Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 3 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 42 2022-11-03

Name

Geoffrey Idelphonce Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Masasi Mjini

Primary Question

MHE. GEOFFREY I. MWAMBE aliuliza: -

Je ni lini serikali itajenga Chuo cha Ualimu Masasi baada ya Chuo cha Ualimu Ndwika kuwa shule ya Sekondari ya Wasichana?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Geoffrey Idelphonce Mwambe, Mbunge Jimbo la Masasi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali ilibadili Chuo cha Ualimu Ndwika kuwa Shule ya Sekondari ya Wasichana kutokana na mahitaji ya wakati huo. Kwa sasa Serikali ina vyuo 35 vya Ualimu vyenye uwezo wa kudahili wanachuo 25,054 ambapo hadi sasa jumla ya wanachuo 22,085 wamesajiliwa. Idadi hii ni chini ya uwezo wa vyuo hivyo katika udahili kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali imeelekeza nguvu katika ukarabati wa vyuo hivyo ili kuweka mazingira wezeshi ya ufundishaji na ujifunzaji. Aidha, Serikali itaendelea kujenga Vyuo vya Ualimu katika maeneo mbalimbali kulingana na mahitaji na rasilimali.