Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 2 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 27 2022-11-02

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. JUSTINE L. NYAMOGA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga bwawa la maji katika Kata ya Nyanzwa kwa ajili ya skimu ya umwagiliaji?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Justine Lazaro Nyamoga, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa Fedha 2022/2023 Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa bwawa na Skimu ya Umwagiliaji Nyanzwa. Aidha, mara baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatenga fedha katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa bwawa na Skimu ya Umwagiliaji Nyanzwa.