Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 2 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 38 2022-09-14

Name

Omar Ali Omar

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Wete

Primary Question

MHE. OMAR ALI OMAR aliuliza: -

Je, wanafunzi wangapi kutoka Zanzibar wamepata mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2020/2021?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia napenda sasa kujibu swali la Mheshimiwa Omar Ali Omar, Mbunge wa Wete kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imekuwa ikitoa mikopo kwa wanafunzi wote wa Kitanzania wenye uhitaji bila kuangalia mwombaji anatoka upande upi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, takwimu za mwaka 2020/2021 zinaonesha kuwa wanafunzi Watanzania wapatao 1,492 wanaosoma katika taasisi sita za elimu ya juu zilizopo Zanzibar walipangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 5.3. Aidha, kwa mwaka 2021/2022 jumla ya wanafunzi wa Tanzania 1,929 wanaosoma katika taasisi za elimu ya juu Zanzibar walipangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 5.8. Nakushukuru.