Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 2 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 21 2022-09-14

Name

Zaytun Seif Swai

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza: -

Je, Serikali inatoa kauli gani juu ya sintofahamu ya utaratibu wa kuwapata wanafunzi wanaorudishwa masomoni?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa Mwongozo wa Februari, 2022 wa kuwarejesha wanafunzi waliokatisha masomo katika elimu ya msingi na sekondari kwa sababu mbalimbali ili waweze kukamilisha mzunguko wa elimu katika ngazi husika.