Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 4 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 63 2022-09-16

Name

Jesca Jonathani Msambatavangu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza: -

Je, Serikali ipo tayari kuanzisha shule maalum kikanda ili kusaidia watoto walioathirika na ukatili wa kijinsia?

Name

Dr. Dorothy Onesphoro Gwajima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jesca Jonathan Msambatavangu, Mbunge wa Iringa Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kuwasaidia Watoto manusura wa ukatili, ambapo imeweka mifumo mbalimbali ikiwemo; Kamati za Jamii za Ulinzi wa Wanawake na Watoto; Madawati ya Jinsia kwenye Vituo vya Jeshi la Polisi na Magereza; Vituo vya Mkono kwa Mkono kwenye Hospitali; Madawati ya Jinsia Vyuo Vikuu na Kati; Madawati ya Ulinzi wa Watoto Shule za Msingi na Sekondari; pia Nyumba Salama kwa ajili ya Manusura kupata huduma jumuishi.