Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 4 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 60 2022-09-16

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO K.n.y. MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga uwanja wa ndege wa Omukajunguti?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Florent Laurent Kyombo, Mbunge wa Nkenge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ina mpango wa kujenga Kiwanja kipya cha Ndege katika eneo la Omukajunguti, mkoani Kagera ili kuwezesha ndege kubwa ziweze kuruka na kutua.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo basi, utekelezaji wa mradi huu utaanza kwa kadri ya upatikanaji wa fedha baada ya Serikali kukamilisha taratibu za utwaaji wa ardhi na ulipaji wa fidia. Ahsante.