Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 5 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 76 2022-09-19

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaondoa wananchi waliovamia Msitu wa Bondo uliopo Kata ya Mswaki, Kijiji cha Mswaki?

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Omari Mohamed Kigua, Mbunge wa Kilindi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nyakati tofauti Hifadhi hii imekuwa ikivamiwa kwa ajili ya shughuli za kibinadamu zikiwemo kilimo, makazi na kuchungia mifugo. Hadi sasa, Serikali imeweka matangazo ya kuwataka wavamizi wote kuondoka ndani ya Hifadhi hiyo ya Bondo kwa hiari yao ifikapo tarehe 30 Desemba, 2022.