Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 87 2022-09-20

Name

Daimu Iddi Mpakate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kupandisha hadhi barabara ya Tunduru – Namasakata – Misechela kuwa ya Mkoa?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Daimu Iddi Mpakate, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007 na Kanuni zake za Mwaka 2009, imeainisha vigezo na utaratibu wa kupandisha au kuteremsha hadhi barabara toka daraja moja kwenda daraja lingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Rais, TAMISEMI inaielekeza Halmashauri ya Wilaya Tunduru kupitia TARURA kufuata utaratibu huo ili kuiweka barabara hiyo katika mpango wa kupandishwa hadhi na kuwa ya Mkoa.