Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 86 2022-09-20

Name

Hamida Mohamedi Abdallah

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Lindi Mjini

Primary Question

MHE. HAMIDA M. ABDALLAH aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatoa fedha kutekeleza mradi wa ujenzi wa soko kuu na stendi ya mabasi Lindi Mjini?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hamida Mohamed Abdallah, Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023 imejumuisha mradi wa soko kuu na stendi kwenye Mpango wa TACTIC unaojumuisha Halmashauri 45 ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ipo katika awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi huo inayohusisha Halmashauri 15 zinazotarajiwa kuanza Januari, 2023.