Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 8 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 131 2022-09-22

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaifanya elimu ya sekondari kuwa ya lazima?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Husna Juma Sekiboko, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inafanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 kwa lengo la kuiboresha elimu yetu ili iweze kukidhi mahitaji ya sasa na baadaye.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali ipo katika hatua ya kupokea na kuchambua maoni ya wadau kuhusu Sera ya Elimu, hivyo suala la elimu ya sekondari kuwa ya lazima itategemea maoni ya wadau na mahitaji ya wakati. Rasimu ya kwanza ya Sera ya Elimu inatarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2022. Nakushukuru.