Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 8 Sitting 1 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 17 2022-09-13

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Primary Question

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA aliuliza: -

Je, ni lini ujenzi wa Chuo cha VETA unaoendelea Wilayani Mkinga utakamilika?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Sayansi na Teknolojia, naomba sasa kujibu swali la Mheshimiwa Dunstan Luka Kitandula, Mbunge wa Mkinga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kukamilika kwa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Mkinga pamoja na vyuo vingine ili viweze kutoa mafunzo yatakayowawezesha vijana wetu kujiajiri na kuajiriwa. Kwa sasa ujenzi wa Chuo hiki upo katika hatua za mwisho za ukamilishaji ambapo ujenzi umefikia asilimia 95. Ujenzi wa Chuo hiki unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Disemba, 2022. Hivyo, Chuo hiki kinatarajiwa kuanza kutoa mafunzo ya muda mfupi kuanzia mwezi Oktoba, 2022 na mafunzo ya muda mrefu mwezi Januari, 2023. Nakushukuru. (Makofi)