Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 4 Sitting 6 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 78 2021-09-07

Name

Haji Makame Mlenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chwaka

Primary Question

MHE. HAJI MAKAME MLENGE aliuliza: -

Je, ni lini Kituo cha Polisi cha Chwaka kitapatiwa gari ili kutimiza majukumu yake kwa ufanisi zaidi?

Name

George Boniface Simbachawene

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibakwe

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Haji Makame Mlenge, Mbunge wa Chwaka, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi linatambua uhitaji wa magari katika Kituo cha Polisi cha Chwaka kama nyenzo ya kutendea kazi. Kupitia mkataba wake na Kampuni ya Ashok Leyland Jeshi la Polisi linategemea kupokea magari 369 toka Serikalini. Pindi magari hayo yatakapofika, kipaumbele kitatolewa kwa maeneo yote ya vituo vya polisi ambavyo havina magari kikiwemo pia Kituo cha Polisi Chwaka.