Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 3 Sitting 55 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 456 2021-06-21

Name

Anastazia James Wambura

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA aliuliza: -

Je, ni lini ujenzi wa shule za sekondari utaanza katika kata zisizo na shule za sekondari nchini ili kuendana na mpango wa Serikali wa kuhakikisha kila kata inakuwa na shule ya sekondari?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anastazia James Wambura, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari itajenga shule mpya 1,000 za sekondari za kutwa nchini kwa kuanza na ujenzi wa shule za sekondari kwenye Kata zote ambazo hazina shule za sekondari. Mradi huo unatakelezwa kwa awamu, na katika Mwaka wa Fedha 2021/2022 Serikali imetenga shilingi bilioni 220 kujenga shule 310 mpya za sekondari za kutwa nchini.