Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 3 Sitting 52 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 434 2021-06-16

Name

Nicholaus George Ngassa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igunga

Primary Question

MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA Igunga?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nicholaus George Ngassa, Igunga kama ifuatavyo: -

Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Igunga ni miongoni mwa vyuo 29 ambavyo vinaendelea kujengwa. Ujenzi wa Chuo hiki unaendelea vizuri na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai, 2021. Aidha, mchakato wa ununuzi wa mitambo na zana za kufundishia unaendelea sambamba na ukamilishwaji wa chuo hiki. Ujenzi wa chuo hiki utakapokamilika udahili wa wanafunzi wa kozi fupi utaanza mara moja wakati ule wa kozi ndefu unatarajia kutafanyika ifikapo Januari, 2022. Ahsante.