Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 3 Sitting 36 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 303 2021-05-25

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza:-

Je, Serikali haioni umuhimu wa kusamehe kodi za miaka ya nyuma Taasisi za Dini zilizokuwa zikiendeshwa kwa utaratibu usiolenga kupata faida na kuziwekea utaratibu Taasisi hizo kuanza kulipa tangu walipojulishwa kutakiwa kulipa kodi?

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Wa Ardhi, Nyumba Na Maendeleo ya Makazi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Joseph George Kakunda, Mbunge wa Sikonge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika kudhibiti na kukabiliana na ujenzi holela mijini wizara imeandaa program ya utambuzi upangaji na umilikishaji wa ardhi yote katika kipindi cha miaka kumi, aidha katika bajeti ijayo wizara kwa kushirikiana na mamlaka za upapangaji imetenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mkakati ya utambuzi na upangaji upimaji na umilikishwaji wa ardhi nchini.

Mheshimiwa Spika, rai yangu kwa mamlaka zote 184 za upangaji kuendelea kutenga bajeti ya kutosha ili kuongeza kasi ya upangaji upimaji na umilikishaji wa ardhi ili kuwa na maeneo mengi yaliyopimwa ili kukabiliana na tatizo sugu la ujenzi holela. Ubunifu wa mbinu mpya ya upimaji ambayo ni shirikishi inayotumia teknolojia rahisi ya simu janja imeongeza kasi na usahihi wa kuimarisha majira nukta kwa kutumia GPS yaani Global Position System.

Mheshimiwa Spika, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2023 maeneo yote yaliyoendelezwa bila kufuata taratibu za ujenzi mjini yawe yametambuliwa na kurasimishwa ambako program ya urasilimishaji ya miaka kumi yani 2013 mpaka 2023 itakuwa imefikia ukomo.

Mheshimiwa Spika, nizitake mamlaka zote za upangaji waongeze kasi ya utambuzi wa maeneo ambayo hayajaendelezwa kwa ajili ya kuyapanga na kuyapima na hivyo ujenzi holela mjini kukoma.

Mheshimiwa Spika, pamoja na jitihada hizi ofisi ya Rais- TAMISEMI pia inatekeleza program ya uboreshaji mfumo wa udhibiti wa ujenzi holela mijini Development Control strategic Program kwa kushirikiana na benki ya dunia. Program hii itawezesha mamlaka zote kuanzia ngazi ya mtaa kusimamia kudhibiti uendelezaji holela na kutoa taarifa za uendelezaji unaokiuka taratibu za ujenzi mijini ahsante.