Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 19 Sitting 5 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 35 2020-04-06

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza:-

Sekta ya Afya nchini inakabiliwa na uhaba wa Watumishi:-

Je, Serikali ina mpango gani wa haraka wa kuziba pengo hili?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi, Mbunge wa Mlalo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuajiri wataalam wa kada mbalimbali za Sekta ya Afya nchini ambapo kuanzia Mei, 2017 hadi Julai, 2019 jumla ya watumishi 8,994 wameajiriwa na kupangwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Aidha, Ofisi ya Rais, TAMISEMI imepewa kibali cha kuajiri Madaktari 610 ambao watapangwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.