Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 19 Sitting 1 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 6 2020-03-31

Name

Asha Mshimba Jecha

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA MSHIMBA JECHA aliuliza:-

Azma ya Serikali ya kuwafikishia wananchi huduma popote walipo ni njema. Aidha, naipongeza Serikali kwa ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi Dunga baada ya jengo la awali kuwa bovu na kuvunjwa.

(a) Je, ni lini jengo hilo jipya litakamilishwa kwa kufanyiwa matengenezo yaliyobaki?

(b) Je, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iko tayari kukipatia Kituo cha Polisi Dunga gari la huduma?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Asha Mshimba Jecha, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Kituo cha Polisi Dunga Daraja C ulianza mwezi Julai, 2018 na ulisimama mwezi Novemba, 2018 ukiwa umefikia hatua ya umaliziaji (finishing) ambayo tathmini yake inakadiriwa kufikia shilingi 49,862,220.

Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi linategemea kupata fedha hizo kutoka katika Mfuko wa tuzo na tozo na zitatumiwa katika mfumo wa nguvu kazi (Force Account).

(b) Mheshimiwa Spika, Kituo cha Polisi Dunga kipo katika Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja. Mkoa mzima una jumla ya magari ya Polisi 17. Wilaya ya kati peke yake ina magari mawili mazima. Jeshi la Polisi limekuwa likigawa magari kwa awamu kwa kadiri yanavyopatikana. Kituo cha Polisi Dunga ni miongoni mwa vituo vitakavyopatiwa magari pindi yatakapopatikana.