Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 15 Sitting 52 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 458 2019-06-25

Name

Hasna Sudi Katunda Mwilima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kusini

Primary Question

MHE. HASNA S. K. MWILIMA aliuliza:-

Vijana wengi wa maeneo ya Nguruka na Uvinza kwa ujumla biashara zao ni pikipiki na Polisi wamekuwa wakiwakamata na kuwatoza faini nyingi vijana hao bila utaratibu:-

Je, Serikali haioni kuwa sasa ni wakati wa kulielekeza Jeshi la Polisi kuacha mara moja kuwasumbua vijana hao wa bodaboda ambao wanajipatia kipato kupitia bodaboda?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hasna Sudi Katunda Mwilima, Mbunge wa Kigoma Kusini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, pikipiki za matairi mawili (bodaboda) na matatu (bajaji) zilianza kutumika kubeba abiria kuanzia mwaka 2008 Tanzania Bara na mwaka 2009 Bunge la Jamhuri ya Muugano wa Tanzania iliridhia vyombo hivyo vitumike kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria.

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua biashara inayofanywa na pikipiki za kubeba abiria na inathamini mchango wao katika kutoa huduma hiyo ambayo imesaidia sana katika kutoa ajira katika mikoa yote Tanzania Bara. Hata hivyo, si wote ambao wanakiuka Sheria za Usalama Barabarani na Kanuni zake.

Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi limekuwa likichukua hatua dhidi ya waendesha bodaboda wote ambao wamekuwa hawazingatii sheria, kanuni na masharti ya leseni za usafirishaji ikiwa ni pamoja na wapanda pikipiki wa maeneo ya Nguruka na Uvinza. Aidha, Serikali imekuwa ikiendelea kutoa mafunzo kwa waendesha bodaboda juu ya matumizi bora ya barabara.