Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 15 Sitting 23 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu 187 2019-05-08

Name

Kiteto Zawadi Koshuma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KITETO Z. KOSHUMA aliuliza:-

Je, Serikali haioni umuhimu wa kuelekeza taasisi zote nchini kuwa sifa mojawapo ya kuajiriwa iwe ni umri wa miaka 21- 35 ili kuwezesha Vijana wengi wanaotoka vyuoni kupata ajira?

Name

Antony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kiteto Zawadi Koshuma, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa mijibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya Mwaka 2004, Kifungu cha 5 kimekataza mtoto chini ya umri wa miaka 18 kuajiriwa isipokuwa katika mazingira maalum yaliyotajwa katika kifungu hiki. Kwa msingi huo, umri wa kuajiriwa ni miaka 18 na kuendelea pamoja na masharti yaliyotajwa katika kifungu cha 5 cha Sheria Na. 6 ya mwaka 2004. Hivyo nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kuendelea kuwahimiza waajiri wote kutii Sheria za kazi na kuhakikiahsa vijana wote wenye sifa wanapomaliza mafunzo yao na kutimiza umri wa kuajiriwa wanaajiriwa kwa kuzingatia fursa zilizopo kwa waajiri na masharti ya kazi husika.