Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 15 Sitting 9 Works, Transport and Communication Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano 71 2019-04-12

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. SELEMAN J. ZEDI aliuliza:-

Je, ni lini ujenzi wa barabara ya Tabora – Mambali – Itobo - Kagongwa yenye urefu wa Kilometa 149 utaanza kujengwa kwa kiwango cha lami? Kwani ni ahadi ya Mheshimiwa Rais na pia imo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015 - 2020.

Name

Eng. Atashasta Justus Nditiye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi Uchukuzu na Mawasiliano, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Selemani Jumanne Zedi, Mbunge wa Bukene, kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza kutekeleza mpango wa ujenzi wa barabara ya Tabora – Mambali – Itobo–Kagongwa yenye urefu Kilometa 149 kwa kuanzia na hatua ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wameingia mkataba na Mhandisi Mshauri NIMETA Consult Ltd. kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Tabora – Mambali – Itobo – Kagongwa kwa gharama ya shilingi milioni 789. Hadi sasa Mhandisi Mshauri amekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na kazi ya usanifu wa kina itakuwa imekamilika kufikia Juni, 2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara baada ya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, gharama za ujenzi pamoja na maandalizi ya nyaraka za zabuni kukamilika, Serikali itatafuta fedha za kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hii. Aidha, wakati kazi ya usanifu ikiendelea, Wizara kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) itaendelea kutenga fedha za matengenezo mbalimbali kwa barabara hii ili iweze kupitika majira yote ya mwaka. Jumla ya shilingi 345 zimetengwa katika mwaka wa fedha 2018/ 2019 kwa ajili ya kazi hiyo. Ahsante.