Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 15 Sitting 1 Education, Science,Technology and Vocational Training, Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi 3 2019-04-02

Name

Susan Anselm Jerome Lyimo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUSAN A. J. LYIMO aliuliza:-

Je, ni fedha kiasi gani zilitumika kujenga mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yajulikanayo kama H.E Magufuli Hostel?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Susan A. Lyimo, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Spika, mradi wa ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yajulikanayo kama Hostel za Dkt. J. P. J. Magufuli ulianza rasmi tarehe 1 Julai, 2016 na mabweni hayo yalikamilika na kukabidhiwa rasmi tarehe 15 Aprili, 2017. Ujenzi huo ulifanywa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kama Mkandarasi na kusimamiwa na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Mheshimiwa Spika, mradi huu uligharimiwa na Serikali kwa kiasi cha shilingi bilioni kumi tu.