Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 12 Sitting 1 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu 02 2018-09-04

Name

Marwa Ryoba Chacha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Primary Question

MHE. MARWA R. CHACHA aliuliza:-
Ili kuinusuru amani ya nchi yetu baada ya Uchaguzi Mkuu ni kuwa na Tume Huru ya uchaguzi:-
Je, ni lini itaanzishwa Tume Huru ya Uchaguzi kwa mujibu wa sheria?

Name

Antony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Marwa Ryoba Chacha, Mbunge wa Serengeti, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 74(1)-(15) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imeainisha na kufafanua kuhusu muundo, majukumu pamoja na uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika utekelezaji wa majukumu yake ya msingi.
Mheshimiwa Spika, tangu kuanzishwa kwa Mfumo wa Vyama vingi vya Siasa nchini mwaka 1992, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeratibu na kuendesha kwa ufanisi chaguzi tano za Rais, Wabunge na Madiwani pamoja na chaguzi ndogo mbalimbali za Wabunge na Madiwani.
Mheshimiwa Spika, kwa muktadha huu, Tanzania tayari inayo Tume Huru ya Uchaguzi.