Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 11 Sitting 18 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Mifugo na Uvuvi 151 2018-04-27

Name

Goodluck Asaph Mlinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ulanga

Primary Question

MHE. GOODLUCK A. MLINGA aliuliza:-
Wilaya ya Ulanga ina ongezeko la mifugo; ng’ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe lakini hakuna huduma za mifugo kama vile majosho:-
Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa majosho?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Goodluck Mlinga, Mbunge wa Ulanga, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inafahamu ongezeko la mifugo katika wilaya mbalimbali nchini ikiwemo Wilaya ya Ulanga inayokadiriwa kuwa na idadi ya mifugo kama ifuatavyo: Ng’ombe 70,000; mbuzi 16,000 na kondoo 6,373.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu imepokea ombi la Mheshimiwa Goodluck Mlinga na kwa kushirikiana na wadau wengine litazingatiwa katika bajeti ya mwaka 2018/2019.