Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 7 Sitting 54 Education, Science,Technology and Vocational Training, Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi 447 2017-06-23

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JULIANA D. SHOZA aliuliza:-
Mkoa wa Songwe ni mpya na unakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Vyuo Vikuu hata vile vya Ufundi.
Je, ni lini Serikali itakuja na mpango wa kujenga hata kampasi ya Chuo Kikuu kimojawapo pamoja na vile Vyuo vya Ufundi?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) hivi karibuni itaanza kutoa mafunzo katika kampasi yake ya Myunga iliyopo Wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe. Vilevile kutokana na gharama kubwa ya uwekezaji inayohitajika katika kuanzisha Vyuo Vikuu pamoja na Vyuo vya Ufundi Stadi, wananchi wanashauriwa kuendelea kutumia Vyuo Vikuu na Vyuo vya Ufundi Stadi vilivyopo nchini.