Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 4 Sitting 8 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 105 2016-09-16

Name

Tauhida Cassian Gallos Nyimbo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAUHIDA CASSIAN GALOSS aliuliza:-
(a) Je, katika bajeti ya mwaka 2015/2016, Serikali imepeleka wanafunzi wangapi kusoma nje ya nchi?
(b) Je, kada gani ambazo zilipewa kipaumbele?

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Tauhida Cassian Galoss, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa masomo 2015/2016, Serikali ilipeleka jumla ya wanafunzi 159 katika nchi za China 84, Algeria 57, Urusi wanne (4), Misri wawili (2) na Uingereza kupitia Jumuiya ya Madola 12.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inapeleka wanafunzi nje ya nchi kwa kuzingatia vipaumbele vya Taifa ambavyo ni masomo ya sayansi, teknolojia na TEHAMA. Hivyo wanafunzi wanaopelekwa nje ya nchi husoma shahada ya kwanza, uzamili na uzamivu katika fani za nishati na madini; mfano masuala ya gesi na mafuta, mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, uhandisi, afya na sayansi shirikishi, usanifu majengo, elimu, uchumi na mawasiliano.