Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Charles John Mwijage (67 total)

Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa hii ya kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Rais.
Awali ya yote, nachukua fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza wananchi wa Wilaya ya Muleba Kaskazini, Jimbo la Muleba Kaskazini kwa kunichagua, lakini zaidi namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwa na imani na mimi kunikabidhi Sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Sekta ambayo ndiyo inabeba kazi kubwa ya sehemu ya kwanza ya Awamu ya Tano ya Serikali yake.
Mheshimiwa Naibu Spika, dhima ya sehemu ya kwanza ya Awamu ya Tano ni kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya uchumi na maendeleo ya watu. Ndiyo kazi ambayo tumepewa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama walivyochangia Waheshimiwa Wabunge, viwanda vitajengeka, lakini nani atajenga? Wabunge tuna nafasi ya mbele, kila Mtanzania ana jukumu na injini kubwa ya kujenga viwanda ni sekta binafsi.
Niwahakikishie, Serikali ya Mheshimiwa Rais amesema itaweka mazingira bora na hiyo ni moja ya kazi ambayo amenikabidhi mimi. Ukisoma taarifa ya Doing Business 2016, Tanzania tumewekwa mahali pabaya, hali siyo nzuri. Bado njoo kesho zipo. Hiyo ni kazi ambayo nitaisimamia na mimi ni tarishi mkuu. Nitatembea Wizara zote, Idara zote, kuhakikisha kwamba wafanyabiashara, wawekezaji, wenye viwanda, wanatendewa sawa na kwa haraka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini tunakwenda kwenye viwanda? Kwa nini tunatoka kwenye uchumi wa uchuuzi? Sifa moja kubwa, viwanda vinatoa ajira kubwa sana. Tuna matatizo na vijana kwa sababu hatuwapatii ajira na Mheshimiwa Rais ameshatoa maelekezo. Nimepewa matrix mezani kwangu, nimeambiwa kila Mkoa kiwanda gani kiende; kila siku natafua wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna maeneo matatu tunayolenga; kuna viwanda vilivyopo sasa nchini, tutahakikisha vinafanya kazi na nitaondoa vikwazo vyote kama tarishi mkuu. Vile vile kuna wawekezaji wa ndani na nje wanaotaka kuwekeza, mimi ni mtumishi wenu, nitahakikisha nawatendea zaidi mnavyopenda ili muweze kuwekeza ili kutengeneza ajira nyingi, lakini nisiwafiche, muweze kuchangia kwa kutulipa kodi ili tuweze kupata maendeleo ya Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, namba tatu, kuna suala ambalo Mheshimiwa Rais amelizungumza kwenye hotuba yake kuhusu viwanda vilivyobinafsishwa. Kuna watu wanasema Mwijage ametoa maelekezo miezi sita sijui wafanye nini. Siyo miezi sita, amri ilishatolewa ya Treasury Registrar, wote mliopewa viwanda mwende mjisalimishe, ueleze hicho kiwanda unakifanyia nini. Niwaeleze, watu wasiwe na mtazamo hasi, siyo kweli kwamba viwanda vyetu vinafanya vibaya, hapana!
Mheshimiwa Naibu Spika, Breweries ilibinafsishwa, inalipa shilingi bilioni 400 kwa mwaka kama ushuru. Mbeya Cement inalipa shilingi bilioni 38 kwa miaka mitano, inafanya vizuri, inakwenda kuzalisha tani milioni moja ifikapo mwisho wa mwaka; na mwezi ujao nakwenda kufungua kinu kipya cha kuongeza usalishaji. Twiga Cement inafanya vizuri, lakini Moro Polister ilikuwa inazalisha kilometa 16 za urefu wa nguo leo inazalisha kilometa 60. Fikiria kilometa 60 ya nguo. Kwa hiyo, tusiangalie upande hasi na upande chanya upo. Aidha, kuna mazingira yasiyokuwa sawia kwa wawekezaji wa ndani, wanazidiwa na vitu vinavyotoka nje. Nitahakikisha kwamba mnatendewa haki ili tuweze kufanya kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimesema Tanzania halitakuwa dampo la taka, substandard products hazitaingia nchini na nitasimamia. Nimemwambia Manager wa TBS ukae standby mimi na wewe tunafanya kazi sahani moja. Ndugu zangu tutahakikisha vipyeo vinakuwa sawia. Mtu analeta mzigo umejaa kwenye meli, anasema nimeleta nusu, amharibie kazi Mzee Mpango. Nitakusaidia kufanya kazi hiyo Mzee Mpango, kwa sababu ndiyo kazi niliyoanzanayo. (Makofi)
Mtu analeta finishing product anasema siyo finished product kusudi ampige magoli Mzee Mpango. Mjukuu wangu nitahakikisha mambo yanakuendea vizuri, kwa sababu hiyo ndiyo kazi ya taaluma yangu. Tutahakikisha uwanja wa ushindani upo sawa kusudi watu wafanye biashara. Watanzania wengi wameshindwa kufanya biashara kwa sababu uwanja wa ushindani haukuwa sawia.
Kwa hiyo, ndugu zangu Watanzania nitawaletea matrix, yule anayejua nini faida ya kwao ya kiwanda, aje aniambie. Shemeji yangu nikwambie, usiwe na wasiwasi, kiwanda cha mbolea kinajengwa Mtwara na wawekezaji wanagombania Mtwara.
Mheshimiwa Naibu Spika, niwatoe mashaka, watu wanaosema Bagamoyo isijengwe Bandari, Bagamoyo siyo Bandari, ni Bagamoyo Special Economic Zone. Ni zaidi ya Bandari! Kuna mji unajengwa Bandari square kilometer 100. Nimekwenda pale na nimewaagiza, Bandari mtengeneze kitu kinaitwa wet port kusudi meli zitakazokwenda kuvua, zikija zing‟oe pale Bagamoyo tuweze kufanya vitu vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitachangia zaidi kwenye Mpango. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa Fedha 2016/2017
WAZIRI WA VIWANDA BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kukushukuru kwa dhati wewe binafsi, ninamshukuru Mheshimiwa Spika na Naibu Spika, kwa kuongoza na kusimamia vema Mkutano huu wa Bajeti na mahususi majadiliano ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji kwa mwaka 2016/2017.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawashukuru pia Waheshimiwa Wabunge wote kwa usikivu na uchangiaji makini kwa hoja za maandishi na kwa kuzungumza katika Bunge lako Tukufu. Natambua na kuthamini dhamira na nia njema iliyotawala mjadala ambao kimsingi ulilenga kuboresha mikakati na mbinu za kisekta zitakazotekelezwa katika mwaka wa 2016/2017.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekee naishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, chini ya Mwenyekiti Mheshimiwa Dkt. Dalaly Kafumu, Mbunge wa Igunga, Makamu wake Mheshimiwa Vicky Paschal Kamata Likwelile, Mbunge wa Viti Maalum kwa ushauri na mwongozo ambao umechangia katika kuboresha mipango ya kuendeleza sekta hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru pia Mheshimiwa Anthony Calist Komu, Mbunge wa Moshi Vijijini, Waziri Kivuli wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa maoni yenye kulenga kujenga, kutoa chachu na hivyo kupanua mawazo katika kuinua ufanisi wa sekta hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa pongezi nyingi za utendaji wa Wizara na taasisi zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge. Sisi kama Wizara tunaahidi kuendeleza jitihada zetu ili kuleta mafanikio endelevu. Aidha, tumepokea ushauri na michango mingi yenye chachu na changamoto ambazo kwetu tunazichukulia kuwa fursa muhimu katika kuleta maendeleo endelevu kwa sekta ya viwanda, biashara, masoko, viwanda vidogo sana, viwanda vidogo, viwanda vya kati na viwanda vikubwa na uwekezaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mawasilisho haya yanatambua na kuzingatia pia, hoja mbalimbali za Sekta yangu yaliyojitokeza wakati wa kujadili na kupitisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais na Makamu wa Rais na pia Wizara zilizonitangulia kuwasilisha bajeti zao hapa Bungeni. Napenda kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge kuwa, ushauri wenu na maelekezo ya Bunge hili katika kujadili bajeti ya sekta hii, tutayazingatia na kuyafanyia kazi ikiwemo kutoa mrejesho na utekelezaji wake.
Aidha, kutokana na muda mfupi nilionao katika kuhitimisha hoja za bajeti hii, maelezo na majibu ya kina ya michango mbalimbali yameandaliwa na yatawasilishwa rasmi kabla ya bajeti ya Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijajielekeza katika kujibu na kufafanua hoja mbalimbali zilizojitokeza napenda kutambua michango ya jumla ya Waheshimiwa Wabunge 117 ambapo kati yao Wabunge 64 wamechangia kwa kuongea moja kwa moja hapa Bungeni na Waheshimiwa Wabunge 53 wamechangia kwa maandishi, ahsante sana msiondolewe hapo.
Baada ya maelezo hayo naomba sasa nijielekeze katika kujibu na kutoa maelezo kwa hoja mbalimbali zilizojitokeza wakati wa mjadala wa bajeti hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo ambayo napenda niyakatae, niweke kumbukumbu sawa! Wizara yangu tangu nikabidhiwe, siwasemei walionitangulia, it is not business as usual. Wizara yangu tangu nikabidhiwe kuna mabadiliko na hata Mzee Komu nikutume Mheshimiwa Dkt. Komu, nenda kamuulize Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation kwamba Mheshimiwa Mwijage mnamuonaje?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimezungumza katika mambo yatakayotekelezwa kwamba nitapigana kufa na kupona kuhakikisha Watanzania wote wanashiriki kwenye uwekezaji, this is not business as usual! Nimekaa na wataalam wangu, nina Profesa mmoja nguli wa uchumi, nina Profesa mmoja ana Ph.D. ya Uhandisi, mainjinia na wataalam wengine. Tumefanya kazi, ngoja niwaoneshe. (Kicheko/ Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mkakati, ngoja niwaambie bwana! Wanasema mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Nimesimamia mimi na wataalam wangu tumetengeneza mkakati ambao Mheshimiwa Bashe anaulilia unaitwa Cotton to Cloth Value Chain Strategy, mkakati huu kazi nimeimaliza tarehe 2 Mei, Mheshimiwa Kabwe Zitto nihurumie nimefanya kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimetengeneza Mkakati tarehe 2 Mei nimeuzindua, nimesafiri usiku kuja hapa. Mkakati unaitwa Sunflower Sector Development Strategy. Natoa maelekezo Wizara yangu naomba mlete mikakati hii muiweke kwenye pigeon holes kabla Waziri wa Fedha na Mipango hajawasilisha, watu wanafanya kazi! it is not business as usual any more. (Makofi)
Mheshimiwa Mweyekiti, tumetengeneza Mkakati unaitwa Leather Sector Development Strategy. Mheshimiwa Mabula anapozungumza kiwanda cha Leather cha Mwanza, nimekwenda Kashenamboni nikakuta kiwanda kile ambacho ukikiangalia unamkumbuka Mwalimu, mtu anaweka makatapila na matrekita, inatia uchungu. Nimetengeza mkakati wa ngozi. Nimemfuata mwekezaji wa ngozi ambaye alikuja hapa akizungushwa, amekwenda kuwekeza Kigali. Nambembeleza arudi hapa mnasema sijafanya kazi. it is not business as usual. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja niwaambie, unajua kuna mambo unapaswa kumwambia mtu usije ukamwambia mtu wa kwetu kwamba hufanyi kazi au hujaenda shule. Ukitaka kumuudhi mtu wa kwetu mwambie hujaenda shule, ndiyo maana nimekuja na mambo haya, ngoja niwaeleze, tumetengeneza mkakati, huu ni mkakati unalenga watu wa Lindi, Value Chain Road Map for Pulses, tarehe 2 Mei, ninao wafanyakazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru Mheshimiwa Faida, naingia saa mbili ofisini natoka saa nne usiku, is not a matter of writing, watu wanaumia na ndiyo maana Mheshimiwa Rais, akaweka Makatibu wawili wote ni nguli. Tunazungumza usiku na mchana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja niwaambie it is not business as usual tumemshawishi mwekezaji toka Singapore, tarehe 23 mwezi wa kwanza nilikwenda Morogoro katika mradi wa AGOA nilikuta watu wa Mazava wanahangaika, hawana mahali pa kufanyia kazi, nikawauliza nikiwapa eneo mtafanyaje, wakasema tutaajiri watu 7000.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimezindua eneo la Star City Economic Zone, ninatengeneza shed tatu, kuna watu wako tayari ku-rellocate kutoka China na Pakstani kuja kuwekeza katika sekta ya nguo, wewe unasema business as usual, haiwezekani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kulisema hilo, niende kwenye suala la pili ambalo nasema na lenyewe siyo sawa. Watu wanasema hatuna mikakati, aah! Mikakati tunayo, kuna mkakati mwingine mdogo unaitwa Development Strategy for Tanzania Textile and Apparel February 2016, italetwa brother Chei. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, we trying to do everything, soma mkakati wa Integrated Industrial Development Strategy 2025, soma hotuba yangu page 24 imeeleza tutafanya nini. Tutawekeza kwenye fertilizer na kwenye petrochemicals. Nimjibu Mheshimiwa Hawa Ghasia, Ferrostaal sasa hivi wako na matarajio, wako Kilwa wanaangalia kujenga kituo cha kuunganisha gesi, kutengeneza mbolea ya gesi kwa kushirikiana na Minjingu. Mtu wa HELM A.G. ambaye anategemea kuwekeza Msanga Mkuu matatizo yake kwa nini hajaanza ni kwa sababu anataka uthibitisho wa maandiko kwamba gesi itapatikana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshatoa suluhisho la kitaalam na gesi itapatikana, mamlaka zitaamua na watu wa Mtwara mtatengeneza mbolea. Waheshimiwa Wabunge niwaambie mambo ya Mtwara, mbolea ya Mtwara ikianza zinazalishwa tani nyingi za mbolea, tutaweza kupata mbolea, muwe na subira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nichukue fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Hawa Ghasia Mbunge wa Mtwara Vijijini. Mheshimiwa Mbunge huyu nilikwenda Misri nilimwakilisha Mheshimiwa Rais kwenye business forum, Business for Africa, nikakutana na mwekezaji anataka kutengeneza Kiwanda cha sulphur, nikamwambia nitampa kiwanja bure yule mwekezaji. Kiwanja mimi Mtwara nimekipata wapi. nikazungumza na Mbunge Mheshimiwa Hawa Ghasia ametoa eneo ambako huyu mwekezaji ataweka kiwanda. Mwekezaji huyu ametoka Misri, amepanda ndege, amekuja hapa, asubuhi ameonekana. Mheshimiwa nakuomba na katika Mstari huo hayuko peke yake, Mheshimiwa Bashe ametoa ekari 200 Nzega kujenga Special Economic Zone. Mheshimiwa Prosper Mbena ametoa eneo Morogoro Kusini. Waheshimiwa Wabunge tufuate namna hiyo, tutengeneze maeneo tutaweka utaratibu wa kuyaendeleza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuzungumza hayo yaliyokuwa yananikereketa, ngoja niendelee kujibu hoja zenu. Eeee! Mtu hawezi kusema we are trying to do everything, we will end up doing nothing, siyo kweli. Katika mkakati tumezungumza ni mbolea, ni mazao ya kilimo, halafu niwaeleze, ukisoma page 24 na ukasoma jedwali namba 16(c) inaeleza na nichukue fursa hii nimpongeze Mheshimiwa Nsanzugwanko na Mheshimiwa Nswanzugwanko usimame uwaambie watu kama siyo mimi Kigoma Sugar, mradi wa kulima miwa kwa ajili ya kiwanda cha sukari ungeanza?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nazungumza sukari soma jedwali namba 16, wananchi wa Mbeya kuna mtu ametoka Marekani anataka kuweka kiwanda wanamzungusha, nimesharipoti kwenye mamlaka. Anataka kutengeneza tani nyingi za sukari halafu unasema you are trying to do everything, you end up doing nothing, usiniambie hivyo siwezi kukubali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa twende kwenye majibu ya jumla. Hakuna tofauti ya takwimu, Mheshimiwa Komu hakuna tofauti ya takwimu. Mheshimiwa Komu, Waziri mwenzangu lakini wewe ni Kivuli, hapa mwenzako aliyetoa hoja ndani ya Kamati yenu, tulipoletewa pesa nyingi kwenye General Tyre hoja ilitolewa na amerudia hapa. Ninyi ndiyo mlimwambia toa pesa hizi, nenda mkajitafakari muweke pesa zinazostahili. Tukatoka kwenye mamilioni yaliyopangwa tukabakiza shilingi milioni 150.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo General Tyre ninachokwenda kufanya nitaleta watafiti nguli waanze General Tyre kwa mtazamo mpya ikiwemo mawazo ya Mheshimiwa Lema, amesema hapa mmemsikia. Sasa Mheshimiwa Komu kuna mtu mmoja ameniambia kwamba Mheshimiwa Komu alipokuwa akisoma ile speech ukimwangalia inaonekana mambo aliyokuwa anasoma alikuwa hakubaliani nayo. Haya ulikuwa hukubaliani nayo. (Makofi)
Kwa hizo takwimu Kamati ni kwamba ilipanga milioni 150, huwezi kujenga kiwanda cha General Tyre kwa shilingi bilioni mbili. Ameshatangaza tajiri namba moja Social Security zote amesema Arusha nenda muone Waziri wa Viwanda awaambie pesa zenu mtaweka wapi muache kutengeneza majengo tu.(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Kivuli mwenzangu, huwa unanishauri na unayonishauri hapa uyasemi. Ananishauri vizuri sana huyu lakini akija hapa anabadilika, kwa hiyo mimi sina matatizo nayo, takwimu zangu ziko sawa sawa. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda tunavyolenga vipo page 24 nimeshavisema na vimezungumzwa kwenye Integrated Industrial Develoment Strategy. Hakuna kitu chochote ambacho hatukusema. Kama alivyosema pacha wangu kwamba ukitaka mali utaipata shambani, lakini ili upate tija yapitishe kiwandani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake nini, anakuja ndugu yangu anasema Mwijage unataka kujenga viwanda kila mahali, ndiyo nataka kujenga viwanda kila mahali. Sifichi, wala sipepesi macho nitavijenga kila mahali. Kiwanda cha kuchakata asali ni dola 40,000, Tabora ni asilimia 36 tu ya asali ya Tabora inachakatwa. Mimi hapa nina order za asali kwenda Oman, siwezi kuzipata. Katavi asali yenu yote haichakatwi. Ni Mbunge gani anaweza kwenda benki kukopa dola 40,000 akanyimwa. Nani anaweza kunyimwa? Nakushukuru, unajua tatizo la Mheshimiwa Lema anachangia mambo mazuri ukiondoa yale aliyoyafuta halafu anatoka nje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nunua kiwanda watakukumbuka. Uzuri wa viwanda, kwa nini mimi napenda viwanda vidogo, unaweza kufanya biashara ya apples au mvinyo wa zabibu, meli ikifika Dar es Salaam unauza kontena bila kuliona, unaweka pesa yako hapa unakwenda Kilimanjaro unashusha mvinyo. Lakini ukitengeneza kiwanda wewe mwenyewe unafaidi na jirani anafaidi. Ndiyo maana Mheshimiwa Magufuli anasema tujenge viwanda, ufaidi wewe mwenye mtaji na jirani afaidi. Mama nipigie makofi umeipenda hiyo. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye kujenga viwanda hakuna itikadi, kwa hiyo tutajenga viwanda vidogo sana na tutajenga viwanda vya kati. Niwasimulie mfano mtakaupenda tena niwaambie ninyi rafiki zangu, Mheshimiwa Lema, ame-order kiwanda cha toothpick kwa ushauri wangu dola 28,000, ame-order kiwanda cha Tomato Souce kwa ushauri wangu, anataka kufuga samaki, mimi nina kiwanda cha kutengeneza chakula cha samaki, the best in this country. Msiogope kumiliki, watu wanaogopa kumiliki, mtu ana malori, anayaficha eti siyo ya kwangu, useme! tatizo ni kwamba uliyapataje? (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo, kwa hiyo ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge mhamasishe watu wetu na tutajenga viwanda. Mheshimiwa Jitu Soni ninakushukuru pia. Mheshimiwa Jitu amesema kujenga Petrol Station moja ni milioni 700, hivyo ni viwanda vingi, mimi nimetoka kwenye oil industry, nawashawishi sasa wale nguli wa oil industry watoke na kundi la kwanza nalipekeka kwenye maziwa. ASAS ni nguli wa petrol amashakwenda kwenye maziwa, Oil com ameshakwenda kwenye maziwa, na nitakwenda kwa Mheshimiwa Lukuvi, Waziri wa Ardhi, ndiyo maana nikamshukuru, nataka kuomba maeneo ya ile nuclear farm kusudi tutengeneze farm. Nina ajenda ya kwenda Musoma, nimekuwa namfuata kila siku Mheshimiwa Vedastus Mathayo Manyinyi, kuna shamba la Utege ili kusudi tutengeneze maziwa. Mnaweza mjiamini, mnaweza Waheshimiwa Wabunge na muwaambie wapiga kura wenu wanaweza, msipothubutu ninyi waliopo nyuma yenu hawataweza kwenda kwenya uchumi wa viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekti, kwamba fedha uliyopangiwa ni kidogo, katika maazimio yangu ambayo nitayaboresha kumridhisha mjukuu wangu Mbunge wa Kigoma amesema uyaboreshe babu, nikasema nitayaboresha. Nitamuwekea kile anachopenda afurahi. Sasa mjukuu kama anapenda kitu mpe.
Katika maelezo yangu nimesema viwanda vitajengwa na sekta binafsi. Kitu kingine niwaambie, maelekezo ya Mheshimiwa Rais anasema tunaanza na viwanda vilivyopo, vizalishe maximum capacity. Kwenye ripoti yangu nimezungumza, viwanda vingi vinazalisha below 40 per cent.
Mheshimwia Mwenyekiti, mtu anaishangaa TANELEC, Mheshimiwa Rais alipokwenda Monduli ile ziara ya kwanza ya Jeshi, Mkuu wa Mkoa ambaye na yeye ni mjukuu wangu wa Arusha, akamfuata akamlalamikia TANELEC. Mheshimwia Rais kwa utaratibu wake akamwambia anayeshughulika na viwanda ni Mheshimiwa Mwijage, akaja na watu wa TANELEC. Mimi lile nikalipeleka kwa Mheshimiwa Muhongo, tatizo la TANELEC ni sawa na East African Cable. Tumetengeneza umeme kwa Mpango wa REA II karibu kilometa 45,000 lakini hakuna waya ulinunuliwa hapa, East African Cable inatengeneza cable zile zile, haijauza kwa miezi 36. Lakini huwezi kunilaumu mimi ndiyo naanza sasa nije nione mtu anaziagiza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema katika hotuba yangu kwamba nitakuwa mboni ya kuhakikisha Wizara yoyote, Mtendaji yeyote, Shirika lolote la Umma linalokiuka nitawasemea na mnajua nitawasemea wapi. (Makofi)
Kuhusu mipango ya Wizara haiunganiki siyo kweli, huyu ni Waziri mwenzangu wa Kilimo, ni pacha wangu, hata juzi Mheshimiwa Mtolea wakati tunahangaika namna gani tulipeleke jembe kwenye makumbusho, tumekutana mimi nilikuwa chairman na chini yangu walikuwepo Makatibu Wakuu watano. Wawili kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Makatibu Wakuu watatu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Tunajadili namna gani tunaweza kupata zana za kilimo, kuzitoa huko tuzitoako, kwa riba nafuu, tukapeleka kwenye vituo ili kusudi jembe libaki kwenye bendara ya chama na watakaokwenda makaburini mlikute basi mambo yawe mazuri Mheshimiwa Mtolea.
Kwa hiyo usiwe na wasiwasi, tunafanya kazi kwa kuunganisha Wizara, lakini kama alivyozungumza mrithi wangu Mheshimiwa Kalemani ni kwamba mimi bila nishati sifanyi lolote, bila barabara sifanyi lolote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wachumi mnaelewa. Kuna kitu kinaitwa production cost na transaction cost. Transaction cost ni zile gharama za miundombinu, unaweza kuzalisha kwa gharama ndogo lakini kama usafiri ni mbaya bidhaa itafika sokoni imeshakuwa mbaya. Ninawategemea watu wa miundombinu na tunafanya kazi wote na ndiyo maana wanasema bajeti ya viwanda ni trilioni 29 kwa sababu sasa tunatengeneza mazingira wezeshi. Miundombinu wezeshi, ni pamoja na maji umeme, barabara na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mradi wa Bagamoyo. Bagamoyo haiwezi kufanya kazi mpaka Kidunda ifanye kazi, litatatengenezwa birika lingine la kuchuja maji, kwa hiyo we are connected, we are related and intergrated. Kwa hiyo, kwamba hatuna mahusiano, hatukuunganika haiwezekani, brother. Mheshimiwa Rais, ana Mawaziri 19 kwenye cabinet, anatuona na ana simu zetu kila wakati tunazungumza, sisi ni timu moja inayokwenda kwa kasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini miradi ya Mchuchuma na Liganga, Engaruka Soda, General Tyre, miradi ya Ngaka inaitwa kuwa ni miradi ya kimkakati. Akaniuliza rafiki yangu, ninampenda sana Mheshimiwa Hussein Bashe, ana michango ya kiuchokozi, amenikumbusha zama zangu nikikaa pale, nilikuwa na michango ya namna hiyo muulize Mheshimiwa Ngeleja. Nilikuwa naweza kutetemesha microphone, ananiuliza uniambie comperative advantage.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika miradi hii kuna comperative advantage, kuna competitive na absolute advantage zote zimeunganishwa hapo. (Makofi)
Kuhusu General Tyre siyo kwa ufahari, General Tyre sina shida na matairi, nataka General Tyre irudi nyuma ichochee kilimo cha mpira Pemba na Unguja, ichochee Morogoro, ichochee Tanga tulime mpira. Lakini General Tyre tuna advantage, tuna population inayokua vijana wa sasa kila mtu akipata mshahara kwa kwanza anapeleka ile salary slip kwenda kununua gari. Niwaambie nimewahi kuwa Mtafiti Msaidizi wa Benki ya Dunia kuangalia usalama wa barabarani, percent kubwa ya hatari za barabarani zinasababishwa na matairi mabovu.
Mheshimiwwa Mwenyekiti, nimeshwamwambia mtu wa TBS, na nitawaonesha show kama mnapenda show, watu wakienda na video mnasema wanakwenda na video, wasipokwenda nazo mnasema business as usual. Nimemwelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa TBS, tutakagua matairi yote hata kama ni mapya, kama hayana siku ya kutengenezwa na siku ya ku-expire tutakwenda kuyateketeza. Piga makofi na hiyo mbona hampigi makofi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu tuambizane, kwa hiyo General Tyre,
comparative advantage, tuliyonayo tuna watu wanaweza kulima mpira, but the comperative advantage we
have, we have a young population itakayopenda kuendesha magari. That is the comparative advantage,
comparative advantage nyingine tuna ardhi, Mheshimiwa Lema amenipa heka
200. Hauwezi kupata heka 200 Ulaya, utaipata wapi? Kwa hiyo, tutaangalia
comparative, competitive na ikibidi tuangalie absolute advantage. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampenda Mheshimiwa Bashe, nililazimika kwenda kusoma Michael Potter, Tom
Peter na Charles Andy kuangalia hivyo vitu vinazungumzaje. Kwa hiyo hii iko vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mchuchuma na Liganga ina maneno. Tunataka chuma pale, ndicho kiwanda mama.
Lakini chuma ya Liganga inasema ukiweza ku-extract yale madini mengine, unapata faidi nyingine.
Ukasema Mheshimiwa Bashe kwamba kuna makando kando ameyaona CAG. CAG alipokuja kuona makando kando
mimi nilishayaona. Tarehe 23 Januari niliwaita watu wa NDC wakafanya presentation.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya maneno nilikuwa nayasikia nikiwa kijiweni, nikawauliza, Katibu Mkuu
ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa NDC wakati anaanza kazi, akaita timu ya wataalam kutoka nje ya
Wizara yangu, wameandika ripoti nzuri, tutaweka sawa, tuondoe makando kando, lakini mkakati wa
Mchuchuma na Liganga uweze kuendelea. Ukitaka kuujua mradi huu muulize Mheshimiwa Dkt. Dalaly
Kafumu, akueleze, ni mradi muhimu. Lakini kuja kumpata huyu mtu haikuchukua siku moja imechukua
miaka mingi, kuna mtu mmoja mshindani alisema naapa Mchuchuma na Liganga haitafanya kazi, kwa
sababu yeye ana migodi sehemu zingine za dunia hii.

Kwa hiyo tupigane Watanzania, kama mtu atakuwa na makandokando tuyaondoe. Watu wa kwetu wanasema
osangile amazi, oshorome eboga yaani unafukia kinyesi kusudi uchukue mboga uende, ukikataa utakula
chakula bila mboga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini viwanda vilikufa, ngoja niwasimulie mlichangia siku mbili siyo
mchezo. Kwenye kitabu changu ukurasa wa nane aya ya 14, nimezungumza ngoja niende taratibu
mnisikie. Mfumo wa kiuchumi ulikuwa mfumo hodhi, ndiyo maana viwanda vilikufa. Huwezi kununua raw
materials mpaka upewe kibali na Kamati Kuu tumemaliza hiyo sasa ni soko huru. Kutozingatia
viashiria vya nguvu za soko katika kuendesha uchumi wa viwanda, ndiyo maana vilikufa, lakini
msisahau lilikuja lile wimbi la globalization (utandawazi), ule upepo tusingeweza kuuzuia na ninyi
mnajua madhara ya
upepo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana upepo ulitaka kupita hapa, alhamdulillah Mwenyezi Mungu akatuokoa upepo ulikuwa umekuja vibaya, upepo ulikuwa umekuja vibaya kwa hiyo huwezi kuzuia upepo. Mpaka akatokea jamaa mmoja akazuia mafuriko kwa mikono, ni mambo ya ajabu ajabu!
Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu nyingine viwanda vililenga kukidhi mahitaji ya ndani, viwanda vililenga kukidhi mahitaji ya ndani tu sasa tumekataa, ni import substitution cum export promotion, nimesema kwenye hotuba yangu wazalishaji wa Tanzania nitawalinda lakini msibweteke, nitawalinda wasibwete walenge kuzalisha katika soko la dunia, hata tairi tutakazozizalisha zitakuwa zinalenga dunia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni menejimenti ambazo hazikuzingatia ujuzi pamoja na study, na technical know who, iliingia pale. Nataka niwaeleze ninayoyajua bila kuwaficha kitu. Mtoto wa shangazi unampa kazi mambo yanaharibika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuyumba kwa uchumi wa Taifa hili, kulikosababishwa na kuyumba kwa uchumi wa dunia, ukumbuke oil crisis ya miaka 70 lakini msisahau na nichukue fursa hii kuwashukuru Watanzania mliokuja kupigana vita ya Kagera hadithi ingekuwa nyingine, vita ya Kagera ilitusumbua, wengine mikanda haijawahi kufunguliwa, kwa hiyo na yenyewe ilituyumbisha. Viwanda vikayumba tukaingia kwenye mgao wa sukari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwaeleze Watanzania haya mnayajua ila mnataka kujifanya hamyajui. Ujenzi na uendeshaji wa viwanda ulitawaliwa zaidi na matakwa au matashi ya kisiasa bila kuzingatia zaidi nguvu ya soko. Kwa hiyo, viwanda tutakavyovijenga, nimeeleza kwenye hotuba yangu itazingatia upatikanaji wa malighafi, soko na teknolojia, lakini na utulivu. Ngoja niwaambie research moja imefanyika, nazungumza na watu mbalimbali Morogoro iko juu katika disciplined labor force worldwide Tanzania nzima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitawaambia mambo yote disciplined work force Tanzania wanasema iko Morogoro, mtoto wa Kiluguru anashuka na mzigo anapanda na mzigo, anaweza kufanyakazi. Lakini ukimchukua mtu kwenye pool table brother amepiga pool table miaka mitatu, umuweke kiwandani saa sita hajazungumza Simba na Yanga au kigodoro, hawezi kufanya kazi. Habari ndiyo hiyo, tutazingatia mambo yote hayo. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, uwekezaji mdogo, under capitalization mtaielewa hiyo, nalo lilikuwa tatizo, utamaduni wa utegemezi wa wahisani kupita kiasi. Donor over dependence syndrome, mmemsikia Mzee Magufuli, anasema hata kama ugali nakula bila mboga ni wa kwangu. Donor over dependence syndrome amelisema Mheshimiwa Magufuli, kwamba itabidi tutembee kwa nguvu zetu na haya yalituangusha, wanakuletea kiwanda wanachotaka kukuletea siyo kile unachokihitaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mahusiano ya kisekta na uratibu wa Wizara nimeyazungumza sina tatizo nayo, kuna vikao vingi vinahusika, dhana kuwa Serikali haina sera na mikakati endelevu kutoka awamu moja hadi nyingine hapana, wenzangu wamelizungumza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vision 2025, ilipokuwa inaandikwa akiwemo Mheshimiwa Profesa Mark Mwandosya, alikuwa bosi wangu mimi nikiwa Meneja wa gas, nilikuwa namuona anaandika imemalizika 1996, haijaanza leo ni Mzee Mkapa huyo. Tunapozungumza sustainable industry development strategy ya 2011/2015 alikuwa Mzee Kikwete, kwa hiyo kuna uendelevu, kinachowasumbua watu ni kutokusikiliza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisikiliza hizi nyimbo zina mafundisho yake, kwa nini Rais wetu anaitwa tinga tinga? Ni kwa sababu yeye ni kama tingatinga, tingatinga likifanya kazi baada ya masaa fulani hufanyiwa service tena kwa gharama kubwa, likimaliza kufanyiwa service linafanya kazi kama jipya, kwa hiyo wanaona kwamba ni mpya lakini ndiyo tabia ya tingatinga, ametoka service brother kwa hiyo tunachapa mwendo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sera zipo zimeandikwa na zote nimekuja nazo ni hizi hapa, sustainable industry development policy ya 1999 inakwenda mpaka mwaka 2020, Rais alikuwa Mzee Mkapa, ngoja niwaoneshe Integrated Industry Development Strategic ya 2011, Rais alikuwa Mzee Kikwete, kwa hiyo kuna uendelevu, ndiyo tabia ya magari makubwa, likiharibika gari kubwa huwa linafanyiwa service linarudi barabarani utadhani gari jipya, gali kubwa halitupwi, CCM ni gari kubwa, huwezi kulitupa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie SIDO. Wanasema SIDO imetengewa Mikoa mitano tu, hapana siyo hivyo, SIDO haijatengewa Mikoa mitano tu, hiyo Mikoa iliyotajwa ikiwemo Arusha tunaweka vitu vinaitwa incubator. Watanzania wakiwemo wanafunzi watakaoonekana na ubunifu, tutawapeleka pale, watawekwa kiatamizi, wataangalia utaalam wao, Canada na India watatusaidia waki-graduate, tukiona wanaweza wanakwenda mtaani, itakuwa Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, zimeandikwa hapo, kwa hiyo pale ni center.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mikoa yote, nitahakikisha kunakuwa SIDO na niwaambie, najadiliana na TAMISEMI Maafisa Biashara wa Wilaya nataka wapewe mamlaka zaidi siyo kukata leseni tu. Wawe wanawafundisha watu namna ya kufanya biashara na ujasiriamali, waingie hata kwenye mikutano ile ya Halmashauri ile Menejimenti ya Halmashauri waingie pale, wafanye kazi, hakuna kwenda kukusanya leseni, unakusanya leseni biashara mtu ulimfundisha? Hiyo tutaizuia, tukubaliane hapa waende wafanye kazi na SIDO atakuwa coordinator wangu, yaani Meneja wa SIDO wa Mkoa, anaripoti kwa Minister moja kwa moja na mambo yanakwenda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawaagiza SIDO watengeneze catalogue za mitambo yote midogo midogo ya milioni kumi, milioni ishirini, milioni thelathini, muwaoneshe Waheshimiwa Wabunge wakawaoneshe wananchi wao namna ya kuchakata maziwa, asali, kuchakata mihogo, kama ndugu yangu Mheshimiwa Bilago wa Kigoma nimemuonesha mtambo wa kuchakata muhogo, unahitaji shilingi milioni12 unatengenezwa Morogoro pale, unachakata muhogo. Kwa hiyo, ndugu zangu vitu vipo ni jukumu la SIDO.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ya Mchuchuma na Liganga na CAG nimeishaizungumzia.
Kuhusu umuhimu wa NDC katika ujenzi wa viwanda nchini. NDC ni kutambua fursa, mimi bwana mkisema napendelea kwetu basi mtanilaumu tu, nirudi tena kuwapongeza watu wa kwetu Kigoma. Watu wa Kigoma wanafanya kazi nzuri, Waheshimiwa Wabunge wa Kigoma na uongozi wao wa Mkoa wameanzisha utaratibu wametambua kaya laki moja, kila kaya ilime mawese heka moja, watengeneze ekari laki moja na nimewaahidi mniombee nidumu kwenye cheo hiki, nitawaletea wawekezaji wawekeze katika kiwanda cha mafuta ya mawese. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndivyo inapaswa kuwa siyo kazi ya Serikali, kwa hiyo ndugu zangu kazi ya NDC niwaeleze watu wa Kigoma, wako Kibaha - Pwani, wanatengeneza shamba la ekari 4,000 na outgrowers watazalisha tani 60,000, mahitaji ya sasa ya mafuta ni 400,000 wanatengeneza 60,000 nimewaagiza waende Mbeya, nimewaagiza waende Rukwa, nimewaagiza waje Kigoma. Mtaalam wa mbegu za miwese nimeishampata anaitwa Mushobozi, anafanya kazi na Koffi Annan yuko Arusha, aje awatengenezee mbegu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu anakuambia business as usual haiwezekani it is not business as usual, ngoja niwaambie, kuna mambo mawili napaswa niyazungumze nimetulia, moja la rafiki yangu Mheshimiwa Sungura. Mheshimiwa Sungura amezungumza maneno makali. Ubora wa vyakula niwasihi msinunue chakula chochote ambacho hakina alama ya TBS, maneno aliyoyasema Mheshimiwa Sungura siyo ya kuchekea, msinunue chakula ambacho hakina alama ya TBS kwamba mtu anachukua chakula sijui anaugua figo, sijui anakwenda kumsubiri Mungu amchukue siyo habari nzuri, kwa hiyo hilo naisemea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni kuhusu utendaji wa CBE, CBE inasaidia kufundisha vijana wetu, CBE ninaisimamia, CBE nitaisimamia, tuhuma alizozisema ndugu yangu Mheshimiwa Waitara, watu hao waliniletea taarifa Ijumaa ile iliyopita nikazichukua mwenyewe nikazipeleka ofisini, nikampa Katibu Mkuu, nikamwambia mambo ya kufanya. Mambo ya kufanya ni pamoja na kumhusisha CAG, lakini mambo mengine ni ya kimamlaka zaidi, ni ya PCCB ni ya Polisi, nikayaancha kule. Waziri hawezi kwenda kupeleleza, na yule msichana aliyeko gerezani tangu mwaka 2012 aitwaye Rose ni mahabusu siyo mfugwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanasema mahabusu huwa hanyimwi mshahara, mimi sijawahi kwenda shule ya sheria na kwa umri huu sitegemei kwenda kwenye shule ya sheria lakini niwahakikishie kitu kimoja, nitaisimamia CBE.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaambie CBE mnisikie sasa, wasionijua wakawaulize niliosoma nao shule. Nitahakikisha CBE inakuwa shule ya viwango, kuanzia muonekano, ukimuona mwanafunzi wa CBE anapita utasema yule anasoma marketing, yule ni mtawala, hakuna mtepesho, hakuna mtu anavaa kama anakwenda kwenye vigodoro, CBE nitahakikisha naiweka kwenye viwango. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo mengine nimeishaweka wataalam Mheshimiwa Waitara tulia. Tukitoka hapa nitakwenda niwaone wajukuu zangu huko. Suala la kuangua mayai Mheshimiwa Waitara wewe una pesa za kununua incubator, incubator ya mayai ya shilingi milioni 20 inatosha ndugu zangu wa kule, nitasaidiana na wewe kutafuta eneo, tutengeneze eneo katika mpango wa Mitaa Mheshimiwa Waitara mimi sina ugonvi na wewe, kuniacha kwenye chama hiki haujakosea, nitakwenda kushughulikia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kuwashukuru Waheshimiwa Mawaziri waliochangia bajeti yangu. Nimshukuru Mheshimiwa Omary Mgumba, mfano wake wa korosho ulikuwa mzuri sana. Ametoa literature ya korosho, lakini tatizo la korosho watu wa korosho, mimi nimepewa maelekezo na Mheshimiwa Waziri Mkuu, mimi na Mheshimiwa Mwigulu, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi tutakaa chini, matatizo mnayo wenyewe. Wamarekani wametoa order ya korosho tani 15,000 wako tayari kununua kwa bei zaidi ya 40,000 kwa kilo iliyokobolewa lakini kwa masharti, kwamba lazima ikobolewe na wananchi, the poor mnaowatetea
Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria nasikia za Chama chenu cha Ushirika zinakataa, imeishafika kwa Mheshimiwa Mwigulu na ninyi mtaitwa wadau na nimezungumza hata na makampuni yanayohusika ORAM walinifuata, nilizungumza hapa wadau wa korosho walinifuata, tutakaa chini jioni tujadiliane twende mbele. Hii sayansi ya korosho ina mambo mengi, ngoja niwaambie sayansi ya korosho, wameniambia kwamba unaweza ukaona korosho iliyotoka Tanzania tani 150,000 korosho iliyotoka Tanzania India, unakuta ni 250,000 nimeyaona. Kwa hiyo, ukubali Shekhe nakushukuru kwa nipigia makofi, mtu akisema business as usual mkatalie. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye hoja binafsi moja moja, nimeishamshukuru Mheshimiwa Omary Mgumba, lakini kuna watu akiwemo Mheshimiwa Nsanzigwanko, wamezungumzia suala hili, suala la ease of doing business. Kama wazungu wakirudi leo, kutupima kwenye wepesi wa kufanya biashara, Tanzania hali imebadilika, mojawapo ya eneo tulilokuwa tunapimwa ni wepesi wa kupata viwanja vya kuwekeza. Kwenye bajeti yangu nimeshukuru TAMISEMI na Wizara ya Ardhi, wamefanya kazi nzuri. Mimi nimepewa hekta 800 kwa kazi ya Mheshimiwa Dkt. Ndugulile na Mheshimiwa Lukuvi, Dar es Salaam.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeisha mwambia Mheshimiwa Muhongo tutoe bomba la gesi kutoka Mbagala, likatishe moja kwa moja liende Kigamboni. Tunaendelea nahangaika, sasa aliyenichekesha kwenye ease of doing business ni rafiki yangu Mheshimiwa Kubenea, akataka kuzungumza Omukajunguti, akasema nimesoma kitabu chote Mwijage hajazungumza Kagera, usinichonganishe. Watu wa Kagera wanajua kwamba Mwijage alilelewa na bibi yake, na bibi yake Mwijage Mko Omwami alimfundisha hadithi 1002, hadithi moja inasema hivi, bibi yangu aliniambia mwanangu ukiamka asubuhi kwanza unawe uso. Uso wangu mimi ni Kagera na wala simfichi mtu, kwa hiyo Omukajunguti itajengwa, tutaishughulikia Omukajunguti, maua yatatoka pale, ufugaji wa samaki nitajisahauje?
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini utaratibu siyo kukimbilia haya, nataka niondoe kwanza mambo ya kwanza, Bagamoyo wananidai pesa sijazilipa nikachukue Omukajunguti niongeze nitaongeza matatizo. Lengo letu kwenye SEZ tutalipa maeneo tuliyopewa kwanza, tukishamaliza tunatafuta wawekezaji kwenye yale maeneo yenye vivutio, kuna watu wanataka ku-relocate kuja Tanzania. Tunataka tuyachukue yale, tuya-service hata kwa kukopa pesa, pesa tutakazopata twende kwenye maeneo mengine, wengine wanasema Mwijage mmekamata maeneo mengi, we are not aiming for the next election, we are aiming for the next generation. Tunakamata maeneo watakaokuja miaka 50 chama ni hiki hiki, watakwenda kwenye hayo maeneo watajenga. Kwa hiyo ndio mpango mzima. It is not for next election, it is for next generation.(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Vietnam nimewaandikia wana Special Economic Zone 150, lakini Vietnam ni moja ya saba ya nchi yetu. Sasa ndugu yangu mimi naota kesho kutwa, ningependa vijana wakija wakiwa wanaangalia waseme alikuwepo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mheshimiwa Charles John Mwijage. Kwa hiyo hilo nimelijibu kwa hiyo ease of doing business tunaijua, na mojawapo ya ease of doing business ni katika kutoa haki. Mheshimiwa Rais ameliona, ametoa pesa za kutosha katika Mahakama kusudi ipunguze, ninacho hiki kitabu, na nimeagiza kiwekwe kwenye website ya Wizara yangu, utakisoma hiki tunapimwa vipi, lakini ndugu zangu wasikudanganye.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimezungumza na Mmarekani mmoja juzi, baada ya hotuba yangu imejadiliwa nchi nzima, na CTI wameijadili. Mmarekani amenipigia simu akasema Mwijage, yote uliyoandika ni bure nikasema eeh bure. Akasema you didn’t include important element nikamwambia what? Akasema peace, amani yetu inatusaidia kufunika haya mapungufu lakini hatutabweteka, haya mapungufu tutayaondoa, na akaniambia kitu kimoja, Tanzania katika Afrika ndiyo nchi ambayo inatembelewa na Marais wengi wa Marekani wastaafu, hawawezi kwenda mahali pengine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Msigwa nakushukuru sana, kwa hiyo fedha ya General Tyre nimeishaijibu, dira ya maendeleo ya Taifa kuifanya nchi yetu kuwa ya uchumi wa kipato cha kati imetimiza miaka 21 bila mageuzi nimeisha lizungumzia. Kitu kimoja ambacho watu hawaelewi, kuna ule mpango wa kuanzia mwaka 2010, mpaka 2025 kipande cha kwanza ilikuwa ni kuondoa vikwazo. Vikwazo vimeondoka, sasa tunakwenda kwenye kujenga uchumi wa viwanda, tukimaliza tunakwenda kwenye ushindani. Kwa hiyo, kazi imeondoka sasa hapa kama ni ndege tunaanza mwendo wa kupaa, tumeshatenga maeneo, nimewaeleza taarifa za ukweli kuna viwanda vina-relocate, vina-relocate kutoka Asia kuja hapa, someni majedwali yangu nyuma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu niingie Ofisini nimekutana na makampuni zaidi ya 32, kuna kampuni inaitwa Goodwill inakuja Mkulanga, muulize Mheshimiwa Mbunge wa Mkuranga, kuna Kampuni inaitwa Goodwill inakuja Mkuranga, itatengeneza kiwanda cha vigae kitakachozalisha square mita 80,000 kwa siku, production ya mwaka itaweza ku-generate dola milioni 150. Lakini kuna kiwanda ambacho mimi niliwezesha kupata ardhi Mkuranga Mzee Lukuvi nitakushukuru mara mia moja, kile kiwanda kitatengeneza ajira za watu 20,000 Mbunge wa Mkuranga anajua. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sina shamba Mkuranga ndio maana nakwenda kule kwa hiyo kazi inafanyika. Kwamba tumefanya nini, basi tulikuwa tunatoka kwenye runway sasa tunapaa, na tukipaa tunakwenda, kwa hiyo muwe na imani. Lakini nimezungumza kwenye mipango ya kazi yangu, kwamba nawaomba tukubaliane twende safari, asitokee mtu akawa na mashaka. Tukifika njiani mkaona tunapotea mniambie tunapotea na niwahakikishie, hii hotuba na michango yenu, kuna michango imeandikwa ya maandishi inastahili kuandikiwa kitabu. Wale ambao michango yenu itakuwa ina mapungufu, nitawarudishia mui-edit vizuri, nitaweka picha zenu pale na nitaandika majina yenu, mchango wa Mbunge fulani ili kusudi muweze kuona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kuangalia suala la Omukajunguti, nimelijibu, uwanja wa ndege utajengwa Serikali isuke upya taasisi zinazoshugulikia viwanda, biashara na uwekezaji ili kuziba mianya ya ukwapuaji fedha za umma ambazo zingetumika kuendeleza sector ya viwanda, ushauri huo naupokea na nitaufanyia kazi.
Kwa hiyo, mwaka 2016/2017 Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano, haijaweka bayana mkakati wa Serikali wa kufufua viwanda 33 vilivyobinafsishwa na kufa. Ngoja niwaambie, viwanda vilivyopo lazima vifanye kazi, na bidhaa mnaziona madukani, lakini vile vilivyokufa vina njia mbili.
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Ahsante sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vile vilivyokufa vina njia mbili, ama ukirudishe ama ukiendeleze na namna ya kukiendeleza tafuta mbia mwenzako. Kwa nini tunavitafuta ni kwa sababu mikataba ya mauziano inasema hivyo lakini faida nyingine vile viwanda vina miundombinu wezeshi na miundombinu saidizi kuliko kwenda kupasua misitu kuweza kujenga sehemu mpya.
Suala la korosho nimelizungumzia, tutakaa chini tulizungumzie, viwanda vya Mwalimu tutavifufua, Serikali itimize ahadi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, aliahidi wakati wa kampeni kuwa kiwanda cha kubangua korosho kitaanzishwa eneo la Mkuranga. Tutakapomaliza matatizo ya korosho na kile kiwanda kitaweza kufanya kazi. Sunshine wako tayari kutengeneza viwanda wana kiwanda kimoja Mtama, wanataka kwenda Nachingwea wako tayari kwenda kokote, lakini muondoe yale matatizo ya msingi yaliyopo kwenye sekta hiyo.
Serikali iwezeshe vijana wasio na ajira ili wasiwe wanatanga tanga, kwa kushirikiana na TAMISEMI tunatenga maeneo, hapa ni mshukuru Mheshimiwa Azzan Zungu, nakubaliana naye mipango ya kurasimisha sekta isiyo rasmi inafanyika na njia mojawapo ni hiyo. Leo nimezungumza na Mheshimiwa Mangungu wa Mbagala, wameshanitegea eneo, nikitoka hapa nakwenda kukutana na Mheshimiwa Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam tukaangalie eneo tutaanzia pale. Kwa hiyo, Mikoa yote imeshaambiwa kutenga maeneo na tunawalenga Vijana. Watu wa BRELA na TRA tutaangalia namna ya kuondoa mambo ya TIN, kumlipisha mtu kabla ili watu waweze kurasimisha shughuli yao. Tutafuata maelekezo yenu ambayo mmetupa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiwanda cha Kioo Mbagala, nitatoa maelezo kwa kuandika. Katika miaka 1970 NDC imechukua eneo la hekta 350, Mbunge wa Nyamagana tuonane, nitakupa maelekezo namna ya eneo hili, tuko tayari kulitoa kwa ajili ya Halmashauri kama mtaona kwamba mtalifanyia kazi vizuri, lakini tafuta wawekezaji tuweze kulifanyia kazi sina tatizo nao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vya chai navishughulikia, nimemaliza cha Lushoto, nitakwenda Lupembe na Mheshimiwa Spika aliyemaliza kipindi chake anafuatilia suala hilo.
Mheshimiwa James Millya suala la Diamond, Tanzanite kule tunalishughulikia nimeshamaliza kulipa pesa zilizokuwa zimebaki zote, kwa hiyo tutakwenda kuangalia namna gani ya kutengeneza Special Economic Zone.
Mheshimiwa Adadi Rajab nimekukubalia kwamba tukutane kesho kutwa leta wawekezaji wako, tuweze kwenda mbele na mpango wa kuwekeza kwenye matunda.
Mheshimiwa Kasuku Samson aliuliza je, viwanda dira ya Rais au ya nchi? Hii ni sera ya CCM hilo sina tatizo nalo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti,wakulima wa Dodoma wasaidiwe kuanzisha viwanda vidogo vya kusindika karanga na alizeti. Mheshimiwa George Malima Lubeleje tutafanya hivyo, nimekubaliana na Serengeti waende waanzie kwenye Jimbo la Mtera, watachukua hekari nyingi wawafundishe wale wakulima wa kawaida watumie matrekta wazalishe mtama, tunawahakikishia kwamba mtama utauzwa Serengeti, kutoka kwa bwana kibajaji kule Mtera, kwa hiyo Mbunge wa Mtera pamoja na swali lako hili, uje unione nitakuunganisha na mtaalam wa Serengeti walime mtama kwako, mwezi wa saba nitakwenda kukagua hilo shamba tulime. Tutawachukua mmoja mmoja muwe na imani tunakwenda ili mradi safari ianze.
Kambi Rasmi ya Upinzani wanasema wafanyabiashara wadogo kuelekezwa katika viwanda badala ya kuonekana kero, tutafanya hivyo sina matatizo.
Kuhusu kuiwezesha SIDO isogeze huduma zaidi Wilayani hadi vijijini, huo ndiyo mpango wangu na itategemea bajeti na Mheshimiwa Elias John Kwandikwa wa Ushetu Wizara isimamie SIDO ili vijana wapate ajira, nitaisimamia SIDO, ipo chini yangu tunaanza na centre kubwa zile tano, ninawaomba Waheshimiwa Wabunge mtembelee SIDO mkaone mambo, kuna mambo mazuri sana.
Kuna hoja kuhusu SIDO itoe elimu zaidi kwa viwanda vidogo ili Watanzania wengi wavianzishe, tutafanikiwa tukiwekeza kwenye viwanda, mchezo upo kwenye viwanda. Baba Mchungaji Mheshimiwa Msigwa mnihukumu kwa viwanda vidogo. Viwanda vya wakubwa vinatumia teknolojia kubwa haviajiri watu wengi, kwa hiyo nitavihimiza hivi nawashukuru sana kwa mchango wenu huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nisingependa kupigiwa kengele michango yote nimeizingatia, natafuta mchango wa Mheshimiwa Msigwa ambaye alitaka kuona kama ninaweza kumwonesha 40 percent. Mimi leo ndiyo ninaomba bajeti, ninamaliza Ilani ya Chama ya 2010-2015 sasa naanza ya 2015-2020. Kwa hiyo niko year zero nina take off, huwezi kunihukumu leo kwamba nimetengeneza wangapi? Lakini nimeandika kwenye maelezo yangu kwamba tutatafuta wajihi wa kila kiwanda na kila kampuni. Lengo la kutafuta profile za kila kampuni ni kuweza kubainisha at every stage kwamba watu wangapi wameweza kupatiwa ajira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini tumeanzisha viwanda? Tumeanzisha viwanda kwa sababu vinaweza kutoa ajira, na ndiyo maana tunalenga viwanda vinavyotumia watu wengi. Mheshimiwa Msigwa akasema Mwijage ninazungumza kama ninapiga kampeni. Nimesema kazi yangu kubwa itakuwa kuhamasisha Watanzania wakubali hii dhima ya kujenga uchumi wa viwanda ili kuleta mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu, inahitaji mhamasishaji na mhamasishaji aliyepewa ni mimi, sasa Mzee Msigwa unauliza makofi polisi? Ndiyo kazi yake. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itafute masoko ya matunda nje ya nchi. Nichukue nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Raza, amekubaliana na mimi atanisaidia kunipatia masoko ya mazao na masoko ya mazao ya matunda yako Oman. Walikuja watu wa Oman Waziri wa Oman nilizunguka naye mjini, watu wake wakaniuliza, Mheshimiwa Waziri, nikasema naam, wanazungumza kiswahili wa Oman, wakasema mnanunua na ninyi matunda kutoka Mombasa? Matunda ya Muheza yanauzwa Mombasa kwa hiyo watu wa Oman wakadhani matunda ninayanunua kutoka Mombasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, soko lipo ninamshukuru Mheshimiwa Raza na TANTRADE nawapa jukumu, lakini Watanzania mchangamke kufanya biashara inawezekana. Tatizo kubwa la Watanzania walio wengi wanaogopa kumiliki, mtu anapita kwenye nyumba yake anaangalia huku, eti wasimwone ana nyumba, kwenye gari lake hawezi kulipanda, anapanda gari nyingine, gari yake inapita. Mmiliki, msiogope kumiliki ili mradi mmiliki kihalali ndiyo utaweza kufaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kutumia fursa za uanachama wa Jumuiya za Kikanda angalia takwimu zangu, Tanzania tumeuza mno East Africa, tumeuza mno SADC, tunakwenda COMESA. Kwa hiyo, Watanzania tujiamini na nitaendelea kuhamasisha mambo ya Kikanda ya bilateral, kikanda, kieneo na ninyi msiogope, Watanzania msiogope kwenda Southern Sudan sasa hivi mchangamkie fursa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania kuna wakati tulikuwa tunashangilia fursa, location advantage, haina maana, ushishangilie fursa, ichangamkie fursa. Katika hilo ndiyo maana viwanda vidogo, viwanda vya kati, tunataka kuanzisha mashindano ya kimkoa ningependa kuona mtu analeta sembe imekuwa packed kwenye mfuko, anasema sembe safi kutoka Ileje, mchele mzuri kutoka Mbarali, tushindane Kiwilaya na tushindane Kimkoa, hii ni asali nzuri ya kutoka Katavi, hilo haliwezekani mpaka muweze kuyahamasisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kusaidia wahitimu kusajili makampuni. Nitaliangalia hili tuweze kuangalia namna gani tunaweza kuwasaidia wahitimu hata ikibidi kuwasajili siku wanafanya mtihani, lakini lazima tuzingatie sheria, na kama kuna vikwazo mtaweza kuondoa ninyi mnaopitisha sheria.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kumaliza tatizo la sekta ndogo ya sukari. Kigoma Sugar amepewa na watu wa Kigoma niwashukuru tena, hekta 47,000; akifanya kazi mpiganie kwa namna yoyote asikwamishwe na mtu yeyote na mimi nitawasaidia. Atazalisha tani 120,000; RAK wameomba ardhi watazalisha zaidi ya tani 60,000; Kagera Sugar anataka kupanua mpaka tani 120,000; lakini Oman wamesema wanataka watumie facilities za Kagera Sugar wazalishe tani 180,000 kama alivyosema Mheshimiwa Zitto Kabwe tunaweza kuzalisha tani 1,500,000 tukapata mamilioni mengi ya pesa. Kwa hiyo hili tatizo la sukari ni suala la muda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaeleze muazime uzoefu wa Wabunge wa Bunge la Kumi, Taifa lilikuwa linasumbuliwa na sekta ya mafuta namna hii, kwa hiyo kinachokuja tutakuwa na coordinated importation kwani kuna suala la quality, kuna suala la quantity, kuna suala la price, ulikuwepo udanganyifu kwa hiyo udanganyifu unakwisha wanaoshangaa kwa nini Mheshimiwa Rais anasema ndiyo, akishamaliza kusema mwenye nyumba sasa mje muone watoto watakavyofanya tutalishughulikia hili, kwa hiyo itakuwa na coordinated importation na msiwe na wasiwasi hakuna Ramadhani sijui sukari itakosa hakuna, kuna wengine sijui Mikoa gani huko, wanachagua maduka mawili ya kata kuuza sukari, sukari itauzwa kila duka na itakuwepo sukari ya kutosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachotaka mwenye sukari, na ukitaka mambo yakuendee vizuri hakikisha sukari inakwenda kwa wananchi, distribute kusudi tuone kwamba hakuna sukari. Lakini sukari ndiyo ilikuwa inakwamisha viwanda vyetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni waambie siri moja, waulize wawekezaji, Kigoma Sugar, muulize hata RAK, Mheshimiwa Jitu Soni anataka kutengeneza kiwanda cha sukari kwenye Halmashauri yake cha kuzalisha tani 50, Abdul Salim aliyekuwa Mbunge wa Kilombero, anataka kutengeneza kiwanda cha tani 50, siyo gharama kubwa ni shilingi bilioni mbili tu unakwenda Benki unaweka guarantee ninakudhamini, wewe Mbunge mimi nitakosa kukudhamini? Ndiyo faida ya Ubunge mnakopa. Msiogope kukopa huwezi kuwekeza kwa pesa yako mwenyewe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo usinipigie kengele, baada ya kuzungumza yote hayo, nimeahidi kwamba mengine yote nitaweza kuyaweka kwenye kitabu vizuri, niwashukuru wote mliochangia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba kutoa hoja.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia nafasi kuchangia taarifa mbili za Kamati. Kipekee niwapongeze Wenyeviti wa Kamati hizi mbili, Wajumbe wa Kamati lakini kipekee Waheshimiwa Wabunge ambao mmeshiriki kuchangia hizi Kamati mbili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesoma sana taarifa hizi mbili, lakini nimesoma kipekee taarifa iliyohusu mahsusi suala la viwanda, biashara na uwekezaji. Ninawaunga mkono, nataka niwaambie pale ninapotofautiana na ninyi. Serikali haina mpango wa kutwaa kiwanda na kukiendesha, haijaandikwa mahali popote wala sijawahi kuelekezwa na mkuu wangu wa kazi au tajiri namba moja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumewaambia wenye viwanda, vile viwanda vihakikishe vinafanya kazi, wasipofanya kazi tutawapa wengine waviendeshe. Ndugu yangu wa Tabora, kwetu kuna methali moja inasema asiyemhurumia chura anasema chura hafi kwa mpini ukimpiga. Nimekwenda kwa Ndugu Rajan mimi, Rajanialikufa nikamfuata mtoto wake wa Uingereza nikaongea naye, kiwanda cha nyuzi kitaanza. Ndugu Gulamali kila siku ananifuata ili kusudi turudishe Manonga. Igembe Nsabo wanakuja hapa kesho kutwa nifanye nini Mwijage? Kwa hiyo, huo ndiyo msimamo wa viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, msiwaoneshe Watanzania kwamba tuna hali mbaya, nimepewa dhamana hii Novemba, 2015 ngoja niwape taarifa. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, TIC wamesajili viwanda 170, BRELA viwanda 180 nina taarifa. Mbali na taarifa ya Kamati na mimi nina taarifa yangu nimefanya nini na nitaiwasilisha. Unapozungumza EPZA viwanda 41, NDC viwanda saba na vitatu vikiwa ni vya dawa. Unapokuja SIDO wameratibu viwanda 1,843 mpaka sasa ninapozungumza nina viwanda 2,169; ndivyo hivyo viwanda. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niwaeleze Watanzania nimefurahishwa na jambo moja kwamba Watanzania tunawahamasisha watu wa nje tunawaacha watoto wa ndani, siwezi kufanya hivyo. Hata nilipokuja hapa saa nane nilikuwa nawahamasisha Watanzania, niwaeleze ndugu yangu Mavunde, kesho kutwa tunakwenda kuzindua kiwanda cha chaki chenye uwezo wa kuzalisha chaki hapa Dodoma, kimetengenezwa kwa gharama ya milioni 20 kitaweza kuzalisha na kiwanda kipo hapa.
Kwa hiyo, ningependa tuzungumze ukweli. Msiwatie hofu ushauri wote utazingatiwa msiwatie hofu Watanzania kwamba hatuendi, tunakwenda mbele.
TAARIFA...
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu ni Mjumbe wa Kamati yangu, taarifa uliyonipa naikubali na naipokea.
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu ni Mjumbe wa Kamati yangu, taarifa uliyonipa naikubali na naipokea. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, dakika zangu zilindwe, kuna kitu kinaitwa mis-conception...
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kinaitwa misconception.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Dkt. Mpango amewaeleza, Serikali haijengi viwanda ila Serikali inaweka mazingira ya kujenga viwanda. Mchuchuma na Liganga ametueleza, Mheshimiwa Ridhiwani amekuambia anakualika ukienda Chalinze usimame uangalie, Mkuranga umealikwa. Mheshimiwa Mchungaji Msigwa hizo nyanya unazolima mimi nina fursa ninaweza nikakupa kiwanda. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu niwaambie kitu kimoja Wabunge waelewe, unajua Wabunge mnajichanganya, mnasema Watanzania wazawa wawezeshwe, wapewe fursa msiagize wageni, lakini ninyi wazawa kuna mzawa kuliko Mbunge, unyanyuke wewe Mbunge. Asubuhi nimejibu swali kuhusu zile taulo za akina dada, niwaeleze kuna Waheshimiwa Wabunge wawili hapa tunahangaika kuleta teknolojia ya kutengeneza vitu, msiogope kuwa na utajiri ilimradi huo utajiri usiuibe. (Makofi)
Waheshimiwa Wabunge mjiandae kumiliki useme kiwanda hiki ni changu na hiki ni changu. Mheshimiwa hapa tumekubaliana alete proposal. Juzi nimeitisha semina hapa ya venture capital nikawaleta hapa, wanasema pesa wanazo. Kuna Wabunge walijitolea wakaja wakaangalia, waliposema dola bilioni kumi kumpa mwekezaji nikawaambia msiwadanganye Wabunge. Mtu akasimama akasema we have money mjitokeze. Hauwezi kulala kitandani ukapewa lift lazima uingie barabarani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie viwanda vilivyobinafsishwa, hali siyo mbaya hivyo, ila yeyote aliyepewa kiwanda kulingana na masharti viwanda vitatwaliwa. Ninayo ripoti ya viwanda kumi ambavyo vinakwenda kwa AG na viwanda vitatwaliwa, Lakini safari yetu ni miaka mitano, ndiyo naanza kazi sasa hivi mnaanza kusema. Hivi unategemea unaweza kujenga viwanda kwa shilingi bilioni 42. Kiwanda cha Mkuranga mnachosikia ni bilioni zaidi ya 80. Serikali haijengi viwanda.Mheshimiwa Mwenyekiti, dakika zangu zilindwe, kuna kitu kinaitwa mis-conception...
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kinaitwa misconception.
MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge naomba utulivu!
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Dkt. Mpango amewaeleza, Serikali haijengi viwanda ila Serikali inaweka mazingira ya kujenga viwanda. Mchuchuma na Liganga ametueleza, Mheshimiwa Ridhiwani amekuambia anakualika ukienda Chalinze usimame uangalie, Mkuranga umealikwa. Mheshimiwa Mchungaji Msigwa hizo nyanya unazolima mimi nina fursa ninaweza nikakupa kiwanda. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu niwaambie kitu kimoja Wabunge waelewe, unajua Wabunge mnajichanganya, mnasema Watanzania wazawa wawezeshwe, wapewe fursa msiagize wageni, lakini ninyi wazawa kuna mzawa kuliko Mbunge, unyanyuke wewe Mbunge. Asubuhi nimejibu swali kuhusu zile taulo za akina dada, niwaeleze kuna Waheshimiwa Wabunge wawili hapa tunahangaika kuleta teknolojia ya kutengeneza vitu, msiogope kuwa na utajiri ilimradi huo utajiri usiuibe. (Makofi)
Waheshimiwa Wabunge mjiandae kumiliki useme kiwanda hiki ni changu na hiki ni changu. Mheshimiwa hapa tumekubaliana alete proposal. Juzi nimeitisha semina hapa ya venture capital nikawaleta hapa, wanasema pesa wanazo. Kuna Wabunge walijitolea wakaja wakaangalia, waliposema dola bilioni kumi kumpa mwekezaji nikawaambia msiwadanganye Wabunge. Mtu akasimama akasema we have money mjitokeze. Hauwezi kulala kitandani ukapewa lift lazima uingie barabarani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie viwanda vilivyobinafsishwa, hali siyo mbaya hivyo, ila yeyote aliyepewa kiwanda kulingana na masharti viwanda vitatwaliwa. Ninayo ripoti ya viwanda kumi ambavyo vinakwenda kwa AG na viwanda vitatwaliwa, Lakini safari yetu ni miaka mitano, ndiyo naanza kazi sasa hivi mnaanza kusema. Hivi unategemea unaweza kujenga viwanda kwa shilingi bilioni 42. Kiwanda cha Mkuranga mnachosikia ni bilioni zaidi ya 80. Serikali haijengi viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la EPZA. Tunalitambua suala la EPZA! EPZA inayoniuma ni Special Economic Zone ya Bagamoyo. Maamuzi yametolewa na Serikali namna gani wananchi wa Bagamoyo watakavyoweza kufidiwa. Liko suala la EPZA, Special Economic Zone ya Bunda, timu yangu imekwenda, nimshukuru Mjukuu wangu, wamekwenda Bunda, wamepewa ushirikiano, wale waliokula pesa za Serikali watakamatwa na watajuana na Mheshimiwa Mwigulu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwaombe kitu kimoja Waheshimiwa Wabunge, viwanda tunavyojenga ni kwa ajili yetu, kamateni maeneo kwa ajili ya familia zenu. Mheshimiwa Simbachawene ametoa maelekezo namna gani katika Serikali ngazi za vijiji na mikoa mtakavyoweza kutunza maeneo na kuweza kuwapa vijana wenu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la kilimo nusu. Katika viwanda vilivyotengeneza ninavyowaambia kuna Kiwanda cha TAMCO, tumeshakibadilisha kuwa kiwanda cha kuunga matrekta na ninavyozungumza sasa vifaa vya kutengeneza matrekta 340 vimeshafika Kibaha na tunalenga kutengeneza matrekta 2004 Kibaha kabla ya mwisho wa mwaka huu na yote nimepewa dhamana nitayagawa mimi. Sasa kama ulikuwa unalima na jembe, nitakupa trekta, ndiyo namna ya kuongeza tija katika kilimo. Kwa hiyo, viwanda ninavyovihesabu ni cha Urususi cha matrekta kiko TAMCO. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kipekee ambalo baadhi ya Wabunge mmezungumza ni viwanda vya dawa na dhamana hiyo iko chini ya Makamu wa Rais. Makamu wa Rais amenielekeza pamoja na Waziri wa Afya, tuandae wawekezaji juu ya kuwekeza kwenye viwanda tiba, ndiyo kazi ambayo tunawaita wawekezaji kutoka Misri, ndiyo kazi ambayo tunawaita wawekezaji kutoka Uturuki, China and the response is good. Kwa hiyo, Waheshimiwa msijione wanyonge Watanzania, ninyi Wabunge mkijiona wanyonge wananchi wenu watanyong‟onyea! Tanzania sasa tunajenga viwanda, msidhani kwamba hamuwezi na mjifunze kumiliki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kuwashukuru watu wa Kigoma. Tunasaidiana na watu wa Kigoma kwenye kilimo cha michikichi na miwa, nichukue fursa hii pia wawekezaji wote waliochukua maeneo ya kulima miwa, kufikia mwezi wa nane atakayekuwa hakufika site nitampeleka kwa Mheshimiwa Lukuvi, tutamnyang‟anya eneo, ikiwemo Kibondo Sugar, ikiwemo Kigoma Sugar. Waheshimiwa kazi zinafanyika, lakini kama nilivyosema hii ni ripoti ya wenyewe na ripoti ya kwangu iko hapa, siku mtakapoiona mtacheka na kufurahi. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie mambo mahsusi, suala la Urafiki. Ubinafsishaji wa Kiwanda cha Urafiki una masharti. Upande wangu kwa dhamana yangu, nilishazungumza na watu wa Foreign Affairs yule mwekezaji aondoke, aletwe mwingine kusudi awekeze kwa malengo. Ule ufisadi mnaozungumza ni historia na mimi nimeukuta, lakini mimi siyo expert wa kufukua makaburi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusu viwanda vya kilimo, uvuvi na mifugo. Nakushukuru Mheshimiwa Nsanzugwanko, ndivyo Mpango wa Pili wa Miaka Mitano unavyosema. Ndiyo maana kuna mkakati mmoja wa mwaka jana niliou-launch mimi na Ndugu Mwigulu, unasema cotton to clothing, unasema leather and leather by products, unasema kuhusu maziwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mbunge wa Njombe anajua, leo nimempa muhtasari wa Kikao cha SAGCOT ambapo ng‟ombe 3,000 wataletwa kupelekwa Njombe ili watoe maziwa, ili maziwa hayo yaweze kutosheleza viwanda vya maziwa vya ASAS na viwanda vya Njombe vya maziwa. Tunafanya kazi, lakini kama nilivyosema asiyehurumia chura, anasema hata ukimpiga kwa jiwe hawezi kufa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mikataba ya Viwanda vya Korosho, kwa kipekee nilikuwa nalishughulikia suala hili, lakini suala hili nakwenda kulimiliki na nitakufa navyo. Viwanda vya Korosho nitakufa navyo, naviperemba nikimaliza nampelekea Waziri wa Fedha ndiye mwenye dhamana. Viwanda vyote vilivyobinafsishwa mwenye navyo ni Treasurer Registrar, kwa hiyo, viwanda vyote tutavishughulikia. Hii kazi nirudie tena, siyo kazi ya mtu mmoja, tukishinda Taifa letu limeshinda na tukishinda tushinde wote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudie kwa mara nyingine niwaeleze; Serikali yetu ya Tanzania katika Taarifa ya Kamati kwamba, Serikali ina matatizo na wawekezaji. Mimi ndiye receptionist, wawekezaji wote wanakuja kwangu kila siku, nimehamia Dodoma kila siku wanakuja hapa. Hakuna mwekezaji amekuja kwangu akashindwa kuhudumiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaambie pale wanapokosea, usijidanganye kwenda kwa tajiri namba moja au Makamu wa Rais au kwa Waziri Mkuu, kama unataka kuwaona wakubwa uje unione mimi. Mimi ndiyo nitakufanyia mpango ukamuone Mheshimiwa Rais, huwezi kutoka huko ukaenda kwa baba bila kupita kwa mwana, njooni hapa nitawafanyia mipango, huo ndiyo utaratibu. Kwa hiyo, Serikali hii ni friendly, inapenda wawekezaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru binti Katimba kwa sababu ya upatikanaji wa malighafi. Mheshimiwa Katimba ngoja nikwambie, nimepata mwekezaji, muulize dada yako wa Uvinza, tunakwenda kule Itamigaze na ndugu yako Mheshimiwa Zitto, tutapanda Migaze Kigoma, lakini Migaze ya leo haiwezi kuzidi ya kesho. Kuna kipindi kirefu, tutafanya kazi sisi ambayo ni manufaa kwa vijana wetu. Waheshimiwa Wabunge, watu wasikate tamaa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwashukuru watu wa Kamati mmenipa changamoto, lakini…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, ahsante sana,
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
WAZIRI WA VIWANDA BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia wote nguvu na afya njema ili kuweza kujadili hii bajeti yetu kwa siku mbili. Hii ndiyo bajeti inayobeba Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wenye dhima ya kuleta mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Nawashukuru sana Wabunge wote mlivyojadili bajeti hii, napenda niseme mmeitendea haki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya kipekee namshukuru Mheshimiwa Stanslaus Nyongo, Mbunge wa Maswa; yeye na Kamati yake kwa jinsi walivyoichambua bajeti yangu na kwa jinsi walivyosimamia Wizara yangu, mpaka kutupelekea kuandika hii bajeti ambayo kila anayeisikia, anaomba nakala halisi pamoja na kwamba iko kwenye mtandao.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, naomba nimshukuru kipekee Waziri kivuli wangu, Mheshimwa Antony Komu kwa hotuba yake ya kufikirisha ambayo inakufanya ufikirie miaka mingi mbele, uende maili nyingi. Waziri Kivuli nakushukuru. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mbali na ushauri mzuri, uliotolewa na Kamati na Waheshimiwa Wabunge kwa ujumla, Wizara na taasisi zilizoko chini yake imepokea pongezi nyingi kwa kuweza kutekeleza masuala ambayo wananchi wamekuwa wakiyatarajia. Hakika pongezi hizo zinatupa hali ya moyo ya kujibidiisha zaidi katika kubuni, kupanga na kuboresha mbinu za utendaji ili Taifa na Watanzania kwa ujumla wanufaike zaidi na matunda ya fursa zilizomo. Nami nawaahidi kuwa tutaendelea kujibidiisha na wala hatutawaangusha.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yenu. Waliochangia kwa kuongea moja kwa moja ni Waheshimiwa Wabunge 44; waliochangia kwa njia ya maandishi ni Waheshimiwa Wabunge 48; waliochangia Wizara hii kwa kina katika bajeti za Mawaziri wenzangu waliotangulia ni Waheshimiwa Wabunge 10, ujumla wake watu 101 wameiunda upya Wizara yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nijitahidi kujaribu kuweka sawa kwa mujibu baadhi ya hoja, lakini ni kweli wataalam wangu wote wako hapa, wamejiandaa watatengeneza majibu ya kina; na kama nilivyosema, mtazamo wetu katika kujenga uchumi wa viwanda mmeujenga upya. Kwa maneno rahisi, mmeuimarisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na swali la kwanza, the misconception, what is not, mawasiliano ya kati na ndani ya Serikali siyo mazuri; the misconception, siyo kweli. Mawasiliano ndani ya Serikali ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ni mazuri. Sina muda wa kuzungumza zaidi, nitawapa vielelezo. Serikali hufanya kazi kwa maandishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni Taarifa ya Wizara yangu ambayo nimemwandikia Waziri wa Fedha baada ya yeye kunitaka kwa maandishi kwamba ni vivutio gani unavitaka ili wawekezaji wako waweze kuwekeza unavyotaka, iko hapa. Akaenda zaidi, ni kodi gani ziongezwe au zishushwe ili mambo yaende vizuri? Ndiyo hayo! Kwa hiyo, mawasiliano ni mazuri na Serikali inafanya kwa makaratasi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, watu wasipate wasiwasi kwamba nchi hii inaingia vitani, hapana! Tunafanya kazi vizuri na nakumbuka, bahati mbaya simu zangu nimezifungia, mawasiliano ya mwisho alinipigia akiwa Marekani kwamba hakikisha andiko hili linapelekwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimempa maelekezo Katibu Mkuu wangu anayeshughulikia biashara na uwekezaji, anayeshiriki kwenye chombo cha Kitaifa kinachopitia bajeti kabla ya kwenda kwa Mheshimiwa Waziri kwamba yale niliyoyapendekeza mimi msiongeze wala kupunguza chochote. Kama mnakataa, andika mmekataa, kusudi siku ya siku waje waone tunavyoshirikiana. Serikali hii ni moja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kifupi, nimeelezea hivyo, lakini nitatoa mifano mingine zaidi. Tunawasiliana!

Waheshimiwa Wabunge, zimekuwepo hoja na mmesema ukweli kwamba kasi ya kujenga uchumi wa viwanda inakwenda taratibu. Napenda nikiri na nitambue mchango wenu, lakini nyie sio wa kwanza. Kuna wakati mimi na Mheshimiwa Waziri Mkuu tulikuwa hatuangaliani machoni; nikawauliza Wasaidizi wake, vipi? Wanasema, haoni viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mama Samia kuna wakati aliniiita nyumbani kwake, akasema Mwijage nataka viwanda vya madawa! Bahati nzuri Mheshimiwa Ummy amekwenda kutafuta viwanda hivyo, hayupo hapa. Tajiri huyo ndio alikuwa hataki kuniona.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nitambue mchango wa Mheshimiwa Katibu Mkuu Kiongozi, Mheshimiwa Kijazi, nikamwambia mzee nifanyaje? Akasema kama hawakuelewi andika! Nikaandika kitabu hiki kinaitwa strategy for fast tracking in industrialization in Tanzania. Yote mliyoyasema yako humu. Wakakipeleka kwa tajiri. Tajiri namba moja; wewe unalinda duka tu, tajiri ni mmoja tu! (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilijuaje kwamba Mheshimiwa Rais ameona kitabu hiki? Tulipowaita wawekezaji, Mheshimiwa Rais alitamka kwamba wakati wa kuwekeza ni sasa na atakayetaka vivutio, aje aniambie. Nikajua ugonjwa umepata dawa. Nimewasiliana, Serikali inawasiliana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo ni vielelezo viwili kwamba the Government is coordinated; na kitabu hiki siyo changu tena, kimeshapelekwa kwenye Kamati ya Wabunge wote na kinakwenda kwenye Baraza la Mawaziri. Kwa hiyo, Serikali inawasiliana. Naweza kutoa ushuhuda, Mheshimiwa Mpina alizungumza nini, tulibishana nini kuhusu hii; na vile vikwazo vyote na gear zote za kwenda kasi, zimezungumzwa humu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushirikiano wa Sekta Binafsi na Serikali. Viongozi wa Sekta Binafsi wako pale; Tanzania Private Sector Foundation, CEO wao Dkt. Simbeye yuko pale. Jana mliona uwanja wote ulijaa suti za bei mbaya! Hao ni wawekezaji hao! Walikuwepo hata wale akinamama wa VICOBA, wote ni wawekezaji. Tungekuwa na mahusiano mabaya wasingekuja. Kwa hiyo, mawasiliano yetu ni mazuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwezi huu tukiwa Bungeni, mimi na Mheshimiwa Mpango tuliitisha mkutano wa wawekezaji wote, mliona; uwanja wa ndege wa Dodoma ulionekana mdogo, ulijaa ndege! Wawekezaji wa Madini walikuwepo; wa umeme walikuwepo, tukakutana, tukajadiliana; na tukawekeana maazimio. Tumekubaliana kila miezi mitatu tuitishe mkutano mkubwa. Sekta Binafsi na Serikali tunafanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, ngazi ya Kitaifa, Baraza la Biashara la Taifa ambalo Mwenyekiti wake ni Mheshimiwa Rais, tumekutana juzi. Wale mnaotumia mitandao, ndiyo ile clip ya Millard Ayo inayozungumza, ikichukua yale maneno matatu aliyoyasema Mheshimiwa Rais, wakati wa kuwekeza ni sasa. Atakayekukwamisha njoo uniambie. Ukitaka vivutio, nitakupa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kama Mheshimiwa Rais anasema ukitaka vivutio nitakupa, wewe unaogopa nini kumfuata? Si anaonekana! Amekwambia ukitaka vivutio atakupa. Nenda kamwambie sasa akupe, si yupo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namba tatu ni viwanda vilivyobinafsishwa. Mheshimiwa Devotha, wewe bado ni rafiki yangu. Usidhani urafiki wangu ulikufa kwa sababu ulifanya hivyo, hapana, bado ni rafiki yangu. Tatizo la Morogoro halipo tena. Nawaomba Waheshimiwa Wabunge, mnitendee haki. Msome kitabu changu, kina majibu ya kila kitu. Moro Canvas karibu mambo yake yatakwisha. Kutoa kiwanda kwenye ownership moja kwenda ownership nyingine kuna mambo ya kimikataba.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikwambie nimetumia nguvu zangu zote na muda wangu wote, mimi nina maslahi. Nimekwambia Mheshimiwa Devotha urafiki wangu na wewe hautakufa. Nilikasirika kipindi, sasa hasira zimekwisha, eeh! Kuna wakati alibadilisha mwelekeo wetu na mimi nikakasirika, sasa nimetulia. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, MOPROCO inaanza mwezi wa Sita. Matatizo ya MOPROCO yamekwisha na nimeshaeleza kwenye kitabu changu kwamba pamoja na ku-crush mbegu ita-crush hata mashudu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, MOPROCO inaanza, haina tatizo na Moro Canvas inaanza. Hivi vingine viwanda vya Ceramic, siyo tatizo, tutavishughulikia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye viwanda vilivyobinafsishwa, nimeandika kwenye mambo nitakayoyafanya kwamba mfumo wa sasa wa kushughulikia viwanda vilivyobinafsishwa utabadilishwa. Lazima tumhusishe Mkuu wa Mkoa, tuhusishe Wizara ya Kisekta, tumhusishe kikamilifu Attorney General na lazima tuihusishe Wizara yangu kama anavyosema bosi wangu wa zamani, jeshi la mtu mmoja. Kwa hiyo, viwanda vilivyobinafsishwa ndiyo hatma yake.

Mheshimiwa Japhary rafiki yangu, Mheshimiwa Rais amekuja juzi anasema viwanda vya Moshi vifanye kazi. Kama Mheshimiwa Rais anasema, mimi nitapingaje? Juzi mtu mmoja amenipigia simu, anataka Kiwanda cha Viberiti. Kwa nini Kiwanda cha Viberiti kilikufa? Mlikuwa mnaagiza viberiti kutoka Pakistan vya bei rahisi wakati vya hapa mnaviacha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, amezungumza Waziri wa Mambo ya Ndani, atanisaidia kuhakikisha smuggled items haziingii nchini. Mheshimiwa Mwigulu nami itabidi niende lindo. Ni hilo naweza kuwaeleza kwenye viwanda vilivyobinafsishwa. Azma ya Serikali ndiyo hiyo, tunaongeza nguvu, kazi ya Treasury Registrer, Wizara za Kisekta, twende pamoja. Mama, viwanda vya Korosho ni chapter inajisimamia yenyewe; tutazalisha na ile kitu ambayo ukiiona unasema astaghfiru Allah. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namba nne; mazingira ya kufanya biashara. Mazingira ya kufanya biashara naomba nilizungumze hili na Waheshimiwa Wabunge tusikilizane, unajua mtu akitusikiliza, lakini hiki ni kikao cha wakubwa, ndiyo maana hata mitandao mingine hairuhusiwi kusikiliza. Kwa hiyo, wakubwa mnaponyukana huko chumbani, mnanyukana mtu wa nje asisikie.

Mheshimiwa Naibu Spika, mtu akitusikiliza atadhani Tanzania hapafai kuwekeza, hapana! Ni kwa sababu tunakopataka siyo hapa. Kwa hiyo, muumini mkubwa wa mazingira mazuri ya kuwekeza ni mimi namba moja. Nikipata muda nitawasimulia. Niliwahi kupoteza kazi yangu nzuri kwa sababu ya mazingira mabovu ya uwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma report ya dunia ya mwaka 2017, wepesi wa kufanya shughuli, Tanzania tuna nafasi ya 132, tulipoanza tulikuwa 139 katika nchi 190. Mzazi yeyote akipeleka mwanaye shule, hawezi kufurahi kwamba mwanawe awe wa 132; lakini siyo sababu ya kupiga kelele au ya kulalamika kana kwamba kuna mtu kafa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ngoja niwaambie sababu moja inayofanya Tanzania kuwa ni sehemu ambayo siyo nzuri ya kuwekeza. Wale wanaotupima, wanaangalia wepesi wa watu kulipa kodi na ule mfumo wa kodi. Sasa watu wengi wanaojadili wanaangalia upande ule unaolipisha kodi, wanaangalia madhaifu ya TRA, lakini hawaangalii wepesi wa mtu kulipa kodi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi nyingine zilizoendelea ambazo ziko better ranked, namba moja, namba kumi, mtu anadai risiti, anasema lazima unipe risiti, unioneshe kodi. Hapa, unamwambia andika kwamba hii bidhaa ya shilingi milioni moja, niandikie laki moja halafu, basi, basi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, wepesi wa kulipa kodi ni kigezo. Kwa hiyo kama ningekuwa mhubiri kama ambavyo mdogo wangu Bashe anaamini ningewaambia tujitazame, tuwe wepesi wa kulipa kodi na tuwaambie wapiga kura na ndugu zetu tuwe walipa kodi wazuri kusudi wawekezaji waje. Mwekezaji makini hawezi kuwekeza katika nchi ambako mmoja analipa kodi, mwingine halipi kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, rafiki yangu pale Mnyampala anasema, mbona makampuni yamekufa? Mbona biashara inakufa? Mbona maduka yanafungwa? Inaitwa paradigm shift. Kama ulizoea kuleta bidhaa yako hulipi kodi, sasa utaratibu ni kulipa kodi, uta-collapse. Kama ulikuwa unalipa chumba Kariakoo kwa kodi ambayo ni kubwa kuliko London, haiwezekani chumba Kariakoo kikazidi London, huo unaitwa uchumi bandia. Sasa ni uchumi halisi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hao wataondoka. Sasa tutahesabu shilingi kwa ya pili, tutajenga uchumi imara na mfanyabiashara atakayelipa kodi ataweza kustawi. Huo ni upande wa pili wa sisi walipa kodi. Upande mwingine ambao walio wengi na mimi nikiwa Mbunge tunausemea ni upungufu wa TRA. Nawaahidi, mimi ni sehemu ya Serikali, tutaishughulikia. TRA ina upungufu, tutaiboresha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma taarifa ya Wizara yangu aliyosimamia Profesa Mkenda, wepesi wa kufanya shughuli Tanzania, walipotu-rank Wazungu na sisi tukaji-rank; unajua mtu akikwambia wewe ni handsome boy, kajiangalie kwenye kioo, kweli wewe ni handsome au anakudanganya? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Wazungu walipotufanyia ranking, nasi tukajifanyia ranking wenyewe. Tukatengeneza zoezi la wepesi wa kufanya biashara. Katika kitabu hiki alichokiongoza Profesa Mkenda, kimehusisha Watendaji wa Wizara zote za Serikali, wote wamehusishwa. Kwa hiyo, NEMC kama anakosea, tunasema anakosea; TBS ana makosa, ana makosa; TFDA, ana makosa, ana makosa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kitabu hiki shangazi, kodi 25 za Kagera zimeandikwa. Rafiki yangu Gimbi anasema umefanya nini nyumbani? Nimepigana kodi 25 zitoke, ngoja aje Tizeba kesho. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma kitabu hiki kinaeleza kwamba kila Waziri aliyepewa mamlaka, yale mambo ambayo kutokana na regulations anaweza kuyabadilisha, ayabadilishe. Ndivyo inavyosema. Kwa hiyo, kero zote tutaziondoa moja baada ya nyingine. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, nashukuru mmepaza sauti. Mlitupa jukwaa kama lilivyo, tumeshughulikia. Tuliyoyaona ndiyo hayo, fast tracking of industrialization lakini vikwazo viko hapa, tumemaliza. Kilichobaki ni utekelezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya point tatu hizi katika 25 nitakazozisema, Waheshimiwa Wabunge kwa point tatu nawaomba mjiandae kwa heshima na taadhima na bashasha na nderemo kunipitishia Bajeti yangu niende kuitekeleza. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, Sera ya Viwanda. Hapana, kwanza niwaeleze viwanda ni nini? Halafu nije niwaeleze Sera ya Viwanda. Mheshimiwa Nape na Waheshimiwa Wabunge wengine wametaka kujua tafsiri ya viwanda. Shughuli yoyote, viwanda vina tafsiri mbili; ile tafsiri inayohusisha mambo ya construction, uzalishaji wa gesi kwamba ni viwanda, mimi siitumiii. Naitumia ile ya manufacturing, ya kuongeza thamani ya kuchukua mawese yakatoa mafuta, mbegu za alizeti kutoa mafuta, cotton kutoa suti nzuri kama niliyovaa leo hii. Hivyo ndiyo viwanda unavyovihesabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ngoja niwaeleze, kiwanda kidogo sana ni kiwanda kinachoajiri mtu mmoja mpaka wanne; na kiwe na thamani isiyozidi shilingi milioni tano. Kiwanda kidogo sana! Watu wanakwenda zaidi, wanasema ukiwa na vyerehani vinne ni kiwanda kidogo. Najua kuna Mbunge mmoja hapa alianza na vyerehani vinne, leo ana vyerehani 30.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Katani, amekuwa mkweli. Amesimama akawaambia, Mwijage alinielekeza nimekwenda, nimeona nimetekeleza. Waheshimiwa Wabunge, tuambizane. Kama kuna kasungura, umwambie na mwenzako.

Mheshimiwa Naibu Spika, huyo ninayemsema Mheshimiwa Mbunge, alianza na vyerehani vinne, leo ana vyerehani 30 na cherehani kimoja ni shilingi milioni tatu, ninety million, anaajiri watu wa kutosha. Kiwanda kidogo kinaajiri watu watano mpaka 49 na kina thamani ya milioni tano mpaka 200. Hivyo ndivyo sisi Wabunge tunavimudu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha kati kinaajiri watu 50 mpaka 99. Shilingi milioni 200 mpaka shililngi milioni 800 na hivi Wabunge tunavimudu. Ndiyo vile viwanda vya akina Mheshimiwa Captain Rweikiza vya kutengeneza nyanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukija kwenye viwanda vikubwa, vinaajiri watu 100 na vinatumia shilingi milioni 800 na kuendelea, ndiyo viwanda vya akina Mheshimiwa Salum, vya Jambo, ndiyo viwanda vya akina La Cairo, vimo humu. Kwa hiyo, hivyo ndivyo viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niwaeleze Sera ya viwanda ambayo nilizungumza mimi na Mheshimiwa Mama Lulida, shangazi yangu. Ni shangazi yangu kweli, tumetoka mbali shangazi Lulida na wengine waliochangia. Sasa niwaeleze, sifa ya Sera kama walivyosema Wabunge na nimshukuru mtangulizi wangu Mheshimiwa Mama Mary Nagu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sera yoyote ina sifa moja kubwa, lazima iishi muda mrefu, lakini na nyie mmechangia, kwamba sera mbona zinabadilika? Kumbe mlisahau, mnataka sera inayoishi muda mrefu, sasa ya 1996 mpaka 2020 huu ni muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, uzuri wa sera hii kuliko yote, inazungumza mambo mawili ambayo mmeyasema. Inasema viwanda visambae Tanzania yote. Nani hataki viwanda visambae Tanzania yote? Kama imepitwa na wakati, kwa hiyo, tuibadilishe viwanda vikae sehemu moja? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia inasema kwamba mikoa ya pembezoni ipewe vivutio; kwamba pamoja na vivutio kwa wawekezaji wote, lakini mikoa ya pembezoni ipewe more incentives. Kuna ubaya gani? Huwezi kwenda kuwekeza Kigoma bila kupewa incentives za ziada! Ni mbali sana! Uipiganie ndugu yangu Wamugabwa. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ndiyo hiyo Sera ya Viwanda ya Mwaka 1996 mpaka 2020. Kutokana na Sera hii, tumetengeneza mkakati wa integrated au fungamanisho la maendeleo ya viwanda, kutokana na Sera hii tumetengeneza vision ya 2025.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakumbuka wakati huo mimi nilikuwa officer, Mwenyekiti wangu wa Bodi Profesa Mwandosya akiwa yeye anashiriki kwenye timu iliyotengeneza vision ya 2025, tumetoka mbali. Nilikuwa nabeba mkoba, sera hii inatengenezwa. Sasa ni mimi, Mr. mimi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, msambao wa viwanda. Viwanda vina namna mbili. Sera inasema viwanda visambae; wawekezaji wanapokuja, Serikali au Waziri uwezo wangu wa ushawishi kiwanda kiende wapi ni mdogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, wawekezaji wanaokuja siyo mbumbumbu, wawekezaji wanaijua Tanzania kuliko tunavyoijua sisi. Akija Mjerumani anajua madini yako wapi. Labda wamwondoe Profesa Muhongo mtaalam wa miamba, lakini mwingine anakuja anakuonesha dhahabu ziko hapa. Ndiyo maana kila mara wanakuja wanajidai kwenda kuangalia makaburi ya babu zao. Wanaangalia yake mambo waliyoyaweka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, viwanda viko vya namna mbili, FDI, nina influence kidogo ya kueleza ziende wapi. Kuna LGI (Local Grown Industries), ndipo tunapokwenda kwamba unaanza na kiwanda kidogo sana, unakilea kinakwenda kuwa kiwanda kidogo, kinakuwa kiwanda cha kati na kiwanda kikubwa. Mdogo wangu Mheshimiwa Kitandula, ni mdogo wangu kabisa, tumefanya kazi wote, nimemlea, nimemfundisha kazi, tumefanya kazi wote. Pole sana na Tanga Fresh.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Mheshimiwa Kitandula angeniambia kwamba barua yake iliyokwenda Hazina hawakushughulikia ningeshakwenda mimi. Naomba anikumbushe nitakwenda Hazina huyo aliyekata aniandikie mimi, I am a Minister, kwa nini alinyamaza? Mimi nilisema mtu huyu hana hatia afunguliwe, yeye akakaa na barua akanyamaza. Angeniambia ningemwambia Mzee Mpango, huyu ni mtu wa Mungu anaelewa. Unajua Mheshimiwa Mpango watu hawamwelewi, unamtegea wakati anatoka kusali unamwambia shida yako, atakusainia tu. (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, viwanda vidogo sana, vidogo na vikubwa ndivyo viwanda tutakavyokwenda navyo ila watu wanavidharau kwa neno la viwanda vidogo. Waheshimiwa kiwanda cha shilingi milioni 200 kinazaa sana. Angekuwepo Mheshimiwa Katani angewaeleza mchanganuo na namshukuru sana Mheshimiwa Katani hata usiku nimemuota. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Katani, amenikumbusha Profesa Aba Mpesha, Baba Mchungaji wa kutoka Michigan University aliyenifundisha biashara ndogo na viwanda vidogo, aliyefanya utafiti wa korosho, watu wa korosho, wanasiasa wa Mtwara ndiyo waliomwekea mtimanyongo. Kama mnamtaka naweza nikampigia simu akatoka Michigan akaja, lakini kama mmejirekebisha. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, ngoja niwaeleze, wawekezaji wanakuja kule kwenye Mikoa na Halmashauri mnawawekea mtimanyongo kama ile kesi yangu ya Tabora. Mwekezaji ametoka China yupo uwanja wa ndege watu wakapiga figisu, wakamwambia umekuja Tanzania hupaswi kwenda Tabora, Tabora siyo Tanzania, yule Mchina akashangaa akarudi kwao. Inabidi niwaambie kusudi mwelewe tunayoyapata. Nichukue nafasi hii kumwombea kijana wangu Mheshimiwa Heche apone vizuri aje afanye kazi, tunafanana sura lakini ana pilikapilika nyingi. (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, ngoja niwaambie suala la Heche limekwisha, wale wawekezaji watakuja, mkitaka taratibu nitasimamia mimi wawekeze Tarime. Yale yamekwisha na nikitoka hapa nakwenda Dar es Salaam nikazungumze naye, mwambie afanye kazi moja mambo yamekwisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini naomba niwaeleze Wabunge kuwapata wawekezaji ni shida, msiwaseme neno baya na Tanzania si nchi peke yake ya kuwekeza. Mimi napoteza wawekezaji wanakwenda Zimbabwe, Mozambique, Ethiopia, Rwanda na baya zaidi wanakwenda kuzalisha Rwanda kusudi sisi tugeuke soko, msiniumize.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimewaeleza FDI na LGI, LGI ndiyo inaweza kusambaa nchi zote.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwongozo wa Tawala za Mikoa, tutafanya nini? Nimewaahidi kwenye hotuba yangu tunamalizia mwongozo, Wakuu wa Mikoa tutawapa mwongozo. Hii imetokana na nini? Baadhi ya Wabunge wananilaumu kwamba mimi napendelea mikoa fulani na mingine naiacha, tarehe 28 nakwenda Tanga. Niwaeleze Wabunge wa Tabora, Mheshimiwa Mwanry ameshafanya booking kwamba nikapige kongamano kule. Mjiandae Waheshimiwa wa Tabora, tupige kongamano na nimemweleza Mheshimiwa Maige rafiki zake wa Geneva awaambie na wenyewe waje watuletee viwanda twende Tabora. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naleta mwongozo kwa sababu imekuwepo kutolingana kati ya mkoa na mkoa. Ukifungua Facebook ni Simiyu, WhatsApp ni Simiyu, sasa tunataka kuwaambia Wakuu wa Mikoa wote waingie kwenye Facebook na Instragram na mitandao yote.

Ndiyo, wawekezaji wanatafutwa, kwa hiyo, nitatoa mwongozo wa kuweza kutekeleza hilo. Kwa hiyo, mwitikio wa mikoa haulingani lakini haya ni maelekezo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, tutaandika mwongozo, nitauweka dibaji mimi, ataweka dibaji Mheshimiwa Simbachawene na Mkuu yeyote ataweka dibaji twende mbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, kasi ya ujenzi wa viwanda, nimeilezea fast tracking. Jukumu la ujenzi wa viwanda linatafsiriwa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda seti kubwa na ujenzi wa viwanda vya subset. Sekta binafsi ndiyo itajenga viwanda, Serikali inaweka mazingira wezeshi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimewaeleza katika kipindi ambacho Mheshimiwa Rais yupo madarakani, viwanda vya sekta binafsi kwa address humu yaani mpaka wenye viwanda nimewawekea simu zao, wamejenga viwanda kwa mtaji wa shilingi trilioni tano, una mashaka wapigie simu, lakini nimeweka picha na beacon za mahali walipo unaweza kwenda ku-trace. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini napenda niwaambie mimi siyo saizi ya kuzalisha viwanda vya shilingi trilioni tano kwa mwaka mmoja, I want more, ndiyo maana nikaleta fast tracking, ndiyo maana nikazungumzia kuweka mazingira bora ya biashara. Kwa hiyo, nashukuru na nyie hamridhiki sio saizi yetu tunapaswa kukimbia. Hatupaswi kuwa soko la watu wengine, tunapaswa kuzalisha tuwauzie watu wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ulinzi wa viwanda. Niwashukuru Waheshimiwa wote waliozungumzia kuhusu ulinzi wa viwanda. Sitaki kurudi nyuma, nimeshampongeza Kivuli changu, unajua ukiona Kivuli kina mashaka hata na mtu mwenyewe ana mashaka, sasa Kivuli changu ni kizuri siwezi kusema zaidi, lakini Nunua Tanzania inaendelea. Mwaka jana ilipigiwa sana kampeni na Mheshimiwa Makamu wa Rais alipozindua 620GS1 lakini tulipokwenda kutoa award za Brand 50 mshindi akawa Alaska Rice, huyo mama Alaska Rice ni mke wa Mheshimiwa Bashungwa, Mbunge mwenzetu, anatengeneza branded product zinapendwa Dar es Salaam Supermarket zote. Hata pilipili, watu wanaokwenda kununua wanasema nataka ile pilipili ya Alaska, branded na Mheshimiwa Mbunge. Jamani Wabunge muwe mnaambizana tunaishi vipi siyo tunakuona unaendesha mtambo mkubwa hutuambii, tuambizane. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ulinzi wa viwanda tunauzungumzia. Ulinzi wa viwanda upo chini ya TBS, Fair Competition na upo chini ya Polisi. Niwahakikishie taasisi zilizopo chini yangu zitafanya kazi sasa kuliko wakati wowote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimehakikishiwa niseme ninachopewa na mimi nimekwenda kuwaambia wakubwa, bidhaa feki inapita, nimezungumza wakaniambia sema unachotaka nimewaambia, kwa hiyo, tutafanya kazi. Niwaeleze wawekezaji wengi kwa mfano kwenye sukari walikuwa wanakataa kwa sababu ya sukari inayokuwa smuggled in, kwa sababu ya mchele ulikuwa smuggled in, sasa watu wana confidence baada ya ku-control. Hata hivyo, namwomba Mheshimiwa Mwigulu tu-control zaidi bado, bado, bado. Kwa hiyo, vitu vya feki na quality tutalizungumzia.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie fungamanisho la viwanda na sekta nyingine. Waheshimiwa Wabunge kuna fungamanisho kuliko maelezo. Ukisoma mkakati wa pamba mpaka mavazi ni fungamanisho. Ndiyo maana Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Mwigulu huwa ananiita pacha. Ni kwamba mimi ndiye niliyebuni mradi wa viatu wa Karanga lakini mwenye dhamana ni Waziri wa Mambo ya Ndani. Nilijua tukitengeneza viatu Magereza vitasambazwa katika majeshi yote na yule mzalishaji anapata soko la kuanzia, kuna fungamanisho hapo. Soma mkakati wa pamba mpaka mavazi kuna fungamanisho, soma mkakati wa alizeti kuna fungamanisho.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa maziwa, soma Ripoti ya SAGCOT inazungumzia mradi wa maziwa. Nikiri kwa masikitiko kwamba hatufanyi vizuri kwenye maziwa, lakini mambo ya Tanga Fresh tutayashughulikia na viwanda vingine vianze. Niwaeleze jambo moja, ASAS ana kiwanda chenye uwezo wa kuchakata lita 50,000 kwa siku lakini maziwa anayopata ni lita 12,500. Kwa hiyo, kuna haja ya kuweza kuwasaidia watu wa Nyanda za Juu Kusini kuweza kuzalisha maziwa zaidi na chini ya hapo atakuja aeleze Waziri wa Kilimo ndiyo tunakuja na mpango wa SAGCOT wa kuleta IFAD kutoka Ulaya kusudi waende kule. Sitaki kusoma hotuba ya mwenzangu ngoja aje aseme mwenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda vya kipaumbele, nitafika baba ikibidi nitaomba muda. Ipo hoja ameuliza Mheshimiwa Mbunge, jina lake nimelisahau kidogo ila ame- declare interest kwamba yeye ni mwana Tanga na mimi Tanga nakwenda tarehe 28, kwa hiyo, huenda tutakutana huko. Nakwenda kupiga, mnaita sound, kuhamasisha viwanda, anasema tuwe na kipaumbele. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha Saruji cha Simba, kimeongeza uwezo kwa tani 750,000, ndiyo alichokizungumza Mwenyekiti wa Kamati yangu kwamba ile nafuu waliopaswa kupewa haijatoka. Mwenyekiti wa Kamati na wewe ni sehemu ya Serikali waambie watu wa Tanga walete karatasi zao tutakwenda Hazina wanieleze mimi kwa nini hawatoi. Kama mtu amewekeza na tani zinaonekana kwa nini msimpe? Halafu unajua watu sijui kwa nini, mkikwama huko mje kwangu, mimi ndiyo Waziri mwenye dhamana nitawapeleka huko mnakoshindwa kufika. Wanasema huwezi kwenda kwa Baba mpaka upite kwa Mwana, Mwana ni mimi. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ukisoma mkakati wa fungamanisho la viwanda, Mheshimiwa Mbunge aliyesema hatuna kipaumbele, kwenye mkakati wa fungamanisho la viwanda imeelezwa na hicho kiwanda kingine cha Tanga kitazalisha tani milioni saba, kitawaajiri watu milioni nane na 60% ya saruji itauzwa nje ya nchi, sisi tutabaki na 40%. Kinawekwa jiwe la msingi, kwa sababu sina mamlaka ya kutamka kinawekwa jiwe la msingi mwaka huu, kitapata vivutio.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa aliyesema kwamba hatuna vipaumbele asome mkakati wa fungamanisho la viwanda liko kwenye website yangu. Tutaweka kwenye viwanda vya sukari, Mkulazi tani 2000, Mbigiri 30,000, tutapanua Kagera Sugar na Kilombero. Juzi mbele ya Mheshimiwa Rais nimemueleza Mheshimiwa Zuma kwamba aisaidie Ilovo iongeze Kilombero One na Kilombero Two waache kutonunua miwa ya wananchi, kwa hiyo tumeyazungumza.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini katika hilo kuna pamba, mafuta ya kula ya alizeti, ngozi na bidhaa za ngozi na matunda. Kwa matunda ndiyo tunazungumza na Kiwanda cha Matunda cha Sayona. Nimewasikia Ndugu zangu wa Tanga, tunazungumzia Kiwanda cha Eveline lakini tunazungumzia Kiwanda cha Matunda cha Handeni, kwa hiyo, tunaendelea na imeainishwa. Tunazungumzia maziwa, tunaweza kuwa hatujatekeleza kama alivyosema Mheshimiwa Kitandula lakini ndiyo dhamira yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunazungumziwa viwanda vya nyama, watu wa Manyara mwambie yule mwana mama aliyekuwa na matatizo ya kiwanda chake cha nyama, matatizo yake yameainishwa kwenye Ripoti ya Profesa Mkenda. Wale waliokuwa wanamkwamisha, sitaki kuwasema wasijisikie vibaya wakashindwa kula, dawa yao imeshapatikana aje tumpeleke wampe nyaraka zake. Unamkwamisha mtu na kikaratasi asitengeneze kiwanda cha nyama, ng’ombe wanakwenda Kenya wanarudi, ningependa tuwe wawazi tuambizane. Hicho ni kiwanda cha Chobo Investment kipo Mwanza, anachinja ng’ombe 600 kwa siku, kijana amejaribu. Matatizo yako yote watayasema kesho kwenye Wizara inayohusika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu viwanda vya chakula na katika hili niwaeleze, nimekuwa nikisema hapa Bungeni, nikiwaambia Waheshimiwa Wabunge hakuna sababu ya kutoa mahindi Katavi kuyapeleka Dar es Salaam, msage mahindi kule, mfanye packaging vizuri, muweke kwenye maroli mpeleke sokoni. Ndiyo maana nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Aeshi ametengeneza kiwanda kikubwa sana cha kusaga nafaka na zitakuja sokoni. Waheshimiwa tuambizane, kama umewekeza mwambie mwenzako wewe umepata wapi namna, tuelezane. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa na rafiki yangu mmoja Kenya nilipotaka kuingia kwenye siasa nikamuaga aliniuliza Mwijage utaziweza siasa. Nikamwambia nitaziweza, I can talk. Akaniambia politics is not about talking. Akaniambia ninyi Watanzania mna tatizo moja. Akaniuliza adui yenu ni nani? Nikamwambia umaskini. Akaniambia mbona mnaogopa utajiri? Ukikutana na mwanasiasa wa Tanzania ukimwambia wewe tajiri anasema mimi maskini bwana, hapana! Mheshimiwa Aeshi amejenga kiwanda cha mfano cha kutengeneza nafaka, tunataka hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wanasema sembe nzuri inalimwa Ileje. Mheshimiwa Mbunge wa Ileje, jasiria, SIDO wanakuja weka kiwanda Ileje, mjini tunataka watu waondoke warudi shamba, zile by-product, mmetoa mfano mzuri wa pumba zibaki kule. Akinamama wapepete mahindi, wafanye packing, wakaangalie watoto wakimaliza pumba wawape mifugo, nazungumzia mifugo ng’ombe sizungumzii astaghfiru Allah. Unajua kuna wengine pumba wanamlisha astaghfiru Allah, hapana. Wamlishe ng’ombe akamuliwe maziwa, akikamuliwa maziwa mama auze na mtoto anywe. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, maamuzi ya Serikali ni kwamba ziliko rasilimali ndiko vitajengwa viwanda. Ndiyo maana Mheshimiwa wa Simiyu, maamuzi yamefanyika kiwanda cha vifaa tiba vitokanavyo na pamba nimeandika kwenye ripoti kitajengwa Simiyu kitatumia pamba tani milioni 50 na kitatuokoa na aibu ya kuagiza vifaa pamba toka nje. Tuna aibu nyingi na tutazimaliza. Tunaagiza hata drip ile ya kumwekea mgonjwa kutoka Uganda, hizo aibu zote tunazifuta. Soma ripoti hiyo, mimi aibu zote nimezianika kusudi mnione halafu mnipange vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, nayasema yote haya ili Waheshimiwa Wabunge wasiwe na tatizo la kuangalia vifungu ila wakubaliane tupitishe moja kwa moja. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu nyingine ni petrol chemicals. Petrol chemicals ni vile viwanda vya Mheshimiwa Muhongo. Kiwanda cha Ferrostaal Mheshimiwa Muhongo amekwenda zaidi mpaka ametaja tarehe ya kwenda Kilwa na mimi nimeshapata mwaliko kutoka Ujerumani, Profesa nitakuwa karibu na wewe. Unajua watu siku hizi wananichanganya na mimi wananiita Profesa, kwa hiyo, tutakuwa wote. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kiwanda Ferrostaal karibu kitaanza na kiwanda cha Helium kitaanza, kwa hiyo ni petrol chemicals zimeandikwa. Nawaeleza vipaumbele mvijue kwa sababu uwekezaji katika kiwanda cha mbolea utatuwezesha kuzalisha mbolea tani 2,600,000 katika viwanda viwili wakati mahitaji ya mbolea Tanzania mnatumia tani 400,000. Kwa hiyo, is a break through tutatumia mbolea zaidi, tutapata tija na viwanda vitafufuka. Ni kwa uwekezaji wa namna hiyo kuongeza tija ginneries zitafufuka, akina Manonga watafufuka pamba ikizalishwa kwa wingi na tukawa na viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo ya uwekezaji, Kurasini Logistic Centre. Kama nilivyoeleza kwenye ripoti yangu inatengenezwa. Mheshimiwa Ngwali, Kurasini Logistic Centre haiwezi kufika mwezi Julai. Nichukue fursa hii kuwaeleza watendaji ninaofanya kazi nao, mimi huwa nasema wazi, nimeshamwambia Waziri Mkuu kwamba performance ya EPZ si nzuri kwenye Kurasini Logistic Centre.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimewaandikia memo Makatibu Wakuu wangu kwamba I am not happy na speed ya EPZ on Kurasini, nimeshamwambia Mheshimiwa Waziri Mkuu baada ya hapo ni kwenda kwa tajiri. Naitaka Kurasini Logistic Centre ianze, namna nilivyokaangwa hapa na rafiki yangu Mheshimiwa Ngwali siwezi kukubali mimi ni mtu mzima. Kurasini Logistic Centre tutakuwa na nafasi nzuri kabla ya Bunge kuwaambia ni kitu gani kinafanyika, ikibidi kuitisha Bodi nitaitisha Bodi. Naitaka Kurasini Logistic Centre, mimi ni mtu wa Temeke nani asiyejua bwana, Mbunge wangu yupo hapa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, Bagamoyo Special Economic Zone, bandari ipo na itachimbwa na mwekezaji. Nimeulizwa kwa nini tumetaka private sector ilipe fidia? Mimi wazo hili nimelipeleka kwa wakubwa nikajenga hoja wakanikubalia. Wewe mtu umemthamini mwaka 2008 unamlipa kidogo kidogo huwezi kuona, tena Kamati yangu ndiyo iliniambia kwamba Mwijage itakuhitaji miaka 30 kumaliza, basi nikawaomba wakubwa tutafute private sector wameingia lakini malipo yote tutayasimamia sisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaeleze nimepata barua sasa hivi, kuna mwekezaji nguli kutoka China ananifuata hapa anataka nimpe eneo la kuweka Special Economic Zone. Nimeshawaeleza watu wote tunaofanya kazi pamoja, watu wa EPZA, Makatibu Wakuu mnahusika, huyo Mchina hata asiponiona mimi mpelekeni Bagamoyo, mpelekeni Kibaha, ninazo hekari 5,000 Kibaha.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaeleze watu wa Pwani, Mheshimiwa Subira Mgalu na Wabunge wote sijawahi kuona ukarimu kama wa Pwani. Mkuu wa Mkoa anachosema ndicho anachosema Diwani. Unajua ngoja niseme niokoke na nitakayemsema msimchukulie hatua yoyote. Watu wa Morogoro waliniangusha na nimemwambia Mzee Mbena. Nimemleta mwekezaji toka Singapore amefika pale Madiwani wanatokea huku wanakwenda huku, tumepoteza viwanda vitano kutoka Mauritius juzi vyenye kuweza kuajiri watu 7,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, niliwaambia nina kiwanja Morogoro, wakienda Morogoro wanatokea hapa wanaingia hapa, mara umeme mara nini. Umeme hauwahusu, umeme mniambie mimi, mimi Mzee Muhongo naongea naye wakati wowote, substation ni shilingi bilioni tatu, mbele ya kuingiza wawekezaji watano wanaozalisha ajira 7,000 ni kitu gani?


Mheshimiwa Devota nisaidie hilo, acha longolongo na mambo ya master plan tunataka eneo lile. Kwa hiyo, Bagamoyo itatekezwa na watu watalipwa haki zao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, TAMCO Kibaha, tunaendelea kutekeleza. Maeneo ya mikoani, Kigoma na Songea kwenye bajeti nimewaweka. Kwenye bajeti inayokuja naomba mnitendee haki msome vitabu vyangu. Mheshimiwa Special Economic Zone, nimesaini kwa mkono wangu Special Economic Zone nane za sekta binafsi, kwa hiyo, Serikali inapenda sekta binafsi. Nitambue nafasi ya Waheshimiwa Wabunge walioniahidi kunipa maeneo, Mheshimiwa Bashe taratibu, kama sikuwekeza leo na kesho ipo, wewe niombe nibaki kwenye nafasi hii. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuwezesha SME, SIDO, TBS na TanTrade wamekuwa wakiwezesha SME. Ninachotaka kuwaambia hatutalegeza viwango hasa kwa wale watengenezaji wa chakula, TFDA atashirikiana na TBS hatutalegeza viwango. Ila katika maelekezo ya Serikali za Mikoa mnapotenga maeneo wale akinamama, watu wamehoji nimesema nini kwa akinamama, akinamama muwajengee mabanda ambayo TBS atawapa mafunzo. TBS atakupa mafunzo na certificate na gharama za certificate atalipa yeye mpaka utakapokuwa mjasiriamali mwenye nguvu. Nimetoa maagizo na mamlaka inaniruhusu kufanya hivyo, akinamama niwapende zaidi ya hapo niwapende namna gani? (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuongeza hisa kwenye makampuni. Jambo ambalo nimekuwa na ushawishi nalo ni Urafiki. Mwekezaji wa Urafiki amekubali kupunguza hisa zake alikuwa na hisa 51. Majadiliano yanaendelea, wanafanya valuation na tumeshapata wawekezaji wa Tanzania. Kwa hiyo, hicho ndicho naweza kusema kuhusu Urafiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu TANALEC, sina mamlaka nayo ila mimi nawashawishi TANALEC waende kwenye Dar es Salaam Stock Exchange. Hata hivyo, katika kulinda uchumi wa viwanda Mheshimiwa Muhongo alishasema na kwenye tenda zake amesema transformer na cables zote zote kwenye REA Awamu ya Tatu zitanunuliwa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge, orodha ya viwanda ni kubwa, kuna kiwanda kimejengwa Tanzania cha kutengeneza waya, kina uwezo wa kutengeneza kilometa 100 za waya kwa masaa nane kiko Mwenge. Viko vitatu kimoja kiko Nigeria, kingine kiko Mwenge na kingine kiko South Africa, ni kijana mdogo ukimwona hutaamini.

Mheshimiwa Naibu Spika, matumizi ya makaa ya mawe. Mheshimiwa Profesa Muhongo amezungumza lakini mojawapo ya faida ya kutumia makaa ya mawe ya Tanzania yamechangamsha uchumi. Pale wanapopita wenye malori, mama ntilie anapika lakini spea na mechanic wanatengeneza Watanzania. Naomba mtuelewe, tumefanya hivyo kwa nia nje lakini hali hiyo imefanya wenye migodi waone kwamba kuna soko wamefungua migodi yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie korosho. Maelezo aliyozungumza comrade Mwambe, unajua ukiwa comrade hata ukijipaka matope mtu akikuangalia tu michango yako ni ya ki-comrade tu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, michango yake Mheshimiwa comrade na mchango wa Profesa Masawe wa Naliendele tutaufanyia kazi na tutamuunganisha na COSTECH kusudi zile bidhaa zinazotokana na korosho tuweze kuzitumia. Suala ni research na Profesa Masawe amefanya research, kuna bidhaa nyingi, brake lining na kile kinywaji ambacho wewe ukikiangalia unasema astaghfur Allah lakini kinaingiza pesa. Kwa hiyo, vyote hivyo tutavishughulikia na naomba tuendelee kufanya kazi wote. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, kipekee kuna faida kwa kuchambua korosho hapa ndani tunaposhughulikia viwanda vilivyobinafsishwa. Kama alivyosema Mheshimiwa Kitandula zile export levy, mabilioni yale, tutakaa tuwaulize wenye dhamana kama tunaweza kuchukua viwanda vya kuanzia kusudi msimu unaokuja tuweze kuanza na baadhi ya viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la CBE. Mheshimiwa Mwita ameleta suala la CBE akalipitisha kwa Mheshimiwa Ngwali akaona haitoshi akalipitisha kwa Mheshimiwa Mwambe akaona haitoshi, ikanipa shida. Nikaenda kutafuta Ripoti ya CAG.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya Mheshimiwa Waitara ni kwamba waliokwenda kukagua CAG hakukagua Dar es Salaam. Nakala niliyo nayo iliyowekwa lakiri na CAG anasema yeye CAG alikagua Dar es Salaam, lakini kwa mamlaka ya kiutawala, Waziri nikishapata ripoti, siruhusiwi kufanya lolote kwa watendaji napitia kwenye Bodi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waitara najua yeye amesoma sayansi mambo ya utawala hayajui. Ukiingilia moja kwa moja watendaji bila kupitia kwenye Bodi akienda mahakamani anakushinda. Kwa hiyo, mimi nimepata ripoti yangu nitaiandikia Bodi na itachukua action isipochukua action ndio mimi kwa mamlaka niliyonayo au kwa mamlaka ya uteuzi naweza kuchukua hatua. Nimhakikishie I have the report anaweza kuisoma, nimemshikilia kwa sababu imeandikwa siri na yeye siyo mmoja wa siri, sisi ndiyo watu wa siri, kwa hiyo mambo ndiyo hayo CBE Dar es Salaam ilikaguliwa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo, naomba nihitimishe kwa kuwashukuru kwa namna ya kipekee Waheshimiwa Wabunge na kupitia kwenu Watanzania wote ambao tunawawakilisha kwa ushirikiano mnaotupa katika kuendeleza sekta yetu na hususan ujenzi wa uchumi wa viwanda. Wizara daima itaendelea kuwa sikivu, kupokea mchango wa mawazo na ushauri katika kuboresha utendaji wa Wizara na sekta kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaombe kuendelea na ushirikiano huo katika kuhakikisha kuwa rasilimali tunazozipata zinatumika kwa umakini mkubwa ili mipango na mikakati ya sekta iweze kuleta matokeo chanya katika kufikia uchumi wa viwanda ifikapo 2025. Ni dhahiri kuwa ushiriki wa sekta binafsi na uthubutu wao ni nyenzo muhimu katika kuleta mageuzi na matokeo yenye ushindani utakaotokana na juhudi za uendeshaji na uanzishwaji wa viwanda, biashara, masoko, viwanda vidogo, biashara ndogo pamoja na uwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni jukumu letu tukiwa ndiyo wawakilishi wa wananchi wetu kuwajengea ufahamu wa mipango, sera, mikakati mbalimbali ya kisekta ili kuwaongoza ipasavyo katika ujenzi wa Tanzania ya viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru wewe binafsi kwa kunipatia fursa ya kuchangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2018/2019, awali ya yote nitoe shukrani na pongezi kwa Mheshimiwa Rais kumaliza miaka miwili na nimshukuru kwa kuendelea kuniamini nipige filimbi ya ujenzi wa Tanzania ya viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza Waziri wa Fedha na Mipango na Naibu wake kwa mpango mzuri ambao ninauafiki. Kwa sababu sitaki kufanya kazi ya kuwasomea watu, kila Mbunge anapaswa kusoma, nitatoa ufafanuzi kidogo juu ya mambo ambayo watu wanayaelewa ndivyo sivyo.

Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kukariri dhima ya mpango wa pili wa miaka mitano. Dhima ya mpango wa pili wa miaka mitano ni ujenzi wa uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Rafiki yangu Mheshimiwa Ummy amezungumzia maendeleo ya watu ambayo yanajikita kwenye elimu, yanajikita kwenye afya, yanajikita kwenye kipato. Sasa mageuzi ya kiuchumi, huu mpango ambao nauunga mkono ni sehemu ya ule mpango mrefu wa miaka mitano ambayo naiunga mkono. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda tunavyovilenga, nimesikia hoja watu hawajajua mpaka leo viwanda tunavyovijenga. Sitaki kuwasomea watu lakini kwa faida, viko viwanda vya makundi manne na vyote tumevishughulikia. Kundi la kwanza ni viwanda vinavyochakata mazao au malighafi ya wananchi, katika kuhamasisha ni jukumu la viongozi wote na wananchi wote, ninapopiga filimbi nawategemea na ninyi Waheshimiwa Wabunge tuendelee kuhamasisha zile malighafi tuzijengee viwanda.

Kundi la pili ni viwanda ambavyo vinaajiri watu wengi. Yupo Mheshimiwa Mbunge ameniambia kwa nini usilete viwanda vya teknolojia ya juu, hapana! Watanzania wote hawawezi kuendesha mitambo ya teknolojia ya Juu, Watanzania wote hawawezi kuendesha LNG Plant, kwa hiyo, nitaendelea kutengeneza viwanda vinavyoajiri walio wengi ili kusudi wale wenzangu na mimi ambao waliishia darasa la saba na darasa la kumi waweze kutumika pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kundi la tatu ni viwanda ambavyo malighafi zake, bidhaa zinazozalishwa zinatumika sana. Katika kundi hili tumefanya vizuri sana katika viwanda ambavyo nilianzisha. Tuna uwezo uliosimikwa wa kuzalisha saruji tani milioni 10.8, tunatumia mahitaji yetu tani milioni
4.87 kwa hiyo tuna uwezo wa kuzalisha kuliko ambavyo tunahitaji kama nchi. Tuna mahitaji sasa ya kujenga viwanda vya tani milioni 10 Sinoma Tanga lakini kuna viwanda vinakuja Chalinze, Mamba na mwenzake Nyati wanaweka viwanda vya tani milioni tatu pale. Kwenye hiyo industry ya bidhaa zinazotumika sana tumefanya vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kundi la nne ni kutumia malighafi ambazo tumepewa faida na Mwenyezi Mungu ya kipekee ndiyo inaangukia suala la viwanda vya mbolea inayotumia gesi. Niwaeleze Waheshimiwa Wabunge mmelizungumza, Ferrostaal ameshapewa clear line na Wizara ya Nishati kwamba atengeneze mbolea. HELM ya Mtwara na ninyi njooni mjadiliane tuko tayari mzalishe mbolea. Tunapojenga Bagamoyo Special Economic Zone viwanda 190 kiwanda kimojawapo kitakuwa cha kutengeneza mbolea. Kwa hiyo, hivyo ndivyo viwanda tunavyoshughulikia. Sasa uhamasishaji ni jukumu lako mimi nikiwa nimetangulia kusudi tujenge Tanzania ya viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mafanikio tuliofanikiwa, tumepata mafanikio. Fanikio moja kila Mtanzania sasa anaimba viwanda. Nchi yote watu wanaimba viwanda na nilifikiria wakati huo nitoe dhana ya isiyokuwa. Unapozungumza Watanzania, kwa mfano viongozi tunazungumza Watanzania kuanzia ngazi ya kwanza ngazi ya juu, ndiyo maana mimi kiwanda kidogo hata vyerehani vinne naendelea kusema ni viwanda vidogo. Kwa hiyo, usijitambue wewe nafasi yako kwa sababu unazo, lazima tuwalee Watanzania wadogo mpaka wale Watanzania wakubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa faida ya yule aliyeuliza swali, viwanda vidogo sana vinaajiri mtu mmoja mpaka wanne na capital yake ni shilingi milioni tano. Cherehani industrial kinauzwa shilingi milioni 3.5 na kinaweza kukutengeneza kipato cha kukutosha wewe na familia yako. Vipo viwanda vidogo vinaajiri watu watano mpaka 49 na mtaji wake ni shilingi milioni tano mpaka shilingi milioni 200. Hivi ndiyo vile viwanda vya kuchakata nyanya, viwanda vya pilipili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna viwanda vya kati vinaajiri watu 50 mpaka 99, vinaanzia shilingi milioni 200 mpaka shilingi milioni 800. Kuna viwanda vikubwa milioni 800 na vinaajiri watu 100 na kwenda zaidi. Hiyo ndiyo naihubiri kwa Watanzania walio wengi. Nikienda kwa wale wenye nazo; kiwanda kidogo wanasema ni shilingi bilioni mbili lakini tunahimiza viwanda vidogo na ukisoma Mpango wa Mheshimiwa Mpango anakuambia SIDO itapewa kipaumbele cha kuongoza katika ujenzi wa viwanda, kwa sababu tunatambua kwamba wananchi walio wengi wataweza kupata faida kwa kushiriki katika kuchakata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaeleze Waheshimiwa Wabunge katika ujenzi wa viwanda sekta inayoongoza ni ya uchakataji (manufacturing) wanaita mediating sector, tunataka tuwalee Watanzania watoke katika uchuuzi wawekeze katika kuchakata katika kutengeneza viwanda. Pale ulipo, uangalie zile factor zinazokuwezesha uweze kwenda mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma ule mpango wa pili wa miaka mitano nafasi ya sekta binafsi ndiyo mhimili kwa hiyo msitegemee Serikali ihamasishe, sekta binafsi ihamasishe, ni jukumu lenu ni jukumu langu na sekta binafsi ndiyo itafanya hayo mambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala ambalo kuna watu wamedokeza nawaheshimu sana rafiki zangu, nitawapiga taratibu. Watu wanasema kwamba Serikali haina mahusiano mazuri na sekta binafsi. Hamna taarifa, Serikali inakutana na sekta binafsi na jana wanaosikiliza taarifa za kiingereza katika kipindi cha This Week In Perspective wamesema wenyewe watu wa Tanzania Private Sector waliokuwa pale kwamba mahusiano ni mazuri sana mpaka Mheshimiwa Rais anawaita wafanyabiashara anazungumza nao. Ila ni kwamba kuna paradigm shift, mambo yamebadilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatengeneza viwanda ili moja; tutengeneze ajira, tunatengeneza ajira, mbili; tuzalishe bidhaa zenye ubora kusudi tuweze kutosheleza mahitaji ya Watanzania na kuuza nje. Lakini tunatengeneza uchumi wa viwanda na viwanda ku-broaden ile tax base. Mwisho yote haya mawili ukiyatengeneza utakwenda vizuri. Lakini mwisho lazima umuone Mzee wa mpango uweze kumpa chochote. Kilicho cha Yesu mpe Yesu na cha Kaisari mpe Kaisari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie masuala maalum. Limezungumzwa suala la Mchuchuma na Liganga. Amezungumza Mheshimiwa Mpango, Mchuchuma na Liganga naisimamia mimi na ni suala la muda. Ile sheria mliyoibadilisha Bungeni ya kuhusu rasilimali zetu tupate kiasi gani inahusu Mchuchuma na Liganga. Nikishamaliza mambo yangu, mwekezaji tayari ana pesa ya fidia anaanza na kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la EPZA watu wanasema tunatumia utaratibu ambao hautumiki dunia nyingine, ndiyo! Mambo mengi tunayofanya Tanzania hayatumiki sehemu nyingine, kama la kuwakoromea wale watu wa makinikia, Marais wachache wanaweza kuwakoromea, kwa hiyo, kuna mambo ni ya kwetu kwetu tu! (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachofanyika kwenye EPZA, tumekubaliana na wawekezaji wa Bagamoyo waje walipe fidia tutengeneze ile Bagamoyo Special Economic Zone. Bagamoyo Sepcial Economic Zone Januari inaanza na nitatengeneza viwanda 190 kwa kuanzia. Tutaharakisha viwanda hivi mwaka 2020 viwe vimeanza. Mwaka 2020 kuna shughuli lazima nihakikishe kwamba viwanda vile vipo ili kusudi niweze kuonesha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee. Suala lingine specific la uhusiano kati ya sekta ya kilimo na viwanda. Waheshimiwa Wabunge, Serikali (mimi ndiyo napiga filimbi) lakini siwezi kufanya kazi bila kilimo, bila mifugo, bila TAMISEMI, bila miundombinu na miundombinu wezeshi ndiyo maana nahitaji umeme, nahitaji maji, nahitaji reli, nahitaji barabara. Ukijumlisha hayo ndiyo yanaitwa uchumi wa viwanda halafu mimi nakuja najenga viwanda.

Kwa hiyo, wanaosubiri milingoti ya viwanda ukiona reli inajengwa, viwanda vinakuja. Ukiona mabomba ya maji viwanda vinakuja, ukiona umeme unavutwa viwanda vinakuja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo ndiyo mahusiano. Serikali ihakikishe upatikanaji wa soko la mazao. Hapa ndipo kuna kazi. Nimei-position kwa maelekezo ya Mheshimiwa Waziri, nai-position Wizara yangu. Wizara yangu imepewa mandate mpya ya kuhakikisha tunatafuta masoko ya mazao, yawe kilimo, yawe wapi ni kazi yangu mpya katika hii awamu mpya kuhakikisha ninapata soko la mazao na nitatoa mwongozo zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viwanda vya kuchakata mazao nimelizungumzia katika zile sekta tatu, watu wanauliza mbona nyama haijazungumzwa? Katika mazao ya wananchi mifugo ni mazao ya wananchi ndiyo viwanda category number one. Viwanda vya mbolea vya Ferrostaal na HELM nimevizungumzia ni kiasi cha kusubiri vinakuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uhamasishaji nimezungumza ni jukumu la sisi wote. Viwanda vilivyokufa tunavifufua na hakuna mjadala. Atakayeshindwa ampe mwenzake na tunahakikisha suala hilo tunalifikiria. Ukisoma Vision 2020 inaelezea kwa nini tulishindwa lakini ukisoma Mpango wa Pili unakueleza kwa nini hatutashindwa. Import substitution come export promotion ni mojawapo ya hatua nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie sekta ya sukari na nizungumze kuhusu Mheshimiwa Mchengerwa. Wale wawekezaji wako watatu siku zao zimehesabiwa, hatutaki watu kuatamia maeneo ya ardhi. Tutashirikiana Wizara ya Ardhi na ile ya Kilimo kuhakikisha kwamba tunazalisha sukari ya kutosha. Watu wa SADC wametusaidia kupata uwezo wa kuzalisha sukari bila kuingiliwa. Tanzania tuna uwezo wa kuzalisha tani milioni mbili kwa mwaka kwa kutumia mabonde yetu yote yaliyopo. Mheshimiwa Rais alipokuwa Kagera ametoa ultimatum kwa wenye viwanda waongeze uzalishaji na hilo mimi nalisimamia. Kwa hiyo, msiwe na wasiwasi tutazalisha sukari lakini uzuri wa sukari uzalishaji wa sukari unatengeneza ajira nyingi. Kwa hiyo, Kigoma kwetu kule nitapeleka viwanda viwili kusudi watu wa Kigoma badala ya kwenda mbali mkate miwa kwenu na mambo yawanyokee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utendaji wa Wizara nimeshazungumzia naipanga upya, lakini jukumu la SIDO kwenye mpango ndiyo inatangulia na niwaambie naanza na Mkoa wa Geita, Katavi, Simiyu, kote huko naweka ma- shade mpya. Kwa hiyo, nataka kuwaonesha tunatengeneza shade, dada tulia na Kagera nitaweka, tunatengeneza shade ambazo mtu unachakata unakwenda pale, ma-shade ninayokujanayo ni mapya, unapewa shade, unafundishwa na namna ya kuchakata, ukihitimu unatoka na kitu chako. Ni miaka miwili, mwaka wa tatu mtaona wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitambue mchango wa Mheshimiwa Saada. Na mimi nitazungumza na counterpart wangu wa Zanzibar namna ya kuweza kuchakata ile karafuu kuiongezea ubora. Napenda kutumia fursa hii kuwaambia kwamba watumie wataalam wangu, SIDO tutaiongezea uwezo iweze kufanya kazi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nizungumzie mchango wa Mheshimiwa Mbowe, aliyezungumza kwamba hatuna sera na kwamba tutengeneze sera moja, huwezi kutengeneza sera moja, sera zote zilizopo ni nzuri. Ile mnayoiita fast tracking ni kuharakisha na fast tracking strategy maana yake ni nini, ni kuondoa vikwazo. Tunayo hiyo na tunayo blue print ambayo ukisoma Easy of Doing Business tuko poorly ranked, sasa kwa sababu tuko poorly ranked tumejitambua sisi tukatengeneza blue print, ile blue print ndiyo inakwambia kasoro yako, usichelewe kutoa kibali, nenda kalipe kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale wanaposema tumepimwa vibaya hata kutolipa kodi wazungu wanatuona ni kasoro. Kwa hiyo, kama mnasema Easy of Doing Business tunarudi nyuma ni kwa sababu watu hawalipi kodi. Sasa huwezi kunihukumu Mwijage eti nimerudi nyuma kwenye Easy of Doing Business ni kwa sababu watu hawakulipa kodi. Hawa watu nitaendelea kuwabembeleza mimi kusudi walipe kodi niendelee kupata ranking nzuri. Kwa hiyo, mikakati iliyopo ni mizuri ila kama mtu anataka nije nimsomeshe, nimwelekeze taratibu, mikakati ile inatosha na niwahakikishie Tanzania sasa tuko kwenye viwanda, siyo kwamba tutajenga viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo machache, naomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Fedha, tutakwenda vizuri, Mpango uko vizuri.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuhitimisha hoja ya Wizara yangu. Hoja zangu ziko kwenye makundi makuu mawili, kundi la kwanza ni hoja kama zilivyowasilishwa na Wabunge kupitia kwenye Kamati inayosimamia Wizara hii, niwashukuru kwa kuleta hoja zao na ninawaahidi kwamba nitazitekeleza. Kundi la pili ni Waheshimiwa Wabunge ambao ama walizungumza ama walikuja kwa maandishi wakichangia bajeti hii. Waheshimiwa Wabunge 50 wameweza kuchangia kwa kuongeza hapa Bungeni na Waheshimiwa Wabunge 39 walichangia kwa maandhishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi Mheshimiwa Spika wakati alipokuwa hapa nawasilisha alitupa dira na nadhani ndiye aliyewapa hamasa Waheshimiwa Wabunge kwamba muijenge upya, mui-shape upya hii bajeti. Hiyo yote yaliyosemwa nakwenda kuandika upya utekelezaji wangu wa mwaka unaokuja. Kwa kukubali kwangu huko niko mbele yenu nikiwaomba mpitishe bajeti yangu nitaitekeleza kama mlivyonishauri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaongozwa na Dira ya Taifa 2020/2025 ambayo kama Taifa tunalenga ifikapo mwaka 2020/2025 Taifa letu liwe Taifa la uchumi wa kati. Uchumi wa kati Watanzania wenye kipato cha kati tungetamani Mtanzania wakati huo 2020/2025 awe na kipato kwa wastani wa dola 3,000, hicho ndicho kipato tunachokitaka ili kufikia hapo kwenye uchumi wa kati uliojumuishi chombo cha kutupitisha mpaka hapo ni uchumi wa viwanda. Dira yetu ya Taifa inajengwa katika mipango mitatu ya miaka mitano mitano iliyoanza mwaka 2011 inayoisha 2026. Mpango wa kwanza ulilenga kuondoa vikwazo, mpango wa pili ni ujenzi wa uchumi wa viwanda na mpango wa tatu kujenga uchumi shindani (the capacitive economy).

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kufika hapo tunaongozwa na mkakati (Integrated Industrial Development Strategy) wa 2011 unakwenda mpaka 2020/2025 unaelelezea yote ambayo Waheshimiwa Wabunge mlikuwa mnanikumbusha yote yameandika mle. Huo ni mkakati mkubwa, ndani ya mkakati mkubwa kuna mkakati mdogo, mkakati mdogo wa kwanza unazungumzia kutoka pamba mpaka mavazi, mwingine unazungumzia fursa ya kutumia mafuta ya kula kutoka kwenye mbegu tuzalishayo hasa hasa alizeti. Kama mlivyosema Waheshimiwa Wabunge mafuta ya kula ni bidhaa ambayo inachukua pesa zetu za kigeni ikiwa namba mbili ikifuatiwa na mafuta ya jamii ya petroli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati mwingine kama mlivyosema Waheshimiwa Wabunge upo unazungumzia namna gani tutengeneze ngozi na bidhaa za ngozi. Wakati mwingine mdogo ni wa madawa, mkakati mwingine ni wa kujitosheleza chakula, mikakati yote hii inajengwa ndani ya mkakati mkubwa wa Integrated Industrial Development Strategy.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunapojenga uchumi wa viwanda kwa maandiko ya mipango hiyo mitatu na kwa maelekezo ya viongozi wakuu, tunaambiwa tulenge mambo matatu, tujenge viwanda ambavyo vinaajiri watu wengi. Tujenge viwanda ambavyo bidhaa zake zinatumika sana, lakini tujenge viwanda ambavyo vinategemea malighafi zinazozalishwa na Watanzania walio wengi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyoeleza viwanda vinavyozalisha bidhaa zinazotumika kwa wingi tumebakiza item moja na mimi na Waziri wa Afya tumeweka kipaumbele kuhamasisha ujenzi viwanda vya madawa. Tutakapokuwa tumefanikiwa kujenga viwanda vya madawa sekta ya bidhaa zinazozalishwa kwa wingi tutakuwa tumevuka. Kama nilivyoeleza tunajitosheleza kwa nondo, lakini Mheshimiwa Bulembo amehoji inakuwaje nondo zinapanda bei.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika soko la dunia chuma kimepanda bei hatujafika Bajeti Kuu ya Serikali tutaangalia namna gani ya kufanya, lakini mtoto mzuri Dangote ambaye mimi namuita mtoto mzuri, alipoharibikiwa mitambo yake ya clinker kutokuwepo kwa Dangote ambaye yeye anazalisha tani milioni tatu kwa mwaka hawa wazalishaji wadogo wakashindwa kulihimili soko. Kwa sababu Dangote alipoleta industry shakeout hawa wazalishaji wengine walikuwa wamerudi nyuma wakizalisha kwa kujikimu, sasa alipoondoka kwenye soko tukabaki na vacuum, lakini Dangote wakati wowote atamaliza mtambo wake wa clinker na wakati huohuo anafungiwa gesi kila kitu tayari atarudi troublemaker, tuweze kurudi kwenye bei zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naelezea viwanda ambavyo bidhaa zake zinatumika kwa wingi ndiyo tuko hapa, tumebakiza madawa, pili tumebakiza mafuta ya kula ambayo nitaelezea suluhisho lake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachofanya siyo kufika uchumi wa kati, ni kufika uchumi wa kati ulio jumuishi na uchumi wa kati ulio jumuishi unaupata kwa kupitia viwanda vinavyotegemea mali za wakulima na ndiyo maana tunazungumza viwanda kuanzia vijijini, ndiyo maana tunazungumza viwanda vinavyochakata malighafi za wananchi, yule anayelima pamba anapata keki yake, anayeivuna anapata keki yake, anayeichakata kwenye ginnery anapata keki yake, anayetengeneza nguo anapata kipande cha keki na anayekwenda sokoni kuuza nguo ndiyo uchumi jumuishi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ilibidi niliendeleze hivyo, ili kujenda uchumi jumuishi ambapo Wizara yangu inakuwa ni kitovo na muhimili nahitaji watu wa kuniwezesha. Nichukue fursa hii kumpongeza Waziri wa Nishati amezungumza, bila nishati huwezi kujenga viwanda, unahitaji nishati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru Waziri wa Nishati umezungumza power mix sipaswi kuirudia, tunahitaji umeme wa kutosha. Hatuwezi kuuza mawese ya Kigoma, Kigoma inaweza kuzalisha mawese lakini soko liko Dar es Salaam, asilimia 50 mpaka asilimia 70 ya bidhaa zote ziliwazo Tanzania huliwa Dar es Salaam. Hivyo mawese ya Kigoma bila usafirishaji mzuri hamuwezi kuyauza Dar es Salaam, ndiyo maana tunajenga standard gauge, kumbe reli miundombinu wezeshi, barabara ni miundombinu wezeshi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mlivyosema bila maji hatuwezi kwenda popote, namshukuru Mwenyezi Mungu Bwawa la Kidunda litawezesha Bagamoyo Special Economic Zone na Dar es Salaam kufanya kazi. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge niwaeleze, tunachofanya tunataka kuwa Taifa lenye uchumi wa kati ifikapo 2025, tuna miaka miwili, tunaweza kuwa tumechelewa, lakini msikate tamaa, your on right truck. Unapokuwa na mashaka na kule uendako umeshaijua njia, haya mashaka mnayoonesha ina maana mmeshaiona njia, kazi mliyoifanya kwa siku mbili imeshanionesha namna gani niendeshe kwa kasi. Nimeona nizungumze hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viwanda vilivyobinafsishwa; kazi niliyopewa moja ni kuhakikisha viwanda vyote bila kujali mmiliki vinafanya kazi vizuri. Viwanda vyote bila kujali mmiliki binafsi na vya Serikali vinafanya kazi vizuri. Ndiyo maana tunazungumza mazingira wezeshi, natambua concern yenu, natambua maelezo yenu katika mazingira wezeshi. Hatuko vizuri kwa muhtasari wa namba, kwamba sisi ni wa 137 kati ya 190, lakini distance to frontier tuko above 50 percent. Sitaki kujivuna na hiyo nitafuata maelekezo yenu na ndiyo maana tunakuja na regulatory reform ya blueprints ambayo hizi taasisi mnazozilalamikia zitalazimika kufanya kazi, inaanza na bajeti mpya kwa sababu ina bajeti implication. Hatukuianza jana kwa sababu ina mambo ya kibajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vilivyobinafsishwa na nimshukuru Shangazi yangu Mheshimiwa Lulida alisema Mwigaje asiwe kondoo wa kafara. Lakini hili la viwanda niko tayari kuwa kafara! Nitahubiri viwanda anayetaka kunipiga risasi anipige risasi, lakini Mheshimwa Lulida unajua mtoto hakui kwa shangazi yake, mimi nilipoelekezwa suala la viwanda, viwanda vilivyobinafsishwa vilikuwa ni 156, tulipokuja kufanya snap shot wakati naambiwa nikiwa Tanga na Mheshimiwa Rais kwamba nimemkwanza, viwanda vilivyokuwa vinafanya kazi vizuri vilikuwa 62, vilivyokuwa havifanyi vizuri tatizo langu vilikuwa 56, vilivyokuwa vina suasua ni 28, vilivyouzwa by stripping (engine peke yake, godown peke yake) vilikuwa kumi. Nikaanza kazi, taarifa niliyowaletea mwezi Machi ndiyo kazi niliyofanya. Katika viwanda 56 troublesome, viwanda 18 vimeshaanza kukarabatiwa na vimekarabatiwa tayari kufanya kazi. Katika kipindi cha mwaka mmoja nawaomba Wabunge mnikubalie muwe na uhakika kwamba nikibaki hapa kufikia mwaka kesho viwanda vinatakuwa vimekwisha vyote. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja nikuambie viwanda 35 vilivyobaki na nitawasilisha kwa Mheshimwa Spika haya ni mambo ya kitaalam, Waheshimiwa Wabunge viwanda 35 vingine havina sifa ya kuwa viwanda, lakini kwa mamlaka niliyonayo siwezi kuvifuta, inabidi niende kwenye ngazi zinazohusika niwaambie jamani mlichonionesha kama ni viwanda 156 hiki haki-qualify. Mfano, lilikuwepo eneo la kiwanda cha kuunga matrekta, nimeambiwa na kiwanda, nikaenda kufanya survey nikakuta wamejenga shopping mall nzuri kabisa, inaajiri watu inaitwa Quality Center, mimi mall naipenda kwa sababu inazalisha ajira, kumbe tumekosa eneo la matrekta sasa nimetengeza maeneo mengine ya matrekta, ugomvi utoke wapi? Mnanishauri nikabomoe ile shopping mall? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna viwanda vingine vilikuwa vya kupasua mbao, nilipokwenda kuangalia misitu imekwisha, sasa huyo mtu nimfanyeje, nimuue huyo mtu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna viwanda vingine ni mali ya Serikali, kuna eneo kiwanda cha maziwa ni mali ya NHIF, sasa kiwanda cha Serikali siwezi kukichukua nimemwambia NHIF pesa unazo unijengee kiwanda cha madawa, yuko kwenye mchakato ajenge kiwanda cha madawa, ndiyo story za viwanda hivi navimaliza kabla ya asubuhi. Waheshimiwa Wabunge mniamini, wengine wanasema Mwigaje he is not serious, siwezi kujiua! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumze suala la sukari, mimi ni mcha Mungu na mcha Mungu yeyote ni lazima atii na aheshimu dini ya mwezake. Mbali na kuwa mcha Mungu mama yangu ni Muislamu apumzike kwa amani, mama yangu aliitwa Mariamu, nikalelewa na bibi yangu anaitwa Mwamini na Zuhura. Kwa hiyo Uislamu ninao, Mjomba wangu anaitwa Sadiki, kwa hiyo siwezi kuhujumu Uislamu. Mama mdogo wangu mwingine yuko pale, sina tatizo, lakini Watanzania niwaambie tunayo sukari ya kutosha. Tunapozungumza sasa kuna tani 43,000, kwenye stock, lakini Tanzania tunatumia tani 40,000. Bandarini nimeshamwagiza Meneja wa TFDA na TBS sukari iliyoko bandarini inaondoka, ninyi Wabunge ndiyo mnawaonea huruma wale wanaokwenda kufunga na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mbunge yeyote, Mbunge wa kwanza ameshaniambia nimpe tani 1,000 nimemruhusu achukue, njooni mchukue sukari, tuna sukari ya kutosha. (Makofi?Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini bandarini tani 22,000 ziko tayari. Mbali na sukari hiyo viwanda vya sukari vyote vimebakiza wiki tatu mpaka wiki nne baada ya dry season vinaanza kuzalisha. Kwa hiyo, asitokee suala la uadimikaji wa sukari ilikuwa ni propaganda na katika propaganda mimi nilisomea propaganda mpaka China ilikuwa ni propaganda sukari ipo, kama ni propagandist mwenyewe ni mimi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kingunge angekuwepo ungemuuliza propaganda alinifundisha Kingunge Ngombale Mwiru. Kwa hiyo, hakuna tatizo la sukari, Wabunge niko hapa na tunafunga kwenye mwezi mtukufu wa Ramadhani atakayekuwa na tatizo aje aniulize tunasambaza sukari kwenda mikoani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzue suala l sukari nchini, suala hili halikuanza leo na linaenda na mfungo wa Ramadhani, linaendana na rain season viwanda vinapofungwa tumekuwa na haja kama nilivyowafahamisha kwenye sababu tatu za viwanda tulenge viwanda vinavyoajiri watu wengi, kama ilivyo pamba sekta ya sukari inaajiri watu wengi. Sekta ya sukari, kwa mfano kiwanda cha Kagera Sugar kinachozalisha tani 75,000 kinaajiri watu 5,000, lakini Tanzania kama nchi ndiyo wale Wabunge mnasema halafu mnakasirika mnasema shame, wakati mwingine mna haki ya kusema hivyo. Tanzania tuna fursa ya kuweza kuzalisha tani milioni mbili za sukari kwenye mabonde yetu, lakini upaunuaji wa mashamba hayo financiers/wanaotoa fedha walikuwa wanakataa kwa sababu ya uingizaji wa sukari holela na substandard. Tatizo lililompata Kenya, uingizaji wa sukari wa Kenya, sukari wanayozalisha imeshuka kwa 40 percent, sasa tulichoamua Serikali ni kwamba gap sugar tani 135,000 wailete wale wenye viwanda ambao wanalalamika kwamba kuna watu wana- dump sukari halafu wale wenye viwanda tukawapa masharti watuoneshe acreage, eneo watakaloongeza la kuweza kulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niwaeleze kwamba Kiwanda cha Mtibwa wanaongeza, British Food walikuwa hapa kwenye Mei Mosi wakija kutangaza mbele ya Mheshimiwa Rais, wame-commit bilioni 500 Kilombero kuwekeza, pamoja na kuongeza Profesa Jay nikuambie, nitahakikisha maslahi ya wafanyakazi waliopunguzwa wanalipwa pesa zao. Watu wa Mtibwa wanatengeneza bwawa la irrigation 29 square kilometres, Mwenyekiti wa Kamati ni shahidi wameanza system ya irrigation na Kagera vilevile. Mheshimiwa Rais amewapa daraja kuvuka kwenda upande wa Kitengule, tunataka kujitosheleza kwa sukari na ninawahakikishia utaratibu huu ni mzuri, atakayekiuka tunamchukulia hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze alizeti, mawese na karanga ili kuziba lile pengo. Nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Munde Tambwe, amesema kwao Tabora na Wabunge wote wa Tabora na Halmashauri zenu eti mje kwangu niwape trekta, nina matrekta 148, mimi ndiye nawajibika, hizo tractor tatu mlizoomba kila Halmashauri mniletee barua ya Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi

wa Halmashauri, Mkuu wa Mkoa asaini, mlete kwangu kwa mamlaka niliyonayo matrekta zikaanzie kule hamuwezi kutoroka ninyi ni Watanzania. Ngoja tukafanye mazoezi Tabora, Mheshimiwa Munde tukafanye mazoezi Tabora tuta- leverage kwenye Mikoa mingine. Maksudi yake ni nini? Tumeshakubaliana na SAGCOT walete mbegu zenye high yield na ninyi Wabunge najua, kuna Wabunge mnalima alizeti, msilime alizeti ilimradi alizeti, kuna alizeti ambazo ukikamua unapata mafuta mengi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, SAGCOT wameshafanya utaratibu, Waziri wa Kilimo ataelezea, tutawapa mbegu lakini ngoja niwaambie na mimi nitakwenda kukamata shamba Tabota nitaanzia Tabora nikikosa Nzega nitakwenda Igunga tulime alizeti, nitahakikisha si mmesema viwanda nivilindwe, nitavilinda viwanda vinavyozalisha mafuta yawe ya pamba, yawe ya alizeti tuondoe hiyo mliyoniambia shame. Nilikuwa naangalia kwenye dictionary, shame ni neno baya mtu akikwambia shame nikamuuliza mwanangu anasema shame maana yake ni nini. Kwa hiyo, nitawahakikishia tunazalisha alizeti na tunapokuwa na alizeti tunaweza kujiokoa na mafuta. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze suala la kulinda viwanda, suala la la kulinda viwanda ni wajibu wangu, lakini Watanzania tukubaliane, waliochangia wengine wamehoji utamaduni wa TBS na FCC. Ukienda bandarini haya mambo ya under invoicing na over invoicing kuna nguo zinapita wakishonewa wanafunzi uniform baada ya wiki tatu nguo inakuwa kama chandarua. FCC akizichoma ndiyo hayo maneno ya Mheshimiwa Munira anasema mnachoma nguo za watu, mniongoze nifanye nini. Sasa kwa sababu mmeniruhusu, atakayeleta bidhaa yoyote, TBS nakwambia na FCC wewe choma usisikilize kilio cha huku kwa sababu Waheshimiwa Wabunge wameniruhusu wenyewe. Hiyo ndiyo namna ya kulinda viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, linahusu valuation ya TRA. Suti niliyovaa mimi hii thamani yake ni dola 600, mtu wa TRA akii-value dola 50 unapigwa 25 percent na 18 percent, sasa wewe unataka ipigwe vipi? Mheshimiwa Mpango wametupa ruhusa atakayeleta suti kama hii niliyovaa akasema dola 50 nakuomba tu-uplift kusudi tuipige bei kubwa, tulinde viwanda vya ndani, nadhani ndivyo mlivyonieleza! Ndivyo mlivyotueleza, ndivyo nilivyo waelewa na ndiyo maana viwanda vyetu vinakufa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamezungumza Mwatex, Mwatex ilikufa kwa sababu tulipenda kanga za China ambazo Mheshimiwa Zainabu Mwamwindi anasema akijifunga haiwezi kumfika vizuri, lakini ukiziangalia watoto wa Pwani wanasema zile ndiyo nzuri wanaziita sijui nini zile, ndiyo wanazozipenda sasa tutahakikisha kwamba substandard product tunazi-control, nitalinda viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye suala la tata la Mchuchuma na Liganga. Waheshimiwa Wabunge mradi wa Mchuchuma na Liganga upo, Serikali ilishaaingia makubaliano na mbia kampuni ya China. Kampuni ya China imewekeza pesa karibu dola milioni 60 wamemaliza, wakasaini kitu kinaitwa performance contract, baada ya kusaini performance contract ikabaki kuanza, ndiyo tukaja na sheria yetu ya kuangalia mara mbili tukakubaliana kwamba tupitie ule mkataba tuboreshe vifungu. Wataalam wakaanza kufikia, sasa watalaam kwa maelekezo wao walitumwa kuangalia kama kuna ukakasi au maslahi mapana ya Taifa, ikakutwa kuna vifungu tunavyojadiliana, lakini mwekezaji yuko tayari. Vifungu vya kujadiliana huu ni mkataba wa siri na silazimiki na siyo vizuri kwa wanaojua sheria kuujadili, lakini mimi ni ninyi, ngoja niwaambie mambo mawili na msiwaambie watu. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ule mkataba wa kwanza, ngoja niwaambie, mkataba wa kwanza mwekezaji alikuwa anataka akusanye VAT, aichukue VAT aitumie baada ya miaka 20 atulipe, akasema baada ya miaka 20 niwalipe, sasa ukikutana na watendakazi wa leo wanataka VAT wakatoe elimu bure, wanataka VAT wakanunue madawa wanapata ukakasi. Kwa hiyo, tukakaa nao, kitu kingine na niwashukuru

Wabunge waliochangia chuma cha Mchuchuma na Liganga. Watalaam wa uchambuzi wa migodi wanasema katika ule mgodi deal siyo chuma, kuna madini mengine ambayo kitarakimu yanatija zaidi, wakatuonesha kwa namba na mimi nikawa m dogo kama piriton.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu mradi niliupigia kampeni mimi tukamwambia mbia mwenzetu atuletee financial modal, amekwenda kutafuta financial modal ya ku-recognize madini yale na madini haya halafu tutakaa chini na namwambia huyo mbia alipo haraka sana alete financial modal tuanze. Katika utaratibu wangu tukakubaliana kwamba twende tukatengeneze barabara za ndani ramani tunaijua, kiwanda kitawekwa hapa, barabara ya kutokea, mlima uko hapa ndiyo nikaomba pesa ambazo ziko mbele yenu shilingi bilioni tano, lakini kuna shilingi bilioni tano nyingine kama walivyosema, ninakwenda kutathmini upya nijue anayepaswa kustahili kulipwa, kama bilioni moja ndiyo fidia, bilioni nne nitazileta nina Kamati inanisimamia, nina CAG ananisimamia ndiyo Mchuchuma na Liganga, ipo na tutaitumia.

Waheshimiwa Wabunge niwaambie, kuna kitu kinaitwa kulila masimanda, unachukuakitu chako unakiuza, unakuja kwa Kiswahili wanakwambia umeuza kwenye throw price. Kuna nchi moja nilioona kwenye clip walifanya mkataba na wawekezaji, mwekezaji akawaambia we will break even after 30 years, huyu akakubali akasema nipata employment, walipoanza kazi miezi sita aka-break, mwaka wa pili madini yamekwisha, wananchi wakamrudia kiongozi huyo. Nisingependa kuliona hilo na naogopa na nilishawahi kuwaambia sitashiriki kwenye maamuzi yoyote ambayo wajukuu wangu watafunga kaburi langu minyororo, ndiyo hiyo Mchuchuma na Liganga, mniamini, niko serious, watu wengine wanasema Mwijage hayuko serious, hivi sura hii iwe serious itafananaje, mtaiangalia? I am serious (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze suala lililozungumzwa sana la mkakati wa pamba mpaka mavazi.

Nimewaita wenye viwanda vya nguo, wenye ginneries nimekaa nao watu wenyewe wa kwenye field, wameeleza maeneo wameeleza maeneo ambayo yana ukakasi, nilikuwa na watu wa Wizara ya Fedha tunayashughulikia, lakini Mheshimiwa Waziri wa Nishati amezungumza, tunapeleka umeme. Kwa hiyo, tunathamini cotton to clothing kama mlivyosema siwezi kusema tena, ndiyo sekta yenye ajira nyingi. Kwa mfano, Kanda ya Ziwa nimeeleza kwenye speech yangu kwamba Social Security Funds wamekwenda kufufua ginneries, tunapambana zinunuliwe zaidi lakini kuna ginneries za sekta binafsi, muulize Mheshimiwa Kishimba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unajua kuna watu wengine anamiliki lakini hataki kujulikana anamiliki, Kishimba anamiliki na anasema anamiliki. Sasa kuna ginneries za Tanzania, uzoefu tulio nao hakuna ginnery ilikuwa inaweza kufanyakazi kwa siku 90, sasa pamba imezalishwa kwa wingi, tunakwenda kuiunganisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kuzungumza kidogo kwa heshima na taadhima, watu waliosema The Government is not coordinated, No! tuko coordinated. Mfano, ni cotton to clothing, ilipopigwa baragumu ya pamba mpaka mavazi, Waziri Mkuu alikuwa Kiranja wetu Mkuu, alikuwepo Charles John Tizeba, Waziri wa Kilimo, alikuwepo Waziri wa TAMISEMI, Jafo tukakimbia wote na Mheshimiwa Selemani Jafo, tukaanza kuzunguka nchi nzima, ndiyo matokeo haya tukisaidiwa na ma-DC, tukigawa kamba, tukapanda, Mungu atatusaidia pamba itavunwa nyingi, lakini tutavilinda viwanda vilivyopo ili viweze kuchakata pamba yetu. Ndiyo nataka kujibu hilo kwamba mniamini. Cotton to clothing tunaijua na nimezungumza kwenye mikakati midogo kwamba na yenyewe ipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaeleze Waheshimiwa Wabunge, kuna Mbunge mmoja kazungumza vizuri kwamba haya mambo yanabadilika, yatakapobadilika wote tupo Tanzania mnieleze. Mimi napatikana, kwa simu napatikana, hata kwenye kahawa nakuwepo tuzungumze. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la kukwamisha Wawekezaji na nizungumze kesi ya Hanang’. Mimi ndiye niliyepewa dhamana na nitahukumiwa kwa kutoakuanzisha viwanda. Kama nilivyowaambia, kufufua viwanda vilivyokufa na vile vilivyopo kuzalisha ukomo lakini kuanzisha vipya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mamlaka niliyonayo nitamtuma Naibu Katibu Mkuu wa Viwanda aende Hanang amtafute yule mwekezaji aliyetaka kutengeneza kiwanda cha saruji nije nisikie mtu anayekataa nitampandia juu, nitampandia juu kwenye mamlaka iliyotuteua! Haiwezekani, huwezi kuchelewesha mwekezaji. Mbunge wa Hanang usiwe na wasiwasi, kiwanda cha saruji tunakihitaji, atakayetaka kujenga kiwanda afanye utafiti na utafiti utafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo TIRDO, nimewaambia ndugu zangu, ukitka kuenga kiwanda kama wewe ni mwenzangu nenda SIDO, kama inafikiri una ubavu nenda TIRDO. Hata uki-hire consultancy, niwaambie tahadhari enyi wawekezaji na Wabunge muwe wawekezaji na niwashukuru wale Wabunge ambao mnakuja kuwekeza na mnaanza kujenga, mnaniletea picha kwa whatsapp, msiniletee picha mnialike mimi nina gari nzuri, nitakuja nifungue viwanda hivyo. Tunadanganyana, kuna watu wanafungua viwanda vidogo, wanapata tija halafu wewe unabaki viwanda vidogo mimi sivitaki, wenzako wanakula ,wewe unasusa. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie suala la mazingira ya biashara. Nawashukuru mlinishauri vizuri, lakini siyo kwamba nchi hii siyo ya uwekezaji. Ninawaahidi nitaboresha zaidi, regulatory reform ikija mtaona mambo yanakuwa mazuri, mambo yatakuwa mazuri.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Lucy Mayenga uliyozungumza yote kuhusu mazingira ya biashara, najua watoto tunawazaa wenyewe. Mimi mtoto wangu anaweza akapata kazi Fair Competition au TBS akikosea siyo mimi. Sasa kama nilivyowaeleza, Mheshimiwa Lucy Mayenga yote mnayoyaona mje mtuambie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, brother umezungumza mambo ya ukaguzi wa bidhaa kule Dubai, njoo uniambie, umekuwa kwenye Wizara hii ukisimami sekta hii unaijua vizuri njoo uniambie. Mabadiliko unayoyasema kama SGS anaongeza gharama nitayatekeleza. Sina maslahi binafsi mtu kukwamisha wawekezaji. Kwanza wawekezaji wanapokuja wengi ujiko unakuja kwangu, mnasema Mwijage umejenga viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze suala la kujenga viwanda. Serikali haijengi viwanda ila inaweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi kuwekeza. Tuko vizuri, soma hotuba yangu nimeeleza nafasi yangu na Tanzania Private Sector Foundation, muulize Mzee Mengi.

Nimezungumza na Mzee Mengi wakati nahamasisha viwanda vya madawa ilikuwa juzi tu tumeweka jiwe la msingi kiwanda chake. Tunazungumza na biashara ni kuzungumza kama mikono miwili ilivyo, mikono miwili ni kunawishana, kwa hiyo hatuna tatizo na private sector. Hii migongano iliyopo mtu anapopata matatizo aje atueleze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Chumi alizungumza suala la mifuko. Hilo suala la mifuko ya plastic ni suala la kiutawala. Katibu Mkuu wangu usimame, angalia hiyo mifuko inakwendaje na uanze utekelezaji bila kuchelewa.

Tumezungumza suala la fidia za EPZA, Mheshimiwa Kawambwa, Kaka yangu twende tukae chini, tuangalie Bagamoyo tutakavyoweza kuiweka vizuri na niwaeleze kuna watu waliandika wakihoji kuhusu Bagamoyo Special Economic Zone. Bagamoyo Special Economic Zone ninavyozungumza sasa mwekezaji yuko Dar es Salaam na timu ya Serikali wanajadiliana. Upande wa viwanda wamemaliza, sasa wanajadiliana upande wa bandari ndiyo taarifa niliyonayo, mambo yanakwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuko mwaka wa pili katika safari ya miaka kumi ya kufika uchumi wa kati. Watu wangependa kufika leo lakini naona muende taratibu tutafika lakini muendelee kunielekeza na kunikosoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la Mheshimiwa Mariam Kisangi. Tumekubaliana na Meneja wa TanTrade kwamba siku za sikukuu wenye biashara mtaingia kuuza bila kujali kama ni Sabasaba au siyo Sabasaba wale wananchi wa Dar es Salaam na watoto wataingia bure. Mheshimiwa Mariam Kisangi amependekeza bembea, sasa tunatafuta nani aweke bembea na atafute mtu binafsi aweke mabembea mtoto kipanda weka shilingi 50, msiwa-charge pesa nyingi, mkitaka profit nitawafukuza, watoto waende kuburudika na watoto hawana pesa au wacheze bure kwa sababu hawana pesa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Benardetha Mushashu umezungumzia suala la viwanda Kagera, namsubiri Waziri wa Mifugo, tumepata mwekezaji ambaye atatengeneza kiwanda cha maziwa, shamba la kutengeneza maziwa kuanzia maziwa kwenda kwenye UHT mpaka maziwa unga. Mheshimiwa Lwakatare anasema Mwijage usikimbie ukapita kwenu. Bibi yangu aliyenilea, alinimbia Mwijage ukiamka unawe uso na uso ni Jimbo langu, uso ni nyumbani, lakini mimi najenga Tanzania. Kwa hiyo, usiwe na wasiwasi Mama Mushashu nitakuja kuwaelekeza namna gani ya kujenga viwanda. Wewe shangazi yangu unielewe, usiogope kuanza na kiwanda kidogo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala la kiwanda kidogo sana nilizungumze, mwenzangu mimi hujawahi kumiliki hata milioni moja, unakwenda kutafuta bilioni 100 utaanguka nayo, anza kidogo. Siri ya kiwanda kidogo maana yake ni nini? Tunataka kurithisha utamaduni wa kumiliki biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie hili, tunataka kujenga utamaduni wa kupenda viwanda. Nimetoa mfano huu siyo wa kibaguzi. Wenzetu Wahindi na Waarabu watoto wao tunasoma nao, lakini kwenye kazi hatuombi na wao. Nilikwenda Manyara kwenye kiwanda cha sukari, nimekuta watu mle wana historia ya viwanda, wameanza kwenye kiwanda kile cha sukari mpaka kinakua, mtoto na watoto wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kueleza maelezo hayo nitayafafanua zaidi nikipata nafasi, naomba kutoa hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mchango wa kuchangia kwa kuzungumza katika Bunge lako Tukufu kupitia maandishi narejea na kuendelea kuchangia Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyoeleza awali msisitizo wangu ni juu ya njia na shughuli zinazoweza kutuongezea mapato ya kutekeleza bajeti yetu na kuendeleza Taifa letu kwa ujumla. Fursa ya kuongeza mapato kwa kuuza bidhaa nje zilizoagizwa kutoka nje na kuongezwa thamani hapa au kuuzwa nchi nyingine kama zilivyo maarufu kama re-export. Bidhaa ya kwanza ni mafuta jamii ya petroli. Katika historia ya biashara ya mafuta kuna wakati makampuni, watu binafsi na idara za Serikali toka nchi jirani walikuwa wanakuja Dar es Salaam kununua mafuta na kuyasafirisha kwa njia ya malori au na mabehewa ya treni. Matumizi ya mfumo huu ni kuwa kampuni ya Tanzania inapo re-export Taifa linafaidika na lile ongezeko katika bei (mark up) ambayo huongeza faida ya kampuni husika na hatimaye kutozwa kodi na tozo nyinginezo kwa manufaa ya Taifa. Lakini uwepo wa utaratibu huu ulioratibiwa vizuri huwezesha Taifa kuwa na hifadhi kubwa ya mafuta bila kuilipia ambayo inapelekea kuwa na mafuta mengi ya kimkakati (strategic stock).

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu huu utawavutia na kuwafunga wateja wa nchi lengwa kwa kuwa na uhakika wa kupata mafuta kwa bei inayojulikana toka kwao, lakini pia uwepo wa volume kubwa ya mafuta toka hapa kwenda nchi jirani itaongeza matumizi ya mafuta (fuel for truck use on safari) yaliyolipiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nifafanue kidogo dhana ya mafuta yaliyolipiwa, mafuta yanayotumiwa na malori yanayokwenda nje ya nchi (transit) au re-export shughuli zake huleta pesa za kigeni ambazo huchangia kununua mafuta mengine. Kwa mafuta yanayotumika nchini wingi au ongezeko lake linaweza kuwa na tija pale inapopelekea kutafuta fedha za kigeni kuagiza mafuta mengine. Ikumbukwe kuwa tuna mahitaji ya kununua mafuta kama bidhaa muhimu na mafuta jamii ya petroli ndiyo bidhaa ya kwanza kuchukua fedha zetu adimu za kigeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, jinsi ya kuchota fursa hii ni kwanza kujipanga kuisimamia ili kuepuka watu wasio waadilifu kuitumia vibaya kwa manufaa yao/kuifisadi. Hili zaidi ni jukumu la TRA na idara zake wakisaidiwa na vyombo na taasisi nyingine za dola. Utaratibu huu ulikuwepo ila kwa kushindwa kuusimamia basi zikatungwa sheria zilizoua fursa hii. Sasa tunao vijana wengi wenye elimu wanaweza kupewa ujuzi na stadi za kusimamia sekta hii na kwa faida ya matumizi ya teknolojia tukachangamsha sekta hii na kupata mapato ya Serikali .

Pili ni kuruhusu hifadhi ya mafuta ya forodha iliyozuiliwa (bonded customs warehouses/terminals). Kama nilivyodokeza mafuta yaliyoko katika hifadhi za namna hii yanahamasisha kampuni husika kuagiza mafuta mengi kwani hawawajibiki kulipa kodi na tozo mara moja, lakini kwa upande wa nchi stock hizi ni kinga ya kiusalama kwani nchi inakuwa na haki ya kwanza kuyatumia inapotokea tatizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, fursa nyingine inayofanana karibu na hiyo ni hifadhi ya mafuta inayoelea (floating stock). Tanzania tunayo fursa ya kufanya biashara hii kwa kuruhusu sekta binafsi kujenga matanki makubwa ya kuhifadhi mafuta nchini kwa lengo la kuuza mafuta hayo popote duniani. Kimsingi mafuta yanayotunzwa katika hifadhi hizi huwa yananyumbulika kufuata bei za soko la dunia. Faida kwa nchi ni kodi na tozo kwa uwekezaji, huduma za bandari na haki ya kuwa mteja wa kwanza. Biashara ya namna hii iliwahi kufanyika kwenye maji ya bahari ya Tanzania kwa kutumia mtindo wa meli mama na mtoto (mother daughter vessels). Chini ya utaratibu huo na kutokana na ukosefu wa matenki makubwa na sheria” za nchi yetu, meli kubwa zenye ujazo wa kati ya tani 150,000 mpaka 200,000 hutinga nanga kwenye maji ya Tanzania ambapo hufaulisha mafuta kwenye meli za ujazo wa tani 40,000. Shughuli hii kulingana mwenendo wa bahari ya Hindi inaweza kufanyika Tanzania usawa wa Tanga-Bagamoyo na Zanzibar kwa usawa wote wa chini ya Jangwa la Sahara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu mafuta ipo fursa ya kuboresha mfumo wa bei elekezi ili kuchota faida kubwa itokanayo na kushuka na kupanda kwa bei za mafuta kwenye soko la dunia (backwardation - contango). Busara yake ni rahisi kuelezeka, bei katika soko la dunia inaposhuka na hapa nchini bei ikashuka kwenye vituo vya mafuta nauli au bei ya bidhaa huwa haishuki. Hii ina maana mlaji wa mwisho hafaidiki mara nyingi na anguko kubwa la bei ya mafuta. Lakini mafuta yanapoanza kupanda na bei elekezi ikaonesha bei ya mafuta kuwa juu kwa kutegemea huo mzigo mpya walaji hawafaidiki endapo kuna stock kubwa ya zamani. Lakini soko la Tanzania kulingana na sheria na taratibu zetu hatuna mipango na mikakati ya kuchota na kuhifadhi mafuta yenye bei nafuu katika mazingira ambayo wazi inaonesha kuwa muda si mrefu bei itapanda. Yote haya yanaweza kufanyika kirahisi kwa kuweka sheria na mazingirra ya kuvutia uwekezani wa namna hiyo kupitia sekta binafsi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie fursa nyingine ya re-export kwa bidhaa zingine zisizo mafuta jamii ya petroli.

Kwanza nieleze kuwa viwanda vya mafuta ya kupikia na ngano vilivyoko nchi za jirani ikiwemo Rwanda, Burundi na hata Uganda vilijengwa huko baada ya wawekezaji waliokuwa wakitumia viwanda vilivyoko Tanzania kushindwa kuhudumia masoko hayo kutoka kwetu. Yote hayo yalitokana na sheria na usimamizi usiowezesha kufanya biashara ya aina hiyo toka Tanzania. Tathimini ya biashara hii itakuonesha kuwa kuna fursa kubwa sana tukijenga sekta hii kwa lengo la kutengeneza ajira, kupata kodi na kuchangamsha uchumi. Kuna wakati re-export kwenda nchi jirani ilifikia dola milioni 840 kwa mwaka lakini kati ya mwaka 2015 mpaka 2020 kiasi cha juu ni dola milioni 340.7 na kiwango cha chini ni dola milioni 143.16 mwaka 2017. Ni imani yangu kuwa kwa kuweka mazingira mazuri re-export value inaweza kufikia dola biilioni 1.5 kwa mwaka katika miaka mitatu ijayo. Hii ni sekta ya re-export, si mauzo ya bidhaa nje (export).

Mheshimiwa Naibu Spika, shughuli nyingine inayoendana na re-export na ambayo inaweza kuchangamsha uchumi kwa kutengeneza ajira na kupanua wigo wa walipa kodi ni vituo vya biashara hapa nchini, kwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na zile zinazotoka nje ya nchi, kwa mfano, soko la Kariakoo kabla ya kuanguka kutokana na sheria na udhibiti. Ni kweli yalikuwepo mapungufu katika biashara hiyo ambayo pamoja na kuzalisha ajira kwa kiasi kikubwa kulikuwepo mianya ya kukwepa kodi, bidhaa hafifu na bidhaa za bei ndogo zinazoathiri viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja hapa ni kuwa mapungufu yanaweza kurekebishwa na faida za kuwa na masoko kama hayo zikaweza kuchotwa kwa manufaa ya Taifa. Mfano wa wazi ni Kariakoo ya Kampala, Uganda iliyoanzishwa baada ya kudorora kwa Kariakoo mwenye jina. Wafanyabiashara kutoka Malawi, Congo, Zambia na kwetu Tanzania wananunua bidhaa Kariakoo Kampala. Hapa kuna hoja tatu, ajira, kodi na kuchangamsha jamii. Ajira inatangulia kodi lakini mwenye ajira analipa kodi iwe moja kwa moja au indirect. Eneo hili liangaliwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ni uhamasishaji wa mauzo nje (export). Kama nilivyoeleza kwenye mchango wangu kwa kuzungumza Tanzania mwaka 2019 tuliuza nje bidhaa zenye thamani ya bilioni 2.9 pesa ya Marekani na 2/3 ikiwa ni dhababu lakini fursa ya mauzo nje (potential export) yetu ni bilioni 2.37 pesa ya Marekani bila kuhesabu dhahabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja hapa ni fursa zilizowazi ambazo tunaweza kuzitumia na kuongeza mauzo nje. Nieleze wazi hapa kuwa kama Taifa lazima tutembee na lengo letu la kuuza bidhaa nje kwani pamoja na kuleta pesa za kigeni linatuhakikishia soko la bidhaa zetu na kuleta ustahimilifu wa sekta zetu za uzalishaji nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika bidhaa/mazao 19 niliyoyarejea sikuona nyama au ng’ombe hai, maziwa, mawese, maharage aina ya soya kwa kutaja baadhi. Uchambuzi wa haraka ni labda watakwimu walichukua bidhaa ambazo zina fursa zaidi ya dola milioni 20.8 kwa mwaka. Hoja yangu ni kuwa iweje nchi yenye fursa ya kufuga tushindwe kuzalisha nyama bora na maziwa kutosheleza soko la ndani na kuuza nje? Iweje Uganda na Botswana wafanye vizuri kwenye sekta hizi kuzidi nchi yetu yenye ardhi na uwanda mzuri wa kufuga ng’ombe. Hili ni eneo muhimu la kuwekeza kwani mbali ya fursa ya kuuza nje sekta hizi zinasaidia kujenga uchumi jumuishi jambo muhimu katika Taifa lenye amani na mshikamano. Pia kwa mazao ya shamba kama mawese au mafuta ya mawese ambayo kimsingi yana soko kubwa DR-Congo na tunakuwa na faida ya kuwa karibu na soko kwani yanalimwa mikoa ya Magharibi, ni muhimu tuongeze jitihada za kuhamasisha sekta hii kuliko tunavyofanya sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, jibu hapa ni kualika sekta binafsi kushirikiana na wananchi kwanza kwa kuhakikisha wanalima mashamba makubwa kwa uwiano wa familia, lakini mwekezaji anayeweza kujenga kiwanda kikubwa kitakachofanyakazi kwa tija kubwa. China wametupa nafasi ya kuuza maharage aina ya soya tani milioni 42 kwa mwaka kwa bei ya shilingi 3,000 kwa kilo ni takribani mauzo ya shilingi trilioni 126. Kiasi ni kikubwa sana hata ingekuwa ni mauzo ya miaka kumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja yangu ni kuwa kwanza Serikali ihakikishe mkataba huu unalindwa, pili lazima iwepo mipango na mikakati ya kuhudumia soko kwa kukidhi viwango vya soko kwa faida kwa wazalishaji. Tatu, ni kuhakikisha wananchi kwa matabaka yote wanashirikishwa hasa kwa kusaidiwa kuingia kwenye mnyororo huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya mazao ya soya ni vizuri tukaielewa kwa ujazo na uzito wake. Tanzania kwa ujumla wake tunazalisha vyakula vya aina zote tani million 19, soya tu ni tani milioni 42; huu ndio ukubwa wa jukumu tulilonalo. Hii ni fursa kubwa na nzito na inahitaji nguvu ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja yangu ni kuwa kwa kuuza nje (export & re-export) kwa kiasi kikubwa tutapata fedha nyingi za kigeni lakini kujenga uhakika wa soko hali itakayochochea sekta za uzalishaji hapa nchini kuzalisha zaidi. Mchakato wa uzalishaji utasaidia kutengeneza ajira, kuzalisha bidhaa, kusaidia kukusanya mapato ya Serikali kwa maendeleo na kuchangamsha uchumi. Pamoja na bajeti hii kama ilivyowasilishwa, tunaweza kufikia mapendekezo haya kwa kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji tukirekebisha sheria na taratibu za utendaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nihitimishe kwa kushauri juu ya usimamiaji wa zuio la sukari la asilimia 15 kwenye sukari ya viwandani na hiyo VAT refund. Nakubaliana na Serikali kwa kukubali kuondoa hiyo 15% kwenye sukari ya viwandani lakini lazima Serikali iendelee na taratibu za kusimamia sukari hiyo. Hupo uwezekano wa sukari ya mezani kuingizwa na kuuzwa kama sukari ya viwandani. Sukari aina hii iratibiwe kwa kuwa na customs bonded rooms kwenye viwanda vikubwa na kwa wawekezaji wadogo iwepo bonded warehouse ya ujumla. Naomba na kushauri wazo la kurudisha kiwango hiki lisifikiriwe kwani madhara yake kwenye sekta ya viwanda hatutakaa tuyamalize makali yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, bado Serikali haijatamka juu ya kikwazo kikubwa cha uendeshaji wa viwanda na uwekezaji kwa ujumla. TRA wawe wazi kubainisha stahili ya PMG - VAT revenue na stahiki ya CG TRA - VAT expenditure. Kama awali tunapopokea VAT au kuratibu VAT ni vema tujue yapi ni mapato ya Serikali na kiasi gani kitarejeshwa kwa mfanyabiashara. Vipo viwanda vya Tanzania vimeshindwa kuzalisha na kuuza masoko ya nje kutokana na mapungufu yetu katika kusimamia VAT refund.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia hii Wizara muhimu, Wizara moja ya sekta za kiuzalishaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesoma sana randama ya Wizara hii. Nimesoma Hotuba ya Mheshimiwa Waziri na nimesoma maandiko yake yote.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kusema, naunga mkono hoja ya Wizara hii. Nataka kusema, naunga mkono hoja Wizara hii ipite.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika randama, Ukurasa wa 17, ukurasa wa 18 na ukurasa wa 32, mara tatu, Waziri ametamka kwamba, yeye migogoro ya Rutoro na Mwisa ameshaachananayo anasubiri huruma ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, waende wapime, wananchi wa Rutoro na Mwisa waishi kwa amani. Amesema mara tatu. Naunga mkono hoja ya Waziri kwa misingi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati tunaingia karne ya 21, tuliandika Dira ya Taifa. Hayati Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema, aliandika dibaji, nitanukuu sehemu ya dibaji, kwamba, “Tunapokwenda kwenye ile karne ya 21 lazima tuwe na nguvukazi yenye ustadi mkubwa na hulka ya kujituma.” Nguvukazi yenye ustadi mkubwa na hulka ya kujituma.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeunga mkono bajeti ambayo Waziri anakiri kabisa kwamba idadi ndogo ya Watumishi katika Sekta ya Uvuvi ikilinganishwa na mahitaji ni changamoto. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, yaani alivyosema Mzee Mkapa mmemsikia; mtu ambaye nimemuunga mkono, amekiri kabisa kwamba, rasilimali watu aliyonayo, haimtoshi. Namuunga mkono Mheshimiwa Rais anaposema kwamba, mifugo na uvuvi ni utajiri mkubwa. Nikipata muda nitawaonesha. Kuwa na utajiri siyo hoja, kuchota utajiri ndiyo ngoma ilipo. Hatuna rasilimali ya kuchota rasilimali zile. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali Wizara hii, nitawaonesha rasilimali zilipo, waongezewe pesa, kwani hizi pesa hazitoshi. Waongezewe pesa kwa ajili ya kutengeneza rasilimali, na zana za kuchota raslimali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilizungumze na hili ni kwa Wizara zote; sekta zote za kiuzalishaji. Mnapotuletea bajeti, mnapojinasibu mahali popote, pamoja na kazi nzuri ambazo Wizara hizi zinafanya, kuleta chakula, kutengeneza ajira, malighafi za viwanda, mtueleze clearly ni kiasi gani tunapata pesa za kigeni? In bolded font.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania tuna-export na kupata pesa za kigeni dola bilioni 10 hazifiki, ni tisa na kitu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ukraine ana-export 68 billion dollars; sisi tunapata nini? Madini tuliwasikia lakini kwa kufichaficha, tunapenda tujue, tuige mfano ule wa Ajenda 10/30. Ajenda 10/30 anakueleza malengo yake atapata kiasi gani kwa dola ambayo na mimi sikubaliani naye, nasema amejiwekea malengo kidogo. Lakini ninapenda hii iwekwe wazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe pongezi kwa kampuni ya maziwa ya Asas. Kazi mliyofanya ujombani Busokelo, Rungwe nzima ni nzuri. Waheshimiwa Wabunge, Kampuni ya Asas inaagiza ng’ombe wa maziwa kutoka Afrika Kusini, ng’ombe mmoja ukimlisha unapata kilo 25, anawakopesha watu wanafuga halafu wamrudishie. Mheshimiwa Waziri, kama unaijua Kampuni ya Asas na tunagombania mwisa, nakuomba mjomba leta Asas Company Ltd. tumpe aardhi awagawie wananchi wa kwetu wa Kagera hao ng’ombe na ajenge viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaeleze watu, hawaelewi; hekta 600,000 za NARCO nusu yake ziko Kagera. Kwa hiyo, wananchi waliozoea kutumia ardhi ile, imetwaliwa. Sasa niko tayari kufanya kazi nao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na wewe nikuombe umweleze Waziri kwamba kwenye mabanda yale wasituoneshe ila waweke na banda la watu kutoa maoni na kubadilishana uzoefu kwa sababu tuna uzoefu tofauti. Tusiende kuangalia, turuhusiwe kutoa maoni yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kuchangia sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wanafanya fujo, nilindie muda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2017 Tanzania tuliuza nje samaki wenye thamani ya dola milioni 193 kwa takwimu nilizonazo. Na hizi ni takwimu za World Fish Center. Rasilimali ya maji tuliyonayo sisi Tanzania siyo wa kuuza kiasi hiki. Mahesabu yanakuonesha wewe kuuza dola milioni 800 inawezekana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Nchi ya Morocco ambayo tunawazidi kwa wingi wa maji wanauza samaki duniani 2.5 billion dollars. Sisi tuna maji mengi kuliko Morocco, ndipo linapokuja suala la rasilimali. Ukiweka shilingi katika sekta hii unapata shilingi 2.5. Serikali muweke shilingi kwenye sekta hii ili tupate pesa nyingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kiburi cha Taifa lolote ni uwezo wa kuuza nje, na imeandikwa hata kwenye Dira ya Taifa, huwezi kujenga uchumi shindani kama huna huo uwezo wa kuuza nje. Kwa hiyo, nilikuwa nawaeleza hiki kitu.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine kwenye sekta hii ni kwamba asilimia 97 ya wanaozalisha hawa samaki tunaowazungumza ni wafugaji wadogowadogo, wavuvi wadogowadogo. Kwa hiyo, Serikali mpeleke pesa kule kwa wafugaji hawa wadogowadogo, kwa wavuvi hawa wadogowadogo, ili hao watu sasa watusaidie kujenga uchumi jumuishi. Uvuvi wa samaki utakaoleta watu wengine wakawatoa hawa ndani ya shughuli patakuwa hapakaliki.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie kwa nini tuko hivi; moja wapo ya changamoto za Wizara hii au sekta hii ni uvuvi haramu. Lakini uvuvi haramu siyo suala la Tanzania tu, hoja hapa siyo kwamba tuna uvuvi haramu, hoja ni kuu-manage, tunau-manage namna gani. Uvuvi haramu duniani, overfishing, unasababisha mapungufu ya 83 billion US Dollars; hizo ni taarifa za World Bank.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, utaona kwamba hii 193 niliyowaambia ya mwaka 2017, tungefanya kazi kwa tija, kwa kuzuia overfishing na uvuvi mwingine haramu, tungeweza kuchupa na kwenda kwenye nafasi nzuri. Nilimueleza Mheshimiwa Waziri nikiwa Goziba kwamba nitakuja nimuoneshe nilichokiona Goziba. Uvuvi haramu umezidi mipanga na Wizara hii peke yake haiwezi kuutatua, mnahitaji kupata msaada wa zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana nikaomba aweke banda la maonyesho pale ili nije wasionioneshe, na mimi niwaoneshe nilichokiona Goziba, Bumbire, Kelebe, Makibwa na Nyamburo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niende kwenye sekta ya nyama, hesabu zangu za haraka – nisije nikakosa muda – sekta ya nyama kirahisi inaweza kutuingizia dola bilioni tano. Kama kuna mtaalam katika Wizara hii ana mashaka, tukakutane kwenye banda pale nimuoneshe kwa mahesabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, huwezi kuwa na ng’ombe milioni 35 halafu ukashindwa kuuza nyama inayofikia bilioni sita kwa mwaka. Hata ungewachinja wale ng’ombe kwa kipindi cha miaka kumi, chukua ng’ombe milioni 35 wagawe namna hiyo, utaona hizo figures. Nitakuwa kwenye banda la maonyesho pale, niwekeeni zulia nije niwaeleze. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunataka kufanya nini; mmeizungumzia NARCO kwamba itawataka wawekezaji waje na business plan; hakuna. Ninyi ndio muwape NARCO masharti watakayoyafuata, wewe ndio uandae business plan. Ndiyo maana hata watu wa estate mtu anajenga nyumba, iwe hoteli, iwe hospitali au klabu, watu waende kucheza. Huwezi kufanya klabu ukaigeuza kwamba ni hospitali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo NARCO ianzishe business plan ili watu waje wafanye nini. Na hiyo business plan iwahusu hawa waliopewa vitalu na wale watakaokuja. Siyo unajenga kitalu cha kufuga ng’ombe mtu analeta ng’ombe analingana na mbuzi; haiwezekani. Ufugaji wa kuweza kufikia malengo niliyowaeleza inatokana na malisho, mbegu utakayoleta na utunzaji wake, ili tuweze kufuga nyama tupate nyama inayoweza kufikia hizo dola bilioni tano ambazo nakueleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, umezungumza Mheshimiwa Waziri nakuunga mkono, watu sasa wanataka nyama inayozalishwa Tanzania. Na jambo la faraja ni kwamba katika nyama wanayohitaji ni wanyama wanaofugwa kirahisi; anaongoza mbuzi, anakuja kondoo, ng’ombe ni wa tatu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kote nilikokwenda kujifunza – siwaambii tena mambo ya Uganda – hapahapa Tanzania, hapahapa Iringa, kuna Watanzania wamefanya maajabu, Asas anawaongoza na wengine wanafuatia.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilisema mwanzo na awali kwamba naunga mkono hoja, naendelea kuunga mkono hoja. Nimemuona Mheshimiwa Waziri wa Ardhi ananiangalia, na yule wa Ofisi ya Waziri Mkuu ananiangalia; naomba kuwasilisha. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Nishati
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipatia fursa ya kuhutubia bajeti ya kimataifa, unajua kuna bajeti ile ya wananchi, ilipita ile bajeti ya kitaifa, sasa hii ni ya kimataifa kwa sababu mambo yake ni dola, ni geopolitical, sijui ni migogoro ni Ukraine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilihudhuria maonesho ya nishati, lakini nimesikiliza vizuri hotuba ya Mheshimiwa Waziri na nimeisoma na viambatisho hivi, napenda nikiri kwamba kuna majibu mengi hapa kuliko maswali niliyonayo kutoka kwenye maonesho na kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri, lakini kabla sijaanza kuhutubia nizungumze jambo moja; mwezi Januari, 2018 nilipata bahati ya kuhutubia Kabare, Uganda; Mheshimiwa Rais Jenerali Kaguta Museveni aliniomba nihutubie tena nihutubie kwa Kinyankole.

Mheshimiwa Mwenyekiti, alikuwepo Mheshimiwa Dkt. Kalemani, nikahutubia lakini Wizara ya Nishati wakanikaribisha Bunazi walikuwepo watu wengi na watu kutoka Nzega walikuwepo na kutoka Tanga walikuwepo na baadhi ya Wabunge, sikuona mahali popote ambako watu wa Uganda na Tanzania wanalalamika kwamba bomba la mafuta la kutoka Hoima kwenda Chongoleani lina matatizo, wala mimi katika Jimbo langu sijawahi kuona mahali watu wanalalamika kwamba watafukuzwa. Sasa hao wanaokwenda kutusemea huko Ulaya wametumwa na nani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mafuta ni ya Uganda, bomba ni la Tanzania; sisi na Uganda ni ndugu, mimi Rais wa Uganda Msita Waitabara ni mjomba wangu na alikuwa anaishi Jimboni kwangu kabla hajaenda kuwa Rais wa Uganda ni ndugu, kwa hiyo, watuache watuache. Lakini wale watu wanaosema bomba lisijengwe nimewapenda kitu kimoja, wanasema tupande miti bilioni tano, mimi ninakubali waje tutawapa eneo watupandie michikichi, watupandie mibuni, watupandie majani ya chai; miti bilioni moja sisi tutakwenda kuvuna wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye nishati; kwenye maonesho nashukuru kwa umeme visiwani off grid watu wa Mazinga, Ikuza, Kerebe, Gumbire, Nyaburo na Goziba suala la umeme nimepata majibu, lakini nimepata majibu kwamba REA II iliyokwama vijiji vya Busingo, Ruwanda yote itakuwa haina matatizo na miradi yote ya TANESCO itatengenezwa, nishukuru kwenye hotuba Mheshimiwa Waziri umekumbuka suala la campsite, vituo vidogo vinavyoondoa matatizo ya distribution ya mafuta, nashukuru Mheshimiwa Waziri ulikuwa Mwenyekiti wangu kwenye Kamati zetu tulilijadili sana sasa upele umepata mkunaji, ulishughulike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe jambo lingine umesema magari ya Wizara ya Nishati yatafungiwa gesi, mimi sikubali, magari yote ya Serikali yaanze kutumia gesi, zipo faida za kutumia gesi, gesi is economical, gesi is available, waanze kutumia gesi hiyo nimeisoma kwenye hotuba yako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nizungumze mambo ya kidunia; suala la mafuta na mwenendo wa mafuta duniani; hili tunaomba uelewa Watanzania wote muelewe suala la mafuta halimhusu Mheshimiwa Rais wala halimhusu Waziri, wala halimhusu Mkurugenzi, ni suala la kidunia, sina muda ningezirudia zile sababu tano zinazosababisha hivyo, zipo nje ya uwezo wetu, na ninapozungumzia hiyo suala la uelewa nipende kuishukuru Serikali na hasa hasa Mheshimiwa Rais, kimsingi hoja sio bei ya mafuta imeshuka, bei ya mafuta haijashuka, bei ya mafuta imeshushwa, ukiangalia kwenye soko la dunia na nilikutana na mtaalam mmoja nilikuwa naangalia bei ya dunia inapanda, ila mamlaka imeshusha bei angalau kwa siku mbili hizi tupate afueni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la uelewa wa Watanzania muelewe huko bado vumbi linatimka, bei ya mafuta inaendelea kupanda, ila mamlaka imeamua bei ishuke na hiyo ninaiita zawadi namba tatu, zawadi ya mama na hii ni zawadi ya mama namba tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze suala moja muhimu ambalo watu hawalielewi katika somo la mafuta; petroleum business management introduction huwa tunafundishwa availability, reliability na availability of mafuta ndio tunafundishwa. Sasa katika suala la availability kuna kitu Watanzania hatukijui, ni siri iliyo wazi kwamba sisi tunapata umeme asilimia 60 inatokana na gesi ya Songosongo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama isingekuwepo kutokana na vyanzo vya maji kutotosha tunge-import mafuta, kama ingetokea tatizo la supply/ disruption of supply ina maana tungeingia gizani mnasema mafuta yamepanda watu wanapiga kelele nawaambia Mungu apishe mbali ikitokea tatizo la umeme 60 percent kila mtu atatafutana. Kwa hiyo, tuipongeze Serikali, tuishukuru Serikali kwa kuwezesha hii gesi na tunapoishukuru gesi lazima uwakumbuke waasisi akina Sylvester Barongo na vijana wake wakati ule akina Mzee Ntomola, akina Kilagani, akina Khalifani na hapo ndipo ninapoipongeza Serikali ya Mheshimiwa Samia kwa kuwarudisha wakongwe kwenye sekta yaani uwarudishe wakongwe waje wakuoneshe njia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haikuwa rahisi kuchukua gesi ya Songosongo, sasa niwaambie kama sisi leo tungeingiza mafuta kwa bei hii, tungetumia trilioni moja kuagiza mafuta ya miezi minne; trilioni moja kuagiza dizeli ya kuendesha mitambo, sasa hoja sio trilioni moja, hoja ni kwamba foreign currency ungeipata wapi. Kwa hiyo wakati tunashukuru punguzo la bei huku kushuka kwa bei tushukuru kwa kuwepo na mfumo wa gesi asilia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze bulk procurement; bulk procurement watu hawaielewi, Tanzania haijawahi kuwa soko la mafuta na nilikuwa nikilisema Tanzania haijawahi kuwa soko la mafuta, huwezi kumwambia international trader kwamba unataka tani 10,000; tani 5,000. Sasa hivi kutokana na bulk procurement consolidation ya maziwa yote makuu, mahitaji kupitia Dar es salaam sasa dunia inatambua kwamba Tanzania kuna soko la mafuta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sisi tunashika mpini wao wanashika makali, watakuja hapa, watakuja hapa, sasa kwakuwa na wingi wa mafuta kama walivyosema Mbunge wa Manonga ndio maana hata mtikisiko unaompata South Africa, unaompata Nigeria, unaompata Kenya hautupati sisi na hiyo ni siri Waziri anajua na nasema Waziri usiisema kwa sababu tupo live watu wengine watakuja kuiba style yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi hatuwezi kuadimika mafuta kwa sababu ya mfumo wetu, asije mtu akakwambia rahisi, what is rahisi? Hakuna kitu cheap, cheap lazima kiwe pegged, kiwe pegged kwenye international kuna watu wamekwenda kuagiza mafuta cheap fedha zimeliwa, fedha zikiliwa za Serikali utamwambiaje CAG, hili Bunge utaliambiaje, lazima tufuate mfumo unaojulikana kama tunapata ya aghali tupate aghali, tuvumilie kesho tutapata nafuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo mengine nataka kuzungumzia ni trading hub, kidogo na hii nazungumza taratibu Mheshimiwa Waziri wasije wakawepo watazamaji kwingine kule, shangazi yangu nikamsalimia akakataa kuniitikia, kuna tofauti kati ya strategic reserve na trading hub.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo ningeomba mlete mjadala, mlete semina sijakubaliana nalo. Strategic reserve inaweza ikawa ni trading hub na ninakupongeza umekubali kwamba tuweke bonded warehouse, sasa zitumie zile bonded warehouse ku-re-export kwenye enabling countries, nchi za Kongo kwenye madini kuna watu wanaweza kununua lita 500,000 kwa mpigo, waambie waje Tanga wanunue, waambie waende Dar es Salaam wanunue, nilikuwa nikifanya kazi hiyo unajua, tuna push volume. Kwa hiyo tuigeuze Tanzania soko, wanapokuja vijana wetu watapata kazi, lakini ile amari iliyopo kwenye ghala letu ndiyo hiyo strategic reserve. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemwambia Mheshimiwa Waziri akatikisha kichwa, tunahitaji mjadala tukae Wabunge tujadiliane na utaratibu utazingatiwa kusudi tunyukane hapa, kwa sababu hatuwezi kukubali hili suala lipite lina uzuri na ukali wake. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kenya juzi wamefanya mjadala juu ya hili walitoka bila kuelewana, OTS walikuwa na mjadala juzi walitoka bila kuelewana. Mambo ya aging, mambo ya kukamatwa na mafuta ya bei kubwa yakashuka, kwa jirani yameshuka wewe una mafuta ya bei kubwa utafanya nini, tunapaswa tuelezane kwa nia nzuri inayofanywa tutoke tumeelewana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine Tanzania tunayo storage capacity ya 1.4 billion liters kwa mwaka tunayotumia tuna storage capacity hiyo, 89 percent ni private sector, ninaiomba Serikali msiiache private sector, ndio iliyotufikisha hapa, hamasisha private sector wawekeze, Serikali weka uratibu, weka wadhibiti waweze kuelekeza. (Makofi)

Suala jingine naomba la utafutaji na uchimbaji wa mafuta, nishukuru unao wataalam Mzee Khalifani bosi wangu amerudi, tutafute mafuta mambo ya kuogopa ASPA sijui nini hakuna, usiogope lazima utapoteza na katika kupoteza utapata, hii ni biashara ya stara kubwa, ni biashara ya gharama kubwa, kwa hiyo, tuhamasishe kutafuta mafuta. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na sasa siyo siri kwa sababu ya kupanda kwa mafuta nchi za Ulaya wanakimbilia Afrika tumesikia hapa Afrika Magharibi, tungependa kusikia wanakuja Tanzania na wakija wape masharti, tunao vijana wamesoma hapa wamekwenda China wakasoma petroleum, mradi wa gesi haukufanya kazi waajiri watoto wale, waingize kwenye sekta ndio masharti kwamba njoo uwekeze, wekeza vijana wa Kitanzania waweze kufanyakazi, tafuteni mafuta, wakati wanatafuta green energy ni hadi 2050 sasa 2050 na sisi tutumie ndiyo maana na ninamuambia mjomba asikie huko aliko Kampala na Entebe tunataka mafuta ya Uganda yapite Tanga kusudi Tanga wafaidi na njia yote tufaidi, tufaidi na sisi tuchome gesi kama wazungu walivyochoma wakati sisi tumelala. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia Mapendekezo ya Mpango. Mapendekezo ya Mpango ni mazuri na kama mnavyojua, lugha ya mjini ni kujenga uchumi wa viwanda ili kufanya mageuzi ya uchumi yatakayoleta maendeleo ya watu na hiyo inawezekana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya upungufu wa muda, ningependa nijibu baadhi ya maswali yaliyojitokeza na nianze na shemeji yangu, kusudi wajomba zangu kule wasijisikie vibaya, baba yao anajua takwimu na mjomba wao anajua takwimu. Kwa nini tunakwenda kwenye viwanda? Tutatengeneza ajira. Ilani ya CCM Ibara ya 32 mpaka 33, inasema asilimia 40 ya nguvu kazi itokane na viwanda, inawezekana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa nini, tunakwenda kwenye viwanda? Tunalenga kwamba asilimia 15 ya GDP basi itokane na viwanda, inawezekana. Kwa nini tunakwenda kwenye viwanda, tunazo rasilimali asilia tulizopewa na Mwenyezi Mungu, sasa ni wakati wa kuzichakata, hizi rasilimali hizo zipitie kwenye viwanda ili pato, tutakalopata liweze kwenda kwenye maendeleo ya watu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini tunakwenda kwenye viwanda? Tunakwenda kwenye viwanda kwa sababu kwa kuchakata viwanda vya Mzee Mwigulu tutaweza kuwashirikisha wananchi walio wengi na wananchi walio wengi wakishiriki ule umaskini utaweza kuondoka. Kwa nini tunakwenda kwenye viwanda? Viwanda tulivyonavyo sasa vimeonyesha utendaji mzuri, export ya bidhaa za viwandani zimeongezeka kwa takwimu sahihi. Sasa tunataka kuongeza zaidi, twende kwenye soko la nje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilizungumza juzi nchi ya India, pamoja na matatizo ya jana, wametufungulia milango kwamba bidhaa itengenezwayo Tanzania na ipelekwe kule. Sasa tunalenga viwanda gani? Tunalenga viwanda vya chuma Mchuchuma na Liganga zichakatwe ziende kule. Engaruka soda ash ichakatwe, mazao ya kilimo na mifugo yachakatwe. Hizo ni shughuli ambazo zitashirikisha watu wengi, lakini edible oil, alizeti, mawese ya Kigoma yachakatwe tuweze kutosheleza soko la ndani. Tanzania tunaagiza tani 350,000 za mafuta ya kula. Napenda mimi nikiwa katika nafasi hii tusiagize mafuta, ila sisi tuuze nje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nijibu swali lingine, nani atafanya hivi? Kama alivyosema Profesa Muhongo ni mimi na wewe Mbunge, ni sekta binafsi. Sekta binafsi ndiyo injini, sekta binafsi ndiyo itasukuma hii. Kwa hiyo, sekta binafsi ndiyo ambayo itatuongoza katika kutekeleza suala hili. Sekta binafsi, nini jukumu la Serikali, Serikali itatengeneza mazingira safi, kusudi wawekezaji tuwaondolee vikwazo. Njoo kesho iishe, ardhi inapimwa pale, unakuja una mgogoro, mahakamani, mambo yanawekwa sawa. Unakuja saa tatu unasajili saa saba, hiyo iko chini yangu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine la kufanya, nini uzoefu wa dunia? Uzoefu wa dunia unaonyesha kwamba asilimia kubwa ya shughuli za ujasiriamali zinamilikiwa na SME, viwanda vidogo na vya kati. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge mjiandae, nilikuwa nagawa nguzo mwaka jana, sasa nitakuwa nagawa viwanda vidogo. Kwa hiyo, tafuteni viwanda vidogo, asilimia 99 ya shughuli za kiuchumi duniani ni viwanda vidogo. Lakini GDP angalia mfano wa Brazil, South Korea, India, coated industry ndiyo inazalisha bidhaa zilizo nyingi. Kwa hiyo, tunakwenda kwenye viwanda vidogo vidogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaambie Waheshimiwa Wabunge, angalieni kwenye Manispaa zote na Miji muangalie, guest house yenye vyumba kumi, ni kiwanda kidogo. Mtaji wa milioni 50, milioni 100 unanunua kiwanda kidogo. Juzi, nimenunua Kiwanda Bangkok Thailand, kitazalisha chakula cha samaki, ambacho kwa mwaka kitazalisha samaki wenye thamani ya bilioni 60, juzi wamekizindua Muleba, mimi nakwenda kukihamasisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rweikiza wa Bukoba Vijijini, amenunua mtambo wa kuchakata nyanya, kwa shilingi milioni 140. Ni Mbunge gani anaweza kukosa kwenda benki akaaminiwa, kwa milioni 140, akawahamasisha wananchi, wakazalisha nyanya, akazichakata. Wale wanaochakata wanaweza kuongeza kipato.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo machache, tutakutana kwenye Mpango na naunga mkono Mpango.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii kuipongeza Serikali na hususani Wizara ya Nishati na Madini kwa kuja na mpango wa bajeti itakayowezesha Taifa letu kuwa na umeme wa uhakika. Sekta ya Nishati ni muhimu katika kutekeleza dhamira ya Taifa ya kujenga uchumi wa viwanda.
Mheshimiwa Naibu Spika, nishauri juu ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini chini ya REA na TANESCO. Tofauti na mipango ya REA katika kusambaza umeme Mkoa wa Kagera una upekee wake kutokana na ujenzi wa nyumba za makazi sehemu za vijijini. Wananchi wa Kagera kila familia hujenga mbali na familia nyingine katika familia ambazo hazijabanana. Kaya moja inaweza kuwa mita 100 – 200 kati ya nyumba moja mpaka nyumba nyingine. Hali hii inapeleka mgao wa kilomita mbili na nusu kila kijiji waishio sehemu ndogo tu ya kijiji. Changamoto hii wananchi na viongozi tumeiwakilisha kwenye ngazi mbalimbali za REA, TANESCO na Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na shukrani kwa kazi nzuri iliyofanyika niombe na kushauri yafuatayo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na vijiji kuwa vikubwa sana na aina ya makazi, tathmini ifanyike na waongezewe wigo wa usambazaji. Usambazaji wa umeme kwenye Jimbo la Muleba Kaskazini utoe kipaumbele kwa Kijiji cha Kahumuko, Kata ya Katoke na Omurunazi, Kata ya Mushabego kutokana na uwepo wa mashine za kusukuma maji ambazo zinatumia diesel.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Nyakatanga, Kijiji cha Bihija hakikutajwa, kihusishwe. Kata ya Rutoro nashauri Kijiji cha Misambya kihusishwe na izingatiwe kuwa kijiji kimoja kimeandikwa mara mbili.
Mheshimiwa Naibu Spika, nishauri pia Kata ya Bumbiile ni eneo kubwa sana, kwa hiyo solar min grid ziongezwe ili kufikia vijiji vingi hasa wananchi wakazi. Kata ya Boziba, Kisiwa maarufu kwa shughuli za uvuvi na biashara ya samaki kisiwa hiki kiongezewe solar min grid ya umeme wenye uwezo wa kuhimili shughuli za kibiashara kadri ya mahitaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016/2017 – 2020/2021
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Mpango wa Pili wa miaka mitano.
Mheshimiwa Naibu Spika, dhima ya Mpango wa Pili wa miaka mitano ni kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Ninaunga mkono dhima hiyo, nikijibu michango ya Waheshimiwa Wabunge, nataka niwaeleze, ukisoma falfasa ya viwanda, watalaam wa falsafa ya viwanda wanakwambia kujenga uchumi wa viwanda ni vita na ukirejea maandiko ya Mwalimu, mnapokwenda vitani lazima wote muungane mkono. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge kwa niaba ya Watanzania niwaombe tuunge mkono ujenzi wa uchumi wa viwanda, asitokee mtu akabaki nyuma.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini ni vizuri kujenga uchumi wa viwanda? Uchumi wa viwanda unatusaidia kutengeneza ajira. Watanzania wenzangu mkubali, Tanzania ni Taifa changa kama Afrika lilivyo continent changa, zaidi ya asilimia 65 ya Vijana wetu au watu wetu wana umri wa usiyozidi miaka 35, maana yake ni kwamba hawa watu wanataka ajira. Sekta inayoweza kutengeneza ajira ni viwanda.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunakwenda kwenye kitendawili cha viwanda gani tunavitengeneza! Kama alivyosema pacha wangu akirejea usemi wa babu, ukitaka mali utaipata shambani. Tutalenga sekta ambazo zitawashirikisha watu walio wengi na watu walio wengi wapo katika sekta zile za kilimo.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo niwashawishi Watanzania, sisi mali tunazo, viwanda vitakavyotutoa ni viwanda ni viwanda vidogo sana, viwanda vidogo na viwanda vya kati, hivi ndivyo viwanda vitakavyotutoa, niwahakikishie Watanzania wanao uwezo wa kufanya hivyo. Badala ya kujenga nyumba ukifanya tathmini ya nyumba zilizojengwa katika Miji, zile zinazoitwa dead capital, dead capital unajenga nyumba yako ya ghorofa unafika ghorofa ya tatu huwezi kuendelea, hiyo inaitwa dead capital, ukiorodhesha nyumba zote ambazo ni dead capital au zile zinazojengwa zikaisha zikawekwa vibao vya tunapangisha kwa miaka sita hizo zote ukijulisha na uka-convert pesa yake ukaiweka kwenye viwanda vidogo na viwanda vya kati, vijana wote watapata ajira.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie fursa hii kuwapa utangulizi wa kazi ambayo nitaifanya kwa miaka mitano ni kuwahimiza Watanzania tubadilishe sasa mtazamo ili tuwekeze kwenye viwanda. Jambo la kuwaambia Watanzania ni kwamba sera ipo, Sustainable Industry Development Policy ipo ya mwaka 1999 mpaka inakwenda mpaka 2020, tunao mkakati unaitwa Integrated Industrial Development Strategy ipo ya 2025.Waheshimiwa Wabunge niwadokeze kitu kimoja kuhusu suala la Kurasini, suala la Kurasini linapotoshwa!
Mheshimiwa Naibu Spika, niwape siri ya Kurasini Logistic Industrial Area tunalenga kwamba sisi tuwe kituo cha mauzo ya nchi zilizotuzunguka, huwezi kuzuia China kuuza nchi za Afrika. China ni soko kubwa sasa tunawaleta hapa. Pia niwape siri msiwambie watu, tunalenga kudhibiti bidhaa substandard tunataka bidhaa zote zitengenezwe Kurasini, bidhaa ambazo ni substandard hazitaingia hapo, ndiyo mpango mzima na wanaotetea wanaogopa hiyo! Hakuna substandard itaingia pale itaanzishwa kitu kinaitwa Total Quality Management (TQM), TBS ambayo iko chini yangu nitawahamishia pale kila kitu kinachoka China kitengenezwe pale na msiwe na wasiwasi kwamba Kurasini itaharibu viwanda.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo nina orodha ya wawekezaji, kuna mwekezaji mmoja anakwenda Tanga anatengeneza kiwanda cha saruji tani milioni 2.5 huyu anazuiliwa na Kurasini? Kuna mtengenezaji wa vigae nimempeleka Mkuranga, muulize Mbunge wa Mkuranga atatengeneza square kilometer 80,000 ambazo zitatosheleza Afrika yote, huyu anazuiliwa na Kurasini? kama walivyosema uulize jambo uelezwe, kwa hiyo, kila kitu kina mpango wake.
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie EPZ. EPZ ni muhimu na inatenguwa kile kitendawili cha wepesi wa kufanya shughuli. Wawekezaji hasa vijana wanaotoka shule wameshindwa kufanyakazi kwa sababu hawakupa maeneo ya kufanyia kazi. Maelekezo ya Serikali ni kwamba kwenye Halmashauri za Miji kuanzia Vijiji, Kata, Tarafa mtenge maeneo mkija ngazi ya Kanda inakuwa ni EPZ na wale wanaodai tunapambana kuhakikisha wote wanalipwa. Hii ina maana kwamba tukitengeza EPZ tukatengeza maeneo, wawekezaji wanaokuja kuwekeza, Watanzania tunawapa maeneo wanaanza shughuli, na wale wanaotoka nje tutawaelekeza kwenye EPZ.
Mheshimiwa Naibu Spika, ngoja niwape taarifa muelewe. Viwanda vya dunia vilivyokuwa Asia sasa vinarudi Afrika. Viwanda vya dunia nzima vilivyokuwa vimekwenda Asia vinakuja Afrika na mtu asikudanganye, Afrika maana yake ni Tanzania! Kwa hiyo, EPZ zimeandaliwa kuwapokea. Ninazo square kilometers 100 ziko Bagamoyo, Songea nitawafidia, napeleka kwetu Kigoma, iko ile ya Manyoni, nakwenda Bunda - Mara kuweka EPZ na wanaodai wote watapewa fidia. Watu wa Tabora wamelalamikia EPZ, EPZ pitieni ngazi ya Mkoa malizeni matatizo yenu, niiteni mimi ndiyo mwenye mamlaka ya EPZ nitawapa.
Mheshimiwa Naibu Spika, watu wa Dodoma wameniuliza pale nje kwamba Dodoma mbona hamna EPZ, Mbunge wa Dodoma usiwe wasiwasi EPZ nitawapa. Mimi ndiyo mwenye mamlaka ya kutoa EPZ. Tengenezeni mazingira, wakaribisheni Wawekaezaji lazima tutengeneze uchumi wa viwanda.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru naunga mkono hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 – Wizara ya Fedha na Mipango
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipatia nafasi hii mimi yangu ni machache, ninakuja kuwaeleza kwamba tunakwenda kwenye kujenga uchumi wa viwanda na nakuja kuwahakikishia kwamba uwezo wa kujenga uchumi wa viwanda tunao, na sekta itakayoongoza ujenzi wa uchumi wa viwanda mhimili wetu ni sekta binafsi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijaenda mbele nichukue fursa hii kwako wewe binafsi, Waheshimiwa Wabunge niwakaribishe kwenye maeneo ya 40 kwenye Saba Saba Mwalimu Nyerere Dar es Salaam International Trade Fair ya 40 itafanyika kuanzia tarehe 1; karibuni nyote mtaingia na VIP pass. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nianzie pale alipoishia Mheshimiwa Makamba. Dhamana niliyopewa ni kuhakikisha kwamba kunakuwepo wepesi wa kufanya shughuli, ni wepesi wa kufanya biashara jambo ambalo ninalisimamia mimi litakalowawezesha wawekezaji kuja hapa, mengine yote yatafuata baadaye. Ikitokea hakuna wepesi wa kufanya biashara mimi nitalaumiwa lakini mimi ndiyo mdogo nitawakumbusha Mawaziri wote kwamba wawekezaji wote tuwape wepesi wa kufanya biashara, mengine ya kodi yanafuata baadaye, kinachotangulia ni wepesi wa kufanya biashara. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la mitumba ambalo mama yangu alilizungumza, hatuna dhamira ya kuwafanya Watanzania watembee uchi, tunajenga uchumi wa viwanda, viwanda vyangu vya nguo ambavyo vinazalisha 40% viende kwenye 100% na tunatengeneza nguo kusudi watu wavae na tunaanza kuwavika watoto wa nyumbani kabla ya kuuza nje. Kwa hiyo, kama tunawavika watoto wa nyumbani hawawezi kuvaa mitumba msiwaombee Watanzania kuvaa mitumba, kwa nini tumeongeza tozo kwenye mitumba, tumeongeza tozo kwenye mitumba tunawa-beep wenye viwanda kwamba sasa tunawalinda, zalisha nguo nzuri, watu wetu wavae na mitumba itapigwa marufuku yenyewe katika miaka mitatu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie mafuta ya kula. Sekta ya mafuta ya kula (the edible oil), mbegu zinazotengeneza mafuta ya kula ukianzia migaze, ukaja karanga, alizeti zinaajiri watu milioni 1.5 lakini Tanzania tunahitaji laki nne mafuta ya kula, sasa mafuta yanalimwa nchini hayafiki 70,000, kiburi chetu ni kwamba tujenge ujasiri wazalishe kiasi hiki kama 70,000, zinatengeneza ajira milioni 1.5 laki nne itatengeneza kiasi gani ndipo mimi nitakpopata ajira ya Watanzania, wenye viwanda vya mafuta Tanzania msikate tamaa, najua wasiwasi wenu ni kwamba mafuta kutoka Kenya na Uganda yatakuwa na advantage kwa sababu kwao yanaingia kwa sifuri, ngoja niwaeleze.
Mheshimiwa Naibu Spika, tangu tarehe 1 Julai, mafuta yatakayoingia Tanzania ambayo hayakupitia kwenye viwanda vya Watanzania wale watatu yatalipishwa asilimia 25 na asilimia 18 nimemwambia Waziri wa Fedha kwamba tuhakikishe mafuta yanayotoka Kenya na Uganda kuingia Tanzania yanalipishwa zaidi kusudi viwanda vya Tanzania viweze kupata advantage. Wenye viwanda nitawalinda, leteni habari kwangu niweze kuwapa wepesi wa kufanya shughuli. Lakini siwafichi nichukue fursa hii kuwapongeza Wabunge wa Kigoma kwa mara ya nne mkiweza kuzalisha migaze kwenye hekari laki moja tutaweza kuzalisha mafuta ya kuweza kutosheleza mafuta yetu. Tunapojenga standard gauge rail kwenda Kigoma maana yake ni nini, treni ikipanda na mizigo ya Congo irudi na mawese kwenye viwanda vya Dar es Salaam. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, limekuwepo swali tata watu wanasema Mwijage umepewa shilingi bilioni 40 utajengaje uchumi wa viwanda? Nitaujenga hivi Jimbo la Jiangsu juzi walikuja kumuona tajiri namba moja, wameahidi kwamba wataleta dola trilioni tano kujenga viwanda, ndiyo maana nachukua fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Mchengerwa, Mbunge wa Rufiji ameandamana kuja kwangu na nimemwambia anipe hekta 15,000 nitamletea mtengenezaji wa kiwanda cha sukari kuzalisha tani 150,000. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama alivyosema Mheshimiwa Makamba, ngoja nikueleze muingie kwenye benzi hii, muingie kwenye treni hii tunaondoka atakayekataa kujiunga na sisi atajuta na kusaga meno. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba bajeti hii ipite, nichukue fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Simbachawene ametoa maelekezo kwenye Wilaya yote na Mikoa kutenga maeneo ya uwekezaji natoa mimi maelekezo kwa wale walio chini yangu SIDO ndiyo itakuwa gateway, na Serikali ya China sisi tuna marafiki zetu bwana, Serikali ya China watatoa dola milioni 100 kusaidia viwanda vidogo zinakuja kwangu. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge SIDO ndiyo itakuwa gateway, tutatafuta mbinu zote kuhakikisha tunaweka mazingira wezeshi kusudi Watanzania wote waweze kwenda vizuri.
Niwaeleze moja, pacha yangu amekwenda Mambo ya Ndani, tumedhamiria kwamba kiwanda cha Karanga Prison, tutawapatia vifaa kutoka Wizarani kwangu kupitia TIB watengeneze sole za viatu ili ngozi zinazotengenezwa Tanzania zitengeneze viatu tuanze kuvaa viatu na kabla Bunge lako halijaisha watu wa Karanga Prison, watu wa Imo Tannaries watakuja kuonyesha viatu vinavyozalishwa, viatu vizuri sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa uchumi wa viwanda ni lazima tukubali sisi wenyewe kuvaa bidhaa zetu, ukipende chako kabla wenzako hawajakipenda na kama nilivyowaeleza ujenzi wa uchumi wa viwanda ni vita hakuna anayecheka kwenye vita wote tunune tujenga uchumi wa viwanda, tuongeze GDP. Kama alivyosema Profesa Muhongo, GDB ikikua ukigawanya kwa watu wetu unapata dola 3000 kwa kila mtu, ifikapo 2025 Tanzania inakuwa uchumi wa kati, uchumi ambao mambo ya umaskini na ujinga itakuwa ni historia. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hayo machache, naomba kuunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Sekta ambayo nimeitumikia kwa miaka 31 nikiwa fundi bomba wa kupaka grease mpaka nilipokuwa Naibu Waziri wa Nishati.
Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa Bajeti na speech nzuri, Naibu Waziri ambaye amevaa viatu vyangu, yaani kama vya kwako kabisa, lakini na Watendaji wote ambao nimeishi nao kwa miaka 31 ambao naamini wanaifanyia vizuri nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijajibu hoja zilizojitokeza kutoka Wizara ya Nishati, nichukue fursa hii kuishukuru Serikali kupitia Wizara hii kwa namna walivyosambaza umeme kwenye Jimbo langu la Muleba ya Kaskazini. Nifikishe ujumbe wa Wanamuleba Kaskazini, asilimia 16 wanaoishi visiwani, Mheshimiwa Profesa Muhongo wanamtegemea kwamba kwa kurudi kwake, Visiwa vya Goziba, Makibwa, Bumbire na Kerebe vitapata umeme, sina wasiwasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kujibu hoja za Waheshimiwa Wabunge zilizojitokeza kwenye bajeti hii ya Nishati na Madini. Suala la EPZ Simanjiro, Tanzanite; tumeshatoa EPZ, tumeshatoa eneo tumefidia. Sasa hivi tunatafuta wawekezaji watakaoweza kutengeneza Tanzania Minerals Business Center. Nikiwaonesha picha yake kama ndoto ikiwa kweli, suala la Tanzanite litakuja kubadilika na kuwa ndoto ya mambo ya zamani.
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Nishati na Madini, mpango wao ni kutengeneza kituo kimoja cha madini na EPZ ilianzishwa nyakati zile kwa misingi hiyo. Kwa hiyo, hilo suala halina tatizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru wewe na Ofisi ya Bunge kwa kuitanguliza bajeti yangu na Wizara ya Nishati ikaja baadaye. Wako waliokuwa wanasema viwanda haviwezekani, sasa angalieni, kuna power generation inaendelea kutokea, kuna power transmition inaonekana, kuna power distribution. Kama nilivyozungumza, tumieni umeme huo mpaka vijijini kwa kuanzisha viwanda.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, muwe na imani, think positive, muione glass ya maji iliyoko nusu kwamba imejaa nusu, msione kwamba iko tupu nusu. Huu umeme unakuja, maneno anayoyasema Mheshimiwa Profesa Muhongo, nina imani naye, ni mambo ya kweli.
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala ambalo limechukua hisia za watu wengi la Mchuchuma na Liganga. Mchuchuma na Liganga, Waraka la Baraza la Mawaziri wa mwaka 96, Waraka Na. 6 ndiyo ulisukuma suala la Mchuchuma na Liganga. Sasa hivi tuko wapi? Nawaomba Waheshimiwa Wabunge, kama kuna mtu yeyote anajua makandokando yanayokwamisha Mchuchuma na Liganga aje aniambie mimi. Mheshimiwa Deo, Mzee wa Njombe njooni wote mnione.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la Mchuchuma na Liganga Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati alijibu swali hapa akasema anaanza kulipa mwezi wa Sita na anayewajibika kulipa ni Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji; yaani mimi ndiyo Waziri mwenye dhamana, niwahakikishie kwamba Tanzania sasa ziko pesa za kutosha za kuweza kulipa hao wananchi. Ninachoomba ni ushirikiano wa Wabunge. Hii sitamwachia mtu, nitashughulika mimi mwenyewe na Makatibu Wakuu na Madiwani wote tuhakikishe watu wanakuwa compensated. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimesema kama kuna mtu anaelewa makandokando yoyote kuhusu mradi huu, anieleze. Hakuna kurudi nyuma, tunakwenda mbele. Tunakwenda na mwekezaji huyo aliyepo, aje alipe. Kama alivyozungumza Mheshimiwa Mbunge ni kwamba, mradi huu katika kuujenga tutaajiri watu 3,000, lakini utakapokuwa umeanza, utaajiri watu 6,000 wa moja kwa moja. Huu mradi utakuwa na indirect employment watu 24,000, lakini utachangamsha maeneo yote ya Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niwaeleze, wananchi wote wataelimishwa namna ya kushiriki. Tuna uhakika sasa amekuja huyu mwekezaji ambaye ni Mbia wa NDC, tumekaa naye na bahati nzuri Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Mheshimiwa Dkt. Dalaly Kafumu alikuwa nami, tumekaa nao, nimewauliza, wakanionesha nyaraka, hii ni ukweli. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tujiweke tayari, tu-think positive huu mradi uweze kuendelea. Kwa hiyo, haki za watu zitalipwa. Nilichozungumza na walioliona kwenye vyombo vya habari, tunachotaka, ni lazima VETA iwepo, iwafundishe Watanzania. Nimesema mbele ya Bunge Tukufu, Watanzania watashiriki kwenye ngazi zote za utendaji kuanzia ngazi za chini mpaka ngazi za juu. (Makofi)
Waheshimiwa Wabunge, nimepata faida ya kushiriki kwenye mchakato mzima wa kampuni. Nimewaeleza nilipoajiriwa TPDC, nilikuwa pipeline operator nikifungua valve, lakini nimepanda mpaka nikawa international trader wa Chevron, nikapanda mpaka Naibu Waziri wa Nishati. Kwa hiyo, nami napenda vijana wa Kitanzania wakachakate chuma watengeneze vyuma. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niwaambie ndugu zangu wa Kilimanjaro; Kilimanjaro Machine Tools inapoanza Mchuchuma na Liganga na yenyewe itaanza kazi. Kwa hiyo, suala la Mchuchuma na Liganga zile historia na hadithi zimefikia mwisho, tunakwenda kwenye reality na mwekezaji, pesa zimeshaingia nchini. Ule mradi utajengwa kwa gharama ya Dola bilioni tatu na Tanzania tunashiriki kikamilifu katika mradi huo. Tutakapokuwa tumefikia kikomo, tutakuwa na hisa asilimia 49.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama kuna mtu anafahamu makandokando yoyote, asiache kuja kuniambia Mwijage ulikosea, aje twende wote. Mchuchuma na Liganga ni mradi kielelezi, kwa sababu wenyewe utachochea viwanda vingine. Badala ya kuagiza chuma ambacho ni bidhaa nzito kutoka huko Amerika na sehemu za Uchina tutakuwa na chuma hapa nyumbani kwetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mradi wa Mchuchuma na Liganga kutakuwepo mtambo mwingine wa kuchenjua madini yanayopatikana ndani ya mtambo huo wa titadium na vanadium yanayoendana na chuma. Ndiyo maana mradi wa Mchuchuma na Liganga ulichelewa. Chuma chake siyo cha kuchukua na kuchakata, kina taratibu zake na huyu mwekezaji amefanya research na amejihakikishia. Kwa hiyo, ndiyo maana ilani ya Chama changu inasema huu ni mradi kielelezi, ndiyo maana mpango wa miaka mitano unaitwa mradi kielelezi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nataka nilifafanue hilo, kwa hiyo, Mchuchuma na Liganga is a reality, lakini umeme unakuja. Watu wengine wanafanya mahesabu kwamba imechukua…
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, naomba umalize. Naomba umalize!
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa muda wa kuchangia bajeti hii. Niwahakikishie kwa kumalizia kwamba, umeme upo wa kutosha. Kauli za kwamba hatuna umeme wa kutosha zinawakimbiza wawekezaji lakini wawekezaji wanaijua Tanzania ndiyo maana sasa kutoka Mtwara kwenda mpaka Dar es Salaam, ukanda mzima wa gesi wa uwekezaji ndiyo sehemu ya preference ya kwanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ndugu zangu tuzungumze vizuri, tuipe imani hii bajeti kusudi wawekezaji waweze kuja, nami niweze kutengeneza viwanda, score card yangu iboreke na tajiri namba moja anione nafaa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono bajeti ya Mheshimiwa Profesa Muhongo.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuwasilisha mpango na bajeti ya mwaka 2016/2017. Sekta hii ni muhimu sana kwa maendeleo na ustawi wa Taifa letu, ardhi ni msingi wa shughuli zote za maendeleo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie kuhusu migogoro ya ardhi. Narejea Jimbo langu la Muleba Kaskazini, tunayo migogoro mikuu miwili katika Kata za Mayombwe na Muhutire kati ya wananchi na kambi ya Jeshi la Wananchi Kaboya. Jeshi la Wananchi kwa maslahi ya Taifa waliamua kuongeza ukubwa wa eneo lao. Mgogoro huu umepitia ngazi zote za uongozi wa nchi ukiondoa mahakama. Uamuzi wa Wizara ya Ardhi na ile ya Ulinzi kwa maelekezo ya Mheshimiwa Rais Kikwete na Rais wa Awamu ya Tano ni kuwa Serikali iwalipe fidia wananchi wa maeneo yote yatakayotwaliwa, lakini mpaka sasa fidia haijalipwa na wananchi wamezuiwa kuendeleza maeneo yao kwa miaka sasa. Katika mwaka 2016/2017, Wizara ya Ardhi ibebe jukumu la uongozi na kumaliza mgogoro huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro wa pili ni katika Kata ya Rutoro. Eneo hili kampuni ya NARCO iligawa vitalu vya ufugaji kwa wawekezaji kwa kuwapatia wawekezaji hao maeneo ambayo tayari vilikuwepo vijiji tena vinavyotambuliwa na Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili limeanza tangu miaka ya 2005, Kamati nyingi zimeundwa kutatua tatizo hili, zilileta mapendekezo bila utekelezaji. Moja ya Kamati iliyotoa mapendekezo yaliyolenga kuleta suluhu ni Kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara sita iliyoteuliwa na Mheshimiwa John Pombe Magufuli, wakati huo alikuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Kamati za Bunge mara mbili zimefanyia kazi suala hili na kutoa mapendekezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais Kikwete wa Awamu ya Nne aliamua kutwaa hati ya NARCO inayohusu eneo la Kata ya Rutoro, iliagizwa eneo hilo ligawiwe upya kwa kubainisha eneo la vijiji na lile la wafugaji. Uongozi wa Mkoa umejaribu kutoa mapendekezo namna ya kutatua mgogoro huo kwa kuazima mapendekezo ya Kamati mbalimbali nilizozitaja hapo juu. Nakubaliana na mapendekezo hayo kwa asilimia 49, sikubaliani na mpango huo pale unapotaka kurudia makosa ya kutoa maeneo kwa watu ambao si raia wa nchi hii na pale wanaposhindwa kutambua kuwa wananchi wa Rutoro ni wakulima na wafugaji. Mgogoro huu hapa ulipofikia ni rahisi sana kuutatua, tuwe objective bila kupendelea upande wowote, tulenge maslahi ya Taifa, tumalize mgogoro huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utendaji uliotukuka kwa kipindi cha miaka minne ya Uongozi wake
MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru. Nami nichukue fursa hii kuunga mkono Azimio la Kumpongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli namna anavyoiendesha nchi hii kuelekea kwenye uchumi wa kati. Ninapofuatilia njia ya Mheshimiwa Rais, napenda niwakumbushe Watanzania wenzangu, tunapokwenda kwenye uchumi wa kati, uchumi jumuishi, tunalenga katika kuwa na maendeleo ya watu ambayo maendeleo ya watu yanapimwa kwa afya na kama walivyosema wenzangu nchi nzima inasheeni, inasheeni vituo vya afya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, zamani kwetu sisi tulikuwa tunaona malori yanakwenda vijijini kusomba kahawa, siku hizi tunaona malori ya MSD yanapeleka madawa. Tunapima maendeleo ya watu kwa kuangalia elimu, siku hizi vijana wanakimbizwa kwenda shule na kila anayekwenda shule anapata elimu inayopatikana. Mheshimiwa Rais anajasiria uchumi wa viwanda na uchumi wa viwanda utakapokuwa umefikia katikati tutaweza kukabili vizuri kipato, wako wasioelewa, ujenzi wa uchumi wa viwanda unategemea miundombinu wezeshi na miundombinu saidizi. Miundombinu wenzeshi ndiyo umeme Stiegler’s Gorge, ndiyo miradi mikubwa ya kusambaza umeme, lakini ndiyo hizo ndege, watu wengine hawajaliona. Tunakokwenda tutakuwa na wataalam ambao asubuhi mtaalam atakuwa Katavi, saa sita atakuwa Dar es Salaam, saa tisa atakuwa Bukoba na huyo mtu atatakiwa kuwa Moshi, huwezi kwenda namna hiyo mpaka uwe na ndege kubwa kama bombadier, dreamliner na nyingine ambazo zinakuja.

Mheshimiwa Spika, dunia ya sasa inakwenda kwenye mazao ambayo hatukuyategemea kama alivyosema Mheshimiwa Kamwele, tunakwenda kuleta ndege kubwa za kupeleka mazao, ina maana asubuhi unachuma njungu mawe na maharage ukiwa Bukoba, unakwenda kwenye ndege uwanja wa ndege wa Chato halafu Muhaya aliyeko London anaweza kupata kisamvu na overcado.

Mheshimiwa Spika, tunakwenda kwenye uchumi wa kati, uchumi jumuishi, mambo haya ndivyo yanavyokwenda, huwezi kuijua ngoma mpaka uicheze. Tunaendelea na ujenzi wa viwanda, lakini ujenzi wa viwanda kama nilivyozungumza unategemea miundombinu wezeshi, ICT, wewe mwenyewe na nichukue nafasi hii kukupongeza, sasa hivi makaratasi yale ya mezani hayapo, tulikuwa tunayaacha hotelini, ni mambo ya kubofya tu, hiyo ndiyo miundombinu wezeshi, miundombinu saidizi, ina maana mtu sasa tunapokwenda kesho kwenye TMS, utakapokuwa umevuna kahawa Bukoba au korosho Mtwara, utaweza kumweleza mteja aliyeko China au Vietnam kwamba kahawa yangu ni kiasi hiki na unajua bei, ndiko huko tunakokwenda.

Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache, naunga mkono Azimio hili na namshukuru sana aliyewasilisha Azimio hili, Mheshimiwa Rweikiza ameliwasilisha vizuri sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipatia nafasi ya kuchangia bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukirejea hotuba yangu ya Wizara ya Viwanda, Waziri wa Ardhi nilimshukuru kwa kumtaja jina na hii ni kutokana na namna Wizara hiyo inavyoshirikiana na Wizara yangu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna moja napenda niliweke wazi, wawekezaji njoo muwekeze Tanzania na ninyi Watanzania mchangamkie kuwekeza, hatuna tatizo la ardhi. Mama mwenye nyumba wangu alipata nafasi ya kuzungumza akasema viwanda mtavijenga wapi, viwanda tuna maeneo ya kutosha. Ukisoma ukurasa wa 135, jedwali namba 11 la bajeti hii, miji kumi tu imeeleza maeneo yaliyopangwa lakini hayo ni hayo tu. Pia ukienda kwenye jedwali la TIC (land bank) kuna hekta 500,900 zinazoonyesha maeneo yaliyotengwa mahsusi kwa ajili ya kilimo na hasa kilimo cha miwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kumueleza Mheshimiwa Kamanda Silinde kwamba mwekezaji niliyekuwa namwambia ameshaweka timu Songwe, anakwenda jimboni kwake, anakwenda kulima miwa na anategemea kuzalisha tani 120,000 za sukari. Nayasema haya kuwatoa wasiwasi watu wasije wakadhani kwamba nchi ya Tanzania haina ardhi na Wizara ya Ardhi haijanitengea ardhi. Niwashukuru sana, nikushukuru na mueleze bosi wako kwamba Mwijage amekushukuru sana ulipokuwa haupo kwenye kiti chako. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumetenga ardhi ya kutosha kwa ajili ya kujenga viwanda vya sukari na kilimo cha miwa. Mbunge wangu wa Temeke leo asubuhi aliniuliza swali likanipa shida juu ya hali ya sukari nchini. Niwahakikishie tunayo sukari ya kutosha.
Tumechukua jitihada za kawaida za kutenga maeneo, kwa mfano lipo eneo la Kigoma ambapo hekta 47,000 zitatengeneza kiwanda cha Kigoma Sugar, nimelizungumza hili la Songwe, tutaendelea na Songwe, lakini Kagera Sugar wanaozalisha tani 60,000 wanapanua eneo la Kitengule wazalishe tani 60,000 nyingine. Aidha, watu wa Oman wataingia ubia na Kagera Sugar ili kuzalisha tani 300,000 kutoka pale. Kwa hiyo, hii adha tunayopita ni kwamba tuliamua kudhibiti uingiaji wa sukari ili kuwajengea hamu wawekezaji waweze kuingia katika shughuli hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, adha iliyokuwepo sasa inakwenda kuisha, tunayo sukari ya kutosha, kuna maeneo yana matatizo, kuna Mbunge wa Mwanza ameniuliza kwamba Mwanza sukari iko wapi? Leo Mwanza hali ni mbaya, kilo moja ya sukari shilingi 4,000. Baada ya kunieleza, Bukoba wanapakia tani 600 kwenda Mwanza na kiwanda cha Kagera Sugar kimeanza kuzalisha leo, ni tani 250 zinazalishwa. Tarehe 25 Mei, Kilombero (K1) inaanza kuzalisha na wakimaliza kuzalisha full swing ni tani 600 kwa siku. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge tuwe na imani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, maamuzi yaliyochukuliwa yalijenga imani na kuwaleta wawekezaji hapa ndani.
Ngoja nitoe maelekezo mama unielewe, niko kazini hapa. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimetoa maelekezo wafanyabiashara wote mnaoshughulika na sukari mkajitambulishe kwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ili sukari mnayopewa Dar es Salaam muifikishe kwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya waione.
Tayari zimeshatoka tani 10,000 kwa ajili ya kusambazwa, lakini kuna tani 31,000 ziko njiani zinakuja. Ngoja niwaeleze jambo moja, matumizi ya nchi ni tani 1,200 kwa siku, Kagera Sugar inazalisha tani 250, Mtibwa inazalisha tani 600, deficit ndiyo hiyo niliyowaeleza iliyoagizwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwahakikishie kwamba maeneo ya ujenzi hayana shida. Nichukue fursa hii kuwapongeza tena wale viongozi mnaokwenda mbele zaidi kutambua maeneo yenu na kuyapeleka Wizara ya Ardhi ili yapimwe. Nichukue fursa hii kuwapa pole Waheshimiwa Wabunge wa Tabora. Wabunge wa Tabora walinipa ardhi, nikatafuta mwekezaji, mwekezaji alipokuwa anapanda ndege akazuiliwa asiende Tabora. Niliwaambia wakati wa bajeti yangu kwamba ujenzi wa viwanda ni vita, kwa hiyo, vita hiyo nitaishinda, nitawasaidia watu wa Tabora, nitamleta hata kwa baiskeli huyo mwekezaji ili twende Tabora tuweze kuwekeza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nisisitize agizo la Mheshimiwa Waziri Mkuu ambalo kimsingi halitafanikiwa kama sisi Waheshimiwa Wabunge hatutalisimamia. Tumeagizwa au imekubalika na Serikali kwamba katika maeneo ya vijiji na kata, tutoe maeneo tuyarasimishe, twende tuyapatie hati ili vijana wetu waweze kuanzisha shughuli na biashara ndogo ndogo. Kuna fursa zinakuja za ujenzi wa silos (godown), maeneo mtakayoyatoa kama alivyozungumza Mbunge mmoja yataweza kutoa nafuu katika ku-acquire ile land na kuweza kuweka infrastructure bila kutumia gharama kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo yaliyotengwa yapo kama nilivyowaeleza, yapo maeneo ya Mkurazi yameelezwa na nimeiona Momba hapa nimeiona imetengwa. Niwaeleze ukweli, nimepewa jukumu lingine bahati mbaya, nimsemee Mheshimiwa Mwigulu. Mheshimiwa Mwigulu maneno anayozungumza siyo hadithi za kufurahisha watu. Tuombe Mwenyezi Mungu atusaidie kabla ya mwaka huu kuisha nitakuwa na mtambo tayari wa kuunganisha matrekta 2,500 hapa Tanzania na matrekta hayo yatakwenda kulima ardhi hizi. Kwa hiyo, tunachopaswa kufanya Watanzania wenzangu, unapopata ardhi isalimishe kwa Mheshimiwa Lukuvi, Wizara ya Ardhi ili ardhi hiyo tuweze kuifaidi Watanzania wote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maelezo hayo mimi niseme Wizara yangu iko vizuri lakini niwatoe wasiwasi wawekezaji, msiwe na wasiwasi ardhi ipo. Nimetoa mfano wa Nzega, Maswa na Kagera ambako wananchi wametoa maeneo. Hata hivyo, mnapotoa maeneo nendeni mkayarasimishe Wizara ya Ardhi ili mpate title ili mwekezaji anapokuja iwe rahisi kuwekeza. Napozungumzia wawekezaji sizungumzii wa kutoka nje, mwekezaji ni pamoja na wewe. Tujenge kiburi, tujiaminishe na sisi tuanze kuwekeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo machache, naomba kuunga mkono hoja ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipatia nafasi hii mimi yangu ni machache, ninakuja kuwaeleza kwamba tunakwenda kwenye kujenga uchumi wa viwanda na nakuja kuwahakikishia kwamba uwezo wa kujenga uchumi wa viwanda tunao, na sekta itakayoongoza ujenzi wa uchumi wa viwanda mhimili wetu ni sekta binafsi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijaenda mbele nichukue fursa hii kwako wewe binafsi, Waheshimiwa Wabunge niwakaribishe kwenye maeneo ya 40 kwenye Saba Saba Mwalimu Nyerere Dar es Salaam International Trade Fair ya 40 itafanyika kuanzia tarehe 1; karibuni nyote mtaingia na VIP pass. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nianzie pale alipoishia Mheshimiwa Makamba. Dhamana niliyopewa ni kuhakikisha kwamba kunakuwepo wepesi wa kufanya shughuli, ni wepesi wa kufanya biashara jambo ambalo ninalisimamia mimi litakalowawezesha wawekezaji kuja hapa, mengine yote yatafuata baadaye. Ikitokea hakuna wepesi wa kufanya biashara mimi nitalaumiwa lakini mimi ndiyo mdogo nitawakumbusha Mawaziri wote kwamba wawekezaji wote tuwape wepesi wa kufanya biashara, mengine ya kodi yanafuata baadaye, kinachotangulia ni wepesi wa kufanya biashara. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la mitumba ambalo mama yangu alilizungumza, hatuna dhamira ya kuwafanya Watanzania watembee uchi, tunajenga uchumi wa viwanda, viwanda vyangu vya nguo ambavyo vinazalisha 40% viende kwenye 100% na tunatengeneza nguo kusudi watu wavae na tunaanza kuwavika watoto wa nyumbani kabla ya kuuza nje. Kwa hiyo, kama tunawavika watoto wa nyumbani hawawezi kuvaa mitumba msiwaombee Watanzania kuvaa mitumba, kwa nini tumeongeza tozo kwenye mitumba, tumeongeza tozo kwenye mitumba tunawa-beep wenye viwanda kwamba sasa tunawalinda, zalisha nguo nzuri, watu wetu wavae na mitumba itapigwa marufuku yenyewe katika miaka mitatu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie mafuta ya kula. Sekta ya mafuta ya kula (the edible oil), mbegu zinazotengeneza mafuta ya kula ukianzia migaze, ukaja karanga, alizeti zinaajiri watu milioni 1.5 lakini Tanzania tunahitaji laki nne mafuta ya kula, sasa mafuta yanalimwa nchini hayafiki 70,000, kiburi chetu ni kwamba tujenge ujasiri wazalishe kiasi hiki kama 70,000, zinatengeneza ajira milioni 1.5 laki nne itatengeneza kiasi gani ndipo mimi nitakpopata ajira ya Watanzania, wenye viwanda vya mafuta Tanzania msikate tamaa, najua wasiwasi wenu ni kwamba mafuta kutoka Kenya na Uganda yatakuwa na advantage kwa sababu kwao yanaingia kwa sifuri, ngoja niwaeleze.
Mheshimiwa Naibu Spika, tangu tarehe 1 Julai, mafuta yatakayoingia Tanzania ambayo hayakupitia kwenye viwanda vya Watanzania wale watatu yatalipishwa asilimia 25 na asilimia 18 nimemwambia Waziri wa Fedha kwamba tuhakikishe mafuta yanayotoka Kenya na Uganda kuingia Tanzania yanalipishwa zaidi kusudi viwanda vya Tanzania viweze kupata advantage. Wenye viwanda nitawalinda, leteni habari kwangu niweze kuwapa wepesi wa kufanya shughuli. Lakini siwafichi nichukue fursa hii kuwapongeza Wabunge wa Kigoma kwa mara ya nne mkiweza kuzalisha migaze kwenye hekari laki moja tutaweza kuzalisha mafuta ya kuweza kutosheleza mafuta yetu. Tunapojenga standard gauge rail kwenda Kigoma maana yake ni nini, treni ikipanda na mizigo ya Congo irudi na mawese kwenye viwanda vya Dar es Salaam. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, limekuwepo swali tata watu wanasema Mwijage umepewa shilingi bilioni 40 utajengaje uchumi wa viwanda? Nitaujenga hivi Jimbo la Jiangsu juzi walikuja kumuona tajiri namba moja, wameahidi kwamba wataleta dola trilioni tano kujenga viwanda, ndiyo maana nachukua fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Mchengerwa, Mbunge wa Rufiji ameandamana kuja kwangu na nimemwambia anipe hekta 15,000 nitamletea mtengenezaji wa kiwanda cha sukari kuzalisha tani 150,000. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama alivyosema Mheshimiwa Makamba, ngoja nikueleze muingie kwenye benzi hii, muingie kwenye treni hii tunaondoka atakayekataa kujiunga na sisi atajuta na kusaga meno. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba bajeti hii ipite, nichukue fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Simbachawene ametoa maelekezo kwenye Wilaya yote na Mikoa kutenga maeneo ya uwekezaji natoa mimi maelekezo kwa wale walio chini yangu SIDO ndiyo itakuwa gateway, na Serikali ya China sisi tuna marafiki zetu bwana, Serikali ya China watatoa dola milioni 100 kusaidia viwanda vidogo zinakuja kwangu. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge SIDO ndiyo itakuwa gateway, tutatafuta mbinu zote kuhakikisha tunaweka mazingira wezeshi kusudi Watanzania wote waweze kwenda vizuri.
Niwaeleze moja, pacha yangu amekwenda Mambo ya Ndani, tumedhamiria kwamba kiwanda cha Karanga Prison, tutawapatia vifaa kutoka Wizarani kwangu kupitia TIB watengeneze sole za viatu ili ngozi zinazotengenezwa Tanzania zitengeneze viatu tuanze kuvaa viatu na kabla Bunge lako halijaisha watu wa Karanga Prison, watu wa Imo Tannaries watakuja kuonyesha viatu vinavyozalishwa, viatu vizuri sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa uchumi wa viwanda ni lazima tukubali sisi wenyewe kuvaa bidhaa zetu, ukipende chako kabla wenzako hawajakipenda na kama nilivyowaeleza ujenzi wa uchumi wa viwanda ni vita hakuna anayecheka kwenye vita wote tunune tujenga uchumi wa viwanda, tuongeze GDP. Kama alivyosema Profesa Muhongo, GDB ikikua ukigawanya kwa watu wetu unapata dola 3000 kwa kila mtu, ifikapo 2025 Tanzania inakuwa uchumi wa kati, uchumi ambao mambo ya umaskini na ujinga itakuwa ni historia. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hayo machache, naomba kuunga mkono hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru, na mimi nipitie mapendekezo ya Mpango na zaidi nitoe ufafanuzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ambalo nataka kufafanua nilieleze Bunge lako Tukufu na niwaambie Watanzania. Jukumu la ujenzi wa viwanda ni jukumu la sekta binafsi. Soma mpango wa pili wa miaka mitano, soma vision 2020–2025, sikiliza hotuba za Mheshimiwa Rais, ujenzi wa uchumi wa viwanda, kule kujenga viwanda ni jukumu la sekta binafsi. Serikali kazi yetu ni kutengeneza mazingira wezeshi, tutatengeneza miundombinu, tutatengeneza maji, tutapeleka umeme, sekta binafsi ndio itajenga viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ilibidi nilizungumze hili. Sekta binafsi ni nani? Ni mimi Mbunge, mwananchi, mfanyabiashara. Niwaeleze ndugu zangu Wabunge muelewe viwanda maana yake ni nini? Mheshimiwa Waziri Mkuu atawasomea hotuba ya taarifa yangu ya Viwanda vilivyojengwa, wengine mtashangaa na wengine mtapatwa kihoro, kazi imefanyika. Kwa tafsiri ya viwanda ya Benki ya Dunia, kuna kiwanda kinaajiri mtu mmoja mpaka watu wanne kinagharimu shilingi milioni nane, kuna kiwanda kinaajiri watu watano mpaka 49 ni cha shilingi milioni tano mpaka 200, hizo ndizo ambazo nasema zinapatikana na benki zipo tayari kutoa pesa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna viwanda vinaajiri watu 50 mpaka 99 vinathamani ya shilingi milioni 200 mpaka milioni 800 hivyo viwanda vinaitwa viwanda vya kati. Nitumie fursa hii kuwaambia Wabunge wote mnaotoka maeneo ya SAGCOT ziko pesa dola milioni 70 za Kimarekani, anayetaka kwenda kujenga kiwanda aje aniambie nipo Dodoma siku tatu hizi nikamuonyeshe namna ya kuomba. Waambieni watu wenu pesa zipo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo tulilolipata katika ujenzi wa viwanda kulingana na taarifa za wataalamu, kama alivyosema ndugu yangu Ulega ni mindset, watu wanalala wanasubiri Serikali ije iwajengee viwanda.
Kwa hiyo hivyo ndivyo vitakavyojengwa na kazi inaonekana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze suala la Kurasini Logistic Center. Kurasini Logistic Center Serikali imeshalipa fidia kilichobaki tutamleta operator, ambapo viwanda vita-assemble bidhaa pale zinazotoka nje kuja hapa, lakini pia na kukusanya bidhaa kutoka kwa wananchi kuzi-assemble kwenda nje kuuzwa, ndio utaratibu huo. Masharti anayopewa operator lazima aajiri vijana wa kitanzania ili wapate ujuzi wanaporudi kwao wajue namna ya kutengeneza viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze suala la TBS. TBS inasimamia viwango na nimewaeleza hata Mawaziri wenzangu hata rafiki zangu sitaandika memo kwa mtendaji yeyote wa TBS eti ampendelee mtu yeyote, you follow the principles unapata huduma, wanaolalamika wana makando kando yao, sitaandika memo yoyote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kiongozi wa wafanyabiashara bwana Minja amenifuata kwa matatizo ya TBS, niwaambia wataalam wangu wawashughulikie wale wafanyabiashara wadogo watashughulikiwa. Lakini ngoja niwaambie mkilegeza TBS utendaji wake viwanda vyangu vitakufa, ni kama nilivyowaambia jana lazima TBS izuie bidhaa dhaifu na isiyolipa kodi isiingie nchini. Vijana wa TBS wanafanya kazi nzuri na nitaendelea kuwaongezea nguvu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mchuchuma na Liganga. Mchuchuma na Liganga Serikali hakuna tatizo wala hamtaweka pesa zenu kwenye bajeti, muwekezaji yupo ameshapatikana, nimeelekezwa na mamlaka kwamba niandike cabinet paper niipeleke hatua zilizobaki ziweze kupata baraka ya cabinet paper, ikishindikana zitaletwa kwenye Bunge. Kwa hiyo, msiwe na wasi wasi kamanda Silinde kwamba tumepanga Mchuchuma na Liganga, Logistic Center, haiwahusu, ninyi mmeshatoa baraka tunalishughulikia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie wepesi wa kufanya biashara (the easy of doing business). Tulikuwa watu wa 139, tumekuwa watu wa 132, sijaridhika. Kwa hiyo, anayesema kwamba sisi tuna mahusiano mabaya na wafanyabiashara aje aniambie wafanyabiashara anayewawakilisha ni nani. Ukiwataka wafanyabiashara njoo uniambaie mimi, kila siku ninakuwa nao wanazungumza vizuri ila wanasema ukikaza ukaze kwa wote. (Makofi)
Mheshimiwa Waziri wa Mipango eti ukaze sawia wote mianya uweze kuibana, kwa hiyo, hatuna matatizo, wafanyabiashara wa kweli ni wenzetu. Lakini Waheshimiwa Wabunge mkubali….


niandike cabinet paper niipeleke hatua zilizobaki ziweze kupata baraka ya cabinet paper, ikishindikana zitaletwa kwenye Bunge. Kwa hiyo, msiwe na wasi wasi kamanda Silinde kwamba tumepanga Mchuchuma na Liganga, Logistic Center, haiwahusu, ninyi mmeshatoa baraka tunalishughulikia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie wepesi wa kufanya biashara (the easy of doing business). Tulikuwa watu wa 139, tumekuwa watu wa 132, sijaridhika. Kwa hiyo, anayesema kwamba sisi tuna mahusiano mabaya na wafanyabiashara aje aniambie wafanyabiashara anayewawakilisha ni nani. Ukiwataka wafanyabiashara njoo uniambaie mimi, kila siku ninakuwa nao wanazungumza vizuri ila wanasema ukikaza ukaze kwa wote. (Makofi)
Mheshimiwa Waziri wa Mipango eti ukaze sawia wote mianya uweze kuibana, kwa hiyo, hatuna matatizo, wafanyabiashara wa kweli ni wenzetu. Lakini Waheshimiwa Wabunge mkubali….
MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwijage naomba umalize.
Taarifa ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo; na Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nizipongeze Kamati zote na Waheshimiwa Wabunge kwa kujadili taarifa hizi. Kuhusu Wizara yangu katika kitabu cha PAC ukurasa wa 63 mpaka 68 imezungumziwa NDC.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninayo mambo machache ya kuzungumzia kuhusu NDC; niwakumbushe kwamba hili ni shirika la kimkakati lililoanzishwa na Mwalimu mwaka 1965, na katika ujenzi wa uchumi wa viwanda NDC tumeipanga kwamba ile miradi ya kimkakati ndiyo itashughulikiwa na NDC. Kumbe wakati tunahamasisha sekta binafsi kujenga viwanda, miradi ya kimkakati itakuwa inashughulikiwa na NDC.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikiri kwamba hatujaweka mtaji wa kutosha ndani ya NDC kama ilivyokuwa mwaka 2015, lakini mipango inapangwa kulingana na kila mradi. Kwa mfano, unapozungumzia mradi wa Engaruka, unautambua mradi, lakini huwezi kuuwekea pesa mara moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kukiri, tunayo miradi mingi kwa sababu NDC kazi yake ni kutambua fursa, kutambua maeneo ambayo wafanyabiashara wa kawaida hawawezi kwenda. Kwa mfano tunapozungumzia Mtwara Corridor, ni kazi yake kuitambua na kuitangaza. Tunapozungumzia TAZARA Corridor, ni kazi ya NDC kuitambua na kuitangaza ili hiyo sekta binafsi, iwe ya ndani au ya nje iweze kuingia.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya kipekee limezungumzwa suala la Mchuchuma na Liganga. Nirudie tena, kila mtu anapenda Mchuchuma na Liganga ifanye kazi na Kamati imezungumza maneno mazuri, kwamba hatufanyi maamuzi, wakati wa maamuzi ni sasa na dhamana hiyo iko chini yangu mimi. Nimeagizwa niandike andiko nipeleke kwenye mamlaka na mamlaka itaamua, nililisema mara ya kwanza na Mheshimiwa Deo alinifuata hapa.
Mheshimiwa Naibu Spika, narudia kusema, Mheshimiwa Deo na Waheshimiwa Wabunge, Mchuchuma na Liganga maamuzi yake yanatoka sasa, nitapeleka andiko kwenye mamlaka na mamlaka itaamua na mamlaka inataka Mchuchuma na Liganga iweze kuanza. Kwa sababu Mchuchuma na Liganga ikianza ni kwamba ndiko ile reli ya Mtwara unaweza kuijenga kwa sababu kutakuwa na mzigo mkubwa wa kusomba.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile tuna potential ya watu 5,000, lakini tuna potential ya kutengeneza megawatt 600 za umeme ambazo haziathiriwi na tabia nchi. Nina uhakika bila kuwa-preempt wanaofanya maamuzi kwamba nitakapokwenda mbele yao na sababu hizo, Mchuchuma na Liganga tutafanya maamuzi na kuondoa mambo mawili, matatu ambayo yamekuwa yakiwafanya watu wasifanye maamuzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, limezungumzwa suala la General Tyre na niwashukuru Waheshimiwa Wabunge mmezungumza maneno mazuri, mmezungumza maneno mazuri kuhusu UDA.
Mheshimiwa Naibu Spika, General Tyre ninayo mimi; zimeelezwa pesa zilizotumika, mimi ndiye niliyezuia kwamba General Tyre hatuwezi kuendelea kuipa bilioni mbili, mnieleze tunahitaji kiasi gani kuweza kuifufua na kuiendesha. Nimelishikilia mimi, nimeweka timu inafanya survey, watanieleza twende vipi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikiwa na uhakika na kitu ambacho nitakifanya General Tyre tutaiendeleza. Tunataka kutengeneza kiwanda cha matairi kwa sababu ndiyo kitakuwa sifa ya nchi hii, tunataka kutengeneza shirika kubwa litakalolipa ushuru mwingi, tunataka kutengeneza shirika kubwa litakalowaajiri watu wengi, lakini tunataka kutengeneza shirika kubwa litakalochochea wakulima wa mpira ili watu wanaolima mpira waweze kupata soko.
Mheshimiwa Naibu Spika, yametajwa mashamba ya mpira yaliyopo Muheza na Morogoro; mvute subira. Kwa sababu tutakuwa na uhakika wa soko la mpira tutakuwa na uhakika sasa wa kuwaambia wananchi waweze kulima zaidi, na mpango wetu sisi ni kuyatumia yale mashamba ya NDC kama nucleus farm na kama road base, lakini tutawahamasisha wananchi watumie outgrowers kuweza kuzalisha mpira zaidi kwa ajili ya viwanda vyetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo vilevile kwa mradi wa Engaruka, nimetengewa bilioni 1.7, lakini ninachopigana nacho ni kuangalia nani atakwenda kuwekeza pale. Pia imeelezwa kwamba NDC anashindwa kufanya feasibility study, anawategemea wawekezaji. Jambo la muhimu tunalofanya ni kutafuta vijana wazuri wanaoweza kwenda sambamba na wale wawekezaji ili kufanya feasibility study. Si jambo la ajabu, hata kwenye petroleum industry tunafanya hivyo, jambo la muhimu ni kuwa-monitor wanafanya nini.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hayo machache, niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba, ushauri wao ni mzuri na tutauzingatia.
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Viwanda Na Bishara
MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia maandiko nichangie bajeti ya Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchango wangu nibainishe kwanza muhimu ya kuzingatia kwanza tunao mpango wa muda mrefu wa kufufua viwanda vilivyobinafsishwa ambavyo havifanyi kazi vizuri au vimekufa kabisa. Naomba na kushauri Serikali ifanye tathimini ni kiwanda gani kinaweza kufufuka na kuzalisha kwa tija kubwa. Viwanda ambavyo haviwezi kufufuka tuachane navyo au maeneo hayo kama yana miundombinu wezeshi na saidizi basi maeneo hayo yatumike kwa viwanda vingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ijikite katika kujenga uchumi shindani kwa kutanguliza lengo kuu ikiwa ni kutengeneza ajira, ikifuatiwa na kuzalisha bidhaa na mwisho kwa umuhimu huo kukusanya mapato. Ni katika mfuatano na umuhimu huo ujenzi wa uchumi wa viwanda shindani utaweza kufikiwa. Kwa maana rahisi shughuli yoyote inayoweza kutengeneza ajira, maslahi ya kukusanya kodi yasitukwamishe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kujenga viwanda tubainishe ni viwanda gani tusijihusishe navyo hasa pale penye uwekezaji wa umma ili kuepuka kupoteza rasilimali adimu za wananchi. Pia ni muhimu Serikali kuchangamsha re-export business na biashara hapa nchini ili kutengeneza ajira na kukusanya mapato lakini muhimu kulinda viwanda vya ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ifanye utafiti ili kujua ni kwa namna gani korosho na pamba izalishwayo nchini inaweze kuongezwa thamani hapa nchini na bidhaa zake kuwa shindani hapa nchini au na kuingia kwenye masoko ya nje na kufanya vizuri. Hoja hapa ni kuzalisha kwa tija na kuingia kwenye masoko mazuri ya nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ichukue jitihada zaidi kuelimisha wananchi na hasa Wabunge juu ya dhima ya mipango mitatu ya miaka mitano mitano. Hii italeta uelewa wa pamoja hali itakayoongeza kasi ya kutekeleza dira ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia njia ya maandishi naomba kuchangia Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Muhutwe – Kamachumu – Muleba (kilomita 53). Barabara tajwa imeainishwa katika Ilani ya CCM ya mwaka 2015 kuwa itajengwa kwa kiwango cha lami. Umuhimu wa barabara hii kwa vipindi tofauti nimeelezea hapa Bungeni. Pamoja na mpango huu kwa sasa barabara hii imeharibika sana maeneo ya Rukono (Muhutwe – Kyabakoba) na Malele (Kyabakoba – Nyawaibewa). Uharibifu ni mkubwa sana kiasi kwamba kuna wakati watu watokao Muhutwe kwenda Kamachumu (15km) wamelazimika kuzunguka kupitia Muleba, umbali wa kilomita zaidi 110.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maombi yangu ni kuwa mradi huu utekelezwe kama ilivyoanishwa katika Ilani yetu. Aidha, kutokana na hali ya barabara kutoruhusu usafiri kuwa salama naomba bajeti ya barabara tajwa kama inavyoonekana ukurasa 286 sehemu kubwa ihamishiwe chini
ya mpango wa upgrading to DSD. Nyongeza za fedha itasaidia kujenga maeneo korofi kwa zaidi ya kilometa sita zilizopangwa sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Bunge lako nieleze kutokuridhika na utendaji usioridhisha katika barabara hiyo kwa mwaka huu (2016/2017) hali iliyopelekea maeneo niliyoyaeleza hapo awali kuharibika. Muhimu watendaji wajiulize ni kwa nini kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 eneo hilo halijapata tatizo kama la sasa katika maeneo ya Rukomo, Ruhanda na Malele. Kutokana na hali ya udongo wa eneo husika mkandarasi atafanya kazi hewa, ufanisi hewa. Kuongeza na kushindilia tabaka la changarawe badala ya kupalula tabaka la changarawe ambalo limewekwa kabla. Siridhiki na utendaji wa eneo hilo na limekuwa chini ya mategemeo ya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mamlaka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADs). Yamekuwepo mawazo ya kuanzisha mamlaka ya kusimamia barabara zilizoko chini ya Halmashauri. Hii ni kutokana na utendaji mzuri na wenye ufanisi wa TANROADs.

Mheshimi Mwenyekiti, utendaji na ufanisi wa TANROADs umefikiwa baada ya kujifunza na uzoefu wa muda mrefu. Hivyo badala ya kuanzisha Mamlaka Nyingine, basi baadhi ya barabara za halmashauri zipandishwe kwenda TANROADs na mgawo wa fedha za Bajeti uongezeke sawia. Halmashauri wabaki na eneo dogo la mtandao wa barabara; na kama nilivyoelekeza awali kwamba mgawo wao kutoka Road Fund upungue. Hata kwa mgao huu kwa halmashauri bado ufanisi wa barabara si wa viwango na si mzuri kutokana na upungufu katika kufanya maamuzi au kutokuwepo mafundi, wahandisi na zana zenye kukidhi viwango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Muleba, Kanyambozo na Rubuja. Kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Muleba kupitia Bunge lako nitoe shukrani kwa Mheshimiwa Rais na Wizara husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa kutoa pole kwa wahanga wa tetemeko Mkoani Kagera Mheshimiwa Rais Dkt.. John Pombe Magufuli, alisikia ombi la wananchi na kuagiza kuanza ujenzi wa barabara ya Muleba Kanyamaboga – Rubya Hospital. Ni maoni yetu kuwa kiasi cha fedha kilichopangwa kwenye Bajeti ya 2017/2018 zitatolewa kwa wakati na mradi utatekelezwa. Aidha, ni mombi yetu kuwa usimamizi makini ufanyike ili tupate ufanisi wa hali ya juu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Hoja ya Dharura kuhusu Mikopo ya Elimu ya Juu Nchini
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia hoja ya Mheshimiwa Ezra Chiwelesa, kuhusu hili suala la malipo wanayolipa wanafunzi wanapokuwa katika vyuo vikuu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Ezra na naomba niichambue kiuchumi na kisiasa. Dira ya Taifa 2025 ina malengo Matano. Mojawapo ya malengo ni kujenga jamii ya watu walioelimika na wenye uchu wa kujifunza. Kwa hiyo, mtu akikuuliza kwamba 2025 tutafika, kwa speed hii tutakwama, lakini kwa sababu tumeona, naona Mheshimiwa Ezra ametusaidia tunakwenda kukwamua ili tuweze kujenga jamii ya watu walioelimika na wenye uchu wa kujifunza.

Mheshimiwa Spika, kiuchumi kwa haraka haraka nimeangalia kipato cha Mtanzania, income per capita, najua kinachomsumbua Mheshimiwa Ezra, mkoa wake ndiyo ambao una pato dogo. Kwa hiyo, wakuu wa vyuo mkoa wa Mheshimiwa Ezra ukumbukwe sana, ndio una pato dogo. Ila per capital income ya Watanzania ni Dola 1,040. Sasa Dola 1,040 angalia mwanafunzi anayekwenda kusoma shule ya milioni tano kwa mwaka, ataweza vipi na mzazi huyo ana watoto nne mpaka watano?

Mheshimiwa Spika, lengo la Taifa ni kuelimisha watu bila kubagua, lakini kuna fani zinazopendelewa. Ninachoshauri, hapa kuna suala la haraka la kuokoa hii hali na suala linalohitaji mchakato wa miezi mitatu, minne, mpaka sita tufanye maamuzi. Suala la haraka kama walivyodokeza wenzangu, kama mjomba Chumi alivyosema, tutafute namna ya haraka, hawa wenye sifa tuwabebe wote kama walivyo waende wasome, waendelee na shule. Wanapoendelea sisi huku tuweze kwenda kutafuta mpango wa muda mrefu, nami mpango wa muda mrefu kwangu ni miezi sita.

Mheshimiwa Spika, kisiasa nimekwazika, kama mfumo huu tukiendelea nao ambao tuliutengeneza kwa nia njema, lakini umekwama; nami sioni tatizo, unatengeneza formation, inakwama unabadilisha, unatengeneza formation nyingine, unatoka na magoli. Mfumo huu kwenye Chama cha Mapinduzi umekwama, tunakwenda kujenga matabaka wana-CCM wenzangu. Huu mfumo unakwenda kutupeleka kwenye matabaka, hawa wapate hawa wasipate.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kanyasu amebahatika mwanaye yuko chuo kikuu wakamwambia, kuna mzazi hana mtoto chuo kikuu, atasemewa na nani? Kwa hiyo, nawasihi, tuweze kutafuta wepesi wa haraka kuwakomboa wote hao wenye sifa waende chuoni, halafu turudi tuje tutengeneze mipango ya muda mrefu. Mojawapo ya sababu za kufanya, naweza nisishiriki kwenye mchakato huo, hizo fani mnazotaka kupeleka watoto za Shilingi milioni tano, hebu fikiria vyuo vya namna hiyo mvipe ruzuku. Yaani course inapewa ruzuku kabla ya mtoto, kwamba ukienda kusoma udaktari wewe, ni shilingi milioni moja au ni laki saba, kusudi watu waende kule. Ukienda kwenye u-pilot ni shilingi laki tatu, kusudi wale watoto wanaomudu waende kule.

Mheshimiwa Spika, langu ni kuunga mkono hoja kwa sababu wanaolia ni wengi, Mheshimiwa Chiwelesa alilolisema ametusemea wote, amewasemea Watanzania wote.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana na nichukue fursa hii kuunga mkono Bajeti Kuu ya Serikali, lakini kabla ya hapo nichukue fursa hii kwako wewe Mheshimiwa Spika na Bunge lako Tukufu kuwakaribisha kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoanza tarehe 28 Juni, 2017 na yatakwenda mpaka mwezi wa saba tarehe 8 Julai, yakishirikisha nchi za Kimataifa kama 30 na makampuni 2,500. Tutaonesha bidhaa ya Tanzania, bidhaa kama nilizovaa, siwezi kutembea, ninacho kiatu kutoka Karanga Prison na hizi nguo kutoka 21st Century Morogoro na mshonaji ana kiwanda kidogo; kwa hiyo, nitumie fursa hii kuwakaribisha Sabasaba, mje muone bidhaa ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, yaliyozungumzwa kwenye Bajeti ya Serikali Kuu. Bajeti hii ni ya ujenzi wa uchumi wa viwanda. Bajeti hii kwa ujumla wake ni ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, si ya ujenzi wa viwanda tu, ni ya ujenzi wa uchumi wa viwanda. Nichukue fursa hii kuwatoa wasiwasi watu waliokuwa na mashaka kwamba hatutajenga viwanda kwa sababu mwaka uliopita Mheshimiwa Mwijage alitengewa shilingi bilioni 40 akapewa saba, lakini viwanda havitajengwa; la hasha angalia upande wa pili nilipopewa shilingi bilioni 40 zikaja shilingi bilioni saba nimetengeneza viwanda vya shilingi trilioni 5.2, kwa hiyo hayo mambo hayahusiani.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo katika kipindi hicho tumetengeneza miundombinu wezeshi na ile miundombinu saidizi itakayopunguza transaction cost na production cost, ndipo uchumi utakavyoweza kuchangamka.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la viwanda kuna watu wana mashaka kwamba hatujui changamoto za viwanda, si kweli tutendeane haki, kama kuna watu wanajua Serikali hii inajua changamoto zote. Tunajua mimi na Wizara yangu tunakutana na wawekezaji kila siku, pia viko vikao vya ubia kati ya mimi na Waziri wa Fedha tunakutana tukiwa wenza kuzungumza na wawekezaji wote, tunajua changamoto zao. Hata hivyo wawekezaji wanaweza kuwa na matakwa yao Serikali haiwezi kuyatimiza kwa wakati mmoja. Bajeti hii naipongeza imejibu hoja za Wabunge na wananchi wote.

Mheshimiwa Spika, nilipokuwa nawasilisha hapa nilikuja na vitabu vingi, nikawaonesha kitabu kimoja cha mawasiliano yangu mimi na Mheshimiwa Waziri wa Fedha na yote yaliyosemwa ambayo yametokana na Dawati la Wepesi wa Kufanya Biashara ambalo nalisimamia mimi mengi mengi yametekelezwa.

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kuwaomba wananchi wote wakiwemo Wabunge na wafanyabiasha, tunaanza upya, leteni mawazo yenu kwa kile ambacho mnadhani akikutekelezwa au kile ambacho kimeibuka. Kwa sababu biashara ni dynamic siyo static upepo unabadilika. Kwa hiyo, leteni mawazo yenu nitayapeleka kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Tumekubaliana na Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mawaziri wengine tutawaalika, tutakutana mara nne kwa mwaka ili kuhakikisha kwamba tunaweza kwenda kwa pamoja.

Mheshimiwa Spika, kuhusu vivutio vikubwa vya uwekezaji ni mazingira bora ya kufanya biashara, the easy of doing business. Naomba nieleze sasa hivi wakaguzi wa wepesi wa kufanya shughuli ndio wanapita kuangalia nchi gani ndiyo inafanya vizuri. Msipige kelele msizungumze kama kwamba nchi hii inawaka moto, hapana, sisi ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri ila tuna tamaa ya kufanya vizuri zaidi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu wepesi wa kufanya biashara timu ya Serikali kwa kushirikiana na private sector imefanya kazi nzuri na ripoti hiyo ndiyo inafanyiwa kazi, yale yote mliyoyasema yataondolewa. Mheshimiwa Tizeba amesema kuna tozo zimeondolewa lakini tunataka ziondoke zaidi. Tutakwenda hatua kwa hatua Idara za Serikali, Wizara zote na wote wawe tayari kuondoa kile ambacho kila Mtanzania ataona kwamba kinamkwamisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lipo suala la bidhaa bandia na bidhaa zisizokidhi viwango. Nilizungumza kwenye bajeti yangu kwamba ndiyo kazi ninayokwenda kuifanya, hii kazi si rahisi, inahusu change of mind na kwamba wale wanaokwenda kukamata na wao lazima uwabadilishe. Hata hivyo niwaambie hakuna jiwe litakalobaki bila kugeuzwa. Kama Jemadari Mkuu anapambana na makinikia mimi nitashindwa je kupambana na panya hawa? Nitapambana nao, bidhaa bandia Tanzania hazitaiingia.

Mheshimiwa Spika, tuna tatizo la vifaa vya vitenzi vinakuja bandia, waende majenerali wapambane kule juu na mimi nitapiga hawa panya.

Mheshimiwa Spika, juu ya aina ya viwanda kwamba sisi hatujui aina ya viwanda hakuna, Mheshimiwa Rais amesema jengeni viwanda ambavyo vinachakata maliasili au mazao ya wananchi, ndivyo tunavyojenga. Kesho kutwa nakwenda Kibaha, Mkuu wa nchi anakwenda kuzindua kiwanda cha kuchakata matunda. Limeni matunda kuna viwanda vimetengenezwa vya kuweza kuchakata matunda yote.

Mheshimiwa Spika, lakini msiende mbali sana, hapa Dodoma kuna Kiwanda cha Asante kinaweza kuchakata matunda yote yanayoweza kulimwa Ukanda wote wa Kati, kwa hiyo tunajua, lakini tumeelekeza tuwekeze nguvu katika viwanda ambavyo vinaajiri watu wengi. Ila niwaeleze kiwanda cha vifaa vya ujenzi kama vigae kinachukua muda mfupi kujengwa kuliko kiwanda kinachoajiri watu wengi. Mpaka sasa nina viwanda ambavyo vikianza kazi Morogoro na Kigoma tutaweza kuzalisha sukari zaidi ya mahitaji ya nchi hii, lakini viwanda vya namna hiyo vinachukua muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mchengerwa nikuambie umesema, umelalamika nimekusikia, Mheshimiwa Waziri Mkuu amekusikia, Waziri wa Ardhi amekusikia waliochukua ardhi Rufiji lazima niende nilale nao mbele kama nikishindwa nitapimwa kwa hilo. Ardhi ya Rufiji inaweza kuzalisha sukari, Mbunge anasema njoo Waziri anasema njoo, nani anapinga? Nakwenda kufanyakazi juu ya Rufiji na Mchengerwa usiache kupinga kelele piga kelele na mimi nakusikia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu Bandari ya Bagamoyo. Tume ya Serikali imeshapokea ripoti ya mwekezaji kuhusu Bagamoyo, Bagamoyo mwekezaji yuko tayari kumaliza kila kitu. Ni juu yetu sisi Serikali kukubaliana naye ili tuweze kumruhusu aendelee.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru karibu Sabasaba, karibu uone bidhaa ya Tanzania. Kwa mara ya tatu tena naomba kuunga mkono hoja bajeti ya Mheshimiwa Mpango na Mama Kachwamba, twende mbele.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana na nichukue fursa hii kuunga mkono Bajeti Kuu ya Serikali, lakini kabla ya hapo nichukue fursa hii kwako wewe Mheshimiwa Spika na Bunge lako Tukufu kuwakaribisha kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoanza tarehe 28 Juni, 2017 na yatakwenda mpaka mwezi wa saba tarehe 8 Julai, yakishirikisha nchi za Kimataifa kama 30 na makampuni 2,500. Tutaonesha bidhaa ya Tanzania, bidhaa kama nilizovaa, siwezi kutembea, ninacho kiatu kutoka Karanga Prison na hizi nguo kutoka 21st Century Morogoro na mshonaji ana kiwanda kidogo; kwa hiyo, nitumie fursa hii kuwakaribisha Sabasaba, mje muone bidhaa ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, yaliyozungumzwa kwenye Bajeti ya Serikali Kuu. Bajeti hii ni ya ujenzi wa uchumi wa viwanda. Bajeti hii kwa ujumla wake ni ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, si ya ujenzi wa viwanda tu, ni ya ujenzi wa uchumi wa viwanda. Nichukue fursa hii kuwatoa wasiwasi watu waliokuwa na mashaka kwamba hatutajenga viwanda kwa sababu mwaka uliopita Mheshimiwa Mwijage alitengewa shilingi bilioni 40 akapewa saba, lakini viwanda havitajengwa; la hasha angalia upande wa pili nilipopewa shilingi bilioni 40 zikaja shilingi bilioni saba nimetengeneza viwanda vya shilingi trilioni 5.2, kwa hiyo hayo mambo hayahusiani.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo katika kipindi hicho tumetengeneza miundombinu wezeshi na ile miundombinu saidizi itakayopunguza transaction cost na production cost, ndipo uchumi utakavyoweza kuchangamka.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la viwanda kuna watu wana mashaka kwamba hatujui changamoto za viwanda, si kweli tutendeane haki, kama kuna watu wanajua Serikali hii inajua changamoto zote. Tunajua mimi na Wizara yangu tunakutana na wawekezaji kila siku, pia viko vikao vya ubia kati ya mimi na Waziri wa Fedha tunakutana tukiwa wenza kuzungumza na wawekezaji wote, tunajua changamoto zao. Hata hivyo wawekezaji wanaweza kuwa na matakwa yao Serikali haiwezi kuyatimiza kwa wakati mmoja. Bajeti hii naipongeza imejibu hoja za Wabunge na wananchi wote.

Mheshimiwa Spika, nilipokuwa nawasilisha hapa nilikuja na vitabu vingi, nikawaonesha kitabu kimoja cha mawasiliano yangu mimi na Mheshimiwa Waziri wa Fedha na yote yaliyosemwa ambayo yametokana na Dawati la Wepesi wa Kufanya Biashara ambalo nalisimamia mimi mengi mengi yametekelezwa.

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kuwaomba wananchi wote wakiwemo Wabunge na wafanyabiasha, tunaanza upya, leteni mawazo yenu kwa kile ambacho mnadhani akikutekelezwa au kile ambacho kimeibuka. Kwa sababu biashara ni dynamic siyo static upepo unabadilika. Kwa hiyo, leteni mawazo yenu nitayapeleka kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Tumekubaliana na Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mawaziri wengine tutawaalika, tutakutana mara nne kwa mwaka ili kuhakikisha kwamba tunaweza kwenda kwa pamoja.

Mheshimiwa Spika, kuhusu vivutio vikubwa vya uwekezaji ni mazingira bora ya kufanya biashara, the easy of doing business. Naomba nieleze sasa hivi wakaguzi wa wepesi wa kufanya shughuli ndio wanapita kuangalia nchi gani ndiyo inafanya vizuri. Msipige kelele msizungumze kama kwamba nchi hii inawaka moto, hapana, sisi ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri ila tuna tamaa ya kufanya vizuri zaidi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu wepesi wa kufanya biashara timu ya Serikali kwa kushirikiana na private sector imefanya kazi nzuri na ripoti hiyo ndiyo inafanyiwa kazi, yale yote mliyoyasema yataondolewa. Mheshimiwa Tizeba amesema kuna tozo zimeondolewa lakini tunataka ziondoke zaidi. Tutakwenda hatua kwa hatua Idara za Serikali, Wizara zote na wote wawe tayari kuondoa kile ambacho kila Mtanzania ataona kwamba kinamkwamisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lipo suala la bidhaa bandia na bidhaa zisizokidhi viwango. Nilizungumza kwenye bajeti yangu kwamba ndiyo kazi ninayokwenda kuifanya, hii kazi si rahisi, inahusu change of mind na kwamba wale wanaokwenda kukamata na wao lazima uwabadilishe. Hata hivyo niwaambie hakuna jiwe litakalobaki bila kugeuzwa. Kama Jemadari Mkuu anapambana na makinikia mimi nitashindwa je kupambana na panya hawa? Nitapambana nao, bidhaa bandia Tanzania hazitaiingia.

Mheshimiwa Spika, tuna tatizo la vifaa vya vitenzi vinakuja bandia, waende majenerali wapambane kule juu na mimi nitapiga hawa panya.

Mheshimiwa Spika, juu ya aina ya viwanda kwamba sisi hatujui aina ya viwanda hakuna, Mheshimiwa Rais amesema jengeni viwanda ambavyo vinachakata maliasili au mazao ya wananchi, ndivyo tunavyojenga. Kesho kutwa nakwenda Kibaha, Mkuu wa nchi anakwenda kuzindua kiwanda cha kuchakata matunda. Limeni matunda kuna viwanda vimetengenezwa vya kuweza kuchakata matunda yote.

Mheshimiwa Spika, lakini msiende mbali sana, hapa Dodoma kuna Kiwanda cha Asante kinaweza kuchakata matunda yote yanayoweza kulimwa Ukanda wote wa Kati, kwa hiyo tunajua, lakini tumeelekeza tuwekeze nguvu katika viwanda ambavyo vinaajiri watu wengi. Ila niwaeleze kiwanda cha vifaa vya ujenzi kama vigae kinachukua muda mfupi kujengwa kuliko kiwanda kinachoajiri watu wengi. Mpaka sasa nina viwanda ambavyo vikianza kazi Morogoro na Kigoma tutaweza kuzalisha sukari zaidi ya mahitaji ya nchi hii, lakini viwanda vya namna hiyo vinachukua muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mchengerwa nikuambie umesema, umelalamika nimekusikia, Mheshimiwa Waziri Mkuu amekusikia, Waziri wa Ardhi amekusikia waliochukua ardhi Rufiji lazima niende nilale nao mbele kama nikishindwa nitapimwa kwa hilo. Ardhi ya Rufiji inaweza kuzalisha sukari, Mbunge anasema njoo Waziri anasema njoo, nani anapinga? Nakwenda kufanyakazi juu ya Rufiji na Mchengerwa usiache kupinga kelele piga kelele na mimi nakusikia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu Bandari ya Bagamoyo. Tume ya Serikali imeshapokea ripoti ya mwekezaji kuhusu Bagamoyo, Bagamoyo mwekezaji yuko tayari kumaliza kila kitu. Ni juu yetu sisi Serikali kukubaliana naye ili tuweze kumruhusu aendelee.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru karibu Sabasaba, karibu uone bidhaa ya Tanzania. Kwa mara ya tatu tena naomba kuunga mkono hoja bajeti ya Mheshimiwa Mpango na Mama Kachwamba, twende mbele.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru. Awali ya yote niwashukuru Wajumbe wa Kamati zote tatu wakiongozwa na Wenyeviti wao kwa taarifa zao nzuri hasa kwa maelekezo na ushauri tutauzingatia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaenda mbali nirekebishe kidogo tafsiri ambayo siyo. Mheshimiwa Mbunge nadhani alikuwa anasherehesha, aliyesema Serikali haijafanya lolote kwenye zao la korosho lakini mwisho akakiri kwamba labda kutafuta bei. Katika biashara ya uchumi kinacho-drive kila kitu ni bei. Panga bei nzuri watu watahangaika wenyewe. Kwa hiyo, nadhani alikuwa anasherehesha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nijibu kidogo hoja zilizozungumzwa lakini nimjibu na mchangiaji mmoja Mheshimiwa Mbunge aliyetafsiri taarifa za wepesi wa kufanya shughuli. Zile takwimu alizoziangalia aende akaangalie na distance to frontier. Distance to frontier inakueleza unapokuwa umepata maksi mbaya ujiangalie wewe ni wa ngapi katika yule aliyekutangulia. Ukiona upo above 50% hupaswi kulala bila usingizi, nakubali hatufanyi vizuri na pale ambapo hatufanyi vizuri tumejitathmini na tumeandika andiko ‘The Blue Print’ maeneo yote yenye matatizo tutayakosoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna mtu ambaye anaweza kukaribisha wageni halafu wageni hao unashindwa kuwawekea kiti au namna ya kuwakirimu. Namna ya kuwakirimu wawekezaji ni kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanya biashara. Mimi binafsi nakiri kwamba ninapopataka siyo hapa, nitaendelea kuhimiza kwa kushirikiana na wenzangu tuweze kwenda kwenye nafasi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la viwanda vilivyobinafsishwa. Siyo mapenzi ya Waziri mwenye dhamana wala mtu yeyote ni Ilani ya Chama inasema viwanda vilivyopo sasa vifanye mpaka ukomo (maximum capacity), viwanda vilivyobinafsishwa vyote vifanye kazi na tuhamasishe viwanda vingine vije. Kwa hiyo, orodha ya viwanda vilivyobinafsishwa kama alivyozungumza Comrade Lusinde nitaileta hapa Bungeni mje muione, kazi inafanyika lakini ngoja niwaambie, viwanda vile lazima vifanye kazi, kama huwezi kufanya kazi mpe mwenzako na tutakapofika wakati wa factoring unaweza kushtakiwa kwa uhujumu uchumi na dhamana yake mnaifahamu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ulinzi wa viwanda. Tunalo jukumu la kulinda viwanda na viwanda tunavilinda kwa ngeli mbili, moja ni kuangalia mpangilio wa kodi katika maeneo ya kikanda tulipo. Bado hilo zoezi linaendelea hatujafanya vizuri na Kenya wanajua kututegea kwenye suala hilo na tunalijadili Serikalini tutahakikisha kwamba hatupangi bei ambazo majirani zetu wana-take advantage, hilo tutalishughulikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ambalo tunakiri upungufu katika shughuli hiyo ni tatizo la under valuation na under declaration na smuggled items. Tunalijua na tutalishughulikia na tutalifanya kazi. Kama alivyosema Comrade Lusinde watu wanaouza hivi vinywaji katika chupa za plastiki kumbe tatizo siyo chupa za plastiki, tatizo ni kuuza katika chupa za plastiki chini ya ujazo uliokubalika. Tatizo la pili ni kuuza bila kuweka ile stampu ya TRA. Kwa hiyo, wale ni

majambazi kama majambazi wengine, naomba mkiwaona mniambia mimi au mwende Polisi mtafute RB. Ulinzi wa viwanda ni jukumu la sisi wote sio jukumu la Serikali peke yake au Waziri mwenye dhamana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kidogo mkakati wa kuendeleza viwanda. Mkakati wa kuendeleza viwanda upo ni Integrated Industrial Development Strategy lakini tumezungumza ni viwanda gani tunavitaka, tunataka viwanda vile ambavyo vinaajiri watu wengi, tunataka viwanda vile ambavyo vinachakata malighafi za wananchi, tunataka viwanda vile ambavyo bidhaa zake zinatumika kwa wingi na imekuja kwa maelekezo ya Mheshimiwa Rais tutengeneze viwanda vitakavyochakata mali za asili ambazo tulipewa kipekee na Mwenyezi Mungu. Ndiyo maana ukuta unajengwa pale kuzunguka Tanzanite. Hivyo ndivyo viwanda tunavyoshughulikia, tumefanya vizuri katika hilo. Jukumu la Serikali ukisoma Mpango wa Pili wa Miaka Mitano ni kuhamasisha sekta binafsi iweze kuwekeza, tunajitahidi, tunafanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mtu asije akadhani kwamba sisi hatujafanya kazi na mambo yote haya yanajulikana tatizo ni mapenzi ya kufika finally wakati ndiyo mchezo unaanza. Tunajenga viwanda na tunategemea come 2025 itakuwa nchi ya uchumi wa kati tukiwa na viwanda, leo ndiyo mwaka wa pili na niliambie Bunge lako kwamba kwa kipindi cha miaka miwili viwanda 3,306 vinafanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania tuna installed capacity ya saruji 10.9 millions tans wakati matumizi yetu ni
4.8 millions tans. Tanzania tunazalisha vigae Kiwanda cha Mkuranga square 80,000, Kiwanda cha Chalinze kinazalisha 50,000, ukienda Rwanda ukipeleka kigae cha China hawanunui wanataka vya Tanzania. Kwa hiyo, msidhani kwamba tuna hali mbaya, tunataka kuwa mbele lakini hapa tulipo hatupaswi kujinyonga kwa sababu hatufanyi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kasi ya utendaji wa miradi ya Serikali. Imetolewa hoja kwamba miradi ya Serikali inakwama, ndiyo, tumelizungumza hapa suala la PPP, tumezungumza hapa suala la hizi sheria kuna upungufu na hayo yote hayo tumeyaona na tunayafanyia kazi. Kwa sababu tukienda bila kuyarekebisha haya na kuyaleta mbele ya Bunge tutakuja kuulizwa tulifanya nini. Tunayafahamu haya, tutayarekebisha ikiwemo suala la Kurasini Logistics Centre na General Tyre.

Mheshimiwa Mwenyekiti, General Tyre tunajua tunataka kufanya nini, lakini sheria sasa inayokuwezesha namna ya kushirikiana na yule private sekta ndipo inapokuja ngoma. Taasisi zinazohusika, watendaji wa Serikali wanashughulikia suala hili ili tuwe na mwendelezo mzuri wa kuweza kufanya shughuli hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, muda siyo rafiki, nakushuru na naomba kuunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Nitachangia kwa kujaribu kujibu hoja za Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote napenda nimpongeze Mheshimiwa Waziri Mkuu, niwapongeze Waheshimiwa Mawaziri wenzangu walio katika Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na watendaji wote wa Wizara hii ambayo kimsingi ni Wizara ya uratibu. Sisi ili tuweze kufanya kazi zetu tunawategemea sana, ahsanteni kwa msaada mnaotupa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo mengi yaliyozungumzwa, niwashukuru Waheshimiwa Wabunge, yananijengea uwezo wa kuwaletea hotuba nzuri ambayo italenga kujibu matakwa yenu. Hata hivyo kuna mambo ambayo ningeomba niyajibu leo kusudi niweze kuchangia vizuri Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la msingi la kwanza ni suala la viwanda. Kuna kutoelewa au tuna kuelewa tofauti juu ya suala la viwanda. Ukisoma Mpango wa Pili wa Miaka Mitano tumeamua kujenga uchumi wa viwanda na dhima yetu ni ujenzi wa uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu ndiyo center.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunalenga ifikapo mwaka 2025 hii iwe nchi ya uchumi wa kati kwa kupitia uchumi wa viwanda. Sasa Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote ili tujenge uchumi wa viwanda kwa mtu ambaye alikuwa hajui viwanda lazima kulingana na matabaka yetu na uwezo wetu twende kwenye makundi manne ya viwanda. Mimi kiwanda ninachokiita kidogo mwenzangu atakiita kikubwa ndiyo maana tunahimiza falsafa ya viwanda vidogo sana, viwanda vidogo, viwanda vya kati na viwanda vikubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwatie shime Watanzania na tuwaangalie waliotutangulia. Nchi ya India ambayo yenyewe ina population ya bilioni 1.256 lakini ina income per capita ya dola 1,800 unaweza kuzidisha ukapata GDP yake. Asilimia 38 yake inatokana na viwanda vidogo. Bidhaa unazozikuta madukani India asilimia 40 inatokana na viwanda vidogo, lakini mauzo ya India nje asilimia 45 inatokana na viwanda vidogo. Sasa ukisoma andiko la Mchungaji Profesa Adam Persia anakueleza kwa nini viwanda vidogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda vidogo hasa kwetu Watanzania ni shule, kama hujawahi kumiliki kiwanda, usianze na kiwanda cha bilioni mia tano, anza na kiwanda kidogo. Kiwanda kidogo kinakufaa wewe muanzishaji, lakini ni shule una-train family, ndiyo maana; napenda niliseme hili; ndiyo maana unakuta family za wenzetu kama Madhvani mimi nimezaliwa nasikia Madhvani mikaa 65 iliyopita Madhvani alikuwepo Uganda, lakini Madhvani mpaka leo yupo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana mkagundua sisi Wabunge, Watanzania wote kwa nini tunasoma na watoto wa Wahindi mashuleni lakini hatuombi kazi pamoja na wao? Ni kwa sababu wanakuwa trained kwenye family business na wanaweza kuendelea miaka mingi na mingi. Kwa hiyo nawasihi muwe mashuhuda, campaigner, mhimize Watanzania wakubali suala hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninapozungumza suala hilo tunakwenda kwenye jibu la viwanda, tuna viwanda vingapi? Nina rafiki yangu mmoja Mbunge wa Monduli anasema viko wapi? Hivyo viwanda 3,306 vipo na viko Tanzania. Nimekwenda kutafuta takwimu za viwanda vile, viwanda tulivyonavyo Tanzania ni zaidi ya viwanda 53,000, vimechapwa kwenye karatasi za A4 karatasi 900. Kwa hiyo vipo, vipo Tanzania na ukiviangalia kila kijiji kina kiwanda kimeorodheshwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivyo viwanda vinafanya kazi gani? Tumeelekezwa kwamba tuanzishe viwanda ambavyo vitachakata mazao ya shamba, mazao tunayoyalima sisi. Faida ya viwanda hivi hata kama ni vidogo vinaongeza life span ya product na vinapunguza post-harvest loss, ndiyo maana ya kuhimiza hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwape mfano mmoja tulionao sasa hivi wa watu wa Dodoma. Dodoma wana zabibu, sasa hivi zabibu inapata tatizo la soko kwa sababu ya mambo fulani ambayo tunayarekebisha, lakini mtu mwenye kiwanda kidogo cha shilingi 500,000 au 600,000 unaweza kuchukua zabibu ukasaga, unapata mchuzi unauweka kwenye gudulia ambapo unasubiri wakati soko likipatikana unaweza kuuza. Mheshimiwa rafiki yangu ambaye ni mkulima wa zabibu anaelewa kitu hicho. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nawasihi toka hapa kabla ya andiko langu halijaja muweze kuhubiri viwanda vidogo. Niwaahidi, nimeandika kitabu kuhusu viwanda vidogo nitakitoa kabla ya bajeti yangu, lakini na bajeti inayokuja ni kitabu cha rejea. Kama hujui viwanda ukisoma bajeti yangu nitakayoiandika utaweza kuelewa suala la viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie mazingira ya biashara. Wengi wamezungumzia mazingira ya biashara. Mimi narudia kauli ya viongozi wangu; Mheshimiwa Rais amelizungumzia, Mheshimiwa Makamu wa Rais amelizungumzia, Mheshimiwa Waziri Mkuu amelizungumzia suala la mazingira ya biashara. Zaidi tumeandika andiko (regulatory reform) ambayo inaitwa almaarufu blue print; tunataka hivi vikwazo viondoke. Hata hivyo ukisoma maandiko hii kazi haikuanza leo. Mpango wa kwanza wa miaka mitano ilikuwa kuondoa vikazo, haikumalizika, tumekwenda nayo na hivi vikwazo vitaondoka na nyingine tusilaumiane ni mind-set. Kuna mtu ukiingia ofisini amezoea kuwanunia watu sasa hilo sio tatizo la Waziri wake au Katibu Mkuu wake ndivyo alivyo na tutawabadilisha hao watu waweze kufanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika suala la viwanda limezungumziwa suala la matrekta ya URSUS au matrekta yaliyoko TAMCO almaarufu kama alivyokuwa akiyaita ndugu yangu Dkt. Mwigulu Nchemba kwamba ni matrekta ambayo yana lengo la kuondoa jembe shambani kulibakiza kwenye ile bendera ya chama anachokipenda na makaburini kusawazisha makaburi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge kwa nini matrekta ya URSUS hayajauzwa, yana maelekezo maalum, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameelekeza yale matrekta yaende kijijini sasa huyo mtu wa kijijini unampaje? Tunatengeneza utaratibu tukishirikiana na Hazina kwamba Wabunge mpewe, wafanyakazi mpewe na ma-DC wapewe yaende vijijini si matrektra ya kuvuta mizigo. Watu walileta matrekta unayakuta airport, au unayakuta bandarini, haya yanakwenda vijijini. Tuna matrekta 2,400 kwa hiyo Waheshimiwa Wabunge, yakija myagombanie kama mpira wa kona myapeleke vijijini, halafu mtaona mwaka 2020 mambo yatakavyokuwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie miradi ya kimkakati. Miradi ya kimkakati inatekelezwa, mnaweza mkawa mnaona uchelewesho, wengine mnasema twende haraka, lakini sheria tuliyoitunga sisi Wabunge mwaka jana ya kuangalia maslahi ya Taifa imetufanya ile mikataba kwa mfano ya Mchuchuma na Liganga iangaliwe mara tatu au nne.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaeleze, mimi nilikuwepo; nilimsikia Rais wa Zambia na wengi mmeona clip za Zambia na kuna nchi nyingine wanalia, waliingia mikataba unakuta kila kitu kimechukuliwa. Naogopa na namkumbuka kaka yangu ambaye alikuwa Waziri hapa. Aliwahi kusema mtafanya maamuzi, maamuzi hayo hata kama mmekufa makaburi yenu yatafungwa minyororo ndivyo alivyosema Sebastian Rweikiza Kinyondo. Nisingependa mimi kaburi langu lifungwe mnyororo.

Kwa hiyo, hii miradi ya kimkakati tusingependa kufanya maamuzi, kwa hiyo tunaipitia na tunapoipitia tunazungumza na ninyi mje mtuhoji mtuelekeze.

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii kuwapongeza Wabunge ambao wametupa information where we are getting wrong, lakini kama nilivyowaahidi nitazungumza nanyi zaidi katika bajeti yangu ambayo nimeahidi kitakuwa kitabu cha rejea. Ahsanteni sana naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru. Awali ya yote ningependa kuwapongeza Wenyeviti waliowasilisha taarifa za Kamati zao, ni Kamati nzuri, ni kioo, kinatuonesha tunafanya nini. Langu ningependa kuanza kuchangia Kamati ya Bajeti, mimi ni Mjumbe wa PIC, nampongeza Comrade Simbachawene na niende taratibu kwa sababu sijawa mzoefu. Nimpeleke ukurasa wa 22 alipozungumzia michezo ya kubahatisha, kwamba mapato ya Serikali kwenye michezo ya kubahatisha



yameongezeka, lakini michezo ya kubahatisha imeleta uzezeta, imeleta uzembe, watu hawafanyi kazi. Sasa hili la kupata mapato kwenye kuangamiza jamii ningependa tuliangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Bajeti nimpeleke ukurasa wa 23 alipozungumzia mafuta ya kula na zile takwimu nzuri za upunguaji wa asilima 90 wakapendekeza zaidi kwamba tubaini endapo uzalishaji wa ndani umeongezeka, ningependa aende zaidi aangalie mchango wa crude palm oil, mchango wa mafuta ya kupikia katika re- export na aangalie mchango wa re-export commodity katika uchumi wa Taifa, aangalie viwanda vimeendeleaje baada ya maamuzi haya, lakini aende zaidi aangalie mafuta haya yalikuwa yanachangiaje kwenye maamuzi ya nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Kamati ya Bajeti nimpongeze kwa pendekezo lao la ukurasa wa 25 alipoitaka Serikali kwamba iwashirikishe kabla haijaenda kwenye CET - Common External Tariff, lakini ningependa aongeze hapo kwamba Serikali inapokwenda kwenye CET wakati inalenga East Africa Community ijue kwamba ina mshirika mwingine anaitwa SADC. Sisi tuko East African Community lakini tuwe waangalifu tusiwekewe magoli na wenzetu wa East Africa katika mchezo ambao sisi tunafaidi kutoka kwenye SADC. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 26 Kamati ya Bajeti imezungumzia suala la udhoofu katika kukusanya mapato ya majengo, kwamba pato katika upande wa majengo ni dhoofu, ningependa kumwuliza au waiulize Serikali kwamba lile pendekezo, ule ushauri Mheshimiwa Rais kwamba watoze kiwango kidogo ili nchi, nyumba zote ziweze kulipa limefikia wapi?



Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye Kamati yangu, Msajili wa Hazina au Taasisi, Kamati yetu inasimamia mashirika 270. Mashirika haya 270 yana fursa kubwa kwenye uchumi wa Taifa, lakini linaloonekana wazi na kama tulivyoeleza kuna under capitalization; mashirika haya hayapewi pesa ya kutosha, lakini yakipewa pesa ya kutosha yatazalisha pato kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kushauri kama tulivyowashauri, huyu ni ng’ombe wa maziwa, tumpe nyasi, tukubali tumpe mashudu, kwetu wanasema atana gatalonda, poteza kusudi uje upate. Katika eneo hili la mashirika 270 kuna fursa kubwa ya ajira, lakini kuna upungufu wa weledi katika kufanya shughuli, si suala la vyeti suala la weledi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwapeleke kwenye ukurasa wa tisa wale wanaofuatilia kitabu cha PIC, ukiangalia makampuni yaliyolipa gawio makampuni 11, kuna kampuni inalipa bilioni tisa, naomba nishauri kwamba hawa ndiyo ng’ombe wa maziwa, kampuni kama NMB, lazima itengenezewe mazingira na ituoneshe namna gani italipa zaidi, kampuni kama PUMA Energy lazima itengenezewe mazingira kusudi iweze kulipa zaidi, kuna kampuni kama Cigarette lazima itengenezewe mazingira na kampuni kama Tanzania Planting au TPC. Kwa hiyo, kampuni zinazofanya vizuri, lazima tuzifuatilie kusudi tuweze kupata zaidi katika mapato hayo. (Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, wale wanaofuatilia kitabu chetu niwapeleke ukurasa wa 28, nataka nilizungumzie alilozungumza Makamu Mwenyekiti wa Kamati yangu kuhusu mtazamo mpya wa SUMA JKT. SUMA JKT ni zaidi ya JKT tunayoijua, Taifa sasa linao upungufu wa watu wenye weledi, lakini iko fursa kubwa ndani ya JKT kukusanya vijana waliopewa mafunzo, wakapelekwa JKT wakapewa mafunzo mazuri na wakaweza kufanya vizuri. JKT Kigoma wana mradi wa mawese, wanaweza kupelekwa Kigoma, wakalima mawese na kuweza kuzalisha bidhaa za sabuni na zingine.



Nashauri na Kamati yetu imeshauri kwamba tuliangalie suala hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine, bandari yetu ya Dar es Salam, Bandari ya Dar es Salam nao ni mgodi na kimsingi sisi bandari ya Dar es Salam hatujaitumia kikamilifu. Kamati yetu iliona Bandari ya Dar es Salam ina matatizo makubwa makubwa matatu. Tatizo la kwanza ni la kisheria na kama mnavyojua Waheshimiwa Wabunge, tuliwahi kutunga Sheria, kwa mfano, ile Sheria ya VAT iliweza kuiathiri Bandari ya Dar es Salam. Pia sasa kuna ile Sheria ya axle weight ambapo mteja wetu namba mbili wa bandari, mteja wa bandari wa nje wa kwanza ni DRC Kongo, wa pili ni Zambia, lakini Zambia sasa inajiandaa kususia Bandari ya Dar es Salam kwa sababu ya Sheria ya axle weight. Kwa hiyo tunapotunga Sheria, kama nilivyosema mwanzoni tuiangalie SADC badala ya kuiangalia Afrika Mashariki tupu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni la TEHAMA, ukiangalia ule wepesi wa kufanya shughuli easily of doing business, eneo ambalo Tanzania tunafanya vibaya sana ni cross border business, cross border business inaanzia bandarini na tatizo mojawapo ni kwamba mifumo ya bandari ya kuhamisha bidhaa haisomani, TEHAMA hazisomani, yule anayetoa mzigo bandarini, anayelipisha anayetunza mzigo, hawasomani. Kwa hiyo ninachotaka kuzungumza ni kwamba tu-improve upande huo kusudi bandari yetu tuweze kuifanyia vizuri.


Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuwekeza kwenye magati, suala lingine ni kuwekeza rasilimali watu, watu wenye weledi na watu wenye motisha. Tukiweza kuwekeza kwenye weledi wa watu wetu tutaweza kuiwezesha bandari yetu. Bandari ya Dar es Salam, ile geographical location advantage inaondoka; Beila, mtu ambaye alikuwa na disadvantage anatumomonyoa taratibu, lakini watu wengine wana-opt kwenda Durban, lakini fursa za nchi tulizonazo, ukiangalia Tanzania inayokuja hali ni nzuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo machache, naomba kuunga mkono hoja yangu ya PIC. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia taarifa za Kamati hizi tatu na nianze kwa kuwapongeza Wajumbe wa Kamati zote tatu na Wenyeviti wao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda kuanza na suala la UKIMWI. Suala hili siyo siri. UKIMWI ulipoingia nchini kwetu miaka ya 80 ungeweza kumgundua mgonjwa wa UKIMWI kwa kumuangalia kwenye macho hivi kwamba huyu tayari, walikuwa wanasema kupandisha kenchi, unamwona mtu mabega yamepanda juu lakini kutokana na kuwepo kwa dawa za kufubaza leo ni vigumu kuweza kumgundua mgonjwa kwa macho. Mtu unamuona anakwenda anadunda kawaida amejaza vizuri lakini kumbe anaumwa, ni kwa sababu ya vile vidonge anavyokula. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, linalonituma kuzungumza suala hili ni utaratibu wa Taifa letu kutegemea wahisani katika kusaidia wagonjwa kwa asilimia 95. Hoja yangu hapa ni kwamba sasa inabidi tujiangalie. Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati, idadi ya watu hawa ni wengi na hawakutaka wenyewe, inabidi Taifa tujifikirie tutafute vyanzo. Wakati mwenzako anapokubeba Waswahili wanasema muangalie kisogo au ujikaze mwenyewe. Kuna hatari hawa watu wakaja kutukwamisha kwa kutukamatia kwenye ugonjwa huu. Napendekeza na Wabunge iwapendeze tuanze ku- allocate pesa nyingi zaidi kwenye tatizo hili ambalo tunalo. Ninalo hilo dogo, imebidi nilichangie. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitachangia kidogo kwenye michezo. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii ambaye amemaliza kuchangia, Mheshimiwa Nkamia, alikuwa anataka kujifanya eti ni wakala ananitafutia mimi timu za kwenda kukimbia, hapana. Hizi mbio za juzi nilikuwa na-test mitambo, mimi siyo mwanariadha. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, lakini jambo ambalo nataka kuungana naye ni kwenye dhana ya utawala bora, naazima msemo wa Rais wa Uganda, Mheshimiwa Kaguta Museveni, walipomuliza kwa nini Museveni uko madarakani, akasema ni vitu viwili; prosperity na security. Kwa hiyo, kwa nini mtu anaweza akawa anatamani kukaa miaka saba, labda anataka kujenga shule kila kijiji. Ikikupendeza mkwe wangu, Mheshimiwa Nkamia, kama una malengo mahsusi kama huyu Rais wa Uganda ambaye anatafuta prosperity na security kwenye nchi yake, basi na iwe hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nianzime maneno ya Mheshimiwa Serukamba, juzi Mheshimiwa Museveni alikuwa anapokea kiwanda kinachozalisha lita 100,000 za maziwa akawa anamkabidhi mkwewe, akasema mimi tangia mwaka 1966 nachukia umaskini akawa anaonesha hiyo. Kwa taarifa Uganda inachakata maziwa lita milioni mbili kwa siku wakati sisi tunachakata lita 150,000 lakini nilipokuwa kule waliniambia tuna fursa ya kuchakata lita milioni 4. Nimeshazungumza na Waziri anayehusika na sisi tunakwenda huko, msiwe na wasiwasi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumze suala la elimu. Tumefungua neema ya elimu ambayo imekuja na changamoto. Mimi kwetu huko kwa kipindi cha miaka mitatu nimeanzisha shule mpya za msingi tano, nimshukuru Waziri wa Elimu alinisaidia kuzi-fast track na kusajiliwa. Changamoto niliyoiona, jengo la vyumba vinne walijitokeza watoto 300 kuanza shule.

Mheshimiwa Spika, nachotaka kuliambia Bunge na Serikali ni kwamba tunapaswa tujiandae, Mwenyezi Mungu ametujalia kupata uzao sasa hao watoto wetu wasiwe bora wingi wa watu ila watu walioandaliwa vizuri. Zitafutwe rasilimali, watafutwe walimu ili waende kufundisha huko. Mimi nakwenda zaidi kwamba ikishindikana kuwaweka kwenye majengo bora hata tutengeneze maturubali ili mradi tuwe na walimu wawafundishe wale watoto kwa sababu mtoto aliyefika umri wa kwenda shule hawezi kusubiri.

Mheshimiwa Spika, Muadhama Cardinal Laurean Rugambwa alikoanzia darasa la kwanza kule kwetu Busita alikuwa kwenye nyumba ya nyasi, it was a shelter ya nyasi, lakini akasoma kwenye jengo lile na akaishia kuwa Kadinali wa kwanza Muafrika. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri wa Elimu wale Wadhibiti Ubora wadhibiti lakini wakikuta watoto wanasoma chini ya miti waruhusu wasome hata kwenye nyumba ya nyasi mpaka siku hiyo tutakapoweza kuwapatia jengo wanalohitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine kwenye elimu, naomba Waheshimiwa Wabunge wenzangu tukubaliane, mtoto ni wa kila mtu, kama ambavyo Mama Kikwete huwa anasema kwamba mtoto wa mwenzio ni mwanao. Sasa huyu mzee aliyekuja na elimu bure tusichukue watoto wetu tukamuachia, yeye alikuja na dhana nzuri kwamba elimu bure sasa tusimrushie mzigo, jukumu liwe la kwetu sisi.

Mheshimiwa Spika, unakwenda kwenye maeneo mengine watu wanajenga shule, unakuta mzazi ambaye mwanaye amekosa chumba cha darasa, hakuna mbao anataka kukuuzia mbao. Sasa sisi Wabunge tuisaidie Serikali, tupige propaganda, tuwahimize mtu awe tayari kutoa, aone kutoa mawe ni fahari, kushirikia kujenga ni fahari kwa sababu Mwenyezi Mungu ametusaidia ametupatia huu uzao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nichangie kidogo suala la afya. Nimesikia Mheshimiwa Kapteni Mkuchika juu ya wataalam, nazijua taarifa nzuri za TAMISEMI wanapojenga majengo. Tunapofanya rationing ya majengo tuangalie ni wapi tunasubiria kupeleka wataalam na wapi tunasubiria kupeleka kituo kipya.

Mheshimiwa Spika, nikukaribishe siku moja uende kwetu Goziba, mimi nikiwa nchi kavu kwetu kwenda Ziwani Goziba nakwenda saa nane, sasa mtu anapokuwa Dodoma anafanya uamuzi wa wapi apelike wataalam, kituo changu ambacho drifting kwenye maji ni saa nane unasema tunasubiri, unakuwa hufikirii kwa kuwaangalia wale wenye tatizo. Ninayo zahanati kwetu Rutoro, ni kilometa 70 kutoka kwetu nilipozaliwa, wale watu wanakwenda kilometa 72 kwenda kwenye Jimbo la Mheshimiwa Rweikiza, unapokaa Dodoma, TAMISEMI, Utumishi wa Umma unasubiri kuja ku-allocate ina maana tunakuwa hatuangalii uhalisia. (Makofi)

Niombe TAMISEMI, Wizara ya Afya, mnapofikiria mnifikirie mimi, nahitaji wataalam Goziba kwa sababu watu wanakufa maji kila siku kule, hawawezi kupata huduma na kuna baradi kali. Keleba hakuna wataalam, tumeshajenga maboma, kwa miaka mitatu nimemaliza maboma tisa, Serikali na mimi mniunge mkono na wananchi wangu, tuna maboma tisa tayari yanahitaji kumaliziwa na yote yapo kwenye critical points ambazo haziwezi kufikiwa bila kutembea kilometa ndefu. Nilitaka nizungumze hilo la afya.

Mheshimiwa Spika, nizungumze na watu wa Utumishi kwamba kuna jambo unaweza kusubiri. Unaweza kusubiri kwenda shule lakini huwezi kusubiri kwenda kupata tiba. Kama tuna upungufu wa wataalam kwa mujibu takwimu tujinyime tuweze kuwaajiri watu, mgonjwa hawezi kusubiri. Utakaa uwe mjinga usijue kusoma na kuandika, sawa, utasoma ukiwa mtu mzima miaka 20 ndiyo uko darasa la kwanza unasoma ‘a, e, i, o, u’, hata usipojua kusoma basi utaangalia wenzako wanakwenda lakini mtu anayeumwa hawezi kusubiri. Maana yangu ni nini? Naiomba Serikali yangu sikivu mjitahidi tupeleke watu wa afya kwa sababu wagonjwa hawawezi kusubiri lakini watu wenye nguvu ndiyo wanaweza kuchangia uchumi.

Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache, naomba kuunga mkono hoja zote. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia Wizara hizi muhimu katika maendeleo ya Watanzania. Awali ya yote, niwashukuru Waheshimiwa Mawaziri kwa wasilisho zuri, masilisho lenye vielelezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siwezi kuchukua muda mwingi kuzungumzia hilo kwa sababu natoka kijijini kama ni shule nimeziona. Wale waliosafiri kwenda kwetu, Kaitu Kaila kuna misemo inasema mtenda kazi ndiye huleta kazi, mtenda kazi aliyeamua watoto wote waende shule ndiyo aliyeleta kazi. Kwa hiyo, ukiona watoto wako wengi shule hawana madarasa ni kwa sababu mtenda kazi amesema wote waende shule na nina imani mtenda kazi atawafuata kule wale watoto atawapatia madarasa, vyoo na mambo yatakwenda mbele. Kama mtenda kazi asingesema muende shule wala msingewaona na hali ingekuwa siyo nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niishauri Serikali miundombinu ya shule inayotakiwa ni mingi, pamoja na jitihada zetu za kujenga miundombinu Serikali itoe vivutio kwa sekta binafsi iingie kwenye kuendesha shule. Vyumba 85,000 Serikali hatutavimaliza kesho sasa sekta binafsi ihamasishwe, ipewe vivutio vya kila namna kusudi na wao waingie kwa sababu vijana hawa hawatasubiri, waweze kwenda kwenye shule hizi walipe pesa kidogo kidogo. Hilo la elimu nimelimaliza na nishukuru kwa kazi zote ambazo mmefanya kwenye Jimbo langu la Muleba Kaskazini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la afya. Napokuja kwenye afya niwashukuru wananchi wangu wa Jimbo la Muleba Kaskazini lakini niwashukuru wadau wangu wa maendeleo, katika Jimbo langu tumetengeneza zahanati 12. Unajua mtoto anapoanza kufyeka shamba mzazi unamwekea msingi, naiomba Serikali katika maeneo yangu yenye maeneo hatarishi kama Kisiwa cha Bumbile ambako kuna shughuli za uvuvi na kuna mapato mengi tunaomba tuwekewe kituo cha afya. Kuna sehemu za low lands upande wa Magharibi mpakani na Karagwe, sehemu za Ngenge tungeweka kituo cha afya kuwasaidia watu wa eneo lile ambao wao wanatembea siyo chini ya kilometa 30, 40 kuweza kupata huduma ama kwenda Muleba au Bukoba Vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napomaliza hilo nizungumzie suala la TARURA, tofauti na wenzangu waliozungumza mimi sitawaliwi na asilimia. TARURA mnapojijenga upya mfanye tathmini ya uhalisia wa barabara zenu mlizo nazo na sisi Wabunge tupewe fursa ya kutengeneza Mfuko wa Barabara za Vijijini. TARURA amepata ngapi, TANROADS amepata ngapi haina tija, tija itokane na kutenga mfuko wa kuweza kutengeza barabara. Kimsingi hata mgao huu unaofanyika unakuta Wilaya moja anapewa pesa nyingi mwingine anapewa kidogo bila kuzingatia uhalisia wa barabara. Kwa hiyo, solution ni mfuko yaani shida ya jirani yako isikufanye wewe ufurahi, TANROADS apate pesa za kutosha na TARURA apate pesa za kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la mikopo wanayopewa vijana na akina mama na hili nizungumze nikihusisha na shughuli ya Wizara hii ya TAMISEMI kuhusu suala la viwanda. Nakumbuka katika kitabu kimoja nimewahi kusoma kinachozungumzia mwongozo wa ujenzi wa viwanda katika Tawala za Mikoa na Vijijini kinaeleza watu weledi na maeneo yako kule vijijini. Kwenye vitabu inaonyeshwa kwamba shilingi bilioni 62 zinatumika kuwapa watoto na akina mama, nashauri Serikali mngechukua shilingi bilioni 62 sehemu yake mkanunua matrekta, kwa sababu vijana wengi wako vijijini wapeni matrekta, muwape viwanda badala ya kuwapa shilingi laki mbili mbili, wanakwenda kugawana umaskini. Nichukue fursa nikushukuru Mheshimiwa Jafo namna unavyoendelea kuhamasisha viwanda. Mimi niliacha viwanda 3,540 nimesikia wewe una 4,000, unanitia moyo, endelea kuhamasisha viwanda. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la watumishi, nichukue fursa hii kuiomba Serikali kwenye sekta ya afya na elimu tuwatafutie watumishi, pelekeni watumishi kule. Mimi chumba cha darasa hakinipi shida, unaweza kutengeneza makuti ukaweka pale. Nimewahi kulisema na nalisema tena, Muadhama Laurean Cardinal Rugambwa yeye alianzisha…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa Duniani na kupewa Tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja iliyotolewa na Mheshimiwa Zainab Katimba kufuatia tuzo aliyoipata Mheshimiwa Rais kwenye kuimarisha au kujenga miundombinu.

Mheshimiwa Spika, nikushukuru na wewe kipekee kwa kutaja jina langu na baada ya kulitaja ukanitamka nikiwa wa mwisho, matokeo yake nitakachosema hapa ni meseji nilizotumiwa na Wanajimbo wa Wilaya ya Muleba kwa ujumla na nyingine nimekurushia wewe.

Mheshimiwa Spika, Muleba wanasemaje kwenye tuzo hii? Wanasema jema lolote, lililoshindikana katika nchi hii sasa kwa Mama litalekelezwa, hiyo ni Muleba, jema lolote katika nchi hii lililofikiriwa na likashindikana kutekelezwa kwa Mama litatekelezwa.

Mheshimiwa Spika, Muleba ni kubwa mno, wanasema Mheshimiwa Rais sio kwamba amejenga barabara, amejenga barabara kule ambako watu hawakufiria. Ukienda kule Muleba kule ambako watu hawakufikiria, alipopaona Mjerumani Muleba kuna barabara, amejenga barabara katika Kata ya Kamachumu na Luanga kupita Kyaraburamula ameshuka akaenda Chuo cha Elimu Katoke akajenga barabara mpaka ziwani Kamugaza. Wanasema Muleba, amejenga madaraja, barabara ya Kyamyolwa kwenda Kimeya, Kumuliza mpaka Kashebuko amejenga barabara. Kimbugo amejenga barabara, Mheshimiwa Rais amejenga barabara Kakindo mpaka Maziba, Mayondwe mpaka Bugasha, Muramura na Kyamyolwa. Mama anafungua barabara anakwenda kule ambako watu hawakufikiria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, amejenga barabara kwenda Ngenge zaidi, wameniambia mama, wanavyosema ni wagandagaza, wagandagaza maana yake nini ukimuona mtu analia, ukampangusa machozi, unaitwa uwagandagaza. Anajenga barabara kwenda Rutoro, kwenye Kisiwa cha Bumbile, mama anafanya mambo tofauti lakini yaleyale yaliyozoeleka. Wananchi wa Muleba na Kagera kwa ujumla wanampongeza na wanasema mama isifike mwezi Oktoba hujafika, haya matatizo madogo madogo ya ardhi yatakuwa yanakuja, uje tusherehekee, wamkumbuke Baba wa Taifa wakati anasema Mwenge.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi/Vigelegele)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia njia ya maandishi nichangie bajeti ya Wizara ya Afya. Awali ya yote nichukue fursa hi kuunga mkono hoja bajeti hii na niwapongeze viongozi na watendaji wote wa Wizara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii kuishauri Wizara iweze kupitia upya upangaji wa watendaji maalum katika wizara hii ili angalau kila mkoa upate hao wataalamu wa msingi. Mfano, mwezi wa tatu Mkoa wa Kagera kwa hospitali zote Umma na binafsi hakukuwepo Mganga kwa ajili ya magonjwa ya akina mama (gynocologist). Hoja hapa ni kuhakikisha kila mkoa unapata wataalamu hawa na hata wakati wa kutoa ajira muhimu, kutoa nafasi kwa utaratibu huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kupitia bajeti hii, nishauri juu ya upangaji na ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na hospitali. Ushauri wangu ni kuwa suala hili lisimamiwe na Wizara ya Afya ambayo katika busara ya kawaida watatumia weledi kupanga maeneo ya taasisi hizo. Nikirejea ujenzi, uboreshaji wa zahanati na vituo vya afya katika Jimbo langu, inasikitisha kuona kuwa maeneo ambayo yalipashwa kupewa nguvu baada ya wananchi kuonyesha juhudi kwa kujenga maboma hayajafikiriwa. Hii inaonyesha ukosefu wa utaalamu katika kubaini wapi paendelezwe, kwani maeneo mengine yanaachwa bila huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Wizara ipitie ujenzi wa zahanati 12 zilizojengwa na wananchi kwa kipindi cha miaka mitatu ili tupate somo juu ya haja ya kuendeleza zahanati na vituo vya afya kwa ulinganifu na kwa kuzingatia zaidi mahitaji, lakini zaidi Serikali itusaidie kwa kuendeleza angalau Zahanati za Rutoro, Bumbire na Crogllo kati ya zahanati hizo 12 kwa kuanzia.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine la kuangalia ni upangaji wa wataalamu wa sekta ya afya. Ili kuepuka tatizo la sasa ambapo sasa kila wizara inataka watendaji wanaohusika na sekta zao walioko katika Halmashauri za Wilaya wawajibike Wizarani. Wizara ya Afya na TAMISEMI wapitie upya usimamiaji wa watendaji hawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa hii ni Serikali moja, unaweza kuwepo utaratibu ambapo wataalamu wa Wizara ya Afya wanaweza kupata miongozo tokea Wizara ya Afya ikiwa ni pamoja na kupata stahili zao wakiwa Halmashauri za Wilaya. Uwepo wa zahanati wa vituo vya afya ambavyo havina wataalamu ni kutokana na upungufu tu wa msimamizi (DED) kutokuwa na uelewa wa mguso wa sekta.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na umakini wa Serikali katika kutoa vibali vya kuajiri, naomba na kushauri vibali vya kuajiri watendaji wa sekta hii ni muhimu vitolewe. Hii italeta umaana wa kujenga miundombinu ya zahanati, vituo vya afya na hospitali.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho lakini siyo kwa umuhimu, nichukue fursa hii kupongeza msimamo wa Serikali katika kuwasimamia watendaji wa Sekta ya Afya. Siyo busara kwa kila atakayesimama amwelekeze na kumkemea Nurse, Daktari au Mtendaji wa Afya. Kazi nyingine unaweza kuzifanya kwa sababu unajua kongea. Sekta ya Afya watendaji wake wanatumia muda mwingi shuleni, wanahitaji utulivu na wanashughulika na afya na uhai wa binadamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia kidogo Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, awali ya yote, nikushukuru na kumpongeza Mheshimiwa Waziri na wasaidizi wake. Kipekee niwapongeze Waheshimiwa Wabunge kwa michango yenu ya Ijumaa na leo.

Mheshimiwa Spika, itoshe mimi leo kuchangia kwamba safari yetu ni kwenda kwenye uchumi wa kati, ulio jumuishi na ili kufika hapo lazima tujenge uchumi wa viwanda, siyo viwanda. Kuweza kujenga uchumi wa viwanda ni lazima tuwe na miundombinu wezeshi na saidizi. Kwa hiyo, Wizara hii ndiyo inayojenga miundombinu wezeshi na saidizi. Twaweza tusione leo hayo tunayoyataka lakini tunapokwenda kwenye uchumi wa kati nina imani hayo tutayaona. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo nalotaka kuzungumzia ni bandari. Watu wa bandari, sitazungumzia suala la Bagamoyo ila Mheshimiwa Ally Saleh, nikukosoe kidogo au nikupe taarifa, Bagamoyo Special Economic Zone itazalisha viwanda 1,000 na watu laki tano watapata ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, watu wa bandari, kuna kiwanda cha Hengia cha Tanga kinachotaka kuzalisha tani milioni saba, nawaomba tukubaliane na wazo la kiwanda kile cha kupata access. Alipokuja Dangote akazalisha tani milioni tatu nchi nzima bei ilishuka, akiingia wa tani milioni saba mambo yatakuwa mazuri. Kama walivyosema wenzangu, twende kasi kwenye maamuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, watu wa TPA niwaeleze kuhusu kitu kinaitwa Port Community. Tunafanya vizuri sana ndani ya bandari lakini wale wanaotusaidia, kwa mfano TRA, TANROADS, hawafanyi kazi vizuri.

Mheshimiwa Spika, nimewaeleza kwa maandishi kwamba ya nini kuweka mzani wa TANROADS Kurasini wakati unaweza kuweka mzani huohuo bandarini na wote wako chini ya Wizara moja? Ndiyo maana kunakuwa na foleni. Niwaombe watu wa bandari tuongeze kasi, tunafanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda nirudie tena; sisi Nacala na Beira si washindani wetu katika bandari, Durban si mshindani, tunatengeneza washindani sisi wenyewe. Yaani ni kama mtu unatengeneza mke mwenza, unashindwa kumhudumia uliyenaye mpaka analazimika kwenda nje kutafuta ushindani. Wanaokwenda Beira na Durban wamelazimika kwenda kule. Tukisawazisha ease of doing business, Nchi za Maziwa Makuu wanapenda kuja hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilikuwa na rafiki yangu mmoja kwenye Serikali ya Kongo iliyomaliza muda, aliniambia wanaweza kutupa robo ya shehena waliyonayo, Bandari ya Dar es Salaam haitapokea mzigo wa Tanzania au nchi nyingine. Kama walivyozungumza tuitumie njia ya Kigoma tuweze kuvuta huu mzigo wa Mashariki ili uweze kuja lakini na Kigoma iweze kuchangamka ili hawa ndugu zangu waache mambo ya kulalamika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie ATCL, niwashauri watu wa Wizara hii tafadhali Uwanja wa Ndege wa Bukoba uangaliwe. Bukoba tunahitaji uwanja mkubwa, hatuhitaji ndege nyingi, sisi shida yetu ni kupakia bidhaa za kwenda kwenye masoko makubwa. Mkoa wa Kagera unamiliki sehemu kubwa ya Ziwa Victoria lakini viwanda vya samaki haviwezi kwenda pale kwa sababu ndege za mizigo haziwezi kuja pale Bukoba.

Mheshimiwa Spika, lakini niwapongeze ATCL hapo mlipofikia, mnachopaswa kufikia sasa ni kutengeneza soko kubwa, kuchangamsha soko na mimi nawaona Watanzania wanakwenda kule. Mnakumbuka kuanzia tarehe 19 Desemba mpaka Januari Bukoba mlikuwa mnapiga trip mbili kwa siku na ilikuwa inajaa. Sasa ninachowashauri ATCL, nimekuwa nikiwaambia muende kwenye utamaduni, mtu akipanda ndege unamkaribisha kwamba karibu kahawa, unampa kahawa, unampa senene ili watu wapande ndege waweze kuzoea ndege. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi hatufanyi mambo ya profit and loss, hii siyo biashara ya maandazi, wazoeshe Watanzania ndege hata kwa kuwapa free ride, wapande ndege na wazipende ili tutengeneze soko kubwa. Haya mambo ya kuongeza destination watu wakishapanda ndege wakazizoea watapanda ndege.

Mheshimiwa Spika, kama alivyozungumza Mheshimiwa Kepteni Abbas, sitaki kuchangia, competitive advantage ya Air Tanzania ni soko la ndani.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa muda huo, mengine ntaleta kwa maandishi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, kupitia njia ya maandishi nichangie bajeti ya Wizara hii muhimu katika ujenzi wa Taifa imara. Rejea ya hotuba ya Mheshimiwa Waziri, kwa sekta zote inaonyesha dhahiri kuwa ujenzi wa uchumi wa viwanda uko kwenye uelekeo sahihi na kasi inayotakiwa.

Mheshimiwa Spika, naomba na kushauri TPA wakamilishe ujenzi wa mradi wa gati la Kyamkwikwi. Ukamilishaji wa mradi huu utawezesha sekta binafsi kujua mipaka ya mradi na kuweza kuendeleza eneo lililobaki.

Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano, kupitia Wizara hii kwa uwekezaji katika vivuko. Naomba Wizara ifikirie maombi ya kupatiwa vivuko (pantoni/ferry).

Mheshimiwa Spika, kuanzia mwaka 2012 nimekuwa nikiomba kivuko kwa ajili ya visiwa vya Bumbiile, Kelebe na Goziba. Kutokana na jitihada na mafanikio ya TPA kukamilisha ujenzi wa gati Kyamkwikwi, ni busara kijamii na kiuchumi kuweka vivuko ili tusaidie na kuokoa wananchi wanaosafiri ziwani.

Mheshimiwa Spika, Tanzania upande wa Mkoa wa Kagera tunayo mahitaji ya uwanja wa ndege mkubwa. Tunaomba na kushauri Serikali kwa njia zote isaidie uchumi wa mkoa huu kwa kuwekeza katika upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba au tujenge uwanja mpya sehemu ya Omukajunguti. Hoja hapa ni kuwa na uwanja wa ndege ambao utawezesha ndege za mizigo kutua. Kagera ina fursa ya kuvutia; viwanda vya samaki na uzalishaji wa matunda na mboga kiurahisi kipindi chote cha mwaka.

Mheshimiwa Spika, nitoe pongezi na maombi kwa TANROADS kupitia kwa Mheshimiwa Waziri na watendaji wake wote. Barabara ya Muhutwe – Kamachumu – Muleba ujenzi unaendelea, hasa sehemu hii ya Muhutwe – Kamachumu. Naomba sehemu hii ya Muhutwe mpaka Kamachumu isimamiwe ili ikamilike kama ilivyopangwa.

Mheshimiwa Spika, vile vile kipande cha Kamachumu/ Ibuga mpaka Rutenge tunaomba kipigwe lami hasa ile sehemu ya Kamachumu Islamic School ambacho ni eneo korofi.

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kuwaomba TANROADS kupitia Wizara kuboresha barabara za TANROADS za Rutenge – Bulyakashaju – Rubale – Izimbya – Kara. Barabara hii ni muhimu kwa kuwa inaunga Wilaya ya Muleba, Bukoba na Karagwe. Eneo ipitapo barabara hii ni mkanda muhimu kiuchumi kwani inalengwa kuwekeza ufugaji wa ng’ombe wa kisasa na kilimo.

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kuipongeza TPA kwa utendaji wa bandari wa sasa. Bandari hii kwa sasa inafanya kazi masaa 24 kwa siku, siku saba za juma. Ushauri ni Serikali kuhakikisha jamii yote za bandari (Port Community) kushirikiana ili kuongeza ufanisi mkubwa. Eneo moja dogo la kutolea mfano ni ukosefu wa ushirikiano wa TPA na TANROAD katika kupima mizigo, hali inayopelekea foleni eneo la Kurasini.

Mheshimiwa Spika, ni rahisi magari yanayotoka bandarini yapimwe yote uzito ndani ya eneo la bandari. Kazi hii inaweza kufanyika chini ya wadau wote wenye maslahi ikiwemo TANROADS na baada ya hapo magari yasipimwe au kusimamishwa mpaka yatoke eneo la jiji. Faida moja kubwa ni kuondoa foleni hali ambayo itaongeza kasi.

Mheshimiwa Spika, yapo madai kuwa bandari za Nakura, Beira, Durban na hata njia za Angola ni washindani wa bandari za Tanzania hasa Dar es Salaam. Kimsingi wateja wote wanaopita njia hizo wamelazimika kupitia huko baada ya njia ya Tanzania kuwa na vikwazo. Nashauri Serikali ziangalie maslahi mapana na kwa pamoja naomba vikwazo hivyo ili kuchangamka kwa biashara ya TPA kulete neema kwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia uzima nikaweza kuwepo mbele ya Bunge lako. Nikushukuru wewe binafsi kwa mambo mawili; moja umefanya kazi yangu au ya Wabunge wengine iwe rafiki kwa kuleta hii Bunge Mtandao, yaani unasoma bila matatizo na mambo yana-flow yenywe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili nikushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia sekta za leo, hizi sekta mbili ndizo sekta mhimili za uchumi jumuishi. Yapo maswali, ziko hoja nyingi za kwamba uchumi unakua, watu wako vipi, ukitaka watu na uchumi ukue lazima uguse hizi sekta hizi, zinaitwa sekta za uchumi jumuishi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kufikisha pongezi zangu mezani kwako, nichukue fursa hii kumshukuru Waziri wa Mifugo, Mheshimiwa Luhaga Mpina. Watu wa Rutoro na vijiji vyake na watu wa Misenyi wanamshukuru kwa kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais. Tumekuwa na migogoro muda mrefu kati ya NARCO na wananchi lakini kwa kauli yake ambayo ni utekelezaji wa ahadi ya Mheshimiwa Rais migogoro ile ameimaliza. Nachoomba kwa Serikali Mheshimiwa Mpina sasa toa maelekezo wa watekelezaji wako ili washirikiane na Serikali ya Mkoa wa Kagera waweze kuonesha wananchi watakuwa wapi wakifanya shughuli zao na NARCO watakuwa wapi wakiendelea na shughuli za mifugo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nichangie mchango wangu katika taarifa hizi za Kamati. Niwapongeze Wenyeviti wote na Kamati zao zote mbili. Napenda nizungumze kidogo kuhusu suala la mifugo. Katika mchango wa Kamati, imeelezea vizuri sana Tanzania ni namba mbili kwa idadi ya mifugo.

Mheshimiwa Spika, napenda nizungumze kwa masikitiko kwamba tuna idadi ya mifugo, hawa ng‟ombe tulionao huwezi kuwapeleka sokoni na Kamati imezungumza tatizo la masoko. Nyama yetu haiwezi kuuzwa kwa sababu tuna idadi ya ng‟ombe kinachotakiwa katika soko la dunia ni nyama quality, kuna watu ambao wanajali afya zao. Kwa hiyo, niungane na Kamati kusema kwamba Serikali inapojenga uchumi jumuishi lazima iwekeze katika mifugo. Wizara hii lazima isaidiwe kama Kamati inavyosema, kusudi tuweze kutengeneza malisho na kuzalisha mifugo yenye tija.

Mheshimiwa Spika, taarifa nilizonazo Tanzania ina fursa ya kuzalisha lita milioni nne za maziwa kwa siku lakini tunazalisha lita laki moja au laki moja na nusu. Tukizalisha lita milioni nne kwa siku maana yake tutaongeza afya ya Watanzania, tunaweza kufikia hatua hata ya kugawa maziwa bure kwa watoto wa shule. Taarifa nilizonazo ni kwamba huu ukanda wa Dodoma, Iringa na Mbeya mnaweza kuchakata zaidi ya lita milioni moja kwa siku, lakini ukanda wa Tanga kwenda mpaka Moshi kuna opportunity ya kuchakata lita milioni moja kwa siku, ukanda wa Kagera kwenda kwenye hizi hifadhi tunazogombania kuna uwezo wa kuchakata lita zaidi ya milioni moja. Ina maana lita milioni nne kwa siku wananchi wote watajumuishwa. Kwa hiyo, hakuna atakayelalamika kwamba uchumi wa vitu unapanda wa watu unadhoofu. Ni kwa sababu, watu moja kwa moja watakaokwenda kuuza maziwa wataweza kuhusishwa katika mchakato huo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala la Kamati ya Bajeti ambalo linahusiana na hapa, suala la mazao. Iko Tume ya Serikali wanasema ilichunguza bei ya ngozi kwamba ngozi zetu haziuzwi. Napenda nichangie katika Kamati hii na Kamati ya Bajeti, ngozi ni bidhaa ya kigolobali, it is a global product, huwezi kuichunguza hapa. Unapochunguza soko la ngozi lazima uangalie Pakistan anafanya nini kwenye sekta ya ngozi na wewe Tanzania unafanya nini? Huwezi kujaza kodi kwenye sekta ya ngozi Tanzania au kwenye industrial sector ya ngozi Tanzania wakati Pakistan anaiacha ngozi iende ishindane duniani ukaweza kushindana naye. Nilipaswa nilizungumze hilo tuweze kulielewa vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niende kwenye sekta ya uvuvi, mimi nusu ya Jimbo langu ni maji, ninavyo visiwa tunafanya shughuli ya uvuvi. Nikubaliane na Mheshimiwa Waziri na Serikali namna mlivyodhibiti uvuvi haramu, nakubaliananalo, nawapa mapendekezo. Njia mnayotumia sasa haiwezi kuwa endelevu, ili kuleta udhibiti ulioendelevu nashauri muwashirikishe wananchi wa sehemu husika. Kabla wavuvi wengi hawajaja, hawa wanaofanya samaki wapotee, katika maeneo ya kwetu walikuwepo wavuvi, kwetu Bumbire, Goziba, Kelebe, Bakibwe wavuvi walikuwepo, sasa huwezi kuja na mapolisi kuzuia uvuvi haramu bila kumhusisha mzee wa mahalia. Huyu mzee wa mahalia pale lazima umuhusishe akuambie mwenye kokoro ni nani, aweze kutoa taarifa. Wewe katika mapato makubwa unayompa lazima urudishe kwa mtu wa pale ili aweze kuona shughuli zinazofanyika na yeye ana manufaa, nilitaka nilizungumze hilo.

Mheshimiwa Spika, lakini tumezungumza katika Kamati ya Kilimo sikuona suala la soko. Tunalo tatizo la soko la mazao, ni kipaumbele na ni kikwazo kikubwa. Nipenda kuzungumzia mahindi na nafaka. Ili tuweze kutafuta soko la uhakika la mazao yetu, hasa nafaka, lazima Taifa lijikite kwenye kujenga storage capacity, hizi silos, ma-godown. Kenya yuko mtu mmoja anao uwezo wa kutunza tani laki saba. Sasa Serikali iige mfumo wa sekta ya mafuta ihamasishe sekta binafsi tuwe na uwezo mkubwa wa kuhifadhi.

Mheshimiwa Spika, jambo lililo wazi katika ukanda wetu wa Afrika haiwezi kupita miaka mitatu hatujapata shida ya chakula, Mungu atunusuru. Haya mafuriko na wale nzige tutapata shida ya chakula hata tufanyeje. Sasa kama tungekuwa na storage capacity kubwa ya kutunza tani milioni nne na Serikali katafuta mfumo mzuri wa ku-finance watu wanaleta mazao yanakuwa managed, halafu benki zinatoa mikopo. Ina maana mazao yangenunuliwa, mkulima kaondoka, halafu kile chakula kikabaki kwenye silos. Haiwezekani, lazima tutapata jirani yetu mwenye shida ya chakula na sisi kwa sababu tuna faida ya uoto tungeweza kuwa-supply hawa wenzetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naishauri Kamati na Serikali kwamba tuwekeze kwenye silos. Kasi ya Serikali kuwekeza kwenye storage ni ndogo sana. Tuongeze kasi ya kuweza kuongeza storage capacity kusudi tutumie hizo finance modalities tuweze kuwa na chakula cha kutosha.

Mheshimiwa Spika, nizungumze kidogo mazingira ya biashara na nimshukuru Mheshimiwa Jitu umenikumbusha Blue Print Regulatory Reform. Nimesikitika tunapokwenda kwenye kuuza mbogamboga, tunapozungumzia avocado, kwenda kuuza avocado Ulaya ukiangalia tozo zinazotozwa inaonekana kama mkulima labda anapewa adhabu. Ni vilevile hata kwenye samaki, mmezungumza samaki hawana soko lakini linganisha tozo na kodi tunazotoza sisi upande wa Tanzania na wanazotoza wenzetu wa Kenya na Uganda, landing fee ya ndege Mwanza na landing fee ya Entebe ni tofauti, lakini kontena la minofu ya samaki linapotoka kwenye kiwanda Mwanza linatozwa kiasi gani na wenzetu wa upande wa Uganda wanatoza kiasi gani.

Mheshimiwa Spika, tunapokuwa tunazungumzia bidhaa zetuna nizungumze hili, ili tuweze kujenga uchumi na shilingi iliyo imara lazima tu-export zaidi. Hatuwezi kulenga kujitosheleza hapa, tulianguka zamani kwa sababu tulilenga kujitosheleza, we must invest in import substitution come export promotion. Kwa hiyo, kujitosheleza-kujitosheleza hakutatusaidia, lazima uuze nje na lazima tuuze nje kwa mazao haya niliyoyasema kwamba ndio yanashikilia uchumi jumuishi. Uchumi jumuishi uko kwenye kilimo, mifugo na kwenye utalii kwa sababu wananchi wazawa wa Tanzania wataweza kuhusika moja kwa moja na kuweza kupata kipato. Kwa hiyo, uchumi wa vitu na wa wananchi utaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache nawapongeza Wenyeviti wa Kamati hizi mbili. Naipongeza Serikali, tuongeze nguvu, mwelekeo wetu ni mzuri.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Kuhusu Shughuli za Kamati Kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia taarifa za Kamati hizi mbili zilizopo mbele yetu, lakini kwa sababu sijavaa vazi la kidiplomasia nitachangia sekta ndogo ya nishati upande wa mafuta na gesi nikikumbuka nguo nilizokuwa navaa miaka 36 iliyopita wakati nafungua valve.

Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Mheshimiwa Waziri. Nilieleze Bunge lako Tukufu kwamba unaweza kuwa na kitu na usijue thamani yake. Kwa watu wanaojua historia ya mafuta nchini wakati watu wanapata mafuta kwa mgao ndiyo utaweza kujua kwamba Wizara ya Nishati leo inafanya kazi iliyotukuka. Nimeisoma vizuri taarifa ya Kamati, inavutia. Tunayo hifadhi ya mafuta ya kutosha miezi mitatu, lakini kipekee hifadhi hiyo imenunuliwa na Private Sector. Ina maana mfumo wa Bulk Procurement unaodhibitiwa na Serikali unaifanya sekta binafsi kuleta mafuta kuwa hapa bila fedha ya Serikali na watu hawawezi kugundua kwamba nchi ina upungufu wa mafuta.

Mheshimiwa Spika, nipongeze suala lingine la bulk procurement ambapo kwa historia, najua hili unalifahamu vizuri; wakati meli zinakuja Dar es Salaam tulikuwa tunaweza kukalisha meli nje tukaingia gharama (demurrage) ya dola 20 mpaka 40. Taarifa ya Kamati inafurahisha, kwamba demurrage charges sasa ni chini ya dola mbili (dola 1.6). Ni jambo zuri sana niwafurahishe wanakamati kwamba muendee hivyo tuweze kwenda kwenye mambo mengine yanayofurahisha.

Mheshimiwa Spika, nitofautiane kidogo na Kamati; kwamba tathmini yao haijatupeleka kwenye malengo ya kuanzisha bulk procurement, pamoja na haya availability of product, affordability na quality ambayo kweli quality tumeiweza hatujaweza kujibu au taarifa yenu haikutueleza. Je, haya mafuta margin yake ni kiasi gani? Mwenyekiti wa Kamati anaelewa kwa sababu mimi ndiyo nilimpokea kazini nikamuonesha dawati na kumfundisha kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kitandula ni kijana wangu nilimpoke kazini mika hiyo kwa hiyo hii success ugomvi wa kuagiza mafuta uko kwenye ile margin. Je, unapokuwa umenunua margin iko kiasi gani, lakini Mwenyekiti wa Kamati nikueleze haujatueleza mafuta yanayopotea. Ugomvi mkubwa wa Wizara ya Fedha ni mafuta yanayopotea kutoka kwenye meli kuingia kwenye matenki, hili suala kamati yenu haijalijibu.

Mheshimiwa Spika, nimweleze Mwenyekiti wa Kamati kwamba kuna suala tata la floor meter, floor meter inayopigiwa kilele ambayo kimsingi mimi mwenyewe kama mtalaam wa shughuli siiungi mkono, lakini solution ya upoteaji wa mafuta ni kuwa na single receiving tanks. Hili suala tata la single receiving tanks Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati haujalijibu, umekuwa wimbo wimbo wimbo wa kila siku.

Mheshimiwa Spika, jambo moja la kufurahisha niwapongeze Mheshimiwa Waziri kwa kuongeza storage capacity, kwamba leo nchi ina uwezo wa kutunza mafuta lita bilioni 1.3 ambayo matumizi ya nchi inakwenda kwenye lita karibu 3.8 bilioni. Jambo la kufurahisha ni kwamba mafuta ya jirani yetu yanayopita Tanzania ni takriban kiasi hicho cha 1.9 billion litters kwa miezi sita. Maana yake ni nini, wakati una mafuta ya kutumia nchini kwa miezi mitatu una mafuta mengine ya jirani yako yanayopita; ina maana hatuwezi kulala njaa wakati mafuta ya jirani yapo. Kwa lugha ya kawaida huwezi kuwa umemuwekea mwenzako mihogo halafu baba hajatoka kuhemea watoto wakalala njaa, hapana utakula mihogo hiyo halafu kesho yake utakuja urudishie. Kwa hiyo niwapongeze Wizara ya Nishati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini wakati nawapongeza tumeshindwa kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inayotuelekeza kwamba Dar es Salaam inapaswa iwe trading hub ya mafuta kwa nchi zilizotuzunguka. Kwa masikitiko watu wa Kenya wanatumia bounded warehouse, watu wa Uganda wanatumia bounded warehouse, Rwanda wanatumia bounded warehouse. Maana yake ni nini, kama mafuta yangeletwa yakazuiliwa Dar es Salaam tungefanya re-export. Ina maana kwenye lita zinazopita hapa 1.9 billion kwa miezi sita tungeongeza cha juu tukaweza kuuza nje. Kwa hiyo tunapoteza fursa ambayo ingetuongezea kodi nyingine Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Yaani unaongeza make up inaitwa cha juu unaweza kuuza. Niwaeleze, watu kutoka nchi zilizotuzunguka hawapendi kununua kutoka nje. Ndicho kitu nilichokifanya kwenye sekta ya saruji; watu wa Rwanda na Burundi walikuwa wananunua saruji Pakstan lakini viwanda vya saruji vilipochangamka wakaja na malori wakanunua saruji kwetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nahimiza kwamba tutekeleze Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kujenga storage tanks zile za Tanga, tengeneza bounded warehouse tusimamie ile damping na whatever tuweze kuongeza kile cha juu 1.9 billion litters ukiweka dola moja moja mambo ya kujenga madarasa tunaweza kufanikisha kwa haraka.

Mheshimiwa Spika, nipongeze wizara na TPDC; katika taarifa yenu mliwahi kuzungumza, mlirashiarashia kidogo. Zipo jitihada za TPDC kuanza kutafuta na kuchimba gesi. Si jambo jipya, mmerudi kule tulikoanzia, TPDC katika historia ya kutafuta mafuta imewahi kuchimba visima, Munazi Bay, Songosongo, akina Mzee Kaaya, akina Mzee Barongo walichimba visima na wakakuta gesi. Kwa hiyo jitihada za sasa ni lazima tuziendeleze. Msiwe na wasiwasi, kazi hii ina gharama kubwa. Kupata mafuta, kuchimba mafuta kwa gharama yako ni kubwa lakini failure ni kubwa. Mtachimba visima kwa gharama kubwa na unaweza kuchimba visima hata kumi usipate lakini ukipata ulichokipata ni cha kwako. Kwa hiyo hapo wanaofanya maamuzi lazima mkae chini mtulie. Libya kuja kupata kisima cha mafuta ya kutosha (economic quantity) walichimba visima zaidi ya 50. Kwa hiyo na sisi tunaweza kuchimba visima vingi lakini tukipata tumepata tunaondoa yale mashaka ya kwamba tunaliwa.

Mheshimiwa Spika, Kuhusu Suala la Utafutaji. Suala la utafutaji lina faida nyingi, utafutaji wa mafuta ni shule. Wako vijana wengi wanafanya suala la geology, petroleum chemicals na whatever, hawa vijana tunawapatia nafasi ya kuweza kujifunza hii sekta. Kitu kimoja kilichodokezwa na Kamati ambacho nawaunga mkono, naiomba Serikali yangu ya Chama Cha Mapinduzi muharakishe kufanya maamuzi na kuzipitia PSA ambayo nina hakika Kamati yetu iliwahi kupitia, kuna Kamati ya Gesi iliwahi kupitia; lakini ukisoma mtu yeyote kuna makandokando ambayo kwa sababu ya kupitwa na muda tunaweza kufanya maboresho. Tufanye maamuzi kusudi watafutaji na wachimbaji waanze kuchimba kwa sababu hizi rasilimali haziko Tanzania peke yake, lakini hizi rasilimali zina rasilimali mbadala kwingine.

Mheshimiwa Spika, sehemu nyingine sasa hizi liquefied natural gas si biashara tena, lakini anayekuwahi sokoni anakwenda kukamata mteja, mteja atakayechukuliwa na Mozambique wewe kuja kumtoa Mozambique uuze gesi yako itakuwa ni tatizo. Kwa hiyo naomba Serikali yetu fanya michakato usiku na mchana, pitia hizo PSA, pitia hizo leseni, waite hao watafutaji na wachimbaji watafute. Mimi nina uhakika Mwenyezi Mungu na sisi ametuwekea mafuta sehemu, ametuwekea gesi mahali, ningependa na sisi tuweze kuyafaidi haya mafuta si kwamba wajukuu wetu waje waseme babu zetu walikuwa wazuri, waliishi na mafuta wakayaacha ngoja sisi tuweze kufanya nini, tuweze kuyatumia. Tukiweza kupata mafuta yakaweza kuchochea zile sekta za kilimo na mifugo zikaziunga mkono tutaweza kwenda kwenye uchumi mkubwa haraka sana kuliko tunavyotegemea.

Mheshimiwa Spika, nilizungumze hili wakati nataka kumalizia. Safari yetu ni ya kwenda kwenye uchumi mkubwa, si uchumi wa kati, uchumi wa kati ni kituo. Kwa hiyo ili uende kwenye uchumi mkubwa unahitaji nguvu nyingi, moja wapo ya nguvu ni nishati na nishati yenyewe ni mafuta na gesi ambayo Mwenyezi Mungu alitujalia. Kwa hayo machache naomba niunge mkono hoja, ahsanteni Mheshimiwa Kitandula kwa repoti nzuri.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia Wizara hii muhimu. Nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mpina na Mheshimiwa Naibu Waziri mjomba Kerebe wanamsubiri, apitie kwenye diary yake kabla hajaenda Kerebe. Jambo la kwanza niwaeleze asilimia 70 ya Halmashauri yangu ni maji, Ziwa Victoria asilimia 70 ya Wilaya yangu ya Muleba ni maji, kwa hiyo mimi ni mvuvi. Sehemu kubwa ya eneo ambalo Wizara hii inajinasibu nalo katika ufugaji wa ng’ombe (NARCO) ni Jimbo langu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia bajeti hii nataka kuzungumzia mafanikio ya kampeni ya uvuvi haramu, ni pale tulipofanikiwa kuweza kupata samaki wale wanaokidhi hata kwenda kwenye ule utamu wa samaki mwenyewe hayo ndio mafanikio. Hakuna aliyejua njia hiyo ndio maana njia zilizotumika mimi siwezi kuziunga mkono, nakubaliana na Waheshimiwa Wabunge wanaosema yale makandokando yaliyofanyika yarekebishwe. Nami nampa Mheshimiwa Waziri makandokando ambayo ningeomba ayarekebishe, atoe amnesty, kuna watu walinyang’anywa injini zao, atamke kwamba wale walionyang’anywa injini zao naziachia, wale waliovunjiwa mitumbwi yao hiyo tuiache. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tena nami nina dhambi hiyo, tuliwahamasisha wana viwanda wa Tanzania wakauze nyavu, tukazuia wana viwanda wa nje, kumbe kuna wana viwanda wa Tanzania wakapeleka nyavu zisizokuwa na viwango, Mheshimiwa Waziri ashirikiane na Mheshimiwa Waziri wa Viwanda waende walete zile nyavu, wenye viwanda waliouza nyavu kanyaboya waweze kuwakamata kusudi mbele ya wananchi tuweze kuonekana ni watu wazuri kwa wananchi. Sio kwamba namchomekea mjomba aende Kerebe kwamba hatarudi, hapana, lakini hawa wavuvi wanaweza kutushangilia kwa mikono lakini moyoni wanaumia. Sasa namna ya kuweza kusawazisha mambo haya ni kukaa pamoja na wao. Mheshimiwa Waziri arudishe injini za watu mambo yaishe, twende mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la nyavu, Jimbo langu linapakana na Uganda kwa maji na linapakana na Kenya kwa maji, milimita sita linavua dagaa kwa watu wa kutoka Uganda na Kenya, wewe unaniambia mpaka nilete milimita nane. Tukae chini tusawazishe mambo haya, tunachekwa. Mganda anatoka Uganda anavua Goziba, anavua Zilagura anachukua samaki, samaki hana mpaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la leseni; sisi tunafuata sheria za Wizara ya Mifugo, hatuwezi kuruhusu mtu aharibu mazingira, tunatunza eneo letu la maji square kilomita saba, siwezi kukubaliana na Serikali kwamba mtu akakate leseni Bunda aje kuvua kwangu, hapana, aende Muleba akate leseni Muleba, ukikata leseni Bunda, kavue huko huko, kila mtu atunze mazingira yake. Hatuwezi kuhakikisha halmashauri hizi tunazinyang’anya mapato, mapato ya Wilaya yangu yanatokana na leseni, kama unaipenda Muleba nenda kwa Shilembi akukatie leseni uvue, kama hutaki nenda huko kwao ambako wanaharibu mazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie cage, ufugaji wa vizimba Uganda wameanza kufuga kwa vizimba, Tanzania mnaweka masharti, haiwezekani, ndio hayo mambo Profesa Kishimba anakwambia nenda na wenzako. Hata hivyo, ni kuna watu wa Maalia, watu wa Bumbire wakati wa mvua tulikuwa tunapiga samaki kwa fimbo mkaleta over fishing kwa teknolojia ya kisasa, wale ambao wamewaondoa kwenye mavuno yao ya asilia, chonde waende wakawape pesa, hizo pesa nyingi wanazovuna warudishe kwa jamii wasaidie vijana waweze kufuga kwa vizimba. Hawezi kwenda mbele akasema amekusanya asilimia 147 hawatamwelewa, hizo kama 147 asilimia 100 wapelekee Mheshimiwa Mzee Mpango atashukuru, 47 arudishe kwa wananchi watampenda sana. Zile njia ambazo wanavuna sizo, hizo waachane nazo, akimnyang’anya nyavu haramu ampe nyavu halali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie Sekta ya Maziwa; Tanzania wanachakata maziwa lita 150,000, wengine wanasema hazifiki, Uganda wanachakata lita milioni mbili. Napenda niwashauri walielewe hili, hii ndio sekta na Mheshimiwa Waziri nazungumza ili kumsaidia, yeye ndiye ng’ombe wa maziwa wa uchumi wa nchi hii. Hizi ndizo sekta za kutupelekea uchumi wa kati ulio jumuishi, ukiwalisha wafugaji, ukawalisha wavuvi, uchumi unachangamka, uchumi jumuishi uko kwenye sekta hizi. Kwa hiyo ni suala la Serikali kupeleka pesa nyingi, watu wa Uganda wanawasaidia watu kuwatengenezea malisho, wanawapa mabirika ya kukusanyia maziwa, wanajengea viwanda. Kiwanda Uganda ni market wanatengeneza lita milioni 2,000,000 kwa siku.

Mheshimiwa Spika, samahani, Mheshimiwa Mwenyekiti, naona unaniangalia nakuchulia mambo mema. Naunga mkono hoja na nitawasilisha kwa maandishi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, pamoja na mchango kwa njia ya kuzungumza, naongeza kuchangia kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, nishauri juu ya uvuvi wa bahari kuu. Baada ya kuanzisha Shirika la Uvuvi (TAFICO), hakuna haja ya kusubiri kununua meli zinazomilikiwa na Serikali, waalike wawekezaji walio tayari kufanya kazi kwa kushirikiana na TAFICO. Walete meli zao, TAFICO ishirikiane nao tupate japo kidogo hicho tunachokosa. Serikali ipitie upya sekta ya uvuvi wa bahari kuu na kufanya maamuzi kwa mwongozo ulio sahihi.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeweza kudhibiti uvuvi haramu. Mafanikio ni kuwa samaki wameongezeka, wale wenye ubora unaotakiwa. Ushauri kwa Serikali ni kuwa Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa uvuvi haramu haurejei tena. Eneo lenye mapungufu ni watendaji wa Wizara na idara za uvuvi, hawa ndio wanaohamasisha uvuvi haramu. Katika Mkoa wa Kagera maeneo ya visiwani, compliance iko juu sana ila sehemu za karibu na nchi kavu uvuvi haramu umeanza kurejea tena.

Mheshimiwa Spika, Niishauri Serikali Juu ya Sekta ya Maziwa. Sekta hii ni moja ya sekta zenye fursa kubwa ya kujenga uchumi jumuishi. Taarifa za wataalam wa sekta ya maziwa nchini Uganda wanasema Tanzania kwa uchache tuna fursa ya kuzalisha na kuchakata lita milioni nne kwa siku. Uganda kwa sasa wanazalisha na kuchakata lita milioni mbili kwa siku ukilinganisha na lita 150,000 kwa siku kwa nchi ya Tanzania.

Mheshimiwa Spika, ili Tanzania iweze kufikia kiwango hicho kwa kuazima uzoefu wa Uganda tunapaswa kufanya yafuatayo; moja, Serikali itenge maeneo sehemu za wafugaji nchi nzima kwa kuanzisha semi free range animal keeping. Wafugaji wasaidiwe kuendeleza maeneo hayo kupewa mitamba huku Serikali ikitegemea kupata uwekezaji wake kwenye maziwa yatakayouzwa.

Mheshimiwa Spika, pili, soko la maziwa ni kiwanda, viwanda vyote vya maziwa vipewe vivutio kadiri inavyowezekana. Punguzo/upotevu wa ushuru/tozo kwenye viwanda vitarejeshwa kutoka kwenye kipato cha wananchi na sekta za kuzalisha maziwa zitakazoshamiri.

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NARCO inaendesha zoezi la kugawa vitalu vya ufugaji Mkoani Kagera. Tatizo langu kwa zoezi hili NARCO na Wizara wanarudia makosa yaliyofanyika miaka ya 2005. Maamuzi ya Serikali ya mwaka 2005 juu ya ranchi za Mkoa wa Kagera tume nyingi ikiwemo ile ya makatibu wakuu sita ziliikataa. Tume ya makatibu wakuu sita iliundwa na Mheshimiwa Dkt. Magufuli akiwa Waziri wa Mifugo na hata akiwa Mkoani Kagera amekuwa akilaani ugawaji huu wa maeneo.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali katika zoezi hili izingatie yafuatayo:-

(a) Imalize migogoro ya ugawaji wa mwaka 2006, kwetu Muleba. Tunashauri vijiji vyetu vinne na vitongoji virudishwe kwa wananchi.

(b) Kabla ya kugawa maeneo, lazima wazingatie mahitaji ya vijiji jirani ambavyo hutegemea mbuga hizo kuchunga ng’ombe wao.

(c) Mkoa wa Kagera unahitaji na kutegemea sekta ya maziwa. Yatengwe maeneo mahususi kwa ajili ya wawekezaji waliotayari kujenga viwanda. Wawekezaji hao wapewe vivutio vya ziada kwani sekta hii inajenga uchumi jumuishi.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Bajeti ya Wizara ya Nishati; na ninapoanza, leo tarehe 28 zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania kufikisha miaka 50, nichukue fursa hii kuwapongeza Watanzania kwa shirika la Kitanzania kufikisha miaka 50. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni mtumishi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania kwa miaka 18, lakini ni mtumishi wa sekta ya mafuta kwa miaka 30. Kwa hiyo ninachokizungumza sikukisoma darasani, ninachokizungumza nakijua ndiyo maana wakati mwingine huwa naona mnyukano nashika kichwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaposherehekea miaka 50 ya TPDC napenda nichukue fursa hii kuipongeza Serikali na pia nilipongeze Bunge hili. Bunge la Kumi lililopita kupitia Sekta ya Mafuta tuliwahi kufanya mambo makubwa, moja wapo ni kutengeneza tozo, la pili kuzuia uchakachuaji na la tatu bulk procurement. Wabunge waliokuwepo watamkumbuka Mheshimiwa January Makamba, Mwenyekiti wetu na Mzee wa SCOPO, Mheshimiwa Mzee Ndassa, haya ni mambo makubwa ambayo tunapaswa kujivunia. Sekta ya mafuta watu wengine wanaweza wasilewe; ni wakala mkubwa wa Serikali kwenye kukusanya kodi; kodi kubwa inakusanywa na TRA hupitia kwenye sekta ya mafuta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine cha kujivunia kwenye sekta ya mafuta, ndiyo sekta nafuu, ndiyo sekta ya kipekee ambako kuna ubia wa sekta binafsi na Serikali. Vituo vya mafuta 1,400 vilivyoko nchini vyote ni vya sekta binafsi, ndipo mahali pa kulea Watanzania ili kuweza kuwaonesha kwamba kumbe sekta binafsi inaweza kufanya kazi. Tanzania tunayo hifadhi ya mafuta ifikayo milioni 1,200 m3, lakini yote hiyo asilimia 89 inamilikiwa na sekta binafsi. Mimi ni muumini wa sekta binafsi nimesimama kuisemea sekta binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kitu kinachoitwa power mix. Tunapokwenda kujenga uchumi wa viwanda ifikapo 2025 nchi hii inahitaji gigawati 25 au megawati 25,000. Kwa hiyo mimi mtu anayejadili Stiegler’s Gorge nashindwa kumuelewa. Mahitaji yetu ni makubwa mno kuliko Stiegler’s Gorge, tunaihitiaji Stiegler’s Gorge na… (Makofi)

(Hapa sauti ilikatika)

MWENYEKITI: Sogea kwenye microphone nyingine. MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii hapa. MWENYEKITI: Muda wake bado upo, anaendelea, dakika kumi.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niseme washindwe na walegee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nazungumza kuhusu power mix. Mahitaji ya nchi hii kufika 2025 ni gigawati 25 ambayo mnaita megawati 25,000. Kwa hiyo suala la Stiegler’s Gorge yenye megawati 2,000 wala si kachumbari, tunaihitaji jana. Lakini ina maana tunahitaji vyanzo vingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka kuwapa uzoefu; niliwahi kwenda huko SADC, Congo DRC wanatengeneza gigawati au megawati 40,000; South Africa ameshaomba 16, Mheshimiwa Waziri ukija hapa uwakumbushe. Ndiyo maana tunatengeneza kitu kinaitwa interconnector, tunatengeneza mtandao wa kutoka Kongo, wa kutoka kaskazini, nchi za Ethiopia. Sasa kama baba anakwenda kuhemea usimshangae mama anayelima viazi. Yaani Stiegler’s Gorge ni kama viazi, chakula bado kinahitajika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ninapenda niwaeleze katika mambo ya nishati kuna vyumba vitatu; chumba cha kwanza kinaitwa availability, cha pili liability na cha tatu affordability. Wawekezaji tunaowatafuta, kama hawajui kwamba una nishati ya kuaminika kesho hawawezi kuja. Kwa hiyo anayejenga Stiegler’s Gorge anawavuta wawekezaji waje. Mwekezaji makini haangalii umeme ulionao leo…

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: …anaangalia keshokutwa utakuwa na…

MWENYEKITI: Mheshibiwa Mwijage, taratibu; taarifa.

T A A R I F A

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nimpe taarifa rafiki yangu anayechangia. Amezungumza mambo ya energy mix; suala la energy mix ni kwamba unakuwa na aina tofautitofauti za umeme, yaani upepo, maji, makaa ya mawe. Sasa hapa anachosema energy mix tayari tuna Mtera, tuna Kihansi, sasa kule tena tunaleta tena mambo ya maji tena, sasa hiyo ni energy mix ipi?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwijage.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema hii sekta siyo mchezo. Huwezi kuisoma umelala, hili si somo la kulala kwenye kitanda ukaanza kusoma. Yaani nimekwambia mwanzo nina miaka 30 kwenye sekta, naweza kuanzia jotoardhi, nikakueleza umeme wa mawimbi, nikakueleza mambo ya mkaa, kwa hiyo watu wengine muwe mnakaa Bungeni mnasikiliza. Mheshimiwa Maige asubuhi ametoa somo la makaa ya mawe na yenyewe nishati tunayo; hiyo taarifa siikubali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na katika hiyo niwaeleze dhana isiyo, kuna dhana isiyo; mtu anasimama anasema bomba la kutoka Mtwara linatumika asilimia sita it’s a failure, it is not! Ukijenga barabara ukamaliza, traffic ika-jam umeshindwa; ile bomba ni barabara tunawavutia wawekezaji wachukue gesi zaidi, ile gesi mmesema itakwenda Uganda, bomba halipaswi kujaa na uwepo wa bomba lile ni kivutio cha gesi ya maji marefu ipitie pale ije huku itumike. Lakini gesi ile ni kivutio cha visima vilivyoko kusini vichimbwe vitatumia bomba ile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie bomba la Uganda. Wako watu hawajui faida ya bomba la Uganda. Faida ya bomba la Uganda linafungua fursa zetu. Nchini Tanzania tuna kitu kinaitwa stranded reserve, sehemu za Kigoma, sehemu za Eyasi, kuna mafuta kule Mungu atatujalia tutayapata, lakini watafutaji hawakuwa na motisha ya kwenda kule. Kwa hiyo kwa kuwepo bomba la kutoka Kabale, Hoima, mpaka Tanga ina maana wawekezaji sasa watavutiwa, watakwenda kuchimba mafuta kule na siku moja nchi yetu itaweza kupata mafuta. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema awali na mwanzo, hili ni somo gumu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti kwa kumalizia naomba niwaeleze mojawapo ya mambo niliyofundishwa. Wanasema wasafiri wenye busara ni wajibu wao kukumbuka wafikapo safari salama au njiani wakiwa, kukitunza chombo chao vyema na nahodha wao kushikilia. Chombo ni Tanzania na nahodha mtajaza wenyewe. (Makofi)
Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020
MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuwa mtu wa kwanza katika kuchangia Hotuba ya Mheshimiwa Rais. Awali ya yote, nisije nikasahau, naunga mkono Hotuba ya Mheshimiwa Rais aliyoitoa hapa na hotuba alizozitoa wakati anaomba ridhaa ya kuongoza kwa mara ya pili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Hotuba ya Mheshimiwa Rais na zile nyingine na hasa Andiko la Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inaonyesha dhahiri nia ya Mheshimiwa Rais ya kuhuisha au kujenga upya Dira ya Taifa ya 2020 – 2025. Mheshimiwa Rais nikimnukuu, anasema Taifa hili siyo maskini, lina rasilimali nyingi na anataka kwenda kwenye uchumi mkubwa. Nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kutembea na maneno yake. Alipochukua fursa ya kuteua Baraza la Mawaziri, akachukua Wizara ya Uwekezaji akaiweka chini ya mamlaka yake, yaani yeye ndiye Waziri wa Uwekezaji na akamteua rafiki yangu awe Waziri wa Nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais amefanya hivyo kwa nia moja. Wawekezaji wako wa kila namna; na kuipeleka nchi hii katika uchumi mkubwa, lazima uchangamshe uwekezaji. Hata mkulima yule wa nyumbani ambaye ametuwezesha kuishi miaka mitano iliyopita bila njaa, naye ni mwekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwa Mheshimiwa Rais, nashauri, ili tuweze kufikia malengo yetu, lazima vile vigezo tulivyovipitia katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na kugundua kwamba vinatuwekea vikwazo, basi vyote avipeleke, aviweke chini yake kama ambavyo Bunge hili liliwahi kumshauri.Namaanisha blueprint. The Blueprint of RegulatoryReform iwekwe chini ya Rais ili Wizara na Taasisi nyingine aweze kuzielekeza namna ya kufanya.

Mheshimiwa Spika, sifungui mjadala, lakini hata ungekuwa mganga wa namna gani uliyebobea, huwezi kujifanyia operation kubwa wewe mwenyewe. Wizara yoyote yenye jukumu la kukusanya maduhuli, haitakubali haraka sana kuondoa hayo maduhuli au kodi mbalimbali mpaka Mheshimiwa Rais mwenyewe aseme wewe punguza hapa, punguza hapa, punguza hapa.

Mheshimiwa Spika, nazungumza sana suala la Wizara hii anayoisimamia Mheshimiwa Rais kwa sababu jitihada ya kufikia ule uchumi wa kati na kwenye uchumi mkubwa linahusisha uwekezaji. Nami napenda nitangaze interest; uwekezaji ninaoushabikia ni wa zile sekta za uzalishaji (the productive sectors).

Mheshimiwa Spika, tumefanya vizuri kwenye miundombinu, tumefanya vizuri kwenye elimu, sasa ni wakati wa kuhakikisha tunazidua sekta za uzalishaji, tunalima kwa tija kubwa; kama alivyoniambia Profesa Mkenda kwamba, kupungua kwa bei ya mazao siyo hoja, lakini kipato cha mkulima kisipungue, hata bei ikishuka. Sasa jibu hilo ni kuongeza tija katika shughuli na kuongeza tija katika shughuli maana yake ni uwekezaji.

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana nina falsafa, nina neno langu ninalolisema kila siku kwamba sasa tuweke flagship project katika shughuli za sekta za kiuzalishaji katika kilimo, uvuvi na katika sekta za namna hiyo. Kwa sababu gani? Hoja siyo kujenga uchumi mkubwa, hoja yetu ni kujenga uchumi mkubwa ulio jumuishi. Unaweza kuzidua mafuta, ukazidua madini ya namna mbalimbali, ukawa na GDP kubwa, ukawa na income per capita kubwa sana, lakini ukawa na watu wenye matambara, ombamba; lakini sekta hizi ni productive sectors ambazo zinahusisha watu wengi.

Mheshimiwa Spika, yote haya yapo, tumeyashughulikia, tumehangaika nayo miaka mitano, sasa ni mwendo wa kupaa. Kwa mara nyingine namuunga mkono Mheshimiwa Rais, nasi wapambanaji wake tuko tayari kupaa naye. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimezungumzia sekta za uzalishaji, lakini jambo moja ambalo nataka niishauri Serikali, katika maandiko iko kauli ya kwamba tuzalishe kiasi cha kutosha na ziada tuuze nje. Kwa heshima na taadhima, napenda kuishauri Serikali yangu tuondokane na falsafa hiyo. Unapokwenda kuzalisha, uende na malengo mawili makuu, ambapo lengo moja haliathiri lengo lingine. Uende kuzalisha kutosheleza soko la nchi hii na uende kuzalisha ili kuuza nje. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukisoma taarifa au Hotuba ya Mheshimiwa Rais, kwa miaka mitano tuliweza kuuza nje dola bilioni nane na kitu mpaka dola bilioni tisa. Ni mtazamo chanya, lakini siyo namba ya kujivunia, kwa sisi waumini sehemu tulipo, locational advantage; tungetegemea nchi hii iuze sana. Kwa hiyo, zalisheni ili kuuza katika nchi hii na kuuza nje kusudi tuweze kupata fedha za kigeni na kupata uzoefu wa masoko ya nje. Ukizalisha leo kutosheleza maisha ya nchi hii au mahitaji ya nchi hii, wenzako wanaokamata soko la nje, hutakaa kuwatosheleza au kuwaingilia kwenye masoko yao wakati wewe utakapokuwa umemaliza hapa.Ninayo mifano mingi, muda siyo rafiki.

Mheshimiwa Spika, namuunga mkono tena Mheshimiwa Rais kwa kauli yake. Tunatambua kazi nzuri tuliyofanya kwa miaka mitano; watoto wengi wamekwenda shule. Mheshimiwa Rais akasema, kipindi hiki sasa ni kuongeza ubora katika sekta ya elimu. Naungana naye, tuongeze ubora katika wanafunzi ambao wameingia katika shule zetu waweze kuwa na ujuzi.

Mheshimiwa Spika, nitakuwa mkosefu wa fadhila na niko tayari kutoa album, siyo single tena; naishukuru na kuipongeza Serikali kwa kuweka jiwe la msingi jengo ambalo limekaribia kukamilika la VETA ya Mkoa wa Kagera, jengo lenye thamani ya shilingi bilioni 22 linaloweza kupokea wanafunzi 800 kwa wakati mmoja. Ndiyo maana nilipofurahi nikakumbuka ule wimbo alionifundisha bibi kwamba senene ni tamu kuliko nyama.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Kicheko/ Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022
MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia Mpango wa Tatu wa Miaka Mitano na Mpango wa Mwaka Mmoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nimpongeze Waziri wa Fedha na Mipango na Serikali kwa kuja na mpango huu maana yake sasa tumefanikiwa kuikamilisha mipango yetu mitatu. Mpango wa kwanza, mpango wa pili ambao tunaumaliza sasa na tunakwenda kwenye mpango wa tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napoanza kuchangia narejea kwenye maandiko, lengo kuu la Mpango wa Tatu ni kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2025 yaani kuwa na Watanzania wenye kipato (income per capita) Dola 3,000, kuwa na jamii ya Watanzania iliyoelimika na yenye uchu wa kujifunza, kuwa na uchumi shindani wenye uwezo wa kuagiza na kuuza nje, utawala bora lakini eneo ambalo sisi tunalimudu la umoja, mshikamano na amani. Nina imani hapa tunafika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kabla hatujaenda kwenye mapendekezo yangu nipitie kwenye dhima tunayomaliza na dhima tunayokwenda. Uzuri wa kitabu hutangazwa na kichwa cha kitabu (the title). Kwa waandishi wazuri kama Mheshimiwa Dkt. Philipo Mpango unaweza kusoma jina lake la kitabu ukajua uzuri wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhima ya mpango wa pili wa miaka mitano ambao tunamalizia, ni kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Ni vitu viwili; kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu lakini kujenga uchumi wa viwanda, ni zaidi ya kujenga viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dada yangu alikuwa anashangaa muhubiri wa zamani aliyekuwa anahimiza watu kutumia cherehani kumbe ni kujenga uchumi wa viwanda siyo kujenga kiwanda, ni kujenga utamaduni (the culture). Rafiki yangu marehemu Shah wa A to Z alianza na cherehani kimoja wakati anakufa alikuwa ana kiwanda cha A to Z na alikuwa mlipaji mkubwa wa kodi kwa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, picha kubwa ni ujenzi wa uchumi wa viwanda unaweza kuanza kidogo kidogo halafu unakua. Watanzania ndicho tunapaswa kufanya kwamba ujenge utamaduni wa kitu kusudi mwisho wa siku uweze kufika kule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhima mpya ni kujenga uchumi shindani (the competitive economy) kwamba katika mawanda yote tuwe na competitive economy. Nakubaliana na jina la kitabu, nakuja kwenye mapendekezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma mipango yote mitatu, huu mpango umeandikwa tulidhamiria kuchangamsha productive sectors (sekta za uzalishaji). Mpango tuliomaliza ilikuwa kutengeneza miundombinu wezeshi na miundombinu saidizi, tumeishaitengeneza, sasa ni kuchangamsha shughuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, imeandikwa ifikapo 2025 hatutaki uchumi wa kati, tunataka uchumi wa kati uliojumuishi. Ili uweze kupata uchumi wa kati uliojumuishi wale watu wanaohusika lazima uwajumuishe. Unawatoa wapi? Ni kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyie mnaoandika mpango mmesema hii ni rasimu lazima rasimu hii ije na miradi kielelezi (flagship projects) kwenye sekta zitakazotujumuisha. Tunaweza kuvumbua madini na kuyazindua, gesi, helium, mention whatever, tukawa na GDP na income per capita ya Dola 15,000 haina maana yoyote chenye maana ni uchumi jumuishi. Uchumi jumuishi ni kuwachukua Watanzania hawa katika shughuli zao wanazofanya ukazizindua kwa nguvu wakaweza kuzipeleka kwenye shughuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda mfano mmoja wa Singida, block farming, Singida wanachukua watu kwenye ekari 6,000 wanakwambia kulima hapa minimum eka 5 ukiweza eka 20 hauna caterpillar wanakuletea. Wanakuwezesha unalima halafu kwenye kuvuna ndipo wanakukata. Tunataka uwekezaji flagship project kwenye miradi hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona katika mipango ya Serikali wanazungumza vihenge, wanazungumza hifadhi. Hoja siyo kuwa na vihenge, tunachotaka kusikia ni uwezo wa taifa wa kuhifadhi bidhaa au chakula kwa kipindi gani. Tuambiwe kwamba tunaweza kuhifadhi mchele wa kulisha nchi hii miaka mitatu, miaka minne ikinyesha mvua likitoka jua hizo ndizo hesabu hoja siyo vihenge. Unaweza kuwa una kihenge ukaita watu 10 wakakila wakakimaliza siku moja. Kwa hiyo, tunataka malengo makubwa mtueleze kwa muda gani. Tunapokwenda kwenye hizi productive sectors kama alivyosema marehemu Ruge, Mungu amrehemu tunaanzia sokoni, mchele una soko wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napoipongeza Serikali kwa dhima iliyopita kuna jambo napaswa nilizungumze. Kuna jambo moja la kuangalia na niko tayari kukosolewa, tumeweza kukusanya mapato kwa sababu ya compliance, namna gani watu wali-comply siyo mjadala wa leo, tumepata trilioni 2, niliwahi kusema tunaweza kupata hata 3 hata 4. Compliance ilipatikanaje siyo mjadala tunapaswa tupate mapato makubwa kutokana na ukuaji lakini ukuaji haupo, sekta binafsi inapaswa ikue haikui. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, compliance ndiyo imetufikisha hapa, walifanywaje watu kulipa kodi mimi sijui, nisiingie kwenye mjadala huo lakini tunapaswa tukue. Hapa ndipo inapokuja hoja ya kujenga sekta binafsi ya Tanzania. Ili tuweze kufika yale malengo sekta binafsi ya Tanzania inapaswa ijengwe. Wasikudanganye popote duniani sekta binafsi hujengwa na haiendi kwa miaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka miwili unaweza kujenga sekta binafsi, mimi mwenyewe mikononi mwangu nimetengeneza mabilionea naweza nikawazungumza hapa na wengine kaka zao wako humu kwamba Mwijage ndiyo alimtengeneza kaka na msishangae hata Monduli Sajenti ndiyo hutengeneza Brigedia. Kwa hiyo, lazima tutengeneze sekta binafsi, tuwawezeshe. Watu wanachelea kwamba watapoteza pesa, usipochafuka utajifunzaje? Wape wapoteze pesa watoke. Kwa hiyo, kuna haja hiyo ya kuweza kujenga sekta binafsi ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niliseme hili tunapoingia kwenye Mpango wa Tatu maana yake ni nini? Dira ya Taifa 2025 inakwisha kesho. Kwa hiyo, kuna jukumu la kuhuisha Dira mpya ya Taifa na hapa tujiangalie, kanuni iliyotupa ushindi leo kesho inaweza isifae. Tunaweza kuwa tunajivuna na rasilimali ambazo kesho zitakuwa ni obsolete. Tunazungumza chuma ikaja dunia isiyohitaji chuma, unazungumza petrol yanakuja magari ya hydrogen na umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, lazima leo katika Mpango huu wa Miaka Mitano tutenge kipindi tuzungumze Dira mpya ya Taifa, tuhusishe watu wengi. Hii ni lazima muiweke kwenye mpango kwa sababu tunapanga kesho ijayo, the fourth industrial revolution inazungumza mambo yanatisha watu wanaanza kulima bila kutegemea udongo, watu wanaendesha viwanda vinavyotumia watu wachache lazima tujipange tunajua tunakwenda wapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napomalizia katika mpango wa mwaka mmoja Serikali wanasema watakwenda kumaliza matatizo ya ardhi Kagera kwa kutoa hekari 7,000 kwa JKT SUMA na hekari 22,000 kwa vijiji vya Misenyi. Kagera haigawanyiki, Kagera ni moja. Huwezi kumaliza tatizo la Misenyi bila kumaliza tatizo la Muleba, Karagwe na Bukoba Vijijini. Huu mpango kama unamaliza Misenyi afadhali uachwe, mnapoifuata Kagera muifuate Kagera nzima. Ukimaliza tatizo la Misenyi litahamia Bukoba utakuwa hujatatua tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachoweza kumaliza mgogoro wa ardhi Kagera siyo pesa ni ushirikishwaji wa wananchi. Sisi Wabunge ndiyo viongozi wa wananchi mtushirikishe, mnahitaji siku 15 mgogoro umekwisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono Mpango wa Tatu wa Miaka Mitano na Mpango wa Mwaka Mmoja tuendelee kuuchakata. (Makofi)
Azimio la Bunge la Kutambua na Kuenzi Mchango wa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa Utumishi wake Uliotukuka Pamoja na Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ya kuunga mkono maazimio mawili. Moja, la kumuenzi Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na la pili la kumpongeza Mheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, nichukue fursa hii kuwapa pole Watanzania wote kwa msiba uliotufika. Pia nichukue fursa hii kuwashukuru wote ambao walichukua jitihada za ziada kuwasiliana nami kunipa pole kwa kuondokewa na kiongozi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na kumuenzi, mtu mwema anapofariki na muungwana akaamua kumuenzi Marehemu, njia nzuri ya kumuenzi marehemu ni kutenda yale mema ambayo yeye alipendezwa nayo. Si mara moja au mara mbili; hasa Bunge lililopita nilimsikia, siyo mimi peke yangu Hayati Dkt. Magufuli akisema nawashukuru sana Wabunge kwa kuniunga mkono nikaweza kutekeleza yale niliyoyatekeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi Wabunge tuna deni. Kama alitushukuru kwa kumuunga mkono sasa tutekeleze kama tulivyotekeleza kwake kwa huyu ambaye amekuwa mrithi wake. Tumuunge mkono Rais mama Samia kama tulivyomuunga mkono Hayati Magufuli. Hili sizungumzi na Wabunge tu, nazungumza na watendaji wa Serikali, nazungumza na wananchi wote Tanzania nzima, Mkoa mzima wa Kagera bila kusahau jimbo langu kwamba yale tuliyotenda kwa miaka mitano dunia ikatushangaa basi kwa kumuenzi na tutende maradufu tunapokwenda kufika mwaka 2025. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, aliyeondoka ni rubani mkuu lakini rubani mkuu alipokuwa anga za juu katika mwendo wa mbali alikuwa na rubani mkuu msaidizi. Kumbe hawa wote tulikuwa nao safarini na sisi abiria tulishajua tunakwenda wapi, tulishajua dira. Mwenyezi Mungu akaamua rubani mkuu akaishiwa pumzi, bila mtikisiko rubani mkuu msaidizi bila kuyumba akaendesha chombo na wakati muafaka akatuambia kwamba rubani mkuu hatunaye lakini hatukutetereka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninapompongeza Mheshimiwa Rais, nampongeza kwa hilo. Watu waliyumba, watu walitetereka lakini rubani mkuu msaidizi akakaa kwenye usukani akaelekeza chombo kule kule. Tunakokwenda Watanzania tunakujua, tunakwenda katika ujenzi wa Taifa imara, siyo uchumi wa juu, Taifa imara, Taifa lililoendelea na uzuri wa bahati, mwenye bahati habahatishi. Kumbe dira ya Taifa mwaka 2010 aliyekaa kupanga mipango mitatu ya miaka mitano mitano ni Dkt. Phillip Isdor Mpango. Sasa yeye anakwenda kuwa rubani mkuu msaidizi chombo kinakwenda kwa kasi ile ile. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vizuri ukauliza watu wanakuonaje. Watu wanapanga matabaka, huu ni uchumi wa chini, huu ni uchumi wa juu; Dkt. Mwigulu Nchemba alisema Tanzania haikwenda kuomba ili iwe uchumi wa kati, haikuomba Tanzania, walikaa huko wakapanga. Ukitaka kujua demokrasia ya Tanzania ni tabaka gani, waulize Waganda, waulize Wakenya, watakwambia sisi ni demokrasia ya daraja la juu, la kati au lipi. Waheshimiwa Wabunge, kipekee niwaombe tunalo deni kubwa, wale nilioweza kuwaandikia niliwaandikia, Mheshimiwa Spika ni shahidi, tunachopaswa kufanya sisi Wabunge ambao ni viongozi wakubwa, wataalam wa mikakati wanasema ni ku- hold yaani tushikilie haya mafanikio.

Mheshimiwa Naibu Spika, yapo mambo katika kujenga maendeleo ya nchi hii kwa miaka mingi iliyopita tulikuwa tunajifunza au tunapambana, sasa yale mafanikio ambayo tumeyapata katika kipindi cha Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tuyahodhi. Tumefanya vizuri katika ujenzi wa shule, tuhodhi. Tunapaswa kuongeza ubora wa watoto mashuleni, tuhodhi twende mbele. Tumeweza kudhibiti ukwepaji wa kodi, tuhodhi. Tumeweza kufanya vizuri, tuhodhi na yote aliyoyasema Makamu wa Rais mtarajiwa, tuhodhi na yote haya yamefanyika kwa mafanikio na kwa ushirikiano wa wote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono na napongeza yote yaliyoletwa mbele yetu. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia hii bajeti ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora. Nianze kwa kuwashukuru watumishi, hawa watumishi wa Umma. Watumishi wa umma ndiyo wapishi wakuu, ndiyo wapishi wakuu wanaofanya mambo haya tunayoyaona. Mafanikio yote yanayosemwa sisi wanasiasa tunakuwa juu na bendera, lakini mpishi mkuu ni mtumishi wa umma. Nimewashukuru watumishi wa umma kama vile nilivyowashukuru wakulima na wafanyakazi waliotuwezesha kupata chakula cha kutosha kwa miaka mitano iliyopita.

Mheshimiwa Naibu Spika, utawala bora na utumishi ni sekta muhimu, ni sekta muhimu kama ambavyo zimeanishwa katika Mpango wa Tatu wa Dira ya Taifa na Lengo la Taifa la 2025. Katika Dira ya Taifa 2025 tunazungumzia utawala bora, lakini tunazungumzia amani, utulivu na mshikamano. Huwezi kuwa na utulivu na amani kama hauna utawala bora.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo wananchi wanapoona amani na mshikamano ina maana nchi hii ina utawala bora. Sitachukua muda kuzungumzia suala la utawala bora kwa sababu kila mtu anafaidi amani ya nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie utumishi, ninayo mapendekezo, mtumishi ukitaka kumpa motisha ili aweze kufanya kazi vizuri kuna mambo muhimu ya kuongelea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninayo mapendekezo, naiomba Wizara hii ibaini mahitaji ya watendaji ya watumishi tujue tunahitaji watumishi kiasi gani; sekta ya afya, watumishi kiasi gani; sekta ya elimu, kiasi gani; ugavi wa kila namna ili tukiwa tunajua watu tunaowahitaji basi tujue mapungufu yetu ni kiasi gani ili nchi hii tuweze kuwa na walimu wanaotakiwa, waganga wanaotakiwa ili wale waliopo waweze kupata motisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, shule yenye mahitaji ya walimu kumi ukitaka kuwa-demotivate waliopo wapange wawili. Ni kama timu ya mpira, timu ya mpira ya watu kumi na mmoja ukitaka kuwa-demotivate weka wacheza mpira saba hawatafanya kazi. Kwa hiyo, pamoja na miradi yetu ambayo lazima iendelee, mradi kielelezo mwingine ni kuajiri wafanyakazi wanaotakiwa kila sekta. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sekta za uzalishaji (the productive sectors) hatutaweza kuzalisha kwa tija kama hatutakuwa na wagani wanaotakiwa. Kumbe Wizara hii ndiyo inahusika na kutoa na kutoa vibali, Wizara hii ndiyo inachakata, inachakata, inachakata ule mchakato mzima wa kuajiri kwa maneno mengine ndiyo waajiri wenyewe. Kwa hiyo, katika sehemu nzuri tunayopaswa kuingalia ni hii ya watumishi na imeandikwa wala sio mjadala.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yoyote ili iendelee inahitaji watu. Unaweza kuwa na madini, unaweza kuwa maji na usiendelee, lakini ukiwa na watu mfano wa Japan, Japan hawana migodi lakini wameendelea kwa sababu wana watu. Ndiyo maana katika Dira ya Taifa ya 2025 lengo letu ni kuwa na watu walioelimika na wenye uchu wa kujifunza ambayo ni kazi ya ofisi hii ambayo tunajadili bajeti yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna mambo madogo ya kuangalia ni msingi, kuna suala ambalo naungana na TAMISEMI wanaposema kwamba watakapoajiri watakuwa wanawapanga watu kwenye mikoa ambako wataweza kutumika na hawataondoka mpaka baada ya miaka mitatu.

Mimi nashauri kwamba kila mkoa upangiwe quota yake; wafanyakazi wangapi waende kule na mtu akubali kuwa anakwenda Rukwa, anakwenda Kagera, anakwenda Dodoma, anakwenda Dar es Salaam na hatatoka si pungufu ya miaka mitano. Hii itatuondolea hii kadhia waliyoisema watu wanakwenda kuchukua check number.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pamoja na hilo nitoe angalizo kuna haja ya kujenga jamii, hapa nazungumzia ndoa changa, haja ya kujenga jamii si busara wanandoa wachanga wenye miaka miwili/mitatu mpaka kumi bwana kukaa Tabora na bibi akakaa Tanga, hii itakuja kutuletea kujenga jamii ya ajabu ajabu. Kwa hiyo pamoja na kupanga watalaam zingatia msiwape kadhia hawa wanandoa, otherwise tutakuja kuzaa watoto, unakuja mtoto unarudi nyumbani mtoto anakuita mjomba. Sasa ina maana nyumbani kila siku walikuwa wanakuja wajomba. (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la ustawi; ustawi wa nchi unapaswa kuwa na nguvu kazi…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwijage hebu subiri kidogo. Walikuwa wanakuja wajomba, kwa hiyo ni upande mmoja tu ambao unahusika au hebu weka vizuri hilo eneo kidogo. (Kicheko)

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, sijui kinyume cha mjomba ni nini? Napenda nikiri kwamba kwetu ni kilometa 1,600 kutoka Pwani kwa hiyo Kiswahili kilichelewa kufika. Mimi najua madhara ya wajomba. Naomba kwa ruhusa yako hilo swali linishinde, nizungumze…(Makofi/Kicheko)

NAIBU SPIKA: Aah, ngoja ngoja, ngoja inabidi tuweke vizuri, labda, lazima uwelewe Malkia wa Nguvu siku hizi tunatunza umalkia kwa wivu kabisa. Eeh ukituambia sisi ndiyo tunaoleta wajomba na ninyi mnaleta mashangazi kwa hiyo lazima sentensi ziwe zinanyooka vizuri. Mama pia anaweza akarudi nyumbani akaitwa shangazi. (Makofi)

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunifundisha msamiati, kumbe kinyume cha mjomba ni shangazi. Napenda ni kiri tena kwamba Kiswahili mimi kwangu ni tatizo, kwa hiyo hoja yangu iko palepale, kwa hawa watu wenye ndoa changa ni vizuri wakakaa pale na sasa hivi kwa hali tuliyonayo Tanzania tunao wataalam wa kutosha.

Nizungumze kuimarisha sekta ya umma, jambo ninalopendekeza kwa Serikali; watumishi wa umma wanapoanza kazi day one ni muhimu Serikali kuwajengea mazingira na kuwaaminisha kwamba leo ni watumishi wa umma, kesho watakuwa watamishi au wadau wa sekta nyingine. Unapokuwa wewe ni mtumishi wa umma, ujue kesho utakuwa kwenye sekta nyingine ambayo ni sekta binafsi ukiwa mwajiri au mwajiriwa; kwa hiyo mazingira yako sasa uweze kujiandaa kwa kwenda sekta nyingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, Lengo langu ni nini! Kama sekta ya umma itastawi watu waliopo nje sekta ya umma watajenga wivu wa kuingia katika sekta ya umma, lakini na wa sekta umma sasa watajenga wivu na wataitendea sawia sekta binafsi. Watumishi wa umma wasiojua kwamba siku nyingine watakuwa watumishi wa sekta binafsi huwaangalia kwa jicho baya watu ambao ni wa sekta binafsi. Kwa hiyo, ukiwa umekaa kwenye sekta ya umma ujue ipo siku na wewe utakwenda kwenye sekta binafsi ukiwa mwajiriwa au ukiwa mwajiri.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia sekta ya elimu, ambayo ni muhimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, nitumie fursa hii kuipongeza Serikali kwa kufanya uamuzi ulioondoa kero katika sekta ya elimu, kero zilizokuwa zinazuia wananchi au baadhi ya wananchi kupeleka watoto shule, hasa hili suala la karo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hizo pongezi, nizungumzie visiwa vya kwetu. Wilaya yangu ya Muleba inazo kilometa za mraba 7,000 ambazo ni maji na ndani yake ziko kata tano ambazo zina watu wanaishi na visiwa karibu 39.

Mheshimiwa Naibu Spika, wazo na pendekezo langu kwa Serikali, Kata za Ikuza na Mazinga wananchi wenyewe wanahangaika kujenga sekondari. Naiomba Serikali kupitia TAMISEMI, Mheshimiwa Ummy na Mheshimiwa Prof. Ndalichako, hawa wananchi wa Ikuza na Mazinga uwasaidie kwa jitihada zao wamalizie sekondari zao. Itatusaidia sisi kuona vifo vya watoto wanaoanguka na mitumbwi wakati wa hali mbaya ya ziwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, unapoondoa Ikuza na Mazinga unabaki na Goziba, Kerebe na Bumbile. Ninalo ombi, na niliwahi kulipeleka kwa Mheshimiwa Rais, Mungu amlazi mahali pema Peponi, najua Mheshimiwa mama Samia atachukua wazo hili alifanyie kazi. Wananchi wa Kerebe, Goziba na Bumbile wana sekondari yao moja iko Bumbile. Tunachoomba, pesa za sekondari ya Kata, mnazotaka kupeleka kwenye kila Kata msizipeleke Goziba, wala Kerebe, zote mzipeleke Bumbile. Mwende Bumbile mtujengee mabweni na madarasa ya ku-accommodate watoto karibu 1,000 ili watoto wa visiwa vyetu 39 wawe wanakaa bwenini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ni mhamasishaji mkubwa wa elimu, lakini huwa nashindwa kuhudhuria misiba watoto wanapozama kwenye mitumbwi. Ukienda pale, watu wanakuangalia wewe, wanakuona ndio mchawi, kwa sababu ndio ulishawishi mtoto aende shule. Sasa mimi siyo mchawi, mnisaidie kwa kujenga mabweni Bumbile na kujenga madarasa watoto wakae shuleni wasome. Watoto wanataka kwenda kusoma, lakini wanatoka kwenye visiwa vidogo vidogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikwambie, Ziwa Victoria kitaalam hubadili hali ya hewa baada ya dakika 25. Unaingia kwenye ziwa liko vizuri, baada ya dakika 25 limebadilika. Mwezi Februari, mimi mwenyewe na wataalam tisa wa Halmashauri tulisalimika kufa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI, umeniskia rafiki yangu, Mheshimiwa Mama Joyce Ndalichako umenisikia. Naomba Bumbile Sekondari sasa iitwe Prof. Joyce uweke shule ya bweni ya Serikali watoto waache kufa, nami nikaonekana mchawi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niende kwenye uboreshaji wa sekta ya elimu. Naunga mkono Serikali kuboresha suala la sheria za elimu, ule Muswada wa Sheria ya Elimu uletwe na kuboresha sera. Ninachotofautiana na ninyi, mnasema mlenge mahitaji ya sasa, ushauri wangu ni kwamba; na Waziri wa Fedha ananisikia; Dira ya Taifa inakwisha mwaka 2025, Dira ya Taifa inapaswa ihuishwe sasa. Dira ya Taifa ya 2025 ni outdated, tunapaswa kuangalia miaka 50 mbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, leteni Dira ya Taifa ya mbele na sheria za elimu, Sera ya Elimu itakayoundwa iwaandae Watanzania kupambana miaka 50 hadi 60 mbele. Mengine yote yako vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie maboresho yanayoweza kufanyika sasa, nakubaliana na Wizara kwamba wataboresha Shule za Ufundi, wakianzia na Ifunda na Iyunga. Wamezitaja shule tisa, hizo shule zilikuwa maarufu miaka ya sabini nikiwa sekondari.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimweleze Mheshimiwa Waziri ajaribu kukumbuka, Ifunda ilipokuwa maarufu tulikuwa na sekondari hazizidi 200 Tanzania. Hizo tisa zilipokuwa maarufu sekondari Tanzania nzima hazikuzidi 200, leo tuna sekondari zaidi ya 4500, kwa hiyo Shule za Ufundi zitengenezwe proportionally kwa uwiano, kuwe na shule za Ufundi proportionally uwiano wa 9:200 sasa 4,500 itakuwa ngapi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimshauri Mheshimiwa Waziri, wamelenga kuleta masomo ya ujuzi, wasiwachanganye watoto, wawafundishe mazingira, kilimo, biashara, ufundi, hapana. Tuige mfano wa zamani, ziwepo shule za mchepuo wa kilimo, mchepuo wa biashara, mchepuo wa ufundi, waliosoma SHYCOM wanajua. Mwanafunzi aliyesoma SHYCOM alikwenda kusoma Chuo Kikuu akirudi CPA anaipiga per seat. Mwanafunzi wa SHYCOM alikuwa na makali yake hata na Waziri wa Ujenzi wa sasa alisoma Chuo cha Ufundi, ndiyo ma-engineer ambao wanatisha sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuige mfano wa zamani, chenga ya zamani si mbaya ilimradi goli linafungwa. Kwa hiyo naishauri Serikali iende kwa mfano huo. Kwa mfano, shule za michezo, wachukue shule ya michezo, mtoto anayejua kucheza mpira na kukimbia wafundishe Hesabu, Kiingereza na Kiswahili basi, kinachobaki asubuhi na jioni anacheza mpira, Kiingereza na Hesabu. Kwa hiyo aende, aende, hiyo ndiyo specialization. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo haisuburi sera, haisubiri sheria ni kunisikiliza na Mheshimiwa Waziri akiniita, anapaswa kuwa na soda, nitamshauri na mambo yanakwenda. Hakuna haja ya kusubiri kubadilisha dira, ndiyo mkakati huo, watoto wanawachosha, wengine wanasema wasome mazingira, wasome na vitu vingi, watasoma mpaka wapi. Mheshimiwa Waziri apunguze ili watu wawe na umahiri (specialization) ili waweze kuelewa zaidi tuweze kwenda. Maisha ya binadamu ni miaka sabini, msiwafundishe kana kwamba wataishi miaka 900. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie VETA, mtaala wa VETA, VETA yetu inapaswa kureke…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Kengele imeshalia.

MHE. CHARLES J.P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie. Tubadilishe mtaala wa VETA ulenge sekta za kiuzalishaji, the productive sectors. VETA si ya kufundisha udereva, udereva wa magari madogo si kazi waende kwenye productive sectors; kutengeneza chakula, watengeneze maziwa, watu wanakula hawawezi kuacha kula, kwa hiyo VETA ibadilike. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia bajeti hii muhimu, neno muhimu linaweza kuonekana la kawaida, lakini hii ni muhimu kwa maana ni muhimu. Unapoona mtu unalala, unaamka unatembea, una amani na utilivu, una usalama ina maana kuna watu wanaumia kwa niaba yako. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mukhtadha huo nishukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa niaba ya Serikali ina maana Amiri Jeshi Mkuu, Mkuu wa Majeshi Makamanda na Wapiganaji wote, kazi yenu ni nzuri sana na Mwenyezi Mungu atawalipa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ulivyohitimisha wakati Mjumbe wa Kamati anamaliza kusoma taarifa, mimi naungana kabisa na mapendekezo yote ya Kamati hiyo ya Ulinzi ingawa mimi sio Mjumbe. Nimeisoma na nimewasikiliza nawaunga mkono. Sasa na mimi nichangie kwenye bajeti hii kwa kusisitiza mambo mahususi yanayohusu Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma yale malengo sita ya Wizara ndio utajua uzuri wa Wizara hii, nimechagua mawili katika sita. Moja ni kujenga uwezo katika tafiti mbalimbali na uhaulishaji wa teknolojia kwa matumizi ya kijeshi na kiraia, nachukua ile ya kiraia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ilivyosema Kamati kitengo chetu cha Nyumbu kilichoasisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kinafanya mambo makubwa, huyu naye ni ng’ombe wa maziwa sioni kwa nini Serikali tunasita kutoa pesa za kutosha kusudi Nyumbu aweze kufanya maajabu. Nimewahi kukaa nao mara nyingi na mimi nilikwenda Jeshini sio wiki mbili mwaka mzima na kwa wale wanajeshi mimi nilifundishwa na Kanali Mtono alikuwa ni commando failure yaani alikwenda kwenye kozi ya ukomando akashindwa, akaja kunifundisha mimi. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo jeshi nalijua kwa hiyo Nyumbu ukiangalia mfumo wa Nyumbu na vitu wanavyotengeneza katika hizi zama za uchumi wa viwanda kama hawa watu wakiwezeshwa, matatizo mengi yanayotusumbua yasingeweza kuwepo. Kamati imezungumza vizuri siwezi kuzungumza zaidi naiyomba na kuishauri Serikali yetu iweze kutekeleza mapendekezo ya Nyumbu.

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwijage, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Ester Bulaya.

T A A R I F A

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumpa taarifa Mheshimiwa Mwijage, babu yangu kwamba hata humu ndani kuna wanajeshi wa akiba mmojawapo ni mimi ambaye nilikuwa kikosi cha JKT Ruvu na akina Mheshimiwa Halima Mdee, kina Silinde, kina Lusinde na wengine nilikuwa nakupa hiyo taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwijage unaipokea taarifa hiyo?

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, amesema yeye ni mjukuu sasa babu usipokubali taarifa ya mjukuu usipochemshiwa maji itakuwaje.

Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo ni moja ya malengo sita ya Wizara kutengeneza jeshi la akiba ndio hilo jeshi la akiba. Kwa hiyo ninachozungumizia mimi hoja iko kwenye Nyumbu, tuna-under utilize uwezo wa Nyumbu nizungumze mimi Nyumba naiona mbali ya kuwa ile teknolojia waliyonayo nyumbu kinapaswa kiwe chuo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ijipange, Wizara ya Elimu, mjipange na Nyumbu mnaweza kuchukuwa wahandisi wetu kutoka kwenye vyuo baada ya kumaliza, badala ya kukuaa mtaani wanatembea na mabahasha wakaenda kuwa attached Nyumbu, wale watu wamakaniko watu wa IT wakafanya practice, watawapikia, watakula, watashiba, unapotoka pale unakuwa na competence iko Nyumbu yako mambo makubwa. Niwashauri Waheshimiwa Waziri wanaohusika na sekta hizo basi na waende wakajifunze Nyumbu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninapoiacha Nyumbu nizungumzie JKT na ninaizungumza kwa upole mkubwa, naishauri Wizara naishauri Serikali tuwe na mtazamo wa JKT, mtazamo ulio mpya. Tuwapeleke vijana wetu JKT awali na mwanzo, tuwaambie wanakwenda kufanya nini. Tanzania inahitaji bidhaa nyingi mojawapo ya bidhaa iliyoko JKT unayoweza kuiendesha JKT ni wana michezo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama kijana anaweza kukimbia, anaweza kupiga ngumi, anaweza kucheza mpira, mpeleke JKT kama nilivyoshauri mwanzoni akafundishwa hesabu na jiogorafia na Kiingereza acheze mpira asubuhi na jioni basi akisha fika kule siku za mwendo asiende JKT asiende JKT timu ya JKT ajiunge na kablu kubwa kama Simba aende Barcelona na Manchester. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo twende specifically tukiwatumia hawa watu tatizo wasiende JKT wakidhani wanataka kwenda Jeshi la Wananchi, hapana, aende kwa mfano mtu anakwenda kujifunza kilimo na nichukuwe fursa hii kuwapongeza Jeshi la Kujenga Taifa, nimeona mashamba yao ya irrigation kule Morogoro, ni mashamba yanaonesha yana tija kubwa. Basi hata tunapohangaikia kutafuta pesa JKT sehemu zake ziwe sehemu za vitengo vya biashara, sio kama hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna rafiki mmoja yuko JKT sitamtaja nilimwambia unapojenga kiwanda JKT usijenge kiwanda cha maji, ningependa kuona majeshi yetu yanawekeza kwenye viwanda vikubwa kama wangekwenda Mchuchuma na Liganga kama wanaweza waende, lakini Jeshi letu nisingependa kuona Jeshi la Wananchi eti wana kiwanda cha maji; kiwanda cha maji mtu yeyote anaweza kutengeneza. Basi vijana wako watakaokwenda jeshini watengeneza viwanda vya maji kusudi uwape jeshi libaki kwenye co-activities ambazo ni very sensitive.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini TAMISEMI niwaeleze tunazo pesa tunazowapa vijana kila mwezi kutokana na Halmashauri, unaweza kupeleke vijana kutoka kwenye Halmashauri wakaenda JKT, wakajifunza kazi mahususi, siku ya kuhitimu, siku ya graduation basi ile Halmashauri ilete vifaa ambavyo mfanyakazi huyo vijana atakwenda kutumia na impe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, yaani mtu anapata mafunzo mahususi anapotoka anakwenda moja kwa moja kazini kwa mfano, sifa ziwaendee tumewaona vijana wanafanya kazi nzuri ya ujenzi, sasa siku ya kumaliza miaka mitatu au sita huyo kijana apewe vifaa na si vifaa tu, apewe na hati kwamba yeye ni mkandarasi daraja la saba au daraja la kumi aende moja kwa moja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kwa sababu ndio wenye miradi kupitia Wizara mbalimbali Ujenzi, Afya tunaweza kuwapa makandarasi vijana ikiwepo sifa ya kwamba ulipitia JKT. Ndio maana ya lengo lenu moja kuwajengea uzalendo unatangaza tender unasema tutakupa wewe mkandarasi sifa mojawapo uwe wewe mwenye kampuni ulikwenda JKT, hapo uje uone vijana watakavyokwenda JKT wao kwa upenzi wao wakitegemewa kuandaliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee kuzungumzia suala moja muhimu; Mheshimiwa Waziri katika kambi ya Kaboya walikolala mashujaa waliopigana vita ya Uganda, kando yao kuna wananchi waliopisha eneo kwa ajili ya jeshi lile wanalalamika na kwa mila za kikwetu ukiwa una marehemu wanalalamika na majirani wanalalamika mambo hayawezi kutuendea vizuri. Nikuombe kabla hatujaenda kufagia makaburi Kaboya, wale wananchi ambao tulichukua ardhi yao kwa sababu nzuri za kiusalama tutafute pesa mimi na wewe tusaidiwe twende tukawafidie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wale waliolala kwenye makaburi wanalalamika acha wananchi wenyewe, waliolala kwenye makaburi wanalalamika kwa sababu wenye ardhi zile wanalia.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja, Mheshimiwa Kwandikwa, usinitupe twende tukafagie makaburi, lakini huwezi kufagia makaburi kama hujalipa fidia ya wale uliowahamisha. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa hii ya kuchangia sekta hii muhimu.

Mheshimiwa Spika, kabla sijaanza kuchangia rasmi, nitumie dakika moja kuliweka sawa jimbo langu. Kama inavyojulikana, mimi ninazo square kilometers 7,000 ambazo ni maji na nina Kata tatu za visiwani. Nitumie fursa hii kuwaomba wananchi wa Bumbile hasa Iyumbo, mtulie. Mamlaka ya TASAC imewazuia wananchi wetu wasipande mitumbwi kwenda kwenye Mwalo wa Kamugaza kwa sababu haujajengwa gati, mtulie. Nimemjulisha Waziri mwenye dhamana, nimemjulisha Mwenyekiti wa Sekta. Sijapata pesa za kujenga gati, lakini nitaomba hata kuuza mali zangu, nitajenga gati. Shida zangu na wananchi wangu nazijui mimi, mwenye shibe hamjui mwenye njaa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC ana shibe yake na wasaidizi wake wana shibe zao, mimi nafanya kazi na Waziri na ikishindikana nitakuja kwako Mheshimiwa Spika. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, naanzia ulikoishia juzi. Juzi wakati tunahitimisha Wizara ya Kilimo, ulitoa mahitimisho mazuri na haya yalitokana na michango mizuri ya Waheshimiwa Wabunge, lakini zaidi mzungumzaji wa mwisho, Mheshimiwa Balozi Dkt. Kakurwa. Katika mahitimisho tulikubaliana wote kwamba sasa hatuwezi kwenda na mwendo huu, ila tunapaswa kuchupa. Ukarejea, tulipofanya mageuzi makubwa katika sekta ya nishati na sekta ya miundombinu. Kwa ruhusa yako nami uniruhusu nianze hapo.

Mheshimiwa Spika, katika Dira yetu ya Taifa 2020 - 2025, tuna mipango mitatu ya miaka mitano. Mpango wa Kwanza dhima yake ilikuwa kuondoa vikwazo, tulipambana. Mpango wa Pili, dhima yake ilikuwa ujenzi wa uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Mpango wa Tatu ni kujenga uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya watu. Kumbe tulikuwa tunafanya nini? Dhima ya kwanza tulikuwa tunajenga msingi; dhima ya pili, tukanyanyua boma na dhima ya tatu ni finishing. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi Wabunge wa Bunge la Kumi na Mbili tunahusika kwenye finishing. Finishing ya kufanya nini? Kuipeleka nchi hii ifikapo 2025 watu wawe na kipato, waondokane na umasikini, wawe na income per capita ya dola 3,000. Ama wasifike, angalau wafike Dola 1,700 kama alivyosema Mheshimiwa Prof. Muhongo. Pia tuwe na uchumi imara na shindani.

Mheshimiwa Spika, nizungumze la muhimu, siyo hiyo income per capita ya 3,000 ila muhimu ni uchumi jumuishi. Sasa unapotaka kwenda uchumi jumuishi, ni sekta za kiuzalishaji ambazo ndizo zinaweza kukupeleka kwenye uchumi jumuishi. Unaweza kuzidiwa mafuta, dhahabu, ukawa na income per capita kubwa, lakini kuna watu wanakula vumbi barabarani. Kumbe ukiimarisha kilimo, mifugo na uvuvi, ndipo unaweza kwenda kwenye sekta ambayo italeta uchumi jumuishi kwa Watanzania wote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, siendi kwenye takwimu kwamba bajeti ni ndogo, hapana. Iwe kubwa ifanye nini? Nataka kuchupa. Bahati mbaya, tujifunze kwa wadogo zetu, lakini siyo bahati mbaya wadogo zetu ni rafiki zetu. Tujifunze Uganda, tujifunze Rwanda. Katika nchi zinazofanya vizuri kwenye mifugo Afrika, ni Mali, Ethiopia, South Africa na Uganda.

Mheshimiwa Spika, Uganda wanauza maziwa na bidhaa za maziwa nje na wanapata Dola milioni 100 kwa mwaka. Tanzania hatupati hata senti 50. Ukiuliza kwa nini? Wanasema ni sera. Kumbe siyo bajeti, kinachotangulia ni sera.

Mheshimiwa Spika, nikishamirisha ule mkakati wako wa kuchupa, tunapaswa tuanze kwa kubadilisha mindset ya ufugaji wetu, tutoke kwenye uchungaji twende kwenye ufugaji. Kwa hiyo, sera ninayoitaka ni sera ya kuwachukua hawa watu; kwa sababu nawasikia watu wanavyochangia. Watanzania na Wabunge walio wengi, hawataki uchumi wa kuwapeleka wachache juu na kuwaacha wengine. Mimi nakuwa makini ninapokuwa nachangia na ndugu yangu Mheshimiwa Balozi Dkt. Bashiru. Yaani ukileta sera ya kuwaacha walio wengi, unaona anaumia kweli. Kwa hiyo, sera inayotakiwa ni ya kuwachukuwa walio wengi.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia, dairy industry ya Uganda, imechangiwa na wananchi walio wachache, lakini Serikali ya Uganda ilikopa pesa nyingi na kulikamata lile eneo lililofanya vizuri na kuwekeza pesa pale. Ndiyo ikafanyika local farming, ikafanya vizuri.

Mheshimiwa Spika, Uganda wanachakata maziwa lita milioni 2.8. Nilipokwenda Uganda ku-understudy, ile nafika walijua najua nakuja ku-understudy. Wakanieleza mambo yote, lakini wakasema Tanzania mna uwezo wa kuzalisha na kuchakata lita milioni nne. Nikasema mnajuaje? Wakasema habari zenu tunazijua. Mnaposema Tanzania nasi tunazalisha lita milioni 2.8, hoja siyo kuzalisha, hoja ni kuzichakata ili zifike kwa mteja. Unaposema unajenga uchumi wa Taifa, ujenzi wa uchumi wa Taifa ambao ni shindani, lazima uwe na kiburi cha kuuza. Hatuuzi nje. Tuna hali mbaya kwenye maziwa. Sasa tunachopaswa kufanya ni kukamata watu kuwafundisha njia mpya za kufuga kama walivyofanya Uganda.

Mheshimiwa Spika, watu wamezuiwa mambo ya kuhamahama; ndama anazaliwa Muleba, akija kuchinjwa ameshafika Lindi. Huyo ng’ombe ukimchinja, wastani wa kilo ni 100. Leo hii katika jimbo la Mheshimiwa Bashungwa kuna ndama wa miezi 18, ukimchinja unapata kilo 600. Waziri ulimwona, Katibu Mkuu wako alimwona na Wabunge niliokuwa nao; na Mheshimiwa Balozi Dkt. Bashiru alimwona na akaweka sahihi nikaiona sahihi yake. Tunapaswa kuipeleka sekta hiyo, ndipo tutakapoweza kuchukua walio wengi na kwenda kwenye level hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie NARCO. Waziri ameizungumza vizuri kwamba asilimia 20 ya NARCO ndiyo ranchi ambazo wanazimudu na kuweka ng’ombe hao. Katika kuchupa, nitoe ushauri kwa NARCO; ubaki na eneo la asilimia 20 uache kupangisha. Haya maeneo unayopangisha uwaachie Halmashauri na Waziri wa Ardhi wawapangie wananchi. Nitapendekeza tuje na kitu kinaitwa Livestock Development Authority ambayo itakuwa na idara ya maziwa na idara ya nyama, kusudi ninyi sasa muwe mna-regulate na kuwaambia watu pasture ziko vizuri, pasture zinakwenda namna hiyo ili tuweze kuhakikisha kwamba sekta ya mifugo na sekta ya uvuvi zinachangia pato la Taifa zikiwa za kwanza.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kaguta Museveni aliniambia, kufika 2022 kama sekta ya maziwa haitakuwa namba moja Uganda, Waziri anapoteza kazi. Leo maziwa ni sekta ya pili baada ya kahawa ukiondoa dhahabu, katika kuchangia uchumi wa Uganda. Waziri wa Mifugo (ni mjomba wangu) aliniambia kwamba 2022 maziwa yatakuwa yanaongoza. Sasa na sisi Taifa tujiwekee mpango kwamba samaki tuta-export kiasi gani? Maziwa kiasi gani? Sisi aibu tumezizoea, hata kwenye samaki; nusu ya Ziwa Victoria ni la Tanzania lakini Uganda wanatuzidi kwa ku-export samaki. Yaani unapata aibu, unakuwa mjinga mpaka unazoea ujinga. Sasa tuchupe. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakimbilia kwenye maamuzi yako kwamba tuchupe, hii hali tuliyomo siyo ya kwetu. Sina shida na bajeti, uwasilishaji mzuri, lakini hii tunaitumia kama maandalizi ya kuweza ku-take off na kuchupa kwenda kwenye anga tunazostahili zenye kipato kikubwa cha watu walioshikamana wenye utulivu, amani na utawala bora tulionao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Nishati
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia bajeti hii ya Wizara ya Nishati na kabla sijaanza kuchangia nipende kutoa taarifa kwa Mheshimiwa Waziri kwamba nimepata simu kutoka kwa Engineer Maro na Engineer Said wa TANESCO na Engineer Fumbuka nashukuru sana wamefika kwetu wanasema Wilaya ya Muleba watashughulikia vijiji 22 lakini nikasema mzee wa Mbongoshi mbona niliomba 28?

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nashukuru kwa 22 na endelea kuomba kwa vile vinane lakini katika vile vijiji vilivyobaki kuna Kijiji kimoja kina utata, Kijiji cha Bugasha, kilichopo kando kando ya jeshi la Kaboya ambacho kinapiganiwa na watumiaji wetu mzee angaliaangalia uwape kipaumbele vijana wale wana kazi kubwa.

Mheshimiwa Spika, nianze kuchangia, ni mdau wa mafuta ni mtoto wa sekta hii na leo nitachangia nishati upande wa mafuta tu. Najua unajua, niliingia kwenye sekta hii mwaka 1984 nikiwa kijana navaa kaki na malapulapu na radio call nikifungua valve la kupima matenki mapenzi ya Mungu nikapanda mpaka nikawa Naibu Waziri Nishati. yaani kutoka kufungua valve mpaka kuwa Naibu Waziri unaweza kuona mambo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mafuta ni jambo muhimu na katika ukusanyaji wa mapato sekta ya mafuta inasaidia Serikali kukusanya mapato kwa kutumia jasho kidogo. Yaani TRA wanakuta pesa zinakuja mezani kwa kutumia sekta ya mafuta, tunatumia lita karibu bilioni 3.14 kwa mwaka, na kwa petrol Serikali inakusanya shilingi 792, diesel shilingi 668 kwa kila lita na mafuta ya taa shilingi 615. Mafanikio ya umeme tumepata mafanikio mazuri makubwa sana katika kusambaza umeme yametokana na sekta ya mafuta.

Mheshimiwa Spika, unakumbuka ukiwa umekaa kiti hicho ukiwa Naibu Spika na mimi nikiwa mjumbe wa kamati nikiwa pale nimeshika microphone tuliweza kutenga pesa zilizoweza kusababisha REA isambaze umeme kiasi hiki. Lakini hata kasi hii tunayoiyona ya RUWASA kusambaza maji kama anavyosema Waziri wa Maji kwamba unapomuona Kobe juu ya mti ujue amepandishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sekta ya maji imepandishwa na sekta ya mafuta kwa sababu ile pesa ring fenced ya mafuta ndio inasababisha kasi hii tunayoiona. Hata sekta nyingine iwe reli, iwe nini wana pesa wanapata kutokana na mafuta. Mheshimiwa imebidi niyaseme hayo ninapokumbuka miaka 37 ya utumishi katika sekta ya mafuta. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie bomba la mafuta niwapongeze marais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Jeneral Kaguta Museveni wa Uganda kwa kufanikisha mchakato wa bomba la mafuta kufika hapa.

Mheshimiwa Spika, kwangu katika bomba la mafuta la zaidi la mno ni kwamba kuwa na mkuza wa bomba la mafuta unasaidia kuamasisha utafutaji wa mafuta kitaalam sisi tunayo mafuta katika bonde la kutoka Albert kushuka mpaka Tanganyika na Rukwa Eyasi Wembele kuja mpaka kwetu huku. Lakini zile wanaziita stranded reserve lakini zile wanaziita stranded reserve yani ni reserve ziko uwezi kuzifikia kwa sababu hakuna miundo kuwepo kwa bomba ili kutatusaidia, ndio faida kubwa ninayoiona ninachoomba kazi kubwa iendelee.

Mheshimiwa Spika, lakini Mheshimiwa wakati napongeza hiyo nipende kuiomba Serikali na hii naiomba Serikali kwa ujumla wake sio Waziri Tanzania tumekuwa na mapungufu katika kutafuta mafuta kumbukumbu zangu haziko sawa sikumbuki kama kutoka mwaka 2011 kuna leseni ilitolewa ya kutafuta mafuta.

Mheshimiwa Spika, huwezi kupata mafuta bila kutafuta lazima kutafuta na kutafuta kuna gharama nimesoma taarifa ya Kamati nimesoma hii hotuba ya Mheshimiwa Waziri atujafanya lolote hizi pesa zilizotengwa katika kutafuta Eyasi, Embele sijui Mnazibay si chochote si lolote kucholonga kisima unahitaji bilioni 100 hizi pesa zilizotengwa si lolote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kazi ya TPDC kubwa ilikuwa kuhamashisha promotion, u-promote kusudi wadau waje wachimbe ukitaka uchimbe wewe kama Taifa utamaliza miaka minne miaka 100 sisi tunataka kuishi leo tuchimbe mafuta leo tuweze kuyapata.

Mheshimiwa Spika, inasikitisha hatujatafuta mafuta kwa zaidi ya miaka 10 hukuna kilichofanyika, hata hii mafanikio ya Embele nimesoma kwenye taarifa Embele hakuna kitu kimefanyika. Tuamue kama Taifa na ninajua utata ulipo nani atachimba atapata nini ni kanuni ya dunia uwezi kuibadilisha ama uende PSA au uwe na pesa umtafute mkandarasi au utumie concession kama unadhani utaliwa wewe tafuta pesa zako utumie contract uchimbe yakikosa inakula kwako.

Mheshimiwa Spika, kisima kimoja bilioni 100 vichimbe 10 vikose tirioni 1 utawaaambia nini watu hapa kwa hiyo ama utumie PSA kama anavyosema mzee mmoja ukitaka kula na wewe uliwe kidogo PSA mgawane mwende mbele. Au uende kwenye concession kusudi mwende ule mlabaa haina ujanja lakini bottom tunataka mafuta leo tuchimbe na huwezi kupata bila kuchimba. Nimeangalia Uganda kutoka mwaka 2002 mpaka sasa wamechimba visima 100 hivi vya Eliyasi, Embele vitatu tena vifupi hatutafika popote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, bomba la kwenda Uganda litapeleka gesi ya kupikia au natural gas Uganda. Na kuna agenda ya kupeleka gesi Kenya, ni muhafidhina katika hilo, na niliwahi kuwa katika kiti cha maamuzi nikiwa Gasco; nilikuwa nakataa gesi kwenda Kenya. Tutapeleka gesi Kenya atatengeneza mbolea tatuuzia mbolea. Yanakuwa yale yale ya parachichi, yanakuwa yaleyale ya mahindi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuchimbe gesi Mtwara, kina kifupi; tuchimbe Lindi; tuchimbe nyumbani Mkuranga, kuna gesi, tutengeneze kiwanda cha mbolea. Kiwanda cha mbolea kina makandokando; haiwezekani tukatafuta makandokando kuyaondoa kwa miaka yote. Tukubaliane leo kiwanda cha mbolea kianze kwa sababu tunahitaji mbolea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie usalama wa mafuta, na amelizungumza mwenzangu, Mheshimiwa Mansoor, na wewe ulilizungumza wakati tunahitimisha ile bajeti ya Mazingira. Tatizo liko wapi?

Mheshimiwa Spika, tunayo sekta ya bodaboda, na wale wanahitaji mafuta kwa sababu mafuta ni upatikanaji wake, waipoyapata watayatafuta vyovyote. Namna ya kufanya – na kweli EWURA mjiangalie – zamani tulikuwa na vituo vya aina tatu; fuel service station, fuel station na cab site. Wale wakongwe wenye faida ya umri kama mimi, ulikuwa ukienda kununua mafuta utayaona yanapanda kwenye chupa wanasonga hivi halafu yanakwisha.

Mheshimiwa Spika, tuanzishe vituo hivyo vidogo ambavyo vinaweza kuwa vijijini, vijana wanatunza lita 100, 200, 300 salama. Yataangalia ubora wa mafuta, usalama wa mafuta na uwezo wa kupatikana kwa karibu walipo watu. Hatuwezi kuepuka biashara ya bodaboda, tunazihita pikipiki leo kuliko siku nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, EWURA – na mnaweza kuja, nitawaelekeza bure – lazima muende kwenye cab site muweze kupunguza gharama ndiyo tutaweza kusambaza vituo mpaka vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie uagizaji wa mafuta. Nimesoma taarifa; yako maendeleo yameonekana. Lakini katika mafuta ninachotafuta ni nafasi ya mafuta kuchangamsha uchumi wa nchi hii. Sisi location advantage ya Tanzania ambayo nasema location advantage siyo faida, faida ni kutumia hiyo location advantage.

Mheshimiwa Spika, sisi tuko kwenye nafasi nzuri ya kuweza kuwauzia wenzetu. Pamoja na taarifa ya Waziri kwamba tumepunguza premium kwenda wastani wa 36 lakini tujipime na Kenya; Tanzania tunaposema premium ya 22, 25, 58, Kenya wanasema 4, 5, 6. Kwa nini premium Kenya zinakuwa nafuu premium Tanzania zinakuja juu?

Mheshimiwa Spika, lakini jiulize; kwa nini unapowaita watu walete bid kuja ku-supply mafuta wanakuja wawili kila siku? Ukimuita ni yuleyule, Magesa na Mwijage, kila siku haohao; kwa nini hawaji kumi? Lazima tujipime tuangalie katika mfumo mzima, kuna nini hapa? Ndiyo maana tunapata mafuta yenye gharama kubwa kiasi kwamba hatuwezi kupata competitive advantage. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia Bajeti Kuu, Bajeti ya Serikali. Awali ya yote naunga mkono bajeti hii, mimi naiita bajeti ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono maoni na Mapendekezo ya Kamati ya Bunge inayoshughulikia bajeti, lakini nijitendee haki naunga mkono mchango wa Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kachwamba alipozungumzia Idara ya Mipango. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi katika mchango wangu nitazungumzia zaidi namna ya kupata mapato. Najua waswahili wanasema kulea mimba siyo kazi, kazi ni kulea mwana, tumehangaika tupo hapa miezi yote hii tangia mwezi wa kumi, vijijini huko tunatengeneza bajeti mtoto huyu Mwigulu Nchemba ameshamtoa sasa tutengeneze mapato, mimi najikita kwenye mapato.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika bajeti yetu tumeongeza shilingi mia.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwijage kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Esther Matiko.

T A A R I F A

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nataka kumpa taarifa ndogo tu kwamba kulea mimba ni kazi sana na kuna kipindi hata wamama tunapata bed rest kwa miezi tisa yote ukilea mimba. Kwa hiyo kulea mimba ni kazi na kulea mwana pia ni kazi vyote kwa pamoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwijage, nadhani hiyo inamaanisha misemo mingi ya Kiswahili itabidi ibadilishwe, maana wanawake tuko kazini safari hii. Tunataka kurekebisha mambo yote ambayo kwake yeye hayajakaa sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Charles Mwijage.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, naikubali sana taarifa hiyo. Kazi ya mwenzio ambayo hujawahi kuifanya usiizungumzie. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, niizungumzie ongezeko la shilingi 100 kwenye mafuta. Ongezeko la shilingi 100 kwenye mafuta, ile tozo si hoja, hoja ni mzigo mzito sasa utakaokuwa unabebwa na kila lita ya mafuta. Kwa ongezeko la shilingi 100 petroli sasa itatozwa shilingi 892, dizeli shilingi 768 na mafuta ya taa shilingi 765. Si hoja na hiyo, hoja ni kuwa sasa mafuta haya kwa kiasi kinachotozwa italeta ushawishi na kivutio cha watu kukwepa kodi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiweza kutoa depot malori 27 ya mafuta utaweza kukwepa shilingi bilioni moja. Kwa viwango vya Mheshimiwa Ummy Mwalimu, hizo ni sekondari mbili kabisa kabisa za Kata.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ninachotaka kuzungumza, katika kuboresha mapato lazima Serikali tujiandae na tujiimarishe katika kuimarisha vitengo vyetu vya upimaji, sina wasiwasi na ways and measure, lakini lazima tujiimarishe. Tujiimarishe na kitengo kinachopewa kazi ya kuangalia kwamba mafuta hayatoki kundi moja kwenda kundi lingine pale tunapozungumzia suala la vinasaba. Lakini tunalo tatizo la miundombinu ya cha wote. Kuna miundombinu muhimu ya mafuta ambayo hakuna yeyote anayewajibika nayo, ambapo mafuta yanapotea na huwezi kumuwajibisha yeyote. Serikali inapaswa kudhibiti maeneo hayo na kumuwajibisha mmojawapo. Lazima ichukuliwa taasisi moja ya Serikali ipewe jukumu la kulinda miundombinu hiyo ambako ndipo mafuta mengi yanaweza kuwa yanapotelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jumla ya yote, nimshauri Mheshimiwa Waziri kwamba kitengo cha TRA kiimarishwe upya kwa kuongezewa watu na kupewa mafunzo ya kudhibiti sekta hii. Kwa sababu utakuja kuona kwamba, katika kuuza lita bilioni 3.14 kwa mwaka kwa kiwango cha wastani wa shilingi 700 kwa lita ni fedha nyingi tutakuwa tunazikusanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pamoja na hiyo, mimi napenda niishauri Serikali, hayo ni mafuta yatakayouzwa ndani, tunapaswa kufanya utaratibu wa kuchochea mafuta mengi yauzwe. Na hapa nazungumzia mafuta ambayo yakiuzwa humu ndani hayatatubebesha mzigo. Kwa sababu kumbuka mafuta haya unayoyatoza tozo utawajibika kutafuta dola kusudi uyanunue; lakini kuna mafuta unaweza kuyatoza pasipo kutafuta dola kusudi kuyanunua. Haya ni mafuta yanayowezesha mizigo kupita Tanzania kwenda nchi za Jirani (transits).

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu, ya sheria zetu na uendeshaji wa shughuli tumekuwa tuki-discourage transit cargo, na ndiyo maana mizigo inakwenda Durban, Beira pamoja na Mombasa. Sasa tunapaswa kuangalia udhibiti na usimamiaji wa mizigo yetu ili mingi ipite kusudi tuweze kupata mafuta ambayo tutayatoza tozo kwa ili tuweze kuongeza pato letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hiyo niishauri Serikali, kwamba muangalie sasa, wakati umefika wa kuweza kuitumia Dar es Salaam kuwa trading hub. Yaani mafuta yawe traded Dar es Salaam yaweze kuuzwa nje. Lita bilioni
2.5 zinapita Dar es Salaam zikiwa transit kwenda land locked countries. Sasa tukigeuza re-export Tanzania ikiwa trading hub ina maana takriban asilimia 30 zinaweza kuwa zinauzwa kutokea hapa, na kila yanapouzwa, unapata mark-up na ile mark-up inaweza kuchangia kwenye mapato ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie suala la uchumi wa nchi. Nimeona mapendekezo katika sekta ulivyopendekeza. Niombe sasa, kwa kila sekta tuanze kuweka vigezo KPI, kwamba kila sekta inaleta nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tunauza nje ya nchi kwenye re-export, tunauza mazao yenye thamani ya dola bilioni 2.9. Katika hiyo theluthi mbili ni dhahabu, lakini ukiangalia potential ya export ni trilioni 2.36 bila kuweka dhahabu. Sasa tunapaswa kuwekeza katika maeneo hayo kusudi tuuze zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilisema hapa kwamba katika fursa ya nyama Tanzania hatu-export chochote ilhali wenzetu Uganda na Botswana wanauza dola milioni 100, dola 135 mtawalia, Uganda anauza maziwa dola milioni 100 kwa mwaka, sisi hatupo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna fursa ya ma- avocado ambayo yanapendwa dunia nzima, na soko la avocado linaendelea kuongezeka duniani. Hata hivyo Tanzania pamoja kuwa na nafasi ya tatu katika Afrika bado kiasi tunachosukuma kwenye soko hili soko kubwa halijaonekana.

Mheshimiwa Naibu Spika, imekuja fursa ya soya beans. Ukihesabu tani milioni 42 tunazopewa na China kuuza kule ni revenue kubwa sana kuliko mazao yote tunayo-export. Sasa, Wizara isaidie sekta hizo kusudi tuweze kutengeneza kipato kikubwa na kuweza ku-supply kwenye iInternational markets. Hiyo ni sekta ya re-export. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niende kwenye mchango wa Mheshimiwa Waziri alipozungumzia matumizi ya LUKU katika kuweza kukusanya Property Tax. Nakubaliana na wazo hilo kwa kuwa lina ubunifu ndani yake, hata hivyo kuna angalizo. kuna mtu ana nyumba ya ghorofa vyumba viwili juu kimoja chini analipa shilingi 5,000. Je, yule mwenye vyumba vitano chini kwa nini umlipishe shilingi 1,000?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna mtu ana vyumba saba, ana wapangaji watatu kila mpangaji ana mita yake atalipa shilingi 3,000. Sasa kwa nini huyu unamlipisha shilingi 3,000 badala ya shilingi 1,000 na ni vyumba 31 vile vile? Lakini kuna mtu ni mstaafu, kama alivyosema Mwenyekiti wa Kamati, kwanini huyo unampa adhabu hiyo? Suala la msingi kuna watu wako tayari kulipa hawajapewa umeme. Kwa hiyo napendekeza Serikali iongeze fedha kwenye REA kusudi wale wanaotaka umeme wapewe umeme. Vilevile Serikali iwekeze katika huo mfumo wa LUKU; na nashauri ikiwezekana tusubiri. Huu utaratibu usije ukashindwa kama ule wa TRA ulivyoshindwa au wa local government ulivyoshindwa katika kuweza kukusanya mapato haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Azimio la Bunge la kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia hoja iliyopo Mezani. Awali ya yote na mimi naunga mkono Azimio la Kuridhia huu Mkataba, kazi ambayo na mimi nimeshiriki sana katika kufikisha maamuzi ya Wakuu wa nchi za Afrika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianzie kwa madhumuni (objectives) ya makubaliano haya. Lengo kubwa ni kutengeneza soko kubwa la Afrika. Wataalam wanasema kufika mwaka 2050 nchi zitakazokuwa na watu wengi ni China, India na African Continent. Kwa hiyo soko ni wingi wa watu.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo tunao watu bilioni moja na milioni mia mbili, kama walivyosema Waheshimiwa Wabunge, lakini kwa takwimu za mwaka 2017 Afrika inaagiza nje chakula chenye thamani ya dola bilioni thelathini na tano. Lakini kufika mwaka 2025 keshokutwa tu, Afrika itakuwa inaagiza nje ya Afrika chakula chenye thamani ya dola bilioni 110, yaani pesa zenye thamani kuliko GDP ya nchi hii leo na itakapofika mwaka 2025. Kwa hiyo, kwa vigezo hivyo sisi hatuna kisingizo chochote, lazima tujiunge na soko kubwa na soko la Afrika.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia misingi (principles) katika Article No. 5 ya hii Africa Continental Free Trade kuna suala la nipe nikupe (reciprocity). Kipengele namba 9, watu watakaokuwa wameelewana watauziana wao. Ni kama leo tunahangaika na mahindi lakini ukienda upande wa Nakonde, upande wa Malawi, malori yamejazana Malawi yanasafirisha mahindi kwenda Southern Sudan, sisi hapa tunatafuta soko tunakosa. Kumbe sasa tutakapokuwa sisi hatukujiunga – na ninawaomba tujiunge, hakuna sababu ya kuogopa nitaielezea, tujiunge ili wale watakaokubaliana wasije wakatengeneza kundi la waliokubaliana na sisi Tanzania tukabaki tunalia. Kama nilivyoeleze population inakuja Afrika, sasa unajitoa Afrika uwe mgeni wa nani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nataka kulizungumza ni kwamba hatuna sababu ya kuogopa. Tumejipanga kwa kipindi kirefu na hususan kwa kipindi cha miaka 15. Mpango wa kwanza wa miaka mitano tuliondoa vikwazo na ndiyo ikaja kuzaa blueprint katika mpango wa pili wa miaka mitano.

Mheshimiwa Naibu Spika, imeelezwa wazi mambo ya vikwazo, sasa vikwazo tunavijua, viondoke. Ninataka nirudie tena, Tanzania haina ukosevu wa wajasiriamali. Tanzania haina shida ya sekta binafsi, sekta binafsi ya Tanzania imefungwa minyororo, ina vikwazo vya kutosha. Kwa hiyo, ni suala la kuwaondolea vikwazo kama ilivyoandikwa kwenye Blueprint Regulatory Reform.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda niseme Blueprint Regulatory Reform ni mkakati wa kujitokeza (emergent strategy), ni kwamba watu walibishana wakabishana vikwazo vipo au havipo, wataalam wakakaa chini wakaweza kuonesha vikwazo ambavyo wote tunavikiri kama alivyosema Mbunge wa Biharamulo, kwamba unaona vikwazo hivi. Yaani mtu anakupa faini kwamba nipe lita kumi za damu, nitazitoa wapi lita kumi za damu halafu niendelee kuishi?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukisikiliza maelekezo ya Wabunge katika Bunge Bajeti la lililopita, Wabunge msiwe na wasiwasi kwamba tutashindwa kushindana. Kama maelezo ya Mheshimiwa Spika ya kufanya mageuzi makubwa katika sekta za kiuzalishaji yatazingatiwa tutakwenda kwenye soko la Afrika tukiwa kifua mbele. Transformation ya productive sectors tunaiweza, hakuna jambo geni. Hatutaki kurudia, hatutaki kubaki kwenye idadi ya ng’ombe wengi, hapana, tunataka kuwa na ng’ombe wengi watakaoweza kutoa maziwa mengi na nyama nyingi na ngozi ya kutengeneza viatu vizuri vya moccasins. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo Watanzania msiwe na wasiwasi. Lakini mjadala wa sekta ya elimu wa kutengeneza elimu inayotufaa, siyo tuitakayo, ni mjadala unaopaswa kwenda haraka sana kama alivyozungumza Mbunge wa Viti Maalum kutoka huko Mbinga, lazima tuwe na watu wabunifu na wanaoweza kuchezea teknolojia. Lazima watoto wetu, siyo kwamba waende darasani, waende darasani wapate maarifa na weledi kwa sababu sasa wanakwenda kushindana katika nchi inayoitwa Afrika.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatutengenezi watu wa kushindana Mbeya, Songea na Kagera, tunaandaa vijana wetu tutakuwa tukipigiwa simu sisi tukiwa wazee nyumbani, mtoto anakupigia simu akiwa Ivory Coast, anatoka hapo anakwenda Cairo.

Mheshimiwa Naibu Spika, na hili la Continental Africa linakuja. Juzi Misri wameamua wata-pioneer wao kujenga reli kutoka Cairo kwenda mpaka Durban, itapita Dodoma na Mbeya. Hiyo ndiyo Afrika inayokuja, ukiwa na wasiwasi utaachwa unazubaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja, naunga mkono Azimio hili. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia mada iliyopo mbele yetu. Awali ya yote, nimshukuru Mwenyezi Mungu, lakini niipongeze Mamlaka, niipongeze Serikali kwa jinsi tulivyoweza kupita kwenye rejea mwaka mzima, wakati nchi nyingine zina uchumi hasi, sisi tumekuwa na uchumi chanya. Watu wanakula, kazi zinafanyika, hili ni jambo kubwa sana, inatosha kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nizungumzie kuchangia kwenye kuboresha vipaumbele vya Mpango na nini tufanye. Jambo moja tunapaswa kufahamu, huu ni Mpango wa Mwaka wa Pili katika miaka mitano ya Mpango wa Tatu wa miaka mitano mitano. Tatizo la miaka mitano hii, ndiyo miaka mitano inayokwenda kutupeleka kwenye kilele cha Dira ya Taifa. Sasa tatizo tulilonalo, yaani ndiyo tunafika fainali hivyo, tunafika fainali ambako tunategemea kuwa tumeondoa umaskini, ile biashara ya income ya per capita ya Dolla 3,000, lakini tunafika finali katika linge lengo la kujenga uchumi imara wa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa unapozungumza kuondoa umaskini ina maana unalenga uchumi jumuishi, wengine wanaita uchumi shirikishi, hapo mimi Kiswahili kinapingana. Uchumi jumuishi, yaani tunataka tufike kwenye uchumi wa kati, Watanzania wote tusiwe tumeachana sana, siyo kushiriki. Unaweza kwenda kwenye harusi ukamwona bibi harusi kule umeshiriki, lakini kujumuika ni kumtunza na kuhangaika naye yule bibi harusi, hapo umejumuishwa. Sasa kuwajumuisha Watanzania wote, lazima Watanzania wote washirikishwe, wajumuike wapate huo uchumi, ndipo inapokuja tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia dhima ya Mpango wa Pili wa Miaka Mitano ulilenga kwenye miundombinu wezeshi na miundombinu saidizi. Ndiyo hii sasa Mheshimiwa Waziri ameibeba tena ikawa vipaumbele vya Mpango wa Tatu. Vipaumbele vya Mpango wa Tatu vilipaswa kulenga zaidi shughuli za kiuzalisha (the productive sectors) hajazizungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri alipotoka, huko nyuma sawa kwa sababu miradi haikukamilika, sawa aje nayo, lakini sasa anapofika hapa kuna wenye shughuli, tunajenga reli, reli inapaswa isafirishe bidhaa, isafirishe maziwa, yapo wapo? Inapaswa isafirishe matunda, yako wapi? Kwa hiyo lazima productive sectors ziweze kushughulikiwa na productive sectors ndizo zitatengeneza ajira, ndiyo zitalisha viwanda na ndiyo zitajenga uchumi wa nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyeki, unapozungumza uchumi imara, unazungumza uwezo wa nchi kuuza nje. Tanzania tuna mapungufu yetu tunapaswa tuyaangalie, kama walivyosema Wabunge wengine kwa kujilinganisha na nchi nyingine. Wamezungumza Uganda, kahawa Uganda wanauza Dola milioni 500 kwa mwaka, sisi 135, lakini sisi tuna potential, tuna ardhi tunaweza kwenda juu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri katika Mpango wetu unapokuja tutengeneze jedwali la kuangalia kila sekta inaweza kutuletea nini. Hatari tuliyo nayo, mapato yetu ya Taifa kwa fedha za nje kwa kiasi kikubwa inategemea uziduaji. Two third ya mapato yetu yanategemea dhahabu na madini ambayo ni hatari, ni kipato kwa Taifa, lakini siyo jumuishi. Kwa hiyo tunapaswa tuwekeze kwenye shughuli za ujumuishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapendekezo yangu. Jambo la kwanza kwenye Sekta ya Mifugo, lazima Serikali iwekeze zaidi katika kuhakikisha kwamba wafugaji wanaacha kuhamahama. Huwezi kujenga Sekta ya Nyama na Maziwa kwa watu wanaohamahama na ili kudhibiti hilo lazima Serikali iweke fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine kwa upande wa kilimo, sisi Tanzania tuna hekta milioni 29 zinazofaa irrigation na tunalima 0.4 million hectors, Serikali wawekeze, waweke fedha, kama Mwalimu Nyerere alivyojenga Mbarali, waweke fedha nyingi watu walime halafu wawaachie, halafu watengeneze Mfuko wa kuwalipisha wale watu ili tuachane na kilimo cha kutegemea kudra za Mwenyezi Mungu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu kitu kingine, ningependa nishauri, limezungumzwa suala la mbolea litatusumbua sana. Nimewahi kulizungumza, naishauri Serikali, juhudi za kuweza kutengeneza Kiwanda cha Mbolea lisisubiri, achana na visima vyenye well and bottleneck, waende wakachimbe visima vingine. Bahati nzuri Sekta ya Nishati naona wamewarudisha wakongwe wa mafuta akina Mzee Halfani wanarudi, wanajua gesi ilipo, waende kuchimba visima tutengeneze gesi, hii bei itapanda na kushuka na kupanda na kushuka ndiyo historia ya gesi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nalifurahia, Serikali wameanza kuzungumza suala la Bagamoyo, wamefanya kazi ya Bagamoyo, waizungumze, siyo siri, tuzungumze Bagamoyo kama Industrial City, tuzungumze Bagamoyo kama Bandari, tuzungumze Bagamoyo kama Logistic Centre. Wamezungumza suala la DRC Congo kwamba Tanzania mnataka kuwa njia, unapotaka kuwa njia lazima uwe na uwezo wa kupokea Panama Versal, uwe na uwezo wa kupokea meli kubwa ziweze kuja hapa. Nalipendekeza hilo waliangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi mwingine ni mradi wa ajira. Ziko nchi duniani zimeendelea kwa kukopa na kuwaajiri watu. Hizi Sekta za Uzalisha, Productive Sectors hazina wafanyakazi, tusione aibu kwenda kukopa. Jambo moja la faida, Productive Sectors ukikopa ni malipo ambayo utayaona katika kipindi kifupi. Ukichukua model ya Swaziland ambao wana ng’ombe laki sita, sisi tuna ng’ombe milioni 33.9, wao wanapata Dola milioni mbili Dola export kwa extrapolation sisi tunaweza kupata Dola karibu milioni 150.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ukiwekeza kwenye sekta hizi unakopa na katika kipindi kifupi unaweza kupata mapato. Kwa hiyo, pamoja na hii miundombinu wezeshi na saidizi, sasa tunapaswa kutupa kwenda kwenye Productive Sectors. Hata hivyo, jambo la muhimu twende tukope, tuajiri watu, watu wafanye kazi. Kwa sababu watakapofanya kazi utaweza kupokea zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mengine nitawasilisha kwa maandishi. (Makofi)
Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuanzia Januari, 2021 hadi Februari, 2022 pamoja na Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa Kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2022
MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia taarifa za Kamati hizi mbili kwa sababu ya muda nitachangia taarifa ya Kamati inayoshughulika na sekta ya kiuzalishaji ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hizi ndiyo sekta za kiuzalishaji na kwa mtazamo wangu mimi ni kwamba naangalia ustawi wa ndani ya nchi, uzalishaji wa chakula na naangalia uwezo wa sekta hizi kuuza nje. Tunapata chakula Tanzania, hatujapata njaa kwa miaka sita au saba na watu wanafurahi, lakini nataka niwaambie Watanzania tunakula chakula cha bei ghali, tunazalisha bila tija, tungetegemea watu wale nyama kwa shilingi 5,000 kwa kilo, wale samaki kwa shilingi 3,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nchi yetu ina export thamani ya dola bilioni sita lakini bahati mbaya 2/3 inatokana na madini na zaidi dhahabu, tunapaswa tu export tukitegemea hizi sekta za kiuzalishaji kwa sababu zina nguvu ya kujumuisha, zinashirikisha watu walio wengi. Lakini ukisikiliza wataalamu ikiwepo Wizara husika hizi, hawa watu wakiwezeshwa Serikali ikiwekeza katika sekta hizi tutaweza ku-export zaidi ya bilioni 10 kutoka kwenye sekta hizi, lakini madhara yake ni kwamba wananchi walio wengi watakuwepo wataachana na hizi tabia za kushukuru vitu vidogo vidogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nizungumze kitu kimoja na nimshauri Mheshimiwa Spika aiambie Serikali iletwe semina na Wabunge tukae kama Kamati tujadili hizi sekta mbili kwa kifupi bila kutafuta maneno mimi sijadili pesa walizopewa, hizi sekta hazijapewa pesa yaani Serikali haijawekeza kwenye sekta hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwape jambo moja la kuangalia, fursa ya samaki wa kufuga world potential ni bilioni 284; hakuna zao tunalima Tanzania kwenye soko la dunia lina kiasi hicho. Lakini ngoja niwaeleze Tanzania sisi tunasifika kwa kuwa na maji mengi, sasa niwaambie aibu, uwekezaji wa Serikali ya Uganda samaki wa kufuga wanauza tani 118,000; sisi tunauza samaki tani 12,000 nasema tani 12,000 lakini nini wenzetu hawa wamewekeza sitaki kuwaletea historia za mzee wangu za Brazil nawaeleza Afrika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Egypt wana samaki tani milioni 1.4; kwa hiyo ujanja ni kwamba kwa sababu tuna water bodies nyingi Tanzania Serikali muwekeze kule na uzuri wa sekta hizi tatu nilizozungumza ukiweka pesa leo, kama alivyosema Mwenyekiti wa Kamati inalipa na tusitegemee benki zetu za commercial mambo ya CRDB na asilimia tisa au TBBA hakuna, twende tukakope kwenye benki za kimataifa, zinazotoza riba ndogo, tuweke mamlaka za Serikali tuwape Watanzania. Sekta binafsi mnayoisema siwezi kukubali sekta binafsi ya kutoka nje hayo ni ya kumlisha mtoto wa kwale wakati watoto wa kuku wanakufa, tuchukue pesa tuwape watoto wetu Watanzania, tuwasimamie waingie kwenye uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi kwetu watu wanasema ziwa liliuzwa kwa sababu hawawezi kuvua kama watu wanaokuja na ….technology, sasa watu wangu mimi lazima tuwatengenezee vizimba, tuwatengenezee miundombinu waweze kushiriki.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho nisaidie nizungumze hoja ya Tume ya Mipango; kuna kitendawili kimoja, kuna Wizara ina shughulikia maji ya binadamu, nyingine maji ya kilimo, nyingine maji ya mifugo, nyingine inazuia mafuriko ya miundombinu tungekuwa na Tume ya Mipango hili suala lingeratibiwa kwa pamoja. Lakini unakuta sasa kuna Wizara sita zinashughulika na kitu kile kile halafu mtu anakwambia eti uchimbe kisima unyweshe ng’ombe huo umeme utautumia kutoka wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tungekuwa tumeratibiwa pamoja tungetengeneza kitu kinaitwa mini leg hawa wa ndugu zangu wa Kaskazini wasingekuwa wanalia, wangekuwa majosho yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia mada iliyoko mbele yetu. Awali ya yote naomba nichukue fursa hii kukubaliana na kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwa mapendekezo haya ya mpango. Mapendekezo haya akizingatia ushauri wa Waheshimiwa Wabunge, hao ambao nimewasikiliza utakuwa mpango mzuri, tutatoka na mpango mzuri ambao tukijituma, na tutajituma na kuutekeleza tutaweza kutimiza malengo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaendelea na mchango wangu, nichukue fursa hii kutoa pole kwa Watanzania na wananchi wa Kagera kutokana na ajali ya ndege ya Shirika la Precision Air, Sina zaidi nianze kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajadili Mpango wa Tatu katika mipango Mitano ya mwaka mmoja mmoja, inayokamilisha Mpango wa Tatu wa miaka Mitano na huu ndiyo mpango wa tatu wa miaka mitano unaomalizia mipango mitatu ya miaka mitano mitano tukiwa tunafikia Dira ya Taifa ya 2025. Kumbe huu mpango wa tatu ndiyo dira yenyewe ya 2025. Ninapochangia nitajaribu kurejea dhima ya mpango wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhima ya mpango wa tatu wa miaka mitano ni kujenga uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya watu. Uchumi shindani ni upi? Uchumi shindani ni ule ambao shughuli zake zinatawaliwa na tija kubwa, shughuli zote zinatawaliwa na tija kubwa. Uchumi shindani ni ule ambao una ujumuishi, umma umejumuishwa, lakini shughuli ya ushindani na ujumuishi inakuwa endelevu. Pamoja na uchumi shindani tunajenga viwanda kwa maendeleo ya watu. Hili la maendeleo ya watu niliseme kidogo, watu wengine huwa na kigugumizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maendeleo ya watu kuna vigezo vingi lakini kuna hili la afya, tunalisema sana, kuna hili la elimu tunalisema sana, lakini kuna lile la kipato. Unasikia watu wengine wanazungumza sasa tunapojipima lazima tujipime kwa vigezo vyote. Baada ya kueleza hayo, mimi nitajikita zaidi kwa sababu natambua mchango wa walionitangulia hususani Prof. Muhongo, nizungumzie utatuzi wa changamoto za kibajeti na mipango au mikakati ya kukabiliana na changamoto na vihatarishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumetengeneza mapendekezo ya mpango tutakuja na mpango lakini huenda tusifikie mpango. Ni kitu gani Wachumi wanaita ceteris paribus yaani unaweka assumption ambazo kama zisipokudhuru unaweza kutekeleza mpango wako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nizungumzie namna ya kukabili vihatarishi. Mojawapo ya vihatarishi Waheshimiwa Wabunge, wengine wamevisema ni suala la mazingira na hali ya hewa. Tumeona nguvu za kidunia mojawapo ikiwa vurugu ya vita ya Ukraine na kupanda kwa bei ya mafuta. Napenda nishauri kwamba Serikali yetu pamoja na kutoa ruzuku lazima tuongeze kasi ya kutumia gesi asilia. Moja, tutumie gesi asilia sana, lakini pamoja na agizo la Mheshimiwa Rais alilolitoa la kutumia gesi kwenye taasisi za Kiserikali, tutumie gesi asilia kwenye taasisi za Kiserikali. Hii itatupunguzia mzigo wa ku-import products hali ambayo itaongeza import bill. Kwa hiyo gesi asilia ni rahisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kilimanjaro Hotel Dar es Salaam wanabeba mitungi kutoka kwenye kituo mama (mother station) ya natural gas, wanaleta ile mitungi, wanakuja kutumia wanairudisha. Ni mtungi mkubwa, tunaweza kufanya hivyo kwa radius ya kufika mpaka Dodoma, tukaweza kufanya hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala jingine ni hili la mazingira na tabianchi. Kuna suala moja, kuna presha za mazingira zinazotoka nje ya nchi lakini kuna presha za mazingira zinazotoka hapa nchini. Ulilidokeza jana, kuna matatizo yanayotupata sasa kwa sababu tumeharibu mazingira. Katika mapendekezo ya mpango huu, vidokezo vilivyotolewa na Serikali haviwezi kutatua tatizo hili. Mojawapo ya eneo nataka kupendekeza, lazima tuje na sera na sheria ya kuiondoa Tanzania katika utaratibu wa uchungaji wa mifugo, tuende kwenye ufugaji ni suala gumu lakini lazima tulizungumzie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala jingine ninalotaka kuzungumzia ni suala la mikakati ya kuongeza mapato. Kuongeza mapato ni muhimu na suala mojawapo la kuongeza mapato ni ku-invest kwenye re-export. Tuna VISA re-export kutoka Tanzania, lakini tuwekeze kwenye viwanda. Ujenzi wa uchumi shindani na viwanda. Viwanda tunavyovilenga ni viwanda vya Kitanzania, siyo viwanda vya Tanzania, viwanda vya Kitanzania. Mheshimiwa Kakosa alisema jana kwamba tutengeneze mamilionea wa Kitanzania – ndiyo! Tutengeneze viwanda vya Kitanzania kwa sababu hawa wawekezaji wanaotoka nje ni watoto wa kufikia, watarudi kwao wakati ukifika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la kusimamia matumizi yetu. Kuna haja ya kuimarisha Idara za Kiukaguzi. Hii idara ya kiukaguzi ipewe uhuru zaidi, rasilimali, itungiwe sheria kusudi Mkaguzi awe na nguvu za kumsimamia yule anayemsimamia. Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri hawezi kusema juu ya Mkurugenzi wake. Hata yule wa Mkoani hawezi, hata Mkaguzi wa Wizarani hawezi kusema kwa Katibu Mkuu. Lazima hii taasisi tuitengenezee sheria, sera na mamlaka na tu-train watu wetu kwenye ukaguzi wa leo, waweze kukagua mifumo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakaguzi wetu wamesomea kukagua makaratasi, hard papers, wafundishwe zaidi kukagua mifumo hii. Kenya wanao Wataalam wa namna hii karibu 1,800,000 sisi tunao Wataalam kama 200. Kwa hiyo lazima tuende kwa teknolojia, ndiko hali inakokwenda. Fedha nyingi zinakuja, zinakusanywa lakini namna ya kusimamia hayo matumizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ni Tume ya Mipango. Tunahitaji Tume ya Mipango, moja ni kwamba tunamahitaji mengi lakini tunahitaji kwenda kwa kasi kubwa. Baada ya hayo, naunga mkono hoja naona mapendekezo haya ni mazuri. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, kupitia njia ya maandishi naomba nichangie makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Awali ya yote niunge mkono mwelekeo wa makadirio ya mapato na matumizi kama yalivyowasilishwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu, mipango na mategemeo yalivyobainisha utekelezaji wake kama tulivyodhamiria utasukuma maendeleo ya Taifa letu kwa kasi kubwa zaidi na kwenda hatua nyingine bora zaidi.

Mheshimiwa Spika, tunapoelekeza nguvu na jitihada zetu katika sekta za kiuzalishaji, nichangie suala la migogoro ya ardhi inayohusisha sekta tunazozitegemea zituvushe.

Mheshimiwa Spika, nianze na utekelezaji wa mipango ya maendeleo inayotegemea sekta za kiuzalishaji; jambo muhimu linalopaswa kuzingatiwa ni kuondoa na kuzuia migogoro kati ya wananchi na wananchi au na wananchi na taasisi za Serikali au wawekezaji. Njia rahisi na ya haki ya kusimamia sekta hii muhimu ni kuzingatia sheria za nchi na kama sheria zina mapungufu basi ziboreshwe.

Mheshimiwa Spika, moja ya maeneo ya kutolea mfano ambayo migogoro inaibuka kila kukicha na usuluhishi wake unachukua miaka bila kupata muafaka ni ile ya Wilayani Muleba. Mgogoro wa ardhi katika Kata ya Rutoro, kata yenye vijiji vinne na vitongoji 16 chimbuko lake ni utendaji usiozingatia sheria za nchi zilizopo. Mwaka 2005/2006 Serikali ilipopima eneo lenye ukubwa wa hekta 50,000 na kutenga vitalu 18 kwa ajili ya kuwakodisha wafugaji vijiji tajwa hapo juu vilikuwepo. Vijiji vilikuwepo vikiwa na watu ambayo ndiyo rasilimali kuu na namba moja ya Taifa, pamoja na kuwepo vijiji hivyo wakati huo vilikuwa vimesajiliwa kisheria. Kijiji cha Rutoro mwaka 1976 kilikuwa Kitongoji cha Kijiji cha Rwigembe wakati Kata ya Ngenge ilianzishwa toka kata mama ya Rushwa. Wakati huo huo vijiji vya Kyobuheke na Misambya vilikuwa vitongoji vilivyosajiliwa chini ya Kijiji cha Ngenge mwaka 1976. Mwaka 1999 Rutoro ilipandishwa hadhi na kuwa kijiji kwa kufuata sheria za nchi. Lakini kwa kufuata sheria za nchi yetu vijiji vinne vya Rutoro, Kyobuheke, Misambya na Byengerere vikasajiliwa na kuunda Kata ya Rutoro.

Mheshimiwa Spika, utaona kuwa hata kwa mtu mgeni wa sheria usimamiaji mbovu wa sheria ndilo chimbuko na kichocheo cha mgogoro wa Rutoro. Kama ilivyo kwa mgogoro wa Rutoro, MWISA II nayo mgogoro wake umeibuka kwa makosa yale yale yaliyofanyika mwaka 2005/2006 Kata ya Rutoro. Mradi wa NARCO kupima vitalu ili kuwagawia wachungaji wa ng’ombe kwenye kata saba zenye vijiji 12 na vitongoji 19 bila kuzingatia sheria ni kuzalisha mgogoro mpya. Utawala bora kwa kuzingatia sheria unaelekeza matumizi bora ya ardhi na uhaulishaji pale inapobidi.

Mheshimiwa Spika, kiu ya NARCO na Wizara mama yake ya kuwa na maeneo mengi ya kufuga inachochea migogoro kutokana na utendaji wake usiozingatia shughuli zenye tija kubwa. Kimsingi NARCO anachofanya ni kuvamia maeneo, kupima, kuwakodisha wachungaji na kudai kodi. Shughuli yenye tija inapashwa kuanza na utendaji unaozingatia sheria, uendelezaji wa maeneo kwa kulenga ufugaji wenye tija au kuwawezesha wawekezaji wazawa ili waendeshe shughuli kwa tija au na kutafuta wawekezaji wenye uwezo mkubwa wa kiuwekezaji ili shughuli iwe na tija kwa manufaa ya wadau wote.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru. Kwanza niipongeze bajeti ya TAMISEMI, kwa taarifa nzuri ya utekelezaji. Utekelezaji unaakisi hali halisi tuliyoiacha huko kwenye Majimbo yetu, lakini napongeza Mpango unatupa matumaini makubwa sana. Nianze na masuala ya Kitaifa kabla ya kwenda Jimboni. Suala la kwanza katika taarifa ya Mheshimiwa Waziri amezungumzia magari yaendayo kasi Mpango wa Dar es Salaam DARTS. Inaelezwa kwamba abiria 180,000 wanasafirishwa kwa siku na tutafikia watu milioni 2,500,000 kwa siku. Ushauri kwa Serikali, wekeza katika magari yanayotumia gesi asilia haraka sana (natural gas vehicles) haraka sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, naishauri Serikali tunayo mahitaji ya watendaji lakini tunao watendaji wengi wamehitimu na hawajapata kazi, lakini jambo la kufurahisha kwa taarifa za uhakika Serikali imeanza kuajiri. Hata hivyo, haiwezi kumaliza kuajiri kwa mwaka huu, lakini kuna uhakika mwaka kesho na mwaka kesho kutwa itamaliza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa pendekezo langu, vijana wote ambao wako tayari waende katika Taasisi iwe afya iwe shule kusudi wajitolee; na wanapojitolea uwepo utaratibu wa kuwa-monitor na kuwa-mentor. Kusudi wanapokwenda kuajiri sasa wamchukue yule mtaalam aliyekwenda kuwa mentored na wataalam kuliko kwenda kuokoteza. Sio sawa mtu ambaye miaka sita amemaliza shule hajawahi kufundisha unampeleka kwenda kufundisha. Hii itatusaidia sisi kwamba wale vijana kuliko kwenda kuzurura wawe na kazi maalum. Huo ni ushauri wangu kwa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye Jimbo langu na Mkoa wangu. Nashukuru kwa ajili ya Jimbo langu la Muleba Kaskazini, yote waliyotekeleza na Mpango wao. Nashukuru kwa niaba ya Wilaya yangu ya Muleba na Mkoa wangu wa Kagera. Nataka niwaeleze katika Wilaya yangu ya Muleba tunazo shule za msingi 250, za sekondari 40, tuna wanafunzi 157,372, kwetu sisi tunao wanafunzi wa sekondari 33,255. Hoja yangu ni kwamba tunahitaji Walimu wa shule za msingi, Walimu tunaowahitaji ni 1,390. Wakati ratio ya Taifa ni 1:60 Muleba ratio yetu ni 1:71, naomba wanapokuja kugawa Walimu sisi watuangalie kwa macho matatu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, sisi Muleba tunao watoto 23,500 ambao wanaingia form one, mwaka kesho katika mwaka kilele wa elimu bila usumbufu. Wanaopaswa kuingia darasa la tisa ni watoto 23,500. Kwa uwezekano wa ushindi wa asilimia 85, Muleba watoto 19,000 watakuwa tayari kwenda shuleni. Naomba watuangalie kwa jicho zuri na nimeiona mipango ya Serikali, tunahitaji vyumba 243 ili kuweza kuwapokea watoto hao. Nimeona mpango wa Serikali kwamba tutasaidiana kujenga na sisi Wabunge wa Muleba tumeshajiandaa, mwezi Mei tutaomba ruhusa kwa Spika tunakwenda kuanzisha ule mchezo wetu wa Bank ya Matofali. Kwa hiyo, watatukuta huko safarini aje atupe lift Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie sekta ya afya. Tunavyo vijiji 166, zahanati 142 lakini vijiji ambavyo havina na kata ambazo hazina, wananchi wameshaanza, kwa hiyo kumbe Mheshimiwa Waziri atawakuta njiani. Jambo ambalo sisi hatuwezi tunao upungufu wa wataalam 505, Mheshimiwa Waziri anapogawa wataalam chonde chonde atuangalie kwa macho matatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee nimpe salamu zake Waziri kutoka Bumbile, Mazinga na Ikuza wanamshukuru kwa kutoa boti ambayo itakwenda visiwani; na nimewaambia hiyo boti inayokuja inaitwa ambulance, atuletee ambulance usafiri mwingine tutajijua. Sisi tuna square kilometer 10,200 wanasema kama kobowagabiyolengelao, wanaomba boti ya pili, 10,200 boti moja haitatosha, lakini tunashukuru kwa hicho kidogo kilipotoka kingine kitaongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende sasa kwenye sekta ya elimu. Kumbe sasa hatua tuliyofikia Tanzania kufikia 2025 watoto wote wa msingi wanaweza kwenda sekondari. Jambo lililonifurahisha katika Wizara hii kuna kauli inasema utawala bora TAMISEMI ya wananchi na Mheshimiwa Waziri wanasema you are walking the talk, kauli yako uliyoitoa juzi, ikamfanya Mbunge wa Nyamagana aende kula chakula na Mkuu wa Mkoa na yule muuza ndizi, you are walking the talk. Hata hivyo, sasa ndugu yangu akipiga watoto awapige watoto wote, yeye vijiji vyake vyote vimeandikwa chini ya TAMISEMI. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kijiji changu kimoja cha Rutoro, kuna watoto asilimia 23 ndio wanafika shule asilimia zaidi ya 77 hawaendi shule, kuna shule nyingine just 53 ndio wanakwenda shule katika watoto 540, kitu gani. Ni kwamba kuna tatizo la utawala bora. Vijiji vilivyoandikishwa vya Kata ya Rutoro wamekuja watu wanafukuza watu kwenye vijiji vilivyoandikishwa. Kama ni utawala bora, a-walk the talk, aende akawaulize vijiji alivyovisajili chini ya TAMISEMI katika maeneo ya Kata nane, ni nani mwenye mamlaka ya kuja kupangua vijiji vile bila yeye kuhusishwa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungependa Wakuu wa Mikoa wote wawe kama Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, mnakaa watu mnajadiliana. Yule kijana aliyekuwa anasukuma ndizi amenipigia simu, anasema ameridhia makosa yaliyotokea amewasamehe wote. Sasa na wengine waambie kama wanasikia Mbunge anahoji, wamuite Mbunge wakae naye wajadiliane, hatuwezi kuishi kwa kebehi. Mtu anakwenda anakatakata mashamba ya watu anasema Muhaya ukimpa heka sita zinatosha, hiyo dharau isiletwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika miaka 100 ya Nyerere, huwezi kusimama kuwabagua watu kikabila, unasema heka sita kwa Muhaya ni nyingi, nani alikuambia Muhaya hawezi kuwa na heka sita. Mimi nina zaidi ya heka 30, sio Muhaya? Hata hivyo, kwa nini tunatafuta ukabila? Hatuwezi kukubali kudharauliana, Mheshimiwa Waziri a-walk the talk, ahakikishe wale wote wanaohusika wakutane wote, Wizara zote zinazohusika, wakamalize matatizo yale, TAMISEMI ya wananchi, lakini sio wale wananchi ambao wanakuwa 75 kwenye ranking za FIFA. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Awali ya yote napenda nitoe taarifa kwamba mimi ni Mjumbe wa Kamati hii, Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji au sekta za kiuzalishaji, kabla sijaendelea nizungumze waliyonituma mabosi wangu ninaowawakilisha.

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Kata ya Rutoro wamenituma kwako nije kukushukuru, wanakushukuru kwa ushauri ulionipa wakati wa kipindi kigumu cha mgogoro wa Rutoro. Pia wanamshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali, unakumbuka nilivyokuja kwako ninahema, lakini wanamshukuru na bosi wangu wa zamani Mheshimiwa Simbachawene.

Mheshimiwa Spika, unajua mgogoro wa miaka 17 uliodumu Rutoro, Mheshimiwa Rais alipokuja Kagera mwezi Agosti kwa ujasiri nilikwenda nikamweleza tatizo la wananchi, alisema Mwijage hilo tatizo nitalishughulikia.

Mheshimiwa Spika, nataka nilieleze Bunge lako tukufu Baraza la Mawaziri walikuja na helikopta, wakasema Mheshimiwa Rais anasema wananchi wakae walime na wafuge wakae kwa amani. Naitwa good boy siku hizi na sio bad boy, lakini wamenituma nikushukuru wewe.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie hii sekta ya uzalishaji; leo tuko kwenye dhima ya tatu ya ujenzi wa dira ya Taifa ambayo inazungumzia uchumi shindani, uchumi uliojumuishi, uchumi wenye shughuli za tija kubwa na uchumi endelevu. Nimeshiriki kwenye Kamati ulikonipanga, tunakwenda vizuri, kwenye maji shughuli zinakwenda, kwenye kilimo shughuli zinakwenda na kwenye mifugo shughuli zinakwenda. Nina mambo ya kuishauri Serikali au Wizara.

Mheshimiwa Spika, tumepeleka pesa nyingi kwenye Wizara hii, lakini tumepeleka pesa ukweli ulio wazi, hakuna watenda kazi kule. Kwa hiyo hakuna watu wa kutenda kazi zile. Naishauri Serikali haraka watendakazi wenye ujuzi na weledi waajiriwe kusudi zile pesa ziweze kuleta tija.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo suala lingine la ajira; unapozungumza wafanyakazi/ajira, watu wa Serikali wanakwambia suala la bajeti. Sawa , lakizi zipo taasisi za Serikali ambazo ukizifanya Strategic Business Unit (SBU), ukamtafuta mtu mahiri ukamkabidhi badala ya wewe kumpa ruzuku atakupa ruzuku. Mojawapo ya taasisi ni NARCO, NARCO wana hekta laki sita za ardhi, hawawezi kufuga, hawawezi kuuza maziwa, sio mabingwa wa kuuza nyama, sio mabingwa wa chochote. Ardhi wanayo, tatizo lake ni under capitalization.

Mheshimiwa Spika, TAFICO, sisi tuna kilometa 1200 za bahari, tuna shirika linaitwa TAFICO - Kampuni ya Taifa under capitalization, hawana neli, hawana kasia, hawana hata mtumbwi. Kwa hiyo, tunapaswa kuleta watu kuwapa, tuwape kazi kwa masharti kusudi waweze kutekeleza na kuilipa, tuajiri watu.

Mheshimiwa Spika, kitu kingine nilichokiona katika miradi hii tumeajiri wakandarasi na wengi wenye miradi mikubwa ni wakandarasi kutoka nje; tunawalipa mamilioni ya pesa wanapeleka wao huko kwao, lakini miradi wanayofanya si ya kiajabu, si miujiza. Tunao vijana wetu kwenye taasisi za Serikali, tunao Watanzania wenzetu tuwakamate hawa watanzania kwa masharti magumu tuwakabidhi kazi, tuwaangalie watengeneze. Hauwezi kutafuta pesa ukamlipa mtoto wa jirani wakati mtoto wako anakufa njaa, tuwasimamie waweze kufanya, ndivyo walivyofanya nchi nyingine, ndivyo wanavyofanya Urusi, ndivyo wanavyofanya Rwanda na duniani kote. Mtoto wako unamrekebisha huwezi kusema mapungufu yam toto wako, Mrekebishe. Ndivyo tulivyofanya kazi kwenye Wizara ya Nishati wakati wa REA na aliiasisi Mheshimiwa Muhongo. Hawa wakandarasi mnaowaona Watanzania walitafutwa, walikuwa hawajui lolote na wakaweza kufanya kazi. Ndio maana hata ndani ya TANESCO iko Kampuni ya TANESCO inapewa kufanya kazi ambazo tungeita watu wageni waje kuifanya hiyo kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo tuliloliona katika Kamati ile…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Sekunde thelathini naambiwa kengele imeshagonga.

MHE.CHARLES P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, nizungumze la mwisho la haraka. Tumepanga pesa kwa ajili ya kutekeleza miradi, lakini utaratibu wetu wa mnyororo wa manunuzi, procedure ya PPRA ya manunuzi; unakuta pesa mmepewa, mchakato wa ku-release pesa kutafuita mkandarasi unakuchukua miezi sita, mwaka umekwisha. Kwa hiyo mradi hauishi.

Mheshimiwa Spika, hizi bureaucracy, necessary devils tujaribu kuzifupisha kusudi miradi iweze kutekelezwa kwa wakati. Ikiwezekana miradi ya mwaka kesho basi tuanze leo kutafuta mkandarasi kwa sababu tunajua pesa tutazipanga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nishukuru kazi iliyofanywa na Wizara ya Kilimo ya kuendeleza Bonde letu la Mto Ngono, tunataka sasa lilimwe wananchi waweze kupewa vizimba waweze kulima na kufuga samaki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono kazi ya Kamati yangu. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Kilimo
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mimi ni Mjumbe wa Kamati lakini ni muumini wa sekta za kiuzalishaji. Naogopa nisije nikasahau, naomba kuunga mkono taarifa ya Kamati pia ninaunga mkono yote taarifa ya mtumishi, mimi naiita bajeti ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitazungumza mambo matatu kwa sababu tumezungumza sana suala hili mwaka jana na tumelichakata kwenye Kamati. Moja nitazungumza kuhusu umuhimu wa kilimo. Suala la pili nitazungumza mtazamo wa Serikali ya Awamu ya Sita kwenye sekta ya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilipokuwa mdogo, nilipoacha ziwa la Mama nilikwenda kulelewa na Bibi yangu aliitwa Zuhura Teshasha. Mama yangu alinipenda sana na watu wengine walikuwa wananiletea zawadi. Pamoja na udogo wangu nilikuwa na uwezo wa kutambua zawadi ya Mama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zawadi ya Mama ingekuja ningesema hiyo zawadi ya mama. Napenda niwaambie, kitendo cha kutoa bajeti shilingi bilioni 294 kwenda kwenye shilingi bilioni 751 hiyo ni zawadi ya Mama. Nimemsikia mtumishi na wewe mtumishi hii siyo ya kwako umetumwa. Hii ni zawadi ya Mama, anasema atawatafuta vijana, atawapa heka tano au heka 10 hiyo siyo ya kwako, wewe ni mtumishi hiyo ni zawadi ya Mama. Wale ambao siyo watumishi wa Mama anachukua watu 10 anawapa heka mbili, huyo siyo mtumishi wa Mama. Mtumishi wa Mama ni kama wewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitazungumza kitu kingine. Hii ni bajeti ya Taifa, ile ya TAMISEMI ilikuwa ni bajeti ya wananchi, hii ni bajeti ya Taifa. Nizungumze suala jingine nikipata muda nitawaambia change of mind, working by targets. Nimemsikia mtumishi kwamba sisi tubadilishe malengo, sikiliza bajeti yake na ninyi Watanzania mnasikiliza, anaweka malengo kwamba ifikapo mwaka fulani sisi tuuze kiasi fulani. Kiburi cha Ukraine anauza nje Dola Bilioni 64, ndiyo kiburi cha Ukraine na angalia anauza nini Ukraine, anauza mazao ambayo na sisi tunaweza kulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine nitakalozungumzia ni suala la uchumi jumuishi. Ziko block farming 110 anasema mtumishi na hii umetumwa na mama nina taarifa. Anasema yeye mtumishi, block farming 110 atatengeneza block farming 10,000 kufikia 2025. Angalizo, hakikisha na Mkuu wa Mkoa wa Kagera unamwambia akutengee hekta 50,000 na vijana wa Kagera waweze kupata ardhi na mimi nitapambana na uongozi wa Kagera kuanzia Kijiji, iwe Wilaya lazima watoe ardhi vijana walime. Siwezi kukubali, siwezi kukubali wananchi wangu kutengewa heka mbili, lazima watengewe heka tano, heka 10, heka 20. Naanza kuchangia. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma gazeti la Business Insider, Business Insider wanasema sababu tano, nazungumza umuhimu wa kilimo. Wanasema umasikini wa Afrika unatokana na sababu tano na sababu mbili ziko kilimo, lakini sababu mbili za kilimo zinaweza kuondoa umasikini kwa asilimia 70 tukizi-address. Mheshimiwa Waziri amezungumza anaweza kuondoa umaskini kwa asilimia 50 kama Mama atampa zawadi na sina wasiwasi. Sina wasiwasi zawadi itakuja, Shilingi Trilioni Mbili zitakuja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mojawapo ya sababu inayotajwa ni tariff berrier na non-tariff berrier. Wale wenye ukwasi mkubwa, mazao yetu tunayolima wanayawekea kodi kubwa na wanayawekea masharti yasiyokuwa ya kikodi. Lakini watu wale wenye ukwasi mkubwa, kitu ambacho wanacho kingine wana ruzuku sana mazao yao yanayoshindana na kwetu hapo ndipo naungana na mtumishi anasema litoke jua inyeshe mvua atatoa ruzuku kwa mbolea. Naomba mumuunge mkono ili kusudi aweze kutoa ruzuku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala jingine Business Insider wanasema inadequate infrastructure and inadequate expertise. Kwamba hatuna miundombinu na hatuna utaalam. Nimewaona jeshi la kilimo limeshajengwa uniform, usiwavike uniform, usiwaruhusu kurudi nyumbani wapige wiki kama mbili hapa uwapige shule na mimi uje uniite mtumishi mwenzako niwape maneno. Kwa hiyo, inadequate expertise is very important. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala jingine ni miundombinu. Nitumie fursa hii kuiunga mkono Serikali, mwaka 1970 Muadhama Raulian Rugambwa na Baba Askofu Kibila na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Kagera waliamua kuanzisha mradi wa Mto Ngono tangia siku hiyo tulijua kwamba tunakwenda kwenye neema, baadae Mzee Byabato wakaanzisha Kagera Basin Organization. Nimesoma kwenye bajeti kwamba Serikali inakwenda kufanya assessment ya irrigation Mkoa mzima wa Kagera.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaambie kama kuna kitu kilisahaulika na sasa hivi wakati wa Mama hakikufufuka, hakitafufuka tena. Wananchi wa Kagera, Kagera Basin inakwenda kurudi halafu niwaambie Ngono Project inakwenda kurudi halafu basin yote ya Victoria inakwenda kulimwa, tunakwenda kuzalisha chakula. Maana yake ni nini? Tunakwenda kuwa exporter wa mazao. Kiburi cha Ukraine ni uwezo wa kuuza nje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimewaambia target lazima mambo yote Wabunge tuyalenge kwenye malengo, unauza nini? Natofautiana na Mtumishi. Hatuwezi kusubiri mpaka 2030 kuweza kuuza nje mazao yenye thamani ya Dola Bilioni Sita no! Lazima kabla ya 2025 tutumie pesa hizi na Mama atakuongeza nyingine ili kusudi uweze kuzalisha zaidi. Kuzalisha zaidi ndiyo kutatuwezesha sisi kuwezakuwa na kiburi. Hatutampiga jirani yetu lakini tutakuwa na kiburi ili hata wale vijana wenye jambo lao kwa sababu tutakuwa na kipato kikubwa tunaweza kubadilisha ile jezi Namba 23 ikawa Namba 46, ni kiasi cha kubadilisha tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja niwaambie. Kiasi cha mafuta tunachotumia nchini lita Bilioni Saba ndiyo mafuta ya alizeti ambayo Ukraine anazalisha. Lakini arable land ya Ukraine ni ndogo tunamzidi mara tatu kwa arable land ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina imani sana, nina imani lakini kuna mazao yenye mashaka, mojawapo ya mazao yenye mashaka ni haya yanayojitokeza. Kwetu sisi tunalima vanila, Serikali itusaidie ku-address suala la vanilla, lakini kwetu sisi tunalima chai, chai ya Kagera irudi kwenye nafasi yake.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwijage, Mheshimiwa Mwijage.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo.

MWENYEKITI: Ninakuongeza dakika moja uhitimishe hoja yako Mheshimiwa. (Makofi)

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Naunga mkono hoja. Lakini jambo la Mama, zawadi ya Mama ukiiangalia utaiona na watumishi wa Mama wanakuja na heka tano kwa mtu siyo heka mbili kwa watu 10.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kujadili bajeti na hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu inaakisi sawasawa hali halisi ilivyo nchini au tulikotoka. Mahususi kwangu, aya ya 62, Mheshimiwa Waziri Mkuu ametamka kazi nzuri ya mpango wa Serikali kujenga Soko la Kimataifa la samaki katika bandari ndogo ya Kyamkwikwi. Napenda nichukue fursa hii kushukuru. Namwomba Waziri wa Mifugo asimamie suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninalo suala lingine dogo la kitaifa linalohusu pension za watu waliowahi kuitumikia Serikali. Wako watu walitumikia Serikali, leo wana miaka 70, 90 na wengine 100, lakini ukiangalia pension wanayopewa na ukatumia ile time value of money, naishauri Serikali tuwaangalie watu hawa. Hawa watu kwa sababu ya umri, wana magonjwa yanayoendana na umri, lakini mfumo wetu wa Bima ya Afya kama NHIF, hawa watu wakienda hospitali bima za afya haziwasaidii. Serikali tuliangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, msiwe na wasiwasi, hesabu za haraka, hawa watu ni wachache. Mnaweza kuwaongezea. Msiwe na wasiwasi, kwa idadi hawa watu ni wachache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuzungumzia uchumi wa dunia na uchumi wa Taifa. Nina hofu muda hautatosha, lakini naipongeza Serikali namna inavyodhibiti uchumi wa Taifa letu. Ukiangalia kwa jirani kunavyofukuta, ukaona nyumbani mmetulia, unaweza kujua kwamba aliyeko jikoni anahangaika kusudi mle. Nitarudi hapo muda ukiniruhusu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze mambo matatu. Mkoa wa Kagera tumepata mapigo matatu. Nasimama hapa kuwaeleza mila za kiafrika. Unapopatwa na shida au kama una shughuli, watu wakija kwako kukuona, inakupa faraja. Ilipoanguka ndege ya Precision Serikali kwa nguvu zote ilifika Kagera, Mheshimiwa Waziri Mkuu ulikuja Kagera; hilo jambo liliwafurahisha watu wa Kagera na Watanzania wote. Tunachoomba, Waziri wa Uchukuzi, imeanguka ndege ni historia, lakini lazima tujenge uwanja wa ndege Kagera, Bukoba, utakaoweza kusaidia Soko la Kagera. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kagera tuna soko la ndege, economically ni viable, lakini uwanja wa ndege Kagera ni suala la kiusalama. Kwa hiyo, mnaweza mkaangalia Omukajunguti, na Kashaba. Naomba pamoja na pole mliyotupa, tuliangalie na hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni ugonjwa uliotukumba juzi, Marburg. Napenda niwahakikishie, mimi nimezungumza na wahusika, nimezungumza na Mbunge mwenye Jimbo, Mheshimiwa Advocate Captain Pilot Rweikiza, Marukuni shwari, Kanyangereko ni shwari. Eneo lote liko shwari, lakini jambo la muhimu kwa wananchi wa Kagera, response ya Wizara ndiyo iliwafurahisha. Ujio wa Naibu Waziri na kufuatiwa na Mheshimiwa Ummy, ndiyo jambo liliwafurahisha, lakini zaidi namna Serikali ilivyoweza kudhibiti ugonjwa ule. Nchi nyingine bado ugonjwa unaendelea na limekuwa dondandugu. Katika mambo ya kujivunia tujivunie hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa zaidi ya hayo, tunaiomba Wizara: Moja, mjenge hospitali kubwa ya rufaa Kagera ya kudhibiti milipuko. Hii milipuko nimemwambia Waziri, ilikuja Juliana ikaua watu, ni mlipuko; ukaja ugonjwa wa Covid, ukaua watu, kwa hiyo, umekuja na huu Marburg umeua watu, ijengwe hospitali ya kimkakati, special yenye eneo kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimezungumza na Waziri, sisi tunapakana na ziwa. Karibu 1/3 ya Ziwa Viktoria liko kwetu na tunapakana na nchi nyingi, kuna mwingiliano. Kuna namna ya kutuangalia kipekee. Katika kata tano za Wilaya ya Muleba kututengenezea vituo vya afya vya kuweza kukabili mapigo haya. Nimeomba na ninadhani Serikali mmenielewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende suala la tatu. Desemba tarehe 17, timu ya Mawaziri ilifika Wilaya ya Muleba. Katika timu hiyo Waziri mwenye dhamana ya mifugo wakati ule na wenzake alioambatananao, namwona Mheshimiwa Silinde, Mheshimiwa Mavunde, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, walikuwepo; wakatamka kwamba, uliokuwa mgogoro wa Rutoro umekwisha kwa sababu, mgogoro ulikuwa kati ya NARCO na wananchi, umekwisha. Serikali itakuja kupima, lakini wakaenda mbele wakasema watu wakae bila kuhasimiana, tukamaliza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu na Serikali yangu, msisubiri kuja kunipimia, mtupimie leo ikiwezekana kesho. Iddi yangu ninayoweza kuipokea, futari yangu inayoweza kunishibisha ni kwenda kuwapimia watu wangu leo. Watu wangu wanateseka, wana-Kagera wanateseka. Aliyozungumza Mheshimiwa Ezra pale, amezungumza kidogo; kuitendea haki sekta ya mifugo, sekta ya ardhi, sekta ya uhamiaji Kagera, ni kuunda tume huru iende ikaangalie watu wanapigwa katika nchi yao, watu wanabakwa katika nchi yao, mashamba yao yanaharibiwa. Mimi nitakuwa mgeni wa nani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ile clip mliyoiona ya kuuaa kwa Aspro, Katibu wa Chama cha Mapinduzi, ilikuwa edited. Ukiuona mkanda mzima unaweza ukakubaliana nami kwamba, Mheshimiwa Mwijage tukapime Rutoro kesho, tukamalize mgogoro wa Rotoro keshokutwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema Mwijage mimi vile ni vijiji na hati za Serikali ninazo hizi. Anatoka mtu, eti ni mteule, anasema pale sehemu ya kuchunga ng’ombe, ndipo hapo tunapoachana. Na kwa umri huu siwezi kuogopa kutofautiana na mtu mimi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema ile ni sehemu ya Serikali na Waziri anasema kwamba pale watu wakae, anatoka mtu anasema mimi sijapewa barua; upewe barua zaidi ya hii? Serikali imeandika yenyewe kwamba hapa watu wanapaswa kukaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoomba – hayo Mungu atatulipia mbinguni – ninachomba, wale watu ni maskini, nendeni muwapimie ardhi yao. Mtu aende aseme communal land. What does communal land mean? Wale ndiyo nchi yao, hawana kwao kwingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, inauma, mtu yuko kwao anapigwa na mtoto wa jirani, unasikia mtoto wa jirani anampia mtoto wako kweli utalala? Watu wanasema Mwijage ni kichaa. Itakuaje wewe umelala na mkeo, mtoto anapigwa na anayempiga anazungumza lugha ya mwezini; unalala baba usingizi unakuja? Na mnaamshana na mkeo wakati watoto wanaumia, haiwezekani. Mtoto wa mjomba nenda kalelewe ujombani, lakini ukifanya shari ujombani watakwambia wewe siyo mtoto wa hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mtusaidie. Na zaidi katika hayo, nimesikia watu wanazungumzia kufuga, kufuga kuna tija. Ninaomba muitumie Kagera kama model ya kufuga, siyo kuchunga. Mwenyekiti ni dhamana yako, uje unite nikueleze. Tuanzie Kagera, hii biashara tunayofanya tunapoteza muda. Anza kufuga kuanzia Kagera mkiiga mfano wa Mbarara. Hatuwezi kuchunga tukaweza kuingia kwenye soko la dunia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo futari yangu na Eid al-Fitr naomba tuandamane twende kwenye vijiji vyangu vinne mkavipime, wananchi watajijua. Nilikuwa nimewaombea chakula, sasa naomba muwapimie wakajilimie wenyewe watavuna wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, kupitia njia ya maandishi naomba kuchangia bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Wizara hii ni muhimu katika ujenzi wa Taifa hili, lakini zaidi ya jukumu hili ni shughuli za Wizara hii zinawagusa Watanzania walio wengi na hasa walioko vijijini. Pamoja na majukumu ya Wizara hii ambayo kwa miaka miwili hii yametekelezwa kwa ufanisi wa kiwango cha juu nashauri na kuomba yafuatayo: -

Kwanza, Wilaya ya Muleba ina kata 43, tarafa tano na vijiji 166. Eneo hili ni nchi kavu na maji ya ziwa kwa uwiano wa asilimia 30 kwa 70 mtawalia. Tuna shule za msingi 250 zenye wanafunzi 158,000 wakifundishwa na walimu 2,287. Tunazo sekondari 70 zenye wanafunzi 47,890 kwa walimu 755. Katika shule tajwa hapo juu, shule 15 za msingi na moja ya sekondari ziko visiwani (square kilometer 7,600) eneo ambalo usimamizi na utendaji katika maeneo hayo ni mgumu na hatarishi. Tunaomba yafuatayo kwa ajili ya Wilaya ya Muleba: -

i. Sekta ya elimu hasa msingi Wilaya Muleba iongezwe toka shilingi milioni tisa mpaka milioni 17 kwa uwiano wa eneo, wingi wa shule, wanafunzi, walimu hudumiwa, lakini ugumu wa kukagua maeneo yote hasa visiwani.

ii. Shule ya sekondari ya Bumbiile ambayo iko visiwani iwe shule ya bweni ya Serikali. Hali ya visiwani ni ngumu sana, wanafunzi hutoka visiwa jirani kuja shule lakini visiwa vingine viko mbali mwanafunzi kumudu kwenda na kurudi. Hata wale wanaokwenda na kurudi kwa kutumia mitumbwi ni kutegemea huruma ya wavuvi na kuangalia hali ya hewa, ikichafuka ziwa halipitiki.

iii. Kwa wingi wa shule, msambao wa vijiji na kata tunaomba tuongezewe walimu kwa shule za msingi na sekondari.

Pili, Wilaya ya Muleba kwa kupitia TARURA imefunguka kwani maeneo ambayo yalikuwa hayapitiki sasa yana barabara za uhakika. Pamoja na kazi nzuri hjyo tayari tulishaleta maombi maalum kwa ajili ya kujenga barabara ya kufungua Kata ya Rutoro na barabara ya Kimeya mpaka Burigi kwa kadirio la shilingi bilioni 4.9. Tunaomba nyongeza ya bajeti hiyo tusaidiwe kufungua maeneo hayo hali ambayo pamoja na kuchochea maendeleo italeta ustawi kwa wananchi.

Tatu, Wilaya ya Muleba ilianzishwa miaka ya 1970 lakini mpaka sasa haina hospitali ya wilaya. Tulipewa shilingi milioni 500 likajengwa jengo la OPD tangu hapo hakuna nyongeza ya pesa mwaka jana hata mwaka huu kwa ajili ya kuendeleza ujenzi hospitali hiyo.

Nne, kwa Jimbo la Muleba Kaskazini tunashukuru uboreshaji wa vituo vya afya vya Kamachumu na Izigo ili kufikia viwango vya vituo vya afya. Tunaomba sana uboreshaji huo uendelee ili vituo hivyo vifikie viwango vya kitaifa vya vituo vya afya. Kituo cha afya kilichoko kisiwa Bumbiile kinachojengwa kwa vyanzo vya ndani kimekwama yaani hakijakamilika. Mbali na utaratibu huo nilioueleza jimbo la Muleba Kaskazini halijawai kujengewa kituo cha afya katika utaratibu huu tunaouona kwa majimbo mengine nchini. Kupitia bajeti hii niombe tupate kituo cha afya Kata ya Ngenge eneo ambalo litahudumia Kata za Bulungula, Rutoro, Mushabago, Nyakatanga, Nsheshe na Ngenge yenyewe. Maeneo haya kwa pamoja hayana kituo cha afya na kadirio la watu ni zaidi ya 80,000.

Mheshimiwa Spika, tano, Jimbo la Muleba Kaskazini wananchi wake wanao utamaduni wa kushiriki maendeleo kwa kujenga shule na zahanati. Kutokana na mrundikano wa wanafunzi katika baadhi ya shule hasa ya msingi na kutokana na hizo shule kuwa na vyumba vichache au vyumba vilivyochakaa wananchi wameanzisha shule mpya ili kurekebisha mapungufu hayo. Tatizo kwa jimbo la Muleba Kaskazini ni kuwa miradi hiyo iliyobuniwa na wananchi haisaidiwi na Serikali na hata tathimini ya maeneo yenye uhitaji inapofanyika hawa walioanza wanaachwa bila kusaidiwa. Mfano; mosi, kutokana na shule ya Ruzinga Kata ya Ibuga yenye wanafunzi takribani 700 kuwa na vyumba vichache na vilivyochakaa, Kijiji cha Rwanda walianzisha shule mpya ya Bwanika ili kupunguza matatizo ya shule mama na kupunguza umbali kwa watu wa upande wa Busingo. Jengo la vyumba vinne na ofisi liko usawa wa kuezeka. Naomba wananchi hawa wasaidiwe.

Pili, kutokana na shule ya Biija Kata ya Nyakatanga yenye wanafunzi takribani 750 kuwa na vyumba vichache lakini kutokana na wanafunzi wake kutoka maeneo ya mbali na shule, eneo la Mulole kuna mradi wa ujenzi wa shule mpya sasa iko usawa wa lenta yenye vyumba vitano na ofisi. Ushauri wangu ni kuwa tathimini ya wahitaji iwaangalie wananchi hawa kwa kupima miradi hii miwili.

Tatu, kutokana na shule ya msingi Nyakatanga yenye wanafunzi 900 kuwa na vyumba vichache tena vidogo kwa size ya mkoloni na kutokana na baadhi wa wanafunzi kutoka mbali sana takribani kilometa 10, wananchi wanajenga shule eneo la Kalengo. Mpaka sasa wamekusanya vionwa na saruji wanayo. Hawa nao tathimini iwaangalie upya.

Nne, kutokana na shule ya msingi Ngenge Kata ya Ngenge yenye wanafunzi 1,000 na zaidi wengi wakitoka mbali shule ya Kalimalimo ilianzishwa sasa iko darasa la nne na wananchi wanajenga vyumba vitatu na ofisi, lakini ipo shule moja ya Kihya inajengwa umbali wa kilometa 13 na wananchi wanapambana kujenga ili kupunguza umbali lakini na tatizo la vyumba shule mama ya Ngenge. Naomba miradi hii mipya wananchi wasaidiwe.

Mheshimiwa Spika, tano, kutokana na wanafunzi kuwa wengi katika shule ya msingi Kata Bumbiile wanafunzi 700, lakini wanafunzi hutoka mbali, shule mpya Kisha imeanzishwa kupunguza tatizo hilo na lile la vyumba. Kuna vyumba viwili tu, wananchi wanapambana kujenga vyumba vinne kwa kukusanya vionwa kwa sababu vyumba hivyo viwili tayari kuna wanafuzi wengi sana. Hawa nao waangaliwe.

Sita, tatizo kama la Bumbiile liko shule ya Mushenyi Kijiji cha Buhaya, Kata ya Kagoma, nao waangaliwe; na saba, kutokana na kuwa na sehemu kubwa Wilaya kuwa ni ziwa (70%), kunahitajika boti salama na ziendazo kasi. Hii itasaidia sekta za afya, elimu, maendeleo na usalama. Tulishaleta mapendekezo na maombi tusaidiwe

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia Bajeti ya Wizara hii ambayo naipenda sana na ninaifahamu. Nina mambo machache ya kuzungumzia.

Mheshimiwa Spika, kabla sijaenda niunge mkono hoja ya Bajeti hii. Takataaje kuiunga mkono? Watu wa Mtelakuza hawatanielewa, na nimemwona Profesa wangu hapo, Profesa Winnie-Esther hatanielewa, kwa sababu hii ndiyo dissertation yangu ya Ph.D iko hapa. Jambo la kwanza, nimekuwa nikizungumza kwamba shughuli zote za kiuzalishaji zitueleze mauzo ya nje. Nampongeza Waziri, ameonesha kwamba Dola bilioni 8.52 anauza nje, na kwa gazeti la Citizens na tarehe 20 Aprili, limeandika, Tanzania tunauza nje shilingi bilioni 12.383. Hiyo tumekubaliana.

Mheshimiwa Spika, nizungumze kidogo kuhusu blueprint. Blueprint imefanikiwa, na mafanikio ya kwanza yalitokana na pale sisi wenyewe tulipokubali kujitathmini. Blueprint tuliiandika sisi wenyewe na ninapenda kusema, architect mkubwa alikuwa Mheshimiwa Profesa Adolf Mkenda. Niwape changamoto nyingine, na hii siyo Wizara tu, ni Serikali, ni wadau wote, ni wananchi wote, tuendelee kujitathmini na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara kwa sababu ina tija kubwa.

Mheshimiwa Spika, namba tatu, kulinda tasnia au kulinda viwanda. Nimemsikia Mbunge wa Tanga anazungumzia viwanda kufa. Kufa kwa viwanda mimi nakujua vizuri sana. Vingine nilijitahidi kuvifufua, aah, nikashindwa.

Mheshimiwa Spika, nitachambua ulinzi wa viwanda na Profesa Winnie-Esther yuko hapo, ananisikia, kwenye marks zangu utaniongezea, nitatumia ngeli Michaek Porter, Profesa wa Harvard Business University kuchambua ni kutumia industry strategy kuwaonesha namna ya kulinda viwanda vya nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiacha viwanda kuna kitu kinaitwa tasnia nitawapa mfano rahisi, chukulia viwanda vya magurudumu ya magari, kama Michelin, Bridge Stone, Ring Long, Fire Stone na Safari, assume viwanda hivyo vingekuwa hapa nchini, unapoangalia industry strategy, unaangalia kitu cha kwanza, unaingiaje kwenye ile industry structure? Unaangalia ile barrier of entry na barrier of exit, lakini unajiuliza, unakwenda kumkuta nani mle ndani? The competitions, the players, lakini unaangalia nani mteja wako (the consumer)? Unaangalia nani supplier wako mle? Unajiuliza, ushindani ukoje? Ni ushindani wa kirafiki au wa kihasama? Au wa kukatana vimeo?

Mheshimiwa Spika, unapokuwa unaangalia mambo hayo kuna watu wana maslahi. Mojawapo ya watu wenye maslahi ni Watanzania kwa kesi ya viwanda hivi nilivyovitaja ambavyo siyo vya ukweli, kwa sababu hatuna viwanda vya magurudumu. Mojawapo, kwanini tunajenga viwanda? Tunajenga viwanda: -

(i) Kutengeneza ajira;

(ii) Kutengeneza bidhaa za kutumia na bidhaa za kuuza nje na yote yanakwenda pamoja. Naipongeza Wizara, inauza nje na inaonekana.

(iii) Kuchangamsha uchumi. Pale penye viwanda, uchumi unachangamka, na ndiyo maana nasikia kilio cha Tanga; na

(iv) Kukusanya mapato ya Serikali kwa ajili ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, unapokuwa unaangalia ES structure ya Michael Porter wakiwemo wadau watano au sita katika ile structure, angalia wanavyofanya kazi. Ndiyo maana unakuta yanaundwa makundi ya watu kutetea wateja wale watano, wale waendeshaji wa shughuli wanaweza kulumbana au wakaungana pamoja wakamuumiza supplier. Unaleta malighafi, wanakupa bei ndogo. Au wakaungana, wakamuumiza mlaji. Wanazalisha bidhaa, wanaziuza kwa bei kubwa. Ama wakashindana wao kwa wao, kwa ushindani unaoitwa ushindani wa kukata kimeo, unakuta wawili wanakufa katika wale watano, watatu wanaobaki sasa, wana conspire, wana-collude na kuongeza bei. Kwa hiyo, walaji mnaendelea kuumia. Au waka-merge, wakaungana mtu na dada yake, unadhani ni players wengi, kumbe ni wale wale, halafu ikatokea kuja kumuumiza mlaji.

Mheshimiwa Spika, nizungumze kitu kingine. Kwanini tunatengeneza viwanda? Kutengeneza ajira. Unapo-merge hawa washindani wa matairi ninaozungumza, wanaweza kuungana watu, kwa mfano, ukitokea mtikisiko katika industry katika shughuli; hawa watano wa matairi wakapatwa na mtikisiko, industry ikafa yote, siyo kwamba mmoja akabaki, kafa. Kitatakachotokea ni nini? Ni kwamba itatokea supply itatoka nje. Mtaagiza bidhaa za matairi kutoka nje. Fikiria, mkiagiza kutoka nje, dola mtazipata wapi? Hiyo ndiyo hatari kubwa. Mnapozungumza measure na acquisition, kama industry ikitikisika na kupasuka, you will end up importing. Now, you will end up using the rare dollars you have. Yaani Dola kidogo mliozonazo mtaweza kuzitumia kwa kuagiza bidhaa. Kwa hiyo, nataka kuwaeleza katika industry unapomwangalia…

MHE. GODWIN E. KUNAMBI: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Mwijage, kuna taarifa kutoka kwa Godwin Kunambi.

TAARIFA

MHE. GODWIN E. KUNAMBI: Mheshimiwa Spika, namuunga mkono mzungumzaji. Nchi inaponunua sana nje na siyo kuuza, kwenye uchumi naye ataniunga mkono, kuna terminology inaitwa cutoff right inflations, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Mwijage unapokea taarifa hiyo?

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, naipokea taarifa ya Mheshimiwa Chifu Kunambi. Unajua maprofesa wako juu hapa, watu wanatafuta kiki ya dissertations huko kwa maprofesa.

Mheshimiwa Spika, ninachotaka kuzungumza ni kwamba, industry ina mambo matatu. Moja, players wachache wanaweza kufa, waliobaki wakaua soko, lakini industry yenyewe inaweza kufa mkaamua kuagiza kutoka nje. Kwa mfano, wa Tanga niwaeleze, industry ya cement ya Tanzania iliwahi kupata tatizo la supply. Anafahamu Profesa Muhongo. Mimi na Profesa Muhongo tulikwenda kuwahakikishia Watanzania (Industrialist) kwamba mkaa wa Tanzania ni bora duniani. Yule tajiri namba moja duniani alipotuona, cv yangu na ya Profesa Muhongo, akakubali kwamba mkaa wa mawe wa Tanzania ni mzuri. Nazungumza kuhusu hawa suppliers.

Mheshimiwa Spika, mimi na Profesa Muhongo tulikwenda kuwahakikishia watanzania, kuwahakikishia industrialist kwamba mkaa wa Tanzania ni bora duniani. Yule tajiri namba moja duniani alipotuona cv yangu na ya Profesa Muhongo akakubali kwamba mkaa wa mawe wa Tanzania ni mzuri.

Mheshimiwa Spika, nazungumza kuhusu hawa supplier matokeo yake ni nini? Hii merge, merge ya Twiga na Simba matokeo yake ni kwamba industry inaweza kufa tukaishia kununua bidhaa nje, kwa hiyo merge pamoja na kuangalia sheria huyo ni mwanasheria mimi sijasoma sheria lakini pamoja na kuangalia maslahi ya wananchi lazima tuangalie kwamba tunapoungana hakuna uwezekano wa industry nzima kufa? Ili baada ya kufa bidhaa itatoka nje na ukuzingatia kwamba Tanzania leo tunahitaji saruji kuliko maelezo.

Mheshimiwa Spika, nimeshiriki kwenye ma–group mengi na nimewashauri, niipongeze Serikali kwa kujenga reli sisi hapa tunajiandaa kwa African Continental Free Trade. Kwa hiyo, vigezo vya kuwa na market share vizingatiwe ili kwa kuwa na market share unazuia watu kukurudi, watu kupanga bei na wakawaumiza wale wadogo wanaoota, matabirio yetu sisi ni kutengeneza Tanzania industry ya cement yenye tani 25,000,000 twende mbele kama anavyosema Baba Askofu Gwajima kwamba tuangalie mbele na kuangalia mbele ni kuangalia ile industry isiweze kuyumba.

Mheshimiwa Spika, kwa hayo naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nami nitajitahidi kuwasilisha kama Mheshimiwa Prof. Muhongo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naipongeza Serikali kwa kutenga bajeti zaidi ya kilimo, lakini nisisitize kwamba, pamoja na pesa hizi, ziendane na kuongeza nguvu kazi yenye ujuzi mkubwa na uthubutu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Serikali kwa kuamua kutenga Mabwawa 100. Kipekee bajeti hii imetaja irrigation kwenye Lake Victoria basin ikiwemo Kagera na Muleba. Kwa misingi hiyo, naunga mkono hoja. Kipekee, miradi ile midogo midogo ya visima 150 kila Halmashauri, yakiwa na matenki ya irrigation kusudi kuwasaidia wananchi wadogo wadogo, kutoka kwenye robo hekta na nusu hekta kuwapeleka kwenye hekta mbili wakilenga mazao maalum kama maharage. Kwa msingi huo, umewafikia wananchi, umewajumuisha, naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi najikita kwenye Tanzania Coffee Industry na niangalie kwa namna gani inaweza kuchangia uchumi wa nchi hii kutupeleka zaidi. Nampongeza Mheshimiwa Waziri, tulikuwa na kipato cha shilingi milioni 944 mwaka 2021 kama export, leo ametangaza kwamba tumefikia shilingi bilioni 1.38, ni hatua moja. Sasa kwa kuchelea, muda usitoshe, naomba katika tasnia ya kahawa na hususan Mkoa wa Kagera nitoe mapendekezo yafuatayo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa visima alivyopanga, na kwa irrigation scheme aliyopanga, tunaomba kwa Mkoa wa Kagera, Serikali iwahimize na kuwahamasisha wananchi wapande zaidi mibuni ambayo ni michanga inayoweza kuongeza kahawa. Pia sisi kahawa ilipoanguka bei tulipanda miti ya hovyo hovyo, naomba sasa Serikali tusaidiane, tuhamasishe wananchi, watumie kanuni za kiuchumi, waondoe ile miti, wapande miti rafiki, wafanye intercrossing na kahawa ili tupate kahawa zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba na kuishauri Serikali kuwa kwa Mkoa wa Kagera uwepo mpango maalumu wa kugawa miche bora angalau milioni 25 mpaka miche 30 kwa mwaka. Nitaeleza kanuni zake za uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri unisikilize, unao mkakati wako wa kahawa 2021/2025, kwa heshima na taadhima wewe ni rafiki yangu, nenda kaupitie upya. Huo mkakati ukapitiwe upya na Katibu Mkuu anisikilize, kama akitaka ushauri, nitamshauri upya. Aupitie mkakati ili utuwezeshe sisi kutumia zao la kahawa kuweza kuzalisha zaidi na kuleta pesa nyingi za kigeni. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naanza kuchangia tasnia ya Kahawa Tanzania. Soko la Kahawa Duniani ni dola bilioni 126.36, sisi Tanzania mazao yetu ya kahawa tunauza nje dola milioni 204. Katika soko la Shilingi bilioni 126 sisi tunachukua Dola milioni 204. Nakupongeza Mheshimiwa Waziri, nimepata habari kwamba South Korea umeingia, nimepata habari kwamba China mazao yako yameingia, nimepata taarifa kwamba Middle East umetufungulia soko, lakini kama wanavyosema watu wa Tanga, ukiona kobe juu ya mti, kuna mtu aliyempandisha. Nampongeza huyo aliyekupandisha kuweza kuingia masoko hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mahitaji ya Kahawa Tanzania yanaendelea kukua, kama nilivyoeleza, tumeshaingia kwenye masoko hayo. Hata hivyo, tuangalie wenzetu kama alivyofanya Mheshimiwa Prof. Muhongo. Kwa mwaka 2021/2022 Uganda waliuza Kahawa ya dola milioni 862, ndiyo maana nasema urudie mkakati wako. Mkakati wako unazungumza quantity, hauzungumzii amount of money. Ukiusoma unazungumza quantity, hatuhitaji idadi, tunahitaji pesa tunazopata. Chini ya Mamlaka ya Kahawa ya Uganda, wanaeleza mamlaka itakachofanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Waganda wana mkakati wao wa kuingiza sokoni dola milioni 300 kwa mwaka, na kwa miaka mitano wanapanga kuingiza dola bilioni 1.5 kwa kutumia kahawa tu. Kwa hiyo, kwa mwaka 2022 mpaka miaka mitano ijayo watakuwa na 1.5 in additional na ile dola milioni 800, yaani watafikia dola 2.362, hiyo ni Uganda.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi naiona Tanzania kama kwa mfano wa Kagera niliokwambia, kama tukiweza kuzalisha miche bora milioni 25 mpaka milioni 30 kwa Kagera ambayo inazalisha asilimia 44 ya Kahawa yote ambayo yote ni Robusta, nina uhakika kwa hesabu za uwiano utaweza kuingiza karibu dola milioni 600.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa uwiano huo kama tasnia nzima ya kahawa Tanzania, ikiweza kuwekezwa kwa nguvu hizo tutaweza sisi Tanzania kuzalisha bilioni 1.56 kutokana na kahawa kwa miaka mitano mpaka kumi ijayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nilikuwa naishauri Serikali, hii miradi ya uwekezaji ielekezwe kwenye zao hili la Kahawa. Kwa mfano; kwetu upande wa Kyelwa, Kyelwa ni wazalishaji wazuri wa Kahawa, wapewe miche zaidi. Lakini Ngara wanasifika kwa kuzalisha Kahawa yenye ubora mkubwa sana. Waangaliwe waweze kushindana na mshindani wetu wa Burundi. Pia bora Mzee Kanyasu ulikuwa Mkuu wa Wilaya pale. Vilevile sehemu ya Biharamulo ambayo ilikuwa sehemu ya BCU ukiunganisha na Muleba ni ukanda ambao unaweza kuzalisha Kahawa kwa wingi. Umekuja na mpango wa irrigation ambako utafanya irrigation sisi kwetu hatuhitaji visima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukianzia ukanda wa ziwa kuanzia sehemu za Mayondwe, kuja sehemu za Kagoma, kuja sehemu za Izigo Kwenda Lwanganilo mpaka Kimwani, sehemu zote unaweza kuweka pump kwenye maji una irrigate kwenye ukanda wote wa ziwa na tunapata Kahawa nyingi. Ndio maana nasema Kagera tunaweza kuzalisha dola milioni 500 kwa kutumia Kagera tu. Kwa uwiano huo pato la kipato cha Mkoa wa Kagera litaweza kuendelea, wala hatuhitaji viingereza wala kitu gani, ni kwamba unazalisha zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na pesa ambazo Serikali imepanga, nimeunga mkono hoja. Lakini kwa kuwekeza pesa hapa utaweka shilingi moja na utapata shilingi mbili, hili ndilo eneo la sekta ya kiuzalishaji ambalo unaweza kuzalisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kuzalisha, liko suala la utumiaji wa Kahawa. Sisi tunatumia 0.07 kwenye kahawa…

NAIBU SPIKA: Ahsante, ahsante.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: …wenzetu wa Algeria wanatumia kilo tatu, tunywe kahawa, kahawa ni burudani.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa ahsante.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, kupitia njia ya maandishi naomba kuchangia bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi. Sekta hii ni sekta wezeshi katika ujenzi na maendeleo ya nchi yetu ikichangia takribani asilimia 26 katika kuleta fedha za kigeni. Hii ni sekta inayoongoza katika sekta zinazounda tasnia ya huduma (service industry). Unapoangalia mafanikio na mchango wa utalii katika kuingiza fedha za kigeni ni vigumu kutenganisha usafiri na usafirishaji na utalii. Pamoja na umuhimu huu hii ni sekta ambayo tofauti na rasilimali zinazokwisha kama madini, sekta hii ni ya kudumu na huleta manufaa kadri inavyoboreshwa.

Mheshimiwa Spika, ninapoandika na kuchangia sekta hii nitambue mafanikio makubwa katika Taifa letu katika mwezi huu, hatua ya kufikia makubaliano kati ya Serikali na wawekezaji katika mradi wa kutengeneza gasi kimiminika (LNG) na matumizi ya gesi asilia katika magari yaendayo kasi jijini Dar es Salaam (CNG) ni jambo lenye tija kubwa kwa sekta hii na Taifa kwa ujumla. Mafanikio haya yanahitaji nguvu na ushiriki mkubwa wa Wizara ili tufikie malengo tunayotarajia.

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kuishukuru Wizara kwa kuboresha uwanja wa ndege wa Bukoba hasa eneo la uongozaji ndege. Nilipongeze Bunge letu tukufu kupitia Kamati inayosimamia Wizara hii kwa kuishauri Serikali ijenge uwanja wa ndege mpya mkoani Kagera. Eneo la mkoa wa Kagera ukizingatia na nchi zinazotuzunguka (location advantage) kuna umuhimu na haja ya kujenga uwanja wa ndege mkubwa maeneo ya Omukajunguti au Kashaba ili kutoa huduma ya usafiri na usafirishaji kwa maeneo haya. Wananchi wa Rwanda, Uganda na DR Congo katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii wanategemea eneo hili.

Mheshimiwa Spika, pamoja na changamoto za uwanja wa Bukoba uliopo sasa, uwanja huu ni miongoni mwa viwanja saba vyenye abiria wengi nchini bila kuhesabu abiria wanaoshuka Mwanza kwa kuogopa kutua Bukoba. Tunaiomba sana, Serikali ijenge uwanja wa ndege mkubwa Kagera.

Mheshimiwa Spika, shirika la ndege la ATCL linaelekea kuanza biashara ya kusafirisha mizigo kwa ndege maalum za mizigo. Naomba na kushauri katika kutekeleza mpango huu ni muhimu kuanzia sasa kuwashirikisha wadau wa kuuza na kuagiza bidhaa toka nje ya nchi kwa lengo la kubaini wingi wa mizigo inayohitaji huduma ya ndege. Tuwe na uhakika sasa kabla ya ndege ya kwanza kuwasili, wazalishaji wa nchini na nchi jirani wahamasishwe kutafuta masoko ya moja kwa moja na maalum.

Mheshimiwa Spika, Serikali imewekeza sana kwa kujenga vivuko katika Ziwa Victoria upande wa Mashariki na Kusini, niombe na kushauri sasa ombi la kujenga vivuko katika Ziwa Victoria upande wa Mkoa wa Kagera litekelezwe.

Mheshimiwa Spika, napongeza mpango na uboreshaji na ujenzi wa maegesho Kisiwa cha Ikuza. Tunaomba na kushauri vivuko kwa kutoa huduma kati ya Magarini na Kyamkwikwi na visiwa vya Ikuza, Mazinga, Bumbiile na Kelebe ipangwe na kutekelezwa. Upo mpango wa siku nyingi wa kujenga na kuweka kivuko Kabango Bay kilometa 42 Kaskazini mwa Mji wa Bukoba. Kivuko hiki ni muhimu katika kuunganisha nchi yetu na Uganda katika dhana hii ya biashara huru katika Bara la Afrika lakini na mahusiano mema na nchi jjrani.

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kuishukuru Serikali na hususani Wizara kwa mipango ya kuboresha usafiri katika Visiwa vya Wilaya ya Muleba. Uwepo wa meli ya Clarias na meli/boat maalum ziendazo kasi utasaidia kuboresha maisha ya Visiwa vya Goziba, Kelebe, Bumbiile, Ikuza na Mazinga na bandari ndogo za Kyamkwikwi na Magarini nchi kavu. Tunashukuru kwa nia ya kupeleka barge Bandari ya Goziba ili kuwezesha meli tunaposubiri gati yetu kuboreshwa. Nashukuru kwa mipango na utekelezaji wa uboreshaji wa Bandari za Bukoba na Kemondo Bay, tunapoendelea na uboreshaji nishauri Bandari ya Bukoba iwekewe mazingira ya kuwezesha meli zaidi kuegesha hasa Songoro Marine. Tunaomba meli za Songoro ziwezeshwe kutoa huduma katika bandari na visiwa vya Ziwa Victoria.

Mheshimiwa Spika, nipongeze na kushukuru kwa ujenzi wa barabara kiwango cha lami kutoka Muhutwe, Kamachumu, Buganguzi, Nshamba mpaka Muleba. Ujenzi umebakiza kilometa 7.4 kukamilika, tunaomba na kushukuru kazi iendelee kwa kumalizia eneo lililobaki. Tunaomba mchepuko wa kilometa tatu kuelekea Hospitali ya Ndolage ufikiriwe kwa kuendeleza kilometa moja iliyojengwa katikati ya Mji Mdogo wa Kamachumu.

Mheshimiwa Spika, napongeza mpango wa ujenzi wa barabara ya Mutukula, Bukoba mpaka Kagoma, ombi na ushauri ni kuwa maegesho ya magari wakati wa kushusha a kupakia abiria yaboreshwe. Sasa hivi barabara tajwa ina mabasi ya abiria mengi sana, tena mengi yakipita maeneo haya usiku na alfajiri, uboreshaji uzingatie eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, mwisho lakini si kwa umuhimu niombe kufungiwa taa za barabarani katika Mji Mdogo wa Kamachumu. Pamoja na eneo hili maboresho ya barabara ya Mutukula mpaka Kagoma yahusishwe kuweka taa Mji Mdogo wa Muhutwe, Kakindo, Izigo, Kagoma na Kikuku.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Nishati
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kuwahisha zawadi yangu kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia bajeti ya Nishati nikiwa mtu wa kwanza.

Mheshimiwa Spika, Mwezi Julai nitakuwa nakamilisha miaka 39 tangu nianze utumishi kwenye sekta hii ya nishati, kwa hiyo kwa kuniteua niwe wa kwanza kuchangia umewahisha zawadi yangu ya miaka 39. Kuna lingine niliseme kwa wapiga kura wangu masuala ya umeme nimeyamaliza jana kwenye maonesho ya umeme ya karne. Maonesho yale yaliyofanyika jana hapa hoja zenu zote nimezipeleka kwa Meneja wa Wilaya na wa Mkoa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitazungumza kuhusu mafuta na gesi tu umeme nimemaliza. Pia nimuombe Waziri ukatafute kitabu kinaitwa Tanzania Oil and gas cha Mzee Sylvester Barongo, kinaelezea historia ya mafuta na gesi kuanzia mwaka 1952, mwaka 1974 tukapata gesi ya kwanza Songo Songo akiwepo, 1982 Mnazi bay tukapata gesi Mzee Barongo akiwepo. Pia nafurahi Mzee Ntomola yuko pale, Mzee Khalifan yuko hapa, Mzee Mwandosya bosi wetu yuko hapa. Kitabu ni kizuri ana kitawasaidia Wabunge waelewe sekta ya gesi Tanzania tunapojiandaa kwenda uchumi wa gesi.

Mheshimiwa Spika, suala la kwanza nizungumzie bomba la mafuta. Nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Rais Dkt. Jenerali Mseveni kwa kuwa na msimamo thabiti kuhakikisha bomba la kutoka Hoima mpaka Chongoleani linajengwa. Ujenzi wa bomba hili pamoja na kuleta faida za ajira litafungua njia za kuweza kuchochea wawekezaji katika sekta ya mafuta waweze kuweza zaidi. Sisi tunayo rasilimali ya mafuta lakini watu wengi wamekuwa hawaji hapa wakijiuliza mafuta ya Kigoma utayafikishaje Dar es Salaam, Eyasi Wembere utayafikishaje Dar es Salaam. Sasa kwa kujenga bomba la mafuta ni kwamba wawekezaji wengi watapata motisha. Kwa hiyo, kwa sababu hiyo mimi ninaunga mkono.

Mheshimiwa Spika, suala lingine kwa kutumia bomba la mafuta ajira zitakazotengenezwa zaidi ya 10,000 ni kwamba vijana wa Kitanzania sasa wanakwenda kufundishwa stadi za Kimataifa, baada ya ujenzi wataweza kutumika katika viwango ya Kimataifa mahali popote duniani. Sambamba na hilo ninaipongeza Wizara na naipongeza Serikali kwa kumaliza rejea ya product sharing agreement, hili suala la OPSA limechelewesha utafutaji mmefanya maamuzi mmeweza kushughulikia suala hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala la bulk procurement ununuaji wa mafuta kwa wingi. Bila kusema mengi naunga mkono mapendekezo ya Kamati iliyopewa dhamana ya kusimamia shughuli hii ya bulk procurement. Kama huwezi kujua adha angalia kwa mwenzako, mwaka mzima tumemaliza pamoja na mitikisiko ya kidunia hatukuweza kupata ukosefu wa mafuta nchini. Majirani wetu wamepata hiyo adha, hata Watasha huko Ulaya wamekosa mafuta lakini sisi tumekwenda vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wenzetu wamehangaika kutafuta njia mbadala lakini ule ulinganisho wa kiasi cha kununua mafuta wengine wananunua bei ghali mara nne. Premium yetu iko kwenye 40 kuna wenzetu wananunua premium ya 160. Kitabu kile cha Mzee Barongo ambae ni bosi wangu kinaelezea namna ya kutafuta premium mkitafute muweze kukisoma.

Mheshimiwa Spika, sasa zaidi niende kwenye mradi wa LNG, nilimwona Mama salma anapiga makofi, anashangilia tunakuja Lindi na mimi nakuja Lindi ujombani nami nifaidi. Mradi wa LNG ni mradi mkubwa wa dola bilioni 42 zaidi ya bajeti au sawa na bajeti yetu ni mradi mkubwa.

Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza, mimi nimesoma suala la maamuzi. Nichukue fursa hii kipekee kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kufanya maamuzi amefanya maamuzi, hivi visima havikuwepo leo lakini imekuwepo dana dana kwa miaka saba kama alivyosema Waziri, lakini Mheshimiwa Rais akatoa maamuzi. Mwezi Juni nilimsikia mwenyewe akasema nendeni mtekeleze haraka. Sasa niko hapa kuwaelekeza kwa nini Mheshimiwa Rais anataka tutekeleze mradi huo kwa haraka? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mradi huu wa LNG utakapokuwa umefanyika uwezo wa Tanzania kuuza nje kwenye masoko ya Kimataifa utaongezeka, tutapata pesa nyingi za kigeni, ulali wa kuuza na kununua Tanzania tutakuwa na advantage tuta-export zaidi. Sasa hivi Tanzania tuna-export bidhaa zenye dola bilioni 12 kwa mwaka. Gesi peke yake itakuwa na uwezo wa kusukuma katika soko la Kimataifa zaidi ya uwezo huo.(Makofi)

MHE. PROF. KITILA A. MKUMBO: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Mwijage kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Profesa Mkumbo.

TAARIFA

MHE. PROF. KITILA A. MKUMBO: Mheshimiwa Spika, nataka nimpe taarifa Mheshimiwa Mwijage, amesema dola bilioni 42 ni sawa na bajeti yetu, actually ni sawa na GDP yetu. Kwa hiyo, ni fedha nyingi ambazo ni pesa nyingi kwa kweli uamuzi anaouzungumza ni uamuzi mzuri na ni uamuzi mkubwa sana, kwa sababu ni fedha nyingi na zitabadilisha kabisa uchumi wetu. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Mwijage, unapokea taarifa hiyo?

MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nizungumze taratibu aliyenipa taarifa ni Profesa na amesema anatoa taarifa kusisitiza Mheshimiwa Rais kufanya maamuzi, weka kwenye mabano nakubali taarifa hiyo. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kwa nini Mheshimiwa Rais amesema tuharakishe? Mafanikio ya kuanza kutumia gesi yataharakisha ujenzi wa uchumi wa viwanda. Siyo ujenzi wa viwanda ni kujenga uchumi wa viwanda ina maana chuma utakayoipata shughuli za kuendeleza sekta ya gesi LNG itatupatia pato, itafundisha watu. Kwa hiyo, tunapozungumzia sekta za uzalishaji iwe kilimo, mifugo, sekta zote tutaweza kuzalisha kwa tija. Pamoja na kuwa na mafuta tutaweza kuwa mabingwa katika dunia kwa kutumia haya mazao ambayo yamekuwa yakitusaidia siku moja, siku nyingine, tutauza kahawa nyingi, maziwa mengi, pamba nyingi ile C to C sasa tutaweza kuwa na viwanda vyetu hapa.

Mheshimiwa Spika, kama ilivyo kwenye bomba la mafuta tunakwenda kutengeneza huo ndioy mfano kwenye chuo cha Lindi, tunakwenda kufundisha vijana wetu wawe wataalam katika sekta za mafuta ili Tanzania sasa miaka ijayo wawekezaji wanakuja kuchukua vijana wetu hapa na kwenda kufanya kazi sehemu nyingine.

Mheshimiwa Spika, kwa kutenegenza huu mradi kwa kukubnaliana sasa wawekezaji mahili wa dunia wanajua kwamba Tanzania sasa ni mahali salama pa kuwekeza. Makampuni yanakuja sisi tuna TCF zaidi ya 68 hizi mlizonazo, mimi sio mtabiri lakini najua kwa uhakika hapa tuna mafuta, hapa tuna gesi lakini hauwezi kuyapata mafuta mpaka uyachimbe.

Mheshimiwa Spika, naomba nitoe sababu nyingine kwa nini tunafaidi kitu hiki. Faida nyingine katika utafutaji wa mafuta ni kwamba sisi Watanzania kwa fursa tuliyonayo tunakwenda kubeba nchi nyingine zilizotuzunguka. Tulikuwa na mradi wa mbolea ulikwama kwa kuangalia gesi tuitumie kwa namna gani, sasa bila kutetereka tutatengeneza kiwanda chetu cha mbolea na kitaweza kufanya kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niwakumbushe Wabunge wenzangu, na Mheshimiwa Jafo naona simuoni na wenzangu niliokuwa sisi ni mahiri wa gesi, sisi tunajua gesi. Gesi inayokuja ni neema tumekaa nayo tumejitafakari. Kwa hiyo, wale wanaofikiria kwamba gesi ni laana ni kwao. Sisi gesi tunaijua tumedhibiti mafuta tunajua namna ya kuitumia. Pia, lengo la nishati hii ni kwa ajili ya mapato na matumizi na ustawi wa Watanzania. Tunakwenda kujenga uchumi imara, uchumi wezeshi na uchumi ulio jumuishi. Kwa hiyo, naunga mkono maamuzi ya Mheshimiwa Rais kwamba tuharakishe ujenzi wa gesi ili iweze kuwafikia wananchi ili kusudi ichangamshe uchumi nan chi yetu iweze kuwa ni nchi yenye ushindani ambayo inakwenda kwenye uchumi mkubwa, uchumi wa Watanzania wote.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono bajeti ya Wizara hii. (Makofi)
Azimio la Bunge Kuhusu Pendekezo la Kuridhiwa Mkataba Baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa Lengo la Kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia mada iliyopo mezani. Kwanza, niunge mkono wasilisho la Mheshimiwa Waziri, lakini niungane kabisa na mapendekezo ya Kamati mbili zilizotuongoza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haya makabrasha na mikataba nimeyasoma sana, na nimshukuru sana consultant wangu Mheshimiwa Advocate Lujwahuka aliyeniongoza kipengele kwa kipengele. Kwa hiyo mambo ya mikataba sitayazungumza ila nitaunga mkono kwa kupitia transport and transportation economics, mambo ambayo mimi nina uzoefu nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la bandari au usafiri na usafirishaji kuna wadau wawili wana maslahi, mmoja ni mwenye mzigo. Maslahi ya mwenye mzigo ni mzigo wake ufike haraka sana na ufike salama. Mdau wa pili ni mwenye rasilimali au mwendeshaji, yeye ni kupata chumo alilowekeza return on investment na faida, na apate faida justifiable, siyo awanyonye wale wanaomtegemea. Kwa hiyo, utendaji wa bandari unakwenda namna hiyo.

Mheshimiwa Spika, lakini nizungumze suala lingine kuhusu ushindani wa bandari (the competitiveness of a port); hii inategemea namna gani bandari inaweza kupokea meli, inaitwa vessel turn around, ikaipokea haraka na kuiondoa ikaondoka haraka, yaani kama mtu anakuja, captain anaingia maji ya Dar es Salaam, anaiita Dar es Salaam, Dar es Salaam mnakuja, wanamwambia karibu. Aingie aende bandarini, ashushe, apakie aondoke; hicho no kipimo moja wapo cha competitiveness of a port. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine linaloleta ushindani wa bandari ni muunganiko wa sekta au miundombinu inayofanya hiyo bandari ifanye vizuri, hapo tuna barabara na reli au mfumo mzima wa logistics.

Mheshimiwa Spika, nitoe mfano mmoja, Bandari ya Dar es Salaam tumekuwa tukishindwa kuuza matunda na chai itokayo mikoa ya Kusini kwa sababu ya udhaifu wa logistics, yaani matunda wanayapeleka Mombasa na chai wanapeleka Mombasa kwa sababu ya competitiveness hiyo.

Mheshimiwa Spika, sasa competitiveness, indicators nilizozungumza ni vessel turn around, lakini kitu kingine ni ukubwa wa mzigo. Bandari inashika mzigo kiasi gani. Kama mzigo ukipakiliwa China au Singapore meli ikajaa, isisimame popote, ina maana mzigo wetu utakuja haraka, kwa hiyo bandari yetu itakuwa competitive.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kama walivyozungumza Wabunge, unakusanya mzigo mzigo kwa sababu huwezi kuwa na mzigo mkubwa na hapo ndipo inapokuja utafute mshirika mwenye uwezo. Siyo siri, DP World anakuja; kwa nini? DP World ameshashika mzigo ulipo, ameshashika Rwanda, ameshashika DR Congo, lakini yeye ni mkusanyaji mzuri wa mizigo huko inakotoka.

Mheshimiwa Spika, kwa nini tunamchukua? Ni ili tupate mzigo mkubwa meli ije moja kwa moja Dar es Salaam, na Dar es Salaam iwe trans-shipment center ndogo. Kama mizigo inafika hapa basi ipakuliwe hapa na kwenda kwenye nchi nyingine.

Mheshimiwa Spika, competitiveness namba tatu ni speed. Basi kama meli imepakia kutoka itokako moja kwa moja Dar es Salaam itakuja kwa speed kubwa, hakutakuwa na trans-shipment ya suala hilo, ilibidi niliseme hivyo.

Mheshimiwa Spika, ninapozungumza hapa, limezungumzwa suala la TEHAMA. Nadhani Mheshimiwa Mwakyembe atakuwa anasikia, katika watu ambao wamehangaika kuweka mifumo katika Bandari ya Dar es Salaam alikuwa ni Mheshimiwa Mwakyembe. Hata kulazimisha watu walipe kuingiza benki watu walipe kwenye benki watu walikuwa wanakataa. Lakini kwa kuweka TEHAMA, mwekezaji anayekuja anakuja kuweka TEHAMA. Maana yake ni nini? Maana yake anapokuja, kontena likifika mteja ataweza kujua kontena lake limefika, lakini na wenye interests zao wataweza kujua kwamba kontena limefika.

Mheshimiwa Spika, sasa niichambue kwa misingi ya kiuwekezaji. Katika uwekezaji tunaangalia suala la kwanza ni ajira, niwatoe hofu na wote walionipigia simu na walionitumia messages. Ukisoma kifungu namba 13 uwekezaji huu utaongeza shughuli, lakini kifungu namba 13 kinasema ajira za Watanzania waliopo kazini zitalindwa, lakini na Watanzania zaidi watafundishwa ili waweze kupata kazi pale. Kwa hiyo, kiuwekezaji mimi sina tatizo.

Mheshimiwa Spika, suala la pili katika uwekezaji, tunakwenda kuzaa bidhaa. Kimsingi katika hii sekta ya uwezeshaji ni service, huduma zitaongezeka kwa sababu meli zitakuwa zinakuja kwa haraka zinachukua muda kidogo, kutakuwepo big volume, the service will improve kwa sababu una-order mzigo wako, mzigo unafika, unaondoa mzigo wako, unakwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine ni kuchangamsha uchumi. Hakuna haja ya kuzunguka, tumezungumza kutengeneza industrial zone, tumezungumza kutengeneza logistics center. Zikitengenezwa watakazi-manage ni wananchi, kwa hiyo uchumi utachangamka.

Mheshimiwa Spika, kipengele namba 18 kimezungumza wazi, uwekezaji lazima utupeleke kwenye kulipa kodi. Kutakuwepo na kukusanya kodi. Sasa makusanyo ya kodi yale tunakusanya kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mengine wamezungumza, haya ya disputes. Lakini niwaeleze wasafiri na wasafirishaji kwamba ukisafirisha mzigo kutoka Dar es Salaam, transporter, ukifika kwenye mpaka wa Congo utakwama. Lakini magari yanayotoka Durban hayakwami kwa sababu gani? Ni kwa sababu anayesimamia mizigo kutoka Durban anawasiiana na yule anayekusanya mzingo ndani ya Lubumbashi, mzigo unakusanywa moja kwa moja unaweza kupita. Sisi madereva wetu wanakaa siku 30, hata siku 40 kwenye mpaka wa Tanzania na DRC.

Mheshimiwa Spika, lakini niwambejambo moja, na hili nakuomba Mheshimiwa Waziri unisikilize; mimi katika Ziwa Victoria nina bandari 13, huyo mtu kwenye phase two, usisubiri phase two, mlete kwenye bandari 13 za kwangu, aende Goziba, aende Rwangamile, aende Kyamkwikwi atengeneze bandari ili marine seaport aweze kusafiri na kusafirisha watu. Songoro Marine anashindwa kusafiri kwa sababu hana port nzuri.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Haya, ahsante sana.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nilisema mwanzoni naunga mkono hoja, lakini Mheshimiwa Waziri umenisikia, mlete huyo mtu atengeneze bandari kwetu, atengeneze bandari Goziba tusafiri. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kunipatia fursa ya kujadili au kuchangia bajeti ya Serikali ya mwaka 2023/2024; lakini na Mpango wa mwaka 2023/2024.

Mheshimiwa Spika, Mpango wa mwaka 2023/2024 dhima yake ni kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha sekta za kiuzalishaji ili kuboresha maisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Rais, lakini na mpishi mwenyewe Waziri wa Fedha. Hii kauli ya kuboresha maisha nimeipenda sana. Kama unaita majina, Mheshimiwa Mwigulu kama uliita jina wewe hili unajua kuita majina, tunataka kuboresha maisha ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, taarifa kama tulivyoisikia na katika maandishi, utekelezaji wake ni mzuri na ni wa kiwango cha juu, ni kutokana na taarifa lakini ni kutokana na kule tunakoishi nchi nzima, uraiani kwetu, mikoani kwetu, utendaji unaonekana.

Mheshimiwa Spika, ziko dalili wazi; miradi ya umeme vijijini inaendelea, ujenzi wa mashule ikiwemo vyuo vya VETA, ninapozungumza VETA Kijiji cha Bushagara, VETA inajengwa inaendelea, lakini jitihada za Serikali za kuweka pesa katika mabenki TIB ili kuwaongezea watu ukwasi na kuweza kukopa. Lakini jitihada za Serikali katika miradi ya maji, tulikuwa na miradi ya maji 586, kipindi tulichomaliza, nimeiona kwa macho yangu katika Jimbo langu, nimeiona popote napopita Tanzania katika kamati ulizotutuma, lakini mpango wa Serikali wa kutengeneza miradi 1,293 mimi inanituma bila wasiwasi kuunga mkono bajeti hii ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, bila kuisahau TARURA niipongeze Serikali kwa mpango wake wa kutenga pesa zaidi kwa idara hii ya TARURA, ili tuweze kutengeneza barabara ziweze kuwafikia wananchi.

Mheshimiwa Spika, linazungumzwa suala la uchumi wa dunia, wanazungumza uchumi wa dunia na kiashiria rahisi cha uchumi wa dunia ni takwimu. Mimi ningependa niwaeleze Watanzania na Wabunge wenzangu viashiria rahisi vya kujua uchumi wa dunia ni mzuri, lakini sisi kiongozi wetu na wasaidizi wake akiwemo Waziri wa Fedha, tumeweza kuudhibiti uchumi. Wakati kuna nchi sio za kutafuta, ndege zilishindwa kuruka, magari yalishindwa kutembea kwa kukosa mafuta, tatizo hili hapa kwetu halikutokea. Wakati kuna nchi watu walilala njaa, Serikali kabisa viongozi wakuu walihangaika wakitafuta chakula sisi hapa hatukukosa chakula. Yupo rafiki yangu aliwahi kuniuliza unamfahamu Waziri wa Kilimo, nikasema yule ni mtumishi mwenzangu akasema kamshukuru. Nilikuwa na shida na njaa kwetu nikamwambia akaandika karatasi NRFA wakapeleka chakula, sisi hatukulalamika na chakula. Kwa hiyo, Serikali imeudhibiti uchumi huu wa dunia kwa tafsiri ya kirahisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mtanzania yeyote ajipime kwa hilo ulikuwa kwenye kituo cha mafuta ukakosa mafuta, haikutokea, lakini kuna nchi zimekosa mafuta, zimekosa chakula. Watu wamekuwa na black out, umeme umeshindwa kuwaka wakataka black out, lakini Tanzania hatukuweza kuingia katika hilo. Baya zaidi kuna nchi katika bajeti zao walisimamisha bajeti za maendeleo, yaani Serikali imetengeneza bajeti mwaka jana kwamba maendeleo yasitekelezwe, lakini Tanzania hakuna mradi uliosimama. Kama anavyosema Mheshimiwa Rais hakuna kilichosimama na kweli hakuna kilichosimama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nipongeze Serikali na Mheshimiwa Waziri umeweka msingi wa bajeti ambao ni kazi kubwa na kazi lazima ifanyike. Msingi mmoja wa bajeti unasema kuongezeka kwa ushiriki wa sekta binafsi kwenye shughuli za uwekezaji na biashara.

Mheshimiwa Spika, ili bajeti yetu iweze kufanikiwa ni lazima kuongezeka kwa ushiriki wa sekta binafsi. Mimi nina ushauri wa mambo mawili. Tunapoizungumzia sekta binafsi tusiangalie wakubwa tu, hata hawa wadogo wanaolima kilo mbili za maharage, wanaolima mahindi na wao twende nao. Sekta binafsi ni mzalishaji yoyote, tusikimbilie wale wakubwa. Suala la pili ninaloomba unapozungumza sekta binafsi kuna sekta binafsi ya Tanzania na sekta binafsi ya Kitanzania.

Mheshimiwa Spika, nimshauri Mheshimiwa Waziri lazima sekta binafsi ya Kitanzania tuifikirie. Tungependa watoto wetu tuwaweke katika shughuli kusudi wasije kuwa watazamaji kwenye mchezo ambao waliuanzisha wao. Niipongeze Serikali hasa Mheshimiwa Waziri, umezungumzia juu ya mamlaka za udhibiti, ukazungumzia na TRA, lazima kama tunaitegemea sekta bonafsi basi mamlaka za udhibiti zifanye mazingira ya kufanya shughuli yawe mazuri, wasiwe kikwazo. Siwezi kuongezea zaidi namna ya kutekeleza hii, ni kutembea na maelekezo ya Mheshimiwa Rais, lakini ni kutembea na maneno yako ambayo uliyatoa kwa maneno yanayoeleweka.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie Tume ya Mipango, tuliomba Tume ya Mipango, Wabunge tumezungumza Tume ya Mipango, hatimaye Tume ya Mipango iko kazini.

Ombi la kwanza Serikali, mamlaka Tume ya Mipango muwape majukumu lakini muwape mamlaka na wawajibike kwayo (authority, responsibility and accountability). Tungependa Tume ya Mipango ituongoze, tunatengeneza dira lakini dira bila Tume ya Mipango haiwezi kufika mahali popote. Unaweza ukawa na mali nyingi, ukakusanya rasilimali nyingi ukazitumia, lakini ukazitumia bila mpango. Sipendi kuzungumza mengi zaidi tuna imani na Tume ya Mipango, lakini Tume ya Mipango iwe wazi ili kusudi watu waweze kutoa mawazo yao.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie dhima ya mwaka wa fedha ujao inayosisitiza kuimarisha sekta za uzalishaji ili kuboresha maisha. Hili neno kuboresha maisha kuna ndugu yangu mmoja anaishi Songwe huko analipenda na mimi nimelipenda zaidi naona Mheshimiwa Waziri ameiga kwako, tuboreshe maisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nizungumzie kidogo kuhusu urari wa biashara ya bidhaa na huduma, katika urali wa biashara wa bidhaa na huduma mwaka huu tunaomaliza tumepata hasi bilioni 3.87, bidhaa na huduma, lakini urari wa biashara na bidhaa tumepata nakisi ya bilioni 6.066, urari wa biashara ya huduma tumepata chanya bilioni 2.199 maana yake nini, tumeokolewa na utalii na sekta za huduma.

Kwa hiyo, kwa kuanzia lazima tuwekeze nguvu nyingi kwenye utalii, lakini hizi sekta za kiuzalishaji tulizozungumza lazima tuwekeze katika sekta za uzalishaji kusudi tuuze zaidi. Maana yake nini? Tuingie kwenye import substitution come export promotion, tuingize pesa zaidi kwa kutoka nje ndio tuweze kuhimili kutekeleza bajeti hii.

Mheshimiwa Spika, naona umeniwashia taa, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia Wizara ya Mifugo na Uvuvi; Wizara ndugu na Wizara ile ya Kilimo ambazo ni sekta za kiuzalishaji. Nilishaeleza mwanzo umuhimu wa sekta hizi, sasa niende kwenye undani wa sekta hizi, the agricultural sector, kwa wale ambao hawakusoma kilimo, inahusu mazao (growing crops) inahusu ufugaji wa ndege na kuku (poetry), inahusu kufuga wanyama (animal husbandry), inahusu kufuga samaki (aquaculture), inahusu maua horticulture na floriculture. Sasa tunazungumza kile kipande kingine baada ya kumaliza kipindi kile cha kwanza kilichokwenda na zawadi ya mama Mkoa wa Kagera. Ngoja nichambue hii nione kama na hapa kuna zawadi ya mama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kwanza suala la ufugaji wa vizimba. Waheshimiwa Wabunge wenzangu wamezungumza na mwaka jana, 2021 nilizungumza, kwamba Misri anafuga samaki tani 1,400,000, lakini maji aliyonayo Misri ni madogo, ni machache kuliko maji ya Tanzania. Nakubaliana kuna kampuni moja ya simu zamani ilikuwa na kaulimbiu inasema: “Now You Are Talking.” Naweza nikasema Government, now you are talking, au now you are coming. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma taarifa ya Waziri anasema atatengeneza vizimba 19,500 na kufanya environment impact assessment ili atengeneze makazi kwa ajili ya ufugaji. Kagera atatupa maeneo tisa, lakini muhimu ni kwamba atazalisha tani 100,000. Kabla ya hapo tulikuwa tunazalisha tani 12,000. Tunatoka tani 12,000 anakwenda tani 100,000. Misri, now we are coming Misri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kuvutia kwamba mapato ya samaki hizo tani 100,000 ni Shilingi bilioni 600. Mauzo ya kahawa ya Tanzania kutoka Septemba, 2020 mpaka Septemba, 2021 ni dola za Kimarekani 163,000 au shilingi bilioni 383. Ina maana kwa kuwekeza kwenye vizimba vya Ziwa Victoria samaki watazidi kahawa, lakini hatutaacha kahawa, tutafanya kahawa, tunafanya na hiyo. Ndiyo hiyo Kamati yetu ilikuwa inalalamikia, ndiyo hiyo Kamati yetu ilikuwa inashauri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ambayo nami natumika naiunga mkono kwa maneno mawili; imeiambia Serikali changamoto za ugawaji wa vitalu zitatuliwe mara moja, nawaunga mkono. Jambo la pili, tuhimize kufuga, siyo kuchunga. Ndugu yangu Mheshimiwa Vita Kawawa kinachomwogopesha ni kuchunga, siyo kufuga. Tuhimize kufuga, siyo kuchunga. Huwezi kujenga uchumi wa nchi hii bila kufuga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze jambo lingine kuhusu upungufu; na katika hili namwomba samahani Mheshimiwa Mama Joyce, naishauri Serikali, simzungumzi mumeo Mheshimiwa Mama Joyce unisamehe, nanyi Wajumbe wa Kamati ya Siasa nazungumza kuhusu Serikali. Taarifa yote hatuzungumzi tutauza nini nje? Niliwaambia juzi, kiburi cha Ukraine anauza nje Dola bilioni 64 kwa mwaka, hatujazungumza hapa tunauza nini nje? Tunahitaji kuuza nje kusudi tuje tuweze kujenga Taifa imara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri katika hotuba yake alitaja jina langu, baada ya kulitaja, simu zikaanza kurindima hapa; Wabaki Wabaki, umekuwaje Mwijage? Umekuwaje? Kwa nini Mheshimiwa Waziri alinitaja?

Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wabunge, katika randama ukurasa wa 42, mimi ni Mbunge wa Muleba. Niliiuliza Serikali, mgogoro wa eneo la Mwisa II utatuliwe ili wananchi na wafugaji waendeshe shughuli kwa tija kubwa na kwa amani. Ndicho nilichoiambia Serikali. Mgogoro wa Mwisa II utatuliwe ili wananchi na wafugaji waendeshe shughuli kwa tija na kwa amani. Katika kuendesha tija kwa amani, wazalishe maziwa na bidhaa nyingine za kilimo, ndiyo nilimwuliza Waziri. Halafu nikasema, katika kumwuliza Waziri na Serikali yake, wananchi wa eneo la Lutoro wapewe ekari sita, siyo ‘angalau’. Lile neno ‘angalau’ sikulisema. Wapewe ekari sita kutoka eneo la Mwisa II lenye hekta 67. Sikusema kutoka eneo la Mwisa II, rejea kwenye komuniki Mheshimiwa Waziri. Ni pale walipo; na pale walipo nitakuja nikupe vifungu hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa akanijibu akasema suala la Mwisa II bado lipo chini ya uwezo wa Wizara, ambapo Wizara itashirikiana na mamlaka husika katika Mkoa wa Kagera kwa kumaliza suala hili. Nakubaliana naye. Kumbe kumaliza matatizo ya Mwisa, Waziri ana uwezo na mkoa una uwezo, mnasubiri nini sasa? Komuniki tuliandika, watu wanalala nje, mnasubiri nini? Watu wanalia, mnasubiri nini? Watu wanachunga kwenye makaburi ya watu, mnasubiri nini? Kumbe Mkoa wa Kagera unaweza, na Waziri anaweza, mnasubiri nini watu na wanalia? Nitaipata wapi zawadi ya mama hapo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, twende Lutoro. Aidha, mahitaji ya wananchi wa Lutoro yalibainishwa na Kamati Maalum ambayo iliwashirikisha wananchi kwenye funga na fungua semi “iliwashirikisha wananchi.” Iliwashirikisha wapi? Wananchi ulikutana nao wapi? Nani alikutana na wananchi? Utakutana na wananchi wa Lutoro bila Mwijage, utawapata wapi? Hujawahi kukutana na wananchi. Kwa pamoja ilibainisha, eti ilibainisha watu wapewe kaya ekari mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Lutoro wanampongeza Mheshimiwa Bashe kwa kusema atatoa ekari tano kwa mtu, hii haijawahi kukaa mahali popote, wanakudanganya. Nimekuomba samahani Mheshimiwa Mama Joyce, umwombee mumeo, huyu ni rafiki yangu. Halafu watasema; nisikilize, jambo la maudhi anasema, watapewa ekari mbili na endapo kutakuwa na mahitaji zaidi, wananchi wanatakiwa kushauriwa kutafuta maeneo hayo nje ya ranchi. Wananchi wanatakiwa kutafuta, watu wa Ngorongoro mbona hamkuwashauri waondoke? Wananchi wangu ndio mnawashauri? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Rutoro ni la kisheria suala la Rutoro ni la utu suala la Rutoro ni la kisiasa! Mwaka 2015 Gymkhana Club Bukoba aliyepanda jukwaa ni mimi hali ilikuwa mbaya kule nenda kwenye video muangalie Rutoro ndio iliamua watu hawawezi kuondoka hiyo ndio iliamua hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja nikwambie nazungumka kwa ajili ya watu ya Kyebitembe naizungumzia Karambi naizungumzia Kasharunga Mubunda na Ngenge naizungumzia Rutoro mimi ni Mbunge wa Muleba ndio mwakilishi wa wananchi asitokee mtu yeyote akasema ndio mwakilishi wa wananchi ni mimi na Kikoyo hakuna wa kuchonga na nikifa mimi nitazikwa kwetu hakuna mwingine. Na niwaeleze watu wanakwenda eti Mheshimiwa Mwijage hamsemei mama unakwenda kwenye eneo la watu unachoma nyumba 280 unawaambia kazi iendelee Samia hoyee! kuna mtu atakujibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyumba 280 zimechomwa Migomba imekatwa halafu mtu anasema Mheshimiwa Samia hoye, sio Mheshimiwa Samia ninaye mjua Mama Samia anatoa zawadi nakubaliana na wewe ninachokueleza tukubaliane…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwijage naomba umalizie sentensi yako.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachosema Wizara yako Wizara ya Ardhi Wizara ya TAMISEMI tukae chini, chini ya Waziri Mkuu tuweze tukatafuta mstakabali wa suala hili vijiji vilivyopo pale vimeandikwa kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Nakaa chini kabla sijakaa naomba mezani kwako niwasilishi mgogoro wa Muleba na Naruko naomba niuwasilishe mezani. (Vicheko/Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. CHARLES J.P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wasaidizi wa Mheshimiwa njooni mchukue hapa.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia fursa hii. Mimi nitachangia Kamati ya Elimu, Utamaduni na Michezo. Kwa kipindi cha miaka hii miwili mitatu, ni wazi kwa kila mtu kwamba tasnia hii imeitendea haki Tanzania. Kwa hiyo, nichukue fursa hii kuishukuru Serikali, lakini na sisi Bunge tujishukuru. Unajua inabidi wakati mwingine ujishukuru, lakini kipekee nawashukuru Wajumbe wa Kamati na Mwenyekiti, kwa kusimamia kazi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niko hapa kushukuru, na anayeshukuru anaomba. Siyo siri na sioni aibu kuomba. Katika haya mengi ninayoyazungumza, maamuzi ya Serikali na Mheshimiwa Rais, mmefanya jambo moja jema, yaani elimu mmeipeleka kwao. Uamuzi wa kujenga Chuo Kikuu Bukoba au Kagera ni kuipeleka elimu kwao, ni jambo zuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo moja nataka kuzungumza, nimepitia Taarifa ya Kamati kuhusu vyuo vikuu vyote. Kuna upungufu wa watumishi, na unaponiambia upungufu wa watumishi chuo kikuu, ni Wahadhiri. Hili jambo lisikae likatokea. Ni kama kujenga hospitali nzuri wasiwepo waganga na wauguzi. Haupaswi kuwa na chuo kikuu ambacho hakina wataalam. Hili jambo linapaswa lijulikane mapema kwamba huyu atastaafu au kuna programu mpya tuweze kutengeneza hawa watu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hospitali bila daktari siyo hospitali, ni majengo tu. Kwa hiyo, hizi mnazoziita changamoto, mimi sikubaliani kama ni changamoto au tuseme ni uzembe. Tuseme ni uzembe, haya mambo yarekebishwe kusudi tuweze kuwa na chuo kikuu, na niwaeleze, watu wengi wangependa kuja kusoma hapa. Kama nilivyosema, kwa kuweka Chuo Kikuu Kagera, Bukoba ina maana watu wa maziwa makuu watakuwa wanakuja kusoma sehemu ile. Pamoja na kutoa elimu, tutaweza kupata utalii wa kielimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusu VETA, VETA imefanya kazi nzuri, naweza kuwa ugomvi binafsi na Kamati na Waziri kwamba kila wanapokuja Kagera kukagua VETA hawaji kwenye VETA ya kwetu. VETA sio ile ya Bukoba tu, kwa hiyo mnapokuja kukagua Bukoba muende na Karagwe kuna VETA mtembelee VETA zote mje na Kamachumu kuna VETA ili kusudi muweze kuona tunakwama wapi. Mimi nina VETA huenda majengo hayatoshi, Karagwe kuna VETA huenda kuna mapungufu, ninyi ndiyo mnaojua. Mje mtukague ili kusudi mjue mapungufu ukienda ugenini lazima uende na zawadi yoyote, mtuletee zawadi yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, muhimu kuhusu VETA, mitaala yenu isiwe ya mchakato, iwe situational. Leo soko linataka mafundi wa pikipiki, leo soko linataka mafundi wa simu. Kwa nini leo msilete Wachina VETA wakafundisha vijana wetu namna ya kuunda simu, kutengeneza simu na kutengeneza pikipiki?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini VETA watu leo wanakula kwa nini msilete VETA wataalamu wa food processing na vinywaji mkatengeneza vinywaji vyenye ubora ili watu wakaburudika na wakala maisha? Kwa hiyo, msitengeneze mchakato mirefu ya mitaala (situational au radical change). Tunataka VETA ya namna hiyo, msiwe mnapenda muda mrefu. Kuna mahitaji vijana wanajifunza. Kwa sababu unampeleka mtoto shule na unamuaminisha atapata kazi by the time anamaliza, kwa sababu ni mtaala wa kimchakato anakuta hiyo fursa imeondoka, tuwe situational, tuwe situational, tuwe situational kwenye hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe kuishukuru TEA (Mamlaka ya Elimu). Mlifika kwetu Kisiwa cha Bumbire mkatujengea nyumba nne za walimu, nawashukuru sana. Lakini mlituahidi kutujengea mabweni, kule ni kisiwani, watoto wanakaa kisiwani. Najua maombi yako mezani, muwasaidie vijana wale wanapata shida, mamba ni wa kwao, mawimbi ni ya kwao. Nimesema leo nimekuja kushukuru, kwa hiyo watu wa TEA tafadhali, mnapoangalia yale yanayobaki muweze kutuzungumzia na sisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nizungumzie mitaala mipya. Mitaala mipya inalenga kumuelimisha mtoto na ina wadau watano. Linalonipa shida, mimi ni muumini wa mitaala mipya kwa madhumuni yake, linalonipa shida ni kwamba, hawa wadau watano hawana uelewa, muwajengee uelewa ili wajue wanakwenda wapi. Kama mtu anaingia kwenye mitaala hii ajue anapofika mwisho wa safari anaweza kujiajiri au kuajiriwa, asifikirie kuajiriwa tu, alijue hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tunapozungumza kwa mfano wadau wote ni pamoja na Serikali, na kwa shule za msingi unaizungumzia TAMISEMI. Kwa mfano mimi katika wilaya yangu tunapokwenda kwenye mitaala mipya nina upungufu wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi karibu 2000. Tunakwenda vipi? Kwa hiyo, ninakuwa na hofu ambayo wataalam wanasema Mwijage unakuwa na hofu isiyokuwa na maana. Lakini mimi nina upungufu wa vyumba 2000, watoto nitawasomeshaje kwenye mtaala wa namna hii?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna watu wengine kwamba labda tunataka kulipua. Tuwaeleze kwa namna gani hatutaki kulipua na kwa namna gani tunataka kufanya vitu vya namna hiyo. Lakini wengine wana upungufu wa walimu, tuwaeleze kwamba, tuna mpango wa kuwaandaa walimu na wameelewa vipi. Hoja ni kuelewa, na mpiganaji yeyote anayejua kwa nini anakwenda kupigana, atapigana vipi na nguvu ya adui, vita ataishinda kabla haijaanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kutokuwa na uelewa wa pamoja kwa sisi hawa wadau watano ambaye ni mwanafunzi, mzazi, jamii, mwalimu, shule na Serikali, wote watano wakiwa na uelewa wa pamoja ninaimani tutaweza kuisimamia hii mitaala mipya, ukweli mimi leo asubuhi nilikimbilia kwa Mkuu wa shule, nilikuwa na wasiwasi na mitaala hii na nikawa nimejipanga kwamba, hapana nakwenda kukataa ili tubadilishe; lakini nilipokaa kwa Mwenyekiti hapa mwanangu akanieleza Baba hakuna hofu, usiwe na hofu, yale uliyokubali mwanzoni ulikuwa sawa, hii mitaala muwaeleze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mimi naweza kutiwa hofu na umahili wangu huu, sasa wengine kule watakuwa na hofu kubwa, lakini tuiombe Serikali iongeze bajeti kama ilivyoelezwa, lakini bajeti iende na mipango isiwe ya ujumla. Kuna watu wa pembezoni tuna hali ngumu, mtu una shule zenye upungufu wa madarasa 2000 huwezi kulingana na mtu ambaye mwingine madarasa yanakaa yamefungwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, niipongeze Serikali na nimpongeze Mheshimiwa Rais, zawadi aliyotutumia ya bilioni 3.8 tumeipokea na tunasubiri maua yake muda ukifika. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2020 (Toleo la Kiingereza)
MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuchangia hii Finance Bill ya mwaka 2021. Langu zaidi ni kuwapongeza na kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa kazi ya jana. Ahsante kwa kupiga kura za ndio nyote kwa sababu takwimu zinaonesha hakuna kura ya hapana zote ni ndio. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapochangia Muswada huu na zaidi nikilenga kuongeza mapato Zaidi, kwa sababu hapa biashara ni kuongeza mapato na namna ya kuwakusanya, nirejee mawazo ya Mheshimiwa Mbunge mwenzetu, Mheshimiwa Balozi Bashiru aliwahi kusema kwamba, tunapaswa tuwe na dialog, tuwe na mijadala, yaani kuna mawazo yanatoka humu mpaka unafurahi unasema na mimi nikachukue PhD ya mawazo yanayotoka humu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na kitu kinaitwa transfer pricing; katika Muswada huu na hotuba ya Mheshimiwa Waziri suala la transfer pricing sisi Wabunge hata wataalam wa Serikali inaonekana tunakwenda kufanya maamuzi bila kujua madhara yake. Sielewi kwanini tunakwenda kupunguza transfer pricing, nini madhara ya transfer pricing wakati bidhaa inatoka au inapoingia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inapoingia bidhaa na transfer pricing, yule mwenye faida ata-trigger price whole, lakini wewe kama mtoza ushuru bidhaa inapotoka, huyu mtu anapotoka, ataweza kukuletea kukwepa kodi. Naona Serikali hii tuna haja ya kukusanya kodi kwa ajili ya kutimiza malengo. Sasa unapokataa kumtishia mtu kum-scare yeye asikwepe hiyo kodi, halafu unamwachia bila kumtoza lolote, hapa naishauri Serikali yangu tuache kipengele hiki kilivyo, tuchukue muda zaidi tuweze kukiangalia zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, Sheria ya Wakala wa Meli, Sura 415; hili suala na lenyewe linapaswa kuangaliwa. Kwanza naiangalia TASAC katika mambo mawili; inakiuka sheria za mchezo kwa kuendelea kuwa operator na kuendelea kuwa regulator. Pamoja na kwamba anakiuka sheria za mchezo, sisi pamoja na kutafuta kodi, tuna maslahi mengine ya ajira, utendaji wa TASAC unaviza ajira, tunaweza kukusanya kodi lakini kama vijana hawana ajira tutapata matatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sikuelewa maelezo yote yaliyoelezwa hapa. Pamoja na kuwaunga mkono watu wa Kamati ya Fedha, lakini TASAC anapokamatiwa bidhaa anasema exclusive right ya ku-handle mafuta, TASAC mafuta Anaya-handle ili yasiweje? Mafuta yameshughulikiwa, vipimo vimewekwa Wakala wa Vipimo na Mizani, ni Serikali, viwango vimewekwa chini ya TBS, bei imewekwa chini ya Bulk Procurement; hizi zote ni Taasisi za Serikali TASAC anakwenda kufanya nini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu ambacho Serikali haikielewi na napenda niwashawishi hawa watu wanaokwenda ku-handle watu wengine wanasaidia kuuza haya mafuta. Nimeandika maelezo marefu kwenye mchango wangu wa maandishi, Tanzania inapaswa kuwa kituo cha kuuza mafuta katika Afrika hii na mafuta utakayoyapeleka transit au mizigo ya transit kupitia hapa ndio yatakupa fedha zile unazochangisha kwenye shilingi. Kwa hiyo uwepo wa TASAC wa kutaka kuchukua kila kitu kwenye mafuta sioni uhalali wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo TASAC atengwe aende kushindana kusudi tuweze kuleta ushindani, tuache kubweteka, TASAC anabweteka, analeta inefficiency. Naomba suala hilo tulipitie upya, tuweze kumtoa kwenye maeneo mengine. La mafuta nina vielelezo vyote, hakuna anachoweza kufanya na niweze kusema hakuna anachoelewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niunge mkono Kamati kuhusu suala la anguko la mafuta, the backwardation and contango; nimemwandikia Mheshimiwa Waziri somo zuri, mtu anaweza akapata degree pale. Hata hivyo, niwakosoe Wajumbe wa Kamati si kila mafuta yanapoanguka bei, makampuni ya mafuta hufaidika, si kweli, anguko la bei tatizo lake ni kwamba halimnufaishi mlaji wa mwisho ndio tatizo lake. Tanzania kuanguka kwa bei hakuwezi kuleta manufaa kwa sababu sisi sio soko huru, ni soko lililodhibitiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimetoa maelezo ya kina na Mwenyekiti wa Kamati nimemwahidi tuje tukae Pamoja, hii ni sehemu yangu ya kujidai. Kwa hiyo kuna mambo yanapaswa kufanyika ili tuweze kupata hiyo faida, lakini nakubaliana kwamba lile anguko lichukuliwe liende TARURA kusudi kuweza kufungua barabara za kwetu ambazo hazipitiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni kuhusu Government loans, grants and guarantee. Langu katika hili, Serikali ikakope na ikatoe guarantee, lakini tujiridhishe tunakwenda kuwekeza wapi.

Niliandika kwenye mchango wa Waziri, hata kwenye mchango wangu wa maandishi kuhusu viwanda. Msiende kuwekeza pale ambapo hapawezi kulipa yaani kuna viwanda vimekufa hata mngedhikiri uchi haviwezi kufufuka. [Maneno Haya Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani kuna viwanda vimekufa hata ungefanyaje, nilijaribu nikashindwa, vikanishinda, hawawezi kuvifufua, Waziri aachane navyo. Kwa hiyo, Waziri wasiweke guarantee pale ambapo hawawezi kupita. Kwa hiyo fedha za guarantee, tuna mafunzo mabaya na guarantee, tusirudi kwenye makosa yale yale, kwa hiyo tuwekeze kwenye maeneo ambayo…

T A A R I F A

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimpe taarifa mzungumzaji hasa aliposema kwamba yeye alijaribu akashindwa nataka nimpe taarifa na mimi nilijaribu nikashindwa Lindi Industries, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwijage unakubali taarifa?

MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubali taarifa ya mjomba wangu. Kwa hiyo tuwekeze pale ambako kuna fursa kubwa, tuwekeze kwenye fursa kubwa, lakini tunapohitaji guarantee…

T A A R I F A

MHE. TABASAM H. MWAGAO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. TABASAM H. MWAGAO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kidogo mjomba wangu Mheshimiwa Mwijage afute kauli yake katika suala la kudhikiri uchi yaani hapo amekwenda kwingine. Naomba sana kwa sababu itaingia kwenye Hansard za Bunge, halafu litaleta taabu hilo neno, naomba alifute, tafadhali. (Makofi)

MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naondoa sentensi hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika guarantee, guarantee ni muhimu, nachelea upande wa kupata kibali cha Baraza la Mawaziri. Nawaomba Waheshimiwa Mawaziri na mamlaka husika tuwe na kasi kubwa ya kuweza kutoa hizo guarantee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namba tatu, kwenye Electronic and Postal Communication Act; nina uhakika kwa watu wote wenye LUKU, mapato ya property tax yatakuwa makubwa kuliko maelezo. Ninachoomba kama nilivyosema mwanzo tunapaswa kujiandaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali, wale ambao hawana LUKU, msiwafuate manually kama zamani, fedha tutapata za kutosha, lakini naomba basi tuchukue fedha za kutosha kama nilivyosema mwanzoni wa-electrify sehemu zilizobaki. Wanaotaka umeme wako wengi, wawape umeme kusudi waweze kupata property tax. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapomalizia kuhusu mambo ya vibali na wale wanaoajiri watu kutoka nje, kama walivyosema Waheshimwia Wabunge, mambo ya filing unaposoma vizuri Blue Print Regulatory Reform moja wapo ya tatizo ni hii kimbia kimbia, kwenda hapa, kwenda hapa, hii filling ingefanyika mara moja kwa miezi sita, filling ya vibali ingefanyika mara moja baada ya mwaka mzima ili tuache watu watulie wafanye shughuli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)