Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Catherine Nyakao Ruge (21 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ili nami niweze kuchangia Wizara hii ya Maliasili na Utalii. Pia napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika Wizara hii Mheshimiwa Ester Matiko kwa hotuba nzuri. Baada ya kusema hayo naombe niende moja kwa moja kwenye kuchangia Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Maliasili na Utalii ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya Taifa hili, ina mchango mkubwa katika pato la Taifa na imeweza kuchangia asilimia 17.5 kwa maana ya GDP. Pia sekta hii inachangia ajira milioni moja na laki tano(1,500,000) katika nchi hii, kwa maana ajira laki tano za moja kwa moja lakini pia ajira milioni moja ambazo si za moja kwa moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Sekta ya Utalii ni sekta ambayo inaliingizia Taifa letu fedha za kigeni. Asilimia 25 ya pesa za kigeni katika Taifa hili zinatokana na Wizara ya Maliasili na Utalii. Sekta hii ya Utalii ni sekta namba mbili katika kuvutia wawekezaji. Mwaka jana 2016 Sekta hii ya Utalii imeweza kuliingizia Taifa letu dola za Kimarekani bilioni 2.1. Kwa kutambua umuhimu, fursa na mchango wa Sekta ya Utalii katika kuwezesha na kuendeleza uchumi wa nchi yetu, ni dhahiri kabisa tunahitaji Sera Wezeshi na mikakati thabiti kuweza kuendeleza na kuboresha sekta hii ya utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wawekezaji na wafanyabiashara wa Sekta ya Utalii wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi, naomba niongelee utitiri wa kodi, ada, leseni na tozo mbalimbali katika sekta hii. Jambo la kusikitisha tozo, ada na leseni hizi hazilipiwi kwenye mamlaka moja, zimekuwa zikilipiwa kwenye mamlaka tofauti na hivyo kuwa kikwazo na changamoto kwa wawekezaji na makampuni yanayowekeza katika sekta ya utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ruhusa yako naomba niseme baadhi ya tozo na leseni mbalimbali na mamlaka mbalimbali zinazolipiwa gharama kwenye sekta hii. Utaambiwa uende TRA ukalipe kodi; nenda Wizara ya Maliasili na Utalii ukalipe leseni na ada; nenda Marine Park Authority ukalipe concession fee, nenda Tanzania Civil Aviation Authority ukalipe leseni ya huduma za anga na ukaguzi; nenda SUMATRA ukalipe SUMATRA vehicle sticker; nenda TANAPA ukalipe motor vehicle guide fee; nenda Ngorongoro Conservation Area ukalipe NCAA vehicle fee. Niiombe Serikali iangalie ada, tozo na leseni ambazo zina tija katika sekta ya utalii ili kupunguza changamoto na usumbufu kwa wawekezaji katika sekta hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee katazo la matumizi ya mkaa na kilio cha wananchi. Naomba nieleweke, sipingi harakati za Serikali katika kulinda misitu yetu kwa utalii endelevu. Lakini, karibu kila mtu anatumia mkaa ikiwa ni pamoja na sisi baadhi ya Wabunge. Serikali haijaja na nishati mbadala ambayo inapatikana kwa urahisi na ambayo ni affordable kwa mwananchi wa kawaida especially vijijini, ambayo inaweza kumsaidia katika matumizi ya nyumbani. Kwa hiyo, niishauri Serikali iweze kuangalia ni jinsi gani inaweza kuja na nishati mbadala ili tuweze kumwezesha mwananchi wa kawaida aweze kumudu gharama za matumizi ya kupikia na taa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna option ya gesi lakini option hii ni ghali sana. Mtungi wa kilo 15 ni shilingi 52,000, siamini mwananchi wa kawaida wa kijijini kule Serengeti ninakotoka mimi anaweza kumudu hii gharama. Pia kuna option ya makaa ya mawe, sijaona kwenye hotuba hii kwamba kuna utafiti wowote umefanyika ambao unaonesha nishati ya makaa ya mawe hayana madhara kwa matumizi ya nyumbani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niishauri Serikali kwa maeneo ambayo ni ya wafugaji, kuna miradi imefanyika ya biogas kwa maana ya kutengeneza biogas kwa kutumia kinyesi cha ng’ombe, tuweze ku-invest katika hii area na ile miradi ambayo imefanywa na wafadhili. Kwa mfano, Serengeti kuna Kata ya Morotonga, Ring’wani kuna miradi imefanywa na wafadhili. Niiombe Wizara ya TAMISEMI kwa kushirikiana na Halmashauri zetu kuona ni jinsi gani inaweza ikachukua hii miradi na kuiendeleza na kui-scale kwenye Wilaya zote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee Mkoa wa Mara ninakotoka. Mkoa wa Mara ni Mkoa ambao una makabila mengi na wenye tamaduni tofauti. Wizara ya Maliasili na Utalii haijaweza kuwekeza kwenye fursa ya utalii wa tamaduni mbalimbali zinazopatikana katika Mkoa wa Mara. Niombe Waziri uweze kuangalia pia ni jinsi gani tunaweza kuwekeza kwenye tamaduni zinazotokana na makabila mbalimbali badala ya kuangalia utalii wa wanyamapori peke yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia 70 ya mbuga ya Serengeti iko Mkoa wa Mara, lakini wananchi wa Mkoa wa Mara wamekuwa wakiishi maisha ya kimaskini kama vile hii mbuga ya Serengeti haiko Mkoa wa Mara. Ni asilimia 10 tu ya watu walioajiriwa Serengeti National Park wanatoka Mkoa wa Mara. Namwomba Mheshimiwa Waziri wakati anakuja kuhitimisha hotuba yako atuambie watu wa Serengeti na watu wa Mkoa wa Mara ni sababu gani ni asilimia kumi tu ndiyo wameajiriwa katika Serengeti National Park, je, ni kwa sababu hatuna watu wenye uwezo ambao wanaweza kufanya kazi kwenye mbuga hiyo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na changamoto ya wanyama wanaotoka mbuga ya Serengeti kuvamia vijiji vilivyo pembezoni ya mbuga ya Serengeti na kufanya uharibifu wa mali za wananchi ikiwemo mashamba, pia kuwadhuru wananchi na kusababisha vifo kwa baadhi ya wananchi ikiwa ni tembo, nyumbu na wanyama wengine wanaokula mazao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua kwamba kuna kifuta jasho na kifuta machozi, lakini kuna wananchi wa vijiji vinavyozunguka Wilaya ya Serengeti ikiwemo Pakinyigoti, Makundusi, Robanda ambao hawajalipwa toka mwaka 2005. Namwomba Mheshimiwa Waziri wakati anakuja kuhitimisha hoja yake atuambie compensation plan ya hawa watu ikoje na watalipwa lini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na changamoto hiyo kuna migogoro kati ya Askari wa Wanyamapori na wananchi wanaoishi pembezoni mwa mbuga ya Serengeti. Askari hao wamekuwa wakiwabambikia kesi wananchi wanaoingia kwenye hifadhi ama kwa kujua au kwa kutokujua kwa sababu hakuna mipaka inayoeleweka. Kinachonisikitisha ni kwamba wananchi hawa wamekuwa wakipelekwa Mahakama ya Bunda na siyo Serengeti wakati Mahakama ya Bunda ina uwezo sawa na Mahakama ya Serengeti. Namwomba Mheshimiwa Waziri atakapokuja kuhitimisha hoja yako atuambie watu wa Serengeti ni kwa nini wanapelekwa Mahakama ya Bunda na siyo Mahakama ya Serengeti.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa ili niweze kuchangia hoja zilizopo mbele yetu. Nitajikita kwenye taarifa ya Kamati ya PAC ambayo ni mjumbe. Kwanza kabisa nitumie fursa hii kuipongeza Kamati ya PAC kwa taarifa nzuri, lakini nimpongeze Mwenyekiti wangu mama Kaboyoka kwa uongozi wake na ujasiri mkubwa aliouonesha wakati wa kipindi chote cha kuongoza na kuandaa taarifa hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo nitaomba kujikita kwenye maeneo machache katika taarifa hii PAC. Kwa kuanza nitaomba kuchangia kwenye mradi wa Mlimani City na kabla sijaanza kuchangia naomba ku- declare interest kwamba nilisoma Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Focus of Commerce ambayo sasa UDBS (University of Dar es Salaam Business School) nilipata degee ya Accounts, Bachelor of Commerce in Accounting.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa Mlimani City una maajabu, una maajabu mengi lakini naomba nizungumzie maajabu saba ya Mradi wa Mlimani City. Ajabu namba moja mtaji ambao uliowekezwa kwenye mradi huu wa Mlimani City. Tangu mradi huu umeanzishwa Mwekezaji ameweza ku-issue shares 100 tu kati ya shares 1,000 ambazo ziko authorized kwenye mtaji wa hiyo kampuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, share hiyo kwa miaka hiyo iliuzwa Dola 0.75, kwa hiyo mtaji mzima wa Mlimani City ulikuwa ni Dola 75 kwa sasa hivi ni 150,000 au 160,000 sikumbuki by then 2004 exchange rate ilikuwa ngapi ambao mnakumbuka mnaweza mka-calculate na mkajua ni kwa kiasi gani mradi mkubwa kama wa Mlimani City uliweza kuwekezwa kwa mtaji kiasi kidogo namna hiyo. Mpaka leo zaidi ya miaka 10 share 900 kwenye kampuni hiyo bado hazijauzwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ajabu namba mbili, ni mbia mwenye share moja anaitwa Transtor, huu mradi una Wabia wawili Highland View na Transtor ameweza kukopesha Kampuni ya Mlimani City dola za Kimarekani 40,000 wakati yeye ana share moja badala ya kuwekeza kwenye ile Kampuni kwa kununua zile share ambazo mpaka leo hazijauzwa tangu kampuni hiyo imeanzishwa ambayo ina share 900 mpaka sasa hivi haziko issued. Hiyo ni ajabu namba mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini unajiuliza ni sababu gani labda ameamua kukopesha badala ya kununua shares. Wahasibu wenzangu sababu ni mbili tu. Sababu ya kwanza ni yeye kuendelea kupata riba au interest income kutokana na pesa anayoikopesha Mlimani City. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu ya pili kwa sababu interest expense inapunguza faida kabla ya kupata net income, kwa hiyo automatically faida ya Mlimani City inapungua na mwishoni kabisa na pesa inayolipwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inapungua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninazo hesabu za Mlimani City Holdings hapa zinaonesha kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017 mwaka mmoja tu financial charges kwa maana interest expenses zilikuwa 1.9 Milioni US Dollars, kwa maana hiyo kwa mwaka mmoja tu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimepoteza mapato karibu Dola za Kimarekani Milioni 2. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ajabu namba tatu ya mradi huu wa Mlimani City, ni uwiano uliopo kati ya gawio la faida na rental income au kodi ya pango ambayo wanalipwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Yaani haya ni maajabu na yanaweza kutokea Tanzania tu. Ukiangalia mapato ambayo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimeanza kulipwa kuanzia Mwaka 2006 mpaka Mwaka 2017, wamelipwa Dola za Kimarekani Milioni 7.5.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hawa Wabia, actually Mbia ni mmoja kwa sababu ana shares 99 na ile moja unaweza ukairudisha ni redeemable anytime unaweza ukai- redeem kurudi kwenye Kampuni. Kwa hiyo, Mbia ni mmoja, huyu Mbia ameweza kujilipa dividend au gawio la faida la 3.8 milion dollars. Hiyo ni nusu ya pesa iliyolipwa kwa Mlimani City kama Rental Income au Kodi ya Pango kwa miaka, kuanzia Mwaka 2006 mpaka leo; miaka 11. It’s can only happening in Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ajabu namba nne, ya Mkataba huu wa Mlimani City na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni kukiukwa kwa masharti ya Mkataba kwa zaidi ya miaka 10 na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekaa kimya. Kinachonishangaza ni kwamba hiki Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndiyo kinazalisha Wanasheria wabobezi, wakiwepo baba yangu Profesa Kabudi, dada yangu Dkt. Tulia, lakini hawakuuona huu upungufu wote mkubwa uliopo kwenye mradi mpaka CAG alivyoenda kufanya Special Audit mwaka jana mwezi wa Nne na akaibua hiyo hoja na wao kuanzia mwezi wa Tano wakaanza kumwandikia mwekezaji kuwa anakiuka masharti. Hiyo ni ajabu namba nne. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ajabu tano, Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba Makamu Mkuu wa Chuo kwa kipindi chote, tunajua nani walikuwa Makamu Mkuu wa Chuo miaka hiyo kuanzia Mkataba umesainiwa mpaka leo. Walikuwa ni sehemu ya bodi kwa maana ni Board Members, ukianza na Profesa Luhanga, Rwekaza Mkandala sasa hivi baada ya Rwekaza kuondoka ameingia Profesa mwingine wote hao ni Maprofesa. Profesa Muhanga, Profesa Mfinanga ameingia sasa hivi ndiyo Board Member amem-replace Mkandala, ana miezi kama miwili au mitatu, walikuwa wanaingia kwenye Bodi ya Mlimani City Holding. Kwa maana hiyo walikuwa ni sehemu ya maamuzi ya Mlimani City Holdings.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa huwa najiuliza, hivi hawa Maprofesa wetu, macho yao yalikuwa yameingia michanga au ni nini, mpaka wanaangalia haya maamuzi ambayo hayana tija kwa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ajabu namba sita, ni going concern ya hii Kampuni ya Milimani City au kuendelea kuwepo kwenye kwa biashara kwa hii Kampuni kwa miezi 12 ijayo au mwaka mzima. Going concern au kuendelea kuwepo kwa biashara kwa Mlimani City Holding kunategemea na ipo kwenye ripoti, ipo kwenye financial statement za Mlimani City Holding, inategemea na uwezo wa shareholders kuendelea kuweka pesa. Willingness ya Shareholders kuweka pesa kwenye huo mradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi mkubwa kama huu unategemea jinsi gani mwanahisa atajisikia kuweka pesa kwenye mradi. Kwa hiyo, akiamka hajisikii ina maana huo mradi utakufa, kwa hiyo, we are not sure hatuna uhakika wa kuwepo kwa hii Kampuni ya Mlimani City kwa miezi 12 ijayo hilo ni ajabu lingine la sita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ajabu la saba na la mwisho, yapo mengi lakini nimechukua haya makuu ambayo naomba Serikali mkayafanyie kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ajabu la saba, ni huyu mwekezaji ambaye ni Mbotswana, mwenye asili ya Kihindi anaishi Afrika Kusini. Mwekezaji huyu tangu ameanza huu mradi hajawahi kuonekana in physical. Sasa sijui ni mzimu au huyu mwekezaji sijui ni nini, yaani unawekeza pesa zote hizo, unakopesha almost 100 billion maana 49 milioni dollars ni zaidi ya bilioni 100, lakini huoni umuhimu wa kuja in physical kufanya negotiation unawatuma wawakilishi, hajawahi kuonekana. Hilo ni ajabu la saba, it can only happening in Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naona Serikali ya CCM ime-fail kusimamia miradi, tunaanzisha miradi mizuri lakini tunashindwa kusimamia. Imeshindwa kufanya oversight na monitoring na mwisho wa siku tumeishia kuvunja Mikataba na kupata hasara kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niiombe Serikali badala ya tukishasaini tu mnaiacha Mikataba, mnaiacha hamuangalii implementation, ni bora tuache kusaini hii mikataba kuliko kuendelea kupoteza pesa za umma, pesa za walipa kodi maskini na kuacha pesa hizi zinapotea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu wa pili ningependa kuchangia kuhusu Dege, mradi wa Dege Eco Village, mradi huu una utata mkubwa. Mradi wa Dege nilipata fursa ya kwenda kuangalia niliumwa tumbo la uzazi, kwa sababu ni Mwanachama wa NSSF nimekua nikichangia zaidi ya miaka 10, kwa hiyo, nina interest kwenye huo mradi wa Dege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu unautata kuanzia jinsi ulivyoanzishwa kwa maana jinsi gani ardhi ilipatikana mpaka implementation ya huo mradi. Tunaambiwa na Mkaguzi CAG anasema eka moja ilinunuliwa kwa milioni 800 Kigamboni. Sijui kwenye ile sehemu kuna gold, I don’t know labda hawa watu waende wakaangalie inawezekana kuna gold. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba sitaki kuongea maneno mengi naomba tu niishauri Serikali. Kwa vile mradi huu ni pesa za Wanachama wa NSSF na nikiwemo, naitaka Serikali na iazimie kwamba Mradi huu, pesa za NSSF zisiendelee kuingizwa kwenye mradi huu kwa sababu mpaka sasa hivi NSSF wameshaingiza bilioni 219 na ule mradi ni mfu mpaka itakapofanyika independent actuarial valuation, kuona kama pesa zilizoingizwa pale zina-reflect investment cost ya huu mradi sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukumbuke kwamba, kila siku gharama zinaongezeka lakini pia depreciation inatokea kwenye yale majengo na hizi gharama zitakuja kulipwa na Wanachama wenyewe.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Usimamizi wa Matumizi ya Fedha za Umma katika Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2017
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii na nimi niweze kuchangia. Napenda kujikita kwenye Taarifa ya Kamati ya PAC na ningependa kuzungumzia issue ya 1.5 trillion. Kabla sijachangia, napenda kumnukuu aliyekuwa Rais wa 16 wa Marekani, Marehemu Abraham Lincolin ambaye alisema; “You can fool all people some of the time, but you cannot fool all people all the time.” (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amelithibitishia Bunge, lakini pia ameuthibitishia umma kwamba kulikuwa na tofauti ya 1.5 trillion kwenye Mfuko Mkuu wa pesa za Hazina ambazo hazikukaguliwa wakati anafanya ukaguzi wake kwa hesabu zilizoishia Juni, 2017. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Kamati ya PAC kwa kumtaka CAG aweze kufanya verification na kujua tofauti ya 1.5 trillion na leo kuleta taarifa ya Bunge ambayo tunaijadili sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na verification kufanyika, badala ya hoja ya 1.5 trillion kufungwa, zimeibuka hoja nyingine na sasa hatuzungumzii 1.5 trillion, tunazungumzia 2.4 trillion. (Makofi) [Maneno Haya Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niweka records clear, siyo kazi ya CAG kusema kama kuna wizi. Kazi ya CAG ni kufanya ukaguzi na kutambua upungufu uliopo na mamlaka husika inatakiwa i-take charge. Kuna hoja mbalimbali ambazo zimeibuliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwenye hii ripoti ya ukaguzi maalum.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa kuna issue ya overdraft ya shilingi bilioni 290.7, Hazina wanasema hii ilikuwa ni overdraft na majibu yao wanasema zilikuwa ni pesa zilizokwenda kwenye miradi ya maendeleo na hazikupita kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina, lakini Mkaguzi hakupata vielelezo kuthibitisha hii hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkaguzi alienda mbali zaidi akaamua kuomba confirmation letter kutoka BOT kuthibitisha hiyo balance ya shilingi bilioni 290.67. Kuna confirmation letter kutoka BOT hii hapa ambayo wame-confirm kwamba kulikuwa na zero balance wakati Hazina inafunga mahesabu yao Juni, 2017. Pia taarifa za Ukaguzi za Hesabu za BOT za Juni, 2017 zinaonyesha balance ya overdraft ya Central Government ilikuwa ni 1.5 trillion. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nina Hansard hapa ya tarehe 20 Aprili, 2018, ukurasa wa 22 mpaka 25. Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango alisimama hapa kutoa maelezo ya Serikali kuhusu tofauti ya 1.5 trillion. Alisema; overdraft ilikuwa shilingi bilioni 79.1. Sasa hapa tuna figure nne za kutoka kwenye Serikali moja, tuamini ipi? ya BOT ya 1.5, confirmation letter ya zero balance, maelezo ya Naibu Waziri ya shilingi bilioni 79.1 au taarifa za hesabu za BOT za 1.5 trillion? Yaani kwa kifupi hapa naona Serikali ilipoteana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya pili, ni kuhusu shilingi bilioni 976.96 ambazo zilifanyiwa reallocation kwenye vote mbalimbali kutoka kwenye mfuko wa Hazina kwenda kwenye vote 20 na fedha hizi hazikupitishwa na Bunge. Lakini pia reallocation hiyo haikupata approval ya BoT. Hizi pesa zimeenda vote 20 ambako ni Ofisi ya Rais. Wote tunatambua, vote 20 haikaguliwi. Kwa hiyo, Serikali imefanya vote 20 ni kama kichaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa masikitiko makubwa, mpaka leo…

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Catherine Ruge, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere.

T A A R I F A

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Catherine Ruge, unaipokea taarifa hiyo?

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika, siipokei, naomba niendelee kuchangia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee nilipoishia. Hizi pesa ninazozizungumza zilizoenda vote 20 hazikupata approval ya CAG pamoja na reallocation iliyotokea. Kinachonisikitisha zaidi, hoja hii haiko kwenye Taarifa ya Kamati, lakini pia, Hazina mpaka leo hawajatoa majibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee kueleza jinsi gani Mheshimiwa Naibu Waziri alilipotosha Bunge lako tukufu aliposimama na kusema kwamba kulikuwa na receivable kwenye pesa ambazo zilikuwa zimekusanywa na Hazina.

MHE. ALLAN J. KIULA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

T A A R I F A

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Catherine Ruge, unaipokea taarifa hiyo?

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika, siipokei hiyo taarifa na ninaomba unilindie muda wangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niseme, ripoti ya PAC ni matokeo ya taarifa ya CAG na taarifa ya CAG ni public document.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee.

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

T A A R I F A

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba niendelee.

Mheshimiwa Naibu Spika, tarehe 20 Aprili, 2018 Naibu Waziri alisimama mbele ya Bunge lako tukufu na kulihadaa Bunge kwa kusema kulikuwa na receivable za shilingi bilioni 687 ambazo zilisababisha tofauti ya 1.5 trillion na akasema hii ilitokana na Hazina kuanza kutumia mfumo wa IPSAS Accrual. Taarifa ya Mkaguzi hii hapa haionyeshi hiyo hoja, haijaongelea kabisa receivable. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa wahasibu na tax administrators tulioko humu ndani, tunajua kabisa, hakuna pesa tarajiwa zinazokwenda kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina. Hakuna non cash item, kule zinakwenda cash tu. Mapato yote yako on basis of cash. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja nyingine ni hoja ya hati fungani. Hazina walikuja na vielelezo ambavyo vilikuwa kwenye excel na CAG amesema hizi taarifa haziaminiki na haziko credible. Naomba ni-quote taarifa ya CAG; “The weaknesses continue during the verification of the difference,
the document were required as to meet numerous types from various department also it took a long time to locate and extract information most of which was in MS Excel spread sheet in different location. Kwa hiyo, kwa statement hii, hakuna credibility ya hii information.

Mheshimiwa Naibu Spika, kinachonishangaza, hivi inakuwaje Hazina inaweza kutumia excel kuweka hesabu zake ambayo inaweza ikabadilishwa, ikaongezwa kitu, ikatolewa kitu bila traces? Sasa kweli tuko serious? Hazina ambako tunaamini inalinda pesa za walipakodi wanyonge, lakini ndiyo tunaona haya matatizo na uongo mkubwa na weaknesses za mfumo na udhaifu mkubwa wa Hazina! Tusipofanyia kazi udhaifu wa mfumo wa Hazina, haya matatizo yataendelea kuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa…

MHE. OMARI M. KIGUA: Taarifa.

T A A R I F A

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Catherine Ruge, unaipokea taarifa hiyo?

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika, siipokei.

MBUNGE FULANI: Pokea.

MBUNGE FULANI: Usipokee.

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika, naipokea hii taarifa na naomba nikwambie, I am a Certified Public Accountant, najua ninachokizungumza. Inawezekana hiyo syllabus yako uliyosoma ilikuwa ya zamani, mimi I am very current. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja nyingine ilikuwa ya hati fungani ambapo hizi hati fungani zilionekana zimeiva na zikawa rolled over. Lakini vielelezo hivyo pia vimeletwa kwenye excel na ukiangalia hii taarifa, ukijumlisha kwanza hizo hati fungani, haziji-figure hiyo ya shilingi bilioni 656, zinakuja shilingi bilioni 853. Angalieni hii taarifa. Kwa hiyo, kuna tofauti ya kitu kilichosemwa na kitu ambacho CAG amekizungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukitaka kujua figure ya bonds unakwenda kuangalia kwenye taarifa ya BOT; na kwenye taarifa ya BOT zimeonyeshwa bonds zote. Sasa naomba Serikali ikija hapa ituambie, hizo bonds zilizo-mature 2016/2017 Juni, ni bonds gani? Za muda gani? Zilikuwa zina kiasi gani na zililipwa lini?

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakusukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia kwa mara ya kwanza kabisa katika Bunge lako hili Tukufu. Napenda kuchukua nafasi hii kutoa pole kwa Watanzania, kwa familia, kwa Wabunge, ndugu jamaa marafiki na bila kusahau Mbunge wa Arusha Mjini Mheshimiwa Godbless Lema kwa msiba uliolikumba Taifa hili siku chake zilizopita, Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo naomba niungane na Waheshimiwa Wabunge wenzangu waliotangulia kuchangia, kwamba Serikali iweze kuongeza bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kuzingatia umuhimu wa maji katika maisha yetu ya kila siku. Serikali inaweza ika-pull resource kutoka kwenye sekta nyingine na tuweze kuipa kipaumbe Wizara hii ya Maji ambayo ni muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nisikitike kusema kwamba pamoja na kuwa na vyanzo vingi vya maji katika nchi yetu, kwa maana ya maziwa, mito, mabwawa na mabonde mbalimbalil changamoto ya maji imekuwa ni ya muda mrefu. Tangu mimi nimezaliwa mpaka sasa hivi bado namwona mama yangu na wanawake wengine wa Kitanzania wakiwa wanabeba ndoo kichwani ikiwa ni zaidi ya miaka 30. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ya maji inawaathiri pia wanafunzi wa kike kwa sababu mashuleni hakuna maji, hasa sehemu za vijijini. Hii inafanya watoto wa kike wakiwa katika hedhi washindwe kuhudhuria masomo kati ya siku tatu mpaka tano, jambo ambalo hupunguza ufaulu wa masomo kwa sababu ukichukua siku tano katika mwaka ina maana wanakosa masomo takriban siku 60 kwa mwaka. Kwa hiyo, niiombe Serikali iangalie jinsi gani inaweza kuboresha miundombinu ya maji katika shule zetu ili tuweze kuwasaidia watoto wa kike waweze kufaulu vizuri kwa kuweza kuhudhuria masomo yao kila siku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie kuhusu miundombinu ya maji katika jimbo la Serengeti ninalotoka mimi. Ukiangalia bajeti hii ya mwaka 2017/2018 ni shilingi milioni 858 tu zilizotengwa katika jimbo la Serengeti. Kuna changamoto nyingi sana ambazo zinalikabili shirika la maji safi na taka la MUGUWASA ambalo lina wakazi 47,000 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ni nyingi ikiwa mojawapo pump ni moja ambayo haikidhi mahitaji, lakini pia kuna tenki moja tu ambalo halitoshelezi kwa wananchi wa Mugumu Mjini, mji ambao ambao unaundwa na kata saba zilizoko pale. Kwa hiyo, niiombe Serikali iweze kuongeza bajeti katika eneo hili ili kuweza kuboresha miundombinu ya maji katika mji wa Mugumu kwa sababu miundombinu ni ya zamani sana na imechoka, lakini pia gharama za uendeshaji ni kubwa sana za Mamlaka ya Maji ya Mugumu Mjini kwa sababu makusanyo ya mwezi ni shilingi milioni saba lakini wanalipa ankara za umeme shilingi milioni 16.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inaonesha kabisa mamlaka ya maji Mugumu Mjini inajiendesha kwa hasara. Kwa hiyo, tuangalie nishati mbadala ambayo inaweza kuendesha ile pump ya Manchira ili tuweze kupunguza gharama za uendeshaji, lakini pia tupunguze gharama kwa watumiaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto nyingine ambayo inaikumba MUGUWASA ni kwamba kuna upungugu wa mita kwa wateja. Kati ya wateja 1,536 ni wateja 509 tu ambao wameunganishiwa mita za maji. Kwa maana hiyo hii inaikosesaha mapato Muguwasa. Kwa hiyo, niiombe Serikali iangalie jinsi ya kuisaidia MUGUWASA kuweza kusambaza mita ili wateja wote waweze kupata mita na hivyo waweze kuchangia mapato ya MUGUWASA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti hii…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga hoja Kambi Rasmi ya Upinzani.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia hotuba hii ya Waziri Mkuu. Nianze na suala la utawala bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yoyote duniani ili iwe na maendeleo, lazima ifuate sheria na taratibu ilizojiwekea kama nchi. Hivi karibuni tumeona sheria zetu zikivunjwa. Mfano, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wamekuwa na mamlaka makubwa na bila kufuata sheria wamekuwa wakitoa amri kwa viongozi mbalimbali wakiwemo Wabunge kuwekwa ndani kinyume cha sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia pia, kuhusu nishati ya gesi. Miaka mitatu iliyopita wananchi waliaminishwa kuwa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam utaenda kutatua tatizo la nishati kabisa nchini, lakini katika hotuba ya Waziri Mkuu jambo hili halijazungumziwa kabisa; na kinachoendelea sasa hivi ni mradi wa Stieglers’ Gorge. Je, ni kwa nini Serikali imeamua kubadilisha kipaumbele chake toka kwenye umeme wa gesi kwenda kwenye umeme wa maji, huku tukifahamu Serikali imeshatumia pesa nyingi za walipakodi kuwekeza kwenye mradi wa gesi asilia?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi huo bado haujawa fully utilised, kwani mpaka sasa ni 6% tu ya bomba la gesi linatumika. Naitaka Serikali iwaambie Watanzania, ni kwa nini imehamisha focus toka kwenye umeme wa gesi asilia kwenda kwenye umeme wa maji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia, kuchangia kuhusu hali ya uchumi iliyozungumziwa ukurasa wa nane katika hotuba ya Waziri Mkuu. Hotuba inaonesha uchumi wa nchi yetu unakua kwa asilimia 6.8 kwa kiwango cha juu kuliko nchi zote za Ukanda wa Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina shaka na takwimu hizo, ila tatizo langu lipo kwenye jinsi gani hali ya uchumi iko reflected kwa wananchi wa kawaida. Wananchi wana hali mbaya sana hata kupata milo mitatu ni tatizo. Je, huo uchumi unaokua unawanufaisha vipi wananchi, kama wananchi hawawezi hata kula milo mitatu kwa siku?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa ili niweze kuchangia. Tunaitazama Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na mafungu yake yote kwa maana ya Fungu la 93 ambalo ni Uhamiaji, Fungu 29 Jeshi la Magereza, Fungu 28 Jeshi la Polisi, Fungu 51 Makao Makuu ya Wizara na Fungu 14 Jeshi la Uokoaji na Zima moto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa miaka miwili mfululizo Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali alipata fursa ya kukagua wizara hii pamoja na mafungu yake yote. Mwaka 2016/2017 CAG aliibua hoja kumi za ukaguzi kutoka kwenye wizara hii ambazo zilikuwa na thamani ya shiilingi bilioni 128.6. Ukaguzi wa mwaka 2017/2018 CAG aliibua hoja 12 za ukaguzi zilizokuwa na thamani ya shilingi bilioni 180.2. Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 40 ya thamani ya hoja zote za ukaguzi kwa maana ya total value of audit queries.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wizara hii imekuja mbele ya Bunge lako tukufu kuomba tena kuidhinishiwa bajeti kwa ajili ya matumizi kwa mwaka ujao. Ninashangaa wizara hii bila woga imeweza kufanya hivyo wakati ikiwa na hoja lukuki za ukaguzi ambazo hazijapatiwa majibu kwa kipindi cha miaka miwili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwaka 2017/18 Bunge hili lilipitisha bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya shilingi bilioni 930. Lakini shilingi bilioni 180.2 zinahojiwa najiuliza wanapata wapi confidence ya kusogea mbele ya Bunge hili na kuomba tena fedha kwa ajili ya matumizi ikiwa kuna hoja nzito sana za ukaguzi ambazo zimekosa majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sioni kama hii wizara ina hadhi ya kuja kuomba pesa tena wakati imeshindwa kujibu ufisadi na pesa nyingi za walipa kodi wanyonge Watanzania zimetumika kwa ubadhirifu mkubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe mifano michache, ufisadi wa kutisha kwenye ununuzi wa mfumo wa utambuzi wa alama za vidole au afisi katika jeshi la polisi. Kulikuwa na manunuzi ya mtambo wa utambuzi wa gharama kwa alama za vidole. Kwanza jeshi la polisi halikuwa na bajeti, lakini hazina ilichepusha kinyemela shilingi bilioni 40.3 kwenda jeshi la polisi kwa kutumia fomu ambazo hazikuwa halisia, afisa aliyehamisha hizo fedha alikuwa hausiki, sasa basi sawa zimekwenda basi zitumike vizuri, maajabu!

Mheshimiwa Mwenyekiti, shilingi bilioni 1.7 ambazo zilikuwa zitumike kufunga vifaa vya utambuzi kwenye magereza 35 hayakufanyika. Malipo hewa ya huduma ya matengenezo na uwezeshaji shilingi bilioni 3.3, malipo ya mafunzo hewa shilingi milioni 600.4, malipo ya vifaa hewa shilingi milioni 594 kulikuwa na vifaa vyenye uwezo sawa, mahitaji sawa na sifa sawa lakini zilikuwa quoted kwa gharama tofauti, kwa bei tofauti na hii ikapelekea jeshi la polisi kulipa zaidi ya shilingi milioni 556. Huku ni kupoteza na ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi. Wote tunafahamu na tunatambua mkandarasi au mzabuni alikuwa ni nani? Alikuwa ni Lugumi enterprises. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nashangaa mpaka leo sioni hatua zilizochukuliwa dhidi ya Lugumi. Nakumbuka mwaka jana Mheshimiwa Kangi ulivyoteuliwa kuwa Waziri ulikuja na kauli nzito na mkwara mzito kweli kuhusu Lugumi na ulim-summon kuja ofisi kwako within 24 hour. Lakini baada ya wiki mbili kuna kitu gani, who is behind Lugumi, tunataka Serikali ituambie mmechukua hatua gani dhidi ya Lugumi na maafisa wote wa Jeshi la Polisi waliohusika na huu ubadhirifu tunataka majibu ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mweyekiti, nasema hivi kwa sababu Serikali hii imekuwa ikijipambanua kwamba ni Serikali ya kupinga ufisadi ya kutetea wanyonge hivi ni ufisadi gani sasa ambao mnaupinga huu sio ufisadi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijielekeze kwenye hoja nyingine, hoja ya Idara ya Uhamiaji. Idara ya Uhamiaji imekuwa ikipata hati zenye mashaka kwa miaka miwili mfululizo. Mwaka huu hati yenye mashaka imesababishwa na Idara ya Uhamiaji kutokurekodi thamani ya ule mfumo ulionunua waki-electronic wa e-migration.

Tunatambua mfumo huu ulinunuliwa, manunuzi yalifanyika kwenye ofisi ya Rais, nashangaa manunuzi makubwa siku hizi yanafanyika kwenye Ofisi ya Rais. Rais amekuwa ndio afisa manunuzi mkuu wa taifa au procurer in chief wakati tunafahamu hatuwezi… [Maneno Haya Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kuhusu Utaratibu.

MWENYEKITI: Kuhusu utaratibu.

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi wote tunafahamu mambo yafuatayo kwa mujibu wa kanuni ya 61(1)(e) lakini kwa mujibu pia wa kanuni ya 61(1)(a). Jambo la kwanza ninalotaka kusema manunuzi ya umma yana sheria yake na yanafata taratibu za kisheria zilizowekwa na Serikali hii. Taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ibara ya 34 inampa mamlaka Rais ya uteuzi wa viongozi watakaowajibika na kusimamia majukumu mbalimbali ya Serikali. Lakini Kanuni ya kwanza, Kanuni ndogo niliyoisema ya (e) inayovunjwa na Mheshimiwa Mbunge anapoleta tuhuma nzito ndani ya Bunge hili, kwamba Rais wetu sasa amekuwa Afisa Manunuzi na anasimamia manunuzi ndani ya Serikali yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili halivumiliki, siyo jambo la kweli, ni uongo uliopitiliza. Namwomba Mheshimiwa Mbunge athibitishe wapi? Lini? Kwa namna gani? Kwa vigezo vipi Mheshimiwa Rais amefanya hivyo? Ninao ushahidi kama Mjumbe wa Baraza la Mawaziri na ninafahamu Mheshimiwa Rais wetu amekuwa akizingatia taratibu na sheria na kuzisimamia sheria za nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba mjumbe afute kauli yake, kama hataki kufuta kauli hii, alete vielelezo vya kuthibitisha kwamba Mheshimiwa Rais sasa amekuwa Afisa Manunuzi Mkuu na amekuwa akisimamia na kufanya manunuzi yeye mwenyewe. (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge,…

MBUNGE FULANI: Kanuni zinasema athibitishe mwenyewe.

MWENYEKITI: Hapana.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, mimi ndio naongoza shughuli na Kanuni ndiyo zenyewe.

Mheshimiwa Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu kasimama vizuri sana kwenye point ya utaratibu na ametaja hizo Kanuni ambazo kwa sababu ya muda sitachukua, niseme tu moja ili mjue yeye yuko katika nafasi ya Waziri na kwa mujibu wa nafasi hiyo, ana nafasi pana sana na uwanja mpana sana wa kupata taarifa na ndiyo maana amelielezea Bunge hili taratibu ambazo zinatumika kwa upande wa manunuzi, kwamba haiwezekani hata siku moja, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania afanye shughuli za manunuzi kama inavyodaiwa. (Makofi)

Kwa maana hiyo, kwa mujibu wa Kanuni hiyo ya 63 ambayo ndiyo inahamisha jukumu sasa, mimi naridhika kabisa kwamba kwa maelezo aliyoyatoa Mheshimiwa Chief Whip wa upande wa Serikali, yanalifanya Bunge liamini kwamba ana taarifa za uhakika. Sasa Mheshimiwa Ruge Catherine una option mbili, na mimi kama Presiding Officer nakupa option ya kufuta kauli yako ili twende mbele au sasa tuingie hatua ya kukutaka uthibitishe.

Nakupa option ya kufuta kauli.

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafuta kauli. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, endelea.

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee kuchangia. Kwa sababu mtambo huu wa kielektroniki wa e-Immigration haukuwa kwenye hesabu za Idara ya Uhamiaji, ilimnyima nafasi Mkaguzi kuweza kukagua manunuzi ya mtambo huu na hivyo kupelekea Idara ya Uhamiaji kupata hati yenye mashaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa namwomba Mheshimiwa Waziri, wakati anakuja ku-wind up atueleze ni kwa nini fedha hizi au thamani ya mtambo huu ambao ulinunuliwa kwa shilingi bilioni 127 haukuweza kuonekana kwenye hesabu za Idara ya Uhamiaji kwa sababu hilo ni takwa la kisheria la IPSAS 31. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka mwaka 2018 hapa, tuliambiwa e-Immigration ilikuwa na component nyingi sana zaidi ya nne ikiwemo e-passport, e-border, e-gate na vitu vingine. Ningependa kufahamu mchakato huu umefikia wapi? Baada ya e-passport zile components nyingine ziko katika hatua gani kwenye mchakato? Kwa sababu nimejaribu kupitia kitabu chake na sijaona amelizungumzia suala hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kuzingumzia manunuzi ya sare hewa ya Jeshi la Polisi ya shilingi bilioni 16. Naitaka Serikali iweze kutoa majibu juu ya suala hili. Pia kuna fedha shilingi milioni 800 ambazo zilitoka Jeshi la Polisi zikawalipa watu ambao siyo Polisi. Tunataka tuambiwe watu hao ni akina nani kama siyo Polisi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa hii fursa niweze kuchangia Wizara hii ya Maliasili na Utalii. Ningependa kuanza na issue za Jimboni kwangu Jimbo langu la Serengeti ninapotoka. Ningependa kuzungumzia suala la kifuta jasho kwa wananchi ambao wanaishi pembezoni ya mbuga ya Serengeti ambao wamekuwa wakipata madhira ya kuvamiwa na Tembo kwa kubomolewa nyumba zao, kuharibiwa mazao pamoja na kupoteza maisha. Naomba nitoe mifano michache tu, mfano mwaka jana Kata ya Machochwe Jimbo la Serengeti karibia asilimia 50 ya mazao yaliharibiwa na mpaka sasa hawajalipwa fidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kijiji cha Makundusi kuna mama alikuwa na mtoto mgongoni aliuwawa na Nyati na yule mtoto alikuwa mdogo wa miezi mitano anatambaa yule mama alifariki na yule mtoto ameachwa yatima mpaka leo hajaweza kulipwa fidia. Kuna wakazi wa kijiji cha Nata wamebomolewa nyumba zao hawajalipwa fidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri naomba unisikilize, kwenye kitabu chako ukurasa wa 31 umeonyesha shilingi bilioni 1.4 zimeipwa kwa wananchi 7320 kwa wilaya 57 kama kifuta jasho na machozi, lakini kuna malalamiko makubwa na mengi kwa wakazi wa Jimbo la Serengeti kuhusu kulipwa fidia au kifuta jasho kwenye mazao yao yaliyoharibiwa, wanakijiji waliopoteza maisha na nyumba zilizobomolewa. Sasa nikuombe Mheshimiwa Waziri naomba nipate list ya watu waliolipwa kutoka katika Wilaya ya Serengeti kati ya hizi shilingi bilioni 1.4 ulizozionyesha, na usipofanya hivyo leo nitaondoka na mshahara wako.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba niende kwenye mambo ya Kitaifa, kwenye taarifa ya Mheshimiwa Waziri ameonyesha kwamba mapato yanayotokana na Utalii ni dollar za Kimarekani milioni 2.4, idadi ya watalii ni milioni 1.5. ukitafuta per- capital spending ya kila mtalii kwa maana ukichukua mapato yale tuliyoyapata dollar za Kimarekani milioni 2.4 ukigawa kwa idadi ya watalii wapatao milioni 1.5 unapata shilingi dollar 1.6 sawa na shilingi 3,500, maana yake ni nini, ni kwamba kila mtalii alitumia shilingi 3500 na ningependa kupata ufafanuzi hizi data ni za kweli au hata wale vijana wa bodaboda wanafika kwenye geti la Serengeti na wao mnawahesabia ni watalii?

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumzie suala la mradi wa Stiegler’s Gorge ambao Serikali imeamua kwenda kuutekeleza katika Bonde la Mto Kilombero pamoja na Rufiji ambako kuna pori la Akiba la Selous. Wote tunafahamu Selous is the World heritage, ni urithi wa Dunia. Lakini pia tunafahamu Utalii wa Southern Circuit unategemea mbuga ya Pori la Selous lakini nasikitika kwamba Serikali imeamua kwenda kuharibu mazingira bioanuai na kuathiri maisha ya Watanzania zaidi ya 500,000 wanaofanya activities na wanaoishi pembeni mwa bonde la Kilombero pamoja na Mto Rufiji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa watu ambao wa umri wangu ambao walisoma Literature wakati nikiwa form three kuna kitabu kimoja kilikuwa kinaitwa Song of Lawino, kwetu sisi Stiegler’s Gorge ni kama Song of Lawino. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwetu sisi tutaimba mradi wa Stiegler’s Gorge kama Song of lawino ili mtanzania, ili Watanzania wote wenye masikio na wasikie kwamba mradi huu una madhara na hautakwenda kuwafaidisha Watanzania. Stieggler’s Gorge is nonstarter project na ninawaomba namuomba Mungu Waheshimiwa Wabunge 2020 tuweze kupata…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa!

MHE. CATHERINE N. RUGE: Namuomba Mungu atujalie Waheshimiwa Wabunge turudi hapa 2020 ili muweze kuthibitisha maneno yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini nasema hivyo, Stiegler’s gorge is non-economically viable, Stiegler’s gorge is not economical viable.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo statement huwezi kurudi Bungeni.

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu kwanza kabisa gharama za utekelezaji wa huu mradi umekuwa under estimated, kuna taarifa ya mtu anaitwa George Hartman amesema amefanya economic feasibility na ripoti yake inasema kwamba mradi huu utatekelezwa kwa trilioni 21 wakati sisi Tanzania tumesema ni trilioni 10.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Benki ambazo tumezifuata kwenda ku-finance huu mradi hazina uwezo Egyptian Banks haziwezi ku-finance huu mradi na tukisema tutumie mapato ya ndani pia hatuna uwezo wa ku-finance trilioni 21 kwenye Stiegler’s Gorge. Pia mradi huu unakwenda kuwaathiri watu zaidi ya 500,000 wanaoishi pembezoni mwa Bonde Mto Rufiji pamoja na Bonde la Selous kwa sababu shughuli zao zinategemea maji yanayotoka katika Mto Rufiji. Pia hatujafanya environmental impact assessment kuona madhara ya muda mrefu kwa ajili ya huu mradi.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utaratibu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Catherine Ruge naomba ukae. Mheshimiwa Subira kanuni iliyovunjwa.

KUHUSU UTARATIBU

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kanuni ilivyovunjwa ni kanuni 64 naomba nisiisome.

NAIBU SPIKA: Endelea Mheshimiwa Subira.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, hatatoa Bungeni taarifa ambazo hazina ukweli wowote Kanuni 64(1)(a). Mheshimiwa Mbunge Catherine anayechangia anatoa taarifa ambazo hazina ukweli wowote, mradi wa Rufiji hydro power ulifanyiwa tathimini na tenda ilivyotangazwa wakandarasi wameomba kwa kadri wanavyoweza kufanya ule mradi na ndio maana tumeingia mkataba nao wa kiasi cha trilioni 6 ambazo wakandarasi na timu ya Serikali ya wataalam iliyondwa kwa pamoja na kwa majadiliano tumekubaliana.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa anaposema kwamba mradi utagharimu trilioni 21 na kwamba Serikali imeingia na mabenki ambapo Serikali utagharamia mradi huo kwa vyanzo vyake vya ndani na imeshatoa asilimia 15 kiasi cha bilioni 685. Sasa anaposema kwamba Serikali imetumia mabenki ambayo hayapo asilipotoshe Bunge Serikali itagharimu mradi huu kwa pesa zake za ndani na imeshalipa asilimia 15 na kazi inaendelea. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge Mheshimiwa Catherine Ruge alikuwa akichangia, Mheshimiwa Subira Mgalu amesimama akionesha kwamba katika mchango wa Mheshimiwa Catherine Ruge ametoa taarifa ndani ya bunge ambazo hazina ukweli kwa mujibu wa Kanuni ya 64(a). Sasa Waheshimiwa Wabunge ukisoma masharti ya hii Kanuni ya 64 na Kanuni ya 63 inanitaka nikiombwa utaratibu kuhusu jambo hili nimtake Mheshimiwa Mbunge aliyekuwa akichangia kwa maelezo hayo yaliyotolewa na Mheshimiwa Subira Mgalu kwa sababu yeye ndio aliyesema hilo jambo si la kweli na amejaribu kuonyesha namna ambavyo yeye taarifa zake alizonazo zinaonyesha kwamba taarifa unayotoa ni tofauti na anayoitoa.

Kwa hiyo, kwa mujibu sasa wa hii Kanuni ya 64 na Kanuni ya 63 inayozungumzia kutokusema uwongo Bungeni Mheshimiwa Catherine Ruge taarifa hiyo ya Mheshimiwa Waziri na taarifa uliyoitoa wewe uyafute hayo maneno labda kama nawe unao ushahidi tutakutaka kwa mujibu wa kanuni hii. Kwa hiyo, unayo hayo mawili, moja ni kufuta kwa mujibu wa kanuni hizi kama unaoushahidi utanijulisha ili niweze kutoa maelekezo mengine Mheshimiwa Catherine Ruge. (Makofi)

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika, haya ni maoni yangu na nimesoma report ya George Hartman inasema hivyo mradi utatekelezwa kwa trilioni 21 hiyo ni research report amefanya utafiti kama hauna hiyo report nitaweza kukupa, lakini pia sheria mpya ya madini inasema…

NAIBU SPIKA: Sawa ngoja Mheshimiwa Catherine Ruge kabla hujaendelea kuchangia tulimalize hili kwanza, kwa hivyo katika yale mawazo mawili wewe unasema unao ushahidi.

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ndio.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kwa mujibu wa hizi Kanuni zetu mchango wa Mheshimiwa Catherine Ruge nimelazimika kumuuliza mara ya pili kama anao ushahidi kwa sababu ameanza kwa kusema yeye ni mawazo yake, lakini sasa amethibitisha kwamba yeye anao ushahidi. Kwa hivyo, nitamruhusu aendelee kuchangia ataleta ushahidi wake ambao ushahidi huo kama taratibu zetu zilivyo ili kumbukumbu zetu zikae sawasawa ushahidi huo utapelekwa kwenye Kamati ambayo itatusaidia kuangalia uhalisia wa hiyo taarifa anayoitoa. (Makofi)

Kwa sababu hiyo Mheshimiwa Catherine Ruge mchango wako kuhusu Stiegler’s Gorge kwa kuwa sasa utapeleka ushahidi kwenye Kamati utaangaliwa wakati huo, naomba uendelee kuchangia kwenye jambo jingine linalofuata. (Makofi)

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee na mchango wangu. Nafahamu Tanzania tuna vyanzo vingi sana vya umeme ambavyo tungeweza kuwekeza huko na tukapata megawatts hizo hizo 2,100 au zaidi, lakini pia nafahamu Wajerumani ambao wamekuwa wakitoa fedha kwa ajili ya kuhifadhi mazingira kwenye Bonde la Akiba la Selou toka mwaka 1959, lakini pia wakitoa pesa kwa ajili ya kuzuia ujangili, walitoa offer kwa Serikali kuweza kuwekeza kwenye alternative source of energy ya geothermo na wakasema wanaweza waka- finance huo mradi wa umeme wa geothermo kupata megawatts 2,000, lakini Serikali imekataa offer hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa tu kufahamu, ni kweli tuna nia ya kupata nishati ya umeme au nia yetu ni kwenda kuharibu Bonde la Selou ambalo limekuwa kivutio kikubwa cha watalii kwa Southern Circuit, lakini pia utalii wa Southern Circuit unategemea sana Mbuga ya Selou. Naomba niseme na iwekwe kwenye hansard, mpaka mwaka 2025 hamtakuwa mmetengeneza hata megawatt moja kutoka kwenye Mradi wa Stieglers Gorge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niende kwenye jambo lingine. Kulikuwa na hoteli za kitalii ambazo zilikuwa kwenye hifadhi ambazo zilikuwa chini ya Serikali, lakini wakapewa watu binafsi, lakini hoteli hizi zimekuwa na hali mbaya kuliko hata zilivyokuwa chini ya Serikali. Jumla ya hoteli hizi zilikuwa 16, lakini nina mifano michache; moja ya hoteli hizo ni Mafia Lodge ya Mafia, Lobo Lodge Serengeti, Seronera Wildlife Lodge, Ngorongoro Wildlife Lodge, Manyara Wildlife Lodge, zina hali mbaya kimiundombinu, mapato, huduma. Ningependa kufahamu msimamo wa Serikali kuhusu hoteli hizi ambazo zilibinafsishwa na hazifanyi vizuri na ni nini sasa way forward kuhusu kuzihusisha hoteli hizi.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Kengele ya pili imegonga Mheshimiwa Catherine Ruge.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia katika Bajeti Kuu ya mwaka 2017/2018.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Kambi Rasmi ya Upinzani kwa hotuba nzuri. Niiombe Serikali iweze kuchukua muda kusoma hotuba hii na kuangalia mambo mazuri ambayo tumeishauri ili waweze kuifanyia kazi kwa mustakabali wa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba hii nitajikita kwenye mambo makuu matano. Bajeti hii imekuja wakati kama Taifa tukiwa na changamoto nyingi, mojawapo ikiwa ni ukame ambao umesababisha njaa katika maeneo mbalimbali nchini lakini pia kuyumba na kufungwa kwa biashara nyingi ambapo zimeathiri uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie kufungwa na kuyumba kwa biashara nyingi nchini mwaka 2016/2017. Wakati Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango akiwasilisha hotuba ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/2017 alikiri katika kipindi cha mwezi Agosti na Oktoba, 2016 biashara 1,872 zilifungwa katika Mikoa miwili ya Dar es Salaam na Arusha. Kama kwa kipindi cha miezi mitatu, biashara zaidi ya 1,000 zinaweza kufungwa basi ndani ya mwaka mzima ni zaidi ya biashara 7,488 zinaweza kufungwa kwa mikoa miwili tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii maana yake ni nini? Tunakwenda kupoteza ajira zaidi ya 15,000 kwa maana ya wastani wa wafanyakazi wawili katika kila biashara. Hii haiathiri wafanyakazi tu, lakini pia familia zao ambazo zinawategemea ukizingatia utamaduni wetu wa nchi yetu tunaishi kwa kutegemeana (extended families). (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango alikuwa anatoa mifano ya jinsi gani kumekuwa na mdororo wa uchumi kwa nchi mbalimbali miaka mingi iliyopita. Nadhani ni vizuri Mheshimiwa Waziri ungejikita katika kuangalia sababu zilizofanya kufungwa kwa biashara hizi na suluhisho ili kuzuia na sisi tusije tukapata mdororo wa uchumi kama nchi ambazo ulizitolea mfano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wafanyabiashara wengi wamekuwa wakilalamika kwamba kuyumba kwa biashara zao kumetokana na jinsi ambavyo TRA wamekuwa wakiwakadiria mapato. Niishauri Serikali iweze kuangalia ni jinsi gani inaweza kujenga mazingira rafiki ya wafanyabiashara kulipa kodi na kufanya biashara zao na isiwe chanzo cha wafanyabiashara kufunga biashara zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ambalo napenda kuchangia ni import and export. Uchumi wa nchi yoyote hauwezi kukua kama mauzo ya biashara tunayozalisha nchini yanapungua siku hadi siku. Kwa mujibu wa Jarida la Uchumi la Benki Kuu ya Tanzania Machi, 2017, linaonyesha kwamba uwezo wetu wa kuuza bidhaa tunazozalisha nchini kwenda masoko ya nje umepungua kwa asilimia 34.6 ukilinganisha na kipindi kama hicho Machi, 2016. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni jambo ambalo inabidi tulitazame kwa jicho la tatu na inabidi Serikali ijiulize maswali yafuatayo. Je, ni kwa sababu bidhaa zetu hazina ubora wa kuweza kushindana na bidhaa za mataifa mengine au ni kwa sababu bidhaa tulizokuwa tunaziuza nje kwa mwaka 2016 na miaka iliyopita zimekosa masoko na hivyo basi inabidi tufikirie bidhaa mbadala ili tuweze kuendelea kuuza nje na kuongeza pato la Taifa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mauzo ya nje yakiwa yameshuka kwa kiwango hicho nilichokitaja lakini pia manunuzi yamepanda kwa asilimia 33.5 kwa mwaka 2016/2017. Hii inanipa wasiwasi kwa kuwa tunaelekea Tanzania ya Viwanda kwamba tunanua zaidi kuliko tunavyouza na hivyo kunakuwa na unfavorable balance of payments. Ili tuweze kuvilinda viwanda vyetu, inabidi tu- promote viwanda vya ndani lakini pia tuweze kuzalisha zaidi na kukidhi masoko ya ndani pia kuweza kuuza zaidi nje ya nchi ili tuweze kuongeza pesa za kigeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la tatu ambalo napenda kuzungumzia ni ajira. Suala hili limeendelea kuwa changamoto especial kwenye kipindi hiki cha Awamu ya Tano ambapo tumekuwa na wahitimu wengi wakiwa wanatoka vyuoni zaidi ya 10,000 kila mwaka, lakini Serikali hii imesitisha ajira pia kuna mazingira magumu ya kufanya biashara na hivyo kampuni nyingi zimepunguza wafanyakazi. Hii imekuwa ni changamoto especial kwa vijana, wamekuwa wakirandaranda mitaani na degree zao na vyeti vyao na kukosa matumaini ya kesho yao na kujiona kwamba wamepoteza muda kusoma degree zao za miaka mitatu mpaka mitano. Mheshimiwa Waziri nikuombe wakati unakuja kuhitimisha hotuba yako uwaeleze vijana wa Kitanzania katika bajeti ya mwaka 2017/2018 unakwenda kuajiri vijana wangapi katika Taifa hili? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, ukisoma kitabu cha bajeti Serikali inaonyesha imelipa madeni ya shilingi bilioni 67.6. Naomba niipongeze Serikali kwa kulipa madeni hayo. Tatizo langu nataka kujua definition ya watumishi katika Taifa hili kwa sababu madeni haya yote ya shilingi bilioni 67.6 wamelipwa walimu. Nikuombe Mheshimiwa Waziri, kuna watumishi wengine ambao siyo walimu wanadai arrears zao za mishahara, stahiki zao za kupanda vyeo, stahiki zao za uhamisho ili uweze kuwalipa kwa sababu kwenye kitabu chako hujaonesha kama kuna ongezeko lolote la mshahara. Hata ile increment ambayo ni kwa mujibu wa sheria wafanyakazi hawa hawajongezewa mishahara yao, namaanisha statutory annual increment kwa wafanyakazi ambayo ipo kwa mujibu wa Labor Laws. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee suala la PAYE kwa maana ya Pay As You Earn. Wafanyakazi wamekuwa wakilipa kodi kwa asilimia 100 kwa sababu hawana loopholes za kukwepa hii kodi ukilinganisha na wafanyabiashara. Kama kuna watu wanalipa kodi genuine katika Taifa hili basi ni wafanyakazi, lakini wafanyakazi wanakatwa kodi kwenye gross pay na siyo net pay. Tukumbuke wafanyakazi pia wana matumizi au expenses mfano na wao pia wanalipa kodi, wanalipa nauli, wanakula chakula pamoja na matumizi mengine katika kutimiza wajibu wao wa kwenda kazini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfanyakazi ambaye yupo kwenye band ya milioni moja na zaidi analipa asilimia 25 au zaidi ya PAYE. Ukiangalia kwa makampuni au corporate companies ambao wanalipa 30 percent kwa net profit kwa maana kuna allowable expenses nyingi ambazo wanakuwa hawazilipii kodi. Kwa hiyo, tunaona kuna burden kubwa sana kwa mfanyakazi wa Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuombe Mheshimiwa Waziri, kama Serikali haiwezi kupunguza Pay As You Earn basi PAYE ikatwe kwa net pay baada ya kutoa housing allowance, food allowance, fuel allowance… (Makofi/Vigelegele)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa ili nami niweze kuchangia Wizara hii nyeti ya Afya. Mwaka 2001 African countries kwa maana ya AU na Tanzania ikiwa mmojawapo walisaini convention ya Abuja declaration na wakuu wote wa nchi walikubaliana kutenga angalau asilimia 15 ya bajeti yote ya nchi kwa ajili ya afya, lakini tukiangalia miaka 17 sasa hivi hilo halijawahi kutokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia bajeti ya mwaka 2017 ukurasa wa nane inaonesha Bunge tuliidhinisha 1.1 trillion lakini pesa zilizopelekwa ni asilimia 57 tu. Pia hii bajeti ya 1.1 trillion ilikuwa ni asilimia 3.5 ya bajeti nzima ya Taifa. Pesa za Maendeleo kwa Wizara ya Afya, pesa zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo, pesa za ndani zilikuwa asilimia 24 tu zilizokwenda ambayo ni almost eight billion na pesa za nje zilienda shilingi bilioni 321 ambayo ni sawa sawa na asilimia 71. Sasa kama tunaweza kutenga pesa kidogo hivyo, kutokana na mapato ya ndani, tunategemea zaidi pesa za nje, hivi kweli tuna nia ya dhati ya ku-improve sekta ya afya? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukija kwenye bajeti ya Afya ya mwaka huu, imepungua kutoka 1.1 trillion mpaka 0.9 almost shilingi bilioni 898 ambayo ni pungufu ya asilimia 22. Hivi kweli are we serious? Tunawezaje kupunguza zaidi ya asilimia 20 kwenye sekta muhimu kama ya afya? Hii ni sekta inayo-deal na afya za watu, tunapunguza pesa kiasi hicho! Napenda Mheshimiwa Waziri wakati anakuja ku-wind up atueleze ametumia criteria gani kupunguza zaidi ya asilimia 20 ya bajeti ya Wizara hii? Ni kwa sababu labda changamoto zimepungua au magonjwa yamepungua? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia ukurasa wa 128 pia pesa zilizotengwa kwa ajili ya Fungu 52 - Wizara ya Afya, bado pia ni kidogo sana na asilimia 67 imetengwa kutoka pesa za nje. Tuna guarantee gani kwamba tutazipata hizi pesa kutoka nje, kama sisi wenyewe we are not committed kutoa pesa za ndani kwa ajili ya afya za watu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie kuhusu vifo vya akina mama wakati wa kujifungua (maternal mortality rate). Taarifa ya Tanzania Demographic Health Survey ya mwaka 2015/2016 inaonesha vifo vya akina mama wakati wa kujifungua vimeongezeka kutoka akina mama 432 mpaka 556 kwa kila uzazi kwa watu laki moja. Moja ya sababu ni zaidi ya nusu ya akina mama wanajifungulia nyumbani. Pia hiyo taarifa inaonesha ni asilimia 46 tu ya akina mama wakati wa kujifungua wanahudumiwa aidha na daktari au muuguzi au clinical officer. Sasa tuna zaidi ya miaka 50 ya uhuru, I think Serikali ya CCM mmekuwa very comfortable ndiyo maana mnacheza na afya za watu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli zaidi ya asilimia 50 ya akina mama wanaojifungua kwenye Taifa hili hawapati huduma wakati wa kujifungua na tunasema tuna nia ya dhati ya kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua, I think we need to be serious. Mheshimiwa Ummy wewe ni mwanamke, wewe ni mama unajua ni jinsi gani mtu anapata shida kubeba mimba miezi tisa halafu anakuja anapoteza maisha au anapoteza maisha ya mtoto wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuomba Mheshimiwa uliangalie hili suala kwa makini kama wewe mwenyewe ulivyoonesha kwenye hotuba yako ukurasa wa saba kwamba mnataka kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo wa Kati 2020/2021, Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2015/2016 na Sustainable Development Goals (SDG) 2030 ambayo tunataka iwe chini ya akina mama 200 wanafariki wakati wa kujifungua; lakini tunaona trend inaongezeka. Sasa kama trend inaongezeka ndani ya mwaka mmoja, akina mama zaidi ya 100 wamefariki, tunafikiaje hiyo less than 200 mwaka 2020. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, niwaombe Wabunge wote akina mama zile shilingi trilioni 1.5 zilizopotea, tumwombe na tumuunge mkono Mheshimiwa Rais zipatikane ili tuweze kuboresha na kujenga vituo vya afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba kuiongelea Hospitali ya Jimbo langu ya Wilaya ya Serengeti. Hatuna hospitali ya Wilaya tangu uhuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ya kilimo mwaka 2018/2019 Serikali ya CCM haina dhamira ya dhati kuendeleza kilimo na haina mpango wa kuwasaidia wakulima. Lengo la MKUKUTA lilikuwa kwamba sekta ya kilimo ikue kwa asilimia sita mpaka asilimia nane kwa mwaka kwa miaka 10 mfululizo ili Watanzania wa vijijini waondokane na umaskini. Hata hivyo hali halisi ni kuwa kati ya mwaka 2011 – 2015 sekta ya kilimo ilikuwa ni wastani wa asilimia 3.4 kwa mwaka. Mwaka 2016 na 2017 miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Tano kilimo kilikua kwa asilimia 19 mwaka 2016 na 2017 ni asilimia 1.3.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uzalishaji wa mazao yote makuu isipokuwa korosho umeshuka katika mwaka 2016/2017; kahawa uzalishaji umeshuka kutoka tani 760,000 mwaka 2015 mpaka tani 48,000 mwaka 2017; pamba imeshuka kutoka tani 50,000 mwaka 2015 mpaka tani 48,000 mwaka 2017; tumbaku imeshuka kutoka tani 87,000 mwaka 2015 mpaka tani 61,000 mwaka 2017 na chai imeshuka kutoka tani 33,000 mpaka tani 27,000 mwaka 2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata mazao ya chakula; wakati mahindi uzalishaji umeongezeka kutoka tani milioni 6.1 mwaka 2016 mpaka tani milioni 6.6 mwaka 2017, bei ya mahindi imeporomoka sana kufuatia Serikali kuzuia mahindi kuuzwa nje ya nchi na Serikali yenyewe kutonunua mahindi kwa ajili ya ghala la Taifa. Hii ni kwa sababu NFRA haikuwepewa fedha za kununua mahindi na hivyo Serikali kuwapa umaskini wananchi na wafanyabiashara wa mazao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ya Wizara ya Kilimo imezidi kushuka, kwa mfano mwaka 2017/2018 pesa zilizoidhinishwa na Bunge zilikuwa shilingi bilioni 221.10. Mwaka 2018/2019 Wizara inaomba kuidhinishiwa na Bunge shilingi bilioni 170.27, hii ni pungufu ya asilimia 23 kulingana na bajeti ya mwaka jana. Hii sio sawa ukizingatia umuhimu wa sekta hii ya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kushauri mambo yafuatayo:-

Moja, kwa ajili ya kujenga uchumi shirikishi ni muhimu kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha kwamba kilimo chetu kinaanza kuchangia vya kutosha katika ukuaji wa uchumi. Serikali iweke shabaha ya kufuatilia ukuaji wa asilimia nane wa sekta ya kilimo.

Mbili, Serikali lazima itambue kuwa kilimo ndiyo shughuli kuu ya kutokomeza umaskini. Shughuli za kilimo ziendeshwe na wananchi wenyewe kwa kuwawezesha kumiliki ardhi, kuongeza tija na kupata mitaji.

Tatu, Serikali itunge stable fiscal regime katika sekta ya kilimo na kuhakikisha kwamba mkulima anabaki na sehemu kubwa ya mapato baada ya mavuno ya mazao yake.

Nne Serikali iunde mamlaka ya kilimo itakayosimamia sekta ya kilimo na kutekeleza mikakati yote ya maendeleo ya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tano na mwisho, Serikali ihusike kikamilifu kwenye uhifadhi wa mazao kupitia soko la bidhaa (commodities exchange) ambao utashirikisha vyama vya wakulima na hivyo kufuta middle men.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu. Sayansi na Teknolojia
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ili na mimi niweze kuchangia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kwanza ninapenda kutoa pole kwa Mwenyekiti wangu wa Kanda na Mbunge wa Tarime Vijijini Mheshimiwa John Heche kwa msiba wa mdogo wake ambaye alifariki kwa kuchomwa kisu mikononi mwa polisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hapo naomba niende moja kwa moja kwenye hoja zangu. Mheshimiwa Waziri Profesa Ndalichako nimesoma hotuba yako na nimegundua mapungufu makubwa matatu. Pungufu la kwanza bajeti hii haina jicho la kijinsia (it is not a gender responsible budget). Nasikitika kwamba wewe ni mwanamke ni Mama lakini umeshindwa kuliona hili. Umeonesha takwimu mbalimbali mfano udahili wa wanachuo, wanafunzi waliopata mikopo elimu ya juu, kwamba unaenda kujenga mabweni, kuboresha miundombinu lakini huonyeshi beneficiaries (wanufaika) kwa kuangalia jinsia. Tunataka kuona rasilimali za nchi hii zikitumiwa sawa na zikiwafaidisha sawa watu wote bila kujali jinsia kwa maana ya jinsia ya wanawake na wanaume lakini huoneshi, kwa hiyo tunashindwa kujua beneficiaries wanawake ni wangapi na wanaume ni wangapi.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pungufu la pili bajeti yako haina consistency kwa maana kwenye takwimu ambazo unazionesha ukurasa huu unaweka asilimia, kurasa nyingine hauweki asilimia, pale ambapo Serikali imefanya vibaya kwa maana ya Wizara hujaonesha kabisa takwimu. Uki-compare na hotuba ya Kamati wamefanya vizuri kuliko bajeti ya Wizara, wakati Wizara ina Wataalam. Wameweza kuonesha asilimia kwenye takwimu zao zote mpaka wametuwekea bar chart na tunaweza kuona ulinganifu wa performance indicators tofauti tofauti. Mpaka natia shaka inawezekana Waziri hii hotuba umekuja kukutana nayo hapa Bungeni kama Wabunge na hukuipitia. Siamini kama kwa umakini wako Madam Professor uliweza kuipitia na ukaliacha hili likaja hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pungufu la tatu bajeti hii haina continuity kwa maana ya muendelezo. Bajeti ya mwaka 2017/2018 na 2019 vitu ulivyoviandika 2017/2018 ambavyo unaona kabisa vinatakiwa kwenye bajeti hii vionekane vinaendelea havina mwendelezo.

Naomba nikupe mfano, ukienda ukurasa wa 10 wa kitabu chako unaelezea kuainisha mahitaji ya nchi katika ujuzi na kuendeleza na ukataja huo mradi ambao unaitwa Education Skills for Productive Job na ukataja maeneo ambayo unaenda kuendeleza stadi za kazi na ujuzi ukasema kilimo, TEHAMA, nishati, ujenzi, uchukuzi na utalii, lakini Madam Professor hakuna statistic, where the statistic Madam? Ukienda ukurasa wa 76 umeenda kuelezea jambo hilo kwamba kuainisha mahitaji ya nchi katika ujuzi na kuendeleza, lakini vile vipaumbele, ukija ukurasa wa 76, 77 kuainisha mahitaji ya nchi katika ujuzi na kuendeleza huku ametaja maeneo ambayo anaenda kuendeleza kwa maana ya elimu, TEHAMA, nishati na kadhalika, lakini huku hicho kitu hakijatajwa kabisa na hamna takwimu. Kwa hiyo, ina maana hii programu imeisha au? Sielewi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ningependa kuzungumzia ni usajili wa watoto wa kike vyuo vikuu. Ukisoma ukurasa wa 35 wa hotuba ya Kamati imeonesha idadi ya watoto wa kike wanaosajiliwa vyuo vikuu ni ndogo sana na wametoa takwimu hapa kwa mfano, Chuo Kikuu cha Mbeya mwaka wa masomo 2017/2018 jumla ya wanafunzi ambao wanafanya Shahada ya Kwanza ni 1,759 lakini kati ya hao ni wanafunzi 344 tu ambao ni wa kike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tunasema tunajenga uchumi wa viwanda na kama tunajenga uchumi wa viwanda haiwezekani, huwezi kumuacha mwanamke lazima mwanamke ata-contribute kwenye uchumi wa viwanda kwa maana ya nguvu kazi kwa kuajiriwa au kwa kujiajiri. Sasa naomba Mheshimiwa Waziri wakati unakuja ku- wind up utuambie mkakati mahsusi wa Serikali wa kuhakikisha tunaongeza namba ya watoto wa kike wanaosoma masomo ya sayansi kuanzia shule za Awali mpaka vyuo vikuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ningependa kuchangia kuhusu ubora wa elimu nchini, bado unazidi kuporomoka kwa miaka Sita mfululizo bado Serikali inazidi kufanya vibaya kwa maana ya shule za Serikali uki-compare na shule binafsi. Ukiangalia ukurasa kuanzia wa 21, 22, 23 wa kitabu cha Kamati wameonesha indicators tofauti za ubora wa elimu. Kwa mfano, asilimia 37.8 ya Walimu ndiyo wana hamasa. Mwalimu mmoja anafundisha wanafunzi 159 upungufu wa walimu bado uko juu, lakini ukiangalia matokeo ya mwaka 2016 katika ukurasa wa 23 wa kitabu cha kamati inaonekana asilimia 73.3 walipata division four na division zero. Napata shaka kwamba miaka 10/20 ijayo tutakosa nguvu kazi, tutakosa watu ambao wanaenda kuajiriwa kwenye hiyo Tanzania ya viwanda kwa maana ya viwanda. Nasikitika pia kwamba tunaweza tukakosa maprofesa, madaktari kama tutaenda kwa mtindo huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mwanafalsafa mmoja anasema if any organization want to be successful it must invest in people. Kwa hiyo, kama tunataka kuboresha elimu yetu ni lazima tu-invest kwa walimu, whether tunataka hatutaki ni lazima tu-invest kwa walimu kwa maana ya kuboresha maslahi yao, kwa maana ya kuongeza namba ya walimu wanaofundisha watoto tufuate ile ratio ya moja kwa 25, kwa maana ya kulipa malimbikizo ya madeni yao, kuwapandisha madaraja kwa wakati na maslahi mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna Mwanafalsafa anasema kama unataka kupata matokeo tofauti lazima ufanye kitu tofauti. Tumeona miaka sita iliyopita bado ni business as usual lazima kama Serikali tu-take initiative ya kufanya vitu tofauti kabisa ili tuweze kupata matokeo bora na kukuza elimu ya watoto wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa pia kuiomba Serikali kujenga shule ya watoto wa mahitaji maalum Mkoa wa Mara kwa sababu mkoa ule hauna shule ya watoto wa mahitaji maalum na wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kwenda kutafuta elimu. Kwa hiyo, hii inawanyima haki yao ya msingi ya kupata elimu, naomba uliangalie hilo na Mkoa wa Mara tunaomba shule ya watoto wenye mahitaji maalum. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa nipende kuzungumzia jinsi mvua ambavyo imeharibu miundombinu mbalimbali ya shule katika nchi hii. Mvua zilizokuja zilikuwa kubwa...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa ili na mimi niweze kuchangia Wizara hii ya Mifugo na Uvuvi.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo kama Taifa tuna-set trend ya kuwa, sekta hii ya Mifugo na Uvuvi haijaliwi na Serikali ya CCM. Kwa nini nasema hivi; tangu Serikali hii ya Awamu ya Tano iingie madarakani hakuna hata asilimia moja ya Bajeti ya Maendeleo iliyoweza kupelekwa kwenye sekta hii. Sekta ya uvuvi pekee inatoa ajira kwa Watanzania milioni tano, hii ni sawa na asilimia 10 ya wananchi wote wa Tanzania. Pia watu milioni nne wanajishughulisha moja kwa moja na shughuli za uvuvi.

Mheshimiwa Naibu Spika, asilimia 7.8 ya sekta ya mifugo na uvuvi inachangia Pato la Taifa. Asilimia 5.9 ikiwa inatoka kwenye sekta ya mifugo na asilimia 1.9 ikiwa inatoka kwenye sekta ya uvuvi. Takwimu hizi zinatoka kwenye quarterly bulletin za BOT 2017.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia sekta hii ya mifugo na uvuvi inachangia zaidi ya sekta ya madini kwenye Pato la Taifa, ambapo sekta ya madini inachangia asilimia 4.8 tu; lakini nasikitika kwamba sekta hii imepuuzwa na imeshindwa kabisa kupewa kipaumbele na Serikali hii ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, take it from me, tukiamua kuwekeza kwenye sekta hii ya mifugo na uvuvi na tukaweza kufikia asilimia 10 tu kuchangia kwenye Pato la Taifa nawaambia nchi hii itakimbia. Solution hapa ni ku-double tu uzalishaji na kuangalia vipaumbele vyetu ni vipi. Je, return ya investment ya ku-invest kwenye ndege ni kubwa kuliko return ya investment ya kuwekeza kwenye sekta ambayo asilimia 50 ya kaya inategemea sekta ya mifugo na uvuvi? Kwa hiyo kupanga ni kuchagua, tuamue tunachagua wanyonge ambao ni zaidi ya asilimia 90 ya Taifa hili au tunachagua asilimia tano ya watu wachache ambao wana uwezo wa kupanda ndege? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tuna ng’ombe zaidi ya milioni 28 lakini ukiangalia Botswana na Ethiopia wanafanya vizuri kuliko sisi. Hebu tukae tujiulize shida ni nini? Maldives, Mauritius uchumi wao unaendeshwa kwa uvuvi, sisi tuna tatizo gani wakati samaki wao wanakuja kwenye maji yetu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sekta hii kwa mwaka mmoja tu imeweza kukusanya maduhuli ya bilioni 26.9; naomba Mheshimiwa Waziri akija atueleze ni kwa nini sekta hii imeshindwa kupata pesa za maendeleo hata asilimia 10 basi wakati imeweza kukusanya kwa mwaka mmoja tu 75 percent ya malengo ya Wizara? Kwa kweli inasikitisha sana; yaani inaonesha tuna chuki, Serikali hii ina chuki kwa wafugaji, ina chuki kwa wavuvi. Hebu tuache hiyo chuki ili tuweze kuwainua wafugaji na wavuvi wa nchi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa pia kuzungumzia viwanda vya ndani vinavyotokana na sekta ya mifugo na uvuvi. Ningependa nianze na kiwanda cha maziwa. Viwanda vyetu vya ndani vina uwezo wa kutengeneza lita milioni 276.6 kwa mwaka, lakini sasa hivi vina uwezo wa kutengeneza lita milioni 56.3 ambayo ni sawa na asilimia 20 tu ya operating capacity.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo viwanda vyetu vya maziwa vina-operate under capacity kwa asilimia 80. Vile vile kinachoshangaza bado wafanyabiashara wa nchi hii wa maziwa na bidhaa nyingine kama cheese, butter wanaagiza bidhaa kutoka nje. Naomba Mheshimiwa Waziri akija atuambie, ni kwa nini viwanda vyetu vya ndani vya maziwa vina-operate under capacity for eighty percent (80%) yet tunaagiza bidhaa za maziwa kutoka nje na tunapoteza kama Taifa almost bilioni mia moja ishirini kwa kuagiza kutoka nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda vya nyama vina uwezo wa kusindika nyama kwa tani 626,922 kwa mwaka, lakini maajabu sasa hivi viwanda vyetu vya nyama vya nchi hii vinatengeneza au vinasindika nyama kwa tani elfu themanini na moja, elfu ishirini na mbili sawa na asilimia 13. Tuna-operate under capacity kwa asilimia 87 na bado tunaagiza nyama kutoka nje kila mwaka. Kutokana na taarifa za Wizara 2016/2017 tumeagiza nyama kutoka nje kwa kutumia dola milioni saba na bado tunasema Tanzania ya Viwanda; hivi kweli tuna nia ya dhati ya kuwekeza kwenye viwanda vyetu vya ndani au viwanda tunavyovizungumzia ni viwanda gani?

Mheshimiwa Naibu Spika, ukija kwenye viwanda vya samaki. Nchi yetu ina uwezo wa ku-process tani 700,000 kwa mwaka, lakini sasa hivi capacity ni tani 350,000 tuna- operate kwa asilimia 50 tu na asilimia 50 bado tunaagiza kutoka nje. Ningependa kupata majibu yanayoridhisha kutokana na production capacity ya viwanda vyetu vya ndani.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimepitia hii hotuba ya Wizara, hotuba haiko solution oriented, haitoi solution kwa matatizo yetu. Ukisoma maneno mengi tunafanya tathmini, tumewatuma wataalam, tutajitahidi, tuta-make sure, tutafanya nini. Ukiangalia ukurasa wa 38, 39 na 40 kuonesha jinsi yeye na wataalam wake Mheshimiwa Waziri ambavyo hamko makini unasema kuhusu NARCO na NICO kwamba, naomba nianze kusoma ukurasa wa thelathini na tisa (39):-

“NARCO haikupata gawio lolote kwa kipindi cha miaka 10 na kwa kuwa hakuna maendeleo yoyote yanayofanyika kwa mujibu wa mkataba wa mipango na biashara na hivyo kutofikia malengo na matarajio ya Serikali, hivyo ili kukamilisha taarifa ya uchambuzi wa mkataba na kuiwezesha Serikali kufanya maamuzi Msajili wa Hazina anaelekezwa kufanya ukaguzi maalum (Special Financial Audit) katika kampuni ya nyama iliyopo Dodoma”.

Mheshimiwa Naibu Spika, labda nikusaidie Mheshimiwa Waziri, Msajili kazi yake siyo kufanya audit. Audit inafanywa na Control and Auditor General ndiye mwenye mandate ya kufanya ukaguzi kwenye Taifa hili, Msajili kazi yake ni kuangalia mali, kwa hiyo aende aka- review hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa pia kuzungumzia suala la tozo mbalimbali na manyanyaso yanayofanywa kwa wafugaji.
Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, ningependa kuchangia mambo machache katika Wizara hii ya Maliasili na Utalii. Jambo la kwanza ni kuhusu mtiririko wa bajeti katika Wizara hii. Mwaka 2016/2017 Bunge liliidhinisha fedha za miradi ya maendeleo kiasi cha shilingi 17,746,682,000; hata hivyo, kiasi kilichotolewa ni shilingi 2,199,870,358 ambacho ni sawa na asilimia 12 ya fedha zote zilizotengwa.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2017/2018 jumla ya shilingi 51,803,204,000 zilizoidhinishwa na Bunge kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo mpaka kufikia mwezi Februari, 2018 Wizara ilikuwa imepokea jumla ya shilingi 27,946,781,302 ni ambayo ni sawa na asilimia 54 ya fedha zilizoidhinishwa. Makadirio ya bajeti ya mwaka 2018/2019 ni shilingi 29,978,082,000 hii inaonesha anguko la bajeti ya Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, mtiririko wa bajeti wa Wizara hii unaonesha bajeti ya maendeleo imekuwa ikitegemea fedha za nje. Mfano kwa mwaka 2017/2018 fedha za ndani zilizotolewa zilikuwa shilingi 11,353,250,489 na fedha za nje ni shilingi 16,593,530,813. Mwaka wa fedha 2018/2019 fedha za maendeleo zinakadiriwa kwa shilingi 29,978,082,000 kati ya hizo fedha za ndani ni shilingi 3,000,000,000 tu.

Mheshimiwa Spika, hili ni tishio kubwa kwa Wizara kwani kuzidi kutegemea misaada kutoka kwa wahisani hakuwezi kamwe kunyanyua sekta hii. Kumekuwa na matamko mbalimbali ya Mheshimiwa Rais, hatutategemea wahisani, ila hali halisi ni kuwa bajeti yetu imekuwa tegemezi kwa zaidi ya asilimia 50. Hii inaonesha kuwa bado Serikali haijakubali kuwekeza ipasavyo kwenye sekta ya maliasili na utalii.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kuhusu ukuaji wa sekta ya utalii nchini. Mwaka 2012/2016 wastani wa ukuaji wa sekta ya utalii ilikuwa asilimia 13.7 mwaka 2017 sekta ya utalii imekuwa kwa asilimia 3.3 kwa sababu ya maamuzi holela ya Wizara hii, unstable policy decisions katika sekta ya uwindaji ambayo imesababisha kushuka sana kwa ukuaji wa sekta ya utalii.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuchangia kuhusu Jeshi la Polisi. Zamani wananchi waliamini Polisi ni sehemu salama lakini Awamu hii ya Tano mambo yamebadilika, Polisi siyo sehemu salama tena maana matukio mengi ya vifo yametokea mikononi mwa Polisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, kuna kijana anaitwa Allen aliuawa akiwa mikononi mwa Polisi Mjini Mbeya. Pia hivi karibuni mdogo wake Mbunge wa Tarime Vijijini, Mheshimiwa John Heche pia amechomwa kisu akiwa mikononi mwa Polisi, tena akiwa amefungwa pingu. Matukio haya yanalidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kukosa weledi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuzungumzia ukimya wa Jeshi la Polisi kuhusu matukio mbalimbali ambayo yametokea katika nchi yetu. Mfano, Mheshimiwa Nape Nnauye alitishiwa bastola mchana kweupe; Mheshimiwa Lissu alimiminiwa risasi 38 mchana kweupe Mjini Dodoma, kifo cha mwanafunzi wa NIT ambaye alipigwa risasi wakati wa kampeni za uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni, mauaji ya Kibiti, kupatikana kwa maiti katika fukwe za Coco Beach, lakini mpaka leo hakuna taarifa yoyote kuhusu matukio haya. Namwomba Mheshimiwa Waziri wakati anahitimisha hoja yake atolee ufafanuzi suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa pia kuzungumzia suala la Askari Polisi kuwashikilia watumishi zaidi ya saa 48 bila kuwapeleka Mahakamani. Ni kwa nini Jeshi la Polisi linafanya hivi? Namwomba Mheshimiwa Mwigulu akija atueleze ni sheria gani ambayo inaruhusu Jeshi la Polisi kuwa- detain watuhumiwa zaidi ya saa 48 bila kuwapeleka Mahakamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na suala la utawala bora; naomba kutumia fursa hii kuikumbusha Serikali ya CCM misingi ya utawala bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, Serikali na taasisi za umma kutekeleza majukumu yake kwa kufuata Katiba, Sheria na taratibu zilizowekwa. Taasisi za Serikali kusimamia rasilimali za umma kwa manufaa ya wananchi, kutengeneza mfumo wa kutoa haki bila upendeleo, kulinda demokrasia, kulinda amani, kulinda haki za binadamu, uwajibikaji, uwazi, utawala wa Sheria kufuta chain of command.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, Serikali ya Awamu ya Tano imeonesha upungufu mkubwa katika kufuata misingi ya utawala bora. Kwa mfano, sasa hivi kila kiongozi anatoa matamko kuanzia Rais, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Polisi wa Mikoa, Wakurugenzi bila kufuata misingi ya utawala bora; tena matamko mengine yamekuwa hayatekelezeki na ya kudhalilisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi Wakuu wa Mikoa na Wilaya wamekuwa na mamlaka makubwa mpaka kufikia kuwaweka Wabunge ndani kwa personal interest. Napenda kuishauri Serikali kuzingatia misingi ya utawala bora ili tuweze kulinda amani, demokrasia na kutoa haki sawa kwa kila mwananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kuchangia hotuba ya TAMISEMI; nimesoma hotuba ya TAMISEMI na nimegundua upungufu katika sehemu tatu. Moja, hotuba hii haina jicho la kijinsia; pili, haina mnyambulisho wa data; tatu, haina consistency.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda ukurasa wa 12 wa hotuba hii inaonesha asilimia 49 ya pesa za maendeleo hazikwenda kwenye halmashauri. Napenda Waziri atakapokuja ku-wind up atueleze ni kwa nini pesa hizi hazikwenda wakati Serikali imekusanya mapato kwa asilimia 86.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kuzungumzia suala la vijana na wanawake. Taarifa ya ajira kutoka National Bureau of Statistics inaonesha jumla ya watu 2,334,969 na youth employment rate is 13.7 percent kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2015/2016. Naomba kufahamu mkakati wa Serikali juu ya ajira kwa vijana. Serikali inasema vijana wajiajiri wakati hawana mitaji watajiajiri vipi? Mapato ya ndani ya halmashauri hayatoshi kuwapa vijana asilimia tano na wanawake asilimia tano. Ukiangalia ukurasa wa 23 wa hotuba ya TAMISEMI ni asilimia 15 tu ya vikundi vya vijana na wanawake waliweza kupata fedha hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu; Serikali iwa- guarantee vijana ambao wamemaliza vyuo vikuu ili waweze kupata mikopo kutoka taasisi za fedha ili waweze kujiajiri kwa kutumia vyeti vyao.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kupata fursa na mimi niweze kuchangia Mpango wa Serikali wa mwaka 2019. Mchango wangu umejikita kwa eneo moja kutokana na umuhimu wa eneo hilo na eneo hilo ni kilimo. Lakini kabla sijajikita kwenye mpango ningependa nitoe takwimu za umuhimu wa kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo kinachangia asilimia 70 ya ajira katika nchi yetu, kinachangia fedha za kigeni takribani 1.2 billion USD ambazo ni sawa na asilimia 35 ya pesa zote za kigeni zinazoingia katika nchi yetu. Lakini pia kilimo kinalisha malighafi kwenye viwanda kwa asilimia 65, kilimo kinatuwezesha kupata chakula kwa asilimia 100 katika nchi yetu, lakini pia kilimo kinachangia asilimia 29 ya pato la Taifa. Pamoja na contribution ya kilimo kwenye Taifa hili lakini Serikali ya Chama cha Mapinduzi bado haijaipa sekta ya kilimo kipaumbele, kwa nini nasema hivyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ya mwkaa jana ilikuwa shilingi bilioni 170 pungufu ya shilingi bilioni 44 kutoka kwenye bajeti ya mwaka 2017/2018. Kwa mwaka mmoja tu bajeti ya kilimo ilipunguzwa kwa asilimia 20.8 wakati wenzetu wa Kenya wanaongeza bajeti ya kilimo kutoka asilimia 2.3 kwenda asilimia tisa ya bajeti ya Taifa sisi tunapunguza bajeti ya kilimo kutoka asilimia 0.8 kwenda asilimia 5.2, are we serious kweli tunataka kutengeneza Tanzania ya viwanda? Na tunasema Tanzania ya wanyonge, Serikali ya wanyonge, hivi kuna wanyonge zaidi ya wakulima?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye ukurasa wa tano wa mpango inaonyesha wka mara ya kwanza kwenye historia ya nchi yetu kilimo kilikua kwa asilimia 1.1 mwaka 2016 baada ya Serikali hii kuingia madarakani, mwaka 2015 kilikua kwa asilimia 3.4 lakini bado bajeti ilipunguzwa. Hii inaonesha Serikali hii ni adui wa wakulima kwa maana wame-focus zaidi na kipaumbele imepewa asilimia tano ya watu ambao wanaweza kupanda ndege na kutokomeza, kuwaweka asilimia 70 ya wananchi wa Tanzania wanaotegemea kilimo kwenye wimbi la umasikini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa niende kwenye mpango. Niliamua nisome vitabu vitatu vya mpango ili niweze kuona trend analysis kwenye sekta tu ya kilimo, lakini pia nlitaka nijue ni kwa nini mipango ya hii Serikali haitekelezeki na badaa ya kusoma nilipata majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina kitabu hapa cha mpango 2016/2017, 2017/2018 na hiki cha taarifa ya utekelezaji wa mwaka huu na nili-focus kwenye kilimo tu kwa sababu najua tukiwekeza kwenye kilimo tunakwenda kuwatoa asilimia 70 ya Watanznaia kwenye wimbi la umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa yaani mambo niliyoyaona ni maajabu. Baada ya kusoma ni kwamba Serikali inatekeleza vitu ambavyo haikupanga, ina-report vitu ambavyo haviko kwenye mpango, inaondoa vitu ambavyo vilikuwa kwenye mpango lakini kubwa zaidi hata pesa za kutekeleza hiyo mipango pia hazipo. Ukiangalia implementation ya bajeti ya maendeleo ya mwaka jana imekuwa implemented kwa asilimia 55 tu na asilimia 45 pesa hazikwenda kwenye bajeti ya maendeleo lakini nawashangaa Waheshimiwa Wabunge, tumeacha jukumu letu tulilopewa Kikatiba la kusimamia Serikali lakini jukumu la stewardship lord tulilopewa na wananchi la kuja kuwakilisha wananchi Bungeni, tumebadilisha majukumu yetu badala ya kuisimamia Serikali tunapongeza na kushukuru, kumpongeza Rais, inasikitisha kwa kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikuoneshe vituko vilivyo kwenye mpango kwenye sekta ya kilimo. Mwaka 2016/ 2017 unaambiwa ukurasa wa 70 mpaka 71 zilitengwa shilingi bilioni 4.35 fedha za ndani kuweza kuzalisha mpunga kwa tani 290,000 na sukari tani 150,000 lakini pia kupatikana kwa hati kwa mashamba makubwa kwenye Mkoa wa Katavi, Rukwa, Tabora, Lindi, Kigoma, Ruvuma, kuandaa kanzidata kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi kwenye eneo la Ludewa na Rufiji hiyo ilikuwa mwaka 2016/2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa njoo 2017/2018, hatua iliyofikiwa, kuandaliwa programu ya muda mrefu na mfupi ya upimaji wa ardhi kwa matumizi ya kilimo. Serikali imetoa shamba la ukubwa wa hekta 10,000 lililoko Mkurunge, Bagamoyo kwa Kampuni ya Bakhresa kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo cha miwa na sukari. Ukiangalia hivi vitu hata havikuzungumzwa kwenye mpango, hiyo ndiyo hatua. Kwa hiyo, mna-implement what you didn’t plan. Haya njoo sasa kwenye taarifa ya utekelezaji ni vichekesho, unaambiwa hivi; kwanza hakuna kabisa hata habari ya hilo shamba ya Bakhresa, hakuna implementation status ya hiyo tani 150,000 ya sukari pamoja na tani 290,000 na mashamba ya miwa hayajazungumziwa kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja eneo la pili, tafiti za kilimo mwaka 2016/2017 milioni 854 za fedha za ndani na milioni 53 zilitengwa kwa ajili ya kuleta tani 10 za mbegu za mpunga, kukarabati na kuimarisha vituo 12 vya utafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nenda sasa mwaka 2017/2018, hatua iliyofikiwa ni kuzalisha mbegu 35 mpya za mahindi haikuwepo kabisa kwenye mpango kule wanasema vitu vingine na huku wanasema vitu vingine. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vituo vya utafiti havijazungumziwa kabisa. Kati ya tani 10 ambazo miliahidi kutekeleza ni tani 2.9. Njoo sasa kwenye taarifa ya utekelezaji ni vituko, hakuna vituo vyovyote vilivyofanyiwa utafiti, habari mpya za mbegu hazijazungumziwa kabisa. Hiyo ndiyo Serikali ya CCM ambayo inajua kupanga na kutekeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nishauri kwa haraka haraka, Serikali ijenge uchumi shirikishi ambao unaweza kuhakikisha ukuaji wa kilimo unakuwa sambamba na ukuaji wa pato la Taifa. Ukiangalia kilimo kinakuwakwa asilimia 2.1 wakati pato la Taifa linakua kwa asilimia 7.1 yaani mbingu na ardhi. Ukiangalia viwanda vinakua kwa asilimia 6.8, kilimo asilimia 2.1… (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuchangia mambo machache kwenye hoja hii iliyopo mezani, mahususi nikirejea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuanza na hoja ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu. Bodi hii imeshindwa kutambua wakopaji wake na wako wapi kwa sababu bodi haina mfumo wa kuwatambua ili kupata marejesho yake. Thamani ya deni hilo ni shilingi trilioni 4.6, rejea ripoti ya CAG 2016/2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Elimu imeshindwa ujenzi katika Chuo cha Ualimu cha Ndala licha ya bajeti ya shilingi bilioni 46 kutengwa na wizara. Niombe Serikali ikatekeleze ujenzi wa chuo hicho cha Ndala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa pia kuchangia kuhusu ukaguzi maalum wa Chama cha Walimu (CWT). CAG alifanya ukaguzi maalum CWT na kuanika ubadhilifu mkubwa katika Chama cha Walimu. CWT ilifanya matumizi ya shilingi bilioni 26.8 bila kuzingatia bajeti; pesa hizi zilichepushwa kutoka kwenye matumizi husika na kufanya matumizi mengine. Malipo ya shilingi bilioni 11.5 yalifanyika bila uambatanisho toshelezi. Matumizi hayo hayakuwa na vielelezo kuthibitisha matumizi hayo, hivyo mkaguzi alishindwa kuthibitisha uhalali wa malipo hayo. Malipo ya shilingi bilioni 3.3 yalifanyika bila kuidhinishwa na Katibu Mkuu na mweka hazina wa Chama cha Walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kuzungumzia suala la Tume ya Huduma za Walimu (Fungu 40). Tume hii ilifanya malipo yasiyo ya kawaida, shilingi milioni 721 kulipa posho, overtime na safari hewa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuchangia mambo machache katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Kwanza nianze na suala la uzazi wa mpango. Kuna msemo unasema if you fail to plan you have planned to fail. Ongezeko la watu katika nchi yetu limekuwa likiongezeka kwa asilimia 27 katika nchi yetu. Tanzania inakadiriwa kuwa na watu milioni 150 ifikapo mwaka 2050. Je, kama nchi tumejiandaa kuhudumia ongezeko hilo la watu ukizingatia ongezeko hilo la watu na limited resources tulizonazo?

Mheshimiwa Naibu Spika, nafahamu dhana ya Serikali ya kuongeza matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango kutoka 32% - 45% ifikapo mwaka 2020, pia kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua kutoka vifo 556 - 292 kwa vizazi hadi vifo 100,000, ifikapo mwaka 2020; kupunguza mimba za utotoni toka 27% - 22% ifikapo 2020. Naomba majibu ya Serikali, sasa hivi tumefikia wapi katika malengo tajwa hapo juu ikiwa tumebakiza mwaka mmoja tu kufika mwaka 2020?

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda pia kuzungumzia suala la Community Health Workers (CHWs)au watoa huduma za afya ngazi ya jamii wamekuwa na mchango mkubwa sana katika kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano. CHWs wamekuwa wakitoa elimu kuhusu lishe ya watoto, akina mama wajawazito na kuhamasisha akina mama wajawazito kwenda kujifungulia katika vituo vua afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano hai ni Kijiji cha Uturo Mbarali hakijaripoti kifo cha akina mama kwa zaidi ya miaka mitano kwa sababu wamekuwa wakiwatumia CHWs katika jamii. Nafahamu mpango mkakati wa IV wa Wizara ya Afya umetambua kada hii na umeonesha kwamba mpaka mwaka 2020 itakuwa imeajiri CHWs 5000, lakini mpaka sasa Serikali haijaajiri hata CHW mmoja licha ya service scheme kukamilika mwaka 2018, Desemba.

Mheshimiwa Naibu Spika, Global Funds walitoa pesa kwa ajili ya motisha kwa CHWs na mradi huu unakamilika mwaka 2020, lakini Serikali imegoma kuwatumia CHWs kwa pesa za Global Funds.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa Waziri akija kuhitimisha anijibu maswali yafuatayo:-

(a) Ni lini Serikali itaajiri CHWs kama ilivyoahidi kwenye mkakati wa IV wa Wizara ya Afya?

(b) Pesa zilizotolewa na Global Funds ziko wapi?

(c) Kwa nini Halmashauri zinazotaka kuajiri CHWs kwa makato yao ya ndani zinakatazwa kuajiri?

(d) Ni nini mkakati wa Serikali kupunguza vifo vya akina mama wajawazito hasa wanaojifungulia majumbani ikiwa Serikali haitaki kufanya kazi na kuwatambua CHWs?

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa niwe mchangiaji wa kwanza siku ya leo kwenye bajeti hii iliyoko mezani, Bajeti ya Sekta ya Mifugo na Uvuvi.

Mheshimiwa Spika, sekta ya mifugo na uvuvi, kwangu ni sekta ambayo imenilea, imenikuza na imenisomesha. Kwa hiyo, nitachangia kwa passion sana kwa sababu, sekta hii ni sehemu ya maisha yangu.

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Mifugo na Uvuvi inaajiri takribani asilimia 50 ya watanzania, lakini inachangia asilimia 6.9 ya pato la TTaifa, kuliko hata Sekta ya Madini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kwa masikitiko makubwa, sekta hii imepuuzwa na Serikali ya Awamu ya Tano. Kama Serikali itaamua kuwekeza kwenye sekta ya mifugo, uvuvi pamoja na kilimo, tutakwenda kwenye uchumi wa kati, kwa sababu sekta hizi ni inclusive, ni jumuifu na zinamgusa kila mtanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninachoshangaa ni kwamba, Serikali imeshindwa kuipa sekta hii kipaumbele, imeenda kuwekeza kwenye maeneo ambayo hayana impacts kwa wananchi wengi, na nitakwenda kuthibitisha hili baadaye. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Tano imerudisha sekta ya mifugo na uvuvi miaka mitano, sita nyuma, wanasema, historia nishahidi mzuri sana, na leo nitakwenda kutumia hisitoria ku-substantiate mchango wangu. Hapa nina hotuba za bajeti tatu, nina hotuba ya bajeti ya mwaka 2013/2014 ya Serikali ya Awamu ya Nne, nina hotuba ya mifugo na uvuvi ya mwaka 2018/2019 na nina hotuba ya bajeti pendekezwa ya mwaka huu.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia kwa mfano tu vitu vichache, kwa mfano maduhuli ambayo yalipangwa kukusanywa kwenye bajeti ya mwaka 2018/2019 na Wizara hii ya bilioni 18.5 yalikusanywa mwaka 2014 na Serikali ya Awamu ya Nne, halafu tunasema tunatekeleza, hivi tunatekeleza kitu gani! Mauzo ya mazao ya uvuvi mwaka 2014 yalikuwa dola za kimarekani milioni 832 lakini mwaka 2017 yameshuka mpaka dola za kimarekani milioni 182. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuko serious kweli? Tunataka kuwekeza kwenye mifugo? kwenye uvuvi! Naomba niende kwenye bajeti ya miaka hii mitatu muone tofauti kubwa na muone jinsi gani tumerudi nyuma kwenye sekta hii ya mifugo na uvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka 2013/2014 bajeti yote iliyopitishwa na hili Bunge lako ilikuwa bilioni 54.5, mwaka 2018/ 2019 bajeti yote ilikuwa bilioni 35.3, yaani miaka mitano baadaye, bajeti ya sekta ya mifugo na uvuvi, inapungzwa kwa bilioni 19.2, sawa asilimia 35, ndiyo bajeti ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka 2013/2014, ilikuwa bilioni 13.8, mwaka 2018/2019, ilikuwa bilioni nukta tano, yaani Serikali kwa miaka mitano, imepunguza bajeti ya wafugaji na wavuvi kwa shilingi bilioni 8.4. Mwaka 2013 bajeti ya maendeleo ilitekelezwa kwa asilimia 40, mwaka 2018/2019 ilitekelezwa kwa asilimia 43. Yaani within six years, implementation ya bajeti ya maendeleo ni asilimia tatu, kwa sekta muhimu kama hii ya uvuvi na mifugo! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, halafu tuje hapa tuwasifie, tusifie nini? This is not a praise and worship team, hili ni Bunge, tunatakiwa kuisimamia na kuiwajibisha Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, njoo kwenye bajeti pendekezwa, mwaka 2019/2020, bajeti hii iliyoko mezani, bajeti yote ni shilingi billioni 64.9, baada ya miaka sita Serikali inaongeza only 10 billion, kwenye sekta ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 50 ya watanzania, lakini kwenye bajeti ya maendeleo ni shilingi bilioni 13.8, wakati mwaka 2013/2014, bajeti ya maendeleo ilikuwa bilioni 14. Yaani ongezeko la milioni 200 kwa miaka sita, are we real serious, kweli tunataka kutoka hapa tulipo, sijui tunakwama wapi!

Mheshimiwa Spika, naomba niende kwenye sekta ndogo ya maziwa, mwaka 2013/2014, uzalishaji wa maziwa ulikuwa lita bilioni 1.92, mwaka 2018/2019 ulikuwa bilioni 2.4, ongezeko la asilimia 20 ndani ya miaka mitano kwa maana ya aslimia nne kila mwaka, hakuna efficiency, tukubali tu, hakuna efficiency. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, twende kwenye usindikaji sasa, mwaka 2013, viwanda vyetu vilikuwa na uwezo wa kusindika lita 135,000 kwa siku, mwaka 2018/2019, viwanda vyetu vina uwezo wa kusindika lita za maziwa 154,000 kwa siku, yaani ongezeko la lita 19,000 kila mwaka, halafu tunasema Serikali ya wanyonge, wanyonge gani tunaowazungumzia? Wakati huo viwanda vilikuwa 67, sasa hivi tuna viwanda 91, hapa hatuzungumzii wingi wa viwanda, tunaongelea uwezo wa uzalishaji wa viwanda vyetu, operating capacity, viwanda vya maziwa vina operate kwa asilimia mbili. 98% ya viwanda vyetu vya maziwa vina operate under capacity, hakuna efficiency kwenye viwanda vyetu. Kwa hiyo, siyo hoja kwa na viwanda vingi, hoja ni uwezo wa uzalishaji wa viwanda vyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunaweza tukawa na viwanda vichache, lakini tukaweza kuzalisha zaidi na uzalishaji ukawa na tija. Kwa maana hiyo, asilimia 98 ya mazao ya wafugaji wa nchi hii, hayana soko, na hii imepelekea wafugaji wa nchi hii wameendelea kuwa maskini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niende kwenye suala la sekta ndogo ya nyama, na hapa ningependa nimnukuu Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Mpina, “Tanzania inaagiza tani 2000 za nyama kila mwaka na wakati huo huo inauza nje tani 2000 za nyama” utaona kuwa kiasi cha nyama tunachouza nje kwa bei rahisi kabisa ndicho kiasi hichohicho tunachoagiza kutoka nje kwa bei ya juu. Natamani kuona wawekezaji wengi wakiwekeza katika sekta hii, kwa sababu fursa zilizopo ni kubwa. Mheshimiwa Waziri, hapa issue siyo kuwekeza kwenye viwanda, viwanda tayari tunavyo, issue ni kuhakikisha viwanda vinakuwa na tija, vinakuwa na efficiency na vonaweza ku-operate at full capacity.

Mheshimiwa Spika, na ningependa, with due respect my brother, wakati unakuja kuhitimisha hoja yako, utuambie, ni kwa nini viwanda vyetu vimeendelea ku-operate under capacity, vyote vya nyama na maziwa! Pia, ni kwa nini kama nchi tumeendelea kuagiza mazao ya mifugo, uvuvi kutoka nje, wakati tuna viwanda katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, tuna viwanda 25 vinavyoweza kusindika maziwa katika nchi yetu na uwezo wake kama vingekuwa vinafanya kazi, kwa uwezo halisi kwa maana ya full operating capacity, vingekuwa na uwezo wa kuzalisha lita tani 626,000 za nyama, lakini sasa hivi zinazalisha tani 81,220 za nyama. Kwa hiyo, vinazalisha chini ya uwezo wake kwa asilimia 87.3. sasa halafu tunaongelea kuongeza viwanda, we don’t need quantity, we need quality. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna…

SPIKA: Ahsante sana ni kengele ya pili.

MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Wakala wa Meli Tanzania wa Mwaka 2017
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa ili niweze kuchangia huu Muswada wa The National Shipping Agency of 2017. Nina mambo machache ya kuchangia, lakini kwa kuanza nianze na section number (5) inayoelezea objective of the Corporation:-

Ukisoma hizo objective zote kuanzia (a) mpaka (e) na ukizichanganua unaona ziko objective za aina mbili; kuna business objective kwa maana ya business entity kwa maana ya operator lakini pia kuna regulatory objective kwa maana regulator, kwa hiyo sioni kama ni sahihi hili Shirika kuwa na objectives mbili kwa maana ya operator at the same time regulator. Ni vizuri Serikali ikachagua kimojawapo, either business entity au regulator kwa sababu huwezi ukafanya biashara na wakati huo huo pia unajisimamia, hii inakuwa ni kama self-review. Kwa opinion yangu nashauri hili Shirika liwe msimamizi au regulator na upande wa biashara tuiachie private sector.

Mheshimiwa Spika, baada ya hapo ningependa kwenda section number (7) ambayo inaelezea so mandate ya corporation; hiki kifungu ukikiangalia katika ulimwengu wa free market economy kinawabana wafanyabiashara au private sector ambao tunaamini hii nchi ni ya uchumi na ni wadau muhimu sana katika maendeleo ya nchi yetu. Kwa hiyo, Serikali kufanya biashara pamoja na private sector inaonekana hakutakuwa na fair grounds in terms of competition au fair competition kwa players wote kwa maana ya Serikali na private sector na naona kama Serikali inakwenda ku-cripple private sector kwa hiyo ni vizuri tukaiachia private sector ikafanya biashara.

Mheshimiwa Spika, baada ya hayo, ningependa kuchangia kuhusu Part Five inayoongelea administration and management of the Corporation; kifungu cha 22(1) kinasema, “The Director General of the Corporation who shall be also the Chief Executive Officer responsible to the Board atakuwa na shughuli za management pamoja na administration function” sina tatizo na hicho kifungu na wala pia sina tatizo na kifungu namba mbili (2) ambacho kwamba “DG atakuwa appointed na President”

Mheshimiwa Spika, tukienda kifungu namba (5) kinachosema, “The Director General shall be appointed to serve for the term of five years renewable once on such terms and condition as shall be set in the letter of his appointment or as may be determined by the Board upon approval of the Minister”.

Mheshimiwa Spika, ningeshauri, baada ya appointed to serve for a term of five years, baada ya renewable iwe renewable on yearly basis according to his performance kwa sababu gani? Huwezi ukamwacha mtu akakaa miaka mitano kama ana-perform vibaya, hilo Shirika litakufa. Kwa hiyo, kama atakuwa ana-perform vizuri, contract zitakuwa renewable on yearly basis na tuna mifano mizuri ambayo ipo kwamba mtu anaajiriwa kwa term labda ya three years lakini kila mwaka mkataba wake unakuwa-renewable baada ya performance appraisal kuwa imafanyika. Kwa hiyo ningeshauri iwe hivyo.

Mheshimiwa Spika, kifungu namba saba (7) kinasema section hiyo hiyo 22; “The Director General shall be the Secretary to the Board”. Director General huyu ni mtu ambaye ana-deal na administration lakini pia management functions, sasa kumpa tena kazi ya ukatibu huyu mtu atakuwa overwhelmed na anaweza akashindwa kutimiza majukumu yake na best practice nadhani suala la ukatibu wa board ungekuwa chini ya Chief Legal Council or Director of Legal Affairs.

Mheshimiwa Spika, tukienda kifungu namba 23 kinachosema; “There shall be a Registrar who shall be responsible for maritime environment and safety, security markers of the Corporation”. Namba (2) inasema, “The registrar shall be appointed by the Minister through competitive procedurea taking into account the Public Service Act…” na kuendelea.

Mheshimiwa Spika, tumeona DG anakuwa appointed na President na yuko accountable to the Board wakati Registrar anakuwa appointed na Waziri wa sekta husika au Wizara husika kwa maana hiyo atakuwa responsible or accountable to the Minister sioni harmone kwenye hii organization kati ya Registrar pamoja na DG na ukiangalia DG ndiyo accounting officer au Afisa Masuhuli na yeye ndiyo mwenye resources sasa sioni harmony. Ningeshauri, Registrar awe accountable to the DG na Registrar office iwe ni sehemu ya department kwenye Shirika lakini siyo kitu kingine kama inavyoonyesha kinajitegemea

Mheshimiwa Spika, lakini pia kifugu cha tisa (9) na 10 kimempa DG mamlaka makubwa sana ya kufanya regulation lakini bado anafanya business na kuweza kuzifutia leseni agencies nyingine. Bado sioni kama kuna fairness kwenye hilo na kama kuna fair grounds kwa sababu anaweza kuamua kuzifungia zile agency ili yeye apate business. Kwa hiyo, ni vizuri pia vifungu hivi namba tisa (9) na 10 pia vikawa reviewed, narudia point yangu ya kwanza kwamba hii agency ibaki kuwa regulator ili kuwez ku-regulate other players in the market badala ya kuwa regulator at the same time awe anafanya biashara ambako hakuna fair competition kwenye hilo.

Mheshimiwa Spika, pia kama tunataka ku-empower private sector ni vizuri tukawaachia wafanye biashara na GDP ya nchi zote zilozoendelea zinakuwa accounted na service industry na hii ni service industry, kwa nini tusiwaachie private secror waweze ku-run hii biashara kwa sababu pia ni biashara kubwa sana itaajiri watu wengi lakini pia ita-push economy na zile indicator zote za macro-economy ili kuweza kusaidia uchumi wetu uweze kukua.

Mheshimiwa Spika, lakini pia wanasema ‘experience is the best lesson’, tumeona haya Mashirika ya Serikali in terms of the quality of service hayafanyi vizuri, in terms of efficiency, effectiveness compared to private sector, kwa hiyo ni vizuri tukaiacha private sector ikaweza ku-run hii business.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii.
Muswada wa Sheria ya Usuluhishi wa Mwaka 2020 (Toleo la Kiingereza)
MHE. CATHERINE N. RUGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa ili nami niweze kuchangia Muswada huu wa Usuluhishi au Arbitration Act of 2020. Mchango wangu utajikita zaidi kwenye sehemu ya 13 ya Muswada huu au consequential amendment. Serikali ilileta Muswada huu kwa hati ya dharura ukiambatana na sheria nyingine nne ambazo zilitakiwa zifanyiwe mabadiliko sambamba na Muswada huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati tuliijadili kwa maana ya Arbitration Act lakini kwa eneo hili la sehemu ya 13 ya consequential amendment tuliishauri Serikali iende ikajipange na ilete sheria hizi kwa ajili ya mabadiliko kwa Bunge lijalo kwa kupitia Miscellaneous Amendment ili Bunge liweze kupata fursa ya kuchambua, kujikita, kujadili na kujiridhisha mabadiliko haya yanayoenda kufanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba ni-register masikitiko yangu kwamba Serikali ilipuuza ushauri wa Kamati na wameamua kulazimisha kuleta sehemu ya 13 Bungeni. Leo tukiwa tunajadiliana asubuhi, Serikali ilikuja ku-table kabla hatujafikia consensus. Wazungu wanasema, the devils are in the details. Ukiangalia kifungu cha 100 cha Muswada huu ambacho kinakwenda kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Permanent Natural Resources Wealth and Resources (Permanent and Sovereignty) Act, 2017 ambayo ililetwa 2017, nitaomba nirejee hiki kifungu cha 11 cha sheria hii ambacho marginal note inasema ni prohibition of proceeding foreign court.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma vifungu viwili vinavyoenda kurekebishwa kwenye sheria hii iliyoletwa 2017 ambayo ilikuwa inajikita zaidi kwenye Sheria ya Madini na Makinikia, ilikuwa inasema, “Desputes relating arising from extraction, exploitation or acquisition and use of natural wealth and resources shall be adjudicated by Judicial bodies or other organs established in the United Republic and accordance with laws of Tanzania. Migogoro yote inayohusiana na Maliasili na Utalii litafanywa kwenye ardhi ya Tanzania na vyombo vilivyoanzishwa hapa na kupitia sheria za Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, sasa Serikali imetumia Muswada wa Arbitration kama kichaka cha kwenda kubadilisha Sheria ya Madini ambayo mlikuja hapa kwa mbwembwe na kusema kila kitu kitafanyika humu ndani kwa kutumia Mahakama zetu na sheria zetu. Leo hii mmeamua… ambapo mlisema kila kitu kitafanyika Tanzania. Kwa kifupi, mmerudi na mmekwenda kupiga magoti kwa mabeberu. (Makofi) [Maneno Haya Yameondolewa Kwa Maelekezo ya Kiti]

Mheshimiwa Naibu Spika, tunajua nyuma ya hiki kitu kuna nini. Ni mkataba au ni makubaliano yaliyofanyika na Barrick. Kama ni uongo, wekeni hadharani. Haiwezekani neno moja tu linaenda kuondolewa (establish) na linaenda kubadili muktadha mzima wa Sheria ya Maliasili ya Mwaka 2017. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kifupi, Serikali hatukuona umuhimu wa jambo hili kufanyika kwa udharura huu. Kwanza hatuna Sera ya Arbitration. Sheria iliyopo ina zaidi ya miaka 80 au miongo minane, lakini leo hii hamjafanya gap analysis kujua ni mambo gani ni changamoto kwenye issue za Arbitration ili muweze kuja na sera na then mje na sheria. Ni kwa nini mnakuja mnakuja haraka haraka kwa hati ya dharura kwa mambo ya msingi kama haya, kwa mustakabali mkubwa wa nchi yetu tunapokwenda kuongelea suala la madini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda kwenye Ibara ya 63(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema, “kazi ya Bunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali,” nasi kama Kamati tulifanya hivyo, tuliishauri Serikali lakini Serikali imekaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika aliwahi kusema, “Bunge hili ni la vijana, hatuwezi kukubali vijana makini twende kuwa rubber stamp kwa mambo ya Serikali. Hilo halikubaliki.” Kwa hiyo, naungana na maoni ya Kamati, Serikali irudi iende ikajipange na ije na huu Muswada mkiwa mmejipanga na Wabunge tupate fursa ya kuweza kuuchambua huu Muswada. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niende kifungu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)