Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Godbless Jonathan Lema (23 total)

Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza kabisa na mimi namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba hii ni awamu yangu ya pili kuwa ndani ya Bunge hili na ninawashukuru sana wananchi wa Arusha, kwa sasa nina Madiwani 34 na Chama cha Mapinduzi kina Diwani mmoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili niwashangae wenzangu wapinzani wanapowalaumu sana Serikali ya Chama cha Mapinduzi, sijui wanategemea nini? Mimi sijawahi kutegemea kitu bora kutoka huko upande huo.
Kwa hiyo, ninavyoona wanatarajia kitu bora kutoka upande huo, nawashangaa. Tutakaa tutaongea ili badala ya kuwalaumu sana, waanze kuwaombea, kwa sababu lawama ikizidi inakuwa laana. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, unapoongelea maendeleo ya nchi ni lazima uongelee stability ya nchi. Suala la Zanzibar mnafanya nalo mzaha. Aliongea Mheshimiwa Mbunge mmoja kutoka Chama cha CUF na akasema kwamba demokrasia inapokandamizwa na watu wanaposhuhudia uonevu, wakaona hawawezi kujitetea, ugaidi na ujasusi utazaliwa katika Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, uliomba na mlimpiga miongozo mingi sana, lakini maneno haya alisema Mandela wakati anakwenda jela. Alisema mtu mnyonge anapozalilishwa na kuteswa, hafundishwi uoga, anafundishwa njia ya kutafuta utetezi. Makundi mengi ya ugaidi duniani ukisoma historia, mwende mkasome, yametokana na ukandamizaji uliofanywa na Serikali zilizoko madarakani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mnafanya mzaha na Zanzibar, mtashinda uchaguzi, mtafanya uchaguzi bila uwepo wa vyama vingine, mtapeleka polisi kutoka Bara, mnaweza mkaazima polisi na Kongo, lakini mtakuwa mmeshinda uchaguzi na mtakuwa mmeharibu the next generation ya Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, anayetakiwa kuongoza Zanzibar aliyeshinda uchaguzi siyo Msudani, ni Mtanzania na ameshafanya kazi kubwa katika Taifa hili na ni Makamu Kwanza wa Rais wa Taifa hili, hamtaki kumpa nchi kwa sababu mna bunduki, mna majeshi na mnaweza mkawazuia watu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niliambiwa miaka ya nyuma iliyopita huko na nilisema hapa Bungeni; unaweza ukazini kwa siri, lakini huwezi kuugua UKIMWI kwa siri. Hiki mnachokifanya Zanzibar kitaleta madhara Tanzania Bara huku. Uchaguzi ulikuwa halali na Rais akapatikana. Mnafikiri kumnyang’anya Maalim Seif ushindi wake ni kutunza Muungano, mnachokifanya sasa, ndio mnabomoa Muungano. Hakuna Jeshi lenye nguvu ya kuzuia umma uliochukia kwenye nafsi. Watu wataanza kutafuta mabomu, kutengeneza mabomu, wataanza kufikiria kujilipua. Taifa hili litakuwa mahali pabaya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunavyoongea, Wazungu ambao ni wafadhili wakubwa wa Taifa hili, watalii ambao wanaingia katika Taifa hili, wakizuia watalii kuingia Zanzibar, Arusha itaathirika, Serengeti itaathirika, mtaua uchumi wa nchi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Zanzibar ni suala la msingi sana na tunapojadili Mpango wa Taifa, stability ya Taifa hili ni muhimu kuliko Mpango wenyewe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa juzi mmezima matangazo ya TBC1 na mna mkakati wa kuzima matangazo mengine; mtafanikiwa, mko wengi sana! Mtafanikiwa kila dhambi, lakini mshahara wa dhambi ni mauti. Kila dhambi mnayoipanga mtafanikiwa, lakini mshahara wake ni mauti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashauri Waheshimiwa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi; tunapotengeza Sheria ndani ya Bunge, tunapo-set precedent za nchi yetu ndani ya Bunge, leo nyie ni Mawaziri, watoto wenu hawatakuwa Mawaziri. Leo ninyi mna ndugu ma-IGP, watoto wenu hawatakuwa ma-IGP. Mheshimiwa Mama Mary Nagu alikuwa ni Waziri leo anauliza maswali ya nyongeza. Mtoto wake huko mtaani atakuwa wa kawaida. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mnapotaka kutengeneza Taifa lenye misingi bora, ni vyema ninyi Wabunge mliopo leo, mkajua nchi hii ina kesho, ambapo hamtakuwa na influence. Shangazi zenu hawana influence mlizonazo, wengine hapa mlitokea kwenye matembe, mkaenda university mmekuwa Wabunge. Tunapokaa Bungeni kuongelea Taifa hili, tunaongelea ndugu zetu, jamaa zetu ambao hawana influence tuliyonayo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mnazuia matangazo live! Wananchi wanapoona hawatetewi, watatafuta utetezi! Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania linapokuwa live… (Makofi)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Godbles Lema, umejenga hoja yako, sasa twende kwenye Mpango usaidie nchi. (Kicheko)
MHE. GODBLESS J. LEMA: Huu ndiyo Mpango. Tulia! (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi kuongoea mpango bila kuongea stability ya nchi. Tulia Mzee, tulia!
Mheshimiwa Mwenyekiti, mmezima matangazo hapa ya TBC1, leo wananchi nje hawajui kinachoendelea humu ndani. Ninyi mnafikiri tukiwasema sana nyie, mnafikiri chama chetu ama vyama vya upinzani vinajenga umaarufu, lakini kimsingi kabisa, vyama vingi vimeleta amani katika Taifa hili, kwa sababu ni alternative ya peace. Wananchi wanapoona tunasuguana ndani ya Bunge, wanakuwa na uhakika wa kesho, wanajua wana watetezi na Serikali ya tender.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mmeondoa matangazo, mnafikiri mko salama? Mmeondoa maangazo tukisema tusisike, mnaweza mkafanya kila kitu. Yesu alisema, watu hawa wasipopiga kelele, mawe haya yataimba. (Makofi)
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, huko tunakoelekea watu hawataongea tena, hiki mnachokifanya hamtakifanya tena! Wakishindwa kuandamana, zitaanza assassination; wakishindwa kuandamana, nyumba zitaanza kuchomwa moto. Haki itatafutwa kwa gharama yoyote ile! (Kicheko/Makofi)
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashauri sana, mkikaa humu ndani, nawe ukikaa hapo juu, unajiona kama ni mdogo wake Mungu, mnakandamiza demokrasia, mnaleta polisi humu ndani, mnadhalilisha watu wanaodai haki! Ipo siku itafika! (Makofi)
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tumekuwa ni alternative ya amani. Wanachama wenu wakichukia, wanakuja kwetu. Siku wakichukia wakaona huku hakuna msaada, wataenda porini. Vijana wenu wakichukia… (Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa
muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Katika Kitabu cha Mithali ambacho ameandika Mfalme Suleiman, hii ni sura ya 30 mstari wa 18 mpaka 19 anasema ifuatavyo: “Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu. Naam, kuna manne nisiyoyafahamu. Mwendo wa tai katika hewa, mwendo wa nyoka juu ya mwamba, mwendo wa merikebu katikati ya bahari na mwendo wa mtu pamoja na msichana.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfalme Suleiman angekuwa anaandika, angeandika; “na utaratibu wa uchangiaji wa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi.” Mnaikataa bajeti muda wote wa kuchangia, halafu mwisho mnaunga mkono hoja. Hili jambo pia lingemshangaza Suleiman. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa namwuliza Mheshimiwa Msigwa hapa, hivi sisi tukija upande huo na nyie mkaja upande huu, tukabadilishana Vyama lakini status quo ikabaki hivyo hivyo, mkabaki Mawaziri, Wabunge lakini mkawa CHADEMA na sisi CCM, mngeweza kubadilisha maisha ya Watanzania? Nikapata jibu msingeweza kwa sababu kimsingi tatizo siyo Chama chenu, ni akili zenu. Msingi kabisa, ni attitude. Attitude…
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, basi attitude ni tusi, naliondoa hilo neno “attitude” kwasababu nyie mnasema ni tusi.
Mheshimiwa Mwenyekiti leo tunaongelea habari ya viwanda..
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachopigiwa kelele hapa ni opportunity. Wabunge wote humu wa Upinzani na wa Chama Tawala, wanapigia kelele opportunities ambazo walipaswa kuzi-cease na ndiyo sababu nilipoanza na neno “attitude” mlipaswa kusubiri. Wabunge wote hapa…
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafuta neno “akili.”
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo la viwanda nchi hii na wala Serikali haiwezi kuleta viwanda vyote ambavyo vitaleta transformation katika Taifa hii. Ukienda nchi zote zilizoendelea, transformation ya viwanda imeletwa na private sector. Kwa hiyo, kama private sector ndiyo imeleta transformation ya viwanda, Waheshimiwa Wabunge wanaodai Serikali ya nchi hii lazima ilete viwanda, Wabunge wao ni lazima waanze kujua tofauti ya liability na Assets.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Wabunge wanachaguliwa wapya. Anachaguliwa Mbunge mwezi wa Kumi; mwezi wa Kumi na Mbili ananunua gari ya shilingi milioni 400 halafu full back position ya kuendesha gari ile ni posho ya kikao. Tatizo hapa siyo kiwanda! Gari moja ya thamani ya shilingi milioni 400 ni viwanda nane China.
Kwa hiyo, tunapoongelea suala la transformation ya viwanda siyo Serikali peke yake, ni pamoja na transformation of the attitude. Wananchi kutoka kwenye negative mentality kwenda kwenye positive mentality na hiki ndicho nilikuwa nataka mwelewe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda hivi mnavyosema hapa, havitakuja. Mtaonea Wizara hizi! Riba leo kwenye Commercial Bank ni asilimia 20 mpaka 22. Ukichukua shilingi bilioni moja Benki leo, utalipa riba ya shilingi milioni 220 kwa mwaka, maana yake ni takribani shilingi milioni 20 kila mwezi. Ndiyo sababu wananchi wengi ama watu wengi hawaingii katika mfumo wa investment, wanaenda katika mfumo wa buy and sell kwa sababu kununua kiwanda, kifike, ukijenge, kianze kufanya kazi upate leseni, ni jambo linachukua takribani zaidi ya mwaka mmoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Benki zetu siyo rafiki na urafiki huu unaondoka kwa sababu base rate ya BOT ni asilimia 16, maana yake Benki zote zinaanza kuanzia asilimia 16 kupanda juu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namna pekee ya kufanya transformation ya viwanda katika Taifa hili, ni lazima Wizara ya fedha na BOT waende wakashushe riba kwa watu ambao wanataka kufanya investment kwenye viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, investment ya Viwanda haiwezekani. Leo ukitaka kufungua Kiwanda, unahitaji kwenda kuchukua fedha Benki, utaenda kuweka property yako.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo watu wengi wanakufa na pressure kwa sababu ya riba. Ili viwanda nchi hii vifanikiwe, nendeni mkaongee. Wizara ikaongee na Wizara ya Fedha na Benki Kuu. Riba ya viwanda lazima iwe tofauti na riba nyingine zote katika uwekezaji. Sasa attitude haitawakwaza tena. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti na Mheshimiwa Waziri, kuhusu General Tyre; niliwashauri kwenye Kamati, wakati General Tyre inajengwa pale palikuwa ni pori, leo General Tyre iko katikati ya residential, huku kuna nyumba za PPF, nyuma kuna mtaa wa Lolieni. Niliwaambia njooni tuongee na Halmashauri ya Jiji na mimi na-control lile Jiji, kila kitu ni mimi Kamati ya Mipango Miji ni mimi, Meya ni mimi kila kitu ni mimi. Kwa sababu mnataka shilingi bilioni 68 ili m-take off, mkija Arusha kuliko lile eneo muendelee kulazimisha kuweka kiwanda pale njooni tuwape heka 100 kilometa 20 kutoka Arusha Jiji na lile eneo muende mkatengeneze iwe ni commercial areas, mtengeneze proper residential.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mnawaza mkauza eneo la General Tyre kwa zaidi ya bilioni 30 ya Kitanzania, ikawa ni ubia wenu mkatafuta partner, lakini leo Mheshimiwa nakushauri ukifufua kiwanda cha General Tyre na mitambo iliyopo, tairi moja utauza shilingi milioni 10, ile mitambo ni mitambo ya siku nyingi, inatumia umeme mwingi na umeme wenyewe huu wa kusuasua, matairi yamebadilika, moulding zimebadilika. Leo kuna tairi za waya, pale kuna tairi za nyuzi, ni bora hiyo fedha mkaitumia kufanya research na analysis, mjue ni kitu gani mnataka kufanya kwenye kiwanda kile lengo siyo kufungua kiwanda, je, kiwanda kitakuwa effective? Lengo ni kiwanda kitakuwa effective.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri njoo Arusha tukubaliane tuwatafutie heka 100 nje ya Mji, tupeni lile eneo tuwatafutie shilingi bilioni 30, pale fedha iko! Lakini leo ukiweka kiwanda cha General Tyre pale na usitoe nje ya Mji pale ni residential, barabara ni nyembamba, unaingiaje kupeleka raw material? Unaingiaje kutoa raw material? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nakushauri sana Mheshimiwa Waziri ukitaka kuleta transformation kwa General Tyre lazima uchukue mwelekeo ninaokuambia mimi. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mishahara ya nchi hii ni midogo, hakuna purchasing power. Leo mtu kuingia supermarket ni prestige, leo mtu akionekana anaingia supermarket nchi hii ama akipanda ndege ni issue yaani leo kupanda ndege it’s a dream! Kwa hiyo, ili muweze kutengeneza viwanda na muweze kutengeneza wawekezaji waone kwamba nchi hii unaweza ukawekeza viwanda lazima kuwepo na purchasing power. Purchasing power, number one inakuwa created na mishahara ya Serikali pamoja na private sectors. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ninaomba sana kwamba Serikali kama inataka kuona viwanda vinakuwepo katika Taifa hili ni lazima Serikali ifikirie kuongeza mishahara ya wafanyakazi. Lazima Serikali ifikirie kuongeza mishahara bora ya wafanyakazi ili kuwepo na purchasing power, siyo kupunguza kama ambavyo mnafikiria sasa, mtu wa shilingi milioni 30 apewe shilingi milioni 15. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Lukuvi hapa kila siku anafuta title na anatangaza! Mnafikiri mnasaidia nchi, msiwanyang‟anye watu ardhi mkatangaza. Mwekezaji mnayemuita kuja kuwekeza kwenye kiwanda halafu anasikia kuna mtu amenyang‟anywa heka 3,000 huyo mtu atarudia Dubai kama alikuwa ana-connect ndege. Msinyang‟anye watu ardhi. Hata kama mkinyang‟anya watu ardhi, imekaa muda mrefu msifanye publicity kwa sababu ina threat wawekezaji wanaotaka kuja kuwekeza. Huwezi kuwekeza kwenye viwanda kama huna ardhi. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo dakika tatu zilikuwa zimebaki kwa sababu ya zile kelele kelele.
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu TRA. Wafanyabiashara wa nchi hii wakiwaona TRA wanawaogopa kama wameona Field Force. Ili wafanyabiashara wawe na malengo ya kufikiria maono makubwa ni lazima TRA ijenge attitude ya kuwa na urafiki na wafanyabiashara na siyo wakali kwa wafanyabiashara. Viwanda na Biashara ni Wizara ambayo imesambaa sana, kilimo kiko ndani yake, Wizara ya Fedha iko ndani yake, kila kitu. Lakini hawa ili waweze kufanikiwa lazima muwape nguvu zaidi ya kufanya connectivity na hizi Wizara nyingine kwa ajili ya harmonize shughuli zao za kila siku. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Mazingira leo anaweza akatoka hapa ama Naibu Waziri wa Mazingira akaenda Tanga akafunga kiwanda kwa sababu tu anataka aonekane kwenye tv bila kum-consult Waziri wa Viwanda na Biashara
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Taifa hili kujadili masuala yote yanayohusu mipango ya maendeleo bila kujadili stability na demokrasia muhimu katika Taifa hili, kinachojadiliwa hapa kilicholetwa na Dkt. Mpango hata kama kingekuwa ni sawa kwa asilimia 100 lakini kwa Taifa ambalo hakuna utawala bora, kwa Taifa ambalo demokrasia imeminywa, kwa Taifa ambalo vyama vya siasa haviruhusiwi kufanya shughuli zake mpaka mwaka 2020, mipango hii ina-create instability katika Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, siku za nyuma tumekuwa tukisema kwamba nchi hii haitawaliki na tafsiri ya upande wa pili ikawa ni kwamba tunasema kwamba nchi hii haitawaliki kwa sababu tumepanga kuingia barabarani kufanya maandamano, kuvuruga Taifa. Maana ya nchi kutokutawalika ni viongozi walioko madarakani sasa ambao ndiyo wanaotawala Taifa hili kushindwa kabisa kujua na ku-predict future ya Taifa hili itakuwaje incase kama watashindwa kusimamia utawala bora na demokrasia katika Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaongelea Mpango ambao una lengo la ku-attract investors. Mwekezaji yeyote mwenye akili hawezi kuleta mtaji kwenye Taifa ambalo limeua vyama vya siasa kufanya kazi zake za siasa. Maana yake ni nini? Lengo la kuua vyama vya upinzani likifanikiwa vilevile litakwenda kuuwa chama tawala chenyewe. Litauaje chama tawala? Ikifika mahali vyama vya upinzani haviwezi kuongea chama hicho ambacho kimefanikisha mpango huo kitazuia watu wake wasiongee na ndiyo sababu baada ya kikao cha asubuhi Wabunge wa CCM wengi walikuwa positive juu ya jambo hili kiliitwa kikao cha party caucus kwenda kuwaelekeza Wabunge namna gani ya kuja kuongea ndani ya Bunge hili badala ya kuongea ukweli ni kubeba Mawaziri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa hili linapoelekea na mambo yote yanayopangwa hapa hayatatekelezaka bila utawala bora. Kwa bahati mbaya sana tunaongea Mpango wa Maendeleo wa Taifa hili katika Taifa ambalo Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi Watendaji hawana confidence. Hakuna mfanyakazi wa Serikali nchi hii ana ujasiri wa kwenda asubuhi kazini ikafika jioni akajua bado yupo kazini. Jambo hilo limeleta wasiwasi na kwa sababu imeleta wasiwasi kwa Wakurugenzi, Makatibu Wakuu na kwa Mawaziri wengine hawajui ni wakati gani watatumbuliwa na ni kwa vigezo gani watatumbuliwa, kwa hiyo imekosekana creativity ndani ya ofisi za kazi na hakuna innovation. Ndiyo maana Bunge lenyewe likikosa pesa badala ya kwenda ku-push pesa zipatikane, Bunge ambalo lilisema lina fedha ya ziada likatoa fedha za madawati likapeleka kwa Rais Bunge hilo leo limeshindwa kuchapisha nakala zake. Sasa unajiuliza hili Bunge lililokuwa na ziada ya fedha likachukua fedha ikampelekea Rais ya madawati mbona leo imeshindwa kuwa na mpango wa kununua hata tonner ya kufanya kazi zake ndani ya Bunge hili? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuongelea mpango bila kuongelea stability ya Taifa hili, demokrasia, ustawi wa jamii katika Taifa hili mipango hii hata kama ni bora kwa kiasi gani haitafanikiwa. Leo tulimuona Mheshimiwa Rais alikwenda kufungua kiwanda cha Bakhresa, akasema tena nimefurahi sana na zile sukari zilizokuwa zimekamatwa Waziri nendeni mkampe. Unajiuliza sasa kama sukari zilikuwa zimekamatwa kinyume na utaratibu kwa nini zilizuiwa na kama zilikuwa zimekamatwa ndani ya utaratibu kwa nini zilizuiwa mpaka Rais afurahishwe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo kwa sababu tukisema Waheshimiwa viongozi ambao ni sisi pamoja na huko nje tumekuwa na hofu kubwa dhidi ya kusema ukweli, dhidi ya kupigania ukweli, leo kila mtu ni muongo na woga ni njia anayotumia shetani kutenda miujiza na imani ni njia anayotumia Mungu kutenda muujiza. Kwa uoga huu ambapo watu hawawezi kuamua, kwa uoga huu hakuna mtu anakwenda kazini akajua jioni atabaki kuwa mfanyakazi, ndiyo maana Rais alisema watu wanaficha pesa, ni kweli kauli yake ilikuwa na uhalali kwa asilimia kadhaa. Mimi kama sina confidence ya kwamba nitakuwa kazini kesho maana yake itakuja ku-minimize gharama zangu za maisha. Mimi niki-minimize gharama zangu za maisha maana yake ni kwamba nakosa spending confidence kwenye jamii ndiyo sababu unaona biashara zinakufa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye kikao cha kodi cha TRA cha Wilaya nilimuuliza mtu wa kodi Arusha peke yake hizi kampuni za biashara ya kati zaidi ya 48 zimeandika barua ya ku-close business itakapofika Novemba mpaka Disemba mwaka huu. Sasa badala ya kumsaidia Rais na kumwambia ukweli na siyo mambo yote anafanya Rais Magufuli ni mabaya, ana courage ambayo watu wengi hawana, lakini courage hiyo ikikosa hekima, maelekezo na ushauri Rais anakuwa kama Mungu, anakuwa yeye ndiyo kila kitu, ndiyo Pay Master General, ndiyo Waziri wa kila kitu, anakwenda kufumania, kila kitu anafanya. Hii imesababishwa na ninyi kutokumwambia Rais ukweli, Rais amekuwa polisi. Imefika mahali hata mtu mdogo kwenye Kamati akiongea Rais anapiga simu mwenyewe, Rais anatoa maelekezo mwenyewe mpaka kwa ma-RPC, hofu kubwa imejengwa katika Taifa hili.
KUHUSU UTARATIBU...
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Namheshimu sana Mheshimiwa Jenista alikuwa Mwenyekiti wangu wa Kamati siku za nyuma, lakini nashukuru kwamba amekiri kwamba Mpango siyo mzuri na kwamba Mpango kutokuwa mzuri siyo intervention ya Mheshimiwa Rais.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hiki kitu tunachokisema ndicho ambacho mkiniambia ninyamaze sitanyamaza. Hili ni Bunge na kazi ya Bunge ni kushauri Serikali, inapofika mahali Bunge linashindwa kushauri Serikali ndiyo hiyo hofu aliyonayo, niliposema Rais ana courage ya kufanya maamuzi mazito na magumu mlipiga makofi, tukisema Rais anakosea hatumuudhi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimesema nimeona maono kwenye maombi, leo nimepelekwa polisi na sasa hivi navyoongea nimeambiwa maelezo uliyotoa hayatakiwi, polisi wa Arusha wanakuja kunichukua kwamba nimeona maono makubwa kwa nini sijalala hata ndani nimepata bail kabla sijawekwa lockup, haya mambo katika Taifa hili yanakwaza. Sasa ninyi ambao mnamuogopa, mimi siogopi, najua Rais ana nguvu, najua hii Serikali ina Usalama wa Taifa, Mimi nikitaka kufa leo nakufa asubuhi I have no weapon lakini hatutaacha kusema ukweli for the sake of this country, hii nchi inakufa, imepandikizwa hofu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, amesema hapa Mheshimiwa Mbunge mmoja kwamba Wakuu wa Mikoa na ma-DC na Wakuu wa Mikoa wanaweka watu ndani saa 48. Kuna mambo mengine tena mkiongea huko tutasema na Mawaziri tunaongea nao mambo haya nayoongea mimi tunawakilisha sisi, lakini haya ni mawazo ya kwenu mnayotuambia sisi, hatuwezi kuendelea na Taifa lenye hofu kwa kiwango hiki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mikoani OC hazijakwenda, hakuna fedha, mambo yanakuwa ni magumu, biashara zinakufa sisi ni wafanyabiashara. Utalii hapa mmempa Profesa ambaye Kinana alimuita mzigo some days ago, leo amekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Novemba peke yake utalii umeanguka kwa asilimia 48. TRA wamekuwa kama polisi, kontena la futi 40 lililokuwa linakadiriwa shilingi milioni 18 hadi 20 wakati wa Awamu ya Nne leo ni shilingi milioni 35 mpaka shilingi milioni 40. Wananchi wakiona TRA wanaona kama wameona wanajeshi kutoka Sudan. Hakuna friendliness kati ya walipa kodi na wanaotoza kodi. TRA wamejisifu wanakusanya kodi kwa muda mrefu, Mheshimiwa walikuwa wanakusanya arrears, leo kuna makampuni yameambiwa yalipe kodi ya miezi sita mbele watakuja kurekebisha baadaye. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Taifa linayumba, hali inakwenda vibaya, mitaani hakuna fedha, Tanzanite imeanguka kwa asilimia 40, utalii umeanguka kwa asilimia 48 kwa mwezi Novemba. Leo watu wanaopita Serengeti na Ngorongoro hata boda boda akipita mnamuweka kwenye database as if ni mtalii amepita. Mheshimiwa Maghembe akienda aka-print anakuja anasema watalii wameingia milioni moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mliongeza VAT na haya mambo alisema Mbunge hapa, mmekaa na Kenya na Uganda mkakubaliana pamoja, tathmini waliotumia watu wanaoshughulika na mambo ya uchumi ni kwamba Kenya International Airport imekuwa listed kama sehemu hatari ya utalii. Kenya juzi wakamleta mmiliki wa facebook wakamtembeza nchi nzima, ana wafuasi zaidi ya mamilioni ya watu, Kenya utalii unakua, Arusha hoteli zinauzwa, hakuna biashara kampuni zinafungwa, hoteli zinauzwa hata wateja hakuna benki zinafunga. Ukienda leo kwenye DSE, CRDB hali siyo nzuri, Twiga Bancorp imekabidhiwa kwa BOT, uchumi unakwenda hivi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haya mambo kwenu ni mabaya ni mabaya kwa manufaa ya nchi hii. Ule UKUTA tuliosema tunautangaza kama hamtarekebisha mfumo wa kiuchumi na kiutawala sisi hatutaingia barabarani ila iko siku mtatuomba tuwaambie watu warudi nyumbani hali itakuwa ni mbaya sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Taifa hili Rais hasafiri kwenda kutafuta partners. Leo amekuja hapa Mfalme wa Morocco juzi kaenda Zanzibar kapiga pensi na tisheti yake ina ganja, ina bangi hapa kifuani huyu, ndiye mwekezaji…
Mheshimiwa hujaona wewe.
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ulinde dakika zangu ambazo Mheshimiwa Jenista alinipotezea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni Mfalme na lile jani la mzaituni ambalo linatumiwa na vijana wengi sana wa mjini. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nachosema ni nini? Nachotaka Bunge hili lielewe ni kwamba kazi ya Bunge hili ni kuisaidia Serikali maana yake ni kwamba Serikali hii itayumba, kumwambia Rais ukweli siyo kumdharau, kumwambia unakosea siyo kumdharau. Mfalme ambaye haambiwi ukweli siku akishtuka mlikuwa mnamdanganya na hamumuambii ukweli atafukuza wote kazi. Kwa sababu huko tunakoenda atashtuka na atauliza kwa nini sikuambiwa ukweli kuna jambo kama hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema Taifa kama hili ambalo limejaa hofu na wasiwasi ambapo hakuna mtu anayejua kazini atakuwepo mpaka kesho ama kesho kutwa ni Taifa ambalo limekosa creativity na innovation.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwanza kabisa niipongeze kwa nguvu zote hotuba yetu ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ni hotuba muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikipigia kelele sana habari ya viwanda lakini katika bajeti inayoishia kati ya shilingi bilioni 42.1, Serikali ilipeleka shilingi bilioni 7.6 asilimia 18 tu. Ndiyo maana Mheshimiwa Mwijage anavyosema cherehani nne ni viwanda halafu watu wakamshangaa mimi nawashangaa wanaomshangaa, ni ukweli viwanda vya Serikali ya awamu hii ni cherehani nne. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ndiyo agenda kubwa ya Serikali ya Awamu ya Tano, viwanda, viwanda, viwanda, kati ya shilingi billioni 42 mnapeleka bilioni saba, asilimia 18. Hamtaweza ku-transform nchi hii ili iende katika kuwa Taifa la viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye maji, maji ni biashara, najiuliza kwa nini nchi hii haijawahi kuona maji ni biashara, tena maji ni biashara ambayo haihitaji matangazo, maji ni biashara ambapo kila mtu anahitaji maji. Mahitaji namba moja ya binadamu anayeishi ni maji. Maana yake mmeshindwa ku-connect pipe, mmeshindwa ku-connect vyanzo na kuweka mita Serikali ikusanye fedha kutoka kwenye maji. Kama mmeshindwa kuona maji ni biashara cherehani nne lazima iwe ni viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maji shilingi bilioni 33 ambayo walikuwa wapeleke wamepeleka shilingi bilioni 2.9 asilimia 8.4. Ukienda kwenye kilimo na mifugo ambayo ni uti wa mgongo unaajiri zaidi ya asilimia 80 ya Taifa hili fedha iliyokuwa inapaswa kupelekwa ni shilingi bilioni 101, wamepeleka shilingi bilioni 3.3 sawasawa na asilimia 3.31. Waheshimwa sio rahisi kukiri kwamba mmechoka, sio rahisi kabisa, lakini Waheshimiwa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi kazi yenu siyo kuitetea Serikali ni kuisaidia Serikali ifikie malengo muhimu ya Taifa letu. Leo kama kwenye kilimo kati ya shilingi bilioni 100 wanapeleka shilingi bilioni 3 hiyo tansformation ya agriculture itatoka wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye mazingira kwanza wamepanga hela ndogo kabisa, wamepanga shilingi bilioni
10.9. Leo ukiongelea tishio lingine la ulimwengu katika vizazi vinavyokuja ni mazingira. Mazingira ambayo yalipaswa kutengewa fedha nyingi kama ambavyo Jeshi la Ulinzi linatengewa. Leo Mheshimiwa January wamempa shilingi bilioni 10 halafu wakampelekea shilingi bilioni 1.2 sawa na asilimia 11.3, maana yake wao ambao wanasema wanajenga amani na imani ya kizazi kinachokuja kama hawawezi kuona mazingira ni jambo muhimu, kama hawawezi kuona mazingira ndiyo yata-sustain future za watoto wenu maana yake ni kwamba hawajui wanachokifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo ni very seriously na Mheshimiwa Dkt. Mpango haya mambo lazima ayaelewe. Leo wanatoa makandarasi wa barabara, mimi niliongea na Mheshimiwa January nikamwambia habari ya mazingira ni habari sensitive na kwenye hotuba yangu ya Wizara ya Mambo ya Ndani niliiweka, nikasema tishio lingine la amani ya Taifa hili ni uharibifu wa mazingira kwa sababu yatakuja kusababisha njaa kali sana tunakoenda na Bob Marley alisema mtu mwenye njaa ni mtu mwenye hasira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara zinajengwa, makandarasi wanaojenga barabara kuanzia sasa wapewe na contract ya kupanda miti. Wakati wanaendelea kujenga urefu wa barabara wapande miti na maji wanayojengea barabara hayo maji wajinyweshee miti. Mti ukiumwagia kwa mwaka mmoja huo mti hauhitaji tena kumwagiwa utakuwa umeota wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba nirudi kwenye mambo ya msingi. Mheshimiwa Dkt. Mpango, kauli zao wanazoongea katika jamii zimefanya wafanyabiashara wamerudi nyuma. Leo hawatangazi tena mapato ya TRA kwa sababu wanajua nini kinaendelea. Ikiendelea hivi mwezi unaokuja Taifa hili litashindwa kulipa mishahara. Lugha za viongozi wa juu ni tishio kwa usalama wa uchumi wa Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba yetu imesema, leo wafanyabiashara hawana amani. Mheshimiwa Mpango amshauri Mheshimiwa Rais na hao watu wa TAKUKURU hii biashara wanapita Mbezi wanaona nyumba nzuri, wanachukua plot namba, wanakwenda kuanza kutishia watu, watu watahamisha pesa. Wakati Rais anasema fedha imehamishwa ilikuwa haijahamishwa lakini sasa ninavyokwambia watu wanahamisha fedha katika Taifa hili kwa sababu mazingira ya investment yamekuwa ni magumu, vitisho vimekuwa ni vingi, Wakuu wa Mikoa na ma-DC wanajiita ni Marais wa Mikoa, ni Marais wa Wilaya. Kila wakienda kutishia wafanyabiashara wanasema kuna maelekezo kutoka juu. Wafanyabishara wamevunjika moyo, wafanyabiashara wanaogopa kufanya investment kwa sababu ya kauli za viongozi, kauli za viongozi zinaua morale na Mheshimwa Mpango anafahamu uchumi ni confidence, kama huna confidence na Taifa, huna confidence na maisha yako mambo yatakuwa ni mabaya sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ukienda magereza watu wote wenye fedha kwenye akaunti mbalimbali wanahojiwa na Polisi na TAKUKURU, wanatishiwa kupewa money laundering. Mfumo wenu ambapo nyie mlikuwa watawala uliruhusu hata mtu kununua round about. Nchi hii miaka iliyopita na hata sasa hata ungetaka kununua round about, hata ungetaka uuziwe Ikulu miaka iliyopita ungeuziwa. Ni Serikali hii ilishawahi kutaka kuuza Mahakama ya Rufaa iwe parking ya Kempinski. Kwa uchumi ulivyoyumba …


T A A R I F A . . . .

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilindie dakika zangu, tuendelee na mambo ya msingi, nilisema toka mwanzo mnamjua huyu kijana. (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachosema siku za nyuma wote mnakubaliana na ndiyo sababu mnauona huu ukali wa Rais kwamba mfumo haukuwa rasmi sana kuzuia baadhi ya mambo. Hawa watu muwa-engage kwenye uchumi, msiwa-disengage. Kama mnafikiri kuna hela chafu zilitoka ndani ya mfumo wa nchi hii, ni muhimu mkafanya engagement na siyo disengagement.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Putin wakati anaingia madarakani alikuta hali kama hii Russia, lakini wale wote ambao walikuwa wamepata hela katika mfumo usiokuwa rasmi hela ambazo zilikwepa kodi, wakiwaza kuwatisha, wakawapa kesi mbalimbali kama money laundering, watahamisha fedha katika njia isiyokuwa stahili na wataogopa kufanya investment katika Taifa hili, watapoteza fedha nyingi sana kupita kiasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe sana Mheshimiwa Mpango hali inavyoendelea sasa, hali ni mbaya kupita kiasi. Namna pekee ya kusaidia uchumi wa Taifa hili namba moja ni lazima wafanyabiashara warudi kwenye confidence waliyokuwa nayo. Leo watu hawalipwi fedha, biashara za ndani hazilipwi fedha. Hapo Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu amekuwa ndiyo Governor, tunajua! Haya mambo tunaambiwa kutoka huko huko kwenye corridor zenu, Katibu Mkuu ndiyo kila kitu. Fedha hazilipwi, mambo hayaendi na kama fedha hazilipwi, Mheshimiwa Mpango yeye ni mtaalam wa uchumi, ili uchumi uweze kupanda lazima watu wa- spend kama watu hawawezi ku-spend watapata wapi kodi? Leo nenda hata kwenye mahoteli hapa Dodoma, pamoja na kwamba Wizara nyingi zimehamishia makazi hapa watu hawana uwezo wa kufanya purchasing, watu hawawezi kununua, hoteli zinafungwa, biashara zinafungwa, watu wanahama kwa sababu wamekosa confidence ya kufanya investment. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana, Mheshimiwa Mpango namwomba sana aelewe confidence ni muhimu katika investment katika Taifa. Leo TRA wamekuwa kama polisi, ukimuona mtu wa TRA ni hatari. Leo TRA wanakwenda kukusanya kodi wakiwa na Usalama wa Taifa na TAKUKURU. Nawahakikishia, hawatajenga uchumi kwa ukali wanaou- pose katika society. Watajenga uchumi kwa wanasiasa ambaye ni pamoja na Rais, kujenga mahusiano mazuri na kuwapa confidence wafanyabiashara. Bakhresa alikuwa anaondoka nchi hii, wakaenda wakampa eneo la bure ili abaki, wanaoondoka ni wengi. Shares za DSE Mheshimiwa Mpango zinaporomoka mpaka kwa asilimia 90, Serikali imekaa kimya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba sana Waziri afanye bidii ya namna yoyote ile arudishe confidence ya wafanyabiashara. Wakati tunawaambia bandarini meli haziji walisema bora zisije, wakaambiwa na TATOA kwamba truck zimepungua kwa asilimia 80, wakasema bora zipungue.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namalizia, naomba dakika mbili za yule kijana aliyekuwa amenipotezea kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie kwa hotuba ya Mheshimiwa Mpango mwenyewe, matumizi kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa mwaka 2016. Kati ya shilingi bilioni 791 zilizoidhinishwa kutumika katika Mafungu yote tisa jumla ya shilingi bilioni 323 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 68 ni fedha za nje. Hadi kufikia Machi, jumla ya shilingi bilioni 18 zimetumika. Kati ya fedha hizo shilingi bilioni moja ni fedha za ndani, shilingi bilioni 17 ndiyo fedha za nje. Sasa hizi fedha za nje bado hata hao Wazungu wanaendelea kuwazingua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha muhimu ambacho ningependa nisisitize kwenye mchango wangu confidence ya wafanyabiashara imepotea, vitisho kwa wafanyabiashara zimekuwa nyingi, wataharibu na kuua uchumi kwa sababu ya sifa na kiki ambazo hazina msingi.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Nitaongea mambo serious, naomba wale watu wenu ambao mmewapanga kwa taarifa waniache nisikilizwe na Serikali ili muweze kulisaidia Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli usiopingika kwamba mazingira ya kibiashara Tanzania yamekuwa magumu sana. Mfanyabiashara yeyote ili aweze kuwekeza anahitaji kitu kinachoitwa confidence. Katika Taifa hili na nimekuwa nikisema mara nyingi na nimemwambia hata personal Mheshimiwa Mpango, mitaji inayohama na watu ambao wana-reallocate biashara zao katika mataifa mengine ya jirani, ukiniambia nikutajie kwa namba makampuni ambayo yanaondoka ni mengi sana. Huwezi kujenga uchumi wa taifa bila kuimarisha private sector. Kiungo muhimu kabisa katika taifa ni private sector. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo katika Jimbo langu la Arusha Mjini kwenye kikao cha kodi ambacho tulikaa mwezi huu ulioisha, watu walio-register kufunga biashara walikuwa ni 650. Ukifanya utafiti wote hawa kitu kinachowasabishia wafunge biashara ni ujasiri katika kuwekeza katika taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hapa zinakuja takwimu za uongo juu ya ukuaji wa uchumi lakini wote ni mashuhuda na wewe ni shuhuda kwa sababu ni Mbunge wa Jimbo la Mjini kabisa Dar es Salaam ya kwamba purchasing power ya Watanzania ime-decline katika kiwango cha hali ya juu. Kwa bahati mbaya sana mnapokuja humu ndani kuongelea inflation kwamba imeshuka mnashindwa kutofautisha inflation na kuanguka kwa soko. Kinachoendelea mitaani ama kinachoendelea katika biashara za bidhaa ni kwamba nguvu ya manunuzi imeshuka na kwa sababu nguvu ya manunuzi imeshuka maana yake ni kwamba watu wanashusha bei bidhaa ili angalau waweze kuuza vitu vyao waepuke hasara ya moja kwa moja sasa huku mkija mnasema ni inflation imeshuka. (Makofi)

T A A R I F A

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, twende kwenye Sera ya Viwanda. Bunge lililopita nilisema hapa kwamba viwanda havijengwi kwa kauli mbiu vinajengwa kwa mazingira wezeshi na mazingira hayo wezeshi wanafanywa na Serikali kwa watu. Leo Sera yenu ya Viwanda 100 kila Mkoa nikiomba Bunge hili Mheshimiwa Waziri aoneshe viwanda viwili, hamuwezi kuonesha. Unajiuliza Serikali hii ambayo inapigia kelele viwanda, inakwenda kupunguza bajeti ya kilimo na wakati kilimo ndiyo malighafi ya viwanda, unajiuliza hawa watu wako serious na viwanda ama ni kelele tu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini viwanda vinasababishwa na demand, hakuna Mtanzania aliyepiga kelele spirit zitengenezwe, pombe aina za spirit zimetengenewa kwa sababu ya demand. Kwa hiyo, ili viwanda viweze kutengenezwa, ili traders waweze kufika kwenye hatua ya kuona viwanda ni vitu muhimu kinachopaswa kufanyika ni watu wawe na mazingira mazuri, uchumi ukue, mishahara bora, kuwepo na purchasing power ili nguvu ya manunuzi ikawaambie wafanyabiashara kwamba kwa hali hii sasa mimi naona sihitaji kuagiza tomato kutoka India nahitaji kuwa na kiwanda cha tomato Iringa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mazingira ya biashara yanatengenezwa na hali nzuri (harmonization) pamoja na demand na hiyo demand wa kwanza kuitengeza ni Serikali. Sasa Serikali yenu imeua workshop, Serikali yenu inawatanzama wafanyabiashara kama maadui, ma-DC na Wakuu wa Mikoa wanaumiza wafanyabiashara, wafanyabiashara wanawekwa ndani. Mheshimiwa Lukuvi kila anapokwenda ananyang’anya watu mashamba, Sheria na Sera ya Ardhi ni mbovu, leo nani anakuja kuwekeza Tanzania mahali ambapo Sheria ya Ardhi inasema ardhi ni mali ya Serikali. Hivi ni nani leo atakuja kufanya investment ya dola bilioni 50 …

WABUNGE FULANI: Aaaaaa.

T A A R I F A

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ni tatizo kubwa sana kuwa na viongozi wanaokuja ndani ya Bunge wakiwa wamelewa, ni tatizo kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana unilindie muda wangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nasema ukiangalia namna Taifa linavyoenda sasa, anzia ma-DC na ma-RC na wote ninyi Waheshimiwa viongozi hapa ni mashuhuda wa behavior za ma-DC na ma-RC kwa wafanyabiashara, hiyo sasa imesababisha watu na viwanda kuondoka. Nilisema katika Bunge hili utajiri ni prestige, kama mimi nakuwa na fedha halafu fedha yangu inakuwa ni adhabu maana yake nitatafuta mahali ambako nina amani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee General Tyre ambayo Kamati yetu imefanya conclusion vizuri sana. General Tyre toka imefungwa ni miaka mingi sana. Nimekuwa kwenye Kamati wakati wa Bunge la Mheshimiwa Makinda, tukaongelea kuhusu General Tyre, leo tunavyoongea General Tyre bado haijafunguliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, demand ya tairi nchi hii ni kubwa katika kiwango ambacho hatuhitaji kiwanda cha matairi Arusha peke yake, tunahitaji viwanda vya matairi zaidi ya viwanda hata kumi. Leo tairi nchi hii zinatoka China, Taiwan, Japan, Marekani na Ujerumani. Hii demand yote ya matairi ndani ya nchi, nchi hii ingekuwa serious, kiwanda cha matairi kisingekuwa mpaka leo hakipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumetoa ushauri kwenye Kamati pale kilipo kiwanda cha General Tyre ni katikati ya makazi, ni elite area, ni karibu heka 70, ukiweza kuuza heka moja pale ni karibu shilingi milioni 300 ama shilingi milioni 400 kwa mnada kwa sababu ni eneo prime. Maana yake ni nini? General Tyre ukiithamanisha kuwa pesa leo pale katikati Arusha ni zaidi ya shilingi bilioni 28 mpaka bilioni 30. Kiwanda cha matairi hakihitaji dola milioni 15 au 20 kuanza. Maana yake ni nini? Mtaji ni eneo lile kuligeuza kuwa pesa, nendeni kwenye maeneo ya EPZ yaliyoko katika Mkoa wa Arusha chukue zaidi ya heka 500 au 100 tafuteni mwekezaji atawakuta na ardhi na pesa, kiwanda tayari kitafunguliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa bahati mbaya huku watu mme-operate manual, watu huku mna-operate kwa woga, mkiingia kwenye vikao mnashindwa kuongea mmekuwa waoga, mmepandikizwa hofu, mnashindwa kuwaza kisasa, mnashindwa kuwaza kibiashara. Ndiyo maana leo hata maana ya broker kuwa katika biashara mmeshindwa kujua. Mnashindwa kuwawezesha ma-broker kwa kuwapa leseni, mnashindwa kuwarasimisha ma-broker kuwapa mizani, leo mnakwenda kutafuta broker Kenya! Ni kijana mmoja kutoka Kenya ana kampuni yake ya thamani ya dola 1,000 za Kimarekani, amevaa suti, amekuja na caravan na wapambe Mawaziri wote mmekimbilia Arusha kwenda kusaini mkataba na broker Kangombo. Kangombo kutoka Kenya amekuwa wa maana kweli kwa sababu tu amekuja suti na private jet, Mawaziri wote mkaacha kazi mnapigwa na style, kwa sababu hamuwazi kimkakati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Watanzania wanafikiria ninyi mnaweza mkawa solution ya nchi hii, waone mawazo yenu na waone michango yenu. Hata angalia dressing style tu ya Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara utajua kabisa huyu hawezi kuleta transformation yoyote katika uchumi wa Taifa hili. (Makofi/Kicheko) [Maneno Haya Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nachosema ni nini? Nachosema ni kwamba biashara haihitaji nguvu, biashara haimhitaji Sirro, uchumi haumuhitaji Sirro, uchumi hauhitaji nguvu. Maduka ya Forex Arusha yamefungwa mpaka leo. Hivi kweli ninyi mna Usalama wa Taifa unawambia...

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa
Mwenyekiti, kuhusu utaratibu.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, leo...

KUHUSU UTARATIBU

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hata huyu anayemalizia kuongea ukiangalia koti lake linaweza likatoa suti za...

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lema, endelea na hoja yako.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee suala la Benki Kuu na maduka ya kubalisha fedha Arusha. Leo navyoongea hapa hakuna duka la kubadilisha fedha za kigeni Arusha linalofanya kazi na Arusha ndiyo center ya utalii katika Taifa hili. Ukitaka kubalisha fedha ya kigeni Arusha Mjini ni lazima uende Kilimanjaro Moshi. Sasa hawa watalii wanaokuja Arusha wanataka kununua bidhaa ndani, wanataka ku-spend unampeleka benki ya NMB, CRDB akapange foleni, anasubiri kubadilisha fedha, mazingira magumu kama haya yanasababisha wale wanaotafuta watalii yaani tourist operator wa-shift destination kutoka Arusha na Tanzania kwenda Kenya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utakuja kuniambia katika Bunge la bajeti high season ya kipindi hiki watalii watapungua wengi sana kwa sababu ya matatizo mengine lakini hata hili la kubadilisha fedha. Unajiuliza, hivi inachukuaje miezi miwili kupata solution ya kurudisha maduka ya kubadilisha fedha yaanze kufanya kazi kama kawaida? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo wamenyang’anywa fedha na wakienda kudai anaambiwa ukiendelea kudai tutakupa money laundry. Kwa sababu kuna ushuhuda wa watu wameteseka na kesi hizi watu wanaamua kuacha kudai fedha zao. Maduka haya kuna Sheria za BoT, sheria hizo zina faini pengine na vifungo, hatujasikia mtu mmoja anapelekwa Mahakamani leo ni mwezi wa pili maduka Arusha yamefungwa. Maduka mengine mmefunga mnasema eti Lema ana Bureau de Change kumi namwomba Mungu anisaidie niwe nazo yaani kama mna Usalama unawaambia mimi Bureau de Change kumi, mnakuja kufunga maduka ya kubalisha fedha eti mimi nina maduka, huo Usalama unawaingiza chaka sana maana yake haujui kitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tanzanite hapa inakufa, mmem-mislead Mheshimiwa Rais tanzanite haichungwi na ukuta, rushwa ni attitude, mtaweka ukuta na kamera wale askari mnaowalipa 700,000 kwa mwezi tutawapa milioni 50 yatapita mawe bilioni moja, fikirieni vizuri. Leo mnasema mnaweka na kamera, tena mmesema kamera ziwekwe bila tenda. Kila mgodi Mererani una fensi, akili ilikuwa ni nini, kama mngekuwa hamuwazi manual, ni kila mgodi mnatoa standard ya kamera, mnaweka internet ninyi, mna monitor migodi yote kutoka Dar es Salam na kutoka Arusha bila ninyi kuweka kamera. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niko hapa naangalia nyumbani nikiwa Dodoma, usiku naamka naangalia nyumbani kwangu, namwambia mke wangu nje kuna watu ponyeza alarm, ita mlinzi, sasa ninyi mnashindwa kuwaza hivyo tu, leo mmepiga ukuta hakuna mawe, sasa hapa itakuwaje, Mheshimiwa watakuwa wanaiba, weka kamera bila tenda, mnaweka kamera bila tenda! Kila mgodi una ukuta, weka kamera, weka mtu pale, TRA wako pale, mgodi ukitoa mawe siyo siri kila mtu huwa anajua, Arusha nzima huwa inajua, maana yake ni kwamba TRA watakwenda pale sasa leo mmeweka ukuta hausaidii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mgodi siyo duka la mkate, mawe hayatoki kila siku. Mwanzo mgodi ulitoa mawe mkakusanya shilingi milioni 800 mwezi unaokuja migodi haikutoa mawe mkamfukuza na Mheshimiwa Angellah, mkakusanya sijui 500,000. Mikataba tunaibiwa, lile siyo duka la mkate ama la colgate kwamba mawe yanatoka kila siku. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilivyokuwa mdogo kaka yangu alikuwa anahudumia mgodi. Nikawa mkubwa, nikawa Mbunge nikahudumia mgodi, nikawa Mbunge kipindi cha pili mgodi ukahujumiwa hatukuwahi kupata hata chembe moja ya mawe. Sasa ninyi mkikaa kule…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Leo nilikuwa nisome hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni; hotuba hiyo kimsingi haikuwa mbaya hata kidogo. Waheshimiwa Wabunge, wenzangu wa Chama cha Mapinduzi tafuteni hiyo hotuba muisome, muitathmini mwone wapi kulikuwa na makosa ya msingi ya kuiondoa Bungeni, kama siyo tu hotuba ile ilikuwa na busara ya kusaidia Jeshi la Polisi na Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja nimwambie rafiki yangu Mheshimiwa Kitwanga, nilimwambia Mheshimiwa Sitta kwenye Bunge hili, kipindi kile Mheshimiwa Lowassa alikuwa yuko CCM. Nilimwambia ukiona Kambi ya Lowassa inakushangilia wewe kuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, maana yake usisherehekee, maana yake ujiulize kwa nini nashangiliwa? Hili jambo linalohusu Mkataba wa Lugumi halikuwa kwa ajili ya kuidhalilisha Serikali, ilikuwa ni kwa ajili ya kuiondolea doa Serikali. IGP anasemwa, Waziri unasemwa, Jeshi lote la Polisi linasemwa na mkataba mchafu wa Lugumi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kitwanga ni rafiki yangu, haya mambo ambayo nimeandika, nimejadiliana naye nyumbani kwake tukiwa tunakula ugali. Nikamwambia mimi ni kipindi cha pili kuingia Bungeni, nazijua siasa za Bunge, nakuomba Mheshimiwa uniambie mimi kama Kambi ya Upinzani naweza nikasaidia mambo gani ambayo Serikali hamwezi kuja nayo direct? Nikamwambia usiponiambia, mimi nitakunyooshea na nitataka majibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeuliza swali ambalo nimeambiwa niliondoe kwamba, hivi Kamati ya Bunge inavyotembea kote huko kutafuta sakata hili la Lugumi, CAG anashindwa kutuambia kama mkataba ule ulikuwa thamani yake ya fedha na vifaa ni okay ama ni no! Anashindwa kujua!
Nikauliza swali lingine ambalo nimeambiwa niliondoe na Kamati; hivi Mheshimiwa Kitwanga wewe ni mbia wa enforce na ni Waziri wa Mambo ya Ndani; na Kampuni hii ya Lugumi iliingia kwenye biashara ukiwa siyo Waziri. Je, kama umekosa taarifa kutoka Jeshi la Polisi ambalo liko chini yako, umekosa pia taarifa kutoka kwenye kampuni ambayo ni mbia, ukijibu haya maswali Bungeni, utaondoa ukakasi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikauliza swali lingine ambalo nimeambiwa niliondoe.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Lema, nakujua wewe ni mzoefu kwenye Bunge, najua uwezo wako. Unatumia njia nyingine kusoma hotuba yako hapo ulipo. Sasa nakusihi, sababu maneno hayo unayosema ndiyo yamekatazwa kuanzia ukurasa wa kumi. (Kicheko/Makofi/Kelele)
Unajua Mheshimiwa Lema, hawa wanapiga vijembe kama mpirani. Referee akipiga filimbi, watu wanalalamika, lakini Serikali, referee anakuwa strict. Jiepushe na maneno yaliyopo kwenye ukurasa wa kumi mpaka wa kumi na nne.
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajiepusha na hayo maneno, lakini Wabunge wa Chama cha Mapinduzi, nikiangalia Wabunge wote hapa ni wapya kwa asilimia 50.
MHE. GODBLESS J. LEMA: Ama seventy. Wabunge tuliokuwepo Bunge lililopita, hatukuwa hawa ninaowaona hapa. Waheshimiwa Wabunge pamoja na itikadi za vyama vyetu vya siasa, inapokuja kwenye suala la maslahi ya nchi yetu, tuache hizi siasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkisema mambo ya msingi kama haya tusiyaongee, ndiyo sababu uliponiita hapo mbele nilisema basi ngoja na mimi tu nimshukuru mke wangu kwa kuja Dodoma. Kama mambo serious kama haya Kambi inakatazwa kuongea, tunaisaidiaje Serikali?
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Wizara ya Mambo ya Ndani, unapokuwa na IGP anayesemwa vibaya na hakuna kauli ya Serikali, unafanya Jeshi la Polisi lidharaulike. Unapokuwa na Waziri wa Mambo ya Ndani anatiliwa mashaka kwa mambo ambayo ama ni ya magazeti au mitandao na hakuna majibu, unafanya Wizara idharaulike. Wizara ya Mambo ya Ndani ikidharaulika, ni nchi imedharaulika usalama wake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba yangu utakuwa umeipata ambayo ina mambo nimeambiwa nisiyasome. Wewe yajibu tu kimkakati ili uwe na amani. Nakwambia jambo hili halimhusu Lugumi. Lugumi is nothing in this Parliament! Mtu anayetafutwa humu ni wewe.
MHE. GODBLESS J. LEMA: Sawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme tu, hii wanataka kutengeneza mlima kutoka kwenye kichuguu. Hii wanaacha pressure iendelee, wanakutafuta wewe. You will tell me my brother, you will tell me! Mimi najua siasa za Bunge humu! Unajiuliza, hii hotuba ina makosa gani? Haina makosa, wanataka pressure iendelee. Wanasema wewe ni rafiki wa karibu wa Magufuli, nawe ndiyo kiherehere mkubwa, kwa hiyo, wanakutafuta wewe! Wanakutafuta!
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais wetu huyu mwema, nikilitumia hivyo kuna shida?
Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais wetu huyu mwema wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni rafiki wa karibu wa Mheshimiwa Kitwanga. Kwa hiyo, nasema kwamba jambo hili siyo jambo dogo, nami maswali niliyokuwa nauliza ambayo nimezuiwa; Waheshimiwa Wabunge, nakatazwa kwenye hotuba yangu hata kuuliza. Jamani leo Mheshimiwa Kangi amenishangaza! Mheshimiwa Kangi anasema, Mheshimiwa Chenge hajawahi kutuhumiwa na scandal ya Rada. Mheshimiwa Kangi!
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, okay. Naongea nini? Mbunge yeyote ndani ya Bunge hili, zawadi pekee ambayo anaweza akaipa familia yake ama wazazi wake ama nchi yake ni kuthubutu kusimamia ukweli unaolinda Taifa hili. Yeyote! Nawaomba Waheshimiwa Wabunge, bendera zetu zisiwe na nguvu kuliko hadhi ya nchi yetu. Tusaidie hii nchi kwa pamoja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niliwaambia na nawaambia tena, hatutashinda uchaguzi kwa sababu ninyi ni wabaya, tutashinda uchaguzi siku ambayo watu wataamua tushinde uchaguzi na kuwepo kwa Demokrasia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna mtu amesemwa kwenye Bunge lililopita na kwenye magazeti. Kuna watu walisema mwaka 2015 kwamba kuna siku tutam-miss Kikwete, mimi nimeanza kum-miss Mheshimiwa Kikwete. Hakuna mtu alisemwa kama Rais Kikwete! (Kicheko/Makofi)
MBUNGE FULANI: Kweli kabisa!
MHE. GODBLESS J. LEMA: …lakini hakuwahi kuingilia Mhimili wa Bunge. Hakuwahi kuingilia shughuli za Bunge. Bunge hili lilikuwa linamsema Rais Kikwete kwa namna yoyote ile, Mawaziri akina Mheshimiwa Jenista mlikuwepo, hamkuwahi kuingilia! (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Waheshimiwa Wabunge wenzangu, tuisaidie hii nchi, tuvuke mipaka ya party caucus zetu tusaidieTaifa hili. Kuna mtu mmoja yuko Magereza huko, alipokuwa jela aliulizwa na Wakili wake; aliambiwa, lakini wewe ulikuwa Waziri, wakati mnapitisha hii sheria ya kwamba ukikamatwa na makosa ya ufisadi wa fedha za umma ni lazima ulipe 50 percent kama bail, ulikuwa wapi? Akasema nilikuwa kwenye kikao hicho lakini sikuona jambo hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vikao hivi tunavyofanya shughuli za Bunge, tunavyohudumu kama Wabunge, iko siku dhambi tunazozifanya humu zitakuja kuwala watoto wetu na watoto wetu kwa sababu tulishindwa kusimamia ukweli.
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Waziri…
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na nafurahi kwamba leo Bunge lina utulivu wa kutosha na taarifa na miongozo pengine jana mlijadili mkasema haina maana sana. Jana nilikuwa natafakari sana, kwamba ndani ya Bunge hili Wabunge wote tuliopo sasa tukapewa fursa na Mwenyezi Mungu ya kuishi miaka 30 inayokuja mimi nitakuwa na miaka 72, wewe utakuwa na takribani miaka 100, pengine Mheshimiwa Jenista atakuwa na miaka mingi zaidi. Maana yake ni kwamba hata kama tutakuwa hai wengine watakuwa hawana nguvu kabisa za kulitumikia Taifa hili. Thamani yetu leo si kulinda Chama Tawala ni kulinda misingi ya haki katika Taifa na ndio wajibu wa kwanza wa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiishi kula leo, kuvaa leo, kuendesha gari leo, halafu usitafakari maisha ya wajukuu wako, ya vitukuu vyako baada ya maisha yako hapa duniani, si tu utakuwa ni Mbunge mkatili, utakuwa ni mzazi mkatilii. Kama kuna kitu tunapaswa kukichunga Wabunge wote bila kuangalia itikadi yetu ni juu ya namna gani tunalisaidia Taifa kuheshimu Katiba hii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ndio msingi tuliokubaliana kwamba kwa sasa tutaishi kwa madhumuni haya na kwa utaratibu huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali yoyote duniani, iwe ni Marekani, iwe ni Venezuela, iwe ni Kenya, ikianza kuishi nje ya utaratibu wa Katiba na sharia, Serikali hiyo inakuwa ni kikundi cha wahuni ila wamevaa suti, yoyote duniani. Namna pekee ya kuthibitisha umahiri wa Maprofesa, Madaktari, form four na watu wote wenye hekima, namna pekee ya kuthibitisha umahiri ni kuishinda hofu linapokuja suala muhimu la haki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtoto wangu mimi na mjukuu wangu mimi natarajia siku moja akutane na Mahakama huru hata kama nitakuwa sipo, same to mtoto wa Mheshimiwa Jenista, same to mtoto wako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunapoona haki inachezewa, lakini inachezewa kwa kwa sababu inatupa fever ni sawa sawa na chloroquine imepakwa chocolate, utaila kwa muda utasikia radha ya chocolate baadaye utakutana na uchungu. Hakuna uovu ambao hautalipwa ni nature, ni karma. Kuna mambo leo yanawatokea watu wa CCM ambao huko nyuma walikuwa untouchable.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikutana na Manji siku moja Karimjee, nikamwambia kwamba kuna kipindi wewe ulikuwa untouchable. Leo kuna watu walikuwa hawaguswi katika katika Serikali hii, walikuwa ni wafanyabiashara wakubwa, walikuwa ni viongozi wakubwa, leo wako magereza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna utawala unaoweza uka-guarantee usalama wa mtu isipokuwa haki, kwa sababu haki haina tu kipaumbele cha system ina kipaumbele cha Mwenyezi Mungu peke yake. Waheshimiwa Wabunge tunapokaa hapa Bungeni kujadili mambo ya msingi; jana nimeshangaa; kwamba suala la mkono wa sweta (govi) linaweza likatolewa na Bunge na TV ya Bunge likapelekwa mitaani halafu masuala mengine ya msingi ya kusaidia nchi kama vile michango ya Wabunge wa Upinzani inanyimwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, michango yetu siyo uhaini…

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawasaidia, leo tunaongea michango yetu si uhaini, michango yetu…

T A A R I F A

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napokea hiyo taarifa. Hiyo ni sehemu ya mfano wa jambo hilo, lakini yako mambo mengi, kwamba leo mawazo yetu ndani ya Bunge si mawazo ya kuiangusha CCM. Mimi leo mkitawala kwa haki, kwa upendo, kwa sheria na mkafuata Katiba, hata mkitawala milele sitakuwa na tatizo. Lengo letu si kuwatoa ninyi madarakani, lengo letu ni kuona ninyi mnatutawala kwa haki na ndiyo maana ya upinzani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo chuki inajengwa, leo kiongozi mmoja m-NEC wa Chama cha Mapinduzi anahutubia anasema Mheshimiwa Lissu siku akitua ashambuliwe, Mheshimiwa Zitto ashambuliwe, leo Mheshimiwa Zitto yuko Bungeni, tumemwondoa juzi, Mheshimiwa Zitto juzi alikuwa anafuatiliwa usiku kwa kazi za Kibunge si za kuuliza madawa la kulevya, si za kubaka mtoto, kwa kazi za Kibunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilitekwa Makuyuni kwa kazi ya Kibunge, wakaua mtu mmoja polisi, kwamba wale ni watu waliokuwa wanakuja kuniteka mimi. Nikapelekwa jela kwenye ile kesi yangu dhidi ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli. Nikiwa jela wale vijana wakaletwa jela, wakapelekwa dispensary nikajifanya naumwa nikapelekwa dispensary nikaanza kuongea nao. Cha ajabu wale vijana waliokuwa jela walitolewa jela siku ya Jumapili na Mbunge, Mheshimiwa Jitu alikuja kuwachukua na gari siku ya Jumapili ambapo Mahakama wala Magereza haifanyi kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa haya mambo yanafanya tulipwe machozi, tunaguna, siyo mimi peke yangu ninayeguna, tumesikia juzi hapa Itigi, Mkurugenzi ameua, ameingia ndani ya Kanisa la Sabato, ame-shoot, mzazi anasema ame-shoot, Mkurugenzi akasema ilikuwa ni kwa bahati mbaya. Tunaona taarifa ya polisi leo inasema Mkurugenzi yule hakuua, walioua ni Polisi wa Wanyamapori waliokuwa nje.

KUHUSU UTARATIBU

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, haya maneno tunaongea hapa kwanza hili suala haliko Mahakamani; lakini siku Bunge hili likafikiri hata jambo lililoko Mahakamani lakini lina mashaka ya damu ya mtu, Bunge hili haliwezi kulijadili tunainajisi legitimacy yetu kama Wabunge. Waheshimiwa Wabunge thamani ya mtu mmoja ni zaidi ya kilometa 10, 000 za lami, thamani ya mtu mmoja, hata kama ni kichaa, ni zaidi ya SGR ya kutoka Tanzania kupita nchi zote za SADC. Kazi ya kwanza ya serikali yoyote duniani ni ku-protect human rights. Kama huu si msingi wetu wa imani, kwamba maisha ya mtu mmoja yanaweza yakawa considered na vitu, thamani yetu ya kuishi haipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wanaendelea kufa, watu wanaendelea kupotea na yote hii ni Katiba. Inawezekana kabisa kuna nia njema ya Serikali, kumsaidia Mheshimiwa Rais kutekeleza majukumu yake ni kumwambia ukweli kwa sababu ukweli ni nguvu. Leo tunavyoongeza kuna watu wanaozea mahabusu. Jamani mimi nikiongea habari ya mahabusu; pasu nimekutaka na Mheshimiwa Profesa Kabudi nimeongea naye; kuna watu wana kesi za money laundering wako mahabusu, Sh.300,000 mtu yuko jela miaka mitano. Kenya leo kila kesi ina dhamana isipokuwa kesi ya uhaini, Uganda leo kila kesi ina dhamana mpaka kesi ya uhaini. Dhamana ni hoja kuu imewekwa kwenye Katiba hii ndiyo Mtobesya. (Makofi)

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

T A A R I F A

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge lenye Wabunge zaidi ya watu 350, hutarajii kumkosa mtu kama huyu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi, mimi napita Magereza zote, kuna kesi inayotumika vibaya, Profesa yuko hapa, ni Mwanasheria. Money Laundering Act; Waheshimiwa sikilizeni tuna miaka miwili kutoka humu ndani, haya mambo ninayowaambia sisemi kwa niaba ya CHADEMA nasema kwa niaba ya watu wote sisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, walioko Magereza leo wengi hawakuwa makada wa Chama cha CHADEMA. Concern yangu hapa nini, leo Mahakama ya Kikatiba ilinusa section 148 ya CPA ambacho kilikuwa kinampa mamlaka DPP ya kuweka watu ndani kwa certificates. Mimi nimekaa ndani kwa certificate, watu wengi wakaa ndani. Sasa haya mambo leo yanaonekana ni CHADEMA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili kundi hili linaweza likaamua leo, tunaamua tu leo kwamba hatugombanii ubunge, tu naacha siasa halafu ninyi CCM mjae huko, then what? Halafu nini kifanyike? Yaani assume huku mmejaa, huko mmejaa Mheshimiwa Waziri Mkuu ni wenu, Mheshimiwa Rais wenu halafu then what, then what? Kimsingi ni sheria, kimsingi ni utaratibu. Ndiyo maana tunasema Waheshimiwa Wabunge turudi turudi kwenye sense. Nawaambia, kwa hali ilivyo leo na nisikilizeni mimi ninyi, Mawaziri mlioko kwenye Baraza hili na Makatibu Wakuu, kwa utaratibu wa sasa ninavyouona jiandaeni, la sivyo badilisheni sheria; jiandaeni ninyi na hamtajua. Kwani, Waheshimiwa viongozi, kwani Magufuli ni CHADEMA, Magufuli si CHADEMA, ni purely CCM. Wakati Magufuli anashinda Urais.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lema, Mheshimiwa Rais utamu-address kwa cheo chake tafadhali.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, samahani na namheshimu sana. Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Mtukufu Magufuli, siyo CHADEMA ni CCM na watu wote leo wamekuwa responsible na matatizo waliyofanya kwenye kazi zilizopita siyo CHADEMA, wengi ni Makada wa Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema hivi, mtafanya mitimanyongo yote mnayoweza kufanya, mtafanya kila mnachoweza kufanya; tunaweza tusirudi Bungeni tena; mtasema tutamweka mtu wetu Profesa Kabudi huyu, atalinda utawala uliopita. Akina Kikwete walifikiri hivyo hivyo, utawala uliopita haulindwi. Walifikiri hivyo hivyo. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachosema, bado dakika tano. Zangu ni 15.

MWENYEKITI: Ahsante. Tayari Mheshimiwa Lema. Ulianza na dakika sita.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Nataka nianze na utawala bora na habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba Juliet Kairuki alikuwa Mkurugenzi wa TIC amefukuzwa kazi kwa sababu ya kutokupokea mshahara. Sasa ile bahasha aliyokuwa anasema msitulipe posho tunaweza tukapita kwenye wimbi hilo la kuvuliwa Ubunge kwa sababu ya kutokupokea posho. Naomba mliangalie vizuri kwa sababu utumbuaji wa majipu umeanza hata kama hupokei hela, this is very serious.
Mheshimiwa Naibu Spika, Rais aliyeko madarakani siyo kwamba kila anachokifanya hatukikubali, tunaiamini nia yake ya ku-restore glory ya nchi hii hasa baada ya sisi ndani ya Bunge hili kupiga kelele sana dhidi ya ufisadi katika Taifa hili. Anachokifanya Rais, siyo vitu vyote ni vibaya kwamba courage yake ya ku-restore glory kwenye utumishi wa umma siyo mbaya lakini utukufu binafsi unapozidi sifa za Mungu, Rais anaweza akakosea.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Rais, Dkt. Magufuli, kuteuliwa na chama chake kuwa mgombea wa Chama cha Mapinduzi kulisababisha public opinion ambayo ilikuwa created na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu alionekana ni kati ya Mawaziri waliokuwa wakifanya vizuri katika Wizara zake ndani ya Bunge hili. Leo mmekuja na mapendekezo ya kuondoa live broadcasting ndani ya Bunge hili, maana yake leo tunaongea hatusikiki nje.
Mheshimiwa Naibu Spika, unaposema ni gharama Wabunge na Bunge kuongea na wananchi wao hizo gharama mna-compare to what? Yaani unaposema ni gharama kulipia matangazo ya Bunge wananchi wasikie Wabunge wanachojadili compared to what, expensive is a relatives. Leo mmekuja na mapendekezo mengine ya Wakurugenzi wa Wizara watoke na mabasi Dar es Salaam, waje Dodoma kwenye vikao sensitive vya Bunge. Mnafikiri ni kubana matumizi, huwezi kubana matumizi kwa kuondoa class, hiyo ni poverty mentality. Nchi hii ina rasilimali za kutosha ifikie mahali muanze kufikiria Wabunge kuja hapa na helicopter siyo Wakurugenzi wa Wizara kuja hapa na mabasi. Haya mambo tulifanya wakati nchi inapata uhuru leo mnataka kuturudishia mnasema ni kubana matumizi? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, huwezi kubana matumizi kwa ku-create poverty mentality kwenye mfumo, huwezi kubana matumizi kwa kumfanya tajiri aishi kama maskini. Rais anatoa kauli, anasema hawa wanaoishi kama malaika wataishi kama mashetani, this is bad na mnashindwa kumshauri kazi ya Rais ni kufanya mashetani kuokoka waishi kama malaika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, huwezi kuwa na wish ya kufanya watu wako kuwa na maisha mabaya lazima uwe na wish ya kufanya watu wako kuwa na maisha mazuri. Sasa kinachoendelea sasa mnafikiri mnakomoa opposition; mnachokifanya mnamtengenezea Rais spirit of dictatorship, mnamfanya Rais anakuwa ni one man show game. Kama Rais angekuwa na nia njema ya ufisadi, kazi nyingi tungemsaidia hapa Bungeni. Kama Rais angekuwa na nia ya kupigana angeacha Bunge liwe live.
Mheshimiwa Naibu Spika, Rais mwenyewe anajua umuhimu wa vyombo vya habari kila anakokwenda amesema mwenzangu hapa anabeba TBC hata kama ana kwenda kufumania bahati mbaya kazini; unashangaa hawa Azam na wenyewe wamejuaje leo Rais anakwenda BoT? Kumbe ni mipango. Kama mnajua umuhimu wa vyombo vya habari acheni Bunge liwe huru. Mnasema Rais wenu anawajibika vizuri cheni basi haya mambo yawe huru.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo mmetoa hela za Bunge hapa mnaita utawala bora, mmeenda kukabidhi kwa Rais, Spika hajui, Spika naye anasoma kwenye WhatsApp, Spika anaangalia mko Ikulu; yuko anaumwa anasoma kwenye WhatsApp, mnafanya maamuzi ya fedha za Bunge bila kushirikisha Kamishina wa Bunge, utawala bora uko wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukitaka tumsaidie Rais ku-restore glory katika Taifa hili, chombo cha kwanza cha kumsaidia ni Bunge kuwa democratic, hili Bunge halina uhuru. Mawaziri waoga leo hakuna innovation kwenye Ofisi za Mawaziri, hakuna innovation kwa Katibu wa Bunge, kila mtu anaogopa, sasa kama hivi usipopokea mshahara unatumbuliwa. Hawa watu kule kazini wako hivi, walikuwa wanafanya kazi bila instrument, walikuwa ni Mawaziri vivuli, hakuna watu wanaobuni, watu wako hivi wanaogopa, maamuzi hayafanyiki kwa sababu mmeshindwa kumshauri Rais.
Mheshimiwa Naibu Spika, utawala bora siyo huu mnaoufanya nyie. Nilishawaambia hapa tena narudia leo, lengo la opposition siyo kutawala nchi hii, lengo la opposition ni pamoja na kuona mnatutawala vizuri. Ingekuwa haya mambo mnayofanya yanaharibu chama chenu peke yenu lakini hayaharibu Taifa letu tungewaachia kwa sababu pengine maisha yenu hayatuhusu lakini mkiharibu, mnaharibu maisha ya watoto wetu ndiyo maana tunapiga kelele. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo nchi inaenda haijulikani, leo hakuna kiongozi wa Serikali anakwenda kazini asitegemee kufukuzwa kazi, leo anakwenda Makonda anamsoma mtu hadharani, unasema nifukuze kazi ama nisifukuze? We don‟t live like that man hatuwezi kuishi hivyo, wale wana wazazi, wana-family, wana ndugu, watu wote wanafanya makosa lakini hauwa-treat hivyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa na wewe umepeleka hela kule Ikulu sijui nani angekutumbua. Ukachukua hela bila hata kumuuliza bosi wako na wewe hapo siku hizi ndiyo unajifanya zaidi ya Spika, yaani wewe ni kila kitu, mnafika humu mnawaamulia Wabunge, magari ya Wabunge hakuna mnampa Mbunge milioni, eeh tabu sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri Muhongo alikwenda bandarini, akamuuliza yule mama nani amekwambia ufungue lile bomba? Mama akasema nimeambiwa na Waziri. Mkamfukuza aliyeagizwa na bosi wake mnaacha aliyeagiza; mnawaonea watu, mnanyonga watu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nirudi kwako kaka yangu Simbachawene, umeongea kwenye television kwamba kuanzia sasa Halmashauri ndiyo zitakusanya mapato, hamjajiandaa …
Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hamjajiandaa. Leo kwa kazi moja ya parking system Arusha Mjini utahitaji watu 220, utawalipa kima cha chini, Pay as You Earn, NSSF, Bima ya Afya, mfanyakazi mmoja aliyekuwa anakusanya parking kwa Sh.80,000 kupitia private sector leo wataigarimu Halmashauri Sh.400,000/=. Mnakwenda kuua Halmashauri kwa sababu ya disengagement ya private sector, angalieni hili suala kwa umakini sana kuhusu private sectors.
Mheshimiwa Naibu Spika, Zanzibar. Mmemaliza uchaguzi mmeshinda mmepiga kura wenyewe mmelinda kura, mlichoshinda Zanzibar mmeshinda tena hapa, kwa ushauri wa Nape, mkionesha Bunge wanaonekana sana hawa. Zanzibar kesi haijaisha, msifikiri mko salama, iangalieni Zanzibar vizuri, ukiona unapiga mnyonge anakaa kimya, Mandela alisema hatafuti kichochoro anatafuta njia ya kujitetea.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie, kuna Mheshimiwa Mbunge mmoja aliongea habari ya Arusha kwamba uchaguzi tumeshindwa, huyo haijui Arusha. Kwanza hatujui anakaa wapi, analala wapi, kama hawezi kuwa na tathmini ya watu ambao anaishi nao kila siku Tanga, Dodoma, Dar es Salaam hawezi kuwa na tathmini ya mkoa. Mwaka jana Wenyeviti sita wa CCM waliniunga mkono mwaka huu tumefanya uchaguzi, tumewanyang‟anya CCM mitaa minne imebaki miwili. Sasa yule dada anasema CCM Arusha inaendelea vizuri kwa kasi ya Magufuli. Ajue kwanza maisha yake na mumewe na wapi anaishi ni Tanga, Dar es Salaam, ni Mara ni Dodoma na anaishi na nani? Akishajua anaweza akajua tathmini ya Mkoa.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naomba kabisa nianze bila kusahau na suala ambalo tulikutananalo Arusha na Mheshimiwa Waziri naomba anisikilize sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikwenda Arusha na Kamati ya Viwanda na Biashara na tulivyofika TANELEC, mahali ambako tunatengeneza transformer, walikuwa na malalamiko ya msingi sana. TANESCO ni shareholder wa TANELEC, yaani kwenye Board ya Directors ya TANELEC, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO ni mjumbe. Cha kushangaza sana ni kwamba, Kenya wananunua transfoma Tanzania, Msumbiji wananunua transfoma Tanzania, mpaka Malawi, lakini Tanzania ambao ndiyo wanaotengeneza transformer na TANESCO ambao ndiyo inafanya biashara ya umeme, inanunua transfoma kwa Manji, kutoka India kwa bei mara mbili ya zinazouzwa TANELEC!
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri, haya mambo ni mambo ya ajabu kweli, kwamba partner, mwenzi wa TANELEC ambaye ni TANESCO kwenye Board anaingia Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, wanakwenda kufanya maamuzi ya manunuzi ya transfoma, wanaacha kununua transfoma Tanzania, wanakwenda kumpa order Manji kuagiza transfoma ya dola 4,000 au 5,000 wakati pale zinatengenezwa transfoma. Sisi na Wajumbe wote wa Kamati tulihuzunika sana na tulimpelekea Waziri wa Viwanda na Biashara tukamwomba akuone! Hili jambo Mheshimiwa, siyo tu ni jipu, hii ni cancer ambayo matibabu yake kwa kweli, lazima yafanywe very serious.
Mheshimiwa Mwenyekiti, madini ya Tanzanite; ninachokielewa na ninachokiona, Mheshimiwa Waziri ni Mtaalam wa Miamba, lakini ukweli ni kwamba, lazima tutafakari kwenye Wizara ya Nishati na Madini tunahitaji Mtaalam wa Miamba ama Mtaalam wa Biashara ya Madini. Tukiweza kulipambanua hilo vizuri tunaweza tukaisaidia sana Wizara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninavyoongea sasa hivi Madini ya Tanzanite yameanguka kwa takribani asilimia 60 mpaka 70! Jiwe lililokuwa likiuzwa shilingi milioni moja mwaka jana mwezi wa 11, leo jiwe hilo linauzwa shilingi 300,000 mpaka shilingi 400,000 hakuna market! Sababu ni moja, kuna confusion kubwa imekuwa created kati ya madini ya tanzanite, ambayo ni cut na madini ya tanzanite ambayo ni rough. Kwa hiyo, nimwombe sana Waziri, waende wakafanye tathmini ya kutosha; watu wote waliokuwa wakinunua madini Arusha wakisafirisha kwenda nje, wote wame-shift position wamekwenda Mombasa, wamekwenda Kenya. Kimsingi ni kwamba, hawataweza kuzuia madini ya tanzanite yasiende kwa njia za panya kufika Nairobi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kitakachoonekana, Nairobi ndiyo watakuwa wana-seal mzigo. Mzigo utaondokea Kenya, kwa hiyo tanzanite yote duniani itaonekana inaondokea Kenya kwenda kwenye Mataifa ambako inanunuliwa kwa sababu, haikufanyika feasibility study vizuri ya kuweza ku-burn hii tanzanite ambayo leo inazuiwa kwenda rough.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Mheshimiwa Waziri wataalam wako wanapokuja kufanya utafiti wa biashara ya madini wasije tu watu waliosomea miamba inavyotoa madini, waje watu ambao wako business oriented. Leo tunavyoongea Arusha watu wameondoka na kwa sababu ya hii kasi ya Serikali hii watu wanaondoka wanahamisha investment. Biashara kubwa inafanyika Mombasa na jiwe la Tanzanite ukipita nalo kwenye kengele hapo, gemstone haipigi kelele. Kwa hiyo, mawe yataondoka yote Arusha, yatakwenda Mombasa, yatakwenda Nairobi, wata-seal mzigo Nairobi, watakwenda Thailand, watakwenda Marekani, itatokea kama ilivyotokea miaka ya nyuma, Kenya ilipewa zawadi ya ndege kwa kuuza madini mengi ya Tanzanite wakati Tanzania haijawahi kupewa zawadi hata ya baiskeli. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu umeme na mazingira. Tanzania kuna takataka nyingi sana. Amesema Mheshimiwa Japhary kwamba takataka siyo disadvantage, takataka ni umeme. Lakini leo nchi hii tuna claim kuwa na takataka nyingi mijini badala ya kuzi-transform takataka hizi kuwa umeme. Wameongea wenzangu hapa kuhusu biogas, kama Wizara ya Nishati na Madini ingekuwa serious na biogas leo misitu inavyokatwa nchi hii inakatwa kwa sababu hakuna njia mbadala ya nishati ya kupitia tofauti na kuni, lakini ukiangalia maeneo yote ya Usukumani kuna ng‟ombe wengi, kuna vinyesi vingi vya ng‟ombe ambavyo hivi vingeweza kuwa transformed kuwa umeme, vingeweza kuzuia sana uharibifu wa mazingira mkubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo suala la biogas siyo suala la umeme peke yake na kupikia chakula. Ukitaka kuokoa Taifa hili na uharibifu mkubwa wa mazingira, Mheshimiwa Waziri ni shahidi ukiwa kwenye ndege unakwenda Dar es Salaam hapa katikati Morogoro kote kumeanza kuisha. Mawaziri na Wabunge tunanunua mikaa barabarani. Ukiongelea future ya Taifa bila kugusa mazingira ni kujidanganya sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana suala la biogas, mimi ni shahidi nyumbani kwetu ninakotoka kijijini kwa mama yangu tumemfungia biogas ana ng‟ombe wawili, tuna miaka mitatu hajawahi kutumia kuni, tuna miaka mitatu hajawahi kutumia umeme wala hajawagi kununua gesi ya madukani. Kwa hiyo, suala la biogas siyo suala tu la nishati mbadala, lakini nishati ambayo inaweza ikazuia uharibifu mkubwa wa mazingira. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, TANESCO wanapobadilisha nyaya utafikiri wametumwa na ibilisi kuja kukata miti. Hakuna watu wanakata miti hovyo kama TANESCO. Kila wanapobadilisha waya wanakata miti, mti mmoja kukua unachukua zaidi ya miaka mitano mpaka 15 halafu TANESCO wanakuja kubadilisha waya imetumika muda mrefu wanakata mti wote. Kupanda mti mwingine mpaka ufike kwenye maeneo ulikofika ni miaka mingine kumi, tunaendelea kutengeneza jangwa. Waya za siku hizi nimeziona, ni waya ambazo zina plastic, ziko covered na plastic. Unajiuliza kuna sababu gani ya TANESCO kukata miti hovyo badala ya ku-prune miti na kuacha waya zipite kawaida na miti iendelee kuwa mapambo ya miji yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakuomba sana Mheshimiwa Waziri, TANESCO waambiwe kabisa wakitaka kufanya pruning ya miti yoyote wawe na link kwanza na Halmashuri husika ili tukubaliane na Mipango Miji hii miti inakatwaje, kwa sababu watu wanafanya jitihada. Mheshimiwa Mbowe amepanda miti kutoka KIA mpaka Hospitali ya Machame mpaka Moshi Mjini, juzi TANESCO walikuwa wanabadilisha waya, wanahamisha nguzo mimi nikawakuta wamekata. Nikasimama, nikampigia Mbunge simu, nikamwambia Mbunge miti uliyopanda, amenwyeshea mwenyewe kila kitu mwenyewe, miti imefika mita tatu, mita tano juu TANESCO wanakata miti na waya zinazopita pale ni waya ambazo zina plastic cover. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe sana Mheshimiwa Waziri kwamba TANESCO wanavyofanya kazi ya kuweka waya mijini na Mheshimiwa Maghembe analijua hilo tukiwa kwenye kikao cha RCC waliliongea hili. Waangalie kabisa kwamba mazingira ni muhimu kuliko kitu chochote katika nchi hii. Hakuna kitu cha msingi kama mazingira. Kwa hiyo TANESCO watusaidie, wa-communicate na Halmashuri, tukubaliane namna gani ya ku-prune miti na waya zipite bila kuharibu mazingira. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri anafahamu, Waziri Mkuu alikwenda bandarini, alivyofika bandarini akakuta ile flow meter imefunguliwa akauliza, alipouliza Waziri Mkuu akawa na hasira kwa sababu anaipenda nchi yake akakamua jipu. Lakini yule mama alisema nimetumiwa message na Waziri, sasa Mheshimiwa Waziri kwa sababu wewe tulikutolea maazimio mwaka jana na bado leo tuko na wewe, ina maana ni huruma yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, basi kama ni Mheshimiwa Waziri alimtuma yule mama aongee tu na Waziri Mkuu yule mama mumrudishe kazini kwa sababu kwa vyovyote vile yule mama kama aliambiwa na bosi wake fungua hiyo flow meter, halafu mama akasema nimeambiwa na bosi wangu, Waziri Mkuu akatumbua jipi bila ganzi. Mheshimiwa Waziri Mkuu mimi nakuheshimu sana, kwa kweli hebu mfikirieni yule mama kama ambavyo sisi ama wenzako huko ambavyo wamekufikiria wewe Mheshimiwa Waziri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mwaka jana tulimfungua na mashati hapa lakini mwaka huu tumekuona umekuja na tunashindwa kuongea vibaya dhidi yako kwa sababu wote waliokuja……
MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ili kuepuka miongozo mingi naomba nianze na neno la Mungu kutoka kitabu cha Ufunuo mstari wa nane, inasema “bali waoga, na wasioamini na wachukizao na wauaji na wazinzi na wachawi na hao waabuduo sanamu
na waongo wote sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto wa kiberiti.” (Makofi)
Mheshimiwa Spika, watu waoga, Biblia imewafananisha na wazinzi; watu waoga biblia imewafananisha na wanaoabudu sanamu; watu waoga
Biblia imewafananisha na waongo na biblia ikasema hawa hukumu yao ni ziwa la moto.
Mheshimiwa Spika, nilipokuwa Magereza nimekuombea sana, Mungu ni shahidi. Ili Bunge hili liweze kutenda haki, wale watu waliotajwa hapa kama wapo, wakatae kufanishwa na wazinzi na waabuduo sanamu.
Mheshimiwa Spika, nchi hii inapokwenda, kama leo Bungeni pasipokuwepo na uhuru wa majadiliano wananchi wataongelea wapi? Tukiongea nje, tunakaa ndani, tunanyimwa dhamana, tunapelekwa Magareza kwa miezi minne. Tukiongea Bungeni haturuhusiwi. Leo haturuhusiwi
kuisema Ofisi ya Rais, mnafikiri mnamsaidia Rais! Ipo siku atatafuta watu makini. Huko mlikuwa wengi sana, wengine sasa hivi wako huku. Atatoka mmoja mmoja na wote mtakuja huku. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, namna ya kuisaidia nchi ni watu kutokuwa waoga. Ni watu kusema ukweli! Leo Taifa linayumba! Hakuna mtu ambaye hakuona Siku ya Sheria Duniani, lakini hapa kila mtu anatetea chakula, anatetea mshahara kuliko utu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, watoto na wajukuu wa Taifa hili wanaangalia kizazi cha Bunge hili kinatunga Sheria za aina gani? Maombi yangu ni kila Mbunge angalau apite jela kwa miezi minne ili mjue ninachokisema.
Mheshimiwa Spika, nasema hivyo kwa sababu gani? Waheshimiwa Wabunge tuisaidie nchi. Kuna siku mke wangu alikuwa anawaambia wanangu, nataka msome sana muwe kama profesa. Mtoto wangu mmoja akamwuliza, kama profesa nani? Mke wangu akasema ngoja ni-google!
Mheshimiwa Spika, tunataka Madaktari na Maprofesa walioko ndani ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi wawe mashuhuda wa kupigania haki ya Taifa hili. Leo msiporuhusu mijadala huru ambayo imeruhusiwa na Katiba hii kwa Wabunge, ndani ya Bunge, tunaenda kuongelea wapi
mambo ya kulisaidia Taifa hili? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Hussein Mwinyi ni mtoto wa Mzee Mwinyi; baba yake leo ana faraja mtoto wake ni Waziri yuko Bungeni. Ben Saanane ni mtoto wa Mzee Focus; Ben Saanane amepotea, hajulikani alipo.
Mheshimiwa Spika, Serikali imemtafuta Faru John kwa gharama zote; imemtafuta Faru John kwa nguvu zote; kuna mtoto anaitwa Ben Saanane, ana wazazi kama ambavyo Mzee Mwinyi ana mtoto anaitwa Hussein; kama ambavyo Mzee Maghembe ana mtoto wake, juzi tumemchagua kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, akampa mkono akifurahi; leo kuna binadamu ana ndugu zake, ana wadogo
zake anaitwa Ben Saanane; baba yake aliniambia maneno haya, “CHADEMA na Serikali nisaidieni kumtafuta mtoto wangu. Ben sio mbuzi wangu, Ben ni mtoto wangu.” (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Serikali imemtafuta Faru John. Leo nimeshangaa yaani wanyama wamekuwa na hadhi katika Taifa hili mpaka leo kuna mnyama anaitwa sijui Yusta na mnyama mwingine anaitwa Ndugai, wewe mwenyewe! Aisee! I am wondering! Yaani mpaka leo wanyama
wanakuwa na thamani mpaka wanabatizwa majina ya binadamu na kuna mtu anapotea hapatikani.
Mheshimiwa Spika, Mawazo aliuawa, Geita. Mawazo ameuawa Geita, mahabusu wale wakalala barabarani wanasema Serikali ilete viongozi wakubwa tuwaambie watu waliomuua Mawazo. Serikali haikuchukua hatua. Faru John ametafutwa kwa nguvu zote. (Makofi).
Mheshimiwa Spika, kuna maiti Ruvu, nilikuwa Magereza nasoma kwenye magazeti, saba; DNA yake haijapimwa, taarifa yake haijatolewa, lakini Faru John na Faru mwingine sijui Yusta sijui nani, ametafutwa kwa nguvu zote.
Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge, haya mambo yanayoendelea mnakaa kimya; mnasikia mtu amepotea mnakaa kimya; mnasikia kuna damu imemwagika mnakaa kimya; mnafikiri hao sio watu; hii damu itanena. Hii damu itanena! (Makofi)
Mheshimiwa Spika, yaliyomkuta Mheshimiwa Nape juzi, yametukuta sisi siku za nyuma, yatamkuta kila mtu. Kama ambavyo wema ni mbegu, ubaya pia ni mbegu, kila mtu anavuna anachopanda. Wakati utafika, leo mko wengi, tulitarajia nyie ndio msaidie Taifa hili kwenda mbele.
Mheshimiwa Spika, leo alikuwepo Mwalimu Mwakasege hapa, wakati tunasali tukawa tuko na Wabunge wa CCM wengi tu, nami nilikuwa karibu na Mheshimiwa Juliana Shonza. Nikafumbua macho kidogo nikaona Wabunge tunasali kwa pamoja. Nikasema hivi zile kura za hapana hawa hawakuwepo! Nikasema hawa kwenye kura za hapana hawakuwepo! (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Spika, nchi hii isipoacha usiasa ndani ya Bunge, upande huu na upande huu, tusipoacha siasa za vyama ndani ya Bunge, Taifa hili tunalipasua! Leo inaonekana Vyombo vya Dola vina nguvu, leo inaonekana mna majeshi. Tumeongea habari ya Mahakama hapa mkasema tusiingilie Mahakama.
Mheshimiwa Spika, mimi nilishawahi kupewa mdhamana na ikasainiwa remand order. Nimekaa jela miezi minne, nina dhamana lakini sina masharti ya dhamana. Hakimu aliyefungwa mikono kuninyima masharti ya dhamana, alifunguliwa mikono kutoa masharti ya dhamana.
Tunapokuja kuongea habari ya Mahakama, hamwezi kujua vizuri mpaka mwende jela.
Mheshimiwa Spika, nimetoka jela, kuna mtu yuko jela mwaka wa tatu kwa kesi ya bangi ambayo akienda akaplead guilty Mahakama Kuu faini yake ni 18,500/=. Kuna Mwanasheria, Mheshimiwa Mwakyembe anamjua, amekaa jela anaanza mwaka wa saba, kesi yake ni money
laundering. Miaka saba! Hiyo kesi akikutwa na hatia pengine ni miaka minne jela. Kuna watu wanaozea jela. Ofisi ya DPP inatumika vibaya, tumetunga kesi mbaya. Nenda Keko, zimejaa watu kesi za money laundering. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna hasira inakusanyika kwenye mioyo ya watu. Hamuwaoni watu wanaandamana barabarani, watu wanaandamana ndani ya mioyo. Ipo siku watatoka barabarani bila sauti ya CHADEMA! Iko siku watatoka barabarani bila sauti ya CUF! Iko siku mtawakuta
barabarani!
Mheshimiwa Spika, Taifa hili litapasuka vipande viwili! (Makofi). Mheshimiwa Spika, huu uonevu mnaotufanyia, hatufanyi mikutano ya hadhara leo. Leo mkutano wachadhara nchi hii tumekatazwa…
SPIKA: Mheshimiwa Lema, muda hauko upande wako. Muda, muda, umekwisha.
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Spika, nina dakika zangu mbili, nilikuwa naangalia hapa. Dakika zangu mbili.
Mheshimiwa Spika, leo tumezuiwa kufanya mikutano ya hadhara. Tunaambiwa tufanye mikutano ya hadhara 2020. Ni sawa na kuliambia Kanisa lifanye Ibada Christmass. Ni sawa na kuuambia Msikiti ufanye Ibada Siku ya Idd! (Kicheko)
Mheshimiwa Spika, nyie mnafikiri ni kwetu, wakishamaliza kutushughulikia sisi, meno yale yale, msumeno ule ule, utakuja upande wenu. Ngoja watumalize kwanza, utakuja upande wenu. Nawaambia, kila mbegu mnayopanda mtavuna na tuko kushuhudia haya na Mungu ni shahidi. (Makofi).
Mheshimiwa Spika, ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge na Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kwanza niulize swali moja, hivi nyie Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lema unamuuliza nani?

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti nakuuliza wewe…

MWENYEKITI: Mwenyekiti haulizwi swali, Mwenyekiti anasikiliza michango…

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachangia.

MWENYEKITI: Haya changia.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nasema hivi sisi ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunapoishauri Serikali hatuishauri kwa sababu tuna chuki, tunaishauri kwa sababu hii ni nchi yetu. Sasa mara nyingi unaona unapoishauri Serikali kwenye mambo critical watu wanasimama kuomba miongozo na utaratibu, hatupo hapa ku-shine, tupo hapa kulisaidia Taifa. Ninyi mna-shine, ninyi ndio mna Serikali, ni Mawaziri tusikilizeni sisi tuwaambie muende mkafanyie kazi haya mambo. Hii nchi ikiharibika, inaharibika yote kama ambavyo mafuriko yakija hayachagui CHADEMA, CCM wala CUF. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, neno utawala bora linachukuliwa kirahisi sana, leo Taifa hili imefika mahali mtu hajatiwa hatiani na mahakama, anpata msamaha kama mtuhumiwa, yaani mimi napelekwa mahakamani leo, ninawekwa jela miaka mitano, ninaitwa nimetakatisha fedha halafu baadaye unatangazwa msamaha kwamba anayetaka kuomba msamaha aje; sijatiwa hatiani na mahakama kuitwa mwizi nasamehewa kitu gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unamkamata mtu mwaka wa kwanza, wa pili, wa tatu, wanne; mimi mwenyewe ukiniweka ndani kama familia yangu haipo stable, mke wangu na wazazi wangu watasema omba msamaha, kubali makosa uza nyumba ukae nje kuna maisha mengine zaidi ya haya. Kuna watu wanaomba msamaha leo si kwa sababu ya hatia, ni kwa sababu familia zao zimechoka kuona watu wakiwa ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu utawala bora tunaouongelea sio wa kwetu, kimsingi waliopo jela wengi ni wakwenu tukiongelea kwa mambo ya itikadi. Utawala bora tunaouongelea leo ni kulinda maslahi ya kila mtu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna uchaguzi mwaka huu, pengine asilimia ndogo sana ya Wabunge watarudi. Kwa namna kesi ya utakatishaji fedha na uhujumu uchumi zinavyoendeshwa sasa, kila mtu hapa ana-qualify kuwa mtuhumiwa na kwenda jela. Mimi nimekwenda magereza kuna watu wana M-Pesa 900,000 wamepewa utakatishaji fedha wapo magereza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, utawala bora sio kujenga barabara na kununua ndege, utawala bora ni kutengeneza misingi ya haki ambayo inadumisha utu katika Taifa hili. Mimi leo ukinipa barabara kilometa milioni moja Jimboni kwangu lakini ukamchukua mtu mnyonge maskini ukamuweka jela, huyu mnyonge kutoka jela ina maana kwangu kuliko barabara; utu ni wa msingi kuliko vitu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunavyosema utawala bora wa haki, tunataka Bunge liwe huru, mahakama ziwe huru na Serikali iwe huru. Tunapopingana na Serikali hatupingani kwa sababu tunamchukia Rais. Na hakuna mtu anasema kila kitu anachofanya Rais ni kibaya lakini nyie sio malaika na ndio maana mnapata usingizi na mnakufa, kwa vile sio malaika mkubali mshauriwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo hali ni mbaya, tunakwenda kwenye uchanguzi Mkuu mwaka 2020. Tumeona matamko huko nje ya UVCCM, matamko yanayotamkwa vijana wa UVCCM nikitamka mimi asubuhi saa 4, saa 6 nipo magereza na bila dhamana. Badala ya Serikali kuchukulia hatua matamko makali kama haya, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi anasema ninawaonya vijana wa UVCCM. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilihudhuria kesi za mauaji ya Rwanda Arusha, watu wote waliotiwa hatiani ni kwa sababu ya matamko. Tulinde Taifa hili kwa upendo, tulinde Taifa hili kwa kuonana sisi ni watu wema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ukikaa kantini Wabunge wanakaa kwa caucus, wanaogopa hata kukaa na sisi wakati wa Jakaya mnafumuana humu ndani, mkitoka nje jioni mnakwenda mnakunywa chai na juice; hiyo ndio ilikuwa siasa, leo siasa imeshindikana. Polisi ndio wanasaidia kuumiza watu; yakija maswali hapa mnakata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitagombania Ubunge mwaka 2020 kesho kutwa, sigombanii kwa sababu nitashinda ama nitashindwa, nagombania kuweka alama ya kwamba wakati demokrasia inapita kwenye majaribu, sikuogopa nilisimama imara nikapigana hii vita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi wote mnaweza mkarudi kwa sababu uchaguzi wenu hauamuliwi na kura, unaamuliwa na bunduki lakini nawaambia mnachojenga katika Taifa hili ni kitu kibaya sana kwa vizazi vinavyokuja. Ni bora Mungu awape hekima leo muone mnachokifanya. Utawala bora leo Mawaziri hawana confidence na ndio maana hakuna innovation. [Maneno Hayo Hapo Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmi ya Bunge]

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuwepo na uwezo…

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utaratibu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lema confidence ya Mawaziri subiri sasa, haya Mheshimiwa Jenista.

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nipo kwenye utaratibu na hilo la confidence ya Mawaziri wala sina shaka, nchi inatuona tuna confidence na tunafanya kazi ya kutosha. Kwa hiyo, hayo ni mawazo ya Mheshimiwa Lema. Mimi nakwenda kwenye suala la kiutaratibu, la confidence wala sitazungumza kwa sababu taifa linatuona confidence yetu na Rais wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba suala la utaratibu, Mheshimiwa Lema amesema hapa na jambo hili hatuwezi kuliacha kwamba ushindi ambao umekuwa ukipatikana kwenye chaguzi ndani ya nchi hizi umeamuliwa na mtutu wa bunduki. Jambo hili kwa mujibu wa taratibu, Kanuni ya 61(1)(a) jambo ambalo Mbunge hana uhakika nalo na si la ukweli hatakiwi kulisema Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua chaguzi zote zinaendeshwa kwa misingi ya sheria na Katiba.

WABUNGE FULANI: Aaaaaa!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mzuri kwa sababu Kanuni ya 63 inanitaka mimi ni-prove hiki ninachokizungumza, kifungu cha 44 cha Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kimesema kama kuna mtu ameona uchaguzi katika eneo lake haukuwa haki na
halali, ana uwezo wa kwenda ndani ya siku 30…

WABUNGE FULANI: Aaaaaa!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Nisikilizeni basi…

MWENYEKITI: Malizia Mheshimiwa, endelea. Waheshimiwa tutulizane basi amalize. Mheshimiwa Jenista naomba uendelee.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha 44 cha Kanuni za Uchaguzi kwa mfano kwenye Serikali za Mitaa tulizomaliza juzi kimeeleza wazi ndani ya siku 30 kama mtu ana ushahidi uchaguzi haukuwa halali aende akashitaki…

WABUNGE FULANI: Na weweee!

WABUNGE FULANI: Huyoooo!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, hatujapata hiyo kesi. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Jenista. Naomba tutulizane basi, Waheshimiwa Wabunge tusikilizane. Utaratibu ni hivi ndio ukweli wenyewe; Tanzania kama nchi haijawahi kupata ushindi wa aina yoyote kwa mtutu wa bunduki.

WABUNGE FULANI: Eeeeee!

MWENYEKITI: Sio hivyo sasa mnakwenda mbali hebu subirini. Tanzania kama nchi haikuwahi kupata sifa hiyo, kama kuna maeneo yametokea hayakufanywa kwa usahihi, sheria zipo hilo ndio lililozungumzwa. Mheshimiwa Lema tumalize hapo, kama umekusudia nchi nzima kwa maana ya Tanzania naomba ufute hiyo kauli.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushauri. Mheshimiwa Jenista kwa jinsi unavyopenda Uwaziri siku ukitumbuliwa unaweza ukafa baada siku mbili kwa sababu huwezi ku-defend kila jambo eti kwa sababu uonekane, kuna saa ku-chill ni wisdom, una-chill tu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe unajua haya mambo tunaongea unafahamu na ni hivi, hatufanyi ili kuwa Mbunge; nimeshakuwa Mbunge awamu mbili, hatufanyi mimi kuwa Mbunge. Tunaposema utawala bora katika Tume huru ya Uchaguzi, naomba niongezee muda tafadhali sana…

MWENYEKITI: Malizia.

MHE. GODBLESS J. LEMA:Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaposema utawala bora ulenge katika Tume huru ya Uchaguzi sio tume ya kuisaidia CHADEMA, tume ya ku-harmonize future ya Taifa hili. Kwamba kusiwepo na mashaka, ni hatari sana watu kufikiria eti huwa mnaiba kura. Hilo tu lenyewe ni hatari yaani tu kufikiria kwamba huwa mnaiba kura ni hatari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa cha muhimu ni nini, ili kuwa na future nzuri, wananchi wanatakiwa wawe na imani na uchaguzi, wananchi wakiondoa imani na uchaguzi, watatafuta alternative. Haya mambo yanahusu wajukuu na watoto zenu, wewe utakuwa mzee ama utakuwa umetumbuliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba hili suala lizingatiwe, sasa tukisema tuanze kuleta ushahidi hapa Pompeo mwenyewe amesema…

MBUNGE FULANI: Taarifa

MHE. GODBLESS J. LEMA: Pompeo amesema kwani hamuona Wamarekani wamesema nyie…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

WABUNGE FULANI: Aaaaa!

MWENYEKITI: Mheshimiwa Jenista.

MWONGOZO WA SPIKA

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mwongozo.

Nimwabie tu Mheshimiwa Lema kwamba humu ndani sisi Mawaziri tunapofanya kazi tunaendelea kulinda heshima na hadhi ya Serikali. Haya maneno ya kutumbuliwa ama kutokutumbuliwa hayatukatishi tamaa, sisi tunaendelea kupambana. Kwa hiyo, kwetu hiyo sio hoja na Mheshimiwa Lema wala asifikiri atanitoa kwenye hoja kwa kunitishia kutumbuliwa, huo utashi utani… (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, narudi kwenye mwongozo bado ninaendelea kusisitiza kwamba Ibara ya 74(7) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinaitamka Tume ya Uchaguzi kwamba ni idara huru. Ibara ya 11 na ya 12 inaeleza mipaka ya Tume ya Uchaguzi kutokuingiliwa na chama wala taasisi yoyote.

WABUNGE FULANI: Aaaaaa!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeomba hapa suala la kiutaratibu kwamba hatuwezi kama Ibara tu ya Katiba inaonesha uhuru wa vyombo tulivyonavyo, hawezi Mbunge humu akaendelea kusimama akadai kwamba uchaguzi tunaoshinda kwenye nchi yetu unatumia mtutu wa bunduki, haiwezekani. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Hivyo hivyo!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimalize kwamba ni lazima jambo hilo liondolewe kwenye hansard vinginevyo hatuwezi kumaliza kikao hiki kwamba nchi hii inashinda kwa kutumia…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. ESTER A. BULAYA: Mwongozo.

MHE. JOHN W. HECHE: Taarifa.

MWENYEKITI: Waheshimiwa ngoja nimalize moja halafu tutaendelea na lingine…

MHE. JOHN W. HECHE: Taarifa kwa Jenista

MWENYEKITI: Aah! Hakuna taarifa kwa Jenista, hakuna taarifa kwa Mheshimiwa Jenista. Mheshimiwa Heche naomba ukae chini…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge hebu tutulizane, Waheshimiwa Wabunge naomba tutulizane. Mnapoteza muda wa kuchangia mambo muhimu, kote nasema naomba mtulizane. Ikiwa kama tunahisi kwamba Katiba inasema ipo sahihi na Katiba lazima wote tunaiamini na ndio tunaapa kwa Katiba hapa. Ikiwa Katiba inasema kwamba tume ni huru na imepewa mamlaka kamili kama kuna Katiba imevunjwa pahala tunajua taratibu zipo wapi, kama hamkwenda mtulie mnyamze mnasema kitu ambacho sicho.

Mheshimiwa Lema nilikwambia pale mwanzo kwamba nchi hii haikuwahi kupata ushindi kwa mtutu wa bunduki kwa maana ya Tanzania. Kwa hiyo, ili umalizie vizuri mchango wako naomba hiyo kauli uifute na kama hujaifuta nitaiondosha kwenye hansard.

MHE. ESTER A. BULAYA:Mheshimiwa Mwenyekiti, mwongozo.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chief Whip naomba utulivu, kwa hilo naomba utulie amalizie kuchangia Mheshimiwa Lema.

MBUNGE FULANI: Taarifa.

MHE. ESTER A. BULAYA: Mwongozo wa Mwenyekiti.

MWENYEKITI: Lema amalize kuchangia…

MHE. ESTER A. BULAYA: Ni haki kama aliyokuwa nayo Jenista Mhagama upande wa Serikali, nijibu mwongozo wa Mwenyekiti.

MWENYEKITI: Naomba amalize Mheshimiwa Lema halafu utazungumza.

MHE. ESTER A. BULAYA: Mwongozo wa Mwenyekiti

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. ESTER A. BULAYA: Mwongozo wa Mwenyekiti, nina haki kama aliyokuwa nayo Mheshimiwa Jenista Muhagama upande wa Serikali Chief Whip. Mwongozo wa Serikali.

MBUNGE FULANI: Ndiyo

MWENYEKITI: Naomba amalize Mheshimiwa Lema nitakupa ruhusa, muache Mheshimiwa Lema amalize.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MWENYEKITI: Nakupa nusu dakika umalizie Mheshimiwa Lema.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nusu dakika ni wewe bora uiondoe kwenye hansad ila mimi siwezi kufuta ukweli. Ni sawasawa na kuanza kujisachi kama mimi ni mwanamke ama ni mwanaume. (Makofi/Kicheko)

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Taarifa.

MHE. GODBLESS J. LEMA: uchaguzi sio huru kwa hiyo kama unaiondoa kwenye hansard hakuna shida lakini mimi siwezi kufuta.

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Taarifa.

MWENYEKITI: Hapana, Mheshimiwa Lema nakwambia hivi kwamba kauli uliyozungumza si kauli sahihi, hata ukienda kwenye Kamati ya Maadili utatuhumiwa kwa kosa lako. Tanzania haikuwahi kupata ushindi kwa mtutu wa bunduki, kwa hiyo naomba ufute hiyo kauli…

MBUNGE FULANI: Hataki

MBUNGE FULANI: Atoke nje, atoke nje.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Tulishinda kesi ya uchaguzi Ndalambo kule Momba na mahakama ilisema polisi walitumia silaha kutangaza…

MWENYEKITI: Hiyo sio Tanzania, ni sehemu ndogo sana. Kwa hiyo, naomba hiyo iondoke nimeshaiondoa kwenye hansard. Malizia mchango wako, haya umeshamaliza basi ukae chini.

MWENYEKITI: Tayari, Mheshimiwa Lema naomba tumalize hapo basi…

MHE. GODBLESS J. LEMA: Nimemaliza?

MWENYEKITI: Naomba ukae chini tumalize basi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Naif Abazeed alikuwa ni kijana mdogo sana kipindi hicho wa miaka isiyozidi 16 na ndiye alisababisha machafuko yanayoendelea Syria sasa hivi. Pia Mohamed Bouazizi yeye ndiye aliyesababisha machafuko yaliyotokea kule Tunisia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mwanaharakati mmoja alisema maneno haya, naomba niyasome:-

“Kitu kimoja tu cha hakika ni kuwa, damu ikimwagika hasa damu ya kimapinduzi hutoa mvuke utakaonyesha na kutiririsha mafuriko katika mito na vijito vya haki. Kama itanyesha mvua ya radi basi itaambatana na mwanga na cheche zitakazowamulika walaghai, watesaji, wakandamizaji wa haki na watetezi wa haki watapata mwanga katikati ya giza totoro la unyanyasaji.” (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maneno haya ni message ya mwisho ya Ben Saanane ambaye hatujui kama ni marehemu ama ni hai, lakini hata kumjadili humu haturuhusiwi, nje mikutano ya hadhara hatufanyi. Kama kijana wa miaka 16 katika Taifa ambalo halina uhuru wa vyombo vya habari, halina chama cha siasa, aliandika maneno machache tu, “Assad must go, Assad will be next,” leo Syria haina amani. Kama kijana mmoja alijichoma moto Tunisia na Tunisia ikaingia kwenye machafuko, vyama vya siasa ni alternative ya amani, uhuru wa habari ni alternative ya amani siyo kikwazo cha amani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wanapoongea wanatema nyongo. Watu wanapoongea wana-release tension, leo tunapotaka kujadili mambo ya msingi mnatumia nguvu na uwezo mlionao, mtashinda. Kila jambo mnalotaka kulipitisha kwa wingi wenu mtashinda. Kila jambo mnalotaka kulifanya kwa wingi wenu mtatushinda. Kwenye mchango wangu uliopita nilisema Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu ndicho avunacho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilikuwa magereza, vijana waliokamatwa kwa makosa ya cyber walioko magereza, makosa ambayo ni bailable offence ni wengi. Wanakamatwa kimya kimya wanapelekwa mahakamani, wanasomewa mashtaka bila ndugu zao kuwepo, wanapelekwa magereza. Vijana wamejaa magereza kwa sababu ya ukosoaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nimeona kwenye mitandao na mimi naomba nipaze sauti kabisa kwamba Kinana naye amefichwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba nimtetee Kinana kama Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani. Kama ni kweli Kinana amefichwa, kwa mujibu wa mitandao kwa sababu hata Ben Saanane kupotea tuliona kwenye mitandao, tukapuuza. Hii ya Kinana kama ninyi mtapuuza, mimi sitaki kupuuza, ni mpiga kura wangu Arusha, naomba nimtetee.
heshimiwa Mwenyekiti, kuna mtoto mmoja alipewa shilingi 200,000 na baba yake akaambiwa akalipe ada. Alipokuwa njiani akaenda aka-bet mchezo kwa shilingi 30,000. Alipo-bet akapata shilingi 3,000,000. Akamtumia baba yake message akamwambia, baba ile pesa uliyonipa ya ada nimetumia shilingi 30,000 nime-bet. Sasa baba kabla hajajua mtoto alipata faida ya shilingi 3,000,000 akaanza kumtukana mtoto, mjinga wewe, kwa nini umetumia fedha kufanya mambo yako ya kitoto? Mtoto akamwambia, baba hapana, nime-bet shilingi 30,000 nimepata shilingi 3,000,000. Baba akageuka akamwambia si unge-bet yote upate nyingi? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, iko siku tutawabariki na mtakataa baraka. Yaani iko siku tutawatetea kabisa na mtakataa utetezi wetu kwa sababu kila mara tunapokuja na mambo ya msingi mnafikiri sisi ni maadui zenu. Ninyi sio maadui zetu, ninyi ni marafiki zetu, nyie ndiyo chama tawala. Leo tumeongea habari ya Ben Saanane mkakataa, nikaongea habari ya Katibu Mkuu wenu hata kama ni tetesi mlitakiwa mzichukulie maanani mseme huyu kijana ana roho nzuri, mmekataa, sasa nimeondoka huko. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uhuru wa habari ni nini? Nimesema kwenye hoja zangu nilizojenga, hatuwezi kuwa na Taifa lenye amani bila kuwa na uhuru wa habari. Mheshimiwa Tundu Lissu amewaambia asubuhi hapa kwamba msifikiri mnatunga sheria ama msifikiri mnatumia wingi wenu kutukomoa sisi, mna watoto na wajukuu wanakua. Mheshimiwa Mkuchika hapa amesema yeye ana umri mkubwa, ni kweli ana umri mkubwa ndiyo maana kuna saa mambo mengine ya msingi yanaweza yakampita, lakini ninachosema ni kwamba Mheshimiwa Mkuchika ana watoto, ana wajukuu nawajua. Tunapopigania uhuru wa habari hatupiganii CHADEMA, tunapopigania uhuru wa habari hatupiganii CCM, tunapigania Taifa bora na Taifa huru. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ndiyo tukasema leo ndani ya Bunge hatusemi na kwenye mitandao hawaongei. Sasa kama kwenye mitandao hawataongea, vyombo vya habari havitasema, huko mitaani mikutano ya hadhara imezuiwa ndiyo maana nikaanza kujenga hoja kwa wale vijana wawili, yule wa Syria na yule wa Tunisia kwamba iko siku watu wataingia barabarani kutafuta uhuru mnaowanyima. Watu hawa hawatakuwa wametumwa na CHADEMA wala hawatakuwa wametumwa na CUF na siku hiyo kila mtu atatafuta nyumba ya kujificha, iko siku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu unapozuia haki, unapozuia uhuru, unapozuia kweli, unatengeneza balaa katika Taifa hili. Tunalalamika kwa sababu familia zetu zinaishi hapa, tunalalamika kwa sababu sisi tunaishi hapa tumejenga Tanzania, tumeishi Tanzania, tumezaliwa Tanzania, tungekuwa na mpango wa kuondoka tungeenda kulalamikia Marekani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukisema miongozo ni mingi na sijui hata hotuba yangu itakuwaje sasa kama hotuba ya Waziri wa Michezo, Habari na Utamaduni mmeifanya hivi, hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani na uzoefu wa Lijualikali alivyokuwa Magereza, uzoefu wangu nilipokuwa magereza mtaanza kuizuia kuanzia kwenye salamu. (Makofi)

Waheshimwa Wabunge mko wengi tusaidieni, Mawaziri tusaidieni huku kuna madaktari, kuna maprofesa tusaidieni, taifa hili tukishamalizwa sisi, narudia tena, tukishamalizwa sisi, msumeno utakaofuatwa utakuwa ni kwenu. Ni nini mnachokipigania Waheshimiwa Wabunge mnakipigania mnafanya kila kitu kinakuwa hovyo, ni fedha?

Mheshimiwa Mwenyekiti, utu wa mtu haupimwi kwa ghorofa, utu wa mtu haupimwi kwa cheo, utu wa mtu unapimwa kwa kazi na wajibu ulioufanya katika ulimwengu na wajibu huo ninyi kama Chama Tawala, mnaweza mkaufanya, sisi tutashindwa. Mimi nilikamatwa nje getini hapo, nikapelekwa Kondoa, nikawekwa lockup saa nne usiku mpaka saa nane usiku. Nikapelekwa Arusha nikatengwa chumba changu peke yangu, nikakaa jela nikatoka baada ya miezi minne. Mnaweza mkafanya hivyo leo, mimi mkitaka kuniua mnaniua leo, kesho ni mbali, mkitaka kumuua yeyote hapa mnamuua leo, kesho ni mbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema hivi haya mambo mnayotuzuia kuyasema mnafikiri tunayasema kwa sababu tunapenda uanaharakati, mimi na watoto na mtoto wangu wa kwanza ana miaka 11 na wa mwisho ana miaka minne, ningependa kuona watoto wangu, ndoa, harusi na elimu ya watoto wangu kwa macho yangu. Hata hivyo, ikibidi nisione hiyo harusi kwa sababu ya kupigania ninachokipigania watakumbuka kwamba maisha yetu Bungeni hayakupigania property yalipigania haki na msingi wa Taifa hili kazi hii ambayo mmeishinda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimwa Wabunge, Waheshimiwa Mawaziri, hapo alikaa Mzee Sitta leo ni marehemu, kila mtu atapita kwa wakati wake. Ni muhimu mkapita mkaacha faraja nyuma, ni muhimu mkapita mkaacha baraka nyuma, acheni kutumia wingi wenu vibaya.

Mheshimiwa Simbachawene wewe una historia, wewe ulikuwa kondakta, Mungu amekuweka hapo ulipo, tulitarajia tukuone wewe unapigania nchi hii, tulitarajia tukuone wewe unakumbukumbu ya haki na msingi, leo unaishi utafikiria umezaliwa kwenye familia Warren Buffet kila watu wakisimama kuongea ukweli …(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Itifaki ya Nagoya ya Kusimamia Upatikanaji na Mgawanyo Sahihi wa Faida zitokanazo na Matumizi ya Rasilimali za Kijenetiki.
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshikiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Nikazie pale alipoishia Mheshimiwa Msigwa na Waheshimiwa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi niwaombe sana, hili Bunge ndiyo think tank ya nchi. Demand yetu ya kupata nyaraka muhimu kwa ajili ya kuishauri Serikali ni kwa sababu ya kutoa opinion ambazo zitawasaidia ninyi na Taifa letu na watoto wa watoto wetu. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, opinion zetu kila mara zinaonekana ni uadui, na hii ndiyo inasababisha kuanza kususiana futari, hii ndiyo inasababisha uhasama unakuwa ni uhasama. Kwa sababu hakuna opinion yetu ya msingi ambayo ninyi mtaichukua kama ni jambo muhimu katika Taifa hili. Sisi sote ni Watanzania, mnapokuja na hizi nyaraka sasa hivi naongea hapa hakuna hata hiyo hotuba ya Kambi ya Upinzani haipo mezani. (Makofi)

Mheshikiwa Mwenyekiti, leo tu asubuhi hapa tumeambiwa tutajadili habari ya Mikataba na Sheria za Madini mpaka Jumatano mwisho. Sheria hizo mnaleta kwa Hati ya Dharura. Wabunge wamekaa hapa miezi mitatu, wamechoka. Binadamu anapochoka ana-loose capacity ya ku-focus, leo tunaenda emotionally. Kwa sababu makinikia na ripoti zimesomwa mbili kwa Rais, television mkapeleka nchi nzima kwenye masoko waone, sasa leo mnataka ku- implement jambo hilo ndani ya siku nne, kinachotokea ni nini? Kitakachotokea mtafanya makosa yale mliyoyafanya kipindi cha mwanzo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi ndiyo Serikali, haya mambo kama yana umuhimu kwa kiwango hiki wapeni Wabunge hizi nyaraka wazisome, wapeni Wabunge hizi nyaraka wazipitie. Sasa kazi ya Mheshimiwa Jenista Mhagama hapa yeye, iko siku atatokea mtu huku aseme amegundua dawa ya UKIMWI, Mheshimiwa Jenista utasimama uombe utaratibu na ukatae kabisa, kama hiyo itakuwa inatibu kwa sababu haiwezekani kila opinion yetu mnaikataa, tunasema hakuna nyaraka mnakataa, tunawaambia hivi mnakataa, sasa tuishauri, futeni basi upinzani tubaki chama kimoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipindi kile CCM mko peke yenu kulikuwa kuna G7 tukiwa wadogo, mlikuwa mnashindana lakini mlikuwa hambaguani, sasa hivi tunaanza kupishana na tunaanza kubaguana. Narudia tena hiki mnachoendelea kupanda kitatoka hapo nje ya Bunge, kitakwenda mitaani. Haya yanayotokea Kibiti msishangae siku moja yakasambaa nchi nzima kwa sababu ya chuki zinazojengwa ndani ya Bunge hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya Mbunge ni kutoa ushauri sasa nitoe ushauri gani zaidi ya huu? Huu ndiyo ushauri, nasema hizi chuki mnazojenga ndani ya Bunge ndiyo zitatoka hapo nje, zikitoka hapo nje zitakwenda mitaani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia tena itafika mahali nchi hii itakuwa ni sehemu mbaya ya kuishi kwa sababu ninyi mlio wengi mmekataa kuchukua opinion zetu za msingi kwa sababu tu tumeitwa Wapinzani, utafikiri tumetoka Sudan sasa leo tunajadili mambo ya itifaki. (Makofi)

Haya mambo ya mazingira, DC wa Hai alikwenda akavunja vunja shamba la Mheshimiwa Mbowe, Sea Cliff Hotel na Golden Tulip ziko baharini sasa kwa sababu issue hapa ni itifaki ya kuridhia mazingira bora ya bahari na hizi hoteli basi zilizopo kando kando ya bahari zipigwe marufuku kabisa, ziwe mita 120 kutoka ufukwe wa bahari, kwa sababu issue kama leo ni itifaki ya mazingira ya bahari ambayo leo mmeilete hapa, ipi ilikuwa ni muhimu? Kwenda kuvunja shamba la mboga ama kuondoa Sea Cliff iliyoko pale kando kando ya bahari ambapo vichungi vya sigara vinatumbukizwa mle ndani? (Makofi)

Kwa hiyo haya mambo ya itifaki nilikuwa nataka tu niwaambie tu hichi ninachowaambia hivi mnavyoishi endeleeni, ila nawaaambia iko siku kama ambavyo sasa hivi hata issue za Kibiti mnaogopa kuzijadili utafikiri hamna kitu kinachiendelea. Kila mtu anaogopa kujadili humu ndani, Waziri wa Mambo ya Ndani naye anaogopa, nani anaogopa, Usalama wanaogopa kwa sababu mkianza kujadili tu ni kwamba jamaa wanaweza wakaja na hii inasababishwa na hasira ya wananchi. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana hasira hizi ambazo mnawapandikizia wananchi, mambo haya mnayotufanyia humu ndani ya Bunge, mnatuzuia tusiseme, mnatuzuia tusitoe opinion zetu, ninawashauri vunjeni siasa za vyama vingi katika Taifa hili mbaki wenyewe na familia zenu na wajukuu zenu.
TAARIFA YA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE KUHUSU SHAURI LA KUDHARAU NA KUDHALILISHA BUNGE LINALOMKABILI MHE. HALIMA JAMES MDEE (MB)
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Sidhani kama naweza nikashawishi Bunge kuondoa adhabu ambayo imeshakuwa proposed na Mwenyekiti wa Kamati. Maneno yafuatayo ndiyo yanamfanya Mheshimiwa Halima apendekezewe adhabu kubwa kwa kiwango hicho. Nnaomba niyanukuu: “Kitendo cha CAG cha kusema kwamba hali siyo nzuri halafu chombo kinachotakiwa kusimamia hali hakifanyi hivyo, ni kitendo cha kijasiri na nina imani kwamba wanaoongoza huo mhimili watakuwa wavumilivu, hawatafikiria kumuita kwenye Kamati ya Maadili kwa sababu tumeitwa dhaifu kwa sababu kweli ni dhaifu. Roho ya mwenendo wa nchi unategemea uimara wa Bunge. Sasa amesema Bunge ni dhaifu ni kweli na mimi kama Mbunge wa vipindi vitatu nathibitisha hilo.” Mimi ni Mbunge wa vipindi viwili nathibitisha Bunge hili ni dhaifu. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lema kwa maneno hayo uliyoyasema na wewe unapelekwa kwenye Kamati ya Maadili na ukae hakuna mchango tena. Kwa sababu tunajadili adhabu kuhusu maneno hayo na wewe unasema unayathibitisha na wewe utaelekea kwenye Kamati ili ukathibitishe vizuri kule. Kwa hiyo, Kamati ya Maadili huyu naye analetwa kwenu kwa utaratibu wa kawaida. (Makofi)

Tunaendelea na Mheshimiwa Goodluck Mlinga.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, huna...

NAIBU SPIKA: Umeshapewa adhabu Mheshimiwa kwa hiyo wewe…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lema, naomba ukae, Mheshimiwa Lema naomba ukae.

Tunaendelea na Mheshimiwa Goodluck Mlinga, tutamalizia na Mheshimiwa Dkt. Christine Ishengoma.
Azimio la Kufuta Hasara itokanayo na Maduhuli ya Madeni ya Nyuma ya Ada na Leseni za Magari, Riba na Adhabu kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni, 2019
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Kwa kuanza nianze na alipomalizia Mheshimiwa Mbunge tumweleze kwa nini Kambi Rasmi ya Upinzani tuna mashaka. Mimi ni Mbunge awamu ya pili ndani ya Bunge hili na miaka yote yalipokuja masuala yanayohusu pesa nyingi kama hizi tulitilia mashaka suala la Meremeta, Kagoda, Escrow na IPTL. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni Wabunge wa upande huo huo walisimama wakasema IPTL ile pesa ilikuwa ni pesa ya watu binafsi na Mheshimiwa Rais akaongea na Wazee wa Dar es Salaam akawathibitishia kwamba wakati huo Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete kwamba ile pesa ilikuwa ni pesa ya watu binafsi haihusiani na Serikali. Leo tunavyoongea Wakurugenzi wa IPTL wako Magereza kwa zaidi ya miaka miwili kwa pesa ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani ilitilia mashaka na mashaka hayo yakapuuzwa ndani ya Bunge na leo kuna watu wanaitwa wezi, wamepewa kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha na wanaendelea kuteseka Magereza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, uzuri jana Mheshimiwa Rais amesema walaaniwe wale wanaowaweka wenzao Magereza muda mrefu. Nami naunga mkono Azimio la Mheshimiwa Rais, kwamba walaaniwe wanaosababisha watu kukaa Magereza muda mrefu, hata kama Mheshimiwa Mbowe alaaniwe na hata kama ni Rais mwenyewe ama ni DPP ama ni wewe Mheshimiwa Spika ama ni mimi tulaaniwe wote tunaosababisha watu kukaa Magereza muda mrefu kwa kesi za kubambikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, najenga kwanza hoja kwa nini mashaka yetu ni ya msingi kwenye pesa kama hizi. Hii Sheria tulipitisha mwaka 2016/2017 ilikuwa ni Sheria ya kuondoa Motor vehicle license kutoka kwenye kulipia dirishani kwenda kwenye mafuta. Sasa wasiwasi wetu nasema uchaguzi ni kesho kutwa na tunaona mnavyolilia hela kwa Mabeberu, sasa tunasema pengine hizi pesa wanataka kwa ajili ya uchaguzi ziwasaidie, pengine hizi pesa kwa sababu Stigler‟s Gorge imewekewa mguu sasa pengine wanataka pesa kwa ajili ya kusaidia mambo yao…

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mmeanza?.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lema kuna taarifa, Mheshimiwa Goodluck Mlinga.

T A A R I F A

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimpe taarifa mzungumzaji anayezungumza kweli tunakubali Mheshimiwa Lema ni Mbunge wa awamu ya pili, lakini katika rekodi zangu hapa zinaonesha muda mwingi alikuwa akitumikia adhabu za Bunge na muda mwingine alikuwa jela kwa hiyo hana uzoefu wa kukaa ndani ya Bunge muda mrefu. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lema…

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, napokea taarifa na wale wale wanaosababisha wenzao wafukuzwe Bungeni kwa kuonewa twende kwenye Azimio la Rais na wenyewe walaaniwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wale wote ambao wanasababisha wenzao wateseke, waondoke ndani ya Bunge lile lile, yaani mtu yeyote anayeonea alaaniwe. Kwa hiyo napokea taarifa yake na tukubaliane kwamba na wenyewe wale kama walihusika kwenye Kamati kama ni Kiti kumwonea mtu walaaniwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nasema hivi haya …

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lema kwa sababu wewe huwa unasoma sana Biblia, hiyo laana lazima uiweke mazingira ambayo hata wewe mwenyewe unayesababisha watu wengine wafanye maamuzi na wewe ikupate, kwa hiyo usiwe mtaalam wa kugawa laana halafu wewe mwenyewe hutaki ikupate. Kwa hiyo na wewe mwenyewe pia ikupate kwa yale ambayo unasababisha watu wafanye maamuzi ya kukuweka ndani maamuzi ya kukutoa nje, yote hayo pande zote mbili inakuwa inapendeza zaidi. (Makofi)

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, mimi kama ni sababu ya watu kupata tabu nilaaniwe na wewe kama ni sababu ya kufukuzwa watu Bungeni, ulaaniwe, haina shida. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ninachosema tunajenga haya mashaka na Waheshimiwa Wabunge watuelewe, haya mashaka tunayajenga kwa sababu moja tu ya kwamba hili Azimio linakuja wakati Assad kaondolewa Ofisini na sisi tuna mashaka makubwa sana na Bunge hili lilikuwa na imani Profesa Assad. Sasa tunasema hizi pesa ni nyingi sana isije ikawa baada ya Bunge hili ama Awamu ya Utawala wenu akatokea Rais mwingine akaandika kitabu kama alivyoandika Mheshimiwa Mkapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mkapa ameandika kitabu amefanya confession, lakini Taifa limeumia Taifa limepata hasara, sasa wasiwasi wangu nina …

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa …

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lema kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Peter Serukamba.

T A A R I F A

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kumpa taarifa Mheshimiwa Godbless Lema, taarifa hii ambayo tunaiongelea ambayo ni Ripoti ya CAG aliyeisaini ni Profesa Assad. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lema kabla sijakuuliza kama unaipokea taarifa hiyo umemtaja hapa Mheshimiwa Rais Mstaafu Mkapa kwamba kwenye kitabu chake kuna jambo amelisema ambalo unaona nchi imeteseka sasa ili uweke kumbukumbu vizuri za Bunge, uwe umelisema na lenyewe maana hicho kitabu hata sisi wengine pia tumesoma ili kumbukumbu zikae sawasawa, maana zisije zikakaa kwamba Mheshimiwa Rais aliyepita alisema jambo lililoumiza nchi watu wanaumia halafu likaachwa hivyo hewani. Kwa hiyo kwanza unaipokea taarifa hiyo ya Mheshimiwa Peter Serukamba?

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, naipokea.

NAIBU SPIKA: Haya.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika…

NAIBU SPIKA: Hilo la pili sasa refusha pale kwenye ule mjadala wako.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mkapa ameongea kuhusu Mauaji ya Zanzibar ambapo leo kuna wajane, watoto na ame-confess mwenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ndiyo, ndiyo kwenye kitabu chake.

NAIBU SPIKA: Aahha. Mheshimiwa Lema kuna mambo mawili umeyazungumza. Hoja ya ku-confess maana yake ameandika na kama kitu kinachoaitwa confession ndio maana huwa tunapenda maneno yatumike ya lugha moja, kinachoitwa confession ni kitu ambacho unakubali kwamba kuna jambo fulani hivi ulishafanya. Confession ni lugha ya Kisheria sasa wewe ukisema ame-confess ni kana kwamba wewe unavyoyaeleza hayo mauaji ame-confess nini kwa sababu mimi mwenyewe kitabu nimesoma? Sasa ili tutunze muda wetu vizuri aidha, uyaondoe hayo uendelee na jambo lingine au kama unataka kuyaweka eleza ame-confess nini kwa sababu kitabu na mimi nimekisoma na ameelezea mauaji ya Zanzibar kwa kawaida tu kama alivyoeleza sehemu nyingine. Ameeleza kwamba yalitokea, kwa hiyo akisema yalitokea ni kwamba ni kweli watu walikufa, hakuna mtu anayekataa kwamba kuna watu hawakufa.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, kile kitabu cha Mheshimiwa Rais Mkapa siyo fiction, ni kitabu ambacho ameelezea maisha yake ya Uongozi na Utawala wake na akasema vitu ambavyo anavikumbuka ambavyo vimetia doa maisha yake ya utawala ni pamoja na hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hata hili la Mkapa ambalo ameandika mwenyewe mnataka kuli-defend? (Kicheko)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lema…

MHE. GODBLESS J. LEMA: Ndio …

NAIBU SPIKA: Lazima uwe tayari kuelewa unachoelekezwa, usitake kupindua unachoelekezwa, hapana. Nimekueleza hivi ukitumia neno confession ni kwamba anakubali jambo Fulani, sasa alichokifanya ameeleza uhalisia kwamba kifo kilitokea na yeye hafurahii, sasa unavyosema ame-confess, ame-confess nini? Kwamba yeye ndiye aliyeua ama alituma mtu kuua. Kwa hiyo uwe unaeleza vizuri jambo namna alivyosema Mheshimiwa Rais kwenye kitabu chake, usiongezee wewe ya kwako kwa sababu kile ni kitabu chake yeye.

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nimekuelewa, naomba niazime maneno yako halafu ndiyo yaingie kuwa mchango wangu kwamba Mheshimiwa Mkapa amesema kama ulivyosema, halafu tuendelee. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni hayo hayo tu, nimeazima lugha yako kwa sababu imekaa kistaarabu, nafikiri unataka niwepo kwenye hili Bunge mpaka mwisho, kwa hiyo nimeazima lugha yako nisiingie hatiani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo mashaka yetu kuhusu hizi pesa najiuliza tu Mheshimiwa Waziri Mpango toka mwaka 2016…..

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa.

WABUNGE FULANI: Hapana jamani. Eeh.

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa.

WABUNGE FULANI: Hapana.

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa, huku kushoto kwako.

WABUNGE FULANI: Hapana.

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, Dkt. Mollel huku.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge leo tuna mambo mengi kidogo hii itakuwa ni taarifa ya mwisho.

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, namwelewa Mheshimiwa Lema anapokuwa na wasiwasi na vilevile yeye kama Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alaaniwe, kwa sababu wakati nina bajeti hapa ya kama trilioni tatu ambayo baada ya ile taarifa yao waliyotoa CHADEMA au Mheshimiwa Mbowe pale Dar es Salaam, walijipanga kwenda kutafuta nje trilioni tatu kuja kufadhili mkakati wao ambao ni mchafu kwenye nchi yetu na ninyi mlaaniwe ambao mnatengeneza mazingira ya fujo kwenye Taifa hili kwa kutumia hela za Mabeberu halafu mnakuja…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa…

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, halafu mnakuja kusema mwisho wa siku mnataka laana halafu…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lema malizia mchango wako …

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niwashukuru Chama cha Mapinduzi kutuchukulia Mheshimiwa Dkt. Mollel, Mungu awabariki sana. Hebu imagine huyu alikuwa kwetu, halafu ukatokea muujuza yuko kwenu kwa hiyo, niwashukuru sana kwa kweli Mungu awabariki sana na kama kuna wengine mmewaona huku wako kama hivyo tafadhali fanyeni kazi kwa bidii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hebu imagine alikuwa ni Mbunge wetu wa Siha. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Endelea …

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, halafu ninyi mkatumia mikakati yote akawa wa kwenu, mimi nikushukuru, nishukuru Chama cha Mapinduzi, nimshukuru Katibu Mkuu, nimshukuru na Mwenyekiti wa Chama Taifa na kama mkiwaona wengine kama hawa kwa kweli tusaidieni ili tuweze kujenga chama kizuri. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninachosema ni nini? Namheshimu sana mimi binafsi Mheshimiwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mpango, ninachosema kwamba 2016/2017, ndiyo tulipitisha hii Sheria sasa 2016, 2017, 2018, 2019 na 2020 miaka minne baadaye ndiyo mnaleta Azimio la kufuta deni la almost half a trillion? Sasa tunasema hapa kuna dili na tukasema hii tabia mmeanza lini?

Mheshimiwa Naibu Spika, ninyi huwa mnapeleka, mlianza kujenga Chato bila Azimio mlihamishia Dodoma hapa bila Azimio, mkaenda huko Stigler‟s Gorge bila Azimio, mkaenda kwenye ndege bila Azimio, sasa hii tabia nzuri mmeanza lini?(Makofi/Kicheko)

NAIBU SPIKA: Muda wako umeisha, Mheshimiwa kengele imeshagonga, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na naomba tu Wizara ifuatilie sana ushauri alioutoa Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna Wizara sensitive kama Wizara ya Mambo ya Nje kwa sababu dunia ya leo imekuwa kijiji. Katika mambo yanayohusu biashara na uchumi wa kidiplomasia kati ya mataifa na mataifa, engagement ya Wizara ya Mambo ya Nje ni muhimu sana kwa ajili ya kutoa ushauri ni mambo gani yanatakiwa kufanyika? Hatua ya kulinda rasilimali za nchi hii ni mtu mwendawazimu anayeweza asipongeze; lakini namna gani unalinda rasilimali za nchi hii, inaweza ikaligharimu sana hili Taifa na kuliingiza kwenye consequences nyingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Taifa hili wote tunafahamu kwamba nchi hii ina mgogoro na Acacia Mining, mgogoro huo kwa sura ya kwanza unajenga hisia na sifa za kisiasa ndani ya nchi, lakini sura ya pili ya mgogoro huu unakwenda kabisa ku-demoralize spirit ya investors walioko nje kuja katika Taifa hili kufanya investment. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo tu Acacia, ukiangalia ardhi kwenye Wizara ya Mheshimiwa Lukuvi, imekuwa ni sifa kunyang’anya watu ardhi na imekuwa ni sifa kunyang’anya wawekezaji ardhi, jambo hili mbele ya safari litalifanya Taifa hili liende likawe kama Zimbabwe. Wakati Mugabe anaanza sera hii ya kunyang’anya watu mashamba, kuwakandamiza investors wa nje, alipigiwa makofi na wananchi wake kama ambavyo leo tunapigiwa makofi, lakini leo ninavyoongea kwenye Bunge hili, Zimbabwe hawana noti yao, hawana fedha yao, ni Taifa ambalo limepoteza hata identity. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri, ni muhimu sana mkamshauri Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia suala la Acacia Mining, linaonekana linapongezwa na kila mtu, lakini consequences zake; leo tuna taarifa kwamba Acacia wanakwenda Mahakamani London. Concequences zake Taifa hili litakuja kuingia kwenye gharama kubwa kama lilivyoingia kwenye ile minofu ya samaki na meli kule Dar es Salaam. Kwa hiyo, ni muhimu tukajenga mahusiano. Siasa na biashara ni vitu vinavyofanana. Mwanasiasa imara, mwanasiasa makini ni mwanasiasa atakayejua maana ya uchumi. Hawa wananchi wanaoshangilia leo, baada ya miezi miwili, mitatu watakosa chakula; wakishakosa chakula itakuwa rahisi kuingia barabarani kuliko wangeingia barabarani kudai mikutano ya hadhara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunashangaa mnafanya nini? Leo uchumi umeyumba. Ukienda hapo Kenya, tumemwona Uhuru Kenyatta amekwenda kwenye mkutano wa G7 Summit. Uhuru anakwenda ku-present paper kuhusu Taifa lake. Leo Peugeot wameweka plant yao kule Kenya, kiwanda cha magari kinakuja Kenya. Unajiuliza, hivi kweli Wizara ya Mambo ya Nje inafanya nini? Ukienda kwenye Ubalozi, Mabalozi wanalia. Kama mishahara yao haifiki kwa wakati, wanawezaje wakafanya hiyo connectivity ya kupata wawekezaji kuja huku? Kitakachoondoa wawekezaji, hata hii bajeti mnayopitisha, mimi mwenyewe ningekuwa ni mwekezaji, nasikia mambo mnayoyafanya kwa hizi multinational companies, ningevuta subira kwanza nione hali inakuwaje? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ni shahidi kwamba Wazungu wanapokuja kufanya investments za mabilioni, wanaangalia pia future ya nchi hiyo kisiasa. Leo nchi hii masuala ya kidemokrasia yamepigwa marufuku, leo nchi hii mikutano ya hadhara imepigwa marufuku. Maana yake, kwa investor yeyote ambaye yuko serious anataka kuja kufanya investment ya hela nyingi atasema Taifa lile hawana political stability. Maana yake ni nini? Maana yake hawatakuja…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo na Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na ninaomba niwakumbushe Wabunge wote kwamba hili ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge ndio watunzi wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge ndio watunga sera za maendeleo ya taifa hili. Unapokuwa na chombo kama hiki na mizaha ya ajabu ajabu kama inayoendelea, this is the very serious humiliation for this country. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kutoa pole kwa Mheshimiwa Spika, nafahamu yuko India kwa ajili ya check-up na matibabu na vilevile Mheshimiwa Lissu ambaye na yeye yuko Ubelgiji kwa ajili ya matibabu. Mheshimiwa Spika anatumia fedha za Bunge za Serikali kwa ajili ya matibabu na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mheshimiwa Lissu tumeendelea kuumkusanyia fedha mitaani kwa vikopo naye vilevile ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekti, hii double standard inayoendelea katika taifa hili, kwamba Mbunge wa Chama cha Mapinduzi anaweza akatibiwa na Serikali, akatibiwa na Bunge, Mbunge anayetokana na upinzani, Chief Whip aliyepigwa risasi Dodoma hawezi kutibiwa na Bunge wala hajapelekewa shilingi mia moja na Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bob Marley ana wimbo unasema only time will tell.

T A A R I F A . . .

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajadili Taarifa ya Utawala Bora Katiba na Sheria. Kuna Chief Whip wa Opposition kapigwa risasi, kifungu namba 24(1) cha Sheria cha uendeshaji wa Bunge kinaeleza ni nani anapaswa kuwa responsible in case Mbunge amepata matatizo, na kama sitaweza kujadili maslahi ya Wabunge si Lissu peke yake ya Wabunge wote akiwa ameumia ama hajaumia, niko tayari nisiwe Mbunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama sisi ni Wabunge hatuwezi kujadili maslahi ya Wabunge, huyu anasimama anaongea mzaha…

MWENYEKITI: Ongea na kiti.

MHE. GODBLESS J. LEMA:… kuna mtu amepotea mpaka leo anaitwa Ben Saanane, kuna watu wanapotea, haya ni mambo yanahusu utawala bora, katiba na sheria, na haya mambo ni ya msingi kuliko madaraja kuliko lami. Uhai wa mtu mmoja unazidi kilometa bilioni moja za lami, haya mambo tukiyajadili kwa mioyo ni msingi imara kwa sababu kuna watu wamepotea, kuna mtu ameumia, yuko hospitali tunapojadili hatuwashutumu tunataka mrudi kwenye sense, mjue kwamba tunajadili damu za watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo sababu nikasema Spika ni Mbunge, anatibiwa na hela ya Serikali, Lissu ni Mbunge anatibiwa na nani hata tunamchangia fedha? Nataka tulirudishe Bunge kwenye sense, kwamba yuko ndugu yetu anaumia, wewe umempiga risasi, si wewe? Kama Bunge tuongee, haya si kuyajadili kwa mioyo, tena tuna hekima kwamba tunaendelea kujadili huku tunalia na tunafanya sala ingekuwa ni nchi nyingine watu wangeweza kuingia barabarani kwa sababu kuna mtu ameumia. Tunajadili mambo haya anaibuka mtu tu kama mrembo huko pepepepe! Wewe! Wewe! Wewe! (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Katiba na Sheria
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Nina mambo ya msingi sana ambayo nataka niliambie Bunge. Taifa lolote duniani linaweza likaendelea kama utawala wa sheria na Katiba utazingatiwa. Kwa bahati mbaya, mambo ya kisheria na kikatiba yanayokosewa sasa watu wanafikiri ni temporary na wengine miongoni mwenu mnasema ngoja haya mambo yapite awamu hii tu, lakini baadae tutakuja kurudi kwenye line nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wasiwasi wangu ni kwamba kinachoendelea sasa ni tabia ambayo inaanza, wa-Spanish wanasema tabia inaanza kama utando wa buibui na mwisho wake unaishia kama lehemu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kujadili masuala ya Katiba na Sheria bila kuwa na utawala unaoheshimu Katiba, bila kuwa na Bunge ambalo linaweza likasimamia Serikali Kikatiba na Kisheria, Taifa hili litaendelea kwenda mahali pabaya sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi, Mheshimiwa Polepole ametoa maelekezo kwenye vyombo vya habari kwamba Mheshimiwa Mbunge Zitto Kabwe akamatwe na polisi kwa sababu ya kuchambua hoja za CAG. Maana yake nini? Maana yake ni kwamba sasa Polepole hana maana amemwongelea Mheshimiwa Zitto, maana yake anaongelea Bunge hili lisiendelee na uchambuzi wa jambo lolote ambalo ni kinyume na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ilianza humu ndani, maoni yetu ya Kambi Rasmi ya Upinzani mnayafanyia screening, tumeacha kusoma. Sasa imefika mahali Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi anaonya na kutoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi limkamate Mbunge anayechambua ripoti ya CAG. Kama kuna wa kwanza kukamatwa, ni aliyepoteza shilingi trilioni 1.5. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongee, nina masuala muhimu sasa kuhusu matumizi mabaya ya sheria hasa Mahakamani na mara nyingi tukiongelea habari ya Mahakama, watu huwa wanakuja hapa wanasema mambo yaliyoko Mahakamani tusiyaongee. Kwa sababu Bunge ndiyo linatunga sheria na Mahakama inakwenda kutafsiri sheria, mambo yaliyoko Mahakamani yasiongelewe kwa kina gani, lazima tafsiri yake ipatikane, lakini uzembe na matumizi mabaya ya sheria Mahakamani, lazima tuyaongee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kuna kesi ya money laundering. Hizi kesi zinatumika kuonea na kutesa wafanyabiashara. Juzi TLS walipitisha azimio Arusha kwa ajili ya kumtetea Wakili Median Mwale. Mwale ana mwaka wa nane Magereza; DPP amesha-enter nolle zaidi ya mara tano. Nolle nyingine imekuwa entered mwaka huu. Huyu mtu mafaili yake yamekwenda mpaka Court of Appeal, vielelezo vimetupwa na Court of Appeal.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni Jaji amemwachia na Ofisi ya DPP ikasema ukimwachia huyu mtu, hatutamkamata tena. Kwa miaka nane Ofisi ya DPP imeshindwa ku-establish evidence ya kumfunga mtu, bado yuko ndani kama mahabusu. Siyo yeye tu, ilipotokea ya Mwale, watu walifikiri ni Mwale peke yake. Leo kuna Dkt. Ringo Tenga, kuna Sioi, kuna akina Kitillya; hawa ni wale ambao magazeti yanawaandika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimekwenda Magereza nimekuta watu wana money laundering ya shilingi 800,000 M-pesa. Nimemkuta mtu yuko Magereza kwa money laundering ya dola 1,500. Ukishapelekwa kwenye Mahakama ya chini, wanasema hatuna mamlaka ya kusikiliza shauri hili. Mtu anakaa jela miaka nane. Suala hili nimeshaongea na Mheshimiwa Waziri mara nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natetea kwa sababu moja, najua mateso ya Magereza. Leo tuna kesi ya Mheshimiwa Mbowe, hii kesi kwenye penal code ikiwa watakutwa na hatia, watakwenda jela mwaka mzima. Hakimu anatoa masharti ya Waheshimiwa Wabunge kuripoti Kituo cha Polisi kila Ijumaa. Haya ni matumizi mabaya ya sheria, matumizi mabaya ya Hakimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiongea hivyo ninyi mnasema hivi, kama hamkuridhika na masharti haya, nendeni kwenye Appellate Court. Kama remedy yetu itakuwa ni kwenda Appellate Court, lakini bila kuwakemea Mahakimu wanao-abuse sheria, wanao-abuse power, maana yake watu wataanza kuiona Mahakama haitendi haki. Mahakama ikipoteza trust, nchi hii itaingia kwenye civil war.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo una Wabunge ambao wana kesi ya mkusanyiko usio halali. Wakikutwa na hatia ni mwaka mmoja jela, unawapa masharti ya dhamana kila Ijumaa Waheshimiwa Wabunge waende Kituo cha Polisi Dar es Salaam. Leo Mheshimiwa Heche ni Mbunge wa Tarime, maana yake kuanzia Jumatano ya kila wiki, kesi ikichukua miaka miwili Jumatano ya kila wiki anaanza safari kutoka Tarime kuja Dar es Salaam. Mambo haya yanaleta maumivu makali sana kwetu sisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nasema hivi, pamoja na kwamba ni kweli Mahakama ni mhimili mwingine, lazima kuwepo na check and balance. Hakimu alinipeleka Magereza mimi kwenye kesi ambayo nilikuwa nimeingia nasikiliza, anamwambia State Attorney usini- mislead kama mlivyoni-mislead kwenye kesi ya Lema. Nimekaa jela miezi minne kwa sababu ya makosa ya Hakimu. Mahakama ya Rufaa inakuja kuamua ndiyo, lakini mtu ameshaumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Sugu, ameomba, huyu kesi yake akikutwa na hatia amefungwa miezi mitano. Alinyimwa dhamana kwenye kesi ambayo akikutwa na hatia anafungwa miezi mitano, Hakimu anasema huyu akae ndani kwa usalama wake. Huyu anamaliza kifungo kesho kutwa, rufaa yake haijasikilizwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaposema Serikali inaingilia Mahakama, ni mikakati kama hii tunayoiona kwamba Mheshimiwa Sugu sasa rufaa yake ikisikilizwa mwezi unaokuja na anatoka tarehe 20, atakuwa amepata remedy gani katika kifungo ambacho alikuwa ametumikia?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge, mambo haya siyo ya CHADEMA, ni yetu wote. Utakapokuwa na Mahakama huru, Ofisi ya DPP huru, Ofisi ya AG huru haiwasaidii CHADEMA. Mimi naweza nikaamua leo nikaja huko CCM, lakini haijalishi. Unapokuwa na Mahakama ambayo haiko huru, unakuwa na mazingira mabaya ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Polisi hawako huru; juzi mmemwona Makonda na sinema yake ya watoto. Leo wamemkamata yule dada waliyekuwa wamempa deal aseme ni mtoto wa Mheshimiwa Lowassa, anakamatwa tena kwa sababu alikanusha juzi. Haya matumizi mabaya ya sheria ambayo sasa yanaingia Mahakamani. Watu wanaozea jela. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, money laundering, Waheshimiwa Wabunge msipolileta humu Bungeni, Bunge liweze kuichambua na kutolea maelekezo mapya, hii kesi haitamwacha Mbunge yeyote salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana nimeona barua ya TRA; mtu kanunua nyumba ya shilingi milioni 80 Sinza. TRA wanaandika barua, wanakwambia badala ya ku-claim capital gain, wanaenda kuandika barua wanasema, tunataka uje utuambie na chanzo cha fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi siku nikifanya hivyo, mkatafuta chanzo cha fedha, Mheshimiwa Jenista Mhagama mimi nitasema umenihonga wewe ama Mheshimiwa Angellah Kairuki, sasa sijui hiyo kesi itaendeshwaje? (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo siyo tu yanaua uchumi, haya mambo yanaondoa confidence kwa wafanyabiashara. Mimi nawaambia, leo watu nchi hii wanahamisha fedha kwa sababu ya sheria za ajabu ajabu. Hakuna tena transaction zinazopita kwenye mabenki. Ukiweka shilingi milioni 20 kwenye akaunti; mimi nili-transfer hela kwenye akaunti yangu wanazuia, tueleze sababu ya ku- transfer hela. Napeleka hela kwa mke wangu unaniuliza sababu? Sababu inaweza ikawa love. Haya mambo yanafanya watu sasa wasiweke hela benki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, TAKUKURU, hizi tax holdings zilizoundwa ambazo ziko chini ya Kamati ya Ulinzi wa Mkoa huko zinafanya watu wanakuwa na hofu. Transaction hazipiti kwenye mabenki, benki wanakosa deposits, benki sasa zinaanza ku-fail.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuomba sana, Mheshimiwa Waziri, punguza uoga.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Niwaombe Waheshimiwa Wabunge ile biashara ya miongozo, miongozo wakati wangu bora muipunguze kwa sababu nataka niongee mambo serious.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo humu ndani wako viongozi wote wa vyombo vya ulinzi na usalama. Unapokuwa na viongozi ambao mshahara na cheo kwao ni msingi kuliko utu na thawabu, lawama wanazozipokea kutoka kwetu lazima zitaendelea kuwepo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya Upinzani na Wabunge ilikuwa ni kutetea ustawi na maslahi ya Jeshi la Polisi, badala yake Wabunge ndani ya Bunge wanaliongea Jeshi la Polisi kama ni kikosi cha mauaji. Kama hawawezi kuiona hii sense kwamba Taifa limepotea kwamba Wabunge wote wa Chama cha Mapinduzi na opposition wakiongea wanalaumu Jeshi la Polisi na Jeshi la Polisi linalaumiwa kwa sababu tumeli-politicize. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo shughuli za siasa zimekuwa ngumu, mimi leo niko upinzani, kama lengo la demokrasia ni Mbowe, Lema na Mwambe na Mbatia na walioko huku, hawa watu wanaweza wakaamua kurudi kwenye biashara zao. Yeyote anayefikiria kuua demokrasia kwa sababu ya ushindi wa chama chake hampendi mjukuu wake. Wakijua msingi wa demokrasia hawawezi kutengeneza mkakati wa kisiasa wa kuua demokrasia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi siyo maadui, leo hatufanyi mikutano ya hadhara, leo vikao vya ndani vimezuiwa, Polisi wamepewa amri na kwa sababu wao wameapa kutekeleza amri leo kazi ya siasa imekuwa ngumu. Tukimalizwa sisi, tukaondoka sisi, hiyo vita itahamia ndani yenu, na nawaambia mwaka 2020 kwenye uchaguzi unaokuja kama sisi tutakuwa tumeshafukiwa, nyie hamtakuwa na kura ya maoni, mtakuwa na kura ya vidole, imeonekana Songea na sehemu nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulinda demokrasia haisaidii chama tawala inasaidia the next generation of this country. Leo wewe ni Mwenyekiti hapa alikuwepo IGP Mangu leo hayupo leo yupo Sirro na kwa utawala huu Mwigulu kesho anaweza yeye akajikuta amekuwa DC kama ambavyo Deputy DGIS leo ni RAS anaenda kukaa kwenye kikao ambacho RCO anakuwa boss wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wajifunze kwamba tunavyotaka kuhimiza demokrasia maana yake ni kwamba ni kwa ajili ya ustawi wetu. Mimi ni mchaga naweza nikaamua kuuza sumu ya panya, naweza nikaamua kuwa na hardware nikaachana na siasa. Siachani na siasa kwa sababu sifikiria uchaguzi unaokuja, nafikiria next generation. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, linda muda wangu, Katibu nakuomba linda muda wangu. Nyie mliopewa zawadi ya kurekodi naomba hii video yangu niipate baadaye kwa sababu siku hizi hamnipi video zangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Nasema hivi Waheshimiwa Wabunge nyie mko wengi, nyie mna kura, nyie mna maamuzi, kuna Mawaziri huko wa nyanja zote saidieni hili Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kila mtu analia, tuna Mashehe Gereza la Arusha, tuna Mashehe Dar es Salaam, tuna Mashehe Songea, unapoweka viongozi wa dini kwa miaka minne bila kumaliza mashauri yao unajenga enemity ya kidini. Hawa watoto wao na wajukuu wao waliokaa kimya hawana maana kwamba wamekuwa wajinga, kuna siku wataamka na siku wakiamka itakuwa ni hatari sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kibiti nauliza lini tumeona Jeshi la Polisi limeita Press Conference ya kusema mambo ya Kibiti, watu wamekufa, watu wanapotea. Hawa watu walitakiwa wapelekwe Mahakamani, wasomewe mashtaka wahukumiwe, leo hakuna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mkristo naogopa uadui unaojengwa kati ya Waislam na Wakristo wako Mashehe 85 karibu kule Arusha mwaka wa nne watu wamekatwa miguu, upelelezi haujakamilika. Huu uadui unaojengwa Waheshimiwa nyie mnaweza mkasaidia nchi hii, nyie mko wengi, kuna Mawaziri huku Maprofesa na namna ya kusaidia nchi hii ni kupuuza vyeo na mshahara against dignity. Dignity ni thawabu kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kesi ya kubambikizwa, mimi najua Mbowe alikuwa anapewa kesi ya mauaji, Halima anapewa kesi ya uhaini, kwa sababu gani! Hakuna Mbunge huku ambaye ana kesi. Kila siku unaona Jeshi la Polisi linapambana na vijana wadogo wa cyber-crime, kijana wa miaka 25 amemkosoa Rais mnakwenda mnamkamata. Mnawapa polisi mzigo ambao ni unnecessary.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi hii ina matatizo mengi baharini, matatizo ya madawa ya kulevya, Sirro anaanza kukimbizana na mtu ame-twitt kwamba Rais Magufuli hafanyi vizuri. Msipomfundisha Rais kukosolewa hamuwezi kupata, mjifunze kukosoana, kukosoana ni tiba siyo balaa”.

KUHUSU UTARATIBU . . .

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Jenista namshukuru kwa sababu pia amekuwa mtetezi wa Mwenyezi Mungu. Mungu akubariki sana, basi nahama kabisa. Sasa dakika 3 .6 nimetumia, Katibu usije ukaleta mambo yako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachokisema ya kwamba kuna matatizo makubwa katika Jeshi la Polisi. Nimesema wabunge wote hapa asilimia karibu 60 wana kesi, wote wana kesi, wote wapinzani wana kesi, sasa haya mambo yanaongewa na Wabunge lawama kwa Jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi likiwa imara siyo kwa faida ya CHADEMA wala CCM ni kwa faida ya generation ya nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwa Mbunge ni thamani kubwa. Mbunge maana yake unawakilisha wananchi, unatunga sheria kuhusu nchi. Nilisema Bunge lililopita Wabunge wote mlioko hapa asilimia 70 hatukuwa wote term iliyopita. Tunapotunga, tunaposimamia maadili na integrity ya Jeshi la Polisi tushikamane pamoja kujenga jeshi imara ambalo hata kama wewe siyo Mbunge litakupa nidhamu, hata kama wewe siyo Rais litakupa nidhamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Jeshi la Polisi leo lina lawama nyingi, mimi nimekaa magereza miezi minne na siku 16 nimeona mambo ya kutisha. Nimeona watu wanaishia magereza, leo polisi kupata dhamana ni mpaka uka-apply habeas corpus Mahakamani. Leo polisi bail haipo, sasa kuna chuki inajengwa kati ya polisi na wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo sababu leo Mheshimiwa Spika alisema mbona Sirro alivyotajwa makofi hayakupigwa upande huu? Siyo upande huu huko nje hawapigi makofi wakimuona polisi, kwa sababu gani, Marekani ukimuona polisi unaomba kupiga naye picha, hapa ukimuona polisi unakimbia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu ninachosema ni kwamba Waheshimiwa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi nawaomba sana hakuna kazi muhimu tutakayofanya kama ya kujenga integrity ya Jeshi la Polisi. Ukiangalia undani kabisa Jeshi la Polisi wao wenyewe wanaharibiwa na sisi wanasiasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kuna uadui kati ya raia wa kawaida na Jeshi la Polisi. Unasikia mtu ameuawa Mbeya, mdogo wake Heche amepigwa kisu akiwa na pingu kwenye gari ya polisi, wanaenda kutupa mwili bodaboda ikaona. Boda boda imeona, watu wakasema, wakapiga kelele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado dakika tano, mimi zangu dakika 10 bado naangalia saa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yuko hapa IGP. IGP ushauri wangu ni huu mimi nimekuwepo Bunge hili nimeona Bunge hili likisema Sethi Harbinder zile pesa za IPTL zilikuwa ni mali binafsi. Nimeona Bunge hili hili wakisema asulubiwe, kabla jogoo halijawika mara tatu hawa watu hawa wanaokutuma kazi leo kuna siku watakuning’iniza, ushauri wangu ni huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwambia IGP, sio kila maelekezo ya kuumiza watu mnayachukua Mheshimiwa Lissu kapigwa risasi hapa, Naibu Waziri Kalamani anang’oa CCTV Camera kwake, kuondoa ushahidi. Ben Sanane kapotea, Azory kapotea, maiti zinaokotwa mchangani Mwigulu Waziri anasema hizi maiti zimeuawa na watu wasiojulikana. Kama wewe ni Waziri wa Mambo ya Ndani, kama kuna IGP maiti zinaokotwa zaidi ya elfu moja, huwezi kujua aliyeuwa unakaa ofisini kufanya nini, nenda kauze maandazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba integrity ya Jeshi la Polisi ni ya msingi kuliko chochote. Waheshimiwa Wabunge nawaambia...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba nimemaliza adhabu yangu vizuri na nimerudi nimewakuta hamjabadilika sana. Kwa hiyo, nawashukuru sana wale waliosaidia kupata adhabu ya muda mrefu, mmehuisha sana roho yangu na thamani yangu kupenda haki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni Bunge la mwisho. Maana yake mwaka huu Bunge hili lote tutaondoka twende kwenye uchaguzi na kwa miaka mitano ambayo tumekaa hapa ndani ya Bunge, Bunge hili kama limefanya kazi ya kusaidia nchi zaidi ya kuipamba Serikali ni kwa kiwango kidogo sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajadili taarifa za Kamati, Viwanda na Biashara. Taifa lolote linalotaka kuimarisha biashara katika nchi yake, kitu cha kwanza ni utawala bora uonekane kwa macho na siyo tu utawala bora; leo utawala bora, utawala wa sheria, demokrasia katika Taifa hili imeonekana siyo sehemu ama siyo part ya mafanikio ya nchi. Juhudi kubwa sana zinafanyika za kuondoa Wapinzani katika uchaguzi unaofuata. Jambo hilo linaweza likafanikiwa, lakini halitafanikiwa na baraka za vizazi vya Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumetoka kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa; ule uchaguzi hayakuibiwa matokeo, uliibiwa mchakato. Mchakato uliibiwa na CCM imeshinda kwa asilimia 100. Mnapiga makofi, mnafurahi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakwenda kwenye Uchaguzi Mkuu Mwaka 2020; kuna commitment kubwa sana ya kuhakikisha kwamba hakuna Mpinzani atakayerudi. Unapoongelea biashara na viwanda, wawekezaji wanaangalia utawala bora ili kuleta biashara ambazo ni sustainable. Unapoongelea viwanda na biashara wawekezaji na watu wa ndani wanaangalia utawala wa sheria uliothabiti ili kuleta mitaji na kuongeza mitaji katika kujenga uchumi wa nchi. Kwa hiyo, ili ku-improve biashara katika Taifa hili na ku-improve viwanda, kitu cha kwanza cha kuimarisha ni utawala wa sheria ambao mtu yeyote hatautilia mashaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, factors za utawala bora katika kuamua uchumi wa nchi ni namba moja. Leo Kenya inawawekezaji wengi kuliko Tanzania. Kenya haina rasilimali nyingi kama Tanzania, lakini wawekezaji wana-confidence na Kenya kwa sababu hata Mahakama za Kenya za ndani zina uhuru wa kutosha wa ku-handle matter za wawekezaji kuliko hata Mahakama za nje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Kenya inapokea watalii wengi kuliko Tanzania, leo Kenya ina vitanda ziada kuliko Tanzania karibu vitanda 30,000 ni kwa sababu ya mazingira ya utawala wa kisiasa wa nchi ile. Mheshimiwa Uhuru leo na Raila wanashikana mikono pamoja kujenga Taifa lenye umoja. Leo Kenya huwezi kujua tofuati ya mpinzani na Serikali kwa sababu wameamua kujenga nchi. Hapa Mpinzani ni Mhaini. Hata akitoa maoni, yanakuja maazimio ya AG; yamekuja maazimio leo hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ningekuwa Serikali, suala la Mheshimiwa Zitto ningelipuuza tu, kabisa! Leo Mheshimiwa Zitto ameandika barua tarehe 22 Januari, maazimio ya World Bank kuhusu mtafaruku wa Sera na Serikali ya Tanzania ni mwaka juzi 2018. Barua ya tarehe 22 Janauri ya kimkakati leo mmeishikia Bango, yanatolewa maamuzi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaambiwa aangalie kama kuna kosa la jinai katika maoni aliyotoa Kiongozi wa Upinzani wa Chama cha siasa. (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utaratibu.

KUHUSU UTARATIBU

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mimi nachnagia Taarifa ya Kamati ya Viwanda na Biashara na hoja yangu ni moja tu, ya kwamba ili kuwepo na biashara ambazo ni sustainable, tunahitaji utawala bora. Sasa mimi ni Mbunge, naishauri Serikali kwamba kwa suala ambalo limetokea leo Bungeni, ambalo wala mtafaruku wake siyo Mheshimiwa Zitto, Zitto anaweza akawa amedandia, mtafaruku wake ni confusion ya policy kati ya Serikali na World Bank.

Sasa ndiyo nikasema, ningekuwa ni mimi, badala ya kuamuru Mheshimiwa Zitto atiwe hatiani, ningesema Mheshimiwa Zitto apuuzwe halafu Serikali mwendelee kujadili na World Bank mfikie consensus. Hiyo ndiyo ingekuwa Utawala. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa maana yake Mpinzani anapotoa maoni sasa internationally naye anatiwa kibano, mnatia mashaka wale watu ambao wanataka kuleta mitaji mingi hapa. Hivi vitu vinakwenda internationally na vikienda Kimataifa watu wanasema ile nchi Bwana, hata Mbunge akitoa maoni huwa anapewa money laundering, tusubiri kwanza tuone utawala upite.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo letu siyo tu kuwatoa madarakani, hata mkibaki madarakani, lakini tukiona Taifa hili linakuwa ni mahali salama pa kuishi, hiyo ni baraka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaongea biashara; leo…

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Tusikilize taarifa. Iwe ni taarifa ya kujenga.

T A A R I F A

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna wakati ilitolewa hoja kiwekwe kipimo, ile alcoholic nini ile, hapo. Ninafikiri kuna haja ya kukirudisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme nini? Ninachowaambia Waheshimiwa Wabunge na Serikali, leo huko mitaani sisi tunafahamu hali ya kibiashara ilivyo mbaya. Tunafahamu jinsi ambavyo watu wanaondoka, ambavyo mitaji inahama na hiyo ni kwa sababu ya mashaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TRA hata wakiongeza kodi kwa kiwango gani, lakini kama Taifa halina uncertainty, bado kodi huwa haiendi kwa yule anayefanya biashara, inakwenda kwa mlaji wa mwisho. Sasa kuna mashaka makubwa. Leo kupata working permit nchi ama business permit, mimi niko Arusha, watu wengi wameondoka kwa sababu ya working permit. Wamekuja Wazungu wanataka kufanya miradi wanaondoka kwa sababu ya working permit. Mimi najiuliza, mtu anakuja na investment ya labda shilingi milioni 10, una…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.
Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari wa Mwaka 2016
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Huu Muswada nikisikiliza Wabunge wenzangu wanavyochangia naona kwamba una-mis kidogo, lakini waliouleta wala lengo, siyo access to information, lengo ni kuzuia vyombo vya habari kuwa huru katika kutetea maslahi ya Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi taarifa zinazoongelewa zikatafutwe, kwamba Diwani, Mwenyekiti wa Mtaa, tayari Sheria ya Local Government inasema kwamba Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa kabla hajaenda kwenye WDC anapaswa kuitisha mkutano wa hadhara na kusoma mapato na matumizi na kuchukua kero za wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo huu Muswada ulivyoletwa na Mheshimiwa Mwakyembe, „Bwashee wangu‟, ameuleta kimkakati sana, lakini lengo lake litatimia kwa sababu hakuna siku mmeacha kupitisha kitu mnachokitaka hata kama ni dhambi. Hii pia itapita, lakini lengo la huu Muswada ni kuzuia uhuru wa vyombo vya habari. Narudia tena Waheshimiwa Wabunge, leo wote hapa tuna influence, tuna namba za simu za Mawaziri, tuna namba za simu za watu wa usalama, watoto wetu hawatakuwa na influence tuliyonayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia huu Muswada ulioletwa, ukiangalia na hukumu iliyoletwa kwamba, in case mtu akitoa taarifa ambazo siyo sahihi, hapa mmesema mara ya kwanza mlisema anapaswa kwenda jela miaka isiyopungua 10! Unajiuliza hivi ni Diwani, ni Mtendaji wa Kata ndiyo amepangiwa miaka 10 asipotoa taarifa za maendeleo ya Kata? Maendeleo ya Kata Diwani anakwenda Halmashauri, kuna vikao kuna Kamati ya Finance inajadili mambo ya siri! Mabaraza yote ya Halmashauri yanafanya Mabaraza kwa wazi na Mabaraza yote yanatangazwa watu waje!
Mheshimiwa Mwenyekiti, huu Muswada hauna maana hii mnayoitaka, huu Muswada ni hamtaki kuona makala za magazeti! Hamtaki kuona taarifa yoyote nyingine! Hili Mheshimiwa utafanikiwa! Kama Mheshimiwa Mwakyembe, Waziri wa Sheria aliweza kabisa kutetea kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara na yeye ni Mwalimu wa Sheria, suala la kikatiba! Huu Muswada wameuleta kwa njia ya mbali sana, utafanikiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema ukweli humu Bungeni tutakaa kwa muda tu, iko siku hizi Sheria tunazopitisha humu ndani zitaendelea kula vizazi vyetu na siku moja utakaa utasema haya mambo nilipitisha mimi. Haya mambo yanakuja kuzuwia vyombo vya habari! Waziri ameshafungia vyombo vya habari zaidi ya vitatu! Kila siku Mheshimiwa Nape akiamka anafungia chombo cha habari! Chombo cha habari chochote kinachomsema Rais! Chombo cha habari chochote kinachosema Viongozi wa Serikali ni chombo cha habari ambacho kinaonekana kina uadui! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa sababu nyie mtatawala milele, niliwaambia huko nyuma, kuna wakati zilitungwa sheria humu. Wakati inapitishwa hapa Act ya Economic Crimes na Money Laundering mlifikiri mnawatungia CHADEMA! Sasa hivi wale wote wanaohojiwa TAKUKURU ni watu ambao walikuwa kwenye madawati haya. Hizi sheria mnazotunga kuzuia haya mambo zitakuja kuwala kwa upande mmoja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nawaambia ukweli, aliulizwa Waziri mmoja akiwa Magereza huko amenyimwa dhamana! Akaambiwa huu Muswada ulikuja kwenye Cabinet, kwa nini hukupinga? Akasema nilifikiri wanatungiwa wale kule nje! Hizi sheria mnazotunga hamtutungii sisi, mnatungia watoto wetu. Hili ni Bunge ambalo linatunga sheria eti ya ku-protect mtu mmoja!
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nimemwambia AG hapa asubuhi, hivi umesoma kutengeneza nuclear ama sheria? AG kwenye vyombo vya habari anaonekana kabisa anashindwa kuitetea Katiba na wote tuko hapa kwa sababu ya Katiba. Mimi leo ni Mbunge kwa sababu ya Katiba, Rais leo ni Rais wa Jamhuri kwa sababu ni Katiba, hawa Polisi wanatusachi hapo nje ni kwa sababu ya Katiba, lakini Katiba hiyo ilipokuja kwenye haki ya kufanya mikutano ya hadhara, mimi naambiwa nifanye mkutano Arusha tu!
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri hajaongea chochote...
MWENYEKITI: Kuhusu Utaratibu!....
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ulinde dakika zangu saba zilizobaki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kanisa halihitaji mtakatifu kumfanya mtakatifu, linamhitaji mwenye dhambi kumfanya mtakatifu, ndiyo kazi ya msingi ya Kanisa. Humu ndani kama Mbunge nina kazi moja tu, kwanza kuwahubiri na kuwaeleza ukweli, huu Muswada wote umeletwa kwa lengo la kuzuwia uhuru wa vyombo vya habari. Kwa sababu, information zote zinazotakiwa na huu Muswada ziko huko chini!
Mheshimiwa Mwenyekiti, Diwani akihitaji BOQ ataipata, Mabaraza ya Halmashauri yako huru tena mijadala yao iko wazi. Hii imefungwafungwa, lengo la huu Muswada ni magazeti yasiandike, redio zifungwe, ndiyo sababu nasema hili jambo mtafanikiwa kwa sababu, wingi wenu unatosha kupitisha sheria yoyote humu ndani, lakini nawakumbusha kwamba, kila sheria inayopitishwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri hampitishi sheria kwa ajili ya kikundi cha watu wachache hiki, mnapitisha sheria kwa ajili ya maisha ya Watanzania hata miaka 100.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimetolea mifano sheria mbalimbali ambazo zimepitishwa, ukitaka kuangalia hata adhabu iliyowekwa ya kifungo kwa mtu ambaye ana-distort taarifa ni miaka 10 jela, hii miaka 10 jela haiwezi kuwa ni kwa Diwani ama Mtendaji wa Kata ama Mwenyekiti wa Mtaa, hii lengo lake ni kwa waandishi wa habari. Tulisema huko nyuma na tunasema tena leo, hii sasa imehama, tuliambiwa tusifanye mikutano ya hadhara, sasa hivi waandishi wa habari wanapigwa-lock, Makanisa na Misikiti wasikie itafuata, watanyamazishwa kwa sababu, tunakoelekea italetwa Miswada mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, huu Muswada hauna maana kuja Bungeni kwa sababu, una lengo la kuua uhuru wa vyombo vya habari. Wanasema access to information, hii maana yake gazeti halitaandika taarifa yoyote, Bunge hili limepata taarifa mbalimbali kutoka hata katika blog mbalimbali za Ulaya kuhusu ufisadi ndani ya Taifa hili na magazeti yakazifanyia kazi na Bunge hili likafanya maamuzi kupitia vitu ambavyo viliitwa vipeperushi! Leo unaambiwa ukitaka habari uandike barua, iende ikae siku 30 Bunge limeshakwisha! Ikionekana huyu Mbunge ana kiherehere ndiyo mwenye hii hoja kwenye uchaguzi asirudi tena, kama alivyofanyiwa Mheshimiwa David Kafulila. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ndugu zangu Waheshimiwa Viongozi sisi ni Wabunge, kila mbegu ya hila inayopandwa na kila atakayehusika kuipanda ataivuna, kama siyo wewe mtoto wako. Huu Muswada umekuja kuua uhuru wa vyombo vya habari. Vyombo vya habari vikinyamaza na sisi tukanyamaza, watakuja watu wengine ambao hawatasikia sauti mnayoisema ninyi, watakuwa ni watu wabaya kuliko sisi tunaopiga kelele na kutuona wajinga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, huu Muswada Mheshimiwa Mwakyembe kwa sababu alishindwa kutetea hata Katiba ambayo ndiyo inatoa right ya kuwepo huu Muswada, huu Muswada hauna maana leo kwa sababu lengo lake ni kuja kuua vyombo vya habari. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesoma hii hapa, kwenye paragraph ya pili aliyoleta Mheshimiwa Mwakyembe, ngoja nikusomee, paragraph ya pili kwamba:
“Mheshimiwa Spika, kupitishwa kwa Muswada huu kutaboresha sana uwajibikaji nchini kwa kila ngazi hasa katika mfumo tulionao na ugatuzi wa madaraka. Sheria hii mpya itampa mathalani Diwani, Mwenyekiti ama Mtendaji wa Kijiji...”
Mheshimiwa Mwakyembe siyo kweli! Eti kwamba, hii sheria mnawatungia Madiwani! Hii sheria hamuwatungii Madiwani, unatungia Mwanahalisi, unatungia Mawio, unatungia Tanzania Daima, unatungia Channel 10, unatungia Radio Five, mtafanikiwa, ila mshahara wa dhambi ni mauti.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017.
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Bunge linapokaa kutunga sheria nafikiri ndiyo wakati sensitive kwa Wabunge kuliko nyakati nyingine zote katika mijadala ya Bunge. (Makofi)


Mheshimiwa Naibu Spika, wewe ni shahidi na Wabunge wote sisi ni mashahidi kwamba Muswada huu umeletwa kwa Hati ya Dharura sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, rai yetu toka mwanzo ilikuwa ni muda wa kutosha, siyo Wabunge wa Upinzani wa kupitia wala wadau. Ni muda wa Wabunge wote kuwa na concentration ya kutosha juu ya mjadala muhimu kama huu ambao unakwenda kutengeneza sheria ya rasilimali za Taifa hili ya watoto wetu, wajukuu na vitukuu. Kwa bahati mbaya sana, pande zote, ushabiki katika masuala ya utungaji wa sheria umekuwa ni muhimu na umekuwa thabiti kuliko umuhimu wa sheria wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge hili hili tulipitisha Sheria ya Money Laundering hapa, kelele zikapigwa hapa ikawa kama wanatungiwa upande mmoja, leo sheria zile zinakula watu wa upande huu kuliko watu wa upande huu. Kwa hiyo, utungaji wa sheria ni issue sensitive siyo issue ya kishabiki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ukiangalia Ripoti ya Makinikia wakati Mheshimiwa Rais anaipokea ulikuwa ukisikiliza hotuba ya Rais unaelewa kwamba analalamika kwamba uongozi uliopita maana yake ni pamoja na Bunge lilifanya makosa makubwa katika utungaji wa Sheria za Madini. Ukimuangalia Rais alikuwa analalamika anasema, jamani tumelipeleka Taifa mahali pabaya, tumetunga sheria mbaya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kama leo tuko serious na kubadilisha sheria hizi kwa ajili ya utawala bora wa Taifa hili, ingekuwa ni vyema Chama cha Mapinduzi ambako kuna Wabunge wengi Muswada wa kwanza ambao mngeuleta kwa dharura ungekuwa ni Muswada wa kuondoa kinga ya viongozi wanapokuwa madarakani. Imethibitika kwamba kwa sababu viongozi wengi wana immunity hiyo ndiyo imesababisha viongozi wengi kufanya maamuzi yasiyozingatia haki katika Taifa hili.

KUHUSU UTARATIBU...

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Hatutarajii kuwashinda sana humu ndani kwa sasa, lakini wakati wa Mungu ukifika mtashindwa na watu wengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna wengine wanataka kuhamishwa Wizara ndiyo maana kila nikisimama wanasimama, kwa sababu wanajua umuhimu wa hizo Wizara. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, labda hujafahamishwa, hizi hapa zote zimekataliwa na majina yao yako hapa nitakukabidhi baadaye.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Nilikuwa nasema ulikuwa ukimuangalia Rais wakati akipokea Ripoti ya Makinikia lawama yake na maelekezo aliyotoa baadhi ya watu kuwajibishwa unagundua kwamba kuna makosa yalifanyika katika mfumo wa utawala huko nyuma. Ndiyo nasema pamoja na Muswada huu kuja kwa haraka, Muswada wa kwanza ambao ungepaswa kuletwa kwa haraka ni wa kuondoa kinga ya viongozi wakuu wa nchi wakiwa madarakani ili mambo haya ambayo yamefanyika huko…

KUHUSU UTARATIBU...

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa sababu umemuelewa. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, hatuwezi kutengeneza sheria bila kutafuta reference za kusaidia Wabunge kufanya maamuzi. Tunanukuu hotuba za Rais wakati anapokea Ripoti ya Makinikia alivyokuwa anasema huko nyuma tumefanya makosa makubwa na ndiyo maana mmeleta Muswada huu kwa Dharura. Dharura ya Muswada huu ni kwamba makosa yasiendelee kufanyika. Sasa tunajenga hoja kwa kuangalia reference. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, habari ya IPTL ni Wabunge hawa na Simbachawene huyu aliyesema hela sio za Serikali, hela ni za watu binafsi, leo mmekamata watu mmepeleka magereza. Sasa tunapojenga hoja, mkae kimya. Wote sisi ni Watanzania. Humu tunafanya nini? Wote sisi humu ni Watanzania tunaongea kwa manufaa yetu wote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jamani mimi nanukuu maneno ya Rais unanyanyuka unasema tusiongelee viongozi wa zamani, tumuongee nani? Shetani wa zamani? Tumuongee nani? Mungu wa zamani? Tumuongee nani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tungekuwa sisi tunatawala mngetusema. Sisi hamuwezi kutusema sana kwa sababu hatutawali, ninyi ndiyo mnatawala, tupeni fursa ya kuwarekebisha na hapa ndiyo pa kusemea. Wewe pia unataka Uwaziri, unaweza ukakaa sana. (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, twende kwenye hoja za msingi. Nataka niamini, nataka nifanye assumption Rais tuliye naye ni mzalendo, nataka niwe na hiyo assumption. Nataka niwe na assumption kwamba Rais tuliye naye anapenda watu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Rais Magufuli alisema hivi, alikuwa ana-beep watu wakapokea. Najiuliza kwa power mliyompa Rais ya kusimamia rasilimali za za nchi hii, siku moja anakuja Rais ambaye sio mzalendo kama Magufuli, nataka niamini hivyo, anatokea hata upande huu, inawezekana akatokea hata CHADEMA kwa sababu huku hawako malaika, anaweza akatokea CUF kwa sababu CUF hakuna malaika, akatokea Rais siyo mwaminifu mmempa power ya ku-manage na kusimamia rasilimali zote na mkawekea Bunge masharti nafuu kuhusu usimamizi huo, Taifa hili litauzwa. Mnapotunga sheria hamtungi sheria kwa kumwangalia Rais aliyeko madarakani, bali mnatunga sheria kwa assumption kwamba anaweza akaja Rais ambaye si malaika kama mliye naye na siku moja Taifa hili likaingia mahali pabaya na hili ndilo angalizo tunataka mliangalie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiongea mnafikiri tunawachukia, tunawachukiaje? Ninyi wote nyie tukikaa kantini maneno mnayoongea ni tofauti kabisa na mnavyo- behave huku na sijui kwa nini. Kama tungekuwa tunawarekodi ninyi maneno tunayoongea kwenye kantini tunampelekea Magufuli, kwenye Kamati tukitoka nje mnaongea tofauti, lisaidieni Taifa hili. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ni Mbunge awamu ya pili, Wabunge wote unaowaona hapa asilimia 70 ni wageni, pengine hamtarudi tena kuwa Wabunge ninyi na kama hamtarudi kuwa Wabunge…

Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge wote ninyi 70% hapa ni wageni, tunasema hivi tutunge sheria hata kama siku moja mtoto wako hatakuwa Waziri, hatakuwa Mbunge, hata kama hautarudi Bungeni sheria hizi bado zinaweza zika ku-protect hata kama huna- influence ama huna connection na mtu yeyote. Sisi tukileta mawazo haya ndugu zangu mkubali kwamba opinion zetu siyo kwa sababu ya kuwashinda bali ni kwa sababu ya kurekebisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunapoanza kulalamikia kwamba hii Miswaada inakuja kwa njia ya Dharura na wakati kuna muda, leo makinikia yamezuia Bandari ya Dar es Salaam, Rais ana mamlaka. Ukweli ni kwamba kutokuiamini Taasisi ya Urais siyo jambo la maana hata kidogo, kutokumwamini Rais siyo jambo la maana hata kidogo, lakini kwa mazingira ya mataifa ya Afrika na demokrasia ilivyo Taasisi ya Urais lazima iwekewe check and balance ili Taifa hili liweze kwenda salama kwa sababu anaweza akaja mtu, siyo kama huyu malika tuliye naye. (Makofi/Kicheko)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)
Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017.
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Bunge linapokaa kutunga sheria nafikiri ndiyo wakati sensitive kwa Wabunge kuliko nyakati nyingine zote katika mijadala ya Bunge. (Makofi)


Mheshimiwa Naibu Spika, wewe ni shahidi na Wabunge wote sisi ni mashahidi kwamba Muswada huu umeletwa kwa Hati ya Dharura sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, rai yetu toka mwanzo ilikuwa ni muda wa kutosha, siyo Wabunge wa Upinzani wa kupitia wala wadau. Ni muda wa Wabunge wote kuwa na concentration ya kutosha juu ya mjadala muhimu kama huu ambao unakwenda kutengeneza sheria ya rasilimali za Taifa hili ya watoto wetu, wajukuu na vitukuu. Kwa bahati mbaya sana, pande zote, ushabiki katika masuala ya utungaji wa sheria umekuwa ni muhimu na umekuwa thabiti kuliko umuhimu wa sheria wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge hili hili tulipitisha Sheria ya Money Laundering hapa, kelele zikapigwa hapa ikawa kama wanatungiwa upande mmoja, leo sheria zile zinakula watu wa upande huu kuliko watu wa upande huu. Kwa hiyo, utungaji wa sheria ni issue sensitive siyo issue ya kishabiki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ukiangalia Ripoti ya Makinikia wakati Mheshimiwa Rais anaipokea ulikuwa ukisikiliza hotuba ya Rais unaelewa kwamba analalamika kwamba uongozi uliopita maana yake ni pamoja na Bunge lilifanya makosa makubwa katika utungaji wa Sheria za Madini. Ukimuangalia Rais alikuwa analalamika anasema, jamani tumelipeleka Taifa mahali pabaya, tumetunga sheria mbaya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kama leo tuko serious na kubadilisha sheria hizi kwa ajili ya utawala bora wa Taifa hili, ingekuwa ni vyema Chama cha Mapinduzi ambako kuna Wabunge wengi Muswada wa kwanza ambao mngeuleta kwa dharura ungekuwa ni Muswada wa kuondoa kinga ya viongozi wanapokuwa madarakani. Imethibitika kwamba kwa sababu viongozi wengi wana immunity hiyo ndiyo imesababisha viongozi wengi kufanya maamuzi yasiyozingatia haki katika Taifa hili.

KUHUSU UTARATIBU...

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Hatutarajii kuwashinda sana humu ndani kwa sasa, lakini wakati wa Mungu ukifika mtashindwa na watu wengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna wengine wanataka kuhamishwa Wizara ndiyo maana kila nikisimama wanasimama, kwa sababu wanajua umuhimu wa hizo Wizara. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, labda hujafahamishwa, hizi hapa zote zimekataliwa na majina yao yako hapa nitakukabidhi baadaye.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Nilikuwa nasema ulikuwa ukimuangalia Rais wakati akipokea Ripoti ya Makinikia lawama yake na maelekezo aliyotoa baadhi ya watu kuwajibishwa unagundua kwamba kuna makosa yalifanyika katika mfumo wa utawala huko nyuma. Ndiyo nasema pamoja na Muswada huu kuja kwa haraka, Muswada wa kwanza ambao ungepaswa kuletwa kwa haraka ni wa kuondoa kinga ya viongozi wakuu wa nchi wakiwa madarakani ili mambo haya ambayo yamefanyika huko…

KUHUSU UTARATIBU...

MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa sababu umemuelewa. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, hatuwezi kutengeneza sheria bila kutafuta reference za kusaidia Wabunge kufanya maamuzi. Tunanukuu hotuba za Rais wakati anapokea Ripoti ya Makinikia alivyokuwa anasema huko nyuma tumefanya makosa makubwa na ndiyo maana mmeleta Muswada huu kwa Dharura. Dharura ya Muswada huu ni kwamba makosa yasiendelee kufanyika. Sasa tunajenga hoja kwa kuangalia reference. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, habari ya IPTL ni Wabunge hawa na Simbachawene huyu aliyesema hela sio za Serikali, hela ni za watu binafsi, leo mmekamata watu mmepeleka magereza. Sasa tunapojenga hoja, mkae kimya. Wote sisi ni Watanzania. Humu tunafanya nini? Wote sisi humu ni Watanzania tunaongea kwa manufaa yetu wote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jamani mimi nanukuu maneno ya Rais unanyanyuka unasema tusiongelee viongozi wa zamani, tumuongee nani? Shetani wa zamani? Tumuongee nani? Mungu wa zamani? Tumuongee nani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tungekuwa sisi tunatawala mngetusema. Sisi hamuwezi kutusema sana kwa sababu hatutawali, ninyi ndiyo mnatawala, tupeni fursa ya kuwarekebisha na hapa ndiyo pa kusemea. Wewe pia unataka Uwaziri, unaweza ukakaa sana. (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, twende kwenye hoja za msingi. Nataka niamini, nataka nifanye assumption Rais tuliye naye ni mzalendo, nataka niwe na hiyo assumption. Nataka niwe na assumption kwamba Rais tuliye naye anapenda watu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Rais Magufuli alisema hivi, alikuwa ana-beep watu wakapokea. Najiuliza kwa power mliyompa Rais ya kusimamia rasilimali za za nchi hii, siku moja anakuja Rais ambaye sio mzalendo kama Magufuli, nataka niamini hivyo, anatokea hata upande huu, inawezekana akatokea hata CHADEMA kwa sababu huku hawako malaika, anaweza akatokea CUF kwa sababu CUF hakuna malaika, akatokea Rais siyo mwaminifu mmempa power ya ku-manage na kusimamia rasilimali zote na mkawekea Bunge masharti nafuu kuhusu usimamizi huo, Taifa hili litauzwa. Mnapotunga sheria hamtungi sheria kwa kumwangalia Rais aliyeko madarakani, bali mnatunga sheria kwa assumption kwamba anaweza akaja Rais ambaye si malaika kama mliye naye na siku moja Taifa hili likaingia mahali pabaya na hili ndilo angalizo tunataka mliangalie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiongea mnafikiri tunawachukia, tunawachukiaje? Ninyi wote nyie tukikaa kantini maneno mnayoongea ni tofauti kabisa na mnavyo- behave huku na sijui kwa nini. Kama tungekuwa tunawarekodi ninyi maneno tunayoongea kwenye kantini tunampelekea Magufuli, kwenye Kamati tukitoka nje mnaongea tofauti, lisaidieni Taifa hili. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ni Mbunge awamu ya pili, Wabunge wote unaowaona hapa asilimia 70 ni wageni, pengine hamtarudi tena kuwa Wabunge ninyi na kama hamtarudi kuwa Wabunge…

Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge wote ninyi 70% hapa ni wageni, tunasema hivi tutunge sheria hata kama siku moja mtoto wako hatakuwa Waziri, hatakuwa Mbunge, hata kama hautarudi Bungeni sheria hizi bado zinaweza zika ku-protect hata kama huna- influence ama huna connection na mtu yeyote. Sisi tukileta mawazo haya ndugu zangu mkubali kwamba opinion zetu siyo kwa sababu ya kuwashinda bali ni kwa sababu ya kurekebisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunapoanza kulalamikia kwamba hii Miswaada inakuja kwa njia ya Dharura na wakati kuna muda, leo makinikia yamezuia Bandari ya Dar es Salaam, Rais ana mamlaka. Ukweli ni kwamba kutokuiamini Taasisi ya Urais siyo jambo la maana hata kidogo, kutokumwamini Rais siyo jambo la maana hata kidogo, lakini kwa mazingira ya mataifa ya Afrika na demokrasia ilivyo Taasisi ya Urais lazima iwekewe check and balance ili Taifa hili liweze kwenda salama kwa sababu anaweza akaja mtu, siyo kama huyu malika tuliye naye. (Makofi/Kicheko)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)