Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Ally Abdulla Ally Saleh (39 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Unapotazama bajeti hii lazima takuwa-impressed na takwimu hasa kwenye kipato ambacho nchi hii inapata. Lakini utakuwa unajiuliza kama mwananchi kwa sababu utakuwa na matumaini kwamba tunaweza kutoka kwa mali ambayo tunayo katika nchi hii, mbali ya mali nyingine za misitu na bahari na kitu gani. Picha ya utajiri tulionao katika nchi kwa upande wa madini haionekani katika picha kubwa ya Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, unaamini kwamba madini yangeweza kututoa kwa sababu wako watu wana madini au wana resource moja, mbili na wametoka na nchi zao zimekwenda mbele sana. Sasa sisi kama nchi ukitazama katika kitabu hiki unaona kuna mapato mengi, lakini unaweza ukajiuliza is this our level best, have we done our best katika suala la madini au la gesi? Kwa sababu siyo tu kuna room to improve, lakini naona kama kwamba unajiuliza, tatizo ni nini? Ni sera, ni mipango, ni utekelezaji, ni kitu gani? Kwa sababu zipo nchi ambazo zimeweza kutoka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Angola ilikuwa na vita kwa muda mrefu, lakini baaa ya kutoka kwenye vita wamejipanga, sasa hivi wana kipato kizuri kinachopita dola 8,000 kwa kila mtu. Botswana nchi ndogo, ina GDP ya 38 au 39 billion dollars. Sasa hivi Mbotswana anapata dola 18,000 per capita yake na resource yao ni chache, uranium kubwa kabisa na vitu vingine vidogo vidogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sisi Tanzania tunayo madini ambayo mtu mwingine katika Nchi nyingine angeweza kujiuliza why are you poor? Tusifananishwe na nchi kama Congo ambayo inautajiri mkubwa. Lakini Congo wana tatizo moja kubwa katika suala la utawala bora, lakini sisi tuna utulivu wa kutosha. Kwa hiyo, pamoja na uzuri wa kitabu hiki lakini ukisoma vitabu vingine viwili vya Hotuba ya Kamati na Hotuba ya Upinzani unaona kwamba kumbe tuna mengi ya kufanya ili tuweze ku-realise utajiri ambao Mungu ametujaalia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, na Mungu ametujaalia utajiri ule, ameuleta kwa sequence. Kila baada ya muda tunavumbua kitu kingine ambacho ni kizuri zaidi kuliko kitu kingine. Tulikuwa na almasi tangu miaka ya boers, imeondoka almasi ikaingia dhahabu sasa hivi Mungu katujaalia kuna madini makubwa zaidi ya graphite, tuna uranium inakuja lakini tunajipangaje katika hivi? Sasa mimi najiuliza, kwa mfano, tuna uranium na graphite ambayo ni madini very strategic, lakini je, tunayo sisi wenyewe strategic mineral policy?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tunavyojua madini yanatumika yanakwisha lakini tunajipangaje madini haya yawe ya kututoa. Je, tunatengeneza sovereign fund kutokana na madini haya? Madini yatakwisha lakini nchi itabakia. Nchi inajitayarisha kwa mfuko ule ambao utaweza kuwa akiba kwa siku za mbele?
Mheshimiwa Mwenyekiti, Qatar kweli ina gesi, Angola kweli ina petroli na vitu vingine lakini wana sovereign fund ambayo wanaweka akiba kwa ajili ya baadae. Sasa utajiri wote ambao tunao hivi sasa tunaojivunia, hatutawekea vizazi vyetu huko mbele lakini pia hatutoweza kufanya uwekezaji wa uhakika kwasababu kama nchi hatuna mfuko wa sovereign fund. Jambo hilo nimelisema hapa kabla na ninalisema tena kwa sababu mtu yeyote anaye study Qatar, Norway na wengine wamefaidika katika hilo. Sasa nilisema ukisoma hotuba ya Waziri, soma na vitu vingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, twende kwenye REA. REA tunasema fedha zake zinajulikana zinapatikana njia gani na zimetengewa sheria kwamba lazima zitumike kwa njia ile. Jana tumeambiwa hapa kwamba shilingi bilioni 73 hazikutumika inavyopaswa. Unajiuliza kama shilingi bilioni 73 hizi zingetumika tungepata umeme kiasi gani kwa vijiji vyetu? Na kwa nini hazikutumika na zimekwenda wapi? Kama ambavyo wamesema watu wengine pia ningependa kumuuliza Bwana Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, makaa ya mawe ya Mchuchuma, Liganga kila mtu Tanzania amekuwa akiisikia. Kama nchi tuliwahi kujitayarisha kutumia sisi wenyewe ndani? Tumekuwa na mkakati wa kuongoza nchi kwamba hatuwezi kutumia makaa ya mawe? Makaa ya mawe haya kwa maana nyingine yapo lakini ni kama, kule Zanzibar wanasema kama joka la mdimu, yapo hayatusaidii kitu. Tumekaa nayo, hatuyauzi nje wala hatutumii hapa ndani kwetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni madini. Kama nilivyosema pale mwanzo, tuna madini ya kutosha, kumekuwa na malalamiko mengi hapa. Hata ile alama ya Tanzania (Tanzanite) bado hatuitumii inavyopaswa. Lakini mbali ya hayo, madini mengine mengi ambayo tunayo katika nchi yetu, hatujayatumia kiasi cha kutosha. Mimi naamini kama tungekuwa tumejipanga basi haya yangeweza kututoa. Tumeambiwa katika report ya Kamati kwamba kipato kwenye madini kimeshuka kwa asilimia 19, unajiuliza kitashukaje kwa sababu madini bado yapo kama kuna mikakati mizuri na mipango mizuri ya kutosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwahivyo mimi naamini tungefanya kazi vizuri katika eneo hili. Eneo lingine kama nilivyosema pale mwanzo, ni uranium na graphite. Tanzania, watu wengine wamesema hapa tunaweza kuwa katika kumi bora wa matumizi ya graphite. Graphite imekuja kama akiba yetu, kama hamadi kibindoni ambayo tunaweza tukaitumia ili nchi tuweze kusimama sawa sawa. Lakini kama nilivyosema mwanzo kama hatujakuwa na strategic mineral policy ambayo itatuongoza namna ya kuzuia vitu vyetu hivi basi hatutafika mbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, jana nilisikia wazo ambalo nililipenda kidogo, wazo la STAMICO. Tunawekeza sana katika STAMICO, na dada mmoja hapa amesema, sehemu nyingine walizonazo STAMICO ziruhusiwe kwa wachimbaji wadogo wadogo; lakini lilikuja wazo zuri hapa. Wazo lenyewe ni kwamba badala ya STAMICO kung‟ang‟ania kuwekeza na kushindana na makampuni makubwa, kwa nini tusibadilishe format, STAMICO ikawa inanunua shares ambazo zitakuwa zina uhakika, kwa hili wazo ililtolewa na upande wa upinzani ambazo zitaweza ku-maintain hii kuliko kung‟ang‟ania kitu ambacho STAMICO hiyo enzi na enzi haijatutoa popote pale na bado tuko pale pale tulipo. Wazo hilo nimelipenda na ningependa Waziri alifikirie.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni kuhusiana na suala la gesi. Ni kweli kama nchi tunajipanga kwamba tunataka kutumia gesi ikifika mwaka 2023. Lakini tujue tunajipanga, tuna majirani zetu Mozambique nao wana gesi ambayo inaweza ku-equal na kile ambacho tumekipata hivi sasa. Kwa hiyo, tujue tutakuwa na ushindani wa karibu, tena maeneo ambayo yamekaribiana. Kwahivyo mtu anaweza akachagua kuja Tanzania au kwenda Mozambique kwa sababu kijiografia ni maeneo yako karibu na kwahivyo kama hatujajipanga sawa sawa hatutaweza kufaidika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ningeshauri, suala la LNG lingetazamwa mapema na namna ambavyo tutafaidika kwa sababu watu wote waliopata gesi wametoka. Qatar, Norway na wengine wote lakini kwa ambavyo mara nyingi naona katika nchi yetu tunaweza kuwa na gesi lakini bado tutakuwa maskini kwa sababu umaskini wa Tanzania kwa sehemu kubwa ni umaskini wa kujitakia. Ndiyo maana nakubaliana na hoja ya Kamati ambao wamesema, Serikali iandae mpango mkakati wa usimamizi wa gesi asilia pamoja na kutafuta masoko mapema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, dunia ya ushindani, tujipange kwa muda mrefu. Gesi na vitu vingine vinaweza kututoa lakini kama sivyo tunaweza tukabakia hivi badala ya kuwa economically giant tukawa economically dwarfs.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa mara ya kwanza nimeitwa jina ninalolipenda la Albeto.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo machache ya kuzungumzia na kwanza nitaanza na mjusi, Wajumbe wengi humu wamepiga kelele juu ya mjusi kwamba, kwa nini harejeshwi Tanzania! Mimi ni katika wale ambao wanaunga mkono arejeshwe, lakini najiuliza kama tuko tayari kumpokea na tunaweza kumtunza; lakini kumrudisha tunaweza. (Makofi)
Mheshimmiwa Mwenyekiti, tayari kuna international precedents nyingi zimetokea za mali ambazo zimechukuliwa katika nchi na zikarudishwa. Mfano wa karibuni kabisa ni wa Ethiopia, kuna mnara unaitwa Obelisk, umri wake ni karibu miaka 1700 na una urefu wa mita kama 24, ulikuwepo Italia kwa miaka 68. Baadaye Ethiopia wameweza kuurudisha na upo nchini kwao na ni sehemu ya utalii wao. Sasa inategemea kama Serikali tunaweza ku-negotiate tukaweza kumrudisha. Hata hivyo, kabla ya hapo ningependa sana tutengeze mazingira ili mjusi huyo asije akaozea kwetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni suala la utalii nitalizungumza kwa undani kidogo kwa sababu ni area ambayo naielewa vizuri zaidi. Kwanza, ningetaka kusema kwamba, tuna haja ya kushambulia emerging markets, emerging markets, markets mpya hizi za China, Urusi, India, Arabia, ni sehemu ambazo zinatengeneza pesa sana na hata ukilinganisha namna ambavyo wanatengeneza mamilionea per day wao wako mbele. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni namna gani utatumia kuwavutia kuja kwetu? Nitatoa mfano mdogo wa namna ambavyo kama tutaweza kufaidika na emerging markets, mfano nitakaotoa ni wa Mauritius. China katika mwaka 2011 walipeleka watalii 15,000 Mauritius. Mwaka uliofuata walipeleka watalii 22,000, mwaka mwingine walipeleka watalii 14,000 na mwaka 2014 wakapeleka watalii 63,000 na ushee. Mwaka 2011 India walipeleka watalii 53,000, ikawa 55,000, ikawa 57,000, ikawa 61,000 na naamini tukisema hivi sasa rate yao itakuwa imepanda. Kwa hivyo, namshauri Mheshimiwa Waziri kwenye Wizara yake ajaribu kwenye emerging markets, hilo la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ni suala la re-branding Tanzania. Tanzania tumepitia process mpya kubwa na ndiyo maana hata tukaona kuna haja ya kufanya katiba mpya kwa sababu kama nchi tumepitia mambo mengi lazima tujitambulishe upya kama Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, branding ambayo tunayo hivi sasa ndiyo ambayo kwa miaka yote imetupa watalii milioni, labda 1,200,000. Hii branding nataka ifanywe upya tujitambulishe tuna vitu gani vya kuuza, vinapatikana wapi, vinapatikana vipi, rates zetu ziko vipi. Kwa mfano, tumetumia brand ya Tanzania, land of Kilimanjaro and Zanzibar kwa miaka yote hiyo, tumepata watalii 1,100,000.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashindwa kupata watalii zaidi kwa sababu sisi hatutaki kujilinganisha na wengine, sisi tuna vivutio vingi, Mauritius wana vivutio vichache kuliko sisi lakini wao wanatupita, wao tayari 2014 walikuwa wana watalii 1,200,000. Ni kisiwa cha watu 1,500,000 lakini wamepata watalii 1,200,000. Kwa hivyo kuna haja ya ku-re-brand. Lakini hiyo re- branding tusiifanye sisi tuwape watu, mashirika makubwa wanaoweza kufanya re-branding ili tuweze kupata faida. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hiyo hiyo na sasa nataka nizungumzie habari ya re-discovering our pontentials. Watu wengi wamezungumza hapa, kuna watu wamezungumza kwamba, inaonekana kama kuna upendeleo au ndiyo culture tuliyoachiwa, kwamba utalii ni kaskazini. Lakini kuna southern circuit ambayo inaweza ikatusaidia sana. Pia kuna sehemu nyingine za pembezoni, kwa mfano Mara, Arusha wameungana na Kenya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tumejipanga vipi sisi utalii wetu kuungana na Uganda, tumejipanga vipi utalii wetu kuungana na Mozambique, kuungana na sehemu nyingine ambazo tunapakana nazo. Nitatoa mfano wa Kagera, kagera tuko na Uganda. Lazima tuwe na package ambayo inamfanya mtu akienda Uganda baadaye akija Kagera ashawishike. Juzi nilifunuliwa macho na Profesa Tibaijuka hapa aliposema kuna ziwa linaitwa Ziwa Burigi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiambiwa chochote dakika ile ile nakwenda kwenye internet. Pale pale nikaenda kwenye internet nikaona how beautiful that place is. Ni mahali ambapo mtu yeyote angeweza kwenda. Tuna game reserve ya Burigi lakini tuna ziwa, lakini hakuna hata kibanda cha mtalii kufika. Pale kwa nilivyosoma na nimetamani, nimemwambia mama Mwigaje hapa nataka niende nikaone, ile picha niliyoipata Ziwa Burigi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo tunaweza tukamshawishi mtalii kutoka Uganda akaja pale, hali kadhalika southern circuit. Kuna fursa nyingi beach sun mpya za Mtwara na Lindi, mnazitumiaje kama sehemu ya southern circuit. Kwa hiyo, tubadilike katika hilo.
Mheshimwa Mwenyekiti, halafu nataka kuzungumzia juu ya advertising. Nchi kama Malaysia, Indonesia, zimepiga hatua kubwa sana katika utalii, lakini bado wanatangaza costing millions to them. Tangazo lao linapendeza, unalipenda, unalisikiliza. Kwa hivyo lazima tuchukue international firms siyo tunapeleka tangazo kwenye Sunderland ambalo linawekwa tu hivi. Tangazo lazima liwe strategic, idadi ya watu wangapi, tunafaidika vipi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija katika nukta hii hii nataka nizungumzie Walking billboard. Tuna Mbwana Samata anacheza mpira Belgium, kwa nini kama Taifa au kama Wizara tusiingie naye mkataba akifunga goli akiinua jezi tu visit Tanzania, ambayo inaonekana dunia nzima na sio Belgium tu, lakini hatutumii potential tulizonazo. Kwa hivyo, ningependa hili tulitazame. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna sports tourism. Nilizungumza na Mheshimiwa Nape juu ya namna ya sisi kujipanga kama Taifa. Nchi hii hakuna international tournament ya golf, hakuna international tournament ya Tennis, hakuna international tournament ya cycling. Nchi kubwa lakini haijajipanga vyovyote vile kimichezo. Kwa hivyo, ningependa kwamba, eneo hilo pia tulitengeneze ili tuweze kuzitumia vizuri tufaidike. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nataka nizungumzie role mpya ya Mabalozi. Mabalozi wote lazima waelekezwe kwamba, hivi sasa tutengeneze tourism diplomacy kuwe na package, watayarishwe, wawekewe na malengo namna ambavyo wanaweza kukuza utalii wetu; lakini isaidie kwamba, watengenezewe package ili tuweze kufaidika ndani ya nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, nataka nizungumzie suala la kutengeneza mnaso wa community kubwa ya wageni wanaoishi maeneo ya East Africa. Mzungu au expert yeyote ambaye yuko East Africa unamtoza visa sawasawa na ambaye amekuja leo kutoka Marekani. Tuwe na package maalum ya expertise kutoka Rwanda, Kenya, Uganda, tuwe na package maalum washawishike kuja kwetu. Mtu mmoja alisema lazima tuweke rates za kuvutia ili watu waje, baadaye tuweze kubadilisha lakini lazima tu-change katika strategy hizi na kwamba, tunatoza kodi nyingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ni very expensive destination, tusijisifu kwa watu wanaokuja, tungeweza kupata watu zaidi kama tutajitengeneza vizuri zaidi. Sisi ni losers, hatuna haja ya kushindana na Kenya, hatuna haja ya kushindana na Uganda, tuweke rates ambazo zinatufaidisha sisi na ndiyo maana tutawashinda. Ndiyo maana kukitokea matatizo Kenya sisi tunafaidika. Kwa hiyo, tusingojee mpaka Kenya wapigane sisi tufaidike. Pia tunaweza tukaweka rates ndogo ili tuvutie watalii zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia ningependa kuzungumzia habari ya standards. Tunakwenda nchi za wenzetu, tuna hotel higher lakini unaona kwamba, bado tuko nyuma, service mbovu. Ningependa tuhakikishe kwamba, tunakuza sekta kwa kuwa hata na masomo ya degree na tuweze …
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Alberto.
Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. ALLY SALEH ALLY: Hayupo, ndiyo maana nikaomba nafasi hiyo nichukue mimi. Hayupo Dodoma.
MWENYEKITI: Hayupo Dodoma. Umejipangia wewe mwenyewe, haya.
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, sikujipangia, nimekuletea ombi la ruksa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ahsante. Tukitazama utekelezaji wa mpango wetu kwa muda wa miaka mitano iliyopita na hata mwaka mmoja uliopita, hatupati picha yenye kutia moyo. Ingawa umetekelezwa lakini kuna upungufu mwingi, ambapo kwa mfano kwenye umeme hatukuweza kufikia kiwango ambacho tulikuwa tumejiwekea cha zaidi ya megawati 4000. Kwenye barabara hatukuweza kufanikiwa ni chini ya asilimia 50, kwenye reli kilometa 174 au 75 zilizoweza kukarabatiwa. Pia kwenye irrigation ambapo jana kuna mtu mmoja alitoa taarifa, nilikuwa sijui kama tuna potentiality ya 20 million lakini kitu ambacho kimefanywa katika target ya milioni moja, tumefikia only 23%, pia Deni la Taifa limeongezeka katika miaka hii kutoka tisa mpaka 19.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, kama Wabunge na kama Serikali tunatakiwa tujiulize wanatupa moyo gani au wanatupa hope gani ya kuweza kutekelezwa kwa mpango huu unaokuja, wakati Mpango ambao umemalizika ulikuwa very much under-performed.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimefurahi kwamba Serikali wame-mention baadhi ya changamoto katika ukurasa wa 13 wa hotuba ya Mheshimiwa Waziri na wamekuja na solution katika ukurasa wa 14, katika baadhi ya changamoto zile imezungumziwa pia sekta binafsi kwamba ni solution mojawapo ambayo inaweza ikasaidia ikiwa suala zima la funding litafanywa kwa uhakika yaani ugharamiaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niiombe Serikali kwamba, wakati wakija na Mpango kamili hapo baadaye, waje na andiko ambalo litaelezea hii sekta binafsi itachangia vipi katika Mpango huo ili kuhakikisha kwamba funding inapatikana ya kutosha ndani lakini pia kutoka nje, baada ya kuwa na andiko ambalo litaonesha namna gani sekta binafsi itaweza kuchangia katika Mpango wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, ningependa pamoja na vile vipaumbele pale vilivyowekwa ambavyo ni vinne, ningependa suala la utawala bora lingewekwa kama mtambuka, kwa sababu tunalo tatizo kubwa la utawala bora ambalo huko mbele tutalizungumzia zaidi lakini katika hatua hii nataka niseme kwamba, sasa hivi Tanzania inadaiwa kuwa kuna suala kubwa la rushwa, inaidaiwa kwamba kuna tatizo la utekelezaji hata wa maagizo kutoka Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, lakini pia kuna madai mbalimbali ya wananchi kunyanyaswa katika sehemu mbalimbali. Kwa hivyo, ili Mpango uwe endelevu na unaoweza kuwa wa uhakika, ningependa katika vipaumbele hivi pia suala la utawala bora lingewekwa katika umuhimu mzuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimevutiwa na Mpango wa Serikali wa kuweka katika yale mambo ya vipaumbele, kuweka miradi ya flagship, miradi ambayo hiyo itakuwa ni miradi kielelezi. Hili ni wazo zuri na ningefurahi kama katika wazo hilo katika mradi mmojawapo ambao unaweza kuwekwa au katika miradi ambayo itafikiriwa suala la Zanzibar liwe incoperative.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu mimi ni Mtanzania lakini nampigia kura Rais wa Tanzania, lakini pia kuna Wazanzibar ambao wanatumikia Serikali, sioni sababu gani Serikali ya Muungano haina specific project Zanzibar zaidi ya zile za kukagua kodi tu au za immigration ambapo kuna jengo kubwa. Hata hivyo, ningependa nione Serikali, inachangia kwa kuwa na mradi maalum (specific) ambao ni wa kutoka Zanzibar, ili Wazanzibar waone kwamba Serikali yao inawajali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo katika miradi ambayo ni ya flagship, ningependa tuweke mradi, eneo letu ni dogo la ardhi, miradi ambayo inaweza ikaweka; nilisema juzi mama Waziri ulikuwepo, nilikwambia suala silicon veiling tunahimiza katika eneo lile la miradi wezeshi, habari ya TEHAMA. Ni vizuri, tukili-consider suala la silicon veiling, Tanzania ina urafiki mzuri na Bill Gates, tungeweza kutumia ushawishi wetu wa kuleta mradi kama huu wa silicon veiling ambao hauhitaji eneo kubwa sana lakini inaweza ikazalisha eneo kubwa. Mpaka sasa katika eneo letu lote la kanda hii hakuna mahali ambapo pana silicon veiling. Kwa hivyo, kwa wazo hilo ningependa tulitumie vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, ningependa kuona kuwa tunatumia bahari yetu. Tuna masafa ya bahari ya kilomita 1,400 kutoka pembe mpaka pembe ya chini. Nchi kama Seychelles nchi ndogo kabisa ambayo ina watu laki moja. Ambayo ina eneo inaingia ndani ya Tanzania zaidi ya mara 2000 wao ndiyo wanaongoza duniani kwa uvuvi, wa pili kwa uvuvi wa samaki aina ya Tuna, sisi tuna bahari hapo hatujaweza kuitumia vya kutosha. Kwa hivyo hili, ningependa lifanyiwe mkazo kwa sababu tuna uwezo mkubwa sana wa kuvuna kutoka baharini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kitu kingine ambacho ningependa tukitumie kama alama ya Tanzania ni excellence in education. Tunaweza tukajipanga vizuri, tukaweza ku-specialize katika maeneo maalum, zamani nakumbuka niliwahi kusikia, katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam masuala ya maji Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilikuwa kina-save almost kanda yote hii hapa. Mtu yeyote akitaka kuja kusoma maji anakuja Tanzania. hata katika East Africa zamani ilikuwa kuna mgawanyiko, ukitaka kwenda kusoma kurusha ndege unakwenda Soruti, ukitaka kufanya kitu gani unakwenda sehemu gani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, ningependa hili tuli-concentrate, nchi kama ya Cyprus nimekwenda Northern Cyprus, uchumi wake mkubwa unategemea education wamejenga vyuo wame-specialize katika maeneo maalum wamejitangaza dunia nzima, wamejitangaza katika kanda mbalimbali, kwa hivyo wao wanavuna sana kutokana na suala zima la education.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, nataka kuzungumzia, nilisema pale nitarudia kwenye suala la utawala bora. Nataka nirudie hili la Zanzibar, kwanza nafadhaishwa sana kuona Mawaziri wetu hapa Waziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa Ulinzi wanakataa, wanakana kama hakuna suala la mazombi na masoksi Zanzibar, inaniumiza moyo sana. Labda kwa sababu ndugu yake, labda kwa sababu jamaa yake, au kwa nafasi yake yeye hajawahi kukutana na mazombi wakamdhuru au wakamfanyia vitu vingine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati haya yakitokea tunakwenda katika Uchaguzi wa Zanzibar ,tunaambiwa kama unarudiwa, lakini ningependa Serikali itazame upya, itazame implication za kurudia uchaguzi huo, socially implication, 2001 siyo mbali, watu 4000 walikimbia nchi hii wakaenda Somalia. Tutazame economic implication, ikiharibika Zanzibar hakuna uchumi Bara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jana alikuwa anazungumza mwenzangu mmoja anasema baada ya uchaguzi hapa hatuji hapa kujadili mpango, tutakuja hapa kujadili namna ya kujitoa kiuchumi. Kukiharibika Zanzibar, mtalii haji Ngorongoro, kwa sababu mtalii anaji-program kuja Ngorongoro kisha anakuja Zanzibar. Kuna security implication, ikiharibika hali ya Zanzibar hapatakuwa salama katika Tanzania, kuna stability implication, hali ya Zanzibar ikiharibika pia hapatakuwa stable hapa. Mnapotupeleka sasa hivi kama watu hawapati nafasi yao, uhuru wao, kupitia kwenye Katiba watatafuta kwa njia nyingine. Hizo njia nyingine ndiyo ambazo tunataka kuziepuka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, ni negative public relation, hivi Tanzania inajijengea sifa gani kwa dunia. Tanzania imekuwa mfano wa dunia, kwamba ni nchi ambayo inaheshimu demokrasia, ni nchi ambayo inaheshimu haki za binadamu, inaheshimu uchaguzi. Kwa nini tunalazimisha kwa Zanzibar, tulazimishe uchaguzi ambao hauna hata mantiki moja. Unarejea uchaguzi ili iwe nini, Tume ile ile, kwa maana ya marefa wale wale, ma-linesmen wale wale waliokufungisha mabao manne halafu unarudia uchaguzi ule ule, mnarudia uchaguzi ili iwe nini, tupate suluhu gani?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri kuna haja ya Serikali kukaa kwa maana ya uchumi, kwa maana ya stability, kwa maana ya security implication, tukae chini tutazame suala la Zanzibar. Kama mnataka kumwokoa Dr. Shein awe Rais lazima utafute njia nyingine. Ahsante sana. (Makofi)
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016/2017 – 2020/2021
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza hakuna mwenye nia mbaya, sote ni wananchi na sote hii ni nchi yetu. Tunachofanya ni wajibu wetu kuikosoa Serikali na kuishauri Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nianze kwanza kwenye deni la Taifa. Jana wakati wa presentation ya Mheshimiwa Mama Hawa hapa, wakati ilipozungumzwa na Kambi ya Upinzani kwamba deni ni kubwa na kwamba kuna haja ya kufanya auditing ili tunapoingia katika Mpango huu ambao utagharimu Shilingi trilioni 107 tujue deni letu kabisa kabla hatujaingia huko, Mheshimiwa Mama Hawa alijaribu ku-defend akatoa vigezo vingi vya kuonesha kwamba deni hili bado ni manageable. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nataka kusema kwamba, wenzetu wengine pia walisema madeni yao ni manageable. Bolivia wana mafuta, walisema deni lao ni manageable, lakini baadaye wakaingia kwenye matatizo makubwa! Argentina wana uchumi mzuri na ndiyo wanaoongoza kwa uchumi wa ng‟ombe duniani, walifikiri deni lao ni manageable na waka-collapse! Hali kadhalika na Greece!
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naungana kwanza na Waziri Kivuli wa Fedha wa Kambi ya Upinzani kwamba ni vizuri Bunge hili likatoa Azimio au tukazungumza kwamba kuna haja ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutufanyia auditing ili tujue tunasimama wapi. Katika hizo Shilingi trilioni 107 za kuendesha Mpango, maana yake pia tutakopa. Tumefika hapa kwa ajili ya mikopo ambayo hairudishwi. Kwa hiyo, ni bora wananchi wetu wajue tuna madeni kiasi gani kabla hatujasonga mbele na vipi tutaya-manage madeni hayo. Hilo ni la kwanza! (Makofi)
Mheshimiwa Spika, la pili ni kuhusiana na kipato. Tumeambiwa kwamba sasa hivi kipato chetu kwa Mtanzania ni wastani wa Dola 1,006. Kipato hiki tunaambiwa kwamba, ndicho ambacho Mtanzania anapata. Tumekuwa tukisema hapa kwamba kipato hiki hakionekani kwa Mtanzania wa kawaida, ni pesa za makaratasi zaidi; na tunaambiwa kwamba, tunaelekea kwenye kipato cha Dola 3,000, ndiyo lengo letu!
Mheshimiwa Spika, kama mwananchi, napenda tufikie huko na nchi iingie katika kipato cha kati, lakini Mpango haukueleza base kubwa zaidi; haujapanua base kubwa zaidi ya namna ya kuelekea kwenye kipato hicho kwa kuamini tu kwamba, viwanda ndiyo vitatuletea kipato, lakini ziko sehemu nyingine nchi hii hazihitaji viwanda wala Watanzania wote hawatafanya kazi kwenye viwanda. Kwa hiyo, rai yangu ilikuwa ni kupanua base.
Mheshimiwa Spika, kwa mfano, naambiwa katika Wilaya ya Lushoto au Mtanzania yeyote anajua kwamba wao wanaongoza kwa mazao ya kilimo, mfano mmoja. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Lushoto wanatoka Wakomoro wanakuja pale wanachukua bidhaa wana-pack kabisa wanazipeleka Comoro na pengine zinafika mpaka Ufaransa! Sasa kwa nini tuwaachie Wakomoro wafanye kazi hiyo badala ya kuimarisha wananchi wetu tukawapa fedha wakaweza kufanya vitu kama vile tuka-add value katika bidhaa zetu za kilimo ili kufikia masoko kama hayo? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, la pili, tumeacha area moja kubwa sana katika nchi yetu; area ya uvuvi. Uvuvi wetu ni wa ndoana, wa hapa karibu karibu. Uvuvi wetu haujawa mkubwa wa kutosha. Nimesema katika Kikao kilichopita kwamba tunashindwa na nchi ndogo ya Seychelles ambayo ina watu 100,000 lakini wanaongoza kwa uvuvi wa jodari! Kwa duniani wao ni wa pili!
Mheshimiwa Spika, tuna ukanda wa bahari wa kilometa 1,400 hatujautumika vya kutosha. Jana nilisikia hapa kwamba kuna taarifa kwamba kwenye benki kuna dirisha la kilimo katika mambo ya ukopaji, napenda nione tunafungua Benki ya Uvuvi, iwe specifically located kwa sababu tuna sekta kubwa sana, uvuvi wa kutoka maziwani mpaka kwenye bahari kuu. Kwa hiyo, napenda Serikali ilizingatie hili ili tu-take fursa ambayo inaweza ikapatikana.
Mheshimiwa Spika, kingine ambacho nataka kusema, ni kuhusiana na Mtwara Corridor au sehemu ya Kusini. Kusema kweli, ingawa hapa Bungeni kwa observation yangu, mara nyingi watu wanajivutia Kikanda.
Mheshimiwa Spika, watu wanazungumzia habari ya Reli ya Kati na utaona wengi wanaozungumzia Reli ya Kati maana yake ni watu ambao wanatokea upande wa huko. Kwa fikra yangu nahisi Mtwara is the next big thing in Tanzania, really! Yaani kwa kanda ile kule! Hivi sasa kuna gesi, viwanda vinakuja na capital chemicals nyingi kutokana na LNG ambayo ukitoa gesi maana yake unapata LNG na viwanda vya aina nyingi.
Mheshimiwa Spika, pia, juzi juzi nimesoma kwamba yamegunduliwa madini ya graphite. Madini haya hivi sasa waliotangaza kugundua ni kampuni ya Marekani na mmoja katika Board Members (Stith) ni mtu ambaye alikuwa Balozi wa Tanzania…
MHE. ALLY SALEH ALLY: Anaitwa Stiff, anasema graphite iliyogunduliwa Tanzania inaweza kuwa ya pili baada ya China duniani, lakini pia inaweza kuwa ya kwanza kuliko hata China. Kwa hiyo, ina maana kuna potential kubwa sana.
Mheshimiwa Spika, jana Waziri mmoja alituambia hapa kwamba kuna mpango wa kilimo cha mihogo ya tani milioni 200 kinakuja na soko lipo, lakini sioni uwekezaji unaofanana; kwa communication, unaofanana na rasilimali zilizoko Mtwara. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa hivi tumefungua Corridor ya Kusini kwa Uwanja wa Songwe. Tuna Uwanja wa Kilimanjaro. Kuna haja sasa hivi ya kuwa na Uwanja wa Kusini wa Kimataifa ili uelekee upande mwingine, tufungue Corridor nyingine, katika kila kona ya Tanzania tuwe tuna uwanja ambao unafanana na uwezo na hali tunayosema tunataka tuwenayo. (Makofi)
Kwa hiyo, nashauri kwamba the next big thing kuitazama ni Corridor ya Kusini, tujipange vizuri tuweze kuitumia vizuri ili tuweze kufaidika na gesi na vitu vingine ambavyo vinaambatana na mambo hayo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kingine ninachotaka kuzungumzia ni kuhusu Shirika la Ndege la Tanzania. Actually mpaka tulipofika hapa ilikuwa ni aibu sana kwamba nchi hii tumekubali Shirika letu la National Carrier kufa na hatukuweza kulitengeneza, mpaka hivi sasa tunataka kutengeneza kwa kuwa na ndege mbili. Tunasema kwamba tunatarajia kuwa na watalii wengi kwa sababu tutakuwa na ndege mbili. Actually kuwa na ndege ni kitu kingine na kupata watalii ni kitu kingine. Unaweza kuwa na ndege, lakini kama huna routes zinazofaa na kama hujapata kununua route kwa watu wengine na kama hujaweza kuiuza nchi upya, bado utalii hauwezi kukusaidia. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, pamoja na kuwa na ndege mbili, ambazo sifikiri kama itakuwa ni kitu kikubwa sana, lakini kwa maana ya kuanzia angalau tumeanza, nashauri pia, kama tunataka kufufua Shirika la ATC, mbali ya kwamba tunatakiwa tufagie ATC yote, lakini pia tutafute strategic partners ambao wanaweza kutupa routes nyingine ambazo tutaweza kuzitumia.
Mheshimiwa Spika, hivi sasa humu ndani routes zetu nyingi tumeshaziuza, tumempa Fast Jet kwa routes za ndani. Sasa utashindanaje na Fast Jet wakati ameshaweza kuji-establish kwa muda wa miaka mitatu ambayo yupo hivi sasa na wewe unakuja na ndege mpya? Kwa hiyo, ni lazima tuingie na Mashirika, tuwe na strategic partners ambao wataweza kutusaidia kutufungulia njia nyingine.
Mheshimiwa Spika, pia tutafute model nzuri ya kuwa na Shirika la Ndege. Ethiopia pamoja na kwamba walikuwa katika kipindi cha Haile Selassie, vita, udikteta, lakini bado ni shirika ambalo lilikuwa haliguswi na ndiyo maana limebaki kuwa shirika la mfano kwa Afrika na linafanya kazi na limekuwa likienda vizuri. Kwa hiyo, tusione aibu kuazima management au kuchukua management ikaja kutuwekea sawa mambo ili Shirika lile liende katika hali inayoweza kufaa na ikatusaidia sote kama nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho nataka kusemea ni suala la usalama na utawala bora. Nina mifano michache sana ya nchi ambazo zimeweza kufanikiwa katika kuingia kuwa nchi za viwanda ambazo zimekuwa hazina utulivu au zimekuwa zikiendeshwa na madikteta. Nchi chache kama Singapore na Lee Kuan Yu mfumo wake wa uongozi ulikuwa ni wa kubana lakini ilifanikiwa.
Kwa hiyo, hili ni eneo ambalo hatuwezi kuliachia hivi hivi. Hatuwezi kuwa na chaguzi ambazo kila mara sauti ya wananchi haisikiki, hatuwezi kuwa na chaguzi ambazo Serikali inapeleka majeshi na inalinda chama kimoja halafu tutarajie kwamba tutapiga hatua katika maendeleo. Kwa hiyo, suala hili ni muhimu sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho ningependa ku-cut across the board ni suala la disability, watu wanaoishi na ulemavu. Hili ni eneo ambalo Mbunge yeyote humu ndani halizungumzi kama vile siyo kesho yeye litamtokea.
Mbunge yeyote hazungumzi, kama vile hatuna asilimia 12 ya Watanzania ambao wana ulemavu wa aina moja au aina nyingine. Kwa hiyo, napenda program yote ya Serikali tusiseme tu katika UKIMWI, lakini pia katika disability, ika-cut across kote ili tuweze kutengeneza mazingira na tuweze kufanikisha ili kuona watu wenye ulemavu wanaweza kuchangia na wanaweza kupata fursa za aina nyingine yeyote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, cha mwisho nataka kusemea juu ya kile ambacho Waziri Simbachawene alikitolea taarifa hapa juu ya mshahara wa Rais. Actually aliye-raise suala la mshahara wa Rais ni yeye mwenyewe Rais. Ame-raise mshahara wa Rais yeye mwenyewe kwa sababu pengine alitaka liwe publicity stunts kwamba yeye ni Rais ambaye anapunguza mshahara na kwamba yuko pro-people na hivi na hivi. (Makofi)
Kwa hiyo, hili suala limekuja hapa siyo kwa sababu sisi tumelianzisha, ni kwa sababu yeye alianzisha. Kama itakuwa ilikosewa, ni kwamba waliomshauri walikuwa wamwambie kumbe hawezi kubadilisha mshahara wake akiwa yeye katika madaraka, lakini wanaofuata wanakuwa na madaraka. Pamoja na kazi nzuri inayofanywa lakini wakati mwingine wananchi wanajua wapi pana publicity stunts na wapi ni sifa ya kweli. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nina mambo machache ya kuzungumza lakini kimoja nitakisema in passing tu juu ya mwenge. Tusipeane majina wala tusipunguziane uzalendo kwa sababu tu hatuukubali mwenge. Mimi kwa bahati nilikuwemo katika Tume ya Warioba na katika kitu Watanzania walichokikataa na wakasema waziwazi uende makumbusho ni Mwenge wa Uhuru. Kwa hiyo, wanaosema kwamba mwenge upumzike au kama msemaji wa sasa hivi aliyesema tutafute modality nyingine mimi ni mmojawapo na hii hainipunguzii uzalendo kwamba mimi ni Mtanzania na naipenda Tanzania yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, sisi kama Taifa tunaishi katika zama za sasa, hatuwezi kuishi sasa kisha tukabakia kizamani. Sasa hivi dunia imepanuka, kuna technology mbalimbali na kuna njia mbalimbali za kuwasiliana. Wakati njia za kuwasiliana zinapanuka na wakati sisi tunapimwa kwa ajili ya kuwa wawazi kwa wanachi wetu na sisi kuwa huru kujieleza, ndipo sisi tunapofunga milango ya uhuru wa habari na uhuru watu wetu kujieleza. Hii hai-augur well na vipimo ambavyo sisi tunapimwa kama nchi na ndiyo maana ripoti ya Amnesty juzi imetu-condemn na kutushusha sisi katika suala la uwazi na uhuru kwa waandishi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi hii katika upande wa habari, mimi maisha yangu yote ni mwandishi wa habari na nimepita wakati ambapo tulikuwa tunabanwa hata kusema tulikuwa hatuwezi. Wakati naripoti Zanzibar naweza kuiandika story leo nikaenda Dar es Salaam nikakaa siku tatu nasubiri mshindo kule Zanzibar utakuwa vipi, tusiishi tena hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi hii wakati tunapanua demokrasia mwaka mmoja tunapitisha sheria tatu za kubana uhuru na kubana watu namna ya kujieleza, nafikiri hii si sahihi. Hii ni dalili ya woga na dalili ya kuogopa watu wako wenyewe wasiseme. Kiongozi mzuri, Serikali nzuri ni ile ambayo inaruhusu watu wao watoe joto lao, wajieleze ili wajue kuna kitu gani katika Taifa. Kwa hiyo, mimi nafikiri tusijivunie kwamba tunazuia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine tu kwa mfano, leo tumezungumza vitu vingi sana kuhusu wasanii na utamaduni, lakini tumejifungia humu ndani. Tumezuia wananchi wetu wasisikilize na wasipate taarifa juu ya mijadala ya Bunge kwa hofu tu kwamba wakisikia watabadilika mawazo, tusiogope hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambacho nataka kuzungumzia ni suala la kiswahili, watu wengi wanazungumzia habari ya kiswahili. Kwa wale ambao hawajui, mimi ni mpenzi sana wa Kiswahili na ni mwandishi wa mashairi lakini pia ni mwandishi wa vitabu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, wakati tunajivuna kwamba Tanzania ndiyo mabingwa wa kiswahili lakini kusema kweli Kenya wametutangulia. Graduates wa Kenya kwa kiswahili hatufiki sisi hata one third yao kwa kila mwaka. Sasa hivi katika mashirika mengi ya kimataifa, translators wengi walioko nje, vyuo vingi vikuu, walimu ni kutoka Kenya na siyo Tanzania. Nchi hii ya Tanzania ambayo inajivuna ina kiswahili niambieni kuna literature prize gani ndani ya nchi hii? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kenya katika zawadi ambayo inaongoza duniani kwa kiswahili ni Cornell-Mabati Kiswahili Prize ambapo mimi mwaka huu nime-submit kitabu changu kinaitwa La Kuvunda. Wenzetu hawa wanatoa zawadi kila mwaka kwa miaka mitano sasa na kuna commitment ya kampuni ya Mabati na Cornell University kuendelea kwa muda wa miaka kumi ijayo, hata hili hatuwezi kubuni ku-approach corporate world ya Tanzania ikashirikiana na chuo kikuu kimojawapo kukawa na literature prize kwa kila mwaka? Hii itaibua waandishi, tutabaki tunaimba tu tulikuwa na Ibrahim Hussein, Profesa Lihamba, Profesa Penina, wako wapi watu kama hao, hakuna tena caliber kama hiyo kwa sababu hatuwatengenezi. Tusitarajie tu kwamba watuzuka bila kutengenezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine ni suala zima la culture ya michezo ya kuigiza. Tunazungumza sana habari ya bongo movie lakini moja katika culture nzuri sana ni michezo ya kuigiza ambapo Tanzania imekufa. Nilipokuwa chuo kikuu ilikuwa wakija wale waigizaji Nkurumah Hall inajaa, sasa hivi hata sijui kama kuna michezo ya kuigiza ndani ya nchi hii kwa sababu hata waandishi wa michezo ya kuigiza hawapo tena na hawatengenezwi na hawatayarishwi. Kwa hiyo, namuomba Mheshimiwa Waziri alitizame hili, tuwe na competition za kila mara ili kuweza kukuza jambo hili. Sasa hivi tuna vyuo vikuu vinafika 50, jambo kama hilo linawezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nije katika area ya michezo ambayo naielewa vizuri sana kama ninavyoelewa suala la habari na hapa nitazungumza zaidi kidogo.

Mimi nafikiri ni katika wale ambao siamini kwamba Wizara au Serikali ndiyo yenye jukumu la michezo, mimi siamini. Mimi naamini Serikali kazi yake ni kutengeneza sera, lakini corporate world ndiyo ambayo inaweza kusimama na kukuza michezo na mfano mzuri ni huu wa Simbu hivi sasa. Niliwahi kuzungumza na Mheshimiwa Nape wakati akiwa Waziri kwamba tuache kumpa mzigo mtu mmoja kumwambia tunataka shilingi milioni 200 kwenda Olympic au shilingi milioni 500 kwenda Commonwealth, unakwenda kwa mtu mmoja mmoja, uache kila corporate imwambie wewe chukua dhamana ya mwanariadha huyu hapa, wewe chukua dhamana ya mwanariadha huyu hapa, tutafika mbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini watu wanalalamika wanasema hatupati timu kubwa za nje kuja Tanzania, wanalalamika kwamba rank ya Tanzania haipandi kwa sababu hatuchezi na timu kubwa. Kucheza na timu kubwa ni gharama kubwa sana, kuileta Brazil mimi mwenyewe nilijaribu, minimum wanataka dola milioni moja za kucheza uwanjani, mbali ya gharama zao. Kuileta Argentina inahitajika kama dola 800,000 kuwaleta wakacheza uwanjani mbali ya gharama zao nyingine za ndege na kila kitu. Kwa hiyo, kama corporate Tanzania hatujaishirikisha vya kutosha ikaweza kuchangia, hatuwezi kuzileta timu kubwa na maisha yatabakia kule kule zero. Maana yake unataka ulete timu lakini kiingilio unataka uweke shilingi 5,000, unasema eti unawajali watu wadogo, haiwezekani, lazima kimojawapo utakikosa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine watu wamezungumzia hapa habari ya vipaji, vipaji vinatengenezwa na tena siyo Serikali yenye jukumu la kutengeneza academy, ni mimi na wewe. Wabunge pia wana uwezo, wana haki na wajibu wa kutengeneza vipaji kwa sababu vipaji ni biashara, unaweza ukatumia shilingi milioni 100 lakini wakati ukiuza mchezaji mmoja unaweza ukapata shilingi bilioni moja. Kesi ya Samata kwa mfano, mimi nilikuwa involved mara nyingi katika biashara zake, najua namna ambavyo amefikia pale.

Kwa hiyo, watu wajue kwamba kuwekeza kwenye riadha, soka, vipaji inalipa kwa mchezaji mmoja tu ukipata, siyo wawili au watatu, mmoja tu inalipa. Kwa hiyo, Wabunge hilo pia mnaweza kulichangamkia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini sikubaliani na msemaji aliyepita hapa kwamba tuwalete wachezaji wengi wa nje wacheze ligi yetu ya ndani. Uingereza wana tatizo hivi sasa hawana timu ya Taifa nzuri kwa sababu wageni ni wengi. Cha kufanya sasa hivi TFF itengeneze kanuni kwamba klabu yoyote kwanza iwe na timu ndogo lakini ilazimike kama vile ambavyo kuna limit ya wachezaji wa nje kucheza watano basi lazima iwe na mchezaji under 20 katika kila mechi yake ya ligi, mmoja, wawili au watatu, hiyo itatusaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kingine naogopa time yangu isiishe nataka nizungumzie juu ya mchezo wa chess. Mheshimiwa Waziri nisikilize vizuri. Chess ni mchezo ambao unaweza kututoa Tanzania kwa haraka sana, kwanza hauna gharama. Mimi ni mshabiki wa chess na nafundisha chess. Ni mchezo ambao ukishapata bao lako la kuchezea, mnakaa watu wawili, ukivaa bukta, kanga, seluni (msuli) unacheza tu. Ni mchezo ambao unaweza kufundishwa na kukuza vipaji vya watoto wetu. Kuna uwezekano pia wa kusaidia kupata masters wa chess wakacheza dunia nzima na tukajulikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi nafikiri tusing’ang’anie tu michezo iliyopo na ndiyo maana hapa nataka kusema Mheshimiwa Waziri lazima hivi sasa tuamue tuwe na priority, iko michezo tumecheza miaka haijatupeleka popote, lakini iko michezo inayoweza kututoa. Kwa hiyo, hata kama utatangaza waziwazi kwamba priority itakuwa ni riadha, soka na kitu fulani na kitu fulani kwa sababu hatuwezi kucheza michezo yote kwa sababu hatuna fedha za kuhudumia michezo yote, lakini lazima tuangalie na hii michezo mingine. Mheshimiwa Waziri tunaweza kushauriana zaidi ukinihitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante nilitaka kuchangia maeneo manne, lakini matatu nimeyaleta kwa njia ya maandishi ambayo ni kuhusu conference tourism, festival tourism na water sports tourism ambayo bado nchi hii haijatilia mkazo na haijawekeza vya kutosha. Lakini eneo ambalo nitalizungumza kwa urefu kidogo na ambalo nina interest lakini ninauzoefu nalo ni sports tourism ambayo hivi sasa inaambiwa ni the still sleeping giant, hii inafaida kubwa duniani na ikitumika vizuri inaweza kusaidia Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa globally sports tourism inatengeneza karibu 90.9 trillion dollars kwa mwaka mpaka 2017. Lakini kutoka 2015 ilikuwa 46.5 trillion dollars kwa hivyo ni biashara kubwa duniani lakini Tanzania bado hatujaitumia vizuri. Lakini hata katika individual sport kwa mfano golf, golf ni biashara kubwa na Kenya wanazungusha a lot of money kwa sababu wamewekeza katika golf. Wana viwanja vyenye kutosha yale mashimo yanayotakiwa vitano ambavyo karibu 35 percent ya watalii wanaokwenda Kenya ni wale ambao wanakwenda kwa ajili ya golf. Halikadhalika na Afrika Kusini nao wamewekeza katika eneo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kwa ujumla golf ni biashara kubwa duniani na wanaongoza duniani ni Ireland ambao wanatengeneza wageni kiasi 165,000 kila mwaka wanatembelea Ireland kwa ajili ya issue ya golf wakati sisi hatujaitumia golf kama mchezo ambao unatusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata kwenye riadha mimi ningetarajia watu wa utalii wangehimiza sana marathon zote ambazo Tanzania wangejitokeza wakazidhamini na wakasimamia, lakini pia wakazikuza. Kuna mchezo kama cycling ambao tuna maeneo ambao unaweza ukatengeneza pengine Dar es Salaam to Tanga tunaona ile Paris mashindano ya baiskeli yanaisaidia sana na yanaitangaza sana nchi ile, Arabuni wanafanya mashindano ya baiskeli lakini sisi bado hatujaanza kutumia michezo katika hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, muhimu ni kwenye individual sports ni rahisi kuwekeza. Kwa mfano Watanzania wote sasa hivi wanajivunia Simbu, Simbu lakini kumbe taasisi za kitaliii zingeweza kutengeneza Simbu wengine kumi kwa sababu kuwekeza katika individual sports ni rahisi kuliko kuwekeza katika team sport. Kwa hiyo, mimi ningewashauri watu wa utalii wawekeze kwa mtu mmoja/mmoja wamdhamini mtu mmoja/mmoja tunaweza tukatengeneza watu hasa watu ambao wanakimbia kwenye marathon.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingini ni kwenye mpira wa miguu na hili tayari naelezea interest yangu nimeshawaandikia TANAPA ni decleare interst nimeshawandikia TANAPA programu ya namna ya kuweza kuileta timu kutoka Ulaya kuja kucheza Tanzania. Eneo la pre-season ambao ni kuelekea kwenye ligu kuu za nchi za Ulaya timu nyingi za Ulaya zinapenda kwenda nje ya nchi zikafanye mazoezi na sisi Tanzania hatujaitumia. Nimekuwa nikisikia kwamba Everton inaweza ikaja hapa lakini tunaweza tukaleta Everton na tukaleta na timu nyingine na nyingine. Kwa hiyo, pia ningetaka watu wa utalii wawekeze katika eneo hili kwa sababu inakuwa na fedha nyingi. Wenzetu Thailand, Singapore na wengine huwa wanafanya kila mwaka na tayari kama nilivyosema nimewapelekea TANAPA pengine wataona kama inafaa wataitumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna timu za ndani hapa tumezoea kuwekeza kwenye Yanga na Simba. Lakini Yanga na Simba at the end of day sio kwa maana ya kuingia watu uwanjani, lakini kwa maana ya kuonekana wanaonekana timu zingine zinaonekana kama timu nyingine katika television hasa Azam Tv ambayo kusema kweli sasa hivi ni globally brand, inafika mbali.

Kwa hiyo, watu wa utalii silazima wawekeze kwenye Yanga na Simba ambao wanapata wafadhili mbalimbali NMB, Sport Pesa na wengine lakini pia wanaweza wakajitokeza kwa mfano timu ambayo najaribu kui-promote timu ya Lipuli au timu nyingine zilizopanda daraja wakawavisha jezi zao wakazi-brand matangazo ya utalii at the end of the day kwa maana ya kuonekana wanaonekana ninety minuties sawasawa wanavyoonekana Yanga na Simba na kwa hiyo, wataonekana dunia nzima. Kwa hiyo, ningependa hiyo pia mlifanyie kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najiuliza tuliambiwa hapa kwamba tulikuwa tunatangaza kwenye klabu za timu za nje hasa ilikuwa Sunderland lakini suala hili liliulizwa mwaka jana halikupata majibu ya kutosha. Na kwa hiyo bado kuna haja ya kutumia matangazo ya nje lakini very strategical, mwaka jana nilishauri kuhusu Samatta siju limefikia wapi lakini…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante,
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa fursa hii na nitaitumia vizuri, Insha-Allah. Nataka nianze kwa premises mbili, kwanza ni ile ambayo umeizungumza sasa hivi kwamba, mara nyingi ukichangia katika hali ya kukosoa unaonekana kana kwamba, unakosa uzalendo hivi. Kana kwamba, wewe unatoka kwenye sayari ya Mars umekuja hapa na huna haki ya kusemea. Ndiyo maana Msemaji wa mwisho akasema inafika mpaka unapewa majina.

Mheshimiwa Mwenyekiti, premises ya pili ninayotaka nisemee ni Serikali kuwa very defensive. Wakati mwingi Wabunge wakitoa michango mara nyingi utasikia, labda pengine hilo lililosemwa sasa hivi lingekuwa limetoka upande huu kungekuwa na miongozo kama kumi, kumi na tano, lakini pengine imetoka upande ule kuna stahamala kidogo. Naomba Serikali isikilize Wabunge, listen up, tusikilizeni mtakuwa na nafasi ya kusema na miongozo haisaidii kitu kwa sababu miongozo at the end of the day Watanzania wanatusikiliza na zile hoja zinabaki palepale tusiwakatize watu kwa miongozo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nataka kusema kwamba, kama Watanzania kama Wabunge tuna- appreciate ambacho kinafanywa na Serikali, si kweli kwamba, kila kitu hatuoni. Tunaona na tunajua, lakini tuna wajibu wa kusemea. Kwa mfano, tunajua kwamba, kuna improvement kubwa ya doing business in Tanzania. Tumetoka nafasi ya 144, according to World Bank hata juzi tu tumekuja nafasi ya 52, which is very good na hiyo ni pongezi kwa Serikali kwa sababu, ina maana kwamba, tunaweza kuvutia watu kuleta mitaji yao kwa sababu it is easier to make business in Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, tuko proud kama Watanzania kwamba, kuna vitu vingi vinafanywa, maendeleo yetu ya kila aina, lakini tunapotofautiana ni kwamba, je, tunapaswa kuyafanya haya yote kwa wakati mmoja? Tunapotofautiana kama alivyosema Msemaji wa mwisho, tunapaswa kutumia resources gani katika kuyafanya haya kwa kipindi hiki? Hiyo ndiyo tofauti yetu kubwa inapokuja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kusoma kwenye mtandao kujitayarisha kwa presentation hii, sina hakika kama hii ni hakika statement ya World Bank or not lakini wanasema projection yetu wamei-down kidogo kutoka 7.1 ya growth mpaka 6.6. Kwa hivyo, matarajio ya kukua kwa uchumi hiki kipindi kinachokuja haitokuwa tena 7.1, itakuwa 6.6.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa Waziri hili aje alizungumzie na vitu gani vitafanya hiyo tushuke, wao wamesema hivyo. “there appears to have been an overall deterioration in business sentiment due to perceived risks resulting from unpredictability of policy actions related to the Government intensified efforts to collect revenue and it is anti- corruption drive.” Kwa maana hali ambayo Serikali na sera zetu za kukusanya kodi, Serikali na sera zetu za kupigana na rushwa kunaweza kufanya mapato katika mwaka unaokuja yakashuka kutoka 7.1 mpaka 6.6 maana yake nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni kwamba tunafanya vitu kwa nia nzuri ya kukusanya kodi, kuondoa rushwa lakini zina boomerang. Wale ambao wanajua maana ya boomerang ni kwamba kule Australia kuna ubao unachongwa unaurusha uende mbali kama usipotahadhari utarudi tena utakupiga wewe mwenyewe. Kwa hivyo, kuna makosa hapa tunayoyafanya na wenzetu wanaona kwamba makosa haya yanaweza kutu-cost. Kama ni suala la kupigana corruption na kupigana na suala la revenue ambalo kuna mashaka katika ukusanyaji wake, mimi kama Mheshimiwa Ally Saleh ningependa kuongeza haya pia yana athari katika uchumi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo hayo ni rule of law, political stability, usalama wa raia na Katiba. Mimi naamini hayo yana relation ya moja kwa moja baina ya uchumi na mambo haya ya utulivu wa kisiasa, utawala wa kisheria, usalama wa raia na Katiba yenyewe. Pengine ingekuwa kila kitu kipo vizuri theoretically hayo yote yamekaa sawa pengine FDI’s, uwekezaji kutoka nje ungekuwa mkubwa zaidi kuliko hali ilivyo hivi sasa, lakini tatizo letu nchi hii tuna tatizo la denial, tunakataa kwamba siasa yetu iko sawa hakuna kinachobadilika; raia wetu wako salama hakuna kinachobadilika, lakini vitu vingine vidogo tu, tunaona katika stock market za nchi nyingine; suala dogo tu linaweza likashusha stock market point tano au sita. Kwa hiyo, haya tusiyadharau nami nitaelezea kwa nini nayasemea hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tunasema tuna utawala mzuri lakini inatokea mtu ambaye ameshutumiwa kwa rushwa, ambaye amesemwa waziwazi kwamba amenunua Madiwani anapandishwa cheo, mtu ambaye ameshtakiwa kwa kesi iko Mahakamani anachaguliwa nafasi kisha Serikali ina-enter nolle proseque. Wasiojua maana ya nolle ni kwamba Serikali kwenda Mahakamani kusema hatuendelei na mashtaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unamchagua mtu ambaye unajua kama ana kesi Mahakamani, unampa cheo kisha unakwenda kufuta mashtaka, what message are you sending? Definitely wa nje wanaona kumbe nchi hii ina utaratibu mbaya wa kisheria. Katika wakati ambao tunapigana na rushwa Serikali inakwenda ina-enter nolle kwa watu kadhaa, msururu wa watu ambao wana mashitaka ya rushwa, wameshakaa miaka mitano, sita, saba jela lakini je, is this a proper timing? Inaonesha nini katika suala la kwamba nchi hii inapigana na rushwa. Kwa hivyo tuna tatizo katika suala la rule of law. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo unajiuliza Serikali what has it show kupigana na rushwa mpaka hivi sasa, kuna kesi gani ya conviction ambayo imeonekana kupigana na rushwa ambayo itamfanya mtu wa nje aseme kwamba nchi hii kweli inapigana na rushwa. Katika doing business je, mfumo wetu uko mzuri kiasi gani wa kuhakikisha kwamba hakuna rushwa kwa sababu hilo tatizo linalalamikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo nataka kuzungumzia ni suala la political stability. Hapa Bungeni tumeshuhudia jinsi gani Chama kimoja kilivyogawanywa. Inafika wakati humu ndani hatuwezi kukaa na kushauriana kama Wabunge pamoja kwa sababu CUF imekatwa katikati. Una-send message gani kwa wengine huko nje kwamba wewe unaendesha siasa vizuri na unathamini mchango wa Wabunge. Ikiwa kama Wabunge wa CUF hawawezi kushirikiana kwa umoja wao unatarajia input gani upande wa CUF ije kwa Serikali ikusaidie? What do you gain?

T A A R I F A ....

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, siipokei kabisa taarifa kwa sababu Bunge limehusika na iko siku nilitaka nikueleze juu ya mgawanyiko huu ukaniambia kwamba nikisema utanipeleka Kamati ya Maadili. Kwa hiyo, Bunge limehusika katika hilo, tuache. Haijawahi kutokezea popote pale unaichukua Kamati Kuu nzima ya Chama unaipeleka Polisi kwenda kuihoji, tuna-send message gani kwa watu wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, chama gani kinaweza kikapelekwa chote Mahakamani wakati chama kina Principals wake, lakini unachotaka kufanya ni kuonesha kwamba unataka kuminya watu kujieleza na hilo hali-hog well na ujenzi wa uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, no, haya yote yanahusiana na mpango kwa sababu mpango hautotekelezeka, mikopo haitokuja, riba haitakuwepo na wananchi watakuwa, haya yanahusika na mpango moja kwa moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo asubuhi tulimsikia Waziri Mkuu hapa anasema kwamba Serikali hii itafanya suala la Katiba wakati Watanzania watakapomaliza matatizo yao. Kwanza siamini kama tutamaliza matatizo yetu kama Watanzania, shida ya maji, elimu na shida nyingine
zitaendelea kuwepo, lakini katiba ndiyo msingi wa huu mpango.

Mheshimiwa Spika, huwezi kuwa na Katiba ambayo wananchi wake wamegawanyika, mambo yake yanabishaniwa katika nchi halafu ukatarajia utakuwa na mpango mzuri wa kuzalisha lakini matokeo yake ndiyo kama haya ambayo tunayaona hivi sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuzungumzia pia kuhusiana na suala zima la Tanzania kama nchi. Najiuliza kama Mtanzania what are our best products, what are we marketing, branding yetu ipo kwenye kitu gani? Kama Mtanzania najiuliza mpaka sasa huwa nachachiwa. Katika production tume-specialize katika kitu gani ambacho tunaweza tukajivuna katika Afrika Mashariki na katika Afrika tukasema kama Sri Lanka wanauza chai basi brand yao ni dunia nzima, kama Israel wanauza vifaa vya umeme basi brand yao ni dunia nzima, mimi sioni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hiyo basi naona Mpango wakati mwingine ndiyo mwenzetu mmoja alisema pale kwamba ni copy and paste ilivyokuja lakini ingekuwa angalau tunaji-specialize katika maeneo madogo ambayo yanatusaidia vizuri tungeweza kufanya vizuri sana kuliko ambavyo tupo tupo hivi sasa. We are master of all lakini vinginevyo sio vizuri. Kwa hiyo, hatuko vizuri sana, ningependekeza basi tuwe na utaratibu ambapo tuna major brands tunazitengeneza ili ziweze kuuzika kama nchi tuweze kumiliki soko la wenzetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la private sector. Amezungumza msemaji wa mwisho kwamba hawaonekani Serikali kama ina nia ya kuwashirikisha private sector kama inavyofaa, hayo ndiyo maoni yangu. Mfano mdogo tu nikitazama kule Zanzibar, pengine Zanzibar ni ndogo lakini unaona impact ya Said Salim Bakhresa, amejenga City na vitu gani vingine lakini huku upande wa Tanzania Bara na pengine hata Zanzibar kwa kiasi fulani ile kuwavuta wale wateja wa ndani siyo sana kama inavyotarajiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tumekwenda kukopa nje na tumekopa commercially Swiss Bank na kwingine kote kwa maana kwamba mkopo ni mkubwa, lakini tunakwenda kukopa mkopo ambao unatakiwa ulipwe kwa asilimia tisa na tumeacha mkopo ambao pengine ungetaka ulipiwe asilimia moja. Mkopo ambao ungetaka ulipwe kwa muda mrefu zaidi tumekwenda kukopa mikopo ambayo inatakiwa ilipwe kwa muda mfupi zaidi, wakati tungeweza kutumia resources za ndani za watu wetu wakaweza ku- absorb baadhi ya zile fedha zikabakia ndani na matokeo yake wao wakiwa ni wawekezaji wa ndani ina maana kwamba yale matunda yanabakia ndani zaidi kuliko kwenda kukopa nje matokeo yake matunda yanakwenda nje zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hao wote wanaokuja hapa at the end of the day ni mabepari ambao kutengeneza faida kwao ndiyo jambo la muhimu kuliko kitu chochote kwa hivyo ni lazima watakuwa na masharti. Ndiyo hao ambao tukikosana nao wanatupeleka Paris au London kwenye Mahakama. Nashauri kwamba tungetazama eneo hilo tukafanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa leo nitachangia hoja moja tu na nitaanza kwa kusoma shairi ambalo nimeliita jina la “Dhima”, linasema hivi: “Dhima ipuuzwapo, dhahiri ikawa, husuda ikaongoza, hutia nyoo doa, awaye yeyote kuwa, ajipaye mno madaraka, izara jadidi itamkuta, iwe leo ama kesho. Fundo za majigambo, fitna kwa jamii zitamrudi. Ubinadamu ni ukosefu, ujue sijibereuze.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeamua kuanza na shairi hili kwa sababu naamini, au kwa kiasi kikubwa nitazungumzia juu ya dhima katika lengo la utawala au katika lengo la Taifa. Neno “dhima” nitalielezea huko mbele, lakini linaanzia na kupewa ridhaa ya kuongoza nchi au kukamata dola.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara nyingi Vyama vya Siasa hufikiri kwamba wakipewa ridhaa maana yake ndiyo mwisho wa kila kitu, kwa maana wanaona uchanguzi ndio unamaliza kila kitu. Uchaguzi au kushinda uchaguzi au kupewa kushika dola ni sehemu ndogo sana ya wajibu wa chama ambacho kipo maradakani. Siyo free hander kama wanaweza kufanya chochote, kile lazima kuna maeneo ambayo wanatakiwa wayatazame katika hali nzuri. Huanza kwa kujenga dhana ya kuongoza na siyo kutawala. Kwa ninavyoona mimi, hapa nchini kwetu CCM inatawala na siyo kuongoza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, inatawala kwa sababu namna wanavyoendesha nchi haikisi human face, haikishi kufungua public space. Nitaelezea huko mbele namna wanavyobana public space. Kwa hiyo, kutawala na kuongoza ni mbingu na ardhi, lakini Kwa CCM tunaona inatawala na siyo kuongoza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tunaambiwa kuna maendeleo yanafanywa in fact kila mtu anakubali maendeleo ni jambo nzuri; iwe Stiegler’s, Standard gauge, ndege, barabara, madaraja, flyovers na madubwasha mengine yoyote mengine ambayo tunaletewa kama maendeleo. Sehemu ya binadamu ina mbili, ina vitu vya kukamata na ina vitu vipo rohoni. Sasa huwezi kumjazia mtu ukamwambia kwamba kwa kuwa nakuletea ndege, nakujenga daraja, kwa hiyo umnyime haki zake zile ambazo kama binadamu angetaka awe nazo; ku-enjoy public space, lakini pia ku-enjoy vitu vingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, studies nyingi zimeonyesha kwamba maendeleo ya vitu siyo maendeleo ya binadamu, lazima kuwa na uhuru wa wananchi kwenye kujikusanya, kwenye maoni, kwenye kujieleza na maeneo mengine. Kwa hiyo, maendeleo bila vitu hivyo, siyo maendeleo kitu. Sasa ili kupewa ridhaa, lazima kuwa na dhima kama chama ambacho kinataka kutawala katika Taifa. Ridhaa ni jambo muhimu sana kwa sababu ndilo ambalo linasimamia vitu vingi. Ni kwamba ukipewa dhima maana yake uendeshe nchi kwa usawa, haki, imani na uadilifu. Bila vitu hivyo basi unakuwa unatawala na huongozi na CCM inatawala, haiongozi, kwa sababu inakosa vitu hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kuongoza nchi siyo utashi, siyo utakavyo, siyo upendevyo, siyo vyovyote vile, lazima uendeshe nchi kisheria na kikatiba. Hilo kusema kweli linaonekana lina doa katika utawala wa CCM ambao tunakwenda nao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, raia wote wanatakiwa wawe na haki sawa wasibaguliwe kidini, kisiasa na kila kitu. Katika hilo tunaliona, raia wa Tanzania hawakuwekwa katika hali sawa. Sasa Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo inatakiwa iakisi uendeshaji wa Serikali. Ningetamani Ofisi ya Waziri Mkuu katika bajeti kama hii au katika uendeshaji wa nchi tungeona ina-reflect kwamba inagomba, inakataza, inasimamia kwa wivu kabisa juu ya suala la haki, usawa, imani na uadilifu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa CCM inatawala, haingozi, hayo hayaonekani. Nataka nim-quote msanii Idrisa Sultan, aliandika juzi katika twitter, ilikuwa ni suala hili la kutaka suala la CAG, akasema yeye anasaini katika watu 15,000 waliosaini juu suala la CAG kwamba Bunge libatilishe maamuzi yake kwamba akasema nasaini kwa sababu nina wivu na kesho, nataka nione Tanzania ya kesho inatengenezwa. Kwa hiyo, Bunge hili pia au Wizara hii ilipaswa ione kesho yetu sisi kama binadamu, ione kesho ya watoto wetu, ione kesho ya wajukuu zetu na ione kesho ya vitukuu vyetu.

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ally Saleh, kuna taarifa.

T A A R I F A

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimwa anayechangia akitaja sana CCM, lakini nilitaka nimwulize kama anapochangia hapo anasimama kama CUF au ACT? Pili, kama ni CUF, anajua kwamba Maalim Seif amekuwa kiongozi Mkuu wa CUF kwa miaka mingapi? Kwa sababu mimi nakumbuka alianza sijui ni enzi ya Mheshimiwa Mwinyi, Mheshimiwa Mkapa, Mheshimiwa Dkt. Kikwete na sasa Mheshimiwa Dkt. Magufuli yupo, sasa anamanisha nini anapozungumzia uongozi na utawala? Ni wapi kuna utawala? (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ally Saleh.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naendelea tu. Nimesema CCM inatawala na haiongozi kwa sababu nina reasons; na reasons zangu siyo za leo, zimekuja kwa muda mwingi sasa. Nitataja mfano, kwa jambo moja tu. CCM katika ilani yake imesema kwamba itakuza vijana ambao wamepata mimba wakati wakiwa shule. Kinyume na Ilani na Sera yake, CCM imebadilika, kwa sababu haina culture ya kuongoza, culture yake ni ya kutawala. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wiki iliyopita tu, chama cha CCM kimefanya mkutano wa ndani Sikonge, tumeona mamia ya watu wamekaa, wamefanya mkutano lakini Serikali hiyo haijawazuia kufanya mkutano. Chama hicho cha CCM kimefanya mkutano NIT, wiki hii iliyopita lakini hatuona kuzuiwa. Vyama vingine, iwe CHADEMA, iwe ACT au CUF wakifanya vitu kama hivyo wanazuiliwa. Kwa hiyo, mimi najiuliza, hii Ofisi ya Waziri Mkuu inafanya kitu gani katika kutazama masuala ya kila siku ambapo uhuru wa siasa unaminywa kila siku? Ambapo kila siku uhuru wa kujieleza unazidi kupungua? Ambapo kila siku watu wanapotea, watu wanatekwa, lakini hatukuona uongozi wowote kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ukiukwaji wa haki za binadamu umekuwa mkubwa nchi hii mpaka juzi Rais Mheshimiwa Dkt. Magufuli akaingilia, mtu ambaye amebambikiziwa makosa na alikuwa ameshakaa kifungoni kwa muda mrefu. Polisi wanazuia vyama vingine kufanya mikutano, tunafika hata maandamano ya amani tunayaogopa. Hivi sasa katika mtandao kuna kikundi kesho kinataka kuandamana kwa ajili ya kueleza hisia zao juu ya kukiukwa Katiba au tishio la kukiuka Katiba uhusiana na CAG, lakini wamezuiliwa wasifanye. Hata maandano ya amani yanakataliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile Wapinzani kuporwa Wabunge wao. Pia tunaona kwamba hata suala la Tanzania katika nyanja ya Kimataifa kwenye mikataba ya Kimataifa ya haki za kibidamu ya utawala bora inajitoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata Bunge haliruhusiwi kuonekana wananchi. Sasa ningetamani Ofisi ya Waziri iakisi katika kuisaidia Serikali kuendesha nchi hii kwa hali ya good faith na public space ili wananchi…

MHE. CHACHA R. MARWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa. Mheshimiwa Ally Saleh unapewa taarifa.

T A A R I F A

MHE. CHACHA R. MARWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kumpa taarifa Mheshimiwa Ally Saleh kwamba jana Tarime Mjini, Mheshimiwa Esther Matiko na Mheshimiwa John Heche walikuwa na Mkutano wa Hadhara. Kwa hiyo, unaposema mikutano inazuiwa, mimi sikuelewi, maana jana walikuwa na mkutano wao na hawazuiliwa. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ally Saleh.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Asubuhi Mheshimiwa Gekul alizungumza kwamba alikuwa upande Gaza, naona bado ana Gaza syndrome ndani ya kichwa chake. Hatuzungumzii individual cases na hao ambao wamefanya mkutano baada ya msukosuko. Kwa nini iwe msukosuko wakati ni haki ya kikatiba? Kwa mfano, kufanya mkutano ni haki ya kikatiba, kwa nini uzuiliwe? That is the question, siyo kwamba amepewa mtu mmoja ameonjeshwa ndiyo tuseme kwamba ndiyo general rule, tunataka tuhakikishe…

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nataka kumpa taarifa mzungumzaji, hivi ninavyoongea sasa hivi, viongozi wa Tarime Jimbo CHADEMA na Mkoa wameshikiliwa na Polisi na wanahojiwa kwa nini walienda kumsindikiza Mbunge wa Chama chao kufanya mkutano jana Tarime? Kwa hiyo, nakupa taarifa. (Makofi)

MHE. ALLY S. ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa inapokelewa kwa mikono miwili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimalizie kwa kusema kwamba we need to change kama Taifa. Sote…

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpe taarifa kaka yangu Mheshimiwa Ally Saleh kwamba watu wanazuiliwa mikutano na maandamano kwa kutokuwa na nidhamu. Kwa mfano, jana mkkutano wanaozungumza wapo watu ambao wamemsindikiza Mheshimwa Esther Matiko ambao kimsingi sio Wabunge lakini walikuwa wakimtukana Mheshimiwa Rais kwenye mkutano ule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile Mheshimiwa Esther Matiko mwenyewe kwenye mkutano wake alikuwa anamtuhumu Hakimu aliyeshughulikia kesi kule Mahakamani akamweka ndani na kwamba amepewa dhamana. Sasa katika mazungumzo kama hayo sheria inakataza. Ni lazima Serikali ingalie utaratibu ulivyo. Ukizuiliwa maana yake hukwenda vizuri. Ukiomba mkutano, ukazungumza mambo yanayopaswa, hakuna ugomvi na Serikali wala vyombo vya dola. (Makofi)

MWENYEKITI: Haya. Mheshimiwa Ally Saleh.

MHE.ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo ni kwamba mambo yanayopaswa siyo mambo ambayo Serikali inayataka, ni yale ambayo kwa uhuru tulionao chini ya Katiba na chini ya Sheria tuna haki ya kusema. Huwezi kumzuia mtu kusema. Kama unamwona ana makosa, mpeleke Mahakamani, siyo umzuilie kusema, siyo utumie utaratibu wa intelijensia kwa vyama vingine lakini vyama vingine unakuwa una madudu kichwani. Lazima tuhakikishe kwamba kama intelejinsia inaonyesha kwamba watu watafanya fujo, basi jukumu la Polisi ni kuwakamata hao ambao wanataka kufanya fujo na siyo kuwazuia wale ambao wana haki ya kukutana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, nimejiwa na wazo ambalo ni kuona uwepo wa haja ya kumwenzi Dkt Salim Ahmed Salim kwa kupewa heshima ya jina la Mheshimiwa kuingia kwenye kumbukumbu ya milele nako ni kumuenzi akiwa hai na kusikia kiwa duniani kuwa Uwanja wa Ndege wa Songwe unapewa jina lake.

Mheshimiwa Spika, ikumbukwe Dkt. Salim ameshika nyadhifa nyingi ambazo ni: Balozi wa Zanzibar , Gairo; Balozi wa Tanzania, Cairo; Balozi wa Tanzania UN, New York; Katibu wa OAU; Waziri wa Nje, Ulinzi; na Waziri Mkuu, naomba hilo lizingatiwe.
Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa Mwaka 2016
Mheshimiwa Ally Saleh Ally, Mheshimiwa Anatropia Lwehikila Theonest ajiandae. Tutamalizia na Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa.
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nianze kwa kusema kuna msemo wa kiingereza unasema kila kitu kinakuja kwa sababu zake na leo asubuhi tulipoanza hapa tulianza na swali kuhusu mambo ambayo yametokea Zanzibar ambayo ya upigaji, uoneaji, unyanyasaji wa wananchi na tukashuhudia Serikali ikisema hata haijui kwamba hayo mambo yanatokezea na ikasema kwamba mambo hayo hata hayajawahi kuripotiwa polisi na kwa hivyo wao hawajui chochote kinachoendelea.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini only two hours later tunaletewa Muswada wa Msaada wa Kisheria kwamba upande mmoja haki zinavunjwa, watu wanakoseshwa haki zao, wananyanyaswa, wanapigwa, hakuna kinachoendelea lakini upande mwingine wanajitengenezea mazingira ya kulinda wananchi wake. Kwa maana hiyo tunaambiwa kwamba kuna raia wa namna mbili nchi hii. Kuna raia wa Zanzibar ambao ni haki yao kuonewa na Serikali kila siku kukataa na asubuhi nilisema hapa Bunge hili imefika wakati iundwe Tume, Waziri akakwepa hakujibu kabisa, lakini upande huu mwingine wanatengenezewa haki ya ku-access justice. Upande ule kule justice is denied to them. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ni Mjumbe wa Kamati hii ya Katiba na Sheria na natahasaf kusema kwamba Muswada huu ni Muswada muhimu sana kwa ajili ya Tanzania na ningetamani Muswada kama huu baadaye uwepo Zanzibar. Umuhimu wake ni kwamba unatengeneza mazingira ambayo watu wetu kwa miaka wamewekwa nyuma sana, elimu ya uraia, elimu ya haki haijafikishwa kwao kiasi ambacho wengi wanadhulumiwa, wanaonewa bila ya kujua waende wapi au wafanye nini.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mbunge mmoja asubuhi hapa alimwambia Waziri wa Katiba na Sheria kwamba alikuwa wapi siku zote, lakini kila kitu kinakuja na wakati wake. Kila kitu na zama zake. Hata hivyo, mimi mwenyewe nilimwambia Mheshimiwa Waziri kama kwamba Muswada huu utakuja vizuri, utamjengea legacy yeye kama Waziri kwamba ameweza kuleta Muswada huu ambao unahitajika sana na Watanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna tatizo moja ambalo litatukabili. Muswada huu unakiuka utaratibu wa Muswada wa mwaka 1969 ambao tulikuwa tunazungumzia masuala ya jinai peke yake. Hapa sasa tunakwenda pia masuala ya madai. Hapa maana yake tunafungua wigo mkubwa sana. Wenzetu Kenya hawakufungua kwenye suala la madai, wenzetu Malawi hawakufungua kwenye suala la madai, lakini sisi tumefungua kwenye suala la madai, maana yake sasa administration itakuwa kubwa, kazi itakuwa kubwa ya kufanya, elimu itahitajika kubwa sana, wakati ukweli kwa mujibu wa watu wenye uzoefu wa legal aid ni kwamba sehemu kubwa yale mashirika makubwa sana yanasimamia kesi kumi mpaka kumi na tano kwa mwaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi tuna mashirika machache sana ambayo yanafika sehemu kubwa. Tuna paralegals ambao watafika au wanafika mpaka vijijini. Hata hivyo, kuna tatizo hilo la kufungua upana mkubwa sana, wanasheria wanaweza wakasema flood gates sasa sijui kama nia yetu tutaweza kuitimiza kuchukua madai na jinai pamoja lakini maadam sheria inawekwa, wacha tuone itafanya kazi vipi, itasimamiwa baadaye. Hilo moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, sheria hii is not the best that we could have done, ingeweza kuimarishwa kwa sababu tumepata bahati hatuku re-invent the wheel. Mheshimiwa Tundu Lissu leo hapa amezungumzia historia ya Marekani ya miaka mingi ya legal aid, lakini tusiende mbali twende hapo Kenya tu, kama tungeweza kwenda ndani wenzetu wamefanya nini, wamekwama wapi? Nafikiri tungeweza kufanikiwa, lakini sheria hii imekuwa katika mchakato kwa zaidi ya miaka kumi hivi sasa, kwa bahati mbaya hawa Kamati ya Katiba inayosimamia hivi sasa haikupata fursa ya kujifunza wenzetu wengine wanafanya nini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, wenzetu waliokwenda Afrika Kusini na kwengine kwenye Kamati hii wote wameondoshwa kwenye Kamati hii, kwa hivyo, hawakutuwezesha kupata uzoefu wowote ule ambao wameupata huko walikokwenda kufanya study.
Mheshimiwa Naibu Spika, ndio maana asubuhi akapongezwa sana Mheshimiwa Tundu Liissu kwa sababu he is the only surviving na analazimisha kuja kwenye Kamati yetu tu, kwa sababu yeye siyo mjumbe wa Kamati yetu; lakini ametusaidia sana kwa sababu he is the only surviving ambaye alikwenda katika training au kufanya utafiti Afrika Kusini na akabakia kwenye Kamati hii. Kwa hivyo, kwa mfano Kenya, board inayosimamia haikufanywa kuwa governmentally, imefanywa kuwa ni board huru ina muhuri wake inaweza kushtaki na kushtakiwa na haiko moja kwa moja kiserikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kenya wamefanya Mkurugenzi wa Board anagombea kwa sifa; hateuliwi. Kwa hivyo, kuna ule uhuru wa board yenyewe, tumekuwa tuki-force, tunasema kwamba board hii inaweza ikafanya maamuzi ya kutetea watu, tunajiuliza je, ikitokea kwamba inayoshtakiwa ni Serikali au kosa lililopo ni kubwa kama kosa la uhaini, kosa la ugaidi huyu mtu ambaye; hii board ambayo mlolongo wake unakwenda mpaka kwa Katibu Mkuu na tuli-attempt hata katika Kamati hata kutaka kum-distance Katibu Mkuu lakini ikaonekana kama waleta hoja wakaona kama ni ngumu. Tukajiuliza inawezekana vipi katika hali kama hiyo, mtu kama huyu kutetewa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ambacho Kenya wamefanya ambacho mimi mwenyewe nilivunjika moyo, ni kujaribu kufanya ushawishi wa kwamba tuhakikishe tunakuwa na legal aid fund; ama kwa kuwa na sheria nyingine au itajwe kuliko ilivyosema section 37 ambayo inaelezea namna ambavyo pesa zitapatikana. Tunajua kuna shida ya ku-approve pesa hapa kwa mashirika haya ambayo ni kama yako pembezoni. Mwaka jana hapa tulilalamika sana watu wa katiba na sheria na hata tukataka kumtetea Mheshimiwa Waziri kwamba Tume ya Haki za Binadamu iongezewe pesa na mpaka mwaka huu haikuongezewa pesa hata ya kufanya activity moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maana tume mwaka mzima huu, itakuwa imekaa ofisini tu, najiuliza tulete mambo haya mengine, kwa maana nyingine tunaweza tukarudia yale yale tena tusiipe legal entity, fedha za kutosha na kwa hivyo haitofanya kazi za kutosha itakuwa kama ile Tume ya haki za Binadamu. Kwa maana nyingine watakuwa wanawategemea wale legal aid provider‟s ambao hao wanakwenda kuomba pesa kwa wafadhili wetu wa kawaida traditionally founders sijui wa-Sweden, wa- Norway ndio wanaotuendesha hivi sasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivyo ningependa kuona kwamba wale Wabunge wanakuwa serious katika Serikali itakapoleta pendekezo, wale wanaoshangilia hapa kwamba sasa watatetewa, watapata haki za kutetewa na kitu gani waje waishike Serikali koo hapa mpaka hiki chombo kipate fedha za kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine ambacho Kenya wamefanya na sisi tungeweza kukifanya ni kwamba sheria yao iko liberally zaidi. Kwa mfano, wameweka utaratibu kwamba kila kituo ambacho ni holding center kama cha watoto, kama ni polisi au kama ni magereza kunakuwa na form za readymade zipo, mtu akifika kama vile Marekani unaposimamishwa unavyoambiwa haki yako ni moja mbili tatu, basi na hiyo iwepo, kwamba ukifika gerezani, ukifika polisi usomewe haki zako, halafu upewe option uambiwe kuna uwezekano wa kupata legal aid, unataka au hutaki, alafu iwe recorded katika register kwamba huyu kapewa fursa hiyo na ameikataa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hivyo Mheshimiwa Waziri akasema lakini hiyo itapita kwenye mamlaka nyingine, Wizara nyingine, tukasema Serikali inasemezana, wasemezane ili hili liwepo tuweze kujua kitu kizuri ambacho wenzetu wameweza kukifanya.
Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ambacho kilitatiza kidogo ni suala la pale mtu anayekwenda mahakamani lakini akashindwa kesi na kwa hivyo hapatakuwa na cost ambazo zitakuwa awarded na Mahakama na kwa hivyo ataondoka pakavu. Sasa sijui Waziri amekuja na pendekezo gani katika hili kwa maana mimi nilipenda statement yake moja alisema issue sio kum- reimburse fully advocate au mtu ambaye anakwenda kumtetea mtu lakini angalau arudie katika hali yake inayofanana kabla hajaenda kule kwa gharama aliyoipata.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri ametuletea amendment hapa inambana Wakili, Wakili atakwenda mahakamani, tunajua sasa hivi aibu kusema hivi sasa anapata kiasi gani, lakini atakwenda mahakamani pengine akishinda kesi, atakuwa awarded cost ambayo tulisema ziwe awarded sio kwa yule ambaye alitetewa lakini ziwe awarded kwa Wakili, lakini akishindwa case anaondoka patupu, sasa huyo sijui hii imefikiriwa vipi kuweza kuhakikisha kwamba inawezekana kuifanyia kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, cha mwisho kabisa ni suala zima la namna ambavyo sasa hivi tulipigania kwamba wale ambao sasa hivi wapo wana-exist sijaona schedule of amendment lakini tumesema wale ambao wana-exist sasa hivi wasiwe labored ku-register upya. Moja kwa moja wachukuliwe kwamba wao automatically ni legal providers na wachukuliwe wawe registered moja kwa moja. Wasiwe labored kuanza tena ku-apply kwa sababu uki-apply ina maana mwenye mamlaka anaweza kukukatalia au anaweza kukubalia.
Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana na nitafurahi kama Muswada huu utatendewa haki ya yale marekebisho ambayo tuli-suggest katika Kamati na naamini utaweza kusaidia sana Watanzania hasa wale wanyonge. Ahsante sana.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.4) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza)
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kabla sijachangia kwenye vifungu, nataka niseme vitu viwili vya mwanzo. Cha kwanza nataka ku-appreciate jinsi ambavyo Serikali imekuwa ikifanya kazi na Kamati yetu kwa maana ya kwamba imekuwa ikisikiliza na baadhi ya mengi ambayo tuliyapendekeza yamekuwa incorporated kwenye sheria hii. Hata hivyo, tulikuwa na mengine ambayo tungependa pia yabadilishwe, hayakubadilishwa lakini ndiyo give and take katika mambo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili nataka niunge mkono maoni ya Kambi kwamba kuna tatizo kubwa la public hearing. Sijui tunakosea wapi msemo wa siku hizi lakini hatupati watu wa kutosha kuchangia katika Miswada. Maana yake ni kwamba hatupati maoni ya kushiba tuwajue wadau wanataka nini ili sheria zikirekebishwa ziwe robust na ziweze kudumu kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nafikiri kuna haja ya Bunge kutafuta utaratibu mzuri zaidi wa kupata maoni pengine Kamati itoke nje ya Dodoma iwafuate watu regionally au vituo maalum kupata maoni kuliko kutegemea wadau waje hapa katika mzunguko huu wa uhaba wa fedha kiasi ambacho pengine inakuwa vigumu kwa wadau kuja Dodoma. Wakati mwingine sheria zinatolewa anakuja mdau anasema mimi nilikuwa nikiandika kwenye gari kwa maana taarifa niliipata juzi, jana niko kwenye gari nasafiri, njiani naandika ndiyo nimekuja kutoa maoni kuliko kuiacha nafasi ikapotea bure. Naomba sana suala hili tulirekebishe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuzungumzia suala la Mawakili ambalo limetajwa katika sehemu mbili kwenye sheria hii. Kusema kweli tulizungumza sana juu ya haja ya Mawakili wa Serikali kuweza kufanya kazi zao kama ambavyo Mawakili wengine wa binafsi wanafanya lakini tukaambiwa kwamba practice hii inafanywa sehemu nyingine ya kuwazuia Mawakili wa Serikali wasiwe engaged katika private businesses lakini Serikali haikuja na chochote kile kuthibitisha Uingereza, Sri Lanka au China wako hivi, hawakuja na mifano halisi. Wamesema tu kwamba hii ni standard practice kwamba Mawakili wa Serikali hawafanyi kazi za binafsi lakini wanasahau kwamba hao Mawakili wa Uingereza wasiofanya kazi za binafsi, Uingereza inajitosheleza kwa Mawakili, Uingereza haina remote places ambazo Wakili hafiki, Uingereza haina sehemu ambazo Halmashauri pengine kuna mwanasheria mmoja naye ni Hakimu lakini pia huko katika Halmashauri zetu au katika vijiji kuna mwanasheria mmoja tu ambaye pengine angeweza kusaidia lakini kwa bahati mbaya au bahati nzuri yuko Serikalini lakini anazuiwa asifanye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona hapa na na- appreciate Serikali kwamba wameweza kutengeneza mazingira kwamba wanaweza kufanya utaratibu huyu Wakili akaweza angalau kufanya kazi kama za viapo, kusimamia masuala ya mikataba lakini pia katika mazingira maalumu anaweza hata aka-practice lakini kwa taratibu zilizowekwa. Tunaomba hizo taratibu zisiwe restrictive, ziwe pana ili kuruhusu uwezekano wa mtu kupata nafasi ya kuwa Wakili binafsi tukizifanya restrictive itakuwa haisaidii kitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hotuba ya Kambi imesema inawezekana siku zijazo tukapata watu wakakataa kuwa Mawakili wa Serikali au waajiuliza mara mbili kuwa Wakili wa Serikali ikiwa tutakuwa na very restrictive Kanuni pengine mtu asiweze kupata fursa ya kufanya vitu kama hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimefurahi kwenye suala la Registrar General kwamba hivi sasa uandikishaji wa masuala ya vizazi na vifo unashuka chini. Kusema kweli this is a very good spirit kwa sababu huko kutasababisha takwimu zikusanywe vizuri zaidi lakini pia vile vyeti vya kuzaliwa vitatengenezwa kwa haraka zaidi kuliko hivi sasa pengine mtu ana sehemu kubwa ya kwenda au anatumia muda mrefu kwenda sehemu hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine nalotaka kuzungumzia ni mali zinazopatikana kwa njia ya uhalifu. Kwanza nitazungumza habari ya Plea Bargaining, hii ni dhana mpya. Tuliiambia Serikali katika Kamati kwamba tungependa tupate mifano ya Plea Bargaining. Wanasema kwamba hii ipo lakini sasa inarasimishwa zaidi lakini sisi Wajumbe wa Kamati kama ilivyo mara nyingi huwa si rahisi Serikali kuturuhusu tudurusu vya kutosha juu ya dhana ambayo wanaileta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli walikuja wakafanya semina, lakini bado mimi binafsi kama Mjumbe wa Kamati sikushiba, sikuona ule uelewa kwamba napitisha sheria hii ili baadaye ije ipate picha gani? Kwa sababu, sikuletewa mifano mingi, naambiwa tu kwamba, inatumika kwingine na kwingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tumeweka vifungu ambavyo tunajitia pingu wenyewe. Tumesema yako maeneo ambayo hayatakuwa katika plea-bargaining tumesema uhaini, makosa ya ugaidi na mengine. Sasa makosa mengine ambayo ningependa yawe katika plea- bargaining ndio yametolewa wakati ukiyaweka katika plea- bargaining unaweza ukapata fursa ya kuyafanyia kazi na ukayaua kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba ya Kambi imesema hapa, kwa mfano kwenye mambo ya drugs ambayo nimefurahi Serikali imeongeza kiwango kutoka shilingi milioni 10 kwenye dawa za kulevya hadi 20 na hali kadhalika kwenye nyara za Serikali imeongeza shilingi milioni 20 ili haya yasemwe katika plea-bargaining.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utavunjaje mitandao ikiwa wewe hutaki kufanya plea-bargaining? Mtu umemkamata drug lord, pengine ana biashara ya shilingi bilioni 50, ana mtandao wa watu 200 wako nchi nyingi duniani, unakataa kuingia naye plea-bargaining unasema kwamba, suala la dawa za kulevya hakuna plea-bargaining, ina maana hata ukimfunga, ndiyo yale yanatokezea kwamba mtu yuko ndani, bado anaweza akapata huduma, anaweza akawa anaendesha biashara yake wakati yuko ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani Serikali ingefikiri sana katika hili ili kuhakikisha kwamba, inawezekana kwamba plea-bargaining isiwe maeneo haya au tusijifunge kuyaondoa yote kwa sababu yanaweza kutusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni mali zinazopatikana kwa njia ya uhalifu. Msemaji aliyepita hapa amezungumzia kwamba, hii sheria ni nzuri, lakini pia kuna ubaya wake kwa sababu, ubaya wake mmoja ni kwamba, inawezekana sasa mtu anakamatwa au unaundiwa kosa na kama ilivyosema hotuba ya kambi kwamba ili wakukamate vizuri wanakwambia mali hii uliyoipata hapa tunaichukua kwa sababu imo ndani ya miaka mitano ambayo wewe unashitakiwa kwa kosa la uhalifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajiuliza, hivi kigezo gani Serikali imetumia kusema miaka mitano? Kwa nini isingekuwa mitatu? Mimi niliuliza kwenye Kamati, kwa nini iwe miaka mitano? You go back so much time. Miaka mitano pengine mtu alikuwa akifanya biashara halali, unazuia mali zake mpaka watakapothibitisha otherwise. Halafu hukuna kifungu au njia yoyote ya kupata fidia ikiwa mali yake ile iliyozuiliwa kwa miaka wakati wa kesi, Serikali ikashindwa kuthibitisha kwamba alikuwa na kosa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ingawa taratibu zitawekwa, lakini ningependa hii iwe very strict na due process itumike ili Serikali ithibitishe Mahakamani beyond doubt kwamba au ithibitishe kwa kiasi kikubwa kwamba shaka ya mali ile iliyopatikana kwa njia haramu inaweza ikatumika na Mahakama kuliko Mahakama kushawishiwa tu kwamba hasa ilivyokuwa ni ex-parte. Serikali itakwenda peke yake itasema mali ya Musa au mali ya Juma tuna shaka imepatikana miaka mitano ndani ya kipindi cha uhalifu, ex- parte peke yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini isifanye basi ikawa argued Mahakamani ili kuthibitisha? Matokeo yake ni kwamba, kwa sababu wanakwenda upande mmoja tu, nayo ni very dangerous, inawezekana ikawa hasara kwamba mtu anakamatiwa mali yake wakati pengine ile mali haikuwa ya uhalifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha mwisho nitakachozungumzia ni suala la Red Cross. Nilihoji kwa nini Red Cross inafanywa suala la Muungano? Nikahoji kwamba kuna sheria nyingi za Kimataifa au Mikataba ya Kimataifa kwa mfano Mkataba wa Watoto, Zanzibar imeweza kusimama yenyewe bila ya kufanywa kwamba ni suala la Muungano ingawa huu ni Mkataba wa Kimataifa. Kwa sababu, tunaongeza mambo ya Muungano unnecessarily. Hakuna haja hata Red Cross kufanywa suala la Muungano, mimi sioni kwa sababu gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli ni Mkataba wa Kimataifa, kweli unatekelezwa Kimataifa, lakini mbona mikataba mingine ya Kimataifa Zanzibar inatunga kanuni zake, ingawa unaridhiwa na Serikali ya Muungano, lakini inatunga sheria zake yenyewe. Kuna ulazima gani Red Cross kuifanya ifanye kazi mpaka Zanzibar?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mna abandon mambo mengi na kama ilivyosema Hotuba ya Kambi ya Upinzani, unaichukua Red Cross unakwenda kupeleka kwa Waziri ambaye sio wa Muungano. Au inapelekwa sehemu ambayo utekelezaji wake utakuwa mgumu kwa sababu mnaongeza mambo ya Muungano pasipo haja ya kufanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, baada ya kusema hayo, nashukuru sana kwamba kwa muda huu tumefanya vizuri sana na upande wa Serikali nashukuru kwamba, walikuwa wasikivu, lakini waendelee kuwa wasikivu ili tuweze kutoa ya moyoni kwa maana ya kujenga nchi. Sote tunajenga nyumba moja tufanye kazi kwa pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza)
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mimi ni Mjumbe wa Kamati na nitakuwa na maeneo machache, kwa sababu kama nilivyosema jana, vitu vingi tumekubaliana na upande wa Serikali, lakini vile ambavyo hatukuweza kwenda sawa inabidi tuviseme na vingine tuvikazie hata kama tumekubaliana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimefurahi kwamba sasa hivi yale mambo kwamba unapigiwa simu unatapeliwa kwa simu inaweza ikapungua kidogo pengine, kwa sababu ya kuweka hii adhabu ya kwamba mtu ambaye anatumia vibaya simcard yake anaweza akaadhibiwa. Tutaona katika utekelezaji inakuwaje. Pia sasa sheria inakaza kwamba kuna wajibu kwa mtoa huduma naye kuhakikisha kwamba laini zake anazihifadhi na zikitoka zinakuwa zile ambazo zimesajiliwa ili watumiaji wake waweze kufuatiliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia sehemu hii inazungumza habari ya namna ya kukusanya mabaki ya simu (e’waste) ambayo tumetumia ambapo baadaye yanaangukia kwenye mito, maziwa na kwenye mashamba yetu, tumeelezwa kwamba utaratibu unatengenezwa ili Serikali iweze kufaidika na kodi ambayo Makampuni ya Simu ya Kimataifa yanayoleta bidhaa zake katika nchi huwa yanapaswa kulipa kodi ya kijani. Kwa hiyo, inawezekana sasa baada ya utaratibu kukamilika tukawa tunaweza kupata, yaani kila Kampuni ya Samsung ikaleta simu yake Nokia ikaleta simu yake, basi Tanzania inapata fedha ya kutumia katika ku- dispose hizo simu ili matumizi yake yawe ni mazuri na siyo yanaharibu mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine kuhusu sheria ya wanyamapori, sheria hii iko very positive, lakini nakubaliana na upande wa Kambi kwamba kuna haja ya kuhakikisha kwamba inatekelezwa katika hali ya uwazi na ya uhakika. Tulipitishwa kwenye semina katika mnada wa vitalu uliofanyika. Kusema kweli ile process ya vitalu ilikuwa so good tulivyoiona kwa macho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, imewekwa amount ambayo unaweza ku-bid automatically ikiwa bid yako ni ndogo inakwambia moja kwa moja kupitia kwenye computer kwamba bid yako ni ndogo, imekataliwa.

Nilichopenda katika mfumo ule ni kwamba mwisho wa process nzima, basi unaoneshwa nani ame-bid shilingi ngapi au dola ngapi na nani ame-bid dola ngapi na kwanini fulani amekuwa mshindi kwamba ame-bid kwa amount kubwa zaidi? Kwa hiyo, ilikuwa ni uwazi kabisa. Kama tulivyoonyweshwa ndivyo ilivyo, chance ya kuwepo na rushwa na kuchezea chezea ni ndogo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni kwamba sheria hii inampunguzia mwananchi akitaka kuwekeza kwenye biashara hii ya vitalu kwamba sasa ataweza kuwekeza kwa asilimia 10 na siyo 25 katika biashara ya kitalu, ingawa hizo asilimia 10 bado pengine ni asilimia 10 ya dola milioni moja au asilimia 10 ya dola milioni mbili. Kwa hiyo, bado ni amount kubwa, lakini angalau imempunguzia mzalendo aweze ku-compete.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia imeweka vitalu kwa wazalendo vitakavyokuwa 15% na vilivyobakia kwa wageni; lakini sheria inatengeneza mazingira kwamba hata hivyo vya wageni 85% bado mzalendo ataweza kwenda kuvi-bid ili aweze na yeye kupata. Ukweli ni kwamba biashara hii ni kubwa sana kwa gharama ya uwekezaji kwa hiyo, siyo rahisi kwamba hiyo asilimia 15 tunaweza kuijaza, kwa sababu ina amount kubwa ya kuwekeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hapa wakati tunataka kupitisha sheria nzuri kama hii, kuna statement ambayo imekuwa ikizunguka kwenye mitandao ya Waziri wa Utalii, Mheshimiwa Kigwangwala juu ya matamshi yake anayotoa ambayo kusema kweli siyo mazuri, ingawa amesema pengine kwa uchungu, lakini it is very unfortunate wakati tunatengeneza sheria hii juu ya kutengeneza mazingira mazuri ya suala ya biashara ya vitalu, Mheshimiwa Waziri anasema kwamba wazi wazi na haja-regret, nami nafikiri angesema kwamba alikosea kusema kwamba anaweza kumpiga risasi mtu ambaye anamwona anaua mnyama specifically akamtaja twiga katika mbuga zetu. That is very unfortunate na ninafikiri kwamba Mheshimiwa Waziri alipaswa alinde matamshi yake kwamba itakavyokuwa huwezi kufananisha uhai wa mnyama na uhai wa binadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ninachotaka kuzungumzia ni kuhusu Baraza la Mitihani. Again sheria hii ya mabadiliko haya yamejaribu kuziba gaps ambazo zimejitokeza. Serikali kwa miaka mitatu, minne hivi sasa imekuwa ikipambana na vyeti feki na sheria hii inakwenda huko ku-address tatizo la vyeti feki ambapo pia Serikali itakwenda katika kujaribu kuziba suala la kuvujisha mitihani. Nimeona mapendekezo hapa ya marekebisho yaliyoletwa na baadhi ya watu na nitafurahi yakiwa-considered, kwa mfano, kuna hili la Mheshimiwa Suzan Lyimo juu ya eneo hili lingefaa kuzungumzwa vizuri

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine kizuri katika sheria hii ni kwamba Serikali imekubali mapendekezo ya Kamati kwamba kuwe na consideration ya watu wenye mahitaji maalum katika muundo wa Baraza la Mitihani kwa sababu ni sisi wenye mahitaji maalum tunaoweza kufikiri nini wenzetu wanaweza kukihitaji. Kwa kuweka condition hiyo kwamba awepo mtu mwenye mahitaji maalum kwa kweli itasaidia sana kwa upande wa watu wenye mahitaji maalum kwa sababu watakuwa na msemaji wao ndani ya Baraza la Mitihani

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni Baraza la Usalama la Taifa. Hapa tatizo nililokuwa nalo na upande wa Serikali halikupatiwa ufumbuzi, nalo hili la Kikatiba. Nilisema kwamba Serikali imekuja na pendekezo kwamba kuanzia sasa watambue nafasi mpya ya Waziri Kiongozi wa Zanzibar ambaye alikuwa tangu mwanzo Mjumbe wa Baraza la Usalama la Taifa, lakini sasa atambuliwe kwa jina jipya la Makamu wa Pili wa Rais, ambapo hiyo ni kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nili-argue very strongly kwamba mabadiliko haya yanakwenda kinyume na Katiba, kwa sababu katiba ya Zanzibar inamtambua Makamu wa Pili na wa Kwanza. Katiba ya Muungano mpaka leo ndani yake kuna Waziri Kiongozi tu. Argument yangu imekuwa kwamba tubadilishe Katiba kwanza ili itambue kuwepo kwa Makamu Wawili na itambue kwa mfano, katika Katiba yetu tumesema kwamba Zanzibar ni nchi, Katiba ya Muungano inasema Zanzibar ni sehemu ya Muungano. Sasa ingekuwa muhimu kwanza tubadilishe Katiba kwanza kukiri angalau hii kwamba kuna Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili katika Katiba ya Muungano. Kusema tu kwa kutumia sheria kwamba yule Waziri Kiongozi sasa atatambuliwa kama ni Makamu wa Pili wa Rais, siyo halali Kikatiba na ni kosa Kikatiba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahadi ya Mwanasheria Mkuu, alisema we are going to treat this in such a way kwamba itaweza kukidhi hiyo haja, lakini hilo halikufanywa. Kwa hiyo, najua katika hatua hii hapatakuwa na la kufanya, lakini I want to register very strong opposition kwamba Serikali katika hili haikufanya sawa, ilisema kwamba itafanya marekebisho, haikufanya, lakini bado tatizo ni kwamba unaisogeza sheria mbele ya Katiba, bado litaendelea kuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Baraza la Sanaa au kuhusu sanaa tumezungumza mara nyingi na tulikuwa na hoja kubwa sana pale kwamba Serikali inasema inataka kuunganisha COSOTA na wengine lakini tukawashauri Serikali kwa nini wasisogeze mbele ili walete sheria comprehensive lakini bado wakaleta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kuna tatizo hapa ambalo limeibuliwa na kambi ambalo naliunga mkono nalo ni power ya Baraza la Sanaa ku-seize kukamata, ningefikiri kwamba hapa ni wrong pengine hata nilipaswa kusema katika Kamati kwamba ni wrong kuipa Baraza haki ya ku- seize na ku-destroy bila ya amri ya Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na mapendekezo ya Kambi ya Upinzani kwamba hili linaweza kutumika vibaya au wapinzani kwa maana ya msanii mmoja na msanii mwingine wakashawishi Baraza kwamba kuna kitu kinafanyika kwa hivyo inawezekana kazi ya msanii ikakamatwa ikawa destroyed pengine ni kwa ajili ya ushindani wa kibiashara. Hivyo, ingekuwa vizuri hapa hatua yote ambayo Baraza linataka kuchukua ipate baraka ya Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ilivyosema Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, basi angalau kuwe na read verse kwa msanii ambaye mali yake imekuwa seized au imekuwa destroyed aweze kupata hatua ya kudai kupata fidia juu ya kile ambacho kimechukuliwa kinyume na sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Wizara ijitazame kuchachua utalii katika maeneo yafuatayo:-

(i) Festival Tourism: Nchi lazima ijipange vyema kuanzisha matamasha mapya na kuimarisha yaliyopo. Nionavyo kama Taifa tutimize na ku-advertise Busara Festival na Zanzibar Film Festival, kwa sababu ya effect yake, tunaweza kuwa promoted katika kiwango cha Taifa. Ni kosa kutotangaza as part of National Tourism Campaign.

(ii) Songkran Festival ya Thailand ambayo ni ya siku tatu huingiza US Dollar 428.08 million. Afrika Kusini 35 percent ya utalii wake ni matamasha ya utamaduni. Tuwe na matamasha ya sanaa na mengine.

(iii) Nyingine ni Conference Tourism ambayo inatarajiwa kuipa Rwanda US Dollar 76 million mwaka huu na kupandisha utalii kutoka US Dollar 1.2 million kwa 2014 hadi US Dollar 1.3 million hapo mwaka 2015; na mapato kutoka US Dollar 318 million to US Dollar 400 million kwa kipindi hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vema sana kwa kuwa Dar es Salaam imepumua kuwa Capital City, sasa tukielekeza jiji hilo kuwa hospitality and commercial city na conference tourism ipigwe jeki kubwa kuifanyia matangazo. Tuhimize uwekezaji wa Multipurpose Convention Centers na hii itaendana vizuri na ujio wa uwanja wa ndege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, water sports ni muhimu pia.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni Wizara muhimu kwa uhai na mustakbali wa nchi yoyote, bado naafiki Jeshi halisi la JKT kimuundo. Ningependa Jeshi letu liende katika usawa kivifaa, lakini imeonekana Jeshi kwa sasa halina powerful public branding ili kusimama kama taasisi yenye chapa ya Kitaifa. Wananchi hupata public relations ya Jeshi only wakati wa sherehe tu, na si vinginevyo na hivyo Jeshi hubakia katika obscurity. Bila shaka mazoezi ya kijeshi ni moja ya njia hizo kama ile amphibious iliyofanywa Bagamoyo. Ningependa Jeshi liji-brand pia kwenye kufanya kazi za dhamana mara zinapotokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa kuna dharura za mvua/upepo lakini Jeshi halijitokezi kikamilifu. Kazi hizo hufanywa kwenye matukio ya big magnitude tu. JKT inapaswa ipitie upya jukumu lile la kujenga uzalendo ambalo linaonekana limeshindwa hata katika hili, inafaa JKT ijitathmini upya.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika, health tourism ni eneo ambalo bado halijafanyiwa kazi vyema wala halijastawishwa sana. Naamini kama tukiweka hili kimkakati, mfano Mbeya kwa Zambia na Malawi; au Kagera kwa Burundi na DR Congo itakuwa vyema. Pia lazima kama nchi tuwe na specialized areas ambazo zitavuta majirani kufuata matibabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumearifiwa kuwa kuna fedha za mkopo wa riba ndugu juu ya early childhood development kiasi cha shilingi milioni 200 kwa miaka mitano na kuweza kusaidia eneo hili. Tunaambiwa the money has been waiting for us - we drag our feet and the 0-5 child is not developed.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, Wizara imetenga partner fund ili Serikali iweze ku- access fund kwenye taasisi, mashirika ya ufadhili ambayo yana masharti hayo? Je, ni kiasi gani hicho ambacho kimetengwa?
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, uchangiaji wangu utakuwa na theme kwamba nchi hii inahitaji mabadiliko ya fikra kwa sababu hapa tulipo tumegota. Kama kilimo tunakipa asilimia chinjo kila mwaka, kama kilimo kinapata asilimia tatu tu katika maendeleo, wakati huo tunasema tunataka maendeleo ya kilimo na maendeleo ya kilimo haya tunataka yaungane na viwanda, nafikiri tunahitaji fikra mpya. Hapa tulipo tumegota. Miaka 53 ya nchi hii haiwezekani tusiweze kujilisha au kusimamia wakulima wetu. Nafikiri tumegota na tunataka mabadiliko ya fikra katika kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tulipo hivi sasa, nchi hii ina ardhi ya kutosha, ina maziwa ya kutosha, ina mito ya kutosha, ina ukanda wa bahari wa kutosha, lakini ni kitu gani tunajitosheleza? Je, tunajitosheleza kwa chakula? Tunajitosheleza kwa uvuvi? Tunajitosheleza kwa mazao ya nyama au maziwa? Sifikiri katika yote hayo kama tunaweza kuyatimiza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukisema hivi mara nyingi tunakuwa tunalaumiwa, lakini nafirikiri badala ya kwenda mbele kwa kilimo tunarudi nyuma. Kwa sababu baada ya miaka 53 haiwezekani kwa mfano, Kenya ambao sisi tunawapita kwa idadi ya ng’ombe kwa zaidi ya mara mbili ya mifugo wana maziwa ya kutosha sisi hatuna au nchi nyingine nyingi ambazo tunapakana nazo. Kwa hiyo, katika utewekezaji wetu wa kilimo, tumeshindwa kupima muda, fursa na rasilimali zetu. Kwa sababu hiyo, ninaamini kwamba tunahitaji fikra mpya, hapa tulipo, tumegota. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tulipo hivi sasa, nchi hii, kwa mujibu wa Ripoti ya Benki ya Dunia ni kwamba tuna ekari ambazo ni arable na ambazo zinalimika ni milioni 13,500,000; tuna ukanda wa bahari wenye maili 1,400; tuna eneo la mikoko ambalo lina hekta za mraba 115,000 lakini kwa mfano kwenye bahari mpaka hivi leo hatujaweza kuvuna rasilimali za bahari na wanaokuja kuwekeza tunawakamata, tunawashitaki na tunawanyang’anya vyombo vyao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna utaalamu ambao hautaki tena kuvumbua; nchi za Philipines Cambordia, Malaysia na nyingine zinatumia mikoko ambao sisi tunaihifadhi tu, lakini kina kitu kinaitwa mud crab farming, yaani ufugaji wa kaa katika mikoko ambao una utajiri mkubwa sana, lakini bado hatujautumia. Naamini tumegota katika fikra na tunataka tupate mapinduzi ya fikra. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine nashangaa katika nchi hii ambayo asilimia 52 ni misitu. Tuna eneo la maji ambalo linaweza kuzalishwa kwa kilimo ni zaidi ya hekta za mraba 61,500; lakini haielekei kama kuna connectivity baina ya Serikali yenyewe na Wizara kwa Wizara, kwa sababu kama kuna connectivity ingekuwa hadi hivi leo isingewezekana rasilimali zote tulizonazo tusiweze kuzitumia vya kutosha. Nafikiri tunataka fikra mpya, sasa hivi Serikali inaonekana kama imeshindwa katika eneo la kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuje katika leather industry. Tanzania ni ya tatu kwa ng’ombe Afrika; ni ya 11 kwa ng’ombe duniani. Ina asilimia ya ng’ombe asilimia 1.67 ya dunia. Tumefaidika nini katika leather Industry? Kama hatuna leather Industry, ina maana hakuna maana ya kufuga ng’ombe maana hatupati maziwa ya kutosha, hatuna viwanda vya maziwa, ngozi yetu hatuitumii vya kutosha. Kwa hiyo, haina maana ya kufuga. Nafikiri tumegota, tunataka fikra mpya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kwenye mazao ya chakula, tumebaki katika yale yale ambayo ni traditional; na vile vile mazao ya biashara ambayo ni traditional. Sasa hivi sisi tunajifunza, tuna hali ya hewa nzuri sana au ya kila namna; ipo joto kidogo, baridi kidogo, ipo ya mchanga kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mazao mapya ambayo tunaweza kuyavumbua, tumeingia kwenye vanilla kidogo kwa Kilimanjaro na Kagera. Hivi sasa bei ya vanilla ni dola 500 kwa kilo moja. Sisi kama nchi tumehiza vipi zao hili? Kuna mazao kama zafarani (saffron) ambayo kilo moja ni dola 4,000. Tumefunguka vipi kama nchi? Nafikiri tumegota na tunataka mapinduzi ya fikra. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna masoko yamejifungua chungu nzima. Tuna Vietnam wamekuja kuingia mkataba na sisi, tuna Wachina, tuna Waturuki; tumefikiria vipi juu ya mazao? India peke yake inaweza kumeza kwa siku 15 mazao yote ya choroko ya Tanzania, kunde zote za Tanzania. Tumewafunza vipi watu wetu kutumia soko hilo? Tunataka mabadiliko ya fikra, tunafikiri CCM mmegota kimawazo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi hii pia hatuoni upya wa mambo ambayo tunayafanya. Walisema kwamba walitaka wamtue mwanamke ndoo, walisema wanataka wamnyang’anye mkulima kijembe cha mkono, lakini kwa miaka kadhaa hivi leo bado ni tradition farming. Niambieni nchi hii, wapi kuna shamba la kilimo la kisasa la mwekezaji ambaye analima kwa maelfu ya heka kuitoa nchi hii katika njaa? Nafikiri mmegota na inabidi tupate mabadiliko ya fikra. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nafikiri kuna haja kubwa ya mabadiliko. Kwa fikra zangu, nadhani sasa hivi irudisheni agenda kwa wananchi, mwaambie wananchi kwamba katika kilimo, mifugo na uvuvi, mmeshindwa; ili baada ya bajeti hii turudi tena kwa wananchi tujadili jambo hili. Kwa sababu nafikiri kunahitajika mapinduzi ya fikra na fikra hamwezi tena kuitoa ninyi kwa sababu mmeshindwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa Mwaka 2019
MHE. ALLY SALEH ALLY: Thank you.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kama walivyosema watu kwamba huu Muswada umekuja kwa dharura lakini sikubaliani na wengi wanaosema kwamba hakuna madhara ya dharura. Madhara ya dharura yapo kwa sababu hatukupata muda wa umakini wa kuupitia. Hata hapa msemaji wa mwisho, Mheshimiwa Ester alimalizia kwa kuuliza swali kwa nini hajui kama ukiwa wewe ni owner huwezi kupata leseni lakini kwa bahati mbaya wadau wa eneo hili hatukumpata hata mmoja.

Kwa hivyo, anayesema kwamba Kanuni inasema kwamba hata bila wadau tunaweza kuendelea madhara yake ndiyo kama haya hatupati mawazo ya kutusaidia ili tuweze kufanya maamuzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pili dharura hii baada ya kufikiri mimi naona imekuja kwa sababu moja muhimu, ni kwa sababu IMF na World Bank walikuja kuuchangia hapa kwenye Muswada wa Takwimu. Dharura ile ikaonekana hata Mwanasheria Mkuu alituambia kwenye Kamati kwamba ilibidi wa-withdraw the whole part ya Statistics wakaiandike upya ambayo sasa imekuja a better version baada ya kuwasikiliza IMF na World Bank. Kwa hivyo, nahisi hiyo ndiyo ilikuwa moja ya dharura kwa sababu tulikuwa tumefika mahali tumekwama na ilikuwa lazima hawa watu tuzungumze nao na wamekuja na kuna slight improvement ya sehemu ya statistics. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nitachangia sehemu mbili au tatu. Kwanza ni Sheria ya Copyright and Neighboring Right, eneo hili nimefurahi kwamba sasa imekaziwa kidogo kwa watu wanaofanya piracy ingawa kama Kambi ilivyosema hii sheria imetungwa wakati sera bado iko kwenye cabinet. Wengine tulikuwa tunafikiri kwamba sera ifanyiwe kazi halafu tuje na a more compressive law ya copyright na neighboring right. Wameweka hapa namna ya kudhibiti na faini, naziunga mkono na nakubaliana nazo itabaki kwenye utekelezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili kwenye Sheria ya Neighboring Right wamezungumza habari ya resale, naona hapa imewekwa kama kupachikwa tu hakuna umuhimu wa kuonekana re-sale hiyo tutailinda vipi ambayo iko nje ya nchi. Katika Kamati kitu kikubwa ambacho tulikuwa tunalilia ni kwamba Serikali presentation yake ya kuleta sheria ni updated kwa sababu wanasema madhumuni na malengo very shallow, I am sorry to say, haina taarifa ya kutosha. Waheshimiwa Wabunge hata katika dhana mpya hatupitishwi through tukaona kwamba dhana mpya zinafanya kazi vipi.

Mheshimiwa Naibu Spika, unasema unataka kulinda haki ya Mtanzania kuhusu re-sale lakini hujamwezesha Mbunge wako ajue duniani wanafanyaje resale. Imezungumzwa habari ya kinyago lakini kuilinda haki yako huko duniani unafanya vipi na best practice ziko vipi? Kuna makosa mengi ya best practice ambapo tumeshindwa kuyafanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikienda kwenye Sheria ya Film, nilipiga kelele sana ya kukosa best practices na taarifa za kutosha katika maeneo haya. Ni namna gani utamwezesha mtu wa Hollywood akuachie raw footage, wapi inafanyika mtu akuachie raw footage hata kama ni copy atajuaje usalama wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nilitaka best practice nyingine kwamba eti ukishamalizana naye akiendelea kupata faida na wewe unapata faida katika filamu yake. Ina maana kaja hapa umemtoza kila kitu bado wewe unataka uendelee kupata faida anapouza filamu, wapi inafanyika na how best can we protect our country katika eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Serikali haikuja na maelezo ya kutosha kutuambia eti baada ya kuisha kulipana kila kitu wewe uwe na haki ya copyright yake yeye uweze kuwa unaitumia kwa kumega vipande unavyoona vitamu uvitumie kwa ajili ya matangazo wakati wewe umeshamalizana naye. Wapi wengine wanaruhusu ili na sisi tuweze kujiridhisha? Serikali haikuja na maelezo ya wapi hili linatekelezeka.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni habari ya makosa, nilisema hapa kwamba watu wanaweza wakafanya makosa lakini tumeweka faini moja kubwa sana ya 5%, Serikali haikurudi kufanya marekebisho. Tunajua hawa watu wakija wanawekeza billions ingawa pengine akija hapa huwezi kujua undani wa bajeti yake lakini bado mtu ambaye anafanya filamu ya shilingi 1,000,000,000 halafu unamwambia kafanya makosa pengine makosa yale si makosa makubwa kama ya kuhatarisha nchi lakini pengine hakuwakatia watu leseni unaweka 5%. Kwa maoni yangu faini hiyo ni kubwa sana na ni mbaya na haitusaidii.

Mheshimiwa Naibu Spika, halafu lingine ni kwenye Sheria ya Kampuni, hapa pana improvement kidogo kwa sababu hoja ilikuwa kwamba kwa nini usipate fursa ya ku- challenge ile sheria na ilikuwa ile sheria kabla ya kufutiwa lakini hapa kuna tatizo. Pia kulikuwa na tatizo ambalo bado lipo juu ya habari ya kutumia watu ambao wamekuwa prohibited immigrant. Tuna wasiwasi sehemu hii kama haikukaziwa vizuri ingawa inasema by operation of law yaani kama mtu amepitia taratibu zote za kisheria, amefukuzwa nchini kampuni yake ifutwe lakini tunajua kwamba inaweza ikatumika vibaya ama kwa watu kutoka kampuni au watu ambao wana ushindani hao kutengeneza mazingira ya watu hawa kufukuzwa nchini. Hii inaweza ikatishia wawekezaji na wakaanza kujiuliza, je, usalama wao uko vipi ikiwa kwa kufukuzwa nchini pamoja na kwamba sheria inasema anaweza mtu akaenda mahakamani baada ya miaka mitano akasajiliwa tena upya lakini bado kuna utata katika hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ni suala la takwimu, eneo hili lina improvement ndogo. Hoja kubwa hapa ilikuwa uhuru wa kutoa takwimu kwa mtu yeyote bila ya kwanza kuipeleka NBS ili wa-verify halafu iwe publishable. Eneo hili lime-improve kidogo kwa sababu nafikiri tumewasikiliza IMF na World Bank wadau wakubwa wa maslahi ya statistics dunia nzima na tumeweka vipengele vime-improve kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, sheria ya sasa inatenganisha baina ya statistic information na survey, hili lilikuwa na utata. Pia tumejaribu kuweka international na national standard. Hili la national standard ziwepo lakini zisiende kinyume sana na international standard kwa sababu takwimu kama sayansi ina vigezo vilevile popote pale ambavyo unaweza kuvitumia kama social science.

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ni namna ambavyo sasa hivi mtu yeyote anaruhusiwa kutoa takwimu na NBS watakuwa na haki au fursa ya kujibu takwimu hizo. Pia Serikali imefanya jambo lingine zuri la kutengeneza technical committee ambayo itakuwa inatizama kama takwimu zile zinakwenda sawa au haziendi sawa siyo kwa maana ya right au wrong lakini kwa maana ya kwamba zimetimiza masharti ya kisayansi. Inawezekana ukawa umetimiza masharti ya kisayansi ukatoa matokeo ambayo Serikali haiyapendi lakini muhimu ni methodology unayoitumia ambapo Serikali imejibana katika sheria imeweka vigezo vitakavyotumika ni pamoja na vya Afrika na vya UN.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ujumla tunaona kwamba sheria hizi zilivyokuja zimetunyima fursa kama kwenye Kamati yetu ya Sheria. Nakubaliana na ukweli kwamba Serikali inaweza kuleta sheria wakati wowote lakini ili urgency imekuwa kubwa sana kiasi tumejadili sheria nane kwa siku mbili lakini sheria nane kwa wadau mbalimbali waliokuja kiasi ambacho ilikuwa ni a bit of pressure. Mimi sikuona sababu ya kufanya hivyo kwa sababu vitu vingine vingeweza kuja baadaye.

Mheshimiwa Naibu Spika, mtu hapa akisema kwamba wapinzani wanapinga hizi sheria au wanapinga mabadiliko haya just for the sake of kupinga hatutendewi haki. We want to have a better laws ambazo zitasaidia wawekezaji wetu na sisi ndani. Kwa hivyo, tukiinuka kwenye Kamati na Bunge hatupingi kwa sababu Muswada huu umeletwa na CCM, Muswada huu umeletwa na Serikali na Serikali ni yetu sote. Tunataka kutengeneza mazingira ili kwanza tusirudi tena hapa kutengeneza sheria hiihii. Pili, tutengeneze mazingira ili wawekezaji, tunasema tunataka Tanzania ya viwanda, Tanzania ambayo ina wawekezaji tutengeneze sheria ambazo zitakuwa friendly kwa wawekezaji na hicho tunachopigania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, kuhusu Sheria ya Filamu nimesema tunataka international standards ili tuweze kuona Bollywood, Hollywood na nchi zingine zinafanya nini? Tumekuwa tukiambiwa kwa maneno pale kwamba nchi hizi zipo, hatukuweza kuona.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda pia nishauri Serikali katika hili kwamba unakuwa na generation mpya ya Wabunge ambao wanahoji sasa, Wabunge ambao wanaweza ku-Google, kufanya utafiti na kadhalika. Kwa hivyo, Serikali ibadilike katika mtazamo wake namna ya kuleta Miswada, ije na taarifa za kutosha ili iweze kutusaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nitaanza na makinikia ambayo kidogo yameelekea kama kutugawa huku ndani kiasi ambacho juzi Mheshimiwa Abdallah Ulega alisema kwamba sisi ni UNITA na kwa kwa sababu hakukatazwa na hakuna kiongozi yeyote aliyemwambia afute kauli hiyo nataka niulize maswali matatu/manne.

Nani UNITA zaidi au upande ule ambao wanafuta matokeo ya uchaguzi na wanaweka watu wasio halali? Nani UNITA zaidi wanaofuga mazombi ambao kila siku wanapiga raia? Nani UNITA zaidi ambao wanatunga sheria za kuzuia watu wasitoe maoni yao na wanafungia magazeti? Nani UNITA zaidi ambao wanaweka Masheikh kwa miaka minne hata bila kesi kufanyika? Hilo nimemaliza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili nilitaka kusema kwamba hii makinikia imekuja ili kutupunguzia uwezo wa kuchangia katika bajeti yetu hapa. Mimi sioni kama ni bahati mbaya kitu ambacho kiko nje ya Bunge kimeletwa hapa ndani kimetupunguzia uwezo wetu wa kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana nilihudhuria kwenye kongamano moja ambalo linasema hapa Tanzania watoto 30.2 wenye uwezo wa kwenda shule hawaendi shule, hatujadili hapa tunaona kama kitu kidogo tu. Jana tumesikia kwamba, asilimia 34 ya watoto wa Kitanzania wana utapiamlo, tumeacha kulizungumzia hapa! Lakini pia, tumeacha kuzungumzia kwamba bajeti yenyewe imekuja na mashimo mengi ambayo yanapaswa yajazwe, pia bajeti yenyewe imekuja ikiwa imetekelezwa chini ya asilimia ndogo ya ile ya mwaka jana, imetutoa katika mood na tumeanza kuzungumza mambo mengine ambayo hayakuwa na umuhimu kuyazungumza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye mambo ya bajeti nina mambo mawili matatu, kwanza ni Deni la Taifa. Mimi siyo katika wanaoamini kwamba deni letu linanyumburika, sijui linafanya kitu gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana nilisema na kusema kweli rate ya mwaka jana imeongezeka mwaka huu kwa hivyo, bado nina maoni kwamba Deni la Taifa linapaswa likabiliwe inavyopaswa na sio kuona kwamba linahimilika kwa hivyo tuliachie liendelee. Mwaka jana nilisema na mwaka huu narudia, ziko nchi zilikuwa zikisema hivyohivyo kwamba deni linahimilika lakini zimesambaratika, Greece, Venezuela, Peru na wengine, hilo la pili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, mwaka jana nilisema na mwaka huu nasema tena. Bado sioni faida ya Serikali ya Muungano kwa Zanzibar katika mambo makubwa. Nilisema mwaka jana kwamba katika miradi kielelezo basi angalao mmoja uwepo Zanzibar. Hii nasema kwa sababu Zanzibar tuko watu 1,200,000 ukipeleka mradi ambao unaajiri watu elfu tano, elfu sita, maana yake umeajiri work force yote ya Zanzibar, lakini bado Serikali ya Muungano inaona kwamba bado haitaki kufanya wajibu, mimi nahisi ni wajibu, inaona haina wajibu kwa Zanzibar. Lakini Zanzibar itafanyaje mambo makubwa wakati uchumi wake unazuilika na upande huu? Kodi zake haziwezi kukusanywa kama inavyotakiwa? Lakini itakavyokuwa vyovyote vile uchumi wa Zanzibar ni uchumi mdogo hauwezi kufananishwa na uchumi wa Bara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ninachotaka kusema ni kile ambcho Mheshimiwa Ulega alisema siku mbili tatu nyuma, nampa credit yake. Alisema kwamba Rais Magufuli anafaa sasa aelekeze kwenye ku-invest kwenye mambo ya bahari, lakini hata leo Mheshimiwa Adadi alisema jambo hilo. Sisi tumezungukwa na nchi ambazo ni land locked, Rwanda, Zambia, sijui wapi, wote wale, tungekuwa tumejijenga kwenye bahari tuna meli za kutosha, tuna uwezo, tungelamba cargo zote za nchi hizo, sio tu wakati wa kuodoa, lakini hata wakati wa kuingiza, hilo moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jingine ni suala la aqua culture. Wiki tatu nyuma nilisema katika Wizara ya Maliasili kwamba bado hatujatumia blue economy na kitu kimoja ambacho kina utajiri mkubwa sana, narudia tena ni bahari, kuanzia Bahari Kuu kule mpaka pembezoni humu. Kwa kuwa watu wengi wameshazungumzia Bahari Kuu, mimi nazungumzia hapa pembezoni; nilisema utajiri wa hapa pembezoni uko katika fukwe pale, kwa maana ya kufuga vitu kama kamba, kufuga vitu kama kaa, ambazo ni billions of dollars. Nchi kama Vietnam ambayo tuna urafiki nayo, nchi kama China, hawashibi kwa mazao ya bahari. Chochote utakachozalisha wewe wanaweza kukichukua kama vile ambavyo India ukizalisha chochote kile cha beans hizi, chochote kile watakichukua. Kwa hiyo, nasema tena Mheshimiwa Waziri, hilo tulifanye. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia lilizungumzwa leo suala la afya. Tungewekeza katika afya kiasi cha kutosha tukawa na hopitali ambazo ni kubwa ni za maana, watu wasingekuwa wanakwenda India. Tuna majirani zetu hapa chungu nzima wangekuwa hii ndio India yao wanakuja kwetu. Serikali najua hii haitafanya kazi muda huu, itandike misingi yakuwezesha hilo lifanyike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kwenye suala la elimu. Suala la elimu wenzetu mfano Northern Cyprus moja katika kipato chao kikubwa ni kwenye elimu au nchi nyingine. Tumekuwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kina brand moja nzuri sana kupita kiasi duniani, lakini kimeshindwa kukua nje ya Tanzania kimebaki hapa hapa, wakati wenzetu kama Marekani utakuta American University iko Misri, iko Lebanon, iko wapi. Na sisi kama tungejipanga vizuri tungeweza kutumia eneo letu hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, Mheshimiwa Mama Rwakatare jana alisema hapa au juzi, kwamba kuna kodi nyingi kwenye elimu kiasi ambacho hatuvutii watu kutoka nje. Nchi kama Cyprus watu kutoka nje ni mataifa 144 wanakwenda kusoma Cyprus, wana wanafunzi zaidi ya laki mbili kutoka nje ambao wanasoma katika nchi yao. Tukifanya hii kama ni sehemu ya kipato, tukatengeneza vizuri, tukapunguza kodi, tukai-streamline, naamini inaweza kutusaidia sana kwenye mapato ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jingine ambalo linaweza kutusaidia ni kwenye diaspora. Mpaka sasa diaspora tunasema in general terms kwamba waje wawekeze. Je, tumeonesha maeneo gani wanaweza kuja kuwekeza? Tumetangaza wao kama diaspora watapata vivutio gani kuja kuwekeza? Kwa hiyo, ina maana kwamba kama tukijipanga vizuri tunaweza kutengeneza hiyo ikatusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine tunajenga reli. Reli kutoka inakotoka mpaka inakokwenda hapa katikati kungeweza kufanywa vitu vya kuweza kusaidia, ili local content iwe na maana, lakini kama tutajenga reli tu ili itoke mwanzo kama ilivyo sasa inatoka Dar es Salaam inakwenda mwisho wa reli Kigoma, hapa katikati hapana chochote kuwasaidia watu wafanye local content itakuwa haina maana yoyote. Kwa hiyo, nashauri kama tunajenga reli hii kubwa, tusilenge tu kwamba tutatoa makaa kutoka kule mpaka kuja huku, lakini pia katikati hapa kuwe na uwezekano wa kuwawezesha watu wafaidi kwa local content. Hali kadhalika katika hili bomba la mafuta linalotoka Uganda kuja Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, alizungumza Mheshimiwa Selemani Zedi hapa katikati watu wapate ajira. Sio ajira tu kwa maana ya vibarua, lakini what after that? Nashauri kwamba kama tunataka tuwatengenezee watu fursa nzuri ya maisha, basi tuwatengenezee local content ili waweze kusaidia, lakini kama tukizubaa hapa chakula cha wafanyakazi wa reli watakaojenga, Waturuki kitatoka Uturuki badala ya kuwawezesha wananchi wetu hapa wakasaidia. Chakula cha wafanyakazi ambao wanajenga hilo bomba kitatoka kwingine, tujipange katika haya ili tuweze kusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nitazungumzia mambo mawili tu, la kwanza ni suala la investor confidence ambalo jana Mheshimiwa Lema alilizungumzia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna tatizo kubwa Tanzania la investor confidence kwa sababu ya kauli nyingi ambazo zinatolewa na Serikali, matendo mengi ambayo yanatendwa na Serikali ambayo katika nchi nyingine athari yake inaonekana moja kwa moja, lakini hapa kwa kuwa athari yake hatuioni moja kwa moja kwa sababu stock exchange yetu haifanyi kazi kama vile ambavyo ingetakiwa tunadharau.

Kwa hiyo, napenda niishauri Serikali na Mheshimiwa Waziri kwamba wakae na Serikali na wajaribu kutengeneza namna ambayo shock ya kibiashara, shock ya uwekezaji inaweza kupata nafasi kidogo kwa kuzuia kauli au matendo ambayo yanapoteza investor confidence, hilo moja. (Makofi)

Mheshimiwa MNwenyekiti, lakini lingine nitalizungumzia kwa undani kidogo ni suala la Mfuko wa Pamoja wa Fedha ambapo leo hii halitochacha mpaka nipate majibu, kwa sababu hili lipo Kikatiba, miaka almost 40 hivi sasa halijafanyiwa kazi, kwa nini linashindwa kufanyiwa kazi? Kama vile ambavyo Mahakama ya Katiba ambayo nchi hii imesema iundwe mpaka leo haijaundwa badala yake tunatatua matatizo yetu ya Katiba kwa kupitia kwa Tume ya Pamoja au whatever. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfuko huu wa Pamoja wa Fedha tokea kuasisiwa hivi sasa tumeshapoteza mamilioni katika kuiendesha na kujaribu kufanya kazi, mabilioni yote ambayo yametumika yamekwenda bure.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfuko wa Pamoja ni white elephant haujaundwa, haujatumika na kwa hivyo bado matatizo ambayo yameundiwa kwayo yako pale pale kwamba Zanzibar inalaumika haichangii katika Muungano, lakini Zanzibar inasema itachangiaje katika Muungano wakati haijui matumizi yapo vipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi ya Bara hayawezi kuwa sawasawa na matumizi ya Zanzibar kwa sababu Zanzibar ni ndogo kama inataka askari, inataka askari kidogo kuliko Tanzania Bara, kama inataka kulinda mipaka Tanzania Bara inapakana na nchi tisa wakati Zanzibar inapakana na Kenya peke yake. Kwa hiyo, kuna mambo mengi ambayo hatuwezi kwenda sawasawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo haitoshi kulikuwa na ripoti nyingi zimefanywa, moja ni ripoti ya black, nyingine ni ripoti ambayo imetengenezwa na Coopers and Lybrand, ikionesha namna gani kunaweza kuwa na formula kwa sababu inaonekana formula ya 4.5 ambayo tunagawana hivi sasa imepitwa na wakati. Kwa hivyo, mfuko huo siyo tu utaonesha Zanzibar ichangie kiasi gani na Tanzania Bara ichangie kiasi gani, kuondoa lawama kwamba Zanzibar inabebwa au Zanzibar inapata bure kila kitu, pia utaonesha namna ambavyo fedha za Muungano, zilizo halali za Muungano hazitumiki kwa Serikali ya Tanganyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tusikatae ukweli, hapa tuna mamlaka tatu, tuna mamlaka ya Zanzibar, tuna mamlaka ya Muungano na tuna mamlaka ya Tanganyika, Tanganyika ipo, haijawahi kuondoka, kwa sababu mfanyakazi wa kilimo wa Tandahimba ni mfanyakazi wa Tanganyika siyo mfanyakazi wa Muungano. Mfanyakazi wa Mbeya, Nachingwea wa Wizara ya Afya ni mfanyakazi wa Tanganyika siyo mfanyakazi wa Muungano, tunajidanganya siku zote. Kwa hiyo, mamlaka ya Tanganyika ipo, imekuwa inatumia fedha za Muungano kwa ajili ya Tanganyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ukiwepo Mfuko wa Pamoja na hizi ripoti zimeonesha ni kiasi gani fedha za Muungano zinakusanywa na hizo fedha za Muungano zinatosha kuendesha Mamlaka Tatu, Mamlaka ya Tanganyika, Mamlaka ya Zanzibar na Mamlaka ya Muungano. Kwa hiyo, mpaka leo mfuko hauundwi kwa sababu watu walioko Tanganyika wana hofu ya ku-expose hiyo, kwamba kuna fedha za Muungano zinatumika kwa Tanganyika, wana hofu ya kuonesha kwamba Zanzibar inaweza kuchangia iwapo kungekuwa na usawa kwa maana ya kwamba Zanzibar itashirikiana kitu gani na Muungano itashirikiana kitu gani. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri leo hii natangaza kabisa, najua mtashinda kwa wingi…(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ahsante. Nimejipanga kuchangia katika eneo moja tu, lakini kumetokezea kitu ambacho itabidi nikiseme ambacho kimetokezea jana usiku na ambacho kinahusiana na hali ya usalama na utata utata na matatizo haya ya kukamatana kamatana bila ya kujitambulisha wanaokamata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana usiku huko Pemba Wete wamekamatwa vijana sita Sued Nassoro, Khamis Abdallah, Abdallah Chumu, Juma Kombo, Said Shomari na Uledi Khamisi, wamechukuliwa na watu ambao wamekataa kujitambulisha lakini wananchi kwa bahati waliziona nambari zao za gari wakachukua na leo asubuhi tulipoanza kuulizia RPC wa Kaskazini na Kusini wote wanasema hawako mikononi mwao. Kwa hivyo, wamekamatwa na watu wasioeleweka, tunaongezea ule msamiati wa watu wasiojulika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu hasa mimi nitabakia katika sukari. Nataka kutazama sukari bigger picture. Sukari kwa maana ya kwamba ni kilio cha Wazanzibari, ni mkusanyiko wa vilio vingi kinaji-manifest katika sukari; kwa maana kwamba kutokana na matatizo, mivutano ya kisiasa au sekeseke la kisiasa ambalo tumekuwa tukiendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muda mrefu pia kumekuwa na tatizo la kiuchumi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Zanzibar au wafanyabiashara wa Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wengi wa Zanzibar wanafikiri kwamba hii ina ukandamizaji, ina unyanyasaji, ina kuipendelea Bara zaidi kuliko Zanzibar lakini pia inaleta sintofahamu ambayo watu wengi wanafikiri inafanywa makusudi ili kuitia Zanzibar kitanzi cha uchumi. Kwa sababu yapo mambo mengine hayana logic lakini yamekuwa yakitokezea, na watu wanauliza au kwa sababu sisi ni Visiwa. Kwa sababu yako mambo mpaka tunafika tunajiuliza au sisi ni visiwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi imekuja hii zana ambayo inaelezwa hapa ya kutojitosheleza; kwamba ikiwa wewe hujitoshelezi katika bidhaa usiuze kwingine, bila kujali uhuru wa soko, bila kujali upana wa soko. Sasa nafikiri hii ni principle mbaya haifai kuendelezwa na inapaswa ikomeshwe mara moja. Maana yake nini, maana yake ni kwamba kama leo unawaambia Wazanzibari hawawezi kuuza sukari kwa sababu mahitaji yao ni tani 17,000 wanazalisha tani 8,000 maana yake kesho utawazuia wasiuze viazi, kesho kutwa utawazuia wasiuze nguo, kesho kutwa utawazuia wasiuze kingine kwa sababu tu mahitaji yao ya ndani hayajajitosheleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri hii ni principle mbaya sana, tunakwenda katika hatua isiyokuwa na msingi kabisa. Tunafanya protectionism ya viwanda au kiwanda cha sukari dhidi ya ndugu yako au kwa sababu sisi ni Kisiwa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhana inayoenezwa ni kwamba pengine Wazanzibari watapenyeza sukari kutoka nje. Kwani hivi sasa sukari haiingii kutoka Malawi, kwani hivi sasa sukari haiingii kutoka kwingine inayoingia kwenye soko la Tanzania ambalo lina starve? Soko la Tanzania hivi sasa linahitaji tani laki tatu na hamsini kwa mwaka. Kila mtu anajua uzalishaji una upungufu wa tani laki moja nzima, sukari inatoka nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sukari ikipitia Zanzibar, hata ikiwa inatoka nje inapita Zanzibar inakuja katika soko la Muungano, kwa nini iwe vibaya kwamba inatoka Zanzibar wakati pia soko la Muungano linaagiza sukari kutoka nje ili kujaza lile pengo? Au kwa sababu sisi ni Kisiwa kwa maana nyingine tunahukumiwa kwa vitu ambavyo kwa kusema kweli vinatuumiza sana moyoni?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi hatukuungana kwa ajili ya kugawana umaskini tu, tumeungana katika kugawana pia na neema. Sasa kama tunazuiana tusigawane neema, mtu anajiuliza Muungano huu una faida gani kwa Wazanzibari?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano ulikuwa unatarajia nini kuungana na Zanzibar ambayo ina eneo la kilomita elfu mbili za mraba vis-a-vis nchi ambayo ina kilomita elfu tisa za mraba? Ulitarajia nini unaungana na Zanzibar ambayo watu wake sasa hivi ni milioni moja na laki tano vis
-a-vis milioni hamsini na tano? Ulitarajia nini kuungana na Zanzibar ambapo upande mmoja una soko kubwa na upande mmoja una soko ndogo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ulitarajia Zanzibar a-survive vipi kibiashara? Ulimfikiria Zanzibar afanye nini aingie katika soko? Kama unazuia Zanzibar asiingie kwenye soko la Tanzania Bara ina maana unamzuia Zanzibar asiingie kwenye soko la Afrika Mashariki. Otherwise tunaingia katika matatizo ambayo kusema kweli kama hatukuyapatia suluhu basi utakuwa mgogoro mkubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari Zanzibar tulizuiliwa Zantel isiingie Tanzania Bara kwa muda wa miaka mitano. That was the first mobile company, the biggest, ikafa. Kwa maana sasa hivi ipo taabani imeshanunuliwa na Tigo. Hata hivyo, hivi sasa bidhaa nyingine zinazuiliwa, kwa mfano ukitoka Zanzibar kuna maji ya drop yanazuiliwa kuja huku. Kwa muda mrefu maziwa ya Bakhresa yalizuiwa kuja Tanzania Bara. Kuna njia inaonekana kuna watu wanafanya makusudi ili kui-starve Zanzibar kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nauliza hivi hatujui kwamba Zanzibar kwa udogo wake inahitaji ipate mahali ipate soko? Itafika lini Zanzibar kwa udogo wake itengeneze magari ya kujitosheleza halafu iuze nje, itengeneze TV za kutosheleza halafu iuze nje? Let use our brain.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wawili watatu hapa, mmojawapo Mheshimiwa Kitwanga jana na leo amekuja na fikra mpya, tufikiri upya, tusifikiri kizamani, tufikiri kisasa, kwa sababu kama hatujatengeneza mazingira ya Zanzibar kusonga kiuchumi unatengeneza bomu lingine. Bomu ambalo likilipuka linaweza kuwa kubwa zaidi kuliko bomu hili la kisiasa ambapo pengine watu wakipewa vyeo wananyamaza, watu wakibebelezwa wananyamaza lakini watu wakiwa na njaa watashindwa kunyamaza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa biashara nyingi Zanzibar zimefungwa kwa sababu ya hii double taxation ambayo mara nyingi inatokezea ikija huku. Imesemwa, imesemwa, imesemwa, lakini mpaka hivi leo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nafikiri ikiwa kwamba tumeungana sisi kwa mambo matatu ambayo yote nafikiri yana shaka katika Muungano huu; la kwanza tumeungana kama vile tunatafutana. Kuna habari nyingi mara nyingi zinazungumzwa kuwa Zanzibar ni kichocho. Hivi kichochoro Zanzibar tu, hakuna mipaka ya Sirari, hakuna mipaka ya Horohoro, hakuna mipaka mingine yote ya Tanzania? Hivi bidhaa zinazopitishwa Zanzibar kuja huku ndiyo ukikusanya zote pamoja itakuwa ndiyo zinapita zile ambazo zinapita katika mipaka yote ya Tanzania? Hilo moja, lakini la pili kwani… (Makofi)

TAARIFA . . .

MHE. ALLY SALEH ALLY: Nafirikiri It is very dismissible amechukua very minor issue, mimi ninazungumzia sukari katika picha kubwa, lakini Waziri anajikita katika swali moja ambalo kwa miaka hamsini ya Muungano halijapatiwa suluhu. Ikiwa mpaka leo Mawaziri wanazungumza miaka hamsini na tano baada ya Muungano kwa maana gani? Bora Waziri angekaa tu akasubiri wakati wako ajibu kwa sababu hapo hajajibu kitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, nafikiri lazima tuwe na mfano wa kuonesha kama uchumi wa Zanzibar haukuwa supported kama vile kwa mfano EU walipoungana na nchi maskini Portigual na Spain walitengeneza mpango maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niulize leo hii hapa Serikali ya Muungano imetengeneza mazingira gani ya kiuchumi ya Zanzibar? Mtu ataniambia Zanzibar kuna Serikali yake. Serikali gani ambayo haina taratibu za kupata mikopo, lazima ipite kwenye Serikali ya Muungano, Serikali gani ambayo sera zake kuu zinafuata sera za nchi, kama ni sera za kifedha, kama ni sera nyinginezo? Kwa hivyo nyingine si kweli kwamba Serikali ya Muungano imeleta tatizo hili, tatizo hili lipo mpaka leo kila siku linaendelea kuwepo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri tukubali tu kwamba Zanzibar ina potential…(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Katika mitaa ya twitter, Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla anajulikana kama Mzee wa Nje ya Box kwa sababu ya falsafa yake ya kufikiri nje ya box. Sasa kwa kupewa Wizara hii, nafikiri sasa siyo tu afikiri acheze nje ya box kwa sababu ni Wizara ambayo inaweza kuitoa Tanzania, inaweza kuifanya Tanzania ikawa power house ya kiutalii kama ilivyo au inavyotarajiwa. Kwa bahati mbaya, amekaribishwa katika hatua mbovu kabisa, ameingia kwa mguu wa kushoto kwa maana kwamba bajeti yake anaingia tu imekatwa by 22 percent kiasi ambacho kinaonyesha Tanzania au Serikali kutokuwa na umakini au kutokuwa na nia ya kuona utalii unakua kwa kiasi kikubwa na hivyo anaanza kwa bajeti yake kupunguzwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, tunataka acheze nje ya box kwa sababu akicheza ndani haonekani. Kwa hivyo, Waziri muelezee Mheshimiwa Rais kama inawezekana ukicheza humu ndani hutafanya chochote. Lazima utoke kama walivyosema wengine uende kwenye maonesho, uende kwa matajiri wakubwa, utembelee nchi mbalimbali ndivyo ambavyo tutapata watalii. Kwa kufikiri tu nje ya box bila kucheza nje ya box tutabaki hapahapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia tunataka ututolee aibu ya nchi hii kwamba inatoa ajira 1,500,000 wakati ina uwezo wa kutoa ajira kubwa na nyingi zaidi. Nchi hii inapata watalii 1,300,000 wakati inaweza ikapata watalii hata milioni 2 na zaidi ikiwa kama Waziri atacheza nje ya box na siyo tu kufikiri ndani ya box. Pia nchi hii utalii unachangia asilimia 17 wakati tunaamini unaweza ukachangia hata zaidi ya asilimia 30 ikiwa Wizara hii itapewa umuhimu unaostahili na kwamba Waziri atapewa mamlaka na kuweza kufanya kazi yake vya kutosha na kuweza kufika mbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mauritius ina watu 1,500,000, watalii wanaopata ni 1,400,000 almost double ya raia wake, halikadhalika kwa Qatar, UAE na Seychelles ambayo inapata watalii 300,000 lakini raia wa nchi hiyo ni 100,000. Mtu anaweza akasema lakini wao ni kidogo lakini katika kupima kitu unapima kwa percentage ya watu au percentage ya kitu haijalishi kama wewe ni nchi kubwa au ndogo. Tanzania inapaswa kupata, kama mnavyoweka lengo zaidi ya watalii 3,000,000 lakini kwa kufikiri tu nje ya box hutafika mbali, cheza nje ya box. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kuhusu sera, tumekaa miaka 20 tangu sera iliyopita, sasa hivi najua kuna sera inatengenezwa kwa bahati nimeweza kuichungulia kidogo. Tumechelewa kufanya vitu vingi kwa sababu tumechelewa kurekebisha sera. Sera hii imetufanya tuwe nyuma katika vitu vingi ambavyo itabidi tutumie nguvu nyingi kuvirekebisha wakati tungeenda kwa wakati tungekuwa tumekwenda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mengi niliyoona katika sera naona ina mwelekeo mzuri. Natarajia kwamba itakuwa shirikishi zaidi na tutakuwa na legislation nzuri na kutengeneza mazingira mazuri. Isipokuwa kitu kimoja sikukiona napenda kushauri nacho ni kuhusu lugha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sera hamkuzungumza suala la lugha. Kama tunataka kuvuta watalii wengi zaidi ni lazima hilo liwe muhimu. Kichina, Kirusi, Kituruki hizo ndiyo lugha ambazo zinakuja hivi sasa na wana raia wengi ambao wanaweza wakaja katika nchi zetu. Ningependa hili liingizwe katika sera kwa sababu linaweza kutusaidia kwa maana kwamba taasisi ambayo inafundisha utalii basi iwe na component ya lugha mojawapo katika major languages au coming major languages. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni kuhusiana na bombardier na utalii. Kumekuwa na dhana hapa ya kuamini kwamba tukiwa na bombardier maana yake tutakuwa na utalii, mimi siamini kwa sababu kuwa na ndege ni kitu kingine na kuwa na utalii ni kitu kingine. Unaweza kuwa na ndege lakini usiweze kui-brand vya kutosha kiasi ambacho tutaingia sisi tu Watanzania tukitoka Dubai tukija hapa au tukitoka Uingereza tukija hapa. Inachukua muda kwa watu kuamini brand ya ndege, muda sana na kwa hivyo mpaka brand ya bombardier iwe sawasawa pengine miaka mitano au miaka 10 mbele huko kama tutakuwa tunakwenda sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitawapa mfano mdogo tu, brand ya ndege ni shirika la nchi, wananchi wake wanapenda kujitambulisha. Chukueni mfano wa Kampuni ya Zantel na Zanzibar. Zantel kwetu sisi Wazanzibar ni brand yetu sisi Wazanzibar, pamoja na maudhi yake yote ya Zantel lakini Wazanzibar wote hapa lazima watakuwa Zantel halafu watakuwa na simu nyingine. Haiwezekani kuna Mzanzibar hana hata simu moja ya Zantel kwa sababu ni ndani ya moyo wake. Kwa hivyo, ukitaka raia wa nchi nyingine aipende bombardier, aje kwa bombardier ni lazima ujue kwamba kuna mapigano ya kupigania routes, alignment ya mtu kama mwananchi kwamba anaipenda nchi yake na kwa hivyo lazima asafiri na ndege ya nchi yake, kwa hivyo, itachukua muda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mmoja, Seychelles walikuwa na Air Seychelles ilikuwa inakwenda Dusseldorf kuingia Ujerumani, ni kituo pale cha utalii cha kupata mashirika makubwa ambayo namshauri Mheshimiwa Waziri charters ndiyo muhimu kuzitumia zile kuleta watalii. Wamekata kwenda Dusseldorf basi ule mwaka waliokata ndiyo watalii wametoka 16% mpaka 29% pamoja na kwamba Air Seychelles haendi Ujerumani. Kwa hivyo, is not about kwamba wewe una ndege yako ya Taifa ndiyo kupata watalii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine nachotaka kuzungumza ni kuhusiana na brand. Leo Mheshimiwa Waziri umetuambia kuwa tutakuwa na hashtag ‘Tanzania Unforgettable’, nimeipenda kwa sababu ile motto ni nzuri na inaweza kuwa na maana ya kusaidia. Nimei-tweet leo na tayari kuna tweet nyingi zinasema kwamba kuwa na hiyo motto siyo issue, issue ni namna ya kui-brand sasa mpaka ikubalike. Kwa hivyo, it takes a lot of money ku-brand motto hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ukifikiri Singapore, Malaysia au India Incredible India zimechukua a lot of money ku-invest. Kama leo hatuwezi kutenga pesa ya kutosha kuweza ku-invest katika brand zetu itabakia vilevile tu haitakuwa na maana yoyote ku-change from Tanzania Land of Kilimanjaro and Zanzibar na kuingia katika motto hii.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nataka kusema kwamba sisi wapinzani hatuna ugomvi na ATCL, hatuna ugomvi na ndege; ndege ni zetu na ATCL ni yetu, tunapokosoa, tunaposema ni kwa ajili ya kulifanya shirika liwe na nguvu zaidi kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mambo yangu matatu nitakayozungumza, nianze kuondosha dhana ambayo inazidi kukua kwamba kukiwa na shirika la ndege ni huduma, hii sio sahihi na kwa bahati mbaya tunapandikiza fikra kwa Watanzania ambao baadaye shirika likifa itabidi tuwajibu kwa sababu kama ambavyo tulikuwa tunasema viwanda vingine ni huduma, viwanda kwa maelfu au kwa mamia vimekufa na faida yake hatukuiona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili ni kwamba, tunapandikiza fikra mbaya kwa watendaji wa shirika letu, kwamba wao hawalazimiki kuliendesha shirika kibiashara, hiyo ni wrong concept. Shirika ni sustainability na profitability, kama hamkufuata hivyo shirika linakufa, pesa ya umma inapotea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ethiopian Airlines – moja ya mashirika ya mfano hapa mitaani kwetu; Ethiopian Airlines mwaka wa fedha 2016/2017, walitengeneza faida ya Dola bilioni 233, mwaka uliofuata yaani 2017/2018, wakatengeneza faida ya dola bilioni 229, wakajiuliza wameshuka kwa bilioni nne, wamefanya inquiry kwa nini wameshuka kwa bilioni nne, sio kwamba wamejiachia tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tusijenge dhana ya kujiachia kwamba ni service, kwa sababu hatimaye shirika likifa tutakuwa na tatizo, kwa hiyo tuiwekee target management ya ATCL kwamba lazima katika muda fulani mfikie lengo fulani. Hilo la kwanza. La pili ni kwamba, lazima wawe na business program ambayo inaonesha wanatoka hapa watafika hapa na growth iwe inaonekana mwaka hadi mwaka, tukiwaachia na kuwajengea dhana kwamba ni huduma tu, basi tutafika pabaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili nimelisikia leo na nimefurahi, juu ya Uwanja wa Ndege wa Songwe. Siku zote nasema kwamba nchi nzuri haiwezi kuwa na gateway moja tu katika nchi yao, inabidi watengeneze gateways nyingi kwa suala la ndege. Uwanja wa Ndege wa Songwe ni gateway yetu ya kusini, tunaweza tukatawala na tukatengeneza biashara kusini ikiwa tutajipanga vizuri kwa uwanja ule, lakini leo nimesikia kwamba angalau sasa tenda imetangazwa ili kuweka taa katika Uwanja wa Songwe ili iwe getaway yetu ya kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Mwanza ni gateway yetu ya Maziwa Makuu, Mwanza ikitumika vizuri ni mahali pazuri sana pa kuweza kutumia kuingia Maziwa Makuu, lakini sioni athari ya kiuchumi ya kujengwa uwanja mkubwa Chato. Nimekuwa najiuliza; hivi Chato ni gateway ya kwenda wapi kwetu sisi? Unaweka kiwanja pembeni ya nchi, hakuna utalii, hakuna biashara ya hivyo, halafu unatumia pesa nyingi badala ya kuimarisha viwanja ambavyo ni gateway…

T A A R I F A

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, siipokei taarifa yake kwa sababu ni ndoto tu anayoyasema.

MWENYEKITI: Endelea na mchango wako.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nafikiri kwamba tungeweza kuwekeza zaidi katika maeneo ambayo yangeweza kuwa na maana kwetu sisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ninalotaka kuzungumza ni kujaribu kui-turn…

T A A R I F A

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubali taarifa hiyo na Mji alioujengea unaitwa Gbadolite na ni kweli kwamba kumekuwa na makazi ya popo na njiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine linaloifanya Dar es Salaam Airport…

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Musukuma.

T A A R I F A

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa imekataliwa kwa sababu udhahiri umejengwa kwa ajili ya upendeleo tu, hakuna kingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema kingine ni kuutengeza Uwanja wa Ndege Dar es Salaam uwe ni hub. Sasa hivi utakuta mtu akitaka kwenda Moroni, akitaka kwenda Seychelles, akitaka kwenda Mauritius…

MHE. JAMES K. MILLYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Millya, kaa chini.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naishauri Serikali…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Mimi nitachangia katika eneo moja tu la utawala bora. Kwanza nataka nianze na msemo usemao, “Mgema akisifiwa tembo hulitia maji”. Sitaki kuufafanua nitauacha hivyohivyo tu uning’inie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuanza kwa kusema kwamba kukosolewa ndiko kunakomjenga mtu. Wanaokusifu hawakusaidii sana, ukikosolewa ndipo unapoona makosa yako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana wakati nafanya research ya nini nitasema hapa nikaona kwamba IMF imetoa taarifa kwamba uchumi wetu utakua kwa asilimia 4 tu mwaka huu na mwaka ujao utakua kwa asilimia 4.2, kinyume na ambavyo tumeambiwa na bajeti inavyosema kwamba utakua kwa zaidi ya asilimia 6. Humu ndani tunajisifu kwamba uchumi unakua, wa pili Afrika, wa tatu Afrika, wa kwanza Afrika Mashariki, hiyo haisaidii kitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nianze kwa kusema kwamba katika upande wa utawala bora kuna vitu vingi vya kuiga lakini tukifika kuwaambia viongozi wetu kwamba tuige hili tunaambiwa Tanzania haiigi kila kitu. Nitakuja na mfano mdogo tu mmoja mmoja kutoka Ethiopia, ndani ya miaka miwili Ethiopia imetoka kwenye dictatorship into democracy and now deep into good governance. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano nitakaoutoa ni wa mwanariadha ambaye anaitwa Feyisa Lilesa ambaye alishinda medali ya silver kule Rio De Janeiro. Yule anatoka Kabila la Oromo ambao ni wengi lakini kule kwao hawana nafasi ya kiuongozi. Alipokuwa kule in protest akafanya alama hii (hapa Msemaji alionesha alama) kuonesha kwamba Waoromo hawana uhuru ndani ya nchi yao wenyewe. Matokeo yake akabakia kulekule Brazil kama mkimbizi kwa miaka miwili. Jana amerudi kwao na ameitwa na Waziri Mkuu ameambiwa njoo nyumbani hata kama uliikosoa nchi yako ukiwa nje, rudi nyumbani uje ujenge Taifa. On top of that akarudishiwa zawadi yake ya Olimpiki ambayo alikuwa apewe ya dola 17,000, look at that level. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi hapa Profesa Assad amekwenda nje na amesema maoni kuikosoa Serikali, tunasema uzalendo, hautakiwi ukosoe nje ya nchi. Utakosoaje ndani ya nchi wakati hakuna nafasi ya kukosoa? Utakosoaje ndani ya nchi wakati uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujikusanya haupo kabisa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tukisema utawala bora tutizame na mengine. Utawala bora siyo maneno tu, utawala bora lazima uendane na haki, usawa, uadilifu na imani, lazima uendane na Katiba na sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza mifano ya kuonesha kwamba we still have a lot to do katika utawala bora. Nianze na uhuru wa kujikusanya, uhuru wa siasa. Kwa mujibu wa Katiba ya nchi hii na sheria, hakuna mwenye uwezo wa kusema kwamba nasimamisha siasa mpaka wakati wa uchaguzi, hakuna kisheria wala kikatiba. Kwa mujibu wa sheria hakuna mwenye uwezo wa kusema kwamba nasimamisha siasa mpaka wakati wa uchaguzi, hakuna kisheria na kikatiba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vyama vipo kufanya siasa wakati wowote. Hata kauli ile itoke juu kiasi gani, ni kauli batili, haramu, mutlaq. Hata kama imetoka juu kiasi gani, huwezi kuwazuia wananchi wako wasifanye siasa eti kwa sababu wajenge nchi. Nchi ni pamoja na kufanya siasa na kukosoa ndiyo kujenga nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi vyama vingine vya siasa haviruhusiwi kufanya mikutano na Polisi mpaka sasa wanashindwa hoja. Hoja yao ni simple intelijensia. Intelijensia yenyewe haionyeshi kama ya kisayansi ya kisasa. Aah, maana yake Chama cha CUF kitazuia vyama vingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano uliotolewa, CUF watazuia ACT wasifanye mikutano. Hivi CUF ni chama cha fujo? Hivi huoni kwamba unakiweka pabaya Chama cha CUF kwamba ni chama cha fujo kinataka kuzuia mikutano ya vyama vingine? Au mnataka kukifuta na CUF vilevile! Kwa sababu kama chama kinafanya fujo kila siku za kuzuia mikutano ya vyama vingine nacho kifutwe? Siamini kama CUF wanafanya hivyo. Hawafanyi hivyo kwa sababu ni their interest vile vile na wao wakifanya mikutano yao wengine wasitumike kuwazuia. Hilo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni jambo ambalo sioni kama linaendana na utawala bora, nalo ni taasisi zetu za kiulinzi kupokea zawadi. Jana nimeona Polisi wanapokea vifaa gani sijui kutoka NMB. Mara utasikia wamejengewa vibanda, mara sijui vitu gani how can you do that? Mtu ambaye anakuzawaidia utawezaje kum-counter? Utawezaje kum-check akifanya makosa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taasisi ya Polisi au Jeshi ama wengine wanawekewa vote; kwa nini waende wakajidhalilishe kwa kupekewa vibanda viwili, vitatu vya kujengwa barabarani? Huo siyo utawala bora, kwa sababu huyo ambaye amekuzawadia huwezi tena kumkagua. Kwa mujibu wa sheria yetu ya rushwa, anayepokea na anayetoa wote ni rushwa. Kwa hiyo, Polisi nao wanapokea rushwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni Miswada; tunakuja hapa ndani ya Bunge letu, Miswada mingi utaona hata haitoi fursa nyingine za kisheria. Unashangaa wanasheria wetu wanaoleta Miswada Bungeni wanayo dhana ya utawala bora ndani ya akili zao? Kama hawana, kwa nini basi muwaache walete Miswada kila siku. Ndani ya Kamati yetu ya Katiba na Sheria tunasema mbona hapa hakuna fursa ya rufaa? Mbona hapa hakuna kitu gani? Utawala bora bado haujaingia katika akili zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo nataka kulisemea ni suala la TAKUKURU. Watu wanashitakiwa kwa very grievous offences kwa mfano utakatishaji fedha au uhujumu uchumi, lakini wanatangaziwa dunia nzima, wanahukumiwa kabla hawajafika mahakamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana nimeona kesi moja, mama mmoja anashitakiwa, anapelekwa mahakamani, TAKUKURU wanatoa Press Conference. Tayari umeshamhukumu mtu yule katika public. Kwa hiyo, huu siyo utawala bora. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni muundo wa kuhoji watu hadharani. Umekuwa mtindo sana katika nchi yetu ya Tanzania kwamba Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa anaweza kuwaita watu akawahoji katika hadhara na hata mkuu wetu wa nchi anafanya. Kusema kweli taratibu za kumhoji mfanyakazi zipo; taratibu za kumkosoa mfanyakazi zipo, zimewekwa kisheria. Sasa kwa nini umwite hadharani, uende ukamuue kwa pressure na kitu gani, unamdhalilisha mbele za watu ajibu maswali papo kwa papo wakati ungeweza kuwa naye ofisini? Huu siyo utawala bora. Siyo utawala bora kabisa kwa sababu humtendei haki mfanyakazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati mwingine, juzi nimeona, nafikiri Mkuu wa Mkoa wa Iringa, anamwambia mtu wa benki aende akafungue benki aje na nyaraka siku ambayo siyo ya kazi. Aende akafungue achukue nyaraka wakati ambao siyo wa kazi. Anamwambia wewe si ndio Meneja bwana, nenda kafungue lete nyaraka hapa. This is not utawala bora. Jamani, utawala bora deserves more than that. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine kwangu mimi, utawala bora ni financial governance. Ripoti ya CAG inaonyesha kwamba utawala bora is far from dream to us. Madudu ambayo yanaendelea ndani ya Serikali katika upande wa fedha yanatisha. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante nitazungumzia mambo matatu kwanza kuhusiana na mikutano ya kisiasa, pili kuhusiana na Mashekhe ambao wapo jela sasa, ramadhani sita wapo jela, kisha nitazungumzia juu ya ajira ya askari wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sote humu tumeapa kuheshimu katiba pamoja na viongozi ambao hawapo humu ndani, na katiba yetu maeneo mengi inaeleza juu ya haki, usawa, uwadilifu, ya namna ya ku- treat haki za watu na mambo mengine. Lakini pia inatupa fursa ya namna ya kujikusanya kujieleza, kujiunga, uhuru huo umetolewa, lakini pia nchi yetu imejiunga na mikataba mbalimbali imesaini mikataba mbalimbali ya kimataifa juu ya haki ya kujikusanya na kujieleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia mwaka 92 kwa hiari yetu tulikubali kwamba tunaingia katika mfumo wa vyama vingi, na CCM kwa nafasi yake iliyokuwa ilikuwa inaweza kukataa kutokuingia katika vyama vingi. Kwa sababu kwanza wale walisema wanataka vyama vingi walikuwa ni kidogo 20 percent lakini ikaonekana busara kwamba 20 percent hawa wanaweza wakawa wamenyimwa haki yao kwahivyo tuwape haki na tukakubaliana tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi. Lakini seven year on haionekani infact it is even going to the extreme. Kwamba CCM sasa wanakataa kilekile ambacho wao walituingiza ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa unashangaa nchi hii kwamba inaamini katika demokrasia, inaamini katika siasa za pluralism kwa sababu haielekei kwamba inaamini hivyo kwa matendo, ndani ya katiba ndani ya sheria tunasema kama tunafuata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema tutazungumza habari ya mikutano ni simple logic it doesn’t need Ph.D au rocket science, kwamba ili mtu afanye siasa lazima aweze kuchanganyika na watu, ili mtu afanye siasa lazima aweze kujikusanya na watu, aweze kuzungumza na watu, aweze kupiga propaganda na sera zake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tumesema mara nyingi kama mnahisi hamuwezi bado mna-majorit just call it off semeni tu mnazo kura za kutosha humu za kusema kuanzia leo hakuna vyama vingi basi tujuwe hakuna vyama vingi tusisumbuane tusitaabishane tusipatishane tabu, kwamba mnataka vyama vingi inaelekeaje mnataka vyama vingi mtu mmoja anasema siasa msimu mpaka msimu mnataka vyama vingi lakini bado hamruhusu watu wafanye mikutano, mnataka vyama vingi lakini bado mnakuja na excuse lame excuses intelligentsia sijui kitu gani kitu gani jamani kama intelligentsia umeipata si ndiyo wewe wakuifanyia kazi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa you’re a failure ukiwa na intelligency you’re a failure sasa kama Waziri unakubali uitwe failure is horrible kama unakubali uitwe failure kila siku unakubali polisi wako wakuwa intelligentsia you don’t question kama intelligentsia kwanini usiwape wape opition. Juzi ulisema hapa katika kujibu swali moja ulisema kwamba kama mkutano leo haufanyiki unakuwa kesho kutwa ufanye nafikiri ilikuwa katika briefing hebu nikuulize, siku gani upinzani walipewa siku mbadala ya kufanya mkutano? Hata siku moja! (Makofi)

Mheshimiwa mwenyekiti, sitaki kuzungumza habari ya CCM wala nazungumzia kuwakilisha wapinzani kwahiyo kama mnahisi hamuwezi call it off. Leo leteni Muswada na sisi tutaunga mkono tutafanya kazi nyingine siyo lazima kuwa wapinzani si lazima kuwemo humu ndani hatukuzaliwa kuwa Wabunge wa upinzani tumezaliwa tuishi tu kuwemo humu ni coincidence tu, kwa hiyo, siyo lazima tubakie humu kama hamtaki wacheni semeni hakuna vyama vingi katika nchi hii mtakutana nao mabwana wa dunia (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni kuhusu mashekhe nimesema hapa kwamba hii ni ramadhani ya sita its six ramadhan they are spending in lockup hata kesi haijaanza kushughulikiwa six years shame on this country, shame on our system. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnatuambia tusiseme nje, tunaitukana nchi yetu humu ndani shame kwa nchi yetu, shame kwa Serikali zetu kwamba miaka sita mtu anachunguzwa hata kesi aijaanza jamani fikirini hata kesi haijaanza fikirini jamani wale binadamu kama sisi next it could be you, it could be mwanao, it could be mtu mwingine, jamani watu wanasema sheria haina huruma miaka sita inatosha jamani, inatosha, inatosha, inatosha miaka sita. Waamulieni kama wana makosa waukumuni hakuna mtu anayesema anaunga mkono ugaidi, nataka kama ugaidi miaka 50 mia 200 wafungwe lakini wawe wameukumiwa kesi i-move, kesi haija-move mnataka nini tuambieni halafu mnasema mna tunza haki nyie watetezi wa wanyonge ninyi its rubbish, hamfanyi chochote kwa haki ya nchi hii. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ally Saleh unayemwambia rubbish ni nani? Hebu mimi nakuheshimu sana hebu tumia ile lugha ya Kibunge tu, futa hiyo kitu.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni aibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ya mwisho namalizia juu ya habari ya kichakaa, kichakaa ni kama utani kule pemba kuna msemo mmoja umesema uchumi wa mudu, uchumi wa panga, panga hutumika kwa kukatakata vitu vingi kulima kufanya nini lakini mwisho hutupwa lisionekane mpaka msimu ujao. Ni sawa sawa na hawa polisi wetu manawatumia katika uchaguzi, mnawatumia katika operation, mnawatumia kuzuia mikutano yetu lakini vyeo vyao hamuwapi haki zao hamwapi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, polisi wa nchi hii wanatumika vibaya wanatumika visivyo lakini haki yao basi minimum wapeni haki zao, wapandisheni vyeo kwa wakati sio kwa kuwa hawana pa kusema, sio kwa kuwa wanapiga salute hawa mabwana wanaitikia mkaona hawasemi wanatuambia mnawafanyia vibaya hamuwapi haki zao hata tukisema mara nyingi polisi wa nchi hii wana lala pabaya hawana mahali pa kulala hawana matunzo mengine yanayostahiki askari jamani vibayeni wanasema wapemba vibayeni, vibayeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kweli sehemu yangu kubwa ya mchango wangu utakuwa ni kuhusu bandari ya Bagamoyo ambayo umeitaja hapo. Lakini kwanza nitapitia in passing tu. Kuhusiana na ATCL nakubaliana 100 kwa 100 na mchango wa Mheshimiwa Kapteni Abbas Mwinyi wa wiki iliyopita ametusemea wengi na amesema mengi na amesisitiza yale ambayo opposition tumekuwa tukisema lakini Serikali ilikuwa haitusikilizi naamini kwa kuwa yametoka kwao sasa labda pengine utasikiliza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili ni kuhusiana na reli nakubaliana na wengi ambao wanaosema kwamba reli ni muhimu lakini haiondoshi kuwepo na taratibu nyingine za usafiri. Marekani mizigo mingi inasafirishwa kwa magari makubwa hata kuliko reli, reli ni ya pili, pia kutegemea reli kwa abiria ni makosa makubwa sana, reli ni mizigo, yupo mtu alisema hapa kuna haja ya kuwa na drive ports kila baada ya eneo ili kurahisisha mizigo kuwa collected ili kwenda sehemu nyingine ya nchi au nchi jirani. Kwa mfano kuwa na drive port Dodoma au kuwa na drive port Morogoro ili mizigo inatuliwa pale kisha reli inabeba. India mizigo ni 80 percent ya reli inatia faida kwa 80 percent. Abiria ni less labda 15 percent, mizigo mingine midogo ndio percent iliyobakia, kwa hiyo tusijidanganye reli ni mizigo bila mizigo hakuna reli itakuwa hasara tupu.

Mheshimiwa Spika, la tatu nataka kuzungumzia juu ya suala la mabaharia, nchi yetu mwaka jana tuliridhia mikataba miwili Maritime Law Conventional na Seafarers ID. Lakini hatukwenda mbali zaidi kuleta sheria kuibaidilisha ile sheria ya meli ili iweze kufaidika. Kwa hivyo kwa maana nyingine tumeridhia conventional lakini hali ya mabaharia wetu 5,276, iko mbovu vilevile bila kitambulisho, bila sheria ya kupitishwa hapa haiwezekani mabaharia wetu wakafaidi malipo mazuri ambayo wanaweza kulipwa na wanaendelea kupunjwa kwa sababu tu kwamba sheria haikufuatiliwa domestication I mean mkataba wa Kimataifa hawakufuatilia domestication ya sheria ili mabaharia wetu wawe na hadhi kamili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya hayo nakwenda kwenye Special economic zone ya Bagamoyo, na naanza kwa kusema kwamba tunafanya makosa kama Bunge na kama nchi kuachia miradi mikubwa kama hii ikafutwa bila kuwepo na public discussion. Vilevile nataka nikushawishi hata wewe kwa nafasi yako unaweza kuunda vyombo au kuunda namna ambayo ya kuweza kuchunguza kwa nini kama nchi tunaacha mradi huu ambao tutauelezea leo hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mradi huu kwanza tunaondokane na dhana kwamba ni bandari, ni zaidi ya bandari ni mji, ni ajira ni kufunguka kwa uchumi wa Tanzania. Kutakuwa au kungekuwa na viwanda 800 ambavyo tayari viko pale pale katika eneo kwa hivyo mzigo unachukuliwa unatiwa katika meli unapelekwa nje au mwingine unatoka pale unakwenda Silama unaunganishwa na reli hii mpya ya SGR inakwenda kwingine inakwenda kuuzwa. Pia utajenga Mji wa Kisasa Bagamoyo kwa maana mbili, kwa maana ya kupata watu kuishi lakini pia Dar es Salaam itapumua, Dar es Salaam ikipumua watu wanakwenda kule kuishi Bagamoyo kwa hivyo nchi inatononoka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu kutakuwa na logistic la tan trade ambayo itafanyika itakuwa kubwa sana bandari ya Bagamoyo kama ingejengwa au kama itajengwa itaweza kuchukua makontena milioni 420 kwa mwaka. Sasa hivi bandari kubwa duniani Rotterdam inachukua milioni 11.87, kwa maana nyingine bandari ya Bagamoyo ingebakia kuwa kubwa pengine kwa miaka 100 ijayo kwa Dunia nzima. Rotterdam wanaingiza meli 3,613,315 kwa mwaka kwa maana ya meli 110, hapa ndipo unaweza kuona suala la locally country linaweza kuwa pana. Imagine meli 100 zinakuja kwa siku wanataka maji, wanataka matunda, wanataka toilet paper, sijui wanataka kitu gani imagine faida ambayo ingepatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia Bandari hii au eneo hili lingeweza kuzalisha ajira zaidi ya 120,000. Eneo la Dar es Salaam kusema una forfeit kule ambako mkopo unatoka China na Oman marafiki zetu wakubwa tuseme pia suala la demokrasia katika hili wanatuunga mkono katika mambo mengi lakini unasema na kuna Dar es Salaam, tayari kuna Banana unatka uje na fourth generation meli ambazo ni kubwa zinashusha zinapakia wenyewe haziwezi tena kuingia Dar es Salaam, pengine kina cha bandari cha Dar es Salaam kitagoma kupokea meli hizo za fourth generation na tukaenda itakuja fifth na sixth generation. Meli moja ya sasa inaweza kuwa na tani milioni 100 inaleta mzigo wa tani pengine milioni mbili, pengine Dar es Salaam isiweze kubeba tena. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa pale Dar es Salaam pameshajaa...

SPIKA: Mheshimiwa Ally Saleh bahati mbaya dakika saba zimeisha.
Azimio la Bunge la Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC na kuendesha vyema Mkutano wa 39 wa Jumuiya hiyo
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nataka kwanza kusema kwamba siyo tatizo kuona fahari kuona fahari kwamba Rais wako anakuwa Mwenyekiti wa Jumuiya kubwa katika Kanda au popote pale. Hiyo siyo issue, kwa sababu ni rotationally. Vyovyote vile angekuwa mwingine yeyote angeweza kuwa Mwenyekiti kesho, kesho kutwa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninachotaka kusema you should not politicize the issue, twende sober mind, tutazame nini tumshauri Mheshimiwa Rais wetu katika hicho kipindi anachokuwa Mwenyekiti, tutafanya nini kama Tanzania? Cha muhimu, tufanye ili legacy yake iwe na maana zaidi na siyo kumpongeza wakati baadaye hatafanya kitu cha maana, ili legacy yake ikumbukwe zaidi ya kuwa Mwenyekiti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, sisi ni member wa SADC, lakini katika mkutano ambao ni wa mwisho kabla Mheshimiwa Rais kuwa Mwenyekiti Serikali yetu imeshindwa kupeleka Wabunge kwenye Mkutano wa SADC uliokuwa Mozambique. Vile vile sisi tukiwa Wabunge wa SADC tumeshindwa katika mikutano mitatu kuhudhuria katika mikutano ya SADC. Picha hii haiwezi kuwa nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi tuna mkutano hapa kwetu, lakini kuna utamaduni wa SADC wa kukaribisha NGOs, tunaambiwa kwamba wana-NGOs wengi walikuwa harassed walipokuwa Dar es Salaam; wakasachiwa wakapekuliwa wakafanyiwa kila kitu. Sisi kama SADC tuna itifaki ya kufanya election observations, lakini katika mikutano uchaguzi kibao hatuendi, tunacha legacy gani kama Taifa? Kuna Model Laws na visions za SADC ambazo zinataka nchi zifanane kwa kadri inavyowezekana. Kama nchi hatufanyi vizuri katika hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hivi SADC inajengwa kuwa Bunge kamili baadaye. Tungeomba Rais wetu asaidie watakaokuja baadaye katika Bunge lingine walikute Bunge la SADC limekaa sawa sawa, role yake iwe nzuri hiyo.

Mheshimiwa Spika, cha pili, nakuja kwenye uwekezaji. SADC ina watu karibu 370 wengine wanasema 350 jumla yake, wana GDP ya milioni 6.07 kwa pamoja, lakini pia SADC inasemekana kwamba ina-perform low by 25 percent ya uwezo wake, kwa maana bado biashara miongoni mwetu iko ndogo sana. Kwa mfano, Tanzania tunafanya vizuri na South Africa pengine na Democratic Republic of Congo, lakini sisi kama Taifa hatufanyi vizuri na nchi nyingine. … Katika hili tulifanye vizuri.

Mheshimiwa Spika, pia kama zone hii kuna tatizo kubwa la zone phobia South Africa. Hii inafanya kusiwe na uzuri wa nchi nyingine kushiriki baina yao pamoja. Tungemshauri Rais wetu hili alisimamie vizuri ili zone phobia na kufungua mipaka kuwe kuzuri na kwa Mataifa yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, pamoja na kusema kwamba tumefurahi kwamba Rais wetu amekuwa Mwenyekiti wa SADC, ni mwaka mmoja tu, lakini muhimu legacy gani ataacha ili tuje tufurahi kama Watanzania ametufanyia chema kwa ajili ya nchi yetu?

Mheshimiwa Spika, ahsante sana Mheshimiwa Spika.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwanza kabla ya yote napenda kwa mara nyingine tena ku-register kwamba bado sioni mantiki ya kutengeneza mpango wetu bila ya kuwa na connectivity yoyote ile na Zanzibar, bado akilini mwangu nataabika. Unawezaje kutengeneza uchumi wa nchi pasiwe na connectivity, hiyo bado najiuliza, na kwanini kila mara hili halifanyiki? Napenda iwepo on record.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili na katika mpango umezungumza…

SPIKA: Connectivity gani Mheshimiwa Ally Saleh, kwa dakika moja tu ili akupate vizuri.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano wakati ule wa mpango wa mwanzo kulikuwa kuna miradi kielekezi, na tulisema angalau mradi mmoja ukiwekwa Zanzibar utasaidia kazi, utasaidia ajira, utasaidia kila kitu. Si kila kitu kiwekwe huku, hata kama cha muungano kikiwekwa kule kinaweza kikasaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano Bandari ya Bagamoyo.Unaweza ukawa na Bandari ya Bagamoyo lakini kuweko na connectivity; kazi fulani inaweza kufanywa Zanzibar; kwa mfano namna ya ku-repair au ya kufanya vitu gani hiyo ndiyo connectivity ambayo nazungumzia lakini huu mpango tunachoambiwa ni kwamba Zanzibar wanampango wao lakini at the end of the day hii ni nchi moja hakuna connectivity, hilo la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni kuhusu dhima; dhima nimeipenda kwasababu inaelezea juu ya kuongeza mauzo ya nje na uwezo wa ushindani, hii ni dhima nzuri sana kwa nchi kujiwekea kwasababu hapa nikieleza itaonekana kwambanaiunga mkono kwasababu gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevie tumechagua maeneo matano ya mkakati ambayo mimi nitataja matatu ambayo yamenipendeza; nayo ni uchumi wa viwanda, uchumi wa watu na uwezeshaji biashara na uwekezaji, na ninataka nianzie hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ningependa kuungana na Mheshimiwa Ally Keissy, Mheshimiwa Wilfredy Lwakatare na Mheshimiwa PeterSelukamba,nafikiri na mmoja mwingine yoyote ambaye amesema. Kwamba kuwepo sisi hapa kama nchi coordinance kadhaa mpaka coordinace kadhaa Mwenyezi Mungu ametaka tuwepo na fursa zimetuzunguka. Kwa mfano amezungumza Mheshimiwa Lwakatare juzi, wanasema walipo wao kuna fursa mpaka South Sudan; leo Mheshimiwa Ally Keissy anasema kwamba tunapakana na moja katika nchi tajiri Afrika ingawa per capitalyake ni dollar 627 lakini wana strength ya watu na pia wanautajiri wanchi.

Kigoma tunapakana na nchi nyingine nyingi pale, pamoja na Kongo je tunazitumia vipi fursa ya uwepo wetu katika maeneo hayo? Kama nchi tunajielekeza vipi maeneo yaliyo pembezoni kwa jina tu lakini ndiyo ambayo yalitu- open up.Kwahivyo bado nahisi hata kama tutatekeleza maeneo ya kilimo, maeneo ya deep sea, uwekezaji, biashara elimu, nishati na LNG inparticularna energy mix, kama alivyosema Mheshimiwa Selukamba bado tunataka outs tunataka tutoe vitu vyetu. Umesema hapa China, lakini it is not only China, kuna nchi nyingi. Urusi per capital yao 24 thousand per person, Uchina yenyewe ni per capital yao 16,000 lakini Uturuki per capital yao ni 26. So, it is not only China. Nakubaliana na mtu aliyesema nikutafuta new markets; kama tunavyotafuta new market kwenye utalii, basi tutafute new market kwenye uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Uturukiis so strategicallylocatedkwa Asia na Europe. Ni njia ya kuingia Europe kirahisi, ni eighthoursfrom Dar es Salaam. Uturuki wanaleta ndege mbili kila wiki, wanaleta ndege tatu kila wiki lakini almost nothing leaves here to go to Turkey kwasababu hatujajitayarisha kibiashara. Pia Uturuki na kama viletunavyokaribisha Urusi, wanauwezo mkubwa sana wa kuwekeza,the money is there forthem wanachotafuta wao ni waziweke wapi. Ssasa mimi nafikiri kuna haja ya kutazama hili hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine; kwamfano tumezungukwa na bahari, kila siku tunasema; tunaambiwa kutakuwa na bandari ya utalii, bandari ya uvuvi.Issue si bandari ya uvuvi,issue ni kuwa na mipango kwanza kabla hujajenga bandari, watu hao wanaokuja kutuvulia ndio watakaotupa pesa ya kujenga bandari. Una uvuvi unaotoza kilo moja unaotoza dola 0.4 kwa kilo moja ya samaki, unawavunja moyo wanaokuja kutaka kuwekeza kwenye habari ya uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo issue si kuwa na mipango, lakini ni kupanuka, ni kutazama fursa mpya. Kila siku fursa mpya zinakuja,kila siku watu uchumi wao unaongezeka duniani; soko la Arabuni Qatar, Dubai pamoja na Oman. Tumefanya nini kama nchi? Kwahiyo mimi nafikiri kama ilikuwa mpango ule upo sasa haupo, kwamba pale mwanzo wa awamu hii walikuwa Mawaziri au safari za nje zilikuwa kidogo kwa watendaji mimi nahisi ni wakati sasa tupanue safari kwa watendaji ili waende wakatafute masoko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu gani utapeleka India kirudi, kitu gani utapeleka India kirudi kitu gani utapaleka China kirudi, kitu gani utapeleka Qatar kirudi, kwasababu wao hawalimi as such.Lakini bado, nchi kama Oman pamoja na kwamba wana utajiri mkubwa na wana gesi wana kitu gani lakini bado hawana kilimo cha kutosha na sisi tunaweza tukajazia mazao yao huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuzungumza hayo, kuna jambo moja ambalo limo katika mpango lakini limetajwa just in passing; kidogo tu limetajwa, nalo ni utawala bora. Dunia ya leo ni wazi kabisa huwezi kuwa na uchumi mzuri kama hujawa na utawala bora, nchi chache tu zimepenya; labda Indonesia zamani, zilizokuwa Tiger zile, walikuwa na ukandamizaji kandamizaji lakini bado wakapenya. Hata hivyo bado, ukiwa na utawala bora ndiyo unakusaidia kwenye uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili la utawala bora bado mimi nina wasiwasi nalo katika nchi yetu. Public space inazidi ku-shrink kila siku, fursa za maoni zinazidi kupotea. Tumetunga AccessTo InformationAct miaka kama 10 nyuma huko au saba nyuma mpaka leo hatujatunga kanuni. Kwa hiyo bado mwananchi hawezi ku-access information ambayo anaitaka kutoka Serikalini. Vilevile uhuru wa vyombo vya habari ambao umekuwa ukilalamikiwa sana. Kwamba vyombo vya habari vinaogopa kuandika, ingawa unaweza ukasema uhuru upo lakini watu wanaogopa. Pia mfumo wa mahakama; tuna mashekhe leo miaka saba wako jela hata kesi haijaanza. Kwahiyo hii inatutia doa kwa watu wengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hivi sasa imekuja hii issue ya Serikali za Mitaa; mimi nahisi hii ni aibu kwa taifa, kwasababu huwezekani unakata asilimia 96 ya wagombea;at least kwa chama cha ACT na CHADEMA asilimia tano; halafu anakuja Waziri na simple statement ambaye kabla yake alisema hakuna kilichobadilika…

SPIKA: Mheshimiwa Ally Saleh naambiwa muda hauko upande wako

MHE. ALLY SALEH ALLY: Ulinipa dakika 10 Mheshimiwa?

SPIKA: Yuko katibu anaangalia

MHE. ALLY SALEH ALLY: Nitaziona katika clip in shaa allah. (Makofi)

SPIKA: Anaangalia hapa maneno; ahsante sana Mheshimiwa Ally Saleh.
Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa FAO wa Kuzuia Uvuvi Haramu kupitia Bandari za Nchi Wanachama pamoja na Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Kuanzishwa kwa Ushirikiano wa Kimataifa wa Nishati ya Jua (The Framework Agreement on the Establishment of International Solar Alliance)
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mimi nitabaki katika hili suala la solar power agreement ambayo imesainiwa miaka michache tuliyopita, lakini nimefurahi kwamba nchi yangu ilikuwa katika nchi za mwanzo na leo hata muda haujapita sana linaletwa Bungeni turidhie. Kwa kweli tumekuwa tukipitwa na maazimio mengi ya kimataifa lakini hili limekuja haraka sana. Nitafurahi spirit hii ya kukipitisha maazimio haraka inavyowezekana ikiendelea.

Mheshimiwa Spika, la pili ni kwamba jana na juzi nilisema kwamba Mungu ameiweka Tanzania kwa makusudi yake. Katika mfano huu wa solar ni kwamba ametuweka katika maeneo kati ya tropical of cancer na tropical of Capricorn ambayo inatajwa katika mkataba huo na katikati inapita IKweta. Kwa maana tumewekwa kwenye sunshine state kama inavyotajwa, na kama anavyosema Narendra Modi wa India. Kwamba tuko katika eneo ambalo jua ni 12 seven, lakini tunalitumiaje? Jua liko wakati wote na liko takriban nchi nzima; sasa tunalitumiaje ndiyo muhimu; kwa hivyo tumekuwa katika pahala ambapo sasa hivi tuna fursa nzuri sana. Nchi ambazo jua si wakati wote kama Ujerumani bado ni katika nchi 10 duniani ambazo zinaongoza kwa solar.

Mheshimiwa Spika, nchi kama ya Norway jua ambalo si siku zote lakini bado inaongoza kwa solar, sembuse sisi ambapo asubuhi mpaka jioni jua.

Mheshimiwa Spika, kikundi hiki cha International Solar Power Agreement sasa hivi ni kundi kubwa la pili la nchi za Kimataifa zinazokutana baada ya Umoja wa Mataifa. Kwa hivyo ni eneo ambalo linakua haraka sana na nafikiri takwimu za mwisho labda kama signatories kama 121 tayari mpaka hivi sasa, kwa hivyo ni kundi kubwa. Hata hivyo si kundi kubwa kwa jina tu, ni kundi kubwa kwa dhamira; kwa sababu kuna mipango mingi ya kufanya ili kuiokoa dunia, linalofanywa hapa ni kujaribu kuiokoa dunia. Ndiyo maana wanataka tufanye kila njia ili tuache kutumia fossil energy badala yake tutumie energy ambayo ni renewable, kwa hivyo sisi tusiiache fursa hii.

Mheshimiwa Spika, nasema tusiiache kwa sababu nina experience, kwamba labda pengine kwa hii sasa kutakuwa na mabadiliko; na ningependa Mheshimiwa Waziri wa Uwekezaji anisikilize katika hili.

Mheshimiwa Spika, na narudia tena hapa Bungeni niwahi kupata ofa ya wawekezaji ambao wako tayari kuwekeza three billion dollar’s kwa ajili ya three thousands megawati za umeme nikataabishwa, nikasumbuliwa mpaka yule muwekezaji akakata tamaa. Hivi sasa nasema, pengine Mheshimiwa Waziri ananisikia, kwamba nina offer nyingine ya mtu ambaye yuko tayari kuwekeza vituo zaidi ya 50 vya solar kwa ajili ya magari, kwa ajili ya vyombo vya umeme, kwa pesa zake; I mean ni self financing. Kwa hiyo kama Serikali watakuwa tayari huu ndio mwanzo mzuri, tunaanza kidogo kidogo ku-phase kwenye petroleum tunaingia katika vitu vingine. Kwa hiyo ningependa baadaye nikae nizungumze na Mheshimiwa Waziri tuone tatafanya kitu gani.

Mheshimiwa Spika, lakini pia ni njia nzuri ya energy mix tunalalamika kila siku juu ya energy mix. Wengine tulisema sana hapa juu ya umeme wa Julius Nyerere; lakini kusema kweli tulikuwa na ushindani. Wengine tunasema kwamba umeme wa solar ni rahisi zaidi, wengine wanasema umeme wa maji rahisi zaidi, lakini namna ya uwekezaji wenyewe. Sasa hivi kumepatakana solution, hawa walioko mbele, kwa mfano India, wao wametenga three fifty billion dollar’s kwa ajili ya kuzisaidia nchi kufanya kazi hii. Pia World Bank wao wanatarajia kuhamasisha uwekezaji wa takriban bilioni 1000 mpaka kufikia 2030 ili nchi zote ambazo zina fursa zipo katika sunshine area ziweze kunufaika. Kwa hiyo sisi tusikae nyuma sasa maadam tulishaingia katika uwanachama huu na tuna fursa.

Mheshimiwa Spika, Dodoma peke yake hapa ikitumika, maeneo ambayo hayafai kwa kilimo, maeneo ambayo hayaoti miti basi tunaweza tukatoa megawati kwa mamia kabisa sembuse nchi nzima, kwa hiyo tutumie fursa hiyo kwa vizuri.

Mheshimiwa Spika, lakini pia sasa hivi kuna nchi; kwa mgano Venezuela, ambazo tayari zinaweza kufikia 100 percent sasa ya mahitaji yao. Kwa hivyo sisi tusiona kwamba Julius Nyerere kama tumefika kwa zile megawati 2000 na ushehe. Bado nchi hii kama tunataka kweli kwenda kwenye viwanda tuondokane na dhana, kama alivyosema Mheshimiwa Mbarouk, ya kuona umeme wa jua si umeme kitu. Umeme wa jua ni umeme kama umeme mwingine na unaweza kuuzalisha viwandani na unaweza ukatumika sehemu nyingine nyingi hata hapa Bungeni.

Mheshimiwa Spika, imagine hapa jua linalopiga kutwa nzima katika paa la nyumba hii na namna paa yaliyopo humu ndani kiasi ambacho pengine tukiweka solar tu humu ndani ya Bunge tunaweza tukakoa mamilioni ya fedha. Kama vile ambavyo tumeokoa karatasi kwa kwenda kwenye tablets na huku tunaweza tukaokoa pesa tukatumia renewable energy lakini pia tukaokoa fedha nyingi kwa kuitandika solar power eneo lote la Bunge au eneo lolote lingine ambalo umeme wake utakuja mpaka Bungeni. Kwa hiyo mimi nasema katika hili Tanzania tusikae nyuma…

SPIKA: Mheshimiwa Ally Saleh nilitaka kukubaliana na wewe katika eneo la Bunge kutumia solar power. Niliwahai kutembelea Bunge la Israel wanatumia 1005 umeme wao kwenye Bunge la Israel solar power. Endelea tu Mheshimiwa. (Makofi)

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, fahari kubwa kukubaliwa wazo langu. Kwa hivyo mimi nafikiri Bunge lioneshe mfano kwamba hiki kinawezekana na taasisi za Kiserikalia kwa mfano Mji wetu wa Mtumba utandikwe solar, inawezekana kufanya, ili Serikali iwe mfano na ili tuwe tunaweza kujiendesha wenyewe kidogo mpaka hapo ambapo wakubwa wa dunia watakapotuona na kuwekeza katika maeneo haya; kwa sababu umeme utaendelea kuhitajika kwa sababu tunasema tunataka Tanzania ya viwanda ahsante sana. (Makofi)
Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya pamoja ya ziada ya Nagoya – Kuala Lumpur kuhusu Uwajibikaji Kisheria na Fidia kwa Madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya Bioteknolojia ya Kisasa katika Kutekeleza Itifaki ya Cartagena (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety) pamoja na Azimio la Kuridhia Itifaki ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika kuhusu Kulinda Haki Miliki za Wagunduzi wa aina mpya za Mbegu za Mimea. (Protocal for Protection of New Varieties of Plants (Plant Breeder’s Rights) in The Southern African Development Community – SADC) pamoja na Azimio la Kuridhia Mkataba wa Marrakesh wa mwaka 2013 unaowezesha upatikanaji wa kazi zilizochapishwa kwa watu wasioona, wenye uoni hafifu au ulemavu unaomfanya mtu kushindwa kusoma (The Marrakesh Treaty to Facilitate Access to Published Work For Persons Who Are Blind, Visually Impaired or Otherwise Print Disabled)
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Jana tulipokuwa katika mafunzo ya watu wanaoshiriki katika Mabunge mbalimbali ya Afrika, tuliambiwa kwamba nchi yetu inachelewa kuridhia mikataba. Kwa mujibu wa viwango vya mikataba hii ambayo imeletwa leo hapa lakini specifically huu wa Marrakesh haujachelewa kabisa kulinganisha na mikataba mingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba huu ni muhimu sana kwa sababu unakwenda kusaidia kundi kubwa la watu wetu. Maelezo yanasema kwamba watu wasioona, wenye uoni hafifu na ulemavu wa kusoma (print disabled) na hawa baadhi ni wale ambao kwa lugha ya kiingereza wanaitwa Dyslexia ambao wanaona sawasawa, wana intelligence sawasawa lakini ni slow leaners. Wale ambao kwenye shule tunasema mbona huyu haelewi, mbona huyu anachelewa kuelewa, nao wamekuwa considered katika mkataba huu. Kwa hivyo, mkataba huu unakwenda ku-cover kundi kubwa katika jamii ambalo hivi sasa linakosa fursa ambazo wangeweza kuzipata kwa kuwa mkataba huu umechelewa kuja kidunia lakini sasa hivi tayari upo na ndani ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo mengi ya kufanya kama nchi. Mojawapo ni kama ilivyosema hotuba ya Kambi ya Upinzani na hotuba ya Kamati kwamba kuna haja sasa kutengeneza sheria kwa haraka kuhusu copyright. Hilo liende sambamba na kuwaambia watu wetu wa ndani kwa mafunzo, maelezo na semina juu ya umuhimu wa kutengeneza kazi hizi na wao wajue kwamba kazi zao zinaweza kukuzwa ili watu kama hao waweze kuzitumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kingine ni namna ambavyo tunaweza kuwa na kanzi data ya uhakika ili wale ambao wanafaa kupewa hizo kazi ambazo zimekuzwa na siyo kutafsiriwa, kutafsiriwa haimo katika hili, ni kukuza maandishi ili waweze kuona basi kuwe na uhakika kwamba wanaopewa ni watu sahihi. Tunaomba pia taasisi ambayo itahusika na labda wengi wetu tunafikiri ni kama Chama cha Watu Wasiiona au Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) ambao wao ni authorized kwa mujibu wa mkataba huu ili na wao waweze kutumia vizuri nafasi hiyo na wasiitumie vibaya kiasi kuweza kuathiri vibaya mkataba huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nafikiri kuna haja, kwa sababu tumechelewa kuingia katika mkataba huu ingawa siyo sana kama watu walivyosema kwamba zaidi ya nchi 70 zilishajiunga, ya kwenda kujifunza kwenye nchi nyingine wamefanya nini hadi hivi sasa. Moja ya nchi hiyo ni Australia ambayo iko mbele sana katika mkataba huu. Naishauri Serikali ikafanya utaratibu, sidhani kama Afrika tumekwenda mbele sana lakini kama ziko nchi zimekwenda mbele sana basi pia tujifunze kwenye nchi za Kiafrika nini wao wamefanya japokuwa tumechelewa kujiunga lakini tusifanye makosa yale tukafanya vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ni haja sasa ambapo tunasema mara kwa mara kutengeneza kanzi data. Kila siku tunaambiwa kuna kanzi data lakini jambo kama hili sasa unakuja umuhimu sana kuonesha kwamba ili tuweze kufanya makisio, ili hiyo kazi ichapishwe kwa haki ya kukuza vya kutosha ni muhimu kuwa na kanzi data juu ya watu wasioona, wenye uoni hafifu na wale ambao wana print disabled.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, ingawa katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri halikuwemo kuhusu suala la Marrakesh, ametuambia hapa kwamba Zanzibar imeshirikishwa lakini ingependeza katika Waraka huu rasmi wa Bunge na record zikaonesha kwamba Zanzibar ilishirikishwa. Hata hivyo, ukisoma Waraka huu hamna maandishi hayo kwamba Zanzibar ilishirikishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, mimi leo nitajikita katika mfungamanisho wa uchumi wa Tanzania (Tanzania na Zanzibar) na Inshallah tutaelewana, leo nitakuwa mtaratibu sana katika kujieleza. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, naanza kwa misingi minne, kwamba tatizo la Muungano ninavyoona mimi hasa ni uchumi mwanzo, siasa na madara yanakuja baadaye. Msingi wa pili kwamba fiscal and monitory policy za Tanzania au za Bara zina direct impact za Zanzibar bila ya Zanzibar kuwa na nafasi ya kujitetea au kupata afua yoyote. Tatu, kwamba Zanzibar imekuwa ikipunjwa katika Muungano na nne kwamba Serikali ya Muungano haifanyi afua yoyote Zanzibar. Haina investments, haifanyi capital investments, haifanyi fidia wala haina afua aina yoyote, imeicha Zanzibar kama ilivyo lakini bado chumi hizi zinaambiwa zimeungana.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa Tanzania Bara inakula mikono miwili, inakula mkono wa michango au kodi ambazo au uwekezaji ambao unafanywa kwa upande wa Tanzania Bara peke yake kwa sababu Tanzania Bara kuna Tanganyika na upande wa pili ni ule ambao Serikali ya Muungano inatumia fedha ambazo zinazalishwa na taasisi za Muungano ambazo Zanzibar nayo ina sehemu yake na ndiyo hapo Zanzibar inapopunjwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikizungumzia taasisi hizo, zenu za ndani ziacheni, TIB, sijui kitu gani, taasisi zenu zote za ndani. Mimi nazungumzia za Muungano, TTCL, ATCL, Bima na vingine vingi kama hivyo, TCRA na nyingine kama hizo. Sasa hizi ndiyo ambazo sisi Wazanzibar tunasema kwamba tunapunjwa kwayo, maana yake zile ni zetu sote, lakini hazitumiki kama zinavyotarajiwa na nitaelezea. Hii inatokana kwamba tumepuuza msingi wa Muungano ambao tumeutengeneza kwamba tuna nchi mbili, Taifa moja na kwamba tuna chumi mbili ndani ya nchi moja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tulikubaliana kwamba kwa mujibu wa Katiba kifungu cha 133 na 134 tutengeneze akauti ya pamoja na tume ya pamoja ya fedha. Sitaki kwenda kwenye historia kwamba muda mrefu hizi hazifanyiwa kazi, kusema kweli inasikitisha kwamba Marais ambao tangu limeamuliwa hilo, Mawaziri ambao tangu limeamuliwa hilo, Mawaziri Wakuu tangu limeamuliwa hili, Maspika tangu limeamuliwa hilo, Wabunge tangu limeamuliwa hilo tumeipuuza Katiba yetu. Kuwepo kwa taasisi hizo mbili za Muungano lakini kwa miaka yote sitaki kutaja miaka mingapi maana yake ni aibu kwamba nchi hii inaweza kupuuza Katiba kwa miaka yote hiyo na ndiyo maana tumefika hapa tulipofika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hali kadhalika taasisi nyingine ambayo imepuuza Kikatiba ni kuwa na Mahakama ya Katiba ambayo pengine Zanzibar ingeweza kwenda kushtaki kama inaona inaonewa, lakini baadaye tumekwenda kup-opt na kuwa Kamati ya Kero za Muungano ambayo kusema kweli ni nje ya Katiba na hata isingestahili kuwepo. Nimesema hapa kwamba tunazungumzia juu ya taasisi za Muungano ambazo mapato yake yanapaswa yagaiwe sawasawa, kwa bahati nilikuwepo katika Tume ya Warioba.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Tume ya Warioba tuliarifiwa, kwa sababu tulikuja mahali ule Muungano wa Serikali tatu tungeutengeneza vipi. Tukaarifiwa kwamba kwa mfumo wa Tanzania kama kungekuwa matumizi ya taasisi za Muungano kutumika kwa Muungano, basi zile fedha za kuanzisha Serikali ya tatu zingepatikana, zingepatikana fedha kwa Zanzibar na zingepatikana fedha kwa Tanganyika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wanaopinga Serikali tatu wapinge kwa mengine lakini wasipinge kwa kiuchumi, kwa sababu kiuchumi fedha tulizonazo zinatosha kufanya hivyo. Taasisi za Muungano zinawezakumudu kuwa na Serikali tatu.

Kwa hiyo Tume ya Warioba tuliambiwa kwamba iliundwa, ilipewa kazi (Pricewaterhousecoopers) ambao wao walihakikisha kwamba hilo linawezekana. Sasa kwa mnajili wa mgawanyo huo wa taasisi za Muungano mapato yanayokusanywa Zanzibar ni 2%, mapato yanayokusanywa Tanzania Bara ni 98%, lakini hizi zinatiwa katika kapu moja kwamba zote ni za Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jana ACT walitoa mchanganuo ambao pengine unaweza ukabishiwa, lakini tumepata mahali pa kuanzia. Wanasema 68% ya fedha ambazo ni za Muungano zinatumiwa na Tanganyika; 32% ndiyo zinatumika kwenye taasisi za Muungano proper. Labda Wizara ya Mama Samia, Wizara gani, za Muungano tu, 68% zinatumika na Tanganyika peke yake. Kwa hiyo, tunasema kwamba kama ingekuwa nchi hii inaendeshwa sawasawa basi Zanzibar ilikuwa ipate mgao wake kutoka 68%. Hesabu zilizotolewa ambazo zinaweza zikabishaniwa lakini mwisho nita-propose kama zinabishaniwa, basi Bunge hili liunde Kamati ifanye njia yoyote ile ya kuhakikisha ukweli uko wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa miaka saba wamefanya utafiti ACT wanasema kwamba 2414 mpaka sasa hivi kwamba kama ingekuwa fedha zile zimegaiwa labda kwa mgao wa formula ya 4.5 ambazo ni fedha Zanzibar wanazipata kutoka mgao wake wa Benki Kuu au mgao wake wa 11% ambayo inatokana na mgawanyo wa mapato ya kibajeti kutoka nje, basi Zanzibar ingepaswa kwa formula ya 4.5, Zanzibar ingepaswa ilipwe trilioni 4.6 kwa Serikali ya Tanzania kwa Zanzibar. Kama ikitumika formula ya mchango wa Zanzibar katika kuunda Benki Kuu yaani 11% basi Zanzibar inaidai Tanganyika hivi sasa 11.1 trillion shillings. Msitupe hizo, tupeni kile ambacho mnaona tutengeneze formula nyingine, lakini lazima tulipwe chetu, kwa sababu chetu kimo katika mashirika ya Muungano. Mimi sizungumzii 4.5 ambayo inatokana hivi sasa, sizungumzii fedha zile za kibajeti, nazungumzia haki yetu ambayo mashirika yale tumeyaunda pamoja na mengi yao yalitokana na Jumuiya ya Afrika Mashariki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo katika hali kama hii ungetarajia kwamba option zipi za Zanzibar, viongozi wetu kama nilivyosema kwa upande wa Tanzania hawajaheshimu Katiba kwa muda wote, viongozi wa Zanzibar hawajaheshimu Katiba lakini pia hawawezi kusema hadharani kama tunaidai Serikali ya Tanzania, wataishia pembeni tu. Hata juzi baada ya bajeti hapa kuambiwa kwamba 18% imeondolewa ya VAT kwamba eti tulitarajiwa tusherehekee. Wakati kitu kile tangu mwanzo hakikuwa halali kufanywa, hakikuwa halali kabisa kufanywa na katika hali kama hiyo basi, mimi nafikiri kwamba kuna haja kama tunasema kwamba uchumi wa nchi hii unataka uende sambamba na haki itendeke, kwamba lazima tufike wakati Zanzibar apate haki yake bila ya tone, bila ya shilingi kupungua. Kwa sababu kama sivyo ni kwamba uchumi wa Zanzibar sasa unadidimia, Serikali ya Muungano haiwekezi Zanzibar, haitoi afua ya aina yoyote ile, lakini fedha zote zile za Muungano zinatumika kujenga Tanzania Bara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, siku moja nilimsikia Dkt. Shein akisema surprisingly anasema ukienda Bara siku hizi utaona barabara zinajengwa, majengo yanajengwa, hamadi; nikasema kama yeye anasema hivyo nani mwingine wa kusema. Wakati yeye alipaswa aseme kwamba hizo fedha zilizojenga barabara na sisi zetu zimo, hizo fedha zinazojenga majengo na za Zanzibar zimo. Yeye anasema kwamba Bara kunaendelea zaidi, nani wa kusema hayo sasa kama yeye mkuu wa nchi hawezi kuyasema hayo. Kwa hivyo tunasema kwamba kama hamkutengeneza mazingira haya, Muungano utaendelea tu kama ulivyo lakini hatuna mapenzi nao. (Makofi)
Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya wa Mwaka 2017
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Sheria hii imekuja wakati mzuri sana na in fact imechelewa kupita kiasi kwa sababu tumepitisha sheria hii mwaka 1995, tukafanya marekebisho mwaka 2015 mpaka hivi sasa lakini bado tunakwenda katika hali ambayo mimi nisingefurahi kwamba inachelewa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ni sheria ambayo ni lazima iakisi mtazamo wa dunia. Tatizo la dawa za kulevya lazima utizame katika picha ya dunia na ni kitu ambacho ni uchumi na ni maisha ya watu hao ambao wanahusika na drugs. Kwa hivyo, ili kupambana na barons wale wakubwa wa biashara hii ni lazima uwe na sheria ambayo ningetarajia ingekuwa better zaidi kuliko ambayo imekuja hivi sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sheria hii inakwenda zaidi kwenye adhabu kuliko taaluma. Kuna baadhi ya wenzetu sisi ambao tunashiriki katika Bunge la SADC wanakwenda kwenye de-criminalization, mtazamo ambao badala ya kutoa adhabu kwa mkosaji/mtumiaji unatafuta njia ya kumfunza, njia ya kumtoa katika utumiaji kuliko kumfunga maana ukimpeleka jela anakuwa sugu na pengine anapata maradhi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wenzetu wengine vilevile wamekuwa wakitazama zaidi katika suala la elimu na suala la utamaduni kwa sababu uki-instill culture ya watu kujijua, kujitambua kutoka ujana wao na utoto wao unatengeneza mazingira mazuri ya mtu kutotumia unga kabla hajautumia lakini hilo linakosekana. Ni kweli tunasikia hapa na pale kuna elimu zinatolewa lakini nafikiri eneo hili lingetiliwa zaidi mkazo lingetusaidia sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesema pale mwanzo lazima uwe na global approach. Msemaji wa Kambi ya Upinzani amezungumzia juu ya utata uliopo kwa mfano baina ya sisi na Kenya kuhusu suala la mirungi. Kama tukichukua joint effort wao kwao mirungi ni halali, lakini pia SADC wanasema effort to fight against drugs is hampered by lack of legal uniformity. Kwa hiyo, hili pia Serikali ilitazame vipi tunafanya kazi na wenzetu otherwise effort yetu itakuwa haina nguvu kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa naona kuna pendekezo la kufanya suala hili la drugs kuchukua ushahidi kwa njia ya online au ya mitandao, lakini pia ningependa sheria hii itazame kipengele kidogo cha kutizama namna ya kupata supply ya drugs kupitia mitandao. Hivi sasa Tanzania si ajabu kupata supply ya sex kupitia kwenye mitandao. Tunaona makundi mbalimbali kwenye mitandao yanatangaza njoo utapata huduma hii, na sasa naona pengine tunaweza tikaelekea huko sasa ikawa mpaka si tu sex, lakini mpaka unga unaweza ukapata kupitia online, ningependa hili litazamwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeona hapa pembeni kuna pendekezo la kuifanya sheria hii iende mpaka Zanzibar; nafikiri hii si sahihi. Jana tu hapa tumetoka kuukataa muswada ambao umesema ufanye kazi Zanzibar wakati jambo hilo si la Muungano.

Kwa hiyo, pamoja na ukweli, na mimi ni muathirika wa matumizi ya unga kwa maana ya watoto wangu, watoto wa ndugu zangu wengi watatu/wanne wameingia hii, lakini bado sioni uhalali wa Kikatiba/wa kisheria jambo hili kulipeleka Zanzibar kwa sababu kule tuna taasisi yetu na mipango yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependekeza kama sheria itaweza kusema kuwepo na joint commission ambayo inaweza ikafanya kazi, ili ifanye kazi kwa pamoja, kwa sababu nakubaliana na hoja kwamba, huwezi kupigana na hiki kitu bila kuwa inclusive sote, lakini haina maana kwamba, ulazimishe sheria ambayo kitu ambacho si cha muungano ukipeleke kwenye mambo ya muungano.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mwisho…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 5) wa Mwaka 2017
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Juzi hapa tulisikia kwamba wanasayansi wa Kenya wamegundua satellite, sasa hivi Kenya wametengeneza satellite yao wenyewe ambayo ita-serve madhumuni yao na si kutegemea satellite za nchi za magharibi ambazo zimetawala anga zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania hatufanyi haki ya kuweka pesa katika research, nazungumza hapa haja ya kuweka pesa kwa ajili ya maprofesa kuwaweka kwa muda mrefu, maprofesa hawa ambao haki yao ya kwenda sabbatical ni ndogo, mazingira ya kuweza kufanya kazi madogo, mazingira ya kuongeza sayansi ya kisasa mdogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hata kama tutaunga mkono kwamba tuongezee muda wataalam hawa, lakini kama alivyosema Mheshimiwa Mollel, kama package ni ndogo basi hali kadhalika wataondoka, au watabaki katika madaraka kwa kuwa tu wanajua kuna kitita kinawasubiri na kwa hiyo matokeo yake watabaki ilimradi wabaki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesoma Wage Bill tuliyoletewa na Serikali ambayo inaelezea kwamba 2.9 billion wanalipwa maprofesa wakubwa, 1.8 wanalipwa maprofesa wadogo na 1.3 kwa jumla 5.5 billion kwa miaka miwili ni mkataba mzima wa wataalam hao. Unaweza ukaziona ni nyingi lakini after reflection ukizigawa unaweza ukaona zile package ni milioni tatu tu kwa kila mtaalam, wakati akienda Botswana anaulizwa how much does he or she want.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ingawa tunaunga mkono kwa maslahi mapana ya Taifa, kwa maana kwamba kuna ukosefu wa wataalam kwa asilimia 50 sasa hivi Tanzania; lakini pia viko vyuo kama UDOM hata profesa mmoja hawana. Kuna ukweli kwamba machapisho yameshuka Tanzania; labda pengine tungeweza kuchapisha machapisho 500, 600 kwa ujumla kwa maana ya nchi nzima, hatuwezi na huwezi sustain academic institutions bila machapisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tayari udororaji wa taaluma yetu unashuka, lakini je, tuna-address vitu hivyo?

Wengine tulihoji katika Kamati hii isiwe njia ya mkato tu ya kupata wataalam; kuna progam gani endelevu ya kupata wataalam? Ni kweli tulikuwa na gap ya miaka 10 ya kutoajiri, lakini tulisomesha? Kwa sababu kama tulisomesha na kama watu walisoma gradually wangeweza kupanda, kwa hiyo hata hii agreement you can’t buy from it kwamba kwa kuwa kulikuwa na gap ndiyo maana sasa hivi kuna uhaba wa wataalam, lakini pia hatukusomesha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia pengine tulifanya uchoyo wa promotion; kwa sababu hiyo inafanyika katika system ya Serikali. Inawezekana mtu ana qualify lakini anacheleweshwa kwa sababu nyingine nyingine tu, mbali ya watu ambao wamekatizwa kwa sababu ya maoni yao pengine kwa sababu ya fikra zao. Hasa katika kuja katika vyama vingi sasa hivi watu wengi academicians wameingia kwenye loggerhead na Serikali, pengine hawakubaliki katika vyuo na kwa sababu hiyo wameona kwamba kuna mgongano wameamua kuacha na kwa hivyo ile gradually ya watu kupanda pengine imesaidia katika kupungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo nakubaliana na Serikali katika hili, kwa maana kwamba kuja na wataalam kuwaongeza kutoka 60, mpaka 65; lakini isiwe kwamba ni mwisho wa mambo. Ukweli ni kwamba tunahitajika kutengeneza mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu nchi nyingine wanatengeneza mazingira wala vijana wao waende wakasomeshe nchi nyingine kama kuna excess. Mwaka jana sisi tuliambiwa kuna excess ya madaktari hapa tukataka kuwapeleka Kenya. Kwa hiyo wakati mwingine ni contradiction ya Serikali, wengine tukataka waenda kule, tuwasaidie Kenya, wakati kumbe sisi wenyewe tuna upungufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ukweli ni kwamba kuna taka tuwe very pragmatic, tuwe wa uhalisia kwamba tatizo hili haliwezi kukamilishwa tu kwa kuzidisha umri, lazima tuwe na program ya kutosha kuweza...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi wa Mwaka 2018
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kusema ukweli hii ni sheria muhimu kwa maana ya progress ya nchi na ni sheria ambayo pengine wengine wanaweza wakasema kwamba ingepaswa ije kabla ya hapa lakini mtu anaweza akajiuliza kwa nini imechelewa muda wote kutangaza Makao Makuu ya nchi. Kwa sababu hii si dhana ngeni imewahi kutokea sehemu nyingi kama ilivyosema hotuba ya Kamati na hata ndani ya Afrika kumekuwa na nchi ambazo zimekuwa zikiamua kubadilisha Makao Makuu yao.

Mheshimiwa Spika, kubadilisha Makao Makuu kunategemea sababu nyingi, inawezekana ya kiusalama, kibiashara au mkakati mwingine wa kuleta maendeleo karibu na watu. Kwa mfano, zipo nchi ambazo kwa kuanzia zilikuwa na mipaka yake karibu na nchi nyingine, wameondosha Makao Makuu kupeleka sehemu nyingine ili kuondoa uwezekano wa matatizo inatokea dharura katika nchi nyingine.

Mheshimiwa Spika, hakuna maelezo ya kina hasa kwa nini tumehamisha kwa maana ya kuja katikati ya nchi lakini tuna-assume kuna sababu ambazo zimeelekea kufanya hivyo. Sehemu kubwa tumejikita katika Tamko la Mwalimu Nyerere la mwaka 1973 kwamba angependa kuona Makao Makuu ya Chama chake cha TANU wakati huo yanakuwa Dodoma na halikadhalika na Makao Makuu ya Nchi yanakuwa Dodoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukumbuke wakati anasema hivyo kulikuwa na Chama cha ASP cha Zanzibar kwa sababu tuliunganisha vyama mwaka 1977 kwa maana ya TANU na ASP. Kwa hivyo, dhana ambayo mimi naweza kuipata ni dhana ya Mwalimu kwa chama chake na siyo dhana ya Tanzania nzima. Kwa maana hiyo, wakati huo alipaswa au
ilitakiwa tuoneshwe tamko ambalo alizungumza kwenda zaidi ya pale. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hivyo, alikuwa anakisemea chama chake.sasa hivi kushikilia hoja hiyo kwamba ndiyo hoja madhubuti ya kwamba tunahamisha Makao Makuu ya nchi kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma kwa sababu ya kauli kama hiyo inaleta utata kidogo kwa sababu wakati ule Mwalimu alitia na suala la chama chake cha TANU. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini vilevile…

T A A R I F A . . .

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, namshangaa swahiba yangu kwamba hajui kwamba mwaka 1973 kulikuwa na Chama cha Afro Shiraz Party - Zanzibar na kulikuwa na Chama cha TANU – Bara. Ndiyo maana nikatangulia kusema kwamba 1977 vyama hivi vikaungana ASP na TANU ikazaliwa CCM na mimi nilikuwepo Zanzibar wakati ule na udogo wangu nilikwenda Uwanja wa Amani kushuhudia. Kwa hivyo, taarifa hiyo siipokei na nakusamehe kwa hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika kuhamisha Makao Makuu ya nchi ungetarajia kungekuwa na kitu cha kuuliza wananchi wanasemaje juu ya kuhamishwa Makao Makuu ya nchi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Siku za nyumba haikuwahi kufanywa lakini ningetarajia sasa hivi kutokana na kupanuka kwa demokrasia na vitu mbalimbali kungekuwa na White Paper Wazanzibar kama walivyoulizwa kuunganisha vyama, wangeulizwa juu ya kuhamishwa mji kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana nikasema tangu mwanzo, dhana ya kuhamisha siyo problem, kwa sababu kunaweza kuwa na sababu nyingi za kimsingi za kuhamisha lakini hizi ni pande mbili za Muungano. Unapohamisha Makao Makuu ya nchi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, ilipaswa pande mbili zishiriki kikamilifu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, taarifa niliyonayo, sina uhakika, sitaki nijinukuu lakini katika corridors tunaambiwa Serikali ya Zanzibar katika hili haikushiriki. Tunaambiwa na watu wetu waliopo katika Kamati walimuuliza Mheshimiwa Waziri anayehusika na jambo hili, vipi kuhusu hili hakuna jawabu la uhakika lililotoka kwamba Zanzibar ilishiriki. Sasa unahamishaje Makao Makuu ya nchi ya pande mbili bila ya popular will ya pande zote mbili zinazohusika? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa tatizo liko wapi? Ni katika mfumo mzima wa sheria wa Tanzania. Serikali ya Muungano inaweza ikaamua chochote kuhusu Muungano, hapa tunaambiwa itapigwa kura kwa maana ya Bunge zima na ni sawa kwa maana ya Bunge zima tupate two third lakini mara nyingi sheria ikishapitishwa hapa inatakiwa iende kuwa tabled katika Baraza la Wawakilishi, unajiuliza tutasema mara ngapi kama nchi kwamba kuna matatizo katika kutunga sheria lakini ikienda kule inaenda kukataliwa, hii ni moja katika sheria ambayo inaweza kukataliwa Zanzibar labda itumike whip ya chama lakini njia rahisi ingekuwa ni kuishirikisha Serikali ya Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, ipo mifano mingi ambapo sheria iliyotungwa huku bila kushirikishwa Zanzibar kule zimekataliwa, mojawapo ilikuwa ni ya Deep Sea. Sheria ile ilipitishwa kwa magube hapa kwa sababu ya huu utaratibu kwamba Serikali ya Muungano inaweza ikafanya lolote lile kisheria hailazimiki kuishirikisha Zanzibar, hilo ni kosa kubwa la kikatiba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mimi nasema binafsi naafiki suala la kuhamisha lakini ninavyoona mimi taratibu hazijatimia, mojawapo ni kujaribu kuwauliza wananchi kwamba wanataka Makao Makuu ya nchi yao yahamishwe yaje Dodoma? Upande wa Zanzibar hatukuwahi kuona kwa maana ya kura ya maoni au njia yoyote ile ya kuwashirikisha wananchi.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2018
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuwa mchangiaji wa mwanzo katika siku muhimu kwa historia ya kiuchumi ya Tanzania. Ni siku muhimu kwa sababu tulikuwa tunatarajia Muswada kama huu ambao utashawishi sasa mitaji ya binafsi kuja kwa masharti ambayo pengine yatakuwa bora zaidi. Umechelewa kuja lakini maadam umeshafika, basi tutaupokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekubali kuwa tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda na Waswahili wanasema kila ngoma ina masharti yake. Ngoma hii ya uwekezaji ina masharti yake. Hatuwezi ku-dictate sisi terms, lazima tutazame terms ambazo zinafanana na ulimwengu ili tuzilinganishe na mazingira yetu, tuzioanishe na tuweze kuzitumia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchumi wa viwanda ni kuwa na sheria imara. Ukishaweka misingi ya sheria, basi utafanya vizuri. Uchumi wa viwanda maana yake ni kuwa na sera ambayo ina mapana, ni wide looking na ni far looking. Kama alivyosema Msemaji wa Kambi ya Upinzani nchi hii siyo tunaoishi sisi tu leo ni pamoja na ambao wataishi miaka mingi baadaye. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa Zambia ina-suffer; kiwanja chake cha ndege kimechukuliwa, shirika lake la umeme limechukuliwa kwa madeni ambayo yamekopwa toka zama za Kaunda. Hali kadhalika, nchi ya Sri Lanka tangu wanapigana wenyewe kwa wenyewe wamekopa kwa Wachina hivi sasa wameanza kufilisiwa. Kwa hiyo, kila mara tukifikiri, tufikiri sisi na wengine wanaokuja ili makaburi yetu yasije yakalaaniwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni pamoja na kuwa na mipango imara. Tuna Mpango mzuri wa Taifa ambao unalenga katika kuimarisha nchi hii, lakini cha muhimi pia ni kubadilisha mindset za watu wetu. Watendaji wengi wa Serikali hawaendi na wimbi la mabadiliko, hawaendi na mtazamo wa kidunia. Kwa hiyo, hiyo ni muhimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ili kuvutia mitaji ni lazima utayarishe umma. Kwa hiyo, haya yote ni maandalizi ambayo yanaweza kutangulia ingawa yanafanywa kwa phases, lakini yakikamilika ndiyo maana unaweza kuwa na watu. Leo ukienda Malaysia, China watu wenyewe wanakaribisha uwekezaji, watu wenyewe wanakaribisha mipango ya nchi yao na wanaipokea na wanaifurahia kwa sababu wameelekezwa katika hali nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sehemu kubwa ujenzi wa viwanda au uchumi wa viwanda au uwekezaji mara nyingi una njia nyingi. Iko njia ya mikopo na njia ya mitaji ya watu binafsi. Hii ndiyo ambayo sheria hii sasa inaelekeza. Uzuri wa sheria hii sasa inasogeza kwamba itakuwa centered pamoja kwamba pengine siyo kila Wizara itakuwa inafanya, lakini imeletwa kwa pamoja, ambapo jambo hili litasaidia kujenga na tutakuwa tunaona taasisi moja inasimamia na uimara wa nchi unaonekana kwa sababu mipango inaweza ikapita katika system, ikaonekana na ikatekelezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi kuvuta mitaji kwa kubakia katika ujamaa ni lazima soko lifanye kazi. Hata Wachina wenyewe ambao mara nyingi wamekuwa ni mfano wetu, wametoka, pamoja na ujamaa wao lakini wakatengeneza economic zones; Dalian, Guangzhou, Wenzhou, Nantong na kwingine kwingi. Kutokana na kile, ndipo wakaweza kutengeneza mazingira yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia soko lina masharti yake na uzuri wake. Uzuri wa kuvuta mitaji ya PPP, maana yake unapata miradi haraka inakuja kwako, investment return ni greater kwa sababu inasimamiwa vizuri. Tendency imekuwa ikionesha, miradi ya kiserikali ina ukakasi mwingi, ina mambo mengi, vichochoro vingi, lakini miradi ikiwa ni ya PPP investiment return inakuja haraka. Vilevile unapunguza risk inakuwa transferred kutoka kwenye Serikali kwenda upande wa private. Ikiwa Serikali imeshiriki, basi risk itakuwa 50, 50 lakini ikiwa ule mradi umekuwa funded moja kwa moja na private ina maana risk moja kwa moja inakwenda private na Serikali inakuwa imeepuka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha muhimu inasaidia bajeti ya nchi kupumua. Kama una miradi ambayo watu binafsi wamechangia, ina maana pesa zako zinapumua unaweza ukazi-direct kwenye mambo mengine. Hapo ndiyo unapokuwa na nafasi nzuri zaidi ya ku-target miradi ya kijamii ambayo ni makosa kuikopea unless iwe ni muhimu sana kukopea miradi ya kijamii kwa sababu mara nyingi wanataka ile miradi ambayo inarudisha pesa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo mengi nakubaliana na Kambi ya Upinzani, kwa sababu katika sharti muhimu la uwekezaji ni predictability, namna ambavyo unaweza kutabiri. Kwa hiyo, haiwezekani unataka miradi lakini leo unafanya hili, kesho unafanya lile, Mkuu wa Wilaya huyu anafanya hivi, Mkuu wa Mkoa huyu anafanya hivi; huyu ananyang’anya passport, huyu anawatia ndani wawekezaji. Kwa hiyo, utakuwa huwezi kwenda sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nakubaliana na Kambi ya Upinzani kwamba mambo tuliyotaka, mojawapo ni time of doing business. Serikali badala ya kupunguza siku za kupitisha miradi imeziongeza kutoka 15 kwenda 21, hakuna sababu ya msingi. Utaalam upo wa kutosha, kuna watu wa kutosha, kwa nini tutoke siku 15 twende 21? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna lingine ambalo limekuja halina maelezo ya kutosha ni suala la kwamba wafunguaji wote wa miradi hii waweke fedha BoT. Hakuna maelezo ya kutosha zaidi ya kwamba tumetangaziwa. Pengine hii ina madhara yake kwa sababu unakwenda kuiweka Benki Kuu ya nchi katika mazingira magumu ya kusimamia jambo ambalo pengine lingeweza kusimamiwa na benki nyingine yoyote ambayo wadau wawili wanaoshiriki katika ule mradi wanaweza kukubaliana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo nitalizungumzia kwa undani kidogo ni suala la unsolicited projects. Hili nitapenda ni-declare interest kwa sababu ya kitu ambacho nimekiona na ndiyo maana nimefurahia kwamba kuna mabadiliko makubwa yanafanywa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri ukurasa wa 4 anasema kwa sasa sheria haikubainisha vigezo au masharti ambayo yanaweza kuruhusu baadhi ya miradi inayoibuliwa na sekta binafsi (unsolicited proposal) kutokushindanishwa. Kwa maana nyingine, katika kifungu cha 10 kinachobadilisha kifungu cha 15, kimetaja hayo masharti ambayo mradi ambao ni unsolicited unaweza kukubaliwa. Mengi ya masharti haya, watu hawa wa nje wanaweza wakayakubali, mtu ambaye anatafuta kuleta mradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni kwa kujua shida ya umeme ya nchi na alternatives za umeme, niliiandikia Serikali kwa Wizara inayoshughulika na Nishati kwamba nina mwekezaji ambaye yupo tayari kuwekeza mpaka one billion Euro kwa kutupatia nchi hii 1,000 megawatts ambazo baadaye anaweza akazisogeza kwa mujibu wa mahitaji ya Serikali. Nimeiandikia Wizara ya Nishati, majibu niliyopata kutoka kwa Katibu Mkuu, anasema kwamba lazima iingie katika competitive process. Mimi katika barua ya pili niliyomwandikia, nikamuuliza competitive process anashindana na nani? Kwani unao watu wengine ambao wameleta offer kama hiyo? Competitive process kwa maana ipi nyingine? Maana nimeshindwa kuelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilifikiri Wizara ile ingeniambia mlete mwekezaji aje ajieleze tuone… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2018
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Juzi nilipokuwa nawasilisha, nilizungumzia juu ya suala la kutokuwepo fungamanishi la kiuchumi baina ya chumi zetu hizi mbili. Pia nikasema chumi hizi mbili hazionekani kusomana kiasi ambacho it is disadvantage of Zanzibar, Zanzibar inaathika sana. Nikasema kuna maeneo matatu; maeneo ya kisera, maeneo ya kibajeti na maeneo ya muundo wenyewe wa Serikali ya Muungano.

Mheshimiwa Spika, sasa hapa leo nitazungumzia jambo moja ambalo linaathiri hayo niliyoyasema kwamba kuna tatizo la kutokusomana chumi zetu kiasi ambacho hatufikiriani kwamba tukifanya hii ni advantage ya huyu; huyu anapata na huyu anapata tukatengeneza win win situation. Nalo ninalotaka kuzungumzia ni suala ya VAT katika umeme.

Mheshimiwa Spika, VAT katika umeme imesemwa sana na Wabunge wengi kutoka Zanzibar, kwamba Wazanzibar wanalipa VAT mara mbili. Wanalipa wakati wa kununua huku kwa sababu wanauziwa kama watu wa kawaida, ZECO, kisha tukifika kule Zanzibar tunalipa tena VAT nyingine asilimia 18. Kwa maana Wazanzibari wanalipia VAT ya umeme ya kitu kimoja asilimia 36.

Mheshimiwa Spika, ni Kanuni ya uchumi kwamba VAT inalipiwa kule inakotumiwa, sasa kwa nini Zanzibar walipe VAT huku kisha waende wakalipe kule asilimia 36? Ndiyo yale, chumi hazisomani. Kwa maana nyingine, upande mmoja wa Muungano unachajiwa VAT asilimia 18, basi, kwa maana ya mlaji lakini kule tunalipa mara mbili. Hasara yake nini? Hasara yake, kwanza biashara inakuwa mbovu Zanzibar kwa sababu tunalipa umeme ghali zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, tunakuwa hatuna competition na kile ambacho wenzetu wanaweza kufanya. Kwa mfano, kama ilikuwa mtu ana Hoteli, anafanya biashara; labda ana biashara Bara, kwa hivyo gharama ya Hoteli Zanzibar itakuwa kubwa zaidi kwa maana ya kwamba tutakimbiza mtalii ambaye angetaka kuja kulala Zanzibar akaamua kulala Dar es Salaam kwa sababu Dar es Salaam is cheaper kulala kuliko Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, pia kama kuna uzalishaji ambao Zanzibar wanataka bidhaa ile wailete huku upande wa pili wa Muungano, kuzalisha inakuwa ghali zaidi Zanzibar kwa sababu unalipa asilimia 36 kulinganisha na huku asilimia 18. Kwa hiyo, kama mtu anazalisha tuseme ana kifungashio fulani anafunga ina maana gharama yake itazidi kwa asilimia 18 kwa sababu ya umeme lakini pia asilimia nyingine ya kusafirisha kutoka Zanzibar kuja huku Bara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu ni kwamba tunayafanya maisha ya Wazanzibari yawe ghali zaidi kwa asilimia 18 ya VAT ya nyongeza. Kwa hivyo hii siyo haki, siyo sawasawa na hii inapaswa irekebishwe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho, tuna unfair treatment katika nchi ambayo ina soko moja, ina chumi moja, ina tax regime mmoja, lakini bado tumekuwa tukiliachia hili bila kujali kwa miaka yote. Naambiwa kumekuwa na
mazungumzo kwa zaidi ya miaka minne hivi sasa, watu wanakwenda, wanarudi, lakini Serikali ya Muungano haioni uchungu na inakataa kulimaliza hili na hatujui kwa sababu gani.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, labda kwa lugha ya Kizanzibar tunasema mpaka kuna kedi ndani yake inafanyika kwa Serikali ya Muungano, hawataki kulimaliza tatizo hili. Kwa hiyo, nafikiri kuna haja ya hili suala la VAT linawezwa kumalizwa humu ndani kwa kauli ya Mheshimiwa Waziri. Halitaki kungojea wala halina ulazima wa kungojea, kwa sababu hatua nyingi zilishapitiwa na inaonekana kwamba kuna makubaliano kwamba Zanzibar katika hili hawatendewi haki. Kwa hiyo, nafikiri kuna haja.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, sasa hivi kwa sababu ya hilo, Zanzibar imekusanya deni kubwa TANESCO ambalo halina umuhimu wowote kuwepo. Hili likirekebishwa Zanzibar inaweza ikapata afuweni. Kwa hiyo, hili tunaweza kulimaliza humu ndani kwa kauli ya Mheshimiwa Waziri na tukasonga mbele.

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho ninalotaka kulizungumzia ni suala Export Levy ya korosho. Kumetolewa compromise leo hapa leo; imetolewa compromise ya Mheshimiwa Katani ya 50:50 kwa maana ya 50 katika zile inazoenda Serikalini, 50 iende kwa Bodi; pili, ilitolewa option na Mheshimiwa Zitto, kaigeuza kinyume nyume asilimia 35 ibakie kwenye Bodi na asilimia 65 iende Serikalini. Options hizi napenda Mheshimiwa Waziri mojawapo tuitumie. Kwa sababu kama ambavyo imeletwa hapa inaweza ikaleta matatizo, tunaweza tukapata watu wakakataa kulima korosho au kukatokea chochote kile katika korosho.

Mheshimiwa Spika, tukilazimisha hii, pengine korosho inaweza kuwa na hasara. Kwa hiyo, nafikiri twende katika compromise mojawapo, hata Mheshimiwa Waziri atakuwa na nyingine. Kuendelea tu kukataa, kusema kwamba yote iende huku na zile hoja zote zilizoletwa hapa kwamba hii korosho inakwenda mikoa 17; kwa hiyo, anayesema
kwamba hii korosho ni kwa ajili ya watu wa Kusini au levy ni kwa ajili ya watu wa Kusini siyo kweli. Inakwenda kwenye mikoa 17 na pengine itakwenda zaidi, tafiti zitaonesha kwamba Korosho inaweza kulimwa sehemu nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, sisi ni Watanzania ni Bunge la wananchi, tuna uwezo wa kufanya maamuzi na maamuzi haya ni kutafuta compromise. Tukishindana, hatuna faida nalo. Tumeona Pemba watu watu walikataliwa mikarafuu, watu waliingia katika magendo ya karafuu. Hatuna haja ya kwenda huko. Kama Taifa napenda uliongoze Bunge hili tutafute compromise, tusitafute kitu ambacho hakina ulazima wa kwenda huko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naanza kwa kunukuu kauli zako mbili ulizosema jana wakati wa Kikao cha Briefing, mojawapo ni ile ya kushangaa kuja kwa Sheria ya Maji kwa namna ilivyokuja ukawa unasema hivi hawa watu wanaishi dunia gani. Pili, nataka nipitie kauli yako ya leo asubuhi au jana pia uliposema kwamba sheria inatungwa kwa kufanya amendments. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nataka nianze kutiririka. La kwanza ni kwamba kwa mshangao mkubwa pamoja na kauli yako ya jana leo asubuhi amendments za Upinzani zimekataliwa kuingia Bungeni. Mpaka sasa sijui kama zimeingia au hazijaingia. Kanuni inasema kwamba tupeleke mapema na tulipeleka mapema lakini tukakwepwakwepwa, nanong’onezwa hapa kama zipo lakini kitendo hicho kimeonyesha nia ovu. Baada ya kusema sisi ndiyo pengine zimekubaliwa.

Mheshimiwa Spika, pili, kuhusu kauli yako ile ya maji inanishangaza kwamba Muswada huu umekuja kama ulivyo, kwamba umepita kwa wataalam, Makatibu Wakuu na Cabinet na ukaja Muswada ambao nitataja kasoro zake hata usingetarajia uje kama ulivyokuwa hapa, hii ni dalili ya nia ovu.

Mheshimiwa Spika, Muswada ule umekuja na vifungu vingi ambayo ni unconstitutional ambapo unashangaa kama umepita hatua zote lakini bado mnaleta Muswada ambao ni unconstitutional. Pili umekuja Muswada una lack view process, sehemu hii ndiyo inampa mamlaka mtu bila ya kuhoji aamue mengine in belief, akiamini tu anaweza akafanya utashangaa kwa nini umekuja hivi lakini kwa sababu kulikuwa na nia ovu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sehemu ya tatu ni criminalization of politics. Vifungu vingi vimekuja ku-criminalize politics wakati tunajua huu ndiyo uwanja mpana wa watu kushiriki na ni politically space inafaa kutumiwa vizuri lakini we have criminalized a big part of it. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitu kingine ni suala la ubaguzi. Utashangaa Muswada ambao umepita kwa Makatibu Wakuu na Cabinet unakuja na vifungu vya ubaguzi, lakini yote kwa sababu ulikuwa nia ovu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka niseme wapinzani hatusemi tusiwe na sheria na anayesema hivyo anajidanganya kwa kusema kwamba wapinzani mnataka nini, tunataka a lot siyo hii, tunataka sheria ambayo itatupeleka mbele. Baada ya miaka 50 ya Uhuru hungetarajia kwamba ungekuwa na sheria ya aina hii. Baada ya miaka kadhaa ya vyama vingi hungetarajia kuwa na sheria kama hii. Kuna mifano mingi ya majirani zetu ya kuitazama, kuna maeneo mengi tu ya kuyatazama, wakija pale wanakupa mifano ya Ghana ukiwaambia kwa nini hukuchua hili wanakwambia kwa nini tuige yote lakini mazuri huwezi kuchukua? What is the harm kuchukua good practice za wengine?

Kwa mfano tumesema unachukua vyama unafanya waungane au unachukua vyama unafanya kitu lakini kuna kitu tume-suggest kizuri tu tribunally disputes certain month tribunally ya vyama ili mtu akikwaza na Msajili awe na pahala pa kwenda, hata hilo mnalikataa? Hata hilo linakataliwa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii kama vile hawa wanaishi nchi nyingine na hawa wanaishi nchi nyingine we are lived in the same country? Na tuna haki ya kufanya siasa kama wengine wanavyofanya siasa. Kama ambavyo kimekuja kipengele kimoja kwa heshima zote kwenye merge tunaambiwa kwamba chama tawala hakitahusika kwenye merge kwa nini kisihusike? Yaani CCM hawatarajii kama wanaweza wakaungana na mtu? Yaani CCM wanafikiri watakuwa hivi hivi kila siku? Alisema Mheshimiwa Mbarouk asubuhi hapa mifano gani, kwani alitarajia kama Mori angeondoshwa, nani alitarajia kama Kaunda angeondoshwa, nani alitarajia kama Kamuzu Banda angeondoshwa, msitarajie msitengeneze mazingira kwa kuona leo look ahead. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tizameni vizazi vyenu, tizameni usalama wa nchi, mnachukua kifungu mnasema kwamba hakuna kuunda Majeshi, nani kasema vyama vya Upinzani vinataka kuunda Jeshi? Katiba ilishasema kwamba hakuna kuunda Majeshi, nani ataunda Jeshi, sasa unawaambia utalindwa, hivi kweli mnatulinda? Hivi kweli nchi hii inalinda Wapinzani, hivi kweli ingekuwa Wapinzani wanalindwa? Hivi kweli kungekuwa na haki Wapinzani wanalalamika pote hapa kwamba wanachotaka angalau minimum. Angalau usalama wao, nani kasema wataunda vikundi vya Kijeshi, kwani Sheria hazipo, kwani usalama wa Taifa haupo, kwa hivyo mnafanya vitu ambavyo mnafikiri mtaishi milele katika siasa.

Mheshimiwa Spika, hamtaishi milele, kuna mwisho wake, kuna kuanguka, wangapi walikuwepo, walikuwepo Firauni, walikuwepo nani anaishi, ameondoka. Kwa hivyo msitengeneze Sheria ambayo inatizamwa leo, tengenezeni Sheria ambayo inakwenda wazi nikupe mifano ya vifungu kuna mambo tulikubaliana na Mheshimiwa Waziri kwenye Kamati ndio maana nikasema hizi gains ambazo tumezipata kwenye Kamati sizikatai lakini zilipaswa ziwepo kwa sababu zimekuja unconfussion zimekuja with a lack of democracy ndio maana tuka-gain kwenye Kamati, Kamati ilitumia akili. Yuko mtu simtaji hapa alisema, vifungu vingine vitaipeleka CCM ikashindwe asubuhi Mahakamani, Mahakamani mtakwenda kushindwa asubuhi hata mchana haifiki. Ndio maana baadhi ya viongozi, katika baadhi ya Viongozi baadhi ya Wabunge mle, wakasema, tusahihishe, na nimefurahi Serikali imekubali, lakini vingine wamekataa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mfano tumezungumza katika suala la kutoa elimu, tumezungumza kwamba kuwe na muda Mheshimiwa Msajili anakujibu, haikuwa-reflected humu ukipeleka mafunzo yako unayotaka kufanya hakuambiwa muda gani atajibu, lakini kingine tumesema kwamba tunataka tupewe orodha ya mambo ambayo hayahusiki katika mafunzo ili orodha ile iwe reference kwetu katika kutengeneza mafunzo, tukaomba iwe schedule iwe na scheduled haikuja hapa, unatarajia tufanye nini sasa tumpelekee Msajili halafu tukae tu tusubiri, achague muda anaotaka yeye kutujibu?

Mheshimiwa Spika, kingine ni suala la merge na coalition, hili ni eneo ambalo pana kichekesho kikubwa sana kwa sababu unatengeneza mazingira unaamini kama vile CCM hutotarajii kuungana na chama chochote kile, unajitoa katika merge unasema kwa hili chama tawala hakihusiki. Lakini unasahau kwamba ilikuwa ni challenge tuliowapa baada ya kuja na sheria Kifungu kibovu katika kifungu hiki, walikuwa wana-argue wenzetu wa CCM kwamba ukisha-merge vyama vife tukawaambia sawa, vyama vitakufa, lakini vyama vikifa na Rais anakufa kwa sababu Rais hana chama, wakasema Rais haondoki kwa sababu Rais analindwa na Katiba tukasema what comes first?

Mheshimiwa Spika, Katiba au Rais wake, au kuwa mwanachama wa chama, definitely unachaguliwa kuwa mwanachama wa chama, mwanachama kisha anachaguliwa, kwa hivyo tutakuwa na President less country ambayo itakuwa ni chaos. Tukasema kingine tukawaambia kwamba merge hi itakwenda kuonesha kwamba wanasema Wabunge ukifika muda wao, wanakufa, tukawaambia sawa wanakufa, lakini je, ikitokea dharura, unataka kuwaita Wabunge, utawaita Wabunge kwa chama gani? Hili halijasahihishwa tunakwenda kwenye merge, CCM ndio wameshasema wao chama dume sijui chama gani, wao hawamo, haya, tuseme tumekubali, lakini hawa Wabunge je, Wabunge kumetokea dharura hakukufanyika uchaguzi, hakujafanyika uchaguzi, utawaita kwa Mamlaka gani? Na wakati umesema vyeo vyao vimekufa? Lakini pili ni kuhusu coalition, coalition tulipendekeza lakini schedule iliyokuja haikupita kwenye Kamati imekuja…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha muda wa Mzungumzaji)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 7) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza)
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza nataka niseme kama ambavyo mara nyingi nasema na pengine Mheshimiwa Susan na Kambi imesema kwamba vitu vinakuja kwa dharura kila mara. Si tatizo kwamba Serikali inafanya mabadiliko kwa sababu ni lazima ifanye mabadiliko, lakini hii dharura kama ambavyo msemaji wa mwisho, Mheshimiwa Sixtus, amezungumza hapa suala la namna ya kukabiliana na ugaidi ambalo hatukatai linaweza kuwa tishio katika nchi yetu, lakini ukileta kwa dharura ina maana unakosa wadau.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano mara hii, wadau tuliopata ni mmoja tu kuhusiana na eneo moja tu la HIV. Tunakwenda kumpa Waziri mamlaka ya kutunga kanuni kuhusu ugaidi, kanuni ambazo zitaishia kutengenezwa na Waziri hazikupitishwa kwenye sheria. Matokeo yake kunaweza kukawa na kanuni halafu zikaja zikatubana kupita kiasi kama nchi au vingine, matokeo yake ikawa kila aliye ndiye anakamatwa na aliye siye anakamatwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kwenye suala la NIDA; hatukupata maoni kutoka kwa wadau, namna gani hizi data ambazo zinawekwa katika eneo hili zitalindwa, wadau wenyewe wana nafasi gani, zinaweza zikatumika vipi, kwa sababu data dunia ya sasa ni suala muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, tunazungumzia kuhusiana, kama alivyosema Mheshimiwa Susan, unaleta sheria hapa kuhusu maziko ya kitaifa, lakini wakati huo huo unasema kwamba mtu anaweza kuona hiari asizikwe katika eneo la kitaifa. Sasa maana yake nini, maana yake nani atakwenda kuzikwa kule? Kwa sababu kama mtu ana hiari yake family itasema hapana, sisi tunataka tumzike Chwaka, tunataka tumzike Tandahimba, hatutaki kumzika katika eneo lililotengwa na kwa hali hiyo…

T A A R I F A

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naelewa hofu ya Mheshimiwa Ally Saleh, ni kwamba tunapoleta kufanya mabadiliko ya mazishi ya viongozi lengo letu sasa ni kufanya mazishi ya viongozi kwa kuzingatia utaratibu wa kimila, utaratibu wa kidini, kila mtu kwa mahali ambapo anataka kwenda kuzikwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja hiyohiyo inakwenda kwamba sasa kama kulikuwa na sheria ya mwanzo inapofutwa lile eneo litafanywa nini na Mheshimiwa dada Susan ameniuliza; yale maeneo yote tulishayarejesha sasa tunarudi kwenye utaratibu mmoja, kila kiongozi atakwenda kuzikwa pale anapotaka kwa kuzingatia matakwa ya familia na taratibu zote zitatafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu sasa wa mazishi hayo ya kitaifa unabaki kwenye Principle Act ambayo imetoa maelezo yote sasa utaratibu wa mazishi yenyewe utafanyikaje hata kama sio pale kwenye makaburi ya kitaifa. Kwa hiyo kila kitu kimekuwa under control na Mheshimiwa Saleh wala asiwe na wasiwasi, mfumo umetengenezwa kwa viongozi wote pande zote mbili za Muungano.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na maelezo yake bado nina wasiwasi; unawekaje mahali pa maziko ya kitaifa lakini bado maziko yanafanyika kwingine? Pale patalala mbwa tu, patalala paka tu kwa sababu hapatumiki, anyway, tunasonga mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo ambalo nataka nilizungumze kwa undani kidogo, ni kuhusu hii Sheria ya UKIMWI na HIV. Tumesema kwamba Serikali imekuja na nia nzuri na naona sio mbaya kutoka 18 kuja 15, lakini mimi binafsi naunga mkono wanaosema 12 na binafsi nilikuwa nimejitayarisha kwa compromise ya 14, lakini nikapigwa technical knockout kwamba nimechelewa dakika tano kupeleka amendment hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nahisi ama 14 au 12 nitaunga mkono lakini kwa sababu amendment iliyopo na kama italetwa humu nitaunga mkono kwenye 12 kwa sababu nimevutiwa sana na hoja za NACOPHA kuliko hoja za Serikali katika suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa takwimu, watoto miaka sifuri mpaka tisa ni asilimia 30 ya population yetu; 10 mpaka 14 ni milioni saba ni asilimia 12; 15 mpaka 19 ni milioni sita, asilimia 10.9. Kwa maana nyingine hao wa miaka 10 mpaka 14, 15 mpaka 19 ni twenty four percent ya population yetu. Kama ni twenty four percent ya population yetu ina maana kwamba humu kuanzia 14 mpaka 12 ni karibu asilimia 18 ya watu wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama tunasema mtu ambaye anaweza kujipima ni kuanzia 15 kwenda juu unamwacha 14, unamwacha wa 13 unamwacha wa 12 wakati tunaamini sote, kila mmoja katika sisi anaamini kwamba watoto miaka 12 wanaingia katika mambo ya ngono, hasa wanawake, ama kwa kubakwa au kwa kushawishiwa au kwa chochote kile. Kwa hiyo tusifanye denial kwamba watoto kuanzia miaka 12 mambo hayo yapo mpaka 14 – 15. Sasa kwa nini tukatae watoto wasijipime wakati hili ni suala la hiari. Tumesema kujipima ni hiari, angalau basi watoto hawa wakiruhusiwa kujipima ina maana tunakuwa na chance ya kuokoa watu wengi ambao ni nje ya 15 kwenda juu. Tukisema tunakataa ina maana tunawaweka watoto wenye miaka 14 kwenda chini at risk.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua sote kwamba mtu akianza kutumia dawa, nafasi ya kuambukiza mtu mwingine inapungua, lakini kama watoto hawa wenye umri wa miaka 12 mpaka 14 ambao wameshaingia katika ngono ambao wanapata HIV au wanapata UKIMWI, matokeo yake ni kwamba unawakataza wasipime, wazazi wao hawawapeleki na kama alivyosema Mheshimiwa Susan kuwa watoto hawa pengine mjomba, ami, kaka anahusika au pengine baba, ina maana kwamba unatengeneza bomu ambalo sasa hivi unaweza ukaona prevalence au incidence ni ndogo, lakini inaweza ikawa kubwa ghafla akifika miaka 15 ndiyo anaanza kupima unaona kuna ongezeko kubwa limeongezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ya Serikali ya kusema kwamba ziko nchi zimefanya taratibu kama hiyo kwa mfano Afrika Kusini lakini bado prevalence imeongezeka, au kusema kwamba zipo nchi zenye kujaribu hilo lakini bado maambukizi yako makubwa, hii haina msingi. Wala haina msingi kusema kwamba kwa mila zetu au kwa utamaduni wetu; kama mila mtoto wa miaka 15 anaruhusiwa kupima kwa nini mila kwa mtoto wa 12 asiruhusiwe kupima?

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sheria za nchi hii hii kwa mujibu wa sheria ya kiislamu, mtoto wa miaka 14 anaruhusiwa kuolewa na wengi wameolewa kwa ruhusa ya wazazi wao. Kama hotuba ya Kambi ilivyosema mtoto anabanwa katika sehemu nyingi za kisheria, sina haja ya kurudia, kama alivyoeleza kwenye kambi, lakini bado kuna haja ya Serikali kutazama suala hili, kwamba tukiwaacha miaka 12 mpaka 14 nje ya net hii, maana yake tunakusanya bomu baadaye wakija wakifika miaka 15 wakiweza kupima matokeo yake yanakuwa ni athari kubwa, bora tuzuie sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sioni tatizo kubwa sana la kusema huyu aende akapimwe na mzazi wake, lakini kama hata kwa mzazi wake haruhusiwi lakini pia haruhusiwi kupima yeye mwenyewe, hili ni tatizo. Ni tatizo kwa sababu mtoto, watu wengi katika umri huo wana usiri mkubwa na kwa sababu hawana uwezo matokeo yake wanaweza wakadanganywa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu vilevile utafiti unaonesha kwamba nchi ambazo zimejaribu kufanya hivyo, ingawa Serikali imetuletea mfano wa Lesotho na South Africa, lakini kuna nchi nyingi ambazo zimeweza kufanikiwa. Sisi kama tunataka kulenga 90, 90, 90 basi 90 ya mwanzo ni muhimu kabla ya 90 ya pili na kabla ya 90 ya tatu. 90 ya mwanzo ina-include watoto wa miaka 12 mpaka 14 ambao pia wamejiingiza au wameingizwa katika masuala ya ngono.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaunga mkono hoja yoyote ambayo inasema twende miaka 12. Ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.8) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza)
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwangu mimi leo ni moja katika siku ya unyonge na it’s a dark day kwa sababu ya sheria ambayo tunakwenda kupitisha na sheria ambayo inaonekana Serikali ikiikazia kuhusu Tanganyika Law Society. Nahisi kila tunavyokwenda tunazidi kuibana taasisi hii muhimu ili isiweze kufanya kazi zake kama inavyotarajiwa na badala yake Serikali iwe na control kubwa sana. Kwa maana nyingine tunazidi kubana public space na tukilaumiwa na wenzetu wengine huko nje kwamba Tanzania tunabana public space tunakuwa tunalalamika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo kwa sababu ya vipengele ambavyo kama ambavyo hotuba ya Kambi ya Upinzani hata katika Kamati tulikubaliana kwa kiasi fulani kwamba kuna tatizo la Serikali kutaka kufanya namna ambavyo taasisi hii ya kitaaluma inavyokutana. Mambo yanayofanywa kwingine kote hayafanywi katika taasisi nyingine za kitaaluma, kwa mfano madaktari wanaweza kukutana kama walivyo wako elfu tano wako elfu sita wanakutana kama walivyo. Lakini kwa upande wa Tanganyika Law Society wanaambiwa wakutane kwa zone, zone hizo hatujui baada ya kupitisha kanuni zitakuwa na mfumo gani. Serikali ilikuja na package ya compromise, lakini haikuridhisha sana kwa mfano, walipoulizwa kwamba asilimia sabini ya wanasheria pengine wapo Dar es Salaam, wakasema inawezekana tukafanya special zone kama vile kuna special zone ya kipolisi na special zone nyingine kwa maana nyingine inawezekana Dar es Salaam kukawa na zone nne.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia kuna tatizo la uwakilishi wenyewe, wenyewe wanasheria wanasema mkutano wao mkuu wakikutana wana mambo mawili; wana mkutano wao wa kujadili masuala yao wenyewe ya kimaendeleo, lakini pia mkutano ule una chagua viongozi, sasa Serikali wanatoa nje ile aspect ya wao kukutana kama wanachama au watu wa aina moja ili waweze kujadili mambo yao, kwa maana nyingine hili pia linapingana na Katiba ya haki ya kujikusanya, kwa sababu wao ni entity moja huwezi kusema uwapeleke kwa mafungu hakuna sababu ya kuridhisha iliyofanywa hivyo. Baada ya mjadala katika Kamati, Serikali ikasema ikaja na lile linaloitwa andiko, andiko lenyewe lilifanywa within two days bila ya utafiti ya uhakika au utafiti mpana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukaja na hoja nyingi ya za kuzungumzia juu ya namna ambavyo kwa nini wana cartel power za Tanganyika Law Society kwa sababu tu haijafanyiwa mabadiliko ya siku nyingi na kwa sababu ni sheria ya zamani sana lakini badala ya kuifungua demokrasia tunafunga kwa sababu tu sheria hii ni ya zamani na kwa sababu Serikali ina hofu ya uanaharakati ambao unatokea ndani ya TLS.

Mheshimiwa Spika, lakini ukweli uanaharakati ule ni suala la muda tu, inawezekana leo Rais wa TLS au Kamati ina uanaharakati lakini kesho au pengine wanaounga opposition, lakini kesho inawezekana Rais wa TLS ambaye anaunga mkono CCM. Kwa hiyo, unazuia nini wakati hata kama atakuwa mwanaharakati bado ni ndani ya haki yake, bado hajavunja sheria bado anatumikia wananchi wa nchi hii. TLS imefanya kazi kubwa, imagine, TLS inakufa kifo cha ghafla ina maana kwamba tasnia nzima ya sheria imekufa ndani ya nchi hii, lakini unachofanya unauwa pole pole tasnia ya sheria kwa sababu ya vikwazo vingi ambavyo vinakuwa created kila siku nafikiri sheria hii haitupeleki mbali bali inaturudisha nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kingine ambacho nataka kusema nje ya jambo hili ni hili la Serikali mashitaka dhidi ya Serikali, Serikali imekwenda kuingia katika mamlaka ambayo tayari yako kwa halmashauri, kwanza imeongeza siku au muda kuomba fear kuishitaki Serikali kufikia siku 90 ambapo pengine huyu mtu aliyeathirika ni muda mrefu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia sasa hivi tunataka kumshusha Solicitor General awe involved ashirikishwe aunganishwe katika kila kesi ya kisheria ambayo iko katika kiwango cha chini na siyo tena kule juu. Rais wa TLS Ndgu Nshalla alitahadharisha katika Kamati alisema kwa maana hii sasa kama Solicitor General anaunganishwa ina maana Serikali Kuu imeingia ina maana mtu part ya grief wakitaka attach mali, wanaweza waka attach mali katika lengo lengo la kitaifa, inawezekana Mtanzania sasa akasema anazuia ndege, akasema anazuia train, akasema anazuia property ya Serikali kwa sababu Mwanasheria Mkuu amekuwa involve katika ngazi ya Halmashauri jambo ambalo hivi sasa halina jambo la kufanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili unajiuliza juu ya utekelezaji wake Halmashauri zipo nyingi, makosa katika Halmashauri yanafanywa kila siku, halmashauri inashitakiwa kila siku, je, huyu Solicitor General atakuwa na manpower ya kuweza kuyafanya yote hayo au itakuwa ni yale yale kwamba wanadumbukiza makesi, raia wanaumia hakuna linalofanywa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na jambo la mwisho nataka kusema juu ya peace mill… (Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Sheria ya Fedha ya Mwaka 2019
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, mara nyingi humu ndani kimekuwa kikitajwa kitu kinaitwa blueprint na siku moja ulitoa agizo kwamba Wabunge tupewe ili tuwe sawa na Serikali katika uelewa wa kilichomo katika blueprint ili tuweze kuifuatilia na tuwajibike Kibunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi mpaka leo sijaiona hiyo blueprint na Wabunge wengine niliowauliza wanasema hawajapata copy ya blueprint, pengine wenzetu wanayo sisi hatuna.

Mheshimiwa Naibu Spika, uchumi una nguzo zake. Ni lazima uzifuate nguzo hizo kwa sababu bila kufuata nguzo za kiuchumi huwezi kufanikiwa. Tupo hapa leo tunapitisha sheria ambayo ni ya lazima, baada ya bajeti lazima tuipitishe sheria hii ili kuipa mamlaka Serikali iweze kutumia.

Mheshimiwa Naibu Spika, ikiwa tunataka kujenga uchumi, lazima uwe uchumi ambao unatabirika. Mwekezaji anakuja hapa anajua kwamba ana uhakika uchumi unaweza kutabirika hakuna mambo yatakayotokezea. Lazima katika nchi kuwe na utulivu wa kisiasa, utulivu kwenye haki za binadamu na mambo mengine. Pia tuwe na ushindani halali. Tukiwa na ushindani halali basi mtu yeyote yule anaweza kuwa interested kuja kuwekeza kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye upande wa kodi, kodi inakusanywa scientifically. Kuna misingi ya kikodi, lazima iwe harmonious, lazima kodi isikusanywe kwa bugudha. Msemaji wa mwisho aliyepita amesema kwamba TRA should pull up their act, wajisafishe, waonekane kama ni wakusanya kodi, mtu asiogope kukabiliwa na mtu wa TRA. Pia tujenge utamaduni wa kulipa kodi. Utamaduni wa kulipa kodi umfanye raia aone kodi yake inatumika vipi. Ukimfanya raia anaamini kama kodi yake inatumika vizuri basi twabaan na yeye atakubali kutoa kodi bila tabu yoyote.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nataka nipongeze kwamba sasa hivi Tanzania tax base ni ndogo sana. Ikiwa tax base ni ndogo sana wanaobeba mizigo mabeba yao lazima yataelemewa, ni vizuri Serikali itafute njia mbalimbali za kuongeza tax base ili walipaji kodi wawe wengi na mzigo uwe mwepesi na ndiyo maana vilevile nikisema hapo nakubaliana na Msemaji wa Kambi ya Upinzani kwamba mfumo wetu wa mara hii haukuja na kitu kipya katika kodi, hakuna innovation, ni zile zile kodi za kawaida zimechezewa hivi zimebadilishwa hivi, hatukuwa na innovation katika Serikali. Tungependa Serikali kila mwaka ije na innovative ideas ili kuwe na hamasa ya kulipa kodi, lakini pia ishawishi watu wengine wajaribu kuwekeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna maeneo mimi nayaona mazuri na ambayo nayaunga mkono mojawapo ni hili suala vifaa vya plastiki, lakini nakubaliana na upande wa Kambi kwamba hili liwekwe sawa, kwenye suala la vifaa vya ujenzi, sekta hii tunajua inaweza ikachangia kiasi kikubwa kwenye uchumi, kwa hivyo ile concern iliyotolewa na Kambi ya kutofautisha ya kujua vifaa vinavyotoka nje na ndani ingekuwa sawa, hili ni eneo zuri

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ni hili la kuondosha kodi kwa majokovu au vifaa vya kuhifadhia. Nakubaliana na Mheshimiwa Mbene kwamba wigo ungepanuliwa tukaenda kwingine zaidi kwenye uvuvi na kwenye vitu vingine. Wakati mwingine hata hizi dry goods zinapaswa ziwe katika temperature maalum, bila kuwa na temperature maalum zitaharibika, kwa hivyo hiyo pia itengenezwe vizuri. Pia hii ya vilainishi na ya tiketi inakusudia kuibeba Air Tanzania, si vibaya, lakini itumike vizuri kwa makampuni yote ya ndege ili ushindani uwe ni fair, kama nilivyosema pale juu unatakiwa tuwe na ushindani fair. Hata hivo, sidhani kama walivyosema kwenye Kambi sidhani kama itaongeza sana kwa sababu ni makaratasi ya nembo na kitu gani, lakini angalau itaweza kusaidia

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ambacho nimekipenda ni Tax Ombudsman, hii ni nzuri na inaweza ikatufaa sana, lakini kuwe na watu impeccable kwa tabia zao, waaminifu wa kutosha, kwa sababu hapo yatakuja yale aliyoyasema Mheshimiwa Japhary unakwenda kupatana, unakwenda kwa tax abuse, matokeo yake watu wanakugeuzia kibao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine nimekifurahia ni kuondosha kodi immediately mtu akianzisha biashara apewe muda wa kujitayarisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine alichokizungumzia ni hili suala lililosemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti kuhusu punda na kodi za punda. Kwa kweli kama tusipoweka vizuri punda wata-disappear na baadaye tutawatafuta kama nyara ya Taifa. Chochote kile kinachowahusisha Wachina it is a big market, kwa hivyo mahitaji yake yanakuwa ni makubwa sana. Labda niseme kidogo kuhusu punda kwa wale ambao hawajui. Punda ngozi yake ikisagwa inatoka powder inaitwa gelatin, gelatin inauzwa kilo dola mia 500 China au Far East kwa ujumla na wao wanaamini ina-regulate menstruation (hedhi), wanaamini inaondosha usingizi, wanaamini inaongeza nguvu za kiume, kwa hiyo kwao ni soko kubwa sana. Kwa hiyo kama hatukuongeza kodi au kutengeneza mazingira kwamba watu ambao wanaweza wakafanya mashamba ya kufuga punda yakawa ni rahisi kuyaendesha, tunaweza baada ya muda tukajikuta kwamba hatuna punda katika nchi hii

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa nataka niseme kwamba, tunasema tunakwenda katika uchumi wa viwanda na uchumi wa kipato cha kati, lakini kuna haja ya kutengeneza mazingira mazuri zaidi ili tuelekee huko. Hali inavyokwenda hivi sasa ambapo bado inaonekana hakuna space kubwa ya wafanyabiashara kutoa maoni yao zaidi ya kwenda kwa Mheshimiwa Rais, tungependa base iwekwe huku kabla ya kumfikia Mheshimiwa Rais, taarifa zinaanza kufika kwa Serikali kwa njia nyingine, kwa sababu Rais hawezi kukutana na wafanyabiashara kila muda mfupi, inachukua muda mrefu sana tuongeze namna ya kutoa maoni wafanyabiashara na wawekezaji ili maoni yao yaweze kufanyiwa kazi, kabla ya kusubiri mpaka Mheshimiwa Rais apate muda.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)