Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Hussein Mohamed Bashe (79 total)

Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa fursa. Awali ya yote, nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha sote salama na kuendelea kulifanya Taifa letu kuwa salama na tulivu pamoja na misukosuko yote ambayo tumekuwa tukikabiliana nayo. (Makofi)
Vilevile nitumie nafasi hii kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Nzega kwa heshima walionipa ya kukichagua Chama cha Mapinduzi na kunichagua mimi kuwa Mbunge wao wa Jimbo la Nzega. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa hotuba aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge. Wataalamu wengi wa utawala wametoa criteria na quality za viongozi ambapo viongozi wa aina mbalimbali na Taifa hili kwa muda mrefu tumekuwa tukiomba kupata kiongozi ambaye ni transformational wa kuweza kutusaidia kui-transform society yetu na kuipeleka mbele. Nitumie nafasi hii ku-copy sehemu ya presentation aliyowahi kuifanya Dkt. Mpango akielezea sifa za kiongozi ambaye ni transformational. Moja ya sifa ya kiongozi ambaye ni transformational ni kiongozi uncompromising katika jambo analoliamini na lenye maslahi ya watu wake. Katika presentation ya Dkt. Mpango alitumia neno moja no gain without pain. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuchangia hotuba ya Rais, wenzetu walisema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano amekuwa akivunja na kukanyaga sheria katika maamuzi ambayo amekuwa akiyafanya sasa. Mimi niseme, moja ya tatizo kubwa linalokabili Taifa letu ni uwepo wa sheria zinazoruhusu watu kuzitumia kuliibia Taifa hili. Sheria hizi zimewapa fursa watendaji wengi kuiibia nchi yetu. Mmeona wizi mwingi ambao umefanyika katika Taifa hili umehifadhiwa katika sheria. Tunahitaji kiongozi mwenye sifa ya Rais Magufuli kuzikanyaga hizi sheria ili tuweze kupambana na wizi wa nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, yalisemwa hapa na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge kwamba Rais amepeleka fedha katika sekta ya elimu bila kuleta mini-budget. Swali tu la mantiki, tulitaka watoto wasiende shule tusubiri Bunge la Februari tuwaleteeni mini-budget mpitishe? Tumeambiwa barabara ya Morocco, fedha zilizokuwa allocated kwa ajili ya sherehe za uhuru zimepelekwa pale bila kufanyika utaratibu wa kumpata mkandarasi. Walitaka tutumie miezi sita kumpata mkandarasi ili barabara ile ijengwe. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niwaambieni, jambo la kwanza ambalo tunatakiwa kulifanya sasa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kaka yangu Mwakyembe kaeni mzipitie hizi sheria hovyo mzilete kwenye Bunge la Aprili tuzifute, Sheria ya PPRA ni wizi mtupu. Leo kujenga tundu moja la choo mkandarasi anakuletea bajeti ya shilingi milioni 25 na imefuata taratibu za evaluation na process zote, kile choo kina nini? Kwa hiyo, nimuunge mkono Mheshimiwa Rais katika hatua anazochukua, Taifa letu liko kwenye dharura, linahitaji aina hii ya leadership ili tuweze kwenda mbele.
Mheshimiwa Naibu Spika, nijikite sasa kwenye hotuba ya Rais. Tumeona political will ya Rais ya kutaka kulifanya Taifa hili kuwa la viwanda lakini yapo mambo ya msingi ambayo tunatakiwa tuyafanye kama Waheshimiwa Wabunge na Watanzania. Jambo la kwanza ambalo naiomba Wizara ya Fedha, nia ya Rais haiwezi kufanikiwa kama Wizara ya Fedha haitakaa chini na kufanya strategic decision ni maeneo gani ya viwanda tunataka kuwekeza ambayo yatakuwa na matokeo chanya kwa watu wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nashauri na ningeomba Waheshimiwa Wabunge na Wizara ya Fedha tukubaliane, nchi hii tunasema ni nchi ya wakulima ni kweli. Hata hivyo, ukitazama takwimu uchangiaji wa sekta ya kilimo katika pato la Taifa kwa mwaka 2014 umeshuka kwa asilimia kumi na nne. Aidha, Watanzania waliokuwa wamejiajiri katika sekta ya kilimo mwaka 2012 walikuwa asilimia 76 leo ni asilimia 66 maana yake ni kwamba Watanzania wamehama kwenye sekta ya kilimo wameenda kwenye sekta zingine. Hii inamaanisha nini? Maana yake tukifanya maamuzi yasiyokuwa sahihi katika uwekezaji wa viwanda, tukaenda katika maeneo ambayo hayatakuwa na matokeo chanya kwa watu wetu wengi, umaskini wa Watanzania utaendelea kuwepo hata tukiwa na viwanda vyingi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili kwenye suala la viwanda, hatuwezi kufanikiwa kwenye suala la viwanda kama hatujamsaidia Mheshimiwa Profesa Ndalichako katika eneo la elimu kuhakikisha kwamba tunawekeza fedha nyingi kwenye sekta ya elimu ili ku-improve skills za vijana wetu waweze kwenda kusaidia uzalishaji katika viwanda. Tusipohakikisha kwamba elimu yetu inatoa majibu sahihi kuweza kufikia lengo la viwanda, matokeo yake ajira nyingi za viwanda hazitachukuliwa na Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nawaomba Waheshimiwa Wabunge, tukaipa kipaumbele Wizara ya Elimu na kuiagiza Wizara ya Elimu ije na mpango mkakati wa namna gani technical schools zetu kama vyuo vya VETA vitatoa wanafunzi ili waweze kwenda kuajiriwa katika sekta ya viwanda vya Agro Based Industries. Hivi ndivyo viwanda ambavyo vitatuondolea matatizo. Textiles Industries, hivi ndivyo viwanda ambavyo vitaajiri vijana wetu wengi. Tunaotoka katika maeneo ambayo pamba inalimwa mmeona wakulima wamepoteza matumaini. Tukiongeza jitihada katika viwanda vya textiles, mazao ya pamba yakawa processed katika viwanda vyetu, wakulima wetu watakuwa na moyo wa kufanya kazi, watakuwa na soko la uhakika na hii itasaidia sana nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo tunazungumzia viwanda lakini hakuna jambo la msingi kama infrastructure ya reli. Nimeangalia Mpango wa Maendeleo wa mwaka mmoja, Waziri amesema tutajenga reli ya standard gauge. Habari ya kujengwa reli imekuwepo kabla mimi sijaja hapa Bungeni, nimekuwa nikiisikia, niwaombe Wabunge, bajeti itakayokuja kama haitatuambia imetenga fedha kiasi gani za kujenga reli ya standard gauge, tusikubali kuunga mkono bajeti hiyo. Kama bajeti ya Serikali itakuja bila suala la reli kupewa kipaumbele cha kutosha tusikubali kuunga mkono.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunapozungumzia suala la uzalishaji wa viwanda, tumsaidie Mheshimiwa Profesa Muhongo. Leo 41% ya uzalishaji wetu wa umeme wanazalisha Independent Power Producers na tunanunua umeme kwa shilingi ngapi, ni ghali. Kwa hiyo, tuisaidie Serikali uzalishaji wa gesi uweze kutusaidia kama nchi. Tufanye maamuzi ya lazima, haya mambo ya 100% owned by private, anakuja anatumia gesi yetu, sisi hatu-own stake katika huu uzalishaji, ameenda kukopa nje hatumsimamii alikokopa, bado tutaununua umeme kwa bei kubwa. (Makofi)
NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Bashe muda wako umekwisha.
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hotuba ya Mheshimiwa Rais. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa fursa ya kuchangia. Nianze kwa kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa kutufanya tuweze kuwa salama na tuweze kushiriki kikao hiki cha siku ya leo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kuwapongeza Mawaziri na nawapongeza kwa jambo moja la msingi. Zamani kabla sijaingia Bungeni nilikuwa nasikia kwamba kumfikia Waziri ni kazi ngumu kweli, lakini Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano naona ni Mawaziri reachable, ni rahisi kuwafikia. Binafsi niwashukuru kwa dhati kabisa Waziri Mheshimiwa Simbachawene na Naibu wake Mheshimiwa Jafo kwa sababu yanayohusu Halmashauri yangu ya Mji wa Nzega wamekuwa wakitoa ushirikiano hata yale ambayo hajakamilika lakini angalau unakuwa una moyo kwamba kesho litakamilika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na jambo la kwanza. Halmashauri ya Mji wa Nzega ni mpya, lakini kwa muda mrefu kwa lugha ambayo nimeisikia Serikalini inalelewa na Halmashauri ya Wilaya ya Nzega. Kwa maana kwamba bajeti ceiling zake zinakuwa zikipitia Halmashauri ya Wilaya ya Nzega. Mheshimiwa Waziri anafahamu matatizo yanayoikabili Halmashauri ya Mji wa Nzega, fedha za OC mnazopeleka Halmashauri ya Mji wa Nzega zinazopitia Nzega DC hazifiki katika Halmashauri ya Mji wa Nzega. Inakuwa ni unfair kwa watendaji walioko pale, Serikali Kuu ina disburse fedha kwenda kwenye Halmashauri ya Mji wa Nzega kupita Halmashauri ya Nzega DC kwa sababu tu ceiling na vote ya Halmashauri ya Mji wa Nzega ilikuwa chini ya Halmshauri ya Wilaya ya Nzega. Mpaka leo fedha mlizotuma kwenda Halmashauri ya Mji wa Nzega 56 million shillings ambazo ni za OC zimetumika katika Halmashauri ya Wilaya na Halmashauri ya Mji haijapata zile fedha, ni tatizo kweli.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Halmashauri ya Mji wa Nzega ipewe vote yake, ijitegemee, ina wafanya kazi wake, ina vyanzo vyake vya mapato, ina kila kitu, for how long Halmashauri ya Mji huu itakuwa chini ya Halmshauri ya Wilaya ya Nzega, ni mateso. Leo hii fedha za Mfuko wa Jimbo la Nzega Mjini tunashindwa kuzipata na hili siyo suala la Wabunge ni la watendaji walioko pale hawako flexible kutumia taratibu zilizowekwa ili fedha zile ziwe disbursed kwenda kwenye Halmshauri ya Mji wa Nzega, hili ni ni tatizo. Nakuomba Mheshimiwa Simbachawene, Halmashauri ya Mji wa Nzega muiondoe kwenye kwapa la Halmashauri ya Wilaya ya Nzega. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo vyanzo vya mapato vya Halmashauri ya Mji wa Nzega vinakusanywa na Halmashauri ya Wilaya kwa hoja kwamba fedha hizi zitahamishiwa katika Halmashauri ya Mji lakini hawahamishi. Kwa hiyo, ningeomba hili jambo litatuliwe kabisa katika Mji wa Nzega. Hilo ni jambo la kwanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, nimeona hapa katika jedwali lililoambatanishwa, Halmashauri ya Mji wa Nzega imetegewa shilingi milioni saba kwa ajili ya kilimo, Halmashauri ya Mji wa Nzega ina kata 10, kata nane zote ni za wakulima na ndiyo zinalisha ule mji lakini tume-allocate only seven million shillings. Bajeti iliyokuwa proposed na Halmashauri ya Mji ambayo tuliomba for development ni 176 million shillings lakini tunapata shilingi milioni saba. Kwa hiyo, naomba mnapo-allocate fedha hizi mnazoweka kwenye majiji makubwa kama Mwanza, Arusha na kwingine kwamba ni ya kilimo hawalimi, hizi fedha pelekeni kwenye maeneo yenye kilimo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mfano katika Mji wa Nzega tuna eneo kubwa la kilimo katika Kata ya Mwanzori, kumekuwepo na irrigation scheme toka miaka ya 1970. Kwa sababu tu hakuna allocation ya resources, sasa hivi ile irrigation scheme katika Kijiji cha Idudumo inakufa. Namuomba Mheshimiwa Waziri waliangalie suala hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ukiitazama allocation ya funds kwenye kilimo kwa Wilaya zote za Mkoa wa Tabora imetengwa 198 million shillings. Mkoa wa Tabora unalima tumbaku na kwa mwaka jana tumbaku ime-contribute over three hundred million US dollars kwenye pato la Taifa, tunawapelekea shilingi milioni 180. Ukiangalia fedha zilizokuwa allocated kwenye Wizara ya Kilimo na zenyewe ni masikitiko. Najua kasungura kadogo wekeni priority sehemu ya kuzi-allocate.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais alipofika katika Mji wa Nzega wakati anaomba kura tarehe 14 Oktoba, 2015 aliahidi mambo makubwa mawili. Jambo la kwanza katika Mji wa Nzega tuna tatizo sugu la maji, tukamuomba Mheshimiwa Rais kwamba kutatua tatizo la maji katika Mji wa Nzega wakati tunasubiri mradi wa maji wa Ziwa Victoria, kwanza nimwambie Mheshimiwa Waziri wa Maji akija hapa atuambie ni lini mradi wa Ziwa Victoria utaanza kwa ajili ya Mkoa wa Tabora. Wasiposema specifically ni tarehe ngapi mkandarasi anaingia pale mimi nitakuwa mmoja kati ya Mbunge wa Chama cha Mapinduzi ambaye hataunga mkono bajeti ya Serikali kwa sababu mradi huu umejadiliwa mwaka 2013, 2014 na 2015.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais, wakati anajadili suala la maji alitupa shorten solution, katika Mji wa Nzega tunahitaji pampu na matenki matano, ukitazama allocation ya maji iliyowekwa ni shilingi milioni nane. Nikiangalia fedha zilizokuwa allocated Wizara ya Maji hazitatui kabisa tatizo la maji la muda mfupi Nzega. Leo tunatarajia maji kutoka Bwawa la Kilimi, chujio liko Bwawa la Uchama, kwa hiyo vijiji vyote vinavyotoka Kilimi mpaka Uchama ambako tunaenda kusafishia maji hawapati maji. Naiomba Serikali kwa heshima kabisa tunapo-allocate hivi vitu kidogo kidogo hatutatui tatizo. Ni lazima tulitatue tatizo kwa ujumla wake.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ningeomba ahadi ya Rais ya kufunga pampu ya maji katika Bwawa la Kilimi na kujenga matenki matano katika Mji wa Nzega ili kutatua tatizo la maji wakati tunasubiri utekelezaji wa mradi wa maji wa Ziwa Victoria itekelezwe na tuone commitment ya Serikali katika jambo hili. For good news, nimwambie Waziri wa Maji yupo hapa kwamba kwa kuwa Rais alisema mkandarasi atakaa pale Nzega kwa sababu ni njia panda kupeleka maji Singida na Tabora, sisi Halmashauri ya Mji wa Nzega tumetenga eneo ambalo Serikali haitataka fidia yoyote hata shilingi kwa ajili ya kuja kumkaribisha huyo mkandarasi ili aweze kukaa pale na kufanya huu mradi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nilimsikia Mbunge mwenzangu mmoja hapa anaongea simkumbuki nadhani ni Mheshimiwa Sannda, namuomba Mheshimiwa Naibu Waziri Jafo na Waziri Mheshimiwa Simbachawene, leo tunaenda kuwaambia wananchi wachangie madawati, wachangie ujenzi wa maabara, Nzega zimeliwa 2.2 billion shillings zilizotolewa na Mgodi wa Resolute ambazo zilikuwa allocated kwa ajili ya ujenzi wa maabara.
Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla aliandamana, alipigwa mabomu, aliwekwa jela ndiyo akapata hako kasungura ka shilingi bilioni 2.2 kalivyoenda Halmashauri waliopiga deal mwingine mme-promote ndiyo kawa Injinia wa Manispaa ya Kagera. Huyu mtu aliharibu Ilala, akahamishiwa Nzega and Nzega is a dumping place kwenye local government, zikaja 2.2 billion shillings akapiga yeye na wenzake maabara zilizokuwa allocated 68 million shillings hazijafika hata kwenye lenta, akahamishiwa kuwa Injinia wa Manispaa ya Kagera, yupo pale.
Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Mji wa Nzega, tena Mheshimiwa Waziri Mkuu nisikilize, aliyekuwa Mweka Hazina wa Halmashauri ya Sumbawanga ana kesi ya uhujumu uchumi akapelekwa Magu, akapata kesi ya uhujumu uchumi, leo kahamishiwa Nzega. Leo tumemkamata yeye na network yake wakiiba fedha za parking, wenzake wamewekwa ndani yeye anazunguka pale, this is unfair. Halafu tunaenda kwa wananchi kuwaambia watuchangie fedha za maabara, mimi nimewaambia wananchi wangu wa Mji wa Nzega hakuna kuchanga fedha ya maabara mpaka wezi wapelekwe mahakamani tutafunika maabara zilizobaki. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, kwa masikitiko kabisa, dhamira ya Rais kumpatia kila mtoto wa nchi hii elimu bora ni dhamira njema, tuione kwenye commitment ya Serikali katika allocational of resources, tumefanya mass expansion ya elimu. Hata ukisoma Mpango wa Miaka Mitano, Waziri Mpango anakiri kwenye document yake kwamba quality ya elimu yetu ni tatizo. Niiombe Wizara ya TAMISEMI, kwa sababu kwa sasa hivi dhamana ya ku-expand infrastructure iko mikononi mwenu, jamani tengeni fedha ya kujenga infrastructure ya elimu, tukiuacha huu mzigo kwa wananchi peke yao hawawezi, tuiombe central government. Nishukuru nimepokea madawati 250 nadhani ni chenji ya rada, nashukuru kabisa na nimeyapokea yako pale. Nitumie fursa hii kushukuru institution ambazo zimetusaidia katika Mji wa Nzega, tumepata madawati 600 kutoka TEA…
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja, ahsante.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia. Kwanza nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa fursa sote kuamka siku ya leo na kuja kutimiza wajibu wetu wa kisheria.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Kanuni ya 106 imesema wazi hatuna mamlaka ya kubadilisha chochote katika bajeti ya Serikali, kwa hiyo niseme, tunachofanya hapa ni kushauri ili mengine yachukuliwe yaweze kufanyiwa kazi kwenye mwaka wa fedha 2017/2018; lakini mengine itakapokuja Finance Bill ili tuweze kuitumia kuitaka Serikali kufanya mabadiliko katika baadhi ya maeneo, hilo ni jambo la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, nishukuru Wizara ya Fedha. Nimeangalia document ya mpango ambayo ilizinduliwa juzi, nimeangalia hotuba ya hali ya uchumi, yapo yale ambayo tumekuwa tukiyasema katika Bunge la mwezi uliopita wakati tunajadili mpango na yapo ambayo tumeyasema katika kipindi hiki wameanza kuya-accommodate. Jambo ninaloshukuru kutoka Wizara ya Fedha, ni kauli ya Waziri kwenye Hotuba yake ya ku-acknowledge kwamba mpango wetu wa mabadiliko kwenda kwenye sekta ya viwanda, wata-accommodate viwanda vinavyotokana na mazao ya kilimo, hili ni jambo la kheri kabisa. Kwenye maisha kutambua na kutekeleza ni vitu viwili. Hatua ya kwanza ni kutambua na ya pili ni kutekeleza. (MakofiI)
Mheshimiwa Naibu Spika, nina baadhi ya mambo ambayo nataka nishauri na tutumie Finance Bill kuweza kufanya hayo mabadiliko.
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ya Serikali kwenye msamaha wa mazao yasiyosindikwa; ningeomba, athari ya jambo hili ni kwa wananchi. Lengo ni kuongeza uzalishaji wa mazao, wametolea mfano, soya, mbogamboga, lakini mazao haya yakisindikwa tu yanakutana na kodi. Hapa ina-work against vision ya Mheshimiwa Rais, kwa sababu mkulima kalima mboga mboga hawekewi kodi, lakini akienda kuisindika anakutana na kodi, hili ni tatizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitolee mfano wa alizeti. Tukipeleka alizeti kiwandani ikawa processed inakutana na VAT, maana yake mafuta haya ya alizeti hayamsaidi mkulima wetu kwenye value addition, tuna mu-encourage mkulima auze raw, hili ni tatizo. Ningeomba hili tusilipitishe Waheshimiwa Wabunge. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ingekuwa inaonesha value addition kwa maana ya kwamba tunafuta kodi zote kwenye mazao yatakayosindikwa maana yake tunashauri na kushawishi wananchi wetu kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo ili mazao wanayolima yaingie kwenye viwanda, wauze finished goods; hili ni eneo moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, tozo kwenye huduma za utalii. Competitors wetu wote dunia au kwenye masoko ya jirani kwa maana ya Kenya, Msumbiji, South Africa bado Tanzania itaendelea kuwa the most expensive destination. Kwa hiyo, ningeshauri Waheshimiwa Wabunge, tusipitishe hii VAT ambayo inachajiwa kwenye utalii kwa sababu haitosaidia kabisa sekta ya utalii, bado destination yetu itaendelea kuwa ghali.
Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na ripoti aliyoisoma Mheshimiwa Waziri, mkitazama Sekta zilizochangia kukua kwa uchumi wa nchi yetu mojawapo ni tourism; ya pili ni usafiri; na ya tatu ni financial services. Sekta zote hizi tumeziwekea kodi, tunatarajia kweli huu uchumi uta-grow kwa 7.2? Nina mashaka, sioni kukua kwa 7.2 kama tutaweka hizi kodi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii Beira, Mombasa, wamefuta kodi za ongezeko la thamani, kwenye goods on transit; sisi tumeweka, nini tunatarajia? Maana tume- tighten taratibu zetu za kukusanya kodi bandarini, ni jambo jema sana, lakini tunaweka kodi, kuna uwezekano wenzetu waliofuta, watu wakakimbilia kule. Kwa hiyo, ningeshauri Serikali ikaachana na kodi hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, kaka yangu Mheshimiwa Zungu kaongelea kodi ya mitumba, niwaombe hatuna viwanda vya nguo vya ku-meet mahitaji ya nchi yetu, lakini tukiweka kodi kwenye mitumba, tuna discourage importation ya mitumba, tutaua small business, tutaua soko la pale Dar es Salaam, Wamachinga wanaojitafutia riziki barabarani, matokeo yake tutaongeza vibaka barabarani. Tujenge kwanza uwezo wa kuzalisha nguo ndani ya nchi ndipo tu-impose kodi kwenye hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Serikali itasema; na mimi hili kidogo nina mashaka Mheshimiwa Waziri. Serikali itasema inatoa wapi fedha? Kwa sababu hizi kodi zina budgetary implication. Ushauri, yapo maeneo ambayo hamna sababu ya Dkt. Mpango kuchukua fedha kutoka kwenye Mfuko wa Hazina kuyahudumia:-
Moja, tumetengea hundred and sixty one billion Shilling, kwa ajili ya kununua vichwa vya treni na mabehewa, ningeshauri kuna sheria zinakuja kwa mwendokasi huku, tutaletewa hapa. Leteni moja ya sheria ya RAHCO, tuifute RAHCO iwe chini ya TRL. TRL ikakope fedha hizi; kwa nini tukulazimishe Mpango uwape cheki ya one sixty one billion TRL wakati wana uwezo wa kujiendesha?
Mheshimiwa Naibu Spika, mwondoeni huyu mzimu unaoitwa RAHACO hili ni chaka la wizi. Mwekeeni hizi mali zote TRL, ataenda kukopa kwenye financial institution. Nimwambie Mheshimiwa Waziri, ana one of the best CEO kwenye TRL Masanja, ametoka Private Sector anajua hela, anajua biashara, amwezeshe kwa kumletea hiyo sheria. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna kodi ya kiinua mgongo cha Wabunge, nataka niishauri Serikali na nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge, Serikali hapa imetuletea kamtego kutaka kutochonganisha na wananchi, kwamba tunajipendelea. Sheria ya The Political Service Retirement Benefit Act ya mwaka 1999, section 24(2) imeelezea exemption; subsection (4) imewa-define those leaders waliopewa exemption, nataka aniambie Waziri wa Fedha kama kweli tunataka kuwa fair kwa nini kamwacha Mheshimiwa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya? Mimi nasema Wabunge tulipe kodi, lakini wawekeni wote.
Mheshimiwa Naibu Spika, it is unfair kutuchonganisha na wananchi, Majaji why not? Wawekeni wote walipe. It will be fair mbele ya macho ya sheria, itakuwa fair mbele ya kila mtu kwamba tunalipa kodi wote kama tumeondoa exemption, achene kufanya division; msitu-divide, wawekeni wote walipe. Eee na Naibu Spika na Spika wote tulipe. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Fedha determination na dhamira yao ya kupeleka asilimia 40 ya fedha ya maendeleo kwa wananchi, ni jambo jema sana, lakini nataka niwaulize swali, hivi unapelekaje fedha Halmashauri ya Nzega, halafu CAG umemkata miguu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimesikia kengele, aaa, ya kwanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, dada yangu Neema kanipa dakika zake.
Eee nashukuru. Mheshimiwa Naibu Spika, tumepeleka 40 percent ya fedha za umma…
Mheshimiwa Naibu Spika, Neema Mgaya, dakika tano.
Mheshimiwa Naibu Spika Ahsante. Waziri Mpango, Hazina, TRA; wanakimbizana barabarani kukusanya fedha wanapeleka 40 percent ya fedha za maendeleo kwa wananchi; jambo jema lakini mnapelekaje fedha bila kumwezesha watchdog? Watch dog wa Serikali na Bunge hili ni CAG, lakini tunampunguzia fedha. Halafu tumempunguzia fedha wanahitaji taarifa za CAG ili wakazitekeleze mfano TAKUKURU tumewapa 72 billion, how? inakuwa vice-versa hii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ningeshauri Serikali na Waheshimiwa Wabunge; Waziri Mpango aliulizwa swali hapa akasema kwamba CAG akiishiwa atakuja kugonga mlango; jamani! Yaani wanataka aende kugonga mlango kwake, Mzee nimeishiwa hela ya mafuta na yeye atampa kutoka wapi Mheshimiwa Waziri?
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ningeshauri CAG aongezewe fedha; zinatoka wapi? Zile bilioni 161 tulizokuwa tukanunue mabehewa na vichwa vya treni tuchukue fedha kule kwa sababu hakuna sababu, RAHCO ivunjwe, TRL wakakope twende huko. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, nashtuka kidogo. Kwenye bajeti ya mwaka 2015/2016 inflow expectation kutoka kwa donors ilikuwa 2.14 trillion Shillings, lakini tuliyopokea ni 65 percent only. Mwaka huu kwenye bajeti tumeongeza kwenda 3.7 trillion. Najiuliza kama zile za mwaka jana wale wale development partner hawajatuletea, tuliyotaka kukopa kwao hawajatupa, mwaka huu kuna muujiza gani watupe three trillion Shillings? Nini madhara yake? Target mliyojiwekea mnaweza msiifikie. Ningeshauri m-review hii, simameni kwenye 1.4 ambayo mliipata mwaka jana. Mkipata ziada ni kheri, lakini ni afadhali kupanga yale ambayo tunaweza kuyafanya.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeweka kodi kwenye crude oil, tunataka tumsaidie huyu mwananchi wa chini, lakini kwenye mafuta ya alizeti yanayosindikwa pale Singida na Shinyanga tumeweka 18 percent, yanayokuwa imported tumeweka kodi, huyu mwananchi wa Nzega ananunua haya mafuta kwa bei ghali. Hatuna sababu ya kuweka kodi kwenye crude oil, wala hatuna sababu ya kuweka kodi kwenye mazao ya kusindika; hasa ya chakula na mafuta.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Mheshimiwa Waziri, kwenye bajeti ametenga, ingawa nimeona kwenye kitabu cha maendeleo ni one trillion ya standard gauge; lakini kwenye hotuba amesema 2.4 trillion, kidogo nashindwa kuelewa. Hata hivyo, nauliza hivi, hivi ni lazima kweli 15 percent ya commitment ya nchi tuweze kutumia fedha zetu za ndani kuweka?
Mheshimiwa Naibu Spika, ningeshauri Serikali iangalie uwezekano, pamoja na kuwa tunajenga reli ya kati, ambayo mimi naiunga mkono, reli ya kati ya mtazamo wa Kitanzania hatuna sababu ya kutumia fedha zetu za mfukoni kufanya hili jambo; hebu tuangalie option ya PPP kama itawezekana, lakini jamani kuna uwezekano wa concession, why should we go for our pocket every now and then? Ningeshauri Serikali kuwaza kufanya kila kitu kutoka mfukoni kwake.
Mheshimiwa Naibu Spika, ameongea Mheshimiwa Profesa Norman na Mheshimiwa Zungu kuhusu suala la ku-impose kodi kwenye transfer ya share. Wenzetu wamefuta halafu bahati mbaya tumeweka kwa foreigners 20 percent, kwa wa ndani 10 percent na ukiangalia listed companies pale ni chache, matokeo yake hawa watu watakimbilia Nairobi Stock Exchange, watakwenda kule kwa sababu kuna incentive. Ningeiomba Serikali, dhamira ya kukusanya ni njema, lakini nakuomba Mheshimiwa Waziri kodi isiwe ni ya kukusanya tu itumike kama stimulus kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Ahsante sana.
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016/2017 – 2020/2021
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nitumie fursa hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutupatia fursa sote kukutana katika kikao hiki, lakini nitumie nafasi hii vile vile kumpongeza na kumtakia kila la kheri Rais wa Awamu ya Tano.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka tu niseme ujumbe mmoja kuna popular speech aliwahi kuitoa Baba wa Taifa Mkoani Tabora, ambayo alikuwa anazungumzia historia na hadithi ya vijana wanaokwenda kuchumbia kwa binti mzuri lakini wakawa wanazomewa zomewa ukigeuka unageuka jiwe. Kwa hiyo, nimwombe tu kelele nyingi zinaweza zikawepo, asikubali kugeuka jiwe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa masikitiko, masikitiko yangu ni kwamba, ni aidha kuna disconnection kati ya vision na mwelekeo wa Rais na walio chini wanaoandaa Mipango mikakati kufikia vision hiyo. Jambo la kwanza ambalo naona wengi wetu tunaimba viwanda, viwanda, tunasahau kwamba viwanda ni matokeo ya efficiency ya sekta zingine, ndiyo tutapata viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nature ya nchi yetu hakuna viwanda kama sekta ya kilimo haitopewa kipaumbele kinachostahili, hakuna viwanda kama sekta ya usafirishaji haitopewa kipaumbele kinachostahili na nianze kuwaambia Wabunge wenzangu tunaosema reli ya kati tunapongeza, hakuna reli ya kati. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesoma kitabu hiki nendeni ukurasa wa kumi na saba mkasome, naomba ninukuu construction of new Central Railway Lane to standard gauge, ukienda chini sehemu inayosema this project is facing number of challenges as follows. Kipengele namba tatu, the choice of route that is Dar es Salam, Tabora, Kigoma with branches to Tabora Mwanza, and Kaliua - Mpanda, Dar es Salaam – Isaka – Kigali – Keza - Msongati has not been decided, and this is the railway we want.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatutaki railway ya project ya ADB, inayotoka Dar es Salaam kwenda Isaka, kwenda Keza, this does not help this country na niwaombe wenzangu wa Kanda ya Ziwa na Mikoa inayopita reli, hakuna reli yetu, haipo! Hilo ni jambo la kwanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, nimesoma Mpango wa Serikali, Mpango wa Mwaka Mmoja unatokana na Mpango wa Miaka Mitano. Serikali inataka kufufua General Tyre, mmeshafanya study kujua kwa nini General Tyre ilikufa, you are going to allocate two billion shillings kwa ajili ya General Tyre.
Swali la kujiuliza hii General Tyre ni wangapi wamewekeza, nendeni kwenye rekodi NSSF iliwekeza nine billion shillings imeshindikana kufufuliwa kile kiwanda, leo mnapeleka fedha za walipa kodi kwenda kuwekeza kwenye dead project lakini study zipo, wamekuja wawekezaji na Waziri Mwijage anajua, wameomba wawekeze sixty billion shillings kwa ajili ya kufanya investment kwenye kile kiwanda, leo mnataka kuchukua fedha za umma kuweka hapo, this is wrong thinking. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema tunawekeza ATC, hebu jamani tufanye study airline industry, Kenya Airways ambayo partner wake ni KLM mwaka jana wame-register two million U.S dollar loss. South African Airline kila mwaka inapoteza one million U.S dollar, sasa hivi wanataka kuunganisha Airlines tatu ku-streamline operation zao, sisi ATC toka Mwalimu Nyerere, kaja Mzee Mwinyi, kaja Mzee Mkapa, kaja Mzee Kikwete tumeshindwa ku- revive!
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba Serikali fedha za umma kupeleka kununua ndege is wrong direction, lazima tufanye business sense decision siyo kila maamuzi jamani ya kisiasa. Hizi ni fedha za walipa kodi, fedha hizi tuzipeleke kwenye huduma za jamii, fedha hizi tuzipeleke kwenda ku-revive Textile Industry, Mwigulu hayupo hapa, yupo nimemuona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Mpango wa Mwaka Mmoja, ukisoma Mpango wa Miaka Mitano, hapa wanazungumzia C to C na hakuna strategy, wanaelezea tu cotton to clothes, hawasemi wanafanya nini, there is no investment kwenye cotton. Niwaambieni watu wa maeneo tunayozalisha pamba hakuna investment kwenye Mpango wa Miaka Mitano, hakuna investment kwenye Mpango wa Mwaka Mmoja. Hatuwezi ku-revive uchumi wa nchi hii kwa kwenda kuwekeza kwenye mpunga, Serikali inatenga fedha kwa ajili ya mpunga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namshauri Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mwigulu, nimekutana nae private as my brother and friend, nchi hii tunazalisha mazao mengi fanya strategic decision. Mazao mengine waachie District Commissioners mahindi, mchele, mbaazi, mananasi tuwaachie kwenye Wilaya. Chukua mazao ya msingi, chukua cotton, chukua kahawa, chukua korosho, chukua katani, chukua tumbaku, mazao haya yata-turn around na kumsaidia Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Mwijage kuweza kufanikisha wazo la kuwa na viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunajadili ufugaji, na-declare interest mimi ni mfugaji, tunajadili kama ufugaji ni jambo la ajabu, mkulima leo akilima heka mbili mwaka kesho akalima heka tatu tunasema growth, mfugaji akiwa na ng‟ombe tatu zikafika saba anaharibu mazingira!
Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa kuwa na mifugo mingi baada ya Ethiopia. Kwa mwaka 2015 Ethiopia kwa tannery industry imewaingizia five hundred million US dollar, leo Kenya wanajenga kijiji cha viwanda vya ngozi, raw material yao sehemu kubwa wanachukua Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, what is the plan? Ukisoma kitabu cha Miaka Mitano Mpango kinaelezea tu tokea tulivyoanza kuzalisha ngozi mpaka tulipofeli, hamna mkakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna umuhimu na mimi nashauri kwamba, kwa kuwa tunataka kujenga viwanda kwanza tukubali kwamba viwanda ni matokeo, ni efficiency ya agro sector ni efficiency ya energy sector, ni efficiency ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mheshimiwa Ndalichako, ni efficiency ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Mbarawa, ndiyo tunampata Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Mwijage! There is no miracle, hakuna muujiza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ukienda pale Mkoa wa Tabora tunalima tumbaku na wakulima wa tumbaku wapo, wanafahamu utitiri wa kodi intermediaries wamejaa kati ya mkulima na mnunuzi kila intermediaries hapa anavuta kidogo mkulima anabaki maskini. Nimeona kwenye Mpango tunazungumzia special zones ambazo tutaweka either viwanda, sijaona Tabora, Tabora tunazalisha tumbaku haijatajwa, ningemwomba Mheshimiwa Dkt. Mpango na Dada yangu Mheshimiwa Ashatu... (Makofi)
MWENYEKITI: Mheshimiwa tunakushukuru kwa mchango wako mzuri, nilifanya makusudi kukuweka wa mwisho kwa jioni ya leo.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuchangia. Jambo la kwanza, ningependa kumwomba Waziri wa Fedha asirudie aliyoyafanya wakati analeta Mpango wa Mwaka 2016/2017. Tutakayomshauri a-take into consideration kwa sababu hii nchi ni yetu sote. Nchi hii siyo ya executive only, ni nchi yetu sote Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili nataka nishauri, ndugu zangu wa UKAWA, nimesoma hotuba aliyoisoma dada yetu Mheshimiwa Halima, kuna a lot of constructive issues. Hii nchi ni yetu sote, mkisema viwanda kizungumkuti kwa maana ya zile abusive language mnatufanya na sisi tuwe defensive na kusahau content mliyoweka ambayo ina substance kwenye maendeleo ya nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi hii iki-develop wote tuna-develop. Kuna mambo mengine mnasema ni ya msingi sana lakini inatufanya tu-defend kwa sababu ya lugha inayotumika. Nimemwambia nje na nasema humu ndani ili iingie kwenye rekodi. Linapokuja suala la Mpango wa nchi tuweke siasa pembeni tujadili Mpango wa nchi. Waziri wa Fedha asipochukua yale tunayoamini ni kwa maslahi ya nchi yetu na watu wetu tuna jukumu la kuungana bila kuangalia vyama vyetu, hili ni jambo la pili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nianze kwa masikitiko, premises alizoziweka Waziri wa Fedha kwa ajili ya msingi wa bajeti anayokuja nayo ni premises ambazo zinatujengea failure. Ukienda ukurasa wa 14, item 2.3.10, ametaja item kama saba ambazo ndiyo msingi wa Mpango na bajeti ya 2017/2018, hii ndiyo pillar. Item ya mwisho anasema, kuwepo kwa sheria na taratibu wezeshi kwa uwekezaji. Ukiangalia taarifa ya Kamati, World Bank Report inatu-rank ni wa 139, doing business in Tanzania is very difficult. Ni jukumu lake Mheshimiwa Waziri akaangalie sheria za nchi hii kama zina-attract investment?
Mheshimiwa Mwenyekiti, item number five anasema, hali ya hewa ya nchi na katika nchi jirani ni nzuri, which is not right! Hali ya hewa ya nchi kwa mwaka 2017/2018 tuna-project kuwepo kwa ukame. Nchi zilizotuzunguka zina hali mbaya ya chakula, taarifa ya TMA inaonesha kwamba kutakuwa na ukame, yeye anasema itakuwa nzuri, we are failing! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, anaendelea kusema, kuendelea kuimarika na kutengemaa kwa uchumi wa dunia, Mheshimiwa Waziri anatoa wapi hii fact? Global trade imeteremka by 0.08! Siyo maneno yangu, ni ya World Bank, ni ya IMF yanaonesha na uki-google report ya World Bank ya tarehe 20 Oktoba, 2016 inasema wazi kwamba bei ya mafuta duniani inapanda, Waziri anasema itaimarika. Tulivyopitisha bajeti iliyopita na bajeti hii mafuta yamepanda kwa zaidi ya dollar 10! Kaka yangu anasema unaimarika, this is very bad! Hii nchi ni yetu sote, tulisema kwenye mpango wa mwezi Februari, tukasema sana kwenye bajeti, yale yote tuliyomshauri humu ndani akaja akatuona humu ndani Wabunge wote hatuna akili, leo tunaathirika kama nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ripoti hii ya Waziri ya Mapendekezo ya Mpango inazungumzia growth ya biashara yetu ya nje by 7.4, very good! Kataja mazao, katani, tumbaku na nyuzi, nimechukua hii document, nimeangalia kwenye agro sector, hakuna sehemu anapanga kuongeza uzalishaji na ku-invest kwenye hizi bidhaa ambazo zimetuingizia fedha, what is this? Anachosema huku na Mpango wake havifanani! Kaka sisi Chama cha Mapinduzi tumewaahidi wananchi, au kwa sababu kaka yangu hajaenda kuomba kura? (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, CEO wa Nokia wakati imekuwa taken na Microsoft alisema, we did not do anything wrong but somehow we lost, sisi tuko excited na historical fact, the world is changing! Tusipobadilika we are going to perish. Soma Mipango, Liganga na Mchuchuma mimi sijaja Bungeni naisikia, iko chini ya NDC, hebu jiulizeni kwenye Mipango, NDC toka lini inapelekewa fedha na nchi hii na mnitajie subsidiary moja iliyo-succeed NDC, nothing! Hakuna subsidiary iliyo succeed! Nashindwa kuelewa what are we thinking? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri anazungumzia, Mungu huyu! Waziri anazungumzia 32, 33 trillion shilling budget, area ya kwanza ni makusanyo ya kodi kuongezeka kwa 16%, maana yake tuna mpango wa kwenda kuongeza kodi na mzigo kwa wananchi by 16%. Tuliwaambia msiweke kodi kwenye money transfer hamkutusikiliza, tuliwaambia msiweke kodi kwenye tourism hamkutusikiliza, tuliwaambia msiweke kodi kwenye maeneo mengi, mnajua matokeo yake? Quarter iliyopita commercial banks zimeshuka profitability by 94%. Implication yake ni moja, income tax itakuwa chini, excise duty zitaporomoka, there is no hope!
Mheshimiwa Mwenyekiti, nini ninachotaka kushauri? Moja, Dkt. Mpango kaka yangu, I respect your academic background; kodi should not be your target kwenye kila jambo. Haina maana kuweka kodi kwenye kila kitu, kwenye maeneo yale yale we are killing the business. Tutumie strategic location ya nchi, nataka nitoe mfano mdogo, it’s not a rocket science, Dubai ime-grow because of airport, tuna best location hapa lakini one of the expensive landing katika dunia hii ni Tanzania, futeni kodi kwenye viwanja vya ndege, fanyeni this is the hub, we will grow! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mnaleta issue ya Kurasini kutengeneza gulio la Wachina mnaua Kariakoo. Maana yake Wachina waje pale waweke bidhaa zao halafu iwe ni free tax kuziweka pale halafu ikitoka ndiyo tuchukue kodi, hatuna hizo control mechanism! If you want to establish a free market with zero tax fungueni soko la Kariakoo waacheni Waswahili wale wauze pale ikitoka tukusanye kodi! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tumekuwa wakusanya ushuru wa Kongo…
(Hapa kengele ya kwanza ililia)
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Muda umekwisha?
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna uwezo wa kutengeneza fedha sana, alisema kaka yangu kwenye Bunge lililopita, Mbunge wa Kahama tuanzisheni soko la madini, yeyote atakayeleta madini yake hapa Tanzania aingize bure, yakiuzwa yakitoka tutapata kodi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuongelea kuhusu agro sector. Nataka niwaambie, tunazungumzia kwamba tunataka kuondoa umaskini, kama hatufikiri sawasawa kwenye kuwekeza zaidi kwenye sekta za kilimo na uwekezaji wetu wa viwanda ukagusa maeneo ya kilimo there is no way tutapambana na umaskini wa nchi hii. Hapa nimesikia Wabunge wanalalamika dawa hamna, Wabunge wanalalamika kuhusu mikopo, nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge, mimi natoka Kamati ya Huduma za Jamii, Kamati ya Guantanamo, ndiyo inayosimamia Sekta ya Elimu na Afya, mtamtoa roho Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla bure, mtamtoa roho Mheshimiwa Ummy, mtamtoa roho Mheshimiwa Profesa Ndalichako, MSD, if we will not rectify our economy hatuwezi kuondoa matatizo ya afya. Sasa kama Wabunge tunataka kweli kusaidia Serikali tu-deal na Wizara ya Fedha. That is the only solution!
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Waziri wa Fedha ha-cherish private sector, wanasheria wanajua kuna kitu kinaitwa law of negligence, huwezi kwenda Kariakoo umeshika burungutu la shilingi milioni 10 unatembea halafu watu wakichukua ulalamike. Tuliacha milango yetu wazi muda mrefu, wafanyabiashara wakatumia opportunity, wakavuta, leo kwa uzembe wetu uliowa-attract wao kukwepa kodi na wizi mwingine ulikuwa masterminded from the Government, it is true!
This is the naked truth. Kwa nini mpaka leo mindset ya Serikali na Wizara ya Fedha ni kwamba business community ni wezi? No one will come to our market. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwape mfano mwingine, Waziri anasema uchumi umekua kwa asilimia 6.7 katika kipindi cha miezi sita ya kwanza na moja ya eneo ambalo limechangia kukua huko ni minerals. Mimi najiuliza sana na nashangaa taarifa zake, najiuliza kuna tatizo Serikalini? Production ya Tanzanite imeshuka by 50% toka tumewauzia wale wahuni ule mgodi, hiyo growth inatoka wapi? Tunasema fedha imekua, imekua kutoka wapi wakati wana-register losses, private sector can not access loans from the financial institution na siyo kwa sababu hawana hela ni kwa sababu hakuna security sokoni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo biashara zina-collapse nchi hii, leo mabenki yanapata hasara. Nataka niitahadharishe Serikali, if we will not be careful na Waziri wa Fedha usipofanya intervention kwenye financial institution, real estate is going down na wengi waliokopa watashindwa kulipa, tutaingia kwenye matatizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa. Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia sote kukutana hapa kutimiza wajibu wetu wa Kikatiba.
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuipongeza Wizara, vile vile nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa jambo moja kubwa sana. Kwa muda mrefu tulikuwa tuna kilio cha reli ya kati. Tulipokuja kwenye Bajeti ya mwaka 2016/2017, Waheshimiwa Wabunge wengi sana tuliijadili reli ya kati ya kutoka Dar es Salaam - Kigoma - Mwanza kwenda Mpanda kwa maana ya reli ya kati yenye tafsiri ya Kitanzania. Kwa hiyo, tumeona jiwe la msingi limeshawekwa na vile vile mkandarasi anaanza kazi. (Makofi)
Mheshimiwa naibu Spika, nianze kuishauri Serikali kwenye hii project. Tunatumia zaidi ya shilingi trilioni mbili kwa ajili ya Mradi wa Reli (Phase I). Ukitazama, kuna lot ya Morogoro mpaka Makutupora, halafu lot ya Makutupora mpaka Tabora. Ninachotaka kuishauri Serikali, kuwa na lot zenye masafa mafupi, cost per unit inakuwa kubwa. Ni vizuri kwa sababu kuna fixed cost whether ni kilometa 100, kilometa 200, kilometa 300, kilometa 600 mobilization cost unaweza ukakuta ni almost the same. Ni vizuri tukaangalia namna gani tunatoa huko mbele lot zinakuwa ni za kilometa ndefu ili angalau gharama iweze kupungua.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, tunatumia fedha za ndani; tunachukua shilingi zetu converting into dollar kumlipa Mkandarasi. Nawaomba Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri na Wizara ya Ujenzi na watu wa TANROADs wapo hapa, waambieni hao Wakandarasi strictly sub-contracting jobs zote zifanywe na local kwa sababu zitasaidia fedha yetu tunayoitoa kubaki ndani. Tusipokuwa makini, tunaweza tukajikuta fedha nyingi zinakwenda nje badala ya kubaki ndani ya uchumi wetu. Hili ni muhimu sana kuliangalia. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nawapongeza watu wa Wizara ya Nishati (REA). REA mkiangalia ilivyoanza, ilianza na foreigners lakini baadaye wali-up grade kuhakikisha sub- contracting jobs zote zinafanywa na local. Lots zilizotoka sasa hivi asilimia kubwa inafanywa na Watanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naishauri Serikali, huu ni mradi mkubwa sana, mkitusaidia kuweka hii condition kwenye kazi na hata tulivyokuwa tunazindua mradi wa maji ya Ziwa Victoria, tumemwomba Mheshimiwa Waziri wa Maji kwamba 600 billions ya mradi wa maji ya Ziwa Victoria, hawa Wakandarasi waliopewa wa kutoka India wahakikishe kazi zote za sub-contracting zinafanywa na Watanzania ili tubaki na fedha ndani. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili katika hili, nataka niishauri Wizara kwamba, mpango wetu ni reli ambayo itatumia umeme na hii ni miezi kama 36. Nawaombeni Serikali, hakikisheni suala la TANESCO na TRL kufikia muafaka namna gani umeme utapatikana. Itakuwa ni hatari sana kwamba tumefika mwisho, mradi umekamilika wa phase ya Morogoro suala la umeme likaanza ku-drag. Kwa hiyo, ni vizuri hivi vitu vyote vikienda vinafuatana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la nne katika hili la mradi wa reli; leteni Sheria ya RAHCO Mheshimiwa Waziri tuifute hapa ndani, haraka sana, ili tuweze kumpa mamlaka TRL. Halafu chagueni financial institutions moja, TIB atafute financial advisor wazunguke duniani kutafuta fedha. Hatuwezi kumaliza huu mradi kwa fedha zetu za ndani tu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nami nina hofu, hata hii phase II anaweza akaomba Mturuki tu peke yake. Kwa hiyo, mtafunga milango ya competition. Watabaki wao kwa sababu wanatu-finance wao, wanaleta mkopo wao kwa kilometa hizo 400 zilizobaki, zitatu-restrict competition.


Mheshimiwa Naibu Spika, tukichukua Benki kama TIB ikatafuta financial advisor mwingine ambaye ni recognised internationally, wakazunguka kutafuta fedha, mtampunguzia kazi Mheshimiwa Dkt. Mpango kutafuta fedha kwenye Mfuko wa Hazina ku-finance hii miradi mikubwa, kwa sababu tuna miradi mikubwa sana ambayo iko katika Wizara yenu, miradi ya ndege na miradi hii ya reli. Tukiamua kuwa strategic miradi hii itatusaidia. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho kwenu ni transfer of knowledge. Nawaomba, hawa Wakandarasi wanaotujengea reli, component ya transfer of knowledge ni muhimu mno. Tutakapokwenda kwenye phase inayofuata kwa sababu tutahitaji kuwa na mabehewa na vichwa vya treni, lazima kuwe na makubaliano kwamba atakayeenda kutengeneza vichwa vya treni na mabehewa, ahakikishe anachukua watu wetu wakati wa kutengeneza ili watakaporudi hapa ndani, hizi kazi za kutengeneza vipuri, assembling zote zifanyikie nyumbani kuliko kufanyika nje. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nawapongeza, mnafanya kazi kubwa sana ya kuifungua nchi na Mheshimiwa Rais ameamua, vision yake it is very costfull. Matokeo ya vision ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Magufuli inaweza ikatuchukua muda mrefu sana kuona matunda yake, lakini I believe baada ya miaka mitano, miaka kumi kazi hizi zinazofanyika sasa hivi matunda yake yataonekana wazi kwenye uchumi wa nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimwambie Mheshimiwa Waziri, mwezi Septemba tarehe 14 Mheshimiwa Rais alituahidi Nzega ujenzi wa kilometa 10. Ahadi hii ilitokea wakati yeye akiwa Waziri wa Ujenzi na Rais Kikwete juu ya ujenzi wa kilometa 10 ndani ya Mji wa Nzega.
Mheshimwia Naibu Spika, nimeangalia kitabu cha Mheshimiwa Waziri hapa hakuna any shillings ambayo imekuwa allocated kwa ajili ya hizi kilometa 10, na ukitazama kwenye bajeti ya 2016/2017, road fund fedha zilizokuwa allocated kwa ajili ya Halmashauri ya Nzega ilikuwa ni milioni 707 lakini tulichopokea ni milioni 190.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nikuombe Mheshimiwa Waziri, na wewe kwenye mwezi Desemba, wakati Rais anaenda Chato, niliongea na wewe kwa simu ukaniambia Hussein sema mbele ya wananchi na Mheshimiwa Rais kwamba daraja la Nhobola na daraja la Butandula tunajenga mwaka huu wa fedha. Shekhe mwaka unaisha, Mheshimiwa Waziri na mwaka huu tumepoteza watu watatu katika mto ule. Mheshimiwa Waziri naomba sana hili jambo lipewe kipaumbele.
Mheshimiwa Naibu Spika, zimekuwepo hoja nyingi sana juu ya priority, na mimi nataka niiombe Serikali, tunapojenga hii reli tufanye cost benefit analysis kwa sababu tunawekeza fedha, ni wapi return on investimate itakuwa rahisi. Mzee Chenge ameongelea northen corridor kwamba wanakwenda speed sana, lakini wanakimbilia wapi? Wanakimbilia wafike Kigali ili waweze ku-benefit na Msongati. Tujiulize kipi kiwe mwanzo? Tufike Mwanza ama twende Kigoma ndio iwe priority? Wizara lazima ifanye hii analysis ili iweze kutuambia Watanzania kwamba tunakwenda Mwanza kwa sababu tuta-benefit mizigo ama tunakwenda Kigoma kwa sababu tuta-benefit mizigo na fedha tulizowekeza kama nchi zitarudi haraka.
Mheshimiwa Naibu Spika, itakuwa ni jambo la upotezaji wa fedha za Watanzania kama tutakwenda Mwanza wakati kuna biashara kubwa Kigoma, Kalemii ama Msongati. Mzigo ulioko Msongati kama tutawahi kufika Msongati kabla ya northern corridor, sisi ndio tutakuwa na competitive advantage kuliko watu wengine. Ni vizuri sana mkafanya maamuzi haya kwa mtazamo wa kibiashara zaidi. Reli si kubeba abiria, abiria ni subsidiary, fundamental ni mzigo unaobebwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie, Mheshimiwa Waziri, kwa heshima kabisa nitakuomba unapokuja kufanya wind up hapa uniambie daraja la Nhobola ambalo imekuwa ni ahadi ya muda mrefu ni namna gani linajengwa. Halmashauri ya Mji wa Nzega na TAMISEMI haziwezi kujenga daraja la Nhobola.
Mheshimiwa Naibu Spika, Tunaweka fedha kwenye Rural Road Agency inayotaka kuanzishwa. Mimi ningeshauri tulitazame sana, TANROADS imekuwa good performer. Kurundika shughuli kwenye TAMISEMI wote tunalalamika, TAMISEMI Elimu malalamiko, TAMISEMI Afya tunalalamika, kila kitu TAMISEMI, ni afadhali tuangalie namna gani Rural Road Agency ni unit ndani ya TANROADS. Kwa sababu safari hii mmeiwekea bilioni 80 hamna kitu haiwezi, lakini TANROADS ina sheria ina vyanzo vyake vya mapato.
Mheshimiwa Naibu Spika, hii Rural Road Agency haina vyanzo vya mapato inapewa kwa hisani, haiwezi kuwa sustainable unless mtuletee sheria hapa. Lakini mimi nadhani kwa technical no how kwa infrastructure iliyopo ni vizuri tukaangalia hii wakala wa ujenzi wa barabara vijijini ikiwa ni sub unit ndani ya TANROADS ambayo inatengewa fedha kwenye bajeti ya TANROADS na TANROADS waisimamie. Kwa sababu TANROADS wana watu, tayari wana ofisi kwenye mikoa na wana kila kitu. Tukianzisha hii agency tutaanza kujenga miundombinu mipya.
Mheshimiwa Naibu Spika nashukuru, naunga mkono hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitumie fursa hii kuwapongeza Waheshimiwa Mawaziri ambao wamebaki kwenye nafasi zao na Mawaziri wapya na Naibu Mawaziri walioteuliwa na Mheshimiwa Rais katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri la hivi karibuni, niwatakie kila la kheri katika kutimiza wajibu wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2016 wakati tunajadili mpango ndani ya Bunge hili nilimtahadhalisha Waziri wa Mipango nikimwambia kwamba mpango unaouleta hatutofikia economic growth ya seven percent kwa sababu Mpango huu unaacha sehemu kubwa ya Watanzania nje, sio mpango inclusive. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2016 wakati tunajadili Bajeti nilirudia maneno haya na mwaka huu wakati tunajadili Bajeti nilimwambia kuna conflict kati fiscal policy ambazo Wizara za Fedha inazisimamia na monetary policy these two policies zinapambana zenyewe na matokeo yake yataonekana. Naomba nitumie takwimu zifuatazo kama alivyosema Ndugu Serukamba uchumi wowote duniani una mirror (kioo) na kioo cha uchumi wowote unaokuwa ama unaosinyaa ama unaoshuka moja ni financial Institution, mbili ni
trade, tatu ni stock exchange. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, personal landing mwaka 2015 ilikuwa ni 50% today ni 8.9 percent. Trade ilikuwa ni 24% this is a landing to trade ilikuwa 24%, leo ni 9% na maneno haya siyatoe kwingine ni ripoti za BOT na quarterly report ya BOT ya inayoishia Juni, lakini taarifa zingine ni mwongozo wa Bajeti alioleta yeye na ni mpango wake aliouleta yeye. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, agriculture leo ni negative nine from six percent land capacity ya mwaka 2015, manufacturing from thirty percent landing to three percent, transport and communication from twenty four percent landing to negative twenty five, bulding from twenty two to sixteen. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, our economy it is said inakua, ukisoma projection ni 6.8. Lakini taarifa ya mwisho ya economic bulletin for the quarter ending June, 2017 imetuambia ni 5.7 sio maneno yangu. Food inflation lets go categorically its 10.1 percent sio maneno yangu taarifa ya Septemba ya BOT hii hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, why are we facing this, it’s not a rocket science. Waziri wa Fedha ukurasa wa sita wa Mpango unasema export naomba iingie kwenye Hansard ya Bunge. Nimeangalia taarifa za monthly za BOT toka mwaka 2011 mpaka Septemba mwaka huu, for the first time in the history hamjaweka performance export and imports, why? Mnaficha nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, alisema ndugu Abdulrahman Kinana, wakati anaongea katika function ya Kigoda pale Universty of Dar es Salaam alisema hivi namnukuu, Katibu Mkuu wa chama chetu; “Jambo muhimu la kiongozi ni kusikiliza watu wake.” Viongozi hamna monopoly right wisdom, viongozi hawana monopoly right ya trueth, viongozi hawana monopoly right ya wao wako sahihi kila siku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna jambo muhimu katika kupanga mipango yoyote duniani kama takwimu. Ukurasa wa saba wa document ya mapendekezo ya Mpango unaonesha mwenendo wa ukuaji wa Pato la Taifa toka mwaka 2011 hadi 2017, 2011 our growth was 9.1 percent. Today its projected 6.8 lakini as per this report ni 5.7.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ninukuu maneno yafuatayo , ukurasa wa saba unasema; kufikia Juni, 2017 export zilikuwa zimeshuka kwa asilimia 29.8. Lakini Waziri anatupa a counseling statement kwamba matarajio ni kurejea kwa exportation, kuongezeka eti kwasabbu tunajenga kukuza viwanda sasa twendeni tukasome hivyo viwanda vya export, siyo maneno yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Mpango Waziri ametaja viwanda, ukurasa wa 26, kiwanda cha kuchenjua madini kulichopo Geita, kusindika nyama Kisivani Shinyanga- Mitobotobo Farmers Company Limited, kuzalisha mafuta ya kula, kuchambua pamba, kiwanda cha kuzalisha vifungashio (Global Packing), kiwanda cha kuzalisha vinywaji baridi (Sunny Food Company - Sayona) hivi ndiyo tuta-export kurudisha asilimia 29. Kuzalisha bidhaa za ujenzi; brother tumeahidi kuondoa umaskini wa watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo maneo yangu mimi na- quote maneno ya Waziri wa Mpango. Twendeni ukurasa wa 68 - sekta ya kilimo look at this, hii ndiyo sekta imeajiri asilimia 65 mpaka 70 ya wananchi wetu na tafiti zilizofanyika Watanzania zaidi ya asilimia 80 walioko kwenye sekta ya kilimo yaani ile 70 percent, 80 percent ya hiyo 70 percent inafanya kazi mbili (dual), inalima na inafuga kama siyo ng’ombe, mbuzi, kuku, bata na vitu vya namna hiyo, anafanya dual, now look at this two things.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya mifugo, Serikali imepanga kufanya uhimilishaji, tunahimilisha, kufanya insemination ng’ombe 450,000. Lakini tunapanga kuzalisha chakula hay. Hay ni yale majani ya ng’ombe, tunapanga kuzalisha chakula kwa mwaka hey 445,000 kitakwimu hay moja ina uzito wa kilo 25, chakula hiki ukikigawa kwa siku 360 kinalisha ng’ombe 1,600 huku unapanga kuzalisha ng’ombe 400,000 lakini unaandaa mpango wa chakula ng’ombe 1,600. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa Wabunge wamejadili suala la kilimo, hakuna sehemu Waziri wa Kilimo ana-plan kuanzisha price stabilization ya mazao ya chakula. Leo kuzalisha kilo moja ya mahindi, gharama ya shambani ni shilingi 357, haya siyo maneno yangu, it is scientifically proved, halafu huyu mkulima anayetumia shilingi 357 kuzalisha kilo moja ya mahindi bado gharama ya kupeleka store, gharama ya kuweka mifuko, gharama ya kuweka dawa halafu atakapoweka store yake kuna kauli inasemwa hapa walanguzi ndiyo wana mahindi, this is total misconception ya business principal. Kote duniani kuna producer, kuna distributor, kuna retailer kwahiyo unataka kuniambia mimi ninayelima Nzega-Nata Mahindi yangu niyabebe, niende nikayauze Nairobi? Kuna intermediaries and this is the duty of your fiscal mono-policies kufanya intermediaries wafanye biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikupe mfano mwingine, profitability ya financial institution imeshuka over 50 percent, Waziri ana hoja moja dhaifu sana anaitumia ndani ya mipango. Money circulation imepungua kutoka bilioni 222 mpaka bilioni 12 na hoja anayosema ni nini? Matumizi yasiyokuwa ya lazima ya Serikali yamepungua. Sasa najiuliza bajeti ya recurrent imepungua? Kutoka mwaka 2011, 2012, 2013 imepungua recurrent budget? No, spending ya government ipo, kwa hiyo nilitarajia kwamba itakuwa wisely tutaiona imeleta positive impact, lakini hakuna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ushauri wangu kwa Waziri wa Fedha Mheshimiwa Dkt. Mpango narudia this is the third time, naheshimu your academic background, sijawahi ku-doubt. Kaka hauwezi kuondoa umaskini wa nchi hii bila kuwekeza kwenye kilimo, never. Hauwezi kuleta mapinduzi ya viwanda bila kuwekeza kwenye kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkulima wa nchi hii ndiyo kageuka punching box ya nchi hii. Tuna-control inflation ya chakula kwa gharama ya mkulima, how come? Haiwezekani, hatuwezi kufanikiwa kwa namna hii. Yaani sisi tunadhibiti mfumuko wa bei kwa kumtia umasikini mkulima, aina gani za economy hizi? (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikupe mfano mdogo tena aangalie, hatuwezi kuondoka kwenye umaskini kama mawazo ya Wizara ya Fedha hayatakuwa ni productive oriented badala ya kuwa tax base approach. Angalia Mpango huu unakuwa financed namna gani. Waheshimiwa Wabunge tuchukue document ya Mpango muusome how are we going to finance Mpango. Page number 29 ya muongozo wa maandalizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilindie dakika zangu dakika moja tu. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri anasema kwamba how to finance, anazungumzia kwamba ata-improve EFD machine, ataanzisha maabara ya TRA, it is all about tax base approach. Haumsikii anasema kwamba tutawekeza bilioni moja kwenye kilimo cha mahindi ili tuweze ku-yield X hausikii, hauwezi kukamua maziwa ya ng’ombe usiyemlisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia VAT, Pay As You Earn zimeshuka hazifikii target aliyojiwekea kwenye bajeti ya 2017 na hapa anasema kwamba makampuni yamepunguza wafanyakazi an unajua ni kwa nini? Is not a rocket science, tulimshauri kwenye Kamati ya Bajeti kwamba unaongeza exercise duty kwenye TBL utapunguza uwezo wa uzalishaji wa hawa watu, hakusikia! Tumemwambia kwenye Kamati ya Bajeti I was there. Tumemwambia Waziri wa fedha unaua viwanda vya soft drink kwa ku-impose 10 percent eti kwa udhaifu wao TRA wa kusimamia sukari inayoingia wameweka asilimia 10 tena on top kwa hiyo Coca cola akiingiza sukari kwenye nchi hii analipa 25 percent instead of 15 percent, what kind of economy is this?(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge hasa wa chama changu, tumepewa dhamana ya nchi hii na Watanzania, let not allow mistake za Waziri Mpango kuharibu nafasi ya kuchanguliwa kwa Rais wetu mwaka 2020. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, samahani nikupe mfano mdogo, kampuni zote za vinywaji baridi zilikuja mbele ya Kamati ya Bajeti na sisi tukawaita Wizara ya Fedha, hawana capacity ya kwenda kukagua bonded warehouse, hawana capacity hiyo madhara yake unajua wamefanya nini? Wameamua kuanzisha kodi mpya ya ku-withold. Sasa hivi private sector inadai TRA over eight hundred billion shillings za returns on tax, hawalipi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Wana-sufocate, this is very wrong na mimi nimalizie samahani, kama Waziri wa Fedha hatobadilika hatuwezi kutoka hapa.
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017- Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuchangia.
Jambo la kwanza nitumie fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais, ameongelea suala la sukari huko alikokuwa anaelekea Arusha, kwa sababu jambo hili ni jambo la dharura, ni jambo kubwa, kwa sababu leo tu pale Choma cha Nkola sukari ni shilingi 5,000, Nzega Mjini ni shilingi 4,000, Igunga Mjini ni shilingi 3,200, Kibaha hapo kwenye mzani ni shilingi 3,000.
Kwa hiyo, naiomba Serikali, alichokisema Mheshimiwa Rais huu mchakato wa kuagiza sukari na sukari kuingia nchini, kwa sababu mwezi wa Ramadhani umebaki siku chache na kwa tabia ya soko bidhaa huwa zinapanda sana na moja ya bidhaa ambayo huwa inapanda ni sukari. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kumwambia kaka yangu Mwijage, mimi nitakuunga mkono leo. Bajeti hii nitakuunga mkono, ila ya mwaka kesho ukija kwa style hii sitakuunga mkono. Nasema hivi kwa sababu moja, ukisoma ripoti ya Kamati ya Viwanda na Biashara katika miradi ya kimkakati iliyotajwa na Mheshimiwa Waziri, moja ni kufufua General Tyre. Serikali inataka kutenga two billion, lakini Kamati inasema ili uifufue General Tyre unahitaji shilingi bilioni 60. Bajeti ya Serikali ni bilioni 80! Kwa hiyo, namwonea huruma Mheshimiwa Mwijage, anaenda kufanya muujiza gani? Mimi namtakia kila la kheri. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hivi? Ukisoma hotuba ya kaka yangu Mheshimiwa Mwijage, page namba 43 mpaka 49 anasema uendelezaji wa viwanda vya kimkakati. Kiwanda cha kwanza nachokitaja ni Kiwanda cha Makaa ya Mawe cha Mchuchuma na Liganga ambacho CAG amesema mkataba wake una harufu ya ufisadi, strategic partnership tunayotaka kufanya na hawa Wachina, ina walakini. Nasema namtakia kila la kheri kaka yangu, Mheshimiwa Mwijage.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa pili ni wa Magadi Soda wa Engaruka; mradi wa tatu ni wa Viwatilifu TAMCO Kibaha. Najiuliza swali dogo, nimeamua kwenda hadi kwenye dictionary kutafuta tafsiri sahihi iliyotajwa katika Mpango wa miaka mitano, lakini vilevile iliyotajwa na Mheshimiwa Mwijage, ya nini strategic industries? Strategic industries kutokana na dictionary ya Cambridge inasema kwa kiingereza, nanukuu; “an industry that a country considers very important for economic development.” Hii ndiyo tafsiri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, I am asking myself, kama tunataka kuuondoa umaskini wa nchi hii, ni wapi pa kuanzia? Engaruka? General Tyre? Ukisoma Mpango alichokisema ukurasa wa 62, flagship project, kipengele cha kwanza, anasema maamuzi ya uwekezaji yote yatakuwa based on the countries comparative advantage.
Mheshimiwa Mwenyekiti, my question is, do we have comparative advantage over others in the world, kwenye uwekezaji huu wa kutengeneza matairi? Hili ni swali najiuliza namtakia kila la kheri kaka yangu Mheshimiwa Mwijage. Huo muujiza mwaka kesho niuone. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulisema wakati tunachangia Mpango Bunge lililopita, nchi hii 65% ya wananchi wetu wako kwenye sekta ya kilimo, kwa nini Processing Industries? Ninayo hotuba ya kaka yangu Mheshimiwa Mwigulu, nendeni page namba 23 pamba; mwaka 2013/2014 uzalishaji ulikuwa 245,000; mwaka 2015/2016 uzalishaji ulikuwa 149,000, una nosedive! Uzalishaji unaporomoka! Tumbaku uzalishaji unaporomoka! Kila sehemu uzalishaji unaporomoka. What are we doing?
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kosa letu la kwanza, ni utangulizi wa kauli yetu ya Mpango wa mwaka mmoja; hili ndilo kosa la kimkakati tulilofanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema hivi, naomba ninukuu; “Mpango unakusudiwa kuwa na maeneo ya vipaumbele vinne, viwanda vya kuimarisha kasi ya ukuaji uchumi, miradi mikubwa ya kielelezo, miradi wezeshi kwa maendeleo ya viwanda ikiwemo barabara, reli, nishati, bandari, maji, mawasiliano, maendeleo ya viwanda; maeneo yatakayolenga kufungamanisha maendeleo ya viwanda na watu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema tunataka maeneo yatakayofungamanisha maendeleo ya viwanda na watu, halafu hayo maeneo hatuwekezi. Hatuwekezi kwenye pamba, hatuwekezi kwenye katani, hatuwekezi kwenye korosho, hatuwekezi kwenye alizeti, hatuwekezi popote, halafu tunatarajia muujiza! Nawaombeni Mawaziri, ushauri wangu wa kwanza kwenu, Mheshimiwa Waziri Mwijage kwanza in your mind, wewe ni mtoto, ni matokeo ya wengine. Mkae mtengeneze strategic unit ili muongee lugha moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeangalia hotuba ya Mheshimiwa Mwigulu, nimeangalia ya kwako, nimekata tama. We are planning to fail kaka zangu! Hatuwezi kujadili kufanya revolution kwenye uchumi wa nchi hii bila kuamua kuweka vipaumbele vya maeneo yanayogusa watu. Tutakuja hapa kusema uchumi wetu umekuwa kwa asilimia nane, umaskini bado upo kwa sababu mipango yetu yote inaacha watu wetu wengi nje. Hakuna inclusion! Hatuwa-include watu wengi kwenye mipango yetu; na hili ni tatizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumzia uwekezaji, nataka nikwambie Mheshimiwa Waziri, nenda kwenye database ya Wizara, miaka minne iliyopita kilo moja ya ngozi, raw, kwa mchunaji machinjioni ilikuwa shilingi 3,000 leo ni shilingi 400.
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, tutakutana mwaka kesho, namuunga mkono kaka yangu.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia bajeti hii. Kwanza nianze kwa maneno yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania wanapoenda kuchagua viongozi na wanapoenda kupiga kura ya kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanamchagua mtu ambaye wanamkabidhi dhamana juu ya usalama wao, uhai wao, usimamizi wa rasilimali zao. Huyu anakuwa custodian wa resources zao ambazo wamekuwa nazo walizopewa na Mwenyezi Mungu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais ameunda Tume mbili na ametusomea findings za Tume zake, lakini huko nyuma Marais nao waliunda Tume mbalimbali. Nataka nitumie Bunge hili kuwaambia Waheshimiwa Wabunge wenzangu, vita ya kupambania rasilimali ya nchi hii siyo vita ya John Pombe Magufuli, vita hii ni vita ya Watanzania wote. Naamini kwamba there is no wrong doing in doing right thing, hakuna kufanya makosa katika kufanya jambo jema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana baada ya kuchangia kaka yangu Mheshimiwa Tundu Lissu mimi nilimfuata kwa heshima kabisa ili anipatie maandiko yake. Mpaka saa tisa usiku jana nimekuwa nasoma baadhi ya maandiko yake. Ukisoma ripoti ya Bomani, ukisoma writing alizoandika kaka yangu Mheshimiwa Tundu Lissu na mkononi hapa ninayo kesi ambayo yeye aliisimamia ya mwaka 2006, this country imeibiwa rasilimali zake kwa muda mrefu. Nataka niombe Bunge hili, let’s not be hostage of the history. Bunge hili limefanya makosa, viongozi wetu huko nyuma wamefanya makosa, leo tumepata mtu anayetu-lead kwenda kupambania haki zetu let us join hands with him. Tumnyooshee mkono akishindwa kutufikisha mwisho wa vita hii, not now! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi natoka Nzega, katika kesi hii kaka yangu Mheshimiwa Tundu Lissu anawafahamu akina Mzee Jumbe Kumega, anamfahamu Mama Fatuma Mhina wa Isungangwanda amewa-cite, these are victims. Leo kama Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini ndugu yangu Mheshimiwa Kigwangalla alipigwa mabomu kwa ajili ya Resolute.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeibiwa na kama alivyosema Mheshimiwa Heche jana na mimi nataka niseme leo, Resolute ameondoka na fedha za Halmashauri ya Nzega ten billion shillings za service levy. Jambo la kusikitisha Serikali imeipa kampuni tanzu ya resolute leseni ya kupewa maeneo ndani ya Jimbo la Nzega, Wallah wabillah watallah, kama hamtafuta leseni ya Mwabangu Miners, mimi nitaongoza wananchi I will not care the outcome! (Makofi)

Mheshimiwa Menyekiti, pili, namwomba Mheshimiwa Mpango, yeye ni Waziri wa Fedha, Resolute wana mgogoro na TRA juu ya kodi! Kuna ten billion yetu kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Kalemani anaijua. Nataka kwenye wind up waniambie ten billion ya Halmashauri ya Nzega inapatikanaje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais amesema nasi lazima tumuunge mkono na katika hili la Resolute nitamuunga mkono kwa jitihada zangu zote. Asiponijibu Mheshimiwa Kalemani, kile chuo walichofungua cha madini naenda kuwaambia wananchi wagawane yale mabati, that is all we can get wananchi wa Nzega. Tumeachiwa mahandaki yenye urefu wa zaidi ya mita 1,000, tunaambiwa yatajaa maji baada ya miaka 200 we will not allow this.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme Rais amekuwa mstaarabu sana, angetangaza kufunga hii migodi, leo kuna Diamond Williamson, walichokifanya Diamond Williamson pembeni kuna uchimbaji unaendelea wa kampuni nyingine ya Hilal, yule Hilal kapewa kazi ya ulinzi wa migodi ya Diamond, wanachukua almasi kutoka kwenye mgodi wa Mwadui wanaenda ku-process kwenye mgodi wa Hilal zinaondoka kwa njia za panya, this has been the game for years, this business has to stop! Lazima tumuunge mkono Rais katika hili, tuje tumnyooshee mkono akishindwa kutufikisha mwisho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nijielekeze kwenye hoja ya kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mpango, sina mgogoro mkubwa na yeye this time, namuunga mkono nina mambo machache ya kushauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nishauri kwenye hotuba ya Mheshimiwa Dkt. Mpango; kwenye page namba 50 ametaja sheria anazokuja kutuletea kwa ajili ya kuzifanyia mabadiliko. Sheria ya kwanza ni Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani Sura ya 148. Hapa tunaona dhamira ya Serikali ya ku-link industrialization na fiscal measures za nchi. Serikali inafuta VAT on capital goods ni jambo zuri, namwomba Mheshimiwa Waziri a-extend hii iwe ni capital goods with processing chemicals, kwa sababu chemicals ambazo tutakuwa tuna-import kwa ajili ya ku-process kwenye viwanda bado zitakuwa na import duty tax.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tunapofuta kodi ya ongezeko la thamani kwenye capital equipment tufute na kodi zinazoendana na chemical goods ambazo zitatumika katika viwanda vifuatavyo: Viwanda vinavyohusika na mazao ya kilimo hasa ya nguo, kwa maana ya viwanda vya cotton vinavyo-process nguo ili tu-link na mpango wa Serikali wa cotton to clothes (C to C) ambao umeandikwa na Serikali. Hilo ni jambo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, tufute kodi ya import duty kwenye chemicals zinazotumika ku-process leather industry. Nchi yetu ni ya pili kwa mifugo, itakuwa it is not helping kama hatutaweza ku-take hii advantage, kwa sababu asilimia 65 ya watu wetu wako kwenye sekta ya kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kodi ya pili ambayo nataka nishauri ni kodi ya mapato. Tumepunguza kutoka asilimia 30 kwenda asilimia 10 ya corporate tax, lakini maeneo gani? Ni assemblies ya matrekta na magari. Namwomba Mheshimiwa Waziri, tu-extend hii docket, tutatoa hii fiscal incentive ya asilimia 10 ya corporate tax kwenye viwanda vyote ambavyo vitawekeza kwenye korosho, vitawekeza kenye mazao ya kilimo kwa maana ya kwamba cotton, korosho, kahawa kwa sababu leo korosho yetu yote inakuwa exported raw kwenda India. Hii haitusaidii, maana yake ajira zinakwenda nje. Kwa hiyo, naomba docket hii iongezwe zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Waziri kwenye VAT, leo mkulima wa alizeti akizalisha alizeti, akisindika tu anakutana na VAT. Ningemwomba Mheshimiwa Waziri, ili tuweze ku-gain advantage ya kukua kwa viwanda, iweze kuchukua watu wengi, mazao ya kilimo yanayosindikwa ndani tufute kodi ya VAT katika mazao haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, Sura ya 20, wenzangu wameongelea sana suala la CESS. Mheshimiwa Waziri nataka niwaombe kuna kodi inaitwa services levy ya asilimia 0.03 ya gross income. Kodi hii inakwenda kinyume na principle of taxations, kwa sababu tunachaji kodi kwenye mtaji, sheria hii ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2012 Sura ya 6, tukasema kila Mtanzania mwenye leseni pato lake la mwaka (Gross income) linachajiwa asilimia 0.03, kwanza ina-attract double taxation kwa sababu service levy hii inachajiwa kule juu lakini kwa mzalishaji, vilevile na muuzaji wa Nzega anachajiwa. Tufanye nini? Tuweke dermacation, tutengeneze levels, kwamba service levy ichajiwe 0.01 kwa wafanyabiashara wadogo wenye leseni, corporate wabaki wachajiwe 0.03. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Sheria hii tumei-impose asilimia 10 kwenye crude oil. Najua kuna a lot of politics kwenye suala la mafuta ghafi, lakini ukisoma ripoti ya BOT ya mwezi Aprili re-exportation imeshuka. Nchi za jirani wenzetu wamefuta! Matokeo yake sisi tunakuwa soko la mafuta kutoka Kenya na maeneo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Waziri, udhaifu wa taasisi zetu za kusimamia shughuli wanazowapa usiathiri uzalishaji, kwa sababu sasa hivi ni kwamba kuna udhaifu inawekwa kodi ili ku-discourage kama walivyofanya kwenye sukari za viwanda. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuomba dakika moja kama muda wangu umekwisha. Naomba niongelee kodi ya railway development…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge, muone baadaye Waziri tunakwenda kikanuni.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Awali ya yote nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kumaliza mwezi Mtukufu wa Ramadhan na sasa tumeanza mwezi wa Shawali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kukushukuru wewe na kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa ushirikiano mlionipa wakati nilivyopata msiba, nawashukuru sana na nathamini support yenu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa maneno yafuatayo; Taifa lolote linapopanga bajeti linatengeneza instrument ambazo zitatumika kuisaidia bajeti hiyo kuweza kutekelezwa na wakati huo huo kuchochea uzalishaji na kuisaidia Serikali kukusanya kodi yake. Kwa dhati kabisa, ni mara chache sana nimempongeza Waziri wa Fedha na mimi kwa dhati kabisa safari hii nimpongeze kwa measures alizochukua kwenye fiscal hasa za kikodi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatua ya kwanza aliyoifanya ya kikodi ni maamuzi ya Waziri wa Fedha kutoa amnesty ya kipindi cha miezi sita kwa watu wanaodaiwa kodi, riba na penalties kwa wafanyabiashara, hii ni taswira njema. Wafanyabiashara wengi wamekuwa na malimbikizo na kumekuwa na kesi nyingi za kikodi katika Tax Tribunal ambazo wengi wanapambana na Serikali kupinga either penalty ama interest, Waziri ametoa amnesty, kwamba watu wanaodaiwa kodi anawasamehe riba na penalty kwa kipindi cha miezi sita.

Mheshimiwa Spika, nimwombe Mheshimiwa Waziri utakapokuja kufanya wind-up naomba atoe flexibility ya kumpa Commissioner General wa TRA kwa sababu ndiye yaliye kwenye daily operations aangalie pale ambapo mtu anapokuja na payment plan, either ni ya mwaka mmoja, inategemea anadaiwa shilingi ngapi ili waweze kumpa hiyo amnesty isiwe restricted ndani ya kipindi cha miezi sita.

Mheshimiwa Spika, yeye mwenyewe anafahamu TRA inadaiwa na wafanyabiashara hawana haki ya kudai interests, hawana haki ya kukupiga penalty. Kwa hiyo kama wanavyosema Wazungu, scratch my back I scratch yours, ameonesha good gesture, nakuomba u-extend hii amnesty ili Mtendaji Mkuu wa TRA aweze kufanya maamuzi kutokana na hali halisi ya mfanyabiashara huyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo nataka niseme, wafanyabiashara na it is natural, kutumia loopholes za kisheria kutokulipa kodi na hii siyo dhambi na Serikali inafanya jitihada ya kuboresha sheria zake. Waziri amekuja na Mfumo wa ETS. Moja ya maeneo ambayo wafanyabiashara hutumia nafasi ya ku-avoid kodi ni kwenye VAT. Eneo hili liko connected na production.

Mheshimiwa Spika, nimesikia mawazo ya Waheshimiwa Wabunge, nami nataka nimwombe Waziri, cautions zote zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge juu ya mambo haya, juu ya hii Kampuni inayoitwa SCIPA, zifanyie kazi. Hata hivyo, practice na studies zinaonesha maeneo ambayo hii Kampuni ya SCIPA imewahi kufanya kazi kumekuwa na positive result.

Mheshimiwa Spika, pale ambapo tunajua kwamba wana kesi Morocco ama wamekuwa wana tuhuma ya rushwa, suala la rushwa ni suala la watu. Kama mfumo utaruhusu watoe rushwa ili waweze ku-yield more, it is our weakness, lakini kama mfumo wao huu utatusaidia kufanya production count, kama mfumo wao huu utatuongezea mapato; nimwombe Mheshimiwa Waziri tunapokuja mwaka kesho ambapo atakuwa na miezi sita ya utekelezaji wa bajeti atuletee taarifa ya performance ya hii kampuni, imetuongezea mapato kwa kiwango gani na kama haijatuongezea mapato aweze kuchukua hatua stahiki.

Mheshimiwa Spika, hatuwezi kuwa na hofu kwa sababu let us accept the reality, wao wana patent right, wao ndio wana teknolojia, sisi tunahitaji huduma yao; tuhofie kwa sababu walitoa rushwa nchi fulani? Kama waliwapa watu rushwa it is their problem na sisi watu wetu wakipewa rushwa it is our problem. Sisi tunahitaji huduma tuangalie mechanism ambayo we can yield more kwa mfumo huu.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo nataka kuongea, ukisoma taarifa hii ya uchumi ya Wizara ya Fedha kuanzia ukurasa wa nne mpaka wa saba, Waziri kaonesha key economic indicators ambapo jibu la failure zote hizi tulizozitaja ni sekta mbili; sekta ya kilimo na ya mifugo. Waziri ameonesha uzalishaji wa viwandani umeshuka kutoka asilimia 7.8 mpaka 7.1; biashara imeshuka kutoka asilimia 6.7 mpaka 6; malazi na huduma za chakula kwa maana ya hoteli na akinamama ntilie imeshuka kutoka 3.7 mpaka 3.2; shughuli za fedha na bima zimeshuka kutoka 10.7 mpaka 1.9; na hii ni analysis ya 2016/2017, ni taarifa ya hali ya uchumi. Shughuli za sanaa zimeshuka kutoka asilimia 8.6 mpaka asilimia 7.6; shughuli za kaya binafsi (household activities) kwa maana ya kuajiri wafanyakazi wa ndani, walinzi na nini zimeshuka kutoka asilimia tatu mpaka 2.7.

Mheshimiwa Spika, hizi indications zote ukienda kwenye mapato ya Serikali tuna-project kupungua kwa mapato yetu ya ndani kwa asilimia 10. Tafsiri yake ni moja tu, kwamba purchasing power ya watu wetu kwa ajili ya kununua bidhaa, kufanya shughuli za kibiashara, zimeshuka.

Mheshimiwa Spika, sasa what is the solution? Nami nimpongeze Mheshimiwa Dkt. Mpango, kwa mara ya kwanza priority yake ya bajeti ya mwaka huu ni kilimo, kwa mara ya kwanza. Solution ni ku-invest kwenye agriculture. Waziri kwenye tax measures alizoweka safari hii ametoa corporate tax incentive ya 20 percent kwenye viwanda vinavyozalisha mazao ya mifugo kwa maana ya leather sector na dawa lakini ni viwanda vipya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuna viwanda saba katika nchi yetu vinavyozalisha mazao ya ngozi na viwanda hivi havifanyi vizuri. Kwa nini; sababu kubwa ni mbili. Sababu ya kwanza ni export levy ya 10 percent, kwamba Mtanzania aki-process wet blue ndani ya nchi yetu kuiuza nje anachajiwa export levy ya 10 percent, kwa nini? Wakati competitors wote, kwa maana ya ukanda wetu wa Afrika Mashariki hawachajiwi 10 percent ya export levy. Ushauri wangu kwa Waziri wa Fedha; tufute 10% ya export levy kwenye wet blue.

Mheshimiwa Spika, ushauri wa pili kwenye Sekta ya Leather; sisi tumeweka 80 percent ya kodi kwa ajili ya ku- export raw, lakini unapoweka export levy ya 80 percent kinachotokea katika maeneo yetu ni jambo moja; bei ya raw nje ni nzuri, kwa hiyo wanachokifanya wafanyabiashara na Wizara ya Fedha inajua na TRA inajua; wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu wanachukua ngozi zetu raw kwenye container ya 40 feet wanaweka just 10 percent ya wet blue wana-declare ni wet blue wakati wame-export raw, matokeo yake Serikali inakosa.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu katika hili; ban export ya raw, aite viwanda vilivyopo vinavyozalisha ngozi ndani ya nchi yetu; na Mheshimiwa Waziri Mwijage anavijua, a-sign nao performance agreement, aondoe export levy ya 10 percent, ban export ya raw. Tunazalisha vipisi milioni nne. Kuna kiwanda kimekuja Tanzania kutoka Ethiopia, ni Wachina, wameweka investment yao pale kwenye EPZA Bagamoyo, wanaomba leo kupewa haki ya ku-import ngozi raw kutoka Ethiopia kwa sababu wao uzalishaji wao kwa siku ni vipisi 30,000, hawavipati ndani ya soko letu because of smuggling. Kwa hiyo ushauri wangu; ili tuweze ku-create value kwenye mazao ya mifugo, achukue hatua hizi mbili.

Mheshimiwa Spika, nimeona ametoa exemption ya VAT kwenye mashudu ya soya; hatukamui soya, sisi tunakamua alizeti, tunakamua pamba, aweke VAT exemption kwenye mazao ya pamba, kitatokea nini? Mifugo yetu na kwenye taarifa hii ya hali ya uchumi uzalishaji wa nyama na consumption ya nyama imeshuka kwa asilimia 14. Ushauri wangu huu ni kwamba Watanzania wataingia kwenye feedlotting.

Mheshimiwa Spika, leo ili uweze kumchinja ng’ombe, hawa ng’ombe wetu wa Kisukuma, Kigogo na Kinyaturu, ili umchinje uuze nyama yake technically anatakiwa achinjwe ng’ombe mwenye miezi 18 maximum miezi 20. Hatuwezi kwa sababu the cost of feedlotting ni kubwa mno. Mashudu ukinunua yana VAT, kwa hiyo ili tuweze ku-create proper value chain kwenye sekta ya mifugo nashauri create an exemption ya VAT kwenye mashudu kwa sababu kinachotokea sasa hivi mashudu yako yote unayozalisha ndani yanapelekwa Kenya, kwa sababu yana exemption kwao yanarudi ndani sisi tunageuka soko kwa raw material ya kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo nataka niishauri Serikali, Wizara imechukua hatua na ni muhimu Mheshimiwa Waziri wa Fedha, kama hatutachochea ufanyaji biashara katika uchumi wetu, mwaka kesho atakuja hapa hajafikia target ya makusanyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hali ya benki zetu, non-performing loans Serikali imechukua measures ambazo mimi kwa kweli naziita cosmetic, samahani akinamama; kwamba mama amekaa kwenye dressing table anachukua poda anaweka haibadilishi alivyo naturally. Cosmetic measures tulizochukua ni nini; BOT imeamua kupunguza some of the regulations zake za deposits na non-performing loans.

Mheshimiwa Spika, lakini unawapa watu extention ya miezi mitatu ambao wameshindwa kulipa mkopo. Wameshindwa kulipa mkopo kwa sababu gani; kwa sababu wameshindwa kufanya biashara. Kwa hiyo ni wajibu wa Wizara ya Fedha kuhakikisha kwamba tunachochea trading na ili tuchochee trading ni lazima tuchochee Sekta ya Kilimo. Kama kwenye kilimo hatutaamua kuanzisha price stabilization; wakulima wetu wanazalisha mahindi, kuzalisha kilo moja ya mahindi; narudia, ni Sh.357.

Mheshimiwa Spika, leo kilo moja ni Sh.150 au Sh.200, mkulima anapata hasara. Ni wajibu wa Wizara ya Fedha kwa kutumia vehicles tulizonazo ambayo moja ni Bodi ya Mazao Mchanganyiko na nyingine ni NFRA. Tuwape fedha wanunue haya mahindi kwa competitive rate kutoka sokoni halafu tuyatafutie soko wauze, kwa sababu hii fedha ni revolving. Nafahamu hofu ya Wizara ya Fedha, imekuwa kwamba wakitoa fedha kwenda NFRA huwa hairudi. Sasa ni udhaifu wetu sisi, kwamba mkulima kazalisha mahindi hana soko, tutachochea vipi biashara? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo kule kwetu Nzega; natolea mfano kwangu Nzega; leo mkulima amelima mazao yake, amevuna anataka kuuza, tunatumia mifumo tuliyonayo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Spika, leo kule Nzega wafanyabiashara wa mazao wanakuwa disturbed. Tumeleta vi-regulation kwamba eti mpunga usiweke kilo 90 kwenye gunia, ukikutwa unaweka faini. Waganda wanaokuja kununua mchele Nzega wanakuwa disturbed, wanahojiwa, kiko wapi kibali
cha kuja kununua mashineni, huna kibali faini 500,000. Tunawanyima fursa wakulima wetu kuuza mazao yao, matokeo yake hawawezi kubadilisha maisha yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimwombe Waziri, kachukua measures nzuri lakini kama hataweka jitihada kwenye sekta ya kilimo na mifugo mwaka kesho tutakuja hapa hatujafikia malengo ya bajeti tuliyotarajia.

Mheshimiwa Spika, nashukuru na naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia. Jambo la kwanza ambalo nataka niseme, Taifa letu kama alivyosema Dkt. Kamala linafanya radical changes katika baadhi ya maeneo, lakini radical changes zozote ambazo tunazifanya kama Taifa, bila kuwa na inclusive plan ya sehemu kubwa ya population, hazitoweza kutuletea matokeo mazuri huko mbele tunakokwenda. Tumekuwa na Wizara ya Fedha katika Kamati yetu ya Bajeti na nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Wataalam waliotoka Wizara ya Fedha na naweza nikasema honestly kabisa kutoka moyoni for the first time nimemwona Mheshimiwa wa Fedha amekuwa very accommodative na anafungua milango ya ushauri na hapa ni lazima tuishauri Serikali kwa ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatumia takwimu za BOT za mwezi Novemba. Ukiangalia takwimu za Benki Kuu kati ya mwezi wa nane, mpaka mwezi wa 11 our forex zimeshuka kwa zaidi ya dola milioni 500, fedha zetu za kigeni zimeshuka kwa kiwango hicho. Pia ukiangalia pressure kwenye shilingi yetu, leo dola kwenye soko inakwenda karibu Sh.2400, maana yake the cost of imports zinakwenda juu, shilingi inakuwa dhaifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia forex tunapata kutoka wapi? Ukiangalia mazao yote yanayotuingia fedha za kigeni, our exports zimeshuka,. Kwa hiyo, tafsiri yake ni kwamba, fedha za kigeni kuingia kwenye soko letu kuna upungufu na trend hii imeendelea kuwepo toka mwaka 2016. Hata hivyo, lakini ukiangalia taarifa ya TRA juu ya makusanyo ya kodi waliyoileta kwenye Kamati, malengo ilikuwa ni kwamba ukuaji wa makusanyo ya mapato yalikuwa ni asilimia 18.5, ndiyo yaliyokuwa malengo yetu, kwa miezi sita makusanyo yetu yamekuwa kwa asilimia mbili tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu ambalo kwa mtazamo wangu naliona ni challenge, mapato ya kodi ya customs yamekuwa kwa negative one percent maana yake yameshuka kwa asilimia moja, tafsiri yake ni kwamba component inayotuingizia asilimia 30 ya mapato, haiendi vizuri. Haya ni indication. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye landing, amesema Dkt, Kamala, segment pekee inayokua ya kukopesha katika commercial banks ni personal landing, mikopo ya wafanyakazi na Waheshimiwa Wabunge tunayokopa ambayo ni one hundred percent haiendi kwenye production. Ukiangalia commercial landing kwenye Agro sector imeshuka, ukiangalia landing kwenye manufacturing imeshuka. Sasa nini ushauri wangu, radical change tuliyofanya kama nchi, tumewekeza kwenye airline, tunajenga barabara, tunajenga viwanja vya ndege katika hifadhi zetu na tourist destination. Ushauri wangu, Wizara ya Fedha, Wizara ya Miundombinu, Wizara ya Tourism, kwa sababu GDP contribution ya Sekta ya Utalii ni asilimia 17, ni lazima Wizara hizi tatu zikae pamoja zije na mkakati wa growth, kwa sababu ukisoma taarifa zote za Wizara ya Fedha hakuna mpango wa kukuza biashara ni mipango ya administrative tu and this is counterproductive. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili tuweze ku-yield mapato kutokana na kwanza nawashangaa watu wote wanaofikiri kwamba tutapata faida kwenye ATC, leo Airline Business kwa Afrika inakuwa projected itapata hasara ya three million US Dola, Sekta ya Airline. Kwa nini nchi zinawekeza kwenye airline, zinawekeza kwa sababu it is means to stimulate growth kwenye sekta zingine. Kwa hiyo ushauri wangu, Wizara ya Fedha na end of the day anayeandika cheque ya kulipa ndege na kulipa cost zote ni Wizara ya Fedha, nimemwambia kwenye Kamati Mheshimiwa Waziri wa Fedha na narudia ndani ya Bunge, its time awe kaka mkuu ni lazima tuone tourism ina-grow kwa zaidi ya asilimia 22 ili iweze kuchangia kwenye GDP ya Taifa letu tuweze kurudisha investment tuliyowekeza kwenye ndege. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ambalo ni muhimu sana tuelewe na mimi nataka niwaombe Serikali kwa heshima, Tanzania Kariakoo ilikuwa ni trading center ya nchi za SADC. Leo tuna advantage kubwa sana na nataka niwaombe Serikali, tunapokuwa kwenye hizi Jumuiya blocks mfano hii EAC, the most important question ya kujiuliza, who is our cash carry? Cash carry yetu ni Kenya the trading partner, cash carry yetu ni Uganda au ni Rwanda? Our cash carry ni Kongo na Zambia. Kwa hiyo all our economic policies ni lazima tutazame soko hilo. Tusipofanya namna hiyo hatutoweza kupata benefit ya kuwepo kwa eneo la Bandari ya Dar es Salam. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni jambo ambalo ni muhimu sana tulitazame, Eastern part ya Congo kuna zaidi ya watu milioni 25, how we are taking advantage of that? Leo amesema Mheshimiwa Mwijage, tunapitisha hii Sheria mnaita sijui axle, kwamba malori ya uzito, atakayekuwa disadvantaged ni sisi kwa sababu our trading partner ni Zambia, watahama wataenda Beila.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitolee mfano kampuni kama PUMA. PUMA Serikali ina-own fifty percent, PUMA kwa mwaka 2011 mpaka 2017 wamelipa dividend Serikalini sixty billion shilling. Naomba msikilize, PUMA wamelipa tozo na kodi kwa miaka miwili for hundred and eighty billion shilling, halafu huyu anaomba leseni ya aviation industry mnamnyima, jamani what is this? Yaani PUMA ambaye tuna asilimia 50, ametulipa kwa miaka miwili bilioni 480 kodi, anaomba leseni ya aviation hapewi, why? Nashindwa kuelewa kwamba tunatafakari namna gani! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Kariakoo is dying...

MHE. DANIEL N. NSANZUGWANKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

T A A R I F A

MWENYEKITI: Mheshimiwa Bashe, taarifa hiyo.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipokea, narekebisha siyo 2011 ni 2009. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachotaka nishauri ni nini? Ni lazima Wizara ya Fedha, fiscal measures zinazotengenezwa na Wizara ya Fedha ziwe production oriented badala ya kuwa more control measures. Mimi ni muumini wa aina moja ya ajabu sana ya falsafa. Naamini kwamba Mchaga wa Kariakoo akikwepa kodi haipeleki Ulaya, hafungui akaunti Uswiss, atakwenda kununua mfuko wa cement upata indirect. Kwa hiyo, why are we controlling these small businesses, tunazi-suffocate? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo lilinishtua sana na namshukuru Waziri wa Fedha aliahidi kulifanyia kazi. Tulipitisha measure hapa ya kuongeza kodi kwenye crude oil, tukaongeza 35% matokeo yake zaidi ya 90% ya mapato katika kipande hicho imeshuka. Tukauliza swali, mbona hamna matatizo ya mafuta nchini? Tukaambiwa wana-import zaidi refined oil. Tafsiri yake ni nini? Viwanda vya ndani, re-export component na taarifa za BoT zimeonyesha re-export imeshuka. One the product ambayo tulikuwa tunafanya re-export ilikuwa ni crude oil tukiingiza nchini, tukisafisha yakawa refined tunayauza Congo na mataifa ya nje. Matokeo yake sasa hivi sisi tunaokaa kwenye boader mafuta yanatoka nchi za jirani, it is counter productive. Kwa hiyo, ushauri wangu kwa Wizara ya Fedha, umefika wakati wa ku-come up na mpango wa kikodi ambao uta-stimulate production.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kuhusu kilimo. Kilimo kinachangia almost 30% ya GDP yetu ukiacha tourism. Umefika wakati kama nchi ni lazima tuje na mkakati wa ku- protect agro-sector. Tusipokuja na mkakati wa kulinda sekta ya kilimo tutarajie maafa huko mbele kwa sababu kilimo kinatuletea mambo mawili; moja food security lakini mbili ni component inayotuingizia forex. Leo tumbaku imeshuka, zao pekee la kilimo linalo-grow kwenye export ni cotton peke yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu wa mwisho kwa Serikali, just a minute, mazao ya mahindi, karanga na kadhalika yaacheni katika regional level. Wizara ya Kilimo ichukue mazao strategic kama Korosho, katani, kahawa, tumbaku ili tuwe na big plan kwa ajili ya ku-increase the export yetu. Bila ya hivyo, traditional crops na non-traditional crops zinashuka export matokeo yake tutapata shida kama nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa. Awali ya yote, nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia sote kukutana katika Bunge hili la bajeti na kutimiza wajibu wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, nitumie nafasi hii tena kumpongeza Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kauli ambazo wamekuwa wakitoa zaidi ya mara moja, mara mbili juu ya namna ambavyo watendaji wa Serikali na Serikali nzima inatakiwa ku-act na ku-behave katika suala zima la uwekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaongelea mambo mawili. La kwanza nitaongelea suala la investment. Suala la pili nitakaloliongelea ni la kilimo. Ukitazama takwimu za World Bank, The Economic Update No.11 iliyotolewa mwaka huu, inaonesha kwamba idadi ya Watanzania walioongezeka katika umaskini toka mwaka 2012 mpaka leo ni Watanzania milioni mbili. Watanzania milioni mbili wameongezeka kwenda kwenye umaskini. Kwa nini? Nitaeleza baadaye.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia asilimia 60 ya population ya nchi yetu au mpaka 70 ipo katika sekta ya kilimo. Mipango yetu yote tunayofanya kama nchi na financing program zetu zote tunazozifanya kama nchi ni lazima ziangalie ni namna gani zina-improve productivity na kuhakikisha kunakuwa na masoko ya uhakika ya wakulima ili tuweze kuondoa watu wetu katika umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukitazama financing ya sekta ya kilimo kwa miaka mitatu mfululizo, tunachowekeza katika sekta ya kilimo kinazidi kupungua kila mwaka. Tunachowekeza na kile tunachoki-disburse against bajeti yetu ya maendeleo, haviwiani. Sekta yetu ya kilimo inachangia asilimia 29 ya GDP ya taifa letu lakini inatengewa less than 5% ya development budget. Wakati huo huo population yetu inaongezeka kwa wastani wa asilimia 3, hili ni tatizo, ni lazima watu wataendelea kuongezeka kwenye umasikini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nini ushauri wangu katika hili? Hakuna njia tunayoweza kuondoa watu kutoka katika umaskini kama hatutofanya mambo matatu. La kwanza, ni lazima tuanzishe Price Stabilization Fund kwenye eneo la kilimo ili wakulima wanapokutana na mtikisiko wowote wa soko la dunia ama unpredictability kwenye bei za dunia tuna njia ya kuwaokoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kunapotokea hili tatizo, mimi ninazo takwimu za toka mwaka 2014 – 2017, zao la pamba msimu wa mwaka 2013 kwenda mwaka 2014 production ilishuka kwa asilimia 30; mwaka 2015 lilishuka kwa asilimia 17; mwaka 2016 lilishuka kwa asilimia 16; mwaka 2017 lilishuka kwa asilimia 18 na mwaka huu lime-grow kwa initiative iliyofanywa na Serikali. Zao la korosho ukiangalia toka mwaka 2014 lilikuwa lina negative trend lakini mwaka 2017/2018 zao hili lime-grow ni kwa sababu tuliwekeza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu, moja, kama nchi ni lazima tuanzishe Price Stabilization Fund kwa ajili ya mazao ya kilimo. Mbili, ni lazima tuanzishe mfuko wa ku- subsidize inputs kwa sababu mazao tunayoyazalisha kwa ajili ya kwenda kwenye export sisi hatuna uwezo wa ku-control bei nje, tuna uwezo wa ku-control uzalishaji na quality. Sasa mzalishaji mfano wa mahindi, kama tutakapompa mbolea, viuatilifu hatutotoa ruzuku katika maeneo haya maana yake gharama ya uzalishaji itakuwa kubwa, soko halipo au halipo la uhakiki, matokeo yake mkulima huyu atakata tamaa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesoma mpango ambao umesomwa na Wizara ya Fedha ambao tutaujadili, ningeshauri katika misingi na maeneo makuu matano ambayo Wizara ya Fedha wamesema, eneo la kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu, hapa wametaja suala la elimu, maji na afya ni lazima tuweke wazi (precisely) component ya kilimo, kwamba ni eneo muhimu la kufungamanisha uchumi na maendeleo ya watu ili liweze kupata priority. Kwa sababu tukianza kulijadili kwa staili hii tutaanza kulitengea fedha tunapokuwa na uwezo. Hili ni eneo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la pili ni la masoko, nini ushauri wangu? Tumeanzisha Tanzania Agricultural Development Bank. TADB kuna tatizo la structure kwa sababu TADB iko chini ya Wizara ya Fedha, Bodi ya Mazao mchanganyiko, NFRA na Bodi zingine ziko chini ya Wizara ya Kilimo, kuna suala la marketing ambalo liko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara na kuna suala la investment ambalo liko chini ya Wizara ya Waziri Mkuu. Ushauri wangu ni lazima kutafutwe njia ya kutengeneza a strategic alliance kati ya hizi Wizara zote kwenye suala la marketing ya mazao ya wakulima ili Bodi ya Mazao Mchanganyiko kama tunaenda kwenye msimu waweze ku-plan nje kuna mahitaji ya mahindi kiasi gani, masoko yako wapi, Serikali isihitaji ku-finance, TADB awa-finance wanapokuwa wamepata contract za kuuza mazao nje. Hii itasaidia predictability ya mazao tunayozalisha. Tusipofanya namna hii, aje kiwanda cha magari na kadhalika, viwanda hivi havita-break even, havitaweza kuzalisha kwa sababu sehemu kubwa ya watu haina purchasing power. Hili ni jambo la pili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tatu ambalo nataka nishauri na mimi niipongeze Wizara ya Fedha nimeona kwenye mpango wameongelea uboreshaji wa mazingira wezeshi kwa uendeshaji wa biashara na uwekezaji. Lazima Serikalini watu wafahamu kwamba suala la mtu kuchukua shilingi mia moja yake kwenda kuiwekeza kwenye nchi au mji number one ni perception kwamba naamini shilingi mia yangu nayoenda kuiweka pale iko salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo Kariakoo is dead na mimi nimpongeze Waziri Mkuu alienda kukutana na wafanyabiashara wa Kariakoo. Nawaomba suala la Blue- print kama linahitaji mabadiliko ya sheria leteni tubadilishe. Suala la Blue-print kama linahitaji harmonization ndani ya Serikali ifanyike. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, World Bank wametoa ripoti, wamesema key areas ambazo zinatumbua sisi Tanzania kwenye suala la investment ni kwamba moja, kuna utitiri wa kodi ndogo ndogo. Mbili, hakuna simplicity kwenye suala la ulipaji wa kodi na tozo. Tatu, wanashauri kuwe kuna simplified system and predictable tax regime. Haya yatatusaidia watu kuja kuwekeza. Jamani, ambalo nataka nishauri na hapa Waheshimiwa Wabunge wengine wamesema, leo inaanzishwa Task Force inaenda Kariakoo pale inasimama, eti ile Task Force ina Polisi, haijui kukusanya kodi. Polisi kasomea wapi ukusanyaji wa kodi? Ina TAKUKURU; TAKUKURU kasomea wapi ukusanyaji wa kodi? Ina watu wanasemwa kutoka Idara nyeti za Serikali, ina watu wa TRA, na kadhalika. Kundi la watu limekaa pale Kariakoo, mtu kanunua mfuko wake anaambiwa leta TRA aah, hii ni feki huyu.

Mheshimiwa Naibu Spika, huyu mtu katoka Kongo anajuaje kama ile karatasi ya EFD mashine yake ni feki? Hawezi kujua, atabebwa, anawekwa Msimbazi Kituo cha Polisi. Next time haji, anaenda Uganda; anaenda nchi nyingine. Hii ni shida. Ni lazima suala la ukusanyaji kodi liachwe mkononi kwa watu waliosomea ukusanyaji wa kodi. Polisi wakafanye kazi yao, TAKUKURU wakafanye kazi yao. Hii ni dis-incentive.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo ukienda kwenye soko letu la hisa, trade volume imeshuka sana, share prices za share zilizoko kwenye soko la hisa zimeshuka. Kwa sababu gani? Sababu ni chache tu. Moja, there is no investors wanaoenda kununua na kuuza shares; wanaoenda kununua shares, watu wameshikilia share zao. Pili, maana yake hakuna surplus, hakuna fedha za ziada ambazo watu wanataka kuwekeza. Tatu, kuna kuwa na unpredictability. Kwa hiyo, tusipofanya haya mambo kuwa na sera ambazo ziko predictable katika suala la investment, hatuwezi kuondoka hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mwisho ambalo nataka nishauri, leo tumewekeza sana kwenye ndege, it is very good. Nami nataka niseme, uwekezaji wa ndege is not for itself, lakini uwekezaji wa ndege ni means to drive other sectors. Tumewekeza kwenye ndege, tumejenga viwanja vya ndege, nami nimshauri Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Waziri wa Fedha ni lazima uwasainishe Wizara wa Tourism Performance Agreement, kwamba wanakuongezea tourists kiasi gani kurudisha investment uliyoifanya kwenye ndege? Ni lazima kwa sababu hizi ndege ambazo tumewekeza, tunajenga viwanja vya ndege kwa kasi sana, tunafungua nchi yetu, ni lazima tuweze kupata return kutokana na hii investment.

Mheshimiwa Naibu Spika, investment hii, hatutaki tuone ATCL; nami kwanza niseme tu wanasiasa, hebu nitajieni Africa Airline gani ina-make profit? Hakuna! They are making loss. It is not true. African Development Bank wame-predict Airline sector Africa globally ita-make 3 million US dollar loss, zote! Sasa hizi Airline zinafanya nini? Zinakuwa ni feeders za sector nyingine. Kwa hiyo, ni lazima sekta nyingine tuzitengenezee utaratibu wa kujua kwamba tumewekeza shilingi 100 kwenye ndege, wao wanaleta shilingi ngapi? Tusiseme tu tuna Bombardier tuna Dreamliner, tuna nini; ni lazima hizi ndege zitusaidie kukuza sekta nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, tunajenga reli. Mimi niseme hapa, nilisikitika sana. Tanzania imewekeza sana Kongo kwenye usalama. Tumewekeza sana. Askari wetu wamepoteza maisha yao. Sisi Rais wa Kongo kaapishwa, nilikuwa nafuatilia, wawakilishi wetu kama nchi wametua, wameenda kwenye kuapisha, wamegeuza.

Mheshimiwa Spika, Kenya katua Rais wa pale na delegation ya wafanyabiashara 60, wamekaa kusaini mikataba, kesho yake kaondoka. The first visit ya Rais wa Kongo is Kenya; and you know what? Wamesaini makubaliano ya Kenya itaenda ku-train civil servant wa Kongo. This is a forex. Katoka pale CEO round table ziliofanyaka Rwanda, kaenda Kigali three days. Naishauri Serikali, ni lazima tuwe business oriented. This is very important. Bila hivyo, Waziri wa Fedha hapa atakuja kudondoka na pressure. Tunaomba maji, tunaomba nini, he cannot do anything.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, nashukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa fursa. Jambo la kwanza nitumie nafasi hii kwanza kwa dhati kabisa kulipongeza Jeshi la Polisi na nawapongeza tukiwa honest sasa hivi katikaTaifa letu wamefanya kazi kubwa sana ya kudhibiti uhalifu na ujambazi mkubwa hasa katika maeneo ambayo yalikuwa yanaathirika ya pembezoni mwa nchi na ambayo yamezungukwa na nchi ambazo zina instability. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi wamefanya kazi kubwa sana ya kudhibiti na kuleta utulivu na amani hasa sisi tunaotoka Mikoa ya Kanda ya Magharibi, zamani ilikuwa ukifikiria kusafiri kukatiza kutoka Dodoma hapa ukaseme ukalale Bukoba, ilikuwa ni mtihani. Kwa hiyo wamefanya kazi kubwa sana tunawashukuru na Mwenyezi Mungu awajalie kwa kazi hii wanayoifanya. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Amina.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, nataka niongee mambo machache kuhusiana na polisi. Polisi wetu wanafanya kazi katika mazingira magumu, ni muhimu sana ndani ya Serikali kuangalia ni namna gani stahiki za polisi na majeshi mengine zinakuwa harmonized, kwa sababu suala la usalama linaanza na intelligence kwa maana ya kukusanya taarifa, lakini suala la kuzuia, suala la ku-enforce, hizi ni kazi ambazo zinashabihiana. Kwa hiyo, kuna umuhimu sana wa kuangalia ni namna gani stahiki za askari wa Jeshi la Polisi zinakuwa harmonized na majeshi mengine ili kuleta uwiano ulio sawa kwa sababu majukumu yao yanategemeana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo askari wetu wanafanya kazi over time, hawapati kulipwa over time, wanafanya kazi masaa 12, akiingia kwenye lindo ni masaa 12 na hii ni kutokana na uchache wa askari katika maeneo yao. Kwa hiyo ni muhimu sana Serikali iangalie. Nataka niishauri Serikali, watafakari, mfano, sasa hivi huwa tunasikia kwenye TV kwamba kutokana na makosa ya barabarani askari wamekusanya bilioni 700, hivi is it not possible ndani ya Serikali wakatengeneza utaratibu katika kila kituo angalau twenty percent ya hizi fedha wanazokusanya zibaki kituoni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka nitoe mfano, pale Nzega kwangu leo ni mwaka wa tatu askari wamekatiwa maji, Jeshi la Polisi. Pale Nzega kwetu LUKU wanaweka kutoka mfukoni kwao na it’s an average ya shilingi laki moja kwa mwezi wanayotumia. Kwa hiyo wananchi wanachanga changa na wenyewe saa nyingine wanatoa fedha zao mfukoni, Mkuu wa Kituo hawezi kukubali usiku pasiwe na taa katika kituo chake cha polisi na ni kwa sababu ya ukata.

Mheshimiwa Spika, pale Nzega tuna household za askari familia 17, leo sisi katika halmashauri tumeamua kuanza kutafuta fedha ili tuanze kujenga makazi ya askari, tunaiomba Serikali iangalie, ni vizuri sana kuangalia hawa watu kazi wanayoifanya ilivyo ngumu iweze kwenda na stahiki zao. Tunaweza tukaja hapa ndani tukawalaumu kuwa wanachukua rushwa, je, tumeangalia, nimemsikia Haonga rafiki yangu amesema tuwape two million, nadhani tusingeanzia kwenye two million, tungeanzia namna gani tunatengeneza uchumi imara ambao utakuwa na mapato imara ili tuwalipe vizuri askari wetu. Hili ndiyo jambo la msingi kabisa, lazima tuanze na kutazama haya mambo in a broader perspective, itatusaidia kama nchi kwenda mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo nataka niongelee, ni vizuri Serikali ikaangalia custodian wa border control ni migration. Je, equipments tunazowapa watu wa Uhamiaji, kwa sababu ndiyo mwenye jukumu la kuangalia mipaka, wanaoingia na kutoka, ni vizuri hili Jeshi la Uhamiaji likawa a unit inayojitegemea, inayojiendesha, iwe na resources zake, iwe na proper plan tujue ndani ya miaka mitano border control zetu zitaendeshwa namna gani. Hii ni muhimu sana ili kuweza kuingiza efficiency katika kazi wanazofanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka niongelee jambo lingine mahsusi. Kwa miaka mitatu ambayo nimekuwa humu ndani ya Bunge na kabla sijaja Bungeni, kumekuwa na mjadala mkubwa sana juu ya suala la Masheikh waliowekwa magereza. Leo ni mwaka karibu wa sita, nataka niiombe Serikali kwa heshima kabisa na mwaka jana walitoa ahadi hapa, hawa watu kama wana makosa wapelekeni mahakamani dunia ijue kwamba hawa watu wana tuhuma moja, mbili, tatu kuliko kuendelea kuwa-hold ndani with no clarity, inaleta maswali mengi, ina distort image, inasababisha watu wengine kupata hoja ya kujadili jambo ambalo halina sababu. Nataka nimwombe Mheshimiwa Waziri atakapokuja kufanya wind up, hebu tuelezeni faits na direction ya suala la Mashekh walioko magereza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili nataka niliombe Jeshi la Polisi na Mheshimiwa Rais alisema hili, alisema Watanzania siyo wajinga, Watanzania wanaona, nami nitaongea kuhusu hili ninalolisema na lingine linaloitwa la task force. Kuna mambo yanasemwa halafu response inayopatikana kutoka kwenye authority is just a political response, kuna mambo ambayo yanatajwa ya ki-criminal yanatakiwa yapate majibu complete. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mfano, imesemwa sana hapa na Mheshimiwa Bwege amewahi kuisema mara nyingi, nataka nimwombe Mheshimiwa Kangi hebu wamwambie Mheshimiwa Bwege awasaidie. Kuna hoja inayosemwa sana sana na inaenda kwa umma, inayozungumzia Masheikh wa Tablih waliopigwa risasi inayosemwa huko Kilwa sijui, this things need answers. Kama ni taarifa za uongo, wanaotengeneza taarifa hizi za uongo wachukuliwe hatua, we should not allow mambo ya uongo yanasemwa semwa, yanaachwa, halafu siku ya mwisho yana-distort heshima na image ya Taifa hili. This country imejengwa katika misingi imara ya utu, hili ni muhimu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine, nataka niseme kuhusu minority society, nataka niiombe Serikali, pale Uhamiaji waanzishe dawati maalum linalohudumia wahamiaji katika nchi hii. Community ambazo ni minority, Idara ya Uhamiaji zimegeuka ni mradi, halafu jambo la kushangaza anakwenda mtu akionekana Msomali anaambiwa wewe siyo raia, leta cheti cha bibi na bibi yako watano, anatoa wapi? Kwa sababu hata huyo Afisa yeye ukimuuliza cheti cha bibi yake wa nne hana, basi fanyeni audit. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Nzega kuna familia tano za Wasomali zinajulikana ambao familia ile hawako watu hata arobaini. Suala la uhamiaji jamani siyo dhambi, today Rais wa Taifa kama Ireland ni Mhindi, kwa hiyo Uhamiaji na migration nataka niwaambie, hivi mnajua neno sukuma! Hawa Wasukuma ni wahamiaji kwenye nchi hii, ni Northerner. Neno sukuma, kisukuma maana yake ni Kaskazini. (Makofi/ Kicheko)

SPIKA: Ilikuwa ni Mheshimiwa Ndassa au nani alisimama! (Kicheko)

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Yupo. (Kicheko)

SPIKA: Au Mheshimiwa Chegeni!

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Wote.

SPIKA: Nilisikia kama taarifa hivi, Mheshimiwa Bashe endelea. (Kicheko)

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, ninachotaka niseme ni hivi, dunia leo you cannot restrict migration, tengeneza proper administrative measures zitakazokusaidia wewe migrants kukusaidia kwenye nchi, because the world is village, hili ni muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo nataka niongelee, Mheshimiwa Kangi nitampa majina. Sasa hivi kuna watu wanahama nchi yetu especially business community na wanasumbuliwa na watu wanaoitwa task force. Kinachotokea na nitampa Mheshimiwa Kangi majina hapa, transporters walioko Wilaya ya Temeke ambao wana asili ya Kisomali na ni Watanzania, mfano mtu anaitwa Abdigul Abdi Kulane ambaye ana kampuni inaitwa Kulane and Sons Company Limited alifuatwa nyumbani kwake Kinondoni akachukuliwa, leo ni miezi miwili hajulikani alipo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna mtu anaitwa Abushir Ally, huyu mtu kachukuliwa, leo hayupo, walichukuliwa wane, wenzao wawili wameachiwa baada ya kutoa fedha na wao walichokifanya, angalia hiki kitu, wametoka wamehamisha Transport Company yao wamehamia Zambia.

Mheshimiwa Spika, kuna mtu anaitwa Abushir Ally, huyu mtu kachukuliwa leo hayupo. Walichukuliwa wanne, wenzao wawili wameachiwa baada ya kutoa fedha na wao walichokifanya, angalia hiki kitu, wametoka wamehamisha Transport Company yao kwenda Zambia. This is happening. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wafanyabiashara hawa wakubwa kwa hizi task force wanachokifanya sasa hivi, wengi wanahamisha biashara. Nakuomba Mheshimiwa Waziri, tazameni hizi task force zinavyoundwa na bahati mbaya Kituo cha Polisi mtu akienda anaambiwa huyo wala usihangaike yuko chini ya task force, wala sisi hatuna control naye. Sasa hizi task force ambazo hazina controls zitaathiri image ya nchi yetu, kazi kubwa inayofanywa image yake itakuwa distorted. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, namwomba Mheshimiwa Kangi, angalieni hizi task force zinazoundwa, lazima ziwe zina TOR, majibu. Watu wasipokuwa na majibu juu ya family members wao, inaleta shida na ukakasi mkubwa sana katika community.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka ni-conclude kwa kuiomba Wizara ya Mambo ya Ndani, mnafanyna kazi kubwa sana ya kulinda usalama wa raia. Niwaombe, moja, angalieni maslahi ya askari kuya-harmonize na majeshi mengine, ni muhimu sana ili kuwajengea confidence askari wetu.

Mheshimiwa Spika, la pili, naomba Idara ya Migration waache kugeuza minority society mradi. Tengenezeni Dawati Maalum litakalohudumia na ikiwezekana familia zilizoko hapa nchini ambazo ni migrants, minority zinaweza kujulikana, it’s easy kuwa na database ambayo itaondoa hii shida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mfano mdogo wangu mimi kaenda siku ya kwanza kapata shida, siku ya pili mmoja kaangalia jina la mwisho alivyoona Bashe akasema wewe ni mdogo wake na Mbunge. Sasa yule ana privilege ya mdogo wake na Mbunge, wangapi hawana? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mimi nataka niiombe Serikali, ni vizuri sana haki za raia zilindwe na mwenye wajibu wa kutoa majibu juu ya masuala yenye ukakasi ni Wizara ya Mambo ya Ndani, toeni majibu juu ya haya mambo yanayosemwa.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia. Jambo la kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuamsha salama na kutufikisha kutimiza wajibu wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, awali ya yote kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwa kuonesha katika bajeti ya mwaka huu dhamira ya kuanza safari ya kufanya reforms katika mambo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na Wabunge na Watanzania kwa muda mrefu. Kwa hiyo, mimi nampongeza sana, hasa suala la kutengeneza demarcation ya line kati ya TBS na TFDA katika hatua ya awali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, nimpongeze Mheshimiwa Dkt. Mpango na Mheshimiwa Profesa Kabudi kwa namna walivyo-handle suala la Airtel na kupelekea Serikali kupata 49% share. Wameli-handle jambo hili in a civilized and professional way. Nataka nimuombe Mheshimiwa Waziri, na niiombe Serikali kwa ujumla wake; tunapo-handle masuala ya private sector this is the best way ya ku-handle wawekezaji wa ndani ama wa nje. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini nisisitize tumepata share asilimia 49 katika Airtel. Ombi langu, kwa kuwa tunakuwa sehemu ya bodi, tunakuwa sehemu ya management, ikija obligation ya investment kwa sababu kwa takwimu, Airtel is not making profit, likija suala la investment na Telecom Sector inabadilika kila siku hakikisheni mnawekeza kama wadau wengine waliokuwa partners katika business, this is very important. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu kuhusu Airtel; Serikali ina TTCL, nimemsikia Mtendaji Mkuu wa TTCL akisema siku moja kwamba utakapokwenda maeneo ambayo hakuna mtandao wa TTCL unaweza ukafanya roaming kwa kutumia Tigo, it is wrong in business. Sisi tutakuwa tunalipa sana kumlipa Tigo kwa sababu tunatumia infrastructure yake. Ninawashauri, ingieni makubaliano na Airtel ambayo mna 49% kama Serikali ili tutakapokuwa maeneo ambapo TTCL haipo itumie infrastructure ya Airtel kufanya mawasiliano kwa sababu itakuwa ni within the circle ambako ninyi mna-stake.

Mheshimiwa Spika, nitoe maoni yangu katika hoja iliyopo mbele yetu. Nimesoma hotuba ya Waziri, nimesoma hotuba za Wizara tatu ambazo tunazitarajia kuwa ndiyo input kuweza ku-attain malengo yaliyoko katika hotuba ya Waziri; nimesoma hotuba ya Wizara ya Wizara ya Kilimo, nimesoma hotuba ya Wizara ya Mifugo, nimesoma hotuba ya Wizara ya Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Nape ameongelea Sekta ya Kilimo, nataka tu on record ukichukua total development budget tuliyotenga mwaka huu ya shilingi trilioni 12, uka-compare na kile ambacho tumekitenga katika sekta ya kilimo na mifugo ambazo kwa ujumla wake zinachangia zaidi ya asilimia 30 ya GDP yetu. Fedha tulizotenga kwa ujumla ni shilingi bilioni 161 wakati development budget ni shilingi trilioni karibu 13. Hii ni sawasawa na asilimia 1.3; hatuwezi kupiga hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hoja yangu ni nini; nimesoma monetary statement, hii hapa ya BOT na ninaomba ninukuu maneno; BOT wanasema; global economy itashuka kutoka 3.6 kwenda 3.3 kwa sababu ya trade war iliyopo kati ya China na Marekani. Sasa sisi kwenye global economy who are our trading partners and what are we selling? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi tunauza mazao ya kilimo na ninaomba niyasome hapa; zao la tumbaku, limeshuka kutoka 1.2 million kgs tuna-project mwaka huu 2018/2019 tutakuwa na tani 50,000 ndiyo tutakayoenda kuuza kwenye soko la dunia. Korosho mwaka 2016/2017 ilikuwa tani 265,000; mwaka 2018/2019 tani 224,000; mkonge kutoka tani 36,000 sasa tuna- project tani 15,000; chai kutoka tani 26,000 tunakwenda tani 19,000; sukari kutoka tani 330,000 tunakwenda tani 327,000; pareto kutoka tani 2,150 tunakwenda tani 1,800. Zao pekee ambalo tuna-project ku-grow ni zao la kahawa kutoka tani 48,000 kwenda tani 61,000; pamba na yenyewe tunajua kinachoendelea.

Mheshimiwa Spika, sasa nini ninachotaka kusema Mheshimiwa Waziri wa Fedha umempa Commissioner General wa TRA target ya kukusanya 1.7 trillion shillings. Mheshimiwa Waziri Commissioner General hawezi kukusanya na huyo utamtumbua. Nasema haya in very good faith kwa sababu ili tukusanye kodi ni lazima tuzalishe, ili tukusanye kodi ni lazima tufanye biashara. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, sasa ushauri wangu ni nini; ukienda kwenye lending, kutoka mwaka 2016 mpaka mwaka wa fedha 2018/2019 sekta ya kilimo uwekezaji wa mikopo umeshuka kutoka asilimia 11 mpaka -4; sekta ya manufacturing kutoka asilimia 20 mpaka 17; sekta ya transport kutoka asilimia 27 mpaka asilimia 4; building kutoka asilimia 9 mpaka -2; trade kutoka 2.2 mpaka -2.1; hotel and transportation kutoka asilimia 7 lending kushuka mpaka -1.6%.

Mheshimiwa Spika, nini kitakachotokea; excise duty zitashuka, VAT zitashuka, consumption taxes zote zitashuka na Mheshimiwa Rais wakati anaongea na wewe Mheshimiwa Waziri na wataalam wakati anaongea na wafanyabiashara, alisema kodi za ndani zinashuka na kodi za ndani ni zipi; kodi za ndani ni VAT on consumption za ndani; kodi za ndani ni PAYE, kodi za ndani ni excise duty, hizi zote ziko related na biashara. Kama hatutafanya proper harmonization na regulation kwenye biashara hatuwezi kutoka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Dkt. Mpango, sasa hatua ya kwanza ninayokuomba na ninajua hii utakumbana na matatizo Serikalini, fanya maamuzi yafuatayo; muite Waziri wa Viwanda na Biashara, kaa naye, muombe mfanye mabadiliko makubwa. Tuna sheria hapa; tuna Sheria ya CARMATEC, tuna Sheria ya TIRDO, tuna Sheria ya EPZA, tuna Sheria ya TanTrade, tuna Sheria ya TEMDO; hizi taasisi zina-contradict zenyewe. Fanyeni harmonization. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili; mtu yeyote anapotaka kusajili biashara hatua ya kwanza anayofanya ni kwenda sehemu inatwa BRELA, BRELA ni kifupi cha Business Registration and Licensing Agency. Ushauri wangu, chukueni Sheria ya BRELA, hizi taasisi zote ziwekeni mle ndani, anzisheni kitu kinachoitwa Business Registration Licensing and Regulatory Authority. Ili mtu anapoingia kusajili biashara, kuchukua leseni, anakutana na kila kitu mle ndani, akitoka anakwenda kufanya biashara yake. Uta-reduce bureaucracy, uta-reduce cost of business. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Bashe una akili wewe.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, la pili angalia kitu hiki Mheshimiwa Mpango GDP contribution, sekta iliongoza kukua ambayo ni ya sanaa inachangia 0.3% hii ndiyo imekua, imeongoza kukua katika uchumi wetu, sekta inayokua ambayo inachangia asilimia kubwa ya GDP, sekta ya kilimo imekuwa kutoka 3.7% kwenda 5% marginal growth is less than population growth, hamuwezi ku-break through.

Ushauri wangu tuhakikishe tuwe na mpango na mimi hili linanisikitisha, ukisoma mpango wa maendeleo huwa hapa tulioupitisha hauna smart objective, tunapozungumzia smart objective ni lazima ziwe measurable, unazalisha pamba kutoka tani 200,000 kwenda ngapi? Unazalisha tumbaku kutoka tani moja kwenda ngapi?Unazalisha kahawa kutoka wapi kwenda ngapi?Usipofanya namna hii hamuwezi kujipima, hatuwezi kujipima...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Malizia Mheshimiwa.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, namalizia kwa neno moja,naomba niseme hivi yupo hapa tulikuwa handsome boy Waziri Mwijage aliasisi cotton to clothes, ule mpango umeishia barabarani, aliasisi mpango wa leather to leather product umeishia barabarani, aliasisi mpango wa mbegu za kunde, mazao ya mbegu za kunde mpango umeishia barabarani. Mheshimiwa Waziri tunawaomba tulifanya mabadiliko mwaka 1967 kwenda kwenye uchumi wa kuhodhi wa Serikali, tukafungua masoko 1990s kwenda 2000 umefika wakati wa kupitia mfumo mzima wa Serikali, badilisha Sheria ya Income Tax, badilisha Sheria ya VAT, badilisha Tax Administration Act, usipofanya namna hii hauwezi kufikia malengo tuliyojiwekea ni lazima tuwe production oriented kuliko tax oriented kwenye uchumi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ombi moja kwa heshima yako na kwa kiti chako, Waziri umetangaza hapa wafanyabiashara wasikamatwe, Nzega kwangu imetua tax force wiki iliyopita na kamji kale kadogo, wamekamata wafanyabiashara saa hizi wako polisi zaidi ya wiki, pale Wizarani kwako Mheshimiwa Waziri na Mwenyekiti niseme Waziri amekuwa mwalimu na dada yangu Ashatu mwalimu, wanajua kwenye maendeleo kuna-primitive way of wealth accumulation, nchi hii huko nyuma watu walipiga dili niwaombe hebu kale kaofisi namba 43 pale Hazina, Dar es Salaam ambako kamekuwa- connected na TAKUKURU ambako wafanyabiashara wanapiga foleni mpaka leo kuhojiwa mambo ya mwaka 2008, 2009, 2010.

Nikuombe Rais Magufuli ni man of decision mpelekee, toeni amnesty, watu waliowahi kupiga deal jamani Mheshimiwa Mpango hawezi kufukuzwa hata siku moja kwa wizi hata siku moja I can bet. Lakini huko nyuma watu walipiga deal, na deal zote zilianzia Serikalini, leo wanao- suffer ni wafanyabiashara, wanauza mali zao kulipa madeni ya miaka ya nyuma, tutawaumiza, wasameheni tangazeni amnesty, atakayeiba kuanzia leo mumshughulikie. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono, ninachokiomba Serikali fanyeni harmonization mipango na bajeti havionani, ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza nishukuru kwa kupata fursa ya kuchangia. Nina mambo machache na ningeomba Bunge hili tumsaidie Waziri na Naibu wake na Katibu Mkuu ili mwaka kesho wakija watuambie wamepunguza vifo vya akinamama kwa kiwango gani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, takwimu zipo na ukitazama vifo vya akinamama vinachangiwa na nini? Moja ni access to health services, wao kutopata huduma nayo ni moja kati ya sababu kubwa inayowachangia kupatikana kwa vifo vya akinamama. Kwa takwimu tunapoteza akinamama 42 kwa siku kama nchi. Kwa hiyo, nilichokuwa nataka niombe ni nini?
Mheshimiwa Spika, nataka niombe Bunge hili tupitishe, tuitake Wizara ya Fedha impatie Waziri wa Afya shilingi bilioni 7.5 mwaka huu ili akinamama wajawazito wote wakatiwe Bima ya Afya ya National Health Insurance Fund. Kutokana na takwimu za nchi yetu, kwa wastani akinamama wanaojifungua kwa mwaka ni average ya akinamama milioni moja na laki mbili, maximum milioni moja na laki tano. Wakipata Bima ya Afya ya average ya shilingi 50,400 ni sawasawa na shilingi bilioni 7.5. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Waziri wa Afya aidhinishiwe fedha hizo, Waziri wa Fedha akatafute fedha hizo popote ili akinamama hawa nchi nzima kwa sababu mama anakwenda kliniki, akienda kliniki anakuwa registered, anakatiwa bima ya afya, baada ya miezi tisa anakwenda kujifungua bila kwenda na gloves, wembe wala kitu chochote na tui-task bima ya afya kuweza kulifanya jambo hili. Hii itakuwa ni njia moja ya kutatua tatizo au kupunguza vifo vya akinamama kwa sababu kila mama mjamzito atakuwa amepata haki ya kuleta kiumbe duniani bila matatizo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nasema hivi kwa sababu sisi sote Wabunge tunafahamu ugumu wa maisha wa watu wetu, nataka nitolee mfano Nzega. Leo theatre iliyoko katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega na nimshukuru Waziri na Katibu Mkuu, katika theatre tatu zilizojengwa na ADB katika Wilaya ya Nzega, theatre iliyoko katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega imefunguliwa, bado theatre ya ndugu yangu Kigwangalla iliyoko katika Kata ya Lusu haijafunguliwa na theatre iliyoko Itogo kwa Mheshimiwa Selemani Zedi haijafunguliwa. Kumtoa mama Bukene kumleta Nzega ni kilometa zaidi ya 50 ili aweze kuja kupata huduma. Kwanza anaingia gharama ya usafiri, lakini bado akifika hospitalini anatakiwa aende na zile accessories ili aweze kupata hiyo huduma.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tukiwapatia bima akinamama nchi nzima, kwanza tutakuwa tumetekeleza ahadi na ilani ya chama chetu, tulisema akinamama wajawazito watapata huduma ya afya bure. Kwa hiyo, tuwakatie bima na ningeomba Waheshimiwa Wabunge tuungane pamoja kuitaka Serikali impatie Mheshimiwa Ummy shilingi bilioni 7.5 ili mwaka huu akinamama wajawazito wote nchi nzima, wakatiwe bima ya afya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo la pili, sera ya afya inasimamiwa na Wizara ya Afya. Hili tatizo wewe umelisema katika lugha nzuri tu kwamba suala la afya ni TAMISEMI na nini; ni sahihi kabisa na ndugu yangu Sugu ameligusia, tutazame, D by D ambayo kama nchi tumei-adopt, kwenye Sekta ya Afya na ikija Wizara ya Elimu na nikipata fursa nitaongea, is it practical? Ningeomba Bunge hili kwa mwaka huu, tumtake Waziri wa afya, akabidhiwe hospitali zote zilizoko katika mikoa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nasema hivyo kwa sababu hii sekta ya afya katika nchi yetu inasimamiwa na Wizara ya Afya, on the other hand TAMISEMI, on the other hand Utumishi, Wizara tatu zinasimamia sekta moja, hatutopata efficiency. Kwa hiyo, ningeomba Bunge hili kwa mwaka huu wa fedha tumkabidhi Waziri wa Afya hospitali zote za Mikoa, siyo tu za Rufaa za Mikoa zote, kila Mkoa ukiwa na hospitali ya mkoa na kama mkoa hauna hospitali ya Mkoa, hospitali moja itambuliwe kuwa ni hospitali ya mkoa, akabidhiwe Waziri wa Afya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hii itatusaidia mambo yafuatayo; itatusaidia suala la usimamizi wa sera, itatusaidia katika usimamizi wa sekta ya afya katika hospitali ile, itasimamia ugharamiaji na uendeshaji, TAMISEMI tumwachie jukumu la ku-develop infrastructure peke yake. Kwa sababu haina mantiki, anayesimamia sera, hata tukienda Nzega pale mimi na Mheshimiwa Kigwangalla, hana mamlaka ya kumsimamia Afisa yeyote katika Hospitali ya Wilaya. Mfano, siku nne zilizopita katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega hakuna umeme, Daktari hayupo, wagonjwa wamejaa OPD. Kwa hiyo, inabidi mimi ama Kigwangalla amtafute Mkurugenzi, bwana watu wako hawapo kazini na hakuna umeme, lakini Waziri hana mamlaka na yule Daktari aliyeko pale na huyu ndiye anasimamia afya.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ningeomba kwa mwaka huu tuwakabidhi Wizara ya Afya Hospitali za Mikoa, bajeti ya mwaka kesho, Wizara ya Afya ije ichukue hospitali zote za Wilaya ziwe chini ya Wizara ya Afya, kwa sababu wao ndio wanasimamia sera na wao ndiyo tutawawajibisha juu ya ubovu wa afya katika nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niwaombe Waheshimiwa Wabunge wenzangu, kama Bunge tuchukue jukumu la kutoa leadership katika nchi hii juu ya suala la D by D. D by D is not practical kwenye sekta ya afya, is not practical kwenye sekta ya elimu. Leo hii nataka nitolee mfano watoto wa form four wakifeli tunasema Wizara ya Elimu ime-perform hovyo, lakini hana mamlaka, hasimamii uendeshaji wala ugharamiaji, ndiyo hivyo hivyo kwenye Wizara ya Afya, Waziri wa Afya anasimamia sera tu. Kwa hiyo anatengeneza sera pale, anaiangalia ofisini kwake, mimi ni mjumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii, nataka niwaambie for my little experience, katika sekta mismanaged katika nchi hii ni sekta mbili, afya na elimu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niseme kama Mbunge wa Chama cha Mapinduzi na nataka nikupe mfano, wazee wa miaka 60 watoto chini ya umri wa miaka mitano, magonjwa sugu yasiyotibika, kwa maana ya kisukari, pressure na UKIMWI na mengine mama wajawazito hawa wote kisera wanatakiwa wapate huduma bora na huduma bure. Ukienda leo kufanya tathimini katika hospitali zetu hawa wana-constitute 70% ya wagonjwa wanaokwenda hospitali, lakini central government hai-subsidize fedha kwenye hospitali hizo. Kwa sababu tumesema kisera wapate huduma bure, lakini watakwenda pale, matokeo yake ataandikishiwa cheti, atafika pale, hatopata huduma, ataambiwa nenda dukani kalete gloves. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ningeomba ili mwaka kesho tuingie kwenye rekodi ya nchi hii, Wabunge wa Chama cha Mapinduzi na Wabunge wa Kambi ya Upinzani, tuungane kumsaidia mwaka huu Mheshimiwa Ummy na Mheshimiwa Kigwangalla, wawaondolee matatizo mama mjamzito katika nchi hii kwa kumpatia bima ya afya. It is doable, naamini Serikali inaweza na ni ahadi yetu kama Chama cha Mapinduzi, tuliwapa Watanzania kwamba mama mjamzito atapata huduma bure na bora. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na mwisho namwomba Waziri pale Nzega, sisi tumejenga OPD mpya, Mheshimiwa Kigwangalla anajua tumeishia njiani, kwa sababu imekuja amri ya maabara na madawati hatuna fedha…
SPIKA: Ahsante sana.
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Tunaomba mtusaidie, ahsanteni.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, nitumie nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa fursa hii na kutujalia sote afya na kushiriki kujadili mjadala huu unaohusu maslahi ya wananchi wa nchi yetu. Vilevile nitumie nafasi hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa dhati kabisa kwa michango yao ya hizi siku mbili na maoni waliyoyatoa.

Mheshimiwa Spika, ili nisipoteze muda, niende moja kwa moja katika hoja ambazo Waheshimiwa Wabunge wametoa. Hoja ya kwanza ambayo imejadiliwa kwa uchungu na maoni mengi ya Waheshimiwa Wabunge ni hoja ya stakabadhi ghalani. Kama unavyofahamu stakabadhi ghalani inatekelezwa kwa mujibu wa sheria. Mfumo wa stakabadhi ghalani ni moja kati ya mifumo ambayo inatumika katika mauzo ya mazao. Wizara ya Kilimo sio mara moja wala mara mbili tumesema hadharani msimamo na mwelekeo wa Wizara ya Kilimo katika suala la stakabadhi ghalani. Naomba nitumie nafasi hii kuliambia Bunge lako Tukufu na kuwaambia wakulima wa nchi hii kwamba msimamo wetu tutalinda haki za wakulima na tutafanya maamuzi kwa maslahi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala hili, hatuwezi kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani katika kila zao. Kila zao lina tabia na mfumo wake. Yapo maeneo ambayo hatuwezi kuuondoa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa sababu umefanya vizuri. Mfumo wa stakabadhi ghalani umefanya vizuri katika zao la korosho, hatuwezi kuuondoa mfumo wa stakabadhi ghalani wala mfumo wa ushirika. Mfumo wa stakabadhi ghalani umefanya vizuri katika zao la tumbaku, hatuwezi kuuondoa mfumo wa stakabadhi ghalani na mfumo wa ushirika katika zao la tumbaku. Tutarekebisha changamoto zilizoko katika eneo hilo lakini sio kuuondoa mfumo wa stakabadhi ghalani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini hatuwezi kutekeleza mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye maeneo ambayo hakuna miundombinu ambayo imeainishwa kisheria na kikanuni. Tumesema hatuwezi kutekeleza mfumo wa stakabadhi ghalani katika Mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara, Songwe na Katavi. Katika mikoa yote hii hatutekelezi siyo kwa nia mbaya bali ni kwa sababu mikoa hii haina mifumo ambayo inaweza kumfanya mkulima akafaidika na mfumo wa stakabadhi ghalani. Ni jukumu letu kuendelea kuijenga mifumo hiyo na wakati ukifika tutatoa elimu na tutaenda kwenye stakabadhi ghalani, lakini siyo sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini yako mazao hatuwezi kupeleka katika mfumo wa stakabadhi ghalani sasa hivi mfano ni ufuta, choroko, dengu na mbaazi. Hata katika mikoa ambayo tuna-practice mfumo wa stakabadhi katika Mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Mara na mikoa ambayo inazalisha pamba, hatutatekeleza mfumo wa stakabadhi ghalani katika dengu wala choroko, tutaweka nguvu katika mfumo wa ushirika na mfumo wa stakabadhi ghalani katika maeneo hayo. Kwa hiyo, nilitaka nimtoe hofu Mheshimiwa Mulugo, hatutatekeleza mfumo wa stakabadhi ghalani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, mwenye mamlaka na instrument na kanuni ya kutoa maelekezo zao gani liingie katika mfumo wa stakabadhi ghalani ni Waziri wa Kilimo. Huyu ndiye mwenye mamlaka. Sisi kama Wizara na nitumie nafasi hii kuwaambia Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote, atakayetoa mwongozo zao gani linaingia katika mfumo wa stakabadhi ghalani ni Waziri wa Kilimo na wala siyo mtu yeyote. Kwa hiyo, nataka niwaombe Waheshimiwa Wabunge ambao walikuwa wamedhamiria kushika shilingi kwa sababu ya hoja ya mfumo wa stakabadhi ghalani kama kulitokea makosa tutarekebisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mfumo wa stakabadhi ghalani kote unatumika kwa ajili ya financing. Sisi kama Wizara tunashirikiana na wenzetu wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa ajili ya kufanya mapitio na kuungalia mfumo huu. Tunafanya pilot na benki za biashara, tumefanya Igunga na Katavi, sasa hivi wakulima wa mpunga wanahifadhi mipunga yao katika ghala, wanapewa risiti, ile risiti inaenda katika benki na kuwa discounted, anakuwa na fedha, akiwa na fedha wakati anasubiri zao lake liongezeke bei ataliuza wakati atakapoamua yeye.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nirudie tena kwamba stakabadhi ghalani itatekelezwa katika maeneo ambayo imeonesha mafanikio. Hatuwezi kuwa na mfumo mmoja ukahudumia mazao yote, tutatengeneza mifumo ya kuuza mazao kutokana na hitaji la eneo na zao lile. Kwa hiyo, niwaombe Waheshimiwa Wabunge walielewe hili na sisi tutaendelea kuwasiliana na wenzetu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wasiweze kubughudhi wanunuzi wanaonunua ufuta katika Mkoa wa Dodoma, wanaonunua mbaazi, choroko na dengu, mazao haya madogomadogo tunayaacha ili competition ichukue nafasi yake yaweze kukua na volume iongezeke. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo tuna zao la soya, kama nchi tumepata mkataba wa miaka mitatu wa kuuza zao la soya katika nchi ya China na wakulima ndio wameanza kwenda kulima. Itakuwa ni jambo la ajabu tunaenda kuchukua zao la soya ambalo linalimwa kule Songea Vijijini, mkulima anapewa na mnunuzi Sh.1,000/= bei ya shambani halafu tunalazimisha liingie kwenye stakabadhi ya ghala ili liingie katika mfumo wa ushirika aanze kukatwa tozo mbalimbali siku ya mwisho anaondoka na Sh.800/=. Hii hatutaruhusu Waheshimiwa Wabunge na ninataka niwape commitment ya Wizara ya Kilimo kwamba tutajenga mifumo ya masoko kutokana na zao na mahitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, korosho iteandelea kubaki katika mfumo wa stakabadhi ghalani katika Mikoa ya Kusini. Tarehe 29 tunazindua mfumo wa kuuza ufuta katika Mkoa wa Lindi na tutauza kwa stakabadhi ya ghala kwa sababu umeonesha mafanikio katika maeneo hayo, hivyo hatuwezi kuua mfumo huu. Niwaombe Waheshimiwa Wabunge tusiuwe mifumo tunayoijenga, turekebishe matatizo yaliyopo katika mifumo bila kuathiri mambo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo limeongelewa na Waheshimiwa Wabunge kwa uchungu mkubwa ni suala la export levy kwenye zao la korosho. Sisi kama Wizara ya Kilimo tunaamini mazao haya ya kilimo yana uwezo wa kujiendesha yenyewe. Takwimu, tathmini na experience imeonesha kwamba wakulima wanaweza kujiendesha wenyewe tukiwajengea mazingira mazuri na sisi ndiyo kazi yetu. Kwa hiyo, nataka niwahakikishie kwanza suala la intervention ku-disturb mifumo iliyojengwa vizuri hatuwezi kulirudia jambo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini suala la export levy, nataka nitoe commitment katika Bunge lako kwamba tunalichukua tunaenda kulifanyia kazi, lakini sasa hivi tunaenda shambani. Tunazo takwimu zao la korosho lilifikia metric tons 320,000 wakulima walipewa pembejeo, uzalishaji wa korosho mkulima akienda shambani ili aweze kuzalisha korosho kwa gharama za input peke yake anatumia Sh.327/= kwa kilo, gharama zake za uzalishaji.

Mheshimiwa Spika, mimi namshukuru sana Mbunge wa Liwale na Mheshimiwa Nape, msimu uliopita baada ya maua ya korosho kuanza kuanguka walipiga kelele tukatuma watu wa TARI Naliendele waende wakafanye study kwa nini maua ya korosho yanaanguka. Spika nawe ni mkulima wa korosho unafahamu changamoto ya kuhudumia zao la korosho, hatuwezi kumuachia mkulima wa korosho mfumo wa huria katika ku-finance input, ni lazima tutafute njia ya kumpunguzia gharama.

Mheshimiwa Spika, dude lile la kupulizia peke yake, mimi nimefika shambani kwako nimekukuta wewe ukihangaika na Afisa Magereza wa Gereza la Mpwapwa, lile bomba peke yake linauzwa shilingi 1,000,000, mkulima gani anaweza kulinunua bomba lile, ni difficult.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge tukiwa wakweli ni lazima tutafute njia ya ku-finance namna hii. Hatua ya kwanza tuliyochukua ni kuanzisha bulk procurement system. Kule Kusini na Bunge lako lifahamu, mkulima wa korosho inapofika wakati wa kwenda kununua sulphur anaenda kukopa. Akienda kujiandikisha kwamba anataka kukopa kuna microfinance ziko kule, sulphur ambayo mkulima anaenda kukopa kwenye market price ni shilingi 32,000 lakini wakulima wananunua mpaka shilingi 40,000 mpaka shilingi 50,000.

Mheshimiwa Spika, akienda kukopa kwenye microfinance anajaza idadi ya mifuko anayotaka halafu yule mwenye microfinance anaenda kwa supplier anamwambia nipe sulphur, yeye anaichukua kwa shilingi 32,000 halafu anampa mkulima kwa shilingi 40,000 halafu ile shilingi 40,000 inatozwa interest ya 2% kila mwezi. Wanao-benefit ni service provider na wala sio farmer. Tumechukua hatua, tumeamua safari hii vyama vyote vya ushirika vimeleta mahitaji, tumekitumia chama kimoja, bei ya sulphur imeshuka mpaka shilingi 29,750. Kwa kukokotoa kwetu huku katika market rate mkulima alikuwa anatumia shilingi 300 kwa kilo kwenye input.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge la kwanza, suala la export levy tunaenda kulifanyia kazi, tumewasikia, tutatafuta solution, lakini wakulima watagawiwa pembejeo zote kutokana na mahitaji yao. Kwa mara ya kwanza mpaka sasa sekta hii inadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 30. Sisi sote tunafahamu, Mheshimiwa Katani na Mheshimiwa Nape wanafahamu, kila mmoja anafahamu kule kwenye korosho mkulima akivuna anaeenda kukopa kwenye chama cha msingi ni Hussein, anayeenda kuuza ni Nape. Matokeo yake sekta yote inadaiwa, mkulima anadaiwa, chama cha ushirika kinadaiwa, Bodi ya Korosho inadaiwa, sekta haikopesheki, taasisi za fedha zinajitoa kuhudumia sekta hii. Kwa hiyo, njia pekee na sisi tuwaahidi kwamba tunaamini katika kuanzisha mifuko ya kuendeleza mazao, hiyo ndio njia itakayomsaidia mkulima. Kwa hiyo, hii hoja ya export levy tunaichukua tunaenda kuifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hapa tumejadili suala la korosho ya Pwani. Kwa muda mrefu humu ndani tunazungumzia korosho ya Pwani haina ubora, kwa nini haina ubora? Majibu yanakuja kwamba inapata unyevu. Korosho ya Pwani inapata unyevu, iki-mature inakuwa nyeusi.

Mheshimiwa Spika, Pwani kuna mvua nyingi. Kwa hiyo, kama Wizara tumechukua hatua gani ambayo tunaanza kuitekeleza sasa hivi? Vyama vyote vya msingi na nimshukuru sana Mheshimiwa Ulega, Mheshimiwa Mchengerwa na Mheshimiwa Twaha, safari hii tumeamua wakulima wote wa Pwani kuanzia mwezi ujao vyama vya msingi vyote tutavigawia maturubai kwa ajili ya kuanikia korosho zao, hili ni jambo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, katika sekta ya korosho kuanzia Pwani, Lindi, Mtwara mpaka Ruvuma wana AMCOS 623, tumeamua kila AMCOS tutaigawia bomba kwa ajili ya kupulizia korosho za wakulima wao kwa sababu watu wana-make profit in the middle. Tutatumia mifuko ya mazao ku-finance na ku-subsidize input kwenye sekta ya kilimo na hili linawezekana. Kwa hiyo, tunaomba Waheshimiwa Wabunge mtupe fursa tuweze kulifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la export levy tumelichukua, sasa hivi tunaenda kwenye msimu na tutalifanyia kazi. Tutajadiliana ndani ya Serikali ili tuweze kupata solution ambayo haitamuumiza mkulima.

Mheshimiwa Spika, niongelee suala la tumbaku. Takwimu zinaonesha tumbaku ilifika metric tons 120,000. Mimi nishukuru humu ndani kwa siku hizi mbili nimejifunza, jedwali lile linaonesha trend ya tumbaku kwa kipindi cha miaka kumi, kuanguka kule kwa tumbaku hakujasababishwa na mkulima hata mmoja. Humu ndani tumekuwa tukisikia kauli kwamba korosho, tumbaku, pamba na kahawa ni mazao ya siasa, sio kweli, haya ni mazao ya kibiashara. Kwa hiyo, let us put aside politics kwenye kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumbaku hii imeporomoka kwa sababu ya policy zetu mwaka 2014-2015 tulienda kushtaki makampuni yote na pressure ilitoka ndani tukayapiga faini ya trilioni saba TLTC aliondoka kwenye nchi hii tunachukua hatua gani. Mwaka jana kupitia Bunge lako Tukufu hili, tulibadilisha sheria ya LCC, tukawaondolea faini zote makampuni haya. Wakalipa tozo ya shilingi dola 300,000 kutoka trilioni saba it was unfair na haikuwa haki, hawa wanafanya biashara matokeo yake makampuni yaka-pull out sekta ya tumbaku ikaanguka mpaka tani 36,000 mwaka jana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kwa hatua tulizochukua mwaka huu wakulima wa tumbaku wamepeleka sokoni tani 67,000 ambazo tumeanza kuziuza. Just kwa maamuzi madogo tu ya kufuta tozo tulizowapiga, faini kuwapiga na kukaa nao mezani wanunuzi wamekuja zao letu tunalouza safari hii ni tani 67,000 kutoka tani 39,000 na sisi tuwaahidi kwamba tutalinda wakulima na tutawalinda wanunuzi wanaonunua mazao ya kilimo hakuna njia nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini jambo la pili ambalo tunafanya kwenye tumbaku, mkulima wa tumbaku zao za tumbaku linakuwa determined na biashara ya dunia unapozalisha tani moja ya tumbaku mnatakiwa mpande miti 600 lazima wanunuzi wajiridhishe. Kinachotokea mkulima anakatwa 0.092 dola kwa kilo kwa ajili ya ku-finance mfumo wa kupanda miti. Nataka nikwambie kwa mwaka wakulima wa nchi hii wanachangia bilioni 25 lakini miche hile haipandwi popote tumechukua hatua tumebadilisha mfumo sasa hivi fedha zile zitakusanywa kwenye one account tutatangaza tender tutaingia makubaliano na TFC miche itapandwa na itaonekana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwasababu hivi zilikuwa ni shughuli za watu wanagawana viongozi Mikoani Mheshimiwa Kakoso anafahamu watu wanaotoka Katavi wanafahamu kilichotokea baada ya maamuzi haya tunabadilisha mfumo wa uharamiaji kwenye tumbaku. Mkulima wa tumbaku anakwenda kukopa yeye na AMCOS yake at the interest of 7 percent USD hawezi kupata faida, atapata hasara tu tumeamua tumebadilisha mfumo kwanza procurement ya input yote tunaagiza kutoka kwa producers hatutotumia watu wa kati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili tumesema kwamba tunatumia LC model kwamba supplier anapeleka pembejeo tunamlipa baada ya siku 360 baada ya mnada mkulima anapata bila riba na tumevizuia vyama vyote vya ushirika kwenda kukopa katika benki zinazozalisha tumbaku kwa dola na kwa riba kwa sababu mbolea tutapeleka, dawa tutapeleka, supplier atapewa LC baada ya siku 360 mtoa huduma atapata fedha yake na tumekubaliana na taasisi za fedha hili tunalifanya.

Mheshimiwa Spika, jambo jingine ambalo nilitaka niliongelee ni zao la pamba, zao letu la pamba lilidondoka mpaka tani 120,000 na sisi wote tunafahamu na graph ile inaonekana tulifika tani 348,000 mwaka 2019 mkulima alivyopewa mbegu alipewa dawa tukabadili policy zao likadondoka, hatua gani tumechukua safari hii, cha kwanza tumewagawia wakulima wa pamba wote mbegu bila kulipia, la pili tumewagawia dawa zote bila usumbufu wowote tumekaa na wanunuzi na vyama vya ushirika lakini tumewapatia input hizi bila wao kwenda kukopa benki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, benki zimetupa LC watoa huduma wamepeleka pembejeo baada ya kupeleka pembejeo zitalipwa pembejeo baada ya mkulima kuuza zao lake. Mwaka huu tunavuna metric tonnes kati ya 350,000 hadi 400,000 na mkulima ataenda kuuza kwa bei ya kuanzia 1050 bila ukatwa hata shilingi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka niliombe Bunge lako Tukufu tupo tayari kufanya mabadiliko, tupo tayari kuchukua hatua tutakubaliana na maoni na ushauri wenu tusaidiane kwa sababu jambo hili hatuwezi kulifanya peke yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo jingine ambalo nilitaka niliongelee ni suala la umwagiliaji ni kweli bila mfumo mzuri wa umwagiliaji hatuwezi kupiga hatua. Wizara kwanini tunafanya tathmini? Tunafanya tathmini kwa sababu experience yetu ya muda mfupi imetuonesha kwamba tunahitaji kufanya mabadiliko makubwa kwenye tume yetu ya umwajiliaji, tutawaleteeni sheria hapa. Tunataka kuibadilisha tume kuwa wakala wa umwagiliaji kuwa agency kama ilivyo TARURA kama zilivyo nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini la pili tunabadili mifumo kwasababu hii mifumo ya umwagiliaji tunatumia gharama nyingi kujenga mradi mmoja tumeamua katika bajeti hii ambayo mtatupitishia Waheshimiwa Wabunge la kwanza tumeanzia kitu kinaitwa irrigation development fund ambayo kwa kutumia fedha zetu za ndani tumetenga zaidi ya bilioni 30.

Mheshimiwa Spika, lakini hatua ya pili tutakayoichukua ni kwamba tume ya umwagiliaji tumewaagiza kwamba watangaze tender kwa ajili ya kununua vifaa, ili kuanzia mwaka huu wa fedha kwenda mbele kazi yetu ya kwanza pamoja na ku-repair miradi iliyopo lakini nikuchimba mabwawa maeneo yote ambayo tunaona kwamba kuna uwezekano wa kuhifadhi maji, hii ndio itakuwa priority yetu tutaangiza vifaa tutakuwa navyo wenyewe tumefanya pilot project kwenye mradi wa Ruaha chini na Mheshimiwa Mbunge yule pale shahidi tumetumia excavator zetu wenyewe bila kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kuu-repair ule mradi.

Mheshimiwa Spika, nilitaka niliongelee jambo jingine kuhusu suala la mahindi, ni kweli mwaka jana mahindi yalifika mpaka kilo 1,000 -1,100 lakini sasa hivi mahindi yameonekana bei imeshuka. Nashukuru nimalizie tu kuwaambia waheshimiwa Wabunge kwamba tunaamini kwamba bila kui-engage sekta binafsi katika sekta ya kilimo hatuwezi kwenda mbele na sisi tutajenga mazingira kuhakikisha kwamba sekta binafsi inakuwa sehemu ya safari ya kilimo ili tuweze kupiga hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Mimi nina mambo machache tu. Nitaunga mkono bajeti ya Mheshimiwa Waziri akinipa majibu juu ya mambo yafuatayo:-
Jambo la kwanza ahadi ya Mheshimiwa Rais Kikwete aliyeitoa mwaka 2005 na baadaye mwaka 2010 katika Jimbo la Nzega na bahati nzuri Meneja wa TANROADS, Mkoa wa Tabora yupo, juu ya ujenzi wa lami kilomita 10 ndani ya Mji wa Nzega, ahadi hii ilikuwa ya Rais Kikwete. Mwaka 2014, Rais Kikwete alifika Nzega akiwa na Rais wa sasa wakati huo Waziri wa Ujenzi aliiongelea barabara hii. Baadaye Rais Magufuli akiwa mgombea aliongelea suala la ahadi hii. Kwa hiyo, naomba majibu kwa Mheshimiwa Waziri juu ya suala hili nijue nini kinafanyika ili niweze kumuunga mkono na yeye anafahamu namheshimu sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, Mheshimiwa Rais aliahidi madaraja mawili katika Jimbo la Nzega na ni kwa sababu Halmashauri kupitia TAMISEMI hawana uwezo wa kuyajenga madaraja haya, daraja la Nhobora na daraja la Butandula pamoja na barabara zake. Hli ni jambo lingine ambalo napenda kupata majibu.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la tatu, nataka niseme kidogo kuhusu Bandari ya Bagamoyo. Mimi naiunga mkono kama strategic investment kwa nchi na study zinaonekana kwamba by 2030-2035, six percent ya mzigo wa dunia wa kibiashara unaopita katika bahari utapita kwenye bahari ya Hindi. Tathmini za kisayansi zinaonesha hakuna bandari itakayokuwa salama duniani kwa gharika mbalimbali kama Bandari ya Bagamoyo. (Makofi)
Mheshimwia Naibu Spika, lakini tatizo langu ni moja kama nchi tunalipa fidia, kama nchi tunachimba kuongeza kina cha bandari hii, what is the stake ya kwetu, share yetu kama Taifa kwenye mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni asilimia ngapi? Kwa sababu the biggest part ya expenses tunafanya sisi kama nchi, kupokea wharfage tu haitutoshi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la nne, Rais Kikwete aliahidi Wilaya ya Nzega wakati anamnadi Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla na Mheshimiwa Selemani Zedi, ujenzi wa barabara ya kutoka Tabora kupita Mambali kufika Itobo kwenda Kahama. Nitaomba majibu kutoka kwa Mheshimiwa Waziri nini kinafanyika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hizi nilizozitaja ni barabara muhimu sana kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora. Vilevile madaraja haya, daraja la Nhobora ni daraja la uhai kwa wananchi wa Jimbo la Nzega kwa sababu hili daraja mto wake ndiyo unaenda ku-connect kule ambako Mheshimiwa Rais Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi alijenga daraja kwa kutumia local engineers Wilaya ya Igunga. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho nilitaka niwaambie Waheshimiwa Wabunge tuna haki ya kukosoa na nataka niwashauri Waheshimiwa Mawaziri, kwa karne hii tumepata the most honest President. Rais Magufuli is honest, ni mkweli, kama hataki jambo atasema, hana siasa. Niwaombe Waheshimiwa Mawaziri mmepata kiongozi wa kufanya naye kazi ambaye ni most result oriented, msaidieni kumshauri, msiogope. Sisi huku mtaani tunasema mna nidhamu ya uoga, tunawaomba kama kweli ipo basi msiifanye hii. Kwa sababu huyu mtu deep in his heart anachokisema ndicho anachokiamini na hata kama kuna makosa amewahi kufanya au anafanya basi tujue deep in his heart hana malicious interest na nchi hii. Mheshimiwa Magufuli ana-represent the true picture ya common Tanzanian na anayajua maisha ya Watanzania, kwa hiyo, tumsaidie kuweza kufikisha nchi hii anakotaka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Mimi nilitaka niseme
kwanza niipongeze Kamati kwa taarifa walizoleta, lakini jambo moja nilitaka niseme.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nchi tumekuwa tukijadili suala la kuwa na viwanda.
Mambo mawili ni muhimu sana, sekta ya miundombinu na sekta ya umeme. Nilitaka niishauri
Serikali, imefika wakati wa ku-embrace private sector (PPP), energy sector mawazo ya kufikiri
kwamba tutatumia fedha zetu za ndani kununua majenereta, kuzalisha umeme sisi, TANESCO
izalishe umeme, ifanye nini, hatutopiga hatua ya kuwa na hizo megawati 10,000 tunazotaka.
(Makofi)
Kwa hiyo, mimi ningeshauri, wizara mnafanya kazi kubwa sana kwenye rural energy,
mnafanya jitihada kubwa sana lakini mfungue fursa kwa ajili ya uwekezaji wa sekta binafsi
kwenye umeme, ili watu waweze ku-compete na kupatikana umeme wa bei rahisi ili Mwijage
atuletee viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini umeme hauwezi kuja bila kuwa na proper incentive
scheme kwenye sekta. Ningewashauri Wizara ya Nishati pamoja na Wizara ya Fedha, na Wizara
ya Viwanda na Biashara, kaeni chini m-develop incentive scheme kwa ajili ya uwekezaji wa
private sector mziweke wazi ili wawekezaji wajue tukienda Tanzania kuwekeza mtaji wetu, these
are the benefits na Wizara ya Fedha iache mindset ya kuweka kodi kwenye inputs. Tarajieni
kuvuna kwenye matokeo hilo ni jambo muhimu sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, nilitaka niiombe Wizara ya Miundombinu, mmeanza jitihada
kubwa sana ya kujenga reli ya kati, kupanua bandari, ni jambo jema. Lakini kule kwetu Nzega,
kama Mkoa wa Tabora kuna barabara; mwaka 2014/2015 mlituwekea fedha kwa ajili ya visibility
study hazikutosha, kwa hiyo ule mpango wa barabara ya kutoka Tabora kupita Mambali
kwenda Bukene, kwenda Itobo, kwenda Kahama mpaka leo imesimama. Ni ahadi ya Rais
Kikwete, ni ahadi ya Rais Magufuli, kwa hiyo, nakuomba kaka yangu Mheshimiwa Waziri wa
Miundombinu, tukumbuke barabara hiyo ni muhimu sana kwa uchumi wa eneo lile. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, kuna Daraja la Nhobola pale Nzega, Mheshimiwa
Waziri unafahamu, tumegonga sana mlango ofisini kwako kuomba haka kadaraja. Sasa hivi
wananchi wa jimbo la Nzega upande wa Nhobola hawavuki kwenda kupata mahitaji katika Mji
wa Nzega, inabidi wazunguke kwenda Tinde kwenda kupata mahitaji Mkoa wa Shinyanga
ambako ni mbali zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwenye uwekezaji wa reli, Mheshimiwa Waziri hakuna
clause muhimu ambayo mnatakiwa muiweke kama Serikali; mambo mawili, commitment ya
nchi ya mapato yetu ya ndani ambayo tunatoa shilingi kulipa mkandarasi yatumike kama
sehemu ya kulipa contract za ndani. Tukitumia zile fedha kumlipa mkandarasi wa nje maana
yake tuta-transfer dola kupeleka nje, zitatuumiza.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kukushukuru kwa kunipa fursa kuweza kuchangia katika Taarifa ya Kamati. La pili niishukuru Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji inayoongozwa na Dkt. Ishengoma kwa ushirikiano na support wanayotupa na wajumbe wote wa kamati kwa ushirikiano na support wanayotupa. Mapendekezo mengi waliyoleta mbele yako na sisi upande wa Serikali tunayaunga mkono na tutaenda kuyafanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, kwanza umenitaka nitoe taarifa kuhusu TARI Ilonga. Ni kweli shamba letu la kuzalisha mbegu za msingi za awali za TARI Ilonga wafugaji waliingia na kuharibu eneo kubwa. Nataka kulitaarifu tu Bunge lako Tukufu ni kwamba kama Serikali tulichukua hatua za haraka. Kwanza kuhakikisha kwamba tunarudisha uzalishaji wa zile mbegu za msingi ambazo ni muhimu kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo, lakini hatua ya pili ambayo tumeamua kufanya kama Serikali ni kwamba mashamba yote ya uzalishaji wa mbegu sasa tunayawekea fence ili kuondokana na hili tatizo la kuvamiwa na mifugo na ambalo limekuwa ni chanagamoto kubwa katika maeneo ambayo tunapatikana na wafugaji; na kuhakikisha kwamba tunaondoa hii changamoto ya kuvamia mashamba na kuweza kuondoa tatizo la magugu kwenye mashamba ya uzalishaji wa mbegu. Kwahi yo nataka nikutaarifu tu na kulitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba hakuna athari yeyote itakayotokana na mpango tuliyokuwa tumeuweka katika mwaka huu wa fedha kwenye eneo la uzalishaji wa mbegu kutokana na matatizo yaliyokuwepo.

Mheshimiwa Spika, nilitaka nichangie maeneo machache. Eneo la kwanza ni la ruzuku ya mbolea. Nikiri kwamba kuna changamoto, na changamoto inatokana kutokana na distribution network na kwanini kumekuwa na changamoto kubwa.

Mheshimiwa Spika, msimu wa kilimo wa 2021/2022 ambao mazao yake ndiyo tunatumia leo nchi yetu ililima jumla ya leo la kilimo hekta million 10.1, ndilo tulilolima kama nchi nzima. Baada ya Serikali kutangaza ruzuku mwaka huu tumelima jumla ya eneo la kilimo hekta million 15,890,362. Na ukiangalia Mikoa mikuu ya uzalishaji, kwa mfano Mkoa kama wa Ruvuma umeongeza eneo la kilimo kutoka eneo la hekta laki sita na elfu thelathini mpaka laki tisa na elfu sitini. Tafsiri yake nini? Tafsiri yake nikwamba distribution network itakuwa na mzigo mkubwa. Sisi kama Serikali hatua ya kwanza tuliyochukua tumehakikisha kuanza kuvisajili vyama vya ushirika. Maeneo ambayo kuna vyama vya ushirika tumevipa status ya kuwa distributor wa mbolea katika maeneo hayo; na hii inatupunguzia pressure na kutuondolea tatizo.

Mheshimiwa Spika, hatua ya pili tunayoichukua, sasa hivi tumeanza kusajili maghala yote yaliyoko vijijini na kuyapa status kama ni selling point kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo ili tutakapifika kuanzia mwezi wa saba, wa nane mbolea za kupandia na mbolea za kukuzia zote zinakuwepo katika vituo vya kuuzia mbolea na wakulima wanapouza mazao yao wanapata mbolea na kurudi. Hii itasaidia kuondoa huu utaratibu wa biashara ya mbolea ambayo waagizaji wote wanaagiza kuanzia mwezi wa tisa. Sasa tumewapa ruhusa, na hivi karibuni mtaona tangazo la pre-qualifications kwa ajili ya bulk procurement kwa mwaka ujao wa fedha. Naamini kwamba utaratibu huu utatuondolea pressure ya distributions network.

Mheshimiwa Spika, nitumie Bunge lako kuwashukuru Wabunge wote ambao wamekuwa wakipata changamoto, tukiwasiliana kwa ajili ya kutatua matatizo haya na wewe mwenyewe Mheshimiwa Spika, mara mbili mara tatu uligeuka kuwa Afisa Kilimo kupita katika maduka na kuwa TFRA Officer na umetusaidia sana, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Spika, nataka niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge, tutakumbana na changamoto, mfumo umeanza tarehe 15 Agosti. Naamini kwamba, maeneo mengi yamekuwa na upungufu, lakini upungufu huu utakwisha katika mwaka ujao wa fedha. Niwatoeni hofu, hatutakuwa na matumizi madogo kuliko ya msimu wa 2021/2022 ya mbolea katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka nichangie eneo la pili, eneo la mfumuko wa bei. Ni kweli bei ya chakula imepanda na ni vizuri Waheshimiwa Wabunge wote tukaelewa kwamba, chakula tunachokula leo ni kile kilichozalishwa msimu wa 2021/2022 ambapo wakulima walienda shambani wakiwa wamenunua pembejeo ghali, mara mbili ya bei iliyoko leo. Gharama za uzalishaji mwaka jana zilikuwa kubwa, pamoja na changamoto nyingine. Sasa hapa swali limeibuka miongoni mwa Wabunge; ruzuku hii inasaidia nini kwenye mfumuko wa bei? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hebu sote tufikiri leo, wakati unga ni shilingi 2,000 mkulima angekuwa anaenda dukani kununua mbolea kwa shilingi 140,000. Serikali imetoa ruzuku ili kumpunguzia ugumu wa maisha mwananchi huyu, leo badala ya kutumia shilingi 140,000, anatumia shilingi 70,000 anakuwa na disposable income ambayo anaweza kutumia kwenye shughuli nyingine. Serikali imempa ruzuku kwenye mbegu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kunti ametolea mbegu aina moja ya Hysun, lakini mbegu ya alizeti ambayo sasa hivi inauzwa kupitia taasisi za Serikali inauzwa kwa shilingi 10,000 ambayo katika bei ya soko la kawaida angeinunua shilingi 20,000. Naamini kwamba, gharama hizi ambazo tunakabiliana nazo sasa na kote duniani, njia bora ya kuondoa mfumuko wa bei ni kuongeza tija na kupunguza gharama za uzalishaji. Serikali inachukua hatua hizo na matokeo yake tutayaona kwenye msimu ujao wa uvunaji ambao tunaanza kuvuna kuanzia mwezi wa Aprili, Mei na Juni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sekta yetu ya kilimo, historically, na bahati nzuri wengine wamo humu walimu wametufundisha, wamefundisha na sisi tumesoma nyaraka mbalimbali; toka tunapata uhuru mfumo wetu wa mawasiliano kwenye kilimo ni kilimo cha kujikimu. Ndio maana kilimo toka nchi hii inapata uhuru kimeshindwa kuwaondoa watu kwenye dimbwi la umaskini. Ni lazima tukiri zama zimebadilika, mahitaji yamebadilika, hakiwezi kuendelea kuwa kilimo cha kujikimu, ni lazima kiwe kilimo ambacho kinamwondoa mtu kwenye umaskini na kumpatia kipato. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ili kilimo kiwe cha namna hiyo ni lazima tuwekeze kwenye tija. Niwaombe sana Waheshimiwa Wabunge watu-hold sisi responsible, Serikali kumsaidia mkulima kuongeza tija ya uzalishaji ili azalishe kwa tija na gharama za uzalishaji zitashuka na gharama za chakula zitashuka na wakulima watakuwa competitive ndani na nje ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo la mwisho, bajeti. Nataka nilihakikishie Bunge lako Tukufu, limetupitishia bajeti ya zaidi ya bilioni 900, eneo la umwagiliaji ni eneo la procurement. Leo hii tunavyoongea kama Wizara, miradi yote ambayo tulitarajia kui-commission kwa ajili ya mwaka huu wa fedha tumesha-procure, wakandarasi wameshapatikana na sasa tumeshasaini mikataba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kinachotokea, tunakojenga wakulima wanalima. Hatuwezi kuwazuia wasilime, tumewapeleka wakandarasi wanasubiri wakulima wavune. Tutaanza kuziona certificates kuanzia mwezi Mei, Juni na Julai, ndio zitakwenda Wizara ya Fedha nyingi kwa ajili ya malipo. Miradi hii ni ya miezi 18, naamini hatuna problem kubwa sana na Wizara ya fedha. Mimi ni mkweli, nakuhakikishia, nikiona nina tatizo nitaenda kwenye mamlaka za juu, lakini as I stand today, sina big problem na Wizara ya Fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu hela ya ruzuku ya mbolea; tumepokea bilioni 50…

SPIKA: Sekunde 30.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, tumepokea bilioni 50. Ruzuku ya safari hii ni tofauti kabisa na ruzuku za zamani, hatuwezi kumlipa importer au distributer fedha kabla ya mkulima kuchukua mbolea. Imetuletea shida na wasambazaji, lakini huu ndio mwelekeo sahihi, tunalipa baada ya mbolea kununuliwa na mkulima na kui-verify na kuona DN, QR Code na namba ya mkulima, ndio importer analipwa fedha yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, fedha zipo bilioni 150 na African Development Bank, dola milioni 41 ambazo zilikuwa kwa ajili ya ruzuku ya mbolea na zenyewe zimepatikana, tutawalipa suppliers wote na tunaubadili mfumo wote wa usambazaji wa mbolea katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, awali ya yote nitumie nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema na nikushukuru wewe na Bunge lako Tukufu kutoa fursa kwa Wabunge wengi kuchangia na pale ilipohitaji hata ratiba ilibadilishwa ili Wabunge waweze kuchangia hoja hii ambayo ni kwa maslahi ya Watanzania wengi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wamechangia Wabunge 88 kwa ujumla. Kwanza nitumie nafasi hii kuwashukuru Wabunge na niwaambie mwaka jana tulivyo-submit bajeti yetu hapa mawazo na ushauri wenu ni sehemu ya kuandaa mpango wetu wa mwaka ujao kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu sisi hatuishi in isolation, kwenye Kijiji tunaishi na watu na tunathamini sana michango yenu. Nataka niwaambie tu kwamba maoni na ushauri na critics zote mnazozitoa kwetu sisi ni sehemu ya lesson na niwahakikishie tunazichukua tunaenda kuzifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, zipo hoja zilizotolewa na Wabunge nyingi, inawezekana nisizijibu zote. Hoja ya kwanza ambayo nilitaka niseme ni je, tuna uhitaji ushirika? Jibu ni ndiyo. Je, tunahitaji ushirika wa namna gani? Tunahitaji ushirika unaoenda kumsaidia mkulima na wala siyo ushirika utakaomnyonya mkulima. Je, ushirika tulionao ni mtakatifu? Jibu ni kwamba ushirika tulionao una changamoto na ndiyo maana kuna Waziri wa Kilimo, kuna Tume ya Ushirika tuna wajibu wa kwenda kusimamia changamoto hizo. Je, upo ushirika unaowatendea haki wakulima kwenye nchi hii? Jibu ni ndiyo upo. Upo ushirika unaowaibia wakulima? Jibu ni ndiyo upo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo hatuwezi kwenda kuua mfumo wa ushirika katika nchi kwa sababu tu tunao washirika ambao siyo waaminifu. Tutachukua hatua na nimhakikishie Ndugu yangu Mbunge wa Mbozi na Wabunge wa Kahawa wa arabica, ilituchukua miaka miwili kujadiliana na kuelewana na wenzetu wa robusta, leo changamoto zilizoko kwenye robusta zimepungua, ushirika una compete na sekta binafsi, wanashindana sokoni, tunawapa mitaji, wanaingia kununua na mkulima analipwa fedha yake on time. Tutakuja kwenu Mbozi na nimwambie Mwenisongole kwa macho yangu nimeona viongozi wa ushirika wa Mbozi walivyowaibia wakulima wa kahawa na mimi nilimkamata, nikamuweka ndani na timu ya Wizara ya Kilimo imeenda, imetuletea takataka zilizoko. Nikuhakikishie tunaenda kufanyia kazi, wakulima wa Songwe, Mbozi mpaka Mbinga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii, Mrajisi wa Vyama vya Ushirika yuko hapa, ni marufuku Chama cha Ushirika kwenda kukopa fedha kabla ya msimu na kusema tunalipa malipo ya awali, halafu mzigo wa riba na gharama za uendeshaji mnaenda kumbebesha mkulima. Hii tabia ife na tutaenda na watu wetu kwenda kulifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, ushirika ni lazima tuuwezeshe. Tunafanya sasa hivi feasibility study ya TANICA. Tutaenda kuipa TANICA shilingi bilioni nane ili kui-capitalize iweze ku-compete na kuweza kufanya value addition, hili linawezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ni irrigation. Je, kuna matatizo kwenye Tume ya Umwagiliaji? Mwenyekiti wa PAC ametoka. Nataka nimwambie, taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imekuwa ni sehemu ambayo sisi ni kama instrument ya kufanyiakazi. Hatutaki kuwa hostage wa matatizo ya mwaka 2017 na 2018, ingekuwa hivyo leo hii kwenye hii nchi kwani TRC haikuanguka? ATCL haikuanguka? Si zilianguka? Hakukuwepo na ubadhirifu au mambo matatizo yaliyokuwepo? Ni jukumu letu sisi kufanyia, kuchukua hatua juu ya matatizo yaliyopo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, irrigation kwenye nchi yetu as a country toka mwaka 2000 hatukuwahi kuweka emphasis kwenye mifumo ya umwagiliaji na usimamiaji wa umwagiliaji katika nchi hii. Ndiyo ukweli! Tulitenga shilingi bilioni 20 na mimi nilikuwa Mbunge nakaa pale alipokaa Mheshimiwa Tabasam. Fedha haziendi, tunataraji kwamba zaidi ya Halmashauri mia moja na kitu, tunatenga fedha za usimamizi za umwagiliaji shilingi milioni 20. Hakuwezi kutokea muujiza! Ndiyo maana kuna hayo matatizo tuliyoyaona. Aliyaona Mkaguzi wa Hesabu za Serikali.

Mheshimiwa Spika, tumechukua hatua gani? Hatua ya kwanza Tume ya Umwagiliaji sasa imeenda kuwa na ofisi kila Wilaya. Pili, Mheshimiwa Rais katupa kibali tumeajiri ma- engineer sasa hivi wana mwezi mmoja tumewapeleka katika Wilaya. Tatu, tumewanunulia vitendeakazi tumenunua gari 53 tunapeleka katika kila Wilaya. Nne, tumeongeza bajeti na sasa hivi hakuna mradi wa umwagiliaji unaofanyika bila feasibility study. Nchi yetu Mwenyezi Mungu kaijalia hekta milioni zaidi ya 29 kwa miaka 60 tume-invest only 2.7 per cent ni aibu! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mama Samia kafanya nini? Kasema wekeni emphasis kwenye irrigation. Kwanza hauwezi kuweka fedha za umwagiliaji bila kutambua maeneo ya umwagiliaji, Naibu Waziri amesema. Tuna maji Ziwa Victoria mita 300 wakulima wanasubiri mvua. Tumefanya nini? Tunafanya feasibility study kuanzia Mara mpaka Kagera. Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu hata asipojenga Samia, atakuja kujenga mtu kwa sababu leo tunajenga Stigler’s waliofikiri juu ya Stigler’s na kufanya feasibility study na detailed design leo hawapo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo sisi plan zetu kama Wizara siyo za kesho, niwaambie Wabunge kama mnafikiri tunawekeza kwenye umwagiliaji kujenga mifereji ya mita mia mia siyo Wizara hii, siyo Waziri huyu. Tunafikiri kufanya miradi ya umwagiliaji ili tumwagilie kiangazi na masika. Tuna mradi wa 55 billion hapo kwa Mheshimiwa Lukuvi. Ule mradi tunaujenga kwa miaka miwili. Mradi ule tu barabara za mashamba ni kilometa 98. Mradi ule mifereji ni zaidi ya kilometa 100. Halafu mnataraji eti kuna hoja hapa kwamba imetengwa shilingi bilioni 300 fedha kwa nini hazijatoka zote? Labda tubadilishe utaratibu tuleteeni pale Wizarani zikae shilingi bilioni 300 na nyie ndiyo mna mamlaka badilisheni Sheria ya Manunuzi hapa, kila kitu iwe force account. Haina shida mimi nitaziweka ofisini, bwana eeh, chukua in advance. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, utaratibu ni kwamba miradi yote tuliyoiahidi mwaka jana mpaka kufikia mwezi Aprili, asilimia 70 tumeshasaini na leo ninavyowaambia miradi ya mwisho tumeipandisha kwenye mfumo. Tunaenda Juni 30 hatutakuwa tunadaiwa mradi mmoja. Wakandarasi wote watakuwa site na miradi hii inajengwa kwa miezi 18 mpaka 24, mwaka kesho ndiyo ina kamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, phase two tumesema miradi yote katika haya mabwawa 100 kwa kuwa tunajenga irrigation scheme sasa phase two kwenye fedha za mwaka kesho tunaanza kujenga mabwawa ili tulime mwaka mzima. Huu ndiyo mwelekeo wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, hapa ameongea Dada yangu Mheshimiwa Halima kasema tunafanya kilimo cha iPad na mimi namheshimu. It is a very good statement, ni kweli! Tunataka siku moja nchi hii na dunia hii watu waingie google wajifunze kilimo kilichofanywa Tanzania. Mimi nashangaa watu wanashindwa kuota, this is the country na mimi nataka niwaambie, sisi ndiyo purity ya nchi, kama sisi tunawaza kimaskini we are in trouble. Niwaambie ukweli! Kama sisi tunawaza kimaskini tena tuna tatizo kubwa mno ambalo linatukabili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna hoja ya BBT. Kwanza naomba ni-clarify. BBT ina-compete na wakulima wadogo waliopo? Jibu ni hapana. BBT imesababisha wakulima wadogo tuwaweke pembeni? Jibu ni Hapana. BBT imesababisha wakulima wadogo wasihudumiwe? Ruzuku ya mbolea ina- target wakulima wadogo. Tunavyopeleka Maafisa Ugani, tuna-target wakulima wadogo.

Mheshimiwa Spika, kwenye bajeti hii tumeweka fedha kwa ili kila Halmashauri tuchukue wakulima au mashamba 150, tutawachimbia kisima bure, tutawawekea pampu kwa kutumia solar technology, tutawawekea tank la kuanzia lita 5,000 na tutawawekea irrigation kit ya ekari 2.5. Huyu ni nani? Mkulima mdogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza nataka niwaambie Wabunge wenzangu, ukiona Taifa lolote asilimia 70 ya population wako shambani, ni Taifa masikini. Ndiyo principle za economics. Haiwezekani the bigger population iko shambani ina-contribute asilimia 25 tu ya pato la Taifa. Ni sign of poverty. Kwa nini? Kwa sababu productivity ni ndogo.

Mheshimiwa Spika, tunachotakiwa sisi leo, kwa kuwa sisi tuko shambani, watoto wetu wasiende kulima hekta moja moja. Tujenge uwezo wa-graduate kutoka kwenye agriculture, waende kwenye service industry na maeneo mengine. Economy zote zilizokuwa duniani, watu wachache wako shambani, wengi wameondoka. Sasa kipato cha mkulima mdogo ni Shilingi ngapi? Haizidi 1.2 million Shillings kwa mwaka.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa nini tumeenda kwenye program ya BBT? Kwanza nataka niwaambie Watanzania wenzangu, ni aibu kuhoji kwamba kwa nini tumemmilikisha kijana ardhi? Leo anakuja Mzungu kutoka Ulaya; juzi ofisini kwangu ilikuja kampuni moja kutoka China, inataka kuwekeza. Condition ya kwanza nimpe ekari 20,000; condition ya pili, nimpe subleasing title ya miaka 60; condition ya tatu, anataka barabara; condition ya nne, anataka umeme.

Mheshimiwa Spika, sasa nikimpa Mtanzania hekta 10, nimemwandalia shamba, nimemwekea irrigation scheme, nimempelekea umeme, nimempimia afya ya udongo, mnasema, kwa nini tumemilikisha? Wawekezaji wangapi katika nchi hii tumewamilikisha ardhi na hawaitumii? What is wrong kummilikisha mtoto wa Kitanzania ardhi? Nauliza hili swali, kuna dhambi gani? Mheshimiwa Halima usiingie kwenye historia ya kuhoji kijana wa Kitanzania ambaye kaenda kurithishwa ardhi…

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, taarifa.

WAZIRI WA KILIMO: Umechangia, give me space.

MHE. HALIMA J. MDEE: Usiniwekee maneno.

WAZIRI WA KILIMO: Nimesema hivi…

SPIKA: Ngoja, ngoja, Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Halima, naomba ukae. Waheshimiwa Wabunge, kwenye ngazi hii, Waziri akiwa amesimama anahitimisha hoja, huwa hakuna taarifa. Kinachoweza kutokea, ukiona kilichojibiwa ni tofauti na ulichokuwa umesema wewe, utatumia kanuni nyingine, lakini kanuni ya taarifa haiwezi kutumika katika ngazi hii.

Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, out of respect, hoja imekuwepo tunawatoa Dar es Salaam. Hivi nimuulize graduate yeyote aliyemo humu ndani, alipomaliza Chuo Kikuu, destination ya kwanza ilikuwa wapi? Nawaulizeni! Mimi nimemaliza Mzumbe, nimeenda Dar es Salaam, sikurudi kwetu kijijini, Nzega. Nimeenda Dar es Salaam, nazunguka na bahasha ya kaki, na kula wali wa shilingi 700 IFM. Leo tunahoji, eti kijana aliyeko Dar es Salaam hawezi kulima! Nani kasema kwamba kijana aliyekwenda Dar es Salaam hawezi kulima? Nani? Tumemjaribu wapi? Hawawezi kulima kwa sababu tunataka kuwa-subject walime kwa teknolojia za 1960, 1970, 1980, it is impossible. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa nini vijana hawalimi? Halafu tunasema sisi viongozi mbele ya Mungu, nami niko honest, I will push BBT, aidha nifanikiwe mimi na wenzangu, ama nikaanguke. Siwezi kusubiri, siwezi kuwa mmoja wa viongozi wanaowanyooshea vidole vijana wa nchi hii kwamba kwa nini hawataki kujiajiri? Tunao wajibu. Tuna moral responsibility ya kuwatengenezea vijana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mazingira ya kujiajiri, na ndicho kinachofanywa na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii nani anaweza kwenda kununua ardhi ya shilingi milioni mbili, milioni tatu hekta moja? Nani, kijana aliyetoka chuo kikuu? Nani anaweza kutumia Shilingi milioni mbili au milioni moja na nusu au milioni tatu kuweka drip irrigation? Yuko wapi huyo kijana? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka nimpe mfano, nami na- focus kwenye hoja ya Mheshimiwa Halima kwa sababu, let me say, nasema ukweli.

MBUNGE FULANI: Unachagua hoja!

WAZIRI WA KILIMO: Yes, nimechagua hoja.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, hebu tusikilizane. Unapozungumza Waziri akiwa amesimama hapa mbele, unataka aongelee hoja anazojibu au muanze kujibizana? Tafadhali naomba utulivu, Waziri anajibu hoja za Wabunge. Yeye wakati ninyi mnachangia aliwasikiliza, mpeni nafasi na yeye ya kumsikiliza. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nataka nitoe hii takwimu. asilimia 74 ya Watanzania walioko mashambani, wana wastani wa ekari mbili. Asilimia 25 tunaowaita medium size, wana ekari tano mpaka 20. Tunaowaita large scale, wana ekari 20 mpaka 100. Hii ndiyo taswira. Wote hawa wanavuna mara moja kwa mwaka, wanasubiri kudra ya Mungu. Lazima tuondokane na hii hali. Hii hali hatuwezi kuondokana nayo kwa msimu mmoja, au miwili, au mitatu, is a long-term process. Lazima tufanye hii kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine niongelee suala la ruzuku ya mbolea. Nakiri kulikuwepo na changamoto za distribution network. Tunachukua hatua. Hatua ya kwanza, tunawekeza kwenye TFC, kampuni yetu wa Serikali. Kwenye bajeti tumeipa shilingi bilioni 40, mwaka jana 2022 tuliipa shilingi bilioni sita, mwaka huu tumeiongezea shilingi bilioni 40, na sasa hivi tuko kwenye negotiation na funding kutoka JICA ambazo zilikuwa ziende ku-support hiyo ruzuku, tutawapa dola milioni 25, itakuwa capitalized.

Mheshimiwa Spika, kwa nini tunai-facilitate kampuni hii? Tunai-facilitate ili tuwe na jicho la Serikali ambalo linaweza kutusaidia kwenye price discovery huko nje. Wata-import mbolea kutoka huko nje na watanunua kutoka huko nje, lakini capacity ya ndani tunaendelea kuijenga.

Mheshimiwa Spika, leo tuna hiki kiwanda chetu cha INTRACOM ambacho kinaendelea kufanya kazi, tunatarajia mpaka mwezi wa Kumi kitafika tani milioni moja. Kwa kuwa program ya ugawaji wa ruzuku ya mbolea; na kwa nini tunafanya hivyo? Hapa nitaijibu hoja ya Mheshimiwa Mpina.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mpina kahoji kachukua idadi ya wakulima tuliowasajili, kagawa kwa mbolea tulizotoa; nadhani ni katika kuelewa. Kwanza wakulima milioni saba wa nchi hii sio wote wanaotumia mbolea. Matumizi ya mbolea katika nchi hii kwa hekta moja sasa hivi, wastani ni kilo 19. SADC minimum standard ni 50 kg.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa nini kuna tatizo la matumizi ya mbolea? Elimu, hilo la kwanza; la pili, taarifa ya afya ya udongo; la tatu, ni availability na affordability. Kwa hiyo, Serikali inaweka ruzuku ili bei iweze kushuka. Siyo sahihi katika hoja yake, nami nimeichukua hoja yake hapa, ninayo, kanipa yeye mwenyewe kwa maandishi. Kuna mambo kama manne kayataja. La kwanza, kasema mfumo wa usajili na mfumo wa ruzuku haukupata approval ya Serikali, umeenda kinyume na utaratibu. Nataka nimwambie, tumepata approval ya Katibu Mkuu Kiongozi, tunayo approval ya e-GA; tarehe 26 Juni, tulipata approval ya e-GA, na tarehe 16 Julai vilevile Katibu Mkuu Kiongozi aliwaandikia e-GA kuwasiliana na Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kutengeneza mfumo wa ruzuku ya mbolea. Barua hii hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni vizuri, nami nataka nimshauri, na ninajua ameenda hadi e-GA. Namwomba kwamba kwa mila zetu hasa sisi tunaotoka huko maeneo ya wafugaji, ni vibaya sana mtu ambaye umefika katika level ya uongozi, kuongea mbele ya Baraza ku-accuse mambo ambayo huna facts. Nataka nimwombe, next time akiwa na jambo linalohusu Wizara ya Kilimo, mlango wangu uko wazi sana. Saa yoyote njoo, tutakusikiliza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja yake ya pili ni kwamba, mfumo wetu ulikuwa haufai, kuna double scanning. Sasa tumegunduaje mfumo kwamba huyu mtu ka-double scan kama mfumo wetu hautoi taarifa? Mfumo wetu unatupatia taarifa, mtu yeyote atakaye-temper na system; na wizi uliokuwa unafanyika, na Bunge hili litumike, uko wa aina nyingi. Mkulima alikuwa akifika dukani, akichukiliwa namba yake ya kusajili na Agro-dealer, leo allocation yake ni mifuko kumi, akilipa mitatu, akiondoka, kwa kuwa Agro-dealer kabaki na ile namba, anaitumia tena ile namba, meseji inaenda kwa mkulima, mkulima anapiga call center ya Wizara ya Kilimo. Sisi tunafanya tracing.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi wanaendelea kuhojiwa. Kuna wengine wamefika, tumewakamata walikuwa wame- double scan mbolea za zaidi ya shilingi milioni 100, wanasema naomba nisamehewe, hiyo shilingi milioni 100 ifutwe, tuendelee. Nataka niwaambie, tulianza tukiwa hatuna mfumo wa kumtambua mkulima nchi hii. Tumeanza safari, sasa tumefika wakulima milioni tatu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitumie Bunge lako tukufu kuwaambia wakulima, tarehe 01 mwezi huu wa Tano, TFRA ilitangaza wakulima kwenda kujisajili na ku-update data zao. Nendeni mkajisajili, mwendelee kutoa taarifa zenu sahihi, mfumo utaendelea kuwa updated, na process ya kusajili wakulima ni ya mpaka mwaka 2025. Tutakamilisha kumjua mkulima jina, GPS ya shamba lake, afya ya udongo wa eneo lake, na kujua mazao anayolima, na kuwa na taarifa sahihi. Kwa muda mrefu tumehudumia wakulima tusiowatambua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, gharama za mradi wa BBT. Wastani wa shilingi milioni 16 kwa hekta. Kwanza, nilitaka niseme jambo moja. Hekta moja ni ekari 2.5, nasi hatuchukui mashamba yaliyoandaliwa, tunachukua mapori, ambapo tunaenda kusafisha. Kusafisha hekta moja ya pori, ni wastani wa 1.5 million shillings. Gharama hizi za shilingi milioni 16, zinahusisha kusafisha, kupima afya ya udongo, gharama ya kupima shamba, ni wastani wa shilingi milioni mbili. Huyo anayekuja, hawezi kuzilipa hizo gharama. Sisi ndiyo tunaolipa gharama za upimaji wa haya mashamba. Tuna-include gharama za kupanda, tuna-include gharama za kupima afya ya udongo, tuna-include gharama za teknolojia itakayotumika, whether ni sprinkler ama ni drip irrigation kama kwenye maeneo ya mabonde kama kule Membe, tunakotumia canal technology.

Mheshimiwa Spika, siku ya mwisho tunapomkabidhi huyu kijana gharama ya hekta moja ambayo ni ekari mbili na nusu, ni karibu Shilingi 16,700,000. Ukigawa, haizidi Shilingi milioni saba kwa ekari. Ni muujiza gani? Mheshimiwa Halima analima pale panaitwa Ihanga, ndiyo mfano wangu leo. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, yeye mwenyewe ameshindwa kuweka the best technology za irrigation, anatumia zile za vijungu, zile traditional. Mmenielewa! This tells the costs ya investment. Mmenielewa lakini? This tells the costs of investment kwamba shilingi milioni 16 is nothing. Shilingi trilioni moja, tukichukua hekta milioni moja kwa ekari milioni 2.5; shilingi trilioni 16 tukiajiri vijana 250,000 na scientifically imedhibitika kwamba ajira moja ya shambani inatengeneza ajira sita kwenye value ya addition; gharama ya kutengeneza hizi ajira, ni shilingi milioni nane. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii jamani ni simple economics siyo muujiza, ni namba. Je, tunatarajia kunaweza kukatokea changamoto? Inawezekana kabisa. Sasa hivi tunafanya mikoa mingapi? Dodoma, tunafanya Njombe ekari 80,000, tunafanya Singida, tunaenda Geita, tunaenda Shinyanga, kote huko tunaenda. Tumepokea maoni yenu kuhusu namna ya kuwapata vijana. Tutaenda kuyafanyia kazi. Hili tutaenda kulifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo lingine la mabadiliko kwenye Tume ya Umwagiliaji, tunakuja na sheria, inaitwa Tanzania Irrigation and Extension Development Authority. Kwa sababu tunapeleka vitendea kazi, tunapeleka watu, lazima tuwe na mamlaka yenye kuwajibika kusimamia shughuli hizi.

Mheshimiwa Spika, kulitolewa wazo la kuwepo na mfuko wa umwagiliaji. Sheria ipo. Tumeanzisha Irrigation Development Fund, tumepata shida kwenye ukusanyaji wa maduhuli, na ziko sababu. Tumeamua kwenda kuzifanyia kazi hizo sababu, kwa sababu hatukuwa na mfumo wa registration wa scheme za nchi. Sasa hivi tunafanya registration ya scheme zote za nchi. Hatukuwa na mfumo wa kuwasajili wakulima walioko kwenye scheme, sasa hivi tunafanya shughuli ya kusajili wakulima walioko kwenye scheme.

Mheshimiwa Spika, niliombe Bunge lako Tukufu kwamba tusi-condemn vijana wa nchi hii. Tusiumie kwa nini mtu amemiliki ekari 10. Nchi hii ina jumla ya hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo. Tulizotumia hazizidi hata milioni 15, bado ardhi ipo. Tuhangaike kuongeza tija ya uzalishaji.

Mheshimiwa Spika, suala la mbegu, ni kweli, kama nchi tuna tatizo la mbegu. Mahitaji yetu ya mbegu ni jumla ya tani 670,000. Tunazalisha asilimia 10, Serikali inachukua hatua gani? Kwanza, tumeanza kuweka miundombinu ya umwagiliaji kwenye mashamba yetu yote ya mbegu.

Mheshimiwa Spika, pili, tunaihusisha sekta binafsi ya nchi yetu kwenye uzalishaji wa mbegu na tumeanza kuwapa mashamba. Tumewapa pale Mbozi, na mwaka huu wamezalisha tani 7,000. Tatu, tuna-acquire land kama Serikali ili tuweze kuwa na ardhi tunayoihitaji ili tujitosheleze kwa mbegu. Nchi yetu inahitaji jumla ya hekta 360,000 za kuzalishia mbegu.

Mheshimiwa Spika, lingine, tunawekeza kwenye utafiti, naongelea issue ya kuwepo kwa maabara za tissue culture, kwa watu wa Kagera kwenye eneo la kahawa. Tunapeleka pale maabara Maruku, tunaenda kuweka maabara kwa ajili ya tissue culture ya migomba na tissue culture kwa ajili ya kahawa.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine, tunapima afya ya udongo wa nchi. Niseme tu jambo moja. Hapa ndani, niwaambieni, hili ndiyo Bunge na sisi ndio Watanzania, na Watanzania wote wajue. Taifa letu toka tunapata uhuru, suala la kupima afya ya udongo, tulikuwa tunategemea makampuni ya mbolea na donors, haiwezekani. Serikali imechukua hatua gani?

Mheshimiwa Spika, kwanza, tumetengeneza mfumo wetu, tumeshaanza na sasa hivi kupima ramani kwa ajili ya kuangalia acidity level kwenye nchi yetu. Hiyo ni ramani ya nchi yetu na hali ya afya yetu ya udongo, lakini database hiyo tunaimiliki wenyewe, tunatengeneza mfumo wa kuhifadhi taarifa za upimaji wa afya ya udongo ili tuweze kujua mbolea sahihi unayoipeleka Nzega is a process siyo jambo la usiku mmoja.

Mheshimiwa Spika, la tatu; uwekezaji kwenye infrastructure za umwagiliaji tutatumia maji ya Ziwa Victoria wala siyo aibu, tutatumia maji ya Lake Tanganyika wala siyo aibu tutatumia na tumeisha tangaza. Sasa hivi feasibility study zinaanza kufanyika na mwaka huu unaokuja katika mabonde yenye jumla ya hekta 306,000. Mwaka huu unaokuja kwa sababu feasibility study zinafanyika ndani ya mwaka huu wa fedha wa 2022/2023.

Mheshimiwa Spika, kuanzia mwaka kesho tutaanza kujenga hekta 300,000 katika kila bonde ndiyo muelekeo wa Serikali. Niwaombe Waheshimiwa Wabunge, transformation ya agriculture naweza nikasema with confidence baada ya Mwalimu Nyerere mimi nakuwa mkweli. Baada ya Mwalimu Nyerere ni Serikali ya Awamu ya Sita ndiyo imeamua kwenda kuwekeza kwenye maeneo ya msingi ya kilimo ndiyo ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mwalimu kaondoka kaacha mashamba 17 ya mbegu ni yaleyale sixty years Mwalimu kaondoka kaziacha maabara zilezile. Leo ndiyo tunawekeza kwenye maaabara za utafiti, leo ndiyo tuna expand tunaanza kufungua mashamba kwa ajili ya kuweka miundombinu ya umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho program ya BBT inahusisha kwenda shambani, inahusisha kutoa financing kwa vijana walioko kwenye mashamba ambao hawamo ndani madarasa sasa hivi. Mwezi uliyopita tumewapa vijana two hundred million walioko mashambani ambao hawawezi kwenda kukopeshwa na taasisi za fedha. Tumeweka eighty hundred million katika mfuko wa pembejeo tutawapatia hawa vijana ambao wanafanya shughuli za kilimo mashambani na wanaofanya value addition. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niongelee issue ya ngano na alizeti. Eneo la alizeti tumesambaza mbegu na nataka niipongeze taasisi yetu ya ASA mbegu walizosambaza safari hii satisfied seed zimeweza kuleta matokeo mazuri na uvunaji umeanza.

Mheshimiwa Spika, ninajua wakulima wa alizeti kuna anguko la bei, nataka niwaambie hivi tunampelekea Mheshimiwa Rais barua ombi la kututeulia Mwenyekiti wa COPRA Mamlaka inayosimamia cereals na other produce. Ambayo kwa mujibu wa sheria hii ndiyo itatoa masuala ya bei elekezi, tutatoa bei elekezi ya alizeti clearly. Hatua ya pili tunawasilia na wenzetu Wizara ya Fedha tumewaomba tuongeze kodi ya mafuta yanayotoka nje ya refine kutoka asilimia 25 kwenda asilimia 35 na wachajiwe VAT ya asilimia 18. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo la ngano sisi tuna import ngano tani milioni moja kwa mwaka. Ili tujitosheleze ngano tunahitaji tani 50,000 za mbegu za kwenda kumpa mkulima alime tumechukua hatua gani? Tumeanza kuzalisha mbegu mama, sasa tunazalisha mbegu za pre basic, tunaenda kuzalisha basic seed 2025/2026 tutazalisha mbegu kwa ajili ya wakuwapelekea wakulima. Tumewaandikia makampni ya ngano yote kwamba waingie MOU na Serikali kwamba kabla ya ku–import watanunua ngabo ya ndani kwanza, wamekataa mpaka sasa.

Mheshimiwa Spika, nataka niseme mbele ya Bunge lako Tukufu, niseme mbele ya Wabunge na mbele ya watanzania kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu 2025/2026 tunaenda kuzalisha ngano mwenye mamlaka ya kuwapa cheti cha ku– import ngano ndani ya nchi ni Waziri wa Kilimo. Kama takuwa kwenye kiti viwanda vitageuka chuma chakavu
hawatoingiza hata kilo moja kama hawajanunua ngano ya ndani ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, watanzania hawatokufa kwa kukosa ngano, haiwezekani unambembeleza mmefanya nao trial, tumewapa mbegu wao wenyewe kwenye maabara zao. Wamesema inafaa alafu wakati wa kusaini MOU wanasema hatutaki over my dead body watasaini mkataba, wasipo saini hatutowapa phytol-sanitary kuingiza ngano watajua watakachofanya na viwanda vyao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haiwezekani 1970, 1980 asilimia 80 ya ngano ya nchini, hii ilikuwa inapatikana ndani tulifungua mipaka. Kwa hiyo, hili walifahamu tutaufunga Mkoa wa Manyara, tunafanya pilot Njombe, tumeona matokeo ni mazuri, tutaweka cluster na sasa tumeishaamua kuwa na korido za mazao. Kuna mazao tutazalisha maeneo maalum maeneo mengine hatutoyaruhusu kuzalishwa ili tuweze economies of scale. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri, dakika mbili malizia.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie kwa kusema kitu kimoja, bila kuongeza tija kila siku tutakutana hapa bei ya mkulima mbaya, bei ya mkulima juu bei ya nini. Lazima tuongeze tija, lazima tumiliki mbegu zetu wenyewe, lazima tuwekeze kwenye umwagiliaji na ni lazima tuwekeze kwenye skimu za umwagiliaji siyo mifereji ya umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ili tuweze kufanya hivi tunahitaji kuwekeza kwa muda mrefu na huu ndiyo muelekeo sahihi kokote kule duniani. Lazima tufungue mashamba ya kuzalisha mbegu, lazima tuhakikishe tunaiwezesha sekta yetu binafsi ya ndani na kwenye bajeti tumeweka bilioni 10 ambayo tutawapatia wafanyabiashara wa kitanzania wanaobangua korosho, wanaoongeza value addition kwenye zabibu, kuwanunulia vifaa kwa ajili ya kununua mazao ya wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho, nataka niwaambie vijana wa kitanzania Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuwafanya wamiliki nyenzo za uzalishaji na kuwamilikisha ardhi. Tutawekeza kwenye eneo la kuwamilikisha ardhi, tutawasapoti waweze kufanya shughuli zao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho niwaambie Waheshimiwa Wabunge maoni yenu tutaendelea kuyafanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsanteni, natoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Jambo langu la kwanza kabisa, kwa dhati namshukuru Waziri wa Nishati na Madini. Namshukuru kwa kuonesha nia ya kushughulikia tatizo lililoko Katika Jimbo la Nzega la wachimbaji wadogo na chuo cha MRI.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimpe taarifa Mheshimiwa Waziri na naomba AG ampe nafasi ili aweze kusikia hili tatizo Mheshimiwa Waziri, kwamba agizo alilolitoa Mheshimiwa Waziri la kumtaka mchimbaji aliyeingia kinyume na utaratibu, aliyeingizwa na MRI katika eneo la Resolute na mwezi mmoja aliopewa, pamoja na Waziri kupeleka delegation kubwa akiwepo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Kamishna wa Madini, yule mtu mpaka leo anaendelea na uchimbaji ndani ya eneo la Mgodi wa Resolute. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niliongea na Naibu Waziri Kalemani na tulishauriana juu ya solution ya jambo hili. Nataka niitahadharishe Serikali, tension iliyoko katika eneo lile, ni tension kubwa. Kwa hiyo, nashauri Waziri awaagize wataalam wake, yule mtu atoke ndani ya lile eneo kwa sababu perception ya wananchi juu ya lile eneo siyo jambo zuri sana. Hilo ni jambo la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, Mheshimiwa Waziri anafahamu, nami nashukuru amenipa commitment, miradi ya umeme iliyokuwa inafadhiliwa na MCC katika Jimbo la Nzega kwa maana ya mradi wa umeme wa kutoa umeme Nzega Mjini kuupeleka Kitangili, kutoka Kitangili kwenda Migua; kutoka Migua kwenda katika Kata ya Mwanzoli, Kijiji cha Kitengwe. Naomba tuhakikishiwe wananchi wa Nzega kwamba mradi hii iliyokuwa inafadhiliwa na MCC itaingia kwenye REA Phase III, kwa sababu kuna upungufu mwingi katika miradi ya REA Phase II katika Jimbo la Nzega. Kwa hiyo, naomba Serikali itoe commitment katika jambo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nataka niseme katika hotuba ya Waziri, wazo la East African Countries kununua share kwa ajili ya kushiriki katika mchakato refinery kwenye project ya uzalishaji wa mafuta katika nchi ya Uganda, mradi huu ni jambo muhimu sana. Strategically ni muhimu kwa sababu maisha ya Watanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki, gharama za mafuta zitashuka.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Muhongo ni jambo la kuisukuma Serikali na sisi Wabunge tumsaidie ili Serikali ya Tanzania iweze ku-play part yake ili tuweze kupata shares zetu katika mradi huu na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa sababu economically litatusaidia sana jambo hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la mwisho, Waheshimiwa Wabunge, nimesoma hotuba ya ndugu yangu Mheshimiwa John Mnyika, kwa heshima Kabisa, tunajua suala la ESCROW mna hoja ya kumhusisha Waziri Muhongo, ni kutaka kumfanya kondoo wa kafara katika jambo hili. Naomba Bunge hili lisifanye makosa ya Mabunge yaliyopita kushughulika na watu dhaifu na kuacha msingi wa matatizo. We all know katika mioyo yetu suala la ESCROW kama beneficiaries wakubwa wa ESCROW wapo, wanajulikana. If we real want to deal with it, tuwafuate hao, lakini tumwache Mheshimiwa Profesa Muhongo atimize wajibu wake. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza nianze kusema kwamba naunga mkono taarifa za Kamati zote mbili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ninukuu Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 mpaka 2020, inasema: “Katika kipindi cha miaka mitano, Chama cha Mapinduzi kitaweka kipaumbele cha kuhakikisha kuwa kilimo nchini kinakuwa endelevu na chenye tija ili kuwezesha Taifa kujitosheleza kwa chakula, kuongeza mapato ya wakulima, kuwa chanzo cha kuaminika cha mapato.” Hii ndiyo ahadi yetu kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mawaziri wanapoapa mbele ya Mheshimiwa Rais, katika kiapo chao wanasema watamshauri Mheshimiwa Rais. Tunapochagua Rais na Wabunge na inapoundwa Serikali inaenda kutekeleza Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi. Humu ndani huwa Wabunge tunagawanyika, tunaotetea wafugaji, tunaotetea wakulima. Nataka niwaambie, hii ni divide and rule. Asilimia 70 ya wakulima wa nchi hii, asilimia 80 ya hii docket inafanya kazi ya kilimo na mifugo. Kwa hiyo, anapoathirika mfugaji ndivyo hivyo anavyoathirika mkulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikupe jambo hili dogo tu; Bajeti ya mwaka 2010/2011 asilimia 7.8 ndiyo ilikuwa bajeti ya kilimo; Bajeti ya 2012 asilimia 6.9 ndiyo ilikuwa bajeti ya kilimo; Bajeti ya 2016/2017 asilimia 4.9 ndiyo bajeti ya kilimo. Angalieni namna gani tunavyo-lose focus. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye mipango ya matumizi ya ardhi tumeweka maeneo kwa ajili ya misitu, maeneo kwa ajili ya game reserves, maeneo kwa ajili ya wanyama, lakini ukija kuna ardhi ya vijiji ambayo imepangiwa matumizi haizidi asilimia 30. Pia tunazo ardhi za miji. Nataka niulize leo, Mawaziri hapa watuambie, ni lini wamekaa chini kuja na master plan ya ku-allocate ardhi kwa ajili ya wafugaji na wakulima ili tuweze kujua namna gani tunawapanga watu wetu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tembo akila mahindi, akiua mtu, kuna kafidia na tembo anaheshimiwa kweli, lakini mwananchi akilima ndani ya reserve ya wanyamapori, ataadhibiwa kwa faini. Akivuna mazao yake, anaambiwa asiuze ili tuweze kudhibiti mfumuko wa bei. Tunatengeneza artificial control mechanisms za kuonyesha uchumi wetu uko vizuri, wakati tunawatia watu umaskini. This is unfair. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nataka niseme kwa Waheshimiwa Wabunge wenzangu wa Chama cha Mapinduzi, we are not fair kwa wakulima, kwa wafugaji, kwa wavuvi, na kwa wamachinga. Who are we expecting kesho kwenda kumwomba kura? Tusikubali kuingia kwenye record ya kukipeleka chama chetu kubovu kwa makosa ya Mawaziri Serikalini. We should not allow kuwatia umaskini Watanzania. Tusiruhusu kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mahindi yanazalishwa tena…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia. Nianze kwa kusema kwamba naunga mkono hoja iliyoko mbele yetu ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza nitumie nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa nafasi. Pili nimshukuru sana Waziri wa Fedha na Wizara ya Fedha kwa ujumla. Katika Hotuba ya Waziri wa Fedha, katika mpango wa mwaka ujao wa fedha amesema wazi kabisa, katika miradi ya kielelezo na miradi ya kipaumbele, miradi ya umwagiliaji itakuwa ni eneo la kwanza ambalo Serikali itaweka fedha. Nitumie nafasi hii kumshukuru sana. Vilevile nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa guidance anayotupa na maelekezo anayowapa wenzetu wa Wizara ya Fedha kuangalia uwezekano wa kuweza kuweka kipaumbele katika eneo hili la kilimo namshukuru sana Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge, wametoa ushauri na wamesema mambo mengi. Kwanza nitumie Bunge lako Tukufu kuwaambia kwamba kwa mara ya kwanza tangu tumepata uhuru uzalishaji wa zao la kahawa tumefika metric tons 82,000 ambazo tumeziuza mwaka huu. Vilevile zao la tumbaku uzalishaji wetu sasa hivi unakwenda tani 120,000. Hizi zote ni effort ambazo Mheshimiwa Rais amefanya na tunaendelea na masoko na masoko yanaendelea vizuri tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hali inavyokwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wengi wameongelea eneo la mafuta ya kula na eneo la ngano. Nataka nitumie nafasi hii kuwaambia Waheshimiwa Wabunge tumewasikia na tumekaa na Wizara ya Fedha tumekubaliana tutakuwa na tax measures na tutakuwa na administrative measures ambazo zitaonekana kwenye finance bill ambazo zitafanya uzalishaji wa mafuta tuweze kuwa na tax ambazo zinaweza kumlinda mkulima. Serikali inaweka fedha tumegawa mbegu nyingi sana za ruzuku na safari hii mashamba yetu yote ya kuzalisha mbegu yatakuwa yanatumia pivot technology. Mwenyezi Mungu akitujalia mpaka kufika mwishoni mwa mwaka huu baadhi ya mashamba ambayo yamefungwa mifumo ya umwagiliaji ya kutumia technology ya center pivot yataanza kufunguliwa ili tuweze kuzalisha mbegu mwaka mzima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nataka niseme kwamba Waheshimiwa Wabunge wameongelea sana suala la tija. Ni ukweli kwamba mchango wa sekta ya kilimo na ukuaji wa sekta ya kilimo hauakisi tamaa tulionayo kama Taifa. Ili tuweze kufikia huko ni lazima tuwekeze kwenye tija. Serikali inafanya jitihada kubwa sasa hivi ya uwekezaji kwenye maeneo ya kuongeza tija. Mmepitisha bajeti ya Wizara ya Kilimo na Bajeti Kuu ya Serikali; na mwaka kesho mtaona tunaanza kutekeleza miradi katika majimbo yenu ya kuchimba visima kwa ajili ya wakulima wadogowadogo na kuwawekea irrigation kit ya hekari 2.5 kila mkulima ili wakulima waweze kuzalisha kwa wingi na waweze kuwa na uhakika wa kuzalisha kuwa na resilience kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ni uwekezaji, tumeshatangaza tender sasa hivi za kufanya feasibility study na detail design kwenye mabonde yote 33. Na ninawashukuru Wizara ya Fedha kwa kutupa kibali. Tumeshatangaza tender na mikataba imeshasainiwa wakandarasi wanaanza kufanya feasibility study kwenye mabonde ya Ziwa Victoria, Lake Tanganyika Lower Basing ya Ruvuma na mabonde ya Rifiji. Yote haya tunayafanyia detail design ili tuweze kuanza mipango ya kujenga miradi ya umwagiliaji ili Mwenyezi Mungu akitujaalia tukikamilisha hizi zaidi ya hekta laki tatu na kitu zitatuongezea eneo kubwa la uzalishaji wa mwaka mzima katika maeneo tunayofanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine Wabunge waliongelea pamba, wakatoa concern yao kuhusu bei. Nataka niwakumbushe mwaka 2020/2021 tulianza msimu kwa bei ya shilingi 800 tulimaliza msimu kwa bei ya 1200. Mwaka 2021/2022 tulianza na msimu kwa bei ya shilingi 1500 tukamaliza msimu na bei ya shilingi 2200. Mwaka huu tumeanza na bei ya 1060 ninaamini kwamba bei ya pamba itaimarika namna ambavyo competition inavyoongezeka na soko la dunia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, njia pekee ambayo tunaongea na wenzetu wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Fedha, ni kutengeneza mfumo ambao utatufanya sisi wakati wakulima wanalima, wanavuna, wanapata assured good price na tunahifadhi, tunaenda katika mfumo wa TMX na kuangalia namna gani tutawasaidia waongezaji wa thamani, waweze kuongeza thamani ya pamba yetu na kutengeneza financing scheme. Tuko kwenye majadiliano na Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara, naamini ndani ya miaka miwili, mitatu tutafika katika eneo hilo. Hii ni safari haiwezi kutokea haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tamaa yetu ya kuwa na stabilization fund, kama mtakumbuka mwaka jana wakati tunapitisha Finance Bill tulianzisha Agricultural Development Fund hapa ndani ya Bunge. Sasa hivi tuko hatua za kukamilisha kanuni ambapo tutakuwa na Mfuko wa Fedha ambao unatumika kwa ajili ya kuwalinda wakulima wetu na changamoto za masoko ili pale ambapo wanapata hasara tuweze kuwa–cover. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo Mheshimiwa Rais alitoa maelekezo na mlimsikia akiwa Mwanza, alitoa maelekezo ya kuiongezea fedha National Food Reserve Agency, tumepata approval ya bilioni 320 na tumeshaanza kuzitumia hizi fedha. Nawashukuru sana Wizara ya Fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini tunaweka fedha kwenye National Food Reserve Agency? Pia sasa hivi tumetangaza feasibility study kwa ajili ya kuongeza uwezo wetu wa kuhifadhi. Mpango wa Serikali katika kipindi cha miaka mitano mpaka minane ijayo tuwe na uwezo wa kuwa na maghala ya kuweza kuhifadhi mazao yasiyopungua tani milioni saba ndani ya nchi yetu. Kwa kutumia njia hiyo ndiyo tutaweza kuwalinda wakulima wetu na kuweza kujiwekea usalama wa chakula katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imetupatia fedha kwa ajili ya Kampuni ya Serikali na niwapeni good news, tulifanya majaribio TFC na Profesa Mkenda ametoka nataka nimshukuru mbele ya Bunge hili, akiwa Waziri wangu ali–champion hili jambo. Leo TFC tumeipatia fedha, baada ya kuipatia fedha imefanya biashara ndogo na imepata faida. Matokeo yake Wizara ya Fedha wametuelewa, wametupatia bilioni 40 kwa ajili ya kuipa TFC na tumepata dola milioni 25 kwa ajili ya kuipa TFC na sasa hivi TFC imeshaagiza mbolea kutoka nje ili tuwe na mbolea ndani ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndoto ya nchi kuwa na blending facility ambayo Serikali ina share, TFC sasa hivi tuko kwenye maongezi ya mwisho na OCP, lakini niwahakikishie Wabunge tusipoelewana na OCP tutawekeza wenyewe facility ya ku–blend mbolea ndani ya nchi na tutafuta wawekezaji wa Kitanzania kuwakabidhi waweze ku–run hilo eneo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwaambie wakulima wa korosho, nimesikia kilio cha kwamba mfumo tuliouweka na equation tuliyoiweka ya miche 100 kwa mfuko mmoja tumeshawaagiza Bodi ya Korosho wafanye review na mgao wa pili utakapotoka watatoa kutokana na idadi ya mikorosho na ukubwa wa mikorosho. Niwaombe Waheshimiwa Wabunge wa korosho, wakulima sasa hivi wanapokea pembejeo kwa kutumia teknolojia ya biometric, tuendelee kuwahamasisha wajisajili. Akijisajili akiwa na namba yake hata wakati wa kuuza korosho atauza korosho kwa kutumia namba yake aliyosajiliwa nayo ili tuwaondoe hawa wote ambao wanachukua mazao ya wakulima katika kipindi hiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo Wabunge wamekuwa wakisema sana. Wabunge wa Nyanda za Juu Kusini, naomba niwahakikishie, Wilaya ya Makete msimu ujao ngano tunawapa ruzuku ya tani 1,000 kwa ajili ya kwenda kufanya pilot. Wamefanya majaribio na niishukuru Halmashauri ya Makete kutoa ten percent kuwapa wale wakulima katika eneo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo niwaombe tu Waheshimiwa Wabunge matarajio tuliyonayo, Rais ana nia na Wizara ya Fedha imekuwa flexible kwa ajili ya kutoa fedha. Ndani ya miaka miwili, mitatu tutayaona matokeo makubwa katika sekta hii kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Kilimo
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuwepo hapa leo kutekeleza majukumu yetu ya Kibunge. Pia nichukue nafasi hii kukushukuru wewe binafsi na Wenyeviti wa Bunge, kwa kusimamia mjadala wa hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha, 2022/2023 ambao tunauhitimisha leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie nafasi hii vile vile kushukuru mchango mkubwa uliotolewa na Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji. Kwa dhati kabisa nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge waliochangia kwani wametoa hoja nzuri sana, zenye malengo ya kuimarisha utekelezaji wa majukumu katika Wizara yangu na kuharakisha mapinduzi ya kilimo. Hii inaonesha umuhimu wa kilimo katika usalama wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutoa shukurani zangu za dhati kabisa kwa Naibu Waziri Mheshimiwa Antony Peter Mavunde, kwa kuchangia hoja hii na kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizojitokeza. Niwashukuru pia Katibu Mkuu, Bwana Andrew Massawe; Naibu Katibu Mkuu, Ndugu Profesa Siza Tumbo na Ndugu Gerald Mweli; pamoja na Watendaji wote wa Wizara na Taasisi zake, kwa ushirikiano na ushauri wanaoendelea kunipa katika kutekeleza majukumu yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa naomba kuwasilisha maboresho katika kitabu cha Hotuba ya Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mwaka wa Fedha, 2022/2023. Aya ya 61 ukurasa wa 35 jedwali Na. 4 mchanganuo wa matumizi ya fedha zilizotolewa kwa Mafungu yote matatu kwa mwaka wa fedha 2021/2022 jumla kuu ni shilingi bilioni 151,863 badala ya shilingi bilioni 272,931. Aidha, matumizi ya shilingi bilioni 151,863 ni asilimia 51.63 ya fedha zilizoidhinishwa na sio asilimia 92 kama zilivyooneshwa katika jedwali. Aya ya 366, ukurasa wa 194 inaonesha kuwa katika kuongeza thamani kipato cha mkulima na kupunguza upotevu wa zao la zabibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianze kujibu hoja za Wabunge ambao wametoa mawazo yao. Hoja yetu imechangiwa na Wabunge 92 kwa kuchangia na vile vile imechangiwa kwa maandishi na Wabunge 10. Naomba nianze kuongelea eneo ambalo Waheshimiwa Wabunge wametoa maoni ya muda mrefu. Naomba nianze na Mheshimiwa mama Anne Kilango Malecela, kwanza nikiri mimi nikiwa Naibu Waziri wakati huo Waziri wangu Profesa Adolf Mkenda, alinituma na nimekwenda Jimboni kwake na nimefanya survey, nimetembelea wakulima wote wa tangawizi. Vilevile nimeitembelea scheme yake ambayo ilijengwa na Baba wa Taifa ya Ndungu na nikaenda mwenyewe kufika pale na kutatua changamoto zile. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimwambie hana sababu ya kuondoka na shilingi ya kijana wake. Nataka nimhakikishie mbele ya Bunge lako na kuwahakikishia wakulima wa tangawizi sio wa Same tu, lakini vile vile wakulima wa tangawizi wa Buhigwe, Wizara ya Kilimo baada ya miaka 38 tumelichukua zao la tangawizi tumelikabidhi Taasisi yetu ya Utafiti ya TARI Mlingano kuanza kufanya utafiti na kufanya multiplication ya mbegu, ili maradhi yanayowakabili wakulima wa eneo lile wanaolima tangawizi tuweze kuliondoa tatizo hili kwa kudumu na mazao yote ya viungo. Kuanzia mwaka huu wa fedha tumetenga fedha kwa ajili ya utafiti wa tangawizi na mazao mengine ya viungo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la pili, nataka tu nimhakikishie Mama Anne Kilango, wataalam wa Wizara ya Kilimo wako Wilaya ya Same, wanafanya kazi kubwa mbili. Ya kwanza, watafiti wa TARI wamekwenda kuchukua sample za udongo na mazao ya tangawizi kwa ajili ya kuyapeleka maabara, tuweze kutambua maradhi halisi yanayowakabili wale wakulima wa pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, watu wetu wa Tume ya Umwagiliaji wanafanya kazi ya kufanya stadi kuitambua mifereji, kujua tufanye design ya namna gani kuweza kuweka mifumo ya umwagiliaji. Ndugu zetu wa Hai walituvumilia na mwaka huu tumeshatatua tatizo lao tumewapelekea fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimwombe mama yangu Mheshimiwa Anne Kilango asiwe na hofu wakulima wa tangawizi wa Wilaya ya Same wanakwenda kutatuliwa tatizo lao. Watu wa Tume ya Umwagiliaji wako kule, wanafanya design ili tuweze kujua tunatumia solution gani kuweza kuvuna maji yale na kuwaondolea matatizo ya muda mrefu ya wao kujiunganishia mipira kienyeji kwa ajili ya kupeleka mashambani kwao. Kwa hiyo, Serikali inalifahamu tatizo, lakini vile vile tunalifanyia kazi hatujawaacha na hatutawatupa mkono. Mwaka kesho kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu aje aniulize ndani ya Bunge hapa na anisute mbele ya Wabunge hawa na Watanzania kwamba, Hussein uliniahidi unakwenda kushughulikia tatizo la wananchi wa Same la tangawizi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo kubwa linalowakabili wakulima wa tangawizi kule Buhigwe, wanavuna hawana sehemu ya kuhifadhi, mwaka huu tumewawekea fedha tunakwenda kuwajengea maghala. Nataka niwaambie wakulima wa tangawizi, Serikali inachukulia mazao yote ya viungo kwa u-serious mkubwa na hatutoyapa nafasi ndogo kama ambavyo miaka 30 iliyopita ilichukuliwa kwa style hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine, nataka niwaombe Waheshimiwa Wabunge wapo waliochangia na kusema kwamba, bajeti ya Wizara ya Kilimo ni ndogo haitoshi, ni kweli lakini kuna hatua ambayo tumepiga. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tulikuwa na bajeti kwa zaidi ya miaka sita isiyozidi Shilingi bilioni 200, leo tunatenga bajeti ya Shilingi bilioni 751, asilimia 88 ya bajeti hii, inakwenda kwenye maendeleo, haiendi kwenye vikao, haiendi kwenye matumizi ya ofisi. Nataka tu nitaje maeneo ambayo tunapeleka. La kwanza tunapeleka kwenye suala la mbegu. Nataka niseme mbele ya Mungu na mbele ya Bunge hili, kama kweli nchi hii tunataka kuondoka kwenye matatizo, kwenye sekta ya kilimo, tusifanye maamuzi ya sekta ya kilimo kisiasa. Kilimo ni biashara, kilimo ni sayansi, kilimo ni teknolojia na kilimo kina basics. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwape hizi takwimu na ni vizuri kwa kuwa sisi ndio wawakilishi wa wananchi tufahamu. Nimechukua mazao 13 na ili food security ya nchi hii iweze kupatikana, tuna mazao mawili makubwa, mahindi na mpunga ndio mazao tunayokula Watanzania wengi. Swali la kujiuliza sisi, toka tumepata uhuru kati yetu tumewahi kukaa kujiuliza swali, tunahitaji mbegu bora tani ngapi ili tumpelekee huyu mkulima mdogo maskini kwa msaada wa Serikali ili aweze kwenda shambani? Nataka niwape hizi takwimu tunahitaji tani 652,000 kwa mwaka ili tuwagawie wakulima, sasa tujiulize swali tunazalisha tani ngapi? Tunazalisha tani 15,000 sisi na sekta binafsi, halafu tunaamini kwamba we are safe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya mahitaji ya tani 652,000 uwezo wetu wa sekta binafsi na Serikali tunazalisha tani 15,000, ndicho tunachozalisha. Sisi kama Wizara na nawaomba mtuunge mkono. Tumekwenda kuongea na Mheshimiwa Rais, tumemwambia mama, cha kwanza kwenye sekta ya kilimo ni tija. Tija haiji kwa jina la Roho Mtakatifu wala haiji kwa kumwomba Mwenyezi Mungu kwa kupitia Mtume Muhammad, ina equation. Equation ya kwanza ni input na input namba moja ni mbegu, ni lazima kama nchi tujitosheleze kwa mbegu na tuwe na uwezo wa kuzalisha mbegu zetu. Sisi kama Wizara ndio tumekipa kipaumbele namba moja. Tunafanya nini? Bajeti ya utafiti imeongezwa kutoka shilingi bilioni 5.0 kwenda shilingi bilioni 43. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti ya uzalishaji wa mbegu tumeongeza kutoka shilingi bilioni 5.0 ya mwaka 2020 kwenda Shilingi bilioni 40.7. Zinakwenda kufanya nini? Cha kwanza, tunakwenda kufanya kazi kubwa moja; kwanza kwenda kuweka miundombinu ya umwagiliaji kwenye mashamba ya mbegu. Haiwezekani mkulima anakwenda shambani na sisi Serikali ndio tunakwenda kuzalisha kwa kudra ya Mungu. Tunawaomba mtuunge mkono ili tupate tani 600,000 tunahitaji kuzalisha pre-basic seed. Kwanza tunatakiwa kufanya breeding tufanye pre-basic seed tuzalishe basic seeds halafu tuwape sekta binafsi na Serikali kwa ajili ya multiplication tuweze kuzipeleka kwa wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni safari, tunaomba watuunge mkono Waheshimiwa Wabunge, tunakwenda kufungua mashamba ya Serikali. Nitumie Bunge lako Tukufu niiombe sekta binafsi ya Watanzania, waje Wizara ya Kilimo, tutawapa ardhi kwa mikataba ya muda mrefu, tutawagawia wazalishe mbegu, tutanunua kama Serikali na tutawagawia wakulima kwa ruzuku. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua ya pili ambayo tumejiamulia kama nchi ni lazima tuwekeze kwenye umwagiliaji. Nataka nimkwambie hiki kipindi mimi ni Muislam, sio hamsa swalawat lakini naswali swali. Mvua zilivyokuwa zinachelewa, wewe tunaswali wote Gaddafi, kila Ijumaa Imamu anatuongoza kuomba dua na kufanya kunuti Msikitini Mungu alete mvua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, licha ya yote, Mwenyezi Mungu katupa akili, Mwenyezi Mungu katupa nafasi, Mwenyezi Mungu katupa ikolojia nzuri, ni suala la kuamua tunawekeza fedha zetu wapi? Tumekwenda kwa Mheshimiwa Rais, tukamwambia mama, naomba tuongezee bajeti ya umwagiliaji. Mheshimiwa Rais tumepata fedha tumeongeza bajeti ya umwagiliaji kutoka Shilingi bilioni 46 kwenda shilingi bilioni 361. Hata hivyo, tumesema nini? Tumeamua na nawaambieni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutayafanya haya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niliombe Bunge hili hata kama Bashe hayuko Wizara ya Kilimo Mungu kamchukua, au kwa jambo lolote, Bunge hili lisimamie vision hii ya irrigation kwenye nchi. Cha kwanza, tulichoamua kwenye umwagiliaji tumesema hivi lazima tufanye comprehensive feasibility study and design kwa mabonde yote ambayo ni ya uhakika na tuanze kujenga mabwawa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeamua kufanya nini? Tunakwenda kufanya feasibility study na design ya Bonde lote la Rufiji, hekta 64,000 tumeweka Shilingi milioni 835. Tumeamua kwenda kuweka feasibility study bonde lote la Mto Manonga na Wembele hekta 57,000. Tumeamua kuchukua bonde lote la Kilombero hekta 53,000. Tumeamua kuchukua eneo lote la Usangule, Malinyi hekta 2,500 na tumeamua kuchukua Mkoa wa Ruvuma Bonde la Mto Ruvuma hekta 26,000. Katika hili nimewaambia wenzangu Wizarani mambo ya joint effort na neighbour’s country, tukikutana nao kwenda pamoja hewala, hawapo sisi tunaanza safari. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hatuwezi kuwa tunakutana mikutano ya pamoja ya joint effort, vikao vya kuitwa Waziri tunakwenda, safari hii nimealikwa kwenye Ruvuma Basin sijakwenda kwa sababu I don’t see a reason, we can do our own design, tunaweza.

Mheshimiwa Naibu Spika, jumla ya hekta 306,000 zinazohusu eneo la Ziwa Victoria kuanzia Mara mpaka Kagera; eneo la Lake Tanganyika; na eneo la Lake Rukwa, tunakwenda kufanya design mwaka huu na tunalifanyia design lote, tutaanza kujenga kuanzia mwaka ujao wa fedha. Tumeamua kujenga mabwawa na nataka kusema ndani ya Bunge hili na iingie on record, nadhani katika Mawaziri ambao, wamekwenda kukaa na Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha mara nyingi, mimi ni mmojawao na namshukuru sana yuko hapa, anaelewa, ana-sympathize na anaunga mkono juhudi hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini tunaweka effort kwenye irrigation? Nimewaambia watu wa Tume ya Umwagiliaji, ni hivi, haiwezekani tunajenga mradi tuna shilingi bilioni 2.0 unampelekea Hussein shilingi milioni 100, John shilingi milioni 2.0 nani shilingi milioni 3.0, mwisho wa siku mmegawana umasikini na hakuna kilichokamilika. Tukijenga scheme ya umwagiliaji tunajenga total package kuanzia water catchment na mifereji, ni heri tujenge scheme mbili kuliko kukaa tunagawana umaskini mdogo mdogo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, priority yetu ya kwanza tunafanya feasibility study na kufanya design ya maeneo yote ambayo ni potential katika nchi, ili tunaposema kwamba mwaka kesho tunajenga nini tunajua tunakwenda kujenga sehemu ambayo hata nchi isipopata mvua mwaka mzima tunayo food basket ambayo inaweza kutulisha na kutuweka salama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, fedha hizi tunazopeleka asilimia 90 zinakwenda kwenye development za irrigation, hakuna fedha inayokwenda kwenye matumizi ya kawaida. Mbali na hapo scheme nyingi zinajengwa katika nchi yetu, baada ya miaka miwili zimekufa. Nataka niwape mfano, Sheria ya Umwagiliaji inatutaka tukusanye Irrigation Development Fund, five percent katika kila scheme ambayo Serikali imewekeza. Niwape mfano Serikali imewekeza 21 billion shillings kwenye scheme ya Dakawa yenye hekta 2,000, turn over ambayo tunatakiwa tukusanye iingie kwenye Irrigation Development Fund ni 600,000,000 million shillings. Tumeamua ku-unlock hili tatizo kwa kufanya nini? Tunafungua Ofisi za Umwagiliaji kila Wilaya na kila scheme itakuwa na Meneja wa Skimu, ili tuweze kuzisimamia na wakulima wasimamiwe, wazalishe mara mbili kwa mwaka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapeleka manpower, tunapeleka vitendea kazi, tunanunua magari kwa ajili ya Irrigation Development iweze kufanyika katika nchi hii. Tunakwenda kufanya Luiche imekuwepo kwa muda mrefu lazima tufanye hivi vitu. Nataka niwaombe Waheshimiwa Wabunge, always na naomba kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, Bunge hili lii-guide Serikali kwenye kilimo kwa kuhakikisha tunawekeza kwenye mambo ya msingi. Moja ni seed multiplication, kama hatuna mbegu zetu, kama hatuna umwagiliaji, kama hatua uwezo wa kum-subsidizing mkulima kwenye input, hatuko salama. Huu ndiyo ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niongelee issue ya mbolea, nitumie Bunge lako hili Tukufu, it is very danger kwenye capacity zetu tunaposimama mbele ya Bunge Tukufu na sisi ndiyo tunaowakilisha wananchi, tunapata air time and then we send a negative message and misleading information. Trend ya bei ya fertilizer duniani na mimi nimeamua niongee hapa. Kuna hoja inasemwa kwa nini Rwanda, kwa nini Malawi, kwa nini Zambia bei ya mbolea iko chini? Nataka niwapeni statistics za bajeti ya Rwanda mwaka huu. Rwanda for the last ten years amekuwa aki-subsidize input yake, hasa mbolea kwa support ya World Bank, WFP, FAO na wengine. Mwaka huu wa fedha Rwanda inatumia Dola Milioni 15 kutoa ruzuku ya mbolea. Ni sawasawa na asilimia 11.7 ya bajeti nzima ya kilimo ya Rwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Malawi anatumia Dola Milioni 131 ku-subsidize mbolea. Ni sawasawa na asilimia 44 ya bajeti nzima ya Malawi. Zambia ana-subsidize mbolea by 30 percent. Tena Zambia package yake ya subsidy ni mbolea na mbegu. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Tanzania?

WAZIRI WA KILIMO: Tumeanza kuchukua hatua. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tutatumia Bilioni 150 kuanzia Tarehe Mosi.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bashe kidogo subiri. Waheshimiwa Wabunge hapa tunazungumza vitu very serious na kurukiarukia maneno ni nje ya utaratibu wa Kibunge. (Makofi)

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niseme haya mambo kwa uwazi na with respect nijibu hoja categorically ya Mheshimiwa Mpina. He has been a Minister katika Serikali, it is very danger kwenye capacity ya mtu ambaye ni Mbunge wa muda mrefu, amekuwa Naibu Waziri, amekuwa Waziri, kusimama Bungeni ku-present issue ambayo totally he is misleading the public. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bei ya mbolea duniani siyo jambo la kuficha ni jambo liko kwenye public domain, it is a commodity like any other commodity. Hata uki-google unazipata taarifa za bei ya mbolea duniani. Nimechukua source yangu hiyo ni taarifa ya World Bank, a reputable organization. Bei ya mbolea Machi, 2018 DAP ilikuwa Dola 549, FOB rate an average price, today ni Dola 948. Urea Dola 134 leo ni Dola 723.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili siyo jambo la siri, liko wazi halifichwi. Nipitie mbele ya Bunge lako nimuombe Mheshimiwa Mpina kama anayo source yoyote ya kunipatia mbolea ya bei rahisi aje nampa mkataba wa tani Laki Nne zote aniletee. Duniani kote wana-subsidize na mimi nataka niwaambie tusipotoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima wa nchi hii tutakuwa tunawaonea, tunawaumiza na hatuwatendei haki na hatulitakii Taifa letu uhai. Tusifanye siasa kwenye mambo hatari. Hii siasa ndiyo imeua kitalu cha mbegu ya pamba katika Jimbo lake. Ninawaomba, mimi ni very open na I am ready to bear any cost, this is what I believe, lazima tutoe ruzuku ya mbolea kwa wakulima wa nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali haijaishia hapo kwenye ku-design ruzuku, tumeamua kufufua Kampuni yetu ya TFC. No where in the world, hii dhana ya kwamba, Serikali can not trade ni dhana iliyopitwa na wakati. Serikali ita-trade kwa sababu mbili, moja ku-make profit when it is necessary, lakini mbili ku-subsidize na ku-stabilize ndiyo maana tunanunua na kuuza. Sasa tumeamua kuifufua TFC tumeipa mtaji wa Bilioni Sita na tutaipa guarantee iende ikanunue mbolea kwenye soko la dunia ije hapa iweze kushindana na private companies. Kama tuta-subsidize lazima tuwe na mkono wetu ndiyo maana kwenye hotuba nimesema subsidy mechanism ya Wizara ya Kilimo safari hii tutawapa priority wazalishaji wa ndani and we will do this. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna siku zote hofu watu wataiba, halafu kuna dhana moja hatari sana, kuwaita wafanyabiashara wezi. Kwani hakuna Civil Servants wezi nchi hii? Big scandals zilizofanywa humu ndani hazijahusisha Civil Servants? Why we call our private sector everyday wezi kwenye nchi hii? Mtu wa sekta binafsi haibi peke yake lazima awe na mtu wa Serikali waibe nae. Kwa hiyo, mimi nataka niiambie private sector iliyoko kwenye kilimo, I will protect you kama ninavyom-protect mkulima wa nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna majadiliano hapa yamesemwa kuhusu ushirika, nataka niwaambie na nimwambie Ndugu yangu Mheshimiwa Sanga, mazao yote yanayopitia mfumo wa ushirika hayana lumbesa. Ili kumlinda mkulima, wakulima hawa wadogowadogo ni lazima tuujenge ushirika. Wanaushirika wapo wanaoiba lakini hatutaufuta ushirika kwa sababu kuna wezi, tutashughulika na wezi wakati tunaendelea kuujenga ushirika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunazo success stories za ushirika, zipo. Ushirika ulikufa because the country decided kwenda kwenye role approach ya privatization, ndiyo ukweli huo na mimi hiyo ndiyo naamini. Leo tumefufua ginneries, tunafanya Chato, they are making profit, tunayo Mbogwe ya Mheshimiwa Maganga mwaka huu imepata profit na tumeifufua mwaka jana. Nikuhakikishie tunawapa 13 Bilioni ya kwenda kununua pamba. Tumefufua CACU, tunaenda kufufua SHIRECU Sola, tunaenda kufufua Nyanza, tunaenda kufufua Manawa, tunaenda kufufua Sola, tunaenda kufufua Lugulu, tunaenda kufufua ginnery ya Sengerema kwa Mheshimiwa Tabasamu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niseme hivi, tutazifufua. Tuliziua kwa sababu tuliogopa kukabiliana na changamoto, tutakabiliana nazo, tutazifufua without any problem na huo ndiyo mwelekeo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna hoja ya Tanzania Agricultural Development Bank. Kisera TADB is a development bank siyo commercial bank. Kazi ya TADB ni ku-de-risk sekta ya kilimo na ku-invest kwenye miradi ya muda mrefu, ndiyo kazi yao. Bahati mbaya kwa sababu ya sera zetu na mifumo yetu ya ukopeshaji ambayo tunayo katika uchumi wetu, ambayo tume-copy na ku-paste huko kwingine tumeileta hapa ambayo hai-acknowledge rural economies ndiyo maana tunampeleka TADB kwenda kumkopesha mkulima ili akapande nyanya auze kesho, badala ya kumpeleka kwenye development projects. TADB anafanya hiyo kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimekusikia Dada yangu Mheshimiwa Jacqueline, nimewasikia Wabunge wote wanaotaka wamuone TADB karibu, tutakaa na commercial banks zote ambazo zimesaini makubaliano na Tanzania Agricultural Development Bank ziwe na madirisha ya TADB kwa ajili ya kutoa guarantees kwenye maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, benki zote ambazo zina asili ya Kitanzania zimeanza kuelewa sekta ya kilimo, zipo benki NMB, CRDB na mimi wala sioni aibu kuzitaja, TADB, Equity, benki hizi zimeanza kutoa fedha kwa ajili ya kilimo, zimeanza, Wizara tutazisaidia na kuzi-support. Benki yoyote, nilisema mbele ya Rais, nasema mbele ya Bunge, benki yoyote ambayo haitakwenda kutoa mikopo ya kilimo kwa single digit kama tulivyokubaliana haitafanya biashara na Wizara ya Kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, misimu inakuja, unakuja msimu wa korosho wa turn over ya zaidi ya Bilioni 500, wanunuzi wote tutawapeleka kwenye benki zinazofanya biashara na sekta ya kilimo. Unakuja msimu wa pamba, unakuja msimu wa kahawa, unakuja msimu wa chai, unakuja msimu wa kakao, nataka niziambie commercial banks, they must play our music. Kwa muda mrefu turn over zao zinabebwa na kilimo, lakini kinachoenda kwenye kilimo hakionekani, tutafanya nao biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia Bunge lako Tukufu kuwaambia commercial banks pelekeni fedha kwenye ushirika wa korosho. Wakopesheni AMCOS, tumeshakubaliana mimi na ninyi na mmetaka barua kwangu nimewaandikia, sasa ambae hatopeleka tutakaa naye mezani. Ninasema categorically tunaenda kwenye msimu atakaye-enjoy fedha ya msimu wa korosho ni yule aliyeenda kwenye korosho kuwekeza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ipo hoja hapa kwamba, kwanini tunaanzisha Benki ya Ushirika, nashauri tuende tukasome mifumo ya ukopeshaji na ya uendeshaji wa Cooperative Society na Cooperative Society Financing Modals. Vyama vya Ushirika haviwezi kukopesheka katika mifumo hii ya commercial approach tuliyonayo kwenye mabenki, ndiyo maana duniani kote watu walioendelea wanazo benki za cooperatives. Niwahakikishie benki ya ushirika haitaenda kuchukua hela ya umma. Tumefanya modal Benki ya Kilimanjaro. Tumeingia benki wameweka mkono wao, wameweka management, tumeanza kupata faida. Tunai-reform Benki ya Tandahimba, tunazi-merge benki hizi mbili tuna-form Cooperative Bank. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima tuwe na negotiating tool. Lazima taasisi za fedha zijue kwamba wakulima wa nchi hii wana benki yao wasiposikilizwa there is somewhere they can go. TADB ni mali ya Serikali, tuiache TADB ifanye kazi yake ya msingi ya ku-invest kwenye long term project, tuziache commercial banks na cooperative bank zitaenda kwenye short term, hii cooperative bank tunashirikiana na commercial bank kuianzisha. Kama zilikufa benki nyingine, zilikufa because tuliamua kuziua kwa kufanya political decisions kwenye mifumo ya ukopeshaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaenda kuanzisha insurance ya wakulima, inakuwa total package. Tumeanza kazi na TIRA na inakuwaje, kwenye production, kwenye storage na kwenye market, mkulima anapata risk kote, tumeamua. Kwa nini tunaenda kwenye eneo hili? Tunaenda ili kumlinda mkulima na siku ya mwisho aweze kukopesheka kirahisi. Tunashirikiana na Wizara ya Fedha, tunashirikiana na TIRA na tutaanzisha na ku-launch scheme ya insurance ya wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la mafuta ya kula. Siku zote toka nimeingia Bungeni tumekuwa tukijisifia mchikichi ulianzia Tanzania, nataka niseme hivi kama tutaendelea na modal tunayoendelea nayo sasa hivi ya mchikichi tusahau kuwa na utoshelevu wa mafuta, tusahau! Hauwezi kuzalisha miche, unai-breed halafu unampelekea Hussein anaenda kupanda kwenye robo eka. Ninamuomba Mbunge wa Kalenga usiwagawie wakulima eka moja-moja kilimo siyo kugawana umasikini, that is wrong approach. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunachukua hatua gani kwenye mchikichi? Hatua ya kwanza tunayoichukua kama Serikali, tumejiwekea lengo la kuzalisha metric tons Laki Tano ya mafuta ya mchikichi. The first approach tunayotaka tunahitaji hekta 154,000. Nimemuandikia barua Mkuu wa Mkoa wa Pwani, nimemuandikia barua Mkuu wa Mkoa wa Tabora, nimemuandikia barua Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, nimemuandikia barua Mkuu wa Mkoa wa Katavi, tunaenda kuchukua maeneo makubwa kama yatahitaji fidia Serikali italipa fidia. Tunaenda ku-clean, kuyasafisha, tunagawa blocks kubwa kubwa na kuwagawia wakulima tumewakabidhi eneo, kama ni eka 20 unampa eka 20, umempandia, mnasimama. Then automatically kitakachotokea processors ndiyo watakuja pale wataanza ku-process. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii wanayofanya Kaka yangu Mheshimiwa Kirumbe kule Kigoma ni kutengeneza michikichi nusu eka, wanaichemsha kwenye pipa na mti, haiwezi kutuondoa, ndiyo ukweli. Tumeamua kuchukua modal ya ku-subsidize kwenye alizeti na ninataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge, tunaenda kuanzisha Tanzania Agricultural Growth Corridors, lazima tufanye hivi. Wazee wetu hawa akina Mheshimiwa Mkuchika na wenzake hawakuwa wajinga kutoa muongozo wa TANU wa maeneo ya kilimo. Leo unalima korosho kutoka kule kwa kina Mheshimiwa Katani unaipeleka mpaka Ngara. Economically does not pay, logically it has no sound. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaambie inawezekana ikawa unpopular decision, lakini lazima tuwe na growth corridors za kilimo katika nchi hii, lazima na ndiyo mwelekeo tunaoenda nao kama Wizara. Ninaliomba hili Bunge yeyote atakayekuja Wizara ya Kilimo mumhoji juu ya Agricultural Growth Corridor, lazima! tusipofanya hivi hatuitendei haki hii nchi kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunagawa mbegu za alizeti, tuna-subsidize, it is a painful decision na Serikali itaweka Bilioni 11. Nitumie Bunge hili kuwambia Mkurugenzi wa ASA, Dada yangu Sofia mmoja wa Civil Servant wanaofanya kazi nzuri sana katika nchi hii, tulivyoamua kugawa tani 2,000 hakulala yule Dada. Ninawaomba Wakurugenzi wa Halmashauri, targets za kukusanya mapato mtazipata kwenye kilimo, m-support kilimo, tutazalisha, tutagawa tani 5,000 msimu unaokuja kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na tutagawa certified seeds, msimu uliopita tuligawa standard seeds, safari hii tunaenda kugawa certified seeds kwa wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tusipogawa mbegu na kuwapa ruzuku wakulima wa nchi hii, Marekani anatoa ruzuku, European Union wanatoa ruzuku, sisi ni akina nani kudhani kwamba eti mkulima atajinunulia kila kitu? We should not be misled. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niliongea sana kuhusu suala la mbegu na ninataka niseme kwamba mwelekeo wa Serikali ni kufanya research and development, kuzalisha mbegu bora za kisasa, tuwe na mbegu zetu ambazo tunazalisha wenyewe. Tukijizalishia wenyewe hizi mbegu bora whether ni hybrid au ni OPV na kwa kuwa tunataka growth rate ya 10 percent by 2030 haya tunayoyaanza leo matokeo yake siyo ya kesho. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wapo watu waliwekeza huko nyuma, leo tuna-enjoy sisi. Let us sacrifice now. Tujitoe, tuwekeze kwenye uzalishaji wa mbegu, tujitosheleze. Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mazao 13 ambayo ni mahindi, mpunga, mtama, alizeti, soya, ufuta na maharage; mazao haya tukiwekeza kwa muda mrefu kwa kipindi cha miaka mitatu tu kwenye eneo la mbegu nchi hii itajitosheleza. Tutakuwa na mbegu zetu wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, narudia tena kuiambia sekta binafsi ya Tanzania, iache tabia ya kuwa traders, wawe investors. Njooni tutawapa maeneo, tutawapa mikataba ya muda mrefu mzalishe mbegu, tutazinunua sisi, tutawapa wakulima wa nchi hii kwa ruzuku. This is the best model, kote duniani wamefanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ameniambia ndugu yangu Mheshimiwa Katani kwamba nawapendelea watu wa tumbaku kwa sababu natoka Tabora kwenye tumbaku. Kwanza sikani, natoka Tabora. Pili,…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba dakika moja. Ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka tu niseme hivi, wakulima wanasajiliwa wote wala msiwe na hofu. Kupitia Bunge lako nimwambie Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho, usipoanza kusajili wakulima, kuanzia mwaka huu tunaanza kugawa pembejeo, mimi na wewe hatutaelewana. Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba ni lazima usajili wakulima. Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa ni lazima usajili wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Katani anasema tumewapendelea watu wa tumbaku; niseme, kwa mwaka huu mmoja…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bashe toa hoja. Ahsante kwa michango mizuri na majibu mazuri.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimalizie. Karatasi ya hela imepotea nini? (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, awali ya yote nitumie nafasi hii kukushukuru kwa kunipa fursa, lakini tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kuwa na a health discussion inayoendelea ndani ya Bunge lako tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba, mimi ni Mbunge wa awamu ya pili, katika Ripoti za CAG ambazo nimewahi kuona zikijadiliwa openly, transparently na healthy, hii ni moja wapo ya ripoti ambayo nimeiona katika kipindi changu cha pili cha Ubunge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, nataka tu nimhakikishie Mheshimiwa Bonny Kwamba, Mawaziri hatuko katika sehemu ya kulinda ubadhirifu wala hatuungi mkono uhalifu wowote unaofanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la jumla, CAG ni jicho na ni jicho la Bunge lako kwa maana ya oversight function. Vile vile, ni jicho kwa sisi tuliopewa responsibility ya kuweza kusimamia na kuhakikisha tunachukua hatua za kulinda rasilimali za nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pale CAG anapokabidhi ripoti kwa Rais na inapokuja Bungeni na tunapotakiwa kwenda mbele ya Kamati, Serikali tunachukua hatua. Kwa mfano, CAG katika ripoti hii ya mwaka 2021/2022, amezungumzia suala la Mfuko wa Pembejeo kwamba, kuna non-performing loans za zaidi ya shilingi bilioni 121 ambazo hazijakusanywa.

Mheshimiwa Spika, vile vile, CAG ametoa recommendation na Kamati yako ya PIC imetoa recommendation. Moja ya recommendation iliyotoa ni kwamba baadhi ya madeni tuyafute. Hata hivyo, sisi kama Serikali tunachukua hatua gani ili kuweza kusimamia rasilimali za umma?

(i) Kama Serikali tumefanya mabadiliko ya taasisi yetu ya Mfuko wa Pembejeo. Tumewaondoa viongozi waliokuwa wanasimamia taasisi zile na tumechukua professionals ambao wengine ni credible. Sasa hivi DG wa Mfuko wa Pembejeo ni Formal Chief Executive Officer wa ECO BANK. Tumemwomba Rais, tumemtoa private sector na tumemleta tumkabidhi ule Mfuko ili aweze kuu-transform. Mfuko ule ni muhimu kwa uchumi wetu na sekta yetu. (Makofi)

(ii) Mfuko wa pembejeo, wote, viongozi na wasiokuwa viongozi wali-take advantage na CAG amesema na ametoa maelekezo. Sisi katika hatua ya kufuta madeni, hatuendi kufuta madeni kwanza, tunataka ku-recover fedha. Toka mwezi Machi alipo-submit report, tumeshakusanya zaidi ya 1.4 billion. Pia, baadhi ya Wabunge, watumishi wa umma pamoja na viongozi wastaafu wanaodaiwa tumeshawaletea notice. Sasa tunakwenda kuwasajili kwenye credit reference bureau ili wakose uhalali wa kukopeshwa kwenye sekta yoyote ile ya nje katika uchumi mpaka waje walipe hela za umma walizokopa katika Mfuko wa Pembejeo. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri, wapo Wabunge wanaodaiwa?

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, yes wapo. Vile vile, wapo hapa kwenye orodha ninayo. Pia ukiniruhusu naweza nikawataja. (Makofi/Kicheko)

SPIKA: Hapana, nimetaka tu hilo Wabunge wafahamu. Maana watu tunaposema CAG amekwenda huko kukagua akakuta madeni makubwa halafu na sisi tunadaiwa humo, tuwe wa mfano, maana sasa tusije tukawa tunawazungumzia wengine huko na sisi wenyewe hatufanyi. (Makofi)

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika…
SPIKA: Mheshimiwa Bashe, muda wako unalindwa. Endelea na mchango wako, nilitaka tu kujua hilo.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, tunakuletea rasmi (formally) ili wakati wa gratuity tuweze ku-recover zile hela. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo la pili ambalo Kamati ya PAC na bahati nzuri Makamu Mwenyekiti wa Kamati ni aliyekuwa Boss wangu, ametupatia ushauri kwenye Kampuni ya TFC…

MHE. HAMISI S. TALETALE: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Taarifa inatoka wapi? Okay, Mheshimiwa Bashe, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Hamis Taletale.

TAARIFA

MHE. HAMISI S. TALETALE: Mheshimiwa Spika, naomba Kaka yangu Bashe, hiyo list uliyoishika ungeitaja kidogo, tungejua umuhimu wa CAG.

SPIKA: Hebu hiyo orodha niletewe hapa mbele. (Kicheko/Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, nataka niletewe hiyo taarifa kwa sababu na ninyi humu ndani mkichangia kuna watu mnawataja. Kwa hiyo, ngoja niletewe hiyo taarifa nione ukubwa wa hilo tatizo. Ahsante sana. Mheshimiwa Waziri endelea na mchango wako.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, Taarifa ninayokukabidhi ni baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliokopa wao binafsi. Vile vile, baadhi ya Wabunge waliowadhamini wananchi wao kama guarantor. Pia vilevile baadhi ya viongozi wastaafu. Kwa hiyo hii hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tatizo linalokabili Mfuko wa Pembejeo katika nchi yetu kwenye hili suala la kukopesha, linaikabili vile vile Tanzania Investment Bank na linaikabili Benki yetu ya Kilimo. Tumeomba katika eneo la Benki ya Kilimo nao tukuletee list ili uweze kutusaidia na TIB iweze kutusaidia kupitia ofisi yako. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo la pili ambalo nataka nichangie ni eneo la maoni ya Kamati kuhusu TFC. Nataka niwahakikishie Kamati, tumechukua recommendation za CAG kuhakikisha kwamba, Kampuni yetu ya Mbolea inanunua moja kwa moja kutoka kwenye source na inafanya trading. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba Serikali isifanye biashara, nataka niwaombe Waheshimiwa Wabunge, duniani kote Serikali inafanya biashara. Tunachotakiwa kujiuliza ni kwamba, taasisi za Serikali zinazofanya biashara, zinafanya biashara efficiently and effectively? Kama hazifanyi ni kwa nini hazifanyi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mfano TFC, tuliiua wenyewe TFC, tukaua viwanda vya kuchakata mbolea, tukavibinafsisha kwa bei holela, lakini leo tumeona umuhimu na sasa Serikali imeipatia TFC zaidi ya bilioni 110. Leo tunavyoongea, TFC inapakua zaidi ya tani 50,000 katika Bandari ya Dar es Salaam ili kuingiza katika soko la mbolea ndani ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumefanya mabadiliko kutokana na recommendation za Mkaguzi (CAG) kwamba, tufanye mabadiliko ya menejimenti. Tumefanya mabadiliko ya menejimenti, imeundwa Bodi, tumeweka CEO mpya, tumeweka Commercial Director mpya, tumepeleka Director of Finance mpya mwenye uwezo. Mabadiliko ya Sheria ya Procurement Act ambayo yamekuwa yakiifunga miguu TFC ku-compete sokoni, tumechukua hatua hizo ili TFC iwe competitive na hivi sasa tume… (Makofi)

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Haya, ahsante sana. Mheshimiwa Bashe, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Kandege.

TAARIFA

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Taarifa ambayo nataka nimpe Mheshimiwa Waziri, pamoja na mchango wake mzuri juu ya sisi kuua taasisi za Serikali. Kwa mfano TFC ni kwamba, waliagiza mbolea lakini yakaja maelekezo wauze below price. Kwa hiyo, kwa vyovyote vile hasara ilianza kupatikana tangu siku ya kwanza. Ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Bashe, unaipokea taarifa hiyo?

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naipokea na nakiri kwamba, TFC na mashirika mengi ya nchi yetu yaliuawa because of political intervention na maamuzi ambayo ni ya kisera na policy ambazo hazikuwa home-grown policies, kwamba, government should not trade. Hii ndiyo ilipelekea kuua na kwa kuwa tumejifunza, naamini hatutokwenda tena siku nyingine kuichokonoa TFC katika nchi yetu. Sasa, TFC tumeipatia fedha inajenga blending facility Kwala. Tumeinunulia eneo na inajenga blending facility ili kuwa competitive.

Mheshimiwa Spika, la tatu, ambalo nilitaka nimalizie, mawili tu ya mwisho ili nimalizie…

MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Maganga.

TAARIFA

MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Spika, mchangiaji, Mheshimiwa Waziri anachangia vizuri sana na namheshimu. Hata hivyo, kwenye taarifa iliyoko hapa mezani, tunajadili ripoti ya CAG. Kuna watu wametajwa majina na wewe umesema kuna majina ya Wabunge pamoja na Mawaziri ambao ni wahusika. Sasa, naomba Waziri afunguke kabisa aache kufumba macho tusije tukaua Chama. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri, dakika moja malizia mchango wako.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie. Pia, kama dakika moja haitatosha nitakuomba unipe hata mbili. Nataka nimalize mambo mawili ya mwisho.

Mheshimiwa Spika, jana kwenye contribution ya Waheshimiwa Wabunge, kuna jambo lilisemwa hapa. kwamba, Ripoti ya Financial Intelligence Unit imeonesha upotevu wa over two hundred trillion shillings. Nimeamua kwenda kuichukua ile ripoti na kuisoma, kuangalia, nilishtuka sana.

Mheshimiwa Spika, mchangiaji alisema, nanukuu: “fedha hizi zinahamishwa kupita mipakani.” Technically ukijiuliza kwa kufumba macho, unaamini kuwa kuna malori yanakatiza pale border na hela.

Mheshimiwa Spika, nimekwenda kuchukua ile taarifa. Sisi ni Wabunge tuna communicate na wananchi nje, ni hivi, Financial Intelligence Unit Report ambayo summary yake hii hapa, imesema hivi: “Taarifa za miamala ya fedha taslimu (cash transactions) ni 7,313, value ya hizo cash transactions siyo value ya hela tu, transactions thamani yake ukijumlisha ni 56 trillion shillings.”

Mheshimiwa Spika, nini maana yake? Any financial analyst anatakiwa afanye analysis. Nini maana yake? Maana yake ni hivi, our economy is dominated with cash transaction. Nimeuza mahindi NFRA nalipwa cash, nabeba nakwenda foleni benki na-deposit. Financial Intelligence Unit wana-capture zile data. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Financial Intelligence Unit wamesema, taarifa za miamala ya fedha kwa njia za kielektroniki 8,784, thamani yake ni trilioni 200. Maana yake, huko mtaani tunapeana cash, tunalipana kwa M-pesa, tunarushiana. Leo kwa taarifa za Benki Kuu, ratio ya formal na informal ni 60:40. Tafsiri yake bado kuna cash nyingi huko mikononi mwa wananchi ambazo haziko katika mfumo rasmi. Kwa hiyo, tunapoziona cash zinatoka kwenye informal kuingia kwenye mfumo wa kibenki ni hatua nzuri kwa uchumi wowote unaokua. (Makofi)

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kwanza taarifa zimekwishafika tatu. Pili, huu muda anaotumia Mheshimiwa Waziri ni wa kumalizia sentensi ili nimwambie muda umekwenda, kwa sababu sasa hivi ni saa nane Waheshimiwa.

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Spika, anapotosha, anachokizungumza anapotosha siyo purpose ya FIU.

SPIKA: Omba utaratibu, kama anapotosha omba utaratibu.

Mheshimiwa Bashe.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, la mwisho, kwenye hii hoja, ninachotaka niseme kwenye hii hoja ni hivi, tusichukue taarifa kwenye document na kufanya literal translation halafu na kuzipeleka mtaani, zina-confuse public.

Mheshimiwa Spika, la pili, leo hapa na wewe naomba nikunukuu, umehoji kitu ambacho tunatakiwa tukijadili as a country. Our governance system, umehoji hivi, baada ya Mheshimiwa Jerry Silaa kutoa taarifa kuhusu nafasi ya Mbunge katika halmashauri kwamba, Mbunge ni Mjumbe wa Kamati ya Fedha. Wewe ukasema, kama Mbunge ni sehemu ya Kamati ya Fedha katika Halmashauri inayotuhumiwa, huwezi kujadili kesi inayokuhusu.

Mheshimiwa Spika, nini maana yake? Maana yake umefika wakati wa kufanya critical analysis ya role ya Mbunge kwenye halmashauri na namna gani anamsimamia Accounting Officer. Waziri anapokwenda kwenye PAC, ambapo PAC inamwita Katibu Mkuu, Waziri hayupo. Nafika hapa ndani ya Bunge nahojiwa kwa kile ambacho wali-differ kati ya PAC na Waziri kwenye kikao ambacho mimi sijashiriki kama Waziri. (Makofi)
SPIKA: Haya, sawa.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, namalizia…

SPIKA: Mheshimiwa Waziri, hoja yako imeeleweka. Umekwishatoa pendekezo kwamba umefika muda wa kufanya hilo jambo, hatuwezi kuchukua muda zaidi ya hapo. Ahsante sana.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuchangia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kusema jambo moja, tulipopata Uhuru mwaka 1961 tulisema na tuli-declare wazi kwamba nchi yetu ni nchi ya wafanyakazi na wakulima. Hii ndiyo ilikuwa kauli na ndiyo iliyotengeneza direction ya nchi yetu, wafanyakazi wakawa na vyama vya wafanyakazi, wakulima wakawa na ushirika na Serikali ikaweka nguvu katika kutunga sheria, kutengeneza sera ambazo zingeweza kuwajengea mazingira bora wakulima na wafanyakazi wa nchi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka ya 1990 tukafanya liberalization tukatambua kundi la tatu katika nchi yetu, kundi la wafanyabiashara tukawapa heshima kubwa na kuwaita wawekezaji, tukawatengenezea sera, tukawatengenezea sheria ili kuwajengea mazingira ya wao kufanya biashara. Mpaka leo kama nchi hatujawahi kuwa na deliberate move ya kuweza kuli-accommodate kundi kubwa linaloitwa la wafugaji. Huko nyuma tumekuwa tukisema kwamba nchi hii ni yetu sote, sungura mdogo tutagawana wote. Nataka niseme leo, Mwalimu Nyerere aliwahi kuongea mwaka 1975 na wafanyakazi, akiwaambia wafanyakazi utii ukizidi unakuwa uoga, na siku zote uoga huzaa unafiki na unafiki huzaa kujipendekeza na hivyo kuzaa mauti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwalimu aliendelea kuwaambia wafanyakazi, kama ninyi watumishi wa umma kwa wingi wenu mmeshindwa kupiga kura ya kuwaondoa viongozi dhalimu ni bora mfe. Na mimi nasema sisi kama CCM kwa wingi wetu tunashindwa kuishauri Serikali kwa ukweli hatuna sababu ya kubaki kuwa madarakani. Nayasema haya kwa moyo mweupe, nikiwa mwanachama wa chama chetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hivi. Hili ni jukumu letu Serikali ya Chama cha Mapinduzi kutafuta suluhisho la migogoro ya wakulima na wafugaji na hili siyo jukumu la Waziri peke yake ni jukumu letu sote kama chama na kama Serikali. Hili siyo jukumu la Mheshimiwa Maghembe, hili ni jukumu la Waziri wa TAMISEMI, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Ardhi, Waziri wa Katiba na Sheria ili tuweze kutengeneza mazingira bora kwa ajili ya wananchi wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikuambie leo hii kaka yangu Mheshimiwa Kakunda yule pale, katika Wilaya ya Sikonge over 70 percent ni hifadhi, hawa wananchi wakulima na wafugaji wanaenda wapi? Mkoa wa Tabora Pori la Ipala linaanzia Nzega linaenda Uyui, linaenda Tabora Manispaa, linaenda Sikonge, hakuna maeneo. Wakulima wetu na wafugaji wetu wanakwenda wapi? Lazima ufike wakati na ningemuomba Waziri wakati unakuja kufanya wind up hapa useme clearly kwamba tarehe 15 mfugaji hatotolewa porini bila kumuandalia maeneo. Maana yake mkimtoa porini mnaenda kumchonganisha na ndugu yake mkulima waanze kuumizana, hili ni jambo la kwanza. (Makofi)
Mheshimwia Mwenyekiti, kwa hiyo ndugu zangu, dhambi hii na Bunge liiagize Serikali, Bunge la Oktoba wanapokuja hapa kama Serikali waje wametoa affirmative action juu ya tatizo la wafugaji na wakulima. Nataka niwape mfano, mwaka 2006 wafugaji waliondolewa Ihefu wakapelekwa tena Mheshimiwa Abdallah Ulega alikuwa DC yule pale, mnampeleka mfugaji eneo la kijiji hamjamwekea miundombinu. Bajeti ya mwaka huu Mheshimiwa Mwigulu hana fedha ya kuchimba hata mabwawa mawili na tumeipitisha hapa, tunataka kwenda kusaidia matatizo ya wafugaji na wakulima hatuwezi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tuiombe Serikali ije na affirmative action na solution ya jambo hili ili tuondoke kwenye mgogoro huu iwe ni leo, ni kesho, kwa kizazi cha watoto wetu na wajukuu zetu huko mbele. Inawezekana hatupendi kuyasikia, lakini ndiyo ukweli wa jambo hili. (Makofi)
Mheshimiwa mwenyekiti, jambo la pili, siongelei wafugaji na wakulima tena. Jambo la pili leo maliasili ukitazama takwimu zilizotolewa na World Travel Tourism Council on Economic Impact in Tanzania ya mwaka 2015, inasema maliasili yaani utalii ume-create ajira mwaka 2014 watu 1,300,000. Wana-project mwaka 2025 watu watakaokuwa wameajiriwa katika sekta hii direct or indirect ni 1.6 million, growth ya 2.7 percent. Lakini investment lile kapu la uwekezaji kutoka nje na ndani kwa mwaka 2014 uwekezaji uliyofanywa katika sekta ya utalii ni trilioni 1.8. Wana-project mwaka 2025 utakuwa 3.7 ambao ni 9.8 growth ya 0.3 percent.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Mheshimiwa Ally Saleh kaka yangu kaongea mambo ya msingi sana. Tunasema tuangalie emerging economics kwa ajili ya uwekezaji, kwa ajili ya ku-attract watalii, swali la kujiuliza ripoti za dunia zinasema uchumi wa dunia kuna slow growth. Nimeisoma hotuba ya Mheshimiwa Profesa, hakuna plan iliyo-accomodate kuwepo kwa kushuka kwa uchumi wa dunia kwa 0.0 percent namna gani utaathiri Utalii wetu wa ndani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma kitabu alichokiandika kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mpango, anakiri Southern part and Western part of this country tourism haiwezi kukua kwa sababu ya infrastructure mbovu. Tunafanya nini kama Serikali? Mbali na hapo hunting (uwindaji) na Serikali ilipitisha katika Bunge lililopita kuwasaidia locals wawekeze katika uwindaji, kati ya vitalu 160 walivyopewa wawindaji, vitalu 50 vimerudishwa Serikalini kwa sababu gharama ya leseni, ushuru ni kubwa mno. One of expensive destination duniani ni Tanzania, eneo lingine hata landing rate za kutua kwenye viwanja vyetu vya ndege ni kubwa watalii wanatua Kenya ndiyo wanakuja Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ningeiomba Serikali iende ikafanye review upya, itazame upya sekta hii ya utalii kwa kuangalia variables zote za dunia, waje na mpango ambao kama watahitaji idhini ya Bunge tuwasaidie, bila ya hivyo growth kwenye sekta ya utalii ukiitazama kwa miaka mitano ijayo mpaka kumi ni 2.5 percent peke yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo...
MWENYEKITI: Ahsante.
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari za Mwaka 2016
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuchangia.
Kwanza ni-declare interest kama taratibu zinavyotutaka, kwa sababu nina maslahi kwenye vyombo vya habari. Vilevile mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii, ambayo tumetumia muda mrefu katika kipindi cha wiki mbili tulizo kaa hapa Dodoma kuupitia muswada huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme moja na kwa dhati kabisa nishukuru Ofisi ya AG na vilevile nimshukuru Mheshimiwa Waziri, tumefanya engagement za ndani na nje kuhusu muswada huu kuweza kufuta mambo ambayo kwa sababu sheria hii inaenda kupata supremacy over other laws when its comes on issue related to media. Kwa hiyo, sheria hii ilikuwa inaenda kuathiri makundi zaidi ya matatu; moja, printer; pili, publisher; tatu, mwandishi na nne, jamii kwa ujumla. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nitumie fursa hii kushukuru kwa sababu moja; sheria iliyoletwa na Serikali kabla haijaingia kwenye mikono ya Kamati ilikuwa ni sheria ambayo kweli kabisa ilikuwa inaenda kuzamisha industry ya media, lakini sheria hii tuliyonayo leo ni sheria bora kabisa kuliko sheria iliyokuwa inaletwa awali na Serikali kwenye mchakato huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wabunge, kwa spirit ambayo tumeiona Serikali imekuwa nayo, kwenye mchakato na Ofisi ya Attorney General, naamini yale machache yaliyobaki ya kufanyia amendment tukijenga hoja sote bila kutumia moyo na tukajadili kwa nia njema Serikali itakubali ku-give in. Na mimi yapo mambo ambayo humu ndani ningeshauri tuweze kuyajadili na kuweza kuyafanyia marekebisho ili kuyaweka kwenye utekelezaji na kufanya kazi hii ya habari kwa ufanisi.
Moja, tuanze na definition ya editor. Ukienda part one, muswada unam-define editor, means a journalist who is in charge of production of content for radio, television, newspaper, journalist and magazine and include online platform for radio, television and newspaper.
Nashauri tungem-define an editor as a person who is incharge of, and determine the final content of the text, kwa sababu editor ndio anayefanya get away ya final content inayoenda nje, huyu ndio editor. Kwa hiyo, naomba upande wa wahandishi tungeweza kufanya re-definition na mimi nitaleta katika schedule of amendment on the definition of the editor. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikia mjadala ulivyokuwa ukiendelea; kwa spirit ya sheria hii na muswada huu, online publications ambazo haziko connected na print media, haziko under this law. Law hii inasimamia online publications ambapo publications hizo zimetolewa leseni na Mkurugenzi wa Habari MAELEZO kwa ajili ya newspaper. Kwa hiyo, Jamii Forum hausiki humu; Millard Ayo, hausiki humu; all these publications ambazo hazitokani na print media hazihusiki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nilitaka nishauri section 7(2) inasema: “A media house shall in the execution of its obligations, ensure that information issued does not undermine;” kwa hiyo, kuna items zimeelezwa hapo, nilitaka niseme item (f); “it should not undermine (f) infringe lawful commercial interest…” inaendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, spirit ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kupambana na ufisadi na rushwa katika nchi hii. Tunapoweka restriction ku-infringe undermine lawful contract; nataka nitolee mifano. Ipo mikataba before the law leo hii inaonekana ni lawful contract lakini ni mikataba ya hovyo ambayo imelinyonya Taifa hili, inaiibia nchi hii, mfano Mkataba wa IPTL, we all know, ni wizi. Kwa hiyo, before the court of law na kwa sheria za kimikataba this is a lawful contract, lakini hapa tunamnyima mwandishi wa habari haki ya kuandika na kuuchambua na kuonyesha mkataba huu kuwa ni wa kifisadi just because umo kwenye sheria hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka nimshauri Mheshimiwa Waziri, atakapoleta amendment na AG Office waweze kukubali kuondoa hiki kipengele. Kwa nini nasema? Kipengele hiki tulikipitisha kimakosa kwenye access to information tukakipitisha humu ndani ya Bunge. Kwa hiyo, kule tumekitengenezea kinga kwenye access to information halafu huku tena tunakitengenezea kinga kwenye sheria, nayo itakuwa shida. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo nilitaka nishauri, na mimi nipongeze, nimeona kwenye obligations of media wameweka haki za waandishi (right of journalist) kwenye amendment ya Serikali. Nataka nishauri kwamba tunapotoa rights hizi za vyombo vya habari kufanya kazi yake na wakati huo huo tuna section namba 49 ambayo imewekwa na kwa spirit ya section 7(2)(f), tunawaweka wahandishi wa habari kwenye hatari kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, twende kipengele namba 20, nashauri tufute kipengele kidogo namba (3) katika kipengele namba 20.
Mheshimiwa Mwenyekiti, an accredited journalist whose name is expunged from the roll of journalists or is suspended shall not be employed or otherwise act in any capacity in the business or career connected to journalism.” Kipengele hiki ni kibaya, naishauri Serikali kipengele hiki tukiondoe ama tukiongezee kipengele cha ziada kwamba wakati mwandishi amenyang‟anywa leseni ya kufanya kazi, aruhusiwe kufanya kazi on the business associated to his profession, lakini wakati huo huo tumpe haki ya ku-appeal against this process. Appeal iende kwa Waziri, asiporidhika, aende mahakamani kutafuta haki. Kwa sababu the highest place ambayo haki hutafutwa ni mahakamani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kipengele kinampa mamlaka Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO kwenye ku-issue leseni, lakini kipengele hiki kinampa mamlaka ya yeye ku-issue leseni na wakati huo huo anaweza akakunyima leseni. Kwa hiyo, tungeweka kipengele ambacho kinanipa haki mimi ambaye nimenyimwa leseni, haki ya ku-appeal against maamuzi ya Mkurugenzi wa Habari, MAELEZO, ili niweze kupata haki yangu, anaweza kuninyima leseni just because kaamua yeye. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naaamini kwa spirit ambayo tumeanza nayo kwenye Kamati, Waziri na Serikali watakubali kutoa haki hii ili tuweze kumpatia huyo mtu haki ya ku-appeal against that decision. Kwa sababu haki hiyo ya kuninyima leseni inaweza ikatumika vibaya kuninyang‟anya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona kwenye amendments za Serikali; kwanza, naishukuru Serikali sana kwa kufuta kipengele cha 50(4) ambacho kilikuwa kina-provide a room for looting. Polisi alikuwa ana uwezo tu wa kuja kuingia kwenye chombo cha habari na kufungua mitambo, lakini katika amendment, unapofuta sub-section (4) automatically unaiondoa sub-section (8). Kwa hiyo, naomba sub-section (8) na yenyewe iondoke kwa sababu itakuwa haina kazi tena uwepo wake pale. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, labda niongelee wasiwasi uliopo kwenye mchakato wa accreditation na kwenye suala la bodi. Bodi itakuwa ina members saba; na tumekubaliana kwamba members hawa saba watatoka kwenye council ya waandishi wa habari, watatoa participants wawili. Vilevile watatoa media owners kwa maana ya wamiliki wa vyombo vya habari, nao watapewa nafasi ya kuweka members wawili. Naishauri Serikali, kwenye mchakato wa kupatikana accredited journalist wa kuingia kwenye Bodi, Waziri apelekewe na council majina kwamba haya ndio tunayoyapendekeza sisi as a council ili mwaingize kwenye bodi ya kusimamia accreditation na masuala ya vyombo vya habari ili kuwapa uhuru wenyewe kuchagua watu wa kuwaleta (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni kitu kinachoitwa national interest na national priorities; ni vizuri kwa sababu issue za national security ziko defined na Sheria ya Usalama wa Taifa. Kwa hiyo, vifungu ambavyo vinazungumzia suala la Usalama wa Taifa tuseme kwenye sheria kwamba kama sheria inayo-guide suala la usalama wa Taifa; lakini hizi national priorities ni vizuri angalau zikawa defined ndani ya sheria yenyewe ili siku ya mwisho kusitokee pale ambapo unapewa instruction kwamba hili ni la national interest, basi uweze kujithibitishia kwamba hili ni jambo la maslahi ya nchi. Kwa sababu naamini hakuna chombo cha habari ambacho hakitakuwa tayari kulinda maslahi ya nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, nitumie nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais kukutana na wanahabari siku ya leo. Naamini kwamba utaendelea kuwa utamaduni wa kila mwaka kukutana nao ili waweze kumwuliza maswali yale ambayo wananchi wanataka kusikia kutoka kwake.
Kwa hiyo, ni jambo jema na hii spirit tunaamini kwamba Mheshimiwa Nape na Ofisi ya Attorney General watakubali ku-accommodate hizi amendments ndogo ndogo ambazo tunashauri ili kuweza kuuboresha muswada huu na kuifanya sheria hii ni practical iweze kwenda kufanya kazi katika mazingira ya vyombo vya habari. (Makofi)
Mheshimiwa mwenyekiti, ahsante sana.
Naunga mkono hoja.
Mkataba wa Ubia wa Uchumi baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya.
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Labda kwanza nianze kwa kumpongeza Waziri wa Viwanda na Biashara na Serikali kwa ujumla kwa kuleta mjadala ndani ya Bunge wa kujadili mkataba ambao Taifa letu lingeingia. Naiomba Serikali, spirit ya kuleta mikataba Bungeni na uangalie namna gani unaweza kutusaidia kupitia ofisi yako, mikataba ikawa inaletwa ili kupata mandate ya wananchi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, labda nianze kujenga hoja yangu; kwa nini Watanzania tunahoji juu ya mkataba wa EPA? From the business perspective, mahali ambapo mnaenda kushindana hakuna kuaminiana, ndiyo maana tunayoosheana vidole. Tatizo la mkataba huu, hali-recognize state as an individual lina-define parties as a group. Hili ni tatizo la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mimi ningesema na ushauri wangu kwa Serikali, kwa sababu section 143 ya Mkataba wa EPA, kama hawa wazungu wana nia njema na uchumi wa nchi yetu, tupeleke amendment; kwa sababu section 143 inaruhusu kupeleka amendment. Tupeleke amendment ku-redefine parties, kila nchi iingie mkataba na EPA kivyake kwa kuangalia maslahi yake. Bila hivyo, hatuna sababu ya kusaini mkataba huu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa nini nasema hivyo? Ukiusoma mkataba huu unanikumbusha wakati nasoma form three historia; triangular trade. This is another triangular trade in a different way. Ni mkataba ambao unatujenga sisi kuwa producers wa raw material and become a market for them. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sababu ya pili, mkataba huu unapingana na dream ambayo Tanzania imekuwa nayo toka tulivyopata Uhuru. Mwaka 1964 tuli-develop thinking ya kuwa na industries, tuka-fail. Vilevile mistrust kati yetu na Kenya jamani tusisahau. Mwaka 2015 kabla ya Bunge, Mawaziri wetu walienda kukaa kwenye East Africa, wakakubaliana mambo ya msingi kama block.
Moja, walikubaliana kuweka kodi kwenye transit goods; sisi tumekuja kuweka, Wakenya wamefuta. Kwa hiyo, how can we trust them? We will never trust them kwa sababu ya historia. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, yapo mambo ambayo tumekubaliana na wao toka tuna Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kwanza, Jumuiya ya Afrika Mashariki ya pili, wenzetu wameshindwa ku-honour kwa kuangalia maslahi yao. Kwa hiyo, hili ni jambo la msingi sana ambalo tunatakiwa tulione. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo lingine ukisoma Article 20 kwenye mkataba huu, unazungumzia issues za tax; import duties, kutoa uhuru na kufungua borders without restriction. Wanakuwekea conditions kabisa kwamba ukitaka kufanya protection on your internal market or internal development, lazima upate approval kutoka kwao. Who are they? Are we not free country?
Mheshimiwa Spika, ili ujue mkataba huu ni shida, wanazungumzia compensation framework ambapo hawatoi commitment. They know we are going to lose money; we are going to lose our development truck, lakini hawaweki commitment, this is the problem. Kwa hiyo, ndiyo maana nasema, tusiseme kwamba tuko kisiwani, tuko kwenye dunia; lakini mkataba lazima uwe win win situation. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nami nataka kumshauri Waziri wa Viwanda, kwa kuwa section 143 inatoa ruhusa ya kufanya amendment; proposal ya kwanza, redefinition of parties, “this has to be a country between EU and Tanzania, not EU with East Africa, that is number one. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, number two, tukubaliane, we have raw material, they have capital, they have technology; tukubaliane kwamba chochote wanachotaka kuuza kwenye soko lao, viwanda vyao wahamishie kwetu, tu-produce ndani. If they want, they sing our song, not their song. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tusipokuwa protective; tusipokubali kama nchi ku-protect interest zetu za ndani, nataka niwahakikishie, tunaletewa; amesema mama yangu Mheshimiwa Hawa Ghasia this is a second scramble of Africa, tunageuka wazalishaji wa raw materials kama wakati ule tulipokuwa wazalishaji wa watumwa.
Mheshimiwa Spika, ukisoma Article 75 kwenye huu mkataba, unazungumzia issue za economic development. Vilevile, wameorodhesha items, wame-avoid kitu kimoja, they know, there is no development, without industrialization. There is no anywhere kwenye huu mkataba mimi nimeusoma page by page. Wanako-require na kukubali kwamba katika transfer of knowledge we will transfer teknolojia za viwanda kwenye nchi ambazo tunaingia nazo kwenye mikataba, lakini EPA Agreement wametugawa kama Afrika. EPA Agreement content zake kwenye West Afrika, hazifanani na East Africa. Kwa hiyo, wametugawagawa kwa maslahi yao.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka niishauri Serikali, hamjakosea kutokusaini na niipongeze Serikali, nimpongeze Mheshimiwa Rais kutokusaini mkataba huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba huu uende uwe ni mkataba kati ya Tanzania...
Taarifa..
Mheshimiwa Spika, naipokea taarifa yake.
Mheshimiwa Spika, namalizia kwa kusema kitu kimoja, East African Community ni historical. Ilikufa kwa sababu ya mistrust na kwa sababu ya economic interest ya individual state members. There is no shame kwa nchi kuingia kwenye block na kujitoa. There is no shame kwa nchi kuingia kwenye block na kulinda maslahi ya watu wake na kuachana na wenzake. Watu huachana na wake zao, huachana na wazazi wao, kwa kuangalia maslahi na yale wanayoamini. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nataka niwatie moyo Serikali, EPA Agreement, if they will not follow our interest we can‟t, kuna Far East, kuna Middle East; kwanza leo tumbaku inadhalilishwa na wazungu; leo hii mazao yetu yanadhalilishwa na wazungu, we should think of another way. Ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa. Nami nitumie nafasi hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuleta sote pamoja katika Bunge la mwaka huu tukiwa salama na afya njema. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kuchangia katika maeneo makubwa mawili. Eneo la kwanza ni eneo la utumishi. Tumeona commitment ya Serikali juu ya kufanya jitihada kubwa ya kurudisha nidhamu ya Watumishi wa Umma, lakini nataka niiombe Serikali kuna two approach, kuna carrot na stick. Nimeona matumizi ya stick yamekuwa makubwa zaidi kuliko carrot mahali ambapo imefikia watumishi wetu wamekuwa waoga sana katika maeneo mbalimbali. Watu wamekuwa hawafanyi maamuzi, watu wameingiwa na hofu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ningeomba Wizara ya Utumishi, commitment ya Serikali kurudisha nidhamu iende na incentive package kwa watu wanaofanya vizuri na wanaofanya maamuzi katika sekta mbalimbali katika utumishi wa umma ili jambo hili liweze kuwatia moyo wale waadilifu. Hatusemi wanaofanya vibaya wasiadhibiwe. Hilo ni jambo la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili katika Utumishi ni suala la ku-develop Institutional capacity. Dhamira ya Serikali ya Rais, mimi nakubaliana sana na approach ya Rais Magufuli. When you are in crisis tumia hiyo mechanism ya crisis ku-sort out problem, wakati una develop Institution zako.
Kwa hiyo, ningeomba mwaka huu mmoja tumetumia fire approach sasa Serikali ifanye kazi kubwa ya ku-develop institutional capacity ili Mheshimiwa Rais atakapomaliza kipindi chake cha miaka kumi taasisi ziendelee. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini ni lazima tujenge capacity za Taasisi? Tunapotegemea sana uwepo wa mtu, anapokuwa hayupo tunarudi kule tulikotoka, tutakuwa hatuisaidii nchi kule tunakotaka kwenda. Kwa hiyo hili ni jambo muhimu sana la kufanya ili tuweze kutatua tatizo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni Wizara ya TAMISEMI, nampongeza Waziri wa TAMISEMI na Naibu wake wanajitahidi, lakini wameondoa vyanzo vya mapato hasa katika Miji na Manispaa. Wajitahidi basi hata fedha za OC ziende. Kinachotokea sasa hivi fedha za OC haziendi ambazo ziko budgeted kabisa na zimepitishwa na Bunge, haziendi kwa wakati, hazifiki matokeo yake fedha za mapato ya ndani sasa zinatumika kuendesha ofisi za Hamashauri, matokeo yake zinaathiri development activity katika maeneo yetu. Kwa hiyo, hili ni jambo muhimu sana Serikali ikaangalia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile mtazame uwezekano wa kurudisha hivi vyanzo vya mapato ambavyo vimeondolewa kwenye Halmashauri. Kwa sababu tunapopunguzia capacity ya Halmashauri ya kifedha maana yake na tumeamua kwenda na approach ya D by D shughuli za maendeleo na hali ya uchumi kwa wananchi wetu ni ngumu. Ni muhimu sana tuone namna gani tunazipa uwezo Halmashauri zetu kutatua changamoto zinazokabiliana nazo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, TAMISEMI kama wenzangu wamesema, TAMISEMI ni kama jalala, lakini sitaki kutumia neno jalala imeamuliwa kwamba kwa approach ya utawala tuliyochagua ni kwamba ndiyo coordination center. Leo tumeunda Tume ya Utumishi ya Walimu (Teachers Commission) imeenda TAMISEMI, ingawa mimi kwa mtazamo wangu naiona haina meno, lakini la pili kuna madai ya Walimu ambayo ni makubwa mno. Lazima tuje na mechanism ambayo itajenga hope kwa Walimu wetu kwamba madai yao haya within this span of period yatakuwa yamelipwa. I don‟t believe mpaka leo bado tunafanya uhakiki, tunahakiki mpaka lini? Hili ni jambo ambalo ni lazima tujiulize. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ajira imekuwa changamoto, wewe ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati yetu unaona Wizara ya Afya ikija, Wizara ya Elimu ikija, suala la ajira linavyokuwa ni mjadala mkubwa na upungufu wa watumishi hasa wa kada ya afya katika Halmashauri zetu. Mheshimiwa Simbachawene na Dada yetu Mheshimiwa Angellah Kairuki, uhakiki wameshafanya for almost one year, hebu wafungulie hizi ajira ili tuondoe watoto wetu wanao graduate mitaani tuweze kuwa-absorb katika ajira, pia tuweze kuondoa kero! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi leo by June katika Mji wa Nzega tutakuwa na zahanati 15 mpya, tutakuwa na vituo vya afya vitatu vipya, hakuna manpower! Leo Nzega tuliamua kuachana na approach ya kushusha vyeo Walimu ambao hawa-perform vizuri na kuwaadhibu, no! Tuliamua kuangalia changamoto zao. Mwaka jana matokeo ya darasa la saba Halmashauri ya Nzega ilikuwa ya mwisho Kimkoa, mwaka huu imekuwa ya pili kwa sababu tulienda ku-tackle matatizo ya Walimu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana Mji wa Nzega haukuwa na division one na division two almost lakini performance ya mwaka huu kidogo ime-grow, Halmashauri ya Mji wa Nzega imekuwa ya 73. It‟s very important tukaangalia hizi crisis katika Local Government na Brother Simbachawene you have a lot of mzigo. Kwa hiyo, ni vizuri kupitia Bunge hili na nimshauri kwenye Bajeti inayokuja matatizo ya Walimu tuje na clear plan kwamba madai ya Walimu ni kiwango hiki, tutayalipa ndani ya kipindi hiki ili Walimu wetu wawe na matumaini kule walipo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, TASAF. TASAF imesaidia sana watu wetu lakini umefika wakati wa approach ya TASAF kubadilika iwe ni developmental approach, kwamba fedha zinazopelekwa kwenye kaya maskini ziwe ni fedha ambazo zina wa-commit wale watu maskini kuja na miradi ya maendeleo ambayo hawa wataalam wa TASAF mwaka kesho kabla hawajakupa fedha wanaangalia performance ya mwaka jana, fedha tuliyokupa na mradi ulioanzisha. Ni muhimu Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Local Government ikafanya kazi very close na wataalam wa TASAF na Watendaji wetu wa Vijiji ili kusaidia kaya hizi maskini badala ya kupewa fedha kwenda kula ziwe fedha za investment ili tuweze kuondokana na umaskini katika Local Government. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumesikia hoja ya asilimia 10 nataka Serikali itafakari. Tuna asilimia 10 katika Halmashauri, tuliahidi kwenye Ilani shilingi 50 million ya kila kijiji. Tuna fedha za Mfuko wa Uwezeshaji, hizi fedha ziko scattered katika maeneo mengi. Umewadia wakati kama Serikali itazame hizi fedha ambazo zina target kwenda kukopesha vijana na akinamama tuziwekee proper framework kisheria ili ziweze kufikia watu kwa wakati. Ukichukua milioni 50 ya kila one basket halafu tukachukua fedha za uwezeshaji zinazowekwa Wizara ya Mheshimiwa Jenista, fedha hizi tukazitengenezea sheria zitatusaidia sana kuondokana na changamoto za financing kwa watu wetu maskini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana na naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa. Kwanza nianze kuipongeza sana Kamati kwa kazi waliyoifanya ingawa taarifa yao ni ya quarter moja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili nataka niishauri Serikali. Siyo dhambi kufanya evaluation ya kipindi cha miezi sita na kurudi kwenye drawing table ili kujipanga upya. Ukisoma taarifa ya Kamati, ukisoma Taarifa ya Hali ya Uchumi aliyoiwasilisha Mheshimiwa Waziri kwenye Bunge hili, ukisoma Taarifa ya BOT waliyoitoa Desemba inatuonesha kabisa tuna kila sababu ya Serikali kurudi kukaa chini kujitathmini na kupanga upya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe indication chache ambazo kwa upande mmoja Kamati wamezi-observe upande mwingine taarifa ya BOT waliyoitoa Desemba wamezionesha. Kwenye taarifa ya BOT na Waziri wa Fedha kwenye taarifa yake aliyoisoma juzi ndani ya Bunge hili, ukisoma kwenye taarifa aliyoisoma kwenye Bunge hili, item number (6) na (7) naomba ninukuu. Kwenye item number (6), Mheshimiwa Waziri anasema:-
“Kiashiria kingine cha jumla cha afya ya uchumi wa Taifa ni mfumuko wa bei ambao unapima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya nchini. Mfumuko wa bei ulipungua kutoa 6.5 Januari mpaka 5.5 Juni 2016”.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda item number (7), Mheshimiwa Waziri anasema:-
“Kuna viashiria vinavyoonesha uwezekano wa kuongezeka kwa mfumuko wa bei kutokana na hali ya ukame uliojitokeza hapa Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki na uwezekano wa kuongezeka kwa bei za mafuta katika soko la dunia” Mheshimiwa Mwenyekiti, item (6) ni viashiria vya kuporomoka wakati item (7), kuna uwezekano wa kupanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa ya Benki Kuu inasema, headline inflation ime-grow kutoka 0.1% kwenda 1.1% na contributing factor ni energy na fuel growth. Kwa hiyo, tafsiri yake ni nini? Ni kwamba kuanzia leo Januari mpaka tunapofika Julai hali ya mfumuko wa bei itakwenda juu. Maisha ya Watanzania yatakuwa magumu. Kwa hiyo, ni vizuri sasa Serikali ikachukua hatua ili ku-rescue situation inayotukabili huko mbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hivi? Kwa sababu sehemu kubwa ya bajeti yetu tuliyopitisha, fedha za maendeleo tulitarajia kutoka nje ya nchi. Hali inavyoonesha tume-attain less than 30% na kuna uwezekano development partner wasitupatie hizi fedha. Tumekimbilia kwenda kukopa ndani ambako tume-burst, tumekwenda 132%. Tafsiri yake mzunguko wa fedha kwenye soko utashuka maisha yataendelea kuwa magumu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuongelea kushuka kwa shilingi. Mheshimiwa Waziri anatuonesha confidence na mimi nayasema haya kufuata maelekezo yako kwamba tujikite kwenye ripoti ya Kamati, najenga hoja zangu hizi za awali ili ripoti ya Kamati ambayo wamei-submit hapa iweze kutu-guide na Serikali ikubali kuna tatizo. Dola ya Kimarekani wameamua wao wenyewe kuongeza kutoka 0.25% interest kwenda 0.5% na wana project by December itakwenda 0.75%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tafsiri yake ni kwamba madeni tuliyokopa kama nchi gharama yake itaongezeka. Serikali inasema deni linahimilika, Mheshimiwa Waziri umefika wakati sasa, ushauri wangu kwenye hili, tuanze kulitathmini deni letu sio kwa GDP tulitathmini deni letu kwa mapato yetu halisi against revenue kwa sababu tunalipa kwa kodi tunayoikusanya kutoka kwa Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nchi, Kamati imesema na Serikali imesema kwamba tumekusanya vizuri kodi kutoka kwa Watanzania, tafsiri yake ni nini? Tumetoa fedha kwenye mifuko ya Watanzania, tumeipeleka Serikalini. Njia pekee ya kutatua hii changamoto ni fedha hizi zirudi kwa shughuli za maendeleo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nami niipongeze Serikali kusaini mkataba wa ujenzi wa reli ya kati na Waturuki wa kilometa 200. Naipongeza sana na nikitazama kwa bajeti ya 2016/2017 achievement zitaonekana kwenye item ambazo hazigusi maisha ya Watanzania moja kwa moja, ndege tuta-attain na hilo ni jambo jema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaelewa sana Wizara ya Fedha wanafanya jitihada ya kutuondoa kwenye consumption based economy kwenda kwenye investment based economy lakini hatutakiwi ku-destroy fundamental pillars tulizozijenga, uchumi wetu muda mrefu umekuwa based on consumption.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niishauri Serikali, tuna dhamira ya kwenda kwenye viwanda, angalieni takwimu zifuatazo. Ukisoma taarifa ya Waziri na taarifa ya Kamati tunasema kwamba tumepunguza importation lakini importation zipi tulizopunguza? Capital goods imports zimeshuka kwa 33%, building and construction zimeshuka kwa 29%, machinery zimeshuka kwa 36%, fertilizers zimeshuka kwa 24%, transport equipment zimeshuka kwa 32%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii tafsiri yake ni nini? Ni kwamba uwekezaji kwenye viwanda haupo! Hakuna mtu anaenda kuwekeza! Kwa hiyo, Serikali sasa hivi inachotakiwa kukifanya na mkubali kwamba bajeti ya mwaka jana tuliyopitisha haikuwa realistic! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri la kwanza na tulisema kwenye bajeti wakati tunachangia mwaka jana kwamba wakati umefika tuwe na realistic budget na vipaumbele ambavyo tunaweza ku-attain kwa muda mfupi. La pili, financial institution, Waziri amesema Benki zetu ziko imara, moja ya benki iliyopata hasara quarter ya pili ni Tanzania Investment Bank, ndiyo ime-lead! Imepata hasara ya 20 billion shillings lakini hoja tunayoisikia sana kutoka Wizara ya Fedha ni kwamba provision zinazowekwa na benki za non-performing loans ni nyingi ndiyo maana wanapata hasara. Kunapokuwa na NPL nyingi sio rocket science ni kwa sababu wakopaji waliokopa wameshindwa kulipa! Kwa hiyo, wanacho-provide ni kwamba hazitakusanyika huko na kwa kuwa hazitakusanyika maana yake mabenki yatapata hasara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tazama Benki yetu ya Kilimo ilikuwa ina 56 billion shillings, wamekopesha only 3.6 maana yake hakuna mikopo inaenda kwenye sekta ya kilimo. Sekta ya kilimo ndiyo uti wa mgongo wa kutuletea fedha zetu za nje pamoja na tourism lakini hali ya nchi inavyoonekana, sekta ya kilimo imeshuka kwa 0.5. Kitakachotokea mavuno ya 2016/2017 itashuka zaidi kwa sababu hatukutenga fedha kwa ajili ya pembejeo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashangaa perception ya Serikali sasa hivi kwamba uwekezaji kwenye pembejeo na researchers wamefanya uchunguzi duniani kwamba msipo-provide fedha nyingi kwenye kilimo kwa kuwekeza kwenye pembejeo ukuaji wa sekta ya kilimo utakuwa ni historia, hatuwezi! Kwa hiyo, ningeiomba Serikali, Wizara ya Kilimo uwekezaji kwa ajili ya pembejeo kwenye bajeti ijayo ufanyike…
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Naunga mkono ripoti ya Kamati.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa fursa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naunga mkono taarifa za Kamati zote mbili. Nataka niseme mambo machache na jambo la kwanza ni suala la maji, ninaiomba Wizara ya Maji mchakato wa maji wa Ziwa Victoria na utekelezaji wake tunatarajia sana watu wa Mikoa ya Tabora na Singida utekelezaji wa mradi huu, tumeusubiri kwa muda mrefu ingawa kuna matumaini madogo, tunaomba, tulitarajia mwezi huu wa pili mkandarasi angekuwa site, tungeomba jambo hili litekelezwe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili kwenye maji fedha zinazoenda kwenye Mfuko wa Maji chanzo chake ni mafuta. Amesema Mheshimiwa Nsanzugwanko ni muhimu sana base ambayo Kamati ya Bunge inayosimamia section hii i-demand kutoka Serikali mahitaji halali ambayo yalitakiwa yaende kwenye mfuko ili siku nyingine wakija kwenye Bunge hapa watuambie matarajio yalikuwa ‘X’ kilichopatikana ni ‘Y’ ili Bunge liwe na picha halisi ya nini kinaendelea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu, narejea nilisema mwezi wa tisa nasema na leo; hakuna dhamira ya Serikali kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji. Nilitahadharishe Bunge kwamba tusiingizwe kwenye mkenge tukadhani hili ni tatizo la Mheshimiwa Tibeza, siyo tatizo la Mheshimiwa Tizeba tu wala siyo tatizo la Waziri wa Ardhi tu na wala siyo tatizo la Waziri wa Maliasili, hili ni tatizo linalotakiwa kuchukuliwa na Serikali collectively. Wizara ya TAMISEMI, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Maji, Wizara ya Mifugo na Wizara ya Ardhi waje kwenye Bunge la Bajeti watuletee mpango wa Serikali juu ya kumaliza mgogoro wa wakulima na wafugaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu na la mwisho ni hii dream tuliyonayo, dream hii imekuwepo toka Serikali ya Awamu ya Kwanza kujenga Taifa la kujitegemea la viwanda, Serikali ya Awamu ya Pili, Awamu ya Tatu, Awamu ya Nne na Serikali ya Awamu ya Tano. Ninachokiona makosa yale ya toka enzi za Mwalimu Nyerere yanafanyika leo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kosa la kwanza tuna-focus kuwekeza kwenye viwanda ambavyo ukitazama objective yake ni import substitution industry, ni wrong. Lazima tufike mahali Serikali ielewe hakuna industrialization kama hatujaamua kuwekeza kwenye sekta ya kilimo. Hakuna industrialization kama Wizara ya Viwanda, Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati na Wizara ya Miundombinu hawatokuja collectively na kuwa na master plan ya kutujengea viwanda katika nchi hii.
Mheshimiwa Mwijage atakuwa anakuja hapa anatuambia njoo nikupe kiwanda. Mimi nimempa eneo hekta 200 Nzega, mpaka leo nataka niwaruhusu wananchi walime hakuna hata hope. Nataka nitoe mfano mwingine, leo hii tumbaku ina tozo na ushuru almost 16 lakini ukizitazama pamoja na silent ziko 19, Mheshimiwa Tizeba anajua.
Mheshimiwa Rais wakati anaomba kura alisema ataondoa tozo kwa wakulima, leo Nzega mkulima wa Idudumo akilima mpunga anaanza kutozwa kuanzia anavyotoka njiani nyumbani kwake na mageti mpaka anafika mashineni kuuza gunia lake moja, tunaongeza umaskini kwa watu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, safari hii hatujaweka bajeti ya pembejeo, niwaombe Waheshimiwa Wabunge, hasa wa Chama chetu cha Mapinduzi, tusiwe tayari ku-fall into the pressure ya Serikali. Tumepitisha bajeti ya ajabu sana ya Kilimo mwaka huu hapa sisi, ambayo haina fedha ya bwawa, Mheshimiwa Dkt. Tizeba Waziri wa Kilimo wala Wizara ya Maji hawana uwezo wa kutujengea mabwawa ya wafugaji, hana fedha za pembejeo, tunasema mawakala walipwe tutaambiwa tu bado wanachunguza, Mheshimiwa Dkt. Tizeba hana lugha nyingine, kaapa yule, lakini hakuna fedha za kuwalipa, this is the bitter truth…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa, mimi nataka nichangie mambo machache na nataka nijielekeze kwenye Kamati ya Mambo ya Nje na Usalama. Mheshimiwa Mwenyekiti, dhana ya usalama ina mitazamo mingi, lakini usalama wa nchi yoyote duniani huanza na raia wake. Raia ndiye mlinzi namba moja wa nchi yake. Unaweza ukawa na jeshi kubwa, lina vifaru vingi, bunduki nyingi, askari wengi lakini raia kama hawako tayari kulinda usalama wa nchi yao, nchi hiyo haiwezi kuwa na usalama, itakuwa na utulivu. Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia kitakwimu duniani, Tanzania ni moja kati ya nchi 20 za mwisho ambazo raia wake wanafuraha. Raia wanapokuwa hawana furaha, kuna mambo mengi yanayochangia. Sasa msingi wa yote haya ni nini, ni haki. Jambo la kwanza ambalo kama Taifa muhimu kabisa kulipa kipaumbele katika kuhakikisha usalama wa nchi yetu unaendelea kushamiri ili mambo mengine yaweze kufanikiwa ni haki za raia kuheshimiwa na haki hizi ni haki za kiraia, lakini vilevile haki za kiuchumi. Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mifano michache. Leo Bunge sisi tunapitisha sheria, nataka nitolee mfano sheria ya SUMATRA. Basi lenye kubeba abiria 40 ili lipate leseni ya SUMATRA linatakiwa kulipa shilingi 80,000. Ukiangalia cost per unit maana yake kila kiti cha abiria ni shilingi 2,000. Lakini bodaboda ili afanye biashara yake anatakiwa alipie SUMATRA shilingi 20,000 maana yake kiti kimoja kile cha abiria yeye anakilipia shilingi 20,000 hakuna haki. Mheshimiwa Mwenyekiti, mwanafunzi wa Chuo Kikuu anaenda chuoni hana uhakika wa maisha yake, mfanyabiashara anayeenda sokoni kufanya biashara yake hana uhakika wa kufanya biashara yake katika mazingira salama. Maana yake tumetengeneza sheria nyingi ambazo hazimfanyi mtu masikini kuweza kuwa na uhakika wa maisha yake, hii ni hatarishi kwa usalama wa nchi yetu. Kwa hiyo, mimi ningeshauri Serikali, hakuna jambo la msingi kuliko jambo lolote kama haki za raia kuheshimiwa. Tunapoanza kujenga msingi wa kukandamiza haki za raia katika nchi, tunajenga Taifa la watu wanaonung‟unika ambao hawatakuwa na uzalendo katika moyo wao, ambao hawatokuwa tayari kulipigania Taifa hili. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu za dunia za United Nations za mwaka 1974, Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi ya 107 katika nchi ambazo raia wake wanafuraha, leo imeporomoka, ni swali muhimu la kujiuliza. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, kama Taifa tulikuwa na heshima yetu katika medani ya kimataifa, heshima ambayo ililijenga na kuijenga taswira ya nchi hii kutokuungana na watu wanaokandamiza watu wao, leo Serikali iko katika mchakato wa kufungua Ubalozi wa Israel. Mwalimu alim-consider Muisraeli kuwa ni mkandamizaji wa haki za watu duniani ambaye amekalia kimabavu Taifa la watu wengine, sisi tumeondoka kwenye msingi uliojenga Taifa hili kwa muda mrefu. Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikitika sana, African Union kuichukua nchi ya Morocco kuiingiza katika Jumuiya ya Nchi za Afrika na sisi kama Taifa hatujatoa stand mpaka leo, ni jambo la kusikitisha sana kama nchi. Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuchangia. Na mimi ni-declare interest kwanza ni Mjumbe wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kusema, kama Taifa tunakabiliwa na mambo matatu makubwa, nina imani sana na Serikali ya Awamu ya Tano, kwamba mambo haya matatu, ukiwa na collective work mambo haya tutayamaliza. Jambo la kwanza ni suala la dawa za kulevya, jambo la pili ni jambo la ushoga, jambo la tatu ni tatizo la elimu ya hovyo kwenye nchi yetu, haya mambo matatu yanaliumiza Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mheshimiwa Rais Kikwete alisema anayo list ya wauza dawa za kulevya, naomba nieleweke Rais Kikwete alisema anayo list ya majina ya wauza dawa za kulevya. Mimi ningeomba kupitia Bunge hili Waziri wa Mambo ya Ndani amfuate Mzee Kikwete pale Msoga akamuombe ile list ili waweze kuungana na kazi ya Makonda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaiomba Serikali, kama alivyosema Mheshimiwa Rais, vita ya madawa ya kulevya, na mimi naamini anachokifanya Mheshimiwa Makonda ana-collect taarifa, vita ya dawa za kulevya siyo vita ya Paul Makonda peke yake, ni vita ya Serikali dhidi ya cartel ya dawa za kulevya. Kwa hiyo, naamini hataachwa Makonda na vita hii kama alivyoachwa alivyoanza kuongelea suala la lesbians na ushoga, alibaki nayo peke yake, kwa hiyo naamini kwamba Serikali itamuunga mkono katika jitihada hii aliyoanza, he started somewhere, ninaamini watumiaji wataachiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili kwenye issue ya dawa za kulevya, nadhani lazima tuelewe, kama nchi tunataka kupigana vita hii tupigane in it’s totality. Kwa sababu tunatunga sheria dhidi ya dawa za kulevya halafu tunaruhusu kuanzisha vituo vya kutibu watumiaji wa dawa za kulevya, you prohibit in the left hand side, unakataza kwa mkono wa kulia unaruhusu kwa mkono wa kushoto, mnaanzisha vita mnaita sober house. Mimi ingekuwa amri yangu ningefunga sober house na kila mtu anayekula unga akienda hospitali apimwe, akionekana anakula aanze kushughulikiwa yeye kutusaidia aliyemuuzia, distributor ni nani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu; nataka tuangalie hizi takwimu Waheshimiwa Wabunge humu ndani tumeongea sana, kwamba madai ya walimu, walimu wana matatizo. Tatizo la msingi la sekta ya elimu katika nchi yetu ni mfumo. Leo elimu yetu inasimamiwa na almost Wizara tano, TAMISEMI, kama Kamati ya Huduma madai ya walimu anayasema sana Mheshimiwa Mwalimu Bilago kwa sababu ni mwalimu, na dada yangu Mheshimiwa Susan na Wajumbe wengine, lakini hili liko chini ya TAMISEMI. Kwa hatua ya awali Bunge hili liazimie, linapokuja suala la elimu, Waziri wa TAMISEMI na Waziri wa Elimu waje mbele ya Kamati kwa pamoja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu matokeo ya mwaka huu asilimia 93 ya shule zilizofanya vizuri ni shule za private, government ni only seven percent. Lakini division one mpaka division three ni asilimia 28 tu ya wanafunzi, asilimia 72 ni division four na division zero. Hali ya vyuo vyetu vikuu tunasema kwamba tunatanua elimu ya msingi matokeo yake idadi ya watoto wanaofaulu ni kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka huu tumeweza kuwapa sponsorship au kuwapa mikopo watoto 25,000 tu kati ya karibu watoto 60,000 ambao walikuwa wamedahiliwa kwenda vyuo vikuu, kuna watoto 35,000 hawajapata fursa ya kwenda higher learning institution ni tatizo. Kamati imesema TCU badala ya kusimamia suala la ubora amebaki kuwa dalali wa vyuo vikuu. Nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge, East Africa Community iliunda commission ya kupitia vyuo vikuu vinavyotoa elimu ya madaktari, vyuo vinne vimefungwa Tanzania kwa sababu quality ya elimu yake iko chini, this is a crisis! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hatutakuwa serious kwenye suala la elimu ya nchi hii hatuwezi kupiga hatua tunayotaka kupiga na mimi niwaombe Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Spika hapa alisema kuna hoja nilipeleka ya kutazama mfumo wa elimu, basi kwa kuanza tu tuazimie, Serikali ikautazame mfumo wa elimu wa nchi hii wote. Vyuo vikuu angalau by standard, wahadhiri wenye Ph.D wanaotakiwa kuwa kwenye vyuo vikuu, tulionao sasa hivi ni only 25 percent wakati standard ni angalau asilimia 60, lakini vyuo vyetu vina asilimia 25 tu ya wahadhiri wenye sifa ya kuweza kufundisha katika vyuo vikuu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sometimes unajiuliza, nimeona takwimu za BEST, ukichukua takwimu za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia za mwaka 2012 mpaka 2016….
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, muda umeisha?
MWENYEKITI: Ndiyo, Ahsante Mheshimiwa Bashe.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa fursa. Kwanza nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia sote kufika hapa kwa ajili ya kutimiza wajibu wetu. Vilevile nitumie fursa hii kukupa pole wewe kwa kuondokewa na mmoja kati ya sisi, Mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mheshimiwa Dkt. Macha ambaye alikuwa Mjumbe mwenzangu wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Mheshimiwa Spika, nianze kwanza kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu. Nampongeza kwa jambo moja kubwa sana, humbleness. Kwa kipindi cha mwaka mmoja ambao amekuwa Waziri Mkuu wetu ame-portray kuwa kiongozi mtulivu, mwadilifu na msikivu. Simpongezi kwa sababu labda ya unafiki au kuna kitu nataka, this is the naked truth. Ni Waziri Mkuu mpole, msikivu na anayesimamia kile ambacho anakiamini. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tumeshuhudia viongozi wa ngazi mbalimbali na Wabunge wamekuwa wakisema katika levels mbalimbali za wilaya na mikoa viongozi wengi kukosa sifa aliyonayo Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Hiki ni kipaji ambacho Mwenyezi Mungu amempa na hatuna budi
kumpongeza kwa kuonesha hilo. Nadhani viongozi wengine katika nchi wana wajibu wa kujifunza jambo hili alilonalo Mheshimiwa Majaliwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niende kwenye kuchangia. Kwanza niipongeze Ofisi ya Waziri Mkuu, ukiangalia kwenye maelezo ya hotuba yake na Kamati, bajeti ya maendeleo wamepata asilimia 44, ndicho walichokipata. Hii ni taswira inayoonesha kwamba Serikali katika Wizara mbalimbali suala la upelekaji wa fedha limekuwa tatizo. Kwa hiyo, ningeshauri kwenye cabinet kabla ya bajeti ya Serikali Kuu haijaja ingawa katika Kamati tumeona wote, mimi kwenye Kamati niliyopo nimeona utekelezaji wa bajeti ulivyo tatizo hasa fedha za maendeleo.
Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Waziri Mkuu ukiangalia ukurasa wa 16, anapoongelea suala la Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana imetoa mikopo ya 1.5 billion shillings kwa vikundi 297 lakini ameongelea Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutoa 4.6 billion lakini tulioshiriki kwenye mchakato huu, mimi nimeenda na Mkoa wangu Serikali za Mitaa kuona ni kiwango gani fedha kutoka Central Government zinavyoathiri upatikanaji wa asilimia tano na asilimia 10.
Mheshimiwa Spika, kwa mfano katika Halmashauri ya Mji wa Nzega, OC iliyokuwa budgeted kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ilikuwa ni shilingi milioni 606, tulichokipokea ni asilimia 27 peke yake. Development budget ilikuwa ni 5.7 billion tulichokipokea ni asilimia 24. Maana yake ni kwamba fedha tulizokusanya katika mapato ya ndani zote zitaenda kusukuma shughuli za uendeshaji wa ofisi, asilimia tano ya akinamama na asilimia tano ya vijana haiwezi kuwa attained. Kwa hiyo, tafsiri ni moja tu, ni lazima tupange realistic budget. Sio vibaya kuwa na uhakika kuliko kujenga matumaini makubwa kwa watu wetu ambayo hayapo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pale Ofisini kwa Waziri Mkuu na mimi nimpongeze kuanzisha hiki kitengo cha ku- track ahadi za Rais, nampongeza sana. Mheshimiwa Waziri Mkuu ningekuomba uende hatua ya mbele zaidi, ile ofisi yako inayo-track ahadi za Rais kwa mfumo wa kidigitali na utekelezaji wake katika kila Wizara tungeomba angalau kila miezi sita Wabunge tugawiwe, kwa sababu sisi ndio tuliokuwepo kwenye majimbo wakati Rais anatoa hizi ahadi. Zipo ahadi za Ilani na zipo ahadi ambazo Rais alitoa pale pale hadharani. Kwa mfano, katika Jimbo langu Rais aliahidi ujenzi wa daraja la Nhobola na sisi katika Halmashauri tukaamua kutoa fedha imefanyika feasibility study na kila kitu tume-submit Wizara ya Ujenzi, kwa sababu uwezo wa TAMISEMI kujenga haupo.
Mheshimiwa Spika, aAhadi ile tuliahidiwa itatekelezwa mwaka huu mpaka leo hatuoni dhamira pamoja na kukutana na Mawaziri katika corridor. Wakati Rais anakwenda Chato Desemba alifanya mkutano Nzega na kwenye podium akasema kwamba jambo hili linashughulikiwa mwaka huu wa fedha, hakuna, wananchi wanaishi kwa matumaini. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwenye hotuba hii ya Waziri Mkuu amezungumzia suala la kukua kwa uchumi kwa asilimia saba na nimemsikia dada yangu Mheshimiwa Janet Mbene amezungumza suala hili. Economic growth na economic development ni vitu viwili tofauti. Tunapozungumzia growth ya uchumi bila kuzungumzia kubadilika kwa maisha ya watu tutakuwa tunajidanganya kwenye takwimu na tatizo liko wapi? Tatizo la kwanza ndugu zangu nimeangalia alichokipresent Waziri wa Fedha hapa hakuna inclusion, kwenye mpango wetu tunaokuja kuupitisha wa 2017/2018 ni ule ule hauna tofauti na 2016/2017. Hakuna focus kwenye agrosector.
Mheshimiwa Spika, hatuwezi kuondoa matatizo ya watu wetu kama hatuwekezi kwenye kilimo. Ni hatari kweli! Mimi nataka niseme, kama hatutokuwa makini kutatua changamoto ya umaskini wa watu wetu kwa kuangalia sector zinazokua, zinazogusa maisha ya watu, it is just a time bomb, iko siku watu watatafuta haki yao mitaani na hii itahatarisha usalama wa nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, angalia sekta zilizo-contribute asilimia saba kutokana na hotuba ya Waziri Mkuu, madini, usafiri, mawasiliano, financial institution. Madini ni yapi? Ni GGM na Acaccia. Ripoti ya Kamati ya Bomani ambayo iliundwa na Serikali ya Awamu ya Nne mpaka leo utekelezaji wa mapendekezo yake its only 30%. Kamati ya Bomani ilipendekeza mrahaba wa 3% - 15% hiyo ndiyo range. Revenue
sharing plan hatujafanya, matokeo yake tumefanya nini? Ndiyo hii tunafanya zima moto. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tunayo mipango, tuna Sera ya Madini ya nchi, tuna mapendekezo ya ripoti ya Bomani hayajatekelezwa, tunafanya hizi kazi za zima moto. Ningeomba Mheshimiwa Waziri Mkuu niishauri Serikali kwa heshima kabisa, kule kwangu Nzega wanaamini yale makontena yaliyoko pale bandarini ndani yana dhahabu yaani kuna zile gold bar. Tunaomba mrekodi hili tukio la uchunguzi mtuoneshe kwenye TV kilichomo ndani ya zile kontena.
Mheshimiwa Spika, mimi ni mmoja wa watu ambao naamini uwekezaji wa migodi mikubwa haujasaidia nchi yetu. Haujasaidia kabisa na mimi ni muathirika natoka Nzega. Yule Resolute kaondoka na 10 billion shillings ya service levy, nimesema humu, TMA wamefanya, nimeandika barua na kwa taarifa yako Mheshimiwa Spika, mwezi wa Sita anapewa certificate na Serikali ya ku-close mradi na kuondoka. Anaondoka na bilioni kumi ya Watanzania na ya wananchi wa Nzega, it is very painful. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niishukuru Serikali kwa kugawa maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo, mimi kwangu wameanza kupata. Hata hivyo, naiomba Wizara ya Nishati na Madini, nimpongeze Waziri na Naibu Waziri kwenye hili wamekuwa supportive. Wale mnaowapa leseni wakija
kwenye Halmashauri zetu angalau mhusishe jamii kwa sababu… Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
SPIKA: Mheshimiwa Bashe, muda hauko upande wako.
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, ahsante.
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru nianze kabisa kwa kuunga mkono hoja.

Mimi nina mambo machache, jambo la kwanza alilisema Mheshimiwa Selemani Zedi, tarehe 19 Januari, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega alimuandikia Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kuitaka kampuni inayoitwa Mokasi Medical Systems and Electronics iliyopewa mkataba wa ku-service x-ray waje waifanyie marekebisho x-ray ya Hospitali ya Wilaya ya Nzega. Mpaka leo ni miezi mitano, ninataka nimuombe Mheshimiwa Waziri anapokuja ku-wind up atuambie kwa nini, kwa sababu nimemsikia hata ndugu yangu wa Mafia amelalamika sana kuhusu hili suala. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini hii kampuni kama ina mkataba na Serikali usivunjwe huu mkataba? Jambo la kwanza. Jambo la pili kwa nini hatua za kisheria zisichukuliwe? Hili ni jambo ni muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega na Halmashauri ya Mji wa Nzega wanapata shida, x-ray ipo, hairuhusiwi kuguswa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe taarifa kwenye Bunge na nimpongeze Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, ninaamini kaka yangu Simbachawene hatamchukulia hatua kwa maamuzi aliyoyafanya huyu Mkurugenzi. Mkurugenzi ameamua kuwasialiana na Hospitali ya Rufaa kwa ajili ya kumpata Biomedical Engineer anaitwa Emmanuel Nkusi kutoka Bugando ili aje aweze kwa sababu ni mtaalamu kushughulikia suala la x-ray ya Hospitali ya Wilaya ya Nzega. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kwamba kwa kuwa mkataba ni Philips huyu mtu amefanya maamuzi kwa kuangalia maslaha mapana ya nchi, nataka niseme kwamba maamuzi haya yamefanyika na mtaalamu amefika na ameshalipwa na amechukua kifaa kuondoka nacho. (Makofi)

Hoja yangu, Mheshimiwa Waziri anapokuja why huyu Mokasi asifukuzwe kufanya hizi kazi, hili ni jambo moja. Jambo la pili mimi ni mpongeze sana Mheshimiwa Rais, mimi ni mjumbe wa Kamati, support aliyoitoa Mheshimiwa Rais kwenye suala la hospitali ya Ocean Road na tunafahamu matatizo ya cancer, na mimi nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri Ummy kwa sababu tupo kwenye Kamati yeye na Mheshimiwa Kigwangalla tunaona tatizo la resource lililopo na namna anavyoweka priority, nataka niombe kwa ushauri, mwaka huu tunamaliza ile Phase II pale Ocean Road na tutakuwa kwenye nafasi nzuri sana kwenye Ocean Road. Niombe jitihada ziongezwe kwenye Hospitali ya Kikwete ya Moyo na Hospitali ya MOI ili ziweze kuongeza utoaji wa huduma katika maeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho nataka niishauri Serikali, Ilani yetu ya uchaguzi it is very clear, kwamba kila kijiji - zahanati na kila kata - kituo cha afya, hii ndiyo commentment yetu kwa Watanzania. Ningeomba kuwepo na proper plan na kuwe kuna strategic unit kati ya Wizara ya TAMISEMI na Wizara ya Afya ni namna gani tunajenga kila mwaka vituo vya afya. Kama kila Halmashauri ikiwekewa condition kwamba kila mwaka wa fedha angalau vijengwe vituo viwili, vitatu vya afya tuna uwezo wa kupata kwa mwaka angalau vituo 200 vya afya. Hii itatusaidia sana kupunguza matatizo katika maeneo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami niwapongeze sana Wizara ya Afya na TAMISEMI, kuwepo kwa Dkt. Chaula pale anayeshughulika na masuala ya afya, angalau anatupunguzia.

Nataka niwaombe Mheshimiwa Simbachawene na Waziri wa Afya, hebu ondoeni haka ka-condition kwa tofauli za nchi sita. Kule kwenye Halmashauri wananchi tumewahamasisha, mfano kwangu sasa hivi tunavyoongea tuna zahanati 15 tunajenga sisi wananchi, zimefika kwenye level ya madirisha, lakini kuna kale ile condition ya kusema kwamba ili ujenge zahanati lazima iwe tofali ya nchi sita. Tofali ya nchi sita kwa kule kwetu Nzega ni 1200, mwaka huu mimi nimegawa matofali 47,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukichukua hiyo twenty percent ya incremental cost ni milioni tisa na laki nne, gharama additional cost. Hivyo, tuwe na flexibility kwenye haya mambo ili angalau kama tulivyojenga madarasa katika kuanzishwa kwa shule za kata, wananchi walijitahidi sana kwa sababu tuliondoa zile condition za ki-engineer. Niombe sana Serikali iangalie namna gani Serikali inaweza kufanya jambo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa kuwapongeza kwa jitihada mnazofanya lakini Mheshimiwa Waziri usipokuja na hoja ya huyu Mokasi Medical Systems.....

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. HUSSEIN M. BASHE: ….nitashika shilingi. Ahsante Mheshimiwa Mwenyekiti.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa. Kwanza nitumie fursa hii kumpongeza kwa dhati kabisa Mheshimiwa Rais kwa ku- revive dream ya kuwa na industries katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 1967 Mwalimu Nyerere aliasisi dhana ya kuwa na viwanda, na focus ikawa import substitution industries, viwanda ambavyo baadaye vilikuja kufa. Kwenye bajeti ya mwaka jana nilimuahidi kaka yangu Mwijage, kwamba tutakutana na nilionesha mashaka yangu juu ya utekelezaji wa dhamira ya yeye kufikia yale ambayo alikuwa ametarajia, na leo tunayaona.

Mheshimiwa Naibu Spika, vision ya Rais ni kujenga uchumi wa viwanda ambao utalijenga Taifa hili kujitegemea, hii ndiyo vision ya Rais. Kwenye battle field, Chief of Staff na Generals wanachora vita kwenye meza, wanaoenda kupiganisha vita hii ni makamanda. Tuna tatizo kubwa la ku-link vision ya Rais na mikakati yetu ya kuweza kufikia malengo aliyokuwa nayo Mheshimiwa Rais ya kuwa na viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nitoe mifano michache, kwa taarifa ya BOT ya mwezi Aprili, manufacturing industry imeshuka kutoka 1.4 million US Dollar mpaka 817 million US Dollar, maana yake tumepoteza dola milioni 500. Re-Export ime-drop kwa dola milioni 80, fish and fish products ime-drop kwa dola milioni 20, lakini on the other hand credits kwenye agro sector zime-drop mpaka kufika negative 9.2, transport and communication zime-drop by negative 21.6, building by negative 3, hotel and restaurant ime-drop by 7%. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, export of traditional crops, bidhaa pekee iliyo-grow ni korosho na not because of volume, because of price. Tobacco imeshuka kutoka mwaka 2015, three hundred and forty three million US Dollar mpaka milioni 281 mwaka 2017 Machi. Cotton imeshuka kwa dola milioni 10, kahawa imeshuka kwa dola milioni tisa, karafuu imeshuka kwa dola milioni 13. Sisal ime-grow only for one million US Dollar. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, capital goods, capital equipments. Capital goods zimeshuka mpaka negative 16.7, transport imeshuka kwa 23.9, building 19.3, machinery 11.3, what is the problem? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, problem ni un-predictability ya sera zetu za kodi. Nitatoa mfano wa Sheria ya Uwekezaji, kifungu namba 19. Sheria hii tumeibadilisha mwaka 2009 kwa kufuta utaratibu wa deemed capital goods, ikashusha investiment. Tukaibadilisha mwaka 2010;tukaibadilisha mwaka 2012; tunafuta na kurudisha, tukaibadilisha 2014 na tumeibadilisha mwaka 2015. This is the same country sheria ile ile, leo unweka incentive kesho unafuta. Mheshimiwa Mwijage hata ahubiri kwa Injili na Qurani, we will never go through. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nichukue mfano, success ya industrialization ni private sector na Mheshimiwa Rais amesema. Nimechukua kitabu cha miaka mitano cha mpango, hakuna hata page moja inayoongelea namna gani private sector itakuwa included kwenye growth of economy of this country. The problem is a Ministry of Finance that is our biggest problem. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nikupe mfano mwingine, ninayo Ripoti ya World Bank iliyoifanya Tanzania Micro Reform for Agri-Business. Ili uanzishe kiwanda kidogo cha kuzalisha maziwa unatakiwa uwe na documents zifuatazo, upate Incorporation Business Licence kutoka BRELA, Premise Registration, Equipment and Truck Registration, Product Testing and Registration, Staff Health Certificate, On Going Inspection, Import Permit/Export Permit, Weigh Measures; ili uzipate hizi zinatakiwa zipite BRELA, TFDA, TBS, Diary Board, OSHA, Ministry of Labour, Weigh and Measure, NEMC, all of these! Nani anakuja kuwekeza hapa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu, Deputy Managing Director of International Monitory Fund alikuwepo Tanzania, amesifia sana uchumi wetu kwa kipindi cha miaka 20, lakini amesema mambo matatu na naomba ninukuu:-

“(i) It is essential to increase investiment in an effective way to address key bottlenecks in the economy and create more jobs.”

Mheshimiwa Naibu Spika, our area to create jobs ni ku-link industrialization na agriculture, tusipofanya namna hiyo hatuwezi ku-create kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe mfano wa Wamachinga, na nimeongea na Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI ameahidi kuipitia hii Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa. Leo tuna Sheria ya Fedha tuliyoifanyia mabadiliko mwaka 2012 ambayo inamtaka mfanyabiashara alipe service levy ya 0.3 percent. Wewe ukiwa unauza coca cola, double taxation angalia hii. Cocacola Kwanza atalipa service levy kutokana na turn over na muuzaji wa Nzega anatakiwa alipe
0.3 on the same product ambayo mmei-tax from the producer mnakuja kum-tax from the agent na mnakuja kum-tax retail seller. How can we grow business like this? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kaka yangu Mheshimiwa Mwijage, utazunguka all over the world. Nataka niwape mfano kuhusu leather industry, waliongea Waheshimiwa Wabunge hapa. Kuzalisha one square feet ya ngozi Tanzania ni senti 14 dola, Ethiopia ni senti 8, India ni senti 7, Pakistan ni senti 8, how can we compete? Na why, kwa sababu, sisi tumeweka export duty ukizalisha ngozi Tanzania kui-export unalipia kodi, uki-import chemicals kwa ajili ya ku-process ngozi unalipa 25% tax, unalipa 18% VAT, how can we grow? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa heshima kabisa nataka niiombe Serikali na Mheshimiwa Waziri wa Fedha, there is no where in the World una-tax inputs. Kodi zote lazima ziwekwe kwenye output, una-tax vipi inputs! Unaongeza cost of production, nani atawekeza? BOT imefanya mabadiliko kwenye mfumo wake wa interest, nani ataenda kukopa? There is no way! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndio maana ripoti ya BOT inaonesha lending imeendelea kushuka kwa sababu hakuna sehemu ya kwenda kufanya biashara. Sasa hivi wanachinga tunakusanya kodi za Halmashauri vibaya mno, hawakui hawa watu, mkulima kodi, mmachinga kodi akianza kufanya biashara yake, mwekezaji kodi. Nataka niishauri Serikali, Mheshimiwa Waziri wa Viwanda toa direction dunia ijue.

Mheshimiwa Naibu Spika, umefanyika Mkutano wa IFC juzi, one week ago, kujadili emerging economies and where to put money kwenye private sector, Tanzania inakuwa discussed ni area ambayo ni unpredictable. Leo mna sheria hii kesho akija Waziri huyu anabadilisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, there is no way kama Wizara ya Fedha haitaelewa kwamba kodi ni secondary, number one is creation of wealth and creation of job.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa muda. Kwanza sina shaka na dhamira na uwezo wa Mheshimiwa Dkt. Tizeba hata kidogo ila nina mashaka na dhamira na focus ya Wizara ya Fedha ambayo asilimia 65 ya Watanzania wanaishi katika sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi lakini development budget tuliyopeleka kwenye kilimo ni asilimia tatu na kwenye mifugo ni asilimia nane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa mkononi ninayo barua aliwahi kuiandika Mheshimiwa Rais Magufuli akimuandikia wakati huo Waziri wa Fedha, Ndugu Mustapha Mkulo mwaka 2009 na nitamkabidhi kaka yangu, nitaomba wahudumu wampelekee Mheshimiwa Waziri. Mheshimiwa Rais Magufuli wakati huo akiwa Waziri wa Mifugo alitaja changamoto saba zinazokabili sekta ndogo ya maziwa katika nchi hii. Mpaka leo zile changamoto ziko hai, unaona ni namna gani Serikalini kuna tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya mifugo kwa maana ya sekta ya ngozi, katika nchi ya Ethopia asilimia 47 ya GDP ya Ethiopia inachangiwa na sekta ya mifugo na sekta ya kahawa. Sisi ni wa pili na ningeomba niweke kumbukumbu sawa humu Bungeni tunasema watatu Sudan imeshagawanyika sasa hivi nchi ya pili Afrika kwa mifugo mingi ni Tanzania. Hata hivyo, hawa wafugaji tunawasaidiaje? Nataka nikupe mifano namna gani Serikali inawafilisi wafugaji wa nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Ngara katika hii operesheni ya kufukuza wafugaji, zaidi ya ng’ombe 2,047 za wafugaji ambao walinyang’anywa mifugo yao zimefilisiwa leo ni watu maskini. Waziri kwenye kitabu anazungumzia mauzo ya hay, yale majani yale yanayofungwa ya thamani ya Sh.55,000,000. Ukipiga hesabu ni sawasawa na hay 20,000, are we serious? Hay 20,000 ni chakula cha ng’ombe kwenye shamba la mtu mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ilani yetu ya Uchaguzi hii hapa, ukurasa wa 14 na 15 unazungumzia namna gani tutaweza kuongeza uzalishaji wa mifugo bora kwa wafugaji. Ilani yetu ya Uchaguzi imeweka target ya kupeleka mitamba 10,000 kwa wafugaji wetu. Waziri anazungumzia mitamba 500 kwa mwaka, Ilani inazungumzia mitamba 10,000. Mabwawa kwa mwaka katika kipindi cha 2015-2020, Ilani yetu inazungumzia kuchimba mabwawa 2000 mpaka sasa bajeti ya mwaka jana na ya mwaka huu hakuna fedha za mabwawa. How can we help this country? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niishauri Serikali, hatuwezi kufikia dhamira ya industrialization kama hatutowekeza kwenye kilimo na ufugaji katika nchi hii. GDP yetu ni Dola bilioni 52, bilioni 15 inatoka katika sekta ya Agro lakini hatuwekezi yaani sekta inayotuingizia bilioni 15 tunapeleka only three percent of our budget. Hii inasikitisha sana na inaenda against our promises kwa wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Waziri akija hapa atueleze, leo tumbaku inaporomoka na ninavyoongea hivi leo gulio la tumbaku limezuiliwa Tabora, ame-project mwenyewe kwamba mwaka huu 2017/2018 yaani Serikali kabisa inapanga kwamba zao la tumbaku litashuka, wana mpango gani kwa hawa wakulima watakaopata umaskini kutokana na zao kushuka na ni namna gani umaskini wao unakuwa compensated kwa mazao mengine, hakuna mpango. Waziri amefanya kazi kubwa ya kufuta tozo ambayo itatusaidia bei yetu kuwa competitive kwenye soko la dunia, jambo jema lakini kama hatuwekezi kwenye production hizo tozo zote anazofuta kaka yangu Mheshimiwa Tizeba hazitakuwa na manufaa yoyote yale kwa wananchi wetu wala uchumi wetu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuweza kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitumie fursa hii kumshukuru kwa dhati kabisa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa initiative na kusukuma Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria ambao sisi wakazi wa Mkoa wa Tabora tumekuwa tukiusubiri kwa muda mrefu. Nimshukuru kwa dhati kabisa Mheshimiwa Waziri na Katibu Mkuu ambao tulishiriki pamoja pale Tabora katika sherehe ya kutia saini mkataba, na kwa taarifa zilizopo ni kwamba mwezi ujao wakandarasi wataanza kazi na kwa sisi tunaochunguza chunguza tayari zile Kampuni za Kihindi zimeshaonekana maeneo ya Solwa kule wakianza kufanya fanya shughuli za awali. Kwa hiyo, nishukuru kwa dhati kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Nzega nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kuanza kutekeleza ahadi ya Rais ya shilingi milioni 200 ambayo ni fedha za awali kwa ajili ya kuondoa tatizo la maji wakati tunasubiri mradi huu wa miezi 36. Sasa hivi Nzega angalau tumeanza kupata maji kwa mgao kwa wiki mara mbili. Mwanzo tulikuwa hatupati, angalau kwa mwezi walikuwa wanapata mara moja. Lakini sasa hvi ime-improve two hundred. Nikuombe Mheshimiwa Waziri utakapokuja kuhitimisha ahadi ya Mheshimiwa Rais wakati anakwenda Christimas ile milioni 200 iliyobaki inafiki lini Nzega? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme jambo moja, pamoja na shukrani zote hizi za dhati, niseme jambo la kusikitisha. Leo Nzega tuna siku tano hatuna maji na sababu ni moja tu, Mamlaka ya Maji ya Nzega ambayo imeanzishwa mwaka mmoja uliopita imekatiwa umeme na Shirika la TANESCO kwa sababu ya deni la shilingi milioni 206 ambalo chanzo chake ni Serikali Kuu kutokupeleka fedha za OC kwa zaidi ya miaka mitano, wananchi wanaadhibiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Bunge hili ningeomba, tunamnyooshea kidole Waziri wa Maji, jukumu na matatizo ya maji haya cause route ya haya yote tunayoyajadili ni Ministry of Finance. This is a biggest problem, kila sehemu tatizo fedha hazijaenda za maendeleo. Nataka niwape mfano mdogo, mimi natoka Kamati ya Huduma za Jamii, tuna matatizo ya x-ray kutokuwa serviced kwa sababu ya deni la Philips. Who is the problem? Ministry of Finance hawajamlipa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Mamlaka za Maji za nchi nzima zinadaiwa shilingi bilioni nane na Shirika la Umeme, lakini mamlaka hizi kwa ujumla wake zinadai taasisi za Serikali shilingi bilioni 39. Watanzania wanalipa bills zao tunawakatia maji kwa sababu taasisi za Serikali Kuu hazijalipa umeme. Anayeadhibiwa ni common man on the street. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo Katiba ya Chama changu hapa. Moja ya dhumuni, wajibu wa mwanachama, Wajibu Namba Tatu; “Kujitolea nafasi yake, kuondosha umaskini, ujinga, maradhi na dhuluma na kwa jumla kushirikiana na wananchi wote katika kujenga nchi yetu.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, sitakuwa sehemu ya dhuluma ya wananchi wa Nzega kukosa maji kwa uzembe unaotokana na maamuzi ya Serikalini, I will never be part of this. Sitaunga mkono Bajeti ya Serikali kwa sababu moja tu, Waziri wa Fedha aje hapa atuambie Waheshimiwa Wabunge anamalizaje deni la TANESCO ili Mamlaka za Maji zisikatiwe umeme kwa uzembe unaotokana na Serikali Kuu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge hapa tumejadili sana kuongeza fedha na mimi nashukuru Waziri wa Fedha popote alipo apigiwe simu au Naibu wake atuhakikishie hapa kwenye Finance Bill wanaongeza tozo la shilingi 50… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa. Kwanza nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha wote hai na salama, tuliopata bahati ya kufika kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Mwenyezi Mungu atujalie tuweze kufunga kwa amani na utulivu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze hotuba yangu na mchango wangu kwa maneno yafuatayo:-

Jukumu la msingi la Wizara ya Fedha kama Wizara ni administrator anayesimamia utekelezaji wa kitu kinachoitwa Fiscal Policy. Fiscal Policy ndiyo instrument inayotumika na Serikali kukusanya fedha na inayo-guide Serikali sehemu ya kutumia fedha hizo kwa lengo moja tu la msingi, kusaidia na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimefanya tathmini yangu kwa kina. Leo tuna mwaka mmoja, nimekaa najiuliza maswali na naongea kwa polepole sana, nini dhamira ya wataalam walioko katika Wizara ya Fedha?

Mheshimiwa Mwenyekiti, usimamiaji na utekelezaji wa jambo hili una vehicle mbili tu, moja yenye dhamira ya kupambana na mfumuko wa bei. Hapo ndipo Serikali itaweka kodi ili kupunguza purchasing power ya watu, lakini katika kuchochea uchumi nyingine ni Serikali kutumia Sera yake ya Kodi ili kupunguza sehemu mbalimbali wanazotoza kodi na kukuza uchumi na hasa pale ambapo biashara zinapokuwa chini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitamtolea mfano mlipa kodi mmoja mkubwa anaitwa TBL. TBL baada ya mabadiliko ya kodi ya mwaka jana, kodi anayolipa kwa Mwaka huu wa Fedha wa 2016/2017 tunaomaliza, imeshuka kwa bilioni 50. Huyu ni TBL kwa nini, kwa sababu ya imposition of Excise Duty.

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa za Wizara ya Fedha zinaonesha kushuka kwa makusanyo ya kodi ya PAYE, taarifa ya makusanyo ya fedha ya Wizara ya Fedha inaonesha kushuka kwa VAT on import goods. Taarifa ya TPA inaonesha kushuka kwa mapato kwa asilimia 13 ya bandari yetu, kwa nini? Kwa sababu ya imposition ya VAT on transit goods. Najiuliza swali, wataalam wa Wizara ya Fedha wanafikiri nini? Mwalimu wangu wa uchumi yumo humu ndani, I am not an economist, lakini nimesoma basics, najiuliza wao wanatoa wapi hizi thinking wanazo-impose?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa za Wizara ya Fedha biashara 7,700 zimefungwa nchi hii, ajira zimepotea! Najiuliza maswali, what is the bottom line? Bottom line ni kukuza uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wataalam wa Wizara ya Fedha wameweka kodi maeneo mbalimbali kwa mwaka wa fedha na ukisiliza business community inalalamika juu ya imposition ya kodi nyingi zinazowekwa na Serikali na huoni dhamira ya Serikali kupunguza kodi hizi, huoni kabisa. A large tax payer ambaye ananunua mazao ya kilimo kutoka kwa Watanzania kama TBL, anaenda Serikalini anapeleka proposal ya kuwaambia jamani, mnavyoweka kodi hii mnapoteza fedha hizi na Serikali at the end of the day inapoteza kiwango hiki cha fedha! Alisema Mheshimiwa Serukamba hapa ni lazima Serikali ijue katika kila biashara ya kila Mtanzania Serikali ni share holder kwa asilimia 30, kwa sababu inachukua siku ya mwisho corporate tax. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe mifano michache, nimeitaja; Domestic VAT imeshuka, VAT on import imeshuka, domestic ya excise imeshuka, PAYE imeshuka, withholding tax imeshuka, corporate tax imeshuka! Where are they going to collect? Wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba kaka yangu Mheshimiwa Mpango nilisema mwaka jana na narudia leo ndani ya Bunge hili. Naheshimu sana his academic back ground, either kuna mambo mawili, kuna slow move ndani ya Wizara ya Fedha juu ya wataalam kuishauri Serikali sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa za Wizara ya Fedha zinaonesha zimefunguliwa biashara mpya laki mbili, unajiuliza swali biashara elfu saba zilizofungwa impact yake kwenye kodi zimeonekana. Hizi laki mbili zilizofunguliwa kwenye uchumi hazionekani, nashindwa kuelewa wapi tunataka kwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niiombe Serikali kwa heshima kabisa, kuna njia mbili za kutengeneza bajeti, anao large tax payer wake Mheshimiwa Waziri, awaite awaambie kutoka wewe TBL anataka corporate tax ya this amount mwaka huu wa fedha amfanyie nini kama Serikali, atamwambia ili a-grow productivity yake atasema nipe one, two, three, four, because the bottom line una-tap mwisho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo vinywaji baridi wiki iliyopita CocaCola Kwanza imepunguza wafanyakazi 130. Jamani ninyi wataalam mliokaa huko nataka niwaambie jambo moja na niseme kwa kuwa mimi ni Mbunge wa Chama cha Mapinduzi, sitavumilia kutoka moyoni kuona technical mistake ambazo haziitaji PhD wala u-professor. We will not allow this! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhamira ya Rais iko very clear, ku-grow uchumi wa nchi hii, kujenga viwanda, ku- create ajira, hatuwezi ku-attain namna hii. Nataka niwape mfano, ukisoma taarifa ya Port Authority ya Kenya mwaka 2014/2015 asilimia 1.4 ya mizigo ya Tanzania ilipita pale. Mwaka 2016/2017 asilimia 2.7 ya mizigo ya Tanzania imepita Mombasa, ina-grow, maana yake wafanyabiashara wanahama, wanaenda kupitishia mizigo yao kwingine, why! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, principal ziko wazi, Serikali inakusanya kodi, haiwezi kukusanya kodi kwa watu maskini, haiwezi kukusanya kodi, nataka niwape mfano, Bunge lililopita Waziri wa Fedha alisema humu ndani Dkt. Mpango tutagawa EFD machines kwa wafanyabiashara Serikali haijagawa to-date, unajua kinachoendelea site, wafanyabiashara wameandikiwa barua waikopeshe Serikali hela…. (Makofi)

(Hapa muda wa kengele ililia kuashiria muda wa mzungumzaji kuisha)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa. Kwanza nitume nafasi hii kuwapa pole familia ya Mzee Kingunge na watu wote ambao kwa njia moja au nyingine wameguswa na msiba huu na nikipe pole Chama cha Mapinduzi na niwape pole kwa dhati kabisa Watanzania ambao wanaufahamu mchango wa mzee huyu katika historia ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kusema jambo moja, umefika wakati kama nchi hasa Wizara yetu ya Fedha kukubali kubadili Sera zake za Kibajeti. Kwa nini nasema hivyo? Nitatoa takwimu chache ambazo ukitazama takwimu hizi zinaonekana katika taarifa za BOT za kuanzia mwaka 2011 mpaka 2017, Desemba. Hata hivyo, taarifa hizi zina complement taarifa iliyotolewa na IMF Januari, taarifa hizi sina complement taarifa iliyotolewa na Economic Intelligence Unit.

Mheshimiwa Mwenyekiti, real GDP growth yetu mwaka 2011 ilikuwa 7.9 sasa hivi tuna- project itakuwa 6.8. Hata hivyo, mzunguko wa fedha umeshuka kutoka asilimia 22 ya mwaka 2011 mpaka asilimia 1.8 ya sasa hivi. Ukiangalia Export ya hasa mazao ya kilimo ambayo ndiyo yameajiri asilimia 70 ya Watanzania, ukichukua zao la kahawa lilikuwa mwaka 2011, growth rate yake ilikuwa ni asilimia 55 sasa hivi asilimia negative 5.4.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile ukichukua cotton mwaka 2012 ilikuwa kwa asilimia 26, kwa sasa hivi imekuwa kwa asilimia hasi 3.8; ukichukua Sisal ndiyo imekuwa na ongezeko la asilimia 2.9 ya mwaka 2011, sasa hivi linakuwa kwa wastani wa asilimia 4.0; ukichukua zao la tumbaku ambalo mwaka 2011 lilikuwa kwa asilimia 56, sasa hivi mwaka 2017 kwa taarifa za BOT limekuwa kwa negative 62.7; na zao la korosho ambalo limekuwa kwa asilimia 70.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niangalie manufacturing, export ya manufacturing na hii ni business export naiongelea. Manufacturing ukichukua mwaka 2011 ili-grow kwa asilimia 96 growth rate. Sasa hivi ime-growth kwa negative asilimia 244. Tuangalie credits kwenye major economic activities; Trade, ilikuwa mwaka 2011 kwa asilimia 34 sasa hivi imekuwa kwa asilimia 16. Agro mwaka 2011 ilikuwa 51.7 sasa hivi imekuwa kwa negative 0.3. Transport ilikuwa imeshuka mpaka asilimia 22.1. Building yenyewe mwaka 2011 ilikuwa kwa asilimia 44 sasa hivi inakuwa kwa asilimia kwa wastani wa asilimia 5.0.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imports za Capital Goods zimeshuka kwa asilimia 15. Tafsiri yake ni ndogo tu. Our fiscal policies hazichochei ukuaji wa biashara na uchumi katika nchi. Nataka niwapeni mfano, takwimu zinaonesha Watanzania tunakuwa kwa wastani inasemekana asilimia mbili point something lakini ukuaji wetu wa kilimo ni 0.4 growth, hakuna matching.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hili ni jambo ambalo hata inawezekana tukasema humu ndani ya Bunge lisifurahishe upande wa Serikali kauli zetu, lakini we have a duty to tell the truth. Pia ni muhimu kabisa Wizara ya Fedha ikakubali kwamba Sera za Kibajeti za Wizara ya Fedha si rafiki katika ku-accelerate uchumi wetu kukuwa katika nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, non-performing loans, sasa hivi zimefikia asilimia 12 na hii ni taarifa ya BOT, lakini taarifa ya BOT iliyoletwa na Treasurer Registry kwenye Kamati ya PIC inaonesha kwamba mapato ya BOT yanayotokana na Trading yameshuka kwa asilimia 63. It is not a rocket science, narudia, this is just a fundamental principal kwamba our Sera za kibajeti haziwezi ku-accelerate uchumi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nini ushauri wangu, jambo la kwanza ambalo namshauri Waziri wa Fedha anapoleta Mpango wake wa mwaka 2018/2019 aje na chapter inayozungumzia Tax Reforms ili tukubaliane humu ndani what is our direction. Number two, ni lazima ije chapter inayoelezea ni namna gani Agro Sector tunawekeza iweze ku-link na industrialization.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunazungumzia na tunapiga makofi jitihada zilizofanywa Serikali kwenye zao la korosho. Leo Mkoa wa Dodoma ni potential kwa ajili ya korosho. Leo Mkoa wa Tabora ni potential kwa ajili ya korosho. Swali la kujiuliza, nini mpango wa Serikali kwa ajili ya value addition kwenye mazao ya korosho. Tutajikuta tumezalisha korosho nchi mzima halafu tunategemea soko la nje la kwenda kuuza raw korosho. Tujiulize, Mwijage atengeneze clear structure ya kuonesha namna gani tunatoa incentive packages kwa viwanda vinavyobangua korosho nje vije ndani ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna ardhi, tuna raw material na naamini tuna cheap labour, what is our problem? It’s our physical measures this is our biggest problem. Nataka nijiulize swali kwa nini tuna-charge 30 percent corporate tax kwa mtu atakayewekeza kiwanda cha mazao ya kilimo? Why? Kwa nini tunaitaka thirty percent? Kwa nini tusimwambie corporate tax zero? Kwa sababu utapata in Direct Tax kutoka kwenye Pay as You Earn, VAT na Excise Duty ambazo watu wata-spend. Why we don’t see this. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Fedha alituambia kwenye Kamati ya Bajeti na wewe ulikuwepo, alisema hivi wakati anamsindikiza Mtendaji Mkuu nadhani wa World Bank or IMF. Alimwambia nchi yenu ina bahati kubwa mbili.

Moja ya bahati tuliyo nayo ni rasilimali za kutosha tulizo nazo katika nchi. Hizi rasilimali tusiposi -turn fursa hazina maana yoyote. Kwa hiyo ushauri wangu ni lazima mentality ya Serikalini iondoke kuwaza kodi, ianze kuwaza uzalishaji.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa. Awali ya yote nianze kwanza kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa namna ambavyo amekuwa akifanya shughuli zake ndani ya Bunge na nje ya Bunge na niwapongeze Mawaziri wanaomsaidia katika ofisi yake, Mheshimiwa Jenista Mhagama na niseme tu Mheshimiwa Jenista lile tatizo la maji Nzega kule mpaka leo mambo muswano. Kwa hiyo, nakushukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nimshukuru sana Mheshimiwa Antony Mavunde kwa kazi anazofanya na commitment anayoonesha na namna ambavyo amekuwa akijituma katika kufanya shuguli zake. (Makofi)

Mheshimiwa Mweiti, nianze kwa maneno yafuatayo. Ukitazama ngao yetu iliyoko mbele yetu pale ina maneno mawili, uhuru na umoja. Mwaka 1957 wazee wetu wakiwa pamoja na kijana wao wakati huo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere walipoanza harakati za kutafuta uhuru kupitia Chama cha TANU waliwaunganisha Watanzania wote kwa makabila yao, dini zao ili kupata umoja ambao utafikia dhamira ya wao kupata uhuru wa Tanganyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo mambo ambayo yanaendelea katika nchi yetu ambayo yanaashiria kuanza kuwepo kwa migawanyiko katika Taifa letu. Mambo haya tukiendelea kuyatazama kwa macho hayaleti taswira njema huko mbele na wala hayataweza kulifanya Taifa hili kuendelea kuwa Taifa moja na kupambana na adui mkubwa ambaye ni umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yanatokea matukio ya kusikitisha katika nchi yetu ambayo ukitazama huoni any concern ya deliberate effort ambayo itawajengea Watanzania imani kwamba, hata mimi mdogo nikikumbwa na zahma basi yupo anayenilinda. Yamekuwa yakitokea matukio mengi yakikosa majibu katika nchi yetu, lipo tukio la kijana anaitwa Allan ambaye ni muuza machungwa pale Mbeya. Mimi ningeiomba Serikali kwa heshima kabisa, matukio ya namna hii yakiendelea kujengeka katika nchi yetu na ku-develop culture ya impunity yana-destort peace iliyopo katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kijana huyu amekufa. Ripoti ya Daktari Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya imesema kwamba kijana huyu kafariki kwa majeraha ya ndani ya mwili wake. Familia yake imesema waliomuua, waliompiga ni Jeshi la Polisi. RPC wa Mbeya akasema hawahusiki! Matokeo yake nini, Serikali imeenda kutoa rambirambi ya shilingi 200,000. Is that the reason? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, matukio ya namna hii yameendelea kuwepo, mimi ningeiomba Wizara ya Mambo ya Ndani na Ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali wakati ina-wind up budget ya Waziri Mkuu waagize kuundwa kwa official independent organ ifanye investigation ya haya mambo. Hatuwezi kuacha this culture of impunity inaendelea katika nchi yetu, it is very sad na ina-destort image. Hii ndiyo inatumika na watu wasiopenda nchi yetu kuendelea kuharibu heshima ya Taifa letu. Hili ni jambo ambalo ninaiomba Serikali ichukue hatua katika jambo hili. Kwa hiyo, hili ni jambo la msingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirejee kwenye hotuba ya Waziri Mkuu, Waziri Mkuu katika hotuba yake ameelezea kukua kwa uchumi. Rais anafanya effort nyingi ku-encourage watu kujenga viwanda katika nchi yetu, kama hatutaamua deliberate kuwa na specialisation hatuwezi ku-specialise katika kila jambo, 70% ya nchi yetu iko katika sekta ya kilimo. Nitoe mfano, mwaka 2015/2016 uzalishaji wa zao la korosho na Serikali imesema kilimo kimekua kwa asilimia 3.6. Uzalishaji wa korosho ulikuwa tani 265,000 msimu huu tunazungumzia tani 313,000 inputs ambazo Serikali iliingiza, investiment ya Serikali ni shilingi bilioni 28 kwenye zao la korosho. Msimu uliopita mapato tuliyoyapata ni bilioni 872. Serikali ilivyoamua ku-invest 28 billion mapato ya korosho sasa hivi yatakwenda
1.18 trillion shillings. Waziri wa Fedha haoni hili? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, it is not a rocket science, narudia. Kilimo tulizungumzia NFRA, Wizara imeomba 86 billion shillings, inapewa 15 billion shillings. Mwaka huu tunazalisha metric tones 900,000 mahitaji yetu ni metric tones
5.9 hii excess inaenda wapi? Tutafunga mipaka ili tu-create artificial control ya inflation tuseme mfumuko wa bei asilimia nne, tunawatia umaskini wakulima. We have to be serious. Inputs kwa ajili ya pamba Wizara imeomba 10 billion Serikali imempa three billion. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo wale wadudu wanaokula mahindi wanaitwa viwavijeshi wameshaanza kushambulia baadhi ya maeneo. Kwa nini, kwa sababu, fedha zilizoombwa na Wizara ya Kilimo kwa ajili ya inputs hawajapata as per the requirements. What do we want? Tunataka nini? Siyo muujiza, tukijenga viwanda kama asilimia 70 ya Watanzania ni maskini, hawana uwezo wa kununua bidhaa za viwanda hivyo, viwanda hivi vitakufa tu na wala siyo muujiza. Nataka niiombe Serikali, nimesoma mpango wa Dkt. Mpango, nitakuja kuongea wakati wa bajeti, it is typical cosmetic measures. Hakuna serious fiscal measure zinazotengenezwa na Wizara ya Fedha kuweza ku-stimulate sekta ya kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunaagiza crude oil karibu tani 600,000. Nini mpango wetu wa kuwekea kwenye mazao ya alizeti, ili tuweze kujitosheleza mafuta? Kama hatutaamua, nitoe mfano wa mifugo. Kwenye hotuba ya Waziri Mkuu amezungumzia suala la chapa na mimi nimpongeze Ndugu yangu Mheshimiwa Ulega kwa mara ya kwanza kajua, zamani ng’ombe alikuwa anaita mnyama siku hizi anaita mifugo, kawajua na ng’ombe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili tuweze ku-improve mazao yanayotokana na mifugo ni lazima tuwekeze kwenye proper breeding programs. Ng’ombe wetu hawajafanyiwa breeding toka mwaka 1982, hakuna investments, leo mzalishaji wa maziwa anayezalisha maziwa, mfano mtu kama ASAS, cost of production ya ASAS ni asilimia 18 juu kuliko mzalishaji anayezalisha maziwa Kenya. Kwa nini? Ni kwa sababu ya mfumo wetu wa kodi. Nataka nijiulize Serikalini kwa nini mnahitaji VAT kwenye vifungashio vya maziwa? Why?

Mheshimiwa Mwenyekiti, zimeisha dakika? Naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naushukuru kwa kunipa fursa. Kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza ndugu yangu Mheshimiwa Jafo na Naibu Mawaziri wote wawili wa Wizara hii kwa kazi kubwa wanazofanya na kujituma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilitaka nianze kwa jambo moja; jamii yoyote inayohitaji maendeleo msingi mkubwa wa maendeleo ni haki na viongozi kujua kwamba wana wajibu wa kulinda uhai na mali za kila raia. Nasema hivi kwa sababu kumekuwa na hii culture ya impunity na matukio madogo madogo yanayoendelea, na mimi kwa mtazamo wangu naamini kwamba it is a high time Serikali ikaja hadharani na kuteka bold decision juu ya haya mambo ambayo yamekuwa yakiendelea katika jamii yetu; kwa sababu yanaharibu taswira na heshima na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nataka niongee kuhusu TAMISEMI. Ukitazama taarifa ya Waziri only 40 percent maximum of 50 percent ya Development Budget ndiyo imekwenda kwenye Halmashauri zetu. Hata hivyo katika Halmashauri zetu mapato yetu ya ndani yanaathirika sana pale ambapo Central Government inashindwa kushusha fedha kwa wakati katika Halmashauri, na kule ndiko ambako kuna burden kubwa iliyopo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kisera tumeamua kuwa na D by D, naomba nitumie takwimu hizi kuwaonesha Waheshimiwa Wabunge. Katika sekta ya elimu ukichukua ratio ya pato letu la taifa vis-a-vis kile ambacho tuna-allocate katika sekta; kati ya mwaka 2006 mpaka 2007/2008 ratio ilikuwa ni asilimia 20 ya pato letu la ndani ndiyo ilikuwa allocated kwenye sekta ya elimu. 2009 na 2010 ikawa asilimia 18. Imeendelea kushuka, mwaka 2017/2018 tumetenga only 15 percent ya pato letu la ndani kupeleka kwenye sekta ya elimu, sasa nini implication yake?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitazama matokeo ya kidato cha nne asilimia 60 ya wanafunzi wanaomaliza mtihani wa kidato cha nne wanafeli; na ni kwa nini? Kwa sababu kwa takwimu, na hizi ni takwimu za BEST, satisfaction ya walimu, job satisfaction only 30 percent ya walimu walioko katika shule zetu za msingi na sekondari ndio wako satisfied na kazi wanayoifanya, maana yeke tunaandaa janga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini fedha za elimu tunazozipeleka TAMISEMI, asilimia 96 ya fedha hizi zinatumika kwenye administrative only, haziendi kwenye development ya education, kwa maana ya kujenga infrastructure na kuangalia stahiki za watoa elimu, hili ni tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna umuhimu mkubwa sana Serikalini wa kufanya replanning, nini focus yetu? Tunataka kujenga uchumi wa viwanda. Ili tujenge uchumi wa viwanda ni mambo mawili tu, moja ni uwepo wa rasilimali kwa maana ya raw material, lakini uwepo wa rasilimali watu. Kama elimu yetu matokeo yake ni haya ni matatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwape mfano wa TARURA; mwaka jana tumetenga shilingi bilioni 246, mwaka huu tunatenga shilingi bilioni 272. Ukitazama mipango yetu ya maendeleo ni urban centric, yote inatazama Dar es Salaam, Mbeya, fedha zinaenda Jiji la Mwanza na vitu vya namna hiyo, lakini kule ambako kuna wazalishaji wa rasilimali, kwa maana ya wakulima, barabara zao tumeziweka chini ya TARURA, hatuzipi fedha ama tunachoki-allocate ni kidogo, tuna matatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kuhusu suala la TARURA; Waheshimiwa Wabunge wamesema tuangalie hela ya mafuta 30 percent kwa ratio ya 70 percent, ninaomba Wizara ya Fedha angalieni kutumia chanzo cha Gaming Board, chanzo hiki kiwe dedicated kisheria, kiende moja kwa moja kuongeza Mfuko wa TARURA. Pamoja na ratio mnayoitumia sasa hivi tumieni Gaming Board kuna fedha, watu wana-bet. Tumeamua kuruhusu watu wacheze kamari, basi tumle huyu nguruwe vizuri aliyenenepa ili matokeo ya kule yaje basi kwenye barabara, hili ni eneo lingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma hotuba ya Mheshimiwa Waziri ukurasa wa 52 anasema; ukuaji wa uchumi na maendeleo ya wananchi Tanzania unategemea kwa kiasi kikubwa sekta ya kilimo. Sekta hii ni mhimili wa uchumi wa viwanda na kuchangia kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati. Ili tuweze kufikia lengo hili ni lazima tuwekeze kwenye sekta ya kilimo, tutoe fedha za pembejeo, tujenge barabara za kutoa mazao kwa wakulima vijijini kuleta kwenye barabara kubwa zilizojengwa na TANROADS, bila kufanya hivi hatuwezi kutatua hili tatizo la kuondoa umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka niiombe Serikali. Leo kule kwenye Halmashauri, na mimi nasema hii kwa nia njema, kule kwenye Halmashauri Serikali kwa maana ya Rais amekuja na vision kubwa kupambana na rushwa, kujenga miundombinu, kuhakikisha kwamba wananchi masikini wanapata haki, lakini ukitazama kinachoendelea katika Halmashauri zetu, ni kero kubwa kwa wafanyabiashara wadogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mkulima kabeba mpunga wake kutoka Katavi kwenye gari la tani 10 kaamua kufunga yale magunia kilo mia-mia badala ya kilo 90, lakini uzito ni tani 10, akifika njiani anapigwa faini. Msafirishaji wa ng’ombe kutoka Nzega kuleta Dar es Salaam, amekatiwa ushuru, ana leseni, ana kila kitu, akifika njiani kasimamishwa kapigwa fine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaongoza Halmashauri na nchi kwa faini, hatuwezi kuwasaidia hawa watu maskini. Ningemuomba Mheshimiwa Waziri Jafo wakati anakuja kufanya winding up hapa atuambie definition, kuna mgogoro mkubwa unaendelea kwenye Local Government. Tulipitisha hapa Waziri wa Fedha alileta Mabadiliko ya Sheria ya Fedha mwaka jana, wenye hoteli ambao wanalipa VAT je, wanatakiwa walipe service levy? Je, wanatakiwa walipe hotel levy?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu sasa hivi kinachoendelea analipa VAT, anapelekewa service levy anapelekewa hotel levy, asipolipa anafungiwa. This is a very bad thing, na mimi nataka niseme Waheshimiwa Wabunge wa chama change, kwamba tunaweza tukajenga standard gauge, tunaweza tukanunua ndege, tunaweza tukajenga barabara, kama kero zinazohusu maisha ya watu ya kila siku hatutakuwa wakali kuitaka Serikali ichukue hatua mapema, sisi ndio tutakaoenda kunyooshewa vidole. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kule kwenye Halmashauri kila mtu ni mbabe. Mtu ana kabisahara ka-shilingi 500,000 anapigwa fine ya shilingi 2,000,000, It is very unfair. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni jambo ambalo nakuomba kabisa ndugu yangu Mheshimiwa Waziri Jafo toka strong statement. Hii tabia ya Wakurugenzi wetu kwenda kufungia watu makufuli, kwenda na polisi kuburuza, unaletewa sasa hivi demand note, in a next one hour umepigiwa kufuli. Demand note inasema nini, hujalipa service levy… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa. Jambo la kwanza nitumie fursa hii kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Nzega kuishukuru Serikali kwa dhati kabisa kwa support ambayo imetupa katika improvement ya Kituo cha Afya cha Zogolo, lakini vilevile mpango uliopo kwa ajili ya vituo vya afya vya Mbogwe na Migua. Pia nimshukuru Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri, na nikushukuru kwa dhati kabisa Mheshimiwa Ummy kwa kazi kubwa unayoifanya kuhakikisha kwamba akina mama wanajifungua wakiwa salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nilitaka nishauri mambo mawili madogo. Improvement tunayoifanya katika referral hospital, kwa mfano kama Muhimbili Serikali imafanya kazi kubwa sana ya ku-improve hospitali yetu ya Muhimbili na dhamira ya Wizara kuhakikisha kwamba akina mama wanajifungua salama nilitaka niiombe Serikali Wizara ya TAMISEMI, Wizara ya Afya na Wizara ya Mzee Mkuchika kutumia takwimu za TASAF, zile kaya maskini, ili tuweze ku- establish akina mama wanaotoka katika kaya maskini kabisa kuona au kuja na mpango wa namna gani wanaweza kupata zile delivery kits ili wasiweze kukumbana na lile zoezi la kuwa wanalipa shilingi 20,000 ama kwenda kununua kwa sababu kuna kaya ambazo ni maskini na kwa takwimu zetu kuna asilimia kama 28 mpaka 30 ya Watanzania ambao wako katika umasikini wa hali ya juu.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili ambalo nilitaka niiombe Wizara, MSD tunatenga fedha za dawa nyingi lakini bado kuna tatizo la out of stock. Nikitolea mfano katika Wiaya ya Nzega na Mheshimiwa Waziri wewe mwenyewe uliliona katika ziara yako hivi juzi tulivyokwenda wote, mtu ana
bima, anafika katika dirisha anakosa dawa, ina-discourage watu kujiunga katika National Health Insurance. Mfano, jambo la pili ambalo ni la kusikitisha, tunaamini MSD wako katika mfumo ambao unawafanya waombaji wa dawa kuweza kupata feedback haraka ya kujua kwamba dawa hakuna lakini kupata ile barua ya kuwaruhusu kwamba we are out of stock, hatuna dawa kwenda kununua dawa katika vendors ambao mmewaruhusu inachukua ages.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi leo hapa mkononi nina barua iliyoandikwa na Daktari wa Hospitali ya Wilaya Nzega tarehe 27 Februari, aliomba idadi ya dawa tofauti 100. Kati ya hizo 100 akakosa 48, ile barua ya kumruhusu ili aende kwa vendors ili aweze kwenda kununua hizo dawa 48 tofauti mpaka leo hawajapata. Matokeo yake inaonekana kwamba fedha tunazotenga, wananchi wanaokwenda kupata dawa katika viuto vyetu vya afya ama hospitali zetu wanakuwa hawapati dawa kwa sababu ya inefficiency ya taasisi zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo mimi nilitaka niiombe Serikali, tunatenga fedha kama Bunge na zile dawa muhimu ukiangalia bajeti ya mwaka jn ni almost asilimia 100 hazina wametoa fedha zake lakini zile dawa kuzipata kwa wakati katika vituo vya afya ni changamoto. Mimi niwa- challenge Serikali, tafuteni solution ya MSD na delivery system katika vituo vyetu vya afya kuhakikisha kwamba kinachoombwa kinapatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi teknolojia imekua mtua anaweza akaomba kutokea ofisini kwake akajua stock iliyopo na ambayo haipo, system ikamruhusu kwenda kuomba katika vendors waliopo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, otherwise mimi nitumie nafasi hii kuwashukuru sana na naunga mkono hoja, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa kwanza nianze kwa kusema kwamba naunga mkono hoja. Lakini nina mambo machache ya kushauri.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza nilitaka nimuombe Mheshimiwa Waziri mwaka 2017 Septemba walitupatia fedha kwa ajili kufanya usanifu wa kilometa 149 barabara ya kutoka Tabora - Mambali - Bukene - Itobo kwenda Kahama. Lakini safari hii na mradi huu unaisha Desemba, 2018 huu nikuombe Mheshimiwa Waziri kwenye financial hiyo inayokuja kwa kuwa mtakuwa mmesha jua gharama mtutengee bajeti kwa ajili ya ujenzi ya ile barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ambalo nataka niombe rehabilitation mmetenga fedha kwa ajili ya Mambali - Tabora na mmetenga fedha tena Mambali - Bukene hamjatenga fedha Itobo - Nzega kilometa 25 ninakuomba Mheshimiwa Waziri muiangalie hii kwa jicho la huruma sana ni muhimu sana msipofanya rehabilitation ile barabara itakatika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo jingine ambalo nataka niseme Mheshimiwa Waziri sekta ya ujenzi inachangia almost asilimia kumi ya pato la Taifa la nchi yetu, na focus ya Serikali ni kufungua miundombinu. Nataka nikuombe Mheshimiwa Waziri leta mabadiliko ya sheria ya TANROADS ili tu-establish kitu kinaitwa preferential treatment kwa local contractors miradi mnayotenga fedha kwa ajili ya aidha, tumekopa ama fedha zetu za ndani angalau local contractors wapewe preference ili ile fedha iweze kubaki ndani ya uchumi wetu kwa kiwango kikubwa. Kwa sheria iliyoko sasa hivi inatoa preference only kama ni fedha za ndani, lakini hata fedha mnazokopa ni fedha za ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nilitaka niongee ni ukisoma hotuba ya Waziri ukurasa wa 170 mimi naunga mkono ujenzi wa standard gauge. Lakini Mheshimiwa Waziri ninachosikitika ni mabadiliko ya mwelekeo, ahadi yetu ya uchaguzi ilikuwa ni kujenga reli kutoka Dar es Salam na naomba ninukuu kidogo tu au kwa sababu ya muda niache ni kutoka Dar es Salaam kwenda Tabora, kwenda Mwanza; kutoka Tabora kwenda Kigoma, kutoka Uvinza kwenda Msongati; kutoka Kaliua kwenda Mpanda Kalemii. Kwenye kitabu chako cha bajeti mwaka huu tunakupitishia one point five trillion unatenga one point four kwa ajili ya phase one na two shilingi bilioni 100 unatenga kwa ajili ya kwenda Isaka kinachonishangaza hii decision basis ni nini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa taarifa ya uchumi ya mwaka 2015/2016 mizigo kwenye bandari ilikuwa tani milioni tano asilimia 34 ni Zambia, asilimia 34 ni DRC, asilimia 12 ni Rwanda, asilimia sita ni Burundi our cash cow ni ku-save Eastern and Western Congo na Burundi kwa nini mnataka kumfanya Mnyarwanda kuwa hub wa Afrika Mashariki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Northen route inajengwa kwenda Rwanda na sisi tunampeleka line ya Isaka kwenda Kigali, kitakachotokea ataunganisha kwenda Msongati yeye ataihudumia Congo, ataihudumia Burundi na mkumbuke tuna East African Protocols ambazo zitamfanya yeye achague kutumia route anayotaka niwaombe kwa heshima tujenge reli yetu kutoka Makutupora Tabora, Tabora - Isaka, Isaka - Mwanza, Tabora - Kigoma, Uvinza - Msongati Kaliwa kwenda Kalemii, baada ya hapo tujenge kipande cha Isaka kwenda Rwanda tutakuwa tuna age over the others. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho tunajenga na reli bottom laini yake ni mzigo. Nataka nikuombe Mheshimwa Waziri tuanze preparation sisi bandari yetu ki-location na masoko tunayoyahudumiwa tuna-complete na Durban na Beira, nataka niwaombe naombeni mkaritafakari hili Mheshimiwa Waziri tuanzisheni, sasa hivi kwa regulation zetu za TRA mafuta ya transit yanakaa kwa siku 30, ni ya kwanza….

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nitumie nafasi hii kwanza kusema mambo machache; mwaka 2016 wakati tunachangia bajeti ya kwanza ya Wizara ya Viwanda na Biashara nakumbuka nilimwambia kaka yangu Mheshimiwa Mwijage kwamba nasubiri nione muujiza na nilitaja miujiza ambayo nilikuwa naisubiri na leo haijatokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, muujiza wa kwanza niliokuwa nausubiri ni kuona namna gani Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji inaweza kuunganisha mambo matatu ambayo Waziri amekabidhiwa. Mheshimiwa Rais alivyokuja na vision ya ku-revive industrialization aliamua kwa makusudi kuunganisha biashara, uwekezaji na viwanda ili kuweza kufikia lengo la industrialization.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka leo bado tunazungumzia General Tyre, mpaka leo tunazungumzia Liganga na Mchuchuma, mpaka leo tunaongelea matatizo ya msingi ya biashara na huoni yakijadiliwa katika hotuba za Waziri na hata kwenye mpango wetu wa mwaka mmoja, miwili na huu ni wa tatu. Tusome ukurasa wa 138 wa hotuba ya Waziri. Waziri ametaja vipaumbele na malengo ya mwaka 2018/2019. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri ametaja vipaumbele kushirikiana na taasisi kutunisha mtaji wa NEDP, kuendeleza miradi ya kieleleza ya Mchuchuma na Liganga, Engaruka Kiwanda cha Matairi, utekelezaji wa eneo la TAMCO, mradi wa kuunganisha matrekta, uendelezaji wa maeneo ya viwanda ya SIDO. This is a hundred percent kwa miaka mitatu tunajadili the hardware part of business, hatujadili the software part of the business. Ili tuweze kuona matatizo tuliyonayo kwenye software part of the business naomba nitaje haya mambo. The software part of business ni regulations na sheria na mfumo wetu wa kodi, huu ndiyo utachochea haya mambo mengine yote kutokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania katika kufanya biashara according to the World Bank Report ni ya 137 kati ya nchi 190 katika mazingira ya kufanyia biashara, Tanzania ili uanzishe biashara ni nchi ya 162 kati ya nchi 190; Tanzania ni ya 150 kwa ajili ya kutoa vibali vya kufanyia biashara. Kama kweli tunataka ku-break through ni lazima Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Fedha wakae kwa pamoja kwa ajili ya kutengeneza the softaware part ya kufanya biashara katika nchi, tusipofanya namna hii tutakuja hapa tutaimba kila siku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikupe mfano wa leather sector; na ndugu yangu Mheshimiwa Mgumba, ameongelea Kiwanda cha Ngozi cha Morogoro. Kwa takwimu kwa mwaka sisi tunazalisha vipande milioni tatu vya ngozi katika nchi. Sasa ili kiwanda chetu cha ngozi kiweze kuzalisha, na nimeona kwenye mpango tunatenga 10 billion kwa ajili ya kuandaa eneo la viwanda vya ngozi, tuna viwanda saba ama vinane havifanyi kazi, halafu tunataka kutenga bilioni kumi nyingine kwa ajili ya kuandaa eneo la viwanda hapa nchini, this is wastage of resources. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikupe mfano, katika uzalishaji wa leather sector tuna-process ngozi kutoka katika hatua ya raw material kwenda kwenye wet blue, kutoka wet blue kwenda kwenye crust na kutoka kwenye crust kwenda kwenye finished, hizi ni levels tatu. Level ya kwanza investment inayohitajika kwa kiwanda cha kati ni 15 million US dollars; kutoa kwenye wet blue kwenda kwenye second level ambayo ni crust unahitaji five million dollars; kutoka kwenye crust kwenye level ya finished unahitaji another five million dollars, this is 25 million dollars. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini angalia kodi za mzigo. Ukizalisha wet blue ili ui-export kwenda nje unalipa ten percent export levy, unalipa wharfage dola 40, unalipa MoFED dola 100 halafu uki-import chemicals unalipa dola 190 kwa ajili ya import duty, lakini bado utalipa 18 percent VAT. Huyu mtu atahitaji apate chemical permit, alipe dola 667, atalipa railway development levy ya 1.5, atalipa, wanaita corridor levy ya 4.9 dollars; lakini bado ana Government taxes, kuna workers’ compensation, kuna municipal levy, kuna tax, kuna Government chemistry fee, kuna OSHA, NEMC, other crises.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hebu compare leather sector na nchi zilizotuzunguka; hakuna export duty ya 10 percent ya wet blue ukienda Kenya na Uganda. Halafu ngozi zetu zinazozalishwa ndani ya nchi huyu mwenye kiwanda hawezi ku-process kwa sababu atakapozalisha kwenda kuuza nje, the cost of processing wet blue square feet moja ni dola 30, na soko la dunia ni dola 30 anauza wapi? Hata tujenge viwanda milioni we cannot. Ni lazima Serikali itambue kwamba number one principle ya biashara ni kutengeneza mazingira condusive ya watu wetu waweze kuzalisha at a competitive rate. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe mfano mwingine, nchi ambayo ilifungua soko lake pamoja na sisi ni Vietnam na Waziri ameshawahi kwenda mwaka 1986. Na Waheshimiwa Wabunge tuelewe, viwanda ni vya aina tatu; tunazungumzia manufacturing, processing and assembling, hivi ndivyo viwanda tunavyovizungumzia. Manufacturing and processing kuna technological advancement kila siku, leo tunazungumzia textile industry, je, tuna raw material ya kutosha kulisha viwanda vyetu tulivyonavyo? Je, tumeweka mpango gani wa ku-invest katika uzalishaji wa raw material? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tunazungumzia mafuta, nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge, kwa mwaka tunatumia dola milioni 240 ku-import mafuta ya kula katika nchi yetu. Lakini tunahitaji shilingi ngapi kuondoa hili tatizo? Mpango uliopo kwenye African Development Bank wa African Edible Oil ili sisi tuondokane na importation ya mafuta ya kula katika nchi we only need 45 million US dollars ili tuweze kulima michikichi ambayo tutazalisha mafuta, tutaondokana na tatizo la ku-import mafuta, where is the plan? Hakuna! Hela ipo kwenye ADB, ni accessible.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jamani, Dkt. Magufuli ataimba, ndiyo maana kila siku anabadilisha sheria huko State House, because the old man is frustrated. Anaongea hivi it seems like yeye yuko mbingu ya saba wengine tuko kwenye ardhi, what is the problem? Wizara ya Viwanda na
Biashara what is the problem? Wizara ya Fedha what is the problem? Wizara ya Kilimo what is the problem? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemsikia hapa ndugu yangu Mheshimiwa Ulega anazungumzia exportation ya nyama. 70 percent ya ngozi tunayoizalisha katika nchi yetu ni grades four, five, six and seven, hatuna ngozi ya grades one, two wala three katika nchi yetu. Why? Because hatujafanya proper breeding ya mifugo. Hakuna mpango, Wizara ya Mifugo ukisoma huu mpango wa mwaka mmoja Waheshimiwa Wabunge Serikali inapanga eti kutafuta madume kumi ya kupanda ng’ombe, hivi mnajua madume kumi ni shilingi ngapi, ni 20 million shillings, this is the plan, it is here, iko humu kwenye mpango. There is no seriousness. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mimi nataka niseme mambo machache sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nataka niwaombe Waheshimiwa Wabunge, bajeti hii tutumie Kanuni ya 69 tuirudishe ili Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha zikakae kuweza kuja na bajeti ambayo inagusa maisha ya watu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitumie takwimu hizi. Tumeandaa bajeti ya shilingi trilioni 32, shilingi trilioni 12 ni fedha za maendeleo. Sekta ya kilimo inachangia almost 30% ya GDP ya nchi yetu, development budget ya sekta ya kilimo ni shilingi bilioni 94 ambayo ni sawasawa na almost 0.8 ya total budget ya maendeleo, kweli? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta inayochangia almost 30% ndiyo inatengewa chini ya asiliamia moja ya bajeti nzima ya maendeleo. Sekta ambayo inaajiri kati ya asilimia 60 mpaka 70 ya Watanzania ndiyo inatengewa chini ya asilimia moja ya bajeti ya maendeleo. Sekta ambayo ina-supply asilimia 70 ya viwanda vyetu inatengewa chini ya asilimia moja ya bajeti ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine la kusikitisha sekta hii imeendelea kuonewa katika nchi hii kwa muda mrefu na siyo sahihi. Sisi Wabunge, hasa wa Chama cha Mapinduzi, tuna wajibu wa kumlinda mkulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shinyanga, Tabora, Kigoma, Mwanza, Simiyu, Katavi, Mara, Rukwa na Ruvuma, huku kuna mkulima na mfugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mikoa hii ndiyo inayolima mahindi, pamba, ndiyo yenye ng’ombe na samaki, halafu ndiyo watu tunaowatesa, it is unfair. Nadhani ni vizuri sisi viongozi wa nchi hii tukatambua hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Uislam Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu kuwa Khalifa, kuwa kiongozi wa viumbe vingine. Mwenyezi Mungu kampa mwanadamu utu na akili ili aweze kuwatendea wema wengine, leo nyavu zinachomwa, leo mifugo ya nchi hii wafugaji wamekuwa wakimbizi, leo wakulima wa nchi hii wanaonewa, tunam-sacrifice huyo bwana aliyekaa hapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikupe mfano mdogo, ili mkulima aweze kulima mahindi heka moja anahitaji input zifuatazo; trekta kulima mara mbili anatumia shilingi 90,000; harrow atatumia shilingi 35,000; kupanda atatumia shilingi 30,000; kupalilia atatumia shilingi 60,000 in total; ili aweze kupanda mahindi anahitaji mfuko wa jumla ya kilo nane ambayo atatumia shilingi 45,000; bado ataweka mbolea ya kupanda na kukuzia, in total anatumia shilingi 550,000. Leo mahindi ni shilingi 150 kwa kilo. Cost per unit ya production yake ni shilingi 500, are we realistic? Turudisheni hii bajeti. This is not healthy for our country. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Tizeba hana problem kaomba 60 billion shillings kwa ajili ya inputs ya tumbaku. Tumbaku mwaka jana tumeteseka wananchi wa Mkoa wa Tabora. Leo tumeletewa pamba mtu anaitwa galagaja, galagaja kule usukumani ni middle man, huu ushirika ulioletwa kwenye pamba hauna mtaji. Ziara ya kwanza ya kiongozi wa ushirika, mmoja alienda Kishapu anauliza eti inakuwaje wafanyakzi wa SHIRECU hawalipwi mshahara, ninyi SHIRECU mna shamba? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri turudishe bajeti hii na mambo yafuatayo yafanyike. NFRA apewe fedha aliyoomba. Suala la pili, kusiweko na condition kusafirisha… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa fursa na nianze kwa maneno yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kabla sijaingia Bungeni kwanza nilipewa kadi ya Chama cha Mapinduzi mwaka 1995, kwa hiyo, mimi ni CCM kwanza kabla ya Ubunge. I am putting this on record. Katiba ya Chama changu sehemu ya kwanza kwenye madhumuni ya kuanzishwa Chama cha Mapinduzi, dhumuni namba saba linasema: “Kusimamia haki na maendeleo ya wakulima, wafanyakazi na wananchi wengine wenye shughuli halali za kujitegemea na hasa kuona kwamba kila mtu ana haki ya kupata malipo yanayostahili kutokana na kazi yake.” (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimesoma dhumuni hili kwa makusudi kabisa ili Serikalini wajiulize swali, je, wanatimiza wajibu wa wanachama wa CCM zaidi ya milioni sita/saba/ nane ambao walikaa kwenye foleni na kuomba kura za nchi hii ili kuweka Serikali madarakani? (Makofi)

Ninarudia, mahusiano yaliyopo kati ya Serikali na wananchi ni mahusiano kati ya principal and agent. Mkataba uliopo kati ya Watanzania na sisi, ni CCM na wananchi na siyo Serikali na wananchi. Chama kimepigiwa kura, tumemnadi Mheshimiwa Rais Magufuli tukampa dhamana ya kuunda Serikali, akasimamie na Serikali yake maslahi ya wananchi wa nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niulize maswali yafuatayo; juzi tumepitisha bajeti na kwa masikitiko makubwa sana tutapisha na hii, ndiyo kawaida yetu. Jana tumepitisha bajeti ya kilimo; kilimo kinachangia asilimia 30 ya GDP ya nchi hii, kilitengewa 0.8% ya bajeti ya maendeleo. mifugo na uvuvi inachangia 7% tumewatengea 0.04% ya bajeti ya maendeleo. Halafu tunakuja hapa tunasema kuna kuharibu mazingira, this is nonsense. Hamna lugha nyingine ya kutumia zaidi ya hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba unisikilize kabisa, leo hii tumezuia wavuvi wasivue, haturuhusu wavuvi wavue kwa kutumia makokoro, sawa, what is the option? Tumetenga shilingi ngapi ya kwenda kuwafundisha wavuvi wetu ili waanze uvuvi wa kufuga wenyewe walioko kando kando ya Ziwa Victoria? Tumewaandaje? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka nikwambie jambo la kusikitisha, mkulima mahindi yake leo shilingi 150 kwa kilo. Na mimi nakushuru sana, umetoa maelekezo kwamba Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha ije kwenye Kamati ya Bajeti. Tumeanza nao vikao, na mimi nakuahidi, tusipoelewana tutarudi humu ndani. Hatuwezi kuendelea na business as usual. Haiwezekani Serikali inashindwa kutimiza wajibu wake, tunaenda kuwaadhibu wananchi. We cannot allow this! Sekta ya mifugo bajeti ya mwaka 2017 development budget tumepeleka asilimia ngapi? Zero! Sifuri. Bajeti ya kilimo tumepeleka asilimia ngapi? Asilimia 18.

T A A R I F A . . .

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, namheshimu na nimefunga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka kushauri mambo yafuatayo: Kwanza, nikizungumzia Sekta ya Mifugo. Ninaongea kuhusu Sekta ya Mifugo kwa mambo makubwa mawili. Moja, nimezaliwa ndani ya mifugo ndiyo sababu naifahamu. Toka mwaka 1983 hakuna proper breeding programme iliyofanywa na Serikali ya nchi yetu. Hakuna!

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Mwalimu Nyerere iliandaa sehemu zinazoitwa holding ground kwa ajili ya breeding programme. Kwangu Nzega na Jimbo la Selemani Zedi, kulikuwa na eneo linaitwa Kisasiga. Kule kwetu tuna ng’ombe zinazoitwa Tarime, Waziri anazijua. Ni ng’ombe ndogo, ngozi yake ni nyembamba, lakini zinaweza ku-survive kwenye ukame. Mwalimu akasema ili nimwongezee value huyu Msukuma, akaleta ng’ombe aina ya borani, akaziweka Kisasiga. Mwaka 1990 ziliuzwa kubinafisisha zote hadi ardhi. Pale pamebaki open, hakuna chochote. Mkoa wa Tabora kuanzia Nzega kwenda Tabora Kaskazini kwenda Urambo, kwenda Sikonge, kwenda Wilaya zote zaidi ya asilimia 60 ni hifadhi. Hawa wafugaji wanaenda wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, unajua jambo linalonisikitisha, nami nataka nirudie humu ndani, Serikalini hatuna nia mbaya na Mawaziri, hapa kuna politics ya ajabu sana, mimi sio mwenyeji ndani ya Bunge, nina miaka miwili tu. Mbunge akisimama akiongea, atakuwa branded a name aidha, anamchukia Mheshimiwa Dkt. Magufuli. Simchukii Mheshimiwa Dkt. Magufuli, I have voted for him, I have campaigned for him for sixty days. Na mimi kama Rais Magufuli asingekuwa mgombea wangu mwaka 2020, I didn’t care. Nisinge-care kusema haya ninayosema ndani ya Bunge kila wakati, but because I know he is my candidate, nitasema as far as nimo ndani ya Bunge hili. Nataka niwaombe hii bajeti turudishe. Bajeti hii irudi na siyo kwa nia mbaya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo wafugaji wanauawa, nataka nikupe kichekesho. Kule Nzega wanakata leseni ya kufanya biashara. Namshukuru Mheshimiwa Waziri, ukimsumbua anakusaidia. Anakata leseni ya kusafirisha ng’ombe, inaitwa kabisa leseni ya kusafirisha ng’ombe nje Mkoa wako, analipa na mapato na kila kitu, akifika hapo Nala anakamatwa. Anakamatwa mama aliyebeba kuku 200 anazipeleka Dar es Salaam, anaambiwa alipe faini ya two million. What is this? Nchi yetu leo mkulima ananyanyasika, mfugaji ananyanyasika, mvuvi ananyanyasika, machinga ananyanyasika na mfanyabiashara ananyanyasika. This is unfair and we should not allow it.

Mheshimiwa Spika, nakushauri unda Tume ya Bunge, mimi sio mtalaam wa Kanuni. Jambo la kusikitisha, nataka nikwambie jambo, Mheshimiwa Nape aliandaa Hoja Binafsi inayohusu wafugaji. Hizi Kanuni za ajabu tuzibadilishe kwa maslahi ya nchi yetu na chama chetu. Tukaitwa kwenye Kamati yetu ya Uongozi ya chama chetu. Nataka nikwambie, hata kama tukifuata kanuni na taratibu zote, hoja zinazohusu wananchi zinaenda kufia kwenye Kamati za Vyama. Why are we here? (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka niseme, kama tumeamua kuwa na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ambapo vyama hivi vinatuleta ndani ya Bunge, tuna mihimili mitatu, kila mhimili utimize wajibu wake kwa maslahi ya Taifa hili.

Mheshimiwa Spika, nataka nimwambie ndugu yangu Mpina, hapa mkononi nina document nitamkabidhi. Leather sector tunaye mwekezaji amekuja ana kiwanda kikubwa sana Ethiopia. Tunasema industrialization, kama hatu-invest kwenye sekta ya kilimo na mifugo, let us forget about industrialization. Wizara ya Fedha inazungumzia 3.9% ya inflation. Mnajua bei ya bati ni shilingi ngapi? Ni shilingi 30,000, ng’ombe shilingi 150,000, mahindi shilingi 150, halafu tunasema tuna-control inflation kwa kuwatia umaskini watu.
We should not allow this. Sekta ya leather…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hatutaanzisha Price Stabilisation Fund, hatuwezi kupiga hatua kama Taifa. Kwa sababu wakulima ambao ndiyo asilimia 70 tunatarajia auze mahindi yake Nzega akanunue bati. Leo mahindi ni Sh.18,000, Sh.20,000, bati bandari moja imeongezeka kwa kipindi cha miaka mitatu almost mara mbili. Kwa taarifa mazao ya kilimo yanashuka bei kwa zaidi ya 20%; ni taarifa za NBS na za Wizara ya Fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitolee mfano zao la korosho, hatuna uwezo wa ku-control bei ya soko dunia sisi, lakini sisi tuna uwezo wa ku-control volumes. Ili tu-control volumes ni lazima tuwape incentives wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mfuko wa mahindi wa kilo mbili ni Sh.12,000, nataka niwape hizi takwimu. Mkulima ninayemuongelea ni huyu anayetumia mbegu ya hybrid ambayo kwenye heka moja atapata magunia 20 ambayo yatampatia kilo 2,000. Sasa ili alime heka moja atatumia tractor kwa Sh.45,000, tuandike, atafanya harrow kwa Sh.40,000, atatumia mbolea ya kupandia kwa Sh.65,000, atapalilia kwa Sh.25,000 mara mbili Sh.50,000, atatumia mbolea ya kukuzia kwa Sh.70,000, atanunua mbegu ya hybrid kilo moja Sh.6,000 kwenye heka moja atatumia mifuko nane ambayo ni Sh.48,000. Mkulima huyu ataweka ulinzi, atavuna, atapakia, ataweka dawa, ukichukua gharama yake ni karibu Sh.650,000. Gawa kwa huyo amepata at the optimal, best production, tani mbili ni Sh.325, bei leo kilo moja Sh.150. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima, tuchukulie zao la korosho, tumbaku sisi imeanguka leo ni mwaka wa pili wa tatu. Nataka nitoe ushauri na ni ushauri tu, it is pure administrative. Leo Mheshimiwa Rais kachukua hatua kasema korosho inunuliwe kwa Sh.3,000, ushauri wangu kwa heshima Mheshimiwa Dkt. Mpango wafanyabisahara wamesema watanunua kwa Sh.2,700 waagizeni nunueni kwa Sh.3,000 sisi kama Serikali tuta-subsidise hiyo Sh.300 mnayopata hasara ili mkulima asipate hasara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuwezi kutoka, this is the practise all over the world. Lazima tutengeneze a buffer plan kwa wakulima wetu. Tusipofanya namna hii madhara wanayoyapata wakulima kitakachotokea demand na purchasing power ya wakulima itashuka, ndio asilimia 60.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe unatoka Dodoma. Zao la zabibu, mimi nitampa Kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mpango World Economic Forum wamefanya Competitive Index Report ya dunia wametu-rank sisi 100. Hii siyo World Bank Report ambayo imetu-rank 140 ambayo tumeporomoka kwa digit 4. Hawa watu wa World Economic Forum wamefanya survey kwa ma-CEO wa Kitanzania. Ma-CEO wa Kitanzania na wafanyabiashara wa Kitanzania wametaja mambo matano ambayo ni matatizo katika nchi yetu kwa ajili ya kufanya biashara. La kwanza wamesema access to financing, la pili right to own properties, la tatu tax rate, la nne tax regulation.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nachoshangaa ni jambo moja, Serikali imechukua hatua nzuri ya kutengeneza document ya blue print, nachojiuliza kwa nini wasilete sheria na kwenye document ya mpango kungekuwa na chapter inayoongelea tax reforms tutakazozifanya kutokana na document ya blue print. Nilitarajia nione hili kwamba tutafanya mabadiliko ya kodi na regulations katika mwaka huu wa 2019/2020 katika maeneo haya baada ya kuandaa document ya blue print, hakuna. Kinachotokea ni nini? Nashindwa kuelewa kwa nini tunaandaa kwa haraka Muswada wa Vyama vya Siasa? Kwa nini tusilete Sheria za Kodi ambazo ni bottleneck to the economy, kwa nini? What is our priority? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi namuonea huruma sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha na nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge, mimi naona kuna tatizo sana Serikalini Mheshimiwa Waziri Mkuu. It is either Mawaziri na wataalam wameamua kutokufikiri ama wameamua kutegeana, hakuna kitu kingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachojiuliza tumbaku inaporomoka, the biggest market ya tumbaku sasa hivi ingekuwa Middle East, what are we doing as a country? Far East, what are we doing as a country? Yaani husikii, tunaambiwa tu tupunguze production, tumbaku imekuwa shida. Leo korosho tunaenda kwenye crisis. Nataka nishauri, sisi hatuna control na bei za dunia, tuna control na volumes za ndani na ili tuweze ku-expand volume lazima tujenge incentives. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namalizia tu. Naomba Wizara ya Fedha njooni na chapter kwenye mpango wa Februari wa namna gani mnaokoa kilimo katika nchi hii kwa kuanzisha price stabilisation, namna gani mnafanya tax reforms ili biashara ziweze kufanyika katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa. Awali ya yote, nitumie nafasi hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu. La pili nitumie kwa dhati kabisa kumshukuru na kumpongeza Waziri wa TAMISEMI na Naibu wake kwa kazi ambazo wamekuwa wakifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda mimi nianzie alipoishia Mheshimiwa Mabula. Nadhani umewadia wakati kama Bunge na kama nchi tutazame mfumo wetu wa bajeti na budget process kwa sababu kwa uzoefu huu mdogo nilionao ambao tumekaa humu ndani, kila mwaka tunakuja tunalaumu kutokufikia malengo. Nadhani umewadia wakati wa ku-reflect na kuangalia, je, mfumo wetu wa kujadili na kupanga bajeti kama nchi unatatua matatizo tunayoyataka?

Mheshimiwa Mwenyekiti, umefika wakati wa kukaa muda mwingi kuangalia revenue side kuliko expenditure side yaani tutumie muda mwingi kuangalia ni namna gani Serikali itapata mapato ili yaweze kwenda kutatua changamoto ambazo zinatukabili. Tusipofanya namna hii tutakuja kila siku hapa kuinyooshea kidole Serikali. Sisi wenyewe ndiyo tunapitisha hiyo bajeti ambayo kila mwaka tunaiona kwamba haifikii malengo lakini hatu-provide solution katika matatizo ambayo tunakabiliana nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nadhani umewadia wakati wa kuisaidia Serikali sisi kama Bunge na tuangalie kanuni zetu na sheria, je, mfumo wetu wa kujadili bajeti unajibu mahitaji yetu? Hili ni jambo la kwanza ambalo nilitaka niseme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili nataka niongelee kidogo kuhusu TAMISEMI. Responsibility zilizoko katika Wizara ya TAMISEMI ni kubwa sana. Mahitaji yaliyoko TAMISEMI ni makubwa sana. Mfano pale kwetu Nzega tumejenga Kituo cha Afya cha Zogoro, Serikali ilitupatia fedha kama 500 million shillings, tumejenga nyumba za watumishi tano, tumejenga instruction zilizoletwa theatre, OPD, wodi ya akina mama, theatre ya akina mama kujifungulia na nyumba za wafanyakazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto inayotukabili leo ni vifaatiba. Wakati tuna majengo yaliyokamilika, vifaa tba hatuna. Naiomba Serikali na Mheshimiwa Waziri alifika pale akaiona, Naibu waziri alifika akaiona washughulikie suala hili. Mimi niwapongeze sana kwa maamuzi ya kutumia force account katika kujenga miundombinu katika kata zetu za vijiji vyetu, imeleta matokeo mazuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka niombe, tufanye stock taking, majengo yaliyopo sasa hivi ambayo yameshajengwa na nguvu za wananchi na mchango wa Serikali yana upungufu kiasi gani ili yaweze kutumika. Nzega tumejenga zahanati katika vijiji 17 ambazo ni nguvu za wananchi na tumefika katika level ya kuezeka. Tumetumia fedha zetu za ndani 700 million shillings kwa ajili ya ku-support infrastructure hizi lakini bado hazijakamilika. Naiomba TAMISEMI i-deploy team katika kila Halmashauri iende ikafanye tathmini ya miundombinu iliyopo ambayo haijakamilika tuweze kuikamilisha halafu tuanze phase two. Tunajua kwamba hatuwezi kuwa tumemaliza changamoto zote lakini angalau tuwe tuna kazi ambazo zimekamilika asilimia 100. Hili ni muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine nataka niongelee suala la TARURA. Umewadiwa wakati Wizara ya Fedha na Wizara ya TAMISEMI kukaa chini kutafuta chanzo sahihi, kwa sababu tusipokuwa na chanzo sahihi ambacho kiko dedicated kwa sheria ambacho kinaelekea kusaidia TARURA bado TARURA itabaki inapata ratio ya asilimia 30 wakati ina mzigo wa asilimia 70 mpaka 80 ya matatizo ya miundombinu. TARURA anachokipata ni kile ambacho kinakuwa shared na TANROADS. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, umefika wakati wa ku-evaluate, TARURA inafanya kazi kubwa sana na ni muhimu upande wa Central Government wakaelewa, wakulima wako vijijini, wanapovuna mazao yao wanahitaji kuyatoa vijijini kuyaleta kwenye barabara za TANROADS kwenda sokoni. Kwa hiyo, kama kutakuwa hakuna miundombinu sahihi ya kutoa mazao vijijini, mazao haya yatabaki shambani, yatakosa soko na tathmini zipo, post-harvest loss ni kubwa sana katika nchi yetu na mengine ni kwa sababu tu ya miundombinu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi ningeshauri wataalam wakae, tutafute vyanzo vya mapato. Tunaona chanzo cha mapato cha Sh.50 cha maji kinavyosaidia suala la maji, ni reliable source inaenda moja kwa moja kwenye Mfuko wa Maji kutatua changamoto za maji. Umewadia wakati wa kutazama reliable source ya TARURA ambayo itakuwa kisheria na ring fenced, itakayoenda moja kwa moja kwenye Mfuko wa Barabara wa TARURA. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka niiombe Serikali, Mheshimiwa Waziri, Nzega tulitengeneza mradi na tukaamua kuanza kuutekeleza kwa fedha zetu za ndani kabla ya kupata support ya kutoka Central Government. Tumeamua kuanzisha a transport hub katika Mji wa Nzega na tumeleta maandishi Serikalini, tume- improve revenue ya stendi ya Mji wa Nzega na sasa hivi tumeanza kuitumia temporary.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshapeleka maandiko Wizara ya Fedha na wataalam wa Wizara ya Fedha wamekuja hadi Halmashauri ya Mji wa Nzega, wametembelea na wameangalia viability ya mradi, tunaomba hizi fedha. Tuko tayari kusaini makubaliano na Wizara ya Fedha ili turudishe hizi fedha ziwe revolving funds kwa sababu tuna uwezo. Mapato tutakayoyapata we can pay back kama loan kutoka sehemu nyingine na hii itatuondolea matatizo katika Halmashauri yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nazungumzia hili kwa nguvu? Ni kwa sababu I am not a believer wa kufukuzana na mama ntilie, bodaboda na watu wadogo wadogo kwa ajili ya kukusanya mapato katika Halmashauri. Sasa hivi Central Government inachukua mapato ya Local Government na mimi ningewashauri chukueni na service levy ije tu Central Government kwa sababu kuna confusion katika Local Government. Service Levy iko kwenye sheria kabisa, anayetakiwa kutathmini na kujua turnover ni TRA, ile figure inapelekwa Halmashauri, Halmashauri aka-compute 0.03% lakini mfanyabiashara akifika kwenye Halmashauri anakutana na kigingi. Watu wa Halmashauri wanamwambia hii tathmini hapana na sisi tuna makadirio yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kumeanzishwa mtindo wa clustering, it is against the law. Kama tunaona Local Government control mechanism ya service levy Mheshimiwa Jafo wakabizini TRA kwa sababu sasa hivi hela zote zinaenda Central Government, wakabizini tu ili tupeleke kwenye Revenue Authority kila kitu, hii ni opinion yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka niombe Serikali, Halmashauri ya Mji wa Nzega tumejenga shule ya wasichana, imekamilika. Tuna changamoto moja, tunaomba uongee na Wizara ya Nishati watupelekee umeme, iko porini wananchi walitoa eneo na wewe unaifahamu na Serikali naishukuru kwa support iliyotupa. Tunaomba ili shule hii ya watoto wa kike ya boarding school ya Mwanzoli mtusaidie umeme ufika ili watoto wetu wa kike waweze kwenda kusoma pale. (Makofi)

Jambo lingine ambalo nataka niiombe Serikali, tumejenga maabara, sisi tumekamilisha tumefikisha juu, tunaomba support kutoka Central Government. Tuna maabara 18, tunaomba mtusaidie kumalizia nyumba za walimu 10 katika Mji wa Nzega ili tuweze kutatua changamoto zinazotukabili katika Local Government.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho naunga mkono hoja, ahsanteni sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa na vilevile nikushukuru kwa dhati kabisa kwa maamuzi uliyofanya ya kuchangia kuhusu Bagamoyo. Ni jambo muhimu sana. Investiment ya Special Economic Zone ya Bagamoyo ilikuwa inatuletea inflow ya 10 billion US Dollar kwenye uchumi wetu na ni jambo ambalo ni vizuri Serikali wakati Waziri anakuja kufanya wind-up watueleze kinagaubaga kwa nini mradi huu unasimama?

Mheshimiwa Spika, nataka niongelee SGR. Kumekuwa na mjadala mkubwa sana na last week kulikuwa kuna mjadala mkubwa hapa ndani ya Bunge kwamba mradi wetu wa SGR kwa nini hauonekani kama unatuletea impact na mzunguko wa fedha kwenye uchumi?

Mheshimiwa Spika, nilitaka nije niombe kwamba wakati Waziri anakuja kufanya wind-up na hasa Waziri wa Fedha, the financing model ya SGR ya Dar es Salaam – Makutupora: Je, itaendelea kuwa hiyo hiyo model ya financing kutoka Makutupora kwenda Tabora; Tabora – Mwanza, Tabora – Kigoma, Uvinza – Msongati? Kwa nini nasema hivyo?

Mheshimiwa Spika, the financing model tunayofanya, which is very good, mimi sipingani nayo katika hatua hii ya awali, kwamba tunatumia fedha zetu kujenga reli hii. Sioni kama tukiendelea hivi mpaka mwisho itatusaidia ndani ya uchumi wetu. Kwa sababu tunakusanya shilingi na tunapomlipa huyu Mkandarasi ni ratio ya 65:35. 35% ya fedha zake analipwa kwa shilingi. 65% analipwa kwa dola.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kinachotokea ni kwamba shilingi inakuwa converted into dollar, halafu dola analipwa Yapi nje, halafu Yapi anarudisha ndani dola ai- convert into shilling kuwalipa local contractors. Kinachotokea ile process ya kuhamisha shilingi kwenda kwenye dola there is a cost, kwa sababu we are losing money in that process. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili kuna tatizo kubwa la Mkandarasi wa Yapi kulipa local contractors. Hili nalo ni tatizo, ni vizuri Wizara ikaliangalia. Hili ni jambo muhimu sana. Tuangalie financial model ya ku-finance mradi wa SGR kuanzia Makutupora kwenda mbele ubadilike. Bila hivyo, uchumi utaendelea ku-suffocate.

Mheshimiwa Spika, sitaki kujadili takwimu za IMF, hizo ni kazi za zao, lakini ninachotaka niwaulize, ukiangalia trend, toka mwaka 2014 construction sector in general, 2014/2015 ili-grow by 16.8%, leo ina-grow katika wastani wa asilimia 13. What is the problem? Shida ni nini wakati tunapeleka fedha nyingi sana za development budget kwenye construction sector? Kuna nini? Hili ni jambo ambalo lazima tujiulize Serikalini.

Mheshimiwa Spika, tuangalie 2014 to date, average growth yetu ya GDP ni asilimia sita point something, imekuwa namna hiyo mpaka leo. Kuna nini wakati tunapeleka fedha nyingi sana kwenye construction? Hili ni jambo moja.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo nataka nitoe ushauri, Mheshimiwa Waziri Kamwelwe, TRC wako pale, washauriane hili. Sisi tunajenga SGR kwenda Mwanza. Our cash cow kwenye reli ni mizigo na ni nchi ya Uganda, Congo, Zambia na Malawi.

Mheshimiwa Spika, nashauri, TAZARA inasuasua, TRC ikodi infrastructure ya TAZARA halafu wanunue wagon kwa ajili ya kuhudumia Zambia na Malawi. Wakati huo tutakuwa tunalipa fee kwa kutumia infrastructure hiyo, TRC wanunue mabehewa na vichwa ambavyo vinaweza kupita kwenye reli ya TAZARA ili wabebe mizigo ya Zambia na Malawi, tutapata revenue.

Mheshimiwa Spika, la pili, leo sisi tunataka kumpelekea huduma Mganda ambaye ana-constitute aslimia 30 ya mzigo wetu. Tujenge kipande cha Port Bell kwenda Kampala ambacho ni kilometa 11, tuweke meli kubwa, mzigo utoke Dar es Salaam mpaka Mwanza, uingie kwenye hiyo meli kubwa ibebe mizigo tupeleke Port Bell. Tutakuwa na competitive age. Kinachotokea, tunaye-compete naye leo ambaye ni Mombasa anamjengea bandari kavu Mganda, Naivasha ili kupunguza distance iliyoko ambayo sisi kwetu ni competitive age. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu, kwenda Msongati ni kilometa 200, ninawashauri achacheni na reli ya kwenda Rwanda, wekeni fedha kujenga Msongati kuja Uvinza. Tujenge kwa SGR. Tukijenga kwa SGR kutoka Msongati kuja Uvinza mzigo utabebwa kutoka Msongati kuja Uvinza kwa Standard Gauge. Kutokea pale tutatumia meter gauge kuja Dar es Salaam. Kwa hiyo, tutaanza kupata fedha kabla ya reli kufika Mwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la nne, we only have 30 kilometers kuhudumia Eastern Congo ambayo ina population ya 22 million people. Ushauri, shaurianeni na Serikali ya Congo tufanye joint effort tujenge gati upande wa Congo tuweze kubeba mizigo kutokea Kigoma kwenye meli kubwa tuvushe kwenda Kalemii ili tuanze kuwahudumia hawa wakati tunasubiri ku-generate revenue. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, this is a question of where to get money. Kwa nini nasema hivi? Leo Mozambique wamejenga reli kwenda Zambia, ili…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Bahati mbaya dakika saba ndiyo hizo.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, naomba Serikali waangalie maeneo ambayo wanaweza kupata fedha. Ahsante, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa kuchangia Wizara hii, jambo moja la kwanza kabisa kabla sijaanza kutoa mchango wangu, nataka niiombe Serikali, Wizara ya Fedha, waangalie huu Mwezi wa Ramadhan, kuna request kubwa za Taasisi mbalimbali za Kiislam ambazo zimeleta tende na vyakula kwa ajili ya kutoa sadaka kwa watu maskini ziweze kupata request ya exemption ambazo wameomba kutoka Tanzania Revenue Authority. Taasisi hizi ziko regulated chini ya BAKWATA na zimepeleka requests zake na wengi wanatoa katika maeneo ambayo watu wana umaskini mkubwa, they cannot afford kupata futari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu utajikita katika maeneo makubwa yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ni suala la kufanya biashara; biashara yoyote duniani, ina mambo makubwa mawili na ninachomshukuru Mwenyezi Mungu, Rais Magufuli alivyoingia madarakani, aliweka vision yake clear, kwamba anataka kujenga nchi yenye uwezo wa kujitegemea ya viwanda. Hii ndiyo vision, ni matarajio yangu mimi na wengine wote tuliomo humu na Watanzania, kwamba wanaomsaidia Mheshimiwa Rais kusaidia utekelezaji wa vision hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, biashara ina mambo mawili, moja kuna software part of business na upande mwingine ni hardware part of business. Hardware part of business, tunajenga barabara, tunajenga reli, tunanunua ndege, tunajenga miundombinu ya umeme, lakini hii hardware part ya biashara, isipokuwa compatible ya software part ya biashara ambayo ni regulation na sheria, hii itakuwa ni wastage ya resources. Kama tutajenga reli, tutajenga barabara, tutaleta umeme, vyote hivi vikakosa biashara ambayo itavifanya hivi vitu viwe effective, havitakuwa na maana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nataka nitoe mifano michache, kwenye Kamati yetu ya Bajeti, walikuja watu wa CTI. CTI kwenye presentation yao, ambayo ninayo hapa na bahati nzuri Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara tulikuwa naye, wanazungumzia existence of multiple Regulatory Authority leading to high costs of doing business, kwa sababu biashara vilevile gharama ni jambo la msingi. Sasa anakwambia an example for the food processing industry is registered by more than 15 authorities, taasisi 15 zina-regulate food processing industry.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pharmaceutical industry, ili aanzishe biashara ya kiwanda kidogo cha pharmaceutical industry na huyu mtu aliyekuja kufanya hii presentation ni mtu ambaye anataka kuweka kiwanda Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kutumia pamba iliyoko pale kutengeneza pamba kwa ajili ya mahospitali. Huyu mtu, anahitaji regulatory authorities zimepe jumla la ya leseni 26 ili aweze kuanzisha huu mradi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, a registered company kwa ajili ya ku-export horticulture products, maua na bidhaa zingine za hotculture, anahitaji kupata jumla ya vibali 45 ili aweze ku-export biashara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwanda kwa ajili ya kuzalisha maziwa ana tozo na kodi na leseni jumla 26 ili anzishe kiwanda hicho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwape mfano, kuna kiwanda kidogo kiko Nanenane hapa Dodoma, mwaka 2016 aliamua kuanzisha kiwanda chake cha ku-process asali ambacho kina uwezo wa ku- process tani 3 kwa siku. Februari 2016 na ninazo barua zake hapa, huyu mwananchi ameiandikia TFDA ije ikague kiwanda chake iangalie mfumo wa uzalishaji na kumpa approval amejibiwa Novemba 6, barua ya kwamba tutakuja kukagua. Mpaka amepata certificate ni Februari 2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu ni mfanyabiashara mdogo, kachukua mkopo Tanzania Investment Bank wa shilingi milioni 200, benki sasa iko mlangoni kwake inataka kuli-recall mkopo wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nini sasa ushauri wangu? Ushauri wangu ni hivi, ile taarifa ya IMF iliyo-leak (unofficial), imetupa mambo mazuri mno na mimi nataka nishauri Serikali ipokeeni kwa sababu imetupa two options, imetuambia kama tunataka ku-grow kwenda 6%, 7% kuna mambo manne ya kufanya. La kwanza improve business environment.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu TFDA, OSHA, taasisi zote hizi anzisheni one building wawekeni pale andikeni business facilitation of whatever ili mfanyabiashara akishachukua leseni yake ya usajili wa Kampuni BRELA, the second place anayoenda anaenda kwenye business facilitation building. Akifika pale analipia taasisi zote na muweke chini pale cage kama za benki, iwe imeandikwa NEMC, TFDA, TBS, ndani ya jengo moja. Yule mfanyabiashara aki-launch application yake pale and the world is connected, akitoka anatoka na document zake anaenda kufanya biashara yake, hili ni jambo muhimu mno. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingne ambalo nataka niulize, TBS ana evaluate standard ya bidhaa na vitu ambavyo tunazalisha. Kama mtu kapata certificate ya TBS anazalisha maziwa kwa nini tena akatafute certificate ya TFDA? Wawekeni hawa watu wote ndani ya one umbrella TFDA awe unit ndani ya TBS ili mtu akiingia afanye kila kitu mule, OSHA awe unit ndani ya NEMC may be ili tuangalie namna gani ya ku-harmonize mambo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe kaka yangu Waziri Kakunda, blueprint leta sheria. Kama kuna mahitaji ya mabadiliko ya sheria jamani mwaka wa fedha huu upo bado hatujamaliza, hata kama ni weekend moja tukae hapa tuwasaidieni kufanya haya mambo yawe rahisi katika kufanya biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe mfano, hapa mkononi nina taarifa leather sector. Sijui kama Kanuni zinaruhusu ni vizuri sana kwenye Kamati ya Bajeti Waziri Jenista awe anakuja, hili ni ombi ili aone mambo yalivyo ndani ya Serikali. Yeye yuko pale kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya ku-coordinate Mawaziri na taasisi za Serikali inakuwa rahisi center of coordination ya shughuli za Serikali kutokea Ofisi ya Waziri Mkuu kuwepo, ni muhimu na nasema hii from my heart kwa sababu kuna mambo yanafanyika unajiuliza are we one Government? Inasikitisha! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikupe mfano, usafirishaji wa ngozi wet blue, mwaka 2016 tulisafirisha ngozi wet blue pieces 1.2 million kwenda nje, leo tuna export wet blue pieces 200,000. Wet blue ni stage ya kwanza ya ku- process, ngozi kutoka raw kwenda wet blue ni stage ya kwanza ambapo tumesafirisha 1.2 pieces mwaka 2016 leo tume export only 200,000 pieces, hii hapa taarifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unajiuliza swali kama tunazalisha pieces milioni 3 kwa mwaka kama nchi hizi zinazobaki ambaz hatujasafirisha ziko wapi? Ukienda kuangalia raw exported only iliyokuwa exported ni pieces 400,000 kuna pieces zaidi ya 800,000 vimeondoka under smuggling na mnajua ni kwa nini? Ni kwa sababu ya one thing, tume impose 10% export levy ya wet blue ambayo competitors wetu wote kwenye East Afrika hawana kodi hiyo, tunayo sisi. Ni kwa sababu gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulienda Arusha tukasaini makubaliano ya Afrika Mashariki tukaingizwa mkenge halafu wao wenzetu hawatekelezi sheria hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, hapa tumesikia suala la Mchuchuma na Liganga, Waheshimiwa Wabunge hebu tujiulize swali, kwenye Mradi wa Mchuchuma na Liganga kuna Mradi wa Makaa ya Mawe, Mradi wa Chuma, Mradi wa Umeme na mradi wa kuchakata product zinazotokana na chuma, sasa wapi tumekwama? Ukisikiliza kabisa kutoka NDC mkwamo unatokana na umeme na chuma. Sasa nauliza kama miradi miwili ina matatizo, kwa nini tunazuia utekelezaji wa mradi wa makaa mawe? Kwa nini hii miradi yote minne tunaifunga pamoja ukifa mmoja they entire project is dead. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama tunaona kuna matatizo tunapeleka barabara Liganga na Mchuchuma, tunapeleka line kubwa ya umeme, why are we spending that money kupeleka kule kama nchi? Kwa nini tusipeleke kwenye madarasa au kwenye maeneo mengine? (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Bashe, nilikuongezea dakika tatu.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia kwenye Wizara hii. Nitumie nafasi hii kwanza nimpongeze Waziri Mheshimiwa Mpina na Naibu wake kwa angalau kuleta awareness ya Sekta ya Mifugo na jitihada wanazofanya. Mchango wangu utakuwa ni kushauri zaidi kwenye eneo la mifugo kwa maana ya ng’ombe lakini vilevile maziwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, dhana nzima ya ufugaji ni dhana ya input na output kwa maana ya kwamba unachokiingiza ndicho unachotarajia kukipata. Kwa hiyo, ukifanya wrong investment na wrong input, utarajie matokeo dhaifu. Ili viwanda vya maziwa viweze kufanya kazi vizuri, hatua ya kwanza ni kuhakikisha kwamba malighafi ya maziwa yanapatikana kwa urahisi, at a competitive rate ili yule mzalishaji wa maziwa aweze kuyanunua na mkulima apate faida.

Mheshimiwa Spika, nitatolea mfano, mfugaji anayezalisha ng’ombe wa maziwa, ng’ombe mmoja anayetoa lita 10 anahitaji kula majani makavu yenye uzito wa kilo 19. Ng’ombe huyu ili aweze kupata ile hay, hay moja inauzwa Sh.2,500 mpaka Sh.3,000, kwa hiyo, kwa siku majani yake ni Sh.3,000; tunamzungumzia mfugaji anayefuga kwa ajili ya kuuza maziwa commercially. Anahitaji kumpa supplement kilo mbili asubuhi na akilo mbili jioni, ina maana kilo nne ya supplement. Kilo nne ya supplement kwa bei ya sasa hivi iliyopo sokoni ni kati ya Sh.470 mpaka Sh.500. Kwa hiyo, kama atampa kilo nne maana yake ni Sh.2,000. Kwa hiyo, kampa majani yenye thamani ya Sh.3,000 halafu kamlisha supplement ya Sh.2,000, gharama yake ni Sh.5,000.

Mheshimiwa Spika, mifugo yetu yote iliyopo katika nchi hii wastani wake wa uzalishaji ni lita 10 maximum, hatuna ng’ombe wanaozalisha lita 20 au lita 30, ni wachache sana na wafugaji wetu katika household wengi capacity ya ng’ombe wao wengi ni ten litres at the best. Kwa hiyo, maziwa anayauza shilingi ngapi, anayauza Sh.900 mpaka Sh.100; kwa hiyo kapata Sh.9,000 wakati yeye kagharamikia Sh.5,000 mpaka Sh.6,000; hizi ni gharama za moja kwa moja. Bado kuna gharama za madawa na maji, matokeo yake ni kwamba bei ya uzalishaji wa maziwa per litre compared na bei ya ununuzi kiwandani, wafugaji hawapati faida yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mfugaji ana-opt kufanya nini? Ana-opt kufanya uchungaji wa kawaida, hata hapa Dodoma ukipita barabarani unaona ng’ombe wa kisasa wanachungwa barabarani kwa sababu hawana uwezo wa kupata input ya kumlisha ng’ombe, kwa hiyo tunaingia kwenye tatizo la feeding. Kinachotokea kwa kuwa ng’ombe hajalishwa vizuri, hawezi kuzalisha vizuri, kwa hiyo viwanda haviwezi kupata maziwa ya kutosha.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nini ushauri wangu kwa Serikali? Ushauri wangu wa kwanza, ni lazima Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mifugo, Wizara ya Ardhi, Wizara ya TAMISEMI wakae chini pamoja kuja na master plan. Ukisoma Tanzania Livestock Master Plan iliyozinduliwa na Waziri, it is centered kwenye Wizara moja na suala la ufugaji ni crosscutting, siyo la Wizara ya Mheshimiwa Mpina peke yake. Leo tuna shamba la Serikali la kuzalisha malisho lipo Dar es Salaam, ni under capacity, haliwezi kuzalisha chakula cha mwaka mzima. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimeona hapa Mheshimiwa Waziri amesema anafanya uhilimishaji wa ng’ombe wa kienyeji milioni tatu kupata mitamba milioni moja. Ni hivi, ukimchukua ng’ombe wa kienyeji Mheshimiwa Mpina anafahamu Tarime ya kule kwetu Tabora na Shinyanga, ukampandisha dume wa Fraiesian atapatikana F1, F1 huyu capacity yake ya uzalishaji wa maziwa is maximum of three and four litres. Ukimpelekea mfugaji akamfanye zero grazing is an economical, haiwezekani, hawezi kumzalisha na kupata mazao. Ili aweze kupata ng’ombe wa kumpatia maziwa mazuri anayetokana na ng’ombe wa kienyeji ni third generation, apatikane F1, F2, F3 ndiyo huyu F3 atafika at least 10 litres kwa sababu genetically ni 25, 50 and 75 yaani generation ya tatu ndiyo tutapata. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu ambao nataka niishauri Serikali, hawawezi kufanya mass insemination nchi nzima, lazima tufanye clustering ni wapi tunazalisha ng’ombe wa maziwa, wapi tunazalisha ng’ombe wa nyama, huu ni ushauri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili kwenye maziwa, leo kiwanda cha maziwa kinahitaji kuzalisha maziwa na wao Wizarani wanajua, walikuja watu wa Tanga Fresh kwenye Kamati ya Bajeti eti waliomba kibali na mimi niwapongeze Wizara ya Mifugo waligoma, wanaomba kibali wa-import maziwa raw kutoka Rwanda.

Sasa what is the success story ya Rwanda? Success story ya Rwanda ilikuwa ni moja, kila kaya ilipewa programu ya ng’ombe mmoja wa maziwa lakini kwenye vijiji zikaanzishwa collection center kwamba wafugaji wote wanaleta maziwa yao kwenye center moja, pale kwenye center, kiwanda kinakuja kuyachukua yale maziwa. Sasa hivi wafugaji wetu wapo scattered, hawezi kusafirisha maziwa yake kuyaleta kwenye center au kumfikishia mtu wa kiwandani kwa sababu gharama ni kubwa na kwa hali hii hatuwezi ku-break through. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu, Asas yupo nyanda za juu, it’s better kukaa chini na Wizara ya Fedha kuangalia incentive za kikodi na kumtengenezea clustering centers kwenye Mikoa ya Mbeya na Iringa, yeye ajenge cooling centers ambazo wafugaji watapeleka maziwa yao pale, yeye ataenda kuyachukulia pale ili gharama zake za uzalishaji ziwe ndogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo nataka niongelee, nataka nimshauri Waziri, ukienda NAIC pale Arusha wana ngo’mbe anaitwa Friesian, wana ng’ombe labda anaitwa Borani, wana ng’ombe anaitwa Ayrshire. Kwenye breeding ya ng’ombe wa nyama the best breed ni aina mbili; ni Borani na Sahiwal, lakini kwa insemination hatuwezi kubadilisha ng’ombe wetu wa Kisukuma na Kigogo na Kimasai.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu; Serikali ianzishe programu, mnunue madume ya Borani; wakati wa Mwalimu Nyerere kulikuwa kuna holding grounds zilikuwa zinatumika kwa ajili ya breeding; kwa hiyo yale madume ya Borani mnayapeleka Nzega, halmashauri inakabidhiwa, katika kila kijiji kunakuwa na centers au kata halafu mnaenda kuhasi madume ya kienyeji, mnaanzisha programu ya kupandisha ng’ombe wa Borani kwenye ng’ombe wa kienyeji, tutabadilisha breed namna hii.

Mheshimiwa Spika, lakini ziki-run parallel ng’ombe wa kienyeji na Borani ambao wanauzwa milioni moja na nusu, milioni mbili, wafugaji hawawezi ku-afford. Ili anunue dume mmoja wa Borani inabidi auze ng’ombe zaidi ya sita wa kienyeji, he cannot afford kwa sababu ana ng’ombe wake kumi anaona anaingia umaskini. Kwa hiyo mimi nashauri Serikali tafakarini…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante, malizia.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, namalizia la mwisho, dakika moja tu nakuomba.

Mheshimiwa Spika, ngozi; rudisheni utaratibu wa zamani, zamani kulikuwa kuna kitu kinaitwa Tanzania Hides and Skin, ngozi zinauzwa kwenye mnada kwenye machinjio. Bila kufanya namna hiyo mazao ya ngozi hamuwezi kuya- control. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa. Kwanza nitumie fursa hii kuishukuru Serikali kwa dhati kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Nzega, kile kimeo cha pale Iguguta kimekwisha Naibu Waziri juzi alienda akazindua, Kashishi wameshatuzindulia, nina maombi machache kwa niaba ya wananchi wa Nzega. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba Mkandarasi anayefanya Mradi wa REA wa Nzega asimamiwe. Mradi tuliowasha katika Kijiji cha Ibushi tukiwa pamoja na Mheshimiwa Waziri, mpaka leo nyumba alizoishia ndiyo hizo hizo, wameshindwa kusogeza nguzo wala kupeleka waya. Kata ya Mbogwe mpaka leo umeme haujafika, Sekondari ya wasichana ya Mwanzoli mpaka leo umeme haujafika tumeshindwa ku-enroll watoto wa kike katika hiyo boarding school kwa sababu ya suala la umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Zahanati ya Idudumo mpaka leo umeme haujafika, wametoa commitment by the end of July ikishindikana by the end July Mkandarasi huyu kufanya kazi na Waziri amekuwa very fair kwake kwa sababu ya jinsia, tunaomba wachukue hatua kama Serikali kuhakikisha kwamba suala hili linatatuliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ambalo nataka niseme, fairly kabisa mimi nawapongeza TANESCO na Serikali, suala la umeme ration na mgao wa umeme umepungua sana katika nchi sasa hivi, wamefanya hatua nzuri sana na ningetumia fursa hii kusema maneno machache.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama taifa tuna plan ya energy mix, na ukitazama focus ya vyanzo vya umeme ambavyo tunatarajia kupata kutokana na maji vyote tukifanya vitatupatia kama megawati 4,000; ukichukua na megawati 1600 tuliyonayo leo jumla tutakuwa tuna megawati 5600, our target ni kuwa na megawati 10,000 by 2025. Ni muhimu kama Serikali kuanza kujadili sasa hivi ni namna gani vyanzo vya solar vinaanza kutumika, na kama inawezekana tufanye PPP ili watu wa private sector waje wawekeze. Namna gani themo tunaanza kutumia, namna gani mradi wa Singida na Mradi wa Makambako unafufuka, namna gani Mradi wa Mchuchuma unaanza kutekelezwa ili by 2025 tuwe na hizo 10,000 megawati.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nataka niseme ni kuhusu Stieglers; kumekuwa na national debate kuhusu stiegler’s; hapa tulipofika ni point of no return stieglers must be implemented. Sasa ushauri wangu kwa Serikali tuna mpango wa kuzalisha 2100 megawati kwenye mradi wa Stiegler’s. Swali la kujiuliza do we have a muster plan ya namna gani tutakapoanza kuzalisha 2100 tuta- maintain kwa kipindi cha miaka 10-15 production 2100?

Mheshimiwa Naibu Spika, kama hatutakuwa na grand plan hiyo maana yake investment yote tunayowekeza pale itakuwa ni waste, ni lazima tuangalie namna gani vyanzo vya maji vinavyoenda kwenye Mto Ruaha na Mto Kilombero vinavyopeleka maji kwenye eneo la Stiegler’s vinakuwa protected na namna gani shughuli za binadamu zilizoko katika upper stream zinakuwa marginalized ili vyanzo hivi vya maji viweze kwenda kule. Tusije kujikuta ata the end of the day baada ya miaka 5 stieglers ina-produce 40 percent ya capacity. Baada ya miaka 10 stieglers ina-produce just 50 percent ya capacity. Tuna experience ya Kihansi, tuna experience ya nyumba ya Mungu, tuna experience ya haya mabwawa ya maji. Ni muhimu sana sasa Wizara ya Mazingira, Wizara ya Ardhi, Wizara ya Kilimo kuwa na joint effort ya kutengeneza a grand plan ya ku-protect mazingira katika maeneo haya. Suala la Stiegler’s is national decision ni maamuzi ya nchi we have to do it na kama tunafanya we do it rightly ili ku-attain efficiency and effectiveness.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru naunga mkono hoja (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa fursa. Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia sote afya na nguvu ya kuja kutimiza wajibu wetu.

Mheshimiwa Spika, mimi nianze kwa maneno yafuatayo; litmus paper ya sera za fedha na fiscal measures ya kwanza ni Revenue Authority, kwamba je, malengo tuliyojiwekea na mimi niingie on record, siyo sahihi na Waziri wa Fedha anajua hili, siyo sahihi kusema Watanzania hawalipi kodi. Labda tuseme ni sahihi kusema kuna Watanzania wachache hawalipi direct tax, kila Mtanzania wa nchi hii analipa kodi whether ni direct or indirect. Kwa hiyo, hii dhana naiona siyo dhana sahihi kwa sababu hakuna Mtanzania hanunui bidhaa, anaponunua bidhaa amelipa kodi. Kwa hiyo, hii ni dhana ambayo ni vizuri sana ikawa inaelezwa vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi mkononi hapa na hii ni Wizara ya Fedha yenye jukumu la kusimamia fiscal measures. Mkononi hapa nina takwimu za miaka kumi zinazoonesha trend ya makusanyo ya kodi ya nchi yetu. Kati ya matarajio na hali halisi, the focus error kwa kipindi cha miaka kumi kwenye Revenue Authority ni asilimia 17 yaani kwa miaka kumi asilimia 17 haijawahi kufikiwa, kila ukitenga shilingi moja kwamba ndiyo tutakusanya maana yake kuna asilimia 17 ya hiyo shilingi moja hatutafikia. Ukichukua focus error ya miaka kumi ya bajeti nzima ni asilimia 27, hizi hapa ni takwimu za Serikali za miaka kumi.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa nini nimesema litmus paper ni TRA? Kwa sababu kule ndiko tunakoenda kukusanya mapato. Sasa unakusanya mapato kutoka wapi? Hapa ndiyo linakuja jukumu la Wizara ya Fedha kusimamia fiscal measures zake. Nataka nitoe mifano, kuna makosa ya kiutawala yanayofanyika katika nchi yetu yana-destroy economy.

Mheshimiwa Spika, ripoti ya IMF ambayo ni leaked ambayo hatupendi kuisikia imezungumzia jambo moja, business environment. Tunapozungumzia business environment ni hatua tunazochukua ambazo nyingi zinakwenda kuathiri TRA function. Mfano, kuna watu wanaingiza sukari za viwandani wanapitisha kwa njia za panya kuziingiza sokoni. Tumeamua kuazisha kodi ambayo ni unconstitutional ya withholding ya 15%. Hili ni suala la administrative, ni suala la usimamizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nini kinachotokea, hivi kweli Waziri, Mheshimiwa Dkt. Mpango, Coca Cola ataingiza industrial sugar aipeleke Kariakoo akauze? Kwa nini wezi watatu tu wanaojulikana, wanaoingiza sukari za viwandani sokoni tunakwenda ku-destroy the entire sector, why? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, yaani mimi hili swali nimeliuliza ndani ya Kamati ya Bajeti kwa miaka miwili halipati majibu. Yaani tunawajua ambao huwa wanaingiza sukari za viwandani ambazo wanaziingiza sokoni, hawazidi watatu katika nchi, tunawajua. Lakini hatua gani tunachukua? Tunaanzisha kodi ambayo inakwenda kuua cash flow za viwanda. It is unfair. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Dkt. Mpango, tunakubebesha dhambi nyingi katika nchi hii, malawama mengi, because you are the one, be bold kaka. Walazimishe polisi, walazimishe Wizara ya Mambo ya Ndani, walazimishe wengine wachukue hatua, don’t kill the sector, sector nzima ina-suffer.

Mheshimiwa Spika, kinachotokea ni hivi, anatakiwa alipe withholding tax ambayo refund yake haipo na tulipitisha kuanzisha Escrow Account na nikwambie mimi nampongeza sana Rais, Dkt. Magufuli, najua anakwenda kukutana na wafanyabiashara kila Wilaya wanakwenda watano. I swear zitakuja sheria hapa za kubadilishwa, kama ilivyokuwa kwenye madini, akienda kuwasikiliza.

Mheshimiwa Spika, mimi nasikitika, it is very painful. The business sector is suffering. Nataka nikupe mfano mwingine, these are administrative issues ambaye anakwenda kuathirika ni Wizara ya Fedha, TRA, kuna kiwanda kinakwenda kupigwa mnada kinaitwa Salahi Company Limited kiko Iringa. Angalia hii movie ya kihindi, kile kiwanda kiko kwenye eneo la EPZA, anazalisha pipi na biscuit, kapata certificate zote na kila kitu input yake mojawapo ni sukari kwa ajili ya pipi na biscuit. Document zote zimeenda amezipeleka Bodi ya Sukari unajua Bodi ya Sukari wamewajibu nini? Sisi hatutambui EPZA hizo incentive wanazokupa, kwa hiyo hatukupi kibali.

Sasa nini kimetokea? Kiwanda hiki kilifunguliwa for trial mwaka 2016 for trial for two months kwa ajili ya watu EPZA kujiridhisha quality na TBS na kila kitu baada ya hapo wakazima wame-importraw material ngano yao sasa hivi iko under bounded warehouse ya TRA imeoza. Sukari waliyo import kwasababu hawajapata kibali cha Bodi ya Sukari angalia bureaucracy hii sukari wamezuiliwa mpaka ime- expire bandarini angalia hili, wananchi 120 wa Iringa mjini waliokuwa wameajiriwa wamerudishwa nyumbani. Benki ya Amana leo ina-recall mkopo, asset zao zinapigwa mnada, he is a Tanzanian ame-invest two billion shillings atapata wapi kodi TRA atapata wapi? (Makofi)

Sasa ushauri wangu, Dkt. Mpango leta kasheria humu mimi sijui procedure. Economic Intelligence Unit iliyoko chini ya TRA ipewe mamlaka makubwa ya kisheria kufanya analysis na kukuletea ripoti na kukupa mamlaka ya kum-summon Waziri yeyote anaye-hinder your productivity ili tuondoke kwenye haya matatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikupe mfano mwingine, mimi nimeamua kuongelea hii tu hebu tuulizane maswali kwa nini tumeenda na ambush na mapolisi na mabunduki kwenda kufunga Bureau de Change, why? hatuna sheria, hamna sheria inayosimamia biashara ya fedha ya nje kwa sababu ya luxity ya watu walioajiriwa kusimamia kazi yao tunatafuta shortcut we are going to destroy the sector matokeo yake tutaandikwa kwenye international news kwamba hawa watu are not friend in business inatu-take ages ku-clean that mess, it’s not because we don’t have laws, we have good laws in this country. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu tumbaku hapa Waziri Mpango ametaja sekta zinazochangia zilizokua kwa haraka, mwaka huu sekta ya kilimo imekuwa kwa asilimia tano na hii imekuwa kwa kudra ya Mwenyezi Mungu, ninarudia kwa kudra ya Mwenyezi Mungu. Mvua mwaka jana zimekuwa nyingi growth yetu imetoka 3.7 to 5% ingawa marginal growth na hili ni jambo muhimu sana wachumi wawe wanafanya analysis tunasema tu sekta imekuwa, imekuwa kwa kiwango gani compared na mwaka jana marginal growth yetu is less than ourpopulation growth, ndiyou kweli sasa nini inatokea tumbaku, Zitto kataja Kampuni ya TLTC.

Mheshimiwa Spika, nataka nikwambie hivi it is a bad news again Alliance One ambaye ananunua tumbaku Mkoa wa Tabora, TLTC ndiyo wanunuzi wakubwa wa kwetu kinachotokea umeona hii karatasi ina page 14 haya yote ni mautitiri ya kodi na nini, crisis VAT returns hawarudishiwi hawa watu wa TLTC leo wanafunga Waziri amejitahidi wa- investment mwezi Aprili amekutana nao, lakini mimi najua hawajafikia muafaka wala kutatua tatizo kwahiyo mwaka huu tumbaku tuliyozalisha mwaka juzi ilikuwa kilo milioni 1.2 imeshuka mpaka 370,000 uzalishaji wa tumbaku unashuka….

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Bashe.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, moja tunimalize nataka niombe kwa heshima kabisa Waziri Mpango unaweza ukawa unaweza ukawa unafanya kazi kubwa tutajenga Stigler’s, tutajenga TRC, tutajenga everything if hatu-encourage productivity na kufanya biashara katika nchi hii miradi mikubwa yote inayoifanya haiwezi kusaidia kukua kwa uchumi, ni lazima Serikali watu, wabadilike TRA rudisheni VAT mna-suffocate economy ya watu na cash flow za wafanyabiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru na naunga mkono hoja. (Makofi)
Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, naomba nitumie nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kupata fursa hii. Vilevile nianze kwa kusema kwamba naunga mkono hoja iliyo mbele yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, zaidi ya asilimia 93 ya Wabunge waliochangia wameongelea sekta ya kilimo. Hii inaonesha ni namna gani sekta hii inagusa maisha ya watu na umuhimu wake. Sisi kama Wizara ya Kilimo tunakiri na kupokea baadhi ya changamoto ambazo wamezisema. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, yapo mambo ambayo katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Wizara na Serikali kwa ujumla imejipanga kuhakikisha tunaondoa hizi changamoto zinazotukabili katika sekta ya kilimo. Changamoto ya kwanza ni mbegu na viuatilifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, siri na future ya sekta ya kilimo ni research and development. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo Ilani imetupa targets za ku-attain katika kila zao ambazo ni lazima tuzifikie na target hiyo siri yake ni mbegu. Kwa hiyo, kama Wizara tutakapokuja katika mpango hatua ya kwanza tuliyoamua suala la mbegu litakuwa ni suala la uzalishaji wa mbegu kwa solution za ndani. Kwa kipindi cha miaka mitano ijayo tutawekeza shilingi bilioni 179 kwa ajili ya research and development and seed multiplication. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa ni vizuri Waheshimiwa Wabunge wakaelewa. Tunapozungumzia mbegu kwanza hili ni suala la dunia na Tanzania ni sehemu ya dunia na sisi hatuwezi kujiondoa katika hiyo seti. Kwa hiyo, tunawekeza katika research kwa ajili ya ku-develop mbegu za aina ya OPV na hybrid lakini wakati huo huo kutunza mbegu zetu za asili na sisi kama Wizara tunakuja hapo mbele Mwenyezi Mungu akitujaalia na sheria maalum ya kulinda traditional seeds ili ziweze kufanyiwa purification na ziweze kufanyiwa maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mara nyingi mbegu tunazozijadili ni nne, ni traditional seed (mbegu zetu za asili), OPV, hybrid na sasa kuna teknolojia ya GMO. Sisi kama nchi tumesema hatutumii mbegu za GMO na hatutaruhusu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeweka utaratibu wa wazi kwamba hybrid seed ambayo inajulikana parent seeds wake (wazazi wawili), labda nitumie lugha rahisi, tunapozungumzia mbegu za hybrid tunazungumzia mbegu mbili za kiume na kike zenye sifa mbili tofauti zinazofanyiwa cross breeding. Hapa msingi wake ni mbegu za asili. Unaweza ukakuta mbegu ya mahindi ya asili A ina sifa ya kuwa na uzalishaji mkubwa lakini haina uwezo wa ku-resist magonjwa. Mbegu B ina sifa ya ku-resist magonjwa lakini uzalishaji wake ni mdogo. Wataalam wetu wanafanya kazi ya kuzi-breed hizi mbegu mbili ili kupata mbegu ambayo inaweza kuwa na sifa zote mbili na kumsaidia mkulima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama nchi potential demand yetu ya mbegu ni tani 371,000. Hii ndiyo potential demand yetu lakini mbegu tunazozalisha za kisasa ni tani 76,000 na tani 11,000 ni mbegu tunazoagiza kutoka nje na mbegu zinazobaki ni mbegu zetu za asili ambazo tumekuwa tukizitumia katika hatua mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano zao kama alizeti, tunakiri kama Wizara tumechukua hatua katika suala la kupambana na gap ya mafuta. Hivi karibuni Mheshimiwa Waziri Mkuu alikuwa Kigoma kuzindua usambazaji wa miche ya michikichi. Tumegawa miche ya michikichi zaidi ya 1,000,000. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sasa hivi kama Wizara tunahitaji uzalishaji wa tani 5,000 za hybrid seed na OPV seed za alizeti ili tuweze kufikia uzalishaji tunaouhitaji wa mbegu za mafuta. Ni kweli viwanda vya kuchakata mafuta vinakabiliwa na changmoto kubwa sana katika suala la uzalishaji wa mbegu. Nilitaka nitoe tu commitment ya Wizara katika eneo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua ya pili ambayo tunachukua, Rais katika hotuba amesema suala la ngano. Nataka nimwambie Mheshimiwa Mbunge wa Hanang, hivi sasa tunavyoongea Wizara ya Kilimo imesaini MoU na wanunuzi na wachakataji wa ngano ndani ya nchi. Tunatengeneza utaratibu ambao tumekubaliana na private sector kwamba hatoagiza ngano kutoka nje kabla ya kununua ngano yote ya ndani. Sasa tunavyoongea tumejiwekea lengo la kuzalisha metric tonnes 150,000 katika msimu huu unaokuja na tutagawa jumla ya tani 36,000 ya mbegu kwa ajili ya kuzalisha ngano katika Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara. Dodoma tumefanya pilot project hapa Bahi ambapo ndiyo sehemu ambayo mbegu ya ngano imeonekana ina-mature kwa muda mfupi kuliko wakati wowote, katika Wilaya ya Bahi na Mkoa wa Rukwa tunagawa hizi mbegu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tulichokubaliana na wanunuzi ni nini? Kilimo ni biashara, lazima u-define volume and price. Kwa hiyo, tulikaa na wanunuzi tukawauliza wananunua ngano kutoka nje kwa bei gani? Tukapiga mahesabu na tukakubaliana watanunua kilo moja kutoka kwa mkulima kwa shilingi 800 bei ya chini mpaka Sh.1,000 kilo moja ya ngano. Sasa hivi wakulima walikuwa wanauza kati ya shilingi 500 na shilingi 600 na walikuwa hawana uhakika wa soko. Nataka nimhakikishie Mbunge wa Hanang hivi sasa tunavyoongea Kampuni ya Bakhresa wako Wilaya ya Hanang, awasiliane na DC wake wanachukua zile tani 400 zilizoko pale. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, secret ya kilimo ni economies of scale. Mimi nataka niseme sisi wote ni wajumbe wa Baraza la Madiwani, niwaombe sana tusipokuwa makini tutajenga Taifa la wachuuzi badala ya Taifa la wazalishaji. Wizara tuko tayari kuwasaidia kwa ajili ya kuanzisha block farming na katika bajeti ijayo tengeni maeneo kama Wilaya ya Manyoni kama kwenye suala la korosho tuweze kuzalisha mazao mbalimbali na sisi tutawasaidia mbegu, wataalam, vitendea kazi ili tuweze kulifikia lengo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nataka niwaambie tu Waheshimiwa Wabunge kwamba kama Wizara ya Kilimo tumejiwekea target...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha Mheshimiwa.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, namalizia tu. Tumejiwekea lengo la kukua kwa asilimia 10 katika kipindi cha miaka mitano ijayo badala ya asilimia 5. Tunawaomba support, ushirikiano wenu na ni lazima tukubaliane kama nchi kuwekeza katika kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote naomba nitumie nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa fursa hii. Kwanza nawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia na kutoa maoni katika masuala yanayohusu sekta ya Kilimo. Sisi kama Wizara tunachukua sehemu kubwa na maoni yao na mabadiliko makubwa watayaona katika bajeti tutakayokuja nayo katika Bunge lijalo Mwenyezi Mungu akijalia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka tu niweze kutoa highlight katika baadhi ya maeneo. Hatua ya kwanza, Waheshimiwa Wabunge wamechangia sana kuhusu suala la udongo, ugani na mbegu na hasa za mafuta. Kuhusu suala la ugani na suala la kupima afya ya udongo, Wizara tutakuja katika bajeti ijayo na mpango wa kuanzisha Agricultural Centre katika kila halmashauri na tutagawa katika kila Halmashauri, lab equipment ambayo ni mobile equipment itakayotumika kupima afya ya udongo na kutoa huduma ya afya ya udongo kwa wakulima bure ili kila mkulima aweze kupimiwa kipande chake cha ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni teknolojia rahisi,; kama Wizara tumeamua kuchukua hatua hii kwa sababu sasa hivi mkulima kupima afya ya udongo, kila sample inamgharimu kati ya shilingi 40,000/= mpaka shilingi 100,000/= kutokana na umbali wa eneo na maabara anayotumia. Kwa hiyo, tutatumia simple technology, lab equipment ambayo itakwenda kufanya soil analysis na soil profile na kumpatia hati mkulima kumwonyesha kwamba udongo wako huu una sifa hizi na unafaa kwa zao hili na unatakiwa kutumia hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua ya pili katika hizi Agricultural Center tutakazoweka katika kila Wilaya, tutagawa pikipiki 7,000 kwa Maafisa Ugani wa Nchi nzima katika msimu ujao na kila pikipiki tutaifunga GPS. Sasa hivi tumeanzisha ile call centre hapa Wizarani ambayo GPS hizi zitakuwa monitored from the centre kuweza kujua Afisa Ugani kama anafanya kazi katika eneo lake na tutawapatia ipad ambayo watakuwa wanajaza taarifa za call sheet za kila siku kuonesha wame-visit shamba gani na kumtembelea mkulima gani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo wameongelea sana Waheshimiwa Wabunge ni suala la research and development na mbegu. Tumeamua kama Serikali suala la research and development kutegemea donor funding, halitakuwepo. Tutaanzisha Research Fund ambayo ipo kwa mujibu wa Sheria ya TARI ili kuweza ku-mobilize fund kwa ajili ya research and development. Kwa kuanza katika bajeti ijayo tutaleta mpango wa kuzalisha tani 5,000 za OPV za alizeti ili katika msimu ujao wa kilimo tuweze kuwagawia wakulima na tuweze kupata metric tonnes, 123,000 za mafuta za alizeti kutokana na input ya hii seed. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la pembejeo, tumeamua kubadili mfumo na nataka niwahakikishie Wabunge tumefanya pilot kwenye pamba na tutaifanya kwenye korosho msimu ujao. Mwaka huu kwenye pamba tumewagawia wakulima mbegu bure. Tumewagawia wakulima dawa bure na gharama za dawa hizi tunazipata kutokana na mjengeko wa bei. Tutafanya hivyo hivyo kwenye korosho, tumeshatangaza tender safari hii tutagawa dawa za korosho kwa wakulima bure na tutawapatia dawa hizo na tumefanya kwa bulk procurement na hii itatupunguzia gharama na tunatarajia sulphur safari hii itapungua bei itakayoenda kwa wakulima na tuta-recover gharama kutoka kwenye mjengeko wa bei. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu zao la chai; tumeanza mchakato wa kuweka soko letu Dar es Salaam ambalo litakuwa ni kwa ajili ya kuuza zao la chai moja kwa moja, lakini vile vile Kiwanda cha Mponde nacho kitafunguliwa na mwaka huu tutasafirisha korosho zote kwa kutumia gunia za katani. Nitumie Bunge hili kumwambia mwekezaji ambaye ana viwanda viwili vya magunia cha Morogoro na Kilimanjaro tunampa kazi, akishindwa tutapeleka mapendekezo Serikalini kumnyang’anya viwanda hivi tuwape wawekezaji wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu irrigation tutatumia…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Muda umekwisha Mheshimiwa, ahsante sana.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: … tutatumia mfumo wa force account na hii itaonekana katika Halmashauri kama tunavyojenga miradi mingine ya shule. Kwa hiyo nataka niwaambie tu Wabunge kwamba waisubiri bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mwenyezi Mungu akitujaalia. Ahsante sana. (Makofi)
Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Viwango vya Afya ya Mimea, Wanyama na Usalama wa Chakula
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nikushukuru kwa nafasi, lakini pili nitumie nafasi hii kuwashukuru Wabunge waliotoa maoni, mengi ni ushauri ambao kama Wizara tutahakikisha tunauzingatia.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka nichangie kwa ufupi sana. Kwanza sisi tunazalisha locally tuna trade globally kwa hiyo lazima zitakuwepo threat na tunai-consider threat waliyoitoa Waheshimiwa Wabunge hasa athari ya hofu ya suala la GMO.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaambie kwamba mwaka jana tumepitisha sheria ndani ya Bunge lako Tukufu (The Plant Health Act, 2020) iliyopitishwa na ukisoma katika definition imesema wazi kabisa hii ni instrument moja tutakayoitumia ku-control vihatarishi vyote vya teknolojia za GMO. Imesema a plant means any living plant all the parts thereof, including seeds and gem plus. Sasa hivi ndiyo tunatengeneza Kanuni na mapendekezo ya Kamati tutaya- consider kwa kiwango kikubwa sana kuhakikisha kwamba tunaitumia sheria hii na mamlaka hii kuwa ni instrument muhimu ya control. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ninataka tu niseme kwamba Tanzania Plant Health Authority inatujengea uwezo mkubwa wa kuwa na maabara zetu ambazo zitakuwa Internationally Certified ambazo mazao yote ya kilimo yanayotoka nje ya mipaka yetu yakipata hati ya uthibitisho kutoka katika maabara zetu hizi itakuwa ni moja kwa moja tunaweza kuingia katika soko la Kimataifa. Kwa hiyo, hili ni jambo ambalo nilitaka niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala jingine ni hoja ya Sera ya Kilimo, tuwahakikishie kwamba tutaihuisha iweze kuendana na mahitaji ambayo ni ya sasa na kuweza ku- accommodate mahitaji yote ya protocol hii. Protocol hii inazungumzia suala la harmonization.

Mheshimiwa Naibu Spika, protocol hii pamoja na kuwa tunaipitisha leo suala la harmonization mnapoenda kwenye meza kama ninyi hamna instrument ambazo zitawafanya m-harmonize na wenzenu hamuwezi ku- harmonize chochote utakuwa out of the game.

Kwa hiyo, kwa kuipitisha leo protocol na sisi kwenda kuhuisha Sera yetu ya Kilimo na uwepo wa hii sheria ambayo imepitishwa na Bunge lako Tukufu na uanzishwaji wa hizi maabara itatujengea uwezo mkubwa wa ku-compete na wenzetu katika soko la Jumuiya Afrika Mashariki, lakini vilevile soko la Kimataifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna hoja wamesema Waheshimiwa Wabunge kuhusu maabara ambazo zipo katika baadhi ya maeneo yaani isiwe kwamba center ya maabara ni moja. Labda tuseme Nyanda za Juu Kusini tuna maabara yetu ya treat ambayo ni ya chai kama Wizara, tumeanza kuiwezesha maabara ile ili iweze kuhudumia na mazao mengine ambayo siyo specifically ya chai mfano, parachichi na mahindi. Maabara zetu za Uyole na maabara zingine tutazijengea capacity ili ziweze ku-meet mahitaji yanayotukabili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie tu kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge kwamba kama Wizara tunajua threat zinazotukabili katika protocol hii, lakini tunazo mitigation solution ambazo tunaweza kupambana nazo na tutakuwa salama huko mbele tunakokwenda.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja, nashukuru. (Makofi)
Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuanzia Januari, 2021 hadi Februari, 2022 pamoja na Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa Kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2022
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, cha kwanza nikupongeze na nikutakie kila la kheri katika kutimiza wajibu wako na kutuongoza katika Bunge ukimsaidia Mheshimiwa Spika.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili niishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ushauri waliotupa na maoni waliyoyatoa. Nataka tu niwaahidi kwamba sisi kwetu maoni, ushauri na mapendekezo yao ni working tool, tutajitahidi ndani ya Serikali kuhakikisha yale ambayo ni kwa maslahi ya nchi tunayafanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, ni kweli, concerns za Waheshimiwa Wabunge zipo, na sisi kama Wizara na Serikali tunazitambua hasa kwenye eneo la umwagiliaji, pembejeo na gharama za pembejeo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la umwagiliaji, nilitaka tu niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge na kuwaambia kwamba mapendekezo ya kuiwezesha Tume ya Umwagiliaji ni jambo ambalo halikwepeki. Tumeanza maongezi na wenzetu wa Wizara ya Fedha na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutapata fedha nyingi sana ambazo zitaenda Tume ya Umwagiliaji na tumekubaliana na Wizara ya Fedha, hivi sasa kuna miradi 19 ya umwagiliaji ambayo Tume ya Umwagiliaji imeshasaini na kupata wakandarasi, na tunaamini kwamba tutakapofika mwisho wa mwaka fedha zitatoka kwa ajili ya ku-facilitate hiyo miradi ambayo tumetangaza tender na kuwapa wakandarasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu eneo la ugani Wizara tayari sasa hivi imepatiwa fedha kwa ajili ya kuwapatia vitendea kazi Maafisa Ugani, na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mwezi wa nne tutagawa pikipiki kwa ajili ya Maafisa Ugani, na sasa hivi tuko kwenye mazungumzo na Wizara ya Fedha kwa ajili ya kuwapatia Maafisa Ugani vitendea kazi. Mara ya kwanza allocation ilikuwa ni kwa ajili ya Maafisa Ugani 1,500 lakini tunaweza kufikia maafisa ugano wote 6,300 walioko nchini ili waweze kupatiwa vitendea kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni kwamba tunabadili muundo wa Tume yetu ya Umwagiliaji ili kuhakikisha kwamba representation ya Tume ya Umwagiliaji itakuwepo mpaka katika Ofisi za Wilaya, kwa hiyo, itakuwa katika structure kama ilivyo TARURA na taasisi nyingine. Kwa hiyo kutakuwa na ma-engineer wa umwagiliaji katika ngazi ya Wilaya ili kuleta usimamizi wa karibu kwenye eneo la umwagiliaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo lingine ambalo halikwepeki, nia kwamba tunatambua Watanzania wengi wako katika sekta ya kilimo. Sekta hii inatakiwa kufanyiwa mabadiliko ya kuwepo kwa sheria inayotu-guide, kwa hiyo tutaleta mabadiliko ya Sheria ya Ushirika, tutaleta Sheria Mpya ya Kilimo katika nchi yetu ambayo itatoa legal framework ya kuisimamia sekta kwenye masuala ya resources, financing na masuala yote yanayohusu mifumo ya kodi ili kuondoa matatizo tuliyo nayo katika sekta.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge wa Arusha kwamba kuhusu subsector ya horticulture, kwamba tuko kwenye hatua za mwisho na Wizara ya Fedha na mashamba yale yatarudi na watawekeza Watanzania kwa priority na watapewa nafasi wawekezaji wa Kitanzania ili wawekeze katika subsector ya horticulture. Subsector ya horticulture ni sekta ambayo tunaipa jicho la karibu sisi kama Serikali kwa sababu ni sekta ambayo inakua na ni lazima tuendane na hali ya dunia inavyokwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie tu kuwaambia Waheshimiwa Wabunge kwamba tunashukuru kwa maoni na tahadhari zilizotolewa. Niwahakikishie tu kwamba sisi upande wa Serikali, suala la majadiliano juu ya kuifanya Wizara ya Kilimo ipate fedha ya kutosha yameshafika katika nafasi nzuri na Mheshimiwa Rais ametoa maelekezo. Tunafanya mazungumzo na Wizara ya Fedha ili Wizara hii iweze kupata fedha inazostahili kwenda kuwahudumia wakulima wa nchi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, na kuhusu kilio cha mbolea na mwelekeo wa dunia unavyokwenda, niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge hili litakuwa ni jambo la mwisho la kujadili katika nchi yetu. Ni lazima tu-subsidize kwenye inputs za kilimo, na huo ndio mwelekeo kwa sababu wakulima wetu ni wakulima wadogo; na hili tunalitengenezea legal framework na financing model ambayo tutakapoenda kutoa ruzuku basi ruzuku hiyo iweze kuwafikia wakulima, na tusifanye makosa ambayo tumekuwa nayo huko nyuma.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mimi nimalizie kuwashukuru Kamati, na niwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa maoni waliyoyatoa. Ahsanteni sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kwanza nakushukuru kwa nafasi na pili naishukuru Kamati ya PAC kwa maoni. Specifically, kwenye eneo la kilimo kulikuwa kuna hoja kubwa mbili. Moja ni hoja ya vihenge na pili ni kuhusu NFRA.

Mheshimiwa Spika, Serikali baada ya kuona mradi wa vihenge umeanza kusuasua na kumekuwa sintofahamu, Serikali iliunda Government Negotiating Team na mwaka 2021 mimi mwenyewe nilishiriki; na wakati huo, Mheshimiwa Kitila akiwa Waziri wa Viwanda ndio alikuwa leader wa ile Kamati na mpaka sasa hivi ile Kamati ipo kazini, tumekutana na wenzetu wa Poland, tumekaa kujadiliana nao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nihakikishie Bunge lako Tukufu kwamba kutakuwa hakuna overspending juu ya framework iliyokuwepo awali. Siyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala beneficiary ambaye ni NFRA haaja-violet mkataba kwa namna yoyote. Part ya YUNA, wenyewe wanaendelea na ujenzi. Sites zao tatu zimeshavuka 90%, wanaenda bila matatizo. Theorem ambaye ndio alikuwa na sites tano, alileta demand ya kuongezewa dola milioni 12 kwa sababu mbalimbali alizozitaka. Serikali imemwomba alete justification, ameshindwa, ameleta barua, anataka kujitoa kwenye ujenzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote kwamba Serikali haitaenda kuingia additional cost kwenye mradi huu. Huu ni mkataba wa kukopa, hatupewi sadaka. Kwa hiyo, mkopo una framework, nasi tutausimamia kwa maslahi ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili ni kuhusu NFRA. Serikali ina njia nyingi ya kutoa fedha kuikabidhi taasisi. Moja, wanaweza wakatoa fedha ambazo wamezibajeti na vile vile unaweza ukachukuliwa mkopo. Mkopo wa NFRA ulitolewa under guarantee ya TR, ni mkopo wa Serikali. Ili usiwe mzigo kwa NFRA baada ya ile maturity ya OD kwisha, interest inabebwa na Serikali na wala siyo NFRA. Kwa hiyo, kutakuwa hakuna burden yoyote kwa NFRA kwa ile shilingi bilioni 50.

Mheshimiwa Spika, nasi kama Serikali tumeamua badala ya ile 15 billion ikifikia ku-mature, kuoandoa ile capital mkononi mwa NFRA, Wizara tutakuwa tunatenga kwenye bajeti yetu ile cost of financing, hii 50 million itaendelea kubaki NFRA na kuifanya NFRA kuwa na liquidity, wakati huo tunaiwekea bajeti ya kila mwaka na kufanya uwezo wa NFRA kuwa mkubwa (aggregative). Kwa sababu kuna njia mbili za NFRA anafanya; pale ambapo tunakuwa na dharura kama nchi, NFRA ndiyo ina jukumu la kutoa chakula cha msaada.

Mheshimiwa Spika, pale ambapo wakulima wanapata shida kuuza mazao, tunaitumia NFRA na CPD kama stabilizing instrument kuweza kwenda kuchukua mazao kwa subsidize rate. Kwa hiyo, naomba niwatoe hofu kwamba maamuzi ya Serikali baada ya Bunge kushauri kununua mazao ya wakulima ya mahindi na model iliyochukuliwa na Serikali ni njia sahihi ambayo haina hasara yoyote na ni njia salama ya capitalize taasisi nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimalizie kusema tunashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa maoni yao, sisi tutapokea ushauri hasa kwenye eneo la mikataba. Mikataba yoyote tunayoingia hasa kwenye sekta ya kilimo niwahakikishie itakuwa ni mikataba kwa maslahi ya wakulima na wananchi na huu ndiyo mwelekeo na maagizo ya Mheshimiwa Rais, lazima kuwe na value for money kwenye any mkataba tunaoingia nao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru na ninaunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kwanza nikushukuru kwa kunipa nafasi. Vile vile niwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa ushauri na maoni yaliyotolewa kwa ujumla na niishukuru Kamati ya PAC na Kamati ya PIC zote kwenye eneo linalohusu Wizara ya Kilimo.

Mheshimiwa Spika, la kwanza nataka kuchangia maoni ya Kamati ya PAC hasa kuhusu issue ya vihenge. Ni kweli kwamba Serikali imekuwa na mkataba na kampuni mbili; Kampuni ya FERRUM na Kampuni ya UNEA, mkataba wenye jumla ya thamani ya Dola milioni 55. Kampuni ya UNEA ilipewa site tatu ambazo zimeshakamilika kwa asilimia 100 na tumeanza kuzitumia. Changamoto iko kwenye mradi unaofanywa na kampuni ya FERRUM, lakini nataka nilihakikishie Bunge lako Tukufu kwamba Serikali imechukua hatua, kwamba Kampuni ya FERRUM ilileta intention ya kutaka kuongezewa fedha zaidi ya Dola milioni 18 over and above the contractual agreement. Serikali ilikataa kutekeleza maombi hayo na mpaka sasa Serikali imeshikilia retention ya Dola milioni tatu.

Mheshimiwa Spika, tunafanya nao mazungumzo, kama hawataweza kutekeleza kutokana na scope iliyopo, tutavunja nao mkataba na tutatafuta mkandarasi mwingine kwa ajili ya kuweza kuendelea na mradi huo. Kwa hiyo, tunalichukulia in a serious note na ninaamini kwamba pamoja na maazimio yatakayofikiwa, tukija next time tutakuta jambo hili limeshaondoka kwenye meza yetu.

Mheshimiwa Spika, la pili lilikuwa ni suala la pamba, ni kweli mwaka 2019 Serikali ilitoa maelekezo kwamba pamba inunuliwe kwa bei ya Shilingi 1,200/= na kulikuwa na clear instruction na mechanism. Serikali ilishalipa hasara ya Shiligi bilioni 14, na mimi mwenyewe Kamati ya Bunge iliniita tukiwa na Waziri wa Fedha, tukakutana na kuongea na Kamati ya PIC na kuwaeleza hatua ambazo tunachukua. Kama Serikali hatua ambayo tutachukua kuliondoa hili jambo la mwaka 2019 ni kwamba tutahakikisha tutakapokwenda kwenye mwaka ujao wa fedha hili eneo tunali-resolve once and for good.

Mheshimiwa Spika, nataka niliombe Bunge lako Tukufu, ni vizuri Waheshimiwa Wabunge, suala la mauzo na manunuzi ya bidhaa sokoni, tukaheshimu soko. Mwaka 2018, 2019 tulichukua hatua ambazo zilitupeleka kwenye hasara kubwa na kutuumiza kama nchi, na leo Kamati ya Bunge na CAG wameweza kuleta mapendekezo haya yaliyotokana na influence iliyotoka ndani ya Bunge.

Mheshimiwa Spika, nashauri huko tunakokwenda turuhusu kuchukua hatua ambazo not more political kwenye masuala ya kibiashara.

(Hpa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri sekunde thelathini.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, sawa. La mwisho, Waheshimiwa Wabunge wame-comment sana kuhusu suala la kupeleka mbolea za ruzuku. Ni kweli Mheshimiwa Rais amezindua, na mimi nilishukuru Bunge lako Tukufu kwa kuweka effort kwenye eneo la kilimo na kuongeza bajeti na Serikali imeanza kutoa ruzuku. Tumetengeneza mfumo ambao una muda wa siku 60 tu.

Mheshimiwa Spika, zipo changamoto, lakini nawaomba Waheshimiwa Wabunge tuendelee kushirikiana pamoja ili kuhakikisha kwamba tunapeleka huduma hii, wakati huo huo tukimlinda mkulima, na wakati huo huo tusiruhusu kwenda kupeleka ili mfumo huu uende kuwafaidisha watu wachache badala ya wakulima.

Mheshimiwa Spika, nashukuru.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitumie nafasi nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Pili, niseme tu kwamba Waheshimiwa Wabunge tumeyasikia maoni yao na ushauri wao na ndoto zao na sisi kama Wizara na upande wa Serikali tutaendelea kuyafanyia kazi kadri ambavyo Mwenyezi Mungu anatujalia na upatikanaji wa rasilimali (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nichangie mambo machache tu. Kwanza ni ukweli kihatarishi namba moja ambacho kinatukabili kama Taifa ni mabadiliko ya Tabianchi. Kama Serikali ukiangalia kwamba ukuaji wa population unakua kwa wastani wa 3.2% na Sensa iliyopita imetuonesha kwamba umri wastani wa Mtanzania ni kati ya miaka 16 na 18 maana yake society ambayo ina watu wenye umri mdogo sana lakini sekta iliyoajiri watu wengi ndiyo ambayo ina mchango mdogo na ukuaji wake ni mdogo ni jambo la ukweli ambalo halipingiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imechukua hatua za maksudi, nalishukuru Bunge, ninamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa niaba ya wakulima, Serikali imeongeza fedha katika mwaka uliopita na tumeanza kuchukua hatua, tunazo ekeri jumla ya Milioni 29 zinazofaa kwa umwagiliaji, huko nyuma kwa muda mrefu tumekuwa tukijenga miundombinu ya umwagiliaji ambayo imekuwa inasubiri na yenyewe kudra ya Mungu mvua inyeshe ndiyo watu waweze kuitumia hiyo miundombinu. Kwa mwaka huu wa fedha tunajenga Mabwawa 13, niwatoe hofu Waheshimiwa Wabunge na Kamati ya Bajeti, hatua ya Serikali kujenga mabwawa katika maeneo ya Kati siyo hatua ya kutilia mashaka. Ni hatua ambayo umefanyika utafiti wa kisayansi na kujiridhisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajenga bwawa kubwa la Msagali liloko Mpwapwa lenye uwezo wa kuhifadhi Milioni 95m3 ambalo litamwagilia eneo kubwa la umwagiliaji. Tunajenga Mabwawa Dodoma, Simiyu, Mwanza, Singida, Tabora, Kigoma na Manyara. Haya ni kwa mwaka huu wa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua ya pili ambayo tumechukua mtaona mwaka ujao wa fedha mlitupitishia fedha hapa ya kwenda kufanya feasibility study na design kwenye Mabonde 22 ya nchi yetu, yakiwemo Mabonde ya Lake Victoria, Mabonde yaliyoko Ziwa Nyasa, Mabonde yaliyoko Mto Ruvuma. Mabonde yote haya sasa hivi tumesha-commission na watu wanafanya feasibility study ambayo tutaanza kuyajenga katika mwaka ujao wa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto inayokabili sekta ya kilimo ni tija na tija ina-equation; Kwanza ni utafiti, Pili ni uzalishaji wa mbegu, Tatu ni extension services, Nne ni kuwa na miundombinu ya uhifadhi na miundombinu ya umwagiliaji. Serikali ya Awamu ya Sita imeanza kuchukua hatua hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye uzalishaji wa mbegu mmetupitishia fedha hapa, kutoka Bilioni 15 kwa ujumla wake mpaka Bilioni 83. Tunafanya nini? Tumeanza kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwenye mashamba ya kuzalisha mbegu, ambayo toka tunapata uhuru hayakuwepo haya mashamba yakiwa na miundombinu ya umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeanza kujenga mwaka huu tunajenga hekta 95,000 kuongeza mtandao wetu wa umwagiliaji. Miundombinu ya DADPs na mingine yote ambayo ilikuwa inasubiri mvua za Mungu na yenyewe tunaijengea mabwawa. Kwa hiyo, nilitaka niwatoe hofu Waheshimiwa Wabunge kwamba hii ni hatua ambayo tunaichukua na niseme hapa kwamba kilimo ni process, hatuwezi kutegemea matokeoya kwenye kilimo kesho, ni lazima tu-invest kwa muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ambalo ninataka niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge msiwe na hofu na mashamba ya block farm, kwa nini? Vijana wengi wanaomaliza Vyuo Vikuu hawaendi kwenye kilimo kwa sababu kubwa tano: Moja, hawana ardhi, Mbili, hawakopesheki, Tatu, Teknolojia zimepitwa na wakati, Nne, suala la masoko ya uhakika. Miradi hii ya jumla ya ekari 188,000 ambayo phase one tunaanza na Dodoma na Chunya itatengeneza ajira za vijana 40,000 watakaoenda kulima shambani. Serikali inatumia Bilioni 200 gharama ya ajira moja ni Shilingi Milioni Tano. Kwa hiyo nilitaka tu niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge maoni yao tumeyapokea, tunayachukua lakini hii ni process ya muda mrefu ambayo tutaenda kufanya kazi pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe hofu Mheshimiwa Sanga ameongelea miradi ya zaidi ya Bilioni Hamsini tuliyoisaini Mbarali miradi ile haijafa. Tunaenda kujenga zile skimu zote ambazo zilisainiwa mbele ya Mheshimiwa Rais. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Haya ahsante sana. Tusaidie tu jambo moja, hayo mabwawa makubwa yanayojengwa yanajazwa na maji kutoka wapi? (Makofi)

WAZIRI WA KILIMO: Ahsante. Mheshimiwa Mwenyekiti kuna njia mbili ambazo tutajaza maji kwenye mabwawa na nitaliomba Bunge lako, Kamati ya Kilimo imeshaenda kutembelea imeona na tutafanya tour ili waone. Kuna njia mbili za kujaza maji na niseme specifically Dodoma najua hofu iko Dodoma.

MWENYEKITI: Wewe nenda hapo kwa sababu muda wetu umeenda Mawaziri wanasubiri nimeuliza swali dogo tu.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna njia mbili tu. Moja tunatega maji ambayo kipindi cha mvua yanasafiri yanayopotea. Nasi wote tunajua hapa katikati ya Dodoma, Morogoro huwa tunakaa masaa mamilioni ya lita ya maji yanapita, hiyo ni njia ya kwanza. Njia ya pili Mkoa wa Dodoma una-water reserve nyingi mno underground. Tunalo Bwawa hapo Chinangali ambalo linajaza lita milioni 32 kwa visima vitatu ambapo shamba la hekta 1000 litahudumiwa kwa mwezi mzima bila kutafuta maji sehemu nyingine. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, awali ya yote nitumie nafasi hii kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi, pili nitumie nafasi hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge na maoni waliyoyatoa kwenye hotuba wakati wanachangia hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na niwape tu commitment kwamba maoni yao na ushauri wao Wizara tunachukua na kwenda kuufanyia kazi na mengi tutayajibu kwenye hotuba yetu ya bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninataka tu niongelee eneo la kwanza kuhusu suala la upandaji wa bei ya mafuta ya kula. Pamoja na kuwa kwamba kuna vitu viwili ambavyo vinasababisha moja ni production yetu ya ndani kuwa ndogo hasa kwenye maeneo ya mafuta kama ya alizeti, lakini kama Serikali tumechukua hatua ya kwanza mwaka huu tumesambaza mbegu zaidi ya tani 2,000 na tunaraji kwamba kwenye eneo la uzalishaji katika Mikoa mitatu ya pilot tunaweza kuongeza katika uzalishaji wetu wa ndani kwa sababu uzalishaji wetu wa ndani ni wastani wa tani 240,000 za mafuta ya kula, wakati mahitaji yetu ni wastani wa tani 600,000.

Mheshimiwa Spika, katika Mkoa wa Singida peke yake mbegu za alizeti zitakazozalishwa kutokana na mbegu tani 1,000 tulizopeleka katika Mkoa wa Singida tunataraji uzalishaji wa wastani wa mbegu mpya tani 300,000 ambazo zitatuingizia kwenye uzalishaji wa mafuta lita 100,000 ya mafuta.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge kwamba mwakani kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mwaka huu tulisambaza standard seeds mwakani tutasambaza certified seeds tani 5,000 za alizeti ambayo itakuwa subsidized. Kwa hiyo, ninaamini kwamba kufika mwaka 2024/2025 tutakuwa tuna uhakika wa kujitosheleza mafuta ya kula ndani ya nchi na hasa kwa kutumia zao la alizeti.

Mheshimiwa Spika, zao la mchikichi tumeamua kwamba tu-encourage uzalishaji wa mashamba makubwa. Tayari tumeshapata wawekezaji wakubwa wawili. Mmoja atawekeza katika eneo la Rufiji na mwingine atawekeza katika Mkoa wa Kigoma na wameshaanza kufanya soil analysis na Wizara tunaendelea kuwasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatua ya pili kama Serikali tunatafakari na kuangaia tax framework ambayo inaweza kupunguza gharama ya mafuta. Mojawapo viwanda vya ndani ili tuweze kuvipunguzia VAT na kuzifanya kuwa zero- rated ili gharama ya mafuta ya viwanda viwe competitive na viweze kupunguza bei ya mafuta siku ya mwisho na kuvifanya kuwa competitive. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge kwamba Serikali itakapo-table bajeti mwezi wa Saba mtaona measures mbili za upande wa uzalishaji, vilevile mtaona measure za kidodi ambazo zitaweza kusaidia uzaishaji wa ndani lakini vile vile hata mafuta tunayo-import kutoka nje kuweza kuyapunguzia bei.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ambalo nilitaka nichangie, niwape uhakika Waheshimiwa Wabunge hatuna upungufu wa chakula ndani ya nchi. Hatuna upungufu wa chakula ndani ya nchi na kama Serikali tuna-reserve ya kutosha ambayo kwa zaidi ya miaka saba hatujawahi kuwa na reserve ya namna hii ya zaidi ya metric tons Laki Mbili ya chakula ndani ya nchi. Tukipitisha bajeti NFRA ataingia sokoni kwenda kununua mazao kwa ajili ya kuhifadhi ili tusiweze kuingia kwenye matatizo ya upungufu wa chakula ndani ya nchi, bila ku-disturb biashara ya mazao.

Mheshimiwa Spika, nishauri Waheshimiwa Wabunge tusi-restrict biashara ya mazao kwa hofu yoyote ile, kwa sababu kama Serikali tutatumia measure tulizonazo kuweza kupunguza mfumuko wa bei pale ambapo mahindi yamepanda, tutapeleka mahindi kwa bei ya Serikali ili kupunguza bei. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niseme jambo lingine kuhusu zao la korosho. Serikali mwaka jana tulifanya intervention ya kutoa pembejeo bila kulipia kwa wakulima, imetusaidia uzalishaji wa korosho msimu huu umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 10 kutoka wastani wa tani 206,000 kukaribia tani 240,000. Mwaka huu tena tutapeleka pembejeo zenye thamani ya Shilingi Bilioni 90 bure kwa wakulima wa korosho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile tutapeleka pembejeo zenye thamani ya shilingi bilioni 56 kwa wakulima wa pamba. Mheshimiwa Rais ametoa maelekezo kuhusu kutafuta njia kuanzia tarehe 01 Julai ya kupunguza bei ya mboleo kwa mazao na Serikali tunachukua hatua ili kuweza kuwapunguzia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu korosho jambo moja nataka nitumie Bunge lako. Vyama vya Ushirika vilikusanya fedha za wakulima ili waweze kuchangia kununua pembejeo, kupitia Bunge lako kuviagiza Vyama vya Ushirika vyote virudishe fedha za wakulima wote. Wakulima watapata pembejeo bila kulipia, kwa sababu Serikali inaitumia export levy kwa ajili ya ku-support zao hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilitaka niongelee hoja ya Mama Kilango.

SPIKA: Sekunde 30.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ok. Nataka tu nimuombe Mheshimiwa Mama Kilango na Wabunge wote wa Mkoa wa Tanga na maeneo yanayozalisha mazao ya viungo. Serikali imeiagiza TARI kupitia TARI Mlingano kuanzia sasa uzalishaji wa mbegu na research zote za mazao ya viungo itafanyika kwenye Taasisi yetu ya TARI - Mlingano na tunaanza uzalishaji wa mbegu kwa ajili ya tangawizi na mazao mengine ya viungo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwaombe kwamba haikuwepo kwenye plan ya Serikali kwa muda mrefu zao la viungo kama zao la kimkakati, sasa limeingia kama component ya mazao ya horticulture na tutatoa utaratibu unaostahili. Nashukuru. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa fursa na naomba nichangie hoja iliyopo mbele yetu. Kwanza nataka nitumie nafasi hii kusema, tumesikia maoni ya Waheshimiwa Wabunge na ushauri waliotupa katika baadhi ya maeneo na sisi kama Wizara tunachukua na kuyafanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza mjadala umekuwa kwenye eneo la ushirikiano katika kutumia Taasisi za Majeshi na vilevile kutumia Vyombo vyetu vya Dola katika kushirikiana kwenye Sekta ya Kilimo. Nataka kuliambia Bunge lako Tukufu hivi karibuni nadhani siyo muda mrefu mtaona kwenye Vyombo vya Habari, Wizara ya Kilimo inasaini MoU na JKT kwa ajili ya maeneo yafuatayo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, uzalishaji wa mbegu. Mbili, kwa ajili ya kutumia maeneo ambayo yanamilikiwa na Jeshi kwa ajili ya strategic crop mazao kama ya mafuta. Vilevile mbali na hapo jambo hili tulishalianza, namshukuru Waziri wa Ulinzi wa sasa na aliyemtangulia, mfano, mwaka huu wametuzalishia mbegu za alizeti tani 500, lakini vilevile mwaka huu tumesaini makubaliano na JKT Mgambo wanatuzalishia jumla ya eka 500 kwa ajili ya uzalishaji wa alizeti. Pia tunashirikiana na JKT Bulombora kwa ajili ya uzalishaji wa michikichi na sasa wameshaanza kusambaza miche ya michikichi itakayoweza kuzalisha jumla ya eneo la ekari 3,400. Kwa hiyo tumeshaanza mahusiano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nilitaarifu Bunge lako Tukufu na Kamati ya Mambo ya Nje, tumeanza ushirikiano mzuri sana na Wizara ya Mambo ya Nje na nimshukuru Waziri wa Mambo ya Nje, tumeshirikiana katika kufungua Soko la Parachichi China na sasa hivi tunashirikiana nao kwa ajili ya kuangalia namna gani tunaingia kwenye masoko ya COMESA hasa katika mazao ya tumbaku. Hivi karibuni pia tunashirikiana nao kwa ajili ya Mradi wa Maghala ambapo kuna wawekezaji wako tayari kuja kuweka. Tunafanya kazi kwa karibu na Balozi zetu zote, ingawa matokeo yanaweza yasionekane kwa haraka, lakini tumeanza ushirikiano mzuri sana na wenzetu wa Foreign.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka niliongelee ni hili eneo la mfumuko wa bei kwa ufupi tu. Serikali inachukua hatua na mpaka sasa tumeshapeleka vyakula katika halmashauri 47 katika mikoa 15 katika nchi yetu na maeneo ambayo tayari yameishaanza uzalishaji tumefunga vituo. Mfano, katika Wilaya ya Sengerema, maeneo ya Buchosa ambayo Wakulima wameshaanza kuvuna tumefunga vituo vya kuuza mazao kwa bei ya nafuu na tunaendelea mpaka sasa tumeshagawa tani 23,000, lakini vilevile tumeweka allocations ya jumla ya tani 40,000 ya mahindi ambayo tutaendelea kuiingiza sokoni na kuiuza kwa bei ya kati ya Sh.700 mpaka Sh.800 ili ku-stabilize. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba na Bunge lako Tukufu lituelewe, hatuwezi kuondoa mfumuko wa bei kwa kuja na shortcut. Ni lazima tuongeze tija na ndiyo maana Serikali inawekeza kwenye maeneo ya umwagiliaji, inawekeza kwenye kutoa ruzuku za mbegu, tunatoa ruzuku ya mbolea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka niseme tu Mradi wa Block Farm wa vijana; tunao vijana ambao wanatoka JKT aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ulinzi alisha-submit majina ya vijana ambao katika phase one tunaanza nayo, tutawachukua hao vijana kwenda nao kwenye hii project, hatuwaachi vijana waliyopo JKT, lakini lazima miradi hii iende parallel, maeneo ya JKT wataendelea kuwa-accommodate vijana na sisi tunaya-develop kupitia Wizara ya Kilimo tutawa-accommodate vijana wote. Ni Mpango ndiyo tumeanza, kunaweza kukatokea marekebisho, tutaendelea kurekebisha wakati tunakwenda mbele. Hata hivyo, la msingi lazima vijana wamiliki ardhi ili kuwafanya vijana wa nchi kuwaondoa kwenye kundi la watu wasio miliki ardhi na kuwaondoa kwenye hatari ya kuwa manamba katika nchi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie eneo la ruzuku ya mbolea. Cha kwanza niwahakikishieni Waheshimiwa Wabunge mfumo wetu wa ruzuku wa mbolea ni mfumo bora kuliko mifumo ambayo tumewahi kuwa nayo huko nyuma. Mfumo wetu wa ruzuku unamtambua mkulima na niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge, hofu ya kwamba tunaibiwa, kama tusingekuwa na Mfumo huu unaomtambua mletaji agrodealer, mkulima, hata mbolea ambazo zinatokea ubadhirifu tusingeweza kuzikamata. Niwahakikishie sitoingia kwenye record ya historia ya nchi kuwatia umaskini wakulima wa nchi hii kama baadhi ya watu walioingia kwenye record ya kuwatia umaskini wavuvi wa nchi hii. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa. Nitachangia katika maeneo makubwa mawili; la kwanza Taarifa ya CAG imeongelea eneo la umwagiliaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli findings za CAG kwenye Miradi ya ERPP na hata iliyokuwa miradi ya DADPUS ni sahihi na ripoti hii ya CAG ndio imekuwa msingi mkuu wa sisi kufanya mabadiliko katika Tume ya Umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Miradi ya ERPP ambayo Mheshimiwa Deus ameitaja ni miradi ambayo ilikuwa funded na World Bank na mfumo ule wa funding ulikuwa unaamua wenyewe namna ya kuwapata hadi Wakandarasi, hili ni jambo la kwanza. Wizara tumefanya mabadiliko sasa hivi ni sisi ndio tuna-design namna gani external funding ziende kwenye miradi ya umwagiliaji na hatutatekeleza mradi wowote wa umwagiliaji ambao hauna visibility study wala detail design. Hili ni jambo la kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili miradi hii ya DADPs na ERPP kwa mfumo ulivyokuwa Tume ilikuwa makao makuu na sote tunafahamu katika Bunge hili. Nimekuwa Mbunge toka 2015, tumepitisha bajeti mbalimbali za Wizara ya Kilimo, tulikuwa hatutengi fedha za usimamizi wa umwagiliaji na sisi ndio tulikuwa tunapitisha fedha. Meneja wa Umwagiliaji wa Mkoa kwa mwaka anatengewa milioni mbili, tunatarajia muujiza. Sote tukiri hatukuweka concentration kwenye irrigation as a country for a very long time. Kwa hiyo tuchukue yale matokeo ya nyuma kama lesson wakati tunafanya reform. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Serikali inafanya nini? Sasa hivi tunaajiri Mainjinia 350, kila Wilaya tutapeleka Injinia wa umwagiliaji na Mheshimiwa Rais mwezi Machi atazindua magari ya Tume ya Umwagiliaji kwa ajili ya kupeleka katika kila wilaya ili tuweze kusimamia miradi ya umwagiliaji na fedha tunazopeleka katika eneo la umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la pili ambalo nataka niseme na Mheshimiwa Katani ametoka na hapa tumekuwa tunajadili. Je, bei inayoonekana sokoni anaipata mkulima ama haipati mkulima? Tumefanya survey kama Wizara na tuko tayari ku submit ripoti mbele ya Bunge hili. Mkulima wa mpunga msimu wa 2020/2021 na msimu wa 2021/2022 bei aliyoipata shambani ni mara mbili kuliko bei aliyoipata msimu wa 2020/2021. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili lazima watu tuelewe, msimu wa 2021/2022 sote sisi tunafahamu tumeishi na wakulima. Mkulima aliyeenda shambani kulima heka moja ya mahindi, alitumia shilingi 300,000 kwa ajili ya mbolea ya kupandia, alitumia shilingi 240,000 kwa ajili ya mbolea ya kukuzia, alitumia shilingi 60,000 kununua mbegu, alitumia shilingi 60,000 kulimia, alitumia wastani wa shilingi 40,000 kupandia na kupiga halo. Cost of production ilikuwa ni shilingi 720,000, tuna expect kitu gani kwamba auze, sisi Serikali NFRA tumenunua mahindi kwa wastani wa shilingi 700 na shilingi 800, haya tunayoyauza kwa shilingi 700 na shilingi 800 tuna- subsidize as a government.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli, wote tunafahamu kwenye commodity trading. Naomba hili nilisema kwa heshima kabisa, mkulima anayelima Nzega au anayelima Mbarali hutarajii ndio afikishe zao Soko la Dar es Salam lazima kuna intermediary. Ni jukumu letu kuviwezesha Vyama vya Ushirika viwe central aggregating na ndio hatua ambayo Serikali inachukua, ndicho tunachokifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaambie ukweli, there is no way tutaondoa intermediaries. Tunachotakiwa kuangalia kama bei ya mlaji imeongezeka kwa asilimia mia kwa mkulima aliyeko shambani ka-benefit kwa asilimia ngapi kutoka kwenye ile asilimia mia, hili ndio la msingi. Sasa hivi Mheshimiwa Esther katolea mfano Tarime, Serikali imefanya nini? Tumevi-unlock Vyama vyote vya Kahawa, Pamba, Tumbaku vyote. Tumevipa mandate mbili ku aggregate cereals na ku-aggregate mazao yao ya biashara yanayoitwa, kwa sababu the biggest business itakuwa chakula. There is no way tutakimbia kwenye huu ukweli. Ni lazima sisi kama Serikali na sisi kama Wabunge, tum-protect mkulima, lakini hatuwezi kum-protect mkulima bila kufanya proper investment kwenye infrastructure. Serikali imetoa fedha mwaka huu, inajenga maghala 70, tuna-revive masoko ya Tarime, tuna-revive soko la Ngara, tuna-revive soko la…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Nimekuongezea sekunde 40 endelea Mheshimiwa Waziri wa Kilimo.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimalizie kwa kusema hivi, hakuna njia tutamwondoa mfanyabiashara kwa mazao, hakuna.

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna njia tutamwondoa mfanyabiashara kwenye mazao. Vile vile hakuna njia tutakwepa forces za demand and supply kwenye soko. Bungeni hapa tuliilazimisha Serikali kwenye Korosho, tumeenda kuwatia hasara wakulima. Bungeni hapa tuliilazimisha Serikali ku-intervene kwenye pamba, tukatoa One thousand and two hundreds ambayo haiko sokoni.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo tuna-struggle na matatizo ya pamba, it was this Parliament iliyoifikisha Serikali kununua pamba kwa shilingi 1,200 ambayo haiko sokoni. Aliyepata hasara ni mkulima. We will never allow this. Never government intervention ku-disturb soko. Tutapunguza gharama za ununuzi, tutapunguza gharama za uzalishaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo ndiyo best practice, tutaongeza tija, tutaendelea kupunguza gharama za production ili mkulima azalishe kwa gharama ndogo, auze anakotaka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nitumie nafasi hii kwa fursa hii uliyonipa; na mimi naomba nichangie. Kwanza nisema naunga mkono hoja. La pili, niwashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa ushauri waliotupa kwa upande wa Serikali na nataka tu niwahakikishie kwamba kwa Wabunge kusema wazi mawazo yao inatusaidia sisi upande wa Serikali kuweza kutambua na kuelewa kwamba kwenye planning zetu tunatakiwa kuchukua hatua zipi za muda mfupi na za muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli kwamba hatujitoshelezi kwenye mafuta ya kula. Lakini ni ukweli kwamba upandaji wa bei ya mafuta ya kula unasababishwa na mambo makubwa mawili. Yapo yaliyopo ndani ya uwezo wetu na yapo ambayo yapo nje ya uwezo wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama nchi tunatumia wastani wa tani 650,000 kwa mwaka ya mafuta ya kula. Uwezo wetu wa uzalishaji ni wastani usiozidi tani 250,000 – 300,000; asilimia 70 ya haya mafuta tunayozalisha yanatokana na mafuta ya alizeti. Linapotokea tatizo duniani kama lilitokea la COVID, Ukraine, upande mmoja ni balaa lakini upande mwingine ni fundisho ambalo sisi kama taifa na watanzania; linatufundisha kwa sababu hapa tulipo ni maamuzi tuliyoyafanya kama taifa miaka ya 90; tulipoamua kuacha ku-protect sekta yetu binafsi na ku-protect viwanda vyetu it was a policy na ilifanywa na watanzania wote; na sheria zingine zilipita ndani ya Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo baada ya matatizo ya COVID nchi inajadili kwa nini hatuna mafuta ya kula? Baada ya matatizo ya Ukraine nchi inajadili kwa nini hatuna mbolea? Si kwamba hakuna rasilimali, Tanzania ilikuwa na Tanzania Fertilizer Company tuliamua; kwa hiyo kama tumeamua kama nchi kutubu kurudi kwenye misingi let us take a responsibility as a country; isiwe kuinyooshea kidole Serikali, isiwe kuinyooshea kidole Serikali, Serikali ilitekeleza maamuzi yaliyopitishwa na Bunge hili hili na sheria zilipitishwa humu humu ndani. Tuliamua kwenda kwenye mfumo wa uholela; tukaua mambo yetu ya msingi kama nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Sita inachukua hatua gani? Moja, tunachukua two policy direction ambazo tunafanya Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha. Cha kwanza, mwaka huu tumefanya pilot ya kugawa mbegu kwa mikoa mitatu; tumegawa kwa ruzuku. Nataka niseme na sisi tuwe wakweli kwa sababu siku ya mwisho we will all die, tutakwenda kuhukumiwa kwa Mungu. Dhana ya kufikiri Serikali haina jukumu la kulinda sekta binafsi kwa ku-protect viwanda vyake vya msingi ni dhana potofu. Kwa sababu sasa hivi all over the country wanainyooshea kidole Serikali and we forgot kuwa ni sisi ndio tuliamua kutokulinda viwanda vyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Sita imeamua ku-protect na Serikali ya Awamu ya Tano ilianza; tume-protect sekta ya sukari kwa uweo wa Mwenyezi Mungu 2025 tutajitosheleza. Serikali sasa hivi kuhusu viwanda vidogo vidogo vya sukari tunafanya nini? Wizara kupitia Bodi yetu ya Sukari kwa kushirikiana na TEMDO tunatengeneza portal types small industries za ku-process metric tons 10 kwa siku ya miwa ambayo itatupatia tani 24 kwa mwezi ili tuweze kuwapa vyama vya Msingi vya Wakulima. Anayegharamia ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kazi hii inafanywa na TEMDO na tutatengeneza hivi viwanda vidogo tutawagawia wakulima ili AMCOS katika ngazi za chini waweze ku-process sukari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekit, tunafanya nini kwenye mafuta ya kula? Tumegawa mbegu tani 3,000 na mwaka huu kwa uwezi wa Mwenyezi Mungu mkipitisha bajeti ya Wizara ya Kilimo tutagawa certified seeds tani 5,000 kama ruzuku kwa wakulima. Lakini kugawa mbegu peke yake hakutoshelezi lazima viwanda viwe competitive; tumejadiliana na Wizara ya Fedha tunachukua hatua za kikodi ili kuvilinda viwanda vyetu vya ndani ili viweze kuzalisha mafuta ya alizeti na siku ya mwisho yaende sokoni. Hatutomaliza tatizo la kujitosheleza mafuta kwa mwaka mmoja; lakini kwa uwezo wa Mungu ndani ya miaka mitatu tutajitosheleza na tutakuwa na mafuta ya kutosha ya alizeti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wameongelea sana sana suala la mafuta ya kula; hatua ya pili tunachukua kwenye palm oil. Ukienda kwa mama ntilie hakaangi vitumbua kwa kutumia mafuta ya alizeti, anatumia mafuta ya mchikichi; ukienda kwa mama ntilie anatumia mafuta ya mchikichi. Sisi kama Serikali hatua tunayochukua wakati tuna-develop kwa muda mfupi mafuta ya alizeti long term tunakwenda kwenye palm. Tumeanza kuwapa wawekezaji wakubwa maeneo makubwa kwa ajili ya kulima mchikichi. Kwa muda mrefu mchikichi na lazima tuelewe kuna kitu kinachoitwa economies of scale. Mchikichi hauwezi kuwa profitable kwa kulima heka moja halafu tukadhani kwamba yule Muha wa Kigoma anaye-crush mchikichi na kuzungusha kwenye pipa siku ya mwisho yale mafuta yataweza kuwa competitive sokoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachukua hatua gani? Tumepata wawekezaji wakubwa ambao tunawapa 10,000 hectares; moja tunampa Bakheresa hekta 10,000 down stream ya Rufiji kwa ajili ya kuweka michikichi, tuta-develop pembeni yake small scale farmers yeye ndiye atakayenunua na ku-crush ndipo pote duniani wanavyofanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kule Kigoma tumegawa michikichi, Serikali inachukua hatua gani? Tutaweka viwanda vidogo katika eneo la Kigoma Manispaa ili miche tuliyogawa mwaka jana na mwaka juzi ambayo inakaribia ku-mature iweze kuweza kupata sehemu ya crushing. Nini nataka nimalizie, mimi nataka niseme jambo moja; suala la kilimo na kujitosheleza kwenye masuala ya msingi hasa mafuta ya kula, fertilizer, sukari ni suala la lazima. Tunawaomba Waheshimiwa Wabuge waiunge mkono Serikali kwenye hatua tunazoanza kuchukua kuanzia mwaka ujao wa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili suala la mbolea; ili viwanda viweze kupata rasilimali lazima mkulima azalishe; gharama za uzalishaji zikiwa kubwa mkulima hawezi kuzalisha na hata atakachozalisha kiwanda hakitaweza kununua. Kwa hiyo, ni lazima tukubali kama nchi tuanze kutoa ruzuku kwenye maeneo ya msingi na tuwaombe Waheshimiwa Wabunge Serikali inachukua hatua ya kupunguza gharama za riba, Serikali itachukua hatua za kikodi kuanzia mwaka ujao wa fedha kwa ajili ya kulinda industries ambazo ni muhimu; Serikali itachukua hatua ya kutoa ruzuku kwenye mbegu za mazao ya mafuta. Tutatoa ruzuku kwenye mbolea ije jua ije mvua tunawaomba mtuunge mkono kwenye hatua hizi; tuache kushauriwa kwamba Serikali haitakiwi ku-intervene kwenye maeneo ya msingi ni lazima tu-intervene this is the small economy, sekta yetu binafsi bado ni changa inahitaji Government intervention. Tutakapochukua Government intervention tunawaombeni mtuunge mkono kwenye masuala ya msingi ya kutoa subsidy. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Hoja Kuhusu Bei ya Kuuza na Kununulia Mahindi
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wenzangu, nataka tu niwahakikishie, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Chama cha Mapinduzi haiwezi ku-institute sera wala utaratibu unaokwenda kummaliza mkulima. Hili ni jambo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, je, Serikali imezuia kuuza mazao nje? Jibu, Serikali haijazuia kuuza mazao nje. Pili, kuna hoja imesemwa na hata dakika tatu zikiisha naomba uniongezee nataka niongee pole pole kwa heshima, kwa unyenyekevu ili wanielewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mfumo wa kutoa export permit unafanya kazi ama haufanyi kazi? Jibu, mfumo unafanya kazi. Jana peke yake tumetoa export permit zenye jumla ya tani 3,640 kwa siku moja. Toka tarehe Mosi mpaka siku ya tarehe 22 tumetoa export permit zenye jumla ya tani 32,000. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa naomba mnielewe, kwa nini tumeweka utaratibu? Wiki iliyopita Wizara ya Kilimo tumepokea notice kutoka Mamlaka ya Afya na Chakula ya nchi ya jirani ikitu-notify kwamba mahindi yetu yaliyoingia kwao moisture content ni 18 percent. Mnataka tuue soko hili? Yaani nataka nijiulize hili swali, ni lini tunataka kuruhusu tuanze kufungua border tupeleke nje ikitokea condemnation moja tu inaua biashara yetu yote, na ni akina nani wanaopeleka? Siyo wafanyabiashara wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Aeshi yuko pale huwa ananunua mahindi Zambia, muulizeni lini kaenda kununua mahindi kama yeye? Lazima apitie kampuni ya Wazambia. Why do you want foreigners to come and go to our farms? Mnataka kuua small business? Yaani mtu atoke nje aingie kwenye mashamba ya nchi hii, aondoke na lori lake nimpe phytosanitary? sitampa phytosanitary, foreigner yeyote anayetaka kununua mazao ya Watanzania aingie asajili kampuni, aingie mikataba na makampuni ya Watanzania, hilo la tatu.

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho. Ni hivi siwezi kuwa Waziri wa Kilimo ambae anataka mkulima akose soko la mazao ya chakula, tutayauza mazao ya chakula kwa utaratibu maalum. NFRA imefungua vituo, leo Magazeti yametangaza vituo 44 katika Mikoa minane na tumetangaza bei ya kununulia kati ya shilingi 600 mpaka 1,000 kutokana na kituo. Kuna hoja kwamba masharti ya NFRA siyo marafiki. Ni hivi, huko nyuma Serikali haikuwa na miundombinu ya kukaushia mazao. Tumeshafungua maghala manane na Mbunge wa Sumbawanga Mjini yule pale shahidi, katika kituo cha kwanza tulichoanza kununu mahindi nchi hii ni Sumbawanga Mjini. Tumenunua mahindi mpaka yana moisture ya 15 tunayaingiza kwenye mashine tunayakausha, ile asilimia tatu inayopotea tunaiongeza kwenye cost of our production, hatuendi kuchambua.

Mheshimiwa Spika, tumewaagiza NFRA mkulima akifikisha mahindi kwa kuwa tunajua wakulima wetu wanapovuna huwa wanapiga kwa fimbo yanakuwa yana uchafu, ten to 15 percent ya hayo mahindi yanakuwa yana uchafu. Tumewaagiza NFRA chukueni mahindi kwa wakulima, kwa kuwa Sumbawanga Mjini, kwa kuwa Manyara, kwa kuwa Katavi, haya maghala na vihenge vimekamilika, tutayapeleka hayo maeneo hayo, tutayakausha yatakuwa na moisture inayotakiwa, tutayasafisha ten percent wastage tunayoipata tunaiingiza kwenye gharama yetu ya ununuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwaombe Waheshimiwa Wabunge na ninataka nitumie nafasi hii kuwatangazia wakulima, usiuze mahindi yako kama uko Mkoa wa Katavi chini ya shilingi 800, usiuze mahindi yako kama uko Kiteto chini ya shilingi 800, usiuze mahindi yako kama uko Sumbawanga chini ya shilingi 800 na Serikali inachukua hatua hii ya kutoa bei elekezi ili competitors wote wanapotaka kuyanunua mahindi wayanunue juu ya bei ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu hoja ya CPB.

SPIKA: Haya Mheshimiwa malizia dakika moja.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kama kuna changamoto tutazirekebisha, kama kuna changamoto lakini tukubaliane asisafiri mtu yeyote kutoka Mkoa mmoja kwenda Mkoa mwingine kama hana leseni ya biashara. Hii dhana ya kuwafanya wafanyabiashara na Watanzania walioko kwenye sekta ya kilimo kulitumia neno “wanyonge” neno wanyonge lisitumike kuhalalisha mambo ya ajabu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwaombe sana, tutarekebisha kama kuna changamoto kama kuna difficulties za mfumo tuliouweka tutaupitia lakini hatujafunga mipaka, hatutafunga mipaka, lakini hatutaruhusu mtu yoyote kutoka nje kuingia shambani anunue kupitia Watanzania, asajili kampuni na yoyote anayetaka ku-trade a-trade kwa mujibu wa sheria za nchi hii na walioingia mikataba na CPB Mheshimiwa Mbunge wa Iringa Mjini…

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri, malizia.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, waliolipa fedha kwa CPB wana mikataba, na mikataba imeonesha kwamba wametoa benki, wale wamekuwa wajanja, walisaini mikataba ya bei ya juu walivyoona mavuno yameanza wanataka kurudi ku-renegotiate, wameshasaini mkataba fedha hazitarudishwa, watayachukua mahindi kwa bei ya shilingi 900 waliyosainia mikataba na tumeshawapa CPB export permit wawape hivyo vibali vya kupeleka nje, lakini watapeleka nje kwa bei ya mikataba tofauti na hapo hatutaruhusu. (Makofi)
Hoja ya Kuazimia Kuwahamisha Maafisa Ushirika katika Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Maafisa Ugani chini ya Wizara ya Kilimo
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, cha kwanza nianze kukushukuru kwa kunipa nafasi na nianze kwa kusema mambo mawili makubwa. Changamoto ambazo mtoa hoja amezitaja ni changamoto ambazo zipo lakini changamoto hizi msingi wake ni changamoto zinazotokana na administration ni suala la utawala. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, dhana ya D by D Wizara ya Kilimo haina mkulima Wizarani. Mkulima yuko wilayani na kule wilayani aliko anatakiwa asimamiwe na Afisa Ugani aliyeko wilayani. Kama Wizara na Bunge lako tukufu lilitielekeza hapa kwamba tulete mabadiliko ya sheria ya ushirika ambayo tunaifanyia kazi ili tuweze kutatua changamoto zilizopo kwa sababu hoja siyo kwamba nani amsimamie nani? Hoja iliyoko ni kwamba afisa kilimo aliyeko katika ngazi ya halmashauri atimize wajibu wake na kufanya kazi inayostahili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi sasa hivi kama Wizara tukishirikiana na wenzetu wa TAMISEMI tunapitia Sheria ya Tume ya Ushirika ambayo itayapitia mapungufu yote ya kiutawala yaliyoko na ya usimamizi katika sekta ya ushirika. Vilevile, tunapitia upya Sheria ya Tume ya Umwagiliaji ambayo inatupa mamlaka ya kwenda kuanzisha ofisi za umwagiliaji katika ngazi ya wilaya na kuweza kuwasimamia maafisa kilimo walioko katika ngazi ya wilaya na vijiji bila kuathiri D by D. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nawaomba Waheshimiwa Wabunge watupe nafasi wasubiiri tulete mabadiliko ya sheria hizo halafu tutatoa ushauri kutokana na jambo…(Makofi)
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Nani anataka kutoa taarifa? Sawa Mheshimiwa Zuberi Kuchauka.

TAARIFA

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, nataka nimpe taarifa mzungumzaji amechangia vizuri. Shida iliyopo ukienda kwenye kata zetu kama mtendaji kata hayupo hachukuliwi mwalimu mkuu akawe mtendaji wa kata wala hachukuliwi mganga mkuu akawe mtendaji wa kata anachukuliwa afisa kilimo ndiyo anaenda kukaimu mtendaji kata kwa maana wanaonekana kwamba maafisa kilimo wa kata hawana shughuli. Halafu hoja nyingine inakuja wanasema hawa maafisa kilimo…

SPIKA: Mheshimiwa taarifa huwa ni moja tu Mheshimiwa. Mheshimiwa Bashe unaipokea taarifa hiyo?

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, taarifa yake ni suala la utawala tu ni suala la usiamamizi, ni suala la maafisa kilimo kutokusimamiwa na kutokufanya kazi na ni suala la maafisa kilimo kutokuwezeshwa. Kwa hiyo, ninachotaka ni-appeal kwa mtoa hoja na ni-appeal kwa Waheshimiwa Wabunge kama Waziri wa Kilimo ninaesimamia sera na masuala ya uratibu wa shughuli za kilimo ninatambua changamoto zilizoko katika ngazi ya halmashauri, ninatambua matamanio ya Waheshimiwa Wabunge na ninatambua matamanio ya wakulima.

Mheshimiwa Spika, niwaombe Waheshimiwa Wabunge mtuache tumalizie kazi tunayoifanya ndani ya Serikali ili kutatua changamoto zilizoko zinazowakabili maafisa ugani na zinazokabili suala la ushirika ambazo… (Makofi)

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Spika, taarifa.

WAZIRI WA KILIMO: na maafisa ushirika ambazo zitatuliwa… nimalizie, ambazo zitatuliwa tutakapoleta mabadiliko ya sheria ya Tume ya Ushirika…

SPIKA: Haya ahsante sana kuna taarifa…

WAZIRI WA KILIMO: lakini tutakapoleta mabadiliko ya sheria ya Tume ya Umwagiliaji bila kuathiri…

SPIKA: Kuna taarifa Mheshimiwa Bashe, Mheshimiwa Ole-Sendeka

TAARIFA

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa niungane na mawazo mazuri sana ya Mheshimiwa Bashe. Naunga mkono hoja ya kutungwa kwa sheria inayowadhibiti hawa maafisa wa ushirika. Mheshimiwa Bashe ni shahidi alipokuja Njombe alikuta ufisadi wa vyama vya ushirika na tukalazimika kuwakamata wale waliohusika ambvapo baadae tulikusanya shilingi bilioni 5.5 kutoka kwa mafisadi wa vyama vya ushirika na SACCOS. Sheria ilikuwa vibaya tulipokuwa tunaomba ushauri wanasheria. Kwa hiyo, sheria ibadilishwe bila kuathiri D by D.

SPIKA: Haya huyu nadhani yeye hajatoa taarifa ameunga mkono unachosema na kengele imeshagongwa, sekunde 30 malizia.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nataka nimalizie kwa kumuomba mtoa hoja kama Serikali tunafahamu tatizo linalokabili Sekta ya Ushirika na tunafahamu tatizo linalokabili Sekta ya Ugani. Watupe nafasi tumalizie michakato hii ya kisheria ambayo itaenda kutatua masuala ya utawala na ugatuaji lakini vilevile itatatua tatizo la upelekaji wa rasilimali na usimamizi wa maafisa ugani. (Makofi)
The Written Laws (Miscellaneous Amendment) Bill, 2016
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia. Jambo la kwanza niseme naunga mkono uswada aliouleta Mheshimiwa Attorney General, hasa katika mabadiliko ya Economic Crimes kwa kuanzisha Division Maalum ya Mahakama ya Mafisadi.
Mheshimiwa Naibu Spika, uanzishwaji wa Division Maalum ya Mahakama ya Mafisadi, unaonesha commitment na dhamira njema ya Serikali ya kutaka kupambana na rushwa. Nina jambo moja tu la kutaka kushauri, kiwango cha one billion shilling ni kiwango kikubwa sana, ingawa dhana na hoja ya Mheshimiwa Attorney General ni kutaka kupunguza kuwepo kwa kesi nyingi na labda Division hii kufanya kazi zake kwa haraka zaidi na kutoa hukumu.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukitazama trend ya ufisadi ilivyo katika nchi yetu, pamoja na uwepo wa rushwa kubwa, kuna rushwa za kati, ambazo nyingi zinaathiri katika level ya Central Government na rushwa hizi zinaathiri moja kwa moja watu wetu. Kwa hiyo, ningeshauri Serikali kuangalia uwezekano wa kubadilisha kiwango hiki, kutoka shilingi bilioni moja kushuka chini angalau kuanzia at least a hundred million kwenda juu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu tutakwenda kurundika kesi katika Mahakama zingine katika hujumu uchumi za milioni 500, 600 kwenda kupambana kwenye Mahakama zetu ambazo zinakumbana na kesi mbalimbali na dhana nzima ya kupambana na rushwa itakuwa kidogo imekosa nguvu. Hapa wataalam wa kula rushwa watakuwa wajanja tu, watahakikisha rushwa zao zinakuwa less than one billion ili wasiende huko.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nafikiri hilo tulitazame, lakini kwa kweli katika jambo jema ni kuanzisha hii Division kwa sababu tunao mfano wa Mahakama ya Biashara, zinakwenda kesi nyingi tu kule, bila kuangalia ambazo zina nanihi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ningeshauri its very important tuangalie kuipa kiwango cha kutosha, wote tunaelewa rushwa kwenye Local Government inaonekana na tukiweka hii loophole ya one bilion wajuzi na wataalam wa kutengeneza besinga kama ambavyo watoto wa mjini wanavyosema, watahakikisha besinga zao zinakuwa divided into less than one billion shillings, wanapata exit door. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ambalo nataka nishauri, its very important ku-maintain dhana ya separation of power na mihimili hii kukaa tofauti na hapa ndiyo naona umuhimu wa Bunge, kuhakikisha tunasukuma kuwepo kwa Mfuko Maalum wa Mahakama kama ambavyo kisheria uko Mfuko Maalum wa Bunge ili Serikali iwe inapeleka fedha kule. Kumwambia Chief Justice anapotaka kumteua mfano, TRA Appealing Board, ile ni Mahakama kabisa na wanaokwenda kwenye dispute pale ni wafanyabishara na Serikali kuhusiana na kodi. Sasa tunapomwambia Chief Justice, katika kumpata huyu Jaji wa kuendesha hii Bodi, ashauriane na Serikali, appointment ya Jaji huyu, itakuwa directed, inaonekana kabisa kuna influence ya Serikali. Kwa hiyo, ili tuipe Mahakama, kwa sababu Bodi hii ni ya Kimahakama, ningeshauri suala hili aachiwe Jaji Mkuu mwenyewe kum-appoint huyu Jaji atakayeendesha hii Appeal Board.
Mheshimiwa Naibu Spika, the same kwenye development za Division, tunamwambia Chief Justice a-consult na Rais, Rais ana mhimili wake, Chief Justice ana mhimili wake. Kwa hiyo, ili kuhakikisha tuna-create separation ya hii mihimili hii, ni muhimu sana kumpa Jaji Mkuu haki ya kuweza kujiamulia katika masuala yanayohusiana na Mahakama asiweze kuingiliwa na Serikali ama Bunge ili mihimili hii iweze kuendelea kuheshimiana na kuhakikisha kwamba tunatenda haki kwa watu wetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ya kwangu yalikuwa ni hayo na hili jambo la kuanzishwa Mahakama ya Mafisadi ni commitment kwa wananchi na tusitoe loophole ya wataalam wa kisheria, Mheshimiwa Naibu Spika wewe ni Mwanasheria, AG ni Mwanasheria na Wataalam wa Sheria wako hapa, mtu hata akiiba anakuja kusema nimeiba, sasa natokaje hapa? Hii ni exit door ambayo wataalm wa sheria wanaweza wakaitumia sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari wa Mwaka 2016
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza niseme tu kwamba nafurahi kuwaona ndugu zetu wamerejea, tuko pamoja ndani na niseme tu kwa ufupi, dunia ina-evolve kama alivyosema kaka yangu Msigwa, dunia na mataifa yanabadilika kwa stage mbalimbali, lakini wanaopambania haki hawakimbii mapambano hata siku moja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninukuu sehemu au ni-copy baadhi ya maneno aliyosema kaka yangu Lema na nayasema haya kwa nia njema kwamba pale ambapo sisi Wabunge tunakuja Bungeni, tunalipwa na nchi hii kwa kodi za watu maskini kuja kuisimamia Serikali na sisi tunalalamika kwamba Serikali imevunja Katiba, imevunja sheria, it is our duty kuisimamia Serikali. Tuunganeni, tufanye kazi yetu kuisimamia Serikali itimize wajibu wake. Siyo fair na ninyi kuwa sehemu ya kulalamika, je, waliotupigia kura? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nayasema haya kwa sababu sisi wote ni waathirika wa kila jambo. Pale ambapo tunataka kujivua responsibility na kutaka kuonyesha kwamba responsibility hii na madhambi haya ni ya Wabunge wa CCM tu, it is your duty also kusimamia Serikali hii. Hata kama yale uliyopendekeza hayajapitishwa, siku ukifa wewe mtoto wako atakuta kwenye kumbukumbu za nchi hii kwamba my father or my mother stood for this. Kwa hiyo, mimi nataka niseme ili kwamba tusisuse, ni ya kwetu sote, it is our duty kuungana kutafuta haki na yale ambayo tunaamini ni ya watu wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nichangie mafupi. Tunazo sheria mbalimbali, kuna umuhimu wa Waziri wa Sheria kwenda kufanya harmonization. Niwaambie Waheshimiwa Wabunge, mimi natoka kwenye vyombo vya habari, sababu ya kuifungia Mseto ni Afisa wa Serikali alipeleka taarifa ya uongo matokeo yake kaadhibiwa Mseto na wala siyo mtoa taarifa. With this sheria, tukisimama firm tuweke clause ya kutaka pamoja na kuadhibu publisher au mtangaza taarifa aliyetoa taarifa naye aadhibiwe, it is our duty.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tunazungumzia access to information tunaweka time ya siku 30, why? Information unayoipata muda umepita is not valid information. Kwa hiyo, mimi ningeomba Serikali hiki kipengele cha siku 30 tukiondoe. There is no need ya kuweka limitation ya information kuiwekea time frame, tusiruhusu hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, section 16(1) inasema:-
“The information holder may defer the provision of access to information until the happening of particular event, including the taking of same action required by law or some administrative action, or until the expiration of a specific time, where it is reasonable to do so in the public interest or having regard to normal and proper administrative practices.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, why do we create monopoly? Why do we create bureaucracy kwamba huyu mtu can just decide kukunyima tu taarifa until happening of an event, who is defining that event? Kuna tatizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukienda kifungu cha 6(3)(b) kinasema:-
“…information relating to national security includes-
(b) foreign government information with implications on national security.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, sijaelewa, nataka clarity on this. Mimi Afisa wa Serikali, nimepata taarifa za foreign nation related to security of the country nikazitoa nje ninaadhibiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini subsection 2(f) of section 6 inasema:-
“Infringe commercial interests, including intellectual property rights of that information holder or a third party from whom information was obtained.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna-restrict commercial interest. Wamesema Waheshimiwa Wabunge hapa, commercial interest zipi ambazo tunazizuia ambazo zinaweza zikaathiri usalama wa nchi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, section 19(3) inasema:-
“Any person agrieved by the decision by the head of institution made under subsection (2) may, within thirty days from the date of receiving such decision, appeal to the Minister whose decision shall be final.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, the highest authority ku-interprete sheria na kutafuta haki ni mahakama. Why tunamwambia Waziri tu ndiyo afanye final decision? Why? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, section 24 inasema:-
“Officers in the service or employment of any information holder shall not be subject to any civil or criminal liability for any act done or omitted to be done in good faith…”
Mheshimiwa Mwenyekiti, nani anaye-define hii good faith? My question is kwa nini kipengele hiki kisim-protect third party aliyefanya taarifa hizi kuwa public in good faith?
Ningemuomba Mheshimiwa Waziri kwa kuwa civil servant huyu au afisa tumempa protection ya civil case or criminal liability, protection hii hii tumpe third party ili huyu third party anapo-publish information in good faith, protection hii hii imlinde. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeshauri Serikali, sisi kule kwenye Kamati yetu ya Huduma za Jamii maarufu kama Guantanamo, tuna sheria inakuja, Sheria ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Kuna umuhimu wa harmonization ya hizi adhabu juu ya distortion of information. Sheria hii inazungumzia fifteen years, sisi kule tumeweka maximum of five years, lakini zipo sheria mbalimbali ambazo zimeeleza suala la adhabu. Kwa hiyo, ningeshauri Serikali kuangalia umuhimu wa kufanya harmonization katika jambo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho niwatoe hofu wenzetu wa UKAWA, media players tumehusishwa kwenye access to information na tumeshiriki kwenye mchakato huu mwanzo mpaka mwisho. Ningeomba Bunge hili tuache kutokuaminiana yaani kutokuaminiana ndani humu ni the highest level, tu-provide benefit of doubt, inawezekana sheria hii ina nia njema. (Makofi)
Kwa hiyo, ningeomba Bunge hili kama tunaamini kuna mapungufu yanafanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ni jukumu letu la Kikatiba kutumia Bunge hili kuisimamia Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hatari pale ambapo tunaamini kwamba sisi ndiyo wajibu wetu kuisimamia Serikali na kama tunaamini mazingira ya ndani siyo mazuri, kanuni hizi zimetungwa na Bunge hili hili, leteni motion tutaungana mkono kubadilisha kanuni. Kama tunaamini kanuni hizi hazitujengei mazingira ya kutimiza wajibu wetu ni hatari, tunatoka nje, tunasusa, tunarudi, kanuni ni zile zile, there is no change! Kama tunadhani kwamba kupitisha mambo kwa majority siyo sawa tuleteni hoja humu tupambane ndani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.
Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Mwaka 2016
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia. Awali ya yote nitumie fursa kwanza kuipongeza Serikali kwa dhati kwa sisi kwenye Kamati tumefanya nao engagement kwa muda mrefu, lakini vilevile wadau wameweka input nyingi sana na mchango wangu utakuwa zaidi sio kwenye vifungu vingi lakini ni general kwenye uanzishwaji wa hii Bodi ya Taaluma na uanzishwaji wa hii agency.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukitazama role na responsibility kubwa ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa hii sheria moja itakuwa ni advisory services kwa regulatory body ambazo zitakuwepo mbalimbali. Na sisi kwenye Kamati tulilitazama sana hili kwamba kusiwe na kuingiliana mamlaka. Lakini vilevile ukitazama part five ya sheria hii section 20(1) anasema “there shall be within the Authority, a laboratory responsible for matters related to forensic science.” Na forensic science ni application ya sayansi kwenye criminal and civil laws whereby forensic scientist watafanya kazi za ku-collect, analyse na preserve scientific evidence during cause of an investigation. Na hapa ndipo inapokuja concept ya kuwepo kwa mtu anayetoka Jeshi la Polisi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niiombe Serikali kwa kuwa kumekuwa na dhamira ya wazi ya ku-empower na kumekuja kwa sheria hii, tatizo linalojitokeza mara nyingi kwenye Serikali jambo linalofanywa na mkono na kulia, mkono wa kushoto wanakuwa hawana taarifa. Kwa hiyo, unaweza ukakuta kesho na kesho kutwa Waheshimiwa Wabunge tunakuja kupitisha bajeti hapa ya kuweka fedha nyingi labda kwenye maabara ya Jeshi la Polisi, lakini function hiyo inaweza kufanywa vizuri kabisa na Unit ndani ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, huko mbele tunapokwenda role ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na kuwa ukiangalia nchi zingine; nchi kama Uingereza Unit hii imewekwa kwenye Idara inayohisika na development for business and energy and industrial strategy. Kwa sababu ita-provide advice kwenye masuala ya viwanda, na kwakuwa Serikali ina dhamira na imeonesha nia ya kufanya nchi hii kuwa ya viwanda kuna obligation kubwa ya kumu-empower Mkemia Mkuu wa Serikali katika kipindi cha miaka mitano na miaka kumi ijayo ili kuifanya maabara hii iweze kutimiza na kufikia malengo ambayo yamekuwa yamewekwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunazo taasisi kama TFDA, nimpongeze Waziri pale ambapo mtu anakuwa na dispute wakati kwenye Kamati limekuja wazo hili, ilikuwa ni kwamba referral point iishie kwa Waziri tu. Lakini nimshukuru na Serikali niwashukuru kabisa na Ofisi ya AG kwa kukubali kumpa mtu haki ya kwenda mahakamani pale ambapo hakubaliani na maamuzi yanayofikiwa na Mkemia Mkuu wa Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna hii bodi ambayo imeanzishwa na kwa kuwa Serikali imeamua kuanzisha hii professional board na kwa sheria kuna kipengele ambacho kinawataka wanafunzi wanaosoma kemia kwenda kwenye practicals na sasa hivi tumeona na tunapowatazama hawa wataalam ndio hao ambao tunao kwenye maabara zetu za hospitali, ndio watakaokuwa chini ya bodi hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaishauri Serikali umefika wakati tunavyopitisha sheria muanze kujua kuna budgetary implication, muanze ku-plan namna gani wanafunzi watakao kwenda field wanaosoma kemia ni namna gani mnawa-accommodate katika bajeti za Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu itakuwa ni unfair daktari yupo Hospitali ya Wilaya ya Nzega ambaye ameenda pale intern analipwa, lakini mwanafunzi aliyeenda pale kwenye maabara ya Hospitali ya Wilaya ya Nzega ambaye anatakiwa kwenda intern kisheria halipwi.
Kwa hiyo, naishauri Serikali sheria hii inawaletea budgetary implication kwenye maeneo mengi, ni vizuri sana kuanza kufikiria inapoanza implementation ya sheria hii hasa wanafunzi tunaowa andaa katika sekta hii waanze kutengewa fedha wanapokwenda kwenye intern wawe wanalipwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho ningeiomba Serikali uharakishwaji wa kutunga kanuni za kwenda kuifanya sheria hii iwe operational. Itakuwa ni jambo la kusikitisha kwamba tunapitisha kama Bunge inaenda kwenye makabati, inaenda kukaa miaka mingine miwili mitatu kuweza kuifanya operational sheria hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mwisho kabisa niishukuru Serikali kwa kuja na jambo hili na kuleta sheria hii ningeomba Waheshimiwa Wabunge kwakuwa tunasema tunajenga taifa la viwanda this is one of the most instrumental item ambayo tunahitaji kui-empower huko mbele. Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ni strategic unit ni muhimu sana, Serikali inapokuja na bajeti mwaka kesho au mwaka kesho kutwa kama itakuwa tayari imekuwa operational iwe ina vote yake. Itakuwa ni ajabu kama itaenda kufichwa ndani ya kwapa la Wizara ya Afya kuwa kama ka-unit kanategemea fedha kutoka Wizarani. Nashukuru, naunga mkono hoja. Ahsante
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa Mwaka 2016
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nataka kuchangia maeneo mawili tu madogo. La kwanza, ni marekebisho ya Serikali kwenye Sheria ya Mazingira. Subsection 15 kuna composition ya trustee ambayo itakayokuwa inasimamia masuala ya mazingira. Mapendekezo ya awali, naomba ninukuu ilikuwa inasema kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, the principal act is amended kwa kuongeza idadi ya members kutoka tisa mpaka 11 kwamba na katika hao members watakaongezwa wengine watatoka katika private sector. Hata hivyo, amendment aliyoleta AG, anasema the Board of Trustee may invite any person, who is not a member to participate in the deliberation of any meeting of the Board of Trustee by any person, so invited shall not be entitled to vote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nini hoja yangu? Hoja yangu ni moja, ningeshauri Serikali, Board of Trustee kwa ajili ya kuijengea credibility na kwa ajili ya kuweza kusaidia ku-mobilize funds kwa ajili ya Mfuko wa Mazingira. Tukielewa kwamba hali ya Serikali na namna ambavyo tunabana matumizi, tunaamini kwamba board hii itaweza ku-source fund kutoka nje ya mfumo wa kawaida wa kibajeti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ningeshauri Serikali, kwamba, waruhusu katika composition ya board waweze kuacha kipengele kilichokuwa proposed waongezwe watu kutoka katika private sector ili kuijengea credibility, board hii kwenda kutafuta fedha nje ya mfumo rasimu wa kiserikali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, kipengele hiki cha invitation kiendelee kuwa retained ambacho Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameleta. Hii itatoa fursa kwa board ku-invite even international organizations kuja kwenye hii Boards of Trustee na itaijengea credibility katika suala la kwenda kutafuta fedha. Hicho ni kipengele cha kwanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kipengele cha pili ni section 12(2) inasema “A person who has paid a fine as penalty for an offence of failing or refusing to conduct an Environmental Assessment Study, shall submit to the Council an environmental management plan, for approval and guidance on how the project shall be implemented”.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya matokeo ambayo yanajitokeza sasa hivi, watu wanafanya environmental assessment, anapopewa certificate nyuma ya environmental assessment certificate kunakuwa kuna guidelines, lakini most of the organizations au taasisi nyingi hazifuati zile guidelines. Kwa hiyo, ninachotaka nishauri, kwa hali ya mazingira ilivyo sasa hivi, mapendekezo ya AG ni ku-delete kipengele hiki, ningeshauri Serikali ikiache.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tungeongeza enforcement kwamba unapokabidhiwa certificate ya mazingira usipokwenda kufuata masharti yaliyoelekezwa katika certificate ile basi uweze kuadhibiwa. Bila ya hivyo kutakuwa hakuna sababu ya kumpatia mtu certificate yoyote ile baada ya kufanya environmental assessment. Hili ni jambo la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, nataka nishauri Serikali, hii Public Service Act, dunia inabadilika, competition ina-grow. Haya mambo ya kuweka ceiling ya mishahara, ku-control remuneration ya watu na sisi leo hii tunakwenda na competition duniani hali inavyobadilka, hebu imagine tutapoteza best brains.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina hofu sana katika jambo hili. Ku-control maposho na namna ya kulipana posho na nini, is a good thing, lakini mshahara, dunia ina competition, leo hii, tunapoweka ceiling kwa Mkurugenzi Mkuu wa ATC, tunapowawekea ceiling, Wakurugenzi au taasisi hizi ambazo tunatarajia watu waende ku-perfom vizuri, waweze kufanya kwa sababu naamini kwamba you pay someone out of productivity na uwezo wake wa kufanya kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka niishauri Serikali pamoja na nia njema, ni vizuri Serikali ikalitazama hili jambo. Is very danger tunapoumiza morali ya civil servant, ni hatari kwelikweli kwa maslahi ya nchi yetu na kwa maslahi ya Taifa hili. Ni vizuri mno tukatafakari mara mbili maamuzi haya tunayoyaweka tuweke frame work lakini lazima tufikiri mara mbili, what do we want to attain, nini tunataka tupate siku ya mwisho. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni-conclude kwa kusema kwamba, hili la Board ya Trustee tunaomba ni vizuri Serikali na AG akakubali wazo lililoletwa na Wizara la kuomba kwamba members wawe 11, kuijengea credibility board hii ili iweze kutafuta fedha nje ya mfumo wa kawaida wa kibajeti. Tumeona hapa namna gani wakati wa bajeti tulivyopata shida kuwawekea fedha katika Mfuko wao wa Mazingira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2017.
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushuku kwa kunipa fursa. Moja niipongeze Serikali kwa boldness na decision ya kuleta Miswada yote hii mitatu kwa Hati ya Dharura.

Mheshimiwa Naibu Spika, unapokuwa kwenye crisis lazima utafute solution kwa wakati huo huo ili kukabiliana na crisis inayokukabili. Kutoa fursa ya kusema kwamba Miswada imekuja kwa hati ya dharura, imefanya nini dharura hii inaondoa fursa ya kutengeneza sheria bora zaidi, nadhani you have to start somewhere ili uweze kufikia kule unapotaka kwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo niipongeze Serikali na binafsi nataka niishauri Serikali. Maamuzi haya tuliyofanya kama nchi ya kuweka rasilimali za nchi mikononi mwa Watanzania, lazima mjue kwamba Mfumo wa Kibepari wa dunia utapambana na dhamira hii iliyoonesha na Taifa letu. (Makofi)

Sasa Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niishauri Serikali nimeona kwenye mapendekezo ya hii Supplement Bill, naomba kwa dhati kabisa Serikali iangalie our fallback position katika mapambano haya ni wachimbaji wadogo. Tutarajie kunaweza kukatokea watu waka-pull out mitaji yao ili waweze kutu- stuff, wakijua kwamba kutatokea multiplier effect kwenye mauzo yetu ya dhahabu nje na shilingi yetu. Kwa hiyo, solution pekee ambayo ningeiomba Commission ambayo itateuliwa na Katibu Mtendaji atakayeteuliwa na Mheshimiwa Rais, lazima aanze effectively kushughulika na suala la wachimbaji wadogo, ku- regulate wachimbaji wadogo ili tuanze kuuza dhahabu yetu kwa wingi kupitia wachimbaji wadogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, niliambie Bunge hili, binafsi kama Hussein Bashe na Mbunge wa Jimbo la Nzega sioni value, sioni value ya uchimbaji mkubwa mpaka sasa katika Taifa letu, sioni! Tutabaki na takwimu kubwa na kuona uwepo wao nataka niwape taarifa Waheshimiwa Wabunge. Miaka ya 1980 nikiwa mdogo, Nzega kulikuwa na daladala zinatoka Nzega Mjini kwenda Isungangwanda kwa wachimbaji wadogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, alipokuja resolute daladala zilikufa biashara ile ikachukuliwa na cater ya kwao, there was no growth kwenye uchumi wetu, matokeo yake leo wametuachia mahandaki, juzi mlimsikia. Duniani is the only country Tanzania mwizi anaweza akaja kwa Wabunge kuwapa ushauri, CEO wa Resolute nae alikuja kutupa ushauri wa namna gani wa kulinda rasilimali zetu na yeye aliondoka na fedha za wananchi na amelipa kodi only two years, over ten years wamechimba dhahabu katika Mji wa Nzega. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge tujiandae hii ni kama vita ya Uganda, lakini in a different way, kwa hiyo tujiandae kujifunga mkanda, we might surfer na tuwe tayari kuungana kwa ajili ya rasilimali za nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niombe tu kwa Mheshimiwa Waziri jambo dogo, tunaye Kamishna wa Madini ambaye atateuliwa na Rais, according to this law, vilevile kutokana na sheria hii atakuwepo Katibu Mtendaji Mkuu wa Commission atakayeteuliwa pia na Rais, hawa watu wawili watakuwa wanafanya function na ukimtazama Kamishna kutokana na mabadiliko ya sheria hii anamshauri Waziri, Katibu atakuwa anafanya day to day activity na kuishauri Commission, wakati huo modal yetu ya uchumi wa madini inahamia kwa wachimbaji wadogo, hili tujiandae kisaikolojia, kufuta Makamishna wa zones, kuwaondoa ambao walikuwa wanaenda kuleta huduma kwa wachimbaji wetu wadogo ita-work against us.

Mheshimiwa Naibu Spika, niishauri Serikali ilitazame jambo hili na namna ya ku-harmonies Kamishna na Mtendaji Mkuu na Zonal Office zitakazokuwa chini ya Makamishna wa Kanda, this is very important.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la mwisho...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja na ahsante.
Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2017.
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa. Kwanza nitumie fursa hii kumshukuru Waziri wa Fedha na Wataalam wote wa Serikali, Kamati na nitumie nafasi hii tu kuwaambia Waheshimiwa Wabunge, Kamati imekuwa na engagement ya almost siku mbili, tatu kuhusu masuala mengi yanayohusiana na Sheria ya Fedha na alignment ya malengo ya Serikali na bajeti iliyosomwa na Mheshimiwa Waziri na Serikali ime-give in kwenye mambo mengi sana. Kwa hiyo, mimi tu binafsi nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri na Serikali katika maeneo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niseme kitu kimoja, Kanuni za Bunge siyo Msahafu wala Biblia, nitumie nafasi hii kuomba Ofisi ya Spika, dunia inabadilika, mazingira yanabadilika na Kanuni zetu zibadilike. Nimemsikiliza Ndugu yangu Silinde akionesha challenge za Kikanuni juu ya Muswada ulioletwa na Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Kwenye notice hapa Waziri wa Fedha amesema this Bill to be submitted to the National Assembly was published as a Bill Supplement No. 3, of 2nd June. Kwamba hii ni supplement ya ile Bill iliyokuwa imeletwa, why supplement?

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaleta bajeti, Wabunge tunachangia siku saba, haina maana kwamba ndani ya siku saba Serikali isichukue mawazo yetu na mawazo yetu yanaathiri sheria, yanapoathiri sheria tuna option mbili, tukubaliane model ya kwamba Serikali ikija na bajeti hapa inakuwa ndiyo Msahafu tunafanya sisi tunakuwa rubber stamp ama mawazo yetu yanaenda kuwa accommodated na kuletwa kwenye Sheria ya Fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, kama kuna upungufu wa Kikanuni, ni wajibu wetu Wabunge ku-demand mabadiliko hayo, ili tuweze kufikia malengo na wajibu wa kufanya kazi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie kwenye baadhi ya maeneo, moja ni eneo la ku-regulate informal sector. Tunawapa vitambulisho tunawa- regulate ma- MC na nani, ningeomba tutakapowa-regulate hawa informal sector kwa kuwa vyanzo vingi vya mapato tumevipeleka Central Government through TRA, nashauri, TRA ikae na Serikali za Mitaa na hapa ndipo Waziri wa Serikali za Mitaa afanye kazi closely na Wizara ya Fedha namna gani chanzo hiki kitaweza kuwa regulated katika Local Government ili baadhi ya mapato yabaki katika Serikali za Mitaa na baadhi ya mapato yaje ya-support Serikali Kuu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Sheria ya Gaming Board, Gaming Board ina vyanzo na vyanzo hivi nadhani Serikali iangalie, tumeshapitisha Appropriation Bill juzi tumefunga, lakini bado hatujawahi kuwa na asilimia 100 ya ku-attain bajeti yetu, ningeomba tuongeze tozo inayoitwa tax on collection kutoka 6% to 12%, tuongeze tozo ya tax on winning kutoka 18% kwenda 25% kwenye Gaming Board, tuongeze license fee.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivi kwa sababu hili ni eneo ambalo wanaita wenyewe, ni kodi za dhambi hatutaki kamali i-grow lakini its growing is there, it is an opportunity. Kwa hiyo, wakati mna-loose morally lazima m- gain economically. Hivyo, ningeshauri vyanzo hivi vya fedha vikusanywe na ikiwezekana Central Government na Hazina muangalie uwezekano wa kupeleka fedha hizi kwenye Mfuko wa Mazingira, if it is possible tupeleke fedha hizi kwenye Mfuko wa Mazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna-demand maji, kuna fedha ile shilingi 40 na Serikali imetupa commitment ya kuhakikisha kwamba hela ya maji itaenda, in a future ili maji yawepo lazima tu-protect mazingira. Kwa hiyo, hili ni jambo muhimu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda kwenye Income Tax Act, kwenye hii Bill iliyoletwa na Serikali page number 14, item number two, section 27 item (b) inasema a corporation with a newly established plant for assembly motor vehicles mpaka mwisho tumetoa incentive ya 10% . Naomba tuongeze item
(c) tuseme kwamba a corporation with a newly established on agro processing industries with the performance agreement with the Government will enjoy a 10% Corporate Tax for the period of five years.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali yetu tuna-grow industrialization, Ukiangalia tumetoa VAT exemption kwenye capital goods, tusipotengeneza structure za kodi, kwa sababu Mwekezaji anapoingia kwenye nchi, jambo la muhimu analolitazama ni tax regimes kwanza. Najua kuna window ya TIC, kuna window za EPZA na kadhalika, tukitengeneza tax regimes ambazo ziko wazi, wawekezaji wanaokuja kwenye sekta ya kilimo, leo ukimwambia mwekezaji wa korosho kwamba njoo u-process korosho yako Tanzania badala ya kui-process India, utapata VAT exemption kwenye capital goods, utapata 10% corporate tax badala ya 30%, utapata zero rated kwenye chemical processing, huyu mtu hatakuwa na sababu ya kwenda kuwekeza nje, pamoja na incentive tulizoziweka TIC na maeneo mengine ni rahisi sana kufanya namna hii.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunayo maeneo ya cotton, ni vizuri hizi incentive zikawa extended kwenda kuwa- accommodate sehemu kubwa ya watu wetu. Kila siku tutakuja hapa tunasema asilimia Saba ya GDP uchumi wetu umekuwa kwa 7.5 hadi 7.8 kama tax regimes zetu hazi-attract investment ya viwanda kwenye eneo la kilimo hatuwezi kufikia malengo tunayoyataka.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nataka nishauri kwenye VAT exemption ambayo tumetoa, ningeomba tuongeze kwenye schedule Namba 21 tuweke schedule Namba 22, ili namba 22 tuongeze chemical processing on agro industries. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie kwa kusema kwamba nawashukuru sana Serikali safari hii wame-give in kwenye mambo mengi. Ahsante sana.
Muswada wa Sheria ya Reli wa Mwaka 2017
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia. Moja niipongeze Serikali kwa dhati kabisa kwa kuunganisha mashirika haya mawili na kuwa shirika moja na kuifuta RAHCO.

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu utakuwa katika mitazamo miwili, moja specific kwenye sheria lakini mwingine utakuwa ni mchango wa jumla. Nikichukua sheria hii iliyoletwa na Serikali, ukienda page number eight, kifungu namba tano kwenye objects of corporation, there is no anywhere kwenye objective za shirika zimesema specifically kwamba tunaanzisha shirika hili kwa ajili ya commercial interest na kutengeneza faida, hakuna. Ukitazama objective na kila kitu kilichooneshwa hapa it is pure service delivery and not profit making organization, na hili ni tatizo from the day one.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ningeshauri, katika kipengele namba tano tungeongeza kifungu, tunasema kwamba; “to invest and generate profit for the United Republic of Tanzania” ili management inapoingia madarakani ijue jukumu lake la kwanza ni kutengeneza fedha kwa ajili ya Serikali, hilo jambo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili nikienda page number ten kwenye composition of Board, ningeshauri tungekuwa specific katika aina ya watu tunaowaweka katika board na mmojawapo wa wawakilishi akawepo wa kutoka private sector kwamba katika board members watakaokuwa wanatengeneza board ya shirika hili mmojawapo atoke katika sekta binafsi, kwa sababu shirika hili linatarajia kufanya biashara na umma ili huyu mtu wa sekta binafsi angalau apeleke the mindset, the perception ya kufanya biashara katika board.

Mheshimiwa Naibu Spika, huu ni ushauri wangu kwamba tunapotengeneza composition tuseme specifically kwamba kutakuwa na uwakilishi wa mtu kutoka katika sekta binafsi ili tusitoe room unaweza wakashangaa wakachanguliwa Makatibu Wakuu wa Serikalini tupu humu ndani, halafu tukarudi kule tulikotoka kwa sababu tuna bad experience.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye functions of the board page number eleven, kifungu namba 13. Tungesema moja ya function ya board ni ku-approve annual strategic plans na ku-evaluate monthly performance ya management, ili kui-commit management kuwa ina-provide monthly report ya performance ya shirika halafu kila quarter board ina- evaluate hizi performance za kila mwezi ili tuweze ku-take corrective measures mapema badala ya kusubiri muda mrefu. (Makofi)

Mjheshimiwa Naibu Spika, eneo jingine nilitaka niende page number 33 na hapa nataka niishauri Serikali kwamba kwenye financial provisions, kwenye Finance Bill tuliyopitisha hivi karibuni tuliweka exemptions ya levy, ningeomba kifungu namba 69(4) ambacho kinasema; “The provision of subsection 3(c) shall not apply to exemption provided under the East African Community Custom Management Act.

Mheshimiwa Naibu spika, hapa tungeongeza exemption tulizotoa kwenye levy ambayo tulikuwa tuna- charge 1.5 percent kwenye mafuta ya ndege, kama mtakumbuka kwenye Finance Bill tulifuta tozo hii ya reli kwenye mafuta ya ndege ili kufanya viwanja vyetu vya ndege kuwa competitive. Tusipofanya hii exemption kipengele hiki kinaenda ku-over rule maamuzi tuliyoyapitisha kwenye Finance Bill and this will be a problem.(Makofi)

Mheshimiwa naibu Spika, ningeshauri kwenye liability za TRC nilitaka niishauri Serikali; tunajenga standard gauge railway system kwenye nchi yetu, we will be competing na watu wengine. Ukisoma liability, shirika limejiwekea protection isiyokuwa na vipimo. Twende page numbe 22 kifungu namba 38 “The Corporation shall not be liable for any loss arising from the delay cause by the failure of any train to start on or complete any journey within set time” nani anaye-determine hii set time? ni shirika lenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni loophole na nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge, the bottom line ya railway business siyo kusafirisha abiria ni mizigo, sasa tuta- compete na wenzetu if this protection tuliyojiwekea haitokuwa competitive na wengine, investment tunayofanya kama nchi itakuwa waste. Tukae tufikirie kwamba kuna another Northern Corridor ina hiyo standard gauge railway system ya Kenya ambayo inaenda hadi Kigali na our objectives ni kwenda ku-save market ya Congo, ku-save market ya Kigali na maeneo ya namna hiyo. Kwa hiyo, ukitazama hiki kipengele tumejifunga sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kipengele namba 40 kinasema hivi naomba Waheshimiwa Wabunge mnisikie:

“The liability of the corporation in respect of any animal, shall not in any case exceed the appropriate amount set out in the tariff book unless at the time of acceptance of such animal by the corporation.” Kwa nini tusiseme; “as per the market rate” ili ku-provide confidence ya mtu anayekuja kuchukua huduma kwamba mkinisababishia hasara mimi

nitakuwa determined na soko siyo tariff book uliyotengeneza wewe, this is not competitive, nataka niiambie Serikali hapa na Mkurugenzi wa TRL yuko hapa ametoka kwenye private sector.

He is running the organization ambayo tunatarajia kwenda kutengeneza fedha. Lazima iwe more competitive, sheria hizi tukae tukijua wafanyabiashara wataangalia sheria yetu ya shirika, wataangalia sheria ya mashirika competitive, haya ni ya upande wa kisheria.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niseme mambo ya jumla wenzangu Waheshimiwa Wabunge wameongelea sana suala la bomoa bomoa. Tabora ni moja ya eneo affected. Zinabomolewa kaya zaidi ya 500 Tabora, miongoni mwao ni watu waliojenga zaidi ya miaka 50, 60, 70, 80 wapo watu waliojenga katika maeneo hayo. Kuna bibi anavunjiwa nyumba ana umri wa miaka 80 hana familia yuko peke yake, alipewa hati na Serikali, alikuwa analipa kodi za Serikali anafanya nini. Ningeomba Waziri pamoja na kuwa hatujaja kujadili, tunajadili sheria, give us a statement of hope kwenye hili jambo because tuna-represent watu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine Serikali inajenga standard gauge na ningeiomba kwa heshima Serikali na TRL sasa tumeipatia assets za kutosha, jamani hatuwezi kujenga standard gauge kwa fedha zetu za ndani, this will be a dream which we will never be realized. Niishauri Serikali sasa mmruhusu TRL aende kwenye dunia kutafuta fedha za ku- invest kwenye standard gauge, hatuwezi kufanya kila kitu kwa fedha zetu za ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunajenga reli kwa hela yetu ya ndani, tunajenga megawatts 2100 za umeme kwa hela yetu ya ndani, tunanunua ndege kwa hela yetu ya ndani, we are going to suffocate this economy, huu ni ushauri. Iruhusuni TRL ikakope ijiendeshe na nimshauri Mkurugenzi wa TRL na Waziri, it is uneconomical kujenga reli kwenda Mwanza kwanza, twendeni Kigoma, twendeni Kalemii, twendeni Uvinza, twende Msongati halafu jengeni Mwanza. Niitahadharishe Serikali msiweke fedha za wananchi for political reasons. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi natoka ukanda huo ningependa nipande Bukene standard gauge, lakini it is not going to pay. Fanyeni cost benefit analysis, wapi tunapeleka, tukienda Lake Tanganyika tutahudumia part of Congo, tukienda Kalemii tutahudumia the Western part of Congo, tukienda Uvinza tukaenda Msongati tutabeba mzigo wa Nikel siku ya mwisho reli hii itajiendesha kibiashara.
Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania wa Mwaka 2017
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa. Labda nianze kwa kusema kwamba Serikali imetuletea Muswada huu wa kuihamisha TTCL from a Limited Company kwenda kuwa Corporation. Kwenye biashara maana yake tumeitoa kwenye uwanja wa mapambano tunaenda kuifungia chumbani ili tui-spoon feed. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini najiuliza tu swali, why corporation and not limited liability company? Naelewa, strategically ni Serikali haitaki kuipeleka kwenye DSE, kwenye soko la hisa, ndio mkakati. Ili tuiweke miongoni mwa mashirika ambayo kwa muda mrefu yameendelea kuwa liability kwa Serikali lakini tatizo la msingi la TTCL ni sheria? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hili ni swali ambalo lazima tuweze kujijibu sisi. Tatizo la msingi la TTCL sio sheria, tatizo la msingi la TTCL ni business model ya TTCL. Kwenye sheria kuna subsidiary company inaitwa TTCL Pesa, money transfer kwenye mobile business ni one of the product. Kama kweli tunataka kuifanya TTCL kuwa strong and effective kwa nini tunaiacha hii subsidiary peke yake? Nani atai-finance? Itabebwa na nani? Sheria haijasema.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nafikiri kama tumeamua kula nguruwe tule aliyenona. Tumhamishe na huyu TTCL Pesa kama tunavyochukua mali zote, assets and liabilities kuziingiza chini ya corporation tuiweke kwa sababu ni moja ya line ambayo italipatia pesa shirika hili. Hilo ni jambo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, sheria hii inampa mamlaka Waziri kuisimamia Bodi na kutoa maelekezo. Siyo nia mbaya lakini nataka niiulize Serikali tuna mtu anaitwa Treasury Registrar, huyu ndiye msimamizi mkuu wa mashirika yote ya Serikali. Humu kwenye sheria Bodi haiambiwi kwamba itawajibika kwake, itapewa maelekezo na Waziri na siyo Hazina, kwa nini?

Mheshimiwa Naibu Spika, kama tuna nia kweli ya ku- transform na model zipo. Ukiangalia Far East Malaysia, Singapore, the powers za Treasury Registrar zilizopo kwenye mashirika ya umma ndiyo maana yame-perform, hata hiyo China mnayoijadili. These are the people wanaisimamia, Treasury Registrar ana right ya ku-hire na ku-fire. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwapeni swali Waheshimiwa Wabunge, tujiulize anayesimamia mashirika ya umma ni Msajili wa Hazina, lakini Msajili huyu wa Hazina hana mamlaka ya kumfukuza kazi Mkurugenzi wa Shirika, hana mamlaka ya ku-appoint Board of Directors, tumezipeleka hizi powers kwa political figures halafu tunategemea results? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri, hapa sina platform ya kuleta ammendments, nashauri kwa Mheshimiwa Waziri, I agree dhamira ya Serikali kwamba tunataka ku-maintain security, communication is very important lakini lazima wajue tunatengeneza monopoly rights kwa TTCL. Inawezekana kuna sababu zipo za kiulinzi na kadhalika, we can agree, but wajenge mazingira ya kulifanya shirika hili liweze kujiendesha kibiashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mazingira haya ili tufanikiwe, ili tuweze kufika tunakotaka, Msajili wa Hazina angepewa hizi mandate anazopewa Waziri. Msajili wa Hazina angepewa mandate ya ku-appoint Board of Directors, hata Mwenyekiti, angepewa haki ya kuweza ku-hire na ku-fire Mkurugenzi ili aweze kusimamia vizuri haya mashirika, aweze kuwa na powers huyu Msajili. Bila ya hivi tutaendelea kuongeza mzigo, tuna mashirika zaidi ya 50 au 60 ni mangapi yanafanya kazi kwa faida? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunatengeneza hili, najua tuna sheria keshokutwa tutaleta ya NASAC ambayo na yenyewe tunaipa mamlaka ya kufanya biashara indirect na yenyewe itataka kupata fedha kutoka Bunge, itataka kupata msaada wa Bunge na yenyewe kuwa shirika. Are we creating environment ya biashara? Kwa nini Waziri anachukua mandate hizi?

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu kwa kaka yangu Mheshimiwa Profesa Mbarawa ni kwamba, wakati ana-wind up hapa, akubali tu hizi powers alizochukua za kusimamia Bodi hii wamwachie Treasury Registrar. Tuangalie uwezekano wa AG kuleta ka-ammendment hapa ili Treasury Registrar tumpe jukumu hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni recruitment process, ukiangalia zote ni appointment. Hivi jamani kwa nini tusiseme kwamba Directors wote wa Bodi wata-apply na wata- compete kama ambavyo private sector inafanya lakini wote tunawa-appoint na hili shirika tunatarajia liende likafanye biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu ni kwamba sioni kama tatizo la TTCL ni sheria, sioni tatizo la TTCL to be called corporation or limited company, aah, aah, hili sio tatizo. Tatizo la msingi la TTCL tunatoka kwenye tatizo
tunaenda kwenye tatizo lingine kwamba tunampa Waziri mamlaka lakini Waziri siyo msimamiaji wa mashirika haya ya umma. Mwenye mamlaka ya kusimamia mashirika haya ya umma hana powers kwenye sheria hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine dogo tu ambalo nataka niliseme, kulifanya kuwa corporation tusilifungie mlango wa kulipeleka kwenye soko la hisa. Tuna window ya makampuni yanayopata hasara, tulipeleke kule, tuliache liende kule ili Watanzania waweze kushiriki. Kuwe kuna transparency ili tuweze kuona books of accounts za haya mashirika ya umma kwa sababu yakienda kwenye soko la hisa tutayaona lakini tusipofanya namna hiyo hili ni tatizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, TTCL haiwezi kufanya kila kitu, ni lazima ikubali ku-define, tunali-empower hili shirika ili likajibu tatizo gani? Likajibu tatizo la kuwa na simu za mkononi, likajibu tatizo la data kwa sababu the future of this business ni data. Lazima tujue tunataka kwenda wapi na ili tuweze kufanikiwa ni lazima tuondoe mfumo wa mashirika ya umma Wakurugenzi, Board of Directors kuwa appointed na Mawaziri, iwe ni competitive mechanism. Yanatangazwa, wana-apply, wanaingia kwenye interview ili waweze kupata nafasi hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, kupokea taarifa kwa miezi sita Mheshimiwa Waziri according to this law is too long. Apate taarifa za shirika hili quarterly, tusisubiri miezi sita. Akipata taarifa hizi quarterly atakuwa na nafasi ya kuweza ku-take corrective measures kwenye shirika hilo kwa muda mfupi kabla ya hasara au matatizo ku-grow.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niseme kwamba tulipo ni point of no return na mwelekeo ni kwenda kuanzisha corporation, Waziri akubali kifungu hiki kinachompa mamlaka makubwa ayapunguze, amuachie TR ili awe na haki ya kuisimamia hii bodi direct. TR apate powers za ku- appoint directors ili aweze kuwa answerable siku ya mwisho kwa Waziri wa Fedha kwa sababu shirika hili likilegalega watarudi kwa Waziri wa Fedha kuomba hela kutoka Hazina na watakuja hapa tutawapitishia lakini jicho la Wizara ya Fedha kwenye mashirika ya umma ni TR ambaye hana powers katika haya maamuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie tu kwa kusema kwamba inawezekana dhamira ni njema sana lakini strategy is very wrong kwa mwelekeo huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru.
Muswada wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma wa Mwaka 2017
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa. Kwanza nitumie nafasi hii kuipongeza sana Serikali kwa kukubali kufanya mabadiliko ambayo Kamati imewashauri kwa kipindi cha siku nane. Kwa kuwa Kamati ya Bunge inafanya kazi kwa niaba ya Bunge, haya yanayokuja katika muswada huu, kwa asilimia zaidi ya 99 Kamati imeshiriki katika mabadiliko haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nayasema haya kwa dhati kabisa na yapo mabadiliko ambayo tumeyafanya. Moja, uwepo wa unemployment benefit; pili, mabadiliko kwenye kifungu cha 29 ambacho kinaelezea mafao na kuipa mamlaka bodi kuweza kufanya maamuzi juu ya aina ya mafao ambayo bodi husika itaona inaweza kuyaongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa kuna cry kubwa ya public juu ya withdraw benefit. Sisi tumeangalia nini? Tuliangalia sustainability ya mifuko hii. Sote tunafahamu mifuko ya hifadhi hii kama ingeendelea kwa utaratibu ambao tumekuwa nao, kuna mfuko kama PSPF uhai wake ulikuwa hauna zaidi ya miaka miwili, ulikuwa unaanguka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, denominator ya 540 ilikuwa ni dialogue kubwa, lakini sisi kama Kamati vilevile tuliona kwamba tu-provide nafasi kwa Serikali na kuiruhusu kutumia kanuni kwenda kuweka equation na kwa kufuata utaratibu wa utatu kwa maana ya waajiriwa, vyama vya wafanyakazi, waajiri na Serikali katika mchakato wa kutengeneza kanuni ili mjadala wa equation itakayotumika kama benefit ya wafanyakazi iweze kuwa considered.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tumeangalia suala la ku-safeguard interest za mifuko ya hifadhi kwa maana ya investment. Kumekuwa kuna uwekezaji mwingi sana ambao ulikuwa ukifanyika huko nyuma ambao umepoteza fedha za wastaafu. Kwa sheria hii, Management, Board of Directors watakuwa accountable juu ya uwekezaji wowote utakaofanyika na wataadhibiwa mpaka kifungo cha miaka mitano juu ya uwekezaji wowote watakaofanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliamua mapendekezo ya Serikali yalikuwa ni kwamba wafanyakazi walioko kwenye private sector, wanaolipa katika mifuko ya kiserikali kama PPF wahame na michango yako. Uhai wa mifuko ungekwisha! Tuliamua kuweka demarcation na kusema kwamba kuanzia sasa mashirika yote ya umma ambayo Serikali ina interest yachangie katika mfuko wa umma. Hii ni ili kuweza kuipa uhai mifuko hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini kabisa kwamba maamuzi ya kisiasa ambayo yalikuwa yakifanyika huko nyuma katika mifuko ya hifadhi, hayatafanyika tena na Serikali. Tumeitaka Serikali kwamba watakapotunga kanuni, ziletwe kwenye Kamati ya Bunge ili Kamati ya Bunge iweze kuzipitia kanuni zile, ili tuone maslahi ya wafanyakazi kama yameweza kutazamwa inavyotakiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo moja tu ambalo naendelea kuiomba Serikali na tumeiomba hata kwenye Kamati, sheria hii imetambua watu wa kada mbalimbali ambao wapo Kikatiba, ambao wametwajwa na sheria, lakini Makatibu Wakuu wameachwa kwa hoja kwamba Makatibu Wakuu ni wengi, lakini vilevile waliokuwa considered ni wale waliotajwa katika Katiba tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu kila Executive ni Permanent Secretaries. Kwa hiyo, ni vizuri kabisa Permanent Secretaries wakaweza kuwa considered kama alivyotajwa IGP, kama alivyotajwa Chief Secretary, kama alivyotajwa Katibu wa Bunge na sheria hii, ili hawa watu ambao ndio custodian wa taasisi zetu za umma waweze kuwa na uhakika wa kesho yao.

Mheshimiwa Mwenekiti, otherwise nimalizie tu kusema jambo moja kwamba attitude iliyooneshwa na Wizara katika mchakato wa kuipitisha sheria hii ni very positive attitude. Tunaamini Serikali inapoenda kutunga kanuni ambazo zitatumika ku-govern sheria hii na kufanya utekelezaji wa sheria hii, kanuni zile zitatungwa katika misingi ile ile ambayo sheria hii imepitia. Misingi ya dialogue, misingi ya kusikiliza vyama vya wafanyakazi, misingi ya kusikiliza vya waajiri ili tuweze kuwa na sheria ambayo itaipa uhai mifuko yetu ya hifadhi ya jamii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kusema kwamba naunga mkono hoja hii, ahsante sana.
Muswada wa Sheria ya Bodi ya Kitaalam ya Walimu Tanzania wa Mwaka 2018
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitumie nafasi hii kutakia heri wanafunzi wote wanaofanya mtihani wa primary school na niwatakie heri specifically wanafunzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega. Matumaini yangu ni kwamba mwaka huu watafanya vizuri kama walivyofanya mwaka 2017 kuwa Halmashauri ya saba Kitaifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, nitumie nafasi hii kuipongeza Serikali kwa dhati kabisa na Mheshimiwa Waziri. Sekta ya elimu inahitaji transformation na transformation tunazofanya ni hatua kwa hatua. Uanzishwaji wa Teacher’s
Professional Board limekuwa ni wazo na ni jambo ambalo limekuwa kwenye mjadala kwa muda mrefu. Bodi hii kwa muundo wetu wa kiutawala katika nchi, anayesimamia utawala na uendeshaji wa walimu ni Waziri wa TAMISEMI lakini anayesimamia sera, ni Waziri wa Elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwepo wa Teacher’s Professional Board unampatia Waziri wa Elimu mkono wa kuweza kuangalia walimu walioko katika shule zetu za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu. Hii itatupatia fursa na kumpa Wizara ya Elimu mtu anayesimamia sera mkono wa kuweza kuwasimamia walimu na kuhakikisha kile ambacho anakitazama yeye kama vision kinafikiwa. Hili ni jambo muhimu sana ambalo sisi kama Wabunge tunatakiwa kuiunga mkono Serikali kwa dhati kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na conflict, nami nimesoma kwa kina hotuba ya Dada yangu Mheshimiwa Susan. Ukitazama ameonyesha a lot of gaps ya Teacher’s Service Commission na Muswada ulioko mbele yetu ni Teacher’s Professional Board. Kumekuwa na maoni na hoja kwamba uwepo ya Bodi ya Kitaaluma hii ni kuongeza mzigo wa gharama katika nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kujiuliza, kama tunataka kupunguza gharama na kama tunataka ku- streamline sekta ya elimu, tujadili mfumo wa D by D. Kwa sababu mfumo wetu wa D by D umemfanya mwalimu kuwa chini ya Mkurugenzi, kusimamiwa na Halmashauri na TAMISEMI, ndiyo maana kuna Teacher Service Commission anayeangalia maslahi ya walimu. Kwa hiyo, kama Sheria ya Teacher’s Service Commission ina upungufu, huo ni mjalada ambao tunatakiwa tuulete, tutazame upungufu uliopo tuweze kuirekebisha sheria hiyo na hilo ni jukumu la Bunge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimeipitia sheria hii, jambo pekee ambalo naiomba Serikali, kwenye functions za Bodi hii mojawapo ni kufanya training. Naomba Mheshimiwa Waziri anapoenda kutengeneza regulations, hizi training za
kila mwaka ambazo mwalimu anapata, ziweze kuwa accounted na kupata score marks ambazo zitamsaidia mwalimu at the end of the year anapoangalia maslahi yake mwisho wa mwaka yaweze kuwa considered katika mapato yake ya mwaka. Kwa sababu mwalimu kama kapata taaluma ambazo zimetolewa na Bodi yenyewe kwa utaratibu maalum uliowekwa kwa mujibu wa regulation, kama ilivyo NBAA, score marks hizo ziwe na positive impact katika maslahi ya mwalimu ili iwe incentive kwa mwalimu kuweza kujiendeleza. Hili ni jambo la muhimu sana likaangaliwe katika regulation. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati anachangia ndugu yangu Mheshimiwa Serukamba ali-rise a very important point juu ya suala la appointment ya Mwenyekiti wa Bodi. Mwenyekiti wa Bodi kutokana na sheria anateuliwa na Waziri. Nami naomba kwenye composition, sekta yetu ya elimu ina composition ya aina mbili, ina upande mmoja unaoendeshwa na private sector na upande mwingine unaendeshwa na Serikali. Kwa hiyo, nafikiri Serikali itazame composition ya ile Bodi; nimeona kwenye amendment ya Mheshimiwa Susan Lyimo naye kaweka, kwamba tuangalie ni namna gani tunaweza kuwaingiza watu wanaosimamia private sector katika Bodi ya profession wawe na uwezo wa kuwa na representation. Ni muhimu tuangalie namna gani composition hii tunaweza ku-add into that. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Mwenyekiti, Mheshimiwa Serukamba alisema kwamba Mwenyekiti wa Bodi ateuliwe na Mheshimiwa Rais kama zilivyo Bodi nyingine. Nimeangalia amendment ya dada yangu Mheshimiwa Susan, pendekezo lake hajasema kwamba ateuliwe na Rais, alibadilisha tu Chairman to chairperson, hakukuwa na issue ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nachotaka nishauri ni kwamba private sector inasaidia sekta ya elimu. Tuangalie namna gani tunaweza kuwaingiza katika composition ya ile Bodi, namna gani uwakilishi wa sekta binafsi uliowekeza katika elimu unaweza kuwemo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ni muhimu sana, Professional Board ya Walimu, naiomba Serikali, kutokana na structure na kazi yake, ni muhimu mno ikapata resource kwa nia njema, kwa sababu jambo hili litakuwa na positive impact kwenye suala la elimu katika nchi yetu lakini isiwe ni njia ya kuingiza chanzo cha mapato hasa hizi fee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, annual fee ambazo mwalimu atatakiwa kulipa for registration, nashauri na naomba humbly na Mheshimiwa Waziri namwomba sana, atakapoenda ku-form regulations iendane na hali halisi ya kipato cha walimu ili isiwe kiwango ambacho kitawa- discourage walimu kukata hizi leseni. Ni muhimu sana kwa sababu walimu wetu wanafanya kazi katika mazingira magumu lakini kipato chao ni kidogo sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie tu kuipongeza Serikali kwa dhati kabisa kwa kuja na Muswada huu. Hii ni hatua muhimu sana ya kuleta reform katika sekta yetu ya elimu na nimpongeza Mheshimiwa Waziri kwa dhati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, ahsante sana.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza).
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa fursa. Awali ya yote nitumie fursa hii kuishukuru kwa dhati kabisa Serikali, lakini vilevile nimshukuru Mheshimiwa Rais kwa maamuzi makubwa aliyoyafanya kukutana na wachimbaji wadogo na kusikiliza kero zao. Jambo la pili, nishukuru Wizara ya Fedha na Wizara ya Nishati na Madini na Ofisi ya AG, tumekuwa na engagement ya siku mbili wame- give in katika mambo mengi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka nitoe ushauri hasa katika zao la zabibu. Tumechukua hatua ya awali ya kutatua changamoto ya zao la zabibu kwa kubadilisha tozo ya excise duty, nataka niiombe Serikali kwa dhati kabisa hii ni asilimia 40 tu ya tatizo la sekta ya zabibu, asilimia 60 bado imebaki katika gharama za import za component zinazohusika kama input kwenye uzalishaji wa mazao yanayotokana na zabibu kama vifungashio na chupa. Kwa hiyo, ningeshauri Serikali kwa kuwa tunaanza kujiandaa na mwaka wa fedha unaokuja, ni vizuri kukutana na wadau hawa kwa kina ili tuweze kulinyanyua zao la zabibu vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo nataka nishauri, kaliongea kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Dalaly Kafumu. Kwa sisi tunaotoka kwenye maeneo ya uzalishaji wa dhahabu, tunafahamu na hii aliiongea kwenye Kamati, kwa mara ya kwanza tumeanza kujadili dhahabu baada ya uhuru kwa uwazi. Ni sawasawa na gorilla fighters mnawatoa porini sasa mnawaleta waje waweke silaha chini waache smuggling.

Mheshimiwa Spika, naiomba kwa dhati Serikali wakati wanaenda kutengeneza regulation ya utekelezaji wa mabadiliko ya sheria hizi, ni vizuri wakafanya engagement ya kutosha na hawa wanaojihusisha katika sekta hii ndogo ya madini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la import license; yaani Serikali tumeongea nao sana na naamini huu ni mjadala wanaweza wakaleta hapa additional amendment. Hivi kifungu hiki kinasema hivi, naomba ninukuu:

“A person shall not import any minerals without a relevant Mineral Import Permit.”

Mheshimiwa Spika, kwa nature ya wafanyabiashara wa madini mtu ana-smuggle kupeleka nje kwa sababu ya gharama za tozo na soko la kwake la ndani. Sasa tujiulize tumezungukwa na Mozambique mtu kalipua shimo lake kapata dhahabu yake, utaratibu uliopo kule ni shida kwa nini hii declaration isifanyikie sokoni? Yeye aingie na dhahabu yake, aingie moja kwa moja sokoni auze. Kwa nini tuna complicate mipaka yetu, hebu tujiulize swali wakati Tanzanite yetu inakatiza kwenda Kenya waliwekewa hii import license barabarani? Sisi tuna become very holy wakati sisi tumepoteza sana rasilimali, wenzetu wamefaidika na rasilimali zetu. Naishauri tuondoe hii, declaration ikafanyikie sokoni, ni muhimu sana tukifanya namna hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la tatu kwenye regulation; kule kwenye uchimbaji wa madini ya dhahabu na Mheshimiwa Waziri wa Madini anafahamu, kule hakuna kulipana mshahara kule mtu akiingia chini ya ardhi hata miezi sita siku akizalisha wanagawana mifuko, huyu hana PML, Dealer License na Broker License. Kwa hiyo, yule mchimbaji (nyoka) aliyepo kule aki-crush dhahabu akapata dhahabu zake ndogo anaweka mfukoni, hapa katikati hana leseni yoyote. Yeye kavumbua Nzega anataka kurudi Dodoma nyumbani kwao ndio akauze. Anaweza kukamatwa na polisi na kufanya nini. Kwa hiyo, nashauri tutakapoenda kutengeneza regulation, tunayo Dealer’s License, Broker’s License, PML, ni vizuri waangalie namna gani hawa wachimbaji wadogo wanaweza kufanya biashara yao bila kuwekewa vikwazo. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Spika, otherwise naishukuru sana kwa hatua hii iliyochukua. (Makofi)
Sheria ya Fedha ya Mwaka 2019
MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia. Kwanza niseme kwamba naipongeza Serikali na naunga mkono hoja lakini nina maboresho machache ambayo ningeshauri Serikali iweze kuyafikiria ili yaweze kuingia katika Finance Bill ya mwaka huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la jumla nilitaka niiombe Serikali kwa dhati, mpaka leo wanunuzi wa pamba hawajaingia kununua zao la pamba katika maeneo yetu. Ningeomba zichukuliwe hatua za haraka sana. Vilevile ningeshauri Serikali utaratibu wa kisheria na ninaamini sheria zinavyotungwa ni kwa ajili ya kumtumikia mwanadamu na wala siyo mwanadamu kuwa mtumwa wa sheria. Kama sheria haiko practical katika mazingira halisi, nashauri itazamwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano, bei ya pamba inakuwa determined na bei ya soko la dunia. Tumetangaza bei ya shilingi 1,200 lakini kwa utaratibu ni kwamba pamba hizi zinatakiwa zinunuliwe kupitia AMCOS pale kwenye AMCOS pamba inapowekwa katika go-down ni mnunuzi ndiyo mwenye gharama ya kubeba ile pamba kurudi nayo kiwandani kwake. Kwa hiyo, kuna additional cost ya transpotation, kuna asilimia 3 ya cess, kwa hiyo, bei ya mnunuzi inazidi shilingi 1,200. Kwa hiyo, wanunuzi wengi hawaendi na Serikali imeonyesha nia ya kutoa guarantee kwa wanunuzi katika financial Institution, financial institution ikiangalia contract ambazo wanunuzi wanazo, inaona kuna risk ya mnunuzi huyu atakwenda kukutana na hasara sokoni.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba niwashauri ule utaratibu wa Ma-DC kuwalazimisha wanunuzi wa pamba kununua pamba kupitia AMCOS, naomba Wizara ya Kilimo na Serikali itoe relief wakulima wapeleke moja kwa moja kwa wanunuzi kwa sababu itampunguzia gharama ya transportation huyu mnunuzi. Hii imetokea maeneo ya Bariadi, wakulima walianza kuuza pamba kwenye ginery, DC akatoa amri ya kumzuia mnunuzi asinunue matokeo yake pamba imebaki mikononi mwa wakulima. Kwa hiyo, naomba Serikali tutafute intervention ya haraka, futeni shilingi 100 ya bodi ili bei ya pamba iweze kuwa affordable kwa mnunuzi kununua, hili lilikuwa la jumla. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niende moja kwa moja kwenye hoja iliyoko mbele yetu, Serikali imefanya effort kubwa sana kutaka kufanya reforms na harmonization mbalimbali lakini naomba nitoe ushauri. Hapa kumekuwa na hoja ya pedi muda mrefu sana, kuna measure inatajwa katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri ambayo imetolewa kwa ajili ya diapers kwamba kwenye ushuru wa forodha tuna exemption inasema kwamba kupunguza ushuru wa forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwenye malighafi ya kutengeneza taulo za watoto (baby diapers). Nawaomba Serikali wekeni hapa na pedi ili i-accommodate two products. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ipo hoja ya Serikali kwamba measure hii imekuwepo siku za nyuma lakini hatukuona efficiency ya measure hii ikionyesha uwezekano wa bidhaa hii kuwa affordable. Inawezekana kuna matatizo ya kiutawala lakini tunawaomba muweke clarity hapa itamke kabisa taulo za akina mama na taulo za watoto. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ambalo nilitaka nishauri, Serikali tumeamua kuwekeza kwenye airline, leo tunawekeza katika airline industry na tumetoa measure ya kutoa exemption kwenye lubricants, nawaomba Serikali muende hatua ya mbele. Nawashukuru mmetoa clarifications ya local operators, mmeweka wazi kwamba local air transporters, nawaomba ondoeni kodi ya withholding ya ten percent pale ambapo mfanyabiashara anapoamua kununua ndege kwa sababu private sector hawanunui ndege kwa cash wananunua ndege kwa credit.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, anaponunua ndege ile kwa credit ile down payment anayolipa kwa mujibu wa sheria zetu anatakiwa alipe ten percent withholding tax. Nawashauri futeni hii, mmefanya effort ya kuweka exemption kwenye lubricants na nafahamu mmefanya effort ya kuweka exemption ya VAT kwenye insurance na spareparts za airline, nawaomba sana muweke exemption ya ku-remove withholding tax on re-payment of principal payment on purchase of aircraft. Hii itatusaidia sisi ku-attract a lot of investors kuja kwenye sekta ya ndege katika nchi yetu na wafanyabiashara wa ndege watakuja hapa kuwekeza kuwe na linkage kati ya Air Tanzania Investment na hizi ndege ndogondogo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe ushauri kwenye suala la ngozi, ameliongea Mheshimiwa Njeza, sekta ya ngozi ina mzalishaji wa ngozi ambaye ni mfugaji na mfanyabiashara wa kuchinja mifugo lakini ina trader na processor na hawa processors wamegawanyika sehemu mbili. Kuna processor aliyeko katika level ya kwanza anaye produce wet blue lakini kuna anaye produce crust na anaye produce finished goods.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu kwa kuwa sisi hatuko kwenye kijiji tuna-compete na other players around the world, taarifa ya Kikosi Kazi cha Wizara ya Mifugo imesema wazi changamoto kwenye sekta ndogo ya ngozi ni mbili. Moja, ni export levy ambayo tunaiweka kwenye ten percent ya wet blue matokeo yake viwanda vilivyoko ambavyo ni viwanda saba katika nchi yetu haviwezi kununua ngozi hizi kutoka kwa wakulima kwa sababu ngozi haziuziki nje. Nawaomba Serikali waiteni wenye viwanda sainisheni nao performance agreement muwasimamie waweze kununua ngozi tuweze ku-process ngozi hii na ku-add value ili tuweze kwenda level ya crust na level ya finished goods. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niipongeze Serikali kwa ku- excise duty mliyopunguza kwenye mazao yanayotokana na mvinyo unaotengenezwa na ndizi na vitu vingine. Ushauri extend hii docket muongeze na mvinyo unaotokana na zabibu. Zabibu inachajiwa Sh.200 per kilo, tume propose Sh.60 kwenye mvinyo unaotokana na mazao yanayotengenezwa na ndizi, nini ushauri wangu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania ni Mkoa wa Dodoma, ndiyo tunazalisha zabibu. Zabibu ina changamoto ya vifungashio kwamba kwa kuwa vifungashio vyote tuna import processor wa mvinyo unaotokana na zabibu anakuwa not competitive outside mipaka ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo wakiongeza hiyo, tukampa na yeye incentive ya Sh.61/=, nimwombe Mheshimiwa Waziri wa Fedha, dada yangu Mheshimiwa Ashatu ambaye yuko hapa kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha, kwenye mpango tunatenga ten billion kwa ajili ya ngozi. Ushauri wangu wa-allocate hizo ten billion kwenye zabibu ili tuweze kupanua sekta ndogo ya zabibu, wakulima walioko Dodoma waweze kufaidika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa, niwaombe sekta ya kilimo ndio imeajiri Watanzania wengi, nawaomba sana pendekezo ambalo tumelitoa kwenye Kamati na wadau wamekuja nalo la kuomba exemption ya VAT kwenye vifungashio kwenye grain drying equipment kwenye sheria wamesema kwamba for a person engaged on agriculture yaani yule mkulima wa Nzega ndio anunue hiyo equipment, nawaomba waongeze for a person engaged on agriculture and the dealers and agent kwa sababu wanao- import hivi vifaa sio mkulima wa Nzega… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)