Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Job Yustino Ndugai (4 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. JOB Y. NDUGAI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba mwelekeo wa usambazaji umeme Wilayani Kongwa kwa TANESCO na REA kama ifuatavyo:-
(a) Vijiji ambavyo havina umeme kama Pembamoto, Mbagilwa, Bangibanyi, Makole, Nguji, Muungano, Mkoko, Kiteto, Masinyeti nakadhalika.
(b) Vijiji vyote ambavyo bado huduma ya umeme haujafika kwenye sekondari, zahanati, visima vya maji, makanisa, misikiti, vitongoji vilivyoachwa.
(c) Miji midogo inahitaji umeme sana Kibaigwa, Kongwa, Mlali, Mkoka, Sagara, Mbande, Songambele, Pandambili.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. JOB Y. NDUGAI: Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba sana kilometa sita zilizobakia kuwekwa lami kati ya Mbande – Kongwa, mwaka huu zifanyiwe kazi. Miaka 20 sasa tunaongelea jambo hili hili kila mwaka, haipendezi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. JOB Y. NDUGAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Halmashauri za Miji Midogo; za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji kuna kanuni za uendeshaji ambazo zinapelekea kuwepo kwa vikao vingi sana kwa mwaka. Kamati ni nyingi mno na malipo ni ya mara kwa mara kwa kila Diwani na zaidi kwa Wenyeviti/Mameya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia wawakilishi hawa ni wengi sana, hivyo ipo haja ya kuangalia kama Kongwa unahitaji Madiwani 30 waliopo plus miji miwili midogo ya Kongwa na Kibaigwa ina Wenyeviti wa Mitaa 30 pia. Kwa Mkoa wa Dodoma kwa mfano, Halmashauri ni Kondoa Vijijini; Kondoa Mji; Chemba; Bahi; Dodoma Jiji; Chamwino; Mpwapwa; Kongwa; Mpwapwa Mji Mdogo; Kibaigwa Mji Mdogo; Kongwa Mji Mdogo, jumla ni 10. Kama wawakilishi ni 30 tu kwa kila Halmashauri kwa kikao kimoja cha Madiwani hao 30 x 10 = 300 na kila mmoja hulipwa shilingi 240,000 kwa kikao, jumla ya kikao kimoja tu ni shilingi 72,000,000 (hii ni minimum). Wajumbe wa Bodi za Afya kila Wilaya ni 100 x 240,000 = 24,000,000. Madiwani wajumbe wa Kamati za Fedha na Mipango wanakaa mara 12 kwa mwaka, kwa vikao vya Kamati hiyo tu na hao hao ni wajumbe wa Kamati nyingine kwa hiyo wanalipwa each siyo chini ya mara ishirini kwa mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja hapa ni kwamba vikao vipunguzwe kwa idadi na malipo yapungue. Patolewe mwongozo maana malipo haya ni kwa fedha za ndani za Halmashauri. Kipaumbele kinakuwa ni vikao vya Madiwani, fedha za maendeleo zinakosekana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. JOB Y. NDUGAI: Mheshimiwa Waziri, tunaomba sanasana tuanze kujenga kwa lami barabara ya Kongwa – Arusha kupitia Olkesmet (Simanjiro). Tuanze hata kama ni kilometa 15 tu.

Mheshimiwa Waziri, Kongwa Mjini tunahitaji lami angalau tupate hata kilometa 5 tu.

Mheshimiwa Waziri, Daraja kubwa la Njoge kwenye barabara itokayo Pandambili ni muhimu mno kujengwa. TARURA wapewe bajeti.