Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Dr. Dalaly Peter Kafumu (24 total)

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017- Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Naomba nianze kwa kumshukuru tena Mungu kupata nafasi hii kutoa na mimi mchango wangu. Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara na Mazingira, na ni Mwenyekiti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nitoe mchango wangu baada ya kuwa nimekutana na wadau wengi sana pamoja na Kamati yangu, tulikutana na wadau wenye viwanda, wafanyabiashara lakini pia tulikutana na mamlaka za udhibiti, ziko nyingi, tulikutana nazo kama 19 hivi. Tulikutana pia na waagizaji wa bidhaa na wale ambao wanapeleka bidhaa nje. Pia tulikutana na Wizara ya Viwanda na Biashara. Kila tulipokutana swali langu la kwanza kwa Waziri lilikuwa ni kwamba hivi tunafanya muujiza gani ili tuweze kutekeleza hii azma ya Mheshimiwa Rais ya kuwa na viwanda katika miaka 10 ijayo? Waziri ni shahidi na hata Wajumbe wenzangu ni mashahidi, tuliuliza sana swali hili na kwa kweli hatukupata jibu kwa maana kwamba yale yote yaliyowasilishwa kwenye Kamati ni business as usual. Kwa kweli ni vizuri sisi Wabunge wote wa Kambi ya Upinzani na sisi wa Chama cha Mapinduzi tutoe ushauri ambao utatutoa hapa tulipo utupeleke mbele. (Makofi)
Baada ya kutafakari, naomba niseme mambo kama sita hivi kwa kifupi, nadhani muda utanitosha. Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano una maneno mazuri sana na unasema vizuri sana, naturing industrialization in Tanzania. Maneno haya ni mazuri na Mheshimiwa Rais ameya-reflect wakati anafanya kampeni na sisi sote lazima tufikirie kwenda huko. Tukifanya kazi kama tunavyofanya tunaweza tusifike.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza, ni lazima tuwe na quick wins sasa, vitu ambavyo tutavifanya kwa haraka tuone mabadiliko. Jambo la kwanza katika quick wins, ni viwanda vilivyopo na wafanyabiashara waliopo; tuwaondolee kero zao, tutengeneze mazingira mazuri, waweze kupanuka badala ya kufa. Walituambia wana kero sana na Waheshimiwa Wabunge wamesema, kero ni nyingi. Regulation ya udhibiti, kila mtu anakuja kudhibiti kiwanda kidogo. OSHA anakuja, nani anakuja mpaka unafunga. Kwa hiyo, Regulatory Authorities hizo bado zinachelewesha huduma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, walisema mambo mengi; utitiri wa kodi, tozo na vitu vingi sana. Jambo lingine walilosema hao wenye viwanda vilivyopo, walisema service wanayopewa na hizi institutions, wakati mwingine wanazilipia kwa bei kubwa. Serikali inatakiwa itoe service hii bure kwa hivi viwanda ili viweze kuendelea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, walilosema miundombinu. Umeme unakatika sana. Pamoja na kwamba tuna mipango mizuri, tunaishukuru Serikali, lakini bado umeme uwe stable, reliable. Siyo unakatika! Kwenye kiwanda ukikata dakika tano, umechelewesha production kwa muda mrefu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia walisema kulinda bidhaa za ndani. Kuna hatua tunaona zinachukuliwa, tunaishukuru Serikali. Tulinde bidhaa za ndani dhidi ya bidhaa za nje. Viwanda na wafanyabiashara waliopo wana mambo mengi sana ambayo siwezi kuyasema, lakini Waheshimiwa Wabunge wamesema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, Serikali mmeonesha vizuri sana kwenye hotuba, lakini pia kkwenye Mpango, viwanda vya kimkakati. Ukisoma kwenye mpango vimejatwa vizuri; viwanda vya chuma, vimetajwa viwanda vinavyotumia mazao ya kilimo na viwanda vingine kama vya mazao ya uvuvi na mazao ya mifugo. Ukienda kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri, unaona ni kiwanda kimoja tu cha chuma ndio cha kimkakati, lakini viwanda vingine; sijui kiwanda cha kutengeneza dawa za kuua mbu, sio cha kimkakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni lazima tuangalie hasa viwanda vinavyotumia mazao ya kilimo. Hivi ni vya kimkakati kweli, sivioni kwenye speech! Kwa hiyo, tunaomba hilo liwe jambo la pili. Tunavyotaka kujenga viwanda vipya, ni hivi vitakavyohamasisha industrialization katika nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu ni kuhamasisha wawekezaji. Tuliongea na wawekezaji wengi wa ndani na nje, wote walisema wanaonekana kama wezi. Mtazamo wa Watanzania wengi na mtazamo wa hata viongozi wengine, mwekezaji wa ndani anayepewa eneo kubwa anasumbuliwa, anaonekana mwizi, yule wa nje ndio kabisa! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana, wawekezaji hawa wanahitaji misamaha. Japokuwa tulipitisha sheria mwaka jana, ile ya VAT ya mwaka 2015 nadhani, na mimi nilisimama hapa nikasema hii VAT ukiweka kwenye vifaa kwa ajili ya kutafuta madini, kwa ajili ya kuanzisha kiwanda, utafukuza wawekezaji. Kwa hiyo, nasema tena, tutazame hii misamaha tusiiogope.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la nne ni kufufua viwanda vilivyokufa. Kama walivyosema Waheshimiwa Wabunge, viko viwanda vya mazao ya kilimo kama pamba. Igunga kule tulikuwa na Manonga Ginnery, ilikufa. Hatutazamii kufufua viwanda vya namna hii. Kule Tabora ndugu yangu amesema; viwanda vya nyama Mwanza, Shinyanga na kadhalika tumeviacha; viwanda vya chuma Tanga na kadhalika, tuvifufue hivi. Kuna viwanda vingine kama CAMATECH na Mang‟ula, vitu vya namna hii tuvitazame, tuvifufue. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, niseme maeneo ya kuwekeza (EPZA), tulipe madeni. Serikali itafute fedha ilipe madeni, Shilingi bilioni 191. Fedha hizi zitafuteni mlipe ili mpate maeneo mengine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, samahani, naomba nimalizie kwa kusema, tulikubaliana na Mheshimiwa Waziri kwamba ili tuweze kupata gist ya mambo haya, tuitishe Mkutono wa wadau na tulikubaliana tuitishe Dodoma kabla ya bajeti. Tulisema wadau ambao tunataka tuwaitishe, tuzungumze tufanye dialogue hii, tujue; tukipata yale maneno ndiyo tuyaingize kwenye mpango.
Mheshimiwa Mwenyekiti, najua mwaka kesho tutakuwa na mpango mzuri zaidi kwa sababu tutakuwa tumepata mawazo ya wenzetu. Kwa hiyo, wadau ambao tulikubaliana, Mheshimiwa Waziri na hii lazima uitishe labda hata wiki ijayo ili tupate mambo haya kwa ajili ya mwaka kesho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja. Ahsante sana.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nihitimishe hoja hii muhimu sana katika historia ya maisha ya Tanzania yetu. Tunataka nchi yetu iwe nchi ya viwanda ifikapo 2025.
Ninawashukuru Waheshimiwa Wabunge mliochangia, tulikuwa na wachangiaji 37, kumi na sita wamechangia kwa maandishi na kwa maneno wamechangia Waheshimiwa Wabunge 21 pamoja na Mawaziri, ahsanteni sana kwa michango yenu. Kamati tunashukuru sana kwa hayo yote.
Waheshimiwa Wabunge, suala la kujenga viwanda katika Tanzania ni suala la kufa na kupona na ndiyo maana liko kwenye awamu hii ya Mpango wa Maendeleo. Tulianza kama Mbunge mmoja alivyosema kuweka mazingira. Tulitakiwa tuwe tumeshamaliza kuweka mazingira ya miundombinu halafu tuanze ku-industrialise lakini hatukuweza. Kwa hiyo, sasa tuna-industrialise wakati huo huo tunaweka mazingira. Kwa hiyo, ni jambo letu sisi wote ni jambo la kufa na kupona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ningependa kusema ni jambo la coordination, Serikali inafanya kazi individualy mmoja-mmoja. Nishati na Madini yuko kwake, Kilimo yuko kwake, kila mtu yuko peke yake. Mimi nilitarajia maprofesa pamoja na madaktari, Serikali ina madaktari na maprofesa, mkutane wote, Wizara zote mkutane mtengeneze road map ambayo itatupeleka, lakini mnapofanya kazi kila mtu peke yake hatutafika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Profesa Waziri wa Nishati umeeleza vizuri sana juhudi ambazo tunataka kuleta umeme, lakini uko peke yako, hufanyi kazi na wenzako. Mheshimiwa Profesa Waziri wa Kilimo ni Daktari wa Kilimo yule na yeye yuko peke yake. Msipokutana tukatengeneza kitu kimoja hatutafika. Kamati tunadhani mkakati wa pamoja wa Serikali nzima unatakiwa ufanyike, vinginevyo hatufiki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la sekta binafsi kuhamasishwa mmesema vizuri sana, Waziri wa Fedha amesema vizuri na baadhi ya Wabunge, huo mtazamo, pamoja na Waziri wa Viwanda hapa, mtazamo wa kwenda kwenye ujamaa hatuutaki. Sasa hivi we are not going back to ujamaa, tunataka sekta binafsi ijenge uchumi. Serikali inaweza kuwa na viwanda vya kimkakati vichache, lakini mnavyofikiria kutwaa viwanda na kuviendeleza, nashukuru Waziri wa Viwanda na Biashara amesema hapa, yeye ni coordinator ili sekta binafsi iweze kujenga viwanda pamoja na Serikali kwa namna ya pekee. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pesa kutokupelekwa limesemwa sana. Waziri wa Fedha ameeleza vizuri pale, wanahangaika na kukusanya, lakini ni jambo ambalo tumelipata kwa wadau, tumelipata kwenye Mawizara ni tatizo letu sisi sote, ni lazima tulichukulie kwa upana wake kwamba, fedha lazima zipatikane na zipelekwe. Tunapopanga Bungeni humu, basi tupange bajeti ambayo ni realistic, tutaweza kupata fedha na kuzipeleka, lakini tunapopanga tu bajeti ambayo haina fedha tunakuwa kama tunawadanganya wananchi, siyo jambo zuri sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la miundombinu limesemwa sana na wadau. Tunamuomba Mheshimiwa Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, pamoja na juhudi zote hizi lakini tatizo bado lipo. Ukienda kwenye kiwanda chochote utakuta wanasema umeme unakatika katika kweli na wengine mpaka wanafunga viwanda, wengine mitambo inaharibika, kwa hiyo, ni jambo lipo. Pamoja na mikakati ya kisayansi na nini, lakini umeme bado ni shida. Tukubaliane kwa kweli, pamoja tuende ili tufike mahali panapohitajika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo Wabunge wamesema ambalo nataka nili-echo tena, malighafi tutumie, tunapojenga viwanda tutumie malighafi ambazo zinagusa watu, kilimo, uvuvi na mifugo. Ukianzisha kiwanda cha tiles kama cha ndugu yangu kule unaweza ukawanavyo 200, lakini wananchi umaskini unaendelea. Kwa hiyo, kuna suala la maendeleo (growth ya uchumi), lakini kuna suala la economic development pia, maendeleo ni tofauti na kukua kwa uchumi, unaweza ukakuza uchumi, lakini wananchi bado wanahangaika.
Kwa hiyo, ni lazima tutumie hizi bidhaa, malighafi za Tanzania za kilimo, mifugo na uvuvi na zingine tuzijengee viwanda. Hii itatusaidia sana na Wabunge wengi wamesema na mimi naunga mkono jambo hilo.
Narudia tena kwa kusema ni lazima mwekezaji akija awe wa ndani au nje, ajisikie amepokelewa. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mheshimiwa Mwijage, wawekezaji wengi bado wanalalamika, pamoja na kwamba upo vizuri, lakini wenzako sasa, mtu akienda ardhi kule anaweza akakimbia, akienda madini kule anaweza akakimbia, akienda kilimo anakimbia, wewe uko vizuri. Kwa hiyo, coordination ni muhimu, lazima m-coordinate mfanye vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mazingira ya kufanya biashara wadau wamelalamika sana. Kwa kweli ni jambo letu sisi sote na sisi Kamati hatukutoa hii ripoti kwa sababu ya kuipiga Serikali, hapana. Tumetoa hali halisi tu inavyoonekana huko kwa wadau ili tushughulikie jambo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, karibu namaliza, jambo kubwa la mazingira. Mazingira ni jambo kubwa kama alivyosema Mheshimiwa Waziri, uharibifu wa mazingira ni mkubwa kuliko tunavyofikiria. Tuna mpango wa kupanda miti lakini hautekelezeki. Tuliliomba Bunge mwaka jana uanzishwe mfuko na fedha za tozo zote ziingie kwenye mfuko. Tumeweka pendekezo, tumeweka Azimio la Bunge kwamba bajeti ijayo tozo zote za kimazingira ziingie kule na mfuko huu uwe na fedha ili tuweze kutunza mazingira, vinginevyo tutaimba sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Ziwa Victoria ni vizuri niurudie, unakamilika mwezi wa 12, lakini effect yake ni ndogo. Naishauri Serikali kama mnaweza kuanzisha mradi mwingine katika viunga vya Afrika Mashariki utakaoshughulikia zaidi mito hii mikubwa ambayo inaleta maji, tunaweza kulitunza ziwa letu vizuri zaidi, lakini uvuvi haramu ni tatizo kubwa sana. Serikali lazima mliangalie hili, Wizara ya Kilimo, wote tushirikiane ili tuweze kuondokana na jambo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mabadiliko ya tabianchi ni jambo kubwa pia. Kuna Mheshimiwa Mbunge mmoja amesema, Tanzania ya mwaka 68 na Tanzania ya leo ni tofauti. Mito imekauka, maziwa yamekauka, vitu vingi vimekauka na sisi wote ni mashahidi. Kwa hiyo, ni lazima tulitazame jambo hili kwa namna ya tofauti na ninaiomba Serikali katika kutengeneza miradi na katika kuzungumza na wadau wa maendeleo ni lazima tupate fedha kwa ajili ya ku-curb jambo hili, tusipolitazama vizuri mambo yetu yataendelea kuwa mabaya zaidi. Nasema suala la mazingira ni mtambuka na lazima tushirkiane kama nilivyosema awali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ni maazimio. Haya maazimio tuliyoyapita, naomba ni-echo yale aliyoyasema Mheshimiwa Nsanzugwanko na mimi wakati nawasilisha hapa nilisema. Maazimio haya ni maazimio muhimu sana, hatutaki yakabaki kwenye shelf za Bunge, hebu tutengeneze utaratibu wa kuyafuatilia kama Wabunge. Tukiunda Kamati Ndogo ya kuyafuatilia, tunajadiliana na Serikali maana hili ni jambo letu wote siyo kwamba tunapingana ni jambo letu wote, tusigombee fito. Tutengeneze Kamati ambayo itafuatilia na Serikali itakuwa inatupa mambo kwa uzuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa nizungumzie viwanda ambavyo vimesemwa na Wabunge. Mbunge wa Mkuranga kasema ana viwanda sijui vingapi 56 na viwanda 11 jumla 67, pia Waziri anasema ana viwanda 1,149 sijui, kama namba nimeishika vizuri.
WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Ni viwanda 1,169.
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda 1,169.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme hivi Mheshimiwa Waziri, Kamati yangu haina taarifa kabisa. Interpretation yetu kama Kamati ni kwamba Waziri hushirikiani na sisi vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu kama kungekuwa na ushirikiano tungekuwa tuna habari, hata kufunguliwa kwa kiwanda cha Mkuranga au wapi, hata Mwenyekiti tu angeenda. Hata Mjumbe mmoja tu hizi habari tungekuwa nazo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge, ninatamuomba Mheshimiwa Rais labda amuongezee Naibu Waziri inawezekana ana shughuli nyingi sana ili tuweze kumpata Waziri kirahisi zaidi. Vinginevyo, Kamati tunafanya kazi peke yetu Mheshimiwa Waziri, sasa hii siyo sawa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa naomba Bunge lako lipokee Taarifa ya Kamati na kuwa maamuzi ya Bunge. Ahsante sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE.DKT. DALALY P. KAFUMU: Mhehimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru Mungu kwa kupata nafasi hii kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu, na nakushukuru na wewe Mwenyekiti kwa kunipa nafasi. Lakini kama wenzangu walivyosema tuwapongeze Waziri na Naibu Waziri, pamoja na wataalam kwa kazi nzuri wanayofanya katika mazingira haya magumu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua wana changamoto nyingi sana, mimi nilikuwa mmoja wao wakati fulani, kwa hiyo najua changamoto walizonazo, wanahitaji kuhudumia wananchi, lakini pia wanahitaji kuhakikisha wawekezaji wanaendelea kuja katika nchi yetu. Mnatakiwa kukaa katikati, ukihamia upande mmoja unaweza kuharibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi nitasema maneno machache ya kutoa ushauri tu kwamba ukiangalia ukurasa wa 62 wa hotubua ya Mheshimiwa Waziri, kipengele 136, naomba nisome, kinasema; “Pamoja na bei ya madini ya dhahabu na nikeli kushuka katika soko la dunia, Serikali imeendelea kuhamasisha uendelezaji wa miradi mikubwa ya madini,” mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana Waziri kwa kusema haya maneno, lakini ningependa sasa haya maneno ya-reflect katika vitendo vya Serikali katika kuhamasisha uwekezaji mkubwa. Sasa hivi ukipita mitaani huko ukisikiliza wawekezaji na wachimbaji wadogo kuna kilio kwamba Serikali imegeuka kidogo. Zile juhudi tulizofanya kuanzia mwaka 1995 Awamu ya Tatu na ya Nne zinakwenda tofauti kidogo, kwa hiyo mimi ningependa niwashauri Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri, hebu ongezeni juhudi za kuhamasisha wawekezaji waje tusipohamasisha hatutakuwa na migodi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi utafutaji na ninyi ni mashahidi umepunga kweli na utafutaji unapopungua maana yake ni kwamba hatutakuwa na migodi siku za usoni, hii migodi ikifungwa basi. Napenda niseme kwamba Kamati ya Bomani ilitushauri tukatengeneza sera nzuri, tukatengeneza na sheria nzuri, tumekosea wapi sasa mpaka tuanze kurudi nyuma? Ukiwasikiliza wawekezaji wengine wanasema Tanzania ninyi mnataka kurudi kwenye ujamaa, ukisikiliza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi nashauri Mheshimwia Waziri, hebu tutoke hapo tulipo, tutengeneze mikakati sasa ya kuhamasisha. Kwa mfano tulikuwa tunaenda sana kwenye mikutano hii ambayo wawekezajiwote duniani wanakusanyika, tunawaalika. Miaka miwili iliyopita hatujaenda na wale wawekezaji wanaona Tanzania haimo tena kwenye kazi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nawaombeni sana tujitahidi tuwahamasishe wawekezaji, wasikate tamaa, ninyi ni mashahidi leseni nyingi sasa hivi zimekaa idle kwa kweli, japokuwa tumetengeneza mfumo mzuri lakini hazifanyi kazi kwa sababu tumekosea wapi, wataalam wa nishati na madini toeni ushauri jamani kitu gani kimetokea? Mimi inaniuma sanamnapoona juhudi zile za Serikali ya Awamu ya Tatu na ya Nne zinakwenda nyuma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia majirani zetu Mozambique hata Malawi walitangaza geophysical results zao mwaka jana, sasa hivi wawekezaji wanaenda kule kutafuta dhahabu hii hii ambayo imeteremka bei. Kwa hiyo, mimi naomba sana na sisi tutazame tena wapi tumejikwaa, tuamke, ni ushauri tu ambao kwa kweli utatusaidia kwenda mbele upande wa madini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine napenda niseme juu ya ushiriki wa watanzania, tunaishukuru Serikali kwa kuwasaidia wachimbaji wadogo kuwapa hii mitaji. Lakini hebu wasaidieni pia na katika kutafuta madini. Geological Survey of Tanzania moja ya kazi yake kwa sera ile tuliyotengeneza ni kuyaangalia hayo maeneo ya wachimbaji wadogo na kuyapa value kidogo ili waweze kufanya kazi zao vizuri. Lakini pia ni kuwasaidia katika environmental impact assessment ili waweze kuwa na tija katika uwekezaji wao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo ningependa kulisema ni ushauri ambao hua natoa kila mwaka na sasa hivi natoa, mnaweza msinielewe sasa lakini baadaye mtanielewa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), ni wakala unaofanya kazi nzuri kama walivyosema, lakini unalipa Taifa hili gharama kubwa kwa sababu unafanya kazi zinazofanywa na taasisi zingine. Ngoja nitoe mfano, wanaangalia kampuni itaweza kulipa kodi, kazi ambayo inafanywa na TRA mnaweza mkasema ni audit, lakini kazi ni ile ile ukimuuliza mwekezaji anayekaguliwa na TMAA, mwekezaji anayekaguliwa na TRA anayekaguliwa na yule mkaguzi wa kisheria kazi wanazofanya ni zile zile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunafumia hela nyingi kufanya jambo moja, ukiangalia wanafanya kazi ya ukaguzi wa mazingira, NEMC anakwenda kufanya jambo lile lile. Wanafanya kazi ya kuangalia madini yanavyopelekwa nje, wametengeneza ma-desk pale kwenye viwanja vya ndege, kazi hii ilitakiwa kufanywa na Ofisi ya Kamishna wa Madini kwa Sheria ya Madini ya mwaka 2010. Mimi nasema skills na taaluma tuliyoijenga pale, hebu tuiweke mahali inapostahili, mimi ningependekeza na nimewahi kupendekeza kwamba hii kazi ifanywe na mtu mmoja sio watu wengi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tunaweza tukaifanya TMAA ikawa Idara ya TRA yenye Kamishna wake wa ukaguzi wa migodi na hizo skills zote tukamuachia TRA, itasaidia sana badala ya kufanya kazi mara mbili. Taarifa ninayoipata lazima iende TRA na kama amekosea mtu, TRA ndio anaechukua hatua, TRA akiacha inakuwaje? Kwa hiyo TMAA imewekwa hapo kufanya kazi za watu wengine ili watu wengine wachukue hizo information. Tunatumia fedha nyingi sana, kufanya jambo lile lile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nishauri tena, sasa hivi naweza nisieleweke nasema lakini siku za usoni nadhani nitaeleweka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kama nitapata muda, nataka nizungumzie mikataba ya madini. Mikataba ya madini watu wengi wanaisema tofauti, Sheria ya Madini…
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Ahsante sana.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Naomba nimshukuru Mungu tena kwa kunipa nafasi hii mara ya nne kuchangia katika Bunge lako.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niipongeze Serikali kwa mambo makubwa mawili. La kwanza, Serikali kutenga fedha nyingi kwenda kwenye maendeleo kwa sababu fedha hizi zitawafikia wananchi.
La pili, azma ya Serikali ya kujenga viwanda (nchi ya viwanda), hili ni jambo zuri na tunalipongeza. Tutakuwa na changamoto nyingi ambazo Waheshimiwa Wabunge wanazisema lakini nadhani tukitekeleza haya mambo mawili nchi yetu itafika mahali pazuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichangie mambo kadhaa. La kwanza ni hili jambo la gratuity ya Wabunge, naomba nianze na hilo. Sheria ya mwaka 1999 ya Political Service Retirement Benefit iliwekwa makusudi kwamba viongozi hawa wa kisiasa spectrum yote mpaka DC, wamefanya kazi kubwa sana ya kuhangaika na wananchi, wanapewa retirement ya namna ile kwa kuwapongeza na kuwapa zawadi na hii ilikuwa ni hekima tangu mwaka 1981 sheria ilipotungwa na kurekebishwa. Sasa leo kama hekima ya Serikali ni kuiondoa, nadhani watafakari vizuri zaidi kama alivyosema Mheshimiwa Ngeleja ili kama ni lazima basi spectrum nzima ya viongozi iweze kulipa kodi kwenye mafao yao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili amelisema tena Mheshimiwa Waziri wangu mstaafu ni kuhusu sekta ya uchimbaji wa madini ambapo kwenye nchi zingine ni injini ya uchumi wa nchi zile. Serikali ilianza vizuri sana miaka ya 1990 mpaka miaka mitano iliyopita kuhamasisha uchimbaji mkubwa pamoja na uchimbaji mdogo, lakini mwaka huu uchimbaji mkubwa sijausikia kabisa. Tutafanya makosa makubwa sana kwa sababu sekta hii ni sekta inayoleta FDI ya kutosha, ni sekta inayoleta ajira na mifano ya Afrika ipo. Botswana, South Africa, Mali, Ghana, Burkina Faso hata DRC Congo ni nchi ambazo uchumi wao unategemea sana madini, sasa sisi tunaacha kuwaalika wawekezaji wakubwa waje kuwekeza katika nchi yetu kufanya kazi hii, tunafanya makosa. Naomba Serikali tutafakari tena kuna kitu gani kimetokea, sheria nzuri tunayo, nilisema wakati nachangia kwenye madini na narudia tena jamani Serikali tuhamasishe uwekezaji katika spectrum yote. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nataka kuzungumzia ni misamaha ambayo walikuwa wanapewa mashirika ya kidini wanapoingiza vitu kwa ajili ya shughuli zao. Serikali inasema watalipa halafu watarudishiwa, mimi nina mifano katika sekta ya madini, unapo-export unasamehewa VAT na unalipa hiyo VAT kurudishiwa ni ngoma. Makampuni yanaidai Serikali hii shilingi bilioni zaidi ya 100, wameshindwa kabisa kurudisha. Tusifikirie kurekebisha jambo kwa kuongeza kodi, turekebishe mfumo. Sisi kila kitu kikiharibika kwenye kodi tunaenda kwenye kodi badala ya kurekebisha mfumo ambao umefanya hii kodi isikusanywe. Kwa hiyo, naomba sana mashirika ya dini yanapoleta vitu kwa ajili ya kuhudumia wananchi wetu yasamehewe kama kawaida, turekebishe utaratibu wa kukusanya hizo kodi.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo nazungumza kidogo kidogo ili niweze kuchangia mambo mengi, jambo lingine ambalo napenda kuchangia ni kuhusu watumishi wa umma. Mheshimiwa Rais alipoingia katika Serikali yake amefanya kazi moja nzuri sana ya kuhakikisha discipline inarudi katika utumishi wa umma. Amefanya ziara za kushtukiza na amefanya mambo makubwa na sisi tunamuunga mkono. Hata hivyo, kuna changamoto imejitokeza kwa wale wasaidizi wa Mheshimiwa Rais wameshindwa kurudi kwa wafanyakazi na kuwapa motisha (morali) ya kufanya kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mtaalam mmoja wa mambo ya psychology ya institutional structures alisema hivi:-
“Leaders must know how to develop their EQ and put into practice to attain emotional intelligence, they need for insparing others to achieve. These emotionally excellent leaders are able to create a heart of an emotionally intelligent organization. An emotionally intelligent organization is one where its leaders and their followers exhibit a high level of emotionally excellence which allows them to connect one another and deliver in the organization.”
Mheshimiwa Naibu Spika, sisi nchi yetu ni organization ambayo viongozi wanaosimamia wafanyakazi na wafanyakazi wenyewe lazima wawe na uhusiano ambao siyo wa paka na panya, uhusiano wa kuogopana, hatutapata mafanikio mazuri katika kufanya kazi.
Kwa hiyo, naomba wasaidizi wa Rais (Mawaziri na wasaidizi wao) hebu warudi kwenye Wizara zao. Mimi nimekaa kwenye Wizara, mtumishi usipompa hamasa ya kufanya kazi atagoma kimya kimya, huwezi ukapata matunda ya kazi yake. Leo hii ukienda kwenye Mawizara watu wameinama wanasema naogopa kutumbuliwa. Viongozi mnaosimamia watumishi, wahamasisheni watumishi wapende kazi yao, wasiogope, wajisikie kufanya kazi kuipenda nchi yao vinginevyo productivity itaharibika, tutaendelea kutumbua lakini hatutapata mafanikio mazuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho nataka niseme habari za Mkoa wa Tabora. Mkoa wa Tabora ni mkubwa kuliko mikoa yote Tanzania na ndiyo maana tumeomba tuugawe. Mkoa wa Tabora una matatizo ya maji kuliko mikoa yote Tanzania. Mkoa huu unahitaji kutazamwa kwa jicho tofauti. Tunaomba ule mradi wa kuleta maji Mkoa wa Tabora kutoka kule Malagarasi utekelezwe ili Tabora tupate maji.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye elimu Tabora tunaonekana wa mwisho, lakini ni kwa sababu ni mkubwa, usimamizi unakuwa ni mgumu sana kwa viongozi wetu. Leo ninavyoongea Mkuu wa Mkoa wa Tabora hana gari, hawezi kutembea kabisa kuzungukia maeneo yake unategemea elimu itakuwaje? RAS naye pia hana gari na ma-DC wetu nao hawana magari.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali iuangalie Mkoa wa Tabora na itusaidie tuweze kufanya kazi kuwahudumia wananchi wetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja na ahsante sana kwa kunipa nafasi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kutoa mchango wangu mdogo. Kwanza nimshukuru Mungu tena kwa kunipa nafasi hii kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu nichangie kama Wabunge wengine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Waziri kwa speech lakini pia nampongeza kwa kazi ngumu aliyonayo mbele yake. Tunajua yeye ni mtaalam ataweza kutusaidia.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichangie mambo mawili tu, na kama nitakuwa na la tatu basi nitachangia. La kwanza, kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri ukurasa wa 31 kifungu 3.4.10 anasema katika mwaka wa 2015/2016 Wizara imepitia Sheria ya Manunuzi ya Umma namba saba ya mwaka 2011 na kupendekeza marekebisho ya Sheria hiyo. Napenda niseme kati ya vichaka au sehemu ambazo zinatumika kumaliza fedha ya Taifa hili ni Sheria ya Manunuzi. Bei za tender za Serikali huwa ni za ajabu kweli, ni kwa sababu ya sheria hii. Kwa hiyo, tunaiomba Serikali kwa kweli sheria hii iletwe kwenye Bunge hili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimesoma sheria ambazo mmetupa tuangalie za marekebisho miscellaneous, hii sheria siioni, mtaileta nini? Maana yake ndiko huko fedha zinakopotelea. Tunaomba kama mnaweza kuileta hata kwa hati ya dharura tutashukuru kwa sababu matumizi ya Serikali yanatumika vibaya kulingana na sheria hii ya mwaka 2011. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ambalo nataka kusema ni juu ya kazi ya BOT (Benki Kuu ya Tanzania) na hili jambo niliwahi kusema na narudia tena, labda baadaye litaeleweka. Ni vizuri kusema sema hata kama ni jambo la uongo linaweza kuwa la kweli. Sisi tunachimba dhahabu katika nchi yetu, tuna migodi minne sasa inayotoa dhahabu. Kazi ya BOT ni kutunza fedha za kigeni lakini kutunza dhahabu safi na dhahabu ina represent utajiri wa nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna wakati tulijaribu kununua dhahabu tukapata hasara kwa sababu tulinunua dhahabu, tulivyoipeleka kwenye smelting ikaonekana ni makapi lakini sasa tuna nafasi nzuri ya kupata dhahabu safi kwa kuwaambia makampuni watulipe nusu ya mrabaha katika dhahabu safi, hatuna tatizo. Hivi tunashindwa nini kuchukua dhahabu safi tukalipwa, tukaitunza ili baadae watoto wetu tutakapokufa tunawaambia bwana dhahabu hiyo mnaona mashimo hayo, ipo pale tani 200, 300 zimekaa. Uzuri wa kuwa na dhahabu kwenye reserve yetu tunaweza kurekebisaha hata thamani ya shilingi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, thamani ya shilingi ikiteremka tuna-release kidogo inakuwa nzuri. Kwa hiyo, tuna wajibu sasa hivi kutunza dhahabu. Najua niliuliza swali mwaka jana, Serikali ikapiga chenga lakini nasema hatuna sababu ya kutokutunza dhahabu kwenye benki yetu. Nchi zingine kama Marekani wana tani 8,000 kwenye reserve yao. Ujerumani wana tani zaidi ya tani 3,000 hata Libya nchi inayopigana ina dhahabu 116 tani. Na nchi nyingi ambazo unaziona ni tajiri zote zina dhahabu kwenye reserve yao. Kwa nini tusifanye hivyo, kwa vile na sisi tunachimba dhahabu. Nchi za Afrika, iko South Africa, ina tani zaidi ya 100 kwenye reserve yao, sisi tuna shida gani? Sisi zero! Kwanini? Kwa hiyo naomba sana Serikali mtafakari jambo hili. Tafuteni wataalam waangalie namna tunavyoweza kufanya jambo hili tukapata dhahabu. (Makofi)
Jambo la tatu, ni matumizi holela ya dola katika nchi yetu. Dola inatumika mahali popote. Ukienda leo mahali popote hata Karikaoo unaweza ukatoa dola ukanunua, hata salon umekwenda kutengeneza nywele ukanunua kwa dola. Dola zetu zinapotea. Haziingii kwenye mfumo halali wa nchi, kwa hiyo dola zinaibiwa, zinapotezwa, zinabebwa kwa sababu tumeruhusu hili jambo. Ukienda South Africa ninyi mashahidi, huwezi kulipa hata hoteli ya kitalii kama huna dola, lazima ukatafute hela yaki-South Africa. Nenda nchi za Ulaya, hivyo hivyo, nenda Thailand, kila mahali. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tuna ruhusu kila mahali dola inatumika, tunapoteza fedha. Serikali tunaomba tena, nilishawahi kuuliza swali mkapiga piga chenga, mimi naomba jamani uchumi wetu unaharibika kwa sababu tuna mifumo ambayo haisimamimii fedha zetu vizuri. Hili ni jambo sio zuri sana. Tunaomba Serikali msimamie jambo hili tungeni sheria. Tungeni sharia tuko tayari sisi Wabunge tutunge sheria ili fedha za kigeni ziweze kubaki kwenye reserve ya Taifa letu vinginevyo tuna kazi kubwa kweli. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda Ubelgiji huwezi ukatumia hela ya nje lazima uibadilishe iwe Euro sasa sisi tuna shida gani?
Mheshimiwa Naibu Spika, la nne na la mwisho, naomba nisipigiwe kengele, leo niko very smart. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuelimishwa kidogo, la kwanza ni ahadi ya Mheshimiwa Rais ya shilingi milioni 50. Amesema mama yangu pale, kwenye bajeti huko kote nimeangalia sioni, hivi tumeiwekea bajeti wapi?
Inawezekana nimeisoma vibaya, kwenye vitabu vyote nimeangalia hakuna mahali ambapo tumeweka fedha kwa ajili ya kutekeleza ile ahadi ya Rais, basi nielimisheni.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo lingine ni MCC. MCC tuliiachia ikaondoka hatuna mradi wa MCC tena, labda kama kuna mazungumzo mapya. Hata hivyo, bado kuna subvote 1007 inasema imeweka hela shilingi milioni 500 kwa ajili ya MCC, ni kitu gani hicho?
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Naibu Spika nakushukuru kwa kunipa nafasi
nichangie kidogo hoja hizi mbili mbele yetu; Taarifa ya Miundombinu na Taarifa ya Nishati na
Madini.
Kwanza napenda kusema kwamba, sekta ya madini kwa kipindi hiki wawekezaji
wamepata shida sana, wengi wanakimbia, wengi wanarudi na sababu kubwa ni kwamba
wawekezaji wengi wana hofu kwamba security of tenure ya leseni zao ziko hatarini wanaweza
kunyang‟anywa leseni wakati wowote, kwa hiyo, nilikuwa naiomba Wizara na Kamati hebu
tujaribu kuishauri Serikali irudishe mazingira mazuri ya kuhamasisha Wawekezaji waje.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, ni wachimbaji wadogo ambao kwa sasa hivi
wamekuwa wachimbaji haramu kwa sababu tozo na kodi mbalimbali za uchimbaji mdogo
zilipandishwa sana katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, kwa hiyo, wameshindwa kulipa na
wengi haramu bado wanaendelea kuchimba. Naiomba Wizara hebu fanyeni review ya
wachimbaji wadogo wanavyolipa.
Mheshimiwa Naibu Spika, la tatu, ni kuhusu mradi wa magwangala. Mheshimiwa
Musukuma amesema, wameweka mahali ambapo kwanza hata hawajapafanyia
environmental impact assessment na kwa sababu hawajui watatunzaje mazingira ya eneo lile,
Mheshimiwa Waziri labda au mtu mwingine alikwenda akachangua tu akasema wekeni hapa,
sasa hayachukuliwi. Maana yake ni nini? Eneo hilo litachafuka kimazingira. Kwa hiyo, sisi
tulikuwa tunaomba, Kamati inayosimamia mazingira huo mradi muusitishe. Tafuteni maeneo ya
kuwapa hawa Wachimbaji wadogo kama alivyosema Mheshimiwa Musukuma, ni vizuri
kushirikiana na mgodi, kushirikiana na wananchi mpate maeneo mazuri zaidi badala ya kufikiria
kuwapa magwangala ambayo hayana Madini. (Makofi)
Mwisho ni kuhusu bandari, Bandari ya Dar es salaam ilipata matatizo kidogo sasa hivi
tunaishukuru Serikali imeanza ku-pick up kidogo lakini kuna tatizo moja kubwa na tutalisema
sana kesho kwamba Mkuu wa Bandari ameamua kubadilisha watumishi pale, wale wasimamizi
wote kawabadilisha wako saba. Kaleta watu wengine ambao hata taaluma ya mambo ya
maritime hawana. Hii inaleta mdororo zaidi wa huduma katika bandari yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tutaiomba Kamati pamoja na Wizara mliangalie hili, watu
waliopewa nafasi pale, Wakurugenzi wote wanaomsaidia Bwana Kakoko pale hawana
taaluma wengi ni wahandisi kutoka TANROADS, tutaendeshaje mambo haya kwa urafiki?
Nashukuru kwa kunipa nafasi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuishauri Wizara itathmini miradi yote iliyokuwa imefadhiliwa na Benki ya Dunia kuboresha baadhi ya zahanati kwa kujenga wodi za wazazi na theater ili kuboresha afya ya mama na mtoto.

Moja ya zahanati hizo ni Zahanati ya Itumba katika Jimbo la Igunga ambayo ilipewa mradi wa kujenga na kuboresha theater na wodi. Mradi huo ulimalizika bila kukamilishwa kwa majengo (miundombinu) hayo kwa miaka mitatu sasa. Naomba Serikali ikamilishe mradi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, naiomba Serikali pia ikiboreshe Kituo cha Afya cha Igurubi ambacho uhudumia kata sita za Tarafa ya Igurubi za Kiningu, Igurubi, Kininginila, Mwameshimba, Itunduru na Isakamaliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi la Polisi Wilaya ya Igunga linafanya kazi nzuri katika kulinda raia, lakini Jeshi hilo lina changamoto nyingi sana zikiwemo ukosefu wa miundombinu kwa ajili ya kutenda kazi zao. Wilaya ya Igunga ina Kata 35, lakini ina vituo saba tu vya Polisi vya Igunga, Nanga, Simbo, Igurubi, Simbo, Sungwizi na Choma. Vituo hivi vyote vinatumia magari mawili tu yaliyopo kituo kikuu cha Wilaya Mjini Igunga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Polisi wetu wanafanya katika mazingira magumu sana. Kuna wakati wanalazimika kukodi pikipiki hata baisketi kwenda kukamata wahalifu. Hii ni aibu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Askari wetu wanaishi Mtaani na wengine wanaishi kwenye nyumba mbaya sana (Line Police). Hii haikubaliki. Naomba sana Serikali ijenge nyumba za Askari wetu kwani wanaishi kwa taabu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Polisi, Igunga hakina jengo la utawala kwa ajili ya upelelezi. Tumeanza kujenga kwa kuchangishana na sasa tumefikia kupaua. Tunaomba Wizara ituunge mkono kwenye ujenzi huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Gereza la Wilaya ya Igunga ni dogo sana. Linahudumia wafungwa zaidi ya 200 badala ya wafungwa 100. Pia kuna Gereza kwa ajili ya akinamama. Kwa hiyo, tunalazimika kupeleka mahabusu na wafungwa Gereza la Nzega. Gereza hilo halina jengo la utawala, pia halina ngome. Ngome yake ni miti, aibu kubwa. Nilishawahi kumwomba Mheshimiwa Waziri atutembelee mara kadhaa lakini sijafanikiwa. Tafadhali Mheshimiwa Waziri aje Igunga ajionee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Viongozi wa Gereza la Igunga wakashirikiane na viongozi wa Wilaya wakiwemo Wabunge. Tumeanzisha ujenzi wa jengo la utawala ili kuondokana na aibu hii kwa kutumia fedha za Mfuko wa Jimbo na michango mingine. Tumekamilisha ujenzi wa msingi. Tunaomba Wizara ikamilishe jengo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, Askari Magereza nao hawana nyumba za makazi. Tunaomba wajengewe nyumba kwani wanateseka sana mitaani. Tafadhali tusaidieni Igunga Gereza letu lipo katika hali mbaya.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kupata nafasi hii tena ya kuchangia hoja hii iliyoko mbele yetu ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Namshukuru sana Waziri Mkuu kwa speech yake nzuri yenye maelekezo mazuri. Naipongeza Serikali kwa kazi nzuri mnazofanya, kazi zenye changamoto nyingi sasa hivi, kwa kweli mna changamoto nyingi lakini endeleeni kuzifanya, endeleeni kulisaidia Taifa hili tuweze kufika mbele. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kutoa mchango wangu, naomba nitoe ushauri mdogo, ushauri unaotuhusu baadhi yetu sisi. Tuna bahati nzuri sana katika nchi yetu katika kipindi hiki cha Awamu ya Tano, tumepata Rais mwenye sifa kubwa tatu, hizi sifa tulizihitaji muda mrefu. Sifa ya kwanza ana nia thabiti ya kuleta maendeleo kwa wanyonge. Sifa ya pili, anaamua papo kwa papo, hacheleweshi na sifa ya tatu anataka watu wafanye kazi, ndiyo maana ya msemo wa Hapa Kazi Tu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sifa hizi baadhi yetu tumezitumia vibaya, tumeshindwa kuzitumia kuzi-harness ili nchi yetu isonge mbele. Nasema hivyo kwa sababu baadhi yetu Wabunge wa Upinzani, Chama cha Mapinduzi, baadhi yetu Mawaziri siyo wote na baadhi yetu Wasaidizi wa Rais tumeshindwa kusema kweli. Tumeshindwa kushauri kwa ukweli, tumekuwa wanafiki, hili jambo litatuua sana, badala ya kutengeneza ushauri uliokamilika, unatengeneza ushauri nusu nusu, unampelekea Rais anaamua palepale unafikiri kitatokea nini? Tunahitaji uchambue ushauri wako uupime, uutengeneze uende umekamilika na Rais wetu huyu anayefanya papo kwa papo akiamua nchi inasonga mbele.
(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi haya yote tunayoyaona ni kwa sababu unafiki umezidi miongoni mwetu, nasema kweli. Mimi ni mwathirika wa mambo haya, mtu anaenda kusema anasema Dkt. Kafumu, Kafumu, Kafumu, jambo hili siyo zuri sana. Tumsaidie Rais kusonga mbele tutafika, tukifanya vinginevyo kwa kweli tutarudi nyuma. Ushauri wangu jamani tumsaidie Rais, tumshauri tumshike mkono. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Baba wa Taifa aliamini katika ujamaa lakini waliomzunguka hawakuamini, tumeufikisha ujamaa wapi, Mzee amekufa ameondoka anaamini peke yake na sasa tuna bahati hii, hebu tuitumie.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maneno hayo, naomba nitoe mchango wangu sasa. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kama ilivyo kwa Wabunge wa Tabora nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, suala la tumbaku lilikuwa linatusumbua kweli lakini umelimaliza ahsante sana. Tunakushukuru sana endelea kuja Tabora kwa watani zako utusaidie na mambo mengine.
(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kifungu cha 46 kinazungumzia miundombinu, haya ninayoyasema nayaleta kwa Waziri Mkuu ili anisaidie kumwambia Waziri wa Miundombinu, Wilaya ya Igunga na Jimbo la Igunga, tuweze kupata miundombinu, tuweze
kupata barabara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo langu sina barabara kabisa, unajua ni kwa sababu za kijiolojia. Miaka 60,000 Kabla ya Kristo Igunga asilimia 80 ilikuwa ni ziwa na ziwa hilo lilipokauka limeacha tope, ukifika Igunga ni mbuga ambayo ukitaka kujenga barabara ni lazima uweke tuta zito kubwa la juu. Halmashauri haina uwezo, tunajikuta hatuwezi kujenga barabara. Ukikwangua hiyo barabara ni ya kiangazi tu, wakati wa masika barabara hakuna kabisa na hasa Jimbo la Igunga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Igunga halina barabara ya TANROADS, kuna kipande cha kilomita nadhani kumi kutoka Itunduru kwenda Igurubi. Hakuna barabara ya TANROADS kwenye Jimbo la Igunga, wakati wa masika lile Jimbo halipitiki kabisa. Naleta hili kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, uwatume wataalam wakaangalie na hasa wakati wa masika wakienda, hatuwezi kabisa. Mimi huwa sifanyi kazi wakati wa masika, nasubiri kiangazi ndiyo niweze kuwafikia wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumzia barabara Jimbo la Igunga tunazungumzia, Kata 16 za Wilaya ya Igunga ambazo hakuna barabara ya TANROADS na wakati wa masika hakuna barabara. Nataka nizungumze habari za barabara Wilaya ya Igunga na nimwombe Mheshimiwa Waziri Mkuu, anisaidie kabisa ikiwezekana atume wataalam wakatembee sasa Igunga. Kwa kweli hakuna barabara na wale waliofika Igunga waliofanya kampeni wanajua hakuna barabara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Mheshimiwa tunatumia ‘mapanda ya ng’ombe’, ni njia za ng’ombe hatuna barabara kabisa. Wakati wote nimeomba kuna barabara ya kutoka Shinyanga, kupitia Igurubi mpaka Igunga, na inapita inaenda mpaka Loya kwa ndugu yangu Mbunge wa Igalula. Hiyo barabara tumeomba ipandishwe hadhi mpaka leo angalau tupate barabara moja ambayo itatusaidia kwa ajili ya wananchi wa Igunga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sitaongelea kitu kingine chochote, nataka niongelee barabara tu, namwomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, tukimaliza Bunge hili, atume wataalam wakaangalie barabara Wilaya ya Igunga hususan Jimbo la Igunga. Kwa kweli kuna shida kubwa sana na nitaomba akiwa hapo akimaliza hii nitaenda hapo pembeni labda kesho kutwa niende kumwonesha vizuri Mheshimiwa Waziri Mkuu. Naomba sana sitaki kusema mambo mengine nasema barabara. Barabara Igunga ni mbaya, barabara Igunga hakuna, barabara Jimbo la Igunga hakuna kabisa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mliofanya kampeni Upinzani huku na huku CCM, mliona barabara hamna mapanda du wanasema Wasukuma, kwa hiyo ni kazi kubwa kweli.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nirudie tena, ningeweza kusema mambo mengi, mambo ya maji lakini naomba barabara, hiki ni kilio cha wananchi na najua wanasikiliza, tuna shida kubwa kweli tusaidieni. Mheshimiwa Waziri Mkuu, naona majirani zangu wananiambia nizungumzie Ziwa Victoria lakini sitaki, naomba barabara, barabara, barabara, barabara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba barabara Mheshimiwa Waziri Mkuu tafadhali sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza sana Serikali kwa usimamizi wa Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kwa kazi nzuri inayofanya kusimamia ujenzi wa miundombinu katika Taifa letu. Kazi yao ni nzuri sana. Namwomba Mungu awape nguvu na afya walipeleke Taifa la Tanzania kwenye nchi ya viwanda yenye miundombinu ya barabara za kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Serikali, Jimbo la Igunga ni Jimbo ambalo halina barabara ya kupitika wakati wote (majira ya masika na kiangazi). Wananchi wa Jimbo la Igunga inapofika wakati wa masika (mvua) huwa hawana miundombinu ya barabara kuwawezesha kufika kwenye vijiji na hata kata za jirani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, wakati nachangia hotuba ya bajeti ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwamba eneo la Wilaya ya Igunga miaka 60,000 kabla ya Kristo lilikuwa ziwa na lilikuwa ziwa na lilikauka kwa sababu za kijiolojia na kuacha tope jeusi ambalo wakati wa mvua huwa tope ambalo hufanya barabara kutopitika kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwezo wa Halmashauri kujenga barabara inayohitaji ujenzi wa tuta kubwa kwa urefu mkubwa ni mdogo sana; matokeo yake barabara zinazounganisha vijiji na kata hazipitiki kabisa. Pia barabara zinazounganisha Wilaya za Meatu na Igunga, Kishapu na Igunga, Uyui na Igunga, hazipitiki kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Igunga linayo barabara moja tu ya lami ambayo ni barabara kuu ya Dar es Salaam kwenda Mwanza inayopita katikati ya Jimbo la Igunga. Pia Jimbo la Igunga lina kilometa zipatazo 10 tu za barabara ya changarawe inayotoka Kata ya Itunduru kwenda Kata ya Igurubi inayohudumiwa na TANROADs.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara zote za Jimbo la Igunga zinahudumiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Igunga yenye uwezo mdogo sana kifedha wa kujenga barabara za changarawe kwenye eneo la mbuga. Kimsingi Jimbo la Igunga halina barabara za vijijini na kwenye kata na hasa wakati wa masika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu mwaka 2012 Halmashauri ya Wilaya ya Igunga iliomba kupandishwa hadhi kwa barabara itokayo Igurubi (mpakani mwa Wilaya ya Kishapu) kupitia Igunga na Itumba kuelekea Loya na kufika Tura katika Wilaya ya Uyui.

Mheshimiwa Mwenyekiti, licha tu ya kuwa barabara hii inapitika katika maeneo makubwa ya uchumi wa Mikoa ya Shinyanga na Tabora, sehemu ambazo wananchi wa maeneo hayo wanalima pamba, mpunga na tumbaku, lakini pia wanafuga ng’ombe kwa wingi. Kufunguliwa kwa barabara hii kutakuza uchumi wa Wilaya ya Igunga na Jimbo la Igunga, lakini pia uchumi wa Mikoa ya Tabora, Shinyanga na Singida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara kadhaa nimewahi kuuliza maswali humu Bungeni juu ya lini barabara hii inaweza kupandishwa hadhi ili kufungua Wilaya ya Igunga na kuunganisha Mikoa ya Shinyanga, Singida na Tabora?

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii ikipandishwa hadhi, inaweza kujengwa kwa kiwango cha lami ikitokea Kolandoto kupitia Ukenyenge katika Jimbo la Kishapu na kupitia Igurubi hadi Mbutu - Igunga na Itumba katika Jimbo la Igunga kuelekea Miswaki - Loya hadi Turu katika Jimbo la Igalula. Barabara hii itaunganisha kwa upande wa kaskazini barabara ya lami itokayo Shinyanga kwenda Mwanza na kwa upande wa kusini barabara ya lami itokayo Manyoni kwenda Tabora. Kujengwa kwa barabara hii kwa kiwango cha lami kutaunganisha barabara hizi kuu za lami nchini kwetu na kufungua fursa za kiuchumi za Mikoa ya Tabora, Shinyanga na Singida. Fursa hizo ni pamoja na kilimo cha pamba, tumbaku, alizeti na mpunga, mazao yanayozalishwa kwa wingi katika mikoa hii. Pia biashara ya mifugo katika minada nayo itaimarika sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba sana Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ifike wakati atume wataalam wakaitathmini barabara hii muhimu kwa mikoa hii na ikiwezekana katika bajeti ya mwaka huu wa fedha 2017/2018 tupate hata fedha kidogo za kufanya upembuzi yakinifu ili bajeti ijayo iweze kupandishwa hadhi na baadaye kujengwa kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, barabara ya Kininginila – Mwabakima – Mwanyagula – Mbutu hadi Igunga nayo inao umuhimu wa pekee sana kwa sababu inaunganisha Wilaya ya Meatu katika Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora. Pia barabara hii inapitia katika maeneo ya kilimo cha pamba na ufugaji wa ng’ombe. Tunaomba barabara hii nayo kupandishwa hadhi kuwa ya TANROADs ili iweze kujengwa kwa kiwango cha changarawe na kupitika wakati wote ili kuwaondolea adha ya ukosefu wa miundombinu ya barabara hasa wakati wa masika wananchi wa Kata za Kininginila, Isakamaliwa, Mwamashimba, Mbutu na Igunga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukosefu wa barabara za kiwango cha changarawe chini ya usimamizi wa TANROADs katika Jimbo la Igunga ni changamoto kubwa inayosumbua na kukera sana wananchi wa Jimbo la Igunga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kwa heshima kubwa, naiomba sana Serikali ilisaidie Jimbo la Igunga kupata barabara za kutosha za kiwango cha changarawe na kiwango cha lami ili kuwaondolea adha ya usafiri wananchi wa Jimbo la Igunga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niongee. Niliomba dakika 10 za kikanuni kwa sababu sijawahi kuchangia kwa mwaka mzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi hii tena kwa mwaka huu ili niweze kuchangia habari za wananchi wa Igunga.

Mheshimiwa Mwenyekiti,, nataka niseme na jambo hili nimeendelea kulisema kila wakati, kijiolojia Jimbo la Igunga ni ziwa lililokauka miaka 60 elfu iliyopita. Narudia hili ili Mheshimiwa Waziri anielewe, kwamba kujenga barabara kwenye eneo hilo la Mbuga ni lazima ujenge tuta kubwa. Halmashauri imeshindwa kujenga barabara hizi kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati mbaya zaidi Jimbo la Igunga halina barabara hata moja ya TANROADS. Tuna kata 13 ziko kwenye jimbo hili, sasa hivi ukienda hakuna hata kata moja ambayo unaweza kufika kwa sababu hapafikiki kabisa. Nimeomba mwaka jana na naomba tena kwa Mheshimiwa Waziri, Igunga hatuna barabara, tunaomba waje watutengenezee barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2014, 2015 na 2016 tuliomba barabara ya kutoka Igurubi kuja Igunga ipandishwe hadhi. Barabara hii inaunganisha wilaya yetu na mkoa wetu na Mkoa wa Shinyanga. Hata hivyo, kwa bahati mbaya sana wakatuambia kwamba wameirudisha TARURA, kwa kweli inatusikitisha sana, jimbo lisilo na barabara yoyote ya TANROADS inayohudumiwa na mkoa halafu wakairudisha TARURA tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii ni muhimu kuliko barabara zote kwenye Jimbo la Igunga kwa sababu sisi Jimbo la Igunga tunalima asilimia 90 ya pamba inayolimwa Mkoa wa Tabora. Sasa hivi ndiyo tunaozalisha mbegu kwa ajili ya wakulima wa pamba Tanzania. Hiyo mbegu au pamba inayozalisha hiyo mbegu inatoka kwenye barabara hii. Ziko kata kama 13 kwenye barabara hii ambazo zimelima pamba mwaka huu vizuri na tunategemea barabara hii ndiyo ibebe pamba hizo kutoka kwenye maeneo hayo, halafu wanatuambia kwamba imerudi TARURA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli samahani sana nashindwa kuongea, naongea kwa uchungu na wananchi wa Igunga wananisikia. Barabara ya kutoka Igurubi kwenda Igunga tuliomba ipandishwe na tunaomba bado ipandishwe TARURA hawaiwezi. Sasa hivi ukitoka Igunga kwenda Igurubi hamna mtu anayeweza kwenda tena. Naomba sana Mheshimiwa Waziri anisikilize safari hii. Kwenye kitabu hiki cha bajeti mimi sina barabara yoyote humo ndani, nasema hapa kwa sababu ni kama vile wananchi wa jimbo lile wamesahauliwa wameachwa. Kuna Wabunge wamesema hapa hivi Jimbo la Igunga tuna matatizo gani au tumekosa nini hasa? Naomba sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara nyingine ambayo tuliomba ipandishwa hadhi ni barabara ya kutoka Igunga kwenda Itumba mpaka Loya. Hii barabara inafungua tena Mkoa wa Tabora inaunganisha na ile barabara wanayoifungua inatoka Tura kwenda Iyumbu na ukiziunganisha hizo barabara unakwenda mpaka Mbeya.

Mheshimiwa Spika, tuliomba ipandishwe hadhi, makaratasi yote tulipeleka na ikakubalika, lakini leo tumeambiwa tena bado iko TARURA na TARURA hawana uwezo. Sasa hivi hiyo barabara ya kutoka Igunga kwenda Itumba kupitia Mwanzugi daraja limebomolewa kabisa na kuna Mkandarasi alikuwa anajaribu kujenga pale, lakini hana fedha ya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi niliuliza swali watafanya fanyaje basi kutusaidia barabara hiyo haipitiki kabisa saa hizi na huko ndiyo nyumbani kwetu, mimi nikifika kule inabidi nitembee kwa mguu kwenda nyumbani kwetu. Naomba tena hii barabara kama wanaweza kuipandisha hadhi ili wafungue Mkoa wa Tabora, wafungue jimbo hili liunganike na Singida na Mbeya, litakuwa jambo zuri kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli naomba tena, Mheshimiwa Waziri kama anaweza kuja kututembelea Igunga aje; pamoja na kwamba kuna barabara moja tu kuu ya kwenda Mwanza kutoka Singida basi aje tumpitishe hata kidogo wakati wa masika aone mambo yalivyo, nadhani anaweza akaelewa hiki ninachokisema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Jimbo la Igunga kwa sasa hivi hawawasiliani kabisa, hakuna mtu anayeweza kutoka Igurubi akaja Igunga, hakuna mtu anayeweza kutoka Itumba akaja mjini Igunga, hakuna mtu anayetoka hata Isugiro pale karibu karibu pale akaja mjini, hali ni mbaya kweli kweli na wananchi wanasema sasa Mheshimiwa Mbunge tunafanyaje? Nikawaambia nitalisemea hili jambo na saa hizi wanaweza kuwa wananisikia. Hamna Bunge live lakini nadhani nitapeleka kibwagizo kidogo wasikilize sikilize haya ninayoyasema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakinisaidia hizo barabara mbili wakafungua tukatoka tunaweza kutoka Kolandoto tukapita Ukenyenge, tukaja Igurubi, tukaja Mwamakona, Mbutu, Igunga tukaenda Itumba tukaenda Loya, Tura tukaenda mpaka Mbeya, watakuwa wamenisaidia sana. Kwanza wamefungua maeneo ya kiuchumi, pamba yote ipo maeneo hayo kama nilivyosema. Upande wa huku chini kuna mifugo, concentration ya mifugo mingi iko kusini mwa Igunga mpaka Loya kwa ndugu yangu wa Igalula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, wakifungua hii barabara tutakuwa na ng’ombe wengi ambao watafikia minada. Sasa hivi tunapeleka ng’ombe kwenye minada ya Singida. Tunaomba sana Waheshimiwa Mawaziri hebu wanisikilize na mimi, naongea taratibu kwa uchungu ili wanisikilize jamani, tafadhali sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nataka kusema kuna madaraja ambayo yanaunganisha kata kwa kata ambayo ni makubwa kiasi ambacho hayawezi kujengwa na halmashauri wala na TARURA. Naomba madaraja hayo nitakayoyataja wayafanye kama walivyofanya daraja la Mbutu. Daraja la Mbutu lilikuwa ni daraja lililokuwa chini ya halmashauri lakini kwa umuhimu wake lilijengwa na mradi maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, madaraja hayo pamoja na daraja la kutoka Igunga kwenda Mwanzugi, mahali ambapo saa hizi pamebomolewa panahitaji madaraja zaidi ya matano, mkandarasi aliyepo hawezi kuyajenga. Tuna daraja la kutoka Bukoko kwenda Mtungulu Mto Ncheli, mto mkubwa sana, watu wa Ncheli kule pamoja na Mtungulu hawawezi kuwasiliana na wilaya, kwa sasa hivi wanakaa huko mpaka mvua ziishe. Ni daraja kubwa kweli kweli linahitaji bilioni kadhaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna daraja la kutoka Itunduru kwenda Kagongwa, wananchi wale wakati wa mvua lazima watembee kwa mguu, wanajaribu kwenda Shinyanga kwa upande wa pili. Kuja huku hawawezi, ni daraja kubwa kweli, halmashauri haiwezi pamoja na TARURA haiwezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, daraja la mwisho, ni kutoka Igunga kwenda Isugiro, ni hapo hapo karibu. Mto Igogo ambao unajaza maji kwenye bwawa la Igogo unapotoa maji unakatisha barabara, haiwezekani kabisa kujenga daraja hilo na halipo hilo daraja. Naomba Mheshimiwa Waziri wanisaidie ili na mimi angalau niwe kama wengine kama kata zingine, kama wilaya zingine, kama majimbo mengine niwe na barabara hata za TANROADS mbili, tatu hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunisikiliza na Mungu awabariki.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi nichangie hoja iliyoko mbele yetu ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze mdogo wangu kwa kazi nzuri anayofanya japokuwa ni kazi ngumu sana, kuna wakati anakimbia badala ya kutembea anawahi kusikoeleweka. Kuna siku nikamwambia mdogo wangu hebu rudi nyuma kidogo, namshukuru alinisikiliza na namuomba aendelee na kazi vizuri sisi tuko nyuma yake tutamsaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nizungumzie mambo mawili tu. Jambo la kwanza ni mbuga ya Wembere ambayo ni hifadhi iliyokuwa imeanzishwa na wakoloni mwaka 1940 kwa ajili ya kutunza wanyama lakini pia ilikuwa ni kwa ajili ya mapito ya wanyama kwa sababu inaunganika na Serengeti. Baada ya uhuru, Serikali iliisahau kidogo hii mbuga, mbuga hii inaanzia Mkoa wa Shinyanga, inapita Mkoa wa Tabora lakini pia iko Mkoa wa Singida, ni bonde la ufa linaloelekea Lake Eyasi. Ilivyotelekezwa wanyama wengi walimalizika kwa sababu waliwindwa bila utaratibu, lakini pia mabadiliko ya tabianchi bonde hili lilikauka mwaka 1974 na wanyama wakaisha kabisa. Lilikuwa pia ni mazalia ya ndege wanaotoka Ulaya, walikuwa wanakuja kuzaa wakati wa kiangazi huku na sasa hivi kwa sababu mazingira yameharibika, hawaji tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mbuga hii imekosa sifa ya kuitwa hifadhi kama ilivyokuwa zamani. Kwa sababu hiyo, wananchi wengi walihamia, hiyo miaka ya 70 mpaka 80 na Serikali ikapima vijiji na kata kwenye mbuga hii. Kwenye mbuga hii kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, kuna kata zaidi ya saba lakini kule Singida na kwenyewe ziko kata nyingi kweli kweli sikumbuki ni ngapi. Ukienda Shinyanga kuna kata kama tatu hivi, kule Meatu, wananchi wako mle ndani. Kutokana na kukosa sifa na watu kukaa mle ndani, shughuli za kilimo zimeongezeka sana. Ndiyo tunapozalisha mpunga, mkipita Igunga mnakuta mpunga mzuri unaonukia au mchele unaonukia, unatoka kwenye mbuga ya Wembere. Pia ufugaji umeendelea kupanuka kwa sababu watu ni wengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu hiyo sasa, ugomvi kati ya wafugaji na wakulima umekuwa mkubwa sana na miaka kadhaa watu wamegombana kama kule Isakamaliwa mpaka wengine wakauawa. Pia, pale Makomelo ukiwa unakaribia Igunga, kulikuwa na ugomvi mwaka jana, watu walijeruhiwa sana. Ukienda Itumba nakotoka mimi kama unaelekea Loya kule kwa ndugu yangu Mheshimiwa Musa Ntimizi na kwenyewe watu walipigana sana kwa sababu watu ni wengi, maeneo ya kuchunga na kulima ni machache. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mwaka 2014, tuliandika barua Wizara ya Maliasili na Utalii ili wabadilishe matumizi ya mbuga hii, waiangalie, wabakize eneo dogo lakini lingine wawaachie wananchi. Mwaka 2012 Serikali iliunda kamati ya wataalam wakapitia mbuga na hifadhi nyingi kuangalia ipi imekosa sifa. Moja ya mbuga ambayo imekosa sifa ilikuwa ni mbuga ya Wembere. Namuomba Mheshimiwa Waziri, nimemwandikia barua tena, naomba akaitazame mbuga hii, karibu Igunga Waziri, tukaitembelee, aje na wataalam wake tuone ni jinsi gani tunaweza tukabadilisha mipaka ili wananchi wetu waweze kupata mahali pa kulima pamoja na kuchunga ng’ombe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo nilitaka kuzungumzia ni ukurasa wa 90 wa kitabu cha Mheshimiwa Waziri, kuhusu Idara ya Mambo ya Kale na anazungumzia majengo ya kihistoria kama ya Dar es Salaam na maeneo ya kihistoria kama Engaruka na kadhalika. Sisi tulikuwa na utawala wa Kitemi na wewe Mwenyekiti ni Mtemi na hata mimi natoka kwenye utawala wa Kitemi wa Usongo. Tuna maeneo ambayo Watemi sasa hivi wameyaacha, ukienda kule Meatu, Igunga, kwa mfano, Igunga kuna Mtemi Shomari Ng’wanaasali nyumba yake bado ipo pale Igurubi. Kuna Mtemi mwingine anaitwa Kasanda wa Unambiu na yeye nyumba yake bado ipo. Kuna Mtemi Ntinginya na akina Humbiziota nyumba zao bado zipo. Ukienda Urambo au tuseme Tabora yuko Mtemi Mirambo na yeye nyumba yake bado ipo na Watemi wengi sana masalia yao bado yapo. Isike pale kuna masalia na sehemu nyingine nyingi lakini Wizara haichukui tahadhari yoyote, haiweki programu yoyote kuyahifadhi maeneo haya. Namwomba Mheshimiwa Waziri, hebu wanzishe mkakati maalum wa kuyatambua maeneo ya Watemi wetu hawa, wayapandishe hadhi, wayahifadhi, Wazungu ambao ni watawala wetu kwa hakika wakisikia kwamba maeneo haya yako tayari na hasa Wajerumani, watakuja kuyatembelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini maeneo hayo pia yaendane na ngoma zetu za jadi. Mheshimiwa Waziri, mkishirikiana na Wizara ya Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe, mnaweza mkaanzisha taratibu hizi kwenye utemi huo, watu wanacheza ngoma, embinabhabha, tunazihitaji ngoma zirudi ili wananchi wetu waendelee kucheza. Namuomba sana Mheshimiwa Waziri anisikilize, nilishawahi kusema last time juu ya jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ambalo napenda kusema ni ng’ombe ambazo zinakamatwa kwenye hifadhi. Kwa kweli tunatambua umuhimu wa kutunza maeneo. Tunatambua na tunataka hifadhi itunzwe lakini namna ambavyo hatua zinachukuliwa kuwafanya hawa watu wasipeleke ng’ombe haziendi vizuri na actually zinafanywa na wale wadogo Mheshimiwa Waziri anaweza asijue. Wale vijana waliomaliza kidato cha nne na kupata hizo kazi wanavaa nguo za kijana, nadhani hata leo wapo wanafanya kazi vibaya. Wengi ni matajiri hao vijana, wamejenga majumba kwa sababu ya hizo ng’ombe na wana magari kwa sababu ya hizo ng’ombe. Kwa hiyo, kuna tatizo katika utekelezaji wa jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri waangalie namna ya kutekeleza jambo hili kama wanataka kulifanya vizuri. Wakilifanya hivi wanavyolifanya kwa kweli wananchi wanajisikia vibaya, wanajisikia wameachwa katika nchi yao. Wako wananchi wengi sana ambao wamechukuliwa ng’ombe wao. Kuna mtu namfahamu yuko hapa, nilikuwa naongea naye, ng’ombe wake 4,000 walichukuliwa na wakauzwa, mzee wa watu ana hali mbaya sana. kuna mwingine ana kesi mpaka mahakamani lakini wakati kesi inaendelea, zikauzwa, wala hawajali kwamba kuna kesi. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri, itazameni upya tena hii program ya kukamata hawa ng’ombe kwenye hifadhi ili muweze kufanya hii kazi vizuri, hatukatai, ni lazima tuhifadhi maeneo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapori mengi sana ambayo yamepitwa na wakati kama mbuga ya Wembere nilivyosema yagawiwe kwa watu waweze kuchunga. Sehemu nyingi sana maeneo yamepitwa na wakati. Kule Nzega kuna sehemu moja inaitwa Ipala na kwenyewe watu wanafukuzwa kwenye hifadhi, kuna mjomba wangu kule mzee Charles alichomewa nyumba zake zote. Nakuomba Mheshimiwa Waziri, tambueni maeneo haya ambayo yamepitwa na wakati muwape wananchi waweze kuchunga na hiyo changamoto ya kuingiza ng’ombe kwenye hifadhi inaweza ikapungua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naona nimefika mwisho, nashukuru sana. Narudia tena, mbuga ya Wembere Mheshimiwa Waziri, tafadhali tupeni mbuga tuweze kuitumia kadiri ya mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya makazi, hifadhi, kilimo na mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naomba kuunga mkono hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. DKT. PETER D. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Pia nimshukuru Mungu kwa kuniwezesha kusimama kuchangia kidogo hoja hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema mambo matatu, lakini kabla sijasema naomba nimshauri kaka yangu Isdori kwamba msalaba aliopewa amepewa na Yesu mwenyewe, kwa hiyo amtegemee Yesu; yeye alisema njooni kwangu ninyi nyote mnaosumbuka na mizigo nami nitawapumzisha, lakini Yesu mwenyewe alipata msalaba mkubwa na alipokwenda Gethsemane alimwomba Mungu akasema nipishie huu msalaba lakini kwa mapenzi yako; na wewe umepewa msalaba huo na Yesu kwa kupitia kwa Mheshimiwa Rais, hebu asinung’unike, afanye kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba nichangie kwa kusema, bajeti ya Mheshimiwa Waziri imeonesha matumaini kidogo safari hii. Kwa sababu ameanza kusikiliza ushauri wa Bunge. Tangu Awamu ya Tano imeanza Bunge limekuwa likishauri mambo mengi; nitatoa mifano miwili tu kuonesha jambo jinsi ambavyo bajeti hii imefanya vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri ambao Bunge limekuwa likisema ni kuwasaidia wawekezaji waweze kujisikia wako nyumbani, kuweka mazingira bora ya uwekezaji; na nashukuru ukisoma kwenye kitabu chake utaona wameunda mpaka blue print maana yake wamewasilikiliza na wanazungumza nao kila baada ya miezi kadhaa. Kwa kweli tunaomba hii blue print basi mtuletee tuisoma na muitekeleze ili mazingira ya uwekezaji katika nchi yetu yaweze kuboreka na kweli uwekezaji uje katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ni mfano ni kuhusu kodi. Mara nyingi tumekuwa tukisema kwamba kodi na tozo zitazamwe na hasa kenye kilimo. Nimeona kuna baadhi ya kurasa hapa, kwa mfano ukurasa wa 46 amepunguza corporate tax kutoka 30 mpaka 20 kwenye mazao ya ngozi, jambo hili litachochea sana ukuaji wa sekta ya ngozi. Naomba basi Mheshimiwa Waziri pamoja na hilo basi apeleke na kwenye mazao mengine ya kilimo, uvuvi na ufugaji ili tuchochee shughuli za uanzishwaji wa viwanda katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo lilitekelezwa mwaka jana ilikuwa ni VAT ilyokuwa imewekwa kwenye huduma za mizigo inayopita. Nakumbuka mimi nilipokuwa Mwenyekiti wa Kamati tulilisema na Serikali ikalisikia. Kwa kweli bajeti hii ya leo inaleta matumaini makubwa sana. Ipo mifano mingi sana ambayo ningeweza kusema lakini itoshe tu kuonesha kwamba bajeti inaleta mwelekeo wa kukuza viwanda katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nitoe ushauri, kwamba pamoja na mwelekeo huo bado kuna mambo makubwa ambayo Wabunge wengi wameyasenma na mimi nataka niseme mawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, ili tuweze kujenga uchumi wa viwanda ni lazima bajeti ya kilimo, Waheshimiwa Wabunge wamesema, iongezwe. Kwenye ukurasa wa 80 amesema ni kipaumbele cha Serikali lakini bajeti ni ndogo asilimia sijui ngapi. Tafadhali Mheshimiwa Waziri hebu ajaribu kuongeza hiyo bajeti, bajeti ijayo kilimo tusikie kwamba kweli tumepewa bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kujenga uchumi wa viwanda pia linahusiana na ile miradi ya kielelezo waliyoiweka; mmoja ukiwa ni mradi wa Makaa ya Mawe na mradi wa Chuma Liganga. Chuma tukiweza kukipata ni dhahiri kabisa tutaweza kuendeleza miradi mingi, hata mradi wa Stiegler’s Gorge, mradi wa kujenga Reli, tutatumia chuma chetu, tutapunguza gharama kweli. Sasa tunauacha tu huu mradi unaendelea, kila siku, kila mwaka tunausema; na kwenye bajeti yako hapa hauoneshi. Kwenye bajeti ya Mheshimiwa Mwijage haukupewa kipaumbele cha kutosha. Najua matatizo yake ni vivutio vya kodi, hebu wamalize hilo jambo; kuna matatizo ya fidia ya wananchi wamalize hilo, lakini pia PPA kwa ajili ya kuzalisha umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo ningependa kusema kwa kifupi ni kuhusu ETS. ETS ni mfumo mzuri, kwa maana ya kuhesabu uzalishaji na hakuna mtu anae pinga humu kwamba huu mfumo ni mzuri kwa sababu tutaweza kupata kodi halisia. Hata hivyo, changamoto zilizopo zilizoelezwa na wadau ni lazima Serikali wazisikilize, wanapotekeleza wasikilize gharama ya uwekezaji kwenye mradi huo. Pia waangalie namna ambavyo wataweza kufanya kiasi kwamba wawekezaji hawa waweze kuwa na gharama ndogo ili wananchi wasiweze kupata kodi kubwa kwenye vinywaji vyao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili kutoka mwisho ni Akaunti Jumuifu (TSA), ni jambo zuri kwa maana ya kuweza ku-control liquidity ya fedha katika nchi. Hata hivyo, kuna changamoto kubwa, kwa sababu ukitekeleza utalazimika ukaangalie na sheria nyingine, unaweza ukaangalia hata Katiba ya nchi yetu tunatawalaje, kwa sababu hii inaonesha kwamba inaweza kwenda kuua Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipokuwa kwenye Kamati ya Bajeti kule niliwaambia nchi ya Marekani ina states 50 na kila state ina Bunge na ina bajeti na wimbo wake wa Taifa. Sasa zile fedha kweli zinapelekwa kwenye Mfuko Mkuu ili zirudishwe kwenye states? Nikasema inawezekana kabisa reporting information ya matumizi lakini si hela ziende na kurudi. Kwa hiyo tunapotekeleza ni lazima tufikirie kurekebisha na sheria nyingine. Kwa hiyo ni jambo kubwa ambalo linahitaji Serikali watazame vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ni hili ambalo wenzangu wamesema; mimi nimetoka kwenye sekta ya madini; jambo la dhahabu. Dhahabu ni fedha na ukiangalia sheria ya BOT inasema inatunza fedha za kigeni lakini inatunza dhahabu safi. Niliwahi kusema nchi zote tajiri zina tani nyingi kweli za dhahabu kwenye central Banks zake, kwa mfano Marekani inatani zaidi ya elfu nane imetunza kwenye Central Bank. Uchina elfu moja mia saba, Ujerumani elfu tatu mia tano, Italy elfu mbili mia tano, Ufaransa elfu mbili mia nne; zote hizi zinaipa nchi ile nguvu ya kuwa tajiri. Sisi tuna dhahabu kwa nini tusitunze dhahabu?...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi nichangie kidogo. Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Bajeti kwa hiyo mambo mengi nimeyachangia huko sasa nataka kusema mambo machache tu madogo.

Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kazi anayofanya na aendelee, niseme tu kwamba nchi inayojenga uchumi na hasa uchumi wa viwanda kuna mambo kama sita ya msingi ambayo yanatakiwa iyafanye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ni kujenga miundombinu ambayo ita-support uchumi huu ambalo Serikali inalifanya vizuri, lakini mazingira ya biashara ya kufanyia kazi na kuwekeza ni jambo muhimu pia. Jambo la tatu ni upatikanaji wa mitaji mikubwa ku-support miradi hiyo na mitaji hii inatoka nje na mingine iko ndani, jambo la nne ni ujenzi wa viwanda mama kama vya chuma, industrial evolutional ya Ulaya ilitokea kwa sababu walijenga viwanda vya namna hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tano ni kuongeza matumizi ya malighafi za ndani tumesikia hapa wananchi wa Bunge wanasema kwa nguvu sana mazao ya kilimo yatumike hapa ndani, kuna mazao ya madini tuyatumie hapa ndani, tu-add value kwenye bidhaa tulizonazo hapa ndani. Na jambo jingine kubwa la mwisho ni matumizi ya teknolojia na wataalam, mafundi mchundo ndio wanaoweza ku-support jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie kidogo sasa kwenye mambo hayo kadri muda utakavyokuwa kutoa ushauri kidogo. Kwenye suala la miundombinu naona mpango unapendekeza vizuri na unafanya vizuri tunaona barabara zinajengwa, reli inajengwa, miundombinu ya bandari inajengwa mambo haya ni muhimu umeme. Lakini kuna changamoto kidogo ambazo zinajitokeza na Wabunge wanasema, kwa mfano kwenye ujenzi wa reli tunafanya vizuri sana, lakini changamoto tuliyonayo ambayo nafikiri Serikali inatakiwa iangalie ni namna jinsi ambavyo tunaweza kupata fedha za kutosha kujenga hii reli kwa haraka, tunapojenga vipande kwa kweli tunaweza tukachelewa, tunaweza tukafika mwisho 2025 hatujafika kule ambako kuna mizigo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naishauri Serikali na Wabunge wengine wamesema tutengeneze huu mradi mmoja mkubwa kama tunaweza na tukope kwa concession kama inawezekana ni vizuri Serikali mkaendelea kuliangalia jambo hili kwa sababu tukiendelea kutafuta hela kidogo namna hii tunaweza kuchelewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni lazima tuendelee kupanua miundombinu ya ndani barabara najua tunafaya vizuri lakini tuongeze juhudi. Kwa mfano kuna barabara moja kule mikoa ya kanda ya ziwa kule inayounganisha mikoa zaidi ya mitano ambayo inapita kwenye sehemu za kilimo cha pamba, barabara hii inapita kwenye kilimo cha mpunga, kwenye mifugo kwenye mazao ya misitu na inaunganisha vipande vingi sana vya shughuli za kilimo. Barabara hii inatoka Korandoto kwenye barabara inayotoka Shinyanga kwenda Mwanza na inapita Ukenyenge kwenye Jimbo hili la Kishapu kwa Mbunge sharp inaingia Jimbo la Igunga inaenda Jimbo la Igalula ikitoka hapo inaenda mpaka Tura inaunganisha barabara kutoka Dodoma kwenda Tabora.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii inapita kwenye maeneo makubwa sana ya uchumi, naomba sana mpango huu kama inawezekana Mheshimiwa Mpango muiweke kwenye mpango, itasaidia sana kilimo cha pamba hata ule mkakati wa C to C (cotton to clothing) tunaweza kuutekeleza vizuri zaidi naomba sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili mazingira bora ya kufanyia biashara ni jambo ambalo limesemwa vizuri sana kwenye mpango, lakini bado kuna changamoto, wafanyabiashara na wajenzi wa viwanda wanahangaika wanapiga kelele kwa kweli, mahusiano kati yao na watendaji ni shida, wote mmesikia TRA mpaka Mheshimiwa Rais mwenyewe akasema TRA msiwe polisi sana, naomba jambo hili tuliendeleze tuhakikishe ushirikiano huu usiwe wa kipolisi na raia uwe wa partner, partnership ni muhimu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naona muda unakwenda jambo la pili ni mitaji kutoka nje na ndani, mitaji mikubwa ni lazima hii tuihamasishe, mazingira ya kufanya biashara wawekezaji kutoka nje tuwahamasishe waje, najua Serikali mmetengeneza blue print basi muitekeleze, mazungumzo na wenzetu hawa wanaowekeza kutoka nje myaendeleze na muwe marafiki zaidi, tusiwaone wawekezaji kutoka nje mara nyingi nimesema kama wanyang’anyi na wezi hapana, hawa ni wadau wetu, watatuletea fedha, tutafanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni ujenzi wa viwanda mama kama nilivyosema Mchuchuma na Liganga ni project ambayo ni mama kweli tukipata chuma leo kwa kweli tutatoka haraka kabisa, bahati mbaya mradi huu umesuasua miaka mingi, kila mwaka maneno ni yale yale. Kamati tumesema jamani huu mradi sasa ufike mwisho, tukipata chuma tukapeleka kwenye viwanda vyote vya nondo na vya misumali tukatumia chuma kujenga reli yetu, majengo haya makubwa tukatumia chuma ya ndani tumetoka kiuchumi vinginevyo tuna kazi kubwa sana tutachelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ni kuhusu teknolojia, matumizi ya teknolojia na watalaam, kwenye mpango Mheshimiwa Mpango umesema vizuri sana, kada maalum za taaluma mnaziendeleza lakini juhudi hazionekani ni lazima VETA hizi tuzipe fedha ya kutosha, tuwapate hawa wataalam na mafundi mchundo wa kwenda kwenye viwanda vyetu, bila kufanya hivyo nchi ya India kwa mfano waliwekeza sana kwenye hiyo shughuli au shule za kuwafundisha mambo haya ya ufundi na wameweza sana kuendeleza viwanda vyao na sisi tunatakiwa tufanye jambo hili kwa nguvu nyingi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie kwa kusema...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

Mungu atusaidie, ahsante.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi nichangie kidogo. Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Bajeti kwa hiyo mambo mengi nimeyachangia huko sasa nataka kusema mambo machache tu madogo.

Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kazi anayofanya na aendelee, niseme tu kwamba nchi inayojenga uchumi na hasa uchumi wa viwanda kuna mambo kama sita ya msingi ambayo yanatakiwa iyafanye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ni kujenga miundombinu ambayo ita-support uchumi huu ambalo Serikali inalifanya vizuri, lakini mazingira ya biashara ya kufanyia kazi na kuwekeza ni jambo muhimu pia. Jambo la tatu ni upatikanaji wa mitaji mikubwa ku-support miradi hiyo na mitaji hii inatoka nje na mingine iko ndani, jambo la nne ni ujenzi wa viwanda mama kama vya chuma, industrial evolutional ya Ulaya ilitokea kwa sababu walijenga viwanda vya namna hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tano ni kuongeza matumizi ya malighafi za ndani tumesikia hapa wananchi wa Bunge wanasema kwa nguvu sana mazao ya kilimo yatumike hapa ndani, kuna mazao ya madini tuyatumie hapa ndani, tu-add value kwenye bidhaa tulizonazo hapa ndani. Na jambo jingine kubwa la mwisho ni matumizi ya teknolojia na wataalam, mafundi mchundo ndio wanaoweza ku-support jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie kidogo sasa kwenye mambo hayo kadri muda utakavyokuwa kutoa ushauri kidogo. Kwenye suala la miundombinu naona mpango unapendekeza vizuri na unafanya vizuri tunaona barabara zinajengwa, reli inajengwa, miundombinu ya bandari inajengwa mambo haya ni muhimu umeme. Lakini kuna changamoto kidogo ambazo zinajitokeza na Wabunge wanasema, kwa mfano kwenye ujenzi wa reli tunafanya vizuri sana, lakini changamoto tuliyonayo ambayo nafikiri Serikali inatakiwa iangalie ni namna jinsi ambavyo tunaweza kupata fedha za kutosha kujenga hii reli kwa haraka, tunapojenga vipande kwa kweli tunaweza tukachelewa, tunaweza tukafika mwisho 2025 hatujafika kule ambako kuna mizigo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naishauri Serikali na Wabunge wengine wamesema tutengeneze huu mradi mmoja mkubwa kama tunaweza na tukope kwa concession kama inawezekana ni vizuri Serikali mkaendelea kuliangalia jambo hili kwa sababu tukiendelea kutafuta hela kidogo namna hii tunaweza kuchelewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni lazima tuendelee kupanua miundombinu ya ndani barabara najua tunafaya vizuri lakini tuongeze juhudi. Kwa mfano kuna barabara moja kule mikoa ya kanda ya ziwa kule inayounganisha mikoa zaidi ya mitano ambayo inapita kwenye sehemu za kilimo cha pamba, barabara hii inapita kwenye kilimo cha mpunga, kwenye mifugo kwenye mazao ya misitu na inaunganisha vipande vingi sana vya shughuli za kilimo. Barabara hii inatoka Korandoto kwenye barabara inayotoka Shinyanga kwenda Mwanza na inapita Ukenyenge kwenye Jimbo hili la Kishapu kwa Mbunge sharp inaingia Jimbo la Igunga inaenda Jimbo la Igalula ikitoka hapo inaenda mpaka Tura inaunganisha barabara kutoka Dodoma kwenda Tabora.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii inapita kwenye maeneo makubwa sana ya uchumi, naomba sana mpango huu kama inawezekana Mheshimiwa Mpango muiweke kwenye mpango, itasaidia sana kilimo cha pamba hata ule mkakati wa C to C (cotton to clothing) tunaweza kuutekeleza vizuri zaidi naomba sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili mazingira bora ya kufanyia biashara ni jambo ambalo limesemwa vizuri sana kwenye mpango, lakini bado kuna changamoto, wafanyabiashara na wajenzi wa viwanda wanahangaika wanapiga kelele kwa kweli, mahusiano kati yao na watendaji ni shida, wote mmesikia TRA mpaka Mheshimiwa Rais mwenyewe akasema TRA msiwe polisi sana, naomba jambo hili tuliendeleze tuhakikishe ushirikiano huu usiwe wa kipolisi na raia uwe wa partner, partnership ni muhimu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naona muda unakwenda jambo la pili ni mitaji kutoka nje na ndani, mitaji mikubwa ni lazima hii tuihamasishe, mazingira ya kufanya biashara wawekezaji kutoka nje tuwahamasishe waje, najua Serikali mmetengeneza blue print basi muitekeleze, mazungumzo na wenzetu hawa wanaowekeza kutoka nje myaendeleze na muwe marafiki zaidi, tusiwaone wawekezaji kutoka nje mara nyingi nimesema kama wanyang’anyi na wezi hapana, hawa ni wadau wetu, watatuletea fedha, tutafanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni ujenzi wa viwanda mama kama nilivyosema Mchuchuma na Liganga ni project ambayo ni mama kweli tukipata chuma leo kwa kweli tutatoka haraka kabisa, bahati mbaya mradi huu umesuasua miaka mingi, kila mwaka maneno ni yale yale. Kamati tumesema jamani huu mradi sasa ufike mwisho, tukipata chuma tukapeleka kwenye viwanda vyote vya nondo na vya misumali tukatumia chuma kujenga reli yetu, majengo haya makubwa tukatumia chuma ya ndani tumetoka kiuchumi vinginevyo tuna kazi kubwa sana tutachelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ni kuhusu teknolojia, matumizi ya teknolojia na watalaam, kwenye mpango Mheshimiwa Mpango umesema vizuri sana, kada maalum za taaluma mnaziendeleza lakini juhudi hazionekani ni lazima VETA hizi tuzipe fedha ya kutosha, tuwapate hawa wataalam na mafundi mchundo wa kwenda kwenye viwanda vyetu, bila kufanya hivyo nchi ya India kwa mfano waliwekeza sana kwenye hiyo shughuli au shule za kuwafundisha mambo haya ya ufundi na wameweza sana kuendeleza viwanda vyao na sisi tunatakiwa tufanye jambo hili kwa nguvu nyingi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie kwa kusema...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

Mungu atusaidie, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi ya kuchangia. Niliuliza swali kuhusu kutokuwepo kwa gereza lenye sifa ya kuwa gereza katika Wilaya ya Igunga. Gereza la Igunga halina ngome, hakuna gereza la wanawake na hulazimika kupeleka wafungwa wa kike kwenye Gereza la Wilaya ya Nzega. Gereza hilo pia halina nyumba za askari na halina ofisi za utawala. Kutokana na hali hiyo tunaiomba Serikali itafute fedha za kufanya mambo yafuatayo:-

(a) Ujenzi wa ngome;

(b) Ujenzi wa jengo la utawala;

(c) Ujenzi wa gereza la akinamama; na

(d) Ujenzi wa nyumba za askari.

Mheshimiwa Spika, sasa tumeanza kuwahamasisha wananchi na viongozi wa wilaya kuchangia ujenzi wa ofisi za utawala na nyumba za askari. Tunaomba sana Serikali ituunge mkono kwenye suala hili ili kuondoa adha wanayopata wafungwa na mahabusu katika Wilaya ya Igunga. Wilaya ya Igunga pia haina vitendea kazi kama magari na computer kwa ajli ya Jeshi la Polisi na hii inasababisha uduni wa huduma inayotolewa na Jeshi la Polisi. Wilaya ya Igunga ina vituo vya polisi katika Tarafa ya Manonga-Chome, Tarafa ya Simbo Simbo; Tarafa ya Igurubi, Igurubi; Tarafa ya Igunga, Igunga na Kituo cha Kata ya Nanga. Vituo vyote hivi vinahudumiwa na gari moja ambalo lipo katika Kituo cha Wilaya ya Igunga. Tunaomba Serikali inunue magari kwa ajili ya Vituo vyote vya Polisi katika Wilaya ya Igunga.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa viongozi wa Wilaya akiwemo DC, Mbunge, DED na wengine tumeanza mchakato wa kujenga Vituo vya Polisi vya Kata za Igunga (Mwanzugi) na Lugubu ili kukabiliana na ongezeko la watu katika maeneo hayo. Tunaomba Serikali ituunge mkono. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa nafasi hii ya kuchangia kwa maandishi. Tunaishukuru sana Serikali kwa kutuletea zaidi ya shilingi milioni 400 kwa ajii ya kuboresha miundombinu ya shule za msingi. Tumeweza kuboresha shule za msingi kadhaa zilikiwemo Shule ya Msingi ya Kisesa, Shule ya Msingi ya Mwakipanga, Shule ya Msingi ya Chipukizi Mjini ya Igunga na shule nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru pia kwa Serikali kutuletea zaidi ya shilingi milioni 800 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Shule za Zekondari Nanga, Bukoko, Igunga na nyingine. Bado changamoto ni nyingi, tumeleta maombi ya kuanzisha shule za high school mbili; Shule ya Sekondari ya Bukoko kwa ajili ya wasichana na Shule ya Sekondari ya Igurubi kwa ajili ya walemavu. Je, Wizara imeliingiza ombi letu hili kwenye bajeti hii?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru tena kwa fursa hii.
Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi Sehemu ya Eneo la Pori la Akiba Kigosi Kuwa Hifadhi ya Taifa Kigosi pamoja na Azimio la Kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji wa Hadhi Sehemu ya Eneo la Pori la Akiba la Igalla Kuwa Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugalla pamoja na Azimio la Bunge la Kuridhia Mkataba wa Minamata kuhusu Zebaki (Minamata Convention on Mercury)
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti,asante. Na mimi naomba nichangie kidogo juu ya mkataba huu ambao unataka kuhakikisha matumizi ya zebaki yanakuwa ya salama. Ulianza kutumika mwaka 2017 na sisi mwaka 2019 tunaridhia, kwa kweli tumewahi, Serikali naishukuru sana kwa kuamua kufanya hili jambo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba huu kama alivyoeleza Waziri una mambo kadhaa unaoelekeza. Mambo hayo ni pamoja na kuhakikisha kwamba zebaki haichimbwi tena, migodi yote ya zebaki ifungwe na mingine ambayo ipo inaendelea ihakikishe kwamba haizalishi tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini matumizi ya zebaki au bidhaa zinazotumia zebaki na zenyewe zisitumike lakini zaidi sana ni matumizi ya zebaki katika kuzalisha dhahabu. Mkataba unaelekeza kuwe na matumizi yaliyoangaliwa, sio matumizi holela, mkataba hausemi kwamba tusichimbe dhahabu kwa uchimbaji mdogo, tusiunganishe dhahabu bila kutumia zebaki, lakini tuhakikishe matumizi haya hayafanyi mazingira yakaharibika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niseme kwamba nilivyokuwa msimamizi wa sekta hiyo ya uchimbaji mdogo, wachimbaji wadogo wengi sana wameathirika na hata watu/watoto wanaozaliwa kwenye maeneo hayo wana hali mbaya sana; wanazaliwa wengine hawana macho na wengine vichwa vikubwa. Kwa hiyo, ni jambo la msingi sana Serikali tutakapomaliza kupitisha huu mkataba, tutengeneze sheria na kanuni ambazo zitahakikisha matumizi ya zebaki kwenye maeneo ya uchenjuaji wa madini yanakuwa ya salama, tusiruhusu kama ilivyo sasa watu wanachenjua tu kwa kutumia zebaki bila control. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho; naomba niombe basi Serikali tu-domesticate huu mkataba kwa kutengeneza sheria, tusibakize zile sheria za zamani hazitoshi, tutunge sheria itakayoelekeza jambo hilo itatusaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja kwa asilimia 100, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili nichangie kidogo hoja hii ya Maji. Namshukuru Mungu kwa kupata nafasi hii kwa sababu ni Mungu pekee anayetupa haya yote. Naishukuru Serikali sana kwa kuliangalia jambo la maji na hasa katika Mikoa ya Tabora, Shinyanga, Simiyu na mikoa mingine kame kwa kutuletea maji ya Ziwa Victoria, ahsante sana Serikali kwa jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Igunga tumekuwa na tatizo la maji la siku nyingi kwa sababu ni wilaya kame, lakini wametuletea mradi huu ambao kwa kweli utatusaidia sana. Mradi huu utafikia kwenye Jimbo la Igunga kata kama sita hivi ambazo ni Kata ya Nanga, Mwamashiga, Bukoko, Itumba, Mbutu na Itunduru. Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuangalia hali ya maji katika jimbo letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama walivyosema Wabunge waliotangulia kuna miradi mingi sana ambayo imetekelezwa, ilitekelezwa ikafikia kiwango cha kufanya kazi, lakini ikatelekezwa ama kwa sababu chanzo cha maji hakikupatikana ama miundombinu haikujengwa vizuri. Kuna mfano wa Mradi wa Maji Kata ya Itunduru, kule Jimbo la Igunga, mradi huu ulijengwa mwaka 2010. Miundombinu ya kupeleka maji kwenye kata hiyo na hasa Makao Makuu ya Kata ilijengwa vizuri ikiwepo tank pamoja na mabomba lakini chanzo cha maji kilikosekana, hata hivyo, mkandarasi alilipwa akaondoka. Wananchi tangu wakati huo leo mwaka wa kumi wanailalamikia Serikali mmetutengenezea mradi tunaangalia tu mabomba tunaangalia tank.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemsumbua sana Waziri wa Maji juu ya jambo hili na naomba niliseme tena, naomba Mheshimiwa Waziri katika kutekeleza Mradi wa Ziwa Victoria atupelekee maji pale ni kuunganisha tu na tumepeleka hata design pamoja na bajeti ni shilingi milioni 100 tu, ukitoa hizo unaweza ukafanya adjustment na mradi wetu ukapata maji, sio mbali sana kutoka bomba kuu la maji. Wananchi wa Itunduru wataishukuru sana Serikali, watafurahi sana na kwa kweli wataipenda Serikali yao, tafadhali sana namwomba Mheshimiwa Waziri anisikilize juu ya jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina mambo mengi ya kusema sana, lakini naomba niseme Wilaya ya Igunga kuna sehemu ambazo hakuna maji ya chini, kwa hiyo kuna vijiji ambavyo tumechimba maji tumepata na tumepewa katika bajeti hii baadhi ya vijiji kuchimba maji. Hata hivyo, sehemu zingine kata nyingi kama kata saba hizi ambazo hazifikiwi na huu Mradi wa Ziwa Victoria hazina maji ya chini, tunajenga vibwawa, tumejitahidi. Namshukuru sana Mheshimiwa aliyekuwa Mbunge kabla yangu mimi alisaidia sana kujenga mabwawa kwenye kila kijiji na hasa kata na mimi nimeendeleza jambo hilo kwa kutumia fedha za Mfuko wa Jimbo. Naiomba Serikali, naomba sana Wizara, wanapoangalia maeneo ambayo yana matatizo ya maji sana kama mikoa ya kwetu ile ambayo ni kame, basi watusaidie kutoka kwenye Mfuko wa Maji kutusaidia kujenga haya mabwawa madogo madogo wakati tunasubiria usambazaji wa maji ya Ziwa Victoria kwenda kwenye kila kijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme jambo la mwisho kuhusu Mfuko wa Maji. Najua Wabunge tumesema sana juu ya jambo hilo kwamba tuwaongeze huo Mfuko ili upate fedha za kutosha kama ilivyo kwenye umeme. Tunasema umeme kwenda kila kijiji na kuna fedha kule REA tumeweza kabisa kabisa, sasa kwa nini tusiwe na REA ya maji ambayo ina uwezo wa kufanya na tuseme maji kila kijiji. Kwa wananchi wetu hili ni jambo kubwa na ni tatizo kubwa sana ambalo tukiweza kulitekeleza hili tutalitendea haki Taifa hili jambo zuri sana, tuweze kuwatua ndoo wananchi wetu, akinamama wa vijijini wanahitaji kutuliwa ndoo kichwani. Kwa hiyo mimi naomba pamoja na kelele ambazo zimepigwa mwanzoni mwanzoni hapa kuomba shilingi 50 ziongezwe, nasema tu kwamba ni lazima tutafute vyanzo hata kama sio shilingi 50, basi tutafute vyanzo ambavyo tutatunisha huu Mfuko uweze kuwahudumia wananchi wetu. Serikali wakilifanya hili la maji vijijini watafanya kazi nzuri sana na wananchi watafurahi sana na wataipenda Serikali yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie kwa kusema, ukokotoaji wa percentage ya coverage ya maji kwenye vijiji haufanywi vizuri, Wabunge wengi wamesema na ndugu yangu, kaka yangu Chiza amesema. Kule kwetu Mwamashimba kule, Mwamakona, Mwanyalali kule na sehemu zote zile ambazo ni mbuga ambako ni ziwani hakuna maji chini, unaona calculation anasema maji asilimia 30. Kweli ukienda kule unakuta visima havina maji vyote au unakuta hakuna kisima kuna kibwawa kimoja kinachokauka lakini asilimia 30 coverage, wanafanyafanyaje? Naiomba Serikali kwenye jambo hili wafanye evaluation ya nchi nzima tena upya ili tuweze kupata percentage ya coverage ya maji inayolingana na ukweli na tukiweza kufanya hivyo tunaweza kutafuta fedha kwa sababu tutajua gravity ya tatizo lenyewe, lakini kwa jinsi hii tunaonekana kama vile maji tumepiga hatua, lakini tuna hali mbaya sana kule vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, naomba niishukuru Serikali tena kwa Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kwenda Nzega, Igunga na Tabora na Katibu Mkuu aliniambia wanaweza kufikisha hata kwenye jimbo la jirani la ndugu yangu Mheshimiwa Mwigulu pale Shelui.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru sana, naomba kuunga mkono hoja. Mungu awabariki sana, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi nichangie kidogo hoja hii ya viwanda, biashara na mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Waziri kwa namna alivyowasilisha ripoti yake na alivyoisoma kwa nguvu mpya na ari mpya. Nakuombea ndugu yangu, mdogo wangu, pambana bwana tunataka viwanda sisi. Tunataka 2025 iwe nchi ya viwanda, nchi ya kipato cha kati, kazi ni kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, niseme Serikali ya Awamu ya Tano ilijipangia mambo kadhaa ya kufanya ili kuipeleka nchi hii kwenye viwanda. Jambo la kwanza ilisema ingeweza kuanzisha viwanda vya msingi ambavyo vinachochea viwanda vingine. Kwa mfano, viwanda vya chuma; Liganga na Mchuchuma, tumesema sana hiyo na tunaishukuru Serikali kwa kuliona kwamba hilo jambo lilikuwa la msingi. Viwanda vya magadi soda kwa mfano kule Engaruka tuliweka kama jambo la msingi. Viwanda hivi vikianzishwa, vingeweza kulipeleka Taifa mahali pazuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Serikali ya Awamu ya Tano iliendeleza shughuli ya gesi na mafuta. Jambo lingine ambalo Serikali ilijiwekea ni ujenzi wa miundombinu. Tunaipongeze sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa jambo hilo, ujenzi wa reli, barabara, bandari, viwanja vya ndege, ndege zenyewe, umeme, nishati na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine Serikali hii ililizungumza sana tangu iingie madarakani ni kilimo. Ilitengeneza mkakati unaoitwa Cotton to Clothes (C2C), lakini ilikuwa na mkakati wa ASDP I na mikakati ya Sekta ya Ngozi. Kwa maandishi, Serikali imekaa vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni mazingira ya kufanya biashara iwe rahisi. Pamoja na hayo, Bunge liliendelea kuishauri Serikali, tangu mwaka 2015 nakumbuka mimi nilikuwa Mwenyekiti wa Viwanda na Biashara, tumeishauri Serikali kama Bunge iyafanye haya mambo ambayo yameandikwa kwenye Mpango wa Miaka Mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema, kwenye mazingira ya kufanyia biashara, tulitaja mambo kadhaa ambayo tunahitaji Serikali iyarekebishe ili biashara iwe sawa sawa. Kwa mfano, utitiri wa kodi, wingi wa mamlaka zinazosimamia, pia mtazamo kuhusu wafanyabiashara na wawekezaji, kuwatazama kama marafiki badala ya kuwatazama kama maadui, wezi na wanyang’anyi. Naipongeza tena Serikali, ilikubali na ilisikiliza ushauri. Natoa vithibitisho vya ushauri kusikilizwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, iliandaliwa blue print, ukiisoma hiyo, mambo yote haya ya uwekezaji pamoja na biashara yamesemwa vizuri sana, tena sana. Changamoto iliyopo Mheshimiwa Waziri, ni utekelezaji. Leo ni mwaka wa pili tuna blue print ipo kwenye shelf na wale buibui wameanza kuitanda sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ule mkakati wa ASDP I nadhani umemaliza sijui miaka mingapi? Mitatu, minne hivi haujatekelezwa. Tunaanza kutengeneza mkakati mwingine, ASDP II. Changamoto kubwa tuliyonayo Mheshimiwa Waziri ni kutekeleza haya mambo ambayo tuliyakubali, tumeyaandika vizuri, mnataka wenzetu majirani wachukue hii mikakati wakatekeleze, sisi tunaangalia tu! Tukiweza kutekeleza hayo, Mheshimiwa Waziri, yaani hatuko mbali kabisa na mafanikio. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka niseme kwamba mchango wangu mkubwa ni kuishauri Serikali sasa, naomba nitoe ushauri ufuatao: La kwanza, Wizara hizi zifanye kazi kwa ushirikiano. Niliwahi kusema zifanye kazi kwa ushirikiano; kilimo, Wizara ya Viwanda na Biashara, Nishati na Ujenzi lazima mkutane. Narudia tena, nilisema mwaka 2016 mtengeneze mkakati wa pamoja wa kutekeleza jambo hili. Wizara ya Fedha nimeisahau, ndiyo inayotoa fedha. Msipofanya hivyo, tutakuwa na mikakati na mipango lakini hatuitekelezi kwa sababu kila mtu anakwenda vya kwake. Ni muhimu sana tukawa pamoja katika mambo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa hizi documents ambazo nimezitaja hapa; blue print, ASDP, C2C na mikakati mingine ipo mizuri mingi kabisa, imejibu hoja zote na matatizo yote ambayo tunayasema humu Bungeni, hebu itekelezeni. Nakumbuka kuna mkakati wa kuzalisha mbegu za mafuta nyingi hapa ili tusiwe na matatizo ya mafuta, tekelezeni. Tukiendelea kila mwaka tunakuja tunatoa story hapa, kwa kweli hatutafika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri mwingine, tuangalie baadhi ya sheria. Kuna sheria nyingine tumezitengeneza nzuri kweli, lakini mle ndani kuna maneno ambayo yamefukuza wawekezaji. Naomba kila sekta angalieni sheria zenu, mbadilishe kidogo. Ngoja nitoe mfano, mnisamehe. Sheria za sovereignty tulizotengeneza ni nzuri kweli zinalinda rasilimali zetu, lakini kuna vipengele mle ndani akisoma tu mwekezaji anabwaga manyanga anaondoka. Naomba sana Waziri wa Sheria na Katiba, Waziri wa Madini na Waziri wa Nishati hebu tazameni, kuna vipengele vichache siwezi kuvitaja, ukivibadilisha tu kidogo unahamasisha uwekezaji wa ndani na wa nje, utakuja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wa nne, tuongeze bidii katika kujenga miundombinu. Hapa tunafanya vizuri sana, tunajenga reli, barabara, viwanja vya ndege, tunatengeneza umeme, lakini tuongeze bidii. Kuna sehemu hatujaenda vizuri. Kwa mfano, tunajenga reli kwenda Mwanza, lakini financing inatupa shida kidogo na Wabunge kadhaa walisema, tuna-finance kidogo kidogo, tutatumia miaka 20 kufika Mwanza. Hebu tutafute mkakati mzuri zaidi tuharakishe jambo hili. Kwa kweli ni jambo zuri, lakini tulifanye kwa speed ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wa tano, tujenge viwanda mama. Liganga na Mchuchuma jamani tungetumia chuma sasa hivi kujenga reli yetu, chuma cha ndani, lakini tumechelewa. Hebu tukazane kidogo hapo. Mheshimiwa Waziri wasiliana na Nishati na Madini hii rasilimali iweze kuchimbwa. Hizo changamoto zilizopo hapo tuzirekebishe, tutaenda vizuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wa mwisho, tulifanya vizuri sana katika kuweka maeneo ya uwekezaji; EPZ pamoja na SEZ. Tume-identify maeneo mengi lakini kuya-develop imekuwa taabu. Moja ya changamoto ni Bandari ya Bagamoyo; ni kitu kizuri kweli na kina maelezo mazuri kweli, lakini tumeenda mpaka sasa hivi kuna kizungumkuti wanasema Waswahili. Kwa kweli Mheshimiwa Waziri hatuelewi kama tunaenda au hatuendi. Maeneo mengi kama Kurasini mpaka leo, yapo mengi tu, mpaka kule Igunga kuna maeneo ya uwekezaji ambayo hayajaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa kusema, tunafanya vizuri sana katika kuandika projects na mikakati lakini hatufanyi vizuri katika kutekeleza. Tunaandika sheria, tunashindwa kuzitekeleza. Sheria ya PPP kwa mfano, tuliitunga mwaka 2018 lakini ina vikwaruzo vingi mle ndani. Nami nikiwa Mjumbe wa Kamati ya Bajeti, nilisema, nilimwambia Waziri wa Fedha kama anakumbuka, kwamba hii tulivyoipitisha kama ilivyo hivi hatutapata mwekezaji hata mmoja kwenye PPP kwa miaka 20 ijayo. Lazima tuirudishe hapa tuibadilishe, kuna mambo ambayo hayakusemwa vizuri humu. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Dkt. Dalaly Kafumu.

MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niunge mkono hoja. Ahsante sana kwa kunisikiliza. Mungu awabariki. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikushukuru kwa kunipa nafasi na mimi nichangie hoja ya Mpango iliyoko mbele yetu. Nianze kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kazi njema anayofanya pamoja na Serikali yake. Kipekee pia namshukuru Waziri wa Fedha pamoja na Naibu wake, tumekuwa tukipambana huko kwenye Kamati ya Bajeti, kwa kweli tunakushukuru wakati mwingine unasikiliza maneno yetu na mapendekezo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango huu tunaokwenda kuutekeleza au tunaouandaa ni mpango wa mwisho kwenye Mpango wa Miaka Mitano; na mambo yote inayoyazungumza yalitokana na Mpango wa Miaka Mitano, ule wa 2016/2017 – 2020/2021. Mambo mengi tuliyojiwekea kule, sasa tunakwenda kumaliza kuyatekeleza.

Mheshimiwa Spika, napenda niseme mambo mazuri ambayo Serikali imeyafanya, ni pamoja na miundombinu. Kama nilivyosema mwaka 2018, ukitaka kujenga nchi ya viwanda ni lazima uwe na miundombinu. Kwa kweli Serikali imefanya vizuri sana kwenye ujenzi wa reli, barabara, chanzo cha umeme na miundombinu mingine inafanywa vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado kuna changamoto kidogo ambapo nitatoa ushauri kidogo kama wenzangu walivyosema, kwamba Serikali ichapue kidogo, iongeze speed kidogo katika kutekeleza ujenzi wa miundombinu. Naomba tena na mwaka 2018 nilisema, Mpango huu basi mwangalie, kuna barabara nyingine za kiuchumi kama barabara ile inayotoka Shinyanga, inapita katikati ya Igunga inaelekea Mbeya.

Mheshimiwa Spika, kuna mabasi huwa yanatoka Shinyanga yanaenda Mbeya kupitia katikati ya Igunga. Hii barabara naomba iwekwe kwenye Mpango, nasema tena kwa sababu barabara hii inatoka Ukenyenge, inakuja Igurubi, inapita Mwamakona, inakwenda Igunga, inaenda Rugubu, inaenda Itumba, inenda Loya, inaenda Tura, inaenda kuunganisha na barabara inayotoka kwa wachimbaji madini kule Mbeya na barabara inafika Mbeya. Najua kwa upande wa kule imeletwa mpaka Rungwa. Naomba sasa iunganishwe barabara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii sasa hivi kuna kipande cha kutoka Igunga kwenda Itumba, kimepewa fedha kidogo, lakini utekelezaji umcheleweshwa. Naomba basi katika Mpango, hii barabara ni ya kiuchumi inapita kwenye pamba, kwenye mpunga na kwenye ufugaji wa ng’ombe. Ni muhimu sana tuharakishe miundombinu ili tuweze kujenga viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la miundombinu ya maji. Kama Waheshimiwa Wabunge wengine wanavyosema, maji ni shida kubwa katika nchi yetu. Tunaishukuru sana Serikali kuanzisha ule mradi wa maji wa Ziwa Viktoria na sasa hivi unakwenda Tabora – Igunga
– Nzega. Ahsante sana Serikali kwa kutukumbuka. Igunga ni nchi kame sana, lakini nadhani maji haya yatatusaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tena kwenye Mpango huu basi tuongeze fedha kwa ajili ya kupeleka kwenye zile kata ambazo zimebaki. Sasa hivi tunapata kata kama nane hivi; zinabaki nane kwenye Jimbo la Igunga. Pia kuna Kata nyingine nyingi zinabaki kwenye Jimbo la Manonga ambalo ni Wilaya ya Igunga. Basi tuweke Mpango mwaka 2010 tumalizie kwani wananchi hawa wako kwenye ukame mkubwa, waweze kupata maji. Tutawashukuru sana Serikali mkitukumbuka mkaweka kwenye Mpango jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la viwanda ni suala ambalo Serikali ilijiwekea kwenye mpango wa mwaka 2016/ 2017 mpaka 2021. Ilieleza mambo machache mle ndani yakiwa ni pamoja na kutekeleza miradi ya kimkakati. Miradi mingi ya kimkakati imeshindikana kutekelezwa. Mwaka wa tano leo au mwaka wa nne tunamalizia, mingi bado inasuasua. Naiomba Serikali tena, tuendelee kuiweka kwenye mpango na tutafute fedha ya kuitekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, miradi ya kuendeleza maeneo maalum, kwa mfano, mradi wa kuendelea eneo la Mtwara ambako kuna gesi; tulianza vizuri, lakini kuna mahali tukalega tukaenda pembeni. Kwa hiyo, mradi wa LNG unahangaika, leo mwaka wa tano haujatekelezeka. Naiomba Serikali, hebu malizieni mazungumzo na hawa wawekezaji. Mradi huu ni muhimu, tutapata gesi ya kutumia ndani na pia tutapata gesi ya kupeleka nje tupate fedha za kigeni. Ni jambo kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, gesi hiyo pia tutaweza kujenga kiwanda cha mbolea, ambacho kimetajwa vizuri sana kwenye Mpango, lakini leo mwaka wa nne tunasema tu. Naiomba Serikali, hebu yaangalieni mambo haya, maeneo haya yako mengi, ila Mtwara kwa kweli, hebu tulitazame vizuri, hii gesi itumike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi mwingine tumeusema sana kwa muda mrefu, ambao ni mradi wa Mchuchuma, Liganga. Pale kuna chuma cha kutosha kinachoweza kututosha nchi hii kujengea barabara zetu, reli, madaraja na kujenga maghorofa kama tukichimba kile chuma. Kwa miaka mitano sasa hatujaweza kutekeleza. Naomba tena kwenye Mpango isisitizwe na tuweke fedha kidogo huu mradi uweze kutekelezeka. Vinginevyo kwa sababu viwanda vinategemea sana viwanda vya chuma, tutaweza kuwa na chuma cha kuenea kwenye viwanda vingine vyote vya chuma katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine lililosemwa kwenye Mpango ule wa miaka mitano na Mpango wa mwaka 2018 na wa mwaka huu 2019, limesemwa vizuri, ni jambo la kufundisha wataalam na kuchukua teknolojia, hasa wataalam wa ngazi ya kati. VETA tunafanya vizuri, tunapata mafundi mchundo vizuri sana. Na mimi Wilaya ya Igunga tumeletwa ujenzi wa VETA, tunashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye ngazi za kati, mafundi sanifu, Vyuo vya Mafundi Sanifu vimekuwa vichache na bahati mbaya wakati mwingine Serikali inavigeuza hivi vyuo kuwa Vyuo Vikuu au inaviruhusu vianze kutoa degree.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mzuri ni Chuo cha Madini Dodoma, kilianzishwa ili kupata mafundi mchundo, nami nilishiriki kukianzisha wakati nikiwa Serikalini, lakini sasa hivi kinalelewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Matokeo yake ni kwamba kitakuwa na hamasa na tamaa ya kuwa Chuo Kikuu na kukibadilisha kuwa Chuo Kikuu. Tutakosa mafundi mchundo watakaoshiriki katika ujenzi wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali mliangalie jambo hili kwa makini kidogo. Nakumbuka nilihudhuria Kamati ya Madini na Nishati, pamoja na Wabunge wengine wa kamati hiyo, tulisema maneno haya kwamba msiwe na hamu na haja ya kubadilisha hivi vyuo kuwa Vyuo Vikuu, mtachelewesha uanzishwaji na uimarishaji wa viwanda vyetu kwa sababu tutakosa mafundi sanifu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kilimo. Ukiangalia kwenye Mpango, tulijiwekea mipango mizuri sana. Kilimo kinaweza kuendeleza viwanda sana kwa sababu malighafi nyingi zinatoka kwenye kilimo. Kwa mfano, pamba; tuna mkakati wa C to C (Cotton to Clothing) ambao unasema tuzalishe pamba kwa wingi, tutengeneze nyuzi hapa hapa na tutengeneze nguo hapa hapa, lakini mpango huo hauendelei kabisa. Hiyo C to C imekuwa document ambayo iko kwenye shelf. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara pamoja na Idara zake na Wizara ya Kilimo kwa umuhimu wake muufufue huu Mpango, pamba itumike kujenga viwanda. Tusifikirie tu kuuza pamba nje. Tunapata taabu sasa hivi hatujalipa wakulima wetu, lakini tungekuwa na viwanda hapa hili tatizo la pamba, tatizo la bei lisingekuwa shida kubwa kwetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala la mifugo kwa mfano na lenyewe kwa kuwa tuna mifugo mingi, tunaweza kuwa na viatu hapa hapa, lakini hatutazami. Mpango huu uyatazame mambo haya tena ya kujenga viwanda kwa kutumia malighafi katika nchi yetu. (Makofi)

(Hapa kengele ililila kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Malizia Mheshimiwa.

MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Naomba niseme tena kwamba, Mpango umalizie yale mambo ambayo umeyaacha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi nichangie kidogo. Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kazi nzuri anayofanya, tunampongeza na tunaomba aendelee kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nataka nichangie mambo matatu tu. Kwanza, ukurasa wa nne wa hotuba ya Mheshimiwa Waziri inazungumzia dira, dhima na majukumu ya Wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa namshauri Mheshimiwa Waziri kwamba hii dhima na dira zikaandikwe vizuri kwa sababu ukisoma zinafanana. Dira anasema ni maliasili na malikale zinazohifadhiwa kwa manufaa ya Watanzania kwa ajili ya kukuza uchumi; hiyo ni dira. Dhima na yenyewe inasema, uhifadhi endelevu wa maliasili na malikale na kuendeleza utalii kwa manufaa ya taifa. Hivi vitu vinafanana, ni vizuri kuandika dira ambayo inaonyesha tunaenda wapi baada ya miaka kadhaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Lakini, dhima iwe ni tunafanyafanyaje kwenda kwenye hayo mahitaji tunayotaka kuyafikia, kwa namna hii imefanana, naomba nitoe huo ushauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni kwamba, Mheshimiwa Rais aliagiza maeneo yote yenye migogoro ya wakulima na wafugaji yafanyiwe kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kweli amesema, iliundwa Kamati ya Mawaziri wanne na wameenda na wamemaliza kazi lakini kuna maeneo hawajafika. Kule kwetu Manonga Wembele Game Reserve Mawaziri hawa hawajafika na wananchi bado wanagombana; nilikuwa naomba nako mfike. Pamoja na kwamba tumeanza kufanya mapatano lakini tunahitaji Waziri aje atoe maelekezo mahsusi ili wananchi waache kugombana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jambo la tatu na la mwisho; ninaiomba sana Serikali na hasa Wizara hii, hebu tujaribu pia ku-develop utalii wa mambo mengine badala ya nature reserve peke yake, badala ya baianuai peke yake. Tanzania tumebarikiwa sana kuwa na masalia ya Watemi na nyumba za Watemi. Ukienda kule Igunga, kuna Mtemi Ng’wanansali wa Igurubi, kuna nyumba yake pale, tunaweza kuitengeneza na watalii wakaja kuona. Ziba pale kuna Mtemi Ntinginya na akina Humbi pale, kuna nyumba yao na makaburi yao, tunaweza kuyafanya; na Mikoa mingi tuna mambo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu ukienda Ulaya haya mambo wameya-develop sana. Kwa mfano Ubelgiji, mimi nimekaa Belgium miaka kumi, kuna mtoto mmoja historia yake alikojolea bomu wakati wa Vita Kuu ya kwanza, sasa yule mtoto ametengenezwa na akawekwa kwenye kila mji anakojoa, watu wanakuja kuangalia na historia inaelezwa pale. Kwa hiyo ni kivutio kikubwa kweli cha utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, basi na sisi mambo haya tuya-develop, yako mengi, kwa mfano, tuna njia ya utumwa sisi, kutoka Bagamoyo mpaka Ujiji tungeweza kui-develop hiyo njia vizuri na wazungu na wenzetu watalii wangependa sana kuja kuipita hiyo njia kuangalia watumwa walivyokuwa wanachukuliwa na sisi tulivyokuwa tunabebwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sisi tumeng’ang’ania zaidi utalii unaohusu wanyama, mimea, milima nakadhalika, hebu twende na huo upande mwingine itatusaidia sana tutaalika watalii wengi zaidi kuliko ilivyo sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi, ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza).
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Nianze kabisa kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwenye jambo hili kubwa alilolifanya la kuiangalia sekta ya uchimbaji mdogo. Kwa kweli amefanya jambo kubwa, wachimbaji hawa wamekuwa na kilio kikubwa, tunamshukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda niseme kwamba Muswada huu ni muhimu sana na ulitakiwa uje kwa Hati ya Dharura na sisi tumeutendea haki kwenye Kamati. Sina maneno mengi sana ya kusema kwenye Muswada huu lakini niseme tutakapokuwa tunatekeleza Muswada huu kuna mambo yanaweza kujitokeza ambayo labda hatukuyatazama vizuri. Napenda niseme mambo mawili tu ambayo nategemea yanaweza kutuletea changamoto wakati tunatekeleza Muswada huo.

Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza, ni Kifungu cha 21(2) ambacho kinazungumzia utoaji wa import permit kwa wanaoleta madini nchini. Najua tumevutana vutana sana, lakini tumerekebisha mpaka hapo tulipofika, lakini bado naamini kuna namna tunaweza tukarebisha zaidi, kwa sababu majirani zetu hawana utaratibu huo unaovuta sana. Kwa hiyo, wao wataweza kuendelea kupata madini yetu kutoka hapa yakienda kwao kuliko sisi. Kwa hiyo, huu utaratibu kadiri tutakapotekeleza ikileta changamoto hizi ambazo nazitegemea, basi msisite kuleta tukarekebisha jambo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunatakiwa anayetaka kuleta madini Tanzania asipate tabu yoyote ajue anaenda kwenye madini atapita vizuri, akipita kwenye soko madini yake yanaandikishwa anauza, lakini tukianzia kuwazuia kule kule mpakani tunaweza tukatapa tabu kidogo. Nasema tu kwamba kwa sasa tupite lakini kama kuna changamoto itajitokeza, tuirekebishe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili na la mwisho ni Kifungu namba 26 ambacho nilichokizungumza ni Kifungu
26(b) sasa nazungumzia Kifungu 21(2). Kifungu hiki kinaweza kabisa kuzuia baadhi ya wachimbaji kufanya biashara kwenye soko la nje kwa sababu wao wamelazimika kwenda kwenye soko tulilonalo. Sasa katika kutekeleza kuna wengine wanaweza kuwa na Dealer’s License basi kwa namna fulani waruhusiwe ku-export madini kama wanaweza badala ya kulazimisha kila mmoja aende kwenye soko, anayeweza kwenda nje basi aende lakini tuhamasishe zaidi watokeze kwenye soko.

Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie kwa kusema naunga mkono hoja na naishukuru sana Serikali kwa kuleta Muswada huu ambao utasaidia sana wachimbaji wadogo. Mungu ibariki sekta ya uchimbaji mdogo, Mungu ibariki Tanzania. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi nami nichangie kidogo hoja ya Waziri Mkuu. Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, speech yake kwa kweli imeeleza juhudi ambazo Serikali imezifanya, ni juhudi nzuri. Kwa kweli mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Serikali imefanya kazi kubwa. Nikiangalia kwenye Jimbo langu, Serikali imetuletea maji kutoka Ziwa Victoria. Kata zaidi ya 11 sasa zina maji. Tumepata fedha shilingi bilioni mbili na zaidi tunajengewa VETA pale.

Mheshimiwa Spika, tumejengewa Kituo cha Afya cha Igurubi, tuna daraja la Ngutu ambalo tulijengewa. Kwa kweli ni mambo mengi mazuri wananchi wa Igunga wanashukuru. Kwa niaba yao, naomba niseme ahsante sana kwa Serikali kutufanyia haya mambo mazuri kabisa.

Mheshimiwa Spika, suala la umeme nisilisahau, bado nina kata tano tu ambazo hazijapata umeme. Naomba basi itakapofika wakati ziweze kupewa umeme. Kwa maana hii, naomba niishukuru sana Serikali, nimshukuru Mheshimiwa Rais pamoja na Serikali yote kwa kazi nzuri hii. Bado tuna changamoto kidogo kidogo ambazo kwa kweli ndiyo wajibu wetu Wabunge kusema. Kama Wabunge wengi walivyosema, nami naomba niseme, hizi changamoto basi tuzifanyie utaratibu.

Mheshimiwa Spika, nianzie na janga hili ambalo liko pamoja nasi, Waheshimiwa Wabunge wamesema, nami naomba kuishauri Serikali kwamba kwa sababu limetukuta tuko kwenye bajeti, ni lazima tunapoendelea kuchakata bajeti yetu tuendelee kuiangalia. Hatujafika mwisho, ikiwezekana tuweke utararibu wa kibajeti kupambana nalo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na maelekezo yote haya ambayo wananchi tunaendelea kuyafuata lakini tusisahau kama Serikali kwamba janga hili ni kubwa na hata ikibidi kubadilisha bajeti yetu kidogo, tusione aibu kwa sababu ni jambo kubwa limetukuta.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie kidogo kuhusu kilimo. Sisi ni wakulima wa pamba kule Igunga, tunazalisha mbegu kwa ajili ya wakulima wa pamba wote Tanzania. Mwaka 2019 tumepata taabu sana ya kuuza zao la pamba na mpaka sasa kuna baadhi ya wananchi bado wanadai hawajalipwa. Zaidi ya shilingi milioni 200 hazijapelekwa kwa wananchi. Tunaomba basi kama inawezekana Serikali imalizie, nadhani siyo Igunga tu, lakini wakulima wa pamba wote hii taabu iliwapata sana. Tukumbukeni Mheshimiwa Waziri Mkuu, wananchi wetu wanakata tama kidogo. Mwaka huu nadhani nilizungumza na Naibu Waziri, kuna marekebisho kidogo kwenye jambo hilo.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ningependa kusema ni madhara ya mvua ambazo zimenyesha. Tunashukuru tumepata mvua na chakula ni kingi kama ulivyosema. Tuna chakula kule kwetu kingi sana, mahindi na kadhalika. Sehemu chache ambazo zilikuwa za chini kule, maji yamechukua mpunga na nini, lakini sehemu nyingi wamepata chakula, ila imeleta madhara makubwa sana. Kweye Jimbo langu kuna barabara ambayo huwa nalalamika kila siku, tulipata fedha, lakini wameshindwa kujenga kwa sababu mvua imenyesha kubwa. Nilikuwa naomba basi tuangalie utaratibu wa kubadilisha, kuongeza bajeti kwenye hizo barabara kwa sababu zimekatika sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la umeme kama nilivyosema, wananchi wa Igunga wanashukuru sana. Bado Kata tano tu; Kata ya Mtungulu, Kinungu, Kininginila, Mwamashiga na Kata ya Isakamaliwa, bado hazijapata umeme hata kidogo. Mheshimiwa Waziri wa Nishati, tunaomba basi mtutazame kwa namna ya pekee.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili kutoka mwisho ni usala la uwekezaji katika nchi yetu. Tunataka kwenda kwenye nchi ya viwanda na Mheshimiwa Chegeni amesema kidogo kwamba tunahitaji sana tuhahamasishe uwekezaji wa ndani na wa nje. Blueprint ile hebu tuitekeleze kama alivyosema Mheshimiwa Soni, ni muhimu sana. Kwa sababu tusipofanya hivyo, tunaweza tusiifikie nchi ya viwanda kwa sababu wawekezaji wengi wanakata tamaa. Wengine wanaondoka, wengine wanaogopa kwa sababu ya matatizo ambayo yako katika kuendesha biashara na kuanzisha biashara katika nchi yetu imekuwa taabu sana.

Mheshimiwa Spika, la mwisho, nizungumze kuhusu Sekta ya Madini ambapo kwa kweli naipongeza sana Serikali. Wamejitahidi wamefanikiwa jambo moja kubwa ambalo sisi lilitushinda la kuwapatia machimbaji wadogo masoko. Serikali imefanikiwa sana na ninawashukuru sana. Jambo moja dogo limebaki ni kuhamasiha Sekta ya Uchimbaji Mkubwa. Sekta ya Uchimbaji Mkubwa imekufa kwa sababu utafutaji umepotea kabisa. Utafutaji ndiyo engine ya kuleta migodi mingine.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali na Waziri wa Nishati na Madini, tutazungumza kwenye Wizara yake, ahamasishe utafutaji mkubwa wa madini kwa watafutaji wa ndani na wa nje ili migodi iweze kuanzishwa siku za usoni. Hii migodi mitatu iliyobaki, ikifungwa hatutakuwa na migodi tena na migodi inaleta ajira kweli. Inaleta zile effects za watu ku- supply migodini, kufanya kazi kule ni muhimu sana. Kuna nchi zinaendeshwa na uchumi wa migodi. Kwa hiyo, nasi tukihamasisha utafutaji, tutakuwa na hali nzuri sana ya kuweza kupata uchumi kutoka katika madini yetu haya. Tumeweza kuya-control, tumeweza kuhakikisha kwamba wachimbaji wadogo hawayatoroshi ovyo ovyo. Kwa hiyo, lazima tuyachimbe kwa ku-benefit uchumi wetu.

Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Naishukuru tena Serikali, endeleeni kufanya hivyo, nasi wananchi tunapokea na tutafanya kazi pamoja nanyi.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na Mungu awabariki. (Makofi)