Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Ahmed Ally Salum (14 total)

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017- Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika hoja hii. Kwanza kabisa, nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri kwa hoja yake. Vilevile nimpongeze msaidizi wake mkuu, Dkt. Meru, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara alikuwa EPZ, ni Katibu Mkuu mmoja mzuri sana, anafanya kazi vizuri, tulikuwa naye, namfahamu atakusaidia sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukitaka kuanzisha kiwanda au ili Tanzania iwe nchi ya viwanda, taasisi ya dunia inayotoa hali halisi ya mazingira mazuri ya kuanzisha viwanda nchi ya Tanzania ni ya 139 kati ya 184. Maana yake utaona Tanzania bado kuna vikwazo vingi sana katika kuanzisha bishara au viwanda katika nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri ameongea hoja nzuri sana lakini naomba nitoe mifano miwili, mitatu ili uone namna gani vikwazo hivi bado viko Tanzania. Ukienda TIC pale wako TRA, kipo Kitengo cha Ardhi na kipo Kitengo cha Uhamiaji lakini wale hawana mamlaka. Unapotuma application ya aina yoyote ili kupata huduma pale lazima sasa utoke tena uende Immigration au Ardhi. Wanasema kuna Benki ya Ardhi hawana, siyo kweli! Ukitaka kuwekeza pale wanaweza wakakupeleka kwenye pori ambalo linatakiwa lilipiwe, ufanye kazi kubwa, uanze kuendesha na mambo mengine mengi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, TIC ni kitengo kizuri sana lakini Mheshimiwa Waziri ungefanya utafiti wa kina sana, One Stop Center siyo vile, ungeongeza na TBS na NEMC na wawe na maamuzi pale, ukipata certificate TIC wanakuambia nenda kafanye kazi, ukienda kuanzisha kiwanda, naomba ni-declare interest mimi nina kiwanda, raha ya ngoma uingie ucheze natengeneza air cleaner zipo hapa, mwaka mmoja na nusu kupata certificate ya TBS, mimi sijapata mpaka leo. Nimeenda kwa Katibu Mkuu na wewe nimekueleza mmenielewa. Sasa kama mimi nasumbuliwa hivi wengine inakuwaje? Kwa kweli TIC inatakiwa iwe ni One Stop Center. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, halafu umesema kuna viwanda zaidi ya 49,000, sawa, umefanya utafiti ni Watanzania wangapi wanamiliki na wageni wangapi wanamiliki? Tusipotazama huko tunakokwenda Watanzania watakuwa wasindikizaji na hauwezi kukataa wawekezaji wa nje kuja hakuna kitu kama hicho. Tunawahitaji kweli lakini kuwepo na mfumo mzuri. Mimi nitakuja na hoja binafsi namna gani bora ya kuwasaidia Watanzania waweze ku-penetrate kwenye suala zima la kumiliki viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niseme vikwazo vingine. Ukiwa na kiwanda cha maji TFDA anaingia humo, ukitaka kupata kibali TBS humo humo, OSHA humo humo na hao wote wanafanya kitu kimoja. Kwa nini wasikubaliane tu kwamba taasisi hii moja ikitoa kibali kwa ajili ya maji basi biashara yangu imeisha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda kwenye cement, ili uweze kuuza cement kwenye soko la Afrika Mashariki unatakiwa upate kibali cha Mkemia Mkuu ambapo unalipa 2.5% ya thamani lakini ukienda Kenya haipo, ukienda Uganda haipo. Unamwambia nini mwenye kiwanda? Ni kwamba ondoa kiwanda chako peleka Kenya, peleka Uganda ndiyo maana yake. Ndiyo maana sisi tumekuwa wa 139. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hapa wenye viwanda vya alizeti walisema wana uwezo wa kuwaajiri Watanzania milioni saba mpaka kumi lakini waondoe vikwazo vya kuagiza malighafi. Ukienda Uganda kupata kibali cha kuagiza malighafi ya mafuta ya alizeti kwa maana ya mbegu za alizeti ni miezi sita, Tanzania miaka saba, huu ni utafiti umefanyika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, namuomba Mheshimiwa Waziri afanye utafiti wa kina sana, anaweza akaongea vizuri sana hapo lakini bado hatuko vizuri sana katika kuwasaidia Watanzania wawekeze. Kutana na wafanyabiashara wenye viwanda, wa kati na wa juu wakupe ya kwao uanzie pale, ukitoka na vile vitu vizuri ukavifanyie kazi kwa mfano suala zima la sera na kubadilisha sheria. Kwa mfano, mtu akiwekeza kiwanda cha mashudu hapa, akiagiza malighafi kwa ajili ya mashudu anapigwa ushuru mkubwa sana lakini ukileta mashudu kutoka Kenya unaingia bila VAT, ni msamaha tu! Maana yake unamwambia nini? Ondoa kiwanda chako cha mashudu peleka Kenya ili mashudu yaje Tanzania, ndio hivyo ilivyo. Kuna contradiction kubwa sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nina kiwanda cha air filter, naagiza malighafi kutoka nchi mbalimbali kama Korea na sehemu nyingine, unapigwa as if ni finished product lakini ukiagiza air filter ni 10% only finished product. Hivi una Mtanzania kweli unamsaidia? Yako mambo mengi tu lakini kwa kweli vikwazo ni vingi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, bandari, Kenya wanatoa container milioni sita na nusu kwa mwaka lakini Tanzania ni container milioni moja na nusu wakati ule.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kuongelea transit containers siongelei container za ndani, hiyo ni biashara. Transit containers ni direct foreign income kwa nchi kama vile utalii tu, mtu ana-container lake anatoka DRC anakuja kulichukua hapa, anaacha pesa yake, anachukua container lake anaondoka.
MHE. AHMED A. SALUM: Tunapofanya maamuzi ndugu zangu, tuwe tunafanya utafiti nchi jirani kama Malawi, ninyi mnajua uhusiano wa Tanzania na Malawi.
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, Malawi ni nchi ambayo mahusiano yetu mnayajua wanatupiga vita kwenye bandari yetu hii, Kenya ni hivyo hivyo wanatupiga vita. Kwa hiyo, tunapofanya maamuzi ya aina yoyote ile tuwe tunatazama huku kwa sababu port ya Dar es Salam ni bandari. Sasa hivi ma-container yamepungua pale ni ma-container ya DRC, Zambia na Burundi yameondoka kwa sababu ya vikwazo vilivyokuwa ndani ya bandari yetu, yameondoka kabisa hivi hivi tu. Tumeweka VAT on the transit goods for what reason kuna checks point sita for what reason?
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkono hoja, dakika kumi ni ndogo sana, ahsante.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwenye Mpango huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naendeleza pale alipoishia Mheshimiwa Bashe, Waheshimiwa Wabunge wa CCM tusipokuwa wakweli hii ni Serikali yetu, ni Serikali ya Chama cha Mapinduzi, tusipomwambia ukweli Waziri wa Fedha tunakwenda kugonga mwamba. Leo tunapoongelea uchumi kuna tatizo la mzunguko wa fedha ndani ya nchi yetu, unajiuliza fedha zimekwenda wapi? Halafu unakuja hapa unasema uchumi mzuri, sijui nini, how! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mabenki yanaanza kufilisika, Twiga tayari imeshakuwa taken over, CRDB tayari imeshapata hasara, TIB tayari imeshapata hasara maana yake nini? Maana yake ni kwamba hizo benki projection ya mbele kule miaka miwili, mitatu zinakwenda kufungwa, inakuwa another crisis of Tanzania. Waziri wa Fedha amekaa tu anatazama hali hii! Waheshimiwa Wabunge, mabenki yakifungwa na huku yametoa mkopo businesses hazirudishi mikopo, hebu angalia crisis na tatizo la uchumi wa ndani ya nchi litakavyokuwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, amesema Mheshimiwa Bashe inawezekana hawa hawakwenda kuomba kura hawaelewi joto la wananchi kule.
Sisi ndiyo tunakwenda, ndiyo frontline. Tatizo lingine unaweza kuwa umeteuliwa na Mheshimiwa Rais, basi kule kuteuliwa tu unajiona wewe bora kweli, hapa lazima useme kweli! (Makofi/Vigelegele)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi natoka Jimbo la Solwa, tuna ahadi tumeahidi na kesho nina swali hapa tutabanana tu na TAMISEMI, unakwenda unaongea, unadanganya mpaka unachoka, yapo mambo unachoka kudanganya! Ameahidi Kikwete ameondoka, amekuja Pinda ameondoka, anakuja Magufuli ataondoka na baadhi ya miradi haitawezekana kufanyika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nishauri, fedha ambazo mmezichukua za hizi parastatals companies, haya Mashirika ya Hifadhi ya Jamii mmekwenda kuziweka kabatini BOT, warudishieni wenyewe wazifungulie akaunti kwenye commercial banks, waachie wenyewe iwe ni kama another income of their source. Zile fedha wao watapata, benki zitaendelea kuzitumia ku-lend kwa customers, uchumi kidogo utaendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wa pili, namwomba Mheshimiwa Waziri wa Fedha alipe madeni ya ndani ili fedha zianze kuzunguka sasa hivi kuna joto. Leo Wabunge si mnaona hapa, jana mlikuwa mnaongea sijui nini, hata Bunge hapa ukata mtupu kwa kwenda mbele. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mbunge wa CCM. Tukienda kwenye party caucus tukafanye maamuzi kweli kwa sababu ya nchi yetu na Serikali yetu hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo lingine, wakati ule niliwahi kumshauri Waziri wa Fedha nikasema Mawaziri watakuwa wanafanya kazi kwa matukio, unasubiri tukio likitokea unaenda ku-deal nalo kwa sababu hatuna Department ya Research and Development. Tunaweza tukaanzia na Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Miundombinu ili research zile zijulikane kwenye sekta ya viwanda na Serikali kwa ujumla wake. Ukiweka juu ya meza unakuja hapa na mpango wako yako mambo ya kubadilisha sheria, ya kurekebisha sera matatizo haya yote yatapungua na wananchi watapata ahueni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Japan mwaka 1980 waliweka 2% ya bajeti yake kwenye R&D yaani unafanya utafiti wa sehemu gani tumekosea, tufanye nini, tuboreshe nini ili uwekezaji ukipita pale uweze kunufaika. Australia 1.5 mwaka 1982 ya bajeti yake na ndiyo iliyowapeleka mpaka leo nchi zile zimeweza kuendelea. Leo unakuja na Mpango umeutoa wapi, umefanya research gani? Tutabaki tunahangaika na tunalalamika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nilikwenda kwenye Kamati ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara walikuja wawekezaji wa nchi nzima, wawakilishi kutoka Bakhresa, Mohammed Enterprises, wafanyabiashara wengi walikuja na kila aliyesimama analalamika, halafu unasema Tanzania ya viwanda, halafu unasema Magufuli ataweza kuleta viwanda, ukiwasikiliza wale wanavyolalamika, ukiona sera na sheria zimepitwa na wakati hatuwezi kufika. Kama ni viwanda kwa style hii hatuwezi kufika kwa sababu kuna mambo ya kurekebisha kwenye viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, TIC, One Stop Center, ukienda pale hakuna cha One Stop Center kuna Many Stop Centers, unaweka document yako pale hakuna maamuzi, documents zinachukuliwa zinaenda TRA, TRA pale wiki mbili tatu, mwezi irudi, unangoja certificate umalize pale, maamuzi yanachelewa, kila mtu hana maamuzi. Tatizo ni kubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niongelee kuhusu viwanda. Tukitaka tu-win kwenye viwanda sheria lazima ibadilishwe baada ya kufanya utafiti wa kina. Kuna tatizo kubwa sana TBS, kuna tatizo kubwa sana NEMC na siyo kwamba wao ni tatizo, tumechukua sheria za nje, tumezi-copy tukazi-paste kwetu, imekuja kwenda tofauti na uhalisia wa wawekezaji ndani ya nchi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi hii wawekezaji watakaoweza ku-win vizuri wale wanaotoka nje, wakubwa, anakuja na dola milioni 50, milioni 200, wale ndiyo watakuja kuimeza nchi hii. Mkitaka Watanzania waweze kuinuka kwa sheria tulizokuwa nazo, kwa watendaji ambao wanafanya kazi kwa mazoea bila kuwa na mfumo rasmi, bila kubadilisha mfumo na sera ya nchi nzima, hatuwezi kufika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nikimwambia Mheshimiwa Waziri wa Fedha alete taarifa ya kodi wanazokusanya kuachana na arrears, kama mtu alikuwa ameuza gari nane au kumi, unamwambia bwana kuna gari 10 uliuza lipa hizo hela, sisi tunakutambua wewe kwa sababu hiyo gari ulinunua kwa jina lako na TIN number yako, unabebeshwa mzigo siyo wako. Sasa ile itafika mahali itakwisha, itafika mahali arrears zitakwisha utabaki na cash revenue ya siku hiyo, hapo ndipo utakapoona kutoka 1.5 trilioni inashuka inakuja mpaka kwenye bilioni 800 ambapo Rais Kikwete ameiacha hiyo. Rais Kikwete ameacha bilioni 850 nchi ilikuwa nzuri mambo yanaenda raha kwa kwenda mbele. (Makofi/Vigelegele)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Magufuli ana vision kubwa ya nchi hii anatamani nchi hii itoke tufanane kama Thailand walivyotoka. Hata hivyo, ninavyoona tatizo ni wasaidizi wake ama mnamwogopa au hamumwambii ukweli, mnaogopa kufukuzwa kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Magufuli tumefanya naye kazi hapa miaka kumi, mimi nimefanya naye kazi namfahamu, ukienda na data vizuri ukamwambia Mheshimiwa Magufuli kwa tatizo la bandari kuna mambo mawili, mimi nataka niongelee kukimbiwa na wafanyabiashara wa nchi jirani sitaki kuongelea mizigo ya ndani ya nchi, kuna vitu viwili pale…
Mheshimiwa Mwenyekiti, kukimbiwa na wafanyabiashara kutoka Zaire, jana Mheshimiwa Waziri wa Miundombinu anajibu kana kwamba yeye ni Waziri wa Zaire ndani ya Bunge la nchi hii. Anasema sisi tumeweka ofisi pale ili Wazaire wawe wanalipa ushuru pale kwa sababu wao wanakwepa ushuru inatuhusu nini mambo ya Zaire sisi humu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwawekea ofisi Wazaire walipe ushuru pale ndiyo iliyowakimbiza. Rais Kabila amekuja hapa kwa Magufuli kama alikuwa anataka Wazaire walipie ushuru hapa angeshindwa? Wangeweka sheria pale Bungeni kwamba mizigo yote isipotoka bandari ya Dar es Salaam haingii Zaire lakini yeye ndiyo amewa-encourage akasema nendeni Mombasa, nendeni kule Beira halafu hamuelewi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawaambia bandari yetu inakufa kwa sababu ya mambo manne, naongelea mizigo ya transit siongelei mizigo ya ndani naomba mnielewe hivyo, tunapoteza revenue billions of money. Sababu ya kwanza ni hiyo Single Custom Territory, toa hiyo! Ya pili ni VAT on transit goods. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiongelea kontena moja moja huwezi kuipata kuna meli kama Impala analeta meli tano mpaka sita, akishusha meli yake pale malori 10,000 yanapakia miezi mitatu yanakwenda lakini leo tunamweleza haelewi. Kenya hawana VAT wamesoma sheria zetu, Mozambique wamesoma sheria zetu wameona Watanzania hawa hawaelewi kitu wapo hivi, wao wakaondoa VAT, sisi siku saba tunawapa free wao wameweka siku 90, sijui Single Custom Territory wametoa, check point sisi tunazo sita wao wameweka mbili, tayari wao wamekuwa kwenye advantage.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunakosa mapato, hoja hapa tunakosa nini?
Billions of billions zinapotea. Bandari hii ingefanyiwa kazi vizuri ina uwezo wa kuingiza shilingi trilioni tano kwa mwaka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Singapore in and out containers milioni 30 kwa mwaka, Dubai milioni 27 sisi 500,000 aibu! Jiografia yetu imekaa vizuri tu, jamani bandari muifanye kama private sector, one of the objective of the business is to make profit, bandari ibadilishwe mfumo ikae pale kama private sector kwa ajili ya kuleta mapato kwa Serikali yetu. Sasa leo Mheshimiwa Waziri wa Fedha anaenda anawabana watu mpaka hawa wenye bodaboda anaenda anawabana anaacha mapato yale, mapato bandarini shilingi trilioni tano anaacha anaenda kubana bodaboda kwa Sh. 50,000 au Sh.100,000 ni nini hii? Waheshimiwa Wabunge tuna vikodi vidogo vidogo vingi sana na ni kero katika nchi hii sasa hivi. Leo hapa traffic wanakamata magari kama kuna vita, ukikamatwa Sh. 30,000, kundi la madereva ni hatari kwenye kura za CCM.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamba inaajiri zaidi ya watu milioni 16. Mimi natoka kwenye Mkoa wa Shinyanga, nimeongea nadhani nimeeleweka, Waziri wa Fedha asiponielewa safari hii itakula kwake baadaye. Sisi ni Wabunge wa CCM kule tutafanya maamuzi magumu tu, hatuwezi kuiacha nchi hii inayumba, nchi imeyumba tuseme ukweli. Kwa sababu tukianza kufichaficha hivi tunamficha nani? Sisi ndiyo tunajua 2020 tutashinda, hatuna tatizo lakini lazima sisi wenyewe turekebishe humu! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa pamba leo inaajiri watu milioni 16, mimi natoka kwenye Mkoa wa Shinyanga, tumeongea viwanda, Serikali itafute wawekezaji, sasa hivi Mheshimiwa Magufuli kwa nia njema tu ametaka haya mashirika yetu ya umma yaingie huko, sasa kama kuna mpango huo, niombe mashirika hayo yalete viwanda kwenye Mkoa wa Shinyanga, viwanda vya nguo vikubwa. China na India kiwanda kimoja cha nguo kinanunua pamba yote ya nchi hii, tunataka viwanda vya aina hiyo. Kiwanda kimoja kiweze kununua pamba yote ya nchi hii na kiweze kutengeneza uzi na nguo na ku-add value ili sasa kutengeneza soko la uhakika kwa wakulima wa pamba wa Mkoa wa Shinyanga.
Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi, kwanza kabisa naunga hoja bajeti hii kwa asilimia 100. Katika hoja ya mpango aliyoleta Mheshimiwa Waziri wa Fedha, tulimshauri mambo mengi, tulimshauri suala zima la bandari kachukua, kaweka mezani kafanyia kazi, tukamshauri masuala haya ya leseni za magari, kachukua, kaweka mezani na kafanyia kazi, tumemshauri mambo mengi sana kwa wakati ule na tuliongea kwa hisia na ndio maana nasema leo Mheshimiwa Waziri wa Fedha naomba nikupongeze sana umekuwa msikivu, umesikiliza ushauri wa Bunge na umelinyia kazi kwa maslahi mapana ya Taifa letu. Hongera sana nakuunga mkono kwa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna mawili machache madogo sana naomba nikudokeze, kuna wenzetu hawa wa bodaboda ambapo SUMATRA wamewaambia mpaka tarehe 30 wasipolipa 22,000 kutakuwa na operation moja kali sana na vijana hawa ndio wanaanza maisha katika Taifa letu hili, hebu lione hili katika kufata kodi hii, ili vijana hawa wa bodaboda waweze kufanya kazi kwa raha zao zote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile sekta utalii, nilikuwa na rafiki yangu mmoja yuko Ulaya pale London na Marekani wakasema inakuwaje watalii wengi wanakwenda Kenya, tatizo ni nini, ukitazama kwenye records za watu wanaosafiri kutoka nchi za Ulaya ni asilimia kubwa sana wanaokwenda Kenya, zaidi ya kuja kwetu Tanzania. Kwa research ndogo tuliyofanya inaonekana, bado tatizo la VAT on tourism sector linaathiri mapato makubwa. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri wa Fedha litizame hili, lichukue nina imani kabisa kwa hekima zako unaweza ukalifanyia kazi, ama kama sio mwaka huu, kwa mwaka wa fedha ujao, lichukue ondoa kabisa wenzetu wa Kenya wanatuingiza mkenge kila mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili tulikaa pamoja na Kenya, Wakenya wakaondoa wakasema sisi hatukujipanga, matokeo yake ni kwamba wametuacha sisi tumeweka VAT wao wameondoa VAT wameongeza watalii wengi sana katika nchi yao ya Kenya. Na hii Mheshimiwa Thailand inachukua asilimia 30 ya mapato yao katika utalii, naomba sana suala hili ni kubwa mno katika kuingizia mapato ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru sana Mheshimiwa Rais, huwezi kuongea bajeti hii kama huongei suala zima la makinikia. Makinikia ndiyo fedha na tunatarajia sana baada ya negotiation hii kwenye bajeti ya 2018/2019 tutakuwa na fedha nyingi sana itaweza kutekeleza mradi wa reli bila mkopo, anaweza akaongeza ndege, tunaweza tukaongeza miundombinu mikubwa ya nchi yetu tukaweza kufanana na nchi zote katika nchi za Afrika zilizopiga maendeleo. Kwa hiyo, nampongeza sana Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru tena kwa mara nyingine Mheshimiwa Rais katika Kijiji cha Nyaligongo, Kata ya Mwakitolyo aliweza kufuta leseni ya mwekezaji na kusema kwamba wachimbaji wadogo wa Kata ya Mwakitolyo wasiondolewe, wachimbe, wanufaike na raslimali zao, kwa bahati mbaya sana mwekezaji aliyefutiwa leseni yake akafutwa akabakizwa mmoja mwekezaji Mchina, Mchina huyu amepewa leseni zaidi ya miaka nane, hakuna alichokifanya, ni utapeli, anachukua leseni anakwenda nchi za nje anapata pesa, anachukua mkopo na kuuza hisa katika mabenki ya nje. Tarehe 08 mwezi uliopita, Ofisi ya Mkoa kwa bahati mbaya sana ni masikitiko makubwa sana, imekwenda Mwakitolyo kwenye Kitongoji cha Mahiga wamewafukuza wachimbaji wadogo wadogo kwa mtutu, kwa polisi kwa kuwatisha na risasi zililia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wamekimbia, wachimbaji wadogo wadogo wamekimbia, watoto watano wamepotea mpaka leo baada ya siku tatu, tathimini inafanywa kwa mtutu. Polisi anakwenda kwa familia anamuambia wewe kama haukubali hii, shauri yako itakula kwako, kwa mtu ambaye hajaja hajakuwepo ananyang’anywa hiyo haki.

Kwanza kabisa nimuombe Waziri wa Mambo ya Ndani kwa hekima na busara zote, polisi siwalaumu kwa sababu wale wanaamuliwa tu, siwalaumu sana Jeshi la Polisi ila namuomba Mheshimiwa Waziri aondoe Jeshi la Polisi kule kwa hekima zote, wananchi hawana raha Kata ya Mwakitolyo, wanakaa kama wakimbizi na nimuombe Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kama alivyowasaidia wanyonge hawa katika Kijiji cha Nyaligongo aendelee kuwasaidia kwenye Kitongoji cha Mahiga, ninaomba sana Mheshimiwa Rais afanye hivyo, namuomba sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, namuomba sana Mheshimiwa Makamu wa Rais na wote wenye maamuzi ya maeneo haya wawasaidie wachimbaji wadogo wadogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo la njaa linapotokea katika nchi hii au upungufu wa chakula Mkoa unaoathirika ni Mkoa wa Shinyanga, namba moja, kwa hiyo kwa bajeti ijayo ninaomba sana, Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwa sababu wewe ni Waziri wa Fedha na vilevile una mpango wa nchi nzima, suala zima la kukabiliana na tatizo la upungufu wa njaa ni kwenye irrigation scheme (kilimo cha umwagiliaji). Kwa mfano mimi nina kilimo cha umwagiliaji pale Nyida, nina kilimo cha umwagiliaji katika Kata ya Bukande ni kubwa zinaweza zikalisha Mkoa wa Shinyanga na mikoa mingine mitatu/minne mitano, kwahiyo ninaomba sana fedha ziweze kutengwa ili kukabiliana na hali ya njaa hii kwa miaka ijayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda, Mheshimiwa Magufuli anataka aitoe nchi hii yaani ingewezekana katika miaka mitano hii, tungeweza kufika mbali sana, lakini kwa bahati mbaya sana yako maeneo ni vikwazo katika speed ya Magufuli, Mheshimiwa Rais ana speed, kuna maeneo yanazuia. Kwa hiyo, nimuombe Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, chukua report ya REPOA, chukua report ya CTI wanafanya kazi nzuri, kutaneni na wawekezaji ili mpate matatizo yanayofanya uwekezaji katika suala zima la viwanda kwenda kwa mtindo wa kinyonga. Ukipata hii Mheshimiwa Waziri wa Fedha, utakuja na bajeti ijayo ambayo utaisaidia na tutarekebisha sheria, ili speed ya Magufuli kwenye suala zima la Tanzania viwanda iende vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tazama mfano wa Ghana, Ghana leo wame demolish VAT on everything on the industry on the manufacture industry wamefuta kila kitu, ukitizama hapa hapa juzi tu Rwanda hawa, wanasajiri kampuni leo masaa manne on line, masaa manne wanasajiri kampuni hawataki kukuona wanakujibu wanakupa registration card wanakupa TIN number, wanakupa VAT, wanakupa kila kitu kwa masaa manne, juzi tu hawa, leo wanatushinda kwa namna gani. Ndiyo maana nasema tufanye research, tupate ukweli mzima kabisa wa namna gani kuweze kwenda speed ya Magufuli kwenye suala zima la viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, TIB tuwaongezee fedha benki hii ili iendelee kutoa mikopo na mnaweza mkawa specifically kabisa Mheshimiwa Waziri wa Fedha unajua ukawa specifically kabisa kwamba tunatoa fedha hizi ziende kusaidia mikopo ya viwanda na utoa riba kutoka asilimia 18 mpaka asilimia nane kama mlivyofanya kwenye kilimo, tunakwenda, tunatoka tu. Kwa hiyo, ni suala la ku-negotiate ni suala la kubadilisha sheria na kuiweka vizuri ili watanzania waweze kunufaika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, majengo, katika Jimbo la Solwa nina majengo mengi sana, mimi na wananchi tumejenga na tumefikisha kwenye usawa wa renta, na suala hili nazani ni la Taifa, la nchi nzima, hakuna Mbunge anaweza akasimama hapa akasema mimi nimekamilisha majengo kwa asilimia 100 hayupo. Mimi nina zahanati zilizofika renta 45, nina Hospitali ya Wilaya moja ambayo imefika renta, nina maeneo mengi ambayo ninahitaji msaada wa Serikali Kuu, sasa kwenye bajeti ijayo, najua bajeti hii itakuwa ni ngumu lakini weka tu kwamba kuwepo na mwongozo kwa majengo yote yaliyo tayari kwenye majengo yote yaliyofika renta vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, hospitali za wilaya, vituo vya afya vyote viwe observed kwenye bajeti ya mwaka ni ili tuweze kumaliza tatizo kwa sababu hayo ndiyo maendeleo ya wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukijenga vyumba vya madarasa, tukajenga nyumba za walimu zilizokuwa zimefika renta, tutakamilisha angalau kupunguza kwa asilimia 50 tutakuwa tumefika.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Viwanda Na Bishara
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii kuchangia leo katika Wizara hii ya Viwanda na Biashara, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri mwenyewe kwa hotuba nzuri sana yenye malengo mazuri ya kuboresha vivutio vya uwekezaji katika Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka tu nimwambie Mheshimiwa Waziri mwaka 2017 aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara wakati huo Mheshimiwa Mwijage kuna kitu walikianzisha kinachoitwa blueprint. Chimbuko la blueprint lilitokana na muwakilishi wa World Bank baada ya kuwa ameongea na aliyekuwa Waziri Mwijage akamwambia bado ninyi Tanzania hamko vizuri kwenye vivutio vya uwekezaji na namna ya kuwekeza ndani ya Jamhuri ya Muungano, walibishana sana. Maana yake ni kwamba Mheshimiwa Waziri wakati ule alienda kufanya utafiti wa kina na kujua kweli Tanzania ni nini kinachofanya wawekezaji wasiweze kuja vizuri kuwekeza ndani ya nchi pamoja na wawekezaji wa ndani ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimefanya utafiti mdogo nikaiona Tanzania katika easy of doing business in Tanzania report ya World Bank Group ya mwaka 2020 Tanzania ni ya 141 nchi ya kwanza kabisa ni New Zealand, nchi ya pili ni Singapore, nchi ya tatu ni Hong Kong kwa maana ya kwamba vivutio vizuri na namna ya uwekezaji mzuri ndani ya nchi hizo ni nchi za kwanza ambazo zinaongoza tatu bora duniani. Lakini Rwanda ni ya 38; angalia Rwanda wako 38 sisi tuko 141. Lakini ukiingia Kenya wenyewe wako wa 56 naongelea hii ripoti ambayo iko ndani ya World Bank Group, Uganda wenyewe ni 116, Zambia 85, Malawi 109 na nchi ya mwisho kabisa duniani ni Somalia ya 190.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake nini? Maana yake ni kwamba tafrisi yake hii ni kwamba Mheshimiwa Waziri unaweza ukawa una mipango mizuri sana, lakini blueprint ambayo iliandaliwa kama hutoifanyia kazi kwa maana kuondoa vikwazo ambavyo vinafanya uwekezaji visiwekeze vizuri, waone ni shida katika kuwekeza katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utaongea sera nyingi sana, mambo mengi sana, huwezi kufanikisha. Ondoa vikwazo chukua hii blueprint lete hapa tupitishe futa kero zote zinazosumbua uwekezaji na moja katika sababu inayofanya Serikali isilete blueprint ndani ya Bunge hili wanaona kwamba TBS watawazuia mapato yao, wanaona NEMC tukitoa hii tutawapunguzia mapato yao, wanaona sijui mamlaka gani tutawapunguzia. Mamlaka iliyochini ya sheria ya kukusanya kodi ni TRA peke yake na siyo hizi zingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TBS kazi yake ni kufanya mazingira mazuri mwekezaji aendelee kuwekeza vizuri na aone nchi hii ni bora, NEMC ni mamlaka ya kumsaidia mwekezaji aone kwamba nchi hii ni nzuri, lakini hawa nao wamekuwa na regulate badala ya kurahisisha uwekezaji wao ndiyo wamekuwa wa kwanza kufanya uwekeaji uwe mgumu ndani ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri utakapokuja kuhitimisha hapa nataka hili la blueprint utueleze vizuri tu utalileta lini ili tulifanyie kazi nchi yetu itoke kuwa wa 141 ipande sasa tuwazidi hata Rwanda tuwe katika top 20 na wanajua wawekezaji nje ya nchi kule wanatazama Tanzania iko rank ya ngapi, shida ni nini, wanatizama, ni kama vile ndege iko juu ya anga, anatizama sehemu bora ya kwenda kuwekeza ni wapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwekezaji kuna ushindani mkubwa leo, Zambia wanataka wawekezaji, Ghana wanataka wawekezaji, Ghana ni nchi ya 116, Kenya wanataka wawekezaji, Tanzania tunataka wawekezaji, Rwanda wanataka wawekezaji, Uganda wanataka wawekezaji, wote wanavuta kila mmoja anatengeneza mazingira mazuri ya mwekezaji kwenda kuwekeza pale. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri hilo namba moja nataka tu utueleze kuhusu blueprint haya yote haya kama hutorekebisha print mipango yote Mheshimiwa Waziri sidhani kama utafanikisha kwasababu vitakwaza na hii blueprint ambayo sisi tumeishauri vizuri Serikali kwenda kuifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vya kimkakati kanda ya ziwa tuna pamba inayoajiri watu milioni 21; ukija hapa Dodoma inajulikana kwa zabibu, ukienda Singida na Dodoma pia inajulikana kwa mafuta pamoja na Kigoma. Sasa tusipokuwa na mikakati kama Mheshimiwa Nyongo alivyosema, tusipokuwa na mikakati ya makusudi kabisa kwani shida iko wapi Serikali ikiingilia chini ya Shirika letu na NDC wakatoa bilioni 50; tukafanya business plan tukaona tukiwekeza kiwanda kikubwa ndani ya Mkoa wa Shinyanga, ndani ya Mkoa wa Mwanza ambayo itakwenda kununua pamba yote ya wakulima hapa tukawekeza zaidi ya bilioni 100, 150 baada ya hapo mkatangaza kuuza kama mpango walivyokuwa wakifanya National Housing walikuwa wakichora michoro, wanaweka pale, wanatangaza, wenye fedha walikuwa wakileta fedha zao wanajengewa wanapewa nyumba. Kwa hiyo NDC wanaweza Mheshimiwa Waziri unaweza ukachukua mpango huu wa Serikali kujenga viwanda vikubwa vitano vya kimkakati ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baada ya hapo unaiuza tu kwa mwekezaji yeyote kwamba sisi tumejenga hii, faida yake hivi, tumemaliza lete bilioni 150 unauza NDC inaendelea kujenga kiwanda kingine Kigoma cha mafuta. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo tunakwenda kuwasaidia wakulima ambao wanapata matatizo ya masoko ya kilimo chao kwa mfano Kigoma hawana masoko mazuri ya mawese, ukija Shinyanga hatuna masoko mazuri ya pamba; na ni kweli kabisa pamba ni zao la kisiasa ndani ya mikoa tunayolima sisi pamba. (Makofi)

Mimi katika Jimbo la Solwa mpaka wakulima bahati nzuri mimi katika Jimbo la Solwa wakulima wengi wanalima dengu wamechukua zao mbadala la biashara katika Jimbo la Solwa wameona hii pamba hii ni shida wameachana nayo, tumewaachia Mkoa wa Simiyu wao wameendelea na pamba sisi tumeendelea, lakini kwa sababu kubwa hatuna masoko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija Urafiki kiwanda cha Urafiki ilikuwa ni joint venture baina ya Serikali na Serikali ya China leo mashine pale zote zimeuzwa. Mimi nilikuwa kwenye kamati ya viwanda na biashara tumeenda pale wamesema wameuza kama scrapper, mimi sidhani kama imeuzwa scrapper; zile mashine ziliuzwa kabisa kwa makusudi kukibomoa kile kiwanda na sasa hivi wanataka kufanya complex ya soko la bidhaa zilizozalishwa China kuja kuuzwa finished product ndani ya nchi yetu ni hatari na siyo nzuri kwa maslahi ya Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushauri Mheshimiwa Waziri umshauri Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu fanya mazungumzo na Serikali ya Kenya; Wachina hawa ambao wako Joint Venture katika kiwanda hiki cha Urafiki waondoke watuachie sisi ili tuone namna bora ya kiwanda hiki tuwekeze kwa namna gani, tuendeleze hiki kiwanda cha pamba, tuendeleze kama kwenye mikakati yako uliyojiwekea hapa, kwamba tuwe na kiwanda ambacho kinaweza kikaunganisha magari au vifaa vya kilimo kupitia JKT na kadhalika. Hayo yatakuja baada ya kwamba China imekubali kutuachia sisi kumiliki Kiwanda cha Urafiki kwa asilimia 100; lakini ukienda pale roho inakuuma sana na mimi siamini kama zile mashine ziliuzwa kama scrapper.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiunda task force utakuta zile mashine ziliuzwa tu nchi fulani hivi wameamua kukivuruga vuruga Kiwanda cha Urafiki kwa maslahi kwamba tutengeneze ajira China sasa badala ya sisi nchi ambayo tunajikongoja kwenye uchumi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, TIC wanafanya vizuri, lakini hawana maamuzi palepale yaani wanakwenda wanakupokea vizuri mno, wanafanyakazi nzuri mno, lakini unapopeleka maombi yako ya usajili wa certificate au kupata approved au msamaha wa bidhaa kwa ajili ya uwekezaji wa kiwanda mpaka tena iende tena Makao Makuu, ikubaliwe, wakae kikao kiendelee, siku zinaenda tu uone tu namna bora kwamba TIC iwe mamlaka kamili. Sasa hivi imepelekwa chini ya Waziri Mkuu, iwe mamlaka kamili kabisa pale unapo-log document zako, wawe na mamlaka ya kisheria ya kufanya maamuzi hapo hapo bila kuchelewa ili tuondoke kwenye hii rank ya 141 tuende sasa kwenye top 20 katika uwekezaji duniani. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa muda wako umemalizika tunaendelea na…

MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru naunga hoja mkono ahsante.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii adhimu kuchangia kwenye hoja ya bajeti yetu hii nzuri bajeti ya kwanza ya Mheshimiwa Rais wetu mama yetu Samia Suluhu na bajeti ya kwanza kwa Waziri wetu Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Waziri wa Fedha. Naomba tu niwasalimie Waheshimiwa Wabunge kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Kazi iendelee!

MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri bajeti hii inakwenda kumaliza matatizo mengi sana na hasa hasa kwenye maeneo yetu ya vijijini na hasa hasa kwa wananchi na wakulima wanaoishi maeneo ya mbali na miji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni awamu yangu hii ya tatu nakwenda ya nne nimekuwa nikisema mara nyingi sana tupate fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma bajeti hii inakwenda kukamilisha maboma. Katika Jimbo la Solwa lina mabomba zaidi ya 150 ukichukua katika zahanati nina maboma 39 sasa hivi ukienda kwenye elimu ya msingi nina maboma zaidi ya 53, ukienda kwenye Sekondari nina maboma zaidi ya 60.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naishukuru sana Serikali ya Samia kwamba kweli kabisa tunakwenda kutatua matatizo haya ya maboma yetu. Lakini vilevile inakwenda kumaliza kabisa matatizo ya barabara zetu, nina barabara zenye urefu wa kilometa 743 TARURA lakini hakuna barabara hata moja ambayo ilikuwa inanisumbua kama barabara ya kutoka Didia kuja Solwa. Fedha hizi tulizopata Mheshimiwa Dkt. Mwigulu pamoja na Mheshimiwa Rais wetu nikushukuru sana tunakwenda kumaliza matatizo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na barabara ilikuwa ni muhimu kweli kwenye kata zaidi ya sita zenye kulima mpunga zinalima mazao mengi sana mpaka watu wa Burundi na Rwanda wanakuja kununua mazao katika Jimbo la Solwa. Kwa hiyo, kwa kweli hapa sasa hivi wakulima pamoja na wafugaji wa Jimbo la Solwa wamekusikia na wamefurahi sana kwa Serikali yao hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie tu Mheshimiwa Waziri wa Fedha tarehe 25 Februari, tulisaini mkataba wa maji Tinde pale kwa agizo la Hayati aliyekuwa Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli mradi huu ulisainiwa Tinde kwa maana mradi mzima unaitwa Tinde package ni mradi wa maji wa vijiji zaidi ya 15 Jimbo la Solwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tangu tumesaini mradi huu mpaka sasa hivi mkandarasi ameshindwa kuendelea kwa sababu ya suala zima ya VAT kwa maana ya GN. Nikuombe Mheshimiwa Waziri wa Fedha lishughulikie hili haraka ili mkandarasi aanze kazi aanze kazi mara moja, na mimi nimelisema hivi ili wananchi kwanza wa Jimbo la Solwa wasikie wakusikie wewe waisikie na Serikali yao kwamba tatizo hili sasa limekwisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda nikushukuru Mheshimiwa Waziri umeigusia sana blue print umeigusia sana sana na nikushukuru sana tu umeondoa ile asilimia 15 kwa suala zima la sukari nakadhalika tunakwenda vizuri sasa lakini kuna VAT refund on export hii bado inazuia export ya bidhaa zetu zinazozalishwa ndani ya nchi yetu matokeo yake nini? Biashara yoyote bidhaa yoyote inayozalishwa ndani ya nchi yetu hii unapokwenda kuuza nchi Jirani au nchi za SADC lazima ulipe VAT unapokwenda kwenda kuomba VAT hii na bidhaa tayari imeshatoka bidhaa ikishatoka unatakiwa urudishiwe ile ili uendelee kuzalisha na kwenda kuuza bidhaa nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hii sisi ni tatizo kubwa wafanyabiashara wengi wamekuwa hawafanyi hawa export na hii tatizo kubwa sana inadumaza export leo ninavyokwambia Mheshimiwa Waziri wa Fedha wafanyabiashara wanaokwenda Rwanda kuwekeza waki- target soko la Zaire. Leo wafanyabiashara wengi wanakwenda kuwekeza Uganda waki-target soko la Tanzania na nchi za Zambia kwa sababu hizo nchi ni nchi nzuri sana na ziko mstari wa mbele ku-refund VAT on export product kutokana na manufacturing. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri hili lichukue lifanyie kazi linadumaza export na ukishadumaza export maana yake unadumaza foreign currencies ndani ya nchi yetu utaona kuna tatizo kubwa sana kwenye suala hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitizama Djibouti leo wana free zone kubwa sana inaweza ikawa the second largest au third largest in Africa baada ya Afrika Kusini wamejenga bandari kubwa wamejenga eneo kubwa kweli kwa ajili ya wawekezaji wa viwanda wanaokwenda kuwekeza pale wanataka sasa kuwa katika Afrika wao wawe kama vile Hong Kong kama vile Dubai wanataka kuifanya Djibouti iwe hivyo na Serikali ya China imeisaidia 3.5 bilioni katika mradi mzima ule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tuwe makini na hapa nikushauri Mheshimiwa Waziri atenge fedha kwa ajili ya research development katika Wizara yake. Tenga fedha kwa ajili ya research and development tusiende kichwa kichwa lazima tuwajue wenzetu na nchi Jirani wa Kenya wanafanya nini, Waganda wanafanya nini, Rwanda wanafanya nini Burundi wanafanya nini, Zambia hawa nchi zote zinazotuzunguka ni wapinzani wetu na usifikiri wanafurahia maendeleo yetu kwa namna moja au nyingine wanatizama sera, wanatizama sheria zetu, wanaziweka mezani wanazifanyia kazi ili wawe advantage Zaidi ya sisi Tanzania ndiyo wanavyofanya tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Kenya hapa wanajenga bandari hapa Lamu bandari kubwa sana ambayo tayari inakuwa competitor ya bandari yetu ya Dar es Salaam na Tanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo nilitaka tu Mheshimiwa Waziri wa Fedha lichukue na ikiwezekana tufanye kama wenzetu Ethiopia wamekuwa na maeneo maalum kabisa yaani na wanavyotenga maeneo kwa ajili ya viwanda wawekezaji wa nje na wa ndani ya nchi kwa mfano wanakuwa na strategic zao tunataka kwenda kumaliza matatizo ya masoko ya pamba katika Mkoa wa Shinyanga na Simiyu tunataka kwenda kumaliza masoko kwa mfano ya mazao ya mawese Singida sijui, Singida hapo tunataka kwenda wanakuwa na strategic wanatenga maeneo, wanajenga maeneo wanaweka barabara wanaweka lami, wanaweka umeme wanandaa hili kwa ajili ya viwanda kwa wawekezaji wa viwanda tu atoke nje akija anataka kuwekeza mafuta anaambiwa bwana mafuta ya kula nenda Singida, nenda Kigoma kiwanja hiki hapa na hati hii hapa biashara imeisha nenda kawekeze ndiyo wanavyofanya wenzetu ukienda Thailand hivyo hivyo, ukienda Ethiopia hivyo hivyo yaani hupati shida kabisa kwenye uwekezaji wa nchi kama hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri wa Fedha ukishakuwa na East Africa Development haya yote yataangukia kwako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine Mheshimiwa Waziri wa Fedha hii blue print ipige overall yote mnaigusa gusa hivi sawa kabisa mimi nakushukuru kwa namna ambavyo hata haya uliyoyachukua umeyafanyiakazi. Lakini ichukue ipige overall yote kabisa tuimalize ili sasa Tanzania iwe katika nafasi nzuri ya uwekezaji Tanzania tuweze kuwavutia wawekezaji wote wa ndani na nje ya nchi. Tanzania tuna jiografia nzuri bandari yetu iko katikati karibu na nchi zote za SADC Tanzania kuna amani tuna advantage nyingi mno ya watu kuja kuwekeza hapa Tanzania tuna resources nyingi tuna mali nyingi ambayo wawekezaji wanaweza wakaja kuwekeza katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hapa Shinyanga Simiyu peke yake inazalisha asilimia 60 ya pamba inayozalishwa Tanzania hii na mnajua pamba inaajiri watu Zaidi ya milioni 21 lakini hakuna kiwanda kikubwa cha nguo Tanzania hii haipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwanda kimoja tu India kinanunua pamba yote ya Tanzania hii, hivi tunashindwaje kuwa na Strategic Plan, TPDC, NDC tukamwambia sikiliza chukua hii bilioni 100 jenga kiwanda kikubwa cha pamba hapa, chukua hii bilioni 100 jenga kiwanda cha mafuta hapa, ukishajenga tangaza, uza watakuja wawekezaji, yaani ukishajenga kiwanda ikakaa vizuri Menejimenti kila kitu tangaza uza, chukua fedha jenga kiwanda kingine, tunakuwa na strategic tu, viwanda vikubwa 10 ndani ya nchi hii, nchi inainuka inakwenda vizuri sana katika maendeleo yetu. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Ahmed ni kengele ya pili.

MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru naunga mkono hoja. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Mimi pia niungane na wenzangu kumshukuru sana Mheshimiwa Mama yetu Mpendwa Samia Hassan Suluhu, kwa hizi fedha ambazo kwa kweli zimekuja kukomboa majengo yetu katika Majimbo yetu. Mimi binafsi nilikuwa na majengo zaidi ya 150 kati ya miaka sita au miaka saba ilifika mahali sijui nifanye nini. Lakini sasa hivi kwa kweli naishukuru sana Serikali chini ya Mheshimiwa Mama Samia, tunakwenda kumaliza matatizo haya ya maboma yetu vizuri na watoto watakwenda kusoma vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemsikia sana Mheshimiwa Kigwangalla na Mheshimiwa Abbas Tarimba, suala zima hapa ukitazama kwa upana wake matatizo yote haya ili kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji katika mpango huu, ninashauri sana blue print ifanyiwe kazi. Blue print leo inaongelewa zaidi ya miaka mitatu, mambo yote ambayo yapo kwenye blue print yakifanyiwa kazi, wawekezaji siyo tu wa nje hata wa ndani watapitia humo humo na wataweza kuwekeza vizuri na kuweza kurudi kwenye ile hali ambayo wanaitaka wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ameongelea hapa Mheshimiwa Kigwangalla katika suala hili la Covid-19 limeathiri sana uwekezaji, biashara na kadhalika. Ukija kwenye hii blue print ni mambo mengi mno ambayo ukiipiga overall, kwa ujumla wake na nikuombe sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha itizame hii. Leo watu wanatoa viwanda vyao hapa wanapelekea Uganda kuna watu wanapeleka Uganda ili azalishe a-export bidhaa tena Tanzania au Congo! Yote hiyo moja katika sababu kubwa sana bado sisi hatupo vizuri sana ku-refund VAT on export product. Tunauza bidhaa nje lakini ku-refund zile VAT tunachelewa mno kuliko Uganda na Rwanda wanavyofanya. Leo Uganda na Rwanda wanafanya vizuri sana kwenye suala hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Rwanda wanapata wawekezaji wengi siyo kwa sababu ya population waliyokuwa nayo Rwanda. Rwanda wana population ndogo mno lakini uwekezaji unaofanyika katika nchi ya Rwanda wana-target nchi kama ya Congo, wana-target nchi za jirani na hata juzi kuna malori yamekwenda kupakia hivi vifaa tiba tu Rwanda wanakuja kuleta Tanzania, hivi ni kweli? Yote haya ni kwa sababu ya blue print hatuifanyii kazi haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni jambo la muhimu sana siyo la kufanyia mzaha tu hivi. Pitia hii Mheshimiwa Waziri wa Fedha wewe mwenyewe na Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri Mkuu uko hapa, angalieni namna ya kufanya yale ambayo hayana madhara kwenye nchi, toeni watu waje wafanye kazi wawekeze mambo yaende na nchi iweze kwenda mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kuhusu uwekezaji kwenye viwanda. Ni jambo jema sana kupata wawekezaji kutoka ndani ya nchi ni zuri tu. Lakini ni hatari sana kama hatutakuwa na mpango maalum wa kuwawezesha watanzania wakaingia moja kwa moja kwenye uwekezaji hasa wazalishaji wa viwanda. Itaweza kufika mahali huko mbele ya safari mkawa na wawekezaji wageni zaidi ya asilimia 80, halafu Watanzania wakawa kama wasindikizaji asilimia 10 au asilimia 15 tu, by then huko wakija kuungana tu wanaweza wakaiyumbisha Serikali itakayokuwepo huko mbele ya safari. Kwa hiyo, ni jambo la muhimu sasa sana tena, Serikali ione namna ya kufanya kuwawezesha watanzania waliopo katika biashara na watakaotaka kufanya kazi hiyo ni namna bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitazama Benki ya Afrika ya Kusini (South African Bank) mtu anakwenda na proposal yake, proposal yake kama ni nzuri wameipenda na haikukamilika, wanaibeba ile proposal wanaifanyia kazi wanakuchukua wewe mwenyewe kuna wataalam pale mpaka wanahakikisha ile proposal imekaa vizuri na fedha wanakupa na kazi inafanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hii tusipofanya hivyo, hivi ukitenga hizi Shilingi Bilioni 500 ukapeleka kwenye hizi Developments Bank kama TIB ukasema sasa Watanzania waende pale, mkapunguza riba hata asilimia 10. Fedha kama ni za Serikali wana haja gani wao Benki kutoza asilimia 18 wakati fedha ni za Serikali. Malengo makubwa ni kuwawezesha Watanzania wawe na viwanda wengi waingie kwenye ushindani huo huo ambao wawekezaji wa nje wanatoka kuja kuwekeza ndani ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mambo mangapi tunayahitaji na unaweza ukaweka strategy tu kwamba, tunatoa hizi fedha katika Benki zetu za Maendeleo lakini tunataka wawekezaji wa aina hii. Wawekezaji wa viwanda vya pamba, wawekezaji wa mafuta, uwekezaji ambao una manufaa kwa nchi na kwenda kujibu masuala majibu ya masoko ya kilimo ambayo wakulima wanazalisha. Kwa mfano, katika Kanda ya Ziwa zao la pamba linaajiri zaidi watu milioni 20 lakini kuna kiwanda gani Shinyanga? Hakuna viwanda vya pamba Shinyanga, hakuna kiwanda cha pamba labda Mwanza. Kuna kiwanda cha Urafiki hapa kimekufa tu, kiwanda cha Urafiki kwa historia yake ni ushirika baina ya Tanzania na China, lakini tunashindwaje kwenda kuongea na Serikali ya China kuwaomba tu bwana hiki kiwanda, naomba mkiache tupeni sisi kirudi kwenye mkono wa Serikali mkitangaze ili watu waje wawekeze.

Mheshimiwa Spika, leo pale kiwanda cha Urafiki imekuwa magofu, yule Mchina anakodisha kodisha tu maduka yale imekuwa ukiingia pale mpaka roho inakuuma, kiwanda kiko vizuri mno yaani pale lakini kimekaa tu. Hatuoni strategy, hatuoni Serikali kufanya intervention kuongea na Serikali ya China watuachie ili tuitangaze aje mwekezaji mkubwa pale na ikiwezekana aje Mtanzania afanye kazi pale. Kwa hiyo ni suala tu… (Makofi)

MWENYEKITI: Pokea taarifa Mheshimiwa Ahmed Salum.

T A A R I F A

MHE. DKT. HAMISI A. KIGWANGALLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpa taarifa kwanza tu kuweka sawa maneno nafikiri alipokuwa anasema viwanda vya pamba Shinyanga, Mwanza kwamba havipo, vipo. Hata mimi mwenyewe tu nimpe taarifa ni Mwekezaji kwenye sekta ya pamba na nina kiwanda cha pamba kipo Mwanza. Tatizo tulilonalo siyo kukosekana kwa viwanda vya pamba, tatizo tulilonalo ni kwenye kilimo. Kulizuka mjadala mzito sana hapa jana kuhusu kilimo ni kweli shida tuliyonayo hatuna uwekezaji wa kutosha kwenye kilimo kwa sababu, viwanda vya pamba vyote vilivyopo hapa nchini vinagombania raw material, vinagombania pamba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo kwamba kuna shida ya pamba na kuhusu kiwanda anachokizungumzia cha textile, changamoto kubwa hapa kwenye nchi yetu ukitaka kufilisika wekeza kwenye kiwanda. Changamoto kubwa umeme, kodi, utitiri wa tozo na involvement ya Serikali kwenye kila hatua ya uwekezaji wako. Ndiyo maana hakuna mtu atawekeza kwenye kiwanda ambacho ni capital intensive kama cha textile hapa nchini na akafaidika. Kila atakayejaribu atafeli kwa sababu, riba za benki ni kubwa na mahali pa kuuza finished goods za kutoka kwenye kiwanda chake ni padogo. (Makofi)

MWENYEKITI: Kwa kuwa unajua hilo kwa nini Mheshimiwa Kigwangalla wewe umewekeza? Mheshimiwa Ahmed Salum unapokea taarifa hiyo? (Kicheko)

MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipokea. Mheshimiwa Kigwangalla namheshimu sana lakini tukisema viwanda vya pamba ni viwanda vya pamba. Kiwanda cha pamba kimoja cha India kinanunua pamba yote ya Tanzania. Viwanda tulivyokuwa navyo hapa Mheshimiwa Kigwangalla ni vya nyuzi tu na ginnery. Kiwanda kama kiwanda ina maana kuna kiwanda ginnery inaunganishwa nyuzi, inakuja inazalisha nguo, hicho ndicho kiwanda. Magari 500 kwa mpigo zikishusha zinaingia pale mashine zinachukua zile pamba zinachakata. Kiwanda kimoja ukitembelea India au China kimoja kinanunua pamba yote ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunataka viwanda vya aina hiyo ambayo vinakwenda kujibu masoko ya wakulima wa pamba, vinakwenda kujibu masoko ya walimaji labda korosho na kadhalika na kadhalika. Yaani unaweka viwanda 10 vya kimkakati ndani ya nchi hii, 10 tu vinatosha kubwa kiwanda kimoja labda Dola Milioni 50, hivyo ndiyo unaongelea viwanda, ambavyo vinakwenda kujibu masuala mazima na maslahi ya wakulima wetu watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye kilimo kuhusu Irrigation (skimu ya umwagiliaji) hapa wewe mwenyewe umesema na watu wote wanajua baada ya muda siyo mrefu, au tuseme sijui mwaka huu sijui mwakani watu wa hali ya hewa wanasema kutakuwa kuna shida kubwa sana ya hali ya hewa. Njaa inaweza ikatokea jua kali sana hakuna, lakini majibu makubwa hapa ni kwenye skimu ya umwagiliaji tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi katika Jimbo la Msolwa kwa mfano na hii uchukue kama mpango Mheshimiwa Waziri wa Fedha na wenzako, tukijikita sana kwenye kilimo cha umwagiliaji, mimi nina skimu za umwagiliaji saba lakini nimshukuru hata Mheshimiwa Naibu Waziri na Wizara yote ya Kilimo. Wamepita pale kwenye skimu moja ya umwagiliaji pale Nyida wamechukua na ninaamini kabisa katika mpango huu na fedha wa mwaka huu, Mheshimiwa Bashe alikuja Naibu Waziri namshukuru sana amejitahidi.

Mheshimiwa Mwenyikiti, imagine tukiwa na mpango mzima wa skimu ya umwagiliaji ndani ya Jimbo la Solwa na maeneo yote yenye advantage kubwa ya kilimo, maana yake nini, tunaweza tukalima hata kwenye wakati ambapo msimu siyo mzuri jua kali wewe pale skimu ya umwagiliaji ipo, bwawa lipo, mnafungulia watu wanalima. Angalau tunaweza tukawa na wakulima wanaweza wakalima kwa wakati wowote ule bila kujali kuna jua ama mvua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuende kwenye wakati huo na kwenye eneo hili la skimu ya umwagiliaji ndiyo tunakwenda kuwasaidia Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru naunga hoja mkono. Ahsante sana. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia. Kwanza kabisa, naunga hoja mkono.
Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijaanza kuongea kuhusu suala zima la bajeti hii na hoja hii ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha, nilikuwa nataka kusema kwamba katika Kata yangu ya Makitorio, kuna tatizo kubwa sana la wachimbaji wadogo wadogo ambao sasa imefikia wakati vurugu inataka kutokea.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mwekezaji anaitwa Barricks ambaye naye katika utafiti wake kafika mahala naye akaliuza, yaani kapewa eneo akaona halifai naye akaenda akaliuza. Sasa katika kuliuza kuna mwekezaji mmoja amenunua, imeleta mkanganyiko mkubwa sana kwenye kata ile, tunashindwa kuendeleza, tunashindwa kufanya kazi. Kwa hiyo, naomba Serikali isimamie na hasa Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Profesa Muhongo, nafikiri nitakuja ofisini kwako ili tuone namna ya kutatua tatizo hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Hospitali ya Wilaya, Rais aliyemaliza muda wake aliahidi mara mbili; kaja Waziri Mkuu, Mheshimiwa Pinda aliyemaliza muda wake, akaahidi; akaja Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, ameahidi. Sasa mimi sina majibu katika suala hili na katika bajeti hii sikupangiwa fedha.
Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri hili ulichukue, sisi tuliomba shilingi bilioni tatu, angalau tupate shilingi bilioni moja na nusu, twende, kwa sababu ina miaka sita. Sisi kama Halmashauri kwa miaka sita tumejenga Hospitali ya Wilaya tumeshindwa kumaliza na sina namna nyingine yoyote. Naomba Mheshimiwa Waziri alisimamie suala hili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kuna maji ya World Bank; nimeuliza swali langu hapa asubuhi. Huu ni mwaka wa pili, mradi umefikia nusu. Mwaka wa pili hatujapata fedha za kuwalipa wakandarasi kumaliza kazi zao na hakuna maji; miradi kumi, tunasubiri zaidi ya two billion na mpaka leo mkienda kule maswali ni mengi; ufinyu wa bajeti. Majibu hayo ya ufinyu wa bajeti kwa kweli inafika mahali yanakuwa hayaridhishi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu ina fedha nyingi. Katika mambo ambayo kama kweli tunataka tujikite vizuri kwenye suala zima la viwanda, sijaona bajeti ya research and development. Hakuna nchi duniani inaweza ikaendelea bila kuwa na bajeti ya research and development. Hapa tunafanya kazi kwa matukio tu, kikitokea kitu hivi, basi au itokee makampuni fulani yameweza kuomba halafu Wizara ya Viwanda na Biashara ithibitishe iite vikao, task force mpaka ije Wizara ya Fedha, ndiyo mwone. Hayo ni mambo tu ya matukio.
Mheshimiwa naibu Spika, sasa mkiweka bajeti ya research and development ikafanya kazi kwa maana ya kwamba tukatambua mfano, eneo lote hili la viwanda, ni vitu gani ambavyo vinatufanya Watanzania tuweze kuendelea haraka? Ukishayatambua yale yakakaa juu ya meza, ni mara moja mno kutatua, kama kubadilisha sheria, sera na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, vikwazo ni vingi katika uwekezaji ndani ya Tanzania hii. Nchi yetu ina amani, hakuna kitu kikubwa duniani kama amani, ndiyo advantage kubwa; na wawekezaji wa nje hawa wanaokuja hapa, kitu kikubwa kabisa wanachokifuata hapa ni amani na masoko, lakini ukiingia ndani ya uwekezaji, vikwazo ni vingi sana. Ukitaka raha ya ngoma ingia ucheze tu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vikwazo ni vingi sana. Nilichangia wakati ule katika Wizara ya Viwanda na Biashara, nikatoa mifano miwili, mitatu, midogo sana. Ukitaka kuuza cement kupeleka Uganda ili upate kibali unalipia 2% ya thamani ya mzigo ule. Wakati Uganda na Kenya hulipii, wao wanaleta tu kama wanataka kuleta. Sasa utaona kwamba vikwazo ni vingi katika kupata leseni, ardhi maeneo na maeneo. TIC pale, EPZ, NEMC, TBS kila mmoja ana mawazo yake na kila mmoja na maamuzi yake. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru tu Mheshimiwa Mpango sasa hivi umekuja kidogo na suala zima la material, umeongea vizuri kuna maeneo pale umeweka mambo yamekaa vizuri. Ila naomba tu na Waheshimiwa Wabunge wote tukubaliane, angalau 1% ya bajeti hii itoke iende kwenye research and development ili sasa Serikali iweze kuona kabisa maeneo gani wayafanyie kazi. Nakuhakikishia ukishayagundua matatizo, mwaka 2017/2018, 2018/2019 nchi ita-take off vizuri sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, nisemee bandari yetu ya Tanzania. Bandari ya Tanzania inapigwa vita bila sisi kujua kama inapigwa vita.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kenya tulikubaliana kwamba waweke Ofisi ya Umoja wa Forodha kwamba mizigo yote ya kutoka Zaire; kontena zote zinazotoka Zaire walipie Kenya na Tanzania tukakubaliana hivyo. Tanzania tukawahi kufanya ofisi hiyo, tukaweka hapa, Wazaire sasa, badala ya kuja kutoa mizigo yao hapa, wameondoka wamekwenda Kenya, wamekwenda na Beira. Wakenya wamefanya utafiti wakaona kwamba tukiweka ofisi hapa ili Wazaire walipie ushuru ndani ya Mombasa hawatopata mzigo hata mmoja. Ndiyo sababu kubwa ya bandari yetu kupungukiwa na mizigo ya transit.
Mheshimiwa Naibu Spika, Umoja wa Forodha Wazaire wamekimbia, sababu nyingine ilikuwa ni suala zima la VAT; mmeweka VAT katika transit goods. Kuna kampuni kubwa sana kama hii Impala, wakileta mzigo, meli zake moja mwezi mzima ma-transporter wanabeba mizigo hiyo ya mbolea kwenda nchi jirani, wameondoka, wanashusha Beira, wanashusha Mombasa. Tume-lose a lot of money. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sababu nyingine ni restriction. Namshukuru Mheshimiwa Dkt. Pombe Magufuli, kulikuwa kuna Beira, kulikuwa na hizi za check points; ukitoka bandarini mpaka border ni check points sita; ameondoa zimebaki tatu, mimi namshauri aweke hata mbili tu. Wakenya wameweka mbili, sasa wenzetu Wakenya wanatufuatilia sisi kuona namna gani tumeweka sheria ili wao waondoe zile sheria.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikupe mfano mdogo, mmekuja hapa na sheria ya kuweka VAT katika masuala ya tourism, mmekubaliana. Wao wameondoa, hili suala la kuweka ofisi kwa ajili ya kulipia ushuru wa Wanazaire, tulikubaliana, wao hawakufanya! Ukitazama Malawi wanatupiga vita; wameenda kuongea na Mozambique, wameweka reli pale, kuna mizigo inayotoka Beira kuja Malawi. Kwa hiyo, tunapigwa vita bila sisi kujua tunapigwa vita kiasi gani. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hii research and development ikiweza kufanya kazi yote, itatambua, itajua matatizo yako wapi na tutafanya kazi vizuri; nchi itatoka. Tuna billions of money! Kenya wana kontena milioni sita kwa mwaka, Singapore milioni 30 kwa mwaka, Dubai milioni 24.5 kwa mwaka, sisi tunaongelea kontena milioni moja kwa mwaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi tukiweza kuwa na kontena milioni mbili tu za transit mara dola 1,000 tuangalie ni fedha kiasi gani tunazozipoteza, simply kwa sababu ya kuchukua maamuzi madogo tu ambayo hayahitaji fedha. Ni kuyatambua matatizo yako wapi, kukaa mezani, kuyaleta pale kwenye Baraza la Waziri, leta hapa tubdilishe sheria ndogo hizi ili hawa wafanyabiashara wa nchi jirani warudi na kujenga imani kutumia bandari yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri wa Fedha unakosa fedha nyingi mno kwenye transit goods, mimi siongelei mizigo ya ndani. Mizigo ya ndani wala sina tatizo nalo, wafanyabiashara hawana tatizo na kulipia ushuru.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika suala zima la viwanda, hakuna maendeleo katika suala zima la viwanda kama vikwazo (restrictions) ambayo yako ndani ya viwanda hayatatoka. Ni mengi mno, nikiyataja hapa ni mpaka kesho.
Mheshimiwa Naibu Spika, niungane na Waheshimiwa waliochangia asubuhi, tumewekewa kodi kwenye mafao haya ya Wabunge. Sasa hilo suala zima naomba lishughulikiwe, lifanyiwe kazi. Kama alivyosema Mheshimiwa Bashe, ma-DC na wengine hawakuwekewa. Sasa huko nje mitaani ni kweli kabisa Waheshimiwa Wabunge tumechongonishwa vibaya sana. Ama itolewe kwa wote ama iwekwe kwa wote kabisa kamili.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, nashukuru sana, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Kwanza kabisa naunga mkono hoja ni hoja ni nzuri. Mheshimiwa Waziri umeeleza vizuri sana wewe na Mheshimiwa Naibu Waziri na timu yako nzima ya Wizara hii ya Maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaendelea na mimi niendelee tu kusema kwamba naunga mkono hii shilingi 50 ambayo ni hoja au ushauri wa Kamati na imeelezwa hapa. Sasa itatoka wapi, inaweza ikatoka kwenye mawasiliano au kwenye mafuta. Hivi mtu anayejaza mafuta kwenye gari lake au mtu anayetumia simu akaona kabisa shilingi 50 hii nailipia kwenye maji, inamuuma kweli? Ni suala la Serikali kuamua tu, ninyi amueni mambo yaishe, wanaojaza mafuta kwenye magari yao au watumiaji wa simu watalipa tena wanalipa wakiwa na furaha kwelikweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine hii ni utekelezaji wetu wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Maana yake tunakwenda kukamilisha ahadi tuliyoiweka kwenye ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi. Kwa hiyo, hili ni jambo jema sana Mheshimiwa Waziri wa Maji lichukue ukalifanyie kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mradi wa Ziwa Victoria ambao unatoka Solwa ambao Mheshimiwa Waziri ameutaja hapo unaokwenda Tabora. Mradi huu umetoka kwenye Jimbo langu unakwenda mpaka Nzega baadaye unakwenda Igunga na maeneo mengine. Ni mradi mkubwa sana, gharama yake nafikiri kwenye dola milioni 270. Ni mradi uliosanifiwa vizuri sana unakwenda kutibu tatizo la maji kwenye zaidi ya vijiji 50 katika Jimbo la Solwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu una uzuri wake sana na niishukuru sana Serikali tena kwa asilimia zote na nimshukuru Mheshimiwa Rais na wewe pia Mheshimiwa Waziri. Hata hivyo, kuna kata ambazo mmeziruka kwa maana ya kwamba ama mmeruka katika upembuzi yakinifu ama mmeziruka kwa maana ya kwamba vijiji vipo nje ya kilometa 12.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka Mheshimiwa Waziri anisikie, athari yake ni kwamba Kata hizo tano ni Bukene, Usule, Nsalala na Usanda maana yake ni kwamba mradi ukipita wanaona wenzao wanatumia maji na wao wamerukwa matokeo yake ni kwamba watakwenda kuhujumu mradi. Sasa hapo tutakwenda Waheshimiwa Wabunge kwenda kuongea nao acheni tunafanyia kazi na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu, una Katibu Mkuu Profesa mzuri sana, tuma timu hata kama vile vijiji viko nje ya kilometa 12 kwenye Kata hizi hasa Usule, Bukene, Nsalala na Usanda zikafanyiwa upembuzi ziingizwe. Hivi kweli mainjinia ambao tunao kweli katika Tanzania hii wanashindwa kwenda kufanya usanifu hata hivyo vijiji ambavyo viko nje ya kilometa 12 na wenyewe wakapata maji? Mimi sidhani na gharama siyo kubwa hivyo ili mradi ukipita upite moja kwa moja na mambo hayo yawe yamekwisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru sana Tinde mmeiingiza ilikuwa imerukwa. Mheshimiwa Aweso nakushukuru sana, Mheshimiwa Waziri tuliongea hayo mambo sasa hivi umetupa kibali Tinde vijiji vyake vyote vinapata maji ya Ziwa Victoria. Jana nimepata taarifa kwa maana ya kwamba tulikuwa tunahangaika kijiji kimoja cha Weleza kinapata maji sasa hii kimoja kimoja hapana, tufanye kwa pamoja mambo yote yaishe kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Solwa litakuwa ni mfano, hata National Housing wanavyojenga nyumba wanajenga nyumba moja wanasema hii ni ya mfano anapokuja mteja anaitizama ili aweze kuvutika kununua nyumba. Jimbo la Solwa mradi huu ukiisha nakwenda kuwa na vijiji zaidi ya 86 vyenye maji ya Ziwa Victoria na ni Jimbo la kwanza kabisa naweza ku-declare tumefika asilimia 85. Kwa hiyo, ni jambo jema sana, niishukuru sana Serikali yangu pamoja na Mheshimiwa Rais wetu. Dkt. John Pombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mradi wa Mwakitolyo na Mwasekagi wa mwaka 2017. Mradi huu uko asilimia 85, tuna fedha kidogo sana imebaki bilioni 150, tume-raise certificate kwa ajili ya shilingi bilioni 63 ili zile kazi ndogo ndogo zikamilike. Sasa hivi wanatumia maji lakini kuna kazi ndogondogo za kumalizia ili mradi huu uishe moja kwa moja katika eneo la Mwakitolyo na Mwasekagi kwenye Kata ya Solwa. Naomba sana hili mlifanyie kazi, Katibu Mkuu unanisikiliza, tulipe hii bilioni 63 mkandarasi akamalize kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Mwakitolyo kwa kipekee kabisa Mheshimiwa Naibu Waziri nikushukuru sana na Mungu akubariki sana na kama una mke mmoja akupe wa pili, wa tatu na wa nne. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri alikuja Mwakitolyo, huu mradi wa maji ni wa shilingi 1,400,000,000, ilikuwa fedha zake zimelipwa na mradi haukuweza kufanya kazi. Umekuja pale, ukaongea na Katibu Mkuu kwa simu na wananchi wanakusikia. Katibu Mkuu akajibu vizuri, nafahamu kazi iko vizuri, Tume imeenda na mpaka sasa mmeshachukua hatua. Ombi langu nataka sana uende haraka kwa maana najua kuna usanifu na design mpya inafanyika itengwe fedha ili wananchi wale wa Mwakitolyo ni wengi, pale kuna wachimbaji wadogo wadogo wengi sana, ni mji unaokuwa haraka sana, una fedha watu wanajenga nyumba za kisasa kabisa, nafikiri umeshanisikia suala hili utalifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosema Mheshimiwa Keissy masuala ya mabwawa kuna changamoto makubwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kengele ya kwanza?

MWENYEKITI: Ya pili, malizia sentensi yako.

MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, duh, naunga mkono hoja asilimia 100, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa naunga mkono hoja yetu hii ya Wizara ya Ulinzi. Imesomwa na Mheshimiwa Waziri, yuko vizuri, yuko sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kabla sijaendelea Amiri Jeshi Mkuu, Mama yetu Mama Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimshukuru sana kwa kazi anayoifanya. Amani ya nchi ina mambo mengi katika kuhakikisha amani inakuwepo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Moja katika kazi kubwa kabisa inayofanyika ni pamoja na Mama kutengeneza au kujenga au kuwa na mahusiano mazuri kabisa na nchi zote za Afrika ikiwemo nchi zilizotuzunguka. Hiyo yote ni sehemu moja katika kuona kwamba, Watanzania wanaishi kwa amani kufungua fursa za nchi, wakishirikiana na Jeshi letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili ni pia, nimshukuru Mkuu wetu wa Majeshi, CDF General Nkunda kwa kazi kubwa anayoifanya pamoja na timu yake nzima, Luteni General Salim Othman, ma-Meja Generals wote, ma-Brigadier Generals wote, ma-Kanali wote, ma-Meja wote kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa ajili ya amani ya Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, amani ina mambo mengi na moja katika eneo ambalo wanatusababishia, ukiacha Mungu mwenyewe, amani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mungu mwenyewe ametupa zawadi kwamba, Tanzania ni moja katika nchi chache Afrika au duniani ambazo mpaka sasa hivi zina amani na tunaishi kwa raha. Kama ni wafanyabiashara, kama ni wafanyakazi, na namna yoyote ile tuko kwenye amani kubwa sana. Moja katika sababu kubwa kabisa ni Jeshi ambalo wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha amani inakuwepo katika Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, taharuki niliwahi kusikia huko Kusini, kuna wakati ilitokea taharuki hapa na pale, kazi kubwa ilifanywa na Jeshi letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuna vijana kule wanakaa 24/7 wanakaa kwenye mapori mazito yale kuhakikisha wako tayari kujitoa muhanga, wako tayari kupoteza maisha yao kwa ajili ya amani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hapa tunapokaa tunaona Bunge hili, Bunge hili linakaa kwa sababu ya amani ya Jeshi hili la Jamhuri ya Muungano wakiongozwa na General Nkunda katika kuhakikisha kwamba, hata Kusini kule taharuki iliyokuwepo Kusini kule amani inakuwepo. Hata wananchi wa Mtwara amani ipo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hivi kuna vijana wetu wako hata Msumbiji wanakwenda kutoa ushirikiano mkubwa sana kwenye Jeshi la Msumbiji ili kushirikiana na Jeshi ambalo liko hapa Tanzania kuhakikisha eneo lile ambalo liko Kusini kule linaendelea kuwa na amani. Amani katika nchi yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kambi zile ambazo ziko Kusini, zote ni Watanzania vijana wako zaidi ya 1,500 ndani ya Msumbiji wakitoa ushirikiano, wakitoa mafunzo na Watanzania wanajeshi wanashirikiana pale kuona kwamba amani inakuwepo.

Mheshimiwa Spika, ninamuomba tu Mheshimiwa Waziri, operation kama hii ni gharama kubwa sana, Jeshi hili linafanya kazi kwa weledi, kwa uzoefu, kwa uzalendo, nikuombe tu kwamba kama kuna namna ambayo kuna mapungufu ya kulihudumia Jeshi hili kwenye aina hii ya operation peke yake huku Kusini, hebu jaribu kuona kwa sababu bado mwezi mmoja, hotuba yako na hotuba ya Kamati imeelezea kwamba, bado kuna fedha wanahitaji ili kukamilisha mambo yao waliyojipangia katika maendeleo yao. Bado sasa hivi ni kama mwezi mmoja mpaka kufikia Tarehe 30 mwezi wa Sita, kuna tatizo gani, kama ni Waziri wa Fedha yuko hapa, mkahakikishe kwa muda huu fedha ambazo zimebaki wakapewa, lakini specifically Mheshimiwa Waziri utakapokuja kuhitimisha hoja yako hapa itapendeza sana, sina mashaka na wewe kabisa Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi, lakini kama watakuwa na mipango ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu, kuboresha Jeshi la Tanzania kutoka tulikotoka tulipo hapa sasa hivi tukawa katika Jeshi bora Afrika na Tanzania. Kwa maana ya kwamba, kubadilisha mitambo, kubadilisha zana, kuwa na mawasiliano, Jeshi likawa la kisasa zaidi.

Mheshimiwa Spika, specifically kwenye operation hii nimuombe Mheshimiwa Waziri kama kuna uwezekano waongezewe fedha angalao hata kama bilioni 150, specifically naongelea kwa ajili ya operation hii ya Kusini mwa Tanzania. Sasa utakapokuja kuhitimisha hapa Mheshimiwa Waziri, kama utakuwa na namna ambayo utaiweza sisi Wabunge tuko hapa na tuko tayari kukuunga mkono. Kama utakuwa na mipango mizuri tutakuunga mkono wala hatuna shida na wala sina mashaka kabisa na wewe pamoja na Serikali ya Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri ameongea hapa kwa maana sasa wamekubaliana kwamba tutaingia partnership na private sector katika kuliendeleza Jeshi. Niliwahi kuongea na niliwahi kushiriki Bunge hili wakati ule, mwaka juzi kwenye bajeti na nikasema Jeshi letu la Tanzania wana uwezo mkubwa mno wa kutengeneza silaha ndogondogo, wana uwezo mkubwa mno wa kutengeneza hata risasi, wana uwezo mkubwa mno wa kutengeneza hata magari, lakini pale ambapo kutakuwa na mpango mzuri wa kushirikiana na sekta binafsi, iwe nje ya nchi iwe ndani ya nchi, uwezo huo upo. Hawa wenzetu wamewezaje?

Mheshimiwa Spika, kuna nchi hapa jirani wanajipambanua hivi, lakini sisi ndiyo tuliowafundisha, tuliowaweka pale na tuliwasababisha wakakaa vizuri. Leo wanakuwa na mipango mizuri kuliko hapa, haiwezekani! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimuombe Mheshimiwa Waziri awe na mipango hiyo. Na uwezo mkubwa kabisa, Jeshi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wapo wasomi wazuri, Jeshi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wana uwezo mkubwa sana, wamo ma- engineer wazuri sana, ni suala tu la kukaa, kuwa na mipango, tunafanyaje, unahitaji fedha, kama kuna private sector inakuja, lete Bungeni tupitishe waende wakatengeneze hayo mambo ambayo watakuwa wamejipangia. Tukianza kutengeneza silaha, tukawa na risasi, tukawa na mambo yote hayo, hata magari, hata zana, hatuwezi kushindwa, lakini tukawa na mpango wa muda mrefu tunakuwa tunajihakikishia kabisa kwamba, tunaweza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nchi kama Egypt leo wanatengeneza silaha nyingi tu, wanatengeneza risasi nyingi tu, tunashindwaje sisi? Tanzania ina historia kubwa ya kuleta uhuru Kusini mwa Afrika, tunashindwaje sisi? Leo hapa nchi jirani hapa tuna mawasiliani mazuri. Jeshi la Tanzania lina historia nzuri sana Afrika, Jeshi la Tanzania lina historia nzuri sana kuleta uhuru nchi zote za Kusini mwa Afrika, tunashindwaje kufanya hivyo, ni suala la mipango tu.

Mheshimiwa Spika, mimi sina mashaka na uongozi wa Jeshi wako vizuri sana, tukiamua kwa pamoja, mkiamua kama Wizara kwa pamoja tutoke kwenye Jeshi lililopo sasa hivi standard hii tuihuishe ipande kabisa liwe Jeshi la kisasa, wawe na mitambo ya kisasa, wawe na mawasiliano ya kisasa, yaani liwe Jeshi la kidijitali kutoka kwenye Jeshi la analogia ambalo tunalo sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu, ukishakuwa na mipango ya kati, mipango ya muda mrefu, Jeshi hili litakuwa Jeshi moja zuri sana. Bahati nzuri sana heshima ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Afrika ni kubwa mno. Suala la kuwa na amani mimi sina matatizo kwa sababu amani ipo, lakini unapokuwa na jeshi zuri ni back up ya kuwa na amani ndani ya nchi na hata nchi jirani wanajua kabisa Tanzania pale Jeshi ni zuri hakuna sababu ya kuleta fyokofyoko, tukileta fyokofyoko tunafyatuliwa. Kwa hiyo, suala la kuwa na Jeshi imara ni moja ya back up kubwa sana kusababisha amani ndani ya nchi, Ukiachana na Mama Samia anavyohangaika kutengeneza diplomasia nchi za Afrika na duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuboresha maslahi ya wanajeshi na hasa hawa ambao wanaingia kwenye operations za moja kwa moja, kuwepo na mipango mahsusi kabisa hawa ambao wanakwenda kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya nchi yetu, hawa ambao wanakaa kule kwa ajili ya nchi yetu, hawa hebu tuone maslahi yao yamekaaje kwa maana ya maslahi yao, kwa maana ya zana za kisasa…

SPIKA: Kengele ya pili imeshagonga Mheshimiwa.

MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Naunga hoja mkono, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi hii kuchangia kwenye hii hoja yetu ya Kilimo. Kwanza kabisa niunge hoja mkono kwa asilimia mia moja na nimpongeze Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Mawaziri kwa kazi nzuri wanazozifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri sana katika taarifa au hoja aliyoisoma Mheshimiwa Waziri amekiri kabisa kwamba, kuna matatizo ya climate change kwenye maeneo mbalimbali ya Tanzania ambayo yanaweza yakasababisha upungufu wa mazao au chakula hasa katika Mkoa wetu wa Shinyanga. Mimi naongelea Mkoa wetu wa Shinyanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukilinganisha mikoa ambayo hali ya hewa ikibadilika kidogo tu mambo yanakuwa tofauti kabisa na watu walivyotarajia katika suala zima la kilimo. Ukilinganisha Mikoa ya Shinyanga na mikoa ya Kusini, mikoa ya Kusini ukiongelea masuala mazima ya umwagiliaji wanakushangaa. Mikoa ile imeneemeka na mvua ni nyingi na watu wanalima vizuri sana, lakini Mkoa kama wa Shinyanga hivi ninavyozungumza hali ya mazao katika Jimbo la Solwa per se, Jimbo la Solwa sasahivi mazao mengi yamekauka. Ukienda Bariadi, ukienda Mkoa wa Simiyu, ukienda kote mambo ni hivyohivyo yanakauka halafu baadaye kidogo tena mvua inanyesha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, suala hili nataka tu nimshauri Mheshimiwa Waziri kwenye maeneo ambayo ni muhimu sana ya kimkakati katika kuyaokoa, sisi katika Mkoa wa Shinyanga tunalima vizuri sana na hatupendi kuomba chakula, kinachohitajika pale ni kutengenezewa miundombinu itakayokwenda kuondoa tatizo hili la tatizo la njaa. Sasa eneo pekee, nimweleze Mheshimiwa Waziri, angechukua Mkoa wa Shinyanga na mikoa mingine ambayo anaiona yeye inafaa kwa kuanzia hizi fedha kwa ajili ya umwagiliaji skimu za umwagiliaji ziende maeneo hayo kwa sababu, hakuna eneo linaweza likatusaidia au kuwasaidia wakulima wa Jimbo la Solwa kama skimu ya umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Jimbo la Solwa tuna skimu sita, lakini skimu ambazo ziko vizuri ni skimu tatu ambazo hata hivyo upembuzi yakinifu ulishafanyika na tumeshaomba fedha kwa ajili ya uchimbaji wa mabwawa kwenye maeneo hayo. Hizo skimu zipo kweli, tunashukuru sana kwanza Serikali ka kufanya kazi kubwa ya kutuletea skimu hizo, lakini skimu ni mifereji ina maana kwamba, mvua ikikauka na yenyewe haina kazi kwa hiyo, ili mifereji ifanye kazi vizuri lazima ujenge bwawa, lile bwawa ndio linanywesha, ndio linamwaga pale kwenye skimu ya umwagiliaji kwenye mifereji, wakulima wanalima hata kama mvua haipo. Hivi ninavyoongea sasa hivi kuna tatizo kubwa sana la njaa, yaani njaa ipo, baada ya miezi miwili mitatu itakuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina skimu ya umwagiliaji ya Nyida ambayo kwenye taarifa hapa kampuni au Shirika la Maendeleo la JICA ndio sasahivi linafanya kazi pale katika kutengeneza ile mifereji. Tunawashukuru sana na tunashukuru sana Serikali kwa kuliona hilo. Gharama inayotumika pale ni milioni 466, urefu wa mita 1,325 itakuwa ni skimu ya umwagiliaji nzuri sana. Kinachotakiwa pale ni kujenga bwawa tu, upembuzi wa bwawa na usanifu ulishamalizika na tulishaomba maombi maalum kabisa ya 2.5 billion ili sasa skimu ile iweze kukamilika, Skimu ya Umwagiliaji ya Nyida katika Jimbo la Solwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Skimu ya Umwagiliaji katika Kata ya Masengwa, Skimu ya Umwagiliaji katika Bwawa la Ishololo, wote huu ni umwagiliaji ambao sasa hivi nataka Serikali kwa jicho la huruma sana, kama ni fedha kwa ajili ya kuwasaidia wakulima, kama ni fedha kwa ajili ya kuondokana na matatizo haya ya njaa katika Mkoa wa Shinyanga, eneo muhimu sana, mimi binafsi namshauri sana Mheshimiwa Waziri tujikite sana kwenye skimu ya umwagiliaji. Kwa hiyo, naomba sana na tayari tulishaomba fedha hizo na tayari iko Wizarani kwako, sasa Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa kujibu hoja zetu Mheshimiwa ni matarajio yangu ataniambia kwamba, fedha zote tulizoomba ameshatupa, ili twende sasa tukawaambie wananchi waende wachimbe mabwawa na Mungu atambariki sana na tunaunga hoja mkono vizuri na Serikali ya Rais, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Skimu ya Masengo ni skimu ya muda mrefu sana. Kuna wakati tuliwahi kupata fedha milioni 900, lakini kutokana na committment nyingi za Serikali fedha hizi hatukuletewa, tukasema haina shida, lakini sasa hivi tunaomba. Bahati nzuri sana usanifu, narudia tena, usanifu ulishafanyika kwa skimu zote tatu hizi, kwa hiyo, suala hapa ni kutafuta fedha tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukienda kwenye Bwawa la Ishololo ambalo nalo ni muhimu sana kwenye Kata ya Usule, bwawa hili lilianza mradi mwaka 2013. Mkandarasi aliyepewa bwawa hili alifikia asilimia 30 na muda wake wa mkataba ukawa umekwisha kwa hiyo, fedha tulizopewa na Bank of Africa wakasitisha wakaondoka. Kwa hiyo, mradi umefika asilimia 30 na umesimama mpaka hivi ninaongea leo. Tumerudia tena usanifu, tumeomba fedha kwa mara ya pili ni 1.2 billion.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninayoongea haya ni miradi ambayo inafanyika, iko njiani tunakwenda kukamilisha, siongelei miradi mipya. Katika hoja yake Mheshimiwa Waziri amesema atajikita zaidi kwenye miradi ambayo haikukamilika, iko kati ya asilimia 30, 50 mpaka mwisho, kwa hiyo, miradi hii ninayomweleza ya Skimu ya Umwagiliaji ya Nyida, skimu ya Umwagiliaji ya Masengwa, Bwawa la Ishololo ni miradi ambayo ipo katika asilimia 30 au 50. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naongea hii Wizara ya Kilimo ina Waziri ambaye namwaminia sana. Mheshimiwa Waziri namwamini sana, najua kabisa atayachukua haya, atakwenda kuyafanyia kazi. Sisi Waheshimiwa Wabunge katika Mkoa wa Shinyanga hakuna kitu kinatusumbua sisi kama mabadiliko ya hali ya hewa. Yaani hali ya hewa ikikataa mvua kidogo tu mazao yanakauka na mambo yote yanakuwa yameharibika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna upungufu wa Maafisa Ugani 56. Maafisa Ugani ni watu muhimu sana, bila kuwa na Maafisa Ugani kwenda kuwaeleza wakulima, wakulima bado wanalima kilimo kilekile cha zamani, kilimo kisichokuwa na tija, kilimo ambacho kwa kweli, wanatumia nguvu kubwa, lakini mafanikio yao yanakuwa ni madogo. Kwa hiyo, pamoja na kuwa tuna upungufu wa Maafisa 56 ni kweli inawezekana kabisa akatuletea 10, 20, ninachoomba atuongezee pale ambapo anaona inampendeza, ili sasa Jimbo la Solwa tuweze kuongeza Maafisa Ugani wazuri waweze kutoa elimu vizuri, hii ni pamoja na usafiri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maafisa Ugani wanapata shida sana kwenda kwa wakulima. Mheshimiwa Waziri atuletee mwongozo tu kwamba, katika bajeti ya mwaka huu tunahitaji, Halmashauri ninyi katika mwongozo wa kilimo kwamba, mpange pikipiki kwa ajili ya Maafisa Ugani hata kwa ngazi ya kata. Tunaweza tukaanzia kwa ngazi ya kata peke yake. Mimi nina kata 26 nikipata pikipiki 26 maana yake tayari tumeshajenga network ya Maafisa Ugani na wakulima, tutakuwa tayari tumewajengea uwezo mzuri mno wakulima kulima kilimo cha kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri sana katika Jimbo la Solwa tuna zao moja la dengu ambalo linatumika kama zao la biashara, lakini zao la dengu wanalima kata kama nne au tano tu. Ukichukua Kata ya Salawe, Kata ya Bhukande, Kata ya Mwakitolyo na Kata ya Solwa ndio wanaolima dengu na hiyo dengu kwa mfano hivi sasa hivi kama kuna matatizo ya mazao, kutokuwepo na mazao hawavuni vizuri wanategemea mazao hayo ya dengu, lakini kata zilizobaki zote wanategemea zaidi mahindi pamoja na mpunga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi sina mengi zaidi ya hapa. Nilikuwa nataka tu kujikita zaidi kwenye masuala mazima ya umwagiliaji na hili suala la umwagiliaji hatuna namna yoyote kabisa katika kuokoa wakulima wa Jimbo la Solwa au Mkoa wa Shinyanga...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa kwa mchango wako.

MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga hoja mkono. Nakushukuru sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia hoja hii. Kwanza naiunga mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Waziri makini sana katika Wizara nyingi na ninaamini kabisa katika Wizara hii ya TAMISEMI, pamoja na wasaidizi wake tunakwenda kufanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka nianze na TARURA moja kwa moja. TARURA ni mamlaka iliyotengenezwa kwa ajili ya kutengeza barabara vijijini. Inafanya vizuri. Katika Jimbo la Solwa kule kwangu wanafanya vizuri sana, lakini shida kubwa kabisa katika TARURA ni upungufu wa fedha watu wanazoziomba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nina kilometa 743, lakini fedha ambazo tunahitaji ni shilingi bilioni saba na fedha ambazo tumepata mwaka huu ni shilingi bilioni 1,100 na something. Utaona kwamba tatizo kubwa kwenye TARURA ni upatikanaji wa fedha tu. Sasa Wabunge wengi katika Bunge hili wamechangia sana na ukienda katika michango mikubwa, hasa katika Wizara hii ya TAMISEMI ni suala zima la TARURA.

Mheshimiwa Spika, nitoe rai, tumekuwa na Mfuko wa Maji, tumekuwa na Mfuko wa REA wa usambazaji wa umeme vijijini, tumekuwa na Mfuko wa Road Fund; sasa mifuko hii inaonekana kama kwa namna fulani wanafanya vizuri. Kwa hiyo, tuendelee na mifuko hiyo hiyo. Sasa tuwe na Mfuko wa TARURA, tuwe na Mfuko wa Ukamilishaji Maboma ya Halmashauri zetu. Tufanye hivyo tu, na fedha zipo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama alivyongea Mheshimiwa Zungu jana, nimemsikia hapa na Waheshimiwa Wabunge, fedha zipo kwenye mitandao, kwenye simu na kwenye mafuta na wananchi hawashindwi kulipa. Kwa maana ukichaji shilingi kumi kwa kila dakika, kwa kila mtu anayepiga simu au kwa kila lita shilingi 50, tutakuwa na mfuko wenye fedha wa kutosha kabisa kwenda kukamilisha miradi yetu katika Halmashauri zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikija kwenye Hospitali ya Wilaya, nashukuru sana, nimepata shilingi milioni 800 kwenda kukamilisha majengo yaliyobaki. Naomba tu Wizara hii ifanye kila itakavyofanya; na kipaumbele cha Wizara hii kwa mwaka huu, nilifurahi sana Mheshimiwa Ummy Mwalimu alivyosema wanakwenda kwenye tiba; vifaa tiba na afya yenyewe. Sasa kwenye hospitali yangu ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Jimbo la Solwa, tunahitaji vifaa tiba ili tuendelee na kazi kwenye Hospitali ya Wilaya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukija kwenye maboma, nataka sasa niongee juu ya maboma haya. Katika Jimbo la Solwa tuna zahanati 42. Naishukuru sana Serikali imetupa shilingi milioni 150 kwa zahanati tatu ambapo sasa hivi tunakwenda kukamilisha zahanati hizo; Zahanati ya Kilimawe, Zahanati ya Mwamedilana, tunakwenda kukamilisha zahanati tatu. Vile vile katika ceiling tuliyoipata mwaka huu ni kwa ajili ya zahanati tisa tu. Maana yake katika 42 ukitoa tisa unabaki na 33. Tukienda kwa bajeti tatu bado tutakuwa na upungufu wa ukamilishaji wa zahanati kwa miaka mitatu mpaka 2024.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa Wizara ione namna ya ukamilishaji wa maboma haya, siyo tu Jimbo la Solwa, hata nchi nzima tuwe na mipango mikakati. Wizara ikinipa shilingi milioni 500 ya ukamilishaji wa majengo ya zahanati, ikanipa shilingi milioni 500 ya ukamilishaji wa majengo ya sekondari, wakanipa shilingi milioni 500 ya ukamilishaji wa majengo ya shule ya msingi, kila mwaka tutakuwa tumekamilisha kweli.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano elimu ya sekondari, nina majengo 63. Nikija kwenye shule za msingi majengo 80, kwenye zahanati majengo 42 yanataka ukamilishaji wa katika Jimbo la Solwa, ambapo tunakwenda kuwa na zahanati zaidi ya 80 out of vijiji 126. Naomba sana, sana tu, Wizara kama Wizara, tunapokuwa na miradi mikubwa, well and good, mradi wa reli safi kabisa; mradi wa umeme kule, safi kabisa; sasa twende kwenye huduma za jamii moja kwa moja. Hizo huduma za jamii ndiyo zinakwenda kusaidia wananchi wenye hali ya chini kule (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukitengeneza maboma haya ya zahanati, shule za msingi na nyumba za walimu tukaenda kwenye sekondari, kama ulivyosema wewe wiki iliyopita, unapowapelekea madawati, mtoto wa masikini anapokaa, ni fadhila kubwa mno kwa Mungu. Sasa ndiyo twende huko. Tujikite sana kwenye maboma na ukamilishaji wa maboma katika Jimbo la Solwa pamoja na nchi nzima kwa ujumla wake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni upungufu wa watumishi kwenye zahanati zetu. Nina upungufu mkubwa mno katika zahanati mno. Serikali izingatie hili kupitia TAMISEMI,

Mheshimiwa Ummy namwaminia sana, upungufu wa watumishi ni mkubwa sana… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Ahmed Salum.

MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Spika, dakika ni chache, unaweza kuniongeza mbili!

SPIKA: Dakika tano ni chache sana. (Kicheko)

MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, Mungu akubariki sana. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Kwanza kabisa, naunga mkono hoja ya Wizara yetu ya Uchukuzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesikiliza michango mingi sana ya Waheshimiwa Wabunge ambayo ni mizuri sana. Moja katika mambo ambayo ni muhimu sana huko tunakokwenda ni suala zima la barabara zetu. Katika Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi barabara ambazo zipo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025 nadhani hizo zipewe kipaumbele namba moja na barabara ambazo ziliahidiwa na Mheshimiwa Rais, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na zenyewe ziwe katika vipaumbe vya Wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, katika Jimbo la Swola kuna barabara inayotoka Manawa - Misasi - Swola - Mwakitolyo - Kahama imefanyiwa upembuzi yakinifu mwaka 2010 na ilikuwa ndani ya Mpango wa Millenium Challenge Funds. Baada ya zile fedha kuondoka barabara hii imesahaulika mpaka leo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, umuhimu wa barabara hii inaunganisha Majimbo ya Mwanza Mjini, Misungwi, Solwa na Msalala kwa maana ya Jimbo la Kahama. Majimbo matano au sita yanaunganishwa na barabara moja hii. Wafanyabiashara wa Rwanda, Burundi na nchi zote jirani huwa wanakuja mpaka Solwa na Nyabukande kwa ajili ya biashara ya mazao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara nyingine ni ya Solwa - Old Shinyanga na yenyewe imo ndani ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi yenye urefu wa kilometa 60. Mimi nipo kwenye Kamati ya Miundombinu na nilimueleza Waziri jambo hili, tupo pamoja sana katika utekelezaji wake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nishukuru sana kwenye hotuba ya Waziri nimeona airport ya Shinyanga Ibadakuli, zimewekwa shilingi bilioni 3.6. Mwaka huu airport ya Shinyanga inakwenda kujengwa baada ya kuilalamikia kwa muda mrefu. Naishukuru sana Serikali kwa kutusikiliza awamu hii. Sasa hivi wananchi wa Shinyanga watakuwa hawaendi tena Mwanza baada ya kukamilika airport hii tutakuwa tunapandia hapo hapo Shinyanga. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini niongelee suala zima la bandari. Tanzania hii kuna bandari 89 lakini 66 zipo kwa mujibu wa Sheria Na.17 ya mwaka 2004 na zinasimamiwa na Wizara moja kwa moja. Kati ya bandari hizi, bandari 12 zipo kwenye Bahari ya Hindi, bandari 24 zipo Ziwa Victoria, bandari 19 zipo Ziwa Tanganyika, bandari 11 zipo Ziwa Nyasa na kuna bandari nyingine ndogo ndogo. Bandari ni kitu kikubwa sana, Bandari ya Dar es Salaam inachangia kwenye Pato la Taifa zaidi ya asilimia 30. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukichukua tani milioni 9 alizosema Mheshimiwa Waziri, ukatoa mizigo ya transit ukaacha mizigo ya ndani, kodi ya bidhaa ni zaidi ya kontena laki moja na elfu arobaini mpaka kontena laki moja na elfu sitini ni 2.5 trillion to 3 trillion per year bandari peke yake inaisaidia TRA kukusanya mapato ya nchi. Kwa hiyo, bandari siyo jambo la mzaha mzaha hivi, ni jambo kubwa lakini ipo kama idara ndani ya Wizara ya Uchukuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukichukua Bandari ya Durban wanahudumia tani milioni 31, Bandari ya Beira wanahudumia tani milioni 7 na target yao ni kwenda tani milioni 11 kwa mwaka, ukichukua Bandari ya Mombasa wanahudumia tani milioni 12 kwa mwaka na hizi bandari ni washindani wakubwa sana wa Bandari yetu ya Dar es Salaam. Nakumbuka wakati ule tuliongea sana hapa ilikuwa kuna tatizo kubwa sana tuliingiza sheria ya kutoza VAT on auxiliary goods kwa maana ya transit ikatusababishia matatizo makubwa mno nchi jirani wote wakaondoka wakaenda kutumia Bandari ya Mombasa. Tulipoongea hapa Serikali yetu ilikuwa sikivu ikaondoa na sasa hivi wateja kutoka Rwanda na Zaire wamerudi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja yangu nataka kumalizia, naiomba sana Serikali na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu afikirie bandari iwe Wizara kamili ili tuweze kutoka kwenye milioni 9 twende kwenye milioni 12, 15 mpaka 20 ili iweze kuchangia kwenye asilimia zaidi ya hamsini ya Pato la Taifa. Bandari siyo jambo dogo, Singapore asilimia 80 ya mapato yao yanatoka kwenye bandari.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)


NAIBU SPIKA: Mheshimiwa, ahsante sana.

MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwanza umeniongezea dakika moja ungenipa dakika mbili ningeshukuru sana. Ahsante sana, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii na mimi nichangie katika Wizara hii Wizara ya Ulinzi. Kwanza nimpongeza kaka yangu, ndugu yangu Mheshimiwa Waziri Kwandikwa, Waziri wa Wizara hii na hoja yake nzuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, zamani ilikuwa nafikiri jeshi lolote duniani kazi yake ni kupigana tu au kulinda mipaka peke yake ya nchi husika. Lakini nimekuja kujifunza Jeshi ndio nchi na nchi ndio Jeshi. Nimpongeze sana General Mabeyo na timu yake yote, wakati wa msiba wa aliyekuwa Rais wetu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Msiba ule waliubeba ilikuwa natazama mimi TV nikasema kumbe jeshi ni nchi na nchi ni jeshi kuanzia hatua ya mwanzo mpaka walipokwenda kumpumzisha aliyekuwa Rais wetu John Pombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi ile sio ndogo na ni kazi moja kubwa sana. Kwa hiyo, mimi nampongeza sana, sana, sana pamoja na jeshi lote kwa ujumla wake walivyosimamia msiba wenyewe, walivyosimamia amani ya nchi, walivyosimamia maeneo yote, ilikuwa naona maeneo tu kule mipakani, kwamba sasa pasitokee na taharuki yoyote katika Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania. Jeshi letu linafanya kazi kubwa, yako mambo hata kwenye hotuba hawawezi wakayasema. Mipaka yetu inalindwa na jeshi twenty-four seven. Kuna watu pale hawalali saa 24 wanatazama mipaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, juzi nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari kuna baadhi ya wakimbizi wanatoka nchi jirani kule wanaanza kukimbilia huku. Kazi kubwa hiyo inayofanywa na Jeshi letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wapo pale. Jeshi wanafanya kazi ya kulinda mipaka yetu, Jeshi wanafanya kazi ya kulinda maeneo mengi, Jeshi wanafanya kazi yanapotokea mafuriko ndani ya nchi yetu hii, kwa mfano, kuna wakati meli ilipunduka katika Ziwa Victoria, walitumwa vijana wa Jeshi kwenda pale, lakini kwa bahati mbaya kwa sababu ya vifaa walikuwa hawana sana, walikuwa na vifaa vichache walichukua zaidi ya siku saba mpaka siku kumi kuokoa ile hali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo hoja yangu hapa Mheshimiwa Waziri pamoja na Jeshi yaani uone namna ya kuongeza fedha zaidi za kutosha kwenye eneo hili la kuokoa maeneo ya hatari au kwenye mafuriko kwenye maeneo yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ikitokea kwa mfano sasa hivi treni imepundika, barabara kubwa imekatika, daraja kubwa limekatika, kimbilio letu ni Jeshi. (Makofi)

Sasa hoja yangu hapa, fedha hizi tunapitisha leo trilioni 2.35 na ngapi zisipungue. Ziende kama walivyojipangia wenyewe ili wakajipange sasa waweze kuweka mambo yao vizuri kwa ajili ya Nchi yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kenya nilisikia wameanza kutengeneza risasi na baada ya mwaka mmoja wataanza kuuza. Sisi tuna karakana kubwa ya Nyumbu alivyosema Mheshimiwa Mwijage pale kubwa mno ile inaweza kuwa ya tatu Afrika au duniani ikawa moja katika sehemu moja kubwa. Hivi tunashindwaje sisi kama Jeshi wakawa na mipango ya kutengeneza risasi na silaha ndogo ndogo. Leo JKT waliwahi ku-assemble matrekta haya wakauza na ikafanya kazi kubwa mno na wakulima wengi wamefanikiwa kutokana na zile treka.

Mheshimiwa Naibu Spika, pale Nyumbu karakana ile inaweza wakaagiza engine tu peke yake wana karakana wanaweza kufyatua ma-mudguard, wakafyatua chassis, wakafyatua mambo mengi pale tukaagiza vitu vichache mno vikawa-assembled ndani ya karakana ya Nyumbu. Nyumbu pale tunaweza tukatengeneza risasi, Nyumbu pale wanaweza wakatengeneza silaha ndogo ndogo hizi ambayo kwa nchi kama nchi tunaweza tuka-export kwa nchi jirani.

Mheshimiwa Naibu Spika, Nyumbu ni kitu kikubwa sana wewe ukienda pale ndio unajua hapa kweli nchi ipo hapa. Ni suala la kukaa kuwekwa teknolojia, kuona bajeti yake, kuhuisha mashine zile wakakaa kama Jeshi, mimi naamini jeshi ni watu wakubwa mno na wanaelimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndani ya Jeshi kuna watu wamesoma kwelikweli, juzi tu pale kwenye msiba wa aliyekuwa Rais wetu zilivyopita zile ndege uliamini kama kuna ma-pilot wa aina hiyo. Ndege inaenda inabinuka inarudi namna hii. Kwa hiyo, utaona jeshi lipo vizuri na wanaweza wakafanya kazi vizuri, yaani mimi sasa hivi nimeona jeshi la umuhimu hapa tunatembea kwa amani tu, kumbe kuna watu kule wamekaa wanatulinda. Huwezi kujua wamekaa kwa muda gani, tunafanya kazi zetu vizuri, tunafanya mambo yetu vizuri, tunafanya biashara vizuri, tunafanya vitu vyetu vizuri, nchi leo ya Tanzania hii ni nchi katika nchi tatu Afrika ambazo mpaka leo hazijawahi kuingia kwenye misukosuko ya mapinduzi kwa sababu ya jeshi letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, historia ya Jeshi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni pamoja na Afrika Kusini, huwezi kusema Uhuru wa Afrika Kusini waliopata kule bila kuwataja Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Huwezi kusema Zimbabwe bila kuwataja Jeshi la Wananchi wa Tanzania, huwezi kusema leo Congo kuna vijana wetu wapo Congo, vijana wetu wapo Central Africa, vijana wetu wapo Lebanon, bila ya kuwataja Jeshi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hiyo ni kazi kubwa mno wanaifanya kwa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mimi nilikuwa nataka watoke hapo tuingie, tuiboreshe Nyumbu iweze kuzalisha magari kwa ajili ya matumizi ya kijeshi, wazalishe risasi kwa ajili ya matumizi ya jeshi, waweze kuzalisha bunduki kwa ajili ya matumizi ya jeshi ndani ya nchi na kuweza kuuza ikiwezekana hata kuingia partnership na mashirika mengine ya private.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda Urusi, risasi hizi na silaha zao zinatengenezwa na private sekta lakini chini ya ulinzi wa Serikali ya Urusi. Ukienda China hizi hizi risasi, hizi hizi silaha na mabomu mengine madogo madogo yanatengenezwa na private sekta lakini chini ya usimamizi wa jeshi la nchi husika na hiyo inawezekana tu, ni suala la kukaa, kupanga, kuona tutoke hapa sasa jeshi letu tuliwezeshe kuwa katika jeshi moja bora katika Afrika Mashariki na Afrika nzima kwa ujumla wake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, maslahi ya wanajeshi; wanajeshi tuwatizamie maslahi yao. Mheshimiwa Msukuma alisema nyumba bora, ni kweli, tuwatengenezee namna ambavyo watakavyoweza kuishi vizuri wanajeshi wetu. Ikiwezekana hata kuwaongezea maslahi bora kidogo. Wanajeshi wanavyofanya kazi, yaani wanakuwa na mazingira, unaweza kukuta mwanajeshi mmoja yuko sehemu huku mke wake labda yuko huku, akihamishwa huku, anatafuta ka-chance kadogo tu, Jumamosi, Jumapili anakwenda kumuona mke wake anarudi kwa ajili ya ulinzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wako katika mazingira magumu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kama kuna namna yoyote ya kuweza kuona maslahi yao, tuweze kuona maslahi yao hata kuwaongeze posho au mishahara au kuwatengenezea malazi mazuri na makazi mazuri, wahisi kwamba wao wapo kwa ajili ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nimpongeze tena General Mabeyo kwa kazi kubwa anayoifanya mungu akubariki sana, tuko pamoja sana, tutasaidiana sana, sisi kama Bunge wala hatua wasiwasi na naunga hoja mkono. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Mimi binafsi naunga hoja mkono kwenye Wizara hii ya Maji. kama kuna siku ambayo mimi binafsi Mbunge wa Jimbo la Solwa sina changamoto nyingi kwenye Jimbo la Solwa kwenye suala zima la maji kama awamu hii awamu ya sita. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nchi yetu ni kubwa na ninajua kabisa Mama yetu Rais wetu mpendwa kubwa anaifanya sana; anaitendea haki Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania. Ninajua sana chini ya Wizara ya Maji chini ya Waziri Mheshimiwa Aweso, Naibu wake na timu nzima ya Wizara ya Maji mnaitendea haki Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Solwa mwaka 2005 tulikuwa tuna vijiji 16 tu vyenye maji ya Ziwa Victoria. Lakini tulikwenda awamu baada ya awamu uvumilivu na ustahimilivu chini ya Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi miradi ambayo inatekelezwa sasa hivi katika Jimbo la Solwa ni mingi.

Mheshimiwa Spika, Ukianza na mradi wa Masengwa package vijiji vinane awamu ya pili wenye gharama ya bilioni 4.7 wakandarasi wako kazini wanafanya kazi. Mradi huu una awamu tatu. Mpaka tunamaliza awamu tatu tutakuwa tuna vijiji 12. Katika Masengwa Package tuna Kijiji cha Ishnabulandi, Bubale, Idodoma, Isela, Ibingo, Mharanga, Mwamara na Nalibanza katika kata ya Mhamara. Tumeshajenga tenki Ishnabulandi na sasa hivi inajengwa tenki Mwamara kwenye kata ya Mwamara.

Mheshimiwa Spika, Ndugu zanguni katika Jimbo la la Solwa tuna vijiji vingine sita ambao unagharimu zaidi ya bilioni tatu Jimbo la Solwa tu hilo Mwandutu, Mwabageu, Maemiru, Mwasenge, Mwongozo, na Mwenge vijiji sita tayari wanakunywa maji ya Ziwa Victoria.

Mheshimiwa Spika, katika Tinde package kuna vijiji 22 hata Makamu wa Rais alipokuja kuzindua ule mradi pale tinde walikuja pamoja na Mheshimiwa Waziri sasa hivi mabomba yanalazwa kwenda kwenye Kijiji cha Jomu kwenye Kata ya Tinde. Kata ya Tinde nadhani Waheshimiwa Wabunge wengi mnaifahamu, ni junction kubwa sana ambayo kila mtu lazima aipite kwa maana ya kwamba kama anakwenda nchi jirani.

Mheshimiwa Spika, vijiji 22 lakini katika Kijiji cha Jomu sasa hivi mabomba yanalazwa. Kwa hiyo mwezi wa sita wataanza kunywa maji ya Ziwa Victoria. Mradi huu una-cost bilioni sita. Kata za Mwamara, Didia, Tinde, Osanga pamoja na Nsalala katika Tinde package hii ambayo sasa hivi nafikiri na nina Imani kabisa Wizara wanafanya mchakato wa kuleta fedha ili tukamilishe. Hoja yangu na ombi langu kwa Mheshimiwa Waziri, tunapoomba fedha kwa ajili ya kukamilishaji kwa ajili ya Tinde package nikuombe sana ije kwa wakati ili miradi hii yote ikamilike kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mwalukwa kuna miradi pia sasa hivi inatekelezwa katika vijiji vitatu, kwa kushirikiana na life water, tunawashukuru sana. Tunaendelea, na mradi utaisha baada ya miezi mitatu minne na wenyewe watakunywa maji ya Ziwa Victoria, lakini pia Kilimawe bilioni 304. Kilimawe kijiji kiko ndani sana lakini tunapeleka maji kwa kuwashirikiana na life water, RUWASA wanasimamia pale. Pia Mwashagi katika zile fedha za COVID tumepeleka maji. Vilevile kwenye Kata ya Mwakitorio, nafikiri hata Mheshimiwa Waziri amekuwa akiitolea mfano sana kwenye mikutano yake yote; ule mradi ulitusumbua sana. Sasa hivi kwenye Mwakitorio wenyewe kijiji hicho wanakunywa maji.

Mheshimiwa Spika, vilevile Mheshimiwa Waziri alitoa maelekezo ya kujenga tenki, tenki limeisha, linachukua lita laiki tano, ambalo litahudumia vijiji vitatu, ambavyo ni Mwakitorio, Nyarigongo, na Nyang’ombe. Hivi ninavyoongea kwa faida ya wananchi wa Nyerigongo na Nyang’ombe niwaambie tu mabomba yameshashushwa pale Ofisi ya RUWASA, wiki hii hii na wiki ijayo tutapeleka mabomba kulaza ili wananchi wa Kijiji cha Nyerigongo na Nyang’ombe wapate maji ya Ziwa Victoria.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi tunaomba fedha kwa ajili ya usanifu wa vijiji 22 vingine. Nimuombe sana Mheshimiwa Waziri, vijiji 22 vingine vya Kata za Ryabukande, Iryamidati, Ilola, Bukene, Usule pamoja na Puni, tulikuomba fedha hizi utuletee ili tukamilishe vijiji 22. Tunajipanga kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Ndani ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi asilimia 85 kupeleka maji vijijini, yaani tuwe tumekamilisha kufikia 2025. Miradi hii yote ikikamilika sasa sisi kwenye Jimbo la Solwa tutafika asilimia 87 kufika 2025, na tutakuwa na vijiji 105 ndani ya vijiji 126.

Mheshimiwa Spika, ni miujiza. Yaani wakati mimi nasoma shule nilikuwa nikitoka Kijiji cha Mhangu ninakwenda, kuna wakati kama kuna ukame, mnachukua gari kwenda kuchukua maji kilomita 30 ambako Serikali ilichimba bwawa moja kubwa sana kwenye Kata ya Nindo pale Selamagazi. Unatoka kule unaenda kuchukua maji wengine walikuwa wanakwenda kwenye Malambo kule.

Mheshimiwa Spika, ukikumbuka enzi hizo wakati nasoma mpaka sasa hivi nimekuwa Mbunge wa Jimbo la Solwa, kwa kushirikiana na chama changu utekelezaji wa ilani chini ya awamu ya sita leo tumefanya maajabu na miujiza mikubwa mno katika Wizara hii ya Maji

Mheshimiwa Spika, mimi niseme tu ndugu zanguni tumpe Mama moyo mkubwa sana katika awamu ambayo mimi nimefanya kazi kwenye Jimbo la Solwa hakuna fedha nyingi zimekuja kama awamu hii ya sita yenye miradi yote ikiwemo miradi ya maji. Vilevile nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri Aweso, Aweso chapa kazi wewe mdogo wangu uko vizuri sana. Sina tu cha kusema. Sisi tukuiingia Mskikitini kuswali tunakuombea dua. Zaidi ya kuombea dua ufanye kazi yako vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine niombe tu Engineer wangu Meneja Eng. Nkopi, anakaimu, hebu ichukue hii tumthibitishe, mthibitisheni huyu. Mimi nimefanya kazi na ma-engineer wengi sana hakuna engineer ambaye unafanya naye kazi unamuelewa anasimamia…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Haya, kengele ya pili imeshagonga.

MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Spika, naomba tu athibitishwe na alatewe gari ili kazi tufanye vizuri na nawashukuru sana katibu mkuu meneja wa maji vijijini, wote kwa pamoja Mungu awabariki sana nawashukuru sana ahsante sana.