Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Answers to supplementary Questions by Hon. Anthony Peter Mavunde (509 total)

MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu mazuri aliyoyatoa. Tatizo la ajira katika nchi yetu, na hasa kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu limekuwa ni kubwa sana, kama kwa mwaka mmoja inaonyesha idadi hiyo bado hawana ajira.


Je, Mheshimiwa Waziri anaweza kuliambia Bunge hili ni lini hasa watakuja na mkakati wa kuanza kutoa labda mikopo midogo midogo ambayo itakuwa ni mitaji kwa hawa vijana ambao wanamaliza Vyuo vya Elimu ya Juu ambao hawana kazi kwa muda mrefu?, hilo swali la kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa sasa inaonekana kwamba Serikali bado haina orodha kamili ya wahitimu wa Vyuo Vikuu ambao hawana kazi.


Je, Mheshimiwa Waziri anaweza kukubaliana na mimi kwamba umefika wakati sasa kuanza kuwa na data bank ya kujua wahitimu wote wa Vyuo vya Elimu ya Juu ili kuweza kujua ni ujuzi wa aina gani na weledi wa namna gani ambao upo katika nchi hii, na kuweza kuwashauri waajiri mbalimbali na sehemu mbalimbali? Nakushukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WALEMAVU - (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, katika hoja ya kwanza ya mikopo midogo midogo Serikali inatambua ya kwamba asilimia kubwa ya wahitimu hawa ambao wengi wangependa pia kufanya shughuli za kujiajiri wanakabiliwa na tatizo kubwa la upatikanaji wa mikopo.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeandaa programu ambayo itasaidia katika upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi waliohitimu elimu ya vyuo vikuu ambapo ziko fedha, ambazo zitatolewa kwa ajili ya wahitimu hao kupitia vikundi vyao na kampuni mbalimbali ambazo zitaundwa.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, ipo Kampuni ya Wahitimu kutoka SUA ambayo inaitwa SUGECO, wenyewe walipatiwa fedha za mikopo na wanaendelea na shughuli za uzalishaji mali. Kwa hiyo, mipango hiyo ipo na itaendelea kuwepo.

Pili, katika suala la orodha kamili ya wahitimu, Serikali imekuwa ikifanya tafiti kila mwaka kuweza kubaini ni asilimia ngapi ya vijana ambao hawana kazi waliohitimu Elimu ya Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu. Ilianza kuanzia mwaka 2006 kutumia utafiti wa labour force survey ambayo ilifanyika mwaka 2006/2014. Utafiti huo unahitaji fedha, kila mara fedha inapopatikana utafiti huu umekuwa ukifanyika na huwa unafanyika kila baada ya miaka mitano.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaendelea kufanya utafiti kupata taarifa kamili ya vijana hao ambao wamehitimu elimu ya juu na hawana ajira ili tuone hatua stahiki za kuchukua.
MHE. ESTHER M. MMASI: Mheshimiwa Naibu Spika, moja kati ya mipango ya Serikali ni pamoja na kuinua ujuzi wa vijana wahitimu kutoka vyuo vikuu kutoka asilimia 2 mpaka 12. Je, nini mpango wa Serikali katika kutekeleza mikakati hii hadi kufika mwaka 2019/2020?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, moja ya mikakati ya Serikali katika kuinua sekta ya ujasiriamali kwa vijana wa Kitanzania ni pamoja na kuwekeza kiasi cha shilingi bilioni 1.6 kupitia Mfuko wa Vijana, Baraza la Uwekezaji la Taifa.
Je, Serikali ina mkakati gani katika kuanzisha Baraza la Taifa la Vijana ili kuongeza ufanisi lakini pia kuongeza fursa nyingi na wanufaikaji wengi kupitia Mfuko huu wa Vijana?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la tatu, kupitia …
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther, maswali ni miwili tu.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WALEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la kwanza aliulizia kuhusu mpango wa ukuzaji ujuzi, nataka tu nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tumekwishaanza mpango mkakati wa kukuza ujuzi ambao utahusisha wahitimu mbalimbali wa vyuo vikuu, lakini na wanafunzi ambao bado katika vyuo vikuu. Katika mpango wetu huu utahusisha pia mafunzo ya uanagenzi pamoja na internship na lengo lake ni kukuza ujuzi kwa wanafunzi na wahitimu wa vyuo vikuu.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini katika swali lake la pili ameulizia kuhusu Baraza la Vijana la Taifa na nataka nimpe tu taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari Serikali na Bunge hili lilipitisha Sheria Na.12 ya Uundwaji wa Baraza la Vijana la Taifa na tayari Kanuni zimekwishakamilika kwa ajili ya kuanza rasmi uundwaji wa Baraza hili ambalo litakuwa likiwakilisha matatizo mbalimbali ya vijana lakini pia litakuwa sehemu ya kisemeo cha vijana katika kuwasilisha matatizo mbalimbali ambayo yanawakabili.
Kwa hiyo, tunaamini kupitia Baraza hili, vijana watakuwa wamepata sauti na sisi kama Serikali tutakuwa sehemu ya kushirikiana nao katika kutatua kero na changamoto ambazo zinawakabili vijana.
MHE. SAUMU H. SAKALA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, sasa Waziri anaweza kukubaliana nami kwamba kuna uhaba mkubwa wa elimu juu ya suala la sheria hizi na kwamba muda umefika sasa Serikali iweze kutilia mkazo juu ya kutoa elimu hii kwa wafanyakazi pamoja na waajiri?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, mpaka sasa Serikali imekwishashughulikia waajiri wangapi ambao kwa namna moja au nyingine wamewabagua wafanyakazi ambao tayari wamejiunga katika Vyama vya Wafanyakazi?
NAIBU WAZIRI WA SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WALEMAVU (MHE. ANTHONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la kwanza la elimu juu ya Sheria za Kazi, Wizara yetu imeendelea kutoa elimu hiyo kupitia Vyama vya Wafanyakazi, pia kupitia makongamano na warsha na semina mbalimbali, kuweza kuwaelimisha wafanyakazi, waajiri na umma kwa ujumla namna ambavyo sheria zetu zinaelekeza mambo gani yatiliwe mkazo. Hata hivyo, tunaendelea kutilia mkazo eneo hili na tutakuwa na vipindi tofauti kupitia katika redio na televisheni ili Umma wa Watanzania uweze kufahamu namna gani sheria hizi zinafanya kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia nichukue wito huu kuwaomba wenzetu wa Vyama vya Wafanyakazi kwa kushirikiana na Wizara, tufanye kazi hii kwa pamoja ili tuweze kuwaelimisha waajiri na wafanyakazi sheria za kazi zinavyoelekeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika sehemu ya pili ya swali lake, amezungumzia kuhusu idadi ya waajiri wangapi tumekwishawashughulikia ambao wamewabagua wafanyakazi. Ofisi yetu kupitia Maafisa Kazi ambao wamekuwa wakifanya kaguzi mara kwa mara, wamekuwa wakipita maeneo tofauti kubaini matatizo haya na kuwachukulia hatua wale waajiri ambao wanashindwa kutii masharti ya sheria, hasa hii Sheria Na. 6 ya Mwaka 2004.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maana ya idadi, nitamtafuta Mheshimiwa Mbunge nimpatie taarifa kamili ni kwa namna gani tumewashughulikia hao waajiri waliowabagua wafanyakazi wao specifically, lakini tumekuwa tukifanya kaguzi hizi na tunayo orodha ya waajiri wengi tu ambao wameshindwa ku-comply na orders zetu ambazo zimefanyika baada ya ukaguzi.
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, lakini nina swali moja la nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, vimetajwa vigezo vingi sana hapa, lakini vigezo hivyo inaweza ikawa ni sababu ya kutoleta maendeleo katika maeneo husuka. Je, Serikali haioni umuhimu kwamba kigezo cha jiografia tu kinaweza kutosha kugawanya Jimbo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Katiba yetu, Ibara ya 75(1) mpaka (6) imezungumzia vigezo na sifa za ugawaji wa Majimbo ndani ya nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, vigezo vilivyotajwa ndani ya Katiba ni pamoja na hali ya kijografia, lakini mwaka 2010 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikwenda kufanya tafiti katika nchi za SADC na kubaini baadhi ya vigezo vingine ambavyo vinasaidia katika ugawanyaji wa Majimbo.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge katika pendekezo lako hilo, kama Serikali tunalichukua, lakini pia viko vigezo vingine vingi vya ziada ambavyo vilikuwa vikitumika katika ku-determine Majimbo yagawanywe katika mfumo upi, vingine vikiwa ni pomoja na hali ya kiuchumi, lakini settlement pattern na yenyewe huwa ni kigezo cha kuweza kutolewa ili Majimbo haya yaweze kugawanywa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, pendekezo la Mheshimiwa Mbunge tunalichukua kama Serikali, lakini nimpe pia habari ya kwamba tumekuwa tukichukua na vigezo vingine ambavyo vimeainishwa katika Katiba yetu, vilevile na utafiti uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, leo muda wetu umebana kidogo kwa ajili ya shughuli zilizo mbele yetu. Kwa hiyo, tunaendelea na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt. Elly Marco Macha, Mbunge wa Viti Maalum, swali lake litaulizwa na Mheshimiwa Amina Mollel.
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini inafahamika kabisa kwamba vyama hivyo vya wafanyakazi vinakuwa vinachukua matakwa na mahitaji ya wafanyakazi wenyewe. Na kwa kuwa Serikali imekuwa ikiwasaidia sana waweze kuingia katika vyama hivi na Serikali hapa imetoa agizo kwamba itawachukulia hatua waajiri ambao wanawazuia kujiunga na vyama hivi.
Je, Serikali inatoa tamko gani kwa sababu baadhi ya wafanyakazi wanakuwa wamefanya kazi lakini wanakuwa na madai yao mbalimbali ambayo hawajalipwa na Serikali. Kwa mfano, Chama cha Walimu Tanzania kina madai mengi sana Serikalini lakini madai hayo bado hayajalipwa. Je, kupitia bajeti hii, Serikali itatoa tamko la kuwalipa walimu madai yao na malimbikizo yao?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu tamko Serikali itasema nini, naomba nirudie katika majibu yangu ya msingi ya kwamba Serikali kupitia Sheria Namba 6 ya mwaka 2004 imeendelea kutoa msisitizo kuwataka waajiri wote kuruhusu wafanyakazi wajiunge katika vyama vya wafanyakazi. Na jambo hili ni la kisheria na Kikatiba, na vilevile sisi Tanzania tumekubaliana na ile ILO Convention Namba 87 ambayo inazungumza kuhusu uhuru wa wafanyakazi kujiunga katika vyama vyao.
Kwa hiyo, nichukue tu fursa hii pia kuwataka waajiri kwa kutoa tamko tena ya kwamba wahakikishe kwamba wanawaruhusu wafanyakazi wao wote kujiunga na vyama vya wafanyakazi kwa sababu hii ni haki yao ya kimsingi ya kushirikiana kama ambavyo imesemwa kwenye sheria na kwenye Ibara 20 ya Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuongezea katika majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri,katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Ni kwamba, katika suala zima la madai ya walimu, tumezungumza kwamba sasa hivi Ofisi ya Rais - TAMISEMI inafanya uhakiki wa madai yote. Lengo letu kubwa ni kuhakikisha kwamba walimu wote ambao wanadai, na si walimu peke yake bali katika kada mbalimbali, katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha unaokuja basi madai yote tuweze kuya-address; kila mtu afanye kazi kwa morale katika mazingira yake ya kazi.
MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Mwenyekiti nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.
Kwa walimu wamejiunga na PSPF lakini walimu hawa wanapoomba mikopo watu wa PSPF wanachelewa sana kuwapa majibu na kuwakamilishia haki yao ya msingi ambapo wengine wanakuwa wamekaribia kustaafu wanataka wajiandae. Je, Serikali inawaelezaje walimu hawa ambao wanakaribia kustaafu na wanahitaji wapate huo mkopo wanawacheleweshea kuwapa mkopo huo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli ni haki ya walimu waliojiunga katika mfuko wa PSPF kupata mkopo pale ambapo wamekidhi yale masharti yanayohitajika, kwa maana umri ule wa kustaafu ambao kwa mujibu wa taratibu za sasa za mfuko ule, tayari wamekwishakuanza kutoa mikopo kwa walimu ambao wamekaribia umri wa kustaaafu kuanzia miaka 55 wakishapeleka maombi yamekuwa yakifanyiwa kazi.
Nichukue tu fursa hii kuwaomba walimu wote ambao watakuwa wamekidhi masharti na vigezo vya kupata mkopo basi wafike katika ofisi zao kwa ajili ya kuweza kupata huduma hiyo.
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, wakulima, wafugaji, mafundi na kila mmoja katika Taifa hili ambaye amefikia umri wa miaka 60 amelitumikia Taifa hili kwa njia mbalimbali. Wakulima ndio waliolima chakula ambacho kinaliwa na watumishi wa Serikali, kwa maana ya kwamba utumishi wao unakuwa pensionable baadaye. Wafugaji ndiyo waliofuga mifugo ambayo tunatumia maziwa, nyama na kila kitu. Wajenzi ndiyo waliojenga nyumba ambazo watumishi wa Serikali wanaishi, lakini Taifa hili limekuwa likilipa watumishi wa Serikali tu pensheni lakini watu wengine waliolitumikia Taifa hili kwa njia moja au nyingine hawalipwi pensheni na mpaka sasa Serikali imekuwa ni mchakato na nyimbo mbalimbali.
Je, Serikali inataka kutuambia kwamba hawa watu hawakuwa muhimu katika utumishi wao kwa Taifa hili ndio maana mpaka sasa hawajaanza kulipwa pensheni? (Makofi)
Swali la pili, wimbo wa mipango, michakato, maandalizi umekuwa ni wimbo wa kawaida katika nchi hii, nataka Waziri atuambie, ni lini sasa Serikali itaanza kulipa wazee hawa ili waache kuteseka, wengine mnaona wanauawa kule vijijini Usukumani huko kwamba ni wachawi kwa sababu tu hawana pesa za matumizi na wana...
MHE. ANTONY P. MAVUNDE - NAIBU WAZIRI (SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WALEMAVU): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa wananchi wote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na inathamini mchango wa kila mmoja. Serikali inafahamu na inathamini mchango wa wazee wetu walioutoa katika ujenzi wa Taifa hili katika nyanja tofauti za kiuchumi, kiutamaduni, kijamii na kisiasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhamira ya Serikali kutekeleza mpango huu kwa wazee wote ambao wametumikia Taifa hili. Nimwondoe tu hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba dhamira ya Mheshimiwa Rais na Ilani ya uchaguzi ya CCM inavyosema mpango huu utatekelezwa kwa ajili ya wale wote ambao walitoa mchango wao kwa Taifa hili bila ubaguzi wowote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili amezungumza ya kwamba imekuwa ikisemwa kila mara mipango, michakato na ni lini Serikali itatekeleza mpango huu. Suala hili la mpango wa pensheni kwa wazee ni suala ambalo lilikuwa linahitaji maandalizi ya kutosha na zipo taratibu ambazo zilikuwa zimekwishatekelezwa na imebaki hatua chache za kuweza kwenda kutekeleza mpango huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimwondoe hofu tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika mchakato huu zipo prerequisites ambazo lazima kwanza zitekelezwe na zifanyiwe kazi, huwezi kwenda tu moja kwa moja mpaka upitie katika utaratibu kwamba ni namna gani kuona mpango huu utatekelezeka. Nimtoe hofu kwamba ni dhamira ya Serikali lakini vilevile ni ahadi ya Mheshimiwa Rais na hili litatekelezeka. (Makofi)
MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri, lakini pamoja na majibu hayo, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa vijana ndio nguvu kazi ya Taifa hili na kwa kuwa vyuo vikuu vinazalisha vijana asubuhi na jioni wenye elimu nzuri ya kufanya ujasiriamali, lakini tatizo ni wapi watapata mikopo kwa njia rahisi zaidi na kwa riba nafuu zaidi? Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia hawa vijana kupata mikopo kwa urahisi na kwa riba nafuu zaidi?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa ajira ambayo ni rahisi kwa vijana na hasa kwa wanawake pia ni kilimo; lakini kilimo kinacholimwa kwa sasa hakina tija; kwanza, masoko hayapo kwa urahisi, mazao mengine yanaoza mashambani; lakini la pili, maeneo ya kulima. Vijiji vingi havijatenga maeneo kwa ajili ya kilimo kwa vijana na hata kwa wanawake ambao wameshajiunga kwenye vikundi mbalimbali. Je, Serikali iko tayari kutenga maeneo na kuzihimiza Halmashauri zetu kutenga maeneo kwa ajili ya vijana na hata kwa wanawake ambao wako tayari kuwa wajasiriamali kupitia kilimo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA) Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza na la kwanza la mikopo na mitaji kwa wahitimu wa elimu ya vyuo vikuu na elimu ya juu, ni kweli natambua kwamba vijana wengi sasa hivi wanapenda kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali hasa kilimo, lakini changamoto kubwa wanayokutana nayo ni ukosefu wa mitaji na mikopo.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeliangalia hili kwa macho mawili na katika mtazamo wa mbali kuhakikisha kwamba vijana hawa wanapata fursa ya mikopo na mitaji kwanza kabisa kupitia Mfuko wetu wa Maendeleo ya Vijana ambao umekuwa ukikopesha makundi mengi ya vijana kupitia SACCOS ambazo ziko katika Halmashauri zetu. Vilevile tumeendelea kuwa na msisitizo kwa kuwataka vijana hawa wajiunge katika makampuni na vikundi mbalimbali ili waweze kupata fursa ambazo zinatokana na mikopo na mitaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia tunayo program maalum sasa hivi kupitia Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi, ambapo tuna program ya Kijana Jiajiri inahusisha young graduates, wanaandika proposals zao wanazi-submit katika baraza na baadaye wanapatiwa mikopo na mitaji. Pia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi imezungumza kuhusu kuwawezesha vijana wakae katika vikundi na makampuni kutumia fani zao na taaluma zao mbalimbali ili waweze kukopesheka.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe tu rai kwa vijana wote wale wa vyuo vikuu na wahitimu wa elimu ya juu kutumia fursa hii ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na mikopo inayopita katika Halmashauri zetu kwa kukaa katika vikundi na makampuni.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, limeulizwa swali kwamba Serikali ina nia gani ya kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za kilimo? Mwaka 2014, Wizara yetu ilikutana na Wakuu wa Mikoa wote nchi nzima hapa Dodoma na likatengenezwa azimio, ambapo moja kati ya kilichoamuliwa ni kutengeneza kitu kinaitwa Youth Special Economic Zone, ni ukanda maalum ambao utakuwa unasaidia utengaji wa maeneo kwa ajili ya shughuli za vijana. Mpaka sasa tayari ekari 8000 zimeshatengwa nchi nzima kwa ajili ya maeneo haya ili vijana waweze kufanya shughuli za kilimo na biashara.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia tumezungumza na Waziri wa Kilimo, yako mashamba makubwa ya Serikali ambayo wanayafanyia utaratibu sasa hivi nayo tuweze kuyatenga kwa ajili ya kuwagawia vijana waweze kufanya shughuli za uzalishaji mali.
MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii adimu. Pamoja na majibu yaliyotolewa na Naibu Waziri, ipo nguvu kazi nzuri sana katika nchi hii iliyotafuta ajira binafsi; vijana wa bodaboda. Hawa vijana wa bodaboda tunawatumia vizuri wakati wa uchaguzi, baada ya uchaguzi, wanapata misukosuko ya kufa mtu. Wanasumbuliwa na Polisi. Bodaboda wangu waliopo Kakonko na nchi nzima, hawa bodaboda tunawalindaje katika ajira zao hizi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, hata mimi nataka nikiri kwamba kundi hili ni kundi ambalo kwa kiwango kikubwa sana, asilimia kubwa tuliopo hapa tuliwatumia katika kampeni zetu na ndio wametufanya tumefika katika jengo hili. Vile vile nataka nikiri tu kwamba, bodaboda ni biashara ambayo sisi tunaamini kwa kiwango kikubwa sana kwamba inasaidia katika kutatua changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali katika eneo hili imefanyaje? Kwanza kabisa, Serikali kwa kushirikiana na mamlaka zile husika hasa mamlaka za Halmashauri ya Manispaa na Majiji, kwanza kabisa kutenga maeneo maalum na kuwatambua na kazi yao iheshimiwe. Pili, tuna program maalum kupitia Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya ukopeshaji wa pikipiki, hizi bodaboda ili vijana wetu hawa ambao asilimia kubwa sana wanafanya kazi kwa watu wapate fursa ya kukopa wenyewe moja kwa moja na pikipiki zile ziwe mali zao na ziwasaidie katika kuinua uchumi wao.
MHE. SAUMU H. SAKALA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Suala hili la wazee kulipwa pensheni kila siku limekuwa likitajwa, lakini nashangaa kidogo nikisikia bado hata hayo maandalizi hayajaanza. Je, Serikali inaweza kusema nini kinakwamisha maandalizi hayo ambayo mpaka sasa hayajaanza na kwa kutambua umuhimu huo wa wazee?
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, maandalizi hayo yataanza lini na yatamalizika lini? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Saumu Heri Sakala, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza limeuliza ni nini kinakwamisha. Kwanza kabisa nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ina dhamira njema kabisa ya kuhakikisha inatekeleza ahadi yake ya kuwalipa pensheni wazee kwa kutambua mchango mkubwa ambao wazee wameutoa katika Taifa hili katika sekta za huduma za jamii, kiuchumi na kisiasa. Kwa hiyo, Serikali inatambua kabisa umuhimu wa wazee.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kinachokwamisha hapa si kwamba kuna jambo ambalo linakwama, lakini mipango ya Serikali ilikuwa kwanza kuhakikisha inatengeneza miundombinu ambayo ndiyo itakwenda kulifanya jambo hili liwe endelevu. Kwa hiyo, katika uratibu wa zoezi zima, awali ilikuwa ni kutayarisha mpango rasmi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba mpango huu unaanza kufanyiwa kazi na tayari mpango huu umekamilika zimebaki hatua chache tu za kuona ni namna gani mpango huu utaanza sasa kutekelezwa pale ambapo mamlaka husika zitahusishwa na fedha zitakuwa zimepatikana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ameuliza ni lini itaanza. Nirudie tu katika jibu langu la msingi kwamba zoezi hili ni kubwa sana ambalo linahitaji umakini mkubwa sana na lengo la Serikali ni kulifanya kuwa endelevu. Hata katika baadhi ya nchi ambazo wamefanya zoezi hili kwanza kabisa walifanya namna ambavyo ilikuwa inawapa picha waanzaje ndiyo baadaye waje walikamilishe kwa uzito wake. Kwa hiyo, na sisi kwa kutambua kwamba jambo hili ni kubwa na linahitaji rasilimali fedha, Serikali imeanza kwanza na ujenzi wa miundombinu ya kuratibu zoezi zima ili baadaye kuweza kuwafikia wazee hawa kwa maana ya kuwalipa pensheni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kufuatilia jambo hili tulikwenda kujifunza katika baadhi ya nchi ambazo zimefanikiwa sana. Ukienda kule Nepal ambao ni kati ya watu waliofanikiwa, wana kitu wanakiita Nepal’s Senior Citizens’ Allowance na wenyewe walianza katika utaratibu huu huu. Walianza kwanza kuwalipa wazee kuanzia umri wa miaka 60 lakini baadaye wakaona namna gani waweze kuingiza na makundi mengine. Kwa hiyo, na sisi tunatafakari mpango huu mzima lengo letu ni kuufanya mpango huu uwe endelevu.
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, napenda kuuliza swali dogo la nyongeza.
Kwa kuwa waathirika wengi wa ulemavu, kama alivyosema Mheshimiwa Amina Mollel, katika migodi hii wanapata matatizo mengi sana wanapojikuta kwamba wanapoteza viungo vyao au wanapata ulemavu wakiwa kazini; na kwa kuwa waajiri wengi na hasa migodi hii wamekuwa hawalipi fidia wafanyakazi hawa wanaopata matatizo, na Sheria Namba 20 ambayo inaanza kutumika kuanzia mwezi ujao Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kwamba ndiyo itaanza kushughulikia masuala haya.
Je, kwa wale waajiri ambao wamekaidi kwa muda mrefu, Serikali inatoa tamko gani ili kusudi wafanyakazi hawa ambao wameumia wakiwa kazini waweze kupata fidia zao?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la msingi Mheshimiwa Mbunge anauliza Serikali inachukua hatua gani au inatoa tamko gani kwa waajiri wote ambao wanakaidi kuwafidia wafanyakazi ambao wameathirika kutokana na magonjwa yanayotokana na kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi, Sheria Namba Nane ya mwaka 2008 ambayo imeunda Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi kupitia kifungu cha tano cha sheria hiyo itaanza kufanya kazi tarehe 1 Julai, 2016.
Mheshimiwa Naibu Spika, lengo kubwa na maudhui ya Sheria hii ni kuhakikisha kwamba wafanyakazi wote wale ambao wamepata occupation diseases wanatibiwa kupitia mfuko huu; na wale ambao watakuwa wamepata ulemavu uliosababishwa na shughuli za kazi na wenyewe wanaweza kufidiwa au kupata mataibabu kutokana na aina ya ugonjwa walioupata kutokana na ripoti ya madaktari Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Serikali sasa inafanyaje? Katika mazingira haya kumtaka mwajiri atimize wajibu wake uko utaratibu ambao uko kwa mujibu wa sheria ambao umewekwa ya kwamba waajiri wote watatakiwa kwanza kuwasilisha michango yao kwa mujibu wa sheria ambapo Sekta Binafsi watatakiwa kuchangia asilimia moja ya wage bill ya kila mwezi, na katika sekta ya umma vilevile asilimia 0.5. sasa kwa wale ambao watakaidi kuchangia maana yake ni kwamba kwanza sheria inasema watatozwa fine ya riba ya asilimia 10 ya kile ambacho wamekichelewesha, lakini pili watapelekwa pia mahakamani na wakithibitika kwamba wameshindwa kuwasilisha michango hiyo adhabu ni kuanzia shilingi milioni 50 au pia kifungo kisichopungua miaka mitano mpaka kumi cha mkuu wa taasisi hiyo.
MHE. ABDALLAH H. ULEGA: Mheshimiwa Naibu Spika nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali fupi la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo la wafanyakazi hasa vijana kufukuzwa kazi kiholela, kutokulipwa stahiki pindi wapatapo ajali kazini, kulipwa ujira mdogo sana wa shilingi 4,500 kwa kutwa ya siku, kufanyishwa kazi kwa muda mrefu kinyume cha sheria na taratibu za nchi lipo pia katika Wilaya yangu ya Mkuranga.
Je Serikali ina mpango gani wa kuwalinda vijana hawa wafanyakazi ili waweze kazi zao kuwa ni kazi zenye staha? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ya kwamba Serikali kupitia Wizara ya Kazi tumekuwa tukisimamia sana Sheria Namba Sita ya mwaka 2004 ambayo imetoa haki na wajibu kwa wafanyakazi lakini na kwa waajiri pia. Sheria hii imetusaidia sana kutatua migogoro mingi mahali pa kazi, hasa pale inapoonekana sheria hii imekiukwa Serikali imekuwa ikichukua hatua stahiki kama ambavyo imekuwa ikionekana katika mazingira hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nikija katika swali lake la msingi sasa ya kwamba Serikali tunawalindaje hawa ambao wanafukuzwa kazi kiholela hasa pale wanapoonekana wamepata ulemavu wakiwa kazini.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nimkumbushe tu Mheshimiwa Mbunge kwamba kupata ulemavu ukiwa kazini sio kigezo cha dismissal na kwamba waajiri wote ambao wamekuwa wakikiuka taratibu hiyo ya sheria, sisi kama mamlaka ambayo tunasimamia sheria hizi kazi tumekuwa tukitoa elimu, lakini na kuchukua hatua stahiki.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia Mheshimiwa Mbunge nikuhakikishie tu ya kwamba tumekuwa tukiendelea kufanya kaguzi nyingi sana za kazi kwa lengo la kubaini haya mapungufu na tumekuwa tukichukua hatua pindi inapobainika kwamba mwajiri amekiuka sheria hizi. Kwa hiyo, sisi kama Serikali tutaendelea kusimamia Sheria Namba Sita ya mwaka 2004 kuhakikisha kwamba tunalinda haki za wafanyakazi na wafanyakazi hawa basi wasipoteze haki zao zile za kuwa wafanyakazi kwa kufukuzwa tu kiholela na mwajiri; na sisi tutahakikisha kwamba waajiri wote wanafuata sheria za nchi zinavyoelekeza.
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa swali la msingi limeeleza jinsi watumishi wa migodini wanavyofukuzwa kazi kiholela, pengine wakifanya kazi kwa miaka minane, saba wanafukuzwa kutokana na magonjwa mbalimbali, na Serikali imeondoa fao la kujitoa kwenye Mifuko ya Jamii ikiweka masharti kwamba mpaka miaka 55.
Je, hawa waliofukuzwa kazi wakiwa na miaka tisa na umri wa miaka 40 wanapataje fao lao kwa kusuburi miaka 50 Maana watakuwa na miaka 100?
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, Sera ya Hifadhi ya Jamii ambayo inaongoza masuala mazima ya Hifadhi ya Jamii katika nchi yetu ya Tanzania inaendana na Katiba ya nchi kifungu cha 11(1) ambacho Katiba ya nchi yetu inataka jamii kuangalia utaratibu mzima wa kuweka hifadhi ya wananchi na hasa pale wanapofikia umri wa uzeeni ama wanapopata matatizo mengine yoyote. Kwa hiyo, sera hiyo imekuwa ikituongoza kuunda mifuko hii ya Hifadhi ya Jamii kwa ajili ya kutoa kinga wakati wa uzeeni.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tumepata matatizo ya namna moja ama nyingine. Kadiri uchumi wa Tanzania ulivyoendelea kukua kumeongezeka sekta za kiuchumi ambazo unapata picha kabisa kwamba wafanyakazi ambao wamekuwa wakiajiriwa katika sekta hizo ni lazima watafanya kazi kwa muda mfupi sana, kama katika sekta za migodi, sekta za mashamba na sekta nyinginezo na hivyo basi kumekuwa na namna moja ama nyingine ya kuonekana kabisa kunahitajika kupitia tena sera ya Hifadhi ya Jamii, na kupitia sheria zetu ambazo zinaongoza Mifuko ya Hifadhi ya Jamiii ili kuyapitia mafao yanayotolewa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Kusudi la kufanya hivyo ndani ya Serikali ni kutazama kama sera na sheria tulizonazo zitakwenda kujibu matatizo ya wafanyakazi kama wa migodini kutokupata ama kupata fao la kujitoa kwa kuzingatia nature ya kazi zao. Haya yote yataongozwa na mikataba ya Kimataifa na sheria tulizonazo nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ninaomba nitoe wito kwa Watanzania na wafanyakazi wote watupe subira, na sisi Serikali tuko tunalifanyia kazi suala hili kwa nguvu. Nitoe onyo kwa waajiri wote wanaokiuka matakwa ya kisheria katika kuchangia mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa faida ya wafanyakazi. Na ninaomba niliarifu Bunge lako tukufu, tumeshaunda kikosi kazi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na tunakaribia kuanza kufanya ukaguzi wa nguvu kwa kuzingatia pia Sheria ya Tanzania Extractive Industries Transparency and Accountability na tutapambana na wale wote wanaofanya udanganyifu katika kuchangia mafao ya wafanyakazi na hasa migodini.
MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nashukuru pia kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kama nilivyosema kwenye swali langu la msingi tuna wataalam wengi katika sekta mbalimbali kama nilivyozitaja; na watalaam hao wapo hapa nchini na wengine wanafanya kazi za chini zaidi kuliko viwango vyao vya utaalamu na ujuzi. Je, Serikali haioni sasa kuna umuhimu wa kurejea Sheria hii ya Ajira kwa Wageni ili kwamba Watanzania hawa ambao wana ujuzi kwenye maeneo tofauti tofauti waweze kupewa au kuajiriwa nafasi hizi za juu kwenye NGOs na taasisi binafsi zilizoko hapa nchini? Swali la kwanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwenye majibu yake Mheshimiwa Naibu Waziri anasema mgeni anapoombewa kibali anarithisha utaalam kwa Mtanzania. Je, Serikali ina utaratibu gani wa kufuatilia kama kweli hawa watu walioajiriwa wanarithisha huo utaalam kwa Watanzania kwa sababu tunaona wanapewa hizi kazi halafu anaendelea kufanya kazi hizo miaka miwili, anamaliza mkataba anaongezewa miaka mitatu mingine, anaendelea nenda rudi. Sasa Serikali ina utaratibu gani wa ufuatiliaji juu ya jambo hili, ili kuhakikisha kwamba Watanzania ambao wako chini ya huyu ambaye atarithisha baadaye…
MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Wanapata hizi nafasi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza ameuliza Serikali haioni umuhimu wa kurejea sheria hii na ihakikishe kwamba inatekelezwa, ili Watanzania waajiriwe katika nafasi zao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema pale awali, Sheria hii Namba Noja ya mwaka 2015 ndio sheria ambayo inatusaidia katika uratibu wa ajira kwa wageni. Kwa hiyo, kabla ya mgeni hajaomba nafasi yoyote katika nchi yetu hii utaratibu ni kwamba, lazima Kamishna wa Kazi ajiridhishe juu ya ujuzi ambao mgeni huyo anao na nafasi ambayo anaiomba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimuondoe hofu tu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba tutaendelea kuisimamia sheria hii kuhakikisha kwa kwamba wale wageni wote wanaokuja na wenye ujuzi ambao unapatikana nchini, basi nafasi zao hizo wasipewe na badala yake Watanzania waweze kuchukua nafasi hizo. Hilo linafanyika na tumekuwa tukifanya kaguzi mbalimbali ambazo tumebaini baadhi ya wageni wengi ambao mwanzo walitoa taarifa za uwongo na baadaye baada ya kubaini kwamba, ni taarifa za uwongo tumefuta vibali vyao na nafasi zao wameendelea kupewa Watanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali la pili, alitaka kujua ni utaratibu gani ambao huwa tunautumia katika urithishaji wa ujuzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Sheria Namba Moja ya mwaka 2015, inaeleza wazi ya kwamba, mgeni yeyote ambaye anapata kibali cha kufanya kazi lazima kitengenezwe kitu kinaitwa succession plan ambayo inawasilishwa kwa Kamishna wa Kazi ya kuona ni namna gani mgeni huyu amekuwa ana Mtanzania ambaye anamu-understudy na anajifunza kupitia kwake. Kwa hiyo, ziko fomu maalum ambazo zinajazwa na kuwasilishwa kwa Kamishna wa Kazi kuthibitisha kwamba ni kweli kuna Mtanzania ambaye yuko chini na kweli ananufaika na ujuzi wa mgeni huyo.
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa vijana hawa wa Arusha ambao wamekuwa wakitumiwa na Mbunge huyu huyu kuandamana hawana ajira lakini inapofikia wakati wa kuwasilisha matatizo yao Bungeni Mbunge huyu akatolewa kwa ajili ya utovu wa nidhamu, je, Serikali haioni sasa ni wakati wa kuwasikitikia vijana wa Arusha kwa kuwapatia mafunzo na mitaji ili waendelee kutoa kura kwa Serikali hii sikivu ya Chama cha Mapinduzi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nataka niwaondoe hofu vijana wa Arusha. Pamoja na kwamba wamekosa kisemeo chao humu ndani kwa maana yule ambaye walimpa dhamana hayupo kwa ajili ya kuwasilisha matatizo yao lakini Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuwajali vijana bila kubagua. Sisi katika utekelezaji wa majukumu yetu mbalimbali tutahakikisha vijana wa Arusha kama vijana wa maeneo mengine na wenyewe wanapata fursa za elimu ya ujasiriamali, mikopo na mitaji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi binafsi nimeshafika pale Arusha na nimeshakutana na vijana wa SACCOS katika soko la Korokoroni na nimewaahidi kwamba nitarudi kwa ajili ya kuendelea kuwasaidia katika kupata mitaji na mikopo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nikuondoe tu wasiwasi ya kwamba kama Serikali vijana hawa tutaendelea kuwaangalia.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri lakini naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Catherine kuwa kisemeo kipya cha vijana wa Arusha na hasa kuendelea kuwa daraja la kutu-link kati ya Serikali na vijana wa Arusha ili waweze kufanikiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya 25 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasisitiza sana kwamba kazi ndiyo kipimo cha utu wa kila Mtanzania. Kifungu cha 28(b) cha Sheria ya Mwenendo ya Mashauri ya Jinai na chenyewe kinasisitiza sana masuala ya kila Mtanzania kuwajibika na apimwe kwa kuwajibika na aweze kukidhi riziki zake kwa kuwajibika yeye mwenyewe.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba niwaambie Waheshimiwa Wabunge, kama kuna Mheshimiwa Mbunge anawatumia vijana na kuwahamasisha wasifanye kazi anaenda kinyume na Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo basi kukiuka misingi yote ya utawala bora. Kwa hiyo, naomba kuwaambia Waheshimiwa Wabunge na vijana wote maelekezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais wetu ni sahihi. Vijana wanaweza kucheza pool katika saa ambazo si za kazi lakini saa za kazi kila mtu awajibike ili kuweza kupata riziki yake na kuweza kujenga uchumi wa nchi yetu ya Tanzania.
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipatia fursa ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa changamoto ya ajira imekuwa kubwa sana nchini hususan kwa upande wa vijana na kwa kuwa Halmashauri zimekuwa zinatenga asilimia 10 kwa ajili ya kukopesha akina mama na vijana lakini katika baadhi ya Halmashauri kumekuwa na changamoto kubwa. Je, Serikali haioni sasa ni muda muafaka kutenga kati ya asilimia 10 - 30 ya tenda zote za Serikali ili kuweza kuwapatia fursa za kujiajiri vijana?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli imekuwepo asilimia 5 ya mikopo katika kila Halmashauri kwa ajili ya vikundi vya akina mama na vijana na ambapo kwa kiasi kikubwa vijana na akina mama wengi wamekuwa wakinufaika kupitia mfuko huu. Pia kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM imeelezwa wazi kabisa kwamba moja kati ya mipango ambayo tunatazamia kutekeleza mwaka huu ni kuhakikisha tunatengeneza utaratibu ambapo kila Halmashauri itatenga asilimia 30 ya manunuzi yake ya ndani kwa ajili ya vikundi vya akina mama na vijana.
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba nimuulize maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, Ripoti ya Nane ya World Bank kuhusu Uchumi wa Tanzania inaonesha Watanzania milioni 12 wanaishi katika umaskini wa kutupwa, wengi wao ni vijana na kila mwaka takribani vijana laki nane wanaingia katika soko la ajira. Napenda kujua Serikali ina mpango wa kuzalisha ajira ngapi kwa mwaka?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, kwa kuwa Mkoa wa Pwani ni wa kimkatati unaounganisha kati ya Bara pamoja na Bandari za Mtwara, Dar es Salaam pamoja na Tanga, hata hivyo vijana wengi wa mkoa huu hawana ajira. Je, Serikali ina mpango gani wa kuelekeza viwanda Mkoani Pwani na ni viwanda vya aina gani? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Hawa Mchafu Chakoma kwa jitihada zake kubwa ambazo amekuwa akizionesha na mapenzi ya dhati aliyonayo kwa maendeleo ya vijana hapa nchini.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza ameuliza ni mipango ipi sasa Serikali imeweka ili kuzalisha ajira zaidi. Katika majibu yangu ya msingi nilieleza wazi kabisa kwamba pamoja na kuwa nafasi nyingi za ajira zinatengenezwa ndani ya Serikali lakini Serikali imekwenda mbele zaidi kuzipa umuhimu sekta za kipaumbele ambazo zitakuwa zinachukua vijana wengi zaidi. Lengo ni kuhakikisha tunawachukua vijana wengi zaidi kwa sababu asilimia kubwa ya wanaotafuta kazi wanajikuta wako katika informal sector, formal sector yenyewe inachukua watu wachache sana. Kwa hiyo, mpango wa Serikali ni kuhakikisha inaongeza fursa zaidi za ajira ili vijana wengi waweze kupata nafasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, sekta hizo za kipaumbele ni pamoja na kilimo kama nilivyosema pale awali lakini vilevile na uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo ambavyo vitakuwa ni labour intensive ili kuchukua vijana wengi zaidi. Hata katika Global Employment Trend ambayo ILO wameitoa mwaka jana inaonesha kwamba moja kati ya maeneo ambayo yanaweza yakachukua vijana wengi kwa wakati mmoja ni eneo la viwanda vidogo vidogo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Serikali imeweka msisitizo na mkazo katika eneo hili na tunajenga uwezo huo ili kuona kwamba vijana wengi wanapata ajira kupitia viwanda vidogo vidogo. Pia kupitia Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) Serikali imekuwa na mikakati na mipango mbalimbali ya kuhakikisha kwamba inawasaidia wajasiriamali wadogo kuanzisha viwanda vidogo vidogo hasa vile ambavyo vina-link ya moja kwa moja na sekta ya kilimo ambapo tunapata forward and backward linkage.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili anauliza Serikali ina mpango gani kwa vijana wa Mkoa wa Pwani? Katika kuongeza ajira siku zote tumekuwa tukisema moja kati ya kazi kubwa ya kwanza kabisa ambayo tunaifanya ni kuhakikisha tunawashawishi vijana wengi sana wakae katika vikundi. Kupitia katika vikundi vyao ni rahisi Serikali kuweza kuanza kusaidia kutokana na mahitaji ya maeneo husika. Kwa mfano, vijana wengi wa Mkoa wa Pwani wanafanya shughuli za uvuvi na shughuli nyingine za viwanda vidogo vidogo. Kwa hiyo, ni vyema Mheshimiwa Mbunge pamoja na ujana wake ajitahidi basi kwenda kuwahamasisha vijana wengi wakae katika vikundi ili baadaye Serikali iweze kusaidia katika uanzishwaji wa viwanda lakini vilevile na kusaidia mikopo na mitaji kwa ajili ya vijana hawa.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Ni kweli kuwa taifa letu lina changamoto kubwa ya ajira kwa vijana. Kwa kuwa vijana hawa wengi wako kwenye mazingira ya vijijini, ni kwa nini sasa Serikali isianzishe Jukwaa la Vijana katika Halmashauri zetu ili vijana wetu walioko vijijini na wale walioko kwenye miji midogo kama Mbulu na kwingineko waweze kujadiliana na Maafisa Uchumi, Maafisa Vijana na Maafisa Maendeleo ya Jamii changamoto na fursa zilizoko na jinsi vijana wetu wanavyoweza kupata ajira zile ambazo si rasmi kutokana na ukosefu wa ajira? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka wa jana ilipitishwa sheria hapa ya uundwaji wa Baraza la Vijana ambayo lengo lake mahsusi kabisa lilikuwa ni kwenda kusaidia kuyakusanya mawazo ya vijana na kuwashirikisha vijana katika kutatua kero na changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili. Kwa sasa Wizara ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa kanuni ambazo zitatoa mwongozo ni namna gani Mabaraza haya yataanzishwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, lengo la Mabaraza haya kuanzia katika ngazi ya kata na kuja mpaka taifa itakuwa ni kusikiliza na kujadili na vilevile kuwa sehemu ya kuwasilisha Serikalini na ushauri na matatizo ya vijana. Nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba pamoja na hayo yote lakini sisi kama Wizara tumeendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa Halmashauri. Kwanza kabisa, kwa kuendelea kusisitiza kwamba kila Halmashauri nchi nzima ihakikishe inaanzisha SACCOS ya vijana ambayo lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba vijana hawa wanapata mikopo na mitaji kwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia mwaka 2014 Wizara pamoja na Wakuu wa Mikoa wote tulikutana hapa Dodoma. Lengo kubwa la mkutano wetu hapa Dodoma lilikuwa ni kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za vijana hasa vijana wa pembezoni kwa maana ya vijijini ili tuanzishe kitu kinachoitwa Youth Special Economic Zone ambayo itakuwa ni sehemu kwa ajili ya vijana kufanya shughuli za uzalishaji mali. Kwa hiyo, nimuombe tu Mheshimiwa Mbunge kwamba aendelee kutupa ushirikano, sisi tupo tayari kushirikiana na Halmashauri kutatua changamoto za vijana.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Napenda kumuuliza Mheshimiwa Waziri, kwa kuwa hizi pesa ni za wananchi ambao ni maskini na zimekaa muda mrefu bila kupata hiyo mikopo. Je, Serikali iko tayari kurejesha hizo pesa au kuongeza riba kwa sababu hizi pesa zimekaa muda mrefu na hawa wananchi hawajapata jibu na hili tatizo limekuwepo Karagwe pamoja na Kyerwa. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, dhana nzima ya kwanza kabisa ya makusudio ilikuwa ni kuwafanya wakulima hawa kuingia katika Hifadhi ya Jamii lakini mkulima aliingia katika mfumo huu baada ya kuchangia kipindi cha miezi sita mfululizo alikuwa anapata sifa ya kuweza kukopesheka kupitia SACCOS katika eneo lake.
Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii tu kumwomba Mheshimiwa Mbunge kama bado kuna matatizo haya katika maeneo yao na kwamba wako wakulima ambao walikwisha kutoa fedha hizi wametimiza masharti na hawajapata mikopo mpaka leo, basi wawasiliane na ofisi yetu ili tuweze kuwasaidia katika upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya wakulima hawa. Vilevile nimtoe hofu tu ya kwamba fedha ile ambayo ilikuwa inachangiwa ni fedha ambayo ilikuwa ni ya mkulima mwenyewe kujiwekea kinga ya kijamii na ambayo ingemsaidia katika mafao tofauti.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama bado wana mawazo tofauti, Ofisi yetu iko wazi kwa ajili ya mashauriano na kuweza kuwasaidia katika kutatua changamoto hii ambayo inawakabili wananchi hawa.
MHE. KISWAGA B. DESTERY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali na kadri ambavyo imeanza kushughulikia jambo hili hasa kwa kuamini kwamba katika Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi tulifanya ahadi na wananchi, lakini ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa wazee hawa wengi ni wakulima ambao wakati wote Serikali inapokuwa na hali mbaya ya chakula huzuia mazao yao kuuzwa mahali popote ili kukidhi mahitaji ya nchi, kwa hiyo, hawa wazee wamechangia sana katika Taifa hili.
Je, ni lini sasa Serikali pamoja na hatua nyingine ambazo imezichukua itakamilisha mpango huu ili wazee hawa waweze kulipwa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa sisi sote tuliopo humu ni wazee watarajiwa, je, Serikali inaweza kutuambia hapa itaanza kwa kutoa kiasi gani kila mwenzi na kwa kila mzee?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye swali la kwanza la mpango huu utakamilika lini, kwenye majibu yangu ya msingi nimesema kwamba hatua ambayo tumefikia hivi sasa ni zile za kuainisha idadi ya wazee wote nchini, kuainisha viwango vya pensheni, lakini baadaye tutakapojiridhisha taratibu zote hizi zimekamilika, Serikali itatoa taarifa ni lini sasa tutaanza kufanya kazi hii ya malipo. Nimuondoe shaka Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua umuhimu wa wazee katika nchi hii hasa kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika ustawi wa Taifa letu. Kwa hiyo, pindi taratibu hizi zitakapokamilika basi tutakuwa tayari kutoa taarifa na kusema ni lini mchakato huu wa kuwalipa pensheni wazee utaanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili la nyongeza ameuliza ni kiasi gani kitakacholipwa. Tumefanya tafiti mbalimbali katika nchi tofauti na tumejiridhisha na mapendekezo yaliyopo sasa katika kiwango cha kwanza cha kuanzia itakuwa ni shilingi 20,000 kwa kila mzee. Utaratibu uliowekwa ni kuanza na wazee wa kuanzia umri wa miaka 70 ambao wako takribani 1,570,000 na baadaye tutaendelea kuona jinsi ya kuongeza umri chini ya hapo kadri uwezo utakavyokuwa unaruhusu.
MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kunipa nafasi na mimi niulize swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa ni muda mrefu Wabunge tumekuwa tukiishauri Serikali kuwalipa wazee kiinua mgongo. Mimi tangu nimeanza Ubunge zaidi ya miaka 20 nadai hivyo na leo Serikali inasema wapo katika mipango, sasa mipango hii ni lini itaisha? Sisi tunaomba kama inawezekana katika bajeti hii wazee waanze kulipwa kiinua mgongo
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia majibu yale yale tu ya kwamba suala la kuwalipa pensheni wazee kama ambavyo imesemwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM Serikali itatekeleza, kilichobaki hivi sasa ni kwamba mpango huu mwanzoni ulikuwa umeshakamilika katika awamu lakini baadaye likaingizwa pia suala la watu wenye ulemavu, kwa hiyo, ikabidi tuanze kuangalia na mazingira mengine ya watu wenye ulemavu. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba taratibu hizi ziko ukingoni kukamilika na Serikali itaanza kuwalipa pensheni wazee. Kwa sababu katika utaratibu wa jambo lenyewe jinsi lilivyo upo muundo wake ambao ni kuanzisha kamati mbalimbali kuanzia chini mpaka Taifa ambazo nazo pia zimeanza kufanyiwa kazi na zitakamilika muda siyo mrefu. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge mtuamini kwamba siyo maneno tu, lakini mikakati hii imeshakamilika Serikali itawalipa pensheni wazee kama ambavyo nimesema hapo awali.
MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Katika jibu la nyongeza imeelezwa kwamba ulipaji wa pensheni kwa wazee hawa utaanza kwa wazee ambao wana miaka kuanzia 70 wakati ambapo watu wanastaafu wengine wakiwa na miaka 55, wengine miaka 60 na umri wa kuishi Tanzania unajulikana. Je, Serikali hii ya CCM haioni kwamba inasubiri mpaka wazee wengi wafe ndiyo waweke mpango wa kuwalipa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuanzia ulipaji wa pensheni kwa wazee ukienda nchi zote duniani huwa wanakwenda kwa categories na huwa wanaangalia hali ya uchumi wa nchi katika wakati husika. Sisi kwetu tumeona tuanzie katika umri wa miaka 70 kwa kutambua kwamba bado wazee ambao wanastaafu katika kazi wanaanzia umri wa miaka 60. Ukienda kwa mfano Uganda wana kitu wanakiita Senior Citizens’ Grants ambayo wenyewe wanalipa kuanzia miaka 70. Ukienda Nepal ambayo ndiyo nchi ya kwanza duniani ambayo imeboresha pensheni kwa wazee na wenyewe walianza kulipa kwa watu wenye umri wa miaka 70 kwanza baadaye walipoona hali inaruhusu wakashuka kwenye 65 na sasa hivi akina mama ambao ni wajane na wenyewe wameanza kulipwa pensheni hii katika umri wa miaka 55.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Mnyika ondoa hofu kwamba hatua hii ya kwanza ni ya kuona kwa namna gani tunaweza tukafanya zoezi hili kwa watu hawa wenye umri wa miaka 70 na baadaye kwa kadri uwezo utakavyoruhusu tutaendelea kushuka ili kuwa-cover wazee wote, nikuondoe hofu tu Mheshimiwa.
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa majibu mazuri.
Swali la msingi linauliza kwamba pesa hizi zitaanza kutolewa maana yake toka mpaka sasa ni kwamba uchaguzi umeshapita, mwaka mzima umeisha quarter ya kwanza ya bajeti imeisha ni lini? Swali la msingi linauliza.
Swali la pili la nyongeza ni kwamba hili Baraza la Mawaziri litakaa lini kupitisha hii pesa kwa sababu tayari ilishajulikana pesa hizi zinakwenda kwa kila kijiji, ni nini kinakwamisha Baraza hili kukaa na kupitisha pesa hizi au mpango huu ili wananchi waweze kupata hizi pesa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake kauliza ni lini, na katika majibu yangu nimesema kabisa ya kwamba katika bajeti ya mwaka 2016/2017 tayari kiasi cha shilingi bilioni 59.5 zimetengwa kwa hiyo kinachosubiriwa hivi sasa ni waraka ule kupelekwa Baraza la Mawaziri na ukishajadiliwa, baada ya hapo katika jibu langu nimesema utekelezaji utaanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka tu nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba jambo hili ni jambo kubwa kidogo na linahitaji maandalizi ya kutosha hasa ukizingatia kwamba tunakwenda kuvigusa takribani vijiji 12,545 vya nchi hii na utaratibu wake huu unawekwa sawa kiasi kwamba tusije tukarudia yale makosa ambayo yalijitokeza pale awali katika usimamizi wa fedha ambao zilitoka ambapo walengwa wale hawakuweza kufikiwa na ndio maana waraka huu unaweka utaratibu mzuri na hatukutaka jambo hili kulifanya kwa uharaka kwa kuzingatia umuhimu wa ukubwa wa jambo hili na ndio maana imeshajidiliwa katika level hiyo na mkumbuke kwamba bajeti hii imepitishwa mwezi wa saba tu, kwa hiyo ni miezi mitatu tayari hapa taratibu zimekwisha kuanza nimwondoe hofu kwamba tunalipa uzito mkubwa na baada ya muda sio mrefu waraka huu utajadiliwa na utaratibu utatolewa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini Baraza la Mawaziri litakaa, Mheshimiwa Mbunge atupe nafasi tu baada ya kukamilisha taratibu hizi za Bunge hapa natumaini wahusika wa kuandaa utaratibu huu utafanyika na tutarudi tena kwa ajili ya kutoa taarifa.
MHE. JOHN P. KADUTU: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu. Swali langu la kwanza la nyongeza ni kwamba, katika ajali hizi mbalimbali zinazowapata wafanyakazi kazini, wapo wanaopoteza viungo vya mwili kwa maana wanapata ulemavu; kwa hiyo, inabidi wapate viungo bandia ili maisha yaweze kwenda. Je, Serikali sasa iko tayari kuweka sheria ili waathirika wa ajali hizi wapatiwe viungo bandia bure?
Pili, kumekuwa na usumbufu mkubwa sana katika malipo haya ya wafanyakazi wanaoumia kazini: Je, Serikali sasa iko tayari kuweka utaratibu mzuri ili wanaopata ajali kazini na kupoteza viungo na uwezo wa kazi waweze kupata malipo yao haya ambayo ni sehemu ya faraja katika maisha yao? Ahsante
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la msingi ameulizia kama tunaweza tukatunga sheria ambayo itawarahisishia hawa wanaopata matatizo wakiwa kazini kupata viungo bandia vya bure.
Mheshimiwa Naibu Spika, labda tu nimwondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, kwa sasa hakuna haja ya kutunga sheria nyingine kwa sababu sheria iliyopo ndicho ambacho imekuja kuki-address. Sheria yetu ya sasa ya Workers Compensation Act, kazi yake kubwa ni pamoja na ku-cure mischief ambayo ilikuwa inatokana na sheria iliyopita, ambapo katika sheria ile iliyopita, fidia yoyote ambayo ilikuwa inalipwa, maximum payment ilikuwa ni sh. 108,000/=.
Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na maboresho ya sheria hii sasa, inakuja kuyajibu hayo matatizo ambayo yalikuwa yakisababishwa na sheria iliyopita kiasi kwamba wafanyakazi wengi walikuwa wanaumia, lakini malipo yao yalikuwa siyo stahili na yalikuwa hayaendani na lile jeraha ambalo amelipata. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge tu kwamba, sheria ipo na itaendelea kutekelezwa na kwa sababu ndiyo kazi imeanza hii, WCF ndiyo wenye jukumu la kufanya hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, Mheshimiwa Mbunge, ameuliza kuhusu usumbufu wa malipo. Nimwondoe hofu pia kwamba Mfuko huu ambao umeanzishwa kwa mujibu wa sheria Na. 5 ya mwaka 2008 umeweka utaratibu mzuri wa malipo ya namna gani malipo yatafanyika ikitokea mtu amepata matatizo akiwa kazini. Kwa hiyo, kwa sababu Mfuko umeanza kazi tarehe 1 Julai, 2016 kwa maana ya kuanza kulipa fidia, nimwondoe hofu tu kwamba wenzetu wa Mfuko wamejipanga vizuri kuondoa usumbufu na kuhakikisha kila mtu ambaye amepata majeraha akiwa kazini anashughulikiwa ipasavyo.
MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa nafasi hii. Pamoja na maelezo mazuri ya Naibu Waziri juu ya Workers Compensation na sheria inayohusika, kuna tatizo moja kutoka chombo kilichokuwa kinashughulikia compensation ambacho kimekwisha na kikachukuliwa hiki cha sasa ambacho ni Compensation Act ambayo imeanza Julai, 2016. Naomba anihakikishie kwamba wale wafanyakazi walioumia kwa sheria ya zamani ambayo ilikuwa inalipa viwango vidogo kama sh. 100,000/= watachukuliwa walipwe na Mfuko huu mpya kwa malipo ya Mfuko huu wa sasa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi, Mfuko huu unaanza kulipa fidia kuanzia tarehe 1 Julai, 2016, hasa baada ya kuwa na kipindi cha mpito cha mwaka mmoja kuanzia mwaka 2015.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia nimkumbushe tu Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa mujibu wa taratibu za kisheria; sheria huwa haiendi retrospectively; kwa sababu hii sheria imeshatungwa katika mazingira haya na kuainisha wale ambao watapata madhara kuanzia kipindi hicho, basi Mfuko huu na sheria hii itahudumia wale tu ambao wanaguswa na sheria kuanzia pale ambapo ilitungwa lakini pia tarehe ya utekelezaji ambayo imetamkwa kwa maana ya kuanzia tarehe 1 Julai, 2016.
MHE. HASSAN E. MASALA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana, lakini pia naomba nitoe pongezi kwa majibu haya ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Sambamba na haya, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa sababu Nachingwea tayari tumeshatenga maeneo na kupitia fedha ya Halmashauri peke yake kwa hizi 5% haiwezi kutosha kuwafikia vijana wengi, sijajua Serikali inatuambia nini ili tuweze kuona namna gani tunaweza kunufaika na fedha zinazotolewa na Mifuko ya Vijana kupitia Taifa badala ya kuachia Halmashauri peke yake?
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini swali la pili, naomba nipate majibu juu ya jitihada gani ambazo zinafanywa kwa vijana wa Mikoa ya Lindi na Mtwara ukizingatia ziko baadhi ya Kanda tayari wameshaanza kuwasogezea huduma za kuwafungulia milango ya kupata ajira ikiwemo Kanda ya Ziwa, vijana wengi wanatakiwa waende kule kwa ajili ya kujiunga na vikundi vya kushona viatu. Lindi na Mtwara tunavyo Vyuo vya VETA, nini kauli ya Serikali juu ya vijana wa kanda hii na hasa vijana wanaotoka Nachingwea ambao hawana chuo cha namna hii? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza amesema kwamba, tayari wameshatenga maeneo kwa ajili ya shughuli za vijana na nichukue fursa hii kwanza kabisa kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea kwa sababu mwaka 2014 Wakuu wa Mikoa wote walikutana hapa Dodoma na likawekwa Azimio la kuhakikisha kila Halmashauri nchi nzima inatenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za vijana ambayo tuliyapa jina la Youth Special Economic Zones. Mpaka sasa hivi ninavyozungumza tayari zimeshatengwa ekari 86,000 nchi nzima na Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea nayo ni mojawapo. Kwa hiyo, niwapongeze kwa hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini swali lake la msingi ni kwamba fedha ya Halmashauri haitoshi, ni kweli! Nataka nikiri kwamba fedha ile haiwezi kukidhi mahitaji. Hata hivyo, tunao Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao umetoa mwongozo wa kukopesha SACCOS za vijana katika kila Halmashauri. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge awaandae vijana wake, tushirikiane kwa pamoja, wabuni miradi, walete maombi kupitia mfuko ule tumekuwa tukitoa fedha kusaidia vikundi mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi ninavyozungumza tumeshakopesha takriban Sh.1,700,000,000 kwa vikundi mbalimbali nchini Tanzania. Ushahidi wa dhahiri kabisa ni katika Mkoa wa Simiyu chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa wa Mheshimiwa Anthony Mtaka, tumekabidhi fedha kwa vikundi viwili vya kutengeneza chaki na maziwa katika Wilaya ya Maswa na Meatu, takriban Sh. 30,000,000 kwa kila kikundi. Kwa hiyo, nimwombe Mheshimiwa Mbunge afanye jitihada hizo, sisi tutakuwa tayari kumuunga mkono. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili anasema ni jitihada gani Serikali imezionesha katika Mikoa ya Lindi na Mtwara. Mheshimiwa Mbunge ni kweli, kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu tuna programu nyingi sana za vijana na sasa hivi tumetangaza programu ya vijana kwenda kupata mafunzo ya kutengeneza viatu na bidhaa za ngozi kule Mwanza lakini siyo kweli kwamba mikoa hii tumeisahau. Mwaka jana tumekuwa na programu kubwa sana katika Mikoa mitano ikiwemo Lindi na Mtwara ambapo tuliwafikia vijana takriban 9,100 kupitia programu inayoitwa Youth Economic Empowerment na mpaka ninavyozungumza hivi sasa vijana wengi wa Lindi na Mtwara walipata mafunzo kupitia VETA na sasa hivi wamejiajiri na wameajiri na vijana wengine. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaendelea kupanua wigo wa programu zetu ili ziweze kufika nchi nzima na vijana wote waweze kunufaika.
MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Wilaya ya Rombo ni moja kati ya Wilaya ambazo zina tatizo kubwa sana la uhaba wa ardhi hapa nchini. Mwaka 1974 Mwalimu Nyerere aliwachukua baadhi ya vijana kuwatafutia ardhi maeneno ya Mpanda kule Mikese na Tanga kule Kilindi. Vijana wa Rombo wana nguvu na wana tamaa ya kujiajiri katika kilimo. Mheshimiwa Waziri yuko tayari nikimletea vikundi vya vijana wa Rombo ambao wako tayari kujiajiri katika kilimo kuwatafutia ardhi maeneo mengine ya nchi ili na wenyewe waweze kushiriki katika kujitafutia ajira kupitia kilimo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika programu chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, moja kati ya mkakati mkubwa ambao tumeuweka ni kuwapeleka vijana katika kilimo cha umwagiliaji na kilimo biashara na katika utekelezaji wa programu hii hatuchagui maeneo. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba niko tayari kushirikiana naye kwa wale vijana wa Rombo ambao wako tayari kufanya shughuli za kilimo tukawasaidia wakapata maeneo na sisi kama Serikali tukawa sehemu ya kuwawezesha ili haja yao itimie. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunao mpango wa kitaifa wa kilimo kati ya Wizara ya Kilimo na sisi Ofisi ya Waziri Mkuu ambao lengo lake kubwa ni kwenda kuyatumia mashamba makubwa ya Serikali yale ambayo hayatumiki, yamekuwa mapori, kwa kuyatengenezea miundombinu ili vijana wengi sana waende kufanya shughuli za kilimo katika maeneo hayo. Kwa sasa tutaanzia eneo la Mkulazi Morogoro ambapo patajengwa Kiwanda cha Sukari kwa ushirika kati ya NSSF na PPF, maeneo yameshatengwa na hivi karibuni tutakwenda kuyasafisha yale maeneo na baadaye vijana watapewa maeneo hayo yakiwa yameshaboreshwa na miundombinu yake imekamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, vijana wa Rombo wakiwa tayari anione tu niko tayari kumsaidia.
MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili na mimi niulize swali moja la nyongeza. Kabla ya kuuliza swali, naomba niwape pole wananchi wa Kitongoji cha Chinyika na Kwamshango kwa maafa waliyopata ambapo watu watano wamefariki kwa kusombwa na maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niulize swali. Kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa na anajua vijana wengi sana katika Wilaya ya Mpwapwa hawana ajira na hizo fedha zinazotolewa ni kidogo sana. Je, Naibu Waziri yuko tayari kuongeza fungu la fedha hizo ili vijana wengi waweze kupata ajira pamoja na wa Wilaya ya Mpwapwa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tuna changamoto ya Mifuko hii ya Uwezeshaji ya Mitaji na Mikopo kwa vijana hasa kwa kushindwa kukidhi mahitaji ya vikundi vingi ambavyo vimekuwa vikiomba mikopo hii. Tunachokifanya kama Serikali ni nini? Sisi kazi yetu kubwa tunayoifanya kwanza kabisa ni kuwatambua vijana nchi nzima kutokana na mahitaji yao na kazi, pili ni kuwarasimisha na tatu ni kuwajengea uwezo wa kifedha kupitia mifuko mbalimbali ya Serikali lakini na kushirikiana na wadau mbalimbali. Nimwahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tunaendelea na jitihada za kuwa-invite wadau wengi zaidi wa maendeleo ya vijana ili watusaidie katika eneo hili la uwezeshaji na kuongeza mfuko wetu ili tuweze kuwafikia vijana wengi zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la mwisho, Bunge hili ndilo ambalo tunapanga bajeti, muone pia haja ya kutuongezea fedha kwa ajili ya Mfuko wa Mendeleo ya Vijana ili tuwafikie vijana wengi zaidi nchi nzima.
MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwa kuwa fedha hizi ambazo zimekuwa zikipelekwa katika Halmashauri ni kidogo sana kiasi kwamba hata hazitoi msaada mkubwa kwa wale vijana. Mheshimiwa Naibu Waziri, kuna ubaya gani kama vijana hawa ambao walio wengi hawana ajira hasa wale wanaotoka kwenye vyuo vikuu na sehemu nyingine wakaanzishiwa Benki ya Vijana ambayo itakuwa rahisi kui-control na kuwapata wale wahitaji ambao kwa kweli wanataka kutumia hizo fedha vizuri hasa sehemu kama za Kilolo na hasa hapa kwake Dodoma, je, atakuwa tayari?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa Serikali ni kuelekea katika uanzishwaji wa Benki ya Mendeleo ya Vijana lakini kabla hatujafikia hatua hiyo tukasema ni vyema kwanza tuwaanzishie vijana SACCOS mbalimbali ili tuanze kuwakopesha kupitia SACCOS hizo, wajifunze nidhamu ya fedha na matumizi yake na baadaye tutaenda kufikia katika uanzishwaji wa Benki ya Maendeleo ya Vijana wakati tayari tumeshaandaa kundi letu kubwa hili la vijana kwenda kushiriki katika masuala ya fedha. Vinginevyo, usipoanza na utaratibu huu wa kuwazoesha mwisho wa siku fedha ile ya mikopo inaweza kutumika katika mambo tofauti na ikawa haijamsaidia kijana huyu. Kwa hiyo, tumeanza katika SACCOS baadaye tutakwenda mpaka kwenye uanzishwaji wa Benki ya Maendeleo ya Vijana.
MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, Baraza hili limekuwa likifanya kazi kwa kusuasua sana. Kisheria linatakiwa lifanye kazi, ama likutane, ama lifanye vikao vyako japo mara nne kwa mwaka, jambo ambalo halijawahi kutokea.
Je, ni nini commitment ya Serikali kuhakikisha kwamba Baraza hili linakutana, ama linafanya vikao vyake kama sheria inavyolitaka? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, agizo la kuundwa kwa hizi Kamati kuanzia ngazi ya Vijiji mpaka Mkoa, ni agizo ambalo limetolewa mara kadhaa lakini kamatii hizi haziundwi. Je, Serikali haioni sasa kwamba ni muda muafaka wa kutoa deadline ya uundwaji wa Kamati hizi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwa mujibu wa Sheria Na. 9 ya Watu wenye Ulemavu ya mwaka 2010, Mabaraza haya yanatakiwa kukaa mara nne kwa mwaka. Sheria Na. 9 ya Watu wenye Ulemavu ya mwaka 2010 imeanza kutekelezwa mwaka 2012.
Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya sheria hii, Sheria ya Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 1982 ilizungumza pia kuhusu Mabaraza haya. Wakati wa Tume ya Marekebisho ya Sheria walipokuwa wakiangalia Sheria za Watu wenye Ulemavu waligundua kwamba mabaraza haya hayakukaa kwa muda mrefu sana, takribani miaka kumi na kitu.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia, katika utekelezaji wa sheria hii, ndani ya mwaka mmoja, tayari Mabaraza haya yameshakaa na yameanza kutoa ushauri kwa Serikali. Baraza la kwanza lilikaa mwaka 2016 mwezi wa nne ambalo alifungua Mheshimiwa Dkt. Possi na Baraza la pili tayari limekaa tarehe 14 Januari, 2017. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba commitment ya Serikali ni kuhakikisha mabaraza haya yanakaa kwa mujibu wa taratibu kama ilivyoelezwa kwenye sheria na tutaendelea kuitengea fedha ili watu wenye ulemavu wapate fursa ya kuishauri Serikali ipasavyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia mabaraza haya, Serikali imekuwa ikipata ushauri mbalimbali na sisi tumekuwa tukiyafanyia utekelezaji hasa kupata ushauri kutoka kwenye haya mabaraza.
Mheshimiwa Ikupa, jambo moja tu la ziada, ukisoma kwenye sheria yetu kifungu namba 46(1)(b) kimetoa mazingira ya kusaidia mafunzo ya ufundi stadi kwa watu wenye ulemavu ambayo imekuwa ni mapendekezo ya baraza hili. Na sisi katika utaratibu wetu, tumeshazungumza na watu wa VETA na wamesha-mainstream mfumo wa utoaji wa mafunzo kwa walimu wao ambapo kwa sasa hivi wanafundishwa elimu ya msingi kabisa ya kuwafundisha watu wenye ulemavu. Lengo letu ni kuweza kuwafikia wengi zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo hili tunao ushahidi wa mtu mwenye ulemavu, ndugu yetu mmoja anaitwa Boniface Kayenzi, ana umri wa miaka 63, amefundishwa VETA, sasa hivi anatengeneza na kuranda mbao na amekuwa akitumiwa katika sehemu mbalimbali za Maonesho ya Kimataifa na Biashara. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili la Mheshimiwa Mbunge, amezungumzia kuhusu uundwaji wa Kamati hizi za watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya Kata mpaka huku juu.
Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa mujibu wa sheria yetu, kuna kitu kinaitwa sectorial plan ambapo inafanya kazi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara nyingine. Mheshimiwa Waziri wa Nchi alikwishaandika barua Ofisi ya Rais - TAMISEMI), ambapo kule chini ndiko wanakosimamia hizi Kamati, kwa maana ya Halmashauri na Mikoa ili sasa agizo hilo lishuke chini. Mheshimiwa Simbachawene alikwisha kuiandika barua hiyo kufika chini ili Kamati hizi ziundwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Mheshimiwa Mbunge, niwaombe tu na Wabunge wote mlioko hapa, sisi Wabunge tunapata fursa kuingia kwenye vikao vya Halmashauri, mtusaidie na ninyi katika vikao vyetu kuendelea kutoa msisitizo ili Kamati hizi ziweze kuundwa.
MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona, na mimi niulize swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania imeridhia Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu (UNCRPD), na mkataba ule unazitaka nchi zilizoridhia mkataba huo kutekeleza, kutatua na kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu. Katika bajeti ya mwaka 2016/2017 Mfuko wa Watu wenye Ulemavu haukutengewa kabisa fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri anatueleza nini kuhusiana na mfuko huu ambao haukutengewa fedha zozote na kwa sababu hakuna fedha, inazokwamisha pia hili Baraza la Watu wenye Ulemavu kushindwa kutimiza wajibu wake. Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Sera ya Huduma kwa Watu wenye Ulemavu ya mwaka 2004, vilevile na United
Nations Conventions of Rights of People with Disabilities na yenyewe imesema namna ya kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum hasa katika kundi hili la walemavu katika kuwasaidia kuboresha maisha yao na shughuli zao mbalimbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba hapo katikati hakukuwepo na fedha za kutosha katika mfuko huu kuwezesha kufanya shughuli zake. Nimuahidi tu Mheshimiwa Mbunge, ya kwamba kwa sasa katika bajeti inayokuja ya mwaka 2017/2018, tumeona umuhimu huo na tumeshaanza kuandaa mapendekezo ya kupeleka katika bajeti yetu hiyo ili sasa mfuko huu uwezeshwe na uweze kukidhi mahitaji na utekelezaji wa mfuko huu.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nikuondoe tu hofu ya kwamba tunafahamu changamoto hiyo ya fedha lakini tumejiandaa this time tuitengee fedha ili iweze kufanya kazi yake kikamilifu.
MHE. MBAROUK SALIM ALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Pamoja na majibu ya Naibu Waziri na mtiririko mkubwa wa mikakati na Kamati ambazo zimeundwa, lakini pia nina maswali mawili madogo tu ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, pamoja na mikakati na kamati nyingi ambazo zimeundwa, lakini uzoefu wa tetemeko la ardhi la Kagera na hili balaa la njaa linaloendelea sasa hivi nchini kote, inaonekana kwamba Serikali inapiga tikitaka jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kujua, kwa sababu mikakati ni jambo moja, lakini pia na utayari. Sasa nataka kujua utayari wa Serikali juu ya kukabiliana na majanga kama hayo yanapotekea.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, kuna tetesi kwamba kwenye miaka ya 1980 kuliwekwa vifaa katika baadhi ya maeneo ya hapa nchini ikiwemo Mbeya, nafikiri na Dodoma na Arusha. Nilitaka kujua uwepo wa vifaa hivyo, lakini pia na shughuli ambazo vinafanya kwa sasa? Nashukuru sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mbarouk Salim Ali, swali lake la kwanza ameuliza utayari wa Serikali kukabiliana na majanga.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika majibu yangu ya msingi nimesema, imeundwa sheria makusudi kabisa kwa ajili ya kukabiliana na jambo hili, lakini ndani ya sheria imetengenezwa miongozo zaidi ya minne ambayo imetawanywa nchi nzima katika maeneo tofauti tofauti.
Lengo la hizi Kamati ni kwamba kupitia miongozo ile, kila maeneo na baada ya kuwa ilishafanyika assessment yako baadhi ya maeneo ambayo ni vulnerable, ambayo yako prone kwenye majanga, hasa hilo tetemeko la ardhi; na Mheshimiwa Mbunge kwa mujibu wa tafiti za kijiolojia zinasema, kwa mwaka mmoja duniani kote yanatokea matetemeko ya ardhi kuanzia 150 mpaka 1,500 ambayo yana nguvu za mtetemo kwa kipimo cha richter 4.5 mpaka 5.2.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, katika mazingira yetu haya na sisi tumeandaa utaratibu huo kupitia miongozo yetu ili kuwafanya watu wetu wawe tayari muda wote.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba kupitia Kitengo cha Maafa, utaratibu huu umewekwa na kutokana na experience mbalimbali sasa tunajiandaa kukiboresha kitengo hiki ili kiendane na hali ya sasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili limeuliza kuhusu vifaa.
Mheshimiwa Naibu Spika, masuala ya matetemeko ya ardhi yanasimamiwa chini ya Wakala wa Jiolojia Tanzania, ambayo ni GST. Ninavyozungumza hivi sasa, katika maeneo yale yote ambayo yako prone na suala hili la matetemeko, tayari tuna vituo tisa hivi sasa tunavyozungumza; katika Mkoa wa Dodoma, Geita, Singida, Kibaya, Kondoa, Mbeya na Mtwara na vituo hivi vinafanya kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba vituo hivi vipo na vinafanya kazi.
MHE. WILFRED M. LWAKATARE: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru sana. Swali langu ni kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi tunavyozungumza hivi sasa wananchi wa Bukoba Town ambao walipata matatizo ya tetemeko, wako katika shida. Mbaya zaidi ni kwamba pamoja na miongozo, kamati hizo, mikakati tunayoizungumza, imepelekea kuona hiyo miongozo haiwasaidii, kwa sababu, hadi hivi sasa pamoja na miongozo na Kamati zenu ni kwamba hata misaada ambayo wamepewa au kuelekezewa na mashirika na taasisi mbalimbali ikiwemo Bunge hili, bado hawajapata misaada hiyo. Hebu uhakikishe hiyo miongozo inawaondolea uhalali wa kupata michango inayochangwa na taasisi mbalimbali, likiwemo hata Bunge hili lililowachangia, lakini misaada hawakuipata.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, miongozo tuliyoitoa ilikuwa ni miongozo ambayo inasaidia katika masuala yote ya maafa na zile Kamati zipo kwa ajili ya jambo hilo. Sasa kwa kesi ya Bukoba, michango iliyotolewa na taasisi mbalimbali likiwemo Bunge hili; na ukisoma hata katika Hansard ya tarehe 13 Septemba, 2016 wakati hoja ya Mheshimiwa Shangazi imesemwa hapa ya kuchangia, maelezo ya mwisho hayakusema michango ile inakwenda kufanya shughuli gani, lakini ilisema michango ile ni kwa ajili ya waathirika, kwa maana ya wahanga.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa twendeni pole pole.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho wa siku, maelekezo yalikuwa ni fedha hizi ziende zikawaguse wale ambao wameathirika (wahanga). Wakati huo huo, katika Kiti cha Waziri Mkuu hapa, alikuwepo Mheshimiwa Lukuvi kama Kaimu na alitoa tamko la Serikali kwamba fedha hizi zitawafikia wahanga, kwa maana ya wale ambao wameathirika.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa turudi katika hoja ya msingi. Serikali ikijenga hospitali, Serikali ikiboresha shule ambazo zimebomoka, mwisho wa siku anayekwenda kuhudumiwa ni yule muhanga ambaye ni mwathirika. Kwa hiyo, siyo kweli kwamba fedha hizi hazijawafikia walengwa. Zimewafikia walengwa kupitia katika huduma za hospitali na katika mashule.
MHE. HALIMA A. BULEMBO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba niulize swali moja dogo la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, changamoto kubwa katika kuanzisha Benki za Maendeleo ni mtaji. Hivi sasa nchini kwetu tumejiwekea utaratibu kwamba kila Halmashauri hutenga 5% kwa ajili ya vijana. Bajeti ya mwaka huu katika Serikali za Mitaa imekusanya takriban shilingi bilioni 600 ambapo katika ile 5% ya vijana ni sawasawa na shilingi bilioni 30. Iwapo fedha hizi zitatumiwa vizuri, tunaweza kuanzisha Benki ya Vijana zenye matawi katika kila Halmashauri na tukiweza katika hili, tutaweza kutatua suala zima la mikopo kwa vijana.
Je, Serikali haioni ni vyema sasa, Halmashauri zote nchini kuwa wanahisa wa Benki za Vijana na kutumia fedha hizi kama mtaji wa kuanzisha benki hii?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Spika, nataka tu nianze kwanza kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwafuatilia vijana wa nchi hii na amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba vijana wengi wanapata fursa ya mitaji na mikopo.
Mheshimwa Spika, katika swali lake la msingi, ni kweli kwamba umekuwepo utaratibu wa utengaji wa 5% za mapato ya ndani kwa kila Halmashauri ambao lengo lake kubwa ni fedha hizi kwenda kuwafikia vijana. Kama nilivyosema kwenye majibu yangu ya msingi, lengo kubwa la uanzishwaji wa benki hii ni kutaka ije imilikiwe baadaye na vijana kupitia SACCOS za kila Halmashauri.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hatua ya kwanza ambayo Serikali tuliianza ni kwamba mwaka 2014/2015 alitafutwa mtaalam kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na baadaye sasa Serikali tukaanza kuchukua hatua; mojawapo ni kuhakikisha kwamba kila Halmashauri nchi nzima inaanzisha SACCOS ya vijana ili baadaye SACCOS hizo za vijana ndiyo zije zimiliki hisa katika hii benki.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nimwondoe hofu tu Mheshimiwa Bulembo kwamba tukikamilisha uanzishwaji wa SACCOS katika Halmashauri, kazi itakayofuata sasa itakuwa ni namna ya kuutafuta huo mtaji na wazo alilolitoa ni wazo jema. Kama Serikali, tunalichukua, tutaona namna ya kuweza kulifanyia kazi.
MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majawabu mazuri ya Naibu Waziri anaweza sasa leo akawaelekeza Halmashauri zote nchini kwamba kila mwaka ni mandatory lazima kutenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa Vijana?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utaratibu wa kuwasaidia vijana kupata mitaji na mikopo, tunayo mifuko mingi sana. Moja wa mfuko ambao nimeusema hapa ni Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao umekuwa ukishirikiana na Halmashauri kupitia SACCOS mbalimbali na vijana wengi wamekuwa wakipata mikopo kupitia katika SACCOS hizo.
Kwa hiyo, nimuondoe tu hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba kupitia Mfuko huo wa Maendeleo ya Vijana, kila mwaka tumekuwa tukikopesha vijana na wengi wamefaidika kama nilivyosema hapa isipokuwa tu katika zile asilimia tano za kila Halmashauri ambazo ni utaratibu mwingine tofauti, nako tumekuwa tukitoa msisitizo mkubwa kuhakikisha kwamba Halmashauri zinatenga asilimia tano za mapato yao ya ndani kwa ajili ya vikundi vya vijana.
MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Mwenyekiti swali la msingi, Mheshimiwa Mbunge aliyeuliza alizungumzia fedha iliyotengwa mwaka 2013/2014 na kiwango ambacho Serikali walikuwa wamekitoa. Nataka kujua ni kiasi gani cha pesa kilitengwa na kimepelekwa katika mwaka huu wa fedha tulionao wa 2016/2017?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, labda kabla sijaenda katika kujibu swali lake nisaidie kutoa ufafanuzi kidogo ili jambo hili lieleweke vyema.
Katika utaratibu wa kuwasaidia vijana nchini iko mifuko mingi ambayo inashughulika na shughuli hii ya kuwasaidia vijana, lakini ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira tunao Mfuko wa Maendeleo wa Vijana ambao pamoja na mfuko huu tunao pia utaratibu wa utengaji wa asilimia tano za mapato ya ndani ya kila Halmashauri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi ndani ya mfuko wetu mpaka hivi sasa ninavyosema tayari tumeshakopesha vikundi vya vijana takribani 309 na wamepatiwa takribani shilingi 1,700,000,000 kwa hiyo, katika utaratibu ulioko hivi sasa, mwaka huu wa fedha tumetengewa shilingi bilioni moja ambako hizo nazo tutazisambaza kwa ajili ya vikundi vya vijana ili waweze kunufaika Nchi nzima.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri naomba kuongeza tu hapo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala zima la Halmashauri mwaka huu katika Bajeti ya Halmashauri kwanza tulitoa maelekezo katika utengenezaji wa Bajeti ya mwaka 2016/2017 ni lazima kila Halmashauri itenge 10% ya tano kwa vijana na tano kwa akina mama ambapo jumla ya fedha zote shilingi bilioni 64.5. Katika fedha hizo sasa kwa hivi sasa katika upande wa Halmashauri tumeenda sasa hivi karibuni shilingi bilioni tano Halmashauri mbalimbali zimeshaanza kutoa hivi sasa niwaelekeze Halmashauri mbalimbali sasa suala lile siyo suala la hiari, ni suala la lazima kila Halmashauri lazima itoe asilimia tano kwa vijana na asilimia tano kwa akina mama na hata hivyo mchakato wa bajeti tunaoondoka nao hivi sasa Halmashauri yoyote tutaizuia bajeti yake mchakato wake mpaka ile commitment tuloiwekea iwe imetekelezeka katika mwaka huu wa fedha.
MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa pamekuwepo na unyanyasaji mkubwa sana wa wafanyakazi katika migodi, ikiwepo tabia ya ku-blacklist wafanyakazi na mfanyakazi anapokuwa blacklisted hawezi kuajiriwa sehemu yoyote katika mgodi, mara nyingi wanapokuwa blacklisted hawapewi nafasi ya kusikilizwa. Napenda kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri ni kwa kiwango gani vyama vya vya wafanyakazi vina uwezo wa kuwatetea wafanyakazi linapoteka tukio kama hili? (Makofi)
Swali langu la pili, migodi mingi imekuwa ikiwashirikisha wananchi wanaozunguka migodi kwa ajili ya ulinzi lakini wananchi hao wamekuwa wakipwewa mikataba ya mwaka mmoja na miezi sita, hawana bima na hawana mikataba ya aina yoyote, hili linafanyika ili kukwepa sheria ya kuwalipia NSSF na faida zao zingine. Je, ni lini migodi hii itaelekezwa kuhakikisha kwamba wananchi hawa wanapewa mikataba na wanalipwa haki zao kama wafanyakazi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la kwanza la unyanyashaji na blacklisting ambayo imekuwa ikifanyika, kama Wizara tumeshapata malalamiko hayo kutoka kwa wafanyakazi wengi walioko katika migodi, ambao wamekuwa wakilalamika kwamba waajiri wengi katika migodi hii hasa baada ya kuwa wafanyakazi hawa wametoka katika maeneo yao, wamekuwa wakiwa- blacklist ili wasipate nafasi yakuweza kuajiriwa katika migodi mingine na makampuni zingine.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali tumeshachukua hatua na tayari katika ukaguzi wetu huu ambao tumeufanya katika migodi yote, moja kati ya taarifa ambayo tunaisubiri ambayo itafanyiwa utekelezaji ni pamoja na jambo hilo na Serikali itatoa maelekezo kwa waajiri wote kwamba wanachokifanya ni kinyume na utaratibu wa sheria za nchi na hairuhusiwi kwa mwajiri yeyote kum-blacklist mfanyakazi. Kwa hiyo, tutaendelea kuwachukulia hatua kwa wale wote watakaoendelea kufanya jambo hili, ambalo linawaondolea haki ya kimsingi kabisa wafanyakazi wa Kitanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili kuhusu mikataba, kwa mujibu wa Sheria Na. 6 ya mwaka 2004 imeanisha vema katika Kifungu Na. 14 aina ya mikataba ambayo mwajiri anapaswa kumpatia mfanyakazi. Kama Mwajiri anakiuka katika eneo hilo, anashindwa kutoa mikataba kwa mujibu wa sheria inavyosema, Mheshimiwa Mbunge nikuhakikishie kwamba kwa sababu umeleta lalamiko hili rasmi tutalifanyia kazi na tutachukua dhidi ya wale waajiri wote ambao wanashindwa kukidhi matakwa ya Kifungu Na. 14 cha Sheria za Kazi.
MHE. JOYCE J. MUKYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kumekuwa na tabia mbaya na chafu ya udhalilishaji wa hawa waajiri wa madini ya kuwapekua wafanyakazi sehemu za siri. Hii imefanyika katika Kampuni ya Tanzanite one kule wanapovuna madini ya Tanzanite, wanawapekua sehemu za siri hasa sehemu za kujisaidia haja kubwa. Je, hakuna njia mbadala ya kufanya zoezi hilo zaidi ya kuwadhalilisha hawa wafanyakazi.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI,VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, anachokisema Mheshimiwa Mbunge, mimi mwenyewe nilikwenda pale Tanzanite one katika mgodi huo, nilikutana na changamoto hiyo kubwa ambayo wafanyakazi waliieleza mbele yangu.
Mheshimiwa Naibu Spika, wakati wa ziara ile nilitoa maelekezo na taratibu zote za namna ya ukaguzi unavyopaswa kufanyika ili usidhalilishe utu wa wafanyakazi ambao wanafanya kazi katika migodi hiyo. Maelekezo yalitolewa ya kwamba zipo taratibu za kufuata katika ukaguzi lakini siyo za kumdhalilisha mtu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimuondoe hofu tu Mheshimiwa Mbunge kwamba maelekezo tayari yapo, kama vitendo hivi vinaendelea basi niwaombe wafanyakazi wale waripoti tuchukue hatua stahiki zaidi.
MHE. RITA E. KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo tu la nyongeza. Kwa kuwa huu udhalilishaji ambao umekuwa ukifanyika na hao wawekezaji siyo katika migodi tu, upo hata katika viwanda vyetu. Nimeshuhudia mara nyingi sana Mheshimiwa Naibu Waziri akienda kusuluhisha migogoro hasa ikihusiana na unyanyasaji wa wafanyakazi. Je, ni adhabu gani kubwa kabisa ambao wamekuwa wakipatiwa hawa waajiri au wawekezaji ambao wamekuwa wakiwanyanyasa hawa wafanyakazi. Kwa sababu nimeona jambo hili limekuwa likijirudia mara kwa mara.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI,VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, kila mwekezaji anayekuja kuwekeza hapa nchini hasa wale ambao wanapitia TIC na wale ambao wamejisajili katika Vyama vya Waajiri. Wamekuwa wakipewa sheria za nchi hii na utaratibu ambao unapaswa kufuatwa na jambo lolote linalojitokeza kinyume chake hapo sisi kama Serikali tumeendelea kuchukua hatua stahiki.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna changamoto kubwa sana kwa wawekezaji raia wa China ambao wengi wamekuwa wakiingia nchini na taratibu za kisheria zimekuwa hazifuatwi, lakini wale ambao wamesajiliwa wako chini ya ATE. ATE wamefanya kazi kubwa ya tafsiri sheria za kazi za nchi yetu kwenda katika lugha ya Kichina. Maana mwanzoni wao walikuwa wanatumia excuse ya kutofahamu sheria, ingawa katika principle zile za sheria katika ile maxim inayosema ignorantia juris non excusat, ambayo inasema muhimu kabisa kwamba hakuna excuse kwa mtu ambaye hafahamu sheria. Kwa hiyo walichokifanya hawa waajiri wametafsiri sheria zile, lakini bado kuna watu ambao wanakiuka taratibu hizi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe tamko tu mbele ya Bunge hili kwamba wale waajiri wote hasa wawekezaji ambao wanafahamu sheria za nchi zetu, wanapaswa kufuata utaratibu ambao wanaendelea na unyanyasaji, tutaendelea kuwachukulia hatua stahiki ili kuhakikisha kwamba, tunaondoa dhana hii ya udhalilishaji na unyanyasaji wa wafanyakazi wetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia adhabu kubwa ambayo tumekuwa tukiichukua ni kwamba, tumekuwa tukiwandoa nchini mara moja wale wote ambao tunawabaini ni wageni wanawadhalilisha Watanzania katika nchi yetu ili tutengeneze kitu kinaitwa deterrence, mtu mwingine yeyote asiweze kurudia kosa hilo.
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, napenda kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa hawa waajiriwa 779 walikuwa tayari wapo nchini wanafanya kazi kinyume na utaratibu jambo ambalo ni batili, ni hatua gani ambazo Serikali ilikwishachukua dhidi yao?
Mheshimiwa Naibu Spika, swal la pili, je, anafahamu kwamba utoaji wa vibali unaoendelea, unaendelea kunyima fursa vijana wengi wa Kitanzania kama alivyokiri kwamba wanazo sifa na wamemaliza vyuo vikuu, lakini wanakosa fursa za kuajiriwa kwa wakati kutokana na waajiriwa wengi kutoka nje kupata nafasi? Nakushukuru sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza anahoji juu ya watu hawa takribani 770 ambao waliomba vibali vya kazi na kwamba uwepo wao ulikuwa ni batili.
Kwa mujibu wa taratibu na sheria yetu inavyosema, watu hawa wakiomba vibali maana yake ni kwamba anaanzia katika Ofisi ya Kazi na baadaye anakwenda kupewa kibali cha ukaazi. Kama alikataliwa katika Ofisi ya Kazi kimsingi hapo yeye hastahili kuwepo nchini kwa sababu hiyo pia inamfanya asipate kibali cha ukaazi. Ndiyo maana tumekuwa tukifanya ziara mbalimbali na kaguzi za kuhakikisha kwamba tunawabaini watu wote wale ambao wanaishi nchini kinyume cha sheria na ambao wanafanya kazi kinyume cha utaratibu.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili kuhusu utoaji wa vibali, kwa mujibu wa sheria yetu pia inamuelekeza Kamishna lazima ajiridhishe kibali anachokitoa ujuzi huo haupatikani nchini au mwajiri athibitishe kwa Kamishna kwamba alitafutwa mtu mwenye fani hiyo hakupatikana. Kwa hiyo, kwa suala la vibali, Kamishna anatoa vibali kulingana na sheria inavyomwelekeza na ni kweli kwamba Kamishna anafanya kazi hii kuhakikisha kwamba vijana wengi wa Kitanzania ambao wamesoma vizuri wao ndio wanufaike na nafasi za kazi za ndani. Ukiangalia katika mtiririko tumejitahidi sana kuzuia wageni katika kazi za kawaida ili vijana wetu wa Kitanzania wapate nafasi za kufanya kazi katika nchi yao.

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa kuwa utaratibu wa Serikali wa kuajiri unaeleweka kwa kufuata taratibu mbalimbali na wapo vijana ambao wana sifa hizo, elimu, uzoefu na vitu vingine. Ni lini Serikali itawapa ajira vijana wa Kitanzania ili kuwaepusha kujiingiza kwenye masuala ya ukabaji, wizi na mambo mengine?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kutoa nafasi za ajira kwa vijana kwa nafasi ambazo zimekuwa zikitangazwa. Pia kupitia Wizara ya Kazi tumeendelea kutoa msisitizo wa kuanza kuwabadilisha mtazamo vijana na kuwaaminisha kwamba si lazima vijana wote waende kufanya kazi za maofisini hii inatokana pia na takwimu iliyofanyika mwaka 2014 (Intergrated Labour Force Survey) iliyotuambia kwamba kundi kubwa la vijana wanaoingia katika soko la ajira kila mwaka ni kubwa zaidi kuliko nafasi za ajira ambazo zinazalishwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama Serikali tumekuja na mipango kadhaa kuhakikisha kwamba tunamfanya kijana huyu wa Kitanzania asiendelee kufikiria kuhusu kuajiriwa tu ofisini mojawapo ikiwa ni kumsaidia kupata ujuzi ili waweze kujiajiri na kuajiri vijana wengine. Pia kuwafanya vijana wa nchi hii sasa washiriki kwenye kilimo, ufugaji na biashara ikiwa pia ni sehemu ya ajira.
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Nimesikiliza kwa makini sana majibu ya Mheshimiwa Naibu Wazir; swali langu la kwanza: Je, ni lini sasa Serikali italeta azimio hilo Bungeni kuweza kupitishwa? Maana amesema kwamba ni nchi mbili tu ambazo zimepitisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; sisi Tanzania tuna Sheria ya Kazi nadhani ya mwaka 2004. Je, ni lini sasa kulingana na mazingira ya sasa mtaileta tena ili iweze kufanyiwa mapitio?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la kwanza ameuliza, ni lini? Katika majibu yangu ya msingi, nimesema Serikali bado tunaendelea kupitia maudhui ya mkataba huu ili baadaye baada ya kujiridhisha tuweze kuuleta kwa ajili ya kuwa ratified.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia Convention hii namba 189; katika utaratibu wa hizi Conventions huwa pia wanatoa vitu vinaitwa recommendation. Katika Convention hii kuna recommendation namba 201 ambayo inatoa mazingira ya nchi zile wanachama kuona namna bora ya kuweza kuandaa baadhi ya mechanism ili mikataba hii iweze kuridhiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa mambo mengi ambayo yapo katika mkataba huu tayari yapo ndani ya sheria zetu. Ukiangalia katika article ya kuanzia 13 mpaka 18 imezungumza kuhusu masuala ya Freedom of Association, masuala ya mikataba ambayo kwa mujibu wa sheria zetu, tayari yako covered.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda katika nchi kama Kenya, ziko baadhi ya Conventions ambazo hawajazi-ratify kwa sababu wanaona sheria yao ni nzuri zaidi kuliko ile mikataba. Kwa hiyo, nasi bado tunaona kabisa kwamba yako maeneo mengi sana ambayo sheria yetu ime-cover.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili ni mapitio ya sheria.
Kwa mujibu wa utaratibu wa masuala ya kazi, sisi tunafanya kazi katika mfumo ambao tunaita ni tripartism kwamba ni Serikali, Waajiri na Wafanyakazi. Inapotokea kwamba kuna jambo lolote ambalo linahitaji marekebisho au mapitio ya sheria, wadau huwa wanafanya taratibu hizo. Nasi kama Serikali mara zote tumekuwa flexible kuhakikisha kwamba sheria zetu za Kazi zinakuwa intact ili ziwe msimamizi mzuri katika masuala ya kazi katika nchi yetu.
MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Pamoja na kusubiri mapitio ya huo mkataba, lakini hapa nchini pana vikundi mbalimbali vya watu vinawakusanya watoto wetu wa nchi hii kwa minajili ya kuwatafutia kazi za ndani nchi za nje. Habari tulizonazo ni kwamba baadhi ya hawa watoto wamekuwa wakinyanyasika, wakiteswa na hata kuuawa. Je, ni hatua zipi za wazi ambazo Serikali inazichukua kwa ajili ya kudhibiti vikundi hivi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge hapa alikuwa anazungumzia wale mawakala wa ajira ambao kwa namna moja ama nyingine, yamekuwepo malalamiko mengi sana ya kuwapeleka mabinti zetu katika nchi hasa za Uarabuni kwenda kufanya kazi za ndani.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu alishatoa agizo na tangazo la kwamba wale wote ambao wanakwenda kufanya kazi nje ya nchi wapitie mfumo ambao upo katika Wizara yetu kupitia Wakala wa Ajira wa Serikali ambaye ni TAESA. Sasa tukibaini kwamba wako watu ambao wanafanya kazi hii kinyume na taratibu, sheria zetu ziko wazi, huwa tunawafutia usajili.
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile tumekuwa tukiwachukulia hatua kuhakikisha kwamba hawapati tena registration ili tuhakikishe kwamba nguvu kazi yetu hii wakienda kufanya kazi nje ya nchi tuwe tumewalinda kwa maana ya haki zao za kimsingi, tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo wako baadhi ya Watanzania ambao hawapitii katika Ofisi yetu na wakienda nje ya nchi wakipata manyanyaso tunakuwa hatuna taarifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia hata Balozi zetu zimeweka utaratibu mzuri; ile mikataba inayotolewa pale, mwajiri yeyote wa nje ya nchi ambaye anamtaka mfanyakazi wa Tanzania lazima apitie katika Ubalozi na Ubalozi unawasiliana nasi kwa ajili ya kuandaa mikataba ili tumlinde na tulinde haki za mfanyakazi wa Kitanzania.
MHE. PETER A. P. LIJUALIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Kwanza nashukuru kwamba Serikali inajua hivi viwanda vimehujumiwa. Tuna viwanda ambavyo vilikuwa vinafanya kazi nzuri sana, lakini hao ambao tumewapa wamekata mashine na kuziuza kama scrapers, hasa kule kwangu MMMT imefanyika hivyo na Serikali inajua. Kitu kinachonishangaza ni huu upole wa Serikali kwenye kuwashughulikia.
Mheshimiwa Naibu Spika, watu waliotuhujumu, walioharibu mali zetu wameharibu vitu vyote, halafu tunawabembeleza! Kwenye jibu la msingi hapa, Serikali inasema kwamba imewaambia hawa waliowekeza waje ofisini wapate mwongozo namna ya kuendesha au kuwapa walio tayari, yaani watu hawa wanabembelezwa. Sasa Serikali hii sijui, naomba nipate majibu, kwa nini watu hawa wanabembelezwa kiasi hiki wakati wameharibu rasilimali zetu? Hilo ni swali la kwanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwenye kiwanda changu cha MMMT kule kuna shida kubwa. Mwekezaji amepewa, amekata mashine, lakini bado ameongeza eneo la kiwanda, amenyang’anya ardhi karibu robo tatu ya kijiji. Serikali kama hamjui, naomba mjue na ninamwomba Waziri twende Ifakara, Mang’ula aende ashuhudie wananchi wa Mang’ula ambao wameporwa kiwanda na pia wameporwa na ardhi yao…
Mheshimiwa Naibu Spika, namuomba Mheshimiwa Waziri twende Ifakara. Je, yuko tayari kwenda au hayuko tayari kwenda?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA (K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI): Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la kwanza kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi, Serikali imeanza kuchukua hatua kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina pamoja na Taasisi ya TIRDO. Sasa hatua ya kwanza tuliyoanza, kwanza inafanyika technical audit katika viwanda hivi vingi sana, maana yake idadi ya viwanda vilivyobinafsishwa ni takriban viwanda 153. Kwa hiyo, tumeanza kufanya uhakiki na tayari tumeshapitia viwanda 110 kwa ajili ya kuvipitia na kupata taarifa zake.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninavyozungumza hivi sasa, Serikali hii haifanyi kazi kwa upole, tarehe 26 Januari, 2016 baada ya Msajili wa Hazina kutoa kusudio la kuvitwaa baadhi ya viwanda, alikitwaa Kiwanda cha Chai cha Mponde kwa sababu mwekezaji alikiuka masharti na tarehe 15 Machi, 2017 pia tumetoa Kiwanda cha Nyama Shinyanga ambacho kilikuwa kinamilikiwa na Triple S na sasa tunaangalia utaratibu wa kuweza kukamilisha taratibu za kumpata mwekezaji mwingine.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Serikali hii haifanyi kazi kwa upole. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tunaendelea kuchukua hatua stahiki na ninavyozungmza hivi sasa tayari viwanda nane vimeshakuwa kusudio la kuweza kuchukuliwa hatua.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la lake la pili, ananiuliza kama kweli niko tayari kuongozana naye kwenda kwenye kiwanda hiki kule Kilombero kuona namna ambavyo jambo hili linavyofanyika kwa mwekezaji kunyang’anya ardhi. Kwa sababu ni ombi maalum la Mheshimiwa Lijualikali, niko tayari kuongozana naye kwenda Kilombero kwa ajili ya kazi hii. (Makofi)
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa matatizo ya Mang’ula yanafanana kabisa na yale ya Mbagala: Je, Serikali ina mpango gani wa kutaifisha Kiwanda cha Karosho (TANITA) Mbagala ili kiweze kuendelea na kazi na wananchi wa Mbagala, vijana na akina mama waweze kupata ajira kutokana na kiwanda hicho? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA (K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI): Mheshimiwa Naibu Spika, ili nisichukue muda wako mwingi sana wa Bunge hili, nirudie majibu ambayo nimeyatoa pale awali.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais tarehe 22 Juni, 2017 alipokuwa katika ziara Mkoa wa Pwani ameshatoa maelekezo kwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhakikisha viwanda vyote ambavyo havifanyi kazi vifufuliwe na apelekewe taarifa mapema.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninavyozungumza hivi sasa, tayari Mheshimiwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango na Waziri wa Kilimo na Makatibu Wakuu wote, baada ya Bunge hili watakaa katika kikao maalum cha kuona namna gani sasa kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina kazi hii ya kuvifuatilia viwanda hivi na kuanza kuvitwaa ifanyike ili lile agizo la Mheshimiwa Rais liwe limetekelezwa.
MHE. HASNA S. K. MWILIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nina masikitiko makubwa sana, itabidi Naibu Waziri anipe uhakika wa hao wafanyakazi 389 walilipwa lini na wapi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninapoongea hivi nina ushahidi, suala hili hata Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali analifahamu. Lilifanyiwa uhakiki, watu walitumwa kutoka Hazina wakaja Uvinza wakafanya uhakiki, wakaona kweli wafanyakazi hawa wana haki hawakulipwa mshahara wao wa mwisho na hawakulipwa nauli.
Mheshimiwa Naibu Spika, kumefanyiwa uhakiki Mwanasheria Mkuu wa Serikali analifahamu bahati mbaya leo hayupo hapa, lakini analifahamu, alihakikisha na akatoa ushauri kwamba hawa wafanyakazi walipwe, wanadai zaidi ya shilingi milioni 320.9; je, Waziri yupo tayari kuniletea ushahidi kwamba walilipwa lini na nani, kwa sababu ninavyofahamu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha anayo haya madai juu ya meza yake?
Swali langu la pili, Kiwanda cha Chumvi hivi tunavyoongea wamiliki wameuza kila kitu, wameuza vifaa vyote, wameuza vyuma, wameuza magari, wameuza matofali, kila kitu. Tunajua kabisa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuimarisha viwanda, vilivyopo na kufufua vingine na kuhamasisha vingine ili viweze kujengwa. Swali langu ni kwa nini, kama dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuendeleza viwanda, leo tunaachia kiwanda kama kile cha chumvi ambacho wananchi wa Uvinza akina mama.....
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu kwa nini wanaachia wamiliki wanaoendesha kiwanda hiki kufunga kiwanda kinyume na utaratibu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza kuhusu kuleta orodha, jambo ambalo linaweza kufanyika hapa ambalo ni rahisi la kuweza kuwasaidia wafanyakazi wetu, katika majibu yangu ya msingi nilisema kama wako wale ambao wanahisi kwamba madai yao hayakulipwa ipasavyo na bado wana malalamiko, mimi na Mheshimiwa Mbunge tunaweza kuchukua hizi taarifa zote mbili tukazioanisha ili tupate muafaka wa kuweza kuwasaidia wafanyakazi hawa wa Kiwanda cha Chumvi.
Kwa hiyo, nimuondoe hofu tu Dada yangu Mheshimiwa Mwilima kwamba nalichukua jambo lako kwa uzito mkubwa sana, na kwa namna alivyozungumza kwa masikitiko makubwa, na mimi niungane nae kwamba tutakwenda pamoja wote kuangalia arodha hii ili kama bado kuna mapungufu tutafanya kazi ya kushughulikia pamoja na taasisi husika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pili kuhusu kufunga viwanda na wakati tunasema nchi yetu ni ya uchumi na viwanda. Nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba hata hili nalo pia linahitaji kuweza kufahamu hasa changamoto ambazo zimepelekea jambo hili kutokea, lakini nimuahidi tu kwamba chini ya Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, tunashughulikia masuala ya kazi na ajira na mategemeo yetu na matazamio yetu makubwa ni kuona kwamba viwanda vingi vinakuwepo, uwepo wa viwanda ndipo ajira zinatengenezwa.
Mheshimiwa Mbunge hata katika taarifa ya ILO ya mwaka 2014 ya The Global Employment Trend inasema ya kwamba ili kuendelea kuongeza nafasi za ajira hasa kwa vijana ni vema tuwe na viwanda vingi zaidi. Ninakachokisema hapa ni kwamba, nakwenda kufuatilia kufahamu changamoto na tatizo ambalo limepelekea kiwanda hiki kufungwa ili tuweze kupata suluhisho la kudumu, vijana wa Kigoma waweze kupata ajira.
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Kwa kuwa suala la Kigoma – Uvinza lipo sawa la Kiwanda cha Magunia Moshi na Kiwanda cha Kiritimba ambapo nimeshauliza swali la msingi hapa Bungeni na Serikali ikajibu kwamba ipo tayari kwenda kuonana na wale wafanyakazi ambao hawakulipwa mafao yao ili waweze kuwaeleza, kwa nini hawakuwalipa na kama wamewalipa, waliwalipa kwa vipi.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali inipe commitment kama ni lini itakwenda kuonana na wafanyakazi wa magunia waliostaafishwa na wafanyakazi wa Kiritimba wa Mkoa wa Kilimanjaro. Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge anahitaji commitment ya Serikali ya lini tutakwenda kuwaona na kusikiliza matatizo ambayo yanayowakabili wafanyakazi hawa, nimuahidi tu kwanza kwa kuanzia Jumatatu nitamuagiza Afisa Kazi aliopo pale Moshi aende kukutana na Wafanyakazi hao na baada ya hapo akishanipatia taarifa kama kuna haja ya Naibu Waziri ama Waziri kwenda kufanya kazi hiyo basi nimtoe hofu Mbunge kwamba tutakwenda kuonana nao na tutatatua matatizo ambayo yanawakabili wafanyakazi hao.
MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana nina maswali mawili ya nyongeza. Kwanza ninaomba Bunge lako Tukufu litambue kwamba nina maslahi katika mifuko yote hii ya hifadhi ya jamii.
Swali langu la kwanza ni kwamba mifuko hii inatofautiana katika kukokotoa mafao ya wafanyakazi wanaoacha kazi au wanaostaafu. Kwanza mifuko inakokotoa kutokana na gross salary mapato yote ya mfanyakazi; pili inakokotoa kutokana na basic salary.
Mheshimiwa Naibu Spika, nini msimamo wa Serikali, ni kuhusu basic salary au gross income ya mfanyakazi?
Swali la pili, fao la kujitoa baadhi ya mifuko hii saba iliyotajwa inaitangaza kama ni fao kwa wafanyakazi wanaoacha kazi na mifuko mingine ni marufuku kabisa kulipa mafao kabla ya miaka 60. Je, ni nini msimamo wa Serikali? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, nitayajibu yote kwa ujumla kwa sababu yanaingiliana. Kuhusu kukokotoa, kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa mwaka 2014 ambao ulianza kufanya kazi tarehe 1 Julai wenye vipengele 15 umeainisha namna ya ukokotoaji wa mafao kwa wafanyakazi ambao wamestaafu. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba mfumo uliowekwa kupitia SSRA ndiyo ambao unatumika na ndiyo ambao umeridhiwa mpaka hivi sasa, lakini kama kuna mapendekezo ya namna bora ya kuboresha, Serikali bado tupo tayari kuweza kusikiliza na kuona namna bora ya kuweza kuwasaidia wafanyakazi wetu ili wapate mafao ambayo wataweza kuwafanya wamudu maisha ya dunia ya leo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nafahamu sana kwamba Mheshimiwa Mbunge ni mdau mkubwa na ana mchango mkubwa sana katika eneo hili na nimpongeze kwa kazi kubwa ambayo ameifanya, naamini kabisa kwamba anayo nafasi kama Mwenyekiti wa ATE kushirikiana kwa pamoja wakaleta mapendekezo yao ili tuone namna bora ya kuweza kufanya. (Makofi)
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri ni mazuri kabisa na juzi tu nilibahatika kupata mafunzo na Wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria kuhusu Mfuko huu. Ni Mfuko mujarabu kabisa kwa watu wengi, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Kwanza Naibu Waziri anaonaje akieneza elimu ya Mfuko huu ambao mafao yake yametandawaa na yanaweza kuwafaa watu wengi sana? Anaonaje kukuza elimu ili wafanyakazi au waajiri wengi waweze kujiunga?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, Serikali haioni sasa ni wakati wa hata Wabunge kuingizwa katika Mfuko huu kwa sababu ya manufaa yake ambayo hayawi-covered na Bunge lenyewe au na Mifuko mingine ya kijamii? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA):
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza kuhusu elimu, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi umeendelea kutoa elimu katika ngazi za Mikoa na mpaka Taifa na kuhusisha taasisi mbalimbali na lengo lake ni kuendelea kuwajengea umma wa Watanzania uelewa juu ya Mfuko huu na vilevile mafao yanayotolewa na Mfuko huu.
Mheshimiwa Spika, kwa taarifa tu ni kwamba Mfuko huu unakuja kutibu lile tatizo la miaka mingi ya malipo ya fidia kwa wafanyakazi ambapo kwa mujibu wa Sheria ya mwaka 1949 malipo ya mfanyakazi aliyekuwa akiumia kazini ilikuwa ni takribani kiasi cha Sh.108,000 lakini sasa sheria hii imekuja kutibu changamoto hiyo na tumeendelea kutoa elimu kuhusiana na Mfuko huu.
Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaendelea kutoa elimu zaidi ili wananchi na hasa wafanyakazi na waajiri wote wauelewe vema na waweze kuitii sheria hii.
Mheshimiwa Spika, swali la pili la nyongeza ameuliza kuhusu Wabunge kuingizwa katika utaratibu huu. Kwa mujibu wa Mwongozo wa Mfuko huu, una-cover both private sector and public sector. Tumepokea maoni ya Mheshimiwa Mbunge ambayo yanahitaji majadiliano, lakini kwa sasa niseme pindi pale jambo hili litakapofanyiwa kazi tutaona namna ya kushirikisha taasisi hizi mbili na kuona uwezekano wake.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza nashukuru kwa majibu, nitakuwa na maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa pamoja na mikataba na vipengele vingi vilivyoratibiwa vizuri hali bado kwenye eneo hili siyo nzuri. Bado wananchi wetu wengi wanaendelea kupata matatizo hasa wanawake wanaokwenda kufanya kazi nchi za Urabuni. Serikali kupitia Ubalozi wetu inalazimika kutumia gharama nyingi za kifedha ambazo zingeweza kutumika katika shughuli za maendeleo, kwa mfano, miundombinu, standard gauge na kutununulia ndege nyingine ya Bombadier. Je, Serikali haijaona kwamba sasa wakati umefika wa kuwakatibisha hawa ma-agent, wafanya mikataba ili kuweza kuweka deposit ya fedha ambazo zitatumika kuwashughulikia wananchi wetu hawa inapobidi kurudishwa wanapokuwa wagonjwa wakati wanapokuwa wametelekezwa na waajiri wao?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa zipo taarifa na malalamiko kwamba baadhi ya wananchi wetu hawa wanaokwenda kufanya kazi huko huambiwa, kwa mfano, wanakwenda kuuza duka wakafika kule wakafanyishwa kazi nyingine kinyume na hilo duka na kinyume na ridhaa yao na pengine kusababisha hatari kwenye afya zao. Je, Serikali inalisaidiaje jambo hili katika kudhibiti na kuhakikisha kama wananchi wetu hawaendi kuongezewa udhalilishaji huko nchi za Kiarabu? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI): Mheshimiwa Spika, la kwanza, Mheshimiwa Mbunge alitaka kujua namna ambavyo Serikali tutaweka mfumo mzuri wa kuweza kuwabana mawakala hawa. Kazi hii ya kuwapeleka Watanzania kufanya kazi nje ya nchi inaratibiwa kwa mujibu wa sheria zetu na mawakala hawa wanasajiliwa katika utaratibu ambao umewekwa. Wakala yeyote ambaye anavunja masharti na matakwa ya sheria hizi tumekuwa tukimchukulia hatua kwa kufuta pia usajili wake ili kumtaka ufuate taratibu za nchi ambazo tumeziweka katika kupeleka wafanyakazi nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika, lakini pia katika eneo hili nitoe rai tu kwa wafanyakazi wote ambao wanafanya kazi nje ya Tanzania hasa katika nchi za Kiarabu hususani Oman kufuata taratibu tulizoziweka kupitia Ofisi ya Wakala wetu wa Huduma za Ajira (TAESA) ambapo tumeweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha kwamba kabla ya mfanyakazi wa Tanzania hajatoka nje ya nchi tunafanya kwanza mawasiliano kufahamu kazi anayokwenda kufanya lakini na mkataba na malipo yake. Matatizo mengi yanakuja kwa sababu asilimia kubwa ya wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi hawapitii katika utaratibu ambao tumeuweka na ndiyo maana wakipata matatizo huwa inakuwa ngumu sana kuweza kushughulikia kwa sababu hawajapitia katika mfumo wetu na hawapo katika kanzidata yetu ya watumishi ambao wanafanyakazi nje ya nchi. Nitoe rai kwa Watanzania wote wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi kufuata taratibu ili wapatapo matatizo iwe rahisi kuweza kuwasaidia.
Mheshimiwa Spika, la mwisho, katika hili eneo ambalo Mheshimiwa Mbunge amelizungumza kuhusu kwenda kufanyishwa kazi kinyume na utaratibu uliowekwa, haya yote yanatokana na iwapo tu wafanyakazi hawa hawatakuwa wamepitia katika ofisi zetu. Sisi tunawabana mawakala ili waje na mikataba ambayo tutaipitia wote kwa pamoja na Ubalozi utabaki na nakala yake ili kuweza kufuatilia. Inapotokea Mtanzania anafanya kazi tofauti na ile ambayo ilisemwa katika mkataba ni rahisi kwenda kuripoti katika Balozi zetu na sisi kuweza kuchukua hatua.
MHE. MWANTAKAJE HAJI JUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu wa Waziri, nina swali dogo la nyongeza. Je, ni nini kipaumbele cha Serikali kiuchumi kwa watu wenye ulemavu kwa sasa na baadaye?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi ya kwamba Serikali tulitunga sheria hii pamoja na sera lengo kubwa ni kusaidia katika kutoa huduma mbalimbali kwa watu wenye ulemavu vilevile kuwajengea uwezo katika masuala ya kiujuzi ili waweze kujitegemea.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, katika mipango mbalimbali ya Serikali tumehakikisha kwamba kundi hili la watu wenye ulemavu wanapewa fursa mbalimbali na kipaumbele; hasa ukizingatia katika Ofisi ya Waziri Mkuu ipo program ya ukuzaji ujuzi kwa ajili ya maendeleo ya vijana nchini ambapo tumetumia fursa hii pia kuwawezesha watu wenye ulemavu kupata ujuzi na wengi wao wameonesha uwezo mkubwa hasa baada ya kuhitimu mafunzo haya na kwenda kujiajiri na kuajiri vijana wengine.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kama Serikali tunawapa kipaumbele sana watu wenye ulemavu na vilevile tutahakikisha kwamba tunaendelea kutoa fursa zaidi ili watu hawa waweze kujitegemea pia.
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii ya maswali ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, ninapenda niulize Serikali; kwa kuwa uwekezaji uliofanywa kwenye kituo hicho wa shilingi bilioni 1.8 ambao ulitumika kujenga majengo mbalimbali ikiwemo nyumba sita za kisasa kabisa ambazo hata Mheshimiwa Waziri Mkuu anaweza akakaa mule, na majengo mengine. Kwa nini Serikali isiharakishe usajili upya wa kituo hicho ndani ya mwezi huu wa Septemba ili tathmini ya kina ifanyike ndani ya mwaka huu wa fedha ili kituo hiki kianze kutoa manufaa kwa vijana walio wengi zaidi?
Mheshimiwa Spika, la pili, kwa kuwa kituo hicho kilizinduliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2014 na hakijaonesha sura iliyokusudiwa wakati kinazinduliwa.
Je, Serikali haioni kwamba upo umuhimu wa kuchukua hatua za makusudi za kiutawala, za kibajeti na kitaasisi ili kituo hicho kiwe na sura ile ambayo ilikusudiwa wakati kinazinduliwa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Spika, katika swali la kwanza la kukamilisha usajili ndani ya Septemba hii, suala la usajili ni hatua na kama Serikali ambacho tutakifanya ni kuhakikisha tu kwamba tunahimiza kazi hii ifanyike mapema zaidi ili kituo hiki usajili wake ukamilike na baadaye sasa ifanyike tathmini ambayo itawezesha vijana wengi zaidi wa Sikonge waweze kunufaika. Kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba tutajitahidi kuhimiza taratibu hizi zikamilike kwa mujibu wa sheria ilivyowekwa ili zifanyike kwa wakati vijana wengi waweze kunufaika zaidi.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu bajeti na muundo wa utawala wa taasisi husika, na hasa ikizingatiwa kwamba kituo hiki kilijengwa kwa ajili ya kuwanufaisha vijana wa Sikonge, nichukue fursa hii tu kumuomba Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa sababu kituo hiki kipo chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ambayo pia Mheshimiwa Mbunge ni Diwani katika eneo husika, wachukue fursa hii kwanza kabisa kuhakikisha kwamba katika ngazi ya halmashauri wanajitahidi kuweka mipango mizuri kufanya kituo hiki kiweze kufanya kazi ili kiwanufaishe vijana.
Mheshimiwa Spika, lakini pia na eneo lingine la masuala ya muundo wa kitaasisi na bajeti pia, nashauri katika mtazamo huu kwamba ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge waone namna bora ya kuweza kulifanya hilo pia. Na sisi katika upande wa Serikali Kuu kwa sababu tunashughulika na vituo vingi vya vijana, pia tutatoa msaada wowote ambao utahitajika hasa katika kuwawezesha na kuwajengea uwezo wataalam hawa ambao watashiriki katika kutoa elimu kwa vijana katika eneo husika.
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri ambayo yamejikita katika kuelezea uhalisia wa mifuko hii na changamoto zilizopo, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.
Kwanza, kwa vile inaonekana wazi kwamba watumishi wengi na hasa wanachama wa mifuko hii wanapokuwa wameachishwa kazi au wametorokwa na waajiri wao wanahangaika sana kuweza kujikimu katika maisha yao na hiyo sio hiari yao isipokuwa wameachishwa kazi au wametorokwa na waajiri. Sasa Serikali haioni kwamba kuna haja hawa watu ambao wanapata dhahama hii, wasaidiwe kuchukua mafao yao ili wajikimu katika maisha yao wakati wakitafuta kazi zingine za kuweza kujipatia kipato?
Swali la pili, kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amekiri kabisa kwamba mifuko hii ina changamoto nyingi sana, ikiwa ni pamoja na gharama za uendeshaji ambayo inakula mifuko ya wanachama hawa, lakini pili kutokana na kwamba mifuko hii imekuwa mingi mno na utitiri ambao mafao yao hata hayana tija kwa wanachama wenyewe.
Je, ni lini sasa Serikali, kufuatia kauli ya Mheshimiwa Rais siku ya sherehe ya Mei Mosi Moshi katika Mkoa wa Kilimanjaro alipotaka Serikali ilete hoja hapa Bungeni, Muswada wa kuweza kuigawa mifuko hii kutoka utiriri huu na kubakiwa na angalau mifuko miwili tu ambayo itakuwa na sekta ya umma au na sekta binafsi?
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba ni lini Serikali itatii maagizo ya Mheshimiwa Rais kwa kuleta Muswada hapa Bungeni ili tuweze kurekebisha suala la mifuko hii? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la kwanza naomba tu nirudie majibu yangu ya msingi ya kwamba katika kuliangalia suala hili la fao la kujitoa kama lilivyokuwa linaitwa, sisi kama Serikali na kupitia maazimio ya Bunge hili mwaka 2012 ambayo ilisema Serikali iangalie utaratibu mzuri wa kushughulika na suala hili la fao la kujitoa.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kama nilivyosema tayari tumekwishaanza maandalizi ya kuja na utaratibu mwingine mbadala ambao utamfanya mfanyakazi wa Kitanzania yule ambaye ataachishwa kazi na hajafikisha umri huo wa miaka 60 wa kuchukua mafao yake, tuone namna ya kuweza kuliweka sawa na kumsaidia asipate shida katika muda huu wote wakati bado anasubiria kupata ajira nyingine.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo kwa sababu jambo hili linakuja Bungeni, nimuombe tu Mheshimiwa Mbunge avute subira. Muda sio mrefu tutawasilisha mapendekezo yetu hayo na ninyi kama Wabunge mtapata nafasi za kuweza kuchangia na kutushauri vema sisi kama Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lke la pili; ni lini tutatii maagizo ya Mheshimiwa Rais ya kuunganisha mifuko hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba sisi baada ya tamko la Mheshimiwa Rais kazi hiyo imefanyika mara moja na katika majibu yangu ya msingi nimesema tayari tumeshakutana na wadau, tumezungumza namna bora ya kuunganisha mifuko hii na muda sio mrefu tutatoa pia taarifa sehemi ambayo tumefikia na tutawapa pia the way forward ya namna ambavyo mifuko hii itakuwa. Hivyo Mheshimiwa Mbunge vuta subira tu, hii yote iko katika mipango na agizo la Mheshimiwa Rais tumelitii na tumelitekeleza. (Makofi)
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Badala ya kuwa na fao la kupoteza ajira, kwa nini Serikali isilete sheria na kuibadilisha katika mafao ya mtu apewe angalau theluthi moja ya mafao yake baada ya kuwa amepoteza ajira?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nirejee tu maneno yangu ambayo nimeyasema pale awali katika jibu la msingi ya kwamba Serikali tutaleta mapendekezo yetu na Bunge hili litakuwa na nafasi ya kuweza kutushauri vema. Mimi nafikiri katika hali hii ambayo tumefikia hivi sasa, Waheshimiwa Wabunge mtuvumilie na msubiri muone mapendekezo ya Serikali na baada ya hapo mtatushauri tuone namna bora ya kuweza kulifanya jambo hili tuondoe matatizo kwa wafanyakazi wetu. (Makofi)
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza sina budi kumshukuru Mhehsimiwa Naibu Waziri kwa maelezo yake mazuri yenye fasaha na yenye kueleweka lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, napenda kujua kwa sasa hivi Mfuko huo unatoa riba ya kiasi gani kwa wastaafu kama gawio lao?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, ingawa jibu la swali langu kipengele (c) ameelezea mapato yanayopatikana kwa wadau lakini hakuelezea mapato yanayopatikana kutoka kwenye miradi inayoendeshwa na taasisi hiyo jinsi yanavyowafaidisha wadau. Napenda kujua wadau wa Mfuko huo wanafaidika nini kutokana na miradi hiyo ya ujenzi wa majumba na kadhalika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Spika, katika swali lake la kwanza ameuliza ni riba kiasi gani wastaafu hawa wanapata. Kwa mujibu wa utaratibu wa mfumo wa hifadhi ya jamii katika nchi yetu, tunatumia kitu kinaitwa defined benefits ambapo mwanachama hulipwa kutokana na michango yake na mafao mbalimbali hupatikana kutokana na mfumo huu.
Mheshimiwa Spika, kuhusu riba ambayo anaipata msaafu kimsingi ni kwamba pensheni anayoipata mstaafu inatokana na michango ambayo amechangia lakini mstaafu huyu anakatwa asilimia 10 ya mshahara lakini mchango wa mwisho kwa maana mafao anayopata ya mwisho ni zaidi ya asilimia 72.5 ya mshahara wake wa miaka mitatu ya mwisho. Kwa hiyo, utaona ni kwa kiasi gani ile fedha ambayo ameiwekeza anakuja kuipata baadaye mara nyingi zaidi ya kile ambacho amekiweka. Anakatwa asilimia 10 lakini malipo yake ya mwisho ni asilimia 72.5 ya mshahara wa miaka mitatu.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili alitaka kujua mapato ya miradi hii inawanufaisha vipi wanachama ambao wamechangia. Katika mfumo huu wa uwekezaji ambapo Shirika la NSSF linafanya uwekezaji katika miradi mbalimbali, fedha inayopatika kwa maana ya mapato ndiyo hiyo ambayo huwa inaingizwa kwenye kikokotoo cha mwisho cha kumpa faida mwanachama ambaye amechangia. Pia tunayo miradi ya dhahiri ambapo kupitia miradi hii, unaona kabisa imeleta manufaa makubwa kwa Watanzania.
Mheshimiwa Spika, mfano, tunalo Daraja la Kigamboni ambalo ni matunda ya uwekezaji wa NSSF, daraja lile limetoa ajira lakini vilevile limeongeza mapato kwa shirika na vilevile watu wengi sasa wamerahisishiwa njia ya kwenda Kigamboni kwenda kufanya uwekezaji mkubwa ambao umeongeza tija katika Taifa letu.
Vilevile tuna uwekezaji katika kiwanda cha Mbigili na Mkulanzi pale Morogoro. Katika maeneo ambayo yametengwa, asilimia kubwa ya wananchi ambao wengine ni wanachama na wengine siyo wanachama watapata fursa kutokana na uwekezaji huu kupata mapato kupitia kiwanda kile cha sukari ambacho kinajengwa pale Morogoro.
MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuniruhusu niulize maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kabla ya kuuliza maswali, naomba nieleze yafuatayo, kwa mara ya kwanza nasema Serikali imeshindwa kujibu swali Bungeni.

Hakuna Mahakama, Mahakama haifanyi kazi miaka kumi iliyopita na majengo yote pamoja na nyumba za wafanyakazi milango imetolewa yote na madirisha yamechukuliwa. Mimi nimefanya kazi ya kupeleka umeme pale kwenye Mahakama ile na Kituo cha Afya, hakuna Mahakama pale.
Mheshimiwa Spika, naomba sasa niulize maswali yangu mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, je, ni kwa nini Mahakama ile imetelekezwa?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, ni kwa nini majengo ya Mahakama hiyo yasitumike na Idara nyingine za Serikali?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA - K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, katika utaratibu wa ufanyaji kazi wa kimahakama shughuli kubwa inayofanywa katika Mahakama ni suala zima la usikilizaji wa mashauri na uamuzi. Nakubalina na Mheshimiwa Mbunge kwamba ni kweli Mahakama ya Mwanzo ya Upuge ni chakavu sana, lakini shughuli za kimahakama zinaendelea wakati tunaendelea kujipanga kama Serikali ili baadaye tufanye ukarabati mkubwa wa kuweza kurahisisha ufanyaji kazi wa Mahakama.
Mheshimiwa Spika, tarehe 12/06/2017 kazi za Mahakama zilianza kufanyika kupitia katika baadhi ya ofisi pale katika Halmashauri na mpaka navyozungumza hivi sasa tayari mashauri 50 yalishawasilishwa pale Mahakamani na mashauri 41 yalishafanyiwa uamuzi. Pia pale katika Mahakama ya Upuge yupo Hakimu, mwanzoni tulikuwa tuna Hakimu anaitwa Bumi Mwakatobe ambaye alikuwa anatembelea, lakini sasa hivi yupo Hakimu wa kudumu anaitwa Jacqueline Lukuba ambaye yuko muda wote pale. Kwa hiyo, kuhusu suala la kwamba wananchi wanakosa fursa ya kupata huduma za kimahakama, wananchi wa Wilaya ya Uyui wanapata huduma hii kama ambavyo nimeisema hapo.
Mheshimiwa Spika, nimuahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwamba nafahamu changamoto tulizonazo kubwa ni kuhusiana na masuala ya bajeti katika Mahakama, lakini tunaendelea na ukarabati wa Mahakama zetu za Mwanzo na Mahakama za Wilaya, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba pindi utaratibu utakapokamilika tutafanya marekebisho makubwa katika Mahakama hii ili wananchi wa Uyui waweze kufaidika na huduma za Mahakama.
MHE. SABREENA H. SUNGURA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kumekuwa na tatizo kubwa la vyumba vya uendeshaji wa shughuli za Mahakama hususan katika Mkoa wetu wa Dodoma na ukizingatia mkoa huu umeshakuwa Makao Makuu ya nchi.
Mheshimiwa Spika, nataka kujua Serikali ina mkakati gani sasa wa kupanua Mahakama ya Wilaya ya Dodoma kwa maana ya District Court ili sasa ule mlundikano wa Mahakimu watatu kukaa kwenye chumba kimoja na kusikiliza mashauri na kesi nyingi kuchelewa, hususan kwa kesi za watoto wanaobakwa na kulawitiwa na hivyo kuathiri masomo yao uweze kwisha? Ni lini sasa Serikali itafanya upanuzi wa Mahakama hii ili kero hii iweze kuondoka kwa wananchi? Nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA - K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimekuwa nikisema mara zote, ni kwamba katika utaratibu tulionao sasa hivi katika utendaji kazi wa kimahakama, tunafanya kazi ya ukarabati wa majengo yetu mengi na upanuzi wa baadhi ya Mahakama. Kwa sababu sasa hivi tumeingia ubia pamoja na Chuo Kikuu cha Ardhi ambapo tunakwenda kujenga katika mfumo mzuri wa Moladi ambao unapunguza gharama, Waheshimiwa Wabunge waendelee kuvuta subira tu, pindi bajeti itakaporuhusu tutaendelea kufanya ukarabati na kupanua Mahakama ili kupeleka huduma za kimahakama zaidi kwa wananchi.
MHE. KHALIFA MOHAMED ISSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri, lakini msingi wa swali langu katika introduction nilikuwa nazungumzia wajasiriamali kuwa hawapati fursa hii ya kukopeshwa au kuweza kujua fursa kwa sababu hawana utaalamu na uzoefu wa kuandika andiko la miradi.
Sasa nataka kufahamu ni lini hasa Serikali itatoa maelekezo na utaalamu wa kuweza kuwafanya wale wenye nia na hamu ya kupata fursa hii kuweza kuitumia vilivyo na kwa kupata taaluma?
Pili, ni kweli kwamba kuna vikundi vingi tu ambavyo vinasaidia ama kwa kujichanganya katika SACCOS hizi au VICOBA, lakini kuna wajasiriamali mmoja mmoja ambao wangependa kutumia fursa hii ya kupata michanganuo na kuweza kupata fursa ya kukopa, lakini pia hawajawezeshwa, wala ile fursa ambayo ipo kiuchumi hawajaweza kuitumia vizuri, kwa sababu ile taaluma bado haijawafikia. Kwa hiyo, ni lini Serikali italeta taaluma hii ili watu wenye hamu na ari ya kuweza kutaka kujikwamua kiuchumi katika maisha yao, waweze kuipata fursa hiyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali la kwanza kwamba Serikali itatoa lini maelekezo ili wajasiriamali wengi waweze kupata elimu hii na wafahamu fursa zilizopo. Kwa taarifa tu ambayo napenda kumpatia Mheshimiwa Mbunge hapa ni kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu ndani yake lipo Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambao kazi yao kubwa kabisa ni kutoa elimu lakini vile vile kuwaandaa Watanzania kushiriki katika uchumi wa nchi yao kwa kuwatangazia fursa mbalimbali zilizopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuanzia, tayari tuna ma-desk katika kila Halmashauri kwa nchi nzima ambapo kuna Kamati ya Uwezeshaji ambapo wao sasa wanasaidia katika kuwapa wananchi elimu, lakini vilevile wananchi wanapata fursa ya kufahamu fursa zilizopo za kiuchumi. Kwa hiyo, kupitia hiyo, ni rahisi wananchi wengi zaidi kuweza kupata elimu na kunufaika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuongezea tu, bado tumeendelea kufanya semina, makongamano na warsha mbalimbali za kuwafanya wananchi wetu wa Tanzania waelewe fursa zilizopo na watumie rasilimali zilizopo kwa ajili ya uchumi wa nchi yetu na tumefanya katika mikoa mingi na tumepata mafanikio makubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili la nyongeza, ameuliza kuhusu namna ambavyo Serikali inaweza ikawawezesha mjasiriamali mmoja mmoja naye akapata fursa ya kushiriki katika uchumi wa nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napenda nitoe taarifa katika Bunge lako Tukufu na ninyi Waheshimiwa Wabunge mnisikilize ili mwende mkawasaidie wananchi wenu, katika nchi yetu ya Tanzania tunayo mifuko 19 ya uwezeshaji ambayo inatoa ruzuku na mikopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mifuko hii ina ukwasi wa kiasi cha shilingi trilioni 1.3 ambayo ni fursa ya kipekee kwa sisi Waheshimiwa Wabunge kwenda kuwaelimisha wananchi wetu kuzitumia fursa hizi badala ya kutegemea Mifuko ya Maendeleo ya Vijana au Mifuko ya Maendeleo ya Akina Mama na mifuko mingine, lakini bado ziko fursa nyingi sana. Kuna watu wanaitwa TFF (Tanzania Forest Fund) ambao wenyewe wanatoa ruzuku kuanzia shilingi milioni tano mpaka shilingi milioni 50 katika vikundi mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wabunge wengine wote, naomba tuichukue hii kama fursa ya kwenda kuwaelimisha wananchi wetu watumie fursa hii kujinufaisha. (Makofi)
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona. Swali langu linahusu umbali wa wananchi hawa na benki zao. Kwa kuwa benki hizo zina nia nzuri ya kuwakopesha, lakini tatizo ni wananchi wanakoishi ni mbali na zile benki, kwa sababu benki nyingi zimefunguliwa mijini na nyingi zinafanya kibiashara zaidi.
Ni lini sasa Serikali itawasiliana na hizi benki zifungue matawi yao kule vijijini zikiwemo kule Mamba Miamba kule Same na kwingineko?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa tunashukuru sana kwa concern yake ya kuona kwamba wananchi wengi wanahitaji huduma hizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kama Serikali hatua ambazo zinaanza kuchukuliwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba mabenki haya ya biashara yanakwenda kutafuta wateja maeneo ya pembezoni ili sasa watu wengi zaidi wapate fursa ya kuweza kupata huduma hizi za kifedha.
Kwa hiyo, naamini kabisa katika mipango ile ya Serikali ambayo mojawapo kubwa lililofanyika mwaka 2015 ni kuhakikisha kwamba fedha ambayo ilikuwa ni ya Mashirika ya Umma ambayo mabenki mengi walikuwa wanaitegemea, ilirudi Benki Kuu sasa ili mabenki waende kuwatafuta wateja wengi zaidi. Kwa kufanya hivyo pia itasaidia sana mabenki haya kwenda katika maeneo ya pembezoni ili kuwahudumia wananchi wengi zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inalichukua hilo na kazi inaendelea kufanyika, kuhakikisha kwamba wananchi wengi wanapata huduma hii ya kifedha.
MHE. AIDA J. KHENAN: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Swali la kwanza, Serikali ya Awamu ya Tano imepunguza wafanyakazi kwenye kada mbalimbali kwa kigezo cha kutokuwa na sifa, ni lini sasa Serikali itatoa ajira kwa kuwapa kipaumbele vijana wa nchi hii ambao kwa sasa ni wengi wamerundikana mtaani? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; Kwa kuwa mikopo hiyo anayoizungumza Waziri, Halmashauri inatenga asilimia tano ambayo kwa sasa haiwezi kukidhi haja kulingana na idadai au wimbi kubwa la vijana waliopo mtaani. Serikali haioni sasa ni muda muafaka wa kuwa na mpango mkakati wa kuwapa mafunzo maalum au kuanzisha vyuo kwenye mikoa yote ili kuwapa ufanisi vijana waweze kujiajiri? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza azma ya kutengeneza nafasi nyingi za ajira hasa kwa kundi kubwa hili la vijana, Serikali imekuja na mipango mikakati mbalimbali, si kweli kwamba tunaweza tukawa tuna nafasi za kuwaajiri vijana wote kwenye sekta ya umma, ndiyo maana kupituia program nilizozisema Serikali imeona ni vyema kuendelea kuishirikisha sekta binafsi, lakini vilevile na kwenda na falsafa ya uchumi wetu wa viwanda, lakini vilevile na kuwahimiza vijana kushiriki katika sekta za uzalishaji mali ikiwemo kilimo, ufugaji na biashara ili kwa pamoja tuwe tumetengeneza nafasi nyingi za ajira kwa vijana kuliko kuendelea kuwafanya vijana wengi wa Kitanzania kuamini kwamba nafasi za kazi ni lazima ziwe za maofisini.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sera ya Ajira, imezungumza vyema kabisa tafsiri ya neno ajira maana yake ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu kipato. Kwa hiyo, Serikali tunachokifanya ni kuendelea kutengeneza nafasi nyingi zaidi za ajira ili vijana wengi zaidi waweze kupata nafasi ya kujiajiri na kuajiri vijana wengine.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili la nyongeza amesema ni lini tutaanzisha mkakati wa kuanzisha vyuo ili kuwajengea vijana hawa uwezo. Kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, tunavyo vyuo vya maendeleo ya vijana ambayo lengo lake ni kuwapa vijana mafunzo, kuwajengea ujasiri na kuwasaidia pia katika kuweza kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji mali.
Mheshimiwa Spika, pia kupitia programu hizi katika Ofisi ya Waziri Mkuu tunao Mpango Maalum wa Ukuzaji Ujuzi nchini ambao lengo lake ni kumfanya kijana wa kitanzania apate ujuzi ambao utamsaidia kujiajiri na kuajiri vijana wengine.
Mheshimiwa Spika, ninavyozungumza hivi sasa kupitia mpango huu tayari tunao vijana takribani 2,000 ambao wanapata mafunzo ya kutengeneza nguo na kukata vitambaa katika Kiwanda cha Tooku Garment pale Mabibo, tunao vijana 1,000 ambao wako tayari Mazava Fabrics, Morogoro ambao wanajifunza kutengeneza t-shirts za michezo na wataajiriwa wote.
Mheshimiwa Spika, pia tunao vijana 1,000 ambao wako DIT - Mwanza wanajifunza kutengeneza viatu na bidhaa za ngozi. Tunao vijana 3,445 ambao wako katika sehemu mbalimbali za Don Bosco ambao wao wanapata mafunzo katika TEHAMA, kutengeneza vitanda kwa maana ya carpentry, masonry, ambao wote hao kupitia programu hii tunaamini kabisa watakwenda kusimama na kujitegemea.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Spika, ahsante.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, Mahakama ya Mwanzo Mtowisa ni mahakama iliyojengwa toka enzi za mkoloni na kutokana na hali hiyo imechakaa na inahatarisha maisha ya wananchi. Ndiyo maana Serikali katika bajeti ya mwaka 2015/2016 ni miongoni mwa mahakama iliyopangwa kujengwa upya. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuipa kipaumbele cha pekee kunusuru hali inayoweza kutokea kwa wananchi? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa vile vikwazo ulivyovieleza vya upatikanaji wa kiwanja na hati miliki vyote vilishakamilika na uongozi wa Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga ulishathibitisha. Je, ni lini sasa Mahakama hiyo itaanza kujengwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU - KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi kwamba katika mipango ambayo Wizara tumejiwekea ni kuhakikisha tunatimiza ukarabati wa ujenzi wa Mahakama kadri ya upatikanaji wa fedha za maendeleo. Hivyo kwa sababu katika mwaka huu wa 2017/2018, Mahakama ya Mwanzo Mtowisa ni kati ya Mahakama za Mwanzo ambazo zimewekwa katika mkakati huu, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba pindi fedha zitakapopatikana jambo hili litatekelezeka.
Mheshimiwa Spika, kwa sababu kwa sasa Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Ardhi na Baraza la Ujenzi la Taifa, baada ya utafiti kufanyika kupitia teknolojia mpya ya ujenzi wa Mahakama kupitia Moladi ambapo imeokoa takribani asilimia 50 ya gharama za kawaida naamini kabisa fedha hizi zikipatikana Mahakama ya Mwanzo wa Mtowisa na yenyewe itaguswa pia.
MHE. MGENI JADI KADIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa Serikali imeondosha kodi ya vifaa hivyo lakini utafiti wa mitandaoni unaonesha watu wenye Ualbino katika nchi yetu hawapungui 17,000 na waliofanyiwa uhakiki ni 7,000 tu na vifaa vilivyopelekwa MSD ni boksi 100 na miwani 50. Je, Serikali haioni vifaa hivi bado havijatosha? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, baada ya kugawa vifaa hivi, je, Serikali inachukua hatua gani kwa wafanyabiashara wale wanaouza mafuta haya kwa bei ya juu ili kulikomesha kabisa tatizo hili? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (WATU WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua mahitaji ya watu wenye ulemavu hapa nchini na imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuhakikisha kwamba mahitaji haya yanapatiwa ufumbuzi. Kwa hiyo, nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba kadiri ambavyo bajeti itakuwa inaongezeka basi mahitaji ya watu wenye ulemavu yataendelea kupatiwa mwarobaini wake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ambalo amesema kwamba kuna watu ambao wanauza kwa bei ya juu hizi lotion za watu wenye ualbino; niseme kwamba Serikali itaendelea kufuatilia suala hili kwa maana si sahihi kwamba kama vitu vinaingizwa bila kodi halafu mtu auze kwa bei ya juu. Kwa hiyo, nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba suala hili litafanyiwa kazi na Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
MHE. AMINA S. MOLELL: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza, pamoja na majibu mazuri kutoka kwa Mheshimiwa Naibu Waziri. Tatizo la watu wenye albinism na hasa wa vijijini kutokana na uhaba wa mafuta haya wengi wamekuwa wakifa kwa ugonjwa wa saratani. Pamoja na majibu hayo, Serikali ina mkakati gani wa haraka wa kuokoa maisha ya watu wenye albinism hasa wale wa vijijini? Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (WATU WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimejibu kwenye jibu langu la msingi na kama ambavyo nimewaagiza Wakurugenzi wote wahakikishe wanaweka haya mafuta kwenye orodha ya dawa wanazoagiza. Kwa hiyo, huo ndiyo mkakati wa Serikali kwamba itaendelea kuagiza mafuta haya kadiri inavyotakikana. Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)
MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipatia fursa hii na nimpongeze Naibu Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwamba swali la msingi linahusu huduma za kuwapatia watu wenye albinism vifaa vyao lakini utakubaliana nami kwamba watu hawa wenye albinism wanaishi katika maisha hatarishi na Serikali kwa muda mrefu imekuwa ikifuatilia lakini bado watu wenye albinism wamekuwa wakiuawa hasa kwa sababu ya masuala mazima ya ushirikina. Je, Serikali ina utaratibu gani kuhakikisha masuala haya yanakwisha ili hata hivi vifaa vinavyoletwa basi viweze kuwahudumia hasa hawa watu wenye albinism? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (WATU WENYE ULEMAVU) Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na hizi imani za kishirikina, Serikali imepiga marufuku utolewaji wa vibali kwa waganga wanaopiga ramli chonganishi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Lyimo hilo ndilo jibu langu la msingi na ndiyo jibu la Serikali kwamba tayari imeshapiga marufuku utoaji wa vibali kwa waganga wa jadi wanaopiga ramli chonganishi. (Makofi)
MHE. RASHID ALI ABDDALLAH: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri naomba kuuliza maswali mawili kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Dodoma kilijengwa kwa mkopo wa shilingi bilioni 44.29 kutoka katika Mfuko NHIF bila ya kuwa na mkataba na bila ya uthinbitisho wa udhamini kutoka Serikalini.
Mheshimiwa Spika, swali langu, je, Serikali haioni kwamba imeshindwa kutekeleza jukumu lake kisheria?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kama Serikali imeshindwa kutekeleza jukumu lake jukumu lake kisheria haioni kwamba inasababisha upotevu mkubwa wa fedha za wanachama kama angetokea mkopaji yule si mwaminifu?
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Spika, nikianza na swali la kwanza, kama nilivyoeleza pale awali katika majibu yangu ya msingi katika taratibu zote hizi za uwekezaji zinasimamiwa kwa miongozo ambayo ipo chini ya SSRA na BOT. Kwa sababu sekta ya hifadhi ya jamii inasimamiwa na SSRA, na upo utaratibu amabo SSRA umekuwa ukiufanya kuhakikisha kwamba yale madeni yote ambayo mifuko inaidai Serikali utaratibu umewekwa wa namna ya kuweza kuyalipa ili mifuko hii iendelee kuwa endelevu.
Mheshimiwa Spika, ndiyo maana katika majibu yangu ya awali nimesema kwamba actuarial evaluation ambayo inajumuisha pamoja na madeni yote, inaonesha kwamba mfuko huu bado unauwezo kuwa endelevu mpaka kufikia mwaka 2040.
Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili la upotevu wa fedha za wanachama maelezo yangu ni yaleyale kama nilivyosema pale awali; kwamba katika utaratibu wa miongozo ambayo imetolewa na SSRA na BOT imetoa namna gani mifuko ifanye uwekezaji na baada ya tathimini kufanyika imeonesha kabisa kwamba mifuko hii bado endelevu. Nataka nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hakuna upotevu wa fedha za wanachama, mfuko huu bado ni utakuwa endelevu sana.
Mheshimiwa Spika, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba kilichofanyika pale juu Dodoma ni uwekezaji mkubwa ambao una tija kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania. Kwa hiyo, hakuna upotevu wowote na Serikali katika hakuna jambo lolote kuonyesha upotevu. (Makofi)
MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize maswali madogo mawili na nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake.
Je, Serikali inasaidiaje kufuatilia wafanyakazi wahamiaji nchi za Uarabuni na kwingineko ambako wanateseka bila kuridhia mkataba huo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa tumekuwa tukishuhudia baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitafutiwa kazi kupitia hizi wakala za ajira (Employment Agency), lakini kumekuwa na malalamiko ya kupunjwa haki zao.
Je, Serikali inachukua hatua gani ili kulinda haki za wafanyakazi ambao wanapata ajira zao kupitia wakala hawa, pamoja na madalali ambao wamekuwa wakiwatafutia wafanyakazi wa majumbani?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi ya kwamba tuendelee kuangalia mazingira bora ya namna ya ku-ratify mkataba huu hasa pale ambapo kama nchi tutakuwa tumejiridhisha kwamba, mazingira ni rafiki na hivyo kuusaini mkataba huo ambao utasaidia sana katika kulinda haki za wafanyakazi wa ndani, lakini vilevile ambao wanatoka nje ya nchi, kwa maana ya Watanzania.
Mhweshimiwa Mwenyekiti, la pili la kuhusu Wakala wa Ajira; kama nilivyokuwa nikijibu katika maswali mengine ambayo yamewahi kuulizwa katika eneo hili, ni kwamba pale katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, ipo taasisi ambayo inashughulikia masuala ya ajira kwa maana ya wakala wa ajira ambaye anaitwa TaESA. Na rai yetu ilikuwa ni kwamba, wafanyakazi wote wa kitanzania ambao wanakwenda kufanya kazi nje ya nchi ni lazima wapitie TaESA, ili tuwatambue tujue na katika nchi ambazo wanakwenda. Tumefanya hivyo kwa sababu wakienda katika njia ambazo si sahihi, sisi kama Wizara si rahisi sana kuweza kufahamu akina nani wako wapi na ndio maana tunawataka kwamba wote wapitie katika ofisi zetu na sisi huwa tunaongea na Balozi husika, ili waweze kushughulikiwa matatizo pale wanapopatwa na matatizo nje ya nchi, ikiwemo ukosefu wa mikataba na haki nyingine.
MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kuniruhusu niulize maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Waziri, mimi nasikitika sana Serikali haisemi kwamba mimi ndiye niliyeleta Muswada Binafsi wa Sekta ya Ulinzi Binafsi (Private Security Industry Bill) wa mwaka 2016.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa je, Serikali iko tayari kunilipia kunirudishia gharama hata nusu ya ghalama niliyoitumia katika utafiti huo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, na la pili, kwa kuwa mchakato wa kuipata sheria hii ya sekta ya ulinzi binafsi unakuwa mrefu sana, je, Serikali sasa iko tayari kutunga GN ambayo itatumika wakati huu wa mpito kwa sababu makampuni haya yalianzishwa bila GN wala sheria yoyote?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI):
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na swali lake la kwanza, awali napenda kuchukua furusa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Maige kwa mchango mkubwa sana ambao amekuwa akiutoa katika sekta binafsi ya ulunzi na hivyo kama Serikali tunathamini sana mchango wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya Mheshimiwa Maige kuwasilisha muswada wake binafsi hapa Bungeni majibu ya Serikali yalikuwa kwamba Serikali itafanya kazi hiyo, kwa maana ya kuleta muswada huo ili ujadiliwe mbele ya Bunge na sheria hii iweze kutungwa.
Kwa hiyo, nimuombe tu Mheshimiwa Maige kwamba ile kazi kubwa aliyoifanya aichukulie kama ni sehemu ya mchango wake kwa Taifa hili; na yeye kama akiwa mzalendo namba moja basi aone kama ni mchango wake katika kusaidia Serikali katika kukamilisha utungwaji wa sheria hii. Ninafahamu sana kwamba Mheshimiwa huyu ni mzalendo, itakuwa ni sehemu ya mchango wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, la juu ya GN, katika majibu yangu ya msingi nimesma taratibu za utungwaji wa sheria zinaelekea kukamilika na hivyo namshauri Mheshimiwa Mbunge kwa sababu tumeshapitia kote huko, hatua hii ilibaki atupe nafasi Serikali kuwasilishwa muswada huu ili sheria hii itungwe na baadaye zitakuja hizo GN zingine kwa ajili ya ku-regulate maswala ya ulinzi katika sekta binafsi.
MHE. RUTH. H. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu Serikali ndiye msimamizi mkubwa wa usalama wa raia na mali zao, ningepa kufahamu ni kwa jinsi gani Serikali inasimamia kwa uhakika hizi sekta binafsi za ulinzi ili kuhakikisha wale wote walioajiriwa hawana historia ya uhalifu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI):
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia taasisi zake mbalimbali imekuwa ikihakikisha kwamba kuanzia katika eneo la usajili wa makampuni haya ambayo pamoja na kwamba utaratibu wa usajili wake ni kupitia BRELA, lakini bado Jeshi la Polisi nalo lina nafasi ya kuweza kupitia na kuyatathimini maombi ambayo yanapekwa ili kujihakikishia. Kwa sababu kazi ambayo inakwenda kufanywa hapa na sekta ya ulinzi binafsi ni kazi ambayo vilevile ni ya kulisaidia Jeshi la Polisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni kwa sababu kwa mujibu wa viwango vya Umoja wa Mataifa askari mmoja anapaswa kulinda watu na 450, lakini sisi kwetu askari mmoja analinda kuanzia watu 1,150 mpaka 1,300. Kwa hiyo, ndiyo maaan kama Serikali tunatoa kipaumbele na ndiyo maana katika shughuli mbalimbali za sekta ya ulinzi binfsi tunahakikisha kwamba tunashirikiana nao katika kutoa elimu, lakini vilevile na kuzisimamia kuona kwamba zinayanya kazi ile iliyokusudiwa ili hatimaye isije ikaleta madhara makubwa kwa sababu na yenyewe pia ni sehemu ya ulinzi katika nchi yetu.
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Swali langu lilikuwa kuhusu ukosefu wa nyumba za polisi katika Mkoa wa Manyara ikiwemo Ofisi ya RPC. Ni lini sasa Serikali itaona kwamba kuna umuhimu wa Jeshi la Polisi kupatiwa nyumba ili waweze kufanya kazi yao kwa ufanisi.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI):
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tunatambua kwamba tunayo changamoto kubwa sana ya ukosefu wa nyumba za askari wetu, lakini katika mipango ya Wizara tumejiwekea utaratibu kwamba pindi pale bajeti itakaporuhusu tutahakikisha kwamba tunaifikia Mikoa yote ili kuwaondolea adha ya ukosefu wa nyumba watumishi wa Serikali hasa wa Jeshi la Polisi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuondolee hofu Mheshimiwa Mbunge bajeti ikikaa vizuri basi tutafikia katika maeneo yote katika kuondoa hadha hii.
MHE. BHAGWANJI MAGANLAL MEISURIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kinipa nasafi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nazipongeza Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano kwa sababu katika Jimbo langu wamejenga kituo cha polisi Chwaka na Jozani. Lakini mimi naomba Serikali, wameniomba nizungumze Serikali ya Muungano pamoja na Zanzibar wapatiwe gari za doria, Chwaka na Jozani.
La kwanza kwa kuboresha wananchi wangu wapate hitaji lao, lakini lingine mimi mwenyewe binafsi nimetoa gari mbili hospitali za Chwaka na Kongoroni. Lakini hii gari ya polisi lazima tuhudumie tupate na mimi nimesaidia Jozani polisi walikuwa wanahitaji computer na nimewasaidia, lakini hii gari mnipatie zote mbili. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI):
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Bhagwanji hakuuliza swali, ilikuwa ni ombi la gari la doria na mimi tu kwa niaba ya Serikali tumepokea ombi lake na tutalifanyia kazi pindi pale nafasi itakaporuhusu basi tutaona namna ya kuweza kufanya.
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninayo maswali mawili ya nyongeza.
Kwa kuwa kibali cha Halmashauri kinatozwa shilingi 16,000, kiwango ambacho ni nafuu, je, zimamoto kutoza 150,000 haioni kwamba kiwango hicho ni kikubwa na hivyo inapelekea wananchi wengi kujenga bila kuwa na kibali?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, mchanganuo wa tozo kwa mjenzi wa nyumba ya kawaida anatozwa hiyo hiyo shilingi 150,000 sawa na mjenzi wa ghorofa, hii imekaaje?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI):
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza ametaka kujua tozo ya shilingi 150,000 kwamba ni kubwa na hivyo inawafanya wananchi washindwe kupata kibali hiki na hivyo kujenga majengo holela. Tozo hizi ni kwa mujibu wa Kanuni na Sheria ambazo tumejiwekea, ukiacha ile Halmashauri ambayo ni shilingi 16,000 anayosema yeye, lakini kwa mujibu wa taratibu ambazo tumejiwekea kwa maana ya Sheria yetu hasa katika Kanuni ile ya [The Fire and Rescue Force, (Fire Precautions in Buildings) Regulations], 2015 Na. 248 imezungumza kiwango ambacho kinapaswa kutozwa ukianzia katika Majiji, Halmashauri, Wilaya lakini vile vile na katika vijiji. Kwa hiyo kiasi kilichowekwa hapa cha shilingi 150,000 ni kwa mujibu wa Sheria yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ametaka kujua kuhusu utofauti wa utozwaji wa tozo hizi. Tozo hizi zinatofautiana kutokana na kiwango cha ukubwa wa jengo au vile vile mita za ujazo wa jengo. Kwa hiyo, haiwezi ikawa kuna mfanano kwa namna ambavyo tozo hizi zimewekwa. Kikubwa kinachoangaliwa hapa ni mita za ujazo. Kwa hiyo, mita za ujazo zinavyozidi kuwa kubwa zaidi ndiyo tozo zenyewe zinazidi kuongezeka.
MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na swali la Mheshimiwa Kapufi kuhusiana na hizi kodi za zimamoto, ninachojiuliza na wananchi wanachojiuliza hasa wa Jimbo la Kavuu wanataka kujua, kwa nini hizi tozo zimeanza kutozwa sasa, na watu gani wameshirikishwa? Kwa sababu zinaoneka zimeibuka, hata kama zilikuwepo kwa ujibu wa Sheria, zimeibuka kiasi kwamba hata wale wenye guest houses sasa hivi zimamoto wamekuwa wakiwavamia na kuwa-charge hizi kodi. Kwa hiyo, tunaomba ufafanuzi ni gazeti namba ngapi zilizoruhusu hizi kodi zianze kutumika?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI):
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi ya awali kabisa ni kwamba tozo hizi zinatokana kwa mujibu wa Sheria na Kanuni ambazo tumejiwekea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwasababu Mheshimiwa Mbunge ameonyesha interest ya kufahamu namba ya GN ambayo siponayo hapa hiyo namba nitampatia, lakini ni kwamba tozo hizi zinafanyika kwa mujibu wa regulations ambayo niliisema pale awali ya The fire and rescue force fire precaution in buildings regulations ya mwaka 2015. Hivyo kinachofanyika hapa hata ilikuwa ifanyike hapo awali lakini utekelezaji wa Sheria unaendelea kuwa ni halali kwa sababu ilikuwepo Kanuni hii na sasa ndiyo utekelezaji wake unafanyika.
MHE. JUMA S. NKAMIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri na ya uhakika ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Nilikuwa na swali moja tu la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya Chemba ni moja kati ya Wilaya kubwa sana katika Mkoa huu wa Dodoma na pengine kwa Tanzania kwa ujumla. Je, Serikali wakati inasubiri kujenga jengo la Mahakama katika Makao Makuuya Wilaya iko tayari sasa kuimarisha mahakama za Mrijo na kwa Mtoro ili kupunguza adha inayowafanya wananchi kutembea zaidi ya kilometa 170 kufuata huduma za mahakama Wilayani Kondoa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli anachokisema Mheshimiwa Mbunge kwamba Wilaya ya Chemba ni kubwa sana, na kwa sababu mahakama hii ya wilaya itaanza kujengwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 niseme tu kwamba nimepokea ombi na mawazo ya Mheshimiwa Mbunge na sisi kama Serikali tutaona namna bora ya kuweza kuimarisha huduma katika maeneo ya Mrijo ili wananchi wasipate shida kutembea umbali mrefu kwa sababu alipokusema huko Mheshimiwa Nkamia ni mbali sana mpaka kufika katika makao makuu ya Wilaya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kama Serikali katika mpango wetu wa kuhakikisha kwamba tunasogeza huduma hizi kwa wananchi tutahakikisha pia tunalifanyia kazi jambo hilo la kuboresha huduma za mahakama katika maeneo hayo ili wakati tunaendelea kujipanga katika ujenzi wa Mahakama ya Wilaya wananchi waendelee kupata huduma katika maeneo ya Mrijo na maeneo mengineyo. (Makofi)
MHE. SONIA J. MAGOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Je, Serikali ina mkakati gani juu ya vijana ambao wamekuwa wakipata ajira za muda mfupi na kushindwa kuendelea na ajira zile, lakini kwa kigezo cha umri wamekuwa wakishindwa kupata mafao yao ambayo yangeweza kuwasaidia katika kuendeleza maisha yao?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa kumekuwa na tofauti ya pensheni za kila mwezi kutoka mfuko mmoja na mwingine. Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha wazee hawa wanaostaafu wanapata pensheni iliyo sawa ya kila mwezi na ambayo inaweza kuwasaidia kuendesha maisha yao? Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la kwanza alikuwa anazungumzia kiujumla kuhusu fao la kujitoa na amewazungumzia vijana ambao bado hawajafikia umri wa kupokea pensheni.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo tumesema awali katika Bunge lako kwamba Serikali inaendelea kulifanyia kazi suala hili la fao la kujitoa. Hivi sasa tupo katika utaratibu wa kushirikiana na wadau ili kutengeneza kwa pamoja mfumo mzuri ambao utawa-cover watu wote katika makundi tofauti tofauti. Hivyo nimwombe Mheshimiwa Mbunge, kwa sababu jambo hili bado linafanyiwa kazi na Serikali tutakuja na mpango mzuri wa kuweza kusaidia kutatua changamoto hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili kuhusu pensheni, tayari SSRA wameshatoa miongozo kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kulipa kima cha chini cha pensheni sawa kwa mifuko yote na ambayo hivi sasa imeanza kutekelezwa. (Makofi)
MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika sekta hizi zisizo rasmi na hapa nawalenga hasa wale wanaofanya kazi za daladala kwa maana ya madereva wa madaladala na makondakta wao na hii ni sekta ambayo imeajiri vijana wengi na watu wengi. Kimsingi wana malalamiko mengi ya haki za wafanyakazi, kwamba hawapewi stahiki zao. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri, atakuwa tayari kukutana na Madereva na Makondakta wa daladala ili asikilize kero zao na uweze kuzipeleka Serikali kwa ajili ya kuzishughulikia, ukianzia Temeke? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kazi hii kama Wizara tumekuwa tukiifanya, tutaendelea kuifanya na nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba nipo tayari kukutana nao na kujadiliana nao kuhusu haki ambazo zinawahusu. (Makofi)
MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Swali langu ni kwamba, kwa kuwa kuna waajiri ambao wanakata mshahara lakini hawapeleki fedha hizi kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Je, Serikali inawachukulia hatua gani?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa sheria kila mfanyakazi aliyeandikishwa na anayekatwa makato yake kwa ajili ya hifadhi ya jamii yanapaswa kuwasilishwa katika mfuko husika. Kinyume na kufanya hivyo ni kukiuka taratibu za kisheria.
Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana baada ya kuziangalia sheria zetu tukafanya marekebisho ya mwaka 2016 katika Sheria Na. 7 ya Mwaka 2004 ambayo inashughulikia masuala ya Taasisi za Kazi ambapo lengo lake ni ku-compound hizo fences na inapotokea mwajiri amekiuka taratibu hizi tutakachokifanya ni kwenda kumpiga faini ya papo kwa papo ili kufanya deterrence na kumpunguzia mzigo mfanyakazi lakini kumfanya mwajiri awe ana-comply na sheria.
Mheshimiwa Naibu Spika, huo ndiyo mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba jambo hili linafanyika kwa mwajiri kuwasilisha mchango wa mwajiriwa wake ikiwa ni haki yake ya mchango ambao ni sehemu ya mshahara wake.
MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Swali la kwanza, Majaji waliostaafu kabla ya mwaka 2013 ambao siyo wengi, hawako kwenye hali nzuri sana wakati wa kupata matibabu. Serikali haiwezi ikatumia busara hili suala likawa ni la kiutawala (administrative) ili bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria ikawahudumia Majaji hawa?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Political Leaders Pension Act ya Mwaka 1981 inaelezea pamoja na watu wengine ambao wanatakiwa kupata pension, angalau wapo kazini kwa miaka 10 ni Wabunge. Je, Serikali haioni busara kuleta Muswada hapa Bungeni ili kufufua Sheria hii ya mwaka 1981 ili Wabunge waweze kupata pension? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la kwanza amezungumza kuhusu Majaji waliostaafu kuanzia mwaka 2013. Kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge ni kweli kwamba, kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha Bima ya Taifa ya Afya, Kifungu Namba 11(3) kinaeleza kuhusu wale watumishi wa Serikali waliokuwa wana-hold Constitutional Office ambao wanaweza kunufaika katika matibabu ya afya. Hata hivyo, katika Kifungu hicho pia, kupitia Sheria hii ya Mwaka 2007 imetamka pia, aina ya watu wanaostahili kupata huduma na stahiki kutokana na sheria ambayo imesomwa ya mwaka 2007.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, katika hili ombi la Mheshimiwa Mbunge la kwamba Serikali ione busara, kwa sababu ni suala ambalo linahusisha pia Sera na Sheria niseme tu kwamba, kama Serikali tunalichukua, lakini siwezi kuweka commitment ya kwamba litafanyika, ni pendekezo limetolewa, linahitaji kwenda kuangalia sera na sheria ambazo zinatuongoza, hasa kuanzia yale mafao ya Majaji, na sheria ambazo pia zinahusika kwa maana ya watoa huduma katika baadhi ya masuala ambayo yanawahusu Majaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili ameuliza kuhusu pension kwa Wabunge. Ombi la Mheshimiwa Mbunge hapa ni kufufua tu sheria, sasa Waheshimiwa Wabunge kwa sababu, masuala haya yanaweza kupitia Tume ya Utumishi wa Bunge na ninyi ndiyo Wabunge, lianzie kwenu kwanza ndiyo lifike Serikalini. Kwa hiyo, hii ni kazi ya Kibunge lianzie katika upande wa Bunge. (Makofi)
MHE. FAIDA MOHAMED BAKAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri lakini kuna kitu amekiongelea, amesema kutibu. Mimi ninavyoona kinga ni bora kuliko tiba; na kwa kuwa Serikali inawatibu vijana hawa baada ya kuathirika lakini ni bora ingewakinga wasiathirike. Je, Serikali itachukua hatua gani za haraka au madhubuti za kuwakinga vijana wake wasitumie madawa ya kulevya badala ya kuwapeleka kwenye sober house wakati wameshaathirika na kuwatibu? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa scanning machine katika maeneo mbalimbali ni muhimu sana katika maeneo kama airport, bandarini na sehemu nyingine zozote. Hata hivyo, kuna maeneo mengine kama kule kwetu Pemba, juzi nimesafiri kuja huku scanning machine yake haifanyi kazi na sehemu hizi ndizo wanazopitisha vitu vyao watu hawa wabaya.
Je, Serikali itachukua hatua gani kuwanunulia mashine nyingine pale airport ya Pemba ama kuwatengenezea ile mashine ili kuepukana na matatizo haya ya kusafirisha madawa haya ya kulevya? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Naibu Spika, kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge ni kweli, kinga ni bora zaidi. Katika utaratibu wa kushughulikia masuala ya dawa za kulevya, hatua ambazo Serikali imezichukua zipo katika mgawanyo wa sehemu tatu.
Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu ya kwanza tunaiita ni supply reduction, ni punguzaji wa upatikanaji wa dawa za kulevya ikiwa ndiyo sehemu ya kwanza kusaidia kumfanya
kijana huyu au mtu yeyote asipate madawa ya kulevya. Ni dhahiri kabisa kwamba baada ya Mamlaka ya Dawa za Kulevya kuanza kazi yake, kuanzia Januari mpaka Desemba, 2017 ninavyozungumza hivi sasa tayari wamefanyakazi kubwa ya kuzuia upatikanaji wa madawa ya kulevya.
Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa takribani kilo 196 za heroin zilikamatwa lakini takribani tani 47 za bangi zilikamatwa, tani 7 za Mirungi zilikamatwa na mashamba ya bangi hekari 542 yaliteketezwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ukiyafanya haya sasa, yanasaidia kupunguza upatikanaji wa dawa za kulevya huko mtaani. Kwa hiyo, kazi ya kwanza Serikali inayofanya ni hiyo ya kusaidia hiyo kitu inaitwa supply reduction.
Mheshimiwa Naibu Spika, kitu cha pili tunachokifanya ni demand reduction, tunapunguza pia uhitaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, ya tatu ni harm reduction. Harm reduction sasa huyu ameshatumia dawa za kulevya hatuwezi kumuacha hivyo hivyo ndiyo maana sasa tunakuja na tiba lakini vilevile kumsaidia mtu huyu aweze kurudi katika hali yake ya kawaida.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa ninavyozungumza mamlaka imefanya kazi yake vizuri sana, hata katika uagizaji wa methadone hapa nchini tumetoka katika kiwango cha kawaida cha kilo 120 mpaka kilo 300, maana yake nini? Maana yake ni kwamba dawa za kulevya sasa hivi mtaani hazipatikani, kwa hiyo, hawa waathirika wanapata tabu kubwa ndiyo maana wanakwenda kutibiwa katika vituo vyetu ambavyo tumeviweka kwa ajili ya kuwatibu waraibu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Serikali inalitambua hilo na ndiyo maana tumekuja na hiyo mikakati tofauti tofauti kuhakikisha kwamba dawa za kulevya hazipatikani na tunawalinda vijana wetu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE):
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Napenda kuongezea kwenye swali la pili la Mheshimiwa Faida Bakar kwamba kwa mujibu wa taarifa tulizonazo kutoka Zanzibar Airport Authority (ZAA), scanner ya Pemba inafanya kazi vizuri kabisa na inafuatiliwa kila siku na kila wakati. Scanners zote za viwanja vyetu vya ndege tunazifuatilia mara kwa mara, ahsante sana.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu yote yaliyotolewa na Naibu Mawaziri kuhusu suala hili, tunatambua umuhimu mkubwa wa kuhakikisha viwanja vyetu vyote vya ndege scanner zinafanya kazi na hizo ndizo zinazoweza kutusaidia kudhibiti tatizo la uingizaji wa dawa za kulevya.
Kwa hiyo, naomba niwaambie Waheshimiwa Wabunge kama kuna tatizo kwenye scanner ya Zanzibar basi tutafanya utafiti wa kina ili ndani ya Serikali tuzungumze ili scanner hiyo iweze kufanya kazi na tuweze kuendelea kudhibiti tatizo hilo la dawa za kulevya. (Makofi)
MHE. HALIMA A. BULEMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii.
Mheshimiwa naibu Spika, mwaka jana tumeshuhudia Serikali yetu ikijaribu kupunguza tatizo la utumiaji wa madawa ya kulevya kwa kuwataja hadharani watumiaji na wauzaji jambo lililosaidia kupunguza lakini siyo kumaliza tatizo hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee. Nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeshuhudia mwaka jana Serikali yetu ikijaribu kupunguza tatizo la utumiaji wa madawa ya kulevya kwa kuwataja hadharani watumiaji na wauzaji lakini jambo hili halikumaliza tatizo bali ilipunguza tu, suala hili bado lipo tena kwa wingi zaidi na wanaoathirika ni vijana wa Kitanzania ambao ni nguvu kazi ya nchi. Je, ni lini sasa Serikali itaona umuhimu wa kujenga rehab zitakazotambulika ili kumaliza janga hili? Nashukuru.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa napenda nichukue fursa hii kumshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Halima Bulembo kwa namna ambavyo anawapigania vijana wa Taifa letu la Tanzania, lakini amekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya vijana. (Makofi)
Mheshimiwa naibu Spika, ni kweli tunafahamu kwamba moja kati ya njia ya kuwarudisha waathirika wa dawa za kulevya katika hali yao ya kawaida ni pamoja na kuwa na sober houses nyingi na rehabilitation centers ambazo zitawasaidia kuwarudisha kururdi katika hali yake ya kawaida. Ndiyo maana katika majibu yangu ya msingi nimesema, moja kati ya mkakati ambao tunao ni uanzishwaji wa tiba ambao inaitwa occupational therapy ambao lengo lake kubwa ni kumsaidia muathirika huyu wa dawa za kulevya kurudi katika hali yake ya kawaida.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika utaratibu huo, waathirika wote wa dawa za kulevya ambao watapelekwa katika vituo vyetu mbalimbali watafundishwa stadi mbalimbali za kazi ili baadaye akirudi asirejee katika matumizi ya dawa za kulevya. Katika mpango wetu huo, Serikali tunaanza utoaji wa tiba hiyo katika kituo ambacho kinajengwa hapa Dodoma katika eneo la Itega. Hali kadhalika tunafanya kazi pia na taasisi na wadau mbalimbali katika kuhakikisha kwamba tunawasaidia vijana wetu wa Kitanzania wasipate madhara zaidi ya matumizi ya dawa za kulevya.
MHE. NURU A. BAFADHILI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa vijana wengi wanaopelekwa katika sober houses wanalipishwa kiasi fulani cha fedha ili waweze kujikimu kwa vyakula. Je, Serikali haioni kuwa ni wakati muafaka kuwasaidia kwa sababu kuna baadhi ya jamii hazina uwezo wa kuwasaidia watoto wale? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli sober houses nyingi zinamilikiwa na watu binafsi na waathirika hawa wa dawa za kulevya wamekuwa wakilipishwa. Mpango wa Serikali ni kuandaa utaratibu sasa ambapo na sisi tutatengeneza sober houses za kwetu ili kufanya huduma hii ipatikanike kwa urahisi na kila mmoja ambaye hana uwezo wa kumpeleka katika sober house za private aweze kupata tiba hii na imsaidie kurudi katika hali ya kawaida.
MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, naomba niulize swali moja la nyongeza, kama ifuatavyo:-
Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini bado wamiliki wa vyombo hivi hawajawapa mikataba waendesha bajaji na bodaboda, matokeo yake wanakubaliana kwa maneno kwamba baada ya mwaka mmoja chombo hiki kitakuwa chako kwa kiasi fulani cha fedha lakini ikifika miezi saba au nane anamnyang’anya kile chombo na kumpa mtu mwingine.
Je, Serikali iko tayari kusimamia zoezi la kukabidhiwa mikataba waendesha pikipiki na wakamatwe waendesha pikipiki waulizwe mkataba aliokupa mwajiri wako uko wapi ili kuwashinikiza wamiliki hawa kutekeleza hii sheria?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo hili aliloliulizia Mheshimiwa Mbunge la mikataba hapa lazima tuweke vizuri na ieleweke. Mikataba aliyokuwa anazungumzia Mheshimiwa Mbunge ni mkataba wa umiliki wa pikipiki hasa baada ya kuwa kuna makubaliano kati ya mwenye chombo na yule dereva ambaye amepewa chombo hicho.
Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Serikali, mkataba ambao tuna uwezo wa kuusimamia wa kwanza kabisa ni mkataba wa ajira ambao upo kwa mujibu wa sheria, kifungu cha 14 cha Sheria Na. 6 ya mwaka 2004 ambacho kimeelezea vyema namna ambavyo kila mwajiriwa anapaswa kupewa mkataba.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili ambalo kalizungumzia Mheshimiwa Mbunge, ni makubaliano ambayo yamekuwa yakifanyika kati ya waendesha vyombo na wamiliki wa vyombo ambapo utaratibu katika maeneo mengi ni kwamba yule mmiliki anampatia muda muendesha chombo akisharejesha fedha yake basi baadaye chombo kile kinabaki kuwa cha yule dereva.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika hilo, nitoe tu wito wa kwamba makubaliano hayo yanaingiwa na pande mbili; mmiliki na mwendesha chombo, ikitokea namna yoyote ambayo haki ya mwendesha chombo huyu inadhulumiwa basi vyombo vya sheria vipo na tuwaombe watu hawa ambao wananyanyasika katika eneo hilo waende kulalamika na hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya hao ambao wanakiuka utaratibu na makubaliano ambayo wameshaingia hapo awali.
MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa vyombo hivi vya usafiri bodaboda na bajaji vimekuwa vikisababisha ajali nyingi na wananchi wengi wanapoteza maisha, lakini kwa hali ilivyo sasa wamiliki wanakatia bima ndogo ambayo haim-cover yule anayeendesha na yule abiria wake. Je, Serikali haioni umuhimu wa kukaa na wamiliki wa bodaboda wakatie bima kubwa (comprehensive) ili kuwalinda wananchi wetu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake ilikuwa ni kwamba Serikali haioni umuhimu wa kukaa ili kutengeneza mfumo mzuri ambao utasaidia na hawa ambao ni abiria lakini vilevile na hawa ambao wanaendesha vyombo hivi kuwa katika hali ya usalama. Limeletwa wazo na sisi kama Serikali tunalichukua kuona utaratibu mzuri ambao utasaidia katika kuondoa adha hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwa kuongezea si tu katika bima tutakwenda mbali zaidi kuwataka pia na hawa waajiri ambao wanawaajiri hawa vijana wajiunge na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa maana ya WCF ili inapotokea tatizo lolote la muendesha bodaboda huyu basi na yeye awe katika sehemu nzuri ya kuweza kupata utaratibu ambao umewekwa na WCF kwa maana ya kuweza kumshughulikia katika matatizo ambayo yanatokana na magonjwa au ulemavu kutokana na shughuli ambayo wanaifanya.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumjulisha Mheshimiwa Gekul kwamba suala hili tunalichukua lakini tutakwenda mbali zaidi kusisitiza kwamba na hawa wanakuwa katika utaratibu huo mzuri.
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, sote tunafahamu kwamba biashara ya bodaboda imekuwa ni sehemu kubwa sana ya ajira kwa vijana, lakini naomba tu kufahamu ukichukulia Jimbo la Nyamagana peke yake zipo bodaboda takribani 6,700 lakini vijana hao wenye uwezo wa kujiajiri ni asilimia 30% peke yake, ni nini mkakati wa Serikali kutumia walau fedha za Mfuko wa Vijana na Fedha za Uwezeshaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu waweze kukopeshwa na fedha hizi watumie kama sehemu ya ajira yao ili kuepusha migogoro na waajiri wao na mikataba isiyokuwa rafiki kwao? Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mabula kwa kazi kubwa anayofanya kupambania vijana wa Nyamagana hasa vijana wamachinga na bodaboda amekuwa akifanya kazi hii vizuri sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mkakati wa Serikali ni nini katika hili? Ni kweli tunatambua kwamba asilimia kubwa ya vijana wangependa kumiliki pikipiki hizi ziwe mali yao lakini kikubwa ambacho kinawakwamisha ni upatikanaji wa mikopo ya masharti nafuu, lakini vilevile na fedha kuweza kununulia vifaa hivi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama Serikali hatua ya kwanza ambayo tumekuwa tukiifanya ni kuhamisisha vikundi vya vijana kwanza wakae pamoja, wajisajili then baada ya pale sisi chini Ofisi ya Waziri Mkuu tunalo Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambalo linaratibu zaidi ya mifuko 19 ambayo inatoa mikopo na inatoa na ruzuku.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, rai yangu ni kuwaomba Waheshimiwa Wabunge ambao naamini kila Mbunge hapa kwake ana bodaboda ambao wana mahitaji haya kwanza kuwahamasisha kukaa katika vikundi, wajisajili na baadae tutawasaidia kuwaunganisha na mifuko mbalimbali na taasisi za kifedha ili waweze kupata mikopo ya aina mbalimbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, ziko programu nyingi ambazo zinafanyika sasa hivi ambapo yule mwendesha bodaboda ana-deposit kiasi kidogo tu katika taasisi ya fedha na anakabidhiwa chombo chake na anakuwa anafanya kazi kurudisha taratibu taratibu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niwaombe Waheshimiwa Wabunge wote, najua ni kilio cha Wabunge wengi hakikisheni kwamba mnahamasisha uundaji wa vyama vya bodaboda na baadaye Ofisi ya Waziri Mkuu, sisi tutafanya kazi ya kuwasaidia kuratibu kwa maana mifuko gani inaweza kusaidia kuwezesha makundi haya.
MHE.USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo ninalo. Naomba kumuuliza Mheshimiwa Waziri ni tatizo gani lililopelekea ripoti zenye umuhimu mkubwa kama huu wa haki za binadamu zisichapishwe kwa wakati ili Wabunge na Watanzania wote kwa ujumla wakaweza kujua hali za haki za binadamu katika nchi yao?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Wabunge kwa upande wa Zanzibar hawapati fursa ya kukagua vituo vya polisi wala vyuo vya mafunzo ili kuwatembelea waliozuiliwa na waliofungwa kujua kama utekekelezaji wa haki za binadamu unafanyika kwa kiwango ambacho kinatakiwa. Je, Serikali iko tayari kuwatengenezea Wabunge wa Zanzibar utaratibu wa kuweza kuvikagua vituo vya polisi na vyuo vya mafunzo ili kuona haki ya binadamu inatendeka kwa kiasi gani? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza amezungumzia kuhusu uchapishwaji wa hizi ripoti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi ni kwamba, ni kweli taarifa hizi zinapaswa kuwasilishwa Bungeni kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameuliza na ndiyo maana tumetoa maelezo yetu kama Serikali kwamba ziko ambazo zimekamilika lakini ziko ambazo zinasubiri ukaguzi wa mahesabu ndipo ziweze kuchapwa na kuletwa Bungeni kwa sababu ndiyo itakuwa taarifa kamili.
Kwa hiyo, nimuondoe hofu tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tunafahamu umuhimu wa taarifa hizi kuwasilishwa mbele ya Bunge na ndiyo maana Tume inaendelea kufanya kazi hiyo kuhakikisha kwamba taarifa hizi zinafika kwa wakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la nyongeza la pili ameulizia kuhusu kuwashirikisha Wabunge wa Zanzibar. Kwa mujibu wa Ibara ya 130(1) na kifungu cha 6 cha Sheria Namba 7 ya Tume ya mwaka 2001, Tume imepewa majukumu kufanya kazi hiyo ya kwenda kufanya ukaguzi yenyewe. Kwa hiyo, kazi hii kimsingi ni kazi ya Tume, lakini ambacho tunaweza tukakifanya kwa sababu ya kuombwa ushiriki wa Waheshimiwa Wabunge katika jambo hili na sisi pia tuko tayari kushirikiana nao ili wapate fursa kufahamu hali zilizoko katika maeneo ya magereza na vituo vya polisi.
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, lakini katika ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi yetu katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano umeongezeka sana.
Je, ni lini Tume hii itatoa ripoti kwa sababu polisi wamekuwa wakikaa na watu mahabusu zaidi ya saa 24 kinyume cha sheria kitu ambacho kinakiuka haki za binadamu. Mimi binafsi nasema haya kwa uzoefu nilionao, mara nyingi nimekuwa nakwenda kwenye custody nayaona haya na naongea kama Mbunge kwamba kuna ukiukwaji wa haki za binadamu, kuna watu wanakaa zaidi ya miezi miwili katika vituo vya poilisi wanakuwa tortured, wanapigwa na wanaumizwa.
Je, Serikali inatoa tamko gani kuhusiana na tatizo hili ambapo kumekuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu katika vituo vya polisi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la msingi la Mhehimiwa Msigwa hapa imebeba hoja, ni lini Tume italeta taarifa kuhusiana na vitendo ambavyo vinavyanywa na Jeshi la Polisi.
Mheshimiwa Mwneyekiti, kazi ya Tume hii inajikita katika maeneo tofauti tofauti, ukiacha masuala ambayo yanahusisha polisi, lakini Tume hii ina kazi nyingi za kufanya kwa maana ya kutoa elimu lakini vilevile kwenda kutembelea katika shule za maadilisho, mahabusu za watoto na kila Tume inapokwenda kufanya kazi hiyo imekuwa ikiandaa taarifa na kuziwasilisha katika taasisi husika na mojawapo ikiwa ni kutoa maangalizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa tu ya Mheshimiwa Mbunge, Tume imekuwa ikifanya kazi hii. Kwa mfano, kipindi cha mwaka jana ilitolewa kauli moja kutoka kule Zanzibar na Jeshi la Polisi la kuzuia baadhi ya wafuasi wasiwakilishwe mahakamani na Tume ilitoa maelekezo na kulionya Jeshi la Polisi kwamba hizo ni haki za kimsingi kwa sababu ukisoma kwenye Sheria ya Mwenedo wa Makosa ya Jinai, kifungu cha 40 kinaelekeza kabisa kwamba kila mtu ana haki ya kuwasilishwa katika kesi za jinai.
Kwa hiyo, Tume imefanya kazi yake kuhakikisha kwamba likitokea jambo lolote lile kuhusu taasisi mbalimbali za Serikali au binafsi ambazo zinaonekana kama zinakiuka haki basi wamekuwa kwakitoa taarifa zake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kwa kumalizia ni kwamba pamoja na ukaguzi unaofanyika taarifa hizi zimekuwa zikiandaliwa na wahusika wamekuwa wakiwasilishiwa na hapa Bungeni taarifa itakuja rasmi kwa sababu ya ile taarifa ambayo tunaitegemea ya Tume ambayo itawasilishwa kwa Waziri mwenye dhamana.
MHE. JAKU H. AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa fursa hii, naomba kuuliza swali dogo la nyongeza lenye kifungu (a) na (b).
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri alipokuwa akijibu swali la msingi alisema Tume imekuwa ikiongeza jitihada kila mwaka kukagua vituo vya polisi na magereza. Je, katika kukagua vituo hivyo hasa vya polisi wameona makosa gani na hatua gani zimechukuliwa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili Kikatiba wanafunzi walioko magerezani…
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa
Mwenyekiti, Mheshimiwa Jaku anataka kufahamu baada ya kaguzi hizi ni makosa gani yameonekana. Nirudie tu majibu yangu ya msingi niliyoyasema kwamba ripoti hii ikikamilika itawasilishwa. Nachelea kusema moja kwa moja kwa sababu iko ndani ya ripoti na ripoti hii itawasilishwa. Kwa hiyo, nimuombe Mheshimiwa Mbunge avute subira ripoti hii ikiwasilishwa ataona ukaguzi uliofanyika na matokeo ya ukaguzi huo.
MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba niipongeze Serikali kwa kazi nzuri na juhudi zinazoendelea kufanyika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tunashukuru kweli tunajengewa Mahakama ya Mkoa pamoja na Wilaya katika jengo moja. Lile jengo limejengwa vyumba vinne tu na Mahakimu wa Mkoa wanahitajika wawili na Mahakimu wa Wilaya wanahitajika wawili. Jaji akija hana ofisi ya kukaa na hakuna sehemu nyingine ya huduma mbalimbali za kiofisi.
Je, Serikali haioni kwamba hilo jengo ni la muda tu siyo la muda mrefu? Serikali haioni kama itapata hasara kujenga sasa hivi na wakati mwingine wajenge tena. Lini sasa Serikali itaongeza lilelile jengo liwe kubwa na la kutosheleza? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, ndani ya Mkoa wetu wa Katavi Mahakimu ni wachache sana, je, Serikali itaongeza lini Mahakimu ndani ya Mkoa wetu wa Katavi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza anazungumza kuhusu jengo hili kuwa na vyumba ambavyo havitoshi na kama Serikali itaingia hasara kwa sababu baadae tena itahitajika kujenga jengo lingine. Nianze kwa kusema jengo hili la Mahakama ya Mkoa linajengwa katika eneo moja ambalo linaitwa Ilembo, Manispaa ya Mpanda. Tumempeleka mkandarasi ambaye anaitwa Moladi Tanzania yuko pale anafanya kazi hiyo, kilichojitokeza ni kwamba baada ya mvua kubwa kunyesha na udongo wa pale Ilembo ni mfinyanzi mkandarasi na consultant wameshauriana tumebadilisha michoro tena ambayo inachorwa upya na lengo hapa ni kuhakikisha tunajenga jengo lenye ubora wa juu ili shughuli za Mahakama ziendelee katika eneo hilo la Ilembo katika Manispaa ya Mpanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni hatua ya kwanza ambayo Serikali imefanya. Mheshimiwa Mbunge naomba ukubaliane kwamba ni hatua kubwa sana ya ujenzi wa vyumba hivyo ambavyo vitawaweka Mahakimu wa Mkoa pamoja na Mahakimu wa Wilaya. Yako bado maeneo mengi nchi nzima ambayo yana mahitaji ya Mahakama. Kwa hiyo, kwa kuanza pale Ilembo ni fursa ya kipekee kwa Mkoa na tushukuru sana Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, upo msemo mmoja wanasema ndege mmoja wa mkononi ana thamani kuliko wawili wa shambani. Sasa tayari pale Mpanda wameshapata majengo haya, waishukuru Serikali ikitotokea bajeti nyingine tutaona namna ya kufanya lakini mahitaji ni makubwa sana kwa nchi nzima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, amezungumza kuhusu Mahakimu wachache, hii ni changamoto si tu katika Mkoa wa Katavi lakini katika Mikoa mingi sana ndani ya nchi yetu. Pindi pale bajeti itakaporuhusu ya kuwaajiri watumishi wengine, Mkoa wa Katavi pia na wenyewe tutauangalia ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa Mahakimu.
MHE. STEPHEN HILARY NGONYANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijauliza maswali mawili ya nyongeza kwa ruksa yako naomba nimpongeze Mheshimiwa Rais, kwa kunipa shilingi bilioni moja kwa ajili ya vituo viwili vya Afya, Kata ya Mkumbala na Kituo cha Afya Bungu, Mungu ambariki sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mwaka 2012 Mahakama hii iliahidiwa kwamba itajengwa, mwaka 2014 iliahidiwa itajengwa, mwaka 2015 iliahidiwa itajengwa, sasa nataka tamko la Serikali mwaka 2020 ni kweli kituo hiki au Mahakama hii ya Mwanzo itajengwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Serikali ilijenga Mahakama ya Mwanzo ya kisasa zaidi pale Magoma katika Tarafa ya Magoma, na nikajitahidi nikakarabati Mahakama moja katika Tarafa ya Bungu, lakini Mahakama hizi mpaka zaidi ya miaka saba hazijafunguliwa.
Sasa naomba Serikali iniambie ni nini sababu zinazuia Mahakama hizi zisifunguliwe wakati wananchi wanapata shida sana kutolewa umbali wa kilometa 30 kwenda kufuata Mahakama sehemu nyingine? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nichukue fursa hii kuanza kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa jitihada kubwa anazozifanya katika kuhakikisha kwamba huduma hii ya Mahakama inawafikia wananchi wake kwa ukaribu zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lakle la kwanza la nyongeza, nataka nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa mwaka wa fedha wa mwaka 2019/2020 Mahakama hii ya Mwanzo itajengwa na nimuondolee hofu kwa sababu hivi sasa, kupitia Wizara tunashirikiana na Chuo Kikuu cha Ardhi na Baraza la Nyumba la Taifa na sasa tuna mfumo mzuri wa ujengaji wa Mahakama kutumia teknolojia ya moladi ambayo inafanya kazi kukamilika kwa muda mfupi na ukuta kuwa imara zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba kazi hiyo itafanyika na hivi sasa navyozungumza. Tunayo miradi takribani 39 nchi nzima ambayo inatekelezwa na kufikia mwaka wa fedha 2018/2019 tutakuwa tumekamisha Mahakama za Mwanzo na Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mkoa takribani 70. Kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba hii ni ahadi ya Serikali na jambo hili litatekelezeka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni kuhusu Mahakama ya Magoma ambayo tayari ukarabati na ujenzi umefanyika lakini mpaka leo haijafunguliwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kumuagiza Mtendaji wa Mahakama wa Mkoa wa Tanga kuhakikisha kwamba anafuatilia na kutupatia taarifa na sisi tutakwenda kufuatilia na tutampatia majibu Mheshimiwa Mbunge, lakini nataka nimuahidi tu kwamba kama hakuna vikwazo vingine vyovyote basi tutahakikisha kwamba Mahakama hii inafanya kazi na wananchi wa Tarafa ya Magoma wanapata huduma hii stahiki.
MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, nina maswali madogo mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, kwa kuwa kiwango hicho ni kidogo ambacho kinapelekea hata nauli; kwa mfano, hata katika mabasi ya mwendo kasi ukipiga hesabu hayamtoshelezi huyu mfanyakazi; hawaoni sasa wafanyakazi hawatafanya kazi kwa moyo na tija kwa sababu ya mshahara mdogo? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa kuna wenzetu wawekeza wa nje hasa Wachina wameingia, wanafanya kazi ambazo Watanzania wanazifanya, tena kwa bei nafuu; sasa Serikali haioni ni wakati wa kuwabana kuhakikisha kwamba zile shughuli zinazoweza kufanywa na Watanzania zifanywe na Watanzania badala ya wawekezaji wanaouza mpaka vocha ambao wameshaingia nchini?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA, NA WENYE ULEMAVU – MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la kwanza Mheshimiwa Mbunge amehoji juu ya viwango hivyo kwamba ni vidogo na katika jibu langu la msingi nimeeleza vyema ya kwamba, Serikali kila baada ya miaka mitatu kupitia Waziri mwenye dhamana, amekuwa akitoa kitu kinaitwa wage order. Wage order ndiyo mshahara wa kima cha chini kwa sekta binafsi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge wage order ya mwaka wa mwisho ilikuwa ni ya mwaka 2013.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, sasa hivi tayari Mheshimiwa Waziri ameshaunda Bodi ya watu 17 ambao wanaanza kushughulikia suala hilo la mshahara wa kima cha chini. Bodi hii itafanya uchunguzi kutoka na sekta husika na wataangalia maisha ya leo jinsi yalivyo na gharama zilivyo na baadaye sasa watapendekeza kwa Mheshimiwa Waziri kima kingine cha chini cha mshahara kutokana na sekta.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, napenda kumwambia Mheshimiwa Mbunge, kwa sababu zoezi hili ndio linaendelea sasa na Mheshimiwa Waziri ameshakamilisha kazi yake, tunasubiri mapendekezo kutoka kwenye Vyama vya Wafanyakazi, Vyama vya Waajiri pamoja na Serikali ili baadaye Mheshimiwa Waziri aweze kutoa amri kwa maana ya order.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia nichukuwe fursa hii kuwasisitiza wenzetu wa Vyama vya Wafanyakazi kuhakikisha kwamba wanasimamia majukumu yao ipasavyo ili waendelee kufanya vikao na waajiri ili katika yale ambayo bado wanaweza wakazungumza na waajiri katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi, basi wafanye hivyo kwa niaba ya wafanyakazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Mheshimiwa Mbunge aliuliza kwamba wako wafanyakazi wengi sana wa kigeni ambao wanaendelea kufanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2015 Bunge hili lilipitisha Sheria ya Kuratibu Ajira kwa Wageni na ninyi wenyewe ni mashahidi, Serikali kupitia Wizara ya Kazi, tumekuwa tukisimamia sana sheria hii kuhakikisha kwamba zile kazi zote ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania na ambazo zina ujuzi ndani ya nchi hii ziweze kufanywa na Watanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, sisi kama Wizara, tutaendelea kuimarisha kaguzi mbalimbali ili kuwabaini watu wote ambao wanafanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania ambapo kwa namna moja ama nyingine kumekuwa kuna tatizo kubwa sana la udanganyifu kwa maana ya kwamba, watu wakiomba vibali wanadanganya nafasi anayokuwa, lakini baadaye unakuta amechukua nafasi ambazo zinaweza zikafanywa na Watanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, sisi kama Serikali tutahakikisha kwamba tunaimarisha ukaguzi ili jambo hili lisiendelee kuwepo na tumekuwa tukichukuwa hatua stahiki pale inapobainika.
MHE. FAIDA MOHAMED BAKAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, mbali na matatizo ya mishahara kwa wafanyakazi wengi wa viwandani, lakini pia kuna tatizo moja sugu la ukatiwaji wa bima, yaani wafanyakati wa viwandani kupatiwa bima. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuvilazimisha viwanda viwakatie bima za maisha wafanyakazi wao?
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA, NA WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa Serikali imegundua kwamba yapo matatizo ya namna mbalimbali ambayo wafanyakazi wanatakiwa wahifadhiwe kwa kufuata mifumo inayotakiwa katika nchi yetu ya Tanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua tatizo hilo, Serikali imeanzisha ule Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi na baada ya kuanzisha mfuko huo na kuwalazimisha waajiri watii takwa la kisheria la luchangia mfuko huo, sasa tunauhakika na ninaomba niwahakikishie wafanyakazi watulie kwa sababu sasa Serikali itakuwa ikiwafidia kupitia kwenye mfuko huo ambao umeanzishwa na Serikali na sisi tutaendelea kuusimamia kuhakikisha wafanyakazi wanafidiwa katika viwango vinavyostahiki kulingana na sheria ilivyo na namna mbalimbali ambazo zitakuwa zimetokea katika sekta zao za kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, Serikali imelisimamia hilo na tutaendelea kulifanyia kazi vizuri.
MHE. ABDALLAH H. ULEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika Jimbo langu la Mkuranga liko tatizo la wafanyakazi wanaofanya kazi katika viwanda hivyo vya Wachina, kulipwa malipo madogo kwa muda mrefu wa kazi. (Makofi)
Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari sasa kuja Mkuranga kuonana na vijana wale wanaofanya kazi katika viwanda vile na kuzungumza nao na hatimaye kuweza kuwapa matokeo ya kuweza kuwasaidia kama Serikali?
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA, NA WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa Naibu Spika naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ulega (Baba Tulia) kama ifuatavyo:- (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Ulega, ni kweli amewaleta hao wafanyakazi mpaka ofisini kwangu na anafuatalia sana suala hilo. Nami kama Waziri, naomba nimhakikishie kwamba tutampa ushirikiano. Tutaangalia Sheria inataka nini na hao wawekezaji ni kwa kiasi gani wanavunja sheria ambazo ziko katika nchi yetu, basi ninathubutu kusema kwamba nitaongozana na Mheshimiwa Ulega (Baba Tulia) kwenda katika maeneo hayo anayoyasema na tutapanga utaratibu. Ila tu tutamwomba mtoto Tulia asiingilie utaratibu wa ziara yangu na Mheshimiwa Ulega kwenda kuangalia matatizo hayo.
MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na nashukuru pia kwa majibu mazuri kutoka kwa Mheshimiwa Naibu Waziri katika Wizara husika, nina maswali mawili ya nyongeza.
Swali la kwanza, kutokuwepo kwa takwimu sahihi hasa maeneo ya vijijini kumesababisha kutokuwepo na mipango mahsusi yenye kuleta maendeleo na tija kwa watu wenye ulemavu. Je, Serikali ina mpango gani wa kupata takwimu sahihi za watu wenye ulemavu zitakazosaidia kuwepo kwa mipango mahsusi itakayowasaidia watu wenye ulemavu hasa maeneo haya ya vijijini?
Swali la pili, uwepo wa Sera ya Taifa ya Huduma na Maendeleo kwa Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004, pamoja na uwepo wa sheria ambayo Naibu Waziri ameitaja Sheria Namba 9 ya huduma kwa watu wenye ulemavu zimesaidiaje kutatua matatizo ya walemavu na Waziri haoni kwamba mfuko wa watu wenye ulemavu ambao ungesimamia Baraza la Watu Wenye Ulemavu kutokutengewa pesa kutasababisha jitihada na mafanikio kwa watu wenye ulemavu yasiwepo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji wake, lakini kwa namna ambavyo amekuwa akitetea na kutushauri hasa katika mambo yanayohusu watu wenye ulemavu.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lililoulizwa hapa ni Serikali ina mpango gani kupata takwimu halisi za watu wenye ulemavu. Serikali tayari imekwishaanza mchakato na wameshazindua utaratibu wa kuanzisha kanzidata ambayo itasaidia kupata takwimu sahihi ya watu wenye ulemavu katika maeneo yote ya mijini na vijijini. Lengo kubwa la kanzidata hii itatusaidia pia kuwatambua watu wenye mahitaji hasa watu wenye ulemavu katika maeneo ya vijijini na kushirikiana na Kamati zile ambazo zimeundwa kuanzia ngazi ya Kijiji, Mtaa mpaka Halmashauri ili iwe rahisi kuweza kuwatambua na pia iwe rahisi kuweza kuwasaidia katika kutatua changamoto zao mbalimbali ambazo zinawakabili.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili ameuliza Sera na Sheria Namba 9 ya mwaka 2010 imesaidiaje kutatua changamoto na kero ambazo zinawakabili watu wenye ulemavu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nikiri kwamba uweo wa sheria hii kwanza kabisa imetengeneza msingi na imetengeneza haki za walemavu na sasa sheria hii imekuwa ndiyo sehemu nzuri na platform ya kuweza kusaidia Serikali katika kutimiza matakwa yake mbalimbali ya kusaidia watu wenye ulemavu.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma katika Sera ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2004 imezungumza moja ya jambo ambalo Serikali imeshaanza kulifanyia kazi hivi sasa, changamoto kubwa sana ya watu wenye ulemavu ilikuwa ni upatikanaji wa vifaa vyao ambavyo gharama imekuwa kubwa hasa kutokana na kodi ambayo imekuwa ikitozwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukifuatilia katika hotuba ya Waziri wa Fedha ambayo aliwasilisha hapa Bungeni Hotuba Kuu ya Serikali ukurasa wa 50, Mheshimiwa Waziri ameainisha bayana kabisa kwamba Serikali sasa inaandaa utaratibu wa kuondoa kodi na kuweka msamaha wa ushuru katika vifaa vyote ambavyo vinawahusu watu walemavu lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba huduma hizi zinawafikia kiurahisi sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia katika sheria yetu, Sheria Na. 9 ya mwaka 2010 ukiangalia kifungu namba 30 mpaka kifungu namba 34 kimezungumza wazi namna ambavyo watu wenye ulemavu na wenyewe wanapaswa kupata fursa za ajira katika taasisi za umma na taasisi binafsi. Kwa hiyo, naamini kabisa uwepo wa sheria na sera imechangia sana katika maendeleo ya watu wenye ulemavu.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nashukuru kwa majibu mazuri yaliyotolewa na Mheshimiwa Anthony Mavunde, Naibu Waziri anayehusika na masuala haya.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu ni kwamba, kutokana na kwamba bado hakujawa na udhibiti wa kutosha wa kuzuia madawa ya kulevya yasipenye na kutokana na tulivyomsikia Mkuu anayeshughulika na udhibiti wa madawa ya kulevya kwamba kule Zanzibar bado kunatumika kama kipenyo cha kupitisha madawa haya ya kulevya. Je, Serikali imejipangaje kuongeza ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi ili kudhibiti na kuhakikisha kwamba kule Zanzibar hakuwi mlango wa kupitisha madawa haya ya kulevya? Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli baada ya jitihada na juhudi kuwa kubwa sana Tanzania Bara, hasa kazi kubwa sana ambayo ilifanywa na Mamlaka ambayo imewafanya wafanyabiashara wengi sana wa dawa za kulevya nchini na wengine kukimbilia Zanzibar, ni kweli sasa Zanzibar imeanza kutumika kama sehemu ya uchochoro wa wafanyabiashara ambao wanakimbia kutoka Tanzania Bara.
Mheshimiwa Naibu Spika, kazi inayofanyika hivi sasa ni kuhakikisha kwamba tunaanza kufanya kazi kwa pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kwanza kutengeneza mfumo mzuri wa kusaidia katika kuhakikisha kwamba tunawabaini wafanyabiashara hata hao wanaokwenda nje Tanzania Bara ambao wanakwenda Zanzibar. Pia vimekuwepo vikao vya mara kwa mara kati ya Mamlaka na wataalam kutoka kule Zanzibar, lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba tunatengeneza mfumo mzuri wa udhibiti.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nimwondolee hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba kazi hiyo inaendelea na tayari tatizo hilo limebainika, naamini muda siyo mrefu sana maridhiano yakikamilika basi tutafanya kazi pia kuhakikisha kwamba tunazuia na upande wa Zanzibar.(Makofi)
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona. Kwa kuwa, Serikali inajizatiti kuzuia suala hili la madawa ya kulevya, Je, itatuhakikishia vipi kufanya kila Mkoa wa Tanzania kuwa na sober house ili kudhibiti matatizo haya?(Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika mikakati ambayo tumejiwekea ya kupambana na kudhibiti dawa za kulevya, moja ya mkakati ni kitu ambacho kinaitwa harm reduction. Harm reduction ni kupunguza madhara kwa watumiaji wa madawa ya kulevya hasa wale ambao wanatumia madawa ya heroin ambao wanakwenda kutibiwa kwa kutumia Methadone.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa Serikali pamoja na kuwa na mpango wa kuweka vituo vingi vya Sober houses lakini tunatumia hospitali katika Mikoa yetu kuwa na madirisha maalum kwa ajili ya kuwahudumia watu ambao wameathirika na madawa ya kulevya. Kwa hiyo, naamini huduma itasambaa Nchi nzima na wengi watapata huduma hiyo kupitia katika hospitali za Mikoa katika maeneo husika. (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WALEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ambayo ameyatoa hivi punde.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue nafasi hii kwanza niliarifu Bunge lako Tukufu kwamba Tanzania tumepewa heshima ya kuwa ni kati ya nchi chache ndani ya Bara la Afrika ambayo inafanya vizuri, kuwa na sheria nzuri na inasimamia vizuri udhibiti wa dawa za kulevya katika nchi ya Tanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hali hiyo, Umoja wa Mataifa umekubaliana kwamba mwaka huu wa 2018, nchi zote za Bara la Afrika, Viongozi wanaosimamia Sheria za Kudhibiti Dawa za Kulevya katika nchi zao watakuwa na mkutano wao mkubwa sana lakini utafanyika ndani ya Tanzania ili waweze kujifunza zaidi ni kwa kiasi gani Tanzania imefanikiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nikiongeza kuhusu suala hili la kutengeneza mfumo wa utengemaa kwa waathirika wa dawa za kulevya, Serikali kupitia Mamlaka kazi kubwa tuliyoifanya katika kipindi hiki kifupi ni kuandaa miongozo na utaratibu wa uendeshaji wa sober houses katika nchi yetu ya Tanzania; miongozo hiyo sasa ipo tayari.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, Serikali kwa kuanza kujifunza model nzuri ya sober houses katika nchi yetu ya Tanzania tumetengeneza tayari tumeshajenga na Mheshimiwa Waziri Mkuu mwaka jana amezindua National Rehabilitation Center katika Mji wa Dodoma na itaanza kufanya kazi baada ya muda siyo mrefu, hiyo itakuwa ni model ya Sober houses na rehabilitation centers nyingine ambazo tunazihitaji katika nchi ya Tanzania za kuwasaidia hawa waraibu wa dawa za kulevya kurudi katika hali yao. Hivyo, Serikali inafanya kazi kubwa sana katika eneo hili. Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. (Makofi)
MHE. ZAINAB M. AMIR: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Tunaona jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali katika kudhibiti suala hili la madawa ya kulevya na wakati yanapokamatwa tunaoneshwa. Je, ni kwa nini cocaine na heroin wakati zinateketezwa hatuoneshwi tunaoneshwa bangi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza namshukuru Mheshimiwa Mbunge kwamba amekiri amekuwa akiona uteketezaji wa mashamba ya bangi ambao kwa kipindi cha Januari, 2017 mpaka Disemba, 2017 takribani ekari 542 za bangi zimeteketezwa na hii ikiwa ni kazi nzuri ambayo imefanywa na mamlaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake alitaka kujua kwa nini hatuoni uteketezwaji wa madawa mengine aina ya cocaine na heroin. Kwa nature ya madawa yenyewe namna uteketezaji wake uko tofauti na utaratibu unaotumika ni utaratibu ambao kwanza kabisa utahakikisha tunalinda afya na mazingira vilevile upo utaratibu ambao mamlaka unautumia katika uteketezaji huu ambao kwa kiwango kikubwa sana haijawa rasmi kwamba inaoneshwa kila wakati, lakini ni kweli kazi kubwa imefanyika katika eneo hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka ninapozungumza hivi sasa takribani kilo 196 za heroin zimeteketezwa ikiwa ni kazi nzuri ambayo inafanywa na mamlaka. Kwa hiyo, siyo kwamba kazi hii haifanyiki inafanyika lakini kwa uangalizi mkubwa sana, inahitaji pia kuangalia na athari za mazingira.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa jibu lake sahihi na niunge mkono kwamba ni kweli madawa mengine yanateketezwa kwa uangalifu sana kwa sababu hata bangi tu nilienda kuteketeza nilipotoka pale ilibidi niende kwa Daktari kuangalia kama haijaniingia na Daktari aliniambia sijavuta. (Kicheko)
MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwanza nianze kwa kuipongeza Serikali kwa kuja na utaratibu mpya wa kutoa huduma hii kwa wananchi kupitia NSSF kwa kushirikiana na Azania Bank. Hii ni mara ya pili nauliza hili swali katika Bunge hili la Kumi na Moja kwa sababu ni jambo mahususi. Ili jamii yoyote iweze kutoka kwenye umasikini, lazima kuwe kuna kitu kinaitwa social safety net na huu mpango ulikuwa mzuri kwa sababu katika huduma hii wananchi wangenufaika na pensheni ya uzeeni, pensheni ya ulemavu, pensheni ya urithi, mafao ya uzazi, mafao ya mazishi, mafao ya matibabu na mikopo ya muda mfupi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuiomba Serikali iwaambie wananchi wa Karagwe, je, tutegemee lini NSSF na Azania Bank watakuja Karagwe ili wale wananchi ambao walitoa ule mchango wa shilingi 20,000 wakasubiri huduma kwa muda mrefu, wategemee wataipata lini? Hilo ni swali la kwanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Serikali inaonaje kufanya pilot study kuanzia Karagwe na sehemu nyingine ili tuone namna ambayo tunaweza tukaleta social safety net along side, jitihada nzuri ya Serikali inayoendelea kutupeleka kwenye uchumi wa kati? Nakushukuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza anauliza ni lini tutakwenda Karagwe?
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi ni kwamba mikopo hii ilisitishwa kwa sababu mbalimbali ambazo niliziainisha pale juu, mojawapo ikiwa ni kwamba fedha nyingi ambazo zilitolewa hazikurejeshwa kwa wakati na hivyo kupelekea Bodi ya NSSF kukaa upya na kutathmini zoezi zima la utoaji wa mikopo na hivyo, baada ya kujiridhisha na utaratibu huu mpya, sasa shughuli ya utoaji wa mikopo itaanza rasmi kuanzia tarehe 1 Julai, 2017 na ninaamini pia wananchi wa Wilaya ya Karagwe na wenyewe watafikiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuliweka hili sawa, katika mpango huu wa utoaji wa mikopo kupitia NSSF unawalenga wale wote ambao ni wanachama wa NSSF. Kwa hiyo, namwondoa hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba tarehe 1 Julai, 2017 zoezi hili litaanza upya kushirikiana na Benki ya Azania.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kuhusu masuala ya pilot study ya social safety net, tumepokea maoni ya Mheshimiwa Mbunge na tutayafanyia kazi ili tuone namna ya kuweza kuwasaidia Watanzania wengi zaidi kupata fursa ya kupata mikopo kupitia katika NSSF.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunapokea ushauri wake na tunamshukuru sana kwa ufuatiliaji na nimwahidi tu kwamba haya aliyoyasema, basi nasi tutashirikiana na wenzetu wa NSSF kuona Watanzania wengi zaidi wananufaika kupitia mikopo hii ya NSSF.
MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba nitambue juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi katika kuhakikisha ustawi wa maisha ya watu wenye ulemavu. Pia naishukuru sana Serikali kwa majibu haya mazuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa kuna watu wenye ulemavu ambao wamejitahidi kuondokana na utegemezi na hivyo kuanzisha biashara zao, je, Serikali iko tayari kuondoa kodi kwenye biashara za watu wenye ulemavu?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa kuna ile 10% ya Halmashauri ambayo inatengwa kwa ajili ya wanawake na vijana; na kwa kuwa Serikali ilishakubaliana na pendekezo langu la kugawanya asilimia hii, kwamba 4% iwe kwa wanawake na 4% iwe kwa vijana halafu 2% iwe kwa ajili ya watu wenye ulemavu, je, ni lini sasa pendekezo langu hili litafanyiwa kazi? Ama ni nini tamko la Serikali kuhusiana na huu ugawaji wa hii 2%?
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge ameuliza kama Serikali ipo tayari kuondoa kodi kwa watu wenye ulemavu wanaojishughulisha na shughuli za kibiashara na ujasiriamali.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, napenda kuchukua fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwasemea watu wenye ulemavu na amekuwa mchango na msaada mkubwa sana ndani ya Wizara yetu. Pia Serikali inawathamini sana na tunaendelea kuwaendeleza watu wenye ulemavu katika kuhakikisha kwamba na wenyewe wanapata ujuzi mbalimbali ili waweze kujitegemea pamoja na biashara mbalimbali. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, tumeweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba watu wote wenye ulemavu ambao wanafanya shughuli mbalimbali, lakini ambao wangependa pia kujifunza masuala mbalimbali katika kila programu chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, tumetenga nafasi maalum ili watu hao wenye ulemavu waweze kupata nafasi ya kushiriki katika programu mbalimbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, programu mojawapo ya mfano kabisa ni programu ya Youth Economic Empowerment ambayo ilikuwa chini ya Plan International ambapo tulitenga nafasi zaidi ya 950 kwa watu wenye ulemavu.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la kwanza, aliuliza kama Serikali ipo tayari kuwaondolea kodi. Mheshimiwa Mbunge ameleta wazo hili, nasi tunalipokea, lakini kwa sasa kwa sababu ya taratibu za nchi zilivyo, siwezi kusemea hapa moja kwa moja lakini kubwa ambalo tutalifanya ni kuhakikisha tu kwamba tunawajengea uwezo zaidi ili na wao waweze kujitegemea. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ridhaa yako, nakuomba swali la pili kuhusu 10% atalijibu Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ikupa kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza namshukuru Mheshimiwa Ikupa, siku ya uwasilishaji wa bajeti yetu alileta hiyo concern ya watu wenye ulemavu na siku ile tuliweka commitment kwamba kwa sababu katika ule mgawanyo wa 10%, kuna kundi la vijana, akina mama na kundi specific la watu wenye ulemavu ambalo halijazungumzwa. Tulifanya commitment siku ile kwamba tutaangalia utaratibu tuone ni jinsi gani tutafanya, hata 2% kutokana na mapendekezo yake; na siku ile liliridhiwa katika bajeti.
Mhehimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, lipo katika mchakato, tutalifanyia kazi na tutatoa waraka maalum katika eneo hilo. (Makofi)
MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa kuwa lengo la kutoa ajira kwa watu wenye ulemavu limekuwa likifuatiliwa na taasisi mbalimbali duniani, na kwa kuwa taasisi nyingi hupewa ulazima wa kutenga idadi ya walemavu watakaoajiriwa na kupewa incentives kwa walemavu wanaoajiriwa.
Je, Serikali yetu iko tayari kujifunza lolote kulingana na utaratibu huo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika Sheria Na. 9 ya mwaka 2010 katika eneo la ajira, Sheria imetoa msisitizo kwamba kila mwajiri nchini ambaye atawaajiri watu kuanzia 20 na kuendelea lazima atenge 3% kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tunafuatilia kuhakikisha kwamba Sheria hii inatekelezeka.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, kwanza naipongeza Serikali kwa kubadilisha utaratibu wa awali kwa sababu utaratibu wa awali wakulima waikuwa hawanufaiki. Nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa msimu wa mvua katika maeneo mbalimbali hapa nchini unatofautiana, kwa mfano, katika Mkoa wa Kigoma mvua za kupandia ni za mwezi wa Oktoba. Je, Serikali iko tayari sasa kuhakikisha mbolea inawafikia wakulima mapema zaidi kuliko ilivyo sasa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, wapo mawakala waliofanya kazi kubwa ya kusambaza mbolea kwa wakulima. Na kati ya mawakala hao wapo waliofanya kazi kwa uadilifu mkubwa na uaminifu, lakini wapo ambao hawakuwa waaminifu na Serikali ilituma watu kwenda kuhakiki madeni kwa mawakala hao nchi nzima.
Je, ni lini Serikali itawalipa mawakala waliofanya kazi kwa uadilifu, ili waweze kulipa madeni waliyokopa katika benki mbalimbali, wakiwemo mawakala wanawake ambao wanateseka sana kudai pesa zao? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza la kuhusu utofauti wa misimu ya mvua na mbolea kuwafikia wakulima kwa wakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuondoe hofu tu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba Wizara ya Kilimo inatambua kwamba pembejeo ya mbolea ni kati ya virutubisho muhimu sana, ili kumfanya mkulima wa Kitanzania aweze kulima kilimo cha tija. Sasa katika mpango wa Wizara ni kuhakikisha kwamba katika mfumo huu mpya ambao tunakwenda nao wa bulk procurement mbolea hizi ziweze kuwafikia wakulima kwa wakati, ili waweze kutumia kwa ajili ya kilimo chao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, na kwa sababu ya Maputo Declaration ya mwaka 2003 ambayo katika Ukanda wa Nchi za Kusini mwa Afrika imesema kwamba Tanzania ni kati ya nchi ambazo zinatumia kiwango kidogo cha virutubisho kwa hekta moja ambayo kwa mujibu wa Declaration hii inapaswa kila hekta moja vitumike virutubisho kilo 50 na sisi tupo katika kilo 19. Kwa hiyo, kwa kuona umuhimu huo Serikali sasa itahakikisha kwamba, mbolea hii inawafikia wakulima kwa wakati, ili waweze kulima kilimo cha tija.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili amezungumza kuhusu uhakiki wa malipo ya mawakala.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosema Waziri wa Kilimo wakati wa bajeti yake ni kweli, wako mawakala ambao walifanya kazi hii kwa uaminifu, lakini ambao bado hawajalipwa malipo yao. Tayari Mheshimiwa Waziri Mkuu ameshaiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kufanya uhakiki kwa Mikoa yote 26, isipokuwa Dar es Salaam peke yake ili ndani ya mwezi mmoja mawakala hawa ambao walisambaza pembejeo waweze kulipwa pesa zao. (Makofi)
MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Kwa kuwa tunaona dhahiri kwamba kilimo kinazidi kurudi nyuma badala ya kusonga mbele, na kwa kuwa tumekuwa sasa wakulima hasa wale wa vijijini wanategemea mbegu za kununua na sio mbegu za asili na mbegu hizi zinaenda sambamba na upatikanaji wa mbolea. Siku hizi kuna mbolea ya kulimia, kuvunia na kadhalika, wakati kilimo cha zamani cha asili tulikuwa tunatumia mfano, mbolea za samadi na mbegu zenye ubora.
Je, Serikali haioni umuhimu wa kurudi nyuma na kujitathmini kwamba tunakoenda siko, tuangalie zile system za zamani za kilimo ziboreshwe zaidi ili wakulima wapate manufaa ya mazao yao? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI,VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa ushauri ambao ameutoa na kama Serikali tumeuchukua.
Katika mpango wa Serikali katika huu mfumo mpya unaokuja wa bulk procurement Serikali itaagiza kwa wingi mbolea ya kupandia ambayo ni DIP na mbolea ya kukuzia ambayo ni urea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mbolea nyinginezo kwa maana ya NPK, MOP, SA na Bio fertilizers na folia zile za maji, hizi zitakuja katika utaratibu wa kawaida. Vilevile ndani ya Wizara ya Kilimo yupo Wakala wa Mbegu ambaye kazi yake ni udhibiti wa mbegu bora ambaye ni ASA na yeye tutamtumia ili wakulima wetu wafanye kilimo chenye tija.
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wahenga wanasema samaki mkunje angali mbichi. Nakumbuka zamani tulikuwa tunajifunza masomo ya kilimo katika shule za msingi na sekondari nchini, lakini kwa bahati mbaya sana masomo hayo yakafutwa. Sasa labda tupate Kauli ya Wizara ya Elimu ni kwa nini masomo haya yalifutwa na tunategemea vijana baada ya kumaliza vyuo vikuu ndio wanaoweza kupata sasa ajira kupitia kilimo na ufugaji wakati hawakuandaliwa tangu mwanzo?
Swali la pili ambalo linasema ni maeneo gani hasa yaliyoandaliwa na yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo kwa ajili ya vijana hawa wanapohitimu masomo yao ya Vyuo Vikuu na kukosa ajira katika maeneo mengine? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajibu swali la pili, la kwanza atajibu Mheshimiwa Waziri wa Elimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge ameuliza kama kuna maeneo ambayo yamekwishakutengwa kwa ajili ya shughuli hizi za vijana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2014 Novemba, Ofisi ya Waziri Mkuu ilifanya kikao na Wakuu wa Mikoa wote wa nchi nzima hapa Dodoma. Katika kikao hicho iliamuliwa kwamba kila Mkoa uende kutenga maeneo maalum ambayo tutayaita Youth Special Economic Zones, ni Ukanda Maalum wa Uchumi kwa ajili ya Vijana, lengo lake ni kuwafanya vijana hawa wahitimu na vijana wengine wote wa Kitanzania ambao wangependa kufanya shughuli ya ujasiriamali, lakini wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maeneo ili kupitia utaratibu huu waweze kupatiwa maeneo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka hivi sasa tayari Mikoa mingi imekwishatenga maeneo haya na zimekwishatengwa tayari ekari 85,000 nchi nzima kwa ajili ya shughuli za vijana.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ningependa kujibu swali la Mheshimiwa Ester Mahawe, kuhusiana na Serikali kufuta masomo ya kilimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kulihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba, Serikali haijafuta masomo ya kilimo, masomo ya kilimo bado yanafundishwa shuleni na hata katika matokeo ya wanafunzi wanaoenda Kidato cha Tano ambayo Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI ameyatangaza juzi wapo wanafunzi waliochaguliwwa kwenda kusoma combination zenye kilimo. Vilevile Serikali na Chuo Kikuu Maalum cha Kilimo cha Sokoine na Serikali ina mpango wa kuendelea kuimarisha masomo ya kilimo katika ngazi zote ikiwa ni pamoja na kuongeza udahili katika vyuo vikuu kwa sababu tunatambua kwamba, kilimo ndio uti wa mgongo wa maendeleo ya Taifa hili. (Makofi)
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Kwa kuwa swali la msingi linazungumzia ajira kwa vijana, kumekuwa na utaratibu wa baadhi ya makampuni kuajiri watu kutoka nje, yakiwemo makampuni ya ulinzi na kuwafanya vijana wa Kitanzania kutengwa kuonekana kwamba, wao hawana uwezo.
Je, Serikali haioni kuendelea kuajiri watu kutoka nje ni kuweka nchi yetu hatarini, badala ya kuajiri vijana wa Kitanzania?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, imetungwa Sheria ya Uratibu wa Ajira kwa Wageni ambayo na sisi kama Wizara, tunaisimamia. Nataka nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba katika utekelezaji wa sheria hii tunahakikisha nafasi nyingi sana zinashikwa na wazawa, ili kuweza kulinda ajira za Watanzania. Kama kuna jambo lolote limetokea kinyume chake hapo, basi tutaelekeza Maafisa wetu wa kazi waende kufanya ukaguzi na wale wote ambao wameingia kinyume cha utaratibu waweze kuchukuliwa hatua ili vijana wetu waweze kupata nafasi za ajira.
MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia fursa hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wazi kwamba uchumi wa nchi yetu ungekua zaidi kama tungewekeza kwenye kilimo, lakini tunaona kwamba kilimo chetu kinaendelea kuporomoka. Huko nyuma kilikuwa kinaingiza asilimia nne, lakini sasa hivi kimeshuka mpaka asilimia 1.7. Sasa nilikuwa naomba kujua Serikali ina mkakati gani kuhakikisha kwamba, vijana hawa wanajiajiri kwenye mashamba ili kuweza kukuza uchumi wetu? Kwa sababu vijana wapo wamezagaa, lakini mapori, mashamba yako makubwa, lakini hakuna chochote kinachoendelea. Je, Serikali kupitia ofisi yako ina mkakati gani?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu tumeandaa mpango mkakati wa Kitaifa, it is a national strategy ya kuwaingiza vijana katika kilimo. Katika mpango huu malengo makubwa ni kuyatumia yale mashamba makubwa ya Serikali ambayo hayatumiki kwa ajili ya shughuli za kilimo kwa vijana.
Kwa hiyo, tunaamini kabisa katika mpango huu kwa muungano huu kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Kilimo, tutafanya kazi pamoja ili maeneo haya sasa tuweze kuwapatia vijana wa nchi hii wakafanye shughuli za kilimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekuwa nikisema, narudia mara nyingine tena leo ya kwamba moja kati ya kazi ambayo tunaanza nayo mapema kabisa tumeamua katika eneo la Mkulazi na Mbigili pale Morogoro ambako Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na PPF wanakwenda kujenga Kiwanda cha Sukari tutawafanya vijana wa nchi hii kuwa ndio out growers ambao watasaidia kulima miwa kwa ajili ya kukilisha kiwanda. Kwa hiyo, tunaamini kabisa kwa kupitia mkakati huu vijana wengi zaidi watapata ajira na waweze kujiajiri.(Makofi)
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Asilimia 67 ya Watanzania wako kwenye ajra ya kilimo na kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kuna mikopo inayotolewa na ndani ya Halmashauri tunatenga asilimia tano kwa ajili ya vijana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kujua upande wa Serikali ni lini watabadilisha hiyo sheria ili ukomo wa umri kwa vijana katika kukopa usiwepo kwa sababu, kumekuwa na changamoto, wengine wamefikia miaka 45 miaka 50, lakini bado wanahitaji mikopo, lakini wanakwamishwa na suala la umri. Ni lini Serikali itabadilisha hiyo sheria?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ya kuhusu lini tutabadilisha umri, hili ni suala la kisera. Siwezi kulisema hapa moja kwa moja, lakini definition ya kijana si ya Tanzania peke yake ni definition ya kidunia na sisi tunakwenda katika definition ambayo inazungumzwa na ILO, lakini kama kuna mahitaji hayo nafikiri baadae, kupitia sera na mahitaji mbalimbali, jambo hilo linaweza likaangaliwa upya, lakini kwa sasa bado tunabaki kuwa na umri huo kuanzia miaka 15 mpaka 35.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala la uwezeshaji; kwenye uwezeshaji ukiacha Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao ndio una-limit umri, mifuko mingine bado iko zaidi ya mifuko 19 ya uwezeshaji ambayo yenyewe haiangalii umri. Kwa hiyo, nikuombe Mheshimiwa Mbunge uendelee tu kuwapa elimu wananchi waelewe mifuko mingine ya uwezeshaji ili waweze kuitumia kwa ajili ya kuweza kujiwezesha. (Makofi)
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Spika, ahsante. nashukuru sana kwa majibu ambayo yametolewa na Serikali. Nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa mwekezaji aliyechukuwa DOWICO alizembea na kufunga kiwanda hicho, hivyo kusababisha uzalishaji mvinyo bora wa Dodoma kutokupatikana katika soko. Je, Serikali haioni umuhimu wa kumpatia mwekezaji mwingine tofauti na huyu aliyepo ili aweze kukifufua kiwanda hicho?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, Serikali imekuwa katika mpango wa kuwezesha uanzishwaji wa Kiwanda cha Kusindika mazao ya Zabibu katika Wilaya ya Chamwino kwa kushirikiana na mfuko wa GEPF. Je, ni hatua gani za haraka zilizochukuliwa na Serikali ili kuharakisha ujenzi wa kiwanda hiki ili wakulima wa zao la zabibu waweze kupata soko? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU - K.n.y WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI): Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la kwanza la kumtafuta mwekezaji mwingine, ndani ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Viwanda TIRDO na kwa kushirikiana pia na Ofisi ya Msajili wa Hazina tumeanzisha kitu kinaitwa Technical Audit na lengo lake kubwa ni kwenda kuvifuatilia viwanda hivi ambavyo vilibinafsishwa na havifanyi kazi na kuvifuatilia kuona namna gani vitaanza kufanya kazi kwa kupitia utaratibu huo wa utafiti ambao unafanyika.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimwondoe hofu tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tunawasiliana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi kwamba tayari ukarabati umeanza, kwa hiyo tutafanya hiyo technical audit ya kufuatilia kuona wanaanza lini kazi hii na baadaye tutatoa taarifa namna ya utekelezaji wake.
Mheshimiwa Spika, nafahamu kwamba jambo hili ni kubwa sana kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma, hasa ukiangalia kwamba zabibu ndio zao pekee ambalo linategemewa sana hapa Dodoma na Dodoma ndio sehemu pekee duniani ambako kuna uwezo wa kuvuna zabibu hii mara mbili. Israel wamejaribu, Afrika Kusini wamejaribu imeshindikana, kwa hiyo tunafahamu umuhimu wa zao hili kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma.
Mheshimiwa Spika, nimwondoa hofu Mheshimiwa Mbunge tu kwamba, hii pia ni Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha kwamba tunaendelea kuwavutia wawekezaji wengi kujenga viwanda vikubwa hasa ukizingatia kwamba mpaka Machi, 2017 tayari tumeweza kuvutia viwanda vikubwa 393 ambavyo vimesajiliwa na tayari vimeshaweka kiasi cha shilingi trillion tano. Kwa hiyo nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba, hata hili nalo litafanyika
Mheshimiwa Spika, la pili ameuliza kuhusu Kiwanda cha Mvinyo pale Chamwino. Nafahamu wakulima wa Dodoma wanategemea sana viwanda hivi vikubwa kwa ajili ya soko la zabibu, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge katika utaratibu wa uwekezaji katika viwanda, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, iliamua kuingia moja kwa moja katika uwekezaji huu. Pale Chamwino Mfuko wa GEPF, WCEF pamoja na TIB kwa pamoja watafanya uwekezaji wa kiwanda cha mvinyo.
Mheshimiwa Spika, ninavyozungumza hivi sasa tayari Bodi za Mifuko hii zimekwisha-approve kiasi cha shilingi bilioni 26 kwa ajili ya kwenda kuanza ujenzi wa kiwanda hiki. Niwaondoe hofu wananchi wa Mkoa wa Dodoma, watapata fursa ya masoko ya zabibu na ukiongozwa na wewe Mheshimiwa Spika, ambaye ni mkulima pia. (Makofi/Kicheko)
MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi nipongeze juhudi na kasi kubwa inayofanywa na Serikali ya kufufua viwanda vile ambavyo vilikuwa vimekufa, lakini pia kuvutia uwekezaji wa viwanda vipya. Sasa swali langu, ufufuaji wa viwanda vya korosho katika Ukanda wa Kusini hasa katika Jimbo la Mtama na maeneo mengine umefanyika lakini kuna kusuasua kwa ukamilishaji wa baadhi ya maeneo ili ubanguaji wa korosho uweze kufanyika kwa kiwango kikubwa na hasa hapa nazungumzia Kiwanda cha Kubangua Korosho cha Nachingwea, kwa kuwa Mwekezaji ambaye amefufua Kiwanda cha Mtama, ndiye ambaye amepewa kazi pia ya kufufua Kiwanda cha Nachingwea. Ni lini sasa kazi hii itakamilika ili wakulima wa korosho wapate mahali pa kuuza korosho yao na thamani ya zao la korosho ipate kuongezeka?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU - K.n.y WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI): Mheshimiwa Spika, ni dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kwamba inafufua viwanda vyote na ndiyo maana Wizara inafanya kazi ya karibu sana na Ofisi ya Msajili wa Hazina pamoja na TIRDO, lengo lake ni kuhakikisha kwamba viwanda hivi vinafufuliwa.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kwa upande wa Mikoa ya Kusini kule Mtwara, Lindi na kwingineko wanakolima korosho, tulikuja na model ambayo tumeiita BOOT ambayo Build on Operate na Transfer na hii ndiyo ambayo tuliitumia hata pale Mtama kwa kumtumia huyu Mwekezaji wa kutoka China ambaye anaitwa Sang Shin industry alifanya hivyo Mtama na ndivyo hivyo tutafanya katika maeneo mengine hasa Nachingwea kuhakikisha kwamba viwanda hivi vya korosho vinaweza kufufuliwa.
MHE. MARY P.CHATANDA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pia nimshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri kwa kutukumbuka Korogwe, Kilindi na Mkinga kwamba mwaka huu wa fedha watatupatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama. Swali la nyongeza, kwa kuwa vile vile Mahakama hizi zimekuwa na upungufu mkubwa wa wafanyakazi hususan Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo. Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kutupelekea Mahakimu Mahakama za Mwanzo Korogwe Mjini na Vijijini? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU:
Mheshimiwa Spika, kabla sijamjibu swali lake napenda nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe kwa hatua madhubuti ambayo wameianza ya ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo ya Mnyuzi na hivi sasa najua wanasubiri tu ramani kuanza ujenzi huo.
Mheshimiwa Spika, kuhusu lini tutawapelekea watumishi kwa maana ya kada ya Mahakimu, nimwondoe tu hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba pale ambapo tutakuwa tuna uwezo wa kibajeti wa kuweza kufanya kazi hiyo tutafanya, kwa sababu tumeanza na ukarabati wa miundombinu, basi jambo hili likikamilika pia tutaona namna ya kuweza kuongezea watumishi katika Mahakama za Korogwe ili nao waweze kupata huduma hii ya Kimahakama. (Makofi)
MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Wilaya ya Karatu ilikuwa na Mahakama za Mwanzo nne lakini hivi sasa imebaki Mahakama moja tu iliyoko Karatu Mjini ndio inayofanya kazi, Mahakama zingine za Mwanzo zimesimama kutokana na upungufu wa Mahakimu wa ngazi hiyo. Je, ni lini Serikali itapeleka Mahakimu wa Ngazi ya Mahakama za Mwanzo ili huduma hiyo muhimu ipatikane kwenye ngazi za Tarafa kule chini? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU:
Mheshimiwa Spika, tumepokea ombi lake na natumaini mwaka wa fedha unaokuja tutayafanyia kazi maombi yake ili na wakazi wa Karatu waweze kupata fursa ya kupata watumishi wa kuwahudumia katika Idara hii ya Mahakama.
MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika, asante sana, Wilaya ya Ulanga pamoja na kuwa na Mbunge kijana machachari lakini haina Mahakama ya Wilaya. Je, wananchi wa Ulanga wanaisikiliza Serikali yao ya hapa kazi tu inawaambia nini kuhusiana na jengo la Mahakama ya Wilaya? (Kicheko/Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU:
Mheshimiwa Spika, ukiangalia katika miaka ya hivi karibuni Serikali imeendelea kujenga Mahakama tofauti na miaka iliyopita na kwa mwaka huu wa fedha unaokuja 2017/2018, tumetengewa kiasi cha shilingi billioni 46 kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge na kwamba ninacho kitabu hapa kinachoelezea Mahakama zitakazojengwa, kwa hiyo nimwombe tu afike katika Ofisi yetu aangalie, ni orodha ndefu sana ya Mahakama na naamini kabisa eneo lake la Jimbo la Kilombelo lilitakiwa pia liwe limezingatiwa ili nao waweze kupata huduma hii.
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Nimesikiliza kwa makini sana majibu ya Mheshimiwa Naibu Wazir; swali langu la kwanza: Je, ni lini sasa Serikali italeta azimio hilo Bungeni kuweza kupitishwa? Maana amesema kwamba ni nchi mbili tu ambazo zimepitisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; sisi Tanzania tuna Sheria ya Kazi nadhani ya mwaka 2004. Je, ni lini sasa kulingana na mazingira ya sasa mtaileta tena ili iweze kufanyiwa mapitio?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la kwanza ameuliza, ni lini? Katika majibu yangu ya msingi, nimesema Serikali bado tunaendelea kupitia maudhui ya mkataba huu ili baadaye baada ya kujiridhisha tuweze kuuleta kwa ajili ya kuwa ratified.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia Convention hii namba 189; katika utaratibu wa hizi Conventions huwa pia wanatoa vitu vinaitwa recommendation. Katika Convention hii kuna recommendation namba 201 ambayo inatoa mazingira ya nchi zile wanachama kuona namna bora ya kuweza kuandaa baadhi ya mechanism ili mikataba hii iweze kuridhiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa mambo mengi ambayo yapo katika mkataba huu tayari yapo ndani ya sheria zetu. Ukiangalia katika article ya kuanzia 13 mpaka 18 imezungumza kuhusu masuala ya Freedom of Association, masuala ya mikataba ambayo kwa mujibu wa sheria zetu, tayari yako covered.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda katika nchi kama Kenya, ziko baadhi ya Conventions ambazo hawajazi-ratify kwa sababu wanaona sheria yao ni nzuri zaidi kuliko ile mikataba. Kwa hiyo, nasi bado tunaona kabisa kwamba yako maeneo mengi sana ambayo sheria yetu ime-cover.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili ni mapitio ya sheria. Kwa mujibu wa utaratibu wa masuala ya kazi, sisi tunafanya kazi katika mfumo ambao tunaita ni tripartism kwamba ni Serikali, Waajiri na Wafanyakazi. Inapotokea kwamba kuna jambo lolote ambalo linahitaji marekebisho au mapitio ya sheria, wadau huwa wanafanya taratibu hizo. Nasi kama Serikali mara zote tumekuwa flexible kuhakikisha kwamba sheria zetu za Kazi zinakuwa intact ili ziwe msimamizi mzuri katika masuala ya kazi katika nchi yetu.
MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Pamoja na kusubiri mapitio ya huo mkataba, lakini hapa nchini pana vikundi mbalimbali vya watu vinawakusanya watoto wetu wa nchi hii kwa minajili ya kuwatafutia kazi za ndani nchi za nje. Habari tulizonazo ni kwamba baadhi ya hawa watoto wamekuwa wakinyanyasika, wakiteswa na hata kuuawa. Je, ni hatua zipi za wazi ambazo Serikali inazichukua kwa ajili ya kudhibiti vikundi hivi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge hapa alikuwa anazungumzia wale mawakala wa ajira ambao kwa namna moja ama nyingine, yamekuwepo malalamiko mengi sana ya kuwapeleka mabinti zetu katika nchi hasa za Uarabuni kwenda kufanya kazi za ndani.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu alishatoa agizo na tangazo la kwamba wale wote ambao wanakwenda kufanya kazi nje ya nchi wapitie mfumo ambao upo katika Wizara yetu kupitia Wakala wa Ajira wa Serikali ambaye ni TAESA. Sasa tukibaini kwamba wako watu ambao wanafanya kazi hii kinyume na taratibu, sheria zetu ziko wazi, huwa tunawafutia usajili.
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile tumekuwa tukiwachukulia hatua kuhakikisha kwamba hawapati tena registration ili tuhakikishe kwamba nguvu kazi yetu hii wakienda kufanya kazi nje ya nchi tuwe tumewalinda kwa maana ya haki zao za kimsingi, tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo wako baadhi ya Watanzania ambao hawapitii katika Ofisi yetu na wakienda nje ya nchi wakipata manyanyaso tunakuwa hatuna taarifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia hata Balozi zetu zimeweka utaratibu mzuri; ile mikataba inayotolewa pale, mwajiri yeyote wa nje ya nchi ambaye anamtaka mfanyakazi wa Tanzania lazima apitie katika Ubalozi na Ubalozi unawasiliana nasi kwa ajili ya kuandaa mikataba ili tumlinde na tulinde haki za mfanyakazi wa Kitanzania.
MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa, mradi huu umeleta mabadiliko makubwa sana hapa nchini hususan Tabora; na kwa kuwa fedha zinazotolewa ni kwa awamu na kidogo kidogo. Je, Serikali iko tayari sasa kupeleka fedha hizo vijijini ambako tayari wananchi wana uelewa wa kutumia masoko hayo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, mantiki hasa ya mradi huu ni kwenda kusaidia katika miundombinu ya masoko na barabara hasa katika maeneo ya vijijini. Lengo kubwa hapa ni kusaidia katika kuongeza thamani ya kile ambacho kinafanywa na wakulima. Kwa hiyo, nimwondolee hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba upelekaji wa fedha katika miradi hii unategemeana pia na vigezo ambavyo vimewekwa kwa kila Halmashauri kuweza kuvifikia. Kwa hiyo, tumeendelea kufanya hivyo na tayari mradi huu kama nilivyosema hapo awali umekwishatoa fedha nyingi sana kwa ajili ya huduma hizi.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika maeneo mengine, wale ambao wamekidhi vigezo, fedha hizi zimekuwa zinatoka kwa wakati kwa ajili ya kwenda kusaidia huduma hizi zipatikane kiurahisi. Nimwondoe hofu kwamba fedha hizi zinafika na zinakwenda kwa wakati katika kusaidia malengo yaliyokusudiwa.
MHE. MACHANO OTHMAN SAID: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza swali dogo moja lenye (a) na (b) kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu wa MIVARF ulikuwa na nia nzuri sana kuwasaidia wananchi wa Tanzania. Kama alivyosema Mheshimiwa Waziri, kwa upande wa Zanzibar tumepata fedha na miradi, lakini katika utekelezaji wake inaonekana miradi hii haikuzingatia sana value for money na barabara ambazo zimejengwa kupitia mradi huu sasa hivi zimeharibika na hazipitiki ndani ya mwaka mmoja. Pia Wizara ya Kilimo ambayo imesimamia bado hawajazikabidhi kwa Wizara ya Ujenzi Zanzibar. Je, Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari kwenda kuzitembelea barabara hizi na kuzifanyia ukarabati?
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia kwa upande wa soko la Kinyasini nalo pia limejengwa chini ya viwango. Je, Mheshimiwa Waziri anasemaje kuhusu suala hili?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, hili la kwanza ameniomba kama nina uwezo wa kwenda kuzitembelea. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba mimi binafsi pamoja na Kamati ya Katiba na Sheria tulikwishafika katika eneo hilo. Tulitembelea na tulitoa maoni ya Kamati ambayo tuliwaagiza Watendaji pale Zanzibar waweze kuyafanyia kazi na hasa katika hili eneo ambalo amelisema la miundombinu, kwa sababu katika baadhi ya zile barabara ambazo tulizitembelea tayari MIVARF kwa maana ya programu na Halmashauri ya Wilaya pale waliingia makubaliano kwamba Manispaa inazichukua kwa ajili ya kuzi-upgrade na kuendelea kuzikarabati.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tayari tulishafika katika eneo hilo, tumeziona na kuna hayo makubaliano ambayo yanaendelea. Pia nami nikipata fursa zaidi nitakwenda kuzitembea na kuhakikisha kwamba yale ambayo tumekubaliana yamefanyiwa kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili la soko la Kinyasini, nilisema katika majibu yangu ya msingi ya kwamba mradi huu pia unatarajia kuchangia kiasi cha shilingi bilioni nne na milioni mia sita, ambazo ukiacha shughuli nyingine zitasaidia katika ujenzi wa ghorofa yenye vyumba vya baridi katika eneo la Kinyasini – Unguja, Tibirizi na Konde pia Pemba.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia ukiangalia katika mradi huu, kazi kubwa sana imefanyika Zanzibar na ukiangalia kuanzia katika sehemu ya Kaskazini Unguja, maeneo ya Donge, Vijibweni, Pwani, Donge Mnyimbi, kote huko shughuli zimefanyika kupitia mradi huu. Vilevile katika maeneo ya Mjini Magharibi kule Mwakaje, Mwera, Fuoni, Kibondeni nako pia kazi hizi zimefanyika. Kwa hiyo, nimwondoe hofu kwamba hata hayo mengine yote aliyoyasema tutakuja kuyapitia na kuona namna gani mradi huu unaendelea kutekeleza. Huu ni mradi ambao una manufaa makubwa sana Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Naibu Spika, mimi naitwa Mheshimiwa Mpakate. Napenda kuuliza swali la nyongeza. Katika maeneo yanayozalisha korosho, mfumo wa stakabadhi ghalani umesaidia sana wakulima kuongeza kipato, lakini moja ya changamoto inayokumbana nayo ni matatizo ya maghala katika vijiji vyetu katika maeneo yote ambayo yanalimwa korosho. Mradi wa MIVARF ungeweza kusaidia kujenga maghala kila Kata angalau ghala moja moja ili kuwapunguzia wakulima gharama ya kusafirishia korosho. Je, ni lini Serikali itatekeleza mradi wa kujenga angalau ghala moja kila kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ili kuwapunguzia wakulima wa Tunduru gharama ya kusafirisha korosho.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli katika mradi huu jambo kubwa ambalo linaangaliwa ni miundombinu ya masoko, barabara, lakini vile vile na huduma za kifedha kijijini. Katika eneo la miundombinu ya masoko jambo ambalo linaangaliwa pia ni suala la ujenzi wa maghala. Sasa katika programu hii yako maeneo ambayo tayari maghala yamejengwa lakini siwezi kutoa ahadi ya Serikali hapa kwamba tutajenga katika kila Kata.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mikoa ile ambayo inazalisha zao la korosho, kwa mfano, Ruvuma na Mtwara tayari maghala haya yapo, lakini kutoa ahadi ya kwamba tutajenga kila Kata Mheshimiwa Mbunge hii inategemeana pia na bajeti na programu jinsi tulivyojiwekea.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuanzia katika ile mikoa ambayo tuliona umuhimu huo na ndiyo maana katika Mikoa ya Ruvuma na Mtwara tayari maghala haya yamekwishajengwa. Kwa hiyo, tunaamini kabisa labda baadaye fedha ya ziada ikipatikana hiyo inaweza ikawa sehemu ya consideration, lakini kwa sasa kama Serikali na kupitia programu hiyo hayo ndiyo maeneo hasa ambayo tumeanzia.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri na ya msingi kabisa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninachotaka kusema hapa, Waheshimiwa Wabunge waielewe programu hii ya MIVARF, programu hii ni shirikishi, Mheshimiwa Mbunge anaomba ni kwa nini programu hii isiwe inajenga maghala tu. Tunachokifanya sisi Ofisi ya Waziri Mkuu, tunatafuta fedha na tunatengeneza plan ya nini kitafanyika kwenye fedha hiyo. Jukumu la kuamua aina ya mradi utakaotekelezwa kwenye Halmashauri husika ni jukumu la Halmashauri yenyewe na sio jukumu la Ofisi ya Waziri Mkuu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunachokifanya sisi, tunapeleka aina za miradi, Halmashauri kupitia vikao halali vya kikanuni inaamua aina ya miradi katika Halmashari yao. Kwa hiyo, tunachotaka kusema hapa kama fedha hii itapatikana tena kwa sababu ni mradi ambao unaenda kwa phases, kama fedha itapatikana tena, Halmashauri zikishapelekewa miradi hii basi waamue aina ya miradi kwa kuzingatia hali halisi ya mazingira waliyonayo na shughuli wanazozifanya na Ofisi ya Waziri Mkuu tutakubaliana nao lakini sio wajibu wetu kuwaamulia wao nini kikafanyike kwenye mradi katika Halmashauri yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge, katika maeneo ambayo miradi imefanyika wametupa ushirikiano wa kutosha. Nawapongeza sana na kama kuna tatizo lolote tunaomba tuendelee kuwasiliana ili miradi hii itekelezwe kwa viwango vinavyotakiwa huku ikisimamiwa na Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. (Makofi)
MHE. AIDA J. KHENAN: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa kuwa, Halmashauri nyingi nchini zinapopelekwa Mahakamani zinashindwa kesi, hali inayoonyesha ni jinsi gani Wanasheria wetu wa Halmashauri wanashindwa kuwashauri vizuri Wakuu wa Idara na kusababisha hasara kwenye Halmashauri zetu. Serikali ina utaratibu gani wa kufuatilia weledi wa Wanasheria wetu kwenye Halmashauri ili kuepusha hasara zinazotokea kwenye Halmashauri zetu? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; katika kesi za usuluhishi nje ya nchi napenda kufahamu, ni kesi ngapi tumeshinda kama Serikali na zipi tumeshindwa ikiwepo ya DOWANS, IPTL na nyinginezo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza anauliza namna ambavyo Serikali inaweza kufuatilia weledi wa Mawakili katika Halmashauri ambao wamekuwa wakisababisha hasara kwa Halmashauri kushindwa kesi nyingi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi ya kwamba Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, imekuwa ikiingilia katika baadhi ya mambo ambayo maslahi ya Serikali yanakuwa yako hatarini na pia katika ushauri ambao tumeuweka hapa tumeshauri taasisi hizi zikiwa zina kesi kubwa ambazo zinahitaji intervention ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa-consult mapema, ili wapate ushauri ambao unaweza kusaidia kulinda maslahi ya Serikali. Katika swali aliloliuliza sasa, nitoe tu rai kwa Wanasheria wote, hasa wale Mawakili katika Taasisi za Serikali katika kila Halmashauri kuendelea kufanya kazi hizi kwa weledi mkubwa na ufanisi, ili kulinda maslahi ya Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itaendelea kuwajengea uwezo Mawakili mbalimbali na pia Halmashauri zitenge fedha kwa ajili ya kuwajengea uwezo Wanasheria wao, ili pindi wanapokwenda kulinda maslahi ya Serikali, basi wafanye kazi hiyo katika weledi na ufanisi mkubwa sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili la kesi ngapi tumeshinda za usuluhishi; Mheshimiwa Mbunge aniruhusu tu nikachukue takwimu na nikishazipata nitampatia ili na yeye aone ni kwa kiwango gani Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imefanya kazi hii ya kulinda maslahi ya nchi yetu. (Makofi)
MHE. AMINA N. MAKILAGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira napenda kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amethibitisha kwamba kweli ziko sheria ambazo zimeshapitwa na wakati na Tume ya Kurekebisho ya Sheria ya Serikali inaendelea kuzifanyia marekebisho. Ningependa kujua ni sheria gani hizo sasa ambazo ziko katika huo mchakato na pia ningependa kujua hizi sheria zinaletwa hapa lini ili Bunge lako tukufu liweze kuzipitisha? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa kumekuwa na kilio cha muda mrefu na hata leo Mheshimiwa Mwenyekiti imethibitisha kwamba kumekuwa na kilio cha muda mrefu cha Waheshimiwa Wabunge Wanawake na Wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumekuwa na kilio kikubwa sana cha wanawake na vijana juu ya kutungwa sheria ya mfuko wa wanawake na vijana na walemavu. Lakini pia kumekuwa na kilio cha muda mrefu cha wakulima wadogo wadogo kwamba kilimo chao hakiwaletei tija kwa sababu hakuna sheria inayoweka mfumo mzuri wa wakulima wadogo waweze kuletewa tija. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kujua sasa. Serikali ina mkakati gani wa kuleta hizi sheria Bungeni. Hili suala la kuwa kila siku tunaambiwa Serikali itaweka msukumo kuhakikisha asilimia 10 ya wanawake na vijana inatengwa ili tuweze kufikia mahali panapohitajika. Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya akina mama nchini na ni kazi kubwa amekuwa akiifanya kwa ajili ya akina mama wa nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza anauliza ni sheria gani zipo katika mchakato. Kama nilivyosema, kazi kubwa ya Tume ya Kurekebisha Sheria ni kupitia sheria na baadaye kutoa mapendekezo kupitia taarifa mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka huu wa fedha Tume inafanya kazi ya mapitio ya sheria za mambo ya jinai (criminal justice) wanafanya pia mapitio ya sheria ya mambo ya evidence law, utoaji wa ushahidi mahakamani, lakini pia wanafanya mapitio ya sheria ya ufilisi (insolvency law) na vilevile wanafanya mapitio ya sheria ya huduma za ustawi wa jamii. Kwa hiyo, hizo ndiyo kazi ambazo zinafanyika katika mwaka huu wa fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika swali lake la pili ameuliza kuhusu lini Serikali italeta sheria mahsusi kwa ajili ya utungwaji wa uundwaji wa mifuko hii maalum kwa ajili ya akinamama na vijana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosema Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI, mifuko ya akina mama na vijana ipo na inaongozwa na miongozo yake tayari na imekuwa ikifanya kazi katika utaratibu huo wa kuchangia asilimia 10 hizo za mapato ya ndani ya Halmashauri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mwongozi tayari upo. Labda ambacho kinaweza kikafanyika ambapo Serikali imekuwa ikijibu hapa ni kuboresha na kuona namna bora ya kuweza kuwafikishia kwa urahisi zaidi akina mama na vijana huduma hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la wakulima wadogo wadogo kutungiwa sheria. Kama Serikali tunaichukua na tutaona umuhimu wake hapo baadaye wa kuweza kulifanyia kazi.
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza.
Kwa kuwa posho ya shilingi 5,000 kwa kila shauri ni ndogo sana ukilinganisha na wakati uliopo kuwalipa hawa wazee. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaongezea posho hawa wazee wa Mahakama za Mwanzo shilingi 5,000 ni ndogo sana? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa wazee wanakuwa kwenye Mahakama kwa muda mrefu sana kusikiliza mashauri hayo. Je, Serikali haioni haja sasa kubadili mfumo wa malipo, badala ya kuwalipa kwa miezi mitatu au minne kwa mkupuo, wawalipe kwa mwezi hadi mwezi yaani kwa mwezi mmoja mmoja? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye swali lake la kwanza la ongezeko la posho kutoka shilingi 5,000 kwanza kabisa nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba wazee hawa wanafanya kazi kubwa kuisaidia Mahakama katika kufikia maamuzi na sisi kama Serikali tunatambua mchango wao mkubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba siwezi kutoa commitment ya Serikali hapa kuhusiana na ongezeko la hii fedha lakini pindi bajeti itakaporuhusu basi tunaweza tukaona namna ya kuweza kusaidia katika kuboresha eneo hili la kipato kwa wazee hawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la pili la malipo ya mwezi kwa mwezi badala ya mkupuo. Kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi ni kwamba inafanyika hivi pia kwa ajili ya kupata kumbukumbu sahihi. Lakini vilevile pia inatokana sana na upatikanaji wa fedha kwa wakati kulingana na bajeti, tunalipokea wazo la Mheshimiwa Mbunge na Serikali tutaona namna ya kuweza kulifanyia kazi.
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Ukonga kwa sasa lina wakazi wanaokaribia 700 na tuna Mahakama ya Mwanzo moja tu pale ya Ukonga na kulikuwa na mpango mwaka jana kujenga Mahakama nyingine mpya ya Mwanzo kule Chanika. Kwa hiyo, ningependa kujua kupitia Mheshimiwa Naibu Waziri kama mpango huo wa kujenga Mahakama nyingine mpya pale ili kupunguza msongamano mkubwa kule Ukonga ukoje? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mpango wa Serikali wa mwaka 2017/2018; 2018/2019; 2019/2020 ni kuendelea kuongeza Mahakama nyingi za Mwanzo na Wilaya ili wananchi wengi waweze kupata huduma kwa wakati. Katika Mahakama ambazo zimeorodheshwa, pia Mahakama ambayo ni katika jimbo la Mheshimiwa Waitara ni kati ya Mahakama ambazo zilikuwa zimeainishwa katika wakati ujao wa fedha ili kuona namna ya kuweza kulishughulikia suala hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwa sababu hivi sasa chini ya Wizara ya Katiba na Sheria utaratibu ulioanzishwa sasa hivi ni ujenzi wa Mahakama kwa kutumia teknolojia rahisi sana ya moladi ambayo imerahisisha sana kujenga Mahakama nyingi kwa wakati mfupi.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge anaweza pia, kuwasiliana na mimi ili kuangalia katika orodha ya ujenzi wa Mahakama zile, Mahakama zake za Ukonga zimepangiwa mwaka gani wa fedha.
MHE. MACHANO OTHMAN SAID: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri kwa jibu lake. Lakini pamoja na jibu hilo naomba kuuliza maswala mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, biashara hii ya dawa za kulevya ina mtandao mrefu, na katika mtandao huo wapo baadhi ya raia ya wa kigeni ambao wanaishi Tanzania wanajishirikisha na dawa hizi. Miaka miwili, mitatu, minne nyuma kuna mwanamke mmoja kutoka nchi jirani alikamatwa maeneo ya Mbezi beach na alikuwa akitumia passport nyingi na majina tofauti.
Je, Serikali ina mpango gani wa kukabiliana na wageni ambao wanaitumia Tanzania kwa uuzaji wa madawa ya kulevya?
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, miongoni mwa waathirika wakubwa watumiaji wa dawa za kulevya ni wasanii wetu. Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wasanii hawa kuondokana na tatizo hili la utumiaji wa dawa za kulevya?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la kwanza, sheria yetu haibagui wenyeji na ugeni. Inapotokea mtu yeyote anajihusisha na dawa za kulevya sheria yetu imekuwa ikitumika kwa kuhakikisha kwamba hatua stahiki zinachukuliwa na kufanya kitu ambacho kinaitwa deterrence ili kuwazuia watu wengine wasifanye biashara hii ya dawa za kulevya. Adhabu kali kali hutolewa na hatua stahiki huchukuliwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili la kuhusu kuwasaidia wasanii; katika mpango tulionao wa kuhakikisha kwamba tunatatua changamo hii ya dawa za kulevya ambayo inawaathiri vijana wengi ikiwemo nguvu kazi ya taifa hili, moja kati ya kazi kubwa tunayofanya ni kuendelea kutoa elimu juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya. Vilevile katika mpango mmoja wapo ni kuhakikisha kwamba tunafanya kitu kinaitwa supply reduction kuhakikisha kwamba madawa hawa hayapatikani na hivyo kutokuwalazimu vijana wengi zaidi kuweza kuyatumia. Tume imefanya kazi kubwa mpaka hivi sasa na wameendelea kukamata na kuteketeza dawa nyingi na hivi sasa kuna upungufu mkubwa sana wa dawa za kulevya katika viunga vya miji yetu mingi ya Tanzania kutokana na kazi kubwa ambayo inafanywa na tume.
MHE. HALIMA A. BULEMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuku kwa kuniona. Kumekuwa na malalamiko mengi ya waathirika wa dawa za kulevya wanapokuwa rehab (rehabilitation) wanakaribia kupona wahusika wanawachoma tena dawa ya kulevya ili wasiweze kutoka na lengo limekuwa ili waendelee kujipatia fedha.
Je, Serikali ina mkakati gani wa kuanzisha rehab zao wenyewe ili kuweza kuwasaidia waathirka hawa dawa za kulevya?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia kubwa ya sober house zinamilikiwa na watu binafsi na hilo lililolalamikiwa na Mheshimiwa Mbunge hatujapata malalamiko rasmi. Hata hivyo niseme tu kwamba kwa kuzingati hizi sober house nyingi ziko chini ya watu binafsi tumeamua sasa kutengeneza miongozo ambayo itasaidia namna bora ya management ya hizi sober house ili inapotokea mazingira ya namna hiyo tuwe tuna sehemu ya kuweza kukabiliana nao, kwa sababu miongozo ile itakuwa inaeleza mtu ambaye ni muathirika wa madawa ya kulevya awe treated vipi. Mpango wa Serikali, katika swali lake, ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na sober house nyingi za Serikali ili kuondokana na changamo hii ambayo wananchi wengi wanaipata hasa kutokana na gharama kubwa ya kulipia katika hiyo sober house.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Tumepokea hii taarifa sasa mara kadhaa na hata wakati wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Waheshimiwa Wabunge wametuarifu kwamba uko mchezo mbaya unaoendelea kwenye sober house; badala kuwasaidia vijana wetu wapone na waondoke ndani ya sober house, lakini taarifa ambazo tumekuwa tukizipokea ni kwamba wamiliki wa sober house wanataka kuendelea kuwaweka vijana wetu pale kwa faida binafsi. Naomba sasa nitoe tena agizo kwa wamiliki wa sober house wote ambao wana mchezo huo ambao umekuwa ukisemekana wauache haraka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, na ninatumia muda huu pia kuiagiza mamlaka sasa kuanza kufanya uchunguzi wa kina na atakaye bainika ana tabia hiyo aweze kuchukuliwa hatua haraka sana na hiyo itatusai kuwaokoa vijana wetu kutokuendea kutumia dawa za kulevya katika nchi yetu ya Tanzania. (Makofi)
MHE. ASHA MSHIMBA JECHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri ninayo maswali mawili ya nyongeza.
Kwanza niipongeze kupitia mradi huu, kwa kweli imejitahidi sana kwa haya waliyoyasema na wanachi tayari wameonesha matunda na uzalishaji umekuwa. Mheshimiwa Jenista ni shahidi alikuja kutembelea maeneo ya Kongoroni na akajionea jinsi gani wananchi walivyoimarika katika uzalishaji wa kilimo cha ndimu. Kwa taarifa niliyonayo sasa hivi kwamba mitambo ya kiwanda cha ndimu tayari imefika na tayari imejaribiwa bado ufungaji tu naamini kazi hiyo itafanyika. Kwa kuwa mradi huu umeonesha maendeleo makubwa na bado kuna maeneo mengine yanahitaji mradi kama huu.
Je, Serikali kupitia mradi iko tayari kuendelea kwa yale maeneo mengine ambayo hayajafikiwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swala langu la pili elimu haina mwisho; kwa kuwa vikundi hivi vineonesha mwelekeo mzuri na bado vingali na changamoto ya kuyafikia masoko lakini hata kuongeza ujuzi wao.
Je, mradi huu uko tayari kuendelea na vikundi hivi ili kufikia lile lengo la kuondokana na uchumi mdogo na kuingia uchumi wa kati katika ulimwengu huu wa sasa hivi wa viwnda? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza kama Serikali kupitia mradi huu utaendelea kuyafikia maeneo ambayo hayafikiwa. Nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba mradi huu ambao una lengo la kwenda kurekebisha miundombinu ya barabara na masoko maeneo ya vijijini na kuongea tija katika mazao unaendelea kuwanufaisha Watanzania, na kadri ambavyo miradi inazidi kuibuliwa basi tutayafikia pia na yale maeneo ambayo bado hayaguswa kutokana na maelekezo na mwongozo wa mradi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili Mheshimiwa Mbunge amezungumza kuhusu suala la mafunzo na kuviendeleza vikundi ambavyo vimeshapatiwa fedha kupitia mradi huu. Kwa mujibu wa utaratibu wa mradi huu wa MIVARF miradi hii ikisha ibuliwa katika halmashauri kazi sisi tunayoyanya ni kuwezesha na baadaye kazi ya kuendelea kuvilea vikundi hivi inabaki katika halmashauri husika. Kwa hiyo niendelee tu kumuomba Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwa sababu tayari mradi huu umeshafanya kazi yake eneo la uendelezaji wa vikundi hivyo pia na wenyewe kwa nafasi yao waweze kushiriki kuhakikisha kwamba vikundi hivi vinakuwa endelevu na viweze kuleta tija kwa Mtanzania. (Makofi)
MHE. MUHAMMED AMOUR MUHAMMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa nami kuuliza swali la nyongeza.
Pamoja na majibu ambayo ni ya kawaida, hayana details za kutosha kutoka kwa Serikali na kwamba yako zaidi kimaelezo, kwenye implementation stage hayaonekani kwamba yako hivyo; je, Serikali imejipangaje kuhakikisha kwamba wanashirikisha ipasavyo; yaani wanaitumiaje PPP ili kuona kwamba tunafika kwenye huo uchumi wa viwanda ifikapo 2025?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili ni kwamba kumekuwa na kero na manyanyaso makubwa sana yanayofanywa na TRA kwa wafanyabiashara hususan hawa wenye maduka kwa kuwapa kodi ambazo hazistahiki. Je, Serikali haioni kwa manyanyaso haya itasababisha hayo malengo ya kufika uchumi wa kati na kwenda kwenye viwanda ifikapo 2025 ni ndoto tu kwa Watanzania? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI): Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo kweli kwamba hakuna mipango inayoshikika ya kuipeleka Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Ni dhahiri kuwa Serikali inachokifanya ni kuandaa mazingira wezeshi ya kuwafanya wawekezaji ambao kwa kiwango kikubwa sana tunategemea sekta binafsi kuja kuwekeza na kuifanya nchi yetu ifikie katika uchumi wa viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, yako mambo ambayo yanaweza yakaifanya nchi ikafikia katika uchumi wa viwanda, mojawapo ikiwa ni masuala ya miundombinu ambayo ni dhahiri kwamba Mheshimiwa Mbunge naye ni shahidi, anaona kazi kubwa ambayo imefanywa na Serikali katika eneo hili, lakini pia katika usafirishaji na maeneo mengine ya utoaji wa huduma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tulichokisema hapa kama Serikali, siyo maneno tu, lakini mipango na mikakati ya kuifanya Tanzania kufikia katika nchi ya viwanda, imeelezwa katika majibu yangu ya msingi na ninaomba nisirudie, lakini tu niseme tu kwamba ni dhamira ya Serikali kuifanya nchi yetu iwe nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye swali lake la pili, ameuliza kuhusu manyanyaso wanayopata wafanyabiashara kutokana na kodi inayotozwa na TRA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kati ya mambo ambayo Wizara tumekuwa tukifanya muda wote ni kuhakikisha tunaweza mazingira rahisi ya kufanya biashara katika nchi yetu ya Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeweka utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara kila baada ya muda mchache kusikiliza kero zao na yale ambayo wamekuwa wakituwasilishia tumekuwa tuliyafanyia kazi. Hivi sasa tuna blue print document ambayo imeelezea namna gani Serikali itasaidia kutatua vikwazo ambavyo vinawakabili wafanyabiashara ili kuifanya nchi hii iende katika nchi ya uchumi wa viwanda. (Makofi)
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Katika majibu ya msingi, Naibu Waziri ametueleza kwamba takwimu za mwaka 2014 miaka minne nyuma zinaonesha kuwa vijana 65,614 hawakupata ajira. Naamini kabisa baada ya miaka hiyo idadi hiyo imeendelea kuongezeka. Swali la kwanza; je, ni nini hasa kinawachofanya wahitimu washindwe kuajiriwa au kujiajiri?
Mheshimiwa Spika, swali l a pili, ni hatua zipi mahususi zinazochukuliwa na Serikali kuwawezesha au kuwajengea wahitimu hao mazingira wezeshi ya kuajiriwa au kujiajiri. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza ameulizia kuhusu ni kwa nini sasa watu hawa wanashindwa kupata fursa ya kuajiriwa au kujiajiri.
Mheshimiwa Spika, jibu lake ni kwamba katika nchi yoyote duniani suala la ajira limekuwa ni suala ambalo limekuja na changamoto nyingi sana, kutokana na kwamba nafasi za ajira zinazozalishwa na idadi ya watu ambao wana uwezo wa kufanya kazi vinakosa uwiano. Kwa hiyo, kama Taifa tunaendelea kuwa na mipango mbalimbali ya kuhakikisha kwamba tunakuja na mipango madhubuti ya kufanya nguvu kazi yetu hii kubwa iweze kupata nafasi ya kuajirika.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa tafiti ya mwaka 2014 ambayo wanaiita Integrated Labour Force Survey inasema takribani watu wa kuanzia miaka 15 na kuendelea ambayo ndiyo working age population, ambao wana uwezo wa kufanya kazi kila mwaka wanaojitokeza ni wengi zaidi kuliko nafasi za ajira.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo katika kujibu swali lake la pili, niseme tu kwamba kama Serikali tumeona kabisa suala la kwanza la kuweza kukabiliana na changamoto hii hasa kwa wahitimu wa vyuo vikuu, tumekuja na utaratibu wa kwanza wa kuzindua mpango maalum wa mafunzo ya uanagenzi na mafunzo ya vitendo ambao Mheshimiwa Waziri Mkuu alizindua mwaka jana ambao unamfanya mhitimu yeyote wa Chuo Kikuu....

Mheshimiwa Spika, kwanza tumekuja na framework hiyo ambayo hivi sasa tutaanza kuwachukua wahitimu wa vyuo vikuu kwa kwenda kuwa-attach katika mashirika mbalimbali, kampuni mbalimbali, waende kwa ajili ya kujifunza na kupata uzoefu, hilo ni eneo la kwanza.
Mheshimiwa Spika, eneo la pili, tumekuja na utaratibu wa kubadilisha mindset kwa mujibu wa sera ya ajira inasema ajira ni shughuli yoyote halali inayompatia mtu kipato. Kwa hiyo, tunawatoa sasa wale wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu kutoka kwenye kufikiria kuajiriwa moja kwa moja ofisini na kubadilisha mtazamo kwenda kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo za kilimo, ufugaji na biashara.
Mheshimiwa Spika, Serikali tumeandaa mazingira wezeshi kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ili vijana hao waweze kupata fursa na kupata mitaji na maeneo ya kufanyia shughuli zao. (Makofi)
MHE. RUTH H. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ni kweli kama wengine walivyosema tuna tatizo kubwa la ajira. Hapa Dodoma nina hakika pia kuna tatizo la ajira. Maeneo ninayokaa mimi kule Kisasa ile mitaro ya maji ya mvua imekuwa ni madampo ya takataka, kumekuwa na nyasi nyingi, kumekuwa kama mazalia ya mbu, barabara ni chafu. Je, Serikali ina mkakati gani wa kukusanya hao vijana ambao hawana kazi katika makundi ili kusudi kuwapa ajira ya kufanya usafi katika mji huu. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Spika, nizungumze Kitaifa mpango ni nini? Kwa kutambua kwamba katika nchi yetu ya Tanzania tunao vijana wengi sana ambao wapo katika ma-group tofauti tofauti, kwa hiyo Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mpango wa Ukuzaji wa Ujuzi kwa Vijana ambao una lengo wa kufikia vijana 4,400,000 ifikapo 2021 tumekuja na utaratibu wa kukusanya makundi haya ya vijana na kwenda kuwapa mafunzo mbalimbali ili wapate sifa ya kuajirika na kujiajiri wenyewe.
Mheshimiwa Spika, ninapozungumza sasa tunao vijana ambao walikuwa wako mtaani hawajawahi kusoma VETA, hawajawahi kusoma Don Bosco, wana ujuzi, tuna program ya kurasimisha ujuzi wao pasipo wao kwenda kusoma, hivi sasa tumeanza kuchukua kundi kubwa la vijana katika maeneo hayo, lakini pia tunao vijana ambao wanaendelea na mafunzo katika vyuo mbalimbali. Lengo lake ni kuwapatia ujuzi stahiki ili waje wasaidie katika shughuli mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, nikirudi katika swali lake la kuhusu vijana waliopo hapa Dodoma. Mwaka jana ilisomwa hapa Bungeni na maelekezo yalitoka ya kuzitaka Halmashauri za Manispaa, Halmashauri za Wilaya kuhakikisha kwamba zinachukua vikundi vya vijana waliopo mitaani na kuwapa mitaani na kuwapa shughuli mbalimbali ambazo zinaweza zikafanywa na vijana kama hiyo aliyoisema Mheshimiwa Mbunge Ruth Mollel.
Mheshimiwa Spika, kama Mbunge wa Dodoma Mjini kwa sababu limenilenga hapa, niseme tu kwamba tunalichukua hilo tuone namna bora ya kuweza kuwakusanya vijana hao katika vikundi ili kuwawezesha na mitaji wafanye kazi ya kuzoa taka na kusafisha hiyo mitaro ambayo itakuwa ni sehemu ya ajira pia. (Makofi)
MHE. ALI SALIM KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba nimuulize Waziri maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosema Waziri kwamba mfumo wa vyama vingi ni mfumo wa kidemokrasia. Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa Tanzania inaelezwa kwamba ni haki ya kila chama kufanya kazi zake za kisiasa wakati wote kwa kutumia sheria na kanuni ambazo zimewekwa. Je, ni kwa nini Serikali imezuia harakati na mikutano ya kisiasa ili vyama visifanye kazi yake?
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ni kwa nini Msajili anaingilia mwenendo wa vyama vya siasa hali ya kuwa vinafanya kazi zake kikanuni, kikatiba kwa kufanya maamuzi kupitia Ofisi ya Msajili na kukataa maamuzi ya vikao halali vya vyama vya siasa kama vile Chama cha Wananchi (CUF). Naomba Mheshimiwa Waziri atuambie ni sheria ipi ambayo inampa mamlaka hayo Msajili ya kutengua vikao halali vya chama ambavyo vimefanywa kwa mujibu wa kanuni na katiba na sheria za nchi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA, NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na la kwanza, si kweli kwamba Serikali imezuia harakati za kisiasa. Kama ambavyo yamekuwa yakijibiwa humu ndani bungeni, umewekwa utaratibu maalum wa kufanya siasa kutokana na sheria mbalimbali hasa ambazo zinaongoza utaratibu wa vyama vya siasa kushughulika katika shughuli za kisiasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme tu kwamba Serikali haijakataza vyama kufanya harakati za kisiasa lakini zimeruhusu vyama kufanya harakati za kisiasa kwa mujibu wa taratibu na sheria ambazo zimewekwa katika nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mujibu wa sheria; ukisoma Sheria ya Vyama vya Siasa Sura namba 258 iliyorejewa mwaka 2002 na sheria ya vyama vya siasa iliyofanyiwa mabadiliko namba 7 ya mwaka 2009 inampa mamlaka Msajili kama mlezi wa vyama vya siasa kuhakikisha anavilea vyama vya siasa na pale panapotokea matatizo awe sehemu ya kusaidia kurudisha harmony katika vyama vya siasa akiwa kama mlezi wa vyama vya siasa.
MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Vyama vya Siasa imeweka masharti ya wazi na yaliyo kamilika namna ambavyo vyama vitapata wanachama wake na vitaeneza sera na itikadi yake, lakini kwa sasa polisi wamekuwa na desturi ya kuzuia vikao vya vyama vya siasa hata vikao vya ndani vinavyopanga mipango ya uendelezaji wa chama. Sasa Serikali haioni kwamba badala ya kusimamia sheria Serikali yenyewe kwa kutumia vyombo vyake inavunja sheria; na kama inataka hayo masharti ya sasa yaendelee ilete hiyo sheria hapa Bungeni ili kuweza kuweka hayo masharti mapya, badala ya kutumika kwa ajili ya kuwapiga wanasiasa mitaani?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA, NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, narejea majibu yangu ya awali kwamba si kweli kwamba Serikali inazuia harakati za kisiasa na hata sheria aliyoisema, sheria hii imetoa uhuru kwa vyama kutafuta wanachama na kufanya mikutano, lakini iko subject na sheria zinginezo ikiwepo sheria ya Police Force na Auxiliary Service Act ambayo pia imeweka masharti katika section namba 44 na 45 ya namna vyama vya siasa vinaweza vikafanya kazi zao hasa katika mikutano na maandamano mbalimbali.
MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Mwaka 2002 mpaka 2004 tulikubaliana kati ya wadau wa vyama vya siasa na Serikali tuwe na chuo cha kitaifa cha kuandaa viongozi bila kuangalia itikadi za vyama wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu. Je, Serikali imefikia wapi kuhakikisha tunakuwa na Chuo cha Kitaifa cha kuandaa viongozi kwa ajili ya uzalendo wa kitaifa bila kuangalia itikadi za vyama vya siasa ili tuwe na Taifa moja lenye malengo yanayofanana?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA, NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Serikali nia na dhamira ni kuendelea kukuza demokrasia ndani ya nchi na makubaliano hayo ya mwaka 2002 tutaendelea kuyafanyia kazi na kuyafuatilia ili lengo hili liweze kutimia la kuwa na chuo cha kuoka wanasiasa ambao tunaamini kabisa kupitia chuo hicho basi tutakuwa tumejenga Taifa la watu wenye uzalendo na ambao watakuwa na ari ya kweli ya kuwatumikia Watanzania. (Makofi)
MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Imekuwa ni kawaida sana kwa migodi mingi na makampuni mengi kukaa na wafanyakazi bila kuwaajiri. Mheshimiwa Waziri umejibu kwamba wale wafanyakazi wameajiriwa, si kweli, wale wafanyakazi hawajaajiriwa. Hii inapelekea wafanyakazi wengi kukosa stahiki zao. Kwa hiyo basi, je, Serikali itaweka mkakati gani madhubuti wa kuhakiki migodi yote na makampuni yote kuhakikisha wafanyakazi hawa wamelipwa stahiki zao? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; Sheria ya Ajira na kanuni zake ya 2003 inasema kwamba; mfanyakazi yeyote anapokuwa anafanya kazi sehemu yoyote kwa muda wa miezi sita anatakiwa aajiriwe na apewe haki zake za kimsingi.
Sasa swali langu linakuja, ni kwamba, Serikali haioni inapoteza mapato kwa kutowaajiri wafanyakazi hao kwa kuwafanya vibarua muda mrefu. Kwa nini Serikali isiingilie kati kuhakikisha wafanyakazi wa migodi wanapata haki zao za kimsingi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA, NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza anasema si kweli kwamba wafanyakazi hao wameajiriwa. Nitamuomba tu Mheshimiwa Mbunge kama anayo taarifa nyingine tofauti atuwasilishie, lakini tarehe 28/4/2018 wakaguzi kutoka Ofisi ya Idara ya Kazi walikwenda kufanya ukaguzi katika Kampuni ya ACACIA na wakagundua idadi ya wafanyakazi na walio na mikataba. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama kuna taarifa tofauti Mheshimiwa Mbunge anaweza kutuwasilishia katika ofisi yetu ili tuweze kulifanyia kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni kuhusu lini tutafanya uhakiki katika migodi. Idara ya Kazi mara zote imekuwa ikifanya kaguzi mbalimbali kuhakikisha kwamba waajiri wote nchi wanafuata sheria ya ajira na mahusiano kazini sheria Namba 6 ya mwaka 2004. Ni kazi yetu kama Serikali kuhakikisha kwamba work places zote hizi tunazitembelea…
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Awali naomba uelewe kwamba haya maswali tunayoyauliza hapa na sisi wawakilishi yanaulizwa kwa niaba ya wananchi wetu, kwa hiyo, hii ni kero ya wananchi. Sasa tunapopata majibu yasiyoridisha na majibu ambayo yana mkanganyiko, tunapata mashaka sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwezi wa Septemba, 2017 niuliza swali hili na Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana alitumia sekunde zisizozidi tano akaniambia Mahakama ya Wilaya ya Liwale itajengwa mwaka 2018. Sasa leo hii naambiwa itajengwa kwenye bajeti ya 2018/2019. Kwa nini wanakuwa na majibu ya kudanganya wananchi wakati sisi ni wawakilishi wao na hizi ni kero wanatupa ili wapate majibu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza…
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, sambamba na Mahakama ya Wilaya ambayo nadanganywa kwamba itajengwa kwenye mwaka ujao wa bajeti, je, Serikali ina mpango gani kujenga Mahakama za Mwanzo katika Tarafa za Kibutuka na Makata? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kwamba huduma za Mahakama zinawafikia wananchi wote nchi nzima kwa ukaribu na pasipo upendeleo wowote na ndiyo maana katika bajeti ambayo Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria ameisoma hapa tumeelezea mahitaji yaliyopo na mpango wa Serikali katika kuhakikisha kwamba Mahakama hizi zinajengwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuondelee hofu Mheshimiwa Kuchauka kwamba Serikali hii si Serikali ya kudanganya kama alivyokuwa ameainisha awali Mheshimiwa Waziri na mimi pia nimesema hapa leo ni kwamba Mahakama hii itajengwa na ipo katika mpango huo kwa sababu hivi sasa tumepata nafasi ya kuwa na ushirikiano mzuri na Chuo Kikuu cha Ardhi na Baraza la Nyumba la Taifa ambapo tunatumia teknolojia rahisi sana ya ujenzi wa Mahakama kupitia teknolojia ya moladi. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba kama Serikali ilivyoahidi, Mahakama ya Wilaya ya Liwale itajengwa. Hivi sasa navyozungumza katika mpango wa bajeti ya mwaka huu tuna mpango wa kujenga takribani Mahakama za Wilaya 29. Kwa hiyo, Mheshimiwa atupe imani, Mahakama hiyo itajengwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kuhusu Mahakama za Mwanzo, ni kweli ni dhamira ya Serikali kuendelea kuzijenga Mahakama za Mwanzo nyingi kadri ya upatikanaji wa fedha kwa sababu kwa hivi sasa tuna upungufu wa Mahakama za Mwanzo takribani 3,304 nchi nzima. Kwa hiyo, nimuondolee hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba pindi pale bajeti itakaporuhusu na fedha zitakapopatikana Mahakama hizo pia zitajengwa ili kuwafanya wananchi wa Jimbo la Liwale waweze kupata huduma ya Mahakama kwa urahisi zaidi.
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Jimbo la Liwale linafanana kabisa na Jimbo Mbulu Vijijini; katika Mji wa Haydom hakuna Mahakama ila kuna kituo kikubwa cha polisi, kwa hiyo, mahubusu inabidi wapelekwe kilometa 86 kutoka Haydom mpaka Mbulu. Je, ni lini sasa pamoja na maombi niliyoleta watajenga Mahakama katika Mji wa Haydom?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nisiweke commitment ya ni lini lakini nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba ni mpango wa Serikali kuhakikisha tunaendelea kujenga Mahakama nyingi za Mwanzo katika nchi yetu. Kwa hiyo, pindi pale fedha zitakapopatikana pia Mahakama ya Mwanzo Haydom itaingizwa kwenye mpango ili wananchi waweze kupata huduma ya mahakama.
MHE. JORAM I. HONGOLI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Lupembe, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ina Mahakama ya Lupembe ambayo ni Mahakama ya muda mrefu sana, jengo lile lilijengwa na wakoloni na mpaka sasa hivi karibu linaanguka. Tayari tulishaleta mihtasari ya kuomba ujenzi wa Mahakama eneo lingine ambalo tayari wananchi wameshatoa na nimeshaandika barua ya kuomba. Nataka kujua ni lini sasa Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama hii ambayo sio muda mrefu itaanguka?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katika majibu yangu yote ya awali ya kwamba Serikali inayo dhamira ya dhati ya kwanza kabisa kuhakikisha kwamba wilaya nyingi zinapata Mahakama za Wilaya pamoja na Mahakama za Mwanzo vilevile na kufanya ukarabati wa majengo chakavu ya zamani.
Kwa hiyo, nimuahidi tu kwamba maombi yao yameshawasilishwa Wizarani, tunaendelea kuyafanyia kazi, pindi pale fedha zitakapopatikana basi tutawasiliana na mamlaka husika ili tuone namna bora ya kuweza kufanikisha ujenzi wa Mahakama hiyo katika Wilaya ya Njombe pia.
MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba nielezee masikitiko yangu juu ya majibu ya Serikali ambayo amenipatia.
Mheshimiwa Spika, majibu ambayo Serikali imeleta yako kisera zaidi, nilitegemea yaje majibu ambayo kidogo yangeleta taswira na mwanga kwa vijana.
Mheshimiwa Spika, nashindwa kuelezea malalamiko yangu kwa vile tuko kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani lakini kwa kweli nimesikitishwa sana na majibu. Baada ya kusema hayo nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, kwa vile Serikali imepanua fursa ya elimu kwa kuongeza Vyuo Vikuu vya Elimu ya Juu na Elimu ya Kati. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuendana basi na mahitaji yaliyopo?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa kiasi gani Mfuko wa Vijana umeweza kuwagusa walengwa ukizingatia na hali halisi iliyopo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa na mipango mbalimbali ya kuwawezesha vijana na akina mama na msingi mkubwa wa uwezeshaji huo unatokana na sera. Kwa hiyo, nimuondoe tu hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba majibu haya kwa sababu ya uwezeshaji na sera inatuelekeza hivyo ndiyo maana yalijikita hapo.
Mheshimiwa Spika, nikienda katika swali lake la kwanza la kujua kuhusu ongezeko la idadi ya wahitimu wa Vyuo vya Elimu ya Juu na Ufundi ikilinganishwa na nafasi za ajira. Kama Serikali na kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2014 ya Integrated Labour Force Survey ambayo imeeleza kinaga ubaga juu ya nafasi za ajira zinazotengenezwa kila mwaka lakini na watu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa mwaka husika kwamba idadi imekuwa ni kubwa tofauti na nafasi za ajira ambazo zinatengenezwa.
Kwa hiyo, sisi kama Serikali tuliona njia nyingine mbadala ni kuanza sasa kuwabadili mitazamo vijana wetu hasa wahitimu wa vyuo vikuu na kuamini kwamba bado wanaweza wakafanya shughuli zingine za kiuchumi ikiwemo kilimo, ufugaji na biashara na sisi kupitia Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kuweza kuwawezesha ili kuweza kufikia malengo yao.
Mheshimiwa Spika, sisi kwetu tafsiri kwa mujibu wa Sera ya Ajira ya mwaka 2008, ajira ni shughuli yoyote halali inayomuingizia mtu kipato. Kwa hiyo, tumeanza sasa kuwabadili mitazamo vijana wetu waanze kuamini kwamba si wote ambao wanaweza kwenda kukaa ofisini, lakini pia tunaandaa mazingira mazuri waweze kufanya kazi za kujiajiri.
Mheshimiwa Spika, la pili ameuliza kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana; ni kweli, kwa mujibu wa Sheria ya Fedha, Sheria Na. 21 ya mwaka 1961, kifungu namba 21(1) kilianzisha Mfuko wa Maendeleo wa Vijana ambao lengo lake ni kuhakikisha tunawagusa vijana wengi zaidi kwa kuwasaidia kupata mikopo na mitaji na mikopo yenye riba nafuu.
Mheshimiwa Spika, mpaka ninavyozungumza hivi sasa, tayari tumeshafikia vikundi vya vijana 397 ambao tumeshatoa kiasi cha shilingi zaidi ya shilingi bilioni nne kwa ajili ya kuwawezesha vijana. (Makofi)
MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona.
Mheshimiwa Spika, mwaka 2015, wakati tukienda kwenye uchaguzi mkuu, kila chama kiliuza sera zake kwa Watanzania. Chama cha Mapinduzi kilitangaza sera kuwapatia wananchi wa Tanzania kila kijiji shilingi milioni 50 sera ambayo iliwavutia sana Watanzania. Je, Serikali ya Chama cha Mapinduzi imeshindwa kutekeleza ahadi yake iliyoweka kwa Watanzania? Kama haijashindwa, ni lini pesa hizi zitapelekwa kwa vijiji vyote vya Tanzania? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, ni kweli katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 tulieleza bayana ya kwamba moja kati ya mkakati mkubwa wa kuwawezesha wananchi kiuchumi ilikuwa pia ni pamoja na utengwaji wa shilingi milioni 50 kila kijiji.
Mheshimiwa Spika, narejea majibu yangu ya awali kwamba utaratibu wa uwezeshaji wananchi kiuchumi huwa unakwenda sambamba na utayarishaji wa miundombinu rafiki ya kufanya mpango huu uweze kuwafikia wananchi kwa wakati. Tulijifunza katika mipango iliyopita ikiwa mabilioni ya JK na hivi sasa tunaendelea na mkakati wa kuona namna bora ya miundombinu ambayo itawekwa ili fedha hizi pindi tutakapoanza utoaji wake, ziwafikie walengwa kwa uhakika na pia iende kufanya kazi ambayo itakuwa imekusudiwa.
Kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa kwamba ni mpango wa Serikali na bado upo katika mchakato wa kuona namna bora ya kuweza kuandaa miundombinu hiyo.
MHE. ZAINAB A. KATIMBA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, pia nashukuru kwa kuchukua mapendekezo haya na kuona umuhimu wa kutunga sera hii ya mafunzo kwa vitendo kazini kwa wahitimu.
Mheshimiwa Spika, nina swali moja la nyongeza, sisi tunafahamu kwamba ili kijana/mhitimu awe na uzoefu, uzoefu hujengwa kwa kuanza. Sasa pamoja na kwamba Serikali itatunga sera hii kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kazini kwa wahitimu, lakini haioni haja kwamba kuna kazi zingine ambazo hazihitaji kuwa na experience, kwa sababu ukiangalia leo hii ajira zilizotolewa utakuta kuna kigezo, two years experience, three years experience, five years experience. Sasa hawa vijana wanaohitimu, wataanza lini kupata huo uzoefu kama kila kazi inayotolewa inahitaji wawe na uzoefu?
Mheshimiwa Spika, sasa pamoja na kwamba Serikali itatunga sera hii ambayo itaweza kusaidia kuondoa hilo umbwe kati ya elimu waliyopata wahitimu pamoja na mahitaji ya soko la ajira lakini Serikali haioni haja kwamba kuna kazi zingine ambazo hazihitaji huo uzoefu na vijana waweze kupata fursa ya kuajiriwa ili na wenyewe waweze kujikwamua na changamoto ya kukosa ajira? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, naomba kwanza nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Zainab Katimba kwa namna ambavyo anawapigania vijana wa Taifa hili la Tanzania na vile alivyokuwa mstari wa mbele kuhakikisha maslahi ya vijana yanalindwa katika nchi yetu.
Mheshimiwa Spika, ni kweli kumekuwepo na changamoto kubwa katika masuala ya uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi ambazo zimeombwa na kama itakumbukwa, wakati wa kampeni mwaka 2015 Mheshimiwa Rais pia aliwahi kulisema hili juu ya kigezo hiki cha uzoefu. Sisi kama Wizara tukaona kwa sababu asilimia kubwa ya vijana wanaotoka katika Vyuo Vikuu na Vyuo vya Elimu ya Juu wamekuwa wakipata taabu sana kwenda kujifunza kivitendo na wengi wao ni mashahidi huwa wanatembea na ile barua ya to whom it may concern na wengine mpaka kumaliza soli za viatu bila kupata eneo la kwenda kufanyia kazi. Kama Serikali tukaona sehemu ya kwanza ya kuanzia ni kuhakikisha tunatengeneza mwongozo huu na mwongozo huu tumefanya kati ya Serikali, waajiri na Vyama vya Wafanyakazi ili tutoe nafasi kwa vijana wale wahitimu wa Vyuo Vikuu wakimaliza masomo yao na tumeshazungumza na haya makampuni yatoa nafasi, tunawapeleka moja kwa moja katika makampuni na taasisi mbalimbali kwenda kujifunza kuanzia miezi sita mpaka mwaka mmoja. Lengo letu ni kuondokana na kikwazo cha kigezo cha experience ili akitoka pale akienda sehemu awe ana reference.
Mheshimiwa Spika, hili ni eneo la kwanza ambalo tumelianzia, naamini kabisa kupitia mpango huu utawasaidia sana vijana wasomi wa nchi yetu ambao wamekuwa wakipata tabu na kikwazo cha uzoefu. Kwa hiyo, hivi sasa atapata nafasi ya kujifunza katika kampuni kwa muda huo wa mwaka mmoja na baadaye tutampatia cheti cha kumtambua ili iwe kama reference yake katika sehemu inayofuata. Tunafahamu ni tatizo kubwa, ni changamoto kubwa lakini kama Serikali tumeona tuanzie hapa kwenda mbele na jinsi Waheshimiwa Wabunge watakavyotushauri tutaona namna nzuri ya kuboresha mpango huu.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika, naomba kuongeza majibu machache katika swali hili na hasa nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ambayo amekwisha kuyasema.
Mheshimiwa Spika, baada ya Serikali kuona tatizo hilo Mheshimiwa Naibu Waziri amesema tumeshatengeneza hiyo miongozo. Tunafikiri sasa kazi yetu kubwa ambayo tumeanza kuifanya ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni kuji-link sisi Ofisi ya Waziri Mkuu na miongozo tuliyonayo na wenzetu wa Wizara ya Elimu, lakini kupitia vyuo vikuu vyote kuhakikisha kwamba tunatambua mahitaji na tunawasaidia hawa vijana kuwaandaa vizuri, ili awingie kwenye soko la ajira.
Mheshimiwa Spika, tumekubaliana pia ndani ya Serikali na ndio maana mmeona hata ajira na matangazo ya ajira yanayotolewa sasa hivi, ajira hizo zinazotolewa sasahivi kwa kweli, kimsingi wengi wanaoajiriwa kwenye ajira hizi ni wale ambao ni fresh kutoka kwenye vyuo vyetu vikuu na taasisi nyingine ambazo zinatengeneza ujuzi. Wakati mwingine tunaweza kuwa tunataka ajira katika position fulani ambazo zina matakwa rasmi. Kwa mfano, Mkurugenzi labda wa kitu fulani kwa matakwa fulani kwa hiyo, huko ni lazima tuone sasa wale walioenda internship, lakini vilevile wale ambao wana uzoefu katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Spika, naomba niwahakikishie vijana wetu kwa kweli, baada ya kuona hiyo gap ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu tumeifanyia kazi vizuri sana, sasa hivi waajiri na Serikali kwa pamoja na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi tumeanza kulifanyia kazi vizuri sana eneo hilo. Na tunawaondoa hofu vijana wetu kwa kweli sasa tunataka kuwapa assurance ya ajira bila kupata vikwazo vyovyote katika nchi yetu ya Tanzania. (Makofi)
MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Majibu ya Serikali ni majibu ya siku zote ambayo yameshindwa kutatua tatizo la ajira nchini. Unaweza kuonesha tu mifano midogo kwa mfano, sera ya uchumi na viwanda kwenye bajeti tu peke yake Serikali imeshindwa kupeleka fedha ambayo ingeweza kuwezesha hivyo viwanda kuanzishwa na wananchi kupata ajira, kipengele cha tano utaona kabisa kwamba inasema kwamba Serikali moja ya mkakati wake ni kuwapa mikopo nafuu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, lakini kwenye bajeti tuliyoipitisha hapa unakuta Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ni bilioni moja wakati vijana ambao wako mtaani ni wengi.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, ni kwa nini Serikali isikubali ama ikashauriana na taasisi za kifedha ili wanafunzi wa Vyuo Vikuu watumie vyeti vyao walivyomalizia elimu ya juu, kama sehemu ya kukopea ili kuwasaidia waweze kujiajiri?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni kwa nini sasa Serikali kupitia Wizara ya Ardhi wasigawe ardhi katika yale maeneo muhimu kabisa bure kwa wanafunzi wote wanaomaliza Vyuo Vikuu ili waweze kujiajiri kwa kufanya hizo kazi na baada ya hapo warejeshe hiyo mikopo yao, kwa nini wasitumie hii mikakati ya muda mfupi ambayo inaweza kuwawezesha hawa watu kupata hiyo ajira au kujiajiri? Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza ni kweli katika taasisi za kifedha moja ya masharti ya mtu yeyote kuweza kupata mkopo ni uwasilishaji wa dhamana (collateral) ili aweze kufikia uwezo huo wa kupata mkopo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Silinde kwamba asilimia kubwa ya wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu bado hawajawa na uwezo wa kuwa na hizo collateral ndiyo maana Serikali na kupitia Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi tumeona njia pekee na bora ya kuweza kusaidia kundi hili la vijana kwa kuanzia, kwanza ni kuwahamasisha kukaa katika vikundi, pili ni kuwawezesha kupitia mifuko mbalimbali ya uwezeshaji ambao chini ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi tuna mifuko takribani 19 ya uwezeshaji inayotoa mikopo na inayotoa ruzuku ambayo ina ukwasi wa kiasi cha shilingi trilioni 1.3 kwa maana ya liquidity.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwa wahitimu wote wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Elimu ya Juu bado wanayo fursa kutumia mifuko yetu hii ambayo ina riba nafuu sana, ambayo pia inaweza ikawasaidia wakabadilisha maisha yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya mfano ukienda pale Sokoine University tuna vijana wana kampuni yao wanaitwa SUGECO ambao walihitimu pale wamekaa pamoja ninavyozungumza hivi sasa SUGECO wanafanya miradi mikubwa ya kilimo hapa nchini na wameanza kuwasaidia mpaka na vijana wenzao kwa sababu walipitia utaratibu huu, Serikali ikawawezesha na sasa hivi wamefika mbali sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kuhusiana na masuala ya ardhi, Novemba mwaka 2014, Mheshimiwa Waziri Mkuu aliwaita Wakuu wa Mikoa wote hapa Dodoma likatengenezwa Azimio la Wakuu wa Mikoa wote kwenda kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za vijana, juzi Waziri Mkuu amesisitiza hilo jambo na mpaka ninavyozungumza hivi sasa zimeshatengwa takribani hekari 200,000 nchi nzima kwa ajili ya shughuli za vijana ambao maeneo haya tumeyapa jina mahsusi kabisa kwamba ni Youth Special Economic Zones (Ukanda Maalum Uchumi kwa ajili ya vijana).
Mheshimiwa Naibu Spika, rai yangu ni kwamba niendelee kuwaomba Wakuu wa Mikoa na viongozi wote katika Tawala za Mikoa kwa agizo la Waziri Mkuu watekeleze kwa kutenga maeneo ili vijana wengi zaidi wapate nafasi ya kwenda kufanya shughuli za ufugaji, kilimo na biashara. (Makofi)
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Kwa kuwa ajira ambazo ni rasmi zimekuwa na ukakasi mkubwa kulingana na idadi kubwa ya vijana na Serikali ilishaanzisha mfumo wa kuwasaidia vijana kupitia ajira zisizo rasmi kwa vijana ambao tayari wana ujuzi, nini sasa mkakati wa Serikali kuwarasimisha vijana hawa ili wapate mafunzo na vyeti wanavyoendelea vitakavyowasaidia, hasa wale ambao ni mafundi gereji, mafundi uwashi na mafundi seremala walioko Nyamagana na nchi nzima kwa ujumla? Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa kazi kubwa anayoifanya kuwatetea vijana hasa vijana wa Jimbo lake la Nyamagana. Pia nimwondoe hofu kwamba chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu tuna mpango wa miaka mitano wa ukuzaji ujuzi kwa vijana ambao lengo lake ni kuwafikia vijana takribani milioni nne na laki nne ifikapo mwaka 2021.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mpango huo moja ya component iliyopo tunaita ni RPL - Recognition of Prior Learning. Huu ni mfumo wa urasimishaji ujuzi kwa vijana ambao wana ujuzi lakini hawajapitia mfumo rasmi wa mafunzo. Hivi sasa tunao takribani ya vijana 22,000 ambao wameomba kupitia ofisi ya Waziri Mkuu kufanya mafunzo haya.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninavyozungumza hivi sasa vijana 3,448 nchi nzima wamenufaika na nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mwaka huu wa fedha tunaendelea pia kuwachukua vijana hawa kwa ajili ya kuwarasimisha katika ujuzi walionao na kuwapa cheti bila kupitia katika mafunzo maalum ya vyuo vya ufundi stadi. (Makofi)
MHE JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Tatizo kubwa la ajira ni mfumo wetu wa elimu ambao hauwapi fursa vijana wetu kuwa creative na innovative, yaani unakuwa na mfumo wa elimu ambao unaangalia miaka 50 unataka uwe na Taifa la namna gani badala ya elimu yetu ya copy and paste. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuhakikisha mitaala yake inaandaa Taifa ambalo linakuwa innovative and creative badala ya copy and paste?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, alichokisema Mheshimiwa Mbunge pia kimeripotiwa na taarifa mbalimbali, moja kati ya changamoto iliyopo ni namna ambavyo tunaweza tukawa tuna vijana wahitimu wenye ujuzi ambao utawapa sifa za kuajiriwa katika soko la ajira.
Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama ofisi ya Waziri kupitia mpango wa ukuzaji ujuzi, moja kati ya eneo ambalo tumelipa kipaumbele ni hilo. Mwaka jana Mheshimiwa Waziri Mkuu alizindua miongozo kwa ajili ya kuhakikisha vijana wetu wahitimu wa Vyuo Vikuu wanapata mafunzo ya vitendo ili waongeze sifa ya ziada kwenda kuajiriwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikirudi katika msingi wa swali lake ni kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Wizara ya Elimu tunafanya kazi hii kwa pamoja ili kuona namna bora kuja na mitaala ambayo itamfanya kijana wa Kitanzania akihitimu elimu yake awe na sifa za kuajiriwa ili apate nafasi ya kuajirika.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama alivyosema kwamba kuna hoja ya kuhakikisha vijana wetu wanakuwa wabunifu ili watakapomaliza vyuo kama hawajapata ajira rasmi waweze kujiajiri. Kwa sasa Wizara ya Elimu ina mkakati mkubwa sana kuhakikisha kwamba tunakuza stadi za kazi ili vijana wanapohitimu wasiwe wanaangalia kuajiriwa tu vilevile waweze kujiajiri.
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara kwa sasa inatekeleza mradi unaitwa ESPJ - Education and Skills for Productive Jobs, mradi ambao unafadhiliwa na Wadau wa Maendeleo kwa dola milioni 100. Moja kati ya malengo yake ambalo ni kubwa, ni kuhakikisha kwamba kwenye shule zetu, vyuo vyetu vijana wanafundishwa stadi za kazi ili wakitoka hata kama hawajapata ajira rasmi waweze kujiajiri.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nitumie fursa hii kuendelea kusisitiza kwamba zamani tunapoenda kusoma shuleni tunafikiria kwenda kuajiriwa, kwa sasa focus tokea mwanzo tunataka watu wajue kwamba ajira ni pamoja na kujiajiri. Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. (Makofi)
MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake, hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa utaratibu huu uliopo hivi sasa na tendency tunayoiona, je, Serikali haioni inanyima fursa uwakilishi wa wanawake hapa Bungeni kutokana na ongezeko la Viti hususani kwa upande wa Chama cha Mapinduzi?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa sababu mwongozo huu unatokana na sheria, sasa ni lini Serikali italeta mabadiliko haya ya sheria hapa Bungeni ili tuweze kurekebisha tuone kwamba idadi ya wanawake inaongezeka hapa Bungeni? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Saada Mkuya, kwa pamoja, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katika majibu yangu ya awali, msingi wa mgawanyo wa Viti Maalum unatokana na Ibara ya 78(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ilivyo ada, pamekuwepo na marekebisho mbalimbali ya Katiba kutokana na mahitaji. Inapotokea haja ya kufanyika hivyo basi Serikali tutaona umuhimu wa kuona jambo hili kwa uzuri zaidi ili iweze kubadilishwa kuendana na mazingira ya wakati husika, lakini kwa hivi sasa msingi unabaki kuwa Ibara ya 78(1) ya Katiba ndiyo ambayo inatuongoza.
MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Katiba yetu ya nchi hii ya 1977, Afisa wa Tume ya Uchaguzi hapaswi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa. Wakurugenzi na Watendaji wanaosimamia chaguzi ni wanachama wa CCM kwa ushahidi. Wengi waligombea Ubunge, walioshindwa wameteuliwa kuwa Wakurugenzi na hakuna sehemu yoyote ambapo wamejiuzulu uanachama wao na ndiyo wanaosimamia chaguzi hizi na imepelekea wagombea wa vyama vya upinzani wanaongombea Ubunge na Udiwani wananyimwa ama fomu ama wakirudisha fomu Wakurugenzi wanajificha. Je, hii ndiyo Tume Huru ya Uchaguzi? Hilo ni swali la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, mimi mwenyewe nimeshiriki kwenye hizi chaguzi. Nimeenda sehemu moja inaitwa Nyabubinza kule Maswa Magaharibi. Mimi Mbunge, Mkuu wa Wilaya, Ma-green guard na Polisi wanadiriki kututeka tunaofanya kampeni kutoka upinzani. Hivi hii ndiyo Tume huru ya Uchaguzi? Huko mnakotaka twende ni wapi? Mnataka mpaka damu imwagike? Mnataka mpaka damu imwagike? Swali la pili… Sawa, naenda.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Marwa Chacha Ryoba, Mbunge wa Serengeti, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza alitaka kujua kama kweli hii ni Tume Huru ya Uchaguzi kwa mifano aliyotoa. Nikirejea katika majibu yangu ya msingi unaipimaje Tume ya uchaguzi ni huru. Uhuru wa Tume ya Uchaguzi unapimwa kutokana na majukumu ya Kikatiba yaliyopo ambapo utekelezaji wake ndiyo unaashiria kwamba Tume hii ni huru au siyo huru.
Mheshimiwa Spika, ukienda kwenye Ibara ya 74(6) imeainisha majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo kimsingi hasa majukumu hayo yakiingiliwa ndiyo unasema Tume hii imekosa uhuru. Jukumu mojawapo ni kubwa ni la kuratibu na kuendesha uchaguzi ambao ndiyo umefanya hata Marwa Ryoba Chacha leo yuko Bungeni. Kwa hiyo, sitaki kuamini kwamba majukumu haya ya Tume yanaingiliwa kwa mujibu wa swali ambalo amelileta. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili anasema kwamba alikwenda kwenye kampeni Maswa wakatekwa na je hii ndio Tume Huru ya Uchaguzi? Waheshimiwa Wabunge wenzangu hapa tuelewane kimsingi kabisa, tukizungumza Tume ya Uchaguzi maana yake ni Tume ambayo inayotokana na Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Unazungumza kuhusu kutekwa jambo ambalo la kijinai na ulipaswa kuliripoti Polisi lichukuliwe hatua na siyo jukumu la msingi la Tume la kushughulika na kutekwa kwa watu. (Makofi)
MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Sisi sote tunafahamu kwamba mahakama ni chombo cha kisheria ambacho kimekuwa kikitoa haki na kuleta amani katika maeneo mbalimbali kwa mujibu wa sheria. Je, Serikali haioni kuchelewa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa watumishi wa mahakama wakiwemo Mahakimu ni kudhoofisha hali ya utendaji kazi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika jibu la Mheshimiwa Waziri la msingi amekiri kama mahakama hizo ni chakavu na majengo mengi ni yale yaliyoachwa na Mkoloni, je, ni nini tamko la Serikali la kuharakisha ujenzi wa mahakama hizo sambamba na ujenzi wa nyumba za Mahakimu? Ahsante.
NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA):
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Serikali inatambua changamoto iliyokuwepo katika ujenzi wa mahakama na kwa muda wote tumeendelea kutenga fedha kwenye bajeti zetu kuhakikisha kwamba tunakabiliana na changamoto hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mpango wa Wizara tumeamua kushirikiana na Baraza la Nyumba la Taifa na Chuo Kikuu cha Ardhi ili kupitia ujenzi wa nyumba za mahakama na ofisi za mahakama kwa kupitia teknolojia mpya ya moladi tuweze kuzifikia mahakama nyingi zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba ni mpango wa Serikali wa kuhakikisha kwamba tunajenga mahakama nyingi kadri iwezekanavyo na hii itatokana na upatikanaji wa fedha. Uzuri tunayo teknolojia mpya ya moladi, naamini tutawafikia wananchi wa Tunduru na wao wapate huduma hii ya mahakama. Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Mwenyekiti, majibu ya Serikali yanaonesha kwamba kumbe Tume ya Uchaguzi haiandikishi watu kwa kufuata vigezo bali inaandikisha yeyote atakatejitokeza na mzigo wa kuangalia nani ana vigezo na nani hana unabaki kwa wananchi kwamba waweke pingamizi, jambo hili siyo zuri.
Sasa Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba Tume ya Uchaguzi inapoandikisha wapiga kura ifuate vigezo vilivyoainishwa kisheria? Hilo moja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kutokana na harakati za kiuchumi sasa hivi zilivyo duniani Watanzania wanaishi katika mataifa mbalimbali na wangependa kuendelea ku- enjoy ule Utanzania (utaifa) wao. Serikali ina mpango gani wa kuruhusu uraia pacha ili Watanzania walio nje na wenyewe waweze kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kama watanzania wanaoishi Tanzania? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, KWA swali la kwanza, si kweli kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikiwa inawaandikisha Watanzania kushiriki kwenye uchaguzi haifuati vigezo vilivyowekwa. Kwa mujibu wa Katiba yetu na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, vigezo vimewekwa vya nani anapaswa kuandikishwa kwenye daftari la kupiga kura na ndiyo maana kifungu cha 24 cha sheria hiyo kimetoa mwanya kwa mtu yeyote ambaye ana pingamizi kwa mtu aliyeandikishwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tafsiri yake si kwamba tume sasa inamchukua kila mmoja tu lakini kwa mujibu wa kifungu hicho imetoa nafasi hiyo ili yeyote mwenye pingamizi awasilishe pingamizi hilo kwa Tume lifanyiwe kazi na kama mtu hana sifa ataondolewa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la uraia pacha limezungumzwa mara zote, suala hili ni la Kikatiba muda utakapofika na itakapoonekana inafaa basi ninaamini sisi sote kama Wabunge na nchi kwa ujumla tutaenda katika mwelekeo huo, lakini kwa hivi sasa Katiba na sheria zetu haziruhusu uraia pacha. (Makofi)
MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana na mimi kuniruhusu niulize swali la nyongeza katika suala hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kuhusu raia wageni kushiriki mambo ya ndani ya nchi yetu katika Jimbo la Mchinga inafanana sana na hali ilivyo katika kambi za wageni katika Mikoa ya Kigoma na Tabora hasa Ulyankulu na Katumba. Katika maeneo hayo wageni wamekuwa wengi wanafanya maamuzi kwa ajili ya Watanzania waliopo pale. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaangalia wakimbizi wale wasifanye maamuzi yanayohusu Watanzania? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria za nchi yetu zimeweka wazi namna ambavyo wageni wataingia nchini na shughuli zao zote zinaratibiwa kwa mujibu wa sheria. Inapotokea kuna wageni wowote wameingia nchini wanafanya mambo kinyume na sheria tafsiri yake ni kwamba wanavunja sheria za nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu limeletwa hapa Bungeni, tunalipokea na tutalifanyia kazi kuhakikisha kwamba wageni wote waliopo huko wafuate sheria za nchi yetu na pia tunawaagiza maafisa wetu wa Serikali kuhakikisha kwamba wanalifuatilia jambo hilo ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na nashukuru kwa majibu ya Serikali, hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia sehemu ya mwisho ya jibu la Mheshimiwa Naibu Waziri anakiri kwamba sekta binafsi wanaruhusiwa hata kuongeza kile kiwango ili kuwapa motisha na tunaelewa kwamba motisha ndiyo kila kitu. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri unaweza ukatuambia ni kwa nini Serikali mpaka leo haijawalipa watumishi wake annual increment ambayo ipo kisheria (statutory) na unakiri kwamba hii inasaidia sana motisha na sisi tunajua motisha ndiyo inaweza kusaidia maendeleo ya nchi hii. Je, unaweza kutupa hiyo ni kwa nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia sekta binafsi pamoja na kwamba wana viwango vya juu lakini pia wana viwango vya chini sana na wale wafanyakzi wa chini wanapata hata pungufu ya shilingi laki moja. Je, Serikali inasema nini kuhusu hili hasa ikizingatia kwamba shilingi laki moja kwa sasa hivi haiwezi kitu chochote? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu watumishi wa umma na nyongeza ya mshahara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili limekuwa likisemwa mara kwa mara hapa Bungeni ya kwamba Serikali si kwamba haitambui kwamba kuna umuhimu wa kufanya annual increment kwa watumishi wa umma, kilichotokea ni kwamba baada ya zoezi lile la uhakiki kuhakikisha kwamba tunatengeneza kanzi data ya wafanyakazi ambao wapo hawana changamoto zile za kwenye masuala ya uhakiki na maelekezo yameshatoka kwamba kuanzia hapo sasa Serikali itaona namna bora ya kuweza kulitimiza takwa hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivi sasa shughuli hii ilikwama kwa sababu mtakumbuka kwa mwaka 2016/2017 zoezi la uhakiki liliendelea na kanzi data hiyo ikishatengenezwa vizuri naamini kabisa kwamba jambo hilo litatimizwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kuhusiana na suala la kima cha chini katika sekta binafsi. Kwa mujibu wa Sheria ya Taasisi za Kazi Na. 7 ya mwaka 2004 kifungu cha 37 kimetoa mamlaka kwa Bodi ya Mishahara iliyoanzishwa kufanya uchunguzi wa kina na utafiti kuhusiana na ongezeko la mishahara ya sekta binafsi na baadaye kumshauri waziri mwenye dhamana ili aweze kutangaza kutokana na hali halisi ya wakati huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nilitangazie Bunge lako kwamba tayari bodi hii imeshaundwa na muda siyo mrefu inaanza kazi yake kuhakikisha kwamba jambo hili wanalifanyia kazi kwa utafiti na baadaye kumshauri Mheshimiwa Waziri ili sasa kuja na viwango vya kima cha mshahara kutokana na hali halisi ya wakati huo. (Makofi)
MHE. SILAFU J. MAUFI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri katika swali langu la msingi, mimi kama Mheshimiwa Mbunge wa Bunge hili la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na bahati nzuri kwa rehema zake Mwenyezi Mungu, jana tu tumepitisha sheria ya kuiwezesha Serikali kuingia ubia na mashirika binafsi katika maendeleo ya wananchi wetu wa Tanzania.
Je, kwa nini Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa wao kuingia ubia na sekta hii binafsi yenye viwanja hivi vinavyomikiwa na hawa watu ambao ni viwanja vyao vya halali? Kwani wamevijenga kwa muda mrefu na wanasuasua katika kuviendeleza viwanja hivi ili waweze kuingia ubia waweze kuvikarabati na watoto wetu wapate afya njema na waweze kupata ajira katika maendeleo yao.
Mheshimiwa Spika, naomba Serikali inipatie majibu kwa hilo swali dogo ambalo nimeliuliza kwa wakati huu. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTHONY P. MAVUNDE K.n.y. WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO): Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kwamba moja kati ya mkakati wa kuendeleza michezo mbalimbali nchini ni pamoja na kuwa na miundombinu rafiki ya kuwafanya washiriki wa mchezo husika kuweza kushiriki kwa ufanisi mkubwa. Ni dhamira ya Serikali kuendeleza viwanja vingi vya michezo hapa nchini.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ushauri uliotolewa na Mheshimiwa Mbunge wa kushirikisha sekta binafsi na wadau mbalimbali, sisi kama Serikali tuko tayari. Lengo letu ni kujenga mazingira rafiki ya kufanya michezo mbalimbali iliyo na miundombinu ambayo itatoa fursa kwa washiriki wake kushiriki kikamilifu.
MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Tatizo la ubovu wa viwanja limekuwa kubwa sana hapa nchini. Sasa Serikali haioni kwamba huu ni wakati sahihi sasa wa kuanzisha Wakala wa Kusimamia Viwanja vya Mpira ili iwe inasimamia ubora wa viwanja vyote vya mpira hapa nchini?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTHONY P. MAVUNDE K.n.y. WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO): Mheshimiwa Spika, chini ya Wizara pamoja na Shirikisho la Michezo Tanzania kwa maana TFF iko Idara maalum ambayo inasimamia ubora na vigezo vya viwanja ambavyo vitatumiwa katika michezo mbalimbali. Utaratibu uliowekwa ni kwamba iko international standard ambayo inavitaka viwanja mbalimba viwe vina sifa zifuatazo:-
Mheshimiwa Spika, kwa mfano, kwa Kiwanja cha Mpira wa Miguu, kwa mujibu wa international standard kinatakiwa kiwe kati ya mita 100 mpaka mita 110 na upana wake uwe ni mita 64 mpaka mita 75. Kwa hiyo, tunayo Idara chini ya TFF na kwenye Wizara ambayo kazi yao ni kushughulikia viwanja ambavyo vitakuwa ni bora.
Mheshimiwa Spika, pia kwa wazo ambalo ameleta Mheshimiwa, naamini kazi kubwa ambayo tutafanya kama Serikali ni kuboresha Idara zetu za ndani ili ziendelee kufanya utaratibu kuhakikisha kwamba tunakuwa tuna viwanja bora zaidi vya watu kuchezea.
MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA: Mheshimiwa Spika, ahsante.
Mheshimiwa Spika, haisikiki. Nashukuru sana. Ninayo maswali mawili ya nyongeza. Ukiangalia swali la Mheshimiwa Anna Richard Lupembe angependa kujua hasa kwa Kata za Ilela na Ilunde nini kinafanyika? Sasa pamoja na kwamba Katavi imetajwa na mipango ipi, ni nini hasa kinaandaliwa kufanywa katika maeneo hayo na ni shilingi ngapi zimetengwa?
Swali la pili; kwa kuwa katika Wilaya ya Karagwe, Biharamulo, Ngara pamoja na Misenyi, TBC haisikiki na wananchi wangependa kuisikia, ni nini kinafanyika kuwezesha TBC kusikika katika maeneo hayo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTHONY P. MAVUNDE K.n.y. WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO): Mheshimiwa Spika, nikianza na swali la kwanza; katika majibu yangu ya msingi, nimeuzungumzia Mkoa wa Katavi kwa ujumla ambao tafsiri yake ni kwamba itajumuisha pia Kata za Ilunde na Ilele ambazo ziko ndani ya Mkoa wa Katavi.
Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha bajeti ya mwaka 2017/2018 Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo tumetengewa kiasi cha shilingi bilioni 33.2 ambapo mpango mkakati tulionao hivi sasa ni kuhakikisha kwamba tunaongeza zaidi usikivu kwa sababu ukiangalia katika mwaka 2016 TBC ilikuwa ina usikivu wa asilimia 54 tu nchi nzima.
Mheshimiwa Spika, ndani ya miaka miwili baada ya bajeti hii kuongezeka, tumefikia usikivu wa asilimia 64. Mkakati uliopo ni kuyafikia maeneo mengi zaidi ili wananchi wapate fursa ya kupata habari kupitia TBC.
Mheshimiwa Spika, nikienda katika swali la pili la katika maeneo ya Misenyi, jibu langu ni hili hili la kwamba kwa mwaka huu wa fedha ambapo tuna kiasi cha fedha nilichokisema hapo tulichotengewa, kazi yetu kubwa ni kuhakikisha kwamba tunaendelea kufunga mitambo mingi zaidi ili wananchi wapate fursa ya kuweza kusikia TBC.
Mheshimiwa Spika, katika maeneo yale ya pembezoni tumeongeza usikivu kutoka kilowati 200 mpaka kilowati 1000 na ninaamini kabisa kwamba kwa mwaka huu wa fedha tutajipanga vizuri zaidi kuhakikisha kwamba wananchi wengi wanaisikia TBC.
MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Spika, naishukuru sana Serikali kwa majibu yake. Nina maswali mawili ya nyongeza.
La kwanza, muuliza swali alilenga hasa katika Sheria ya Usalama Barabarani. Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya marekebisho katika sheria hiyo?
Swali la pili; natambua kazi nzuri inayofanywa na Tume ya Kurekebisha Sheria; je, Serikali inaweza kwa wakati muafaka ikatoa report za kazi ambazo zimefanywa na Tume hiyo kama mapendekezo kwa Bunge lako tukufu? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA (MHE. ANTHONY P. MAVUNDE K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Spika, nikianza na swali la kwanza, ni kweli kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Tume ya Kurekebisha Sheria Sura Na. 171 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, moja kati ya kazi ya Tume ni kuandaa report ambayo hupelekea mabadiliko ya sheria au kutungwa kwa sheria mpya.
Mheshimiwa Spika, katika Sheria za Usalama Barabarani tayari Tume imeshafanya kazi yake na tunayo report ya Tume ya mwaka 2004 ambayo imeshawasilishwa kwa Mheshimiwa Waziri. Pindi pale itakapoonekana kuna mahitaji ya kufanya marekebisho katika sheria husika, sharia hii itawasilishwa hapa Bungeni kwa ajili ya kuweza kufanyiwa marekebisho kama ambavyo Mheshimiwa muuliza swali amesema.
Mheshimiwa Spika, la pili, kuhusiana na report za Tume kuwasilishwa katika Bunge; kwa mujibu wa sheria Tume hii inapaswa kutoa taarifa yake ya kila mwaka ya namna ambavyo imezipitia sheria. Tunao mpango mkakati wa kuanzia mwaka 2013 mpaka mwaka 2018 wa marekebisho hayo ya sheria.
Mheshimiwa Spika, suala la uwasilishwaji wa taarifa hii, itakuwa ni kati ya Serikali na Bunge kuona namna bora ya kuwasilisha, lakini kwa hivi sasa taarifa zetu zinapatikana katika mitandao yetu mbalimbali na utaratibu mwingine wa Kiserikali kuhakikisha kwamba wananchi wengi wanazipata.
Mheshimiwa Spika, kwa maombi ya Mheshimiwa Mbunge, kama Serikali tumesikia na tutaona namna bora ya kuweza kulifanyia kazi jambo hilo.
MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Namshukuru Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri aliyoyatoa hivi sasa. Kwa kuwa hakuna ucheleweshwaji wa mishahara, napenda kuuliza maswali yangu mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, Serikali inasema nini kuhusu uongezaji wa mishahara kwa watumishi hao?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Serikali inasema nini kuhusu upandishaji wa madaraja mbalimbali kwa watumishi wa umma?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mwantumu Dau Haji, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza ameuliza Serikali inasema nini kuhusu uwekezaji wa mishahara ya wafanyakazi. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba mshahara ni mali halali ya mfanyakazi mwenyewe hivyo kuhusu uwekezaji ni mfanyakazi mwenyewe anaamua mshahara wake nini aufanyie, akitaka kuuwekeza wote yuko huru kufanya hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusu upandishwaji wa madaraja, Serikali yetu siku zote imekuwa ikiwatendea haki wafanyakazi wetu kwenye upandishaji wa madaraja na kila mwaka wafanyakazi hupandishwa madaraja.
MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, inasikitisha kwamba sheria imetungwa tangu mwaka 2007 lakini mpaka sasa Serikali haijaanza kutoa msaada wa kisheria.
Sasa kwa kuwa mazingira ya Tarime ni maalum; kuna Mgodi wa North Mara pale Nyamongo na wananchi wengi wanabambikiziwa kesi za unyang’anyi na mauaji kutokana na mgogoro na mgodi; kuna mbuga ya Serengeti pale na wananchi wanabambikiziwa kesi za mauagi na unyang’anyi kutokana na mgogoro na mbuga, je, Serikali iko tayari kuagiza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakati huo mwongozo ukisubiriwa iende Gereza la Tarime ili ufumbuzi wa haraka uweze kupatikana?
Mheshimiwa Mwenyekitil, swali la pili, nilikuwa mahabusu ya Segerea na matatizo haya ya ubambikiziwaji wa kesi yapo Tarime lakini yapo Segerea na mahabusu nyingine. Sasa kwa kuwa hali hii imekithiri magereza mengi sana, ili hali hii ya kubambikiza kesi iweze kukoma Serikali ni lini itaanza kutoa fidia kwa wananchi waliobambikiziwa kesi ili utamaduni huu wa kubabikiwa kesi ukome? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTHONY P. MAVUNDE K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza, kwanza nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge si kweli kwamba Sheria hii ya Huduma za Kisheria imetungwa mwaka 2007.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria hii ni ya mwaka 2017, imepitishwa mwaka jana ni Sheria Namba Moja ya mwaka 2017, kwa hiyo na hivi sasa ndiyo imeanza utekelezaji wake. Hoja iliyoletwa hapa kwamba kuiomba Tume ya Haki za Binadamu kwenda katika eneo la Tarime kwa ajili ya kwenda kushughulika na hawa ambao wamebambikiziwa kesi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu uliopo ni huu kwamba huduma za msaada wa kisheria hizi zinatolewa na organization mbalimbali ambazo zimesajiliwa kwa mujibu wa sheria hii. Mpaka sasa ninavyozungumza tayari tunazo 66 ambazo zinafanya kazi hii. Kinachosubiriwa hapa ni muongozo kati ya Polisi na Wizara ya namna bora ya kuweza kutoa huduma ya kisheria kwa mahabusu walipo vituoni kwa mujibu wa kifungu cha 36(1) cha sheria, lakini si kweli kwamba watu hawapati huduma za kisheria.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia katika historia ya nchi yetu mpaka ninavyozungumza hivi sasa ni kazi kubwa sana imefanyika katika eneo hili. Kwa sababu huduma hii ya kisheria imeanza mwaka 1969 ikianzia katika Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lakini baadae ikatungwa sheria Namba 21 ya mwaka 1969, lakini baadae mwaka 1984 kwenye Katiba yetu tukaingiza Bill of Human Rights ikawa enshrined na baadae ikatungwa sheria hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ukiangalia Serikali imekuwa ikifanya kazi hii kwa kiwango kikubwa sana, na mpaka hivi sasa ninavyozungumza tayari wananchi wameweza kupata huduma za kisheria kupitia hizo organizations.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, ameuliza kuhusu watu wanaobambikiziwa kesi na namna ambavyo Serikali inaweza kuwalipa fidia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa kimahakama uko wazi na unajieleza vizuri kabisa. Inapotokea mtu yeyote ameshitakiwa mahakamani na baadae ikagundulika kwamba amebambikiziwa kesi utaratibu wa kisheria upo wa kumtaka yeye kufungua kesi ya madai, lakini Serikali hailipi suo moto moja kwa moja. Kwa hiyo wale wote wanahisi wamebambikiziwa kesi utaratibu upo na wafuate sheria.
MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu ya Serikali, lakini ninapenda kujua, kwa kuwa kilimo ndiyo bado ni uti wa mgongo wa uchumi wetu na vijana ni nguvu kazi safi sana, wana nguvu ya kufanya kazi hawa, wakiwezeshwa wakapewa matrekta, pembejeo, utaalam kidogo kwenye makambi kule watafanya kazi nzuri sana tutapata mazao mengi sana tutauza ndani na nje ya nchi tutapata fedha nyingi sana, vijana watajikomboa na nchi itapata utajiri mkubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini mpango huu haujaanza rasmi ili uweze kujulikana kwaba ni mpango wa vijana makambini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, wali la pili, jambo hili lipo kwenye Ilani ya CCM ya mwaka 2015 baada ya mimi kulisema Bunge lililopita 2010 - 2015, liko kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM, tangu ilani hiyo tumeshafanya bajeti tatu, 2016, 2017 na hii ya juzi, sijaliona kwenye mpango wa Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa nini?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTHONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nichukue fursa hii kwanza kabisa kumuelezea Mheshimiwa Mbunge kwamba moja kati ya maeneo ambayo yanasaidia sana kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana ni pamoja na kilimo na hata katika Jarida la mwaka 2016 la The Global Employment Trend, limesema moja kati ya maeneo katika nchi zinazoendelea ambayo yakitumiwa vyema yatatatua changamoto ya ukosefu wa ajira ni kilimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Serikali, kwa swali lake ambalo ameuliza kuhusu pembejeo kwa makundi ya vijana rai yetu ni kwamba tumeendelea kuwahamasisha vijana kwa makundi na mmojammoja wale wote ambao wanafanya shughuli za kilimo waendelee kutumia mifuko yetu ya uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na Benki ya Kilimo kwa ajili ya kupata mitaji na fedha kwa ajili ya pembejeo. Tukiamini kabisa kwamba mifuko hii ipo kwa ajili ya kuwasaidia kuweza kufikia malengo yao. Nitoe rai tu kwa vijana wote, hasa wale ambao wanapenda kushiriki katika shuguli za kilimo, waitumie mifuko yetu hii kwa ajili ya uwezeshaji; na wapo vijana ambao wamefanikiwa kupitia mifuko hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ni kuhusu kwamba mpango huo, pamoja na kwamba upo kwenye ilani lakini haujaonekana katika hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa miaka kuanzia 2016 mpaka leo. Ukiangalia katika taarifa ya Waziri Mkuu kwa maana ya hotuba, hili jambo limesemwa na ndiyo maana tumekuja na mpango mkakati wa ukuzaji ujuzi nchini moja wapo ikiwa ni kuhakikisha kwamba vijana wetu kwanza tunawabadilisha mtazamo waone kwamba kilimo ni sehemu pia ya kufanya shughuli ya kiuchumi. Lakini la pili, tumeamua sasa kuja na mpango madhubuti wa kuwa na vitalu nyumba kama njia ya kwanza kuhamasisha vijana wafanye shughuli za kilimo, kwa hiyo tumelisema na lipo kwenye mpango na tunaanza utekelezaji.
MHE. WILFRED M. LWAKATARE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kuanzisha Makambi ya vijana ni jambo linaloonekana linaweza kuwa na tija. Lakini je, kutokana na experience ya makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa kwamba wako vijana ambao wanamaliza Jeshi la Kujenga Taifa lakini wanaachwa idle. Je, Serikali haioni kwamba kuna haja kwanza kuimarisha mafunzo yanayotolewa JKT na kuwa-accommodate vijana wanaomaliza JKT ili tujifunze kutokana na JKT kabla hatujaingia kwenye mpango huo wa makambi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTHONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli katika makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa zimekuwepo programu mbalimbali za mafunzo ya ujasiriamali pamoja na kilimo na kupitia mafunzo hayo vijana wengi wameanza kuhamasika kufanya shughuli za kilimo na sisi Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, tumeanza majadiliano na mpango kati ya kwetu sisi na JKT ili vijana hawa wote ambao wanapata mafunzo baadaye tuwasaidie katika uwezeshaji ili wafanye shughuli za kilimo. Kwa hiyo, mpango huo upon a tunaendelea kufanya mazungumzo na JKT.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nashukuru sana kupata majibu hayo ya kina ambayo yameelezea vizuri sana juu ya miradi muhimu kama hiyo REA, Standard Gauge na bomba la mafuta lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, je, ni kwa nini Serikali isije na utaratibu wa kuwachukua vijana hawa moja kwa moja kutoka kwenye vyuo ili kuwapunguzia mihangaiko ya kuzunguka na barua za maombi na kushinda mitandaoni kama ilivyokuwa kwenye sekta nyingine, mfano, afya na elimu ambapo watu hupata ajira kwa wepesi zaidi kutokana na taaluma zao?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, Wizara hii na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ina mikakati gani kutengeneza mazingira wezeshi ikiwemo Incubation Centres za uhakika za kutosha, mitaji, vitendea kazi kwa wahitimu hawa ili waweze kupata wepesi wa kujiajiri na vilevile kwenda na Sera yetu ya Tanzania ya Viwanda, Inawezekana? Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Asha Abdullah Juma, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la kwanza la kuwachukua vijana hawa wahitimu wa vyuo vya ufundi moja kwa moja, tunachokifanya kama Serikali kwanza kabisa kwa kushirikiana na sekta binafsi ambazo pindi nafasi zinapopatikana huwa tunawaunganisha moja kwa moja na vyuo vyetu vya ufundi ili vijana hawa waweze kupata nafasi za ajira za moja kwa moja. Pia baadhi ya vyuo, kwa mfano, Chuo cha Don Bosco kimekuwa kina utaratibu wa kila mwaka kuandaa Kongamano la Waajiri ambapo wamekuwa wakiunganisha wahitimu hawa moja kwa moja na waajiri na vijana wengi wameajiriwa kwa kupitia mfumo huo. Kwa hiyo, naamini kabisa wazo la Mheshimiwa Mbunge ni jema, nasi kama Serikali tutaona namna ya kuweza kuviunganisha vyuo vyetu vya ufundi pamoja na waajiri ili vijana hawa wapate nafasi za ajira za moja kwa moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, suala la incubation kwa ajili ya kuwandaa vijana hawa, kuwalea na kuwapatia mitaji, sisi Ofisi ya Waziri Mkuu tunavyo Vituo vya Vijana. Kipo Kituo cha Vijana Sasanda-Mbozi, Ilonga pale Kilosa na Kilimanjaro. Vituo hivi viko kwa ajili ya kuwalea vijana na kuwandaa kuwa na sifa za kuajiriwa. Pia vijana hawa wanawezeshwa kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Vijana ambao umekuwa ukitoa mikopo kwa vikundi vya vijana lakini vilevile na asilimia 5 za mapato ya ndani ya Halmashauri yamekuwa yakisaidia katika kuwakomboa vijana kwa kuwapatia mitaji.
MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Tatizo hili la ajira halipo tu kwa wahitimu wa vyuo vya ufundi, lipo pia kwa wahitimu wengine wa vyuo vikuu hapa nchini. Kwa kuwa wahitimu wengi wa vyuo vikuu tayari ni wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu, kwa maana hiyo ni watu ambao wanaaminika. Kwa nini Ofisi ya Waziri Mkuu isishirikiane na Wizara ya Elimu kuandaa mikopo ya wahitimu ya kuanzia maisha pale ambapo wanamaliza masomo yao ili waweze kujitengenezea fedha ambazo zitasaidia kuendesha maisha yao lakini kurejesha mikopo waliyokopa wakiwa vyuoni. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mtolea, Mbunge wa Temeke, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhamira ya Serikali kuendelea kuwakusanya vijana wahitimu wa vyuo vikuu katika makundi tofauti tofauti na mmoja mmoja ambao wanaweza kufanya shughuli za kiuchumi na lengo letu ni kuweza kusaidia kufikia malengo yao. Chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu tunalo Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, ambapo ndani ya Baraza lile tuna mifuko zaidi ya 19 inayotoa mikopo na grants. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, natoa rai kwa vijana wote nchi nzima hasa wahitimu wa vyuo vikuu wenye mawazo mbalimbali ya kibiashara, watumie fursa ya uwepo wa Mfuko wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na mifuko mingine ili waweze kujikwamua kiuchumi. Naamini kabisa kwa kutumia Baraza hili itasaidia sana wao kuweza kupata sifa ya kupata ajira lakini vilevile na kutengeneza kipato.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo hili huwa napenda kutoa mfano na naomba nirudie mfano wangu, tunao vijana waliomaliza Chuo Kikuu cha Sokoine pale Morogoro ambao walipohitimu walijiunga pamoja, wakaunda kampuni, sisi kama Serikali tukawapa dhamana ya mkopo na hivi leo wanafanya kazi kubwa sana katika kilimo cha mboga mboga hapa nchini na wameanza kuwaajiri mpaka vijana wenzao. Kwa hiyo, natoa rai kwa vijana wengine wote kufuata mfano huo na inawezekana kabisa kutimiza malengo yao.
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa kuwa tunaamini kwamba wazee ni hazina ya Taifa letu, kama ilivyotengwa kitengo kwa ajili ya vijana, asilimia tano ya vijana na wanawake, Wizara haioni sasa ni busara kutenga pesa kwa ajili ya kuwalipa wazee wetu iwe kama…

Mheshimiwa Spika, nakushuru. Tunaamini kwamba wazee ni busara ya Taifa na ni hazina ya Taifa letu. Kwa kuwa asilimia tano imetengwa kwa ajili ya vijana na wanawake, Wizara sasa haioni ni busara kutenga fedha kwa ajili ya kuwalipa wazee wetu kama baraka katika Taifa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, nimshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri aliyotoa kuhusu masuala ya wazee. Kama Serikali na kama ilivyosema katika Ilani ya Uchaguzi miundombinu yote ya kuwezesha wazee hawa kuweza kulipwa imekwishaandaliwa. Kama Naibu Waziri alivyosema ni taratibu za ndani zinaendelea na pindi taratibu hizi zikikamilika, basi Serikali itatekeleza azma yake ya kuweza kuwalipa wazee pensheni kama ilivyosema katika Ilani ya Uchaguzi. Mheshimiwa Spika, nashukuru.
MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kama sikosei taarifa ya mwisho ya Bodi hii ilitolewa katika kipindi cha pili cha Awamu ya Nne. Hii ni bajeti ya tatu tunaijadili katika Awamu ya Tano na tunasema katika awamu hii uchumi umekua. Naomba niiulize Serikali, ni lini Bodi hii itatoa ripoti yake ili kuwezesha kupandishwa mishahara ya wafanyakazi ambao hivi sasa hata morali yao inashuka kwa sababu ya hali ngumu ya maisha? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, pamoja na mishahara, statutory increments ambazo ziko kisheria nazo hazitolewi. Ni lini takwa hili la kisheria litatolewa ili Serikali isionekane kwamba inavunja sheria ambayo tumejiwekea wenyewe? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Joseph Selasini, Mbunge wa Rombo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza na swali lake la kwanza la lini ripoti ya Bodi ya Mishahara itatoka. Kwa mujibu wa kifungu cha 35(1) cha Sheria Namba 7 ya Mwaka 2004, Sheria ya Taasisi za Kazi imeelezwa uundwa wa Bodi ya Mshahara ambapo watapewa teams of reference na Mheshimiwa Waziri na baadaye kuwasilisha kwa ajili ya maamuzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, navyozungumza hivi sasa kwa muda wa tangu mwaka 2015 Bodi hii imeshaundwa na taratibu ambazo zimewekwa ni kuhakikisha kwamba Bodi hii inapewa kwanza mafunzo na kwa mujibu wa sheria wanapewa nafasi ya kufanya kitu kinaitwa investigation kabla ya kwenda kumshauri Mheshimiwa Waziri. Katika mwaka wa fedha 2018/2019, tumetenga fedha kwa ajili ya Bodi hii iweze kufanya kazi, kwa hiyo, naamini fedha hii ikitoka na wakimaliza kazi yao ripoti hii itawasilishwa kwa Mheshimiwa Waziri kwa ajili ya maamuzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili kuhusu annual increment, ni dhahiri kwamba na Mheshimiwa Mbunge anafahamu limekuwepo zoezi la uhakiki wa wafanyakazi ambalo kwa kiwango kikubwa sana lengo lake lilikuwa ni kujaribu kutengeneza mfumo mzuri wa utumishi wa umma na kujenga utaratibu mzuri wa Serikali katika kufanya mambo ambayo wamepangwa kwa ajili ya watumishi wa umma na mojawapo likiwa ni hilo la ongezeko la mshahara. Kwa hiyo, nimuahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa sababu taratibu hizi zimeshafanyika na zinaendelea basi pale Serikali itakapokuwa tayari kwa maana kibajeti hilo takwa la kisheria litafanyika.
MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Ni vizuri Serikali kwa hili la mishahara na stahili za watumishi wakawa tu wakweli. Mfano zoezi la uhakiki limeathiri madaraja kutokupandishwa na watumishi wengine wakastaafu wakati Serikali inaendelea na uhakiki jambo ambalo limeathiri pensheni zao. Naomba nifahamu Mheshimiwa Naibu Waziri, hawa walioathirika na zoezi hili wakastaafu na pensheni zao zimeathirika Serikali inawafikiriaje ili walipwe stahiki zao kwa sababu wao hawakupenda hilo zoezi lifanyike na wao wameathirika sasa? Naomba nifahamu Serikali inasema nini?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Pauline Gekul, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika zoezi kama hili ambalo lilifanyika mwisho wa siku lazima kutakuwepo changamoto mbalimbali ambazo zimejitokeza. Niseme tu, Serikali ambacho inaweza kukifanya ni ku-deal kwa case by case. Inapotokea mazingira kama hayo, Ofisi ya Utumishi iko wazi kwa ajili ya kujadiliana na kuona namna bora ya kuwasaidia watumishi hawa wameathirika na mpango wa Serikali wa uhakiki wa vyeti. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba bado nafasi ipo kwa wote ambao wamepitia katika mazingira hayo kufanya majadiliano na Serikali na kuona namna nzuri ya kuweza kurekebisha changamoto hiyo.
MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, kwanza nashukuru kwa kutupa matumaini kwamba kuna siku mshahara utapanda.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niulize swali dogo kwamba watakapokuwa wanapandisha mishahara, je, watakuwa tayari kuzingatia watu wenye ulemavu hasa wa macho ambao wenyewe huhitaji msaidizi? Wanapolipwa mshahara sawa na wengine wao wanakuwa wanapata mshahara kidogo kwa sababu hauwatoshi. Je, Serikali itakuwa tayari kuwapa motisha au kuwapa kitu cha ziada ili iwasaidie? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Venance Mwamoto, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo amekuwa mtetezi na mpigania haki wa watu wenye ulemavu. Katika hili, kwa sababu mshahara na stahiki na haki za wafanyakazi zinaongozwa kwa mujibu wa sheria, niseme tu kwamba kwa hivi sasa sheria ambayo imewekwa ndiyo utaratibu wake utaendelea kufuatwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kama unavyofahamu pia kuna Sheria ya Watu Wenye Ulemavu ambayo inalinda haki zao na kwa namna moja ama nyingine pia kumekuwepo na incentives mbalimbali za kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanapata haki kama watu wengine. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inajali watu wenye ulemavu lakini katika hili la mishahara kwa mujibu wa sheria; sheria yetu inatuongoza katika utaratibu ambao umewekwa hivi sasa.
MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna vijana wengi sana pale Tunduma wamejiajiri kwa ajili ya kufanya escort ya magari yaliyobeba copper kutoka Congo na wamefanya kazi kwa muda mrefu lakini mpaka sasa hivi hawajapata mikataba kutoka kwenye kampuni hizo. Serikali inasema nini kuhusiana na vijana hao kwa sababu imeonesha kwamba kampuni hizo zinavunja sheria; kwa sababu wamefanya miaka mitatu wengine mpaka miaka nne lakini mpaka leo hawana mikataba kabisa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Frank Mwakajoka, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Sheria Namba 6 ya Mwaka 2004, kifungu cha 14 kimetoa sharti la kila mfanyakazi kupewa mkataba. Kama vijana hawa wanaofanya kazi Tunduma hawana mkataba maana yake waajiri wamevunja sheria. Natoa maelekezo kwa Afisa Kazi wa Mkoa wa Songwe kuhakikisha kwamba anakwenda kufanya ukaguzi katika eneo hilo na taarifa itakayotoka tutaifanyia kazi ili vijana hao waweze kupata mikataba ya ajira.
MHE. ZAINAB M. AMIRI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Katika madaraja yaliyopo nchini kwetu Tanzania yote huvuka bure isipokuwa daraja la Kigamboni na NSSF ilikusudia daraja hilo kutumika bure mara baada ya marejesho. Je, ni lini Serikali sasa itasitisha tozo la kupita daraja la Kigamboni ili liweze kutumika kama yalivyo madaraja mengine ya Mkapa, Kilombero, Ruvu, Wami na mengineyo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, kuna adha kubwa ya usafiri kwa wananchi wa Kigamboni hususan mabasi ya daladala na daladala ili ivuke inalipa Sh.7,000 ikivuka mara 10 ni Sh.70,000. Kwa hiyo, wamiliki wa daladala huona hakuna haja ya kupeleka route ya Kigamboni, Machinga Complex na wananchi wanapata adha sana ya Usafiri. Je, Serikali haioni haja sasa kutafuta vyanzo vingine ili kuweza kulipa deni la NSSF watu wapite bure kuliko kufanya biashara maana imekaa kibiashara zaidi kuliko huduma?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA : Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niyajibu maswali yake kwa pamoja. Nikianza na swali la kwanza la kuhusiana na uwekezaji uliofanyika hapo, naomba tu ieleweke kwamba daraja hili ni sehemu pia ya uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii na fedha iliyotumika kwa ajili ya uwekezaji huo ni fedha ya wanachama ambao mwishoni pia ndiyo fedha hii hii huwa inatumika kwa ajili ya kwenda kulipia mafao kwa sababu ni sehemu ya uwekezaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninachotaka kukisema tu ni kwamba, Shirika linategemea sana daraja hilo kwa ajili ya kupata kipato na hatuwezi katika hali ya kawaida kufuta kabisa tozo na watu wakapita bure katika eneo hilo kwa sababu ni eneo la investment. Kwa hiyo, nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba huu ni uwekezaji ambao unafanywa na shirika na hii ni michango ya wanachama ambayo baadaye inarudi pia kwa ajili ya kulipia katika mafao mbalimbali.
Mheshimiwa wenyekiti, ukienda duniani kote utaratibu ndiyo uko hivi kwa sababu hii fedha ya uwekezaji, fedha lazima ipatikane kuja kulipia katika shughuli mbalimbali za shirika.
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru Serikali imetoa majibu kwamba na wamekiri kwamba kweli sheria ya mtoto ya kuolewa kwa maiaka 15 ipo na inaendelea kuwepo na wanasema kwamba wanataka kumlinda mtoto huyu asiolewe akiwa na umri huo wakati sheria inasema kwamba anaweza kuolewa akiwa na umri huo. Mkoa wa Tabora ni moja kati ya mikoa ambayo ndoa nyingi za utotoni na watoto kujifungua watoto wenzao wakiwa na umri mdogo na kusababisha vifo vingi vya watoto. Serikali ina mpango gani wa kuibadilisha sheria hii ili watoto hawa waweze kuendelea na masomo yao kisheria? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, asilimia 63 ya wanaoathirika na ndoa za utotoni ni watoto wa kike, kesi nyingi zimekuwepo mahakamani kuhusiana na suala hili, lakini kutokana na sheria kuwepo ya watoto kuolewa na umri wa miaka 15 wanaofanya makosa hayo wamekuwa hawaadhibiwi kwa sababu sheria haisemi ni adhabu gani wanaweza wakapatiwa, Serikali inasemaje kuhusiana na suala hili ili kunusuru watoto wetu wanaolewa wakiwa na umri mdogo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA) : Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali la kwanza amezungumza kuhusu mkinzano na kuitaka Serikali kubadilisha sheria. Suala hili limekwishazungumzwa sana na Serikali mkishatoa maelezo yake na ikumbukwe kwamba yalitolewa maamuzi ya kesi Na.5 ya mwaka 2016 ambayo ni kesi kati ya Rebeka Jumi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Serikali imekata rufaa, kwa hiyo tunasubiri maamuzi ya kesi hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa uchache anachokisema Mheshimiwa Mbunge kama mkinzano, mkinzano huu haupo kwa sababu suala la umri, umri wa mtoto unatafsiri katika sheria tofauti na katika maeneo tofauti. Kuna umri biological, kuna umri contextual na kuna umri situational.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndio maana tunasema hapa katika sheria zetu hizi sheria ambayo anahisi yeye inakinzana hakuna upinzani wowote, Kwa sababu mwanafunzi yoyote ambaye yuko shuleni ambaye akipata ujauzito pale Hatuangalii biological age yake tunaangalia umri wa muktadha, ndio maana tunasema hata kama akiwa yupo form six ana miaka 18 akipewa ujauzito sheria ambayo tulifanya wenyewe marekebisho hapa Bungeni ukienda kwenye Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 kifungu imeongezwa kifungu cha 60A imeweka adhabu ya kwamba mtu anayefanya akosa hilo adhabu yake ni miaka 30. Kwa hiyo hakuna mkinzano katika eneo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili, Mheshimiwa Mbunge amezungumza kuhusu Serikali ifute sheria na amesema kwa sababu ndio sehemu pekee ya kuweza kulinda haki ya mtoto wa kike hasa katika eneo ambalo ametokea yeye kutokana na kwamba kulikuwa na idadi kubwa sana ya watoto ambao wanapata ujauzito na akasema ni sheria gani ambayo inamchukulia hatua mtu huyu ambaye anafanya kosa hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria hii imesema dhahiri kabisa ukienda kwenye Sheria Na. 21 ya mwaka 2009, sheria ambayo inalinda haki ya mtoto imezungumza juu ya kosa hilo la mtu yoyote ambaye anatenda kosa la kuzuia haki ya mtoto, baadaye sheria hiyo inaweza kuchukua mkondo na kuhakikisha kwamba mtu huyo anatiwa katika mikono ya sheria. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa kwamba si kweli kwamba Serikali hatu fahamu na hatulindi haki za mtoto na ndio maana tumechukua hatua mbalimbali kuhakikisha kwamba tunalinda haki ya mtoto na watupe muda tuendelee kufanyia kazi suala hili. (Makofi)
MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Nimemsikiliza vizuri Mheshimiwa Naibu wakati akijibu swali nilikuwa nataka nimuulize tu ikitokea mwanafunzi wa kiume akamchukua Mwalimu wa kike sheria inasemaje?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Sheria ya Elimu ya Mwaka 1978 na kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, Sura ya 353 imezungumza katika kifungu cha 60A(2) kwamba ni kosa pia kwa mtoto wa kiume yeyote ambaye yuko shule kuoa. Kwa hiyo, kosa linabaki pale pale na kwa upande wa wanaume imezungumza kama ni kosa, kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge Mheshimiwa Ndassa bado inabaki pale pale mtoto wa kiume pia na yeye akioa akiwa bado yuko shuleni ni kosa pia.
MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Watoto wakike wengi wanaoshindwa kuendelea na masomo baada ya kumaliza kidato cha nne na cha sita wanaolewa kwa kukosa fursa ya kujifunza katika vyuo vyetu vya ufundi. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuanzisha kambi la vijana ili hawa watoto wanaomaliza kidato cha nne wakiwa wadogo na hawaruhusiwi wakiwa chini ya miaka 14 au wakiwa na miaka 14 wakajifunze shughuli za ufundi, ufugaji bora wakajifunze ujasiriamali na mambo mengine?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA) : Mheshimiwa Mwenyekiti, ofisi ya Waziri Mkuu ina program ya ukuzaji ujuzi nchini ambao lengo lake kubwa ni kuhakikisha tunaisadia nguvu kazi yetu hasa vijana wengi kupata fursa ya kujifunza kwa vitendo hasa katika mafunzo mbalimbali ya ufundi. Program hii inaendelea na mpaka ninavyozungumza hivi sasa takribani vijana 22,000 nchi nzima wameshawasilisha maombi. Kwa hiyo, ni program ambayo inawagusa watu tofauti tofauti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba ni program endelevu mpaka mwaka 2021 tutaendelea kuwachukua watoto wengi hasa wa kike kuingia kwenye program hii kujifunza ili waweze kujitegemea. (Makofi)
MHE. MARYAM S. MSABAHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kumuuliza Naibu Waziri suala dogo la nyongeza. Kwa kuwa kuna watu wazima ambao wana akili zao timamu na wana kazi zao, lakini wamekuwa wakikiuka maadili na kuwachukua hawa mabinti wakiwa katika umri mdogo na sana kuwazalisha watoto na kuongeza ongezeko la watoto wa mitaani. Je, Serikali ina mikakati gani kuchukua sheria na mikakati ili kuhakikisha tunakomesha vitendo hivi na hawa watoto wa kike kupata haki zao stahiki?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA) : Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa sheria imeeleza vyema ni katika mazingira gani mtoto wa kike anaweza kuolewa na kinyume chake maana yake ni kosa linatengenezwa. Kwa hiyo, kwa wale wote ambao wanafanya vitendo hivyo vya kukiuka sheria, sheria zetu zipo, watachukuliwa hatua na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria ili haki ionekane imetendeka kwa mtoto huyu ambaye anakuwa amekatishwa shughuli mbalimbali ikiwemo masomo.
MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu katika nchi za nyingine Afrika Mashariki wako makini sana katika jambo hili na mashauri mengi yamekuwa yakiamuliwa kwa haraka tofauti na sisi. Kucheleweshwa kwa maamuzi ya mashauri haya kunaweza kukapelekea fikra kwamba rushwa inatumika zaidi katika kuamua haya mashauri. Sasa, je, ni lini Serikali itakamilisha huo mchakato wa kuongea na wadau ili maamuzi haya yaweze kufanyika haraka iwezekanavyo kunusuru maisha ya watoto wetu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, sheria inataka mali za watuhumiwa wa madawa ya kulevya zitaifishwe. Uwezekano wa kuzitaifisha ndani ya nchi upo, lakini ni utaratibu gani unaotumika kutaifisha mali hizi kama ziko nje ya nchi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katika majibu ya msingi, kinachofanyika hivi sasa ni wadau wa haki jinai ambao ni mhimili wa mahakama na pamoja na sisi upande wa Serikali kutafuta namna bora ya kuanza utekelezaji wa shughuli ya kushughulikia masuala ya kesi za madawa ya kulevya katika maeneo ya viwanja vya ndege na mipaka ya nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu jambo hilo ni la kisheria tunalifanya kwa umakini mkubwa. Hivi sasa ninavyozungumza tayari Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Dawa za Kulevya na Jaji Kiongozi Feleshi wameshaanza mazungumzo ya kuja na namna bora ya kuweza kuwa na mahakama hizi ambazo zitakuwa tembezi, ili inapotokea kwamba kuna mhalifu yeyote amekamatwa na madawa ya kulevya basi aweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa utaratibu ambao unakuja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ugumu unakuja kwa sababu ukiangalia kesi hizi nyingi za madawa ya kulevya zina masharti yake pia kwa maana ya kisheria. Kwa sababu ni kesi ambazo zinatakiwa zipitie hatua moja mpaka nyingine; kwa maana zinakwenda Mahakama Kuu na zikienda Mahakama Kuu maana yake ni kesi ambazo utaratibu umewekwa kwa mujibu wa sheria zianzie katika Mahakama za Mwanzo. Kwa hiyo si rahisi sana kufanya maamuzi hayo ya kiharaka, ndiyo maana tukasema kwamba kupitia utaratibu huu utarahisisha sana mashauri haya yaweze kusikilizwa kwa wakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia tu nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge, imeanzishwa Mahakama ya Mafisadi kwa mujibu wa marekebisho ya Sheria Na.3 ya Mwaka 2016 ambayo imeonesha tija sana na mpaka hivi sasa ninapozungumza tayari kesi 7,517 zimeshaamuliwa kwa uharaka sana na tunaamini kabisa zoezi hili likikamilika basi tutaweza kuwahudumia Watanzania kwa kuhakikisha kwamba wale wahalifu wote wanakamatwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, ameuliza kuhusu namna ya utaifishaji wa hizi mali nje ya nchi. Nchi yetu imesaini makubaliano na tulishirikiana na baadhi ya nchi na tumekuwa na ushirikiano mzuri na nchi nyingi ambazo kupitia utaratibu wa makubaliano hayo, ikitokea suala la namna hiyo basi mamlaka zote mbili zinafanya kazi kuhakikisha kwamba mhusika ambaye mali zake ziko nje ya nchi pia utaratibu ufuatwe wa kisheria ili ziweze kutaifishwa.
MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kuchelewesha haki ni kunyima haki na si kesi za madawa ya kulevya pekee kuna mashtaka ambayo watuhumiwa wakipelekwa kule ni kama wanasahauliwa. Kuna kesi za ugaidi na kuna kesi …
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujua ni kwa nini mashtaka ya kesi aina hii zinachukua muda mrefu kupelekwa mahakamani na kuhukumiwa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utaratibu wa makosa yote ya kijinai na kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20 umewekwa utaratibu wa namna gani kesi hizi zishughulikiwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kesi hizi zinahitaji umakini mkubwa sana, si rahisi kwa namna yoyote ile kuziharakisha pasipokuwa uchunguzi wake umekamilika. Ndiyo maana nawaomba Waheshimiwa Wabunge waendelee kuvuta subira mamlaka zetu zinafanya kazi sasa hivi kuhakikisha kwamba kesi zinapungua na Mahakama imeweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba kesi nyingi zinasikilizwa kwa wakati ili haki ionekane imetendeka.
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kuniona ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia kuchelewa kwa kesi hizi ni vidhibiti kutopelekwa maabara kwa Mkemia Mkuu haraka ili kuthibitisha. Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua changamoto hii?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa marekebisho ya sheria yaliyofanyika mwaka 2017, hivi sasa Sheria ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya Kifungu cha 4(n) ambacho kimeongezewa baada ya marekebisho kimeweka utaratibu wa kwamba hivi sasa kwa kuzingatia kwamba kuna mashauri mengi ambayo yanasimama kwa kusubiri vidhibiti kutoka katika Ofisi ya Mkemia Mkuu, sasa kupitia sheria hii imeanzishwa laboratory katika Ofisi ya Kamishna Jenerali ili kuhakikisha kwamba mamlaka pia nayo iwe na wajibu huo wa kuchunguza na kutoa taarifa ili kujaribu kusaidia expedite kesi hizi zisichukue muda mrefu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimwondolee hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ilichukua hatua kwa marekebisho hayo ya sheria na hivi sasa ukiacha Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Jeshi la Polisi lakini... kazi hiyo pia.

MHE. KHADIJA N. ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nashukuru pia kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, hotuba ya Wizara ya Viwanda na Biashara ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/2019 ilieleza kwamba tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani imeshajenga viwanda 3,036. Je, ni vijana wangapi wameweza kuajiriwa katika viwanda hivyo mpaka sasa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, pamoja na juhudi nyingi ambazo Serikali inazifanya katika kuhakikisha vijana wanapata ajira na nyezo za kujiajiri. Ripoti ya UN Tanzania ya 2018 inaonesha kwamba kati ya vijana 87 ni vijana wanne tu ambao wanaweza kujikimu kiuchumi, hili suala linazidi kuwa baya au linazidi kuwa gumu siku hadi siku. Je, Serikali sasa ina mpango gani wa dharura kuweza kuwanusuru vijana katika udumavu huu wa kiuchumi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kusema tu kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Khadija kwa kazi kubwa anayoifanya kuwasimamia vijana wa nchi hii na amekuwa mtetezi wa kweli wa vijana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza, ametaka kujua idadi ya vijana walioajiriwa katika viwanda. Nimwombe tu Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa sababu idadi hii ya walioajiriwa kwenye viwanda siwezi kuipata hapa ndani Bungeni hivi sasa, lakini nitakachokifanya nitahakikisha kwamba tunafanya coordination na wenzetu kuweza kujua katika viwanda hivyo ambavyo vimeanza kutoa ajira kwa vijana ni asilimia ngapi ya vijana ambao wameshapata ajira mpaka hivi sasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na mchango mkubwa wa sekta ya viwanda, tunaamini kabisa kundi kubwa la vijana ndiyo hasa waliopata nafasi ya kuajiriwa kwa sababu katika nguvu kazi yetu ya nchi Tanzania tuliyonayo asilimia zaidi ya 65 ni vijana, kwa hiyo automatically hapa kundi kubwa ambalo watakuwa wamepata ajira ni vijana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ni namna gani Serikali tunakuja na mpango wa kukwamua vijana kutokana na udumavu wa kipato…
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mipango tuliyonayo mikubwa kabisa ni kuhakikisha kwamba tunawashirikisha vijana katika shughuli mbalimbali za kiuchumi. Lengo letu ni kuwapatia fedha za Mifuko ya Uwezeshaji ili wafanye shughuli za kiuchumi za kuweza kujisimamia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, huo ndiyo mkakati mkubwa wa Serikali kwa sasa. (Makofi)
MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Miongoni mwa vijana wapo pia vijana wenye ulemavu na tunaposema kwamba tatizo la ajira kwa vijana, basi vijana wenye ulemavu ndiyo waathirika namba moja. Nataka kufahamu katika mkakati huu wa sasa kwamba Tanzania ya viwanda. Je, ni mikakati gani ya haraka Serikali inaandaa katika kuhakikisha kwamba vijana wenye ulemavu nao wanakuwa ni sehemu ya ajira na hawaachwi nyuma katika kuendeleza gurudumu la maendeleo hapa nchini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.(Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mipango yote ya Serikali hasa ya ukuzaji ujuzi, yenye lengo la kumfanya kijana wa Kitanzania aweze kusimama kiuchumi na aweze kuwa na sifa za kujiajiri na kuajiri vijana wengine. Mkakati wetu ni kuhakikisha kwamba katika kila mpango kundi la watu wenye ulemavu wanajumuishwa ili na wao pia wapate fursa ya kupata ujuzi stahiki ambao watautumia katika uchumi huu wa viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba katika progamu iliyoko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya ukuzaji ujuzi kwa vijana ambao lengo lake ni kuwafanya vijana hao kuwa na sifa za kwenda kufanya katika viwanda, kundi la watu wenye ulemavu wanajumuishwa na tumetenga asilimia kadhaa kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kila programu imguse na mtu mwenye ulemavu.
MHE. ADAMSON E. MWAKASAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Katika hii Mifuko ambayo wanakopeshwa vijana, kumekuwa na tatizo kubwa la wale wanaokopeshwa kurudisha mikopo hiyo ili na wengine waweze kukopa. Je, Serikali ina mpango gani mahsusi kuhakisha wale wanaokopeshwa wanarudisha ile mikopo ili na wengine waweze kukopeshwa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA) Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tunao Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao umekuwa ukitoa fedha za mikopo kwa makundi mengi ya vijana na kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge wapo baadhi ya vijana kupitia makundi hayo wameshindwa kurejesha fedha hizi kwa wakati. Tunachokifanya ni kuwasiliana na Halmashauri husika ambao tunafanya kazi kwa pamoja kuhakikisha kwamba wanaendelea kutoa elimu kwa makundi haya ya vijana kwa sababu fedha ile si fedha ambayo inatakiwa tu watu wapewe na ibaki hivyo hivyo, ni pesa ambayo ni revolving. Kwa hiyo, tunaendelea kutoa elimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tumekuwa tukifanya kaguzi za mara kwa mara kuwahimiza vijana hawa kuendelea kurejesha fedha, mpaka ninavyozungumza hivi sasa makundi makubwa ya vijana wameelewa na wameanza kurudisha fedha hii kwa ajili ya kuwafanya vijana wengine waweze kukopeshwa pia.
MHE. RUKIA KASSIM AHMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini bado nina maswali mawili ya nyongeza.Kwa kuwa viwanda vingi vimeshindwa kujiendesha kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa, kama vile kodi kuwa nyingi pamoja na bei ya umeme kuwa ghali hata ukilinganisha na nchi jirani zetu hapa Afrika ya Mashariki. Je, Serikali iko tayari kupunguza hizi kodi pamoja na gharama za umeme ili iwe kivutio kwa wawekezaji wengine kuweza kuja kuwekeza na hivi tulivyonavyo vijiendeshe kwa faida ili vijana wetu waweze kupata ajira?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali pili, kwa kuwa viwanda vingi ambavyo Serikali ina lengo la kuvifufua miundombinu yake ni ya kizamani. Je, Serikali ina mpango gani wa kuvifufua viwanda hivi ili viende na hali tuliyonayo na vijiendeshe kwa faida na vijana wetu waweze kupata ajira.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza la kuhusu gharama za uendeshaji na mazingira wezeshi ya kufanya biashara nchini, nimwondoe tu hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba hata wakati wa usomaji wa bajeti wa Wizara, Mheshimiwa Waziri alieleza mipango na mikakati ya Kiserikali ya kuhakikisha tunaweka mazingira wezeshi ya kuweza kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje kufanya biashara nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kati ya jambo kubwa ambalo linaendelea hivi sasa ni matayarisho ya mpango ambao unaitwa Blue Print to Emprove Business Environment in Tanzania ambao lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba tunaweka mazingira wezeshi ya kuwafanya Wawekezaji wote wavutike na kuja kuweka katika nchi yetu ya Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia katika swali lake la pili alitaka kufahamu kuhusu ufufuaji wa viwanda kutokana na miundombinu chakavu. Wizara inaendelea na mchakato huo na kama ambavyo imekuwa ikitolewa taarifa mara kwa mara, tumepitia katika maeneo mengi ya viwanda ambavyo vilishabinafsishwa na maelekezo yalitoka ili vifufuliwe, viweze kuajiri vijana wengi zaidi, kwa sababu lengo hapa kubwa ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2025 kundi kubwa zaidi ya asilimia 40 lipate ajira kupitia viwanda.
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kumuuliza swali moja Mheshimiwa Waziri. Kwa kuwa, moja ya mbinu za kuhamasisha wawekezaji ni kushauriana nao na hasa sekta binafsi; na kwa kuwa nafahamu Serikali ilianza mashauriano ya kila mwezi na wawekezaji, naomba kufahamu kitu gani hasa kimejadiliwa na mwelekeo wa Serikali ni nini kwenye jambo hilo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali sasa imekuja na mpango wa kuhakikisha kwamba tunakaa na sekta binafsi kujadiliana changamoto zilizopo, mpaka sasa tunavyozungumza vimeshafanyika vikao vitatu ambapo viwili vilifanyika Dar es Salaam na kimoja Dodoma. Kikao hicho sasa ndiyo kimetengeza hasa hii Blue Print kutokana na changamoto ambazo walizisema sekta binafsi ambazo zinawakwaza kwenye ufanyaji wa biashara, Serikali ikaichukua na ndiyo maana tumetengeneza hiyo document kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunaweka mazingira wezeshi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba, kama Serikali tunafahamu kwamba ni muhimu sana kuitunza na kuilea sekta binafsi kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu.
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Naomba kuuliza swali dogo la nyongeza; je, Serikali ina mpango gani wa kuwavutia zaidi wawekezaji ambao wakija watawekeza kwenye viwanda vya kuongeza thamani mazao yetu kuliko viwanda vingine vyovyote.(Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda nimpongeze kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatetea wananchi wake hasa kwenye suala la viwanda ambalo linahusisha masuala la vitunguu na tangawizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili niseme kwa ufupi ya kwamba, kama Serikali tumeona ni vema kuendelea kutumia Balozi zetu, vilevile tumeona ni vema kufanya makongamano mbalimbali ili kuwavutia wawekezaji wengi zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa ninavyozungumza mwaka jana Desemba, tulifanya mazungumzo na kongamano kubwa na Wafanyabishara kutoka China. Mwezi Desemba pia tulifanya kongamano kubwa na wafanyabiashara kutoka Jordani, tarehe 18 mwezi wa Nne tulifanya Kongamano kubwa sana na wawekezaji kutoka Ufaransa kwa lengo hilo hilo. Vile vile tarehe 23 - 24 Aprili tulikutana na watu kutoka Israel.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo letu kuwavutia wawekezaji wengi zaidi na kuwaomba kuja kuwekeza hasa katika maeneo haya ya kuongeza thamani. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba kazi hiyo Serikali inaendelea kuifanya. (Makofi)
MHE. ESTHER M. MMASI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Swali langu kwa Serikali; Vijana wanaohitimu nchini Tanzania ni takribani laki sita mpaka laki nane kwa mwaka lakini vijana wanaoingia kwenye ajira rasmi na zisizo rasmi ni takribani ni asilimia kumi mpaka 25.
Mheshimiwa Spika, nini kauli ya Serikali kutokana na masuala mazima ya retrenchment yanayoendelea nchini Tanzania. Kwa sasa tunayo taarifa ya kwamba kampuni ya TTCL ina mpango wa down size wafanyakazi zaidi ya 500; lakini pia ukienda kwa taasisi zisizo za Kiserikali mfano TBL tumeshuhudia hapa miezi michache iliyopita kwamba wali- retrench zaidi asilimia 80 na wakati huo huo wakihamishia sehemu kubwa ya operations mfano payroll function, lakini pia siyo hivyo tu finance Department ilipelekwa Mauritius; swali langu la kwanza; nini kauli ya Serikali haswa ukiangalia hali halisi ya ombwe kubwa la vijana wanaohitimu pasipo kuwa na ajira?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kumekuwa na utamaduni mbaya sana unaoendelea kwenye taasisi za kifedha ambapo taasisi hizi zinakuwa zinajisajili Tanzania lakini sehemu kubwa sana ya majukumu ya IT yanakuwa yanafanyika nje ya nchi. Mathalani benki ya Stanchart (Standard Chartered), Baclays, lakini Citi Bank pamoja na Stanbic bank, wamekuwa na utamaduni wa sehemu kubwa ya IT zinakuwa zinafanyika nje ya nchi. Ukiangalia NBC, supply of payment inafanyika South Afrika; ukiangalia Stanchart account opening na pia transaction process zote zinafanyika nchini Kenya. Ukiangalia Baclays function management zinafanyika nchini India, swali langu kwa Serikali. Nini kauli ya Serikali hasa ukiangalia uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali kupitia Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi hawa wanaohitimu shule ya TEHAMA? Naomba kupatiwa majibu stahiki na Mheshimiwa Naibu Waziri, ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Spika, nikianza na swali la kwanza la kuhusiana na retrenchment. Ni dhahiri kwamba sisi kama nchi katika Sera ya Ajira tunaendelea kulinda ajira za vijana katika nchi yetu kwa kuhakikisha kwamba vijana wengi zaidi wanapata fursa ya kuweza kuajiriwa.
Mheshimiwa Spika, alichokisema Mheshimiwa Mbunge, kwa mujibu wa Sheria Na. 6 ya Mwaka 2004 imeweka vigezo ni katika hatua gani mwajiri anaweza akafanya retrenchment. Sheria ile pia imetoa nafasi kwa vyama vya wafanyakazi kushiriki moja kwa moja katika majadiliano kabla jambo hili halijafanyika.
Mheshimiwa Spika, rai yangu kwa waajiri wote ni kwamba waendelee kufuata sheria inavyozungumza ya namna ya kuweza kuwaondoa wafanyakaza kazini kwa kuwa jambo hili lipo kisheria.Kazi yetu kama Wizara ni kuhakikisha kwamba taratibu za kisheria zimefuatwa ili Watanzania wengi haki zao za kimsingi zisiondolewe katika utaratibu huu wa uachishwaji wa kazi ambao wa sheria imeuzungumza vizuri.
Mheshimiwa Spika, katika swali lake la pili, kuhusu kazi nyingi kufanyika nje ya nchi. Kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu anachokisema Mheshimiwa Mbunge na sisi tulikiona tumefanya ziara ya ukaguzi tumekwenda makampuni mbalimbali; na hivi sasa tumeshatoa maelekezo ya kazi hizi namna gani zifanywe.
Mheshimiwa Spika, moja ya changamoto kubwa kwenye eneo la TEHAMA pia ni kwamba ukiruhusu mambo hayo yote yafanyike nje ya nchi ni hatari pia kwa usalama wa nchi. Kama Serikali tumechukua hatua na tumetoa maelekezo kuwataka waajiri wote kurekebisha eneo hili. Sasa hivi tunafanya follow up na vile vile tunafanya kaguzi ili kukagua waajiri wote ambao wamekiuka agizo letu tuweze kuwachukulia hatua.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE ENG. ATASHASTA J. NDITIYE):
Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri ningependa niongeze kipengele kidogo kuhusu masuala ya TEHAMA.
Mheshimiwa Spika, kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Serikali imeanzisha Tume ya TEHAMA ambayo pamoja na majukumu mengi kabisa iliyonayo inakwenda kuanzisha Bodi ya kutambua wana TEHAMA wote ili wana TEHAMA hao watambulike kutokana na elimu yao na ujuzi wao wanalionao kama wanavyotambulika Mainjinia, Madaktari na Wahasibu.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa kufanya hivyo tunaamini kwamba tutapata taaluma stahiki za kufanya kazi kwenye maeneo ya TEHAMA. Ahsante.
MHE. MUSSA A. ZUNGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa swali. Kwanza niipongeze Serikali kwa jitihada zake za mikakati ya ajira kwa vijana na Sera ya Vijana.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo liko eneo ambalo Serikali kama wakitilia mkazo na kulifuatilia; sehemu ya hand- looming. Huu ni mtambo mdogo sana ambao unatumika hasa na nchi ya India ku-create ajira kwa vijana na wananchi wa kawaida kwa kufanya biashara ndani ya vyumba vyao. Haihitaji umeme wala teknolojia yoyote zaidi ya kuwa na chumba na mtu mmoja unapata nyuzi wanatengeneza gray cloths na vile vitambaa wanauzia viwanda vya kutengeneza nguo; na matokeo yake wanapata kati ya laki moja na nusu mpaka laki mbili kwa siku. Je Serikali ina mkakati gani wa kutazama eneo hili la ku-create ajira badala ya kuacha vijana wengi ambao sasa hivi hiyo nguvu kazi zinapotea? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Spika, tunapokea ushauri mzuri wa Mheshimiwa Mbunge wa lengo la kuongeza ajira hasa kwa vijana. Kwa kuongezea tu na sisi kama Serikali tuliona pia tuna jukumu la kutengeneza mazingira wezeshi kwa vijana wengi. Ndiyo maana kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu hivi sasa tunaendesha programu ya kukuza ujuzi nchini ambayo imeanza mwaka 2016 mpaka 2021 lenye lengo la kuwafikia takribani vijana milioni 4.4 nchi nzima ili vijana kupitia ujuzi mbalimbali waweze kujiajiri na kuajiri vijana wengine.
Mheshimiwa Spika,kwa hiyo fursa aliyosema Mheshimiwa Mbunge tunaichukua na tutaiboresha ili vijana wengi zaidi waweze kupata ajira.
MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pia napenda kumshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa vile bado malalamiko ya waajiriwa ni mengi sana nchini na bado utaratibu haujafafanua vizuri ni namna gani ambavyo waajiriwa hawa wanaweza kupata stahiki zao na usalama wao wakati wakiwa katika maeneo ya kazi, Serikali ina kauli gani juu ya hili?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa vile bado ajira zetu za ndani hazina sheria ya moja kwa moja ambayo inawalinda waajiriwa, Serikali pia inasema nini juu hili?

Mheshimiwa Spika, ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, AJIRA NA VIJANA): Mheshimiwa Spika, katika swali la kwanza kuhusu malalamikio, Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa ikiyafanyia kazi malalamiko na taarifa mbalimbali zinazowahusu wafanyakazi kwa kufanya kaguzi mbalimbali ambazo lengo la kaguzi hizi ni kutaka waajiri wote nchini wafuate utaratibu wa sheria unavyoelekeza kwa maana ya Sheria Na. 6 ya mwaka 2004 na Sheria Na. 7 ya mwaka 2004 ambazo zimetoa haki na wajibu kwa wafanyakazi pamoja na waajiri.

Mheshimiwa Spika, ofisi yetu imeendelea kuchukua hatua kwa waajiri wote ambao wanakiuka sheria na mpaka ninavyozungumza hivi sasa, tayari tumeshawafikisha Mahakamani zaidi ya waajiri 19 katika kipindi cha mwaka 2017/2018 ambao wamekiuka utaratibu wa sheria. Ndiyo maana Ofisi ya Waziri Mkuu itaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuepukana na malalamiko haya ya wafanyakazi.

Mheshimiwa Spika, sehemu ya pili ya swali lake Mheshimiwa Mbunge alitaka kujua kuhusu sheria ya kuwalinda wafanyakazi. Kwa mujibu wa Sheria Na. 6 ya Mwaka 2004, imeainisha bayana haki za mfanyakazi na wajibu wa mwajiri. Sheria hii ndiyo inayotumika katika kuwalinda wafanyakazi. Ndiyo maana Bunge lako Tukufu mwaka 2016 lilifanya marekebisho ili kuongeza meno zaidi katika Idara ya Kazi katika kuwalinda wafanyakazi kwa kuhakikisha kwamba ikitokea mwajiri anakiuka taratibu za kisheria kuhusu mikataba na masaa ya kazi, Afisa Kazi akienda kumkagua atakuwa na uwezo wa kumtoza faini hapo hapo ambayo ni kiasi cha fedha, ambapo pia baadaye atakuwa na compliance order haya yote yaende kwa pamoja. Lengo ni kufanya sheria hiyo iwe na meno na wafanyakazi wetu waweze kulinda haki zao.

Mheshimiwa Spika, ahsante.
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Naomba kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza; kwa kuwa Serikali inakiri kwamba zoezi hili litaanza siku za hivi karibuni na ni ukweli kwamba tumebakiza muda mchache kuelekea uchaguzi mkuu na kwa kuzingatia tumekuwa na utaratibu wa kuandikisha kupata vitambulisho vya Taifa kupitia NIDA, kumekuwa na changamoto nyingi na watu wengi kukosa na vitu kama hivyo.

Kwa muda huu mchache uliobaki na kwa ukubwa na jiografia ya nchi hii na kwakweli kuna uhitaji wa watu wengi kuandikishwa ili wapate fursa ya kupiga kura, je, Serikali kweli inania ya dhati ya kuanzisha zoezi hili na kuhakikisha watu wote wenye vigezo na sifa wanapata fursa hiyo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, mara ya mwisho tulivyofanya maboresho haya ya Daftari ya kupiga kura kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kulikuwa na changamoto nyingi za ubovu au uhafifu wa vifaa vya uandikishaji, mfano zile mashine za finger printzilikuwa wakati fulani hazifanyi kazi kwa ufanisi na kamera zilikuwa hazifanyi kazi kwa ufanisi.

Je, Serikali ipo tayari sasa kupitia changamoto zilizotokea huko nyuma kuwa na vifaa vya uhakika na vya kisasa kuhakikisha kwamba changamoto zilizojitokeza haziwezi kutokea tena ili kila Mtanzania mwenye fursa aweze kupata fursa hiyo ya kuingia kwenye maboresho ya Daftari ya kupiga kura na kuingia kwenye uchaguzi mkuu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, nikianza na swali lake la kwanza la hofu yake juu ya ukubwa na jiografia ya nchi yetu na muda uliopo, kwa mujibu wa Sheria kifungu cha 15(5) kinazungumza kwamba Tume ya taifa ya uchaguzi itafanya maboresho ya Daftari mara mbili kabla uchaguzi mwingine kwa maana kwamba kabla ya nomination day.

Mheshimiwa Spika, jambo ambalo nataka lieleweke kwa Mheshimiwa Mbunge kwanza kabisa, ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania kushiriki kwenye uchaguzi na kama Serikali tutahakikisha kwamba kila Mtanzania mwenye sifa ya kushiriki kwenye uchaguzi anashiriki kwenye uchaguzi.

Mheshimiwa Spika, pia kuhusu hofu ya kwamba watu ni wengi sana, tumefanya hivi kwa sababu ya changamoto zilizotokea wakati uliopita, tuliona ni vyema kwanza tukaboresha miundombinu na mifumo ya ndani ili changamoto zilizojitokeza wakati uliopita, hivi sasa tuweze kuzitatua na moja wapo ilikuwa ni kuanzisha kanzidata maalum ambayo itatupa nafasi ya kuweza kuwafikia watu kwa urahisi.

Mheshimiwa Spika, katika eneo hili pia si kwamba tutakwenda kuwaandikisha watu upya tunakwenda kuboresha wale ambao wanasifa kwa wakati huo. Kwahiyo, tunategemea kwa mwaka 2019 huo kuandikisha zaidi ya wapiga kura milioni nne wapya wenye sifa na wale ambao wanapata changamoto kwa wakati uliopita na pia mapema mwakani mwaka 2020 tutafanya marejeo tena kwa kwa ajili ya kuwapa watu wenye sifa.

Mheshimiwa Spika, la pili kuhusu vifaa, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, Serikali inafahamu kwamba ni lazima kila mtu mwenye sifa ya kushiriki uchaguzi ashiriki uchaguzi. Kwa hiyo, moja kati ya maandalizi ambayo tunayafanya ni kuhakikisha kwamba tutakuwa na vifaa bora na vya kisasa ili kila Mtanzania aweze kushiriki haki yake ya kimsingi na yakikatiba.
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa Wilaya ya Tanganyika ni Wilaya kubwa na tarafa zake zimekaa kwa mtawanyiko. Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kuharakisha kujenga jengo la mahakama katika wilaya hiyo? Ili kuweza kuwasaidia wananchi ambao wanapata tabu sana kutoka eneo lingine kwenda lingine kwenda kutafuta huduma za mahakama?

Swali la pili, kwa kuwa Mahakama za Mwanzo zimekuwa katika mazingira mabaya na hayana kivutio cha aina yoyote kwa watumishi wanaofanya kazi kwenye maeneo hayo. Serikali iko tayari kwenda kukarabati jengo la Mahakama ya Mwanzo eneo la Karema na maeneo ya Mishamo ili waweze kupata huduma iliyo sahihi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kwamba huduma ya kimahakama ni huduma ambayo kila mwananchi anastahili. Ni kweli katika mazingira ambayo ameyasema ya Wilaya ya Tanganyika wananchi wanatembea umbali mrefu. Lengo la Serikali ni kuhakikisha kwamba katika mpango huu kama nilivyosema hapo awali katika jibu langu la msingi kwamba kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Serikali itaanza ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Tanganyika ili wananchi wengi zaidi waweze kupata fursa ya kupata huduma za kimahakama.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu Wizara yetu ya Katiba na Sheria tumeingia makubaliano na Chuo cha Ardhi pamoja na Taasisi ya masuala ya nyumba tunajenga mahakama hizi kwa teknolojia ya kisasa ya moladi ambayo inatumia muda mfupi sana. Kwa hiyo, imani yangu ni kwamba na zile Mahakama za Mwanzo alizozisema, kutokana na bajeti ilivyo basi tutaanza Mahakama ya Wilaya na hizi zingine pia na kutokana na mfuko wa bajeti ulivyo. Lakini nimhakikishie kwamba Serikali inatambua kilio hicho na tutayafanyia kazi kadri bajeti inavyoendelea kupatikana.
MHE. JAMES F. MBATIA: Ahsante sana, Mahakama za Mwanzo za Kilema lile jengo limebomoka kabisa na haifanyi kazi na Marangu inayofanya kazi hali ni mbaya sana na inahatarisha Hakimu na watendaji wote. Serikali inaji-commit itafanya lini ukarabati wa mahakama hizi na kujenga hii nyingine upya kwa sababu utoaji wa haki unakuwa ni mgumu sana katika Jimbo la Vunjo na Wilaya ya Moshi Vijijini?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, swali hili la Mheshimiwa Mbatia litajibu pia maswali ya Wabunge wengi ambao walitaka kusimama. Serikali inatambua upungufu wa Mahakama za Mwanzo nchi nzima na ndiyo maana katika mpango wa miaka mitano tuliyojiwekea katika Wizara wa uboreshaji wa miundombinu, tunakwenda kuyafikia maeneo yote kadri ya bajeti itakavyopatikana.

Mheshimiwa Spika, lakini pia niwaombe Waheshimiwa Wabunge katika Wizara ya Katiba na Sheria tumetengeneza majedwali ambayo yanaonesha Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Mkoa lakini na vilevile ukarabati na ujenzi wa Mahakama Kuu. Kwa hiyo niwaombe Waheshimiwa Wabunge watakaopata nafasi basi waweze kupitia jedwali lile waangalie katika eneo lake ni lini wamepangiwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo, ya Wilaya na Mkoa.
MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza kabisa, niipongeze Serikali kwa juhudi zake katika kuwaendeleza wananchi kiuchumi na niwapongeze pia kwa kutoa shilingi bilioni 22 kwa ajili ya kuendeleza SACCOS hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuipongeza Serikali lakini pia ninayo maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri lakini niseme kwamba pamoja na Serikali kuingia mikataba na benki na kufikia uamuzi wa kusaini kwa ajili ya kuwaendeleza wakulima hawa kwa kuwapatia mikopo lakini bado benki za Zanzibar zimekuwa zikisuasua kuhusiana na suala la mikopo hiyo. Je, Serikali iko tayari kuzisimamia benki hizi ili kuweza kufikia utekelezaji ili wananchi hawa waweze kupata mikopo hiyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, nataka kusisitiza tu Serikali kwamba SACCOS zetu mara nyingi hazina elimu za kuendeleza biashara zao kimitaji na kimasoko. Kwa hiyo, naiomba Serikali kufika Zanzibar kuwapa elimu wananchi wa Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Maida Hamad Abdallah, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na swali la kwanza, ni kweli Benki ya Kilimo (TADB) ilikwishaingia makubaliano na benki nilizoziainisha pale awali ikiwemo Benki ya Watu ya Zanzibar. Kwa hiyo, rai yangu ni kuziomba taasisi za fedha kwa upande wa Tanzania Visiwani kwa maana ya Zanzibar kuichangamkia fursa hii ili wakulima wengi zaidi wa Zanzibar waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na benki hii kwa sababu ipo kwa ajili yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ufupi tu niseme kwamba kwa upande wa Zanzibar tunaendelea pia na hatua za kuviwezesha vikundi hivi. Hivi sasa tayari vikundi kwa maana ya SACCOS 231 zimeshafikiwa na tayari zaidi ya shilingi bilioni 24 ziko katika mzunguko kwa ajili ya ukopeshaji. Kwa hiyo, nichukue fursa hii kuziomba na kuzitaka benki za Zanzibar kuchangamkia fursa hii ili wananchi wengi zaidi waweze kunufaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye swali la pili kuhusu elimu, katika Programu hii ya MIVARF, kabla ya kuanza utoaji wa fedha na uwezeshaji iko package ambayo inahusisha masuala ya mafunzo hasa nidhamu ya matumizi ya fedha na utunzaji wa fedha. Kwa hiyo, ombi kuhusu suala la elimu ni kwamba ni sehemu ya mradi huu na imekuwa ikifanyika na ninavyozungumza hivi sasa tayari vikundi 57 vya uzalishaji mali kule Zanzibar wameshapewa elimu ya kutosha juu ya matumizi bora ya fedha na namna ya kukopa.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba tu niongeze majibu ya ziada kwenye swali zuri sana la Mheshimiwa Maida na hasa faida ambazo wanaweza wakazipata wenzetu wa upande wa pili wa Muungano yaani kule Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulichokifanya mpaka sasa ni kuhakikisha kwamba Mradi huu wa MIVARF unakuwa ni
kielelezo kizuri cha Muungano wetu katika nchi yetu. Kwa sababu inaonekana upande wa pili wa wenzetu bado mikopo hii hawajaifahamu vizuri na bado hawajanufaika nayo, naomba niliahidi Bunge lako Tukufu, tutafanya ushirikiano na mawasiliano ya karibu na Waziri mwenye dhamana ya Vijana na Uwezeshaji kule Zanzibar ajue uwepo wa mikopo hii ili aweze kutusaidia kusimamia na kuhakikisha kwamba wenzetu wa upande wa pili wa Zanzibar na wao wanafaidika na wanajua uwepo wa mikopo hii kupitia benki yao ambayo itawahudumia kupitia Mpango wa MIVARF.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona. Kumekuwa na masharti magumu sana katika kupata mikopo ukizingatia vikundi vya vijana wengi wanakuwa bado hawana zile dhamana ambazo zinahitajika. Serikali inatuambia nini ili na sisi vijana ambao hatukidhi vigezo hivyo tuweze kufaidika na mikopo hiyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Khadija Nassir Ali, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo anashughulikia masuala ya vijana na kuwa mstari wa mbele kuwatetea vijana wa Taifa hili la Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua kwamba ipo changamoto kubwa sana ya upatikanaji wa mikopo katika kundi hili kubwa la vijana, Serikali kupitia Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na mifuko mbalimbali ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, imedhamiria kidhati kabisa kuwasaidia vijana wa Taifa letu kwa kuwakopesha fedha pasipo masharti magumu kama ambavyo wanayapata kupitia taasisi za kifedha. Tunao Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao mpaka hivi sasa umeshakopesha zaidi ya shilingi bilioni 4.5 katika vikundi 237 vya vijana nchi nzima. Kwa hiyo, ni fursa ambayo vijana wanayo kupitia mfuko huu ambapo wanaweza kukopa bila masharti mengi ambayo yapo katika taasisi nyingine za kifedha. Kwa hiyo, nitoe rai kwa vijana wote nchi nzima ambao wanapenda kufanya shughuli za uzalishaji mali kuutumia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa ajili ya uwezeshaji.
MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza nimshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Sasa naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, ni ukweli usiopingika kuwa bodaboda zimetoa ajira nyingi sana hapa nchini. Je, Serikali haioni sasa kuwa kuna haja kubwa ya kuwawezesha vijana hawa mikopo kwa wakati kuliko ilivyokuwa sasa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa vijana wengi wamejiunga na vikundi na hawajawahi kupata mikopo, je, Mheshimiwa Naibu Waziri, yupo tayari kuongozana na mimi kwenda kuona vikundi vile vya vijana na kuwapatia mikopo ambayo hawajawahi kuiona wala kuisikia, hasa kwa vijana wa Wilaya ya Lushoto?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shaabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nikianza na swali la kwanza la uwezeshaji kwa wakati kwa vikundi hivi vya bodaboda. Kama nilivyojibu katika jibu la msingi ni kwamba Serikali inachokifanya hivi sasa ni kushirikiana na Mamlaka za Halmashauri, Manispaa, Wilaya na Majiji ili kuona namna bora ya kusaidia uundwaji wa vikundi hivi kwa sababu ni ngumu sana kumwezesha bodaboda mmoja mmoja pasipo kukaa katika vikundi. Ndiyo maana sasa hivi kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani tumeendelea kufanya maandalizi kuhakikisha kwamba vyama hivi vya bodaboda katika mikoa na katika ngazi ya Taifa vinasajiliwa ili tupate namna bora ya kuweza kuwahudumia.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mikopo linategemea utayari wa wahusika kwa maana ya kuunda vikundi na kuunda katiba ili wawe tayari kwa ajili ya kukopeshwa. Nitoe rai kwa vikundi vyote vya bodaboda nchini ambavyo viko rasmi watumie fursa ya mikopo inayotolewa na Serikali na taasisi mbalimbali za fedha, hasa ukiwemo Mfuko wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi ambao umelenga katika kuwapatia maendeleo vijana.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, ni kuhusu vijana wa Kilindi. Nitoe tu rai kwanza kwa Waheshimiwa Wabunge wote, wale ambao wana vikundi vya vijana na wangependa kunufaika na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, sharti moja kubwa ambalo lipo ni uanzishwaji wa SACCOS ya vijana katika halmashauri husika. Hivyo, nipo tayari kwenda Kilindi pamoja na Mheshimiwa Omari Shekilindi kwenda kuangalia vikundi vya vijana. Vilevile kama watakuwa wamekidhi mahitaji ya uwezeshaji wa Mfuko wa Vijana basi tupo tayari kuwawezesha vijana wa Kilindi ili nao waweze kunufaika na fursa zilizopo katika nchi yao.
MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Kwa kuwa katika majibu yake Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kwamba SUMATRA imefanya maboresho na inatoa leseni kwa waendesha bodaboda, nataka kujua ni kwa nini kumekuwa na restriction kwa bodaboda kuingiza bodaboda zao katikati ya Jiji la Dar es Salaam, lakini vilevile ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hairuhusiwi? Naomba majibu ya Serikali.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Susan Lyimo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli katika Mkoa wa Dar es Salaam uongozi wa mkoa uliweka utaratibu wa namna vyombo hivi vya usafiri vitakavyoingia katikati ya mji kutokana na changamoto ambazo zilijitokeza awali likiwemo suala la msongamano pamoja na usalama. Tayari kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wameanza kuratibu zoezi hili katika umakini mkubwa ili kuona namna bora ambavyo wafanyabiashara hawa pia watafanya biashara zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo katika maeneo mengine zipo sababu za kimsingi za kwa nini yametokea masuala hayo lakini kubwa limekuwa ni suala la kiusalama. Ndiyo maana Serikali hivi sasa imeanza kuyatambua maeneo rasmi ya maegesho na kuwapatia vitambulisho ili likitokea jambo lolote la kiusalama tuweze kujua ni wapi limetokea na tuweze ku-trace ili kuondokana na dhana hii kwamba boaboda ni wahalifu.
MHE. PASCHAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa mtumishi anapokuwa anaajiriwa, mara ya kwanza na kwenye salary slip yake inaonesha muda atakaostaafu, hivyo inakuwa siyo suala ambalo ni la ghafla, lakini Serikali imekuwa ikichelewa sana kuwalipa watumishi hawa: Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka inapokuwa wamesababisha ucheleweshwaji wa mafao kwa watumishi wa Umma inataikiwa walipe kwa riba?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika Halmashauri ya Mbozi kuna watumishi 35 wamestaafu toka Septemba, 2018, hadi sasa hawajalipwa fedha zao na wanaidai Serikali na wanaishi maisha magumu sana: Je, ni lini sasa Serikali itaacha kuwatesa watumishi hawa wanaoishi maisha ya taabu sana kwa sababu ya ucheleweshaji wa fedha zao?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa
Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza Mheshimiwa Haonga amezungumza kuhusu ucheleweshwaji wa ulipaji wa mafao. Kwa mujibu wa sheria ambayo tumeipitisha hapa ndani Bungeni hivi sasa, inautaka mfuko kulipa mafao ya mstaafu ndani ya siku 60.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zilikuwepo changamoto nyingi hapo awali, nyingi sio kwambwa zinasababishwa na mfuko husika lakini pia wale wastaafu katika namna moja ama nyingine katika uandaaji wa nyaraka na kufuatilia taarifa zao imekuwa pia ikileta changamoto. Baada ya kuunganisha mifuko hii na kwa kutumia sheria mpya, hivi sasa PSSF wameweka utaratibu na motto wao ni kwamba wanalipa mafao tangu jana.

Mheshimimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba hivi sasa zoezi la ulipaji wa mafao kwa wastaafu linafanyika kwa kiwango kikubwa sana na kwa idadi ambayo nimesema tayari imeshalipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kuhusu watumishi katika Jimbo lake la Mbozi, kwa sababu hii inakwenda case by case, nisilisemee kwa ujumla, lakini nichukue tu fursa hii kumwambia Mheshimiwa Haonga kwamba ofisi yetu iko wazi, kama kuna madai ya watumishi ambao mpaka hivi sasa bado hawajalipwa mafao yao, basi anaweza kuyasilisha ili sisi Ofisi ya Waziri Mkuu tuweze kufuatilia mkoa husika tujue changamoto ni nini na baada ya hapo tuweze kutatua changamoto yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhamira ya Serikali kulipa mafao yao kwa wakati kabisa ili kuwafanya watumishi hawa waishi katika maisha ya amani.
MHE. SUZANA C. MGONUKULIMA: Mheshimiwa Spika, kutokana na majibu ya Mheshimiwa Waziri nitakuwa na maswali ya nyongeza mawili. Swali la kwanza, kutokana na maelekezo ya kuwa mtu mwenye ulemavu wa macho atamwomba Msimamizi wa Uchaguzi karatasi ya nukta nundu. Je, Serikali imetoa elimu kiwango gani kwa watu wasioona ili wajue wakifika kwenye kituo hicho wamuone huyo mtu atakayetoa karatasi?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ni miaka 58 ya uhuru wa nchi yetu, ni mwaka 2015 kama Mheshimiwa Naibu Waziri alivyokiri Serikali iliweza kutoa makaratasi ya nukta nundu kwa watu wenye ulemavu wa macho napo kwa kumchagua Rais tu. Je, Serikali haioni haiwatendei haki watu wenye ulemavu wa macho kutokumchagua Mwenyekiti, Diwani na Mbunge hatimaye kupata set ya Serikali ambayo anaitarajia imuongoze?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI,VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Suzana Mgonukulima, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, la kwanza la kuhusu elimu kwa watu wenye ulemavu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu kwa pamoja, tutafanya kazi ya kutoa elimu kwa makundi mbalimbali likiwemo kundi hili la watu wenye ulemavu ili waweze kutimiza haki yao ya Kikatiba ya kupiga kura. Hivyo nichukue fursa hii kuwaondoa hofu watu wote wenye ulemavu wa macho, kwamba wakati wa uchaguzi wa mwaka 2020 watapata fursa ya kupiga kura kwa kupata elimu kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na shirikisho ambao tunafanya nao kazi kwa pamoja.

Mheshimiwa Spika, suala la pili, kuhusu haki za watu wenye ulemavu kuwapigia kura wagombea wengine zaidi ya mgombea wa urais. Katika majibu yangu ya msingi nimeeleza kwamba mwaka 2015 ilikuwa ni fursa hiyo tu ya kuweza kumchagua mgombea wa urais, lakini kwa mwaka 2020 nataka nilihakikishie Bunge lako kwamba tunaweka utaratibu mzuri ili pia watu wenye ulemavu wawe na haki ya kuchagua viongozi wote kwa ngazi zote kama majibu yangu ya msingi yalivyosema.
MHE. YUSSUF HAJI KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kumwuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ongezeko la Majimbo yaliyoongezwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar mwingiliano wake unaleta usumbufu na kupunguza kasi ya maendeleo. Nataka kujua: Je, Tume ya Taifa iko tayari kuongeza Majimbo manne ili yaende sambasamba ili tufanye kazi vizuri?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili ZEC ni Wakala wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi; NEC kwa Zanzibar kwa Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Wabunge, lakini wanatumia daftari moja, kura inapigwa siku moja katika chumba kimoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Uchaguzi wa 2015 ZEC walifuta matokeo ya Uchaguzi wakati ambapo Wawakilishi na Madiwani walishatangazwa katika Majimbo yao na wamepewa hati zao za ushindi, katika mazingira kama hayo, nataka kujua: Je, NEC wametumia sheria gani ya kukubali uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Wabunge kutoka Zanzibar?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa
Mwenyekiti, nikianza na swali la kwanza kuhusu Majimbo manne ya Uwakilishi, kama katika majibu yangu ya msingi yalivyosema, suala hili la ugawaji wa Majimbo yanafanyika kwa mujibu Ibara ya 75(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na katika maneno yaliyotumika ni baada ya kufanyika uchunguzi na kugawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa mujibu wa Katiba hii, ni kwamba pindi pale matakwa ya Katiba hii na hasa katika Ibara ya 98(1)(b) ambayo inasomwa pamoja na Orodha ya Pili ya Nyongeza item Na. 8 ya kwenye Katiba ambayo inahitaji ongezeko la Wabunge wa Zanzibar, lazima pia ipitishwe na theluthi mbili ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na wenzetu kutoka Zanzibar. Kwa hiyo, kwa mujibu wa Katiba, jambo hilo linawezekana baada ya taratibu hizo kufuatwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kuhusiana na matokeo ya uchaguzi; kwa mujibu wa Katiba yetu inazungumza vyema kabisa kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina jukumu la kusimamia Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge kwa upande wa Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, chaguzi nyingine zote zinakuwa chini ya ZEC ambao pia kwa mujibu wa Katiba nao wana majukumu ya kusimamia uchaguzi katika ngazi hiyo. Kwa hiyo, jambo ambalo limetokea ambalo Mheshimiwa Mbunge amelisema, maana yake ni kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitumia mandates yake ya Katiba ambayo inampa mamlaka ya kusimamia uchaguzi huo.
MHE. MAFTAHA A. NACHUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kuna Wilaya ambazo zina Majimbo mawili na Wilaya hizi ziligawanywa Majimbo kwa sababu ya ukubwa wa zile Wilaya na idadi kubwa ya watu, lakini hivi sasa kuna tetesi ambazo zinatembea chini kwa chini huko Serikalini kwamba yale Majimbo ambayo yaligawanywa kutokana na ukubwa lakini pia na wingi wa watu yanataka kurudishwa kuwa Jimbo moja moja.

Je, kama hilo ni kweli, hatuoni kwamba Serikali ita-hinder utendaji wa Majimbo hayo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa
Mwenyekiti, kama Mbunge mwenyewe alivyoli-phrase swali lake kwamba ni tetesi, naomba nami kwa upande wa Serikali tusijibu tetesi, ikiwa rasmi itasemwa kama ni rasmi.
MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB: Mheshimiwa Spika, nashukuru, kwa kuwa watumishi wengi hasa wanaoanza kazi wamekuwa wakiunganishwa kwenye mikataba ya wafanyakazi bila ya ridhaa yao.

Je, Serikali haioni haja sasa ya kutoa mwongozo kwa maafisa utumishi juu ya kulinda haki za watumishi hao?

Swali la pili, Serikali ina mkakati gani wa kujiondoa kuwa mawakala wa makato ya wafanyakazi?

SPIKA: Swali la pili liweke vizuri.

MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB: Mheshimiwa Spika, Je, Serikali ina mkakati gani wa kujiondoa kuwa mawakala wa vyama vya wafanyakazi?

SPIKA: Kivipi yaani, ili ujibiwe swali lako.

MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB: Mheshimiwa Spika, kwenye majibu yake ya msingi, amesema vyama vya wafanyakazi, naomba ninukuu” watumishi wa vyama vya wafanyakazi licha ya kuwa na mamlaka nchini, wafanyakazi husika, vyama vya wafanyakazi hupitia vikao vyao , katiba kwa kufanya mabadiliko katika…

SPIKA: Ahsante sana Munira, Mheshimiwa Waziri jibu hilo swali la kwanza.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, utaratibu wa wafanyakazi kujiunga katika vyama vya wafanyakazi ni utaratibu ambao umewekwa kwa mujibu wa sheria na kuna uhuru wa wafanyakazi kujiunga ambapo chama husika kwa kuzungumza na mwajiri, hufanya mikutano na kutoa elimu mbalimbali na baadaye ndiko wafanyakazi wanajiunga.

Mheshimiwa Spika, hivyo, niseme tu kwamba wafanyakazi wengi wanajiunga kwa mujibu wa taratibu za kisheria ambazo zimewekwa na Katiba na katika mazingira ambayo wafanyakazi wanalazimishwa kujiunga pasipo wao kufahamu na ridhaa yao, hiyo ni kinyume na utaratibu na nitoe tu maelekezo kwamba vyama vyote vya wafanyakazi vihakikishe kwamba vinazingatia sheria za kazi ili wanachama wote wanaojiunga wawe wanajiunga katika uhuru na ridhaa yao.
MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Spika, pamoja na sheria kuelekeza umri wa kuajiriwa kazini, bado ajira nyingi zinapotangazwa hapa nchini hutoa sharti la kuwa na uzoefu wa kazi, kuanzia umri wa miaka mitano na kuendelea, na hivyo hii huwaondolea fursa vijana wengi wanaotoka vyuoni kutokupata ajira.

Mheshimiwa Spika, hivyo, naomba Serikali itoe majibu hapa kwamba ni lini itatoa tamko kwa waajiriwa kuondoa sharti la vigezo ili kuwapa fursa vijana wanaotoka vyuoni, isipokuwa tu kwa zile ajira ambazo zinahusu nafasi za juu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, kwa kutambua kwamba kumekuwepo na changamoto kubwa sana kwa vijana wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu kupata kazi kwa kikwazo cha uzoefu. Ofisi ya Waziri Mkuu katika utekelezaji wa programu ya ukuzaji ujuzi nchini, imeanzisha program maalum kabisa ambayo Mheshimiwa Waziri Mkuu alizindua miongozo yake ya mafunzo ya Uanagenzi na mafunzo ya Vitendo Kazini (Internship). Ambayo hivi sasa kwa mujibu wa utaratibu tuliouweka, tunawachukua vijana kutoka vyuo vikuu, kutokana na fani walizonazo na makubaliano ambao.

Mheshimiwa Spika, sisi Serikali tumeingia na chama cha waajiri na sekta binafsi, tunawapeleka katika kampuni husika kwenda kufanya kazi kivitendo, ambako wanakaa miezi sita mpaka miezi 12 na baadaye mwajiri katika eneo husika, anampatia cheti cha kumtambua kama ni mwanachuo ambaye amekaa kwake katika fani husika kwa miezi 12 ili baadaye ikitangazwa nafasi ya ajira ya kazi ambayo ameifanyia kwa vitendo, iwe pia ni sehemu ya yeye kumsaidia kupata ajira, kwa maana ya kutumia ule utambulisho wa kwamba tayari ameshafanya kazi katika mwajiri husika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kama Serikali na sisi tumeliona jambo hilo, na ndiyo maana tumeweka nguvu kubwa sasa hivi katika kuhakiksiha kuwa tunawajengea ujuzi vijana wetu ili waweze kuwa na sifa za kuajirika na baadaye kuwasaidia kupata ajira pasipo kikwazo cha uzoefu.
MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante pamoja na majibu yaliyotolewa na Mheshimiwa Jenista na Mheshimiwa Naibu Waziri suala la Local content ni muhimu sana katika nchi yoyote ili uchumi ubakie ndani na sio utoke nje. Lakini inahitaji maandalizi kama alivyosema. Sasa hivi sasa tuna sectoral individual locally content policies. Je, Serikali iko tayari sasa kuja na sera kubwa na mabadiliko ya sheria juu ya local content na pia sheria hiyo iwemo na vifungu ambavyo vinaweza kuwawzesha wananchi kifedha ili wafaidi localy content?
MHE. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa swali la nyongeza lililoulizwa na Mheshimiwa Ally Saleh na Mheshimiwa Ally Saleh anafahamu kwenye Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria tumekuwa tukitoa taarifa hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeshaanza hiyo kazi nzuri baadhi ya sheria ambazo zimekwisha kutungwa kwa mfano Sheria ya Mafuta na Gesi, hizo zote zimeshawekewa misingi ya kisera ya local content na imeshaanza kufanya kazi kwenye kanuni na sheria hizo. Lakini naomba nimhakikishie ili kufanya maandalizi hayo muhimu Ofisi ya Waziri Mkuu imeshatoa mwongozo wa local content katika miradi yote ya kimkakati ambayo inaendelea kwa sasa ndani ya Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo hii miradi yote ujenzi wa reli na miradi mingine yote mikubwa ya kimkakati sasa hivi mwongozo wa local content umekuwa ukitumika na sisi kama Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi tunasimamia kwa karibu sana kuhakikisha wazawa wanafaidika na miradi hii mikubwa ya kimkakati ndani ya Taifa letu.
MHE. HASSAN E. MASALA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini pamoja na majibu hayo, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri anakiri kabisa kwamba jengo lile halihitaji tu kufanyiwa marekebisho isipokuwa kujengwa; na kuwa kuwa pia tathmini imeshafanyika toka mwaka 2017/2018, kuna sababu gani sasa za kutenga fedha au kulipeleka jengo hili kwenye mpango wa kujengwa 2020/2021 badala ya mwaka 2019/ 2020?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, naomba kujua nini mpango wa Wizara ya Katiba na Sheria katika kuongeza idadi ya watumishi katika Mahakama zetu hasa Mahakama za Mwanzo? Nachingwea tuna kituo pale kinaitwa Ndomoni, kwa muda mrefu sasa kimefungwa na wananchi hawapati huduma pale. Hivyo, wanalazimika kutembea umbali mrefu kwenda Nachingwea Mjini kufuata huduma ya Mahakama.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA): Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mpango wa Mahakama wa Miaka Mitano wa Kuboresha Huduma za Mahakama hapa Nchini, imeweka pia vipaumbele vya ujenzi. Baada ya taratibu zote hizo kukamilika, limetengenezwa jedwali ambalo ndiyo linaipelekea Mahakama hii kuanza kujenga hizi Mahakama.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa pande wa Nachingwea, kwa sababu tathmini ilikuwa inaendelea kufanyika katika jedwali letu, Nachingwea wenyewe ujenzi utaanza katika mwaka wa fedha 2020/2021 hasa kutokana na kwamba ilikuwa lazima taarifa hizo zikamilike na tayari kuna baadhi ya Mahakama ilikuwa imeshaingia katika mpango wa ujenzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, ni kweli tunatambua changamoto hiyo lakini kwa sasa kwa sababu Wizara tumeingia makubaliano na Baraza la Ujenzi wa Taifa katika ujenzi wa Mahakama kupitia teknolojia mpya na bei nafuu ya Moladi naamini kabisa kwamba pindi fedha itakapopatikana tutaanza ujenzi wa Mahakama ya Nachingwea ili kuwaondolea usumbufu wananchi wa Wilaya ya Nachingwea.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika swali lake la pili la kuhusu watumishi, ni kweli tuna changamoto katika baadhi ya maeneo, lakini nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inaendelea kulifanyia kazi kwa maana ya kuajiri watumishi wengine ambapo tunaenda kupata kibali toka utumishi. Kwa hiyo, pindi ajira hizi zitakapotangazwa na kupatikana, pia Wilaya ya Nachingwea itaangaliwa katika kutatua changamoto hii ya ukosefu wa watumishi katika eneo hilo ili wananchi wa Nachingwea waweze kupata huduma za Mahakama kwa ukaribu lakini na kwa ufanisi zaidi.
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri. Nina maswali mawili madogo ya nyongeza:

Mheshimiwa Spika, tunajua Muungano wa Kikanda au wa Kimataifa kama vile SADC una faida kubwa nzuri sana kwa vijana hususan kwenye kupata ujuzi pamoja na mafunzo. Je, huu mkutano uliopita hivi karibuni nini vijana watafaidika na SADC?

Mheshimiwa Spika, swali la pili kuna maazimio gani ambayo tayari yaliyopo aidha kwenye EU umoja mwingine wa Kimataifa ambayo yatasaidia vijana zaidi kwenye suala lile la mikopo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Spika, kwanza kwenye Mkutano wa SADC uliomalizika hivi karibuni tuchukue fursa hii kuwashukuru sana Wakuu wote wa nchi pamoja na Mwenyekiti wetu wa SADC kwa azma na kauli yao thabiti ya kuhakikisha kwamba vijana wanashiriki katiak sekta ya uchumi wa viwanda.

Mheshimiwa Spika, katika Mkutano uliomalizika agenda kubwa ilikuwa ni kuwashirikisha vijana katika uchumi wa viwanda na kwa Tanzania vijana walipata fursa ya kutembelea na kuona fursa mbalimbali na kujifunza kupitia Mataifa mengine na tunaamini kabisa kupitia Mkutano huu liko jambo ambalo limeongezeka katika fikra za vijana hasa katika kwenda kuwekeza kwenye uchumi wa viwanda. Kwa hiyo ni Mkutano ambao ulikuwa na tija na vijana wamehamasika na tunaamini kutokea hapo vijana wengi zaidi watashiriki katika uchumi wa viwanda, moja kwa moja au isivyo moja kwa moja.

Mhehsimiwa Spika, swali lake la pili alitaka kujua Maazimio ya Kikanda kupitia AU. Katika Azimio la 601 la mwaka 2017 katika moja ya nguzo iliyosemwa ni uwezeshwaji wa vijana na Serikali ya Tanzania tunayafanya hayo kupitia Mifuko mbalimbali ya Uwezeshaji wa Vijana na kuwajengea vijana uwezo hasa katika kuwajengea ujuzi ili waweze kujiajiri na kuajiri vijana wengine.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo Serikali ya Awamu ya Tano inayafanya hayo kuzingatia maamuzi yaliyofikiwa na Wakuu wa nchi katika Umoja wa Afrika.
MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naomba uniruhuru niipongeze sana Serikali kwa hatua ambayo sasa imefikia kwa sababu kilio kikubwa kwa wakulima wapamba ni kwamba pamba hiyo inatakiwa iongezewe thamani.

Sasa swali langu nimesema kwamba upembuzi tayari umeshakamilisha na viongozi wakuu wa mifuko hii wako Mwanza nasikia, sasa ni lini sasa baada ya hiyo Februari kwa sababu majibu haya yanaweza kusema kwamba ni Februari kumbe ni mwezi mwingine, ni lini sasa hasa ujenzi wa vinu hivi vitatu kwa maana ya hii Nyambiti Ginnery, Ngasamo Ginnery pamoja Kasamwa Ginnery.

Lini vitaanza kujengwa ili zao la pamba lipate thamani zaidi? Nakushuru.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTHONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, niruhusu kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo anawapigania wakulima wa pamba wa Kanda ya Ziwa na amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba zao hili linaongezwa thamani. Kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema leo wakurugenzi wote wa uwekezaji wa mifuko hii wako Mwanza na kesho kuna kikao cha Wakurugenzi Wakuu ambao kupitia kikao hicho tutapata way forward ya lini taratibu hizi zitaanza kwa sababu kesho wanakutaka kwa ajili ya mambo ya kitaalam, hivyo nimuombe Mheshimiwa Ndasa awe mvumilivu tusubiri taarifa ya Wakurugenzi Wakuu kesho ili tujue way forward ni nini. Nashukuru.
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, nasikitika sana swali langu halijajibiwa kama nilivyokuwa nimeuliza. Katika majibu ya Naibu Waziri anasema kwamba wao wametenga zaidi ya ekari 217 ambazo ziko katika mikoa mbalimbali lakini hajaainisha ni mikoa ipi na wilaya zipi makambi hayo yapo ili tuweze kujua kwa sababu sisi ndiyo wawakilishi wa hao vijana na tunawaona jinsi ambavyo wanapata adha huko tuliko. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wamesema kwamba kuna programu mbalimbali na mazingira ambayo wamewawezesha, ni program zipi na mazingira yepi ambayo wameyaweka ili hawa vijana tukawaona wanafanya kazi. Amekiri kabisa hakuna hata sensa waliokwisha kuifanya ya kufahamu ni vijana wangapi ambao wanafanya kazi hizo mchana na usiku kwa maana ya kwamba hakuna wanachokijua kuhusu vijana wetu na tunawaona wakiwa wako na hali ngumu na hawana ajira na ajira hazijapatikana. Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Grace Victor Tendega (Viti Maalum), kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo lake la kwanza amehoji kwa nini hatujaainisha maeneo yote ya ekari 217,882 ambayo yametengwa. Katika utaratibu wa uwasilishaji wa majibu nimetoa majibu ya jumla kuonyesha ekeri zilizotengwa lakini bado hii haizuii Mheshimiwa Mbunge kupata taarifa ya maeneo ambayo yametengwa. Kupitia TAMISEMI tutawasilisha orodha ya maeneo yote haya ambayo yametengwa ili Waheshimiwa Wabunge pia wafahamu ardhi ambayo imetengwa kwa ajili ya shughuli za vijana kwa ajili ya kilimo, viwanda na ufugaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili anahoji kuhusu program ambazo tunaziendesha. Ofisi ya Waziri Mkuu kwa 2016/2021 tunaendesha Programu Maalum ya Ukuzaji Ujuzi Vijana yenye lengo la kuwafikia vijana milioni 4.4 kwa mwaka 2021 ili vijana hawa wapate ujuzi waweze kujiajiri na kuajiri vijana wengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ameomba azisikie program, kwa ruhusa yako naomba nimtajie chache tu ili ibaki kwenye kumbukumbu sahihi za Bunge hili. Program ya kwanza ambayo tunaifanya inaitwa RPL (Recognition of Prior Learning), ni mfumo wa Urasimishaji wa Ujuzi kwa vijana wenye ujuzi ambao hawajapitia mfumo rasmi wa mafunzo ya ufundi. Ukienda leo mtaani kuna vijana wanajua kupaka rangi au kutengeneza magari lakini hawajawahi kusoma VETA wala Don Bosco. Serikali inachokifanya inarasimisha ujuzi wao na kuwapatia vyeti. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna Program ya Greenhouse ambapo kila wilaya tunawafikia vijana 100 katika awamu ya kwanza. Mpaka sasa nchi nzima tumeshafikia vijana 18,800. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna Program ya Mafunzo ya Ufundi kupitia vyuo vya Don Bosco na vyuo shirikishi. Takribani vijana 8,800 katika awamu ya kwanza wamenufaika na tunaendelea na awamu ya pili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna program ambayo inaendeshwa DIT Mwanza ya Viatu na Bidhaa za Ngozi ambako vijana wanapata mafunzo na kuweza kunufaika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, program ziko nyingi sana kwa sababu ya muda, naomba niishie hapa lakini Mheshimiwa Mbunge atapata taarifa zaidi.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, nampongeza sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri tena ya kina kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kuongeza jambo dogo tu, Mheshimiwa Tendega amelalamika hapa kwamba hakuna chochote kinachofanyika na haelewi chochote. Ili kumsaidia zaidi Mheshimiwa Mbunge akumbuke kwamba kila tunapopitisha bajeti za Serikali kila Wizara inaeleza program zote zitakazofanyiwa kazi kwenye bajeti ya Serikali.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuliweka suala hili, vizuri namwomba Mheshimiwa Tendega arejee kwenye bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, hizo program zote, utekelezaji wake kwenye ripoti ya Kamati upo na mambo yote yaliyofanyika yako wazi na yanaeleweka. Kwa hiyo, hatujaficha na siyo kwamba hakuna kinachojulikana. (Makofi)
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya kisiasa ya Mheshimiwa Waziri, sasa hivi watu wanaomaliza elimu ya shule ya msingi, sekondari, diploma na digrii ni takribani 900,000. Wengi wao wanaingia kutafuta soko la ajira wakati huo huo Serikali imekuwa ikitoa elimu ambayo inapishana na soko lililoko. Sasa mipango unayosema, ukilinganisha na idadi ya vijana wengi ambao hawana kazi na idadi ya vijana ambao Serikali inasema inawa-train na kuwapa hizo fursa ni chache sana ukilinganisha na uhitaji wa watu. Sasa kuna mkakati gani wa makusudi au mpango maalum wa Serikali wa kutoa elimu ambayo itakwenda kukutana na soko wanapokwenda kukutana huko mtaani ukiachilia mbali hayo waliyoyasema?
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza ya Mheshimiwa Mchungaji Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ningemwomba Mheshimiwa Mbunge aende ku-revisit tena takwimu zake alizonazo kumekuwa na upotoshaji juu ya watu wanaoingia katika soko la ajira kila mwaka, anasema wahitimu lakini kwa mujibu wa takwimu kutoka NBS ya Juni, 2019 inasema watu wenye uwezo wa kufanya kazi kuanzia miaka 15 na kuendelea, the working age population. Kwa hiyo, siyo hicho ambacho amekisema Mheshimiwa Mbunge, kwa hiyo, namshauri aende ku-revist takwimu zake.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kulijibu swali lake, ni kweli hauwezi ukawa una suluhisho moja kwa matatizo mbalimbali ya vijana. Tulichokifanya kama Serikali, katika vijana ambao wengi ni wahitimu wa darasa la saba, kidato cha nne ambao kwa kiasi kikubwa sana tunaamini kwamba wakipata ujuzi wanaweza kujiajiri na kuajiri vijana wengine, Serikali inatekeleza Programu Maalum ya Mafunzo ya Ufundi Stadi ambako tumeanza mwaka juzi kushirikiana na Don Bosco. Mheshimiwa Msigwa katika Jimbo lako la Iringa Mjini wako vijana ambao wamenufaika na program hii kupitia ukuzaji wa ujuzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunachokifanya ni kwamba Serikali sasa inaingia kuwafadhili vijana kupata mafunzo ya ufundi stadi kama sehemu ya kuwafanya kuweza kujiajiri. Tunafanya program hiyo Don Bosco Oyster, Don Bosco Mafinga, Don Bosco Iringa, Don Bosco Shinyanga na Don Bosco Dodoma na maeneo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa vijana ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu, Serikali ilichokifanya ni kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu amezindua program maalum ya mafunzo ya internship na uanagenzi ambako hivi sasa kwenye kuondoa changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kigezo cha uzoefu, hivi sasa Serikali inawachukua vijana wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu, tunakwenda kuwa- place katika makampuni na viwanda mbalimbali wanajifunza kwa miezi sita mpaka miezi kumi na mbili. Akitoka hapo anapewa certificate of recognition ambapo akienda kuomba kazi hiyo itakuwa ni kigezo kwamba kijana huyu tayari ameshapata uzoefu na imesaidia kwa kiwango kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ziko program nyingi sana na nitapata nafasi kuwaelezea Wabunge vizuri zaidi ili waweze kuzielewa program za Ofisi ya Waziri.
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na ahsante kwa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri pamoja na kazi nzuri ya urasimishaji wa ajira lipo kundi la madereza na makondakta wa daladala wamekuwa kwenye ajira kwa muda mrefu sana lakini ajira zao zimekuwa hazithaminiwi kwa maana ya kupewa thamani ya mikataba na wao kuwafanya waweze kuwa na akiba kwenye mifuko yetu ya hifadhi pale wanapokuwa wameacha kazi hii. Ni lini Serikali itahakikisha ajira hii na yenyewe inakuwa rasmi na kutambuliwa kwa mujibu wa sheria?
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza ya Mheshimiwa Stanslau Mabula, Mbunge wa Nyamagana, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo anawapigania sana waendesha bodaboda na daladala katika eneo lake la Nyamagana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake anasema Serikali tuna mkakati gani wa kuhakikisha kwamba madereva wa daladala na bodaboda wanakuwa na mikataba na kufanya kazi zenye staha. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Jenista Mhagama amekwishatekeleza agizo la Mheshimiwa Waziri Mkuu la kuwaita na tumekaa nao kwa pamoja wamiliki wa vyombo mbalimbali vya moto pamoja na Chama cha Madereva katika kutengeneza mpango wa pamoja wa kurasimisha ajira za madereva. Mpaka hivi sasa tunaendelea na ushirikiano mzuri pamoja na wamiliki wa vyombo hivyo na tumepeana muda ambapo baadaye tutafanya ukaguzi kujiridhisha kwamba makubaliano yetu yamefikiwa ili tuhakikishe kwamba Tanzania nzima madereva wote wa magari makubwa, mabasi, magari madogo wanapata mikataba ya ajira kama sheria inavyoelekeza katika kifungu cha 14 cha Sheria Na.6 ya mwaka 2004.
MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza, naomba nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri lakini pamoja na pongezi hizi naomba niulize maswali madogo mawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, ni mkakati gani ambao umewekwa na Serikali wa kuwawezesha vijana kupata mafunzo ya ujasiriamali ili waweze kujiajiri?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, tumekuwa tukishuhudia vijana wengi wanajishughulisha na shughuli za kilimo. Je, Serikali haioni kwamba iko haja sasa ya kuona wale vijana ambao wanajishughulisha na shughuli za kilimo waweze kupata mafunzo na kwa kuwa tunafahamu kilimo ni uti wa mgongo ili waweze kufanya kazi zao kwa umakini na waweze kupata tija? Ahsate.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Sikudhani Chikambo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nichukue fursa hii kumshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo anafuatilia masuala ya vijana na akina mama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza la mkakati, ni kweli kwa kutambua kwamba ujasiriamali hivi sasa ni nguzo muhimu ya kumfanya kijana aweze kujiajiri, hivi sasa tumeshatambulisha mtaala wa ujasiriamali kuanzia ngazi ya chini mpaka elimu ya vyuo vikuu. Pia mkakati wa Serikali hivi sasa ni kuendelea kuwapitia wajasiriamali wote nchi nzima kwa kuwapa mafunzo katika kila Mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, navyozungumza hivi sasa tumeshakamilisha mikoa zaidi ya 14 katika awamu ya kwanza na tutakwenda kumalizia awamu ya pili ambapo kila mkoa tumekutana na wajasiriamali zaidi ya 500 katika kuwapa elimu na ujuzi wa namna ya kuweza kufanya biashara zao.

Kwa hiyo, Serikali inatambua umuhimu huo wa wajasiriamali na ndiyo maana katika moja ya mkakati wetu ni kuwapa elimu na kuwasaidia pia kuweza kupata mikopo ya masharti nafuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kuhusu vijana kushiriki kwenye kilimo, Ofisi ya Waziri kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo tunao mkakati maalum wa kuwahusisha vijana katika kilimo ambao tumeanza kuutekeleza. Navyozungumza hivi sasa tunayo programu ya kilimo cha kitalu nyumba ambacho kitawafikia vijana 18,800 nchi nzima ambako kila Halmashauri nchi nzima vijana 100 watafundishwa kuhusu kilimo cha kitalu nyumba na vijana 20 watapata ujuzi wa kuweza kufundishwa kutengeneza green house. Lengo letu ni kuhakikisha kwamba vijana wengi wa Kitanzania wanashiriki moja kwa moja katika uchumi wa viwanda kupitia sekta hii ya kilimo. Lengo letu ni kuwafikia vijana 47,000 katika mwaka huu wa fedha.
MHE. MARIAM D. MZUZURI: Mheshimiwa Spika, napenda kwanza kumpongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ambayo yana tija kwa vijana wa Mkoa wa Dodoma; na kwa vile yeye mwenyewe ni mtu sahihi, ni Waziri kijana, ni kijana na ni Mbunge anayetokana na Mkoa wa Dodoma, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, moja ya mazao ya biashara yaliyoonyesha kuwa na tija kwenye kilimo biashara Mkoa wa Dodoma ni pamoja na zao la zabibu, lakini mara baada ya Dodoma kutangazwa kuwa Makao Makuu ya Nchi, wageni wengi hususan kutoka katika nchi jirani za Afrika Mashariki, wameonekana kuvutiwa na uwekezaji kwenye zao la zabibu kama zao la biashara. Je, Serikali haioni umuhimu wa kutenga ardhi na pembejeo kwa vijana wa Mkoa wa Dodoma ili wawezeshiriki rasmi kwenye Sekta ya Kilimo cha Biashara kwenye zao la zabibu? (Makofi)

Swali la pili. Kwa kuwa kuna vijana tayari wamejiajiri kwenye ujasiriamali wa mazao, hususan katika zao la biashara la ufuta, lakini hivi karibuni kumetokea sintofahamu kwa Mkoa wa Dodoma hasa kwenye Wilaya ya Kondoa kuwazuia vijana hawa wasinunue ufuta kutoka kwa wakulima kwa kisingizio cha kuwa na stakabadhi ghalani, jambo ambalo halipo katika Mkoa wa Dodoma:-

Je, Serikali inatoa tamko gani kuhusu vijana hawa ambao wameamua kujiajiri?

Mheshimiwa Spika, nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY PETER MAVUNDE): Mheshimiwa Spika, naomba uniruhusu kwanza nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge Mariam Ditopile kwa namna ambavyo anawasimamia vijana wa nchi yetu ya Tanzania na hususan Vijana wa Mkoa wa Dodoma. Mwenyezi Mungu akubariki sana.

Mheshimiwa Spika, ni kweli, baada ya tangazo la Makao Makuu na pia baada ya Serikali ya Awamu ya Tano sikivu kufanya marekebisho katika ule mchuzi wa zabibu ili kuwavutia zaidi wakulima wa zabibu kuendelea kuilima zabibu, mwamko umekuwa mkubwa kwa vijana na kama Serikali mkakati wake katika eneo hili ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, la kwanza, yalitoka maelekezo mwaka 2014 kutoka kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, ya kila Halmashauri nchi nzima kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya shughuli za vijana kufanya kilimo. Kwa Mkoa wa Dodoma na hasa katika maeneo ambayo yanalima zabibu, tayari maelekezo yalishatoka na katika master plan ya Jiji la Dodoma, ambayo itakwenda kukamilika hivi karibuni, yametengwa maeneo maalumu ya kuhakikisha kwamba zao hili la zabibu halipotei.

Mheshimiwa Spika, hivyo, vijana pia watapata fursa ya kuweza kunufaika kupitia maeneo hayo ili nao waweze kulima zabibu na kujiongezea fursa ya kuendeleza mitaji yao na biashara zao.

Mheshimiwa Spika, kubwa zaidi kuliko yote ni kwamba, Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika maeneo yake ambayo wametenga kwa ajili ya shughuli za vijana, wameshapeleka wataalam kwenda SUA kukaa na wataalam wa SUA kwa ajili ya kuja na mpango mzuri endelevu wa kilimo cha zabibu ambacho kitakuwa kimefanyiwa utafiti ili vijana wengi zaidi waweze kunufaika.

Mheshimiwa Spika, siyo zabibu tu, kwa Dodoma hapa, vijana wengi hivi sasa wanafanya biashara za mazao, kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema; na hivi sasa tayari tunavyo viwanda ambavyo vimeanza kufanya kazi. Kwa mfano, Kiwanda cha Mazao Mchanganyiko ambacho kwa mwaka kitahitaji tani 12,000 za mahindi na tani 6,000 za alizeti. Kwa hiyo, tunachukua fursa hii pia kuwaalika vijana kushiriki katika kilimo hicho.

Mheshimiwa Spika, swali la pili la Mheshimiwa Mbunge, analijibu Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo ambaye ameandaliwa kwa ajili ya kulijibu swali hilo.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kwanza napenda nichukue nafasi hii kumpongeza Naibu Waziri kwa majibu mazuri ambayo ameyatoa. Ni kweli kabisa kumetokea sintofahamu katika zao la ufuta katika maeneo mengi hapa nchini na hasa katika mikoa ambayo inazalisha kwa kiwango kikubwa sana. Utaratibu ambao tumeweka kama Serikali, ni kwamba tunatumia ule utaratibu wa mwaka 2018 wa kuhakikisha, mtu yeyote anayetaka kununua ufuta, anaruhusiwa kwenda kununua maadam afuate taratibu zinazostahili; na wote wanaruhusiwa na hatujaweka masharti yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hivi kumetokea katika baadhi ya mikoa, wanasema kwamba tunatumia mfumo wa soko la bidhaa yaani TMX na kuna maeneo mengine wanalazimisha kwamba wanaoruhusiwa ni hawa, hatujaweka huo utaratibu. Kila mtu anaruhusiwa kwenda kushiriki na huo utaratibu wa soko la bidhaa utakapokamilika, tutatoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili kuanza kutumia huo mfumo. Kwa mwaka huu kwa sababu mfumo hatujaukamilisha sawasawa, basi mfumo wa zamani unaendelea kutumika.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nimshukuru sana Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri. Pamoja na majibu hayo nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, pamoja na Serikali kuanzisha programu mbalimbali lakini bado kuna tatizo la masoko. Je, Serikali ina mkakati gani sasa kuwasaidia vijana hawa katika upatikanaji wa masoko?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, vijana 32,563 waliopata mafunzo idadi yao ni ndogo sana ukilinganisha na vijana ambao wako maeneo mbalimbali vijijini.

Je, Serikali ina mkakati gani sasa wa kuongeza idadi ya vijana wengi zaidi, walau waweze kufikia hata asilimia 50 ili kusudi waweze kuacha kukimbilia mijini? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA: Mheshimiwa Spika, nikianza na la kwanza kuhusu masoko; moja kati ya mpango ambao tunautekeleza ni mpango wa kuwashirikisha vijana kwenye kilimo ambao tunaufanya kwa pamoja na Wizara ya Kilimo.

Mheshimiwa Spika, kwa vijana wanaofanya shughuli za kilimo hivi sasa kupitia maelekezo ambayo yalitolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa Mheshimiwa Waziri wa Nchi ambayo na mimi pia nimeshushiwa kwa ajili ya kuyatekeleza, hivi sasa tumeanzisha programu maalum ya kuanza kutafuta masoko ya bidhaa hasa bidhaa za kilimo za vijana wetu ambao wanafanya shughuli hizo kupitia viwanda vya ndani.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa tunatarajia kwenda kutengeneza shamba kubwa la mfano katika eneo la Mboga, Wilaya ya Bagamoyo ambapo kipo Kiwanda cha Sayona ambacho kimekubali kununua matunda kutoka kwa vikundi vya vijana ambao sisi tutawatayarishia mashamba, lakini vilevile pamoja na kuwatafutia mbegu pamoja na Wataalam wa SUA wameshafika katika eneo hilo. Kwa hiyo, katika upande wa kilimo tumeanza kuzungumza na viwanda na makampuni makubwa, ili pia iwe sehemu ya soko kwa bidhaa za vijana wetu.

Mheshimiwa Spika, lakini pia kwa wale vijana ambao ni mafundi, wameunda makampuni, wanafanya shughuli mbalimbali za utoaji huduma, hivi sasa yalitoka maelekezo kwamba, kila Halmashauri nchi nzima itenge asilimia kadhaa ya manunuzi yake ya ndani kwa ajili ya vikundi hivi vya vijana. Na ninavyozungumza hivi vijana wengi wanaofanya shughuli za ufundi seremala ambao wanatengeneza madawati walipata kazi Halmashauri nyingi nchini kusambaza madawati, ikiwa pia ni sehemu ya soko, lakini pia kama Serikali tunaweka mpango mkakati mzuri kuhakikisha kwamba tunaweka mfumo endelevu wa vijana hawa kupata masoko ya uhakika. Hayo ni maeneo mawili tu ambayo nimeyatolea mfano.

Mheshimiwa Spika, swali la pili ilikuwa ni kuhusu idadi ndogo ya vijana. Ofisi ya Waziri Mkuu inatekeleza Programu ya Ukuzaji Ujuzi nchini ambayo imeanza mwaka 2016 mpaka mwaka 2021 yenye lengo la kuwafikia takribani vijana milioni nne ifikapo mwaka 2021.

Mheshimiwa Spika, nilichokisema hapa ni component moja tu katika utekelezaji wa mradi huu, lakini tunawafikia vijana wengi na lengo letu ni kuwafikia vijana zaidi ya milioni nne ifikapo mwaka 2021.

Kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ni kwamba tunafahamu vijana ni kundi kubwa, tunaendelea kuwafikia kwa kupitia programu mbalimbai, ili wote waweze kunufaika na urasimishaji ujuzi huo.
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika, ahsante nashukuru sana kwa nafasi.

Mheshimiwa Spika, napenda kumuuliza Mheshimiwa Waziri kwa kuwa, kule Lushoto sisi tayari tumeshajiandaa na tuko tayari tunavuna matunda mengi sana, lakini masoko yake kwa kweli sio mazuri kiasi kwamba yanashawishi vijana kuachana na kilimo cha matunda na kwenda mjini.

Je, Serikali ina mkakati gani kusaidia kutupatia masoko ya uhakika wakulima wa matunda kule Lushoto?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA NA VIJANA: Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa namba ambavyo anawapigania vijana katika eneo lake na niseme tu kwamba katika majibu yangu ya awali niliyoyasema eneo mojawapo ambalo pia tutalifikia ni eneo la Lushoto lenye matunda mengi sana na tayari tumeshaanza mazungumzo na mwekezaji mkubwa kabisa Ndugu Bakhresa kwa ajili pia ya kuona namna ambavyo tunaweza tukasaidiana naye tukapata mahitaji ya matunda ambayo anayahitaji kule kiwandani, ili vijana wa Lushoto kupitia utaratibu ambao tumeuweka tuwawezeshe waweze kulima na baadae soko liwe ni kupitia Ndugu Bakhresa na kampuni nyingine za vinywaji hapa nchini.
MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu haya mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri na nichukue nafasi hii kuwapa pongezi wawekezaji wa ndani, wazawa kwa kujenga viwanda hivi ambavyo vimepunguza tatizo la soko. Lakini pamoja na uwepo wa viwadna hivi viwili tatizo la soko bado ni kubwa sana na msimu uliopita mananasi yaliozea shambani na tatizo linaongezeka kwa utaratibu uliopo sasa hivi wa ununuzi wa mananasi haya ambao utaratibu huu unahushisha madalali kusababisha usumbufu mkubwa na wakati mwingine kupoteza mapato kwa wakulima.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, je, Serikali iko tayari kuwahamasisha wawekezaji hawa ili waweke utaratibu rafiki utakaowawezesha wakulima kuuza zao lao la nanasi kwa urahisi zaidi na kwa kuwapatia kipato? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa vile zao hili ni zao la kibiashara na linafanya vizuri, linaipatia kipato Serikali pamoja na wakulima, sasa swali langu, je, Serikali iko tayari..., samahani pamoja na kufanya hivyo vizuri mkulima inabidi apambane yeye mwenyewe kwa hatua zote kuanzia kuandaa shamba, kupanda, kupalilia mpaka kuvuna na kadhalika na kubeba gharama zote.

Je, kwa kutambua umuhimu wa zao hili Serikali iko tayari sasa kuwaunga mkono wakulima hawa kwa kuwapa ruzuku katika pembejeo kama vile mbolea na pembeje zingine? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA):
Mheshimiwa Naibu Spika,ni dhamira ya Serikali kuhakikisha wakulima wa mananasi wa Bagamoyo wananufaika na kupata tija kupitia kilimo cha mananasi. Kumekuwepo na utaratibu wa katikati hapo kuingiza watu wa kati ambao mwisho wa siku wanawafanya wakulima hawa wasiweze kunufaika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama Serikali tutaendelea kuweka mipango madhubuti na miundombinu rafiki ili kumfanya mkulima huyu wa nana wa Bagamoyo apate soko la uhakika moja moja kupitia kiwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninavyozungumza hivi sasa na Mheshimiwa Mbunge ni shahidi yangu niliwahi kuzungumza naye pale Bagamoyo katika Kijiji cha Dutumi, Kata ya Dutumi tumeshazungumza tayari na muwekezaji Sayona Fruits Company Limited ambao wako tayari kushirikiana na Serikali na tumeanza kuwaandaa vijana na tayari ekari 50 imeshatengwa na tutachimba visima viwili na watu wa SUA wameshakwenda pale Dutumi, wameipima ardhi, wamejua mwekezaji anataka nini, baadae tutaanza utaratibu mzuri sasa kuhakikisha kwamba ile mbegu itakayokwenda kupandwa pale kwa matunda ambayo mwekezaji anahitaji atanunua moja kwa moja kutoka kwa wakulima Kijiji cha Dutumi na hivyo itakuwa soko kuwa la uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili amezungumza kuhusu ruzuku na kuwawezesha wakulima. Niseme tu chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu inaratibu pia mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika hatua hii ya awali ningeshauri kwanza wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo kuitumia benki yetu ya kilimo ambayo pia ina fursa ya kuwawezesha kupata mikopo ambayo itaongeza tija katika uzalishaji wao ili baadae basi wasipate shida katika uzalishaji wao. (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na mimi nipende tu kuongezea majibu mazuri ya Mheshimiwa Mavunde Naibu Waziri. Lakini kwanza nipende kusema kwamba tumemsikia Mheshimiwa Kawambwa lakini pia na Wabunge wote ambao wamekuwa wakizalisha mazao ya matunda pamoja na mboga mboga, na nipende tu kusema kwamba kwa sasa tumeandaa kongamano maalum la uwekezaji katika nyanda za juu Kusini ambao tutalifanya Mbeya Jumatatu na Jumanne. Lakini nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge Kawambwa tutafanya hivyo pia katika Mkoa wa Pwani tukitambua kwamba na wenyewe wana kilimo cha matunda na mboga mboga na tutaenda pia katika kanda zingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili tunakusudia pia kuandaa kongamano maalum la kuvutia uwekezaji katika kilimo, mifugo na uvuvi na tutashirikiana na Benki ya Kilimo pamoja na Wizara husika, kwa hiyo tuombe tu Wabunge tushirikiane endapo kuna mahitaji mahusui basi tuweze kupata ili tuweze kushirikiana katika kuvutia uwekezaji huu, nakushukuru. (Makofi)
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Spika, nashukuru, nishukuru vilevile kwa majibu ya Serikali, lakini naomba niulize swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, pamoja na jitihada kubwa za Serikali za kuwezesha vijana katika maeneo mengi, lakini bado kuna Sekta ambayo inaajiri vijana wengi sana kama vile sekta ya uvuvi na kilimo lakini hasa kwenye sekta ya uvuvi vijana wengi wameajiriwa maeneo haya lakini wanakutana na vikwazo vingi sana vinavyowafanya washindwe kufaidika na shughuli zao hizi za uvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha kwamba vijana wanaojiajiri na kuajiriwa kwenye sekta kwa mfano ya uvuvi wanaondolewa vikwazo wanatambuliwa na kuwezeshwa ili waweze kufanya shughuli hizi na kufaidika na shughuli hizi za uvuvi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Lakini, swali la pili kilimo ni sekta muhimu sana inayoweza kuwasaidia sehemu kubwa sana ya vijana, lakini bado sioni kama Serikali imefanya juhudi za kutosha za kuweza kuwatambua vijana walio na mahitaji ya kuweza kujiajiri kwenye sekta hii ya kilimo na kuwawezesha kwa kuwapa mtaji ili wafanye shughuli za Kilimo zenye ufanisi, nini mpango wa Serikali kutumia Kilimo kama sehemu kubwa inayoweza kuajiri vijana wengi kwenye nchi hii?

Mheshimiwa Spika, nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA, AJIRA: Mheshimiwa Spika, katika swali lake la kwanza Serikali inatambua ya kwamba moja kati ya sekta ambayo inachangia katika kutoa nafasi za ajira ni pamoja na sekta ya uvuvi.

Mheshimiwa Spika, mpango uliopo hivi sasa na ambao tumeanza kuutekeleza ni kuendelea kuwaweka vijana wote wanaofanya shughuli za uvuvi katika ushirika na vikundi mbalimbali ili waweze kupata fursa kukopesheka kupitia Mifuko ya Mendeleo ya Vijana lakini vilevile Mifuko ya Uwezeshaji na hivi sasa tumeshafanya kazi hiyo katika baadhi ya Mikoa ikianzia Mkoa wa Geita kwenye Wilaya ya Chato, lakini vilevile na Mkoa wa Tanga katika Wilaya ya Pangani tumeanza kufanya kazi hiyo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nimuondoe hofu tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua na tupo katika mkakati wa kuhakikisha kwamba tutaishirikisha na Benki ya TADB ili waweze kupata mikopo.

Mheshimiwa Spika, la pili, kuhusu kilimo, Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ushirikiano na Wizara ya Kilimo tunatekeleza kwa pamoja mpango wa kuwashirikisha vijana kwenye kilimo ambao una lengo la kuwafanya vijana hao kutumia fursa ya kilimo kama sehemu ya ajira.

Mheshimiwa Spika, mpaka ninapozungumza hivi sasa tayari mpango huu umeanza kutekelezwa na vijana wengi hivi sasa wameshaanza kubadili mtazamo na kukichukulia kilimo kama pia ni sehemu ya ajira tofauti na pale awali ambako kilimo ilikuwa ni last resort. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mpango huu unatekelezwa kwa pamoja na tumeanza hivi sasa katika Mpango wa Kitalu Nyumba ambao utashirikisha vijana 18,800 nchi nzima, lakini vilevile kampuni za vijana zinazofanya kilimo pia zimeanza kushiriki moja kwa moja katika kuhakikisha kwamba wanaanza kutoa msukumo na mtazamo kwa vijana wengine wengi kuingia kwenye kilimo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunatambua jambo hilo na Serikali tunaendelea kulifanyia kazi.
MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini bado kuna malalamiko makubwa sana kwa Madereva wa malori na mabasi na karibu asilimia 90 ya Madereva hao hawana mikataba ya kazi na kwa sababu Serikali inasema kwamba Mikataba yao ilitakiwa iboreshwe toka mwaka 2015 na mpaka sasa mikataba yao bado haijaboreshwa na bado hawajapewa mikataba.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuharakisha jambo hili ili wafanyakazi hao waweze kufanya kazi yao vizuri kwa sababu wakiwa na mawazo sana wanaweza wakasababisha ajali na Watanzania wengi wakapoteza maisha?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kumekuwa na tatizo kubwa sana kwa sisi ambao tunaishi mipakani na mmeona kuna migomo mingi sana inatokea pale Tunduma watu Madereva wanapaki malori kwa sababu tu ya migongano kati ya wamiliki wa mabasi na malori kwa ajili ya mikataba hiyo? Sasa Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba jambo hili linakwisha haraka kwa sababu ni muda mrefu sasa na Serikali ipo, inatoa majibu humu Bungeni lakini utekelezaji unakuwa hakuna? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Frank Mwakajoka, Mbunge wa Tunduma, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, maswali yake nitayajibu yote kwa mkupuo. Katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 na katika ahadi ambayo Mheshimiwa Rais aliitoa akiwa Kahama mwaka 2015 juu ya Mikataba ya Wafanyakazi na hasa Madereva, Serikali inakuja na mpango mkakati ufuatao, hatua ya kwanza ilikuwa ni kuwataka Wamiliki wote wa Mabasi na Malori ambao watakwenda kuomba SUMATRA leseni ya usafirishaji wahakikishe kwamba wanawasilisha na Mikataba ya Wafanyakazi kama eneo la kwanza la kuhakikisha kwamba Madereva hawa wanapata mikataba yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kutekeleza hili, Serikali tumekuja na mkakati tofauti tumeona kwamba mkakati huu ulikuwa una mianya ya utekelezaji wake hivyo, siku mbili hizi zijazo Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, watatoa tamko na maelekezo ya kuanzia tarehe moja mwezi Julai ni hatua gani zitachukuliwa. Kuanzia hapo nina hakika kwa mkakati huo ambao wameuweka ni kwamba kila Dereva wa nchi hii atakuwa na mkataba wake na tutahakikisha kwamba pia kila Mmiliki wa Chombo cha Usafiri anafuata masharti ya sheria kama Kifungu cha 14 cha Sheria za Ajira na Uhusiano Kazini kinavyosema. Kwa hiyo, nimwondoe tu hofu Mbunge kwamba si maneno tu lakini mkakati umeshawekwa vizuri kabisa na tumekaa na wenzetu wa Jeshi la Polisi muda siyo mrefu kuanzia tarehe Mosi, Julai mtaona cheche za Wizara.
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nachukua nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mafupi ambayo bado hayajaondoa kabisa hamu ya wananchi wa Singida Mashariki kutumia banio hili. Kwa kuwa kilimo cha umwagiliaji kimeonekana ni kilimo chenye tija na hapa Bungeni tumekuwa tukizungumza mara kwa mara; na kwa kuwa soko la mbogamboga lipo kubwa sana kwenye mgodi wa Shanta Gold Mine pale Mang’onyi ambapo tunategemea utaanza hivi karibuni, ambalo litakuwa ni soko kubwa la mbogamboga na matunda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Serikali haioni umuhimu wa sasa kutenga fedha ambazo zilikadiriwa shilingi milioni 580 ili kuweza kukamilisha upande uliobakia kumalizia banio hilo lililokuwa limeandaliwa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kwa kuwa chanzo cha maji na Bwawa la Mwiyanji alilolieleza limejaa tope na kusababisha maji kuwa siyo ya kutosha; na kwa kuwa tumekuwa tukipiga kelele kuhusiana na mabwawa hapa nchini yajengwe mengi ili kuongeza uwezo: Ni lini sasa Serikali itaweza kutenga fedha kwa ajili ya kuondoa tope za bwawa hilo la Mwiyanji ili liwe na kina cha kutosha na maji mengi na kuweza kujenga bwawa lingine ambalo litajengwa katika Kijiji husika cha Mang’onyi? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaruru, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza na la msingi ni kwamba Serikali inatambua umuhimu wa kilimo cha umwagiliaji. Kwa kuwa kilimo hiki kinagusa pia sekta ndogo ya mbogamboga, Serikali itaendelea kuweka mkazo mkubwa kuhakikisha kwamba mradi huu unakamilika kwa hekta zilizobaki ili wananchi wa eneo la Mang’onyi waweze kupata huduma hii ya kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakika ni kwamba, katika bajeti inayokuja tutatenga fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huu ili wananchi waweze kulima kupitia kilimo cha umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ili mradi huu uweze kutekelezeka vizuri, na Mheshimiwa Mbunge bahati nzuri amelieleza jambo hili vizuri na amekuwa mtetezi wa kweli kwa wananchi katika jambo hili, lazima katika fedha ambazo zitatengwa zijumuishe pia namna ya kuweza kuondoa tope katika Bwawa la Mwiyanji ili maji yaweze kutiririka kwa urahisi ili wananchi waweze kupata huduma hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nikuondoe hofu; pia mimi na wewe tumepanga kwamba baada ya hapa tutakwenda kutembelea na kuzungumza na wakulima ili kuona skimu nzima na kuona namna Serikali inaweza ikawasaidia kwenye skimu hiyi.
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Kwa kuwa Wilaya ya Lushoto ni maarufu sana kwa kilimo cha mbogamboga na matunda, lakini kilimo hicho kimeendelea kusuasua kutokana na kilimo hicho kutegemea zaidi mvua za asili: -

Je, ni lini sasa Serikali itaandaa mpango wa kuvuna maji ya mvua ili baadaye yaweze kutumika katika umwagilia kipindi hicho cha ukame?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Husna Sekiboko, Mbunge wa Viti Maalum, kutoka Mkoa wa Tanga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kwamba ili kilimo chetu kiweze kuendelea, hatupaswi kuendelea tena kutegemea maji ya mvua. Kwa hiyo, kilimo cha umwagiliaji ndiyo tiba na ndiyo mwarobaini wa changamoto tuliyonayo. Kwa wakulima wa Lushoto, kazi inayofanyika pale kubwa ni lazima kuwajengea uwezo kwa kuhakikisha kwamba wanapata skimu hizo za umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Kilimo pamoja na Waziri wa Fedha wiki mbili zilizopita walifanya mkutano pamoja na Benki ya BADEA kwa ajili ya kupata mkopo wa kuja kujenga skimu kubwa za umwagiliaji ambazo zitasaidia sana kutatua changamoto katika maeneo mengi ndani ya nchi hii. Hivyo Waheshimiwa Wabunge tuendelee kuiunga mkono Wizara yetu katika hatua ambayo tumefikia, basi fedha hizo za BADEA zikipatikana tuweze kujenga miradi mingi na mikubwa katika nchi yetu ili kilimo cha umwagiliaji kiweze kupata nafasi yake.
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Zipo skimu zilizoanzishwa na Serikali ikiwemo skimu ya Karema ambayo ilianzishwa toka miaka iliyopita kama saba hivi. Skimu hiyo haijafanya kazi na zipo nyingi nchini zinazofanana na ile skimu: -

Je, ni lini Serikali itakwenda kukamilisha miradi iliyoanzishwa huko nyuma ukiwemo mradi wa skimu ya Karema?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kakoso, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Kilimo ameshatoa maelekezo kwa Tume ya Umwagiliaji Nchini kwa kuhakikisha ina take stock ya scheme zote nchini kwa zile zinazofanya kazi na ambazo zinahitaji ukarabati na zile ambazo zinahitajika kujengwa mpya. Hivi sasa kazi hiyo inaendelea na katika maeneo hayo pia tutaigusa skimu hiyo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameisema ya Karema; na tutatoa pia maelezo ndani ya Bunge letu hatua ambazo tumezifikia kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii mikubwa.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Hai kwa asilimia 78 tunategemea kilimo cha umwagiliaji, lakini pia tunazo skimu
25 za kimkakati ambazo tukizitumia tutabadilisha kabisa maisha ya watu na sisi kushiriki katika pato la Taifa. Tarehe 21Januari, 2022 Mheshimiwa Rais akiwa anaelekea Moshi Mjini alisimama pale Bomang’ombe, nami nilipata nafasi ya kumwomba atujengee skimu hizi. Alituahidi atatujengea kwa kutambua umuhimu mkubwa wa skimu hizi.

Swali langu, ni lini sasa Serikali itatekeleza agizo la Mheshimiwa Rais? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Saashisha Mafue, Mbunge wa Hai kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahadi ya Mheshimiwa Rais ni maelekezo kwetu na tumeipokea na tutaitekeleza kwa kadri ambavyo fedha zitaruhusu, kuanzia mwaka ujao wa fedha. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tumepokea ahadi ya Mheshimiwa Rais na tutaitekeleza kadri ambavyo fedha zitakuwa zinapatikana ndani ya Wizara.
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Kama nchi, ni muhimu kuwa na zao la kimkakati ambalo tuna uhakika wa kutupatia fedha za kigeni. Sasa kwenye zao la mbogamboga, horticulture hususan parachichi, sasa hivi kila mtu anajua kwamba kuna demand kubwa sana ya parachichi duniani na tafiti zilizofanyika karibuni, zinaonesha kwamba Tanzania ni kati ya nchi ambazo zinatoa parachichi bora kabisa duniani. Sasa kuna mikoa ambayo inalima parachichi, lakini ina mabonde ya asili yenye maji; ukizungumzia Njombe, Mbeya, Iringa, baadhi ya maeneo ya Songea na Songwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu kwa Serikali, kwa kuzingatia maeneo haya yana mabonde ya asili, maji yanapatikana kiurahisi sana; kwa nini kusiwe na mkakati mahsusi, ukizingatia demand kubwa ya parachichi duniani, haya mabonde yakaendelezwa kwa gharama nafuu, wananchi wakapata maji, kwa sababu parachichi ili liwe bora linahitaji maji na mbolea ili wananchi wapate na Serikali ipate: Sasa nataka majibu, katika hiyo mikopo ambayo mnasema mnazungumza, kuna mikakati gani mahususi ya kuendeleza mikoa hii mitano ili wakulima wanufaike na Serikali inufaike? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Halima Mdee, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sekta ndogo ya mazao ya mbogamboga na bustani, moja kati ya zao ambalo tumelipa kipaumbele kama Wizara hivi sasa ni zao la parachichi, kwa sababu tunatambua ya kwamba hivi sasa soko lake ni kubwa. Pia tumeshafungua masoko ya parachichi katika nchi za India pamoja na Afrika ya Kusini huku mawasiliano na majadiliano yakiendelea katika nchi za China na Marekani. Kwa kutambua umuhimu huo, katika mkopo huu ambao nimeuzungumza, moja kati ya maeneo ambayo yatakwenda kuguswa pia ni maeneo ambayo yanagusa mikoa hii ili kuhakikisha ya kwamba zao hili linapata huduma stahiki kutokana na upatikanaji wa maji mengi ya kutosha na pembejeo ya mbolea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo letu kubwa katika hili ni kuifanya Tanzania ijulikane kwa parachichi kama zao la kipaumbele. Hatua ambazo zimeshachukuliwa kwa hivi sasa ni kwamba Mheshimiwa Waziri ameshatoa maelekezo ya ujenzi wa common use facility katikati ya mikoa ya Mbeya na Iringa ambayo itasaidia kulima parachichi yetu kwa ufasaha. Vile vile parachichi itakayovunwa itapelekwa kwenye park moja ambayo tutafanya sorting, grading na packaging na kuifanya parachichi yetu ni produce of Tanzania kuliko hivi sasa ambapo parachichi yetu katika baadhi ya maeneo inaonekana kama inatoka nje ya nchi ya Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hii ni hatua kubwa ambayo tumeichukua katika hatua ya awali kabisa, lakini lengo letu kubwa kabisa ni kuhakikisha kwamba tunaendelea kufungua masoko ya parachini lakini vilevile kuwajengea wakulima uwezo na kulipa kipaumbele zao la parachichi. (Makofi)
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Jina langu ni Shally Josepha Raymond. Namshukuru Mungu sana kwa nafasi hii ya kupatiwa majibu haya mazuri na Serikali na nikuombe sasa niulize maswali yangu mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa katika jibu la msingi Mheshimiwa Naibu Waziri amenieleza wazi, kuwa sasa hivi wakulima wanalima kutokana na wao wenyewe walivyoamua. Maamuzi hayo ni mazuri sana, lakini swali langu la kwanza la msingi; kwa kuwa Serikali imeamua sasa kila mazao yanayolimwa yawe zaidi kibiashara na nchi hii utakuta kwamba shida kubwa ni mbegu. Wakulima wako tayari kulima sasa hasa mazao ya mbogamboga na TAHA iko kazini masaa 24 kutoa msaada kwa wakulima wa mbogamboga. Je, Serikali iko tayari sasa kutoa ruzuku kwa mazao hayo yakiwemo maparachichi, alizeti, mbogamboga zozote ambazo zinalimwa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wanawake wa Kilimanjaro wako tayari kulima kwenye vihamba vyao na Taasisi za Kilimanjaro za elimu, yakiwemo mashule yana mashamba ambayo yanalimwa mara moja tu mahindi lakini mwaka wote mzima yanakuwa hayana kitu. Je, Serikali iko tayari sasa kuwasaidia wakulima hao na wakina mama wa Kilimanjaro, kulima maparachichi kwa wingi na Taasisi hizo kuchimbiwa mabwawa ili mashamba yale yasikae idle mwaka mzima? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shally Josepha Raymond, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza la kuhusu mbegu na ruzuku, ushauri huo tumeupokea tutakwenda kuufanyia kazi. Isipokuwa tu nataka nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tumeendelea kukiimarisha Kituo chetu cha Utafiti wa Kilimo kwa maana ya (TARI). Hata ukiangalia bajeti imeendelea kuongezeka kwa sababu tunataka tufanye utafiti wa mbegu bora na zenye tija, ili mkulima wa Tanzania anufaike na kilimo kiwe cha tija.

Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba eneo hili pia tumelipa kipaumbele na tunaendelea kuhakikisha kwamba, TARI inajengewa uwezo ili kuja basi na tafiti ambazo zitatusaidia katika kilimo bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili la kuwasaidia katika eneo la maparachichi hasa katika Taasisi zenye mashamba ambayo hayatumiki muda wote. Kama nilivyosema dhamira ya Serikali katika sekta ndogo hii ya kilimo cha mazao ya bustani na mbogamboga ni kuhakikisha tunaipeleka mbele parachichi. Kwanza kwenye kuongeza uzalishaji wetu kwa sababu hivi sasa kama nchi tunazalisha tani 48,000 kwa mwaka. Lakini lengo letu ni kwamba ifikapo mwaka, 2025 tufikishe tani 140,000 ya parachichi na tuongeze pia ku-export parachichi nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ili hayo yote yaweze kutokea lazima tuweke mkazo mkubwa kuhakikisha kwamba tunasaidia kilimo hiki kukua. Hivyo, kwa wanawake wa Kilimanjaro ambao Mheshimiwa Mbunge amewaulizia swali hili, nataka tu nimwahidi ya kwamba, mimi niko tayari kuandaa ziara maalum katika maeneo yote ambayo umeyataja, tuyapitie kwa pamoja na vile vile tuimarishe vituo vyetu ili mpate miche ya kutosha, basi waweze kulima parachichi kwa sababu soko limeshakuwa kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kuuliza swali dogo la nyongeza ambalo limejikita kwenye sekta hii hii ya zao la parachichi.

Nilisimama Bungeni hapa nikaomba kuhusu ugawaji wa miche ya parachichi kwa wakulima wetu. Kwa sababu, wakulima wetu wa Mkoa wa Njombe, Mkoa wa Mbeya, Mkoa wa Iringa wamejiwekeza sana kwenye kilimo cha parachichi, tukasema, kama ambavyo Serikali imefanya kugawa miche bure ya michikichi, miche bure ya pamba, miche bure ya korosho ili ku-boost wakulima wa mazao hayo, nikaiomba Serikali kuona ni mkakati upi ufanyike kwenye zao la parachichi ambapo wakulima wengi hawana fedha za kununua miche, lakini ni zao linaloonekana ni dhahabu ambalo sisi tunaita dhahabu ya kijani Mkoa wa Njombe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu, je, Serikali ina mkakati upi wa kuandaa vitalu ili iweze kugawa miche bure kwa wakulima ku-boost zao hili, kutoka kwenye kilimo cha kawaida kwenda kwenye zao la biashara ambalo kwa sasa ni hot kwenye Taifa letu? (Makofi)
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu aliyoyatoa ya ufasaha. Nataka nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Festo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Serikali imetoa ruzuku katika miche ya kahawa, tumetoa ruzuku katika miche ya korosho. Nataka nilihakikishie Bunge lako Tukufu kwamba sasa hivi Serikali inafanya mapping katika mikoa mitano, inayozalisha parachichi na kwa kutumia Taasisi zetu za TARI na TOSCI, tumeanza kutengeneza Regulation na Standardization ili kuondoa tatizo la miche inayouzwa na kila mwananchi barabarani ili tusije tukaua zao la parachichi na hivi karibuni tuta-launch hizo guideline. Tunaanza programu kupitia private sector partnership kama Serikali kuanzia mwaka ujao wa fedha. Tutazalisha miche, tutagawa kwa subsidized rate kwa sababu sasa hivi najua wakulima wananunua kati ya shilingi 5,000 na shilingi 6,000 kwa mche mmoja ambao ni ghali sana. Kwa hiyo, tutaanza kugawa miche ya ruzuku ya parachichi katika mikoa yote inayolima parachichi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili tutakalofanya kama Serikali katika eneo la parachichi ni kwamba, kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri, tutajenga common use facility tatu, moja tutaiweka kati ya Iringa na Njombe nyingine tutaiweka Dar es Salaam na nyingine tutaiweka Mkoa wa Kilimanjaro. Hizi zitatumika, wale wanunuzi wanaotoka nje watanunua parachichi, watafika katika hizo facility, watapata huduma kwa kuzilipia na zitawekwa alama ya kwamba ni product za Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu umwagiliaji. Timu yetu ya Umwagiliaji sasa hivi inafanya mapping katika mikoa hiyo ili tuone ni wapi ambapo tutaweza ku-facilitate kuweza kugawa mipira na nini ambako wananchi wamewekeza. Kwa sababu ni zao ambalo linahitaji uwekezaji wa muda mrefu na linahitaji government intervention, niwahakikishie tu Waheshimiwa Wabunge tutafanya strong intervention kwenye parachichi kwa sababu tunaamini tunazo competitive aids zote. (Makofi)
MHE. HUMPHREY H. POLEPOLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Tanzania ni mojawapo ya nchi mbili Ulimwenguni ambazo zimepewa baraka na Mungu ya kuzalisha organic phosphate. Organic phosphate ni mojawapo ya madini muhimu yanayotumika kutengeneza mbolea. Organic phosphate ulimwenguni inapatikana Tanzania na Australia peke yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali, je, Serikali ina mpango gani wa kuzuia ku-export organic phosphate kama ambavyo inaendelea kufanyika sasa hivi, ili ibaki hapa nchini na kuendelea kuzalisha mbolea ili wakulima wetu wapate mbolea hapa na pasipo na kuhangaika kutoka maeneo mengine? Natambua kiwanda kinakuja Dodoma lakini kuna tamaa kubwa sana ya ku-export organic phosphate kwa sababu ni nchi mbili tu ulimwenguni ambazo zinatoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Polepole, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kama nchi tunakuwa guided na WTO Regulation za Trade. Kwa hiyo, ku-declare openly tunazuia export au biashara yoyote sidhani kama katika misingi ya kibiashara ni jambo jema. Hilo la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili sisi kama Serikali tumeshafanya comprehensive analysis kuangalia deposit yetu ya phosphate iliyopo katika nchi yetu. Tunazo taratibu za kuruhusu mahitaji yanapohitajika kwenda nje tunazo guidance zinazotu-guide. Haturuhusu export ya holela katika phosphate. Hilo la pili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la tatu kwa kuwa tumeshapata Mwekezaji ambaye anawekeza na atatumia phosphate katika Kiwanda cha Mbolea, kinachojengwa hapa Dodoma ambacho kinazalisha tani 600,000 na kitaanza mwaka kesho mwezi wa pili kuanza kuzalisha. Nataka niwahakikishie tu wakulima kwamba tuta-regulate matumizi ya rasilimali hii kwa maslahi ya Watanzania bila kuathiri mahusiano yetu ya kibiashara na nchi zingine. (Makofi)
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa Mawakala wengi nchini wamekuwa wakisaidia sana wakulima kwa kuwakopesha mbolea na hivyo kuleta nafuu sana kwenye upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima; sasa suala hili limechukua miaka sita. Kwa mfano kwenye Jimbo langu kuna mama mmoja anaitwa Mama Renata Mbilinyi, anadai shilingi milioni 600 na sasa hivi amekaribia kufilisika: -

Je, Serikali haioni haja ya kuharakisha, kwa sababu jambo hili limechukua muda mrefu, ili kuleta nafuu kwa wakulima wetu? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jackson Gedion Kiswaga, Mbunge wa Kalenga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama maelezo yangu ya awali yalivyosema, ni kwamba hatua za uhakiki zipo mwishoni na pindi zikikamilika, Mawakala wote watalipwa. Kilichochelewesha, kulikuwa na documents zilizokuwa zina- miss, baadhi ya Mawakala wengi walishindwa kuziwasilisha na Serikali iliona kuna umuhimu wa kuwapa muda zaidi kuziwasilisha ili iweze kutenda haki na mtu asidhulumiwe.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba hatua zipo mwishoni, zikikamilika Mawakala wote watalipwa.
MHE. JULIUS KAMOGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Utaratibu wa ruzuku ulitoa nafuu kubwa sana wa bei za mbolea wakati huo. Hivi tunavyozungumza, bei za mbolea bado ziko juu na hii changamoto bado haijatatuliwa: Je, Serikali inasema nini kwa Watanzania kuhusu bei za mbolea ambapo hadi sasa wanashindwa kuzimudu?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Nyamoga, Mbunge wa Kilolo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge, bei ya mbolea ipo juu tofauti na bei ambazo wakulima walinunua katika misimu miwili au mitatu iliyopita. Hata hivyo, Serikali imeendelea kuchukua hatua kuhakikisha kwamba tunampunguzia maumivu mkulima.

Mheshimiwa Spika, katika hatua ya awali kabisa ambayo tumeanza nayo ni kwamba, hivi sasa tumeanza mazungumzo Pamoja na zile kampuni za usambazaji wa mbolea kutoka katika source yenyewe badala ya kuwatumia watu wa katikati, Mheshimiwa Waziri alifanya kikao na Makampuni kutoka Saud Arabia, China Pamoja na Urusi. Lengo letu ni kuhakikisha kwamba tunaipata mbolea moja kwa moja kutoka kwenye source kuja katika nchi yetu ya Tanzania ili tusiwape nafasi katikati hapa watu ambao wamekuwa wakiongeza bei.

Mheshimiwa Spika, swali la pili; katika bajeti inayokuja tumejiandaa kutenga fedha kwa ajili ya stabilization fund kuhakikisha kwamba tuna-control bei ya mbolea ili wakulima wasipate taabu.

Mheshimiwa Spika, la mwisho, tumeendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya mbolea. Ninavyozungumza hivi sasa, kiwanda cha ETRACOM pale Nala Dodoma, kinakamilika mwezi Julai. Kikikamilika kiwanda hiki kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 600,000 za mbolea kwa mwaka na hivyo tutakuwa tumeondoa changamoto hii ya bei ya mbolea kwa wakulima wetu. (Makofi)
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; kazi kubwa katika kusimamia vyama vya ushirika ipo kwenye wilaya zetu. Je, vifaa hivi vilivyozungumziwa vinaelekezwa kwenye Wilaya au Mikoa? (Makofi)

Pili, Taarifa ya Shirika la Ukaguzi (COASCO) ya mwaka 2019/2020 inaonesha ni vyama 6,021 vilifanyiwa ukaguzi, kati ya vyama hivyo ni vyama 289 nivyo vilivyopatiwa hati safi, sawa na asilimia 4.8.

Je, Serikali haioni kwamba ipo haja ya kuwawezesha maafisa ushirika ili waweze kufanya kazi hiyo kwa ufanisi zaidi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Josephine Genzabuke, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, pikipiki hizi 137 zimeelekezwa katika Halmashauri za Wilaya na kama nilivyosema hapo awali, pamoja na hiyo pia Wizara imeona kuna umuhimu wa kuanza kuandaa bajeti ya kutenga fedha za kununua magari kwa ajili ya kusaidia zoezi la ushirika katika mikoa yetu. Kwa hiyo nimuondolee hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba kazi hii ya ushirika tunaipa thamani kubwa na tunatambua umuhimu wake katika kumuendeleza mkulima wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, la pili ni linalohusu kuiwezesha COASCO kufanya ukaguzi ili kuweza kupata hali halisi ya vyama vyetu vya ushirika hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, katika bajeti yam waka 2021/2022 Serikali tumetenga shilingi milioni 700 kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunavifikia vyama vingi vya ushirika na kufanya ukaguzi. Lengo lake ni kuweza kufikia maeneo mengi zaidi kuliko ilivyokuwa awali.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo Serikali tumeona umuhimu na tumeendelea kuongeza katika eneo hili.
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali imekuwa ikisisitiza uanzishwaji wa vyama vya ushirika, je, Serikali haioni kwamba umefikia wakati kuwahamasisha wananchi wa Mkoa wa Dodoma wakaanzisha ushirika ukizingatia kwamba zao la zabibu ni zao la biashara na ni zao la kimkakati?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Fatma Toufiq, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Dodoma kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, miongoni mwa mazao ambayo Serikali iliyaongeza katika mazao ya kimkakati ni pamoja na zabibu. Serikali inatambua umuhimu wa zao la zabibu katika Mkoa wa Dodoma na manufaa makubwa ambayo wananchi wamekuwa wakiyapata kupitia zabibu. Hivyo, katika kuharakisha maendeleo ya zao la zabibu katika Mkoa wa Dodoma hivi sasa tayari Mrajisi ameanza na zoezi la usajili wa Vyama vya Ushirika vya Msingi 11 na ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wataitisha mkutano wa majadiliano kupitia kamati ambayo imeundwa kwa ajili ya kuja na Chama cha Ushirika ambacho kitasimamia vyama vya msingi, lengo letu ni kuendelea kuipa thamani zabibu ya Dodoma.

Mheshimiwa Spika, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba tayari mchakato umeanza na muda si mrefu tutakamilisha zoezi hili, na wakulima wa zabibu wa Dodoma watapata nafasi ya kuwa na chombo ambacho kitasimamia zao hili la zabibu katika Mkoa wa Dodoma.
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana nashukuru kwa majibu ya Serikali, lakini pamoja na majibu hayo ni ukweli usiofichika kwamba changamoto kubwa kwa uzalishaji wa kahawa ni hayo magonjwa uliyoyataja na mbegu zilizozalishwa bado hazijaweza kupambana na hayo magonjwa mia kwa mia.

Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kuanzisha mfuko wa maendeleo ya kahawa ili wakulima waweze kupata pesa za kununua pembejeo wapambane na magonjwa haya?

Mheshimiwa Spika, swali la pili je, kwa kuwa tumehamasisha sana uzalishaji wa kahawa, Serikali haioni pia ni muhimu kuanzisha programu za kuboresha mifereji ya asili ili wakulima waweze kupata maji ya kumwagilia kahawa zao? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Profesa Patrick Aloyce Ndakidemi, Mbunge wa Moshi Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza sisi tunaona Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo ambao tumeutamka katika bajeti yetu unatosha kwa ajili ya kushughulikia mazoa yote. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba zao la kahawa pia ni kati ya mazao ambayo yanashughulikiwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo na hivi sasa utaratibu ambao unaendelea ni kutenga kila shilingi mia moja kwenye zao la kahawa aina ya robusta na shilingi mia mbili kwa arabica kwa ajili ya kuchangia katika mfuko huu, kwa hiyo mwisho wa siku pia utakwenda kuhudumia zao la kahawa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mifereji, nakubaliana na wewe Profesa nami nimefika katika baadhi ya mashamba katioka Mkoa wa Kilimanjaro, hilo tumelichukua tunaendelea kulitekeleza, tutalifanyia kazi ili mwisho wa siku liweze kuleta tija kwa wakulima wetu. (Makofi)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Swali langu ni fupi. Je, Serikali itatumia mkakati gani na ni lini itaanza kugawa hizo mbegu mnazosema tutagawiwa za ruzuku za miche ya kahawa kwa sababu muda unakwenda?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Kimei, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, zoezi la ugawaji wa miche chotara linaendelea na tumeshagawa katika Mikoa ya Kagera, Mbeya, Songwe pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro, pia hata Mheshimiwa Ndakidemi ni shahidi katika eneo lako miche hii imeshagawiwa. Zoezi ambalo tunaendea nalo ni kuhakikisha kwamba, tunazalisha kwa wingi ifikie miche Milioni 20 ili tuweze kubadilisha ile mibuni iliyokaa muda mrefu tui-replace na hii mipya ili kuondokana na changamoto ambayo wakulima wengi wanaipata.
MHE. KASALALI E. MAGENI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Je, Serikali haioni kwamba, umefika wakati sasa wa kuwekeza kwenye uzalishaji wa mazao ya choroko na dengu kwa kutoa pembejeo na mafunzo kwa wakulima badala ya ambavyo sasa Serikali imewekeza zaidi kwenye kusimamia mauzo badala ya kusimamia uzalishaji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kasalali Mageni, Mbunge wa Sumve, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Kasalali kwa namna ambavyo amekuwa akiyasimamia mazao haya, hii ni hoja yake ambayo amekuwa akiisema mara kwa mara.

Mheshimiwa Spika, nataka nimhakikishie mbele ya Bunge hili ya kwamba, tutaendelea kuyapa kipaumbele mazao yote, katika maoni na ushauri ambao Mheshimiwa Mbunge ameusema tumeupokea tutakwenda kuufanyia kazi ili mwisho wa siku wakulima wa choroko na dengu pia walime kwa tija na masoko ya uhakika wayapate pia. (Makofi)
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, msimu wa korosho unaanza mwezi wa Kumi. Je, Serikali haioni haja ya kuweka bei dira kwa zao la korosho kama ilivyo mazao mengine kama pamba?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, Yahya Mhata, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika kikao cha wadau tulichokifanya katika Manispaa ya Songea, katika kikao hiki mwongozo uliotolewa na ambao pia Serikali tunausimamia ni kwamba, utaratibu wa zamani wa bei ya korosho utaendelea ambapo ni utaratibu ule wa kulaza sanduku na baada ya hapo bei itakwenda kutangazwa ili mwisho wa siku wakulima waweze kuipata bei yao katika ufunguzi wa sanduku lile. Kwa hiyo, yale ambayo tulikubaliana na wadau na Waheshimiwa Wabunge pia walikuwepo ndiyo sehemu ya utekelezaji ambao Serikali tutausimamia.
MHE. CHARLES J. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika, naomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza: -

Mheshimiwa Spika, kutokana na kwamba, sasa Tanzania ni soko la chakula, naomba Serikali itueleze kasi ya Serikali katika kuwekeza kwenye umwagiliaji kwa kutumia sekta binafsi katika mito ambayo ina maji yasiyokauka, mito kama mabonde ya Kagera, basin ya Viktoria, Ruvuma na maziwa yetu? Hilo ni swali la kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Katika maelezo ya hizo hekta 95,000 zinazozungumzwa naomba Serikali inihakikishie hekta 11,000 za Mto Ngono na zenyewe zimo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Charles Mwijage, Mbunge wa Muleba Kaskazini, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, katika Jedwali la Sita katika Kitabu cha Bajeti iliyosomwa na Waziri wa Kilimo limeelezea mabonde 22 ambayo Serikali imeamua kuyafanyia upembuzi yakinifu na usanifu ili mwisho wa siku nchi yetu kuanzia Mashariki, Magharibi, Kusini na Kaskazini yote tufanye kilimo cha umwagiliaji. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, mpaka hivi sasa ninavyozungumza tayari kazi hii imekamilika na tuko katika hatua za kuwapata Wakandarasi kwa ajili ya kufanya kazi hii.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, katika maeneo yote hayo mabonde yale makubwa, yaani kuanzia Bonde la Ziwa Viktoria, Malagarasi, Mto Manonga, Ifakara, Idete, Mto Songwe, Rufiji Basin Kwenda mpaka Mkoazi maeneo yote haya tutayagusa. Lengo letu ni kufanya kilimo cha umwagiliaji na mwisho wa siku tufikie malengo ambayo tumejiwekea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu Mto Ngono, kwenye hili la Mto Ngono nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ambaye amekuwa akilisimamia sana jambo hili, katika yale mabonde 22 ambayo tunayafanyia upembuzi yakinifu na usanifu, Mto Ngono pia upo. Kwa hiyo, ekari zile 11,000 zitakuwepo kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge suala la Mto Ngono tumelichukulia katika umakini mkubwa sana. (Makofi/Kicheko)
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, hizi zimekuwa ni namba tu ambazo zikisomwa kila mwaka; lakini ukienda kwenye uhalisia kabisa huwezi kukuta mkulima mfano wa pamba ana kitambulisho cha usajili, hata kwenye korosho huwezi kukuta mkulima kwenye korosho ana kitambulisho cha usajili. Ukiangalia hata Chama chetu cha Mapinduzi juzi tu kimesajili wanachama wake, lakini tayari wamepewa kadi. Sasa mimi nataka nijue kauli ya Serikali ni lini sasa hawa wakulima wa mazao ya kimkakati watapewa kadi za usajili ambazo zitakuwa kama vitambulisho kwao?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; tumekuwa zikiagizwa pembejeo nyingi ambazo zinakuja kwa wakulima lakini madhara yake zinakuwa zinabaki kwa sababu uhalisia kamili wa wakulima waliosajiliwa bado haujajulikana. Nataka nipate majibu ya Serikali.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Emmanuel Peter Cherehani, Mbunge wa Ushetu, kwa pamoja kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hivi sasa Serikali tunaendelea na zoezi la usajili wa wakulima nchi nzima ambapo mfumo unaotumika hivi sasa ni mfumo ambao unampa kila mkulima utambulisho maalum kwa maana atakakuwa na namba yake maalum ambayo ndiyo utakuwa utambuzi wake. Zoezi hili linaendelea katika maeneo mengi kwa ukamilifu mzuri na uratibu unaendelea vizuri na tunaamini kabisa likikamilika litatibu changamoto zote ambazo wakulima wanazipata hasa katika utambuzi wao kwa sababu kila mkulima atapata namba yake maalum ya utambuzi; na tunaamini kupitia hapo sasa hata zile huduma muhimu watazipata kwa rahisi zaidi.

Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba zoezi hili linaendelea na linaendelea vizuri na mwisho wa siku tutakuwa na kanzidata ya wakulima wote nchini kila mtu kwa maeneo yake alipo pamoja na maeneo ambayo anayamiliki na mazao anayalima na yields anazipata.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kunipatia fursa ya kuuliza maswali mawili madogo nyongeza.

Mheshimiwa Spika, hizi Skimu za Buhangaza, Kyota na Kyamyorwa ni za muda mrefu, zilijengwa kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania lakini hazijakamilika kwa maana hiyo tumezamisha fedha za walipa kodi lakini hakuna tunachokipata.

Je, hizi skimu nataka kupata commitment ya Serikali ni lini zitakamilishwa ili ziweze kutumika kama ilivyokusudiwa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Kagera tumebarikiwa kuwa na bonde Mto Ngono, ni bonde kubwa linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji maji. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuanza kulitumia hilo Bonde la Mto Ngono kwa kilimo cha umwagiliaji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Oscar Ishengoma Kikoyo, Mbunge wa Muleba Kusini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika majibu yangu ya msingi nimeeleza mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kwanza tumefanya tathmini ya kina ya skimu hizi kufahamu gharama halisi na baadaye utekelezaji wake utaanzia mwaka 2023/2024.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili la kuhusiana na Bonde la Mto Ngono, niliwahi kutoa maelezo hapa naomba niyarudie; ukiangalia katika jedwali la saba katika kitabu cha bajeti cha Wizara ya Kilimo tumeainisha mabonde 22 ambayo Serikali itakwenda kuyapitia kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina likiwemo Bonde la Mto Ngono.

Mheshimiwa Spika, nataka niwaondoe hofu Waheshimiwa Wabunge wanaotoka Mkoa wa Kagera nafahamu hili ni eneo ambalo mmekuwa mkilipa kipaumbele kikubwa sana, tumeanza na upembuzi yakinifu tutajenga skimu katika Mto Ngono na umwagiliaji utafanyika na wananchi wa Kagera watanufaika na bonde hilo. (Makofi)
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Pamoja na majibu yenye matumaini kutoka Serikalini, naomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, utambuzi wa Bonde la Mititi na Ilembo ndani ya Jimbo la Kwela kwa ajili ya kuanzisha skimu umefanyika muda mrefu. Sasa nataka kujua, ni lini Serikali mtaleta fedha kwa ajili ya usanifu kuanzisha skimu hizo?

Swali la pili; skimu ya umwagiliaji iliyopo Kata ya Ilemba kwa maana ya Kijiji cha Sakalilo, imetumia muda mrefu sasa, imetumia zaidi ya Bilioni Moja, na bado fedha karibia Milioni 800 kukamilisha skimu hiyo. Nataka kujua ni lini wataleta fedha hiyo ili iweze kukamilisha skimu hii ya Sakalilo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Kwela, kwa pamoja kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mipango hiyo tumeiweka katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 na imekuwa ni kilio cha Mheshimiwa Mbunge. Ahadi yetu ni kwamba tutafanya utekelezaji katika mwaka huu wa fedha na kuendelea.
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri, ni lini Mkandarasi wa kujenga Skimu ya Umwagiliaji ya Makwale Wilayani Kyela kutumia Mto Rufilio ataanza kazi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ally Jumbe, Mbunge wa Kyela, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, maelekezo ambayo tuliyatoa kwa Wakandarasi wote wale ambao walisaini mikataba wakati wa sherehe ya Nanenane pale Mbeya ni kwamba wanapaswa kuwa site kuanzia tarehe 15. Lakini tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwa hoja yake mahsusi, basi tutahakikisha kwamba tunamharakisha Mkandarasi huyo aende kuanza kazi mapema kama ambavyo maelekezo yalitoka Wizarani.
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa ardhi ambayo inafaa kwa umwagiliaji ambayo inatumika sasa hivi kwa miradi ya umwagiliaji ni pungufu ya asilimia Tano. Je, nini mkakati wa Serikali kushirikisha sekta binafsi katika kuhakikisha maeneo yote ambayo yanafaa kwa umwagiliaji yanajengewa skimu? Nashukuru.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dennis Londo, Mbunge wa Mikumi, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, katika Jedwali Na. 6 la Kitabu cha Bajeti cha Wizara ya Kilimo, imeelezwa mahsusi kabisa kwamba Serikali imejipanga kuyafanyia upembuzi yakinifu na usanifu mabonde yote makubwa 22 ndani ya Nchi yetu ya Tanzania kuhakikisha yote yanafanya kilimo cha umwagiliaji, yakiwemo mabonde ya Mto Songwe, Ifakara, Idete, Pangani, Rufiji, Chamanzi na Malagarasi pamoja na Ziwa Victoria.
MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Naishukuru Serikali kwa kutoa fedha kuchimba bwawa la umwagiliaji katika Kata ya Chunyu, Namhambi: Je, ni lini kazi hii itaanza?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa George Malima, Mbunge wa Mpwapwa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mkandarasi anayejenga mradi wa skimu ya umwagiliaji ya Msagali, hivi sasa yuko site ameanza mobilization na ni kati ya wale Wakandarasi 21 ambao walisaini mikataba pale Nanenane Mbeya na tunategemea muda wowote aanze kazi hiyo. Vile vile bwawa ambalo linajengwa pale likikamilika litakuwa na uwezo wa kutoa lita za mita za ujazo milioni 92. Kwa hiyo, ni habari njema kwa wana-Mpwapwa na kwa bahati nzuri mkandarasi yuko site tayari. (Makofi)
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nashukuru kwa majibu ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, shilingi 93,476,190 ni fedha za wakulima wangu wa ufuta 89: Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba fedha hizi zinakwenda kulipwa kwa wakulima hawa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kutokana na changamoto zilizopo katika uendeshaji wa bodi zetu pamoja na vyama vyetu vya msingi na changamoto wanazozipata wakulima kwa uongozi usiokuwa madhubuti, Waziri atakuwa tayari kuambatana nami baada ya Bunge hili kwenda Nanjirinji kuzungumza na wakulima? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ally Mohamed Kassinge, Mbunge wa Kilwa Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, la kwanza la kuhusu malipo kwa wakulima, namwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushirika Tanzania kuhakikisha anafuatilia na mwisho wa siku wakulima hawa waweze kulipwa madai yao haya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili kuhusu kuongozana na Mheshimiwa Mbunge, nimwahidi kwamba niko tayari, baada ya vikao hivi vya Bunge tuongozane mimi na yeye kwenda Kilwa kwa ajili ya kuhakikisha kwamba mambo yanakwenda vizuri. (Makofi)
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana nishukuru sana kwa majibu ya Serikali, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina swali moja la nyongeza.

Je, Serikali haioni imefikia wakati wa kutenga bajeti maalum ili kuweza kuwapeleka baadhi ya wataalam wa kilimo katika zile nchi ambazo zimekuwa zikizalisha zabibu kwa wingi ikiwemo Afrika ya Kusini, China na Spain? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba tunawajengea uwezo wataalam wetu na hivi sasa tumekamilisha mazungumzo na wenzetu wa Afrika ya Kusini, Ufaransa na Israel kwa ajili ya kuwapeleka wataalam wetu kwenda kujifunza maeneo mbalimbali, ikiwepo ubunifu na uzalishaji wa mbegu bora na udhibiti wa magonjwa wa wadudu pamoja na mbinu bora za kilimo za shambani yaani agronomy.
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nimuulize maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, bei ya kuuzia tumbaku ni muhimu sana kwa mkulima; je, wakulima wenyewe wanashirikishwaje katika kufikia uamuzi wa bei gani tumbaku yao iuzwe?

Swali la pili tunaishukuru Serikali kwa kutupa ruzuku, lakini naomba Serikali ituhakikishie sisi watu wa Urambo; je, mbolea ya tumbaku ni miongoni mwa mbolea zilizopata ruzuku? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta Mbunge wa Urambo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ushiriki wa wakulima, kwa mujibu wa Sheria ya Tasnia ya Tumbaku Namba 24 ya mwaka 2021 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009 na kanuni zake za mwaka 2011 Kifungu cha 43 (1) kimeweka masharti ya ushiriki wa wakulima kupitia vyama vyao vikuu katika majadiliano ya bei na pembejeo. Hivyo, nidhahiri kwamba kupitia sheria hii wakulima wanashiriki kupitia vyama vyao vikuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kuhusu mbolea ya ruzuku; katika mwongozo ambao tumeutoa kwenye mbolea ya zuruku, mbolea ya ruzuku ni kwa mbolea zote ikiwemo mbolea ambazo zinahusiana na zao la tumbaku. Kule kwenye tumbaku wanatumia mbolea hasa za NPK na CAN ambapo hadi hivi sasa kwa mujibu wa maoteo ni jumla ya tani 37,000 zitahitajika na tayari zipo kwenye utaratibu huo kuingia kwenye suala hili la ruzuku.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi hii. Mto wa Ngainanyuki katika Wilaya ya Longido ni muhimu sana kwa kusaidia kilimo cha umwagiliaji: Je, Serikali ina mkakati gani wa kusanifu miundombinu ya mto huu ili kuwasaidia wananchi wa Longido? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zaytun, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika moja ya mikakati ambayo Wizara tunayo ni kuhakikisha ya kwamba tunatumia ipasavyo vyanzo vya maji katika maeneo yote ya mabonde ili tuweze kufanya kilimo cha umwagiliaji. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwa hili ambalo limewasilishwa litakuwa ni sehemu ya mipango yetu na tunaielekeza Tume ya Umwagiliaji kuweza kufika na kuliangalia eneo hilo mara moja kwa ajili ya kuendelea na taratibu nyingine.
MHE. SOUD MOHAMMED JUMAH: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza: Kwa kuwa Herbarium ya TPRI, Arusha ni kituo muhimu cha uhifadhi na utafiti: Je, Serikali ina mpango gani wa kuweza kuajiri na kuzalisha wataalam zaidi ili kuweza kukusanya data nchi nzima badala ya ku-concentrate na mikoa miwili tu hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili: Kwa kuwa wenzetu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, hususan misitu, wana utaalamu mkubwa wa usimamizi wa Herberium: Kwa nini tusiangalie uwezekano wa kuhamisha usimamizi wa hii National Herbarium kuipeleka maliasili au angalau kuwa-engage watu wa Maliasili wakasaidiana ili kuboresha au kuongeza wigo wa uhifadhi, utafiti na utalii katika herbarium zetu? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Soud Mohammed Jumah, Mbunge wa Donge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, la kuhusu kuajiri, kwa sababu, nimezungumza pale awali kwenye majibu yangu ya msingi kwamba hii tayari imeshahamia ndani ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu, ambayo tumeanza kupitia pia muundo wake na hivi sasa tunahakikisha kwamba tunawapatia nafasi pia kuweza kuajiri wataalamu zaidi kwa sababu muundo huu tunaupitia. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba na hilo pia litakuwa ni sehemu kati ya priorities kuhakikisha kwamba, tunakuwa na wataalamu wa kutosha katika eneo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, kuhusu kuhamisha, jambo hili lipo kisheria na hivyo linahitaji marekebisho ya sheria, lakini tumepokea kama Serikali hoja ya Mheshimiwa Mbunge. Nakushukuru sana.
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; changamoto bado ni kubwa sana hususani soko la ndani kwa wakulima wa zao la mtama na uwele. Je, Serikali ina utaratibu gani wa kuhakikisha kwamba yenyewe inashughulika kununua mazao haya kupitia NFRA ili mradi kupunguza tatizo la changamoto ya soko la ndani?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kuna tatizo kubwa la ndege aina ya kwelea kwelea ambao wamekuwa wakishambulia sana mazao haya ya mtama pamoja na uwele na Serikali yetu ina tatizo la kutokuwa na ndege ambayo ni maalum kwa ajili ya kushughulikia ndege hawa waharibifu wa mazao haya. Je, Serikali haioni haja ya kuhakikisha kwamba inanunua ndege yake ili mradi iweze kushughulika kwa karibu na ndege hawa waharibifu ambao wanashambulia mazao haya?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Nyangindu Boniphace Butondo, Mbunge wa Kishapu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, la kwanza, namshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo amekuwa akiwapambania na kuwasemea wakulima wa mtama pamoja na uwele kutoka Mkoa wa Shinyanga.

Mheshimiwa Spika, kuhusu uhakika wa soko la ndani, maelekezo tayari NFRA wanayo ya kununua mazao hayo ikiwemo mtama pamoja na uwele. Kwa hiyo nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba NFRA anaendelea na zoezi la kununua mtama hivyo wakulima wa Shinyanga ni sehemu ya wanufaika wa soko hili la ndani kupitia NFRA.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, kuhusiana na ndege. Katika bajeti yetu ya mwaka huu tumetenga Shilingi bilioni tatu ya kununua ndege mpya kwa ajili ya kunyunyizia wadudu kwenye sehemu ya kukuza kilimo anga. Ninavyozungumza hivi sasa tuko katika due diligence, tunazo kampuni tatu, mbili kutoka Marekani na moja kutoka Afrika ya Kusini ambako baadaye sasa tutafanya maamuzi ni wapi tununue ndege hiyo.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, tunayo ndege yetu pia ya survey ambayo iko Nairobi Kenya, imekamilishwa matengenezo yake na yenyewe pia itakuja kuungana kuimarisha kilimo anga ili kuondokana na changamoto hii ya wadudu waharibifu.
MHE. KASALALI E. MAGENI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na namshukuru pia Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri, lakini ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; Serikali imekiri kwamba imeanza mchakato na inagawa mbegu bora za kilimo cha alizeti kwa wakulima. Je, ni lini sasa Serikali itahakikisha mbegu hizi zinafika kwenye Jimbo la Sumve kwenye Kata za Lyoma na Malya ambazo zimeonyesha uwezo mkubwa wa kuzalisha alizeti kuliko maeneo mengi ya nchi hii?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; uzalishaji wa mazao haya ya alizeti na upelekaji wa mbegu bora unategemea pia upatikanaji wa mbolea. Katika Jimbo la Sumve mbolea ya ruzuku ambayo tunaitegemea sana kwa mazao haya mpaka sasa haipatikani. Je, ni nini tamko la Serikali juu ya upatikanaji wa mbolea hii ya ruzuku ambayo imekuwa ni changamoto kubwa sana kwa wakulima wetu?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kasalali Mageni, Mbunge wa Sumve, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza kuhusu mbegu bora za alizeti kuwafikia wakulima wake, nikitoka hapa nakwenda kumpigia simu na kumwelekeza Mtendaji Mkuu wa ASA ahakikishe wakulima wa Sumve na wenyewe wanapata mbegu bora hii ya alizeti.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu mbolea, ni kweli kumekuwepo na changamoto katika mfumo wa usambazaji, lakini tumeshatoa maelekezo kwa ndugu zetu wa CPB ambao wanashirikiana na wadau wengine kuhakikisha kwamba mbolea hii inawafikia wakulima kwa wakati. Kwa hiyo nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, zilikuwepo changamoto, tumeendelea kuzifanyia kazi na muda sio mrefu CPB pamoja na mawakala wengine watasaidia ufikishaji wa mbolea kwa wakulima pasipo na usumbufu wowote kwa wakulima wetu wa Tanzania.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa nini sasa Serikali isipeleke mbegu bure kabisa kwa wakulima wa alizeti ili waweze kuzalisha alizeti kwa wingi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya mafuta hapa nchini?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Cherehani, Mbunge wa Ushetu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, dhamira ya Serikali ni kuona tunaongeza uzalishaji wa zao la alizeti, kila jambo linakwenda kwa hatua. Hatua ya kwanza tumeanza na ruzuku ya kuuza mbegu ya kilo moja kwa Sh.5,000 ambayo katika hali ya kawaida mkulima angepata kwa Sh.35,000 mpaka Sh.40,000. Kwa hiyo kwa hatua hii, ni hatua nzuri ambayo Serikali imeianza na huko mbeleni tutalifikiria ombi la Mheshimiwa Mbunge.
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa miaka miwili mfululizo Serikali imekuwa ikiahidi, lakini kiasi kinachotolewa kwa ajili ya usambazaji huwa hakiendani na kile ilichoahidi, hivyo kusababisha upungufu wa pembejeo kwa wakulima. Je, Serikali inatoa kauli gani kwamba ahadi hii ya leo ya pembejeo ya unga na dawa za maji kwamba zote zitapatikana kwa wakati na zote zitafika kwa wakulima?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ni ongezeko la pembejeo. Tunatarajia kwamba kutakuwa na ongezeko la uzalishaji wa korosho na tumeona pia kwenye soko la korosho bei inazidi kuporomoka. Je, Serikali ina mkakati gani kwamba ongezeko hili la uzalishaji litaendana na bei nzuri ambayo ina tija kwa mkulima wa korosho? Nakushukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuhusu kauli ya Serikali bahati nzuri kwenye kikao cha wadau wa korosho ambacho mimi nilikuwa sehemu ya washiriki na Waheshimiwa Wabunge walikuwepo mle ndani, tumekubaliana kwamba viuatilifu vyote na pembejeo zote ziwafikie kabla ya msimu na kwa idadi ambayo Vyama vya Msingi vitakuwa vimewasilisha katika Kamati ile ya Pembejeo. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge na kwamba Serikali itasimamia kuhakikisha viuatilifu hivi vinawafikia wakulima kwa wakati ili kuondokana na changamoto ambazo zilikuwa zinawakumba wakulima katika misimu iliyopita.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu namna ambavyo uzalishaji utaongezeka na Serikali imejipangaje katika kuhakikisha kwamba soko linakuwepo? Moja ya mkakati tulionao mkubwa ni kuhakikisha tunawawezesha wabanguaji wadogo ili kuongeza ubanguaji wa korosho ghafi na kutengeneza masoko ya uhakika ya korosho ambayo imechakatwa.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa tumeendelea kutafuta masoko nje ya nchi na wiki iliyopita mimi mwenyewe nimekwenda uwanja wa ndege kusindikiza kontena la korosho iliyobanguliwa ambayo tumepata soko Marekani na kilo moja kule inauzwa 90,000/= ambayo ni uhakika mkubwa kwa mkulima wa korosho. Hivyo mkakati wa Serikali ni kuhakikisha tunawawezesha wabanguaji wadogo na kuwajengea uwezo ili tuachane kuhangaika na soko hili la Vietnam na India ambalo limekuwa na changamoto kubwa sana ya bei.
MHE. NANCY H. NYALUSI: Mheshimiwa Spika, skimu ya umwagiliaji ya Mgololo ambayo ina hekta 700 ilijengwa na Serikali kwa shilingi bilioni 1.9 ambayo ilikamilika mwaka 2012, mwaka 2013 ikaanza kutumika na mwaka 2013 hiyo hiyo mifereji ikaanza kuvujisha maji kwa sababu ilikuwa ni mibovu.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kumaliza kujenga mifereji hiyo ili kuokoa pesa yake iliyotolewa, lakini pia kwa sababu mradi huo haujakamilika na haujawanufaisha wananchi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nancy Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli Skimu hii ya Mgololo ni muhimu kwa sababu inahusisha Kata mbili za Makungu na Kiyowela na humo ndani kuna vijiji zaidi ya tisa ambavyo vinanufaika na mradi huu. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika bajeti yetu inayokuja tutauingiza mradi huu kwa ajili ya utekelezaji ili kuweza kurekebisha mapungufu yote na uweze kuwanufaisha wananchi, hasa wa Vijiji vya Lugolofu, Kitasengwa, Lugema, Mabaoni, Makungu na Lole.
MHE. DANIEL A. TLEMAI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi; je, Serikali itajenga lini skimu ya umwagiliaji katika Bonde la Eyasi ili kuboresha kilimo cha umwagiliaji unaoendelea kwenye bonde hilo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Daniel Awack Tlemai kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika bajeti yetu ya mwaka huu wa fedha Skimu za Eyasi zimebainishwa kuwa ni sehemu ya utekelezaji katika bajeti hii na katika utekelezaji wa mradi huo hivi sasa tupo katika hatua ya manunuzi ya kumpata mkandarasi ili utekelezaji uanze mara moja.
MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, ni nini mkakati wa Serikali wa kuwasaidia wananchi na wawekezaji katika Kata ya Mtunda kwenye Jimbo la Kibiti katika miundombinu ya umwagiliaji ukizingatia kwamba kuna uwekezaji mkubwa sana wa kilimo cha mpunga umefanyika pale na unaendelea wa ekari zisizopungua 20,000?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Twaha Mpembenwe, Mbunge wa Kibiti, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo tumekuwa tukisema hapa tunatambua kwamba Bonde la Rufiji ni kati ya mabonde muhimu katika kilimo cha umwagiliaji hapa nchini Tanzania na ndiyo maana katika mkakati wetu wa mwaka huu katika bajeti yetu, tumeamua kuyapitia mabonde yote 22 likiwemo Bonde la Rufiji kwa lengo la kuhakikisha kwamba tunafanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili baadaye tuje tutekeleze miradi mikubwa ya umwagiliaji ambayo pia itawagusa wananchi wa Mheshimiwa Mbunge.
MHE. KENNETH E. NOLLO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa na mimi nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Skimu ya Kongogo ni moja ya skimu ambazo ziliwekwa kwenye bajeti ya 2022/2023; je, Serikali imefikia wapi katika kuanza utekelezaji wa ujenzi wa skimu hiyo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kenneth Nollo, Mbunge wa Bahi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli Skimu ya Kongogo ipo katika bajeti ya mwaka huu na hatua ambayo tumeifikia, mkandarasi ameshapatikana na muda wowote kuanzia hivi sasa atakwenda kuanza utekelezaji wa ujenzi wa skimu hiyo.
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, Skimu ya Arusha Chini iliyopo Halmashauri ya Mji wa Nanyamba ni miongoni mwa skimu ambazo zitafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu kwa mwaka huu wa fedha; je, ni lini kazi hiyo itaanza?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, Mbunge wa Nanyamba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli skimu hii ilibainishwa na kuwekwa katika mpango wetu wa utekelezaji katika mwaka huu wa fedha. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba hivi sasa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeendelea kufanya kazi ya kukamilisha taratibu zote kwa ajili ya manunuzi na hatua nyinginezo ili kazi hizi zianze kwa uharaka.

Mheshimiwa Spika, kufikia Disemba mwaka huu tutakuwa tumefika hatua kubwa sana katika miradi yote, na hivyo nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba katika kipindi hiki cha muda mfupi, eneo lake hilo pia litajumuishwa na tutaanza kazi hiyo ya usanifu na upembuzi.
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwenye Mradi wa Songwe River Basin kuna package inayounganisha eneo la umwagiliaji la hekta zaidi ya 3,500 pale Kyela.

Je, Serikali imefikia wapi kuungana na Malawi kuanza kutekeleza mradi huu?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ally Mlaghila Jumbe, Mbunge wa Kyela, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama alivyosema muuliza swali, Mheshimiwa Mbunge, amelitaja Bonde la Mto Songwe ambalo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huu. Kazi ambayo Wizara inafanya hivi sasa ni kuhakikisha tunaendelea na kazi ya upembuzi yakinifu wa haya mambonde yote, lengo letu kubwa ni kuwa na miradi mikubwa ambayo itahusisha miradi ambayo pia Mheshimiwa Mbunge ameitaja.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo mwaka huu wa fedha tayari tumeshawapa kazi washauri elekezi kwa ajili ya kuanza kazi hii na tunategemea kwamba mabonde yote yale 22 kuanzia Bonde la Ziwa Victoria, Malagarasi, Manonga, Wembele, Bonde la Ruvuma, Bonde la Rufiji, Bonde la Mto Songwe, Ifakara Idete, Kilombero, Mkomazi, haya yote yapo katika mpango na yatakwenda kukata kiu ya wakulima wa Tanzania. (Makofi)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, nafurahi sana.

Je, Mheshimiwa Waziri anaweza akaniambia ni lini ukarabati wa skimu zilizo kwenye Kata ya Kahe Magharibi na mifereji iliyo kwenye Kata za Marangu Mashariki, Kirua Vunjo na Kilema utafanyika?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Charles Stephen Kimei, Mbunge wa Vunjo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tuna orodha ya miradi mingi sana ambayo mwaka huu wa fedha tunaifanyia kazi. Hivyo, nitaomba mimi na Mheshimiwa Mbunge tukae tuangalie maeneo ambayo tutayafanyia utekelezaji mwaka huu katika Mkoa wa Kilimanjaro ni yapi, na ya mwaka unaokuja ni yapi, ili kama hayapo katika mwaka huu wa fedha basi tuyaingize kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha. Lakini lengo letu ni kuhakikisha mifereji yote hii inafanyiwa kazi na wakulima wa kutoka Jimboni kwa Mheshimiwa Kimei wanapata fursa ya kilimo cha umwagiliaji.
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru.

Mheshimiwa Spika, Skimu ya Umwagiliaji ya Kidoka ni kati ya skimu zilizopo kwenye Mkoa wa Dodoma, lakini skimu ile miundombinu yake imekuwa chakavu na wakulima wetu wamekuwa wakijiendesha kwa hasara sana kutokana na gharama kubwa za umeme wanazozitumia ku-pump maji.

Je, ni lini sasa Serikali mtakwenda kuweka miundombinu rafiki ya skimu ile ili wananchi wetu waweze kujiendesha vizuri kwa faida? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kunti Yusuph Majala, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, moja kati ya kazi kubwa ambazo tuliwapa watu wa tume ni kuhakikisha wana-take stock ya miradi yote ambayo imekwama na yenye changamoto, na tumekamilisha zoezi hilo. Hivi sasa ni kuanza kupitia na kuona namna gani tunaweza tukaboresha skimu hizo.

Mheshimiwa Spika, nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba nitatoa maelekezo kwa watu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha Jumatatu wawepo katika eneo la Kidoka kuangalia changamoto ni ipi na tuone namna ya kuweza kurekebisha skimu hiyo.
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Kalenga lina skimu 19 na nyingi ni chakavu; je, ni lini sasa Serikali itatenga bajeti kwa ajili ya ukarabati huo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Jackson Gedion Kiswaga, Mbunge wa Kalenga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema wakati najibu swali la Mheshimiwa Kunti, tunayo stock ya miradi yote ambayo ina changamoto na nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaingiza miradi yake pia katika mpango wetu na tutaipitia kuona inahitaji marekebisho gani.

Mheshimiwa Spika, lakini lengo letu kubwa hasa; sisi tulifanya kazi ya kupitia miradi yote, tunataka tufanye kilimo cha umwagiliaji kwa hiyo hatutaliacha eneo lolote, tutayafikia maeneo yote. Lengo letu ni kwenda katika kilimo cha umwagiliaji. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge.
MHE. FRANCIS L. MTEGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Wakulima wa skimu za umwagiliaji Matebete, Chosi, Herman, Isenyela wanapata shida sana wakati wa uhaba wa mvua kwa kupeana zamu usiku, na wengi wao wanazunguka na mapanga usiku kucha.

Je, Serikali itawaboreshea skimu hizi lini ili kuondoa adha hii na waweze kulima kwa tija?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika eneo la Mbarali tuna miradi ya umwagiliaji ambayo tumeitengea fedha ya kiasi cha shilingi bilioni 61 ambayo inahusisha Herman Chosi, Bonokuva Gigolo na kwenda katika Matebete, tunakwenda Ifenyela na Uturo. Haya yote niliyoyataja wakandarasi wameshapatikana na muda wowote kazi ya utekelezaji wa miradi hii unaanza.
MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Spika, wananchi wa Tarafa ya Malangali hususan Kata za Nyololo, Maduma, Ihoanza, Idunda mpaka Mbalamaziwa wanafuatilia kwa umakini sana pengine kufahamu commitment ya Serikali, ni lini sasa kwa maana kama ni mwezi au kama ni mwaka wa fedha watapata matumaini ya kupata huu mradi wa umwagiliaji kutokana na changamoto kubwa sana ya ukame kwenye maeneo yao?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kilimo cha umwagiliaji na Serikali pia inatambua kwamba eneo la Mufindi ni kati ya maeneo ambayo kuna wakulima wengi na uzalishaji wake utaongeza tija kwenye kilimo cha nchi yetu ya Tanzania. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika bajeti inayokuja kwa maana kuanzia mwezi Julai tutatenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba uhakiki huo unakamilika, tukisha-establish mahitaji baada ya hapo sasa tutakwenda kwenye hatua inayofuata ambayo itakuwa ni hatua ya ujenzi kutokana na mahitaji.

Mheshimiwa Spika, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge na kwamba zoezi hilo litaanza mapema mwezi wa Saba ambapo uhakiki huu utafanyika na baadaye tutaenda katika hatua ya ku-establish mahitaji.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Bwawa la umwagiliaji la Edayaya Tlawi katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu ilifanyiwa usanifu toka 2009; je, ni lini sasa Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hilo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zacharia Issaay, Mbunge wa Mbulu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, moja kati ya mikakati ambayo tumeiweka hivi sasa kama Wizara, tumeiagiza Tume ya Umwagiliaji wa Taifa ku-take stock ya miradi yote ya umwagiliaji katika nchi yetu ya Tanzania ile ambayo ilishafanyiwa upembuzi yakinifu ambayo ilishafanyiwa usanifu na baadaye kinachofanyika ni kwamba tutakwenda katika mradi mmoja baada ya mwingine iko miradi ambayo inahitaji fedha kidogo na iko miradi ambayo inahitaji fedha nyingi.

Mheshimiwa Spika, kupitia maelekezo haya ambayo Mheshimiwa Waziri ameyatoa, Tume hivi sasa wameanza zoezi hilo. Tutaipitia miradi yote na hivi sasa tunayo miradi 51 ambayo imeshatangazwa kupatikana kwa wakandarasi, naamini kupitia utaratibu huu ambao tumeuanzisha, tutaifikia miradi yote ikiwemo mradi ambao Mheshimiwa Mbunge ameusema.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa katika Manispaa ya Iringa katika Kata ya Isakalilo kuna Mradi wa Mkoga katika Kata ya Kituli kuna Mradi wa Kitwilu. Hii miradi ni ya muda mrefu sana. Je, ni lini Serikali itaona umuhimu wa kutoa pesa ili wananchi hasa akinamama na vijana waweze kujiajiri kupitia hii miradi kwa kulima mbogamboga na matunda?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ritta Kabati, Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Iringa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katika majibu yangu ya awali kwamba miradi yote hii na hasa katika Mkoa wa Iringa tumeshatenga fedha tayari kwa ajili ya Tume yetu kukamilisha kazi hii ya uhakiki. Bahati nzuri Mheshimiwa Rais ametuongezea bajeti kutoka shilingi bilioni 17 mpaka bilioni 51, nataka nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba katika kuelekea ajenda 1030 ya kukuza kilimo katika nchi yetu, moja ya kipaumbele ni kilimo cha umwagiliaji, hivyo hatutaacha mradi wowote nyuma, miradi yote tutajenga tukipata fedha ambazo zitatuwezesha kufikia malengo hayo.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi hii. Naomba nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri; je, mifereji iliyo kwenye Kata ya Kilema na Kirua Vunjo na ile skimu ya Kahe wanaifahamu? Mbona haijawahi kuangaliwa siku za karibuni? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Charles Kimei, Mbunge wa Vunjo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, miradi yote ya umwagiliaji nchini inafahamika na ndiyo maana katika maelezo yangu ya awali nilisema tunayo miradi mingi sana. Tumeielekeza Tume badala ya kuendelea kukumbatia miradi mingi ambayo haifanyi kazi, tunaanza ku-take stock kupata mradi ambao unahitaji marekebisho madogo, mradi ambao unahitaji marekebisho makubwa, baadaye tuweke nguvu kukamilisha miradi hii ikiwemo mradi wa Mheshimiwa Mbunge.
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niulize swali dogo la nyongeza. Kuna bwawa kubwa pale Kijiji cha Nyamgogwa, Kata ya Shabaka tumeshafanya upembuzi yakinifu na tumeshapeleka andiko mezani kwa Mheshimiwa Waziri, tunahitaji milioni 500 kwa ajili ya kulifufua ama kuliandaa bwawa hilo ambalo linanufaisha zaidi ya vijiji 20. Je, Waziri anatoa majibu gani kuhusu andiko letu hilo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hussein Amar, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge andiko lake kweli lipo mezani na hivi sasa kwa sababu ya ufinyu wa bajeti tumekuja na mfumo mwingine ambao pia umesaidia ujenzi wa skimu hizi ambao tunakwenda kuutambulisha mfumo huu. Nimuahidi tu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba na yeye pia tutamuingiza kwenye mfumo huo ambao tumeufanya na tumeanza kuufanya kwa Mheshimiwa Mtaturu pale katika miradi ya Magonyi.

Mheshimiwa Spika, mfumo huu tutamchukua benki, tutamchukua na off taker wa mazao ya wakulima na kwa pamoja tunamwomba benki arekebishe miundombinu ya eneo lile, halafu mazao yatakayolimwa katika eneo lile tutamtafuta muuzaji ili basi itumike gharama hiyo ya benki kurekebisha. Wakati huo huo wauzaji wapate uhakika wa mazao yao ya kilimo na mwisho wa siku tutakuwa tumetatua changamoto ya ukosefu wa masoko ya wakulima wetu, lakini pia mradi huu utakuwa umekamilika. Mfumo huu unaitwa Tripartite Agreement ndiyo ambao tunaenda kuutekeleza katika miradi mingi ya skimu za umwagiliaji. (Makofi)
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwa sababu miradi mingi ambayo Serikali inaiongelea ni ile ambayo ilijengwa miaka ya zamani na teknolojia ambayo imekuwa ikitumika ni ile ambayo ni ya mifereji ambayo inatumia maji mengi sana na inaharibu maji unnecessary. Kuna teknolojia mpya ambayo inatumika na tunaona katika nchi za jirani. Je, Serikali iko tayari kwenda kutumia teknolojia mpya ambayo inatumia maji kidogo lakini inakuwa na ufanisi zaidi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Josephat Kandege, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama Serikali tupo tayari kuendelea kutumia teknolojia ambayo italeta ufanisi katika kilimo cha umwagiliaji na hivyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, bahati nzuri Mheshimiwa Waziri na mimi mnatuona pale ni vijana ambao pia ni wa kidigitali, kwa hiyo tutahakikisha ya kwamba tunapitia kuona mifumo mbalimbali hasa yenye kuleta ufanisi ambayo naamini kabisa kama ni mfumo ambao Mheshimiwa Mbunge ameuzungumza hapa ambao utaleta tija kwa wakulima wetu sisi tuko tayari kuutumia mfumo huu na tutaelekeza pia Tume ya Umwagiliaji kuhakikisha kwamba inafanya utafiti wa kugundua teknolojia mbalimbali ili kumletea tija mkulima wetu wa Tanzania. (Makofi)
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya swali la nyongeza. Kwa kuwa wananchi wa Tarafa ya Gonja katika Wilaya ya Same kwa takriban miaka kumi sasa wameomba kujengewa Bwawa la Yongoma ili lisaidie umwagiliaji katika Kata kame za Ndungu na Maore na design ilishafanywa na wajapan tangu 2012. Je, ni lini Serikali itajenga bwawa hili? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kaboyoka, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika bajeti inayokuja mwaka 2022/2023 tumetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa 19, natumai pia na bwawa la Mheshimiwa litakuwemo ndani ya ujenzi huo. (Makofi)
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nashukuru kwa majibu ya Serikali. Ninayo maswali mawili ya nyongeza: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa katika Bajeti ya mwaka huu Serikali ya Awamu ya Sita imeongeza fedha hadi kufikia takribani shilingi bilioni 954; ni kwa nini Serikali haikuweka kipaumbele cha ujenzi wa soko hili katika hizo fedha?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Mkoa wa Songwe ni moja ya mikoa ya kimkakati, ambayo inapakana na nchi mbalimbali jirani na ambao unaongoza katika uzalishaji wa chakula, ni mkoa wa tatu kwa uzalishaji wa chakula.

Je, ni upi mkakati wa Serikali wa kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa soko hili muhimu kwa wananchi wa mkoa huo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Japhet Ngailonga Hasunga, Mbunge wa Vwawa, kwa pamoja kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza tunampongeza Mbunge kwa kazi kubwa aliyoifanya kuhakikisha kwamba eneo lile linapatikana kutokea TACRI. Pili, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba tunatambua umuhimu wa Mkoa wa Songwe katika kilimo cha nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba suala hili tutalipa kipaumbele katika bajeti inayokuja ili basi wananchi wa Mkoa wa Songwe na hasa wakulima wa mazao mbalimbali waweze kupata fursa hii ya kuwa na kituo cha mazao; na kwa sababu pia Songwe inaungana na nchi nyingine, itakuwa ni fursa ya kipekee kwa wananchi wetu kupata masoko ya uhakika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tunalipa kipaumbele na ataona katika bajeti inayokuja.
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Serikali iliahidi kujenga Soko la Kimataifa katika Kijiji cha Itetemya, Kata ya Karema ambacho kingewasaidia kuunganisha kati ya nchi ya DRC Congo na wananchi hao: Je, ni lini huu mradi ambao iliahidi takribani miaka mitano iliyopita utatekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Moshi Kakoso, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Serikali ilishatoa ahadi juu ya ujenzi wa soko katika eneo hilo. Nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba hivi sasa kati ya maeneo ambayo tunayapa kipaumbele ni ujenzi huu wa masoko. Nimwondoe hofu kwamba katika mikakati yetu inayokuja tutaunganisha masuala ya miundombinu ya masoko tunayoyafanya na ujenzi wa masoko hayo, pamoja na kumkumbuka katika eneo lake. Hivyo Mheshimiwa Mbunge atupe nafasi katika bajeti inayokuja pia tutaikumbuka katika eneo lake hilo.
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kuniona niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Kuna Soko la Kimataifa lililoanza kujengwa katika Kitongoji cha Nzaza Kata ya Kabanga Wilayani Ngara 2014 na ujenzi huo ukasimama ghafla: Je, ni lini Serikali itamalizia ujenzi huo wa soko hilo kwa manufaa makubwa ya wananchi wa Ngara na wakulima kwa ujumla? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza Mheshimiwa Oliver Semuguruka, Mbunge Viti Maalumu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, soko lilopo pale Kabanga katika Wilaya ya Ngara ni kati ya masoko sita ambayo Wizara imepanga kuyamalizia katika mwaka huu wa fedha. Hivyo soko hili lipo katika mpango na litatekelezwa.
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kuuliza maswali mawili. Kwa kuwa mwaka 2021 tulipitisha bajeti kubwa na tukasema kwamba sasa mbegu zitatolewa na ruzuku, lakini mpaka sasa hivi mbogwe hatujaona kitu chochote. Majibu yake yakoje?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; nina imani hujawahi kufika katika Wilaya ile: Je, uko tayari kuongozana nami baada ya Bunge ili ukaangalie maeneo ya Mbogwe, maana ni maeneo yanayofaa sana kwa kilimo? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Nicodemas Henry Maganga, Mbunge wa Mbogwe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la ruzuku la mazao hasa ya kimkakati yanaendelea kuratibiwa na bodi husika. Natoa maelekezo kwa bodi husika kuhakikisha kwamba wakulima wa pamba katika mikoa ambayo ameitaja Mheshimiwa Mbunge waweze pia kufikiwa na ruzuku hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kuhusu mimi kwenda Mbogwe, baada ya kikao hiki cha Bunge, niko tayari kuongozana na Mheshimiwa Mbunge kwenda kuangalia suala la kilimo katika eneo lake la Mbogwe.
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa nafasi hii. Serikali iliahidi kufanya ukarabati wa Skimu za Chikuyu na Udimaa: Je, ni lini sasa Serikali itatekeleza ahadi hii? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Pius Chaya, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Skimu za Chikuyu na Udimaa ni skimu ambazo kama Naibu Waziri nimeshakwenda kuzitembelea, nimeziona na tumebaini changamoto yake. Ninavyozungumza hivi sasa, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Umwagiliaji na timu yake wanaelekea katika maeneo hayo kwa ajili ya kukamilisha kazi ya kupitia upya michoro na kuanza utekelezaji wa miradi ambayo itawafanya wananchi waendelee na kilimo cha umwagiliaji.
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza; je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Skimu ya Kata ya Endagaw ilhali tayari ilishatoa zaidi ya shilingi milioni 800 na bado haijaanza kufanya kazi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Asia Halamga, Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Manyara, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Skimu aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge ipo katika utekelezaji wa Bajeti ya mwaka huu, zoezi la utekelezaji linaendelea.
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi. Je, ni lini Serikali itamalizia ujenzi wa skimu zilizojengwa katika Jimbo la Mhambwe, ikiwemo Nyendara, lumpungu, Kigina, Mgondogondo, Kahambwe, lili ziweze kuwasaidia wakulima wa jimbo hili?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika moja ya mikakati tuliyonayo katika mwaka huu wa fedha ni kuhakikisha tunakarabati na kukamilisha skimu ambazo tulizipitia na kuona zinahitaji marekebisho madogo ili wananchi waendelee kutumia kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba katika baadhi ya skimu katika Jimbo lake zitatekelezwa mwaka huu na nyingine katika mwaka ujao wa fedha. (Makofi)
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Swali langu la kwanza; ili zao hili liweze kufufuka na kuleta tija sio kupeleka mbegu bora tu ni pamoja na kutafuta masoko mazuri nay a uhakika ili wakulima waweze kuuza. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha masoko ya uhakika yanapatikana?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; sisi Mkoa wa Mtwara muhogo ukilimwa unastawi kweli kweli lakini tunashindwa kulima kwa sababu hakuna kiwanda cha kuongeza thamani ya zao la muhogo. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha inajenga kiwanda yenyewe ama kushirikiana na sekta binafsi ili kuongeza thamani ya zao la muhogo? Nakushukuru.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Tunza Issa Malapo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika swali la kwanza la kuhusu masoko hivi sasa Wizara tumeendelea kuimarisha huduma za masoko kwa kuhakikisha kwamba mazao yetu mengi tunayatafutia masoko, ili wakulima wetu wakilima kwa tija mwisho wa siku mazao yao yaweze kupata masoko ya uhakika. Nataka nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba moja kati ya mkakati tulionao hivi sasa ni kufanya muhogo kama sehemu ya malighafi kuu katika viwanda vyetu ambavyo tumeanza mazungumzo nao kwa ajili ya kutengeneza wanga ambao hivi sasa tunaagiza karibuni tani 8,000 kwa mwaka. Kwa hiyo, tumeanza mazungumzo na viwanda vilivyoko hapa nchini kwa ajili ya kufanya muhogo kama malighafi ya utengenezaji wa wanga. Zoezi hilo linakwenda vizuri na mwitikio umekuwa mkubwa na ndio maana sasa tumeendelea kuhamasisha wakulima wengi zaidi kulima muhogo.

Mheshimiwa Spika, la pili, kuhusu viwanda. Ni kweli mwisho wa siku kama Wizara katika mkakati wetu ni kuhakikisha kwamba tunaongeza thamani ya mazao yetu na kwa upande wa muhogo viko viwanda ambavyo mwanzoni vilionesha nia ya kuanza kufungua katika upande wa kule Kusini. Kwenye Kijiji cha Malamba katika Jimbo la Mtama ipo kampuni ambayo ilifungua kiwanda, Kampuni ya Cassava Starch of Tanzania Corporation bahati mbaya sana walipata changamoto ya mtaji na hivi sasa wana administration order ya Mahakama ya Biashara Management wameamua kukichukua kiwanda kile na wanatafuta wawekezaji. Wameshakuja wawekezaji kutoka Japan na maeneo mengine na sisi kama Wizara tunaendelea kuwasaidia kutafuta wawekezaji ili kiwanda kile kifufuliwe na kiwe sehemu ya uchakataji wa muhogo ya wakulima wa Mkoa wa Mtwara, Mkoa wa Lindi na Mikoa yote ya Kusini. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali iliahidi Bilioni 150 katika kutoa fedha kwenye ruzuku na imetoa Bilioni 50 tu, sasa haioni sababu ya kuongeza hiyo Bilioni 100 iliyobaki ili mbolea iweze kupatikana kwa wingi zaidi?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, tunaomba Serikali iongeze speed kusajili mawakala ambao watasaidia mbolea ipatikane kwa wingi, kwa maana mawakala waliopo ni wachache na inakuwa na uzito mkubwa sana wa kupeleka mbolea mpaka kule vijijini. Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Sophia Hebron Mwakagenda, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza kuhusiana na fedha za ruzuku, kama ambavyo yalitolewa majibu na Mheshimiwa Waziri hapa, fedha zinaendelea kuletwa kwa ajili ya kushughulikia suala la ruzuku ya mbolea na nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba yale yote ambayo tuliyaahidi tutayasimamia ili wakulima wetu waweze kupata mbolea na Wizara ya Fedha wameendelea kushirikiana nasi kwa ukaribu sana.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu speed ya usajili wa mawakala, tumetoa maelekezo hivi sasa ya kuwataka Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa katika maeneo amabako mbolea hazifiki kwa wakati na wakulima wako mbali, kuanza kusajili vituo vingine vipya ili kuwarahisishia huduma wakulima na mbolea hizo ziweze kuwafikia kwa uharaka. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba zoezi hilo linaendelea na usajili umeendelea kusajili vituo vingine vipya.
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, ninaishukuru Serikali kwa mbolea ya ruzuku lakini kwa kuwa mbolea hii tangu tumepitisha bajeti hapa, maeneo kama ya Kagera ambao tunakuwa na msimu wa kilimo umeshapita na mbolea haikupatikana kwa wakati kwa sababu mawakala hawapo kabisa.

Je, ni nini kauli ya Serikali kwa wananchi hususan wa Wilaya ya Bihalamuro ambao wamekosa kabisa mbolea hii ya ruzuku ili kipindi cha msimu unaofuata waweze kuwa na matumaini ya kupata mbolea hii kwa wakati?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ezra Chiwelesa, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli tulipata changamoto ya mfumo wa usambazaji, ambao hivi sasa tumeendela kuurekebisha na hivi sasa tumeruhusu pia usajili wa vyama vya ushirika, kuwa kama sehemu ya wasambazaji wa mbolea vilevile na vyama vya wakulima vilivyosajiliwa na pia tutatumia baadhi ya maghala yaliyokuwa katika mradi wa MIVARF kama sehemu ya usambazaji wa mbolea hizi. Kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba katika kipindi kinachokuja changamoto hii haitajirudia tena, tutahakikisha kwamba mbolea inawafikia wakulima kwa wakati lakini katika maeneo yao walipo pia.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Msheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kumekuwa na malalamiko na changamoto kadhaa kwa upatikanaji wa mbolea na bei kuwa juu. Je, Serikali ina mpango gani wa kushajihisha kilimo hai ambacho kinatumia mbolea asilia na kina gharama nafuu ambazo pia hakitumiii kemikali na vilevile ina uwezo wa kuhuisha afya ya udongo na afya zetu?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Asha Juma, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Wizara tumekuwa tukifanya jitihada mbalimbali za kuwakaribisha wadau mbalimbali wanaozalisha mbolea ambao ni organic na habari njema tu ni kwamba nilipata nafasi ya kwenda katika maonesho ya kilimo hai Ujerumani na tukakutana na wawekezaji wengi ambao wameonesha nia ya kuja uwekeza hasa katika Mkoa wa Lindi na Mtwara. Hivyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba mbolea hii pia inazalishwa ili kupunguza gharama hii kwa wakulima.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Zao la pamba ni kati ya mazao ya kimkakati hapa nchini lakini wakulima wake bado wanazalisha kilo 300 mpaka 400 kwa heka moja.

Je, ni nini mkakati wa Serikali sasa kwa wakulima hawa waweze kuzalisha kilo 500 mpaka 1,000 kwa heka moja?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika napenda kujibu swali la Mheshimiwa Emmanuel Cherehani, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, anachokizungumzia Mbunge hapa ni tija na sisi tumejipanga katika Wizara kuhakikisha wakulima wetu wanalima kwa tija. Kwanza, kabisa kuwasaidia kupata viuatilifu sahihi; pili, kuwasaidia kupata teknolojia za kisasa za kilimo cha pamba; na tatu, ni kuhakikisha kwamba wanajifunza kanuni bora za kilimo kama ambavyo hivi sasa tumeona kule kupitia TARI na Balozi wa Pamba juu ya mfumo mpya wa spacing ambao umesaidia sana kuongeza uzalishaji katika zao la pamba.

Kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba, tunatambua changamoto hizo na tumejipanga kuhakikisha kwamba mkulima wa pamba anazalisha kwa tija.
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninayo maswali mawili ya nyongeza. Swali kwa kwanza; kwa kuwa tayari ipo Sheria ya Mbegu ya Mwaka 2003 ambayo ilifanyiwa maboresho mwaka 2014, je, kwa nini Serikali ianzishe upya mchakato wa kuleta sheria mpya badala ya kuongeza kwenye hii Sheria ya Mbegu iliyopo ya mwaka 2003 utambuzi wa mbegu za asili kwa kuwa sheria hii inatambua mbegu za kisasa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; naipongeza Serikali imeanzisha hiki Kitengo cha Taifa cha Kuhifadhi Vinasaba vya Mimea ikiwemo mbegu za asili, lakini tokea mwaka 2005 zaidi ya miaka 15, Sheria ya National Plant Genetic Resource Act bado haijawahi kupitishwa, kwa hiyo kitengo hiki kimsingi hakina meno wala hakiwezi kutambua wala kulinda mbegu za asili ikiwemo na hivi vinasaba na ikiwemo pia kulinda hakimiliki ya mbegu zetu za asili…

NAIBU SPIKA: Swali.

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Je, Serikali itailleta lini Bungeni Sheria hii ya National Plant Genetic Resource ili tuweze kuhakikisha kwamba kitengo hiki kinafanya kazi ipasavyo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Neema Kichiki Lugangira, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo anakuwa mfuatiliaji mzuri wa masuala haya, lakini swali lake la kwanza ni kwamba, tumepokea wazo lake la maboresho ya sheria iliyopo lakini pamoja na hiyo sheria aliyouliza katika swali lake la nyongeza ni sheria ambayo ndio itakuja hasa kuja kuzitambua na vilevile kuzungumzia usajili wa mbegu za asili, ambao sheria hii mpaka hivi sasa ipo katika ngazi ya IMTC. Tunaamini kabisa taratibu zinaendelea vizuri na sheria hii italetwa hapa Bungeni ili iweze kupitishwa na basi tuwe tuna sheria ambayo itakuwa inatambua lakini vilevile ambayo itakuwa ina usajili mbegu za asili kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge.
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa niulize swali moja la nyongeza. Korogwe Vijijini inazo Tarafa tatu ambazo zina jiografia ngumu sana, Tarafa ya Magoma, Mombo na Bungu. Mheshimiwa Mbunge Mnzava anataka kujua kwa nini Serikali isiweke kituo kingine cha pili katika eneo la Makuyuni ambako ndio Makao Makuu ya Halmashauri ili iweze kuhudumia Tarafa zilizobaki za Mombo na Mashewa.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu Mheshimiwa Reuben Kwagilwa, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo hilo la Makuyuni tutaipeleka hii selling point yetu na niwaondoe hofu wananchi wa Korogwe Vijijini watanunua mahindi kupitia eneo hilo la Makuyuni.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Tunaishukuru Serikali kwa kutoa chakula cha gharama nafuu. Je, Serikali ina mkakati gani kwa kaya ambazo hazina uwezo wa kununua chakula kwa sasa ili itoe chakula cha msaada?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, zipo taratibu ambazo huwa zinapelekea Serikali kufikia hatua hiyo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameiomba, nimwombe tu Mheshimiwa Mbunge kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, zipo taratibu za kwenda ofisi ya Waziri Mkuu ambayo pia wao wamekuwa wakiwasiliana nasi juu ya namna ya kupeleka chakula hiki cha msaada katika baadhi ya maeneo.
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Katika Jimbo langu la Kalenga hasa Tarafa ya Kalenga tulipata shida ya mvua na tayari kata zile tumeshaleta maombi. Je, ni lini sasa Wizara itatupelekea chakula kwa haraka ili wananchi wangu wasife?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kiswaga, Mbunge wa Kalenga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama maombi yake yamekwishawasilishwa ndani ya Ofisi ya NFRA, nataka nimhakikishie ndani ya siku mbili zijazo, mahindi yatamfikia katika jimbo lake.
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa upandaji wa chakula unategemea gharama kubwa wanazozitumia wananchi katika kulima kwa maana ya kuchelewa kupeleka mbolea. Je, ni nini mkakati wa muda mrefu wa Serikali katika kuhakikisha wanapeleka mbolea kwa wakati ili wananchi waweze kulima kwa faida?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tumepata changamoto katika msimu huu wa upatikanaji wa mapema wa mbolea hasa ile ya kupandia, kukuzia na kunenepeshea. Nataka nimwondoe hofu kwa mfumo ambao tumeuweka kwenye msimu ujao, tutahakikisha wakulima wanapata pembejeo hizo kwa wakati ili waendane na msimu.
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya yangu ya Nanyumbu inakabiliwa na njaa kubwa kutokana na shambulio la panya ndani ya Wilaya yangu. Tuliandika barua tupatiwe chakula cha bei nafuu hadi sasa hivi hatuna majibu. Je, ni nini kauli ya Serikali?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Yahya Mhata, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nikimaliza kujibu maswali haya mimi na Mbunge tutakaa nione barua yake imefikia wapi, lakini nataka nimuahidi kwamba nitampelekea mahindi.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri aliyoyatoa Naibu Waziri, Mheshimiwa Antony Mavunde, nataka tuweke jambo hili vizuri kuhusiana na suala hili la njaa. Maeneo mengi Waheshimiwa Wabunge wamekuwa wakitoa taarifa kwamba, kuna shida ya upungufu wa chakula na kwa sababu hiyo sisi kwa mujibu ya Sheria ya Maafa, masuala ya chakula au upungufu wa chakula tunayachukulia kama ni maafa. Kwa tafsiri hiyo utaratibu wake ni kwamba, Halmashauri, Mkurugenzi anaandika barua kwa utaratibu wa kuleta kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu kupitia Mkoani, halafu barua ile inapelekwa kwa Waziri Mkuu, kwa ajili ya kupata kibali sasa ili chakula kile kiweze kutolewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu unaotumika sasa ni kama kila mmoja anaenda tu kiholela hivi, lakini kimsingi jukumu la kutoa kibali cha kwa ajili ya chakula ya bei nafuu au cha msaada ni jukumu la Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Waziri Mkuu itakachofanya ni kuwaelekeza Wizara ya Kilimo ili Wizara ya Kilimo sasa waielekeze NFRA kwenda kuangalia maeneo ya kupeleka, kuuzia kile chakula au mtu atakayenunua kile chakula na kwenda kukiuza kwa bei nafuu iliyopangwa. Kwa hiyo niwaombe sana ni kutokana na kukiukwa utaratibu huo, ndio maana mambo hayaendi pamoja na kuwa kwamba barua zimeandikwa.
MHE. HAMISI S. TALETALE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Moja ya changamoto kubwa ya wananchi wa Morogoro Kusini Mashariki na Morogoro Vijijini kwa ujumla ni ukosefu wa mitaji. Je, Serikali ina uratatibu gani wa kutuletea mitaji wana Morogoro Vijijini?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge Hamisi Shabani Taletale, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mitaji kwa wakulima ni suala ambalo tunalipa kipaumbele Serikali, tupo tayari kukaa na Mheshimiwa Mbunge pamoja na ushirika wa wakulima hawa ili tuangalie fursa ambayo wanaweza kuipata kuimarisha mitaji yao.
MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Skimu ya Mwakijembe wananchi wamekuwa wanasubiri kwa takriban miaka 14 sasa. Na kwa kuwa Bunge hili lilipitisha fedha mwaka huu kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu.

Je, Waziri yuko tayari kwenda kusimamia jambo hili ili upembuzi huo na usanifu ukamilike ndani ya mwaka huu tuliotengea fedha na mwaka ujao wa fedha kazi hii ya ujenzi iweze kuanza?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili skimu hii ilitumia zaidi ya bilioni moja na milioni mia mbili, fedha ambazo ni kama zilipotea kwa sababu skimu haijaweza kufanya kazi.

Je, Wizara iko tayari kwenda kuangalia kwa kina design itakayofanyika ili design hiyo ihusishe ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji na ujenzi wa mifereji ili skimu iweze kutumika kwa uhakika?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza kwa pamoja ya Mheshimiwa Dunstan Luka Kitandula Mbunge Mkinga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikiri Mheshimiwa Mbunge amekuwa mfatiliaj mzuri wa jambo hili; na ni kweli skimu hii imekaa muda mrefu. Kulikuwa na changamoto nyingi na hasa kutokana na kwamba katika miaka mingi iliyopita tume yetu haikuwa na uwezo mzuri sana ya kuweza kuisimamia miradi hii mikubwa. Hata hivyo tumefanya mabadiliko makubwa ambapo hivi sasa tumeshamwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha ya kwamba wanaipa kipaumbele skimu hii. Lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunafanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili changamoto zilizokuwa zinajitokeza katika miradi iliyopita zisiweze kujirudia, na ikiwemo hoja ambayo Mheshimiwa Mbunge ameisema, ya ujenzi wa mabwawa ili kuhakikisha upatikanaji wa maji wa mwaka mzima na wakulima wa eneo hilo waweze kufanya kilimo kwa mwaka mzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimwahidi Mheshimiwa Mbunge ya kwamba tutasimamia kwa ukaribu kabisa kazi hizi zifanyike mapema ili basi tutenge fedha kwa ajili ya ujenzi na wananchi waweze kunufaika na mradi huu.
MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Arumeru hususan Kata 13 ambayo ndio imekubwa na njaa imepakana na Longido, Ngorongoro na Monduli. Katika Wilaya hizo za Ngorongoro, Monduli na Longido chakula kimeuzwa shilingi 700 kwa wananchi, lakini katika upande wa Arumeru Magharibu chakula wananchi wanaambiwa wanauziwa shilingi 885.

Je, ni kwa nini bei katika Wilaya zingine ni shilingi 700 na Arumeru Magharibi ni shilingi 885 na wakati tuko sehemu moja na hali ni hiyo hiyo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa kuna hilo tatizo Waziri haoni haja ya kufika katika Jimbo la Arumeru Magharibi au Wilaya ya Arumeru ili aweze kuona hali halisi ilivyo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Noah Lemburis Saputu, Mbunge wa Arumeru Magharibi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, jambo ambalo Mheshimiwa Mbunge ameliuliza hapa tulishawasiliana naye na tulitoa ufafanuzi ambao nataka niurudie hapa.

Mheshimiwa Spika, hoja ya kwanza ya Mheshimiwa Mbunge ni juu ya kituo kuwepo katika eneo ambalo haligusi katika jimbo lake na hivyo wananchi katika eneo lake wanachukua umbali mrefu na bei imekuwa ikiongezeka sana kuweza kupata ile bei ambayo maeneo mengine wanapata.

Mheshimiwa Spika, nilishasema hapa Bungeni ya kwamba katika mazao haya ya mahindi ya bei nafuu, chakula cha bei nafuu kama Mheshimiwa Waziri alivyosema tunapeleke kwenye Halmashauri ya Wilaya na vituo ndiyo vinatengenezwa hapo, lakini ikitokea kwamba katika baadhi ya maeneo kuna umbali mrefu, NFRA tumeshawapa maelekezo ya kusogeza vituo hivyo ili kuweza kuwahudumia watu wote kwa ukaribu zaidi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo katika maelezo ya awali kama katika eneo lake alikuguswa mimi nitatoa maelekezo siku ya leo kuhakikisha kwamba NFRA wanaongeza vituo ili na jimboni kwake pia paweze kuguswa na iweze kupunguza pia hali ya bei kwa sababu moja kati ya changamoto kubwa inayosababisha pia ni kwa sababu ya umbali ambao wamekuwa wakiupiga NFRA.

Kwa hiyo, kwa ujumla wake tumwachie Mheshimiwa Mbunge ya kwamba tutahakikisha pia katika uongezaji wa vituo tutagusa na jimbo lake ili wananchi wake wasiende umbali mrefu na bei pia isiweze kuwa kubwa kama ilivyo hivi sasa. (Makofi)

SPIKA: Ameuliza kuhusu kwenda kujiridhisha.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kuhusu kwenda kujiridhisha hiyo ni kazi yangu mimi kama Naibu Waziri, nilitaka nimhakikishie kwamba nipo tayari baada ya Bunge hili nitakwenda katika eneo hilo kwenda kujiridhisha katika hali ambayo ameisema. (Makofi)
MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa kuwa Serikali imetuletea mahindi kwenye vituo viwili kwa maana ya Segese na Isaka na kuacha kata zingine 16 ambazo ziko umbali mrefu kutoka kwenye kata zile.

Mheshimiwa Spika, ahsante. Ni lini Serikali itawatuma NFRA kuja kuongeza idadi ya vituo kwenye kata ambazo ziko mbali na maeneo hayo husika?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Iddi Kassim, Mbunge wa Msalala kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, utaratibu wa chakula cha bei nafuu Halmashauri husika huwa wanatuambia eneo ambalo limeteuliwa, lakini kutokana na changamoto za wananchi wetu wanatoka maeneo ya mbali tumeishatoa maelekezo kwa NFRA kuhakikisha kwamba wanaongeza vituo zaidi ili wananchi wengi waweze kuhudumiwa kwa ukaribu. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba katika Jimbo la Msalala tutazingatia pia hiyo ili wananchi wake wasitembee umbali mrefu kufuata chakula hiki cha bei nafuu.
MHE. ROBERT C. MABOTO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, Halmashauri ya Mji wa Bunda kuna wananchi wanaishi zaidi ya kilometa 40 kuja Kata ya Bunda Store ambapo ndipo kituo cha kuuzia mahindi kilipo.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza kituo kingine cha usambazaji mahindi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Chacha Maboto, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kwamba kutokana na mahitaji hayo nitatoa maelekezo kwa Wakala wa Hifadhi ya Chakula kuhakikisha wanaongeza kituo kingine zaidi ili wananchi wasitembee umbali mrefu.
MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, ningependa kujua kwa vile kuna taasisi ya ASA ambayo Serikali iliipa dhamana ya kutoa mbegu katika msimu wa mwaka 2020/2021; zile mbegu hazikufanya vizuri na wakulima wengi ambao wamezitumia zile mbegu wamepata hasara.

Je, nini kauli Serikali katika kuwafidia wale wakulima ambao wamekula hasara kutokana mbegu zile za taasisi ya ASA? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Serikali mmejipangaje sasa kuhakikisha haitokei tena wakulima wadogo wadogo ambao wanapata mbegu kutoka taasisi ile ya ASA wakaingia tena hasara ili wakaendelea kuwa maskini zaidi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Chumbuni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli katika msimu alioutaja Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) alisambaza mbegu za alizeti ambazo katika baadhi ya maeneo zilifanya vizuri na pia katika baadhi ya maeneo hazikufanya vizuri.

Mheshimiwa Spika, ziko sababu nyingi zilizopelekea kutokufanya vizuri hasa kutokana na misimu ya kupanda na changamoto zingine zilizosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Iko mikoa ambako mbegu hizi zilistawi vizuri na wananchi wamevuna, wamepata mavuno makubwa na tumekuwa tukichukua kama sehemu ya kielelezo.

Mheshimiwa Spika, katika kuitatua changamoto hii katika mwaka huu wa fedha wa 2022/2023 Serikali imetenga fedha kuhakikisha kwamba tunazalisha mbegu, tunazigawa kwa ruzuku kwa wakulima ambazo ni certified seed tofauti na zile ambazo zimewekwa awali na lengo letu ni kuhakikisha kwamba wakulima wazipate mbegu hizi kwa bei rahisi ya ruzuku kwa kilo mbili kwa shilingi 10,000 ili ziweze kuwasaidia kutokana na changamoto ambayo waliipata.

Mheshimiwa Spika, vilevile tumehakikisha kuanzia hivi sasa tumempa maelekezo ASA tutaanza kuzalisha certified seeds ili wakulima wetu waweze kulima na waweze kupata tija kutokana na kilimo cha alizeti.
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, nilitaka kufahamu ni lini Serikali itakamilisha mchakato wa kuimarisha soko la zao la vanila mkoani Kagera? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Neema Lugangira, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli zao la vanila hivi sasa limeanza kupata muamko mkubwa na wakulima wengi wamehamasika kulima zao hili na sisi kama Serikali tumeendelea kufatilia hatua kwa hatua kuhakikisha kwamba tunaweka mazingira bora na wezeshi kuwafanya wakulima wetu waweze kunufaika na zao hili.

Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba ni sehemu pia ya mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba tunatengeneza miundombinu rafiki na mazingira rafiki ili wakulima wetu waweze kunufaika na uzalishaji wa zao la vanila.
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika ahsante, kwa kuwa zao la chikichi linastawi vizuri katika Bonde la Tanganyika na kwa kuwa chikichi inazalisha mafuta, lakini pia malighafi kwa ajili ya kutengenezea sabuni lakini pia mabaki yake yanatumika katika uzalishaji wa chakula cha mifugo.

Je, ni mkakati upi Serikali inauweka kutafuta wawekezaji wakubwa kama wale wa mashamba ya miwa katika bonde hili ili angalau kuziba nakisi hii? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, mkakati wa Serikali ni kuanza kuzungumza na wawekezaji wakubwa walionesha nia kuwekeza katika eneo ikiwemo Kampuni ya Wilmar, Kampuni ya Bakhresa na Mohamed Enterprises na mazungumzo yanakwenda vizuri na wako tayari kufanya uwekezaji huo pindi pale mashamba makubwa yatakapopatikana na tayari mashamba hayo hivi sasa wataalamu wetu wa Wizara ya Kilimo wapo kule kwa ajili ya upimaji wa afya ya udongo ili tukijiridhisha basi tuweze kukaa chini kuzungumza na hawa wawekezaji watumie mashamba hayo makubwa kwa ajili ya uzalishaji wa chikichi.
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Spika, ahsante; nini mkakati wa Serikali wa kuzalisha zao la karanga ili kuweza kuchakata mafuta ya karanga na kupunguza uagizaji mafuta kutoka nje? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge Fatma Toufiq, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mkakati mkubwa tulionao hivi sasa ni kuendelea kuisisitiza taasisi yetu ya kilimo (TARI) katika kuendelea kufanya utafiti na uzalishaji wa mbegu bora ili wakulima waweze kulima kwa tija na mwisho wa siku kama nchi tuweze kufikia malengo ya kuondokana na changamoto ya uagizaji wa mafuta.

Kwa hiyo, mazao ambayo tumeyapa kipaumbele katika kukamua mafuta ni pamoja na karanga, mchikichi pamoja na alizeti. Kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge nisehemu ya mkakati wa Wizara.
MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, mnamo mwezi Januari, 2008 Serikali ilituma wataalam kwenda kupima udongo katika vijiji hivyo vinne vya Mheza, Mpirani, Kadando na Maore; wananchi wanalipata matumaini makubwa sana, lakini mpaka sasa hivi hakuna kitu chochote kinachoendelea; nini kauli ya Serikali kwa wananchi hawa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; zao la mpunga ni zao la biashara ambalo wananchi wengi wanategemea katika maeneo hayo kwa ajili ya chakula pamoja na biashara ili kujikwamua kiuchumi.

Je, Serikali haioni umuhimu sasa wakufanya uharaka wa wa kuwajengea skimu hizo ili wananchi waweze kujikwamua kiuchumi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, la kwanza; kazi kubwa ambayo tuliifanya kama Serikali ni kuhakikisha tunaipitia miradi yote ya umwagiliaji na kujua changamoto zake.

Mheshimiwa Spika, hatua ya pili ilikuwa ni kwenda katika utengaji wa fedha ili kuweza kutatua changamoto hizo. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba pamoja na huo mwaka alioutaja, lakini tumeielekeza Tume ya Taifa ya Umwagaliaji kwa ajili ya kwenda kufanya upembuzi yakinifu ili miradi hii ijengwe katika kiwango ambacho kitakuwa kinakidhi mahitaji na mwisho wa siku tusirudie kulekule tulipotoka kurekebisha skimu hizi mara kwa mara.

Kwa hiyo, nimuondoe hofu yakwamba kazi inaendelea kufanyika hivi sasa ni kutenga fedha kwa ajili ya upembuzi yakinifu ili tujenge mradi huu kwa ukamilifu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu uharakishaji wa jambo hili; na sisi tunafahamu ya kwamba moja kati ya mazao makubwa ambayo tunayategemea sana ni mazao ya mpunga kwa ajili ya chakula na hivyo tutahakikisha kwamba tunaharakisha zoezi hili ili wakulima wa maeneo hayo waweze kulima kwa wakati na mwisho wa siku tuisaidie nchi yetu ya Tanzania kupata chakula cha uhakika.
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi; zao la chai linahitaji sana umwagiliaji, ni lini Serikali italeta hizo scheme kwenye maeneo ya Igominyi, Tarafa ya Igominyi kwa ajili ya umwagiliaji wa chai?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nimepokea swali la Mheshimiwa Mbunge, tutawaelekeza wenzetu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuyapitia maeneo hayo ili kama kuna uwezekano na maeneo hayo yanaruhusu kuweka skimu hizo tuweze kuifanya kazi hiyo kwa uharaka.
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itajenga Skimu ya Mogahay, Dirimu na Yaeda Chini?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hivi sasa tupo katika taratibu za kupitia skimu zote hizo kwa maana ya kuangalia status zake na hatua za kuchukua. Nimuahidi Mheshimiwa Mbunge ya kwamba pindi wataalamu wetu watakapopita na kuona hali ambayo imefikia tutaweka katika bajeti yetu ili tuweze kutekeleza mradi huo.
MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Spika, nini mkakati wa Serikali kuboresha na kuhimarisha umwagiliaji wa Agricultural Seed Agency (ASA) na hasa ikizingatiwa kwamba msimu wa kilimo uliopita wakulima walipata hasara kubwa kwani maji yalikuwa hayafiki kwenye mashamba yao?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Stella Ikupa kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika ni kweli tunayo mashamba kumi na saba yaliyo chini ya Wakala wa Mbegu Tanzania na hivi sasa baada ya kuongezewa bajeti katika eneo hili kutoka shilingi bilioni 10.5 mpaka shilingi bilioni 43 hivi sasa tunaweka mifumo ya umwagiliaji katika mashamba yetu na tumeanza katika Shamba la Nsimba pale Kilosa ambako tunajenga centre na lateral pivot kwa ajili ya kuhakikisha kwamba ASA anakuwa na uwezo wa kumwagilia mbegu katika mashamba yake mwaka mzima pasipo kutegemea mvua.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa nimekuwa nikifuatilia sana mbegu za parachichi katika Bunge hili kwa kipindi kirefu; na kwa kuwa leo nimeambiwa itazalishwa miche milioni 20 ya ruzuku; na kwa kuwa wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro ikiwemo Siha, Hai, Rombo, Mwanga, Same na Moshi Vijijini, wote wanasubiri miche hiyo kwa hamu, naomba kujua, mgao wetu ni miche mingapi kwa hii awamu itakayotoka? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa parachichi lina wadau wengi sana, naomba pia kufahamu, Serikali imejiunganishaje na wadau hao ili kupata soko la uhakika la parachichi ambalo ni perishable, kwa kipindi hicho ambacho kipo na kinachoendelea katika soko la nje na ndani? Naomba kufahamu. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shally Josepha Raymond, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna anavyowapigania wakulima wa parachichi katika Mkoa wa Kilimanjaro. Katika maswali yake; la kwanza, mgao utatokana na mahitaji. Siyo rahisi sana kutamka hapa Bungeni kwamba nitapeleka miche mingapi katika Mkoa wa Kilimanjaro, lakini mahitaji yataamua miche mingapi iende katika Mkoa wa Kilimanjaro. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge avute Subira, tukianza zoezi hili, najua tutakuwa pamoja, yale mahitaji ya wakulima Mkoa wa Kilimanjaro tutahakikisha kwamba tunayafikia ili wakulima waendelee kulima kwa tija. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili kuhusu soko la uhakika, katika eneo ambalo tumelifanyia kazi la utafutaji wa masoko katika mazao yetu ni pamoja na parachichi. Hivi sasa tarehe 25 Novemba, 2011 Mamlaka ya Afya ya Mimea India walitupatia kibali cha kupeleka parachichi India, na hivi sasa wakulima wetu wameanza kupeleka parachichi India. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile tunauza parachichi yetu Afrika ya Kusini. Pia tunakamilisha mazungumzo na China juu ya phytol-sanitary, tutaanza pia kupeleka parachichi yetu pia China. Hivi sasa ninavyozungumza, wazalishaji wetu wadogo wadogo wameshapata masoko ya uhakika kule Hispania na Marekani pia.

Mheshimiwa Spika, kuhusu masuala ya soko, soko la uhakika lipo, isipokuwa tulikuwa tuna changamoto moja ambayo tumeshai-address hivi sasa, ilikuwa ni lazima zao letu li-meet international standard, na hivi sasa tunayo maabara yetu pale Arusha ambayo tumeiboresha na hivi sasa tumepata accreditation ambayo ni namba 17025. Kwa hiyo, zao lolote ambalo linatoka Tanzania hivi sasa lina uhakika soko nje ya mipaka ya Tanzania. (Makofi)
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kuniona niulize swali dogo la nyongeza. Pamoja na kugawa mbegu bure ambapo tunashukuru, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha kwamba wananchi hasa wakulima wadogo wadogo wanapata utaalam hasa kwenye maeneo ya dawa na magonjwa yanayoshambulia zao hili la parachichi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Deodatus Mwanyika kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema pale awali katika majibu yangu ya msingi, zao la parachichi ambalo ni dhahabu ya kijani tunalipa kipaumbele kikubwa na tunakuja na mkakati madhubuti wa kuhakikisha tunawasaidia wakulima wetu kuanzia huduma za ugani mpaka upatikanaji wa pembejeo na waweze kuzalisha kwa tija. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba ni zao ambalo tunalipa kipaumbele na tutahakikisha kwamba wakulima wetu wanapata elimu ya kutosha na kanuni bora za kilimo ili waweze kulima kwa tija. (Makofi)
NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa Naibu Waziri amekiri kwamba kuna uzalishaji holela wa miche hii ya maparachichi na katika mikoa inayolima parachichi, Songwe pia ni mkoa mmoja kati ya mikoa inayolima parachichi: Ni nini mkakati wa utoaji elimu kwa wananchi na wakulima ili waweze kuepukana na hawa matapeli, wazalishaji wa hizi mbegu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Neema Mwandabila, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kupitia mwongozo ambao tutautoa, utatoa mfumo mzima wa upatikanaji wa miche bora na yenye kuleta tija kwa wakulima wa parachichi na hivyo itaondoa changamoto iliyopo hivi sasa ambapo katika baadhi ya maeneo kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi, kuna chongomoto ya upatikana wa miche bora ya parachichi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kupitia mwongozo huu wa TOSCI, maana yake utakuwa ndiyo mwongozo utakaomfanya mkulima yeyote wa Tanzania ambaye anataka kulima parachichi ataufuata na itakuwa ni sehemu salama kwake kwa sababu ni taasisi ya Serikali ambayo itafanya kazi hii ya kuhakikisha kwamba wakulima wote wanapata miche bora.
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, kigezo cha bei ya mche kinatokana na umri wa mche, kwa sababu hata sasa hivi kuna miche bora kabisa inapatikana kwa shilingi 3,000. Sasa swali langu; Serikali imetumia kigezo gani; ama itatumia kigezo gani cha umri, ili huo mche wa shilingi 2,000 usiwe tofauti na miche ya sasa ambayo inauzwa shilingi 3,000 kwa sababu umri wake ni mdogo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Halima Mdee, mkulima wa parachichi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, zao hili la parachichi ni zao ambalo hivi sasa limeanza kukimbiliwa na wakulima wengi sana kwa sababu limeleta soko la uhakika na vilevile watu wameanza kunufaika kwa kiwango kikubwa sana.

Kuhusu suala la miche ambayo tutaizalisha, ni kweli liko suala la umri wa miche, lakini ni lazima tunanzie sehemu. Sehemu yenyewe ni kwamba, uzalishaji wetu wa miche kama nilivyosema, ni ule ambao tunaamini kabisa wakulima wa parachichi kupitia miche ambayo tutaizalisha chini ya vituo vyetu vya TARI, ambavyo itakuwa ni ya ndani ya muda mfupi pia, wapate kwa bei hiyo hiyo ambapo miche ile mingine ya muda mrefu imekuwa ikiuzwa.

Mheshimiwa Spika, lengo letu kubwa ni kuhakikisha kwamba, ni lazima tuanzie sehemu, lakini mbele tutaboresha kuhakikisha ya kwamba, basi wakulima wetu wawe wana bei ambayo ni standard, ambayo kila mmoja anaweza akai- afford na mwisho wa siku tunaongeza tija katika kilimo chetu cha parachichi na hasa katika eneo ambalo Mheshimiwa Mbunge analima huko. (Makofi)
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa wananchi wa Jimbo la Hai, wamehamasika sana kulima zao hili la parachichi na zao la kahawa: Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa ruzuku ili wakulima hawa waweze kufanya kazi hii kwa ufanisi? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Hai, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi, kutokana na umuhimu wa zao hilo la parachichi, Serikali tumedhamilia kuweka ruzuku ya kutosha ili kuwafanya wakulima waendelee kulima kwa tija na kupata miche hii kwa bei nafuu.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Mkoa wa Kilimanjaro, tunashirikiana pia na wadau kama Africado na wadau wengine kama vile KEDA kule Rombo ambao pia kwa pamoja tunafanya kazi ya uzalishaji wa parachichi. Tumesema katika bajeti ya mwaka 2022/2023, tutazungumza kuhusu ruzuku ambayo tumeitenga kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wakulima hawa wanapata miche kwa bei nafuu.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali madogo mawili. Kwanza nashukuru kwa majibu ya Serikali. Kilimo cha uhakika ni kilimo cha umwagiliaji. Napenda kufahamu hatua iliyofikiwa kwa utekelezaji wa miradi ya Mgombilenga iliyopo Kata ya Kitwiru na Mradi wa UNI wa Kata ya Nyanzwa, kwa sababu hii miradi, Wabunge wa Iringa ni muda mrefu sana tumekuwa tukiifuatilia.

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, katika Wilaya ya Mufindi Kaskazini tuna skimu ya Igoma, Kata ya Sadani na Ikwea. Hii miradi kwa mfano hii ya Ikweha ililetewa shilingi milioni 800, lakini utekelezaji wake mpaka sasa hivi bado haujaweza kueleweka. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri atujibu, Mkoa wetu wa Iringa ni wa kilimo. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Ritta Enespher Kabati, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuhusu miradi ya Mgombilenga na Nyanzwa iliyopo Wilaya ya Kilolo, katika bajeti ya mwaka 2022/2023 Serikali itakwenda kuikabarati miradi hii na kuitekeleza. Hivyo nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye swali la pili la mradi wa Ikweha, ni kweli pale tuna mradi ambao mpaka hivi sasa umeshatumia shilingi milioni 800 ambazo zimetokana na fedha za DADPs pamoja na DIDF. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tunafahamu changamoto iliyoko pale, hivi sasa Serikali tunatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa bwawa. Vile vile mimi mwenyewe nitakwenda kutembelea mradi huu ili kutatua baadhi ya changamoto zilizopo pale na kuwafanya wakulima wawe na amani na kufanya kilimo cha umwangiliaji katika eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, namwahidi tu Mheshimiwa Mbunge, kama Serikali, tunafahamu changamoto iliyopo pale na tunatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa bwawa.
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, Mradi wa Umwagiliaji wa Izazi uliyopo Jimbo la Isimani una changamoto ya uchakavu wa miundombinu pia. Ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya kukarabati miundombinu hiyo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Grace Tendega, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mirada yote ya umwagiliaji tuliyonayo hapa nchini hivi sasa tumeweka mpango mkakati katika mwaka wa fedha ujao kuhakikisha kwamba Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, inaipitia miradi yote nchini Tanzania, tufanye uhakiki, tujue miradi gani inafanya kazi, ipi haifanyi kazi na ipi inahitaji marekebisho ya kiwango gani?

Mheshimiwa Spika, katika uhakiki huo pia tutagusa na miradi ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja.
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Sisi tuna mradi wa Skimu ya Shitage, iligharimu fedha nyingi sana, haifanyi kazi. Lini ahadi ya Mheshimiwa Waziri ya kutengenezwa hiyo skimu itatekelezwa ili wananchi wapate faida ya mradi ule?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Almas Maige, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema pale awali, tunafahamu kwamba kilimo cha umwagiliaji ndicho kilimo hasa ambacho kitamkumboa mkulima wa Tanzania. Kwa umuhimu huo, tumeamua kwa dhati kabisa kuipitia hii miradi yote ikiwemo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameisema. Nimwondoe hofu ya kwamba tumejipanga kuhakikisha miradi hii inafanya kazi.

Kwa hiyo, katika eneo lake pia tutapita na hivi sasa tunaendelea kutafuta fedha na mtaona kwenye bajeti yetu inayokuja, nguvu kubwa hivi sasa imewekwa kwenye Tume ya Umwagiliaji kuwawezesha ili tuweze kufanya kilimo cha umwagiliaji. (Makofi)
MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Jimbo la Mwibara ni kama limezungukwa na maji, lakini hatuna hata mradi mmoja wa umwagiliaji maji: Je, ni lini Serikali itajenga miradi hiyo katika Kata ya Namuhula, Igundu, Iramba na Kasuguti? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Charles Kajege, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ni jambo ambalo ameliwasilisha hapa, nami nitaelekeza wataalam wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakalitembelee eneo hilo na baada ya hapo waone namna ya kuwasaidia wananchi katika eneo hilo kufanya kilimo cha umwagiliaji.
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Pale Ruaha Mbuyuni kuna mradi wa umwagiliaji ulikarabatiwa na Wizara kwa force account, lakini sasa mto ule umeanza kuchepuka tena: Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari tuongozane ili tuweze kuangalia tunafanyaje katika kuukarabati?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Justin Nyamoga, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, namwahidi tu kwamba Mheshimiwa Mbunge, kabla mimi na yeye hatujaongozana Jumatatu, Afisa wetu wa Tume ya Umwagiliaji walioko pale Iringa atakwenda kuukagua kwanza na kutupa taarifa, nami na yeye pia tutakwenda pamoja.
MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Jimbo la Tunduru Kusini kuna miradi miwili ambayo ilifanyiwa kazi na imechukua hela nyingi zaidi ya shilingi bilioni tatu kutengenezwa pamoja na barabara, lakini miradi ile haifanyi kazi. Je, Serikali inampango gani wa kuweza kukamilisha miradi ile, mradi wa Mishaji pamoja na mradi wa Madaba, uliopo Azimio?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Daimu Mpakate, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katika majibu yangu ya awali, tumejipanga kuhakikisha miradi yote hii inafanya kazi. Hivyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba katika uhakiki ambao tutaufanya, tutapitia pamoja na maeneo yake ili kuona miradi hii changamoto yake ni nini; na mwisho wa siku tuweze kuikwamua na wananchi waweze kufanya kilimo cha umwagiliaji.
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, ningependa kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa katika Wilaya ya Mbeya, kuna madini ya aina ya calcium carbonate kwa wingi na NDC katika miaka ya 2006/2007 walikuwa na mkakati wa kuanzisha kiwanda ili watengeneze mbolea, CAN: Je, ni lini Serikali itaanza kujenga kiwango hicho kwa kushirikiana na NDC?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa bei hizi za mbolea zinatishia upungufu mkubwa wa chakula: Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha inarudisha ruzuku kama ilivyo kwenye nchi nyingine za SADC na Afrika Mashariki?

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Oran Manase Njeza, Mbunge wa Mbeya Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza la ujenzi wa kiwanda, ni dhamira ya Serikali kuona ujenzi wa viwanda vingi zaidi vya mbolea vinakuwepo hapa nchini ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa mbolea na kupunguza bei ya mbolea na kupunguza bei ya mbolea kama ilivyo sasa. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba sisi kama Wizara pamoja na wenzetu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, tutakaa pamoja ili tuhakikishe kwamba wazo hili ambalo lilianzishwa mwaka 2006 liweze kukamilika na kuwapungizia adha wakulima.

Mheshimiwa Spika, la pili, ni la kuhusu ruzuku. Katika bajeti yetu ambayo tutaisoma mwezi ujao na pia katika utekelezaji ambao utaanza mwaka ujao wa fedha, tumedhamiria kutenga mfuko maalum (price stabilization fund) kwa ajili ya kudhibiti upandaji wa bei ya pembejeo ikiwemo na bei za mazao.

Mheshimiwa Spika, hivyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba hii ni sehemu ambayo pia tunaipa umuhimu mkubwa na Serikali imedhamiria kuanzisha mfuko wa ruzuku ambao utahakikisha unasaidia kupunguza maumivu ya wakulima na hasa katika upatikanaji wa bei ya mbolea ambayo itakuwa ni rafiki kwa mkulima.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali na kwa kuwa viwanda vilivyotajwa ni viwili tu nchini: Je, Serikali haioni kuwa ni wakati muafaka sasa wa kuhamasisha wawekezaji wengine ili uzalishaji wa mbolea nchini uwe mkubwa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zacharia Issaay, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema awali, moja kati ya mikakati tuliyonayo hivi sasa ni kuendelea kuwakaribisha wawekezaji wengi zaidi wa viwanda vya mbolea ili kwa pamoja tusaidiane kutatua changamoto iliyoko hivi sasa ya upatikanaji wa mbolea. Tunaamini katika misimu michache inayokuja, kiwanda cha Itracom na Minjingu ambacho sisi kama Wizara tumewasaidia kuzungumza na Benki za TADB na CRDB kuongeza expansion, tutakuwa tumetatua changamoto hii ya upatikanaji wa mbolea kwa kiwango kikubwa sana. Pia bado tunakaribisha makampuni mengine, na kama Serikali tunaendelea pia kukaribisha makampuni mengi zaidi ili tuondokane na changamoto hii ya upatikanaji wa mbolea hapa nchini.
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ya udharura na kwa ruksa yako naomba kwanza niwape pole wananchi wa Njombe kwa ajali kubwa iliyotokea na iliyouwa watu nane siku ya juzi.

Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa suala la gharama na hasa zao la Parachichi lina ushindani mkubwa sana kwenye soko, na suala la gharama ni suala la muhimu sana kuzingatiwa kwa maana ya kupunguza gharama hizo.

Je, Serikali itatuhakikishiaje kwamba mamlaka hii inayoenda kuundwa haitaongeza gharama kwa wakulima wadogo kwa kupitia tozo na gharama za uendeshaji?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Je, ni lini sasa hayo mabadiliko yatafanyika kwa kuletwa Muswada hapa ndani. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Deodatus Phillip Mwajika Mbunge wa Njombe Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kwamba inakuza tasnia hii ya mazao ya mbogomboga na mazao ya bustani na hivyo moja kati ya maeneo makubwa ambayo tutayasimamia ni kuhakikisha kwamba mkulima hapati changamoto kubwa ya tozo nyingi ambazo zitamfanya akate tamaa ya kilimo chake.

Mheshimiwa Spika, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba Serikali katika uanzishwaji wa mamlaka hii itahakikisha kwamba inalinda maslahi ya mkulima na mkulima anufaike na kilimo chake.

Mheshimiwa Spika, pili kuhusu ni lini tutaleta mabadiliko haya ya sheria, mchakato umeshaanza ndani ya Wizara ya kuanza kupitia marekebisho haya ya sheria na pindi itakapokamilika kwa mujibu wa taratibu za Bunge utawasilishwa hapa Bungeni kwa ajili ya majadiliano na kupitishwa.
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Ninayo maswali mawili ya nyongeza pamoja na majibu mazuri yaliyotolewa.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza katika skimu hizi ikiwemo hii ya Mgambalenga lakini pia skimu za Ruaha Mbuyuni na nyingine gharama za ulipiaji wa vibali katika bonde zilipanda kutoka Shilingi 70,000 hadi Shilingi 150,000 zaidi ya asilimia 100. Sasa ningependa kujua ni mpango gani wa Serikali wa kupunguza hizi gharama maana gharama za kilimo zimeongezeka kwa hiyo inakuwa ni vigumu wakulima wale wa kujikimu kuweza kumudu kulipia vibali kwa ajili ya umwagiliaji? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili katika Kata ya Nyanzwa skimu ya umwagiliaji iliyoko pale ambayo ni ahadi ya Mawaziri Wakuu kadhaa bado haijatekelezwa, pamoja na juhudi kubwa za kuifatilia zilizofanywa na mimi mwenyewe hata Diwani wa kule amekuja kufuatilia. Sasa ningependa kujua kwa sababu ndiyo uhai wa watu wa kule kwenye kilimo cha vitunguu.

Je, ni lini Serikali itajenga ile skimu kwa kuzingatia pia mwaka huu hali ya umwagiliaji imekuwa ngumu na hali ni mbaya, ni lini Serikali itafanya ujenzi wa skimu ya umwagiliaji Nyanzwa? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Justin Lazaro Nyamoga, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika swali lake la kwanza kuhusu gharama ni kweli kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge gharama zimekuwa juu tofauti na ile gharama ya awali ambayo ilikuwepo. Tumeielekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kukutana na mamlaka ya bonde husika kukaa na kuangalia uhalali wa gharama hizo ili tumpunguzie adha mkulima.

Mheshimiwa Spika, pili ni kuhusu mradi wa Nyanzwa ni kweli mradi huu Mheshimiwa Mbunge amekuwa akiufuatilia sana na ninampongeza sana kwa hili. Tayari pale tuna miundombinu ya hekta 300 na tunachangamoto kubwa ya uhaba wa maji ya umwagiliaji, katika bajeti ya mwaka 2022/ 2023 Tume itafanya usanifu wa kina wa bwawa kuvuna maji ya mvua na usanifu huo pia utahusisha eneo la hekta 9,000 ili kuwahudumia wakulima wengi zaidi na baadae tutajenga kama ambavyo usanifu utakuwa umeelekeza.

Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana. (Makofi)
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, skimu ya umwagiliaji iliyopo katika eneo la Chikopelo Wilaya ya Bahi imeacha kufanya kazi kwa muda mrefu baada ya mwekezaji kuondoka. Nini kauli ya Serikali katika kuifufua skimu hii ili kuwaondolea umaskini wananchi wa eneo hilo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Fatma Toufiq, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli tunafahamu ya kwamba moja kati ya eneo ambalo litasaidia sana kukuza kilimo chetu katika nchi yetu ya Tanzania ni kilimo cha umwagiliaji. Namuahidi Mheshimiwa Mbunge ya kwamba Wizara tumejipanga kuhakikisha tunazipitia skimu zote ili kuweza kufahamu status zake kwa maana tujue ni miradi ipi haifanyi kazi, ipi inafanya kazi lakini ipi imekwamishwa na nini, ili tuitatue na kuwafanya wakulima wetu walime kilimo cha umwagiliaji. Moja wapo ya maeneo ambayo tutayapitia ni pamoja na eneo la Chikopelo.
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.

Katika Wilaya ya Kakonko ambako Jimbo la Buyungu lipo zipo skimu za Katengera, Gwanumpu, Ruhwiti na Muhwazi ambazo miundombinu yake imeharibika na haifanyi kazi vizuri.

Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu hiyo ili waweze kuendelea na kazi kama ilivyokusudiwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Aloyce kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika miradi aliyoisema Mheshimiwa Mbunge ukiacha mradi wa Ruiche hii miradi mingine miwili tutaiingiza katika mipango yetu kuhakikisha kwamba inafanya kazi katika utaratibu ambao nimeuanisha awali wa kuipitia nakuona changamoto ulizonazo.

Mheshimiwa Spika, mradi wa Ruiche tumeshapata no objection na hivi sasa tutaelekeza kazi ya usanifu ifanyike ili baadae tuanze kazi ya ujenzi.
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Katika Kata ya Itilima, Wilaya ya Kishapu kuna Kijiji cha Mwamala na katika Kata ya Mwaduiluhumbo kuna kijiji cha Nyenze, katika Wilaya hii ipo miradi ya skimu za umwagiliaji ambayo Serikali ilitoa pesa lakini baada ya kutoa pesa zile hazikutosha, katika Jimbo hili la Kishapu wakinamama katika maeneo haya wanapata shida sana kutokana na hali halisi ya ukame katika maeneo haya.

Je, ni lini Serikali itatupatia pesa katika skimu hizi mbili za Nyenze pamoja na Mwamala ili wananchi waweze kufaidika? Kwa sababu skimu hizi za umwagiliaji endapo kama zikikamilika maji yatasaidia mifugo pamoja na binadamu. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Lucy Mayenga, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji amekuwa akifanya ufuatiliaji mara kwa mara ofisini kwetu na ninamuahidi kwamba katika bajeti yetu ambayo tutaisoma mwezi ujao tutaainisha miradi ambayo itafikiwa na miradi hii pia tutaifikia. (Makofi)
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, maharage ya soya niliyokuwa namaanisha ni maharage ambayo yanatumika kukamua mafuta ya kula, lakini katika majibu ambayo yametolewa na Serikali naamini wanamaanisha maharage ya kula kama mboga.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pamoja na majibu hayo, lipo tatizo kubwa sana la upatikanaji wa mbegu za maharage ya soya ambayo yanatumika kwa ajili ya kukamua mafuta. Utakubaliana na mimi kwamba sisi kama Taifa tumepata soko kupeleka maharage haya China.

Swali langu; je, Serikali inafanya mpango gani mahususi wa kuhakikisha kwamba mbegu hizi zinapatikana kwa ajili ya wananchi wa Mikoa ya Rukwa, Ruvuma na mingine yote Tanzania ili tuweze kujitosheleza katika kilimo cha mafuta? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni ukweli usiopingika kwamba kuna formular ya synergy, kwamba moja kujumlisha moja ni tatu na siyo mbili, kwa sababu soya meal inayopatikana ni chakula kizuri sana kwa ajili ya mifugo ikimaanisha ng’ombe, samaki na kuku.

Je, siyo wakati mwafaka kwa Serikali, kwa sababu Wizara ya Mifugo bado bajeti yake haijaja ikahakikisha kwamba ina-inject kiasi cha fedha ili mbegu bora zipatikane ili wakulima na wafugaji wetu wasihangaike ili wawe na uhakika wa chakula kwa ajili ya mifugo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kandege kwa ujumla wake kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli moja kati ya changamoto kubwa tuliyonayo hivi sasa ni upatikanaji wa mbegu bora za soya na Serikali imeanza kuchukua hatua na hatua za kwanza ambazo tumezichukua ni kwa kushirikiana na Taasisi za TOSCI pamoja na ASA kuruhusu uingizaji wa mbegu kutoka nchi za karibu za Malawi na Zambia ili tuweze kufanya seed multiplication na lengo letu kubwa ni kuhakikisha kwamba tunasambaza mbegu hizi kwa wakulima wengi zaidi na zipatikane kwa urahisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa kunayo changamoto hiyo kubwa, lakini TOSCI na ASA wameshakaa chini na kukubaliana na uingizaji wa mbegu hizi katika hatua ya awali na lengo letu kubwa ni kufanya wananchi wengi zaidi waweze kuzipata kwa urahisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli liko soko kubwa sana la mahitaji ya soya beans duniani na hasa kule nchini China, mahitaji ni zaidi ya metric tons milioni 100, na kama nchi tumejiandaa pia kulifikia soko hilo. Na katika maeneo ambayo tutayapa kipaumbele ni maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja na hivi sasa Mkurugenzi Mkuu wa ASA yuko njiani anaelekea...

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: ...anaelekea kwenda katika Mikoa ya Rukwa na Katavi kwa ajili ya kupata mashamba mengine makubwa kwa ajili ya uzalishaji mbegu ambayo yatakidhi mahitaji ya maeneo husika.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha wanafanya vizuri sana kwenye zao la vitunguu hapa nchini na hata Afrika Mashariki; je, Wizara ina mkakati gani wa kuwasaidia wakulima hawa ili waweze kuongeza tija na pia kupata masoko ya uhakika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zaytun Swai kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya mikakati tuliyonayo hivi sasa ni kuhakikisha kwamba wakulima wetu wanalima kwa tija na ili waweze kuyafikia masoko mbalimbali ya ndani na nje ya nchi; na kwa kuanzia tumeanza kuwapa maelekezo Maafisa Ugani kwa mazao mahususi ikiwemo vitunguu ili kuwasaidia wakulima waweze kuzalisha kwa tija.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Mikoa ya Iringa, Ruvuma, Njombe na Rukwa ilikuwa inajulikana kama The Big Four kwa kilimo cha mahindi, lakini wakulima wengi sasa hivi wametetereka sana kutokana na bei kubwa ya pembejeo.

Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha kwamba bei ya pembejeo inapungua ili mikoa hiyo iendelee kulima kilimo kikubwa kabisa cha mahindi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ritta Kabati, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua ambayo Serikali tutaichukua kumpunguzia maumivu ya pembejeo mkulima katika bajeti inayokuja tutaanzisha Mfuko maalum, (Price Stabilization Fund) ambao ikitokea pembejeo zitakwenda juu Serikali itatoa ruzuku ili mkulima asiumie sana katika upatikanaji wa pembejeo.
MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nishukuru Serikali kwa majibu mazuri juu ya kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Mto Ruichi. Nina swali moja la nyongeza. Jimbo la Buhigwe lina skimu mbili, skimu ya Rukoyoyo na skimu ya Mugera ambazo nazo hazijawahi kupata msaada wowote kutoka Serikalini.
Je, Serikali ina mpango gani wa kuziendeleza skimu hizi za Rukoyoyo na Mugera zilizoko katika Wilaya ya Buhigwe?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kavejuru Eliadory Felix, Mbunge wa Buhigwe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mpango mkakati, tulioweka Wizara ya Kilimo ni kuhakikisha skimu zote za umwagiliaji hapa nchini zinafanya kazi. Hivyo nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, ya kwamba katika bajeti yetu inayokuja itakayosomwa wiki ijayo wataona miradi mingi ambayo tumeainisha kwa ajili ya kuifufua, kuikarabati na kujenga upya ambapo pia naamini itagusa katika mikoa mingi ikiwemo Mkoa wa Kigoma. (Makofi)
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Serikali iliahidi kukamilisha miradi ya umwagiliaji ya skimu ya Karema na skimu ya Kabaki. Kupitia kwa Waziri aliyekuwpepo aliahidi kuwa atakamilisha hiyo miradi.

Je ni lini itakuja kukamilisha hiyo miradi miwili ndani ya Wilaya ya Tanganyika?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Moshi Seleman Kakoso Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, skimu alizozitaja Mheshimiwa Mbunge, mimi nimefika na nilitoa pia ahadi hii mbele ya wananchi wake katika mkutano wa adhara ambao tuliufanya pale kijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika bajeti inayokuja ya mwaka 2022/23 miradi wa skimu hizi imeainishwa na itatekelezwa kupitia bajeti hiyo inayokuja. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tuliipokea na tunaendelea na utekelezaji wa miradi hiyo.
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Serikali iliwekeza zaidi ya milioni 700 kwenye Bonde la Miogwezi lililoko kwenye Kijiji cha Igongo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, lakini mradi ule umesimama.

Je, Mheshimiwa Waziri huu nao ni kati ya miradi itakayotekelezwa kwenye mwaka wa fedha 2022/ 2023?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mkundi, Mbunge wa Ukerewe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, zoezi linaloendelea hivi sasa ambapo ni maelekezo wamepewa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kuhakikisha kwamba miradi yote hii inafanya kazi. Tumewapa jukumu la kupitia miradi yote nchi nzima kujua status yake, tuone ipi inafanya kazi, ipi inahitaji marekebisho na ipi inahitaji over whole, kwa maana ya kuanza upya katika mradi husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, kwamba katika bajeti yetu ambayo tutaisoma wiki inayokuja tutaainisha miradi ambayo itatekelezwa na imani ni kwamba katika mradi aliosema tutaingiza katika utaratibu wa utekelezaji katika bajeti inayokuja.
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Katika Kata ya Msia pana bwawa dogo ambalo lipo katika Kijiji cha Msia. Bwawa hili linaweza kutumika sana katika kilimo cha umwagiliaji hasa katika mashamba ya kahawa. Na kwa muda mrefu limekuwepo kwenye bajeti lakini Serikali haijaweza kutekeleza. Ni lini Serikali itaanza kutekeleza lile bwawa ili liweze kutumika katika kilimo cha umwagiliaji?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hasunga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha ya kwamba ifikapo mwaka 2025 tumekuwa na eneo la umwagiliaji la hekta milioni moja na laki mbili yakiwa ni maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, ya kwamba katika kufikia azma hiyo ni lazima pia tutekeleze miradi mingi kadri iwezekanavyo ili wananchi wengi waweze kunufaika. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba bwawa alilolisema tutaelekeza wataalamu katika bwawa la pili pia kulipitia ili waje watushauri vizuri namna ya utekelezaji wake lakini ni jambo ambalo ndani ya wizara tunaona kwamba ni jambo muhimu na hivi sasa changamoto kubwa ni upatikanaji wa mabwawa yenye uhakika wa maji. Kama bwawa lipo tayari ni njia rahisi zaidi ya kuanza utekelezaji wa mradi. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge tutalisimamia hilo na mradi utatekelezeka.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa vile utaratibu unaotumika sasa ni wa mkataba wa mwaka mmoja mmoja. Swali la kwanza; je, Serikali ina mkakati gani sasa ya kuwafanya wakulima hawa waweze kutambua ni kampuni ipi nzuri ili waweze kuingia nayo mkataba?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; kwa kuwa Bodi ya Tumbaku na ndiyo msimamizi mzuri wa zao hili, lakini haina fedha kabisa haina magari hata ya kwenda kwenye masoko, je, Serikali ina mkakati gani sasa wa kuweza kuiopatia fedha Bodi ya Tumbaku ili iweze kusimamia vizuri masoko ya tumbaku hapa nchini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza kwa sababu Bodi ya Tumbaku ina ofisi katika mikoa yote ya tumbaku na Bodi ndiyo custodian wa taarifa zote za makampuni ya ununuzi wa tumbaku tumekuwa tukitumia nafasi hiyo kuendelea kuwapa taarifa sahihi wakulima kupitia ofisi zetu hizo ili watambue mnunuzi mzuri wa kuingia naye kwenye mkataba. Sambamba na hilo, pia tunayo taarifa za wanunuzi wote katika tovuti ya Bodi.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili la bajeti kilifanyika kikao cha wadau wote wakakubaliana kwamba ili kuijengea Bodi uwezo kuanzia msimu unaokuja tutaanza kuchaja shilingi thelathini katika kila tumbaku mbichi kwa ajili ya kuiboresha Bodi yetu ya Tumbaku ili iweze kufanya ufatiliaji na kuendeleza zao hili la tumbaku.
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza na pia napenda nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa jibu lake zuri na pia kumpongeza Mheshimiwa Rais, kwa kutoa ruzuku kwenye pembejeo za kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mikakati mizuri iliyowekwa na Serikali lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, hiyo mikakati hasa utoaji wa ruzuku utakuwa ni endelevu kiasi gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa sababu ruzuku ilikuwa kwenye mbolea lakini kuna pembejeo zingine kama mbegu hasa za nafaka, je, Serikali ina mkakati gani pia wa kutoa ruzuku kwenye pembejeo aina ya mbegu pamoja na viatilifu kwa ajili ya kilimo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa ruzuku ya mbolea unategemeana sana na bei ya mbolea duniani na namna ambavyo wakulima wetu wataweza kumudu gharama hizo. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mpango huu ni endelevu kwa muda wa miaka mitatu na tutakuwa tunaendelea kuangalia bei za dunia na kama ikitokea kwamba wakulima wanazimudu gharama, mpango huu pia hautaendelea kwa sababu ni mpango wa kumsaidia kumlima kuondokana na machungu ambayo ameyapata kutokana na kupanda kwa bei.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili kuhusu mbegu za nafaka. Moja kati ya mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kwamba, tunawafikia wakulima na kuwafanya wakulima wetu waweze kuzalisha kwa tija na eneo mojawapo ambalo tumekuwa tukiliangalia ni ruzuku kwenye eneo la mbegu na katika mwaka huu wa fedha tumefanya katika zao la ngano. Vilevile katika mahindi kupitia Wakala wa Mbegu Kilimo Tanzania, tumefanya hivyo kwa kushusha bei ambayo ni tofauti na bei iliyoko sokoni. Kwa mfano Mbegu za OPV za STUKA M1 zinapatika kwa Sh.2,750 tofauti na bei ilivyo sokoni, lakini mbegu za high breed za UH 6303 inauzwa kwa Sh.4,000 tofauti na bei iliyoko sokoni ya Sh.7,000, kwa hiyo ni sehemu pia ya ruzuku.
MHE. MUHARAMI S. MKENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Benki ya Kilimo Tanzania imekasimu madaraka yake kwa Benki mbalimbali ikiwemo CRDB pamoja na NMB kwa ajili ya utoaji mikopo, lakini masharti yaliyokuwepo katika ukopaji huo ni magumu sana ikiwepo na kutoa asilimia ishirini na tano ya kile unachotaka kukopa, kutoa dhamana ya nyumba pamoja na cash flow ambayo inaelea katika benki ya mwaka mmoja. Je, ni lini sasa Serikali itapunguza masharti haya ili wakulima wapate nafuu kwa ajili ya kilimo na hasa wakulima wangu wa Bagamoyo ambao ni maskini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikiri ni kweli kumekuwa na changamoto ya wakulima wetu kukopesheka kirahisi na ndiyo maana Serikali tumechukua hatua madhubuti za kuhakikisha kwamba tunakaa na taasisi za fedha waelewe mfumo wa ukopeshaji katika kilimo ambao ni tofauti na maeneo mengine. Kwa hivi sasa tumekuja na mfumo mzuri ambao tumeu–design mikataba ya utatu ambayo imetusaidia sana kupunguza masharti mengi ambapo anakaa mkulima, anakaa off taker, anakaa na benki kwa upande mmoja ili mkulima aweze kukopesheka kutumia mikataba aliyonayo pasipo kutumia hati za nyumba na sababu zingine ambazo zinamfanya asiweze kufikia kwenye ukopeshwaji huo. Kwa hiyo nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, kama Serikali tumeliona hilo na tunaendelea na mikakati hii kuhakikisha kwamba mkulima wetu anakopesheka kirahisi. (Makofi)
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Naipongeza sana Serikali, naishukuru Serikali ya Chama cha Mapinduzi kutupatia mbolea ya ruzuku kipindi hiki. Hata hivyo, mbolea ile Jimboni kwangu ilifikia tu kwenye Makao Makuu ya Jimbo na wananchi wote kwenye Jimbo zima walikuwa wanasafiri kuifuata Mbungu. Je, Serikali ina mpango gani wa uhakika kwamba kipindi kijacho mbolea hii itafika sehemu zote ambako wananchi wanalima? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli wakati tunaanza mfumo huu kwa mara ya kwanza, tumepitia changamoto hizo, lakini kama Wizara tumekaa, tumetafakari na kuzipitia changamoto zote na kuja na mkakati wa kudumu wa kuhakikisha kwamba mbolea hizi zinawafikia wakulima katika maeneo yao pasipo kutembea umbali mrefu. Mkakati huo ni kama ifuatavyo: -

(i) Hivi sasa tumeshawaagiza TFRA kuendele kusajili vituo vya mawakala karibu na maeneo ya wakulima;

(ii) Tutatumia pia Vyama vya Ushirika kwa ajili ya usambazaji wa mbolea; na

(iii) Tunatumia maghala ya Serikali yaliyoko katika maeneo mbalimbali kuhakikisha kwamba mbolea inafika katika maeneo ya uzalishaji ili wakulima wasitembee umbali mrefu. (Makofi)
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana; zao la kahawa limevamiwa na ugonjwa wa mnyauko ambao unaweza ukasababisha zao hili kutoweka zao hili muhimu: -

Je, Serikali imechukua hatua gani za haraka ili kulinda zao hili muhimu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; zao la kahawa ni zao la kimkakati lakini bado halijaweza kumnufaisha mkulima ipasavyo: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuweka masoko mazuri ambayo yatamnufaisha mkulima apate bei nzuri?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa swali la kwanza, kahawa inaathiriwa na magonjwa makubwa matatu chulebuni, kutu ya majani pamoja na mnyauko fuzari. Mnyauko fuzari ndio umekuwa ni changamoto kubwa sana. Hatua ambazo tumezichukua, kituo chetu cha utafiti wa zao la kahawa TaCRI hivi sasa kinakuja na variety mpya ambayo itakuwa ni himilivu katika magonjwa, hasa ugonjwa huu wa mnyauko fuzari. Pia tumeendelea kutoa elimu kwa wakulima juu ya kufanya palizi ; kwa sababu moja ya changamoto kubwa ni mashamba kuwa machafu, vilevile kung’oa miche yenye changamoto na isipandwe kabla ya miezi sita ndio elimu tumekuwa tukizitoa.
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza kwa niaba ya Mheshimiwa Mpina.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mpango gani wa kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima wa tumbaku? Hilo swali la kwanza. Swali la pili: Je, Serikali inajipangaje kuhakikisha wakulima wanapata mbolea mapema ili kuweza kuwaruhusu mazao yote yale ya umwagiliaji yaweze kupata mbole kwa wakati?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli katika mpango wa msimu uliomalizika, wakulima wa zao la tumbaku hawakuwepo katika mpango wa ruzuku kwa sababu katika utaratibu wa manunuzi ya pembejeo kwenye sekta hii ya tasnia ya tumbaku wamekuwa na utaratibu maalum ambao ulianza kabla ya mfumo wa ruzuku. Hata hivyo, tumeendelea kukaa nao kuangalia pia utaratibu bora ili na wao waweze kunufaika na utaratibu wa ruzuku ambao unaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili la kuhusu mbolea kupatikana mapema; tumeshakaa na waagizaji na wazalishaji wa mbolea wote hapa nchini kuhakikisha kwamba kuanzia mwezi wa Saba mbolea ianze kuingizwa nchini ambayo itawakuta wakulima wakiwa bado na uwezo wa kununua kwa kuwa watakuwa wamevuna ili wakulima wetu itakapofika kipindi cha kuanza msimu mbolea iwepo yote hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tumebaini upungufu katika msimu uliopita, tumeyarekebisha, tutahakikisha kwamba wakulima wanapata mbolea kwa wakati katika msimu ujao.
MHE. FATMA HASSAN TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa nchi yetu ina mifugo mingi ya kutosha, hivyo uwezekeno wa kuwa na mbolea ya samadi ni mkubwa, nini mkakati wa Serikali katika kuboresha na kuhamasisha matumizi ya mbolea ya samadi ili ilete tija? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa kwa hapa Dodoma tunacho kiwanda cha mbolea kinaitwa ITRACOM ambacho kinazalisha mbolea inayoitwa Organo Mineral ambapo zaidi ya asilimia 50 wanatumia samadi na imekuwa kichocheo kikubwa na soko la uhakika kwa wafugaji wetu wengi hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba ilikuwa ni mkakati wa Serikali, na kiwanda kipo hivi sasa na kinatumia malighafi hiyo kama sehemu ya kutengeneza mbolea hapa nchini.
MHE. VENANT D. PROTAS: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Uchache wa mawakala ulileta usumbufu wa upatikanaji wa mbolea kwa msimu uliopita. Je, Serikali haioni haja ya kupeleka mawakala angalau kwa kila kijiji ili wasiendelee na usumbufu walioupata wakulima kwa msimu uliopita? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kati ya changamoto ambazo pia tulizibaini wakati wa msimu uliopita ilikuwa ni hiyo ya uchache wa mawakala. Tumeshatoa maelekezo kupitia TFRA kuongeza idadi ya usajili wa Mawakala ili wakulima wapate mbolea katika maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, tumeamua kuyatumia maghala yote makubwa ya Serikali kwa ajili ya uhifadhi na kupeleka mbolea karibu na wakulima; na tatu, tumeruhusu Vyama vya Ushirika pia kuwa sehemu ya Mawakala ili kufanya huduma hii ifike kwa ukaribu zaidi kwa wakulima.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Uhalisia wa upatikanaji wa mbolea kwa wakti kwa wakulima wetu bado ni changamoto kubwa; na inasemekena mbolea hizi zinatumika kusafishia madini kwenye migodi. Sasa nilitaka kujua, ni Serikali itafanya tafiti za kina kujua matumizi ya ziada ya mbolea hizi nje ya kilimo ili kuweza kuwa na bajeti halisia ya kuwafikia wakulima kwa wakati kulimo ilivyo hivi sasa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi ya msingi ya mbolea yanafahamika, ni kwa ajili ya kilimo. Kama kuna jambo lingine la ziada kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema, sisi na wenzetu wa madini tutakaa tushirikiane ili kuweza kulifanyia utafiti wa kina na kuweza kupata majibu stahiki katika eneo hili ili mwisho wa siku tuwe na mbolea kwa mahitaji halisi yanayohitajika katika kilimo chetu cha msingi Tanzania. (Makofi)
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Nashukuru sana kwa majibu ya Serikali; pamoja na kitu kizito alichopigwa nacho Mheshimiwa Naibu Waziri jana Mkapa, lakini anaweza kutoa majibu ya kina. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali imefanya uhakiki kwamba viuatilifu hivi 44 vilivyobainishwa vimeweza kutokomezwa na kwamba notice ya katazo au ya ku- deregister au zuio inabainika kwa uwazi na kwa ufasaha kabisa kwa wanunuzi, watumiaji na wanaohusika wote? (Makofi)

Mheshimwa Mwenyekiti, swali lingine: Je kuna mpango gani wa Serikali kupima mboga mboga zinazoingia sokoni na kuwajulisha watumijai na walaji kama vile tunavyofanya kwa mazao yanayouzwa nchi za nje? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Asha Abdullah Juma, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza kwa mujibu wa Sheria Na. 4 ya Afya ya Mimea ya Mwaka 2020, ni wajibu wa kimsingi wa mamlaka kuhakikisha kwamba inafanya kaguzi za mara kwa mara ili kuweza kubaini viuatilifu ambavyo vimesitishwa na kuweza kuchukua hatua sambamba na kutoa taarifa kwa watumiaji ili isiweze kuleta madhara zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili la kuhusu upimaji wa mazao ya mboga mboga, Serikali inapima uwepo wa masalia ya viuatilifu vilivyotokomezwa katika mazao yote. Hivi sasa tumenunua Rapid Test Kit ambayo pia itasaidia kupima masalia ya viuatilifu katika mazao ya mboga mboga ili kuweza kumlinda mtumiaji. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo pia tunahamasisha na kilimo hai, kuondokana na changamoto hizi ambazo zinajitokeza na matumizi ya viuatilifu.
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Kumekuwa kuna changamoto kwa wakulima hasa wa zao la mahindi msimu huu, mahindi yamevamiwa na wadudu lakini mkulima anatumia dawa nne, sita mpaka nane, anazichanganya lakini bado hazi-react kwa wadudu hao na elimu kwa wananchi wetu bado ni ndogo: Nini mkakakti wa Serikali kuhakikisha kwamba dawa sahihi kulingana na wadudu husika ambao wamevamia mazao inapata tiba kwa wananchi wetu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Mamlaka ya Afya ya Mimea na viuatilifu (TPHPA) Serikali imekuwa na utaratibu wa kuhakikisha kwamba viuatilifu vyote vinavyoingizwa nchini ni vile ambavyo vinakidhi mahitaji na matakwa ya changamoto ambazo zinawakabili wakulima wetu. Hivyo ambacho tutakifanya zaidi, ni kuendelea pia kutoa elimu kwa wakulima wetu juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu hivi ili viweze kuleta matokeo chanya na viweze kumsaidia mkulima katika kupambana na uhalibifu wa mazao.

Mheshimiwa, Mwenyekiti, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba Serikali inatambua changamoto zilizojitokeza na kuendelea na ukaguzi ili tukibaini kwamba kuna changamoto kama hiyo katika baadhi ya maeneo, tutaweza kuchukua hatua stahiki na tuweze kufuta mpaka usajili katika wale ambao wanahusika. Sambamba na hili, uhakika tu ni kwamba tutahakikisha kwamba mkulima wetu anapata viuatilifu ambavyo ni sahihi kwa wadudu sahihi.
MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninayo maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa Mkoani Kagera kilimo cha vanila kilianza kwenye miaka ya tisini lakini hadi leo hakuna mfumo unaoeleweka wa kilimo cha vanila nchini. Je, ni lini Serikali sasa italeta mwongozo juu ya namna ya kulima, wakatoa huduma za ugani na wakaelekeza juu ya masoko?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa huko ulimwenguni katika nchi nyingine kilo ya vanilla inanunuliwa kati ya 800,000 mpaka 1,000,000 wakati mkulima wa Kagera anauza vanilla kwa 20,000, 15,000 mpaka 30,000 tu. Je, ni lini sasa Serikali kwa kutumia balozi zetu za nje wataweza kututafutia masoko yanayoeleweka ili kuweza kumnufaisha huyu mkulima kupata bei nzuri ya vanilla?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Benardeta Kasabago Mushashu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, wiki mbili zilizopita Wizara ya Kilimo pamoja na wadau wa zao la vanilla tulikutana tukafanya mkutano wa pamoja hapa Dodoma kwa lengo la kuandaa na kutengeneza mwongozo.

Mheshimiwa Spika, nilihakikishie Bunge lako kwamba tuko katika hatua za kuanza kuandaa mwongozo huo ambao utajumuisha masuala ya utafiti, kalenda ya mazao, mfumo wa bei, masoko na uzalishaji bora wa vanilla ambao unakidhi mahitaji ya soko la dunia, hasa ile ambayo ina vanillin na moisture content ambayo inahitajika kimataifa.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu masoko; baada ya mkutano huo wa wadau, sisi kama Wizara ya Kilimo tumeshawaandikia Ubalozi wa Tanzania Nchini China ikiwa ni moja ya sehemu ya masoko makubwa ya vanilla kuanza mazungumzo na ufunguzi wa soko hilo na tutafanya katika maeneo mengine ili kumsaidia mkulima wa vanilla aweze kupata soko la uhakika.
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; tatizo ni muda, mwezi Juni na mwezi Mei mwishoni wakulima wa kahawa wanaanza kuvuna kahawa yao kupeleka kwenye hivyo Vyama vya Msingi, sasa Waziri anaposema mwezi ujao, kwa nini hili suala lisifanyike mapema kabla ya msimu wa kuuza haujaanza ili hayo makato yaondolewe na wakulima wapate chao?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; niipongeze Serikali kwa uamuzi wa kuwafutia leseni mawakala wa mbolea 700. Kwa kweli hii ni hatua nzuri na naomba wasirudi nyuma wakaze buti, hatuwezi kutishwa na watu wasiokuwa waaminifu, ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, bahati nzuri wakati naingia hapa Bungeni taarifa imekwishafika Wizarani, kwa hivyo tutaanza kulifanyia kazi mwezi huu ili kuuwahi msimu.
MHE. NDAISABA G. RUHORO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Naomba sasa kuiuliza Serikali swali la nyongeza. Je, Wizara ya Kilimo ina mkakati gani wa kuhakikisha wakulima wa kahawa wa Wilaya ya Ngara wanaendelea kuuza kahawa yao kwa bei nzuri kama ilivyokuwa kwenye msimu uliopita? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Mbunge kwa kazi nzuri ambayo anaifanya kwenye zao hili la kahawa, nataka tu nimhakikishie kwamba utaratibu ambao tulioanza nao ulimpa mkulima bei nzuri, tutaendelea nao. Vilevile tutahakikisha kwamba tunamsaidia mkulima kupata masoko ya uhakika na azalishe kahawa yenye ubora ili iweze kumpatia bei nzuri sokoni. Kwa hiyo nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba wakulima wa kahawa Mkoa wa Kagera na maeneo mengine wataendelea kunufaika na utaratibu ambao tumeuweka hivi sasa.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Kama ilivyo kwa zao la kahawa kuwa na tozo nyingi; je, ni lini, Serikali itafanya marejeo tena kwa zao la parachichi hasa katika Mikoa ya Njombe na Wilaya ya Rungwe?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza ambalo tumelifanya kwenye parachichi ni kukaa na wadau na kutengeneza mwongozo wa pamoja wa zao ambao pia ndani yake tutajadili makato yote na namna ya uendeshaji wa zao hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba na lenyewe pia tumelipa kipaumbele kwa sababu parachichi ndio dhahabu yetu ya kijani, kwa hiyo tunaiangalia katika jicho la kipekee sana.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Wakulima wa tumbaku wamekatwa makato makubwa sana ya upandaji wa miche ya miti ambapo ni zaidi ya shilingi 813 kwa kila mche mmoja.

Sasa kwa nini, Serikali isiondoe kabisa makato haya kwa wakulima wa tumbaku ili waweze kupanda miti kwa hiari yao bila makato yoyote?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, tumepokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge na tuna kikao cha wadau ambacho tutajadili mambo haya na kuweza kukubaliana kwa pamoja. Kwa hiyo tumeuchukua ushauri wa Mheshimiwa Mbunge.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, ahsante. Swali la kwanza, kwa kuwa katika majibu ya msingi ameitaja Boloti ambayo iko Siha na Ikuini ambayo iko Rombo tu; lakini kwenye swali langu niliuliza tambarare yote ya Mkoa wa Kilimanjaro. Sasa, ni lini wataweza kujenga mabwawa hayo Undugai katika Wilaya ya Hai, Arusha chini kule Chekereni Wilaya ya Moshi Vijijini na Kahe na kule Mwanga ikiweko na Ruvu kule Same?

Mhehimiwa Spika, swali la pili; ni lini mabwawa hayo yanayojengwa na yanayotarajiwa kukarabatiwa yatatumika kufundishia wananchi kutumia drip irrigation ambayo ni umwagiliaji wa matone ili uweze kuwa na tija kwa mazao ambayo yatakuwa yameoteshwa wakati wa ukame?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha maeneo yote yanayofaa kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa tuweze kuyafanyia kazi ili wananchi wetu waweze kulima mwaka mzima, ni muondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba katika bajeti yetu ambayo tutakuja kuisoma hapa tumeitengea eneo hili fedha za kutosha kuhakikisha kwamba tunapitia maeneo yote ikiwemo Mkoa wa Kilimanjaro katika maeneo ambayo ameyataja.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, teknolojia ya umwagiliaji wa matone ni kati ya teknolojia ambayo inatumika katika maeneo mengi sana hivi sasa nchini, na sisi kama Wizara ya Kilimo tunaiunga mkono. Isipokuwa tu katika Mabwawa ambayo ameyatamka teknolojia hii huwa inaendana na aina ya mazao yanayolimwa. Kwa hiyo kama mazao yanayolimwa yatakuwa yanahitaji teknolojia hii tumeshaanza, na ukienda katika Bwawa letu la Chinangali hapa Dodoma tayari kuna umwagiliaji wa matone katika zao la Mzabibu.
MHE. FRANCIS L. MTEGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa mabwawa sita Wilayani Mbarali ili kuboresha kilimo cha mpunga?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika miradi yetu yote sita iliyoko Mbarali tumemaliza taratibu zote na miradi mingine wakandarasi tayari wako site. Miradi kama ya Utuo, Isenyera, Gonakuvagogoro, Helmanichosi yote yana mkandarasi na kazi inaendelea. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kujenga miradi hiyo na kazi inaendelea.
MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kuna changamoto kubwa sana kwenye ukanda wa joto wa Mufundi kwenye zile kata Saba nadhani unazifahamu Mheshimiwa Naibu Waziri, Nyororo, Maduma, mbalamaziwa, Ihoanza, Itandula pamoja na Idunda;

Je, ni lini sasa Serikali watatuletea scheme za umwagiliaji ili wananchi wa pale waweze kulima kipindi chote?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika,napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, moja kati ya kazi kubwa ambayo tutaifanya katika mwaka wa fedha ujao ni kuhakikisha scheme zote za umwagiliaji tunazozijenga zinakuwa na chanzo cha maji ili wakulima waweze kulima mwaka mzima. Mheshimiwa Mbunge katika bajeti inayokuja maeneo uliyo yataja tutachimba mabwawa kwa ajili kuanza scheme za umwagiliaji ili wananchi wetu waweze kulima mwaka mzima.
MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Katika Mkoa wa Morogoro kuna maeneo mengi yana maji ya kutosha;

Je ni lini sasa Serikali itajenga scheme ya umwagiliaji katika maeneo ya Mvomero na maeneo ya Mofu katika Halmashauri ya Mlimba?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli Mkoa wa Morogoro una maeneo mengi yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na tunayo miradi mingi ambayo inaendelea. Maeneo ambayo ameyataja nayachukulia kwa uzito mkubwa na hivyo nitaagiza wataalam wangu waende kuyaangalia, ili kama yanafaa basi tuyaingize katika mpango wetu ili kuhakikisha kwamba wakulima wanalima kupitia kilimo cha umwagiliaji.
MHE. NDAISABA G. RUHORO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, kwa kuwa Serikali ilikuja kujenga miundo mbinu ya umwagiliaji kwenye bwawa kwenye Bonde la Bigombo liliko Ngara mwaka 2013 na kwa kuwa Serikali ilitelekeza bwawa hilo na miundombinu yake mwaka huo huo wa 2013;

Je, ni upi mkakati wa Serikali wa kuja kujenga lile bwawa na kulikamilisha?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nimesikia kilio cha Mheshimiwa Mbunge juu ya mradi wa scheme ya Bigombo ambayo ameutaja. Namwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na timu yake nzima kwenda kuliangalia bwawa hilo na scheme hiyo ili kujua changamoto iliyopo tuweze kuitatua. Kwa hiyo nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, timu yangu itaelekea huko kwenda kuangalia,
lengo letu ni kuhakikisha kwamba wananchi wetu wanafanya kilimo cha umwagiliaji.
MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza;

Je, ni nini mpango au Mkakati wa Serikali kujenga scheme ya umwagiliaji katika ukanda ule wa delta kule kwetu Kibiti?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha tunayatumia mabonde yote makubwa nchini kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji. Tarehe 30 mwezi wa tatu mwaka 2023 mbele ya Mheshimiwa Rais, wakandarasi 22 walisaini mkataba wa mabonde yote ya kimkakati likiwemo bonde la Rufiji, Mto Ngono, Mto Manongawembele, Ziwa Victoria, Mto Luhuhu, Mto Songwe, Mto Ruvuma, Ifakara Idete na mpaka Litumbandio kwa Mheshimiwa Benaya Kapinga.
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kunipa nafasi. Mradi wa umwagiliaji wa Arusha chini upo katika bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya kufanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu lakini hadi sasa kazi hiyo haijafanywa. Je, ni lini kazi hiyo itafanyika?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema ipo miradi ambayo tuko hatua za mwisho za manunuzi ikiwemo mradi huo. Kwa hiyo nimwondoe hofu kwamba ilikuwa imeshapangwa na itatekelezwa kama ilivyopangwa, ahsante.
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, Swali langu nilikuwa nataka kujua, Serikali itueleze kiujumla imejipangaje kuendeleza kilimo cha umwagiliaji kimkakati kitaifa katika mabonde yale ya kimkakati kitaifa yakiwemo na mabonde ya Namtumbo katika Bonde la Mwangaza, Liyuni, Likonde, Kitanda, Lusewa, Amani, Namahoka na Nambecha?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nimetoka kusema hivi sasa, kwamba Serikali tunayo dhamira ya dhati kabisa kuhakikisha kwamba tunayatumia mabonde yote ya kimkakati katika kilimo cha umwagiliaji ili kuwawezesha wananchi wetu kulima mwaka mzima na zaidi ya mara mbili katika mwaka na maeneo ambayo ameyataja ni katika Mkoa wa Ruvuma.

Mheshimiwa Spika, eneo la Namtumbo pia tumeliweka katika mkakati wetu lakini kwa hivi sasa katika Mkoa wa Ruvuma tayari tunalo Bonde la Mto Luhuhu ambapo pale tuna zaidi ya hekta 3700; ambayo tumeanza kuyafanyia kazi, pamoja pia na bonde la Mto Ruvuma. Kwa hiyo sehemu ya Namtumbo ambao ameitaja Mheshimiwa Mbunge tutakwenda kuyapitia ili kuona, kama yanafaa tutayaingiza katika utaratibu wa kilimo cha umwagiliaji.
MHE. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi; nataka kujua ni lini scheme ya umwagiliaji itajengwa Makwale Wilayani Kyera?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, scheme ya Makwale Wilayani Kyera ni moja kati ya scheme muhimu sana kwa wakulima wa Wilaya ya Kyera. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, kwamba tarehe 25/4/2023 tunakwenda kusaini mkataba na mkandarasi na kazi itaanza mapema kwa ajili ya ujenzi wa scheme hiyo.
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante, scheme ya umwagiliaji ya Mkoka ni moja ya scheme ambazo zimeharibiwa na mvua zilizokuwa zinaendela na hivyo kuleta kero kwa wakulima; Mheshimiwa Waziri unatusaidiaje kwa ghafla au kwa dharula?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika,napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nitaelekeza timu yangu ya wataalam kuangalia athari iliyojitokeza na tuweze kukarabati scheme hiyo ili wananchi waendelee na kilimo cha umwagiliaji.
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwa kwenye majibu ya Mheshimiwa Waziri eneo ambalo tayari limeshafanyiwa upembuzi yakinifu liko Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Morogoro Vijijini.

Je, Serikali haiko tayari sasa kuja kufanya upembuzi yakinifu kwenye Jimbo la Kibaha Vijijini kwenye Kata za Ruvu, Dutumi, Kwala, Gwata, Kikongo ili tuweze kuona namna bora ya kuwahudumia wakulima wadogo katika eneo hilo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Tunaposema wakulima kwenye Bonde la Ruvu ni wakulima wadogo, ni wadogo kweli kwa sababu wanatumia umwagiliaji kwa kutimia mashine ndogo na keni za mkono; na kuna katazo la watu kufanya umwagiliaji kwa kutumia Mto Ruvu. Je, Serikali inatoa tamko gani kuwasaidia watu wa Jimbo la Kibaha Vijijini kuendelea na umwagiliaji wa kutumia keni kwa kuwa hawajawa na mabwawa ya kutosha? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, tarehe 20 Machi, 2023 tuliingia mikataba na washauri waelekezi kwa ajili ya kwenda kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika mabonde 22 hapa nchini Tanzania likiwemo Bonde la Mto Ruvu. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba katika skimu alizizozitaja zitaingia ndani ya mpango huo wa Serikali ambapo kazi inaanza mwaka huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kuhusiana na katazo; kwa mujibu wa sheria inayoongoza matumizi ya maji na sheria za mabonde, imeweka utaratibu wa matumizi ya maji kupitia kibali maalum. Sisi kama Wizara tutakaa na wenzetu wa bonde kuweka utaratibu mzuri ili mwisho wa siku wakulima wetu wale wadogo walime kupitia taratibu zote za kisheria na kutunza mazingira pia. Kubwa zaidi ni kwamba tutaweka miundombinu mikubwa zaidi ili wananchi waachane na changamoto hiyo ya kubeba makopo kwenda kumwagilia.
MHE. KENNETH E. NOLLO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, msimu wa mwaka jana Mkoa wa Dodoma hatukupata mbegu za mtama mfupi lakini vile vile mbegu ya alizeti hatukupata na nataka kupata majibu ya Serikali. Serikali ina mkakati gani kwa msimu unaokuja ili kwanza tupate uhakika wa mbegu ambao tumekuwa hatupati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la jingine la pili ni kwamba Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kwamba yapo mabwawa saba ambayo miongoni yatajengwa Dodoma. Je, mabwawa hayo ni yapi na yataanza kujengwa lini?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza la kuhusu mbegu za alizeti na mtama mfupi nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika msimu ujao wa kilimo wakulima wa Mkoa wa Dodoma pia watanufaika na utoaji wa mbegu hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili la kuhusu mabwawa. Katika jibu langu la msingi nimetamka mikoa mitatu kwa maana ya Tabora, Dodoma pamoja na Singida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mabwawa ambayo tunayo mpaka yanaendelea hivi sasa ni mabwawa ya Msagali pale eneo la Mpwapwa, Bwawa la Membe ambalo litakuwa lina uwezo wa kuzalisha maji mita za ujazo milioni 12 lakini vile vile Lyamalwaga ambayo iko Nzega, vile vile Kongogo ambayo iko Bahi na mengine akiyataka kwa orodha nitamtajia yote katika Mkoa wa Dodoma, kwa sababu ya muda naomba niyataje haya machache. (Makofi)
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kuuliza swali la nyongeza. Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza tija kwenye zao la korosho ambao kwa msimu uliopita imeuzwa kwa bei ya chini na ya kutupa na kuwaletea hasara wananchi wa Mtwara? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Sera yetu ya Kilimo ya mwaka 2013 kipengele cha pili (2)(3) likiwa ni lengo la pili la malengo 10 ya sera ya kilimo imeeleza kuhusu tija katika mazao yote ya kilimo hapa nchini. Yako mambo lazima tuyafanye kama Serikali ili wakulima wetu waweze kulima kwa tija. Jambo la kwanza ni kuhakikisha tunapima afya ya udongo kutambua virutubisho ndani ya udongo ili tuwashauri vizuri wakulima wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha pili ni kuimarisha utafiti na cha tatu ni huduma za ugani na ugawaji wa pembejeo. Nataka nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwenye korosho tunajua kuna changamoto nyingi na jana tulikuwa na kikao cha tathmini tumeyaona na tutayafanyia kazi ili wakulima wa korosho na wenyewe waweze kulima kwa tija tuweze kufikia malengo na matarajio ambayo tumejiwekea kama nchi.
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru kwa majibu ya Serikali japo niseme nina imani sana na Mheshimiwa Bashe na Mheshimiwa Antony Mavunde kwa sababu skimu hii imekuwa ni muda mrefu imetelekezwa bila mafanikio. Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, skimu hii imeshatumia zaidi ya shilingi milioni 944 ambazo hazikuleta tija yoyote. Je, ni nini commitment ya Serikali kuhakikisha kwamba sasa inaumalizia mradi huo na unakuwa na tija kwa wananchi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Wakulima wa eneo hilo walisimamishwa kuendelea na ulimaji katika skimu hiyo mwaka 2013, leo ni miaka 10 tunapoongea hakuna chochote kinachoendelea. Naomba Serikali itoe matumaini kwa wananchi hao kuweka commitment kwamba sasa skimu hii inaenda kukamilishwa na wananchi wanarudi pale kwa ajili ya kulima kilimo cha umwagiliaji na kuleta tija katika maisha yao?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza ni commitment. Nataka nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, ni dhamira ya Serikali ya kuhakikisha ya kwamba tunaendeleza kilimo cha umwagiliaji kupitia miradi mbalimbali. Mradi wa Kyakakera ambao umekaa muda mrefu ni mkombozi mkubwa wa wakulima. Tumekwisha mwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha wanalipitia eneo hili na tulikamilishe kwa haraka ili wakulima wetu waanze kutumia mradi huu kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, sisi wenyewe hatupendi kumwona Mkulima amekaa bila kufanya kilimo lakini mradi huo ulikuwa chini ya DADP na ziko changamoto ambazo zilijitokeza katika utekelezaji wa hii miradi na hivi sasa tumejikita kuhakikisha kwamba tumejenga miradi ambayo itakuwa ni bora na ya kudumu muda mrefu ili wakulima wetu wasipate shida. Miaka 10 ya wakulima ni mingi nataka nikafute kilio hicho kwamba Mkurugenzi Mkuu akienda huko aifanye kazi hiyo vyema wakulima hao waweze kuanza kulima mapema kabisa katika msimu unaokuja hivi karibuni.
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasi hii kuishukuru Serikali kwa kutenga zaidi shilingi milioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Endagaw. Kwa sasa mkandarasi ameweza kusimamishwa. Je, ni lini Serikali itatuletea mkandarasi ili aweze kukamilisha ujenzi wa skimu hiyo na uweze kuleta tija kwa fedha za Serikali lakini kwa wananchi pia? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru Mbunge amekuwa mfuatiliaji mzuri katika eneo hili. Ni kweli mkandarasi aliyekuwepo Endagaw tulimsimamisha na kumwondoa lakini tuko katika hatua za mwisho za kumpata mkandarasi mwingine ambaye atakwenda kukamilisha kazi hiyo kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge wape tu matumaini wakulima wako kwamba kazi itakamilika na watafanya kilimo cha umwagiliaji.
MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwa bajeti inayoendelea sasa Bunge hili lilipitisha uanzishwaji wa Skimu ya Ibanda Geita na Igaka Sengerema. Ni lini utekelezaji wa skimu hii utaanza?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa Ibanda ni moja kati ya miradi muhimu sana katika Mkoa wa Geita na hususan Jimboni kwa Mheshimiwa Kanyasu. Habari njema ni kwamba tumekwisha kutangaza juu ya Bwawa la Ibanda na muda siyo mrefu pia tutatangaza kumpata mkandarasi kwa ajili ya skimu.
MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, vijana wanaoshughulika na kilimo katika Mkoa wa Kigoma wana changamoto ya mitaji.

Je, ni lini Serikali itawaongeza mitaji ili kuongeza tija katika shughuli za kilimo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; je, ni lini eneo la Mradi wa BBT lililotengwa na Serikali katika Mkoa wa Kigoma, mradi huu utaanza kutekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza la kuhusu mitaji kwa ajili ya vijana wanaofanya shughuli za kilimo. Ni dhamira ya Wizara ya Kilimo na Serikali kwa ujumla kuhakikisha tunawawezesha vijana wote ambao wanashiriki katika kilimo ili waweze kufikia malengo na matarajio yao. Kupitia Mfuko wa Pembejeo hivi sasa tumeshaanza kutoa matangazo ya kuwakaribisha vijana wote ambao katika shughuli za kilimo kuja kuomba mikopo na mikopo yetu itakwenda katika riba ya chini kabisa ili vijana wengi waweze kunufaika.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, katika eneo la Kasulu tunayo mashamba ya kilimo kwanza ambayo katika Kijiji cha Kwitanga na tunayo mashamba pia ya Makere ambayo katika vijiji vya Mgombe na Mvinza. Yote yana ekari elfu tano tano. Nataka nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba, baada ya vijana hao kumaliza mafunzo, tutaanza utekelezaji mara moja na vijana wa Kigoma watanufaika kupitia mradi huo.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa fursa hii. Kwanza kabisa naomba niipongeze Serikali kwa jitihada zake zinazofanya kuhakikisha vijana wanashiriki kikamilifu kwenye shughuli za kilimo kupitia programu hii ya BBT. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha akinamama ambao ni wazalishaji wakubwa kushirikishwa kwenye mpango kama huu kama akinamama wa Mkoa wa Arusha? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiiangalia hii Programu ya BBT pia inahusisha na akinamama. Kwa hiyo akinamama wako ndani katika programu hii, natumai kwamba akinamama wa Mkoa wa Arusha pia watachangamkia fursa hii ya kushiriki kwenye kilimo. (Makofi)
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa kuwa maeneo haya yana jumla ya hekta zaidi ya 490 na Serikali iliwekeza kama ilivyosema bilioni 1.260 lakini sasa maeneo haya imekuwa wafugaji wanafanya kama maeneo ya malisho na kuharibu mazingira katika maeneo yale. Je, Serikali inaweza kuharakisha kazi iliyokusudia ili kumaliza miundombinu yake na kuweza kufanya kazi ya kilimo cha umwagiliaji kiweze kuendele kwa mwaka mzima?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Serikali kuu inaweza kutusaidia kuondoa wafugaji hawa katika maeneo yale ili yabaki kama eneo la kilimo kama lilivyokusudiwa na kwa kuwa Serikali iliwekeza fedha nyingi?
NAIBU WAZIRI KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa Mbunge wa Namtumbo kama ifuatanvyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la kwanza la kuharakisha nataka nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika miradi ambayo tuliipitia nchi nzima na kuangalia hatua ambayo imefikia na imekwamia wapi ni pamoja na miradi hii ambayo ipo Kata za Liyuni na Limamu nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, kwamba katika mwaka huu wa fedha tutahakikisha kwamba tunafanya upembuzi yakinifu ili kazi ya ujenzi ianze mara moja na wananchi waanze kufanya kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ya kuhusu wanyama, hili liko ndani ya Uongozi wa wilaya husika na sisi tuko tayari kusaidia nao kuhakikisha kwamba eneo hili linalindwa hivyo nitoe rai kwa uongozi wa Wilaya kuhakikisha kwamba maeneo haya yanasimamiwa vizuri na yanalindwa ili yabaki katika matumizi ambayo yamekusudiwa. (Makofi)
MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nilikuwa na maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza: -

Je, ni lini sasa mchakato huu wa Serikali utakwenda kukamilika?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa maeneo haya ni maeneo ya asili ya makazi ya wananchi, kwa mfano, maeneo ya Mtunda, Moyoyo, Nyafeja Pamoja na Nguwalo.

Je, Serikali ina mkakati gani sasa kuweza kuhakikisha wakati wa kugawa maeneo haya wananchi hawa wanakwenda kupewa kipaumbele, kupata maeneo ya kulima ili waweze kuendesha maisha yao na vilevile kuchangia Pato la Taifa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza ni lini mchakato huu unakamilika? Tarehe 23 Mei, 2023 tunategemea taratibu zote za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ziwe zimekamilika na tutaanza ujenzi katika mwaka wa fedha unaoanza 2023/2024, kwa maana kuanzia tarehe 1 Julai mwaka 2023.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili la kuhusu maeneo haya kugaiwa kwa wakazi wa maeneo hayo. Ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhakikisha kwamba wanufaika wa kwanza wanakuwa ni wakazi wa maeneo hayo. Kwa hiyo nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba wananchi wake watapata maeneo katika mashamba haya.
MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwanza naipongeza na kuishukuru Serikali kwa kutupatia fedha kwa ajili ya bonde hili moja. Tunaiomba Serikali itupatie fedha kwa mwaka unaofuata kwa ajili ya Bonde la Kwamngumi pamoja na Bonde la Kwamsisi kwenye Halmashauri yetu ya Korogwe Mjini.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, Dkt. Alfred James Kimea kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tumepokea maombi yake na kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi, tayari Kwamngumi tumeshaingiza katika Mpango wa mwaka 2023/2024 kwa ajili ya upembuzi yakinifu. Hivyo nimwondoe hofu, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kwamba inawekeza katika miundombinu ya umwagiliaji. Tutapitia tena na maeneo mengine ambayo ameyataja hasa katika eneo la Kwamsisi.
MHE. MARTHA F. MARIKI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa. Je, ni lini mradi wa umwagiliaji wa Mwamapuli uliopo Halmashauri ya Mpimbwe utaanza kujengwa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ukisoma katika kitabu chetu cha kwenye bajeti kiambatisho Na. 6, kimeelezea skimu ambazo tunakwenda kuzifanyia kazi kwa maana ya ujenzi kwa mwaka 2023/2024.

Mheshimiwa Spika, skimu ya Mwamapuli yenye hekta 12,000 Wilaya ya Mpimbwe ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa katika mwaka wa fedha unaokuja. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge skimu hiyo inakwenda kutekelezwa.
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, ahsante naomba tu kujua Serikali itaenda lini kuangalia skimu ya umwagiliaji ya Kisango na skimu ya umwagiliaji ya Mariwanda ili kuifanyia kazi. Lini mtaenda kuangalia skimu hizo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha skimu zote zinafanyakazi ili tuongeze eneo la kilimo cha umwagiliaji. Nataka nimuhaidi Mheshimiwa Mbunge, kwamba nitawaelekeza watalamu wangu kwenda kupitia maeneo ambayo ameyataja ili tuweze kupata picha halisi na tuingize kwenye mpango. (Makofi)
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Je, ni lini Serikali itaendeleza Ujenzi wa skimu ya Kijiji cha Mwagrila baada ya kutumia shilingi bilioni 1.2 na haikuwa kwenye mpango wa Serikali? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nataka nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tulituma watalamu kupitia skimu zote nchi nzima, zile ambazo zilikwama na zile ambazo zinahitaji marekebisho tumeishatengeneza picha nzuri ya kuzijua zote pamoja na hiyo ambayo ameitaja nataka nimtoe hofu ya kwamba ipo ndani ya mipango ya Serikali tutaitekeleza.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza je, ni lini mradi wa Mgambalenga katika kata ya Ruaha Mbuyuni utakamilika, kwa sababu toka mwaka 2014 umeanza kujengwa lakini haupatiwi pesa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika skimu 42 ambazo zilifanyiwa upembuzi yanikifu na usanifu wa kina katika mwaka wa fedha 2022/2023 ni pamoja na skimu ya Mgambalenga. Hivyo katika Mwaka 2023/2024 skimu hii itaendelea kufanyiwa ukarabati wa miundombinu na kazi itafanyika kwa uharaka zaidi ili wakulima waweze kupata fursa ya kufanya kilimo cha umwagiliaji. (Makofi)
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru nina maswali mawili ya nyongeza. Ningependa kupata kauli ya Serikali, kule kwetu Muleba wakulima wanafukuzwa wanakamatwa wakisafirisha kahawa kutoka kata moja hadi kata nyingine na katika tarafa hadi tarafa nini kauli ya Serikali?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; nilitaka kujua kahawa ni mali ya nani? Ni mali ya Serikali au ni mali ya mkulima? Na ni lini ile hadhi inabadilika? Nashukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge Dkt. Kikoyo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, kauli ya Serikali ni marufuku kwa wakulima wa kahawa walioko katika eneo moja kukamatwa na kuzuiwa kufanya biashara yao kwa sababu biashara hii inafanyika kwa mujibu wa Sheria Na. 23 ya mwaka 2001.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, zao la kahawa kama alivyouliza Mheshimiwa Mbunge, katika hali yake ya kawaida Serikali inafanya uratibu lakini mazao haya ni ya wakulima. Najua alikuwa anaelekea wapi, lakini lengo kubwa la Serikali ni kuhakikisha kwamba tunasimamia na kumfanya mkulima wa kahawa aweze kunufaika. Kwa hiyo kama Serikali tutaendelea kuhakikisha kwamba tunaweka mazingira wezeshi ili mkulima wa kahawa aweze kunufaika.
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, mnada wa Kahawa wa Songwe ni tofauti kabisa na mnada wa kahawa uliopo kule Kagera. Mazingira ya pale Songwe siyo rafiki, hauko wazi na kuna uhuni mwingi unaofanywa na baadhi ya wanunuzi kwa kushirikiana na watu wa bodi kuchezesha bei ya kahawa kwenye mnada ili wakulima wasipate bei inayostahili.

Je, kwa nini Serikali isiboreshe mazingira ya mnada wa kahawa wa Songwe ufanane kama mnada wa kahawa wa Kagera ambao uko wazi fair na hakuna uhuni wowote unaoweza kufanyika?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge George Mwenisongole, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Kagera inalimwa robusta, Songwe inalimwa arabica. Haya ni variety mbili tofauti. Ukienda kwenye soko ili uweze kuuza kahawa ya arabica lazima pia ionjwe ndio unapata radha na quality inayokwenda ku-determine bei. Tumesikia hoja ya Mheshimiwa Mbunge naelekeza bodo ya kahawa kuhakikisha kwamba wanaweka mazingira wezeshi ili pia mkulima wa Songwe aweze kunufaika na bei ya kahawa.
MHE. INNOCENT M. BILAKATWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Zao la kahawa limevamiwa na ugonjwa wa mnyauko.

Je, Serikali iko tayari kuongeza miche yenye ubora ili zao hili muhimu lisije likafutika?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhamira ya Serikali kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa; na katika bajeti yetu ya mwaka 2023/2024 tumeongeza miche kufikia miche milioni 20 ili wakulima waweze kupata miche bora ambayo pia itakuwa na ukinzani wa magonjwa ambayo yanaathiri zao la kahawa.
MHE. FRANCIS I. MTINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri sana ya Serikali yanayotia moyo; hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Halmashauri ya Mkalama inategemea sana vitunguu kwa mapato yake ya ndani.

Je, Serikali haioni haja ya kwamba mpango huu mzuri ufanyike kwa mtindo wa build and design ili uweze kwenda kwa haraka zaidi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa pale Mwangeza kuna mradi wa ASDP two ambao ulibomoka;

Je, Serikali haioni sasa haja ya kuukarabati mradi huo haraka ili wananchi wa pale mwangeza waendelee kupata umwagiliaji wakati wakisubiri hili bonde la vitunguu kufanyiwa design?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika miradi yote ya umwagiliaji ambayo tumeipita nchi nzima utaratibu unaofanyika hivi sasa ni kuhakikisha kwanza tunaanza na upembuzi yakinifu na baadaye ndipo unakuja usanifu wa kina na kisha twende kwenye ujenzi. Hii ni kwa sababu tulipata changamoto ya miradi mingi sana ya miaka iliyopita ambayo haikupitia hatua hii na hivyo imekuwa ikibomoka kwa haraka sana. Lengo la Serikali ni kuhakikisha kwamba miradi hii inakuwa endelevu na ya kudumu ili wakulima waweze kunufaika. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge wavumilie taratibu hizi zikamilike mradi huu utajengwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili la kuhusu Mwangeza. Katika kiambatisho cha saba katika jedwali lile la bajeti yetu eneo la Mwangeza ni kati ya maeneo ambayo yanakwenda kufanyiwa upembuzi yakinifu na baadaye pia tutajenga skimu na kukarabati ili wakulima waweze kupata fursa ya kushiriki katika kilimo cha umwagiliaji. Kwa hiyo ni eneo ambalo lipo ndani katika mipango ya Serikali tayari.
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kuniona. Jimbo la Kalenga lina skimu 19 za umwagiliaji ambazo miundombinu yake yote ni chakavu.

Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba miundombinu hii inaboreshwa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika bajeti yetu ya mwaka 2023/2024 tumetenga maeneo zaidi ya 80 ambayo yanakwenda kufanyiwa ukarabati zikiwemo skimu zilizo katika Jimbo la Kalenga. Kwa hiyo nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, anaweza kupitia akaangalia orodha yetu na akaona kama maeneo yao yapona aweze kujiridhisha.
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii; je, ni lini Serikali itajenga bwawa na mifeji kwa ajili ya umwagiliaji katika Kata za Shambalaiguruka na Majengo kwa lengo la kupunguza athari za mvua na mafuriko ya Mto Nduruma na Mto Chiplepa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika bajeti yetu inayokuja tumetangaza kwamba tunaenda kujenga mabwawa 100 ambayo yatagusa takriban maeneo yote nchi nzima. Hivyo katika wilaya ya kwake Mheshimiwa Mbunge tunakwenda kuangalia maeneo ambayo amaeyataja. Kama si hayo basi tutaichukua kama sehemu pia ya kuifanyia kazi ili katika wakati mwingine ujaotuweze kuyajenga pia.
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, pia nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri. Ni kweli kitalu kiko tayari na wakulima wanaendelea kupata miche ya kahawa. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa zao la kahawa ni zao ambalo linaingiza fedha nyingi za kigeni: -

(a) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha zaidi zao hili la kahawa hapa nchini?

(b) Je, ni lini Serikali itaruhusu bei ya zao la kahawa kuamuriwa na nguvu ya soko?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na swali la kwanza la kuboresha na kuhakikisha kwamba tunatafuta masoko ya uhakika. Ni dhamira ya serikali ya awamu ya sita kuhakikisha kwamba zao la kahawa linaendelea kuwa na mchango mkubwa katika kuingiza fedha za kigeni na kubadilisha maisha ya wakulima wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa tunaendelea na kuitangaza kahawa yetu nje ya mipaka ya Tanzania kwa sababu wanunuzi wakubwa wanatoka nje ya mipaka ya Tanzania. Tunashirikiana na Balozi zetu mbalimbali na kupitia matamasha na maonesho mbalimbali tumekuwa tukiitangaza kahawa yetu na jambo hili limetuletea tija kubwa sana. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaendelea kuhakikisha kwamba tunaweka miundombinu wezeshi ili zao hili liweze kupata soko la uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili la kuhusu bei ya kahawa kuamuliwa na nguvu na soko. Mwenendo wa masoko rejea ya kahawa duniani ndiyo ambayo huwa yanaamua bei ya kahawa. Masoko haya ni masoko ya New York kwa kahawa ya arabika na Euronex Uingereza kwa ajili ya robusta. Sisi kama Serikali tumehakikisha kwamba mara zote tunahakikisha wakulima wetu kupitia taarifa hizi wanapata taarifa sahihi na mwisho wa siku waweze kupata bei ambayo itamnufaisha. Kwa hiyo kama Serikali tumeacha nguvu hiyo ya soko iamue, lakini tunawasaidia wakulima wetu kuzalisha kahawa bora ambayo itasaidia pia kuongeza tija katika Soko hilo la Kimataifa. (Makofi)
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa fursa. Nina maswali mawili ya nyongeza. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali na kwamba mmeanza kugawa miche ili tuboreshe uzalishaji wa Kahawa. Kwa kuwa mmegawa miche; je, sasa Serikali ina mikakati gani ya kuboresha zile skimu za umwagiliaji za asili ili tuweze kuongeza tija kwenye kuzalisha kahawa, kwani bila maji hata hiyo miche haitakuwa inafanya vizuri sana?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Je, Serikali ina mkakati gani wa kusindika kahawa aina ya Arabica kwa sababu kahawa hii ina soko zuri sana katika soko la Dunia na kuna teknolojia nyingi za kawaida tu ambazo zinaweza zikatumika tukapata chapa au brand yetu: Je, Serikali ina mkakati gani wa kutusaidia kusindika kahawa hizi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza la kuhusu skimu za umwagiliaji wa mifereji ya asili, tunao wakandarasi ambao wako katika Mkoa wa Kilimanjaro, wanaotekeleza miradi ya umwagiliaji, wameshapata maelekezo watakwenda kukarabati na kujenga mifereji yote ya asili inayogusa jimboni kwa Mheshimiwa Ndakidemi, kwa Mheshimiwa Saashisha pamoja na kwa Mheshimiwa Dkt. Kimei.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, Serikali inao mkakati wa dhati kabisa kuhakikisha kwamba tunaendelea kusindika kahawa yetu na tusiuze kahawa ambayo haijasindikwa. Hivi sasa Bodi ya Kahawa imeshatoa zaidi ya leseni 20 kwa ajili ya wasindikaji ili kuchochea usindikaji wa zao la kahawa na mwisho wa siku tutengeneze masoko ya uhakika. Hivi sasa tumepata nafasi kahawa yetu inauzwa sana na kupekekwa Japani ikiwa ni sehemu ya kazi nzuri ambayo imefanywa katika hatua ya awali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, kazi hii inaendelea.
MHE. MUHARAMI S. MKENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nina maswali mawili ya nyongeza. Bonde la Mto Ruvu katika sehemu ya Bagamoyo lina wakulima wengi sana ambao wanatokea Kata za Yombo, Magomeni na Makurunge: Je, ni lini sasa Serikali itawaombea wananchi hawa kupata eneo la Magereza ambalo ni kubwa na halina kazi yoyote inayoendelea ili waweze kufanya kilimo na kupata mahitaji yao?

Swali la pili. Mheshimiwa Waziri ni lini atakuja Bagamoyo kutembelea skimu ya umwagiliaji Ruvu inayojulikana maarufu kama JICA ili kuweza kuja kuzungumza na wakulima pale na kutupa matumaini kwa ajili ya kutengeneza skimu ile? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli pale kwenye eneo la Gereza la Kigongoni tunazo hekta zaidi ya 1,350 na kumekuwa na changamoto juu ya matumizi ya wananchi katika ardhi ya eneo hilo. Nachukua fursa hii kumwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji waende kukaa na uongozi wa gereza ili waone namna ambavyo wananchi wa kata ulizozitaja wataweza kushiriki kilimo katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili la kuhusu kutembelea Bagamoyo baada tu ya vikao vya Bunge la Bajeti, mimi na wewe tutakwenda kuzungumza na wakulima ili tuweze kusikiliza changamoto zao na tuweze kuwatatulia ili wafanye kilimo cha umwagiliaji.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Je, ni lini skimu ya umwagiliaji ya Kwamtonga iliyopo kwenye Kata ya Sungaji Wilayani Mvomero itafanyiwa uboreshaji kusudi wananchi wengi waweze kulima kwa mwaka mzima kwani maji ya kutosha yapo? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kiambatanisho Na. 8 katika bajeti ya Wizara ya Kilimo aliyosoma Mheshimiwa Waziri, tumeorodhesha skimu zote ambazo tutazifanyia ukarabati na ikiwemo skimu ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja. Nimwondoe hofu, hii kazi itafanyika.
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Skimu ya Umwagiliaji ya Ndungu, Jimboni Same Mashariki, imepoteza ubora wake kabisa. Ni skimu ambayo wananchi wanaitegemea sana katika Tarafa ya Ndungu: Je, Mheshimiwa Waziri ni lini utakuja kuiona ili uone pamoja na Mto Saseni? Vipo karibu.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ahadi ya Serikali kupitia Bunge lako Tukufu ambayo tuliitoa humu ndani kwamba tutakwenda kuzitembelea skimu hizo, lakini kabla sijafanya hivyo, nitamwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Umwagiliaji pamoja na wataalam wake wapite kwanza kuangalia, nami na Mheshimiwa Mbunge tutaongozana pamoja kwenda kuzungumza na wananchi na kutatua kero ambazo wananchi wanazo katika eneo hilo.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Wananchi wa Ushetu wametenga hekta zaidi ya 5,000 ambazo ni nzuri na zina mtiririko wa maji kwa ajili ya umwagilijaji: Serikali inakuja lini kuwajengea skimu ya umwagiliaji wananchi wa Jimbo la Ushetu?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niwapongeze Halmashauri kwa kutenga eneo kubwa hilo kwa ajili ya umwagiliaji. Maelekezo yangu ni kumwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kupeleka wataalam kwenda kuliangalia eneo hilo kama linafaa kwa ajili ya kuweka miundombinu basi, Serikali itahakikisha kwamba inaweka miundombinu katika eneo hilo. (Makofi)
MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona. Kata ya Litumbandyosi tulipata skimu katika bajeti hii. Ni lini sasa skimu hii inaenda kuanza ujenzi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bonde la Litumbandyosi ni kati ya mabonde 22 ambayo tarehe 20 mwezi wa tatu mwaka huu tulisaini mkataba na wakandarasi kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na kazi hii inaendelea. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba kazi hii inakamilika mwaka wa fedha huu ambao unaishia. Kuanzia Julai kazi itaanza ili kuwafanya wananchi wako waweze kufanya Kilimo cha Umwagiliaji.
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Halmashauri ya Mji wa Bunda inazungukwa na Ziwa Victoria na hatuna uhaba kabisa wa maeneo. Je, Mheshimiwa Waziri, ni lini mtatujengea skimu ya umwagiliaji ikiwa ni moja ya mkakati wa kuhamasisha vijana kujihusisha na kilimo?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti yetu tumeeleza vizuri kabisa, maeneo yote ambayo yana vyanzo vya uhakika vya maji hasa ikiwemo mito na maziwa tutahakikisha tunawawezesha wakulima wa maeneo hayo kufanya kilimo kupitia umwagiliaji. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge juu ya eneo lake la Bunda, pia tutafanya kazi hiyo kuhakikisha kwamba wakulima wa Bunda wanafanya kilimo cha umwagiliaji.
MHE ENG. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali madogo mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, mbegu za kisasa tunazozitumia unaweza kuzitumia mara moja tu na ni bei ghali. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuendeleza mbegu zetu za asili ambazo unaweza kuzitumia zaidi ya mara moja ili kupunguza gharama kwa wakulima?

Swali la pili, mwaka 2020 Wizara ya Kilimo ilikuja Jimboni Hanang’ na baadaye wakanunua ngano, tukielezwa kwamba zile ngano zilizoko Hanang’ ni bora na zinafaa kuwa mbegu. Je, Serikali ina kauli gani juu ya upatikanaji wa mbegu bora za ngano Nchini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la kwanza mbegu za asili, mbegu hizi zimeendelea kutambuliwa na Taasisi ya Utafiti ya Kilimo Tanzania (TARI) inaendelea kuzifanyia utafiti, vilevile Mamlaka ya Afya, Mimea na Viuatilifu Nchini (TPHPA) na yenyewe sasa iko mbioni kwa ajili ya kutunga Sheria ya Nasaba za Mimea ili kuzitambua, kuzitunza na kuzitumia kwenye utafiti. Kwa hiyo, Serikali inaipa umuhimu suala hili la mbegu za asili.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ni kweli mwaka 2020 tulifanya utafiti huo na tulichukua sampuli ya mbegu 22, tano zikiwa kutoka nje ya nchi na 17 za ndani ya nchi, kwa ajili ya kwenda kuangalia ubora wake. Katika tafiti hii zaidi ya mbegu 10 zimeonekana zinafanya vizuri na zina kiwango kikubwa cha gluten kwa maana ya protein ambayo inazidi asilimia 10, hivi sasa zimeanza kusambazwa katika baadhi ya maeneo kuweza kutumika ili kusaidia upatikanaji wa mbegu bora za ngano.

Mheshimiwa Spika, katika mbegu hizi ziko mbegu za Kariege, Sasambua, Sifa, Chiriku pamoja na mbegu nyingine ya Mbayuwayu ambayo imeonekana kuwa na soko kubwa sana.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Je, Wizara ya Kilimo inaonaje ikitumia muda huu kufungua dirisha la kuwakopesha wakulima mbegu, mbolea, viuatilifu na vitendea kazi vingine ili kujiandaa na msimu wa kilimo ambao unakuja? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hivi sasa Wizara ya Kilimo kupitia Wakala wa Mbegu tupo katika utaratibu wa kuanza kusambaza mbegu kwa msimu unaokuja, kwa kufungua madirisha kupitia hayo maeneo tofauti tofauti. Vilevile tunao Mfuko wetu wa pembejeo ambao nao ni mahsusi kwa ajili ya kuwasaidia wakulima kuweza kupata pembejeo hizi kwa wakati na kwa bei nafuu. Hivyo nitumie fursa hii kuwaomba wakulima wote nchini Tanzania kutumia madirisha haya mawili kwa ajili ya kuweza kupata pembejeo hizi kwa wakati ili wakati wa msimu wawe tayari wanazo na kuanza kutumia kwa ajili ya kilimo.
MHE. NDAISABA G. RUHORO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ninaomba kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba ni kwa nini Serikali wanaendelea kufanya utafiti wa mbegu za asili ambazo zimetukuza wote mpaka hapa tulipo badala ya kuzalisha kwa wingi na kuzisambaza? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika majibu yangu nimezungumza kwamba tayari Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu pale Arusha wanayo benki na wanaendelea kuzitunza mbegu hizi kwa ajili ya usambazi. Kwa hiyo, zoezi la usambazi na kwenye kilimo utafiti haukomi vitakwenda sambamba lakini mwisho wa siku ni kuhakikisha kwamba mbegu hizi zinawafikiwa wakulima kwa wakati. Kwa hiyo, mamlaka inafanya kazi hiyo vilevile utafiti hauwezi kukoma kwa sababu ni kila siku mambo mapya yanajitokeza.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo iliahidi kupeleka mbegu bora za soya kwenye vijiji vingi vilivyopo Jimbo la Ndanda ikiwemo Kijiji cha Mumburu kwa sababu soya ilikuwa inalimwa hapo zamani, ni mwaka wa tatu sasa mbegu hiyo haijaenda.

Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi yake ya kupeleka mbegu kwenye maeneo hayo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nimesikiliza hoja ya Mheshimiwa Mbunge, nimeichukua. Tutakwenda kuifanyia kazi ili wakulima wake waweze kupata mbegu za soya. (Makofi)

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, ahsante.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tatizo hili katika Jimbo la Moshi Vijijini limekuwa kubwa sana; je, Naibu Waziri upo tayari kuambatana na Profesa Ndakidemi kwenda kutatua changamoto hiyo?

Swali la pili, katika Jimbo la Hai SACCOS ya Kware, SACCOS ya Lyamungo, Masama Mula, Mudio na Lemira, wananchi walihamasishwa kujiunga na SACCOS hizi baadae viongozi wale walitoroka na fedha za wanachama.

Je, ni lini Serikali itakwenda katika Wilaya ya Hai kutatua changamoto hizi ikiwa ni Pamoja na kurudisha fedha za wanachama wa SACCOS nilizozitaja? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la kwanza nipo tayari kuongozana na Mheshimiwa Mbunge kwenda katika Jimbo lake kuangalia changamoto zilizopo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, natumia fursa hii kumuelekeza Mrajisi wa Vyama vya Ushirika kuhakikisha kwamba anatuma timu yake kwenda kufanya uchunguzi wa awali juu ya jambo hili na baadaye hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wale wote ambao wametoweka na fedha za wanachama.
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika nakushukuru, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Kumekuwa na ongezeko au utitiri wa viuatilifu vita kwenye zao la korosho; je, Serikali sasa haioni umuhimu wa kutoa elimu kwa wakulima wakati wa ugawaji wa viuatilifu hivi?

Swali la pili, naipongeza Serikali kwa kuanza mfumo wa usajili wa wakulima wa korosho ili kutoa pembejeo na viuatilifu kwa wakulima lakini kuna kundi kubwa la wakulima ambao mpaka sasa hawajasajiliwa.

Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya usajili kwa wakulima hao?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, swali la kwanza la utitiri wa viuatilifu, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi viuatilifu hivi huwa vinatokana na aina ya magonjwa vilevile wadudu waharibifu ambao wanapelekea matumizi ya viuatilifu hivyo. Jambo kubwa ni kwamba kama Serikali kupitia kituo cha utafiti cha TARI-Naliendele pamoja na Bodi ya Korosho tutaendelea kutoa elimu kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu hivi ili mwisho wa siku viweze kuleta tija na tuongeze uzalishaji wa zao la korosho.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili kuhusu usajili wa wakulima. Zoezi la usajili wa wakulima linaendelea. Ni kweli wapo baadhi ya wakulima bado hawajasajiliwa, tunaongeza nguvu kupitia bodi kuhakikisha kwamba tunaongeza idadi ya rasilimali watu ambao watasaidia kufanikisha zoezi la usajili huo wa wakulima ili wakulima wote waweze kusajiliwa na wapate viwatilifu kwa wakati kwa sababu hivi sasa ni takwa la lazima kwamba wakulima tuwe tumewasajili ili waweze kupata viuatilifu kwa urahisi.

Mheshimiwa Spika, hivyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, tunaongeza jitihada kubwa kuhakikisha kwamba zoezi hili linakamilika kwa wakati.
MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, pamoja na kusema kwamba tusitoe pongezi naomba uniruhusu nitoe pongezi kwa Serikali kuhusiana na suala zima la zao la mbaazi. Mbaazi tulikuwa tunauza kilo mpaka shilingi 100 lakini kwenye mnada wa mwisho tumeuza shilingi 2,130. Haya ni mafanikio makubwa sana.

Mheshimiwa Spika, swali langu kwa Serikali, je, bei hii itakuwa ni endelevu ili kuhakikisha kwamba wakulima wanaongeza uzalishaji wa zao hili?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kwamba wakulima wanaendelea kunufaika na kilimo. Tutahakikisha tunaendelea kuweka miundombinu rafiki ili bei hii iendelee kumnufaisha mkulima na hasa wakulima wa mbaazi kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema.
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nichukue nafasi hii mimi pamoja na wananchi wa Kata ya Endagaw na wananchi wa Wilaya ya Hanang, kuiomba Serikali kuhakikisha kwamba ujenzi huo wa mifereji unafanyika sasa na sio kipindi cha masika kwa sababu sisi tunajua uhalisia wa jiografia tunapotoka.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; kwa kuwa wananchi wa Wilaya ya Hanang ni wananchi ambao wanalima sana. Je, Serikali haioni haja sasa ya kuendelea kuongeza mabwawa ili wananchi wa Wilaya ya Hanang waweze kulima kilimo cha uhakika na chenye tija? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, baada ya kumwondoa mkandarasi aliyeshindwa kufanya kazi yake vizuri, hivi sasa tunahakikisha kwamba mkandarasi ambaye tutamtangaza aifanye kazi hii kwa haraka na kuwahi msimu huo ambao umekuwa na athari kubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Waziri, la pili, ni kweli Wilaya ya Hanang ina wakulima wengi. Katika mpango wa Serikali, mwaka huu wa fedha tutakwenda kuchimba bwawa eneo la Laganga ambapo zaidi ya hekta 600 za umwagiliaji zitapatikana na wakulima wa eneo la Hanang watapata maeneo ya kilimo chao cha umwagiliaji. (Makofi)
MHE. NDAISABA G. RUHORO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Serikali kupitia Wizara ya Kilimo mradi wake wa DASP walifika Ngara mwaka 2015, wakaanza kujenga Skimu ya Umwagiliaji ya Vigombo, wakaitelekeza ikiwa imefika katikati kwa zaidi ya miaka nane iliyopita. Je, ni lini Wizara ya Kilimo itafika Ngara na kuja kukamilisha Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Vigombo? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha miradi yote ya umwagiliaji inakamilika na ndiyo maana tumewekeza fedha nyingi kwa ajili ya ukarabati na kuipitia. Nichukue fursa hii kumuahidi Mheshimiwa Mbunge ya kwamba nitampa maelekezo Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji aelekee katika eneo la Rulenge pale Vigombo ili aangalie mradi huu na tuone namna ya kuweza kuwakwamua wananchi ili wafanye kilimo cha umwagiliaji.
MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itakamilisha kujenga miundombinu ya umwagiliaji, hasa kusakafia mifereji mikuu katika Skimu ya Mangisa na Diri iliyoko Wilayani Mbulu?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, tumeendelea kuipitia miradi yote ya skimu za umwagiliaji ambayo ilikuwa ina changamoto na tumetenga fedha za mwaka huu na mwaka wa fedha ujao. Hivyo, nitakaa na Mheshimiwa Mbunge kuangalia katika mwaka huu kama haijawekwa kwenye bajeti hii, basi tuitengee bajeti inayokuja ilimradi tu wakulima waweze kupata fursa ya kufanya kilimo cha umwagiliaji.
MHE. FRANSIS K. NDULANE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naona majibu ya Mheshimiwa Waziri yamekuwa mepesi sana. Hii changamoto ya funza mwekundu iligundulika kwenye miaka ya 1940, sasa ni miaka zaidi ya 80 imepita bado hatujapata solution kuhusiana na changamoto hii. Je, Serikali ina mikakati gani madhubuti, ningeomba tuelezwe kwa kutumia teknolojia ya kisasa kuweza kutatua changamoto hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; ningependa kujua, kuna mazao mengina ya michungwa, ufuta na minazi ambayo yanalimwa sana katika Wilaya ya Kilwa, ningependa kutaka kujua, je, Serikali imeishirikisha vipi taasisi TARI katika kutatua matatizo ya magonjwa ya mazao haya?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli mdudu huyu alitambulika muda mrefu na kama Serikali tumeendelea kuwekeza katika kufanya utafiti kushirikiana na wadau wengi wa kimataifa. Lengo letu ni kuhakikisha kwamba tunamtokomeza mdudu huyu ambaye kila muda anaendelea kujipa maumbo tofauti tofauti lakini wataalam wetu wa TARI pamoja na wataalam wengine tunaendelea kuifanya kazi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo kubwa ni kuhakikisha tunamtokomeza mdudu huyu ambaye ana athari kubwa katika uzalishaji wa zao la pamba. Hivyo, nimwombe Mheshimiwa Mbunge, kwa sababu hivi sasa Mheshimiwa Rais ametoa fedha nyingi kwenye utafiti, tunaamini kupitia fedha hizi wenzetu wa TARI pamoja na mashirika mengine tutafanya kazi hii kwa uaminifu mkubwa kabisa ili mwisho wa siku tupate suluhisho la mdudu huyu na wakulima hao kama ambavyo dhamira yao ya kulima basi tuwe tumemtokomeza mdudu huyu.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la pili, bajeti yetu ya eneo ya utafiti miaka miwili iliyopita ilikuwa ni shilingi bilioni 11.6. Hivi sasa bajeti yetu ni shilingi bilioni 43 kwenye utafiti. Moja ya maeneo makubwa ambayo tumeyapa kipaumbele ni kuhakikisha pia tunakuja na namna bora ya udhibiti wa magonjwa na wadudu wasumbufu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimhakikishie Mbunge kwamba, TARI imewezeshwa na hivi sasa inaendelea kufanya tafiti ili kuja na suluhisho la kudumu la magonjwa ambayo yamekuwa yakitatiza sana michungwa na minazi. (Makofi)
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri nina maswali mawili ya nyongeza. Tumekuwa tukiona wanunuzi kutoka nje ya nchi wakija kununua mazao moja kwa moja wakiwa na magari yao ambayo yana namba za nje ya nchi; na tumekuwa tukiona wananchi wanauziwa kwa bei za chini sana, hasa mazao ya parachichi na mazao mengine kwa sababu hawana mtu anayewasimamia vizuri. Je, mnunuzi anapoenda kununua mazao hayo moja kwa moja kwa sasa hizo data wanazichukuwaje?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa Serikali imekiri kabisa inaendelea kuboresha huo mfumo wa ATMIS na TANCIS ni lini maboresho hayo yatakwenda kukamilika kwa sababu tumeona kwamba, bidhaa zinaenda nje ya nchi na tumekuwa hatujui mchango kamili wa kilimo kwa fedha za kigeni.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la kwanza, ni kweli kumekuwepo na baadhi ya wanunuzi ambao wanakwenda moja kwa moja mashambani, ndiyo maana Waheshimiwa Wabunge mtakumbuka tulileta utaratibu wa namna ya ununuzi wa mazao ili wale wote ambao wanataka kununua mazao nchini Tanzania wafuate utaratibu na mwisho wa siku sisi kama Serikali tupate takwimu sahihi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mkakati wa Serikali ni nini katika hili. Jambo la kwanza, katika eneo la mazao ya nafaka, hivi sasa tunataka kuboresha, kutengeneza masoko ili bidhaa zote zipelekwe katika masoko na wanunuzi wakanunue katika masoko yanayotambuliwa ili kupata takwimu sahihi.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, kwenye mazao ya mbogamboga na matunda, hivi sasa tunajenga common use facilities tatu za kuanzia katika eneo la Nyororo, Hai na Kurasini, ambapo kwa mfano parachichi yote itakusanywa, tutafanya grading, sorting na packaging ambayo itatupa pia uhakika wa kujua ni parachichi kiasi gani imekusanywa na kupelekwa nje ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, swali lako la pili kuhusu mifumo hii, kama mnavyofahamu Waheshimiwa Wabunge mifumo hii siyo jambo la siku moja. Tunaendelea kuiboresha kutokana na maendeleo ya teknolojia vilevile na ukuaji wa soko.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano kwa hivi sasa, tunao mfumo wetu ukiacha hii mifumo mingine wa kutumia mamlaka ya afya, mimea na viuatilifu, ambao wao wanawajibu wa kutoa phytosanitary kwa bidhaa zozote ambazo zinatoka nje ya nchi, cheti cha usafi wa mazao pia na wenyewe ni mfumo ambao tumewaunganisha kutupa takwimu sahihi. Kwa hiyo, hakuna mtu aliye na uwezo wa kusafirisha mazao nje ya nchi kama hajapata export permit na phytosanitary certificate ambayo pia inatupa nafasi ya kuweza kujua ni mazao kiasi gani yamesafirishwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tutaendelea kuboresha mfumo huu ili tupate takwimu sahihi ya mazao yetu.
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze Serikali katika eneo ambalo imeongelea la kudhibiti kweleakwelea, viwavijeshi, nzige na wanyama wengine waharibifu, lakini katika eneo hilo suala la ngedere ni ngumu sana kulidhibiti kwa aina ya kupitia kilimo anga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Wilaya ya Missenyi imekuwa ni janga kubwa na sisi kama wananchi kupitia juhudi za Mbunge na Waheshimiwa Madiwani tulitafuta suluhisho la kununua dawa aina ya carbofuran ambayo inaua ngedere hao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua mchango wa Waheshimiwa Madiwani na Mbunge kununua dawa hiyo; je, Serikali haioni kuna haja ya ku–support juhudi hizo kuchangia hizo fedha au kuelekeza Halmashauri ikatenga bajeti kwa ajili ya kununua dawa hiyo ili wananchi sasa wakilima waweze kuvuna?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Tunajua Serikali imefanya kazi kubwa katika kupambana na suala la mnyauko, lakini mpaka sasa hivi bado unaleta usumbufu katika maeneo yetu.

Je, ni hatua gani ambayo Serikali imefikia katika kufanya utafiti ili sasa tuweze kupata suluhisho la kudumu la ugonjwa wa mnyauko? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hili la kwanza la kuhusu dawa ambayo inatumika pale Missenyi nataka nichukue fursa hii kumuelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya waende kuangalia dawa hiyo ambayo inatumika, na kama ina ufanisi sisi kama Serikali pia, tutaunga mkono kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kuhusu mkakati wa kudumu; kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi, moja kati ya kazi kubwa ambayo tunaendelea kuifanya hivi sasa ni kuhakikisha kwanza kabisa tunang’oa na kuchoma moto mashina yale yote ambayo yalikuwa yana ugonjwa wa mnyauko ili ugonywa huu usisambae, lakini la pili, tunawajengea uwezo Kituo chetu cha Utafiti wa Kilimo cha TARI - Maruku, ili waweze kufanya utafiti na badae kuzalisha miche bora ambayo itakuwa na ukinzani na ugonjwa huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka ujao wa fedha tumetenga shilingi milioni 800; shilingi milioni 400 inakwenda kwa ajili ya utafiti na uzalishaji wa miche bora ya migomba. (Makofi)
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kuniona niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini Serikali itakuja na mkakati wa uzalishaji miche kwa kutumia teknolojia ya chupa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti yetu ya mwaka 2023/2024 zimetengwa shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuwajengea uwezo TARI – Maruku ili waweze kuanza teknolojia mpya ya uzalishaji wa miche safi kupitia tissue culture ambayo itasaidia sana katika kutatua changamoto hii ya ugonjwa wa mnyauko.
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zao la kitunguu linalolimwa sana Wilayani Kilolo limekumbwa na ugonjwa unaoitwa kaukau kwa lugha ya mtaani ambao haujulikani na vitunguu vinakauka mara tu vinapokuwa vimepandwa.

Je, Serikali iko tayari kutuma wataalamu ili kufanya uchunguzi na kutafuta suluhisho katika ugonjwa huu?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa taarifa hii, Jumatatu wataalam kutoka Wizara ya Kilimo watakuwepo jimboni kwake kwa ajili ya kushughulikia tatizo hilo. (Makofi)
MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nimshukuru waziri kwa majibu yake mazuri sana aliyoyatoa hapa hivi sasa, lakini nina maswali yangu mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa suala hili ni la muda mrefu, je, Serikali inaweza kutuambia nini hali halisi kwa sasa pamoja na mifano?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; kwa kuwa ongezeko la thamani, mazao yetu hapa nchi kuna maboresho ya mazao yetu, je, Serikali iko tayari kutengeneza viwanda vidogovidogo katika wilaya zetu?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hali halisi ya upatikanaji wa masoko ya mazao yetu. Nataka nikiri mbele ya Bunge lako kwamba hivi sasa katika baadhi ya mazao hasa mazao ya nafaka soko la mazao haya limekuwa ni kubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na hivyo kuwawezesha wakulima wetu wengi kuwa na masoko ya uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hivyo katika matunda na mbogamboga pia na kwenyewe tunafanya vizuri hivi sasa parachichi letu limepata nafasi ya kwenda katika masoko ya Hispania, China, Marekani, pamoja na Afrika ya Kusini hii ni ishara njema kuonesha kwamba kuna kazi imefanyika kwenye kutangaza mazao yetu, lakini pia kwenye kahawa na korosho na mazao mengine pia tunafanya vizuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili la kuongeza thamani, ni mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba tunaendelea kuongeza thamani ya mazao yetu ya kilimo. Mkakati uliopo hivi sasa ni kuhakikisha kwamba tunajenga uwezo kwa uanzishaji wa viwanda vidogovidogo kuanzia kule katika eneo la korosho na mazao mengine ya nafaka. Hivi sasa bodi ya mazao mchanganyiko yenyewe tu imeshaendelea kuwekeza katika vinu vingi vya kusaga mazao ya nafaka ili kuongeza thamani ya mazao yetu. Hii ni hatua ya Serikali lakini pia na sekta binafsi wanatuunga mkono.
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona. Nataka kujua kauli ya Serikali kuhusu kuporomoka kwa zaidi ya asilimia 50 kwa bei ya alizeti kwa wakulima na hali nchi ina upungufu mkubwa wa kujitosheleza katika uzalishaji wa mafuta ya kula?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli bei ya alizeti imeporomoka na imesababisha kuwakatisha tamaa wakulima, lakini sisi Wizara ya Kilimo pamoja na Wizara ya Fedha tumekaa chini na kuangalia namna bora ya kuweza kutatua changamoto hii ikiwemo kuangalia sera zetu za fedha na hasa katika kuliboresha eneo la kuongeza kodi kwa mafuta ambayo yanaagizwa kutoka nje ya nchi ili kuweza kuwalinda wakulima wetu wa ndani. (Makofi)
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Kwa kuwa asilimia 72 ya zao la tangawizi inalimwa ndani ya Jimbo la Same Mashariki na kwa kuwa bei ya zao hili kwa wananchi bado siyo rafiki kabisa. Sasa naomba Mheshimiwa Waziri aniambie watatumia mkakati gani wa kuwafanya hawa wananchi wapate bei ambayo itawatia moyo wa kuendelea kulima zao hili muhimu nchini?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua kwamba tunao wajibu kama Serikali kuhakikisha kwamba wakulima wanapata bei bora ya mazao yao, Serikali imeanzisha mamlaka maalum ambayo inaitwa COPRA kwa ajili ya usimamizi wa masoko na bei ya wakulima ikiwemo wakulima wa tangawizi. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutahakikisha tunashirikiana sisi na yeye ili wakulima wake waweze kupata bei bora na kilimo kiweze kuimarika katika eneo lake hilo la Same.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi ya kuuliza swali la nyongeza. Mheshimiwa Waziri, Chuo cha TARI Naliendele zaidi ya miaka 20 sasa wamekamilisha utafiti unaoonesha kwamba kutokana na nipa inayopatikana kwenye korosho ina uwezo wa kuzalisha ethanol methanol pamoja na alcohol kwa matumizi ya burudani pamoja na hospitali, lakini pia kuongezea kipato wakulima na kupunguzia Taifa hili hasara. Je nini mkakati wa Serikali kuhakikisha sasa nipa inakuwa rasmi kwa ajili ya kupunguzia hasara Taifa letu?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumesikia hoja ya Mbunge, tutaishirikisha TARI pamoja na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili ikibainika kwamba nipa hiyo inaweza ikatumika katika maeneo ambayo ameyataja, basi sisi kama Serikali kwa kushirikiana na TARI tutasaidia kuongeza mnyororo wa thamani wa zao la korosho.
MHE EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kuwa wakulima walihamasika sana kuhusu alizeti na bei imeteremka na wakati wanaangalia sheria ili wazuie mafuta yanayotoka nje, kwa nini Serikali isifanye commitment au kununua alizeti yote ambayo wakulima wamelima?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tumepata changamoto ya bei kuporomoka na ndiyo maana kwenye bajeti yetu Mheshimiwa Waziri alitamka kwenye kitabu chake cha bajeti uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo (ADF) Agricultural Development Fund ambayo kazi yake nyingine ni kwa ajili ya price stabilization.

Mheshimiwa Mwenyekiti, habari njema ni kwamba tumeshapata amri kutoka Wizara ya Fedha ya uanzishwaji wa Mfuko huu na Mfuko utaanza kufanya kazi, natumai katika changamoto ambazo zitajitokeza baadaye basi Serikali kupitia Mfuko huu inaweza kufanya kazi hiyo kwa ajili ya kuwa rescue wakulima. (Makofi)
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

Kwanza baada ya Serikali kuanza kutoa ruzuku za pembejeo baadhi ya benki zimeacha kabisa kutoa mikopo kwa wakulima wakati gharama ya zao la korosho sio pembejeo tu, kuna gharama ya matayarisho ya mashamba na gharama za uvunaji.

Je, Serikali inatoa tamko gani kwa benki hizo? (Makofi)

Swali langu la pili, changamoto ambazo zinawakabili wakulima wa mazao ya kimkakati, pamba, korosho, chai, alizeti zingeweza kutatuliwa na mfuko wa maendeleo ya kilimo.

Serikali inaweza kutoa tamko, je, ni lini sasa Mfuko huo utaanza kufanya kazi rasmi ili kuwasaidia wakulima hawa. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu uwezeshwaji wakulima kupitia taasisi za fedha, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi Serikali pamoja na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, tutakaa kwa pamoja na taasisi za kifedha kuona namna bora ya kuweza kuwawezesha wakulima hasa wa korosho na hivi sasa tumeanza hatua za awali, tumeshakaa na benki, ziko changamoto ambazo zimejitokeza hasa za urejeshaji wa mikopo hii, lakini hii ilitokana na changamoto kwamba wakulima wengi walikuwa hawajasajiliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa tumeanza kuwasajili wakulima, kila mkulima atatambulika eneo lake alipo, shamba lake lilipo na ukubwa wa shamba ili kuirahishia benki namna bora ya kuweza kuwapatia mikopo na tunaamini kupitia njia hii wakulima wengi zaidi watapata mikopo katika taasisi za fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kwa mujibu wa Sheria za Fedha za Umma Sura Namba 347 Kifungu cha 17 (1) cha Sheria ile, kimetoa amri ya uanzishwaji wa Mfuko wa maendeleo ya kilimo. Mfuko tayari tumeshapata amri ya kuanzisha, umeanza kazi na tumeshateua na Meneja wa Mfuko na Mhasibu Mkuu, punde tutaendelea kuhakikisha kwamba tunapata vile vyanzo vya kuutunisha Mfuko huu ili basi inapotokea changamoto mbalimbali na hasa katika kuwawezesha wakulima kuweza kupata huduma mbalimbali Mfuko huu uweze kutumika.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.

Sswali la kwanza, kama ni hivyo ni kwa nini sasa mbolea hizo kwa vifungashio ulivyovitaja hazipo madukani? (Makofi)

Swali la pili, kwa kuwa mvua za kwanza ni za kupandia. Je, katika Mkoa wa Kigoma kwa mwaka huu mbolea zitafika Mkoa wa Kigoma mwezi gani? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema mbolea hizi za ujazo tofauti tofauti hutokana na mahitaji halisi ya maeneo husika na aina ya mazao yanayolimwa. Kwa sababu imeonekana kuna mahitaji hayo, kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Ubora wa Mbolea Tanzania - TFRA tutatoa maelekezo kwa wazalishaji na waingizaji wa mbolea hapa nchini kuhakikisha kwamba wanatoa mbolea kulingana na mahitaji na hasa katika hoja ambayo Mheshimiwa Mbunge ameisema ya kuanzia kilo tano, 20, mpaka 10 na kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusu mbolea kufika lini. Tulishasema ndani ya Bunge lako Tukufu ya kwamba tunataka tuhakikishe changamoto za msimu uliopita safari hii zisijirudie na mbolea ifike nchini kwa wakati, wakati wakulima wetu wakiwa bado wana nguvu ya kuweza kununua hasa baada ya kuwa wametoka kuuza mazao yao. Ni commitment ya Serikali kwamba tutahakikisha ndani ya mwezi wa Saba mbolea imefika hapa nchini na wakulima waanze kununua kwa ajili ya msimu ujao. (Makofi)
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu ya Serikali hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza. La kwanza kwa kuwa kuna uhaba mkubwa sana wa ardhi maeneo ya Kata ya Luponde ambako ndiko shamba kubwa hilo lipo na mashamba makubwa ya chai yako kule, na vijana ni wengi sana ambao wanauhitaji wa ardhi;

Je, kwa nini Serikali isifikirie ndani ya eneo hili ikagawa sehemu kuwapa vijana katika mpango wa BBR au BBT?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kituo cha utafiti cha Igeri ambacho ndicho kimekuwa na shamba hili kwa muda mrefu sana kimekuwa dormant kwa miaka mingi sana hakujakuwa na uwekezaji, na vile vile kituo kidogo cha Ichenga ambacho ni cha utafiti eneo hilo hilo na chenyewe cha matunda kimekuwa dormant na hakina fedha na hakifanyi shughuli yoyote wakati tuna zao la parachichi ambalo linahitaji sana utafiti;

Je, Serikali ina mpango gani kutoa fedha za kutosha kwenye vituo hivi vya utafiti?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza kuhusu vijana na ushiriki wa vijana kwenye kilimo. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ya kwamba ni dhamira ya Serikali kuhakikisha vijana wengi zaidi wanashiriki kwenye kilim,o na ndio maana tumekuja na programu ya BBT. Na kwa kuwa kuna changamoto ya ardhi kama alivyosema, mimi nitaandaa safari kwenda jimboni kwake Mheshimiwa Mbunge tukakae na uongozi wa wilaya kwa pamoja tutafute namna bora ya kuweza kuwawezesha vijana hao washiriki kwenye kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili la kuhusiana na kituo hiki cha utafiti. Kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi, mwaka wa fedha unaokuja wa 2023/2024 tumetenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunalima eneo lote kwa ajili ya kutayarisha mbegu zile ambazo ni pre-basic seeds na basic seeds ili baadaye tusaidie kwa ajili ya kuzisambaza, hasa kwenye zao la ngano na zao la pareto. Kwa hiyo nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba hatujakitelekeza, tumeshakitengea fedha, kitaanza kuwa operational kuanzia mwaka wa fedha ujao.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa changamoto kubwa ya wakulima wetu nchini ni upatikanaji wa mbegu bora; je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba mbegu bora zinapatikana kwa wakati ukiwemo Mkoa wangu wa Iringa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mkakati wa Serikali kwa kutumia Wakala wa Mbegu Tanzania (ASA) na wazalishaji binafsi kuhakikisha tunazo mbegu za kutosha kuweza kuwahudumia wakulima wa nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mahitaji ya mbegu za kilimo katika mpango wetu ule wa Agenda kumi thelathini ifikapo mwaka 2030 ni kuwa na uzalishaji wa tani takriban laki sita na Hamsini elfu. Hivi sasa tupo katika uzalishaji wa tani 61,000 kama asilimia kumi ya mahitaji yetu katika mwaka 2030.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, hivi sasa kwenye mashamba yetu yote ya ASA tumeweka mifumo maalum ya umwagiliaji ambayo itatuhakikishia uzalishaji wa mbegu zaidi ya mara mbili ndani ya mwaka mmoja, na hivyo wakulima wetu watapata mbegu kwa wakati kwa sababu hivi sasa tumeboresha mashamba yetu 16 na mbegu zitaanza kuzalishwa zaidi ya mara moja ndani ya msimu.
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Wilaya ya Chemba imetenga maeneo kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu na tafiti, na tunafahamu Taifa hili lina changamoto ya upungufu wa mbegu;

Je, nini mkakati wa Serikali wa kuyatumia maeneo haya?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Mbunge pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwa utayari wao wa kutenga ardhi kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu na utafiti. Hivi sasa tuko nao katika mazungumzo ya mwisho kwa ajili ya kuanza kuanzisha shamba kubwa la uzalishaji wa Mbegu za mtama mfupi ambao una soko kubwa kwa kampuni ya bia Tanzania pamoja WFP na wakulima wakubwa wanapatikana ndani ya Mkoa wa Dodoma na Singida. Kwa hiyo shamba hili ndani ya Chemba litakuwa kama mwokozi kwa wakulima wa kanda ya kati.
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia vijana wa Wilaya ya Nyang’hwale kupitia mpango wake wa kuwanyanyua vijana kupitia kilimo? Wilaya ya Nyang’hwale hatuna mazao ya kudumu ya kibiashara; je, Serikali ina mpango gani wa kuchukua udongo na kufanya utafiti ili na sisi tuweze kuwa na miche ama mazao ya kibiashara?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mkakati wa Serikali wa kuhakikisha ya kwamba tunawahusisha vijana wengi kwenye kilimo na ndio maana tumekuja na programu hii ya BBT. Hatua ya awali ambayo tunaifanya kwanza kabisa tunashirikiana na mamlaka za mikoa husika kwa ajili ya utengwaji wa maeneo; na eneo la pili hivi sasa tumeanza kuichora ramani ya Tanzania kwa afya ya udongo ili tujue sehemu gani wanaweza kulima zao gani na sisi tuwasaidie jambo gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, habari njema ni kwamba katika mwaka ujao wa fedha tumekwenda kununua mitambo ya kisasa ya upimaji wa afya ya udongo. Badala ile ya mahabara tu tutakuwa pia na mobile laboratory ambazo zitakuwa zinatembea kupima afya za udongo. Tukija kukupimia kwako mkulima tutapima hapo hapo na nitakupa cheti hapo hapo kitakwambia kwamba katika udongo huu unaweza kulima mazao ya aina gani na utumie mbolea aina gani, na hiyo ndio itakuwa mkombozi kwa wakulima wan chi yetu ya Tanzania.
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Wilaya ya Kishapu na Mkoa wa Shinyanga unajihusisha sana na kilimo cha zao la kimkakati la pamba, lakini zao hili katika msimu huu limeshuka sana bei, kutoka shilingi 2,200 hadi shilingi 1060. Wakati huo gharama kubwa za uendeshaji ama uzalishaji wa zao hili umekuwa ukiongezeka ikiwemo pembejeo na gharama zingine;

Je, ni nini mpango wa Serikali wa kuhakikisha kwamba inafanya kila jitihada kuona kwamba bei hii inapanda ili kumtia moyo na kumhamasisha mkulima ilimradi aweze kuondokana na gharama ya uendeshaji wa zao hili na hivyo kupata manufaa kutokana na zao hili la pamba?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto ya bei ya mazao mengi hapa nchini inatokana na kwamba wakulima wetu wanatumia nguvu kubwa ya wanachokiingiza shambani na wanachokipata havilingani. Sisi kama Serikali tumekuja na mkakati ufuatao. Tunaamini kabisa mkulima wa Tanzania akilima kwa tija suala la bei halitakuwa changamoto kubwa sana. Kwa hiyo mkakati wetu wa kwanza kabisa wa kuanzia ni kuhakikisha kwamba wakulima wetu wanalima kwa tija na hivyo tumefanya yafuatayo;

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha kwanza tunasaidia kuendelea kufanya utafiti kwa ajili ya kuwapatia mbegu bora, cha pili ni kuwasaidia pia katika teknolojia ambayo itamsaidia mkulima aweze kulima kwa tija, na cha tatu ni usambazaji wa pembejeo kwa wakati ili mkulima aweze kufikia malengo yake. Hii itatusaidia sana kwenye kuhakikisha kwamba wakulima wetu wanalima kwa tija na hatimaye hata akienda sokoni bei ikiwa imeporomoka lakini atakuwa na uwezo mkubwa wa kuweza kufidia changamoto ambayo anaipata katika uwekezaji alioufanya shambani.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kunipa nafasi kuuliza swali;

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga benki ya kuhifadhi mbegu asilia zisije kupotea kabisa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, mamlaka ya afya mimea na viuatilifu pale Arusha tayari tunayo benki ya uhifadhi wa mbegu za asili, na tunaendelea kufanya utafiti. Lengo letu ni kuzitunza na kuhakikisha kwamba zinaendelea kutumika na kuwaletea tija wakulima wetu wa nchi ya Tanzania.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri yenye kutia matumaini, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu Serikali imekiri kwamba upatikanaji wa pembejeo ndiyo shida mojawapo inayofanya zao hili lisilete tija iliyokusudiwa. Je, Serikali haioni pamoja na kwamba mwakani itatusambazia hizo mbegu bure, je na pembejeo zingine kama mbolea tutazipata?

Swali la pili, kwa kuwa tunayo Bodi ya Pareto, je, Serikali haioni umuhimu wa kuiwezesha hiyo Bodi ya Pareto kwa kuwaongeza bajeti na kuwaongezea watumishi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema pamoja na usambazaji wa miche bora ambayo itasaidia katika kuongeza tija pia wakulima wa pareto wanaingia katika mpango wa mbolea ya ruzuku. Kwa hiyo ni wanufaikaji na watanufaika pia kupitia mbolea hii.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili kuhusu bajeti kwenye Bodi ya Pareto tunaendelea kulifanyia kazi suala hili, tumeendelea kuijengea Bodi uwezo tofauti na miaka miwili iliyopita, lengo letu ni kulikuza zao la pareto ambalo limekuwa na manufaa makubwa. Kwa hiyo, Bodi tutawajengea uwezo kuhakikisha kwamba bajeti yao inaongezeka pia. (Makofi)
MHE. ALLY J. MAKOA: Mheshimiwa Spika, ninakushuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu yenye kuridhisha ya Serikali nataka kujua sasa, Je, hizo shilingi milioni 300 ambazo zilitengwa kwa kufanya kazi zilizotajwa na Mheshimiwa Waziri hapo, zilitolewa na zikafanya kazi iliyokusudiwa ama walifanya tafiti tu za awali?

Swali la pili, kwa kuwa Serikali ina makusudio ya kufanya kuanza ujenzi mwaka ujao wa fedha, kwa kazi ya kuhuisha sasa hii skimu na hizi ripoti na tafiti, Wizara safari hii imetenga kiasi gani kwa ajili ya kazi hii? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusu matumizi ya fedha shilingi milioni 300 kama zilitoka au la. Madhumuni makubwa ya fedha hizi zilikuwa ni kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ndiyo maana katika majibu yangu ya msingi nimesema katika kupata tathmini halisi, tumetenga fedha tena mwaka huu kuhakikisha ya kwamba tunalipitia eneo lote ili kupata taarifa sahihi na kuanza ujenzi wake kwa sababu tumepata changamoto miradi mingi ilipata changamoto kubwa, kwa sababu usanifu wa kina haukufanyika na imekuwa siyo ya kudumu muda mrefu na hivyo kuleta athari kubwa kwa sababu mara kwa mara imekuwa ikibomoka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba tunakwenda kurudia kufanya kazi hii kubwa katika umakini mkubwa zaidi na ku-involve wataalam wengi zaidi ili tupate kitu ambacho kitaleta tija kwa wananchi wa Kondoa Mjini.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili kuhusu fedha kama zimetengwa. Kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi ya kwamba tunajiandaa kufanya zoezi hili katika mwaka wa fedha 2023/2024 ili ujenzi uanze katika mwaka wa fedha unaokuja 2024/2025. Kwa hiyo, nimtoe hofu tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaangalia namna ya kuweza kulifanikisha kwa uharaka kwa sababu tunajua wananchi wa Serya na eneo la Mongoroma ni wakulima wazuri hatutaki kuwachelewesha, tutafanya kwa uharaka ili wafanye kilimo cha umwagiliaji katika eneo lao. (Makofi)
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuniona. Je, ni lini Serikali itajenga Skimu ya Umwagiliaji Muhuruzi - Nyakahura Wilaya ya Biharamulo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwenye kitabu chetu cha bajeti, kiambatisho Namba 11 Ukurasa wa 206 tumeitaja Skimu ya Muhuruzi katika Wilaya ya Biharamulo kama sehemu ambazo zitajengwa katika mwaka huu wa fedha unaoanza Julai. Kwa hiyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kazi inafanyika katika mwaka wa fedha ujao.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Katika Halmashauri ya Kasulu Vijijini ipo miradi ya umwagiliaji katika Kata ya Titye na Rungwe Mpya. Miradi hiyo haijakamilika kutokana na ukosefu wa fedha.

Je, ni lini Serikali itapeleka fedha ili kukamilisha miradi hiyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kazi ya kwanza ambayo tuliifanya kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ni kuhakikisha tumepitia miradi yote ambayo haijakamilika na ili tujue changamoto ambazo zimefanya imekwama na tuweze kuikwamua. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ya kwamba katika orodha ya miradi hiyo, miradi anayoitaja pia imo. Tutaikwamua ili wananchi wafanye kilimo cha umwagiliaji. (Makofi)
MHE. DANIEL A. TLEMAI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Je, ni lini Serikali itajenga skimu katika Bonde la Eyasi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, tarehe 20 Machi, 2023 tulisaini mikataba ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mabonde 22 ya kimkakati hapa nchini Tanzania likiwemo Bonde la Eyasi. Kwa hiyo maana yake skimu zote za Eyasi zitajengwa katika mwaka wa fedha unaokuja.
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Pamoja na majibu ya Serikali ambayo hayajakidhi swali langu, kwa sababu Skimu za Katengera, Ruhwiti na Muhwazi ambazo nimezitaja, siyo skimu mpya, ni skimu ambazo zimekuwepo na zimekuwa zikifanya kazi. Tatizo miundombinu yake imeharibika na hivyo hazifanyi kazi sasa.

Mheshimiwa Spika, swali; Je, lini mtapeleka fedha kwenye skimu hizi kwa ajili ya ukarabati ili ziweze kufanya kazi inayostahili?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; wananchi wetu wakulima hawana taaluma juu ya utumiaji wa miundombinu ya umwagiliaji kwa maana ya kwamba hawana taaluma;

Je, ni nini kauli ya Serikali kuhakikisha kwamba wanakuwa na maarifa na taaluma ya kutosheleza kutumia miundombinu ya umwagiliaji?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Aloyce John Kamamba, Mbunge wa Buyungu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika majibu yangu ya msingi nimeeleza vyema kabisa tunayo mabonde 22 ya kimkakati. Katika Mkoa wa Kigoma tunafanyia kazi Bonde la Mto Malagarasi na Bonde la Ziwa Tanganyika.

Mheshimiwa Spika, katika maziwa na mito hii miwili ambayo nimeisema ndani yake skimu hizi zinapatikana. Kwa hiyo Serikali imeamua ifanye kazi kubwa kwanza ya upembuzi yakinifu kwenye mabonde haya ambayo pia ndani yake itajumuisha skimu ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitamka. Kwa hiyo nimwondoe hofu kwamba skimu ambazo amezitamka ni ndani ya mkakati wa Serikali katika utekelezaji wa haya mabonde ambapo kazi imekwisha kuanza na ujenzi utaanza mwaka wa fedha ujao.

Mheshimiwa Spika, kuhusu elimu; tumeajiri wahandisi wa umwagiliaji wa kila wilaya. Hawa watakuwa na jukumu pia la kuhakikisha kwamba wanawapa elimu wakulima wetu juu ya matumizi sahihi ya maji katika kilimocha umwagiliaji. Hivyo wananchi pia wa Jimbo la Buyungu watanufaika na huduma hii kupitia wahandisi wetu walioko wilayani.
MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Spika, ahsante; je, ni lini Serikali itapeleka pesa kwa ajili ya kukamilisha miradi ya umwagiliaji katika Kijiji cha Misyaje na Madaba kilichopo Jimbo la Tunduru Kusini?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni mkakati wa Serikali kuhakikisha tunakamilisha skimu zote za umwagiliaji ili wananchi wafanye kilimo cha umwagiliaji. Nitakaa na Mheshimiwa Mbunge kuangalia skimu alizozitaja kama hazipo kwenya mpango wa mwaka wa fedha unaokuja basi tuziingize kwenye mpango ili wananchi waweze kushiriki kwenye kilimo cha umwagialiaji.

MHE. INNOCENT E. KALOGERIS: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itapeleka pesa kukamilisha mradi wa Lubasazi Kata ya Kolelo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema ninayo orodha ya miradi mingi ambayo tunaitekeleza hivi sasa inawezekana nitashindwa kumpa moja kwa moja mradi wake katika hatua iliyofikia lakini mimi nitakaa naye ili tuangalie katika jedwali letu tuone kama mradi huo haupo basi tuweke katika vipaumbele vyetu.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Je, ni lini Serikali itajenga skimu za umwagiliaji katika maeneo ya Mavimba, Lupilo, Minepa, Kivukoni, Namilela katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tumeainisha maeneo mengi ambayo tunakwenda kuyafanyia kazi katika mwaka wa fedha ujao. Nitakaa na Mheshimiwa Mbunge kuangalia maeneo ambayo ameyataja kama hayajajumuishwa basi tuweze kuyaweka katika mpango wetu ili kuhakikisha wananchi hao pia wanafanya kilimo cha umwagiliaji.
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi;

Je, ni nini mkakati wa Serikali kuanzisha miradi ya umwagiliaji kwenye maeneo ya wakulima wadogo wadogo wa chai eneo la Igomini Tarafa ya Igomini Halmashauri ya Njombe?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nataka kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hii ni hoja ambayo Mheshimiwa Mbunge alishaifikisha katika Wizara ya Kilimo na tumemuahidi baada ya Bunge hili la bajeti namwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ndugu yangu Raymond Mndolwa waongozane na Mheshimiwa Mbunge kwenda kufanya tathmini katika maeneo yaliyotajwa ili tuweze kuwasaidia wakulima wa chai katika eneo hilo.

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Spika, Je, ni lini skimu ya umwagiliaji ya Mwamapuli itaanza?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika skimu zaidi ya 42 ambazo tutakwenda kuzijenga katika mwaka wa fedha huu ambao unaishia na ambao unaendelea ni pamoja na Skimu ya Mwamapuli. Kwa hiyo nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba jambo hilo liko ndani ya utekelezaji wa Serikali.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika, Je, ni lini Serikali itajenga skimu za umwagilaiji kwa kutumia maji ya Mto Rwiche katika manispaa ya Kigoma Ujiji?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kwenye mradi wa umwagiliaji kutumia Bonde la Rwiche tunachosubiri hivi sasa ni ile barua ya kutokuwa na kipingamizi ambayo baada ya hapo tutanza utekelezaji mara moja. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba taratibu zimeshakamilishwa ndani ya Serikali tumebakiza kutoka kwa Mhisani tukipata letter of no objection tunaendelea.
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. Ishengoma Kikoyo, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza: -

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa malengo ya Serikali ni kuhamasisha uchumi ambao ni shindani katika ununuzi wa kahawa;

Je, Serikali haioni sasa itoe kibali cha wanunuzi binafsi kushindana na AMCOS kununua kahawa moja kwa moja kutoka kwa wakulima?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa kahawa inaendeshwa kwa Bodi ya Kahawa;

Je, Serikali haioni kwamba ni muda mwafaka kuleta Sheria ya Bodi ya Kahawa hapa Bungeni ikafanyiwa marejeo ili kuendana na uchumi wa sasa? Nakushukuru.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi, Serikali imeweka utaratibu ambao unaruhusu pia wawekezaji binafsi kununua kupitia katika AMCOS, ambapo wao wanakusanya. Na ninaomba tu niliweke wazi hapa lieleweke vizuri; AMCOS hanunui kahawa, anachokifanya yeye ni ku-aggregate na baadaye ndipo wanunuzi binafsi wanakwenda kununua kupitia kahawa iliyokusanywa. Kwa hiyo tutakachokifanya ni kuboresha mazingira zaidi ili wakulima wanufaike na bei lakini vilevile na waagizaji binafsi wapate uhakika wa kahawa yao.

Mheshimiwa Spika, la pili, kuhusu marejeo ya sheria; kutokana na kuwa na Agenda Maalum ya 10/30, hivi sasa tunafanya marejeo katika sheria zetu zote ili kuhakikisha kwamba zinaendana na mipango tuliyonayo ya kukuza sekta ya kilimo kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030, ikiwemo sheria ambayo pia inaongoza zao la kahawa.
MHE. KENNETH E. NOLLO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bwawa la Chikopelo linategemewa na Kata za Chali na Kata ya Nondwa. Bwawa hili limekuwa na uwezo wa kutunza maji msimu wote, hata hivyo lina changamoto ya kupungua kwa kina kutokana na kujaa kwa matope.

Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati bwawa hili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lingine dogo ni kwamba Kilimo cha Zabibu ni kilimo kinachotegemewa hapa Mkoa wa Dodoma hata hivyo kilimo hiki bado kinategemea kwa kiasi kikubwa mvua. Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka utaratibu ili tuanze kupata umwagiliaji kwa ajili ya kilimo na kupata tija? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza kuhusu Bwawa la Chikopelo. Katika hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo kiambatisho namba 13 tumelitamka Bwawa la Chikopelo kati ya mabwawa ambayo tunakwenda kuyafanyia kazi mwaka ujao wa fedha. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge na Kata za Nondwa alizozitaja na maeneo ya jirani kuwa bwawa hili linakwenda kufanya kazi na wananchi watanufaika kwa kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusu zabibu, tunatambua kwamba Dodoma ni kati ya eneo ambalo lina uzalishaji mkubwa sana wa zabibu hapa Tanzania na hivyo kuna umuhimu pia wa kuunganisha zao hili na kilimo cha umwagiliaji. Kwa kuanzia tunao tayari mfumo wa umwagiliaji katika eneo letu la Chinangali ambapo tunalo shamba kubwa la umwagiliaji kwa ajili ya kilimo cha zabibu. Sambamba na hilo hata hili Bwawa la Chikopelo pia na lenyewe tutaangalia ikolojia yake kama ita-support kilimo cha zabibu pia tutaunganisha mifumo hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni kwamba tumetamka hapa tunakwenda kuchimba visima 150 kila Halmashauri nchi nzima hivyo wakulima wa bahi pia watanufaika na visima hivi kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji cha zabibu.
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa na mii swali la nyongeza. Je, Serikali imefikia wapi kwenye ujenzi wa Skimu za Umwagiliaji Wilayani Mbarali? Ahsante.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tumekuwa na miradi ya umwagiliaji katika Wilaya ya Mbarali na ninavyozungumza hivi sasa Wakandarasi wapo site katika mradi wa Msesule, Isenyela, Matebete, Hemanichosi na Gwanakubagogolo kote huko tayari wakandarasi wako site na kazi inaendea. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba kazi inaendelea na wananchi watanufaika na kilimo cha umwagiliaji.
MHE. SYLIVIA F. SIGULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Mkoa wa Kigoma ni kati ya Mikoa iliyobarikiwa kuwa na vyanzo vikubwa vya maji lakini bado suala la umwagiliaji halijapewa kipaumbele. Nataka kujua, wananchi wa Kasulu, Buhigwe na Uvinza ni lini watanufaika na miradi hii ya umwagiliaji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hotuba yetu ya bajeti kiambatisho namba tano tumeyatamka mabonde 22 ambayo tunakwenda kuyafanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya umwagiliaji. Bonde mojawapo ni Bonde la Mto Malagarasi ambalo lina hekta 7000 na litahudumia eneo la Buhigwe, Kasulu pamoja na Uvinza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo katika eneo la Kasulu tuna miradi miwili pale ambayo tunaifanyia kazi katika mwaka ujao wa fedha mradi wa Ahsante Nyerere na Kilimo Kwanza ambayo ina jumla ya hekta 3,500 ipo ndani ya mpango itafanyiwa kazi na wakulima wa Kigoma watafanya kilimo cha umwagiliaji.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naomba niulize swali moja dogo la nyongeza.

Ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya kuwapatia skimu ya umwagiliaji watu wa Mkinga?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua kwamba lazima tufanye kilimo cha umwagiliaji ili tuweze kuleta tija kwenye kilimo. Katika eneo la Mkinga pamoja na Lushoto tumeanza kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa bonde la Mto Umba ambalo lina hekta zaidi ya 5,560 na tunaamini kabisa kwamba wananchi wa eneo la Mkinga watanufaika na mradi huu mkubwa ambao unakuja kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru Waziri kwa majibu yake. Sasa swali la kwanza, sehemu kubwa ya bonde la Kilombero imechukuliwa kama hifadhi, maeneo ambayo wakulima walikuwa ndio wanalima kupata chakula.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka miradi ya umwagiliaji ya kutosha ili chakula kisipungue?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kuwa na ghala moja la chakula naona kama ni risk.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza ghala jingine la chakula hasa kuliweka katika mikoa ile inayozalisha sana ikiwemo Mkoa wa Ruvuma?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Katika swali lake la kwanza, katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji katika Mkoa wa Morogoro kupitia bajeti yetu tulitangaza hapa ndani Bungeni kwenye kiambatisho namba tano cha bajeti yetu. Tumelezea vizuri kabisa kwamba Serikali inakwenda kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mabonde ya kimkakati 22, na mabonde matatu yatatoka ndani ya Mkoa wa Morogoro, yaani kwa maana ya bonde la Kilombero ambalo lina hekta 53,340. Tuna bonde la Usangule ambalo linakwenda kuhudumia mpaka Malinyi ambalo lina hekta 2,500 na tuna bonde la Ifakara - Idete ambalo linagusa Wilaya yote ya Kilombero.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo katika eneo lake la Malinyi tunao mradi ambao unaendelea mradi wa Itete wa scheme ya umwagiliaji ambao pia utasaidia kutatua changamoto hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili, Serikali inayo dhamira ya dhati kabisa kuhakikisha ile mikoa mitano ambayo ndio Ghala la Taifa la Chakula kuendelea kuimarisha huduma mbalimbali, hasa katika upatikanaji wa huduma za ugani lakini vile vile na upataikanaji wa pembejeo za mbolea ili wakulima wetu waweze kulima na kuongeza tija, ikiwemo Mkoa wa Ruvuma ambao ni kati ya Mkoa unaofanya vizuri sana kwenye kilimo cha mazao ya chakula.
MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kunipa fursa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iliongeza zao la parachichi kama zao la kimkakati na katika kutimiza ajenda hiyo, iliamua kuanza ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata parachichi kilichopo Nyololo Mufindi ili isaidie mikoa yote ya Nyanda za juu Kusini. Hata hivyo mpaka sasa hivi ujenzi haujaanza.

Je, ni ipi kauli ya Serikali juu ya mradi huu muhimu sana kwa wananchi wa Mufindi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli katika bajeti yetu ya mwaka 2022, 2023 tuliweka mpango wa kujenga common use facilities mbili. Moja itajenga Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro na moja inajengwa nyololo Jimboni kwa Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimpe taarifa njema Mheshimiwa Mbunge kwamba tumekamilisha taratibu zote za awali na muda si mrefu mkandarasi atapatikana na kazi ya ujenzi wa common use facilities itaanza. Kazi hii ikianza itawapa nafasi wakulima wote wa parachichi kukusanya maparachichi yao sehemu moja, tukafanya collection, tukafanya grading na sorting na baadaye packaging ili maparachichi yetu ya Tanzania ionekane duniani kwamba ni produce of Tanzania kuliko hivi sasa ambapo maparachichi mengi yanakwenda katika nchi za jirani. (Makofi)
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ni kwamba maghala mengi yamejengwa maeneo ambayo mikoa inazalisha chakula, tunakubaliana nayo. Lakini pale kuna mikoa mingine uzalishaji wa chakjula ni kidogo sana na mvua ni za shida. Inapotokea shida ya chakula kunakuwa tena kuna gharama ya kusafirisha; gharama ya fedha na gharama ya muda kutoka maeneo yanayozalisha chakula kwenda kwenye maeneo yasiyozalisha chakula.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuweka maghala vile vile katika maeneo ambayo mikoa inazalisha kidogo chakula kama Mkoa wa Simiyu na hasa maeneo amabayo yana shida ya chakula? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti yetu ambayo inamalizikia tumetenga shilingi 25 kwa ajili ya ujenzi wa maghala na tumeangalia maeneo yote. Kwa mfano katika Mkoa wa Simiyu hivi sasa kupitia mradi wa TANIPAC wa sumu kuvu tumebadilisha matumizi ya ghala lile ili ibaki kuwa sehemu ya ghala kuhudumia Mkoa wa Simiyu na mikoa Jirani ambao uzalishaji wake si mkubwa sawa na mazao ya chaklula ili inapotokea changamoto ya chakula cha msaada basi tuweze kukipeleka kwa uharaka zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tumezingatia pia jiografia hiyo na uzalishaji katika maeneo husika.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kwamba wakulima wanapata soko la uhakika. Lakini inapofika kipindi cha mavuno ya kahawa kumekuwepo na vitendo vya kuwakamata wakulima wanaotoka kata A kwenda kata B kuvuna kahawa kwa kuwanyang’anya kahawa na kutaifisha ile kahawa;
Je, ni nini tamko la Serikali juu ya vitendo hivi ambavyo havifai?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Mibuni mingi mkoani Kagera imekauka kwa sababu ya ugonjwa wa mnyauko. Tumeangalia kwenye bajeti tumetengewa mibuni (miche ya kahawa) michache;

Je, Serikali iko tayari kuongeza miche mingine ya kahawai li kukidhi mahitaji ya wakulima wa Mkoa wa Kagera?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, haikubaliki na hairuhusiwi kumkamata mkulima mwenye mazao yake anayoyatoa sehemu moja Kwenda sehemu nyingine ndani ya Wilaya husika, isipokuwa kama mkulima anayatoa shambani kupeleka kwenye AMCOS kwa ajili ya Kwenda kufanya aggregation hapo ni makosa kumkamata. Vile vile kama kuna mfanyabiashara ambaye pia na yeye anatoa mazao hayo kutoka kwenye AMCOS kupeleka kwenye viwanda lazima tuhakikishe awe ana nyaraka ambayo inamruhusu ili kuondokana na usumbufu. Lakini katika ujumla wake Serikali haiwezi kuwa sehemu ya kuzuia maendeleo ya mkulima; na ninatoa maelekezo katika uongozi wa maeneo husika kuhakikisha kwamba wanawalinda wakulima na wasiwanyanyase wakulima katika mazao ambayo wanayalima wao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili la kuhusu mibuni. Ni kweli mibuni mingi hivi sasa imeshatimiza zaidi ya miaka 25 na kimsingi imezeeka na inapunguza sana uzalishaji. Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa maana ya TaCRI pamoja na Bodi ya Kahawa tunaendelea na uzalishaji wa miche ya kahawa. Mwaka huu tumeendelea kuzalisha miche 20,000,000. Vilevile tutaongeza uzalishaji wa kahawa kupitia teknolojia ya chupa ili kuongeza wigo mpana zaidi na wakulima waweze kupata miche mingi na kwa uharaka zaidi ili kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa.
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali. Mwaka jana Jimbo la Mbulu Vijijini na Jimbo la Babati na Mbulu Mji wakulima waliahidiwa kukopeshwa kulima vitunguu, mahindi katika eneo hilo. Kwa bahati mbaya hawakukopeshwa mpaka msimu umeanza mpka leo.

Je, ni nini kauli ya Serikali kuhusiana na jambo hili?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nilichukue jambo hili la Mheshimiwa Mbunge niende kulifanyia kazi na kufahamu nini ilikuwa ni changamoto ili tuweze kulitatua na changamoto hiyo isijirudie tena.

MHE. MWANTUMU M. ZODO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Zao la mkonge ndiyo dhahabu yetu ya Mkoa wa Tanga kwa sasa. Zao la mkonge linachukua miaka mitatu toka kulihudumia mpaka kuanza kuvuna. Wakulima wengi wadogo wadogo wanaoanza wanashindwa pale mwanzo kwa sabbau ya kusubiria miaka mitatu kabla ya kuvuna;

Je, Wizara haioni haja sasa ya kuja na mkakati wa kuwawezesha wakulima wadogo wadogo ili kuedelea kuleta hamasa kwenye zao hili?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye zao la mkonge Serikali imefanya yafuatayo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha kwanza, tumeendelea kuongeza uzalishaji wa miche ya kutosha kupitia TARI Mlingano pale Mkoa wa Tanga, na hivi sasa tunajenga maabara ya tissue culture kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa miche hii ya mkonge ili wakulima wengi zaidi waweze kuhamasika. Pili; tunahakikisha ya kwamba katika mwaka huu wa fedha tunanunua decorticators mbili, ile corona, kwa ajili ya uchakataji wa mkonge ili mkonge mwingi zaidi uweze kuchakatwa na kuongeza hamasa ya wakulima kulima zaidi; na la tatu, tunaendelea kuunganisha wakulima wetu na taasisi mbalimbali za kifedha ili waweze kukopesheka na kuongeza tija katika uzalishaji wa zao la mkonge. Na la mwisho, kwa sababu katika ulimaji wa mkonge kuna spacing tumekuwa pia tukiwahamasisha pale katikati kulima mazao mengine ya haraka ili yawasaidie kuiongeza tija na kuongeza kipato katika aina ya zao ambalo wanalilima.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa muda wa kuuliza maswali mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, huu mradi umechukua muda mrefu sana kwenye utekelezaji wake, na Serikali tayari ilikuwa imeshaweka zaidi ya shilingi milioni 800 katika mradi huu. Wananchi wa Mufindi Kaskazini wameusubiri kwa muda mrefu sana. Je, Serikali sasa katika bajeti hii iko tayari kufanya huo upembuzi yakinifu na kuanza ujenzi wa mradi huu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, utekelezaji wa maagizo ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Comrade Chongolo alipotembelea Mradi wa Umwagiliaji wa Ruaha Mbuyuni katika Wilaya ya Kilolo kwa sababu ulikuwa una changamoto kubwa sana? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwenye swali lake la kwanza; ni kweli zmetumika shilingi milioni 800 katika hatua ya awali ambayo kazi yake kubwa ilikuwa ni ujenzi wa banio, njia ndefu ya kilometa 3.5 pamoja na vivuko, lakini katika Mwaka wa Fedha unaokuja tumetenga fedha kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, ili kupata chanzo cha uhakika cha maji katika skimu hii, ili iweze kufanya shughuli za umwagiliaji mwaka mzima.

Mheshimiwa Spika, jambo hili pia, tulikaa na Mbunge wa jimbo, Mheshimiwa Kigahe, tulizungumza kwa pamoja namna ya kuweza kuboresha skimu hii na hasa katika kuhakikisha kwamba, tunajenga bwawa hilo kwa ajili ya chanzo cha maji cha uhakika.

Mheshimiwa Spika, la pili la kuhusu Ruaha Mbuyuni; tulipokea maelekezo ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi na tayari mimi na Mheshimiwa Aweso tulishatuna timu ya wataalamu kwa ajili ya kwenda kuangalia, kufanya marejeo ya usanifu wa eneo lile na hasa kurudisha Mto Lukosi katika njia yake ya asili, ili iweze kusaidia maji yale yaende katika mashamba ya wananchi na yasilete athari. Na hivi sasa kazi inaendelea, naamini baada ya muda mfupi ujao tutapata gharama halisi na utekelezaji utaanza mara moja.

MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Je, ni lini Serikali itajenga Mradi wa umwagiliaji katika Kata ya Mwanyahina katika Jimbo la Meatu?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge alishawasilisha jambo hilo ofisini kwetu na tumekubaliana kwamba, nitawaelekeza wataalam wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwenda kuangalia lile bwawa lililoko pale kama litakuwa ni chanzo kizuri cha maji kwa ajili ya umwagiliaji. Na baada ya hapo tutawatengea fedha kwenye bajeti inayokuja ili waanze kilimo cha umwagiliaji.

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona:-

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Kalenga lina skimu ambazo ni chakavu sana. Nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba, skimu hizo zinafufuliwa na zinakuwa zinahudumia wananchi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha miradi yote ya umwagiliaji inafanya kazi. Ninataka nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunaendelea kuipitia miradi yote, tutakwenda pia katika Jimbo la Kalenga kuangalia na pia, wataalam wetu watafanya kazi tutahakikisha kwamba, miradi hiyo inafanya kazi na wakulima waweze kufanya kilimo cha umwagiliaji.
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mkakati gani wa kutumia vyanzo vya uhakika vya maji kama maziwa na mito kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, tarehe 20 Machi, 2023 mbele ya Mheshimiwa Rais tulisaini mikataba 22 kwa ajili ya kuyapitia mabonde yote ya kimkakati nchi nzima na hasa yale yenye mito na maziwa. Nataka nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba, tumezingatia hoja ya Wabunge humu ndani na tutalitumia Ziwa Victoria, Mto Malagarasi, Mto Ruhuhu, Mto Songwe, kule Litumbandyosi, pamoja na Kilombero, Mto Ngono, Mto Rufiji, hii yote tutaitumia kuhakikisha kwamba, tunafanya kilimo cha umwagiliaji. (Makofi)

MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi ya swali la nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, nini mpango wa Serikali kufufua skimu ya umwagiliaji iliyoko Kijiji cha Makangaga, Kata ya Kiranjeranje, Jimbo la Kilwa Kusini?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema pale awali ni dhamiravya Serikali kuhakikisha skimu zote za umwagiliaji zinafanya kazi. Nitashirikiana na Mheshimiwa Mbunge kuangalia kama katika jedwali letu skimu hiyo haipo katika mwaka huu wa fedha, basi tutaitengea fedha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, inafanya kazi na wakulima wanatumia skimu hiyo kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Malinyi lina maji mengi sana yanayopotea bure. Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha skimu ya umwagiliaji katika Kata ya Malinyi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, eneo lote la Malinyi linaingia katika mradi huu mkubwa ambao tunaendelea nao wa Bonde la Kilombero na Ifakara Idete. Kwa hiyo, ndani yake humo tutapata nafasi ya kujenga skimu nyingi za umwagiliaji na wabanchi wa Malinyi watanufaika kupitia mradi huu mkubwa unakuja.
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana:-

Mheshimiwa Spika, katika Kijiji cha Takwa, Kata ya Kinyomshindo, Jimbo la Chemba, kuna skimu ambayo imetelekezwa sasahivi. Siku za nyuma imepata fedha kutoka Serikalini. Ni nini mkakati wa Serikali wa kuifufua skimu ile ya umwagiliaji? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nitahakikisha nashirikiana na Mheshimiwa Mbunge pamoja na wataalam wangu kwa sababu, ipo karibu hapa twende tukaiangalie muda wowote tutakaopata nafasi katikati hapa, ili tuweze kutoa maamuzi sahihi ya utekelezaji wa skimu hii, lakini lengo kubwa la Serikali ni kuhakikisha kwamba, skimu zote zinafanya kazi, ndio dhamira kuu. Kwa hiyo, kama hiyo ndio dhamira kuu maana yake hiyo skimu aliyoitaja ipo ndani ya mpango wa Serikali, baada ya kukaa na wataalamu wetu kuona namna ya kuweza kutekeleza mradi huo.
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana:-

Mheshimiwa Spika, katika jimbo ambalo mimi ndio mwakilishi wao, Halmashauri ya Itigi, kuna skimu moja tu. Je, Serikali sasa iko tayari kuyatumia Mabonde ya Ipalalyo na Bonde la Mnazi kwa ajili ya kutengeneza skimu nyingine?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, tupo tayari na tutashirikiana na Mheshimiwa Mbunge kwa ajili ya kufanya hilo.
MHE. ABEID R. IGHONDO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, pamoja na majibu haya mazuri ya Serikali ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwanza je, Serikali sasa ina mpango gani mahususi wa kuwapatia wakulima nchini zana za kisasa za kilimo hususani matrekta ambapo sasa hivi tunaona wananchi wetu wanatumia jembe la mkono katika maeneo mbalimbali?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Serikali ina mpango gani mahususi wa kufanya kilimo cha umwagiliaji kuwa ni ajenda ya kitaifa ambapo wananchi wetu sasa waweze kulima mara mbili kwa mwaka kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua. Tuna maeneo mengi yenye maji kama Singida Kaskazini, lakini bado hayajatumiaka ipasavyo. Tunaomba mkakati mahsusi wa Serikali kuhusu ku–mechanize kilimo chetu.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nikianza na swali la kwanza la Mheshimiwa Mbunge kuhusu zana za kilimo kama alivyosema tunaendela kufanya mageuzi katika matumizi ya zana za kilimo za kisasa ili wakulima wetu waweze kuzalisha kwa tija na hivi sasa tunashirikiana na CARMTEC na Shirika la TEMDO katika kuja na teknolojia mbalimbali na zana mbalimbli za kusaidia katika uzalishaji katika sekta hii ya kilimo. Lakini kubwa kuliko yote ni kwamba tunakwenda kuanzisha mechanization hub katika ikolojia mbalimbali za nchi yetu ya Tanzania kikanda ili wakulima wetu pia waweze kutumia fursa hiyo ya kuweza kutumia mitambo hiyo ya kukodisha badala ya mkulima kwenda kukopa trekta huko ana ekari mbili na kuingia gharama kubwa, tunaweka vituo hivi kwa ajili ya ukodishaji wa zana za kilimo za kisasa.

Mheshimiwa Spika, la pili kuhusu mipango mahususi katika eneo la umwagiliaji, kama nilivyokuwa nikisema hapa ndani ni dhamira ya Serikali kuhakikisha ya kwamba tunatekeleza kwa dhati kabisa eneo hili la umwagiliaji kwa kuweka mipango madhubuti na mkakati mkubwa hivi sasa ni kuhakikisha scheme zetu zote za umwagiliaji nchini zinafanya kazi, lakini hatua kubwa na ya kwanza ni kuhakikisha kwanza tunaweka vyanzo vya uhakika vya maji ili scheme hizo ziweze kufanya kazi na wananchi waweze kuhudumia mashamba yao zaidi ya mara moja ndani ya mwaka mmoja.
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi, pamoja na mkakati uliosema wa kugeuza kilimo kama cha biashara.

Je, kuna mkakati gani kwenye eneo la Yaeda Chini na Eshkesh ambayo ni kame unavyojua kuyageuza maeneo hayo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, tunakwenda kuanzisha ukanda wa kilimo wa kikanda nchi nzima ili kuweza kuyafikia maeneo yote kutokana na ikolojia, kwa hiyo, na maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja kupitia utaratibu huu tutaweza kuyafikia na kuwasaidia wakulima wetu kulima kwa tija.
MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Spika, Serikali ina mikakati gani ya kuhakikisha kuwa mbolea na pembejeo za kilimo zitafika mapema kabla ya mvua za mwanzo hazijanyesha? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, Serikali imekwisha kutamka narudia tena huku kwamba tutahakikisha wakulima wetu hawapati changamoto zilizojitokeza katika msimu uliopita, mbolea ya kupandia na kukuzia itaanza kuingia mwezi wa saba mapema kabisa ili wakulima waweze kununua na uhifadhi kwa ajili ya msimu unaokuja. (Makofi)
MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pia naomba niipongeze Serikali kwa kuchukua jitihada kuhakikisha kwamba shirika hili linafanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa shirika hili muda mrefu halijafanya kazi, ni wazi kwamba kuna upungufu mkubwa sana wa wafanyakazi. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba inaongeza wafanyakazi katika shirika hilo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kama nilivyosema awali kwamba ni muda mrefu TFC haijafanya kazi, ni obvious kwamba miundombinu ya maghala ambayo yalikuwa yanatumika kuhifadhia mbolea yana hali mbaya: Serikali imeandaa mpango gani kuhakikisha kwamba maghala haya yanakarabatiwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunda, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la wafanyakazi, ni kweli kampuni hii inahitaji wafanyakazi. Wiki iliyopita, management yote ilikuwa hapa kwa ajili ya kwenda kuutetea muundo kwa ajili ya kuanza kuboresha eneo hili na kupata wafanyakazi wapya. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba kazi hii inaendelea ya kupata wafanyakazi wengine wa kusaidia kuendesha Kampuni yetu ya TFC.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili kuhusu maghala, ni kweli tunayo maghala ambayo yamekuwa na changamoto kwa kiwango kikubwa sana, lakini hivi sasa tunashirikiana na Halmashauri za wilaya husika kwa ajili ya maghala yale ambayo yapo katika maeneo yao tuweze kuyatumia. Pia sisi tunayo maghala yetu ambayo tunayaboresha hivi sasa ili yaanze kufanya kazi hii. Katika fedha ambayo tumeipanga mwaka ujao wa bajeti, pia tumeongeza eneo la kuboresha maghala yetu ili yaweze kutumika vizuri.
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kampuni yetu ya Mbolea ilikopesha wananchi, watu binafsi, vyama vya ushirika na Serikali zaidi ya Shilingi bilioni 18 ambayo ilisababisha kampuni ikawa na mtaji hasi: Je, Serikali ina mpango gani wa kukusanya haya madeni ili kuiongezea nguvu Kampuni yetu ya Mbolea?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, suala la madeni ni kweli na moja kati ya kazi ambazo tumeipa management hivi sasa ni kuhakikisha inafuatilia madeni yote na kuhakikisha kwamba madeni haya yanalipwa ili kuongeza mtaji wa Kampuni ya TFC.
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Msimu uliopita wananchi wa Wilaya ya Tarime walipata shida sana kupata mbolea. Walikaa mpaka wiki tatu pale Tarime waking’ang’ania mbolea: Naomba nipate kauli ya Serikali kwamba msimu ujao wa kilimo watu wa Tarime watapata ile shida au itakuwa imeisha? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli katika msimu uliopita tulikuwa tuna changamoto ya upatikanaji wa mbolea kwa wakati, lakini Serikali imechukua hatua. Tumeshamwelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA na timu yake nzima kuhakikisha kwamba wanaongeza vituo vya mawakala wa uuzaji wa mbolea sambamba na kutumia vyama vya ushirika kama sehemu ya usambazaji wa mbolea.

Mheshimiwa Naibu Spika, kubwa kuliko yote, nataka niwaondoe hofu Waheshimiwa Wabunge kwamba mbolea itaanza kuingia nchini mapema mwezi Julai ili wakulima waanze kuinunua mapema kujiandaa na msimu unaokuja.
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu lakini ninayo maswali mawili kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Lulindi ni mzalishaji mkubwa wa malighafi hya hivyo viwanda wanavyoahidi kuvijenga. Je, Serikali itajenga viwanda vingapi kwenye Jimbo la Lulindi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kilimo cha korosho, zao hili pekee yake ndiyo linalochangia mfuko wa kilimo. Je, Serikali haioni sababu ya kutumia kiasi cha pesa zilizoko katika mfuko huu kwa ajili ya kutengenezea bima ya bei ya korosho? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza nataka nikiri ni kweli eneo la Lulindi ni kati ya wazalishaji wakubwa wa korosho. Kwa kutambua hilo Serikali pamoja na sekta binafsi itaendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya kubangua korosho katika eneo hili la Lulindi ili wakulima wengi zaidi waweze kunufaika na hatua hii ya uchakataji wa korosho.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili kuhusu bima, tumeshafanya mazungumzo na Shirika la Bima la Taifa kwa ajili ya kuhakikisha ya kwamba wanaingia katika zao hili la korosho ili tuweze kumlinda mkulima pale bei inapoporomoka. Hivi sasa tupo katika hatua nzuri na baadhi ya maeneo tumeanza majaribio naamini itawafikia wakulima wengi zaidi na itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wakulima wa korosho nchini Tanzania.
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Naishukuru Serikali kwa kututengea fedha kwa ajili ya mradi huu. Kwa kuwa Mkurugenzi wa Umwagiliaji aliahidi kwenda yeye mwenyewe, nataka kujua: Je, Mheshimiwa Naibu Waziri, atamwelekeza lini aende kutembelea mwenyewe mradi huu wa Kisawasawa kwa sababu aliahidi wakati wa Bunge hapa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa Kijiji cha Lungongole Tarafa ya Ifakara nako wana eneo linalofaa kwa umwagiliaji hasa wakati wa kiangazi: Je, ukimwagiza aende Kisawasawa, uko tayari kumwagiza aende na Lungongole ili tathmini pia ianze? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nitamwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kufika Kilombero mapema kadiri iwezekanavyo. Kuhusu eneo lake la pili, bahati nzuri tulisaini mkataba hapa wa kuajiri Washauri Waelekezi kwa ajili ya kuyapitia mabonde yote nchini likiwemo Bonde la Ifakara - Idete. Kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tunayo Kampuni pale ya Clemence na Vibe International Company Limited wako tayari na wako 13% ya kufanya usanifu katika eneo hilo. Kwa hiyo, mradi huo pia utajumuishwa katika skimu ambayo itatengenezwa hapo katika Bonde la Ifakara.
MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru majibu ya Serikali. Bwawa hili la Chemba ni bwawa kubwa sana na likikamilika lina uwezo wa kwenda kuhudumia kata zangu tisa za Jimbo la Ulyankulu na bwawa hili lina maji mengi sana baada ya upembuzi yakinifu na tayari Serikali imeshatutengea milioni 750 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hili kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Sasa Je, upi ni mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba maji haya yataendelea kutumika pia kwenye shughuli za umwagiliaji?

Lakini swali lingine la pili, Je, Mheshimiwa Naibu Waziri upo tayari kuongozana na mimi ili Bunge linapokwisha hapa uende uone hali halisi ya bwawa hilo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katika majibu yangu ya msingi ya kwamba kwa kutambua kwamba tunalo bwawa kubwa ambalo ni chanzo kizuri cha maji kwenye kilimo cha umwagiliaji, Serikali itahakikisha kwamba katika mwaka wa fedha ujao tunafanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili maji yale pia yatumike kama sehemu ya kilimo na yaguse eneo kubwa zaidi ya kata tisa za Ulyankulu ili wananchi waweze kunufaika na bwawa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili niko tayari kuongozana na Mheshimiwa Mbunge kwenda jimboni kuangalia jambo hili pamoja na watalaam wetu ili kuweza kuharakisha zaidi ili wakulima wa Ulyankulu waanze kulima kupitia chanzo hiki cha maji kupitia mfumo wa umwagiliaji.
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuweza kuuliza swali la nyongeza. Je, Serikali ina mkakati gani wa kutumia bonde la Kiru na Magara kwa ajili ya umwagiliaji?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye kiambatanisho namba tano cha bajeti yetu tuliyoisoma hapa ndani tumeyataja mabonde 22 moja kati ya mabonde yaliyotajwa ni mabonde ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja na yapo katika hatua ya mshauri mwelekezi hivi sasa akikamilisha kazi tunaanza ujenzi mara moja ili wananchi wa Mkoa wa Manyara waweze kunufaika na skimu hizi za umwagiliaji.

MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Jimbo la Igunga tuna skimu kubwa ya umwagailiaji ya Mamapuli iliyopo pale Mwanzugi na kwenye bajeti inayotembea, Serikali iliahidi kutupatia fedha. Je, ni lini Serikali itatupatia fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ili kuboresha miundombinu kwa ajili ya kuwahudumia wakulima waliopo ndani na nje ya skimu? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, skimu hii ni kati ya skimu 42 ambazo tumezitengea fedha na nimtoe hofu tu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba tutakamilisha yale ambayo tuliahidi ndani ya Bunge hili kuhakikisha kwamba skimu ile inafanya kazi na inarekebishwa ili wananchi waweze kufanya kilimo cha umwagiliaji kupitia skimu hiyo.

MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza nataka kujua mkakati wa Serikali wa kuhakikisha unawapatia mbegu bora kwa ruzuku wakulima wa mazao haya mengine.

Swali langu la pili, nataka kujua kuna changamoto kubwa sana ya masoko hasa ya zao la muhogo pamoja na mbaazi wakulima wanalima lakini wanakosa masoko ya uhakika. Nataka kujua mkakati wa Serikali kuhakikisha masoko ya mazao haya yanapatikana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu upatikanaji wa mbegu kwa ajili ya wakulima kwa mfumo wa ruzuku. Sisi kama Serikali tuko tayari kuhakikisha kwamba tunaongeza uzalishaji wa mazao haya na pindi pale mahitaji yakiainishwa kupitia TARI na ASA tupo tayari kuwapatia wakulima mbegu hizi katika mfumo wa ruzuku ili waweze kuongeza uzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu masoko ya uhakika, nikianza na mbaazi, kwenye mbaazi tayari tumeshaingia makubaliano ambayo bado tuko katika hatua za mwisho na Serikali ya India ya kuchukua zaidi ya tani 150,000 na hivi sasa ninavyozungumza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo yuko India kwa ajili ya kufatilia jambo hili hili kuhakikisha kwamba tunapata soko la uhakikia la wakulima wa mbaazi ili kuondokana na changamoto hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo hili pia kupitia TARI na MDT ambayo ni taasisi inayo jishughulisha na masuala ya masoko ya mazao, tumeendelea kutoa elimu na mafunzo juu ya matumizi ya ziada ya mbaazi ikiwemo lishe lakini pamoja na matumizi mengine ya viwanda kwa ajili ya kuongeza soko la zao hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Muhogo tunao mkakati wa kitaifa wa kuendeleza zao la muhogo wa mwaka 2020 mpaka 2030 ambao ndani yake pia umeainisha mikakati mbalimbali ikiwemo kuwahusisha watu wenye viwanda kwa ajili kutengeneza wanga kupitia muhogo, industrial of starch wanaita ili tuongeze soko la muhogo wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tupo katika mawasiliano na ubalozi wa China, Rwanda na Burundi kuongeza wigo mpana wa soko la muhogo ili kuwaondolea changamoto wakulima juu ya upatikanaji wa uhakika wa soko la muhogo.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Je, Serikali imejipangaje kushajihisha, kuongeza uzalishaji wa mazao ya nafaka asilia kama fiwi, mtama, uwele, ufuta, dengu,choroko na mbaazi kwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya kilimo hiki?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tumejipanga kuanzisha kanda za kilimo Tanzania Agricultural Growth Corridor ambalo lengo lake kubwa ni kulima mazao kutokana na afya ya udongo itakavyoruhusu. Kwa hiyo, tunaendelea na kazi ya upimaji wa afya ya udongo, yale maeneo ambayo mazao uliyosema yanastawi tutayapa kipaumbele na tutatenga maeneo ili wakulima wapate maeneo ya kutosha na waweze kunufaika zaidi kupitia mazao hayo.

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa. Je, Serikali ina mpango gani wa kuendelea kugawa miche bora ya kahawa yenye ukinzani dhidi ya magonjwa sugu ya kahawa kwa wakulima wa Jimbo la Moshi Vijijini?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu Mibuni tuliyonayo asilimia kubwa imeshakaa zaidi ya miaka 25 na hivyo kupunguza uzalishaji, hivi sasa Serikali kupitia TAKRI na wadau wengine kama bodi ya kahawa tutahakisha kwamba tunazalisha miche ya kutosha na hasa kupitia teknolojia ya chupa ili wakulima wengi zaidi wapate miche iwafikie kwa urahisi na waweze kuongeza uzalishaji ikiwemo wa kulima wa jimboni kwa Mheshimiwa Prof. Ndakidemi.
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Zao la pamba ni miongoni mwa mazao yanayofanya vizuri katika Mkoa wa Mtwara lakini zao hili limezuiliwa kulimwa Mkoa wa Mtwara kutokana na ugonjwa ambao upo kwenye zao la Pamba Nchini Msumbuji Jimbo la Kabodayogado. Je, ni lini Serikali itaondoa zuio hili?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tunalo tishio la funza wekundu ambao wanapatikana katika nchi za Msumbiji pamoja na Zambia na maeneo mengineyo. Kwa sababu ya tishio hilo tumeendelea kuweka quarantine na tuna sisitiza tu wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuendelea kulima mazao mbadala kama ufuta, korosho lakini kwa hivi sasa kwenye pamba tunayo changamoto kubwa na hatuwezi kuachia hivi sasa kwa sababu ya tishio la hao funza wekundu.

MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Kumekuwa na ucheleweshaji wa mbegu kwa wakulima na hivyo wakulima kukosa tija kwenye kilimo chao. Ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha mbegu zinapelekwa kwa wakati ili waweze kulima kwa tija? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli, changamoto kubwa ya upatikanji wa mbegu kwa wakati ilikuwa ni kwamba mzalishaji mkubwa wa mbegu ASA alikuwa na yeye alikuwa anategemea mvua kama ambavyo mkulima kuzalisha mbegu. Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mama Samia Suluhu Hassan tumetenga fedha kuhakikisha kwamba tunaanza kuweka miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba yetu ya mbegu ili tuwe tuna uwezo wa kuzalisha mbegu mwaka mzima na wakulima wazipate kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuanzia katika mashamba yetu makubwa nane ya awali tumeweka miundombinu center na lateral pivot kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunamwagilia mashamba haya na mbegu zinapatikana kwa mwaka mzima na zitawafikia wakulima kwa wakati na msimu ukianza watakuwa nazo.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza kwa niaba ya Mheshimiwa Stella Fiyao. Mji wa Tunduma ni mji ambao unavuna sana mahindi, na uko mpakani na nchi ya Zambia: Ni lini Serikali itawekeza pale kuhakikisha wakulima wale hawauzi kwa hasara ndani, wapeleke hata nje kwa sababu wao wako karibu na nchi ya Zambia?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Zao la kokoa ni zao ambalo hapa Tanzania ni la pili kwa Afrika kwa ubora; na inasemekana zao hili linanunuliwa sana katika nchi ya uingereza: Ni lini mtamsaidia mkulima wa Kyela aweze kuuza zao la kokoa kwa bei nzuri ambayo yeye kama mkulima atanufaika kuliko madalali wa katikati wanaonufaika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli mpaka wa Tunduma ni kati ya mipaka ambayo imekuwa ikitumika sana kusafirisha mazao. Nataka tu nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba, hivi sasa tunawekeza nguvu kubwa kuhakikisha tunawasaidia wakulima wetu ili mwisho wa siku waweze kunufaika na mazao yao na hasa katika utaratibu wa kurasimisha biashara ya mazao na urahisi wa usafirishaji mazao ili mkulima aweze kunufaika na mazao yake ikiwemo katika mpaka huu wa Tunduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili la kuhusu kokoa. Ni kweli katika eneo la kokoa tunafanya vizuri, lakini mkulima pia ana haki ya kupata bei nzuri kutokana na ushindani wa kimasoko uliopo. Kama Serikali tutahakikisha kwamba tunaweka miundombinu rafiki ili kuwaruhusu wakulima wetu kutafuta masoko makubwa nje ya nchi ambayo yatawasaidia pia kupata bei ya uhakika na hasa katika kilimo hai cha kokoa ambacho bei yake imekuwa ni kubwa sana kimataifa.
MHE. DANIEL B. SILLO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali moja la nyongeza. Wananchi wa Babati Vijijini wanatumia sana zao la mbaazi kama zao lao la biashara: Ni nini mkakati wa Serikali wa kutafuta soko la zao hili la mbaazi kwa ajili ya manufaa ya kiuchumi ya wananchi wa Babati Vijijini?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeendelea kutafuta soko la uhakika la mbaazi na hasa kwa kuishirikisha Serikali ya India, ikiwa ni mmoja kati ya wanunuzi wakubwa. Wiki moja iliyopita, tulimtuma Naibu Katibu Mkuu wetu wa Wizara ya Kilimo, kwenda India kwa ajili ya kufuatilia yale makubaliano ya awali yaliyokuwepo ya soko la mbaazi na majadiliano yanakwenda vizuri ili tuweze kuwahakikishia wakulima wetu masoko ya uhakika, hasa ya mbaazi ambapo India wamekuwa wanunuzi wakubwa.
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni Serikali imeweka zuio la kuu za mahindi nje ya nchi. Hali hiyo imesababisha bei ya mahindi kushuka. Kwa mfano, kwenye Jimbo langu la Mbozi debe sasa hivi ni shilingi 8,000 na bei inazidi kushuka; nini kauli ya Serikali ili kuwaokoa hawa wakulima ambao kwa sasa wamevunjika moyo na kuporomoka kwa hii bei?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kati ya changamoto kubwa ambayo tunaipata katika biashara ya mazao ni uholela. Serikali ilichokifanya siyo kuzuia moja kwa moja. Imetoa mwongozo na kuweka utaratibu wa namna ya kufanya biashara ya mazao nchini Tanzania ambapo tumeelekeza kwamba, hivi sasa kila mfanyabiashara wa mazao, ahakikishe kwanza kabisa anapata Business License; pili, awe ana TIN; na tatu, kabla hajaenda mpakani kusafirisha mazao, ahakikishe kwamba ameshapata kibali cha kusafirisha mazao nje ya nchi (Export Permit).

Mheshimiwa Mwenyekiti, lengo la kufanya hivi ni kuweka takwimu sawa, kwa sababu kumekuwepo na wafanyabiashara ambao wanakwenda mashambani moja kwa moja kwa wakulima kwenda kununua mazao na hivyo Serikali kupoteza mapato mengi sana. Serikali ipo kwa ajili ya kuwalinda wakulima na kuhakikisha kwamba wakulima wanapata bei bora tukishawasimamia, kwa sababu ndiyo azma ya Mheshimiwa Rais kuhakikisha kwamba mkulima ananufaika na kilimo chake. (Makofi)
MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, Serikali ina mpango gani wa kuzuia uuzaji wa mazao ghafi nje ya nchi, badala yake yaongezwe thamani kwa kusindikwa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, anachokisema Mheshimiwa Mbunge ni sahihi na ndiyo mkakati wa Serikali. Hivi sasa tunajielekeza katika kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa nchini badala ya kuyapeleka ghafi nje ya nchi. Kwa mfano, katika eneo la zao la korosho hivi sasa tunaweka mkakati mkubwa kuhakikisha kwamba, zaidi ya asilimia 60 ya korosho yetu ifikapo mwaka 2025 iwe inabanguliwa hapa ndani na kuongezewa thamani. Hivi sasa tumeshaandaa eneo la Nanyamba kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha ubanguaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika maeneo mengine ikiwemo parachichi na mazao mengine pia, mkakati ni huo huo wa kuhakikisha kwamba tunaweka miundombinu rafiki kwa kushirikiana na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ili tuwe tuna mnyororo mzima wa kuongeza thamani ya mazao yetu ya kilimo na mwisho wa siku kuliongezea Taifa mapato kupitia mazao haya.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi. Liko soko kubwa sana la mazao ya kilimohai, kwa mfano pamba yetu ya Tanzania iko namba tatu: Je, ni lini Serikali itaweka angalau kitengo mahususi cha kushughulikia kilimohai katika Wizara ya Kilimo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli, mazao mengi ya kilimohai yana soko kubwa na yana uhakika sana wa masoko nje ya mipaka ya Tanzania. Kama Serikali, tumekuwa ni sehemu ya washiriki katika kuhakikisha kwamba tunafanikisha wakulima wetu kuweza kuyafikia masoko hayo makubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndani ya Wizara ya Kilimo pia tunaweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha kwamba tunashirikiana na wadau wakubwa wa kilimohai kwa kuweka kitengo maalum ambacho tutakuwa tunashirikiananao ili mwisho wa siku tufanye kazi kwa pamoja, maana wadau wakubwa wa kilimohai ni taasisi nyingi za binafsi ambazo zimekuwa zina mchango mkubwa. Nasi kama Serikali lazima tuhakikishe pia tunashirikiananao. Kwa hiyo, tunao watu ambao ni focal person katika Wizara ya Kilimo. Tutaendelea kuwaimarisha ili wafanye kazi kwa pamoja na sekta binafsi kwenye kilimohai.
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu ya Serikali, lakini bado nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mkakati wa Serikali unaonekana hawajafanya utafiti wa kuweza kujua ni kwa kiasi gani uzalishaji wa mbegu unahitajika nchini: -

Je, Serikali ipo tayari sasa kutengeneza mkakati, angalau wa miaka mitano, wa kuhakikisha kwamba wanafanya utafiti wa kujua ni idadi kiasi gani ya mbegu zinatakiwa ili uzalishaji huo wa miche milioni 20 kwa mwaka angalau upande hadi kufikia miche milioni 50?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa TaCRI na Bodi ya Kahawa peke yao hili zoezi hawaliwezi: -

Je, Serikali ina mkakati gani mahususi wa kuhakikisha kwamba inaihusisha sekta binafsi katika eneo hili la uzalishaji wa mbegu ili sasa hili zao la kahawa tuweze kulifufua kote nchini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi, Mbunge wa Mlalo, kwa pamoja kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la utafiti kwenye kahawa ndiyo kazi ambayo imekuwa ikifanyika muda wote kupitia TaCRI ili kuwezesha kuongeza uzalishaji katika zao letu la kahawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uzalishaji wa miche ya kahawa unaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na mahitaji. Kwa hivi sasa tumetoa maelekezo kwa wenzetu wa TaCRI pamoja na wakulima pia kuhakikisha ya kwamba tunang’oa ile mibuni yote iliyofikisha zaidi ya miaka 25 ambayo imezeeka na kupanda miche mipya ili kuongeza uzalishaji. Hivyo, itatulazimu kuongeza uzalishaji mkubwa sana wa miche ya kahawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana sisi kama Serikali peke yetu hatuwezi kufanya, tumewahusisha pia sekta binafsi ili kwa pamoja tuweze kuzalisha miche mingi zaidi, na lengo hapa ni kuwa na miche mingi ya ziada ili wakulima wetu waweze kuipata kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa tumeongeza mkakati mwingine wa kuhakikisha kwamba tunatumia teknolojia ya chupa (tissue culture) kwa ajili ya kuongeza uzalishaji miche mingi zaidi ya kahawa, iwafikie wakulima kwa wakati, na tuweze kuongeza uzalishaji wa zao hili la kahawa hapa nchini.
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza ajira zaidi kwa wanawake kwa kuwa hawa 241 bado ni wachache katika zao la korosho Mkoani Mtwara? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa Mkoa wa Mtwara haujapata block farming katika zao la korosho; Serikali ina mkakati gani wa kuwatengenezea vijana programu mahsusi katika mnyororo wa thamani kwa zao la korosho ili vijana wa Mtawara waweze kunufaika na project za Wizara ya Kilimo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 zaidi ya asilimia 60 ya korosho inayozalishwa ndani iweze kubanguliwa na hivyo kutunza ajira zetu za akina mama na vijana kuliko ilivyo hivi sasa ambavyo ajira nyingi zinasafirishwa nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mkakati huo pia hivi sasa tunatazamia kuanza maandalizi ya ujenzi wa industrial park katika eneo la Nanyamba ambako tutajenga viwanda vya ubanguaji wa korosho na zaidi ya tani 300,000 zitabanguliwa na akina mama na vijana hawa wataunganishwa katika mfumo uliyosehemu pia ya ajira yao na kutatua changamoto hiyo ya korosho kutokubanguliwa.

Mheshimiwa Spika, la pili la kuhusu mashamba makubwa ya pamoja, utaratibu huo chini ya Bodi ya Korosho umekwisha kuanza na umeanza kuwapanga wakulima katika mashamba makubwa na ninaamini kabisa kwamba wakulima wa Mtwara wakiwemo akina mama na vijana watanufaika na mpango huo mkubwa sambamba na mkakati mkubwa wa ujenzi wa miundombinu ya skimu za umwagiliaji katika mabonde ambayo pia tutayaweka maeneo kwa ajili ya umwagiliaji wa kilimo cha korosho na hakika pia kupitia utaratibu huu akina mama na vijana wa Mkoa wa Mtwara watanufaika katika mfumo wa mashamba makubwa ya pamoja.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa kuwa uhitaji wa kuongeza thamani kwenye zao la korosho Mtwara unafanana kabisa na uhitaji wa kuongeza thamani kwenye zao la ndizi Kilimanjaro.

Je Serikali ina mpango gani kuwasaidia wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro mashine hizo za SIDO ili waweze kuongeza thamani kwenye zao la ndizi kwa kutengeneza clips na vitu vingine vinavyotokana na ndizi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha ya kwamba mazao yetu ya kilimo yanachakatwa ili kuongeza thamani na vilevile kuongeza kipato kwa wazalishaji au wakulima wetu na tupo katika mkakati wa pamoja sisi pamoja na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhakikisha kwamba tunatumia taasisi zetu za ndani kama CAMARTEC, TIRDO na SIDO kutengeneza mashine ndogo ndogo na ambazo zitakuwa zina bei rahisi ili kuweza kuwafikia wakulima wengi zaidi kuongeza thamani ya mazao haya.

Kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba wakulima pia wa ndizi wa Mkoa wa Kilimanjaro hasa akina mama na wenyewe pia tutawaweka na kuhakikisha kwamba na wenyewe wanafanya kazi ya uchakataji.
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Spika, kwanza niishukuru Serikali kuwa na mkakati mzuri wa kuboresha kilimo cha nazi nchini. Nitaomba niwe na swali moja tu la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Dar es Salaam pembezoni kwa maeneo ya Kibamba, Segerea na Ukonga pamekuwa na vikundi vingi vinafanya kilimo cha mbogamboga; je, ni upi mkakati wa Serikali kuwawezesha hawa ili wafanye kilimo bora cha mboga mboga?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali hivi sasa imeweka mkazo mkubwa kwenye kuhamasisha kilimo cha mboga mboga na matunda ili kuongeza uzalishaji ambao kwa mwaka uliopita kupitia mazao haya yametuletea fedha za kigeni zaidi ya dola milioni 750 na lengo letu kufikia dola bilioni 1.2 kwa mwaka 2030. Hivyo kwa hivi sasa tunaendelea kuwawezesha wakulima wadogo wadogo kwanza kabisa katika upatikanaji wa green houses ambao utasaidia katika uzalishaji mkubwa au vilevile mbegu bora ambayo pia itasaidia katika kuzalisha kwa wingi na sambamba na hilo pia tunatafutia masoko kupitia mwamvuli wa TAHA ambao hivi sasa tumeshafungua masoko mengi na wakulima wengi wameanza kuuza mboga mboga na matunda nje ya nchi kupitia mwamvuli huu wa TAHA.

Kwa hiyo, kama Serikali pia tutahakikisha masoko ya uhakika yanapatikana ili tuendelee kuhamasisha vijana wengi zaidi kushiriki katika kilimo hiki cha mboga mboga.
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona.

Katika Wilaya yetu ya Kilwa zao hili la minazi limekuwa likiabiliwa na changamoto ya magonjwa mbalimbali na hivyo kupelekea uzalishaji kushuka na umaskini kuongezeka kwa wazalishaji wa zao hili la minazi.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kutatua changamoto ya magonjwa ya minazi katika Wilaya ya Kilwa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kupitia Kituo cha Utafiti cha Kilimo Mikocheni hivi sasa tunaendelea kufanya utafiti wa kuja na miche bora ambayo itakuwa kinzani ya magonjwa na hasa ugonjwa wa manjano ambao unaathiri sana nazi na kufifisha uzalishaji na kwa hivi sasa tunaendelea na uzalishaji wa mbegu mbili kubwa ya East African Tall pamoja na dwarf ambazo zenyewe zina ukinzani mkubwa wa magonjwa naamini pia wakulima wa Kilwa watanufaika na mbegu hizi na wataongeza uzalishaji kwa sababu kazi ya utafiti imekwisha kufanyika.

MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kutokana na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri amesema ataleta mbegu bora za minazi.

Je, katika uletaji wa mbegu bora za minazi mtaangalia na zile mbegu za asili ambazo zilikuwa ni bora zaidi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA) pale Arusha tunayo benki ya kutunza vinasaba vya mbegu zikiwepo mbegu za asili, kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba tutayazingatia hayo yote pamoja na mbegu za asili ili mwisho wa siku tuhakikishe kwamba uzalishaji unaongezeka, lakini vilevile tunazitunza mbegu zetu hizi kwa sababu zimekuwa zina manufaa makubwa kwa wakulima wetu kwa miaka mingi kabla hatujaleta mbegu hizi ambazo zinatumika hivi sasa.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuendeleza kilimo cha michikichi kwenye Mkoa wa Songwe kwa sababu uoto wa eneo hilo unakubali zao hili?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kwamba zao la mchikichi linaendelea kulimwa katika maeneo yote ambako tumepima afya ya udongo na inakubali na kwa Mkoa wa Songwe kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema sasa hivi tuko katika uzalishaji wa miche na wenyewe pia tutauweka katika mpango wa kuhakikisha kwamba wakulima wa Songwe wanapata miche ya michikichi na wanafanya uzalishaji kama katika haya maeneo mengine.

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Spika, ahsante pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri kidogo yanatia moyo, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza wezi wa kuku, wezi wa ng’ombe na mbuzi wakikamatwa wanafikishwa mahakamani, na kufungwa jela, lakini hawa wa Vyama vya Ushirika wanaambiwa tu warudishe fedha na ndio sababu hili tatizo limeota usugu sana Wilayani Mbozi. (Makofi)

Sasa ni lini hawa viongozi watafikishwa mahakamani na kuchukuliwa hatua za kisheria? Swali la kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Afisa Ushirika ambaye ametajwa kwenye hii tuhuma kwamba alishirikiana na hawa viongozi wa Vyama vya Ushirika nashangaa mpaka sasa hivi bado yuko kazini, sasa ni lini na yeye hatua hii itamchukulia? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, baada ya kufanya uchunguzi taarifa hii imekabidhiwa kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na vyombo vingine vya kisheria kwa ajili ya kuweza kuchukua hatua na ninavyozungumza hivi sasa tayari zaidi ya shilingi milioni 77.6 zimerejeshwa na baadhi ya viongozi wameondolewa na wengine tumewakabidhi TAKUKURU kwa ajili ya hatua za kijinai.

Mheshimiwa Spika, hivyo kazi yetu ilikuwa uchunguzi tumekamilisha, tunasubiri vyombo vingine vya Serikali na vyenyewe vifanye kazi, lakini tu niseme katika hili tumekuwa tukitoa maelekezo mbalimbali, hatutamvumilia mtu yeyote ambaye atafanya ubadhirifu katika Vyama vya Ushirika na kuwakosesha wakulima mapato yao, Serikali ipo macho tutachukua hatua na hakuna ambaye atapona. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge taarifa iko pale, vyombo vitafanya kazi yake.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Afisa Ushirika ambaye yuko chini yetu kwa sababu hii taarifa imeshawasilishwa ili kuendana na uwezo wetu tutachukua hatua stahiki pale ambapo itabainika kupitia taarifa ambayo imewasilishwa kwamba ni mhusika moja kwa moja huyu yuko ndani ya uwezo wetu tutachukua hatua stahiki juu yake.
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa kuwa katika msimu wa mwaka jana ambao unaishia sasa hivi baadhi ya wakulima wa zao la kahawa wanavidai Vyama vya Ushirika vingi tu ambavyo bado havijawalipa. Lipi tamko la Serikali kuhusiana na madai hayo ya wakulima?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, biashara ya mazao ni biashara kama biashara nyingine yoyote. Vyama vya Ushirika vyote ambavyo havijafanya malipo kwa wakulima vinapaswa kufanya malipo kwa wakulima kwa wakati ili kumsaidia mkulima huyu aendelee na shughuli zake za kilimo, hivyo natumia jukwaa hili la Bunge lako tukufu kuwataka wale wote ambao hawajafanya malipo kwa wakulima wafanye mara moja ili kuwaruhusu wakulima kuendelea na msimu unaokuja wa kilimo.
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri, nataka kumkumbusha tu kwamba, pamoja na kwamba nchi yetu kuwa na ukubwa wa eneo lenye square kilometer 947,300 eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta milioni 44 tu.

Je, Serikali haioni wakati umefika kuharakisha kutunga sheria itakayolinda eneo hili la kilimo ili lisije likavamiwa kwa shughuli nyingine? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kumjibu Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kuilinda ardhi kwa ajili ya kilimo. Kama nilivyosema hapa, tumeamua kupitia baadhi ya sheria ili mwisho wa siku tuje na sheria ambayo imekamilika. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaharakisha mchakato huu ili mwisho wa siku tupate sheria yetu ya kilimo, tutunze ardhi ya kilimo.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwanza namshukuru Naibu Waziri wa Kilimo kwa majibu yake mazuri aliyoyajibu kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, lakini nilichotaka kusema tu ni kwamba, Wizara ya Ardhi pamoja na Wizara ya Kilimo tumeshaanza mchakato wa kuyatambua yale maeneo ambayo yanafaa kwa kilimo. Kwa hatua ya kwanza itakayofanyika ni kuya-gazette ili yasiweze kuingiliwa na watu wengine. Kwa hiyo, stage nyingine itakayofuata ndiyo hiyo ya kutunga sheria ili kuyalinda kwa ajili ya uhifadhi wa kilimo. (Makofi)
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsnate. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali langu la kwanza, mmesema Serikali imejipanga kuipa kampuni yetu ya TFC mtaji wa bilioni 40 na sasa hivi tumebakiwa na miezi mitatu tu tufike kwenye high season ya kuhitaji mbolea. Je, mtatumia muujiza gani kuhakikisha mmeagiza mbolea na mnaisambaza nchi nzima?

Swali langu la pili, ni kwa nini CPB hawataki kuwarudishia wakulima fedha, walizoahidi kuwapa mahindi wakati Serikali imezuia CPB isitoe mahindi, na fedha zao hamtaki kuwarudishia ni kwa nini na mnarudisha lini hizo fedha?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nilitoa taarifa humu ndani Bungeni na naomba leo nirudie ya kwamba Serikali imejipanga kuhakikisha ifikapo mwezi wa saba mbolea zote za kupandia na kukuzia ziwe zinapatikana kwa wakulima ili waanze msimu na mbolea zikiwemo.

Mheshimiwa Spika, nakata nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba TFC walianza maandalizi haya mapema na hivi sasa tuko katika hatua za mwisho kuanza kupokea shehena za meli ambazo tutashusha mzigo huo, pia tunayo mbolea ya kutosha kuanzia kwa wakulima katika msimu unaoanza hivi karibuni. Kwa hiyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba jambo hilo litafanyika.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, nimesikia hoja yake ya CPB na wakulima, naomba nikae na Mheshimiwa Mbunge nipate hayo madai ya wakulima, mimi na CPB tutakaa tuone namna ya kuweza kutatua jambo hili, ili mwisho wa siku tuweze kuhakikisha kwamba wakulima wanapata haki yao.
MHE. AMEIR ABDALLA AMEIR: Mheshimiwa Spika, ahsante sana; kwanza teknolojia hii ya habari na mawasiliano ina mchango mkubwa sana katika kuziba lile pengo la uhaba wa Maafisa Ugani wetu kwa muda mfupi na kwa eneo kubwa, sasa Wizara ina mpango gani sasa wa kuanzisha Apps au mifumo mbalimbali ya TEHAMA, ambayo mifumo hii itawasaidia wakulima wetu wadogo wadogo kupata taarifa kwa wakati na kwa usahihi?

Pili, Wizara sasa haioni kuna umuhimu wa kuyashawishi makampuni mbalimbali ya simu kutoa kifurushi maalum cha huduma za wakulima, ambapo sasa wakulima wetu watakuwa wanapata taarifa hizi wakiwa maeneo mbalimbali? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kwa pamoja kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Wizara inatambua matumizi ya teknolojia ambapo ndiyo dunia ya leo inapoelekea, katika kurahisiha utoaji wa huduma kwa wakulima na hasa kupitia Maafisa Ugani, tunao mfumo ambao tunauita N-Kilimo ambao mpaka hivi sasa tumeshasajili Maafisa Ugani 9,725, ambao kazi yao kubwa ni kuhakikisha kwamba tunasambaza taarifa hizi kwa wakulima kupitia programu hii. Pia tunayo call center yetu ya Wizara ya Kilimo ambayo pia wakulima ambao wanapata changamoto mbalimbali wamekuwa wakipiga simu na kupata ufafanuzi na kujibiwa baadhi ya changamoto ambazo wanakabiliaba nazo.

Mheshimiwa Spika, nitoe tu rai na kuwaomba wakulima wote nchini Tanzania kuendelea kuitumia namba yetu ile ya 0733 800 200 kwa ajili ya kuweza kupata huduma mbalimbali za kilimo kupitia teknolojia hii.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ushauri tunaupokea wa kukaa na kampuni za simu kurahisisha utoaji wa huduma hizi za ugani kwa wakulima wetu. Ushauri huo tumeupokea ni mzuri, tutaona namna ya kuweza kuboresha ili wakulima wetu waweze kupata taarifa kwa wakati. (Makofi)
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa katika taarifa yao ya Wizara ya Kilimo walisema sasa hivi wakulima watakuwa wanapimiwa udongo kupitia Maafisa Ugani kwa vishkwambi. Elimu hiyo sasa wakulima wanayo maana yake nimeona bado hawajaanza kutumia hiyo teknolojia ya kupimiwa udongo katika mashamba yao?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni mkakati wa Serikali kuhakikisha tunapima afya ya udongo ya ikolojia zote saba nchi nzima ili wakulima wawe na taarifa sahihi za afya ya udongo katika maeneo yao.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa Serikali kupitia Maafisa Ugani tumewapatia scanners za kwenda kupima afya ya udongo ambayo itasaidia kutoa taarifa kwa wakulima. Vilevile katika mwaka wa fedha unaokuja tutakwenda kununua mobile lab ambazo zitakuwa pia zinapita kwa ajili ya kuwapimia afya ya udongo wakulima. Kwa hiyo, tutakuwa tunao uwezo wa kupima afya ya udongo kupitia maabara na kupitia katika magari pamoja na kit ambacho tumewapa Maafisa Ugani ambapo mkulima akipimiwa afya yake ya udongo hapo hapo akiwa shambani atapata cheti chake ambacho kitaonesha katika udongo huo kuna nutrients za aina gani na anahitaji nini kupanda zao gani na atumie mbolea ya namna gani, ambayo itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wakulima wa nchi yetu ya Tanzania. (Makofi)
MHE. MASACHE N. KASAKA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini sisi tunapenda kujua kwamba Serikali mradi huu wa maji wa Skimu ya Kata ya Ifumbo ulianza toka mwaka 2006 ni mradi wa muda mrefu na umetumia fedha nyingi sana za Serikali na kila siku Serikali imesema itakuwa inatenga fedha.

Je, ni lini sasa Serikali itatenga fedha kwa ajili ya mradi huu uweze kuanza?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Mto Lupa unaopita kwenye kata nyingi pamoja na vijiji vingi una maeneo mazuri sana yanayofaa kwa kilimo cha umwangiliaji.

Je, Serikali haioni haja sasa ya kutuma wataalamu wake waweze kulitembelea hili bonde na baadaye waweze kuweka kwenye mpango na baadaye skimu iweze kujengwa kwenye Kata ya Mto Lupa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Masache Njelu Kasaka, Mbunge wa Rukwa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli tunatambua kwamba mradi huu ulikuwa ni wa muda mrefu na iko kazi ambayo inapaswa kufanyika ikiwemo ya ukarabati wa mfereji mkuu tumebakiza mita 750, lakini na mifereji ya shambani. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwa sababu ya umuhimu wa mradi huu tutaangalia pia vyanzo vingine vya fedha kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Umwagiliaji ili tuweze kukamilisha maeneo machache yaliyobaki ili wananchi waweze kutumia eneo hilo kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji hasa hekta 141 ambazo zimebaki.

Mheshimiwa Spika, swali la pili la kuhusu kuwatuma wataalam, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba ndani ya wiki hii watendaji wa Tume ya Umwagiliaji nchini watakwenda kuangalia eneo hilo ili pia waje watushauri namna ya kuweza ya kuweza kutekeleza skimu hiyo. Nakushukuru sana. (Makofi)
MHE. ZAINAB A. KATIMBA: Mheshimiwa Spika, ahsante, nina swali moja la nyongeza.

Je, ni lini Serikali itakamilisha mradi wa umwagiliaji wa Bonde la Mto Ruichi uliopo Kigoma Mjini ili wanawake na wananchi wa Jimbo la Kigoma Mjini waweze kufaidika na kilimo cha kisasa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zainab Katimba, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Ruichi hivi sasa tumeshapata no objection kutoka Kuwait Fund na utaanza utekelezaji wake mwaka huu wa fedha 2022/2023.

MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Kwa kuwa skimu za umwagiliaji za Udimaa, Ngaiti na Chikuyu za Wilaya ya Manyoni ni chakavu sana, jambo hili limepelekea shughuli za kilimo cha mpunga kusimama.

Je, ni lini Serikali itakarabati skimu hizo ili shughuli za kilimo ziendelee? Nakushukuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Aysharose Mattembe, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Singida kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Wabunge wote ni mashahidi na wameona kazi kubwa ambayo Mheshimiwa Rais ameifanya na dhamira njema ya kuongeza bajeti ya kilimo hasa kwenye eneo la umwagiliaji.

Mheshimiwa Spika, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge yakwamba timu yetu inaendelea kupita na kuyapitia maeneo mbalimbali ili kuweza kufahamu status ya miradi hii ya umwagiliaji. Lengo letu ni kuhakikisha miradi yote inafanya kazi. Halikadhalika kwa Singida pia kwa maeneo ambayo ameyataja nimuondoe hofu, tutakwenda kuyapitia na kuweza kuyafanyia kazi katika mwaka huu ujao wa fedha. (Makofi)
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana; Bonde la Mto Songwe lina eneo la kilometa za mraba 3,500 kwa ajili ya umwagiliaji.

Je, ni lini Serikali sasa itaanza kutekeleza mradi huo ambao unahusisha ujenzi wa dam pale kwenye Bonde la Mto Songwe?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ally Jumbe, Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ukiangalia katika bajeti yetu ambayo tumeiwasilisha jedwali la kwanza yako mabonde 23 ambayo tunakwenda kuyafanyia upembuzi yakinifu na usanifu kwa ajili ya kuanza utekelezaji wake likiwemo Bonde la Mto Songwe. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ni sehemu ya mipango ya Serikali na tumedhamiria mabonde yote kuweza kuyafikia. (Makofi)
MHE. ABUBAKAR D. ASENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba kwa kuzingatia kuwa Mkoa wa Morogoro ni ghala la Taifa na katika Jimbo letu la Kilombero kuna miradi mingi ya umwagiliaji; Mradi wa Kisawasawa, Mkula na Sanje inasuasua. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari kuambatana na mimi angalau weekend moja akajionee kusuasua kwa miradi hii ili Serikali ichukue hatua haraka za kuinusuru?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abubakar Asenga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, niko tayari kuongozana naye, tutakwenda kuangalia ili tuone namna ya kuweza kukamilisha miradi hii.
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Wakulima wa mpunga wa Wilaya ya Nkasi pamoja na Bonde la Ziwa Rukwa changamoto yao kubwa ni skimu za umwagiliaji pamoja na soko la uhakika. Nini mkakati wa Serikali kwa kuzingatia msimu wa safari hii mavuno sio mazuri sana ili wapate soko la uhakika?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Aida Khenani, Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, moja kati ya mikakati ambayo tumeiweka katika kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga ni kuzikamilisha skimu nyingi za umwagiliaji ambazo zinagusa maeneo aliyoyasema Mheshimiwa Mbunge. Bahati nzuri mimi mwenyewe nimekwenda kama kule Mwamapuli na maeneo mengine Kata ya Kilida kuangalia uwezekano pia kuongeza skimu hizi ili kuongeza tija katika zao letu la mpunga.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwondoe hofu na kwamba tumejipanga vyema ili kuongeza uzalishaji na ukiangalia mpunga hivi sasa ndiyo unatutangaza vizuri nje ya mipaka ya Tanzania na uzalishaji umeongezeka sana. Kwa hiyo katika maeneo ambayo tutawapa priority ni pamoja pia na skimu za umwagiliaji katika maeneo ambayo wanalima mpunga ikiwemo katika mkoa ambao Mheshimiwa Mbunge ameusema.
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa wananchi wa Mkoa wa Njombe wengi wao ni wakulima wa zao la chai. Nataka kuuliza wizara mmejipanga vipi kwa kushirikiana na Wizara ya TAMISEMI kuhakikisha kwamba mnaboresha miundombinu katika mashamba ya chai ili tuweze kupata chai nyingi zaidi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo napenda kujibu swali la Mheshimiwa Neema Mgaya Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Njombe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tuna changamoto katika baadhi ya maeneo ya uzalishaji kutokuwepo kwa miundombinu Rafiki lakini tunayo miradi ambayo tunaendelea kuitekeleza kupitia Agree connect ambayo pia imejihusisha na utengenezaji wa miundombinu. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutashirikiana na TAMISEMI kuhakikisha maeneo yote ya uzalishaji yanapitika kiurahisi ili tuweze kuimarisha na kukuza zao letu la chai katika Mkoa wa Njombe.

MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA: Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Je, Serikali ina mkakati gani wa kufanya kilimo cha zao la mpunga la umwagiliaji katika maeneo ya Malinyi, Ulanga, Mlimba, Kilombero na Kilosa kuwa endelevu badala ya kutegemea msimu wa mvua?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha soko kuu la mpunga katika Wilaya ya Kilombero?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Aleksia Asia Kamguna Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli ya kwamba tunatambua kilimo cha umwagiliaji ndio suluhu katika kuboresha na kuimarisha kilimo cha mpunga katika Mkoa wa Morogoro. Nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba katika bajeti hii inayokuja yako mabonde makubwa na miradi mingi ya umwagiliaji ambayo itatekelezwa katika Mkoa wa Morogoro ambao pia utagusa katika maeneo ambayo ameyataja.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili la kuhusu soko kuu ni wazo zuri, wazo jema tumelichukua na tutakwenda kuchakata ndani ya Serikali kuona uwezekano wake.
MHE. GHATI Z. CHOMETE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa nafasi, kama ilivyo katika zao la mpunga, kahawa aina ya Arabica inalimwa Mkoani Mara katika Wilaya ya Tarime na hasa Tarime Vijijini. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwawezesha wakulima wale ili waweze kuongeza uzalishaji katika zao hilo ili kuinua uchumi wao na uchumi wa nchi yetu.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, moja kati ya mikakati tuliyonayo na kukuza zao la kahawa mojawapo ni uzalishaji na usambazaji wa miche bora ya kuwafanya wakulima wengi waweze kuzalisha kwa tija.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka huu tumejipanga kuzalisha miche milioni 20 kuwafikia wakulima wengi kadri iweekanavyo na hivyo pia tutawagusa wakulima wa Mkoa wa Mara.

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa wananchi wa Jimbo la Hai wamehamasika sana kulima zao la kahawa na kwa kuwa tumepewa taarifa pale TaCRI miche ya kahawa imekwisha. Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha wananchi wa Jimbo la Hai msimu huu wanapata miche ya kahawa?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Hai, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika majibu ya swali la kahawa ambalo limeulizwa humu ndani, pamoja na changamoto aliyosema Mheshimiwa Mbunge, lakini tumeamua kuzishirikisha pia sekta binafsi ili tuwe tuna uhakika wa uzalishaji wa miche hii kwa maana ya TaCRI pamoja na sekta binafsi. Naomba nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba zoezi hilo linaendelea na usambazaji wa miche hii kama ambavyo Serikali imeahidi utafanyika na wakulimna watanufaika na miche hii.

MHE. ABBAS G. TARIMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Napenda niiulize Serikali, kwenye upande wa kuhamasisha na kuleta wawekezaji wakubwa katika ukulima mkubwa kwa maana ya large scale farming hasa katika ngano. Ni nini mtazamo wa Serikali katika zao hili? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abbas Tarimba, Mbunge wa Kinondoni, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha tunakuza kilimo cha nchi yetu ya Tanzania na ni ukweli ulio dhahiri kwamba ili kukuza kilimo chetu lazima tukubali kwamba dunia ya leo inahitaji uwekezaji mkubwa. Kwa sasa mlango uko wazi kwa ajili ya majadiliano na kuwakaribisha wawekezaji na Mheshimiwa Mbunge yeyote ambaye anaona kuna wawekezaji wanakuja kuwekeza nchini na kuna tija, tuko tayari kuwasikiliza na kuweza kuwasaidia ili jambo hili liweze kukamilika.

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, kwanza niishukuru Serikali kwa kutenga fedha kwa ajili ya kufanya usanifu kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Mheshimiwa Spika, swali langu la kwanza kwa kuwa ekari zilizoorodheshwa hapa kwenye jibu la msingi ni 120 lakini kuna eneo kubwa ambalo linazunguka Kijiji cha Ngonja, Arusha Chini na Arusha Juu.

Je, Serikali ipo tayari kujumuisha eneo hilo wakati wa kufanya usanifu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini swali langu la pili, je, Naibu Waziri yupo tayari kuambatana na mimi baada ya kuahirisha Bunge hili la Bajeti ili akajionee uhalisia wa Mradi huu? Nakushukuru.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, Mbunge wa Nanyamba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tupo tayari kutoa maelekezo kwa timu yetu ambayo itafanya usanifu kuhakikisha kwamba inaligusa eneo kubwa kadri iwezekanavyo, kwa sababu ni maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kwamba ifikapo mwaka 2025 tuwe tuna eneo ambalo linamwaagiliwa la hekta 1,200,000. Kwa kuongezeka kwa eneo ni sehemu ya tija ya uzalishaji kwetu pia, kwa hiyo wataalam wetu pia wataangalia eneo ambalo halijajumuishwa liweze kujumuishwa.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, niko tayari Bunge hili likifikia ukomo wake kwa maana ya vikao hivi vya Bajeti, kuongozana na Mheshimiwa Mbunge kwenda kuangalia uhalisia wa Mradi husika.
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Katika Mkoa wa Morogoro eneo la Chita kuna hekari 12,000 zenye miundombinu ya umwagiliaji ambapo sasa hivi zinamilikiwa na JKT, lakini kwa uwezo wao wameweza kulima ekari 2,500. Je, ni lini Serikali itawekeza nguvu yake pale ili kuweza kusaidia usalama wa chakula na kuongeza pato la Taifa? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Felista Njau kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika Fungu Namba 05 la Tume ya Umwagiliaji katika Randama ukiangalia Jedwali la Nne limeainisha moja kati ya miradi ambayo tutakwenda kuitekeleza katika mwaka ujao wa fedha ni mradi wa JKT – Chita. Kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge mradi upo katika mpango na utatekelezwa katika bajeti inayokuja.
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii ya swali dogo la nyongeza.

Kwa kuwa, skimu ya umwagiliaji wa Ilemba usanifu wa kina umekamilika kwa asilimia 100. Je, ni lini Serikali mtaanza ujenzi wa skimu hii ambayo ni muhimu sana kwa uchumi wa wananchi wa Kata ya Ilemba?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Deus Sangu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mradi ambao Mheshimiwa Mbunge ameusema upo katika utekelezaji wa mwaka wa fedha unaokuja, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba mradi huo utatekelezwa.

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Serikali kwa muda mrefu sana imeahidi kuhusu ujenzi wa bwawa kwenye Bonde la Mto Mkomazi. Je, ni lini ahadi hii sasa itaanza kutekelezwa rasmi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Timotheo Mnzava, Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli utekelezaji wa mradi wa Bonde la Mto Mkomazi umekuwa ni wa muda mrefu na Mheshimiwa Mbunge amekuwa akifuatilia sana, nataka nimhakikishie mbele ya Bunge lako Tukufu ya kwamba ifikapo mwezi wa Saba taratibu za awali za kumpata mshauri mwelekezi zitafanyika ili kazi ya usanifu na upembuzi yakinifu uanze na baada ya hapo tutaanza utekelezaji wa mradi huu mkubwa ambao wananchi wa Korogwe wanausubiri kwa hamu kwa sababu unagusa zaidi ya Kata 11 na una manufaa makubwa sana. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge tutaanza mwezi wa Saba mapema kabisa kumpata mshauri mwelekezi. (Makofi)
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kijiji cha Kidoka na Takwa wanayo miradi maarufu ya umwagiliaji lakini mpaka leo Serikali haijawekeza chochote. Naomba kujua commitment ya Serikali katika kuwekeza kwenye miradi ya vijiji hivyo, ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mohamed Monni Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikirudia mara nyingi kusema ya kwamba tumedhamiria kuyagusa maeneo mengi ambayo yanafaa kwa ajili ya umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa mazao katika nchi yetu ya Tanzania, hatua ambayo inafanyika hivi sasa ni kwamba timu yetu imeendelea kuyapitia maeneo yote kufahamu status ya kila maeneo ambayo yanafaa kwa ajili ya umwagiliaji. Katika eneo ambalo Mheshimiwa amelitaja la Kidoka mimi na yeye tutatafuta muda hapa katikati tutaongozana pamoja na wataalam kwenda kulitembelea na kuona uwezekano wa kufanya uwekezaji katika eneo hilo. (Makofi)
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona na kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Kwa kuwa, Serikali imeongeza kwa kiwango kikubwa bajeti ya umwagiliaji kutoka Shilingi Bilioni 46 mpaka Bilioni 361 na kwakuwa Wilaya yetu ya Bagamoyo tunayo skimu ya umwagiliaji - Ruvu inaitwa Chauru yenye wanachama zaidi ya 900 lakini inayo changamoto kubwa ya uchakavu wa miundombinu.

Je, Serikali inatoa ahadi gani kwa wanachama wa skimu hii ya umwagiliaji Chauru katika ukarabati wa miundombinu? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Subira Mgalu Mbunge, kama ifuatavyo.

Mheshimiwa Spika, mradi huo tunaufahamu na changamoto iliyopo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba katika miradi ambayo Tume imepanga kuifanyika kazi katika bajeti inayokuja mradi huo pia umeainishwa, kwa hiyo wakulima wa eneo hilo watapata nafasi ya kuweza kufaidika na uboreshaji wa miundombinu hasa baada ya kuanza utekelezaji kupitia bajeti inayokuja.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, niendelee kumshukuru sana Rais na nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakulima hawa wa tumbaku wamekuwa wakipangiwa uzalishaji na makampuni na mwisho wa siku wanachozalisha kinakuwa kidogo tofauti na matarajio yao na hasa wakulima hawa wadogo; na wanachozalisha cha ziada mwisho wa siku kinashindwa kununuliwa na mwisho wake kinaitwa jina la makinikia; nini kauli ya Serikali? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali langu la pili, kumekuwa na makato makubwa sana ya upandaji wa miti kwa wakulima hawa wa tumbaku. Fedha nyingi zinaishia kwa makampuni hayo na nyingine zinaishia benki na mkulima anaondoka bila fedha na mfano tu tosha mwaka jana wakulima hawa wa tumbaku wameweza kukatwa zaidi ya dola milioni tatu za miti ambapo ni zaidi ya bilioni sita. Nini kauli ya Serikali ili hao wakulima sasa tuwawekee mazingira mazuri waweze kuzalisha kwa wingi na weweze kupata faida kubwa na Serikali yetu iweze kupata fedha za kigeni? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Emmanuel Peter Cherehani, Mbunge wa Ushetu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye eneo la kwanza ni kweli imekuwepo hiyo changamoto na ndiyo maana Serikali tumeendelea kuhakikisha kwamba tunafungua milango kuwaleta nchini wawekezaji wengi zaidi ili kupata soko la uhakika la tumbaku yetu. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba Serikali itaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kwamba zao hili la tumbaku linapata soko la uhakika na wakulima mwisho wa siku tumbaku yao inanunuliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili la kuhusu makato, hii ni concern ambayo Mheshimiwa Mbunge amekuwa akiisema mara kwa mara na tumeshamuelekeza Mkurugenzi wa Bodi ya Tumbaku, kukaa na wadau wote kuona namna bora ya uendeshaji wa shughuli ya biashara ya tumbaku ili mkulima anufaike na kila ambacho anakilima shambani.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba jambo hili tunalichukua kwa umakini mkubwa na tunaendelea kulifanyia kazi ili mwisho wa siku mkulima aweze kunufaika na tumbaku yake.
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakulima wa Bulamata AMCOS wa eneo la Mishamo walilima tumbaku zao na kuwauzia Kampuni ya Naile Leaf Limited wanaidai kampuni hiyo dola za Kimarekani 600,000. Ni lini Serikali itawasaidia hawa wakulima wadogo ambao wamedhulumiwa haki zao za kimsingi na walipewa leseni na Serikali?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge Moshi Kakoso kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuna madai ya wakulima dhidi ya hii kampuni, Mheshimiwa Waziri aliwaita makampuni yote yanayodaiwa na akatoa mwongozo wa malipo; moja kati ya kazi ambayo Mkurugenzi wa Bodi anaendelea kuifuatilia ni kuhakikisha kwamba wakulima hao wanalipwa lakini pia tumewapa sharti kwamba hatuta-renew leseni yao mpaka pale watakapokamilisha malipo ya wakulima.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Wizara ya Kilimo tunahakikisha kwamba tunasimamia kwa dhati ili wakulima hawa waweze kulipwa na jambo hili lipo ndani ya meza ya Mheshimiwa Waziri, kazi inaendelea kuhakikisha kwamba malipo haya yanafanyika.
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, kwa kuwa kumekuwa na changamoto nyingi sana kwenye huu mfumo wa stakabadhi ghalani; je, nini mpango wa Serikali sasa kutoa elimu kwa wakulima wa choroko na dengu kabla ya mfumo haujaanza?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili, mfumo wa stakabadhi ghalani unahitaji uwepo wa warehouse (maghala); nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba wanaanzisha maghala katika halmashauri zote ambazo huu mfumo unakwenda kufanyakazi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO, Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Pius Chaya kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la kwanza la kuhusu elimu, Wizara tumejipanga kutoa mwongozo ambao ndani yake pia unajumuisha masuala ya elimu na masuala yote ya muhimu kabla ya kuingia katika Mfumo wa Stakabadhi za Ghala. Lengo letu ni kutatua changamoto ambazo zimekuwepo na hivyo kupitia mwongozo huu utakuwa umetibu tatizo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili kuhusu maghala, tunafahamu kwamba moja kati ya requirement kubwa ya stakabadhi za ghala lazima kuwepo na maghala. Katika bajeti yetu ambayo tumeisoma kupitia Wizara ni kwamba katika mwaka wa fedha unaokuja tunakwenda kujenga maghala mengi katika maeneo ya uzailishaji, lengo letu ni kuhakikisha kwamba nchi yetu inakuwa na maghala kuanzia katika ngazi za vijiji ambapo wanazalisha kwenda juu. Kwa hiyo katika eneo hilo, Serikali imeona imeona umuhimu na tumetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa maghala.
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, msimu wa kilimo cha mazao ya choroko pamoja na dengu wa mwaka 2021/2022 katika Mkoa wa Shinyanga wakulima wa dengu walipata changamoto kubwa ya kupatiwa fedha kwa wakati; na hii ni kutokana na mfumo mzima kutokuwa na maandalizi mazuri ya ulipaji wa fedha katika Vyama vya Msingi ambavyo vilinunua mazao haya kupitia Vyama hivyo vya Msingi; je, Serikali imejipanga vipi kuhakikisha kwamba fedha ziwe zinafika kwa wakati kupitia Vyama vya Msingi vilivyopo katika ngazi hiyo ya ushirika ili mradi kuondoa hata na changamoto hii ya wakulima wa dengu na choroko katika maeneo hayo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Butondo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika majibu yangu ya awali, kwa kutambua changamoto hizi tumeamua kuja na mwongozo maalum ambao utawajumuisha wadau wote. Lengo la mwisho ni kuhakikisha ya kwamba mkulima anafaidika na mazao yake na tunaondoa changamoto hasa za ucheleweshaji wa malipo. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba ndani mwongozo huu tutakwenda kutatua changamoto zote zilizopo katika mfumo wa stakabadhi za ghala.
MHE. SLYVIA F. SIGULA: Mheshimiwa Spika, kwanza ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Wizara na tunashukuru kwa kupata hizo shilingi bilioni mbili tunaishukuru sana Serikali, lakini nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kutokana na uhaba wa mafuta ulioko nchini na hamasa iliyofanywa na Mheshimiwa Waziri Mkuu wananchi wa Kigoma wamehamasika sana katika kuingia kwenye zao la michikichi lakini kumekuwa na uhaba wa upatikanaji wa miche ya michikichi inafikia hatua mche mmoja unauzwa hadi shilingi 5,000.

Je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kutoa ruzuku ya miche ya michikichi katika vyama hivi vya ushirika?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Slyvia Francis Sigula, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni maelekezo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ya kwamba tutoe miche bora ya michikichi kwa wakulima wa Mkoa wa Kigoma ili kuongeza uzalishaji na ninavyozungumza ni kwamba zoezi hili linaendelea katika Kambi ya JKT Bulombola, lakini vilevile pamoja na Gereza la Kitwanga ambapo jumla ya mbegu zilizozalishwa mpaka hivi sasa ni milioni tisa na miche iliyopo kwenye viriba ambayo bado kugaiwa milioni moja, lakini kwa wananchi tumeshagawa miche 970,000 ikiwa ni elekezo la Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Spika, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge haya ni maelekezo ya wananchi hawa watapatiwa miche hii bure, isipokuwa tu kwa sharti la kwamba lazima wawe katika mashamba makubwa ili tuweze kui-trace miche hii na kuona inaleta tija katika nchi yetu.
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kuuliza swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa zao la michikichi limekuwa likifanya vizuri katika mikoa ya Kigoma, Rukwa pamoja na Katavi lakini pia hata kule Kyela inafanya vizuri sana.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba miche bora inagawiwa katika mikoa yote hiyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Josephat Kandege, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli katika mikoa aliyoitaja na yenyewe ikolojia inakubali kuzalisha michikichi na mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kwamba tunaongeza uzalishaji wa miche ili kuweza kufikia maeneo haya yote na nichukue fursa hii pia kutoa rai kwa Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa katika mikoa ambao umeitaja kutenga maeneo makubwa ya mashamba makubwa tumeanza kuwaleta wawekezaji wakubwa kwenye mchikichi. Kwa hiyo, nitoe rai kwa wakuu wa mikoa kuhakikisha kwamba wanakuwa na maeneo ya kutosha ili wakija wawekezaji hao wawe na maeneo ya kuwapeleka na naamini kabisa kwa mkakati tulionao tutakwenda kutatua changamoto hii ya upungufu wa mafuta ya kula hapa nchini.
MHE. SAASHISA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuniona; kwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo wa wakati huo Mheshimiwa Bashe alifanya kikao Mkoa wa Kilimanjaro na akatoa maelekezo kwamba Vyama vya Ushirika vya Wilaya ya Hai badala ya kubaki na zao la kahawa peke yake viingie na mazao mengine ya mbogamboga na mazao ya biashara kama vile mgomba, vanilla na mazao mengine.

Je, ni lini Serikali itapeleka waraka maalum wa kuonyesha mfumo wa uendeshaji vyama hivi vya ushirika ili kuweza kuchukua mazao hayo yote kwa Warajis Wasaidizi na Kata zile za Boma Ng’ombe, Bondeni, Mnadani, Weruweru ziweze kunufaika na vyama hivi vya ushirika? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Saashisa Mafuwe, Mbunge wa Hai kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli Mheshimiwa Waziri wa Kilimo Hussein Mohamed Bashe alitoa kauli hiyo ndani na inatekelezwa na mimi niirudie tena kwa msisitizo na kuwataka Warajis Wasaidizi wote kuhakikisha jambo hili linatekelezeka la kwamba Vyama vya Ushirika vinaruhusiwa kusimamia zao zaidi ya moja katika maeneo yao ili kuondoa multiplicity ya vyama vingi katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kuhusu waraka Tume inafanyia kazi jambo hilo ili kutoa maelekezo mahsusi ambayo itawafanya Warajis Wasaidizi wote waweze kuyasimamia maelekezo hayo.
MHE. HAMIDA M. ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza nishukuru kwa majibu ya Serikali, lakini ningependa kujua katika eneo la Ngongo, sisi Manispaa tulishatoa hekari 120; nini msukumo wa Serikali kuhakikisha kwamba fedha zinapatikana na kuwawezesha Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuja kujenga Chuo cha Kilimo campus ya Lindi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hamida Mohamed Abdalaah Mbunge wa Lindi Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nachukuwa fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge amekuwa akilifuatilia sana jambo hili na hii si mara ya kwanza kuliulizia. Sisi kama Wizara ya Kilimo tumefanya mawasiliano na wenzetu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia jambo hili limeshaanza na ndani ya muda mfupi ujao wataendelea na taratibu za kuhakikisha kwamba mchakato huu unakamilika, ili ujenzi uanze mara moja.

Kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba Serikali inafanya kazi kwa pamoja na wenzetu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia chini ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam wako tayari kuendelea na mchakato huu na hatua zimefikia sehemu nzuri.
MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti nashukuru kwa kuniona na kunipa nafasi.

Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha nia ya kuimarisha na kuboresha kilimo na kiasi kwamba tumeongeza bajeti yetu ya kilimo; je, Serikali iko tayari kwa kushirikiana na Vyuo vya Kilimo kutusaidia sisi wananchi huko vijijini kwa kutuletea wale wanafunzi ambao wanakuwa kwenye mafunzo ya vitendo ili waje kushirikiana na wananchi katika kuimarisha nakuboresha kilimo?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Cosato Chumi, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa na programu hiyo ya kuwahusisha wale vijana ambao wako chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia programu ya uhanagenzi na tutaendelea kuifanya hivyo kuhakikisha kwamba wanafikia maeneo mengi zaidi lengo hapa ni kuhakikisha kwamba wanawafikia wakulima wengi zaidi, na wakulima wanapata elimu ya kilimo bora ili kuongeza tija na kufikia malengo ambayo tumejiwekea ya kukuza Sekta ya Kilimo kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.
MHE. KHADIJA HASSAN ABOUD: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kwanza naipongeza Serikali katika kuhamasisha kilimo na huduma za ugani suala langu Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imenunua pikipiki kwa ajili ya Maafisa Ugani, lakini bado pikipiki hayo hayajagawiwa ili kuepusha uchakavu, ni lini Serikali itayagawa pikipiki hizo kwa walengwa ili yakafanya kazi kwa wakulima? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Khadija Hassan Aboud kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli bajeti ya Wizara ya Kilimo na hasa katika eneo la huduma za ugani, imeongezeka kutoka shilingi milioni 600 mpaka shilingi bilioni 15 kwa ndani ya miaka miwili kazi kubwa ambayo Mheshimiwa Rais ameifanya na ndani ya bajeti hiyo pia na sisi tulinunua vifaa kwa maana ya pikipiki, kwa ajili ya kuwapatia Maafisa Ugani.

Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba zilikuwepo na taratibu za ndani za kuzifuata ambazo zimekamilika na kuanzia jana zoezi la usambazaji pikipiki limeanza, jana Mkoa wa Dodoma wamechukuwa pikipiki 264, leo Singida watachukuwa 161 na kesho kutwa Tabora na maeneo mengine wataendelea kuzichukuwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge nikuondoe hofu pikipiki zile ndani ya muda mrefu zitaondoka eneo hilo ili ziweze kuwafikia Maafisa Ugani.
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kuwa Kanda ya Kati hususani Mkoa wa Singida na Dodoma ni miongoni mwa mikoa ambayo ni ya kimkakati hususani kwenye zao la alizeti ukiwemo mkoa wa kwako Mheshimiwa Naibu Waziri.

Je, Serikali haioni haja ya kuhakikisha kwamba sasa tunapata Chuo cha Kilimo kwenye Kanda ya Kati kuhakikisha kwamba fedha zinazotengwa na Serikali zinakuwa na tija?
NAIBU WAZIRI KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Nusrat Hanje, Mbunge wa Viti Maaalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Vyuo vyetu vya kilimo vimegawanya katika kanda na Kanda ya Kati pia yenyewe inapata huduma kupitia vyuo hivi, lakini sambamba na hizo tunazo taasisi mbalimbali ambazo zinafanya kazi katika Mkoa wetu wa Dodoma pamoja na Singida ambazo lengo lake kuu ni kuhakikisha kwamba tunawajengea uwezo wakulima wetu kulima kilimo cha alizeti kwa tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba tumezingatia sana ikolojia ya Dodoma na Singida na tumeweka nguvu ya kutosha kuhakikisha wakulima wetu wanapata elimu ya kutosha juu ya kilimo cha alizeti na mwisho wa siku tuondoe tatizo la upungufu wa mafuta ambalo tunalo hapa nchini.
MHE. KENNETH E. NOLLO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali hususani kwanza kufanya upembuzi yakinifu na baadaye utekelezaji wa bajeti 2023/2024.

Swali langu nilitaka niulize Serikali Mkoa wa Dodoma umekuwa unapata mvua kidogo, lakini pamoja na mvua kidogo tumekuwa na maji mengi ambayo yanapotea; je, nini ni mkakati mahususi hasa katika kuongeza mabwawa haya ya skimu hizi za umwagiliaji kutoka kwa Serikali ukoje? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kenneth Ernest Nollo, Mbunge wa Bahi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge hii imekuwa ni hoja yake na ameisema sana hapa Bungeni na sisi Wizara ya Kilimo kwenye bajeti inayokuja tulizingatia hilo. Tuna ujenzi wa mabwawa makubwa mawili katika Wilaya ya Chamwino eneo la Membe na Msagali Mpwapwa, kama sehemu ya kuanzia katika kuhakikisha kwamba tunakuwa na-reserve kubwa ya maji ili tuweze kufanya kilimo cha umwagiliaji. (Makofi)
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa nafasi, Skimu ya Umwagiliaji ya Kitua Nimwezayo Kongriti iliyoko katika Kata ya Lunguza imeshatengenezewa usambazaji wa maji kutoka kwenye banio hadi kwenye mashamba katika hatua ya awali.

Ni lini hatua ya pili ya kutoa maji kwenye mifereji kuyaingiza kwenye mashamba itaanza?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Rashid Shangazi, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua ya kwanza tuliyoifanya ilikuwa ni kurudisha njia za asili za Mto Umba ambao kazi hiyo imekamilika. Hatua ya pili itakuwa ni kufanya tathmini ya gharama halisi za ukarabati wa mifereji ili tupeleke maji hayo shambani. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba hatua ya pili itafanyika ili maji hayo yaweze kufika shambani. (Makofi)
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Kwanza nishukuru sana Mheshimiwa Rais kutupatia shilingi 711,000,000 kwa Skimu ya Magisa, lakini skimu ile sasa inakwenda kuharibika kwa sababu ya uchakavu na uliniahidi kwamba utakuja kufanya ukarabati.

Je, ni lini utatekeleza ahadi ya Serikali ya kufanya ukarabati kwenye Skimu ya Magisa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Flatei Massay, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli skimu hii inahitaji ukarabati hasa baada ya kuwa tulituma timu yetu ambayo imepitia miradi yote na katika bajeti inayokuja, tumepanga miradi ya ukarabati natumai pia mradi huu ambao Mheshimiwa Mbunge ameusema utakuwemo katika kazi hiyo. (Makofi)

MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi na mimi niweze kumuuliza Mheshimiwa Waziri swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Skimu ya Umwagiliaji ya Chinangali ni kati ya skimu kubwa na kongwe katika Mkoa wa Dodoma na skimu hii Serikali tayari mlikuwa mmeshaanza suala zima la ukarabati ili wakulima wale waweze kupata maji kwa ajili ya kukidhi kilimo chao.

Je, ni lini sasa Serikali mtaanza rasmi na kukamilisha ukarabati wa skimu ile, ili wakulima wetu wa zabibu waweze kupata tija katika kilimo chao cha zabibu mkoani hapa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kunti Majala, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Skimu ya Chinangali ni kati ya skimu kubwa ambazo zinazalisha sana zao la zabibu na Serikali kupitia TARI na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji tuliamua kwa dhati kabisa kuifufua skimu hiyo na hivi sasa ninavyozungumza kazi inaendelea na tunategemea mwaka wa fedha ujao kwa maana ya tarehe 1 Julai kazi zitaendelea kukamilisha skimu hii kubwa ili mwisho wa siku wakulima wa zabibu wa Dodoma waweze kuzalisha kwa tija na kwa malengo ambayo tumejiwekea kukuza zao hili la zabibu Mkoani Dodoma. (Makofi)

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii; kwenye Jimbo langu la Korogwe Mjini tuna skimu kubwa mbili za umwagiliaji Bonde la Mahenge Nagoo lakini pamoja na Bonde la kwa Mngumi. Mwaka huu Serikali ilituahidi itatupatia shilingi milioni 600 kwa ajili ya ukarabati wa Bonde la Mahenge pamoja na Nagoo, lakini mpaka muda huu ninavyoongea hatujapata hata shilingi moja kwa ajili ya ukarabati huo.

Je, Serikali inawaambia nini wananchi wa Korogwe Mjini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Alfred Kimea, Mbunge wa Korogwe Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, sababu za kwa nini fedha hazijafika mpaka hivi sasa ni kwamba skimu hizo mbili alizozisema zinategemea sana Bonde la Bwawa Mkomazi. Kilichofanyika hivi sasa ni kwamba tumeamua tuanze na zoezi kubwa la upembuzi yakinifu na usanifu wa Bonde la Mkomazi kwanza ili baadaye tuweze kuzifikia hizo skimu mbili. Nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tarehe za mwanzo kabisa za mwezi wa saba consultant atapatikana kwa ajili ya Bonde hilo la Mkomazi na baadaye kazi hiyo ikikamilika tutaendelea na hizo skimu mbili ambazo amezitaja kwa Mkumbo na ile nyingine. (Makofi)
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa. Skimu ya Umwagiliaji ya Naming’ong’o iliyoko kwenye makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Momba, Chitete ndio skimu ambayo tunaitegemea sana katika kuhakikisha wakulima wetu wanaweza kulima kwa ufasaha.

Je, ni lini Serikali itafanya maboresho ya skimu hii ya Naming’ong’o ili iweze kuleta tija ukizingatia mwaka huu hakukuwa na mvua na wakulima wengi wamekausha sana mpunga?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Condester, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, moja kati ya kazi kubwa ambayo tumeipa Tume ya Taifa Umwagiliaji ni kuhakikisha inazipitia skimu zote nchini Tanzania ili kufahamu status yake, kujau ipi inahitaji marekebisho na ipi ifanyike nini iweze kuboreshwa. Nimwahidi Mheshimiwa Mbunge na skimu aliyoitamka tumeweka katika mipango yetu kwa ajili ya utekelezaji ndani ya Serikali.
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa na mimi nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Skimu ya umwagiliaji ambayo inaendeshwa na umoja wa umwagiliaji katika Kata ya Magoeko katika Jimbo la Tabora Mjini ilitengewa fedha mwaka 2022/2023; fedha hizo sasa zimehamishiwa kwenda wilaya nyingine ya Uyui na Mheshimiwa Waziri nilishakukabidhi malalamiko hayo. Sijui Serikali inasemaje kuhusu wanakijiji hao ambao tayari wameshachanganyikiwa kwa sasa hivi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mwakasaka, Mbunge wa Tabora Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Mheshimiwa Mbunge amewasilisha jambo hili mezani na kwa sababu amelileta wiki iliyopita tu Alhamisi, naomba anipe muda, tutakaa mimi na yeye pamoja na tume ili tutafute ufumbuzi wa kudumu na mwisho wa siku tuweze kuwahudumia wananchi wote wa Mkoa wa Tabora.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, kwanza nichukue nafasi hii kuipongeza sana Serikali, Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri wa Kilimo na Naibu wake pamoja na watendaji wa Wizara ya Umwagiliaji. Kwanza nichukue nafasi hii pia kumwomba Mheshimiwa Waziri je, ni lini atafanya ziara katika eneo hilo la skimu ya umwagiliaji?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zacharia Paul Issaay, Mbunge wa Mbulu Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, tunashukuru kwa shukrani na pongezi. Nimuahidi tu baada ya Bunge la Bajeti tutakwenda pamoja kuangalia mradi huo.
MHE. DKT. DAVID M. DAVID: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. La kwanza; ningemuomba Mheshimiwa Waziri pengine baada ya Bunge tuweze kutembelea katika skimu hizi ili tuweze kuziona zile ambazo kwa kweli ndizo zinazotakiwa zitengewe fedha kwa ajili ya upembuzi yakinifu.

Mheshimiwa Spika, la pili, katika Kata ya Makanya kuna korongo ambalo wakati mvua inanyesha ndilo linategemewa sana katika umwagiliaji. Ningeomba Serikali, hasa Waziri tuweze kutembelea naye pamoja ili aweze kuliona hilo Korongo ili na lenyewe liwekwe katika mpango wa kufanyiwa upembuzi yakinifu ili wananchi wa Makanya waweze kupata chakula kwa mwaka mzima. Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, Dkt. David Mathayo David, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nipo tayari kuongozana na Mheshimiwa Mbunge kwenda kutembelea skimu hizo kuziangalia na ukarabati ambao unahitajika. Vilevile kwa sababu nia yetu ni kuhakikisha hatupotezi maji, Kata ya Makanya kwenye eneo ambapo kuna korongo kubwa ambalo linatuamisha maji tutakwenda pia kuona. Lengo letu ni kuyatumia maji ipasavyo kwa ajili ya kilimo cha nchi yetu.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona. Mto wa Motale unahudumia Kata ya Masama Magharibi na Masama Kati na ni skimu kubwa sana inayotegemewa ndani ya Jimbo la Hai. Je, ni lini Serikali itafanya ukarabati wa skimu hii ikizingatiwa sasa hivi ndani ya Jimbo la Hai kuna changamoto kubwa ya ukosefu wa mahindi? Kwa hivyo, mto huu unaweza kutumika kuweza kufanya kilimo cha umwagiliaji. Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Hai, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli tunafahamu umuhimu wa Mto Motale katika kuhakikisha kwamba wakulima wa Wilaya ya Hai wanafanya kilimo cha umwagiliaji. Jambo alilolisema la ukarabati, namwahidi Mbunge kwamba mimi, yeye na watalaam wetu tutaongozana kwa ajili ya kwenda kuangalia eneo husika. Baadaye baada ya kushauriwa vyema, basi tunaona namna ya kuingiza katika mpango wa Serikali ili wananchi wa Hai waweze kunufaika na kilimo cha umwagiliaji. (Makofi)
MHE. VITA RASHID KAWAWA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali la nyongeza. Naomba kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba, ni lini watakamilisha Mradi wa Umwagiliaji wa Bonde la Liuni ambao ulianzishwa muda mrefu lakini haujakamilika Likonde na kufanya ukarabati katika kilimo cha umwagiliaji Kijiji cha Nambecha?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Vita Kawawa, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyatamka ni maeneo ambayo yapo katika mkakati wa Wizara kuhakikisha tunawezesha wakulima wa eneo hilo kulima kupitia kilimo cha umwagiliaji. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutatuma wataalam wetu kwenda kuyaangalia maeneo hayo ili baadaye tuingie katika mpango wetu wa Serikali kuhakikisha kwamba tunakarabati skimu hizo.

MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mradi wa Chela ni mradi wa muda mrefu sana. Swali langu, je, ni lini sasa Serikali itakwenda kuweka fedha za ukarabati wa Mradi wa Umwagiliaji wa Chela pia na kukarabati mitaro ile na miundombinu kwa ujumla?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Iddi Kassim, Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hili naomba niliseme katika Bunge letu Tukufu kwamba, kwa kutambua kuna umuhimu mkubwa sana wa ukarabati wa miradi mbalimbali ya umwagiliaji; Wizara tumeiagiza Tume ya Maendeleo ya Umwagiliaji kuhakikisha inaipitia miradi yote nchi nzima kwa ajili ya kufanya tathmini na kujua status zake, tujue ipi inahitaji ukarabati mkubwa, ipi inahitaji ukarabati mdogo, ipi inatakiwa tuanze upya, lengo letu ni kuhakikisha miradi hii inafanya kazi.

Mheshimiwa Spika, kwa Mheshimiwa Mbunge nimwaahidi tu kwamba, katika hayo ambayo ameyasema pia tutaingiza katika mpango wetu ili tuhakikishe kwamba wananchi wake wananufaika na kilimo cha umwagiliaji.
MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali langu la kwanza; ni vituo vingapi vya rasilimali za kilimo vilikwishabadilishwa matumizi katika Serikali za Mitaa na kwa maagizo sasa ya Waziri ni vingapi sasa vimerudishwa ili kuendelea na matumizi yake ya kawaida?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; Serikali ina mpango gani sasa kuwateua waratibu watakaoratibu mafunzo katika Vituo hivyo vya Rasilimali za Kilimo ili kuratibu mafunzo kwa wakulima na wafugaji na kwamba vitengewe bajeti kidogo ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Yustina Arcadius Rahhi, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, ni kweli nahitaji takwimu, nitaomba nimpatie Mheshimiwa Mbunge takwimu sahihi baada ya kuwa nimejiridhisha ni vituo vingapi ambavyo vimebadilishwa matumizi. Hata hivyo, tayari tumeshawaandikia wahusika kwa maana ya kurudisha vituo hivi kurudi katika matumizi yake ya awali kwa ajili ya kuwa ni sehemu ya rasilimali za kilimo. Kwa hiyo, baadaye nitampatia taarifa sahihi Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Spika, la pili la kuhusu uteuzi wa Waratibu, tunapokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge, tutalifanyia kazi ili kuwepo na waratibu katika vituo hivi na lengo kubwa ni kuhakikisha kwamba tunatoa elimu ambayo itamfikia mkulima kwa wakati.
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Pale Jimboni Kibaha kwenye Kitongoji cha Disunyala kipo Kituo cha Rasilimali za Kilimo kilichoanza kujengwa tangu mwaka 2007 na mpaka leo hakijakamilika kujengwa. Je, nini mpango wa Serikali kumalizia kituo kile?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Michael Mwakamo, Mbunge, kama ifutavyo: -

Mheshimiwa Spika, jambo hili Mheshimiwa Mbunge alishalileta ofisini, tumezungumza na tulimpa ahadi ya kwamba lengo letu ni kuhakikisha kwamba tunakamilisha Vituo vyote vya Rasilimali za Kilimo vipo katika Kata ili mwisho wa siku tuweze kuwafikia wakulima kwa ukaribu. Katika baadhi ya maeneo tumelenga kuvifanya vituo hivi kuwa ni mechanization center ambayo itasaidia wakulima kwenda kukopa au kukodisha vifaa vya kilimo kupitia centers hizo. Kwa hiyo, nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba, pale kwake pia tutakamilisha ili mwisho wa siku malengo yaliyokusudiwa yaweze kutimia.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kata ya KIA kumekuwa na viashiria vinavyoonesha kwamba, kuna Madini ya Tanzanite green na madini mengine na ikizingatiwa tuko ukanda mmoja na Arusha ambapo yanapatikana madini haya ya Tanzanite. Sasa ni lini, Serikali itafanya utafiti mahsusi kwenye madini ya aina hii ili tuweze kujiridhisha kama kweli yapo na tuweze kuyazalisha? (Makofi)

Swali langu la pili, kwa kuwa Serikali imebaini kwenye Kata ya Masama Rundugai kuna madini aina ya chokaa; je, Serikali ipo tayari kubainisha umahsusi wa eneo linalopatikana chokaa hiyo na kututafutia mwekezaji aanze kuvuna madini haya?
WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na swali la kwanza la kuhusu utafiti. Tunao mpango kiongozi wa kuhakikisha tunalifanyia utafiti wa kina eneo kubwa zaidi la nchi yetu ya Tanzania na tumeligawa katika blocks sita kubwa, ikiwemo block ambayo inahusisha eneo la Mererani pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro ikiwemo Wilaya ya Hai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba, katika utafiti huu tutagusa eneo kubwa na kwa kuanzia mwaka huu wa fedha, tunaanza majaribio kupitia ndege nyuki katika eneo la Mererani, ili kuweza kubaini uwepo wa madini ambapo itakuwa imetapakaa katika maeneo ya Wilaya ya Hai. Hivyo taarifa za awali pia zitakuwa ni sehemu ya kuongoza wananchi wa Wilaya ya Hai katika eneo hili la uchimbaji wa madini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili, kama Serikali ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, tunawapatia maeneo wachimbaji, tuko tayari kuwaongoza kwa ajili ya upatikanaji wa leseni ili wananchi wa Hai waanze kuchimba madini haya ya chokaa.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa, Mheshimiwa Naibu Waziri alipotembelea Machimbo ya Nyakabangala katika Jimbo la Isimani, aliwaahidi kuwaleta watafiti na kuwapatia vifaa ili wananchi waweze kuchimba kwa uhakika zaidi.

Je, ni lini sasa ile ahadi itatimia? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli, hivi sasa tumeanza kuwatawanya sana wataalam wetu kupita maeneo tofauti tofauti ya nchi, na lengo letu ni kuhakikisha kwamba tunawaongoza wachimbaji waweze kuchimba katika kanuni na taratibu za kisheria pasipo kubahatisha. Kwa hivi sasa tumeanza kusambaza pia mitambo yetu ya uchorongaji ambayo itawasaidia wachimbaji wadogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kanda ya Mikoa ya Iringa, Njombe pamoja na Mkoa wa Mbeya tayari tuna mtambo ambao uko kule. Tutatoa maelekezo kwamba uwafikie pia na wachimbaji wa eneo hilo ambalo Mheshimiwa Mbunge amelisema ili nao waweze kupata huduma. (Makofi)
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ni lini Serikali itawapa wachimbaji wadogo eneo namba moja, Kata ya Mang’onyi, Jimbo la Singida Mashariki, ambao wameondolewa tangu mwaka 2015?
NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo ambalo amelitaja Mheshimiwa Mbunge, nitakwenda kufanya ziara eneo hilo kwa sababu nina ziara katika eneo hilo. Pia, moja kati ya jukumu langu kubwa ni kwenda kuzungumza nao na hasa katika kuhakikisha kwamba tunaendelea kuwapatia maeneo wachimbaji wadogo kwa sababu, haya ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba nitafika mwenyewe katika maeneo hayo na kuona namna ya kuweza kutoa utaratibu mzuri kama ambavyo tumefanya katika Mlima wa Sekenke na maeneo mengine ya Sekenke ambayo tulitoa leseni kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kata ya KIA kumekuwa na viashiria vinavyoonesha kwamba, kuna Madini ya Tanzanite green na madini mengine na ikizingatiwa tuko ukanda mmoja na Arusha ambapo yanapatikana madini haya ya Tanzanite. Sasa ni lini, Serikali itafanya utafiti mahsusi kwenye madini ya aina hii ili tuweze kujiridhisha kama kweli yapo na tuweze kuyazalisha? (Makofi)

Swali langu la pili, kwa kuwa Serikali imebaini kwenye Kata ya Masama Rundugai kuna madini aina ya chokaa; je, Serikali ipo tayari kubainisha umahsusi wa eneo linalopatikana chokaa hiyo na kututafutia mwekezaji aanze kuvuna madini haya?
WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na swali la kwanza la kuhusu utafiti. Tunao mpango kiongozi wa kuhakikisha tunalifanyia utafiti wa kina eneo kubwa zaidi la nchi yetu ya Tanzania na tumeligawa katika blocks sita kubwa, ikiwemo block ambayo inahusisha eneo la Mererani pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro ikiwemo Wilaya ya Hai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba, katika utafiti huu tutagusa eneo kubwa na kwa kuanzia mwaka huu wa fedha, tunaanza majaribio kupitia ndege nyuki katika eneo la Mererani, ili kuweza kubaini uwepo wa madini ambapo itakuwa imetapakaa katika maeneo ya Wilaya ya Hai. Hivyo taarifa za awali pia zitakuwa ni sehemu ya kuongoza wananchi wa Wilaya ya Hai katika eneo hili la uchimbaji wa madini.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa, Mheshimiwa Naibu Waziri alipotembelea Machimbo ya Nyakabangala katika Jimbo la Isimani, aliwaahidi kuwaleta watafiti na kuwapatia vifaa ili wananchi waweze kuchimba kwa uhakika zaidi.

Je, ni lini sasa ile ahadi itatimia? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli, hivi sasa tumeanza kuwatawanya sana wataalam wetu kupita maeneo tofauti tofauti ya nchi, na lengo letu ni kuhakikisha kwamba tunawaongoza wachimbaji waweze kuchimba katika kanuni na taratibu za kisheria pasipo kubahatisha. Kwa hivi sasa tumeanza kusambaza pia mitambo yetu ya uchorongaji ambayo itawasaidia wachimbaji wadogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kanda ya Mikoa ya Iringa, Njombe pamoja na Mkoa wa Mbeya tayari tuna mtambo ambao uko kule. Tutatoa maelekezo kwamba uwafikie pia na wachimbaji wa eneo hilo ambalo Mheshimiwa Mbunge amelisema ili nao waweze kupata huduma. (Makofi)
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ni lini Serikali itawapa wachimbaji wadogo eneo namba moja, Kata ya Mang’onyi, Jimbo la Singida Mashariki, ambao wameondolewa tangu mwaka 2015?
NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo ambalo amelitaja Mheshimiwa Mbunge, nitakwenda kufanya ziara eneo hilo kwa sababu nina ziara katika eneo hilo. Pia, moja kati ya jukumu langu kubwa ni kwenda kuzungumza nao na hasa katika kuhakikisha kwamba tunaendelea kuwapatia maeneo wachimbaji wadogo kwa sababu, haya ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge ya kwamba nitafika mwenyewe katika maeneo hayo na kuona namna ya kuweza kutoa utaratibu mzuri kama ambavyo tumefanya katika Mlima wa Sekenke na maeneo mengine ya Sekenke ambayo tulitoa leseni kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nina swali la nyongeza; kwa kuwa Bwawa la Kalemawe lililopo Jimbo la Same Mashariki lililojengwa na wakoloni mwaka 1958/1959 limejaa tope sana na hili lilikuwa linasaidia sana wakulima wa kata ya Kalemawe, Kihurio na Bendera. Je, Serikali ina mpango gani kusaidia kutoa tope hilo ili ikusanye maji ya kuweza kusaidia kwenye kilimo cha umwagiliaji?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Naghenjwa Livingstone Kaboyoka, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaelekeza timu ya wataalam waende kuangalia eneo hilo ili wapate tathmini halisi na baadaye waweze kufanya utekelezaji katika eneo hilo.
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali la nyongeza.

Katika Jimbo la Manyoni Mashariki tuna Bwawa la Mbwasa ambalo tayari upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ulishafanyika. Je, nini kauli ya Serikali kuhusu lini itaanza ujenzi wa bwawa hilo? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Pius Chaya, Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bwawa la Mbwasa liliwekwa katika mpango kupitia Benki ya BADEA na hivi sasa tunajiandaa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa lenyewe, lakini vile vile na skimu za umwagiliaji katika bajeti ya fedha ya mwaka 2023/2024.
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Pamoja na ahadi ya Mheshimiwa Waziri kutembelea Jimbo la Kalenga ambalo najua Waziri ataifanya, lakini napenda kujua ni lini sasa atatupa fedha za haraka angalau turekebishe Bwawa la Wellu katika Kata ya Ruanda ili lisaidie wananchi pale katika kilimo cha umwagiliaji?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kiswaga, Mbunge wa Kalenga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamuahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaelekeza timu ya wataalam kufika katika eneo husika, mimi mwenyewe pia nitafika, ili tuone hali halisi na tuone namna ya kuweza kuwakwamua wananchi katika eneo hilo kwa sababu tumejipanga kuhakikisha kwamba sekta hii ya umwagiliaji inachukua hasa kipaumbele katika bajeti yetu inayokuja. Kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, mimi mwenyewe nitafika na wataalam watafika kuoa namna ya kuweza kuwa-rescue wananchi katika eneo hilo.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Jimbo la Ndanda tuna skimu mbili za umwagiliaji ambazo ni Mkwera, Kata ya Nanganga pamoja na Skimu ya Ndanda, skimu hizi ziko kama zimekuwa abandoned, sasa nimuombe Mheshimiwa Waziri, kwa sababu ya uwekezaji mkubwa ambao ulifanyika pale, nini malengo ya Serikali na skimu hizi mbili ili ziweze kufanya kazi iliyokusudiwa vizuri?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Cecil Mwambe, Mbunge wa Ndanda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja kati ya kazi kubwa ambayo tumeipa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ni kuhakikisha inapitia miradi yote ya umwagiliaji nchini Tanzania kwa maana ya kufahamu status zake, tujue ipi inafanya kazi, ipi imekwama na ipi inahitaji namna gani iweze kutoka hapo ilipo iendelee kufanya kazi. Kwa hiyo, nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba siyo dhamira yetu kuiacha na kui-abandon miradi hiyo mikubwa ya umwagiliaji, tutaifanyia kazi kuhakikisha kwamba inafanya kazi ili tutimize lengo la kuwa na eneo kubwa la umwagiliaji hapa nchini.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bwawa la Bolutu lililopo Kata ya Masama Magharibi lilifanyiwa tathmini na kugunduliwa lina maji mengi sana, lakini Bwawa la Kikafuchini kwa Tito na lenyewe lina maji ya kutosha.

Je, Serikali ni lini itajenga mabwawa haya ili yaweze kuwasaidia wananchi wa Jimbo la Hai?
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Hai, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepokea rai ya Mheshimiwa Mbunge, tutajielekeza katika eneo hilo sisi na wataalam wetu kuona namna ambavyo tunaweza tukayafanya mabwawa hayo yatumike kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na wananchi waweze kunufaika. Kwa hiyo, nimuondoe hofu Mheshimiwa Mbunge, maelekezo yangu ni kwamba mtaalam wetu wa pale Mkoa wa Kilimanjaro atafika kwa ajili ya kuangalia na kufanya tathmini na baadae tufanye utekelezaji.
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kujua baada ya utafiti huo wa awali kuna muendelezo gani katika ugunduzi huo wa madini?

Swali langu la pili, ni kwa kiasi gani wananchi wa Mkoa wa Mtwara wanafahamu maeneo hayo yenye madini ili waweze kuitumia fursa hiyo kujipatia kipato? Nakushukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa hatua zinazochukuliwa baada ya madini kutambulika maeneo yenye madini hayo, Afisa Madini ya Mkoa anao wajibu wa kupeleka taarifa hizo kwa Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya, aidha kupitia machapisho ambayo GST wanaandaa. Mwaka huu mwezi wa Tano waliandaa kitabu cha madini yapatikanayo katika Wilaya zote za Tanzania, wananchi hufikishiwa taarifa pia kupitia mafunzo mbalimbali ambayo Wizara inatoa na kupitia utaratibu huo wananchi wengi wamejitokeza kwenda kukata leseni za utafiti na uchimbaji wa madini yaliyobainika katika hayo maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa swali lake la pili kwamba wanayafahamu maeneo hayo? Jibu ni ndiyo kwa sababu ya taarifa ambazo Wizara inasambaza kupitia GST na taasisi zingine za Wizara na ndiyo maana sasa hivi madini ya graphite yameanza kuchimbwa na wachimbaji wadogo ambao wamepata leseni na wanaendelea na utafiti.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha katika maeneo yenye dhahabu kama Nanyumbu na Masasi wachimbaji wadogo wameendelea kufaidika na Wizara sasa hivi iko katika mchakato wa kufanya utafiti wa kina zaidi ili wajue kiasi na aina ya madini na ubora wa madini yanayopatikana katika maeneo yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)