Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Desderius John Mipata (57 total)

Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwenye hoja iliyoko mbele yetu. Niungane na wenzangu kwanza kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa kutujalia uzima. Vilevile niwashukuru wananchi wa Jimbo la Nkasi Kusini kwa kunirejesha tena kwenye nafasi hii. Nawaahidi nitawatumikia kwa heshima. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naungana na wenzangu wote wanaounga mkono hoja hii. Katika kuchangia, naomba nianze na kuiangalia hotuba ya Mheshimiwa Rais. Katika ukurasa wake wa 16, alijaribu kubainisha maeneo ambayo yakishughulikiwa yanaweza kuwa na mchango mkubwa sana katika kuinua uchumi wa nchi hii.
Vilevile alielezea namna ambavyo sekta mbalimbali zinavyochangia katika uchumi wa Taifa na kutoa ajira. Sekta hizo ni kilimo, uvuvi na ufugaji bila kusahau wachimbaji wadogowadogo. Tunafahamu kwamba kilimo kinachangia kuwapatia ajira Watanzania kwa zaidi ya asilimia 75. Vilevile kwenye GDP kilimo kina mchango wa zaidi ya asilimia 25 na kinasaidia kutuingizia fedha za kigeni kwa zaidi ya asilimia 30. Kwa hiyo, kwa wachumi na maafisa wetu wanaopanga mipango, hapa ndiyo mahali ambapo pangezingatiwa tungeweza kuubeba mzigo mkubwa na kuhakikisha kwamba tunaboresha uchumi wa nchi yetu ambao umezorota kwa kiwango kikubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuanzia napenda kuangalia katika suala zima la kilimo. Ninavyoona mimi kilimo hatukiendeshi vizuri licha ya sera nzuri ambazo tumeziweka kwenye kilimo za kuchangia pembejeo mbalimbali, lakini bado kumekuwa na uchakachuaji ambao umesababisha matarajio kutofikiwa. Inaonekana hakuna anayesimamia kilimo kwa karibu. Nashukuru kupata Waziri wetu, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, naomba ajielekeze kwenye kilimo. Ametueleza kwenye historia yake kwamba ametoka kijijini na amekuwa mtoto wa mkulima sasa adha zile alizozipata na aka-fluke kwa kubahatisha mpaka kufikia hapo alipo leo, ndiyo zimewabana Watanzania wengi. Akikaa vizuri kushughulikia kilimo, anaweza akawatoa watu wa aina yake wengi ambao wamekosa fursa kwa sababu kilimo hakishughulikiwi na watu wengi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali iangalie sekta hii, wakulima, wafugaji na wavuvi, hawapati incentive zinazotakiwa kutoka Serikalini. Ruzuku inayotengwa kwa wakulima haziwafikii wakulima, kuna watu wako katikati hapa wanachakachua na inaonekana ni kama tunawashindwa. Nawashangaa Wizara hii ambayo imesheheni wasomi mnashindwaje kutatua changamoto hizi ambazo zinatusumbua kila mwaka? Katika miaka kadhaa tunahangaika jinsi gani ruzuku itawafikia wakulima, mbolea zinachakachuliwa, fedha zinatengwa na tumeona takwimu hapa lakini hatuoni tija, ni jambo la kushangaa. Naomba tuielekeze Serikali yetu ihakikishe wakulima wanatazamwa kwa macho mawili na changamoto zinazowahusu zishughulikiwe vizuri kwa sababu zinabeba Watanzania wengi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa wakulima wamegawanyika, tunaposema wakulima wako wavuvi pia. Katika Jimbo langu vijiji zaidi ya 30 viko mwambao wa Ziwa Tanganyika. Hawa ndiyo wamesahaulika kabisa, hawajasaidiwa chochote, Serikali haijaonyesha juhudi kuwasaidia wavuvi. Wavuvi wanaishi tofauti na mazingira yao, mazingira yanaonyesha kuna utajiri mkubwa lakini maisha yao bado ni hafifu sana. Maeneo mengi ya wavuvi utakuta ni watu ambao wanatumikia watu wengine licha ya kwamba rasilimali zinazowazunguka zinaonyesha utajiri mkubwa lakini wameshindwa kwa sababu hawajasaidiwa inavyotakiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali yetu isaidie kwa kuwapa vifaa vya kisasa vya uvuvi na ikiwezekana kuwapelekea vitu ambavyo vinaweza kuwa vichocheo vya uwekezaji na kichocheo kimojawapo ni umeme. Suala la umeme lingefanyiwa utaratibu tukapata umeme wa kutosheleza katika maeneo ya Ziwa Tanganyikia maana yake tungeweza kuwavutia wawekezaji katika sekta hii. Ule ukibarua wanaofanya sasa hivi wa kupeleka samaki na dagaa nje ya nchi kwenda kuuza wangeweza kuwekeza hapahapa na tungeweza kuwa tumewasaidia vizuri kuliko ilivyo sasa. Naomba suala hilo liangaliwe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya pili ambayo napenda kuchangia ni suala hili hili la umeme lakini nazungumzia kupatiwa umeme mkubwa zaidi kuliko uliopo sasa. Katika bajeti ya mwaka jana kulikuwa na utaratibu wa kusafirisha umeme kwenye Gridi ya Taifa kutoka Nyakanazi kuleta Kigoma, Mpanda na Sumbawanga. Lengo kubwa lilikuwa ni kuunganisha Mikoa hii na umeme mkubwa zaidi kwa kujua kwamba ni mikoa ambayo kwa kweli ni tajiri na ina bahati nzuri ya kilimo na ingeweza kusaidia pia ku-attract wawekezaji ambao wangeweza kutusaidia.
Kwa hiyo, nia hii naomba iendelee, tusiiachie maana katika mipango hii iliyowekwa sasa hivi sijaona kama kuna mwendelezo huu. Kwa hiyo, naiomba Serikali ione wazo hili linapewa kipaumbele na tunaenda nalo ili kuwasaidia wananchi wa maeneo haya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine la msingi na la mwisho ni barabara. Katika kuunganisha mikoa yetu, ipo miradi ya barabara inayosuasua. Barabara ya kutoka Sumbawanga kwenda Mpanda ni barabara ya muda mrefu na hatuwezi kuzungumzia masuala ya uchumi kuwasaidia wananchi kama hatuwezi kuboresha miundombinu hii kwa kasi inayotakiwa, sasa hivi ujenzi wake unasuasua sana. Nashauri Serikali kuongeza kasi katika ujenzi wa barabara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Serikali isisahau barabara zinazoenda kwa wakulima. Katika Jimbo langu kuna barabara ambazo zinaelekea kwenye vijiji vya Katani na Myiula. Vijiji hivi vinazalisha kwa wingi lakini inafika wakati barabara zinajifunga. Kwa hiyo, juhudi ambayo wananchi walikuwa wamewekeza kwenye kilimo inakosa faida kwa sababu hawafikiwi na masoko na wala huduma muhimu kama za pembejeo kwa sababu barabara zimefunga. Kwa hiyo, muone uwezekano wa kuongeza fedha ili kushughulikia barabara zinazoenda kwenye maeneo ya uzalishaji kama maeneo ya Myiula, Chonga, Charatila ambayo katika Jimbo langu ni muhimu sana kwa uzalishaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ni muhimu kulizungumzia ni suala la maji. Maji katika maeneo yetu yamekuwa ni tatizo na hapa tumekuwa tukizungumza juu ya miradi mbalimbali ya maji ikiwepo mradi wa King‟ombe. Mradi wa King‟ombe ulitengewa zaidi ya shilingi 500,000,000 kwa kijiji kimoja lakini mpaka fedha hizo zimekwisha kijiji hicho hakijapata maji. Jambo hili tumelizungumza kwenye Bunge lililopita, Mheshimiwa Keissy amezungumza sana hapa, hakuna anayesikia suala hili. Mpaka mwisho tunakuwa na wasiwasi pengine hawa watu tunaowaambia ni sehemu ya tatizo.
Naomba mliangalie suala hili. Ukienda King‟ombe kama kiongozi na mdau wa kisiasa watakufukuza, hata wakati mwingine wanawafukuza watalaam kwa sababu wanaona fedha nyingi zimeingia lakini hazina tija, hawapati maji jambo ambalo ni hatari sana. Kuna wizi mkubwa umefanyika lakini hakuna mtu anayefuatilia jambo hili. Naiomba Serikali ijaribu kufuatilia...
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa
muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Mheshimiwa muda wako umekwisha.
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kupata nafasi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza natoa pongezi kubwa sana kwa spidi na kasi nzuri sana ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano. Naunga mkono juhudi zote anazozifanya na kasi hii inatakiwa iungwe mkono na viongozi wote na wananchi wote kwa ujumla. Anatibu majipu, anatibu matatizo ambayo yamekuwa sugu katika jamii na kwa namna hii, natabiri kwamba, nchi yetu sasa hivi italeta mapinduzi makubwa sana kiuchumi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nipitie hotuba ya Waziri Mkuu kuwasilisha ombi la Mji Mdogo wa Namanyere kuomba kuwa Mamlaka ya Mji wa Namanyere. Wilaya ya Nkasi iko pembezoni na mara zote mmekuwa mkitutolea mfano kwamba tuko pembezoni na maendeleo yetu yako chini. Namna ambayo mnaweza kutusaidia na kutuimarisha ni kutusogezea maeneo ya kiutawala. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mji wa Namanyere una zaidi ya watu 135,000, eneo la kilometa za mraba zaidi ya 16,000, ina bajeti zaidi ya shilingi milioni 359, ina Makao Makuu ya Tarafa, Makao Makuu ya Wilaya, Polisi, Sekondari saba, Chuo cha St. Bakhita kinachokusanya watu karibu 1,000 na ina Hospitali ya Wilaya. Kwa msingi huo, tunakidhi vigezo vingi vya kuwa Halmashauri ya Mji.
Tunajua mkitupa Halmashauri ya Mji mtakuwa mmetusukuma na kutusaidia katika matatizo mengi yanayotukabili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kupitia nafasi hii ya kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, niwasilishe ombi rasmi na lishughulikiwe na maombi tumeshapeleka mezani. Tuna Kata 10 tayari na Madiwani tumeshafanya uchaguzi. Kwa hiyo, kwa sasa tuna uwezo kabisa wa kuwa Halmashauri. Hilo ni ombi la kwanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni sekta ya kilimo. Mimi wapiga kura wangu wengi ni wakulima. Miaka mitano yote niko Bungeni lakini sijaona mabadiliko makubwa katika sekta hii. Tumekuwa tunazungumza tunagusagusa na matatizo sugu hayajawahi kushughulikiwa inavyotakiwa. Kwa mfano, suala la utawanyaji wa pembejeo sijaliona kama limekuwa likienda vizuri na nimekuwa nikichangia hapa kila mwaka mabadiliko sijawahi kuyaona.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wetu wanapelekewa pembejeo muda sio muafaka, wananchi wetu wanaoitwa walengwa pembejeo za ruzuku hawapati. Namwomba mtumbua majipu aelekeze nguvu zake eneo hili la pembejeo za wakulima wanyonge. Haki yao haifiki inavyostahili, haifiki hata kidogo.
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Nashangaa hata ruzuku ya mifugo haifiki inavyotakiwa, wavuvi hawapati ruzuku yoyote, hii sekta yote ni kilimo kwa ujumla wake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie nafasi hii kuwaombea wakulima ruzuku ipatikane kwa wakati. Pia mtafute mwenendo mzuri, mbuni mbinu nzuri kama mnavyobuni za kukamata hawa mafisadi, mnavyokamata wauza madawa ya kulevya sasa hivi, hii Serikali ina mbinu ambazo hata hatukuzitegemea kuwepo, ni kama kitu kimekuja ambacho hatukukitarajia, naomba muelekeze nguvu hiyo kwenye kilimo ili mboreshe kilimo. Kilimo kinatuajiri Watanzania 75%, kilimo kinatuchangia hela nyingi za kigeni, kilimo kinaleta utulivu na amani ya nchi kwa kuwepo kwa usalama wa chakula, kwa hiyo, kina kila umuhimu. Sisi Mkoa wa Rukwa ni wakulima na maeneo yote ambayo yanalima wasaidiwe kuangalia kwamba vigezo kama hivi vinazingatiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo haya ya kilimo yanahitaji kupata miundombinu ya usafiri. Barabara zinazoelekezwa katika maeneo ya kilimo bado ni mbovu. Barabara ya kutoka Sumbawanga kwenda Mpanda inayojengwa kwa kiwango cha lami imekuwa ikicheleweshwa tu.
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Miaka saba tuko hapa Bungeni hatuioni hiyo barabara inakwisha kwa nini? Tukitembea sehemu nyingine nchini tunakuta kuna wakandarasi wenye nguvu na miradi inakwenda kwa speed zinazotakiwa, kwa nini kwetu kwa sababu ya upembezoni? Naomba mliangalie, Sumbawanga, Rukwa, Mpanda kote huku barabara haziendi vizuri kwa sababu ya upembezoni wake, lakini sasa ni awamu nyingine mtazame wanyonge. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni maji. Matatizo ya maji katika Jimbo langu na vijijini kwa ujumla ni kubwa sana mliangalie kwa umakini. Nikitolea mfano katika Jimbo langu kuna mradi wa kutoka Kate kupeleka maji Isale ambayo yangeweza kusaidia vijiji karibu saba vya Ntemba, Ntuchi, Isale katika mtiririko mzima wa njia hiyo ya maji. Naomba mradi huu pamoja na miradi mingine iliyoko King’ombe ambayo haijakamilika, tumepeleka zaidi ya shilingi milioni 500 amesema Mzee Keissy hapa kwamba kuna pesa zinatumika visivyo, zaidi ya shilingi milioni 500 lakini huoni maji hata kidogo yanatoka. Nafikiri muangalie yapo majipu kweli kweli. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, upo mradi wa maji Vijiji vya Nkundi na Kalundi bado haujakamilika, upo mradi Kijiji cha Chala bado haujakamilika, Kijiji changu cha Kasu hakuna mradi wa kutosha wa maji kakamavu kama tunavyoweza kuona katika sehemu nyingine. Kijiji cha Wampembe, Kijiji cha Namansi bado kote huko kuna matatizo ya maji naomba mtusaidie kupitia bajeti hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia bajeti hii naomba pia suala la mtandao wa mawasiliano. Nashukuru Serikali kwa kazi nzuri iliyofanyika katika Kata ya Ninde na ya Wampembe. Bado kuna dosari ndogo ndogo ili kukamilisha kazi hiyo, lakini Kata ya Kala ambayo ina tatizo kubwa zaidi bado kuna nini? Bahati nzuri Waziri ni yule yule ambaye alikuwepo. Sasa nakwambia katika bajeti yako siwezi kupitisha kama huwezi kupeleka au kunipa majibu mazuri ya kupeleka mtandao Kala. Sehemu zingine hizi umejitahidi vya kutosha lakini nataka kujua Kala kwa nini? Pembezoni kila siku tunakuwa wa mwisho, kwa nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, ni suala la umeme. Mwambao mwa Ziwa Tanganyika katika Vijiji vya Kata ya Wampembe, Ninde na Kala hazijafikiriwa kabisa katika suala zima la umeme. Katika Jimbo langu la Nkasi Kusini maeneo kama vile Vijiji vya Kate, Katani, Nkomolo II, Kisura na Malongwe tulikwishasema kwamba sasa hivi wangeweza kupata umeme, lakini mpaka sasa navyosema umeme haujawashwa. Wanapelekwa Wakandarasi goigoi hawafanyi kazi inavyotakiwa. Naomba muwabadilishe mlete wenye nguvu ili waweze kuleta matarajio ya wananchi haraka. Kilimo hakiwezi kwenda vizuri kama hata umeme wenyewe unasuasua namna hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, upo mradi wa kupeleka umeme mkubwa katika mikoa ya pembezoni ikiwa ni pamoja na Rukwa, Kigoma na Katavi kutoka kwenye grid ya Taifa. Naomba isiishie maelezo tu ambayo tunayasikia hapa kwamba utafiti unaendelea. Tunataka tuone angalau katika bajeti hii umeme mkubwa ufike Sumbawanga ili mazao na mahindi yaliyopo ya wakulima wale yaweze kuchakatwa vizuri, ili samaki ambao wako mwambao mwa Ziwa Tanganyika minofu yake iweze kuchakatwa vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tunakuwa watumwa wa watu wa Zambia, minofu yetu inapelekwa Zambia, halafu inasafirishwa Afrika Kusini kwa sababu tu hatuna umeme wa kutosha. Wavuvi wetu kule wanakuwa maskini wakati hawastahili kuwa maskini kwa kweli wanacheleweshwa kwa nini? Naomba umeme safari hii ufike Kirando, Wampembe, Ninde, Namansi kwani itakuwa ni ukombozi mkubwa sana wa wananchi wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ni barabara za Halmashauri. Zipo barabara ambazo nilikuwa nasaidiwa sana na Mheshimiwa Rais ambaye alikuwa Waziri. Barabara ya Kitosi – Wampembe, barabara ya Ninde, barabara ya kutoka Kasu - Katani - Nyula, barabara hizi Halmashauri haiziwezi. Tunaomba msaada zaidi kwa sababu sasa hivi karibu zitafunga, bila juhudi za ziada kutoka Serikalini tutaaibika. Naomba ni maeneo ya wakulima wengi na tunatakiwa kuhakikisha kwamba barabara zinapitika. Hii ni pamoja na barabara kutoka Milundikwa - Kisula pamoja na Malongwe. Ni barabara sumbufu na zinasumbua sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kwa sababu muda unaniruhusu ni suala la zahanati. Tumesema kila kijiji kipate zahanati, lakini zipo zahanati ambazo zilishajengwa hazijafunguliwa bado kuna nini? Ipo Zahanati ya Nkomolo II na Msilihofu bado hazijafunguliwa rasmi ili ziweze kuwekwa kwenye utaratibu wa kuletewa dawa hizo zinazoweza kupatikana kwa njia ya kawaida.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tuangalie sana Hospitali ya Wilaya ya Namanyere. Hospitali ya Namanyere ni DDH, iko chini ya Kanisa la Roman Catholic. Utaratibu wa huduma umezorota kupita kiasi. Naomba Serikali itimize wajibu wake kwa hospitali hii lakini na wale wanaohusika juu ya uchunguzi na uangalizi…
MWENYEKITI: Mheshimiwa muda wako ndiyo huo, tunakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima, pili niwashukuru wana Nkasi Kusini kwa kunichagua. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nami niungane na wenzangu wanaounga mkono hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo na naunga mkono pia jitihada zote zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naanza na kuangalia utekelezaji wa bajeti iliyopita, Fungu namba 99, Mifugo na Uvuvi. Katika fungu hili Serikali ililenga kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 25.9 kutoka kwenye maeneo haya kama kwenye naduhuli ya Serikali. Hadi Machi 2016 eneo la uvuvi, Serikali imekusanya zaidi ya bilioni 12 sawa na asilimia 108. Katika eneo la mifugo ilikusanya zaidi ya asilimia 70. Kwa ujumla katika fungu hili mafanikio ya maduhuli yaliyokusanywa ni zaidi ya asilimia 85.7, ni mafanikio makubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hoja yangu ni nini? Ni kwamba katika miradi ya maendeleo katika fungu hili zilitengwa jumla ya shilingi bilioni 40. Kati ya hizo zaidi ya asilimia 40 ilielekezwa kwenye maendeleo ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 19.3. Kwenye utekelezaji, maendeleo ni sifuri, hakuna chochote kilichokwenda. Sasa hapa ndiyo unaweza kuona namna ambavyo sekta ya mifugo na uvuvi haikushughulikiwa kabisa kwa asilimia mia moja. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ni rahisi kukusanya na wamekusanya fedha kirahisi tu, lakini katika mwaka uliopita hawajapeleka kitu chochote kuimarisha uvuvi, hawajapeleka kitu chochote kuimarisha ufugaji, trend hii ni hatari. Kwa msimamo huo, kama tutaendelea kujidai kwamba bajeti ya maendeleo ni asilimia 40 na Mheshimiwa Rais aliwatangazia wananchi kwenye sikukuu ya wafanyakazi kwamba ameweka mkazo kuhakikisha kwamba asilima 40 inaenda kwenye maendeleo, kwa utekelezaji huu hakuna kitu, tuwe na nidhamu katika utekelezaji wa bajeti. Kwa kuwa na nidhamu ya bajeti itatusaidia sana, nashauri tusiendelee na utaratibu huu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ya kilimo, mimi Jimbo langu limegawanywa katika maeneo mawili, kanda ya juu na kanda ya ziwani. Kanda ya ziwani ina Kata nne za Kizumbi, Wampembe, Ninde na Kala, zote zinategemea uvuvi. Mpaka ninavyozungumza hivi hawajawahi kuona hata mara moja ruzuku yoyote inayoelekezwa kwenye mambo ya uvuvi, ni historia, kwa hiyo, tusiwe tunazungumza tu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mwigulu atanisaidia sana, nina miaka mitano hapa Bungeni na nimekuwa nikizungumza jambo hili, lakini mpaka sasa ninavyosema hakuna hata harufu ya mchango ulioelekezwa kwa wavuvi wa mwambao wa Tarafa nzima ya Jimbo langu katika Kata nne. Hakuna mialo iliyojengwa, hakuna barabara zinazotengenezwa, hakuna fedha zinazotengwa kwa ajili ya kuwakopesha watu wapate vyombo vya uvuvi wa kisasa, kwa hiyo ni changamoto kubwa. Watu wanapoona pengine nguvu zinaelekezwa kwenye kilimo peke yake hawaelewi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, Mkoa wa Rukwa na Mikoa mingine ya Nyanda za Juu Kusini inategemea mahindi kama zao kuu na eneo lile ni conducive kwa uzalishaji wa mahindi. Kwa maana hiyo, mahindi kwetu ni chakula na ni biashara. Usipotusaidia katika suala la mahindi katika mambo ya uzalishaji na uuzaji wake hujasaidia Kanda hiyo nzima na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla.
Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa napitia bajeti ya mwaka jana, nimekuta kwenye akiba yetu tulikuwa na tani 370,973.6 za akiba ya chakula kwa mahindi kabla ya kupeleka kwenye soko na kusaidia maeneo yenye njaa. Mpaka sasa ulivyotoa umebakiza stoo tani 61,315, kwa maana hiyo kuna sababu ya mwaka huu kununua mahindi ya kutosha kwa sababu maghala yako wazi sasa na mahindi yanahitajika kama unavyoona mwaka jana yalivyotumika mengi, kwa hiyo, kuna sababu ya kununua mahindi mengi.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka huu nimesikia japo siyo rasmi kwamba Serikali imepanga kununua tani 100,000 hii maana yake nini? Serikali hii ndiyo inaingia madarakani, wapiga kura wengi walikuwa ni wakulima na wafugaji hawa. Unaposema unanunua tani 100,000 maana yake unawaacha wakulima ambao wanachangia population ya Tanzania kwa asilimia 70 na shughuli yao kubwa ni kilimo, wanaendesha kilimo lakini hawajui namna watakavyouza mazao yao.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali isijiondoe kwenye jukumu lake la kutafuta soko la wakulima, mkifanya hivyo mtakuwa mmekosea. Tunahimiza, tunatoa mbolea za ruzuku ili watu wazalishe, sasa uzalishaji upo na Sumbawanga upo, Namanyere kwa Nkasi peke yake tutakuwa na zaidi ya tani 55,000, sasa usipozinunua hatuwezi kuelewa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni kuhusu Ranchi za Taifa. Kule kwetu kuna Kalambo Ranchi, wafugaji wachache wamepewa blocks kadhaa lakini block hizo zimekuwa zinaachiwaachiwa yaani mtu akikosa uwezo anamuachia mwingine kienyeji kienyeji, kwa hiyo, inapoteza maana, naomba utaratibu mzuri uwepo kushughulikia ranchi hizi.
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile Ranchi ya Kalambo inashangaza, wananchi walifukuzwa katika maeneo hayo kuanzisha ranchi ili wafuge, lakini sasa hivi wao wanakodisha ranchi hiyo kwa wakulima wakubwa. Sasa hivi kuna mkulima amelima zaidi ya ekari 1,000 na kuleta malalamiko kwa vijiji vya Nkana, Sintali, Nkomanchindo na Ntaramila kwamba kwa nini wao walifukuzwa badala yake Serikali imetafuta mwekezaji ambaye amelima ekari zaidi ya 1,000 maeneo ya ufugaji, dhana ya kufuga na kulima haieleweki sasa kwa hapo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, naomba kuchangia kuhusu SAGCOT. SAGCOT inalenga kuimarisha kilimo kwa maeneo ya Kusini mwa Tanzania ikiwa ni pamoja na kupeleka mbolea, kuimarisha barabara na vitu kama hivyo ili kuboresha kilimo, lakini katika bajeti hii sijaiona.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba mtusaidie kuhakikisha kwamba miradi inayoanzishwa isiwe inatajwatajwa, iwe inaanza kushika kasi, SAGCOT inatamkwatamkwa hakuna kitu kinachoendelea. Maeneo ya wakulima yasipofikika, tutapataje pembejeo? Sasa hivi tunahimiza sana utumiaji wa pembejeo zinazopatika hapa nchini kama Minjingu, kwa nini tusione umuhimu wa kuboresha miundombinu ya usafiri wa maeneo haya ili kufikisha pembejeo hizo kwa maana ya mbolea za kupandia na mbegu.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna kila sababu ya kuhakikisha kwamba mbegu zinazalishwa katika maeneo ya uzalishaji. Ipo tabia ya kutoa nje mbegu za mazao ya wakulima, kwa nini? Wakati ardhi ya kutosha tunayo na wataalam ninyi mpo na wafanyabiashara wapo. Kwa nini tusiweke utaratibu wa kuzalisha katika maeneo yetu sisi wenyewe ili kujihakikishia usalama wa mbegu na ubora wake kuliko hali ya sasa ambapo unataka mbegu kutoka Kenya na sehemu nyingine, mwisho tunapata mbegu zenye tabia ambazo hazihimili mazingira yetu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Pia nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kutujaalia uzima. Vilevile nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anazozifanya na kujitoa kwa moyo kutumikia Watanzania. Kazi anayoifanya tunaiona, tuko nyuma yake na kila mwenye macho anaona. Kwa hiyo tunamuunga mkono, hayuko peke yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza pia Mawaziri wote wawili mzee wangu Mheshimiwa Mkuchika na Mheshimiwa Jafo, pamoja na Manaibu Waziri Mheshimiwa Kandege, Mheshimiwa Waitara na Mheshimiwa Mwanjelwa Machuche. Wamekuwa wakitusaidia sana na siku zote wanatusikiliza na mara tunapofikishia hoja zetu wanatusaidia vizuri kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na miradi ya afya. Kazi nzuri sana imefanywa na Wizara hii ya TAMISEMI hasa katika eneo hili la afya, sisi kwetu tumefanikiwa kupata vituo vya afya vitatu na sasa wanatuongezea kimoja lakini pia tumepata Hospitali ya Wilaya tumepata hela za kutosha bilioni moja na milioni mia tano mwaka jana na mwaka huu wametuongezea milioni mia tano, jambo hili ni zuri sana. Kwangu mimi nimeweza kupata pia kituo cha afya cha Wampembe ambacho Mheshimiwa Jafo aliweza kutembelea alipotushauri, tunamshukuru sana sana, kazi pale imefanyika vizuri na ushauri aliotupa tunaendelea nao vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, niseme changamoto moja, vituo hivi vinapokamilika kuna jambo bado linabaki kuwa ni tatizo kwa akinamama wetu hata wale wa vijiji vya jirani. Ningeshauri wazo hili liendelee kwenye vituo vyote vinavyokamilika, tuwe tunaweza kujenga jengo la kuwafanya akinamama wajisubirie pale, maternity waiting home, itatusaidia kufanya wale ambao wako mbali kidogo wasogee na waweze kujisaidia vizuri zaidi na kupata huduma inayotakiwa. Vinginevyo habari ya kujifungulia nyumbani itaendelea hata kama vituo vipo kwa sababu gharama zile wanashindwa kujimudu kwenda kukaa pale na kukaa kwa ndugu ni ngumu kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajenga vituo vya afya vingine Ninde, tunajenga kituo cha afya na wananchi wamejenga majengo mazuri, vyumba kumi wamekamilisha lakini King’ombe tunajenga kituo cha afya, Kate pia wanajenga kituo cha afya, Kasu wanajenga kituo cha afya, tunaomba wanapopata nguvu tena waweze kutusaidia kwenye maeneo hayo. Hata hivyo, Kata ya Kala iko mbali sana na akipatikana mgonjwa kule anapata shida kufika kwenye kituo cha afya hasa akinamama na watoto, naomba tupate gari ya wagonjwa ili isaidie katika kuhudumia katika eneo hilo. Tumejenga zahanati nyingi zipatazo 10, zote zimefikia mtambaa panya, hatujapata uwezo wa kuweza kuezeka, lakini tunahamasisha wananchi ili tujenge. Naomba mtusaidie ziko zahanati ya Kisambala, Kantawa, Kipande, Kalundi, Nkomachindo, Ifundwa, Tundu, Kilambo, Ntuchi na Nchenje zimeezekwa, ni pesa kidogo tu zinatakiwa ili kuzikamilisha wananchi waanze kupata huduma. Naomba Serikali itusaidie na kama haiwezi kutusaidia itusaidie hata kuibana Halmashauri zaidi ili watusaidie katika zahanati hizi ambazo karibu zinakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba vilevile nizungumzie kuhusu Bima ya Afya. Bima ya Afya nzuri na inasaidia sana wananchi na mara nyingi watumishi wa taasisi mbalimbali na wa Serikali ndio wanaosaidiwa zaidi. Mpango wa kuwezesha wananchi wote kwa ujumla Watanzania wapate huduma ya Bima ya Afya umefikia wapi? Naomba nihimize Serikali ione umuhimu wa kufanya hivyo. Sambamba na hilo niwaombe, nichukue nafasi hii kuwashukuru sana watumishi wa Bima ya Afya hasa waliojipanga kuhudumia Wabunge yupo Flora Mtabwa na Felister Mabula, hawa watu wakipata dharura wanachukua kwa haraka sana na wanatusaidia na wanajipanga vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile niseme kuhusu hospitali ya Muhimbili, Muhimbili sasa hivi huduma zimejipanga vizuri, watu wanafanya kazi kama mchwa, ukipata dharura ndio unaweza ukajua kumbe sasa tuna hospitali ya Taifa yenye kiwango na inahudumia vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Waganga hatuna, tunaomba Wauguzi kwetu kule Nkasi hatuna hasa pembezoni. Mheshimiwa Kandege na Mheshimiwa Jafo watusikilize na Mheshimiwa Waziri anapajua, bahati nzuri umeshafika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni kuhusu TARURA. TARURA kama wenzangu wanavyosema naunga mkono tuwape asilimia 50 kwa 50, lakini sisi leo hii kutokana na TARURA hatuwezi kufikika kwenye vijiji kadhaa, Kijiji cha Kisula siweze kufika kwa sababu barabara imekatika na mvua na hakuna fedha za dharura. Kwa hiyo TARURA haina hata uwezo wa kukabili dharura yoyote inayotokea mpaka waombe. Sasa jambo hili sio zuri sana, kwa hiyo naomba sana Serikali itusaidie kuhakikisha kwamba TARURA wanapata pesa za kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna daraja la Ninde, Kata nzima haiwezi kufikika kwa sababu ina barabara moja, daraja limevunjika hakuna pesa na tumeshatuma maombi, lakini bado hatujapata pesa, sababu hawana pesa, kwa hiyo tunaomba. TARURA pia hawana watumishi, watumishi wake wako kwa mkataba, naomba waajiriwe, kama ni kujaribiwa wamejaribiwa muda wa kutosha ili watu waweze kujiamini. Sasa hivi wanafanya kazi kwa mikataba ya miezi mitano mitano au sita sita haiwezekani! Wapeni uwezo full mandate waweze kufanya kazi vizuri itasaidia. Vilevile hawana magari ya supervision hasa kule wilayani, lakini vilevile hata huku hawana pesa za kutosha, naomba watusaidie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendee katika eneo la maji. Kuna miradi ya maji ambayo inatekelezwa ya vijiji kumi hivi vya Benki ya Dunia. Miradi mingi imefanya kazi bila utafiti wa kutosha, usanifu wake haukuwa mzuri, Kijiji cha Nkundi kina mradi umegharimu zaidi ya bilioni mbili, lakini maji hayatoki. Naomba Serikali ione utaratibu wa kuwezesha vijiji kama hivi viweze kupata wataalam wa kutosha au kuona vikwazo gani vinafanya maji yasitoke katika gharama yote hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kijiji cha Kisula vilevile maji bado ingawaje wao wanaendelea na mradi. Miradi wa Mpasa, mradi wa Isale una zaidi ya bilioni tano katika Jimbo langu, lakini unaendelea vizuri, tumeshafanya kazi za kutosha, mkandarasi anaendelea vizuri, ila certificate tuliyoomba bado haijarudi ili kazi iweze kuendelea vizuri zaidi. Kwa hiyo, naomba Serikali itupe hela ambayo tulishaomba ili Mkandarasi aendelee na kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la umeme, kuna vijiji vilirukwa katika awamu ya kwanza na ya pili, nikienda kule naonekana kama kichekesho; Kijiji cha Katani, Kijiji cha Malongwe, Kijiji cha Nkana, Kijiji cha Sintali, Kijiji cha Nkomachindo, ni vijiji ambavyo vinanitesa, nashindwa hata namna gani niweze kwenda. Naomba nitumie hadhara hii Mheshimiwa Waziri wa Nishati anisikie, vijiji hivi ni kero, nikienda jimboni, sina raha hasa kwa sababu wamezungukwa na vijiji vyote vyenye umeme. Ingawaje bado kuna vijiji vingi kabisa ambavyo havina umeme, lakini hivi ndio zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho kama nitapata muda ni kilimo, kilimo kikiboresha ndio halmashauri zinaweza kupata mapato ya kutosha. Kwa sasa hivi natoa ushauri kwamba ruzuku iliyokuwa imewekwa kwenye kilimo, irudi kwa sababu ilikuwa inabeba watu wa chini zaidi. Ruzuku iliyoko sasa hivi inawabeba wakubwa wakubwa tu, wenye uwezo wa kwenda kununua pembejeo madukani, lakini wale wenzangu na mimi inakuwa ni ngumu sana kupatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia masoko ya mazao ya wakulima, Mkoa wa Rukwa bila kuwa na masoko ya kutosha, wataalam mko wapi? Tutafutieni masoko ya wakulima kwa sababu tunawahimiza wakulima walime, wanatupa sayansi za kuvuna vizuri zaid, sasa tukishavuna tunaweka vyakula vinaharibika na vinauzwa kwa bei ya chini, watu wanakufa moyo. Kwa hiyo naomba sana…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na naunga mkono hoja. Natambua sana kwamba Serikali ya Mitaa zinafanya kazi vizuri. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kuunga mkono hoja na Wizara ipokee kwa makini sana mchango wangu ufuatao:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Nkasi Kusini lina matatizo ya kijiografia linalosababisha wakati wa kufanya mitihani ya darasa la saba watoto hulazimika kuhamia shule nyingine, karibuni shule zaidi ya kumi huathirika na suala hili. Kwa nini Wizara isisimamie kukomeshwa kwa adha hii au basi vyombo vya usafiri majini vinunuliwe ili vitumike kuwasafirisha wasimamizi ambao wanaogopa kutumia usafiri wa boat zinazotumiwa na wakazi wa eneo la Mwambao wa Ziwa Tanganyika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, uhaba wa Walimu Wilayani Nkasi, hasa eneo la Mwambao wa Ziwa Tanganyika. Jimbo la Nkasi Kusini lina uhaba mkubwa sana wa Walimu wa shule ya msingi na sekondari na hasa eneo la Mwambao wa Ziwa Tanganyika ambako Walimu ni wachache kwa kila shule. Walimu hawa pia hawana nyumba za kuishi pamoja na ukosefu mkubwa wa madarasa katika shule.
Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu maalum. Wapo watoto albino na walemavu wengine, mashuleni kwetu sekondari na hata shule za msingi pia. Naomba kuwapa msaada wa visaidizi ili waweze kumudu masomo, nina maana wakisajiliwa katika shule ifanyike assessment kujua mahitaji yao na shule zielekezwe kuwatimizia mahitaji hayo kutoka kwenye ruzuku hiyo hiyo inayotolewa mashuleni kote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, takwimu za walemavu zitunzwe na tuhimize shule na vyuo walikosoma kufuatilia maendeleo yao ili hatimaye waje wapate ajira. Mtiririko huu uzingatiwe pia mara zinapotoka ajira mbalimbali ili kupunguza utegemezi wa walemavu walioendelezwa na kuwa na sifa za kuajirika, watengewe nafasi kabisa na ziwekwe wazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, albino walindwe, wapewe mafuta ya kuwasaidia na wajulikane walipo na Kamati za Ulinzi na Usalama. Wao au familia zao wapewe simu na Kamati za Usalama za maeneo yao ngazi ya wilaya kwa ajili ya mambo ya dharura kiusalama. Nao hawa wajulikane wanaoendelezwa ili kuwekwa kwenye akiba ili zitokeapo nafasi za ajira wajulikane kwa nafasi walizotengewa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu wanafunzi waliositishwa masomo kwa makosa yaliyofanywa na Board, haikubaliki na lazima Wizara itafute ufumbuzi mwingine na siyo hatua yake ya kuwafukuza vijana vyuoni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, matatizo ya madawati katika shule za msingi ni kubwa na kuacha halmashauri au wilaya kutafuta wenyewe namna ya kumaliza upungufu kutaathiri miradi mingine mawilayani kama ilivyokuwa kwenye mpango wa ujenzi wa maabara. Ushauri; lazima Serikali itenge fedha kushughulikia tatizo hilo na siyo maagizo ya kutia hofu na kuwafanya Wakurugenzi na ma-DC kutafuta mbinu mbadala, hivyo fedha itafutwe Hazina.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo cha Maendeleo Chala, Wilayani Nkasi. Chuo hiki tangu miaka miwili iliyopita kilianza kutoa mafunzo ya VETA; naomba kiwe miongoni mwa chuo cha kutoa mafunzo hayo rasmi na kiendelezwe katika miundombinu yake na hasa ukizingatia Mkoa wa Rukwa hauna chuo chochote cha ufundi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maendeleo ya watoto wa kike shuleni. Nashauri, pamoja na changamoto zilizopo mtoto wa kike asinyimwe fursa ya kusoma kwa njia au mfumo rasmi pale anapopata mimba ili atimize malengo yake na pale inapotokea adhabu ya upande wa mwanaume anayesababisha mimba apewe adhabu ya kutosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, shule za msingi ziendelezwe au kila kijiji kianzishe shule ya sekondari kwa sababu elimu ya sekondari itakuwa elimu ya lazima kufikiwa kumbe tujiandae mapema kuandaa majengo, uamuzi huu wa Serikali kuwa kila mtoto afikie form IV bila malipo utakuwa na matokeo ya kukosa vyumba vya madarasa na miundombinu ya kiwango cha sekondari. Nawasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, napongeza utendaji wa Wizara kwa kazi inayoendelea kutendeka. Nkasi Kusini kuna vijiji kadhaa ambavyo vinadaiwa na Lwanfi Game Reserve kuwa viko ndani ya reserve yake, vijiji hivi vilikuwepo kabla ya hata reserve kuanzishwa. Vijiji hivi ni kama ifuatavyo:-
(i) Kijiji cha Kasapa, Kata ya Sintali;
(ii) Kijiji cha King‟ombe, Kata ya Kala;
(iii) Kijiji cha Mlalambo, Kata ya Kala;
(iv) Kijiji cha Ng‟undwe, Kata ya Wapembe; na
(v) Kijiji cha Namansi, Kata ya Ninde.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vipo vijiji pia vimepakana na Lwanfi na kuna migogoro ya hapa na pale kama vile kijiji cha Nkata na kijiji cha China, Kata ya Kate. Kwa msingi huo, naomba Waziri achukulie hii ni migogoro na sijaiona ndani ya kitabu chake cha migogoro.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ninalopenda kuchangia ni kuhusu mashamba ya wawekezaji. Mipaka ya mashamba ya wawekezaji wawili Jimboni Nkasi Kusini ina migogoro na wananchi wanaozunguka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mashamba hayo yanamilikiwa kihalali lakini kutokana uhaba wa ardhi wananchi wanakosa ardhi ya kutosha kulima. Mashamba hayo ni yale ya Nkundi na China. Ni mashamba makubwa, Serikali ione namna ya kuzungumza na wawekezaji hawa ili kuwaachia wananchi sehemu za mashamba hayo kutokana na uhaba wa ardhi walionao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ranchi ya Kalambo inapakana na vijiji vya Nkana, Sintali, Mkomanchindo na Kasapa, pamoja na sera ya kugawa vitalu kwa waliobinafsishiwa, vitalu havitumiki vizuri na wananchi hawana ardhi. Nashauri ardhi hii igawiwe kwa wananchi kwa sababu hawana ardhi katika vijiji nilivyovitaja, hii ni muhimu sana.
Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwenye hoja iliyoko mbele yetu. Niungane na wenzangu kwanza kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa kutujalia uzima. Vilevile niwashukuru wananchi wa Jimbo la Nkasi Kusini kwa kunirejesha tena kwenye nafasi hii. Nawaahidi nitawatumikia kwa heshima. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naungana na wenzangu wote wanaounga mkono hoja hii. Katika kuchangia, naomba nianze na kuiangalia hotuba ya Mheshimiwa Rais. Katika ukurasa wake wa 16, alijaribu kubainisha maeneo ambayo yakishughulikiwa yanaweza kuwa na mchango mkubwa sana katika kuinua uchumi wa nchi hii.
Vilevile alielezea namna ambavyo sekta mbalimbali zinavyochangia katika uchumi wa Taifa na kutoa ajira. Sekta hizo ni kilimo, uvuvi na ufugaji bila kusahau wachimbaji wadogowadogo. Tunafahamu kwamba kilimo kinachangia kuwapatia ajira Watanzania kwa zaidi ya asilimia 75. Vilevile kwenye GDP kilimo kina mchango wa zaidi ya asilimia 25 na kinasaidia kutuingizia fedha za kigeni kwa zaidi ya asilimia 30. Kwa hiyo, kwa wachumi na maafisa wetu wanaopanga mipango, hapa ndiyo mahali ambapo pangezingatiwa tungeweza kuubeba mzigo mkubwa na kuhakikisha kwamba tunaboresha uchumi wa nchi yetu ambao umezorota kwa kiwango kikubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuanzia napenda kuangalia katika suala zima la kilimo. Ninavyoona mimi kilimo hatukiendeshi vizuri licha ya sera nzuri ambazo tumeziweka kwenye kilimo za kuchangia pembejeo mbalimbali, lakini bado kumekuwa na uchakachuaji ambao umesababisha matarajio kutofikiwa. Inaonekana hakuna anayesimamia kilimo kwa karibu. Nashukuru kupata Waziri wetu, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, naomba ajielekeze kwenye kilimo. Ametueleza kwenye historia yake kwamba ametoka kijijini na amekuwa mtoto wa mkulima sasa adha zile alizozipata na aka-fluke kwa kubahatisha mpaka kufikia hapo alipo leo, ndiyo zimewabana Watanzania wengi. Akikaa vizuri kushughulikia kilimo, anaweza akawatoa watu wa aina yake wengi ambao wamekosa fursa kwa sababu kilimo hakishughulikiwi na watu wengi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali iangalie sekta hii, wakulima, wafugaji na wavuvi, hawapati incentive zinazotakiwa kutoka Serikalini. Ruzuku inayotengwa kwa wakulima haziwafikii wakulima, kuna watu wako katikati hapa wanachakachua na inaonekana ni kama tunawashindwa. Nawashangaa Wizara hii ambayo imesheheni wasomi mnashindwaje kutatua changamoto hizi ambazo zinatusumbua kila mwaka? Katika miaka kadhaa tunahangaika jinsi gani ruzuku itawafikia wakulima, mbolea zinachakachuliwa, fedha zinatengwa na tumeona takwimu hapa lakini hatuoni tija, ni jambo la kushangaa. Naomba tuielekeze Serikali yetu ihakikishe wakulima wanatazamwa kwa macho mawili na changamoto zinazowahusu zishughulikiwe vizuri kwa sababu zinabeba Watanzania wengi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa wakulima wamegawanyika, tunaposema wakulima wako wavuvi pia. Katika Jimbo langu vijiji zaidi ya 30 viko mwambao wa Ziwa Tanganyika. Hawa ndiyo wamesahaulika kabisa, hawajasaidiwa chochote, Serikali haijaonyesha juhudi kuwasaidia wavuvi. Wavuvi wanaishi tofauti na mazingira yao, mazingira yanaonyesha kuna utajiri mkubwa lakini maisha yao bado ni hafifu sana. Maeneo mengi ya wavuvi utakuta ni watu ambao wanatumikia watu wengine licha ya kwamba rasilimali zinazowazunguka zinaonyesha utajiri mkubwa lakini wameshindwa kwa sababu hawajasaidiwa inavyotakiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali yetu isaidie kwa kuwapa vifaa vya kisasa vya uvuvi na ikiwezekana kuwapelekea vitu ambavyo vinaweza kuwa vichocheo vya uwekezaji na kichocheo kimojawapo ni umeme. Suala la umeme lingefanyiwa utaratibu tukapata umeme wa kutosheleza katika maeneo ya Ziwa Tanganyikia maana yake tungeweza kuwavutia wawekezaji katika sekta hii. Ule ukibarua wanaofanya sasa hivi wa kupeleka samaki na dagaa nje ya nchi kwenda kuuza wangeweza kuwekeza hapahapa na tungeweza kuwa tumewasaidia vizuri kuliko ilivyo sasa. Naomba suala hilo liangaliwe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya pili ambayo napenda kuchangia ni suala hili hili la umeme lakini nazungumzia kupatiwa umeme mkubwa zaidi kuliko uliopo sasa. Katika bajeti ya mwaka jana kulikuwa na utaratibu wa kusafirisha umeme kwenye Gridi ya Taifa kutoka Nyakanazi kuleta Kigoma, Mpanda na Sumbawanga. Lengo kubwa lilikuwa ni kuunganisha Mikoa hii na umeme mkubwa zaidi kwa kujua kwamba ni mikoa ambayo kwa kweli ni tajiri na ina bahati nzuri ya kilimo na ingeweza kusaidia pia ku-attract wawekezaji ambao wangeweza kutusaidia.
Kwa hiyo, nia hii naomba iendelee, tusiiachie maana katika mipango hii iliyowekwa sasa hivi sijaona kama kuna mwendelezo huu. Kwa hiyo, naiomba Serikali ione wazo hili linapewa kipaumbele na tunaenda nalo ili kuwasaidia wananchi wa maeneo haya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine la msingi na la mwisho ni barabara. Katika kuunganisha mikoa yetu, ipo miradi ya barabara inayosuasua. Barabara ya kutoka Sumbawanga kwenda Mpanda ni barabara ya muda mrefu na hatuwezi kuzungumzia masuala ya uchumi kuwasaidia wananchi kama hatuwezi kuboresha miundombinu hii kwa kasi inayotakiwa, sasa hivi ujenzi wake unasuasua sana. Nashauri Serikali kuongeza kasi katika ujenzi wa barabara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Serikali isisahau barabara zinazoenda kwa wakulima. Katika Jimbo langu kuna barabara ambazo zinaelekea kwenye vijiji vya Katani na Myiula. Vijiji hivi vinazalisha kwa wingi lakini inafika wakati barabara zinajifunga. Kwa hiyo, juhudi ambayo wananchi walikuwa wamewekeza kwenye kilimo inakosa faida kwa sababu hawafikiwi na masoko na wala huduma muhimu kama za pembejeo kwa sababu barabara zimefunga. Kwa hiyo, muone uwezekano wa kuongeza fedha ili kushughulikia barabara zinazoenda kwenye maeneo ya uzalishaji kama maeneo ya Myiula, Chonga, Charatila ambayo katika Jimbo langu ni muhimu sana kwa uzalishaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ni muhimu kulizungumzia ni suala la maji. Maji katika maeneo yetu yamekuwa ni tatizo na hapa tumekuwa tukizungumza juu ya miradi mbalimbali ya maji ikiwepo mradi wa King‟ombe. Mradi wa King‟ombe ulitengewa zaidi ya shilingi 500,000,000 kwa kijiji kimoja lakini mpaka fedha hizo zimekwisha kijiji hicho hakijapata maji. Jambo hili tumelizungumza kwenye Bunge lililopita, Mheshimiwa Keissy amezungumza sana hapa, hakuna anayesikia suala hili. Mpaka mwisho tunakuwa na wasiwasi pengine hawa watu tunaowaambia ni sehemu ya tatizo.
Naomba mliangalie suala hili. Ukienda King‟ombe kama kiongozi na mdau wa kisiasa watakufukuza, hata wakati mwingine wanawafukuza watalaam kwa sababu wanaona fedha nyingi zimeingia lakini hazina tija, hawapati maji jambo ambalo ni hatari sana. Kuna wizi mkubwa umefanyika lakini hakuna mtu anayefuatilia jambo hili. Naiomba Serikali ijaribu kufuatilia...
MWENYEKITI: Mheshimiwa muda wako umekwisha.
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Na mimi niungane na wenzangu kuchangia hotuba ya Wizara hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima, lakini vilevile nawashukuru wana Nkasi Kusini kwa namna ambavyo wananipa ushirikiano wakiwepo viongozi wangu wa Chama cha Mapinduzi, Mkurugenzi wangu Kaondo, DC wangu Kimantra na wananchi kwa ujumla.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naungana mkono na watu wote wanaosema kazi ya Wizara hii ni nzuri na Mheshimiwa Muhongo pamoja na Naibu wake Mheshimiwa Kalemani wana uwezo wa kutosha na wanafanya kazi vizuri sana. Mimi bahati nzuri niko kwenye Wizara hii, naona uongozi wanaoutoa kwetu sisi ushirikiano kama wana Kamati, lakini pia kwa Wizara nzima. Kwa hiyo, tunawatia moyo na kuwapa big up, waendelee.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine la muhimu ni kwamba katika kazi ya kupeleka umeme vijijini, yapo maeneo yamebaki nyuma. Kwa mfano, tunaposema umeme mkubwa Gridi ya Taifa, Mikoa kama ya uzalishaji ya kilimo kama vile Rukwa na Katavi wamechelewa na Kigoma pia hawajapata. Tunaomba Wizara ifanye juhudi kuhakikisha kwamba tunapata umeme mkubwa ili tuweze kusisimua maendeleo katika maeneo yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo ya Mkoa wa Rukwa yako hodari kwa kilimo, namna pekee ya ku-attract wawekezaji katika kuongeza thamani ya mazao yetu ya kilimo ni kupatikana kwa nishati ya uhakika. Vilevile katika maeneo ya Namwele, Komolo II pale kwenye Jimbo langu, kuna deposit ya kutosha ya makaa ya mawe, muichunguze, ambapo inaweza ikasaidia kuongeza umeme katika Gridi ya Taifa kama inapita sehemu hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo mengine ambayo tunahitaji kupata umeme ni vijijini kwa kupitia REA. Kusema ukweli utekelezaji wa REA Awamu ya Kwanza na ya Pili kwa Wilaya yangu na Jimbo langu, umetia moyo sana wananchi kwa utekelezaji wa Serikali hii. Kwa hakika ni kitu ambacho tumejivunia hata kurudi hapa Bungeni. Nawapongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kosa tu ninaloliona ni kwa Serikali kutopeleka pesa ya kutosha inayotengwa kwa REA. Hiki kimekuwa kikwazo kikubwa ambacho kinarudisha juhudi kubwa zinazofanya na watendaji wakuu hawa wa Wizara huko vijijini. Umeme unakuwa hauendi kwa wakati. Sasa tunaweza tukajidanganya tena, leo tumetenga hela za kutosha, lakini kama mtindo ni huu wa kutowapa pesa, bado tutarudi nyuma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, azma ya kupeleka umeme vijijini, wenzangu wamesema, ni ya muhimu sana, inatusaidia hata kuokoa suala la mazingira. Umeme utakapofika vijijini kote, tutaokoa tatizo la uharibifu wa mazingira kwa sababu litapeleka nishati, ukiachilia mbali ajira na mambo mengine ambayo yametajwa na wenzangu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwangu, mwaka 2015 tulitarajia kupeleka umeme katika Makao Makuu ya Jimbo, Kate, kupitia vijiji vya Kalundi, Miula, Komolo II, Katani, Chonga lakini mpaka sasa umeme haujawaka. Bado vijiji ambavyo vimeorodheshwa tena katika awamu hii, naomba na vyenyewe vifikiliwe, navyo viko katika vijiji vya Tuchi, Kitosi, Sintali, Nkana Mkomanchindo, Kasapa na Kata tatu za Mwambao wa Ziwa Tanganyika. Mheshimiwa Waziri kata tatu za mwambao wa Ziwa Tanganyika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kata tatu za mwambao mwa Ziwa Tanganyika naomba uziwekee umuhimu wa mbele sana, ni maeneo ambayo hayana barabara na kila mara huduma tunawafikishia kwa kuchelewa na wakati mwingine hawapati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi ninavyozungumza, Kata hizi hazina mawasiliano ya simu, hazina barabara nzuri, lakini juhudi na uthubutu wa Wizara hii nafikiri mnaweza mkawahi ninyi. Nawaomba kwa heshima niko chini ya miguu yenu, naomba mwapelekee wananchi hawa ili waweze kuonja neema ya nchi yao. Wananchi hawa wa Kata hizi wamekuwa wakizalisha samaki, wanavuna sana samaki, lakini wanazipeleka Zambia kufuata soko, kwa sababu hatuna uwezo wa kuchakata minofu. Utakapopeleka umeme utatusaidia sana kuhakikisha kwamba sasa wanaweza wakapata wawekezaji ambao wanavutiwa na nishati hii muhimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni geological survey. Mkoa wa Rukwa, una miamba na mazingira yanayofanana na sehemu nyingine nchini, lakini hatuna bahati ya kupata aina yoyote ya madini tunayoshughulika nayo kule.
Kwa hiyo, inaonesha kwamba utafutaji wa madini katika maeneo yale, kazi hiyo haijafanywa kwa juhudu ya kutosha; na tunaona mahali ambapo juhudi zimefanywa watu wanapata ajira, mzunguko wa pesa umekuwa mwingi na wawekezaji wamepatikana katika maeneo ambayo tumeona madini yamepatikana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nawaomba kitengo kinachoshughulika na kazi hiyo, kijaribu kutafuta kwa nini Mkoa wa Rukwa tu pasipatikane madini yoyote ambayo tunashughulika nayo kwa sasa? Hebu tujaribu kuona katika nchi yote, ni eneo gani tunaweza tukanufanika? Ni aina gani ya madini yanaweza yapatikana katika maeneo hayo? Zipo traces na watu wengi wamekuwa wakija wanazunguka zunguka, siyo maalum sana, lakini wanapata na wanasafiri wanarudi. Kwa hiyo, inaonekana kama juhudi ikifanyika ya kutafuta madini, tunaweza tukapata madini ambayo yanaweza kutusaidia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzangu wamesema hapa jiografia inatueleza kwamba maumbile ya miamba yaliyoko Rukwa na yale ambayo yako kwenye eneo la Ziwa Albert kule Uganda ambako kulipatikana mafuta, yana asili moja. Sasa kama yana asili moja, maana yake, juhudi ikifanyika zaidi tunaweza tukanufaika na jambo hilo la kupata mafuta katika Bonde la Rukwa. Kwa hiyo, tufanye hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana kama siyo mwaka juzi, Wizara ilitueleza kwamba kuna leseni ya kutafuta mafuta katika maeneo ya Ziwa Tanganyika, hasa katika Jimbo langu au kule juu; na nimeona juhudi ya hawa watu waliokuwa wanatafuta, lakini sijaona kama imeripotiwa humu kwenye hotuba yako na ningependa kupata maelezo hawa watu hoja yao imeishia wapi? Walisema mnataka leseni msizitoe ili watu waweze kuanza kutafuta mafuta katika maeneo hayo. Sasa ni kitu kimekaa kimya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nikizunguka kwenye ziara yangu, wananchi wananiuliza, nitakosa kupata majibu, kwa sababu wameona ambavyo watu wameenda, wamezunguka sana, lakini sasa nimeona kwenye bajeti hii hakuna kitu kilichotajwa kama hicho.
Mheshimiwa Waziri, naamini udhubutu wako unaweza, tuhakikishe kwamba ziwa lile Tanganyika nalo tukilifanyia kazi vizuri tunaweza tukafanikiwa kupata aina fulani ya madini, kama siyo mafuta na tukanufaika kama hao wengine wenzetu ambao sasa hivi Mtwara wameonesha kabisa matumaini kwamba pamoja na kwamba walikuwa wamebaki nyuma kidogo, sasa hivi wanakuja juu na uchumi wao utapanda kwa haraka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nawashukuru sana, naomba umeme ufike katika Jimbo langu la Nkasi Kusini uwashwe, waya umeshafika lakini bado kuwasha na pengine mnawapa wakandarasi goigoi. Huyu Mchina ambaye anajenga huu umeme kupeleka kwenye Jimbo langu, hata kwa Mheshimiwa Malocha amezungumza hapa, ni mtu nadhani hana uwezo wa kutosha. Mjaribu ku-recruit watu ambao ni wenyeji wetu. Muwatafute wazawa ambao watakuwa na uchungu pia wa uzalendo. Hawa wenzetu, hata mimi nina wasiwasi na vifaa vyenyewe havina specification ya kutosha, wanakuja vina-bounce, vinakuwa haviwezi kufanya kazi vizuri...
MWENYEKITI: Ahsante, tunaendelea.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kupata nafasi. Niungane na wenzangu kuipongeza Wizara kwa hotuba nzuri na naiunga mkono.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo kadhaa ya kuchangia, kwanza ni migogoro ya vijiji vinavyozunguka kando kando ya hifadhi. Nkasi tuna Hifadhi ya Rwamfi Game Reserve, hifadhi hii ilikuwa mali ya Halmashauri, Halmashauri waliamua baada ya kuzidiwa kwamba hawawezi kuitunza wakaipa Serikali, lakini kulikuwa na vijiji kadhaa ambavyo vina migogoro na mipaka ambavyo ni Kasapa, King‟ombe, Mlambo, Mundwe, Namasi, Kata, China na Mlalambo. Vijiji hivi vinaambiwa kwamba viko ndani ya hifadhi, lakini vimekuwepo kabla hata ya hifadhi. Tunaomba sheria ziangaliwe upya ili waweze kurekebishiwa mipaka wapate maeneo mazuri ya kulima kwa sababu watu wameongezeka na kwa uhakika wanahitaji namna ya kuendeleza maisha yao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nilitaka kuzungumza ni suala la uhifadhi, namna ya kuendeleza maeneo ya utalii. Ninyi wenzetu mnaangalia huku tu, jaribuni kuangalia katika mikoa ya pembezoni na Rukwa ni mojawapo. Ukienda kwenye Ziwa Tanganyika kuna ufukwe mzuri sana, ufukwe ambao ni wa ajabu, una kingo za aina aina, mawe yaliyojipanga vizuri, visiwa vizuri lakini hakuna watu wanaowekeza. Nimeona tu kampuni moja kule Kipili kwa Mheshimiwa Keissy ndiyo amewekeza kutoka Arusha, lakini ni maeneo mazuri sana na hayatangaziki kwa sababu Wizara hamfanyi hivyo, barabara zenyewe zinazoteremka katika maeneo haya hazitoi hata motisha kwa mtu kwenda kufika. Kwa hiyo, mtusaidie kuangalia maeneo haya yakitumiwa vizuri yanaweza kutusaidia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, karibu Namanyere kuna eneo linatoa maji moto linaweza likatumika vizuri kwa utalii. Ukienda njia ya Wampembe kuna mahali kuna maporomoko mazuri sana, Halmashauri wameweza kutembelea pale. Ukienda Jimbo la Kalambo kwa Mheshimiwa Kandege kuna eneo linaitwa Kalambo falls, yale maporomoko ni mazuri sana. Wenzetu wa Zambia wamekuwa aggressive wamejenga barabara nzuri wamefika pale wanafikia kirahisi, mwisho watu wanaamini labda Kalambo falls iko Zambia lakini sisi tumeshindwa kujenga barabara tu kusongeza pale na kuweza kuitangaza vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunayo ngome ya Bismark pale Kasanga bado haijatangazwa vizuri na mambo mengine mengi tunaweza tukayaangalia kwa upya, vilevile lugha yetu ya Kiswahili, humu Bungeni tunaiharibu lugha, tungeizungumza vizuri lugha ya Kiswahili ingekuwa kivutio duniani hapa na Bunge lingetoa nafasi ya kuitangaza vizuri zaidi. Tukija humu sasa tunavuruga vuruga tunazungumza Kiswahili siyo Kiswahili tunachanganya na Kingereza basi tunakuwa tunaharibu, bado tungekuwa na utalii mzuri tu katika hili jambo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Utalii lazima iwe dhana pana iangaliwe katika mitazamo mbalimbali, wakati Halmashauri tunajenga miradi mbalimbali tuangalie maeneo ambayo tunayapa vipaumbele. Tuwe na timu ambayo inashauri hata uwekezaji binafsi kwa mfano, kule Nkasi, Kipili, kuna watu wenyewe wanaamua kujenga nyumba za wageni. Je, mnachukua initiative zozote kuwashauri ili wajenge waje na kitu kinachofanana na jengo ambalo mtalii anaweza kufikia?(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wantumia mitaji sawasawa tu inalingana na mataji wowote ambao mtu anaweza akajenga lakini wanakosa utaalam na ushauri wa kitaalam ambao uwekezaji ule ungeweza kufanywa na mtu binafsi lakini ukaleta vivutio au mahali pa kulaza kwa watu ambao wanatutembelea katika maeneo hayo. Kadhalika katika miradi mingine yOyote tungekuwa na dhana pana katika suala zima la utalii, tusiangalie katika eneo moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine la tatu na la mwisho ni huu mogogoro ambao ninauita mgogoro lazima tusiukwepe, mgogoro baina ya wahifadhi, wafugaji na wakulima. Mgogoro huu watu wengi wanauzungumza na tunazungumza hapa katika mitazamo miwili, mitazamo yote iko sahihi. Kuna wanaosema wafugaji wanafanya makosa, wanatuharibia sijui ardhi, wengine wanasema maliasili wanafanya makosa. Serikali lazima myapokee haya, sisi tumechaguliwa na wakulima, wapo waliochaguliwa na wafugaji, lakini haya yote matatizo tumeona athari zake kutokana na Operesheni Tokomeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepata ripoti hapa, tumeangalia madhara ambayo huwezi kuyavumilia. Sasa kama Serikali na jambo hili lazima lije hapa Bungeni lipatiwe muafaka, hiki chombo hakiwezi kukwepa kulizungumza hili jambo, lazima liishe na tuzungumze hapa na msikwepe wajibu, watu wetu wana kufa, watu wetu wanaumia. Vilevile mazingira yanaharibika, mito sasa haitiririshi maji kwa sababu ya ufugaji wa hovyo, kwa nini msije na suluhisho mbona mambo mengine mnasuluhisha?
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali hii naiamini kwa kujenga mikakati ambayo imeshindikana, kwa mfano nimeona katika Serikali hii tumeanza kukusanya mapato mengi kitu ambacho kilikuwa ni tatizo kubwa sana, katika Serikali hii nimeona ufisadi unaanza kupungua, nidhamu kazini imeanza kurejea hili litawashinda. Kaeni muone namna mtakavyoweza kuja na mawazo ambayo yatatusaidia kuondoa tatizo hili. Haiwezekani tatizo likawa linaumiza watu wetu, linaumiza wafugaji, linaumiza wakulima na Serikali isije na suluhisho, mimi siamini katika hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kushindwa kutoa suluhisho katika hili ni kushindwa kutekeleza wajibu wako Mheshimiwa Waziri, ninasema wazi kwamba ni lazima ukae na Wizara zilizo na mahusiano na Wizara yako ili jambo hili ambalo limekuwa kero kwa watu wote liweze kupatia suluhu, hatuwezi kuendelea katika mazingira hayo. Lazima mje na utaratibu, ndugu zangu ni kweli kule Rukwa tulianzisha Azimio la Mto Wisa, tunamkumbuka Mkuu wetu wa Mkoa alikuwa anaitwa Jaka Mwambi, namkumbuka mpaka leo. Mkuu wa Mkoa aliweza ku-manage kuweka wakulima na wafugaji wakakaa pamoja bila ugomvi wowote na wakahitajiana wote, kilichotakiwa kufanyika ni wale wafugaji waliokuwa wanafuga bila kuelewa wafanye nini mifugo yao, wakapata elimu wakaanza kuwekeza, kusomesha watoto, kujenga nyumba nzuri, kuwekeza katika maeneo mbalimbali na hivyo kuvuna mifugo ile ambayo ilikuwa inazidi.
Kwa hiyo, bado hilo linaweza likafanyika, baada ya kuondoka yule Mkuu wa Mkoa, mifugo imefurika kule Rukwa, Mheshimiwa Keissy hapa alizungumza vizuri sana, imezidi uwezo wa ardhi yetu kubeba, lakini kama Serikali wala hatujaona tatizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo hili tumeliona tangu wakati wa enzi ya Serikali ya Awamu ya Kwanza, Awamu ya Pili, Awamu ya Tatu, Awamu ya Nne tulilizungumza sana na kwa wakati fulani nilisikia Rais anasema lazima litafutiwe ufumbuzi. Awamu hii ya Tano kama tutakosa kupata ufumbuzi tutashindwa kuelewa na wananchi watakimbilia wapi? Wataendelea kuuawa? Mtaendelea kuridhika tu watu wanauawa? Kama kweli utakuwa unaendesha Wizara na watu wanazidi kuuawa na hatua zozote hazijachukuliwa sioni kama ni vizuri. Ni vizuri hata kusema nimeshindwa ukaondoka kwenye nafasi, kwa sababu haiwezekani kabisa watu wanauawa tukatoa, lazima tutoe suluhisho na nafasi hiyo lazima ukae ujenge hoja ya msingi, wewe ndiyo sasa tumekupa dawati la mbele la kusuluhisha hili. Wizara yako na wengine wote Serikalini lazima mliangalie hili hatuna namna ya kufanya, hatuwezi kumwambia mkulima ndiye aje hapa aseme, hapana ni lazima tuseme na chombo cha kusemea ni sisi hapa. Hatuwezi kukaa katika makundi mawili tunashindana hapana ni kukaa mezani na kutafuta suluhu ya jambo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja, naomba suala hili liwe na mwisho wake inawezekana mkiamua, kama hamjaamua haiwezekani. Ahsante.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na niunge mkono hoja mapema.
Mheshimiwa Naibu Spika, naanza na kumpongeza Waziri pamoja na Naibu Waziri na watalaam wake wote kwa kutuandalia Bajeti nzuri. Inaonyesha wazi kwamba, Mheshimiwa Rais anaanza kutembea kwenye kauli zake wakati wa kampeni za kuleta maendeleo kwa haraka. Kitendo cha kutenga asilimia 40 ya Bajeti yetu na kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo, kinataka Tanzania iruke, kwa maana ya kuleta maendeleo ya haraka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pesa nyingi zimeelekezwa huku, nishauri kabla sijatiririka kwenye miradi. Nidhamu ndiyo muhimu, tunaweza tukajidanganya tukatenga pesa nyingi, lakini kama nidhamu itakuwa kama nilivyozoea kuona katika miaka miwili, mitatu iliyopita haitotusaidia na Wizara ya Fedha hii ndiyo imekuwa ikichelewesha kupeleka fedha za miradi katika maeneo mbalimbali. Kwa hiyo, naomba nidhamu iwe ndio kitu cha kwanza kabisa cha kuangalia. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la Kilimo, Serikali au Bajeti yetu imetenga zaidi ya Shilingi trilioni 1.56 sawa na asilimia 4.9. Pesa hii, kwangu naona ni ndogo hasa ukiangalia Matamko mbalimbali ya Kimataifa ambayo tumeridhia ikiwa mojawapo ni Tamko la Maputo kwamba, nchi zetu zinatakiwa zitenge angalau asilimia 10. Kwa hiyo, asilimia nne, bado tuna safari ndefu na naangalia asilimia nne imepungua hata kwa kulinganisha na mwaka jana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kilichopo hapa ni kwamba, kilimo hakijapewa mkazo na huku hiki kilimo ndicho tunachotegemea kukomboa nchi yetu. Kupitia kilimo, tumeajiri zaidi ya watu asilimia 70 ya Watanzania wetu, kupitia kilimo ndiyo sasa tunaingiza pesa nyingi za kigeni, lakini ndio Pato la Taifa zaidi ya asilimia 25 tunapata kupitia kwenye bidhaa za kilimo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba juhudi ifanyike kama hatutaweza mwaka huu, basi mwaka ujao tuongeze pesa zaidi katika kilimo. Kilimo hiki kina-support watu wa vijijini, ndiyo wapiga kura wetu hao waaminifu na ambao wamekuwa wakitekeleza sera zetu kwa utaratibu mzuri zaidi kuliko sehemu nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, watu hawa wamekosa maji, watu hawa wamekosa zana bora za kilimo, wamekosa kupata pembejeo kwa wakati. Nategemea Bajeti hii itajikita katika maeneo hayo na kuhakikisha kwamba, tunapata huduma bora katika wakati muafaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, lipo suala la Afya; katika maeneo yote nchini tumeshakubaliana kwamba tujenge Vituo vya Afya, tujenge Zahanati na huduma zitolewe. Katika eneo langu la Mkoa wa Rukwa na kupitia Taasisi mbalimbali za Kitaifa, imebainika akinamama na watoto, vifo vyao viko juu. Plan International, Africare pamoja na Taasisi zingine kama Benjamin Mkapa, wamebaini kwamba, vifo vya akinamama na watoto viko juu sana. Taasisi hizo wameweza kujenga Zahanati, Vituo vya Afya kadhaa, tumebaki sisi Serikali kuweka vifaa katika vituo vya afya na mojawapo ni Kituo cha Afya cha Kala ili huduma ziweze kupatikana za kuokoa akinamama ambao wanapoteza maisha bila sababu za msingi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba bajeti hii iende kujibu matatizo haya, tuitafisiri bajeti katika kuona kwamba, Zahanati zinaongezeka, Vituo vya Afya vinaongezeka, Watalaam wanaongezeka; hawa ni pamoja na Waganga, Nurses na Watalaam wa Maabara tuwaone wameongezeka katika vituo vyetu vya afya, watoe huduma bora ili wananchi waweze kupata afya nzuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine ni eneo la elimu, eneo la elimu limetengewa pesa nzuri. Naipongeza Serikali zaidi ya asilimia 22.1 ya bajeti, juhudi hii ni kubwa. Tafsiri yake ningependa kuona, tuione kuanzia Shule za Msingi kwamba Walimu hawa wanaokaa katika mazingira magumu, sasa miundombinu yao inaanza kuboreshwa kuliko ilivyo sasa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Jimbo langu, Mwambao wa Ziwa Tanganyika, Walimu ni wachache, hawana nyumba, ofisi zao hazipendezi, kwa hiyo, kwa uhakika huduma inayotolewa inakuwa haitoshelezi, naomba juhudi hizo zifanyike. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mwisho ni umeme, mwaka jana tulitenga pesa nzuri sana kwenye umeme lakini matokeo yake hatukuweza kufanikiwa kwa sababu pesa hazikutolewa kwa haraka. Naomba kupitia bajeti hii, ambayo kwa hakika tumetenga hela nyingi kwenye umeme basi ielekeze katika maeneo ambao yako remote zaidi. Mwambao mwa Ziwa Tanganyika kuna umaskini mkubwa, lakini kuna Ziwa Tanganyika ambalo limesheheni samaki wengi na wananchi wa eneo hilo wote wanapeleka samaki Zambia.
Nimelisema hili mara kwa mara, naomba mikakati iliyopo ya Wizara ya Nishati na Madini waanzie katika eneo la Ziwa Tanganyika katika Jimbo la Nkasi Kusini kuhakikisha kwamba umeme unafika huko ili wananchi hawa waachane na hali ya sasa ya upagazi ya kupeleka samaki Zambia badala ya kupeleka katika nchi yao. Tuweze ku-attract wawekezaji katika eneo letu, itatusaidia zaidi katika kuboresha uchumi wa nchi yetu lakini pia uchumi wa Taifa zima kwa ujumla. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niungane na wenzangu kusema kwamba, ile kodi inayotokana na mafao ya mwisho ya Waheshimiwa Wabunge haikubaliki. Haikubaliki na wenzangu wameieleza kwa ufundi mzuri zaidi, tutafute vyanzo vingine bado tunaweza tukavipata, tunaweza tukapata na itatusaidia. Vilevile pesa iliyotengwa kwa CAG ni ndogo, namna ya kukabiliana na ubadhirifu itakuwa ngumu sana na itakuwa kitendawili. Naiomba Wizara iangalie kwa umakini zaidi ili pesa…

NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Mipata, muda wako umekwisha. Mheshimiwa Ignas Malocha, atafuatiwa na Mheshimiwa Prosper Mbena.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kuunga mkono hoja. Jimbo la Nkasi Kusini lina mbuga iitwayo Rwamfi Game Reserve. Katika mipaka ya mbuga hii kuna migogoro kati yake na vijiji jirani kwa Jimbo la Nkasi Kusini, vijiji vya King‟ombe, Mlambo, Kasapa, Ng‟undwe, Namansi na vijiji vya China na Nkata.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vijiji vyote hivi vimekuwepo kabla ya kuanzisha Hifadhi hii, lakini wahifadhi wamekuwa wakidai kuwa wananchi wanaishi ndani ya hifadhi. Naishauri Serikali ije na mkakati mpya kuangalia kwa upya mipaka ya mbuga hii ili kuleta uelewano na vijiji jirani na kuondoa usumbufu unaotokana na wahifadhi kusumbua wananchi ikiwa ni pamoja na kuwapiga. Wananchi hawaelewi kwa nini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hifadhi imevikuta vijiji hivyo vyenye haki na huduma zote za kijamii ikiwa ni pamoja na shule za sekondari, zahanati na vingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la vijiji hivi halitoshi pia kwa shughuli za kuendesha maisha. Tunaomba sehemu ya mbuga hii ipunguzwe kutoa eneo la kilimo kwa kilimo zaidi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kuunga mkono hoja. Nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa utendaji mzuri, yeye na Naibu Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara na Watendaji Waandamizi wa Wizara. Kazi inayofanywa na Wizara inaonekana na inaheshimiwa kwa umma wa Watanzania. Hongera sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimboni kwangu nina barabara mbili za Kitosi - Wampembe yenye urefu wa kilometa 68 na ile ya Nkana – Kala yenye urefu wa kilometa 67. Barabara hizi zote mbili za Mkoa wa Rukwa, kupitia Bodi ya Barabara na RCC tuliomba zipandishwe hadhi na Kamati ya Kitaifa ilikuja na kuridhia. Aliyekuja ni Katibu Mkuu wa sasa wa TAMISEMI (Mussa Iyombe), lakini hazijapandishwa licha ya Serikali kupandisha hadhi barabara nyingi nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba zipandishwe hasa ya Kitosi na Wampembe. Mheshimiwa Rais alitoa ahadi kusaidia barabara hizi na wakati alipokuwa Waziri, aliweza pia kutoa fedha shilingi milioni 500 kwa barabara ya Kitosi na Wampembe kuboresha matengenezo. Nashangaa hamjaipatia fedha ya kutosha na inaenda mipakani. Naomba iongezewe fedha, sh. 84,000,000/= hazitoshi. Inaweza kusababisha barabara kufunga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Kata ya Kala ipate mawasiliano ya simu. Ni Kata iliyoko mpakani mwa Ziwa Tanganyika. Nimefanya ufuatiliaji mkubwa bila mafanikio. Je, ni lini Mheshimiwa Waziri atanisaidia Kala iwe na mawasiliano?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bandari Kata ya Ninde, Wampembe na Kala ziko kando ya Ziwa Tanganyika, hazina bandari hata moja. Kuna umuhimu mkubwa kupata Bandari Wampembe na pia kujenga Gati Ninde na Kala ili wananchi waweze kupata huduma ya usafiri wa meli kwa usalama. Kwa hiyo, nawasilisha maombi Serikalini kuwa bandari ijengwe Wampembe na gati zijengwe Ninde na Kala. Ahsante.
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba ya Wizara hii ni nzuri na Waziri na Naibu Waziri wanafanyakazi vizuri kabisa. Tunawatia moyo muendelee kuwa wabunifu na kusimamia maadili ya wafanyakazi walio chini yenu. Pamoja na kuunga mkono hoja nina mambo yafuatayo kuishauri na kuiomba Wizara kwanza Nkasi tuna uhaba wa watumishi wa afya yaani madaktari, wauguzi na wataalam wa maabara. Kwa vile tuko pembezoni hali siyo nzuri, tusaidieni watumishi hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Nkasi huduma hutolewa kwenye zahanati chache kabisa, wananchi wamejenga maboma zaidi ya 30 Wilaya nzima hayajamaliziwa yanahitaji kuezekwa, tunaomba bati ili wananchi waielewe Serikali iliyowahimiza wajenge na majengo yao yataezekwa.

Mheshimia Mwenyekiti, Hospitali ya Wilaya iliyopo inamilikiwa na Wamisionari na usimamizi wa huduma siyo mzuri kabisa. Naomba mtusaidie tujenge hospitali yetu, huduma hazitolewi kwa msingi ya maadili hata mchango wa Serikali hauwanufaishi wananchi wa Nkasi ipasavyo.

Mheshimia Mwenyekiti, Nkasi bado kuna ukoma hasa maeneo ya mwambao mwa Ziwa Tanganyika. Naomba Wizara itambue jambo hilo na kuongeza huduma katika eneo hili. Pia dawa bado hazitoshelezi, nashauri fedha za dawa ziongezwe zaidi. Aidha, walemavu wawekewe utaratibu wa kutibiwa bure, hii ikiwa ni pamoja na walemavu wa ngozi (albino), walemavu wa ngozi wanashida sana huko vijijini na hapajawa na ufuatiliaji toka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya nchini kote. Naomba ufuatiliaji uwe unafanyika, watambuliwe na wasimamiwe huduma za ushauri na matibabu yao.

Mheshimia Mwenyekiti, Nkasi kuwa pembezoni kuna vifo vingi vya akina mama na watoto. Hatuna vituo vingi vya afya hasa Jimbo la Nkasi Kusini. Naomba Serikali iweke miundombinu kwenye kituo cha afya cha kata ambacho kilijengwa na Benjamin Mkapa Foundation ili huduma ziweze kuanza kutolewa kama ilivyokusudiwa.

Mheshimia Mwenyekiti, nina maombi maalum, naomba gari ya wagonjwa katika kata ya Kala lipatikane ili kupunguza vifo vingi vinavyotokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu ni watumishi wa afya walioonekana wana vyeti visivyokuwa halali wachunguzwe vizuri ili wale wenye weledi wasaidie kupunguza upungufu kwa masharti mapya, wale wasiofaa waachishwe kazi kabla ya kufukuzwa, haya ni maoni yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Kitengo cha MOI kinachotoa matibabu ya mifupa, kiangaliwe hakina huduma nzuri na wauguzi na hata madaktari hawana maadili kabisa. Watu wanapoteza maisha wakati mwingine bila sababu za kutosha, nina shaka huenda kuna shida ya kuhitaji visenti ingawa sina ushahidi, hii ni kutokana na urasimu uliopitiliza wa kupata kitanda hata kwa mgonjwa ambaye hajiwezi kabisa.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Nishukuru pia Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza Viongozi wa Kamati zote mbili kwa namna walivyotoa taarifa zao nzuri na inaonekana kwa kweli ni taarifa nzuri za kufanyia kazi. Katika kuunga mkono nina maeneo mawili ya kuchangia na nikipata nafasi naweza nikachangia eneo la tatu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la kwanza ni suala la Utawala Bora. Suala la utawala bora kwa kadri wenzangu walivyokwisha kulisema kwa kweli ni kitu ambacho siyo cha ku-acquire mtu hivi, ni kitu ambacho lazima mtu aandaliwe. Ni vizuri Viongozi wakapata mafunzo, bila kuwapa mafunzo mambo yataenda mchakamchaka lakini athari zake mtaziona kubwa mno. Hii haitatusaidia katika nchi. Watu wapate mafunzo katika ngazi zote kuanzia Vijiji, Wilaya Mikoa na Taifa, ni muhimu sana. Natoa mfano mmoja wa jambo ambalo limeniathiri, katika eneo langu ambalo nadhani ni maagizo ya kupokea halafu watu hatuwezi kukaa tukaona athari ili tuone tunaweza tukashauri ngazi za juu namna gani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kwanza, nina shule yangu moja inaitwa Mirundikwa, shule ya Sekondari. Shule hii imejengwa kwenye majengo ambayo yaliachwa na Jeshi miaka ya 1998. Kwa kutoa barua kukabidhi vijiji kwamba eneo hilo linaachwa na Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ligawiwe vijiji na mimi nilikuwa kwenye Kamati mojawapo ya kugawa vijiji vinavyozunguka eneo lile lililobaki. Eneo hilo lilikuwa ni shamba la Mirundikwa State Farm zamani, Wanajeshi walipoingia mwaka 1998. Walipoingia na kukomesha shughuli zao mwaka 1998 wakaliacha eneo na Halmashauri mwaka 2000 wakaanza kulitumia, tukagawana na kuanza kujenga miundombinu, tukajenga shule nzuri sana ya sekondari katika suala la kuondoa kero hizi za elimu kulingana na jinsi mnavyotuagiza. Tumejenga shule nzuri sana, imefikia kiwango cha form six.
Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi tumeambiwa kwamba tarehe 1 Januari shule hiyo inafutwa, itafutwe sehemu nyingine Wanajeshi wanaenda pale. Shule hii ilikuwa inafanya vizuri sana katika Wilaya ya Nkasi, ni moja kati ya High School iliyokuwa inafanya vizuri sana. Takwimu zinaonesha tu hapa mwaka jana kulikuwa na mchepuo wa HGK, HGL na HKL, wasichana peke yake walikuwa 32, division one tulipata wanne shule ya kwanza hiyo, division two tukapata 14 na wote waliobaki ni division three. Kwa hiyo ilikuwa ina-perform vizuri sana na wananchi wakaiunga mkono wakaendelea kujenga miundombinu mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa wametuparaganyisha kwa maagizo ya haraka kwamba sasa shule itoke ili lianzishwe jeshi hapo. Sisi tunaomba mtuachie hii shule tumeijenga wenyewe, katika kutafuta wananchi wetu waweze kupata elimu, waweze kuishi maisha bora. Hata hao wanaotoa maamuzi kama wasingepitia shule, wasingekuwa na ubavu wa kutoa maamuzi haya. Jambo hili mimi limeniumiza sana katika eneo langu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka kusema kwamba, athari zimepatikana kubwa zaidi ya watoto mia tatu hamsini na kitu hawana pa kwenda, wamepata athari ya kisaikolojia, wanaanza kwenda shule moja, moja wamegawanywa kwenye shule mbalimbali za Wilaya yetu jambo ambalo litapunguza sana performance yao. Sasa jambo hili lazima kuliangalia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi inalazimika leo kutenga bajeti yake imetumia zaidi ya milioni 50 kutoka kwenye vyanzo vyao kwa hiyo haiwezi kuendesha shughuli zake zingine. Kwa mujibu wa Mthamini ni zaidi ya milioni 871 zinatakiwa, hii milioni 871 zinatakiwa ili kurejesha miundombinu kwenye shule ambayo tunaijenga upya ambayo tunajenga katika eneo la Kasu. Sasa wananchi waliokuwa wamemaliza shughuli zao, wamemaliza wakaanzisha mpaka shule ya high school leo wanaanza upya, Serikali haina mchango hata kidogo, kwa kuanza upya hii ni athari kubwa sana na watu wameathirika na kwa namna hiyo hawawezi kuipenda Serikali yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maamuzi ni mazuri lakini utaratibu huu unaweza kuwa na lengo zuri la kiusalama lakini athari zinazopatikana kwa wananchi mziangalie nazo. Halafu shule hii ni ya wananchi, tumejenga wenyewe na hawajatushirikisha kutoa mawazo ili shule hii iendelee. Naomba Waziri anayehusika hili jambo aliangalie kwa makini sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tuna athari kubwa, Halmashauri na wananchi wana kipato kidogo, walijikusanyia wakajenga miundombinu mingi mpaka ikawa shule nzuri yenye Kidato cha Sita sasa hakuna shule tena. Maeneo ya Jeshi yapo, ungesema acheni sekondari tafuteni maeneo mengine sisi tungewapa eneo lingine, kwa nini msifanye hivyo mchukue shule yetu? Haiwezekani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pale Luwa Sumbawanga kuna eneo ambalo lililkuwa la Jeshi zamani na halijaathirika chochote na lipo mpaka sasa, waliliacha kama la kwao na wala hawakulikabidhi kwa wananchi. Kwa nini wasichukue hata eneo hilo lingeweza kufanya hiyo kazi? Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Rais aisikie habari hii na Viongozi wote ambao mnahusika mtuchangie, kama mnataka lazima iwepo shule Wizara ya Elimu leteni hela. Wizara ya Ulinzi ambayo mnataka tujenge sekondari pale leteni hela! Waziri Mkuu uliyeamua katika utekelezaji wa shughuli za Serikali shule yetu ifutwe tuliyojenga wenyewe tuletee pesa tujenge kwenye Sekondari yetu ya Kasu. Wananchi wanafanya kazi za kilimo na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni suala hili la Utawala Bora. Kuna kijiji changu kinaitwa kijiji cha Kasapa, ni kijiji cha asili kilianzishwa miaka ya 1960. Mwaka 2010 kwa Tangazo la Serikali Na. 301 kimekuwa kijiji kamili na sisi tunategemea kilimo. Juzi tarehe Mosi mwezi Januari watu wa TFS wameenda kusema kijiji hiki kiko kwenye msitu wao, maeneo yote ya watu wanayolima ambayo ni mashamba wamesema ni maeneo yao, kwa hiyo, mazao yamefyekwa katika maeneo yale! Katika kipindi hiki ambacho hali ya chakula ni tete!
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimejaribu kuongea nao na wakati huo nikaenda hata kwa Mkuu wa Mkoa kuona uwezekano wa maeneo hayo ambayo zaidi ya hekta 2000 zimelimwa mahindi wayaachie angalau miezi minne ili waweze kuvuna na kuondoka kama ni lazima wakati taratibu nyingine zinafanyika. Wamenikatalia, sikusikilizwa hata na Mkuu wa Mkoa kwa kweli!
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili limenifadhaisha na limefadhaisha wananchi. Kijiji kile kilitupa kura sisi, mimi na Mheshimiwa Magufuli kiwango cha juu, tuseme watu wote walitupatia kura. Leo hii wanashangaa kuona Mbunge wao hana uwezo wa kutetea jambo hilo angalau kwa miezi michache! Hatujasema tumekataa, tumesema angalau miezi ambayo watu wamelima mazao tayari! Kwa nini wafyeke mazao yote! Nimeenda kushuhudia wamefyeka ekari 15 zaidi ya hekta 2000 kwa mujibu wa Mhifadhi mwenyewe na yenyewe wamesema hakuna mtu wa kuingia na hakuna mtu anayeingia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Kaya 395 zimeathirika na wala hawaendi shamba wamekaa tu. Watu zaidi ya 2000 ambao wanategemea kilimo katika kijiji kile hawatakuwa na chakula, mjiandae kutuletea chakula.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimejitahidi kwa kadri nilivyofanya, nimeshirikiana na DC, nimeshirikiana na Mkuu wa Mkoa, lakini haikuzaa matunda! Nikaenda kumwona Mtendaji Mkuu wa TFS nikamwelezea hoja anaielewa, lakini anakuwa mwoga nadhani bila shaka, baadaye alisema hapana, imeshindikana! Hii ni kuogopa! Mazingira yanayofanywa na Watendaji mimi nafikiri ni ya uwoga bila sababu kwa sababu, Mheshimiwa Rais ni Kiongozi ambaye anataka utawala wa uwajibikaji…
MWENYEKITI: Ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii namshukuru pia Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima, naungana na wenzangu kuchangia katika taarifa za Kamati hizi mbili. Mimi ni mmoja kati ya Mjumbe wa Kamati ya Nishati na
Madini. Nianze na taarifa hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Waziri na watendaji wake wote pamoja na Naibu Waziri kwa kazi nzuri wanayoifanya na kwa hakika inaonekana kwa Watanzania, isipokuwa kitu kinachokwamisha ni pesa zinazotolewa zinawafanya majukumu yaliyopangwa yasifikiwe kwa
wakati, lakini juhudi tunaiona. Kwa hiyo, niishauri Serikali kuhakikisha kwamba katika eneo la usambazaji umeme na kwa vile tumejitangazia kila mahali umeme ufike pawepo nidhamu ya utoaji wa fedha kuendana na utaratibu wa kibajeti kwa mwaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu wananchi tulishakubaliana kwamba tunatoa tozo kwenye mafuta, pesa ambayo ingeenda kwa mwananchi, tunamkamua ili pesa iende kwenye usambazaji wa umeme. Kwa hiyo, hatuna sababu ya kukosa pesa kwa jukumu hili. Lakini nisifie kwamba katika usambazaji wa umeme sisi Wilayani Nkasi tumepata umeme katika vijiji vya Kundi, Kibande, vijiji vyote mpaka kufika Namanyere kwa barabara hiyo, lakini bado tatizo la usambazaji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukifika pale Nkundi, Kipande, Katawa, Milundikwa, Chala, Kasu, Kacheche na Kanondokazi, wapo wananchi wengi wanahitaji umeme na wanagombana leo haujawafikia. Umefika kijijini, lakini haujafika angle ile pale na ile pale.
Pawepo utaratibu maalum wa usambazaji, ili wote wanaohitaji umeme waweze kupata, hilo la kwanza. Na wengine hapa wanaingiza siasa, yupo Mwenyekiti wangu mmoja wa Nkundi pale anasema aliyezuwia tusipate umeme upande huu hapa ni Mheshimiwa Mipata, lakini ana
sababu zake. Naomba tugawane, ni sungura mdogo lakini tugawane wote. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, yapo maeneo pia ya kupeleka umeme ambayo bado katika eneo langu, kama Kata ya Sintali, Kata ya Ntuchi, Wampembe, Ninde, Kizumbi, Kala na vijiji ambavyo vilisahauluka katika Awamu ya Pili, vijiji hivyo ni Katani, Malongwe, Komolo IIpamoja
na Kisura. Ni vijiji ambavyo viko jirani sana na maeneo umeme unapita kwa hiyo, wanauangalia tu hivi. Jambo hili si jema sana, linawatia simanzi na wanaona wakati mwingine ni kama tumewafanyia jambo ambalo sio lenyewe, kumbe sio kwa nia mbaya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri alipotutembelea niliweza kumfikisha kijiji cha Wampembe na njiani kote huko aliona jinsi watu wanavyohitaji umeme. Na wamebaki na matumaini na kila mara tukiwaambia Awamu ya Tatu inafuta machozi yenu wote, wote
wamekuwa hawaamini. Kwa hiyo, naomba awamu hii ianze mara moja ili maeneo haya niliyoyataja yote yaweze kupata umeme, hasa njia ndefu ya kupeleka mwambao wa Ziwa Tanganyika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kipo Kitengo cha Utafutaji wa Madini, mimi kama Mjumbe wa Kamati hii tumekuwa tukizunguka huku na kule tunaangalia jinsi wananchi wanavyopata ajira katika uchimbaji wa madini mdogo mdogo.
Mheshimiwa Naibu Spika, wachimbaji wadogo wadogo inaonekana ni ajira ambayo kwa kweli, fursa hiyo sehemu nyingine hatuna, naomba kitengo hiki kije kitafute Mkoani Rukwa, tuna madini yakutosha, lakini hawajatafuta. Tumemuomba Waziri kwenye Kamati kwamba watupe potentials zilizopo ili wananchi wenyewe waangalie na kama kuna mashirika mengine ambayo yanaweza yaka-chip in waweze kuangalia katika maeneo haya kwa sababu tumeona ni muhimu sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni barabara. Naungana na wote wanaosema kuna kazi nzuri ya barabara inayofanyika na sisi tuna barabara ya lami kutoka Sumbawanga kwenda Kibaoni inajengwa vizuri sana kwa kiwango cha lami na kasi imeongezeka. Sasa hivi
barabara inasogea pale Kichala na nyingine inatoka Kibaoni, imeshafika Namanyere tayari kwa hiyo, bado kipande kidogo sana. Naomba wasisimame, kasi hii iliyopo sasa iendelee ili wakamilishe hiyo barabara tuweze kunufaika na wananchi waweze kunufaika na matunda ya
Chama cha Mapinduzi, wasisimame, watusaidie. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hizi pia zipo za Halmashauri ambazo zinatusumbua. Kuna barabara ya Kitosi - Wampembe, ambayo Mheshimiwa Rais kabla hajawa Rais aliweza kunipa shilingi milioni 500, nayo inaanza kusuasua na wataalam wameanza kuitengea hela
kidogo kidogo, naomba waendelee kuitengea. Alipokuwa kwenye Wizara walitenga hela ya kutosha, sasa hivi hawatengi, nitawashitaki kwake. Hakikisheni kwamba mnatenga ya kutosha. Iko Barabara ya Ninde - Namanyere na Barabara ya kutoka Kasu kwenda Myula, bado
inasuasua sana hii, mtusaidie bila kuacha ile ya kupeleka Chamiku pamoja na maeneo mengine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lipo suala la mtandao wa simu. Suala la mtandao wa simu kwa kweli limekuwa ni huduma muhimu. Kata yangu moja ya Kala imekuwa haina kwa kipindi kirefu na sasa hivi wanaonekana kama wametengwa na wanajimbo wengine na Watanzania kwa
ujumla.
Naomba nitumie nafasi hii kumuomba Waziri, amekuwa akitoa ahadi kila wakati, lakini wananchi hawajapata eneo la Kala, hata wale wa eneo la Wampembe na Ninde wamekuwa wakipata on and off; on and off! Wakati mwingine unasimama wakati mwingine unapatikana!
Sasa haitusaidii sana, tunaomba huduma hii imekuwa muhimu kibiashara, katika huduma za jamii, katika kuhimiza mambo ya kiafya kwa hiyo, ni muhimu iende kila mahali sawia itatusaidia sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo naomba nimalizie kwa kusema kero moja, kijiji changu, kijiji cha Kasapa wananchi wake wamelima mashamba, yale mashamba yamefyekwa na wahifadhi wa Msitu wa TFS. Jambo hili limekuwa kero sana na nilipojaribu kufuatilia sana wale jamaa ni wakatili sana, wameshindwa hata kuwaruhusu wananchi wakatunze mazao zaidi ya hekta 2000 ambazo wameshalima. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, wanakijiji wote wanashinda kijijini hawaendi kutunza mazao yao, jambo ambalo ni kero kubwa sana na kwetu kwa kweli mvua zinanyesha vizuri, naomba sauti hii ifike kwa wahusika wote, waruhusiwe tu wakatunze saa hizi mazao yao ili
wasife njaa, hawana kimbilio lingine lolote zaidi ya kilimo ambacho wanatumia jasho lao. Zaidi ya kaya 395 na watu 2,500 wanakaa hawaendi shamba kwa sababu msitu umezunguka. Na sababu ni kwamba, msitu wenyewe walikuwa hawajaweka vibao. Juzi ndio wanatuwekea
vibao mpaka mlangoni, jambo ambalo wananchi hawapati nafasi hata ya kutoka mlangoni kwenda kulima. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hii ni kero na kijiji hiki kwa kweli kilifanya vizuri hata kwenye uchaguzi. Mimi nilipata kura zote, Mheshimiwa Rais alipata kura zote. Leo hii wanapoona matendo kama haya yanayofanywa na watendaji wao wanakuwa wanasema kwa kweli,
labda Serikali imetuchukia, kumbe Serikali hii ni ya wanyonge, inasikia sauti, nafikiri sauti hii ataisikia Mheshimiwa Rais na atatoa maelekezo. Nimeenda kumuona Mkuu wa Mkoa hajanisaidia katika hili. Naomba maelekezo yatolewe ili waweze kusaidiwa angalau wakavune mazao yao. Sisemi wakae siku zote, hii ni masika na ajira yao ni hiyo, kwa hiyo, mashamba zaidi ya hekta 2000 yamekaa bila kutunzwa tutegemee kutakuwa na njaa ya ajabu Mkoa wa Rukwa ambayo sio stahili yake.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo nakushukuru sana kunipa nafasi hii, Mungu akujalie sana. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mwenyezi Mungu na nakushukuru wewe kunipa nafasi. Naomba nichukue nafasi hii kutoa shukrani za dhati kwa Ofisi ya Spika, Waziri Mkuu, Wabunge wenzangu, kwa salamu za faraja mlizotupatia tulipompoteza Mama yetu mwezi wa Pili. Tulipokea msaada mkubwa sana tunashukuru sana, hasa ule mfuko wa faraja Mungu awabariki na
tunamwombea mama yetu apate mapumziko ya milele. Amina.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kabisa kuunga mkono hoja na nina sababu; kwanza natambua kazi nzuri zinazofanywa na Serikali hii ambazo ni kushughulika na mambo mengi ambayo yalisuasua zamani. Tumeona wahenga wanasema kila zama na kitabu chake, ni hakika
kitabu cha Awamu ya Tano kitakuwa cha pekee kidogo na upekee wake ni namna Serikali ilivyojipanga kushughulikia matatizo mbalimbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona suala la madawati lilikuwa sugu mashuleni limepata ufumbuzi wa haraka kabisa. Tumeona ubadhirifu Serikalini umepata ufumbuzi wa haraka kabisa ingawaje unaendelea, Utumishi wa Serikali umekuwa na nidhamu, uamuzi wa kuhamia Dodoma wa haraka kabisa, umesuasua miaka mingi. Tumeona dawa za kulevya zikishughulikiwa kwa haraka. Kwa hakika wananchi wa
Jimbo la Nkasi Kusini wameniambia niunge mkono juhudi zote zinazofanywa na Serikali hii kama mabosi wangu walionileta hapa kuwawakilisha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ajenda yetu sasa ni viwanda na katika Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ukurasa wa 19, Ibara ya 28, imezungumza suala la uchumi wa viwanda. Katika uchumi huu wa viwanda, historia inatuambia mahali ambapo viwanda vilianzia kulikuwa na maandalizi muhimu sana kwanza na mojawapo ni elimu. Elimu lazima iwe na msisitizo wa sayansi na teknolojia, masomo ya kisayansi lazima yawekewe msisitizo mkubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ninavyozungumza hapa Wilaya yangu ya Nkasi, Walimu wa Sayansi wako 14 tu katika shule 22, kati ya hizo nyingine zina kidato cha kwanza mpaka cha sita. Kwa hiyo, hatuwezi kufanikiwa kama walimu wa sayansi hatuwapati, walimu wa ufundi hatuwapati, hatuwezi. Kwa hiyo, naomba tuleteeni walimu ili tushiriki katika uchumi ambayo ni ajenda yetu ya sasa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile hatutaweza kufanya vizuri katika kilimo. Kilimo kinahitaji elimu, kilimo kinahitaji sayansi na jinsi kilimo kinavyosukumwa katika nchi hii, niko miaka sita sasa Bungeni, sijaridhika. Naona kilimo kama kinasuasua kila siku, kinaenda ili mradi kiende, wakati kilimo mchango wake kwa pato la Taifa ni mkubwa, mchango wake kwa ajira ya Watanzania ni mkubwa na kilimo ndicho kitakachoendeleza ajenda hii ya viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika uanzishwaji wa viwanda Ulaya, kitu cha kwanza ilikuwa mapinduzi katika kilimo ili kutengeneza ready market. Maana watu wakilima vizuri watakula chakula, watazaliana, watakuwa sasa wananunua chakula hicho, bidhaa mtakazozalisha kwenye viwanda, watakuwa na afya na nguvukazi itakuwepo. Sasa kwa nini kilimo kinasuasua miaka yote na kinabeba watu wote wanyonge? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeshauri watu wanaopelekwa kwenye kilimo kusimamia wawe wakakamavu na hatua zichukuliwe. Kwa nini mkulima apate mbolea kwa kuchelewa? Sababu zinakuwa zinatolewa lakini zote hazitoshi zote. Naomba ufike wakati tuchukue hatua kakamavu, hasa katika suala la ucheleweshaji wa pembejeo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mchezo pia katika utoaji wa pembejeo zinakuwa fake, wenzangu wamesema. Mwaka huu mimi ni mmojawapo wa watu walioathirika, nilinunua madawa fake ya kupalilia, ya magugu, jambo hili si jema sana na wasimamizi mpo, vitu hivi vinarudisha wakulima nyuma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maeneo ya utafiti wa mambo ya kilimo, ukurasa wa 21; Wilaya ya Nkasi tuna Kituo cha Utafiti Mirundikwa, hakijasaidiwa vya kutosha, hakina pesa ya kutosha. Naomba tusaidiwe ili tuweze kujitahidi kupata mbegu kwa karibu, sasa hivi mbegu tunaagiza nje bila sababu za kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni nilikuja hapa nikatoa kilio changu juu ya kunyang’anywa Shule ya Mirundikwa! Leo hii nipende kuishukuru Serikali, nimepata pesa zaidi ya milioni 259 kwa ajili ya kujenga bweni na kuendeleza madarasa. Niikumbushe Serikali, nilisema wakati ule kwamba, miundombinu iliyokuwepo wakati ule ilikuwa na zaidi ya thamani ya milioni 871 kwa mujibu wa Mthamini wa Serikali kwa hiyo, bado kuna safari ya kutosha ingawa si haba, lazima tushukuru. Ninaposema Serikali hii ikiambiwa jambo inatekeleza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nililia hapa kila mtu aliniona, sauti yangu niliipaza, nikapata nafasi ya kumwona Mheshimiwa Rais na kumweleza kwa nafasi mbalimbali, lakini sasa napata matokeo chanya. Sasa kwa nini niseme hafanyi kazi? Kwa nini niseme hashughulikii matatizo ya wananchi? Nitakuwa mtu wa ajabu sana. Kwa hiyo, anafanya kazi vizuri sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa katika maeneo niliyoyasema waangalie, Mawaziri watusaidie. Waziri wa Elimu upungufu wa walimu kwangu ni 647, hatuna walimu 647. Upungufu wa nyumba na vyumba vya madarasa ni 1,100. Upungufu wa nyumba za walimu 900, ni mkoa na wilaya iliyo pembezoni kabisa! Mtutupie macho. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho Mji wa Namanyere umeshakua vya kutosha, tunaomba uwe ni Halmashauri ya Mji. Mheshimiwa Malocha amekuwa akizungumza upande wake na wenyewe huko. Hiyo inatakiwa iwe wilaya ni sehemu kubwa. Mwisho zaidi tunaidai NFRA zaidi ya milioni 200 kwenye Halmashauri yetu. Halmashauri yetu sasa haiwezi kufanya kazi kwa sababu, mapato hayatoshelezi. Kwa hiyo, kama mtatusaidia mtusukumie hili jambo liwezekane ili Halmashauri ipate nguvu na uwezo wa kufanya kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niungane na wenzangu wote waliozungumzia juu ya asilimia 10 kwamba, hazitoki. Kama kuna mtu aliziona basi labda ni kwa sababu kwetu hazitoki. Tunaiomba Serikali ihakikishe kwamba asilimia 10 zinatoka ili ziende kwa vijana na akinamama kwa mwaka huu. Kwenye bajeti ya mwaka huu zimeingizwa, lakini sasa tulikuwa hatuzipati na hatuzipati kwa sababu ya mapato machache ya Halmashauri, wanaona vipaumbele wanavyokuwanavyo vinawafanya wasizitumie pesa hizi kupeleka kwa vijana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikia wanamsifu sana Mheshimiwa Mavunde. Hiyo habari yako ya mikopo kwa vijana kuwezesha vikundi mbalimbali kwetu haijafika. Tusaidie au tupe namna ambavyo tutaweza kushiriki twende kwa pamoja na wenzetu ambao wanasifia kwamba
unafanya vizuri katika eneo hili. Binafsi, kwangu mimi bado elimu haijafika na vijana wangu wote ni wachapa kazi wanahitaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho niongelee suala zima la uchapaji kazi, kama ilivyo Serikalini muangalie na kwenye kilimo. Kilimo, kuna watu wanajiita wakulima, lakini ni wazururaji tu na hakuna mtu anayewaangalia! Hili haiwezi kutuletea tija! Wasimamizi, hasa watawala, tujitahidi
kuhakikisha kwamba, kila mtu katika eneo lake awe anafanya kazi inayotambulika na kufanya kazi kwa bidii kwa masaa mengi. Isiwe kama ni ajenda ambayo haina msimamizi; tutakuwa tunazungumza kila wakati kwamba tunaondoka hapa tulipo kiuchumi, kumbe tunafuga watu
ambao… (Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Nami niwe mmoja kati ya watu ambao wanapongeza maandalizi mazuri ya hotuba ya Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri pamoja na Watendaji wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri amekuwa hodari kusikiliza matatizo ya wananchi hasa tunapomwendea sisi Wabunge ni muungwana. Nina hoja zifuatazo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, Wilayani kwetu tuna mbuga inaitwa Rwamfi Game Reserve, mbuga hii imepakana na vijiji kadhaa na kabla ya mbuga hii haijakuwa Serikalini ilikuwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi. Kutokana na umuhimu wa uhifadhi tunaoujua tuliamua kuipeleka Serikalini, Serikali ikaitwaa ikaanza kuihudumia. Katika kipindi ambacho Serikali inahudumia tumeziona faida kwamba kwa kweli wanyama wameongezeka na mbuga inatunzika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo changamoto ambazo tunaziona kwa wahifadhi wenyewe, kwamba hawana vitendea kazi vya kutosha, hawana idadi ya watumishi wa kutosha na kwa maana hiyo tunaiomba Serikali iwaletee gari, maana yake naliona pale gari bovu sana la muda mrefu, kwa hiyo haliwapi nafasi ya kufanya kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia pamekuwa na migogoro baina ya mipaka na vijiji vinavyopakana. Kuna vijiji vya Kasapa, vijiji vya King’ombe, vijiji vya Mlambo, vijiji vya Ng’undwe, vijiji vya Mlalambo, Kizumbi, Kata, Namansi na vinginevyo. Vijiji hivi vimekuweko kabla hata ya kuanza kwa pori lenyewe, vijiji vya kiasili, lakini kwa sasa vinaonekana kwamba viko ndani ya pori na kwa hiyo kuna mgogoro tayari kwamba wahame nao, kwa hivyo hawana nafasi, hawana maeneo ya kulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo Kamati ya Kitaifa ambayo imeshaundwa inatembea kila mahali, kwetu haijafika naomba wafike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni nilifika hata Ofisini kwa Waziri nilimwelezea juu ya mgogoro wa Kijiji cha Kasapa ambao ulipelekea wananchi kufyekewa mazao yao kwa kiwango kikubwa, zaidi ya hekta 20, kitu ambacho kwa mwaka huu ni shida kubwa sana hakuna chakula, ingawaje Waziri alinipa ushirikiano mkubwa na kuwaambia wahifadhi kwamba ni vizuri wawe wanawasiliana kuliko kuchukua hatua kali za namna hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe, Mheshimiwa Waziri ameshaniahidi kwamba baada ya Bunge tutaenda huko ili kwenda kuiona hii changamoto. Namshukuru sana, bila shaka ataiangalia kwa makini na kuona jinsi inavyoweza kusuluhishwa kwa vijiji vyote ni changamoto kubwa kwetu. Namna nzuri ya kuikabili changamoto ni kuangalia kama yapo maeneo ambayo yanaweza yakaachwa kwa wananchi kwa ajili ya kuendeleza shughuli za maisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto nyingine ambayo naiona katika Rwamfi ni mpaka wake na Kalambo ranch. Kalambo ranchi ni ranchi ya Taifa na kuna blocks ambazo wamepewa wawekezaji, wawekezaji hawa katika eneo hilo hakuna mipaka inayoonekana wazi, kwa hiyo pemekuwa na migogoro ya hapa na pale, jambo ambalo linafanya wawekezaji hawa wa-face migogoro mingi na wahifadhi. Kwa hiyo, jambo zuri hapa ni kuweka mipaka iwe wazi ili wananchi hawa ambao wanalipa kodi ya Serikali wasibughudhiwe pia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni vivutio vya utalii. Wilayani kwetu hasa Jimbo la Nkasi Kusini kuna vivutio vya utalii vingi. Ukiwa kwenye mwambao mwa Ziwa Tanganyika kuna ukanda mzuri sana, kuna mawe mazuri ambayo yamepangika kwa namna yake na kuna visiwa vizuri ambavyo vikiendelezwa vinaweza vikawa ni utalii wa namna yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, naishauri Wizara itembelee maeneo hayo ione utajiri uliopo ya utalii waone utajiri uliopo wa utalii ambao ukiendelezwa unaweza ukachangia sana. Siyo tu kwetu kwa Mkoa mzima kuna maeneo kama vile ukienda Kasanga kuna Ngome ya Bismark, ikiendelezwa ile inaweza kuwa nzuri sana, kuna Kalambo falls ambayo sasa hivi nimeona kama Wizara inaizingatia, ikiiendeleza inaweza ikaleta pesa nyingi ya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kama unaenda Kala kuna eneo ambalo ilikuwa ni makazi ya Zwangendaba ambaye alikuwa maarufu sana katika historia ya Tanzania kutoka Kusini. Aliuawa maeneo hayo na kuna majengo ya Mjerumani pale ambaye ndiye alimdhibiti kwenye eneo hilo na alizikwa eneo hilo. Kwa hiyo, inaweza ikasaidia sana kwa watu wanaotaka kujua mambo ya kihistoria katika suala zima la utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ni muhimu sana katika maeneo ya utalii kwetu ni eneo la Kijiji karibu na Mji wa Namanyere. Kuna maji moto ambayo yanatoka kiasi kwamba yakiendelezwa pale kijijini inaweza ikasaidia sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi niishauri Serikali, katika kuendeleza utalii nchini waangalie miji ambayo inawekeza katika ujenzi hasa ambayo ni ya kimkakati katika suala zima la utalii kama Mikoa ya Rukwa, Katavi na maeneo mengine. Majengo yanayojengwa pawepo na ushauri wa kitaalam wa kuangalia Halmashauri ambazo zinasimamia ujenzi ili angalau viwango viwe vinafikia ili changamoto ya mahali pa kufikia wageni ambao wanajielekeza kwenye utaliii isiwe ni changamoto inayokinzana na suala zima la utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba bado suala la mkaa kama wenzangu walivyolisema liangaliwe upya. Sasa hivi bado hatujawa na nishati mbadala ambayo inaweza ikakidhi mahitaji ya watu kwa sasa. Kwa hiyo, pamoja na uhifadhi na umuhimu wake, lakini pawepo na ustaarabu wa kuangalia jambo hili kwa umakini zaidi, vinginevyo tunaweza tukazua migogoro ambayo italeta shida kwa wananchi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Lwanfi Game Reserve iko Nkasi Kusini, hatujawahi kupata mchango wowote katika shughuli zozote za kijamii licha ya ukweli kuwa vijiji kama nane vimepakana na mbuga hii. Vijiji hivi ni Kasapa, Kiing’ombe, Mlambo, Kilambo, Ngundwe, Mlalambo, Kizumbi, Nkata, Namansi na vinginevyo kote huko tuna shida za kujenga miundombinu ya huduma za jamii ikiwemo ujenzi wa madarasa, zahanati, nyumba za walimu na shida ya maji tunaambulia vipigo vya mbwa mwizi pale ambapo mwananchi anapokamatwa na mbao moja tu. Tunaamini tuna mchango katika uhifadhi wa Lwanfi Game Reserve.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna ukatili uliopita kiasi, licha ya umuhimu wa maliasili zetu kulindwa na askari wanyamapori lakini sheria hazifuatwi. Askari hawa huchukua sheria mkononi kwa kufanya matendo mabaya ikiwepo kuua, kutesa, kupiga sana na kadhalika. Jambo hili si la kistaarabu, tujaribu mara zote kufuata sheria labda kama mazingira yanahatarisha usalama wa wahifadhi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa misitu ya TFS; mamlaka hii kama imezinduka toka kusikojulikana, wameweka mipaka kwenye vijiji vyetu hadi ndani ya vijiji na kufanya vijiji vingine ambavyo vipo miaka mingi kisheria kuonekana havina ardhi kabisa. Maeneo yaliyokuwa yanalimwa na wananchi yametwaliwa na kukosa mahali pa kulima, wananchi wanalima, mnafyeka mazao. Kijiji cha Kasapa, Msitu wa Kalambo ni mfano unaothibitisha hali hii ambayo ni ukatili. Wananchi hutengeneza Serikali, mnawaadhibu namna hii, haikubaliki hata kidogo. Kamati ya kutathmini migogoro ije Nkasi tafadhali.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa mchango kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni Serikali imefuta shule ya sekondari ya Milundikwa ikiwa na kidato cha kwanza hadi cha sita na kuua kabisa matarajio ya watoto katika ngazi zao mbalimbali walizokuwa wamefikia bila kuangalia performance nzuri sana ya shule hii. Ikiwa na miundombinu yenye thamani ya shilingi milioni 871. Naitaka Wizara inisaidie kurudisha miundombinu mbalimbali iliyokuwa imejengwa na wazazi ikiwemo madarasa, mabweni, maabara, vyoo, maji na mambo kadhaa ambayo sasa wanafunzi wameyakosa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaishauri Wizara itafute wadau mbalimbali kokote wanaoweza kupatikana ioneni kwa jicho la huruma, Mheshimiwa Waziri mpaka sasa sijaona mchango wa Wizara yako, kazi zinazoendelea kwa sasa ni kiduchu tu, bado kazi ni kubwa kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni miundombinu ya elimu Wilayani Nkasi (Nkasi Kusini kwa upekee) ni hatari na pamoja na mchango huu, naomba kuambatanisha na hali ilivyo mbaya kwa takwimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shule za msingi idadi ya watoto darasa la awali hadi darasa la saba ni watoto 80,604. Idadi ya walimu mahitaji ni 1,791; waliopo 1,089 na upungufu ni asilimia 39. Takwimu za vyumba vya madarasa mahitaji ni 1,791; vilivyopo 655; upungufu ni 1,136 ambao ni sawa na asilimia 63.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wamejenga maboma 273 vya vyumba vya madarasa ili kukabiliana na hilo tatizo, tunaomba tupanue kupunguza kero hiyo, kadhalika takwimu za nyumba za walimu, mahitaji 1,089 zilizopo ni 392 upungufu 697 upungufu asilimia 64. Wananchi tumejenga maboma mengi bado kupauliwa, tunaomba mtusaidie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu sekondari; idadi ya shule ni 23 na 22 ni za Serikali moja tu ni ya binafsi. Jumla ya wanafunzi waliosajiliwa mwaka 2017 wanaume ni 1,345 na wanawake 1,174 jumla ni 2, 519. Idadi ya kutoka kidato cha kwanza hadi cha sita wanaume ni 3,854 na wanawake ni 3,141 na jumla ni 6,995.

Mheshimiwa Mwenyekiti, walimu wa sayansi waliopo kwa sasa ni 14 tu wanahitajika walimu 95 tusaidie. Takwimu za nyumba za walimu, mahitaji ni 366, zilizopo 89, upungufu 277, sawa na asilimia 75.6. Tuna maboma 36 tunaomba tusaidie kupaua. Maabara mahitaji ni 66 zilizopo ni tano upungufu 61. Kila sekondari kuna ujenzi wa maabara wameshindwa kumalizia tunaomba msaada.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtoto wa kike kushindwa kumaliza shule kwa tatizo la mimba tulishughulikie kama Zanzibar, tusiwahukumu watoto wa kike mbona watoto wa kiume wanawapa mimba na wanaendelea na kusoma nani atamsaidia binti wetu asome? Pia walemavu wasaidiwe.

Jimbo la Nkasi Kusini linapakana na Ziwa Tanganyika kwa upande wa Magharibi ambapo kata zilizoko kando kando ya ziwa zina changamoto nyingi zikiwemo, mawasiliano ya simu (kata ya Kala).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mawasiliano ya barabara ambazo siyo nzuri, nyumba za walimu na madarasa; mambo haya yote yamekuwa yakifanya watumishi wengi kutokupendelea kwenda kufanya kazi maeneo hayo. Hivyo ni eneo lenye uwiano wa walimu usiolingana na maeneo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mchango huu, tunaomba kupata walimu zaidi hasa katika shule za maeneo haya, sekondari na msingi pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vipo vijiji visivyofikika kwa gari, mfano, Kijiji cha Kasanga - Kata ya Ninde; Kijiji cha Msamba - Kata ya Ninde; Kijiji cha Izinga - Kata ya Wampembe na Kijiji cha Mwinza - Kata ya Wampembe. Vijiji hivi pamoja na vingine hulazimika kwenda kufanya mitihani ya darasa la saba katika shule nyingine kwa sababu wasimamizi hawako tayari kwa usafiri wa majini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali itafute ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kusidia wananchi katika jitihada zao za kilimo na kufungua barabara za maeneo ya wananchi hawa. Tusikubali jambo hili liendelee siku zote, tutafute suluhu kwani itawezekana pia watoto wanaosafirishwa majini mara kwa mara wakapata shida japo hatuombei jambo hilo; tahadhari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanafunzi wamekuwa wakisafirishwa kwa makundi makubwa/idadi kubwa kwenda kufanya mitihani maeneo yanayoruhusiwa au basi, shule zote zipate fursa ya kufanya mitihani kwa kupata vyombo vya usafiri kwa usimamizi ili shule zote ziweze kufikika wakati wa mitihani, watoto wafanye mitihani kwa utulivu shuleni kwao walikozoea.

Maeneo ya pembezoni kama Jimbo langu naomba yapewe upendeleo kwa nyumba za walimu na madarasa ili kuwakomboa wananchi hawa ambao wanatakiwa kushikwa mkono ili wasogee. Watoto yatima waruhusiwe kusomeshwa kama watakuwa wamefaulu vizuri, maana wengi wao wamekuwa wakirudi nyumbani kwa kukosa msaada zaidi au vinginevyo ianzishwe taasisi itakayoiangalia changamoto hii kwa umahiri mkubwa (yatima kusoma).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nashukuru kupokea shilingi 259,000,000 Kasu sekondari ili kuendeleza miundombinu ya shule mpya kufuatia kufutwa kwa Mihudikwa sekondari na watoto kuhamishiwa Kasu.

Tunaomba Chuo cha Chala kiboreshwe kiwe VETA kamili ili wananchi wa Nkasi wapate ujuzi hasa wale wanaofuzu darasa la saba na sekondari pia. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
MHE. DESDRIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kuunga mkono hoja iliyoko mbele ya Bunge lako Tukufu. Nampongeza Mheshimiwa Waziri, mchapakazi, mtulivu na mwenye tabia ya pekee kimaadili. Hongera kiongozi, unakubalika ukiitwa mtoto wa Rais Mstaafu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni Serikali ilifuta Shule ya Milundikwa Sekondari kupisha makazi ya Kambi ya Jeshi JKT. Pamoja na kukubaliana kwa shingo upande, uamuzi huo umetuathiri wananchi wa Kata ya Nkandasi na Jimbo la Nkasi Kusini kutokana na miundombinu mbalimbali ya elimu kutwaliwa pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tuna sekondari changa sana ile ilikuwa inajitosheleza kwa miundombinu mingi ikiwa ni pamoja na maabara, mabweni ya wasichana na wavulana, madarasa na nyumba za walimu pamoja na kisima cha maji.

Pamoja na msaada wa nguvu kazi kwa wanajeshi, tunaomba Wizara hii inisaidie kujenga mabweni na maabara kwa kadri wanavyoweza ili kutuwezesha kukamilisha miundombinu pungufu. Pia Serikali izingatie familia za askari wetu, nao pia watasoma katika shule hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi la pili ni kwamba Jeshi lisitwae eneo lote, yale maeneo ambayo wananchi wanalima wasiwafukuze, wawaachie waendelee kulima kwa yale ambayo yako mbali na Kambi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi la tatu, naomba Wizara isaidie kujenga mnara wa mawasiliano katika Kata moja ya mpakani mwa Congo DRC; Kata ya Kala ili kuimarisha ulinzi wa mpakani na vilevile kuboresha mawasiliano ya simu za mkononi. Hii ni Kata pekee iliyobaki bila mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kazi nzuri sana ya wanajeshi, zipo dosari ndogo ndogo mfano, Wilayani Nkasi imewahi kutokea kama mara mbili wanajeshi kuwapiga wananchi na mara nyingi ni ugomvi wa mapenzi na mara zote raia huumizwa na wakati mwingine kuuawa. Siyo jambo zuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hapa Dodoma imewahi kutokea mahali pengine nchini. Naomba wapewe somo la maadili, kwani siku zote raia akimwona mwanajeshi huona kama mkombozi wake, huu ndiyo utamaduni wa Kitanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza wanajeshi wote.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Na mimi niungane na wenzangu kusema kwamba tozo zilizofutwa kwenye kilimo, mifugo pamoja uvuvi zinawafariji wadau zaidi wa maeneo hayo hasa wananchi wetu. Nipongeze Serikali kwa hatua hiyo. Lakini nitapongeza zaidi kama tabia ya kuchelewesha pembejeo itaachwa mara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzangu wamepitia vizuri kwenye vitabu na wameeleza kwamba kama kilimo ni tegemeo letu kwa nini sasa pesa zinazotengwa kwenye kilimo zinakuwa chache. Nimeangalia na nimeona kila mwaka pesa tunazotenga kwenye kilimo ni kidogo, lakini hata utoaji wa fedha zenyewe zile za kwenye bajeti zinakuwa kidogo zaidi, zile za wafadhili zinakuwa zimeongezeka yaani kama sisi wenyewe hatujaona umuhimu wa kilimo licha ya takwimu kuonyesha kwamba kilimo kinategemewa na Watanzania wengi. Kilimo ni mhimili wa uchumi wa Taifa letu na ni mhimili wa chakula katika nchi yetu kwa asilimia mia moja. Kwa hiyo, ni vitu vya kuangalia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mpango wa Uendelezaji wa Kilimo Awamu ya Pili umelenga kuongeza thamani ya chakula na tija zaidi kwa wakulima. Naishauri Serikali mpango huu uelekezwe zaidi kwenye vijiji vya uzalishaji mali kwa kuangalia miundombinu ya barabara. Kuna vijiji vyangu pale kwenye Jimbo langu, kijiji cha Milundikwa kwenda Kisula kuna barabara ya uzalishaji na si nzuri sana.

Mkiiweka kwenye mpango huu wa kuboresha maeneo ya kilimo kwa utaratibu wa kuboresha barabara zao inaweza ikatusaidia. Ipo barabara pia ya kutoka Katani kwenda Myula, barabara ya kutoka Kasu kwenda Malongwe ni maeneo ambayo yanatusaidia sana katika suala zima la uzalishaji katika maeneo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka nizungumzie pia juu ya Ranchi za Taifa. Kupitia kitabu cha Mheshimiwa Waziri nimeona ni kama Ranchi ya Taifa (NARCO) ni kama haina mtaji wa kutosha kuwezesha kusaidia Ranchi zetu za Taifa. Nikitolea mfano juu ya Ranchi yetu ya Kalambo ambayo ina ukubwa wa hekta za eneo 23,000 yenye uwezo wa kuwa na ng’ombe zaidi ya 7,000; lakini leo hii Kalambo ina ng’ombe 700, sasa utaona kama ipo under utilized.

Kwa hiyo, ni vizuri Serikali itusaidie kuimarisha ranchi zetu hizi ili iwe ni mfano wa kuigwa kwa wafugaji wanaozizunguka. Kwa sasa mchango huo huuoni kwa wananchi wanaozunguka ranchi hizo, nadhani ndiyo ilikuwa maana kubwa ya Serikali ya kuweka ranchi hizi katika maeneo mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wanaohudumiwa na Kalambo hasa katika blocks zile zilizobinafsishwa sasa hivi wana mgogoro pia wa mpaka kati ya Rwamfi Game Reserve na Kalambo yenyewe. Wanapoendeleza shughuli zao na huku wanalipa kodi ya Serikali lakini Serikali bado inawafanyia fujo kwenye mipaka ile ya Rwamfi Game Reserve. Kwa hiyo, kuna sababu ya kupitia mipaka upya ili kutowasumbua wananchi hawa ambao wanalipa kodi. (Makofi)

Vilevile kwenye uzalishaji wa mifugo (ng’ombe), kuna shida ya kupata madume, madume ni machache. Tungetegemea madume yazalishwe kwa wingi ili wananchi walio katika block hizi waweze kunufaika na breed hizi mpya za kisasa zenye kuleta tija za ufugaji. Hii ingeweza kutusaidia kuliko ilivyo sasa hivi madume tunategemea uhaimilishaji ambao wananchi hawajauzoea na wakati mwingine wanaona kama ni gharama kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napenda kuongelea chanjo na dawa za mifugo. Katika Mkoa wa Rukwa imetajwa Wilaya ya Nkasi hapa kwamba ni eneo ambalo mnataka mliendeleze liwe free kwa magonjwa lakini dawa tunapata kutoka Arusha, ni mbali. Hakuna center ya karibu ya kupata dawa na chanjo ili wakulima na wafugaji waweze kupata dawa katika maeneo ya karibu. Hii ingeweza kutusaidia kuboresha eneo la ufugaji kwa maeneo ya Mkoa wa Rukwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuhusu soko, wafugaji wanafuga lakini hakuna soko la karibu la kuuza nyama kwa bei nzuri. Tuna kiwanda pale cha Mheshimiwa Mzindakaya, tungeweza kuona Serikali kama kuna changamoto yoyote kiweze kuboreshwa ili kiweze kuhudumia center ya eneo letu katika suala zima la mifugo yetu ambayo tunaizalisha pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie kuhusu suala zima la uvuvi. Katika eneo la uvuvi hatujafanya vizuri. Wakati tunaongeza uchangiaji wa ruzuku kwenye kilimo lakini wavuvi kidogo tumewaacha nyuma. Naomba Serikali tuongeze zaidi kuwachangia wavuvi katika vifaa ambavyo vinaasaidia na mikopo ambayo inaweza ikawasaidia. Hivi karibuni mlitueleza hapa kwamba wavuvi wangeweza kuweka utaratibu wa mfuko wao wa kuwakopesha lakini huo mfuko sijauona kama umetusaidia kwa kiwango chochote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ziwa Tanganyika lile lina mwambao mkubwa sana na wavuvi wengi wanaokaa kule ni maskini lakini hatujasaidiwa vya kutosha na pesa yoyote iliyotoka Serikalini kwa ajili ya kusaidia vikundi vya wavuvi ili waweze kuboresha maisha yao. Wamezungukwa na rasilimali ambazo ni tajiri sana, lakini bado naona kama ni maskini. Naiomba Serikali ione uwezekano wa kutoa pesa za kutosha kusaidia wavuvi kama vile tunavyosaidia wakulima na wafugaji wakati mwingine wanasaidiwa kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba kuunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kuunga mkono hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ina mpango mzuri lakini fedha inayotengwa kwenye Wizara ni ndogo mara zote na wakati wote fedha ya ndani ni ndogo zaidi. Fedha ya nje ni kubwa kidogo. Vilevile fedha inayopatikana kwenye bajeti zinazotengwa ni fedha kidogo sana na mara nyingine fedha ya nje inatolewa nyingi kidogo kuliko ya ndani. Maana yake ni kwamba kama Taifa tunaiacha sekta muhimu kuipa umuhimu wake, tunategemea wafadhili ambao wangependa kuona uchumi wetu hautengemai ili tubaki tegemezi kwa kila jambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imekuwa kama ni mazoea kuwa kila mwaka pembejeo huwafikia wakulima kwa kuchelewa. Je, ni matarajio yapi yanayokusudiwa kuleta mapinduzi ya kilimo kwa utaratibu huu? Naomba Serikali itusaidie namna ya kumaliza kabisa tatizo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa yapo makampuni yanayojitangaza kuzalisha na kusambaza mbegu na dawa mbalimbali za kilimo, mengi yanakuwa fake na hakuna hatua zinachukuliwa hasa kwa dawa za kuua wadudu na palizi (kuuwa magugu).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Programu ya Kuboresha Kilimo (ASDP) inayokuwa na malengo ya kuongeza tija kwa mkulima, kuongeza uzalishaji ili kuhuisha viwanda, kuwezesha mkulima wa chini, kuongeza kipato na kuongeza thamani ya mazao ili wakulima na kilimo kwa ujumla kiwe ni kazi yenye kuleta manufaa makubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali iratibu katika mpango huu kuboresha barabara katika maeneo ya uzalishaji katika Jimbo la Nkasi Kusini. Barabara zifuatazo ni muhimu kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo, nazo ni barabara ya Milundikwa – Kisu - Malongwe ni muhimu kwa kilimo Jimboni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Kasu – Katani – Myula ni muhimu sana kwa maendeleo ya kilimo Wilayani. Vilevile barabara ya Nkomo II – Kipende, nayo ni muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Nkasi Kusini tuna mabonde mawili yanayofaa kwa umwagiliaji, nayo ni Bonde la Kate lenye hekta 1,500 na Bonde la Namansi lenye ukubwa wa hekta 440. Mabonde yote yameombewa fedha na Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi lakini bado kupata fedha ya kuanza kujenga miundombinu ya kumwagilia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ranchi ya Karambo ina ukubwa wa hekta za eneo 23,000 lina ng’ombe 710 tu, kondoo 215, farasi nane, uwezo wake ni ng’ombe 7,000. Under-utilized.

Mheshimiwa Mwenyekiti, please Serikali iongeze mtaji.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Naomba kupongeza kazi nzuri zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na Wizara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, Nkasi Kusini tuna miradi ya maji inayoendelea. Miradi hiyo imekuwa ya muda mrefu na imeacha matumaini yakipotea kwa wananchi. Naomba Serikali iione miradi hii kwa namna ya pekee na ilete tija kwa wananchi wake. Naitaja kama ifuatavyo:-

Mradi wa Maji wa Bwawa la Kawa ni wa muda mrefu, umetumia fedha zaidi ya bilioni mbili, wananchi bado hawajaanza kupata maji katika Vijiji vya Frengelezya, Nkuudi na Kalundi. Pia natoa mapendekezo kuwa, mradi huu utakapokamilishwa upeleke maji Sekondari ya Kipande na Kijiji cha Myula.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji wa kutoka Kate Milimani kwenda Vijiji vya Nkata, Ntemba, Kitosi, Ntuchil, Ifundwa, Msilihofu na Isale ni mradi muhimu, uanze mara moja. Najua kwa sasa mtaalam mshauri yuko site, tuna fedha kwenye bajeti.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji King’ombe. Mradi una upungufu kwenye njia zake, mradi una mabomba yako nje nje, dosari zirekebishwe na naomba ukamilike na nashauri wananchi waulinde mradi wao. Nitamshambulia sana mtu anayehujumu njia ya maji, gharama ya mradi ni kubwa, zaidi ya milioni 720.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji wa Kijiji cha Mpasa naomba uanze kutekelezwa. Wananchi wanasubiri kwa muda mrefu na imani inawatoka sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Chala Mji Mdogo. Nimeona Wizara imetenga bilioni mbili kwa ajili ya upembuzi wa kina kushughulikia miji kadhaa ukiwepo wa Chala.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba fedha hii iongezwe, sidhani kama inatosha. Angalia Ukurasa wa 164(31) wa Hotuba. Mji wa Chala una shida ya maji kwa kiwango cha juu sana na mamlaka yake imeanza haina mapato yoyote kwa kuwa hakuna maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji wa Kisura (Kijiji). Kazi inaendelea vizuri kwa sasa, japokuwa ilichelewa sana. Kasi hii iendelee hadi mwisho wa mradi, wananchi wanapata shida.

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi la Kutafiti Maji kwenye Vijiji vya Kasu, Katani, Milundikwa na Kantawa. Vijiji hivi havina maji ya uhakika, naomba Serikali ifanye kazi ya kutafiti ili kusaidia vijiji vyote na Sekondari za Kasu na Kambi ya Jeshi, pia Milundikwa. Naomba vilevile Kata za Wampembe, Ninde na Kizumbi wafanyiwe utafiti maji ya mseleleko yanaweza kupatikana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza nakushukuru wewe na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima. Naunga mkono watu wote wanaosema pesa za maji ziongezwe kwa sababu ya umuhimu wenyewe. Mimi kwangu nina matatizo katika miradi kadhaa inayoendelea. Jimboni kwangu kuna miradi ya maji ya vijiji 10. Mradi wa Kawa umetumia zaidi ya shilingi bilioni mbili na nusu, lakini maji hayajaanza kwenda kwa wananchi. Hii ni hasara kubwa. Kwa hiyo, wananchi hawaoni tija wala thamani ya pesa ambayo imetengwa kwao. Naomba Wizara isukume jambo hili liwezekane. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kadhalika kuna Mradi wa King’ombe. Katika mradi huu tumetumia zaidi ya shilingi milioni 720, lakini mradi huu bado una shida katika maeneo mbalimbali, hasa katika maeneo ambayo bomba lake liko juu. Naomba Serikali ihakikishe kwamba maeneo ambayo bomba linaonekana linakatwakatwa ovyo ovyo, waweke sehemu ile chuma ili huduma ya maji iwafikie kwa uhakika. Wananchi wote wanaohujumu, mimi nalaani vitendo hivyo na hatuwezi kuviunga mkono hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, upo mradi wa siku nyingi sana wa maji kutoka Kate kwenda Isale, unapita Vijiji vya Ntemba, Kata, Ntuchi, Ifundwa na Msilihofu. Huu mradi ni muhimu sana, umekuwa ukiahidiwa na Maraisi wote wawili, akiwepo Jakaya Kikwete na huyu ambaye tupo naye kwenye madaraka sasa. Pesa zilitengwa zaidi ya sh.2,800,000,000/=. Naomba, sasa hivi Wilaya ya Nkasi mlitutengea pesa sasa hazionekani. Naomba mradi huu nao uanze kufanya kazi mara moja ili wananchi wa vijiji hivyo waweze kupata maji ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile upo mradi wa Kijiji cha Kisura. Mradi huu nao umekuwa ukisuasua, una zaidi ya shilingi milioni 400. Naomba Wizara itoe msukumo wa kutosha katika jambo hili ili maji yaweze kupatikana. Vijiji vyote kwa ujumla kwa Kata ya Nkandasi, Kata ya Kipande na vile vile Kata ya Nsintali bado maji ni taabu kubwa sana. Naomba pia utafiti ufanywe katika maeneo haya ili maji yaweze kupatikana katika vijiji vinavyohusika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nije katika mradi wa umwagiliaji. Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ina Majimbo mawili; Jimbo la Nkasi Kusini na Nkasi Kaskazini. Miradi inayotajwa hapa kwenye umwagiliaji, yote miwili imekaa kwenye Jimbo moja. Jambo hili nimekuwa nikilizungumza kila wakati. Sisi kwenye Jimbo la Nkasi Kusini tulishabainisha uwepo wa Miradi ya Bonde la Mto la Kate na Bonde la Mtisi lililopo Kijiji cha Namansi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumetoa mapendekezo, tunaomba tu pesa za kuanza kujenga miundombinu, lakini sijawahi kupata hata wakati mmoja. Naomba ufike wakati haki itendeke. Maana yake, ninapimwaje mimi? Tupo Jimbo moja lakini miradi ipo sehemu mbili, inapata pesa lakini iliyopendekezwa upande wa pili haipati pesa. Naomba na hilo mliangalie kwa umakini sana ili kutujengea pia siasa nzuri. Bila kufanya hivyo, maana yake tutakwama.

Mheshimiwa Naibu Spika, mapendekezo yote yaliyokwishafanywa na Halmashauri, kinachotakiwa sasa ni kuomba pesa ili miundombinu ianze kujengwa hasa katika bonde hili la Kate ambalo kwa kweli ni kubwa la kutosha na linaweza kuzalisha chakula ambacho kitakuwa ni msaada mkubwa sana, mkijua kwamba mazingira yetu sisi Mkoa wa Rukwa ni wazalishaji wazuri sana wa chakula.

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Ahsante
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kuunga mkono hoja. Mchango wangu ni kama ifuatavyo:-

(i) Wizara ya Fedha iangalie sera zake za kutoa fedha za miradi iliyopitishwa na Bunge, fedha zinachelewa na wakati mwingine hazitolewi kabisa na miradi ya maendeleo haikamiliki.

(ii) Wizara ya Fedha ilitazame kwa makini suala la road licence ni kero kwa wananchi. Naomba kodi hiyo iwekwe kwenye mafuta ambako kila mtumiaji chombo kinachotembea barabarani ataweza kulipa na itakusanywa kiurahisi sana.

(iii) Huduma kwa wastaafu, kwanza wanacheleweshwa kupewa stahili zao na nashauri maslahi yao yaongezeke kwani hali ya maisha inapanda na wanahitaji mlo mzuri kuweza kukabiliana na hali zao.

(iv) Mgawanyo wa fedha za ruzuku uangalie maeneo yaliyo nyuma zaidi ili kuyavuta mkono kwa makusudi ili wasogee maana kuna changamoto nyingi zaidi.

(v) Mikopo ya fedha ielekezwe zaidi kwenye kukuza kilimo kama tegemeo la wananchi wengi nchini na mchangiaji mkubwa wa pato la Taifa.

(vi) Walipa kodi ni wadau muhimu wa maendeleo, naomba pawepo staha zaidi katika kufuatilia kodi na wananchi waelimishwe zaidi kwa makala na matangazo mbalimbali juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari.

(vii) Benki ya Kilimo iwezeshwe, kilimo kitakua kama mitaji itaelekezwa huko.

(viii) Sheria itungwe kuwasaidia watumishi ambao hujikuta wamelazimika kukopa fedha kwa wakopeshaji wasio rasmi wanaotoza riba kubwa inayofikia 30% kwa mwezi yaani ukikopa Sh.10,000,000/= tarehe 1 - 31 Desemba wanalipa Sh.13,000,000/= ongezeko la Sh.3,000,000/= na akichelewa inalipa pamoja na Interest kwa Sh.3,000,000 ni Sh.300,000, watu wanaibiwa sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. DESPERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. Pia nampongeza Waziri, Naibu Waziri, kwa kuchapa kazi, wamejitahidi kufanya kizalendo na wametatua migogoro mingi sana. Wananchi wamekuwa sasa na imani na Serikali yao kuhusu namna migogoro ya ardhi inavyoshughulikiwa. Wito wangu waendelee kufanya kazi na kusimamia haki za wananchi katika masuala ya ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Nkasi Kusini lina mashamba na hifadhi nyingi za kufanya wananchi kukosa ardhi ya kilimo. Nashauri Wizara kuona kama mashamba yaliyopo Jimboni yanaendeshwa kwa ufanisi au la ili kuweza kutoa uamuzi wa kuongeza ardhi kwa wananchi.

- Shamba la Nkundi linalotumiwa na Mheshimiwa Mzindakaya. Wananchi jirani hawana ardhi ya kutosha na sehemu kubwa halitumiki ipasavyo lipunguzwe wapewe wananchi wangu.

- Shamba la Kalambo Ranchi lina ukubwa wa hekta 23,000, lakini lina ng’ombe 710 tu. linatumika chini ya kiwango eneo kubwa halitumiki. Lipunguzwe wapewe wananchi wangu.

- Shamba la Milundikwa kwa eneo walilopewa JKT mwaka jana ni kubwa lote halitumiki na wananchi wengi wanalima ndani bila kuruhusiwa kwa sababu ya ukosefu wa ardhi ya kilimo, lipunguzwe wapewe wananchi.

- Shamba la China linatumika lakini tuone kama lazima lote liwe kwa mtu mmoja wakati watu wengi hawana ardhi ya Kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mamlaka ya Misitu ya TFS imepora ardhi ya Kijiji cha Kasapa na kufanya kijiji kukosa kabisa eneo la kulima. Naiomba Wizara ione namna ya kuwasaidia wananchi wa kijiji hiki. Maeneo yao ambayo wamekuwa wakilima miaka yote, tangu miaka ya 1956 yametwaliwa na kufyeka mazao yao. Wizara inisaidie kutatua mgogoro huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Vijiji vya King’ombe, Mlambo, Ng’undwe, Mlalambo, Nkata na Kasapa vinadaiwa kuwa Ndani ya Mbuga ya Lwanfi Game Reserve, kwa hiyo, wananchi hawana ardhi na wanapata usumbufu mkubwa. Kamati ya Migogoro ya Ardhi itembelee kuona shida iliyopo.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kupata nafasi na mimi nitoe mchango wangu katika hotuba yetu ya mpango. Mimi nina maeneo matatu/manne na la kwanza ni kilimo. Tunapoingia kwenye uchumi wa viwanda hatuna namna ya kukwepa kuendeleza kilimo na wachangiaji wengi wameeleza. Manufaa ya kilimo yanaonekana na yako wazi, kwanza ina mchango mkubwa sana kwenye uchumi wa Taifa, lakini pia imewaajiri Watanzania wengi. Kilimo kinaweza pia kikatusaidia kwenye soko la ndani la bidhaa zinazotokana na viwanda. Kwa hiyo, kwa vyovyote vile hatuwezi kukwepa. Sasa ninavyoona mimi kwenye Mpango huu na Mipango yote iliyopita hatujatia mkazo wa kutosha kwenye kuimarisha kilimo chetu, ninaomba hili jambo lizingatiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano sisi Mkoa wa Rukwa katika msimu uliopita tumezalisha zaidi ya tani 710,602; mahitaji yetu sisi ni tani 257,553. Kiasi cha mahindi ambayo sisi tumetoa nje ya mkoa na kwa sababu tuna utaratibu wetu kwenye njia zinazotka nje ya mkoa; tumetoa tani 50,189. Ziada tuliyonayo leo ni zaidi ya tani 402,859.

Kwa hiyo nina wasiwasi hata takwimu za Mheshimiwa Waziri; tulikuwa tunaongea nae leo kwamba anasema Taifa lina ziada ya tani 700,000 za chakula kwa sasa ikiwa sisi Mkoa wa Rukwa tu tuna tani 402,859.62.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa wananchi wetu mahindi ndiyo kila kitu. Ndiyo kwenda shule, mahindi ndiyo afya zao na ndio uchumi wao. Kwa hiyo, usipoweka mfumo mzuri wa masoko katika mahindi sisi umetuumiza. Nilikuwa nafikiri kama Taifa tuangalie, kwa sababu uzalishaji wa mahindi utaendelea kuwepo, haiwezekani kila mwaka tunakuja hapa kuzungumza kwa kutoa mishipa mingi, kukaza maneno ya hovyo, Wabunge kuweka vikundi vikundi. Lazima kama Taifa mjue kwamba kuna wakulima wa mahindi na mahindi yataendelea kulimwa. Sasa ni lazima tuwe na mfumo unaoeleweka, mkaanzisha hata kitaasisi au NFRA ikaimarishwa, ikapewa hata mtaji ili iwe inanunua katika maeneo ambayo kilimo kinafanya vizuri halafu baadaye inaweza ikafanya biashara ama nje ya nchi au sehemu ambazo kuna upungufu wa chakula katika mataifa mengine kuliko kuwa na jambo lisilo na majibu ya uhakika kila mwaka. Hii nafikisi si nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuimarisha kilimo nina kata yangu ya Nkandasi. Kuna shamba la Milundikwa State Farm limenyang’anywa na Jeshi na wananchi sasa zaidi ya 2000 hawana shughuli ya kufanya. Sasa watachangiaje katika Mpango huu? Ninaiomba Serikali itume wataalam wake wakaone jinsi wananchi hawa ambao wamekaa miaka 18 katika eneo hili lakini leo wanakuja kufukuzwa na Jeshi bila sababu za kutosheleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, waagizeni viongozi wakafanye utafiti waone haki iko wapi kwa sababu eneo hili walipewa kihalali na maandishi yapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la maji. Nimeona Mipango mizuri sana katika ukurasa wa 53 katika kitabu chetu cha Mpango na nimeona pia Wizara inavyojitahidi katika kushughulikia suala hili kwa kipindi hiki, hasa baada ya Bunge kuamua kushughulikia suala hili kikamilifu.

Mheshimiwa Mwneyekiti, dosari niliyoiona ni utoaji wa pesa. Zile pesa ambazo zinapatikana moja kwa moja kutoka Wizarani, zinazokwenda kwenye Wizara kwa maamuzi ya Bunge zinakwenda vizuri kwenye kusukuma miradi. Lakini zile ambazo zinapatikana kutoka Wizara ya Fedha zinachelewa na hazitusaidii sana kusukuma miradi, hii iangaliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niweke vizuri, Wilaya ya Nkasi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi na mimi nichangie Kamati hizi mbili. Wenzangu wamelisemea sana suala la kilimo ambapo na mimi nawakilisha wakulima, hivyo ni lazima niwasemee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninavyoona, Wizara ni kama imewatoroka wakulima, wamebaki peke yao. Wakulima sasa hawana msaidizi na tumewatelekeza. Mwaka 2017 Mheshimiwa Waziri alitembelea Wilaya yetu na Mkoa wa Rukwa wakati wa masika, tukifikiri analeta suluhisho ama la mazao yetu yaliyokosa soko au pembejeo zilizochelewa. Yote mawili aliondoka bila suluhisho lolote na tukashuhudia uchelewaji mkubwa sana wa pembejeo. Mbaya zaidi mpaka sasa pembejeo hamna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni nilimsikia Mheshimiwa Rais akikemea kwamba maeneo ambayo yanafanya vizuri kwenye kilimo, yapelekeeni mbolea. Siku mbili, tatu watu wakamdanganya Mheshimiwa Rais wakaleta mbolea nyingi Rukwa, lakini hamna mbolea. Leo ninavyozungumza hakuna Urea, wafanyabiashara wanachokifanya, wanatafuta mbolea, wanaagiza malori na lori likisimama tu, mbolea yote inaisha. Hiyo ndiyo habari iliyoko Rukwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ndugu zangu, kilimo sasa mnakiua, lakini mnawatia zaidi umasikini wananchi ambao wanategemea kilimo kwa kila kitu. Hii hatuwezi kukubali, lazima tuwasemee. Serikali msikwepe wajibu; chukueni wajibu wenu vizuri mhakikishe kwamba mnawasaidia wakulima wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni suala la maliasili, mwaka 2017 Mheshimiwa Maghembe pia alitembelea Wilayani kwetu na akapata nafasi ya kutembelea kijiji kimoja ambacho kina mgogoro wa ardhi kutokana na uhifadhi. Ninavyosema hivi mpaka sasa migogoro iliyokuwepo wakati
ule haijasuluhishwa kabisa na tumeambiwa hapa kwamba kuna Kamati ya Wizara nyingi ambayo ilikuwa imeundwa kwa ajili ya kuangalia migogoro. Kamati hii haimalizi kazi? Ni lini matatizo ya wakulima na hifadhi yataisha? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina vijiji vingi, kuna Vijiji vya Kasapa, King’ombe, Mlambo, vyote viko tunaambiwa viko kwenye hifadhi, wakati vimekuwepo tangu enzi. Yote hii ni kwa sababu Kamati hii haijakamilisha kazi yake. Ninaomba migogoro hii iangaliwe, lakini wapo wahifadhi wa TFS, ni wakatili sana kwa wakulima na kwa wananchi wetu. Mkaa hata debe moja akikamatwa nalo mtu anafanywa vibaya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunavyojua, hakuna nishati nyingine mbadala zaidi ya mkaa, tunaweka nafasi gani ya kuwasaidia wakulima hawa wa ngazi ya chini? Mawaziri wetu waliangalie kwa makini sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni wakulima kutofikiwa na barabara za uhakika. Nina wakulima wangu wa Kata ya Kala hawafikiki kwa barabara na wala hawana mtandao wa simu. Maneno haya nimeyasema kwenye Bunge hili katika vipindi vyote viwili na leo nilikuwa naongea na Mheshimiwa Waziri, Kata ya Kala haina mawasiliano ya simu, ni vipi watafikia masoko? Hawafikiki kwa barabara za uhakika, ni vipi mazao yao yataweza kuuzwa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naiomba Serikali yangu, waone umuhimu wa kupeleka mawasiliano ya simu katika Kata ya Kala pamoja na kutengeneza barabara. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Naibu Spika, nichangie kuhusu mawasiliano ya simu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Kala iliyoko mpakani kando kando mwa Ziwa Tanganyika ina vijiji vya King’ombe, Mtambo, Kilambo, Mpasa, Kapumpali, Tundu na Kala. Vijiji vyote hivi havina mawasiliano ya simu licha ya kuwa na zaidi ya watu 2,000 na ikumbukwe kuwa hawana barabara ya kuaminika. Mheshimiwa Waziri Mbarawa nimekuja kwako siyo chini ya mara sita au saba, nimeandika barua mbili na nimechangia hapa Bungeni zaidi ya mara 10 sijasikilizwa, je, ni kwa nini hasa?

Mheshimiwa Naibu Spika, binafsi sijaelewa kwa sababu pia hujawahi kunipa sababu ya msingi ya suala hili kutokuwezekana kwa muda wa miaka saba nikiwa hapa Bungeni. Naomba Wizara inisaidie kwani sieleweki kwa wananchi hawa. Vilevile kuna Vijiji vya Kasapa, Kata ya Sintali na Vijiji vya Kisambara na Msamba – Kata ya Ninde.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Katongoro – Ninde; barabara ya Kitosi - Wampembe; barabara ya Nkana Kata zote zimefunga kutokana na mvua nyingi zinazonyesha huko Mkoani Rukwa na TARURA hawana fedha ya dharura. Naomba Serikali itoe fedha za dharura TARURA Nkasi vinginevyo wananchi hawapati huduma mbalimbali ikiwepo matibabu na bidhaa zingine za madukani.

Mheshimiwa Naibu Spika, niombe barabara ya lami toka Chala kuendelea kuunga Paramwe barabara ya lami imezunguka Makao Makuu ya Wilaya na kuacha barabara ya zamani ya kwenda Mpanda ambapo Vijiji vya Londokazi, Miombo, Mashete Mtenga na Mwai vimebaki na barabara ya vumbi na vijiji vya uzalishaji mkubwa wanaomba waunganishwe kwa barabara ya lami.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaunga mkono nikipata majibu ya mtandao Kata ya Kala, Nkasi Kusini.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Niungane na wenzangu kumshukuru Mwenyezi Mungu kutujalia uzima, lakini pia nimpongeze Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kuja na hotuba nzuri sana. Hotuba hii ni nzuri sana, tofauti na wenzangu wanaosema ina matatizo. Mimi niko hapa Bungeni kwa muda wa kutosha, miaka sita, nasema hotuba hii ni nzuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaendelea, nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anayoifanyia Tanzania. Rais huyu ni wa pekee! Waswahili wanasema, “Kila zama na kitabu chake.” Kitabu cha Mheshimiwa Rais Magufuli kitaandikwa kwa wino wa dhahabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utendaji huu ni message kwa wanasiasa wengine wanaotafuta nafasi kama ya kwake. Una kiatu cha kujaa hapo? Una mguu? Kiatu chako kinatosha? Mguu wako unatosha hicho kiatu? Ni message kwa Watendaji Serikalini, huyu Rais anataka Watendaji wa namna gani kwenye Serikali yake? Ni message kwa wananchi wote. Tumuunge mkono kwa sababu dhamira yake ameiweka wazi, ni ya kizalendo kupita kiasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile ni message kwa nchi nyingine kwamba Tanzania kuna viongozi wana macho na wanajua kulinda nchi yao. Nampongeza sana Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye bajeti. Bajeti hii ni nzuri, imekonga mioyo ya Watanzania wengi. Imefuta ada ya motor vehicle licence, imepunguza ushuru wa mazao ya biashara kwa wakulima wadogo wadogo na wafanyabiashara wadogo wadogo ambao mara nyingi wako kwenye wigo wa gunia 10 hizo hizo. Imemfanya mkulima sasa ajisikie kwamba kile anacholima kina thamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri pia tuone kwenye ushuru kama dagaa na samaki na zenyewe tunaziachaje? Isiwe kimya namna hii, ili kama ni ushuru, basi tuwapunguzie wale wafanyabiashara wa samaki na dagaa katika kiwango kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti hii inaenda kutekeleza ahadi za Mheshimiwa Rais alizoziweka. Tena aliweka ahadi ya kwanza kabisa kwamba anataka nchi yetu iende kwenye uchumi wa kati. Bajeti hii imeweka mipango mizuri kabisa ya kuboresha ujenzi wa barabara zetu, ujenzi wa reli katika standard gauge, ujenzi wa mifumo ya usafiri wa anga, majini lakini vile vile mfumo wa uendelezaji umeme ambao ni muhimu sana katika uchumi wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoweza kushauri ni kwamba utendaji lazima uwe makini; tutumie fursa tulizonazo hasa za kijiografia kuhakikisha kwamba haya mazingira tunayoyaweka tunafanya uzalishaji mzuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Mkoa wetu wa Rukwa ni wa kilimo. Leo hii hali ya hewa ni nzuri sana Mkoa wa Rukwa, lakini bado kilimo siyo kizuri sana vile tunavyotaka. Bado hatujaingia kwenye kilimo cha kutumia matrekta, kilimo cha kibiashara ambacho kinaweza kikatukomboa na lazima watumishi waangalie, Mawaziri mjue kwamba kilimo kinabeba watu wengi; kinaajiri watu wengi. Ukiimarisha kilimo, kwa vyovyote vile unakuwa na wigo mpana wa kubadilisha uchumi wa nchi na kusaidia watu wengi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba bajeti hii ambayo naiunga sana mkono inisaidie mambo yafuatayo katika Jimbo langu. Vipo vijiji ambavyo vilisahaulika kupelekewa umeme na sikuviona kwenye orodha na niliweza kupata nafasi ya kumwona Mheshimiwa Waziri lakini na Mtendaji Mkuu wa REA. Vijiji hivi ni vijiji vya Katani, Malongwe, Nkana, Sintali, Ifundwa, Nkomachindo na Nchenje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba umeme pia uende Kata ya Ninde iliyo na vijiji saba; Kata ya Kala ina vijiji saba, Kata ya Wampembe ambayo Waziri alitembelea mwenyewe ina vijiji vitano na hawa ni wavuvi wamekuwa wakivua samaki zao wanapeleka Zambia. Akiwapelekea umeme hawa amewakomboa na bajeti hii ni ya ukombozi. Kwa hiyo, naomba umeme ufike katika Kata hizi za mwambao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia bajeti ninayoiunga mkono sana iniunge mkono katika juhudi ya maji katika Jimbo langu la Nkasi Kusini. Tuna tatizo la maji katika Kata ya Nkhandasi ambayo ina Vijiji vya Kasu, Milundikwa, Malongwe, Katani na Kisula. Vijiji hivi vimekuwa na shida ya maji muda mrefu sana na juzi tumehamisha Shule ya Milundikwa tukapeleka kwenye Kata hii hapa. Kwa hiyo, naomba…

TAARIFA . . .

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naikubali sana taarifa yake na nilikuwa naendelea huko. Kwa hiyo, Vijiji vya Chonga, Makupa, Talatila na Miyula vina shida kubwa ya maji na ina mitambo na mtandao wa maji unafika pale. Kwa hiyo, ni suala la kufufua na kuanzisha. Namshukuru sana Mheshimiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado ipo miradi ya maji katika Vijiji vya Nkundi na Kalundi. Vijiji hivi vina bwawa la Kawa ambalo tumekuwa tukilizungumza muda mrefu. Hatua zake ni nzuri, naomba Serikali ikamilishe ili wananchi waweze kupata matunda ya jasho la Serikali yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi mwingine ni mradi wa maji wa Zuma, Isale ambao utahudumia vijiji vya Ntemba, Kitosi na Ntuhuchi. Mradi huu uko katika hatua za mwanzo. Naomba Watendaji waharakishe ili pesa ambazo tulitengewa kwenye bajeti ya mwaka 2016 zisirudi kwa sababu zipo za kutekeleza mradi huu. Kwa taarifa nilizozipata sasa hivi, karibu utekelezaji uanze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, bajeti hii inisaidie kutenga pesa kwa ajili ya Vituo vya Afya. Kipo Kituo cha Afya cha Kandasi, wananchi wameamua kujenga wenyewe, tunachohitaji hapa ni nguvu za Serikali, mtusaide. Kipo Kituo cha Afya cha King’ombe, Kata ya Kala. Kata ya Kala iko na umbali wa zaidi ya kilometa 150 kutoka Makao Makuu ya Wilaya. Akinamama na Watoto wamepoteza maisha yao kwa sababu ya umbali wa barabara isiyofikika. Bajeti hii ninayoiunga mkono leo ikawe mkombozi kwa vifo vya akinamama na watoto kutoka Kata ya Kala na Kituo cha Afya cha King’ombe kiweze kujengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia Kituo cha Afya kijengwe Kate na Ninde na wananchi tumewahimiza na wako na utayari wa kutosha katika kuanza kujenga majengo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti hii ninayoiunga mkono, naomba ikawe mkombozi wa kuleta uchumi kwa wafanyabiashara wadogo waliotambuliwa leo, wasinyanyaswe tena ili pamoja na kutambuliwa kwao, basi Serikali ione namna ambavyo inaweza ikatumia vyombo vya fedha kuwasaidia watu hawa kwa kutoa mikopo midogo midogo ili waweze kupata mitaji na kuchangia katika uchumi wa Taifa pamoja na uchumi wa familia zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Nkasi Kusini ni miongoni mwa Jimbo ambalo liko kwenye maeneo ambayo yana changamoto nyingi. Zipo barabara za Kitosi - Wampembe; barabara ya Kana - Kala; na barabara ya Namanyere – Ninde. Barabara hizi zimekuwa na changamoto kubwa sana, ukiziachia Halmashauri peke yake haiwezi kumudu kuwasaidia wananchi. Nomba bajeti hii ninayoiunga mkono sana, mtutengee pesa pia ya kuweza kuhakikisha kwamba barabara zetu zinapitika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti hii naomba itusaidie pia kuhakikisha kwamba mazao ambayo tumelima sisi watu wa Rukwa yanapata ununuzi kwa bei nzuri kidogo. Sasa hivi bei siyo nzuri sana, lakini gharama ya uzalishaji imekuwa kubwa. Mkipandisha bei mnatusaidia zaidi katika kuweka bei elekezi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa uzima anaotujalia. Nichukue nafasi hii pia kuishukuru Serikali, Mheshimiwa Rais na uongozi wa Bunge kuniwezesha kwenda kutibiwa India na leo nimepona. Najisikia niko vizuri, namshukuru sana Mungu. Naishukuru sana Serikali yangu kwa huruma hiyo na sasa niko kazini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapema kabisa naunga mkono hotuba iliyotolewa na Waziri Mkuu hapa mbele yetu kwa sababu imejaribu kuangalia maeneo muhimu mengi. Kusema kweli Waziri Mkuu na viongozi wanaomsaidia akiwemo Waziri Mheshimiwa Jenista Mhagama pamoja na Mawaziri wengine, wanafanya kazi vizuri na wanatusikiliza vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina hoja chache ambazo naziwasilisha hapa Bungeni. La kwanza, ni suala la shamba la Milundikwa ambalo nimekuwa nikilizungumza sana katika Bunge hilo. Shamba hili lilikuwa la Serikali na lina ukubwa wa ekari 26,500 baada ya kuacha shughuli zake wakaja Jeshi kwa muda. Wanajeshi walikuja mwaka 1994 baadaye walisimamisha shughuli zao na kuwaachia wananchi. Shamba lile liligawanywa katika vijiji mbalimbali, Kijiji cha Milundikwa kilipewa ekari 12,000, Kasu walipewa ekari 6,000, Kisulu walipewa ekari 2,000, Malongo walipewa ekari 1,000 na zikawa zimebaki ekari 5,500, tukashauriwa eneo hilo libaki kuwa eneo la Halmashauri tuendeleze utunzaji wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri kwa busara na namna walivyofanya wakaamua eneo hili kuanzisha Sekondari ya Milundikwa ambayo nayo niliipigia kelele sana hapa kwamba Serikali ilitwaa, lakini lazima nishukuru kwamba Serikali ilikwishatoa pesa nyingi zaidi ya shilingi milioni
360 na sasa tunaendeleza sekondari nyingine japo miundombinu bado haijatosha, tutaendelea kuiomba Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shida yangu ni nini? Wanajeshi walivyoingia kwenye eneo hili sisi tulidhani watachukua eneo hili la ekari 5,500 ambalo lilibaki kwa Halmashauri badala yake wamedai eneo lote lililokuwa shamba la Milundikwa ambalo wananchi wa vijiji nilivyovitaja vyote walipewa kwa barua na kwa maelekezo ya mkoa na mimi wakati huo nilikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nilienda kutembelea kwenye vijiji hivi ni kilio, wananchi hawana mahali pa kulima na wamefukuzwa katika maeneo yao, wamebakiwa na ekari 4,000 tu. Kwa hiyo, takriban wananchi 5,000 hawana mahali pa kulima na ni wakulima. Habari hii nimewahi kuipeleka kwenye Ofisi yake Mheshimiwa Waziri, nimeshapeleka pia Ofisi ya Waziri Mkuu, jambo hili nimekuwa nalizungumza peke yangu sijaona kama naungwa mkono na mtu yeyote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili nimejaribu kuliongea kwenye vikao vya mkoa, nikaambiwa nisiendelee kuongea hilo ni uamuzi wa Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Rais kwanza ni mtu mwenye huruma. Inawezekana sisi wote hatusemi lugha moja, tukilifafanua jambo hili na athari zinazoonekana kwa wananchi, naamini kabisa Mheshimiwa Rais ataona umuhimu wa kuligawa eneo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wanajeshi hatuwakatai wapate eneo lao na wananchi ambao ni wapiga kura wetu lakini ndiyo wakulima na hawana namna nyingine ya kujikimu ni kutegemea kilimo waweze kupata eneo la kulima. Naomba hili lichukuliwe kwa umuhimu wa pekee kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni eneo la elimu. Wilaya yetu ya Nkasi chini ya Mkuu wetu wa Wilaya Said Mtanda, wengi wanamfahamu, tumekuja na sera ya kuitikia kwa vitendo elimu bure. Tumejenga madarasa matatu matatu kwa kile eneo ambapo kuna shule ya msingi na sasa tuna madarasa zaidi ya 348, lakini wananchi hawana uwezo wa kuezeka, wananchi wameshaitikia vizuri, wametimiza wajibu wao. Naiomba Serikali, kwa namna yoyote mtakavyoweza kutusaidia ili wananchi wasivunjike moyo tuweze kumaliza kuezeka madarasa haya ili yaweze kuleta maana ya kuhamasisha wananchi wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la lingine ni afya. Nchini kwetu kuna sera mbalimbali na nashukuru sana jana katika swali langu, kusikia kwamba Serikali imekubali sasa ombi letu la muda mrefu mimi na Mbunge mwenzangu Mheshimiwa Ally Keissy la kujenga Hospitali ya Wilaya katika Wilaya ya Nkasi. Jambo hili ni faraja kwetu, tumelipokea vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini bado vituo vya afya tumekuwa tukivijenga kila mahali. Kwenye Jimbo langu wananchi wanajenga vituo vya afya vinne, tumewahamasisha. Licha ya ahadi tuliyoipata jana lakini bado kuna vituo vya afya vitatu na zahanati zaidi ya 15, zote hizi tumewahamasisha wananchi na sasa wanatimiza wajibu wao, lakini tunaomba Serikali iweze kutusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la umeme. Katika vijiji vyetu imeonekana tutapelekewa umeme katika vijiji karibu vyote lakini wakandarasi wamechelewa. Kuna eneo muhimu sana ambalo nafikiri kama inawezekana wakandarasi waanzie ambapo ni Vijiji vya Sintali, Nkana na Mkunachindo. Vijiji hivi vilisahaulika mara ya kwanza, vikisaulika mara ya pili tena inaweza kuwa sio vizuri sana. Naomba sana hilo liangaliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni juu ya watumishi ambao leo hii tunaambiwa utumishi wao usitishwe kwa sababu wana elimu ya darasa la saba. Jambo hili ni maumivu makubwa sana. Nikiwa Mwenyekiti wa Halmashauri karibu miaka 17, nimeshirikiana na hawa kujenga Wilaya ya Nkasi, kujenga zaidi ya sekondari 23 na sasa niko Mbunge, naendelea kushirikiana nao. Unapowaambia wanaondoka bila kufahamu au kutambua juhudi ambazo wamechangia kwenye maendeleo ya Wilaya, Serikali na wananchi kwa ujumla hii ni dhambi. Hivyo, naiomba Serikali hii sikivu na yenye huruma iweze kuliangalia suala hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kilimo kwetu ndiyo alfa na omega na kwenye hotuba hii nimeona maendeleo ya kilimo na juhudi zinazofanywa na Serikali ikiwemo kuunganisha matrekta. Ni juhudi nzuri zinazotupeleka kwenye kilimo ambacho kitaleta tija zaidi kwa sababu tunatumia mashine. Hata hivyo, uunganishaji huu ungefanyika hata Mkoa wa Rukwa ambako tunalima, pengine ingependeza zaidi kulikoni tunafanyia sehemu ambayo hata kilimo hakifanikiwi vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile changamoto za kilimo amezieleza mwenzangu hapa ni kwamba sisi Mkoa wa Rukwa msimu wetu wa kulima unaanza Oktoba, mbolea tunapata mwezi Februari, suala hili ni kilio kwa wakulima. Nilifanya ziara hivi karibuni, kwa kweli ni kilio. Naomba Waziri na Serikali itambue, nchi hii ni kubwa, inawezekana hatujui misimu mbalimbali, sisi kwetu tunahitaji pembejeo zitufikie Septemba ndiyo tutaweza kufanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile mtuhakikishie pembejeo hizi zinapatikana kwa wingi. Mwaka huu pamoja na Mheshimiwa Rais kuingilia kati jambo hili lakini bado pembejeo ziliisha ikabaki wakulima wanalima bila pembejeo na sasa hivi sisi Mkoa wa Rukwa chakula hakitakuwa kingi sana kwa sababu hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile masoko ni muhimu sana. Tulitembelea Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko huko Iringa, pamoja na majukumu mengine kumbe kuna jambo muhimu ambapo ingeweza kuwasaidia wakulima. Wajibu wake ni pamoja na kutafuta…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kupongeza hotuba ya Waziri Mkuu, napongeza utendaji wake na utendaji unaofanywa na Rais, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika mambo mbalimbali ya kuongoza nchi, tuko nyuma yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wa kilimo katika pato la Taifa na katika kutoa ajira nchini ni mkubwa, hauwezi kupuuzwa na mtu yeyote. Hata hivyo, namna kilimo kinavyoendelezwa hapa nchini hakileti matumaini ya kuleta maendeleo ya haraka katika uchumi wa nchi na vilevile kutoa ajira kwa asilimia 75 ya wakazi wa nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu ya kusema hivyo ni kwamba bado pembejeo hazipatikani kwa wakati hasa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na wakati mwingine pembejeo hazipatikani kabisa. Naomba Serikali ijue misimu ya kilimo ya kanda mbalimbali ili kuhakikisha pembejeo zinawafikia wakulima kwa wakati muafaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kipatikane chombo kitakachopewa wajibu wa kuratibu changamoto mbalimbali za wakulima zikiwemo pembejeo, masoko na utafiti ili kuleta tija kwa wakulima badala ya kufunga mipaka ya nchi kuuza mazao nje. Wakulima wa Rukwa wanapata hasara ya uwekezaji wao katika kilimo pale Serikali inapofunga mipaka na kufanya mazao yao kukosa masoko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani wakulima wa mazao ya nafaka wapate hasara kwa hofu ya nchi kupata upungufu wa chakula wakati mazao ya biashara yanayolimwa na mikoa mingine inapata masoko kama kawaida. Ushauri wangu ni kwamba wakulima waendelee kulima na kuruhusiwa kuuza popote mpaka pale utaratibu muafaka utakapowekwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, ni ukosefu wa ardhi kwa wananchi wa Kata wa Nkandasi, Vijiji vya Mihindikwa, Kasu, Kisura na Malongwe ambapo ardhi yao imetwaliwa na Jeshi la JKT. Takribani ni wananchi 4,000 wa vijiji hivi wamekosa ardhi huku ardhi hiyo ikiwa imekaa bila kutumiwa na mashamba yaliyonyang’anywa wanajeshi mmoja mmoja wanalima huku wananchi wamekaa kushangaa na bila kwenda shamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili limezungumziwa sana lakini hakuna aliyelisikia. Naomba Serikali ilione kwa macho mawili. Kama Mbunge wananchi wamenituma niwaletee Bungeni na mimi nimetekeleza wajibu hivyo wahusika walifanyie kazi vinginevyo watabeba dhambi ya lawama ya mateso ya ukosefu wa ardhi kwa wananchi waliofukuzwa kwenye ardhi waliopewa kihalali na Serikali yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matatizo yanayowakabili wananchi wa Jimbo la Nkasi ni kama ifuatavyo:-

(i) Maji ni tatizo na miradi inayoendelea bado haijatoa matokeo chanya kwa wananchi;

(ii) Suala la mtandao wa simu za mkononi Kata ya Kala iliyoko mpakani mwa DRC, eneo la Ziwa Tanganyika ni kero kubwa kwa wananchi hao; na

(iii) Barabara ya Kitisi - Wampembe chini ya TARURA zinafunga kupitika kwa kukosa matengenezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu elimu, jimbo langu lina takribani vijiji 60 na kila kijiji tumehamasisha wananchi kujenga madarasa matatu. Wote wameitikia kabisa na sasa tuna madarasa 180 hayajaezekwa. Naomba ombi maalum kwa mwitikio mzuri wa wananchi wapewe fedha ya kuezeka madarasa hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la afya, jimboni kuna kata 11 ambapo kata nne wameanza kujenga vituo vya afya. Kata hizo ni Nkandasi, Kala, Ninde, na Kate, takribani zahanati 12 zimejengwa tunaomba msaada wa Serikali.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, napenda kuchangia kuhusu usikivu wa Redio Tanzania. Nkasi Kusini eneo Tarafa ya Wampembe kandokando ya Ziwa Tanganyika hawapati matangazo ya TBC na hali hii inawasononesha sana. Naomba Serikali ilifanyie kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nashauri gharama za matangazo mbalimbali ipungue kwani wananchi wangependa kutangaza matukio mbalimbali lakini tatizo ni gharama. Hata biashara hazikui kwa kasi bila matangazo. Kumbe gharama zikipungua uchumi wa wananchi utaweza kukua na kuwezesha nchi na wananchi wake kuishi maisha yaliyo bora.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
HE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. Nampongeza Waziri na Naibu Waziri wake kwa uchapakazi wao zaidi kwa hotuba iliyoletwa kwetu imeandaliwa vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Nkasi kuna zaidi ya sekondari 22 zinazofanya kazi lakini zote zinakabiliwa na changamoto mbalimbali, za upande wa Nkasi Kusini jimboni kwangu zina shida sana za walimu wa sayansi. Naomba Serikali ituletee walimu hawa kila wanapopatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, majengo ya maabara bado hayajakamilika katika shule nyingi zikiwemo shule za sekondari za Milundikwa, Chala, Ninde Wampembe, Sintali, Kala, Kipande, Nkundi, Kate na Ntuchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maalum kabisa shule ya sekondari ya Milundikwa iliyohamishwa toka makazi ilipokuwa na kupelekwa Kasu ina shida ya kukosa hata nyumba moja ya mwalimu na ukizingatia ni shule ya boarding kwa kidato cha tano na sita. Watoto wa kike wanakaa peke yao mabwenini, hawachungwi kabisa na matron wakati wa usiku wakipata shida. Naomba nyumba hata moja tu. Vilevile miundombinu yake yote iliyobaki hakuna mabweni ya watoto wa kiume, lakini madarasa bado hayatoshelezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shule zote za kata hazifanyiwi ukarabati zikijengwa. Serikali haizipatii fedha ya ukarabati zinaharibika tena, upo umuhimu kuzipa fedha ya ukarabati. Tunaomba Wizara iwe inatembelea shule hizi za pembezoni kuona hali mbaya iliyoko huko ili waweze kubuni namna ya kuwapa motisha watumishi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, walimu waliohamishwa kwenye shule ya sekondari ya Milundikwa iliyotwaliwa na Jeshi kwa maelekezo ya Serikali hawajalipwa haki zao. Naomba walipwe ili waendelee kuchapa kazi kwa moyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Chuo cha Maendeleo ya Wananchi cha Chala naiomba Serikali kutofanya ukarabati wa chuo kwenye majengo yake ya sasa kwani si mali yetu na Askofu wa Jimbo la Sumbawanga ambaye ndiye mwenye majengo ametoa ilani ya kufukuza chuo ili ayatumie majengo yake. Wananchi kupitia vikao vya WDC tumeamua kutoa majengo ya iliyokuwa iwe shule ya sekondari Isoma ambayo ina majengo mengi yanayotosha kuanzia na ukarabati ukifanyika pale itakuwa ni sahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, shule za sekondari nyingi hazina miundombinu ya maji na mfumo wa maji machafu. Shule zote nilizotaja hazina maji ya uhakika na hivyo miundombinu ya maji ya usafi wa vyoo na matumizi yake ni changamoto mfano Nkundi secondary school.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafadhali mtekeleze yote niliyoyachangia hapo juu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, nadhani ninazo dakika kumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kupata nafasi pia namshukuru Mwenyezi Mungu kutulindia afya zetu. Natambua sana kazi za Mheshimiwa Rais anazozifanya katika nchi yetu lakini pia natambua kazi nzuri inayofanywa na Wizara. Mheshimiwa Waziri anafanya kazi vizuri Manaibu wake wawili pamoja na watendaji wa Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mchango kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina shida kubwa sana ya mtandao katika Kata ya Kala na jambo hili nimekuwa nikizungumza zaidi na Mheshimiwa Waziri, vile vile na watendaji. Kata ya Kala ina Vijiji vya King’ombe, Kilambo, Mlambo, Kapumbuli, Mpasa, Lolesha, Tundu pamoja na Kala, vijiji vyote hivi havina mtandao na vijiji viko mpakani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ukiacha tena hiyo kuna vijiji viko Kata ya Sintali, Kijiji cha Kasapa, Kata ya Ninde, Kijiji cha Kisambala na Msamba, lakini vilevile Vijiji vya Nundwe, Mlalambo, havina mtandao, naomba Serikali itupelekee mtandao mara moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Mheshimiwa Waziri atusaidie vilevile barabara. Barabara sasa hivi sisi baada ya TARURA kuanza tulikuwa na mategemeo makubwa sana, lakini bajeti ya mwaka huu ya TARURA haipendezi hata kuiona kwa wale ambao wameziona. Unaweza ukaona hata halmashauri wakati fulani waliweza kuchukua hata own sources wakafungua barabara zinazojifunga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninavyozungumza hivi barabara zangu kadhaa zimejifunga. Naomba fedha za dharura zipelekwe, ili ziweze kupitika. Kuna Barabara ya Kisura – Junction – Malongwe, kuna Barabara ya Nkana – Kala kilometa 68 mabasi hayaendi, Barabara ya Kilambo – Mpasa – Junction haipitiki sasa, kuna barabara ya Kitosi – Wampembe, Barabara ya Katongoro - Namasi, barabara zote hizi hazipitiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile niishukuru Serikali imetupatia hela kidogo kujenga barabara ya Katali – Miyula ambapo Vijiji vya Katani, Chonga, Makupa, Chelatila na Miyula vitaweza kuunganishwa vizuri na ni eneo la uzalishaji mzuri sana. Naomba Serikali ujenzi uanze mara moja ili kazi iweze kukamilika na wananchi wafaidi matunda ya Serikali yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Nkasi Kusini vilevile lina miji midogo iliyoko mwambao wa Ziwa Tanganyika; kuna Mji wa Kala, kuna Mji wa Wampembe. Mji wa Wampembe umeshakuwa mkubwa kiasi kwamba kuna shughuli nyingi za kibiashara na tunaomba tupate bandari, sio gati, tupate bandari Wampembe. Ni muda muafaka sasa, kuna biashara nyingi na ni makutano ya watu wa kutoka nje. Vilevile Kala kuna shughuli nyingi tunaweza tukapata bandari, kama sio bandari, basi tupate gati, itaweza kutusaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona juhudi za Serikali katika kuimarisha usafiri wa majini. Nimeona nia njema ya Serikali ya kuimarisha usafiri wa majini kwani, katika kitabu chake Mheshimiwa Waziri tumeona kwamba, tarehe 18 mwezi huu kuna zabuni ya ununuzi wa meli mpya ya Ziwa Tanganyika imefunguliwa. Kwa hiyo, naomba mchakato huu uendelee, lakini vilevile nimeona kuna mchakato unaoendelea wa kutengeneza meli ya zamani ya Lihemba, jambo hili ni jema tunalifurahia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia, nifurahi kusema kwamba, tumeona juhudi ya kututengenezea uwanja wa ndege wa Sumbawanga ambapo tumetengewa zaidi ya bilioni 12. Hii sio kazi ndogo, kazi inayoenda kufanyika hapa ni fidia, kujenga uwanja pamoja na maeneo ya parking, ambapo ukikamilika tutaanza kuona Bombadier zinatua sasa. Ambazo sasa ni matunda ya Mheshimiwa Rais na Wanarukwa ambao hatujawahi kufaidi kwa kule, sasa tukitengenezewa huu uwanja wataweza kupata nafasi ya kufaidi na kuziona Bombadier. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia kusema kwamba, pamoja na ujenzi wa barabara ya lami kutoka Sumbawanga kwenda Mpanda kuna vijiji vilirukwa kwa barabara ya zamani iliyokuwa inaenda Mpanda. Kuna Vijiji vya Londokazi mpaka pale Palamayo kuna vijiji vingi hapa katikati, Vijiji kama vitatu vinne vya Mtenga, Mwai, Mashete, ni vijiji vya uzalishaji mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona pia kwenye bajeti hii kuna pesa nyingi inatengwa kwa ajili ya ukarabati wa eneo lile, Serikali ingefikiria eneo hili nalo iwekee lami. Kuna wananchi wa Londokazi waliniambia wanafurahi, tuwaombee kwamba, kwa vile lami imefika Chala ipite tu pale iunganishe, ili wananchi wote wa pale wanaolima mazao ya chakula katika maeneo hayo waweze kupata usafiri wa uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudie kupongeza utekelezaji wa ilani unaofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Rais wetu ni Rais wa Kimataifa kwa msingi kwamba, anazungumzwa ndani ya nchi na nje ya nchi na mikakati yake ni ya kipekee. Yale mambo ambayo yalionekana kushindikana wakati ule ndio hayo yameweza kushamiri na kufanya kazi vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hatushangai wanapompinga kupindukia kwa sababu, hoja zinaendelea kwisha, hawana namna nyingine ya kufanya lazima kupinga. Kwa sababu, kama wewe kazi yako ni kupinga hata jambo zuri utaendelea kupinga tu. Unaweza ukapinga kununua ndege, unaweza kupinga kujenga reli katika standard gauge, unaweza ukapinga mambo mazuri yanayofanywa katika nchi hii, jambo ambalo sio zuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba kuunga mkono hoja, naomba Mheshimiwa Waziri ahakikishe kwamba, ananipelekea mawasiliano Kata ya Kala na TARURA ipewe hela za dharura. Barabara hizo zimejifunga na ni wakulima, hawana namna nyingine ya kufanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi. Namshukuru pia Mwenyezi Mungu kwa kutupa uzima, ninayo machache katika Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitambue kazi nzuri sana inayofanywa na Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara hii wamekuwa wakitusikiliza vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ninayo michango miwili, ama mitatu kutoka Jimboni kwangu. Kwanza ni mradi wa Kawa uko Nkundi. Mradi huu unasimamiwa na Wizara moja kwa moja na umeanza miaka minne, mitano iliyopita wananchi wanasubiri maji. Umetumia zaidi ya shilingi bilioni tatu, tangu ujenzi wa chanzo chake, wananchi tumewaaminisha kwamba mradi huu karibu wanapata maji, mpaka sasa Mheshimiwa Waziri bado hawajapata maji. Ujenzi wake umekamilika na nilifika ofisini kwako kukuelezea juu ya changamoto zinazojitokeza, leo hii nilikuwa naongea na wannchi bado maji katika kijiji cha Nkundi hawajapata maji, lakini Kalundi wamepata maji na wao wanasema maji yanachukua muda mrefu sana kujaa kwenye tank kwa hiyo kwa vyovyote vile kuna changamoto ama za kimfumo, mfumo wa kusukuma maji au njia yenyewe.

Kwa hiyo, ninaomba watalaam wa Wizara wausimamie huu mradi vizuri kwa sababu umetumia pesa nyingi na ikiwezekana mradi huu ukitoa maji vizuri upeleke na maji kijiji changu cha Miula itakuwa imesaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, upo mradi mwingine wa mradi wa Isale. Mradi huu una changamoto ya fedha, mkandarasi amesha-raise certificate sasa hivi tunaomba pesa, nilikuja hapo Wizarani Mheshimiwa Waziri ukaniahidi kwamba hivi karibuni utatoa. Tunachotaka kuwaeleza ni kwamba huu mradi ni muhimu sana unabeba vijiji zaidi ya sita na kama mkiupa pesa maana yake ile asilimia ambayo tunatoa maji katika Wilaya yetu itapanda kidogo. Vijiji vya Nkata, Ntemba, Kitosi, Ifundwa na Ntuti vinakusudia kunufaika na mradi huu, shida yake ni pesa. Mtuharakishie pesa ili mkandarasi aweze kuendeleza ujenzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi mwingine ni Mradi wa Mpasa mradi huu wa pia unaendelea vizuri. Mkandarasi sasa hivi amesimama kidogo kwa kukosa pesa lakini anadai vilevile certificate yake ili aweze kuendeleza mradi wenyewe. Mradi huu tunaomba utakapokamilika utapeleka maji King’ombe, Kilambo, Mlambo na tunaomba upeleke Kilambo upeleke na Kapumpuli utatusaidia sana. Maeneo haya ya mwambao huwa yanapata kipindipindu kila wakati, kwa hiyo utakuwa msaada sana na ni muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo maombi pia mapya, niliwahi kuzungumza hapa Bungeni, katika Vijiji vya Kasu, Katani, Milundikwa na Kantawa ili ku-support pia sekondari mpya ya Milundikwa, mradi huu unahitaji watalaam na timu ya watalaam iende nimeandika na barua kwa Wizara, naomba itusaidie kupeleka timu iende ikachunguze, siyo huu tu wajaribu tena kunisaidia katika Kijiji cha Nkana, kijiji cha Sintali na kijiji cha Mkomachindo ambao wana sekondari pia hawana maji ya kutosha yanayoweza kusaidia. Kijiji cha Sintali muda mrefu sana wanatumia maji ya Madimbwi, wana chanzo kizuri lakini haijawahi kusaidiwa. Naomba Wizara iniangalie katika hilo na nimeandika barua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi mwingine muhimu ni mradi wa maji ya Mserereko wa Wampembe. Mji mdogo wa Wampende hauna maji na una kituo cha afya na watu wengi wa kutosha, lakini ndiyo maeneo ambayo chanzo cha magonjwa ya kipindupindu yanaanzia kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika. Mradi ule Halmashauri wameanza kuufanyia kazi, tunaomba support ya Wizara ya kitaalam na kifedha ili uweze kusaidia Vijiji vya Kizumbi, Ng’anga, Katenge, Wampembe na Ng’undwe unaweza ukatusaidia sana. Lakini vijiji kama Mwinza, Izinga, Lusembwa na Itanga hawana maji, naomba sana watusaidie. Vipo vijiji pia vya Kacheche na vijiji vingine vina visima ambavyo tunaomba pia mtusaidie katika uchimbaji na ukamilishaji wa visima vile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mji Mdogo wa Chala una chanzo kizuri cha maji, kinatakiwa kiongezewe tu, kuna kisima kilichochimbwa muda mrefu kiongezewe kwenye chanzo kinachotoa maji sasa ili maji yaweze kutosheleza Mji wa Chala na jambo hili ni pesa kidogo tu itahitajika kwa sababu kisima tayari kimeshachimbwa na miundombinu ipo inayotumika mpaka sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine la mwisho ni suala la umwagiliaji. Nimezungumza juu ya bonde la Mto Kate, bonde la Mto Namansi kuna vyanzo vya umwagiliaji na miundombinu yote na michoro na utaratibu wote wa kihandisi ulishafanywa na Halmashauri kwa gharama kubwa na kuletwa kwenye Kanda, tunachosubiri ni pesa ili tuanze ujenzi wa miundombinu. Nilitegemea kwenye bajeti hii nitaona huu mradi sasa sijui kwa nini. Ninaomba Wizara na watalaam wa Wizara wawe wanapitia michango ya Wabunge, haiwezekani mradi mmoja unazungumzwa mara kumi. Nazungumza kila wakati huu mradi kwamba Halmashauri imetumia gharama kubwa saa katika mradi huu lakini bado hatujaanza umwagiliaji katika maeneo yote mawili ya Kate pamoja na Wamanse.

Mheshimiwa Mwenyekiti, otherwise Wizara inafanya kazi vizuri, naunga mkono hoja na ninapongeza utendaji mkubwa sana wa Wizara na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja na nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa uchapa kazi wake. Hata hivyo, nina mchango ufuatao:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, J.K.T. Hivi karibuni ilianzishwa kwenye eneo la shamba la Milundikwa la zamani ambapo shamba hili lilipomaliza/sitisha kazi zake eneo hilo lilitumiwa na JKT na baadaye Serikali iliamua kuwarudishia wananchi ambao hapo kabla eneo lilikuwa mali yao. Shamba lina ekari 27,000 na katika kurudisha kwa wananchi vilipewa vijiji vya Milundikwa ekari 12,000, Kasu ekari 2,000, Kisura ekari 2,000 na Malongwe ekari 1,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ekari zaidi ya 7,000 ziliachwa kwa Halmashauri ya Wilaya kwa maelekezo ya kupanda miti na utunzaji wa mazingira. Wananchi wameendelea kutumia ardhi hiyo toka mwaka 1998 hadi mwaka jana 2017 ambapo wameondolewa; na zaidi ya watu 4,000 hawana mahali pa kulima na kuna mali zao mbalimbali kama miti, nyumba na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali isichukue eneo lote, wachukue ekari 7,000 ili wananchi waendelee kulima maeneo waliyopewa na Serikali na ieleweke si wavamizi bali walipewa. Tunahitaji uwepo wa Jeshi lakini tunaomba tusaidiwe eneo la kulima. Eneo lote halitumiki, limekaa bila matumizi hata kama patakuwepo matumizi. Naomba Serikali ipokee ombi letu na kulitafakari kwa manufaa ya ustawi wa jamii yetu kiuchumi na kijamii pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi pia iendeleze mila na desturi yake ya kukaa na jamii kwa amani ili kuwawezesha wananchi kunufaika na uwepo wake, kuiga matumizi ya sayansi na teknolojia mbalimbali ikiwemo kilimo, biashara, michezo na mchango wao wanaoutoa kutatua tatizo la upungufu wa walimu kwenye Sekondari ya Milundikwai na wafanye hivyo hata kwenye zahanati zetu za vijiji vinavyozunguka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kunipa nafasi. Kulingana na muda niende moja kwa moja kwenye hoja. Nitazungumzia hoja chache. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo cha mahindi, Mkoa wa Rukwa unalima mazao mengi na hali ya hewa inakubali kuzalisha mazao mengi lakini mahindi yanalimwa kwa asilimia 43 ya mazao yote yanayolimwa pale na ardhi yote. Ndio kusema kwamba kilimo cha mahindi kwa Mkoa wa Rukwa ndiyo maendeleo yao kwa kila kitu kielimu, afya, watoto kwenda shule na kila kitu, lakini sasa tunaanza kukwama kutokana na kilimo kutokwenda vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kilimo hiki kinakwama kwenda vizuri kwa sababu ya mipango mimi niseme mibovu ya kuendeleza kilimo, haiwekwi vizuri. Sasa tunaanza kuona mwaka hadi mwaka hali inakuwa inabadilika, lazima tusimame tupaze sauti. Wakulima sasa wanangamizwa na ndiyo hao wanakaa kijijini ndiyo wanatuchagua na kutuweka kwenye madaraka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali ibadilike, mtazamo wa kilimo sasa si sawa hata kidogo. Kuna mawakala wamehudumia kilimo, si sawa kufikiria kwamba wote walikuwa wezi na kwamba kazi waliyoifanya haina maana, siyo sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie muda mfupi huu kuwasilisha kilio cha wakulima wa Vijiji vya Kasu, Kisula, Milundikwa na Malongwe. Wakulima hawa hawana shughuli nyingine ya kufanya kutokana na uamuzi wa Serikali wa kutwaa maeneo ya jeshi, wamekosa ardhi kabisa. Nitatumia muda mwingi kulisemea hili na leo nashukuru nimefanikiwa kumuona Waziri Mkuu nikamfikishia, najua limefika Serikalini, Serikali najua inasikia. Kwa huruma ya Serikali naomba jambo hili lizingatiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo ni muhimu sana, leteni mbolea; Minjingu sisi hatuitaki, Minjingu haitakiwi, anayesema Minjingu fanyeni utafiti. Basi kama mnaitaka iwekeeni subsidy, muilete kwenye soko halafu wananchi waende kwa kupenda au kwa ubora wake na si kwa kulazimisha. Minjingu katika Mkoa wa Rukwa ni kitu ambacho hakitakiwi na hakizalishi vizuri, labda sehemu nyingine ambayo wameweka wakaleta utaratibu mzuri zaidi, wakafanye utafiti, kwa utafiti uliopo sasa hivi haina matokeo mazuri na mimi ni mkulima ninayesema hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaweza ikatoboreshea Minjingu lakini ituwahakikishie iweke subsidy kidogo, iwekwe kwenye soko ilete ushindani na mbolea halafu baada ya miaka miwili, mitatu wananchi wataamua wenyewe sio kuwala… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasita kuunga mkono hoja Wizara hii ya Kilimo kwa sababu zifuatazo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, sijaona juhudi za kuimarisha kilimo hata kidogo hasa wakulima ambao ndio wapiga kura wa nchi hii, hawajasaidiwa vya kutosha. Mbolea haipatikani kwa wakati, bei yake haieleweki, wala masoko ya mazao hayapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mbolea nashauri Serikali itumie waagizaji wa pamoja (bulk procurement system) lakini waagizaji watakiwe kwenye masharti wafikishe mbolea kwenye mikoa ya uzalishaji na kwa kiwango cha mahitaji, usambazaji uanzie pale Makao Makuu ya Mikoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri mbolea ya Minjingu isilazimishwe kwa wakulima, ifanyiwe utafiti na Serikali iiwekee ruzuku ndogo ili wananchi waitumie miaka miwili au mitatu, wakiipenda wataendelea kuitumia. Mbolea nyingine kama DAP iendelee kuwepo kwenye soko.

Aidha, mawakala walioisadia Serikali kutoa pembejeo wasidhulumiwe, wapewe kile kitakachoonekana ni haki yao. Siyo sahihi kuona kuwa mawakala wote ni wezi na hawapaswi kulipwa. Mbolea ije kwa wakati, Mkoa wa Rukwa leta mbolea mwezi Agosti mpaka Septemba. Mbegu ziwe za viwango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu masoko, wakulima wa Nkasi Kusini wanalima kwa gharama zisizolingana na soko la mahindi kwa sasa. Inakatisha tamaa. Mfumo wa commodity exchange system inaonekana unafanya vizuri. Nashauri NFRA inunue mahindi hata kwa kutengeneza siasa na hawa wakulima, ni muhimu sana. Hawa ndio waliotuamini na kutuweka madarakani. Sasa mambo yao hakuna hata moja lenye nafuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muujiza gani utafanyika kuinua uchumi wa viwanda huku umeacha kilimo nyuma? Hii siyo sawa kabisa, Serikali ishughulikie mambo ya wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi ambao ni wakulima wa vijiji vya Kasu, Kisura, Milundikwa na Malongwe wamenyang’anywa mashamba waliyopewa kwa utaratibu wa kawaida na sasa hawana mahali pa kulima. Zaidi ya watu 4000 wameathirika kwa jambo hili, hawaendi kulima maana wao ni wakulima na sasa watashindwa kusomesha watoto, kujenga nyumba bora, kupata matibabu bora, kuvaa nguo nzuri na kupata chakula cha afya. Serikali iangalie hili jambo.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na nina mchango ufuatao:-

Mheshimiwa Spika, Wizara hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii na ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi. Hata hivyo, fursa nyingi hazitumiki vizuri na wananchi wa ngazi ya chini yaani wananchi wa kawaida wanashambuliwa badala ya kuelemishwa. Maafisa waliopewa dhamana ya kulinda na kusimamia sheria wameondoka kuwa binadamu na sasa wanapomkuta binadamu anatumia rasilimali hii, kwa namna ya makosa haelimishwi badala yake ananyanyaswa.

Mheshimiwa Spika, nashauri elimu ikitolewa vizuri binadamu atakuwa mlinzi mzuri wa rasilimali za majini. Tabia ya kuwashambulia, kuwaka na kuwatesa sababu ya samaki wawili/watatu si sawa. Walitoka wapi hawa, wanaagizwa na nani?

Mheshimiwa Spika, kuhusu ufugaji wa samaki haujajionesha kama ni kipaumbele, naomba Wizara ijitahidi kutoa elimu.

Mheshimiwa Spika, Ranchi za Taifa, Nkasi tunayo Kalambo Ranch, haina mtaji wa kutosha na mifugo iliyopo ni michache sana. Ranchi ni kubwa lakini mifugo ni michache na hakuna mtaji na miundombinu mingine ya kuimarisha ufugaji. Ranchi haina gari, watumishi wachache na vilevile haitengewi bajeti ya maendeleo na Serikali ili kuboresha ufugaji.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mikopo kwa wavuvi, katika Jimbo la Nkasi Kusini wavuvi hawajapata mikopo ya kuboresha uvuvi na hivyo uvuvi unaoendeshwa ni wa kizamani sana na hauna tija.

Mheshimiwa Spika, ufugaji wa samaki, naishauri Wizara kutenga bajeti kuwasaidia wananchi wa Kata za Ninde, Kizumbi, Wampembe na Kala walioko kandokando ya Ziwa Tanganyika, waelimishwe namna ufugaji wa samaki ili kunusuru maisha yao kwani operation zinazoendelea wananchi hawa wanatii sheria na katazo la Serikali.
Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na ninachangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika Jimbo langu la Nkasi Kusini kuna Vijiji vya Kusapa, King’ombe, Mlambo, Kilambo, Ng’undwe, Namansi, Kizumbi na Mlalambo, vilevile Kijiji cha China na Kijiji cha Nkata mipaka ya vijiji vyao na hifadhi havieleweki na vijiji vingine viko ndani ya pori na kuwa pori lilikuta vijiji hivyo na kuvizingira, kwa hiyo hawana ardhi ya kutumia kwa ajili ya kuendeleza maisha yao ya kila siku.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali kupitia Kamati ya Wizara mbalimbali itoe matokeo ili kusuluhisha jambo hili. Naomba matokeo yawe wazi na wananchi wajue hatma ya jambo hili.

Mheshimiwa Spika, Kijiji cha Kasapa kwa mfano, kimezingirwa na maeneo ya hifadhi mawili pori la TFS na Lwanfi Game Reserve ambapo Wizara ilitembelea kwa juhudi yangu. Waziri mstaafu Mheshimiwa Maghembe aliweza kuona jinsi wananchi walivyokosa eneo la kulima maana mipaka iko mita zisizozidi 300 pande zote nne yaani Mashariki, Magharibi, Kusini na Kaskazini. Wizara ilete mapendekezo ni namna gani Wizara imejipanga kuwasaidia wananchi baada ya kutembelea kila kijiji wamekaa kimya, why?

Mheshimiwa Spika, matatizo ya wanyama (tembo) wanasumbua wakulima wa Vijiji vya King’ombe, Mlalambo, Ng’undwe na Mlalambo na Vijiji vya Kisumbaka na Kasanga Wilayani Kalambo, tembo wameuwa watu zaidi ya watatu kwa miaka miwili mfululizo. Wananchi wa eneo hilo wanasema hawana mtumishi hata mmoja wa kuzuia tembo wasilete maafa hayo. Tunaiomba Serikali ipeleke watumishi wa Maliasili Kisumba kuzuia maafa haya. Naiomba Serikali itusaidie kupunguza ukubwa wa pori hili ili wananchi wa vijiji nilivyovitaja wapate ardhi ya kulima ili waendeleze maisha yao hapa duniani.

Mheshimiwa Spika, Mlalambo, Ng’undwe wananchi wanapekuliwa hovyo hovyo, hawawezi kujenga nyumba eti mbao kutoa wapi? Wananchi wanachapwa viboko, Mlalambo na Ng’undwe si sawa eti huo ubao wa mlango katoa wapi? Haya ni malalamiko niliyopewa nilipoenda kwenye ziara, naomba tuliangalie jambo hili.

Mheshimiwa Spika, kuna ardhi ya wananchi ya Kakumbu inatumika chini ya kiwango iko wapi Kamati ya Wizara tano ambayo tumeipatia migogoro ya watu wa Sintali, Nkama na Nkomanchindo.
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, napenda kuunga mkono kwa mchango ufuatao:-

Mheshimiwa Spika, fedha za miradi haitoki, hivi karibuni Serikali iliitisha mkutano wa Wenyeviti wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wakurugenzi na Maafisa Mipango kuainisha miradi michache ambayo itakuwa muhimu kutoa fedha, iliorodheshwa lakini mpaka sasa hakuna fedha iliyotolewa na Serikali. Mara kadhaa inasema fedha ipo, naomba ipelekwe kwenye miradi hii.

Mheshimiwa Spika, tuliwatangazia wananchi kuwa sasa Serikali yao imewakumbuka, pelekeni fedha ya miradi kwenye Halmashauri ambako miradi ya afya, miradi ya vituo vya afya, miradi ya zahanati, miradi ya maji vijijini, miradi hii imeathirika vibaya.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha haitoi fedha zinazoidhinishwa na Bunge kwenye miradi mingi ikiwemo ya maji, ile miradi ya vijiji kumi na REA pia imeathirika sana. Wizara ya Fedha isijichanganye, mwaka jana tuliambiwa mkulima atasafirisha mazao gunia kumi nchi nzima, Halmashauri wanadai, wafanyabiashara wadogo wanaosafirisha mazao tani moja na walitoa barua ya ufafanuzi ikidai mkulima pekee ndiyo inamhusu, tena siyo mchuuzi mdogo mdogo, ipi ni ipi tuelezeni tuelewe.

Mheshimiwa Spika, mikopo kwenye mabenki imebana sana, trend ya uchumi kwenye mabenki yote yanapiga kelele kudorora na mikopo midogo midogo haipatikani. Tunaomba masharti yapozwe kidogo ili wananchi waione fedha kwenye mzunguko wa kila siku. Wizara itoe fedha ya kununulia mazao ya wananchi ili wakulima wapate maendeleo na viwanda vipate kuanzishwa kwa vile malighafi itaweza kupatikana. Wizara ya Fedha ilipe madeni ya Mawakala wa Pembejeo.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha itoe kipaumbele kwenye utoaji wa fedha za kibajeti zote. Hatuwezi kukaa Bungeni kupanga bajeti za Wizara unafika mwisho wa mwaka unakuta Wizara imetoa fedha wakati mwingine chini ya asilimia 20 ya bajeti, kwa nini?

Mheshimiwa Spika, nataka kuona fedha za Wizara zote ikiwemo ya Kilimo, Maji, Nishati, Afya na kadhalika, kulingana na matamko ya kitaifa na mikataba tulioridhia. Malipo ya makinikia, malipo ya watumishi mbalimbali kama walimu.
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, napenda kuunga mkono kwa mchango ufuatao:-

Mheshimiwa Spika, fedha za miradi haitoki, hivi karibuni Serikali iliitisha mkutano wa Wenyeviti wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wakurugenzi na Maafisa Mipango kuainisha miradi michache ambayo itakuwa muhimu kutoa fedha, iliorodheshwa lakini mpaka sasa hakuna fedha iliyotolewa na Serikali. Mara kadhaa inasema fedha ipo, naomba ipelekwe kwenye miradi hii.

Mheshimiwa Spika, tuliwatangazia wananchi kuwa sasa Serikali yao imewakumbuka, pelekeni fedha ya miradi kwenye Halmashauri ambako miradi ya afya, miradi ya vituo vya afya, miradi ya zahanati, miradi ya maji vijijini, miradi hii imeathirika vibaya.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha haitoi fedha zinazoidhinishwa na Bunge kwenye miradi mingi ikiwemo ya maji, ile miradi ya vijiji kumi na REA pia imeathirika sana. Wizara ya Fedha isijichanganye, mwaka jana tuliambiwa mkulima atasafirisha mazao gunia kumi nchi nzima, Halmashauri wanadai, wafanyabiashara wadogo wanaosafirisha mazao tani moja na walitoa barua ya ufafanuzi ikidai mkulima pekee ndiyo inamhusu, tena siyo mchuuzi mdogo mdogo, ipi ni ipi tuelezeni tuelewe.

Mheshimiwa Spika, mikopo kwenye mabenki imebana sana, trend ya uchumi kwenye mabenki yote yanapiga kelele kudorora na mikopo midogo midogo haipatikani. Tunaomba masharti yapozwe kidogo ili wananchi waione fedha kwenye mzunguko wa kila siku. Wizara itoe fedha ya kununulia mazao ya wananchi ili wakulima wapate maendeleo na viwanda vipate kuanzishwa kwa vile malighafi itaweza kupatikana. Wizara ya Fedha ilipe madeni ya Mawakala wa Pembejeo.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha itoe kipaumbele kwenye utoaji wa fedha za kibajeti zote. Hatuwezi kukaa Bungeni kupanga bajeti za Wizara unafika mwisho wa mwaka unakuta Wizara imetoa fedha wakati mwingine chini ya asilimia 20 ya bajeti, kwa nini?

Mheshimiwa Spika, nataka kuona fedha za Wizara zote ikiwemo ya Kilimo, Maji, Nishati, Afya na kadhalika, kulingana na matamko ya kitaifa na mikataba tulioridhia. Malipo ya makinikia, malipo ya watumishi mbalimbali kama walimu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja kwa mchango ufuatao:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, napongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri ya kulinda amani na usalama. Nashauri pamoja na kazi nzuri inayofanywa, Polisi wasichukue sheria mkononi mwao kama vile anapotokea mhalifu badala ya kumpeleka Mahakamani hupigwa na kufia mikononi mwa Polisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vitendo hivi vimeshamiri na pia imetokea kwenye Jimbo langu Kijiji cha Kilambo, Kata ya Kala ambapo mtuhumiwa wa wizi kijana alipigwa na Polisi na akapoteza maisha. Haya yanatokea sehemu mbalimbali nchini na yanalalamikiwa sana. Nashauri Polisi wasitumie nguvu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo malalamiko kuwa watu wanapotea, wanatekwa na wengine hawajapatikana. Vitendo kama hivi siyo utamaduni wa Tanzania. Tanzania irejeshe taswira nzuri iliyojengeka miaka ya matumizi ya vyombo vya kutafsiri sheria, yaani Mahakama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napongeza kazi nzuri ya kuendelea kulinda raia na mali zao ambapo mpaka sasa raia na mali zao wapo salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri Waziri anipe bati kwa ajili ya kuezeka kwenye vituo vya polisi vilivyojengwa na wananchi vya Tarafa ya Kate, Mji Mdogo wa Kate na Tarafa ya Wampembe, Kata ya Kala na Kijiji cha Mpasa wananchi wasikate tamaa maana wao wameona umuhimu wa kuwa na huduma ya Polisi lakini wameshindwa kuezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Polisi Nkasi hawana nyumba za kutosha. Pia Polisi Nkasi hawapati fedha ya mafuta na badala yake wanakuwa wanaomba omba wakipata dharura. Naomba Polisi Nkasi waongezewe gari ili ipelekwe Wampembe kwani ni mbali na Makao Makuu na ni mpakani.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Naibu Spika, napongeza hotuba ya Kamati ya Madini, lakini pia naipongeza hotuba ya Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Rukwa hakuna shughuli za uchimbaji mdogo mdogo wa madini wala uchimbaji mkubwa. Hii ni kutokana na kutokufanyika kwa utafiti wa kujua aina ya madini yanayoweza kupatikana kule. Naamini kazi ya utafutaji ingefanyika wananchi wa Rukwa wangeweza kunufaika na rasilimali hii muhimu, tafadhali Wizara fanyeni hiyo kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Mheshimiwa Rais kwa usimamizi wake muhimu katika eneo hili. Leo tanzanite inaanza kulitangaza Taifa. Udhibiti uliowekwa kwa kujenga wigo utapandisha mapato ya nchi kwa tanzanite.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kujua, ni lini fedha za makinikia zitapatikana? Je, ndiyo mwisho? Kwa vile Serikali ilituambia hapa kuwa kutapatikana fedha ingetamkwa wananchi wajue ili waone juhudi za Serikali yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kuna mgodi wa makaa ya mawe jimboni kwangu unaitwa Mkomolo unaofanywa na mwekezaji Edenville. Naomba utaratibu ufanyike ili ikiwezekana waweze kufua umeme na uingie kwenye Gridi ya Taifa. Hii itasaidia kuwa na vyanzo tofauti tofauti vya nishati na huenda kwa kufanya hivyo bei ya nishati ya umeme inaweza kupungua na kuimarisha huduma ya upatikanaji wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, Rukwa Kusini kuna helium, Tanganyika kuna mafuta, tuanze basi kuchimba rasilimali hizi ili kukuza uchumi wa taifa na Mkoa kwa ujumla.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napongeza kazi nzuri sana inayofanywa na viongozi wa Wizara hii na Rais wetu. Mheshimiwa Rais amekuwa mzalendo na mtu ambaye yuko tayari kufa kwa ajili ya kutekeleza kazi za kizalendo kwa nchi yake. Tumeona hatua mbalimbali alizozichukua kwa kunusuru uchumi wa nchi hata zile ambazo zinahitajika uamuzi mgumu, ni Rais mwenye maamuzi na anasimama kidete kulinda msimamo wake ambapo mara zote ni wa kizalendo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Selemani Jafo ni kijana shupavu mwenye kufanya kazi kwa weledi mkubwa, mara zote anakonga nyoyo za Watanzania. Mheshimiwa Jafo hakika amejaa kwenye nafasi yake hongera sana Mheshimiwa jafo. Nawapongeza pia Manaibu Mawaziri wawili Mheshimiwa Kandege na Mheshimiwa Kakunda, wote kwa hakika wanakonga nyoyo za Watanzania kwa uchapakazi wao. Mheshimiwa Rais ni kweli ana macho mengi kubaini wateuzi wake kuwa watendaji wanaoakisi barabara mwelekeo na kasi ya Mheshimiwa Rais mwenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze kwa dhati ya moyo wangu Katibu Mkuu wa Wizara, Mheshimiwa Mussa Iyombe, kiongozi mzoefu wa siku nyingi kwa kazi nzuri sana anayofanya kuongoza Wizara, lakini pia kupata nafasi ya kusikiliza Wabunge katika changamoto mbalimbali, Mungu akuzidishie maisha aendelee kutoa uongozi kwa Watanzania. Mwisho, niwapongeze Manaibu Waziri na Katibu Mkuu kwa kazi nzuri sana; ndugu Zainabu Chaula na Tixon Nzunda, Wizara iko vizuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, elimu, Wilaya ya Nkasi tumejenga vyumba vya madarasa vitatu, kila shule ya msingi kuna madarasa yapatayo 348 yote yamefikia mtambaa panya yaani yamekamilka katika ujenzi wa ukuta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi walihamasishwa na sisi viongozi tukiongozwa na kamanda wetu DC Said Mtonda, watusaidie wananchi watashindwa kutuelewa. Tunaomba watupatie fedha ili juhudi hizi ziwe na manufaa yaliyokusudiwa na nadhani Nkasi inaweza kuwa ni Wilaya ya kwanza nchini, naiomba Wizara ilipe fedha ili pia iwe na maana ya kutupongeza na kuhamasisha maendeleo nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, tumekosa watumishi wa kutosha katika sekta ya elimu hasa shule za msingi bado Walimu hawatoshi hasa maeneo ya mwambao mwa ziwa, Kata za Kala, Wampembe, Kizumbi na Ninde.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, nyumba za Walimu hazitoshi kwenye shule za msingi na sekondari pia tunaomba fedha ili watumishi hawa muhimu wapate mahali pa kuishi ili watulie kazini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nne, wananchi wa Jimbo la Nkasi Kusini wamejitahidi kujenga maabara katika sekondari zote na sasa yamebaki magofu, watusaidie kutoa fedha ili kukamilisha ujenzi wa maabara ili pia majengo yatumike kupata wataalam wa sayansi kama Walimu wa Waganga na wataalam wa maabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tano, fedha za miradi kwenye halmashauri yetu hazijakuja hasa kwa miradi iliyopitishwa mwaka jana. Fedha iletwe haraka kukamilisha miradi iliyopendekezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sita, kilimo, kwa Mikoa wa Nyanda za Juu Kusini msimu wa kilimo huanza Oktoba kumbe pembejeo zifike Agosti kila mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, saba, Mawakala wa mbolea wapewe masharti ya kufikisha pembejeo kwenye mikoa ya uzalishaji siyo kurundika Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nane, Serikali itenge fedha kwa ajili ya top up kuwezesha bei za pembejeo zisibadilike badilike katikati ya msimu kutokana na mabadiliko kwenye bei ya dunia ili kutoleta usumbufu kwa wananchi. Hii ni muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tisa, wananchi wa Vijiji vya Kaso, Milundikwa, Kisura na Malongwe wameathirika sana na ujio wa jeshi ambapo ardhi yao waliyopewa kihalali na nyaraka zipo wamenyang’anywa. Naishauri Serikali kuliangalia jambo hili vizuri na Mheshimiwa Waziri naomba amwagize Mkuu wa Mkoa akafanye tathmini ili kuona hali iliyojitokeza zaidi ya watu 5,000, hawana pa kulima kabisa na ni wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumi, naomba gari ya kusaidia kazi ofisi ya kilimo ambao hawana fedha kabisa za kufanya matengenezo ya mara kwa mara gari yao mbovu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, afya hali ya huduma za afya kwenye zahanati zetu siyo nzuri kwa tatizo la ukosefu wa watumishi hatuna Waganga, Manesi na watumishi wengine. Tunaomba watusaidie kupata watumishi, zahanati nyingi zinaendeshwa na Wauguzi. Wananchi kujenga zahanati katika Vijiji vya Kautawa, Kipande, Kalundi, Mkomanchimbo, Mlambo, Tundu, Kisambara, Ifundwa, Nchenje, Ntuchi na zinginevyo, watusaidie kumaliza zahanati hizi. Wananchi pia wanajenga Vituo vya Afya vya Kasu Kala, Kate na Ninde. Tunaomba kusaidiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakushukuru sana kuona Serikali imeweka kwenye bajeti yake, ujenzi wa hospitali ya wilaya, nampongeza kwa hatua hiyo, lakini nashauri kutekeleza ujenzi kwa mtindo wa force account, impact itaonekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, gari ya wagonjwa Wilaya ya Nkasi ina majimbo mawili, gari mbili zimetolewa kwa jimbo moja, mimi sijapata jambo hili halina afya kwa siasa za jimbo. Naomba gari moja Kala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ya maji, jimboni ina kasi ndogo, mwanzo kazi zilikuwa zinaenda vizuri, lakini kwa sasa kazi yake imepungua sana Serikali itoe usimamizi zaidi kwa miradi yote ya maji ikiwepo ya Kisura, Kawa, Mpasa na Isake ili kasi iongezeke na rasilimali zitumike kwa manufaa ya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TARURA hawana gari ya supervision, hawana fedha ya kutosha kwa matengenezo ya dharura, hali siyo nzuri barabara zifuatazo zimefungwa na zingine kupitika kwa tabu kabisa, barabara hizo ni:-

Barabara ya Kitosi- Wampembe kupitika kwa shida na daraja la Kizumbi limekatika na hakuna fedha. Barabara ya Ninde- Kala inapitika kwa shida sana makalvati yamekatika hakuna matengenezo na fedha hakuna. Barabara ya Namanyere- Ninde ijengwe ili kunusuru fedha iliyotumika kujenga madaraja na makalvati, lakini pia kufungua Kata ya Ninde iliyoko kandokando ya mwambao mwa Ziwa Tanganyika.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kupata nafasi, na nimshukuru vilevile Mwenyezi Mungu kwa kunijalia uzima, kama nitapata nafasi nitaweza kuchangia maeneo matatu, eneo la kilimo, afya na elimu na kama nafasi itaruhusu na mambo yanayohusu barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niungane na wenzangu wanaotoa pongezi nyingi sana kwa hotuba nzuri ya Mheshimiwa Mpango na utendaji mzuri sana wa Serikali ya Awamu ya Tano na hapana mashaka juu ya utendaji huu, umejidhihirisha juu ya mambo mengi ambayo ushahidi wake nitauelezea baadae.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende moja kwa moja kwenye kilimo. Nakubaliana sana na taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti juu ya mapendekezo anayotoa juu ya kuboresha kililimo katika kitabu chake ukurasa wa 18. Kwamba ili tuweze kwenda lazima Serikali itenge fedha za kutosha katika kuhudumia kilimo na hasa ukiona mwelekeo wetu ni mwelekeo wa viwanda, sasa huwezi kukwepa na historia inatuambia nchi zote duniani zilizofanya vizuri kwenye viwanda zilianza kuboresha kilimo, kwa hiyo hatukwepi hapo. Na kwa mtazamo wangu naona ni kama tunaenda hatujazingatia sana suala la kuimarisha kilimo. Katika kuimarisha kilimo ni lazima upatikanaji wa pembejeo uwe wa uhakika na kwa wakati na kwa bei nafuu zinazokuwa affordable kwa wakulima, zinazowezekana kununulika na uchumi ulipo sasa kwa wakulima.

Lakini pia kuendeleza vituo vya utafiti ili viweze kuleta matokeo bora kwa mbegu na mazao tunayofanya. Lakini vile vile kuhakikisha kwamba upatikanaji wa nyenzo za uvuvi zinapatikana bora na kwa bei nafuu na kuimarisha masoko ya kilimo na ufugaji. Mambo haya kama yatazingatiwa, kilimo kitakwenda. Lakini ninavyoona ni kama kilimo kwetu hapa Tanzania tunaacha sekta binafsi ikiongoze, ukiwaachia sekta binafsi kwa mawazo yangu mimi, nashauri Serikali si sawa ni hatari kwa usalama wa chakula lakini pia kwa usalama wan chi yetu kwa sababu kilimo kinaajiri Watanzania wengi, na ukiachwa kiendeshwe kwa matumaini ya kusema sekta binafsi ndio itakuwa inawawezesha pembejeo na masoko unafanya makosa makubwa. Tuje na mkakati utakaowezesha kubuni mbinu za kuwezesha upatikanaji wa haya niliyoyasema kwa wakulima, kwa uhakika na kwa wakati, lakini vilevile masoko yao. Na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ni chombo ambacho kikitumiwa vizuri na kikiwezeshwa, kinaweza kikaleta neema ya wakulima. Kikatafuta masoko ya ndani ya nchi nan je ya nchi nab ado mambo yakaenda vizuri kwenye kilimo. Kwa hiyo ndugu zangu naomba Mheshimiwa Waziri, uhakikishe kwamba suala la kilimo inakuwa kipaumbele cha kwanza. (Makofi)

La pili, katika kilimo kuna uvuvi. Suala la uvuvi linavyoendeshwa na wavuvi wanaonekana kama ni balaa sasa hivi, Ziwa Tanganyika sasa hivi kuna taharuki kubwa na wananchi hawavui wamekaa na maisha ya kule nature yao wanategemea ziwa. Ukishaweka utaratibu ambao huwawezeshi kuingia Ziwani maana yake wanakufa kabisa. Naomba kwa kutumia hotuba hii, Waziri anaehusika ajaribu kuangalia vijana wake aliowatuma kule, wanachokifanya sio hicho. Kwa sababu mtu anapokiuka utaratibu lazima watu wapige kelele wanajua haki zao, kwa hiyo nawaomba Serikali itupie macho kule. (Makofi)

Sasa hivi wavuvi wanahamia ng’ambo ya DRC na kwa maana hiyo Halmashauri yetu ya Wilaya ya Nkasi leo hazina mapato sasa kwa mwezi huu wa Oktoba na wananchi wana taharuki kubwa na wananchi wa maeneo hayo hawapati hata kitoweo cha samaki. Kwa hiyo, itakuwa shida kubwa, naomba Serikali iliangalie hili na ifuatilie kwa haraka sana hali ni mbaya sasa hivi. (Makofi)

Suala lingine ni suala la Afya, ndugu zangu suala la afya nchi nzima tumeona juhudi kubwa sana itanayofanywa na Serikali yetu hasa kwenye vituo vya afya na mimi kwenye Jimbo langu nimeweza kupata Kituo cha Pembe na sehemu zote. Lakini niseme tu juhudi hii ni upendo wa Serikali kuonesha kwamba ikiwa kipaumble ni afya maana yake watu watakuwa na afya na wataweza kuendeleza shughuli zingine. Niombe haya maboma yote ambayo yapo kupitia mpango huu ukajibu ukaweza kuyaezeka na kukamilisha, nchi nzima kuna zahanati nyingi sana zimejengwa, kuna vituo vya afya vingi tu, sasa kupitia mpango huu tuone kama vinaendelezwa na kujengwa. Kwenye Jimbo langu tu peke yake kuna zahanati zaidi ya 12 zilizojengwa na wananchi ziko katika hatua mbalimbali, wananchi hawaja anza kupata huduma. Kwa hiyo na tumewahamasisha na wakahamasika, sasa itakuwa tunapoenda kwenye uchaguzi kipindi kijacho itakuwa kazi kubwa sana kuelezea haya. Lakini vilevile vituo vya afya viko. Vingi tu nchi nzima kwenye Jimbo langu tu viko zaidi ya vinne Kasu, Kate, Namansi kule, Mbinde, Wampembe, Kala bado vinatakiwa visaidiwe na wananchi wa Kala wana shida kubwa zaidi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. Nampongeza Waziri Mkuu na Mawaziri walioko chini yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napongeza kazi nzuri zinazotekelezwa na Serikali yetu ya Awamu ya Tano. Naridhishwa sana namna miradi mingi ya kipaumbele kwa Taifa inavyotekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya PIC, tumeweza kutembelea miradi mingi inayotekelezwa kwa kipindi hiki. Miradi hii ni pamoja na SGR ambao ni mradi wa ujenzi wa reli kwa kiwango cha kimataifa. Kazi inaenda vizuri sana na ujenzi unaenda kwa kasi na naamini ifikapo Novemba, 2019 huduma ya usafiri itawezekana kuanza kupatikana kwani hadi Morogoro kazi ni nzuri kabisa (Dar – Morogoro). Nampongeza Rais wetu na watendaji wote wakiongozwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi mwingine ni ujenzi wa Kituo cha Kufua Umeme cha Kinyerezi I and II. Tumeweza kuona vituo vyote na kuona kiasi cha umeme kinachopatikana katika maeneo yote mawili, ni kazi kubwa imefanyika. Tumepata maelezo kuwa kwa sasa MW 1,650 zinapatikana kiasi hiki kinatosheleza mahitaji ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kuna utaratibu wa ujenzi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Stigler’s Gorge ambapo tutaweza kupata MW 2,100. Kiasi hiki ni kikubwa kuliko hata kiasi cha umeme tulichoweza kufanikiwa kupata tangu tupate uhuru. Kazi hii nayo imeanza katika hatua ya awali, inatia moyo na inaonyesha Mheshimiwa Rais alivyo mtu wa kuthubutu na sina shaka tutafanikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi mwingine ni ununuzi wa ndege na ujenzi wa viwanja vya ndege nchini. Nampongeza sana Mheshimiwa Rais adumu na Mungu ampe afya atimize malengo yake ambayo yamepokelewa vizuri sana na Watanzania wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwingine ni miradi ya ujenzi wa vituo vya afya, hospitali za Wilaya na Mikoa. Hizi ni juhudi kubwa kabisa, naipongeza sana Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada kusema hayo, naomba nichangie mambo ya jimboni kwangu. Naomba Serikali inipe Kituo cha Afya katika Kata za Ninde, Kijiji cha Ninde. Wananchi wamejenga kwa nguvu zao jengo la vyumba 10, naomba tuwaunge mkono.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile naomba Kituo cha Afya katika Kata ya Kala. Kata hii iko umbali wa zaidi ya kilometa 150 toka Makao Makuu ya Wilaya. Ni muhimu sana wapatiwe kituo cha afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Vijiji vya Kasapa King’ombe, Mlambo Ng’undwe na Mlalambo mgogoro wao wa mpaka na Lwanfi Game Reserve utatuliwe. Naomba utatuliwe ili wananchi waweze kuishi kwa amani na kuzalisha uchumi kwa manufaa yao na Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mgogoro wa Shamba la Milundikwa JKT na vijiji vinavyozunguka vya Kasu, Milundikwa, Kisula na Malongwe. Nashauri wananchi waongezewe ardhi ya kulima ili wafanye kazi za kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba vijiji vya Katani, Malongwe, Sintali, Nkana Kasapa na Mkomanchindo viwe vya mwanzo mwanzo kupata umeme ili kuweka vizuri mazingira ya kisiasa na maendeleo jimboni. Naomba umeme uende katika vijiji hivyo kwa awamu hii ya tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Shule ya Sekondari ya Kala miundombinu yake ya nyumba za walimu itazamwe. Pia mabweni ya watoto wa kike hakuna na iko maeneo ya mwambao ambako mwamko wa elimu bado ni duni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Namanyere - Ninde naomba ikamilishwe. Daraja la Kizumbi, Kata ya Kizumbi lijengwe kwani maombi yalishaletwa kwa maombi maalum lakini ni muda mrefu halipitiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Kata ya Kala wapate kituo cha Afya. Wananchi wako tayari kutoa nguvu zao kushiriki katika ujenzi huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Kata ya Sintali pia hawana maji katika vijiji karibu vyote vinne. Naomba utafiti ufanyike kuona chanzo kizuri cha kusaidia wananchi hawa ambao vijiji vyao viko karibu karibu yaani Sintali, Nkana na Mkomanchindo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nashauri katika suala la kilimo Serikali ione namna ya kuendelea kutoa ruzuku kwa wakulima wa chini bila hivyo hali inaendelea kuwa mbaya sana katika uzalishaji na kumudu maisha kwa wakulima hawa. Pembejeo zitolewa hata kwa watu wachache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile masoko ya mazao ya wakulima hasa mahindi Mkoa wa Rukwa na mikoa yote inayolima zao hilo yatiliwe maanani vinginevyo wakulima watakata tamaa. Naiomba Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi ilete mageuzi kwenye kilimo kama inavyofanya katika maeneo ya miundombinu mbalimbali kama ujenzi wa SGR, ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, afya na elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naona kama Mheshimiwa Magufuli ni zawadi kwa Watanzania toka kwa Mungu. Ana maono na uthubutu na kweli anatatua yale yote yaliyoonekana kushindikana. Kama vile madawa ya kulevya; uzembe wa kazi Serikalini; wizi wa mali ya umma; urasimu na kuchelewesha maamuzi na uonezi hasa kwa watu wa chini. Mungu amzidishie aweze kufikia malengo yake kwa Watanzania.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili nipate kuchangia kwenye Wizara hii muhimu sana, Wizara ya Elimu. Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na vile vile napongeza sana utendaji mzuri wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kazi zote wanazosimamia, Mheshimiwa Rais anatembea kwenye ahadi zake, lakini nimpongeze Waziri kwa uchapakazi wake, Waziri na wasaidizi wake bila shaka. Mheshimiwa Waziri amekuwa akitusaidia sana, ukimwona anakusaidia shida mara moja, lakini pia ametutembelea, ametembelea Rukwa, ametembelea Wilaya ya Nkasi na Jimbo letu ametembelea na kutokana na ziara yake tumenufaika. Nimeona hapa kwenye hotuba yake kunaanza ujenzi Chuo cha VETA Rukwa, ni jambo jema sana tunampongeza, tunaomba tu kasi ya ujenzi iwe nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kuanza kwa ukarabati wa Chuo cha Wananchi Chala ambacho kipo Jimboni kwangu na nimekuwa nikikisemea sana hapa, tunampongeza na tunashukuru sana. Naomba nishauri hapa, chuo hiki kikarabatiwe, kinapokarabatiwa ukarabati huu uelekezwe kwenye majengo ambayo wananchi waliyatoa maana yake eneo ambalo chuo kipo ni eneo la majengo ya Baba Askofu, Jimbo Katoliki la Sumbawanga na ameonesha nia ya kutumia majengo yale na wananchi walishaamua kujenga majengo mengine eneo la Isoma kwenye shule moja ya sekondari tunayotaka tuianzishe ya Isoma na tumekubali chuo kihamie pale. Kwa hiyo naomba huo ukarabati aliotutengea hapa uelekezwe hapo, atakuwa ametusaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kukushukuru kwa kutenga fedha mwaka huu kuanza ukarabati wa majengo ya kuanzisha Chuo cha Ufundi Stadi – Nkasi. Mambo haya yatasaidia sana vijana wetu wanaomaliza darasa la saba na wale ambao wanashindwa kuendelea baada ya kumaliza form four.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeomba pia pesa na umetusaidia, nishukuru Shule ya Sekondari Milundikwa umetupatia zaidi ya shilingi milioni 190 na Shule ya Sekondari ya Nkundi tumepata zaidi ya shilingi milioni 130 na Shule ya Sekondari ya Nduchi tumepata shilingi milioni 91, zote hizi ni za kujenga miundombinu ya sekondari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile shule za msingi tumeweza kupata pesa katika Shule za Msingi Kasu na Chala. Tunaomba waendelee kutusaidia, naomba Shule za Sekondari za Sintali, Kala, Kipande, Kate na Ninde zina hali ngumu sana ya miundombinu ya majengo, madarasa pamoja na maabara. Tunaomba utakapopata nafasi uweze kutusaidia katika maeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuone umuhimu pia wa kusaidia katika maeneo ya Shule za Sekondari za Sintali, Kala na Wampembe. Wizara inahimiza ubora wa elimu lakini katika kuhimiza ubora wa walimu, yapo maeneo katika jimbo langu ya mwambao wa Ziwa Tanganyika miundombinu ya elimu ni mibaya kabisa. Jimbo hili lina tarafa zaidi ya tano lakini Tarafa ya Wampembe miundombinu yake ni migumu sana na ni kandokando ya Ziwa Tanganyika. Kuna vijiji vipatavyo 23, katika vijiji hivi walimu wana hali ngumu sana ya ukosefu wa nyumba, madarasa ya kutosha na usafiri katika eneo lile ni mgumu sana, inafanya hata wakati mwingine wa mitihani vijana kuhama shule moja hadi shule nyingine kwenda kufanya mitihani, kwa hiyo, mazingira kwa ujumla ni magumu sana. Kwa hiyo, walimu wa eneo hili wakati mwingine wanatakiwa kuangalia kwa namna ya pekee maslahi yao. Ni hao ambao wanafuata mishahara yao umbali mrefu sana na hawana namna nyingine ya kuweza kuwasaidia kimaisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna shule chache ambazo tumezianzisha kwa sababu ya wingi wa wanafunzi, Shule za Loleshia, Itanga, Lusembwa, Lupata na Mkiringa. Shule hizi tumezianzisha baada ya kutembelea pale kukuta vijana wengi hawana namna ya kusoma na fedha zilizoanzisha shule hizo ni nguvu za wananchi na Mfuko wa Jimbo peke yake, hatujapata pesa za kutosha. Tunaomba watengewe pesa ili shule hizi ziweze kupata kasi ya kutoa elimu kama shule zingine vinginevyo tutapata shida kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia kuhusu walimu. Walimu wetu wa shule za msingi wana shida kubwa mno. Shida kubwa ambayo tunaiona hapa ni maslahi pamoja na upandishwaji wa vyeo vyao. Unakuta mwalimu anakaa katika cheo kimoja muda mrefu sana na wakati mwingine hawapati uhamisho wa hapa na pale ili kubadili mazingira na kufanya kazi vizuri zaidi na kwa kufanya hivyo unakuta kazi zinaanza kufanywa kwa mazoea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba mageuzi katika suala zima la taaluma yaanze pia kwa watendaji wenyewe hawa ambao wako shuleni. Kitengo cha Ukaguzi kiimarishwe hasa katika shule za msingi. Kitengo hiki kimeachwa bila vitendea kazi vya kutosha, hawana magari wala watumishi wa kutosha na kwa maana hiyo shule zote ambazo tunataja hapa hazitembelewi na hivyo huwezi kuona matokeo mazuri katika mitihani kwa sababu shule hizi haziangaliwi mara kwa mara na walimu wake sasa wanafanya kazi kwa mazoea. Kwa hiyo, naomba sana kitengo hiki nacho kiboreshwe sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo napenda kuchangia ni vijana ambao wanasoma elimu maalum maana yake watu wenye ulemavu, albino na watu wengine. Vijana hawa wanapata changamoto nyingi sana katika shule mbalimbali ambazo wanasoma, nyingi hazina miundombinu ya kuwasaidia lakini wanapomaliza hakuna mfumo unaoeleweka wa kuwaajiri vijana hawa japo inatajwa kwenye sera kwamba asilimia kadhaa katika nafasi zinazotolewa wawe wanaajiriwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kuwe na ufuatiliaji (cross check) kuona katika ajira kadhaa zilizokwishatolewa, je, watu wenye walemavu wamezingatiwa kwa kiwango gani? Kama itakuwa tu ni sera lakini waajiri hawazingatii inakuwa haina maana sana. Naomba kila nafasi za ajira zinapotolewa kiwepo kitengo cha kuhakikisha kwamba watu hawa na wenyewe wanatengewa nafasi zao na tunahakikisha kwamba wamepewa lakini siyo kuacha tu kama sera ilivyo, inakuwa haitusaidii sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, nishukuru kwa mchango mzuri ambao umetolewa na wenzangu hasa katika shule za private kwamba shule hizi zina msaada mkubwa sana na kama kuna haja ya kutoa namna yoyote ya usaidizi hasa katika maeneo ambayo wameona kwamba ni changamoto waweze kufanya hivyo kwa sababu ni washika dau kama wengine, wanatoa elimu kama watu wengine. Kwa hiyo, ni wadau muhimu katika utoaji wa elimu katika nchi, isionekane kama ni wafanyabiashara tu peke yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naona kama ni watu ambao wanasaidia kubeba mzigo mkubwa huo wa utoaji elimu katika nchi na kwa hivyo ni wadau muhimu sana na hii ndiyo inaweza ikatusaidia kwenda kwa pamoja. Kwa sababu tunasema PPP ni muhimu sana katika maendeleo ya Taifa letu bila kuimarisha sekta binafsi tukaiachia Serikali peke yake sidhani kama tutaweza kufikisha malengo ya Kitaifa yanayotakiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana jkwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia kwenye Wizara hii muhimu sana, Wizara ya Maji. Nimshukuru Mwenyezi Mungu kutujaalia uzima na niende moja kwa moja kumpongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri kwa uchapakazi. Wametutembelea kwenye wilaya yetu, lakini pia wametutembelea kwenye majimbo yetu yote mawili, tumeona mchango wao na umetusaidia sana. Nipongeze watendaji wa Wizara, wanatusikiliza vizuri na tunaomba waendelee kutusikiliza sisi wawakilishi wa wananchi pale tunapowapelekea maelezo sahihi juu ya miradi ambayo inatekelezwa kwenye majimbo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze na miradi mitatu ya Benki ya Dunia. Mmoja ni Mradi wa Kisura, Mheshimiwa Naibu Waziri aliutembelea mradi huu lakini mpaka sasa wananchi hawajapata maji. Alipokuja, tunakushukuru sana aliweza kutusaidia tukapata milioni 150 na mradi umejengeka umekwisha. Kinachotakiwa sasa ni nishati tu, sasa kile kijiji kinapata umeme lakini Wizara wametupendekezea tununue generator, sasa generator haiwezi kutusaidia kwa sasa, tunaomba hilo tusifikirie, wabadilishe mawazo ili umeme unaokuja pale watusaidie pesa tufunge mashine pale tupeleke umeme kwenye chanzo, itatusaidia sana. Ni kisima ambacho kinatoa maji mengi na ya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa pili, ni Mradi wa Mpasa. Mradi wa Mpasa una maneno mengi, lakini naomba wanisikilize vizuri. Mradi ule unaenda vizuri na uko asilimia 80. Wamejenga miundombinu mizuri kabisa na unaenda vizuri kiasi kwamba unatia moyo na wakati mwingine tukiwaharibu watu wakati wana spidi nzuri ya utekelezaji tunawavunja moyo, uko asilimia 80, wamejenga matenki yote, sasa hivi wamejenga DP karibu zote. Sasa hivi bado kuunganisha tu kidogo kutoka kwenye njia kuu kupeleka kwenye vijiji. Pale ndiyo wamepata hela kidogo, tena itakuwa certificate ya mwisho na utakuwa umekwisha kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa yanapokuwa maneno mengi mara nyingi mradi huu unakwama wanachelewa kutupa pesa na wametuma tume nyingi kama tatu au nne, hawatuamini tukisema kwamba unaenda vizuri, DC yupo, Mkuu wa Mkoa yupo na anatufuatilia vizuri na mimi nipo. Kwa hiyo watuelewe vizuri, mradi huu unaenda vizuri. Sisemi hivi kwa kumpendelea mkandarasi, hapana, lakini mradi unaenda vizuri na spidi iko vizuri na mimi ndiyo nauangalia kwa karibu. Ulikuwa na matatizo na matatizo yanaweza yakawepo ya kawaida kama sehemu nyingine, lakini spidi ya mradi huu ni nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, upo Mradi wa Isale; mradi huu pia Mheshimiwa Waziri amekuja kuutembelea, ameuona jinsi unavyokwenda, tunamshukuru Mungu unaenda vizuri, mpaka sasa uko asilimia 50. Mradi huu ni wa shilingi bilioni tano na milioni mia tano, ni mradi mkubwa. Mkandarasi amejenga asilimia 50 mpaka sasa na amepokea shilingi bilioni moja na milioni mia moja na sasa wamempelekea milioni 400, kazi inaenda vizuri. Mheshimiwa DC pale anasimamia vizuri, ameshirikisha vijiji vile vya jirani, wanachimba mitaro, wanapata visenti kidogo pale na vinasaidia kwenye miradi ya vijiji. Kwa hiyo mradi huu nao unaenda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatarajia mradi huu upeleke maji Nkata, upeleke maji Kitosi, Ntuchi A na Ntuchi B pamoja na Ifundwa, pamoja na Isale na Msilihofu. Kutakuwa na kakijiji kamoja kamebaki hapa China, nilimwambia Mheshimiwa Waziri alipokuja kwamba wataalam wanasema kwamba design haioneshi kwamba maji yale yanaweza yakaja pale, pana mwinuko, naomba kwa sababu ndiyo bomba linapita kwenye Kijiji hicho cha China, atufanyie utaratibu wa kisayansi utakaowezesha watu wale wapate maji, bila hivyo miundombinu inaweza ikahujumiwa jambo ambalo litatupa shida sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi mwingine ni Mradi wa Nkundi. Bwawa la Nkundi, la Kala Mheshimiwa Naibu Waziri na Waziri walilitembelea wakaona changamoto zilizokuwepo. Nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri juzi ametoa uamuzi, ametuletea milioni 65 na sasa hivi ninavyosema nilitembelea pale nimekuta wameweka umeme tayari, kwa hiyo nishati ile iliyokuwa inasuasua sasa tatizo lile litakuwa limekwisha. Nina imani kama kikwazo kilikuwa ni nishati, mradi huu sasa wananchi wataanza kupata maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nilikuwa naongea na Engineer, wananchi wa Kalundi wameanza kupata maji lakini Nkundi kuna tatizo, bado maji hayafiki. Sasa inaelekea Nkundi hapa kuna shida katika BOQ, inawezekana ujenzi wa BOQ haukuzingatia design ya Wizara katika ujenzi wake. Nimewahi kusikia fununu hii kwamba mkandarasi atakuwa aliwarubuni labda vijana wetu, wakaweka BOQ ambayo haikuwa imependekezwa na Wizara ili maji yaweze kufika pale, kwa sababu kuna mwinuko, wamepeleka bomba jembamba, sio kubwa, design ya Wizara inasema bomba linalotakiwa kuanzia pale kwenye chanzo mpaka kule liwe ni inchi tano, sasa nasikia wamepeleka tatu, kwa hiyo maji yanafika kwa shida na wakati mwingine una-pump siku mbili, tatu ndiyo maji yafike, hayawezi kukusaidia. Wafuatilie kwa makini kama Mheshimiwa Waziri alivyokuja wakati ule akafuatilia na Mkuu wetu wa Mkoa yuko makini sana, ataweza kufuatilia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi mwingine wa maji wa Wampembe. Wampembe ni Makao Makuu ya Tarafa na kuna mwinuko na chanzo kizuri cha maji ya kutiririka. Wataalam wangu wamefanya utafiti wakasema kwamba wametoa mapendekezo Wizarani japo hawajafikisha hapa, tunaomba wataleta mapendekezo hivi karibuni, tukipata ule mradi utalisha vijiji karibu vitano na ni maji ya mteremko. Awali halmashauri ilikuwa imefunga huo mradi, miundombinu yake ikafa, ukifufuliwa utakuwa umetusaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa mwisho ambao nafikiri utatusaidia ni wa Kijiji cha Chonga; Kijiji cha Chonga kinakosa maji. Wataalam wangu wameleta mapendekezo hapo na inaonekana kwamba shilingi milioni 300 ndiyo zinatakiwa ili kijiji hiki kiweze kupata maji. Tayari miundombinu kama tenki lipo, limeshajengwa muda mrefu, ni njia tu ya maji kutoka pale Kijiji cha Nchenje kuja Chonga kama kilometa nne hivi, lakini tenki lipo na linaweza kufanya kazi vizuri. Naomba kwa unyenyekevu mkubwa na uchapakazi wao wanisaidie nipate shilingi milioni 300 ili mradi uweze kufanya kazi. Niwatoe wasiwasi, pesa za maji pia zinasimamiwa Wilaya ya Nkasi, si vile kama zinapotea potea, maana wanakuwa na wasiwasi na wakati mwingine, haziji kwa wakati, wanaunda tume nyingi nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba wakati fulani DC yupo, Mkuu wa Mkoa yupo, Usalama wa Taifa wapo, PCCB wapo, wote wapo ni watu wanaoangalia miradi ya Serikali. Hakuna mtu ambaye atakaa tu pesa zinapotea bila kuangalia, hili tuliangalie sana, lisitie Wizara kigugumizi cha kutuletea pesa Wilaya ya Nkasi. Zinasimamiwa na sisi wenyewe Mwenyekiti wa Halmashauri yupo, Mkurugenzi yupo, wote tunasimamia vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi hii, mchango wangu ni huo. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Nampongeza Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu kwa hotuba nzuri ya Wizara ya Afya. Nampongeza Waziri kwa utendaji mzuri na kuiongoza Wizara vizuri. Nampongeza Naibu Waziri, Mheshimiwa Dkt. Ndugulile kwa uchapakazi wake na watendaji wakuu wa Wizara ya Afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Jimbo la Nkasi Kusini kupatiwa gari la wagonjwa liende Kata ya Kala ambayo iko kilomita 150 kufika Makao Makuu ya Wilaya. Umbali huu umesababisha vifo vingi vya akina mama na watoto hasa wanapopata uzazi pingamizi kwa vile huduma zilizopo Kata ya Kala ni za kiwango cha zahanati ambapo wataalam hawapo lakini pia hakuna gari la wagonjwa ili kunusuru wazazi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi Desderius John Mipata tuko Wilaya moja na Mheshimiwa Keissy ambaye alipewa ambulance mbili. Nina wakati ngumu sana wakati kiuhalisia Jimbo langu kijiografia ni gumu zaidi. Kwa heshima na taadhima namwomba Mheshimiwa Waziri anipe gari moja tu la wagonjwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi la pili, watumishi wa afya Wilayani Nkasi ni wachache sana. Pale Wilayani namuona Dkt. Mwakapimba pekee ndiyo yuko active zaidi na mwenye uwezo mzuri wa kielimu na anafanya kazi sana sana. Yeye ni Medical Officer, wapo AMO’s wengine lakini kiutendaji utagundua kuwa MD’s ni muhimu waongezeke asiwe yeye pekee maana Mkuu wa Idara mara nyingi yuko kwenye mambo ya utawala zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, manesi yaani wauguzi ni wachache sana. Pia clinical officer ni wachache sana, zahanati nyingi zinaendeshwa na manesi na wahudumu. Watumishi wa usingizi ni wachache sana Nkasi au niseme hatuna. Naomba suala hili la kupatiwa watumishi lipewe kipaumbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, vitambulisho vya wazee kutibiwa bado Halmashauri hawajatoa kipaumbele licha ya kuagizwa na Madiwani mara kwa mara. Naomba uwaagize na kufuatilia hasa Nkasi District Council.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, nawaombea Waziri, Naibu Waziri na watendaji wote wa Wizara Mungu awajalie afya na nguvu ili muendelee kusaidia Watanzania. Kwa ujumla Watanzania wanaridhishwa na utendaji kazi wa Wizara hasa upatikanaji wa dawa, mmefanya vizuri sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa mchango ufuatao:-

Mheshimiwa Spika, naomba barabara ya Kitosi – Mwampembe yenye urefu wa kilometa 67 ambayo ni mkombozi kwa Tarafa ya Wampembe ichukuliwe na Serikali au la, iwe inapewa fedha ya kutosha toka TANROADS. Wizara inatoa shilingi 90,000/=, inatosha nini? Tafadhali naomba tuwe tunaipa fedha zaidi.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Nkara – Kala ni ya Halmashauri/TARURA lakini haipewi fedha. Adha zinazowapata wananchi wa Kata ya Kala inatakiwa iondolewe na Serikali. Tafadhali ongezeni fedha TARURA ili iwe na uwezo wa kusaidia wananchi vijijini.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Katongoro kwenda Ninde haipitiki kabisa, kisa hakuna fedha ya kuhudumia barabara hiyo ya kwenda Ninde na kata yote isifikiwe. Tafuteni fedha kuimarisha TARURA.

Mheshimiwa Spika, lingine ni kuhusu mitandao ya simu. Naomba vijiji vifuatavyo vipate mawasiliano ya simu: Kijiji cha Kasapa, Kata ya Sintali, Kijiji cha Msamba Kata ya Ninde, Kijiji cha Kisambara Kata ya Ninde, Kijiji cha Lupata Kata ya Wampembe, Kijiji cha Izinga Kata ya Wampembe na Kijiji cha Mlalambo Kata ya Kizumbi.

Mheshimiwa Spika, Serikali ijenge magati ya meli katika vituo vya Namansi (Kijiji), Kijiji cha Ninde, Kijiji cha Msamba na bandari katika Mji mdogo wa Wampembe. Mji huu una biashara za kutosha na wasafiri wengi. Hali ilivyo inapokuja meli ni hatari kwa wasafiri na matukio kadhaa yanatokea.

Mheshimiwa Spika, nashauri Bandari ya Wampembe na barabara toka Sumbawanga hadi Wampembe ikijengwa ni rahisi kupata soko la nafaka ya mahindi Kongo Kusini.

Mheshimiwa Spika, nawasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa mchango ufuatao:-

Mheshimiwa Spika, mifugo itasaidia Watanzania zaidi iwapo uchumi wa viwanda utashika kasi. Cha kushangaza ni kuwa hata viwanda vilivyopo sasa havitumiki kabisa. Nikitolea mfano, Kiwanda cha Nyama cha SAAFI kilichopo Sumbawanga kinasemekana ni miongoni mwa viwanda bora kabisa vya nyama, lakini baada ya uwezo wa mwekezaji mzawa kutetereka Serikali imeshindwa kabisa kuweka mipango ya kukiendeleza, badala yake ng’ombe wanasafirishwa toka Sumbawanga mpaka Dar-es-Salaam na wakati mwingine ng’ombe hupelekwa Zambia kwenye viwanda vya nyama.

Mheshimiwa Spika, naishauri Wizara ione namna ya kukitumia kiwanda hiki. Nilipata nafasi ya kutembelea kiwanda, ni kiwanda kizuri kina miundombinu ya kisasa mingi inayowezesha mifugo wote na masalia yake yote kuongezewa thamani, ikiwemo damu, ngozi, kwato, mifupa na kadhalika. Serikali iliweza kutaka kushirikiana na mwekezaji ili aweze pia kulipa deni la Serikali na kutafuta masoko duniani. Masoko ya nyama yalipatikana sehemu mbalimbali ikiwemo Comoro, Shelisheli, Uarabuni na kadhalika, hata hivyo Serikali imekaa kimya bila kutoa uamuzi. Naomba watusaidie kiwanda kile kikifanya kazi ng’ombe wa wafugaji wa Rukwa, Katavi, wangepata soko na kuvutia ufugaji. Naomba sana Serikali isaidie kiwanda hiki kipate mtaji wa kazi na ikiwezekana isimamie yenyewe na mwekezaji yuko tayari sasa PPP na Sera ya Viwanda tunaitekeleza kweli namna hii.

Mheshimiwa Spika, wavuvi wananyanyasika kupita kiasi; Maafisa hawajengi mahusiano baina yao na wavuvi, mahusiano ni ya paka na panya. Nashauri Serikali ifanye mabadiliko katika kusimamia sekta ya uvuvi iwe rafiki kwa wadau wote.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo
MHE. DEUSDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kupata nafasi. Nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uzima, lakini pia niwapongeze Mawaziri na Naibu Mawaziri kwa hotuba nzuri sana hii waliyotuletea, lakini pia kwa kazi nzuri wanayoifanya. Mchango wangu utakuwa katika maeneo mawili.

Mheshimiwa Spika, la kwanza, ni juu ya upatikanaji wa pembejeo na bei zake, sijaridhishwa sana na jinsi mbolea au pembejeo za kilimo zinavyopatikana kwa wakulima bado kuna changamoto nyingi. Mbolea hazipatikani kwa wakati, pembejeo za mbegu na madawa feki ni nyingi kupita kiasi na wakulima wanakula hasara sana na kwa sababu ni shughuli ambayo na sisi wenyewe tunafanya Wabunge nami ni mmojawapo, nashuhudia kwa ushahidi mimi mwenyewe wakati mwingine unanunua madawa yatafanya kazi na wakati mwingine hayafanyi kazi kabisa. Kwa hiyo bado kuna changamoto kubwa sana katika suala la utafiti na wataalam wetu waweze kufanya kazi vizuri zaidi.

Mheshimiwa Spika, katika maeneo hayo nataka niwe na mchango ufuatao, kwamba, vituo vya utafiti viimarishwe, tusitegemee sana vituo vya utafiti au mbegu na pembejeo za kutoka nje, hizi zinatusumbua na zinaleta hasara kubwa sana kwa wananchi wetu. Pale kwetu Rukwa pale kuna kituo cha Utafiti cha Mirundikwa kina changamoto nyingi sana, tuna ardhi ya kutosha lakini hawana wafanyakazi wa kutosha, hawana fedha, hawana matrekta, wakisaidiwa hawa watasaidia wakulima wa Mkoa wa Rukwa vizuri zaidi.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo nafikiri ni muhimu sana katika hii ni pembejeo. Matrekta tumeambiwa yapo hapo Bagamoyo yapo matrekta mengi, lakini hii habari haijafika vizuri kwa wakulima wetu, hawajui, utaratibu uliowekwa na Serikali ni mzuri sana, lakini watu hawana information ya kutosha juu ya namna ya kupata hayo matrekta na kwa utaratibu uliowekwa na Serikali ni mzuri kabisa. Kwa hiyo, bado kuna habari ya hamasa ifike kwa wakulima. Kule kwetu kuna vikundi vingi sana hasa Mkoa wa Rukwa vikundi vingi sana vinajihusisha na kilimo, Nyanda za Juu Kusini kwa ujumla wake, lakini hawajapata habari kwamba kuna trekta zipo ambazo wakijiunga kwenye vikundi vikiandikishwa wanaweza wakapata na wakaboresha kilimo chao. Kwa hiyo niipongeze Serikali kwanza kwa uamuzi huo, lakini natoa wito kwa Serikali wataalam wetu watoe wito na elimu zaidi kwa wakulima namna ya upatikanaji wa hizo trekta ili waweze kunufaika na wazo hili zuri la Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni masoko ya mazao; Nyanda za Juu Kusini sisi ni maarufu wa kulima nafaka, lakini siku zote katika miaka miwili mitatu hii yamekuwa ni mateso. Watu wanalima na wanaendelea kukata tama, kwa sababu hatuoni soko la mazao, tunajua wazi kwamba Serikali si wajibu wake kutafuta kununua mazao ya kilimo kama wanavyotusaidia NFRI lakini ni wajibu wa wataalam wetu kuhakikisha kwamba mazao yanayolimwa na wakulima wetu yanapatiwa masoko nje na ndani ya nchi yake. Hakuna sababu kufunga mipaka, mwaka huu ni mbaya sana, nafaka inaweza kuwa kidogo, lakini wazo watakalokuwa wanalifikiri sasa hivi watu wa Serikali ni kufunga mipaka badala ya kuacha watu wanufaike na uzalishaji ambao sasa umetolewa kwa muda mrefu. Naomba kabisa kabisa mwaka huu msithubutu kufanya jambo hilo. Wawaachie watu wanaofanya kazi waweze kunufaika na mazao yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, natoa mchango kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, REA awamu ya III ilipanga kupeleka umeme Wilaya ya Nkasi vijiji 51. Wilaya yenye Majimbo mawili ya uchaguzi lakini Jimbo langu lilipata vijiji 12 tu; pamoja na maombi ya nyongeza nimekuwa napewa maneno ya faraja bila utekelezaji wowote.

Mheshimiwa Spika, Mawaziri na wataalam lazima wajue sikujileta hapa, nililetwa na wananchi lazima wagawe resources za nchi kwa usawa. Mara zote nikionesha maombi ya kunisaidia napewa maneno ya kufariji tu, hakuna hata kijiji kimoja kilichoongezwa katika vijiji 15 nilivyoomba vya nyongeza. Naomba Waheshimiwa Mawaziri wangu nawapenda sana na nimeisemea hapa Bungeni Wizara nikiwa Mjumbe wa Kamati.

Mheshimiwa Spika, hadi sasa wanipe Vijiji vya Katani, Malongwe, Wampembe, Izinga, Ng’undwe, Sintali, Nkana, Mkomanchindo, King’ombe, Mlambo, Kilambo, Mpasa, Tundu, Lolesha, Kala, Mwinza, Lyapinda, Lupata, Msamba, Kisambara, Ninde na Nakasanga ili kuleta usawa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, naanza kwa kuunga mkono hoja.

Mheshimiwa Waziri Mkuu Jimbo la Nkasi Kusini lina Tarafa moja ya Wampembe yenye kata nne, mawasiliano ya barabara ni magumu yaani hakuna kabisa barabara, kwa hiyo kuna shule za msingi zipatazo kumi shule hizi zina hali mbaya na hazitembelewi na wataalam wa ubora wa elimu hawafiki huko zaidi nafika Mbunge na wakati mwingine Mheshimiwa DC.

Kwa hiyo, shule hazijatembelewa miaka yote mitano ni Mbunge nimekuwa nikiwatembelea, ofisi za walimu ni chini ya mti. Shule hizo ni Lupata, Mkiringa, Mlalambo, Lusembwa, Itanga, Tundu, Lolesha na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, hoja ya pili; bajeti ya mwaka jana ilionesha kuna mipango ya kununua meli mpya katika Ziwa Tanganyika na kuwa meli ya Liemba itakarabatiwa, lakini katika bajeti hii haijanipa matumaini na tulishawaambia wananchi. Leo hakuna fedha wala mwendelezo wa mipango iliyosemwa katika bajeti iliyopita.

Mheshimiwa Spika, wavuvi wa Ziwa Tanganyika wanasumbuliwa sana na zaidi wanachanganywa na wataalam wa Wizara husika wanaambiwa nunuweni nyavu size fulani wakinunua kwa maelekezo yao wanasema nyavu hazifai na zinachomwa, wananchi wanapata hasara. Tuelezeni kwa nini mnafanya hivyo. Mheshimiwa Waziri Mkuu lione jimbo hili.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Nimshukuru pia Mwenyezi Mungu kutujaalia uzima na atujaalie atuvushe na janga hili la corona na naomba Watanzania wasikilize maagizo yaliyotolewa na Serikali pamoja na wataalam.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni miaka mitano sasa, hii ndiyo bajeti ya miaka mitano tangu tumeingia hapa Bungeni. Mimi nilibahatika pia kuwepo katika miaka mitano iliyotangulia. Nimeona utumishi uliobadilika sana nikilinganisha na vipindi hivi viwili ambavyo nilikuwepo kwenye Bunge.

Katika kipindi hiki ni lazima niseme mambo yafuatayo ili Watanzania wajue na wananchi wajue kwamba mabadiliko makubwa yaliyofanywa na Mheshimiwa Rais katika maeneo ya utumishi wa umma yameleta heshima kubwa sana kwa Taifa na sasa wananchi wanahudumiwa vizuri kupita wakati wowote ule.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tumeona ameokoa pesa nyingi sana katika fedha za umma kwa kufuta safari za nje, kwa kurekebisha Sheria ya Manunuzi ambayo ilikuwa inatumika vibaya, lakini vilevile amesaidia sana kuhakikisha kwamba rasilimali hizi zilizokuwa zinaokolewa zinakwenda kwenye uwekezaji wa wananchi kama vile madawa yameongezeka, shule nyingi zimejengwa na kwa uchache nitaelezea shule zangu zingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu kwamba ipo pia miundombinu mingi na ya nguvu iliyojengwa kwa kipindi hiki. Kwa mfano, ujenzi wa reli katika kiwango cha standard gauge, ujenzi wa Bwawa la Nyerere ni miradi ya kimkakati ambayo ingeweza kujengwa katika Awamu ya Pili, ingeweza kujengwa katika Awamu ya Tatu, ingeweza kujengwa katika Awamu ya Nne lakini huyu Bwana kwa sababu ana maamuzi magumu na anachukua hatua za mara moja ameamua yeye mwenyewe. Ndiyo maana tunamuita sasa ni Bulldozer kwa sababu miradi yote hii Mungu akimsaidia sana atakaa miaka 10 tu kwenye nafasi hii lakini miradi hii itadumu kwa karne, Watanzania watakuwa wamepata Mtu wa pekee kwa sasa kuliko wakati wowote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vizuri Watanzania wajue, leo tuna Rais ambaye anatolewa mfano ndani ya Tanzania, nje ya Tanzania na duniani pia. Sasa ni wakati wa kumtumia vizuri na wakati mwingine kumpa nafasi zaidi na katika miradi amesema yeye mwenyewe kwamba katika suala la maendeleo hakuna siasa wala itikadi na wenzangu wa upande wa pili nimekuwa nikiwasikia wanasema amechukua ajenda zetu, sasa kiongozi afanye nini? Ameona kwenu kuna jambo zuri na ya kwake mazuri akayachukua, pamoja akatekeleza. Kwa hiyo, ni nafasi sasa tumwache katika miaka mitano ijayo ili atende kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ujio wa Mheshimiwa Magufuli kuwa Rais haukutarajiwa na watu wengi. Ni kama maongozi ya Mwenyezi Mungu kwa sababu tumekuta nchi yetu iko katika hali ngumu sana; rushwa, madawa ya kulevya na vitu vingine. Ameingia mtu ambaye amekuwa jasiri katika mambo hayo na ameyashughulikia sawasawa na sasa Taifa liko na Heshima. Tanzania imepata heshima miongoni mwa Mataifa, anasikika kila mahali. Kwa hiyo, kiongozi wa namna hiyo ukimpata, ni vizuri Watanzania kufikiri mara mbili. Ni wachache kupatikana hawa watu. Watu wanaothubutu, wenye uthubutu wa nguvu kama huu na kwa kweli watu wote mmeona madawa ya kulevya kwaheri, rushwa nchini kwaheri, maliasili zetu zimetunzwa vizuri, miundombinu inajengwa kwa nguvu zote. Kwa hiyo niseme tu kwamba miaka mitano hii iliyopita Serikali yetu imefanya jambo kubwa sana miongoni mwa Watanzania na miongoni mwa Mataifa yanayotuzunguka na ndiyo maana nchi zote ambazo zinatuzunguka wanasema tupate Magufuli wetu. Kwa hiyo tumepata kiongozi ambaye ni mfano katika Afrika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hilo, niseme tu kwamba, katika Jimbo langu nimepata pesa za kutosha katika elimu. Katika elimu tumepata pesa za kutosha, Shule ya Sekondari ya Milundikwa nilisimama hapa kuomba na kila mtu alisikia nimepata zaidi ya milioni 700 na ni shule ya mfano kabisa. Shule ya Sekondari ya Hundi tumepata zaidi ya milioni 130 na tumejenga, Chuo cha Maendeleo-Chala ambayo sasa ni VETA ambayo inapiganiwa tumepata milioni 636 na sasa tayari majengo yanaisha. Miundombinu, barabara yetu ya kutoka Sumbawanga kwenda Kanazi, kwenda Kibaoni imekwisha kuwekewa lami. Tunamaliza hivi, tumeanza Shule ya Sekondari mpya ya Myula na tumepata pesa, kwa hiyo kila mahali tumeweza kufanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hayo, naomba kueleza matatizo yafuatayo yaliyopo Jimboni kwangu.

(Hapa baadhi ya Waheshimiwa walizungumzia bila kufuata utaratibu)

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni changamoto, lazima yawepo hakuna wakati matatizo yote yatakwisha. Naomba fedha zaidi katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kasu ambacho tumekuwa tukikisema kila wakati, naomba fedha zaidi katika Kituo cha Afya cha Kala ili kiweze kufanikiwa.

Naomba vilevile niweze kupata fedha katika Kituo cha Afya cha Ninde ambacho tayari wametupatia pesa milioni 200 waongeze hela nyingine kiweze kukamilika lakini kwa vyovyote vile tumefanya kazi kubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hapo, naomba matengenezo ya barabara ya Nkana-Kala, Milundikwa- Kisura, Namasi-Ninde, Kitosi-Wampembe, naomba umeme katika Kata ya Kala, Kata ya Wampembe, Kata ya Kizumbi na Kata ya Ninde. Kazi hii nzuri najua kwa maombi haya na Serikali yetu yote haya yatawezekana.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya, nawashukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)