Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Prof. Norman Adamson Sigalla King (23 total)

Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. DKT. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kuchangia, naomba nichukue nafasi hii kipekee kabisa kumshukuru Mungu kwa sababu ya kutuwezesha sisi sote kushinda uchaguzi mwaka jana na kuingia kwenye Bunge hili. Kipekee kabisa nipongeze Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya na Vyombo vyao kwa kusimamia uchaguzi huo vizuri. Kwa kufanya hivyo, wameniwezesha mimi na mdogo wangu Mchungaji Msigwa, kuingia kwenye Bunge hili. Ahsante sana Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie kidogo katika Mpango uliowasilishwa. Kwanza, natambua kabisa kwamba yako maeneo mengi ambayo Mpango umejielekeza na hasa upande wa barabara na reli. Mimi kama Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, naomba nisisitize tu kwamba sisi Watanzania tunaamini kwamba uboreshaji wa Reli ya Kati ile tunayoijua yaani ya kwenda Kigoma – Mwanza baada ya pacha ya Tabora ndiyo tunayoisema na matawi yake ya kwenda Mpanda. Mikoa kumi na tano itanufaika na suala hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nieleze kwa ufupi, Tanzania ilivyo na hasa Wilaya ya Makete na Mkoa wa Njombe, ni Mkoa ambao ni tegemeo kubwa sana kwa sababu ya uchumi wa Tanzania na hasa uzalishaji wa mazao ya chakula. Naomba sana barabara inayotoka Njombe - Mbeya kupitia Makete ipewe kipaumbele kwa sababu hata Ilani ya CCM imeiweka barabara hii ni barabara ya kwanza. Umuhimu wa barabara hii si tu kwa sababu Norman Sigalla King anatoka Makete ni barabara muhimu kwa maana ya uchumi wa Tanzania kwa sababu Hifadhi ya Kitulo ndiyo hifadhi pekee ya maua Afrika. Hifadhi hii ili iboreshwe ni lazima miundombinu ya barabara za lami iwe bayana na hii itasaidia kukuza utalii ndani ya hifadhi hii na si tu kukuza utalii lakini pia kuboresha uchumi wa Wilaya ya Makete. Kwa sababu Wilaya ya Makete pamoja na uchumi wa mazao ya chakula pia ndiyo Wilaya ambayo inaongoza baada ya Mafinga kwa mazao ya mbao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ni jambo la muhimu sana, niishukuru Serikali ya CCM kwa kazi nzuri inayoifanya ya kuboresha elimu. Wilaya ya Makete pale tuna Chuo cha VETA, bahati mbaya sana yako madarasa lakini hakuna mabweni. Wilaya ya Makete kwa jiografia yake haiwezekani wanafunzi wa kutoka Tarafa za Matamba, Ikuo, Lupalilo, Ukwama, Bulongwa kwenda kusoma kwenye chuo kilichoko Iwawa-Makete. Ni muhimu sana Serikali ijenge mabweni ili kunufaisha wananchi wa Tarafa zote ikiwemo Taarifa ya Magoma. Hili nimeliwasilisha kwa Waziri mhusika, naomba sana kwenye Mpango wetu wa Maendeleo tufasili kwa vitendo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa elimu pia naomba nisisitize jambo moja. Mtihani tulionao sasa ukisikiliza hotuba ni kana kwamba muhimu kwa Watanzania ni kupata shahada ya kwanza, ya pili ama ya tatu. Mtihani tulionao sasa ni aina ya elimu tunayowapa watoto na watu wetu. Sote tunajua nguvu ya uchumi wa Tanzania ni kilimo, asilimia 77 ya watu wetu wanategemea kilimo. Hata hivyo elimu yetu kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu hakuna mahali ambapo mwanafunzi anakutana na kilimo. Ni hatari sana!
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wamarekani na nchi zilizoendelea nguvu yao ni kwenye teknolojia ndiyo maana mtoto wa Kimarekani wa miaka nane au kumi anacheza na komputa, ana-feed data na analipwa. Kwao Wazungu wanasema hiyo siyo child labour lakini Mwafrika, Mtanzania akibeba jembe akiwa na miaka kumi na mbili, kumi na tatu tunamfundisha kilimo ambacho ndiyo nguvu yetu tunasema child labour. Tunaingia kwenye ugonjwa huu, matokeo yake tutakuwa na wanafunzi wanao-graduate kwenye level ya digrii ya kwanza, ya pili na ya tatu lakini hawana mahali pa kutumia elimu hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu kwa Serikali, baada miaka ile mitatu ya kujua kusoma na kuandika kwa watoto wetu ni muhimu sana watoto hawa wajifundishe ABC ya kilimo, siongelei kilimo nadharia, kilimo vitendo. Mtu anatoka Kanda ya Ziwa basi ajue akifika darasa la saba ni jinsi gani ya kutumia mbolea kulima pamba, kama anatoka Nyanda za Juu Kusini kwa mfano ajue kwa nini tunatumia DAP na kwa nini tunatumia urea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, dozi hiyo ya course inaongezewa uzito anapomaliza kidato cha Nne ili tuwe na Watanzania ambao wakihitimu kidato cha nne hawana haja ya kutafuta shahada maana elimu waliyonayo inatosha kujitegemea. Nafikiri hili Wizara ya Elimu iliangalie kwa namna ya kipekee sana maana vinginevyo tutajuta kwa sababu tutakuwa na watu wengi walio-graduate, lakini hawana mahali pa kutumia elimu hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nipende kusisitiza umuhimu wa Bwawa la Lumakali. Kaka yangu Mheshimiwa Profesa Muhongo yuko hapa. Mto wa Lumakali ambao uko Bulongwa, Wilaya ya Makete, ni kati ya mito michache katika Tanzania ambayo haipungui maji kwa miaka 40 sasa ya utafiti. Document ambayo ni official ya TANESCO inaonyesha kwamba umeme unaotakiwa kuzalishwa kwa kutumia mto ule ni megawatts 640 hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba sana Serikali itekeleze mradi wa Lumakali kwa sababu utasaidia sana kutoa ajira kwa wananchi wa Makete, Mbeya na Njombe kwa sababu ni bwawa kubwa lakini pili utasaidia sana kuongeza umeme wetu. Mheshimiwa kaka yangu Profesa Muhongo chondechonde, naomba sana Mto Lumakali upewe nafasi yake ya kipekee kabisa ili Wilaya ya Makete ipate kufanikiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nihitimishe hotuba yangu kwa kuongelea umuhimu wa kuunganisha barabara ya kutoka Ludewa - Mlangali. Niipongeze Serikali kwa sababu ya kufungua barabara hiyo lakini ni vizuri ifunguliwe kwa kiwango cha lami kutoka Mlangali - Lupila kutokea Ikonda - Makete, kutoka Chimala - Matamba - Kitulo - Mbeya, kutoka Mbeya - Ishonje - Makete - Njombe na kutoka Makete – Bulongwa – Iniho - Ipelele - Isonje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia Mungu akubariki na naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 na Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017.
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nawashukuru sana Waheshimiwa Wajumbe wote ambao wametoa michango yao. Naomba uniruhusu niwatambue kwa majina hasa wale ambao wameandika, kwa sababu wale ambao wamechangia hapa ndani wote mliwaona.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumshukuru Mheshimiwa Ritta Kabati, Mheshimiwa Shelukindo, Mheshimiwa Oran Njeza, Mheshimiwa Juma Othman Hija, Mheshimiwa Aida Joseph Khenani, Mheshimiwa Eng. Ramo Makani, Mheshimiwa Rhoda Edward Kunchela, Mheshimiwa Silafu, Mheshimiwa Mashimba Ndaki, Mheshimiwa Mary Deo Muro, Mheshimiwa Lucia, Mheshimiwa Zainab na Mheshimiwa Lucy Owenya.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuweka kumbukumbu sawasawa, nadhani ni Mheshimiwa Shekilindi badala ya Mheshimiwa Shelukindo. Umetaja Shelukindo hapo, nadhani ni Mheshimiwa Shekilindi. Sasa sema ili kumbukumbu rasmi za Bunge ziwe na jina linalotuhusu kwa sasa.

MHE. NORMAN A. SIGALLA KING - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na michango mingi ya Wabunge pia nichukue nafasi hii kipekee kuwapongeza Mawaziri kwa maana Waziri Mheshimiwa Profesa Mbalawa pamoja na Naibu wake kwa michango yao kwenye hoja hii. Nitoe ufafanuzi katika mambo machache. Kwanza Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia wameipongeza Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kazi kubwa inayofanya, nasi tunapokea pongezi hizo. Pia wengi wameongelea umuhimu wa kuunganisha barabara za lami, nashukuru kwamba Mheshimiwa Wazirri amefafanua vizuri jambo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna hoja ya kuangalia uwezekano wa kuunganisha barabara za mikoa, nashukuru Mheshimiwa Waziri pia ametoa ufafanuzi mkubwa kwenye hilo. Pia kuna hoja ya uwanja wa Chato na pia hoja ya kujenga uwanja Mkoa wa Mara; nafikiri haikujibiwa na ni vizuri nitoe ufafanuzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vizuri Waheshimiwa Wabunge na Bunge lako lifahamu; mimi nimeshiriki kwenye uwekaji wa jiwe la msingi uwanja wa Chato. Shilingi bilioni 39 zilizotajwa ni gharama za ujenzi mradi ukikamilika. Kilichofanyika Chato ni kuweka jiwe la msingi. Kuhusu fedha za bajeti kwa mwaka huu wa fedha kwa mfano, 2018/2019, wale Wajumbe watakaokuwa kwenye Kamati ya Miundombinu wataona bajeti hiyo. Kinachoonekana sasa ni kama vile umeshajengwa. Haujajengwa, tulichofanya ni kuweka jiwe la msingi. Hilo ni la kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, pia aliuliza vizuri rafiki yangu, Mbunge wa Sengerema kwamba kwa nini uwanja haujajengwa Mkoa wa Mara? Je, kwa nini Serikali inapeleka nguvu upande wa Chato?

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge na Bunge lako Tukufu, ni vizuri watu wafahamu, mpaka Mwalimu Nyerere anatoweka tarehe 14 Oktoba, 1999 viwanja ambavyo vilikuwa vimejengwa Tanzania hii ni vichache sana na hasa viwili vikubwa ni uwanja wa KIA na uwanja wa Dar es Salaam. Viwanja vingine vya Kigoma na Tabora na kwingineko, wote tulikuwa tunatua na ndege kwa mashaka, siyo kwa kujengwa. Kwa hiyo, lawama ziende kwa nani?

Mheshimiwa Naibu Spika, Rais Dkt. Magufuli ameingia wakati Mheshimiwa Rais wetu Mwasisi wa nchi hii alishaondoka katika nchi hii. Kwa hiyo, siyo sawa hata kidogo kwa hekima yote ile kupeleka lawama kwa Rais wa Awamu ya Tano wakati, Rais wa Awamu ya Pili alikuwepo, ya Tatu alikuwepo, ya Nne alikuwepo na muda huo viwanja havikujengwa kwa sababu ya uwezo wa uchumi kuwa mdogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utangazaji wa tenda labda nayo niifafanue kidogo. Ni vizuri Bunge lako Tukufu likafahamu, utangazaji wa tenda wa viwanja au miradi mingine ya Serikali imegawanyika katika sehemu kuu mbili; unaweza ukafanya kitu kinachoitwa open tender kwa maana ya kwamba unatafuta Mkandarasi wa ujenzi wa uwanja au jambo lolote ndani ya Serikali au restricted tender.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati gani unatumia restricted tender? Ni pale ambapo Wakandarasi ambao tayari unao wanafanya miradi mingine; unataka mradi mwingine unaofanana na kazi ambazo tayari Wakandarasi wapo, unataka utekelezwe. Badala ya kupoteza muda kufanya open tender, unafanya kitu kinachoitwa restricted tender, kwa maana ya kwamba unachagua katika wale ambao tayari wapo na unaangalia nani mwenye bei ndogo halafu unampa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Procurement Act iko wazi na wala siyo kwamba ni jambo linafanywa kwa kificho, liko wazi kwenye kufanya hivyo, kwa hiyo, chochote utakachofanya katika hivyo, ni sahihi. Kwenye Halmashauri zetu tunafanya hivyo na kwenye Serikali Kuu tunafanya hivyo pia.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitumie dakika chache kupongeza kwa dhati taasisi ambazo Kamati hii inazisimamia. Nianze na taasisi kama TCRA; siwezi kuzitaja zote 37 na CEOs kokote waliko wajue kwamba nazitaja hizi tu kama mfano. TCRA, Kamati iliagiza kwamba watekeleze utaratibu wa TTMS ili tuwe na hakika ya mapato ambayo Serikali inapata. Wameshirikiana na wenzao wa TRA na sasa kazi inafanyika vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilielekeza TPA kwamba wajaribu kurekebisha kero za Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na ucheleweshaji na siku zinazochukuliwa katika kupakua na kupakia pamoja na tozo mbalimbali. TPA wamerekebisha jambo hilo na sasa mambo yamekwenda vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, wanaoagiza mizigo kwa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa watakuwa ni mashuhuda kwamba hata vitu vilivyokuwa vinanyofolewa kwenye magari au kwenye magari tunayoagiza, sasa hivi wizi huo haupo tena. Pongezi sana kwa TPA pongezi sana kwa CEO wa TPA pia.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Tanzania Buiding Agency (TBA) ambayo ndiyo taasisi iliyopewa madaraka ya kujenga miradi mbalimbali ya Serikali na hasa majengo, imefanya kazi nzuri sana. Kwa mfano, imejenga hostel pale Chuo Kikuu Dar es Salaam. Gharama za kampuni ya Kichina iliyokuwa ime-tender ilikuwa shilingi bilioni 80 kumaliza mradi ule. Wao wametumia shilingi bilioni 10. Pia ukienda kwa mradi wa hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndiyo kama hivyo, lakini ukienda mradi mwingine kama wa Ihungo, wengine wali-tender shilingi bilioni 60, lakini wao wamemaliza kwa shilingi bilioni 11. Wameenda hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nenda Mlonganzila, hivyo hivyo; wamekwenda wakitekeleza miradi mingi kwa karibu ten percent of the entire total ukilinganisha na Wakandarsi wengine. Lazima tuwapongeze sana TBA na CEO wake kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya katika kutekeleza miradi mbalimbali. Unakuja bodi za Wakandarasi na za Wahandisi; wote wamefanya kazi nzuri sana. Wakandarasi ambao wamekuwa wakizembea kutimiza viwango wameondolewa kwenye roster ya Wakandarasi Tanzania. Ni kazi nzuri sana inayofanywa na taasisi hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikitaja MSL pale Mwanza, ameteuliwa Kaimu Mkurugenzi. Kwa muda mfupi tu wa miezi michache aliyokaa, ameweza kuifanya meli ya MV. Liemba ambayo ilionekana kama haifai pale Kigoma na ilikuwa inaripotiwa kwamba imeleta hasara kila trip ya shilingi milioni nne. Yeye kwa trip moja ameweza kusimamia na kupata shilingi milioni 15. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge wa Bunge lako Tukufu, kwa hiyo, hii inaonesha kwamba kuna vitu viwili muhimu ambavyo lazima Wizara hii iendelee kufanya. Moja, ni uteuaji kwa kufuata weledi wa Watendaji wanaosimamia taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara hii; lakini pili, kufuatilia kwa makini ili kuona jinsi gani ambavyo tunaweza kuisaidia Tanzania na Serikali kwa ujumla kupata maendeleo. Ndiyo maana nimesema nizitaje taasisi kwa uchache.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, nitakuwa nimekosa fadhila kama nisiporudia kusema nashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wa Bunge hili kwa michango yao kutoka pande zote kwa vyama vyote. Michango yenu imekuwa ya muhimu sana na tumeichukua, tutazidi kuisheheni na kuiweka vizuri ili kwamba kwenye vikao vijavyo tuweze kuisaidia Serikali yetu kutekeleza mipango yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba sasa kutoa hoja kwamba taarifa ya utekelezaji ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa kipindi cha Januari, 2017 hadi Januari, 2018 sasa ipokelewe na Bunge lako Tukufu kama taarifa rasmi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. PROF. NORMAN A.S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza nianze kwa kuishukuru Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kazi kubwa na nzuri inayofanywa chini ya uongozi wa Rais wetu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuimarisha miundombinu na kutengeneza mazingira sahihi ya uwekezaji Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya eneo zuri sana ambalo Mheshimiwa Rais amefanya ni kuimarisha Benki ya Uwekezaji (TIB) na matawi yake ambapo sasa Mtanzania anayetaka kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji kinachohitaji mitaji mikubwa, benki zetu sasa zinaweza kufanya; ukitaka kuwekeza kwenye viwanda benki zetu sasa zinaweza kufanya; na uchimbaji wa mabwawa benki zetu sasa zinaweza kufanya. Kwa hiyo, naomba sana Watanzania kwa ujumla wao wale wanaopenda kuwekeza watembelee benki zetu za TIB ili waweze kutumia fursa hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, ni salamu za wananchi wa Makete. Wanampongeza Rais hasa kwa kutenga vijiji 51 katika ya 67 vilivyoko Makete ili waweze kupata umeme ambao utafasili uanzishwaji wa viwanda na matumizi mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hili naomba nisisitize jambo moja. Wilaya kama Makete ambazo tunafahamu mchango wake kwenye nchi yetu ya Tanzania na hasa upande wa maji yanayozalisha umeme ikiwemo bwawa tarajiwa na mradi mzima wa Stigler’s Gorge, Makete ndiyo hub, ndiyo catchment mama ya mito hiyo ya Ruaha Mkuu ambao baadaye unabadilika majina unaitwa Kilombero na baadaye kuitwa Rufuji. Naomba sana Serikali ipeleke maendeleo ili kuwazuia wananchi wa Makete wasije wakaingia kwenye jaribu la kuharibu vyanzo vya mito.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unapelekaje maendeleo? Kwa mfano, badala ya kupeleka umeme katika vijiji 51 ilikuwa ni kumaliza vijiji vyote 67 vilivyoko Makete ili wasikate miti, wasiharibu vyanzo vya mito ambapo kama wasipoharibu tunajihakikishia kwamba miradi tunayoifikiria na kuitekeleza kama Stiegler’s Gorge, Bwawa la Mtera, Kihansi pamoja na Kidatu watapata maji kwa uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, namwomba sana hasa rafiki yangu Mheshimiwa Waziri, sera zetu za uwekezaji zisikilizane na vitendo vyetu. Mipango yetu na nyimbo zetu za uwekezaji zisipingane na vitendo vyetu. Kwa mfano, sote tunafahamu kwamba maduka ya kubadilishia fedha kwa maana ya Bureau De Change tulianza na mtaji wa shilingi milioni 20 tukapanda kwenda shilingi milioni 40, shilingi milioni 80, shilingi milioni 100, lakini sasa nafahamu mtaji wa kuanzisha duka la kubadilisha fedha ni shilingi milioni 300. Tunataka watu wawekeze kwenye maduka ya kubadilisha fedha au wafunge maduka? Kwa vyovyote vile siyo dhana sahihi hata kidogo. Unapomtaka Mtanzania wa kawaida awe na duka la kubadilisha fedha lakini mtaji wake unasema shilingi milioni 300 siyo sawa. Ushauri wangu kwenye hili, mtaji wa kuanzisha maduka haya uwe kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda Serikali ifahamu, ufa uliokuwepo kwenye maduka ya kubadilishia fedha ilikuwa ni mamlaka za Serikali kutokufuatilia kama hawa wabadilishaji wa fedha wanatoa risiti. Kwa sababu hakukuwa na risiti ambazo ziko centralized kwamba mtu
nikibadilisha dola 100,000, BoT au Hazina wanajuaje kwamba Bureau A amebadilisha fedha? Kwenye nchi nyingine ukishabadilisha, aki-punch tu, Hazina wanajua kwamba Bureau ya Norman ameshabadilisha fedha. Tujitahidi huko ili kupata kodi stahiki, siyo kubana. Tutafunga watu wengi na tukifunga maduka haya mengi, maana yake tutapoteza ajira nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo sasa, niiongeze tu hapo hili la kuhusu mitaji. Leo mtu anaulizwa umepata wapi shilingi milioni 300 za kufungua Bureau De Change? I keep on asking myself, hili swali linaisaidia Serikali kupata mapato? Sielewi!

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri, juzi tarehe 4 Mei, 2018 nilikwenda kwenye Mkutano wa Uwekezaji pale Dubai. Niliyeambatana naye alikuwa ni rafiki yangu mfanyabiashara wa nchi jirani, alikuwa na cash money dola 400,000. Alipofika Dubai alipoambiwa a-declare akasema 400,000 USD. Pale pale wakampa pass ya VIP na kumwambia Sir, do you want us to facilitate your protection while in Dubai? Unataka tukulinde ukiwa hapa? Akasema hapana, I am comfortable. Je, unapenda tujue hoteli unayofikia? Akasema ndiyo, akataja hoteli yake. Akapewa heshima tofauti na Norman Sigalla King aliyekuwa na Dola 350 za kulipa tu hoteli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii nini maana yake? Maana yake ni kwamba mwekezaji anapoleta fedha, it is immaterial kuhoji ametoa wapi? Ametumiaje ni sahihi kuuliza. Ndiyo maana kwenye mchango wangu mwingine nimesema, mtu kama anataka kuangusha Serikali yetu, huyo mfuatilieni. Dunia ya leo unaweza uka-track matumizi ya fedha bila kunihoji kabisa. I will feel comfortable kwamba this is the correct avenue ya ku-invest. Nitasema hapa ndiyo mahali pa kuwekeza, kwa nini? Siwi disturbed, sisumbuliwi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sana tufuatilie matumizi ya fedha wanazoingia nazo watu. Kwa vyovyote vile fedha ni jambo la msingi zikiingia kwenye nchi yetu isipokuwa matumizi yake ndiyo yanaeleza ushetani wa fedha. Sisi Wachungaji Makanisani huwa tunapokea kila sadaka bila kuuliza inakotoka kwa sababu ni matumizi ya hela ndiyo yanayoeleza uovu wa mwenye hela na siyo vinginevyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili la haraka haraka ni sekta ya kilimo. Sekta ya kilimo ndiyo uti wa mgongo kwa Watanzania. Kwenye bajeti ya rafiki yangu Mheshimiwa Dkt. Mpango anaeleza wazi kwamba asilimia 66 ya Watanzania wanategemea kilimo. Ombi langu, moja, tuanzishe kiwanda cha kutengeneza mbolea ambayo itakuwa branded kutoka kwenye uzalishaji kwamba this is not for export, ni kwa ajili ya wakulima wa Tanzania na mfuko wake ni Sh.20,000 kwa yeyote anayetaka, bila kuweka categories.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, NFRA kwa jinsi ilivyoanzishwa, bahati nzuri ni part ya andiko langu ndiyo lililoanzisha NFRA. Anayependa asome kitabu changu kinachosema ‘Maendeleo ni Vita, tufanyeje’. Tulichopendekeza ni kwamba NFRA ipewe fedha nyingi za kutosha ili i-act kama backup ya wakulima wanapokuwa wamelima mahindi, wawe na assurance ya price, wajue bei yake kwamba naenda kukopa benki kwa sababu najua kilo moja ya mahindi ni shilingi fulani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muhimu kwa Serikali, afadhali Serikali ipoteze shilingi bilioni 30 au shilingi bilioni 40 kwa kuwagawia wakulima waliolima kiukweli kuliko vinginevyo. Naiomba sana Serikali, fedha za kununulia mazao kama ya mahindi zipelekwe kwa wingi na tulazimishe wafanyabiashara wote kununua NFRA au kama hiyo Tume ya Mazao au whatever wanunue huko, lakini kwa mkulima tu-ensure price yake kwamba the minimum price you will get is this much, kwa hiyo, tupeleke fedha kwenye eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwa haraka kwenye huduma za afya. Sasa hivi tunajikita kwenye kupeleka madawa, naomba sana Serikali ibadili sura. Sasa tupeleke elimu kwenye kula vyakula bora. Mwezi uliopita tumekwenda Korea, tulikuwa tunakohoa tukauliza kwa mtu mwenye miaka 74 kama anaweza kutuonyesha kituo cha afya kiko wapi, anasema hafahamu kituo cha afya popote. Tukamwuliza, kwa nini? Akasema sijawahi kuugua, kwa hiyo, hajui lakini siri ni aina ya vyakula anavyokula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unafahamu, leo hii tunagombania sukari, tunaongelea habari ya mafuta, nchi za wenzetu, mafuta yanayoitwa sijui mawese na mafuta yoyote ya kupikia kwao zilipendwa. Hakuna wanaotumia mafuta hayo sasa, yanarushwa kwetu nchi changa. Kwa nini? Kwa sababu wanajua kuwa ni madhara kwenye afya zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nihitimishe na jambo la pili kutoka mwisho kuhusu umuhimu wa kutekeleza Mradi wa Stiegler’s, chonde chonde, naiomba Serikali yangu ya CCM, mradi wa Mchuchuma na Liganga upewe kipaumbele.
Nilisema wakati…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. PROF. NORMAN A.S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema wakati fulani hapa kwamba ndiyo mradi pekee ambao Tanzania ina hakika kwamba utalipa fedha tulizowekeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nachukue nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kunipa heshima ya kuchangia nafasi hii muda huu. Jambo la pili, kama wenzangu walivyosema, nachukua nafasi hii kumpongeza Rais wetu mpendwa, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kazi kubwa na nzuri anayoendelea kufanya kwa ajili ya Taifa letu hili. (Makofi)
Tatu, namshukuru Waziri mwenye dhamana hii ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, rafiki na ndugu yangu Mheshimiwa Mwigulu Nchemba kwa kazi kubwa ambayo ameendelea kufanya na wasaidizi wake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesimama kwa masikitiko makubwa sana, pamoja na kazi kubwa anayoifanya Waziri wetu, niliposikiliza pamoja na kusoma kitabu cha hotuba yake hii sijaona akisema chochote kuhusu Shamba la Mifugo la Kitulo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwalimu Nyerere pamoja na Mzee wetu Karume, mara baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kazi kubwa waliyoifanya ni kuhakikisha uchumi wa Tanzania wanaugawanya kufuata mahitaji. Moja ya walichokiamua ni kuanzisha shamba maalum la mifugo Kitulo, Wilaya ya Makete ili kusaidia wakulima wetu kuachana na kuchunga ng‟ombe, waanze kufuga, wameamua hilo mwaka 1965.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali zilizofuata ni masikitiko makubwa, hazijapeleka mkazo kwenye shamba hili. Kumbe waasisi wa Taifa hili waliona kwamba ni vigumu sana kutenga eneo la wachungaji, wakasema ili tubadilike ni lazima tuanzishe kituo cha kujifunza kufuga na shamba hili liko Kitulo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama shamba hili lingepewa haki, kwa maana ya kupelekewa fedha kwa ajili ya kuendeleza, ni wazi kabisa kwamba uchumi wa Watanzania kama walivyo wote maana Mikoa inayochunga ng‟ombe, Kanda ya Kati na Kanda ya Kaskazini wangeenda kujifunza Makete jinsi ya kufuga. Ng‟ombe mmoja wa maziwa, ni wazi fedha anazozalisha ni zaidi ya mara 20 ya ng‟ombe wa nyama kama ukithaminisha gharama za kuchunga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wafugaji na Waheshimiwa Wabunge wengine wako hapa wanajua, ng‟ombe mmoja kwa kawaida ili avunwe anachukua kati ya miaka mitatu mpaka saba. Ukichukua wastani wa miaka mitano ili umuuze, ambapo ng‟ombe wengi wanauzwa kati ya shilingi 300,000 mpaka shilingi 1,000,000.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikichukua bei ya wastani wa shilingi 500,000, kama ukimuuza baada ya miaka mitano, ni kwamba huyo mchungaji alikuwa analipwa shilingi 8,333 kwa mwezi, kwa miaka mitano yote aliyokuwa anachunga ng‟ombe huyo. Amemuuza ng‟ombe baada ya miaka mitano, lakini akimuuza kwa shilingi 500,000 maana yake kila mwezi alikuwa anapewa ujira wa shilingi 8,333. Ikitokea msimu ng‟ombe amedhoofu kidogo ukamuuza kwa shilingi 400,000 maana yake alikuwa anapewa mshahara wa shilingi 6,666.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wazi na ni lazima tufike mahali kama Serikali tuamue kwamba majibu ya kujenga uwezo wa wachungaji wa mifugo ni Shamba la Kitulo lililopo Makete. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wabunge, nyie mnafahamu, hata kama ukisema kwamba mchungaji huyu yeye kipato chake ni dola moja, yaani shilingi 2,200 basi kwa miaka hiyo mitano atatumia shilingi 5,600,000 lakini atakuwa amepata fedha ambayo ni shilingi 400,000 mpaka shilingi 500,000 kwa huyo ng‟ombe mmoja. Huyo ng‟ombe amekula shilingi 5,600,000 au shilingi 3,600,000 lakini amepata kati ya shilingi 400,000 na shilingi 500,000 kwa miaka mitano kwa ng‟ombe mmoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, amekula shilingi 5,600,000 au shilingi 3,600,000 lakini amepata kati ya shilingi 400,000 na shilingi 500,000 kwa miaka mitano kwa ng‟ombe mmoja. Ombi langu kwa Serikali, ifike wakati sasa ione umuhimu wa kuendeleza shamba la Kitulo, sambamba na kujenga miundombinu inayofanya shamba la Kitulo liweze kufanya kazi. Namsifu rafiki yangu Mheshimiwa Mwigulu, tulipomwomba aje kwenye shamba hili la Kitulo alishangaa sana, maana ni shamba ambalo lina ekari 12,000, ng‟ombe waliopo ni 750, shamba lina uwezo wa kuwa na ng‟ombe 4,500 na kama hii ikifanikiwa ni kila nyumba ya Nyanda za Juu Kusini itakuwa ina uwezo wa kuzalisha maziwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, chonde chonde naiomba sana Serikali, lazima tuone umuhimu wa kuenzi waasisi wa Taifa hili kwenye vitu ambavyo vinaleta uchumi chanya kwa wananchi wetu, badala ya kuenzi wakubwa hawa kwa vitu ambavyo kimsingi you can not quantify in terms of economic benefits. Ni muhimu sana! Mojawapo ni shamba la Kitulo la Makete, ardhi ipo ni mali ya Serikali, tatizo ni nini? Wanahitaji shilingi bilioni 7.7 ili shamba hili lirudi asilimia 100 kwa full fledged ni shilingi bilioni 7.7
Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hii pia kuchangia upande wa mbolea. Moja ya mkakati ambao hatujautekeleza vizuri, kama Serikali ya Chama Tawala ni upande wa mbolea ya ruzuku. Naomba sana badala ya kuendelea na mpango huu, ni vizuri Serikali yetu iamue kujenga Kiwanda cha Mbolea, mifuko iandikwe kabisa Not For Export, iuzwe locally kwa bei ya shilingi 10,000, kila mtu mwenye uwezo wa kulima anunue, bila kubagua nani apewe na nani asipewe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mtu binafsi anajenga Kiwanda cha Minjingu pale Manyara, kwa nini Serikali isifanye hivyo? Tunajenga kiwanda kama Serikali, lakini mifuko inaandikwa Not For Export.
Kwa hiyo, kila mkulima mwenye uwezo, anakuwa na uwezo wa kununua. Utaratibu uliopo sasa unamfanya mwenye uwezo wa kulima sana asipewe. Maana Kanuni inasema, anayetakiwa kupewa ni mwenye ekari moja au mbili; ninalima ekari 500 then sistahili kusaidiwa. Sasa swali ni hili, nani ananufaisha uchumi wa Taifa hili? Bila shaka ni yule mwenye ekari nyingi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hili, naomba niseme kidogo upande wa watendeji wetu yaani Maafisa Ugani. Vijiji vyetu vina Maafisa Kilimo, utaratibu uliopo sasa haufanyi maafisa hawa wawajibike kwa wakulima wetu.
Ombi langu kwa Serikali, Afisa Ugani wajibu wake mmojawapo uwe kuwatembelea wakulima na kujua kwamba ametembelea wakulima wangapi, atoe hesabu hiyo ngazi ya Kata mpaka Wilaya ili tuwe na hakika wakulima wangapi wamefikiwa na wataalamu wetu. Vinginevyo mtu anaweza akaajiriwa leo na asitoe ushauri kwa mkulima yeyote, bado akapata mshahara wake. Ni lazima aseme amemshauri nani? Ametembelea wakulima wangapi? Tukifanya hivyo, nchi yetu itabadilika na itafanikiwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba sana, ukitaka kufanikisha kilimo, ukitaka kufanikisha ufugaji, jibu ni shamba la Kitulo lililoko Makete. Liwe Shamba Darasa la Tanzania nzima. Mungu awabariki sana, Amina. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
MHE. PROF. NORMAN A. SIGALLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kunipa nafasi. Kwanza kabisa nianze kumpongeza Waziri Mheshimiwa Mbarawa na msaidizi wake kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya, lakini na mtihani mkubwa walionao wa kuhakikisha kwamba nchi hii inabadilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie maeneo machache kwa haraka haraka. Umuhimu wa Kuunganisha RAHCO na TRL. Wabunge wengi wamechangia, lakini nimepitia sheria ya uanzishwaji wa TRL pamoja na RAHCO, ambacho nimebaini majukumu ya RAHCO bado ni majukumu ya msingi sana.
Pendekezo langu ni muhimu sana RAHCO aondolewe kwenye kusimamia reli ya kati, kwa sababu aliikuta, irudi TRL lakini majukumu ya RAHCO yaendelee kwenye reli mpya zote ambazo hatujajenga ikiwemo reli ya Mtwara Corridor. Miundombinu ya reli zote mpya ambazo hazijajengwa zibaki kwa RAHCO lakini aondolewe kwenye kusimamia reli ya kati, Reli ya kati ibaki TRL. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo naomba nisisitize umuhimu wa ujenzi wa reli ya kati kama wenzangu walivyosema kwa kutoa dimension tofauti kidogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, uchumi wa sasa duniani kote concession agreement ndio utaratibu wa uchumi wa dunia hii, uchumi wa tender ni wa kizamani kidogo nachelea kusema. Watu wanaotafuta biashara duniani anakushawishi, niko tayari kufanya a, b, c, kwa faida hii na mimi nitakupa hivi. Hivi ndivyo walivyofanya Kenya, Rwanda, Uganda, Djibouti na Ethiopia kujenga reli zao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, na kwa utaratibu wa concession agreement nchi haingii kwenye hasara ya kulipia kwa sababu deni linalipwa na uendeshaji wa mradi husika, ndiyo maana ni muhimu sana viongozi wetu wanaoisimamia Wizara hii walione hili kwa namna ya kipekee sana ili kuharakisha ujenzi wa reli ya kati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo niweke mfano mwepesi ili twende pamoja na wenzangu. TRL yenyewe kabla ya uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa sasa ilikuwa inaenda hovyo. Baada ya kuteuliwa CEO wa sasa ndugu Masanja TRL Inafanya vizuri, hii inakupa picha kwamba si wakati wote tatizo ni mfumo, kuna wakati mwingi na sehemu kubwa ya Waafrika tatizo letu ni watu wanao-execute nafasi hizo. Ukichagua CEO mbaya shirika linaweza likafa siyo kwa sababu ya mfumo, ndio maana TRL leo inafanya vizuri hakuna kilichobadilika. Sheria ni zile zile lakini baada ya kubadilisha CEO tu TRL inaenda vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashawishika kusema ni wajibu wa Serikali kuangalia kwamba competency based on recruitment, promotion and appointement become the key in terms of allowing other people to execute these positions. Lazima tuteue, tuajiri na tuwapandishe vyeo watu wetu kwa kufuata weledi usiotia mashaka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kidogo habari TRA na TPA na hasa utaratibu wa kutoza kodi mbili (storage charge na wherehouse charge). Ni vizuri sana Wizara iharakishe kuondoa kabisa TRA asitoze tozo la kutunza mizigo libaki TPA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo ni vizuri sana niongeze kusema habari ya simu fake.
T A A R I F A...
MHE. PROF. NORMAN A. SIGALLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kidogo kuhusu simu fake. Watu wengi fasili ya simu fake wanadhani kwamba ni simu za shilingi 30,000; shilingi 25,000 ndizo simu fake. Ukweli ni kwamba simu nyingi za bei ndogo ni simu genuine. Mpaka sasa hivi, baada ya TCRA kuanzisha utaratibu huu ni asilimia 14 tu ya simu ambazo hazijahakikiwa. Wengi wanasema kwa nini waagizaji hawakufanya hivi kabla ya hapo?
Naomba niseme kwamba hili limetokana na kwamba TCRA haikuwa na mitambo ya kutambua simu fake na simu original. Baada ya kupata mitambo ni lazima tuingie sasa kwenye utaratibu wa kuhakiki simu hizo. Wengi mnajua simu fake madhara yake ni nini. Ninaweza kukupigia simu wewe nikakugombanisha, nikakufanyia madhara na mfumo wa utambuzi ukashindwa kutambua, ndiyo maana ni lazima tuwe na simu halisia ili kulinda afya na ulinzi wa watu wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nichangie kidogo kuhusu barabara. Niipongeze Serikali kwa kutenga fedha kwenye barabara, lakini naomba nisisitize barabara zinazounganisha mikoa kwa mikoa chonde chonde, ni Katavi kwenda Tabora, Kigoma kwenda Tabora barabara ya Njombe kwenda Makete kwenda Mbeya, barabara ya kutoka Chimala - Matamba kwenda Hifadhi ya Kitulo ni muhimu sana zikapewa kipaumbele kwa sababu ya uchumi wetu na kuimarisha uchumi wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo niombe sana Wizara ikamilishe viwanja vya ndege hasa vile ambavyo kwa sura ya kijiografia vinaunganisha na nchi jirani. Viwanja vya Songwe - Mbeya, Mwanza, Kigoma, Mtwara na viwanja kama hivyo. Baada ya kusema hayo naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. DKT. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Waziri Lukuvi na Naibu Waziri Angeline Mabula pamoja na wasaidizi wake wote kwa kazi nzuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kazi nzuri, Hifadhi ya Kitulo imechukua hata eneo ambalo kimsingi halitumiki kwa utalii wa maua. Kwa hiyo hifadhi imepora eneo ambalo ndilo tegemeo kwa kilimo cha wananchi wa Tarafa za Matamba, Ikuwo, Lupalilo na Magoma, hasa kata zifuatazo Mfumati, Itumbu, Kigala, Ipelele, Mlomwe na Kitulo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Waziri ashirikiane na Waziri mwenye dhamana ya Utalii kurekebisha mipaka ya Hifadhi ya Kitulo ili kuondoa malalamiko ya wananchi na kuwasaidia kuendeleza mashamba yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri ifahamike kuwa ulinzi wa Hifadhi ya Kitulo unategemea wananchi hawa. Ni muhimu wailinde huku wakiwa na eneo lao kwa ajili ya kulima. Mheshimiwa Waziri alishughulikie jambo hilo hasa miezi ya kuanzia Juni mpaka Septemba wakati wa kiangazi. Nawasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. PROF. NORMAN A. SIGALLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nashukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia kwenye Wizara hii.
Kwanza kabisa napende kumpongeza Mheshimiwa Sospeter Muhongo na msaidizi wake na timu yake nzima kwa kazi kubwa ambayo wanalifanyia Taifa hili kuhakikisha kwamba nishati ya umeme inapatikana. Sambamba na hilo, napongeza kwa sababu ni ukweli ulio bayana kwamba kwa sasa Tanzania ni moja ya nchi ambazo zinafanya vizuri zaidi Afrika, kwa maana ya coverage, yaani kwenda kwa kasi katika kusambaza umeme. Hongera sana Mheshimiwa Waziri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua uwezo wako na weledi wako, lakini nimesikitika sana ulipokuwa unawasilisha bajeti yako, hasa baada ya kuona Mto Lumakali ambao uko Makete ambao study yake ya kwanza imekamilika mwaka 1998 ikionesha kwamba tuna uwezo wa kuzalisha umeme megawatts 222; ikarudiwa tena mwaka 2002, ikaonesha kwamba tuna uwezo wa kuzalisha megawatts 340.
Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ni mto pekee ambao study kwa miaka 60 inaonesha kwamba maji yake hayapungui. Ninatambua changamoto tuliyonayo kwenye mito mingi iliyoko Tanzania, ni kupungua kwa maji. Ndiyo maana wakati nachangia Mpango wa Serikali nilisema Mheshimiwa Sospeter Muhongo anaonekana ana ugonjwa wa gesi; bila shaka nilimtania, lakini najaribu kusema kwamba upo umuhimu mkubwa wa kupeleka nguvu kubwa kwenye mradi wa maji wa Mto Lumakali unaopatikana Makete, ni muhimu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu unajumuisha kuweka kingo za bwawa. TANESCO wameshafika mara nyingi kule, makampuni ya Afrika Kusini, China yamefika kule, yameshawaweka tumbo joto wananchi wangu wa Makete kwamba mpaka hapa tutakuwa na bwawa. Wameendelea kusubiri toka mwaka 1998 bwawa hilo halitokei.
Naomba sana Waziri mhusika aone umuhimu wa kipekee sana kupeleka bwawa hili. Bwawa hili pamoja na uzalishaji wa umeme litakuwa muhimu kwa uchumi wa Nyanda za Juu Kusini na Tanzania kwa ujumla. Utakuwa umepanda zao jipya la samaki kuvunwa katika bwawa hili la Lumakali pamoja na Mto wenyewe wa Lumakali. Kwa hiyo, ni muhimu sana jambo hili likatekelezwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tena Wizara ione umuhimu wa kupeleka maeneo yaliyosalia umeme wa REA na hasa Kata za Lupila, Mbalache, Ukwama, Mang‟oto, Kipagalo, baadhi sehemu za vijiji vya Tarafa ya Magoma, Tarafa ya Ikuo, Tarafa ya Matamba na Tarafa ya Lupalilo. Ni jambo la msingi sana ili wananchi wa Makete wapate kuleta maendeleo kwenye nchi yetu. Kwa bahati nzuri unatambua, wananchi wa Makete kwa asili ni wachapakazi, kwa hiyo, nishati ya umeme kwao ni nguzo pekee ya muhimu itakayowezesha tukimbizane na maendeleo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie kidogo eneo la madini. Sheria ya Madini ni muhimu sana ikafanyiwa marekebisho. Utaratibu uliopo sasa wa kupata leseni Makao Makuu na kupewa eneo Makao Makuu bila ushiriki wa Halmashauri husika, hautendi haki. Ni muhimu sana tutengeneze mahusiano kati ya Mamlaka ya kutoa leseni na Halmashauri mama yenye kumiliki ardhi ambayo inaangukia kwenye eneo hilo ili kuondoa migongano isiyo na sababu lakini pia ili kuwapa faida wananchi ambao maeneo haya kimsingi ni ya kwao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie EWURA. Wenzangu wallyotangulia walikuwa wanasema kwamba wana interest na maeneo hayo; nami kwenye madini pamoja na mafuta nina-declare interest.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Makete pale mjini ina vituo vinne vya mafuta. Wamekwenda Maafisa wetu wa EWURA kufunga vituo vyote. Makete hakuna transit, kwa maana ya malori yanayobeba mafuta kupita Makete. Mafuta haya yanatwaliwa Dar es Salaam kwenye depot. Ni muhimu sana Maafisa wetu wa EWURA wajikite kwenye ku-control quality Dar es Salaam yanakotoka mafuta. Wajikite kwenye kufanya mahusiano stahiki na mamlaka nyingine zinazohakikisha kwamba mafuta yanayokwenda nchi jirani yanakuwa monitored ili kwamba mafuta hayo yasipelekwe mitaani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo sahihi hata kidogo, inaonekana kama ni uonevu hivi kidogo, pale ambapo mafuta yanatoka Dar es Salaam, muuzaji wa mafuta yuko Makete, kilometa 900 kutoka Dar es Salaam, hakuna barabara inayopita kule kwenda nchi jirani, barabara yenyewe ni mbovu, halafu wafanyabiashara hawa wanafungiwa vituo vyao kwa sababu tu ya maafisa wetu wa EWURA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa labda nimwombe Mheshimiwa Waziri, ninaamini sana katika competence based recruitment, ninaamini Sheria ya EWURA ni nzuri, kwenye hili, tatizo ni la watu. Tusioneane haya kwenye hili. Tatizo ni la maafisa wetu. Ni muhimu sana, maafisa wetu, sheria hata ingekuwa nzuri, kama an official ni corrupt ata-jeopardize the entire system.
Kwa hiyo, ni muhimu sana maafisa wetu hawa waangaliwe ili wanapofanya maamuzi, basi waone madhara ya uchumi pia. Tukisema hivi, hatumaanishi kwamba sasa watu waendelee kuvunja sheria, hapana. Tunachojaribu kusema ni kwamba mafuta yanakotoka yanajulikana, ni Bandari ya Dar es Salaam pekee inayoingiza mafuta Tanzania. Kwa hiyo, eneo la ku-control linajulikana. Inaumiza sana kuona watu wa Makete nao wanafungiwa vituo vyao kwa sababu tu ya maafisa hawa wanaoshindwa kuzingatia umuhimu wa kuzingatia mafuta.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nisisitize kusema kwamba Tanzania kwa sasa ninafahamu, tunakoelekea ni kuzuri, tena kuzuri sana na kazi hii kwa vyovyote vile nitakuwa nimekosa nidhamu kutokumsifia Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa maamuzi yake ya kuongeza bajeti ya jumla ya maendeleo kufikia asilimia 40. Leo Waziri mwenye dhamana anatuambia, asilimia 94 ya bajeti yake inakwenda kwenye maendeleo. Mungu aibariki sana Tanzania na Mungu aibariki sana Serikali ya CCM kwa jambo hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja, Mungu awabariki sana. Ahsante.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi nichangie. Kwanza kabisa nianze kumshukuru Mungu kwa kutupa Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa Rais wetu wa Awamu ya Tano na mikakati yake ya kuiendeleza Tanzania. Kwa vyovyote vile ametumia weledi stahiki wa Marais waliomtangulia ili kuhakikisha kwamba nchi yetu inakuwa nchi ya neema.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, niseme mambo machache. Mimi ni mmoja wa waumini wa kodi, nashukuru wenzangu waliotangulia wamesema pia kuhusu kodi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na kodi za kawaida za VAT kwenye maduka yetu na huduma zingine za mahoteli, mpaka sasa nchi yetu, kwa maana ya TRA hawajaitendea haki Tanzania kwa maana ya ukusanyaji wa kodi kwa wanaotakiwa kulipa kodi. Ingia maduka ya jumla yaliyoko Dodoma, ingia maduka ya jumla yaliyoko Dar es Salaam, migahawa mikubwa iliyoko Dodoma na of course Tanzania ona ni wapi ambapo wanalipa kodi? Hawatoi risiti, TRA wapo;na kwa sababu kutokulipa kodi ni criminal offence, naomba niishauri Serikali kwenye hili hakuna awareness creation. Huwezi ukahamasisha watu kulipa kodi, ni lazima ufanye coercion, ni lazima utumie nguvu.
Mheshimiwa Naibu Spika, badala ya Jeshi letu la Polisi kukaa barabarani na kusimamisha magari yanayokwenda kasi, waingie mtaani kukamata watu wasiolipa kodi na hasa kwenye maduka. Ni lazima wote tukubaliane kwamba tutengeneze nchi ambayo inaabudu kulipa kodi na kwa kuanza hiari haipo, haiwezekani. Huwezi ukasema unatoa tangazo redioni ili mtu alipe kodi, haipo, ni lazima uende kwa shuruti, mtu aone adhabu ya mtu anayopata baada ya kukwepa kodi ndipo wengine wanaanza kulipa kodi.
Mheshimiwa Naibu Spika, wakati fulani nilikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai pale. Wachaga wakawa wananiambia kitu gani kiliwafanya wao walime kahawa. Wakasema haiwezekani ukahamasisha watu walime zao ambalo wao hawalijui. Wakasema wakoloni walichofanya ni kushurutisha watu ili walime kahawa, lakini baada ya kukomaa ile kahawa wameuza, wale Wazungu wakawaambia sasa haya mapato ni ya kwenu ndiyo waka-induce spirit ya kupenda kulima kahawa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninachotaka kusema ni kwamba, kwenye kodi hakuna lelemama, ni lazima kama nchi tukubaliane, kwamba Jeshi letu la polisi tunalo, tunajua maduka hata hapa Dodoma hawalipi kodi, Dar es Salaam tunajua miji yote hawalipi kodi lazima tulipe kodi. Kodi ndiyo itakayoifanya nchi yetu isonge mbele. Kwa hili TRA lazima waongoze, lakini Police Force nayo ifundishwe jinsi ya kufuatilia kodi zetu badala ya kwenda kwenye vitu ambavyo kimsingi havizalishi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Bajeti ya Waziri wa Fedha, ameonesha kuanzisha kodi kwenye transfer of shares, yaani unapouza hisa zako, basi wewe utozwe kodi. Nasikitika Mheshimiwa Philip Mpango rafiki yangu na Waziri wetu its unacceptable from all economic point of view; haipo.
Mheshimiwa Naibu Spika, huwezi ukatoza kodi kwenye transfer ya hisa; NMB kwa mfano ilipouza hisa mara ya kwanza iliuza kwa sh. 150, zikapanda mpaka 5000, zimeshuka mpaka 1,500 uliyemtoza capital gain kwenye transfer ya hisa ilipofika 5000; anapo encounter capital loss Serikali itamfidia? Anataka kuuza hisa zake alizonunua kwa 4,000 na bei ya soko ni shilingi 1,000 utafidia hiyo difference ya 3,000? Huwezi kufanya hivyo. Kwa hiyo, siyo ya kiuchumi wala siyo ya kinadharia wala siyo ya kivitendo.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kenya, Rwanda, South Africa hawafanyi, kwa maana ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hakuna anayeifanya hiyo ninyi mnaitoa wapi? Kenya waliiweka kwenye sheria wakaiondoa hata kabla hawajaitekeleza na tukumbuke ni vizuri Waziri afahamu, moja ya sababu ya kuanzisha Soko la Dar es Salaam ni kuhamasisha uwekezaji. Unaposema mtu akiuza unamtoza kodi unafukuza wawekezaji kwenye nchi yetu, chonde chonde naishauri Serikali iachane kabisa na hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, kodi ya miamala ya simu. Kaka yangu Mheshimiwa Zungu ameliongelea sana, naomba nisisitize. Bahati nzuri mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; chonde chonde Watanzania kodi hii ni lazima itozwe. Ni kweli miamala hii ni kati ya trilioni 40 mpaka 50 kwa mwaka, Serikali inakosa fedha nyingi kwenye hili. Naomba sana katika hili tuiunge mkono Serikali iendelee kutoza.
Mheshimiwa Naibu Spika, niunge mkono haraka haraka Kamati ya Bajeti ya kupendekeza ongezeko la Sh. 50 kwenye mafuta ili tuwe na maji. Hivi ni nani ambaye atakataa kwenye hili? Ndiyo maana sioni kigugumizi cha Serikali kinatoka wapi; Wabunge tunapoongea, tunaongea kwa niaba ya wananchi wa Tanzania; this is the feeling of Tanzanians, tunajua kabisa ukiongeza sh.50, kama ukituma salamu kwamba ni kwa ajili ya maji hakuna atakayekataa kigugumizi kinatoka wapi?
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nisemee kidogo milioni 50 kwa dhima ya Rais wetu. Marais wote duniani wana-dictate vision, lakini kufasili vision ni wajibu wa watendaji kama Waziri na sisi Wabunge kwa nafasi zetu. Rais, Magufuli alichosema kila kijiji atatoa milioni 50, mwenye kufasili utekelezaji huo sio Rais wetu, siyo kazi yake, ni Mawaziri, ni sisi Wabunge. Hakuna uchumi duniani wa kugawa hela.
Mheshimiwa Naibu Spika, pendekezo langu, kwa mfano, Wilaya ya Makete ina vijiji 103, ukikipa kila kijiji milioni 50 maana yake ni Sh. 5,150,000,000/=; Bilioni tano zinatosha kuanzisha Community Development Bank ya Makete na kwenye Tarafa zake sita ukaweka ofisi kwa sababu mtaji wa Community Development Bank ni bilioni tatu. Kwa hiyo, bilioni tano zangu Wilaya ya Makete, ukiwapelekea wakope kwa riba nafuu, hao wote mnaotaka vijiji vikope sasa zitakwenda kwenye Community Development Bank, mtaji ni wa Serikali, wa bilioni tano na Community Development Bank bilioni tano, kwa hiyo Wilaya nzima itanufaika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama si hivyo, ukiwauliza Wabunge wanajua, kwangu mimi ukipeleka bilioni tano ambazo zinatakiwa kwa milioni 50 kila kijiji, umemaliza kabisa tatizo la maji Makete. Badala ya kugawa milioni 50 waulize wananchi wa Makete watakwambia tunataka lami, tunataka maji. Bilioni tano zinatosha kufuta tatizo la maji, kutengeneza benki Wilayani Makete na Wilaya nyingine za Tanzania ili tuweze kupata maendeleo. Sina hakika kama ni kengele ya kwanza ama ya pili.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, niseme naunga mkono hoja na Mungu ambariki Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wake ili twende kwenye haya tuliyopendekeza. Amina.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama wenzangu walivyochangia, nimpongeze Profesa Maghembe na wenzake kwa kazi nzito waliyonayo. Mmoja alisema mzigo mzito mpe Mnyamwezi nadhani kwa mzigo huu hata Mnyamwezi anaweza akashindwa kuubeba. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jana nimemsikiliza sana Waziri mwenye dhamana, Mheshimiwa Profesa Maghembe nikafikiri sikumsikia vizuri. Nikaisoma hotuba yake nikaridhika kwamba nilichosikia jana ndicho kilichoandikwa. Nimesikitika sana kuona katika kitabu chake chote ameacha hifadhi pekee ya maua kwenye Bara letu la Afrika lakini ukisoma kitabu chake, utalii Tanzania unapungua. Yeye hasemi chochote kabisa kuhusu habari ya kuendeleza Hifadhi ya Kitulo iliyoko Makete, hasemi chochote kabisa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Makete wa Kata za Mfumbi, Mlondwe, Matamba, Kinyika, Ikuwo, Kigala, Ipelele pamoja na Kitulo yenyewe, wamehamishwa ili kupisha hifadhi hii muhimu. Sasa miaka inakwenda Wizara haifanyi chochote na bahati mbaya sana kwenye hotuba ya Waziri hasemi chochote kabisa juu ya mkakati wake wa kuendeleza Hifadhi ya Kitulo. Nimesikitika sana na nasikitika sana, kwa vyovyote vile sitaunga mkono hoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wazi utalii katika nchi yetu unachangia kiasi kikubwa sana cha Pato la Taifa lakini mkakati wa Wizara ni nini kuongeza watalii? Hasemi chochote juu ya kuboresha Hifadhi ya Kitulo, hasemi chochote juu ya kuboresha miundombinu ili angalau sasa watalii waone Makete kwenye Hifadhi ya Kitulo ni sehemu ya kukimbilia. Sikutaka kushawishika kwamba Mheshimiwa Profesa Maghembe yeye anaziona hifadhi zilizoko Kaskazini tu, sikutaka kufika huko, lakini naanza kushawishika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niombe sana, ni lazima Waziri aje na majibu ni jinsi gani anafanya kwenye bajeti hii kuwafanya wananchi wa Makete ambao wanaitunza hifadhi hii, wamehama kuacha maeneo yao wasilime ili kuheshimu Pato la Taifa, basi wagawane Watanzania wote, maana wangelima wao mapato yale ni ya kwao. Wamepisha ili sasa hifadhi hii iwe mali ya Watanzania wote. Waziri atoe majibu hapa anaifanyia nini hifadhi hii ili kuongeza pato la Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nafahamu kwamba Ngorongoro na Serengeti zimetajwa lakini Waziri anafahamu moja ya sifa zilizopelekea Hifadhi zetu za Ngorongoro, Serengeti na Manyara kuongeza watalii ni baada ya kuboresha miundombinu hasa barabara ya kutoka Arusha kuelekea Manyara na Monduli pia kuelekea kwenye lango la Ngorongoro, Kitulo mnafanyaje? Ni wazi ni lazima barabara ya kutoka Chimala – Matamba – Kitulo - Makete ijengwe kwa kiwango cha lami ili kuimarisha utalii kwenye hifadhi hii, ni muhimu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima tufikiri heuristically kwa sababu ni kweli utalii ni leisure, utalii ni burudani, siyo mateso. Hakuna mtalii atakayekwenda Kitulo kama miundombinu mingine haionyeshi kuwasaidia wao. Sambamba na hilo, ndiyo maana nilimfuata Mheshimiwa Profesa Maghembe nikasisitiza umuhimu wa TANAPA kuweka hoteli au kutengeneza mazingira ya kuweka hoteli za kitalii eneo la Matamba ili kuboresha au kuongeza Pato la Taifa, kwenye hotuba yake, kimya!
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kidogo kuhusu mwingiliano wa mipaka kati ya mifugo pamoja na hifadhi zetu. Kwa suala hili ni lazima Serikali ijipange, bahati nzuri mimi natoka wilaya ambayo ina wachungaji wa ng‟ombe, ina wafugaji wa ng‟ombe, ina wakulima na pia ina hifadhi. Narudia, ina wachungaji, ina wafugaji na ina wakulima lakini hifadhi pia inayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani dhana hapa, pia weledi kidogo unatofautiana kwenye kufasili kwa usahihi juu ya wachungaji wa ng‟ombe. Duniani kote inajulikana, ukisema unafanya kuchunga, wachungaji wote wanafuata malisho, nchi zetu hizi ni za ki-tropic, kwa hiyo mvua ina kiangazi na masika. Wakati wa kiangazi lazima mchungaji, siyo mfugaji, mchungaji atahama na mifugo yake kufuata malisho, lazima ugomvi na wakulima utakuwepo tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana naunga mkono hoja iliyotolewa na Mbunge wa Mbinga Mjini, Mheshimiwa Sixtus kwamba Wizara lazima wakae, and on this you must be strict. Hamuweze ku-compromise na Wabunge kwa sababu its impossible, kama anatoka eneo ambalo watu wanachunga nitatetea wananchi wangu na ndiyo sifa kwangu. Ninyi lazima mje na ukweli kwamba pamoja na kwamba unatetea wachungaji wako lakini dunia ya sasa ni ya kufuga siyo ya kuchunga, lazima tuelewane hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Wizara husika ishirikiane na Wizara nyingine kutengeneza mkakati ambao ni endelevu. Ni lazima tutafika mahali tutachagua, tunataka hifadhi au tunataka ng‟ombe wa kuchungwa. Kama tunataka wa kufuga, yes you can set aside a piece of land kwa ajili ya kuchunga lakini huwezi kutengeneza eneo kwa ajili ya kuswaga ng‟ombe, haiwezekani, kiangazi kitaingia lazima watatafuta malisho. Sisi ambao tumetumika sehemu mbalimbali kwenye eneo ambalo ni la wafugaji zikiwemo Wilaya za Hai, Siha, Mbeya, Songea na Makete kwenyewe tunajua, uko mtihani mkubwa wa ku-harness kati ya ufahamu wa kuchunga na kufuga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalize hoja yangu kwa kusema, ndiyo maana nilisema Mwalimu Nyerere na Mzee Karume wamezikwa kaburini lakini wana hekima kuliko sisi, wao waliweka shamba la mifugo Kitulo ili wachungaji wakajifunze kufuga Kitulo. Bahati mbaya Serikali haisemi chochote kuhusu hili. Ni muhimu sana shamba lile lifufuliwe ili wachungaji, waswagaji wa ng‟ombe wajue kwamba zama za sasa ni kufuga siyo kuchunga siyo kuswaga.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ifufue shamba la mifugo la Kitulo lililopo Makete pamoja na hifadhi ile ili liwe shamba darasa kwa mikoa yote Tanzania. Tutapona na tutaondoa migongano kati ya wafugaji na wakulima, vinginevyo haiwezekani, narudia, vinginevyo haiwezekani. Ukitaka kutibu hili ni lazima ukumbuke shamba darasa ni shamba la mifugo kule Makete, lakini Hifadhi ya Kitulo ipewe kipaumbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nisisitize, nakusudia kushika shilingi kama Waziri, Mheshimiwa Profesa Maghembe hatakuja na majibu ya kwa nini katika mpango wake Hifadhi ya Kitulo ameiacha kirahisirahisi tu, ameiacha tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza kwa dhati ya moyo wangu Mheshimiwa Profesa Maghembe (Waziri) pamoja na wasaidizi wake wote. Masikitiko yangu makubwa ni juu ya mambo mawili:-
(i) Kutoweka mikakati ya kuendeleza Hifadhi ya Maua ya Kitulo. Hifadhi ya Maua Kitulo ni muhimu sana, lazima uboreshaji wa miundombinu ya utalii ikiwa ni pamoja na barabara za lami kutoka Chimala – Matamba – Kitulo; Mbeya – Kitulo – Makete; Njombe – Makete – Kitulo. Pia kuweka hoteli ya kitalii Matamba na Makete ili kuongeza utalii.
(ii) Ugomvi wa wachunga ng‟ombe na Hifadhi ya Taifa. Ni muhimu sana kutambua kuwa haiwezekani ukatenga eneo la kuchunga ng‟ombe, unaweza kutenga eneo la kufuga tu. Watu wetu sisi ni wachungaji ambao tabia yao kuu ni kufuata malisho. Nchi yetu ni ya kitropiki ina misimu ya hali ya hewa mikuu miwili yaani masika na kiangazi. Wakati wa masika migogoro ni michache kwa kuwa malisho ni mengi, wakati wa kiangazi migogoro ni mingi kwa kuwa wachungaji wataswaga ng‟ombe kufuata malisho. Muhimu ni Wizara kuamua kisayansi, haiwezekani kutenga eneo la kuchunga ng‟ombe, ni lazima wachungaji wafundishwe kufuga na hili ni muhimu kufanyika kupitia kufufua shamba la mifugo Kitulo.
(iii) Shamba la mifugo Kitulo. Shamba hili likifufuliwa litatumika kama eneo la kutoa mafunzo kwa vitendo juu ya ufugaji wa ng‟ombe wa maziwa na nyama. Shamba hili lilianzishwa mwaka 1965 na Mwalimu Nyerere pamoja na Mzee Karume, walijua huwezi kutenga eneo la kuchungia ng‟ombe, lazima twende kwenye uchumi wa kufuga ng‟ombe wa maziwa na nyama. Ng‟ombe wa maziwa wana faida kubwa kwa binadamu kiuchumi na kiafya.
(iv) Sheria ziwekwe na zisimamiwe kwa ukali. Waheshimiwa Wabunge bila shaka baadhi wana ng‟ombe wanaoswaga, hivyo hawawezi kuunga mkono hoja hii lakini sheria zisimamiwe kwa ukali. Mfano huruhusiwi kuswaga ng‟ombe kutoka Wilaya moja kwenda nyingine bila kibali, sheria hizi zizingatiwe.
(v) Trespass kwenye hifadhi. Ni vizuri Wizara ifahamu kuwa watu wanaochunga ng‟ombe kwenye buffer zone, baadhi yao ndiyo hubadilika na kuvuna pembe za ndovu. Kwenye hili, Wizara lazima isimamie hifadhi hizi kwa ukali. Nchi jirani ya Kenya, ukipeleka mfugo au binadamu kwenye hifadhi unapigwa risasi na wamefanya hivi kwa sababu ni vigumu kutofautisha jangili na mchunga ng‟ombe kwenye hifadhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hifadhi ni muhimu sana kwa Taifa letu, si tu uchumi wa Taifa bali kiikolojia. Hifadhi ni msaada mkubwa wa kuhifadhi ikolojia ya mvua. Kama tukiruhusu uvamizi wa hifadhi, nchi yetu itakuwa jangwa. Serikali isimamie sheria kwa ukali, no compromise.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo heshima kuipongeza Serikali ya CCM kwa kazi nzuri. Kipekee kumpongeza Waziri Mkuu kwa kazi kubwa anayoijenga Serikali na kuwafanya Watanzania wajisikie vizuri. Naomba nitoe ushauri ufuatao ili kuongeza ufanisi wa Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, uteuzi wa kada mbalimbali kwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Makatibu Tawala na Wakurugenzi uzingatie faida ya wateuliwa hao na ni vizuri wafanyiwe usaili (interview) ili kujiridhisha uwezo wao. Mfano Katibu Tawala Mkoa au Wilaya ni wakuu wa Watumishi wote wa Umma katika maeneo yao. Watendaji wa nafasi hizo ni lazima au vizuri, wawe na ueledi na uamuzi unaoashiria kuwa wao ni Wakuu wa Watumishi wa Umma. Mheshimiwa Waziri Mkuu, DAS wa Makete alikuwa mtunza fedha (cashier) kampuni ya TiGO, ndiye sasa Mkuu wa Watumishi wa Umma wote wa Wilaya ya Makete.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu, yapo madhara hasi kwa kuteua wateule ambao watumishi wa mahali pale wanaona kiongozi wao hatoshi. Morali wa watumishi wa umma inakuwa chini kwa maana wanakuwa hawaungi mkono Serikali. Hili ni kubwa sana kwa kuwa Serikali yoyote lazima iangalie madhara ya kutoungwa mkono. Pamoja na nia nzuri ya Rais wetu na wewe mwenyewe Waziri Mkuu, wateuliwa wanaotoka nje ya mfumo wa Serikali, nachukua muda mrefu kujifunza na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa letu na kuipunguzia kukubalika Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wateuliwa kama Wakuu wa Mikoa na Wilaya, wanajikuta wanakosa weledi katika kutumikia nafasi zao. Kwa bahati mbaya kila ubaya unaofanywa na viongozi wa Serikali anayeadhibiwa ni CCM. Jambo la pili. ninaomba ofisi yako Mheshimiwa Waziri Mkuu au Ofisi ya Rais iunde timu ya watu waliopewa neema ya kufikiri. Nakumbuka wakati mzee Malecela akiwa Waziri Mkuu mwaka 1991-1994 aliunda Kamati ya Mipango ambayo kazi yake ilikuwa ni kuisaidia Serikali kufikiri. Kufikiri ni kipawa haimaanishi kuwa mtu akiwa na elimu kubwa basi uwezo wake wa kufikiri unaongezeka. Bali ujuzi wa eneo alilojifunza ndio unaongezeka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati hii inaweza kujumuisha watu mbalimbali hata baadhi ya Mawaziri (kama wana zawadi ya kufikiri) ili kuisaidia Serikali kutoa ushauri wa kiuweledi bila kusukumwa na maneno yasiyo na mashiko. Timu hii itasaidia kutoa weledi kwenye uwekezaji, siasa na
kadhalika. Jambo kubwa ni kuwa, moja kati ya changamoto ambazo Serikali karibu zote duniani zinapata, ni uhakika wa taarifa inazozipokea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naipongeza sana Serikali yetu ya CCM kwa kuangalia vipaumbele ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kati na barabara mbalimbali katika nchi yetu Tanzania. Nami nawaombea viongozi wote mpate kuwa na afya njema na utashi mkuu. Ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. PROF. NORMAN A. SIGALLA KING – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE
YA MIUNDOMBINU: Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue nafasi hii kipekee kabisa kwanza
kupongeza wachangiaji wote 15 ambao wamechangia kwa maandishi na 22 wamechangia
hapa Bungeni. Mambo machache tu niangalize.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema shukrani hizo, Waheshimiwa Wabunge
nichukue nafasi hii kipekee kabisa kumpongeza Waziri mwenye dhamana na wasaidizi wake
wote kwa sababu kwa muda wote ambao Kamati imekuwa ikifanya kazi zake wamekuwa
wakitupa ushirikiano mkubwa sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, mambo machache ambayo mmesisitiza ni pamoja na ujenzi
wa reli ya kati, barabara mbalimbali, bandari zote kwa maana ya Dar es Salaam ,Mtwara,
Tanga na Bagamoyo; lakini pia mmesisitiza upande wa ATCL. Pia Waheshimiwa Wabunge
wamesisitiza sana juu ya ajira pale bandarini na kwamba wako watu walioajiriwa ambao
wamefukuzwa kama hivi; sisi kama Kamati tumepokea taarifa hiyo na Wizara imesikia na sisi
wajibu wetu tutafuatilia kuona kwamba Serikali inafanya inavyopasa kama lililofanyika
halikupaswa kufanyika hivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge nitumie nafasi hii kusema mambo
machache tu, na hasa juu ya mradi huu wa reli ya kati. Ninaipongeza sana Serikali kwa sababu
dhamira yake na haya maneno niliyasema Dar es Salaam wakati wa kusaini mkataba juzi wa kutoka Dar es Salam kwenda Morogoro. Nikasema kwa sababu mipango yetu ya kwanza ya reli
yetu haikuwa kilometa 160 kwa saa, kuchelewa huku ndiko kumetupelekea kwenye kilometa
160 kwa saa. Nikasema kama kuchelewa ni huku basi ni kuchelewa kuzuri, maana sasa
tumeenda kwenye spidi kubwa zaidi yenye manufaa zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini muhimu kabisa ambalo Wizara ni vizuri ifahamu ni
kwamba kukamilika kwa reli ya kati ni jambo moja, muda wa kukamilika reli ya kati ndio muhimu
zaidi. Kwa sababu zilezile kwamba mzigo tunaotegemea ili uweze kurudisha mkopo wao wote
wa reli ya kati ni ule ule ambao Kenya, Uganda, Rwanda, DRC na Zambia wanautegemea.
Ndio maana nasisitiza tena na Kamati inasisitiza tena kwamba vyovyote itakavyokuwa tumieni
mkandarasi yoyote mnayemjua kwa vipimo mnavyovijua, muhimu reli hii ikamilike haraka kabla
wenzetu hawajakamilisha, hilo ni muhimu kwetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, na nisisitize tu kusema pia kwamba naunga mkono vizuri sana,
Mheshimiwa Waziri amesema amegawa vipande vingi vingi kwa maana ya ujenzi wa reli ya kati
na sisi Kamati hatuna tatizo na hilo lakini bado tunasisitiza kwamba standard ya reli na
upatikanaji wa funding ndio unaotengeneza hot cake ya project yoyote. Narudia, project
yoyote haiwi viable kama funding haipo; kwa hiyo ni funding inapokuwa available ndio
inafanya mradi kila mkandarasi aone ni hot cake. Unayejua umuhimu wa kuchukua mizigo
Kigoma au kuchukua Kalemi kule Mpanda ama Mwanza ni wewe Mtanzania; mjenzi
anachoangalia ni funding. Ndiyo maana Serikali mjipange ili kufasili kwa usahihi kwamba
funding iko vipi na kwahiyo tunaelekea wapi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo nichukue nafasi hii tena kuomba sasa
kutoa hoja kwamba Bunge lako tukufu lilidhie taarifa ya Kamati ya Miundombinu iwe maelekezo
rasmi kwa Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kushukuru kipekee kabisa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge wote ambao walikuja kuniona nilipokuwa nimelazwa pale Hospitali ya Muhimbili, nasema ahsante sana wote mliokuja na ambao hamkuja wote mlifanya kazi moja ya kuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mambo machache tu ambayo ninataka kuchangia ni Mradi wa Matamba na Kinyika, Wilaya ya Makete ambao Wizara imeandika barua ya kwamba kupewa no objection. Mpaka sasa hivi hatujapewa no objection na mradi huu ni wa bilioni 4.6, ni vizuri Mheshimiwa Waziri akaupa no objection mradi huu ili mambo yaende mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi mwingine ni wa Bulongwa ambao unajumuisha Bulongwa, Iniho, Kapagalo, Usililo, nayo ni umeshakamilika unahitaji milioni 264, lakini huyu mtu amemaliza kufanya kazi hiyo, fedha hajapewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi mwingine ni Mradi wa Lupalilo- Tandala ambapo zinahitajika milioni 161, mpaka sasa hivi bado hajapewa, naomba sana Mheshimiwa Waziri ukumbuke kufanya jambo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi mwingine ni Mradi wa Igumbilo ambao ni milioni 308 zinahitajika ili ziweze kutekeleza mradi huo, naomba sana sana Wizara iweze kutoa fedha hizo ili mradi uweze kutekelezeka. Zaidi ya hapo nipongeze sana sana Serikali ya CCM, Mheshimiwa Waziri Profesa Mbarawa, Katibu Mkuu Profesa Kitila Mkumbo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwezesha miradi hii kutekelezeka. Mungu awabariki sana. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kuungana na wenzangu kutoa pole kwa ajili ya msiba mkubwa ambao Taifa letu limepata na bila shaka Mungu atawatunza watoto hawa maana ni wenye haki mbele zake.

Mheshimiwa Spika, nianze kuchangia kwenye eneo la timu yetu ya Taifa. Mwaka 1985/1986 mimi ni mmoja wa wachezaji walioitwa kwenye Timu ya Taifa ya vijana. Wakati huo tulikuwa tunafundishwa na kaka yetu Joel Bendera, sifa ya kujiunga na timu hizo ilikuwa ni ubora wa wachezaji hao waliotafutwa Sekondari na kwingineko, maadam umri wao ulikuwa chini ya miaka 24.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi watu wengi wanapoongelea timu ya Taifa, wanaongelea kana kwamba tatizo kubwa la Timu ya Taifa kufanya vibaya ni kwa sababu hakuna timu za watoto wadogo. Ni tabia yetu kutokukumbuka historia ya mafanikio yetu.

Mheshimiwa Spika, ni vizuri Waziri afahamu kwamba ili ufanye vizuri, cha kwanza ni wachezaji bora, lakini cha pili ni Mwalimu mwenye weledi. Nijikite hapo kidogo. Timu yetu ya Taifa kwa miaka nane mfululizo imekuwa ikifundishwa na kocha ambaye kwenye timu yake binafsi, yaani klabu yake hajawahi chukua ubingwa. Yaani kocha kwenye timu yake anakuwa katika tano za mwisho, lakini anapewa Timu ya Taifa ili ishinde, it is impossible! Haiwezekani! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukitaka kocha mzawa afundishe Timu ya Taifa ni lazima uchukue the best coach. Unampataje? Aliyefanya vizuri kwenye ligi! Sasa kocha amepewa timu, ameshika nafasi ya mwisho au tano mwishoni kwa miaka karibu nane, tisa, kumi; bado kwa sababu ya vyeti vizuri tu, ndiye awe kocha wa Timu ya Taifa; haiwezekani kushinda.

Mheshimiwa Spika, Mwalimu wa timu ya mpira wa miguu kama ni mzawa ni lazima achukuliwe katika makocha waliofanya vizuri na ndiyo maana ni maoni yangu kwamba kijana wetu Mecky Mexime pamoja na kwamba ni kijana mdogo, lakini as of now, ndiye kocha mzawa ambaye kwa miaka minne, mitano mfululizo timu alizoshika amefanya vizuri. Yanga au Simba akichukua ubingwa, anachukua ubingwa akiwa na foreign coach, lakini kocha mzawa anakuwa yeye. Hata akishika utatu, lakini that is the best coach.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba sana Mheshimiwa Waziri afahamu kwamba ni muhimu sana unapo-dedicate team kwa Mwalimu, ni lazima awe ni Mwalimu mwenye good performance. Bahati mbaya sana siyo wakati wote vyeti vinaashiria uwezo na hasa unapoongelea kupima mpira, siyo wakati wote.

Mheshimiwa Spika, ni muhimu niongelee kidogo viwanja vya mpira. Wizara inayosimamia michezo ni vizuri sana ishirikiane na Wizara ya TAMISEMI ili kuona ni jinsi gani wanaweza wakaboresha viwanja vyetu hasa vya shule za sekondari na msingi.

Mheshimiwa Spika, ukienda kwenye Majimbo yetu na Tanzania nzima ni viwanja vichache sana vya shule za sekondari au msingi ambavyo vina vipimo vizuri na ambavyo level yake unasema atapatikana hapa mchezaji mzuri. Viwanja vingi ni vibovu, kwa hiyo, havitoi tafsiri ya kwamba watoto wanaoandaliwa katika viwanja hivi, watakuwa ni wachezaji bora.

Mheshimiwa Spika, ni muhimu sana viwanja vyetu angalau viwe na level ile inayoonesha kwamba watoto wetu watajifunza mpira; na vile vipimo pia vifanane na huko wanakokwenda. Hili likifanyika kwa ushirikiano wa TAMISEMI pamoja na Wizara inayosimamia michezo, itasaidia sana kupika wachezaji ambao ni wazuri.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, unaweza ukakumbuka kwamba wakati amekuja kocha Maximo, yule wa Brazil, moja ya vitu ambavyo vilimsaidia yeye kufanya vizuri ni kwa sababu alipewa ushirikiano mkubwa na Serikali; malipo mazuri. Ndiyo wakati pekee ambapo wachezaji walijifunza hata kulala kwenye hoteli za kitalii au hoteli kubwa kama Golden Tulip kwa mwezi, miezi miwili au mitatu. Hamasa hiyo ilitosha timu hiyo kuipa nafasi ya kufanya vizuri.

Mheshimiwa Spika, ombi langu; ni muhimu sana Wizara ikishakabidhi timu kwa kocha mzawa, vile vile facilities ikiwa ni pamoja na malipo kwa kocha huyo yafanane na makocha wa kigeni ambao tunawaenzi. Mbona inawezekana kuwalipa makocha wa kigeni fedha nyingi? Tunashindwa nini kufanya hivyo hivyo kwa makocha wanapokuwa sio wa kigeni? Hili likifanyika itakuwa muhimu kutia ubani na kutia nguvu kwa makocha wetu kuweza kufanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nisingependa nichukue muda mrefu kwenye hili. Nisisitize tu kwamba Timu yetu ya Taifa na michezo kwa ujumla ndiyo heshima yetu. Bahati mbaya sana mchezo unaopewa heshima kila wakati ni mpira wa miguu. Naomba sana, Wizara ipeleke nguvu pia kwenye michezo mingine. Iko michezo mingine kama michezo ya ngumi ambayo wengine tunaicheza, ni rahisi kufanikiwa kwa sababu michezo yote ambayo inajali uwezo wa mtu binafsi ndiyo michezo rahisi kushinda.

Mheshimiwa Spika, wewe ni mwanamichezo, unafahamu. Mpira wa miguu ndiyo mpira mgumu zaidi katika michezo kwa sababu akikosea mtu mmoja mnafungwa wote. Anakosea mtu mmoja, mnafungwa wote hata kama mmecheza vizuri, lakini mtu mmoja akizembea tu mnahesabika Tanzania mmefungwa; lakini ngumi, ukikosea wewe, unapigwa wewe. Ndiyo michezo mepesi kufundisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, michezo kama table tennis, kwa maana ya singles, ni rahisi! Table tennis ni rahisi, long tennis ni rahisi maana ukikosea wewe unafungwa wewe na ndiyo rahisi kufanikiwa na kushinda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nisije nikaketi bila kukumbuka kuipongeza timu ya Taifa zima kwa jina la Simba Sports Club kwa kazi kubwa ambayo wanafanya ya kufanikiwa kucheza michezo ya Kimataifa kila wanapowakilisha nchi yetu, wamekuwa wakituwakilisha vizuri na hawajawahi kutuangusha. (Makofi)

Mungu ibariki Simba Sports Club na Mungu wabariki wanamichezo wote. Ahsanteni.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizari ya Maji na Umwagiliaji
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Kabla sijaendelea na mchango wangu, ni vizuri nitambue kama Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ya kuimarisha miundombinu Tanzania. Wananchi wa Makete wamenituma niseme ahsante kwa sababu anashughulika na barabara yao ya kutoka Njombe, Makete kwenda Mbeya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, pia nitumie nafasi hii kupongeza uteuzi wa rafiki yangu na mdogo wangu Profesa Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilipokuwa nasoma kitabu hiki, nimerudia chote mara mbili, mara tatu nilishindwa kuamini. Nimeshindwa kuelewa kama Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana ya Maji na Naibu na Wasaidizi wake wanaifahamu Wilaya ya Makete vizuri na mchango wake wa maji kwenye nchi hii. Labda nimkumbushe Mheshimiwa Waziri. Wilaya ya Makete ndiyo inayotoa mto unaoelekea au kumwaga maji Mbarali katika mashamba ya Kapunga yanayolima mpunga pamoja na bonde la Usangu. Ni mto ambao chanzo chake kiko Wilaya ya Makete, Tarafa ya Matamba na Ikuwo. Ni maji hayo hayo yanayokwenda kwenye Hifadhi ya Ruaha, yanatoka Makete.

Mhedhimiwa Naibu Spika, ni maji hayo hayo yana kwenda kwenye bwawa la Mtera. Umeme wa Tanzania unategemea Makete. Ni maji hayo hayo yanabadilishwa jina lake yanaitwa Ruaha Mkuu ambapo eneo la Ruaha Mbuyuni wanalima vitunguu na nyanya, yanatoka Makete. Ni maji hayo hayo yanayotoka Makete yanayokwenda Kilombero na kuzalisha miwa, sukari wanayotumia Watanzania, yanatoka Makete.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile ni maji hayo hayo yanayotoka Makete yanakwenda Rufiji na kubalishwa jina na kuitwa Mto Rufiji. Pamoja na kazi kubwa ya wananchi wa Makete kuachia eneo la kilometa za mraba 465.4 ili angalau Watanzania milioni 8.9 waweze kupata na kutumia maji kutoka Makete, lakini Makete yenyewe haina maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, juzi nilihudhuria kikao cha Makamu wa Rais, pale Iringa ilikuwa bayana kwamba maji yanayotoka Makete yanNufaisha Watanzania milioni 8.9, lakini Tarafa ya Matamba na Ikuwo haina maji. Mheshimiwa Waziri ana ugomvi gani na wananchi wa Makete? Wanafanya kosa kuhama kilometa 465.4 ili waachie vyanzo vya maji ili Watanzania wapone, lakini wao wasipewe maji. Je, ni kosa lao wananchi hawa kuwahurumia Watanzania wengine? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kilimo unachokiona chote kwenye bonde hili ninalolisema mpaka Rufiji, maji yake yanatoka Makete. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri, hebu awe na jicho la huruma. Ni vizuri bajeti yake itambue ya kwamba wananchi wa Makete na hasa Tarafa ya Matamba na Ikuwo wanahitaji maji na ndiyo zawadi pekee atakayowapa. Haiwezekani wao waachie eneo kwa ajili ya maji ya Watanzania wengine, lakini wao wenyewe wasipewe maji. Hivi ni dhambi gani wamefanya wananchi hawa wa Makete? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Tarafa ya Bulongwa, ukiongelea Kata ya Kipagalo, Luhumbu na Bulongwa yenyewe, nenda Kata ya Vijiji vya Tanala, Mang’oto, Mbarache, Kigala na Mfumbi maji hakuna, lakini wameachia eneo.

Mheshimiwa Naibu Spika, unafahamu kilometa hizi ninazozisema sehemu nyingine ni Jimbo zima. Kilometa za mraba 465 Makete halikaliwi na mtu wameacha ili Tanzania ipate kuneemeka, Tanzania iwe na maji mengi. Juzi wakati Waziri Mkuu alipofanya ziara pale Makete, aliambiwa kwamba tatizo, kuna mradi wa maji ambao Wizara ya Maji ilisimamia pale na ikaufanya vibaya mradi ule. Kwa hiyo, umepelekea Vijiji vya Kinyika, Matamba, Mlondwe na Itundu kukosa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, huo ni mradi uliosimamiwa na Wizara siyo wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete. Waziri Mkuu aliahidi wananchi wa Makete ya kwamba atamtuma Waziri mwenye dhamana aende autembelee mradi ule ili asahihishe makosa ambao Wizara yake ilifanya. Mpaka hivi ninavyoongea, rafiki yangu, kaka yangu Mheshimiwa Engineer Lwenge, Mheshimiwa Waziri hajafika Makete. Naamini ujasiri wake, natambua uwezo wake, najua ataitembelea Makete.

Naomba sana, awakumbuke wananchi wa Makete kwa sababu ya kazi yao nzuri ya kutunza vyanzo vya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, unafahamu, leo hii tunapoongelea vyanzo vya maji, ni vigumu sana kupata eneo ambalo linazalisha maji kwa wingi kama Makete, sijui kama lipo. Ndiyo maana marefu ya mto wote huu angalau leo Watanzania mnajua sasa kwamba kimsingi mto huo asili yake ni Makete.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja za wenzangu ambao wanasisitiza umuhimu wa bajeti hii kuongezwa na hasa shilingi 50 inayosemwa kwa lita ya mafuta, ni muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vitu vingine vyote siyo watu wote wanavitaka, lakini unapoongelea maji ni kila mtu. Ndiyo maana tukaja na sentensi inayosema, “maji ni uhai” kwa sababu bila maji, hakuna uhai. Huwezi kula bila maji, huwezi kufanya chochote bila maji, ndiyo maana ni muhimu sana bajeti ya maji ipate kuongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nafahamu Mheshimiwa Waziri atakaposimama atalijulisha Bunge Tukufu kwamba hitimisho lake kwenye bajeti yake anaonesha shilingi bilioni 672, lakini ni vizuri asome pia ukurasa wa 173 katika hotuba yake, unaoeleza fedha za kutoka India dola milioni 103 ambazo ni sawa na trilioni 1.1 kwamba: Je, zimo kwenye bajeti au la! Kama zimo, basi bajeti ya maji itakuwa ni shilingi trilioni 1.762 na siyo bilioni 672.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri atakaposimama ni vizuri kutoa ufafanuzi ili kulifanya Bunge lielewe kwa usahihi kwamba shilingi milioni 503.04 iliyopo ukurasa wa 173 kwenye hotuba yake, je, imejumuishwa kwenye bajeti au la.

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Kwanza kabisa nianze kuishukuru Serikali yangu ya CCM kwa kuendeleza elimu katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haraka haraka nichangie mambo machache yafuatayo. Ukisoma hotuba ya Waziri wa Elimu na jitihada zetu zote za elimu inaonesha kupelekea kuimarisha au kutengeneza kitu kinaitwa quality education lakini bila kuangalia sana relevance of the education system. Niiombe sana Serikali yangu, tatizo tulilonalo Tanzania na nchi nyingi za kiafrika sio issue ya quality education tu, ni elimu stahiki kwa kiwango gani elimu inawezesha kupambana na mazingira tuliyonayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, wote tunajua Tanzania 77% ya wananchi wetu ni agricultural population kwa hiyo ungetegemea shule ya msingi na sekondari zifasili kilimo, ungetegemea shule za sekondari na msingi yaani basic education zi-articulate hiyo, zibebe mzigo huo wa changamoto ya kilimo lakini haiko hivyo. Mwanafunzi anaanza darasa la kwanza mpaka anafika form six hajakutana na kilimo lakini akimaliza form six tunamtaka aende akalime haiwezekani, haiwezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pendekezo langu ni moja. Ni muhimu sana masomo ya darasa la kwanza mpaka kidato cha nne yawe yamebeba elementary education ya kilimo yaani unatumiaje mbolea ya UREA, DAP, Minjingu, unalimaje mahindi, kahawa, korosho na mazao mengineyo. Turidhike mwanafunzi akiishia kidato cha nne atakuwa amepata elimu inayomtosha yeye kujiajiri ili wanaoenda vyuo vikuu wawe ni wale tu wanaostahili kwenda vyuo vikuu, sio kulazimisha kutanua wigo hata wale ambao hawajafaulu kwa kukidhi viwango vya vyuo vikuu tushushe alama za kuingia chuo kikuu ili tu watu wengi waende, tutakuwa tunapoteza rasilimali za Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niiombe Serikali yangu ilione jambo la vyuo vikuu binafsi. Vyuo vikuu binafsi kwa mujibu wa ownership ni private institutions lakini establishment yake ni public instutions. Ni sera ya Serikali ndiyo iliyoanzisha vyuo vikuu binafsi. Ni kwa nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, unafahamu vizuri na Waziri anafahamu vizuri Serikali ya Awamu ya Tatu na ya Nne ndiyo waliopelekea kuanzisha vyuo vikuu binafsi kwa sababu tulipoanzisha shule za sekondari za kata swali likaja watakapomaliza wataenda wapi, tukafungua utaratibu wa kuanzisha vyuo vikuu binafsi. Niiombe sana Serikali yetu hasa TCU kupeleka wanafunzi kwenye vyuo vikuu binafsi sawa na vyuo vikuu vya umma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wengi nadhani hawajui vizuri, ni lazima tufahamu hata wakuu wa vyuo vikuu binafsi wametokana ama na Chuo Kikuu Dar es Salaam ama Sokoine ama Mzumbe. Kwa hiyo, elimu inayotolewa kwenye vyuo vikuu binafsi ni sawa kabisa na inayotolewa kwenye vyuo vikuu vya umma. Naomba sana tusivitizame vyuo vikuu binafsi kama vile vipo vipo tu au kama vimejileta tu hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo naomba fedha za mishahara zinazokatwa kwa walimu wa vyuo vikuu binafsi kwenda kuchangia Loan Board na contribution zingine zote wanazotozwa vyuo vikuu binafsi ziondolewe. Treatment ya vyuo vikuu binafsi iwe sawa na treatment ya vyuo vikuu vya umma. Ni jambo la muhimu sana kwa sababu vyuo vikuu binafsi ndivyo vinavyopelekea kutengeneza ajira kwa watu wetu, lakini pia vinakidhi haja ya kuhakikisha kwamba watoto wetu wanapata maeneo ya kusoma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichangie kwenye entry qualification na hasa kwa walimu wa vyuo vikuu. Ukisoma maelekezo ya TCU ili uingie kuwa mwalimu kwa vyuo vikuu kwa kawaida ni lazima uwe ama na first class or upper second ya GPA kati ya 3.6 or above. Naomba sana TCU mkumbuke kabisa kwamba kwa wale waliosoma zamani hasa walio-graduate vyuo vikuu miaka ya 90 au nyuma kidogo, darasa tulikuwa tunakuwa wanafunzi 60 au 30 lakini first class anakuwa mwanafunzi mmoja au wawili ndiyo tulivyokuwa tunafaulu hivyo. Tumefaulu ni mwanafunzi mmoja ni kwa first class, upper second, good upper second, lakini kuna watu ambao baada ya kumaliza wamekwenda kwenye field.

Mheshimiwa Mwenyekiti, an engineer ambaye ame-graduate kwa lower second Chuo Kikuu Dar es Salaam huyu ni civil engineer akaenda ku-practice 10 years anaporudi kutaka kufundisha sasa ameshapata degree yake ya uzamili (master degree) bado unamtaka awe na 3.6 GPA, unasahau added value aliyo-accrue kwenye ku-practice engineering inamzidi aliyeko chuoni. Ndiyo maana naomba sana TCU pamoja na kuweka hivyo vigezo wekeni dirisha la watu wale wenye sifa za ziada walio-practice ili kuwa sasa na walimu ambao si tu wamejikita kwenye kufundisha theory lakini wanaweza kufundisha theory na practice kwa sababu kwanza wame-practice.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hili litakuwa muhimu sana kwa sababu hivi tunavyosema inakuwa ni mtihani mkubwa pale ambapo mwalimu amemaliza degree ya kwanza, akamaliza master degree na degree ya uzamivu akiwa shuleni, kwa hiyo, yeye ni master of a school. Sasa ni muhimu sana ku-recruit Walimu ambao wako nje ya mfumo wa vyuo vikuu ambao wame-practice kwenye field hizo ili waweze kuwafundisha wanafunzi wetu elimu ambayo ni ya vitendo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiongelea hiyo relevance of education, niombe sana ni vizuri primary education kama wenzetu wa Kenya walivyo tutoke darasa la kwanza mpaka la nane sio six years. Kwa sababu lengo letu ni lazima u- manage kati ya wanao-graduate na your ability to employ those people. Mfumo wa elimu uliopo sasa hivi wote sisi shahada zetu zimejikita kwenye kuajiriwa sio kujiajiri. Ndiyo maana ni vizuri Mheshimiwa Waziri aelekeze vyuo vikuu vitoe au vitengeneze mitaala yenye kutosha wanafunzi kujiajiri. Hapa tulivyo hata waki-graduate watu 100,000 what next? Serikali haina uwezo wa kuajiri na degree zetu si za kujiajiri ni za kuajiriwa. Tusipobadilisha hili tutakuwa na graduates ambao hawalisaidiii Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kwa kifupi kidogo kuhusu wanafunzi wanaopata mimba. Nisikitike kidogo, maana yake najiuliza kidogo, sasa hivi ilivyo ni kwamba mwanangu mie ambaye anasoma sekondari akipata mimba yuko form one, form two, form three anaachishwa shule, lakini kama mimi baba yake nadhani kwamba bado anahitaji kusoma nitampeleka kwenye shule ya private ninayotaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huo mfumo upo. Maana yake majadiliano mengi ni kama vile mfumo huo haupo aah upo. Binti yako amepata mimba anaachishwa shule lakini akiishalea mtoto ukitaka mpeleke form one shule nyingine ni ruksa, ukitaka mpeleke kwenye mfumo mwingine wa elimu ni ruksa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu nataka tutazame vizuri, ukiangalia tatizo la mimba kwa mfano primary education mwaka jana kwa maana ya taarifa ya BEST ni wanafunzi 251 kwenye lakini utoro ni 82,850, sasa Wabunge wengi tunajikita kwenye kuangalia 251 vis-a-vis 100,000. Ni vizuri ifahamike vizuri, hivi mwanafunzi wa miaka 12 tunamlea kwa do not au kwa counseling. Maana yake mwanafunzi ukimwambia mwanangu ukipata mimba aah unaendelea na shule, the yes kwenye mapenzi zitakuwa nyingi kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana mimi nasema wale wanaowapa mimba wanafunzi wapewe adhabu kali mbali na miaka 30 wapewe jukumu la kuhakikisha hatma ya elimu ya huyo aliyepewa mimba. Sheria iweke clearly kwamba you shall be responsible on the fate of that girl including handover yake ya education. Maana watoto hawa ni wadogo, kwa hiyo ukifungua paradox seriously utaingia darasani kufundisha watoto thelathini wana mimba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Kabla sijaendelea nichukue nafasi hii angalau kwa dakika moja kuendelea kumshukuru Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayofanya ya kuiendeleza Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie mambo machache kwa haraka haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri Waziri afahamu kwamba ili uendeleze kilimo na ufugaji ni vizuri Hazina (treasurers) za Serikali na hasa mashamba maalumu yaliyotengwa kwa ajil ya ufugaji ya Serikali yatumike ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais wetu mstaafu baba wa Taifa hili Mwalimu Nyerere pamoja na mzee Karume mwaka 1965 walikaa kutafakari na kuona ni jinsi gani wataondoa ugomvi kati ya wakulima na wafugaji, ndipo wakaja na wazo la kusema ni lazima mashamba ya mifugo yaanzishwe ili wanaochunga ngo’mbe wajifunze kufuga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inasikitisha sana hawa wazee, wameshalala wametangulia mbele za haki, lakini bado hekima zao na akili zao zinaonekana ziko juu sana ya upeo wetu leo. Kwa mfano Shamba la Kitulo ambalo liko Makete uwezo wake ni kuchukua ng’ombe 4,500 sasa hivi wako ng’ombe 750 tutawezaje, tutawezeshaje wananchi wa Tanzania kufuga ng’ombe na kupata maziwa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Mifugo aliyepita Mheshimiwa Mwigulu Nchemba alitembelea Wilaya ya Makete akabaini hazina kubwa iliyopo pale, akaridhika kwamba ni muhimu sana zitafutwe bilioni 7.6 ili shamba lile liweze kufufuliwa ili Watanzania kutoka kaskazini na pande zote za Tanzania waweze kujifunza namna ya kufuga, tuondoe ugomvi wa kuswaga ng’ombe. Mpaka leo hivi ninavyoongea Waziri hajaenda tena kuweza kujibu hoja hii ya wananchi wa Makete kwamba ni lini hao ng’ombe watakwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji aliposimama hapa kwenye mada yake alisisitiza kwamba ng’ombe 3,000 wameagizwa kutoka nje, mpaka leo hao ng’ombe hawajaenda Kitulo. Kwa hiyo hazina ile inapotea wakati ingeweza kujibu haja ya migogoro ya wakulima lakini pia ingeweza kuboresha uchumi wa Watanzania wala si Makate peke yake, ni Watanzania wote; maana wangejifunza kule namna ya kufuga wangepata maziwa, wangepata ajira, afya zingeboreshwa na uchumi ungeboreshwa pia. Ni muhimu sana Wizara izingatie hili ili kuendeleza uchumi wetu lakini pia kuboresha mifugo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, iko shida ya kufasili namna bora ya kuboresha kilimo chetu. Soko limeachwa kwa wakulima ambao weledi wao uko kwenye kulima na hauko kwenye masoko. Niiombe sana Wizara, Mheshimiwa Waziri Wizara yake ni muhimu kabisa ijikite kwenye kutafuta, la kwanza masoko, ili mkulima anapolima awe na uhakika wa bei atakayouza, siyo ilimradi kuuza lakini bei atakayouza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo la pili, ni vizuri Mheshimiwa Waziri ajikite kwenye kutafuta mbegu bora. Pale Makete na Njombe nzima tunalima sana viazi, lakini leo viazi tunavyolima havina soko kwa sababu viazi vinavyozalishwa nchi jirani ya Kenya vinauzwa kwa bei ndogo Sh.50,000/=, wakati sisi uzalishaji bei ya chini ya uzalishaji ni Sh.80,000/=. Kwa sababu hiyo kwa vyote vile tukitaka kuuza hivyo lazima tuuze kwa bei ya hasara. Tatizo haliko Kenya, tatizo liko kwetu, kwamba Wizara inafanya nini kutoa majibu ya mbegu bora ili wakulima wetu wa viazi, watumie mbegu bora hatimaye wapate viazi vingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilifurahi sana rafiki yangu Mhandisi Tizeba alipoteuliwa kushika Wizara hii. Nilifurahi kwa sababu kwanza yeye ni mkulima, hata kama yeye ana fani ya uhandisi lakini ni mkulima, naamini ataitendea haki Wizara hii; kwa sababu hatusemi vitu ambavyo ni vya nadharia kwake yeye anavi-practice, analima, anajua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe sana rafiki yangu Mheshimiwa Tizeba apeleke nguvu kwenye kutafuta mbegu bora za viazi, pareto na mazao mengineyo, tukifanya hivi tutaharakisha maendeleo ya nchi yetu na hasa kwenye eneo la ukulima bora; vinginevyo wakulima wetu wataendelea kulaumu sana Serikali ya Chama cha Mapinduzi, watadhani kwamba tunazembea. Sasa mtu mmoja akizembea ni vizuri sana ajue kwamba ni yeye aliyezembea. Nami naamini

Mheshimiwa Waziri si mzembe, kwa vyovyote vile atafanya jitihada ili kuhakikisha kwamba analigeuza hili jambo ili kwamba mbegu bora zipatikane na wakulima wapate kulima vizuri na twende mbele zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zao la pareto ni moja ya mazao ambayo miaka ya 80 Wilaya ya Makete ilikuwa inaongoza kwa zao la pareto. Likapoteza mwelekeo kwa hiyo bei yake ikashuka. Sasa hivi angalau bei ya pareto inarudi, niombe sana Wizara, kama nilivyosema awali isipuuze soko kuachia wakulima, hawa ni wakulima wa kawaida weledi wao ni wa kawaida, hawana weledi wa kutafuta masoko. Niombe sana Mheshimiwa Waziri aichungulie Makete ili aweze kuona ni jinsi gani ataharakisha kazi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nihitimishe mchango wangu mfupi kwa kusema kwamba kama Mheshimiwa Waziri atakapokuja kuhitimisha hatasema neno kuhusu jinsi ya kulifufua shamba la Kitulo ili wananchi wale waone faida ya kuachia hekta 12,000, kama asipokuja na majibu hakika nitashika shilingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, anafahamu rafiki yangu, sina jinsi ya kushawishika isipokuwa atoe majibu jinsi ya kuwafanya wananchi wa Makete ambao wamenituma kwenye Bunge hili waone faida ya kutunza eneo hilo na waone faida ya ng’ombe hao kuwa wamesambaa kwenye kata zote 23 za Wilaya ya Makete.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, Mungu Ibariki sana Serikali ya CCM, siungi mkono hoja mpaka atakapotoa majibu. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwanza kwa kuwapongeza Mawaziri wenye dhamana, dada yangu Mheshimiwa Ummy pamoja na rafiki yangu Mheshimiwa Dkt. Ndugulile, kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kwenye Wizara hii. Katika kufasili kwa usahihi matamshi na matarajio ya Rais wetu waliweza kuandaa kongamano au mkutano kwa ajili ya kupata wawekezaji tarehe 4 Aprili ambapo na mimi nilihudhuria, nawapongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa haraka, jambo la kwanza, pamoja na jitihada nzuri za Serikali za kununua vifaa na hasa Hospitali zetu za Muhimbili pamoja na Mloganzila, naomba sana Serikali ijikite kusomesha madaktari hawa nje ya nchi, nasisitiza Madaktari Bingwa wasome nje ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi ya India kwa mfano na Hospitali zake za Apollo, idadi kubwa ya madaktari wake, actually asilimia 94 ya madaktari ambao tunawaona kwenye Hospitali za Apollo India, hawajasoma India. Kwa hiyo, ni muhimu sana na sisi tujenge uwezo kwa kufanya hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, ninaomba sana, pamoja na kwamba Serikali inaweza ikapata shida kwenye taulo za kike, lakini utafiti uliofanywa kwenye Wilaya ya Makete wanafunzi wa Wilaya ya Makete hasa darasa la sita na la saba na sekondari wengi wao ni yatima kwa sababu orphanage rate kwa maana ya Tanzania hii Makete tunaongoza. Wanahitaji kuangaliwa kipekee ili taulo za kike waweze kupewa watoto hawa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu vituo vya afya; ninaipongeza Serikali kwa kazi nzuri ya vituo vya afya, lakini naomba sana Wilaya zile ikiwemo Makete, ambazo zina mtandao wa barabara au wa eneo kubwa zipewe upendeleo wa vituo vya afya. Kwa mfano, Tarafa ya Ukwama inahitaji kituo cha afya na gari la wagonjwa, Tarafa ya Bulongwa, vivyo hivyo Tarafa ya Ikuo, kitu cha afya na ambulance, kwa sababu inachukua karibu kilometa 105 kutoka kwenye kata hizi kwenda Makao Makuu ya Wilaya. Jambo hili likifanyika mtakuwa mmefasili kwa usahihi matatizo wanayoyapata wananchi wa Wilaya ya Makete na Watanzania wengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, itoshe kusema tu kwamba kazi nzuri inayoendelea kufanywa sasa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi ya kuendelea kuongeza bajeti Wizara ya Afya ni kazi kubwa na nzuri ambayo wananchi wa Makete tutaendelea kuiunga mkono kwa nguvu zote. Na kwa hili, kipekee kabisa nimpongeze sana Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na timu ya wasaidizi wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo naomba niongelee kidogo Hospitali ya Misheni ya Ikonda. Makete tunayo Hospitali ya Ikonda, hospitali hii inahudumia mikoa takribani nane lakini Serikali inapaswa kutia jicho la kipekee na kuwapa ahueni na hasa malipo ya Madaktari Maalum ambao wanatoka Ujerumani na Italia kwa ajili ya kwenda kuhudumia wananchi wa Wilaya ya Makete na Watanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hili, tumeandika barua mara nyingi kwa maana ya Hospitali ya Ikonda na mimi kama mwakilishi wao kwa Waziri kuomba favour na hasa ya madaktari hao, wasiwe wanatozwa fedha kwa sababu wanakuja kuhudumia Watanzania hawa na kwa kweli hata malipo yanayotozwa Watanzania kwenye hospitali hii ni malipo madogo sana. Niombe sana Waziri aweze kuiangalia Hospitali ya Ikonda ya Misheni kwa jicho la kipekee ili kuendelea kuwasaidia Watanzania zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia umealikwa Mheshimiwa Waziri ili utembelee Hospitali ya Ikonda ukajionee mwenyewe. Pale tuna kituo kikubwa cha viungo bandia ambavyo huwezi kupata eneo lingine lolote Tanzania hii, tunaomba sana utenge muda utembelee ili uone shida za wananchi wa Makete.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, ninaunga mkono hoja, Mungu ibariki Serikali ya CCM.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Spika, naomba sana ahadi ya barabara ya kutoka Njombe – Makete - Mbeya ifanyike. Kutoka Makete ni barabara ya kutoka Makete - Bulongwa – Mbeya na Makete- Ivalalila - Ujuni kuunganisha barabara ya kutoka Bulongwa.

Mheshimiwa Spika, pia kwa ajili ya kuwezesha Hifadhi ya Kitulo ni muhimu barabara ya kutoka Chimale- Matemba au Mfumbi kuja Matamba ijengwe kwa lami. Pia ili kuboresha ujenzi wa barabara za Ludewa, Kipengele- Mbalache - Lupila kwenda Ludewa ijengwe kwa lami.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mawasiliano Kata za Mang’ota, Ikuwo, Kigala, Lupila na Ukwama zipewe mawasiliano ya Voda, Airtel, Halotel na Tigo. Hili likifanyika litasaidia sana kutupa mawasiliano.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sekunde tano nimpongeze sana Waziri na wasaidizi wake wote kwa kazi nzuri wanayofanya lakini harakaharaka niende kwenye Wilaya ya Makete.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kazi nzuri ambayo Wizara inafanya niombe sana Mheshimiwa Waziri kwenye shule ya sekondari ya Iwawa majengo yamechakaa sana na barua zimekuja kwako ambapo karibu shilingi bilioni 2.6 zinahitajika ili kuweka sawa shule ile. Ikumbukwe shule ile ilikuwa ya kwanza kimkoa wa Njombe na ni shule ya Serikali, ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia shule ya sekondari ya Lupila, ni A-Level, chondechonde uikumbuke. Shule ya sekondari ya Kipagalo uikumbuke na shule ya sekondari ya Ikuo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo niseme tu kwa ufupi. Tumekuwa tukijadili sana kuhusu elimu na ubora wa elimu. Kabla sijachangia, nihoji maswali mawili au matatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu bora ni ile ambayo inatoa majibu ya matatizo tuliyonayo katika nchi au katika jamii, ndiyo elimu bora na siyo vinginevyo. Swali linakuja, je, elimu tuliyonayo leo kutoka darasa la kwanza mpaka vyuo vikuu inafasili matatizo ya Watanzania? Maana nguvu ya Watanzania ni kilimo, uvuvi na ufugaji lakini toka darasa la kwanza mpaka vyuo vikuu hakuna mahali ambapo elimu hiyo inatiliwa mkazo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa lugha nyingine hata kama wanafunzi wa kidato cha nne wote Tanzania wangekuwa daraja la kwanza kwa ufaulu, kidato cha sita wakapata daraja la kwanza na vyuo vikuu wakapata daraja la kwanza, kwa maana ya first class, utawapeleka wapi? What next? Hawawezi kujiajiri na hawawezi kuajiriwa. Kwa hiyo, hoja leo si suala la quality education as far as our education system is concerned, ni issue ya relevance of education system. Elimu tuliyonayo ni irrelevant, kwa nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu mwanafunzi wa kidato cha nne hakuna anachoweza kufanya, kidato cha sita hakuna anachoweza kufanya, hata tukimpa wa shahada ya kwanza hakuna anachoweza kufanya. Ndiyo maana ninapandekeza lazima tufanye overhaul of education system. Tutengeneze masomo kuanzia darasa la kwanza mpaka hilo la saba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ninashauri darasa la kwanza liende mpaka darasa la nane, kwa nini? Kwa sababu masomo ya darasa la sita na la saba kwa kiasi kikubwa ndiyo yanayosomwa form one na form two, isipokuwa ni lugha inabadilika. Tukienda darasa la kwanza mpaka la nane tuende sasa darasa la tisa mpaka la kumi na mbili inaishia hapo, tunaondoa five na six. Sababu ya kuondoa five na six ni kwa sababu hakuna uhusiano wa masomo ya kidato cha tano na sita na degree yoyote ndani ya nchi yetu. Ukimchukua leo mwanafunzi wa kidato cha nne ukampeleka kuanza degree ya kwanza atafanya vizuri tu, mkitaka jaribuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili haraka haraka ni la lugha. Jamani Mheshimiwa Mwenyekiti na Wabunge wenzangu ni vizuri mfahamu kiswahili, kiingereza, kireno, kijerumani ni lugha ambazo tumeamua kuzifuata kwa sababu ya kutawaliwa. Hakuna mtu ambaye amezaliwa
kabila lake wanaongea kiswahili au kiingereza ama kireno ama kifaransa. Kama mwalimu Nyerere na wenzake wangeamua Tanzania tuongee Kingereza tungekuwa tunaongea kiingereza hivi hivi na tungekuwa tunajivunia kwamba ni lugha yetu. Kwa hiyo, kiswahili siyo lugha ya kwetu ni lugha iliyotokana na kutawaliwa na waarabu, sawasawa na kiingereza, kireno na kifaransa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali la kujiuliza, je, hawa watawala wetu walifanya uchaguzi wa maana? Kwa sababu kiswahili as of today nchi hazizidi nne zinazoongea Kiswahili kwa ufasaha lakini kiingereza Afrika peke yake ni nchi 25, kihispaniola ni nchi zaidi ya hizo. Kwa hiyo, ni wajibu wetu sasa kufikiri kwa usahihi kwamba walimu wanaomaliza vyuo vikuu wapewe dossier ya kufundisha primary schools ili walimu wenye shahada waanzie shule za msingi kufundisha Kiingereza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi natoka Makete, baba yangu ni Mahanji mama yangu ni Mkinga, kwa hiyo, naongea kwa ufasaha kikinga na kimahanji. Naongea kwa ufasaha pia kimagoma, kiwanji, kibena, kikisi kwa sababu ndio makabila yanayopatikana Makete. Je, kwa kujua kiswahili ambayo ni lugha mpya, nimeweza kuharibu lugha yangu ya baba na mama? The answer is no. Kiswahili hakijaharibu kimahanji, kikinga, kimagoma changu na Wabena, Wasukuma na Wachaga vivyohivyo. Kwa hiyo, kujua kiingereza hakuharibu kiswahili chako bali kinakuongezea nguvu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nilikuwa kwenye mkutano pale Dubai, mimi ni Financial Advicer. Pale Dubai kuna madereva 12,000 kati ya hao wanaoendesha tax, 2,700 ni Wakenya, sababu wanajua lugha. Sisi kwetu tunawa- barred, tunawa-deter madereva wetu kwa sababu ya lugha, lugha is a problem. Kwa dunia ya sasa ukiwa conversant na lugha nyingi ni mtaji.

Mheshimiwa Mwneyekiti, kwa hiyo, niombe sana mliangalie hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haraka haraka niende kwenye elimu ya juu. Naomba sana fedha zinazopelekwa COSTECH kwa maana ya Tume ya Sayansi zioanishwe na shahada za uzamili na uzamivu kwenye vyuo vikuu. Kwa lugha nyingine Serikali i-identify maeneo ambayo wanataka kufanya utafiti COSTECH wa execute hiyo programu, vyuo vikuu vya private na vya Serikali viombe ili mtu akifanya utafiti wake anaisaidia Serikali kupata majibu ya maeneo wanayotaka lakini wakati huohuo unaongeza idadi ya shahada za uzamivu na uzamili ili twende kwa pamoja. Tukifanya hivyo, tutaongeza sana idadi ya wanazuoni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa TCU, tusipoangalia itakuwa ni tume ya chuo fulani kimoja kwa nature ya waajiriwa wake. Niombe sana viongozi wa TCU ni lazima wawe na weledi hiyo moja na wawe wamesoma vyuo mbalimbali ili akiwa pale asitizame chuo kimoja. Pili, awe pia amefundisha vyuo mbalimbali ili pia awe na weledi wa anachotaka kusukuma vinginevyo itakuwa ni Tume ya Vyuo Vikuu lakini kwa kweli inayokuwa dictated na chuo kimoja, itakuwa ni mbaya sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo TCU waongoze weledi na hasa kwenye kutambua watu wanaomaliza shahada kwenye nchi zilizoendelea. Watoto wetu wanapomaliza vyuo vikuu vya nje…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Kwanza naishukuru Serikali ya CCM na Waziri wa Viwanda na Biashara kwa kazi kubwa waliyonayo mbele yao, lakini pia kwa kazi kubwa ambayo wanafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie tu kidogo, jambo tunalojadili ni muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu; viwanda na biashara. Lakini duniani kote viwanda, biashara na uwekezaji ukiwemo ndani yake cha kwanza kabisa ni lazima mwekezaji awe anaamini kwamba wewe Serikali unamtazama yeye kama ni muhimu. Perception on investors lazima iwe very very positive.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa lugha rahisi ni kwamba lazima Mheshimiwa Mwijage rafiki yangu na wenzake wakiona watu wana fedha nyingi kwenye akaunti zao, wafurahie. Lazima wafurahie, ndiyo dunia ilivyo. Ni vizuri pia tufahamu mitego ya uchumi na biashara tunayosoma vyuoni na vile tunavyo-practice, mara nyingi havioani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii hata wewe mwenyewe ukiwa na shilingi trilioni moja, uka-deposit kwenye akaunti za US au Switzerland hakuna atakayekunyooshea mkono kwamba hii ni money laundering, lakini ukizitoa kwenye uchumi mkubwa ukazileta Tanzania, utaambiwa hela chafu. Nchi changa ni wajibu zijifunze juu ya mtizamo hii. Tukiweka fedha kwenye nchi zilizoendelea, hatuambiwi hela chafu, ukizitoa hizo hizo ulizoweka kwao, ukizileta Tanzania ni hela chafu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda pale Mexico wanalima dawa za kulevya, ukienda China wanalima dawa za kulevya, ukienda Afghanistan wanalima dawa za kulevya na ukienda Colombia wanalima dawa za kulevya. Wakubwa wa dunia hii huoni wanagombana na mataifa hayo juu ya dawa za kulevya. Nini tunajifunza? Maana yake uchumi na menejimenti ya uchumi na biashara duniani ni tricky, lazima ufikiri mara mbili kama unataka uwekezaji ukue.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naiomba sana Serikali kwa wawekezaji wenye fedha nyingi tuwaelekeze kwa kuwekeza, kwa sababu namna ya kupata fedha kwenye dunia hii ziko nyingi, ni ngumu hata kuzieleza. Siyo linearly, yaani ukichukua mtazamo wa linearity kwenye kutazama biashara, uta-fail kwa sababu biashara haiko hivyo, ina vitu vingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wako watu hapa, tupo ambao msingi wa fedha zetu ni commission kwa sababu ni consultancy. Mzee Chenge pale Mwenyekiti yule, nguvu yake kubwa ni Mwanasheria mbobezi wa muda mrefu, kwa vyovyote vile anaheshimika ndani na nje ya Tanzania. Fedha zake za consultancy huwezi hata kuzitaja, lakini kama Mtanzania akijua kwamba akiweka fedha zake kwenye akaunti za Tanzania atahojiwa, hataweka, ataweka Kenya na kwingineko. Maana yake ni nini? Kutakuwa na homa ya uwekezaji na watu kuikimbia Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, chonde chonde namwomba rafiki yangu Mheshimiwa Mwijage, watu wakizileta fedha, tuhoji sana matumizi yake. Tukiona wameingiza fedha kutaka kuiangusha Serikali yetu, tuhoji. Ila fedha zikiingia, tuwaelekeze, wekeza kwenye minofu ya samaki, wekeza kwenye kiwanda hiki, wekeza kwenye kiwanda kile, ndiyo uchumi wa dunia ulivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie kidogo kuhusu Mchuchuma na Liganga. Chuma dunia nzima sasa uzalishwaji wake unapungua sana. China, Australia na USA ndiyo magwiji wa uzalishaji wa chuma. Mtaji tulionao wa chuma Liganga na Mchuchuma hakuna mradi; naomba niweke vizuri, hakuna mradi tulionao wa Tanzania leo ambao una uhakika wa fedha kwa maana ya kurudisha fedha kama Liganga na Mchuchuma. Bila kuuma maneno kabisa, hatuna project yoyote ya uwekezaji Tanzania ambayo inazidi mradi wa Liganga na Mchuchuma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwangu mimi naelewa hata ilipotengwa shilingi bilioni 13 kwa ajili ya compensation, who is going to be paid? Ni Mtanzania. Let them be paid. Nashangaa Wabunge wanahoji juu ya mtu wa Ludewa kulipwa fidia. Akilipwa mtu wa Ludewa, sana sana anawekeza Ludewa, Songea na Mwanza. Hakuna shida na hilo. You don’t upper the economy kwa ku-shift fedha kutoka BoT au Hazina kupeleka kwenye mifuko ya Mheshimiwa Mwijage anayowekeza Mwanza. Hakuna deterioration ya economy kwenye hilo. Is just good, ni jambo zuri kufanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sana Liganga na Mchuchuma ipewe kipaumbele chake, lakini tukisema hivyo ndiyo maana tunasikia hadithi kwamba mafuta yamefika bandarini, I keep on wondering kwamba mtu anahoji kwamba point of origin hakuna documents. Serikali hupati chochote kwa declaration ya point of origin. Mwisho wa siku Mheshimiwa Mwijage wewe unachopata ni kodi. Kwa nini unauliza kama mafuta yametoka mbinguni au yametoka Kenya? Mafuta yameshafika bandarini, piga kodi, pata pato lako leta mafuta Tanzania. Simple as that. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unafahamu leo Tanzanite Kenya ni ya pili duniani, kwani Mheshimiwa Uhuru Kenyatta anahoji Tanzanite mnatoa wapi? Anauza, anapata kodi yake anaendelea na kujenga uchumi wake. India wanaongoza kwa kuuza Tanzanite, Rais na machinery ya India haihoji Tanzanite mnapata wapi? Siyo kazi yao. Ninyi pigeni kodi, leteni mafuta, kwa sababu sisi tunapata mafuta kwenye kodi, siyo kwenye documentation. Documentation hatusemi ni mbaya, zinakusaidia ku-facilitate upate kodi inayostahiki, siyo ikuzuie sasa kupata hata hela. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukishakalisha mafuta bandarini ni wazi yakija mtaani huku bei yake itakuwa kubwa. Kwa hiyo, tutazidi kuumiza wafanyabiashara na sisi wenyewe kujiumiza na Serikali kuiumiza. Kwa hiyo, lazima tuwe na correct perception jinsi ya kufanya tunavyoweza kufanya ili kuongeza uchumi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nampongeza sana Mheshimiwa Mwijage, niseme naomba sana aunde Kamati ya kumsaidia kwenye Wizara yake. Kamati ile siyo sisi, wafanyabiashara wamsaidie kufikiri namna bora ya kuwekeza. Mungu akubariki sana Mheshimiwa Mwijage. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumpongeza Waziri pamoja na Naibu Waziri kwa Mpango mzuri waliouleta. Hawa ni rafiki zangu na wameleta Mpango mzuri sana, nawapongeza sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, nampongeza sana Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri ambayo imemfanya apate sifa Afrika na dunia nzima ya kuekeleza na kusimamia mipango ya maendeleo yetu wenyewe kwa fedha zetu wenyewe. Mipango ya ujenzi wa bandari, viwanja vya ndege, maji Mtwara na mipango mingi mizuri inayofanywa na Rais wetu, inampa sifa na heshimia duniani kote. Mungu ambariki sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichangie kidogo maeneo machache. Unapoongelea kukuza Pato la Taifa ni vizuri kuangalia katika sura mbili. Sura ya kwanza ni ile inayomgusa mtu mwenyewe mmoja mmoja, fedha inayomgusa mtu mmoja mmoja. Kwa hiyo, naomba sana kwenye eneo hili, benki zetu hizi za kilimo kama Tanzania Investment Bank tuweke riba ndogo sana kwa wakopaji wanaomaanisha kwenda kuwekeza kwenye kilimo angalau asilimia 10 lakini sio 17 au 19, haifai kwa sababu ni kilimo. Kwa hiyo, naomba sana wawekezaji wa kilimo wanapokwenda kukopa Tanzania Investment Bank wakope kwa asilimia angalau 10. Tukifanya hivyo basi tutaona maparachichi yakipandwa kwa wingi kule kwetu Makete, Rungwe na kila sehemu yatapandwa kwa wingi kwa sababu ukopaji utakuwa umerahisishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni dhahabu yetu. Kwa sisi wachimbaji wadogo wa dhahabu ni vizuri sana Geological Survey Institute inayoongozwa na Profesa Mruma ikapewa fedha kwenda kufanya explosion test ili tuwe na uokaji wa dhahabu tunayoijua kiwango chake. Geological Survey Institute inayongozwa na Profesa Mruma ipewe fedha ili kwenda kufanya kazi hizo za kuhakiki kiwango cha dhahabu kilichopo kwenye ardhi kwa kila mchimbaji wa dhahbu mdogo mdogo. Tukifanya hivyo, tutasaidia wananchi walio wengi kupata dhahabu yao na fedha zao kwa wingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni upande wa elimu. Kwa mfano, shule za msingi Makete ni wastani wa walimu watatu kila shule sasa wanafunzi hao watasomaje? Naomba sana Wizara ipeleke walimu wa sekondari kwa mshahara wa sekondari wakafundishe shule za msingi, wale waliomaliza wapelekwe shule za msingi kwa mshahara wa sekondari. Wanachotaka wao ni fedha (mshahara), wapelekwe kwa mshahara wa sekondari lakini wafundishe shule za msingi. Shule za msingi orientation yake ni ndogo, figisu figisu na michanganuo ya kusema kwamba ufanye hivi, ufanye hivi, wanapewa elimu ya mwezi mmoja, wanahamasika halafu tunajenga shule zetu vizuri kwa sababu sasa hivi ni tatizo kubwa sana kwa shule za msingi za elimu wilayani Makete. Walimu watatu ndiyo wastani wa walimu kwa shule zangu, hali ni mbaya sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo, nihitimishe kwa kusema kwamba kama mipango yote hii tukiifanya, upande wa elimu tukawapeleka walimu wengi katika shule za msingi, upande wa kilimo tukawapa wakulima mikopo ya asilimia ndogo, asilimia 10 kwa mfano, Upande wa dhahabu tukapeleka fedha Geological Survey kwa Profesa Mruma akaweza kuhakika kiwango cha dhahabu kila sehemu basi tutakuwa tumesaidia kukuza uchumi wa nchi hii. Nafahamu kwamba Geological Survey team walikuwa wameshapewa fedha kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, sasa hivi hazipo lakini walikuwa wameshapewa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho nizungumzie kuhusu ujenzi wa reli. Ujenzi wa reli ni jambo muhimu sana lakini naomba sana, reli ninayoikazia hapa ni ya Uvinza - Msongati, kwa sababu Msongati kuna chuma tani zaidi ya 3,000,000. Watazamaji wote wa reli hii wanafikiria kwamba ile reli itakuwa inameza chuma kile kwa kusomba chuma kile ili tonnage yetu iwe ya maana. Tonnage inayopelekwa Mwanza na Bakhresa ambaye ndiye mpelekaji mkubwa, akipeleka mara moja tu Uganda tonnage yake yote itakuwa imeisha, meli imeenda mara moja inakuwa imeisha lakini tonnage ambayo ni ya uhakika ni ya Msongati kwa sababu pale pana chuma na tayari tunao mkataba walioingia Mawaziri waliopita wa Burundi na Tanzania wa jinsi ya kushirikiana na DRC-Congo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mungu awabariki sana, ahsante sana, naunga mkono hoja. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021
MHE. PROF. NORMAN A. SIGALLA KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kupata nafasi hii kuchangia kidogo kuhusu Mpango huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natanguliza kwanza shukrani kwa Rais wangu, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri anayoendelea kufanya mpaka sasa hivi. Mungu ambariki sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nikapata nafasi ya kushiriki ziara ya siku 21 ya mafunzo ya uendeshaji wa ndege, bandari pamoja na reli (SGR) pale China. Nilichojifunza ni nini? Nilichojifunza ni kwamba Bandari ya Bagamoyo ni mpango halisi wa Wachina wa kutaka kuisaidia Tanzania kujikwamua kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafahamu kwamba Serikali ina macho/sura nyingi inavyoangalia jambo hili lakini jambo lenyewe hili usahihi kabisa ni kwamba niliongea na Wachina wakanionesha michoro ile, wakaonesha jinsi ambavyo Bandari ya Bagamoyo itakuwa inalenga kukwamua uchumi wa Tanzania. Pia wakaonesha kwamba tayari kuna makubaliano ya Mawaziri wetu wa Uchukuzi na nchi za Burundi na DRC Congo ya jinsi ya kuhakikisha kwamba wana-ferry chuma Msongati kwa kutumia Bandari ya Bagamoyo. Kwa hiyo, wao walipokuwa wanapeleka nguvu kuhakikisha kwamba wanajenga reli ya SGR wanafikiria zaidi kwenda Uvinza, Msongati, Burundi kwa sababu tayari kuna makubaliano ya kimkataba ya nchi ya Tanzania na Burundi. Pia kuna makubaliano ya mkataba kwenda Kalemi kwa sababu ya nchi ya Congo DRC na Tanzania pia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema kwamba suala la Bandari ya Bagamoyo ni ni muhimu sana kwa Tanzania. Sina hakika kama Serikali ina taarifa sahihi kuhusu jambo hili kwa sababu tumekaa pale siku 21, siku 21 za mafunzo ni nyingi sana kwa mtu mzima lakini tumekaa pale tukajadiliana na tukaoneshwa waziwazi jinsi ambavyo Bandari ya Dar es Salaam itazidiwa nguvu kama chuma cha Msongati kitachimbwa inabidi kipelekwe Bandari ya Bagamoyo ifanye ferrying ya chuma kile. Kwa hiyo, nafikiri ni vizuri sana ijulikane hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata Mradi wa Chuma wa Mchuchuma na Liganga na nimesema mara nyingi hapa, huu ndiyo mradi ambao sisi Watanzania ni wa kujivunia. Napata shida sana kuelewa kwa nini Serikali inapata shida kupeleka fedha na kutia saini mikataba ya Chuma cha Mchuchuma na Liganga kwa sababu mradi huu upo wazi. Ni kweli kabisa kama mchangiaji mwingine alivyosema kwamba miradi hii inasaidia sana kuongeza ajira za watu wetu kwa wingi sana. Bandari ya Bagamoyo, Mchuchuma na Liganga ni miradi ambayo itaongeza ajira kubwa sana kwa watu wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia ni kweli you cannot do anything now without China, ndio ukweli. Ukweli wa mambo kwa uchumi wa sasa hivi ukifanya skeleton ya uchumi wa dunia unavyokua huwezi ukajitenga na China, haiwezekani. China kwa sasa hivi is a leading country kwa uchumi. Nasikitika sana kusema hivyo kwa sababu China walinifikisha mahali ambapo waliona nafaa kuwa Mwenyekiti wa nchi 16 walioenda China lakini pia waliniona mimi kama ni unique person kwa sababu natoka Tanzania nchi ambayo wao wanaipenda. Kwa hiyo, wakaniambia kwamba wanakusudia kuifanya Tanzania kuwa ndio hub ya uchumi wa China Afrika kwa sababu reli inayojengwa Nigeria (Enugu) kuja Bujumbura inaunganishwa na reli inayokuja Msongati kwenda Bagamoyo, ndiyo master plan yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, wao walikusudia kwamba Tanzania itakuwa ndio hub ya uchumi wa China Afrika. Walisikitika sana kuona kwamba Kenya wamekuja of late wamekubaliana kutengeneza reli ya kutoka Mombasa kwenda Nairobi kwa sababu mpango ulioanza ni wa kwao wa Dar es Salaam kwenda huko tunapopeleka lakini Kenya wakaja nyuma yake wakajenga reli ya kutoka Mombasa mpaka Nairobi na imeshakamilika na wanatengeneza fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sana Serikali iangalie kwa makini sana juu ya China. China ni nchi ambayo inatupenda sana sisi na sisi tuna mahusiano ya damu na China, sio mahusiano ya kubahatisha. China kama akikosea tunaweza kuwaambia, tukiwaambia wanakubali na wanaelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Tanzania na China tuna mahusiano ya muda mrefu, mahusiano ya Mwalimu Nyerere na Mao Tse Tung ni ya muda mrefu. Kwa hiyo, ni hawa hawa waliojenga SGR hii ta TAZARA ya Dar es Salaam kwenda Zambia na wamejenga miaka hiyo wakati hatuna uwezo. Kwa hiyo, leo hii kwa nini tuone kwamba wao ni shida? Nafikiri lazima Serikali iangalie vizuri ili kufika mahali ambapo tunaweza tukafanya vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukifanya hivyo tutafanikiwa sana. Tanzania ni nchi bora sana lakini tutumie kwa usahihi nafasi na fursa ambazo tunazo. Tusipotumia kwa usahihi fursa tulizonazo tutapata shida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni muhimu sana ku-resort into these plans ili tuweze kwenda nazo mbele, tusisikie maneno ya watu. Maneno ya watu wengi ni kutufanya sisi Tanzania tusifanikiwe. Wanasema China imefanya hivi, wanatoa mifano ya China kununua mgodi wa Zambia, tunaoujua vizuri uchumi wa China tunasema siyo kweli, kilichotokea Zambia ni kingine na Tanzania tunafanya vingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni muhimu sana Serikali yangu ya Tanzania ikubali ushauri huu iutekeleze mradi wa Bagamoyo na chuma Msongati. Mungu awabariki sana. Amina. (Makofi)