Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. John Wegesa Heche (26 total)

Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue nafasi hii kwa sababu ni mara yangu ya kwanza, kuchangia, nimshukuru sana Mwenyezi Mungu, ambaye ametupigania mpaka leo tupo hapa. Jambo la pili niwashukuru sana wananchi wa Tarime ambao kwa miaka mingi na miaka yote wameonesha imani kwangu walinichagua, kuwa Diwani wa Kata ya Tarime Mjini nikiwa Mwanafuzi wa Chuo Kikuu, lakini vilevile pamoja na mapambano makali yaliyokuwepo kwenye uchaguzi huu mpaka mauaji yaliyofanyika tarehe kumi mwezi wa Tisa, wananchi walisimama imara na wamenileta hapa na nataka niwahakikishie nitawawakilisha na nitasimamia kero zao kwa nguvu zangu zote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jana usiku nilijitahidi sana kusoma na ku-google nchi mbalimbali kuhusiana na Uongozi, nikajaribu kuangalia mambo yaliyofanyika siku za hivi karibuni hapa Bungeni, ya Polisi kuingia ndani ya Bunge wakiwa wamevaa Head gear, bunduki, sijui mipini kujaribu kupiga Wabunge waliokuwa hawana silaha. Nikagundua kwamba hata Idd Amini, hata Adolf Hitler, hakuwahi kuingiza Polisi kwenye Bunge kujaribu kupiga watu wanaopinga. Kwa hiyo, hapo mtajaza wenyewe kwamba mna uongozi wa aina gani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuwezi kuongoza nchi hii kwa takwimu za uongo. Hapa Dkt. Mpango naomba unisikilize vizuri, nimesoma vitabu vya Mpango hivi, takwimu zilizoko hapa, ni takwimu feki, na kwa takwimu hizi hamuwezi kufanya kitu chochote hata muwe na nia njema. Kwa nini nasema hivyo, kwa mfano, maji vijijini kitabu hiki kinaonesha cha Mpango kwamba kuna maji Vijijini kwa asilimia 68.
MHE. JOHN W. HECHE: Nimejaribu kuangalia kwenye Jimbo langu peke yake…
MWENYEKITI: Taarifa Mheshimiwa Naibu Waziri!....
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ulinde muda wangu, naamua kuwapuuza wote niendelee tu. Nilikuwa nazungumzia kuhusu takwimu. Takwimu za maji kwa mfano vijijini wamesema maji yapo kwa aslilimia 68, lakini nimeangalia Jimbo langu ni Jimbo la Vijijini tuna Kata 26, katika Kata 26 hizo asilimia 68 ya 26 ni Kata 17 ina maana kwa mujibu wenu kwenye Kata 17 kuna maji hivi sasa tunavyozungumza, kitu ambacho ni uwongo na hakipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Mijini mmesema kuna maji asilimia 95, hii ni aibu ina maana kila watu 10 watu tisa wanapata maji, au kila watu 100, watu 95 wanapata maji, lakini pale Dar es Salaam ni kielelezo, kipindupindu kinawaumbua kila siku, kwamba hakuna maji na takwimu mnazoleta humu ni za uongo. Kwa hiyo, kama mnataka kulitoa Taifa hili hapa ni lazima tuwe na takwimu ambazo zinaeleza ukweli, na takwimu ambazo zitawasaidia kujenga kwenda mbele, lakini mkija na takwimu za uongo hapa mnajidanganya wenyewe na wananchi wanawaona.
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu barabara, zetu ni mbovu
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa!
MWENYEKITI: Taarifa...
MHE. JOHN W. HECHE: Nawashauri Mawaziri tulieni msikilize, kwa mujibu wa sera ya maji ya Taifa hili, maji ambayo mnahesabu kwamba watu wanapata wapate ndani ya mita 400 kutoka wanapokaa, sasa kwenye hivi vijiji mimi ninavyosema watu wanafuata maji mpaka kilometa moja, mbili, sasa unatoa taarifa gani hapa. Tulia usikilize tukueleze wananchi watapima kule anasema nani uongo kama maji yapo au kama hayapo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara, barabara zetu ni mbovu, kwa mfano barabara za Tarime. Kutoka Tarime kwenda Serengeti ambako kuna Mbuga kubwa ya wanyama. Inapita Nyamongo kwenye eneo la Mgodi wa Nyamongo, barabara ni mbovu, na mimi ninamwomba sana Waziri achukue hii hoja ya barabara hii iwemo kwenye Mipango ya Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu nishati; leo mnakuja hapa kuzungumza kuendeleza Taifa, wakati watu wanapikia kuni. Dar es Salaam peke yake, ambayo mkaa unakwenda pale magunia tani na tani, mngeweza kama kweli mnataka kuendeleza Taifa hili, kuliko kurukaruka hapa, mngechukua Dar es Salaam ile peke yake, mkazuia utumiaji wa mkaa na magogo na kila kitu mkapeleka gesi pale kwa bei rahisi watu wote watumie gesi pale Dar es Salaam, Arusha na Mwanza, tayari mngekuwa mmesaidia misitu ya Taifa hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mnakuja humu mnaimba tu misitu tuta-conserve misitu, mazuia watu. Kama kule Jimboni kwangu naona eti Afisa Misitu anazuia watu wasitumie mkaa, nimemwambia wananchi watakuchapa wewe! Wapelekee kwanza gesi ndiyo uwazuie kutumia mkaa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Makusanyo ya Serikali; nataka mtuambie hapa, hicho mnachojisifia kwamba mmekusanya mwezi wa 12 ni arrears au ni vyanzo vipya mmeleta na mmekusanya. Kwa sababu msije mkajisifu hapa tumekusanya tirioni 1.4 kumbe ni arrears za huko nyuma ambazo ni za watu ambao ni majipu na majipu wengine wako humu mnawajua wanatakiwa walipe na ni madeni. Sasa huko mbele mmetengeneza vyanzo gani, mmvionesha wapi kwenye Mpango huu, vyanzo vipya. Leo mnataka mchukue pesa kwenye Halmashauri na hili msithubutu Mheshimiwa Waziri, Halmashauri watu wakusanye pesa wao wenyewe, wakupelekee Benki Kuu, halafu wewe ndiyo urudishe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, tunaidai Serikali pesa za ardhi ambazo ni asilimia 30 miaka karibia sita zaidi ya milioni 500, tunapeleka pesa zetu wakati wa kurudi hazirudi. Leo ndiyo wamerudisha milioni 27, leo tena tuchukue pesa zetu za mapato ya ndani tuwapelekee na nyie mnajua, kama mnataka kuendeleza uchumi wa watu kule vijijini mabenki yaliyoko kule Wilayani ndiyo yanakopesha watu wanaofanya biashara ndogondogo na benki hizi zinategemea pesa kutoka kwenye Halmashauri, leo mnataka mchukue pesa zitoke Halmashauri mabenki yakose pesa, yashindwe kukopesha watu wetu kule chini, biashara zife kule chini, halafu mnasema mnataka kuendeleza Watanzania au mnataka kuwa-suffocate.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mmekuja hapa mnasema viwanda, kila mtu anasimama hapa viwanda. Viwanda gani, viwanda vinategemea foreign direct investment, Wazungu hawa mnaoenda kukinga mabakuli wamesema wako concerned na mambo yaliyofanyika Zanzibar, hakuna amani, Zanzibar kule kuna Nkurunziza. (Makofi)
Mmechukua hamtaki kutoa nchi kwa mtu aliyeshinda, kwa maana hiyo Wazungu wanakwenda kuzuia hiyo misaada sijui mtapata wapi pesa za kuanzisha hivyo viwanda.
MWENYEKITI: Mheshimiwa muda wako umemalizika naomba ukae.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili na mimi niweze kuchangia kwenye mpango huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nafikiri isingekuwa sahihi sana kama Wabunge wengine ambavyo wamezungumza kuanza kuchangia kwenye mpango huu au mipango mingine yoyote ya Serikali kabla ya kufanya tathmini ya mpango uliokuwepo ambao tunaendelea nao sasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuko kwenye quarter ya pili ya bajeti, Halmashauri hazijapelekewa pesa, hazijapelekewa OC, watu wanalia, mnataka wakusanye mapato lakini hamjawawezesha kuweza kukusanya hayo mapato, kwa sababu bila OC sijui mnataka watu watembee kwa miguu kwenda kwenye minada kukusanya pesa, haiwezekani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kusema hivi, mimi sio mtabiri, lakini nataka nikuambie Waziri Mpango baada ya Waziri aliyetumbuliwa hapa unamkumbuka, anayefuata ni wewe, wewe ndio utakuwa wa pili kutumbuliwa na Mheshimiwa Rais Magufuli. Na kwa nini utakuwa wa pili ni kwa sababu mambo yanapokwama, mipango mliyopanga yote inapokwama wewe ndio utabebeshwa zigo hilo ili aonekane yeye yupo sawa wakati mnakosea wote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ajira; mnaleta hapa kuzungumza mipango hii, mlisema hamuajiri kwa sababu mnafanya tathmini ya watumishi sijui kutafuta watumishi hewa, haya mmetafuta hewa mwaka mzima, vijana wamesomeshwa na baba zao watu maskini wako mitaani, dada zetu wanajiuza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mikopo nayo sijui mnatafuta wanafunzi hewa. Kilimo hakuna pembejeo mnatafuta majembe hewa, mnatafuta wakulima hewa? Jambo la msingi ni kwamba mseme Serikali yenu imefilisika na haiweze kutekeleza chochote msaidiwe kuliko mnakuja hapa mnasema watumishi hewa, watumishi hewa mnatafuta mwaka mzima, wakulima hewa mnatafuta mwaka mzima, kilimo kimesimama. Wanafunzi mkawapa mikopo mwaka jana, mambo ya aibu kweli kweli! mwaka jana tumewapa mkopo leo mtu anaingia mwaka wa pili hamtaki kumpa mkopo, wengine wanaingia mwaka wa tatu hamtaki kuwapa mikopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali yenu hii mlitoa matumaini mnasema hapa kazi tu, hapa kazi nini sasa watu hawana mikopo wanafunzi wanalia, mnatoa mtoto kijijini anakwenda chuo anafika pale hana pa kuishi, hakuna mkopo, ni matatizo kwenye familia. Sasa mimi nakutabiria Mpango unakaribia sana kutumbuliwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye elimu; elimu yetu wakati anazungumza pale Mheshimiwa Mapunda, amesema vitu vinne ambavyo vinahitajika kuwepo kwa viwanda amezungumzia personnel au man power, ni man power ya aina gani ambayo imeelimika ili iweze kuajiriwa kwenye hivyo viwanda?
Leo elimu ni majanga; mama yangu Profesa Ndalichako mimi nilikuwa nakuheshimu sana ukiwa Katibu wa Baraza; umewahi kutoka pale unaonesha watu wamechora ma-zombie kwenye mitihani, wewe umepewa Wizara hii umechora zombie kubwa kuliko wale wanafunzi. Na sijui hata wizi wa mitihani utazuiaje kama wewe Profesa ulitoka hapa kwenda kuiba kura Kinondoni, sijui. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika elimu hivi baada ya wewe kutoka hapo na Uprofesa wako na ni kwa nia njema tu, kwa sababu hili Bunge mmelifanya kama idara fulani ya pale Ikulu labda hata ya umwagiliaji maji pale, kumwagilia maua ndio maana leo Wabunge wanasimama hapa wanasema ukweli hali halisi ya uchumi ni mbaya, wengine wanasimama wanatetea. Jana tu walikuwa wanazungumza hapa wanapiga makofi, sasa hivi wamegeukana na mimi nilijua hamtafika mwisho. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya uchumi ni mbaya hata kwenye kununua vocha tu, ukinunua vocha ulikuwa unapewa GB sita leo ni GB 2.5 kwa shilingi 10,000; yaani hata mtu ambaye hajaenda shule anajua. Kwahiyo, hali ya mazingira ya mtaani elimu inazidi kuporomoka.
Tumetengeneza madawati tumepeleka, maeneo mengine madawati yapo nje yananyeshewa hapa kwenye mpango hamjaonesha mkakati wowote wa kujenga vyumba vya madarasa ili yale madawati tuliyopeleka yaingizwe ndani, yataoza kwenye miti, mwakani tena tuanze kukamatana kupambana na watu wanunue madawati. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitegemea kwenye elimu hapa Profesa Ndalichako ungekuja na mpango ambao utaondoa elimu yetu hii kwenye mkwamo, ambao tutajua kutakuwepo na maandishi yanayoeleweka kwamba elimu tunayoenda nayo ni ya aina hii, tutoke kwenye elimu ile ya akina Mungai ambayo tulikuwa tunaunganisha hesabu sijui na historia na wewe unaendelea huko huko. Leo mnafanya hivi kesho mnafanya hivi, keshokutwa mnatoa vigezo hivi, siku nyingine mnatoa vigezo hivi. Mimi nawaasa vijana Watanzania wote ambao Serikali hii imewatosa haitaki kuwapa mikopo wajue wana nguvu nyingi sana za kuunganisha kura yao ili mwaka 2020 waondoe Serikali hii kwa sababu hakuna matumaini katika maisha yao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viwanda; amezungumza vizuri sana Mheshimiwa Chegeni hilo ndio jina la yule bwana sio sisi tunaosema ni wananchi. Ukikutana naye hapo nje ukamsimamisha Waziri vipi, nikupe kiwanda? Anaingiza mkono mfukoni, anataka kuchomoa kiwanda mfukoni akukabidhi. (Makofi/Kicheko)
Mpango wenu hamjajenga kiwanda hata kimoja mpaka sasa, mmebaki mkisikia Bakhresa anataka kufungua kiwanda mnakimbia pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viwanda Mheshimiwa Waziri Mpango wewe unajua, ni msomi na uwe unasikiliza watu hapo unaelewa. Kiwanda ndiyo kinaajiri kuanzia mama lishe mpaka engineer kiwandani peke yake. Kwa sababu mama lishe atakuwa pale atawauzia wabeba mizigo wa viwandani, atawauzia madereva wanaobeba mizigo kwenye kiwanda. Kiwanda kitaajiri engineer wa kuendesha mitambo, kiwanda kitaajiri mhasibu, kiwanda kitaajiri kila mtu.
Leo umekuja hapa, kwanza ninyi wenyewe Serikali hii ambayo sasa inataka kufuta eti siyo yenyewe, Serikali hii ya CCM ikaua viwanda, ikauza viwanda. Mmerudi mmeimba Serikali ya viwanda, leo tunaelekea mwaka mmoja na siku kadhaa hata kiwanda cha pini hamna mpango nacho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkisikia Bakhresa anazindua kiwanda chake mnakimbia pale mnasema sukari tuliyokunyang‟anya tunakurudishia na shamba tunakupa zawadi. Halafu mnatoka pale kwamba tumefungua kiwanda. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna taarifa mnakataa hapa kwamba Serikali haijaishiwa kuna taarifa mnatisha wafanyabiashara, mtu amelipa ushuru ana risiti mnamwambia hizo ni risiti fake, Serikali iliyokuwepo ilikuwa inatoa risiti fake. Mnawalipisha watu kodi mara mbili.
Leo Benki zinatangaza hasara, wewe ni msomi utuambie nini implication ya benki kutangaza hasara, CRDB wamesema, nini implication yake kiuchumi? Maana msituambie tu kwamba uchumi unakuwa vizuri, uchumi unakuwa vizuri watu wanalia mtaani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mmewaruhusu traffic, Wabunge walikuwa wanalia hapa kila traffic ameambiwa kwamba kwa siku ni lazima apeleke makosa matatu. Leo makosa ya barabarani ni chanzo cha uchumi kwa Serikali ya CCM, aibu. Makosa ambayo yanatakiwa kuzuiwa watu wasifanye makosa ninyi mna-encourage ili mpate uchumi….
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU: Kuhusu Utaratibu!..
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naomba unilinde kidogo muda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hivyo? Leo wakuu wa traffic nchi nzima wanatangaza mapato yaliyopatikana kutokana na makosa kwamba mwezi wa tisa tumepata bilioni kadhaa kutokana na makosa, nini maana yake? Kama hamu-cherish yale makosa kwamba ni chanzo cha mapato cha Serikali hii?
Mheshimiwa Mwenyekiti, makosa yale nafikiri yamewekwa ku-discourage watu kuendelea kufanya makosa, lakini unapotangaza unajisifu kwamba ma-traffic wamekamata makosa kadhaa ina maana ni chanzo mmeweka pale. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nasema siyo kwa nia mbaya ni kwa ajili ya kuwaambia hawa watu wasikie waelewe kwamba waliambiwa hapa tukikosa mapato yanayotokana na bandari mtaanza kufukuzana na bodaboda, watu walisema humu mkatuzomea. Sasa leo tunaposema haya hamtaki tena, mnataka tukae wapi? Tukisema hili ninyi kwenu baya, tukija hapa ninyi kwenu baya mnataka nini sasa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliwaambia mkipoteza mizigo nchi hii haitawezekana. Leo eti TRA wanataka wawe TRA ya Congo pia wamesema Wabunge wengine hapa, yaani mnataka kujipa majukumu ya kukusanyia Congo kodi. Kwani kama Congo kule wanakwepa kodi ninyi inawahusu nini? Wamepitisha hapa, wamewalipa mapato yenu, mnachukua mnafanyiakazi, mnataka kuwakusanyia Congo ili wawape nini? Mmekuja hapa mnaongea na Rais wa Congo anawahakikishia mizigo itaongezeka, imeongezeka? Kwa sababu hana mandate ya kuwaambia wafanyabiashara lazima wapitie hapa na wao wamehamia Beira, wamehamia Mombasa sasa wote tunapiga miayo hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunadanganyana tumepandisha bajeti kutoka shilingi trilioni 22 desperately kabisa kwenda shilingi trilioni 29 eti mnataka hadi Mama Lishe alipe kodi, Mheshimiwa Mpango, mama lishe alipe kodi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, vijana mnawaambia hawana ajira eti wajiajiri, wewe mwenyewe umeshindwa kujiajiri umeomba Ubunge hapa unataka kijana wa mtaani ajiajiri. Wabunge wote hawa tumeshindwa kujiajiri tukaenda kuomba ajira kwa wananchi, wengine Profesa sijui na nini. Kijana aliyemaliza mwaka wa kwanza mnamwambia nenda ujiajiri kule! Vijana hawawezi kutengeneza ajira!
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jukumu la Serikali yoyote duniani kulinda watu wake na ni aibu kwamba leo nchi hii wakati wa hapa kazi tu hakuna madawa kwenye mahospitali; miradi yote mliyoweka ya kielelezo haiendi, barabara hamtengenezi tena na wengine hapa walikuwa wanaitukana Serikali ya…
MWENYEKITI: Ahsante.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikushukuru sana kwa kunipa nafasi hii na mimi niweze kuchangia kwenye hotuba hii kwenye Mapendekezo ya Mpango wa Mheshimiwa Waziri Mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nianze kwa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu ambaye anatulinda, ambaye yeye si binadamu, yeye anatupenda hata kama wengine wanatuchukia na Mwenyezi Mungu ameokoa maisha ya Tundu Lissu napenda sana kumshukuru. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika miaka yangu miwili ambayo nimekaa hapa Bungeni kumekuwa na Mpango wa mwaka 2016/2017 na bajeti yake, kukawepo na Mpango wa mwaka 2017/2018 na sasa Mapendekezo ya Mpango wa mwaka 2018/2019 na bajeti zinakuwa zinapitishwa. Pia mojawapo ya kazi ambazo Bunge hili limekuwa likifanya ni kutunga sheria na mambo mengine yote ambayo yapo kwa mujibu wa vitabu na katiba ya nchi hii na sheria zetu kwa ajili ya kufanywa na Bunge hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini najiuliza na kila Mbunge hapa aende ajiulize kama kuna sababu yoyote ya kuendelea kuwa tunaleta hiki kinachoitwa mpango, hiki kinachoitwa bajeti na sheria tunatunga humu tunatumia pesa za walipa kodi maskini wakati Serikali na Rais mwenyewe hafuati hiki kinachoitwa mpango, hafuati sheria na hafuati bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na mambo ya mwanzo mawili. La kwanza Mheshimiwa Mpango kila kitu mnachopanga kwa ajili ya wananchi mwisho wake kinaishia kwenye vijiji au vitongoji au mitaa. Bahati mbaya hao Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji na Mitaa wanachaguliwa na wananchi, wanapigiwa kura kama sisi Wabunge kama Madiwani na kwa kampeni.

Kwanza jambo la kwanza hawana security of tenure, anakwenda tu Mkuu wa Wilaya anaweza akamfukuza Mwenyekiti wa Kijiji aliyechaguliwa na wananchi kwa kumsimamisha. Anamfukuza kazi wakati Mkuu wa Wilaya huyo hajateuliwa, hajui hata kura aliyogombea pengine kura za maoni akapigwa, anamfukuza Mwenyekiti wa Kijiji bila kufuata utaratibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili mmekuwa mkiwaaidi kwenye mipango yote, na mnategemea hawa watu ndio wasimamie kazi zile za kuendeleza maendeleo ili mpande kwenye majukwaa mjisifie. Unamlipa Mtendaji wa Kijiji, unamlipa Mtendaji wa Kata lakini haumlipi Mwenyekiti wa Kijiji ambaye ndiye bosi wa Mtendaji. Kwa hiyo, mimi nataka niwaambiwe Wenyeviti wote wa Vijiji wa CHADEMA na wa CCM; hapa ni issue ya maslahi yao, wajue Serikali hii ya CCM haitaki kulipa maslahi yao na inawadharau. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, ni aibu wakati mwingine Serikali inakuja inazungumza hapa na inasema uongo na wananchi kule chini wapo wanaona hivi vitu.

Unajua wakati mwingine kuna vitu mnaweza mkasema tumefanya, ukasema tumenunua ndege kwa pesa zetu wenyewe kumbe umekopa, hiyo wananchi wa kawaida hawatakuewa. Lakini ukija ukasema kuna madawa hospitali na siku hizi bahati nzuri tv zipo, wananchi wakiwa hospitali wanaona na wakati hakuna madawa, hivi wewe Mheshimiwa Waziri unavyojibu hapa wale wananchi waliopo kule hospitali wanakuelewaje? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 13 dereva wangu alikatwa panga saa nne usiku, na mimi nilimpeleka kwenye Hospitali ya Wilaya ya Tarime, hakuna gloves, hakuna gozi, hakuna hata sindano ya dawa ya ganzi. Sasa mimi namshangaa Mheshimiwa Waziri wa Afya anakuja hapa anasema madawa yamejaa tele. Sasa labda mtuambie kuna maeneo mnapeleka na maeneo mengine mnayabagua, lakini kama sivyo si vyema mkaja hapa mkazungumza mambo ambayo mnajua Serikali yenu hii imeshindwa na hivyo vitu haviko kule vijijini. Haviko kwenye vituo vya afya, haviko kwenye Hospitali za Wilaya, haviko wala kwenye zahanati na hizi zahanati wanajenga wananchi wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua Mheshimiwa Mpango ni mchumi. Huwezi kufanya maendeleo kwa kuharibu maendeleo yaliyokwishafikiwa, yaani huwezi leo ukakuta mtu amejenga nyumba yake, ukabomoa nyumba yake halafu akawa analala barabarani kama watu wa Kimara walivyo sasa hivi na maeneo mengine ya nchi hii, halafu ukasema umefanya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo ni kurudisha watu nyuma. Na unawaambia kwa kiburi kabisa kwamba hakuna fidia yoyote watakayoipata, watu wameishi tangu mwaka 1974, tangu miaka 1980 leo unakuja unapomoa nyumba zao, watoto wa watu wanalala nje. Hebu jiulizeni miongoni mwenu kama ni wewe Mpango kama mtu mwingine yeyote, hebu jaribu kujiweka kwenye hiyo picha, umeangaika umejenga na ndiyo maisha yako yote kesho unajikuta umelala barabarani, jaribu kujiweka hapo kwa sababu sisi pia ni binadamu kama wao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekit, miji ya watu inachomwa huko vijijini kwa kisingizio kwamba mnahamisha watu kutoka kwenye mapori. Mnachoma nyumba za watu moto. Watu maskini wamejenga nyumba za miti na majani ma-DC wanakwenda wana-set fire kwenye miji ya watu, watoto wanabaki wanabaki nje unga unaungua madaso, vitaa na vitanda kama anakagodoro kanaungua anarudi kuwa maskini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mifugo ya watu ya watu maskini, alizungumza jana Mheshimiwa Ryoba hapa, wanakamata mifugo, Serikali hii ya CCM inakamata mifugo ya watu. Sisi Wakurya kwa mfano unakuwa na ng’ombe ndiyo unatumia ng’ombe hao kwa kufanyia kazi ya kulima. Unalima chakula, unakuwa nacho kwenye ghala ng’ombe ndiyo wanatoa maziwa unatumia kama mboga. Leo unakamata ng’ombe wa mtu wote unauza, tena kwa shilingi 70,000 na unamshitaki huyo mtu unamfunga na haya yamefanyika mpaka kule Chato mpaka maeneo mengine ya kwa kina Mheshimiwa Doto kule Bukombe wanajua hili ninalolizungumza. Mnarudisha watu kwenye umaskini, ufukara, mnawaambiwa watu mnawaendeleza subiri hasira yake mtaiona mwaka 2020. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala haya yakuwa yanafanyika bila kufuata mpango wa Serikali wala bila kufuata utaratibu. Ukichukua kitabu cha mwaka 2016/2017 zilitengwa pesa shilingi bilioni mbili kwa ajili ya upembuzi yakinifu wa uwanja wa ndege wa Chato. Juzi nikaona kwenye tv kwamba zimeshatolewa shilingi bilioni 39 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja na uwanja umejengwa umefikia kiwango cha asilimia 63; running way yake ina ukubwa wa kilometa tatu wakati uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salamu una running way ya kilometa 3.3; uwanja huu unazidi uwanja wa ndege wa Mkoa wa Kagera, unazidi uwanja wa Dodoma, unazidi uwanja wa Mwanza.

Sasa nataka Mheshimiwa Mpango aje awajibu Watanzania, kama tuna haja ya kuwa na Bunge hili ambalo halijapanga mipango, lakini Serikali ya CCM na Rais wanatekeleza. Ni lini tender ya uwanja ule ilikuwa floated na ni nani na nani walishindana kwenye hiyo tender ili wapate huo uwanja? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi pesa shilingi bilioni 39 zimetoka kwenye bajeti gani ya Serikali ambayo haikupitiwa na Bunge hili? Hizi shilingi bilioni 39 zimetoka kwenye chanzo gani? Tunataka Mheshimiwa Mpango atujibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini mimi sina chuki yoyote na uwanja kwenda Geita sina chuki hiyo, wala Chato lakini uwanja huu ungewekwa walau Geita kwenye maeneo ya Geita au…

T A A R I F A . . . .

MHE. JOHN W. HECHE Mheshimiwa Mwenyekiti, sihitaji hata kupokea hiyo taarifa kwa sababu haelewi kwamba uwanja wa Musoma uko Makao Makuu ya Mkoa kama Geita ambapo kama ungewekwa Geita ungekuwa Makao Makuu ya Mkoa ambako ndiko kwenye economic activites kubwa zaidi kuliko Chato Wilayani, ambako kwanza labda haelewi, kutoka Mwanza Mjini kwenda Geita ni kilometa 105, ambako kuna uwanja mkubwa. Kutoka Chato kwenda Geita ni kilometa 185. Nini maana ya uwanja huu kupelekwa kule? Wanakwenda kubeba nini? (Makofi)

Mnakwenda kubeba ng’ombe mle ndani ndiyo maana mmeweka taa za kuongozea gari barabarani wakati hakuna gari hata tatu zinazopita kwenye ile barabara? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachoangalia huu uwanja unatengewa pesa nyingi za watanzania mabilioni nikiwemo mimi. Lazima values for money ionekane, lazima uwanja huu uonekane utabeba nini na utazalisha nini, siyo tuchukue uwanja tupeleke kama Mobutu alivyo…

T A A R I F A

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilindie muda wangu kidogo tafadhali. Huyu ni Naibu Waziri ambaye hajui kwamba KIA ni uwanja wa ndege wa Kilimanjaro na uwanja wa Arusha ni wa Arusha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi ninachojaribu kuzungumza, wala sina chuki na watu wa Geita, ninachozungumza ni kwamba uwanja huu uweze kufungamanishwa na uchumi, unategemea makao Makuu ya Mkoa ndiko kwenye economic activities nyingi; na kama kuna uwanja wa karibu mtu ata-opt kushukia Mwanza badala ya kwenda kushukia Chato ambako ni kilometa 180.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili nami niweze kuchangia kwenye kamati hizi kwa mwaka huu. Kabla sijaanza kuzungumza, juzi kuna propaganda imesemwa hapa na tunajua Bunge hili ni chombo cha wananchi na lina heshima kubwa. Sasa kama propaganda inaweza ikaja mpaka humu na ikaacha kujibiwa matokeo yake inaweza kuaminika na ikaleta uchafuzi. Ni bahati mbaya sana kwamba propaganda hiyo ilizungumzwa na kiongozi mwenyewe wa mhimili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi Tarime hatujawahi…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Heche subiri kidogo. Hayo maneno yalizungumzwa humu ndani na Kikanuni kama Mheshimiwa Mbunge ana shida na kilichozungumzwa na Kiti hapa, utaratibu uko kwenye Kanuni ya 5. Kwa hivyo, Mheshimiwa Heche endelea na mchango wako, usizungumzie yale ambayo Kiti kilisema kwa sababu Kanuni zetu zimeweka utaratibu. Kama kuna jambo lilizungumzwa na Kiti hapa Mbunge hakuridhika nalo Kanuni ya 5 inatoa maelekezo ya nini cha kufanya. Kwa hiyo naomba ujielekeze kwenye mchango wako na sio yale ambayo yalizungumzwa na Mheshimiwa Spika.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba unilindie muda wangu huo mkubwa uliouchukua. Nazungumza kwa sababu tuko kwenye Kamati ya Nishati. Cha kwanza kama Mbunge wa Tarime nataka kusema hatujawahi kupewa pesa yoyote bure na mgodi, haijawahi kutokea. Pesa ambazo Halmashauri ya Tarime inapewa au iliyokusanya ni pesa zinazoitwa service levy. Service levy ipo kwa mujibu wa sheria; na kwa miaka mitatu tukizijumlisha ndiyo tumepata bilioni 9.3. (Makofi)

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Heche kuna taarifa, ukae upokee taarifa hiyo. Mheshimiwa Dkt. Mollel.

T A A R I F A

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba fundisheni watu kuwa maana ya Wabunge wa Chama Tawala, mjiheshimu kama mnaoongoza nchi ili tujadiliane mambo ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pesa tulizopokea ni pesa za service levy ambazo ni kodi; na kodi ya service levy ina sheria yake ya matumizi. Sheria inasema unapokuwa umepokea pesa hizo 60 percent inakwenda kwenye development, 40 percent inakwenda kwenye uendeshaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi Halmashauri ya Wilaya ya Tarime tumepeta hizo pesa tukasema hatuwezi kupeleka 60 percent, tukapeleka development 80 percent, tofauti na wengine wote. Nataka nikutajie miradi michache tuliyofanya ili mjue Tarime ni Wilaya. Pesa za vijana na walemavu tumepeleka shilingi 1,219,000,000, TARURA tumepeleka milioni 700, madarasa kwenye vijiji… (Makofi)

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa.

NAIBU SPIKA: Kuna Taarifa Mheshimiwa Heche, Mheshimiwa Getere.

T A A R I F A

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, sijui kama ni kuhusu utaratibu au ni taarifa? Mimi nasema maendeleo tuliyoyafanya; madawati Tarime tumetengeneza 12,500 hakuna mtoto anakaa chini. Vituo vya afya tumetengeneza saba kwa miaka mitatu, vingine hamjaleta Madaktari, zahanati 24. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nataka niseme kwa kifupi tu na mengine mengi. Kwa kumalizia CAG ametoa hati safi mara tatu mfululizo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime inayoongozwa na CHADEMA, Tarime chini ya Mbunge Heche. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nije sasa kwenye REA. Serikali ya CCM walisema wao ni Serikali ya wanyonge na kwenye wanyonge tulisema tuwapelekee maji na umeme. Kwenye maji wammeshindwa kwa sababu, Mheshimiwa Silinde alitoa hapa takwimu, sasa mimi nakuja kwenye umeme. REA Awamu ya Tatu iliyoanza mwaka 2017/2018, 2018/2019 tulipanga kupeleka umeme kwenye vijiji 3,559, leo tunavyozungumza vijiji vilivyopelekewa umeme ni 322 chini ya asilimia 90. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tulipanga kuunganishia wananchi laki moja na themanini…

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Heche kuna Taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Subira Mgalu.

MHE. JOHN W. HECHE: Tulieni dawa iingie.

T A A R I F A

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, anachangia. Kwanza grid extension au densification anaijua ambayo wao wanasema mabeberu, walikuwa wanawatukana mabeberu, yote grid extension inafadhiliwa na Norway ambao ni mabeberu anayoizungumza yeye pale. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tulilenga kuunganishia umeme wananchi 180,766, waliounganishiwa hivi tunavyozungumza ni wananchi 7,300 peke yake chini ya asilimia tatu. Hizi pesa mfadhili wake ni nani? Financer wa pesa za REA na ninyi wote ni Wabunge, kama mnataka kurudi humu lazima muwe wakweli. Financer wa pesa za REA ni wananchi wenyewe wanaonunua mafuta, wanaonunua umeme na hizi pesa zilikuwa ring fenced. Sasa nataka watwambie, Mheshimiwa Waziri atwambie hapa, je, hizi pesa ndio wamechukua wakaenda kununua watu au wakaenda kujenga miradi mingine ambayo haikukusudiwa kufanyika? Kwa sababu, pesa za REA ziko ring fenced na zinaeleweka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa leo kama tumewaunganishia wananchi umeme asilimia 3.8 peke yake; na Mheshimiwa Waziri namsikitikia, kwa sababu ukihesabu vijiji, kuna vijiji tumeenda, mimi ni Mjumbe wa Kamati, umeme umepelekwa kijijini lakini umepita kwenye nyumba nne tu kijijini, nyumba nne peke yake; halafu wanahesabu tu vijiji, wanakimbia wanahesabu vijiji. Sasa kama leo ni miaka miwili ya REA Phase III wameunganisha vijiji 322 kati ya 3,500, wanafaa kuendelea kuongoza nchi hii? Wanafaa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nije kwenye Stieglers Gorge. Kwanza kuna watu wanaimba humu Stieglers Gorge! Stieglers Gorge! Wamekuwa kama makasuku. Stieglers Gorge Gorge kupata umeme wake ni mwaka 2027…

MHE. ALLY M. KEISSY: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE: …kwa sababu, kuna wengine wanafikiri utawaka kesho umeme wa Stieglers Gorge.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Heche kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Ally Keissy.

T A A R I F A

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niondoe, wanaimba vyovyote wanavyoimba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, umeme wa Stiegler’s ni bilioni 700; hivi tunavyozungumza pesa ambazo zimekwenda ni bilioni 26…

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE: …sasa kama umeme huu kujenga hili bwawa ni trilioni 7.1, trilioni 7.1 kwa bilioni 700 tunahitaji miaka 10 kujenga…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Heche kuna taarifa nyingine. Mheshimiwa Dokta Mollel.

T A A R I F A

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, unafanya, una-allow Kikao cha Bunge kiwe soko. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivi Stiegler’s Gorge pesa zilizotengwa ni 700 billion, pesa zilizokwenda ni bilioni 27. Kampuni iliyopewa tenda ya Arab Contractors ni kampuni inayohusika kujenga nyumba, haijawahi kujenga bwawa popote duniani, haijawahi. Kampuni hii imetafuta mtu wa kum-subcontract inayetaka kumpa 80 percent ya mradi, watu wanakataa wanaiambia nipe kazi yote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hii nchi ni ya kwetu…

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utaratibu.

MHE. JOHN W. HECHE: …na sisi tunasema...

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utaratibu.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, kuna source nyingi…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Heche kuna Kanuni inavunjwa. Mheshimiwa Subira Mgalu, Kanuni inayovunjwa?

MBUNGE FULANI: Aitaje.

KUHUSU UTARATIBU

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nirudie; na ilifaa utafute Hansard uone nilichosema. Kampuni ya Arab contractors, haina uzoefu wa kujenga mabwawa, nimesema hivyo. Nimerudia kusema na sitatoa neno langu, inatafuta ma-subcontractors wa kuingia kujenga bwawa. Ndicho nilichosema.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI: Taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Angellah Kairuki, naomba ukae kwanza tumalize hili la utaratibu. Mheshimiwa Heche.

MHE. ANGELLAH J. KAIRUKI: Anadanganya.

MHE. JOHN WEGESA HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, siondoi neno langu hata moja.

MBUNGE FULANI: Iletwe Hansard.

NAIBU SPIKA: Naomba ukae.

Waheshimiwa Wabunge, nimetoa maelezo marefu, sikusudii kuyarudia. Kwa mujibu wa Kanuni ya 63 na hiyo Kanuni ya 64 Mheshimiwa Subira Mgalu nitakutaka utuletee mkataba. (Makofi/Vigelegele)

Waheshimiwa Wabunge, tusikilizane. Mheshimiwa Heche, wakati huo naye atatuthibitishia, tukishapata huo uthibitisho kwamba nani anasema uongo? Kwa sababu hiyo, mchango unaohusu Stiegler’s Gorge na mjenzi aliyepata hiyo kazi kuhusu asilimia anazoweza kufanya kazi na uwezo wake wa kufanya kazi, mjadala huo hautaendelea mpaka hili jambo litakapokwisha. (Makofi)

Kwa maana hiyo, Mheshimiwa Heche ataendelea na mchango wake ukiondoa hilo jambo la utendaji kazi wa mjenzi wa Stiegler’s Gorge na uwezo wake wa kazi. (Makofi)

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nisaidie Taifa kwa mambo mengine. Bomba la gesi ambalo tulikopa na tukajengea, mpaka sasa hivi utilization ni seven percent peke yake. Mtwara, alikuwa anazungumza hapa Mbunge wa Mtwara, tuna uwezo wa kupata umeme wa megawatt 300, Ruhunji tuna uwezo wa kupata Megawatt 350 na Kinyerezi III megawatt 350.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia hizi pesa in total ambazo tungeweza kupeleka na tukapata umeme mwingi kweli kweli na wa haraka, kwa sababu umeme wa Stiegler’s Gorge ni mpaka 2027. Tunaweza tukapata umeme na wa haraka na wa bei nafuu, tumezichukua tunakwenda kuzi- dump sehemu ambazo hatuwezi kuzipata matokeo leo na tunakwenda kuharibu mazingira kweli kweli.

Mheshimiwa Naibu Spika, LNG.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
kunipatia nafasi ili niweze kuchangia kwa niaba ya watu wa Tarime. Kwanza nimesoma hiki kitabu cha bajeti na hotuba ya Waziri na niseme tu kwa niaba ya watu wa Mkoa wa Mara, nina masikitiko makubwa sana, na watu wa Mkoa wa Mara, hawataunga mkono bajeti hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni kwamba Rais alichoahidi wakati wa kampeni akiwa Mkoa wa Mara mzima, aliahidi uwongo, kwa sababu nimesoma kitabu hiki, Mkoa wa Mara mzima umepewa 0.8 kilometa za lami, haikubaliki; watu wa Mkoa wa Mara ndiyo wenye mbuga kubwa kuliko zote, Mbuga ya Serengeti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wa Mkoa wa Mara ndiyo waliokuwa na mgodi wa Buhemba, ambao umechimbwa umekwisha madini pale, wana mpaka wa Sirari, wana Ziwa Victoria wanatoa samaki pale, wana Mgodi wa Nyamongo ambao unaendeea kuua watu. Halafu inapofika kwenye maendeleo, hamuwapelekei pesa haikubaliki, haitakubalika kwa viwango vyovyote vile. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nitamtaka Waziri aje atujibu hapa na nimesoma kitabu cha Mpango hiki hapa, Mheshimiwa Waziri amepeleka kiwanja cha ndege Geita Wilaya ya Chato; kutoka Geita Mjini kwenda Chato kwanza ni kilometa zaidi ya 100 na kitu, sijui amepeleka kwa kujipendekeza kwa Rais au ni Rais mwenyewe amemwagiza akipeleke nyumbani kwake sijui hilo atatujibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwangu hapa ni kwamba, Mkoa wa Mara ambao una mbuga ya wanyama ya Serengeti, ina ziwa pale Musoma tunashindwa kujenga uwanja wa Mkoa wa Mara, uwanja wa ndege na kuuboresha uwe wa Kimataifa, wazungu washuke pale walete uchumi kwa watu wa Mkoa wa Mara. Tunachukua mikoa mipya ambayo imeanza juzi, tunaitengea mabilioni ya pesa kwenda kujenga viwanja ambavyo havina muunganiko wowote wa kiuchumi, ni viwanja vya watu kusafiri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, uwanja huu wa Mkoa wa Mara tunauhitaji kwa kweli; naomba sana Waziri anapokuja kuzungumza hapa azungumze hili, kwa sababu ni aibu kwa watu wa Mkoa wa Mara ambapo Mwalimu Nyerere anatoka kule na kila siku mnamsifia, lakini kutendea watu hawa haki hamfanyi hivyo. Hivi kweli watu ambao tunachangia madini yetu mnachukua, samaki wetu mnachukua, kila kitu mnachukua pale, wanyama mnachukua. Jana Mheshimiwa Maghembe alikuwa anasema hata kuchunga hataki tuchunge, anasema ng‟ombe wetu ni tatizo, kwenye ardhi ya kwetu wenyewe, ng‟ombe anasema ni shida; tunachoambulia na mbuga ile ni ng‟ombe wetu kupigwa risasi, ni watu wetu kubaki vilema. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuwezi kukubali hali hii, unapofika wakati wa kutuletea pesa, hospitali ya Kwangwa pale imekuwa wimbo. Haya ni matusi na nitaomba Waziri aje atuambie ni lini mnakwenda kujenga uwanja wa ndege wa Mkoa wa Mara ili kuunganisha watalii waje Serengeti na sisi tuna ziwa pale, watalii wanapenda beach, sisi tuna beach pale, watakuja kuogelea pale, mtuunganishie mtuletee uchumi, hilo ni la muhimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni kuhusu barabara. Barabara ya kutoka Tarime kwenda Serengeti ni barabara muhimu. Wote mnajua watu wa Serengeti chakula wanachokula kinatoka Tarime na hii barabara bahati nzuri inapita kutoka Tarime Mjini inakwenda inapita Nyamongo, mnakochukua mawe ya pesa, lakini mnataka wale watu waendelee kufa na vumbi, wakati dhahabu yao mnachukua, na kila siku wanapigwa risasi na jana walipigwa risasi pale, hata kuwapelekea barabara, hamuoni aibu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Tarime nzima hakuna hata mita moja ya lami ambayo mmetujengea pale, wakati madini yanatoka pale. Kwa hiyo, nataka Mheshimiwa Waziri aje atujibu, hii barabara ndiyo inalisha watu wa Musoma, ndiyo inalisha Bunda, ndiyo inaleta ndizi Mwanza, tofauti na zile zinazotoka Kagera. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri anapokuja kujibu atuambie na hili siyo la kwangu ni ahadi ya Mheshimiwa Rais wakati akihutubia Nyamwaga na wakati akihutubia Nyamongo, aliwaahidi watu hawa barabara hii ya lami ya kutoka Tarime mpaka Serengeti. Tunaomba Mheshimiwa Waziri aje atuambie. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna vitu vingine vinafanyika unashangaa, nimeona hapo mnafumua barabara ya lami hapa Dodoma, yaani watu wengine wanalala porini siku hata 10 hawana hata barabara mbovu, hiyo mnafumua eti imetoboka, mnaweka lami mpya. Hivi haya maamuzi mnayafanya mkiwa wapi? Kwa nini mnafanya maamuzi ya aina hii? Tunahitaji mje mtuambie majibu hapa, ni kwa vipi watu hawa wanapata barabara nzuri ya kiwango cha lami.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Ndege; nchi hii ni miongoni mwa nchi zinazotia aibu kweli kweli, karibu kwenye kila kitu, leo Rwanda nchi ambayo hailingani hata na Mkoa wa Mara, ina ndege zinaruka dunia nzima. Sisi ndege yetu ni Fast Jet ambayo hata Waziri anajua ukienda hata na begi unalipishwa. Nimelipishwa begi shilingi 200,000 kwenye ndege, Taifa halina hata ndege ya kuruka ndani kwa ndani hapa, acha kwenda Kenya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka 55 ya uhuru hatuna ndege, sasa Waziri anakuja kutuambia hapa kwamba watanunua ndege, mtazitunza vipi, wakati watu wanahujumu, wanauza ndege ambazo zingefanya kazi wanauzia trip ma-fast jet, sijui wanahongwa. Kuna watu wako pale Air Tanzania wanakaa kwenye ofisi asubuhi mpaka jioni wanasubiri mshahara, halafu hawafanyi kazi, aibu, yaani hawarushi ndege hata moja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mhasibu, kuna Engineer sijui kuna pilot sijui wanarushwa popo mle ndani? Labda kuna popo wanaendesha mle, wanaruka mle ndani, ndiyo ma-pilot wa hao popo.
Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri, anapokuja hapa utoe majibu kwa Watanzania, ni kwa vipi au wana mpango gani wa kwenda kufufua Shirika lao la Ndege na lirushe ndege kwa nchi nzima. Kwa nchi ambayo tuna Maziwa tuna kila kitu, ndege haiwezi kuwa anasa kwa Watanzania kusafiria. Haya ni majibu ambayo Watanzania wanahitaji na tunahitaji kuyasikia hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati mbaya sana bajeti ya nchi yetu imekuwa ni formality tu; watu wanakuja hapa wanapiga kelele, mwaka baada ya mwaka, kuwa Serikalini, liwe jipu ni la CCM, uwe usaha ni wa CCM, viwe vyombo vya kutumbulia ni vya CCM, hatuna sababu yoyote ya kutetea majipu, yaani haipo kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichokuwa nasema, ni kwa nini mpaka sasa watu wa TANROADS ambapo hata mtoto anajua wamejenga barabara ambazo ni sawasawa na zile sahani tunazotumia kwenye hoteli zile disposable yaani barabara ukipiga teke hivi lami inaruka juu. Wamejenga barabara za kiwango kibovu cha aina hiyo, lakini mpaka sasa hatujasikia hata mtu mmoja ametumbuliwa kutoka TANROADS au ni kwa sababu mkubwa ambaye mmesema asiguswe humu alikuwa hapo? Hivi anashindwa vipi kuungamanishwa na hilo? Leo mmetumbua mpaka watu wa nyuki lakini watu wa TANROADS hatujaona wakitumbuliwa. Hatuwachochei mtumbue, tunataka mtumbue waliokosea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nami leo niweze kuchangia kwenye hizi bajeti mbili za TAMISEMI na Utawala Bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumpongeza sana CAG Prof. Assad, kwa kweli Prof. Assad ameitendea haki na ametendea haki uprofesa wake na ameonyesha ni kwa nini hasa kulikuwa na wingu la kutaka kumchomoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilifikiri Serikali yenu ambayo kwa miaka miwili imekuwa ikijitangaza kwamba inapiga vita ufisadi. Mtu ambaye alitakiwa kukumbatiwa na Serikali na kulindwa kwa gharama zote ni huyu Prof. Assad ambaye ameleta taarifa ambayo mpaka mama yangu kule Kijijini anasema sasa nimejua kwa nini CAG yupo na CAG anafanya kazi gani. Kwa hiyo, ningependa nianze na hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nimnukuu kidogo Mwalimu Nyerere kwenye kitabu chetu cha TANU na Watu Wetu. Anasema, “Viongozi wa TANU hawana budi watokane na watu, kwa sababu TANU ni chama cha watu na sababu ya pili ni kwamba kazi ya TANU ni kuwatumikia watu. Sitaki kueleza mambo yanayofanywa na Serikali kama vile kujenga shule, hospitali, barabara na kadhalika. Nataka kusema juu ya shida za watu za kila siku.” Mwisho wa kunukuu. Mengine tuendelee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ambayo Serikali inakutana na shida za watu za kila siku ni kwenye Halmashauri zetu. Halmashauri ndizo zinasozimamia shule ambazo watoto wa wananchi masikini wanasoma; sio watoto wetu hapa. Hakuna Mbunge hata mmoja humu anasimama aseme mtoto wake anasoma kwenye shule za msingi za Serikali, hayupo hata mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hospitali, ndiyo kwenye watu wetu, wanakwenda kutafuta madawa kule na kutibiwa…

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE: Akina mama wanajifungua kule.

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa Mheshimiwa Heche

T A A R I F A

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimpe taarifa mdogo wangu hapo, asiseme kwamba hakuna Mbunge ambaye anasomesha. Mimi kuna wajukuu zangu wanasoma kwenye hizo shule. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche, naomba uendelee.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, unilindie muda wangu ni kidogo nizungumze matatizo ya nchi, tafadhali.

MWENYEKITI: Endelea Mheshimiwa

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kaka yangu sina sababu ya kumjibu kwa sababu…

Mheshimiwa Mwenyekiti, shule za msingi na shule za sekondari zipo kwenye Halmashauri, hospitali zinasimamiwa na Halmashauri, matatizo ya kila siku ya watu ambayo Mwalimu Nyerere aliyasema kwenye kitabu cha TANU yapo kwenye Halmashauri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwanza na Halmashauri yetu ya Tarime, Kwa masikitiko makubwa; na nimpongeze Mheshimiwa Jafo kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akiifanya na aangalie hili. Halmashauri yetu ya Tarime, huu ni mwezi wa Nne vikao vimesimamishwa kinyume cha utaratibu wa kisheria. Hili suala la utawala bora la kudhibiti Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wanajifanyia vitu vyovyote ambavyo wanaamua, eti kwa kisingizo kwamba kuna ufisadi umefanyika. Fine!

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ufisadi umefanyika, kuna watu waliofanya huo ufisadi. Mkuu wa Mkoa achukue hatua kwa hao watu waliofanya ufisadi. Sasa leo unazuia vikao vya Halmashauri; Finance Committee haikai, Baraza la Madiwani halikai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tulikuwa na watoto 1,030 wameshindwa kwenda sekondari tangu mwezi wa Kwanza, hakuna vyumba vya madarasa, tukatenga zaidi ya shilingi milioni 250 kwenda kujenga madarasa. Hizi pesa tunazo, ni pesa za wananchi wa Tarime ambao wamekusanya wenyewe kwenye nyanya na vitunguu, tunazo zipo kwenye akaunti. Mkuu wa Mkoa amezuia kwamba vikao havikai, anataka sisi tuwe tunamwandikia barua yeye kumwomba pesa kinyume cha utaratibu wa sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa kisheria, watu wenye mamlaka ya kugawa pesa ni hili Bunge na Bunge la wananchi ambalo ni la Halmashauri pale Wilayani. Sasa Mkuu wa Mkoa anataka kujigeuza Pay Master General wa Mkoa. Yeye ndio anataka sisi tuwe tunamwomba. Nimesema hakuna siku tutamwomba hizo pesa. Mwangalie kama hizi hujuma mnazowafanyia wananchi wa Tarime kwa kuwabagua kwa makusudi ni sawa sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini kama wateule wa Rais; leo hapa Assad amezungumza kuhusu upotevu wa zaidi ya shilingi bilioni 16 kwenye uniforms za Askari, mbona hamjazuia Jeshi la Polisi lisifanye kazi? Jana Gilles Muroto alikuwa anasema hapa atapiga watu mpaka wachakae, mbona hamjawazuia wasifanye kazi kwa sababu kuna ufisadi kwenye Jeshi la Polisi. Amezungumza mambo mengi hapa, mbona hamjazuia hao watu wasifanye kazi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi simtetei mwizi na nipo clear; na Mwenyekiti wa Halmashauri yangu katika kupigania hili aliwekwa ndani siku 11 kwa sababu ya kupigania ufisadi uliofanywa na wateule walioteuliwa na Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Mheshimiwa Jafo naomba atengue agizo batili hili, wananchi wa Tarime wapate haki ya Baraza lao la Madiwani ku-deliberate kwenye issue na wafanyiwe maendeleo. Hilo la mwanzo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nije kwenye ajira. Tumeona hapa vijana wetu wako vyuoni wanasoma. Hawa vijana wanahitaji ajira. Kila siku nyie mnazungumza humu. Nyie mmeajiriwa na wananchi, mnalipwa mamilioni ya pesa, wanahitaji ajira hao. Watoke mwatengenezee mazingira mazuri kama ni kujiajiri, wajiajiri na mikopo iwepo. Kama ni ajira za Serikali, zitoke; kama ni private sector, iajiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa miaka minne mfululizo Serikali hii inayotudanganya inakusanya kuliko wote haijaajiri wananchi. Juzi mmetangaza ajira 4,000 za Walimu, vijana walio-apply ni 11,300. Mnaweza kuona crisis iliyopo. Mnatangaza ajira 4,000 wanajitokeza vijana 11,300 na nyie mpo hapa mnasema kila kitu kinaenda sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye afya. Bajeti iliyopita tulitenga shilingi bilioni 561, pesa ambazo mmepeleka mpaka sasa ni shilingi bilioni 89 peke yake. Hakuna madawa, hakuna gloves wala nyuzi. Serikali yenu inayokusanya kuliko zote, kwenye madawa mmetoka hapa na rhetoric za kisiasa mmepeleka chini ya asilimia 15. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnasema ninyi ni Serikali ya viwanda; kwenye viwanda mlitenga shilingi bilioni 90, pesa ambazo zimekwenda zimetolewa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya viwanda ni shilingi bilioni 5.4, asilimia sita peke yake. No wonder mnasema cherehani tano ni viwanda, kwa sababu kama shilingi bilioni 90 mmetenga, mnapeleka shilingi bilioni 5.4 kwa nini msiseme kiwanda cha cherehani ni kiwanda na gongo ni kiwanda. Kwa nini msiseme hivyo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo kinaajiri Watanzania asilimia 70, kinatoa chakula kwa Watanzania asilimia 100, kinatoa malighafi za viwandani asilimia 80; mmetenga shilingi bilioni 98.1, zimekwenda shilingi bilioni 42. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye maji ambayo mmesema mnamtua mama ndoo kichwani, Mfuko wa Maji tulipitisha hapa kwa mbwembwe mkapigiana makofi, shilingi bilioni 299, pesa zilizokwenda kutoka kwenye Mfuko wa Maji ni shilingi bilioni 1.62… (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa…

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE: Tulia Mheshimiwa Waziri utapata nafasi ya kujibu, subiria.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche, taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE: Tulia.

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

T A A R I F A

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpe taarifa kaka yangu Mheshimiwa Heche, katika bajeti ya mwaka 2018 tulitengewa shilingi bilioni 100,058 katika Mfuko wa Maji. Mpaka mwezi Februari tumepokea zaidi ya shilingi bilioni 93. Kwa hiyo, namwombe tu ajiridhishe katika kuhakikisha halipotoshi Bunge letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche taarifa hiyo.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, sources za maji zipo tatu…

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utaratibu.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi sizungumzii pesa za wahisani za kutoka India. Mimi nazungumzia…

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utaratibu.

MHE. JOHN W. HECHE: Mimi nazungumzia pesa za Mfuko wa Maji na Mheshimiwa Waziri anajua ninachokizungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ambayo tunakuja kupitisha hapa kila mwaka, ina maana tuna matatizo ya wananchi tunataka kwenda kuyatatua. Kama tutakuja hapa watu watalipwa pesa, halafu utekelezaji ni zero; general budget utekelezaji ni chini ya asilimia 30. Leo tunakwenda kupitisha bajeti nyingine kwa sababu gani? Hapa Mawaziri wamejua kila siku wakisimama… (Makofi)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE: …ni kutukana CHADEMA mnapiga makofi mnasahau matatizo yaliyowaleta hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu. Tangu kuwepo na elimu bure, enrollment kwenye shule ni asilimia 17…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE: …lakini miundombinu ni asilimia moja peke yake mme-improve. Matundu ya vyoo zaidi ya asilimia 63. Kwa wasichana hakuna, vyoo wanajisaidia vichakani… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche muda wako umemalizika.

MHE. JOHN W. HECHE: Matundu ya vyoo kwa wavulana hakuna; hakuna mabweni… (Makofi)

MWENYEKITI: Umemalizika muda wako Mheshimiwa Heche.

MBUNGE FULANI: Taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE: Je, mnapaswa kuchaguliwa tena au mwondolewe kwa... (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche muda umeisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia. Na mimi pia nimshukuru Profesa Muhongo kwasababu kwenye Bunge la mwanzo mwezi wa pili aliunda kamati ya kwenda kuchunguza suala la Nyamongo na ndugu yangu Agness pale anasema aliniteua, mimi sikuteuliwa na Profesa ni vyema nikaweka wazi haya mambo yakajulikana.
Kwa hiyo, nampongeza Profesa kwa ile kazi na wananchi wa Nyamongo wanasubiria majibu yao kwa matatizo yale makubwa ambayo yamekuwa pale kwa miaka yote. Leo nilitaka tu niseme kidogo kuhusiana na historia ya mgodi ule wa Nyamongo na utofauti wake na migodi mingine ili Profesa uelewe unapokwenda kutoa majibu ya wale wananchi, utoe majibu ukijua hilo kichwani kwako.
Kwanza ule mgodi ni tofauti na migodi mingine ambayo wazungu wanakwenda wanapata eneo porini huko, wanaanzisha uchimbaji, wanafanya exploration na wanaanza kuchimba. Ule mgodi ni mgodi wa wananchi tangu mwaka 1911, watu wa pale walianza kuchimba madini pale kabla hata ya ukoloni na kabla ya Uhuru. Watu wa eneo lile hawana hata eneo la kulima, kwa hiyo waalikuwa maisha yao yote yanategemea uchimbaji wa madini ya Nyamongo, ndivyo maisha yao yalivyokuwa kwa miaka yote. Mwaka 1994, Serikali haya maamuzi ya kuamuliwa Dar es Salaam; Serikali ikachukua leseni ikawapa wazungu. Ina maana ikabadilisha economic activity ya watu, kama mimi nafanya biashara ya duka, leo unakuja unafunga duka langu, hunioneshi kazi nyingine mbadala ya kufanya. Kwa hiyo, Serikali ikachukua leseni ikawapa wazungu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wazungu wakaja wakatwaa eneo na ule mgodi uko katikati ya makazi ya watu. Wakatwaa eneo, migogoro ikaanza tangia mwaka 1994. Mauaji kila mwaka, tena siyo kila mwaka, karibia kila siku na juzi tarehe 7 mwezi huu umesikia ndiyo mauaji ya mwisho yametokea. Wananchi wale tumebadilisha uchumi wao, hatutaki kuwaandalia njia mbadala, hatujawapa hata mita moja. Nimesoma hapa Profesa uje ufafanue, umesema kwenye ukurasa wa 50 kwamba mmewatengea eneo, liko wapi? Hilo eneo mmewapa wachimbaji wapi? Kwa sababu mimi na wewe tulikuwa pale na demand yao ni hii na mimi najua hujatoa taarifa, hujapeleka taarifa ile kwa wananchi lakini umesema ukurasa wa 50 kuna eneo limetengwa kwa wachimbaji wale, akina nani? Hilo eneo halipo na hii ndiyo imekuwa mgogoro siku zote Profesa, pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wanataka kuingia pale wachukue kwa sababu hawawezi kufa kwa njaa, wakati mali yao wanachukua wazungu wanaondoka nayo, haiwezekani, ni lazima kutafuta suluhu. Tangia mwaka 1994 Watanzania wenzetu zaidi ya 400 wameuawa pale mgodini. Watu wamebaki na vilema vya maisha, wengi tu ambao hawana idadi. Na hili suala ni suala ambalo kama hatutatatua kwa kuwapa wananchi eneo la kuchimba, hakuna suluhu pale. Wale wazungu wametumia shilingi bilioni 21 kujenga ukuta, yaani badala ya kutengeneza mahusiano na wananchi kwa kupeleka hizo pesa kwenye maendeleo wamejenga ukuta zaidi ya kilometa 10 na kitu, shilingi bilioni 21 ukuta mrefu na bado haiwi suluhu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi Mkuu wa Wilaya anasema kwamba mtu aliyepigwa risasi alikuwa ameenda rompad kuiba madini. Eti anasema rompad kuna madini. Mimi nimefanya kazi pale mgodini Nyamongo, rompad hawaweki madini, wanaweka mawe na mawe yanakuwa pale zaidi ya tani 2,000, 3,000. Mtu anaenda na kamkoba kuchukua jiwe pale ambalo halifiki hata kilo moja unampiga risasi una-justify kifo chake eti alikuwa ameenda rompad kuchukua madini, hata hajui amekurupuka tu. Mkuu wa Mkoa anakuja bila heshima anasema waliopigwa risasi ni wahuni kwamba wananchi wa Tarime wanauawa halafu mnawaita wahuni? na nilitamani Waziri Mkuu awe hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatutakubali kauli za aina hiyo kwa wananchi wa Tarime ambao mali yao imechukuliwa, inasafirishwa kila siku na Profesa hapa leo mimi nimekuwa mpole sana kwa sababu nategemea utatoa majibu ambayo ni positive, lakini kauli kama zile za Magesa Mulongo kwa watu wa Tarime na watu wa Mkoa wa Mara; Profesa wewe unajua sisi sio wanafiki – nyeupe ni nyeupe. Nilikuwa naona wengine wanakupongeza huko ambao tu walitumika mwaka jana kuku-crucify. Bora sisi ambao tumesema na msimamo wetu umebaki pale pale. Sisi si wanafiki. Wengine ooh Profesa tunashukuru Mungu amekuleta tena, hawa hawa! (Makofi/Vicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Profesa, ninakuomba tatua mgogoro wa watu wa Nyamongo. Nilipokuwa form two nasoma historia wanasema sababu zilizosababisha kukua kwa miji kama Johannesburg, ni kuwepo kwa madini pale. Lakini wewe umeenda Nyamongo pale hata mita moja ya lami tangu mwaka 1994 hakuna. Halafu mnataka Wakurya waendelee kupigia makofi mambo yale, madini yanaondoka. Tunabaki na mashimo, milima, unakuta vijana zaidi ya 2,000 wako kule juu ya mawe. Siku mgodi ukifungwa sijui watakwenda wapi? Mkoa wa Mara hautakalika. Serikali haioni, sisi tunaolia kila siku saidieni hawa watu. (Makofi)
Mheshimiwa wenyekiti, Waziri Mkuu angekuwa hapa asikie, Waziri wa Mambo ya Ndani na Mawaziri wengine msikie. Mgodi unalipa mpaka askari, mimi naamini askari analipwa kulinda mwekezaji na analipwa na Serikali. Lakini mgodi sasa hivi unalipa askari kila siku shilingi 50,000, askari wanaokwenda kulinda ule mgodi na ndiyo maana wamekuwa loyal kwa mgodi. Mtu wa mgodi akiwaamrisha kupiga Mtanzania risasi wanapiga tu, hawajali. Askari wamekuwa wanyama pale. Juzi wanakwenda kwenye Kituo cha Afya, wanapiga risasi Kituo cha Afya? Kuna watu wanafanyiwa upasuaji pale, kuna watu wana pressure pale, wanapiga mpaka mama ambaye anachukua dawa pale, na Tanzania mambo haya mnaona ni sawa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nasema na hii ni kauli yangu na ni kweli tupu, lazima yale mauaji yakome pale. Yasipoisha askari wenu wale wataniua mimi, nawaambia ukweli. Wataniua mimi kabla sijamaliza Ubunge wangu. Siwezi kukubali tena waendelee kuua wananchi pale. Nitawapelekea wananchi laki moja pale, watatupiga risasi hawatatumaliza, watajiua wenyewe baadaye. Tangu mwaka 1994 Wakurya wanauawa kama wanyama hata Profesa Maghembe hapa ukigusa swala pale porini hawezi kukubali. Huyu hapa na TANAPA yake gusa swala mle ndani uone kama atakubali, sembuse mtu? Watu wanauawa kama wanyama halafu sisi tukae hapa tunapiga makofi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakuomba Profesa tunaomba suala la wachimbaji wadogo lile lipatiwe ufumbuzi. Watu wapate eneo kwa sababu mzungu amekuja akawakuta wanachimba Nyabirama, amewakuta wanachimba pale Nyarugusu, amechukua lile eneo hamjatengea wananchi maeneo. Bila kufanya hivyo mgogoro ule hautaisha, tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu, tutaunda kamati na kamati. Achilia mbali DC amekwenda pale amehamisha mto, tulikuwa na wewe unaona pale, umemuhoji bila aibu DC anafanya maamuzi ya kuhamisha mto sasa ule mto mvua ikinyesha una flood kwenye mazao ya watu kwa sababu ya maslahi ya wazungu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, DC anakuja pale siku mbili anajifanya mkali, wazungu wanamchukua wanamweka mfukoni tayari anaanza kuimba nyimbo za wazungu kama yule wa pale. Sasa hivi ukigusa mgodi anasema ua, ndiyo suluhu anayoona. Kwa hiyo ninakuomba Profesa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili yale magari ya mgodi yanayosomba mafuta, tuko karibu kuyawekea magogo kuyazuia yasitembee kwenye barabara zetu, kwa sababu yale magari wazungu wale hawarekebishi barabara, Halmashauri tunahangaika na barabara kwa vifedha vyetu vidogo wao wanatembeza mzigo mkubwa. Kama wanataka warekebishe ile barabara yao ya chini ya mgodi, ile ya kule chini watembeze magari yao. Wakipita huku juu ntawahamasisha wananchi wataweka magogo watayapiga mawe. Hatuwezi kukubali watembeze pale, hawaleti hela pale wanataka watembeze, wanatembezaje magari kwenye barabara yetu pale? (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mwisho, Profesa kuna uamuzi unaweza ukafanya ambao hautakusababisha upigiwe makofi sana…
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Heche, muda wako umemalizika.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge hili ni chombo cha wananchi na nataka niseme Bunge hili lingefanya kazi yake kama chombo cha wananchi na siyo vikao vya vyama, hii bajeti ya Mheshimiwa Maghembe ilikuwa haipiti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri alikwenda kwenye tv anasema wafugaji wanatembea nyuma ya mikia ya ng‟ombe. Waziri anasema ng‟ombe hawana faida, kwanza faida yao Pato la Taifa wanachangia asilimia nne tu! Kwamba utalii sijui unachangia asilimia 22. Sasa unajiuliza hivi leo tungekuwa tumeondoa ng‟ombe wote katika nchi hii, kama sukari tu imetushinda kuagiza, nyama ninyi mngeweza kuagiza watu wakala nyama? Sukari peke yake imetushinda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kila kitu kwenye ng‟ombe ni pesa, maziwa, kwato, kila kitu! unachotupa pale labda ni sauti tu peke yake. Kila kitu kwenye ng‟ombe ni pesa. Tumeshindwa wenyewe kusimamia ng‟ombe hawa, leo watu wanasimama kwenye Bunge la Watanzania wanasema ng‟ombe wanaharibu mazingira, kwamba mifugo inaharibu mazingira. Ni utafiti wa wapi huo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Dar es Salaam watu wanatumia mkaa, nchi nzima ni mikaa. Watu wanakata miti kwa ajili ya mikaa, watu wanatumia nishati, tumeshindwa kupelekea watu nishati tunasema mifugo inaharibu mazingira. Hata mkiua ng‟ombe wote nchi hii halafu mkaacha watu wakaendela kutumia mkaa, nchi hii itakuwa jangwa. Pelekeeni watu nishati Dar es Salaam, pelekeeni watu nishati rahisi Arusha na Mwanza, Majiji matatu peke yake mki-control watu wasitumie mkaa kesho yake nchi hii itakuwa kijani tupu. Leo mnakuja kusema ng‟ombe anaharibu mazingira, ng‟ombe anakata mti? Hiyo haikubaliki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri Maghembe ukumbuke kwenye Bunge la Katiba aliwaita wafugaji nyumbani kwake akawanunulia chakula anawashawishi wapigie Katiba kura, leo unawaita kwamba wanaharibu, unasema ng‟ombe anaambukiza magonjwa, hauli nyama ya ng‟ombe wewe? Utakula pundamilia kila siku kweli? Hilo ni vyema likaeleweka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna vijiji vimeingia kwenye migogoro na TANAPA na mbuga kwa sababu watu wa mbuga wana extend mipaka yao. Vijiji vya Nyanungu, Kegonga, vijiji vya Masanga, hivi vijiji mpaka mwaka 1963 vilikuwepo na vina GN! Baada ya mwaka 1963 mipaka ya mbuga imekuwa extended, ni migogoro kila siku watu wanauawa.
Mheshimiwa Waziri ninaomba Kata tatu hizo nilizozitaja, Kata ya Kwihancha, Kata ya Nyanungu, Kata ya Masanga - Gorong, I mean uende pale ukatatue ile mipaka, vile vijiji vilikuwa nje ya mbuga na mipaka ya TANAPA ndiyo imekuwa extended kufuata mwananchi na mnawahamisha hamna sehemu wanayochungia ndiyo maana inaleta migogoro. Kwa hiyo, hilo nilitaka niliseme.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo leo tungekuwa tuna Bunge la Wananchi tusingepitisha bajeti hii ni Operesheni Tokomeza. Nina picha hapa, naomba karatasi moja ije mezani kwako na nyingine iende kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2013 watu waliuawa, watu walichomewa nyumba zao, mifugo ilipigwa risasi, ng‟ombe anauawa, ng‟ombe anaua tembo. Mbuzi waliuawa, watu wakabaki wanalala nje, Bunge likaja likajadili hapa, mkasema watu walipwe fidia. Kuna watu waliuawa kinyama, panga linachomwa moto mtu anaambiwa akanyage kwenye panga, akikanyaga akitoa mguu nyama inabaki pale, watu walipigwa misumari. Bunge likaja likajadili hapa, hakuna kitu chochote mpaka sasa kilichozungumzwa kwenye bajeti hii ya Serikali kwamba hawa watu wanakwenda kulipwa vipi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana Serikali wanapokuja ku-wind up hapa watuambie hoja ya operesheni tokomeza, ambayo ilitokomeza watu wetu, watu maskini! Madiwani, Wenyeviti wa vijiji na mpaka leo majangili wakubwa hawajaguswa na operesheni hii. Hawakuguswa na hawajaguswa. Ninyi wote ni mashahidi mnakumbuka hapa, Al Jazeera walitangaza na BBC kwamba Rais wa China alipokuja Tanzania aliondoka na meno ya tembo. Hamkuwahi kukanusha. Wachina kila siku ndiyo wanakamatwa kwa sababu Serikali yetu inakwenda kupiga magoti kwa Wachina kila siku hamtaki kushughulika na Wachina. mnakuja kushughulika na watu wanyonge! watu maskini. Leo mnasema utalii, utalii huu, mimi sikatai kwamba utalii uwepo na unachangia kwenye Pato la Taifa lakini utalii unagusa mwananchi wa kawaida kule chini kweli kwa maisha yake? Mpaka pesa hizi zije kwenu, mje mzishushe ziende kwa wananchi, mzunguko wenu, mnaweza kweli? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu akiwa na matatizo atauza ng‟ombe wake, atatibu mke wake, atasomesha mtoto wake, atafanya maendeleo yake binafsi kwa pesa zake. Lakini pesa ambazo zinaingia Serikalini hatukatai, tunahitaji pesa hizi zije Serikalini, lakini ni lini mtazishusha ziende kwenye maendeleo ya mtu mmoja mmoja kule kijijini? Ng‟ombe ana mfungamano au mifugo ina mfungamano na maisha ya watu moja kwa moja ya kila siku.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba anapokuja ku-wind up hapa Waziri atuambie, hatukatai wafugaji watengewe maeneo, wapate maeneo yao ya kulisha, lakini leo tusije hapa tunawapaka rangi kana kwamba wafugaji hawafuati sheria, wafugaji siyo watu wazuri, wafugaji wanahonga Mahakama, yaani kila anayesimama hapa, kuna watu wanafikiri ng‟ombe ni mdudu lakini nyama ya ng‟ombe wanataka kula. Wamesimama huku wanazungumza mpaka wanatetemeka, wanasema tupigwe risasi. Tupigwe risasi kwenye nchi yetu? Tuna kosa gani sisi? Sisi ndiyo tunawaletea nyama mnakula kila siku hapa kantini nawaona pale mnabugia nyama, supu, makongoro sijui nini, yanatoka kwenye ng‟ombe hayo na maziwa, usipoletewa chai ya maziwa unalalamika, unafikiri maziwa ya mbwa hayo? Hayo ni maziwa ya ng‟ombe ni lazima yatoke kwenye ng‟ombe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ninaomba watu wasizungumze hapa kudhalilisha watu wengine na wakazungumza kana kwamba hii nchi ni ya kwao peke yao. Hatukatai tunahitaji wakulima walime, tunahitaji na wafugaji tupewe nafasi ya kufuga katika nchi yetu.
Ninaomba sana Mheshimiwa Maghembe unapokuja hapa utuambie hawa watu waliouawa kwa mfano kule kwangu waliuawa Peter Maseya alipigwa vibaya sana na akauawa na familia yake mpaka sasa iko traumatized. Aliuawa Nicholas Wegesa Moserega, Mheshimiwa Waziri uje hapa utuambie nyumba zilizochomwa moto, ng‟ombe waliouawa kwenye Kata zile tatu zaidi ya ng‟ombe 184, uje utuambie majibu yake ni nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais aliunda Tume ya Majaji kwenda kuchunguza na mnachukua vitu hivi kwasababu mmeshawaona Watanzania ni wasahaulifu, mnachukua mnavitunza, mnaunda Tume, hamtoi majibu mnakalia yale majibu. Tunataka hayo majibu tuambiwe ni nini findings za hayo majibu na ni kwa vipi tunakwenda kuondoa matatizo yaliyojitokeza.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii adimu ili nichangie na kwa sababu siku hizi maisha yangu yamekuwa mahakamani kwa muda mrefu, leo nimepata fursa ya kuchangia niseme machache.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii nchi ni yetu sote na hata kama mtafanya kiburi na kudharau wenzenu na kufikiri mna mamlaka ambayo hayajawahi kutokea duniani hapa, hakuna jambo jipya hapa duniani. Mwaka 2016 tulijiwekea mipango kwenye kitabu hiki ambacho kina mpango wa 2016/2017 - 2020/2021 ambapo kwenye kitabu hiki ndiyo tunatohoa mpango wa mwaka mmoja mmoja ambao tunaujadili leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamezungumza sana wenzangu, nami ningependa miongoni mwa maeneo ambayo nataka nichangie ni kwenye hili eneo la ukurasa wa 11. Najua Mheshimiwa Dkt. Mpango tunakuonea sana huna mamlaka na haya mengine yanaagizwa.

Hata hivyo, kwenye mambo ambayo mliahidi kwenye malengo hapa ni kuhakikisha kuwepo kwa mgawanyo wa madaraka, kukuza demokrasia, uvumilivu wa kisiasa na kijamii. Kwa mara ya kwanza kwenye historia ya nchi hii tangu kuanza mfumo wa vyama vingi hata mwaka 1995 ambapo ndiyo introduction ya mfumo wa vyama vingi ilikuwa inaanza kwa mwanzo kabisa ambapo watu walipaswa kuwa na hofu, mambo yaliyofanyika kipindi kile hayakuwa mabaya kama yanayofanyika leo miaka 27 baada ya mfumo wa vyama vingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkuki kwa nguruwe kwa binadamu ni mchungu sana na what goes around comes around. Watu wa chini kabisa akinamama, vijana na wazee, wamekwenda kuchukua fomu za kugombea ujumbe wa Serikali ya Kijiji, Uenyekiti wa Kitongoji na Uenyekiti wa Kijiji ngazi ya chini kabisa ambapo migogoro mingi wakati mwingine inatokea huku kwenye levels za Ubunge na nini haiwagusi moja kwa moja kule chini, kule chini kuna watu wanachaguliwa siyo kwa sababu ya vyama vya kisiasa, uchaguzi wa kitongoji wakati mwingine hauangalii chama unaangalia ni nani aliyesimamishwa kwenye eneo husika na ana nguvu kiasi gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mathalani, tunaishi kitongoji kwenye kijiji chetu pale Kitagasembe kinaitwa Chelela, Kitongoji cha Chelela, baba yangu alikuwa Mtemi, alikuwa na wanawake wanane, sisi peke yetu kwenye familia ya mzee Heche tupo zaidi ya watu 90 pale; chukua vijana ambao wameoa, wameolewa pale. Kwa hiyo, ukichukua basically kile kitongoji ni watu wa ukoo mmoja tu. Leo kwa sababu mnajiona mna nguvu eti mnataka muende ku-impose mtu kuongoza watu ambao hawamtaki, anashirikiana nao vipi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na watu wazima na akili zetu tumekaa humu juzi Mkurugenzi ameita watu Chuo cha Ualimu Tarime pale wanapitia fomu, Mkurugenzi anafundisha mtendaji kufanya forgery. Maswa Wilaya nzima ya Maswa yenye Majimbo mawili watendaji wamekimbia kwa siku saba hawaingii ofisini eti watu wapiti bila kupingwa na nyie mpo humu mnaona ni kitu cha kawaida kinachofanyika kwenye nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka niwaambie, mmechukua chuki mmeipeleka mpaka kwenye level ya kitongoji na kwa sababu ya kiburi hamtaelewa haya ninayoyazungumza lakini mwanzo mzuri utaanza tu mwakani na nyie wenyewe ndani yenu na mtai-feel. Na hilo linatosha na niishie hapo lakini nataka niwaambie kwanza mmejitia aibu ambayo haijawahi kutokea…

DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE: Na kwa mara ya kwanza inathibitika kwamba CCM pamoja na kujifanya ni chama kikubwa…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche…

MHE. JOHN W. HECHE: Na ni chama chenye nguvu na ni chama ambacho…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche naomba usubiri taarifa, kuna taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, please!

MWENYEKITI: Kuna taarifa, Mheshimiwa Dkt. Mollel taarifa…

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, please!

T A A R I F A

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kumpa taarifa Mheshimiwa Heche kwamba yeye hafikiri kwamba kile kikao chetu tulichokaa kwa Mheshimiwa Komu tukijadili wizi wa rasilimali za chama na tukasema hilo litatuathiri kwenye uchaguzi na uwezo wa sisi kusimamia uchaguzi kwa sababu ukiangalia hata makatibu wa CHADEMA wilaya zote na kata walishindwa kuwezeshwa ili kufika chini kuweza kuwasaidia na kusimamia utaratibu mzima wa ujazaji fomu na vitu..

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche naomba uendelee

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: ndio sasa madhara yake haya ambayo tulitaka kumpindua Mbowe kwa ajili hiyo wewe ukatusaliti wakati ule huwezi kufikiri?

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri hata anaweza kuaminika kidogo baada ya kusema hayo, sio?

MWENYEKITI: Taarifa hiyo sema wewe kwamba umepokea au hujapokea.

MHE. JOHN W. HECHE: Anaweza kuaminika kidogo baada ya kusema hayo?

MWENYEKITI: Usiniulize mimi sema wewe umepokea au hujapokea?

MHE. JOHN W. HECHE: Ndio namuuliza sasa kupitia wewe. Kwa hiyo…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche hiyo taarifa umepokea, hujapokea?

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, please hiyo sio taarifa, haihusiani na tunachozungumza.

MWENYEKITI: Basi endelea.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa kuna mambo ya nchi ambayo tumejiwekea malengo ya kuyatekeleza na yapo kwenye vitabu vyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimesema mambo haya ya kihuni, mambo ya forgery, aibu mnayoyaleta na mnafundisha watendaji wa Serikali wakianza kufanya forgery kwenye mambo ya kiserikali kule chini ikiwemo kuiba pesa za wananchi, sitegemei kuona mnalalamika kwa sababu nyie wenyewe ma-DC na RC wamekaa wanafundisha watu kufanya forgery, hilo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili…

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utaratibu.

MWENYEKITI: Kuhusu utaratibu, Mheshimiwa Chief Whip.

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kutumia kanuni ya utaratibu lakini inayoendana na kanuni ya 64 lakini vilevile itaambatana na kanuni ya 61, nitakwenda kwenye 61(a) na nitakwenda pia kwenye kanuni ya 61(f).

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashindwa kuendelea kumvumilia Mbunge anayechangia. Mbunge anayechangia anataka kulithibitishia Bunge hili kwamba Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi huko walipo wameitisha vikao na kuwafundisha watu kufanya forgery, tuhuma hizi ni nzito na kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuwezi tukakaa hapa ndani ya Bunge tukatoa tuhuma kubwa kama hizi kwa viongozi wenye madaraka walioaminiwa ndani ya Serikali kuwahudumia wananchi na Mbunge mmoja tu humu ndani kwa interest zake…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, anayezungumza sasa ni Mbunge mmoja sio wote…

WABUNGE FULANI: Wote

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Akaamua kujenga
tuhuma hizo nzito na tukamuacha amalize mchango huu bila kutumia kanuni hiyo ya utaratibu ndani ya Bunge, tunachokijua wote utaratibu unaongozwa na sheria na kanuni. Na kwa mtu yeyote ambaye anaona utaratibu umevunjwa na Waziri wa TAMISEMI ameshatoa maelekezo mazuri na kila mtu ana haki…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: …ya kupeleka tuhuma hizo kwa msingi wa utaratibu wa kisheria, ninamuomba Mheshimiwa Heche ama atoe uthibitisho wa hao Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi waliokuwa wamewafungia watu na kuwafundisha kufanya forgery kwa kuzingatia kwamba kwa mujibu wa sheria hao wote anaowataja wanatambulika kisheria kwenye dhana nzima ya uchaguzi huu ama afute kauli yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini vilevile, ninaendelea kukiomba kiti chako Mheshimiwa Heche atumie lugha yenye heshima ambayo haitadhalilisha watu wengine ndani ya Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba mambo haya ya utaratibu niyalete mbele yako Heche afute hiyo kauli na kama hafuti atuletee uthibitisho. (Makofi)

MWENYEKITI: Asante Mheshimiwa Chief Whip, Mheshimiwa Heche nilitegemea baada ya kuzungumza hivyo utakuwa na ushahidi hapo mkononi wa kutuonesha hayo uliyasema. Kwa vile huna ushahidi kwa hiyo naomba ufute hiyo kauli yako na usiendelee tena kutoa tuhuma nzito ambazo huna ushahidi hapo ulipo na vinginevyo nitakuzuia kuzungumza.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, sitashangaa kama utanizuia kuzungumza na sitashangaa kama utavunja kanuni, kanuni inasema mnipe muda nithibitishe. Nimesema hapa Wilaya nzima ya Maswa watendaji siku saba, Majimbo mawili hawakuingia ofisini. Nimesema Tarime Mkurugenzi ameita watendaji baada ya kupokea fomu wamekaa nao chuo cha ualimu, naweza kuwathibitishia, give me time? Sasa ndio kanuni inavyotaka sasa unaniambia sina ushahidi una uhakika gani kwamba sina ushahidi? (Makofi)

MWENYEKITI: Hukusema kama unao, endelea haya.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, tafadhali sana. Kwa hiyo, jambo la pili…

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa sasa umeanza usumbufu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche naomba usubiri.

MHE. JOHN W. HECHE: Ndio kanuni ilivyo

MWENYEKITI: Naomba usubiri, Mheshimiwa Chief Whip taarifa.

T A A R I F A

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimetoa jambo la utaratibu, ninarudi jambo la taarifa kwa mujibu wa kanuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kumpa taarifa Mheshimiwa Heche na Wabunge wengine wote katika dhana hii ya kusimamia uchaguzi, vyama vyote vilishirikishwa, vikapewa maelekezo…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: …na vikapewa maelekezo lakini licha ya kupewa maelekezo…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MWENYEKITI: Waheshimiwa naomba mtulie amalize taarifa.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: …na wewe mlokole?

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge naomba tusikilizane kila mtu atasikilizwa, Mheshimiwa Jenista naomba uendelee.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, sauti za mlango huwa hazimzuii mwenye nyumba kulala kwa hiyo hazinisumbui sauti zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninarudia kusema wapo wajumbe na wagombea, naomba nieleweke, wapo wagombea kupitia hata kwenye vyama vingine ambao walikutana na kupewa maelekezo ya kujaza fomu lakini ni hivyohivyo utaratibu wa kutoa maelekezo kwenye chaguzi zozote ni lazima msimamizi atoe semina na maelekezo kwa wasimamizi wake.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa
Mwenyekiti, ninataka hawa wanithibitishie katika vikao hivyo vya maelekezo Mheshimiwa Heche ana uhakika vikao vya maelekezo vilikuwa ni vya kufundisha forgery?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba mwongozo wangu wa utaratibu uzingatiwe na ninaomba kumpa taarifa Heche, vikao ni mahali popote katika kutoa maelekezo na sio kufundisha forgery.

MWENYEKITI: Waheshimiwa tusikilizane…

MHE. JOHN W. HECHE: Dakika saba za Mheshimiwa Heche zipo!

MWENYEKITI: Zipo dakika zako lakini urudi kwenye mpango kwa sababu huko unapokwenda Serikali za Mitaa na mambo mengineyo sio ishu muhimu kama hivyo unasema, Serikali inafanya kazi yake na hizo tuhuma ulizonazo hazina uthibitisho kwa sasa hivi huna wewe hapo ulipo. Kwa hiyo, kama unazo utaleta kwa wakati wako lakini wakati unatayarisha hizo tuhuma endelea na mpango mwingine.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, now that’s leadership, nakushukuru sana kwa sababu wanakupa pressure anyway.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo ukurasa wa 111 kwenye hiki kitabu, kujenga demokrasia, kuimarisha uvumilivu, kujenga mihimili ya Serikali kuheshimiana sasa ndio maana Serikali wao wanafikiri wana nguvu kuliko Bunge humu, ndio kiburi wanachopata. Ukiona hayo yote ni kwa sababu wanajiamini wao labda wapo…

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utaratibu.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine…

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utaratibu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbatia subiri.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utaratibu.

KUHUSU UTARATIBU

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninaamini heshima ya kusikilizana ni jambo la heri sana na maandiko yanasema kujibu kabla ya kusikiliza inaweza ikawa sio nzuri kwako, nisingependa kuendelea zaidi hapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo anayozungumza Mheshimiwa Heche nilitaka nimpe tu taarifa kwamba ushahidi wa hao Wakurugenzi wanayoyafanya upo hapa kwa halmashauri nzima ya Wilaya ya Moshi nina vielelezo na Waziri ana vielelezo vyote hivi tangu jana mambo gani yanayofanyika. Kwa hiyo, haya mambo ni kweli yanafanyika na sio Tarime tu kwa hivyo nimempa Heche anayechangia taarifa hiyo ili aweze kujua kwamba ni sahihi kwa ajili ya ustawi, amani na utulivu wa nchi yetu ili tuweze tukaisimamia Serikali vizuri na kuishauri Serikali vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimempa taarifa hiyo. (Makofi)

MHE. JOHN W. HECHE: Asante sana.

MWENYEKITI: Sawa kabla hujaendelea Mheshimiwa Heche, Mheshimiwa Mbatia unasema kwamba vielelezo hivyo Mheshimiwa Waziri anavyo tayari, kwa hiyo kama anavyo tayari ina maana Serikali tayari imeshajua na kuna ruling yake ambayo imeshatolewa kwa hiyo sioni kwa nini mnazungumza tena hilo tena. Kwa hiyo, Mheshimiwa Heche naomba uendelee na mengine.

MBUNGE FULANI: Serikali imekataa, mbona imekataa mbele ya…

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante napokea taarifa, nashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, kuhusu Mchuchuma na Liganga; kwenye hiki kitabu Mheshimiwa Dkt. Mpango ulituambia kwamba Serikali yenu imekusudia kuendeleza mradi wa Mchuchuma na Liganga. Huu mradi mwaka 2009 Serikali iliingia mkataba na Kampuni ya Sichuan Hong Gold ya China na tukaunda kampuni moja kati ya kampuni ya China ya kwetu ya Watanzania na Serikali. Serikali ikiwa na 20% na kampuni ya Sichuan Hong Gold ikiwa na asilimia 80, mwaka 2009.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mwaka 2010 ndio mradi huu ilikuwa uanze, tuna mashapo ya makaa ya mawe pale tani milioni 428, tuna chuma pale tani milioni 125. Ule mradi ulikuwa una investment ya dola bilioni 3, zaidi ya trilioni 6.8, in fact ndio ungekuwa mradi mkubwa kuliko miradi mingi yote ambayo imeingiwa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ule mradi ulikuwa unaleta ajira kwa Watanzania direct zaidi ya 5000 na ulikuwa unaleta indirect ajira zaidi ya 30,000. Tangu mwaka 2009, leo tunazungumza miaka 10 baadaye mradi ume-delay, hakuna kinachoendelea, tunaandikiana kila mwaka Mchuchuma na Liganga lakini Watanzania ambao mliwaahidi kwenye uchaguzi kwamba mtawapa ajira hakuna ajira mnazotoa, watoto wa watu wamemaliza shule wamerudi vijijini hawana kazi ya kufanya na nyie mnakalia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnataka Watanzania waliopo kule kwetu waliomaliza ualimu na wao waanze kuimba flyover, ndege ambayo ndege nyie wenyewe mmethibitisha kwamba mmenunua ndege kwa zaidi ya trilioni 1 na bilioni zaidi ya 500 halafu kwa miaka 3 eti imewaingizia bilioni 30.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yaani mmenunua ndege trilioni 1 na bilioni zaidi ya 500 miaka 3 juzi Waziri anaulizwa na Rais anasema tumeingiza dola milioni 14, bilioni 30 wa miaka 3 kwa investment ya trilioni 1. Kwa hiyo, mtachukua miaka zaidi ya 80 kupata trilioni 1 na bilioni 500 ambazo mme-invest pale. Na mnataka Watanzania wote tukae tunaimba ndege ndege. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Heche.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Kuhusu Shughuli za Kamati Kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kwa kunipatia nafasi leo ya kuchangia kwenye Kamati hizi, nami nitajikita zaidi kwenye Kamati ya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa miaka ni 50 baada ya uhuru wetu tunapozungumza suala la umeme. Rafiki yangu Mheshimiwa Kalemani nampenda sana kwa sababu ni mtu msikivu, lakini tunapozungumza suala la umeme nchi hii, Watanzania waliounganishiwa umeme ni 2,800,000; yaani kwa miaka yote ambayo CCM wako madarakani wameunganishia umeme Watanzania 2,800,000. (Makofi)

SPIKA: Chanzo cha data yako Mheshimiwa.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, hizi ni data za Kamati. Mimi ni Mjumbe, naomba nichangie, baadaye wataniuliza. (Kicheko)

SPIKA: Ni vizuri tuwe tunaelewana. Kaya 2,000,000 au watu 2,000,000?

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, ukisema kaya, ukisema wateja, ndiyo wateja hao!

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, mimi nazungumzia wateja.

SPIKA: Kuna tofauti kubwa kati ya kaya na watu.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, nazungumzia wateja ambao wameunganishiwa umeme na ndiyo takwimu tulizonazo. Mmeunganishia umeme wateja 2,800,000 tu.

SPIKA: Hiyo takwimu ina makosa makubwa ya kiuandishi.

MBUNGE FULANI: Ndiyo hivyo.

SPIKA: Kaya moja inaweza ikawa na watu 20 humo ndani na kila chumba kina umeme, lakini TANESCO watahesabu kwamba huyo ni mteja mmoja. Kwa hiyo ukichukulia kwamba ni watu milioni mbili kwa kweli is wrong lakini endelea. Mtunze muda wake. (Makofi)

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, naomba sana muda wangu tafadhali.

SPIKA: Ninasisitiza muda tu.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, hiyo ni taarifa ya Wizara kuhusu wateja waliounganishiwa umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukisema hata kaya, kwani nchi hii ina kaya ngapi? Ni nyingi tu. Ukichukua kama tuna wateja 2,800,000 na hapa hatuzungumzi kwamba tuna-shortage ya umeme. Hivi tunavyozungumza tuna excess ya umeme zaidi ya megawatt 200 na kitu au 300.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, watu wapo wanahitaji umeme na leo wakati Mheshimiwa Waziri wa Maliasili anajibu swali hapa, amezungumza kuhusu jinsi ambavyo nchi yetu misitu inakatwa kwa wingi sana, nchi inaendelea kuwa jangwa kwa sababu watu hawana nishati mbadala, wanategemea mkaa, kuni na hata Wabunge humu asilimia kubwa tunapika kwa kutumia mkaa na kuni kwa sababu hatuna umeme wa kutosha wa kupelekea watu nishati kule vijijini waache kupeleka hii nchi kuwa jangwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nafikiri huu ni mwaka wa uchaguzi na lazima mjipime kwamba kwa miaka 50 wateja 2,800,000 na umeme mnaufanya kuwa kitu cha anasa, yaani kwamba mtu akiunganishiwa umeme anaonekana yuko privileged. Watu wapo, wanahitaji umeme. Hata hili suala la kusema sijui kuna gharama ya kuunganisha umeme, hivi wewe TANESCO unafanya biashara, mtu yuko tayari umuunganishie umeme, unamuunganishia kwa gharama ya kufanyia nini? Mara sijui nunua nguzo, mara sijui; huyu si ni mteja atakulipa bili kila mwezi! Kwa nini umwambie kwamba kunahitajika gharama? (Makofi) (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, sasa haya ndiyo yanafanya tunasema CCM na Serikali yake mmeshindwa, mnapaswa kutoka madarakani waingie watu wengine ambao watapeleka umeme bure na watafikisha umeme kwa watu wengi kwa kipindi kifupi. Hilo la kwanza hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, hii nahamia kwenye masuala ya madini. Mheshimiwa Doto mwaka 2019 mwezi wa 12 mmewapa watu barua pale matongo…

SPIKA: Mheshimiwa kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Waziri.

T A A R I F A

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, napenda tu kumpa taarifa Mheshimiwa Mbunge anayezungumza, nimemsikiliza kwa makini sana kuhusiana na takwimu anazozitoa ambazo tunaamini zinaweza kupokelewa na wananchi zisieleweke vema.

Mheshimiwa Spika, kwanza ni kweli unapohesabu wateja haulinganishi na idadi ya watu, hilo ni jambo la kwanza. Unaweza ukawa na mteja mmoja lakini umeme unaotumiwa na watu katika mteja huyo mmoja wakawa 100 au 200. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hiyo taarifa ikae vizuri kwamba tunapozungumza wateja hatulinganishi na idadi ya watu. Hilo ni jambo la kwanza. Jambo la pili, access ya umeme kwa sasa mijini umeongezeka kutoka asilimia 97 mwaka 2015 hadi 92.2 mijini na umeongezeka kutoka asilimia 49.5 vijijini hadi asilimia 72.5. Hii ni access ya kutumia umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ili kuweka kumbukumbu pia vizuri kwamba Serikali pamoja na hayo; na pamoja na umeme wa access unaobaki wa zaidi ya Megawatt 280 siyo kwamba Serikali haiendelei kujaziliza ule umeme mwingine, tunaendelea kuzalisha umeme na ndiyo tumeanza na mradi mkubwa wa Julius Nyerere wa megawatt 2,215 ili kufanya sasa umeme nchini kuwa wa uhakika ili wananchi waweze kufanya shughuli za kiuchumi kwa ajili ya shughuli za viwanda.

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, amechukua dakika mbili uniangalizie…

SPIKA: Aah dakika zako nazitunza kabisa.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

SPIKA: Anakusahihisha tu kwamba umewahi kusoma takwimu huko nyuma, yaani ukaelewa statistics? Endelea kuchangia Mheshimiwa.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, Mawaziri wakianza kujibu sasa hivi sijui watafanya kazi gani mwishoni wakija ku-respond! (Makofi)

SPIKA: Anaweka sawa sawa hesabu yako.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, kwani amezungumza nini tofauti na nilichosema?

MHE. ESTHER N. MATIKO: Eti!

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, amesema kuna wateja 2,800,000…

SPIKA: Amesema kwamba unaweza … Amesema kwamba …

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, wateja 2,800,000 miaka 50 …

SPIKA: Subiri kidogo …

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Aje Waziri!

SPIKA: Amesema unaweza ukawa na mteja mmoja ana kiwanda lakini ana watu 500 ameajiri ndani ya kiwanda kile. (Makofi)

Kwa hiyo, ukimchukua huyo mteja kama ni mmoja na ukalinganisha na idadi ya watu, ulinganisho huo siyo sahihi.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, naomba niendee, Watanzania watasikia. Wateja 2,800,000. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimemwomba Mheshimiwa Doto, watu wa Matombo mmewaandikia barua na sasa hivi Serikali ina hisa kwenye Barrick, mmewazuia kuendeleza maeneo yao, watu wanashindwa kuzika ndugu zao pale kwenye maeneo yao kwa sababu wakizika baadaye mtasumbuana.

Mheshimiwa Spika, wanashindwa kuendeleza nyumba zao tangu mwaka jana, 2019. Naomba muwalipe wale watu, msitengeneze mgogoro mwingine kama ile iliyokuwa inatengenezwa baadaye mnawaita tegesha. Lipeni wale watu tafadhali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, mwaka 2017 iliundwa Kamati ya Mruma na Mheshimiwa Rais. Kamati ikaenda kuchunguza baada ya makontena kukamatwa kwamba yalikuwa yanasafirisha madini yetu, wana-under revalue wanatoa gharama ya chini kuliko ambacho walikuwa wanauza na kupata mwaka 2017.

Mheshimiwa Spika, baadaye ikaundwa Kamati ya Osoro ikiwa na wanasheria na wachumi kwenda kuangalia gharama halisi ya madini yaliyokuwa mle. Tukaambiwa baadhi ya madini ni ya thamani mno hata ambayo tulikuwa hatujawahi kuambiwa hapa na ikasemekana kwamba kwa miaka yote Barrick wametorosha, wamekwepa kodi dola bilioni 190 ambazo ni sawa sawa na shilingi tririoni 400 na kitu.

Mheshimiwa Spika, TRA wakafanya assessment wakathibitisha Kamati ya Osoro ilichokisema kwamba kumetoroshwa shilingi trilioni 420 na hiyo ikapelekea kuletwa sheria nyingi, baadaye nitazizungumza hapa. Sheria mbili; Sheria ya Permanent Sovereignty of Natural Resources na nyingine.

Mheshimiwa Spika, naanza na shilingi trilioni 426 tulizoambiwa. Juzi ambapo Mheshimiwa Rais alikuwa anasaini mikataba tisa walikuwa wanaingia agreement na Barrick, hatujasikia popote wanazungumza kuhusu shilingi trilioni 426. Sasa nataka wanijibu, hizo fedha mmezisamehe? Mmesamehe mabeberu shilingi trilioni 426 za Watanzania? Je, kama hamjasamehe, hiyo Kamati ya akina Mheshimiwa Kabudi iliyokuwa inafanya majadiliano, ina mamlaka hayo. Kwa sababu Sheria ya TRA Kifungu cha 14 kinasema, kama assessment imeshafanyika, hamwezi tena kufuta hiyo assessment mpaka Bodi ya TRA ikae na Waziri a- gazette. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Heche nakukumbusha tu, siyo wewe peke yako na wachangiaji wengine; ni vizuri sana kuzijua taratibu za Kibunge. Taarifa iliyoko mezani, aliyetoa hoja ni Mwenyekiti wa Kamati. Sasa baadhi ya michango: Je, huyo Mwenyekiti wa Kamati ndiye aliyeingia huo mkataba? Yaani kweli Mwenyekiti atakuja kujibu haya maswali unayosema au ni kitu gani? Kwa sababu hoja hii siyo ya Waziri, ni hoja ya Mwenyekiti wa Kamati kuhusiana na kazi za Kamati za mwaka mzima. (Makofi)

Kwa hiyo, tunapochangia hapa, tuwe tunaelewa hoja hizi tunazielekeza kwa nani. Kwa hiyo, nikumbushe tu, hoja hizi mbili tunapokuwa tunachangia tunazielekeza kwa Mwenyekiti wa Kamati, tunaishauri Kamati, tunalishauri Bunge na Serikali pia. Kwa hiyo, nilitaka tu kuweka hilo vizuri.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana…

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Spika, naye ni mjumbe wa Kamati…

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, najua Mawaziri wanapata muda wa kuchangia...

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mpaka dakika 20, 30...

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, mpaka dakika 20, 30 Mheshimiwa Mkuchika alifanya hivyo jana hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi ni Mjumbe wa Kamati, haya ni mawazo ambayo nilitoa kwa sababu unajua wingi wetu mle kwenye Kamati. Kwa hiyo, naomba nichangie.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunahitaji majibu kuhusu hilo, kwamba shilingi trilioni 426 sita ziko wapi? Zimesamehewa au hazijasamehewa?

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, kuna kitu kinaitwa kishika uchumba, dola milioni mia tatu zaidi ya shilingi bilioni 600 na kitu, hizo mlisema kwamba zitalipwa na mabeberu haraka sana kabla ya mjadala. Hizo shilingi bilioni 600 Serikali imekubali sasa kwamba walipwe kwa installment kwa kipindi cha miaka saba na ukiangalia zaidi ya shilingi bilioni 240 zinakwenda kwenye VAT, refund hakuna cash yoyote inayoingia kwenye Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nauliza, wale wazalendo waliokuwa wanapiga vigelegele kwanza walipaswa waone aibu hapa kwa sababu walichokuwa wanasema hakipo na hakijapatikana. (Makofi)

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Wazalendo bandia hao!

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, jambo la tatu, smelter. Tuliambiwa…

SPIKA: Ushakula nusu ya muda, sasa chunga huko unakoenda.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, tuliambiwa na sheria ikatungwa kwamba kuanzia sasa madini yote ghafi hayatasafirishwa nje ya nchi, smelter itajengwa hapa hapa na madini yatachakatwa hapa hapa ili tuyape value ndiyo yasafirishwe.

Mheshimiwa Spika, hiyo smelter iko wapi? Tunataka mtujibu hiyo smelter mmejenga wai?

WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Taarifa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba Mheshimiwa Heche ambaye ni Mjumbe wa Kamati anafahamu kila kitu kinachoendelea, kwa sababu amekuwa akiuliza maswali kwenye Kamati, mimi najua nia yake ni pamoja na kunogesha, na kuweza kupata fursa ya kusema. Nataka nimweleza kwamba smelter anayozungumza si kama kujenga kibanda, ni teknolojia kubwa ambayo ukishatoa leseni ujenzi wake hauhitaji wiki mbili au mwezi mmoja. Minimum requement ya time ya kujenga smelter moja kwa watalamu wote walikuja duniani kupresent Wizara ya Madini ni miezi 24. Sisi tumeshatoa leseni yakujenga smelter pamoja na kujenga refinery. Sasa kama tunataka kuzungumza kwa sababu tu tumeamua kuzungumza; mimi nataka Mheshimiwa Heche ajielekeze kwenye haya mambo kwa kusema ukweli walau kwasababu anaufahamu ukweli wenyewe.

MBUNGE FULANI: Mwongo huyo.

SPIKA: Ni ushauri huo ummepewa.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, miezi 24 nafikiri tangu mwaka 2017 imeshapita sasa hivi tunaelekea miezi 26 na kitu. Mimi nichozungumza, kama smelter inajengwa hapa kwa nini juzi mnasema kwamba makontena yatafute mteja yasafirishwe? Kwanini msisubiri mpaka smelter yetu ijengwe makontena yote yale 117 yabaki Tanzania? Kama mnajenga smelter? Ilhali sheria iliyotungwa humu Bungeni kifungu cha 11 ilisema wazi kabisa, sheria, kwamba itakuwa ni marufuku kusafirisha madini nje ya nchi na juzi Rais amesema wateja watafutwe na madini yasafirishwe? Kwanini mnafanya hivyo wakati mnajua mnajenga smelter mnaijenga?...

WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

MHE. JOHN W. HECHE:… No! no! no!

T A A R I F A

SPIKA: Mheshimiwa Waziri, Dotto Biteko, nimekuona.

WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Spika, kwanza sifurahi kujibizana hivi, lakini ikitokea uongo unasemwa hadharani inanisumbua. Nataka nieleze ni kweli sheria ya madini imezuia kusafirisha madini ghafi nje ya nchi, sheria hiyo hiyo kifungu cha 59 kimetoa mamlaka kwa Waziri wa Madini kutengeneza kanuni ya kusafirisha madini yaliyoongezwa thamani kwa kiwango fulani. Kanuni hiyo imechapishwa kwenye gazeti la serikali na kanuni hiyo hiyo imetoa kipindi cha mpito wakati hatujawa na hizo facility kuwe na utaratibu maalumu wa biashara hizo kuendelea, ndio maana biashara zinaendelea kufanyika ndani ya nchi. Ingekuwa ni sheria inayozungumza leo marufuku kesho tungekuwa tunazunguza habari nyingine. Mheshimiwa Heche na sheria hizo anazifahamu ninaomba azungumze kwa kusema ukweli. (Makofi)

SPIKA: Ndiyo maana siku moja niliwahi kuzungumza humu ndani kwamba hili neno upinzani lile neno lina shida, kwamba ni vizuri tukafikia mahala pa kuwa na ushindani badala ya upinzani. Kwa sababu upinzani hata kitu ambacho anakijua fika lazima apinge kwa kupotosha.

Kwa hiyo mnapokuwa ninyi ndio wajumbe wa Kamati ambao mmekaa huko mwaka mzima, Mheshimiwa Heche na wewe ukiwa mjumbe wa Kamati halafu mnatoka baada ya mwaka mnatupotosha sisi ambayo hatukuwa wajumbe wa Kamati sasa where we are going to? Itakuwa ni jambo lisilofaa hata kidogo. Lakini endelea tu, malizia dakika zako.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, mimi nasikitika kwamba sheria ya kifungu cha 11 inaweza kufutwa na kanuni ya Waziri hivi hiyo ya wapi hiyo? Unaojua tunaozungumza huku sio kwamba hatuna akili tunajua hivi vitu tuna akili timamu. Wala hatupigi makofi sisi, tunazungumza jambo mlilolileta hapa na sisi tukawaambia na Lissu akawambia hamtapa hata mbuni iko wapi mbuni mliyopata hapa iko wapi kati ya tirion 400 mlizoandika tukawa laughing stock huko duniani; ipo wapi mbuni moja mliyopata muwaambie watanzania hapa. Sasa mnakuja kama kawaida mnayumba kama upepe kama kesho mpo huku mnapiga makofi tu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tulisema hapa, kwamba mlitunga nyie wazalendo mkasema ninyi you’re a sovereign country; kwamba hakuna kesi itakayokwenda kufanyika nje ya nchi, mlisema humu ninyi wenyewe, tukawaambia nyie mmesaini mikataba mmesaini MIGA na hamtaweza ninyi. Sasa hivi mmeleta Sheria ya Arbitration Act mnakuja kuondoa, mmeruhusu na wamewapa Barrick waiver ya kwenda kutushitaki popote wanapotaka. Sasa hayo mambo Heche akisema kwamba...

SPIKA: Hivi unajua kuna Waheshimiwa Wabunge nawatafuta siwaoni. Mheshimiwa Mwita Waitara yupo wapi leo? Samahani Mheshimiwa Heche endelea bwana. (Makofi/Kicheko)

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, mimi chuma usinione hivi. Unajua wazungu wamekwenda mwezini wamerudi, sisi Waafrika bado tupo kijiji hata aliyeko mjini mawazo yake yapo kijiji vilevile. Sisi tunachozungumza hapa ni mambo tuliyojadili humu; kwamba tulikuja hapa tukatamba tukawatangazia Watanzania.

Mimi nilitegemea juzi mnaposaini mikataba msimame pale pale muwaambie Watanzania eeeh! Trilioni 420 hizi hapa noah kila mtu apate. Sasa mmekosa mpaka kishika uchumba, kishika uchumba mmekosa. Sheria ambazo mlituambia you’re a sovereign country hamuingiliwi mmekwenda kupiga magoti kwa mabeberu mmerudisha sheria humu kuja kuzibadilisha. Nilitegemea Wabunge wengi wa CCM, ambao ndio wengi, muone aibu kwa sababu nyie mliyumba kipindi kile. We told you, tuliwaambia hapa, mkasema oooh sisi tunatumiwa na mabeberu. Sasa sisi na nyie nani anatumiwa na mabeberu?... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Mheshimiwa Heche muda wako umeisha.
Taarifa ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo; na Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi nashukuru kupata nafasi hii na namshukuru sana Mheshimiwa Paresso kwa kunipa muda wake nitumie kuchangia.
Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi niseme mambo machache na niseme pale Wabunge wenzangu walipoishia. Tatizo kubwa ninaloliona mimi hasa kwenye uendeshaji wa Serikali za Mitaa ambazo kimsingi ni Serikali kamili, zimepewa mamlaka yake Kikatiba. Leo kila mtu aliyesimama hapa analalamika, aidha, kwa Wakuu wa Wilaya au Wakuu wa Mikoa kuingilia mamlaka za Halmashauri. Hii inafanyika kwa sababu kila mtu anafukuzia kumfurahisha bosi, Mtukufu Rais.
Mheshimiwa Naibu Spika, yaani watu wanafanya madudu pale na imekuwa utaratibu kwamba watu waliofanya madudu wanapandishwa cheo. Sasa na wengine kule Wilayani anatafuta na yeye nitoke vipi. Mkuu wa Wilaya anatembea nyuma kuna kamera utafikiri anaenda sijui kufanya shooting? Mkuu wa Mkoa naye akitembea nyuma kuna kamera, nionekane huko, Mtukufu anione jioni kwenye taarifa, matokeo yake ni kwamba tunaua Serikali za Mitaa. Tunaendesha nchi hii kama duka. Unajua ukiwa na duka asubuhi unasema ile paketi ya sigara iliyokuwa hapa iko wapi, inatafutwa. Ndiyo hayo yanayotuletea matatizo. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nilikuwa Diwani, leo Madiwani wote wazuri wanakataa kugombea na hili Mheshimiwa Simbachawene unalijua, watu wazuri wanakataa kugombea kwa sababu hawalipwi mshahara, wanalipwa posho. Leo hata ile posho ambayo wanalipwa, Mkuu wa Mkoa anaona ni shida anaenda kuwaondolea posho Madiwani wakati yeye mwisho wa mwezi analipwa mshahara. Kama yeye ni mzalendo kiasi hicho kwa nini asiache mshahara wake? Sasa hii ndiyo level ya unafiki ambayo tunaiwea hapa kwamba Mkuu wa Mkoa anataka kuondoa posho ya Madiwani wakati yeye analipwa mshahara, wao hawana mshahara na mnataka wasimamie fedha ambazo mnapeleka Halmashauri, haitawezekana. Ni lazima tuweke heshima kwa Madiwani, hilo la kwanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili fedha zote zinazopelekwa Halmashauri zinakwenda kwenye vijiji, vitongoji, kule ndiyo kuna watu. Serikali hii ya CCM tumeimba miaka yote kwa nini hamtaki kuwalipa Wenyeviti wa Vijiji fedha kama malipo? Hakuna anayetoa majibu. Wenyeviti hawa wa Vijiji ambao wanafanya kazi kwa hisani kila siku utasikia Mkuu wa Mkoa nimekufukuza kazi, nimewaweka ndani, unawekaje mtu ndani kwa vitisho ambaye humlipi hata senti tano? Kwa hiyo, mimi nafikiri tuliangalie hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, fedha za CAG kufanya ukaguzi. Nyie wenyewe mnasema mnataka kutumbua majipu, kumbe ni unafiki mnataka kujificha madudu yenu myafichie ndani humo. Kheri Mheshimiwa Kikwete aliyeweka wazi watu wakajua, ninyi mnaficha hamtaki kujulikana maovu yanayofanywa, mnamnyima CAG fedha. Wananchi wa nchi hii wajue kwamba Serikali hii ni Serikali isiyotaka kukosolewa ndiyo maana haimpi hata CAG fedha ili aende akakague aone hawa Wakuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya mliyopeleka, walioshindwa kura za maoni za CCM madudu watakayofanya kwa miaka hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, wote mliopeleka ni wale walioshindwa kura za maoni za CCM yaani bora wangewachukua ninyi mlioshinda wakawapeleka kuwa Wakurugenzi kuliko kuchukua mtu aliyeshindwa, amekataliwa na wanachama wenzake kwamba wewe huwezi kuongoza, halafu unamchukua unampeleka eti kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri matokeo yake hajui chochote anayochotakiwa kufanya.
Mheshimiwa Naibu Spika, sitatumia muda wangu kuharibu kwa kumjibu yule najua anachofukuzia nitaharibu sana. Naomba niendelee. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mifuko ya Hifadhi za Jamii watu wameweka fedha zao, wewe unakatwa mshahara wako unaenda pale. Leo inasemekana fedha hizi zilipopelekwa Benki Kuu mmechukua mmeenda kununulia Bombardier, mnawakataza watu kuchukua fedha zao ambazo wamehifadhi. Yaani kijana amefanya kazi mgodini, ameteseka maisha yake amehifadhi kule, anataka kujitoa au amefukuzwa kazi achukue fedha ajengee watoto wake, mnamwambia mpaka miaka 60. Mnamkataba na maisha? Akifia hapa katikati huko mtampa nani?
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa matokeo haya ya kuchukua fedha ambapo tunaendesha nchi kama duka, kila kitu mnataka kiwe centralized, Halmashauri mnaua, Mifuko ya Hifadhi za Jamii mnaingilia, kila kitu na fedha mpaka za wananchi wa kawaida mnataka muwe mnachukua kwenye mifuko yao, ni lazima ikome.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakusukuru kwa sababu hata nikianza hii hoja hautanivulimia, ahsante.
Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Nianze kwa kuwashukuru sana wote ambao mliniombea wakati nilipokuwa naumwa. Nashukuru uongozi wa Bunge na Wabunge wote, nawashukuru sana wananchi wa Tarime, nawaambia nimepona. I am back firing.

Mheshimiwa Spika, nianze kwanza kwa kodi ya majengo (Property Tax). Essence ya kuweka Property Tax mijini ilikuwa ni kuweza kukusanya kodi ili isaidie kusafisha majitaka mijini; kwa ajili ya zimamoto, kwa sababu watu wanaomiliki nyumba, wanalipa kodi ya ardhi na kodi ya pango la ardhi. Sasa Mheshimiwa Waziri amepeleka kodi mpaka vijijini pale ambapo tu ili mradi mtu amejenga nyumba ya tofali na bati ambapo Serikali hawajamnunulia hawajamchangia kwenye tofali, hawajamchangia kwenye cement na vitu vyote hivi alinunua vimelipiwa kodi, wanataka waende kuwachaji watu maskini wa vijijini kodi ya nyumba.

Mheshimiwa Spika, hili ni jambo baya na halikubaliki na ni lazima kwa kweli walingalie, wa-recitify hili, huwezi leo kwenda kuwachaji watu ambao huwapelekei huduma ya zimamoto wala huduma ya majitaka, unakwenda kuwachaji pesa ya kodi ya property tax, unawachaji kwa sababu gani?

Mheshimiwa Spika, la pili, wanaondoa Property Tax kwenye Halmashauri ambapo kama leo wanafuatilia Kenya; jambo ambalo linamtikisa Uhuru Kenyatta na linataka kumtoa madarakani ni mambo mawili tu. Ni kodi, ni kushindwa kugatua pesa kwenye kitu wanachoita County. Wanashindwa kushusha pesa kule chini ili ziende kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa leo wanachukua pesa ambazo kule chini tuna Madiwani, wanalipwa ili wakae vikao, wajadili, wapange huduma kule chini; wanazichukua, wanazileta zote mjini. Leo wanataka watuambie kuwa Serikali hii ina uwezo wa kujadili Kitongoji kimoja kimoja! Kwa mfano, kule Kehero kwetu Kemakorere; wajadili maji kutoka Dar es Salaam yaende kule, haiwezekani. Ndiyo maana tulianzisha Halmashauri ziwe karibu na wananchi zione huduma ndogo ndogo pale. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, choo kikibomoka kwenye Shule ya Msingi, asubiriwe Mheshimiwa Waziri kwa sababu amechukua Property Tax ndiyo apeleke pesa choo kiende kutengenezwa, watu waende kutumia! Hilo halitawezekana Mheshimiwa Waziri. Hilo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, ni Road License. Hii ni aibu! Leo wanataka kuwapelekea akinamama vijijini Road License wanaotumia mafuta ya taa kwenye koroboi, yaani maana yake ni kwamba kibatari wanatakiwa kukilipisha Road License, hii itafanyika Tanzania peke yake. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri hili ni muhimu akaliangalia.

Mheshimiwa Spika, la tatu, uporaji wa ardhi Tarime. Kuna kiwanda kimeletwa pale, nami nimesema na mwingine alikurupuka humu, hana research, akaongea wakati nikiwa naumwa.

Mheshimiwa Spika, sipingi kiwanda, lakini napinga utaratibu wa ardhi ya wananchi wa Tarime ambayo ni ndogo sana inavyotaka kuchukuliwa kwa nguvu. Wanakwenda wanaweka beacon kwenye ardhi za watu, mashamba ya watu ambapo Sheria Na. 5 ya mwaka 1999 inasema, ili uchukue ardhi ya mtu, ni lazima umlipe fare prompt and adequate compensation.

Mheshimiwa Spika, hilo halijafanyika, wanatumia nguvu, wanatengeneza makinikia nyingine pale Tarime. Nasi watu wa Tarime mnatufahamu; kwenye ardhi tunailinda kwa nguvu zote. Tutailinda!

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni vyema wakaangalia hilo la ardhi. Juzi wamemwingiza Makamu wa Rais kwenye mkenge kwa makusudi, wanataka kupora ardhi waweke pale kiwanda, mwisho wa siku itakuwa kama hili la makinikia ambalo tumelisema miaka yote, unamchoma mtu kisu halafu unachomoa unamchekea, yaani CCM iliwachoma Watanzania kisu kwenye madini sasa imechomoa kisu halafu inashangilia. Hayo ndiyo yanayotaka kufanyika pale. Kwa hiyo, ni muhimu yakaangaliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la nne, ni suala la madini. Kama kuna watu wameumizwa, kama kuna watu wana vilema, kama kuna watu wana kilio cha madini kwenye nchi hii, ni watu wa Tarime, ambao wamezika ndugu zao miaka na miaka, kwa sababu ya kupigania madini yao yaliyokuwa yanaporwa na sasa wamethibisha yale tuliyoyasema kwamba madini yalikuwa yanaporwa miaka yote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika hili nashauri kama Rais yupo serious alete constitution amendment hapa tuwaondolee kinga Rais Mkapa na Rais Kikwete wachunguzwe kwenye suala hili la madini. Baraza la Mawaziri, wanajua wanavyofanya kazi, huwezi kuniambia kwamba Mheshimiwa Daniel Yona aliondoa fifteen percent yetu peke yake bila concert ya Rais.

Mheshimiwa Spika, haiwezekani kama leo Rais anavyonunua Bombadier, haijapitishwa kwenye utaratibu wa kibajeti, haiko popote, uje uniambie kwamba kuna Waziri hapa anaweza kumwambia Rais tusifanye hivi? Au Rais mwingine mwaka unaokuja aje amkamate Mheshimiwa Mbarawa bila Rais kuchunguzwa! Kwa hiyo, tunataka constitution amendment, hawa watu wachunguzwe waonekane nini mkono wao kwenye hili suala? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine, kwa sababu wamedhibitisha kwamba Acacia ni kampuni fake, ni kampuni hewa ambayo haipo na iko Tarime inawaibia wananchi wa Tarime, kuanzia leo nawaambia wananchi wa Tarime wajiandae tuingie mle mgodini tuchukue kila kilicho chetu. Nami hili nalisema humu na nitalifanyia kazi na sidanganyi kwa sababu wananchi wa Tarime wameumizwa na kampuni ile Rais amesema ni fake na hakuna formula ya kukamata mwizi.

Mheshimiwa Spika, mlisema wenyewe na Bunge limesema, formula ya kukamata mwizi ni kupambana naye. Sisi hatutaruhusu madini yatoke pale. Ndege ikitua, itapigwa mawe na hilo linaendelea na organization pale. Magari yao tutayakamata. Kwanza tunawadai fidia nyingi kweli kweli, pale Tarime. Tunataka hayo mambo yafanyike sasa hivi.

Mheshimiwa Spika, sisi tulitegemea tumwone Rais anaagiza kwamba kuanzia sasa madini yoyote yasiondoke nchini mpaka hayo mambo yote yapitiwe, tutazuia mchanga, dhahabu inaondoka. Hili halieleweki!

TAARIFA .....

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, sipokei. Nami nilijua tangu mwanzo kwamba hamtavumilia tupigane vita hii. Mnafanya mambo ya ukinyonga.

Mheshimiwa Spika, mwizi hana formula. Mheshimiwa Rais amesema Acacia ni mwizi. Yaani wewe unataka tupate utaratibu wa kukamata mwizi Tarime? Sisi watu wetu Mheshimiwa Spika wewe unajua ukiwa Naibu Spika, wameumia na maji ya sumu. Ngombe wamekufa, watu wamepigwa risasi kwa mujibu wa ripoti ya Waziri wa Nishati na Madini; watu wa Tarime zaidi ya 64 wameuawa; na hao ni kwa mujibu wa ripoti ya Mheshimiwa Waziri peke yake. Wameuawa pale mgodini Serikali hii ikilinda wezi wa Acacia. Ndiyo maana nasema watu wengine tuna machungu na tuna maumivu na hili.

Mheshimiwa Spika, mimi nasema na kama mtanikamata, Watanzania watajua hamko tayari kupigana vita hii ya kuokoa rasilimali hizi. Watu wa Tarime wajiandae waanze maandalizi, tuone atakayeenda kulinda mwizi pale, tumwone! Kama Serikali hii itaruhusu Polisi waende kulinda magari ya mwizi.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine kwenye haya ya madini, rasilimali za nchi hii zinazoibiwa siyo madini peke yake, wala siyo Acacia peke yake inayotuibia. Geita Gold Mine inatuibia, magogo ya nchi hii yanasafirishwa nje bure. Twiga walisafirishwa kutoka kwenye nchi yetu hii, wengine wako humu tunawafahamu, waliosafirisha twiga wako humu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, watu wa Loliondo wanalia mpaka sasa hivi kwa rasilimali zetu zinazoibiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Wakati Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli anaingia madarakani miongoni mwa miradi ambayo aliwatangazia Watanzania na dunia kwamba ni miradi ya kifisadi ni mradi wa NIDA, mradi wa vitambulisho vya Taifa wa NIDA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama unakumbuka wakati akina Dickson Mwaimu wanawajibishwa, Rais Dkt. Magufuli alisema kwamba kitambulisho cha kupigia kura ambacho kilikuwa na ubora kuliko kitambulisho cha NIDA kilitengenezwa kwa Sh.3,000 na akasema kwamba vitambulisho milioni 23.5 vya kupigia kura vilitengenezwa kwa bilioni 70.

Mheshimiwa Mwenyekiti, akawa anashangaa inawezekana vipi kitambulisho cha kupigia kura ambacho kina ubora kuliko wa NIDA kikatengenezwa kwa bei ya chini huku kitambulisho cha NIDA kikitengenezwa kwa Sh.17,000 na akina Dickson Mwaimu wakachukuliwa hatua sitaki kwenda huko. Akampeleka pale mtu anaitwa Ndugu Kipilimba, kukaimu nafasi ya Ndugu Dickson Mwaimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitambulisho kile ambacho kilikuwa Sh.17,000 kikapanda kwa kampuni ile ya kwanza iliyotuhumiwa kupewa tenda kuongezewa muda, kampuni iliyotuhumiwa kutengeneza kitambulisho kwa bei ya juu na watu wakachukuliwa hatua, ikatengenezwa addendum ikaongezewa muda kisanii na kitambulisho hiki kikapanda kutoka Sh.17,000 mpaka Sh.26,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nahitaji maelezo ya Serikali na Mwenyekiti wa Kamati atuambie ilikuwaje taarifa hii ikaondolewa? Huu ni ufisadi na siku zote tumesema kwamba Serikali hii ya Chama cha Mapinduzi inalea ufisadi na inajaribu kufunga watu midomo wasiseme ufisadi unaotokea wakati huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili jana…

T A A R I F A . . .

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naongea mambo mazito sana sitaki kufanya comedy hapa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo nahitaji maelezo, siku zote na Watanzania wajue kabisa kwamba kuna mambo mengi tu yanafanyika kwenye Serikali hii ambayo yana ufisadi kuliko hata Serikali zilizopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye kitu ambacho kimezinduliwa jana kinaitwa E-Passport, huko nyuma uliwahi kufanyika utafiti wa jinsi ya kuleta kitu kinaitwa E-Migration, E-Migration ilikuwana zaidi ya components sita, ilikuwa na E-Passport, E-Visa, E-Border na E-Visa kitu kikubwa kilichokuwa mle ni kwamba mtu anapokata visa akiwa hata Marekani vituo vyetu vya immigration hapa nchini watu waweze kusoma na wakajua ili kudhibiti mapato. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana imezinduliwa E- Passport na ule mradi mzima uliokuwa na components sita ulikuwa ni wa dola milioni 180, jana imezinduliwa kitu kinaitwa E-Passport ambacho kina component moja tu kwa dola milioni 50, tenda yake hatujui imetangazwa lini, nani na nani walioshindanishwa. Hii nchi ina sheria na taratibu, tunaruhusu vipi nchi yetu hii miradi ya kifisadi inatokea kila leo, kila kesho na Serikali hii inayojinasibu kwamba inashughulikia ufisadi watu wachache wanatengwa wengine wanaruhusiwa kuendelea kupiga ufisadi kwenye nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Serikali za Mitaa.

Amezungumza hapa Mheshimiwa Bobali kwamba Serikali za Mitaa Wakurugenzi waliowekwa ni Wakurugenzi ambao ni dhaifu na wengi ni walioshindwa uchaguzi katika kura za maoni za CCM. Mimi sitaki kulizungumzia hili, nataka tu nimwambie rafiki yangu, Mheshimiwa Bobali, haya ni makusudi ya Serikali hii kuua Serikali za Mitaa, imekusudia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana hata wakati watu wanazungumza hapa kuhusu Wakurugenzi na matatizo ya Wakurugenzi, amezungumza hapa Mheshimiwa Mzee Selasini, hakukuwa na Waziri hata mmoja hapa anayeshughulika na hilo, kwa sababu nia yao ni kuua hizi Serikali za Mitaa. Ndiyo maana hata mapato ya Serikali za Mitaa yametolewa na hayarudishwi. Mapato ya mabango, kodi za nyumba zilizokuwa zinakusanywa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nam-challenge kaka yangu pale atuambie, mkitoa pesa mnazochukua kwenye mabango ninyi mapato yenu ni kiasi gani, mtuambie ni shilingi ngapi mnazopata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 na Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017.
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii ya kuchangia ili niweze kusema kidogo kuhusu hoja zilizoko mbele yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya matatizo makubwa ambayo nchi yetu imekuwa ikikabiliwa nayo ni ufisadi mkubwa unaolelewa na Serikali hii ya CCM. Ufisadi huu umekuwa kwenye miradi mbalimbali ya Serikali na kila mipango inayopangwa ukiangalia ndani yake unakuta kuna mkono wa kifisadi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2010 mpaka mwaka 2013/2014, kulikuwa na msukumo mkubwa sana kuhusu suala la gesi kule Kusini. Msukumo wa hali ya juu kweli kweli, wananchi kule wakapigwa, wakawekwa ndani, likapelekwa mpaka Jeshi, watu wakawa tortured kwelikweli. Wakati ule hapa Bungeni kikaingizwa kitu tunaambiwa kwamba sasa tunataka ku-shift kutoka kutumia umeme wa hydropower tunakwenda kwenye umeme wa gesi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo ni Serikali ya Kikwete na ilikuwa ni mipango ya Serikali ya Kikwete. Watu wakalazimishwa kule likajengwa bomba pesa zikakopwa kwa walipa kodi maskini wa nchi hii wakawekewa kitu kwa kubambikiwa. Wananchi wa Kusini hawakukubali lakini mkatumia nguvu nyingi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo baada ya miaka mitatu, minne tume-shift tena tunaambiwa sasa tunakwenda kwenye Stieglers Gorge. Serikali iliyoingia hii sasa na yenyewe inatafuta jinsi ya kupiga, tutapigia wapi, sasa tupigie kwenye Stieglers Gorge. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, bomba la gesi lililojengwa kwa gharama kubwa kweli kweli matumizi yake tumeambiwa kwenye Kamati ni mpaka sasa ni asilimia sita tu peke yake na tuliaminishwa na Watanzania wakaaminishwa kwamba sasa hatutaki tena kutumia umeme wa maji kwa sababu is not anymore reliable. Sasa umeme unaoaminika ni umeme wa gesi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Serikali hiihii, ya Chama kilekile, Rais aliyeko ndiye alikuwa Waziri kwenye Serikali hiyohiyo, alikuwa kwenye Baraza la Mawaziri linalopanga mipango, leo amekuja anatuambia sasa tunaenda Stieglers Gorge. Stieglers Gorge haijawahi kuingia kwenye bajeti. Ukisoma kitabu cha bajeti cha mwaka jana hakuna kitu tulichojadili kuhusu Stieglers Gorge. Hakuna pesa zilizopangwa kwa sababu Bunge hili ndilo lipo kwa niaba ya wananchi kupanga mipango na ku-authorize matumizi ya pesa kwa niaba ya wananchi wa nchi hii ambao ndiyo walipa kodi. Bunge hili halikuwahi kupanga hicho kinachoitwa Stieglers Gorge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sawa ni mradi mzuri na wote tunautaka, lakini kama tuliwekeana utaratibu na kama mwaka juzi tu tumechukua pesa za walipa kodi tukapeleka kwenye bomba, kwa nini tusi-utilize bomba kwa matumizi ya asilimia mia moja kabla hatujahamia kwenye hiki kinachoitwa Stiglers Gorge? Kama siyo kwamba kuna wingu la kaufisadi kapya kanatengenezwa hapa kwa sababu ufisadi uliokuwepo sisi hatukugusa? Kwa nini leo tunachukua pesa wakati bomba hili tunalitumia kwa asilimia sita peke yake? (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nafikiri ni lazima Serikali ije hapa na majibu, iwaambie Watanzania kwamba gesi tuliyowaaminisha miaka miwili, mitatu, iliyopita kwa Serikali hii hii ya Chama kilekile ni nini kimeikumba gesi. Kwa nini gesi inatumika kwa asilimia sita na sasa tunahama tena kurudi kwenye hydro ambayo tuliwaambia wananchi kwamba haiko reliable kwa sababu mvua zetu haziaminiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili bwawa tumeambiwa juzi kwenye semina tarehe 3 lina urefu wa kilometa 100 yaani kama unatoka Chalinze mpaka Dar es Salaam na upana wake ni kilometa 25. Mimi ninachotaka kutoka hapa Waziri atuambie hizo pesa ambazo angalau wamefikiria kwamba wanataka kuzitoa kwa ajili ya ujenzi wa hili bwawa, wanakadiria kutoa shilingi ngapi na kwenye bajeti ipi na waliipitisha wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu wamesema within three months tayari kutakuwa na mobilization inafanyika pale kwa ajili ya kuanza kujenga bwawa. Sasa huyo aliyewapitishia hizo hela ni nani? Nani anatoa mamlaka ya pesa nyingi hizo kupitishwa kinyemela hivyo bila Bunge hili? Ni nini kazi ya Bunge hili ambalo wananchi maskini kila siku wanatoa kodi, wanajinyima kwelikweli, mama zetu hawawezi hata kununua vidonge lakini wanalipa kodi kutulipa sisi mamilioni ya pesa tukae hapa tujadili mipango yao na hatufanyi hiyo kazi, tuna haja gani ya kuendelea kuwa hapa? Tunataka Waziri atuambie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuje kwenye REA. Mwaka jana tulizindua kitu kinaitwa REA wakaja wakandarasi na Naibu Waziri wakati ule sasa hivi Waziri rafiki yangu kweli, tulikuwa naye pale Bunda. Wakaja wakandarasi wakatuaminisha kwamba kufikia Desemba, kwa mfano, miradi ya densification, Waziri ni rafiki yangu na yeye yuko hapa atathibitisha ninachokisema, kwamba densification Desemba umeme unawaka. Kwanza ilikuwa Oktoba baadaye ikasemekana sijui imekuwaje Desemba.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo tunazungumza maeneo kwa mfano ya Sirari kwenye mji ambao una population ya watu 45,000, hawana umeme pale. Hata mradi wa densification wenyewe tulioahidiwa hakuna kitu wala hakuna hata nguzo zilizopelekwa mpaka sasa hivi mradi tulioambiwa Desemba utakuwa umewaka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hizi pesa za REA Mheshimiwa Waziri ziko wapi? Kwa sababu hizi pesa siyo za bajeti wala sio za nini, ni pesa za walipa kodi maskini ambapo kila siku tunanunua petrol tunakatwa Sh.50. Mama kijijini kule akinunua mafuta ya taa mnamkata pesa au hizi pesa tena mnachukua mnaenda kununulia Madiwani wakati hizi pesa zinatakiwa zilete umeme? Zinaenda wapi pesa ambazo ziko ring-fenced? Pesa ambazo zinatolewa kabisa zikiwa na matumizi, mtu anaenda kununua mafuta anajua matumizi yake ni kwamba zituletee umeme wa REA, ziko wapi na ni kwa nini haziendi kwenye REA? Nataka Waziri atuambie hizo pesa ziko wapi? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo wamesema TANESCO inadaiwa na sisi wote ni wajumbe tunajua TANESCO inadaiwa. TANESCO hiyo ambayo inadaiwa iko hoi, wameenda tena kubomoa na jengo lake linalokadiriwa kufikia bilioni 54, sijui ni la kwake au walikuwa wamepanga au nini. Yaani mgonjwa ambaye yuko mahututi kwelikweli anaweza kufa sasa wamenyang’anya hadi sehemu ya kulala ananyeshewa na mvua. Sasa hawa hivi mipango yao ni ipi? Ni kwenda mbele au wanaenda mbele hatua mbili, wanarudi kumi na tano nyuma wanajipongeza? Kwa sababu sasa hivi wamedhibiti vyombo vya habari, wanadhibiti hata Wabunge kuongea, wakiongea tu wanashughulikiwa yaani wao wenyewe wanajifungia wanafanya maamuzi ambayo miaka mitatu ijayo mbele au kwa sababu wanajua mwaka 2020 hawarudi sasa wanataka tukiingia Serikalini tusikute chochote hapa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu kama leo wanakwenda kukopa kwenye benki za kibiashara kuwekeza kwenye mradi mkubwa kama wa Stieglers Gorge wanalipaje hizi pesa? Kama siyo kwamba wanataka Serikali itakayokuja ishindwe kufanya kazi yake?
Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari wa Mwaka 2016
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi hii uliyonipa nami niweze kuchangia kwenye muswada huu wa upatikanaji wa taarifa. Sasa kumekuwa na contradiction kubwa sana hapa, wengine wanasema Muswada wa Upatikanaji wa Habari, wengine Muswada wa Upatikanaji wa Taarifa. Ni kwa sababu mambo haya yalivyokuja yalikuja kinyumenyume.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa baadaye tutamhitaji Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe atuambie ni nini hasa ambacho walikusudia kuleta kwa sababu mwanzoni hata kwenye Order Paper ilivyoonekana ni tofauti na tunavyoijadili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii nchi ni yetu sote. Wakati fulani kuna mambo ya msingi yanaletwa hapa, lakini watu wakitaka kuyajadili wanakwekwa na watu wengine baadaye wa kujibu vijembe, wanatoa vijembe upande wa pili bila kusikiliza kile watu wengine tunachokisema. Hata hapa tunajua kwamba kuna watu wameandaliwa, baadaye watachomekwa tu ili waje kushambulia yale tunayozungumza. Mimi sijali, nataka nizungumze na nishauri. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa ikitolewa ndiyo inasababisha upatikanaji wa habari. Sasa taarifa ikiwa imetolewa, ikienda kwa public inakuwa habari.
Sasa huu Muswada wa upatikanaji wa taarifa ambao mwisho itakuwa habari umekuja wakati ambapo Taifa letu lipo kwenye majaribu makubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tupo kwenye wakati ambao tunajadili Muswada huu ambao kuna mtu mmoja, tunapokuja hapa tunapitisha bajeti yeye anakwenda anapitisha yake huko mtaani. Kama jana mliangalia vyombo vya habari vingi vilionesha, Mheshimiwa Rais alikuwa pale Magomeni, anasema atatoa shilingi bilioni kumi kujenga nyumba pale ambazo hatukupitisha kwenye bajeti. Kwa hiyo, hii ni test kubwa sana kwa sheria zetu. Unakuja wakati ambao sheria inaonekana siyo muhimu kwa Taifa hili. Muswada huu unakuja wakati ambao tunajadili mambo hapa, tunayapitisha yanaenda yanapindishwa huko. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tupo katika wakati ambao nafikiri na wananchi wenzangu wafuatilie haya. Je, kuna sababu zozote za Bunge hili kuwa linakaa hapa katika kipindi kama hiki au vipindi hata vya bajeti likatumia mabilioni ya pesa za Watanzania tukajadili jambo ambalo tunajua hatutalifanyia kazi? At least kwenye hii kwa sababu ina vipengele vingi vya kukandamiza, najua hii mnaweza kuifanyia kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo yupo Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe, mwanasheria nguli, yupo Mwanasheria wa Serikali hapa, sheria zinapindishwa; watu wamezuiliwa kufanya mikutano kinyume cha sheria; Mwanasheria Mkuu wa Serikali yupo, kaka yangu Masaju tena anatoka Mkoa wa Mara. Sasa watu wa Mkoa wa Mara sisi huwa hatuogopi kusema ukweli na kushauri pale panapostahili. Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe yupo, mwanasheria nguli, lakini wote hao wanapiga makofi tu; wanampigia mtu mmoja makofi ambaye anavunja sheria hizi. Sasa ndiyo najiuliza, hivi kuna sababu gani ya kukaa hapa, tukatumia pesa nyingi kujadili mambo ambayo tunajua mwisho wa siku hatutayafanyia kazi kama hii sheria? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nirudi kwenye huu muswada. Ukija kwenye kipengele cha 6(6) wamezungumza wenzangu; “mtu yeyote atakayetoa taarifa iliyozuiliwa kinyume cha mamlaka ya umma kisheria hii, atatenda kosa na endapo atatiwa hatiani atatumikia kifungo cha miaka 15 au 20.” Yaani mtu ametoa taarifa ambayo inakwenda kuwa habari kwa wananchi na Katiba hii Ibara ya 18(c) imetamka kabisa kwamba wananchi wana haki ya kupata habari, mnamfunga miaka 20 Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe, huyu mtu ameua mpaka mumfunge miaka yote hiyo? Yaani kwa kutoa taarifa tu!
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkisema taarifa za Usalama wa Taifa, taarifa za Majeshi; hizo sisi hatuna tatizo nazo; lakini taarifa, leo hata Mtendaji wa Kijiji akizuia taarifa sisi tukaitoa, kwa hiyo tufungwe miaka 20. Sasa nafikiri hii siyo sahihi.Ni lazima unapokuja Dkt. Mwakyembe uoneshe Udaktari wako hapa.
Usiunde tu watu nyumanyuma kuja kujibu hapa vijembe. Rekodi hizi zitabaki kwenye vitabu vya Bunge hili na watu wengine watakuja wasome wakati sisi hatupo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kipengele cha 19(3) unasema mtu yeyote ambaye hajaridhishwa na uamuzi wa Mkuu wa Taasisi uliofanywa, yaani ya kunyimwa taarifa, hajaridhishwa. Mimi nimekwenda nimenyimwa taarifa na Katibu Mkuu wako, sijaridhika, nikate rufaa kwako, yaani hii ni sawa na ile waswahili wanasema kesi ya ngedere unampelekea nyani. Hakuna kitakachopatikana hapa. Kwa hiyo, hivi vitu ni lazima kama kunatakiwa kuwepo na checks and balances muweke vyombo vingine ambavyo ni huru viweze kuwahoji au kuwalazimisha ninyi mtoe taarifa hizi ambazo zina manufaa ya umma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa unataka wewe mtu wa chini yako amekunyima taarifa na katika kipindi hiki ambacho nyie ni waoga vibaya sana, akishasema kule hata kama mnajua imevunjwa Katiba mpo kimya!
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilimwona pale kaka yangu Mheshimiwa Masaju na amekuja hapa alivyokuwa anahangaika Mwanasheria mzima kutetea uovu anashindwa; wanahabari wanambana hivi anasema hivi; aibu tupu, kwa sababu tu sheria zipo lakini hamtaki kuzifuata sheria hizi. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naona siyo sawa kwamba mtu wa chini ameshindwa, tukate rufaa kwako sijui na kwa mtu wa juu yake, hii naona siyo sawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu cha 21 kinasema eti mmiliki wa taarifa ambaye maombi ya kupata taarifa yatatumwa kwake anaweza kutozwa ada iliyowekwa kwa ajili ya kutoa hiyo taarifa. Yaani kweli Katiba inasema ni haki ya mwananchi kupata habari na taarifa kwa mambo muhimu yanayohusu nchi yake, leo mnatuambia mtuuzie taarifa, yaani mnataka kweli kabisa Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe umeweka hapa kwamba taarifa inunuliwe, yaani vyombo vya habari vinataka taarifa za Serikali wawatangazie ninyi wananchi wajue mnachofanya, mnataka eti wanunue kutoka kwenu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi kwa nini tunatengeneza vitu vya aina hii? Mimi huwa nakaa najiuliza na wakati mwingine mnatunga haya mambo kama mnatukomoa sisi; lakini waangalieni wenzenu akina Basil Pesambili Mramba na wenzake, walikuwa Wabunge humu na Mawaziri tena waliokuwa wanaheshimika. Sasa hivi wananyea ndoo. Akina Harry Kitilya walikuwa watu wakubwa kwenye nchi hii, lakini wako mle ndani sasa hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mnapotunga hivi vitu kama mnafikiria kukomoa watu, muwe mnawaza pia kwamba ipo siku kama historia haitawahukumu nyie wenyewe, watoto wenu hawatakuwa na nafasi hizo mlizonazo au wajukuu zenu hawatapata nafasi hizo mlizonazo, watakutana na mambo haya ya ajabu mliyoyaweka kwa ajili ya kubana watu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana nipo hapa kushauri na tunashauri kwa nia njema. Mmwambie hata Mheshimiwa Rais na ninyi wote humu mnajua na mnalalamika. Hatuwezi kuwa na Rais ambaye akienda huku, watu tunashika vichwa, leo atasema nini? Yaani hatuelewi! Anakuwa Zanzibar anasema watu watafia kwenye madimbwi ya maji.
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na ninaona maturity yako, nakushukuru sana, kwa sababu watu wengine wako humu wanafikiri tukimtaja Mheshimiwa Rais tunamchukia. Hatumchukii, sasa namtaja kwa Utukufu wake, Mheshimiwa Mtukufu Rais. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema, akienda sehemu hatujui ataongea nini; juzi, Mheshimiwa Ummy alikuwa hapa anakanusha taarifa, amesema watu wazae tu. Mheshimiwa Ummy amekanusha; sasa hilo lilikuwa linajulikana ataongea nini? Mtukufu Rais amesema, machinga waingie popote, Mheshimiwa Simbachawene yule pale, akakanusha juzi tu. Labda watu hawa hawana kumbukumbu na hawafuatilii. Ndiyo maana tunasema wala siyo kwa nia ya kurushiana vijembe wala kudhihaki mtu. Tunasema Taifa hili ni lazima tuliweke kwenye utaratibu wa kisheria na mambo yote yawe kwenye chain ya sheria na Katiba ili kila mtu ajue kwamba nikivuka mipaka hii, awe Mheshimiwa Rais, awe Mtukufu Rais kwa sababu nikisema Rais napigiwa kelele; awe nani, ajue nikivuka mipaka hii, sheria za nchi yetu hazitakubali, Katiba ya nchi yangu haitakubali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, madhara yake, kuacha mambo yanajiendea, ndiyo maana unaona hata Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Makonda anatoa amri eti Mikoa yote tarehe moja ipande miti, yaani Makonda naye ni Rais kwenye nchi hii! Uropokaji wa ajabu! (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna sheria zinaeleza tuendesheje nchi; mtu anakaa Dar es Salaam kwa sababu amesifiwa mara mbili, amejiona na yeye ni kila kitu, anatoa amri; tarehe 1 mwezi Oktoba watu wote wapande miti nchi nzima. Na yeye anatembea na Wanajeshi, ana Polisi. Sasa tukisema haya hatusemi kwa nia mbaya, tunasema kwamba tunakaa hapa tunatunga sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mnaaibisha professional zenu, yaani mnatia aibu! Hii nchi inatia aibu kweli kweli! Wasomi wa Vyuo Vikuu hawazungumzi, wako kimya…
MWENYEKITI: Ahsante sana kwa mchango wako.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi hii ili nami niweze kuchangia kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu wananchi wa Tarime wanichague nimekuwa na miaka mitatu hapa Bungeni. Nimejifunza mambo mengi sana na wakati mwingine fikra nilizokuja nazo hapa na kitu ninachokiona kinafanywa hapa ni tofauti kabisa na inasikitisha sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 1994 Rwanda iliingia kwenye machafuko makubwa sana yaliyosababisha mauaji ya zaidi ya watu milioni moja. Ukiangalia na ukifuatilia mauaji yale, kulikuwa na visasi, kupuuzwa watu, watu kuonewa, double standard na watu wakafika sehemu wakachoka kweli kweli, yakatokea matatizo makubwa kama yale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hapa Tanzania kule Musoma mwaka 2010 yaliwahi kutokea mauaji mabaya ya kulipiza kisasi. Watu zaidi ya 16 kwenye familia moja wakauawa, wengi mnajua. Mbuzi wakauawa, ng’ombe, mpaka kuku na mbwa wakauawa kwa sababu ya visasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nchi hii watu wanapigwa kwa sababu wengine wanafikiri wako salama na kwa sababu wanafikiri wako kwenye madaraka, wanaona ni sawa hawa kufanyiwa hivi. Katibu wetu wa Kata ameuawa, watu wanaona ni sawa. Tundu Lissu amepigwa risasi, watu wanaona ni sawa; watu wanaonewa, mnaona ni sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi wengine tunajua tuko kwenye list ya kuumizwa. Sisi wengine tumeziambia familia zetu kwamba hata kama ni baada ya miaka 10 kwa watu watakaotufanyia ubaya, lazima familia zao ziwajibike. Hili liwe kwenye record kabisa. Hatuwezi kuwa kwenye nchi ambayo imejaa upendeleo, double standard. Tunazungumza kuhusu utawala bora hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumza kuhusu utawala bora. Utawala bora tunaouzungumza Mzee Mkuchika ni utawala wa aina gani? Utawala ambao leo mnakamata mtu, Polisi wanazungumza kwamba huyu mtu amejiteka, lakini yeye mnamzuia kuwaambia Watanzania kwamba yeye hakujiteka au alijiteka. Utawala bora upi? Utawala bora leo tunajua, Serikali leo duniani ni chombo cha mabavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumza Bunge ndiyo chombo cha wananchi, dunia nzima ndivyo ilivyo. Leo mtu anatoa opinion yake kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 18 anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake. Jambo tunalopaswa kufanya kama Bunge ni kumjibu kwamba hili Bunge haliko hivyo kwa kuandika makala kinzani. Au huyu mtu mnafikiri kwa nini anatuona hivyo? Kwa nini hakuliona hivyo Bunge la Mama Makinda? Kwa nini hakuliona hivyo Bunge la Mzee Sitta? Kwa nini hakuona hivyo katika Mabunge mengine? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge hili likiwa sehemu ya kutoa hukumu kwa watu wanaotutazama nasi hatuwezi kulazimisha kila mtu atuone kama tunavyojiona. Watu wana haki ya kutuona tofauti. Kila mtu ana macho yake na wewe utaona umevaa suti umependeza, mwingine atakwambia hujapendeza umevaa suti mbaya. Kwa hiyo, huwezi kuanza kumchapa kwamba amekwambia umevaa suti mbaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nafikiri kama Taifa, nasi tunaongea hapa, watu wanafikiri sisi ni walalamikaji. Tumewaambia mambo mengi. Mwaka juzi mligusa hapa sukari, “oh, sukari, watu wanaingiza sukari, sijui sukari, sukari! Tutaishusha bei! Sukari imepanda kutoka Sh.1,800/= aliyoiacha Mheshimiwa Kikwete, leo ni Sh.2,800/=. Mnajifanya kama hamjui, yaani mmejisahaulisha. Eti mmejisahaulisha kwamba sukari haijapanda bei. Yaani mnafikiri Watanzania hawawaoni. Hakuna anayezungumza, yaani mmejisahaulisha tu, hamjui kwamba sukari hii mlitibua bei nyie. Tukiwaambia, ooh, hawa ni watu wabaya. (Kicheko/ Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa kwenye kitabu, msije mkasema maneno ya Heche; kitabu chenu hiki hapa cha Mheshimiwa Waziri Jafo, cha sasa hivi; Vituo vya Afya tunavyo asilimia 15. Yaani kati ya vituo 4,220, tuna vituo 696. Hapo hatujazungumzia ubora wake, hatujazungumzia vifaa vyake, hatujazungumzia wahudumu, 696 na viongozi wa dini mliowatukana kati ya hivyo vituo 600, vya kwao 183.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mtemi nakuamini, nakushukuru sana. Naomba niendelee. Mama nafikiri nikimsema itakuwa mbaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nasema, Mwalimu Nyerere ambaye ni Muasisi wa Taifa hili kama hamumheshimu, aliwahi kusema maendeleo ya vitu siyo maendeleo ya watu. Maendeleo ya watu ni pamoja na watu kuwa na afya. Mimi nawaambia CCM nyie mnaopiga kelele, Vituo vya Afya tangu uhuru kati ya 4,420 mna Vituo vya Afya 696.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa hivyo Vituo vya Afya kwa mujibu wa kitabu hiki cha hotuba ya Mheshimiwa Waziri, 183 ni vituo vya Makanisa na madhehebu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema, kama ni kujenga reli, Wakoloni walijenga hata kabla ya uhuru.

T A A R I F A . . .

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. You are always firm. Nasema hivi, miaka 59 vituo vya Serikali 513; ili tujenge vituo 4,422 tunahitaji miaka 600. Mnahitaji mtoke madarakani nyie. Ndicho ninachosema hapa, a simple logic. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunakuja hapa mtu anatuambia SGR. Wakoloni walijenga reli hii. Wakati ule ndiyo ilikuwa standard gauge ya sasa hivi, wakati wakoloni wanajenga ile (Wajerumani). Watanzania na Watanganyika walikataa kwa sababu walikuwa wanawa-oppress. Kitu ambacho mnafanya nyi, leo mnatu-oppress. Sisi tukizungumza kuhusu nyie mnatuweka Polisi, mnatupeleka Mahakamani. Mheshimiwa Rais akizungumza kuhusu sisi, mkitukashifu, nyie hakuna pa kupelekwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo tunasema, hata watu wa Afrika Kusini walizungumza na Makaburu wakawaandikia barua, wakafanya nini, lakini ilifika sehemu wakaunda MK kukataa ushenzi uliokuwa unafanywa na Makaburu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunachozungumza hapa ni kwamba ni lazima tuheshimiane. Ni lazima tuelewe; leo unamshtaki Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbowe, Mheshimiwa Mchungaji Msigwa, mimi na Mheshimiwa Ester, eti sisi tulisababisha kifo cha mtu (Akwilina). Yule Mkurugenzi aliyetunyima viapo ambavyo vipo kwa mujibu wa sheria, alisababisha nini? Haya mambo ndiyo tunayozungumza.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nianze kwa kusema hivi, mwaka jana, mwaka juzi na miaka mingine yote iliyopita tumezungumza hapa kuhusu uwanja wa ndege wa Mkoa wa Mara. Tumesema, tumesema, tumeonesha umuhimu wa huu uwanja ukilinganisha na viwanja vingine ambavyo vimetengewa mabilioni ya pesa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu uwanja ni muhimu kwa Taifa hili kwa sababu Mbuga ya Serengeti yote unayoijua iko Mkoa wa Mara, ambayo ndio inayoingiza watalii wengi kuliko sehemu nyingine yoyote ya nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisikia mtu ametoka Ulaya anasema anakwenda Serengeti, mambo ya Ngorongoro na mambo mengine huwa yanafuata baadaye, lakini kichwani kwa watu wanaotoka nje mara nyingi wanasema wanakwenda Serengeti, tumeimba hatusikilizwi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ndio mkoa ambao anatoka Mwalimu Nyerere, niliwaambaia hapa wakati fulani, lakini hatusikilizwi. Pesa zinachukuliwa, tena zingine haziko hata kwenye utaratibu wa kibajeti, hazijapitishwa na Bunge hili zinapelekwa kwenye maeneo ambayo hayana muunganiko wa kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wa Mkoa wa Mara ni watu wa misimamo na wanaona mnayoyafanya. Ukichukua barabara za Mkoa wa Mara kwa mfano ukaangalia barabara ya lami tuliyonayo mkoa mzima wa Mara ni barabara inayotoka Mwanza kwenda Sirari, iliyojengwa miaka ya 90 na kitu, hakuna barabara nyingine yoyote ya lami ambayo tuliyonayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tukiwaeleza ni kama wametutupa, lakini mali inayotoka Mkoa wa Mara inachangia pesa nyingi sana kwenye pato la Taifa. Nafikiri ni lazima Mawaziri waangalie haya mambo ya msingi yanayohusu maisha ya watu wa Mkoa wa Mara. Hilo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nizungumze kuhusu ufufaji wa ATCL na kila mara tunapozungumza hapa watu wanafikiri sisi tunapinga nchi hii kununua ndege. Hakuna mtu miongoni mwetu anayepinga tusinunue ndege, hakuna mtu miongoni mwetu anayekata tusifufue shirika letu la ndege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachosema, kama tulivyosema wakati wa makinikia, kama tulivyozungumza wakati ule walikuja hapa wakatuambia kwamba tunaletewa trilioni 450, tunazisubiri hapa. Tuliwashauri humu, wakatuzomea, tuliwaambia wao ndio walioliingiza Taifa hili kwenye matatizo makubwa ya mikataba mibovu wakasababisha nchi hii inaibiwa na wazungu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadaye wakaja hapa wanatunga sheria, tunawashauri njia ya kwenda nayo hawakusikia, wakatubandika majina ooh vibaraka wa wazungu, sijui vibaraka wa mabeberu. Sasa wao wenyewe aibu yao, hakuna pesa hata Sh.100 hata ile ya bia kishika uchumba haijaja ile ya balimi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ndivyo tunavyowashauri kwenye shirika hili la ndege tunawaeleza kwamba tusiende kununua ndege za nchi hii, mali ya Watanzania wote kama mtu unakwenda kununua machungwa ya nyumbani, kwako bila kushirikisha Bunge, bila kushirikisha bajeti ya Taifa hili, bila kufuata mipango na mikakati ya maendeleo ya nchi hii, hawataki kusikia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawaaambia hasara ambazo watasababisha kwa kununua ndege kwenye mashirika tofauti tofauti na utengenezaji wake na service yake itakavyokuwa ngumu, hawataki kusikia. Sasa leo na hapo Waziri atakuja ajibu, hatujui kama ni kwa mistake au ni kwa makusudi ATCL, ukaguzi wa CAG umefanyika lakini performance yake haijakaguliwa, performance audit haijakaguliwa, tunataka tujue kwamba pesa zilizochukuliwa ni kiasi gani na...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. JOHN W. HECHE: Shukrani sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nianze kwa kusema hivi, mwaka jana, mwaka juzi na miaka mingine yote iliyopita tumezungumza hapa kuhusu uwanja wa ndege wa Mkoa wa Mara. Tumesema, tumesema, tumeonesha umuhimu wa huu uwanja ukilinganisha na viwanja vingine ambavyo vimetengewa mabilioni ya pesa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu uwanja ni muhimu kwa Taifa hili kwa sababu Mbuga ya Serengeti yote unayoijua iko Mkoa wa Mara, ambayo ndio inayoingiza watalii wengi kuliko sehemu nyingine yoyote ya nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisikia mtu ametoka Ulaya anasema anakwenda Serengeti, mambo ya Ngorongoro na mambo mengine huwa yanafuata baadaye, lakini kichwani kwa watu wanaotoka nje mara nyingi wanasema wanakwenda Serengeti, tumeimba hatusikilizwi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ndio mkoa ambao anatoka Mwalimu Nyerere, niliwaambaia hapa wakati fulani, lakini hatusikilizwi. Pesa zinachukuliwa, tena zingine haziko hata kwenye utaratibu wa kibajeti, hazijapitishwa na Bunge hili zinapelekwa kwenye maeneo ambayo hayana muunganiko wa kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wa Mkoa wa Mara ni watu wa misimamo na wanaona mnayoyafanya. Ukichukua barabara za Mkoa wa Mara kwa mfano ukaangalia barabara ya lami tuliyonayo mkoa mzima wa Mara ni barabara inayotoka Mwanza kwenda Sirari, iliyojengwa miaka ya 90 na kitu, hakuna barabara nyingine yoyote ya lami ambayo tuliyonayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tukiwaeleza ni kama wametutupa, lakini mali inayotoka Mkoa wa Mara inachangia pesa nyingi sana kwenye pato la Taifa. Nafikiri ni lazima Mawaziri waangalie haya mambo ya msingi yanayohusu maisha ya watu wa Mkoa wa Mara. Hilo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nizungumze kuhusu ufufaji wa ATCL na kila mara tunapozungumza hapa watu wanafikiri sisi tunapinga nchi hii kununua ndege. Hakuna mtu miongoni mwetu anayepinga tusinunue ndege, hakuna mtu miongoni mwetu anayekata tusifufue shirika letu la ndege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachosema, kama tulivyosema wakati wa makinikia, kama tulivyozungumza wakati ule walikuja hapa wakatuambia kwamba tunaletewa trilioni 450, tunazisubiri hapa. Tuliwashauri humu, wakatuzomea, tuliwaambia wao ndio walioliingiza Taifa hili kwenye matatizo makubwa ya mikataba mibovu wakasababisha nchi hii inaibiwa na wazungu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadaye wakaja hapa wanatunga sheria, tunawashauri njia ya kwenda nayo hawakusikia, wakatubandika majina ooh vibaraka wa wazungu, sijui vibaraka wa mabeberu. Sasa wao wenyewe aibu yao, hakuna pesa hata Sh.100 hata ile ya bia kishika uchumba haijaja ile ya balimi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ndivyo tunavyowashauri kwenye shirika hili la ndege tunawaeleza kwamba tusiende kununua ndege za nchi hii, mali ya Watanzania wote kama mtu unakwenda kununua machungwa ya nyumbani, kwako bila kushirikisha Bunge, bila kushirikisha bajeti ya Taifa hili, bila kufuata mipango na mikakati ya maendeleo ya nchi hii, hawataki kusikia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawaaambia hasara ambazo watasababisha kwa kununua ndege kwenye mashirika tofauti tofauti na utengenezaji wake na service yake itakavyokuwa ngumu, hawataki kusikia. Sasa leo na hapo Waziri atakuja ajibu, hatujui kama ni kwa mistake au ni kwa makusudi ATCL, ukaguzi wa CAG umefanyika lakini performance yake haijakaguliwa, performance audit haijakaguliwa, tunataka tujue kwamba pesa zilizochukuliwa ni kiasi gani na...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. JOHN W. HECHE: Shukrani sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Napenda nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuipitisha familia yangu katika kipindi hiki kigumu ambacho mdogo wetu Suguta alichomwa kisu na polisi kwenye Kituo cha Polisi akiwa amefungwa pingu na akafariki dunia.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo moja linalonisikitisha, sijui ni kwa makusudi au ni kwa bahati mbaya, haijatoka official statement ya Serikali kwa maana ya Waziri anayehusika kukemea au kulaani kitendo kile kiovu kilichofanywa na polisi. Kwa hiyo, hilo namuachia Mungu na kwa sababu wao wanafikiri wako salama waache wajidanganye.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali hii inashauriwa mara nyingi na mimi nasikitika mipango ya Serikali ya CCM ni mipango ya miaka miwili au mwaka mmoja na ndiyo maana mipango mingi ina-fail. Mngekuwa mnachukua mawazo hapa na mnayafanyia kazi mmengekuwa hampati matatizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama mnakumbuka wakati mnajenga kituo cha DART pale, Mheshimiwa Mnyika aliwaambia kwamba hapa huwa panajaa maji na wakati ule Rais huyu wa sasa akiwa Waziri. Mmejenga pale kituo kwa mabilioni ya pesa za Watanzania, leo kinajaa maji. Hiyo ndiyo mipango yenu, miaka miwili haijapita kituo kinajaa maji pale mafuriko. Sasa nimeona gazeti la leo linasema mnataka mhamishe kituo pale mpeleke Ubungo, pesa mlishawekeza pale, nani analipa hizo pesa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hili suala la maji na tuelewane vizuri, Mheshimiwa Kamwelwe wewe umeenda Tarime ukakimbia hukutuambia sisi, ukaenda. Kuna miradi pale Waziri Mkuu amekuja ameiona, mradi kwa mfano wa Gibaso shilingi milioni 900 imepelekwa hautoi hata tone la maji. Leo watu wanasema hapa tuunde Tume ya Kibunge ipitie miradi nchi nzima ilete taarifa Bungeni siyo kwa ajili yako, kuangalia hawa watu waliopelekewa pesa na wamekula pesa za walipa kodi wengine wanasimama hapa wanapinga, sasa mnapinga nini yaani hata hamueleweki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu miradi imepelekewa pesa, pesa zimeliwa leo mnakuja hapa Wabunge mnasema muweke tozo shilingi 50 kwa wananchi maskini ambao mmeweka kwenye REA, pesa za REA mmeweka shilingi 50 haziendi mpaka sasa, miradi ya densification na miradi ya REA imesimama. Pesa hizi muweke kwa mama anayesaga kwa mafuta ya dizeli, mama ambaye anapanda bodaboda kijijini, mama ambaye ananunua mafuta ya taa mumuwekee ongezeko la shilingi 50, mumuumize wakati tunajua na tuna uhakika hamtapeleka maji wala hayo maji hayatapatikana. Sasa hii kitu haikubaliki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndio maana tunasema Engineer Kamwelwe uliambie Bunge hili, mwaka jana ulituambia kuna dola milioni 500 kutoka Serikali ya India, zipo wapi hizo pesa? Kama umesahau sisi wengine tuna kumbukumbu, tunakukumbusha, zipo dola milioni 500 ambazo mlituambia kwamba zipo kwa ajili ya maji vijijini, zipo wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo nimesoma kitabu hiki cha kwenu, mama Makilagi amesimama pale anachangia Mbunge aliyepita sasa hivi amezungumza hata kwa Mwalimu Nyerere hakuna maji. Mimi nimezaliwa Tarime maji yapo, miaka ya 1980 watu wanatumia maji ya bomba. Kadri tunavyoenda mbele tunarudi nyuma yaani leo mwaka 2018 hakuna maji ya bomba, mwaka 1980, 1985, 1986 kuna maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa sisi tukiwaambia bora wakoloni kuliko ninyi Serikali ya CCM hivi mnapinga nini? Kama wakoloni waliacha mabomba, leo hata mabomba waliyoacha yamekufa, yamewashinda, hivi ninyi mnapinga nini sasa hapo yaani mnapingana na nini kwa sababu Serikali yenu imeshindwa.
Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hii na namuomba sana Mungu leo aniwezeshe nisije nikalia humu kwa jinsi watu wa Tarime wanavyoteswa na Serikali hii.

Mheshimiwa Spika, watu wa Tarime wameteswa sana kwenye masuala ya madini, mpaka na sasa wanateswa sana kwenye suala la mbunga na mambo ya TANAPA.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu Waziri wa Ardhi yuko humu atuambie ni nani hasa kati yake au kati ya Wizara yake na watu wa TANAPA au Wizara ya Utalii wanaohusika na masuala ya ardhi ya nchi hii? Kwa sababu leo tunavyozungumza na nataka niunge mkono taarifa ya Kamati iliyosema mambo yanayoitwa vigingi vinavyowekwa kwenye miji ya watu na kwenye ardhi za watu yasitishwe mara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sijui kama nchi hii tunafikiria vizuri kwamba leo wafugaji wa nchi hii wakiamua hata kwa siku 10 peke yake kuzuia mifugo yao kuuzwa kwa ajili ya nyama mtatoa wapi nyama katika nchi hii? Sijui kama tumewahi kulifikiria hilo. Leo wafugaji ambao ni zaidi ya milioni 10 wamekuwa watumwa katika nchi hii, wanaishi kama watu ambao hawatakiwi katika nchi hii, Serikali yao wenyewe inawatesa watu hawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wiki moja iliyopita watu wa Tarime, Kata ya Kwihancha wameenda watu wa TANAPA na DC na group la watu wake anajua alipolitoa, wanakwenda kwenye vijiji, Mwenyekiti wa Kijiji hajui, Diwani hajui, wanavamia, wanaweka kitu kinaitwa buffer zone mpaka ndani ya shule, zahanati, ndani ya miji ya watu, kwenye vungu za watu wanaingia wanachimba ndani wanaweka buffer zone, ndani kwenye mji wa mtu.

Mheshimiwa Spika, Kijiji cha Gibaso kina kaya 120 zote ziko ndani, wanaambiwa watoke hapo, wameishi tangu mwaka 1975 na kijiji hicho kina usajili. Vijiji vya Karakatonga, Gibaso, Nyabirongo, kaya zaidi ya 200 zinaambiwa zihame. Ukienda Kata ya Gorong’a, Vijiji vya Kenyamosabi, Masanga, Nyanungu, Nyandage na Kegonga kaya zaidi ya 2,000 zingine zinaambiwa zihame. Hawa watu hawafuati utaratibu, hawafuati GN, hawafuati chochote. Ukienda pale kuna GN Na. 235 ya mwaka 1968 iliyosainiwa na Mwalimu Nyerere inaonesha mipaka yote kuanzia chini mpaka juu upande wa ile mbuga, they just don’t care. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wanakwenda pale, wanavamia, wanapiga watu, wanaswaga ng’ombe za watu wanaingiza mbugani. Mwanakijiji mmoja ng’ombe wake 250 wameswagwa wameingizwa mbungani, hii hapa risiti aliyoandikiwa ya shilingi milioni 25. Ng’ombe 250 wakiwemo ndama ambao hawana thamani ya shilingi 20,000 analipishwa shilingi milioni 25. Fikiria hata Mbunge mwenyewe ambaye anapata mshahara hapa aambiwe kutoa shilingi milioni 25!

Mheshimiwa Spika, ukichukua hizi karatasi, mwingine ana ng’ombe 54 analipishwa shilingi 540,000, mwingine ana ng’ombe 54 hao hao analipishwa shilingi 5,400,000, risiti fake. Watu wanalipishwa mpaka shilingi milioni 100. Hebu imagine katika nchi hii shilingi milioni 100 unamlipisha mfugaji? Ng’ombe zaidi ya 15,851 wamekamatwa na watu wa TANAPA. Kijana mmoja baba yake alikamatwa …

SPIKA: Wamekamatwa kwenye buffer zone au ndani ya hifadhi?

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, nazungumzia masuala ya buffer zone. Kijana mmoja ng’ombe wao 400 wamekamatwa, baba yake akapata mshtuko akafa, mama yake naye akafa anasoma Mzumbe wakarudi wakazika. Wamefanya kesi, wamefika mpaka High Court, High Court ime-rule kwamba wapatiwe ng’ombe wao 400 amekuta ng’ombe 25 peke yake. Huo ndiyo unyama ambao watu wa nchi hii wanafanyiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, watu wa Tarime wamepigwa risasi, Chacha Gasaya, Wang’enyi Muhere, Marwa Goyagwe, Chirawe Marwa Sira, hawa ni watu ambao wamepigwa risasi na wamekufa. Thobias Waitara, Chacha Gioto, Marwa Ryoba, Kebacho Kebacho, Mwera Muhere hawa ni watu ambao wameuawa kwenye mipaka hii ambayo ipo na watu wameishi hapo, vijiji vimesajiliwa tangu mwaka 1974. Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa bila aibu wanadanganya. Adam Malima ambaye juzi ametishiwa pale Dar es Salaam akapiga yowe dunia nzima ikasikia anakwenda kuwaambia watu wa Tarime kwamba atawashughulikia na Jeshi yaani kwamba Rais amempa mamlaka hayo ili akawashughulikie watu wa Tarime badala ya kuwasaidia.

Mheshimiwa Spika, naongea haya kwa uchungu mkubwa sana halafu wanasema uongo, wanasema watu wamewarushia mishale. Mimi nimemuuliza Waziri, pale Nyanungu kijiji kizima kina watu zaidi ya 5,000 warushe mishale kwa watu 14, mshale hata mmoja usimpate hata mtu mmoja miongoni mwao. Wamerusha mawe hakuna hata gari moja lililopatwa na jiwe yaani kijiji kizima hakina shabaha kiasi cha kushindwa kulenga hata kwenye kioo cha gari moja. Wamekamata watu 100, wamekaa nao siku nne Polisi, DC anawaimbisha nyimbo kwamba sisi ni wahalifu, akina mama, watoto wanaimba Kituo cha Polisi wanapiga makofi, sisi ni wahalifu, tunapaswa kufungwa, kwenye nchi hii. Mazao ya watu yanaharibiwa na ng’ombe wa watu wanataifishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa namuomba Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla, msilete machafuko na chuki kubwa kwenye Taifa hili. Haya mambo yanaumiza kweli kweli, yanatia simanzi kweli kweli.

Mheshimiwa Spika, watu wa Tarime tumelinda hiyo mbuga kwa miaka yote, haina faida yoyote na watu wa Tarime. Haijawahi kutujengea darasa au bati moja. Naomba msilete machafuko kati ya watu na mbuga. Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla nenda kaondoe zile buffer zone kaweke kule ambako beacon zinaonesha zinatakiwa kuwa. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri chukua GN Na. 235 iliyoachwa na Mwalimu Nyerere fanyia kazi. Msitake kuua watu wa Tarime, tumechoka kuuawa, tumechoka kufanywa wanyama katika nchi hii, kila kitu kwetu ni hasara tu. Madini hayajasaidia watu wa Tarime, mbuga nayo imegeuka kuwa mauaji kwa watu wa Tarime. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mbuga hii hapa ya Selous leo Serikali imetoa kibali cha kwenda kukata zaidi ya miti milioni tatu, hamuoni hilo ni tatizo? Hamuoni kama ni uharibifu wa mazingira lakini ardhi yetu waliyoacha mababu zetu, tunaishi pale watu wamezikwa kuna makaburi wanakwenda kuchimba kwenye kaburi la mtu wanaweka kigingi, juu ya kaburi mtu anaweka kigingi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, analeta GPS, GPS ilikuwa wapi mwaka 1968? Kulikuwa na GPS katika Taifa hili mwaka 1968? Watu wamepigwa hapa, kuna wazee wako hapa wa Kisukuma wanalia, wengine anatoka kwenye Jimbo la Mheshimiwa Doto na Majimbo mengine, watu wanateswa.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali ichukue hatua kwenye masuala haya yataleta machafuko mabaya sana. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana nami kwa kunipa nafasi ya kuchangia bajeti yetu hii ya mwaka huu. Nianze na jambo la kwanza la ugatuaji wa madaraka, yaani D by D na Halmashauri. Niliwahi kuwa Diwani, kwa hiyo, nazungumza kitu ninachokifahamu na umuhimu wa Halmashauri hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, iwe kwenye record kabisa kwamba Mheshimiwa Dkt. Mpango atakuwa Waziri wa kwanza na Serikali hii kuua Halmashauri za nchi hii. Nchi hii ina vijiji 18,000. Jimbo langu peke yake lina vitongoji 500. Hawa watu mwaka 2017 walianza na waraka wa kuzuia Madiwani kuwachukulia Watumishi wa Halmashauri hatua. Ilikuwa namba moja kuua Halmashauri zetu. Wakaja na kuondoa pesa zote kutoka Halmashauri kupeleka Hazina then Benki Kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, wakaja kuchukua vyanzo vyote vya Halmashauri ikiwemo mabango na property tax wakapeleka kwenye ukusanyaji wake. Wakaja na mfumo wa kuondoa ripoti za Halmashauri kutoka quartely kwenda kwenye nusu mwaka na sasa kwenye kitabu chake hiki anaanzisha Akaunti ya Pamoja, kwamba pesa zote ziwe zinakusanywa zinawekwa kwenye akaunti. Tarime tukitaka kufanya matumizi asubuhi, tunampigia simu Mheshimiwa Dkt. Mpango ndiyo atuletee tuzibe tundu la choo lililobomoka kwenye Kijiji ha Kemakorere, kwenye Kitongoji cha Nyangasare; vijiji 18,000. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Sera ya Afya ya nchi hii ilivyo, tukiwa na zahanati kwenye kila kijiji, tuna zahanati 18,000. Tukienda na shule, tuna shule 18,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukienda kwenye Kata tuna Kata zaidi ya 7,000. Tukiwa na Kituo cha Afya kila Kata, tuna Vituo vya Afya 7,000. Bulb ikiharibika kwenye nyumba ya mtumishi wa zahanati ya kitongoji fulani, tuombe pesa kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. Mpango, Dar es Salaam. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanataka ku-centralize waongoze nchi hii kutoka Dodoma, hii siyo Rwanda na hawataweza.

La kwanza hilo. Kwa sababu, wame-copy kutoka Rwanda, kutoka Namibia na kutoka Uganda. Rwanda ni mkoa kama Mkoa wa Mara. Tarime peke yake nimesema tuna vijiji 88. Hii nchi ina vijiji 18,000; Mheshimiwa Waziri atakaa hapo awe anapigiwa simu kwamba tundu la choo limeharibika kijiji fulani anapeleka pesa, anaweza hilo? Wasitake kuua nchi hii. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna kichaka Serikali hii imekuwa ikitumia kwa miaka yote kufanya ufisadi, ni kichaka cha umeme. Hapa kwenye ukurasa wa nane, katika kitabu cha Mheshimiwa Dkt. Mpango hiki, anasema, nampongeza Rais kwa ujenzi wa umeme wa Megawatt 2,100 sijui wa Bonde la Rufiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ufisadi mkubwa wa umeme Richmond ulikuwa ufisadi wa umeme wa CCM; Tegeta Escrow ufisadi wa umeme wa CCM; Songas, ufisadi wa umeme wa CCM; na mpaka leo nchi hii haijawahi kupata umeme wa kudumu. Leo ukiwauliza hata Waziri Mheshimiwa Dkt. Mpango na Mawaziri wote hao, kulikuwa na kelele kubwa sana hapa kuhusu wizi wa Tegeta Escrow.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Bunge na Bunge lilikaa mpaka usiku wa manane hapa, likataja watu. Leo walioko gerezani, nami nataka Mheshimiwa Waziri aje anijibu; ni Harbinder Singh na Rugemalila peke yao. Je, hao ndiyo walioiba bilioni 309 za nchi hii? Nataka waje watujibu hapa. Kwa sababu anatengeneza ufisadi mwingine wa kwenda kuiba pesa za Watanzania zaidi ya shilingi bilioni 10 kwenye Stieglers Gorge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nimuulize Waziri, Mheshimiwa Dkt. Mpango, hivi ni utaratibu wa kawaida, leo wanakwenda kwenye nishati wanaonesha kwamba wanahitaji shilingi bilioni 700 kwa ajili ya mradi ambao hatujui na Bunge hili halijui ukamilishwaji wake utakuwa wa shilingi ngapi? Total amount ya kukamilisha ule mradi ni kiasi gani ili tujue tunapoidhinisha shilingi bilioni 700 bado Bunge hili litadaiwa kiasi gani ili ule mradi ukamilike? Sasa wanataka kuanza kuleta shilingi bilioni 700, kesho shilingi bilioni 800, keshokutwa shilingi bilioni 900 Tegeta Escrow, Escrow nyingine na Richmond nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Gujarat India, juzi walisema linakwenda kuzalisha umeme wa Megawatt 5,000 kwa umeme wa Solar kwa gharama ya Dola bilioni 3.384 ambazo ni sawa na shilingi trilioni saba. Mimi, Mheshimiwa Kitandula na Waheshimiwa Wabunge wengine mwaka 2017 tulikwenda Marekani na hii initiative ya Power Africa, tumekuwa na Mheshimiwa Kitandula pale na Waheshimiwa Wabunge wa CCM walikuwepo; nchi hii ina potential ya umeme kutoka kwenye Solar na kwenye wind. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wind peke yake ukichukua Makambako, Singida na Same, tuna uwezo wa kupata umeme Megawatt 24,000. Solar ambayo India wanatumia shilingi trilioni saba kupata Megawatt 5,000 sisi tunakwenda kutumbukiza shilingi trilioni 10 kwenye Megawatt 2,100
ambazo India wamepata zaidi Megawatt 2,900 zaidi kwa bei ya chini ya shilingi trilioni mbili. Huo umeme hautapatikana, wataua viumbe hai pale Selous, wataua pori la Selous na hawatakaa wapate huo umeme wa Megawatt. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka Mheshimiwa Dkt. Mpango aje atuambie hapa, dunia nzima kwenye viwanda wanatumia umeme wa gas na wanatumia nuclear power. Mheshimiwa Waziri viwanda vyake hivyo vya kutumia umeme wa maji ambao alikuwa na Bwawa la Kihansi, Hale na Mtera, hayakudumu hata miaka 30 ukajaa udongo mle na hayafanyi kazi. Atuambie hilo bwawa lao la Stieglers Gorge la shilingi trilioni 10 za Watanzania life span yake ni miaka mingapi? Ili tuweze kulinganisha hizi shilingi trilioni 10 na life span ya hilo bwawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri anakuja hapa anatuambia SGR, hawawaambii Watanzania ukweli. Mapato yetu kwa mwaka mmekusanya maximumly wamepata shilingi trilioni 14.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mishahara ni shilingi trilioni saba, deni la nje shilingi trilioni tisa, wana nakisi ya shilingi trilioni mbili. Hizo pesa za SGR ambazo wanasema ni za kwao za ndani, ziko wapi kwenye hizi shilingi trilioni 14? Wawaambie watu ukweli, SGR wamejenga wapi hata mita moja? Watuoneshe! Wanaenda wanaweka vizimba, wanazindua. Wale Wakandarasi wameshindwa kuwalipa hata petrol, wameondoka. Wawaambie Watanzania ukweli. (Kicheko/ Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri anakaa hapa anakuja anatudanganya hapa eti tunamsifia Mheshimiwa Rais kwa kujenga ukuta wa Mererani, hivi watu pale wanaiba kwa mikataba au wanaiba kwa kupora Tanzanite na kuondoka nayo? Wale wale ambao
tuliwalalamikia; wale wale waliolalamikiwa na wachimbaji wadogo wa Mererani wamewarudisha mle mle ndani ya ukuta, yaani ni jambo la ajabu! (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamewapa nini? Watuambie Mheshimiwa Dkt. Mpango. Watuambie kwamba wanawadanganya Watanzania; leo anakuja hapa anatuambia apandishe bei ya bidhaa. Sisi kwa mfano, tunaishi mpakani, tuna advantage hiyo ya kuishi mpakani. Leo sukari kutoka Kenya Sh.1,200/= Tanzania pale Sirari. Sukari ya kutoka Kagera Sugar Sh.2,200/=, anataka mtu wa Tarime aumie kwa expense yako? Mfuko wa cement wa Bambuli Sh.4,000/=, mfuko wa cement wa Twiga Sh.22,000/=, hawataki Mtanzania wa Tarime anunue mfuko Kenya? Kama wanataka viwanda vyao vishindane, vilete cement kwa bei competitive na ya Kenya, Watanzania wenyewe wachague watanunua wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawawezi kuzuia Watanzania kupata vitu vya bei rahisi na vyenye ubora eti kwa expense ya viwanda vya Wahindi ambavyo siyo vya Serikali hii. Siyo vya kwao, wao hawana hata kiwanda cha nanii; ana viwanda cha tofali, cherehani tano, sijui viwanda vya maandazi, hivyo ndivyo wanavyoweza Serikali ya Awamu ya Tano. Hakuna viwanda vingine, hakuna.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 1966 Chinua Achebe aliandika kitabu cha A Man of the People na kwenye kile kitabu kuna character mmoja anaitwa Chief Nanga. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chief Nanga alikuwa mwalimu na baadae akawa Waziri. Na nikiangalia ile picha ambayo Chinua alikuwa anajaribu kui-portray kwenye uandishi wake na nikiiangalia Tanzania leo, namuona Chinua Achebe alikuwa anaandika kuhusu Tanzania. (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri Mpango ameleta vitabu hapa, vingi sana anazungumza kuhusu mipango ya Taifa ya maendeleo ambayo kila mwaka tunaijadili hapa. Kwenye mipango yake Waziri Mpango, mwalimu hajazungumza kuhusu kuongeza mishahara ya watumishi ambao ndio anategemea wampe ufanisi kwenye utendaji kazi wake. Hajazungumza kuhusu ajira mpya, huyu Waziri Mpango na Serikali yenu, mmekuwa leo ni propaganda. Watu wakitaka kuzungumza mnageuza lile jambo, lionekane ni jambo baya kwenye society na watu waonekane wanatumiwa na mataifa ya nje. Kuna kauli imekuwa maarufu sana, wanatumiwa kuhujumu uchumi na watu wasiopenda Taifa letu. Hawa watu hamuwataji lakini wapo mnawajua ninyi.

Sasa Waziri Mpango wewe unaishi maisha mazuri kama uzalendo ni kuwa masikini kuishi vibaya, kuendesha gari mbaya tuoneshe wewe mfano huo wa uzalendo, kwa nini wewe huutaki huo uzalendo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huo uzalendo wa kutokukaa sehemu nzuri ambao mnataka muwaanimishe Watanzania kwamba uzalendo ni umasikini, kwa nini wewe huupendi huo uzalendo? Kwa nini unaendesha V8 ya Serikali, mafuta ya Serikali, una wasaidizi, nyumba nzuri wote humu Bungeni. Hampendi uzalendo ninyi, mnataka uzalendo huo kwa watumishi wa umma tu. Watoto wa watu wamemaliza

shule. Mwaka 2015 Serikali yenu hii inayokusanya mapato kuliko Serikali zote zilizopita haijaajiri mwaka 2015, hamjaajiri mwaka 2016, hamjaajiri mwaka 2017, hamjaajiri mwaka 2018. Na mnakunakusanya kuliko wote.

Sasa tuje kwenye takwimu zenu, Serikali tukufu mnaokusanya kuliko wote, mwaka 2016/2017…

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mwaka 2016/2017 Serikali hii inayokusanya kuliko zote ilitenga bajeti ya maendeleo shilingi trilioni 11.8 kwa mujibu wa kitabu cha Kamati. Pesa za maendeleo zilizokwenda ni shilingi trilioni 6.4 ambayo ni asilimia 55.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana ni nini, maana yake ni kwamba asilimia 45 ya miradi yote ya maendeleo iliyopangwa haitafanyika kwenye mwaka huo asilimia 45 ya miradi ya maendeleo. Ina maana shule asilimia 45 hazikujengwa, maji asilimia 45 hayakwenda kwa wananchi, barabara asilimia 45 hazikutengenezwa, miradi yote iliyoibuliwa kutoka kwa wananchi 45% haikutekelezwa, Serikali Tukufu inayokusanya kuliko zote ya akina Mpango. Mkikaa hapa mnaimba Stiegler’s Gorge, SGR, flyover kana kwamba mwananchi wa kijijini kwangu kule Nyamwaga au Nyanungu anajua SGR maana yake ni nini au mwananchi wa kijijini kwetu kule Sirari anajua flyover ya Dar es Salaam inamsaidiaje. Leo mmekuja hapa unatuambia kwenye kitabu chako Mpango kwamba kilimo kimekuwa 7.2; sasa mimi nakuuliza Mpango, kilimo kilichokuwa kwa asilimia 7.2 mmenunua mahindi kiasi gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inayokusanya kuliko zote mmeingia mmekuta gunia la mahindi shilingi 100,000, sasa hivi gunia la mahindi haliwezi kununua hata mfuko mmoja wa mbolea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili ununue mfuko mmoja wa mbolea, unahitaji kuuza mahindi gunia tatu, Serikali inayopigania wanyonge, wanyonge mnaojiita ni ninyi mnaoendesha V8. Lakini mnyonge wan chi hii hakuna mnyonge hata mmoja mnaempigania, na mimi nilitegemea Mheshimiwa Mpango muingie hapa, msijisifu Serikali ya wanyonge tuambieni mlikuta wanyonge milioni ngapi, na kwa miaka mitatu mmepunguza wanyonge milioni ngapi, mnataka ku- indoctrinate watu mambo ya ajabu, mnataka kuwaaminisha watu kwamba eti umasikini ni sifa, wakati nyie wenyewe mnaogelea kwenye maisha mazuri. Mnakuja hapa mwaka uliofuata mmetenga bajeti ya maendeleo shilingi trilioni 12 na bila aibu kila mwaka mnaongeza digit na namba hazidanganyi. Mwaka huu mmetenga shilingi trilioni 12 mkatoa ile ile shilingi trilioni sita asilimia 57, sasa mimi najiuliza hizo pesa Mheshimiwa Mpango mnazotuambia mmekusanya kuliko wote mnalia au ziko wapi? (Makofi/Kicheko)

Kwa sababu kwa wananchi hazipo, kwenye ajira hamna, kwenye barabara hatuoni, kwenye Halmashauri leo mnaondoa Capital Development Grant (Local Government Capital Development Grant) mmeiondoa kwa sababu kila siku inawaletea query hamjapeleka hata shilingi mia moja, Tarime mwaka 2016 hamkupeleka, mwaka 2017 hamkupeleka, mwaka 2018 hamkupeleka. Pesa zote tunazofanyia maendeleo tumejenga vituo, tumejenga barabara, own source ya wananchi wa Tarime hakuna shilingi mia moja mlioleta Mpango, pesa hizo ziko wapi? Ziko wapi hizo pesa ambazo mnakusanya?

Haya mmekuja hapa wewe Mpango unaesema unakusanya sana na mkasema mnaweza kununua kama mnanunua ndege mtanunua korosho na wakulima jana, wanunuzi wa korosho jana wametoa statement kwamba hawatanunua tena korosho na mimi namtaka Waziri Mpango wakati anajumuisha hapa atuambie wananunua korosho za wakulima zote ambazo ziko kwenye maghala, kwa sababu hili jambo mliambiwa hapa wananchi walipanga kufikia mwezi wa tisa huu, mwezi wa kumi, mwezi wa 11 wao wameuza korosho zao wapeleke watoto wao shule. Wawe wameuza korosho zao wanunue walau bodaboda, wengine walipe kodi za nyumba, wengine wafanye nini, tunataka Waziri Mpango unapokuja hapa jibu la kwanza utuambie kwa sababu mlisema mtanunua korosho, utuambie mnaanza lini kununua korosho na kwa bei ya shilingi 3,000 kwenda juu hakuna kushuka hata shilingi 100. (Makofi)

Ninyi msifikiri Watanzania hawawaoni haki za binadamu zina tolerate, watu wameuawa Waziri pale anasimama anasema aseme Waziri, aseme polisi aliyeua mtu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi mdogo wangu ameuawa kituo cha polisi halafu mnasimama hapa mnasema eti polisi hawaui watu! Mheshimiwa Zitto juzi ametoa taarifa polisi wameua watu wengi hamjaita kuhoji, mmeita kumtishia na yuko hapa na Zitto mimi nataka uendelee kusema humu Watanzania wajue hatusemi uongo. Mnatishia watu wanaowashauri, mnawawinda wengine tunaishi kwa kuhamahama kwa sababu mnatuwinda kila dakika.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa dakika tano na mimi niseme kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, Prof. Mbarawa ulikuwa na Mheshimiwa Rais pale Nyamongo na nafikiri ndiyo agizo kubwa nchi hii ukipewa na Rais sidhani kama kuna agizo jingine unategemea kusikiliza. Rais alisema maji kwa sababu watu wa Nyamongo madini yanatoka pale yanachangia pesa nyingi kwenye pato la Taifa, ni aibu watu wale kuendelea kunywa maji ya sumu au ya visima vya kuchimba kwa majembe na Mto Mara na Ziwa Victoria lipo pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunajadili maji kwenye Mkoa wa Mara, Mkoa wa Mwanza na Mkoa wa Kagera ambako kuna ziwa linatoa maji yanaenda huko mbali na watu wanapata maji, ni mambo ambayo hayaeleweki kweli kweli kwa wananchi. Kwa hiyo, mimi nafikiri Profesa tuna watu 42,000 pale Nyamongo wanahitaji maji. Mji ule kutokuwa na maji, mji mdogo kama ule mkubwa vile ulivyokuwa na una watu, population yake 42,000 ni sawasawa na Majimbo mengi tu ya watu ambao wapo humu, hauna maji mpaka leo sielewi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili; wote tumekubaliana tatizo la maji ni kubwa kwenye nchi hii lakini tunatofautiana kwenye sehemu ndogo tu kwamba tatizo ambalo linatukumba ni priorities. Tunapangaje vipaumbele vyetu na sisi Wabunge tunasimamiaje Serikali kwenye kutekeleza hivyo vipaumbele. Sasa leo kila Mbunge anasimama humu na ni kwa mara ya kwanza naona Wabunge wanashabikia kwenda kuwawekea wananchi maskini mzigo eti tozo za shilingi 50, inanishangaza sana. sielewi kwamba leo solution kwa sababu hatuna walimu, hatuna barabara, madawati, choo hatuna kwenye shule sijui nini tuweke tozo shilingi 50, hayo mafuta si yatafika 4,000 na nani atasafiri kwenye hayo magari kama mafuta yakifika shilingi 4,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachosema Serikali lazima ije na mpango kwanza zile pesa tulizotenga zenyewe kwenye bajeti kwa nini hazijaenda, kwa nini hazikwenda? Je, na tozo hizo mnazozungumza tumeweka kwenye REA zimekwenda shilingi ngapi kwenye hiyo tozo ya REA? Kwa sababu pia usimamiaji wa bajeti, je tunasimamia na tunatekeleza bajeti kama tulivyozipanga hapa au sisi Wabunge tumekuja tunapiga kelele humu baadaye wanaenda wanakaa kikundi cha watu 4/5 wanatengua kila kitu ambacho Wabunge walipitisha hapa halafu mnataka tuje hapa tupige makofi eti shilingi 5; mimi hata senti moja kuongeza kwenye mafuta napinga na napinga kwa sababu inakwenda kuongezea wananchi maskini mzigo... (Makofi)

T A A R I F A

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru huyu mganga wa meno anajifunza bado Bunge linavyofanya kazi, kwa hiyo, sina haja ya kumjibu. Hapa tunazungumza mambo ya wananchi kwamba watu wana matatizo ya maji na tutoe solution kwamba Wabunge tusikwepe majukumu ya kuisimamia Serikali itoe pesa, kwa sababu wananchi hawapo humu ndiyo wanyonge wenu mnataka leo muwapelekee mzigo; kila mtu anayesimama hapa weka shilingi 50, tukija hapa hiyo shilingi 50 haijaenda nani atasimama humu aseme shilingi 50 haikwenda? Kama mna uwezo huo mbona pesa za REA hazijaenda na hampigi kelele hiyo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi nasema Wabunge…

T A A R I F A

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Hao wenzetu bado wanataka kuaminika, kwa hiyo endeleeni mtaaminika tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninachosema, hoja ya maji wote tunaunga mkono lakini hoja yangu ni kwamba Wabunge wajibu wetu ni kuisimamia Serikali, amezungumza vizuri sana hapa mama Mheshimiwa Conchesta, amesema haya mambo ya kuja hapa tuna-beg naomba tumekuwa Matonya humu na vikombe, naomba piga magoti, hapana lazima Serikali ijue Wabunge wanapozungumza hapa wanawawakilisha walipa kodi wa nchi hii ambao wamejikamua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo tunasema hapa tuongeze shilingi 50 kwenye mafuta ya taa kweli? Hivi ninyi mnajua vijijini wananchi wanaoishi kijijini ambaye kutoa shilingi 2,000 ni tatizo kweli kweli na kama mna uchungu kiasi hicho, nani ame-volunteer mshahara wake humu, mnalipwa mamilioni; anzeni nyie kwamba tukatwe milioni moja moja kila mwezi iende kwenye maji kama kweli mna uchungu kiasi hicho... (Makofi)

MHE. DKT. GODWIN O. MOLLEL: Acha ufisadi kwanza wa madini wewe…

MHE. JOHN W. HECHE: Hatuwezi kukubali tuje kubana wananchi wanyonge eti ndiyo wanyonge wetu kwa sababu hawapo humu, tunakwepa majukumu shilingi 50. Na hiyo itakuwa siasa ambayo tutaizungumza kwa wananchi, muelewe kabisa, shukrani. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nianze na jambo moja hapa. Hakuna kanuni yoyote ya Bunge hili ambayo inamzuia Mbunge kuzungumza kuhusu Waziri yeyote kwenye hili Bunge. Kwa hiyo naomba tafadhali tanapokuja hapa tunalipwa pesa za walipakodi wa nchi hii ili tufanye kazi yao. Sasa haya mambo ya kusumbua watu wakati wanachangia sio mazuri. La kwanza hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, tumezungumza sana kuhusu kilimo, wazungu walipotaka kuanza kuendelea Agrarian Revolution ndio ilikuwa ya kwanza karne ya 16. Kati ya mambo makubwa mawili ambayo Serikali yenu kuyasabishwa yamedharaulika katika nchi hii ni kilimo na ualimu, ambayo ni mambo ya muhimu kweli kweli. Ukiangalia mwanafunzi anayekaribia kufeli shule utasikia familia yake inamwambia ameshindwa hata ualimu, ndipo mlipoufikisha ualimu wa nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo, mtu akikaribia kuonekana hawezi kusoma vizuri wanamwambia utarudi kupiga jembe, kilimo ndicho kinawatajirisha watu na ndicho kinachotoa chakula cha 100% kwa watu, kinatoa ajira 80%, kinatoa malighafi za viwandani na kilimo ndio kila kitu. Sasa wamefanya vice versa na ndio maana tukiwaacha kuendelea kuiongoza nchi hii hata miaka 1,000 hamuwezi kutuondoa hapa, hata miaka 1,000. Ndio maana mwaka 2015 wakati Serikali hii inayojiita ya wanyonge inaingia madarakani, bei ya kahawa pale Tarime ilikuwa Sh.2,200. Sasa hivi tunavyozungumza Mheshimiwa Hasunga bei ya kahawa ni Sh.800, are we moving forward au tunarudi nyuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama bei ya kahawa ni Sh.800 kwa wakulima ambao wameanza kujitegemea, kwa wakulima ambao alikuja Naibu Waziri Tarime, wamechukua kahawa ya wakulima watu maskini Kata za Muriba, Itiryo, Mbogi, kata nyingi tangu mwezi wa Saba mwaka jana hawajawalipa mpaka leo na wanasema wao ni Serikali ya wanyonge. Halafu wanasimama watu humu kwa sababu wao wanalipwa pesa za kodi ya watu maskini, wanafungiwa mikanda kwenye gari, wanajisahau wanajiona ma-queen na ma-king, wanasahau kwamba hizo ni pesa za walipakodi maskini, sasa wanasimama huku, wanawafanyia maudhi Watanzania waliowapa huo ukubwa wanaotamba nao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni aibu kwamba Waziri anaweza kusimama hapa akapinga kwamba Watanzania hawazidi kuumia kwa sababu ya aina ya jinsi mnavyochukulia Kilimo. Sasa leo mmechukua kahawa ya watu, mwezi wa saba. Nani angeambiwa hapa tangu mwezi wa saba hatulipwi posho au hatulipwi mshahara kama mngekanyaga hapa, hata hela za mafuta. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na Watanzania wajue, mpaka mafuta mnayokwenda nayo Bungeni na kurudi mnalipwa na Watanzania. You are being paid millions of money za walipa Kodi maskini; sasa tunaposimama hapa, hebu tuwafikirie pia waliotusababisha tukaja hapa, la kwanza hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kuhusu Korosho. Katika hili naanza kwa kuweka mezani kwako hapo watu wako wachukue, gazeti la Daily Nation la Kenya la tarehe 12 lilisema Serikali ya Tanzania yaingizwa chaka na kampuni ya kihuni ya Indo power, ambayo leo mnataka mui-protect. Ninataka niwaambie, hamtai-protect mkii-protect humu tunazungumza nje. (Makofi) (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kujua, hiyo zabuni ya kuanza kuzungumza na hiyo Kampuni ilitangazwa wapi? La kwanza hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nani aliyekuwa anafanya mazungumzo ya awali na hiyo Kampuni ya Indo power, ambayo gazeti hili la Daily National linasema halina hata ofisi kule Kenya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa na hili ni jambo la aibu, na tunakuja humu mambo makubwa tunayafanya mambo madogo kwa sababu ya mizaha. Sasa nataka mtuambie hivi kama gazeti mwandishi mmoja tu anaweza kufanya uchunguzi akajua hii Kampuni haina ofisi, ni Kampuni ya kitapeli, Serikali nzima mnampeleka Gavana wetu wa Benki Kuu pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnapeleka Mawaziri watano, mko hapa kwenye picha, mlikuwa pale, akiwemo Profesa Palamagamba Kabudi, ambaye mnam-protect hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nani alianza kuzungumza na hiyo Kampuni? Nataka mtuambie je, hiyo Kampuni, yaani gazeti la Daily National la mwandishi lina uwezo wa kuchunguza kuliko Serikali yetu? Muwaambie Watanzania, muwaambie Watanzania na kama si hasara mtuambie; unakuja unatuambia hapa Kabudi anasema eti huyu mtu alikuja na ndege, so what? Mimi na Esther Matiko tunakodi helicopter tunaenda Tarime, kwa hiyo sisi ni wawekezeji? (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eti, kwani, yaani mawazo yenu, Waziri kabisa anasimama, eti hii ni Kampuni nzuri kwa sababu huyu mtu ni Mwekezaji, serious amekuja na ndege. Freeman Mbowe huyu anamiliki Caravan, Godbless Lema anamiliki Ndege ya watu 16, sasa na yeye ni Mwekezaji? (Makofi/Kicheko)

MBUNGE FULANI: Gwajima.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Gwajima, amepaki pale Helicopter yake. (Kicheko/Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche, Mheshimiwa Heche ongea na Kiti wewe, changia, changia. Jielekeze kwenye hoja sasa, mambo, jielekeze kwenye hoja. (Kicheko)

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Hii Kampuni ilipatikanaje?

MBUNGE FULANI: Dakika za Heche….

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ni mambo ya muhimu tunataja kujua, nani alianza kuzungumza nao? Tunataka kujua; common sense ya kawaida, ukimsikia Profesa Palamagamba Kabudi, na Gavana wa BOT Profesa common sense inakataa, kwamba hawawezi kufanya maamuzi ya vile, kama si rushwa basi hawawezi kuongoza hata kibanda cha kuuza nyanya hawapaswi kuongoza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawapaswi kabisa, na hili suala Watanzania maskini…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Heche, hivi mnataka nifanye nini sasa? Nimeshaitolea uamuzi, you may not like my ruling lakini ndio uamuzi wangu.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa. Kule Kusini kuna Watanzania wenzetu ambao ni wakulima wa korosho, na sisi Wabunge tuko hapa ku-protect watu wetu. Kuna Watanzania kule korosho ndio mshahara wao, kama ninyi mnavyolipwa kila mwisho wa mwezi. Korosho ndiyo karo ya watoto wao, Korosho ndiyo malipo ya benki wanayodaiwa wamekopa wamejenga. Kwa hiyo tunapozungumza haya masuala tuyazungumze kwa uzito huo. Ndiyo maana sisi tunasema, kama alivyosema mtu anayekaimu nafasi Waziri Mkuu; kama kweli Serikali nzima, mna collective responsibility na mnakubali kwamba kosa la kuingiza nchi kwenye aibu gazeti la Kenya linatuandika. Pamoja na mambo yote tunayoweza kufanya humu, Rais wa nchi, nje ya nchi ni Symbol ya nchi, na tutam-protect. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa gazeti hili limesema, pamoja na kwamba umesema hivyo, wewe tunaamini kauli yako ni ya Waziri Mkuu. Leo kama mna uadilifu wa kutosha, Serikali nzima resign kwa sababu mmeaibisha nchi yetu vya kutosha kwa kwenda kuingia na Kampuni…. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Madini
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa nafasi hi ya kuchangia. Kwanza napenda nimpongeze sana Mheshimiwa Kapufi, nimemsikiliza vizuri sana, amezungumza kwa kweli mambo mazuri kwa ajili ya nchi yetu na nilipokuwa namsikiliza nilifikiri anarejea Sera ya CHADEMA ya Julai, mwaka 2018 inayozungumza kuhusu madini.

Mheshimiwa Spika, wenzetu kule Norway wanapochimba gesi yao na mambo ya madini, wameweka benki, wanaweka akiba kwa ajili ya vizazi vijavyo na sisi kuendelea kuwa na kauli hizi kwamba madini yabaki chini hayaozi hayafanyi nini, siafiki utaratibu huo, ninachokubaliana nacho, ni kwamba, madini haya yanayochimbwa, yachimbwe vizuri na fedha zinazotokana na madini haya zitunzwe kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi almasi duniani, 40% ya almasi inayovaliwa duniani ni almasi ya kutengenezwa. Sasa tunapokwenda kuendelea kusema sijui tuna almasi, wao watu wanaonunua haya madude baadaye wakija waka, hasa haya ya mapambo, wanaweza kuja kuyabadilisha wakaanza kutumia vitu vingine ukabaki na tanzanite na almasi ambazo hazina thamani yoyote. Kwa hiyo, nafikiri tuangalie lakini tuna-insist kwamba, kila tunapotoa rasilimali hizi zibaki kwa ajili ya vizazi vingine, tusitumie sisi wenyewe na tukamaliza.

Mheshimiwa Spika, suala la pili ambalo nahitaji maelezo kutoka kwa Mheshimiwa Waziri, wachimbaji wadogo, wanalipia environmental impact assessment, milioni tatu mpaka milioni sita, lakini kuna mtu wa mazingira yuko halmashauri, kazi yake ni nini yule mtu wa halmashauri pale, mpaka hawa watu wanalipia hizo fedha. Mbona mtu wa kilimo tunapokwenda kuomba consults hatulipii na tusipofanya environmental impact assessment, ambayo nakubali ifanyike, unapigwa faini. Kwa hiyo, nataka kujua kwa nini wachimbaji wadogo wanalipia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la tatu, sumu iliyotiririka kwenye Mgodi wa Nyamongo, nimeizungumza vizuri kwenye hotuba na ningependa hotuba yangu nzima Mheshimiwa Waziri ajitahidi kuisoma na aijibu. Kuanzia mwaka 2017, watu wamekufa, mali za watu zimepotea, Mto Tigite uliharibika na huu mto unatiririka mpaka Mto Mara, pote kwenye maeneo karibu ya kata sita. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, miaka yote hii, tumekuwa tukiambia Serikali, kwa ushahidi, kwamba kuna watu wanababuka ngozi kwa kuoga maji, viumbe vinakufa, nyasi zinakauka, wakati wote huo Serikali ilikuwa ikisema, hakuna kitu, hakuna kitu, hakuna kitu. Mheshimiwa Waziri alikuja pale akaona maji yanavyotiririshwa, eneo la Kwinyunyi, Kwimange na kule Kegonga, kitongoji kizima watu wamehama, wameacha maeneo yao, hayazalishi chochote kwenye kilimo. Eneo ambalo ulikuwa unalima unapata labda gunia 100, leo ukilima hupati hata gunia 10 kutokana na madini, tembo kuathiri lile eneo.

Mheshimiwa Spika, asa nataka, Mheshimiwa Waziri, kwanza, Serikali wamepiga faini pale, hivi wao wameathirika nini? Kwa sababu walioathirika ni wananchi wanaoishi yale maeneo. Tunataka hizo fedha walizopiga faini, ziende kulipa wananchi ambao wameathirika, wananchi wa Tarime ambao wamekunywa maji ya sumu, ndiyo wakalipwe fidia. Ng’ombe waliopotea, watu waliokufa na tunataka ifanyie assessment mpya, kujua madhara ni kiasi gani na wale wananchi wapate fidia inayostahiki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Waziri ni rafiki yangu, nimekuwa nikimshauri kufuata sheria, Sera ya Madini ya Mwaka 2009, inasema, unapohamisha watu kutoka eneo la mgodi, unawalipa fidia, compensation, unawajengea makazi, yaani unafanya reallocation na unawalipa gharama za kuwahamisha. Hakuna, watu wote waliolipwa fidia Tarime, imekuwa ni kidogo na mgodi umekuwa ukisema, ooh ni kubwa sana, lakini hakuna mtu ambaye amewahi kufanyiwa resettlement kwa kujengewa nyumba na kupewa makazi, watu wachache tu waliofanyiwa resettlement, halafu hawakulipwa fidia, wakajengewa vinyumba tu, Waziri aliviona na Kamati ya Waziri Muhongo ilisema, vibomolewe na vijengwe upya, ukipiga teke kanadondoka. Sasa tunataka kujua ni kwa nini, hawa watu hawafanyi hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la Mchuchuma na Liganga, amelizungumza vizuri sana ndugu yangu hapa Neema. Kampuni ya Hongda Sichuan, mwaka 2019 ilisaini mkataba na Serikali na mkataba wa zaidi ya dola bilioni tatu, ambazo ni trilioni 6.8, ambazo zilikuwa zimekuja kufanyiwa investment hapa, Watanzania zaidi ya elfu tano walikuwa wanakwenda kupata ajira za moja kwa moja kwenye huu mgodi. Mpaka sasa imekuwa ni kizungumkuti, Serikali ime-delay fedha hizi zote ambazo zingekuja kusaidia uchumi wa nchi yetu, nataka Waziri atuambie, ni kwa nini kumekuwa na delay tangu mkataba huu usainiwe na Wachina na tukaunda kampuni. Kwa nini mpaka sasa investment hii haija-take off! Tunataka kujua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, service levy; makampuni yanayofanya kazi pale kwenye mgodi na mgodi wenyewe, umekuwa ukilipa 0.03% ya service levy kwenye halmashauri, lakini kampuni ambazo zinalipwa fedha nyingi sana ni kampuni za insurance. Insurance wanachukua fedha nyingi, wana-insure kuanzia dhahabu, mitambo yote mbayo ni ya gharama kubwa na migodi yenyewe, lakini kampuni zote za insurance, hazilipi hata senti moja ya service levy kwenye maeneo ambayo halmashauri zinatoka.

Mheshimiwa Spika, sasa nataka Waziri aje atuambie, kuna vikampuni vya Watanzania, mtu anafanya kazi ya kujenga kadaraja pale kwenye mgodi, kazi ya milioni 100, analipa 0.03% na siku hizi halmashauri kwa sababu hazina mapato, hata kwenye maduka tu, haya ya wananchi, mtu ana kioski cha milioni mbili, anafukuziwa na 0.03% ya service levy. Ni kwa nini makampuni makubwa ya insurance ambayo yanachukua matrilioni ya fedha kutoka Tanzania, hayalipi service levy kwenye migodi! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la mwisho ni kuhusu smelter. Kwa nia njema kabisa sisi tulizungumza hapa wakati sakata la makenikia linakuja mnatuambia mtatuletea Noah, na Watanzania hawajasahau na tunataka mjibu Noah ziko wapi? Kwa sababu tuliambiwa mambo mengi hapa tukaambiwa na smelter inajengwa, mwaka 2017 hakuna smelter. Amezungumza Mheshimiwa Kafupi pale, watu wanazidi kupata hasara; 2018 hakuna smelter, 2019 hakuna dalili, 2020 hakuna dalili; smelter mtajenga lini hapa? Kwa sababu tuliambiwa hapa tumeibiwa sana makenikia haziendi na sisi tunasema thank you very much, now we want a smelter here, tunataka smelter na watu waanze kufanya uchenjuaji wa madini hayo hapa tuone faida kwenye nchi yetu hii. Kwa sababu hizi kauli za kisiasa ambazo zimekuwa zikifanyika kila siku kufanya kuwahadaa Watanzania sisi ni wazalendo kuliko watu waliokuwepo sijui na nini, tunataka sasa uzalendo huo uonekane kwa vitendo, na tunataka wananchi waanze kunufaika na madini hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na nazungumza hivi kwa sababu watu wanaotoka kwenye maeneo ya madini wameathirika sana. Jana tulikuwa kwenye semina fulani hivi na mtu mmoja akaanza kusema pale, sitaki kumtaja, ni Mbunge na alikuwa Waziri hapa anasema eti tuambiwe benchmark ya faida ni nini, kama hatujanufaika tumepata sijui kodi ya trilioni moja. Hivi mzee Ryoba Ilondo ambaye ng’ombe wake zaidi ya 500 wamekufa unamwambia mgodi una faida gani kwake?

Kwa sababu yeye alizoea ng’ombe wale asubuhi anafunga kwenye jembe anakwenda kulima pale Matongo, anavuna, anakamua maziwa watoto wake wanakula; maisha yanaendelea. Alikuwa kwenye nyumba ambazo zimeezekwa kwa majani fine, lakini yeye maisha yake yalikuwa yanaendelea, hawajawahi kulala njaa; lakini leo ng’ombe wake wamekufa analala njaa; unamwambiaje mgodi una ufaida, na madini haya yanafaida? kwa hiyo Mheshimiwa Waziri hayo ni mambo serious tunaomba majibu kwa ajili ya watanzania,ahsante sana.(Makofi)
Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi wa Mwaka 2018
MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia. Nianze kwa kurejea Ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hasa kile Kipengele cha (c) ambacho kinasema sehemu ya Pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambacho kitakuwa na madaraka kwa niaba ya wananchi kusimamia, kushauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipengele (c) kinasema kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutunga Sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katiba hii ambayo wote tuliapa kuilinda akiwemo Rais inasema kwamba Bunge hili ndicho chombo chenye Mamlaka ya kujadili mpango wowote wa muda mfupi na wa muda mrefu na kuutungia Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti asubuhi na nimewasikiliza Wabunge wote wa CCM na kwa kweli sisi hakuna mtu yeyote anayesema suala la kuhamia Dodoma ni suala baya, hakuna miongoni mwetu anayesema kuachilia mbali wachache wanaofanya spinning kwa sababu ya manufaa yao ya kisiasa kwa sababu wanaweza kuona hapa leo tu hata kesho yake hawawezi kuona.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumesema kwamba Mpango wa Taifa ambao tulijadili hapa tulipokuja hapa Bungeni na tukaupitisha na tukautungia Sheria. Mpango wa Taifa wa mwaka mmoja tumewapa challenge akina Mheshimiwa Jenista kwamba tuonesheni kwenye mpango huo sehemu yoyote mliyoandika kwamba mna mpango wa kuhamia Dodoma kipindi hiki. Wamebaki wanaanza kusema, Dodoma ni katikati, Dodoma ni katikati, Dodoma ni katikati, Dodoma ni katikati ya nini? (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunachotaka watuambie kwa watu walioenda Dubai mwaka 2004, ilikuwa ukifika Dubai mnaona Billboards kubwa zinaonesha Dubai itakavyokuwa baada ya kuwa New Dubai imejengwa na leo ukienda ukaona picha ulizoziona kwenye Billboards na Dubai ndivyo ilivyo sasa hivi. Sasa hawa karne ya 21 wanaleta Bunge hili hapa watu wanajadili vitu petty petty tu, yaani hakuna kitu karne ya 21 hakuna mpango, hakuna utaratibu, hakuna nini, Rais akishasema kesho tunahamia kule kwetu Nyamwaga, kesho wote mnabeba mabegi tupo Nyamwaga, eeh! Nyamwaga hapa ndio penyewe sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanatafuta sababu za kuokoteza, mara kuna usalama Dodoma, Mheshimiwa Lissu amepigwa risasi hapa, hapa hapa Dodoma kapigwa risasi hapa wanapopaita sehemu ya usalama, mpaka leo hawajawahi kukamata hata mtu mmoja na hawajawahi kusema nani aliyempiga risasi. Sasa wanaletewa hoja hapa kwamba nchi hii watu wana matatizo ya Vituo vya Afya. Nchi hii tangu kuanza kwake sera ya afya ya kwetu inasema kila Kata itakuwa na Kituo cha Afya, tunapozungumzia Kituo cha Afya tunazungumzia chenye uwezo wa kulaza mtu, chenye uwezo wa kufanya operation na chenye uwezo wa kutoa matibabu ya vipimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tarime nina Kata 26, tuna vituo vitano na vinne tumejenga kipindi hiki halmashauri inapoongozwa na CHADEMA, tulikuwa na kituo kimoja tu basically. Nchi hii mpaka leo Mbunge anasimama anasema tuna Vituo 200, eti Vituo 200 miaka 56, ndio tukae hapa tupigiane makofi kati ya vituo zaidi ya 4,600 wakati huo wanachukua pesa, pesa za walipa kodi maskini eti wanahamia Dodoma, wakati tuna majengo Dar es Salaam, yaani nawashangaa no wonder leo wanatafuta watu waunge mkono hoja wanachukua zaidi ya bilioni 80 za watu wanapeleka kwenye uchaguzi wakati watu wanakufa mashuleni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, asubuhi hapa nilimwona Mheshimiwa Waziri anajibu wanachukua bilioni 80, wanapeleka kwenye uchaguzi, Wabunge wanaenda kufanya sijui nini ile, eti kutafuta bilioni mbili. Tunatakiwa kupimwa sijui tunafanyaje kazi kwa kweli yaani bilioni mbili mnaenda pale sijui nini ile, wanaenda kutafuta bilioni mbili wakati bilioni 80 zinachukuliwa kwa kufanya mchezo watu wanaunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watoto hawana madawati, asubuhi tumeona mama Kikwete anasema shule moja ina watoto 4000 shule moja ya msingi, sio watoto wetu, watoto wenu hawasomi hapo kwa sababu tu ni nanii wanakuja hapa kwa sababu watoto wenu hawasomi hapa makofi kwa kila kitu makofi kujipendekeza, unafiki, kutokujadili mambo ya msingi, tunachukua pesa tunaleta hapa hatuna Vituo vya Afya, hatuna maji .

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi, Muswada huu najadili kwamba gharama za kuhamia hapa ni kubwa mno ukilinganisha na mahitaji tuliyonayo. Ndicho ninachosema kwamba unapokuwa Kiongozi uko nyumbani kwako una watoto, una elfu 10 mtoto anaumwa na wewe unataka kunywa bia, utapeleka mtoto hospitali kuliko unywe bia ndicho ninachosema, simple! Utakuwa mzazi wa ajabu kweli kweli mtoto wako anaumwa wewe una elfu 10 ya kununua dawa, ukaenda kunywa bia halafu unarudi unasema bia ile ilikuwa muhimu sana kwa sababu nilikuwa na mawazo leo. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo ndio maamuzi yenu nyie mpo wengi na mnaweza kufanya spinning mnaweza kudhibiti Vyombo vya Habari mkazungumza nyie peke yenu, lakini ukweli wa Mungu utasimama na sisi sio kizazi cha mwisho hapa Tanzania. Nataka niwahakikishie haki ya Mungu kabisa Rais mwingine atakuja, atarudisha hii Dar es Saalam mimi nawaambia, tupo hapa Mungu atuweke wazima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema hivyo,? Nasema kwa sababu wanafanya mambo ambayo ni unplanned yaani wanataka Bunge hili lote Watanzania wamewalipa posho wamekuja kukaa hapa wanakula vizuri mshahara wa Mwalimu ni Sh.300,000/=, tumelipwa hapa Sh.300,000/= kwa siku tunakuja kujadili vitu petty tu ambavyo havina msingi wowote kwa maendeleo ya watu wa nchi hii, hakuna reasoning, hakuna mipango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiona Abuja watu walikuwa wanahama kuna mipango. Mwalimu Nyerere mwaka 1973 alisema baada ya miaka 10 kuna mpango mwaka mmoja, mwaka wa pili tutaweka Ofisi, mwaka wa tatu tutafanya hiki, sasa wameleta familia za watu hapa, mama yupo Dar es Salaam, baba yupo hapa, halafu wanadai wamelipa watu wote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukweli ni huo, Mungu anajua na hata wakitumia mabavu na sisi wengine ambao tunasema ukweli tunajua kwamba hawakuwa na mpango wameshtukizwa tu Tamko, si tunaongea na nyie tu hata kwenye chai. Tamko tu sasa wameleta watu wanaenda kurundika UDOM, yaani Chuo kilijengwa watu wasome, eti wamefanya Ofisi na Waziri kabisa eti anaamka anakwenda UDOM pale kwenye madarasa ya watoto, wamekata na ceiling board eti niko Ofisini hapa. Haya mambo ya kuendesha nchi hii kama imezaliwa leo na inaisha kesho, haya mambo…(Kicheko/Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)