Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Fedha na Mipango

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Fedha na Mipango

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi. Niungane na Mheshimiwa Nsanzugwanko kuhusiana na barabara ya Nyakanazi tokea nimekuwa Mbunge hapa nasikia Kigoma-Nyakanazi toka nimekuwa Mbunge kipindi cha kwanza, kwa kweli watu wa Kigoma mnaonewa inabidi tuwasaidie, mpigiwe debe, mpo porini sana, mmetengwa. Nadhani Wizara watasaidia kidogo, ilikuwa mara ya kwanza kufika Kigoma kwa kweli mko nje ya Tanzania.

Mheshimiwa Spika, nikirudi kwenye Wizara hii; naamini Wizara hii ya Fedha na Mipango ni Wizara ya Fedha na Mipango, lakini kwa mtazamo wangu naona wamejikita zaidi kwenye fedha kuliko kwenye mipango na kwa kuwa wao ni Wizara ya Fedha na Mipango walipaswa wawe ni Dira kubwa ya Taifa ili kuliongoza namna gani ya kupata hizo fedha halafu kisha wakusanye, lakini Wizara hii katika utendaji wao wamekuwa kama vile ambavyo wanataka wamkamue ng’ombe ambaye hawamuandalii mazingira mazuri ya kutoa maziwa.

Mheshimiwa Spika, Wizara hii ndiyo inayosimamia Dira ya Taifa, Wizara hii ndiyo inasimamia Mpango wa Miaka Mitano wa Taifa, lakini kwa bahati mbaya toka Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani kuna mipango mingi ambayo inatekelezwa na Wizara hii ni ile ambayo haipo kwenye Mpango wa Miaka Mitano wa Taifa.

Mheshimiwa Spika, sasa mimi siyo Mchumi, I am Theologian by professional, inanichanganya kidogo kwamba sasa hiyo mipango ni ipi wanayoisimamia kwa sababu tunakuwa na priorities, tunaweka mikakati, lakini mwisho wa siku tunapokuja kwenye utekelezaji wanaleta vitu vingine kabisa ambavyo havikuwepo kwenye mpango wa nchi, wanaanza kufanya vitu ambavyo havipo.

Mheshimiwa Spika, mfano mzuri, hakuna mtu anayekataa move ya kuhamia Dodoma, lakini haikuwepo kwenye Mpango wa Miaka Mitano, it was more of a political than economical, imetulete shida, tunahangaika, hatukuwa na Ofisi, imechanganya mambo mengi sana katika kuendesha nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, nirudie tena, hatukatai kuhamia Dodoma lakini hatukuwa na mpango huo, hela tumeitoa wapi? Natoa mifano kama hiyo.

Mheshimiwa Spika, mpango mwingine ambao naweza kusema, mipango hii ambayo inafanywa ambayo haikuwepo kwenye mpango wa nchi, inaleta tabu katika nchi yetu. Nitoe mfano mmoja wa haraka haraka, kwa wastani TRA wanasema kwa sasa hivi wanakusanya wastani wa trilioni 1.3 mapato kwa mwezi. Hata hivyo, mapato haya ukiangalia wao wamekuwa kama Wakala tu, hela nyingi wanazokusanya siyo za kwao.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, wanachukua wharfage, wanachukua hela zote za halmashauri, property tax kwa mfano za majengo wamechukua, wamechukua zile VAT refundable, wamechukua mpaka zile levy za korosho, wamechukua hela nyingi ambazo siyo za kwao halafu wanapita mitaani, barabarani kwa wananchi kisiasa wanasema sasa hivi tumedhibiti mapato yanakuwa mengi. Wakati huo huo hizo hela walizotunyang’anya kwenye halmashauri zetu mnazi-ground halmashauri, hazifanyi kazi vizuri, yaani hadi hela za REA nazo wanasema za kwao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wamezi-ground halmashauri, sasa leo hiyo mipango una-match vipi mipango na jinsi ambavyo wanakusanya hizo pesa. Matokeo yake katika halmashauri wameshindwa kupeleka wataalam wazuri, wameamua tena ku-centralize ambapo ni mipango iliyoshindikana toka tumepata uhuru, tulijaribu tukakwama.

Mheshimiwa Spika, kwenye Majukwaa wanasimama kwamba wanakusanya pesa nyingi, lakini zile pesa ambazo wametunyang’anya kwenye halmashauri hazirudi kwa sababu hakuna mipango mizuri. Nilitegemea Mheshimiwa Waziri katika mipango yake angeishauri Serikali hii kwamba kupeleka watendaji katika halmashauri ambao hawana weledi, ambao wameenda kisiasa kunaharibu utendaji wa kazi kwa sababu nchi hii mtu akiwa Mwanasiasa anaaminika kwamba anajua kila kitu.

Mheshimiwa Spika, nakumbuka siku moja Katibu aliyeondoka Dkt. Kashilillah alisema hapa Wabunge tukianza hapa kuzungumzia masuala ya nuclear tutataka tuchangie hata kama hatuyajui. Pia tunaamini kwamba mtu akiwa mwanasiasa anajua kila kitu na nategemea Wizara ya Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Dkt. Mpango ingekuwa ndiyo dira ya kuishauri Serikali hii. Tumekuwa na mipango mingi ambayo iko nje ya bajeti.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia wakati wa Dkt. Kikwete, Dkt. Kikwete ameondoka hapa tunakusanya 900.0 billion 900.0 ambazo hakukusanya hizi hela za wengine. Inaonesha yeye system zake zilikuwa zinafanya kazi vizuri lakini wao wame-intefere maeneo mengine yote, wanataja pesa kubwa hii lakini bado utekelezaji haupo. Sasa wanatangaza hizo pesa zote zipo zinakusanywa, kwa nini kwenye pesa za maendeleo pesa hazirudi kwenye maeneo yetu tunapotoka kama hizi pesa zote wanazikusanya? Mfano mzuri, kwenye kitabu cha Kamati wamezungumza mpaka Disemba, 2017 Serikali ilikuwa imekusanya 7.6 trillion na mpaka Februari, 2018 walilipa deni la nje trilioni 5.5 maana yake tulibakiwa na trilioni mbili.

Mheshimiwa Spika, sasa tunaendeshaji hii nchi kwa utaratibu huo kama hela zote tunazokusanya tunalipa madeni na bado kwenye kitabu cha hotuba cha Mheshimiwa Waziri ukisoma ukurasa wa 96 amezungumza na hawa wamesema, anasema kwamba deni bado linahimilika lakini mzigo mkubwa bado anabeba mwananchi wa Tanzania. Wakitoka nje kisiasa wanasema kila kitu kipo safi, tunapongezana hapa, mtumbwi unazidi kuzama, kiuhalisia tuna-suffocate, hakuna oxygen katika nchi hii bado tunazama. Kila mtu anaamua anavyotaka, tutapigiana makofi hapa lakini hela hamna. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukienda kwenye kila Wizara kama ni Wizara zipo zimepata pesa zaidi ya asilimia 50 na kitu ni chache sana, zote ziko chini ya kiwango. Kama tunakusanya mapato hayo Waziri, Mheshimiwa Dkt. Mpango, kwa nini Wizara zote zinapata pesa chini ya kiwango? Haya ni masuala ambayo anatakiwa atujibu na ningeomba katika suala hili anijibu hela halisi ambayo anakusanya kodi ya TRA bila kuchanganya na hizi nilizomtajia, wharfage zile za Halmashauri, sijui VAT refundable za watu wengine ambazo wanashika ni shilingi ngapi? Tujilinganishe na Serikali iliyopita na ya sasa kama tunakwenda pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine kama nilivyozungumza, mipango mingi anayotekeleza sasa hivi Mheshimiwa Waziri haikuwepo kwenye Mpango wa Miaka Mitano. Hatukuwa kwenye mpango wa miaka mitano kwamba we will move from Dar es Salaam to Dodoma, kwenye mpango wa miaka mitano hatukuwa na standard gauge, where are we getting the money?

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, hizi hela ukiangalia kiutaratibu wamekopa mikopo ya commercial ambayo ni very expensive. Tunakopa mkopo kwa sababu commercial unakopa mkopo, unaanza kulipa mkopo huo mapema kabla ya ule mradi wa longterm haujaanza kuzalisha sasa ku- service huu mkopo tuta-service kupata hela, itatoka wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri atupe majibu hapa. Ukiangalia Ethipoia au Kenya wao walipata concession loan ambayo ukikopa wale watu watamaliza ule mradi, halafu wakishamaliza ule mradi, unapoanza kufanya kazi ndipo unaanza kulipa. Ni kitu gani kimesababisha wasiende kwenye mikopo hiyo, wameenda kwenye mikopo hii ya commercial loan? Mheshimiwa Waziri, Dkt. Mpango ningeomba anijibu. Kwa hiyo, kuna mipango mingi ambayo tunafanya lakini haikuwepo kwenye utaratibu.

Mheshimiwa Spika, tumeenda kwenye mambo ya Stiegler’s gorge hapa, tatizo la Tanzania siyo kwamba tuna tatizo la umeme, tatizo ni kuuhamisha umeme ulipo kwenda kwa walaji. Hizo megawatts zote tunazozitaka tunataka tuzifanyie nini? Ambapo tutachukua hela ya sasa, kwenye longterm loan ambazo zinakuwa ni mzigo kwa Watanzania wakija hapa wanasema mkopo bado unabebeka. Haya ni mambo siyo suala tuje tushangiliane hapa. Bado nam- challenge Mheshimiwa Mpango yeye ndiye dira ya nchi yetu. Hii mamlaka inatoka wapi ya kwamba wanaleta mipango ambayo haipo kwenye mipango ya miaka mitano? Haya ndiyo yanayotuchanganya, yanatuchanganya kama Taifa hatuelewi tushike lipi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, yote yaliyofanyika, sasa hivi nimezungumza hapo mwanzo kwamba, tumefika mahali tuna-centralize kila kitu ambapo hayo mambo yalishindikana hapo mwanzoni, sasa hivi halmashauri zote tumezi-ground tunarudi kule kule ambako tulishindwa. Ilitumika pesa nyingi sana kuunda Serikali za Mitaa, kuzi-empower Serikali za Mitaa tulitumia pesa nyingi sana hizi D by D leo tena tumerudi kule kule kitu kinafanyika Dar es Salaam, kila kitu wanataka kifanyike sijui Dodoma ambako tumezi-ground Halmashauri.

Mheshimiwa Spika, hii mipango inekuwa ina-empower watu wa kule chini inge-empower watu wa chini waone kama wana-own, wame-complicate. Naamini na elimu yangu ndogo hii niliyonayo, elimu hai-complicate mambo, elimu ina-simplify mambo, lakini ukiangalia mipango yote tunapiga mapambio mengi kwenye vyombo vya habari. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jana wakati nasoma report hapo nimesikia kwenye report wenzangu walifanya siwa-challenge lakini nilishangaa wanashangaa mtu analipwa milioni 96 (Dola 40,000) tunashangaa mtu analipwa eti Dola 40,000, this is poverty mentality. Yule mtu kwanza ameingia mkataba na wale watu, zile hela siyo za kwetu, akilipwa milioni 96 kwanza atalipa kodi milioni 30 si zitakuja hapa nchini, tuna hasara gani sisi? Kodi milioni 30 zitakuwa hapa nchini, tutawaaminisha Watanzania kwamba mtu akilipwa milioni 40 kama ni laana, that is poverty mentality.

Mheshimiwa Spika, watu wangelipwa hela zaidi ya hizo ilimradi hawavunji sheria, sasa kwa mfano, waki-import expert ambaye huwezi kumpata tena ni wa gharama utamlipa Sh.200,000 tunazolipana lipana hapa? Wachezaji wa mpira wanalipwa hela nyingi kwa sababu ya professionalism walizonazo, sasa tusifike mahali tunakuwa sadist, tunawachukia watu wanapolipwa hela nyingi badala ya ku-encourage watu walio chini walipwe zaidi, sisi tunasema analipwa zaidi, kwa hiyo ashuke chini, are we serious?

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka niseme kwa ujumla, I am Theologian anyway I am not an economist lakini nataka kusema Mheshimiwa Mpango atuongoze, atusaidie.