Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

Hon. Ali Hassan Omar King

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Jang'ombe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii ya kuweza kuchangia hotuba ya bajeti ya Wizara hii ya Katiba na Sheria ili kuweza kuboresha mambo yetu ya kisheria katika nchi yetu ya Tanzania kwa maslahi ya wananchi wetu wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, awali namshukuru Mwenyezi Mungu kwa mara nyingine kutujaalia kufika hapa kuja kuchangia mambo ya Watanzania. Watanzania hawa wana matumaini na sisi sana, kwa hiyo niwaombe Waheshimiwa Wabunge tuchangie kwa mujibu wa mahitaji ya Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tumesikiliza hotuba tofauti hapa, tumemsikia Mhesimiwa Waziri, tumesikia Kamati, tumewasikia na Wapinzani, siku zote sitegemei kwamba kutatoka jambo zuri upande wa Upinzani hata siku moja! Mheshimiwa Waziri angesema hapa kwamba jamani kuna Mungu aliyetuumba mimi naamini wangesema hakuna Mungu aliyetuumba, hicho ndicho kitu ambacho kwao wao ni cha msingi.
Katika hoja ambazo zinajadiliwa hapa, wengi wamejikita katika kuzungumza mahusiano haya katika Muungano, wako wanaosema kwamba Zanzibar ni koloni la Tanganyika, nilikuwa najiuliza huyu aliyesimama akasema yeye ni nyapara? Maana yake na yeye katokea Tanganyika sasa ikiwa kwamba Zanzibar ni koloni la Tanganyika ina maana kwamba yeye huyu ni nyapara. Ametumwa aseme hivyo. (Makofi/kicheko)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo huyu nyapara tunamwambia kwamba huu ni Muungano halali na Muungano unaojulikana, lakini kuna msema husema kwamba nyapara huwa ana nguvu kuliko bwana na hao wanazungumza hivi maksudi kwa sababu nafikiri hawaelewi. Humu ndani tutatofautiana kwa mengi sana, hata tukiulizana uhuru umepatikana lini basi pia tutatofautiana humu kwa sababu tu ya kusema kwamba labda kuna upinzani na utawala, lakini tunachojadili hapa ni maslahi ya wananchi, kwa hiyo tujikite katika kuchangia vitu ambavyo vitafanya maslahi kwa wananchi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna msemi mmoja pale kwetu Jang‘ombe alisema hivi alitumia lugha moja; ―kuendesha siyo lazima kupitia kwenye haja kubwa, inawezekana kuna wengine wanaendesha kwa mdomoni.‖ Kwa hiyo tumewaona hao, kwa sababu leo tukitazama maneno ambayo yamezungumzwa, hiyo ni kuendesha kupitia mdomo au kwa jina la haraka haraka kuharisha. Kwa hiyo, tumepokea na tutamsafisha na atasafishika. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nizungumzie suala la haki za binadamu. Suala hili la haki za binadamu na utawala bora kule kwetu iko Tume ingawa mwanzo ilikuwa Zanzibar, kuna tatizo kidogo lakini ikaja pakarekebishwa. Kwa hiyo, tunachoomba kwa sasa hivi ile Tume ya kule kwetu ifanye kazi vizuri sana, kwa sababu yako mambo ya kuzingatiwa na ni muhimu yafanyiwe kazi kwa haraka kwa sababu tunataka kuimarisha masuala ya haki za binadamu.
Mheshimiwa Spika, Tanzania tujue kwamba tumesaini Mikataba ya Kimataifa, hizo nazo zinahitajika kulindwa, hususan haki za watu ambao wanaishi katika Magereza, zimetajwa, kwa hiyo zifuatiliwe na zifanyiwe uchambuzi watu waweze kupewa haki zao. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kingine ambacho ni cha muhimu sana kukizungumza hapa ni suala la Katiba Mpya. Mheshimiwa Waziri aligusia, amezungumzia katika kurasa za mwanzo kuhusiana na Katiba Mpya na ameeleza kwamba taratibu zimegusa sekta tofauti ikiwemo Tume zetu za Uchaguzi, tunaomba jambo hili lifanywe haraka ili liweze kukamilika.
Mheshimiwa Rais alivyokuja kulihutubia Bunge hapa alizungumza kwamba atamalizia kiporo, kwa hiyo maana ya kiporo ni pale kilipofikia, kinapashwa moto tunamaliza. Nafikiri mchakato ulikwenda vizuri, palipobakia tuje tumalize kwa kuzihusisha Tume zetu hizo ili tuwe na Katiba Mpya.
Mheshimiwa Spika, nizungumzie jambo lingine ambalo limezungumzwa hapa kuhusu vibaraka. Mimi nilishangaa sana kwamba kuna vibaraka kule Zanzibar ambao wameweka Serikali...
MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Spika, Taarifa.
SPIKA: Mheshimiwa, Taarifa
TAARIFA....
MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Spika siipokei, hata ningesema kuna Mungu, yule angesema hakuna. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naendelea. Alizungumzia habari ya vibaraka na akataja pande mbili kana kwamba hazina mahusiano kwamba je, tungewauliza na wao hawa ambao wamekuwa wana ndoa hii ya mkeka hii ambayo siyo rasmi watu wote wanaijua je, yeye anakuwa kama nani wakati anayasemea haya? Kwa sababu hata na yeye huyu mimi simkumbuki kama labda ametokea katika Majimbo ya kule kwetu sijui atakuwa ni nani, lakini ndiyo wale niliosema kwamba nyapara siku zote huwa ana nguvu kuliko bwana. Amejaribu kulinganisha uhusiano, anakubali Mwafrika wa Tanzania kwamba ukoloni ulikuwa bora kuliko uhuru, huyu mtu sijui tumuite mtu wa aina gani? Lakini siku zote ukitaka kumjua mtu ambaye amezoea kulamba makombo ya sahani ya bwana siku zote atakuwa yuko chini yake. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo hawa ni watu ambao wamezoea kulamba makombo ya sahani ya bwana, watakumbuka tu kwamba wao wanahitaji kulamba. Hakubali uhuru, mimi nashangaa sana tunamwita mtu kwamba utakuja kuwawakilisha wapinzani, unakuja kutoa hoja kama hizi, kwamba uhuru siyo bora kuliko ukoloni. Unauponda uhuru ambao umepatikana umerudi kwa watu wengi, Waafrika wenyewe una-support kwamba bora usingepatikana wewe ni mtu wa aina gani, kwa kutaja nukuu nyingi, kutaja nukuu nyingi siyo kujua, ni kwenda kusoma hata magazeti ukaja ukanukuu hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo hicho tunajaribu kusema kwamba wajaribu kukiangalia na wakitathmini, upinzani siyo wa aina hiyo hapa tupo kwa ajili ya wananchi, tumeingia humu kwa sababu ya uhuru na tumo humu tunajadili kwa sababu ya uhuru. Uhuru na Muungano ndiyo uliotuleta hapa, utakapozungumza kinyume na hivi Watanzania watakushangaa, hawahitaji haya, ndiyo maana mnapokosa televisheni huumwa ninyi. Product kama hii ingerushwa kule kwenye televisheni watu wangeonaje kitu kama hicho? tujaribuni kufanya kwa ajili ya Watanzania wote. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ningelipenda kuchangia, tunajua kwamba zipo Tume, Haki za Binadamu, Tanzania tuna mahusiano ya Kimataifa, pia kuna masuala mengine ya kupata fedha pengine za kutoka nje katika kuhuisha masuala haya ya haki za binadamu. Tujaribu katika fedha zetu za maendeleo tuwe japo kidogo tunazipata ziwe zinatokana na sisi wenyewe, kuliko zaidi kutegemea kutoka kwa wafadhili. Bila ya hivyo tutakuja kujikuta kwamba wakati mwingine tunaweza tukaja tukakwama katika utekelezaji wa masuala ambayo tumejipangia wenyewe.
Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ni muhimu, tumo humu katika Bunge kama chombo cha kutunga sheria, basi tujaribu tukubali ukweli kwamba Watanzania wanatutegemea na wanatukubali na ndiyo maana wametuchagua kwa hiyo tusiendeleze mambo ambayo yanaweza yakatuletea mfarakano ambao utakuwa hauna maana...
SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa.
MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri.