Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Hon. Marwa Ryoba Chacha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI anisikilize kwa makini maana Jumatatu nitaondoka na shilingi yake. Mheshimiwa Waziri wa Afya alinipa barua inayoonesha Kituo cha Iramba, Kijiji cha Nyagasense, Kata ya Kenyamonta inapata milioni mia saba; na Waziri wa Afya alituma wataalam wakaenda kule wakahamasisha wananchi wakachangia viashiria wakapeleka mchanga wanasubiria milioni mia saba. Mpaka leo TAMISEMI wamepindua milioni mia saba wamepeleka kwenye jimbo lingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Kenyamonta walimpa Mheshimiwa Magufuli kura, wanataka kutwambia 2020 wasimpe, si ndiyo? Kwa hiyo, nataka majibu Jumatatu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, mwaka jana Mheshimiwa Jafo ulikuja Serengeti tukampeleka Hospitali yetu ya Wilaya ya Serengeti tunayojenga kwa nguvu za wananchi na wadau mbalimbali na tumemaliza wing ya kwanza; akatuahidi na akaniahidi tutapata milioni mia saba, lakini hatukupata. Mwaka huu tena sijaona chochote ingawa ameniahidi kwamba ameweka vizuri na kwamba tutapata milioni mia tano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, amekuja pale Mheshimiwa Waziri, tumempeleka kwenye ile hospitali na ameona jitihada zetu. Amekuja Mheshimiwa Makamu wa Rais tumempeleka pale akaahidi kutusaidia; juzi tumempeleka Mheshimiwa Waziri Mkuu, sijaona chochote. Hebu naomba Mheshimiwa Waziri aseme kwamba katika Hospitali ya Wilaya ya Serengeti ambayo itahudumia mpaka watalii hawaoni sababu ya kutenga chochote kwa ajili ya wilaya ile? Kwa hiyo, nataka majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niingie kwenye elimu, naomba niongelee elimu bure. Serikali ya CCM sasa hivi kila mtu akisimama anasifia elimu bure. Wametenga na wanapeleka shilingi bilioni mia moja sabini na mbili kwenye elimu. Ukienda kuna matatizo chungu nzima kwenye shule zetu za msingi, watoto kwenye darasa moja wamerundikana, hakuna madarasa ya kutosha. Tuna upungufu nchi nzima wa madarasa laki 264,594.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya vyumba vya madarasa ni mbaya. Kwa nini wasingetumia pesa hizi kujenga madarasa? Ukienda kwenye shule zetu hali ya elimu ni mbaya, hakuna Walimu, wameamua kutoa Walimu wa sekondari wanawapeleka katika shule za msingi, kweli wataweza ku-deliver? Wata-deliver nini? Watafundisha nini? Hali ya Walimu ni mbaya na ukienda kwenye hali ya Walimu wa sayansi ni tatizo kweli kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba tumpigie makofi Mheshimiwa Kikwete, alifanya kazi kubwa sana. Mimi ni mojawapo ya matunda ya Mheshimiwa Kikwete, nilienda crush program baada ya kumaliza form six, nikasoma mwezi mmoja nikaenda kufundisha. Baada ya miaka miwili nikaenda chuo kikuu nikafanya Bachelor of Science and education nikamaliza nikaenda kufundisha, nilikuwa nafanya vizuri na nina wanafunzi wangu sasa hivi ni madaktari; nilifanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kikwete alikuwa very creative kwenye suala la ualimu; ndipo Mheshimiwa Kikwete alipoona kwamba kuna tatizo la Walimu wa sayansi akaanzisha program maalum chuo kikuu cha UDOM ili kukabiliana na tatizo la Walimu wa sayansi. Serikali ya CCM; yuko hapa ndugu yangu Mwalimu wangu Mheshimiwa Ndalichako, hivi kweli wanawapenda watoto wa nchi hii?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekondari ukienda hakuna Walimu wa hesabu hakuna wa fizikia, hakuna wa kemia, hali ni mbaya, are you serious, mko serious kweli? Mimi ni
Mwalimu, wakati wa likizo nakwenda kufundisha kule, hali ni mbaya. Wanasema Serikali ya viwanda wanatoa wapi Walimu? Lazima muwe na special program kwa ajili ya Walimu wa sayansi, lazima watengeneze incentives za kuwavutia wanafunzi kusoma sayansi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hata ukiwa Mwalimu wa sayansi haina maana, ndiyo maana hata mimi niliondoka huko, mimi ni Mwalimu wa kemia na baiolojia. Yaani Mwalimu wa sayansi ukienda kwenye shule za sekondari, Mwalimu kwa mfano wa kemia ni Mwalimu mmoja, labda kemia na baiolojia; unafundisha kuanzia form one mpaka form four, wanafunzi karibu 2,000, wewe mwenyewe, hakuna incentives yoyote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, akina Mheshimiwa Jafo washauri Mheshimiwa Rais aje na special program kwa ajili ya sayansi. Ndugu zangu tunawashauri bure mkiona ni la muhimu chukueni mkiona halina maana... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)