Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hon. Haji Khatib Kai

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Micheweni

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. HAJI KHATIB KAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na ardhi, kwa kuniamsha salama siku ya leo na kuweza kutoa mchango wangu wa maandishi, vilevile nimtakie rehema kipenzi cha Allah Mtume Muhammad (S.A.W).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu E.T.D Passport; kwa muda mrefu Serikali ilikuwa ikiwawezesha Watanzania kusafiri kupitia Idara ya Uhamiaji kusafiri nchi jirani na zisizokuwa jirani kwa kutumia ETD- Passport kwa muda wa mwaka mmoja, lakini kwa bahati mbaya sana sasa hivi Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji imebadilisha utaratibu huo na sasa passport ya ETD imekuwa ni Single journey, jambo ambalo linaleta usumbufu mkubwa na manung’uniko makubwa kwa Watanzania ambao hawana uwezo wa kumiliki E-Passport ambayo kwa sasa gharama yake ni 150,000/= tofauti na ile ya zamani ambayo ilikuwa ni 50,000/=.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo haitoshi usumbufu ambao unapatikana ni pale Mtanzania anapotaka kwenda nchi jirani kwa kutumia ETD- Passport na ikawa katika shughuli zake au matembezi yake anahitaji kuyafanya zaidi ya mwezi inakuwa vigumu kupata muda huo haiwezekani
na kwa sababu passport yake imeonesha single journey inakuwa vigumu kupata muda huo na badala yake hupatiwa muda wa wiki moja tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu juu ya hili ni kwamba, ni vema Serikali ikarudisha utaratibu ule wa zamani ili na Watanzania wanyonge waweze kuitumia fursa ya soko la Afrika Mashariki, hasa ukizingatia ETD-Passport kabla ya utaratibu huo ilikuwa inapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000 tu lakini kwa utaratibu huu mpya ni Sh.20,000/=.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu passport ya Afrika Mashariki; Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji ilisimamisha kwa ghafla utoaji wa passport ya Afrika Mashariki bila maelezo yoyote kwa Watanzania, jambo ambalo wapo ambao walikamilisha utaratibu wote wa kupata passport hizo, pamoja na kulipia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kulipia ili kupata passport hizo ili ziweze kuwarahisishia shughuli zao katika nchi za Afrika Mashariki hawakuzipata. Nitamwomba Mheshimiwa Waziri, wakati wa kufanya majumuisho aniambie; je, kuna utaratibu gani kwa Watanzania ambao walikamilisha utaratibu na kulipia na hawakupata passport hizo. Je, kuna utaratibu gani wa kupatiwa huduma ambayo waliilipia?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Police Marine; kumekuwa na operation ambayo inaendelea baharini inayosimamiwa na vyombo vya ulinzi wakiwemo Police Marine. Operation hiyo inahusu uvuvi haramu na ugaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni wavuvi wapatao 54 walikamatwa na meli inayofanya operation hiyo wakitokea bandari ya Shimoni nchini Kenya. Wavuvi hao baada ya kushikwa na meli hiyo waliulizwa ninyi ni nani na mnatoka wapi? Wavuvi walijitambulisha wao ni Watanzania na wanatoka Dago Kenya na walithibitisha kwa kuonesha passport zao. Hata hivyo, pamoja na kuonesha passport waliambiwa watoke kwenye boti ambayo walikuwepo na walipelekwa Tanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo haitoshi, pamoja na kushikwa wavuvi hao katika eneo ambalo ilikuwa ni karibu sana na Pemba waliomba ikiwa wana hatia basi wakabidhiwe kwenye Vyombo vya Ulinzi vya Pemba ili kama ni sheria kuchukua mkondo wake na hasa ukizingatia vyombo vya ulinzi ni Muungano basi wakabidhiwe huko Pemba, lakini walikataliwa na kupelekwa Tanga, ambapo kutoka Tanga na maeneo ya Pemba waliokamatwa ilikuwa ni mbali sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba tena Mheshimiwa Waziri atakapohitimisha aniambie je, kulikuwa na ulazima gani wa wavuvi hao kupelekwa Tanga badala ya Pemba? Mambo kama haya ndiyo ambayo yanaleta manung’uniko yasiyo na sababu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.