Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hon. Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha maelezo yangu binafsi kuhusu hoja iliyopo mbele ya Bunge Tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, takriban mwaka mzima nimekuwa nikiomba Jeshi la Polisi likague Kituo cha Polisi Mlalo ili baada ya kukaguliwa tuweze kupata silaha. Nimejaribu kufuatilia jambo hili kwa muda mrefu lakini Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya na Mkoa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Niombe sasa Wizara, jambo hili lifanyike kwa wakati ili kuimarisha ulinzi na usalama katika eneo letu la Wilaya ya Lushoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Mlalo lenye Tarafa tatu, Kata 18, Vijiji 78 na Vitongoji 600 lina vituo viwili vya Polisi, lakini kwa bahati mbaya vituo hivyo havina silaha. Ni jambo baya sana hasa ikizingatiwa kuwa Jimbo lenyewe liko katika mpaka na nchi jirani ya Kenya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Gereza la Kilimo Mng’aro limechakaa sana kwa sababu limejengwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza. Pia, gereza hili lina upungufu wa wafungwa chini ya ikama. Uwezo wa gereza ni kuweza kuweka wafungwa 100 lakini kwa sasa wafungwa wapo 38 hivyo kulifanya gereza hili kufanya kazi zake chini ya ufanisi hasa ukizingatia ni gereza la kilimo.