Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Charles Muhangwa Kitwanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia bajeti hii. Kwanza nianze tu kwa kusema, kwa kweli bajeti hii ni bajeti iliyotengenezwa, ikapikwa, ikawekwa, ikachujwa na ikatoka kuwa bajeti ya uchumi wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kabla sijaendelea naipongeza Serikali kwa kile inachofanya na Mheshimiwa Mpango pamoja na Naibu wake na wafanyakazi wote katika Wizara nawapongeza sana, bajeti yao ni nzuri kwa Taifa letu. Nianze kwa kutaja tabia za pesa. Tabia za pesa ziko hivi.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa complement hiyo.

Mheshimiwa Spika, tabia ya pesa ziko mbili ya kwanza pesa huwa hazitoshi, pili pesa huwa haiishi utamu. Kwa hivyo, ndugu zangu wa mkono wangu huku wa kulia kila siku wanapokuwa wanalalamika kwamba tuna madeni ni kwa sababu pesa siku zote haitoshi na utamu hauishi. Ni jambo ambalo lazima tujivunie kwamba bajeti hii imelenga katika ule mpango wa 2025, tuwe uchumi wa kati vilevile tuwe na viwanda.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia mapunguzo katika elimu hii ni katika kuhakikisha kwamba tunakuwa na resource inayoitwa human capital. Hawa watu tutakaokuwa tunawahitaji kwenye viwanda vyetu wasiwe ma-expert tuwajenge kutoka hapa, kwa hivyo tunapopunguza katika daftari, tunapopunguza katika vifaa vya elimu tunataka tuwe na wataalam wa kwetu, Watanzania watakaoweza ku-serve katika viwanda vyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa tufanye nini cha ziada, kwanza tuache hizi biashara ndogondogo, naipongeza sana Serikali kwa kile ilichokifanya hasa kwa upande wa simu. Nakumbuka nilipokuwa Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia mwaka 2011 nili- suggest kwamba tuweke mitambo TCRA itakayo- monitor matumizi ya simu ili tuweze kujua kila senti inayotumika je, inalipiwa kodi, tumechukua miaka mingi kidogo.

Mheshimiwa Spika, nikiwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini mwaka 2013 nilipendekeza kufunga flow meter kwenye upakuaji wa mafuta, nikapendekeza vilevile tukawa tumeunda timu ya kuweza kusaidia tuwe na single off-loading point, najua ndani yetu humu ndani wako Wabunge wengine ambao wanafanya biashara za mafuta na wanaipinga sana hiyo single point off-loading, naomba hili tulitilie mkazo sana.

Mheshimiwa Spika, flow meter zifungwe na iwe ni sehemu ya off-loading kwenda kwa wale matenki ya watu siyo pale wanapopokea, kwa sababu wanasema na wanadanganya kwamba kuna evaporation, kuna asilimia kubwa inatokea kwamba mafuta yanapotea, tuhakikishe kwamba tunachukua pesa zetu pale tunapowapelekea hawa wauzaji. Kwa hivyo, mafuta yatakapokuwa yanapakuliwa kutoka kwenye meli yaende sehemu moja, halafu kutoka kwenye sehemu hiyo sasa tunawapelekea hawa sijui OILCOM, MOIL sijui PUMA ndipo wapelekewe na tunapowapelekea tayari tumeshachukua pesa zetu. Nadhani hili litatusaidia sana kuweza kuongeza mapato katika Serikali yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile niiombe Serikali kwa ujumla to work as a team, naomba ndugu zangu wa viwanda na biashara, ndugu zangu wa ardhi na ndugu zangu wengine tuwe na ushirikiano. Mwekezaji anapokuja isichukue siku 40, miezi miwili mpaka anapata kibali cha kuanzisha kiwanda. Inashangaza pale ambapo mwekezaji anataka kutengeneza magari anaacha kuwekeza Tanzania anakwenda anawekeza Rwanda! Wakati ukitaka kupeleka vitendea kazi pamoja na raw material Rwanda ita-incur cost nyingine kuvisafirisha kwenda kule.

Mheshimiwa Spika, nadhani tuliweke incentive sana kwenye madini, incentive hizo tuziweke kwenye viwanda. Halafu niwaambieni kitu kimoja madini resources kubwa iko ardhini kwetu, akishachimba akaitoa haiwezi kurudi, lakini resources kubwa kwenye viwanda ni capital yake atakayoileta na akishajenga kiwanda hawezi kukibeba akakitoa akaenda nacho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hivyo lazima tuwe na mipango na sera ambazo ni za kuvutia zaidi kwa sababu after all hatuko stationary lazima kuwe na mabadiliko, tukimrahisishia akaleta kiwanda hapa, pale ambapo tutaona kwamba upande wetu labda hatukuwa tumefanya vizuri sana, bado we can negotiate, we are negotiating now kwenye madini, lakini tutaendelea kuwa mtu akiwa ameleta kiwanda atakuwa ame-employ watu wetu, atakuwa amelipa tax, hawa watu walikuwa employed na wenyewe watakuwa wamelipa tax kupitia kwenye pay as you earn.

Mheshimiwa Spika, tutumie uzoefu wa sehemu zingine kuweza kuona kwa nini sisi ukiangalia Kenya, ukiangalia Tanzania, Kenya bajeti yao ni 30 billion USD, Tanzania ni 14 billion USD why? Nasi tu wengi na vilevile ni nchi kubwa! Kwa hivyo ni lazima tuhakikishe tunaweka miundombinu inayopendeza au inayovutia ili tuweze kuwashinda wenzetu.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, PPP imezungumziwa sitaki kuirudia, kwa mfano tumezungumzia reli ya kutoka Mtwara kwenda Mbamba Bay sijui muda gani.

Mheshimiwa Spika, labda niseme tu kwamba, tuhakikishe kwamba hiyo reli inavutia, uzoefu aliousema Spika umenikutanisha na watu wengi sana. Pale ambapo tutahitaji kusaidiana maana yake Mtanzania lazima ui-serve nchi yako kutokea mahali popote. Mimi nina watu wa kutosha zile contacts zangu nikiwa Bank of Tanzania bado ninazo na naweza nikawapa watu wapo wengi tu wanaotaka kuwekeza hasa kwenye reli hiyo na maeneo mengine mengi.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Spika, lakini sijasema kitu kimoja tu, naunga mkono hoja asilimia 108. (Makofi)