Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Nishati

Hon. Charles Muhangwa Kitwanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Nishati

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze tu kwa kusema kwamba unapozungumzia Serikali ya viwanda halafu huna umeme ni sawasawa na binadamu anayeishi halafu hakuna hewa. Hilo ni wazi, kwa hivyo niipongeze sana Serikali ya Mheshimiwa Rais John Joseph Pombe Magufuli kwa juhudi wanazozifanya za kuhakikisha kwamba tunajenga Serikali ya viwanda na umeme upo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kikubwa ambacho nitakizungumzia na nitatoa ushauri, kwanza ni namna gani tuwe na umeme wa kutosha. Huu mlolongo wa kusema megawatt 20, megawatt 40 forget about it, zungumzia megawatt 2,000 za Stiegler’s Gorge, sasa hivi tuanze mpango mkakati wa kuweka umeme wa makaa ya mawe megawatt 5,000. Haya mambo tunayoambiwa eti tukienda kwenye makaa ya mawe tutachafua hewa, nenda Marekani, Uingereza umeme wanaotumia percentage kubwa ni upi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, teknolojia imebadilika, tuwe na mpango mkakati wa ku-generate umeme mkubwa wa makaa ya mawe na tutajenga teknolojia inayoweza ku- absorb zile fusion ili zichukue zile fumes zote kusiwe na matatizo. Faida kubwa tutakayopata, wananchi wengi watapata kazi katika maeneo hayo, miji iliyopo karibu na pale itakuwa imeendelea na umeme tutakaokuwa tuna- generate ni wa bei nafuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, duniani umeme wa bei nafuu ni maji na mkaa. Halafu hao Wazungu wanao-generate umeme wa mkaa wanatudanganyadanganya hapa, danganyweni ninyi siyo Kitwanga. Ni lazima tufikirie, tuwe na uwezo wa kujua teknolojia hii tutaipataje lakini kila siku tunalalamika hapa, ninyi mmekuwa watalaam sana kuliko Wazungu ambao wana umeme wa makaa ya mawe miaka nenda rudi na bado wanaishi tu na wana afya nzuri hata wakati mwingine kuliko hata sisi? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jamani lazima mje hapa na mpango mkakati, hatutaki hizi megawatt 200 ama 300, tunataka big. Tumepanda kutoka megawatt 1,450 mpaka 1,517, hilo Mheshimiwa Waziri mdogo wangu usilitaje, hilo siwezi kukusifia nalo. Come with big kama ulivyo big, you are a good person and you are doing wonderful job na hii miradi midogo mingi, it is costing us a lot kui-manage. Yaani una-manage mradi wa megawatt 20, una Afisa Utumishi, Engineer na mambo mengine mengi.

Ninaongea na Mwenyekiti, tatizo kubwa la watu wa huku wanapenda kusifia vinavyofanywa na CCM wao wamelala tu. (Kicheko/ Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi REA kila mtu anasifia lakini nazungumza with this feeling because I love my country. I am ready to die for it and there is nobody can change me on that. Kama ulikuwa hujui kwamba najua Kizungu njoo nikufundishe Kisukuma. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala ambalo lipo hapa kila mtu analisema, ukosefu wa pesa, hivi kwa nini unakosa pesa? Wewe kama ni Waziri wa Fedha halafu unasema hatuna pesa, ondoka hapo. Wewe kama ni Mbunge wa Jimbo fulani wananchi wako wanasema unajua kuna matatizo, ondoka hapo. You are been a human being and you are given that opportunity to save that place, because people trust you and you must think. No thinking, get out of that place. (Makofi/Kicheko/ Vigelegele)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, niwaombe ndugu zangu Wabunge jambo la kwanza ambalo litatufanya tuisaidie nchi yetu ni ku-think and implement. Work hard, be ready to die for what you requested for.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, niwaombe ndugu zangu wa REA, we are here and we have brain. Mkiwa na upungufu wa mawazo tupo. Watanzania lazima tuweze kusaidia mahali popote, tuache kulalamika. Unalalamika kwa nini, hujala? Kula, shiba, fanya kazi. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata mimi asubuhi sikuwa na hela, nimekwenda kufanya kazi nimepata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.