Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Riziki Saidi Lulida

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nikushukuru na nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia na mimi kuchangia katika hoja iliyoko mezani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nataka ni-declare interest kwamba mimi ni Mwenyekiti wa Kupambana na Ujangili na Kusimamia Uhifadhi ndani ya Bunge na Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla alikuwa Katibu wangu katika taasisi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nishukuru nilipata nafasi ya kuizungukia Tanzania nzima katika masuala ya uhifadhi na kuangalia mwenendo wa ujangili Tanzania, kwa kweli nimejifunza mengi. Niliomba katika Bunge lililopita, Wabunge walishiriki kuzunguka kutembelea Selou, akiwemo Mheshimiwa Keissy, Mheshimiwa Susan Kiwanga, waliyoyaona na yanayozungumzwa Bungeni mengine mengi ni ya uzushi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitazungumzia masuala ambayo mimi nimeyaona na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge ni mashahidi na ndiyo maana namuomba Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla, atoe fursa Waheshimiwa Wabunge wazunguke wakaone haya yanayoonekana kuhusu mifugo, masuala ya mipaka watakuja na uelewa tofauti. Kuna wengine watakuwa wanafuata mtu ameongea nini na yeye anafuata mkumbo wa kuongea lakini ukienda kuangalia kiuhalisia mengi yanayozungumzwa utaona si ya ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nishukuru Pato la Taifa katika suala la utalii limeongezeka kwa asilimi 17.6. Huu ni uchumi ambao tunaotegemea na katika maeneo ambayo tunafaidika ni TANAPA na Ngorongoro, upande wa uwindaji mpaka leo pamekuwa na utata. Sasa watu wanaangalia uwindaji lakini mnapata nini, wanyama wanakwisha, wanyama wanatoroshwa, matokeo yake mnatetea uwindaji ambao hauna faida. Inabidi tusimame pamoja tuangalie kandanda ya uwindaji kuna nini? Maana tumewamaliza wanyama Selous, corridors zote zimekuwa intervined binadamu lakini leo ukiangalia katika hunting kuna nini ndani ya hunting, hakuna.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitaka kujua tathmini leo nitakwambia TANAPA wameingiza shilingi bilioni 237 na wamepeleka Serikalini kama ruzuku shilingi bilioni 37 lakini huwezi kupata jibu katika uwindaji. Nitakwambia Ngorongoro walichokipata na walichokipeleka Serikalini, lakini leo utajiuliza TANAPA kwa nguvu zote inazozifanya hapa Serikali imeshindwa kuisaidia TANAPA ili iweze kujiendesha kwa mwaka mzima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mfano, inatoa asilimia 15 kupeleka Serikali, inatoa asilimia 30 TRA lakini akijenga barabara inabidi alipie ushuru, akipeleka umeme analipa ushuru na asilimia 3 inakwenda Kurugenzi ya Utalii lakini wenyewe wanashindwa hata kuzunguka kwenda kufanya promotion na marketing ya TANAPA yao. Huwezi kumuachia mwenzako akutangazie, ni lazima na wao wenyewe waende wakatangaze. Leo mmewafunga mikono, TANAPA hawaendi kutangaza utalii. Niwashukuru kwa kazi waliyoifanya akina Ndugu Kijazi sasa hivi shilingi bilioni 237 zinaingia ndani ya TANAPA na inasaidia kwa ajili ya Watanzania lakini ndani ya uwindaji hakuna kitu. Tusishabikie vitu vingine unaona kabisa vinaukakasi ndani yake, mtanisamehe kwa hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitazungumzia corridor za wanyama. Tanzania kulikuwa na mipaka ya wanyama. Rukwa – Rukwati wanyama wanatoka Zambia wanaingia mpaka Rukwa wanakwenda mpaka Kibaoni. Wanyama wanatoka Nyasa wanaingia Selou wanakwenda mpaka Kaskazini lakini njia zile zote zimevurugwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nailaumu Serikali kwa sababu waliuachia uozo huu. Wananchi wamevamia corridors za wanyama, mnyama atakwenda wapi? Mnyama hana mtu wa kumtetea lazima wapatikane watu wa kuwatetea kama Riziki Said Lulida. Mimi ni mtetezi wa wanyama kwa kujua kuwa tulikua nao, mimi nimezaliwa Selou, tumezaliwa na tembo, walikuwa wanapita katika njia zao, njia mmeziharibu mnategemea nini? Mnategemea wale wanyama watakwenda wapi? Hata tukisema tutakula, je, utalii au vizazi vyetu vitakuwa na uwezo wa kuona wanyama hawa baada ya miaka 100? Tunataka tuwe na sustainable tourism ili watoto wetu katika miaka 100 waje waone kizazi cha tembo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika research iliyofanyika hivi karibuni wamesema kwamba kama Tanzania hatutasimamia wanyama baada ya miaka 100 hakutakuwa na tembo, ile the big five yote itapotea. Ni kweli leo unakwenda Serengeti unamtafuta simba na chui, ni kwa sababu ya binadamu. Binadamu wanaingia ndani ya mbuga wanatafuta vimolo, wanachinja wanyama ilhali wakijua wanyama wale wale watalii wanatoka nchi mbalimbali kuja kuangalia utalii wetu na kwa kweli tumeuboresha umefikia katika mazingira mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema tunatafuta kuongeza kipato. Leo TANAPA wanafanya utalii wa msimu tu, ikifika kipindi cha masika daraja zote zimejaa maji. Ningeomba Serikali itengeneze daraja au iwape mkopo watengeneze Madaraja ya Kilawira, Kogatende, Grumeti na mengineyo ili angalau watalii wawe wanaweza kuja Tanzania mwaka mzima maana kuja kwa msimu tunapoteza tozo nyingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwashukuru watu wa hoteli (TATO), tulileta kelele sana kwa sababu walikuwa hawataki kulipa concession fee. Nimepata taarifa kwamba sasa hivi wanalipa concession fees. Penye haki semeni haki na penye uozo lazima tuwaambie pana uozo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaizungumzia Selou. Selou ina ukubwa wa kilomita za mraba 153,000, Ruaha ina ukubwa wa kilomita za mraba 44,000, Serengeti ina ukubwa wa kilomita za mraba 12,500. Zimeletwa hela za World Bank, narudia tena, nilizungumzia katika hoja ya Waziri Mkuu, zililetwa hela na World Bank kwa ajili ya Selou. Unapozungumzia Selou unaizungumzia Lindi, Mtwara na Ruvuma. Zile hela zimetolewa zimepelekwa upande wa pili, barabara ya kutoka Kilwa kwenda Liwale haipo, huyo mtalii atapitia wapi? Wanasema tunataka kuendeleza utalii Kusini ....
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)