Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo

Hon. Anastazia James Wambura

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo

MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwa maandishi. Kwanza niipongeze kazi nzuri inayofanywa na Waziri, Mheshimiwa Dkt. Tizeba na Naibu wake Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa ya kuiongoza Wizara ya Kilimo kwa umahiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri, Wizara iongeze kasi katika kuhimiza uwezeshaji wa kuzalisha high nutritional value crops kama mboga na matunda kwa ajili ya kuimarisha lishe ya jamii. Viazi lishe vyenye vitamin ‘A’ kwa wingi, mbegu yake inatafutwa na wananchi wengi lakini haipatikani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Wizara iwezeshe uzalishaji wa mbegu za viazi lishe ili iweze kupatikana kwa wingi, wananchi waipande na kutumia viazi hivi ili kuimarisha lishe zao. Inasikitisha na kushangaza kuona mboga mboga kama karoti, nyanya na pilipili hoho zinaingia nchini kutoka nchi jirani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara iielekeze Idara za Mipango Miji katika Halmashauri zetu ili Halmashauri ziweze kutenga maeneo ya kutosha katika miji na vijiji kwa ajili ya urban farming ili wakulima na hasa vikundi vya vijana, waweze kulima mboga na matunda ambayo yatawezesha upatikanaji wa malighafi kwa viwanda vidogo mijini na vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maafisa Ugani wahimizwe kwenda kwa wakulima badala ya kubaki ofisini. Wakatoe elimu ya mbinu za kilimo bora, jinsi ya kupambana na visumbufu vya mazao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.