Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii kuchangia katika hotuba hii ya Waziri wa Kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa scenarios tatu ambazo zinanifanya niwe na mashaka kwamba Wizara hii ya Kilimo itaweza kusaidia kupatikana kwa malighafi za kuingia kwenye viwanda. Najua kwamba Wizara hii inategemea Wizara nyingine ili waweze kufanikiwa, matokeo yake ni kwamba Wizara hii hata ingewezeshwa kiasi gani, kama haya matatizo ambayo nitayazungumzia hapa hayakuangaliwa, sioni itakavyoweza kusaidia kwamba asilimia 65 ya malighafi iingie kwenye viwanda vyake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, wananchi tunajua kwamba sasa hivi miwa imekomaa sana, iko mashambani, lakini inashindikana kupelekwa kwenye viwanda kwa tatizo la kwamba barabara hazipitiki. Kwa maana hiyo, ni kwamba wakati Serikali inajenga viwanda, wakati Serikali inawekeza katika mashamba makubwa ya miwa, Wizara ya Ujenzi haina habari kwamba kunatakiwa kuwe na barabara ya kutoa malighafi mashambani kufika viwandani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi viwanda vya sukari ambapo sukari ingekuwa iko nyingi sasa hivi nchini, haiwezi kutengenezwa kutokana na kwamba miwa hii inaozea shambani sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaiuliza Serikali, kama hakuna jinsi ya kukaa pamoja na kuona tunawezaje kufanya sustainability ya hivi viwanda tunavyotaka kuanzisha, tutafanya nini ili basi tuweze kujikwamua? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuangalie tunapopata ukame. Katika ukurasa wa namba saba, Mheshimiwa Waziri amesema mwaka 2016/2017 kumekuwa na ukame, kwa hiyo uzalishaji ukaanguka. Miaka yote tunazungumzia umwagiliaji, lakini ni wazi kwamba Idara ya Umwagiliaji iko Wizara ya Maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Maji haina mpango wa kuona kwamba je, kuna mashamba gani makubwa ya uzalishaji ambayo yanatakiwa huu umwagiliaji ukafanywe kule? Imekuwa ni wimbo wa Taifa kila mwaka tunazungumzia Kilimo cha Umwagiliaji lakini matokeo yake, Wizara ya Kilimo inafanya vyake, Wizara ya Maji na Umwagiliaji inafanya vyake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukija scenario ya tatu, ni kwamba wakati hali ya hewa inakuwa nzuri, production inakuwa kubwa kama tulivyoona kwenye mahindi na mbaazi, yamevunwa mavuno mengi. Tatizo, hatuna soko, haturuhusiwi kuuza nje. Sasa swali langu ni kwamba kukiwa na mvua nyingi, kuna mafuriko, mazao hayawezi kutoka kwenda viwandani, kukiwa na ukame hakuna maji ya kumwagilia kuweza kuzalisha mazao, kukiwa na hali nzuri wananchi wakazalisha sana hakuna jinsi ya kupata masoko ya kuuza hizi products. Sasa nauliza hivi hapa tunafanya ngonjera, utani au tuko really serious? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napata shida sana kwamba ni lipi bora kwetu? Kwenye mafuriko hatuangalii kwamba siku moja kutakuwa na mafuriko, kwa hiyo, mashamba kama ya miwa yatengenezewe structure ambazo zinaweza kutoa miwa mashambani kwenda kwenye viwanda. Matokeo yake tuko tayari tutoe pesa ya nchi hii ikaingize sukari kutoka nchi za nje kuliko kutengeneza miundombinu yetu. Sasa hapa sustainability na hivyo viwanda tunavijengaje? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, hii Idara ya Umwagiliaji, labda sijasoma vizuri, lakini sijaona mahali ambapo Mheshimiwa Waziri anapendekeza kwamba Idara hii ya Umwagiliaji kwa vile inakwenda kwenye kumwagilia mashamba, ihamishwe kutoka Wizara ya Maji iingie kwenye Wizara hii ya Kilimo ili wanapotengeneza mkakati wa kwamba ni mashamba gani yalimwe, basi ionekane kwamba maji yatakuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii scenario ipo hata kule kwangu Jimbo la Same Mashariki. Tunaweka kiwanda sasa hivi kikubwa cha tangawizi, barabara hakuna, maji hakuna, lakini tuna-invest a lot of money kwa ajili ya kutengeneza hiki kiwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi kweli tutaweza kumsaidia Rais, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli afikie azma yake ya kuifanya nchi hii ya viwanda na uchumi wa kati kama kila Wizara inafanya contrary? Yaani hakuna complementarity, hakuna mawasiliano kwamba priorities ziende huku wakati wa kutengeneza barabara na wakati wa kutengeneza mashamba makubwa ya kumwagilia. Tunafanya kazi kwa compartments, kila mmoja anaangalia kwake na haangalii kwamba kweli huu uchumi tunaufikiaje kama tunataka kufikia uchumi wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niulize, hivi kwa mfano mbaazi, kwa nini tume-rely kwenye soko moja tu la India ?