Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Dr. Immaculate Sware Semesi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Katika Wizara hii maoni yangu yatajikita katika elimu ya msingi na sekondari. Nimeamua ku-concentrate hapa kwa leo kwa sababu hawa ndiyo foundation. Tunasema elimu ni ufunguo wa maisha na hawa ndio foundation yetu, ni msingi wa kile tunachokizalisha katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwa mwaka huu uliopita ni asilimia 60 ya wanafunzi wetu wa elimu ya msingi na sekondari wamefeli. Nita-specify katika kidato cha pili na cha nne kwa mwaka 2017, wanafunzi hawa wamepata division four na division zero. Ni janga wala siyo dogo, lakini Serikali inatakiwa iliangalie sana na kati ya hawa waliobaki asilimia 40 ya waliofaulu 90% wametoka katika shule binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna changamoto kadhaa za wamiliki wa hizi shule binafsi wanakuwa wanakandamizwa na Serikali. Mifano miwili kutoka kwa wanafunzi wale wanafunzi wanaosoma katika hizi shule binafsi hawana ruhusa au hawawezi kwenda kusoma shule za government kama kukatokea tatizo lolote. Pia hawa wanafunzi wanaosoma shule binafsi hawapati mikopo kwa ajili ya kupata access ya elimu ya juu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika shule binafsi ambazo sasa zinatuokoa katika elimu zetu za msingi na sekondari, wana maeneo ambayo yanawakandamiza. Moja kati ya hayo wanasema kwamba wanalipishwa service levy na Halmashauri husika. Wanalipishwaje service levy wakati hawa tayari wanatoa service ya elimu? Naomba muwaangalie kwa jicho la kitofauti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo shule binafsi wanakandamizwa sana ni kwenye malipo ya property tax, wanalipa viwango sawa kama vile ni kumbi au ni hoteli wakati hawa ni watoa huduma wa elimu. Kwa hiyo, kama kuna umuhimu wa kulipia property tax basi wawe kwenye certain criteria/category ya kuangalia hawa ni watoa huduma lakini siyo wafanyabiashara wa moja kwa moja kulipisha madarasa au kumbi za shule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mawazo mengi mbadala yametolewa na Kamati husika imetoa maoni mazuri sana naomba yazingatiwe. Moja kati ya hayo ni kujifunza kwa nini shule binafsi zinafanya vizuri ukilinganisha na shule hizi za Serikali. Majibu yapo pale, walimu na wanafunzi wanakuwa treated vipi na miundombinu inakuwa treated vipi. Huitaji rocket science kusema kwamba kwa nini tunafeli kwa sababu mazingira ni hafifu katika shule zetu za Serikali. Naomba tujifunze kutoka private sector na tusiwa-treat kama competitors bali tuwa-treat kama ni partners, ni wadau ambao wanaliokoa Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapoongelea maendeleo pia yanakuwa reflected kwenye bajeti ambazo tunazi-set aside kwa ajili ya maendeleo. Umuhimu wa elimu wala hauhitaji mjadala, kwa mfano ukienda kwenye subvote 2001, kwenye Basic Education Office, item ya 4321, Primary Education Development Programme LANES, mwaka 2016/2017 mliwatengea shilingi bilioni 65, mwaka 2017/2018 mliwatengea shilingi bilioni 39 na 2018/2019 mmewatengea shilingi bilioni nne tu. Sasa tujiulize lengo hapa la Serikali ni nini? Tayari tunafanya vibaya sana, hamuoni kama hii ni alert inabidi tujibadilishe. Tayari kuna tatizo, lakini hatuweki nguvu ambayo inakuwa reflected kwenye bajeti husika ili kuinua kiwango cha elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto nyingine ambayo imeimbwa sana ni issue ya walimu, kwenye elimu ya hawa wanaoelimisha ambao ni walimu pamoja na idadi yao. Ratio yetu ya sasa hivi mnasema ni uwiano wa 1:50 wakati inayotakiwa ki-standard ni uwiano wa 1:25. Hapo hapo tunasema kwamba baadhi ya walimu wa sekondari wanaenda kufundisha sasa primary school, inakuwaje wakati tayari kuna upungufu wa walimu na bado mnataka tena kuwatoa kwenye level nyingine kuwapeleka kwenye level nyingine ambapo hawa walimu hawajasomea kwa sababu ule ualimu ni taaluma ambayo ina level mbalimbali, aidha, ni wa sekondari, chuo kikuu au nursery. Naomba tuliangalie kwa uangalifu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo linguine ambalo nataka niligusie ni kuhusu continuous assessment. Tunajikita kuwa grade hawa wanafunzi wetu kwa mitihani mikuu labda ni darasa la nne, form two, form four au form six lakini kati ya hawa wanafunzi ambao tunawa-grade ambao tunawapa siku moja au mbili kuwa-assess na kubadilisha maisha yao, tunakuwa hatuwatendei haki na baadhi ya hawa wanafunzi katika…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)