Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Asha Mshimba Jecha

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. ASHA MSHIMBA JECHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia leo kusimama hapa katika Ukumbi wako huu wa Bunge, pia nikushukuru wewe kwa kunipa nafasi ya kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri na kubwa anayoifanya, tunaiona na mwenye macho haambiwi tazama. Pia nimpongeze Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunamwona na yeye anavyoshiriki katika kuleta maendeleo ya Tanzania yetu. Niwapongeze Mheshimiwa Waziri Mkuu, Waziri wa Afya, Naibu Waziri wa Afya pamoja na Watendaji wake wote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnafanya kazi nzuri, Tanzania ni kubwa changamoto haziwezi zikaisha kwa siku moja, Wizara ya Afya ilivyokuwa jana siyo ya leo na tunavyoendelea itazidi kubadilika hatua baada ya hatua, c chapeni kazi Mwenyezi Mungu atawalipa kwa wema wenu mnaoufanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kuchangia kuhusu Bima ya Afya. Tanzania bima ya afya kwa wote inawezekana, Mheshimiwa Waziri naomba tukae na taasisi mbalimbali na vikundi mbalimbali kuona jinsi gani wananchi wanaweza kujiunga na bima ya afya. Wananchi wengi wakiweza kujiunga na Bima ya Afya itaweza kupunguza matatizo mengi ya kiafya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyozungumza Mheshimiwa Azza asubuhi hapa, akasema kwamba sasa hivi inaelekezwa kwenye vikundi mjiweke pamoja, lakini kuna watu hawana vikundi kweli ila pesa wanazo, naamini watu wengi wakijitokeza kujiunga mmoja mmoja Wizara wanaweza mkakaa au taasisi zinaweza zikakaa zikawakusanya ule wingi wa vikundi ambao wanautaka. Kwa hivyo, mwananchi asikose bima ya afya kwa sababu hana kikundi cha kujiunga pamoja na kupata ile fursa ambayo wanavikundi wanaweza wakaipata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusiana na afya ya uzazi, kwa kweli mwanamke anastahili kuenziwa, kutunzwa, kukingwa na unyanyasaji wowote ambao anaweza akaupata, kwa sababu bila ya mwanamke dunia hii isingeweza kuendelea. Kuna matatizo mengi ambayo yanamkumba mwanamke tumeona katika kitabu chako

Mheshimiwa Waziri umezungumzia tezi ya shingo ya kizazi lakini mwanamke wakati huo huo anakumbwa na fistula yote yanamkosesha raha mwanamke. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suluhisho la hili wamesema wanzangumkwamba huduma hii isogezwe karibu na wananchi. Huduma kuifuata Dar es Salaam na sehemu nyingine kwenye hospitali za Kanda wananchi Tanzania hii wanaishi mbali sana na huduma wasipoipata kwa kweli uhai wao uko matatani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ugonjwa huu wa saratani ya mlango wa kizazi siyo tatizo la muda mfupi linachukua muda mrefu linahitaji uwe na hela, kama huna hela huwezi kufuatilia huduma hii na unakuta watu wengine wanashindwa kupata huduma hii, kutokana na ukosefu wa hela. Tunaomba Mheshimiwa Waziri pamoja na juhudi Serikali yetu inayochukua lakini tuzidi kuangalia, kuokoa vifo ambavyo umezungumza humu kwamba asilimia kubwa akinamama wanakufa kutokana na saratani ya shingo ya kizazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie unyanyasaji wa watoto, Mheshimiwa Najma Giga amezungumza, kwa kweli watoto wananyanyasika sana. Mheshimiwa Waziri pamoja na juhudi tuliyochukua tumeridhia maazimio kanuni, matamko, sheria ya kumlinda mtoto bado tunawaona watoto wananyanyasika. Basi katika mikoa yetu tuanzishe sehemu maalum ya watoto hawa kuweza kuwasaidia, unawakuta watoto pamoja na kwamba tunasema wana wazee wao, wanahangaika mitaanim wanazurura mitaani, watoto wale wanasaidiwa saa ngapi, wakiugua wanatibiwa na nani na tunaona saa nyingine mtoto anafika mpaka kwenye vyombo vya habari anatangaza au anatangaziwa kusaidiwa ugonjwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli imefikia mahali katika mikoa yetu kuwe na sehemu ambazo wale watoto kama wameshindwa kutibiwa na wanahitaji kusaidiwa basi usaidizi wao uwe wa karibu, tusiende mpaka kwenye vyombo vya habari kutangaza ugonjwa kwa kweli ile hatumtendei haki yule mtoto ambaye anahitaji tumsaidie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo naomba nichangie katika Wizara hii ni uzazi salama kwa mama. Mheshimiwa Waziri pamoja na jitihada kubwa iliyochukuliwa na Serikali yetu lakini bado tuendelee kuokoa maisha ya mama na mtoto. Akinamama wengi wanapoteza maisha wakati wa kujifungua au wakati wa ujauzito, pengine inawezekana ni lile tatizo la asili la ukosefu wa lishe bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, ipo haja ya kuwatumia Maafisa wa Afya au Maafisa wa Maendeleo ya Jamii kuihamasisha jamii juu ya lishe bora ili wakati wa kujifungua basi akinamama waweze kujifungua salama na kupunguza gharama kubwa ambayo anaweza akaitumia wakati ule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri mimi sina zaidi isipokuwa naendelea kuipongeza Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi. Kwa kweli tumeona maendeleo makubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kumalizia katika kudumisha Muungano wetu, basi siyo vibaya kuwa tuna mashirikiano ya karibu sana na upande wa Zanzibar kwa sababu Wizara ya Afya najua siyo Wizara ya Muungano, lakini magonjwa hayana mipaka na utaalam hauna mipaka, kwa hivyo siyo vibaya kuongeza ushirikiano wetu wa karibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.