Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Saada Salum Mkuya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. SAADA S. MKUYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kupata hii nafasi. Kwanza lazima tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kukupa afya njema na tumekuwa pamoja leo hapa, kwa kweli kama haupo huwa tuna-miss kule kutokukuwepo kwako, kwa hivyo lazima tunamshukuru Mwenyezi Mungu Alhamdulillah rabbil- aalamina, Mwenyezi Mungu aendelee kukupa afya njema.

Mheshimiwa Spika, la pili vile vile nachukua fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, lakini vile vile pamoja Mawaziri Dada yangu Mheshimiwa Jenista Mhagama kwa kazi nzuri ambayo anaifanya na Manaibu wake wanafanya kazi nzuri sana sana na wanahitaji pongezi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sina hoja nyingi, ni chache. Kwanza nashukuru kwamba hotuba yetu hii ya Mheshimiwa Waziri Mkuu imelizingatia vile vile suala la Muungano, lakini kwa uchache wake imeeleza sana ni kwa jinsi gani hizi activity za kutafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali za Muungano wetu. Tunashukuru kwa ku-note hiyo, lakini nadhani itakuwa busara zaidi tukiendelea mbele ku-note vile vile achievement ambazo zimepatikana katika Muungano wetu huu ambao kesho kutwa tu tunatimiza miaka 54. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati wazee wetu walipokuwa wanaunga, Mzee wetu Karume pamoja na Mwalimu Nyerere waliungana wakijua wanaungana na kila mmoja alikuwa anajua wanaungana katika context ipi. Wakati tunaungana Zanzibar ilikuwa ndogo hata leo wakazi wake nadhani kwa takwimu labda tunaweza kuwa tumefika kama milioni moja na laki tano ni kidogo ukilinganisha na wakati huo ilipokuwa Tanganyika hata leo Tanzania zaidi ya watu milioni hamsini, lakini ilikubalika kwa spirit ya kuwa Muungano wetu utakuwa na mutual benefit katika maeneo ambayo tumekubaliana.

Mheshimiwa Spika, sasa pamoja na mambo mengi ambayo yalikuwa yamezungumzwa hapa na nakuomba sana Mheshimiwa Spika, hili ni Bunge ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ikiwa Zanzibar haimo hili haliwezi kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Neno la Jamhuri ama jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatokana na uwepo wa Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, wiki iliyopita kulitoka mijadala mingi sana hapa na mjadala ambao unazungumzwa na anayezungumza ni mwana CCM anavyoi-portray Zanzibar as if Zanzibar hakuna mamlaka. Sasa naomba leo kupitia Bunge lako Tukufu tunaomba hizi statements za kuidogosha statements za kuidhalilisha Zanzibar ziishe. Lazima tu- recognize Zanzibar ina Serikali inayoongozwa na Dkt. Ali Mohamed Shein, Zanzibar kuna chombo cha kutunga sheria ambacho ni Baraza la Wawakilishi, lakini Zanzibar kuna Mahakama.

Mheshimiwa Spika, unapozungumza kwamba Zanzibar ama Kiwanda cha Mahonda ambacho kinazalisha sukari isiingie kwa sababu si sukari inayozalishwa Mahonda nadhani kuna mis-conception kubwa sana hapa. Nitaomba sana Waheshimiwa Wabunge tunaposimama ni lazima tuwe tuna takwimu sahihi.

Mheshimiwa Spika, tunakubaliana theory zote katika dunia hii za uchumi, theory zote zinasisitiza kuhusu masuala ya production, kwa sababu ndiyo yanayojenga long term growth. Sasa vile vile kwa upande wa Zanzibar ilipokuja sera ama ilipokuja hoja ya viwanda; uchumi wa viwanda ni uchumi wa viwanda kwa Tanzania nzima; na Zanzibar nayo ikajitutumua ikasema na sisi tuna kiwanda.

Mheshimiwa Spika, sasa kupitia Bunge lako vile vile naomba Waheshimiwa Mawaziri namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu tunamshukuru kwa ziara yake aliyoifanya, lakini nadhani itakuwa busara zaidi akifanya special visit kwa ajili ya ku-visit kile Kiwanda cha Sukari Mahonda. Hatukatai walanguzi wapo na walanguzi si peke yao wanatoka Zanzibar hao wanaokwepa kodi wako kila sehemu na Alhamdulillah Serikali zote mbili zinajitahidi katika kupambana nao.

Mheshimiwa Spika, nami naungana na Waheshimiwa wenzangu kwamba hawa watu wasiachiwe, lakini ukianza kuitengeneza Zanzibar as if wale ambao wanakwepa kodi, wale ambao wanakuja na majahazi, wale wanaotembea ni kwamba ndio Zanzibar na ndiyo character ya Wazanzibari, nadhani hili siyo sahihi hata kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hizi biashara zipo tunafanya, mimi nadhani katika Muungano wetu hakukuwa na kikwazo hiki cha Inter-trade tunafanya biashara. Kule Zanzibar kuna viwanda vya maji, lakini vile vile vina-compete na viwanda utakuta Kilimanjaro ipo Zanzibar imejaa. Kwa hiyo sisi hatuku- withdraw ipo.

Mheshimiwa Spika, utakuta maji mengi ambayo yanazalishwa Dasani yote yapo na biashara inakwenda, why this so special to sukari? Bidhaa zipo mbalimbali na nadhani statement zinapotoka namna kama hizi, hawa ni watu ambao hawautakii mema huu Muungano wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, huu Muungano wetu tunauhitaji sote, wazee wetu walipoungana wameungana kwa spirit ya umoja, lazima sisi tuwe wamoja. Leo unaposimama ukaizungumza Zanzibar huwezi kusimama ukaizungumza Kenya au Burundi namna kama ile. Unapomzungumza ndugu yako kwa maneno ambayo si ya kweli huwezi hata kumwambia mtu mwingine yuko mbali; hili siyo sahihi wenzangu.

Mheshimiwa Spika, ubaya wa mambo tunaozungumza wengine wengi ni wana CCM ambao hata Zanzibar chama kinachoongoza ni Chama cha Mapinduzi.

Tuna Serikali ambayo inaongozwa na Chama cha Mapinduzi. Sasa unapoongea, sasa hivi nimemsikia kuna Mheshimiwa anasema wafanyabiashara kwa sababu ya sheria kali wamehamia Zanzibar, do you know Zanzibar?

Mheshimiwa Spika, tukizungumza Zanzibar maana yake ni kwamba sisi Waheshimiwa tumekwenda asubuhi jioni tumerudi. Kuna sheria zake, sheria zipo na Serikali inajitahidi, changamoto hazikosi na ziko kila sehemu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Bunge lililopita tumeambiwa, kuna Mheshimiwa alisimama hapa anasema Zanzibar haijawahi kukamata hata kilo moja ya Cocaine, lilizungumzwa ndani ya Bunge hili. Ukiniambia hivyo unadharau mamlaka, unadharau Serikali, unadharau jitihada ambazo zinafanyika. Hawa watu kila siku wanakamatwa na hizi juhudi zinafanyika katika pande mbili zote.

Mheshimiwa Spika, tumeambiwa Mawaziri wanakutana, Mawaziri hawa wanazungumza na wanakuwa wana jitihada zao wenyewe wanazungumza. Sawa changamoto zinatokea tunakubali, lakini si katika context hii ambayo inazungumzwa, lazima tuheshimu.

Mheshimiwa Spika, trust me, Zanzibar ikiwa inazungumzwa kiasi kama hiki sisi Wabunge ambao tunatoka Zanzibar tunajiona humu ndani kama second class MP’s which is not fair. Sisi ni Wabunge kama Wabunge wengine, unapoizungumza Zanzibar na sisi tunapata uchungu kwa sababu kinachozungumzwa si sahihi.

Mheshimiwa Spika, tunawaomba haya mambo ya kukaa ukaanza kudharau mamlaka nyingine ambayo zimo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaomba sana, tunapata tabu sana kule nyumbani, wanatushangaa sana wenzetu, what are you doing there? Kwa sababu kinachozungumzwa kinakuwa hakina fact.

Mheshimiwa Spika, tunaomba jamani tuheshimiane, tuwe vizuri kwa sababu tuna spirit moja katika chombo cha dola ambacho tunakutana na tuna-converge hasa kwenye context ya Muungano ni Bunge lako la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunakuwa wamoja sote tunasimama kwa pamoja tofauti zetu za kiitikadi zipo, lakini when it comes to United Republic of Tanzania hiki ndicho chombo ambacho kina-portrait.

Mheshimiwa Spika, sasa…

T A A R I F A . . .

MHE. SAADA S. MKUYA: Mheshimiwa Spika, namheshimu sana ndugu yangu, nilichokizungumza hapa kilichokuwa kimezungumzwa Bunge lililopita Zanzibar hakujawahi kukamatwa hata kilo moja ya unga. Kwa hivyo ninapozungumza vilevile awe ananisikiliza vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, context hii ya ujenzi wa viwanda inasaidia sana katika ujenzi …

T A A R I F A . . .

HE. SAADA S. MKUYA: Mheshimiwa Spika, naipokea.
(Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa pamoja na hayo hizi ni katika changamoto za maendeleo ya nchi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. SAADA S. MKUYA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.